Top Banner

Click here to load reader

Romans 2 · Web viewWAFU KATIKA DHAMBI, HAI KATIKA KRISTO Katika sura hii jambo kuu ni umoja wetu na Kristo katika kifo chake, kuzikwa, na kufufuka. Wakati ukweli huu unapoeleweka

May 29, 2018

Download

Documents

nguyentuong
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript

Romans 2

NEEMA MASOMO YA BIBLIAWARUMI 2

MATOKEO YA HAKI

SURA YA TANO

FOUR

Sura hii inafundisha misingi ya ukweli wa wokovu. Mistari mbali mbali hapa inaweza kutumika kumwongoza mtu kwa Kristo. Pia tunajifunza Baraka za kiroho kuwa ni sehemu ya wokovu huu mkuu.

Soma Warumi 5:1-5 __________(hakikisha)

1.(mstari 1) Tokeo la kuhesabiwa haki katika imani ni nini? ____________________________________ Amani hii ilitengenezwa na Kristo kwa damu yake pale msalabani. (Wakolosai 1:20)

Uadui kati ya ya Mungu na wenye dhambi umefikia kikomo na uhusiano mpya umeanza kama zao la imani katika kuteswa kwa Kristo.

2.(mstari 2) Tuna ziada gani kwa imani yetu katika Kristo Yesu? __________________________________

Tuna furaha ndani ya nini? _______________________________________________________________

3. (mistari 3 - 4) Tunafurahi katika dhiki (mateso) tukijua ya kuwa dhiki inaleta nini?

4. ___________________

______________________________________________________________________________________

5.

Ushindi katika Dhiki ni neno la kuangalia miongoni mwa Wakristo wanaokua. Kama tabia ndani ya motto inavyokua kwa adhabu na majaribu, hili hufanyika hata zaidi katika ukuaji wa kiroho wa Mkristo.

6. (mstari 5) Namna gani tumaini letu kwa Mungu halitavunjika? _____________________________________

________________________________________________________________________________________

Hii ni mara ya kwanza ya kutajwa kwa Roho Mtakatifu katika Warumi. Ana kazi kubwa ya kufanya katika maisha ya waamini, kama tutakavyogundua ndani ya sura chache zijazo. Haki ambayo Mungu ametoa, sasa inapaswa izoezwe. Roho Mtakatifu sasa anaishi ndani yetu na anaonyesha upendo wake kutupitia sisi.

5(mstari 6) Mambo yapi mawili ni ya kweli kuhusu hali yetu wakati Kristo alipokufa kwa ajili yetu? ________________________________________________________________________________________

6.(mstari 8) Mungu alionyeshaje upendo wake kwa wenye dhambi?

_________________________________

________________________________________________________________________________________

7.(mstari 9) Tutawezaje kuokolewa na ghadhabu ijayo?

___________________________________________

8.

Sura nzima ya tano, inaonekana yote tuliyonayo ni kwa sababu ya kifo cha Kristo na kufufuliwa.

Mstari 10 unasema kuwa wakati tulipokuwa ______________________ na ____________________

kwa mauti ya Mwana wake na tutaokolewa katika uzima wake. Tuna haki mbele ya Mungu sababu tupo ndani ya Kristo.

Kumbuka: Mistari ya 12 mpaka 21 inaonyesha tofauti kati ya dhambi na kifo kuwa vilikuja kumpitia Adamu na haki na maisha kuwa vilikuja kumpitia Kristo.

Tunasoma kutokutii kwa Adamu katika Mwanzo 2 na 3. Adamu, kama kiongozi na mwakilishi wa jamii yetu, alileta kifo na hukumu kwa familia yote ya wanadamu. Kuanzia kipindi hicho na kuendelea, watu wote wameishi chini ya hukumu ya kifo, siyo kwa sababu tumeivunja sheria ambayo Mungu aliyompatia Musa, inayojadiliwa katika mistari 13 na 14, bali kwa sababu sisi ni uzao wa Adamu (katika Adamu). Kwa kuokolewa tu katika Kristo ndipo Wazawa uzao wa Adamu wanapata neema na haki.

