KUTATHIMINI MATUMIZI YA LUGHA NA DHAMIRA KATIKA
TAMTHILIA ZA KINJEKETILE NA NYERERE NA SAFARI YA
KANAANI: UTAFITI LINGANISHI
CYPRIAN FIDES
TASNIFU ILIYOWASILSHWA IKIWA NI SEHEMU YA MASHARTI YA
KUPATIWA SHAHADA YA UZAMILI YA (M.A KISWAHILI) YA CHUO
KIKUU HURIA CHA TANZANIA
2017
ii
UTHIBISHO
Aliyetia sahihi hapa anathibitisha kuwa amesoma tasnifu hii iitwayo,Kutathmini
matumizi ya lugha na dhamira katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na
Safari ya Kanaani: Utafiti linganishi na kupendekeza ikubaliwe na Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania kwa kwa ajili kukamilisha masharti ya Shahada ya Uzamili ya
Kiswahili (M.A) ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
..…………………………………………..
Prof. Emmanuel D. Y. Mbogo
(Msimamizi)
…………………………………………
Tarehe
iii
HAKIMILIKI
Tasnifu hii au sehemu yake yoyote hairuhusiwi kukaririwa, kuhifadhiwa,
kubadilishwa kwa mbinu yoyote ile: kieletroniki, kimekanika, kunakilishwa,
kurudufiwa kwa utaratibu wowote ule katika hali yoyote ile bila idhini ya maandishi
kutoka kwa mwandishi wake au kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, kwa niaba
yake.
iv
TAMKO
Mimi, Cyprian Fides, nathibitisha kwamba tasnifu hii ni kazi yangu halisi na
haijawahi kuwasilishwa katika chuo kikuu kingine kwa ajili ya kutunukiwa shahada
yoyote.
……………………………………….
Saini
…………………………………………
Tarehe
v
TABARUKU
Kazi hii ninaitabaruku kwa wazazi wangu, familia yangu, walimu na wanafunzi
wenzangu ambao wamejitoa kwa hali na mali katika kufanikisha malengo yangu ya
kitaaluma ambayo yamenifikisha hatua hii ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika
Kiswahili.
vi
SHUKURANI
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai, nguvu na uwezo wa kukamilisha
kazi hii. Nawashukuru wote waliokuwa wakinipa ushauri na mawazo mbalimbali
hasa walimu wangu wa shahada ya uzamili. Ni vigumu kuwataja wote ila sina budi
kuwaomba radhi wale nisiowataja. Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa
msimamizi wangu Profesa Emmanuel D. Y. Mbogo ambaye hakusita wala kuchoka
kunishauri katika hatua zote za ukamilishaji wa kazi hii. Kwa hakika alijitoa sana
katika kuniongoza, kunishauri, kunikosoa na kunielekeza katika hatua mbalimbali za
utafiti wangu.Hivyo kutokana na ushauri wake ilinilazimu kutumia muda mwingi
kutafakari na kufanyia kazi maelekezo yake yaliyonisaidia kukamilisha utafiti huu.
Nakushukuru sana Profesa Mbogo, nakuombea kwa Mungu akupe maisha marefu
yenye baraka, amani na furaha tele. Pia napenda kuwashukuru wazazi wangu
wapendwa, Bwana Cyprian Abel Moshy na Bi Josephine Jacob Tengia kwa
kunisomesha hatua mbalimbali hadi kufikia kusoma Shahada ya Uzamili. Mungu
awabariki awape afya, amani na furaha katika maisha yenu yote.
Aidha napenda kumshukuru mume wangu mpendwa Bwana Sixbert John Mahundi
kwa kunipa msaada wa hali na mali na kuniwezesha kukamilisha kazi hii. Pia
nawashukuru watoto wangu Alice, Stanley na Charles kwa kunipa ushirikiano katika
kusoma kwangu na kuniwezesha kukumilisha kazi hii ya uzamili.Vilevile
nawashukuru wanachuo wenzangu wa shahada ya uzamili, kwa ushirikiano
walionipa kwa kunihimiza na kunitia moyo bila kuchoka ili niweze kumaliza
shahada yangu ya uzamili Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
vii
IKISIRI
Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini matumizi ya lugha na dhamira zilizojitokeza
katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani: Utafiti linganishi.
Ili kufanikisha utafiti huu, mtafiti ametumia mbinu za maktabani katika kukusanya
na kuwasiilisha data kimaelezo. Pia marejeleo mbalimbali kutoka tamthiliya za
Kiswahili yalipitiwa. Nadharia ya fasihi ya jamii ndiyo iliyotumika katika
kufanikisha utafiti huu. Nadharia hii imemsaidia mtafiti kuweza kubaini mawazo
mbalimbali ya waandishi katika tamthiliya zao za utafiti linganishi. Matokeo ya
uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti. Tamthiliya hizi teule
zimebainisha jamii yetu kabla ya uhuru na baada ya uhuru. Dhamira za uongozi
mbaya, rushwa na usaliti zimejitokeza. Matokeo mengine ni dhamira ya ukombozi
iliyomfanya mkoloni aondolewe katika ardhi ya jamii ya watu wa Kusini ili wawe
huru, kutumia ardhi yao na mali nyingine zilizopatikana katika jamii yao. Pia
uzalendo ulitakiwa kwa jamii kwa kuwapeleka vijana kwenye mafunzo ya Jeshi la
Kujenga Taifa na tohara. Tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya
Kanaani zina mchango mkubwa katika jamii kwa kuwasilisha ujumbe ambao ni wa
kihistoria unaoiwezesha kujua matukio mbalimbali ya nchi kabla na baada ya uhuru
viii
YALIYOMO
UTHIBISHO ............................................................................................................... ii
HAKIMILIKI ............................................................................................................ iii
TAMKO ..................................................................................................................... iv
TABARUKU ............................................................................................................... v
SHUKURANI ............................................................................................................ vi
IKISIRI ..................................................................................................................... vii
ORODHA YA MAJEDWALI ................................................................................ xiii
SURA YA KWANZA ................................................................................................. 1
UTANGULIZI ............................................................................................................ 1
1.1 Utangulizi ......................................................................................................... 1
1.2 Usuli wa Mada ................................................................................................. 2
1.3 Tamko la Tatizo la Utafiti ................................................................................ 4
1.4 Malengo ya Utafiti ........................................................................................... 5
1.4.1 Lengo Kuu ........................................................................................................ 5
1.5 Maswali ya Utafiti ............................................................................................ 5
1.6 Umuhimu wa Utafiti ......................................................................................... 6
1.7 Mipaka ya Utafiti ............................................................................................. 6
1.8 Uzingativu wa Maadili ..................................................................................... 6
1.9 Vikwazo vya Utafiti ......................................................................................... 7
1.10 Utatuzi wa Vikwazo ......................................................................................... 7
1.11 Muundo wa Tasnifu ......................................................................................... 8
1.12 Hitimisho .......................................................................................................... 8
ix
SURA YA PILI ........................................................................................................... 9
MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA KIUNZI CHA NADHARIA ................. 9
2.1 Utangulizi ......................................................................................................... 9
2.2 Dhana ya Fasihi Linganishi .............................................................................. 9
2.3 Tafiti kuhusu Tamthiliya za Kiswahili ........................................................... 11
2.4 Pengo la Utafiti ............................................................................................. 14
2.5 Matumizi ya Lugha ........................................................................................ 14
2.5.1 Tamathali za semi ........................................................................................... 14
2.5.2 Kejeli .............................................................................................................. 16
2.5.3 Sitiari .............................................................................................................. 16
2.5.4 Tashihisi ......................................................................................................... 17
2.5.5 Tashibiha ........................................................................................................ 17
2.5.6 Takriri ............................................................................................................. 17
2.5.8 Tashtiti ............................................................................................................ 18
2.5.9 Mdokezo ......................................................................................................... 18
2.6 Dhana ya Dhamira .......................................................................................... 19
2.7 Kiunzi cha Nadharia ....................................................................................... 20
2.7.1 Nadharia ya fasihi ya jamii ............................................................................. 21
2.8 Hitimisho ........................................................................................................ 22
SURA YA TATU ..................................................................................................... 23
MBINU NA NJIA ZA UTAFITI ......................................................................... 23
3.1 Utangulizi ...................................................................................................... 23
3.2 Eneo la Utafiti ................................................................................................ 23
3.3 Kundi Lengwa ................................................................................................ 23
x
3.4 Usampulishaji ................................................................................................. 24
3.5 Sampuli .......................................................................................................... 24
3.6 Mbinu za ukusanyaji data .............................................................................. 24
3.6.1 Mbinu ya Usomaji Matini mbalimbali ........................................................... 24
3.7 Zana za Utafiti ................................................................................................ 25
3.7.1 Matini ............................................................................................................. 25
3.7.2 Kompyuta ....................................................................................................... 26
3.7.3 Simu ya mkononi ........................................................................................... 26
3.8 Hitimisho ........................................................................................................ 26
SURA YA NNE ......................................................................................................... 27
UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA .............................................. 27
4.1 Utangulizi ....................................................................................................... 27
4.2 Vipengele vya Lugha katika Tamthiliya Teule ............................................... 27
4.3 Mdafao wa Ujitokezaji wa Vipengele vya Lugha katika Tamthiliya za
Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani .............................................. 28
4.4 Uteuzi na Matumizi ya Tamathali za Semi .................................................... 29
4.4.2 Nidaa .............................................................................................................. 31
4.4.3 Tashibiha ........................................................................................................ 33
4.4.4 Tashihisi ......................................................................................................... 34
4.4.5 Sitiari .............................................................................................................. 35
4.4.6 Takriri ............................................................................................................. 37
4.4.7 Tashtiti ............................................................................................................ 38
4.4.8 Tanakali Sauti ................................................................................................. 39
4.4.9 Kejeli .............................................................................................................. 40
xi
4.4.10 Mdokezo ........................................................................................................ 41
4.5 Misemo ........................................................................................................... 42
4.6 Methali ........................................................................................................... 44
4.7 Nahau ............................................................................................................. 45
4.8 Tamathali za Semi katika Tamtiliya ya Kinjeketile .................................. 46
4.8.1 Nidaa .............................................................................................................. 47
4.8.2 Takriri ............................................................................................................. 48
4.8.3 Sitiari .............................................................................................................. 50
4.8.4 Tashibiha ........................................................................................................ 51
4.8.5 Kejeli .............................................................................................................. 52
4.8.6 Tashtiti ............................................................................................................ 53
4.8.7 Tashihisi .......................................................................................................... 54
4.8.8 Mdokezo ......................................................................................................... 54
4.9 Methali ........................................................................................................... 55
4.10 Misemo ........................................................................................................... 56
4.11 Kuwasilisha Dhamira kuu za Tamthiliya ........................................................ 57
4.12 Kulinganisha na Kulinganua Vipengele vya lugha katika Tamthiliya za
Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani ................................................ 59
4.13 Kufanana ........................................................................................................ 59
4.14 Kutofautiana ................................................................................................... 61
4.15 Kufanana au Kutofautiana kwa Dhamira Zilizojitokeza katika Tamthiliya
Teule ............................................................................................................... 62
4.15.1 Matabaka ........................................................................................................ 62
4.15.2 Uongozi Mbaya .............................................................................................. 63
xii
4.15.3 Nafasi ya Mwanamke ..................................................................................... 63
4.15.4 Umaskini ........................................................................................................ 64
4.15.5 Rushwa na Usaliti ........................................................................................... 64
4.15.6 Mapenzi .......................................................................................................... 65
4.15.7 Ukombozi ....................................................................................................... 65
4.15.8 Hitimisho ........................................................................................................ 66
SURA YA TANO ..................................................................................................... 67
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO ........................................... 67
5.1 Utangulizi ....................................................................................................... 67
5.2 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti .................................................................. 67
5.3 Hitimisho ........................................................................................................ 71
5.4 Mapendekezo ................................................................................................. 73
MAREJELEO .......................................................................................................... 74
xiii
ORODHA YA MAJEDWALI
Jedwali Na 4.1: Vipengele vya lugha katika Nyerere na Safari ya Kanaani ........... 27
Jedwali Na 4.2: Vipengele vya Lugha katika Tamthiliya ya Kinjeketile ................... 28
Jedwali Na 4.3: Mdafao wa Ujitokezaji wa Vipengele vya Lugha katika
Tamthiliya ya Kinjeketile na Nyerere na Safari yaKanaani ............ 28
Jedwali Na 4.4: Ujitokezaji wa Tamathali za Semi katika Tamthiliya ya
Nyerere na Safari ya Kanani ............................................................ 30
Jedwali Na 4.5: Mdafao wa Ujitokezaji wa Tamathali za Semi katika
Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani .................................. 30
Jedwali Na 4.6: Mifano ya baadhi ya Nidaa katika Tamthiliya ya Nyerere
na Safari yaKanaani ......................................................................... 32
Jedwali Na 4.7: Tashibiha katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani ...... 33
Jedwali Na 4.8: Baadhi yaTashihisi Zilizojitokeza katika Tamthilia ya Nyerere na
Safari ya Kanaani ............................................................................ 35
Jedwali Na 4.9: Sitiari katika Tamthiya ya Nyerere na Safari ya Kanaani ............... 36
Jedwali Na 4.10: Ujitokezaji wa Takriri katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari ya Kanaani ............................................................................ 37
Jedwali Na 4.11: Ujitokezaji wa Tashtiti katika Tamthiliya ya Nyerere
na Safari ya Kanaani ........................................................................ 38
Jedwali Na 4.12: Matumizi ya baadhi ya Tanakali Sauti katika Tamthiliya
ya Nyerere na Safari yaKanaani ..................................................... 40
Jedwali Na 4.13: Ujitokezaji wa Kejeli katika Tamthiliya ya Nyerere
na Safari yaKanaani ......................................................................... 41
xiv
Jedwali Na 4.14: Ujitokezaji wa Mdokezo Katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari yaKanaani ............................................................................. 42
Jedwali Na 4.15: Ujitokezaji wa Misemo katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari yaKanaani ............................................................................. 43
Jedwali Na 4.16: Ujitokezaji wa Methali katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari yaKanaani ............................................................................. 44
Jedwali Na 4.17: Ujitokezaji wa Nahau katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari ya Kanaani ............................................................................ 45
Jedwali Na 4.18: Mdafao wa Ujitokezaji wa Tamathali za Semi katika
Tamthiliya ya Kinjeketile ................................................................. 47
Jedwali Na 4.19: Ujitokezaji wa Nidaa katika Tamthilia ya Kinjeketile ................... 48
Jedwali Na 4.20: Ujitokezaji wa Takriri katika Tamthiliya ya Kinjeketile ................ 49
Jedwali Na 4.21: Ujitokezaji wa Sitiari katika Tamthiliya ya Kinjeketile ................. 50
Jedwali Na 4.22: Ujitokezaji wa Tashibiha katika Tamthiliya ya Kinjeketile ........... 51
Jedwali Na 4.23: Ujitokezaji wa Kejeli kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile ..... 52
Jedwali Na 4.24: Ujitokezaji wa Tashititi katika Tamthiliya ya Kinjeketile............. 53
Jedwali Na 4.25: Ujitokezaji wa tashihisi katika Tamthiliya ya Kinjeketile............ 54
Jedwali Na 4. 26: Ujitokezaji wa Mdokezo katika Tamthiliya ya Kinjeketile ........... 55
Jedwali Na 4.27: Ujitokeazji wa Methali katika Tamthiliya ya Kinjeketile ............. 56
Jedwali Na 4.28: Ujitokezaji wa misemo katika Tamthiliya ya Kinjeketile .............. 56
Jedwali Na 4.29: Ujitokezaji wa Dhamira katika Tamthiliya Teule .......................... 57
Jedwali Na 4.30: Ujitokezaji wa Dhamira katika Tamthiliya ya Kinjeketile ............ 58
Jedwali Na 4.31: Vipengele vya Lugha Vinavyofanana katika Tamthiliya Teule ... 60
Jedwali Na 4.32: Vipengele vya Lugha Vinavyotofautiana katika Tamthiliya
xv
Teule ................................................................................................. 61
Jedwali Na 4.33: Kufanana kwa Dhamira Zilizowasilishwa na Vipengele
vya Lugha ......................................................................................... 62
Jedwali Na 4.34: Kutofautiana kwa Dhamira zilizowasilishwa na Vipengele vya
Lugha................................................................................................ 64
1
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI
1.1 Utangulizi
Sura hii tangulizi inatoa usuli wa mada katika utafiti huu. Sura hii inahusu usuli
wa mada, tamko la tatizo la utafiti,malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu
wa utafiti, mipaka ya utafiti, uzingativu wa maadili, vikwazo vya utafiti, utatuzi wa
vikwazo, muundo wa tasnifu na hitimisho. Kabla ya kuanza tupate historia fupi ya
wasanii wa tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani.Tamthiliya ya
Kinjeketile imetungwa na msanii Ebrahim Hussein (1969) ambaye ni msanii
aliyeandika kazi hii ya kisanii kwa kutumia tukio la kihistoria lililotokea Kusini
mwa Tanzania. Wananchi wa Kusini walipambana na Mjerumani ili kumwondoa
katika ardhi yao. Mwandishi ameonesha jinsi wananchi walivyoamini kuwa maji ni
kinga ya vita kwa kuwa itafanya risasi kuwa maji. Kinjeketile aliaminiwa na
wananchi wa Kusini na kuweza kuwaunganisha makabila ya Kusini kuwa kitu
kimoja na mshikamano na kupambana na Mjerumani. Mwandishi ameendelea
kuonesha kuwa maji yalikuwa ni ishara ya umoja kwa kuwa kupitia imani ya maji
wananchi waliweza kuungana na kupambana na Mjerumani. Msanii E. Hussein
anafaa kuigwa kwa mchango wake katika fasihi ya Kiswahili.
Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani imetungwa na msanii Emmanuel
Mbogo (2015) ambaye ameandika jambo la kihistoria baada ya Tanzania kupata
uhuru. Msanii ametuonesha baada ya uhuru watu wachache walijilimbikizia mali
kwa muda mfupi na kuwa matajiri. Hvyo watu hawa walikuwa wamepingana na Rais
2
Nyerere. Profesa E. Mbogo ni maarufu kwa uandishi wa Drama na Fasihi ya
Kiswahili na mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
1.2 Usuli wa Mada
Katika fasihi yoyote ni lazima iwe na fani na maudhui. Katika fani kunakuwa na
mtindo, lugha, mandhari, na wahusika. Wasanii wa kazi za tamthiliya wanapenda
kutumia vipengele mbalimbali vya lugha katika kazi zao ili kufikisha ujumbe kwa
jamii. Kazi yoyote ya msanii ili iweze kueleweka vizuri lazima lugha ichambuliwe
kufuatana na jinsi ilivyotumika katika vipengele vyake mbalimbali kwa pamoja ili
kuleta maana kamili iliyopo katika kazi hiyo. Kila msanii ana ubunifu wake katika
kuandika kazi yake kwa kubuni mtindo atakaoutumia katika kazi yake kwa mfano
katika kuteua msamiati muundo na lugha. Katika kuchunguza kazi ya msanii ili
kupata ujumbe wa kazi hiyo hatuna budi kuhusisha vipengele vya lugha katika kazi
husika.
Katika utafiti huu tumechunguza matumizi ya lugha iliyotumika kulingana na
vipengele vyake na dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya ya Kinjeketile
iliyoandikwa na Ebrahim Hussein na tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
iliyoandikwa na Profesa Emmanuel Mbogo. Katika kazi hii utafiti umetathmini
matumizi ya lugha iliyotumika katika tamthiliya hizi ikiwa ni pamoja na vipengele
vyake na dhamira zilizojitokeza katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii kwa
kuwalinganisha na kuwatofautisha waandishi hawa wawili. Utafiti huu umekuwa
wa kihistoria umetumia lugha kwa kupitia vipindi mbalimbali kuonesha mchango
wa waandishi hawa katika kazi ya sanaa ya uandishi. Waandishi hawa wamechangia
kukuza historia ya nchi yetu na kuiwezewesha jamii kuona umuhimu wa kusoma
3
tamthiliya za kihistoria ili kupata maarifa ya kihistoria yaliyopo na kuweza kuona
nchi imetoka wapi.
