Top Banner
KUJENGA MISINGI YA IMANI Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika Yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika Yeye (Wakolosai 2:6-7a) Kimetafsiriwa na Edson Kamenya kutoka katika toleo la Kiingereza Liitwalo Laying Foundations Copyright © 2002 by Cornerstone Church Kitabu hiki chaweza kunakiliwa chote, au kwa sehemu katika mfumo wowote ule (wa maandishi, katika kanda za video au za sauti au njia nyingine sawa na hizo) Bila kupata kibali cha mchapishaji, Kwa sharti moja kwamba nakala zote hazitumiwi kibiashara. Kimechapishwa na Kanisa la Cornerstone la Afrika ya Kusini +27 11 616 4073 [email protected] ______________________________________________________________________ Maandiko yamenukuliwa kutoka katika BIBLIA TAKATIFU, SWAHILI UNION VERSION (SUV) Copyright © 1960 (isipokuwa ilipoelezwa vinginevyo) Toleo hili ni haki miliki za Chama cha Biblia cha Kenya na Chama cha Biblia cha Tanzania Katika kitabu hiki vifupisho kwa vitabu vya Biblia ni kama ifuatavyo:
106

KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Feb 24, 2018

Download

Documents

phamkhuong
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

KUJENGA MISINGI YA IMANI

Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika Yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika Yeye

(Wakolosai 2:6-7a)

Kimetafsiriwa na Edson Kamenya kutoka katika toleo la Kiingereza Liitwalo Laying Foundations

Copyright © 2002 by Cornerstone ChurchKitabu hiki chaweza kunakiliwa chote, au kwa sehemu katika mfumo wowote ule (wa maandishi, katika kanda za video au za sauti au njia nyingine sawa na hizo)

Bila kupata kibali cha mchapishaji,Kwa sharti moja kwamba nakala zote hazitumiwi kibiashara.

Kimechapishwa na Kanisa la Cornerstone la Afrika ya Kusini+27 11 616 4073

[email protected]

______________________________________________________________________

Maandiko yamenukuliwa kutoka katika BIBLIA TAKATIFU, SWAHILI UNION VERSION (SUV) Copyright © 1960 (isipokuwa ilipoelezwa vinginevyo)

Toleo hili ni haki miliki za Chama cha Biblia cha Kenya na Chama cha Biblia cha Tanzania

Katika kitabu hiki vifupisho kwa vitabu vya Biblia ni kama ifuatavyo:

Page 2: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Mwa Mwanzo Mat MathayoKut Kutoka Mk MarkoLaw Walawi Lk LukaHes Hesabu Yn YohanaKum Kumbukumbu Mdo MatendoYos Yoshua Rum WarumiAmu Waamuzi 1 Kor 1 WakorinthoRut Ruthu 2 Kor 2 Wakorintho1 Sam 1 Samueli Gal Wagalatia2 Sam 2 Samueli Efe Waefeso1 Fal 1 Falme Flp Wafilipi2 Fal 2 Falme Kol Wakolosai1 Nya 1 Nyakati 1 The 1 Wathesalonike2 Nya 2 Nyakati 2 The 2 WathesalonikeEzr Ezra 1 Tim 1 TimotheoNeh Nehemia 2 Tim 2 TimotheoEst Esta Tit TitoAyu Ayubu Flm FilemoniZab Zaburi Ebr WaebraniaMith Mithali Yak YakoboMhu Mhubiri 1 Pet 1 PetroWim Wimbo Ulio Bora 2 Pet 2 PetroIsa Isaya 1 Yoh 1 YohanaYer Yeremia 2 Yoh 2 YohanaOmb Maombolezo 3 Yoh 3 YohanaEze Ezekieli Yud YudaDan Danieli Ufu UfunuoHos HoseaYoe YoeliAmo AmosiOba ObadiaYon YonaMik MikaNah NahumuHab HabakukiSef SefaniaHag HagaiZek ZekariaMal Malaki

UTANGULIZI

Page 3: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kuweka Misingi ya ImaniKadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu

Kristo, ndivyo kunavyokuwa na maeneo mengi maishani mwetu yanayohitaji kurekebishwa na hata kubadilika. Waumini wa mwanzoni walilifanya hili kama tusomavyo katika Matendo 2:42 “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.”

Sisi sote tunataka kufikia hatua ya kukomaa kiimani, lakini ni hatua zipi tunazohitajika kuzipitia kwanza? Kitabu cha Waebrania 6:1-2 kinaelezea hatua hizi za mafundisho ya msingi kama ifuatavyo: “Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.”

Masomo yote katika mafunzo haya ya msingi yameandaliwa ili kukusaidia uweze kulifikia lengo hili. “Mafunzo ya kwanza..” au ya “msingi” yote yanayopatikana katika kifungu hiki cha Biblia yamepanuliwa. Mafunzo haya yameandaliwa yawasaidie zaidi wale wanaopitia mafunzo ya Kuweka Msingi wa Imani katika Kanisa la Cornerstone maana yake kwa ni Kiswahili Kanisa la Jiwe la Pembeni. Mafunzo haya yanawawezesha kulenga zaidi katika kile wanachoweza kukipokea katika mafunzo yenyewe kwa kuwa wataweza kuyakumbuka yote ambayo hawataweza kuyaandika katika wakati wa somo kupitia kitabu hiki. Vilevile, endapo mwalimu atakosa kulifundisha somo kama ipasavyo, basi kitabu hiki kitawapa mtazamo utakaofidia mapungufu.

Mwisho wa kila sura kutakuwa na mfululizo wa vifungu rejea vya Maandiko vitakavyoweza kuwa msaada kwako, hasa pale utakapotafuta kujifunza zaidi na hata kuwashirikisha wengine imani yako.

Mwongozo huu pia umekusudiwa kuwa kitabu chenye msaada kwa Wakristo na makanisa kila mahali, na kinatolewa ili kiweze kunakiliwa na kugawanywa kwa watu wengi kadiri inavyowezekana kwa sharti moja tu kwamba yale yaliyomo hayabadilishwi, na pia kitolewe pasipo kutozwa gharama yoyote. Hata hivyo, yapasa isisitizwe kwamba, mwongozo huu ni mfano ambao umeandaliwa kwa ajili ya wakati huu. Mafunzo yenyewe (uchaguzi wa masomo yanayofundishwa wakati wa kila somo, na walimu au wanenaji katika masomo haya), ni mambo yanayobadilika kwa haraka.

Tunatarajia kwamba mafunzo haya na hata mwongozo huu vitakuwa baraka kwako, na hivyo kuweza kuchangia angalau kidogo, katika jukumu zima la kuuendeleza na kuupanua Ufalme wa Mungu.

Kauli Yetu Kuhusu Imani.Tunaamini katika kweli za msingi wa Ukristo kama ulivyofunuliwa katika

Page 4: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Maandiko pamoja na haya kama ifuatavyo:

• Umoja wa Utatu Mtakatifu - Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. (Kum 6:4, Mat 28:19, 2 Kor 13:14)

• Mamlaka na enzi ya Mwenyezi Mungu katika uumbaji, ufunuo, ukombozi na hukumu ya mwisho. (Mwa 1:1, Ebr 1:1-2, Tit 3:4-5, Mdo 17:31)

• Uvuvio kamili wa Agano la Kale na Jipya kama kila moja lilivyotolewa mwanzoni, na kwamba Maandiko haya ndiyo yenye mamlaka ya mwisho katika maswala yahusuyo imani na mwenendo. (2 Tim 3:16, 2 Pet 1:21, 1 Kor 2:13)

• Hali ya anguko la mwanadamu kupitia dhambi ya Adamu, hali inayomuweka mwanadamu kuwa chini ya hasira na hukumu ya Mungu. (Rum 5:12, 2 The 1:7-9)

• Ukombozi kutoka dhambini kupitia kifo cha kidhabihu (sadaka takatifu) na cha kipatanishi cha Bwana wetu Yesu. (Rum 3:25-26, 5:15-21, 2 Kor 5:19, Mk 10:45)

• Ufufuo wa kimwili wa Mwokozi wetu, kupaa na kuketishwa kwake katika utukufu mkono wa kulia wa Mungu Baba. (1 Kor 15:4, Ebr 8:1)

• Roho Mtakatifu aliye nguvu ya utendaji wa Mungu ambaye kwa njia yake mtu mwenye dhambi anahuishwa, na muumini kuwezeshwa katika maisha na huduma. (Yn 3:5-6, Rum 8:9, 2 The 2:13)

• Kuhesabiwa haki kwa njia ya neema ya Mungu pekee. (Gal 2:16, Efe 2:8-9)

• Kanisa moja tu ulimwenguni lililo mwili wa Kristo linalowaunganisha ndani yake waumini wote wa kweli. (Efe 1:22-23, 1 Kor 12:12-13, Mdo 2:41-47)

• Tumaini la baraka la kurudi tena kwa Kristo katika nguvu na utukufu. (Mdo 1:11, Ebr 9:28, 2 Pet 3:10)

Sisi wenyewe tunaweza tukajiita kuwa ni “kanisa la kiroho”, lakini tunatambua umuhimu wa kuepuka kujiweka katika mafungu ya utambulisho. Tunaamini katika vipawa au karama za Roho Mtakatifu (1 Kor 12) na kuendelea kujazwa na Roho Mtakatifu. (Efe 5:18)

Tumejitoa kwa dhati kutimiza wajibu wa “kuwafundisha mataifa” (Mat 28:19-20, Mdo 1:8), na kwa hiyo wewe utapata mafundisho na pia kuambukizwa maono haya.

Yaliyomo

Page 5: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kwanza: Wokovu 1

A. Hitaji la Mwanadamu la Wokovu 1B. Mungu Ametuletea Mwokozi 2C. Nani Awezaye Kuokolewa? 3D. Mtu Anaokolewaje? 3E. Kuufanya Wokovu Uonekane Nje 4F. Uhakika wa Wokovu – Hisia. 4G. Mnyororo wa Wokovu 5H. Uhakika wa Mnyororo wa Wokovu 5

Sura ya Pili: Ubatizo wa Maji 6

A. Ubatizo ni nini? 6B. Kwa nini Yatupasa Kubatizwa? 6C. Nani Astahiliye Kubatizwa? 7D. Wakati Gani Inapotupasa Kubatizwa? 7E. Tukabatizwe Wapi? 8F. Nani Awezaye Kubatiza? 8G. Tunabatizwaje? 8H. Hitimisho 8I. Mnyororo wa Ubatizo wa Maji 8

Sura ya Tatu: Ubatizo wa Roho Mtakatifu 9

A. Roho Mtakatifu ni Nani? 9B. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni Nini? 11C. Ninapokea Ubatizo Huu kwa Njia Gani? 12D. Nani Abatizaye, Wakati Gani, Na Lipi Litokealo? 12E. Kuna Nini Katika Kunena kwa Lugha? 13F. Mnyororo wa Ubatizo Katika Roho Mtakatifu. 15

Sura ya Nne: Kiini cha Ubaba wa Mungu 16

A. Utangulizi 16B. Kwa Nini Mungu Awe na Moyo wa Ubaba? 16C. Nini Kinachotusukuma Kumtumikia Mungu? 18D. Kuupokea Upendo Alionao Mungu Kwetu 18E. Baba Yako Amefunuliwa 19F. Mnyororo: Moyo wa Ubaba wa Mungu 22

Sura ya Tano: Tumaini Letu 23

A. Utangulizi 23B. Uelekeo Wetu 23C. Mnyororo wa Ufufuko 25

Page 6: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

D. Vipi Kuhusu Hukumu, Thawabu na Jehanamu? 25E. Mnyororo wa Hukumu ya Milele 26F. Je, “Hizi ni Siku za Mwisho”? 26

Sura ya Sita: Ibada 28

A. Moyo wa Ibada 28B. Vielelezo vya Ibada Katika Agano la Kale 29C. Vielelezo vya Ibada Katika Agano Jipya 30D. Hitimisho 32E. Mnyororo wa Ibada 32

Sura ya Saba: Maombi na Kufunga 34

A. Maombi ni Nini? 34B. Kwa Nini Twapaswa Kuomba? 34C. Mifano ya Maombi 35D. Mafundisho ya Yesu Juu ya Maombi 36E. Tuombeje? 36F. Vikwazo Dhidi ya maombi 37G. Mnyororo wa Maombi 39H. Kufunga 39I. Kufunga ni Nini? 39J. Kwa Nini Tunapaswa Kufunga? 40K. Kufunga - Tufungeje? 41L. Tufunge Wakati Gani? 42M. Tahadhari na Miongozo Katika Kufunga 43

Sura ya Nane: Biblia 44

A. Kile Tukiaminicho Kuhusu Biblia 44B. Muundo wa Biblia 46C. Kwa Nini Tujifunze Biblia – Sababu kumi 48D. Itupasavyo Kuikaribia Biblia 48E. Hitimisho 50F. Mnyororo wa Biblia 50

Sura ya Tisa: Fedha na Utoaji 51

A. Mungu Ndiye Chanzo cha Vyote 51B. Utoaji 53C. Fedha na Uaminifu 56D. Kutengeneza Mambo ya Nyumba Zetu 58E. Thawabu au Tuzo za Utii 58F. Mnyororo wa Fedha na Utoaji 59

Page 7: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kumi: Kanisa 60

A. Sura ya kanisa Ndani ya Barua kwa Waefeso 60B. Utume na Agizo 65C. Kanisa Ulimwenguni na Kanisa la Mahali 65D. Wewe na Kanisa 66E. Mnyororo wa Kanisa 67

Sura ya Kumi na Moja: Kuwekewa Mikono 68

A. Kutoa Baraka, Mamlaka na Uponyaji 68B. Kupokea Roho Mtakatifu na Vipawa vya Kiroho 70C. Watumishi Kuwekwa Wakfu 72D. Mnyororo wa Kuwekewa Mikono 73

Sura ya Kumi na Mbili: Unabii 74

A. Maandiko na Roho ya Unabii 74B. Unabii Kwa Watu Binafsi 74C. Hamu ya Kuwa na Huduma ya Kinabii 75D. Je, Hivi Twaweza Kutarajia Kumsikia Mungu Akinena? 76E. Kuitambua Sauti ya Mungu 76F. Ni Wakati gani Mungu Anasema Nasi na Kwa Njia Gani? 77. Tunafanya Nini na Neno la Mungu? 78H. Hitimisho 79I. Mnyororo wa Unabii 79

Sura ya Kumi na Tatu: Uenezaji Injili 80

A. Njia Ngumu ya Mashaka Kuelekea Uinjilishaji 80B. Tabia Tatu za Uenezaji Injili 80C. Kanuni Zifaazo kwa Uenezaji Injili 83D. Dondoo Zinazoweza Kusaidia Kwa Uinjilishaji 83E. Mnyororo wa Uenezaji Injili 84

Sura ya Kumi na Nne: Vita ya Kiroho 85

A. Utangulizi 85B. Vita 87C. Maombi (Sala) na Kufunga 90D. Hitimisho 90E. Mnyororo wa Vita ya Kiroho 90

Sura ya Kumi na Tano: Maono, Mali na Magari Yetu 91

A. Utangulizi 91B. Kichwa (Uongozi/Mamlaka) 91C. Moyo Wetu (Kiini au Roho ya Utamaduni Wetu) 94

Page 8: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

D. Tumaini (Maono) 95E. Vyombo vya Kusafirishia Maono, Thamani 98F. Muhtasari na Hitimisho 98

Page 9: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kwanza: Wokovu

Lakini andiko limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo. (Gal 3:22.)

A. Hitaji la Wokovu Kwa MwanadamuNia aliyokuwa nayo Mungu mwanzoni ilikuwa ni kuwa na uhusiano wa kiagano na wa-nadamu. Hata hivyo, “anguko” na “dhambi” vilisababisha utengano na hivyo kuwezesha kifo kitawale. Hitaji la wokovu kwa mwanadamu ni matokeo ya dhambi, kwa kuwa Mungu mtakatifu hawezi kuigusa dhambi.

A.1. Dhambi Hutenganisha

“Lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu” (Isa 59:2a)

A.2. Dhambi ni Tatizo Kwa Ulimwengu Wote

“Hakuna mwenye haki hata mmoja.” (Rum 3:10b)

Wanadamu wote wameishiriki dhambi:

• Kwa kuzaliwa:

“Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi.” (Rum 5:12)

“Na kama kwa kutotii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi.” (Rum 5:19)

“Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.” (Zab 51:5)

Kwa hali hii, dhambi ni urithi wetu wa kuzaliwa tangu hapo anguko lilipotokea.

• Kwa tendo:

“Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Rum 3:23)

A.3. Ipo Adhabu Kwa Ajili ya Dhambi

Adhabu ya dhambi ni hukumu ya Mungu na kifo. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti;” (Rum 6:23a)

“Roho ile itendayo dhambi itakufa.” (Eze 18:4b)

A.4. Muhtasari

1

Page 10: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Wanadamu wote wako chini ya dhambi. Dhambi humtenga mwanadamu ikimuweka mbali na nia ya Mungu ya uhusiano wa kiagano na ukaribu. Dhambi hukiwezesha kifo kitawale.

B. Mungu Ametuletea Mwokozi

B.1. Mwanadamu Hana Uwezo wa Kujiokoa

“Matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi.” (Isa 64:6a)

“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” (Efe 2:8-9)

B.2. Hali Hii Haituachi Tukiwa Hatuna Tumaini

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” (Yn 3:16)

“Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetu-pasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu....” (1 Yn 3:16a)

B.3. Nini Kimpacho Yesu Uwezo wa Kuondoa Dhambi?

• Alizaliwa toka kwa mwanamke bikira na hivyo hakuwa chini ya dhambi iliyoende-lezwa kwa njia ya urithi toka kizazi hadi kizazi (dhambi ya asili, angalia, kwa mfano, Rum 5:12).

• Yeye mwenyewe hakupata kufanya dhambi yoyote (Ebr 4:15).

• Yesu alivumilia mateso ya adhabu (ghadhabu) ya Mungu kwa ajili ya dhambi. Kwa kulifanya hilo alifanyika kuwa dhabihu au sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi na kusimama kama afanyaye malipizi badala ya wanadamu watenda dhambi: “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.” (Rum 5:8-9)

“Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu.” (Isa 53:5a/Mat 4:12)

• Aliiharibu nguvu ya kifo kwa kuwa alifufuka kutoka katika wafu. (angalia 1 Kor 15:3-6 na Ebr 2:14-15).

B.4. Muhtasari

Mungu alimuumba mwanadamu, mwanadamu akaanguka dhambini, na hivyo watu wote wako chini ya nguvu ya dhambi. Mungu ametupatia Mwokozi awe suluhisho: Mwokozi alikufa akiwa dhabihu au sadaka mbadala kwa mwanadamu mtenda dhambi. Ni jambo lililo wazi, hata hivyo, kwamba ukombozi huu haumuhusu kila mmoja kwa sababu Biblia inatamka wazi kwamba baadhi ya wanadamu watatupwa katika jehanamu ya moto pindi wakati wa hukumu utakapowadia.

2

Page 11: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

C. Nani Awezaye Kuokolewa?

Uwezekano upo, kwamba watu wote wanaweza kuokolewa. Yategemeana na mwitikio wao binafsi juu ya ufunuo ambao Mwenyezi Mungu ameutoa. Ni hamu ya Mungu kuona kwamba watu wote wangeokolewa (1 Tim 2:4), Yesu alikufa kwa ajili ya “ulimwengu” (Yn 3:16). Lakini, kwa hali halisi si kila mmoja ameokolewa. Swali ni kwamba, “Mtu ana-pataje kuokolewa?”

D. Mtu Anaokolewaje?

Paulo aliwasihi na kuwatia moyo watu “wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.” (Mdo 20:21). Yesu alianza mahubiri yake kwa kusema, “Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.” (Mk 1:15). Vifungu hivi viwili vyote vinaonyesha mahitaji makuu mawili ya kibiblia yanayohitajika ili mtu aweze kupata wokovu: toba na imani (angalia pia Ebr 6:1-2). Mahitaji haya yanajumlisha mambo gani?

D.1. Toba

Neno la Kiyunani “metanoia” maana yake ya moja kwa moja ni “ni mtu kubadili mawazo/akili/nia.” Hii ina maana kwamba toba si hali ya kujisikia vibaya au kusikitika bali ni hali ya uamuzi, uamuzi wa kubadilika. Ni tendo la dhamira na wala si la hisia. Ni kweli kabisa, kwamba tendo lenyewe laweza kuandamana na hisia kali lakini toba yenyewe ni mabadiliko ya mawazo, akili au nia.

Mabadiliko haya ya mawazo, akili au nia na hatimaye mabadiliko ya maisha yetu katika kila eneo ni:

Utambuzi wa hali yetu halisi ya dhambi.

Uamuzi wa kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa ajili ya watu wake wateule.

“‘Wakati umetimia,’ Yesu alisema. ‘Tubuni na kuiamini Injili!’ ” (Mk 1:15; Mdo 2:38a)

D.2. Imani

Hii inatutaka tuweke tumaini letu ndani ya Yesu – na kujiambatanisha na ufunuo wa Yesu Kristo kama Mwokozi. Hakuna kazi au tendo ambalo mtu aweza kulifanya lina-loweza kumfanya astahili kupewa haki na Mungu.“Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” (Efe 2:8-9a)

Zawadi haifanyiwi kazi, inaweza tu kupokelewa.

“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani.” (Rum 5:1a) Kufanywa kuwa waadilifu au kuhesabiwa haki ni neno la kisheria linalotumika kwa wale ambao hatia yao imeondolewa. Ili kuondolewa hatia iliyo juu ya wanadamu wote mtu lazima awe na imani katika kazi ya uokozi ya Yesu Kristo. Imani, kwa hivyo ni kuliamini Neno la Mungu.

3

Page 12: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

“Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye…” (2 Kor 5:21)

Neno la Mungu ni Kweli (Yn 17:17) na halina uongo hata kidogo. Kwa hivyo tunaweza kulitumainia kwa mioyo yetu yote.

E. Kuufanya Wokovu Wako Uonekane Nje

Toka wakati ule tunapotubu na kumwamini Yesu, tunaingia ndani ya ufalme wa Mungu.Tendo hili linaelezwa kama “kuzaliwa upya au kuzaliwa mara ya pili ” (Yn 3:3). Tokea kip-indi hiki cha kuingia ndani ya ufalme hadi mwisho wa maisha yetu duniani, tunakuwa na wajibu wa kuishi maisha yetu katika hali ya toba (hali ya kuendelea kujiweka chini ya Neno la Mungu) na kuwa na imani kwa Yesu Kristo kama Mwokozi.

Yesu alisema katika Yn 10:27-30, “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja.” Hivyo, mara tunapokuwa tumeokolewa wokovu wetu unalindwa na Yesu – hakuna yeyote awezaye kutuibia wokovu huo. Lakini Biblia inatuonya katika 2 Tim 2:12b, “Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi.”

Kwa hivyo tunatiwa moyo kuvumilia tukidumu katika imani yetu hadi kufa, au hadi Kristo arudipo. Waebrania 10:35-36 inatuambia, “Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi.” Tunapovumilia tukiishi katika uadilifu, matendo mema, uaminifu na mateso, tunalipwa kwa kupewa hazina za milele na Mungu mwenyewe (angalia, kwa mfano, Ebr 11:26, Mat 6:1-6, Mat 6:16-21, Mat 10:41-42, Mat 16:27 na Lk 6:22-23).

F. Uhakika wa Wokovu – Hisia.

Maisha ya Kikristo hayahusu tu kujizoeza katika imani pasipo kujipatia "uzoefu". Muumini anaweza kuhisi na kuwa na hisia au misisimko inayompa kujua kwa hakika kwamba yeye ni mtoto wa Mungu. Biblia inatuonyesha wazi kwamba Roho Mtakatifu aweza kushuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu katika Warumi 8:16, “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.” Uzoefu wa jinsi hii utahusisha hata hisia zetu pia.

Hata hivyo, ni lazima tusisitize wazi kwamba misisimko hii na hisia si vitu vya kuendelea au vya kudumu. Misisimko na hisia hizi ni MATOKEO tu ya imani katika Neno la Mungu na kuifanyia kazi Kweli iliyo katika Neno lenyewe. Nyakati huja ambapo Mkristo binafsi hujihisi kama mtu ambaye hajaokolewa. Misisimko au hisia zetu zinaathiriwa na hali ya mazingira yanayotuzunguka, na tunaweza kujikuta tukiwa wapweke sana, na nyakati zingine hata tukajiona kuwa Mungu mwenyewe ametuacha. Katika nyakati kama hizi hatuwezi kuzitegemea hisia zetu, lakini katika hali ya ukomavu wa kiroho tuziambie nafsi zetu kwamba tunapaswa kuliamini Neno la Mungu.