Hapa chini umepewa sehemu ya kwanza ya mistari ya 15 hadi 21. Hii inaonyesha matokeo ya dhambi ya Adamu na kutotii. Kuanzia sehemu ya pili ya kila mstari, andika matokeo ya utii wa Kristo Yesu kwa Baba yake.

Mfano: (mstari 15) Kupitia dhambi ya Adamu wengi walikufa.

Thawabu ya neema ya Mungu, kwa mtu mmoja, Kristo Yesu, ilimiminika kwa wengi

9. (mstari 16) Hukumu ilifuata dhambi ya Adamu na ikaleta adhabu. __________________________________

________________________________________________________________________________________

10.(mstari 17) Kwa dhambi ya Adamu mauti ilitawala. _____________________________________________

_______________________________________________________________________________________

11.(mstari 18) Matokeo ya kosa la Adamu ilikuwa adhabu kwa watu wote. _____________________________

_______________________________________________________________________________________

12.(mstari 19) Kwa kuasi kwake Adamu wengi waliingizwa katika hali ya dhambi. ______________________

_______________________________________________________________________________________

13.(mstari 20)

Sheria iliingizwa ili dhambi iwe kubwa. ____________________________________________

14.(mstari 21) Dhambi imetawala katika mauti.

__________________________________________________

_______________________________________________________________________________________

Mstari 21 unatuambia faida iliyopokelewa kutoka kwa Kristo. Anatoa neema, haki, na uzima wa milel kwa wote waaminio. Unaishi katika Adamu kama mwadhibiwa wa dhambi au katika Kristo aliyesamehewa kabisa na amehesabiwa haki? Kama hujampokea, chukua muda, katika maneno yako mwenyewe umwambie Bwana ungependa kupokea zawadi ya wokovu.

Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka (

Matendo 16:31).

SURA YA SITA

WAFU KATIKA DHAMBI, HAI KATIKA KRISTO

Katika sura hii jambo kuu ni umoja wetu na Kristo katika kifo chake, kuzikwa, na kufufuka. Wakati ukweli huu unapoeleweka na kuaminiwa unatupatia uhuru toka mzigo wa dhambi na sheria. Unatuweka huru kumtumikia Mungu kwa sababu tunashukrani kwa yale aliyotutendea. Tafadhali soma sura ya sita. ________ (Hakikisha)

1.(Mstari 2) Kwa sababu tumeokolewa kwa neema (kama inavyofunuliwa katika sura ya 5), swali linaulizwa, Je, tuendelee katika dhambi, ili neema ijae tele? Tafadhali tumia maneno yako mwenyewe.

____________

________________________________________________________________________________________

Kumbuka: Neno batiza maana yake kuwekwa ndani ya au kutambuliwa na. Katika barua za Paulo, ubatizo wa kiroho umetajwa mara nyingi. Anarejea kazi ya Roho Mtakatifu ambaye hubatiza ndani ya Kristo. Ubatizo huu humfanya mtu kuwa mshiriki katika kifo cha Kristo, kuzikwa na kufufuka. Tulibatizwa katika mauti yake. Paulo angeweza kusema Nimesulubiwa pamoja na Kristo (Wagalatia 2:20). Na kwa sababu tulibatizwa ndani ya Kristo na Roho Mtakatifu, sisi ni sehemu yake, washiriki wa Mwili wake. Kifo chake kilikuwa kifo chetu, kuzikwa kwake kulikuwa kuzikwa kwetu, na kufufuka kwake kulikuwa kufufuka kwetu.

2. Mstari 3 unasema kuwa waamini wote walibatizwa na Roho Mtakatifu (siyo maji) ndani ya Kristo. Wanabatizwa ndani ya nini tena?

__________________________________________________________

3.(Waefeso 4:5) Kuna ____________ mmoja, ___________ moja, ____________ mmoja.