Katika kutathmini matumizi ya lugha utafiti huu umewalinganisha wasanii wawili
ambapo ni msanii E. Mbogo ambaye ni msanii nguli aliyebobea katika kuandika
drama na kuielimisha jamii kupitia tamthiliya zake. Kwa utafiti huu tumetumia
kitabu chake cha Nyerere na Safari ya Kanaani (2015) ambapo ameelezea Nyerere
na harakati za kuimarisha vijana kabla ya kuanza kazi wawe wazalendo kwa
kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa. Vilevile kuwawezesha vijana kujitegemea hata
pale ambapo hawatapata ajira.Tumefanya utafiti pia kwa kutumia tamthiliya ya
Kinjeketile iliyotungwa na msanii Ebrahim Hussein ambaye katika uandishi naye pia
anaibua hisia za usomaji kwa kuandika tamthiliya za Kiswahili. Mwandishi
anaonesha Kinjeketile alivyokuwa akiwaunganisha wananchi wa Kusini wakati
wakipambana na Wajerumani akitetea uhuru wa Waafrika, akilaani uonevu wa
wakoloni kwa Waafrika katika nchi yao kwa kubaguliwa na kutengwa kabisa na
wazungu (Wajerumani). Kinjeketile alionesha maji yalivyotumiwa kama kinga dhidi
ya mashambulizi ya risasi zilizokuwa zikipigwa na Wajerumani. Kinjeketile alitumia
maji kwa kuwaunganisha wananchi kuwa kitu kimoja ili waweze kumshambulia
Mjerumani kwa urahisi. Na alifanikiwa kuyaunganisha makabila ya Kusini mwa
Tanzania na kuwa na imani kuwa watamshinda Mjerumani.
Tamthiliya hizi za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani ni tamthiliya za
kihistoria kwa kuwa zinawazungumzia watu au wanaharakati wa kihistoria katika
nchi yao waliokuwa wakitetea wanachi kutoka katika makucha ya
wakoloni.Wanaharakati hawa walikuwa na uchungu na nchi yao kwa uzalendo
4
waliokuwa nao bila woga walitetea waziwazi uhuru wa nchi yao. Kupitia tamthiliya
hizi jamii imejifunza jinsi nchi zilivyopitia misukosuko katika kuleta mabadiliko
katika nchi yao.
Kupitia kwa wasanii hawa jamii imeendelea kujifunza historia ya nchi kutoka kizazi
kimoja hadi kingine kwa kuwa historia hubaki kuwa historia wakati wote. Hivyo
wasanii huchangia kwa kiasi kikubwa muendelezo wa matukio mbalimbali ambayo
yatabaki kuwa ni historia.Utafiti huu umechunguza na kutathmini matumizi ya lugha
na dhamira ikiwa ni pamoja na vipengele vya lugha kwa kulinganisha tamthiliya ya
Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaan. Aidha umechunguza kutofautiana au
kufanana kwa wasanii hawa katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
1.3 Tamko la Tatizo la Utafiti
Katika kuelezea jambo la kihistoria katika jamii waandishi wa kazi za sanaa
wanaweza kutumia lugha kufikisha ujumbe uliokusudiwa kuwezesha kizazi kimoja
hadi kingine kujifunza historia.Waandishi wa wana jukumu la kutumia lugha
inayomwezesha msomaji kupata ujumbe uliokusudiwa.
Tatizo la utafiti ni kwamba tamthiliya za kihistoria hazijafanyiwa uchunguzi wa kina
na kuweka wazi jinsi lugha na vipengele vyake vinavyoweza kumtofautisha na
kumfananisha msanii mmoja na mwingine katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii.
Kwa utafiti huu tutaweza kuainisha matumizi ya lugha na dhamira zinazojitokeza
katika tamthiliya teule.Pia kulinganisha na kulinganua matumizi ya lugha na dhamira
zilizojitokeza katika tamthiliya hizo.
5
1.4 Malengo ya Utafiti
Utafiti huu umetathmini matumizi ya lugha na dhamira katika tamthiliya za
Kinjeketile (1970) na Nyerere na Safari ya Kanaani (2015) katika kuwasilisha kwa
namna tofauti ujumbe uliokusudiwa kwa jamii.
1.4.1 Lengo Kuu
Kutathmini matumizi ya lugha na dhamira katika tamthiliya teule ili kubaini
vipengele vinavyotofautiana na vinavyofanana katika kutumia lugha kufikisha
ujumbe katika mkabala wa fasihi linganishi.
1.4.2Malengo Mahsusi
Utafiti huu una malengo mahususi yafuatayo:
(i) Kuainisha vipengele vya lugha katika tamthiliya teule.
(ii) Kulinganisha na kulinganua vipengele vya lugha katika tamthiliya teule
kufikisha.
(iii) Kuainisha dhamira zinazojitokeza katika tamthiliya teule.
(iv) Kulinganisha na kulinganua dhamira zinazojitokeza katika tamtiliya teule.
1.5 Maswali ya Utafiti
(i) Ni vipengele vipi vya lugha vinajitokeza katika tamthiliya teule?
(ii) Uteuzi wa vipengele vya lugha katika tamthiliya teule unafanana au
kutofautiana vipi katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii?
(iii) Ni dhamira zipi zinajitokeza katika tamthiliya teule?
(iv) Uteuzi wa dhamira katika tamthiliya teule unafanana au kutofautiana vipi
katika kufikisha ujumbe kwa jamii?
6
1.6 Umuhimu wa Utafiti
Utafiti ni sayansi ya uchunguzi ambao ni muhimu kwa jamii. Katika uchunguzi wa
matumizi ya lugha katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyrere na Safari yaKanaani
utafiti umesaidia kuelimisha jamii kuona jinsi gani hawa wapigania haki Nyerere na
Kinjeketile walivyokuwa wazalendo na dhamira ya ukombozi katika nchi yao.Utafiti
pia umeonesha jinsi Nyerere na Kinjeketile walivyohamasisha watu wao kupigania
uhuru wao. Kukataa kutawaliwa na kuonewa pasipo na sababu za msingi. Pia
umegundua jinsi wananchi walivyokuwa na umoja katika kupigania uhuru waohadi
kujikomboa na kujitoa katika makucha ya wakoloni.
Aidha utafiti huu utakuwa changamoto kwa watafiti wengine kufanya utafiti juu ya
tamthiliya za Kiswahili zilizojikita katika historia ya mambo mbalimbali yaliyotokea
katika jamii.
1.7 Mipaka ya Utafiti
Utafiti huu umetathmini matumizi ya lugha na dhamira zilizojitokeza katika
tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani.
Zipo tamthiliya nyingi za kihistoria lakini kwa sasa nimeshughulikia tamthiliya za
kihistoria za Kinjeketile iliyoandikwa na Ebrahim Hussein na Nyerere na Safari ya
Kanaani iliyoandikwa na Emmanuel Mbogo. Vipengele vya lugha tamathali za
semi,misemo, methali na nahau ndivyo vimetumika katika kujenga hii kazi ya fasihi.
1.8 Uzingativu wa Maadili
Katika utafiti huu kipengele hiki cha uzingativu wa maadili umejadili masuala
yaliyomwezesha mtafiti kuzingatia, na kudumisha maadili yake kabla na baada ya
7
kukusanya data. Masuala ya kimaadili huibuka katika aina zote za utafiti usio wa
kitakwimu na ulio wa kitakwimu, Padget (2002) katika kipengele hiki mtafiti
ametakiwa kuzingatia usiri,uwazi, utii, ushiriki wa hiari au kujitolea kwa watafitiwa
bila kulazimishwa, kutokuwa na lugha chafu au kali, uvunjivu wa amani, na kuomba
ruhusa ya utafiti wake katika maeneo aliyoyafanyia utafiti.
Aidha mtafiti wa utafiti huu aliomba kibali kilichomtambulisha kuwa yeye ni
mwanachuo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania cha kuingia katika maktaba ili
kuweza kusoma tafiti za Kiswahili na machapisho mbalimbali yanayohusiana na
utafiti huu.
1.9 Vikwazo vya Utafiti
Vikwazo vya utafiti ni jumla ya changamoto mbalimbali zilizokabili utafiti huu.
Changamoto hizo ni uhaba wa fedha kwa ajili ya kufanya utafiti huu. Pia mtafiti ni
mwajiriwa wakati huo huo anasoma hivyo amekabiliwa na changamoto ya muda wa
kutafuta marejeleo, vitabu vya tamthiliya teule na kukutana msimamizi kwa
maelekezo.
1.10 Utatuzi wa Vikwazo
Mtafiti alijiwekea mikakati mizuri ya kukabiliana na changamoto hizo ili aweze
kufikia malengo ya utafiti wake. Ilibibidi mtafiti kubana matumizi kulingana ufinyu
wa bajeti kutokana na pesa kidogo ya kugharamia utafiti huu. Pesa ilitoka kwa
mtafiti mwenyewe na siyo kwa mfadhili. Hapa mtafiti ilimbidi kutumia pesa
aliyoiandaa kwa usahihi. Mtafiti aliangalie safari zake kwa umakini ili kuepuka
gharama zisizo za lazima. Aidha kuhusu suala la muda, mtafiti alifanya shughuli hizi
8
jioni baada ya kazi na wakati mwingine ilimlazimu kuomba ruhusa ili aweze
kuonana na msimamizi kwa maelekezo juu ya utafiti wake.
1.11 Muundo wa Tasnifu
Utafiti huu umegawanyika katika sehemu tano. Sura ya kwanza inahusu utangulizi
wa jumla wa utafiti, uchunguzi umeonesha kuwa tatizo la utafitilimejadiliwa na
kutolewa maelezo kwa undani. Sura ya pili inahusu usomaji wa kazi tangulizi na
mkabala wa kinadharia, ambapo sura ya tatu imejadili mbinu za utafiti, mbinu za
ukusanyaji data, na zana za utafiti. Sura ya nne imeonesha uwasilishaji na uchambuzi
wa data za utafiti huu. Aidha sura ya tano imewasilisha muhtasari wa matokeo ya
utafiti, hitimisho na mapendekezo ya mtafiti.
1.12 Hitimisho
Sura hii imejadili juu ya usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali
ya utafiti, umuhimu wa utafiti, mipaka ya utafiti, uzingativu wa maadili vikwazo vya
utafiti, utatuzi wa vikwazo na muundo wa tasnifu. Sura inayofuata
inawasilishamapitio ya kazi tangulizi na kiunzi cha nadharia.
9
SURA YA PILI
MAPITIO YA KAZI TANGULIZI NA KIUNZI CHA NADHARIA
2.1 Utangulizi
Katika sura hii maandiko na tafiti mbalimbali zinazohusiana na mada ya utafiti
zimejadiliwa kwa kina na mwisho kuibua pengo la utafiti ambalo limeweka
msukumo wa kufanya utafiti huu. Sura hii imeelezea dhana ya fasihi linganishi.
Sehemu ya pili inahusu tafiti kuhusu tamthiliya za Kiswahili. Aidha sura hii
imefafanua, pengo la utafiti, matumizi ya lugha, kiunzi cha nadharia, na hitimisho.
2.2 Dhana ya Fasihi Linganishi
Jilala (2016) akiwanukuu Wallek na Warren (1948), anasema fasihi linganishi ni
mbinu itumiwayo na wahakiki wengi wa fasihi hata wanasayansi kwa kujadili njia
maalum ya usomaji wa sanaa mbalimbali ulimwenguni. Ulinganishi unaweza kuwa
wa fasihi ya Kiafrika na kizungu, ama fasihi ya kizungu dhidi ya Kihindu n.k.
Guyard (1964) anasema kuwa fasihi linganishi ni tawi la historia ya fasihi ambapo
anadai ni somo la mahusiano, mapatano na maelewano ya kimataifa baina ya kazi na
maisha ya waandishi wanaotoka katika fasihi tofauti.
Jilala (2016) akimnukuu Wamitila (2003), ameizungumzia dhana ya fasihi linganishi
kwa kusema kuwa ni mbinu ya kuchunguza, kuchambua na kueleza sifa mfanano
zilizopo katika matini ya fasihi. Na kwamba dhana yenyewe huenda sambamba na
dhana ya ulinganuzi. Ulinganuzi ni mbinu ya kuchunguza, kuchambua na kuonesha
sifa zinazotofautiana baina ya matini zaidi ya moja za kifasihi. Kwa hiyo ulinganishi
10
na ulinganuzi sharti uzingatie fani na maudhui. Fasihi ya Wamitila inatupatia jambo
jipya kuzingatia upamoja wa dhana za kulinganisha na kulinganua.
Kwa upande mwingine Van Tieghem kama alivyonukuliwa na Wallek (1988)
anafasili fasihi linganishi kuwa ni somo linalojishughulisha na uhusiano wa vitu
viwili. Vitu hivi vinaweza kuwa kazi ya mtu binafsi, waandishi wa kundi la
waandishi au kundi la waandishi na binadamu au fasihi kwa ujumla. Kwa upande
wake Wallek (1988) anaiona fasihi linganishi kuwa ni somo la fasihi nnje ya mipaka
ya nchi moja ni kujifunza uhusiano baina ya fasihi kwa upande mmoja na eneo
jingine la maarifa, sanaa, falsafa, historia ya sanaa za jamii, sayansi na dini. Kwa
upande mwingine anaielezea kwa ufupi kuwa ni ulinganishi wa fasihi na fasihi
nyingine na ulinganishi wa fasihi mzunguko wa maelezo ya binadamu.
Ponera (2014) anasema fasihi linganishi ni kitendo cha kulinganisha au kufanya
tathmini ya vitu viwili au zaidi ili kujua ubora, kufanana au kutofautiana kwavyo.
Mtu yeyote anayehitaji kulinganisha au kufanya linganisho lazima atahitaji kwanza
kuwa na mahitaji kwa ajili ya kazi hiyo. Mosi, anhitaji kuwa na maarifa na ujuzi juu
ya vilinganiswavyo. Pili, kuwapo kwa vitu viwili au zaidi vinavyolinganishwa. Na
tatu, kuwapo kwa kigezo au vigezo maalum vya kulinganishia.
Bassnett (1993) anaiona fasihi linganishi kuwa ni taaluma ya usomaji matini za
tamaduni tofauti ili kubaini mazingira yanapokutana na yanapoachana. Nao Wallek
ona Warren (1996) wanaielezea fasihi linganishi kuwa ni mbinu itumiwayo na
wahakiki wengi wa fasihi, hata wanaulimbe kujadili njia maalum ya usomaji wa
sanaa mbalimbali ulimwenguni.
11
Fasihi linganishi hujihusisha na ulinganishaji wa fasihi na kazi nyingine ambazo ni
za kisanii, kwa mfano mlinganishi anaweza kuchunguza uhusiano wa filamu na
fasihi, kazi za sanaa ya uchongaji, uchoraji na uhunzi na fasihi. Aidha, kwa kutumia
fasihi linganishi, tunaweza kulinganisha kazi za fasihi za mwandishi mmoja katika
vipindi tofauti ama katika kipindi kimoja cha kihistoria. Kwa mfano tunaweza
kulinganisha kazi za fasihi za Shaaban Robert katika vipindi tofauti vya uandishi au
kulinganisha kazi za fasihi za Semzaba za kipindi cha miaka ya sabini na kipindi cha
miaka ya elfu mbili. Hii itatuonesha kufanana, kutofautiana na kuhusiana kwa uteuzi
na matumizi ya lugha na maudhui yanayowasilishwa na namna yanavyowasilishwa.
Pia katika fasihi linganishi, tunaweza kulinganisha kazi za fasihi za wasanii
wanaotoka katika maeneo tofauti ya kijiografia, au eneo moja la kijiografia au
wenye utamaduni mmoja. Kwa kufanya hivyo tunaweza kuibua matumizi ya lugha
na vipengele vyake na dhamira zinazojitokeza ambazo zinawafananisha au
kuwatofautisha wasanii. Tunaweza kusema kuwa fasihi linganishi ni mbinu
inayohusisha ulinganishaji wa kazi za fasihi kwa lengo la kuchunguza jinsi kazi hizo
zinavyofanana, na kutofautiana katika matumizi ya lugha na vipengele vyake na
dhamira zinazojitokeza. Hivyo utafiti huu ni utafiti linganishi unaolenga kutathmini
matumizi ya lugha na dhamira katika tamthiliya za Kinjeketile (1969) na Nyerere na
Safari yaKanaan (2015). Lengo la utafiti huu ni kubainisha vipengele vya lugha na
dhamira pia kuona jinsi vinavyofanana na kutofautiana.
2.3 Tafiti kuhusu Tamthiliya za Kiswahili
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu tamthiliya za Kiswahili lakini nyingi zilijikita
katika kuchambua lugha na maudhui kwa ujumla na si kutathmini matumizi ya lugha
12
na dhamira ambazo zimetumika katika utafiti huu. Kazi hizo ni za Kinge’i (1987),
Ligembe (1995), Ramadhani (2005), Saleem (2013) na Mkuhwili (2014).
Kinge’i (1987 utafiti wake ulikuwa juu ya tamthiliya za msanii Ebrahim Hussein.
Katika utafiti wake Kinge’i alimtaja Hussein kuwa ni miongoni mwa watunzi
maarufu wa tamthiliya za Kiswahili.Tamthiliya za Hussein amabazo Kinge’i
amezichambua ni Alikiona (1970), Wakati Ukuta (1970) na Arusi (1980) na kuona
kuwa msanii huyu ana uwezo mkubwa wa kutumia lugha kama chombo cha
kusafirishia ujumbe au maudhui yake katika jamii. Katika nadharia tumeona kuwa
lugha ndiyo inayobeba kazi yote ya fasihi kutegemeana na jinsi lugha hiyo
ilivyotumika. Utafiti huu unatofautiana na utafiti wa Kinge’ i kwa kuwa utafiti huu
ni linganishi unaolinganisha kazi mbili za wasanii tofauti waliobobea katika ya
uandishi wa fasihi zaidi ya miongo mitatu. Katika tamthiliya zao tumetumia
tamthiliya moja ya hivi karibuni ya Mbogo (2015) Nyerere na Safari ya Kanaani na
tamthiliya ya iliyoandikwa zamani Hussein (1969) Kinjeketile katika kutathmini
matumizi ya lugha na dhamira zilizojitokeza katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
Ligembe (1995) alichambua sitiari katika kazi ya tamthiliya ya Lina Ubani
iliyoandikwa na Penina Mhando. Katika utafiti wake amejadili muundo na umbo la
tamthiliya na kubainisha aina za sitiari. Amebainisha kiungo kifananishi na
kizungumzwa na kuelezea mchango wake katika uelewa wa tamthiliya. Katika utafiti
wake hakuonesha uhusiano uliopo baina ya aina ya sitiari na ujenzi wa maana katika
tamthiliya. Tofauti na utafiti wa Ligembe, utafiti huu ni utafiti linganishi ambao
ulilenga kulinganisha na kulinganua kazi za tamthiliya za waandishi wawili ili
13
kubaini vipengele vya lugha vinavyowafananisha na kuwatofautisha katika
kuwasilisha ujumbe kwa jamii.
Ramadhan (2005) alifanya utafiti kuangalia matumizi ya sitiari katika tamtlhiiya ya
Morani iliyoandikwa na Mbogo na Mashetani iliyoandikwa na Hussein. Alitumia
utafiti linganishi kwa kutumia nadharia ya elimumtindo ambapo amelinganisha
tamthiliya mbili. Alihitimisha kuwa sitiari hutumika katka ujenzi wa dhamira
mbalimbali katika tamthiliya zote mbili. Tofauti na utafiti alioufanya Ramadhan
utafiti huu ulijikita katika kutathmini matumizi ya lugha na dhamira zilizojitokeza
katika tamthiliya teule, kwa kutumia nadharia ya fasihi ya jamii kwa kuwa inahifadhi
historia ya jamii.
Saleem (2013) alifanya utafiti linganishi katika wa tamthiliya za Mashetani na Kivuli
Kinaishi. Katika tasnifu yake ya uzamivu alibaini tamthiliya ya Mashetani na Kivuli
Kinaishi zinafanana na kuhusiana katika mbinu za kimtindo na maudhui yake.
Tofauti na utafiti wa Saleem, utafiti huu ulihusisha kutathmini vipengele vya lugha
na dhamira zilijitokeza katika tamthiliya teule kwa kulinganisha na kulinganua
vipengele hivyo.
