MIUJIZA KATIKA MIILI YETU HARUN YAHYA Mfasiri: IBRAHIMU H. KABUGA © Islamic Centre for Research P.O.BOX 76644 Dar es Salaam – Tanzania Phone: +255 712 566595 / 0763348213 E-mail: [email protected]
Sep 30, 2014
MIUJIZA KATIKA MIILI YETU
HARUN YAHYA
Mfasiri:
IBRAHIMU H. KABUGA
© Islamic Centre for Research
P.O.BOX 76644 Dar es Salaam – Tanzania
Phone: +255 712 566595 / 0763348213
E-mail: [email protected]
Ewe mwanaadamu! Nini kilichokughuri ukamwacha Mola wako Mlezi
Mtukufu?
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, katika sura yoyote
aliyoipenda akakujenga. (Surat al-Infitar: 6-8)
YALIYOMO
Utangulizi
Kiwanda kikubwa kisichoonekana kwa macho: seli
Mtandao mkubwa unaoizunguka miili yetu
Ubongo unafanya kazi namna gani?
Safari ya chakula mwilini
Safari ya damu katika mishipa
Kiunzi cha mifupa
Mota ndogo sana zilizopo katika mwili: misuli
Kiboresha hewa kinachofanya kazi katika miili yetu bila kusimama
Hitimisho
KUHUSU MWANDISHI
Akitumia jina la uandishi la HARUN YAHYA, alizaliwa mjini Ankara mwaka
1956. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi na sekondari mjini Ankara, alisoma
masomo ya sanaa (arts) katika Chuo Kikuu cha Mimar Sinan cha Istanbul na masomo
ya Falsafa katika chuo kikuu cha Istanbul. Tangu miaka ya 1980, amechapisha vitabu
vingi kuhusu masuala ya kisiasa, kisayansi na kiimani. Harun Yahya ni maarufu sana
kwa kuandika vitabu muhimu vinavyofichua ulaghai wa waenezaji wa nadharia ya
mageuko (evolutionists), madai yao batili, na mahusiano ya giza kati ya u- Darwinist na
aidolojia nyingine za kikatili kama vile ufashisti na ukommunisti.
Jina lake la uandishi linaundwa na majina ya Harun na Yahaya, katika
kuwakumbuka Mitume wawili watukufu waliopambana na ukosefu wa imani wa watu
wao. Muhiri wa Mtume (s.a.w) katika majalada ya vitabu vya mwandishi huyu ni ishara
maalumu na ina uhusiano na kile kilichomo. Ishara hiyo inawakilisha Qur’an
(Maandiko matakatifu ya mwisho) na Muhammad (s.a.w), Mtume wa mwisho. Kwa
muongozo wa Qur’an na Sunnah (mafundisho ya Mtume), mwandishi anafanya lengo
lake kuwa ni kubatilisha kanuni ya msingi wa itikadi za kikafiri na kutoa “neno la
mwisho”, ili kunyamazisha kabisa pingamizi zinazotolewa dhidi ya dini. Anatumia
mhuri wa Mtume wa mwisho, ambaye alikuwa na hekma ya hali ya juu na ukamilifu wa
kimaadili, kama alama ya kusudio lake la kutoa neno la mwisho.
Vitabu vyote vya Harun Yahya vina lengo moja: kufikisha ujumbe wa Qur’an,
kuwahamsisha wasomaji kuyatamaali mambo ya msingi yanayohusu imani kama vile
kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, Umoja na maisha ya Akhera, na kufichua misingi
dhaifu ya mifumo ya kikafiri na itikadi potovu.
Vitabu vya Harun Yahya vinasomwa sana katika nchi nyingi, kuanzia India mpaka
Marekani, Poland mpaka Bosnia, na Hispania mpaka Brazil. Baadhi ya vitabu vyake
vinapatikana katika lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kijerumani, Kihispania,
Kitaliano, Kireno, Kiurdu, Kiarabu, Kialbania, Kirusi, Kiserbo-Croat (Kibosnia), ki -
Polish, ki – Malay, ki – Uygur, Kituruki, na ki- Indonesia.
Kutokana na kukubalika ulimwenguni kote, vitabu hivi vimekuwa chombo
muhimu cha watu wengi kuimarisha imani yao kwa Mwenyezi Mungu na kupata
maarifa ya kina kuhusu dini yao. Hekima na ukweli wa vitabu vyake, pamoja na mtindo
wa kipekee unaoeleweka kiurahisi, kwa pamoja humuathiri yeyote anayevisoma. Wale
wanaovizingatia kwa dhati vitabu hivi, hawawezi kupendelea tena ukanaji Mungu
(atheism) au itikadi yoyote potofu au falsafa za kidunia, kwa sababu vitabu hivi vina
sifa ya kipekee ya kumuathiri mtu kwa haraka mno, kupata matokeo ya moja kwa moja,
na kutopingika. Hata kama wataendelea kufanya hivyo, itakuwa ni msisitizo wa kihisia
tu, kwa sababu vitabu hivi vinabatilisha itikadi hizo kuanzia chini kabisa kwenye
mizizi. Harakati zote za sasa za wakanaji zinashindwa kiitikadi, kutokana na vitabu
vilivyoandikwa na Harun Yahya.
Bila shaka haya ni matokeo ya hekma, udhahiri na uwazi wa Qur’an Tukufu. Kwa
unyenyekevu kabisa, mwandishi anakusudia kutumika kama njia ya binadamu kuitafuta
njia ya kweli ya Mwenyezi Mungu. Hakusudii kupata faida ya kidunia katika
uchapishaji wa vitabu hivi.
Wale wanaowahamasisha wengine kusoma vitabu hivi, kufungua akili na nyoyo
zao na kuwaongoza ili wawe waja wa kweli wa Mwenyezi Mungu, hupendelea kutoa
huduma yenye thamani kubwa mno (kuliko faida ya kidunia).
Wakati huohuo, itakuwa ni kupoteza muda na nguvu za bure kueneza vitabu
vingnine vinavyotengeneza hali ya mkanganyiko katika akili za watu, kuwaongoza
kwenye vurugu za kiitikadi, na hivyo kutokuwa na athari madhubuti na imara katika
kuondosha shaka katika nyoyo za watu, kama ambavyo pia ilithibitishwa katika uzoefu
wa huko nyuma. Vitabu vilivyotungwa kwa ajili ya kuonyesha nguvu ya kiuandishi ya
mtunzi husika badala ya lengo lake tukufu la kuwaokoa watu dhidi ya kupoteza imani,
haviwezi kuwa na athari kubwa kama hiyo. Wale wenye shaka na hili wanaweza kuona
wazi kuwa lengo pekee la vitabu vya Harun Yahya ni kuushinda ukafiri na kueneza
tunu za kimaadili za Qur’an. Mafanikio na athari ya huduma hii yanaonekana kwa
kusadikishwa na wasomaji.
Nukta moja yapaswa kuzingatiwa: sababu kuu ya kuendelea kwa ukatili,
migogoro, na misukosuko mingine inayowakumba watu wengi inatokana na kuenea
ukafiri kiitikadi. Hili linaweza tu kukomeshwa kwa kuushinda ukafiri kiitikadi na kwa
kutangaza maajabu ya uumbaji na maadili ya Qur’an ili kwamba watu waishi kwa
kuifuata. Kutokana na hali ya ulimwengu hivi sasa, inayoongoza kwenye shimo la
mzunguko wa vurugu, uovu na migogoro, ni wazi kwamba huduma hii inatakiwa
kutolewa kwa kasi na kwa umadhubuti, la sivyo tunaweza kuwa tumechelewa mno.
Katika juhudi hii, vitabu vya Harun Yahaya vimeshika hatamu. Inshallah, vitabu
hivi vitakuwa njia ambayo watu katika karne ya ishirini na moja watapata amani,
uadilifu, na furaha iliyoahidiwa ndani ya Qur’an.
KWA MSOMAJI
Katika vitabu vyote vya mwandishi huyu, masuala yanayohusu imani
yamefafanuliwa kwa muongozo wa Aya za Qur’an na watu wanapewa wito kujifunza
maneno ya Mwenyezi Mungu na kuishi kwa mujibu wake. Mada zote zinazohusu Aya
za Mwenyezi Mungu zimefafanuliwa katika namna ambayo haiachi shaka au alama za
viulizo katika akili ya msomaji. Mtindo wa ukweli, uwazi na ufasaha uliotumika
unamhakikishia kila mtu wa rika lolote na wa kundi lolote la kijamii kuwa anaweza
kuvielewa vitabu hivi kwa urahisi. Simulizi hii halisi na yenye kueleweka kwa urahisi
itakuwezesha kuvisoma kwa mkupuo mmoja. Hata wale wanaokana vikali mambo ya
kiroho huvutiwa na mambo ya hakika yaliyoelezwa katika vitabu hivi na hawawezi
kuyakana maelezo yake yenye ukweli.
Kitabu hiki na vitabu vyote vya mwandishi huyu vinaweza kusomwa na mtu
mmojammoja au katika vikundi wakati wa mazungumzo. Wasomaji wanaotaka
kufaidika na vitabu hivi watakuta kuwa mfumo wa majadiliano unafaa sana kwa maana
kwamba wataweza kuwaeleza wenzao juu ya hisia na uzoefu wao.
Aidha, itakuwa ni mchango mkubwa kwa dini kugawa vitabu hivi wakati wa
kuwasilisha na usomaji wa vitabu hivi ambavyo vimeandikwa kwa kutaka radhi ya
Mwenyezi Mungu pekee. Vitabu vyote vya mwandishi ni vyenye ushawishi na mvuto
mkubwa. Kwa sababu hii, mojawapo ya mbinu zenye athari kubwa kwa wale
wanaowahubiria dini watu wengine ni kuwahamasisha vitabu hivi.
Inatarajiwa kuwa msomaji atatumia muda wake kupitia vitabu vingine vilivyo
kwenye ukurasa wa mwisho wa kitabu hiki, na atautambua utajiri mkubwa wa
machapisho juu ya masuala yanayohusu imani, machapisho ambayo ni yenye kufaa
sana na yenye kufurahisha kuyasoma.
Katika vitabu hivi, tofauti na baadhi ya bitabu vingine, hutokuta mawazo binafsi
ya mwandishi, maelezo yatokanayo na vyanzo vyenye kutia shaka, mtindo usiochunga
heshima na hadhi ya mada adhimu, na wala hutokuta maelezo dhaifu, yenye kuibua
shaka, na yasiyokuwa na matarajio mema ambayo hutengeneza mikengeuko ndani ya
moyo.
UUTTAANNGGUULLIIZZII
Wanangu wapendwa, jiandaeni kuingia ndani ya ulimwengu mpana na wenye miujiza
kwa muda mfupi. Kwa hakika ulimwengu huu utawashangaza sana. Japokuwa mpaka
sasa mnaweza mkawa hamuelewi, lakini matrilioni ya wafanyakazi wa ulimwengu huu
wamekuwa wakikutumikieni bila kukoma. Mnashangaa, sio?
Ulimwengu huu wa ajabu ni mwili wako na wafanyakazi hao wanaokutumkia ni seli za
mwili wako. Kila eneo la mwili wako linaundwa na seli. Wakati huu, kuna matrilioni ya
seli katika mwili wako zinazokutumikia. Zinafanya kazi hata wakati unaposoma kitabu
hiki. Kwa mfano, seli za macho yako zinatekeleza michakato kadhaa bila kusimama ili
kukuwezesha kusoma. Unapopumua, seli katika koo yako na kisha seli katika mapafu
huingia kazini. Wakati huohuo, seli katika tumbo lako zinayeyusha chakula ulichokula
saa chache zilizopita.
Tuliyoyataja hapa ni machache tu katika kazi zinazofanywa na mwili wako bila
kusimama. kazi hizi zote hutokea bila hata wewe kuwa na taarifa yoyote wala kuhisi
kama zinatokea. Matrilioni hayo ya seli yanaungana vipi, kujua la kufanya na
kushirikiana katika kazi? Aidha, hakuna matatizo yoyote yanayotokea wakati wa
michakato hii. Hakuna seli inayojaribu kufanya kazi tofauti au kukataa kutekeleza kazi
yake. Mbali na hilo, kazi zote hizi hufanyika kwa kasi isiyokuwa ya kawaida.
Katika kurasa zijazo, tutachunguza jinsi kazi za kila siku, kama vile uyeyushaji wa
chakula, kupumua, kuona na kusikia, zilivyokuwa za ajabu sana. Tutashuhudia kwamba
wakati fulani seli zetu hufanya kazi kama mkemia kuzalisha vitu vya kikemikali, wakati
mwingine hufanya kazi kama mhandisi kufanya mahesabu na wakati mwingine hufanya
kazi kukidhi mahitaji ya seli nyingine.