Huu tena ni ubatizo wa kiroho (siyo maji) na ni kiunganishi kikuu cha kanisa, kwa kuwa huwafanya waamini wote WAMOJA katika Kristo.

4.(Warumi 6:4) Tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake. Kwa nini?

_______________

________________________________________________________________________________________ (Kama Paulo alisema katika Wagalatia 2:20, Nimesulubiwa pamoja na Kristo...).

5.(mstari 5) Kama tulivyounganika naye katika mauti yake

_________________________________________

_______________________________________________________________________________________

6. (mistari 6-7) Maneno utu wetu wa kale yanamaanisha anguko la zamani, asili ya dhambi.

7.

8. Mungu anachukulia asili hii kuwa imesulubiwa pamoja na Kristo. Nini matokeo ya neema hii?

9. _________________

________________________________________________________________________________________

Mistari 8 na 9 inaeleza kufufuliwa kwa Kristo kutoka wafu. Wakolosai 2:12

inasema kuwa Tumefufuliwa pamoja naye kwa kuziamini nguvu za Mungu.

7.(mstari 8) Ikiwa tulikufa pamoja na Kristo tutaishi pia pamoja na Kristo? _____ Ndiyo _____ Hapana

8.(mstari 10) Kristo alifia _______________________. Amwishia _______________.

9.(mstari 11) Sisi pia ni wafu kwa ______________, bali hai kwa ___________________________.

10.(mstari 12) Kwa sababu ya kweli hizi, tufanye nini juu ya dhambi? Tafadhali jibu katika maneno yako mwenyewe. _________________________________________________________________________

Kumbuka: Kikwazo cha dhambi kilichomtenganisha Mungu na mwanadamu kilikwisha kuondolewa kupitia msalaba wa Kalvari

(2 Wakorintho 5:19).

Kutoamini tu ndiko kunasababisha mwanadamu asipatanishwe na Mungu. Upatanisho ni kwa wote, bali wale tu waliompokea Yesu Kristo kama Mwokozi wameokolewa kweli. Huduma ya upatanisho imetolewa kwa waamini wote katika uwakili wa neema kusimama katika nafasi ya Kristo kuutetea ulimwengu uliopotea Upatanishwe na Mungu. Ndiyo agizo moja kwa leo. Soma 2 Wakorintho 5:17-21.

Soma Mwanzo 2:15-17, tathimini ya uasi wa Adamu, na Mwanzo sura 3. _______Hakikisha. Wakati Adamu alipotenda dhambi, asili yake ilikuwa chafu na familia yote ya mwanadamu ilirithi asili hii ya uchafu. Kuanzia kipindi hicho na kuendelea, watu wote wameishi chini ya hukumu ya mauti, siyo kwa sababu waliivunja sheria ambayo Mungu alimpa Musa, ambayo ilikuja baadaye (angalia Warumi 5:13-14), bali kwa sababu ni uzao wa Adamu. Sisi ni wenye dhambi sababu tumezaliwa wenye dhambi, siyo kwa sababu tumetenda dhambi tu. Kutenda dhambi hatukufanyi wenye dhambi. Kunadhihirisha kuwa sisi ni wenye dhambi.

11.(mstari 13) Tusijitoe viungo vyetu/miili yetu kuwa silaha za ___________; bali kwa kuwa hai toka wafu, tujitoe kama silaha za ___________.

12.(mstari 14) Kwa nini dhambi haitawali ninyi? __________________________________________________

13.(mistari 16-22) Neno watumishi maana yake Watumwa (mstari 16) Kwa hiyo sisi ni watumwa wa yule tunayechagua kumtii ikiwa __________ ambayo mwisho wake ni ____________

au __________ ambao mwisho wake ni ___________.

14.(mstari 17) Paulo anawaandikia wale waliokuwa watumwa wa dhambi. Walifanya nini kinachomfanya Paulo ashukuru?