Mkuhwili (2014) alifanya utafiti linganishi katika tamthiliya za Ngoma
yaNgw’anamalundi na Kivuli kinaishi. Lengo lilikuwa ni kulinganisha katika
tamthiliya hizo. Alibaini kuwa wasanii hawa wanatofautina na kufanana katika
baadhi ya vipengele vya kifani. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya elimumtindo
ambao unamtofautisha msanii mmoja na mwigine katika mtindo wa uandishi wa
14
kazi ya fasihi.Tofauti na utafiti wa Mkuhwili, utafiti huu umetathmini matumizi ya
lugha na dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya teule.
2.4 Pengo la Utafiti
Tafiti zimekwishafanywa juu ya ulinganifu wa kazi za tamthiliya. Utafiti
haukutathmini matumizi ya lugha na dhamira katika fasihi linganishi kwa
kuwasilisha jambo la kihistoria. Utafiti huu unahitajika ili kuweza kutathmini
matumizi ya lugha na dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya tofauti na waandishi
tofauti. Utafiti huu ili ufikie lengo umetathmini matumizi ya lugha na dhamira
zilizojitokeza katika kuwasilisha ujumbe, mtafiti ametumia tamthiliya za Kinjeketile
na Nyerere na Safari ya Kanaani.
2.5 Matumizi ya Lugha
Jilala (2016) anasema lugha ni kipengele muhimu katika kazi za fasihi kwani ndiyo
daraja linalounganisha hadhira na msanii katika mawasiliano. Katika kazi ya fasihi
lugha hubeba dhamira, migogoro na ujumbe mbalimbali aliokusudia mtunzi kwa kazi
hiyo ya fasihi. Ni kipengele muhimu sana kwa sababu hutofautisha fasihi na sanaa
nyingine kama vile uchoraji na uchongaji. Tunapojadili matumizi ya lugha katika
kazi za fasihi tunazingatia vipengele vifuatavyo: misemo, nahau, methali tamathali
za semi na lugha za wahusika, hasa lahaja zao (Senkoro, 2011). Sehemu inayofuata
inajadili vipengele vya lugha
2.5.1 Tamathali za semi
Jilala (2016) tamathali za semi ni maneno au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii
wakati wanapofanya kazi ya fasihi ili kutia nguvu katika maana na hata sauti katika
15
maandishi ama maneno. Wakati mwingine tamathali za semi hutumiwa kwa njia ya
kuipamba kazi ya fasihi na kuongeza utamu katika lugha. Ni semi zenye kupanua,
kupuuza au kubadilisha maana dhahiri au za kawaida za maneno ili kuwasilisha
ujumbe na maana iliyokusudiwa na mtunzi kwenda kwa hadhira.
Wamitila (2003) anasema tamathali ya (za) semi hutumika kuelezea fungu la maneno
au hata neno ambalo limegeuzwa maana yake ya kiurejezi au asilia na kuwa na
maana nyingine. Kwa ujumla tunaweza kusema tamathali za semi ni vifananisho au
viwakilisho vya dhana fulani kwa kutumia dhana nyingine tofauti au zinazofanana
nazo ambazo hutumiwa kwa lengo la kupanua, kupuuza, kubadilisha maana za
dhahiri au za kawaida, ili kuwasilisha ujumbe na maana iliyokusudiwa kwahadhira
au jamii mahsusi.
Senkoro (2012) anaainisha tamathali za semi kuwa ni sitiari, tashibiha, metonomia,
tashihisi, majazi, ishara, taashira na kejeli.Tamathali za semi huweza kutumika
katika ulinganishi wa kazi za fasihi kwa kulinganisha na kulinganua jinsi
zillivyotumika katika kazi moja na nyingine. Mulokozi na Kahigi (1979) wanasema
kuwa tamathali zinazotumika zaidi katika ushairi ni tashibiha, tashihisi, kejeli,
metonimia, na sitiari.
Na tamathali zinazotumika zaidi katika kazi za kifasihi hasa katika tamthiliya na
riwaya ni tashibiha, takriri, tanakalisauti, nidaa, sitiari, kejeli, tashihisi, tafsida,
tashtiti na mdokezo. Katika sehemu hii mtafiti ameeleza maana ya tamathali chache
zitakazotumika katika utafiti huu, ili kuwasilisha ujumbe kwa jamii iliyokusudiwa.
Sehemu ifuatayo inajadili kuhusu tamathali za semi.
16
2.5.2 Kejeli
Hii ni tamathali ambayo maneno yake huwa kinyume kabisa na maana
inayokusudiwa mfano mtu ni mchafu hukuna mfano wake lakini anaambiwa yeye
ndiye msafi kuliko wote. Kamusi ya Kiswahili sanifu (1981:105) wanasema kuwa
kejeli ni maneno ya dharau, fanyia mzaha wa kuchosha.
Kamusi ya Wales (2001:224) inasema, kuwa kejeli hutokea pale ambapo maneno
yanayotumiwa yanaelekea kukinzana na maana inayohitajika katika muktadha
maalum inayokusudiwa na mwandishi, msemaji au mtumiaji. Huangalia mbinu ya
ulaghai, kinyume cha mambo, udanganyifu au masimulizi yasiyo ya kweli ndani
yake katika kuzungumzia kumkebehi au kumteta mtu fulani.
Short (1980:277) anafafanua kuwa mbinu ya kejeli ni ushirikiano kati ya mwandishi
au msemaji na msomaji au msikilizaji au hadhira. Mbatiah(2001) anasema kuwa
kejeli ni maneno yanayotumiwa katika matamshi kwamadhumuni ya kuchoma,
kukata, au kutia uchungu.Wamitila (2008:410) anaendelea kusema kuwa kejeli ya
kiusemi inaelezwa kama ni kejeli ya kimsingi sana na hutokea pale ambapo pana
mkinzano fulani baina ya kile kinachosemwa na uhalisia wenyewe.
2.5.3 Sitiari
Jilala (2016) anafafanua sitiari ni tamathali ya semi inayolinganisha vitu viwili bila
vilinganishi vyovyote. Ni ulinganishi wa moja kwa moja mfano Bwana Juma ni
simba. Muundo wa sitiari una vipengele vitatu yaani kile knachozungumzwa,
kifananisho na kiungo (Lakoff na Johnson 1980). Ili kuelewa dhana ya sitiari tutumie
mfano huu Juma ni simba. Katika mfano huu Juma amegeuka kuwa simba yaani
17
mnyama; bali sifa za simba zinahamishiwa kwake. Yaani simba ana sifa ya ukali
unaosababishwa na simba anahusishwa na ukali wa Juma. Muundo wa sitiari una
vipegele vitatu: kizungumzwa, kifananisho na kiungo (Lakoff & Johnson, 1980;
Kahigi 1995). kizungumzwa ni kitajwa, ambapo katika mfano wetu ni Juma;
Kifananishi ni kitu kinachohusishwa na kizungumzwa na katika mfano wetu ni
simba na kiungo ni tabia au sifa zinazounganisha kizungumzwa na kifananishi hapa
ni sifa ya ukali.
2.5.4 Tashihisi
Katika tamathali hii vitu visivyo na sifa walizonazo binadamu hupewa sifa hizo
mfano baridi kali ilimkaribisha alipofika Makambako. Wamitila (2003) anasema
tashihisi ni tamathali ya semi vitu visivyokuwa na uhai huwasilishwa kwa namna
sawa na binadamu na kuweza kufikiri na kuhisi sawa na afanyayo binadamu.
2.5.5 Tashibiha
Senkoro (1982) anafaili tashibiha ni tamathali ya semi ambayo watu ama vitu viwili
au zaidi hulinganishwa kwa kutumia vilinganishi kama vile mithili ya, mfano wa,
kama, sawa na, kama kwamba mfano Juma ni mweusi kama mkaa. Hapa tashibiha
imetumika kulinganisha rangi ya bwana Juma na mkaa. Dhana hii ya ulinganishaji
hutumika tabia, sifa zinazolinganishwa hivyo weusi wa bwana Juma unalinganishwa
na mkaa.
2.5.6 Takriri
Ni mbinu ya kurudiarudia maneno kwa ajili ya kusisitiza jambo, mfano kwenye
nyimbo na mashairi, tamathali hii hutumika zaidi. Jilala (2016), akiwanukuu Kahigi
18
na Mulokozi (1979), anaielezea takriri kuwa ni uradidi yaani urudiaji wa sauti, neno,
kirai, kishazi na hata sentensi katika kazi za kifasihi.
2.5.7 Nidaa
Huu ni msemo ambao unaonesha kushangazwa kwa jambo fulani na kuambatana na
matumizi ya alama ya mshangao, mfano Lo! Kumbe! La hasha!.Senkoro (2011)
anasema kuwa nidaa ni msemo uanoonesha kushangaa au kushangazwa na jambo
fulani, mfano Haa! Hicho ni kifurushi cha mafumbo!.
2.5.8 Tashtiti
Tashtiti ni mkazo wa maneno yasemayo au kuandikwa. Msanii hutumia mbinuya
kuuliza maswali kwa jambo ambalo analolifahamu jibu lake. Lengo ni kusisitiza
jambo na kuleta mshangao (Msokile 1992:62).
2.5.9 Mdokezo
Mdokezo ni tamathali ambayo mtu hudokeza kitu fulani na kukiacha
bilakukikamilisha kwa maana kwamba kinaweza kukamilishwa na mtu mwingine
kisanaa. (J.P.OCompany2008:45). Jilala (2016) akiwanukuu Cuddon (1998),
anafasili kuwa mdokezo ni mbinu ya msanii kuishirikisha hadhira yake uzoefu fulani
wa maisha.
Mara nyingi msanii wa kazi ya fasihiatumiapo mdokezo katika kazi ya fasihi
anakuwa na lengo la kumfikirishamsomaji au hadhira juu ya jambo analolizungumza.
Hivyo ni jukumu la hadhira kufikiri na kukamlisha wazo la msanii katika kazi yake
kifasihi.
19
2.6 Dhana ya Dhamira
Kwa mujibu wa Jilala (2016), anasema dhamira ni jumla ya mambo yanayojadiliwa
katika kazi ya fasihi. Senkoro (1982) anasema dhamira za kazi za fasihi hujitokeza
kulingana na matukio ya jamii, wakati, mabadiliko ya jamii na historia ya jamii. Kwa
mfano dhamira zilizoibuliwa kipindi cha ukoloni zililenga kuibua suala la ukoloni na
unyonyaji.
Senyamanza (2012) anaeleza kuwa dhana ya dhamira isichanganywe na dhana ya
maudhui kwa sababu dhana hizo ni tofauti. Hivyo aliwanukuu TUMI (1992), kuwa
dhamira ni kiini cha suala linalozungumzwa na mwandishi katika kazi yake.
Dhamira ni sehemu mojawapo tu ya maudhui ya kazi ya fasihi. Kwa ujumla dhamira
kuu ndiyo husindikizwa na dhamira ndogo ndogo na hizi ndizo zijengazo dhamira
kuu. Wazo kuu ambalo hasa ndilo libebalo wazo kuu hutoa dhamira kuu.
Naye Madumula (2009) anaunga mkono mawazo ya TUMI, akielezea kuwa dhamira
ni wazo kuu katika kazi ya fasihi. Anaendelea kuelezea kuwa Senkoro
anatahadharisha kuchanganya dhamira na maudhui jambo ambalo hutokea kwa
wengi. Dhamira ni sehemu tu ya maudhui. Na aghalabu dhamira kuu ndio
husindikizwa na dhamira ndogondogo. Wazo kuu hubeba funzo kuu.
Kwa mujibu wa Jilala (2016), katika kipindi cha janga la UKIMWI duniani, wasanii
walielekeza jicho la kisanii katika kuibua dhamira zenye lengo la kuonesha matatizo,
chanzo, dalili, uenezaji na namna ya kujikinga na athari ya UKIMWI katika jamii.
Dhamira ni kipengele ambacho kinaweza kuhusishwa katika ulinganishaji wa kazi za
fasihi. Dhamira hutusaidia kuonesha wasanii wanavyotofautiana katika kuibua
20
matukio ya kijamii na kuimulika jamii kwa tochi ya kisanii. Kwa kulinganisha
dhamira za kazi mbalimbali za fasihi tunaweza kubaini muingiliano na mahusiano
ya dhamira za duniani, kuhama kwa dhamira na kusambaa kwa dhamira kulingana na
wakati, mazingira na muktadha.
2.7 Kiunzi cha Nadharia
Jilala (2016) anasema nadharia ni wazo ambalo huibuliwa kama mwongozo kwa
msomaji ama mchambuzi na hata mwanafasihi linganishi katika kutoa majumuisho
ya kazi za fasihi. Aidha ni wazo kuu, fikra kuu, mwongozo wa mtu au watu jamii ya
mahali fulani wakati fulani kwa lengo maalum. Nadharia humwongoza mtu kutenda
jambo fulani kwa utaratibu mzuri. Kwa hiyo nadharia ndiyo msingi mkuu wa kuweza
kueleza jambo fulani ili liweze kukubalika, kuaminika na kufanyiwa kazi na watu wa
jamii husika ama taaluma ya fani husika.
Wanjala (2011) anasema nadharia ni mwongozo au maarifa yanayotumiwa na
binadamu kwa kukabiliana na mazingira yake. Au nadharia ni mfumo wa mawazo au
maarifa yanayofasili taaluma mahsusi kwa kutoa mtazamo au falsafa juu ya
matumizi na taratibu za utafiti.
Sengo (2009) anasema nadharia ni wazo kuu, fikra, mwongozo mkuu wa mtu au
watu (jamii), wa pahala fulani wakati fulani kwa sababu fulani. Kuna nadharia za
aina mbalimbali zinazotumika katika kuchunguza na kuchambua kazi mbalimbali za
fasihi. Nadharia fulani inaweza kufaa kutumika kuchambua kazi ya fasihi na
nadharia nyingine isiweze kufaa kutumika kuchambua kazi hiyohiyo kulingana na
21
malengo ya utafiti huo. Baadhi ya nadharia zinazoweza kuchambua kazi za fasihi ni
ufeministi, umuundoleo, umaksi, elimumtindo, nadharia ya fasihi ya jamii na
mwitkio wa msomaji.Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya fashi ya jamii.
2.7.1 Nadharia ya fasihi ya jamii
Uhusiano wa fasihi na jamii umethibitishwa kupitia fasili nyingi za fasihi na
uhusiano wa taasisi hizi mbili hauwezi kupuuzwa hivyo fasihi ni taasisi ya jamii.
Mmoja wa wanaounga mkono dhanna hii ni Escarpit (1974), ambaye anasema, fasihi
ni lazima ichukuliwe kama iliyo na uhusiano usiotatanika na maisha ya jamii. Fasihi
ni taasisi ya jamii kwani hutumia lugha ambayo ni wazo la jamii kwamba fasihi ni
sehemu ya maisha ya jamii. Maisha kuhusu uhalisiya wa jamii, hata kwa mtu binafsi
ni mambo ambayo fasihi inazingatia. Kwa hiyo fasihi inayo dhima kuu katika jamii.
Nao Wallek na Warren (1949), wanashadidia kwa kusema, “Uhusiano kati ya fasihi
na jamii hujadiliwa kwa kuanza na kauli aliyoitoa De Bonaid kwamba “Fasihi ni
kielelezo cha jamii.” Kwa kutumia nadharia ya fasihi ya jamii tumeona kuwa utafiti
huu uliweza kuonesha vipengele vya lugha vilivyotumika na dhamira zilizojitokeza
na pia kufananana na kutofautiana kwake.
Kwa kupitia nadharia hii, moja ya kazi za fasihi ni kuhifadhi historia ya jamii hiyo.
Mfano, vipindi maalum vya mfumo wa maisha ya jamii. Morani (Mbogo 1993) na
Kivuli Kinaishi (Mohamed 1990) ni mfumo wa unyonyaji. Unyanyasaji, rushwa na
uongozi mbaya kwa jamii ya Tanzania. Zote hizo ni mifumo ya jamii katika Nyanja
za maisha pamoja na matumizi ya lugha na vipengele vyake. Hivyo basi mtafiti
anaona kwamba kauli ya fasihi ina uhusiano mkubwa na jamii ni dhima yenye
mashiko. Tunasema ni muhimu kuichukulia fasihi kama zao la jamii ambalo
22
nalohathiri na kuathiriwa na jamii hiyo. Nadharia hii pia inatoa mchango kwa
kuonesha historia ya jamii hiyo matukio mbalimbali yaliyotokea na jinsi jamii
ilivyojifunza, ilivypambana na mafanikio yaliyopatikana.
2.8 Hitimisho
Katika utafiti, sura hii ni ya muhimu sana kwa kuwa imeonesha katika kazi za
kifasihi jinsi watafiti wengine walivyofanya utafiti. Na katika kazi hizo mtafiti
alichagua baadhi ya kazi zinazohusiana na utafiti huu. Kupitia kazi tangulizi mtafiti
aliweza kugundua watafiti wengine walifanya nini na jinsi walivyochambua data,
tatizo la utafiti lilikuwa nini, pengo la utafiti na maarifa yaliyoweza kutumika katika
kazi ya fasihi. Sura hii imeanza na kazi tangulizi kwa kuchunguza dhana ya fasihi
linganishi. Kupitia wataalamu mbalimbali kwa mawazo yao. Vilevile mtafiti
amepitia tamthiliya za Kiswahili ambapo aliweza kuona tafiti nyingi zilichunguza
fani na maudhui. Kupitia tafiti hizo imebainika kuwa tafiti linganishi katika lugha na
vipengele vya vyake na dhamira katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na
Safari ya Kanaani hazijafanyika, hivyo kumfanya mtafiti awe na ari ya kufanya
utafiti huu. Pengo la utafiti limeonekana wazi ambalo ndilo limewezesha utafiti huu
kufanyika.
Pia sura hii imeangalia kiunzi cha nadharia ya fasihi ya jamii ambayo ndiyo
imetumika kuchunguza matumizi ya lugha na vipengele vyake na dhamira katika
tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani. Sura inayofuata
inawasilisha mbinu na njia za utafiti.
23
SURA YA TATU
MBINU NA NJIA ZA UTAFITI
3.1 Utangulizi
Sura hii imejadili mkabala wa utafiti, mbinu na vifaa ambavyo vilitumika katika
utafiti huu. Utafiti huu umetumia mkabala wa kitakwimu na usio wa kitakwimu
katika kukusanya na kuzichambua data zilizopatikana. Utafiti wa kitakwimu na usio
wa kitakwimu hujazilizana na kukamilishana (Kombo na Tromp, 2006) (Opie, 2004)
anasema mbinu na njia zina maana ya mikakati inayowekwa katika kukusanya na
kuchambua taarifa kwa kupata ukweli, ili kusuluhisha jambo, kujibu swali au kutatua
tatizo. Hivyo mbinu ni mpangilio maalum wa mikakati anayoiandaa mtu kwa ajili ya
kufanikisha jambo fulani kwa urahisi. Katika utafiti huu, mtafiti alitumia mbinu na
njia tofauti ambazo zilimwezesha kupata data za matokeo sahihi na zenye ubora wa
kufikia mwisho mwema. Miongoni mwa mbinu hizo ni usomaji matini mbalimbali
zilizohusiana na utafiti huu.
3.2 Eneo la Utafiti
Utafiti huu ulifanyika katika eno la jiji la Dar es Salaam ambapo utafiti ulifanyika
kwa kusoma katika maktaba mbalimbali kama vile Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili na Maktaba
Kuu Tanzania.
3.3 Kundi Lengwa
Kulingana na Kothari na Brayyman (2004), Komba na Tromp (2006) wanasema
kundi lengwa ni jumla ya watu wote ambao huhusishwa katika utafiti. Katika utafiti
24
huu kundi lengwa ni tamthiliya za Kinjeketile iliyotungwa na msanii E.Hussein na
Nyerere na Safari ya Kanaani iliyotungwa na msanii E. Mbogo.
3.4 Usampulishaji
Usampulishaji ni kitendo cha kouchaguloiowa kupoata kikundi fulani ili kuwakilisha
kundi lengwa. Katika utafiti huu mtafiti ametumia usampulishaji lengwa. Hiio ni
aina ya sampuli ambay watafitiwa ama vitafitiwa ambavyo mtafiti amejiridhisha
kwamba watafitiwa hao watampatia data zitakazomwezwsha kutimiza malengo ya
utafiti wake (Yin, 1994). Aina hii ya usampulishaji imetumika katika kuteua
tamthiliyoa za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani.
