-
ISSN 0856 - 3861 Na. 1137 SHAWWAL, IJUMAA , AGOSTI 8-14, 2014
BEI TShs 500/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz
Mapinduzi Daima hayana maana ikiwa hatuna Zbar
Mansour aonja Sunna ya Dunni, MaalimPole mpiganaji. Jussa
ahimiza utulivu, amani
MANSOUR Yussuf Himid. ISMAIL Jussa.
Tunahitaji afya, uwezo na nafasi kutekeleza nguzo ya Hijja.
Rasilimali hizi Ametupa Allah tuzitumie Anavyotaka Yeye. Hakuna
mwenye uhakika wa kufi ka mwakani. Majuto mjukuu, unangoja nini?
Usimwendekeze shetani (iblis). Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa
mipango mizuri na huduma bora. Gharama zote ni Dola 4,500. Wahi
kulipa uitakase mali yako na uboreshe Hijja yako. Tafadhali
wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0655/0765/0682/0777 - 462022;
Zanzibar: 0777468018/0685366141/0657606708.
(13) AFYA, UWEZO, NA NAFASI.
Mujahidina John McCain!Al-Shabab adui, lakini ISIS wa Iraq rafi
ki!Sheikh Kilemile, Sheikh Abu Idd, mna kazi
JOHN Sidney McCain.SHEIKH Mohamed Idd.
Uk. 4Kazi iliyokuwa ikifanywa na Israel Gaza - kuua watoto - Uk.
9
Semina ya Kimataifa kufanyika Chuo Kikuu cha Waislamu Moro
Rais Shein, Bilal, wageni rasmiKujadili Epistemolojia ya
KiislamWasomi wa Kimataifa kushirikiPROF. Hamza Njozi.
-
2 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14,
2014AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148,
0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]
zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
WA I S L A M U W i l a ya n i K i b a b a , w a m e t a k i w a
kujishajihisha katika kutoa michango, sadaka na zaka ili
kuharakisha mipango yao ya kimaendeleo chini ya kituo chao cha
Darul Arqam Leaning Centre.
Wito huo umeto lewa na Mudir wa kituo hicho, Muhamed Tundia,
wakati akitoa ripoti kwa Waislamu juu ya maendeleo na mipango
pamoja na mikakati yao katika sherehe za Idd hivi karibuni.
A l i s e m a , Wa i s l a m u wanapaswa kutambua kuwa chanzo
kikubwa cha uchumi katika Uislamu ni sadaka na zaka pamoja na
kujitoa kikamilifu kwa nafsi zao na mali zao na kwamba, kufanya
hivyo watapiga hatua kwa haraka.
C h a n g a m o t o k u b wa kwetu katika kukamilisha mipango
yetu ni uchumi, kwani kuna ugumu katika upatikanaji wa fedha
kufikia malengo, hata hivyo lazima m u e l e we k u wa c h a n z o
kikubwa cha uchumi katika Uislamu ni sadaka na zaka. Alisema Mudir
Tundia.
Alisema maendeleo yote yanayopangwa, utekelezaji wake
unategemeana na
Waislamu Kibaha wajipanga kwa maendeleo ya kijamii
Walaani unyama wa Israel huko GazaNa Bakari Mwakangwale
Waislamu wenyewe jinsi wa t a k a v y o a m u a k u t o a kwa
wingi na kwa wakati ili mambo yaende haraka n a k w a m b a , v i o
n g o z i wanatakiwa kuonyesha uadilifu kwa kusimamia k u h a k i k
i s h a Wa i s l a m u wanafika pale walipokusudia.
Akizungumzia maendeleo ya eneo lao la ardhi la Mwanalugali,
Mudir Tundia a l i sema kwamba sua la hilo lilishafikishwa katika
Halimashauri ya Mji (Kibaha)
kwa lengo la kupata vibali ili liweze kufanywa kituo cha
elimu.
A l i s e m a e n e o h i l o l i m e s h a p i m w a n a
Halmashauri ya Mji huo na kwamba hivi sasa linaitwa Boko Timiza
(Block D, No. 103), na wapo mbioni kupata hati miliki na
kukamilisha masuala ya RITA.
Aliongeza kuwa ardhi waliyonayo, wameipata kupitia nguvu za
Waislamu
Mudir wa kituo Darul Arqam Leaning Centre, Muhamed Tundia.
SIKU chache kabla ya kurejea vikao vya Bunge Maalum la Katiba
mjini Dodoma, gumzo kubwa kwa Watanzania lilikuwa juu ya hatima ya
Bunge hilo, kufuatia mpasuko m k u b w a u l i o t o k e a miongoni
mwa wajumbe wa Bunge hilo, uliotokea k a t i k a m k u t a n o wa
kwanza wa Bunge hilo kabla ya kuahirishwa kupisha vikao vya Bunge
la Bajeti.
Mpasuko uliotokana na hitilafu katika kujadili rasimu hususana
katika kifungu kilichozungumzia muundo wa serikali katika m u u n g
a n o , a m b a p o wabunge wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya
Watanzania wanaunga m a p e n d e k e z o y a muundo uliopendekezwa
katika katiba ambao ni serikali tatu, yaani ya Zanzibar, Tanganyika
na ya Muungano. Lile la Wabunge wa CCM na washirika wao wanaojiita
Ta n z a n i a K w a n z a , wakipinga mapendekezo katika eneo
hilo, wakitaka muundo wa serikali mbili ubakie kama ulivyo katika
katiba ya sasa.
Kwa kifupi pamoja na mambo mengine, jambo hili la kihitilafiana
katika muundo wa serikali katika muungano, ndio chimbuko la baadhi
ya wajumbe kususia vikao vya Bunge hilo.
Wakat i Bunge h i lo likirejea vikao vyake Agosti 5, wajumbe wa
Upande wa UKAWA wameendelea kusimamia msimao wao wa kutoshiriki
katika vikao vya Bunge hilo, hadi pale pendekezo muhimu la muundo
wa serikali katika rasimu litakapoachwa kwa ajili ya kujadiliwa ili
kuboresha na sikubadilisha kipengele hicho cha rasimu na kukifanya
cha serikali mbili, kipengele ambacho kimeonekana kuwa msingi
muhimu zaidi wa rasimu hiyo.
Hata hivyo, wakati siasa za nchi hivi sasa zikitawaliwa na
mijadala ya Rasimu ya Katiba Mpya, tayari yameibuka matukio mengine
ambayo k wa m t a z a m o we t u , yanaonekana kuwa na
Kesi ya Mansour, Sheikh Hadkuhamisha agenda ya Katiba?
athari kwa kiasi fulani katika uga wa kisiasa nchini.
Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa gumzo kubwa kwa Watanzania
kipindi hiki, ni kuhusu hatma ya hiyo Katiba Mpya inayojadiliwa
huku kukiwa na mivutano na mpasuko mkubwa kati ya wajumbe
wanaowakilisha wananchi na wananchi wenyewe.
Kimsingi tunaweza kusema kwa jinsi hali ilivyo, suala la Katiba
Mpya limeibua mzozo wa kisiasa hapa nchini. Mzozo ambao hai
jafahamika suluhu yake kwa kuwa hakuna hatua zilizochukuliwa n a wa
h u s i k a k u l e t a maafikiano, badala yake, wapo wanaoona bora
liende ilimradi vikao vinaendelea kama ilivyopangwa.
Hata hivyo, wakati kukiwa na mzozo wa kisiasa juu ya rasimu ya
Katiba Mpya, tayari tumeshuhudia yakitokea matukio mengine, ambayo
nayo yana mtizamo wa kisiasa pia.
Tumeshuhudia Waziri wa zamani wa Serikali ya Zanzibar, Mansour
Yusuph Himid, akifikishwa mahakamani Zanzibar akikabiliwa ma
mashitaka ya kukutwa na bunduki na risasi.
Tunakumbuka kwamba Bw. Mansour alifukuzwa u a n a c h a m a k a
t i k a Chama cha Mapinduzi na kuvuliwa Ubunge kwa kudaiwa kukiuka
taratibu na kanuni za chama.
L a k i n i m u h i m u l i n a l o k u m b u k w a n i k w a m
b a k w a k i a s i kikubwa Bw. Mansour alikuwa akipigia chapuo
kudai serikali kamili ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na muundo wa
Muungano wa serikali tatu, sera ambayo ni kinyume na msimamo wa
CCM
K u s h i t a k i w a B w . Mansour kumezua gumzo na hisia za
kisiasa hususan Zanzibar.
H a l i k a d h a l i k a , kiongozo wa taasisi ya Uamsho na
Mihadhara ya Kiislam Zanzibar, Sheikh Farid Ahmed Hadi na wenzake
19 walikamatwa na kufikishwa kat ika mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu
jijini Dar es
Salaam. wakikabiliwa na tuhuma za ugaidi.
Tunakumbuka namna viongozi wa Jumuia ya Uamsho, walivyokuwa
mstari wa mbele katika kuwahubiria Wanzanzibar juu ya Zanzibar huru
yenye serekali yenye mamlaka k a mi l i . Ama k u h u su M u u n g
a n o U a m s h o walikuwa wakipendekeza k u we p o m u u n d o wa
muungano wa mkataba. Yaani serikali ya Zanzibar, Tanganyika na
Muungano wa mkataba.
Fikra hizi za uamsho z i l i w a i n g i z a k a t i k a m t a f
a r u k u m k u b w a Z a n z i b a r , k i a s i c h a kukabiliwa
mashitaka ya uchochezi na kusweka ndani kule Zanzibar kabla ya
kuachiwa kwa dhamana na kushinda baadhi ya kesi zilizokuwa
zikiwakabili.
Katika kesi ya Safari hii ya akina Sheikh Had kudaiwa kuwaingiza
watu nchini kufanya ugaidi, p a m o j a n a k w a m b a makosa
yanayodaiwa kutenda yalihusu zaidi upande wa Zanzibar, eneo la pili
la Muungano, lakini wameshi takiwa bara ,
bila shaka kwa sheria za Jamhuri ya Muungano.
Mara kadhaa tumezoea kuona panapotokea tukio linagusa idadi
kubwa ya watu na hususan linapoihusisha serikali, kunakuwepo na
dhana ya kuhamisha agenda katika jamii ya Watanzania.
Kwamba linapokuwepo tukio l ina lo t ik i sa na kugusa hisia za
wananchi wengi na likaihusu zaidi serikali, basi inaaminiwa kuwa
huwa kunabuniwa tukio mbadala ambalo l i t a w a s h u g h u l i s
h a wananchi na kusahau kufuatilia hatma ya tukio
lililotangulia.
Tu n a v y o o n a , k w a kuwepo kesi za akina Mansour na
Sheikh Hadi, ambazo zinaridima wakati huu wa kufuatililia hatma ya
muswada wa Katiba Mpya Bungeni huku baadhi ya wajumbe wakishiriki
na wengine wakisusia, kunaweza kuleta dhana hii ya kuhamisha agenda
kama tulivyozoea.
H a t a h i v y o k w a msimamo walio nayo akina Mansour na
Sheikh Hadi
kuhusu masuala haya ya kisiasa, kesi zao zinaweza kuongeza hisia
zaidi juu ya katiba mpya, muungano na Zanzibar huru.
Tunasema hivi kwa mfano, wengi wanahoji i w e j e S h e i k h H
a d i ashitakiwe bara badala ya Zanzibar? Bila shaka watahusisha
mazingira haya na hitilafu za sasa za kisheria katika muungano. Kwa
maana hiyo bado wat aende lea k uweka mawazo juu ya katiba mpya,
ambayo kimsingi w a n a a m i n i i n a w e z a kuondoa hitilafu za
namna hii kama itapita kama ilivyopendekezwa.
Kwa maana nyingine, kesi ya Sheikh Hadi, hasa kwa kushitakiwa
bara badala ya kule anakodaiwa kutenda kosa ambako nako kuna
mahakama huru, k u n a w e z a k u o n g e z a hisia zaidi za
wananchi hasa Zanzibar, kuhitajika z a i d i m u u n g a n o u n a
o p e n d e k e z wa n a rasimu ya Katiba Mpya kuliko kutimia dhana
ya kuhamisha agenda.
Inaendelea Uk. 3
-
3 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014Habari
WAISLAMU wameelezwa kuwa ni wajibu wao kuzihifadhi amali njema
walizozichuma katika ibada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
uliomalizika hivi karibuni.
Wito huo umetolewa na Ustadhi Rashid Mponda, katika hotba yake
ya ibada ya swala ya Ijumaa aliyoitoa wiki iliyopita katika Msikiti
wa Sunni, Kibaha Maili Moja.
Lengo la kufaradhishiwa funga ya Ramadhani limetajwa na Allah (s
w), hivyo kama tumeshanufaika nalo, lililo mbele yetu sasa ni
kuwajibika kuhifadhi amali njema ambazo tumezichuma ndani ya mwezi
wa Ramadhani. Alisema Ust. Mponda.
Alisema vitendo ambavyo Allah (sw) anavipenda ni vile ambavyo
mja anadumu navyo, lakini kinyume chake wapo Waislamu ambao
wamejiwekea utaratibu
I M E E L E Z W A k u w a mmomonyoko wa maadi l i uliokithiri
katika jamii unatokana na watu kushindwa kufuata mwenendo wa
maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Hayo ya mebainishwa na Ustadhi Ally Omari, mapema wiki hii
akizungumzia hali ya mmomonyoko wa maadili katika jamii na mwenendo
wa tabia njema.
Al isema, h iv i sasa jami i inahangaika kila kona kujaribu k u
z u n g u m z i a s u a l a l a mmomonyoko wa maadili na
kulitafutia ufumbuzi wake bila mafanikio.
Mmomonyoko wa maadili unapojitokeza katika jamii ni d a l i l i
z a k u o n ye s h a wa t u w a l i v y o s h i n d w a k u f u a t
a mwenendo wa yale tuliyoelekezwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Alisema Ust.Omari.
Ust.Omari, alisema maasi mara nyingi huwa hayana mwisho mzuri
kwani Mwenyezi Mungu aliweza kuwashushia adhabu watu katika umma
zilizopita kwa kukithirisha maswi.
Al isema, ukiona sehemu ambapo maadili yameporomoka, basi ujue
kuwa hao watu hawana msimamo kwa maana watakuwa wameiweka dini
pembeni na kutumia akili zao ili kuweza kuendesha mwenendo wa
maisha yao.