Inashangaza sana kuwa yote haya hufanywa na seli ambazo ni ndogo sana zisizoweza
kuonekana kwa macho. Zaidi ya hivyo ni kwamba, seli zilizo katika miili yetu hufanya
kazi hizi kubwa bila kusaidiwa hata kidogo. Kumbuka kuwa seli hizi sio binadamu kama
sisi. Haziwezi kuonana, kusikia wala kuamua kufanya kazi ya busara. Hazina masikio
wala ubongo. Hazijasoma kemia, lakini, kama tutakavyoona katika hatua za baadaye,
zinajua formula mbalimbali za kemikali na zinaweza kuzalisha mada (substances)
mbalimbali kulingana na formula hizi. Zinawezaje kufanya yote haya?
Utajawa na mshangao utakaposoma na kugundua kuwa seli hazitendi kazi hizi zote kwa
akili zake zenyewe. Lazima utakuwa unajua kwamba haiwezekani ziwe zinajua
kutekeleza kazi hizi ndani ya wakati kwa bahati bahati.
Bado tuna deni kubwa la uhai wetu kuyafahamu matendo ya viumbe hivi vidogo sana
ambavyo hatuwezi kuviona hata kwa macho. Kwa hakika katika seli hizi kuna jambo
muhimu sana kwetu kulitambua. Kuna yule mwenye kumiliki hekima na busara za juu
zaidi ambaye anazifanya seli zetu zitekeleze kazi zote hizi na kuzielekeza kipi cha
kufanya. Mmiliki wa hekima hii ya milele ni Mwenyezi Mungu, aliyeumba kila kitu,
anatupenda na anaujua udhaifu na mahitaji yetu yote.
Kila seli moja miongoni mwa matrilioni ya seli zilizo katika miili yetu hutekeleza kazi
zake kikamilifu kutokana na mpangilio kamili wa Mwenyezi Mungu, ili kwamba tuweze
kuendesha maisha yetu bila shida yoyote. Unapoamka kila siku asubuhi na kwenda shule,
unapoonja ladha tamu ya asali, unapopumua na kuvuta hewa bila tabu,
unapokimbiakimbia katika bustani la shule yako na kucheza na marafiki zako,
unapoandika, unaposoma na mambo mengine unayofanya ni kwa huruma na rehma ya
Mwenyezi Mungu.
Kama ilivyo kwa vitu vingine vyote ardhini, Mwenyezi Mungu amekuumba katika
namna ya ukamilifu na kukupatia kila kitu unachokihitaji. Unachotakiwa kufanya kwa
hisani hii ni kumshukuru Mola wetu aliyekupatia neema zote hizi zenye thamani sana
kuliko zawadi nyingine yoyote ile unayoweza kuwa nayo katika huu ulimwengu.
Kwa sababu hii, tunahitaji kuyatafakari kwa kina yale tuliyojaaliwa na Mwenyezi
Mungu. Katika aya mbalimbali za Qur’an Tukufu, Mwenyezi Mungu ametoa mifano
mingi ili watu waitaamali na kuitafakari. Ifuatayo ni mojawapo ya aya hizo:
Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na
mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji
anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha
ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika
mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na
ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanaozingatia. (Surat al-Baqara: 164)
Katika kitabu hiki, tutatafakari juu ya miili yetu. Tutaangalia jinsi Mwenyezi
Mungu alivyouumba mwili wa mwanadamu kwa ukamilifu na kwa uangalifu.
Utakaposoma kitabu hiki, utazidi kumpenda Mwenyezi Mungu na kumshukuru.
Utashangazwa na mghafala wa watu wanaokuzunguka, ambao hawatafakari, na
utakuwa na hamasa ya kuwaambia kile unachokijua ili nao pia wawe wasikivu.
KIWANDA KIKUBWA KISICHOONEKANA KWA MACHO: SELI
Kama tulivyoeleza mwanzoni mwa kitabu hiki, miili yetu inaundwa na matrilioni ya seli.
Idadi hii haitakiwi kupuuzwa. Kwa kweli trilioni ni namba kubwa sana na isiyokuwa ya
kawaida. Kila mwili wa mtu mzima una seli zipatazo trilioni 100. Lakini kutokana na
ukweli kwamba seli hizi ni ndogo sana, miili yetu haina ukubwa wa kutisha. Mfano
tutakaoutoa utakusaidia kuelewa namna seli zilivyokuwa ndogo. Mamilioni ya seli za
mwili yanapokusanyika pamoja, hutwaa nafasi isiyozidi ukubwa wa ncha ya sindano.
Lakini licha ya udogo wake, muundo wa seli bado haujaeleweka kikamilifu.
Wanasayansi bado wanaendelea kufanya tafiti juu ya mifumo ya seli.
Seli ya kwanza iliyokutengeneza ilitoka katika tumbo la mama yako kwa muunganiko wa
seli mbili, moja ikifyatuliwa na mwili wa mama yako na nyingine ikitokana na mwili wa
baba yako. Muda mfupi baadaye seli hii iliendelea kugawanyika na kuwa kipande cha
nyama. Kisha, huku seli zilizotengeneza nyama hii zikiendelea kugawanyika ili
kutengeneza seli mpya, mwili wako ulikuwa ukitengenezwa kidogokidogo.
Kila seli mpya ilichukua umbo tofauti. Huku baadhi zikiwa seli za damu, baadhi zikawa
seli za mifupa na nyingine zikawa seli za neva. Katika miili yetu kuna aina 200
tofautitofauti za seli. Kwa kweli, hizi seli zote zina vijenzi vyenye kufanana sana
(identical components), lakini kila seli inafanya kazi tofauti. Kwa mfano, seli za misuli
katika miguu yako ni kama kamba iliyosukwa ili kwamba uweze kutembea na kukimbia.
Kutokana na muundo wa seli hizo, misuli ya mikono na miguu haichanikichaniki
kutokana na kunyooka kulikozidi wakati unapocheza mpira. Kwa umbo, seli zako za
damu ni mviringo (blobular), kazi yake ni kusafirisha oksijeni inayohitajika katika mwili
wako, kwa kutumia mirija (vessel) ya damu. Kutokana na muundo wake, zinaweza
kutiririka kiurahisi kupitia ndani ya mirija ya damu zikiwa pamoja na oksijeni
ziliyoibeba. Kwa upande mwingine, seli za ngozi zimebanwa pamoja na kupangiliwa
katika msitari mmoja kwa ukaribu. hivyo ngozi yako haipitishi vijidudu (microbes) na
maji.
Kadhalika, seli zote nyingine pia zina maumbo kamili yanayofaa kwa majukumu yake.
Hata hivyo, seli hizi hazikupata maumbo haya kwa bahati tu. Angalia kompyuta, magari
au ndege. Kuna mtu aliyebuni maumbo na mifumo muhimu kwa ajili ya ufanyajikazi wa
vifaa hivi. Mambo yote yamezingatiwa na kupangwa na wanateknolijia wa makampuni
husika. Magari yametengenezwa ili kuhakikisha safari ya raha na salama; televisheni
imekusudiwa kusafirisha picha na sauti nzuri na zenye ubora wa hali ya juu kwenda kwa
watazamaji. Jambo hili halihusu vifaa vya kiteknolojia pekee, bali linahusu pia vitu vyote
tunavyovitumia. Meza, viti, nyumba unayoishi, penseli unayotumia, vyombo vya ndani
kama vile vijiko au uma jikoni kwako ... kila kimoja ni matokeo ya ubunifu maalumu.
Kila kimoja kimepangiliwa kwa undani kabisa na hakuna kilichotokea kwa bahati nasibu.
Kama ujuavyo, ili usanifu na bidhaa fulani iwepo, panahitajika chanzo cha ujuzi.
sasa tuzitafakari seli za miili yetu. Seli zetu zina mpangilio na kazi za hali ya juu kuliko
televisheni au chombo kingine chochote cha kiteknolojia. Aidha, vikosi hivi vya
kimuundo vyenye sifa zisizokuwa za kawaida, ni vikosi hai. Kama tulivyoeleza hapo
mwanzo, wanasayansi hawajaugundua kikamilifu mfumo wenye kushangaza uliopo
katika vikosi hivi vidogo vidogo.
Unastaajabu jinsi usanifu huo, ambao akili ya binadamu hijaweza kuugundua kikamilifu,
ulivyotokea katika uwanda huu mdogo?
Hii yatuonyesha kuwa seli zetu zilipangiliwa na ziliumbwa na mwenye ujuzi wa hali ya
juu. Mmiliki wa ujuzi huu ni Mwenyezi Mungu aliyetuumba kwa ukamilifu na kwa
undani wa hali ya juu.
MTANDAO MKUBWA UNAOIZUNGUKA MIILI YETU
Je umewahi kujiuliza maswali yafuatayo?
Je nipumue sasa hivi?
Je kiwango cha damu kinachosukumwa na moyo wangu kinatosha?
Ni seli na kiungo kipi katika viungo vyangu inayohitaji kiwango gani cha
nishati?
Ni wakati gani tumbo langu linatakiwa kusaga chakula nilichokula?
Je nguvu ya mwanga inayoingia katika macho yangu ina uwiano?
Ni misuli gani ninayotakiwa kuiangalia ili nihamishe mkono wangu?
Maswali haya yanaonekana kuwa ya ajabu, au siyo? Ni kwa sababu huwa
hatujiulizi maswali kama hayo. Zaidi ya hilo, wengi wetu hawajui hata utendaji kazi
wenye kuendelea wa michakato hii. Miili yetu hufanya kazi zote hizi kwa kujiendesha
yenyewe (automatically). Na inatumia mtandao wa neva kufanya hivyo. Mtandao huu
unaundwa na muungano wa matrilioni ya seli za neva, ambayo waweza kuyaona katika
kurasa hizi. Mtandao huu wa neva unaofika kila kona ya mwili wetu, tunaweza
kuulinganisha na barabara ya magari (motorway). Kutokana na mtandao huu, seli katika
ubongo wetu huunganishwa na seli zilizopo miguuni, na seli zote zinawasiliana
zenyewe kwa zenyewe. Lakini, mfumo wetu wa neva una mfumo mkubwa sana kuliko
kilomita za barabara za magari zenye njia panda nyingi na sehemu nyingi
zinazotenganisha barabara za magari yanayopita upande wa pili. Kama ambavyo magari
hutembea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine juu ya barabara, misukumo ya
kiumeme ya neva husafirishwa katika mtandao wa neva katika miili yetu. Misukumo hii
hupeleka ujumbe kutoka eneo moja kwenda jingine.
Misukumo hii hutembea mwilini mwako kwa kasi kubwa sana zaidi ya unavyoweza
kufikiria. Kwa mfano, kiamshi/kichocheo cha kiumeme huondoka na kuanza safari
kutoka katika ubongo wako pindi unapotaka kukunja mkono wako. Wakati wa safari hii
ngumu, kichochea husimama kwanza kwenye neva kuu (spinal cord). Kisha huendelea
kwenye kiungo husika ambacho ujumbe unatakiwa kufika. Misuli ya mkono wako
hunywea kwa ujumla na unaukunja mkono wako kwenye kiwiko (elbow). Mtiririko huu
wa kazi hutokea kufumba na kufumbua (a mere thousandth of a second). Ukizingatia
kuwa inachukua takriban sekunde kuyafunga na kuyafungua macho yako, unaweza
kuelewa vema jinsi muda wa kufumba na kufumbua (thousandth of a second) ulivyo
mfupi. Vivyo hivyo, vichocheo (stimuli) hutumwa kutoka katika mwili wote kwenda
kwenye ubongo kwa kutumia neva. Kutoka kila eneo moja la mwili wako ujumbe
huendelea kutumwa kwenda kwenye ubongo wako na kwa kasi ya ajabu. Ni kwa sababu
hiyo kwamba waweza kuongea, kucheka, kukimbia, kuonja ladha ya ice cream, kucheza
… michakato na kazi zote hizo hutokea bila kuwepo na uingiliaji kati wa aina yoyote;
unafanya jambo papo hapo unapolifikiria. Unakiona kitu wakati unapokitazama, unasikia
maneno wakati huo huo unapoyatamka, unatambua kitu kama ni cha moto au cha baridi
mara unapokishika. Yote haya yanatokana na uelewano uliopo baina ya ubongo wako na
mfumo wa neva.
Kwa yakini, wakati huu huu pia misukumo ya neva inafanya kazi mwilini mwako. Neva
katika ncha za vidole vyako zinatuma ujumbe kwenye ubongo wako kuhusu uzito wa
kitabu ulichokibeba mkononi mwako, ili kwamba ukiinue kitabu hiki kwa nguvu
inayolingana na uzito wake. Vile vile wakati huohuo, vichocheo vinatumwa kutoka
machoni, puani, masikioni, miguuni na maeneo mengine mengi ya mwili wako kwenda
kwenye ubongo.