3.5 Sampuli
Sampulini istilahi inayotumika kumaanisha watu walioteuliwa kujibu maswali ya
utafiti katika kundi husika (Kothari, 1990). Hivyo katika utafiti sampuli ilikuwa ni
vipengele vya lugha na dhamira zilizojitokeza katika tamthiliya teule.
3.6 Mbinu za ukusanyaji data
Katika utafiti mbinu mbalimbali huweza kutumika katika kukusanya data, kama
Scale (2012) na Silvaman (2010) wanavyounga mkono hoja wanasema kuwa kuna
mbinu mbalimbali za kukusanya data lakini si kila mbinu inafaa kwa kila utafiti.
Mbinu itakayotumika itategemea na mazingira, wakati na aina ya utafiti. Katika
utafiti huu mtafiti alitumia mbinu ya maktaba na usomaji matini mbalimbali.
3.6.1 Mbinu ya Usomaji Matini Mbalimbali
Maktaba ni mkusanyiko wa vitabu vilivyohifadhiwa kwa ajili ya kusoma, TUKI
(2004). Mtafiti alitumia njia ya usomaji taarifa mbalimbali zinazohusiana na utafiti
25
huu ambazo zimekwishaandikwa vitabuni, magazetini na kwenye majarida na kazi
za tafiti zilizohusu tamthiliya za kiswahili. Vitu vingi hupatikana katika maktaba
ambavyo mtafiti alitarajia kuvitumia, kulingana na malengo ya utafiti wake.
Mbinu hii ilitumika katika utafiti huu ambapo mtafiti alisoma na kuchambua vitabu
vya Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani, pamoja na vitabu vingine vya
ziada ili kumwezesha mtafiti kupata data muhimu katika utafiti huu, na kukidhi
mahitaji ya utafiti uliolengwa. Kwa kusoma vitabu vitakavyopatikana katika maktaba
mtafiti aliweza kutathmini matumizi ya lugha na dhamira katika tamthiliya hizo
ambapo ilimwezesha kugundua namna vipengele vya lugha vinavyofanana au
kutofautiana na jinsi lugha ilivyotumiwa kuwasilisha ujumbe kwa jamii.
3.7 Zana za Utafiti
Mulokozi (1983) anaeleza kuwa zana za utafiti ni vifaa vya utafiti hutegemea aina
ya utafiti. Aghalabu baadhi ya vifaa hivi kama si vyote hutumika, kalamu, karatasi,
shajala ya uwandani, tepu rekoda na vifaa vyake, kamera na vifaa vyake, kompyuta,
daroubini, vifaa vya kupimia, kuhesabu, matini, nakadhalika.
Zana za utafiti ni muhimu sana kwa mtafiti ambazo ni kalamu na karatasi kwa ajili
ya kuandika na kutunzia kumbukmbu muhimu zitakazopatikana wakati wa kusoma
katika maktaba(Kabuk 1987). Zipo zana za aina mbalimbali za utafiti, ilamtafiti
katika utafiti huu alitumia baadhi ya hizo ambazo zimefafanuliwa hapa chioni:
3.7.1 Matini
Hivi ni vitabu vilivyotumika katika utafiti huu kwa ajili ya kutathmini matumizi ya
lugha na dhmira ambavyo ni Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani pamoja
26
na vitabu vingine vya kiuhakiki ambapo matini hizi zilitoa mchango katika utafiti
huu kwani data za matumizi ya lugha na dhamira zilipatikana na kuufanya utafiti
ufikie lengo la kuwasilisha ujumbe kwa jamii au hadhira iliyokusudiwa.
3.7.2 Kompyuta
Kompyuta ilitumika katika kutafutia matini kutoka katika tovuti na wavuti, na pia
kuhifadhi taarifa mbalimbali zilizohusiana na utafiti huu. Data zilizohifadhiwa
hutolewa mahitimisho.
3.7.3 Simu ya mkononi
Mtafiti alitumia simu ya mkononi ambayo ilimsaidia na kumrahisishia kupata
mawasiliano na msimamizi kwa ajili ya kupata maelekezo na jinsi yakuwasiliana
naye na kufanya masahihisho.
3.8 Hitimisho
Sura hii imejadili mbinu na njia za utafiti ambapo eneo la utafiti limebainishwa ,
kundi lengwa, mbinu ya ukusanyaji data, na zana za utafiti. Katika ukusanyaji wa
data mtafiti alitumia mbinu ya maktaba kwa kusoma vitabu na machapisho
mbalimbali ya kazi za fasihi. Aidha mtafiti alionesha umuhimu wa zana za utafiti na
jinsi zilivyotegemeana na kuweza kufanikisha utafiti huu. Sura inayofuata
inawasilisha uwasilishaji na uchambuzi wa data.
27
SURA YA NNE
UWASILISHAJI NA UCHAMBUZI WA DATA
4.1 Utangulizi
Sura hii inawasilisha uchambuzi wa data zilizokusanywa katika utafiti huu. Sura hii
imegawanyika katika sehemu nne. Kipengele cha kwanza kinazungumzia lugha na
vipengele vyake katika tamthiliya teule. Kipengele cha pili inazungumzia damira
zilizojitokeza katika tamthiliya teule. Tatu kulinganisha na kulinganua vipengele ya
lugha. Mtafiti ameendelea kulinganisha na kulinganua dhamira zilizojitokeza katika
tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na safari ya Kanaani. Na kipengele cha
mwisho ni hitimisho.
4.2 Vipengele vya Lugha katika Tamthiliya Teule
Kati ya malengo mahsusi ya utafiti huu ni kulinganisha vipengele vya lughakatika
tamthiliya teule. Vipengele hivyo ni methali, nahau, tamathali za semi na misemo.
Vipengele vimechambuliwa kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa hadhira. Mbinu ya
usomaji wa machapisho imetumika ili kuweza kupata data na kuweza kuchambua
tamthiliya teule. Pia mtafiti amepata data kupitia maandiko mbalimbali. Mtafiti
amebainisha vipengele vya lugha vilivyotumika katika tamthiliya teule zaKinjeketile
na Nyerere na Safari ya kanaani, baadhi yake ni kama ifuatavyo:
Jedwali Na 4.1: Vipengele vya lugha katika Nyerere na Safari ya Kanaani
Namba Kipengele cha lugha
1. Methali
2. Nahau
3. Tamathali za semi
4. Misemo
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanani
(2016)
28
Data za utafiti huu zimedhihirisha mwandishi huyu ametumia methali, nahau,
tamathali za semi, na misemo katika utunzi wa kazi hii ya kifasihi. Vile vile mtafiti
amechambua vipengele vya lugha katika tamthiliya ya Kinjeketile, katika Jedwali
namba 4.2.
Jedwali Na 4.2: Vipengele vya Lugha katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Kipengele cha lugha
1 Tamathali za semi
2 Methali
3 Misemo
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Data zinaonesha kuwa msanii huyu ametumia tamathali za semi na misemo katika
utunzi wake wa kazi ya fasihi. Utafiti umegundua kuwa msanii Husseni ametumia
vipengele vitatu vya lugha katika ujenzi wa kazi yake. Mtafiti wa utafiti huu
amechunguza matumizi ya vipengele hivyo kwa lengo la kufanya utafiti linganishi
katika tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na safari ya kanani.
4.3 Mdafao wa Ujitokezaji wa Vipengele vya Lugha katika Tamthiliya za
Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani
Utafiti huu ulichunguza mdafao wa ujitokezaji wa vipengele vya lugha katika
tamthiliya teule za kihistoria kama ifuatavyo:
Jedwali Na 4.3: Mdafao wa Ujitokezaji wa Vipengele vya Lugha katika
Tamthiliya ya Kinjeketile na Nyerere na Safari yaKanaani
Namba Kipengele cha lugha Mdafao waUjitokezaji
Nyerere Kinjeketile
1 Methali 1% 0.25%
2 Nahau 1% -
3 Tamathali 96% 97.75%
4 Misemo 2% 2%
Chanzo: Data za Utafiti kutoka Nyerere na Safari yaKanani na Kinjeketile (2016)
29
Jedwali namba 4.3 linawasilisha mdafao wa ujitokezaji wa vipengele vya lugha
katika tamthiliya teule. Data zinadhihirisha kuwa msanii ametumia tamathali za semi
katika Nyerere na Safari ya Kanaani kwa asilimia tisini na sita (96) na asilimia
zilizobaki ametumia katika vipengele vingine vya lugha. Pia data zinadhihirisha
katika Kinjeketile tamathali za semi zimetumika kwa asilimia tisini na saba nukta
saba tano (97.75) na misemo kwa asilimia mbili (2) na methali asilimia sifuri nukta
mbili tano (0.25). Utafiti katika tamthiliya hizi za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya
Kanani ulichunguza ujitokezaji wa vipengele kwa kila tamthiliya na jinsi
zinavyotofautiana kwa kila moja ya tamathali hizo.
4.4 Uteuzi na Matumizi ya Tamathali za Semi
Tamathali za semi ni usemi wenye kupanua, kupunguza,au kubadilisha maana za
dhahiri au za kawaida za maneno ili kuleta maana maalum ya kishairi iliyokusudiwa
na msanii au mtunzi (Kahigi na Mulokozi,1979). Tamathali za semi ni maneno au
sentensi ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo
na sauti katika maandishi au kusema (Senkoro, 2011) tamathali hizi za semi ni kama
ifuatavyo;
4.4.1 Tamathali za Semi katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
Jedwali hapo juu linaonesha tamathali za semi zilizojitokeza katika tamthiliya ya
Nyerere na Safari ya Kanaani. Utafiti huu ulichunguza ni kwa kiwango gani kila
tamathali ya semi imetumika katika tamthiliya ya Nyerere na Safari yaKanaani.
Mtafiti alitaka kujua tamathali ya semi iliyotumika mara nyingi zaidi katika kujenga
kazi yake ya fasihi. Kwa kuchunguza matumizi ya lugha pia mtafiti amebaini
30
tamathali za semi zilizotumiwa na msanii katika kufikisha ujumbe kwa hadhira.
Matokeo yameonesha kama ifuatavyo katika jedwali.
Jedwali Na 4.4: Ujitokezaji wa Tamathali za Semi katika Tamthiliya ya Nyerere
na Safari ya Kanani
Namba Tamathali za Semi
1 Tashihisi
2 Sitiari
3 Tashibiha
4 Tashititi
5 Takriri
6 Tanakali za sauti
7 Kejeli
8 Mdokezo
9 Nidaa
Chanzo: Data za Utafiti kutoka Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani (2016)
Jedwali Na 4.5: Mdafao wa Ujitokezaji wa Tamathali za Semi katika
Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
Namba Tamathali za semi Mdafao wa ujitokezaji
1 Tashihisi 15
2 Sitiari 17
3 Tashibiha 17
4 Tashtiti 7
5 Takriri 14
6 Tanakali sauti 1
7 Kejeli 3
8 Nidaa 234
9 Mdokezo 53
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
31
Jedwali hapo juu linaonesha kuwa nidaa ni tamathali ambayo ilijitokeza kwa kiasi
kikubwa zaidi ya tamathali nyingine kwa mdafao wa 234., ikifuatwa na mdokezo
kwa mdafao wa 53, tashibiha na sitiari kwa mdafao wa 17. Tashihisi kwa mdafao
wa 15. Takiriri nayo ilijitokeza kwa mdafao wa 14, tashtiti kwa kwa mdafao wa 7,
tafsida kwa mdafao wa 6, ikifuatiawa na kejeli kwa mdafao wa 3 na mwisho
tamathali iliyojitokeza kwa mdafao wa 1 ni tanakali sauti. Hii inadhihirisha kuwa
msanii ametumia nidaa kwa kiwango kikubwa katika kujenga kazi yake ya
kihishoria.
4.4.2 Nidaa
Mtafiti wa kazi hii alibaini kuwa msanii wa tamthiliya ya Nyerere na Safari
yaKanaani ametumia nidaa kwa kiwango kikubwa na kuona kuwa nidaa
ndiyoiliyobeba ujumbe wa kazi hii. Msanii wa kazi hii, ametunga kazi hii ili
kuonesha vijana wa Taifa kujenga uzalendo katika nchi yao.Vijana watambue
kuangalia maslahi ya Taifa na kudumisha amani ya nchi. Kwa kujenga uzalendo huo
vijanawamalizapo kidato cha sita au chuo kikuu walitakiwa kutumikia Jeshi la
KujengaTaifa kwa mujibu wa sheria. Na wawapo katika mafunzo ya Jeshi la
Kujenga Taifa hujifunza mambo mbalimbali ya ujasiriamali na kazi nyingi za
kujitegemea. Nidaa ni msemo ambao huonesha kushangaa na kushangazwa na jambo
fulani. Misemo hii huambatana na alama ya kushangaa katika kukubali kuchukia au
kuonesha heshima maalumu.(Msokile,1992:63) Nidaa ni msemo unaonesha
kushangaa au kushangazwa na jambo fulani. Mfano Aa! Mbona unaondoka
ghafla!Utafiti huu ulibaini baadhi ya nidaa katika tamthiliyahiiya Nyerere na Safari
ya Kanaani kama ifuatavyo:
32
Jedwali Na 4.6: Mifano ya baadhi ya Nidaa katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari yaKanaani
Namba Nidaa
1 Siyo mchongameno! Anaitwa Hambiliki!
2 Aa! Mbona unaondoka ghafla!
3 Hapana! Nenda kwa Farida!
4 Anazo dawa kimbia mama nakufa!
5 Aa! Hufi, nakwambia!
6 Ukienda kumwita Farida haraka, sitakufa ---- Aaa!
7 Martini mwanangu, mwanamke!?
8 Niachie basi usiubofye mwili wangu, usije ukanipasua mwenzio!
9 Aa! Watu wanatia chumvi tu!
10 Haiwezekani! Kwenda JKT miezi sita, kisha kukatwa 60% ya mshahara
kwa miezi 18. Nani atakubali?
11 Mjinga we1 Babaako akitaka kukucharaza viboko, kwa utovu wa
adabu, huwa anakupeleka kwa daktari kwanza?! Mimi nawacharaza
nyote leo kama babaenu. Ninyi watoto wadogo?! Juzi tu mlikuwa
mnavaa nepi na kutoka kamasi, ndiyo mnatutukana sisi, ninyi?! Lala
chini Martin!
12 “We Zebedayo nini sasa! Tohara! Tohara! Kama wao wanapendana,
wewe inakuhusu nini!”
13 Me, I am exicited! Huu msamaha naukumbatia kwa mikono miwili
14 Mgonjwa! Mgonjwa! Mtoto laana tupu! Haya! Na ninyi ingieni ndani.
Upesi! Nyama nyie!
Chanzo: Data za Utafiti kutoka Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
Msanii wa tamthiliya Nyerere na Safari ya Kanaani kutokana na data hizo hapo juu
nidaa zilitumika kuwasilisha ujumbe wa kwa jamii au hadhira. Msanii alituonesha
kuwa mwanamke anaweza, pale Martini alipomwambia mama yake akamwite
Farida aje kumtibu. Mama yake alisita kwa kuona kuwa mwanamke hawezi, ni bora
aende kumwita daktari aliyestaafu ili kumtibu mwanaye. Mfano; “Hapana! Nenda
kwa Farida anazo dawa. Kimbia mama nakufa! Aaa! Hufi nakwambia! Ukienda
kumwita Farida haraka, sitakufa --- Aaa! Martini mwanangu mwanamke!? Tunaona
hadi leo hii bado mwanamke haaminiwi katika jamii kwa kiasi kikubwa. Hata katika
33
chaguzi mbalimbali mara nyingi wanawake wanaangushwa kwa kutokuaminiwa na
jamii husika.
4.4.3 Tashibiha
Ni tamathali ya semi inayotumia sentensi kwa kulinganisha vitu viwili au zaidi kwa
kutumia vilinganishi, kwa mfano mithili ya, kama kwamba, sawa, kama vile, na
kama. Mulokozi, (2002); Kahigi, (1995); Senkoro, (1982); wanasema tashibiha ni
tamathali ya semi inayotoa mfano wa vitu unaojengwa kwa maneno kama vile
kulinganisha vitu viwili au zaidi. Kwa kutumia vilinganishi kwa mfano mithili ya,
kama vile, kama kwamba, sawa na mengineyo. Ujitokezaji wa baadhi ya tashibiha
katika tamthiliya ya Nyerere naSafari ya Kanaani uliochunguzwa na kubainishwa na
utafiti huu umeoneshwa kwenye jedwali kama ifuatavyo:
Jedwali Na 4.7: Tashibiha katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
Namba Tashibiha
1 Amesimama imara kama mlima Kilimanjaro hatikisiki
2 Ndiyo katika nchi maskini kama hii mishahara yetu ni minono mno
3 Kurudi Misri kwangu mimi ni sawa na kumlazimisha mwislamu kula
nguruwe
4 Macho haya yanayong’ara kama pacha ya nyota zinazowaka na
kumeremeta juu ya mbingu samawati katika majira ya kiangazi
5 Hata akinikuta sebuleni ananipita tu kama hanijui. Ananiona kama
shetani, kidudu kalikopotea njia
6 Rais gani duniani anaweza kuvumilia na kuyafumbia macho na masikio
matusi na kebehi kama zile?
7 Tutawapata vijana majabari, wenye nguvu kama kifaru
8 Niko ngangari kama jabari la jibrota
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katikaTamthiliya ya Nyerere naSafari ya Kanaani
(2016)
34
Msanii alitumia tashibiha katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
kuwasilisha ujumbe wa kazi hii ya fasihi kwa hadhira. Kwa mfano “ Kurudi Misri
kwangu ni sawa na kumlazimisha mwislamu kula guruwe. Ni kama kumlazimisha
Mungu kumsamehe Lusifa.” Nyerere alimwambia Kambona haya maneno kwa
kuonesha msimamo wake wa kuiteteta na kuijenga Tanzania ya Ujamaa wa kweli.
Wananchi wanatakiwa kuwa wazalendo wa kuijenga nchi kwa uaminifu na kwa
kushirikiana pamoja kwa nia moja. Wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii,
juhudi na maarifa kila mmoja kwa uwezo alionao ili kuinua uchumi wa nchi yetu ya
Tanzania.
Aidha mtunzi wa tamthiliya hii aliendelea kutumia tashibiha kama vile “Amesimama
imara kama mlima Kilimanjaro.” Nyerere alikuwa na msimamo kuhusu vijana
wamalizapo kidato cha sita na vyuo waende kutumikia Jeshi la Kujenga Taifa kwa
mujibu wa sheria, kwa lengo lakuwajengea uzalendowa nchi yao. Vijana hawa
wakimaliza kutumikia Jeshi la Kujenga Taifa waweze kujitegemea, kutetea nchi na
wananchi wake kwa ujumla. Wawapo katika Jeshi la Kujenga Taifa wanafundishwa
kufanya kazi mbalimbali, wanapewa mafunzo juu ya ulinzi wa nchi na hao ndio
askari wetu wa akiba katika nchi yetu.
4.4.4 Tashihisi
Utafiti ulibaini kuwa msanii wa Nyerere na Safari ya Kanaani alitumia tashihisi
kuwasilisha ujumbe aliokusudia kwa jamii. (Senkoro, 1982), anasema tashihisi ni
tamathali ya semi ambayo wakati mwingine huitwa tamathali ya binadamu. Kwa
kuwa tamathali hii vitu visivyo na sifa walizo nazo binadamu hupewa sifa hizo.
35
Mfano “Kunguru hao walikuzomea wakisema, Babu jinga hiloooo!!!
Bwegedayooo!!! huyooo!”
Jedwali Na 4.8: Baadhi yaTashihisi Zilizojitokeza katika Tamthilia ya Nyerere
na Safari ya Kanaani
Namba Tashihisi
1 Akili zina breki kichwani; lakini hisia ni gurudumu, lenye wazimu
halidhibitiki, bali huenda kasi na pengine hata kugonga mwamba.
2 Kunguru hao wakikuzomea, wakisema: “Babujinga hiloooo!!!
Bwegedayooo!!! huyooo!”
3 Maguruwe pori toka ughaibuni yataletwa yaje kuuziwa rasilimali za nchi
kwa bei chee.