Ust. Omari alisema, matokeo yake ndio huu mmomonyoko wa maadili
uliokithiri ambao unatafutiwa dawa lakini mpaka sasa hakuna dalili
ya kupatikana kwa dawa hiyo nje ya mafundisho ya Mtume (s a w).
Ili kuikabili hali hii, alisema ni bora jamii ikajikita katika
kuamrishana mema na kukatazana mambo mabaya.
Alisema, tayari Mwenyezi Mungu ameeleza kwamba umma huu unacho
kigezo chema kutoka kwake, lakini umma wenyewe umekuwa ukitafuta
ufumbuzi wa kuondoa mmomonyoko wa maadili nje ya kigezo hicho.
Kwa hiyo pale tunapodai kwamba tunatafuta dawa za maadili mema
nje ya kumfuata Mtume Muhammad hayawezi kupatikana katika sekta
nyingine yoyote bali nusra ni kurejea mafunzo yake kama ambavyo M w
e n y e z i M u n g u a l i v y o amrisha. Alisema Ust. Omari.
Waislamu waaswa wasiitupe RamadhaniNa Bakari Mwakangwale wa
kufanya ibada kwa msimu,
Ramadhani hadi Ramadhani au Idd mpaka Idd.
Ust. Mponda, alisema yule ambaye a l ikuwa akiabudia R a m a d h
a n i , m w e z i h u o umeshamalizika, haupo tena, ama yule ambaye
alikuwa na yakini anamwabudia Allah (s w), basi ajue Mwenyezi Mungu
yupo hai na wala hafi, hivyo hana budi kuendelea na ibada hata
baada ya mwezi wa Ramadhani.
Al isema kuwa Mwenyezi M u n g u a m e e l e z a l e n g o l a k
u f u n g a s wa u m u , p a l e aliposema katika Quran kuwa
amefaradhisha juu yao swaumu, kama walivyofaradhishiwa wale
waliopita kabla yao, ili wapate kuwa wacha Mungu.
Alisema kuwa endapo Muislamu alifunga swaumu, kwa kuzingatia
lengo lake na kufuata vile alivyo elekeza Mtume (saw), kwa hakika
mfungo huo utakuwa umemuacha katika ucha Mungu wa kweli.
Ust. Mponda alisema kwa
muda wa mwezi mmoja uliopita, Waislamu wamekuwa katika wema,
wakisaidiana, wakiongea maneno mazuri, wakitoa sadaka na kusoma
sana Qur an, hivyo akasema matendo hayo ambayo wametekeleza ndani
ya mwezi wa Ramadhani hawana budi kuendelea nayo.
Tuepukane na ile hali ya ibada za msimu na kuacha kufanya ibada
hizo baada ya kukamilika kwa mwezi wa Ramadhani, wanaofanya hivyo
ni sawa na wale ambao Allah anawataja kuwa wanafuata matamanio ya
nafsi zao au wale walioamini kisha wakakufuru, watu wa namna hiyo
watajieleza vipi mbele ya Allah (sw). Alihoji Ust. Mponda.
Ramadhani imetufundisha, imetupa semina na kutudarasisha mambo
mengi kabisa , yale tuliyoyapata sasa tuyafanyie kazi katika miezi
mingine ili Allah akitufisha, tufe tukiwa katika ucha Mungu
tuliokuwa nao ndani ya Ramadhani. Aliasa Ust. Mponda.
Maadili mema yapo katika Dini
Na Bakari Mwakangwale
Waislamu Kibaha wajipanga kwa maendeleo ya kijamiiInatoka Uk.
2na wamekusudia kujenga vituo vya kutoa huduma mbalimbali za
kijamii kama vile zahanati, shule za awali, msingi na sekondari na
masomo ya dini.
Tulichokusudia katika eneo hili ni kujengwa zahanati, shule za
awali, msingi hadi sekondari (O-level, A-level) lakini pia kutakuwa
na shule ya dini kuanzia hatua ya Iptidai hadi Thanawi. Alifafanua
Mudir Tundia.
Mudir huyo alibainisha kuwa milango ipo wazi kwa watu wenye
ujuzi, ushauri na maarifa katika masuala mbalimbali katika
kutekeleza malengo yao, kufika katika ofisi zao kutoa ushari wao
ili kuweza kufikia mipango iliyokusudiwa.
Aidha alisema kuwa Waislamu wa eneo hilo wamekusudia kujenga
Misikiti mine na kwamba, mpaka sasa wameanza na miwili ambayo ipo
katika hatua za awali na baadae wataendelea kujenga Misikiti
mingine kupitia mifuko yao.
Ujenzi wa Misikiti hiyo unatarajia kwenda sambamba na ujenzi wa
madrasa katika kila Msikiti kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vijana
wa Kiislamu katika maeneo husika, ili watoto hao wapate elimu ya
Quran na ile ya awali (nursery).
M u d i r T u n d i a , a l i s e m a zitakapoimarika shule za
awali katika Misikiti yao, watakuwa na fursa nzuri ya kuandaa
vijana wao na kuwaendeleza katika mpango wao wa kituo cha elimu,
pale kitakapokamilika.
Katika hatua nyingine, Mudir huyo alisema Waislamu wanaumia na
kupata uchungu mkubwa kutokana na udhalimu na ukatili wa Israel
dhidi ya Waislamu wa Gaza.
Hali ilivyo ni kwamba watoto wadogo, kina mama na Waislamu kwa
ujumla wanauawa kwa mabomu, unyama huo unafanyika kwa
makusudi huku hata yale mazingatio ya vita yakiwa hayafuatwi.
Alisema Mudir Tundia.
Alisema, Waislamu hawana budi kuungana kuwaombea ndugu zao wa
Gaza, kutokana na kukandamizwa na mikono ya Kizayuni.
Akizungumzia hali ilivyo hivi sasa nchini, alisema Taifa
limeingia katika
fitna, kufuatia matatizo ya mabomu ambayo athari zake zimemkumba
pia Sheikh wa Ansar Muslimu Youth tawi la Arusha na Moshi, Sheikh
Soud, akiwa nyumbani kwake.
Alisema Umma wa Kiislamu unalaani matukio hayo kwa kuwa ni
katika mambo mabaya yasiyokubalika katika Uislamu.
Semina MUMSEMINA ya Kimataifa juu ya epistemolojia (ufahamu) ya
Kiislamu na ukuzaji mitaala, inatarajiwa kuanza kesho katika Chuo
Kikuu cha Waislamu, Morogoro.
Ikiandaliwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu (MUM), na taasisi ya
Kimataifa, The International Institute of Islamic Thought (IIIT),
semina hiyo itawakutanisha wasomi bingwa wa Kiislamu katika Nyanja
mbalimbali katika ngazi ya vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu
ya juu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa n a M U M j a n a , s e m i n
a h i y o itafunguliwa rasmi kesho mchana na Makamo wa Rais,
Mheshimiwa Gharib Bilal na kufungwa siku ya Jumatatu na Rais wa
Zanzibar, Mheshimiwa Ali Mohammed Shein.
Miongoni mwa wazungumzaji wakuu katika semina hiyo wametajwa
kuwa ni Dr. Ahmad Totonji kutoka IIIS, Riyadh, Saudi Arabia,
Profesa Omar Hassan Kasule (Faculty of Medicine, King Fahad Medical
City, Riyadh, KSA), Prof. Shaukat Abdulrazak, Dr. Salisu Shehu,
Prof. Jurnalis Uddin, Dr. Mahmud Adesina, Dr. Nura M.Musa na YB.
Dato Seri Anwar Ibrahim (President of Ke-Adilan Party and former
Deputy
Na Mwandishi Wetu Prime Minister of Malaysia).Wengine ni Prof.
Ahmad Sengendo
(Uganda), Dr. Ismail A. Musa, Dr. Sunus Iguda, Dr. Abuyaasir
Mbwarali Kame, Dr. Aisha Garba, Dr. Oladosu-Uthman Habibat, Dr.
Mariam Hamisi, Dr. Haider Pestamgy na Dr. Afis A.Oladosu.
Wasomi na wazungumazaji hawa wanatoka katika nchi mbalimbali za
Afrika, Asia na Uarabuni, zikiwemo N i g e r i a , U g a n d a , M
s u m b i j i , Zimbabwe, Zambia, Afrika Kusini, Indonesia,
Burundi, Kenya, Saudi Arabia, Malaysia, Sudan Kusini n.k.
Wazungumzaji kutoka ndani ya nchi ni pamoja na Mkuu wa Chuo,
Hajjat Mwatumu Malale, Makamo Mkuu wa Chuo, Prof. Hamza Mustafa
Njozi, Prof. Mwajabu Possi, Prof. Hamisi Dihenga, Mr. Mnyero J.Ibnu
Sheikh Gunda na Prof. Mussa J. Assad ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza
la Chuo, MUM.
Taarifa zaidi zinafahamisha kuwa wakuu wa shule na taasisi za
kielimu za Kiislamu nchini, ni katika jumla ya waalikwa wa semina
hiyo ambapo inatarajiwa kuwa ufahamu watakaotoka nao wataweza
kuboresha program zao za kuelimisha ummah wa Kiislamu.
-
4 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014Makala
M O H A M E D E l B a r a d e i ameandika kitabu chake akikipa
jina The Age of Deception: Nuclear Diplomacy in Treacherous
Times..
Akiwa Mkurugenzi mstaafu wa Tume ya Kimataifa ya Nishati ya
Nyukilia-International Atomic Energy Agency (IAEA), humo anaonesha
jinsi mambo mengi katika siasa za ulimwengu wa leo, zilivyotawaliwa
na udanganyifu, propaganda na watu kupumbazwa wakidhani jambo
fulani lipo hivi, kumbe sivyo kabisa. Mambo yapo kivingine kabisa.
Anatoa mfano jinsi mataifa makubwa yalivyoghushi nyaraka kuonyesha
kuwa Iran inatengeneza silaha za nyukilia ili ipatikane sababu ya
kuiadhibu nchi hiyo.
Waislamu wanapohimizwa kusoma, pamoja na kui jua Elimu ya
Mwongozo na elimu ya mazingira, ni pamoja na kujua s iasa na ul
imwengu unaowazunguka unavyokwenda. Wajue mazingira wanamoishi.
Wajue siasa zake. Wawajue maadui zao pamoja na mbinu zao ili waweze
kuweka mikakati munasibu ya kukabiliana nao.
Ukizungumzia Waislamu kujielewa na kujua mazingira
yanayowazunguka na kuwajua maadui zao, ni pamoja na kufahamu
yanayotendeka hivi leo katika hizi zama za deception na proxy war.
Kwa hakika itakuwa ni ujinga wa kutisha, kuwa hamnazo na
kutokujitambua na kutotambua yanayojiri katika siasa za dunia ya
leo, iwapo Muislamu atadhania kuwa maadhali yeye nia yake ni
kupigana Jihad, basi hata akitumikia proxy war, itakuwa Jihad yake
imesibu na itakuwa ni kwa faida ya Uislamu na atapata fungu lake
kwa Mwenyezi Mungu. Mungu katuletea Mwongozo unaotufundisha pamoja
na mambo mengine kuwajua maadui na mbinu zao. Kisha ametupa akili
na akatuhimiza kuzitumia kwa kukariri mara kwa mara katika Quran,
Hamuoni?, Hamfikiri?, Hamna akili? Kwa nini Mwenyezi Mungu atoe
msisitizo huu?
Yupo msomaji mmoja (0773 526 254) kaja na hoja. Anasema
kuwa:
Wapiganaji wa chini (foot soldiers) wanakuwa ni mujahidina kwa
sababu wako kidhati kuleta sheria za Mungu japo wakuu wao ni agents
(mawakala wa Marekani/makafiri). Ndivyo Uislamu unavyohukumu NIA
yako si malengo ya mabeberu au lengo la agents.
Lakini msomaji huyu huyu (0773 526 254) kaja na hoja nyingine,
kuwa kamanda wa ISIS Ni Khalifah wa Waislamu kwa hiyo anayekataa
kumtii kamanda wa ISIS ni halali kupigwa risasi kwa sababu kakataa
kufuata amri ya khalifah.
Mei 2013, Seneta wa Arizona (Republican) na Veteran wa vita
Mujahidina John McCain!!!Al-Shabab adui, lakini ISIS wa Iraq
rafiki!Sheikh Kilemile, Sheikh Abu Idd, mna kazi
SHEIKH Mohammed Idd.
Na Omar Msangi
ya Vietnam, John Sidney McCain aliingia Syria kupitia mpaka wake
na Uturuki akakutana na wapiganaji wa Kiislamu wakiwemo wale wa Al
Nusrah na ISIS. Na alipokuja kuhojiwa baadae alisema kuwa ni kwa
maslahi ya Marekani kwamba mujahidina ( j ihadists) hao wanasaidiwa
kwa fedha, silaha na mafunzo na kila aina ya msaada kufikia malengo
yao.
B a a d h i ya v y o m b o v ya habari na wachambuzi wa siasa za
Marekani, walishangaa na kuhoji, inakuwaje McCain na kwa maana
hiyo, serikali ya Marekani kushirikiana na jihadists?-watu ambao
kwao ni magaidi?
Kwa kutumia k i s ing iz io cha ugaidi, Marekani ilivamia
Afghanistan na kuuwa mamia ya maelfu ya Mujahidina kwa madai kuwa
serikali ya Kiislamu
inayoongozwa na Taliban, ni ya kigaidi. Marekani ikiitumia na
kuiwezesha Ethiopia, ilivamia Somalia na kuondoa serikali ya
Kiislamu ya Umoja wa Mahakama za Kiislamu kwa kisingizio kuwa ni ya
kigaidi. Marekani imeunga mkono jeshi la Misri kuondoa madarakani
serikali ya Mohammed Morsi kwa madai hayo hayo.
Kama huo ndio msimamo wa serikali ya Marekani, leo inakuwaje
isimame kusaidia ISIS kwa silaha na mafunzo ili isimamishe Khilafah
Iraq na Syria? Al-Shabab adui, lakini Al Nusrah, rafiki!! Taliban
na akina Morsi na Mullah Omar magaidi, lakini Islamic State of Iraq
and Syria (ISIS) na kamanda wake Abu Bakr al-Baghdadi,
rafiki!!!