Ubongo wako huvitathimini vichocheo/viamshi (stimuli) hivi na kutuma majibu
muafaka (relevant responses) kwenye maeneo husika ya mwili wako, ambayo hufanya
kazi kulingana na majibu haya. Sasa jaribu kukumbuka kazi zote hizi. Michakato mingi
hutokea ndani ya mwili wako kwa pamoja. Unasoma kitabu wakati huo huo ukisikia sauti
kutoka ulimwengu wa nje, unahisi manyoya laini ya paka wako anapopita katikati ya
miguu yako, unaonja ladha ya juisi ya matunda unayokunywa, moyo wako unaendelea
kudunda na kazi nyingine nyingi zinatokea mwilini mwako.
Kitu gani kingetokea iwapo ungetakiwa kuyadhibiti mambo yote haya kwa sekunde
kadhaa? Bila shaka usingeweza kuyadhibiti yote haya kwa wakati mmoja. Lakini, kutokana
na ukamilifu wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu, ubongo wako na maeneo mengine ya
mwili wako hufanya kazi kwa pamoja na kutekeleza kazi zote hizi bila haja yoyote ya wewe
kuingilia kati. Aina zote za taarifa zinasafirishwa kutoka mwilini kwenda kwenye ubongo
katika namna ya vichocheo viamshi (stimuli) ambavyo vinahitaji kutafsiriwa. Ni hapo tu
ndipo unapoweza kutambua ulaini wa manyoya ya paka wako, ubaridi wa upepo, ladha ya
juisi ya pichi, harufu ya viazi vilivyokaangwa. Sasa basi, je unadhani kuwa ubongo wako,
ambao ni kipande cha nyama chenye uzito usiozidi kilo 1.5, kuwa unaweza kufanya yote
hayo wenyewe? Bila shaka hapana? Kutokana na uumbaji adhimu wa Mwenyezi Mungu,
ubongo wako unaweza kutekeleza kazi zote hizi kwa wakati mmoja.
Utapepesa macho yako iwapo rafiki yako atakukaribia kimyakimya na kupiga makofi
ghafula wakati ukiwa huna taarifa ya ujio wako. Hakuna njia nyingine, kwa sababu hiki
ni kitendo kisohiari (reflex). Kitendo kisohiari ni itikio la papo kwa hapo litokealo bila
hiari ya mtu. Sababu ya kuwa ya papo kwa hapo ni kwamba katika hali hiyo
vichocheo/viamshi (stimuli) havisafirishwi kwenda kwenye ubongo na itikio (response)
litakiwalo hupokelewa moja kwa moja kutoka kwenye neva kuu. Hii ni tunu muhimu
ambayo Mwenyezi Mungu aliiumba kwa ajili yetu kwa sababu, kutokana na vitendo
hivyo visohiari (reflex), tunalindwa dhidi ya hatari nyingi. Kwa mfano, unaweza
kuondosha mkono wako haraka unapogusa bilauri ya moto. Kitendo kisohiari (reflex) ni
chombo cha ulinzi ambacho Mwenyezi Mungu amekiumba kwa ajili ya ulinzi wa miili
yetu. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, vichocheo vya neva husonga mbele mwilini
mwako kwa kasi ya takriban kilometa 9 (maili 6) kwa sekunde na kwa hiyo unalindwa
dhidi ya hatari nyingi.
UBONGO UNAFANYA KAZI NAMNA GANI?
Tawanya vipande mbalimbali juu ya sakafu kwa namna isiyokuwa ya utaratibu na kisha
chukulia kuwa (vipande hivyo) ndio maarifa yote kuhusu ulimwengu. Kwa mfano,
baadhi ya vipande viwakilishe mwanga, vingine viwakilishe rangi na vingine pia
viwakilishe sauti. Sasa vichukue vipande hivyo kimoja baada ya kingine na kisha anza
kuvikusanya ili kutengeneza picha. Kitu unachoweza kukifanya kwa kukifikiria kwa
kina, kwa muda mrefu na kwa undani hufanywa na ubongo ndani ya sekunde moja kwa
mamia ya mara. Ubongo huo hufanya kazi kwa nguvu na amri (inspiration) ya Mwenyezi
Mungu. Je washangazwa na jinsi kazi hiyo inavyofanyika?
Ubongo hukusanya taarifa zinazotoka kwenye macho, pua, masikio, ngozi, mdomo, n.k
na kuzitafsiri. Kinachofanya tafsiri hii ni mkusanyiko wa seli za neva bilioni 100 zilizopo
ndani ya ubongo wako. Seli hizi hufanya kazi bila kuchoka na kukuwezesha kuona rangi
ya tunda unalokula, kutambua sauti ya rafiki yako na kuitambua harufu ya chocolate.
Picha iliyopo katika ukurasa ujao inaonyesha baadhi ya watoto wanaoongea, kusikia,
kuvuta harufu, kutembea na kulala ndani ya ubongo. Lakini picha hii ni ya kufikirika tu,
ambayo imekusudiwa kuonyesha sehemu fulani katika ubongo pamoja na kazi zake. Kwa
uhalisia, ubongo unaundwa na seli za neva, ambazo zinaweza kuonekana tu kwa kutumia
hadubini (microscope). Unadhani seli za neva zinaweza kuuona mwanasesere wako
unaoupenda au kuonja ladha ya ice cream ya chocolate? Bila shaka hapana. Hiyo ni kwa
sababu seli za neva zinaundwa na vipande vyembamba vya nyama (fine pieces of flesh).
Hivyo lazima awepo Mwenye nguvu aliyeuumba ulimwengu huu wa ajabu (wa seli).
Muumbaji huyu ni Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu, Mmiliki wa kila kitu,
ameumba kila kitu kwa ukamilifu na kumpa kila mmoja wetu maisha mazuri.
Tunachotakiwa kukifanya (kwa zawadi hii ya uhai) ni kumshukuru Mola wetu.
Mwenyezi Mungu ameyafanya macho na masikio yetu kuwa mfano na akatwambia
tumshukuru kwa kutupatia neema hiyo:
Na Yeye ndiye aliyekuumbieni kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni
kuchache mno kushukuru kwenu! (Surat al-Muminun: 78)
SSAAFFAARRII YYAA CCHHAAKKUULLAA NNDDAANNII YYAA MMIIIILLII YYEETTUU
Tunapata nishati inayohitajika kwa ajili ya miili yetu kufanya kazi kutoka kwenye
vyakula na vinywaji mbalimbali. Hata hivyo, kila chakula tunachokula, kama vile pasta,
nyama au ndizi, kinahitaji kusagwa kwanza ili kiwe tayari kutumika katika mwili.
Vyakula hivi hutumiwa na seli za mwili baada ya kusagwa. Sukari inayopatikana ndani
ya ndizi au tofaa hutoa fueli/kichocheo kwa ajili ya seli zako na kuongeza nguvu/nishati
(energy) yako; protini zinazopatikana ndani ya nyama ni muhimu kwa ukuaji wa seli
zako, na hivyo mwili wako hupata kukua. Jaribu sasa hivi kurudi nyuma kwenye utoto
wako.
Ulipozaliwa ulikuwa na takriban kilo 2 – 3. Ukifikisha miaka 10 uzito wako utaongezeka
na kufikia kilo 30 – 35, ukifikisha miaka 15 utakuwa na uzito wa kilo 40 – 50, na
ukifikisha miaka 20 – 25 utakuwa na kilo 50 – 60.
Sababu ya hii tofauti kubwa ni kwamba mada (substances) zinazopatikana katika
chakula unachokula huongezwa mara dufu katika mwili wako. Miongoni mwa vyakula
hivi hukupatia nguvu unayoihitaji kwa ajili ya kuendesha baskeli yako, kukimbia na
kucheza, huku vyakula vingine hurudufiwa katika mwili wako na kutengeneza nyama na
mifupa. Vile visivyotumika / vilivyoharibika huondolewa mwilini. Mchakato wote huu
hufanywa katika mfumo wako wa usagaji (digestive system). Viungo na tezi (glands)
mbalimbali ikiwa ni pamoja na tumbo lako, matumbo (intestines) na kongosho (pancreas)
vina majukumu katika usagaji chakula.
Utendaji kazi wa mfumo wa usgaji ni sawa na utendaji kazi wa kiwanda cha kusafisha
mafuta ghafi. Mafuta yasiyosafishwa (ghafi) yanapofika kama mali ghafi kwenye
kiwanda cha kusafishia hufanyiwa mchakato na kusafishwa na mashine ili yaweze
kutumika. Chakula tunachokula huwa ni mali ghafi katika hatua yake ya awali na kisha
husafishwa na tumbo ili kitumiwe na mwili. Baada ya kuvunjwa vunjwa ndani ya tumbo
na matumbo (intestines), chakula huwa tayari kutumiwa kama kirutubisho (nourishment)
cha seli na kupelekwa kwenye maeneo husika ya mwili kupitia mirija/mishipa ya damu.
Kitu chenye asili moja (single parent substance) husafishwa katika kiwanda cha
kusafishia mafuta na kutoa aina mbalimbali za bidhaa kama vile petroli ambayo ni
kichocheo (fuel) cha motokaa, au mpira unaotumika kama soli ya viatu vyako. Vivyo
hivyo, virutubisho ndani ya chakula huvunjwa vunjwa na kuwa mafuta (fats), sukari na
kabohaidreti/chakula cha wanga ndani ya tumbo lako. Lakini kumbuka kuwa
kinachotokea ndani ya tumbo lako baada ya kula sandwichi tamu ni kazi ngumu zaidi
kuliko kazi inayofanyika katika kiwanda cha kusafishia mafuta. Aidha, mlolongo wa kazi
tutakaoujadili hivi karibuni haufanyiki katika kiwanda kikubwa mno, bali hufanyika
katika eneo dogo la mwili wako wewe mwenyewe.
Urefu wa njia yote ambayo ndani yake chakula hupata kusagwa ni mita 10 (futi 30). Hii
ni mara 6 -7 ya urefu wa wastani wa mwanadamu na inashangaza sana jinsi urefu huo
ulivyowekwa na kuenea katika miili yetu. Mfereji huo mrefu umewekwaje ndani ya
mwili wa binadamu? Jibu la swali hili linaonyesha kwa mara nyingine kuwa kuna usanifu
maalumu katika kuumbwa kwa miili yetu.
Kwa kuwa njia ya chakula, kama unavyoweza kuona katika picha kwenye ukurasa
wa kushoto, imeviringiswa, imeweza kuwekwa katika eneo dogo licha ya urefu wake.
Umbo hili maalumu ni usanifu uliokamilika wa Mola wetu, aliyeumba kila kitu. Tabia hii
ya mfumo wa usagaji chakula ni moja tu katika maajabu mengi ambayo Mwenyezi
Mungu ameyaumba ndani ya miili yetu.
Je wajua kwanini meno yako yana maumbo tofauti tofauti?
Sababu ya kwanini meno yana umbo tofauti ni kwamba kila jino lina kazi yake
tofauti. Kwa mfano, meno yako ya mbele ni makali, ili kwamba uweze kung’ata tunda
kwa urahisi. Ingekuwaje kama meno yenye umbo la bapa (molars) yangekuwa mbele?
Usingeweza kung’ata kipande cha tunda kwa meno yako ya bapa. Vivyo hivyo, kama
meno yako ya mbele yengekuwa nyuma, usingeweza kusaga chakula unachokula.
Kama ilivyo kwa kila eneo moja la mwili wako, meno nayo yamepangwa na Mwenyezi
Mungu kwa mpangilio unaofaa na wenye faida na manufaa kwa ajili yako.
BB aa kk tt ee rr ii aa ww ee nn yy ee mm aa nn uu ff aa aa nn aa mm ss aa aa dd aa hh uu ii ss hh ii nn yy uu mm aa yy aa uu ll ii mm ii
ww aa kk oo
Kwa ujumla Bakteria hujulikana kuwa wanazalisha maradhi na ili watu wajikinge
na madhara yake, wanatakiwa kuwa waangalifu kuhusu usafi wa mavazi na mazingira
wanamoishi. Lakini hivi karibuni, wanasayansi wamegundua uwepo wa baadhi ya
bakteria wenye faida ndani ya mwili wa binadamu, hususan nyuma ya ulimi. Ndiyo,
hujakosea kusoma; kuna bakteria wenye faida katika mwili wako. Kazi ya bakteria
wanopatikana nyuma ya ulimi wako ni kuua vijidudu hatari (harmful microbes) katika
tumbo lako. Lakini kwa hakika hii sio kazi rahisi na inahitaji mlolongo wa kazi.
Kwanza kabisa, bakteria huibadilisha nitrati/chumvi (esta) ya asidi nitriki inayopatikana
katika mboga za majani (green – leafed vegetables) kama vile letusi/saladi na kuwa
asidi/nitriti (nitrite). Hata hivyo, kazi bado haijamalizika. Asidi/nitrite kwa kuunganisha
na mate ya mdomoni, huwa na athari dhidi ya vijidudu. Kwa maneno mengine bakteria
walioko nyuma ya ulimi wako husaidia kuzalisha mada inayoua vijidudu (microbe –
killing substance). Kama ujuavyo, vijidudu husababisha maradhi. Kutokana na bakteria
hawa wenye faida ambao huzalisha kitu kinachoua vijidudu unapata kukingwa dhidi ya
maradhi mengi. Bakteria hawa ni moja tu katika ishara za huruma ya Mola wetu
aliyeiumba miili yetu katika namna bora yenye ukamilifu mkubwa. Mwenyezi Mungu
ametupatia neema na tunu nyingi. Kwamba neema na tunu hizi ambazo hazihesabiki
zimeelezwa ndani ya aya ya Qur’an kama ifuatavyo:
Na mkizihisabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu. (Surat an-Nahl: 18)
TUMBO LINASAGA VIPI CHAKULA?