4 Pengo kati ya nguruwe na walala hoi litakuwa bonde la ufa.
5 Kuwa kiongozi ni kuchagua utakatifu. Kukaa Ikulu ni kuchagua utakatifu.
Chanzo: Data za utafiti kutoka Katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
Data katika jedwali namba 4.8 zinaonesha msanii alivyotumia tashihisi katika
tamthiliya ya Nyerere na Safariya Kanaani ili kuwasilisha ujumbe katika jamii.
Mfano “Maguruwe pori toka ughaibuni yataalikwa yaje kuuziwa rasilimali za nchi
kwa bei chee.” Hapa msanii anamwonesha Nyerere alivyokuwa na uchungu na nchi
ya Tanzania. Aidha aliwataka wanachi wasije wakaingiza watu wa nje kututawala
ambapo tashihisi imewapa nguruwe sifa za binadamu. Msanii amewasilisha dhana ya
uzalendo ambapo kila mwananchi wa Tanzania anatakiwa kuwa na uzalendo wa
kujenga nchi, kuilinda dhidi ya maadui na kujenga umoja wa kweli.
4.4.5 Sitiari
Sitiari ni tamathali ya semi inayotumika kuumba picha fulani inayoamsha mwtikio
fulani kutoka katika hadhira . (Mulokozi, 2002). Utafiti huu ulibaini kuwa mtunzi
36
wa tamthiliya hii ya Nyerere na Safari ya Kanaani ametumia sitiari, kwa kuwa
sitiari ni tamathali inayohamisha maana toka kitu au dhana moja hadi kitu au dhana
nyingine. (Kahigi, 1995), anasema katika sitiari kinachohamishwa ni tabia au umbo
au kazi ya kitu kwa kuhusisha na tabia au umbo au kazi ya kitu kingine. Baadhi ya
sitiari zilizojitokeza katika tamthiliya hii ni kama inavyoonekana katika Jadwali
namba 4.9.
Jedwali Na 4.9: Sitiari katika Tamthiya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
Namba Sitiari
1 Vyama vya upinzani vingekuwa kidhibiti-mwendo cha mseleleko wa
kuelekea uimla wa chama tawala.
2 Kufutwa kwa vyama vya upinzani ni yai la mamba kisiasa.
3 Vitabu na maarifa ni chakula kisichoshibisha.
4 Tohara ni kama tupa na kinoo kinachoongeza makali ya mkuki na ufanisi
vitani
5 Japokuwa wewe hukuwa chaguo la baba; lakini uchumba wetu
haukulipua kombora la hasira ndani yake kiasi hichi.
Chanzo: Data za utafiti kutoka katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
Sitiari zilitumika katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani. Utafiti ulibaini
kuwa msanii alizitumia sitiari ili kuwasilisha ujumbe kwa hadhira. Mfano “Vyama
vya upinzani vingekuwa kidhibiti mwendo wa mseleleko wa kuelekea uimla wa
chama tawala.” Hapa Kambona alimwambia Nyerere vyama vya upinzani viendelee
kuwepo ili viweze kukisoa chama tawala. Pia aliendelea kumweleza Nyerere kwa
kusema “Vyama vya upinzani ni dira ya kukuonesha makosa na uweze kujisahihisha
pale unapofanya makosa ya kibinadamu au hata makosa ya makusudi.” Hivyo vyama
37
vingi vinaruhusu mtu kukosolewa anapoenda kinyume na matakwa ya wananchi ili
wananchi hao waweze kupata haki zao.
4.4.6 Takriri
Takriri ni tamathali ya semi ambayo hurudiarudia sehemu ya neno au senntensi ili
kuonesha msisitizo katika kila kinachozungumzwa au kinachoandikwa. Hivyo utafiti
huu ulibaini mtunzi wa tamthiliya ya Nyrere na Safari ya Kanaani alitumia baadhi ya
takriri kama jedwali linavyoonesha.
Jedwali Na 4. 10: Ujitokezaji wa Takriri katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari ya Kanaani
Namba Takriri
1 Lakini “Musa! Musa!” Musa ni sawa.
2 Chwa! Chwa!
3 Sirudi! Sirudi! baba sirudi! Tukimbie!
Chanzo: Data za utafiti kutoka katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaan
(2016)
Takriri katika Jedwali namba 4.10 zilitumika na msanii kuonesha jinsi alivyoweza
kuwasilisha ujumbe kwa jamii. Mfano “Nitamcharaza mwanangu hapahapa mbele
yako…” “Lala chini! Nasema lala chini Saigoda!” “Chwa! Chwa! … Hapa mzee
Mwajombe mzazi wa Saigoda alikasirishwa na kijana wake kuwa mtovu wa nidhamu
kwa Rais Nyerere kwa kuungana na wenzake katika maandamano ya kupinga
kwenda kutumikia Jeshi la Kujenga Taifa. Mzazi huyu anaonesha ushirikiano wa
yeye na serikali katika kumlea kijana wake. Mzazi huyu anaonesha kuwa tuwalee
watoto kwa kuwajengea maadili ya kuwa na nidhamu. Vijana wawe na utii na
38
kuwaheshimu viongozi wanaowaongoza, endapo kuna haki wanayoidai basi wafuate
utaratibu unaostahili ili kujenga uzalendo unaotakiwa.
4.4.7 Tashtiti
Katika tamthiliya hii ya Nyerere na Safari ya Kanaani utafiti umebaini pia
ujitokezaji wa tashtiti ambazo msanii alizitumia kuwasilisha suala la kihistoria katika
jamii. (Msokile, 1992: 62),anasema tashtiti ni mkazo wa maneno yasemwayo au
yaandikwayo. Msanii hutumia mbinu ya kuuliza maswali kwa jambo ambalo
analifahamu jibu lake, kwa lengo la kusisitiza jambo na kuleta mshangao. Ujitokezaji
wa baadhi ya tashtiti katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani kama
Jedwali 4.11 linavyoonesha .
Jedwali Na 4.11: Ujitokezaji wa Tashtiti katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari
ya Kanaani
Namba Tashtiti
1 Unataka kusema nini Oscar Kwamba mimi ni dikteta?
2 Yule Musa bwana! Anataka kutupeleka Kanaani; nchi ya maziwa na
asali!
3 Aa ! Bwana Oscar, naona kama umechukia vile?!
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
Katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani msanii alionesha uongozi
ambao sio wa kidikteta kwa Nyerere kumwuliza ili kuweka msisitizo Mfano
“Unataka kusema nini Oscar? Kwamba mimi ni dikteta?” Haya maneno Nyerere
alikuwa anayasikia lakini akauliza tena kwa ajili ya kuweka msisitizo. Nyerere ni
kiongozi mzalendo mwenye uchungu na nchi yake. Nyerere alikuwa kiongozi
aliyejali watu wake, alipenda ujamaa na kujitegemea na ndio maana alianzisha
39
mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa . Vijana wamalizapo mafunzo ya Jeshi la Kujenga
Taifa walitumikie taifa kwa moyo. Lakini Kambona alikuwa anaupenda ubepari ili
wananchi waendelee kunyonywa na kunyanyaswa kwa sababu ya uongozi wa
kidikteta.
Aidha msanii ameonesha jinsi Kambona alivyokuwa amekasirika kwa sababu
Nyerere alimwambia habari za siasa ya ujamaa na kuwapeleka vijana katika Jeshi la
Kujenga Taifa baada yakumaliza vyuo na kidato cha sita. Kwa kuonesha msisistizo
anasema,”Aa! Bwana Oscar naona umechukia vile? Tashtiti hii inasisitiza kwa
kuonesha mtazamo uliojengwa kwa Nyerere ambaye ni mwenye msimamo na
habadilikibadiliki kama kinyonga. Nyerere alikuwa kiongozi aliyesimamia haki
kwa wananchi na hatimaye kuwajengea vijana uzalendo kwa kuwapeleka vijana
katika Jeshi la Kujenga Taifa.
4.4.8 Tanakali Sauti
Utafiti huu umechunguza na kubaini kuwa msanii wa tamthiliya yaNyerere naSafari
ya Kanaani alitumia tamathali ya semi ya tanakali sauti ili kufikisha ujumbe kwa
hadhira. Hii ni tamathali ya semi inayotoa au kuiga mlio wa vitu au wanyama
(Senkoro, 2011). Naye Wamitila (2010) ansema ni uigaji wa sauti fulani. Msingi
mkuu wa mbinu hii ni kuhakikisha kuwa hali fulani inaelezwa kwa njia kamilifu, pia
hutumiwa kujenga na kukuzia hisia fulani. Tanakali sauti ni mbinu ya kutumia
maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kinavyofanyika.
Msanii wa tamthiliya hii ametuonesha kuwa Nyerere hakubaliani na maandamano ya
vijana wa chuo kikuu na kuamua kuwachapa viboko viongozi wa wanachuo hao.
40
Mfano alianza Martini ambaye alikuwa rais wa wanachuo na ndiye alikuwa mstari
wa mbele kuongoza na kuratibu maandamano waliyoyafanya.
Jedwali Na 4.12: Matumizi ya baadhi ya Tanakali Sauti katika Tamthiliya ya
Nyerere na Safari yaKanaani
Namba Tanakali Sauti
1 Lala chini Martini! Viboko: Chwa! Chwa! Chwa!
2 Nasema lala chini Saigoda!Viboko: Chwa! Chwa!
Chanzo: Data za Utafiti kutoka Tamthiliya ya Nyrere na Safari ya Kanaani(2016)
Rais Nyerere alimwamuru Martini alale chini na kuanza kumchapa viboko “Chwa!
Chwa! Chwa!” Msanii amemwonesha Nyerere kuwa mwenye msimamo,
anachoamua kisikilizwe na kifuatwe. Aidha mzee Mwajombe baba yake Saigoda
alionesha ushirikiano wa kumlea kijana wake. Baba yake Saigoda alichukua jukumu
la kumwadhibu kijana wake mbele ya Rais Nyerere na umati uliokuwa katika
viwanja vya Ikulu. Vijana walitakiwa wawe na nidhamu na utiifu kwa viongozi
vilevile wawe na moyo wa uzalendo wa kujenga taifa.
4.4.9 Kejeli
Mbatiah (2001) anasema kejeli ni maneno yanayotumiwa katika matamshi kwa
madhumuni ya kuchoma, kukata au kutia uchungu. Utafiti ulichunguza na kubaini
kuwa msanii wa tamthiliya teule alitumia kejeli kufikisha ujumbe kwa jamii. Jedwali
linalofuata linaonesha ujitokezaji wa baadhi ya kejeli katika tamthiliya ya Nyerere na
Safari ya Kanaani.
Msanii alitumia kejeli katika tamthiliya hii kuwasilisha jambo la kihistoria kwa
hadhira. Mfano “Ama kweli wewe Julius ni nabii Musa arap Hambiliki.” Hapa
kiongozi anatakiwa abadilike awe anawasikiliza wananchi au jamii inayomzunguka.
41
Jedwali Na 4.13:Ujitokezaji wa Kejeli katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari
yaKanaani
Namba Kejeli
1 Kama u-mwanaume kweli, bwana Bweged…
2 Ama kweli Julius ni Nabii Musa arap Hambiliki
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
Kiongozi anatakiwa awape wananchi nafasi ya kutoa maoni kujadiliana nao ili na
wao washiriki katika kuleta maendeleo ya nchi. Kejeli hiyo ilimfanya Nyerere
abadilike hata pale alipoamua kuwafukuza wanachuo, baadaye aliwasamehe na
kuwarudisha chuoni kuendelea na masomo yao.
4.4.10 Mdokezo
Msanii wa tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani ametumia mdokezo ili
kuiwezesha hadhiara kufikiria kumalizia sentensi ambazo hazijakamilika kisanii.
(Company 2008:45), wanasema mdokezo hudokeza humfanya mtu kudokeza kitu
fulani na kukiacha bila kukikamilisha kwa maana ya kwamba kinaweza
kukamilishwa na mtu mwingine kisanaa. Mfano “Ila nataka kusema hivi…
leo…leo…,” Jedwali linalofuata utafiti ulibaini ujitokezaji wa baadhi ya mdokezo
kama inavyoonekana:
Jedwali namba 4.15 linaonesha baadhi ya mdokezo ulivyotumika katika tamthiliya
ya Nyerere na Safari ya Kanaani kuwasilisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii.
Mfano “Haiwezekani kama amekosa kazi yako ni kumcharaza viboko Nitamcharaza
mwanangu mwenyewe mbele yako .” Msanii ametuonesha kuwa wazazi wengine
42
wanashirikiana na walimu kukuza maadili ya vijana wetu. Kitendo alichokifanya
mzazi wa Saigoda kinatakiwa kuigwa na wazazi na jamii kwa ujumla katika
kuwajengea vijana maadili na uzalendo kuanzia nyumbani.
Jedwali Na 4.14: Ujitokezaji wa Mdokezo Katika Tamthiliya ya Nyerere na
Safari yaKanaani
Namba Mdokezo
1 Watanzania wanakufa wakipigana na Makaburu na Mreno huko
Msumbiji, Angola, Namibia, Zimbabwe, Afrika ya Kusini …ila ninyi
wendawazimu wakubwa mnasema: Afadhali wakati wa mkoloni!
2 Haiewezekani kama amekosa kazi yako ni kumcharaza viboko …
Nitamcharaza mwanangu mwenyewe mbele yako ….
3 Mawaziri wangu… Oscar! John! Kassim! Bibititi na wengine wote:
Niseme hivi… niseme… Najaribu… Natafuta maneno mwafaka
yanayoweza kulieleza hili… Kwamba nchi hii ya Tanzania
ITAJENGWA NA WENYE MOYO.
4 Nimewafukuza! Mtakaa vijijini miaka mitatu…Ndiyo….!
5 Tanzania haitajengwa na ubinafsi; haitajengwa kwa choyo; haitajengwa
kwa tama ya kujilimbikizia mali… Wananchi; Tanzania itajengwa na
wazalendo wenye moyo wa kuijenga Tanzania… Comrades!
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
4.5 Misemo
Mtafiti katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani amebaini matumizi ya
misemo. Wamitila (2010) anafananisha misemo na viungo ambavyo ni sawa na
viungo vya upishi kwani hufanya lugha ya mwandishi huwa na mvuto mkubwa wa
kisanaa. Hivyo mtafiti anaungana na Wamitila (2010) kuwa ni misemo ni fungu la
maneno lililofumbata maana kimafumbo ambayo imekusudiwa kutoa funzo kwa
43
jamii. Kauli hizi huelezea ukweli fulani. Katika Jedwali linalofuata limewasilisha
baadhi ya misemo iliyojitokeza katika tamthiliya teule.
Jedwali Na 4.15: Ujitokezaji wa Misemo katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari
yaKanaani
Namba Misemo
1 Tohara ni utakaso wa mwili na roho.
2 Vitabu na maarifa ni chakula kisichoshibisha.
3 Yule daktari yuko tayari siku yoyote umwone ili aondoe hilo zu lakini
wewe hutaki.
Chanzo: Data za utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
Katika utafiti huu data katika Jedwali 4.15 zinawasilishaji ujitokezaji wa misemo
katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani. Msanii wa tamthiliya hii
amewasilisha ujumbe wa jambo la kihistoria kwa hadhira. Mfano “Tohara ni usafi
nao utakaso wa mwili na roho.” Msanii amelinganisha tohara na jeshi la kujenga
Taifa. Vijana wanapoenda kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa wanapata mafunzo ya
aina mbalimbali pamoja na maadili. Kwa kuwa jeshini kuna utii wa sheria na
nidhamu ya hali ya juu, vijana wanaotoka huko wanakuwa wakakamavu, wenye utii
na uzalendo katika nchi yao. Msanii anaposesma tohara ni usafi na utakaso wa
mwili na rooho anamaanisha kijana anapomaliza kulitumika Jeshi la Kujenga Taifa,
anaweza kufanya kazi za aina mbalimbali za kujitegemea.
Aidha kijana anapofanyiwa tohara anapewa mafunzo ya ujasiri na maadili jinsi ya
kulinda jamii yake dhidi ya maadui na kuwa na upendo kwa watu wote. Msemo
mwingine ni “Vitabu na maarifa ni chakula kisichoshibisha.” Msanii amemaanisha
kujifunza hakuna mwisho. Pia msanii ameonesha kuwa binadamu anahitaji kupata
44
maarifa mapya kila wakati. Vijana wetu wanatakiwa wamalizapo kidato cha sita au
vyuo wakaongeze maarifa zaidi juu ya mambo mabalimbali ya ujasiriamali,
ukakamavu na uongozi bora wakati wakiwa katika Jeshi la Kujenga Taifa. Kwa hiyo
taifa litapata vijana wenye maarifa ya kutosha, wakakamavu, wabunifu na viongozi
waadilifu.
4.6 Methali
Msokile (1992) anasema methali ni semi zinazotokana na ujuzi, kanuni na tabia za
jamii ambazo kwa kawaida hushauri na kufundisha mambo mbalimbali kwa
wanajamii. Methali hufuatilia maisha ya kila siku ya jamii kwa kujihusisha na
migongano ama usuluhishi wa masuala mbalimbali katika jamii. Mulokozi (1989),
oanaelezea methali kuwa ni semi fupifupi zenye kuelezea kwa muhtasari fikra au
mafunzo yatokanayo na uzoefu wa jamii.
Methali ni maneno au sentensi zinazotolewa zenye mafundisho ndani yake ya
kuelimisha jamii. Utafiti huu umebaini kuwa msanii wa tamthiliya ya Nyerere
naSafari ya Kanaaniametumia methali katika kuwasilisha ujumbe kwa hadhira.
Jedwali linalofuata linaonesha ujitokezaji wa baadhi ya methali katika tamthiliya ya
Nyerere na Safari ya Kanaani
Jedwali Na 4.16: Ujitokezaji wa Methali katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari
yaKanaani
Namba Methali
1 Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
2 Mvumilivu hula mbivu.
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
45
Jedwali namba 4.16 data zimeonesha kuwa msanii wa tamthiliya ya Nyerere na
Safari ya Kanaani ametumia methali kufikisha ujumbe kwa hadhira. Mfano “Mtaka
cha mvunguni sharti ainame.” Kila mtu afanye kazi kwa bidii ili aweze kupata
mafanikio. Aidha ili nchi iweze kufanikiwa na kuendelea ni lazima kila mtu
awajibike kwa nafasi aliyo nayo. Hivyo kila mtu aikifanya kazi kwa bidii na kuwa
mzalendo kwa kujituma na kuzingatia maadili ya kazi, nchi yetu itapata maendeleo
endelevu.
4.7 Nahau
Nahau ni fungu la maneno ambayo yakipangwa pamoja huleta maana isiyo ya
kawaida ya kuonekana wazi mfano kula mwiba maana yake kupata tabu. Tia chumvi
maana yake danganya (Kamusi ya Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, 1981).
Msanii wa tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani ametumia nahau kulingana na
utafiti uliofanywa. Msanii ametumia nahau kwa lengo la kufikisha ujumbe
alioukusudia kwa hadhira. Ujitokezaji wa baadhi ya nahau unaonekana katika
jedwali linalofuata.
Jedwali Na 4.17: Ujitokezaji wa Nahau katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari
ya Kanaani
Namba Nahau
1 Kusalimu amri.
2 Wanatia chumvi.
Chanzo: Data za utafiti kutoka katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
(2016)
Msanii ametuonesha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu walikaidi agizo la Rais
lililokuwa likiwataka waende kulitumikia Jeshi la Kujenga Taifa kwa mujibu wa
46
sheria. Na baada ya mafunzo hayo wawe wazalendo, wafuate maadili ya kazi ili
walete ufanisi katika kazi. Wanachuo hawa wakaamua kuandamana ili kupinga
agizo hilo. Hivyo Rais akawaadhibu kwa kuwachapa viboko viongozi wa wanachuo
hao na hatimaye kuwafukuza chuo. Liboma ailikwenda kwa Martini ambaye
alikuwa rais wa wanachuo na kumsisitiza kuwa wasipotimiza masharti watakuwa
wamejifuta chuo.
Aidha Liboma aliwaambia Rais Nyerere akisema, amesema hata Oscar Kambona
“Kasalimu amri.” Maana yake Kambona alikuwa akimpinga Rais kwa muda mrefu
kwa kuwa yeye alitaka kufuata siasa za ubepari hivyo alitorokea nje ya nchi kwa
kuwa uamuzi wa Rais Julius Kambarage Nyerere ulimshinda. Ilitakiwa wanachuo
watii amri ya kurudi vyuoni wakamalizie masomo yao.