Kama Muislamu hutazami matukio yote haya akili yako ikatanabahi,
unakuwa nyuma ya mawakala wa mabeberu unasema maadhali nia yako ni
Jihad, nia yako ndiyo itatizamwa, hii iitwe nini?
Suala kuwa ISIS imeanzishwa na inasaidiwa na Marekani, NATO na
Israel zikishirikiana na Saudi Arabia na Qatar, si la paukwa pakawa
(Tazama: Washingtons Hidden Agenda, Americas War on Terrorism zote
zikiandikwa na Profesa Michel Chossudovsky. Tazama pia Daily
Telegraph, June 12, 2014, Londons Daily Express na rejea nyingi tu
zinazungumzia suala hili).
Jambo hili limeandikiwa sana na ushahidi mwingi kutolewa. Aidha,
ni kwa nini inafanyika hivyo, ikaelezwa pia kuwa kinachodaiwa kuwa
ni Jihad ya kusimamisha Khilafah katika Iraq na Syria, hiyo ni
agenda ya muda mrefu yenye malengo kadhaa. Moja ni kuleta machafuko
katika eneo la Mashariki ya Kati ikihusisha Sunni na Shia.
Wakati serikali ya Baghdad yenyewe imewekwa na Marekani na jeshi
lake linaimarishwa na Marekani (US proxy government) itakuwa
ikiuziwa silaha kali kali ili kupigana na ISIS, Islamic State of
Iraq and al-Sham nao wanapewa silaha kutoka huko huko Washington.
Kisha, acha wapigane na kuuwana wenyewe kwa wenyewe.
Machafuko hayo yamepangwa pia kuwa yafikie lengo la kuigawa Iraq
katika vinchi vitatu: A Sunni Islamist Caliphate, an Arab Shia
Republic, and a Republic of Kurdistan.
H i i i t a p e l e k e a k w a n z a urahisi wa kudhibiti na
kuwa na kauli juu ya maeneo yenye mafuta na gesi katika nchi hiyo.
Tunaambiwa kuwa hivi sasa tayari Kurdistan wanapeleka na kuuza
mafuta Marekani na Israel bila kupitia serikali ya Iraq. Na hiyo
imewezeshwa na kazi iliyofanywa na ISIS, japo mpango wenyewe
haujakamilika bado, lakini wenye proxy war yao, wanaanza kuvuna
walichopanda.
Inaendelea Uk. 11
Veteran wa vita ya Vietnam, John Sidney McCain.
MOHAMED ElBaradei.
-
5 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014Habari za
Kimataifa
KAMANDA wa Jeshi la Marekani , Meja Jenerali Harold Greene,
ameuliwa katika kambi ya Q a r g h a n c h i n i Afghanistani.
Imeripotiwa kuwa Jenara l i Greene n i askari wa cheo cha juu
jeshi la Marekani kuuliwa Afghanistan t ang u kuanza kwa operesheni
za kijeshi dhidi ya Taliban nchini Afghanistan na pia akiwa ni
askari wa cheo cha juu kuuliwa tangu vita vya Vietnam.
Habari zinaeleza kuwa Jenerali Greene aliuliwa k a t i k a s h a
m b u l i o lililofanywa na askari wa Afghan katika kambi i n a y o
e n d e s h wa n a Uingereza jirani na mji wa Kabul, wamesema
maofisa wa Marekani.
K w a w a s t a n i askari 15, wawili wa Kiingereza na baadhi wa
Marekani na Ujerumani n a A f g h a n i s t a n wamejheruhiwa
katika shambulio hilo.
Maofisa wamesema a s k a r i h u y o w a Afghanistan alifyatua
risasi katika shambulio hilo, aliuliwa katika tukio hilo.
J e n e r a l i G r e e n e alikuwa Makamu wa Kamanda Mkuu wa
Combined Securi ty Transition Command, a k i h u s i k a k a t i k
a maandalizi ya kuondoka
Jenerali wa jeshi la Marekani auliwa Afghanistan
Meja Jenerali Harold Greene.
vikosi vya ushirika kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Waandishi wa habari w a m e s e m a k u w a shambulio hilo
limeibua m a s h a k a k u h u s u uwezo wa Nato kutoa mafunzo ya
vikosi vya Afghanistan kabla ya vikosi vya Magharibi kuondoka.
Pentagon wameelezea shambul io hi lo la ndani kuwani tishio la
makusudi.
Mtangazaji wa BBC, David Loyn alisema kuwa Wizara ya Ulinzi ya
Ndani ya Afghanistan imethibit isha kuwa askari kadhaa wa kigeni
wali jeruhiwa katika tukio hilo.
T a a r i f a z a i d i zinadai kuwa askari huyo alikuwa askari
aliyepokea mafunzi kwa miaka mitatu iliyopita, kimeeleza chanzo cha
Wizara ya Ulinzi ya Afghan kilipoieleza BBC.
Ulinzi umimarishwa katika hiyo ya kambi ya Qargha, i l iyopo
Magharibi mwa mji wa Kabul baada ya kutokea tukio hilo.
K a m a n d a m m o j a wa Afghanistan katika kikosi kil icho
chini ya kambi ya maofisa wa jeshi la Uingereza, G e n G u l a m S
a k h i , n i m i o n g o n i m wa waliojeruhiwa.
WANAWAKE katika kambi ya wakimbizi iliyopo katikati mwa Jamhuri
ya Afrika ya Kati, wamelalamikia v i t e n d o v y a ukatili wa
kijinsia wanavyofanyiwa na askari wa Umoja wa Afrika nchini
humo.
Mtandao wa habari w a A f r i c a T i m e , umeripoti habari
hiyo ukiwanukuu wanawake hao ka t ika mj i wa Bambari, katikati mwa
nchi hiyo wakilalamikia vitendo hivyo.
I m e d a i w a k u w a
Askari AU watuhumiwa kubaka wanawake A.Kati wasichana katika
kambi hiyo wanakabiliwa na hali mbaya kutokana na vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia na maudhi wa n a y o f a n y i wa n a
askari hao wa kikosi cha kul inda amani cha Umoja wa Afrika
MISCA.
K u f u a t i a h a l i h i y o , w a n a w a k e hao wameitaka
AU kuwalinda kutokana na vitendo hivyo.
Wa s i m a m i z i w a U m o j a w a A f r i k a ambao
wanatazamiwa kuanza shughuli zao
nchini humo mwezi S e p t e m b a m w a k a huu, wameonyesha kus
ik i t i shwa kwao kutokana na hali hiyo.
R i p o t i n y i n g i n e zinawataja wapiganaji wa Kikristo wa
Anti-B a l a k a , k u wa n a o wanafanya vi tendo hivyo vya
kikatili dhidi ya wanawake.
Hivi karibuni Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF)
lilitangaza kuwa wakimbizi wa Kiislamu nchini Jamhuri ya Afrika ya
Kati bado wanakabiliwa na hali mbaya.(irib.iri)
JAMHURI ya Kiislamu ya Iran, imeilalamikia Misri kwa kukataa
kutoa kibali kwa n d e g e z a I r a n zenye misaada ya kibinadamu,
kuingia Misri i l i kuweza kufikishwa misaada Palestina kwa ajili y
a k u w a s a i d i a w a a d h i r i k a w a hujuma za Wazayuni
katika Ukanda wa Gaza.
N a i b u W a z i r i wa Mambo ya Nje wa Iran, Hussein-Amir
Abdullahian,
Misri yadaiwa kuzuia misaada kufika Gazaamesema kuwa ni jambo
lisilostahili kwa Misri kuzuia misaada ya Iran inayojumuisha dawa
na chakula, kwa aj i l i ya watu wanaodhulumiwa huko Gaza.
Bw. Abdullahian, ametoa wi to kwa wahusika nchini Misri kuchukua
hatua za haraka za kutoa kibali kwa ndege hizo za Iran, ziingie
nchini humo ili misaada hiyo iwafikie Wapalestina haraka
iwezekanavyo.
Ameongeza kuwa hivi sasa kuna idadi kubwa ya majeruhi huko Gaza,
wakiwemo watoto na wanawake ambao wanasubiri msaada wa ndege hizo
za Iran, ili waweze kusafirishwa kwa ajili ya kupataka matibabu
katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameelezea matumaini yake
kuwa, Misr i itatekeleza wajibu wake wa kibinadamu, Kiislamu,
kihistoria, na Kiarabu katika kukabiliana na jinai za utawala wa
Kizayuni wa Israel huko Gaza
kwa kufungua kivuko cha mpakani cha Rafah haraka iwezekanavyo, i
l i k u r a h i s i s h a upelekwaji misaada katika eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa Misri ndio nchi pekee ya Kiarabu yenye mpaka wa
pamoja na Ukanda wa Gaza. Hata hivyo watawala wa Misri wamekuwa
wakikataa kufungua mpaka huo hata pale kunapohitajika msaada w a d
h a r u r a k w a wapalestina, ambao w a m e z i n g i r w a n a
kuwekwa kifungoni na Israel.
Hii ina maana kuwa hakuna kinachoingia wala kutoka Palestina
hususan Gaza, bila idhini au ridhaa ya Israel.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo y a N j e w a I r a n M o h a m
m a d J a va d Zar i f , ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuanzisha
kampeni ya kupeleka misaada ya dharura Ukanda wa Gaza.
W a z i r i h u y o a m e ya s e m a h a y o katika mazungumzo
ya simu na mwenzake wa Malaysia, Dato Seri Anifah Aman.
(irib.ir)
-
6 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014Makala
MANSOUR Yussuf Himid, ameungana na wanasiasa wengine wakongwe wa
Zanzibar ambao yaliwakuta walipotofautiana na utawala.
Mansour sasa anasota rumande hadi tarehe 18 Agosti kesi yake
itakapotajwa tena baada ya kunyimwa dhamana.
Mansour ambaye alikuwa Waziri katika SMZ na Mwakilishi wa jimbo
la Kiembe samaki kupitia CCM, alifikishwa katika mahakama ya Mkoa
Vuga, akikabiliwa na tuhuma za makosa matatu ikiwemo kukutwa na
silaha, risasi na marisau.
Mwendesha mashitaka Maulid Ali alidai mbele ya Hakimu K h a m i
s R a m a d h a n i k u wa mtuhumiwa huyo mnamo Agosti 2, mwaka huu
majira ya saa 7.18 huko nyumbani kwake Chukwani nje kidogo ya mji
wa Zanzibar alikutwa na silaha aina ya pistol yenye namba F76172
W.
Ikadaiwa kuwa hiyo ni kwenda kinyume na kifungu cha sheria no
6(3) na 34 (1) (2) cha sheria ya silaha na risasi No 2 ya mwaka
1991 sura ya 223 sheria ya Jamhuri ya Muungno wa Tanzania.
Katika kosa la pili ikadaiwa kuwa Mansour alipatikana na
Pole MansourJussa ahimiza utulivu
Na Mwandishi Wetu
risasi za moto 295 za pistol jambo ambalo pia ni ni kosa
kisheria.
Na kwamba, kosa la tatu ni kupatikana na marisau 112 ya bunduki
aina ya short gurn
(gobore) baada ya marisau 50 aliyotakiwa kuwa nayo kisheria.
Mtuhumiwa Mansour aliyakana makosa yote hayo matatu.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo
Khamis Ramadhani alisema kuwa makosa mawili ya mtuhumiwa yana
dhamana lakini kosa la kukutwa na s i l aha ha l ina dhamana.
Kwa aj i l i hiyo akaamuru m s h i t a k i w a k u r e j e s h w
a rumande hadi Agosti 18 kesi hiyo itakapotajwa tena.
Kufuatia kadhi hiyo, Katibu wa Kamati ya Maridhiano, Ismail
Jussa, amewataka wananchi wa Zanzibar kuwa watulivu wakati suala
hilo linashughulikiwa kisheria na kwa njia za amani.
Nasaha na wito huo wa Jussa umekuja kufuatia minongono na
mazungumzo mitaani miongoni mwa wananchi kuwa yote hayo yanamkuta
Masour kutokana na msimamo wake juu suala la hadhi ya Zanzibar na
muundo wa muungano.
Mansour, ni kat ika wale wanaopigania Zanzibar huru kama nchi
yenye mamlaka kamili, msimamo ambao unaonekana kutofautiana na ule
wa CCM.
K a t i k a s u a l a l a k a t i b a mpya, Mansour yupo na wale
wanaopigania serikali tatu, msimamo ambao ndio pia wa Kamati ya
Maridhiano.
Wengine wanaotajwa kufikwa na majanga baada ya kutofautiana na
msimamo wa Chama Tawala, ni viongozi wa Chama cha Wananchi, CUF,
wakiwemo Maalim Seif Shariff Hamad, Juma Duni Haji na wengineo.
UKOMBOZI wa kweli wa wa n a n c h i u t a a n z a k wa m a b a d
i l i k o m a k u b w a yatayosimamia haki, usawa, ihsani na
uadilifu hususan katika vyombo vya sheria na vile vinavyobeba
dhamana ya usa lama wa ra ia na wananchi wake. Huwezi kuuita
ukombozi ikiwa bado wananchi hawako huru kimawazo, na wanapothubutu
kusema ya moyoni hukuzwa, yakapewa wito maalum wa kuwakomoa.
Siasa za aina hii zimekuwa zikiendeshwa visiwani kwa muda mrefu,
bila ya kutazama athari ya bomu la chuki l ina lokuzwa. Muungano
nao pia na tuseme ukweli, haukuwahi kusimamia haki h a s a k wa wa
n a n c h i wa visiwani wenye maoni tafauti. Nathubutu kwa ushahidi
mkubwa kusema kwamba taasisi ya muungano iliojengwa kwa heshima na
udugu wa Kiafrika, imejidhatiti katika kufitinisha na kuwakingia
kifua pande zinazokwenda kinyume na haki badala ya kusimamia usawa
na heshima ya wote.