Sasa tuchunguze zaidi kazi ya usagaji chakula. Tafakari juu ya upumuaji,
kuogelea, kuendesha baskeli, kula … Yote haya ni ni sehemu ya maisha yetu ya kila
siku, lakini mara nyingi hatutafakari hata kidogo namna yanavyotokea. Miili yetu
inahitaji nishati. Tumekwishaeleza kuwa nishati hii tunaipata kutoka katika vyakula
tunavyokula. Lakini virutubisho vinavyotakiwa na mwili vinatakiwa viwe vyepesi na
vipande vidogovidogo ili kwamba viweze kupita katika mirija/mishipa ya damu.
Tofauti na hivyo haviwezi kupenya/kuenea katika seli. Lakini vyakula tunavyovitumia
ni vipande vikubwa vikubwa. Hivyo, tunahitaji mashine maalumu ili kuuwezesha mwili
kukitumia chakula hicho. Kwa kweli, kwa ufupi hii tunaweza kuiita mashine ya kusaga,
ambayo kimsingi hukipunguza chakula tunachokula na kuwa vipande vidogo zaidi.
Mashine hii ya kusaga iliyopo katika mwili wako inaitwa “mfumo wa usagaji”
(digestive system).
Mfumo huu, kama mifumo yote ya mashine, huundwa na viungo/vijenzi (components)
mbalimbali na kutokana na utendaji kazi kamili wa kila kimoja katika viungo hivyo,
ndipo tunapoweza kusaga chakula. Ni muhimu kwamba viungo/vijenzi vya mfumo wa
usagaji viwe vyenye kuchukuana/kuafikiana na viwe kamili kwa sababu mfumo mzima
hauwezi kufanya kazi mpaka viungo hivyo viwe hivyo.
Hapa tunatoa mfano ili kubainisha kwa nini vijenzi vyote vya mfumo wowote lazima
viwe kamili kwa ajili ya utendaji kamili wa mfumo husika:
Gari inayoendeshwa kwa mtambo maalumu (remote – controlled car) inaundwa na vifaa
mbalimbali kama vile magurudumu, kifaa kinachotawala (controlling device), mota,
betri, gia, koili, antenna, n.k. Vivyo hivyo, mfumo wa usgaji chakula unaundwa na
vijenzi mbalimbali. Vijenzi hivyo vinajumuisha meno, ulimi, umio wa chakula
(oesophagus), tumbo na matumbo (intestines).
Sasa tafakari. Je gari inayoendeshwa kwa mtambo maalumu yaweza kufanya kazi
kama haina antenna au magurudumu? Bila shaka hapana. Gari hiyo inaweza tu kutembea
iwapo itakuwa na vifaa vyake vyote. Hali ni hiyo hiyo kwa mfumo wa usagaji chakula.
Uwepo wa tumbo hautokuwa na maana yoyote mpaka upatikane pia umio wa chakula
(oesophagus), kwa sababu kinachobeba chakula na kukipeleka tumboni ni umio wa
chakula. Katika namna kama hiyo hiyo, Matumbo (intestines) hayawezi kuwa na faida
yoyote mpaka liwepo tumbo, kwa sababu chakula kinachosagwa hupitshwa katika
matumbo, ambapo hupewa muundo kamili ili kupelekwa kwenye seli za mwili.
Hii inaonyesha wazi kuwa Mola wetu, Muumba wa kila kitu, aliumba kwa ajili yetu
mfumo ambao ni kamili katika kila nyanja. Hii inaonyesha tena kuwa hakuna mungu
zaidi ya Mola wetu:
Hakika Mungu wenu ni Allah, Mwenyezi Mungu, tu. Hapana Mungu isipo
kuwa Yeye. Ujuzi wake umeenea kila kitu. (Surah Ta Ha: 98)
MASHINE YA USAGAJI CHAKULA YAANZA KAZI…
Usagaji chakula huanza mdomoni. Kabohaidreti zipatikanazo katika chakula
unachokula huvunjwa vunjwa kwanza na kuwa vipande vidogo zaidi kwa mate
yaliyopo mdomoni mwako. Kwa mfano, mkate uliokula wakati wa kifungua kinywa
ulianza kumeng’enywa kwanza. Lakini itachukua muda kwa jibini uliyokula na mkate
huo kumeng’enywa.
Virutubisho vinavyomeng’enywa mdomoni hupitia katika umio wa chakula na
kufika tumboni. Tumboni kuna hali nyingine ya ajabu ya utulivu na mlingano. Usagaji
wa chakula tumboni hufanywa na kimiminika / kioevu (fluid) chenye nguvu sana.
Kimiminika hiki ni asidi ya haidrokloriki (hydrochloric acid). Kama ujuavyo, asidi ni vitu
vinavyoharibu. (Asidi hizo) zinaweza kuyeyusha kile kinachogusana nazo. Kwa mfano,
mama yako hutumia kitu chenye asidi ili kusafisha tundu iliyoziba. Kumeng’enya vile
vichafu na vilivyoharibika ambavyo vimeziba bomba, asidi hizi huziondosha. Ni
kutokana na asidi yenye nguvu inayopatikana tumboni kwamba chakula kinachokuwa
katika vipnde vikubwa vinapofika kwanza tumboni humeng’enywa na kuwa vipande
vidogo zaidi vinavyoweza kutumiwa na mwili. Lakini kuna nukta moja zaidi inayohitaji
kueleweka.
Tumeeleza kwamba chakula kinacholiwa humeng’enywa katika vipande
vidogovidogo kwa tumbo au asidi ya tumbo. Sasa inakuwaje hii asidi isiliharibu tumbo
lenyewe, ambalo nalo limetengenezwa kwa nyama? Sasa tafakari kuhusu jambo hilo.
Asidi ya tumboni inaisaga nyama, mathalan, uliyokula wakati wa chakula cha mchana,
lakini inaliacha tumbo ambalo nalo ni kipande cha nyama. Kwa nini inakuwa hivyo?
Katika nukta hii, ubora katika uumbaji wa Mola wetu unadhihirika kwa mara nyingine.
Mwenyezi Mungu aliyeumba kila kitu kwa ukamilifu aliweka ulinzi maalumu ili kwamba
tumbo lenyewe lisimeng’enywe.
Ulinzi huu unaweza kuelezwa kwa mukhtasari kama ifuatavyo; kimiminika
kingine kiitwacho “mucous”, huwekwa ndani wakati wa umeng’enyaji ili kuizuia asidi
ya haidrokloriki (hydrochloric acid) isilimeng’enye tumbo. Utando maalumu wa
kimiminika cha mucous huufunika mzunguko wa ndani wa tumbo na kulizuia tumbo
lisiharibiwe na asidi hii yenye nguvu. Hivyo tumbo halijimeng’enyi lenyewe.
Sehemu inayofuata ya safari ya umeng’enyaji wa chakula ni matumbo (intestines).
Virutubisho humeng’enywa na kuwa vidogo zaidi na kufanywa kuwa vyenye kutumiwa
na mwili pindi vinapopita kwenye matumbo (intestines) mawili, utumbo mpana na ule
mdogo. Kile chenye manufaa katika hivi virutubisho huingizwa kwenye mkondo wa
damu na mabaki yasiyofaa hutolewa nje ya mwili kwa mfumo wa utoaji taka za mwilini.
Hatua/awamu ambazo chakula hupitia ndani ya matumbo nazo pia ni muhimu sana.
Umeng’enyaji huendelea ndani ya matumbo kama ilivyokuwa kwa hatua ya tumboni.
Virutubisho huendelea kumeng’enywa na kuwa vidogo zaidi. Na sasa vinakuwa vidogo
mno kiasi kwamba hufyonzwa na mirija ya damu inayoyazunguka matumbo na
kuingizwa katika mkondo wa damu kwa ajili ya kusafirishwa kila eneo la mwili wako.
Hakika mmetambua kuwa mfumo wa usagaji chakula umepangiliwa moja kwa
moja na kwa ukamilifu. Wakati wa safari hii inayoanzia mdomoni na kuendelea ndani
ya umio la chakula, tumboni na hata kwenye matumbo/utumbo, chakula husika hupitia
hatua/awamu kadhaa wa kadhaa. Na hatimaye virutubisho vinavyohitajiwa na seli za
miili yetu hupatikana. Virutubisho hivyo hufyonzwa ndani ya matumbo/utumbo na
kupelekwa mwilini kupitia mkondo wa damu. Usagaji wa chakula ungekuwa mgumu
sana kama mfumo huu usingefanya kazi kikamilifu. Kwanza kabisa, kama tungekuwa
hatuna meno tusingeweza kutafuna chakula chetu vya kutosha na kisingeweza kupita
kooni. Hata kama kingepita kingeumiza sana umio wa chakula. Kama tumbo letu
lisingekuwa na uwezo wa kusaga chakula, kila kitu tulichokula kingebaki kuwa
kikubwa ndani ya tumbo, jambo ambalo lingeleta usumbufu sana. Aidha, kutokana na
kushindwa kusaga chakula, miili yetu isingepata virutubisho inavyovihitaji. Mwili
usiokuwa na virutubisho hukosa nguvu baada ya muda mfupi na seli za mwili huanza
kufa. Mfumo huu bora na wa kushangaza hufanya kazi bila hitilafu na bila ya sisi
wenyenyewe kuwa na taarifa juu ya ufanyaji kazi huu. Ubora huu katika uumbaji
umeelezwa ndani ya aya ifauatyo:
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye
majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni
Mwenye kushinda, Mwenye hikima. (Surat al-Hashr: 24)
SAFARI YA DAMU NDANI YA MISHIPA /VENA (VEINS)
Katika sura zilizotangulia tuliuangalia mtandao mkubwa wa neva unavyofanya kazi
ndani ya miili yetu. Kuna mtandao mwingine wa ajabu kama huo. Mtandao huu unaundwa
na mishipa ya damu. Kama ilivyo kwa mtandao wa neva, mishipa ya damu nayo
inazunguka ndani ya mwili. Mishipa hii ni mirefu sana kiasi kwamba urefu wake unaweza
kuwa takriban kilometa 100,000 (maili 62,000) kama zikitandazwa kwenye eneo la
tambarare. Kwa kweli, sio jambo gumu hata kidogo kuelewa kuwa kuna mishipa ya damu
kuuzunguka mwili wako wote. Hata mkwaruzo mdogo tu kwenye kiungo chochote cha
mwili wako huweza kutiririsha damu haraka. Hii inathibitisha kwamba damu huzunguka
sehemu zote za mwili wako. Kuna umuhimu mkubwa wa sisi kuwa na mishipa ya damu
katika kila eneo kwa sababu, kama ilivyoelezwa katika sura iliyotangulia, kirutubisho
kinachohitajiwa na seli za mwili husafirishwa kupitia mishipa ya damu. Oksijeni ambayo
seli zinaihitaji ili kuziwezesha kufanya kazi kikamilifu nayo pia hupelekwa kwenye seli kwa
kutumia damu inayotiririka ndani ya vena (vein).
Usafirishaji wa kirutubisho katika mishipa ya damu yaweza kulinganishwa na
usafirishaji wa shehena kwa kutumia meli. Kabla ya usafirishaji wa bidhaa, kwanza mizigo
yote hupakiwa bandarini. Mizigo inatakiwa ipakiwe na kupangwa vizuri. Baada ya mizigo
yote kupakiwa, meli huanza safari kuelekea kwenye bandari inayopelekewa mzigo huo.
Inapofika bandarini, mizigo hupakuliwa na kusambazwa kwenye maeneo husika. Katika
mishipa ya damu, kirutubisho nacho husafirishwa hivyo hivyo kwenda kwenye seli, kama
meli zinavyosafirisha mzigo baharini. Oksijeni, mafuta/shahamu na asidi amino hutiririka
katika mkondo wa damu katika vifurushi na kuvipakua kwenye seli zinazolengwa
kupelekewa shehena hiyo. Kamwe utaratibu huu wa usafirishaji haushindwi hata kidogo.
Kiwango cha shehena kinachotakiwa hufikishwa kwenye seli husika kwa wakati
unaotakiwa. Tofauti na hivyo, mathalani, kama seli fulani inayohitaji oksijeni badala yake
ikapelekewa mafuta, seli hiyo itakufa. Ifahamike kuwa hata kosa dogo katika mfumo huu
linaweza kusababisha madhara makubwa. Lakini, makosa kama hayo huwa hayatokei
isipokuwa katika hali zisizokuwa za kawaida kwa sababu mambo haya hayakutokea kwa
bahati nasibu. Mwenyezi Mungu, Muumba, aliumba mfumo huu katika namna ya ukamilifu
ili ututumikie.