Tamthiliya ya Kinjeketile
4.8 Tamathali za Semi katika Tamtiliya ya Kinjeketile
Utafiti huu ulichunguza na kubaini kuwa msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile
alitumia tamathali za semi katika kazi yake. Msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile
alitumia lugha nyepesi inayoeleweka kwa urahisi na wasomaji kuliko msanii wa
tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani.
Msanii wa Kinjeketile alitumia tamathali za semi, methali na misemo wakati msanii
wa Nyerere naSafari Kanaani alitumia nahau zaidi ya msanii wa tamthiliya ya
Kinjeketile. Utafiti katika tamthiliya ya Kinjeketile ulichambua tamathali za semi
zilivyotumika na kwa kiwango gani kila moja kama jedwali linavyoonesha.
47
Jedwali Na 4.18: Mdafao wa Ujitokezaji wa Tamathali za Semi katika
Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Tamatahali za Semi Mdafao wa Ujitokezaji
1. Nidaa 166
2. Takriri 54
3. Mdokezo 46
4. Sitiari 30
5. Tashibiha 23
6. Kejeli 5
7. Tashititi 3
8. Tashihisi 2
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Utafiti ulibaini kuwa katika tamthiloiya ya Kinjeketile msanii alitumia tamathali ya
nidaa kwa kiwango kikubwa cha mdafao wa 166, ikifuatiwa na takriri ambayo ina
mdafao wa 54, mdokezo kwa mdafao wa 46, sitiari kwa mdafao wa 30. Tashibiha
kwa mdafao wa 23, kejeli kwa mdafao wa 5,tashititi 3 na tashihisi kwa mdafao wa 1.
4.8.1 Nidaa
Msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile alitumia nidaa kama utafiti huu ulivyobaini
katika jedwali linalofuata. Baadhi ya nidaa zilizotumika katika tamthiliya ya
Kinjeketile.
Msanii alitumia nidaa kuwasilisha ujumbe kwa jamii. Watu walihamasisha kupigana,
waweze kumwondoa mkoloni katika ardhi yao. Mfano “Sasa kupigana ! sasa vita tu,
akuna jingine!” Watu hawa wamenyanyaswa na mkoloni, kiasi kwamba wamechoka
wanataka uhuru wao. Kumwondoa mkoloni inatakiwa umoja wa kweli ambapo watu
48
hawa chini ya uongozi wa Kinjeketile waliungana na makabila ya Kusini mwa nchi
yetu ili waweze kumwondoa Mjerumani.
Jedwali Na 4.19: Ujitokezaji wa Nidaa katika Tamthilia ya Kinjeketile
Na Nidaa
1 Kitunda mimi nimemuona leo!
2 Sasa kupigana! Sasa vita tu, akuna jingine!
3 Wewe mwanamke ! wamatumbi waoga!
5 Tokeni! Tokeni!,wanawake wakubwa nyi!
6 Niacheni! Niacheni! mnaniumiza! niacheni niende!
7 Sote tutakuwa kitu kimoja. Maji !
8 Nilizigusa zilikuwa kavu kabisa!
9 Umetudanganya sote !
10 Mtanipa siku moja zaidi !
11 Kama hatukuleta shauri, tutachelewa ! nasema –tuanze!
12 Kwanza shamba la kinoo!
13 Ua udongo mwekundu!
14 Chuki na gazabu iliyotujaa!
15 Au unaogopa! Toka mwanzo alikuwa mwoga! Yeye ni yule muongo.
Kinjeketile njia moja!
16 Namimi mwenyewe nimemfundisha kushika silaha!
17 Shika silaha nikuoneshe nani anaweza kuitumia, muoga we !
18 Si kiongozi ! Ngulumbayo tuongoze! Ndiyo tuongoze!
19 Sema ! Tuna watoto sisi. Tufikirie watoto !
20 Nyamaza usiseme kitu!
21 Sitaki kuongea habari ya kesho!
22 Hapana ! Sitasema neno hilo!
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
4.8.2 Takriri
Utafiti huu baada ya kuchunguza na kuchambua tamthiliya ya Kinjeketile ulibaini
kuwa takriri imetumika katika kuwasilisha ujumbe ya kazi yake kwa jamii. Takriri
imetumika kama mbinu ya kuhamasisha harakati za ukombozi na kuhimiza ushujaa,
mfano “ Tokeni! Tokeni!” Msanii hapa alitumia takriri ya tokeni tokeni kwa
49
kuwahamasisha wanachi watoke kwenda kupambana na mkoloni wasiwe waoga.
Jedwali linalofuata linaonesha ujitokezaji wa baadhi ya takriri katika tamthiliya ya
Kinjeketile.
Jedwali Na 4.20: Ujitokezaji wa Takriri katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Takriri
1 Hodi! Hodi! Fungua. Hodi fungua.
2 Tokeni! Tokeni.
3 Anka! Anka!.
4 Niache!Niache!
5 Talatibu! Talatibu!
6 Nyamaza! Nyamaza!
7 Tutatambaa.Tutatambaa.Tutatambaa. Tutatambaa
8 Ua-Ua-Ua-Ua.
9 Vita! Vita! Vita!
10 Afazali kisa hiki.Afazali kisa hiki.
11 Tupo tayali! Tupo tayali! Tupo tayali!
12 Tuanze1 Tuanze! Tuanze! Tuanze!
13 Maji, Maji, Maji ya maisha ---- Maji ya maisha
14 Haifai, haifai jamaa
15 Kinjeketile muuwe! Muuwe!
Chanzo :Data za Utafiti kutoka katika Tamtiliya Kinjeketile (2016)
Msanii wa tamthiliya hii alitumia takriri ya maji kuwajengea wananchi imani na
kuwaaminisha kuwa yale maji yangewapa ushindi wa vita. Kwa imani hiyo ya maji,
Kinjeketile aliweza kuwaunganisha watu wa makabila ya Kusini kupigana vita ya
kumwondoa mkoloni. Mfano “Haya maji ni silaha yetu, maji ya maisha, maji haya
yatamlainisha simba, maji haya yataifanya risasi kuwa chembe ya mchanga juu ya
vifua vyenu”. “Ndugu tumepewa maji ndiyo, ndiyo maji tumepewa, maji ya maisha”.
Watu walihamasishwa na takriri hizi ambapo msanii aliweka mkazo au msisitizo ili
wananchi wa kusini wawe na imani kubwa juu ya maji ya maisha aliyoyatoa
50
kiongozi wao yaani Kinjeketile na ndipo wananchi walitaka ukombozi kupitia
muungano wa kupigana vita kumpiga mkoloni.
4.8.3 Sitiari
Sitiari ni tamathali ya semi inayotumika kuumba picha fulani inayotoa athari fulani
au inayoumba mwitikio fulani kutoka katika hadhira. Ni uhamishaji wa maana toka
kitu au dhana moja hadi kitu kingine. Utafiti huu uligundua kuwa msanii wa
tamthiliya ya Kinjeketile alitumia sitiari katika kuwasilisha ujumbe wa kazi yake.
Jedwali lifuatalo linaonesha baadhi ya sitiari zilizotumika.
Jedwali Na 4.21: Ujitokezaji wa Sitiari katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Na Sitiari
1 Wewe mwanamke
2 Udongo mwekundu
3 Una maana kusema mimi nitaweza kuwauzeni nyinyi nyote pamoja na watu
wangu?
4 Ningelikuwa ntu wa nzungu ningelikuwa hivi?
5 Kuna moshi, naona moshi! Penye moshi pana moto kalibu kutakuwaka moto
6 Wanawake wakubwa nyie
7 Tukifika daraja hili tutakuwa kitu kimoja
8 Haya ni maji ya maisha, hii ni silaha yetu. Huu ni usinga wa nguvu
9 Usilete taa kalibu. Ondoa muangaza walisema wataleta muangaza ... kutoa
giza...lakini nimetambua muangaza wao una hatali zaidi. Afazali kiza.
Afazali utumwa wa mwili kuliko utumwa wa akili unaoletwa na muangaza
10 Kwa nini anataka kutuuza sisi watoto wake kwa mabwana wengine?
11 Leo tumepata nguvu mpya.Leo tumepata moyo mpya
12 Wanaimba majimaji huku wamefyekwa na lisasi
13 Mala ilianza kutema lisasi
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Msanii alitumia sitiari kuwasilisha ujumbe katika kazi yake mfano “Udongo
mwekundi” Dhana ya mwandishi ni kuonesha kuwa mkoloni ni lazima aondolewe
51
katika ardhi ya watu wa Kusini. Mkoloni hafai katika kututawala kwa sababu
anawakandamiza wananchi. Wakoloni wanapora ardhi ya wananchi, na kuwafanya
wao ndio watumwa wa kuwatumikia wao. Aidha wakoloni ndio mabwana katika
ardhi ya wananchi. Hiyo lazima mkoloni aondolewe katika nchi yetu, kwa kupigana
vita ambapo makabila ya kuishi yaliungana na kuanza kupigana dhidi ya Mjerumani.
4.8.4 Tashibiha
Utafiti huu ulichunguza na kubainisha kuwa msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile
alitumia tashibiha kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii.Jedwali Linalofuata
linaonesha ujitokezaji wa baadhi ya tashibiha katika tamthiliya ya Kinjeketile.
Jedwali Na 4.22: Ujitokezaji wa Tashibiha katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Tashibiha
1 Nimemuona mtu kama yeye ….yeye hasa, lakini kwa mbali.
2 Sisi kama wanawake tumekaa tunatazama
3 Nimesikia habari ya bunduki inayomwaga lisasi kama mchanga
4 Afazali kufa kuliko kukaa hivi tunatawaliwa, tunalimishwa kama
wanyama
5 Nnakuja kama wezi kuja kunisaidia
6 Imekuwa bahati kwenu kuwa mambo haya yametokea siku kama ya leo
7 Nendeni kama upepo kusini, kaskazini, mashariki, magharibi
8 Mbona wanitazama kama hunijui
9 Nakuona kama siye Kinjeketile
10 Na kama mibaazi tutambaa
11 Lakini ikiwa kolelo na Hongo kwa kweli ni wamoja kama wanavyosema
watu wengine huko kwetu basi sisi tayari kuwa pamoja na nyinyi
12 Unafikili wale hawajui kama tumekuja
Chanzo:Data za Utafiti kutoka katika tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
52
Msanii ametuonesha jinsi wananchi walivyokuwa wakikata tamaa wakati
mwingine. Mfano “sisi kama wanawake tumekaa tunantazama tu” wanaume hawa
wajilinganisha na wanawake kwa vile katika jamii nyingi wanawake wanadharauliwa
na hawapewi nafasi ya kutoa maamuzi katika jamii hata kama yawe maamuzi yenye
tija kwa jamii. Hivyo wanaume walishindwa kuchukua hatua kwa Mjerumani
ambaye alikuwa akiwanyanyasa siku zote.
4.8.5 Kejeli
Msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile, alitumia kejeli katika kuwasilisha ujumbe wa
kazi hii ya kisanii kwa hadhira kama utafiti ulivyobaini. Jedwali linalofuata
linaonesha ujitokezaji wa kejeli katika tamthiliya ya Kinjeketile.
Jedwali Na 4.23: Ujitokezaji wa Kejeli kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Kejeli
1 Vijitu viwili vinawatishieni –nyinyi nyote. Eti nyinyi wanaume kweli
kweli wamatumbi. Hata kidogo. Wanawake tu nyinyi.
2 Mpe panya mwanamke huyu
3 Sema kama wewe mwanaume
Chanzo: Data kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Msanii alitumia kejeli katika tamthiliya Kinjeketile kuwasilisha ujumbe wa kazi yake
ya kifasihi. Mfano “sema kama wewe mwanaume.” Baada ya kitendo cha kupigwa
na wanyapala hadi kuishiwa nguvu, mke wake yaani Bi Kitunda aliwadharau
wanaume wa jamii yao na kuwafananisha na wanawake ambao katika jamii
wanadharauliwa siku zote. Hapa anatuonesha jinsi gani jamii hii ilikuwa
53
ikinyanyashwa na Mjerumani kwa kuwafanyisha kazi, na kuwapiga wanapodai haki
zao. Kwa ujumla wananchi hawakuwa na haki katika ardhi yao hivyo ilikuwa ni
lazima kumpiga Mjerumani ili kujitoa katika makucha yake. Wananchi hawa
walilazimika kuungana na kuwa wamoja ili waweze kupigana na kupata uhuru wa
kuishi katika nchi yao kwa amani.
4.8.6 Tashtiti
Tashititi ni mkazo wa maneno yasemwayo au yanayoandikwa ambayo yanayoweza
kuwa muundo wa swali au maelezo kwa jambo linalofahamika jibu lake, lengo ni
kusisitiza jambo na kuleta mshangao. Utafiti huu ulichunguza na kubaini kuwa
msanii alitumia tashititi katika kufikisha ujumbe wa kazi yake ya kisanii. Jedwali
linalofuata linaonesha ujitokezaji wa tashititi katika tamthiliya ya Kinjeketile.
Jedwali Na 4.24: Ujitokezaji wa Tashititi katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Tashtiti
1 Eti nyinyi wanaume kweli?
2 Watu wamekufa?
3 Ujinga? Maji ujinga?
Chanzo: Data kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile alitumia tashititi kuwasilisha ujumbe wa kazi
yake ya kihistoria kwa hadhira. Mfano “Eti nyinyi wanaume kweli” swali hili
wanaulizwa wanaume, ambapo jibu lake lipo. Lengo la swali ni kuweka msisitizo
wa wanaume kuwa jasiri na shujaa wa kutoa maamuzi ya haraka ya kuamua
kupigana vita ili kuondoa unyanyasaji waliokuwa wakifanyiwa na Majerumani.
54
4.8.7 Tashihisi
Utafiti huu ulichunguza na kubaini kuwa msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile
alitumia tamathali ya tashihisi kujenga ujumbe wa kazi yake ya kisanii. Tashihisi ni
tamathali ya semi ambayo sifa ya uhai huamishiwa kwenye kitu kisicho na uhai na
kuvipa uwezo wa kutenda kama binadamu. Jedwali linalofuata linaonesha ujitokezaji
wa tashihisi katika tamthiliya ya Kinjeketile.
Jedwali Na 4.25: Ujitokezaji wa tashihisi katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Tashihisi
1 Kisasi cha siku nyingi kilituvaa mala moja
2 Mapenzi haya yatatuunganisha tutakuwa kitu kimoja
Chanzo: Data kutoka katika tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Msanii alitumia tamathali ya semi ya tashihisi kuwasilisha dhamira ya mapenzi
katika nchi, mfano “Mapenzi haya yatatuunganisha tutakuwa kitu kimoja “.Mapenzi
yamepewa uwezo wa kuunganisha watu ili wawe na umoja. Msanii alituonesha
kuwa watu wa kusini waliungana na kuwa kitu kimoja kwa lengo la kumwondoa
Mjerumani ambaye alikuwa amewachosha wananchi kwa kuwanyanyasa na
kuwakandamiza, na kukosa haki na uhuru katika ardhi yao.
4.8.8 Mdokezo
Katika tamthiliya ya Kinjeketile baada ya uchunguzi na uchambuzi ulibaini kuwa
msanii alitumia mdokezo katika kufikisha ujumbe wa kazi yake ya kisanii. Jedwali
linafuata linawasilisha ujitokezaji wa baadhi ya mdokezo katika tamthiliya ya
Kinjeketile.
55
Jedwali Na 4.26: Ujitokezaji wa Mdokezo katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Mdokezo
1 Moshi ule … Kinjeketile anafanya kafala
2 Nimemwona mtu kama yeye … yeye hasa, lakini kwa mbali
3 Jamani mbona haludi, ntu hawezi kukaa ndani ya maji …
4 Nilikuwa natiwa ziki ziki katika moyo wangu na jambo hili …
5 Ondoa mwangaza … walisema wanaleta mwangaza … kutoa kiza ...
6 Mimi sikuleta maji, mimi …
7 Mumetoka mbali, tumeshastahimili mengi …
8 Tafazali kesho moja …
9 Na kama mibaazi …
10 Neno likintawala ntu badala ya ntu kulitawala neno …
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile alitumia mdokezo kufikisha ujumbe kwa jamii.
Dhamira ya wananchi ni kuondoa unyanyasaji uliofanywa na mkoloni, mfano
“Nzungu afukuzwe lakini kabla ya kufukuzwa” Shauku ya wananchi ilikuwa ni
kupigana vita kumwondoa mkoloni, ili wapate kuishi kwa amani katika nchi yao.
“Sote tunalo shauli moja lakini” Msanii ametuonesha shauri ni moja, kumwondoa
mkoloni.
4.9 Methali
Baada ya uchunguzi kufanyika ulibaini kuwa msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile
ametumiamethali katika kufikisha ujumbe kwa jamii. Msoikile (1992) anasema
methali ni semi zinazotokana na ujuzi, kanuni na tabia za jamii ambazokwa kawaida
hushauri na kufundisha mambo mbalimbali kwa wanajamii. Jedwali linalofuata
linaonesha ujitokezaji wa methali katika tamthiliya ya Kinjeketile.
56
Jedwali Na 4.27: Ujitokeazji wa Methali katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Methali
1 Halaka halakahaina balaka.
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Knjeketile(2016)
Msanii wa tamthiliya ya Kinjeketile ameonesha msisitizo wa kuvuta subira hadi
wajipange katika kumpiga Mjerumani, lakini wananchi walikuwa na haraka kwa
kuwa walikuwa na maji ya maisha. Wananchi hawa walikuwa na haraka ya kupigana
kwa imani ya kumshinda Mjerunmani kwa maji wailiyokuwa nayo. Kitunda
anamwambia Kinjeketile “Tuanze, Tuanze,Tuanze,Tuanze!” Kwa maana kwamba
waanze kupigana lakini Kinjeketile hakuwa tayari. Kinjeketile anamsihi Kitunda
avute subira kwa kusema “Halaka halaka haina balaka” Msanii ameonesha msisitizo
kwa jamii kupanga malengo au mambo yao vizuri kabla ya kuamua na kutofanya
maamuzi ya haraka ili waweze kufanikiwa.
4.10 Misemo
Msanii wa tamthiliya Kinjeketile alitumia misemo kuwasilisha ujumbe aliokusudia
kwa hadhira kutokana na utafiti huu ulivyobainisha. Jedwali linalofuata linaonesha
ujitokezaji wa baadhi ya misemo katika tamthiliya Kinjeketile.
Jedwali Na 4.28: Ujitokezaji wa misemo katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Na Misemo
1 Hata kama kitu cha kula anakataa.
2 Udngo mwekundu atapigwa na atatolewa nchini.
3 Moshi kulikuwa na moshi, ukungu, kulikuwa na ukungu.
4 Afazali kisa hiki! Afazali utumwa wa mwili kuliko wa akili unaoletwa na
mwanga.
Chanzo: Data za utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
57
Msanii alitumia misemo katika kufikisha ujumbe wa kazi yake ya kisanii kwa jamii.
Mfano “Udongo mwekundu atapigwa na atatolewa nchini,” Msanii alitumia udongo
mwekundu kama mtu mbaya ambaye aliwanyanyasa wananchi. Udongo mwekundu
alifananishwa na mkoloni ambaye alikuwa Mjerumani alyeitawala Kusini mwa
Tanzania. Msanii aliwajengea dhamira ya kumwondoa Mjerumani ili wapate
ukombozi. Wananchi walipigana kujikomboa na kupata uhuru katika nchi yao.
4.11 Kuwasilisha Dhamira kuu za Tamthiliya
Msanii alitumia vipengele mbalimbali vya lugha kuwasilisha ujumbe wa kazi za
kifasihi. Katika tamthiliya ya Nyereroe na Safari ya Kanaani, msanii aliwasilisha
dhamira kwa kutumia vipengele mbalimbali vya lugha kama inavyoenekana katika
Jedwali namba 4.32.