Tutazame namna machafuko
Muungano huu pia hausimamii haki za WazanzibariNa Mwandishi
Maalum ya kis iasa yal ikuzwa na
kulindwa na nani kama si taasisi ya muungano inayoonekana kwenda
kinyume na matakwa ya heshima na haki kwa wote na usimamizi
madhubuti uadilifu wa uongozi kwa wananchi na nchi. Haya yameanza
tokea wakati wa Mwalimu, mfano mdogo tu ushahidi uliopo wa namna
Kassim Hanga alivyodhalilishwa hadharani na Mwalimu kwa kuwa tu na
mtazamo kinyume na wengine. Dhambi ya fitna, udhalilishaji, uhasama
wa kukuzwa na kukomoana itaendelea kuwa chanzo cha kuzima maendeleo
ya nchi na uhuru wa kweli wa wananchi. Upande mmoja huwezi kuilaumu
sana taasisi ya m u u n g a n o k wa v i l e muundo wenyewe uliopo
ni wa kimaslahi zaidi. Pande moja ikitegemea ubabe wa muungano
kuwalinda na kuendelea kibri cha kuzima ukuwaji wa haki na usawa,
na mwengine ukifaidika na utulivu wa siasa za msingi wa mabadiliko
wenye asili ya visiwani ambao unaweza kutumika katika induced
effect kwa upande wa bara. Hili naliamini sana kama ndio sababu kuu
ya kusisitiza status quo inabaki kama ilivyo kwa
vile Mwalimu aliweza kwa miaka na dahri kuzima hisia zote za
mabadiliko na kuzipa nguvu za kipekee fikra za Mwenyekiti kiasi ya
kwamba kumpinga ni dhambi. Ukuwaji w o w o t e wa d e m o k r a s i
a vis iwani , au mabadi l iko makubwa ya kimaendeleo visiwani
yatakuwa ni chachu k u b wa ya m u a m k o wa wananchi na
mabadiliko ya utawala.
H a t u t a w e z a a b a d a n kusimamia mageuzi makubwa yenye
tija kwa wananchi bila ya mabadiliko makubwa sana katika vyombo vya
sheria na usalama nchini. Na kipindi hichi cha sasa ndio
kinachozidi kunipa ari ya kuamini hakuna yeyote miongoni mwetu
aliye huru kwa vile tu vyombo vya kusimamia haki, heshima na
uadilifu wa mwananchi bado vimejengwa katika misingi mikuu ya
kikoloni yenye ajenda ya kuzima maoni huru na haki ya kuzungumza
bila ya jitihada za kukomolewa.
Nasikitishwa na wengi ambao wamelibeba hili la kukamatwa kwa
Mansour kama kielelezo cha furaha yao kwa mtu ambae ninaamini
kilichomponza ni kimoja tu: imani yake kwa katiba ya nchi
inayompa
uhuru wa fikra na matamshi. Mazingira yote ya kukamatwa kwake
yana misingi mikubwa ya kuwa mstari wa mbele katika kuhuisha
mabadiliko yanayoweza kutoa afweni kwa wananchi wa pande zote
mbili. Narudia tena kwamba siasa za namna hii zitatumaliza kwa vile
chuki ya vizazi vinavyoona dhulma kwa wazee wao haitamaliza, na kwa
namna ya mgawanyiko wa kiitikadi hususan visiwani, tutaendelea kuwa
katika gurudumu la kukomoana, kutiana ndani na kudhalilishana huku
tukisahau kwamba mwisho wa yote tutasimama mbele ya hakimu wa haki
na kujibu tuhuma za dhulma tunazozitenda.
H a k u n a k a t i y e t u asiyefahamu umuhimu wa sote kuwa
chini ya sheria za nchi, lakini tunapoanza kutafuta sababu za
kuwekana ndani kwa makusudi na kunyimana hata haki ya dhamana kwa
watuhumiwa, basi tutaendelea kuishi katika giza totoro ambalo
halitachaguwa nani atakefuatia katika kadhia ya dhulma. Leo hii
sitashangaa kuona mkono mrefu zaidi wa kukomoana na nongwa za
kijahilia zikishika hatamu kiasi kwamba visasi
Inaendelea Uk. 7
MANSOUR Yussuf Himid akishuka katika gari la Polisi na baadaye
kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.
-
7 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014
UTABIRI wangu katika siku ya sherehe za Muungano tarehe 26
Aprili 2009 kwenye ukumbi wa Taasisi, Zanzibar kwa wajumbe wa
kongamano li l i lokuwa limeandaliwa na Jumuiya ya Uamsho na
kuendeshwa chini ya uwenyekiti wa Muhammad Yussuf, ulikuwa ni huu
na ambao bado naamini ulikuwa sahihi:
Sasa tul ipo, kwa maoni yangu, ni katika hatua ya pili ya
mapinduzi, ambapo mfumo mkongwe wa Muungano usio na maslahi kwa
Zanzibar unaelekea kuporomoka. Kawaida kipindi hichi ni matokeo ya
kupotea kwa uongozi (leadership vacuum) ndani ya kundi la watawala,
a m b a p o m g a w a n y i k o wa makundi humfanya kila mmoja
kutenda vyake. Mara nyingi hatua hi i hai f ikiwi mpaka ajitokeze
kiongozi anayejiona kuwa mwanamageuzi kutaka kuunusuru mfumo
mkongwe; na akafeli. Turgot na Necker walijaribu kuunusuru ufalme
wa Ufaransa kabla ya mwaka 1798 na Stolpyin akafanya jaribio kama
hilo nchini Urusi kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia, lakini wote
walishindwa (Khan & McNiven, 1990).
Huwa ni wakati ambapo, kutokana na mtikisiko wake, mfumo mkongwe
huwa kama tayari umeshakufa kitambo, lakini kwa kuwa watu
wanaothubutu kuyathibi t isha maut i yake hawajatokea, basi
huendelea kuwepo tu ukiendea upepo na kudura ya Mungu. Nabii
Suleiman (A.S) alifariki siku nyingi, lakini watumishi wake
wakaendelea kutumika wakidhani bosi wao amekaa kitini akiwasimamia,
hadi mchwa alipokuja kuila fimbo yake. Kuna watu waliojuwa kuwa
Awamu ya Tatu ya Serikali ya Ufaransa imeshakufa tangu mwaka 1934,
lakini maziko yake yalikuja kufanywa mwaka 1940.
Wazo ninalojaribu kuliwasilisha kwenu hapa ni kwamba, kuna siku
yale yale matakwa ya Wazanzibari, kama yalivyoelezwa kupitia Ripoti
za Tume za Jaji Nyalali na Jaji Kisanga, ndiyo yatakayoiongoza
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wala sio Katiba hizi zilizopo
sasa; na viashiria vya utabiri huo vimeanza kujengeka sasa.
Changamoto iliyo mbele yetu kwa sasa ni ukweli kwamba hatua za
tatu, nne na tano zinakuja kwa kasi na, yumkini, hatuna matayarisho
mazuri kuzikabili. Kwa mfano, hatua ya tatu, ambayo ni ya
kuharibika kwa mahusiano makongwe, kwa mintarafu ya kuharibika kwa
muundo wa sasa wa Muungano, ina matatizo yake. Mojawapo ni kwamba,
wenye maslahi na mahusiano haya hivi sasa, watajitahidi kutumia
nguvu zao za ziada kuzuia yasiharibike. Na ingawa, kutokana na
matakwa ya kiwakati hawataweza kufanya hivyo, lakini kama ilivyo
kawaida
Mapinduzi Daima hayana maana ikiwa hatuna Zanzibar
Mohammed Ghassani
ya mti mkubwa unapoanguka, husababisha maafa kwa pale u n a p o
n g o k e a ( p a n a w e z a kuchimbika shimo kubwa) na kule
unakoangukia (unaweza kuelemea nyumba au wapita njia na kuwajeruhi
kama si kuwatoa roho zao).
Wakati huu ambapo mahusiano makongwe baina ya Syria na Lebanon
yanaharibika, kwa mfano, ni Lebanon ndiyo inayoonekana
kulipia gharama za kipindi hiki kwa wale wanaharakati wake walio
mstari wa mbele katika kusaidia maharibiko hayo, kukabiliwa na
vitendo vya kigaidi vinavyoaminika kusimamiwa na kuongozwa na Syria
ndani ya ardhi ya Lebanon.
Lakini mara tu kipindi hiki kinapoanza, hutanguliwa haraka sana
na kipindi cha ujenzi wa mahusiano mapya. Huu ni
mfano wa ujenzi wa nyumba mpya juu ya kongwe, ambapo mwenye
nyumba huendelea kujenga nyumba mpya, huku yeye akiwemo ndani.
Huvunja kiambaza kimoja kwanza na kusimamisha kipya mahala pa
kilichovunjwa, kabla hajakwenda kat ika kiambaza chengine. Ingawa
huweza kuchukua muda mrefu kwa nyumba kukamilika, kutegemea na
uwezo wa kifedha, kiufundi na mazingira ya ujenzi; lakini ni staili
ya ujenzi ambayo ina faida moja kubwa: hakuna wakati ambapo mwenye
nyumba analazimika kulala nje, hata kama katika kipindi cha ujenzi
huwa hakai katika makaazi mazuri sana.
Hapo ndipo, kwa maoni yangu, nchi hii inapoelekea. Muungano huu
utaingia kwenye kuvunjika na kuundika kwa wakati mmoja, yaani
tunakwenda katika kipindi ambacho hatutasema kuwa hatuna Muungano
moja kwa moja, lakini pia hatutakuwa na Muungano huu.
Mwisho tutaingia kwenye kuimarisha mahusiano mapya
tutakayoyajenga; maana ukweli ni kwamba Zanzibar na Tanganyika,
bali pamoja na mataifa mengine ya karibuni, yataendelea kuwa katika
mahusiano dumu daima. Lakini tafauti na sasa, mahusiano yajayo kwa
sababu ya mapinduzi haya, yatakuwa na sura nyengine na matakwa
mengine.
H a t a h i v y o , t u z i n d u k e Wazanzibari, kwamba jambo
pekee linaloweza kutufikisha hapo ni moja tu, nalo ni mkono mmoja
kuyashikilia Mapinduzi yetu na mwengine kuishikilia Zanzibar yetu.
Yaani isiwe tu Mapinduzi Daima, lakini iwe pia Zanzibar Daima;
maana Mapinduzi Daima hayana maana ikiwa hatuna Zanzibar!
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein
(kulia) akisalimiana na Masheikh visiwani humo.
Makala
Muungano huu pia hausimamii haki za WazanzibariInatoka Uk.
6vitaendelezwa na kupasiana kwa wengine na kuzidisha nuksi
inayoitawala nchi kwa kukosa msimamo wa haki na uadilifu.
N a s i k i t i k a s a n a k w a yanayomkuta Mheshimiwa Mansour
na jinsi gani dhamira mbovu, chuki na hasada imebebwa na baadhi
wakifikiri wanaweza kuzima nuru ya maisha ya mwengine. Si mara ya
kwanza kulalamikia maafa ya sheria tulizorithishwa na wakoloni,
tulianza wakati wa kukamatwa kwa masheikh k wa v i l e t u m a o n
i ya o yaliudhi wengine, na baya zaidi walisekwa ndani kwa muda na
hadi hii leo bado hakuna mashitaka dhidi yao. Ninaamini katika
misingi ya demokrasia pana inayotoa uhuru wa maoni na kuwa na
sheria thabiti inayotumika
kwa uadilifu hata makosa yanapotokea, hushughulikiwa tena kwa
haki na usawa kwa wote.
Sitaki kukata tamaa na kiu ya mabadiliko nyumbani, kwa vile hilo
pekee litasimama kama ishara ya ushindi kwa madhalimu wa ihsani,
haki na uadilifu kwa wananchi. Nina hakika ya faraja kubwa baada ya
dhiki na misukosuko ya aina hii si ya kwanza kwa wapigania
mabadiliko na haki ya kuishi kwa heshima na usawa.
N i n a m u o m b e a d u w a Mheshimiwa Mansour na wengine wote
waliotoswa katika mahabusu huku kwa misingi tu ya kunyima haki zao
za kuishi kwa heshima ya ubinaadamu. Ninawaombea duwa Mungu akupeni
nguvu za kutokubal i kuyumba katika misimamo thabiti ya
haki, heshima na usawa, na kukufanyeni kuwa mashindi wa
mabadiliko tunayoyataka ya uhuru wa kweli kwa wananchi wote. Umma
unayaona yote yanayoendelea kutendwa na umma uko na wale wenye
kusimama na ukweli hata katika kipindi kigumu cha maisha yao.
Natudia tena ni vigumu kuzima ari ya waliojitolea kuhuisha
mabadiliko, na baada ya dhiki ni faraji. Iko siku historia
itawatazama wote mashujaa waliosimama na maoni ya umma kuhuisha
mabadiliko yatayojenga uhuru wa kweli wa wananchi wote.
Niimani yangu pia kuwa kwa hakika mahakama itatenda haki katika
tuhuma zinazomkabili Mansour nikiamini kuwa hicho ni chombo huru
cha kutoa haki.
-
8 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014Makala
Maandamano Washington DC Agosti 2 kuilani Israel kwa unyama wake
GazaMaandamano Washington DC Agosti 2 kuilani Israel kwa unyama
wake Gaza
-
9 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014MakalaEye
on the prize - Free Palestine, John Rees akizungumza mbele ya
ubalozi wa Israel, London, ametoa wito kufanyika maandamano ya
makubwa ya aina yake kesho Jumamosi Agosti 9.
Yakiitwa, National D e m o n s t r a t i o n f o r Gaza,
maandamano hayo yatakayoanza saa sita mchana (12 Noon), yataanzia
BBC Portland Place kuelekea
Hyde Park kupitia mbele ya ubalozi wa Marekani.
Kama msemaji wa taasisi ya Stop the War Coalition, John Rees
anasema, No excuses, hakuna dharura.
Ni lazima kila mtu kushiriki maandamano hayo, i l i kuyafanya
kuwa makubwa kuliko maandamano yoyote yaliyowahi kufanyika
Uingereza.
K a t i k a k u f a n y a taratibu za kuwawezesha watu wengi
kushiriki, watu binafsi na taasisi mbalimbali zimetakiwa kuandaa
taratibu za usafiri kuwatoa watu kutoka kona zote za Uingereza
kuwaleta katika maandamano hayo ya London.
A i d h a , w a t u
Gaza inakuhitaji
Maandamano ya karne keshoHakuna kukosa. Hakuna dharuraFika ukiwa
mzima au mgonjwaFika tulani pamoja ushenzi wa Israel
wametakiwa kusambaza ujumbe na taarifa za m a a n d a m a n o h
a y o k w a w a t u m i j i n i , vijijini, sehemu za kazi,
mashambani, shuleni na vyuoni.