Misisimko na hisia ambazo ni matunda ya imani kwa kweli ni ziada tu au nyongeza, ni kama, "rojo ya maziwa inayowekwa juu ya keki". Haitakiwi tuifanye kuwa msingi wa imani yetu, wala hatutakiwi tuifanye misisimko hiyo na hisia kuwa ndiyo lengo letu. Ina-kuja yenyewe pale sisi tunapotafuta kulitii Neno la Mungu, lakini ITAKUJA, na tunaweza

4

Page 13: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

kutegemea kujipatia uzoefu wa hisia zinazosisimua, hali ya amani na kujiona kuwa na maisha yenye utoshelevu.

G. Mnyororo wa Wokovu

Yn 3:16Rum 3:23Rum 6:23Yn 14:61 Yoh 1:9Yn 1:12Efe 2:8-9Rum 10:9-10

H. Uhakika wa Mnyororo wa Wokovu

1 Yoh 5:13Yn 1:12Yn 3:36Yn 5:24Yn 6:47Rum 1:17Rum 8:16Yn 10:27-29

5

Page 14: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Pili: Ubatizo wa Maji

“Tazama, maji haya; ni nini kinachoni-zuia nisibatizwe?” (Mdo 8:36b)

A. Ubatizo ni Nini?

A.1. Ishara ya Nje

Ubatizo ni ishara ya nje inayoashiria tendo la ndani na lisiloonekana, la kuzaliwa mara ya pili au kuzaliwa upya. Wakati wa uongofu wetu tunabatizwa kwa kuunganishwa na “Kristo” (Gal 3:27), na hivyo ubatizo huonyesha maana ya ubatizo wa kiroho ndani ya mwili wa Kristo. Ubatizo wa maji unakuwa kama taswira au picha ya kile kilichomtokea mtu ambaye amekuwa Mkristo. Wanapozamishwa chini ya maji wanaashiria kifo cha Kristo na hali yao ya kufa kuelekea matakwa ya nafsi zao wenyewe. Wanapoinuliwa juu ya maji wanaonyesha picha ya ufufuko wa Kristo na kufufuka kwao wenyewe kwa kuingia katika uzima mpya (Rum 6:1-14).

Katika Agano la Kale, tukio katika kitabu cha Kutoka la kuvuka bahari ya Shamu lilikuwa ni mfano wa Ubatizo ambao kupitia huo Wana wa Israeli waliwekwa huru toka katika utumwa wa Misri (1 Kor 10:2, 1 Pet 3:21).

A.2. Ukiri Hadharani

Ubatizo ni ukiri wa hadharani wa hali ya ndani ya kujitoa kwa mtu binafsi. Katika maisha ya waumini wengi, hutokea kwamba mara tu baada ya kubatizwa mateso makali hu-waandama kutokana na hali halisi ilivyo ya ukiri huu wa imani.

B. Kwa Nini Yatupasa Kubatizwa?

B.1. Utii

Yesu aliamuru ubatizo: “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuy-ashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari” (Mat 28:19-20a).

B.2. Kufuata Mfano wa Yesu

Yesu alionyesha mfano kwa kubatizwa na Yohana Mbatizaji (Mat 3:13-17). Yohana Mba-tizaji alipojaribu kumzuia Yesu asibatizwe yeye alimjibu, “Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.”

Ubatizo ulionyesha kwamba Yeye alikuwa amejitoa wakfu kwa Mungu na sasa alikuwa amekubaliwa “rasmi” na Baba (jambo linaloonekana katika kushukiwa na Roho Mtaka-tifu, na maneno aliyotamka Baba kumthibitisha).

Ilikuwa wakati wa ubatizo wake, pale Yohana Mbatizaji alipomtangaza mbele ya watu wote kwamba Yeye ndiye aliyekuwa Masihi. Yesu alijifananisha na mwanadamu

6

Page 15: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

mwenye dhambi japo Yeye mwenyewe hakuwa na hitaji la kutubu. Ubatizo wake ulikuwa ni mfano kwa wafuasi wake.

.B.3. Mfano wa Kanisa la Kwanza

Waongofu wa kwanza katika Yerusalemu (Mdo 2:37-41).Wasamaria (Mdo 8:12-13).Towashi (Mwethiopia) Mkushi (Mdo 8:36-38).Paulo (Mdo 9:17, Mdo 22:16).Kornelio pamoja na nyumba yake (Mdo 10:33-48).Mwanamke Lidia pamoja na nyumba yake (Mdo 16:13-15).Askari wa gereza Mfilipi (Mdo 16:31-34).Krispo na Wakorintho wengine (Mdo 18:8).

Ni muhimu kuelewa kwamba ubatizo wenyewe peke yake, hauwezi kumwokoa mtu yeyote, lakini wenyewe huo ni hatua ya utii wa nje iliyo ya lazima kwa ajili ya kuthibitisha toba ya ndani.

C. Nani Astahiliye Kubatizwa?

Waumini wote sharti wabatizwe: Si ubatizo wa watoto wala ubatizo wa watu wazima, bali ubatizo wa wote waaminio. Ni waumini pekee wanaopaswa kubatizwa. Ubatizo ni ishara ya mabadiliko yaliyopo na wala si kisababishi cha mabadiliko.

C.1. Vipi Kuhusu Ubatizo wa Vitoto Vichanga?

Watoto hawawezi kutubu. Yesu hakubatizwa akiwa mtoto mchanga, bali aliwekwa wakfu kwa Bwana katika Luka 2:22. Watoto wenye umri wa kuielewa injili na kuonyesha kuwa na imani yao binafsi wanaweza kubatizwa. Jambo hili laweza kutokea katika umri mdogo sana kwa sababu injili ni rahisi kiasi cha mtoto kuweza kuielewa. Waumini wanaorudi nyuma hawapaswi “kubatizwa upya” wanapomrudia Kristo kwa kuwa ubatizo ni tendo lifanyikalo mara moja tu, sawa na vile ambavyo tendo la kuzaliwa linatokea mara moja maishani.

D. Wakati Gani Inapotupasa Kubatizwa?

Ni wakati tunapopata uongofu. Katika kanisa la kwanza watu walibatizwa mara tu wali-poamini. Katika siku ya Pentekoste, “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.” (Mdo 2:41). Paulo alibatizwa mara tu baada ya kuamini. Uongofu na ubatizo vilikuwa vitu viwili vilivyokwenda sambamba katika kanisa ka kwanza, mara nyingi vyote viwili vikitokea katika siku moja. Angalia, kwa mfano, Matendo 10:47-48.

E. Tukabatizwe Wapi?

7

Page 16: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Popote! Hatuhitaji vyombo maalumu vilivyojengwa kwa ajili ya kubatizia. Maji yoyote ya-liyo karibu na hapo mtu apatiapo uongofu yanafaa. Angalia kwa mfano, Matendo 8:38-40.

F. Nani Awezaye Kubatiza?

Muumini yeyote aweza kubatiza. Si lazima awe mzee au kiongozi. Filipo aliyembatiza towashi wa Kiethiopia alikuwa muenezaji wa injili (muinjilishaji).

G. Tunabatizwaje?

G.1. Kwa Kuzamishwa

Tunabatiza kwa kuzamisha, na si kwa kunyunyizia (Mdo 8:38-39). Filipo na towashi, wote walishuka na kuingia majini na Filipo akambatiza. “Walipotoka majini.” (Mdo 8:39a). Neno “ubatizo” linatokana na neno la Kiyunani, “baptiso”, lenye maana ya “kuzamisha, kuchovya, kutumbukiza au kuzika” na daima hutumika likiwa katika muundo wenye nguvu unaoonyesha tendo la kuzamisha kitu kabisa.

G.2. Katika Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu

Sisi hubatiza katika jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu (Mat 28:18, Gal 3:27). Msisitizo ulikuwa kwamba huu ulikuwa ubatizo wa Kikristo , na si wa Kiyahudi, ki-pagani au ubatizo wa Yohana Mbatizaji.

H. Hitimisho

Kwa kuhitimisha, ubatizo ni tendo rahisi la utii kwa Neno la Mungu lililofunuliwa. Tendo hili hukaribisha baraka za Mungu ndani ya maisha yetu na kutuweka hali imara juu ya msingi wa kimungu. “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafanan-ishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” (Mat 7:24)

I. Mnyororo wa Ubatizo wa Maji

Mdo 2:38-39Mat 3:13-17Mat 28:19-20Mdo 10:47-48Rum 6:1-14Kol 2:9-151 Pet 3:21

8

Page 17: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Tatu: Ubatizo wa Roho Mtakatifu

“Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua vi-atu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtaka-tifu na kwa moto.” (Mat 3:11)

Hakuna “hatua” tatu za mtu kupata kuwa Mkristo, bali ipo hatua moja tu: toba inayooan-damana na imani. Hata hivyo, Biblia inazungumzia ubatizo wote wa aina mbili, yaani wa maji na wa Roho Mtakatifu kuwa ni majaliwa ambayo mwongofu wa kweli sharti apitie. Kwa hali hii, kupata ubatizo wa Roho kunafanya “mchakato” wa uongofu uwe umeka-milika.

Itakuwa vigumu kukielewa na kukitamani kitendo hiki kitokee maishani mwetu endapo kwanza tutakuwa hatuna maarifa ya kumjua Roho Mtakatifu ni nani, naye hufanya nini. Kwa hiyo tunatakiwa kuanza kwa “kumtambulisha” Roho Mtakatifu.

A. Roho Mtakatifu ni Nani?

A.1. Nafsi Yake

Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu aliye nafsi tatu, ni mshiriki aliye sawa na aliye wa milele sawa na Baba na Mwana. Kwa karne nyingi Yeye alikuwa nafsi ya Utatu Mtakatifu iliyosahauliwa na kanisa; lakini katika wakati huu wetu amerejezwa katika na-fasi anayostahili ndani ya mawazo na uzoefu wa maisha ya Kikristo.

Roho Mtakatifu si nguvu ya hivihivi tu au nguvu fulani ya Mungu inayofanya kazi ulim-wenguni (wazo potofu la kawaida la wengi), lakini yeye ni nafsi hai: Biblia inamzun-gumzia kama “Yeye” na “Yake,” na wala si “kitu” na “ya kitu” na Biblia inamwonyesha akiwa na tabia za mwenye nafsi (akili na mawazo, usemi na lugha, kama vile pia hisia na misisimko) akifanya vitendo vya aliye na nafsi (kwa mfano, kuonyesha njia, kuon-goza, kutenda kazi, kutoa, kufanya ushirika, kutia hatiani, kufundisha, kufariji, kushauri na kuomba).

Roho Mtakatifu si mdogo kuliko Mungu (wazo lingine lililokuwa potofu) bali ni Mungu kamili. Anaitwa Mungu katika Maandiko yaliyo wazi na ndani ya mengine ambayo kuto-kana na utendaji wake katika Maandiko hayo inakuwemo maana iliyojificha inayomwon-esha kama Mungu kamili; Anazo sifa za kimungu (kwa mfano, kuweza yote, kuwa ma-hali pote, kujua yote na kutokufa) na anatenda au kushiriki katika kazi ya Mungu (kwa mfano, uumbaji, kufunua, kuonyesha hatia, kubadilisha, kutakasa na kufufua).

Roho Mtakatifu ni mwenye nafsi na pia Mungu, na kwa kuwa yeye anayo nafsi twaweza kuwa watu wanaohusiana naye au wasio na uhusiano naye (hatuwezi kuhusiana na nusu ya mtu mwenye nafsi), na kwa hali hii hatuwezi kuuliza swali “Hivi, mimi nina kiasi gani cha Roho Mtakatifu?” Lakini badala yake swali linalofaa ni “Roho Mtakatifu ana-tawala kiasi gani cha maisha yangu”

Kwa sababu Yeye ni Mungu anayefanya kazi maishani mwetu kwa kuangalia matakwa yake na si yetu. Yeye hufanya apendavyo na hivyo haiwezekani tumuamrishe afanye tutakacho; Yeye ni mtakatifu na hivyo hataweza kukijaza chombo kisicho safi.

9

Page 18: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Ufahamu mwingine juu ya Roho Mtakatifu waweza kupatikana kutokana na majina mengi anayoitwa katika Maandiko na pia alama zinazotumika kumuelezea (moto, upepo, maji, mafuta na hua).

A.2. Kazi Yake

Yeye kama sehemu ya utatu wa Mungu, Roho Mtakatifu anahusika katika kazi zote za Mungu. Yeye alihusika na alikuwa mwenye sehemu muhimu katika kazi ya uumbaji, kutoa ufunuo, katika matendo makuu ya Mungu kwa Israeli na pia katika tendo maalumu ambalo kwa hilo Kristo alifanyika kuwa mwanadamu. Anashughulika ndani ya kanisa; Anakaaa ndani yake, analiunganisha, anatoa vipawa kwa washiriki na pia anaujenga mwili, anawaweka na kuwawezesha viongozi wake, na kuelekeza katika lengo la utume wa kanisa. Atakuwa mwenye kuhusika kwa karibu katika matukio ya siku za mwisho, na pia katika milele ijayo.

Kwa vyovyote vile, kazi ya Roho Mtakatifu inaonekana zaidi katika kipindi hiki kwa kule kuhusika kwake ndani ya maisha ya muumini binafsi. Hata kabla ya wokovu ni Roho Mtakatifu ampaye mwanadamu kujiona ni mwenye hatia na kumfanya amkaribie Kristo (Yn 6:44, Yn 16:8-11). Wakati mtu kupata anapoongoka, Roho ndiye afanyaye ma-badiliko ndani ya roho ya mtu huyo na kumfanya azaliwe mara ya pili (Yn 3:5-8, Tito 3:5). Tangu wakati huo na kuendelea, kila muumini hukaliwa ndani yake na Roho Mtaka-tifu (Rum 8:9) na kwa hali hii, anakuwa amepigwa muhuri na Yeye Roho: ambaye uwepo wake ni kama malipo ya kwanza yanayokuwa ni dhamana kwa ajili ya malipo kamili ya (wokovu) yatakayotolewa mara Kristo ajapo (Efe 1:13-14, Efe 4:30, 2 Kor 1:22).

Baada ya kupata uongofu kwa maisha yote ya mtu husika, Roho Mtakatifu anatembea na muumini, akimpa uhakika, akimtakasa, akishirikiana naye, akimwongoza, akimshauri, akimfundisha, akimvuvia na kumpa vipawa. Tunaweza kusema kwamba Roho Mtakatifu huchukua jukumu la msingi kwa ajili ya maisha ya muumini, akichukua hatua kwa hatua, toka mwenye dhambi aliyetiwa hatiani hadi kuwa mtakatifu aliyekamilishwa na kufik-ishwa katika kilele cha wito wake.

Huu hasa ni utambulisho wa kukupa uelewa juu ya Roho Mtakatifu tuliyepewa na Yesu (Yn 14:16-18). Yeye ni mfariji/mshauri/mtetezi (hakuna tafsiri maalumu kwa neno la Ki-yunani “parakletos,” linalomaanisha ‘mmoja atembeaye nasi akitupa ushauri katika kila hatua tunayoipiga njiani). Yesu aliposema “nitawatumia msaidizi mwingine” neno la Ki-yunani lililotumika siyo heteros (lenye maana ya mwingine), bali neno “allos” (neno la Kiyunani lenye maana ya “mwingine aliye sawa kabisa).Kwa hivyo kama ilivyo kwamba kumjua Yesu ni kumjua Baba (Yn 14:7-9), vivyo hivyo, kumjua Roho ni kumjua Yesu (na kinyume chake).

Roho Mtakatifu hutuwezesha kuzitimiza amri za Kristo kwetu na kutupa vipawa ili kutupa uwezo wa kuyatimiza yale tuliyoitwa kuyatimiza. Kugundua vipawa vyetu tulivyopewa ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya kutembea na Bwana, na jambo hili litatiliwa maanani katika majadiliano yatakayofuata.

Sasa kwa kuwa tumemjua Roho Mtakatifu ni nani na ni nini anachokitaka kukifanya kupi-tia katika maisha yetu, tutakuwa na uwezo zaidi wa kuelewa, kutamani na kuupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu.

B. Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni Nini?

10

Page 19: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Tayari tumeweza kuona kwamba Roho Mtakatifu anakaa ndani ya kila muumini tangu wakati wa kuzaliwa mara ya pili, yaani kubadilishwa au kuokolewa. Lakini ushahidi wa Maandiko na uzoefu wa mamilioni ya waumini ni unaonesha kwamba huwa kuna uzoefu wa kumpokea Roho Mtakatifu unaotokea baada ya kuokolewa, uzoefu unaozidi ile hali ya Roho Mtakatifu kukaa tu ndani ya mtu.

Yesu, Mungu-mtu mkamilifu, alikuwa kwa hakika akikaliwa na Roho Mtakatifu tokea ku-zaliwa kwake. Lakini hata hivyo alihitaji kupakwa mafuta na Roho (kumpokea katika hali iliyo kamili na tofauti) kabla ya kuanza huduma yake ya wazi (Mat 3:16). Inaelekea Wa-nafunzi walimpokea Roho Mtakatifu kabla ya Yesu hajapaa (Yn 20:22). Lakini hata hivyo iliwapasa kusubiri Yerusalemu kwa ajili kujazwa kwingine ambako kungefuatia kabla ya wao kuingia katika huduma yao ya wazi (Lk 24:49, Mdo 1:4-5, Mdo 1:8, Mdo 2:1-4).

Wasamaria waliamini (hii ina maana, waliokolewa au kupata uongofu) wakati Philipo ali-powahubiria, na kutokana na hilo, tangu wakati huo walikuwa watu wanaokaliwa na Roho (Mdo 8:12). Hata hivyo Petro na Yohana waliona kwamba ilikuwa ni muhimu wawaombee “kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.” hii ikihusu uvuvio na ujazo unaofuatia tendo la uongofu au kuok-olewa (Mdo 8:14-17).

Paulo katika Matendo 9:17 na pia katika Matendo 18:24-26, na waumini wa Efeso (Mdo 19:1-6) wao pia walipata hali ya kujazwa na Roho iliyofuatia tendo la awali la kuamini na kupata uongofu.

Kwa hali hii basi, licha ya kukaliwa na Roho Mtakatifu kwa kila muumini baada ya kuok-olewa, lipo tukio halisi litokealo wakati Roho Mtakatifu ajapo juu yetu na kutujaza, akitu-paka mafuta na kutupa uwezo na kila tunachokihitaji kwa ajili ya maisha (kutuwezesha kuishi kama Mungu apendavyo tuishi), na huduma (kutuwezesha kufanya yote atakayo tuyafanye). Yohana alitabiri kwamba Yesu angetubatiza kwa Roho Mtakatifu (Mat 3:11, Yn 1:33), na Yesu mwenyewe aliutambua ubatizo huu wenye nguvu ya nyongeza kama ubatizo katika Roho Mtakatifu (Mdo 1:5). “Ubatizo” (neno lenye maana ya “kuzam-ishwa”) hapa linatumika kwa maana ya kinahau: katika ubatizo wa maji tunakuwa kweli tumezamishwa katika maji wakati katika ubatizo wa Roho Mtakatifu jambo linalotokea mara nyingi linakuwa lenye uzoefu unaotuzidi uwezo wetu wa kuhimili na linatubadilisha kabisa kiasi kwamba, tunakuwa kama watu ambao wanaendelea tena na tena kuzam-ishwa katika Roho.

Ubatizo wa Roho Mtakatifu unatuletea kiwango kipya cha uwepo halisi wa Mungu na nguvu zake maishani mwetu. Hatuwezi kutimiza wito wetu wa kimaisha na huduma am-bayo Mungu ameikusudia bila hilo kutokea. Kwa hiyo, tutakuwa tunatenda tendo la ki-jinga kama tutakosa kuutamani ubatizo huu (tukijiweka kinyume na maagizo ya Yesu na Maandiko yanayotutaka tuutafute). Twaweza kuupokea ubatizo huu mapema iwezeka-navyo, mara tu baada ya uongofu au kuokolewa kwetu (angalia Mdo 10:44). Hatupaswi kusubiri kwanza hadi “tufuzu” kama Wakristo.C. Ninapokea Ubatizo Huu Kwa Njia Gani?Japo kubatizwa katika Roho Mtakatifu ni uzoefu wa tendo la kimungu kabisa, hatupaswi kulifanya tendo hili lionekane kama kufuatilia mambo ya kimiujiza au uzoefu wa mambo ya kimashetani. Hapa chini kuna masharti (au hatua) zinazoweza kutusaidia kupokea.

C.1. Ongoka/Badilika

11

Page 20: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Twapaswa kuwa waumini waliozaliwa mara ya pili. Ni wazi Roho Mtakatifu hataweza kumjaza mtu yeyote kwa namna hii ambaye maisha yake hayajatolewa kabisa kwa Mungu.

C.2. Amini

Tunapaswa kuiheshimu na kuitafuta kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya maisha yetu. Hasa tunapaswa kuamini katika ubatizo wa Roho Mtakatifu, na pia katika uhitaji wetu wa uba-tizo huu.

C.3. Jitakase

Roho aliye mtakatifu hawezi na hatajaza chombo kisicho safi. Tunapaswa kutubu dhambi zote zilizo maishani mwetu (tukidhamiria kuziacha) na kuzikana shughuli zote za uovu (kwa mfano, kujihusisha na mambo ya kichawi) mambo ambayo yaweza kuzuia au kutatiza kuja kwake.

C.4. Jiachilie

Kujazwa hasa na Roho Mtakatifu maana yake ni kutawaliwa naye. Kama tunataka ku-jazwa kabisa hatuna budi kuachilia kila sehemu ya maisha yetu kwa Mungu.

C.5. Kiu

Angalia Yohana 7:37-39.

C.6. Omba

Angalia Mathayo 7:7 na Luka 11:11-13.

C.7. Tulia na Kupokea

Mbali na msaada huo ulio wa kawaida, hakuna njia inayoweza kutolewa kwamba ukiifu-ata hiyo ndiyo utaupokea ubatizo huu.

D. Nani Abatizaye, Wakati Gani, na Lipi Litokealo?

Watu wanaweza kubatizwa wawapo peke yao au wakati wa huduma kwa vikundi vidogo, au wanapokuwa sehemu ya kusanyiko la waumini katika tendo la kuabudu pindi Roho anapotembea kati yao. Yaweza kusaidia wanapokuwepo watu wanaotia moyo, wakion-goza na kutuombea japo si lazima iwe tu kwa njia hii. Wale wanaohudumu wanaweza kufanya huduma ya kuwekea mikono (huu ni mfumo wa Kimaandiko wa kupokezana Roho) lakini pia kwa hili si lazima iwe hivyo. Mkristo yeyote anaweza kuhudumu katika kuwawezesha wengine wapate ubatizo wa Roho Mtakatifu (Mdo 9:10,17) ilimradi tu wawe ni watu wakweli (Mdo 8:21). Si lazima watu hao wawe viongozi. Lakini wale wa-naohudumu ni mfano wa mfereji tu. Yesu ndiye pekee abatizaye, Yeye humwomba Baba atoe Roho Mtakatifu na kisha kumumimina juu yetu.

Kuna njia nyingi tofauti ambazo Roho Mtakatifu anazitumia kuwajia watu, na vile vile jinsi watu wanavyoitikia na kudhihirisha ujio wake (Yn 3:8). Huja kama upepo wenye nguvu na vilevile huja kama upepo mwanana au mtulivu, huja kama mkondo wa maji wenye nguvu na vilevile huja kama umande. Ukweli kwamba Roho Mtakatifu atujiapo, huwa

12

Page 21: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

kuna matokeo ya kiroho, kihisia, kiakili au hata ya kimwili, hautakiwi kutushangaza. Utu wetu ulio na mipaka katika ustahimilivu wake unakuwa umejazwa na Mungu asiye na kikomo! Lakini miitikio hutofautiana baina ya mtu na mtu; baadhi hucheka, wengine hu-lia; wengine huwa kimya, wengine hujidai hata kwa majivuno; wengine hushuhudia tendo la kuwa wenye furaha isiyo na kikomo, wengine hujawa amani, upendo au uhuru.

Lakini kwa namna fulani, tutajua kwamba tumeweza kuguswa na Mungu. Kwa hali hii, wakati tunaweza kuamini na kuwa na imani kwamba Mungu amesikia na kujibu maombi yetu ya kutaka atubatize katika Roho Mtakatifu. Tunapaswa kuangalia kwamba hatuingii katika mgogoro pindi tuonapo “hakuna chochote” kisicho cha kawaida kilichotutokea mara baada ya kuomba na kuamini. Daima huwa tunawatia moyo watu wavumilie katika kiu yao na kuomba hadi wanapofikia kupokea baraka wanayoisubiri. Wakati Roho Mtakatifu anapokuja na kutujaza, jambo linalotokea hatuwezi kukosa kulielewa. Ukweli ni kwamba litaeleweka wazi!

E. Kuna Nini Katika Kunena Kwa Lugha?

Vipawa mbalimbali vya kiroho huweza kutolewa kwa mwamini anapobatizwa katika Roho Mtakatifu na kwa kawaida vipawa vingi kati ya hivi hugunduliwa baadaye. Hata hivyo, watu mara nyingi huanza kwa kunena katika lugha (moja ya vipawa vya Roho) mara baada ya kubatizwa (Mdo 2:4, 10:44-46, 19:6). Jambo fulani lahitajika kusemwa juu ya kipawa hiki katika somo lolote lihusulo ubatizo wa Roho Mtakatifu.