_________________________________________________________________________

15.(mstari 18) Walipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi wakawa _______________________________

16. (mstari 19)

17. Enzi za zamani tulijitoa kutumikia uchafu na uasi/dhambi, bali sasa tunaambiwa kujitoa miili/viungo vyetu ________________________ tufuate ______________________________

17.Tofautisha tunda (matokeo) ya dhambi katika mstari 21 na tunda linalotokana na kumtumikia Mungu katika mstari 22.

mstari 21 Tunda gani hutokana na kuitumikia dhambi? ________________________________________

mstari 22 Tunda gani hutokana na kumtumikia Mungu? ________________________________________

mstari 22 Mstari huu unafupisha faida zinazopokelewa kutoka kwa Kristo. Hutoa neema, haki, na uzima wa milele kwa wote wanaoamini.

18.Mstari 23 ndio wa kukariri. Tunapataje uzima wa milele?

________________________________________

_______________________________________________________________________________________

SURA YA SABA

HURU KUTOKA KATIKA SHERIA

Katika sura hii tunagundua kushindwa kwa mtu mwenye haki kupata utakatifu kwa kujaribu kuifuata sheria baada ya kuwa amekwisha kuokolewa kwa imani. Mwanzoni, Paulo anawahubiri Wakristo wa kiyahudi waliokuwa chini ya sheria ya Musa kabla ya kumpokea Kristo kama Mwokozi. Ingawa mataifa hawakuwahi kuwa chini ya sheria, kanuni inaweza kuwafaa pia.

Please read Chapter 7Tafadhali soma sura ya 7. _________CheckHakikisha.

1.(mstari 1) Sheria humtawala mtu kwa muda gani? ____________________________________________

2.(mstari 2) Mwanamke amefungwa na sheria ya mume wake kwa muda gani? _______________________

______________________________________________________________________________________

3.(mstari 3) Je, yuko huru kuolewa kama mume wake akifa? _______________________________________

Kwa maneno mengine, YUKO HURU KUTOKA KATIKA SHERIA kwa kifo cha mume wake. Kifo huhitimisha uhusiano, kikimweka huru mmoja kuingia katika mahusiano mapya. Kwa hiyo Paulo anahitimisha katika mstari wa 4 kuwa tuliifia sheria kwa njia ya mwili wa Kristo, hivyo tu mali yake katika mahusiano mapya, yeye aliyefufuliwa kutoka wafu badala ya kuwa chini ya sheria.

7. ( mstari 4)

8. Waamini wameifia sheria kwa njia ya Mwili wa Kristo msalabani na wanaungana na mwingine.

9. Nani? __________________________________________________________

Kumbuka: Umoja na Kristo unaleta matunda mema katika maisha yetu.

Tafadhali soma Wagalatia 5:22-23. _________(Hakikisha)

5.Taja matunda matano ya Roho kama yanavyoonekana katika maisha ya mwamini.

1. ___________________________ 2. _________________________ 3. _________________________

4. ___________________________5. __________________________

Tafadhali soma Wagalatia 5:19-21. _________(Hakikisha)

6.Taja kazi tano za mwili.

1. __________________ 2. ___________________ 3. __________________________

4. _____________________________ 5. _______________________________

Kumbuka:

Utofauti ambao mwili unazaa ndani ya wasiookoka na kile Roho Mtakatifu anazalisha ndani ya waamini.

7.(mstari 6) Bali sasa tumekwisha kufunguliwa katika sheria, waamini wa kiyahudi walikuwa huru kumtumikia Mungu _____________

na siyo katika _________________________,

yaani, katika kufuata kila jambo la sheria ya Musa. Uhuru katika Kristo utakuwa huduma laini zaidi kuliko kufungwa chini ya sheria.

Kutakaswa si kwa sheria. Soma Warumi 7:7-14 ________(Hakikisha).

Katika sehemu hii Paulo anaeleza uamini wake wa mwanzo kama myahudi na jinsi alivyojaribu kuwa mtakatifu kwa kujaribu kuifuata sheria baada ya kuokolewa kwa imani. Paulo hakusumbuliwa juu ya msamaha toka dhambini. Alionyesha katika sura zilizopita kuwa imani katika Kristo ilidumisha msamaha

.