Damu inapokuwa inazunguka katika mwili wote, ndivyo inavyotekeleza kazi zake. Na
sasa tuangalie kwa mukhtasari kazi hizi.
USAFIRISHAJI WA SHEHENA
Tumekwishaeleza kuwa aina zote za shehena zinazohitajiwa na miili yetu hufikishwa
kwenye viungo husika kwa njia ya damu. Wakati huohuo, seli za damu hukusanya vile
vilivyoharibika, kama vile kaboni dayoksaidi na kuhakikisha kuwa vinatolewa mwilini.
Katika namna fulani, damu hufanya kazi kama mashine ya kusaga uchafu/taka (garbage
grinder). Kwa kuipitia mara kwa mara kila seli katika seli trilioni 100 kwa siku nzima,
damu huziachia seli kile zinazokihitaji na wakati huohuo hukusanya kile kisichohitajika.
Damu ambayo ni kimiminika tu, inaweza kufanya kazi inayohitaji umakini na
uwajibikaji kama huo bila kukosea. Inajua kila kitu ilichokibeba, kitatumika kwa ajili gani
na mahali kinapotakiwa kufikishwa. Kwa mfano, damu haikosei kuipelekea seli kaboni
dayoksaidi iliyoichukua kwenye seli nyingine kama uchafu. Mara zote inazipatia seli
oksijeni na kuondosha kaboni dayoksaidi. Damu hufanya kazi hii bila kukosea au kuchoka,
kwa sababu ni sehemu ya mpango kamili ambao Mwenyezi Mungu ameuumba ndani ya
mwili wa binadamu. Wakati zikisalimu amri moja kwa moja kwenye mfumo ulioumbwa na
Mola wetu, seli za damu hutekeleza kazi zake bila kufanya makosa yoyote.
ASKARI NDANI YA DAMU
Kila siku miili yetu hupambana dhidi ya bakteria, virusi na vijidudu vingi. Baadhi
huzuiliwa visiingie mwilini, huku vingine vikiweza kuingia. Lakini kuna seli maalumu
za ulinzi ndani ya miili yetu zinazopambana navyo ambazo hujulikana kama “seli za
kinga” (immune cells). Seli hizi, ambazo ni kama askari wanaopambana dhidi ya adui
na kuilinda miili yetu dhidi ya hatari mbalimbali, hupita katika mkondo wa damu.
Panapokuwa na shambulio la adui, huweza kufika kwenye eneo husika la mwili kupitia
mishipa ya damu na kupambana kwa urahisi zaidi dhidi ya adui. Seli za kinga
hazikujifunza majukumu yake zenyewe. Ziliyajua majukumu hayo tangu zilipoumbwa.
Huanza kutekeleza jukumu lake na kuulinda mwili tangu pale mtoto anapozaliwa. Haya
yanaelezea ubora katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Mola wetu amezifundisha seli
ambazo haziwezi kuonekana kwa macho ujuzi muhimu sana na akazifanya zitutumikie.
MAWASILIANO
Damu pia hufanya kazi kama nyezo ya mawasiliano katika mwili. Kuna wajumbe
mbalimbali wanaochukua ujumbe kutoka sehemu moja ya mwili kwenda sehemu
nyingine. Wajumbe hawa wanaojulikana kama homoni, husafirisha ujumbe kwenda
kwenye viungo husika kama mfanyakazi wa posta apelekavyo barua. Kazi nyingi za
muhimu, ikiwa ni pamoja na ukuaji wa mwili, kiu, jasho na udhibiti wa kiwango cha
sukari ya damu hutokana na ujumbe huo mbalimbali unaofikishwa kwa wakati.
DAMU INAYOPONYA MAJERAHA
Bila shaka utakuwa umeshaona kuwa jeraha dogo la ngozi hukoma mara moja
kuvuja damu baada ya muda mfupi. Kwa hakika jambo hili ni lenye kukanganya kwa
sababu, kwa hali ya kawaida, kimiminika kinachotiririka kwenye tundu hakiwezi
kuacha kuvuja kwa matakwa yake. Ili kulielewa zaidi jambo hili, fikiria mfano kwamba
una puto lililojazwa maji. Ukitoboa tundu dogo kwenye hilo puto kwa kutumia sindano,
maji yataanza kuvuja. Je yataacha kuvuja baada ya muda bila wewe kuyaziba? Bila
shaka hapana. Maji yataendelea kuvuja mpaka maji yote yaishe katika puto. Jambo hili
linavihusu vimiminika vyote vilivyowekwa katika maeneo yaliyofungwa.
Damu hupita katika mzunguko uliofungwa wa vena na huvuja pindi inapotokea
jeraha hata dogo sana. Lakini, ni muhimu sana damu hiyo ikome kutiririka kwa
manufaa ya afya yetu. Utakuwa umewahi kusikia kuhusu watu wanaokufa kutokana na
kupoteza damu nyingi katika ajali au oparesheni/upasuaji. Sasa basi, kitu gani
kinachosababisha damu kuacha kuvuja muda mfupi baada ya jeraha kuanza kutoa
damu?
Jambo hili hujulikana kama ugandaji wa damu (blood clotting), ambalo ni
mojawapo ya mifumo ya kiulinzi inayojiendesha yenyewe ndani ya miili yetu. Baadhi
ya mada zinazopatikana ndani ya damu huikatisha na kulifunga jeraha. Kutokana na
uwezo wa damu kuganda, uvujaji mkubwa wa damu hupata kuzuiliwa. Baadhi ya seli
hutaarifiwa juu ya vena iliyoharibika na huelekea mara moja kwenye eneo hilo.
Kwanza hujikusanya kwenye jeraha na kuzuia mtiririko wa damu kwa kutengeneza
utando. Utando huu hukauka ndani ya muda mfupi na kutengeneza kitu tunachokiitwa
“scar” (kovu).
Sasa tutafakari kwa pamoja. Je mlolongo huu wa kazi zilizopangiliwa unaweza
kutokea kwa bahati nasibu? Inakuwaje baadhi ya seli za damu zipate taarifa juu ya
jeraha mahali fulani katika mishipa ya damu, ambayo ni kama ulimwengu mkubwa
mno kwa kulinganishwa na ukubwa wake? Kwa nini zinapambana kuzuia utiririkaji wa
damu? Zinajuaje kwamba zinatakiwa kulifunga jeraha ili kuzuia upotevu wa damu?
Nani aliyezifundisha seli hizi kwamba zinatakiwa kufunga jeraha?
Seli zisingeweza kuyajua yote haya kwa bahati nasibu na wala zisingeweza
kuyakamilisha zenyewe binafsi. Hata binadamu wenye akili hawawezi kutengeneza
mfumo mpana kama huo na kuzifundisha seli kipi cha kufanya. Kwa hakika, uelewa
mkubwa unaoonyeshwa na seli hizi sio milki yao. Mwenyezi Mungu huzifunulia na
hufanya kazi kulingana na mpangilio uliokamilika.
Mwenyezi Mungu anatueleza kuhusu ubora wa uumbaji Wake kama ifauatavyo:
Aliyeumba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji
wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha nadhari! Unaona kosa lolote? Tena
rudisha nadhari mara mbili, nadhari yako itakurejea mwenyewe hali ya kuwa
imehizika nayo imechoka. (Surat al-Mulk: 3-4)
KIMIMINIKA CHA AJABU KISICHOKUWA NA MFANO WA
KUTENGENEZWA UPYA: DAMU
Wanasayansi wamefanya tafiti nyingi ili kutengeneza kimiminika sawa na damu.
Lakini, wakiwa wameshindwa kufanya hivyo, walikata tamaa na wakaacha kabisa kujaribu
(utengenezaji wa) kuiga na wakajikita katika kufanya utafiti wa nyanja nyingine.
Wanasayansi hawana uwezo wa kutengeneza mfano wa damu kwa sababu sampuli
za damu zinazochukuliwa kutoka kwenye mrija/mshipa wa damu huganda mara moja na
muundo wa damu unakuwa haufai tena kwa uchunguzi/kipimo. Aidha, ni kazi bure
kutunza sampuli za damu katika glasi za mirija ya vipimo (glass test tubes), kwa sababu
seli za damu haziishi hata kidogo katika mirija (tubes). Hivyo, wanasayansi walilazimika
kuzitenganisha seli na damu na kuzipima pekee yake. Bila shaka, hii ni miongoni mwa
maelezo yasiyoingia akilini kabisa duniani kudai kwamba mada (substance) hiyo
iliyoumbwa kwa ukamilifu, ambayo haiwezekani hata kuiga mfano wake pamoja na
taarifa zote ambazo binaamu wamezikusanya kwa miaka mingi, kwamba iwe ilitokea
mara moja na kwa bahati nasibu. Mwenyezi Mungu aliumba damu kama kitu
kisichokuwa na mfano. Seli ya damu yenye vipawa vingi vya kustaajabisha ni moja tu
katika ishara za hekima isiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu ndani ya mwili wa
binadamu.
MM OO TT AA YY AA MM WW II LL II :: MM OO YY OO
Je umewahi kufikiria namna lita za damu zinavyozunguka bila kusimama ndani ya
miili yetu juu na chini? Kila kifaa kinahitaji mota ili kiendelee kutembea. Magari,
ndege, motaboti na hata mwanasesere wako wa gari unaoendeshwa kwa rimoti
hutembea kwa kutumia mota. Vivyo hivyo, mzunguko wa damu ndani ya miili yetu nao
pia unahitaji mota. Mota inayosukuma damu yetu usiku na mchana, kwa muda wa
miezi na hata miaka ni moyo.
Weka vidole vyako kwenye kifundo chako (cha mkono) na subiri kwa muda.
Utahisi mapigo ya moyo wako. Moyo wako hupiga mara 70 kwa dakika, na husukuma
kiasi cha lita milioni 152 (galoni milioni 40) za damu katika kipindi chote cha uhai wako.
Kiwango hicho cha damu kinakadiriwa kuwa sawa na kiasi kinachoweza kubebwa na
meli 10,000 za mafuta. Takwimu hizi zinashanga, au sio? Sasa fikiria kwamba unatakiwa
kuchota kikombe cha maji kutoka kwenye ndoo moja kwenda kwenye ndoo nyingine,
mara 70 kwa dakika. Mwishoni mkono na misuli yako itauma na utahitaji kupumzika.
Lakini moyo wako hufanya kazi hii kwa kipindi chote cha uhai wako bila kupumzika
hata kidogo.
PPAAMMPPUU BBOORRAA ZZAAIIDDII IILLIIYYOOKKAAMMIILLIIKKAA
Pampu iliyotengenezwa kwa ubora zaidi kushinda yote duniani sasa hivi inapiga
kwenye upande wa kushoto wa moyo wako. Kutokana na muundo wake wenye
kushangaza na utendaji kazi wake wa bila kusimama, moyo wako huifanya damu yote
katika mwili wako ikamilishe mizunguko kamili 1,000 kwa siku.
Moyo ni pampu iliyotengenezwa kwa nyama yenye ukubwa wa takriban sawa na
ngumi ya mtu. Lakini ndio injini yenye nguvu zaidi, yenye kudumu zaidi na madhubuti
zaidi kuliko injini zote ulimwenguni kulingana na uwezo wake. Tunazo sababu nyingi za
kuielezea nguvu ya moyo katika namna hii. Sababu kubwa kabisa, moyo hutumia
kiwango kikubwa sana cha nishati/nguvu wakati unapopiga. Kutokana na nishati/nguvu
inayotumiwa na moyo, damu inaweza kuruka kwa kiwango cha mita 3 juu. Itafaa zaidi
kama tukitoa mfano ili iwe rahisi kuelewa uwezo wa moyo. Kwa saa moja moyo
unaweza kuzalisha kiwango cha nishati/nguvu inayotosha kunyanyua gari ya wastani kwa
umbali wa mita moja juu kutoka kwenye uso wa ardhi.
Pampu halisi katika moyo
Moyo, ambao ni kiungo chenye nguvu na ukubwa wa sawa na takriban ngumi ya mtu,
unaundwa na nusu mbili. Kuna pampu mbili katika sehemu hizi. Pampu ya upande wa
kushoto, ambayo ndiyo yenye nguvu zaidi, husukuma damu yenye oksijeni kwenda kwenye
maeneo yote ya mwili. Pampu ya upande wa kulia ni dhaifu kuliko ile ya kwanza na
husukuma damu isiyokuwa na oksjeni kidogo (oxygen-poor blood) kwenda kwenye
mapafu. Safari hii ya kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu ni ya umbali mfupi na
kwa hivyo hujulikana kama “mzunguko mdogo” (small circulation). Ule wa awali
unajulikana kama “mzunguko mkubwa” (large circulation).
Kila moja katika hizi nusu mbili za moyo imegawanyika katika sehemu mbili zaidi.