Vipawa vyote au karama za kiroho, vinapotumiwa na mtu fulani, vimetolewa kwa ajili ya kuuimarisha mwili wa Kristo. Kunena kwa lugha kwa sehemu ni tofauti na vipawa au karama nyingine: wakati kipawa hiki kina matumizi ya wazi na faida zake, yapo pia ma-tumizi binafsi na faida binafsi kwa mtu mwenye kukitumia kipawa au karama hii. Ni jambo lisilowezekana kuikuza baraka ya matumizi “binafsi” ya kunena kwa lugha. Inam-jenga muumini (1 Kor 14:2; 14:4) na kuinua kiwango cha mtu kuabudu (Yn 4:24) na huduma yake ya maombezi (Rum 8:26).

Maandiko hayaonyeshi (kama wengine wanavyodai) kwamba watu walinena kwa lugha kila mara walipobatizwa katika Roho. Kwa hali hii sisi hatuwezi kusisitiza (kama vile wengine walivyofanya) kwamba watu sharti wanene katika lugha mpya ikiwa kweli wamebatizwa katika Roho au, kinyume chake, kwamba hawajabatizwa katika Roho ikiwa wao hao hawajanena kwa lugha. Maandiko yanasema wazi kwamba si kila Mkristo sharti anene kwa lugha au atanena kwa lugha. Lakini twaamini kwamba kila muumini aweza kunena kwa lugha (na kwa hali hii kipawa au karama ya kunena kwa lugha iko tofauti na vipawa au karama nyingine za kiroho) na kwa sababu zifuatazo:

Vipawa au karama nyingine hulijenga Kanisa na kwa hali hii si kila muumini atatakiwa awe nazo ili aweze kufaidika nazo. Matumizi binafsi ya kipawa cha kunena kwa lugha humfaidisha mwenye kunena na kwa hiyo kila mtu binafsi yafaa awe nacho kwa Faida yake binafsi. (Hatufikirii kwamba Mungu anaweza kutaka baadhi ya waumini wawe na kipawa hiki, na wengine wasiwe nacho.)

Paulo alitamani kwamba wote wangeweza kunena kwa lugha (1 Kor 14:5). Yeye asin-geweza kulisema hili kama hilo lingekuwa jambo lisilowezekana.

Sisi hatujawahi kumjua mtu yeyote aliyekitafuta kipawa hiki, na hatimaye hakukipata. Ikiwa kama ni kweli kwamba kila muumini aweza kunena kwa lugha, na kama faida ipa-tikanayo kutokana na matumizi ya kipawa hiki ni kama tulivyoieleza, basi, kama ilivyo kwa kipawa au karama yenyewe, laweza kuwa jambo la kijinga kabisa kuamua tusikita-

13

Page 22: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

fute kipawa au karama hii. Mtazamo wetu haupaswi kuwa, “Hivi, ni lazima mimi ninene kwa lugha?”, bali, “Ikiwa Mungu anacho kipawa anachotaka kunipa, mimi nakitaka!” Hivyo muombe Mungu akupe kipawa hiki unapomwomba akubatize katika Roho Mtaka-tifu. Mungu hawezi kulazimisha usemi huu kupitia midomo yako iliyofungwa na isiyo-jishughulisha! Kunena kwa lugha ni ushirikiano unaotokana na uhusiano kati ya Roho na muumini. Unanena kwa lugha kadiri Roho anavyokuwezesha (Mdo 2:4). Kwa hiyo via-chilie viungo vyako vinavyotumika kwa kauli Mungu avitumie. Anza kumwomba katika lugha yako ya asili na ufanye uamuzi wakati fulani wa kuacha kuomba katika lugha yako ya asili ili unene ukitumia maneno mapya ambayo Roho atakupatia. Baadhi ya watu huingia katika lugha yenye maneno mfululizo wakati wengine wakianza kwa maneno yanayowawia magumu mwanzoni nao huwabidi wawe wavumilivu. Katika hali zote ina-tupasa tuendelee na jitihada, na tunakua katika kipawa au karama hii kadiri muda un-avyoendelea. Uzuri wake ni kwamba tunakuwa tumeanza safari itakayoyafanya maisha yetu yote yawe ya baraka.

E.1. Ninawezaje Kudumu Nikiwa Nimejazwa Roho?

Hali ya kubatizwa katika Roho Mtakatifu ni mwanzo tu wa kuwa na maisha yaliyojaa Roho. Kitenzi (verb) cha Kiyunani alichokitumia Paulo katika kusema “mjazwe Roho Mtakatifu” (Efe 5:18) kina maana ya “endeleeni kuwa hali mmejazwa.” Hii ina maana kwamba kujazwa na Roho Mtakatifu ni zoezi linaloendelea, na hasa ni jambo tunalo-takiwa kulitafuta kila siku katika maisha yetu yote.

Roho Mtakatifu ni nafsi ya Mungu tunayoishi nayo katika uhusiano ulio wa ndani sana. Hali ya kutotii uongozi wake na mambo yale anayotuambia itauvunja uhusiano huo na sisi kubaki “tukitembea peke yetu.” Uhusiano huu uliovunjika sharti urejezwe kwa njia ya toba na azma mpya ya kuishi maisha yenye utii kwake. Tunapaswa kutembea hatua kwa hatua na Roho Mtakatifu (Gal 5:25) na wala hatupaswi kumhuzunisha Roho Mtakatifu (Efe 4:30). Pia hali mpya zinazojitokeza na kuingia katika huduma kutahitaji ujazo/upako mpya. Kuendelea kujazwa huku kunafanyika katika njia mbili kuu, nazo ni kama ifua-tavyo:

Kuna Kujazwa upya kunakotokea kidogo kidogo bila wenyewe kujua kunavyofanyika, na kule kutokanako na kuwa na muda pamoja na Mungu (mtu awapo peke yake au katika ushirika wa ibada pamoja na wengine) na katika kutembea hatua kwa hatua na Roho ukimpa nafasi atawale katika kila hatua (yamkini Paulo alifikiria kujazwa kwa jinsi hii ali-poandika Efe 5:17-20).

Kujazwa kunakotokea katika vipindi fulani kunaweza kulinganishwa na ilivyokutokea wakati ulipobatizwa katika Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza. Kusisitiza kwamba hilo laweza tu kutokea mara moja ni kupingana na Maandiko (Mdo 2:4; 4:31) na kujizuilia baraka zaidi na kuwezeshwa zaidi pasipo sababu yoyote. Kupitia njia hiyo ya kidogo ki-dogo, inayotokea bila sisi kuwa na habari na huko kujazwa kunakokuwa kama kuzam-ishwa, tunatakiwa kuendelea kutafuta kujazwa “Roho Mtakatifu” siku zote za maisha yetu ili tuweze kuyapata na kuyafanya yote Mungu ayatakayo kwa ajili ya maisha yetu. Maisha ya kuwa tumejazwa Roho (kutawaliwa na Roho) ndiyo ukamilifu na ufunguo wa maisha makamilifu ya Kikristo.

F. Mnyororo wa Ubatizo Katika Roho Mtakatifu.

Lk 24:49Mat 3:11

14

Page 23: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Mdo 2:1-13Mdo 2:39Lk 11:13Yn 7:38Efe 4:30Gal 5:25Efe 5:18

15

Page 24: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Nne: Kiini cha Ubaba wa Mungu

Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. (1 Yoh 3:1)

A. Utangulizi

Ubaba wa Mungu ni ukweli wa Kibiblia wa msingi ulio muhimu kwetu kuuelewa ili tujue jinsi ya kumuitikia Mungu, aliye Baba yetu wa mbinguni. ‘Agape’ (upendo wa Mungu uo-nyeshwao katika kujitoa kwake) katika maneno ya Leon van Daele, “ni nguvu moja yenye uwezo kuliko nguvu zote ulimwenguni”. Ni upendo huu unaousukuma moyo wa Mungu utuelekee sisi. Upendo wa Mungu ni wa tofauti kabisa na kila upendo wa kib-inadamu ambao tumewahi kuujua: hautolewi kwa masharti yoyote. Ni upendo ambao sisi wanadamu tusingeustahili, na ni upendo ulio mkamilifu kabisa. Hatutakiwi tufanye kazi ili kuupokea upendo huu ulio mkuu. Hili ni jambo ambalo sisi kama wanadamu, hu-tuwia vigumu kulielewa au kulipokea.”

Tabia ya upendo imeelezewa katika 1 Kor 13:4-7. Wanazuoni wakuu wa Biblia wana-kubaliana kwamba, katika sehemu hii ya Maandiko si upendo wa kibinadamu unaoe-lezewa bali upendo wa Mungu. Ni jambo lisilowezekana kwetu kuwa na upendo wa jinsi hii – ni upendo tunaoweza kuupokea tu kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ni upendo unaoe-lezea upendo wa kimungu ulio mkamilifu: upendo alio nao Baba yetu wa mbinguni kutu-elekea sisi, watoto wake.

Mungu aliuonyesha upendo wake mkuu usio kifani kwa kuchagua Mwanaye pekee afe, ili sisi kama wanadamu tuliokuwa katika laana ya anguko tuweze kupata faida ya kumjua Yeye kama Baba yetu wa mbinguni, na kuishi milele pamoja naye (Mat 11:27).

B. Kwa Nini Mungu Awe na Moyo wa Ubaba?

Kuna sababu gani tutumie sura nzima ya kitabu hiki kuangalia Moyo wa Ubaba wa Mungu? Ni kwa sababu Mungu ni mwenye nafsi. Anaweza kuingia katika mahusiano binafsi na watu, ambayo kati ya hayo, uhusiano ulio rahisi sisi kuuelewa kama wa-nadamu ni ule wa “ubaba.” Yesu aliwafundisha wale waliokuwa wameingia katika ufalme wa Mungu wamchukulie Mungu kama Baba yao. Aliwafundisha wanafunzi wake kumwita Mungu “Baba yetu wa mbinguni” (Mat 6:9). Mafundisho yote ya Yesu yanajenga uhusi-ano ulio wa ndani sana, wa karibu sana na Baba, na uliojaa huruma sana. Tunapaswa kuelewa kwamba Mungu kama Baba ni Baba mkamilifu; anatamani kwa hamu kubwa kuona kwamba tunamtegemea kwa ajili ya:

• Matunzo na mahitaji hata yale yaliyo ya kawaida kama vile chakula na mavazi (Mat 6:25-34).

• Ulinzi (Mat 10:28-31).

• Kupewa vitu vyote vilivyo vizuri (Mat 7:7-11).

Si watu wote tuliobahatika kuwa na akina baba wanaomcha Mungu. Wengi wa baba zetu wametufadhaisha kwa njia nyingi na mara nyingi, na kamwe hawako karibu na ukamilifu. Dhambi imeharibu mahusiano mengi ya mtoto na baba kiasi kwamba mahusi-

16

Page 25: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

ano ya baba kwa mtoto yanabaki kuwepo katika macho ya nje tu, lakini katika matukio mengi, uhusiano huu unavunjika kwa mfano kutokana na uzinzi, talaka, ulevi, ud-halilishaji wa kijinsia au tabia za kuwapuuza.

Katika kitabu cha Mwanzo tunaona kwamba Mungu aliwaumba wote yaani mwanaume na mwanamke kwa mfano wake, na hivyo wote wawili ni sehemu ya asili yake na tabia zake. Ili familia iweze kupokea baraka za ufunuo kamili wa upendo wa Mungu, baba na mama wanahitajika wote wawili kwa pamoja, kwa sababu wawili hao kwa pamoja wanawakilisha kipekee sura na tabia ya Mungu. Mahali palipo na familia yenye mzazi mmoja tu ni jambo lenye maana kujua kwamba Mungu aweza kufidia pengo la upendo linalotokana na kukosekana kwa mzazi mmoja.

Kwa kuwa kuna hali inayoendelea ya kukabiliwa na shida ya mababa wenye mapun-gufu, ufahamu wetu kuhusu baba anavyotakiwa awe unakuwa na mapungufu ambayo sisi kwa kujua au pasipokujua tunayaingiza katika uhusiano wetu na Mungu.

Ni katika hatua hii tunapotakiwa kufikiria mawazo yanayoingia akilini mwetu tunaposikia neno ‘baba.’ Je ni wazo la mtu mwenye upendo, mpole, mchangamfu, mwenye kusa-mehe, kulinda, kutoa mahitaji, na Baba anayekuwa kila mahali anayefunuliwa na Maan-diko, au tumeruhusu hali ya ubaba wetu wa kibinadamu na wa wale walio na mamlaka juu yetu uwe kama pazia linalotuzuia tusimjue Mungu kama alivyo Baba yetu?

Angalia hali hizi kama picha za mambo yanayotokea mbele yako:

• Mvulana mdogo anatumia masaa yote ya mchana akichonga kitu anachoamini kwamba ni farasi kutoka katika kipande cha ubao. Mwisho wa siku anamsubiri baba yake aje nyumbani ili amwonyeshe kazi yake ya sanaa. Baba aliyechoka hatimaye anaingia ndani, akiwa amelemewa na mambo mengi kiasi hawezi hata kuinua jicho amwangalia mwanaye pale alipokaa.

• Kijana anayeinukia mwenye umri wa miaka kumi na kitu hivi, anatoka usiku aende kutembea na rafiki zake, na kabla hajatoka anasimama mbele ya baba yake akisubiri kwa hamu, kwamba baba ataonyesha kuwa na hamasa katika yale kijana anayojihusisha nayo. Anachokifanya baba ni kuingiza mikono ndani ya po-chi yake na kumwuliza ni fedha kiasi gani anazohitaji.

• Baba wa mtoto anayetambaa anamuweka mtoto juu, sehemu ya kuwekea cha-kula kilicho tayari kuliwa ndani ya chumba cha jiko. Kisha anamwambia ajirushe naye atamdaka. Huyo mtoto mchanga anapomwamini baba na kujirusha, baba anamgeuzia mgongo na kumwacha aanguke chini. Hili jambo linatokea mara tatu hivi, na mwishowe baba anamwambia mtoto maana ya zoezi hilo: “Mwanangu, kamwe usimwamini mtu yeyote!”

Mifano hii inatupa picha ya mzazi asiye na muda, mzazi asiyejali na mzazi ambaye hawezi kuaminiwa.

Tunahitajika kumwomba Mungu atusaidie kuweka pembeni mawazo potofu tuliyonayo, pamoja na uzoefu tulioupata katika uhusiano wetu na baba zetu wa kimwili, ili tuweze kuhusiana naye kama alivyokusudia. Katika maneno ya Floyd McClung, “Kamwe, wala usichukizwe na kushindwa kwa wazazi wako wa kimwili. Wao nao ni watoto waliokua na hata wakapata watoto. Badala yake, furahia upendo wa Baba Mungu ulio wa ajabu.”

Katika Mungu tunaye Baba aliye mkamilifu. Tunaweza kumtumainia bila kikomo tukijua kwamba kamwe hawezi kubadilika. Tabia na sifa zake zinabaki kama zilivyo na kwake hakuna kigeugeu (Mat 5:43-45; 7:9-11; Yak 1:17). Tofauti na akina baba waliotajwa ka-tika matukio ya hapo juu, Baba yetu wa mbinguni daima ana muda kwa ajili yetu, ana-

17

Page 26: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

tufurahia, akitamani kwamba tutamjia si wenye mikono iliyokunjamana, bali iliyo wazi na anatamani kwamba sisi tutaweza kuweka tumaini letu lote kwake. Maandiko yana hali inayoendelea ya kutufasiria upendo wa Mungu uliojaa hamasa na wema kuwaelekea wanawe. 2 Kor 6:18 inaeleza, “Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.”

C. Nini Kinachotusukuma Kumtumikia Mungu?

Hofu? Kujipatia faida za binafsi? Hamu ya kutaka mafanikio? Hitaji la kuwa mwenye ku-kubalika kwa wengine? Hakika, kama misukumo ni hii basi hatumjui Mungu!

Yeye ni Baba yetu na sisi ni watoto wake. Yeye alitupenda kwanza (1 Yoh 4:19) na kama namna ya kuitikia matunzo na ulinzi wa kimungu anaotupatia, tunahitajika kumtii na kumtumikia. 1 Yohana 5:3a yasema, “maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake.”

Ikiwa kama tunamjua Mungu wetu kama Maandiko yanavyomfunua, na pia upendo al-ionao kwa ajili yetu sisi watoto wake wa kike na wa kiume, hapo kumtumikia halitakuwa jambo linalotokea lenyewe tu, bali litakuwa jambo litakaloonekana kuwa la faida na heshima ya kipekee kwetu. Fikiria jinsi mtoto mdogo anavyomwangalia baba yake kwa mshangao wa ajabu, anavyomtetea na kujivuna kwa ajili ya baba yake mbele ya watoto wengine rafiki zake: “Baba yangu ni mkubwa zaidi kuliko baba yako,” “Baba yangu ana akili kuliko baba yako,” na hivyo mabishano yao huendelea.

Tunahitajika kuwa kama watoto: tunahitajika kumpenda na kumtumikia Baba yetu wa mbinguni kwa sababu tu Yeye alitupenda kwanza. Tunahitajika kuzitafuta nafasi za ku-weza kujivunia sifa zake, na kuwaambia wengine habari za upendo wetu kwake.

D. Kuupokea Upendo Alionao Mungu Kwetu

Tunaishi katika ulimwengu unaoenda kwa kubahatisha. Jamii inayowaza “Je, ikiwa … halafu …” ambamo kukubaliwa kwa mtu kunatokana na yale anayoyafanya na hivyo ku-wepo kwa upendo wenye masharti. Watoto wengi wanafikiria kwamba wanaweza tu ku-pokea upendo wa wazazi wao pale tu wanapopata matokeo mazuri ya mitihani shuleni, ikiwa kama watafanikiwa katika michezo, au kama watafanya kazi za nyumbani kwa bidii sana. Ufahamu wao juu ya upendo ni kwamba upendo hupatikana kwa masharti: ikiwa kama utafanya vizuri, basi utapendwa na kukubaliwa.

Upendo wa Mungu wetu wa ‘Agape’ ni upendo ulio tofauti kabisa—Mungu ni upendo (1 Yoh 4:16). Kwa sababu Yeye ni pendo, basi kumbe asili yake mwenyewe hailazimishi kwamba sisi tufanye chochote ili kumfanya atupende. Anachokitaka tu kwetu ni kwamba tukae katika uwepo wake na kulipokea pendo lake. Kama ilivyo kwa uhusiano wowote wa upendo/mapenzi, kunahitajika hali ya kutoa kwa upande mmoja na kupokea kwa upande mwingine.

Je, mwitikio wako kwa Mungu ni upi anapokuambia kwamba anakupenda? Je, kwa uta-ratibu kabisa unaupokea upendo wake au unajishughulisha kwa kutafuta njia ambazo unaona kwa hizo utaweza kustahili kukubaliwa naye? 1Yohana 3:1a inatumia maneno haya, “Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo.”

18

Page 27: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Endapo labda wewe ulifadhaishwa na baba yako wa kimwili, basi jiingize kila siku katika Maandiko yanayoonyesha sura ya sifa za Baba yako wa mbinguni—kwa kuwa ni kweli pekee itakayokuweka huru (Yn 8:32).

E. Baba Yako Amefunuliwa

Baba yako halisi anasubiri kwa hamu aweze kujifunua kwako; Yeye anachokitamani ni kukusikia wewe ukimwomba afanye hivyo.

E.1. Baba Anayetufanya Tuwe Wanawe

Efe 1:4b-5a Katika pendo … alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo.

Efe 1:11a Na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye.

Yn 1:12-13 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

Rum 8:15a Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa aletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana.

2 Kor 6:18 a Mimi nitakuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa wanangu, waume kwa wake,

E.2. Baba wa Yatima na Mtetezi wa Yatima

Zab 68:5a-b Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane

Kum 10:18a Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki.

Zab 146:9a Bwana ….huwategemeza yatima na mjane

Zab 68:6a Mungu (huwakalisha wapweke nyumbani) huwapa fukara makao ya kudumu.

E.3. Baba Atunzaye Agano

Isa 54:10 Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema Bwana akurehemuye..

Isa 61:8b-9 Nitaagana nao agano la milele. Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika kabila za watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana.

E.4. Baba Atoaye Thawabu

Ebr 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwen-deaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.

19

Page 28: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Mat 6:3-4 Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Mat 10:41-42 Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye am-pokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki. Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.

Mat 5:12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Efe 6:7-8 (Mkitenda) kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu; mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru

E.5. Baba Ajibuye Maombi

Lk 11:9-13 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bish-eni, nanyi mtafunguliwa. Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafu-taye huona; naye abishaye atafunguliwa. Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, ba-dala ya samaki atampa nyoka? Au akimwomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wam-wombao?

Yak 4:2d Mwatamani, wala hamna kitu

Yn 14:13-14 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.

Yn 16:23-24 Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa ham-kuomba neno kwa jina langu

E.6. Baba Mtoaji

Mat 6:25-33 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? ….kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Zab 37:4 Uitafute furaha yako kwa Mwenyezi-Mungu, naye atakujalia unayotamani moyoni.

Zab 34:9 -10 Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, yaani, wamchao hawahitaji kitu. Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; Bali wamtafutao Bwana hawatahi-taji kitu cho chote kilicho chema.

Mat 7:11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wam-wombao?

20

Page 29: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

E.7. Baba Anayesamehe na Kukomboa

1 Yoh 1:9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondo-lee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

Lk 15:21-24 Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. Lakini baba aliwaambia wa-tumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kido-leni, na viatu miguuni; mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye ame-fufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.

Mat 6:14 “Maana mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni ata-wasamehe nyinyi pia.

Sala aliyoiomba Yesu pale msalabani ilionyesha jinsi msamaha wa Mungu ulivyo!

E.8. Baba Aadhibuye (Afundishaye Nidhamu)

Ebr 12:7-11 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.

Mith 3:11-12 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kuru-diwa naye. Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.

Nidhamu afundishayo Mungu kama Baba huzaa haki, amani na furaha. Zaburi 66:18 huuonyesha ukimya wa Mungu kama fundisho lake la nidhamu. Endapo utakuwa hum-sikii Mungu, jiulize mwenyewe: Je ulitii kufanya alichokuambia huko nyuma?

E.9. Baba Mwenye Upendo

Yn 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

1 Yn 3:1 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

Yn 15:13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

1 Yoh 3:6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakum-wona yeye, wala hakumtambua.

21

Page 30: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Rum 8:35-39 Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba,

“Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa,Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.”

Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliy-opo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala ya-liyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.

Zab 33:18-19 Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake.Yeye huwaponya nafsi zao na mauti, na kuwahuisha wakati wa njaa.

Sisi ni “mboni ya jicho lake” (Kum 32:10, Zab 17:8, Zek 2:8), watu wake wateule (Kut 19:5). Dunia itakapofikia mwisho wake wana wake wa kike na wa kiume watakuwa ni urithi wake: bibi arusi (Ufu 21:9-10) kwa ajili ya Mwanaye milele.

Angalia pia Lk 15:11-32 kwa ajili ya habari ya mwana mpotevu.

F. Mnyororo: Moyo wa Ubaba wa Mungu

Ukitumia Maandiko yaliyoonyeshwa hapo juu, chagua yale yaliyougusa sana moyo wako na kuyatumia kujitengenezea mnyororo wako mwenyewe.

22

Page 31: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Tano: Tumaini Letu

Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alitu-zaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio ta-yari kufunuliwa wakati wa mwisho(1 Pet. 1:3-5)

A. Utangulizi

Wokovu wetu ni tendo la ajabu zaidi na lenye umuhimu mkubwa kuliko yote yatokeayo maishani mwetu! Tunaokolewa kutoka katika dhambi na maisha yaliyotengwa na Mungu na kuingizwa katika maisha mapya yenye uhusiano na kusudi pamoja na Mungu – maisha ambayo tayari Mungu aliyaandaa tangu huko mwanzo kwa ajili yetu. Sura hii in-aelezea yale yanayotusubiri katika siku zijazo.

B. Uelekeo Wetu – Makazi ya Milele.

Mbinguni Ndiko Nyumbani Kwetu

Biblia inatuambia kwamba Ufalme wa Mbinguni ni mahali Mungu aishipo na kutawala na kwamba sisi ni raia wa ufalme huo. Bwana wetu Yesu Kristo ni mtawala wa viumbe vy-ote na amepewa mamlaka juu ya kila kiumbe. Ukweli huu umeelezwa katika Barua kwa Waefeso 1:20-23 kama ifuatavyo:

“….Akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwen-guni humu tu, bali katika ule ujao pia; akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”

Uhusiano wetu na Yesu ni wa ndani sana kiasi kwamba tunaelezewa kuwa “ndani ya Kristo” (Angalia Efe 1:3-13 na Kol 3:3.) Kwa sasa tunaishi kama “wageni” hapa duniani lakini wenyeji wetu ni huko Mbinguni (Fil 3:20).