N o e x c u s e s . O n Saturday 9 August we need to fill the
streets of London with a huge outcry at the carnage being
perpetrated by Israel, with the support of David Cameron and his
government.
A n a s e m a R e e s , akimaanisha kuwa hakuna dharura
itakayokubaliwa kwani maandamano ya kesho yanatakiwa kujaza mitaa
ya London kupaza kilio dhidi ya ukatili na ushenzi (Israel's
barbaric onslaught) unaofanywa na Israel, ikiungwa mkono na Waziri
Mkuu, David Cameroon na serikali yake.
Anaongeza akisema kuwa siku 25 zimeshuhudia jeshi la Israel
linalotajwa kushika nafasi ya tano kwa umahiri duniani, likifanya
kazi ya kuchinja raia 1,800 wa Gaza wengi wao wakiwa watoto na
wanawake huku ikiacha majeruhi 9000.
H o s p i t a l i , s h u l e , mitambo ya umeme, na miundo
mbinu mingine imeangamizwa. Watu h a wa n a p a k we n d a , hawana
pa kukimbilia kwa sababu wamefungiwa by Israel and Egypt's inhumane
siege.
Gaza inakuhitaji. Ni kesho Jumamosi Agosti 9. Pamoja na
maandamano y a L o n d o n , m i j i mbalimbali ulimwenguni wa t a
a n d a m a n a p i a (si jui Dar, Mwanza, A r u s h a , Z a n z i
b a r , Tanga???????).
Sema utakuwepo kuungana na wenzako kusema, uhalifu wa Israel
dhidi ya binadamu ukome. Sema utakuwepo kuungana na wenzako
kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza.
-
10 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014
K U H A M A S I S H A m a j e s h i kupigana ndiyo njia pekee i
n a y o w e z a k u t u m i wa n a watawala wa nchi za Waislamu k a
t i k a k u k a b i l i a n a n a maangamizi ya watu wasio na hatia
yanayoendelea kwenye ukanda wa Gaza. Kinyume cha hivyo, ni
kuwasaliti ndugu zetu wa Palestina. Maangamizi makubwa ya raia kama
yale, yanahitaji nguvu za kijeshi kuyakomesha, badala ya vikao,
maandamano na matamko ya kulaani!
Ukisema maneno kama hayo, baadhi ya watu wenye makengeza ya
akili, wanaweza kukuona ni mtu wa vurugu unayeshabikia shari badala
ya kheri. Lakini ukweli siku zote unasimama wenyewe kama ukweli ,
na porojo zinabaki kuwa porojo! Maangamizi ya Wapalestina wasio na
hatia yanayofanywa na majeshi ya Israel kwenye ukanda wa Gaza,
hayawezi kukomeshwa kwa "mazungumzo ya amani", bali nguvu za
kijeshi!
Huwa nawashangaa sana watawala wa nchi za Waislamu,
wakiunganishwa na Jumuiya ya 'Arab League' wanapoishia kulaani tu
maangamizi ya Wapalestina yanayofanywa na Mayahudi bila ya kuchukua
hatua za kijeshi zinazofaa. Watawala hawa wanahisi wametimiza
wajibu wao, kwa kuitaka dunia kukomesha maangamizi ya Wapalestina
yanayofanywa na mayahudi!
Wa i s l a m u u l i m w e n g u n i wanatambua kwamba watawala
h a w a h a w a , w a n a p e l e k a wanajeshi chini ya bendera ya
Umoja wa Mataifa, mahali popote ulimwenguni, kwenye operesheni za
kulinda amani, ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Marekani. Lakini
wanapoambiwa k u w a k o m b o a n d u g u z a o
Waislamu,wanaoangamizwa na
Majeshi yahitajika Gaza siyo porojo!Na Said Rajab makafiri,
wanajitia uzito katika ardhi. Hata Mwenyezi Mungu pia
anawashangaa:"Enyi mlioamini! Mna nini
mnapoambiwa "Nendeni (kupigana) kwa ajili ya dini ya Mwenyezi
Mungu"Mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmekuwa radhi na maisha ya
dunia kuliko ya Akhera"? Qur(9:38).
Ni jambo la wazi kabisa, Qiblah cha watawala hawa wa nchi za
Waislamu, ambazo zina nguvu kubwa za kijeshi, ni Washington na wala
siyo Kaabah. Na nyoyo zao zimeungana zaidi na makafiri wa Magharibi
kuliko ndugu zao Waislamu. Ndiyo maana hawana msaada wowote kwa
Wapalestina, licha ya uwezo mkubwa walionao. Wao ni maajenti tu wa
CIA na Mossad!
Maangamizi yanayowakumba Waislamu wa Palestina, huku dunia nzima
ikiwa upande wa waangamizaji, yanapaswa
k u wa k u m b u s h a Wa i s l a m u ulimwenguni kote, kwamba
wao ni taifa lisilo na dola (a nation without state). Ili kuweza
kujilinda kutokana na maangamizi kama haya yanayofanyika Gaza,
Waislamu wanahitaji kuwa na dola yao wenyewe.
Wiki ya nne sasa, Israel imekuwa ikiangusha mabomu mazito katika
baadhi ya maeneo ya Gaza kutokea angani, ardhini na majini, kwa
kizingizio cha kuwashambulia wapiganaji wa Hamas, lakini maiti
tunazoshuhudia kupitia picha za televisheni ni za wanawake, watoto
wadogo na watu wengine wasio na hatia. Mpaka mwishoni mwa wiki
iliyopita, zaidi ya Wapalestina 1600 walishauliwa na maelfu wengine
kujeruhiwa.
Waislamu wa Gaza wamekuwa wakikabiliana na maangamizi hayo kwa
ujasir i mkubwa, wakiwa peke yao bila ya msaada wowote
unaohitajika, kutoka
Inaendelea Uk. 12
Makala
-
11 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14,
2014Makala
Mujahidina John McCain!!!Inatoka Uk. 4La kuzingatia hapa ni kuwa
wakati msomaji wetu 0773 526254 anadai kuwa hawa wapiganaji foot
solidiers (mujahidina wasiojitambua) wanapigana Jihad kwa sababu ya
nia zao, kwa akina MacCain hawa ni terrorists. Ni foot soldiers of
the Western military alliance ambao baada ya kumaliza vita
waliyotumwa, watajikuta hakuna walichoambulia zaidi ya kuwatia
Waislamu wa maeneo husika katika tabu na machafuko yasiyo na
kikomo.
Lakini jingine linalotazamiwa kupatikana ni kuikokota Iran, nayo
iingine katika mgogoro huu kwa lengo la kuwasaidia marafiki Shia.
Ikinasa katika mtego huu, itakuwa ndio mwanzo wa kudhoofika Iran,
nayo kubakia kama chui wa karatasi kama ilivyomalizwa Pakistan,
nchi iliyofikia kuwa na nyukilia, lakini sasa imefanywa kuwa
takataka tupu.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema kuwa Iran, sio wajinga.
Wanafahamu kuwa huu ni mchezo wa Marekani. Kwamba hawa ISIS sio
wapiganaji huru wala sio mujahidina kwa maana ya hiyo
wanavyojitangaza. Ila ni:
Terrorist proxy controlled by the CIA. It is a creation of US
intelligence. It is a US intelligence asset, an instrument of
non-conventional warfare.
Na kwa hiyo, wanapiga hesabu zao vizuri. Wameweka kando ile
kauli yao ya awali kuwa watashirikiana na Marekani katika
kukabiliana na kitisho cha ISIS.
Ukibaraka na utumiwaji huu wa ISIS, unaelezwa pia na mkuu wa
Idara ya Usalama wa Saudi Arabia, Prince Bandar bin Sultan bin
Abdulazia bin Saud ambaye katika kuishawishi Urusi isimuunge mkono
Bashar Assad, alikwenda Moscow kukutana na Rais Vladmir Putin.
Katika mazungumzo yao akampa Putin biashara nono ya mamilioni ya
dola-kwamba Saudi Arabia ingenunua silaha toka Urusi za mamilioni
ya dola. Lakini pia akasema kuwa wao ndio wanaowadhibiti hao
mujahidina na kwamba mwisho wa yote watatumika tu, ila malengo
yatakayotimia sio hayo yanayoelezwa na ISIS.
Hata hivyo inaelezwa kuwa kwa kuwa Putin naye ana masilahi yake,
aliona masilahi ya Urusi hayapo katika kukubaliana na mpango wa
Marekani kupitia Saudi Arabia, akamtimua Prince Bandar bin Sultan
bin Abdulazia bin Saud ofisini kwake, katika Kremlin. Tazama:
(Saudi Prince Bandar back in action in Riyadh. , Bandar ibn Israel
na Bandar Bush Buys Votes for War on
Rais Vladmir Putin wa Russia.Syria)
Msomaji wetu 0773 526254, anasema kuwa Muis lamu akikataa kuunga
mkono sheria za Mungu na akikataa kutambua dola ya Kiislamu hukumu
yake ni kupigwa risasi na kuuwawa.
Kwa nini baadhi ya Waislamu wanauwawa (na ISIS)?, Jawabu ni kuwa
hawataki kumtii Khalifa. Kama ni hivyo, basi ni haki yao kupigwa
risasi. Anasema msomaji 0773 526254.
Kisha anahi t imisha kwa kusema: Wakumfanyia dawah ni kafiri ila
Muislamu ukiyakataa hayo auwawe.
Anachosema huyu bwana ni kuwa mfano jaaliya mazingira kama ya
Zanzibar, Muislamu yeyoye kama hafanyi ibada, labda haswali,
hafungi, hana kauli nzuri na jirani zake, anafanya ghishi katika
biashara, basi huyu hakuna tena fadhakkir kwake wala kumuelimisha
arejee katika twaa ya Allah. Hukatwa shingo ama kupigwa risasi.
Huuliwa. Kama ni nasaha watapewa Wakristo, makomunisti na waabudu
mizimu (na wale wa mwaka kogwa) kama wapo!
Jingine analosema ni kuwa akiibuka Abu Dawd kutokea huko atokako
Kahama na kudai kuwa yeye ni Khalifah, basi hakuna kuhoji,
ukimpinga ana haki ya kukuuwa. Akitokea Abu Yasir kutoka Kirando,
Rukwa au Nungwi, nakudai kuwa yeye
Khalifah, ukimpinga, haki yako kuuliwa!!!
Kwa uoni kama huo, ndio anasema kuwa Abu Bakr al-Baghdadi na
wapiganaji wake wa ISIS, wana haki ya kufanya mauwaji wanayofanya
Iraq na Syria hivi sasa kwa sababu wanaouliwa ni wale wanaompinga
Khalifah al-Baghdadi!
Nafikiri hapa niseme mambo matatu: Moja ni kuwa hii ni kielelezo
cha upotoshaji na mkorogo (confusion) uliopo ndani ya jamii ya
Waislamu. Na hili litaendelea kutugharimu kama hakutakuwa na juhudi
za makusudi na za kina za kujinasua katika kuchanganyikiwa huku. Na
hakuna njia ya mkato. Elimu.
Pili, nadhani hii ni kipimo pia cha mafanikio cha maadui wa
Uislamu katika kuhamisha vita iwe ni miongoni mwa Waislamu w e n y
e w e k w a w e n y e w e halikadhalika kuwa askari mahiri wa
kupigana proxy war kwa faida ya mabeberu.
(Tazama: 1. Genesis Of Islamic Radicalism: The US Textbook
Project That Taught Afghan Children Terror, 2. The CIA's "Operation
Cyclone" - Stirring The Hornet's Nest Of Islamic Unrest, 3.
Americas Jihad and Counter-jihad in Afghanistan and Pakistan)
Tatu ni kuwa kwa hakika tuna dhima kubwa na hasa Masheikh wetu,
akina Sheikh Kilemile, Muharami Doga, Maalim Ally
Bassaleh, Kundecha, Mohammed Idd Abu Idd, Salim Barahiyani, na
wengineo, mbele ya Mungu.
Kwa muktadha wa makala yangu ya leo mimi niseme jambo moja tu.
Kwa mtu mwenye akili na anayefuata taratibu za kawaida tu za
binadamu asiye mvivu wa kufikiri, baada ya kuibuka kamanda al
Baghdadi, anatakiwa kujiuliza, ni nani huyu Baghdadi aliyeibuka na
kudai anapigana Jihad? Ametokea wapi? Pana ukweli gani wa
anayoyasema?
Alipoibuka al-Baghdad kama kamanda wa ISIS, aliyekuwa mkuu wa
gereza la Bucca-Camp Bucca (ambalo lilikuwa kambi ya Marekani -
U.S. detention camp in Iraq), Col. Kenneth King, alijuliza
imekuwaje? Katika kujiuliza anasema anakumbuka kuwa huyu bwana siku
anaachiwa katika gereza hilo alimuaga akimwambia I will see you
guys in New York.
N i f a f a n u e . A l - B a g h d a d i wakati Marekani
imevamia Iraq mwaka 2003, a l ikuwa miongoni mwa maafisa katika
serikali ya Saddam Hussein aliyekamatwa na kuwekwa katika kambi ya
Marekani ya Bucca. Wakati wenzake wakipelekwa Guantanamo na
magereza mengine, yeye akaachiwa. Na siku mkuu wa kambi hiyo
alipopewa amri ya kumwachia, anasema j a m a a a l i m p u n g i a
m k o n o akimwambia See you guys in New York.
Mkuu huyo wa gereza anasema kuwa hakuelewa kauli hii ilikuwa na
maana gani. Lakini baada ya kuibuka ISIS na Baghdadi akiwa ndio
kamanda, huku misaada na silaha zikitoka Marekani, anasema ndio
sasa anapata picha na kuelewa maana ya ile see you guys in New
Yok.
Kanuni ya msingi ya Kiislamu inatuambia kuwa zinapotufikia habar
i , tuchunguze tus i j e tukawadhuru watu kwa ujinga. Leo anaibuka
mtu anakwambia anapigania Jihad, lakini Jihad yenyewe inaonekana
kuwa na mkono wa Marekani, Mayahudi na NATO, wewe badala ya
kuchunguza ukajua ukweli wa mambo, unasema kuwa foot soldiers
watalipwa kwa nia yao! Unashawishi watu wanakwenda wakidhani
wanapigania Khilafah, katika kufanya hivyo, wanauwa watu wasio na
hatia na wao wenyewe wanajiangamiza na kuuangamiza Uislamu.