8.

(mstari 7) Katika Warumi 3:20 tulijifunza kuwa ...kwa sheria dhambi hutambuliwa.

Paulo alitiwa hatiani na amri gani ya sheria? __________________________________________________________________

9.(mstari 9) Paulo alidhani yuko hai (hahukumiwi) hadi alipojua sheria.

Sheria ilimfunulia dhambi zake na akawa chini ya hukumu ya kifo. Kwa hiyo katika mstari 10, alikuta ile amri badala ya kuleta uzima, hakika ilifanya nini? ____________________________________________________________________________

10.(mstari 12) Katika mstari huu nini kinasemwa kuhusu sheria?

_____________________________________

________________________________________________________________________________________

11. (mstari 13) Sehemu ya mwisho ya mstari huu inatoa lengo muhimu la sheria. Lengo ni nini?

______________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

Sheria ilifanya dhambi mbaya sana kwa kuihukumu. Tafadhali soma Wagalatia 3:24-25 ________(Hakikisha).

12.(Wagalatia 3:23-24) Tunaambiwa kuwa lengo la sheria ilikuwa nini.

Elezea kwa maneno yako mwenyewe, sheria ilikuwa na kazi gani. ____________________________________

_____________________________

Hili ni muhimu sana kuona, maana Paulo hakuelewa hili katika maisha yake ya kikristo ya mwanzo, na kama anavyoendelea kulinganisha katika Warumi 7. Paulo alijaribu kujirudisha nyuma chini ya sheria ili kupata utakatifu na alishindwa. Tazama jinsi Paulo anavyobadilika wakati anapofahamu zaidi mahitaji ya sheria.

USHINDANI KATI YA ASILI MBILI ZA MWAMINI.

Kila mwamini wa kweli ana migongano miwili kwa asili moja. Moja inapatikana kwa kuzaliwa kwa asili na anaitwa mwili. Nyingine ni asili tunayoipokea tunapozaliwa mara ya pili iitwayo roho.

Wagalatia 5:17 inatuambia

asili ya dhambi inahitaji lililo kinyume na Roho, na Roho lililo kinyume na asili ya dhambi. Kwa maana zinapingana hata hamwezi kufanya mnayotaka. Hii inamaana, huwezi kutenda dhambi kama hujaamua toka ndani.

Tafadhali soma Warumi 7:15-25. _________(Hakikisha)

13.(mistari 15-17) Paulo anaonyesha kuwa mwamini ana upinzani kati ya asili ya kale na asili mpya.

(mstari 17) Nini kinamsababisha Paulo kufanya ubaya (dhambi)? __________________________________

14.(mstari 18) Je, Paulo anataka kufanya mema? __________________________________________________

15.(mstari 19) Je, anaweza kupata nguvu za kulifanya? _____________________________________________

16.(mstari 21) Sheria gani ni ya kweli kuhusu Paulo? ______________________________________________

_______________________________________________________________________________________

17.(mstari 22) Mtu wa ndani anafurahi katika nini? _______________________________________________

18.(mstari 24) Paulo anajielezeaje? ____________________________________________________________

19.(mstari 25) Alikombolewaje kutoka kwenye upinzani huu? _______________________________________

________________________________________________________________________________________

Tazama maneno ya sifa Namshukuru Mungu wakati alipogundua kuwa kuna ukombozi.

SURA NANE

MAISHA KWA NJIA YA ROHO

Sura ya nane ni moja ya sura zinazopendwa sana katika Biblia. Hapa tunakuta mafundisho kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya waamini na kwa mwamini. Sehemu ya mwisho ya sura, mistari ya 29-39, inatufundisha kuhusu wito, nafasi, na usalama tulionao katika Kristo.