Yesu aliwaahidi wanafunzi wake kwamba angerudi na kuwachukua ili awapeleke hadi katika mahali ambapo amewaandalia. Katika Yohana 14:2-3 Yesu anasema, “Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda ku-waandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakar-ibishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.”

B.2. Tunamuona Uso Kwa Uso

23

Page 32: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Lengo letu la kuwa ndani ya Kristo ni kuweza kumjua Bwana kwa namna ambayo kuna-kuwa hakuna kitu kinachotutenga naye hadi itakapofika siku tutakapomwona Bwana uso kwa uso. Katika 1 Wakorintho 13:12 tunasoma, “Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.” Katika siku zetu za baadaye tutamjua Yeye na kumfurahia milele.

B.3. Kunatokea Nini Wakati wa Kifo?

Wakati muumini anapokufa, mwili wake wa kidunia unakoma kufanya kazi zake pale nafsi yake itokapo, na wakati huo huo nafsi ya mtu huyo inakuwa pamoja na Mungu (2 Kor 5:4-8). Kifo si maangamivu yanayotowesha uhai au kikomo cha maisha, bali “kuishi” milele katika uwepo wa Mungu (Mat 22:31-32). Ni wazi kabisa, kwamba kuwepo katika uwepo wa Mungu ni jambo linalofaa kutamanika zaidi kuliko kuishi katika ulimwengu huu ulioharibika kutokana na dhambi. “Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi.” (Fil 1:21). Maisha tunayoishi katika uwepo wa Mungu ni tofauti sana na maisha tuishiyo hapa duniani. Biblia huzungumzia Mbinguni kama mahali ambako kutakuwa hakuna usiku tena, hakuna kulia, machozi au huzuni (Ufu 22:3). Huko tutamwona Mungu uso kwa uso na huko tutayajua majibu ya maswali yote tuliyokuwa nayo wakati tukiishi duni-ani (1 Kor 13:12). Japo mbinguni ni tofauti kabisa na duniani kuna pia hali ya kuendelea kwa maisha kunakoanzia katika maisha yetu duniani. Soma 1 Wakorintho 15 ili uweze kuiona sura nzima ya jambo hilo.

Kanuni ya “mbegu” inayoonyeshwa katika 1 Wakorintho 15:35-58 inatufundisha juu ya asili ya kile kitokeacho baada ya kifo.

Kuna hali inayoendelea kati ya kile kinachopandwa na kufa na kile kinachochipuka. Nguvu ya uhai uliokuwa ndani ya mbegu ya kwanza iliyopandwa inakuwamo bado katika mmea unaochipuka ukitokea katika mbegu iliyopandwa.

Mabadiliko yanayoweza kuonekana hutokea katika mmea unaokua ukitokea katika mbegu iliyopandwa, mabadiliko yanayoonekana katika hali ya muundo na sura yake. Asili ya mbegu iliyopandwa huamua juu ya asili ya mmea utakaokua ukitokea katika mbegu hiyo.

Mfano huu una maana kwamba mtu anayezikwa katika hali ya kuwa “mpotevu” ata-fufuka katika hali ya kuwa mpotevu kwa Mungu - mtu “aliyekombolewa” atafufuka ili aishi katika uwepo wa Mungu.

B.4. Ufufuko wa Wafu.

Ukweli wa kibiblia juu ya “Ufufuko wa Wafu” ni wa tano kati ya “mafundisho ya awali/ya msingi” katika Waebrania 6:1-2, na ukweli huu unatakiwa uwe sehemu ya msingi katika maisha ya waumini.

Ufufuko wa Yesu ni wenye maana sana, na unamtenga Yesu kutoka kwa makristo na manabii wote wa uongo kwa sababu hakuna yeyote kati yao aliyefufuliwa kutoka katika wafu (Rum 1:4). Tunaona wazi kabisa katika 1 Wakorintho 15:20-23 kwamba Yesu ni mwanzilishi na mtangulizi wa waumini wote, ambao nao watafufuliwa kama alivyofufuka Yeye.

Wakati wa ufufuo miili yetu itabadilishwa na kufufuliwa kama miili isiyoweza tena kuhar-ibika (1 Kor 15:51-53). Mungu atatengeneza kutoka katika mabaki ya miili hii na kutu-fanyia miili mipya ya utukufu.

24

Page 33: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kutakuwa na ufufuo kwa wote, wema na waovu (Mdo 24:14-16; 1 Pet 1:3-5). Yohana 5:28-29 inasema, "Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”

Jambo hili ni lenye umuhimu mkubwa kwa ajili ya imani yetu, kwa kuwa linatupa mtazamo wa milele kwa ajili ya maisha – TUMAINI LETU!

C. Mnyororo wa Ufufuko

Ebr 6:1-2Yn 5:28-291 Kor 15:20-23Yn 11:25-26Fil 1:211 Kor 15:35-581 The 4:13-18Ufu 20:1-6Ufu 20:11-15

D. Vipi Kuhusu Hukumu, Thawabu na Jehanamu?

Tumejifunza katika sura iliyotangulia juu ya Moyo wa Ubaba wa Mungu na kujua kwamba Yeye ni mwenye neema na rehema, si mwepesi wa hasira na ni mwenye utajiri wa upendo. (Zab 145:8). Tunaona katika Waebrania 12: 23b kwamba, mnasimama mbele ya Mungu aliye “mwamuzi wa watu wote,” na kwamba Mungu ndiye mwenye Mamlaka iliyo kuu juu ya VYOTE na WOTE – mbinguni, duniani, juu ya malaika na wa-nadamu (Zab 145:17).

Wote aliowaumba watatoa hesabu ya vitendo vyao na kuhukumiwa kulingana na matendo yao. Warumi 3:23 yatuambia kwamba wote sisi tumetenda dhambi. Wale am-bao hawakupata kusikia juu ya sheria watahukumiwa pasipo ile sheria wakati wale wali-otenda dhambi wakiwa chini ya sheria watahukumiwa kwa ile sheria (Rum 2:12). Tuna-soma Warumi 3:19, “Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu”

Kwa sababu tumo “ndani ya Kristo”, tayari tumekwisha kutangazwa kuwa “wasio na ha-tia” na tuko huru na adhabu ya kifo, kwa kuwa Kristo amehukumiwa kuwa “mwenye ha-tia” badala yetu alipokufa juu ya msalaba kwa ajili yetu (Kol 1:21-23; Isa 43:25).

Hii haina maana kwamba hatutatoa hesabu kwa ajili ya maisha yetu mbele za Mungu. Warumi 14:10b-13 inasomeka hivi, “Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu..” Waumini watahukumiwa na thawabu zitatolewa baada ya “kazi” zetu kuwa zi-mepimwa (1 Kor 3:13-15). Kupimwa huku kutafanyika si kwa ajili ya kuamua hatima ya wokovu wetu bali thawabu zetu (Angalia pia Mat 25:14-30).

Wote wasioamini, mpinga kristo na malaika walioasi wote watahukumiwa katika hukumu ile ya mwisho (Ufu 20:11-15). Wale ambao majina yao hayataonekana katika kitabu cha uzima watatupwa katika ziwa la moto. (Angalia pia Mat 25:31-46).

25

Page 34: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

E. Mnyororo wa Hukumu ya Milele

Ebr 6:1-2Ebr 12:22-24Yn 5:22-301 Kor 3:11-15Mat 25:14- 46Ufu 20:11-15

F. Je, Hizi ni “Siku Za Mwisho” ?

Sisi kweli tunaishi katika siku za kusisimua sana! Yesu alisema kwamba tuonapo dalili fulani tunajua kuwa mwisho unakaribia. Baadhi ya dalili hizo ni: mapinduzi, vita na tetesi za vita, matetemeko ya ardhi, njaa, milipuko ya maradhi, makristo wa uongo, manabii wa uongo, ishara za uongo, wapinga Kristo, Mpinga Kristo, uasi, dhuluma na mateso, ushuhuda mkuu (Uamsho?), Injili kuhubiriwa kwa mataifa yote, mtikisiko wa nguvu za anga (ishara kuu mbinguni), wimbi la maanguko hata kati ya Wakristo waliosimama imara. (Angalia Mat 24, Mk 13, Lk 21, 1 Tim 4, 2 The 2).

Yesu aliahidi kwamba angerudi duniani kuwakusanya waumini wote na kwamba kun-gekuwa na matukio ambayo yangetangulia mbele ya tukio hilo, matukio ambayo tuli-takiwa kuyatarajia.

Matukio hayo yanaonekana kama ifuatavyo japo mfululizo huu hauna uhusiano na vile yanavyoweza kutukia yakifuatana:

Unyakuo, Miaka Elfu Moja, Kurudi kwa Kristo Mara ya Pili, Mbingu Mpya na Nchi Mpya Dhiki Kuu, Harusi ya Mwanakondoo, kufufuliwa, Hukumu Mbele ya Kiti Kikuu cha Enzi Cheupe, Vita ya Armagedoni.

Sisi tunaishi katika kipindi kati ya kuja kwa Kristo kwa mara ya kwanza (Advent) na kuja kwa Kristo kwa mara ya pili (Parousia). Yesu amefufuliwa na kuketishwa mkono wa kuume wa Mungu na amepewa mamlaka yote juu ya wakati huu na ujao (Efe 1:20-23).

Hatujui ni wakati gani atakaporudi tena lakini tunatakiwa tuishi katika matarajio kwamba inawezekana ikawa ni leo (2 Pet 3:8-10). Maisha yetu hayatakiwi kunaswa na kusongwa na shughuli za kawaida za ulimwengu huu. Tunatakiwa kuishi kama wageni wanaopita tu (1 Pet 2:11-12).

Petro anaonya katika barua yake ya pili akisema, “Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vita-fumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake. Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo,fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.” (2 Pet 3:11-14).

26

Page 35: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

27

Page 36: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Sita: Ibada

Msifuni kwa mvumo wa baragumu;Msifuni kwa kinanda na kinubi;Msifuni kwa matari na kuchezaMsifuni kwa zeze na filimbi; Msifuni kwa matoazi yaliayo;Msifuni kwa matoazi yavumayo sana. (Zab 150:3-5)

Neno la Mungu linatuhimiza kuishi maisha yetu yote kama tendo la ibada (Rum 12:1). Kusudi la sura hii ni kufundisha baadhi ya kanuni zilizo za muhimu juu ya ibada ya kibib-lia pamoja na muziki na nyimbo, mambo yanayomchochea msomaji aingie katika uhusi-ano wa kina zaidi na Baba. Kwa walio wengi, eneo la ibada linatawaliwa na matakwa yao binafsi na pia pale wanapojisikia vizuri, lakini ni kusudi letu sisi kama wazee kuu-fanya ukweli wa Maandiko uumbe umbo hili la uhusiano pamoja na Baba.

A. Moyo wa Ibada

“Nitakuletea kilicho zaidi ya wimboKwa kuwa wimbo peke yake si kile unachokitamani.Wewe unapeleleza hadi undani wa kina cha mwisho,

Jicho lako linapenya kuonekana kwa mambo,Wewe unaangalia undani wote wa moyo wangu.

“Ninarudi katika kiini cha kina cha ibada,Kwa kuwa yote inakuhusu wewe,

Yote inakuhusu wewe, Yesu.Ninasikitika, Bwana, kwa vitu ambavyo nimeifanya ibada iwe,

Kwa kuwa yote inakuhusu wewe, Yesu!”(Matt Redman na Martin Smith)

Ibada haiwezi kukamilika katika wimbo tu, wala haiwezi kupunguzwa na kufanywa iwe maandamano yanayoongozwa na muziki. Hapana, ibada ni jambo linaloyazidi hayo yote kwa mbali. Mapigo ya moyo wa ibada ni mtiririko halisi wa uhusiano wetu na Baba. Mwanadamu angependa kuiwekea vitambulisho na pia kuipangilia, lakini vielelezo vya nje peke yake havielezei ukamilifu wa ibada kama Mungu alivyoikusudia iwe. Katika uhalisi wake, ni kielelezo cha upendo wetu unaowaka ukiitikia upendo mkubwa alionao kwetu, ni hali yetu ya kumgundua pale anapofunua maajabu yake kwetu. Ibada ni tendo la uhusiano. Basi ‘tusileweshwe’ na vitambulisho, badala yake ‘tulewe’ upendo wa Bwana wetu. Tukumbuke kwamba tunampenda na kumwitikia kwa kumwabudu kwa sa-babu “Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.” (1 Yoh 4:19). Sasa tutaji-funza kuona baadhi ya vielelezo vya ibada tunavyovikuta katika Agano la Kale na Jipya.

B. Vielelezo vya Ibada Katika Agano la Kale

28

Page 37: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Yapo maneno kadhaa ya Kiebrania yanayoonekana katika Agano la Kale ambayo yote yametafsiriwa kwa neno la Kiingereza linalotafsiriwa kwa Kiswahili chetu na neno ‘sifa’. Maneno yenyewe ni haya yafuatayo: “barak”, “Yadah”, “towdah”, “shabach”, “zamar”, “halal”, na “tehillah”. Basi na tuyachunguze maneno haya ili tuweze kupata uelewa mpana wa maana ya ibada kibiblia. Utaona jinsi maana ya maneno haya inavyojimimina yenyewe ndani ya Agano Jipya.

B.1. Barak (Zaburi 96:2)

“Kubariki, kulala kifudifudi au kupiga magoti kama tendo la kusujudu au kuonyesha up-endo mkubwa mno.”

“Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, nitaingia nyumbani mwako; na kusujudu kwa kicho,nikilielekea hekalu lako takatifu.” (Zab 5:7) Hii inaonyesha mfano wa ajabu sana wa jinsi ambavyo Daudi, mtu aliyeweka mfano wa ibada katika Biblia, angeingia ndani ya nyumba ya Bwana na kusujudu akionyesha hali ya kumcha Mfalme wake. Mifano pia yaweza kuonekana katika Agano Jipya, kwa mfano, Ufu 4, 5 na Ufu 7.

B.2. Yadah (Zab 28:7)

“Kuonyesha heshima au kicho ama kuabudu mikono ikiwa imeinuliwa juu.”

Mfano mwingine katika Agano Jipya unaonekana katika 1 Timotheo 2:8 mahali ambapo Paulo anawatia moyo wanaume wasalishe “huku wakiinua mikono iliyotakata” wana-pomkaribia Bwana.

B.3. Towdah (Zab 50:23)

“Kutoa dhabihu ya sifa na shukrani katika hali ya kuwa umeinyosha mikono yako mbele.”

B.4. Shabach (Zab 63:3)

“Kusifu kwa sauti kubwa au ya juu.”

Kupiga kelele si dalili ya kukosa kicho, bali jambo linalotakiwa na Baba. Maandiko mengi hunena juu ya jambo hili. Kwa mfano fikiria tu Maandiko haya, Zab 47:1 na Zab 66:1, japo yapo mengi mengine. “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu…” (Ebr 5:7).

Kujinyenyekeza na kuwa mchaji ni uelekeo wa moyo, na si lazima hali hiyo iendane na kuinyamazisha misisimko au uzuie kwa nguvu kuonekana kwa hali hiyo kwa nje.

B.5. Zamar (Zab 108:3)

“Kuabudu kwa kutumia ala ya muziki.”

Mungu ameweka nafasi ya vifaa vya namna nyingi na sauti za namna nyingi pia. Tuna-ona kwamba ala zetu za muziki zinageuka kuwa vielelezo vya utashi wa mioyo yetu. Ala tulizonazo katika viungo vya miili yetu, ndizo kwa hakika zilizo ala muhimu kuliko zote, nazo zaelezea uelekeo wa mioyo yetu. Warumi 12:1 yatuhimiza sisi tutoe maisha yetu kama tendo la ibada lenye maana na hili linajumuisha kila kitu tunachokifanya. Angalia pia Zaburi 150.

29

Page 38: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

B.6. Halal (Zab 35:18)

“Kung’aa, fanya kama mwenda wazimu, piga kelele na fanya ghasia na kuwa mjinga. Kuachana na jambo la kujilindia heshima yako.”

Daudi akiwa amejifunga kizibao cha kuhani kiunoni mwake alicheza kwa nguvu zake zote mbele ya Mwenyezi-Mungu. Hivyo, yeye na Waisraeli wote walilipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu hadi katika mji wa Daudi kwa shangwe na sauti kubwa ya tarumbeta. (2 Sam 6:14-15)

Daudi alikuwa mtu aliyejua kunyenyekea sana katika hali ya kicho, lakini pia alielewa jinsi ya kumheshimu Bwana kwa kuwa mwenye mori ya vielelezo vya nje vya kucheza na kusifu.

Jambo hili lilikuwa na maana kwamba heshima yake yeye kama mfalme na kila jambo alilopenda kulifanya lilitakiwa liingizwe katika tendo la ibada. Hata hivyo alijua kwamba kufanya hivyo lilikuwa jambo lililostahili!

B.7. Tehillah (Zab 22:3)

“Kuimba ‘halal’ zako. Aina ya ibada ambayo Mungu hupendelea kukaa ndani yake.”

B.8. Hitimisho

Muziki, kucheza na kuonyesha shamra shamra za nje kama vigelegele na kadhalika, vilikuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Israeli. Vielelezo vyote hivi vilihusishwa na shughuli zote za kijamii, iwe ushindi vitani au kushindwa, shughuli za kiunabii, kutoka ndani na kuingia. Kwa hali hiyo, walipomsifu Bwana lilikuwa ni jambo la kawaida kwao.

Upo pia utulivu na ukimya wa kuinama mbele ya Mfalme mtukufu, na pia hamasa na changamko la furaha tunapounganika naye katika kushangilia (Sef 3:17). Kama tukijitoa nafsi zetu katika hali ya kielelezo kamili cha ibada na tusitoe nafasi kwa woga wetu au mashinikizo ya wanadamu, kwa hakika tutafurahia na kujipatia uzoefu wa pumzi ya uzima ambao Baba ameukusudia kwa ajilli ya watoto wake wanaomwabudu!

C. Vielelezo vya Ibada Katika Agano Jipya

“Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora.” (Ebr 8:6)1

Tunapaswa kuelewa kwamba Yesu hakuondoa vielelezo vya ibada vilivyokuwa vinapati-kana katika Agano la Kale, lakini badala yake alijenga juu yake akileta ukamilifu uliokuwa hauwezi kupatikana katika zile zama za sheria ya Musa. Ni kwa namna iyo hiyo kwamba sisi hatuiondoi elimu yetu ya sekondari mara tupatapo elimu ya chuo kikuu (bali inatumika kama daraja linalotupa kusonga mbele) vivyo hivyo vielelezo vya ibada vya kwanza vinasalia na bado vinafaa, vikifanya uwepo msingi kwa ajili ya ibada iliyo kuu.

Hatuna budi pia tuelewe kiwango cha ibada aliyoileta Yesu. Kabla ya kifo chake na kufufuka kwake, Sanduku la Agano la Bwana (mahali ambapo uwepo na utukufu wa Bwana ulikaa) lilikuwa limetengwa na Waisraeli kwa utando (pazia) uliokuwa kati yao na Sanduku hilo. Sanduku lilisalia Patakatifu pa Patakatifu pa hekalu na kuhani mkuu peke

30

Page 39: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

yake ndiye aliyeruhusiwa kuingia mahali lilipokuwa mara moja tu kwa mwaka kwa niaba ya watu wote.

Mungu alizuia ufunuo wa uwepo wake kwa watu kutokana na dhambi, kwa kuwa dhambi ni lazima ihukumiwe machoni pa Mungu aliye mtakatifu. Kufunuliwa kwa uwepo wake kwa hali hii kungesababisha kifo kwao mara moja na pasipo kuchelewa. Dhabihu ya Yesu aliyoitoa ili kuleta upatanisho kwa ajili ya dhambi za wanadamu, ilifanya njia iwepo kwa ajili ya wote wanaompokea Yesu kama Bwana na Mwokozi waingie kwa uhuru ndani ya uwepo wa Mungu aliye juu sana. Yesu alipasua pazia la utengano wakati wa kifo chake na hivyo akaifungua njia kuelekea kwa Baba!

“Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; na kuwa na ku-hani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.” (Ebr 10:19-22a)

“Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini.” (Mat 27:50-51a). Angalia pia Mk 15:38 na Lk 23:45.

Tukio hili muhimu kabisa lilileta matokeo ya kuwepo hali ya ibada kamilifu ambayo daima Baba amekuwa akiitamani: yaani ibada inayotoka katika kina cha uhusiano wa ndani. Kabla kazi ya Yesu msalabani haijafanyika, ukaribu huu wa ndani ulikuwa umegubikwa na upungufu ulioletwa na wingu la dhambi. Lakini sasa, hayo yote yamebadilika.

“Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli..” (Yn 4:23-24)

Katika nukuu hapo juu, Yesu anazungumzia aina ya ibada ambayo Baba anaitafuta. Neno la Kiyunani ambalo hapa limetafsiriwa kama ‘ibada’ ni ‘proskuneo’ neno ambalo maana yake ya moja kwa moja ni ‘kusogea mbele upate kubusu’ neno linaloonyesha moyo wa Mungu wenye ukaribu na uhusiano wa ndani ambao Yesu pekee alikuwa na uwezo wa kuuleta. Ukaribu huu wenye nguvu kupita kiasi, mara nyingine unakuwa kik-wazo kwa yale ambayo yangekuwa matakwa yetu binafsi na “mipaka ambayo tunge-penda kuilinda” na kwa hivyo inahitajika kukua katika uhusiano huu ili tufikie mahali am-bapo tutaufurahia kabisa.Siyo tu kwamba Yesu alileta uhusiano wa ndani wenye nguvu kama kiini cha ibada, lak-ini pia alitaka ibada katika ‘kweli.’ ‘Kweli’ ina maana ya ibada kutoka moyoni na inayoju-muisha pamoja na kuishi maisha ya uchaji wa Mungu. Warumi 12:1 ni wito wa maisha ya ibada: “Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana” Siyo tu Jumapili wakati wa ibada kanisani, bali kila siku katika kila hali na kwa yale yote am-bayo Mungu atakuwa ametupatia.

“Ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo.” (1 Pet 4:11b).

“Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” (1 Kor 10:31).

Maandiko yafuatayo yanatupatia maarifa kwamba ibada ilikuwa sehemu muhimu ya maisha katika kipindi cha Agano Jipya: Mat 26:30; Mk 14:26; Efe 5:19,20; Kol 3:16; Mdo 16:25;Yak 5:13; 1 Kor 14:15-17; Ebr 2:12; Lk 19:37; Fil 4:4; Lk 15:25 na Fil 3:3.

31

Page 40: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kitabu cha Ufunuo kinatuonyesha picha ya ajabu sana ya uhusiano wa ndani na uchaji (Ufu 4-5, Ufu 7, Ufu 11, Ufu 14), ikionyesha kwa hali ya wazi ukamilifu wa ibada ya Agano Jipya.

Ufunuo 4:8-11 inafunua kile ambacho ibada yapasa kuwa hali ya kupata ufunuo unaoongezeka wa uwepo wake, kuinama kwa kusujudu na kuzitupa ‘taji’ zetu tukistaja-bishwa na kutangaza utukufu wake na nguvu! “Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza”

D. Hitimisho

A. W. Tozer aliwahi kusema mara moja kwamba tuliumbwa ili tumwabudu Baba yetu: ikiwa na maana ya kuwa na uhusiano wa ndani na moto wa upendo unaowaka. Tuna-paswa kumwabudu vile atakavyo Yeye na katika namna inayolistahili jina lake. Na tusije tukakutwa tunampa Mungu kilicho pungufu ya hiki katika eneo hili.

Ukumbuke kwamba hakutakuwepo tena kuhubiri, kufundisha, uenezaji wa injili au uan-zishaji wa makanisa mapya huko mbinguni, kwa kuwa hakutakuwa tena na mahitaji kama hayo. Ni kitu kimoja tu kitakachosalia tutakapokuwa tunauangalia uzuri wa utukufu wake na maajabu ya uweza wa mkono wake: sifa itokayo katika mioyo iliyohamasika, na kutokana na mazuri yake Mungu itamiminika ikitokea vinywani mwetu wakati tukimwabudu Mfalme wetu Mkuu. Basi na tuchukue nafasi hii kugundua viwango vyake, tuishi maisha yanayowastahili waabuduo, na kufurahia, kwani ibada ni huduma yetu ya milelel!

E. Mnyororo wa Ibada

Rum 12:1Yn 4:23-241 Kor 10:31Efe 5:19,20Kol 3:161 Kor 14:15Fil 4:4Zab 150

32

Page 41: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

33

Page 42: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Saba: Maombi na Kufunga

Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tum-witapo? (Kum 4:7)

A. Maombi ni Nini?

Kamusi yaweza kukupatia maana iliyo kavu, lakini Biblia inatupatia picha katika mfano wa utenzi wenye maana ya maombi kuwa ni ushirika wenye nguvu kati ya wanadamu na Mungu aliye hai – Yeye ambaye Yesu alimfunua kama Baba kwetu. Mungu yule yule ali-yetembea na Adamu katika masaa ya jioni “wakati wa jua kupunga” (Mwa 2-3) anata-mani kuwa na ushirika wa karibu pamoja nasi leo.