Damu iliyopo baina yake hupita kwenda kwenye eneo lingine kupitia kwenye vali za moyo
(heart valve). Pampu hizi hufanya kazi bila kukoma kwa kiwango kikubwa cha nishati,
kutokana na mizunguko ya damu inayofanywa katika miili yetu mara 1,000 kwa siku.
MOYO HUJITUNZA WENYEWE
Mashine huhitaji matengenezo ya mara kwa mara. Wakati mwingine ni muhimu
kuyafanyia matengenezo baadhi ya maeneo ya mashine au kubadilisha vifaa ambavyo
vimechakaa. Mashine inahitaji kutibiwa kwa mafuta baada ya kufanya kazi kwa kipindi
fulani cha muda, ili kupunguza uchakavu unaotokana na msuguano.
Kama mashine, moyo ambao huendelea kufanya kazi muda wote nao pia unahitaji
matengenezo. Lakini, moyo hujifanyia matengenezo wenyewe; hujilainisha wenyewe.
Unadhani moyo unajilainishaje wenyewe? Jibu la swali hili linapatikana ndani ya
mfumo wa uumbwaji wake. Eneo la nje la moyo limefunikwa na kifuko chenye
utando/viwambo viwili. Baina ya tando hizi kuna majimaji/kimiminika chenye
kuteleza. Majimaji haya (yenye utelezi) hufanya kazi kama mafuta ya mota huwezesha
moyo kufanya kazi kwa urahisi. Muundo huu wa kujilinda unaopatikana katika moyo
unaonyesha kwa mara nyingine namna usanifu wa Mwenyezi Mungu ulivyo mkamilifu
katika uumbaji wake.
KIUNZI CHA MIFUPA
Kuna mifupa 206 katika mwili wako. Unaweza kudhani kuwa kiwango hiki ni
kikubwa mno, lakini kwa mfano tutakaoutoa, utaelewa jinsi ilivyo muhimu kuwa na
mifupa mingi kiasi hicho. Hebu tuviangalie vidole. Iwapo kila kidole kimoja kingekuwa
na mfupa mmoja tu usingeweza kubeba hiki kitabu kama ufanyavyo sasa. Hii ni kwa
sababu mfupa usio kunjufu hauwezi kupinda na bila shaka ukiulazimisha utavunjika.
Kwa kuwa huwezi kuvikunja vidole vyako, hutoweza kushika au kukamata vitu. Wala
hutoweza kuandika au kula. Kinachokufanya uweze kubeba kitabu hiki kwa urahisi na
wakati huohuo kunywa juisi yako ya matunda ni uwepo wa mifupa 27 iliyoingiliana
ndani ya mkono wako ikiwemo ile ya vidole vyako.
Kama ilivyoelezwa hapo awali, kuna mifupa 206 katika miili yetu, ambayo
imeungana kama ile iliyopo katika mikono yetu. Kila mfupa miongoni mwa mifupa hii
umekaa mahali pake kulingana na mpangilio wa hali ya juu. Kutokana na mpangilio
huu kamilifu unaweza kuupinda mwili wako mbele, unaweza kupiga magoti na
unaweza kukizungusha kichwa chako. Lakini usikosee: huwezi kufanya yote haya kwa
kutumia tu mifupa yako, kwa sababu mifupa haiwezi kukunjika. Kuna maungio kwenye
eneo la makutano ya mifupa yako. kutokana na maungio haya, unaweza kuukunja
mkono wako kwa urahisi, unaweza kunyanyua mguu wako na unaweza kutumia vidole
vyako.
Ngoja tukupe mfano ili uweza kuelewa jinsi maungio yalivyo na umuhimu katika
usogevu wa mifupa yetu:
Chukulia mfano umetengeneza karagosi wa mbao. Utafanyaje ili mikono yake
isogee? Mikono yake haitosogea mpaka uweke maungio sehemu ambayo mikono
hikutana na mabega. Utafanyaje ili miguu yake iwe ni yenye kusogea? Lazima utumie
kiungio tena mahali ambapo miguu inakutana na pingiti. Hapo ndipo unapoweza
kuisogeza mikono na miguu ya karagosi wako wa mbao. Vivyo hivyo, kama
ukitenganisha ubao ulioutumia kutengeneza mikono na miguu na kuwa vipande vipande
na ukaweka viungio, au maungio, baina ya vipande hivi, hapo mikono na miguu ya
karagosi wako nayo pia itaweza kukunjika kwenye viwiko na magoti kwa pamoja.
Kama ulivyoelewa wazi kwenye huu mfano, kuwa na mifupa mingi na maungio
yaliyowekwa baina yake inatuwezesha sisi ktembea na kusogea kwa urahisi.
RASILIMALI ZA MIFUPA ZISIZOWEZA KUIGWA
Kuna aina mbalimbali za maungio katika mifupa yetu. Huku baadhi ya maungio
yakiiwezesha mifupa kwenda mbele na nyuma, maungio mengine huiwezesha mifupa
kusogea upande upande. Sasa tuyaangalie maungio na mifupa kwa undani zaidi.
Mifupa yetu ina majukumu mbalimbali ya kutekeleza na kuilinda miili yetu. Kwa
yakini, imeumbwa ikiwa na uwezo na uimara wa kutekeleza majukumu hayo.
Mifupa yetu ni myepesi na imewekewa matundu madogo madogo katikati kama sega
la nyuki. Lakini ingawa ni myepesi kutokana na muundo huu nywelevu, pia ni imara sana.
Hata hivyo hii haimaanishi kuwa ni rahisi kuvunjika. Kinyume chake, ni imara sana kiasi
kwamba ukichukua kiwango hichocho cha mfupa na chuma, utakuta kwamba mfupa ni
imara mara 5 zaidi ya chuma. Kwa mfano mifupa ya paja katika miguu yetu, ina uwezo
mkubwa wa kuinua juu tani moja ya mzigo ikiwa imesimama kuelekea juu. Unaporuka au
kuchupa kutoka upande mmoja kwenda mwingine, mfupa huu huwekwa kwenye uzito ulio
sawa na mara 3-4 ya uzito wa mwili wako. Lakini hupati madhara yoyote kutokana na
uimara wa mifupa yako.
Kitu gani kinachoifanya mifupa iwe imara kiasi hicho? Kwa kweli, jibu la swali hili
linapatikana katika mfumo wa uumbaji usiomithilika wa mifupa, ambao tumeuelezea kwa
ufupi hapo juu. Mifupa imetengenezwa kwa tishu nywelevu iliyo kama sega la nyuki. Ni
kutokana na muundo huu kwamba ni imara sana na myepesi kwa matumizi rahisi. Kama
ingekuwa kinyume, yaani kama sehemu za ndani ya mifupa zingekuwa ngumu na zikawa
hazina uwazi (spaces) wowote kama sehemu ya nje, mifupa ingekuwa mizito sana. Aidha,
kwa kuwa isingekuwa nyumbulifu hata kidogo ungeona mifupa ikivunjika au kupata ufa
kwa kupigwa na kitu kidogo tu, mathalani ukiupiga kidogo mkono wako kwenye ukingo wa
kabati. Lakini, Mwenyezi Mungu ni Mwenye huruma na aliiumba mifupa yetu katika
namna hiyo ili kwamba iweze kukabiliana na tatizo la kimwili na kuwa na ulinzi.
Kile ambacho mifupa imetengenezwa nacho kimewashangaza na kuwavutia sana
wanasayansi na wamejaribu kuiga kwa kutengeneza tishu ya mfupa kwa miaka mingi.
Tishu hii, ambayo ni imara sana, licha ya kuwa nyepesi, na ambayo inaweza kujikarabati
yenyewe, inaweza kukua yenyewe binafsi. Sababu ya urefu wa mwili wako wa sasa
kutokuwa sawa na urefu wako ulipokuwa na miaka 4-5 na sababu ya kuwa tofauti
utakapokuwa na umri wa miaka 19-20 ni ukuaji mifupa yako. Kwa ajabu kabisa, ukuaji huu
umepangiliwa kwa uwiano na urari mzuri sana. Mikono yako hukua wakati miguu yako
ikikua; vidole vyako vya mkono na vidole vya mguu hukua kwa pamoja na ukuaji wa kila
mfupa hukoma katika kipindi fulani cha muda. Aidha, hili halitokei tu katika mwili wako
bali hutokea pia kila mwili wa mtu mwenye siha. Kila mtu ana mifupa yenye kubeba sifa na
tabia hizi.
Wanasayansi wanafanya utafiti ili kutengeneza malighafi (substance) kama ile
inayounda mifupa ya mwili wa binadamu. Lakini, hakuna ambaye ameweza kutengeneza
malighafi (substance) yenye sifa na tabia za hali ya juu kama za mifupa.
Ni kutokana na huruma ya Mola wetu kwamba mifupa yetu inatuwezesha kuishi
maisha yetu kwa urahisi na kutembea sana bila kupata shida na bila kupatwa na maumivu
yoyote.
MIFUPA INAYOJITUNZA
Tulieleza kuwa kuna maungio mahali ambapo mifupa hukutana. Kwa mfano,
tunaweza kuikunja na kuinyoosha mikono na miguu yetu kutokana na maungio
yaliyopo kwenye viwiko na magoti yetu. Japokuwa hutembea katika kipindi chote cha
maisha yetu, maungio haya kamwe hayahitaji kuwekewa kilainisho. Lakini, mashine
zinahitaji matengenezo ya mara kwa mara. Kwa mfano, unatakiwa kuweka kilainisho
kwenye pedali au mnyororo wa baskeli yako mara kwa mara kwa sababu kiwango cha
mafuta hupungua kadiri yanavyotumika, jambo ambalo hatima yake ni kuizuia baskeli
isitembee. Vivyo hivyo, maungio ya mifupa yako hutumika wakati wote, lakini huna
haja ya kuyawekea kilainisho. Kwa nini?
Jawabu la swali hili limetafutwa na wanasayansi, ambao hatimaye waligundua
ukweli ufuatao: katika maungio, kuna tishu imara, ya mpira ainayoitwa “gegedu”
(cartilage) ambayo huyakinga/huyalinda maishilio ya mifupa katika sehemu
inapokutana. Kuna utando/kiwambo kinachoyazunguka maungio yote ambacho ndani
yake kuna majimaji maalumu. Pindi mfupa unapotumia shinikizo kwenye maungio,
majimaji haya hulazimishwa kutoka kwenye kiwambo hicho na maungio hupata
“kulainishwa”.
Mambo haya yote yanatuonyesha kuwa mwili wa binadamu ni matokeo ya usanifu
wa ajabu na uumbaji bora. Ni kutokana na usanifu huu wa ajabu kwamba tunaweza
kufanya harakati nyingi kwa urahisi na kwa haraka. Tabia hizi za mifupa zimeumbwa
na Mola wetu. Mwenyezi Mungu anawaita watu kwenye kutafakari juu ya uumbaji wa
mifupa:
... Iangalie hii mifupa yake jinsi tunavyoinyanyua kisha tunaivisha nyama ...
(Surat al-Baqara: 259)
MIFUPA ILIYOVUNJIKA INAPONAJE?
Tumeeleza kuwa mifupa ni migumu na imara. Lakini inaweza kuvunjika pindi
inapopatwa na pigo kali. Sasa kitu gani hutokea? Mfupa hujikarabati wenyewe.
Madktari huuandaa mfupa na kuuwekea bandeji ya piopi ili kwamba mfupa uweze
kujiunga sawa sawa. Hakuna kazi inayobaki kwa madaktari kwa sababu mfupa
wenyewe una utaratibu wa kujirekebisha wenyewe. Ni ajabu na muujiza kwamba
mfupa uliovunjika hujiponyesha na kuwa imara zaidi kuliko hata mwanzo. Muujiza
huu hufanya kazi kama ifuatavyo:
Damu inayouzunguka mfupa uliovunjika huganda na kutengeneza "haematoma",
ambayo ni kiwango kikubwa cha damu iliyoganda. Ugandaji huu ni utandu ambao ni
sawa na kigaga kitokeacho kwenye ngozi yako baada ya jeraha. Madini yapatikanayo
ndani ya seli zinazotengeneza mifupa huubadilisha mgando huu na kuwa mfupa imara.
Awamu hii inapokamilika, seli za ufifishaji wa mifupa huingia kazini. Zikifanya kazi
kama mtaalamu wa metali (sculptor), seli hizi huupunguza mfupa huo mpya kwa asidi
ya haidrokloriki, ambayo ni asidi kali sana, na kuupa mfupa huo umbo maalum.
Mchakato huu huendelea mpaka mfupa huo unaporudi katika umbo lake la asili. Hata
baada ya mwaka mmoja, seli hizi za ufifishaji wa mifupa huendelea kuupunguza mfupa
kama wataalamu wachapakazi wa metali ili kuupa umbo.