Roho Mtakatifu ndani ya mwamini. Soma Warumi 8:1-18 ________(Hakikisha)

1.(mstari 1) Watu gani ambao hawana hukumu? ___________________________________________________

Kwa kadiri mwamini anavyohusika na Yesu Kristo hukumu imekwisha pita. Pale Kalvari, Kristo alimaliza hukumu ya dhambi zetu. Msimamo wa mwamini ni salama sababu unategemea juu ya Yesu Kristo na kazi yake iliyokwisha.

2.(mstari 2) Ni kutokana na sheria gani ambayo sheria ya roho inamweka huru mwamini? __________________

Dhambi na mauti vililetwa ulimwenguni kwa njia ya uovu wa Adamu. Soma tena Warumi 5:12-15.

3.

3. ( mstari 3) Sheria hii inatupeleka kwenye sheria ya Musa au Amri Kumi.

4.

Tazama kuwa kulingana na mstari huu sheria haikuweza kuzaa utii uliohitajika. Je, inawezekana mwili wa dhambi kuitii sheria takatifu? __________________________________________

Lile ambalo sheria haikuweza kufanya Mungu alifanya _____________________________________________

_________________________________________________________________________________________

Neno mwili lililotumika katika mistari ya 3 hadi 13 linamaana ya asili yetu ya dhambi. Katika mstari wa 3 sheria haikuweza kutufanya kuwa wenye haki sababu mwili haukuweza kuitii.

4.(mstari 4a) Kwa nini Mungu aliihukumu dhambi katika mwili? Tafadhali tumia maneno yako mwenyewe.

_________________________________________________________________________________________

Kumbuka: Kuwa haki ya sheria imetimizwa katika maisha ya mwamini, siyo na mwamini. Ni Roho Mtakatifu ndani ya mwamini ambaye hutimiza haki ya sheria.

5.(mstari 4b) Mwamini ni yule asiye _____________________________________________________________

Kuenenda kulingana na mwili ni kukana zawadi ya wokovu kwa njia ya Kristo na kutafuta kuanzisha haki kwa matendo.

Soma Warumi 8:5-8 _______(Hakikisha). Katika mistari hii tunaona utofauti wa njia mbili za maisha:

Mwili (asili ya dhambi) na Roho. Kuwa katika mwili ni kutawaliwa au kuongozwa na mahitaji ya mwili.

6. Mistari ya 5 na 6 inaonyesha utofauti mkubwa kati ya wale wanaoweka akili zao juu ya mwili na wale wanaoweka akili zao juu ya Roho.

7.

8. Matokeo haya tofauti ni yapi? Tumia maneno yako mwenyewe. ____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

9.

10.

7.(mistari 7-8) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe andika mambo matatu yasemwayo kuhusu akili ya mwili.

1. ___________________ 2. _________________________ 3. ______________________________________

8.(mstari 9) Mwamini aliyezaliwa mara ya pili hatawaliwi na asili ya dhambi bali ________________________

Ikiwa mtu hana Roho, je ni mtu wa Mungu? ____________________________________________________

Soma Warumi 8:10-13 _______(Hakikisha)

9.( mstari 10) Kama Kristo yuko ndani yako, mwili wako unakufa kwa sababu ya dhambi, lakini _____________

_________________________________________________________________________________________

10.(mstari 11) Nani huleta uzima? ________________________________________________________________

______________________________________________________________________________________________

Roho Mtakatifu hutuchochea (au hutufanya hai kwa Mungu) na hutupatia nguvu ya kuushinda mwili (dhambi).

Roho Mtakatifu huja maishani mwetu wakati kwa imani tunapompokea Yesu Kristo kama mwokozi wetu. Soma Waefeso 1:13-14. Yeye mwenyewe hututia mhuri na kuwa mlinzi wa WOKOVU wetu (yaani, kununuliwa kwetu na Mungu kwa damu ya thamani ya Kristo) Angalia 1 Petro 1:18-19. Nafasi yetu katika Kristo ni salama.

11.(mistari 12-14) Ukiishi kwa mwili kutatokea nini? ________________________________________________

Ukiishi kwa Roho kutatokea nini? Kwa nini?