Hii akili gani! Uislamu toka awali ungekuwa umepokewa na watu
walio na ufahamu wa chini kiwango hiki, hapana shaka wasingeweza
kukabiliana na vitimvi vya Makuraishi na Mayahudi na usingetufikia
hivi leo.
-
12 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014
Majeshi yahitajika Gaza siyo porojo!Inatoka Uk. 10kwa Waislamu
wenzao duniani. Watu wa Gaza wamebeba roho zao mkononi. Wengi wao
wamekufa shahidi na mamia kutiwa vilema.
N d e g e z a a d u i z i n a f a n ya d o r i a z a kiusalama
kwenye anga la Gaza, kwa uhuru mkubwa bila ya hofu yoyote ya k u t
u n g u l i w a , w a l a kukabiliana na ndege nyingine ya
kuisumbua. M a j e s h i ya n c h i z a Waislamu zilizo jirani na
Gaza, ambayo yana silaha bora za kisasa, hayawezi kuwasaidia
kijeshi ndugu zao wa Gaza. Watawala wa nchi zao wamewatiwa pini.
Ndege zao za kivita, vifaru na zana nyingine ni kwa ajili ya
maonyesho tu na mapambo!
Ndiyo maana ndege za Mayahudi ziko huru kuvinjari anga la
Palestina na kuangusha mabomu m a h a l i wa n a p o t a k a bila
ya hofu yoyote ya kutunguliwa. Nani wa kuzuia hujuma zao dhidi ya
raia wasio na hatia!?
Watawala wa nchi za Waislamu duniani wamefanya kosa kubwa pale
walipokubali suala la Palestina kuhamishwa kutoka kuwa suala la
Kiislamu na kugeuzwa kuwa suala la Waarabu, na baadaye kuwa suala
la Wapalest ina. Sasa nao wamesimama kama watazamaji tu wasio na
upande katika mgogoro wa Palest ina, ambao unawahusu moja kwa moja
kama Waislamu!
Wakati adui anapofanya maangamizi ya watu wasio na hatia, kama
ilivyo sasa katika mauaji ya Gaza, watawala hawa wanaziangalia tu
ndege za wavamizi wa Kiyahudi z i n a v y o u a r a i a w a
Palestina, miili ya ndugu zao Waislamu waliouawa i k i s h a z i k
w a , n d i y o wanaanza mashindano ya kuonyesha huzuni zao, kwa
kutoa matamko yasiyo na tija ya kulaani maangamizi hayo!
K a m a w a l i v y o mabeberu wa Magharibi, n a o w a n a k i m
b i l i a "mazungumzo ya amani", yenye lengo la 'kutafuta' n j i a
ya k u k o m e s h a m a a n g a m i z i h a y o , kama vile
suluhisho la mzozo huo halifahamiki! Mabeberu wa Magharibi, Umoja
wa Mataifa na 'Arab League' hawawezi kuleta ufumbuzi wa maangamizi
ya Gaza. Wao ni sehemu ya tatizo hilo.
I n a s h a n g a z a s a n a kuona watawala wa
nchi za Waislamu, nao wakihangaika kulipeleka suala la
kuangamizwa ndugu zao wa Gaza, k w e n y e B a r a z a l a Usalama
la Umoja wa M a t a i f a , wa k i t a f u t a a z i m i o l a k u
u n g wa mkono Palestina, kutoka kwa nchi wanachama wa Baraza hilo,
ambazo ndizo zilizounda dola ya Kiyahudi, na kuisaidia kwa hali na
mali, kupora ardhi tukufu za Palestina! Hiyo ni akili gani!?
Jawabu linalohitajika k w e n y e m a u a j i yanayoendelea ya
Gaza l i n a j u l i k a n a . I s r a e l i n a t u m i a v i s i
n g i z i o hewa na udanganyifu. Tunajua wanaohofia sana
ushirikiano wa makundi ya Wapalestina ya Hamas na Fatah. Hiyo ndiyo
sababu ya maangamizi wa n a y o f a n ya G a z a , na wala siyo
kutekwa na kuuawa kwa vijana w a K i y a h u d i k a m a w a n a v
y o l a z i m i s h a . Suluhisho la jambo hilo siyo vikao wala
mikutano mirefu ya majadiliano.
Wais lamu dunian i wanapaswa kutanabahi kwamba mgogoro wa
Palestina unawahusu na ufumbuzi wake uko mikononi mwao kama umma.
Mabeberu wa Magharibi hawawezi k u l e t a u f u m b u z i . N i m
a t a p e l i t u , wanaochezesha akili za walimwengu, kwa lengo la
kuhamisha mazingatio yao kutoka kwenye kiini halisi cha mzozo
huo.
W a k i s h a t a m b u a hilo, ndipo Waislamu watakapoweza
kutekeleza kikamilifu maelekezo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kuhusu
maadui h a t a r i w a n a o v a m i a maeneo yao, kwa lengo la
kuwaangamiza, kama vile inavyofanyika Gaza:
" P i g a n e n i n a o , M w e n y e z i M u n g u awaadhibu
kwa mikono yenu, na awafedheheshe na akunusuruni juu yao, na
avipoze vifua vya Waislamu (vifurahi)" Qur(9:14)
Hivi ndivyo msaada k wa wa t u wa G a z a u n a v y o t a k i wa
u we . Na hivyo ndiyo j insi y a k u k a b i l i a n a n a
maangamizi ya wasio na hatia Gaza. Na ndivyo M w e n y e z i M u n
g u atakavyovipoza vifua vya waja wake wema. Matamko ya kuilaani
Israel peke yake hayasaidii sana. Na mazungumzo yasiyokwisha ya
amani ni geresha tu ya kuendeleza d h u l m a d h i d i y a
Wapalestina!
Ni majeshi tu ndiyo yanayoweza kuwalinda raia wasio na hat ia ,
d h i d i y a m a j e s h i mingine ya uvamizi yanayokalia kimabavu
nchi yao. Nchi za Kiarabu zinazoizunguka Palestina, zina nguvu za
kutosha za kijeshi kuzikomboa ardhi zote za Wapalestina zilizoporwa
na Mayahudi na kukomesha unyanyasaji huu wa raia wa Palestina.
Kuna zaidi ya wanajeshi milioni mbili Waislamu katika eneo la
Mashariki ya Kati, wanaotumia zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni
100 kwa mwaka, kwa ajili ya kununulia silaha. Misri peke yake ina
zaidi ya ndege 200 za kivita, aina ya F - 16 na askari wapatao
450,000.
Sasa kama mna nguvu kubwa ya kijeshi kama hiyo, lakini hamuwezi
kuitumia kumpiga adui yenu, basi ninyi ndiyo mnakuwa walinzi halisi
wa adui huyo na wala siyo mataifa ya Magharibi! I wa p o n c h i h
i z o z a Waislamu zitaishambulia I s r a e l n a k u i w e k e a
mzingo (siege), kama vile Israel inavyofanya Gaza, unadhani mataifa
ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani yatakimbilia UN na kutoa
matamko ya kulaani tu!? Nina hakika wa t a p e l e k a m a j e s h
i na kuingia vitani i l i kuwanusuru ndugu zao!
U f u m b u z i w a kudumu wa maangamizi y a W a p a l e s t i n
a yanayoendelea Gaza uko mikononi mwa umma wa Kiislamu. Siyo
Jumuiya ya Kimataifa wala nchi za Kiarabu. Nchi za Kiarabu z ik i s
imama kama Waislamu, ndipo zinapoweza kuwanusuru ndugu zao wa Gaza.
Uislamu una suluhisho la migogoro kama hiyo.
A l h a m d u l i l l a h , tumeshuhudia Waislamu duniani na
wapenda a m a n i u l i m we n g u n i kote, wakiungana kihisia na
watu wa Gaza katika kipindi hiki kigumu, kupitia maandamano yao,
misaada ya kibinadamu na kauli zao za kuilaani I s r a e l . W a t
u h a o wanaonekana kuwa tayari kuchukua hatua zaidi za kuwanusuru
Wapalestina kuliko maneno, lakini nao hawana uwezo , kama walivyo
watu wa Gaza. Hili jambo linahusu utawala na majeshi, siyo raia wa
kawaida.
12 MAKALA/Mashairi
WATU zaidi ya 20,000 waliandamana na kupita m b e l e ya I k u l
u ya Marekani, White House, Washington DC kupinga mauwaji
yanayofanywa na Israel huko Gaza.
Free Palestine, let Gaza live, watu walipaza sauti mbele ya
White House, Jumamosi iliyopita.
20,000 waandamana Washington kulani Israel
Y a k i a n d a l i w a n a k u o n g o z w a n a
Washington-based anti-war coalition ANSWER, ikishirikiana na
taasisi nyingine kama Council o f American- Is lamic Relations,
American-Muslim Alliance, New Yo r k M u s l i m L e g a l Fund of
America na Islamic Circle of North America, yalikusanya
waandamanaji kutoka miji na majimbo mbalimbali ya Amerika.
Israel has terrorized the region and world since 1948. Stop
genocide in Gaza. Free Palestine.
Yalisomeka baadhi ya mabango yaliyokuwa y a m e b e b w a n a
waandamanaji.
M w a n d a m a n a j i Thomas, akibeba bango l i l i l o a n d
i k wa : F r e e Palestine, let Gaza live, alisema:
The diversity in this square shows the great desire for justice
and compassion toward the humanitarian crisis in Gaza.
A k i m a a n i s h a kuwa ule mkusanyiko uliowajumuisha watu wa
kada mbalimbali, dini na mataifa mbalimbali, unathibitisha kilio
cha wengi na huruma ya wengi, kutaka haki kwa
wananchi wa Gaza.Obama, responsible for
massacre. Stop all U.S. aid to Israel. Ni ujumbe katika mabango
mengine.
Waandamanaji walipita pia mbele ya ofisi za gazeti la The
Washington Post, ambalo walilishutumu kuwa lina msimamo wa
kumpendelea na kuwa
upande (pro-Israeli editorial policy) wa dhalimu Israel.
We protest the editorial vision of the Washington Post, which
continues to promote Israeli occupation and apartheid policies that
are the root of the conflict. Shame on you!
Walipaza sauti baadhi y a w a a n d a m a n a j i walipofika
langoni mwa ofisi za gazeti hilo likiwa l inalindwa na askari wenye
silaha kali.
K i l i chovut ia za id i katika maandamano hayo ni uwepo wa
Mayahudi wakiwa na mabango yao yakisema:
Judaism rejects the Zionist Israeli State and its
atrocities.
K w a m b a d i n i y a K i ya h u d i ( J u d a i s m )
inapinga Uzayuni na unyama unaofanywa na Israel.
T h e I s r a e l i s t a t e has been perpetrating genocide
against the P a l e s t i n i a n s w h i c h Judaism would never
accept.
Alisema mwandamanaji wa Kiyahudi rabbi David Fieldman
akimaanisha kuwa serikali ya Israel i m e k u w a i k i f a n y a
mauwaji ya kuangamiza k w a W a p a l e s t i n a jambo ambalo
Uyahudi haulikubali.
-
13 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14,
2014MAKALAALLAH (sw) amemuumba mwanadamu katika umbile bora zaidi ,
amempa aki l i inayomtofautisha na mnyama na akampa maarifa ya
kutengeneza mavazi.
Allah (sw) anasema. Enyi wanadamu, hakika
tumekuteremshieni nguo zifichazo tupu zenu na nguo za mapambo,
na nguo za utawa ndizo bora. Hayo ni ishara za Allah (sw) ili watu
wapate kukumbuka.
Enyi Wanadamu, shetani (Ibilisi) asikutieni katika matatizo kama
alivyowatoa wazee wenu katika pepo, akawavua nguo zao ili
kuwaonyesha tupu zao. Hakika yeye pamoja na kabila lake
wanakuoneni, hali ya kuwa wao hamuwaoni. Bila shaka sisi
tumewajaalia mashetani kuwa marafiki wa wasioamini. (Aaraf:
26-27).
Watukufu Waislamu, watu wengi wataingizwa motoni kwa kumfuata
kwao Ibilisi na kufuata matamanio ya nafsi zao. Ibilisi amekula
njama kuwapoteza wanadamu kwa kuwashawishi wavue nguo zao na waende
uchi, ili wachukiwe na Allah (sw), kama yeye alivyochukiwa na
waingizwe motoni pamoja na yeye. Na ni njia hiyo aliyoitumia
kuwapoteza wazee wetu Adam na Hawa.
Basi Allah (SW), anatuonya tusimfanye shetani ndiyo kipenzi
chetu tukapotea. Allah (sw) anasema, (Hali ya kuwa Allah sw)
ameliongoa kundi moja na kundi jingine limethibitikiwa na upotofu.
Kwa hakika waliwafanya mashetani kuwa walinzi wao badala ya Allah
(sw) na wanadhani kuwa wameongoka. (Aaraf: 30).
Muislamu asi je akadhani kwamba yeye bado hajajaaliwa kufanya
mema, au Allah (sw) ndiye alivyomtaka apotee, ila kila aliyepotea
amejitakia mwenyewe upotofu kwa kumfuata shetani na amepotoka kwa
hiari yake, kwani amepewa akili na uhuru wa kuchagua haki au
batili. Na mtu akifanya maasi mwisho wake atajiona yuko sawa, ndiyo
leo wanawake wanaokwenda uchi, wote hao wanajiona wameendelea sana
na wanakwenda na wakati, hasara yao duniani na akhera.
Makureishi walikuwa wanatufu Alkaaba uchi na walijiona wako
sahihi. Allah (sw) akasema, Sema ni nani aliyeharamisha mapambo ya
Allah (sw), ambayo amewatolea waja wake. Na (nani aliyeharamisha)
vitu vizuri katika vyakula? Sema vitu hivyo amewahalalishia
Waislamu (hapa) katika maisha ya dunia, (na) vitakuwa vyao peke yao
siku ya kiama. Namna hivi, tunazieleza aya kwa watu wajuao.
(Aaraf:32).