Yesu anasema katika Marko 12:30 kwamba amri iliyo ya muhimu kuliko zote ni amri hii: “Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.” Maombi halisi kwa hali hiyo yanahusiana na ushirika na wala hayana uhusiano na vitendo vya kidini ambavyo havitoki katika ma-husiano yenye kina, na hasa kule kufuata mapokeo tu yasiyo na chembe ya uhusiano – ni uhusiano wa upendo unaohusisha mazungumzo yenye pande mbili yaani kati ya mwanadamu na Mungu.

Mwanadamu ni taji ya uumbaji wa Mungu, ameumbwa kwa mfano wake, ili awe na ushirika naye. “Nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu.” (Kut 6:7) ni maneno yanayojirudia kama mwangwi wa kibwagizo kila mahali ndani ya Maandiko.

Kumbuka kuwa Biblia inatuonyesha kwamba kupitia uasi wa Adamu sisi tumezaliwa tukiwa wenye dhambi na kwamba dhambi inatutenganisha na Mungu (dhambi haiwezi kuukaribia utakatifu wa Mungu). Lakini Mungu alitupenda mno kiasi kwamba alimtuma Mwana wake Yesu afe msalabani kwa ajili yetu. Kifo cha Yesu kinatuletea upatanisho na hivyo msamaha kwa dhambi zetu, na kutupa mlango wa kupitia kwenda kwa Baba (Yn 3:16-17). Wakati sisi tulipokuwa bado ni wenye dhambi Mungu aliunyoosha mkono aka-tushika na kutuokoa. Je, si zaidi sana sasa kwa kuwa tumekuwa waumini, warithi wake pamoja na Yesu, na Yeye ni Baba yetu wa mbinguni anayetujali sana.

Katika Agano la Kale, ni kuhani mkuu pekee aliyeingia Mahali Palipo Patakatifu Zaidi, ikiwa na maana kwamba ndiye aliyeweza kuingia katika uwepo wa Mungu, na hata hivyo mara moja tu kwa mwaka, na hapo ni baada ya taratibu ngumu za ibada za kimapokeo kuwa zimetimizwa.

Chini ya Agano Jipya, kifo cha Kristo kinampa kila anayemwamini nafasi ya kuingia ndani ya uwepo wa Mungu. Kitabu cha Waebrania kinafafanua ni kwa nini makuhani maalumu hawahitajiki tena kusimama kama wapatanishi kati yetu na Mungu. Kristo mfufuka, Kuhani wetu Mkuu aliye Juu, ambaye sasa ameketi mkono wa kuume wa Baba, ni mpatanishi wetu. Anatupa uhakika wa kuja kwa ujasiri mbele ya kiti cha enzi cha neema ili “tupokee huruma na neema ya kutusaidia wakati wa shida.”

Yohana 1:12 inanena kuhusu Yesu: “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufany-ika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.” Ni jambo la kustaajabisha sana

34

Page 43: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

pale tunapotambua kwamba Muumbaji wa vitu vyote anatamani kuwa na uhusiano bi-nafsi na sisi, na kwamba anatujua kila mmoja kwa jina lake.

Katika Mathayo 6:7-8 Yesu anasema: “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya ma-neno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.” Upendo wa Mungu na hali yake ya kutujua sana inasisi-tizwa hapa. Sisi si wageni kwake kwa sababu alituumba katika pendo lake nasi twaweza kumgundua na kujipatia ujuzi wa kumjua zaidi kwa njia ya maombi.

Katika Mathayo 6:9 Yesu anatupatia mfumo wa kufuata katika maombi. Kila kitabu kizuri cha fafanuzi ya Biblia kitaelezea kanuni ya maombi iliyo katika mfumo huu. Mstari unao-tufungulia kanuni hii ni “Baba yetu uliye mbinguni.” Kumuona Mungu kama Baba ilikuwa kanuni isiyo ya kawaida kwa watu wa siku zile za Yesu. Matumizi yake ya neno la Ki-aramu lenye maana sawa na neno watoto watumialo kuita “Baba” likionyesha hali ya upendo wa kina kati ya baba na mwana “Abba”, neno lililokuwa na maana ya “Daddy”, kama watoto wa kizungu waitavyo baba zao lilikuwa ni tendo la kimapinduzi.

Katika injili ya Yohana 20:17b tunasoma, “nakwenda juu kwa Baba yangu na Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.” Jinsi ilivyo heshima ya kustaajabisha mtu kuja kwa Muumbaji wa ulimwengu wote na kupokelewa kama mtoto Wake.

B. Kwa Nini Twapaswa Kuomba?

Katika kila sehemu ndani ya Maandiko tunamwona Mungu akitamani kuwa na uhusiano na watu wake. Tunahitaji kuomba kwa sababu bila ya mawasiliano hakuna uhusiano. Isaya 55:6 inatutia moyo “Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu.” Waefeso 6:18a inasihi, “kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho.” Wafilipi 4:6 inanena, “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.” Wakolosai 4:2 inatuhimiza “Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu.” 1 Wathesalonike 5:16-18a inanena: “Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo.”

Tunahitaji kudumu ndani ya Kristo kwa kuwa pasipo Yeye hatuwezi kufanya jambo lolote (Yn 15:5), na tunalifanya hili kwa njia ya maombi yanayoongezeka. Kadiri tunavyoomba katika Roho, Yeye huyo hutusaidia kutuweka sambamba na matakwa ya Mungu mais-hani mwetu, kwa kuwa Roho Mtakatifu ni Mwalimu wetu. “Nayo twayanena, si kwa ma-neno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.” (1 Kor 2:13). Sala au maombi huusukuma mkono wa Mungu na kubadilisha hali ya mambo yanayotuzunguka. Ndani ya sala tunapata neema kwa ajili ya kusamehe, ujasiri kwa ajili ya kuonya, vilevile nguvu ya kuvumilia na hamasa ya kukimbia katika shindano la mbio ambalo Mungu ameliweka mbele yetu.

C. Mifano ya Maombi

C.1. Mifano Katika Agano la Kale

35

Page 44: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

• Abrahamu (Mwa 18:22).• Yakobo (Mwa 32:24).• Musa (Zab 90).• Yoshua (Yosh 10:12).• Hanna (1 Sam 1).• Eliya (1 Waf 18:36).• Hezekia (2 Waf 19:14).• Yona (Yona 2:1).

C.2. Mifano ya Yesu Kuomba

• Faraghani (Lk 5:16).• Mbele za watu (Yn 11:41).• Katika mahali pa siri (Mk 1:35, Mat 14:23).• Kukesha akiomba (Lk 6:12).• Alfajiri (Mk 1:35).• Wakati wa matatizo (Mat 26:36-44).• Baada ya ubatizo wake (Lk 3:21).• Kabla ya kuchagua wanafunzi (Lk 6:12).• Kwa kulia kwa sauti na machozi (Ebr 5:7).• Akiwa msalabani (Lk 23:46).

D. Mafundisho ya Yesu Kuhusu Maombi

Mfano Funzo Andiko Hu-sika

Rafiki anayekwenda kukopa mikate

Kuomba bila ku-kata tamaa

Lk 11

Mwanamke na hakimu dhalimu Ushupavu Lk 18:1-8

Farisayo na mtoza ushuru wakiomba

Unyenyekevu/Toba

Lk 18:10-14

Mtumishi asiye na huruma na mdeni wake

Fadhili/Msamaha

Mat 18:21

Kuomba sirini ukitumia ma-neno rahisi pasipo kujionyesha kwa watu

Kuishi maisha yasiyo na makuu

Mat 6:5,

Kusimama imara, kukesha na kuomba kwa saa moja

Bidii inayoende-lea bila kukoma

Mat 6:6

Wawili, au watatu wakipatana kwa jina la Yesu

Umoja Mat 18:19

Unapoomba, amini kwamba umepokea

Kuomba kwa matarajio

Mat 6:6

36

Page 45: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

E. Tuombeje?

Kristo ndiye mfumo wetu wa kufuata. Paulo anatuambia kwamba yafaa tumfuate yeye kama yeye anavyomfuata Kristo (angalia1 Kor 11:1; 4:16, Ebr 6:12; Ebr 13:7 na 1 Yoh 2:6). “Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.” (Yn 8:28-29) Sisi nasi tunahitajika kuwa hivyo, tukijua kwamba sala katika uhalisi wake ni moyo ambao umemgeukia Mungu ka-tika nyakati zote. Paulo anatuhimiza kuomba pasipo kukoma.

Maandiko yanawaonyesha watu wakiomba kwa njia nyingi tofauti.

• Kwa maneno yanayoeleweka (Neh 1:5-11).

• Kuomba wakinena kwa lugha mpya (1 Kor 14:2).

• Kuomba kwa kuugua (Rum 8:23, 1 Sam 1, Kut 2:23).

• Kuomba kwa kuimba shairi au wimbo (angalia Zaburi na mifano mingi).

• Kwa vilio (Ebr 5:7, Mat 27:46).

• Kimyakimya (Neh 2:4).

F. Vikwazo Dhidi ya Maombi

Biblia inafundisha kwamba vipo vitu vinavyomzuia Mungu asifanye kazi ya kujibu maombi yetu. Japokuwa Biblia inatuhamasisha tumgeukie Mungu kwa njia ya sala kwa sababu anatusikia na kufanya kazi kwa njia ya maombi yetu, yapo maonyo katika Biblia dhidi ya vitu fulani vinavyozuia kukua kwa uhusiano wetu wa maombi kwa Mungu. Hapa chini kuna mifano michache. Ikiwa tutakuta vikwazo kama hivyo katika maisha yetu ita-tupasa tuanze kufanya mabadiliko.

F.1. Kutokusamehe na Uchungu

Mathayo 5:22-24 inafundisha kwamba tusibaki katika kuwakasirikia ndugu (kimsingi Wakristo wenzetu). Pia inatufundisha kwamba kabla hatujaja kwa Mungu tukimletea vi-pawa vyetu tunapaswa kwanza tushughulikie maswala yaliyopo kati ya ndugu zetu na sisi, hata kama uchungu huo unatoka kwa ndugu mwingine kutuelekea sisi. Pia, 1 Timotheo 2:8 inatufundisha kwamba hatupaswi kuwa na magomvi au hasira kati yetu na wenzetu wakati tusalipo.

F.2. Mizozo Isiyotatuliwa ya Mahusiano ya Nyumbani

Katika 1 Petro 3:7 tunafundishwa kwamba tunapaswa kuyaweka mahusiano yetu ya nyumbani katika hali ya Kimungu ili kuhakikisha kwamba hakuna vikwazo katika maisha yetu ya sala. Mizozo isiyotatuliwa na inayoendelea, hasa kati ya wanafamilia (na hasa mume na mke) yaweza kuwa kikwazo kikubwa katika maisha yetu ya sala.

F.3. Dhamira Mbaya

Tunapomkaribia Mungu tunaweza kuanguka katika mtego wa kujifananisha sisi na watu wengine (Gal 6:3-4). Tunapaswa kuwa makini sana na jambo hili kwa sababu laweza

37

Page 46: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

kuifanya shughuli yetu yote ya kidini kuwa kazi isiyo na faida yoyote ndani yake. (Anga-lia Lk 18:10-14 na 2 Nya 7:14). Katika Yakobo 4:3 anatuambia pia hatupokei kutoka kwa Mungu tunapoomba kwa dhamira mbaya. Tunahitaji kuomba katika jina la Yesu (na hivyo kulingana na tabia zake) ili maombi yetu yaweze kuwa yenye manufaa.

F.4. Ubaya/Udhalimu

Katika Mika 3:4 tunaona jinsi Mungu anavyochagua kutojibu sala za watu wake kwa sa-babu ya mitindo yao ya maisha ya udhalimu na uovu. Dhambi inatutenga na Mungu (Mat 27:46, Zab 22:1-5), na tunahitajika kuhakikisha tunaondokana na kila mfumo wa dhambi ulio maishani mwetu ili uhusiano kati yetu na Mungu uweze kukua: kisha Mungu ata-kuwa msikivu kuelekea sala zetu (Zab 34:15-16).

F.5. Dhambi za Makusudi, Zisizoungamwa

Tukichagua kumkimbia Mungu tunapokuwa tumefanya dhambi, tunakuwa tumejitenga na Mungu na kwa hali hiyo Yeye hawezi kusikiliza sala zetu (Zab 66:18). Badala yake, tunapotenda dhambi hatuna budi kumgeukia na kumwomba msamaha, naye atatuonye-sha rehema zake (Mith 28:13). Hatutakiwi tuendelee kutenda dhambi za makusudi tuki-firia kwamba Mungu atazidharau tu dhambi zetu kwa sababu ya pendo lake kuu (Ebr 10:26). Yeye ni mtakatifu na anatamani kuona sisi pia tukiutafuta utakatifu.

F.6. Kutompa Mungu Nafasi Anayostahili Maishani Mwetu

Ni jambo jema kwetu kujitengea muda maalumu kwa ajili ya Mungu (Mk 1:35). Katika Malaki 1:6 -10 Mungu anatuambia kwamba hapendezwi na matoleo ya daraja la pili – Anataka kupokea kile kilicho bora kabisa kutoka kwetu. Anahitaji muda wetu ulio bora zaidi na juhudi zilizo kubwa zaidi. Luka 14:26 hutufundisha kwamba tunapovilinganisha na Mungu, vitu vyote huchukua nafasi ya pili – hata vitu vile vilivyo vya muhimu sana. Mungu hataki kanisa lililo “vuguvugu” (Ufu 3:16). Kweli kabisa, twaweza kuomba kila tu-patapo muda wa ziada, lakini Mungu anahitaji zaidi ya muda wetu wa ziada. Muda unao-tengwa kwa ajili ya sala humpendeza Mungu.

F.7. Kutokuomba

Yakobo 4:2b hunena jambo ambalo ni wazi: “hamna kitu kwa kuwa hamwombi!” Hatu-wezi kulalamika kwamba hatupati majibu ikiwa kama hatujakuwa hata na muda wa kuomba tusaidiwe. (Angalia pia Fil 4:6).

F.8. Kutokuwa Wasikivu

Mwanzoni twaweza tusiwe na uzoefu wa kuisikiliza sauti ya Mungu (1 Sam 3:7-11). Lak-ini tutapaswa kuvumilia na kumuomba Mungu azungumze nasi kupitia Neno lake na Roho wake. Baada ya muda tutaweza kumsikia zaidi na zaidi. Sisi kama kondoo tuna-paswa kuisikia sauti yake (Yn 10:27). Tunaposoma Neno na kuomba zaidi tunajenga uwezo wa kumsikia Mungu.

F.9. Hitimisho

Amosi 7:4-6 inaonyesha kwamba tunapokuwa katika msimamo wenye mapatano na Mungu maombi yetu yanakuwa yenye nguvu na mafanikio. Tamaa yetu ni kudumu katika hali hii kwa sababu hatutaki Mungu ayafunge masikio yake kiasi cha kutosikiliza sala au

38

Page 47: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

maombi yetu (Zab 28:1-2). Kwa sababu tunajua kwamba Mungu ni Mungu mwenye up-endo anayetamani kukutana nasi na kutusikiliza, tunakuwa watu wenye ujasiri tuna-poingia katika uwepo wake kwa njia ya maombi (1 Yoh 5:14-15). Kwa sababu tunata-mani kuwa karibu naye, basi tunafanya mabadiliko katika maisha yetu. Tunaweza kuya-fanya haya kwa njia ya kutumainia neema yake na kufanya maamuzi yanayoendana na ufunuo wa Biblia.

G. Mnyororo wa Sala

Mat 6:9Fil 4:61 The 5:16-18aYn 15:51 Kor 2:131 Tim 2:81 Pet 3:7Ebr 10:26Yak 4:2b

H. Kufunga

“Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema…” (Mdo 13:2)

John Wesley alisema, “Wengine wameliinua tendo la funga ya kidini na kuliweka juu hata kuliko Maandiko na fikra njema; na wengine wamelipuuza kabisa.” Mlingano ufaao kati ya mielekeo hii miwili isiyofaa, unapatikana katika Neno la Mungu.

Zingatia pia kwamba mwenendo wa maisha ya mtu lazima yaendane na nia ya mtu ya kufuata matendo ya kiimani mojawapo likiwa hili la kufunga (Isa 58). Kufunga si jambo linalotakiwa kuwa badala ya azma ya kuishi maisha ya ucha Mungu, bali tendo litakiwalo kuandamana na azma hiyo ya maisha ya kumcha Mungu.

I. Kufunga ni Nini?

Kufunga ni nidhamu ya Kimaandiko inayotakiwa kila Mkristo ajihusishe nayo afikiapo kipindi fulani katika maisha ya Kikristo. Tunapenda kutoa ufafanuzi ulio rahisi na tu-naoweza kuufanyia kazi.

Kufunga ni kujizuia dhidi ya kuridhisha tamaa mbalimbali za kimwili kwa ajili ya sala na kumtafuta Mungu.

Tendo hili laweza kujumlisha kujizuia kula vyakula vigumu, vya majimaji,kujipaka mafuta ya ngozi, tendo la ndoa kwa wanandoa au kujinyima kati ya hivyo vilivyotajwa hapo juu kwa pamoja. Umuhimu wa kifungu hiki, “kwa ajili ya sala,” kinachopatikana katika ufa-fanuzi hapo juu ni kwamba kufunga si tendo linalolinganishwa na kuacha kula kwa sa-babu ya matatizo ya kimwili kama kupunguza uzito au kufuata matakwa ya kisheria au kuendesha mgomo wa kula unaofanywa na wanafunzi, wafungwa, n.k). Pia, ni lazima ieleweke wazi kwamba, kufunga hakuwezi kutumika kama njia ya kumlazimisha Mungu afanye lile asilotaka kulifanya. Badala yake, ni njia ya kuhuisha ufahamu wetu wa kiroho

39

Page 48: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

na kuyatia nguvu maisha yetu ya sala, na mara zote hufanywa katika utiifu wa Neno la Mungu.

J. Kwa Nini Tunapaswa Kufunga?

Yesu anashughulikia tendo la kufunga katika hotuba yake ya Mlimani (Mat 6). Katika se-hemu hii ya Maandiko alizungumzia kufunga katika kiwango kilicho sawa na sala au kutoa sadaka. Twajua kwamba mambo haya ni sehemu ya mtindo mzima wa maisha ya mtu. Ni kweli uadilifu huwa haupatikani kutokana na kazi zetu wenyewe, bali hupatikana kwa imani katika Yesu Kristo. Hata hivyo, ukiangalia maana ya maelezo yake kwa ujumla katika sehemu hii ya Maandiko, utaona kwamba Yesu alitarajia wafuasi wake waige kufanya baadhi ya funga katika maisha yao.

Katika Mathayo 6:16-18 Yesu alisema “mnapofunga” na wala hakusema “endapo mta-funga,” ikiwa na maana iliyojificha ndani kwamba wanafunzi wangekuwa na mfumo wa maisha ambao unahusisha kufunga pia.

Katika Mathayo 9:14, wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walimjia na kumwuliza ilikuwa ni kwa nini wao na mafarisayo walifunga lakini wanafunzi wake hawakufunga! Yesu alijibu kwa kusema kwamba wasingetarajiwa kufunga wakati bwana arusi akiwa pamoja nao (akiwa na maana ya kuwepo kwake pamoja nao), lakini wakati ungefika ambapo Bwana Arusi angeondolewa kutoka kwao, na tangu wakati huo wanafunzi wake wangefunga. (Bila shaka kwa kusema hivi hakumaanisha siku tatu ambazo alikuwa kaburini kwa kuwa wanafunzi walifunga baada ya kupaa kwake. Katika Matendo 13 tunaona kwamba vion-gozi wa kanisa la Antiokia walifunga. Hili lilionyesha kufunga baada ya kupaa kwa Yesu). Yesu sasa ameketi mkono wa kuume wa Baba huko mbinguni ambako amekaa akituombea (Rum 8:34), na anawatarajia wafuasi wake kuingia katika mfumo wa maisha alioufundisha. Mfumo wa maisha alioufundisha ni pamoja na kufunga.

Na sasa kwa kuwa tumeshajadili kwamba Yesu alitarajia wanafunzi wake kufunga, basi hebu tupate muda wa kuangalia kwa ufupi juu ya faida za kufunga.

J.1. Kufunga Huinua Kiwango cha Utambuzi wa Kiroho

Kutokana na uzoefu wa kulifanya tendo hili, pia kutoka katika maelezo ya Maandiko juu ya funga ya Yesu (Lk 4:1-13), tunagundua kwamba kujinyima au kuzuia tamaa za kuuti-mizia mwili mahitaji yake kunaumba hali ya utambuzi kuelekea uhalisi wa mambo ya ki-roho. Ni tendo linaloongeza uelewa wetu juu ya yale yanayotokea katika ulimwengu wa roho. Kwa hivyo, tendo la kufunga ni lenye umuhimu mkubwa katika maisha yetu ya sala.

J.2. Kukabiliana na Adui

Kwa mara nyingine, kutoka katika uzoefu wetu wenyewe na uzoefu katika ile funga ya Yesu, tunagundua kwamba kufunga kunaweza kulazimisha itokee hali ya kukabiliana au pia kushindana na adui, au kufunga kwaweza kutokea kutokana na vita anayopitia mtu kati yake na adui. Inatokea hivi kwa sababu upenyo unapokaribia sana kupatikana, sisi tunakuwa dhaifu kimwili na hivyo kuwa katika hatari ya kuangukia katika majaribu, pia, kwa upande mwingine shetani anaogopa athari ya maombi yetu. Kukabiliana huku mara nyingi kunachukua sura ya vita katika akili zetu pindi adui anaposhambulia yale tu-nayoyaamini kuhusu Mungu, anatamka mashtaka akitulaumu juu ya makosa kadhaa ambayo sisi tunakuwa tukiyafanya na hapo hapo kututangazia hukumu kama kutuonye-sha kwamba hatima ya uhusiano wetu na Mungu imefika na hatuwezi kuhusiana naye

40

Page 49: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

tena. Kama vile Yesu alivyofanya katika wakati wake wa kufunga, sisi pia tunatakiwa kupingana na mashambulizi haya kwa kutumia Neno la Mungu.

J.3. Kufikia Mafanikio ya Kiroho

Wakati Yesu anaporejea akitokea nyikani alikokuwa katika funga na maombi, Luka anaandika maneno haya: “Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.” (Lk 4:14).

Mara nyingi tunapofunga na kuomba, Mungu huachilia nguvu ije katika mazingira yote yanayotuzunguka. Katika Agano la Kale kuna maelezo ya matukio ya ushindi mkuu Mungu aliowapa watu wake wa Yuda akiwashindia juu ya “majeshi makubwa ya maadui.” Yehoshafati alitangaza funga ya kitaifa na watu wote wa Yuda wakaomba msaada wa Bwana. Mungu alinena kiunabii kupitia Yahazieli juu ya ukombozi wa Mungu kwa watu wake. Baada ya hapo Mungu alileta upenyo katika vita iliyowakabili. Maelezo ya tukio hili yamehifadhiwa katika 2 Nyakati 20:3-24.

J.4. Kufunga Huondosha Sumu Zilizo Mwilini

Katika kipindi cha kufunga, hasa funga zinazoendelea katika vipindi virefu, wengi huamini kwamba mwili hupata nafasi ya kutoa sumu zilizokuwa zimejengeka ndani yake katika vipindi vya miezi inayotangulia funga. Wengine huamini kwamba kwa sababu hii funga yetu ndefu ya kwanza inaweza kuwa yenye shida nyingi, ikijumuisha kuumwa ki-chwa na hata kupata kizunguzungu.

J.5. Kukomboa Muda Kwa Shughuli za Kila Siku

Kwa wastani watu hujiwekea matumizi ya masaa 2-4 kwa kula na shughuli zihusianazo na tendo hili kila siku. Tunapokuwa na funga ya kujizuia kunywa maji tunakomboa wakati ambao waweza kutumika katika sala au kujisomea Maandiko na kujifunza. Kwa hesabu rahisi, ndani ya juma moja la kufunga, tunajipatia ziada ya masaa 3 kila siku na masaa 21 ambayo huweza kutumiwa katika sala au kujisomea Neno

J.6. kupumzisha Viungo Muhimu vya Mwili

Wengi huamini kwamba katika muda wa kufunga, tumbo na viungo vingine muhimu vya mwili hupewa muda wa kupumzika. Hii ni sababu mojawapo inayowafanya madaktari wengi waseme kwamba kufunga ni tabia ijengayo afya yetu.

K. Kufunga - Tufungeje?

Mfumo wa kufunga ndani ya Maandiko waweza kugawanywa katika aina tatu zinazoe-lezwa katika sehemu hii, nazo ni kama zifuatavyo:

.K.1. Funga ya Kawaida

Mfano wa kutokula vyakula vigumu umetajwa katika Luka 4:1-2. Wasomi wakuu wengi wa Biblia wanakubaliana kwamba kwa mtafsiri wa Biblia wa Kiyahudi funga hii ingekuwa kama funga ya kutokunywa maji peke yake. Hata hivyo, wengi wanaliona hili kama funga ya vyakula vya majimaji tu, hii ina maana ya kujinyima vinywaji vya aina nyingi.