Kama ulivyoona, kazi zote hizi zinazofanywa na seli za mifupa ambazo ni ndogo
mno kiasi cha kutoonekana kwa macho, ni dalili na alama za utaalamu na ajuzi wa hali
ya juu. Hiyo ni kwa sababu seli hazina macho, lakini zinaweza kujenga mifupa. Aidha,
zinaweza kuelewa ni wakati gani nafasi baina ya vipande hivyo viwili inatakiwa kujaza
na hivyo zinaweza kuamua wakati wa kuacha. Kisha seli zinazofifisha mfupa
zinafahamu kuwa mfupa uliojengwa upya unahitaji kusawazishwa, na huanza
kuupunguza. Ili seli ziweze kufanya hivyo, zinatumia asidi kali kuusawazisha mfupa na
kuupa umbile kwa kutumia asidi hii kwa kiwango kidogo au kikubwa kadiri
inavyotakiwa.
Kama unavyoweza kuona, seli zote za mifupa zinaelewa vizuri jambo la kufanya
na jinsi ya kulifanya. Mfumo uliotengenezwa kwa ajili ya kuiponya mifupa yetu
hufanya kazi kikamilifu na kuiwezesha mifupa kujikarabati. Kwa miaka mingi,
wanasayansi wamestaajabishwa na uwezo huu wa mifupa wenye kushangaza.
Seli za mifupa zilipata vipi uwezo huo wa ajabu unaofanya kazi moja kwa moja
bila mhusika kujua? Seli zinajua vipi kinachohotajika kukarabati mfupa uliovunjika na
hatua gani za kufanya ili kuuponya? Wakati baadhi ya seli zina uwezo wa kujenga
mifupa, nyingine zina jukumu la kuisawazisha na kuipa umbo. Nani aliyezipa kazi na
majukumu hayo? Inakuwaje kwamba hakuna vurugu na vipi kila moja inatekeleza kazi
zake kwa wakati muafaka unaotakiwa? Je seli za mifupa zilijua mambo yote haya
zenyewe?
Kwa hakika kazi hizi za ajabu haziwezi kutekelezwa kwa hiari ya seli
zisizoonekana kwa macho. Wala hazikuweza kuzijua kazi hizo. Ikifanya kazi kwa
muongozo wa Mwenyezi Mungu Mwenye hekma, seli za mifupa yetu zinaweza kuipa
umbo mifupa yetu kama afanyavyo mtaalam wa metali.
Je umeshangazwa namna seli za zinavyotengeneza mifupa?
Maumbile ya zaidi ya mifupa 206 iliyo katika miili yetu yanatofautiana. Tofauti
hii ilianza pindi mifupa hiyo ilipotokea kwa mara ya kwanza, yaani, ulipokuwa katika
tumbo la mama yako. Seli, ambazo zilikuwa zikiongezeka kidogo kidogo kwa idadi,
zilichukua maumbo mbalimbali kutokana na eneo husika la mwili ambalo kila seli
ilitakiwa kukaa.
Baadhi ya seli ziligawanyika ili kuunda mifupa yako, nyingine kuunda ini,
nyingine kuunda mafigo na nyingine kuunda macho yako. Lakini seli zitakazounda ini,
mifupa au macho hazijikusanyi tu pamoja. Zinahitaji kugawanyika zaidi na zaidi. Kwa
mfano, seli za mifupa zinatakiwa kujua eneo la mfupa zitakazouunda ndani ya mwili.
Zinatakiwa kwenda kwenye eneo sahihi kikamilifu na kuchukua umbo sahihi.
Seli za mifupa ndani ya miguu yako hufanya kazi kama mtaalamu wa metali na
kuunda kikamilifu mifupa ya mguu iliopinda pamoja mibonyeo na uchomozaji wa
vidole vya miguu. Kana kwamba zainajua ukubwa wa ubongo, seli za mifupa
zinazotengeneza fuvu lako hujenga kiunzi laini cha mifupa ambacho huuhifadhi
kikamilifu ubongo wako. Sio dogo sana na wala sio kubwa sana, hivyo haliubani
ubongo na wala halifanyi upate shida kukiinua juu kichwa chako.
Nini chanzo cha utambuzi huu wa seli zinazoipa mifupa umbile kamili zikijua
muundo zinaotakiwa kuuchukua na tishu gani zinayotakiwa kuiunda?
Mola wetu ameuweka mpangilio huu tata ndani mwao. Ujuzi Mkuu wa Mwenyezi
Mungu umeashiriwa katika aya zifuatazo:
Na vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamt'ii Yeye.
Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na
jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu
na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima. (Surat ar-Rum: 26-27)
MOTA NDOGO SANA ZILIZOPO KATIKA MWILI: MISULI
Misuli ni vituo vya umeme (power stations) vya miili yetu. Kazi ya misuli ni
kubadilisha nishati kuwa umeme, kazi ambayo huifanya kikamilifu katika kipindi chote
cha uhai. Wakati fulani jambo hili huliona, lakini muda mwingi hatuitambui. Kwa
mfano, baadhi ya misuli hunywea (contract) ingawa hatufanyi juhudi yoyote kwa
uangalifu. Misuli ya moyo na ya tumbo ni ya aina hii. Kazi zake ziko juu ya uwezo na
udhibiti wetu. Misuli ambayo hunywea (contract) kwa utashi wetu imeshikamana na
kiunzi chetu cha mifupa (skeleton). Kuna misuli 650 inayofanya kazi (voluntary) katika
mwili wa binadamu. Tunapotembea, misuli hii hunywea (contract) na kulegea pamoja
na mifupa iliyoshikamana nayo.
Misuli huendeshwa na mirija ya damu na neva. Mirija ya damu hubeba oksijeni na
virutubisho kwenda kwenye miuli, huku neva zikiongoza mwendo wa misuli.
Ingekuwaje kama ungeachiwa wewe udhibiti wa misuli moja kwa moja? Fikiria,
kwa mfano, kwamba misuli ya moyo wako kuanzia leo na kuendelea inashikamana na
udhibiti wa utambuzi pekee. Hutoweza kufanya chochote zaidi ya kumakinika kwenye
unyweaji na ulegezaji wa misuli ya moyo wako. Hii ni kwa sababu kama misuli ya
moyo wako isingenywea hata kwa muda, ungekufa. Na usingeepuka kifu unapokuwa
usingizini, kwa sababu usingeweza kuudhibiti ufanyaji kazi wa moyo wako. Lakini hilo
halitokei kwa sababu huhitaji kufikiri kuhusu mambo hayo kutokana na mfumo kamili
wa udhibiti katika mwili wako.
Tunachotakiwa kufanya kuliko mambo yote ni kumshukuru Mola wetu Mwenye
huruma, aliyekifanya kila kitu kuwa rahisi kwa ajili yetu, na tufanye mambo katika
namna inayomridhisha. Mwenyezi Mungu anatupa amri ya kumuabudu Yeye pekee
yake katika aya ifuatayo:
Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila
Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa
kila kitu. (Surat al-An‘am: 102)
Misuli hufanya kazi kwa uelewano
Je wajua kuwa kuna misuli 17 usoni mwako inayonywea (contract) kwa pamoja
pindi unapotabasamu? Kama isingenywea au kufanya kazi nyingi, usingeweza
kutabasamu. Aidha, usingekuwa na muonekano wowote usoni mwako.
Kuna misuli 28 inayodhibiti muonekano wa uso wako. Kwa mnyweo wa pamoja
wa misuli hii, unaweza kutengeneza mamia ya mionekano mbalimbali. Kutokana na
misuli hii, unaweza ukaelezea na kuonyesha ghdhabu, mkanganyiko, furaha na
burudani na mionekano mingine mingi. Mbali na misuli ya usoni, pia misuli mingine
katika mwili wako hufanya kazi kwa uelewano. Kwa mfano, ili kupiga hatua moja,
misuli 54 hufanya kazi wakati mmoja. Kwa namna hiyo tunaweza kupiga mamia ya
hatua kwa urahisi, jambo linaloonekana kuwa la kawaida kwetu. Lakini baada ya
kuyasoma yote haya, mtu anatakiwa kusimama na kutafakari, kwa sababu watu
hawachangii chochote katika utendaji kazi wa misuli hii. Kama misuli isingefanya kazi
kikamilifu, isingewezekana kupiga hata hatua moja, achilia mbali kukimbia, kuogelea
au kuendesha baskeli. Kwa hiyo, tunatakiwa kuweka akilini mwetu jambo moja la
muhimu sana: Mwenyezi Mungu aliumba mfumo kamili katika mwili wa binadamu. Hii
ni zawadi kutoka kwa Mola wetu. Tunachotakiwa kufanya ni kutafakari juu ya rehma
ya Mwenyezi Mungu isiyokuwa na kikomo, kukumbua ukuu Wake na kumshukuru.
Mikono hubeba kila kitu kwa ustadi
Kugeuza kurasa za kitabu, kufungua mlango wa gari, kuosha mikono ... Haya ni
mambo machache sana tunayoyafanya kila mara kwa kutumia mikono yetu, bila kupata
tabu yoyote. Tunatumia mikono yetu katika kufanya mamia ya matendo.
Mkono wa mwanadamu ni imara sana kiasi kwamba unaweza kutumia shinikizo
kwenye kitu chenye uzito wa kilogramu 45 (paundi 100) bila hata kukunja sana ngumi.
Mbali na nguvu hizo, tunaweza pia kuitumia mikono yetu katika matendo mzuri na
yenye kupendeza sana kama vile kutunga uzi kwenye sindano kila tunapotaka kufanya
hivyo. Wakati kundi moja la matendo likihitaji kiwango kikubwa cha nguvu, mengine
yanahitaji usahihi wa hali ya juu (strict accuracy). Hata, hatutambui hata kidogo kazi
kubwa inayofanywa na mikono yetu katika uhalisia wake. Kamwe hatuamui kutumia
nguvu ya gramu 500 (paundi 1.1) kwa ajili ya kunyanyua juu karatasi kutoka kwenye
meza au kutumia nguvu ya kilogramu 5 (paundi 11) ili ktupa mpira. Tunafanya yote
hayo moja kwa moja (automatically) bila kuwaza, kwa sababu Mwenyezi Mungu
alituumba katika namna ya ukamilifu. Ufanisi huu mkubwa wa mikono yetu ni matokeo
ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu usiokuwa na kifani.
Je wajua kuwa mojawapo ya majaribio makubwa ya wanasayansi imekuwa ni
kutengeneza mkono bandia ulio sawa na mkono wa binadamu? Mikono ya roboti
iliyotengenezwa imekuwa sawa na mkono wa binadamu katika upande wa nguvu, lakini
imekosa hisia ya kushika (kugusa) na uwezo wa kufanya kazi nyingi wa wakati mmoja.
Kwa hakika, wanasayansi wengi wana maoni kwamba haiwezekani kutengeneza
mkono wa roboti wenye uwezo wa kufanya kazi zote za binadamu. Mhandisi Hans J.
Schneebeli, aliyebuni mkono wa roboti unaojulikana kama "The Karlsruhe Hand",
alieleza kwamba kadiri alivyozidi kufanya kazi ya kutengeneza mikono ya roboti,
ndivyo alivyozidi kuustaajabia mkono wa binadamu. Aliongezea kusema kwamba
watahitaji muda mwingi kuweza kushughulia hata kazi ndogo zinazofanywa na mkono
wa binadamu.
Mikono yetu, ambayo haiwezi kuigwa hata na teknolojia ya kisasa,
imetengenezwa kwa ufanisi na Mwenyezi Mungu. Mikono hii ni ishara ya ukamilifu wa
ustadi wa uumbaji wa Mwenyezi Mungu.
Hakuna muumba mwingine tofauti na Mwenyezi Mungu. Katika aya ifuatayo,
Mwenyezi Mungu anatuhabarisha kwamba hakuna mungu mwingine isipokuwa Yeye
tu na anawaambia wale wasiouona ukweli huu:
Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu.
Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao
hawajifai wenyewe kwa jema wala baya? Sema: Hebu kipofu na mwenye kuona
huwa sawa? Au hebu huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi
Mungu washirika walio umba kama alivyo umba Yeye, na viumbe hivyo
vikawadanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na
Yeye ni Mmoja Mwenye kushinda!.’ (Surat ar-Ra‘d: 16)
KIBORESHA HEWA KINACHOFANYA KAZI NDANI YA MIILI YETU BILA
KUSIMAMA
Kupumua ni mojawapo ya matendo unayoyafanya kwa siku nzima bila kutambua.
Michakato mingi hutokea katika hatua hii, ambayo pua, koo na mapafu yanahusika.
Kwa kweli, kuvuta pumzi ina maana ya kuzalisha seli za mwili wako kwa oksijeni. Seli
haziwezi kuishi mpaka zipate oksijeni. Ndiyo maana unaweza kuizuia pumzi yako kwa
muda mfupi pekee. Iwapo muda huo utakuwa mrefu, seli zako zitakufa na hatimaye
mwili wako utakufa.
Hewa unayovuta husafishwa kwanza ndani ya pua yako. Pua yako, ambayo
hutekeleza kazi ya kuboresha hewa, imewekewa nywele zinazofanya kazi kama chujio.