Allah (sw), amesema (Na Allah sw) amekufanyieni nguo
zinazokukingeni na joto na (baridi na amekufanyieni) nguo za chuma
zinazokukingeni katika vita vyenu. Namna hivi anakutimizieni neema
zake ili mpate kutii. (Nahl: 81).
Tunapata mafunzo kwamba Allah (sw) ndiye aliyetupa elimu ya
kutengeneza nguo, magari, computer nk. ili tupate kuzidi kuwa
watiifu kwake, kinyume chake kila tunaponeemeshwa, sisi ndio
tunazidi kukufuru!
Stara ya mwanamke Muislamu
Mavazi ya wanawake.Allah (sw) anasema, Ewe
Mtume! waambie wake zako na mabinti (watoto) wako na w a n a w a
k e w a K i i s l a m u , wajiteremshie vizuri "Jalaabab", kufanya
hivyo kutawapelekea upesi wajulikane (kuwa ni watu wa heshima ili)
wasiudhiwe. Na Allah (sw) ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa
rehema. (Ahzab: 59).
Aya hii imekuja kulazimisha wanawake wa Kiislamu wote kuvaa
hijaab, ni wajibu kama ilivyo swala. La kushangaza ni kuona
wanawake wengi wa Kiislamu wanapuuza fardhi hi i kwa makusudi,
halafu wanategemea kupata pepo kwa kumuudhi huyo anayemiliki pepo
hiyo.
Allah (sw) anasema tena, "Na waambie waumini wanawake w a i n a
m i s h e m a c h o y a o na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe
uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya
vifua vyao, wala wasionyeshe mapambo yao, ila kwa waume zao, au
baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume
zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au
wanawake wenzao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi
wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo
yaliyohusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane
mapambo waliyoyaficha. Na tubuni nyote kwa Allah (sw) enyi waumini,
ili mpate kufanikiwa. (Nuur: 31)
Aya zimekuja kulazimisha wanawake wa Kiislamu kuvaa buibui na
shungi, na anasema Jabir (ra) kwamba aya hizi ziliteremshwa kwa
wanawake waliokuwa wakienda kifua wazi, na miguu wazi
wakionesha
m a p a m b o ya o k wa wa t u , ambao si maharimu wao. Basi aya
zinakataza kwa mwanamke kuonekana mwili wake ila uso na viganja vya
mikono. Na wamekatazwa kujipamba na kutoka nje kuonesha mapambo yao
kwa watu wa mbali, ila kwa watu waliotajwa kwenye aya.
(Nuur:31).
Wanachuoni wa Kiislamu wameorodhesha sharti za hijaab kama
ifuatavyo: Nguo iwe ya halali Muislamu anatakiwa chumo lake liwe la
halali lisitokane na zinaa, ulevi, kamari, wizi, riba, udanganyifu,
kuuza vinyago, muziki na biashara za haramu. Allah (sw) amewahimiza
Mitume pamoja na waumini wao kula rizki za halali na kuchuma
halali, na Muislamu anayechuma chumo la haramu, basi dua na ibada
zake nyingine hazitokubaliwa, kwani Allah (sw) ni mtakatifu,
hakubali ila halali.
Allah (sw) anasema, Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na
fanyeni mema. Hakika Mimi ni mjuzi wa mnayoyatenda. (Muuminuun:51).
Akasema tena Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni, na
mumshukuru Allah (sw), ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.
(Baqarah:172).
Amesimulia Abuu Hurayra (ra), kuwa Mtume (saw) amesema Allah
(sw) ni mzuri hakubali ila vitu vizuri, na Allah (sw) amewaamrisha
waumini mambo a l i y o w a a m r i s h a M i t u m e , aliposema
Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na fanyeni mema. Hakika Mimi ni
mjuzi wa mnayo yatenda.
Akasema tena Enyi Mlioamini! Kuleni vizuri tulivyo kuruzukuni na
mumshukuru Allah (sw) ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu kisha akataja
mtu aliyesafiri masafa marefu mwenye manywele timtimu, aliyejaa
vumbi anainua mikono yake mbinguni, akisema ewe Bwana ewe Bwana, na
chakula chake ni haramu na nguo zake ni haramu na amekulia kwenye
haramu vipi atakubaliwa?.(Muslim na Tirmidhy).
Hadithi inahimiza kula halali na kuvaa nguo za halali na
anayekula haramu na kuvaa nguo za haramu hatokubaliwa ibada
zake.
Nguo isitiri mwili mzima: Sharti jingine ni kwamba nguo yenyewe
iwe ni Jalaabab, yaani guo zito, pana lenye kusitiri mwili mzima
isipokuwa uso na viganja vya mikono. Hijaab ina sehemu mbili
ukiacha nguo za ndani (sketi na blauzi n.k.), nje avae buibui pana
lisilombana wala kuonyesha mikatiko ya mwili wala lisipasuliwe,
halafu avae shungi litakalofunika uso na kuteremka mpaka kifuani
chini ya matiti yake. Tofauti na vile vitambaa vinavyofunika kichwa
tu na vikaitwa hijaab. Vitambaa hivi vivaliwe ndani kabla ya kuvaa
shungi, Mtume (saw) alimwambia Bibi Asmaa (ra), Ewe Asmaa! Hakika
mwanamke akishafikia kuwa na hedhi (akibaleghe) haisihi kwake
aonekane (na mwanamme ajnabi) ila hapa na hapa, akaashiria uso
wake
na viganja vya mikono.(D4104 hadithi hii imedhaifishwa na
Ghuthaymin na ikasahihishwa na Albany)
Katika hadithi hii pia tunajifunza kwamba Bibi Asmaa (ra) alivaa
nguo inayoonesha ndani, kwa hivyo haifai kuvaa nguo hiyo. Pia kuna
hadithi nyingi zaidi zenye kuonesha kuwa wanawake wakati wa Mtume
(saw) walijifunika mwili mzima ila macho tu kama alivyosimulia Ibn
Abbas (ra) na kupokelewa na Bukhari (SB 4759).
Aisha (ra) anasema kwenye Hija, wanawake walijifunika uso
walipopitiwa na misafara ya wanaume. (Mj 1833).
Wamehitilafiana Ulamaa katika suala la kuonekana uso, baadhi yao
wanaona si lazima kufunika uso, na wengine wanaona ni lazima. Ama
wanawake watakaonekana nywele, kwa kusukana nje, au kichwa au
sehemu yoyote ya mwili ukiacha uso na viganja vya mkono, hao wako
uchi kisheria na wanapata dhambi ya kukaa uchi.
Amesimulia Abii Hurayra (ra) kuwa amesema Mtume (saw), makundi
mawili ya watu ni watu wa motoni, sijawaona (katika wakati huu),
watu wenye mijeledi kama mikia ya ngombe wanawapigia watu, na
wanawake waliovaa nguo lakini wako uchi, wamejipamba na kujitakisha
kwa wanaume, nao wanaume wanawafuata kwa machafu, katika vichwa
vyao mna kama nundu ya ngamia iliyolala, hawatoingia peponi wala
hawatonusa harufu yake, pamoja na kuenea harufu yake masafa kadha
wa kadhaa (masafa ya meli hamsini elfu) (SM 2124).
Hadithi inaonesha miujiza mikubwa ya Mtume (saw) kuwajua wale
askari wanaopiga raia kwa marungu bila makosa. Na kuwajua wanawake
ambao wanavaa nguo zenye kubana na kuonesha maumbile ya mwili, na
wanaotoka nje wamejipamba kwa lipstick, piko, hina na nguo
walizovaa ni za marembo marembo, na katika vichwa vyao, wana nundu
ya ngamia, yaani nywele zilofungwa na kuwekwa help me, na kumfanya
mwanamke awe na vichwa viwili kimoja cha kimaumbile na cha pili
kama nundu ya ngamia, na hiyo ni dalili moja ya watu wa motoni.
Nyengine ni kule kutoka nje wamejipamba na kuonesha mapambo yao kwa
wanaume na kwenda kwa maringo, wakitikisha viuno vyao ili watakiwe
na wanaume, wanaingia pia wanawake wanaokata viuno katika dufu na
ngoma na miziki mbele ya wanaume, kwa hivyo wanenguaji wote ni watu
wa motoni.
Mtume wetu Muhammad (saw) alioneshwa watu hao wa motoni na Mola
wake, kabla yeye kuwaona kwa macho, kwani wakati wake kulikuwa
hakuna askari wapigao watu marungu bila kosa, wala wanawake wenye
nundu za ngamia vichwani mwao, ndiyo kwanza sasa yanaenea hayo
mahelp me, ila yeye aliyaeleza haya zaidi ya miaka elfu moja
nyuma.
-
14 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014
UKILITAMKA neno Srebrenica hapa Ulaya , na hasa kat ika sehemu
za Balkan, mwili wa mtu husisimka. Hilo ni jina la mji, kaskazini
mashariki ya Bosnia, ambalo linawaibisha watu wa Ulaya juu ya
unyama uliofanyika ndani ya bara lao. July mwaka 1995 mauaji
makubwa yalifanyika ndani na pembezoni mwa mji huo na yakachukuwa
roho za zaidi ya Waislamu wa Bosnia 8,000, wengi wao wakiwa
wanaume. Wauwaji walikuwa wanajeshi wa Kiserbia kutokea Bosnia
wakiongozwa na Jenerali Ratko Mladic. Walishiriki wanamgambo
kutokea Serbia na hata watu waliojitolea kutoka Urusi. Umoja wa
Mataifa uliyaelezea mauaji hayo ya kiholela kuwa ni mabaya kabisa
kuwahi kufanyika Ulaya tangu kumalizika Vita Vikuu vya Pili vya
Dunia.
Vi t a v ya B o s n i a v i l i k u wa vinaendelea wakati huo
kutokana na kusambaratika kwa lililokuwa Shirikisho la Yugoslavia.
April 1993 Umoja wa Mataifa ulitangaza kwamba Srebrenica ni Eneo la
Usalama. Hata hivyo, July 1995 jeshi la Umoja huo, likiwakilishwa
na wanajeshi 400 wa kuweka amani kutokea Uholanzi, liliwachia mji
huo utekwe na Waserbia. Mbele ya macho ya wanajeshi wa Kiholanzi,
na tena mchana kweupe, wanajeshi wa Kiserbia waliwatenganisha raia
wa Kiislamu walio wanaume upande mmoja na wale wa kike upande
mwingine. Hatima ya wanaume ilikuwa kupigwa risasi na kuzikwa
vichakani ndani ya makaburi ya halaiki. Wengi wa wanawake
walimalizikia kama mashine za ngono kuwaburudisha wanamgambo wa
Kiserbia.
Mwaka 2004 Mahakama ya Kimataifa ilioundwa na Umoja wa Mataifa
kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita katika Yugoslavia ilisema
kilichofanyika Srebrenica ni mauaji ya kimbari, uhalifu chini ya
sheria za kimataifa. Mahakama hiyo ilisema kwamba kuwahamisha kwa
nguvu Wabosnia 25,000 hadi 30,000, wanawake, watoto na wazee, zoezi
lililokwenda sambamba na mauaji hayo, ni ushahidi tosha juu ya nia
ya kuuwa waliokuwa nayo maafisa wa juu wa jeshi la Waserbia wa
Bosnia. Wenyewe Umoja wa Mataifa ulikiri kwa kusema kwamba japokuwa
lawama kubwa ya mauaji hayo inawaangukia watu waliotenda pamoja na
wale waliowasaidia na kuwalinda, hata hivyo, mataifa makubwa ni ya
kulaumiwa pia kwa kushindwa kuchukuwa hatua zifaazo. Pia ilitajwa
kwamba Umoja wa Mataifa ulifanya makosa makubwa ya kutochukuwa
maamuzi barabara, hivyo maafa ya Srebrenica yatawasuta walimwengu
na kuzibakisha hisia zao zikiugua.
Orodha ya watu waliopotea Srebrenica ni 8,373 hadi July 2012, na
kati ya hao 6,838 wameshatambuliwa kupitia vipimo vya uchunguzi wa
kinasaba, DNA, uliofanyiwa mafupa yaliofufuliwa kutoka kwenye
makaburi. Miili 6,066 imezikwa katika Uwanja wa Potocari ambako
kila mwaka maelfu ya Wabosnia huenda
Haki kwa mama wa wahanga wa SrebrenicaNa Othman Miraji
hapo kuwaombea dua marehemu ndugu zao. Rais wa Serbia aliwahi
kuomba radhi kwa mauaji hayo, lakini hajaenda umbali wa kuyaita
kuwa ni ya kimbari.
Licha ya karibu miaka 20 kupita sasa tangu kutokea mkasa huo,
bado Ulaya inatembea na zimwi la Srebrenica, maafa yaliotoa picha
ya udhaifu wa Umoja wa Mataifa kushindwa kuwa chombo cha kulinda
usalama wa watu walio dhaifu.
Wiki iliopita mahakama ya kiraia ya Uholanzi iliamuwa kwamba
nayo serikali ya Uholanzi inabeba dhamana ya kuuliwa zaidi ya
Waislamu wa Kibosnia 300. Ilitajwa kwamba nchi hiyo iliokuwa na
kikosi chake katika jeshi la kuweka amani la Umoja wa Mataifa huko
Bosnia, ni mshirika wa makosa pia kwa vile wanajeshi wake
waliwaachia wanamgambo wa Kiserbia waingie katika kambi iliotengwa
kuwalinda raia wa Kiis lamu wa Bosnia . Inasemekana Waislamu hao
300 walitaka ulinzi katika kambi hiyo walikokuwa wakikaa wanajeshi
wa kulinda amani wa Uholanzi karibu na Potocari. Lakini badala ya
kupewa ulinzi, Waholanzi waliwakabidhi raia hao kwa jeshi la
Jenerali Mladic na kuuliwa.
Lakini mahakama hiyo ilisema serikali ya Uhoanzi si dhamana wa
moja kwa moja wa mauaji yote yaliotokea Srebrenica ambapo zaidi ya
Waislamu 8,000 waliuliwa. Licha ya hayo, wanajeshi wa Kiholanzi
walilaumiwa kwa kwenda kinyume na sheria na kuchangia kuwahamisha
zaidi ya raia 300 kutoka jengo lao la kijeshi.