____________________________________________________

__________________________________________________________________________________________

Soma Warumi 8:15-17 ________(Hakikisha) Cheo kipya

12. (mstari 15) Nani anayetupa uhakika kuwa sisi ni watoto wa Mungu? _________________________________

Tazama: Aba ni neno kama baba, litumikalo na watoto kuonyesha imani kamilifu.

13. (mstari 16) Roho Mtakatifu hufanya nini na Roho zetu? ____________________________________________

__________________________________________________________________________________________

14.(mstari 17) Sisi ni warithi wa Mungu na warithi pamoja na Kristo tunashiriki urithi wake kama tunashiriki naye

__________________________________________________________________________________________

Soma Warumi 8:18-25 ________(Hakikisha) Uumbaji Uteswao

15.(mstari 18) Mateso wa wakati huu si kitu ukilinganisha na nini?

_____________________________________

16.(mistari 19-23) Mistari hii inamaana ya mateso ya viumbe vyote (mara nyingine inatafsiriwa tofauti)

kwa sababu ya dhambi na mauti. Mstari 21 unasemaje kuhusu wakati ujao wa viumbe?

_____________________

____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

18. (mstari 23) Tunateswa pia, tukisubiri nini?

19. ______________________________________________________

18.(mistari 24-25) Je neno tumaini linamaanisha nini kama lilivyotumika hapa?

__________________________

__________________________________________________________________________________________

Ukombozi wa mwili ni tumaini la wakristo. Tumaini linatazamiwa na kutarajiwa. Je unalisubiria tumaini hili kwa uvumilivu?

Soma Warumi 8:26-28 ______ (Hakikisha) Jibu sentensi zifuatazo Ndiyo au Hapana.

19.Roho Mtakatifu atatusaidia katika mdhaifu yetu._________

20.Tunajua nini tunatakiwa kukiomba._________

21.Roho Mtakatifu huomba au hututetea sisi._________

22. Roho Mtakatifu huomba au hututetea sisi apendavyo Mungu

23. _________

24.

25. Mungu hufanya mambo yote pamoja na wampendao katika kuwapatia mema._________

24.Mungu hakuwa na lengo la kutuita (kutuokoa) sisi_________

Soma Warumi 8:29-31 ______(Hakikisha)

25.(mstari 29) Je Mungu alitujua kabla hatujazaliwa? _____________

26. (mstari 29) Nini lengo la Mungu katika maisha yetu? ______________________________________________

27.

28.

27.(mstari 30) Kwa vile aliwajua na walichaguliwa tangu asili na Mungu, wao pia

1. ______________________________

2. ______________________________

3. ______________________________

28.(mstari 31) Paulo anasema basi, Tuseme nini juu ya haya?

Kama Mungu yupo ___________________, ni nani awezaye kuwa _____________________

29.(mstari 32) Hakumwachilia ___________________________, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote.

30.(mstari 32) Hutukirimia _____________________________________________________________________

31.(mstari 34) Kristo ndiye yuko ________________________________________________________________

32.(mstari 37) Sisi ni zaidi ya ___________________________________________________________________

33.(mistari 38-39) Taja mambo matano yasiyoweza kututenga na upendo wa Mungu uliokatika Kristo Yesu.

1. __________________________________________________________________________________

2. __________________________________________________________________________________

3. __________________________________________________________________________________

4. __________________________________________________________________________________

5. __________________________________________________________________________________

Tumia nafasi hapa chini kwa maswali au maoni:

_________________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________________

_________________________________________________________________________________

Rudisha somo hili kwa:

Neema Masomo ya Biblia

SLP 6170

Mbeya, Tanzania

Namba yetu ya simu: 0769032609

Tarehe: ___________________________________________________________________

Jina: __________________________________________________________________

Anuani: ________________________________________________________________

Mji: _____________________________________________

Namba ya Simu:________________________________________

Lesson II - 1

B

C

F

B

C

F