Nywele hizi huifanyia mchakato hewa iliyochafuliwa au hewa baridi ili kuifanya
ikubaliane na mapafu. Ni kutokana na nywele hizi kwamba hewa tunayoingiza ndani
huwa imechujwa, imesafishwa, imewekewa unyevunyevu (humidified), imewekewa
uvuguvugu na kutakaswa dhidi ya bakteria. Kwa hakika, nywele hizi nyembamba
huilinda miili yetu dhidi ya chembechembe zipatazo bilioni 20 za vitu vinavyotoka nje
kila siku.
Bilioni ishirini ni karibu mara 3 ya idadi ya watu wote ulimwenguni. Ni mchakato
mkubwa sana ambao pua inautambua na ni kwa jinsi gani inavyochambua
chembechembe nyingi kiasi hicho zitokanazo na mada (matter) za nje. Chembechembe
bilioni ishirini za mada za nje haiyumkini zitambuliwe na zizuiwe kuingia puani kwa
bahati nasibu/sadfa. Hii inaonyesha wazi ukuu wa uwezo wa uumbaji wa Mwenyezi
Mungu. Hata hivyo, baadhi ya watu hudai kuwa mambo haya hutokea kwa bahati
nasibu, hata kama wanaujua vyema ukweli. Watu hao wanaoiamini nadharia ya
mageuzi yenye kuendelea (evolution theory), wanadai kuwa viumbe hai vyote, ikiwemo
kila kitu tulichokizungumzia hapo nyuma katika hiki kitabu, vilitokea mara moja/papo
kwa papo na kutokana na matukio yasiokuwa na utaratibu maalumu yaliyotokea hapo
zamani. Je, wajua kwa nini wanadai hivyo? Wanadai hivyo ili kukanusha uwepo wa
Mwenyezi Mungu. Na ili kufanya hivyo wanadhani kuwa kuna njia moja tu, nayo ni
kudai kuwa kila kitu hutokea kwa bahati nasibu. Lakini, ni rahisi sana kuelewa jinsi
madai hayo yasivyokuwa na maana. Sasa tuufanye mfumo uliopo ndani ya pua kama
mfano ili kukanusha madai haya.
Mfumo wa kuboresha hewa (air conditioning system) unaopatikana ndani ya pua
ni eneo lingine lenye kushangaza la mwili wa binadamu. Kwa hakika mfumo huo
unaofanya kazi kwa ukamilifu usingetokea kutokana na bahati nasibu/sadfa. Kufanya
ulinganisho kutatusaidia kuelewa vyema namna jambo hilo lisivyowezekana. Fikiria
kiyoyozi/kiboresha hewa (air conditioner), kinachodhibiti hali ya joto ili kukulinda
dhidi ya joto kali wakati wa majira ya joto / kiangazi na kukupatia joto wakati wa
majira ya baridi, na mabacho kinaendeshwa na kifaa maalumu. Je mfumo huo unaweza
kuwa umetokea kwa bahati nasibu? Kitu gani kitatokea iwapo vifaa vyake
vitatenganishwa na kuachwa katika hali hiyo? Je vitaweza kujileta pamoja na
kubadilika kuwa kiyoyozi kamili?
Kwa hakika hapana. Kwani ili mashine yoyote iwepo, lazima mtu fulani mwenye
utaalamu aitengeneze. Hili ni jambo lisilopingika hata kidogo. Achilia mbali mashine,
hata katika fumbo la mlinganisho (jigsaw puzzle) lazima mtu avikusanye vizuri vipande
husika ili kupata picha. Pua yako, ambayo hufanya kazi kama kiyoyozi, nayo pia
inaundwa na vijenzi (components) na ina mfumo uliokamilika zaidi kuliko kiboresha
hewa /kiyoyozi chochote ulimwenguni. Kama ambavyo kiyoyozi hakiwezi kutokea kwa
bahati nasibu, hata pua ambayo ni ya hali ya juu zaidi haiwezi kuwa hivyo. Ukweli huu
unatuonyesha kuwa kiungo hiki kijulikanacho kama "mfumo bora wa uboreshaji hewa
kuliko mifumo yote ulimwenguni", kimeumbwa na Mola wetu. Mwenyezi Mungu
anasisitiza juu ya sifa yake ya kuwa Muumba katika aya ifuatayo:
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mtia sura, Mwenye
majina mazuri kabisa. Kila kilioko katika mbingu na ardhi kinamtakasa, naye ni
Mwenye kushinda, Mwenye hikima (Surat al-Hashr: 24)
NN yy ww ee ll ee kk oo oo nn ii zz ii nn aa zz oo ww ee zz aa kk uu tt oo aa mm aa ee ll ee kk ee zz oo bb ii ll aa
kk uu kk oo ss ee aa
Hewa inayosafishwa puani husonga mbele kupitia kwenye mashine ya kupumlia
(respiratory tract). Eneo la pili kwa hewa iliyovutwa baada ya puani ni kooni. Katika
hewa hii bado kunakuwa na mada kutoka nje - kama vile vumbi - ambazo zina madhara
kwa afya ya mtu. Kwa hiyo, ni muhimu hewa iliyovutwa ipite katika ukaguzi mwingine
wa kiuslama kabla haijafika kwenye mapafu. Usalama huu hutekelezwa na tabaka lenye
utelezi lililopo juu ya mashine ya kupumlia (respiratory tract). Utando huu hujulikana
kama mucous layer.
Utelezi (mucous), unaounda utando huu, huzitambua chembechembe ndogo kama
vumbi ambazo tumezivuta pamoja na hewa na huzizuia zisiweze kuingia kwenye
mapafu. Lakini, mbali na hayo, mada hizo zilizoingizwa kutoka nje lazima pia
ziondolewe mwilini. Katika hatua hii, mtambo mwingine wa usalama huingia kazini.
Mtambo huu unaundwa na vitu vidogovidogo vinavyofanana na nywele vijulikananvyo
kama cilia, ambayo iko chini ya mucous layer. Nywele hizi ndogo ndogo hupiga juu
kwa mpangilio kuelekea mdomoni. Hii inaweza kufananishwa na mashuke ya ngano
zinazopeperuka angani kwa uelekeo mmoja. Kutokana na harakati hii ya cilia
(vinyweleo), mucous, ambayo huzishikilia mada kutoka nje, hupandishwa juu kooni.
Pindi mada hizi ngeni zinapopelekwa juu kooni, moja kwa moja unahisi kuwa
unataka kuzimeza. Hivyo mada zote ngeni ambazo zingeweza kuidhuru afya yako
hupelekwa tumboni ambapo huko humomonyolewa na kuharibiwa na majitumbo
(gastric juice).
Vinyweleo (cilia) vilivyopo kooni havina macho ya kuona wala havina ubongo wa
kuvipa uwezo wa kiakili. Lakini vinaweza kutambua eneo la koromeo ambalo liko
mbali sana kwa kulinganisha ukubwa wa vinyweleo hivyo. Aidha, vikiwa vinajua
uwezekano wa madhara ya mada ngeni, haviziruhusu kuingia mwilini. Licha ya miaka
mingi ya utafiti wa kisayansi, utaratibu wa ufanyaji kazi wa nywele hizi
haujagunduliwa kikamilifu. Lakini kumbuka kuwa hizi nywele, ambazo mfumo wake
bado haujagunduliwa kikamilifu, zimekuwa zikifanya kazi kwa ukamilifu kama ilivyo
kwa vijenzi vingine vya mwili tangu mwanadamu wa kwanza alipoumbwa kwenye uso
wa ardhi.
HEWA ILIYOVUTWA SASA IKO MAPAFUNI ...
Hewa inayokuja mapafuni iko tayari kwa matumizi baada ya kusafishwa na
unyevunyevu wake umedhibitiwa ndani ya koo. Kwa njia ya mzunguko wa damu
kutoka kwenye mapafu, hufikishwa kwenye seli zote za mwili ili izirutubishe. Wakati
huohuo hupokea kaboni dayoksaidi, ambayo ni mali ghafi isiyotumika (iliyoharibika).
Tunapotoa pumzi, tunatoa nje hii kaboni dayoksaidi inayokusanywa kutoka kwenye seli
zetu.
Waweza kudhani kuwa kupumua ni mchakato rahisi, lakini mabadilishano
muhimu ya oksijeni na kaboni dayoksaidi hufanyika katika kina cha ndani ya mwili
wako. Yote haya ni zawadi za Mwenyezi Mungu kwetu sisi; aliviumba vyote na
kuvifanya vitutumikie. Fikiria ingekuwaje lau kama hata upumuaji mdogo ungewekwa
chini ya udhibiti wetu. Tusingeweza kufanya kazi hii bila kukosea. Tungechoka na
hatimaye baada ya muda mfupi tungeacha. Mola wetu anajua kwamba hatuwezi
kufanya kazi hii sisi wenyewe. Hivyo akaumba mfumo wa upumuaji unaofanya kazi
kikamilifu kama ilivyo kwa mifumo mingine tuliyoielezea ndani ya kitabu hiki. Hii ni
mojawapo ya tunu ambazo Mwenyezi Mungu ametujaalia katika hii dunia. Kama
anavyoeleza katika aya hii:
Na akakupeni kila mlicho muomba. Na mkihisabu neema za Mwenyezi
Mungu hamwezi kuzidhibiti. Hakika mwanaadamu ni dhaalimu mkubwa,
mwenye kuzikufuru neema. (Surah Ibrahim: 34)
HITIMISHO
Ndani ya kitabu hiki tumetoa baadhi ya mifano na kueleza kuwa kuna kazi nyingi
zinazofanyika ndani ya miili yetu bila ya sisi kuwa na taarifa hata kidogo. Kila kiungo
na kila seli ya miili yetu hukimbia kwa kasi ya ajabu na wakati huo huo ikifanya kazi
kwa ukamilifu. Vyote hufanya kazi vilivyopangiwa kwa uelewano. Damu huendelea
kuzipelekea seli kirutubisho kinachohitajika ili ziendelea kuishi. Tumbo na matumbo
hukivunjavunja kirutubisho hiki katika vipande mbalimbali na kukifanya kiwe ni
chenye kufaa kwa matumizi ya seli. Seli za neva huendelea kutuma viamshi (stimuli)
kwenye maeneo yote ya mwili; ubongo huvitathmini viamshi hivi, na matokeo yake
tunaweza kuona, kusikia, kuonja na kutambua hisia nyingine zote.
Mojawapo katika kazi hizi inapocheleweshwa au kutofanywa, nidhamu ya
kawaida ya utendaji kazi wa mwili huharibika. Kama seli za neva zikiathirika/
kupungua nguvu midomo yetu haitafanya kazi; kama seli za tumbo zikiathirika,
hatuwezi kusaga chakula tunachokula; kama seli zilizopo katika ulimi zikiathirika,
hatuwezi kuonja keki za chocolate, machungwa au ndizi tunazokula. Lakini hakuna
hata kimoja kinachotokea, isipokuwa katika hali fulani ya maradhi. Kila kiungo cha
mwili wako kinaendelea kufanya kazi zake za kawaida bila kusimama huku wewe
ukiendelea kufurahia maisha yako ya kila siku. Ukamilifu ambao umejaaliwa katika
kila hatua ya maisha yako bila shaka ina chanzo na sababu. Hakuna kinachoweza
kujianzishia chenyewe na kuwa na mfumo kamili na usiokuwa na kasoro kama huo.
Runinga, friji, kompyuta, kalamu unazotumia kuandika, kwa ufupi kila kitu kina
aliyekibuni na kukitengeneza. Gari au ndege haiwezi ktokea yenyewe. Utendaji kazi
wake umewezeshwa na wahandisi na mafundi waliovibuni na kuzitengeneza. Hali
ikiwa hivyo, haiwezekani kabisa kwa mfumo kamili kama wa mwili wa binadamu
utokee kwa bahati nasibu.
Lazima utakuwa unashangaa kwamba inakuwaje baadhi ya watu wanadhani kuwa
miili yao inafanya kazi kwa ukamilifu wa namna hiyo kutokana na bahati nasibu. Kwa
hakika madai haya ndiyo madai yasiyoingia akilini hata kidogo kuliko madai yote
yanayoweza kutolewa. Nidhamu bora katika mwili wa binadamu isingeweza kutokea
kwa bahati nasibu. Nidhamu hii bora inathibitisha kwamba imewekwa na Mwenye
uelewa na hekma ya hali ya juu. Ni uumbaji wa Muumba mkuu, Mola wetu.
Mwenyezi Mungu anatuhabarisha ndani ya Qur'an kuwa Yeye ni Mwingi wa
rehma na huruma kwa waja wake. Tunachopaswa kufanya ni kuwa wenye kujisalimisha
kwake, kumtii moja kwa moja na kumshukuru kwa neema zote ambazo ametujaalia.
Katika aya ya Qur'an, Mwenyezi Mungu anatueleza yafuatayo:
Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila
Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa
kila kitu. (Surat al-An‘am: 102)