Jedwali Na 4.29: Ujitokezaji wa Dhamira katika Tamthiliya Teule
Namba Dhamira
1 Kujenga uzalendo
2 Demokrasia
3 Umaskini
4 Matabaka
5 Uongozi mbaya
6 Unyonyaji
7 Mapenzi
Chanzo:Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya ya Nyerere na safari ya kanaani
(2016)
Vipengele vya lugha katika Nyerere na Safari ya Kanaani vimewasilishwa na
msanii na kuonesha dhamira mbalimbali zilizojitokeza katika tamthiliya hii. Msanii
ameonesha jinsi Nyerere alivyotaka vijana wawe wazalendo kwa kuwapeleka katika
58
Jeshi la Kujenga Taifa aidha ikumbukwe vijana wanapofanyiwa tohara ni sehemu ya
mafunzo na maadili ya maisha. Pia aliruhusu vyama vya upinzani ili kudumisha
demokrasi katika nchi. Utafiti umegundua kuwa dhamira za vipengele vya lugha
vilivyotumika katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani havina tofauti
kubwa na vipengele vya lugha vilivyotumika katika tamthiliya ya Kinjeketile.Jedwali
namba 4.33 linaonesha ujitokezaji wa dhamira katika tamthiliya ya Kinjeketile.
Jedwali Na 4.30: Ujitokezaji wa Dhamira katika Tamthiliya ya Kinjeketile
Namba Dhamira
1 Umaskini
2 Umoja
3 Ukombozi
4 Umaskini
5 Rushwa na usaliti
Chanzo:Data za utafiti kutoka katika tamthiliya ya Kinjeketile (2016)
Msanii alitumia lugha inayozingatia vipengele vya lugha katika jedwali hapo juu
kuwasilisha dhamira za tamthiliya ya Kinjeketile. Vipengele vya lugha vilivyotumika
katika tamthiliya hii vimewasilisha harakati za ukombozi na changamoto
zilizowakumba. Mfano Na Mmatumbi akipigwa, Mzaramo ndiye atapiga kelele za
maumivu. Hapa msanii anaonesha jinsi wananchi walivyokuwa wakihimiza umoja
ili waweze kumwondoa mkoloni katika nchi yao.
Vipengele vya lugha vilevile vinaonesha jinsi wananchi walivyokuwa maskini, kwa
kunyimwa ardhi ya kulima au kuchimba madini katika ardhi yao na kubaki kuwa
watumwa kwa kuwafanyia kazi wakoloni na kuendelea kubaki maskini. Aidha utafiti
huu ulibaini kuwa vipengele vya lugha vilivyotumika katika tamthiliya ya
59
Kinjeketilevimewasilisha dhamira. Dhamira zimewasilisha ujumbe wa kazi ya
kifasihi, kuelimisha jamii, kuikosoa, kubainisha uovu na kuamsha jamii. Katika
tamthiliya ya Kinjeketile msanii ameonesha jinsi kulivyokuwa na changamoto katika
maisha ya wananchi, wanapowahamasisha wenzao kwa kutoa habari kwa Mjerumani
kupitia wanyapala, Hivyo kufanya umoja wao usiwe imara.” Utakachofanya askari
au mnyapala kashasikia, yaani hakuna siri. Tumeshikwa na njaa, na njaa hii
inatufanya tuuzane, tuna maadui na katika sisi wenyewe kuna maadui”. Katika
tamthiliya hii njaa ni umaskini walionao wanachi ambao inawafanya watu wapokee
rushwa na kuwasaliti wenzao.
4.12 Kulinganisha na Kulinganua Vipengele vya lugha katika Tamthiliya za
Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani
Katika tamthiliya ya Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani, utafiti huu
ulichunguza na kubaini jinsi wasanii wa tamthiliya hizi teule walivyotumia vipengele
vya lugha katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii kuona kuwa wanafanana au
wanatofautiana.Yafuatayo ni matokeo ya utafiti kama yalivyowasilishwa katika
vipengele vifuatavyo.
4.13 Kufanana
Katika tamthiliya ya Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani, utafiti huu
ulichambua na kubaini kuwa tamthiliya hizi zinafanana kimaudhui na kifani. Katika
tamthiliya hizi teule zinafanana kimaudhui na kifani kwa kuwa zote wasanii wake
walitumia mandhari halisi isiyo ya kubuni inayopatikana hapa Tanzania. Wasanii wa
tamthiliya hizi walipangilia maneno katika sentensi kwa kuzingatia kanuni za lugha
60
ya kiwsahili. Aidha tamthiliya hizi zinafanana kwa kuwa zinawasilisha masuala ya
kihistoria ingawaje kwa mbinu tofauti za kisanii vilevile kwa vipindi tofauti vya
kihistoria.
Jedwali Na 4.31: Vipengele vya Lugha Vinavyofanana katika Tamthiliya Teule
Na Kipengele cha Lugha Nyerere na Safari ya Kanaani Kinjeketile
1 Nidaa
2 Kejeli
3 Sitiari
4 Tashihisi
5 Tashibiha
6 Takriri
7 Tashtiti
8 Mdokezo
9 Misemo
10 Methali
Tukichunguza jedwali hapo juu linaonesha kuwa wasanii wa tamthiliya teule
wanafanana katika vipengele vya matumizi ya lugha. Watunzi wote wametumia
vipengele vya lugha ambavyo ni tamathali za semi kama vile nidaa, kejeli, sitiari,
tashihisi, tashibiha, takriri, tashtiti, mdokezo na tanakali sauti. Vilevile watunzi hawa
wametumia vipengele vingine vya lugha ambavyo ni methali na misemo. Katika
tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani msanii amemwonesha Nyerere kuwa ni
mtu mwenye msimamo kwa kusema amesimama imara kama mlima Kilimanjaro
hatikisiki. Nyrerere hapa alikuwa ni mtu mwenye msimamo habadiliki na wala
61
hasikilizi maneno yasiyo na mwelekeo mzuri wa kuiletea nchi maendeleo. Aidha
tumeona msanii wa KinjeketileamemwoneshaKinjeketile kuwa na msimamo wa
kukataa kutawaliwa na wakoloni mfano “Afazali kufa kuliko kukaa hivi
tunatawaliwa, tunalimishwa kama wanyama” Kwa kutumia nadharia ya fasihi ya
jamii hii misimamo na mapambano dhidi ya mkoloni na mambo yanayotokea katika
jamii unyonyaji na rushwa yanahifadhiwa na kubaki kuwa historia.
4.14 Kutofautiana
Jedwali Na 4.32: Vipengele vya Lugha Vinavyotofautiana katika Tamthiliya
Teule
Namba Kipengele cha lugha Nyerere na Safari ya Kanaani Kinjeketile
1 Tanakali sauti
2 Nahau
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya teule (2016)
Tukichunguza jedwali hapo juu linaonesha kuwa wasanii wa tamthiliya teule
wametofautiana katika matumizi ya vipengele vya lugha. Msanii wa tamthiliya
Nyerere na Safari ya Kanaani ametumia kipengele cha lugha cha tamathali ya
semiya tanakali sauti wakati msanii wa Kinjeketile hajatumia kipengele hicho. Aidha
msanii wa Nyerere na Safari ya Kanaani ametumia kipengele cha lugha nahau lakini
msanii wa Kinjeketile hakutumia. Kwa hiyo msanii wa tamthiliya ya Nyerere
naSafari ya Kanaani Mbogo ametumia vipengele vya lugha vine ambavyo ni
tamathali za semi, misemo, methali na nahau wakati msanii wa Kinjeketile Hussein
ametumia vipengele vitatu vya lugha ambavyo ni tamathali za semi, misemo na
methali
62
4.15 Kufanana au Kutofautiana kwa Dhamira Zilizojitokeza katika
Tamthiliya Teule
Tamthiliya ya Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani zimetungwa kwa
umahiri, katika kujadili masuala ya kihistoria yaliyojitokeza katika jamii.
Jedwali Na 4.33: Kufanana kwa Dhamira Zilizowasilishwa na Vipengele vya
Lugha
Namba Dhamira Kinjeketile Nyerere na Safari ya Kanaani
1 Matabaka
2 Umaskini
3 Nafasi ya mwanamke
4 Uongozi mbaya
5 Rushwa x
6 Mapenzi x
7 Ukombozi x
4.15.1 Matabaka
Wasanii wa tamthiliya ya Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani walionesha
dhamira ya matabaka. Katika tamthiliya ya Kinjeketile msanii alionesha matabaka
pale Mjerumani alipowagawa watu . Kuna Mjerumani (mkoloni) ambaye alikuwa na
maisha ya hali ya juu, halafu mnyapala ambaye yeye ndiye anayesimamia wenzake
wafanye kazi na wale wanaotumikishwa na Mjerumani. Hivyo hapa kulikuwa na
tabaka la mabwana na watumwa. Katika tamthiliya ya Nyerere naSafari ya Kanaani
kulikuwa na tabaka la matajiri na la maskini kwa sababu baada ya kupata uhuru
miaka michache watu walianza kujilimbikizia mali na kuwa matajiri. Ndipo
lilipotokea tabaka la matajiri na maskini.
63
4.15.2 Uongozi Mbaya
Msanii katika tamthiliya ya Kinjeketile alionesha uongozi mbaya pale ambapo
Kinjeketile aliwapa wananchi maji ya kujilinda wakati wa vita lakini akawa hatoi
maamuzi ya kupigana na Mjerumani. Katika Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya
Kanaani msanii alionesha uongozi mbaya pale wanafunzi wa vyuo vikuu walipotaka
kuzungumza na Rais kwa ajili ya suala la Jeshi la Kujenga Taifa na kukatwa asilimia
60% ya mshahara kwa muda wa miezi 18 watakapoajiriwa. Rais Nyerere alikataa
kukutana nao na kusikiliza maoni yao ndipo walipoamua kuandamana na kubeba
mabango yenye malalamiko yao hadi viwanja vya Ikulu.
4.15.3 Nafasi ya Mwanamke
Katika tamthiliya zote mbili nafasi ya mwanamke imebainishwa. Katika tamthiliya
ya Kinjeketile msanii amemwonesha mwanamke kama ni mtu tegemezi. Mwanamke
alimtegemea mume wake kwa kila hali hata pale ambapo waume zao walienda
kufanya kazi kwa Mjerumani wao, walikuwa wanasubiri bila kufanya kazi na
mwishoni tatizo la njaa likajitokeza.
Katika tamthiliya ya Nyerere na Safari yaKanaani msanii amemwonesha Farida
kuwa na uamuzi wa kumchagua mchumba wake mwenyewe. Baba yake Farida
alikuwa hampendi Martini kwa sababu alikuwa hajafanyiwa tohara. Zebedayo baba
yake Farida alikuwa amesikitika kwa sababu ya msimamo wa Farida wa kutaka
kuolewa na Martini. Mfano Zebedayo alisema “Niko katikati ya bahari
machafukoge.Milima ya mawimbi ya bahari karibu kunizika. Silioni tumaini la
kumwepusha binti yangu Farida dhidi ya hii nakama.
64
4.15.4 Umaskini
Msanii katika tamthiliya ya Kinjeketile ameonesha umaskini uliosababishwa na
wakoloni. Wakoloni hawa walichukua wananchi kwenda kuwalimia mashamba na
kazi mbalimbali.Wakati walipokuwa wakifanya kazi kwa wakoloni, walishindwa
kuzalisha mali kwa ajili ya familia zao. Kwa hiyo uzalishaji kwa ajili ya familia
ulikuwa ni kidogo hivyo kupelekea wanachi kuwa maskini kwa kukosa chakula na
mahitaji yao mbalimbali.
Katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani msanii ametuonesha Martini
alipowasilisha umaskini, alipokuwa akisoma risala mbele ya Rais Nyerere baada ya
maandamano. Alisema wazazi wao ni maskini na wanawategemea wao wasome
wapate kazi ndipo wakawasaidie.Badala yake serikali inawaambia baada ya
kumaliza vyuo ni lazima walitumikie Jeshi la Kujenga Taifa kwa wa miezi sita. Na
watakapoajiriwa kazi wakatwe asilimia sitini ya mshahara kwa muda wa miezi kumi
na nane.
Jedwali Na 4.34: Kutofautiana kwa Dhamira zilizowasilishwa na Vipengele vya
Lugha
Namba Dhamira Nyerere na Safari ya Knaani Kinjeketile
1 Rushwa na Usaliti
2 Mapenzi
3 Ukombozi
Chanzo: Data za Utafiti kutoka katika Tamthiliya teule (2016)
4.15.5 Rushwa na Usaliti
Katika Jedwali namba 4.37 kujitokeza kwa dhamira kumetofautiana. Rushwa na
usaliti vimejitokeza katika tamthiliya ya Kinjeketile wakati katika tamthiliya ya
65
Nyerere na Safari ya Kanaani hakuna. Wananchi wao kwa wao wanatoa sirina
kuwasaliti wenzao ambapo inapelekea umoja waokukosa nguvu na wakati mwingine
adui amekuwa akipata siri zao na hii inawapelekea kutokushinda vita kwa urahisi.
4.15.6 Mapenzi
Katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani msanii aliongelea mapenzi ya
Farida na Martini ambayo hayakuwa ya siri. Wawili hawa walipendana kwa dhati.
Martini alikuwa hajafanyiwa tohara lakini kwa kuwa Farida alikuwa na mapenzi ya
dhati kwake alimhimiza atahiriwe ili waweze kutimiza ndoto yao ya kuoana. Hata
pale walipofanya maandamano na Rais Nyerere akawafuza chuo waliendelea na
mapeni yao. Walipokuwa kijijini kwao Martini alitahiriwa kwa nguvu bado
aliendelea kumhudumia na baadaye walirudi chuoni kumalizia mafunzo yao.
4.15.7 Ukombozi
Katika tamthiliya ya Kinjeketile msanii ameonesha harakati za mapinduzi na
ukombozi zilizofanywa na wananchi wa Kusini mwa Tanzania.Wananchi hawa
walipambana na Mjerumani ili kumwondoa katika nchi yao. Katika tamthiliya ya
Nyerere na Safari ya Kanaani mkoloni alikwishaondolewa na dhamira ya ukombozi
hapa haipo. Kilichokuwepo Nyerere alikuwa anajenga jamii mpya isiyokuwa na
wanyonyaji wanaojilimbikizia mali na kujenga matabaka katika jamii ya walio nacho
na wasokuwa nacho.
66
4.15.8 Hitimisho
Sura hii imejadili data za matokeo yaliyopatikana kulingana na malengo mahsusi ya
utafiti huu. Mtafiti ameonesha vipengele vya lugha ambavyo vimetumika katika
tamthiliya teule.
Aidha utafiti huu umebaini kuwa tamthiliya ya Kinjeketile imetumia lugha ya
kawaida inayomwezesha msomaji kuelewa kwa urahisi ujumbe wa kihistoria
uliowasilishwa na msanii. Vilevile utafiti umebainikuwa tamthiliya za Kinjeketile na
Nyerere na Safari ya Kanaani zimetumia vipengele vya lugha ambavyo vimetumia
lugha ya kitamathali zaidi ili kufikisha ujumbe kwa hadhira. Vipengele vya lugha
vilivyotumika katika tamthiliya teule vimeeleza kuwasilisha dhamira kuu za
tamthiliya hizo, ambazo ni harakati za ukombozi na mapinduzi, nafasi ya
mwanamke, unyonyaji na ukandamizaji, rushwa na usaliti. Tamthiliya teule
zinawasilisha suala la kihistoria kwa vipindi viwili tofauti, Kinjeketile imewasilisha
harakati za watu wa Kusini mwa Tanzania katika kupambana na mkoloni kabla ya
uhuru. Watu hawa wa Kusini waliamini kuwa risasi zitageuka kuwa na wao maji na
wao kupata ushindi kwa urahisi. Tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani
imewasilisha historia ya nchi baada ya uhuru ambapo imejadili harakati za
kupambana na ukoloni mambo leo. Tanzania baada ya uhuru, kwa muda mfupi watu
walijilimbikizia mali na kujenga tabaka la matajiri na maskini, ambapo Rais Nyerere
hakukubaliana na jambo hilo. Sura inayofuata inawaslisha muhtasari, hitimisho na
mapendekezo.
67
SURA YA TANO
MUHTASARI, HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
5.1 Utangulizi
Sura hii ya mwisho hutoa muhtasari, hitimisho na mapendekezo ya utafiti
uliofanyika. Sura hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo, sehemu ya
kwanza inahusu muhtasari, sehemu ya pili inahusu hitimisho na sehemu ya tatu
inahusu mapendekezo ya utafiti huu.
5.2 Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti
Utafiti ulilenga kutathmini matumizi ya lugha na dhamira katika tamthiliya za
kihistoria za Kinjeketile iliyoandikwa na Ebrahim Hussein na Nyerere na Safari ya
Kanaani iliyoandikwa na Emmanuel Mbogo. Lengo ni kutaka kuibua matumizi ya
lugha na vipengele vyake na dhamira vilivyotumika katika kuwasilisha ujumbe
katika jamii na kuvilinganisha kutoka kwa msanii mmoja na mwingine.Tatizo la
utafiti huu ni kutathmini vipengele vya lugha na dhamira katika tamthiliya teule ili
kuweza kuona jinsi gani wasanii wa tamthiliya hizi wanafanana au kutofautiana.
Lengo la utafiti huu kama lilivyobainishwa katika sura ya kwanza. Ilikuwa ni
kutathmini vipengele vya lugha kwa kulinganisha tamthiliya ili kubaini vipengele
vinavyowafananisha na kuwatofautisha wasanii wa tamthiliya hizi. Malengo mahsusi
ya utafiti huu yalikuwa : Kutathmini matumizi ya lugha na dhamira katika tamthiliya
teule na kulinganisha na kulinganua uteuzi wa vipengele vya lugha katika
kuwasilisha ujumbe kwa hadhira. Ili kufikia malengo hayo utafiti huu ulikusudia
kujibu maswali haya yafuatayo: Je, ni vipengele vipi vya lugha vilivyojitokeza katika
68
tamthiliya hizi? Uteuzi wa vipengele vya lugha katika tamthiliya teule unafananana
au kutofautiana kwa vipi katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii? Ni dhamira zipi
zilizojitokeza katika tamthiliya teule? Uteuzi wa dhamira katika tamthiliya teule
unafanana au kutofautiana kwa vipi katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii? Kuna
tafiti nyingi zilizofanywa za kulinganisha kazi za tamthiliya lakini ulinganishaji huo
haukuzingatia masuala ya kihistoria. Aidha tafiti nyingi zilijikita kulinganisha fani na
maudhui ya kazi za fasihi. Utafiti unahitajika kufanyika juu ya kutafiti jinsi matumizi
ya lugha na dhamira vinavyoweza kumtofautisha msanii mmoja na msanii
mwingine, pengo ambalo utafiti huu umekusudia kuliziba.
Kulingana na malengo ya utafiti huu, nadharia ya fasihi ya jamii ndiyo iliyotumika
na kuongoza katika kuchunguza na kuchambua data za utafiti huu. Utafiti ulikusanya
data kwa kusoma machapisho katika maktaba. Mbinu hii ya usomaji katika maktaba
ilisaidia kuchambua vitabu vyote viwili na kubainisha matumizi yalugha na
vipengele vyake na dhamira zilizojtokeza. Wananchi au wasomaji waliweza
kuelimika kupitia masuala ya historia yaliyowasilishwa na wasanii wa tamthiliya
hizi.
Baada ya utafiti imebainika kuwa wasanii wa tamthiliya teule wametumia vipengele
vya lugha kuwasilisha ujumbe kwa jamii ambavyo ni methali, nahau, misemo na
tamathali za semi. Baadhi ya tamathali za semi ni kama sitiari, kejeli,mdokezo,
tashibiha, takriri, tashihisi, nakadhalika. Vipengele vya lugha vilivyotumika
vinamtofautisha msanii wa tamthiliya moja na tamthiliya nyingine. Katika kujibu
swali la kwanza la utafiti huu ni kuwa utafiti ulichunguza matumizi ya lugha katika
tamthiliya ya Kinjeketile. Utafiti uligundua kuwa msanii alitumia lugha rahisi
69
inayomwezesha msomaji kuelewa kwa urahisi. Tamathali za semi zilitumika ambazo
ni sitiari, tashibiha , tashihisi, takriri, kejeli, tashtiti, na nidaa. Utafiti ulichambua na
kugundua kuwa tamthiliya ya Kinjeketile ambayo imeawasilisha masuala ya historia
ya tukio ambalo lilitokea kwa wananchi wa Kusini mwa Tanzania. Wananchi wa
Kusini walipigana vita kumwondoa Mjerumani na utawala wake.