41

Page 50: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

K.2. Funga Nusunusu

Mfano wa kujinyima vyakula vitamuvitamu, nyama, mvinyo au divai kwa majuma matatu unapatikana katika Danieli 10:2-3. Kwa kuacha kwa muda mahusiano ya kindoa kwa mapatano kati ya mke na mume. Angalia 1 Kor 7:3-5.

K.3. Funga Kali au Funga Kamili

Kwa ajili ya mifano ya funga za kutokula au kunywa, angalia Ezra 10:6, Esta 4:16 na Matendo 9:9. Funga hizi zinaendelea hadi siku tatu na si zaidi ya hapo. Juu ya suala la Funga Kali au Funga Kamili, mwandishi Richard Foster, aliyeandika kitabu kiitwacho “Celebration of Discipline” (Kusherehekea Nidhamu), anaandika: “Ni lazima ionekane kwamba funga kali au funga kamili ni funga isiyo ya kawaida na hutakiwa mtu anayei-fanya awe na uhakika kwamba Mungu amemwamuru aifanye funga hiyo, na inapokuwa hivyo basi isizidi kipindi cha siku tatu mfululizo.”

L. Tufunge Wakati Gani?

Tunatoa miongozo mitatu ya msingi yenye manufaa ya kumsaidia mtu ajue ni wakati gani impasapo kufunga.

L.1. Kuitwa na Roho wa Mungu Kuingia Katika Funga

Katika Luka 4:1-2 tunaona kwamba Yesu aliongozwa na Roho aingie katika kipindi chake cha kufunga.

L.2. Kuitwa na Viongozi wa Kanisa Tuingie Katika Funga

Waebrania 13:17 inatuambia tuwatii viongozi wetu. Wakati viongozi wanapomsikiliza Mungu na kuliongoza kanisa liingie katika funga, tunatii neno la Mungu kwa kuutii uon-gozi. Mfano wa kiongozi anayetangaza kuwe na funga waweza kuonekana katika kitabu cha Ezra 8:21.

L.3. Kuamua Kufunga

Huku huwa ni kuchagua tarehe na kuitenga kama sehemu ya mtindo wa maisha yenye uthabiti wa kuwa mfuasi wa Yesu. Tahadhari lazima iwekwe mahali hapa kwa watu wenye tabia za kuona kwamba kila kitu kiletacho furaha maishani ni kibaya na wale wenye tabia ya mfano wa kuishi maisha yanayotawaliwa na sheria.

M. Tahadhari na Miongozo Katika Kufunga

Kufunga kunahusisha ndani yake kipengele cha maombi au sala. Kujizuia kula pasipo sala au maombi ni mgomo wa kula, na siyo kufunga. Kufunga ni sehemu tu ya mtindo wa maisha ya mwanafunzi wa Kristo.

Katika kuanza, waweza kujaribu funga za muda mfupi, au funga zinazohusisha baadhi tu ya vyakula na kadhalika. Hiyo ni njia ya kujijenga ili uweze kufikia funga za muda mrefu. Unaweza kujizoesha hata ukaweza kufikia uwezo wa kuwa na funga ndefu ya kujinyima maji. Endapo utakuwa na sababu za kiafya zinazoweza kukuzuia kufunga, au hata kama unahisi tu kwamba kuna sababu ya kiafya inayofanya isiwe vyema wewe

42

Page 51: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

kufunga (kwa mfano, ujauzito au ugonjwa wa kisukari), basi muone daktari ili akupe ushauri. Kama kukiwa na funga ya watu wengi na wewe ukawa na tatizo la kiafya, labda wewe ni mja mzito au unafanya kazi nyingi za kutumia nguvu, tafadhali ongea na wazee wa kanisa. Kwa njia hii bado unaweza kushiriki kwa njia fulani na pia ukaweza kufurahia faida za funga ya jamii unayoishiriki.

Ni muhimu kufikiria kuacha shughuli za mazoezi ya viungo na kazi nyingine ngumu uwapo katika funga. Mtindo wa maisha ya kufunga una faida za kiroho za ajabu sana na pia baadhi ya faida za kimwili.

M.1. Ushauri Kwa Wale Wanaojiandaa Kwa Funga Ndefu

Katika kujiandaa kwa ajili ya funga ndefu unapaswa kuchukua tahadhari na kuacha kula vyakula vigumu hatua kwa hatua. Kama mwongozo wa jumla, unatakiwa kupunguza vyakula vifuatavyo katika mpangilio ufuatao:

Vyakula vyenye protini nyingi: nyama nyekundu na samaki.

Vyakula vya aina ya maziwa na mayai.Nafaka, wali na ngano.Mboga za majani na matunda.

Wale wanaoingia katika funga ndefu kwa mara ya kwanza sharti waonywe kwamba ku-sikia hali ya kizunguzungu na maumivu ya kichwa ni jambo la kawaida.

M.2. Kufungua

Katika kufungua kutoka katika kufunga, mtu kwa kawaida atafuata mchakato wa maan-dalizi katika mfumo wake wa kinyume:

• Kwanza kula: Mboga za majani na matunda.

• Halafu fuatisha: Nafaka: wali na ngano.

• Baadaye mwisho: Vyakula vya aina ya maziwa na mayai kisha vyenye protini nyingi: nyama nyekundu na samaki.

Zingatia kwamba jambo la kufungua kutoka katika funga ya siku 3-40 kwa namna isiyo-faa laweza kuleta mshituko ndani ya mfumo wa mwili na hivyo kuwa jambo la hatari.

43

Page 52: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Nane: Biblia

Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, la-faa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. . (2 Tim 3:16-17)

A. Kile Tukiaminicho Kuhusu Biblia

Tunaamini kwamba ni jambo la maana na lenye kukubalika akilini kwamba Mungu aliye-viumba vitu vyote angeweza kuamua kuwasiliana na mwanadamu (kiumbe wake), na kwamba mwanadamu, aliyeumbwa na Mungu angeweza kuyaelewa na kuyaitikia ma-wasiliano yale kwa njia fulani.

Mifano ya njia ambazo Mungu amekuwa akizitumia kuwasiliana na mwanadamu ni kama ifuatavyo:

• Uumbaji (Zab 19:1-4, Rum 1:18-20).

• Dhamira (Rum 1:32; 2:14-15).

• Yesu (Yn 14:7-9, Ebr 1:3a).

• Biblia (2 Tim 3:15-17, 2 Pet 1:20-21).

Kwetu sisi Biblia ni yenye umuhimu usio na kifani kwa kuwa ni njia ya uhakika zaidi, na yenye mpangilio uliokamilika na ulio wazi zaidi wa ufunuo wa Mungu kuhusu tabia yake, mpango wa wokovu na kweli nyingine. Kwa kutumia maneno ya Nigel Day-Lewis, “Biblia ni kitabu kilichoandikwa na watu waliovuviwa na Mungu chenye kumbukumbu zisizo na mapungufu au makosa, kumbukumbu zenye ufunuo wote wa Mungu kwa wanadamu, na kwa hivyo Biblia inayo mamlaka ya mwisho kwetu katika mambo yote yahusuyo maisha na mafundisho. Biblia ina kila kitu tunachohitaji kukijua juu ya wokovu, na hakuna cho-chote kinachohitajika kuondolewa ndani yake au kuongezwa juu yake.” Biblia iliandikwa kutokana na uvuvio wa kimungu na kwa hivyo haiwezi kukosea au kuwa na kasoro. Nadharia tano juu ya uvuvio ni kama zifuatazo:

1. Nadharia ya ujuzi au maono ayapatayo mtu akilini pasipo kuanza kuyafikiria, inasema, Maandiko yalitokana na mawazo ya watu wengi washika dini wal-iokuwa na vipawa vya akili vya hali ya juu.

2. Nadharia ya Kuangaziwa; inasema, Roho Mtakatifu huvinyanyua juu vipawa vya kawaida vya waandishi ili waitende kazi yao na kwamba hakukuwa na mawasili-ano yoyote katikati yaliyowasilisha kweli maalumu kwa watu hao.

3. Nadharia ya Nguvu inayoendesha inadai kwamba Mungu aliwaongoza waandishi katika kanuni alizotaka ziandikwe, lakini akawapa ruhusa ya kutumia maneno wanayoyataka.

4. Nadharia ya Imla; inasema kwamba Mungu aliongoza uandishi wa Biblia kwa waandishi wanadamu neno kwa neno.

44

Page 53: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

5. Nadharia ya Matamshi Kamili; inadai kwamba Mungu aliwaongoza waandishi wa Maandiko kwa kiasi kwamba kile walichokiandika kilikuwa ni Neno lake kamili kupitia katika maneno yao na kila sehemu ya yale yaliyomo ndani yake imevu-viwa uwezo wa kimungu.

Ni mtazamo huu wa mwisho, ambao kwa usahihi kabisa unaikamata maana ya Uvuvio wa Maandiko.

Kuna mitazamo minne inayoelezea hali ya Biblia kutokuwa na kosa: Mtazamo unaoshikilia kwamba Biblia haina kasoro yoyote unashikilia kwamba yote isemayo ni mambo ya kweli hata katika mambo ya kisayansi na kihistoria.

Mtazamo wa Biblia kutokuwa na kosa au kasoro unashikilia kwamba japo lengo kuu la Biblia si Sayansi au historia, maelezo yote itoayo ni sahihi, na kamilifu kabisa.

Mtazamo wa Biblia kutokukosea katika kiwango chenye mipaka unashikilia kwamba Bib-lia haikosei katika kipimo cha mafundisho yake lakini inapogusia masuala ya kisayansi na kihistoria huonyesha tu uelewa wa wanadamu juu ya masuala hayo katika kipindi Biblia ilipoandikwa.

Mtazamo wa kutokukosea katika lengo lake unashikilia kwamba pasipo kukosea katika lengo lake Biblia inakamilisha lengo la kuwaleta watu katika uhusiano wa moja kwa moja na Kristo.

Kwa sababu Biblia imevuviwa na Mungu na ni yenye ufunuo mkamilifu kwa mwa-nadamu, tunapaswa kuipa mamlaka ya juu kabisa katika maisha yetu kwa kadiri inavy-owezekana (kumbuka ile nukuu tuliyoisoma hapo juu, “… mamlaka yetu ya mwisho ka-tika masuala yote ya maisha na mafundisho”). Vitabu vingine vinavyoandikwa, matamshi ya kiunabii au maongozi ya kiroho yanayopingana na Biblia hayawezi kabisa kuwa ya kweli ikiwa yanakwenda tofauti na kweli ya Mungu isiyobadilika.

Kwa kuwa Biblia ina mamlaka kamili ndani ya maisha ya Mkristo, ni jambo linalotakiwa kwamba tuipe kipaumbele katika kuisoma na kujifunza kanuni zake kadiri tuwezavyo, ili mawazo yake tuyaingize mawazoni mwetu, hata misisimko yake na moyo wenyewe wa Mungu ufanyike kiini cha maisha yetu.

B. Muundo wa Biblia

Biblia ni maktaba yenye vitabu 66, ambavyo mpangilio wake haufuati mfululizo wa vip-indi vilipoandikwa (kama ambavyo tungetarajia), lakini mara nyingine vimepangiliwa kwa kufuata mitindo ya kiuandishi. Kwa hali hii vitabu vilivyoandikwa katika mtindo wa ki-ushairi na vile vya kinabii vya Agano la Kale vyaweza kuonekana katika mpangilio wa vitabu vya historia vyenye matukio yaliyozunguka kipindi vilipoandikwa. Barua au nyaraka zinaonekana katika mazingira yaliyozunguka uandishi wake ndani ya kitabu cha Matendo ya Mitume. (historia ya Agano Jipya).

Hapa chini kuna chati inayoonyesha mpangilio au umbo la msingi la Biblia, chati inayoo-nyesha hata idadi ya vitabu vyote vya Biblia.

Mtindo wa Kiuandishi Majina ya Vitabu JumlaSheria Mwanzo – kumbu-

kumbu5

45

Page 54: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Historia Yoshua-Esta 12Mashairi Ayubu-Wimbo Ulio

Bora5

Kinabii Isaya-Malaki 17Jumla ya Vitabu vya Agano la Kale

39

Mtindo wa Kiuandishi Majina ya Vitabu JumlaInjili Mathayo-Yohana 4Historia Matendo ya Mitume 1Barua (Nyaraka) Warumi-Yuda 21Kinabii Ufunuo 1Jumla ya Vitabu vya Agano Jipya

27

Jumla ya Vitabu Vyote 66

Biblia haikuanguka tu kutoka mbinguni kama ambavyo watu wangedhani. Hatua kwa hatua ilikusanywa na kuwekwa pamoja katika kipindi cha miaka 2,000, na mkusanyiko wote ni mchango wa takriban kama waandishi 40. Vitabu vya Biblia kila kimoja kilichun-guzwa na kuhakikiwa na kamati mbalimbali na hata mabaraza ili kuthibitisha uhalisi na uvuvio wake.

C. Kwa Nini Tujifunze Biblia – Sababu Kumi

C.1. Biblia Inamfunua Mungu Kwetu

Hakuna njia rahisi, au iliyo bora zaidi na ya hakika zaidi ya kuweza kumjua Mungu kuliko kupitia katika Neno lake. Amefunua tabia zake wazi wazi kila mahali ndani ya Biblia, na njia pekee kwa sisi kupata kujua jinsi Mungu alivyo ni kwa kuisoma.

C.2. Biblia Hutia Uhai Mpya Akilini Mwetu

Tunaishi katika ulimwengu uliojaa na kulemewa na ugonjwa wa dhambi, ulimwengu am-bao kila kunapokucha unagandamiza mifumo yake ya dhambi juu ya akili zetu. Mawazo yetu huamua juu ya matendo yetu na kwa hali hii ni jambo la lazima kuhakikisha kwamba tunaendelea kuzijaza akili zetu kwa mawazo ya Mungu. Njia pekee ya kuyapata mawazo ya Mungu ni kwa kulisoma Neno lake (2 Pet 3:1). “Basi, ndugu zangu, nawa-sihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kum-pendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu ya-liyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.” (Rum 12:1-2).

C.3. Biblia ni Msaada Wetu Katika Vita vya Kiroho

46

Page 55: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Neno la Mungu linaelezewa kuwa ni upanga wa Roho. Kwa hali hii ni silaha ya vita dhidi ya ibilisi. Tunahitaji kujifunza namna ya kulitumia kwa njia hii kama vile Yesu alivyolitu-mia wakati alipojaribiwa jangwani. (Angalia Efe 6:17 na Mat 4:1-11).

C.4. Biblia ni Msingi Imara Kwa Ajili ya Maisha

Nyuma ya Neno la Mungu kuna uaminifu wa Mungu mwenyewe. Kama tukiishi maisha yetu kwa hali ya utii kwa Neno la Mungu, hatutaanguka mbele ya dhoruba za magumu na nyakati ngumu za majaribu zitujiapo kwa sababu uaminifu wa Mungu kwa neno lake utatushika. Ufunguo wa mafanikio siyo tu kulisikia Neno la Mungu, bali kulifanyia kazi kwa kulitii. Angalia Mat 7:24-27 na Yak 1:23-25.

C.5. Linatujenga Ili Tutende Kazi Njema

“Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” (Efe 2:10)

Mungu ametayarisha kazi njema kwa ajili yetu sisi tuzifanye, lakini kama sisi hatuan-daliwi na kuwezeshwa, hatuwezi kuzitimiza kazi hizo kama inavyopasa. Kwa kusoma na kujifunza Neno la Mungu tunajengwa kuwezeshwa kutimiza makusudi ya Mungu. “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe ka-mili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” (2 Tim 3:16-17)

C.6. Biblia Inatuwezesha sisi Tujitambue Tulivyo na Inaifunua dhambi

Tunapolisoma Neno, tunaona kiwango cha maisha Mungu alichokiweka, na pia katika hali ya maumivu mengi tunapata kuyaona maeneo fulani fulani maishani mwetu tunapo-jikuta katika hali ya kupungukiwa. Ni kama kujiangalia kwa kioo na kugundua kuwa wa-naotuangalia wanaona wajihi wetu hauvutii. Hii hutuwezesha kubadilika na kufanya marekebisho ili tuweze kuwa watu ambao Mungu anatamani tuwe. (Ebr 4:12)

Yakobo, alisema, “Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Lakini iweni waten-daji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.” (Yak 1:21-25).

C.7. Biblia Hutakasa Maisha Kuyafanya Yaondokane na Dhambi

Tukiisha kufahamu kuwepo kwa dhambi maishani mwetu, hakuna njia nyingine iliyo bora zaidi ya kuondokana na dhambi kuliko kusikia kile asemacho Mungu kuhusu dhambi yenyewe, na kisha kuliruhusu Neno la Mungu lifanye kazi. Kwa njia hii tutajifunza kuichukia dhambi kwa ukali kabisa (sawa kabisa na Mungu aichukiavyo) na matokeo yake ni kwamba maisha yetu yatatakaswa. (Angalia Yn 15:3; 17:17 na Efe 5:26).

C.8. Biblia Hutuzuia Tusifanye Dhambi

Siyo tu kwamba Neno la Mungu hufichua na kuyatakasa maisha yetu yaondokane na dhambi, lakini pia Biblia husaidia kutuzuia tusiingie katika kutenda dhambi. Ikiwa kweli tunakuwa tumejawa na Neno la Mungu na tukakabiliwa na jaribu, tutakuwa na nafasi

47

Page 56: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

kubwa ya kutoka katika jaribu hilo tukiwa tumepata ushindi (1 Yoh 2:1). Zaburi 119:9 huuonyesha ukweli huu kwa njia hii, “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?Kwa kutii, akilifuata neno lako.”

C.9. Biblia Hutuwezesha Kuhubiri na Kufundisha

Tunapolijua Neno la Mungu na kwamba yale tunayoyahubiri na kuyafundisha yana msingi katika Neno la Mungu hapo tunakuwa wenye uwezo wa kunena tukiwa na ujasiri na mamlaka kwa sababu tunajua kwamba uaminifu wa Mungu uko upande wetu (2 Tim 3:16-17, 2 Tim 4:2). 1 Petro 4:11a inasema, “Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu.”

C.10. Biblia Hujenga Imani

Kwa sababu Mungu ni mwaminifu, tunajua kwamba Neno lake ni kweli. Kamwe Mungu hatashindwa kutimiza ahadi zake. Kwa hali hii, sisi tunapata uthibitisho mkuu na ujasiri wa kuweza kumtumainia kutokana na kulisoma Neno lake. Warumi 10:17 yasema, “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo”

D. Itupasavyo Kuikaribia BibliaUsomaji usiofaa waweza kumkatisha tamaa mtu yeyote anayekuwa ameanza kutaka kuisoma kwa shauku kubwa. Hata hivyo, njia sahihi ya usomaji itaongeza ari ya mtu ka-tika nyakati za mtu kujifunza Biblia na kumuepusha na kukata tamaa kusiko kwa lazima. Dondoo zifuatazo zitakusaidia katika Kujifunza Biblia kwa manufaa endapo utazifuata.

D.1. Isome Biblia Kitabu kwa Kitabu

Chagua kitabu unachopenda kukisoma.

Tafuta kujua mazingira ya kihistoria yanayokizunguka kitabu husika. Unapoelewa maz-ingira ya kisiasa, kitamaduni na kiroho ambamo ndani yake kitabu chenyewe kiliandikwa utaanza kukielewa kitabu hicho kwa urahisi zaidi kwa sababu utaanza kumwelewa mwandishi pamoja na watu waliokuwa walengwa wa ujumbe wake. Kwa wasomaji wa Kiswahili tunapendekeza toleo la Kiswahili la Union Version (1960) na Biblia Habari Njema (Toleo la Kiswahili cha Kisasa (na matoleo ya Biblia kama NIV Study Bible na ITCC Bible Survey kwa wasomaji wa Kiingereza).

Kisome kitabu chote kwa mpangilio wake, badala ya kukisoma katika visehemu baadhi, kuruka sehemu nyingine au kusoma huku na huko pasipo mpangilio wowote. Kwa njia hii utaweza kuufuata mtiririko wa mawazo ya mwandishi na hii itakusaidia wewe kue-puka kuitumia mistari nje ya matumizi yake au kuifanya iseme mambo ambayo mwan-dishi kamwe hakuyakusudia.

Kumbuka kwamba siyo sura zinazotumika, mistari (aya) au vichwa vinavyowekwa juu ya sura mbalimbali vilivyo na uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivi viliongezwa baadaye ili vi-fungu viweze kutofautishwa na kunukuliwa kwa urahisi. Mara nyingi wazo la mwandishi analotaka kuwasilisha laweza kutekwa nyara pale wasomaji wanapokatiza mtiririko na kuuwekea hitimisho katikati bila ya kuangalia kuna nini mwisho wa kifungu au sura. Ni bora kabisa kuangalia kwa viashirizi vilivyo wazi ndani ya kifungu vitakavyoonyesha kwamba wazo ambalo mwandishi alikuwa akiliwasilisha limeendelezwa na kufikia tamati, na kwamba wazo jipya limeanza baada ya lile lililotangulia kabla ya kuacha kusoma.

48

Page 57: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

D.2. Kujifunza Kuyaelewa Maneno Yaliyotumika

Ni muhimu kuzingatia kwamba Roho Mtakatifu aliwavuvia waandishi wa Biblia kadiri walivyoendelea kuandika katika lugha zao za asili (Agano la Kale: Kiebrania na Kiaramu, Agano Jipya: Kiyunani) na kwamba tafsiri katika lugha mbalimbali zilizopo siku hizi hazi-wezi kila mara kuwasilisha utajiri wa maana kamili ya wazo lililoelezwa katika lugha ya asili iliyotumika kwanza kukiandika kitabu husika. Kwa hali hii, mara nyingine ni jambo linalosaidia kuweza kujiingiza katika kujifunza maneno yaliyotumika katika lugha za asili. Vipo vitabu rahisi vinavyoweza kumsaidia msomaji kujifunza maana zilizomo katika ma-neno haya. Siyo jambo la lazima kujifunza lugha ya Kiyunani cha kale.

Thamani ya kujifunza maana za maneno ni kwamba tunakuwa katika kuwezeshwa “kuchimba mfano wa madini yachimbwavyo migodini” utajiri wa ufunuo wa Mungu, kwa kuchukua kipande cha Maandiko (kwa kawaida kipande kifupi tu) na kwa kutumia vitabu kama Itifaki ya Biblia, au Vine’s Expository Dictionary kwa wasomaji wa Kiingereza na vingine vingi kama hivyo, utaweza kuliona kila neno la asili na maana kamili ya neno hilo. Kufanya hivi humpa mtu uelewa ulio wa wazi zaidi unaomsaidia kujua ni nini mwandishi alichotaka kukisema.

D.3. Kujifunza Kwa Kufuata Mpangilio Maalumu wa Masomo

Thamani ya kujifunza Biblia kwa kufuatia masomo maalumu ni kwamba unaweza kuya-kusanya pamoja Maandiko yote yanayohusiana na somo utakalolichagua. Ukiisha ku-soma kila kitu kinachosemwa na Biblia kuhusiana na somo fulani au mada fulani, hapo utakuwa na wazo lililo wazi zaidi kuhusu Mungu afikiriavyo au kuhisi juu ya jambo hu-sika.

Mfumo unaotumika ni rahisi: chagua somo au mada na kisha fuatia neno au maneno katika kitabu cha Itifaki ya Biblia (concordance), ambacho hutoa orodha kamili ya Maan-diko ambamo neno hilo hupatikana. Baada ya hapo unaweza kusoma kila Andiko ndani ya Biblia, ukililinganisha kila moja na lingine na kuyaandika pembeni mambo muhimu unayoyapata au mada mpya zinazojitokeza. Mwishoni kabisa, waweza kuyaweka yote uliyojifunza katika mpangilio unaoleta maana na kuyahifadhi katika mfumo ambao baa-daye utakuwezesha kujifunza kwa urahisi.

D.4. Kusoma Kwa Kuamsha Fikra Njema za Ibada

Laweza kuwa jambo lenye kujenga sana unapochukua sehemu ndogo ya Andiko na kulisoma taratibu, ukifanya mfano wa kulicheua kwa kulitafakari mawazoni na kuwa ka-tika hali ya sala. Kwa mtazamo kama huu, lengo kuu ni kulichukua Andiko na kulitumia ndani ya maisha yako.Maswali muhimu unayohitaji kujiuliza wewe mwenyewe kutokana na kila Andiko uliso-malo ni kama ifuatavyo:

Ninajifunza nini kumhusu Mungu?Ninajifunza nini kunihusu mimi mwenyewe?Andiko hili linanitaka mimi nifanye nini?Ni mahali gani ninaposhindwa?Ninawezaje kulitumia hili maishani mwangu?