Jumuiya ya Mama wa Watoto Wal ioul iwa Srebrenica ndio
iliofungua kesi hiyo. Ilitaka serikali ya Uholanzi ibebeshwe
dhamana moja kwa moja kwa kutekwa eneo hilo na wanamgambo wa
Kiserbia na kuuliwa jamaa wa akina mama hao. Ilivokuwa mahakama
hiyo haijaenda umbali wa kuyakuba madai
yote, akina mama hao wamesema watakata rufaa mbele ya Mahakama
ya Ulaya mjini Strassburg. Akina mama hao wanautaka Umoja wa
Mataifa ubebeshwe pia dhamana juu ya mkasa huo.
Mwaka jana Mahakama Kuu huko Uholanzi ilisema kikosi cha
wanajeshi wa U h o l a n z i k i l i c h o k u we k o Srebrenica
kinabeba dhamana ya kuuliwa wanaume watatu wa Kibosnia ambao
walikataliwa kuingia katika kambi ya wanajeshi hao na baadae watu
hao wakauliwa na Waserbia. Mwaka huu serikali ya Uholanzi
imewafidia jamaa wa marehemu hao kwa kulipa Euro 20,000 kwa kila
mtu mmoja aliyeuwawa.
Hukumu iliotolewa The Hague wiki iliopita imezusha masuali kwa
mabingwa wa sheria za kimataifa. Ina maana kwamba japokuwa
mwanajeshi wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa atakuwa na kinga ya
kutoshitakiwa kwa uhalifu kutokana na kibali ambacho Umoja wa
Mataifa inacho, hata hivyo,
serikali ya nchi ya mwanajeshi huyo inaweza kubebeshwa dhamana
kwa kitendo cha mwanajeshi huyo. Kwa umbali gani tafsiri ya hukumu
hii itakavotumiwa katika operesheni za kijeshi za Umoja wa Mataifa
ni jambo la kungoja na kuona.
Kuna hatari kwamba kutokana na hukumu hii, huenda hamna nchi
yeyote isiokuwa na maslahi katika eneo la mzozo itakayokubali
kutuma wanajeshi wake huko kulinda amani. Madola kama Marekani na
Ujerumani yalikwepa kutuma wanajeshi wa kulinda amani nchini
Bosnia. Na ingekuwa hakujapelekwa kabisa wanajeshi wa kulinda amani
huko Bosnia wakati huo, bila ya shaka idadi ya watu ambao wangekufa
katika vita hivyo ingekuwa kubwa zaidi. Raia wengi pia wangekufa
kwa njaa. Kwa ufupi: ninavoona mimi ni kwamba kanuni za kimsingi za
utu lazima ziwe juu ya ule muongozo uliowekewa operesheni ya
kulinda amani. (Kwa hisani ya Othman Miraj)
TANGAZOUnahitajika msaada kwa kijana (Mtoto) wa Kiislamu (miaka
14), aliye mlemavu wa miguu, kuendelezewa eneo lake la ardhi, kwa
kiwango ama chumba kimoja au viwili.
Eneo hilo lipo Potea, Kigamboni Jijini Dar es Salaam, alipewa na
Muumini mmoja (Mama) wa Kiislamu, toka mwaka 2011, ikiwa ni
Sadakatul-jaalia kwa kijana huyo baada ya kumuona.
Mama mzazi wa kijana huyo, hana uwezo wa kuliendeleza eneo hilo.
Ikiwa msaada huo utapatikana utaweza kumsaidia kukabiliana na
changamoto ya kukidhi malengo yake ya kumpeleka katika masomo ya
Dini, Mkoani Tanga.
Kwa maelezo/msaada piga namba:- 0686 82 36 96, 0659 27 16
49.
WAPALESTINA wakienda kuzika ndugu na jamaa zao kufuatia
mashambulizi ya majeshi ya Israel huko Gaza. Je, Waziri Mkuu wa
Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau anaweza kufikishwa The Hegue
kujibu tuhuma za mauaji ya raia wasio na hatia wa Kipalestina.
MAKALA
-
15 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14,
2014MAKALA
S E R A ya n c h i z a n j e ya Marekani hailengi kuzuia kuenea
kwa Uislamu wa siasa kali. Kwa uhakika, ni kinyume chake. Kielelezo
cha kukua kwa 'Uislamu wa siasa kali' wakati wa vita ya kiitikadi
ya dunia katika iliyokuwa Urusi na Mashariki ya Kati inaendana na
agenda iliyojificha ya Marekani. Inalenga zaidi uendelezaji na siyo
kupambana na ugaidi wa kimataifa, kwa nia ya kutangua mifumo huru
ya kitaifa na kuzuia kuenea kwa harakati za mabadiliko ya kijamii
zinazolenga ukiritimba wa kiuchumi wa Marekani. Watawala jijini
Washington wanaendelea kuunga mkono - kwa kutumia operesheni
kificho za CIA - kukua kwa Uislamu wa kikereketwa, kote Mashariki
ya Kati, katika iliyokuwa Urusi pamoja na nchini China na
India.
Kote katika nchi zinazoendelea, kukua kwa vikundi vya itikadi
kali, za sehemu ndogo za jamii na ny inginezo , z inasa id ia
kutimiza malengo ya Marekani. Makundi haya na yale yenye silaha
yamekuzwa, hasa katika nchi ambazo taasisi za kitaifa zimeporomoka
chini ya mzigo wa matakwa ya kurekebisha uchumi yaliyolazimishwa na
shirika la fedha la kimataifa, IMF.
Makundi haya ya kikereketwa ya n a c h a n g i a k u h a r i b u
n a kuvuruga taasisi za kiraia.
Ukereketwa wa Kiislamu unajenga migawanyiko ya kijamii na
kikabila. Inapunguza uwezo wa wananchi kuungana kupambana na
ukiritimba wa Marekani. Makundi haya au mikusanyiko, kama Taliban
nchini Afghanistan, mara kadhaa huanzisha harakati dhidi ya 'Uncle
Sam.' (mjomba wa Marekani, mfadhili wao) kwa njia ambayo haijengi
hatari yoyote kwa maslahi mapana ya Marekani kiuchumi au kushikilia
maeneo tofauti duniani.
Kufuta historia ya Al Qaeda: Tangu Septemba 2001, historia ya Al
Qaeda kimsingi imefutika. Uhusika wa serikali kadhaa za Marekani na
'mtandao wa kigaidi wa Kiislamu' ni nadra kutajwa. Vita kubwa
katika Mashariki ya Kati na katika Asia ya Kati, inayosemekana ni
'dhidi ya ugaidi wa kimataifa,' ilianzishwa Oktoba 2001 na serikali
ambayo ilikuwa inafuga ugaidi wa kimataifa kama agenda mojawapo ya
sera ya nchi za nje. Kwa maneno mengine, sababu muhimu ya kuanzisha
vita dhidi ya Afghanistan na Irak zimeundwa tu, kijanja. Wananchi
wa Marekani wamedanganywa na kupotezewa mwelekeo kwa
Agenda iliyofichika ya MarekaniNa Profesa Michel
Chossudovsky
JIMMY Carter, Rais wa zamani wa Marekani.
makusudi na serikali yao. Uamuzi wa kuwadanganya wananchi wa
Marekani ulichukulia hapo Septemba 11, 2001, saa chache baada ya
shambulio la kigaidi dhidi ya majengo ya Kituo 'cha Biashara cha
Kimataifa, Bila ushahidi wa kuyakinisha, Osama alikuwa tayari
ametajwa kama 'mtuhumiwa mkuu.' Siku mbili baadaye, Septemba 13 -
wakati uchunguzi wa FBI ndiyo kwanza unaanza - Rais Bush akaahidi
"kuiongoza dunia kufikia ushindi."
Wakati CIA inakubali kwa mbinde kuwa Al Qaeda ilikuwa ni 'amana
ya kiinteligensia' wakati wa vita ya itikadi na Urusi, uhusiano
halisi unasemekana kuanzia mbali, katika enzi zilizopita. Habari
kuhusu Septemba 11 zinaelekea kusadiki kuwa uhusiano kati ya CIA na
Al Qaeda ni wa kipindi cha vita vya Urusi na Afghanistan
(vilivyoisha 1988). Mahusiano hayo yanaonekana kuwa yalikuwa ni
tofauti na kuelewa kilichotokea Septemba 11 na 'Vita ya Dunia dhidi
ya Ugaidi.' Hata hivyo miezi michache tu kabla ya Septemba 11,
kulikuwa na ushahidi wa uhusiano wa karibu kati ya wanajeshi wa
Marekani na makundi ya Al Qaeda yanayoshiriki mapambano nchini
Macedonia.
Ikiwa imefunikwa na mkondo wa historia ya hivi karibuni, nafasi
ya CIA katika kuunga mkono na kuinua makundi ya kigaidi ya
kimataifa wakati wa
vita ya kiitikadi (Vita Baridi) na baada ya hapo, inaachwa
pembeni au kupuuziwa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi.
Kielelezo cha wazi cha uvurugaji wa habari kuanzia Septemba 11 ni
dhana ya 'kujirudi,' ambako dhamana za ki inte l igensia (za ki
jasusi) zinasemekana 'kuwarudi walioziunda kuwa kile tulichokiunda
kinaturudia na kutupiga machoni.' Katika kuonyesha mfano wa mantiki
iliyopinda, utawala wa Marekani na CIA vinaonyeshwa kama
waathirika, wahanga wa hali hiyo:
M b i n u z a h a l i y a j u u zilizofundishwa Mujahidina, na
maelfu ya tani za silaha zilizopelekwa kwao na Marekani - na
Uingereza - sasa vinazitesa nchi za Magharibi katika kile
kinachoitwa 'kujirudia,' ambako mkakati wa kisera unawageukia wale
walioutunga.
Vyombo vya habar i vya Marekani, hata hivyo, vinakiri kuwa
"kuingia kwa Taliban madarakani (mwaka 1996) kwa upande fulani
kulitokana na Marekani kuwaunga mkono Mujahidina, kundi la
Afghanistan la siasa kali, katika miaka ya 1980 wakati wa vita
dhidi ya Urusi. Lakini pia inafuta ushawishi wa hoja zake na
matamshi rasmi na kufikia tamati, kama wimbo, kuwa CIA imedanganywa
na ujanja wa Osama. Ni kama mwana kwenda kinyume na baba yake.
'Vita dhidi ya Ugaidi' baada ya Septemba 11: Dhana ya 'amana
kujirudia' ni ya kutunga. CIA haikuwahi kuondoa mahusiano yake na
'mtandao wa Kiislamu wa siasa kali.' Kuna ushahidi wa kutosha kuwa
Al Qaeda imebaki kuwa amana ya kijasusi inayofadhiliwa na Marekani.
Al Qaeda inatajwa kama mhunzi wa Septemba 11 bila hata mara moja
kutaja mahusiano yake ya kihistoria na CIA na taasisi ya kijasusi
ya jeshi la Pakistan, ISI.
Wakati Al Qaeda imeendelea kubaki chini ya udhibiti wa mashirika
ya kijasusi ya Marekani, utawala wa Marekani umesisitiza muda wote
kuwa 'adui huyu wa nje' atashambulia tena, kuwa 'Septemba 11 ya
pili' itatokea kwingineko Marekani au katika nchi za Magharibi.
"Kuna dalili kuwa mashambulio mengine siku za usoni yanaweza
kushindana au kuzidi yale ya Septemba 11...
Na ni wazi kuwa mji mkuu wa nchi na jiji la New York zitakuwa
katika orodha yoyote ile ya mashambulizi mengine" (kwa mujibu wa
Tom Ridge wakati wa Christmas, 2003).
"Unajiuliza: Hivi ni hatari kiasi hicho? Ndiyo, unaweza kusema
na kuweka rehani hata maisha yako. Watu hawafanyi hivyo kama siyo
jambo la hatari kabisa," kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi
Donald Rumsfeld, wakati huo huo.
Taarifa za uhakika zinaonyesha kuwa Al Qaeda inaendelea na
mipango yake ya kufanya s h a m b u l i o k u b wa n c h i n i
Marekani katika juhudi za kuvuruga mpangilio wetu wa kidemokrasia.
....Hii ni habari ya kustua kuhusu wale ambao wanataka
kututayarishia mabaya. Lakini kila siku tunaimarisha ulinzi wa nchi
yetu." (Rais George W. Bush, Julai 2004)
"Adui aliyeshambulia Septemba 11 amepasuka vipande na kupungua
nguvu, lakini bado ana nguvu nyingi, akiwa na dhamira ya
kutushambnulia tena," alisema aliyekuwa makamu wa rais Dick Cheney,
Julai 2006.
"Septemba 11 nyingine ingetoa sababu na nafasi ya kujibu mapigo
dhidi ya walengwa kadhaa wanaofahamika," kwa mujibu wa ofisa wa
Wizara ya Ulinzi ya Marekani, akizungumza na gazeti la Washington
Post, Aprili 23, 2006.
(Hii ni sehemu ya makala ya Profesa Michel Chossudovsky,
aliyoipa jina Washingtons Hidden Agenda. Imefasiriwa kwa Kiswahili
na Anil Kija)
-
16 AN-NUURSHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 201416
MAKALA
Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105
na kupigwa chapa na POA Printing Works Limited, S.L.P. 4605 Dar es
Salaam.
AN-NUUR16 SHAWWAL 1435, IJUMAA IJUMAA AGOSTI 8-14, 2014
Soma gazeti la
AN-NUUR kila Ijumaa
ZILE tuhuma juu ya watoto wa Kiislamu kat ika skul i ya Eden
International S c h o o l , k u w a w a n a s o m e s h w a U t a t
u , s a s a zimethibiti.
Hata hivyo, watoto hao wameelezea masikitiko yao kuwa wakati
Waislamu ndio wanaofanya idadi kubwa ya w a n a f u n z i w a skuli
hiyo, hakuna somo la Maarifa ya Uislamu, wala mwalimu anayekuja k u
w a s o m e s h a Uislamu.
T a a r i f a y a Mrajis wa Elimu, Zanzibar imesema kuwa,
uchunguzi uliofanyika skulini hapo umebaini kuwa
Wanafunzi wasoma UtatuMwalimu wa Islamic hakuna
Na Mwandishi Wetu watoto wa Kiislamu wanalazimishwa kusoma Ukr
is to na kuvaa mavazi yasiyostahiki.
Akizungumza na vyombo mbalimba