Aidha katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani msanii alitumia vipengele
vya lugha ambayo ni pamoja na methali, nahau, misemo na tamathali za semi
ambazo ni sitiari, tashihisi, tashibiha, tashtiti, na takriri. Matumizi haya ya lugha na
vipengele vyake ambavyo msanii alitumia kwa lengo la kuwasilisha ujumbe kwa
jamii. Wasomaji wakisoma tamthiliya hii waweze kujua kwamba kumbe kulikuwa
na tohara na Jeshi la Kujenga Taifa katika jamii iliyokuwepo awali. Data za utafiti
huu zilizokusanywa, zimechambuliwa kwa uchambuzi linganishi. Katika kujibu
swali la pili la utafiti huu ambalo lililenga kubainisha matumizi ya lugha na
vipengele vyake vinafanana au kutofautiana kwa vipi katika kuwasilisha ujumbe kwa
jamii katika tamthiliya teule. Utafiti huu ulibaini dhamira zilizojitokeza katika jamii
na kufikisha ujumbe katika jamii. Hivyo vipengele vya lugha katika tamthiliya hizi
zinaelimisha, kukosoa na kuamsha jamii. Katika dhamira, vipengele vya lugha
vimetumika kujenga jamii katika kazi za fasihi. Kwa mfano nafasi ya mwanamke,
harakakati za ukombozi, uongozi mbaya, rushwa, imani za jadi na usaliti.
Kujibiwa kwa swali la nne ni kutokana na data zilizopatikana katika utafiti kama
ifuatavyo: Ni kulinganisha na kulinganua dhamira na jinsi zilivyotumika na wasanii
wa tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari yaKanaani katika kuwasilisha
ujumbe katika jamii husika. Utafiti ulibaini kuwa katika uteuzi wa vipengele vya
70
lugha wasanii wa tamthiliya hizi wametofautiana. Tamthiliya hizi zinatofautiana
katika uteuzi wa matumizi ya vipengele vya lugha. Katika tamthiliya ya Kinjeketile
msanii alitumia lugha ya kawaida inayomwezesha msomaji kuelewa ujumbe uliopo
kwa urahisi. Kwa mfano “Wewe mwanamke, Wamatumbi waoga! Sisi sote tunataka
Mjerumani aondoke.” Katika mifano hiyo lugha iliyotumika iko wazi, msomaji
anaelewa ujumbe uliopo moja kwa moja. Tofauti ya Nyerere na Safari ya Kanaani
ambapo msanii ametumia lugha ambayo msomaji ni lazima afikirie ili kupata wazo
la msanii. Mfano “Tohara ni roketi” Hapa lazima msomaji atafakari ili aweze kupata
wazo au dhamira ya mtunzi ndipo apate ujumbe uliopo.
Katika utafiti huu ulibaini kuwa mbinu za matumizi ya lugha ambazo zinatofautisha
tamthiliya hizi katika kiwango cha utumizi na kubainisha upekee wa msanii kutokana
na athari za kimazingira na kihistoria. Kwa mfano katika tamthiliya ya Kinjeketile ni
tamthiliya iliyojikita katika utunzi wa kiaristotle, kwa sababu inazungumzia juu ya
mhusika mkuu ambaye aliaminiwa na watu na baadaye kupata anguko. Katika
tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaanimsanii ameonesha suala la kutumikia
Jeshi la Kujenga Taifa kama mafunzo katika jamii. Kwa hiyo msanii wa Nyerere na
Safari ya Kanaani amejikuta akitumia zaidi vipengele vya lugha kuliko Kinjeketile.
Kufanana kwa tamthiliya hizi ni kwa sababu zote zinawasilisha masuala ya kihistoria
ingawa ni mbinu tofauti za kisanaa na vipindi tofauti vya kihistoria. Hivyo inakuwa
vigumu kutoa hitimisho kuwa tamthiliya hizi za Kinjeketile na Nyerere na Safari
yaKanaani zinafanana.Utafiti huu uligundua kufanana kwa tamthtiliya hizi katika
matumizi ya tashihisi,tashibiha, tashtiti, sitiari, takriri, kejeli na mdokezo. Pia
kufanana kwa tamthiliya hizi ni katika kuwasilisha dhamira mbalimbali kwa kutumia
71
vipengele vya lugha. Mfano wa dhmira hizo ni uongozi mbaya, umaskini,
matabakana nafasi ya mwanmke. Wasanii wa tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na
Safari ya Kanaani wanafanana kwa kuwa wametoka jamii zenye historia
zinazofanana, itikadi moja, siasa na zinafanana kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.
Kutofautiana kwa tamthiliya hizi msanii wa tamthiliya ya Nyerere na Safari
yaKanaani ametumia vipengele vinne vya lugha ambavyo ni tamathali za semi,
methali misemo na nahau wakati msanii wa Kinjeketile ametumia vipengele vitatu
vya lugha navyo ni tamathali za semi, methali na misemo. Katika tamathali za semi
msanii wa Nyerere na Safari ya Kanaani ametumia tanakali sauti ambapo Kinjeketile
hakutumia. Kutofautiana kwa dhamira zilizojitokeza Nyerere na Safari ya Kanaani
kuna mapenzi ya Farida ambaye alimpenda Martini kwa dhati wakati Martini
alikuwa hajatahiriwa lakini katika tamthiliya ya Kinjeketile mapenzi hayapo.
Dhamira za rushwa na ukombozi zilijitokeza katika tamthiliya ya Kinjeketile wakati
katika Nyerere na Safari ya Kanaani hazikujitokeza. Wanachi wa Kusini
walipambana na mkoloni ili kjikomboa kutoka katika makucha yao ya kunyanyaswa.
5.3 Hitimisho
Utafiti huu umejadili matumizi lugha na vipengele vyake na dhamira zilizojitokeza
zilivyotumika katika tamthiliya zilizochunguzwa za Kinjeketile na Nyerere na Safari
ya Kanaani. Katika utafiti huu uamebaini kuwa tamthiliya Knjeketile imetumia
vipengele vya lugha ambavyo ni pamoja na tamathali za semi, methali, na misemo.
Aidha msanii wa tamthiliya hii ametumia lugha ya kawaida na ya wazi ambayo
inamrahisishia msomaji kuelewa au kupata ujumbe uliowasilishwa.
72
Katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani utafiti umebaini kuwa msanii
ametumia vipengele vya lugha ambavyo vimebebwa na lugha zaidi yaKinjeketile.
Vipengele hivyo vya lugha ni kama vile tamathali za semi, methali, nahau na
misemo. Hivyo utafiti umebaini kuwa tamthiliya ya Nyerere na Safari yaKanaani
imetumia lugha ya kitamathali zaidi katika kufikisha ujumbe kwa hadhira. Pia
msanii ametumia lugha inayomfikirisha msomaji ili aweze kubaini ujumbe
uliokusudiwa. Utafiti umebaini kuwa tamthiliya hizi zinatofautiana katika
kuwasilisha suala la kihistoria, kwa kuwa wasanii hawa wanawasilisha historia ya
jamii kwa muda tofauti.
Msanii wa Kinjeketile amejadili kwa uhalisia juu ya jamii ya Kusini kabla ya uhuru,
katika kupambana kwa kupigana vita na Mjerumani. Watu wa Kusini waliamini
kuwa maji yanaweza kubadili risasi kuwa maji na kuweza kumwondoa Mjerumani
katika ardhi yao. Aidha katika tamthiliya ya Nyerere na Safari ya Kanaani msanii
amewasilisha historia katika kipindi baada ya uhuru , hivyo kujadili historia ya
harakati za kujenga ujamaa na uzalendo baada ya wakoloni kuondoka.
Wasanii wa Tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani wanafanana
kwa ujumbe wa kazi zao kwa kuwa wamejadili mambo yaliyopo katika jamii kama
vile harakati za ukombozi, rushwa, usaliti, na nafasi ya mwanamke. Pia wamejadili
vipengele vya lugha katika tamthiliya teule. Aidha utafiti umebaini kuwa tamthiliya
hizi zimeandikwa na wasanii wa jamii moja ambao walishuhudia na kupata
masimulizi ya historia ya jamii yao. Hivyo wanafanana katika kuwasilisha ujumbe
kwa jamii.
73
Utafiti huu umeleta faida kwa taaluma ya fasihi kwa wasomi kwani utatajirisha
maktaba za Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Wanachuo watakaosoma utafiti huu
watapata rejea ya mambo mbalimbali ya kimtindo na wengine watatumia kwa
kuandika katika tangulizi ya kazi zao. Pili utafiti huu umetoa mchango wake kwa
jamii umuhimu wa historia ya nchi au jamii, ni kwa namna gani kazi za fasihi
zinavyobeba historia ya nchi. Tatu, utafiti huu umesaidia kukuza lugha kwa kuwa
vipengele vyake vimefafanuliwa namna vilivyotumika katika kazi hizi, za kifasihi
kama matumizi ya tamthali za semi, methali, nahau na misemo. Hivyo kuwafanya
watakaosoma kazi hizi kukuza msamiati na uwezo wa kutumia lugha kisanaa. Nne,
utafiti huu utachochea ari ya tafiti tofauti tofauti za kifasihi zikiwemo tamthiliya za
Kiswahili hasa zile zinazozungumzia historia fulani ya nchi au jamii.
5.4 Mapendekezo
Tamthiliya za Kinjeketile na Nyerere na Safari ya Kanaani zimewasilisha suala la
kihistoria kwa nyakati mbili tofauti. Utafiti umeweza kizilinganisha tamthiliya hizi
na kuonesha zinavyotofautiana katika uteuzi wa vipengele vya lugha. Utafiti huu
unapendekeza kuwa kuna haja ya kufanya utafiti wa hali ya juu kabisa juu ya kazi
nyingine zilizoandikwa juu ya historia ya nchi au jamii. Pia unapendekeza watatafiti
wajitokeze katika kufanya utafiti unaohusu kazi za kisanaa za kihistoria. Wasanii
wajitokeze katika kutunga kazi za fasihi zinazobeba historia ya nchi au jamii hasa
tamthiliya za Kiswahili. Aidha tafiti mbalimbali ziendelee kufanyika ambapo
zitakuza matumizi ya lugha na kuibua dhamira ili kuwawezesha wanachuo kupata
rejea ya kazi zao.
74
MAREJELEO
Alderson, C. G. & Berretta, A. (1992). (Wah.) Evaluating Second Education:
Cambridge Applied Linguistics. London: Cambridge University Press.
Bachman, R., & Schutt,R. (2007). The Practice of Researchin Criminology and
Criminal Justice(Toleo la 3). London: Sage Publications Inc.
Baker, T. (1994). Doing social research. Singapore: McGrwa-Hill.
Bakiza, (2010). Kamusi ya Kiswahili Fasihi. Nairobi: Oxford University Press East
Africa, Ltd.
Basnell, S. (1993), Comparative Literature: A Critical Introduction, Oxford:
Blackwell.
Berg, B. L. (2004). Qualitative Research Methods for the Social Science. (Toleo la
5.). Boston: Pearson Education, Inc.
Bryman, A. (2004). Social Research Methods. (Toleo la 2) Oxford: Oxford
Univerity Press.
Best, J. W., & Kahn, J. (1993). Research in Education. New York: Allyn Bacon Inc.
Cohen, L, Manion, L., & Morrison, K. (2000). Research Methods in Education.
(Toleo la 5). London: Rutledge Falmer.
Corbetta, P. (2003). Social Research: Theory, Methods and Techniques. London:
Sage Publications Inc.
Crystal, D., & Davy, D. (1969). Investigating English Style. London: Green and Co.
Limited.
Cuddon, J. A. (1998). Dictionary of Literarry Terms and Literary Theory.London:
Blackwell Publishers Ltd.
75
De Vaus, D. A. (1993). Surveys in Social Research (Toleo la 3.). London:University
College London Press.
De Vaus, D. (1985). Surveys in Social Research. (Toleo la 5.). London: Routledge.
Eagleton, T. (1983). Literary Theory: An Introduction. Cambridge: Blackwell.
Escarpit, R. (1974). Sociology of Literature. London: Frank Cass and Co. Ltd.
Hollway, L. (1997). Basic Concepts for Qualitative Research. Oxford:Blackwell
Science.
Hussein, E. (2003). “Hatua mbalimbali za Kubuni na Kutunga Tamthiliya Kufuatana
na Misingi ya Ki-Aristotle.” Katika Makala za Semina yaKimataifa ya
Waandishi wa Kiswahili 111 FASIHI. TUKI. Dar es Salaam.
Hussein, E. (1969), Kinjeketile. Nairobi: Oxford University Press.
Jilala, H. (2016). Misingi ya Fasihi Linganishi, Dar es Salaam, Daud Publish
Company.
Kahigi, K. K. (1995).Kioo cha Lugha:Jarida la Kiswahili, Isimu na Fasihi. Dar es
Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kezilahabi, E. (1976). Ushairi wa Shaaban Robert. Nairobi: East African Literature
Bureau.
Kiango, S. D. (1980). “Tamthiliya ya Kiswahili na Mabadiliko ya Dhamira1957 -
1975” Tasnifu ya Umahiri.,Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kiango, S. D. (1982), “Tamthiliya ya Kiswahili: Dhamira Chapwa na Usuli katika
Uchapwa,” Jarida la Kiswahili, Isimu na Fasihi.Dar es Salaam: Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
Kiango, S. D. (1990). “Mwelekeo wa Tamthiliya za Kiswahili.” Jarida laKiswahili,
Dar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
76
King’ei, J. K. (1987). “Usanifu wa Lugha katika Uandishi wa Hussein.” Katika
Mulika. 19, 19- 35.
King’ei, K., na Catherine, N. M (2005). Msingi wa Fasihi Simulizi, Nairobi: Kenya
Literature Bureau.
Kombo, D. K., & Tromp, D. L. A. (2006). Proposal and ThesisWriting:
Introduction, Nairobi: Paulines Publications Africa.
Kothari, C. K. (1990), Research Methods: Methods and Tecniques. New Delhi:
Willey Eastern Ltd.
Kothari, C. R. (1993). Research Methods : Methods and Tecniques (Toleo la 2). New
Delhi: Willey Eastern Ltd.
Kvale, S. (1996). Interviews An Introduction to QualitativeResearch Interviewing.
London: Sage Publications Inc.
Lakoff, G., & Johnson, M. (1980). Metaphor We Live By.Chicago: University of
Chicago Press.
Lakoff, G. & Johnson, M. (1988), Metophors we Live By (Toleo la 2): Chicago:
Chicago University Press.
Lee, R. M. (1993). Doing Research on Sensitive Topics. London: Sage Publications
Inc.
Mahenge, E. (2014). Nelson Mandela, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Dar es
Salaam.
Mauya, A. B. (2006). Semi Maan na Matumizi. Dar es Salaam: Tasisi ya Uchunguzi
wa Kiswahili.
Maxwell, J. A. (2005). Qualitative Research Design: An Interactive Approach.
London: Sage Publications Inc.
77
Mazrui, A. M., & Syambo, B. K. (1992), Uchambuzi wa Fasihi, Nairobi: East
African Educatinal Publishers Ltd.
Mbogo, E. (1993). “Matumizi ya Dhana na sanaa katika Sanaa za Maonesho za
Jadi katika Tamthiliya ya Leo. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
Mbogo, E. (2015), Nyerere na Safari ya Kanaani, Dar es Salaam: Karljamer Print
Tecnilogy.
Mlacha, S. A. K. (1981). Methali kama Chombo Muhimu katika Jamii, Makala za
Dar es Salaam: TUKI.
Mlama, P. O. (2003). “Utunzi wa Tamthiliya katika Mazingira ya Tanzania,” Katika
Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili I I I FASIHI. Dar
es Salaam: TUKI.
Msanjila, Y. P. Kihore, Y. M., na Massamba, D. P. B. (2010). Isimu Jamii:
Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: TUKI.
Msokile, M. (1992). Misingi ya Hadithi fupi, Dar es Salaam: Dar es Salaam
University Press.
Msokile, M. (1993), Misingi ya Uhakiki wa Fasihi, Nairobi: East African
Educational Pubilshers.
Mugenda, O. M., na Mugenda, A. G. (2003). Research Methods: Qualitative and
Quantitative Approaches. Nairobi: Acts Press Kenya.
Mulokozi, M. M., na Kahigi, K. K. (1979), Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar
es Salaam: Tanzania Publishing House.
Mulokozi, M. M. (1989). Tanzu za Fasihi Simulizi, Mulika namba 21. Dar es
Salaam: TUKI.
78
Mulokozi, M. M. (1996). Utangulizi wa Fsaihi ya Kiswahili, Dares Salaam: Taasisi
ya Uchunguzi wa Kiswahili.
Mutembei, K. A. (2012). Korasi katika Fasihi: Nadharia Mpya ya Uhakiki. Taaluma
ya Taasisi za Kiswahili. Daar es Salaam: Chuo Kikuu cha Dar es laam.
Mutembei, K. A. (1997). “Korasi na Uhusiano Wake na Sanaa za Maonesho:
Uchambuzi wa Kidaikronia” Katika Kioo cha Lugha Juzuu. 1(2),67 – 72.
Mutembei, K. A. (2008). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu, Nairobi: Jomo
Kenyatta Foundation.
Njogu, K., na Chimerah, R. M. (1999). Ufundishaji wa Fasihi.Dar es Salaam:
Oxford University Press.
Nkwera, F. V. (1979). Sarufi na Fasihi: Sekondari na Vyuo, Dar es Salaam:
Tanzania Publishing House.
Padget, D. (2002). Qualitative Methods ni Social Work Research; Challenges and
Rewards. London: Sage Publications Inc.
Patton, M. (2002). Qualitative Research and Evaluation Method (Toleo la 3).
London: Sage Publications.
Ponera, A. S. (2014). Utangulizi wa Nadharia ya Fasihi Linganishi, Nairobi:
Karljamer Print Tecnology.
Powell, R. R., & Lynn, S. C. (2004). Basic Research Methods forLibrarian. (Toleo la
5.). London: Sage Publications Inc.
Punch, K. F. (2005). Introduction to Social Research: Qualitative and Quantitative
Approaches. (Toleo la 2.). London: Sage Publications Inc.
79
Ramadhan, D. (2005). The Uses of Metaphors in Mbogo’s Ngoma ya
Ngw’anamalundi and Hussein’s Morani. A Stylistic Comparison.Tasnifu ya
Umahiri. Dar es Salaam: University of Dar es Salaam.
Richard, M. N. (2007). Nadharia na Uhakiki wa Fasihi.Nairobi: The Jomo Kenyata
Foundation.
Schutt, R. K. (2006). Investigating the Social World: The Process and Practice of
Resarch . London: Sage Publications Inc.
Semzaba, E. (2003). Tamthiliya ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Dar
es Salaam. Tanzania.
Sengo, T. S. Y. (2008). Sengo na Fasihi za Kinchi,Dar es Salaam: AERA
Publishers.
Senkoro, F. E. M. K. (1982). Fasihi. Dar es Salaam: Press and Publicity Centre.
Silverman, D. (2005). Doing Qualitative Research: A Practical Handbook (Toleo
2.). London: Sage Publicatins Inc.
Totosy de Zepetnek, S. (1996a). “Essays in Reader-Oriented Theory, Criticism, And
Pedagogy,” Katika jarida la International Pesrspectives onReading, Mh.
Steven Totosy de Zepetnek, Michigan Tecnological University, Michigan.
Totosy de Zepetnek, S. (1996b). “Thematic Cluster Canadian Review of
Comparative Literature,” katika jarida la Comparative Literature: History and
Contemporaneity,juzuu ya Utangulizi wa Fasihi Linganishi.
TUKI, (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.
Wafula, R. M. (1999). Uhakiki wa Tamthiliya: Historia na Maendeleo Yake. Nairobi:
Jomo Kenyatta Foundation.
80
Wallek, R., na Warren, A. (1948). Theory of Literature, Harcourt, Brace and
Company. New York.
Wamitila, K. W. (2003).Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus
Publication Ltd.
Wamitila, K. W. (2010), Kanzi ya Fasihi 1: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi.
Nairobi: Vide-Muwa.
Wamitila, K. W. (2010), Kichocheo cha fasihi, Simulizi na Andishi, Nairobi: Focus
Books.
Wamitila, W. K. (2002). Uhakiki wa Fasihi, Misingi na Vipengele Vyake. Nairobi:
Phoenix Publishers.
Weiss, R. S. (1994). Learning from strangers: The art and method of qualitative
interviewing. New York: Free Press.