D.5. Jinsi ya Kuitafsiri Biblia (Hermeneutics)

Wasomi wakuu wa Biblia wamekubaliana juu ya “sheria” kadhaa au “kanuni zinazoon-goza”, zinazomsaidia msomi wa Biblia mwenye kumaanisha kuitafsiri Biblia kwa namna

49

Page 58: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

ifaayo. Hili ni somo pana linalohitaji muda mrefu wa kujifunza kwa kina kwa sababu kuna “sheria” nyingi.

Kanuni moja au “sheria” yastahili itajwe, nayo ni sheria inayoitwa sheria ya maana rahisi. Hii ina maana kwamba unaukubali ukweli kuwa Biblia inamaanisha kile inachokisema (hii ina maana kwamba Andiko linachosema ndicho linachomaanisha), isipokuwa tu pale kunapokuwa na hali halisi ndani ya sehemu husika inayoonyesha kuwepo maana tofauti. Baadhi ya watu wasioelewa wamejaribu kulichukulia kila Andiko ndani ya Biblia kiroho na wakajikuta wameangukia katika makosa na maangamivu.

E. Hitimisho

Biblia ni ufunuo wenye mamlaka na uvuvio wa Mungu kumuhusu Yeye mwenyewe. Bib-lia ni kiongozi wetu pekee asiyeweza kukosea anayetuongoza kumjua Mungu, kujielewa sisi wenyewe ipasavyo na kuishi maisha yanayomtukuza Mungu. Kila Mkristo anapaswa atoe muda maalumu wa kulisoma na kujifunza Neno la Mungu.

F. Mnyororo wa Biblia

2 Tim 3:16-172 Pet 1:20-21Yak 1:23-25Ebr 4:12Yak 1:21-25Efe 5:262 Tim 4:2Rum 10:17

50

Page 59: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Tisa: Fedha na Utoaji

akawapa mafungu kumi ya fedha, aka-waambia, Fanyeni biashara hata nitaka-pokuja.” (Lk 19:13b)

A. Mungu Ndiye Chanzo cha Vyote.

Katika Zaburi 24:1 tunasoma, “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,dunia na wote wakaao ndani yake.” Andiko hili linatukumbusha kwamba umiliki wa kila kitu ni wa Mungu na kwamba kila tulichonacho tumepewa naye. Hali kadhalika, 1 Nyakati 29:10-13 inatuambia kwamba utajiri na heshima hutoka kwa Mungu. Hii ina maana kwamba kamwe hatuwezi kuwa wamiliki wa chochote na hivyo sisi ni mawakili wa vyote Mungu alivyoviweka mikononi mwetu.

Mtazamo wetu kwa kila tulichonacho unapaswa uwe wa kuachilia kila kitu kwa Mungu na tumruhusu atuongoze katika matumizi yote ya mali zake Mungu. Mungu anamiliki vingi zaidi kuliko zaka au fungu la kumi! Sisi kama mawakili tutatakiwa kuwajibika kwa vile tunavyoufanyia kazi uwakili wetu (Mat 25:14-30).

Tumeitwa ili tulenge na kukazia katika Ufalme wa Mungu na makusudi ya Mungu kuliko kujiachia tutekwe na kufungiwa ndani ya mfumo wa ulimwengu wa kumiliki na kujilimbi-kizia mali (Angalia Mat 6:19-34).

A.1. Fedha Haina Uovu Ndani Yake

“Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha.” (1 Tim 6:10a) Hali ya kupenda fedha na choyo/uroho ndio uovu, na wala siyo fedha yenyewe. Fedha haina upande ilikolemea, yaweza kutumika ama kwa mema au mabaya. Tunahitaji kuwa na Wakristo matajiri waliozama katika masilahi ya ufalme na wanaoutafuta ufalme wa Mungu kwanza na haki yake yote (Mat 6:33). Kuwa tajiri siyo uovu, bali ni baraka. Kili-cho muhimu zaidi kwa Mungu ni jinsi uipatavyo na pia vile unavyoitumia mali hiyo. Clive Pick alilisema hili kwa njia hii: “Mungu anataka sana kutuona kuwa watu waliokomaa ka-tika masuala ya kifedha kuliko kuwa na urahisi au unafuu katika mambo yahusuyo fedha”. Katika Agano la Kale, utajiri ulikuwa ni baraka ya utii wakati huo huo umaskini ukiwa ni laana itokanayo na kumuasi Mungu (Kum 28).

1 Timotheo 6:17-19 inatoa maelekezo kwa watu wale walio matajiri. Utajiri una hali ya uwiano na hivyo tunaamriwa kuwa makini na waangalifu na vile tufanyavyo na utajiri wetu. Hatuwezi kumtumikia Mungu na wakati huo huo tukatumikia mali (Lk 16:13). Kuna njia mbili za kujipatia kiasi cha kutosha: njia moja ni kujilimbikizia zaidi na nyingine ni kuwa na tamaa ya vichache. Fedha haina thamani ya milele na wala haitupi hakika ya mafanikio maishani. Ni jambo la muhimu zaidi kujiwekea sisi wenyewe hazina mbinguni.

Hatutakiwi kulenga kuwa na maisha ya anasa bali kuwa na mtindo wa kuishi maisha ya kuwa wenye kutosheka.

“Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupun-gukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Fil 4:11-13)

51

Page 60: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

“Baraka ya Bwana hutajirisha,Wala hachanganyi huzuni nayo.” (Mith 10:22)

Pia angalia Mith 8:17-21.A.2. Mungu Hahitaji Kitu

“Sitatwaa ng'ombe katika nyumba yako,Wala beberu katika mazizi yako. *

Maana kila hayawani ni wangu,Na makundi juu ya milima elfu.” (Zab 50:9-10)

“ ‘Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi.” (Hag 2:8)

Mungu hahitaji fedha zetu. Dhahabu ni mali yake, fedha ni mali yake, ng’ombe juu ya vilima elfu ni mali yake, na, kama ambavyo ingetegemewa, Mungu anasema kwamba hata vilima elfu moja ni mali yake. Tunapotoa, tunatoa kwa Bwana, siyo kwa wanadamu (2 Kor 8:5), siyo kwa sababu Bwana anakihitaji kipawa chetu, bali tu kwa kusudi la ku-jikumbusha kwamba hicho tunachompa Mungu ni mali yake (Kum 8:18, Kum 15:15, Kum 24:17). Tunafanya kazi kwa sababu Mungu alituumba ili tufanye kazi, na wala siyo kwa sababu Mungu hawezi kutupa mahitaji yetu au Mungu ana uhitaji sana wa fedha zetu. Hata kama unahisi kwamba Mungu anahitaji kukuona ukijishughulisha katika ulim-wengu wa biashara katika kipindi hiki, huhitaji kukubali kukosa kujihusisha kiroho na shughuli za kanisa lako ati kwa sababu uweze “kuwa na kipato kikubwa zaidi kwa ajili ya kutoa zaka kubwa”. Kama katika mawazo yako unaona kwamba Mungu anahitaji fedha yako zaidi ya anavyohitaji moyo wako. Mungu hahitaji watu matajiri kwa ajili ya kuende-leza ufalme wake, bali anahitaji watu walio tayari kwa ajili yake.

A.3. Mungu wa Baraka na Mafanikio

“Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo...” (3Yoh 2 )

Katika kifungu hiki neno “mafanikio” (Kwa Kiyunani, “evodoo”) maana yake ya moja kwa moja “kusaidia njiani au barabarani” au “kufanikiwa katika kufikia.” Moja kwa moja neno hilo lina maana kwamba, mafanikio ya kimungu si jambo linalotokea kipindi fulani na ku-timia bali hali ya mafanikio endelevu na ustawi.Mafanikio yamekusudiwa kwa ajili ya kila eneo katika maisha yetu: ya kiroho, kimwili, misisimko ya hisia zetu na vitu vinavyoonekana tunavyovimiliki. Hata hivyo, Mungu hataki mtu yeyote aweke msisitizo juu ya eneo mojawapo kati ya hayo, mtu lazima aweke ulinganifu katika uwiano wa maeneo yote hayo.

• Mafanikio ya KirohoAngalia Lk 4:18 na 6:27-38.

• Mafanikio ya KiakiliAngalia Fil 4:6.

• Mafanikio ya KimwiliAfya: angalia 1 Pet 2:24, Mk 16:15-20 na Yak 5:16.Mali: angalia 2 Kor 9:8, Lk 6:38 na Efe 6:8.

52

Page 61: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

B. Utoaji

Tunamtumikia Mungu aliye mkarimu kiasi cha kustaajabisha. Sisi tunahitaji kuionye-sha tabia hii kwa kuishi maisha ya ukarimu. Kuna vifungu vingi sana ndani ya Maandiko vinavyotuhimiza tuishi maisha ya ukarimu. “Ni heri kutoa kuliko kupokea.” (Mdo 20:35b) Waumini wa kwanza katika Matendo 2:45 na hakuna yeyote kati yao aliyekuwa na hitaji lolote. “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.” (Lk 6:38). “Lakini nasema neno hili, Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu..” (2 Kor 9:6). Kuna misemo mingi inayohimiza utoaji katika Maandiko.

B.1. Zaka

Huu ni utoaji unaofanyika pale sehemu ya mapato yako (kwa kawaida hiyo huwa ni se-hemu ya kumi) inapotolewa kwa kanisa lako. Kanuni hii ya kutoa kwa uwiano wa kipato ulifanyika hata kabla ya kipindi cha sheria ya Musa Abrahamu anampa zaka Melkizedeki aliyekuwa mfalme (Mwa 14:20). Yakobo anaweka nadhiri kwa Mungu kwamba angempa moja ya kumi ya kila kitu ambacho Mungu angempa (Mwa 28:20-22). Amri ya Agano la Kale iliyoamrisha utoaji wa zaka inapatikana katika Walawi 27:30-33. Hata hivyo, Zaka ilikuwa ni sheria ya uadilifu na siyo sheria ya sherehe au ibada, na kwa hali hiyo sheria hiyo bado inafanya kazi mpaka leo. Yesu aliipitisha sheria ya utoaji zaka kama inavyoonekana katika Mathayo 23:23 na Luka 18:12. Kukosa kutoa zaka kunaonekana kama tendo la kumwibia Mungu na tendo hilo linatuweka katika hatari ya kupata hasara. (Angalia Mal 3:7-12.) Hili ni Andiko muhimu sana. Kuna sheria inayolingana uliwenguni kote ya kupanda na kuvuna: unapopanda mbegu ardhi hutoa mazao, unapoweka fedha katika benki nayo benki hutoa faida kwa ajili ya fedha yako. Unawezaje kumtarajia Mungu aheshimu matakwa yako ikiwa wewe utakuwa hujaonyesha kuiheshimu amri yake ya kutoa, kulingana na Malaki 3?

Mtu yeyote aweza kuona kutoka katika hayo hapo juu kwamba zaka halikuwa suala la sheria, kwamba zaka ilitangulia kabla ya sheria ya Musa, kwamba zaka iliruhusiwa na sheria na pia ikapitishwa na Yesu iendelee kutumika.

Ni matakwa na mfumo wa Kibiblia kwamba watu wanaojishughulisha na huduma kama kazi yao kamili na ya pekee, wapokee msaada wa kifedha kutokana na akiba ya zaka inayotolewa na wale wanaopokea huduma ya watu hao. Katika Agano la Kale Mungu aliamuru kwamba Walawi wapokee zaka kwa sababu wao walikuwa watumishi maalum wa Bwana (Hes 18:21-24). Wao hawa hawakupewa urithi maalumu kama vile ardhi au wanyama, na wala hawakulipwa mshahara.

Yesu alisaidiwa na watu waliotaka kurudisha fadhila kama wale wanawake katika Luka 8:2-3 na Mathayo 27:55. Bwana Yesu hakujipatia mahitaji yake na ya wanafunzi wake kwa njia za kimiujiza. Yuda alikuwa mkurugenzi wake wa hazina na aliangalia vipawa vyote vilivyotolewa na watu. Yesu alisema kwamba mtenda kazi alistahili ujira wake (Mat 10:9-10). Katika Matendo 4:35 tunaona kwamba fedha iliwekwa miguuni pa mitume ili iweze kugawanywa. Tunasisitizwa kuvishiriki vitu vizuri tulivyonavyo na wale wanao-tufundisha (Gal 6:6). Paulo alifadhaika kwa sababu ni kanisa la Filipi pekee lililompa mi-saada mwanzoni mwa huduma yake (Fil 4:15). Paulo anauweka ukweli wazi kwamba fedha ya Bwana ni sharti sisi tuishiriki pamoja na wale wafundishao na kuhubiri Neno la Mungu (1 Tim 5:18). Yeye anatoa hoja kali kwamba ni haki yake kuvuna baraka za kim-wili toka kwa wale aliowatumikia kiroho. Bwana ameamuru kwamba wale wahubirio injili waishi kutokana na injili (Angalia 1 Kor 9:1-15).

53

Page 62: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Twapaswa kutoa zaka mahali pale tunapopokea baraka yetu ya kiroho. Fundisho la Agano Jipya ni kwamba katika hali ya kawaida kila kanisa liweze kujiendesha lenyewe. Zaka ilitolewa kwa mfumo wa mwaka kwa mwaka katika Agano la Kale wakati katika Kipindi cha Agano Jipya ikitolewa juma hadi juma. Inategemea na wakati unapolipwa na malipo hayo yanatakiwa kuwa ni tunda la malimbuko (yaani, malipo ya kwanza unayoya-fanya). Angalia, kwa mfano, Kut 23:19a, Hes 18:12 na Neh 10:35-38.

Kwa muhtasari: zaka kwa ufafanuzi ni sehemu ya kumi ya mapato yote ya mtu (pato kabla ya kodi) mapato yanayowekwa wakfu kwa Mungu. Zaka si jambo la utoaji, ni malipo ambayo sharti yalipwe. Kusema kwamba “tunatoa” zaka ni kupendekeza kwamba zaka ni jambo la hiari wakati Maandiko matakatifu yanaonyesha kwamba ki-nyume cha jambo hilo ndiyo kweli. Fedha hii inatumika kwa ajili ya watu walio katika utumishi wa Mungu. 1 Timotheo 5:17-18 inasema, “Wazee watawalao vema na wa-hesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.” Hivyo, zaka inatakiwa iletwe katika kanisa lako la mahali (ghalani), na siyo kutolewa kwa huduma nyingine au makanisa mengine.

B.2. Matoleo

Fedha hii inatakiwa itumiwe kwa ajili ya “vitu.” Kwa mfano tu, basi tuangalie Kut 25:2 na Kut 25:8-9, “Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya. Nao na wafanye sanduku la mti wa mshita; urefu wake na uwe dhi-raa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.” Angalia pia 1 Nya 29:3-9, Mal 3:8, 2 Kor 8 na 2 Kor 9.

Kwa hiyo kutoa matoleo ni utoaji wa hiari, na ni matoleo yatolewayo kama nyongeza baada ya zaka kulipwa. Biblia hufundisha kwamba Mungu anadai zaka yetu na wakati huo huo akistahili matoleo yetu. Matoleo hayadaiwi yatolewe ndani ya Maandiko. Ni ma-toleo ya hiari.

Kwa muhtasari, tunatumia matoleo kwa ajili ya kununulia “vitu” wakati zaka ikitumika kwa ajili ya “watu.” Mfano unaoonyesha vile matoleo yawezavyo kutumika ni pale yana-potumika kununulia vipaza sauti vipya au matengenezo kwa jengo la kanisa.

B.3. Sadaka

Sadaka ni vipawa vitolewavyo kwa maskini. “Ila neno moja tu walitutakia, tuwakumbuke maskini; nami neno lilo hilo nalikuwa na bidii kulifanya.” (Gal 2:10) “maana imewapen-deza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yeru-salemu walio maskini....” (Rum 15:26).

Kuna Maandiko mengine mbalimbali yanayosisitiza juu ya daraja hili la utoaji:

• Mdo 6:1-4 Kutoa kwa wenye mahitaji.

• Mdo 19:21 Kuuza ulivyonavyo na kuwapa maskini mapato kutokana na uuzaji huo.

• Lk 3:11 wale wenye vingi wakivishiriki na wale wasio na kitu.

• Mdo 11:27-30 Kutoa vipawa kwa wazee ili wavigawe kwa wanaohitaji.

• Rum 12:8 Kutoa kwa ajili ya mahitaji ya wengine.

54

Page 63: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

• Efe 4:28 Kufanya kazi ili tuwe na vitu vya kushiriki na wale wasio na kitu.

• Yak 2:14-17 Kutoa kama kielelezo cha matendo mema yanayoambatana na imani yetu.

• 1 Yoh 3:17 Kuwahurumia wale walio na mahitaji. Tunaamini kwamba wale wenye mahitaji kati ya wanafamilia (1 Tim 5:8) na wenye mahitaji waliopo katika kanisa letu wanayo nafasi ya juu ya kuwa walengwa wa kupokea sadaka inayo-tolewa. Ni jambo la hekima kutoa chakula, mavazi na mahali pa kulala kuliko fedha.

B.4. Kutoa Kiutume

Huku ni kutoa fedha zetu kwa lengo la kuueneza ufalme wa Mungu katika mataifa. Tunapaswa kutoa kwa ukarimu sana kwa ajili ya kufanikisha kusudi la Mungu na kue-neza injili ulimwenguni. Sisi ni watenda kazi pamoja na Mungu (1 Kor 3:9). Tunapaswa kuwa watu wanaomsaidia Yeye atimize mpango wake wa kuukomboa ulimwengu. Tuna-paswa kuona matoleo yetu yakienda ulimwenguni kote, yakiibeba kweli na kuifikisha kwa mataifa. Paulo, mtume, alipokea vipawa kutoka katika makanisa mengi mbalimbali (Fil 4:14-18).

Paulo hakuitumia haki yake ya kupokea misaada ya kifedha kwa kuwa alifikiria kwamba jambo hilo lingekuwa kikwazo kwa watu kushindwa kuipokea injili katika mji wa Korintho (1 Kor 9:16-18). Na kweli tunaona katika baadhi ya Maandiko (Mdo 18:3, Mdo 20:34, 1 Kor 4:12, 1 The 2:9, 2 The 3:8) kwamba Paulo hakuona aibu kuifanya kazi yoyote am-bayo ingemsaidia katika kazi ya kuieneza injili.

Hakutaka kuwategemea wengine na kuwalemea. Ushirika wa Cornerstone, kama kanisa, hutoa kwa huduma iitwayo New Covenant Ministries International(NCMI) na huduma nyingine na huduma zilizo jirani zinazofikia maeneo ya mbali, na kila mshiriki anatiwa moyo kufanya hivyo, ikiwa ni pamoja na kuwabariki wale wanaoanzisha makanisa mapya.

B.5. Dondoo Za Kusaidia

• Toa zaka asilimia kumi (10%) ya mshahara wako wote (kiasi kinachotozwa kodi) kwa kanisa lako la mahali.

• Zaka inatakiwa iwe ni malimbuko. Toa zaka pale upatapo mshahara wako, malipo ya kibarua au mapato mengine.

• Weka alama ya wazi juu ya bahasha inayoonyesha moja ya mafungu haya manne: zaka, matoleo, sadaka au ya kiutume. (kwa mfano, unaweza kuweka alama inayoonyesha kwamba nusu ya matoleo ndani ya bahasha iliyowekwa ka-tika chombo cha sadaka ni zaka wakati nusu nyingine ni sadaka ya kawaida.)

• Usitoe kwa sababu watu wengine wamekufanya utoe, bali utoe kwa sababu una-ona ni vema kutoa.

• Mungu humpenda atoaye kwa moyo wa ukarimu (2 Kor 9:6-8). Usitoe kwa kusi-tasita.

• Fikiri kabla ya kutoa ahadi kwa sababu baada ya kuitoa utalazimika kuitimiza

B.6. Muhtasari

55

Page 64: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Moyo wa Agano Jipya ni hali ya kuwa watoaji wakarimu katika kila aina ya matukio (hali ya kuwa wenye mtindo wa maisha ya utoaji).

Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee,Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa

Wala mzao wake akiomba chakula.Mchana kutwa hufadhili na kukopesha,Na mzao wake hubarikiwa. (Zab 37:25-26)

“Heri atendaye fadhili na kukopesha;Atengenezaye mambo yake kwa haki. (Zab 112:5)

“Mtu mkarimu atafanikishwa,amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa.” (Mith 11:25)

“Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa;Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.” (Mith 22:9)

Angalia pia 2 Kor 9 na 1 Tim 6:18.

C. Fedha na UaminifuKile tunachokifanya na fedha zetu, ni vitu avitumiavyo Mungu ili kutujaribu aone kama tutakuwa ni watu waaminifu au la: kuamua ni nani anayestahili ashughulikie utajiri wa kiroho: “Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwa-minifu katika mambo makubwa. Kama basi, ninyi si waaminifu kuhusu mali mbaya za dunia, ni nani atakayewakabidhi zile mali za kweli? Na kama ninyi si waaminifu kuhusu mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewakabidhi mali yenu wenyewe?” (Lk 16:10-12). Endapo tutakuwa waaminifu kwa kidogo tutaweza kuaminiwa kwa kupewa zaidi—soma mfano wa talanta katika Mat 25:14-30:

Uaminifu wetu katika suala la fedha hupata mfano unaokuwa kielelezo kwa namna tunavyopangilia matumizi na kutumia mali tunazopewa na Mungu.

C.1. Mpangilio wa Mapato na Matumizi

Mpangilio wa matumizi siyo zaidi ya mpango unaoonyesha matarajio ya kipato chako na matumizi yatakayotokana na kipato hicho. Wote tunapaswa kupangilia mapato na ma-tumizi yetu kama njia ya uwakili wetu kwa Mungu utakaoonyesha jinsi tunavyotawala fedha zetu.

C.2. Kwa Nini Tupangilie Mapato na Matumizi

Kupangilia mapato na matumizi hutusaidia kuweka kipaumbele kwa ajili ya matumizi yetu. Tunapaswa kufanya uamuzi ni matumizi gani yatakayohitajika kulipiwa kwanza na matumizi hayo ni ya aina gani, labda ni matumizi yasiyobadilika mwezi kwa mwezi au yanayotofautina (kutegemeana na matumizi kwa mfano kutegemeana na vipimo vya umeme unavyotumia kwa kila mwezi husika), mfano matumizi ya umeme na maji.

56

Page 65: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kupangilia mapato na matumizi kunatusaidia kuwa makini na mapato yetu na pia ku-tawala mtiririko wa kutoka na kuingia kwa fedha zetu, jambo hili likitupa kuona kwa upana zaidi hali yetu ya kifedha. Kupangilia mapato na matumizi hutusaidia kupanga mipango yetu ya baadaye.

Sababu zinazofanya tusiweke mpangilio wa mapato na matumizi ni ama uzembe, uvivu, kutokujua, hofu au mchanganyiko wa vyote hivyo. Mpangilio wetu wa mapato na matu-mizi unapaswa kutumiwa kama mwongozo. Nidhamu za kifedha na maamuzi ya kifedha ya kila siku yanapaswa yaendane na mwongozo katika mpangilio wetu wa mapato na matumizi.

Mchakato huu unahitajika ili kuhakikisha kwamba unaishi sawasawa na uwezo wa kipato chako. Kanuni inayotakiwa kutawala mambo yote inatakiwa iwe kwamba matumizi yetu na maamuzi ya kifedha yataambatana na fedha tunayolipwa kama mshahara au tunay-opokea. Endapo tutakuwa hatuishi kwa kufuata kanuni hii itakuwa na maana kwamba tunatumia fedha tusiyokuwanayo na hii ikiwa na maana kwamba tunaishi katika deni.

C.3. Deni

Deni hutuweka chini ya mamlaka ya wengine na kutufanya tushindwe kuwa na uhuru wa kujiamulia chochote ambacho Mungu aweza kututaka sisi tukifanye. Deni hutusababisha tuwaangalie wanadamu na mfumo wa ulimwengu kwa ajili ya mahitaji yetu badala ya kumwangalia Mungu. Biblia ina mengi ya kusema juu ya deni.

“Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.” Rum 13:8.

“Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu.” 1 Kor 7:23

“Tajiri humtawala maskini, naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.” Mith 22:7

“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtu-mikia Mungu na mali.” Mat 6:24

Unapokuwa tayari umo katika hali ngumu ya kifedha, tendo hili la kumuasi Mungu kwa kukopa madeni hukuingiza katika deni zaidi (Kum 15:5-6; 28:1-2,12 )

D. Kutengeneza Mambo Ya Nyumba Zetu

“Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, ‘Tengeneza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona” (2 Fal 20:1).

Kuweka hali yetu ya kifedha ni jambo la kipaumbele. Tunapoanza kufanya kile Mungu anachotaka tufanye katika eneo hili tunaonyesha utiifu wetu na hivyo kufungua mlango kwa ajili ya baraka za Mungu. Tunahitaji kujiwekea akiba kwa ajili ya matukio ya dharura na vifo.

