NSURANC TH IN HEALT NHIIF 0 7avang guaity bealtk Cr ISO 9001:2015 CERTIFIED MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MACHINGA AFYA Machinga Afya ni nini? Ni utaratibu wa bima ya afya unaowalenga wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga walio katika umoja unaotambuliwa na mamlaka za Serikali. Utaratibu huu unawawezesha Wamachinga hao kuchangia huduma za afya kwa um Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhudumia wanachama wake ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. wao na kunufaika na bima ya afya kupitia mtandao mpana wa vituo zaidi ya 7,700 vilivyosajiliwa na Wanufaika ni akina nani? Wanufaika ni Wamachinga walio katika umoja, wenza wao na watoto wasiozidi wanne wa kuzaa au kuasili wenye umri chini ya miaka 18. Madhumuni ya Mpango wa Machinga Afya a) Kutoa fursa kwa Wamachinga kujisajili na kunufaika na huduma za bima ya afya zinazotolewa na Mfuko kupitia umoja wao. b) Kulinda kipato cha wanachama kwa kuwapa uhakika wa matibabu kupitia kadi ya bima ya afya. Jinsi ya Kujisajili na Mambo Muhimu ya Kuzingatia a) Mwanachama anatakiwa kujaza fomu ya kujiunga ambayo inapatikana katika ofisi zote za Mfuko nchi nzima na Tovuti ya Mfuko www.nhif.or.tz. Mwanachama anaweza kusajiliwa pía kupitia mtandao baada ya kikundi chake kuwasilisha taarifa za wanachama wote b) Usajli utafanyika kwa wanachama wote katika shirikisho/umoja uliosajiliwa na kutambulika na mamlaka za Serikali. c) Utaratibu wa Machinga Afya utahusisha usajili wa kundi zima na siyo mwanachama mmoja mmoja na fomu za uanachama, viambatanisho na taarifa zote muhimu za wategemezi zitawasilishwa kwenye Mfuko kupitia Umoja wao. d) Mchango wa kila mwanachama ni Shilingi 100,000 kwa mwaka. Aidha, mwanachama atamlipia mwenza Shilingi 100,000 na mtoto Shilingi 50,400 pindi atakapotaka kuwaunganisha. e) Michango ya wanachama wote italipwa kwa mkupuo kupitia kwa shirikisho au umoja husika Mwanachama anatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa au namba ya kitambulisho cha uraia wakati wa usajil. 9) Mwanachama atapata kitambulisho cha matibabu kwa kuzingatia vigezo na masharti ya mpango wa MACHINGA AFYA Kwa maelezo zaidi wasiliana na ofisi ya Mfuko iliyo karibu na wewe au wasiliana nasi kupitia simu ya huduma kwa wateja bila malipo 0800 110063