Kama tutakuwa watu wasiofikiria na kujiwekea akiba kwa ajili ya baadaye tunaweka mzigo mkubwa juu ya wale watakaojikuta wanawiwa kuja na kuyaweka vizuri mambo ya nyumba zetu. Tendo la kuandaa Wosia ni jambo la muhimu sana na la lazima katika ku-timiza ada ya uwakili wetu.

57

Page 66: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Pia ni jambo la muhimu kufanya nakala za hati zote muhimu, mfano vyeti vya utam-bulisho (vitambulisho), hati za kusafiria (paspoti), hati za ndoa, n.k. na kuziweka mahala palipo salama. Hakikisha kwamba wanafamilia wote wanajua mahali hati hizo zilipo en-dapo dharura yoyote itatokea.

E. Thawabu au Tuzo za Utii

Mungu huheshimu utii kuliko dhabihu/sadaka (1Sam 15:22). Yeyote atoaye kutokana na maelekezo ya Mungu atapokea baraka na tuzo ambazo hazifikiriki kwa mawazo ya kib-inadamu.

Kumbuka Malaki 3:10: Mungu anaahidi baraka nyingi, za kimwili pamoja na za kiroho pia. Pia atazilinda mali zetu (Mal 3:11, Kumb 11:13-15; 28:12) dhidi ya maadui zetu, wadudu waharibifu, hali mbaya ya hewa, falme na mamlaka za giza.

Kulingana na Malaki 3:12, mataifa yanayotuzunguka yataziona baraka zitokanazo na kumtolea Mungu kwa ukarimu. Katika maisha yetu ya kibinafsi na kifamilia, watu wataweza kuona utajiri wa kiroho na baraka tunazozipokea.

Kusudi la Mungu juu ya Kanisa ni kwamba tuweze kuwa kama nchi ya kupendeza: Paradiso izaayo matunda tele. Ahadi ya Mungu kwamba atatumwagia baraka imejengwa juu ya sharti kwamba sisi tuwe watiifu kwa Neno lake na pia tuwe watoaji. Hii ni hali pe-kee katika Maandiko ambamo ndani yake tunaambiwa tunaweza kumjaribu Mungu (Mal 3:10).

Angalia pia Mith 19:17, Mith 25:22, Eze 44:30, Mat 5:43-48, Lk 6:35; 12:33; 14:12-14, Rum 12:13, Ebr 13:2, 1 Pet 3:9 na 3 Yoh 8.

Jim Elliot, mtumishi wa Mungu aliyekwenda katika huduma ya kitume kwa kabila la Waauka, kabila lililoishi katika bonde la mto Amazon huko katika Bara la Amerika ya Kusini, alisema maneno haya kipindi kifupi kabla ya kuuawa kwake na watu wa kabila hilo, akiwa bado na umri mdogo wa miaka 29; “Hawi mpumbavu mtu atoaye kitu ambacho hana uwezo wa kukihifadhi, ili apate kile ambacho hataweza kukipoteza.”

58

Page 67: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

F. Mnyororo wa Fedha na UtoajiKwa kutumia Maandiko yaliyonukuliwa katika sura hii, chagua Maandiko ambayo yameugusa sana moyo wako na uyatumie kujitengenezea mwenyewe mnyororo wako.

59

Page 68: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kumi: Kanisa

Ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho (Efe 3:10)

Moja ya mitazamo ya msingi na iliyo ya muhimu zaidi juu ya kuwa Mkristo ni ushirika na kujihusisha katika shughuri za kanisa. Kwa sababu hiyo tunataka kuchunguza ili kuona kanisa ni nini, linafanya nini na kwa nini hilo ni muhimu kwa ajili yetu.

Neno “kanisa”, ni tafsiri kutoka katika neno la Kiyunani “ecclesia (eklesia),” neno lenye maana ya kusema “watu walioitwa,” likiwa na maana ya wale walioitwa na Yesu kutoka katika jamii yote ya kibinadamu iliyoanguka, yaani ya ulimwengu: wale walionunuliwa naye, watu ambao ni mali yake.

Neno hili hutuambia angalau mambo mawili yaliyo makubwa na muhimu:

• “Kanisa” halina maana ya jengo au shirika fulani isipokuwa tu lina maana ya kundi la watu. Kwa hivyo swali siyo, “Kanisa ni Nini?” bali, “Kanisa ni Nani?”

• Kanisa lina chanzo maalumu na utambulisho.

Biblia (na hasa kitabu cha Waefeso) inatupa sura au taswira au picha (mifano) kadhaa za kanisa ambazo zikiwekwa pamoja hutupa uelewa kamili wa utambulisho na tabia zake zinazolitofautisha na jumuia za namna nyingine, pia mfumo, uongozi pamoja na utume au kusudi teule la kanisa.

A. Kanisa Lionekanavyo Ndani ya Kitabu cha Waefeso

A.1. Watu/Taifa

“Kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo…” (Efe 2:12-13)

“Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na wataka-tifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.” (Efe 2:19)

“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamku-pata rehema, bali sasa mmepata rehema.” (1 Pet 2:9-10).

Sura hii inayoonekana kutokuwa na madhara kuliko sura zote za kanisa yamkini ndiyo iliyo yenye nguvu kuliko zote. Katika Agano la Kale majina haya yanayoonyesha daraja au cheo yalilindwa kwa wivu mwingi na yalijulikana kama vyeo vilivyolielezea taifa la Is-raeli. Ni Israeli peke yao kati ya mataifa yote ya ulimwengu waliojulikana kama watu wa Mungu, waliokuwa wameitwa kutoka kati ya mataifa ya dunia (Kut 19:5-6). Asili yao hiyo ya kipekee (ya kuchaguliwa na Mungu) iliwapa nafasi ya pekee na ya heshima, utam-bulisho, kusudi na hatima ya uelekeo wao (nafasi kama kuwa na agano na Mungu, kuwa

60

Page 69: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

wapokeaji wa ufunuo maalumu, kuwa na jukumu la kitume kwa mataifa na kuwa taifa ambalo ndani yake uzao wa Masihi ungetokea).

Sasa Agano Jipya bila kuchelea, linavitumia vyeo vyote hivi kwa kanisa. Juu ya hesabu ya Wayahudi wenye kuamini kumeongezwa juu yake watu wa Mataifa wanaoamini ili kufanya Agano moja Jipya la watu wa Mungu (Efe 2:14-18), Kanisa, ambalo sasa li-naitwa “Israeli wa Mungu” (Gal 6:16). Kanisa ni Israeli mpya (wa kweli), utimilifu wa watu wa kale wa Mungu katika siku za mwisho (eschatological). Unapoliangalia hili katika mpangilio wa muda, Kanisa linafuata baada ya kuwekwa na kuwepo kwa taifa la Israeli la kale; lakini uteuzi wa kanisa kuwepo ulitangulia ule wa Israeli wa kale: hilo la kwanza lilikuwa la maandalizi, na sasa limeshazidiwa kwa ubora na hilo la karibuni—sawa na ilivyo kwamba Agano la Kale lilikuwa ni maandalizi na sasa limeshazidiwa kwa ubora na hilo Jipya (chunguza kwa makini uone jinsi 1 Pet 2:9-10 inavyochukua maneno ya kitabu cha Kutoka 19:5-6 na kuyatumia kwa kuelezea Kanisa).

Hivyo, Kanisa kama Israeli wa Agano la Kale, lina asili maalumu ya kipekee na ya kimungu (kuchaguliwa na Mungu: lilianzishwa na Mungu mwenyewe aliyelichagua kwa mapenzi yake mwenyewe kutoka katika mataifa yote ya ulimwengu). Kwa hali hii, Kanisa lina utambulisho au cheo cha kipekee na cha kimungu (agano), wajibu (utume) na hatima ya uelekeo (mbingu mpya na nchi mpya). Kupitia kipindi chote cha historia, Mungu amekuwa akitafuta watu watakaokuwa washirika wake wa Agano, watu ambao anaweza kuwa na ushirika nao na kuwafanya walishiriki pendo lake na uhai wake wa milele. (kile kijulikanacho kama mpango wa agano, kwa maneno, “Nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu,” ni kauli inayojirudia sana ndani ya Maandiko matakatifu.) Agano Jipya ni agano lililo kamili na la mwisho, na watu wa agano hili – Kanisa – ndiyo watu hao!

“Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao wata-kuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.” (Ufu 21:3)

Sura hii ya Kanisa inatuonyesha kwamba:

• Wakati ambapo kanisa kimsingi siyo sawa na shirika fulani, linahusisha kuwa na muundo na hali ya kiutawala ndani yake; viongozi wa kanisa hutawala, kuonyesha uele-keo na kushughulikia mambo muhimu ya kiutawala kati ya watu wa Mungu (kusimamia hali ya utaratibu/mpangilio, uadilifu na haki).

• “Raia” huwa na vyote viwili yaani wanazo haki zao na pia wajibu kuelekea jamii wa-nayoishi ndani yake (sawa na raia wengine katika jamii yoyote ile kati ya mataifa duni-ani).

A.2. Familia/Nyumba

“Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na wataka-tifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.” (Efe 2:19).

“Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; * na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.” (Rum 8:16-17)

Angalia pia Rum 8:14-17 na Gal 3:26-4:7.

Kanisa juu ya mambo yote ni familia ya waumini. Hii inamaanisha kwamba wao ni kundi la watu wanaounganishwa kimsingi na uhusiano na wala siyo mfumo au mpangilio, wala utendaji au kushiriki imani moja na matendo au kushiriki maono mamoja au kuwa na

61

Page 70: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

tathmini moja ya mtazamo kuhusu maana au thamani (japokuwa baadhi ya hivi huon-geza kuimarika kwa umoja). Hii ndiyo sababu kuna methali zisemazo: “Kanisa ni kitu chenye uhai na wala siyo shirika au chama” na “urafiki kabla ya utendaji.”

Sisi sote tu watoto wa Mungu (Yn 1:12, 1Yoh 3:1-2) na pia ni warithi wake. Yesu ni kaka yetu nasi tunarithi naye. Sisi ni kaka na dada kwa waumini wote wengine. Familia ya kawaida ya wamchao Mungu, ni mahali penye mazingira ya upendo kwa wote, mahali ambapo kila mwanafamilia anakubalika, mahali penye pumziko na uhuisho, na ni mahali ambapo ndani yake watu wanaweza kukua wakiwa salama na huru, mbali ya mazingira yenye vitisho kadiri wanavyopokea maelekezo, kutiwa moyo, kusaidiwa, kusahihishwa wanapokosea na nidhamu au kuadibishwa. Yote haya yanatakiwa yawe ni hali zilizo za kweli ndani ya mazingira ya kanisa. Ndani ya sura hii viongozi hutenda kama wazazi, wanaolea na kukuza watoto wao wa kiroho—lakini hata walio wadogo kuliko wote wanaweza kuwa na msaada kwa “ndugu zao” katika njia tofauti japo pengine itakuwa ni misaada midogomidogo.

A.3. Jengo/Hekalu

“Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu ka-tika Bwana.” (Efe 2:21)

“Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.” (1 Kor 3:16-17)

Angalia pia 1 Pet 2:4-8.

Kanisa ni jengo ambalo Yesu ni jiwe kuu la pembeni au la msingi, na pia Yeye ni mjenzi wake mkuu. Kwa hali hii anahakikisha kwamba linakua na kuwa katika hali ya umoja. Anajenga akifuata mpango/ramani ambayo imeandaliwa tayari (chochote kisichojengwa juu ya jiwe la pembeni/msingi sahihi si Kanisa. Analisafisha na kuliweka vizuri kila jiwe kabla hajaliingiza katika mahali pake ndani ya lile jengo; neno la Kiyunani lililotumiwa na Petro kumaanisha “jiwe” siyo “petros” (neno lenye maana ya “mawe yasiyochongwa”) bali neno “lithos” (lenye maana ya mawe yaliyochongwa kwa ustadi): kwa hali hiyo jengo linakua kwa kuongezeka ubora na ukubwa. Viongozi wa kanisa ni wajenzi wasaidizi, wakisaidia katika kusafisha na kuyaweka mawe yaliyoandaliwa mahali pake na kwa hali hiyo kusaidia kuliinua juu jengo lote. Sura hii inalionyesha kanisa kama kitu kilicho imara, cha kudumu na kinachoonekana kwa ulimwengu.

Zaidi ya hayo, Kanisa ni aina maalum ya jengo, kwa maana ya hekalu (“hekalu takatifu,” “Nyumba ya Mungu” na “nyumba ya kiroho”). Katika Agano la Kale hekalu lilikuwa ma-hali Mungu alipokaa (kwa hali hiyo lilikuwa takatifu na lenye utukufu) na mahali mataifa yote walipokuja kukutana na Mungu na kupata wokovu. Sasa Kanisa ndilo hekalu la Mungu, mahali akaapo kwa njia ya Roho wake. Kwa hali hiyo, Kanisa ni takatifu (Neno la Kiyunani lililotafsiriwa “hekalu” katika mistari hii siyo “hieron,” linalotumika kuonyesha uwanja wote wa hekalu, bali “naos,” lenye maana ya Palipo Patakatifu Sana), ni mahali ambapo utukufu wa Mungu huonekana (2 Kor 3:18), na mataifa ya ulimwengu yalipaswa kufika hapo ili yaweze kupata ujumbe unaohusu wokovu wao (1 Tim 3:15).

A.4. Ukuhani

“Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.”(1 Pet 2:5)

62

Page 71: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

“Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Pet 2:9)

Angalia pia Ufu 1:6.

Kanisa siyo tu hekalu yaani mahali Mungu akaapo, bali pia Kanisa hilo hilo ni ukuhani unaomhudumia Mungu ndani ya hekalu hilohilo. (Sura hii imejificha ndani ya Barua kwa Waefeso lakini iko wazi kabisa kila mahali penginepo.) Tofauti na ilivyokuwa katika Agano la Kale, ambamo ni baadhi tu ya watu wa Mungu waliokuwa makuhani, katika Agano Jipya watu wote wa Mungu ni makuhani, hii ina maana kwamba, Kanisa lote ni ukuhani; waumini wote ni makuhani wanaomhudumia Mungu, waumini wenzao na ul-limwengu. (tumekwisha kuona kwamba waumini wote ni sehemu ya hii “naos” mpya, yaani Mahali Patakatifu Sana, na kwamba waumini wote wanaweza kuingia na kuabudu katika sehemu hiyo.) “Dhabihu za kiroho” watoazo ni pamoja na nafsi zao wenyewe, sala, sifa, fedha, na uenezaji wa Injili. Kanisa, zaidi ya hayo, ni “ukuhani wa kifalme” kwa sababu limetengwa na kuwekwa wakfu na Mfalme linayemhudumia na pia Kanisa hilo hilo ni “ufalme wa makuhani” kwa sababu Mungu anatawala juu ya Kanisa na kwa sa-babu kutokana na huduma yake Kanisa linaupanua ufalme wa Mungu na kutawala pa-moja na Kristo. Kama vile makuhani wa Agano la Kale walivyohudumu kwa niaba ya ndugu zao Waisraeli waliokuwa hawawezi kuingia hekaluni, waumini katika Agano Jipya wanahudumu kwa niaba ya wale ambao hawawezi kuingia ndani ya uwepo wa Mungu —hii ina maana, watu wasioamini—kwa njia ya sala, vita vya kiroho, uenezaji wa injili na huduma za vitendo.

A.5. Mwili

“Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.” (Rum 12:5)

Angalia pia Efe 4:1-16, Rum 12:3-8 na 1 Kor 12:12-27.

Mwili wa Kristo ni sura inayotawala ndani ya Agano Jipya na sura hii inabeba takriban kweli kuu nne ambazo ni muhimu sisi tuzijue.

• Kila mwili ni lazima uwe na kichwa. Kichwa cha mwili huu ni Yesu (Kol 1:18). Yesu si kichwa cha kawaida tu, au kichwa cha jina tu kinachokuwepo lakini kisiwe na kazi (kama mtu anayepewa heshima ya kuwa raisi wa maisha au wafalme/malkia katika dola za ki-falme ambazo mamlaka za serikali zinakuwa chini ya mawaziri wakuu), bali yeye ni kiongozi halisi wa siku kwa siku, kiongozi aongozaye na kutenda ipasavyo, kichwa cha Kanisa na mwenye uwezo. Kuwa kwake kichwa kuna maana kwamba analitawala Kanisa (Efe 1:22-23) na (kama ilivyo kwamba kichwa cha mto ni chanzo chake) Yeye ndiye chanzo cha uzima wa Kanisa, mwenye kulilisha na kulidumisha (Efe 4:15-16, Kol 2:19). Yesu ni kichwa pekee: hakuna mwingine awezaye, na anayeweza hata kujaribu, kujiweka mwenyewe juu ya Kanisa kama kichwa (mwili wenye vichwa viwili ni jitu!). Ki-nyume chake, mahali ambapo Yesu anakuwa haruhusiwi kuwepo kama kichwa, hapo hapana mwili tena: hii ina maana kwamba, mahali Kanisa linapoondoka na kwenda mbali na utawala na mfumo wa kichwa, Kanisa hilo hukoma kuwa mwili wa kweli wa Kristo (nao mwili usio na kichwa ni jitu!).

• Kama ilivyo kwamba mwili waweza tu kuwa na kichwa kimoja, vivyo hivyo kichwa na-cho chaweza tu kuwa na mwili mmoja. Lipo Kanisa moja tu la kweli (kichwa chenye viwi-liwili vingi ni aina ya tatu ya jitu!), na vyovyote vile kuonekana kwake kulivyo, Kanisa hilo lina umoja unaotokana na kuwa na kichwa kimoja.

63

Page 72: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

• Kama ilivyo kwamba mwili wa kawaida una viungo vingi vilivyo tofauti, na kila kimoja kikiwa ni cha muhimu kwa ajili ya utendaji wa mwili mzima, vivyo hivyo mwili huu wa ki-roho unafanywa na watu wengi tofauti, ambao kila mmoja ana vipawa na huduma tofauti lakini ambao mchango wao ni wa lazima kwa ajili ya utendaji mzuri na mafanikio ya Kanisa zima.

• Kanisa, kama mwili wa kiroho wa Kristo, linaendeleza katika kipindi hiki kazi yote ali-yoianza Yesu alipokuwa duniani katika mwili. Sisi ni vifaa ambavyo kupitia hivi Yesu an-aendeleza kazi yake katika jamii ya wanadamu.

Hapa viongozi ni kama mfumo wa mishipa ya fahamu, wakipitisha maamrisho ya kichwa na kuyapeleka katika kila sehemu ya mwili. Wao wanahakikisha kuwepo kwa hali ya afya na utendaji mzuri kwa kila kiungo.

A.6. Bibi Arusi

Angalia Efe 5:22-32.

Kanisa ni bibi arusi wa Yesu. Alikuja kumchumbia na kumfanya ampende (Pendo lake linawavuta watu kwake) na alilipa mahari iliyopasa kwa ajili yake (Aliwakomboa watu ili wawe watu wake); sasa anawakamilisha na kuwafanya wakomae; mwisho wa nyakati atarudi ili aoe na kusherehekea pamoja na bi-arusi wake karamu ya arusi ya mwanak-ondoo (Ufu 19:6-9). Kama bwana arusi wa kale katika nchi za mashariki, baada ya karamu ya arusi atamchukua bi-arusi na kwenda naye hadi nyumbani kwa Baba yake (Yn 14:2-3) na hapo ataishi naye milele (Ufu 21:1-3). Sura hii inaonyesha upendo mkubwa na wa karibu uliopo kati ya Yesu na Kanisa, pendo linaloonyeshwa katika ibada za Kanisa, lakini pia katika maisha na matendo yote ya Kanisa, yanayotokana na up-endo wa Kanisa kwa Yesu. (Pendo hili linaonyeshwa katika kivuli cha kiunabii katika adhimisho kubwa la mahaba na penzi la kimwili kati ya Mpenzi na Mpendwa wake katika Kitabu cha Wimbo Ulio Bora.) Kama sura nyingine, sura hii inafichua uteuzi wa Mungu kutokana na mapenzi yake mwenyewe, na pamoja na uteuzi huo kuna faida (nafasi ya upendeleo, Yesu akijitoa kwa ukamilifu pasipo kusaza kwa ajili ya bibi arusi) na wajibu (kumtii, kumtumikia na kumtukuza Bwana Arusi). Na kwa kadiri uhusiano huu ulivyo wa ajabu katika kipindi hiki, bado hiki ni kipindi cha uchumba: arusi, kamilisho la uhusiano wa ndoa na maisha ya pamoja bado yanatusubiri! Katika sura hii viongozi wa kanisa hu-fanya kazi kama matowashi (wanaume waliohasiwa wasiwe na nguvu za kiume, wasio-thubutu kumchafua bibi arusi kwa tamaa yao wenyewe bali wakifanya kazi ili wamfikishe bibi arusi akiwa mkamilifu kwa Bwana Arusi.

A.7. Jeshi

Angalia Waefeso 6:10-18.

Mungu ni mpiganaji (Kut 15:3); Yesu anafanya vita (Ufu 19:11). Kanisa ni jeshi la Mungu, linalousukuma nyuma ufalme wa giza na kuupanua ufalme wa nuru. Kanisa linafanya haya katika kila eneo la maisha yake na huduma: katika uenezaji injili, uponyaji, katika maombi ya ukombozi na maombezi kwa waliofungwa hali hii ya vita inakuwa jambo lililo wazi (Mat 12:29; 16:18, Mk 16:15-18, Lk 10:17-19, 2 Kor 10:3-5). Lakini Kanisa katika mafundisho yake (kuwaweka watu huru kwa kuwaletea ukweli, kukanusha mafundisho ya uongo na upotofu na kuhuisha akili), uchungaji (kuponya maisha yaliyopondeka au kuvunjika) vitendo kwa jamii (kwa mfano, kupambana na umaskini aidha kwa kuwalisha maskini au kupigana na vitendo vya ukandamizaji vinavyosababisha umaskini), pia Kanisa kwa kuyafanya hayo linajihusisha na vita vya kiroho. Kwa kifupi, kama vile Kanisa linavyoendeleza kazi zote za Yesu, vivyo hivyo Kanisa linaendelea kuziharibu kazi za yule mwovu (1 Yoh 3:8).

64

Page 73: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Ukweli kwamba Kanisa ni jeshi linalojihusisha na vita unaleta maana nyingine ya maisha ya Kanisa na huduma yake kama vile: maarifa ya kumjua adui (malengo yake na mi-kakati); mafunzo na hali ya uimara; ghala la silaha na silaha zenyewe; mbinu za kushambulia; nidhamu na utiifu kwa amri. Katika sura hii viongozi wa Kanisa ni maafisa wanaoongoza na kuliamrisha jeshi katika hatua mbalimbali za vita vyake.

B. Utume na Agizo

Sura nyingine za Kanisa, ziwe zinazoonekana wazi au zilizojificha, zaweza kupatikana ndani ya Maandiko – kwa mfano, Kanisa kama kundi la Mungu, shamba, wasafiri, mtu-mishi na adhimisho takatifu (sakramenti) – lakini sura hizo saba zilizotajwa hapo juu zita-tosha kwa sasa. Kwa pamoja zinatupa wazo lililo wazi kuonyesha Kanisa ni nani na ameitwa kufanya nini. Tunajiona kama wenye kuingia katika hatari ya kurahisisha mambo kuliko ipasavyo, lakini tunaweza kusema kwamba Kanisa lina kusudi moja au mawili katika kuelekea kila moja ya pande nne za mahusiano yake:

• Kumwelekea Mungu: ibada na sala.

• Kati yetu sisi wenyewe: ushirika na kuelekezana.

• kuuelekea ulimwengu: Uenezaji wa injili na huduma za vitendo.

• Kumwelekea shetani (na washirika wake): vita vya kiroho.

Kanisa linaendeleza kazi ya Yesu. Kila kitu alichokuja Yesu kukifanya: Alikuja kuuan-zisha ufalme wa Mungu. Hivyo kifupi,Kanisa limeitwa kuuendeleza ufalme (utawala) wa Mungu. Katika kuwepo kwake, Kanisa linakuwa kama mfano wa ufalme; katika kunena kwake, linautangaza ufalme; katika vitendo vyake, linafanya kazi kwa ajili ya ufalme. Kanisa ni pamoja na uthibitisho wa kibao chenye tangazo linaloashiria, pia kanisa ni wakala mahsusi wa Ufalme. Mafanikio ya kusonga mbele kwa kanisa ni mafanikio ya kuja kwa ufalme wa Mungu katika kipindi hiki tulichonacho.

C. Kanisa Ulimwenguni na Kanisa la Mahali

Mahali popote Agano Jipya linapozungumzia “kanisa” lina maana moja kati ya hizi mbili:

C.1. Kanisa Ulimwenguni

Kanisa ulimwenguni, ambalo mara nyingi huitwa Kanisa (herufi ya kwanza kubwa), ni jumla ya kundi lote la waumini wa kweli walioko mahali pote ulimwenguni na wote wale waliokuwepo duniani huko nyuma lakini sasa hawapo (wale ambao majina yao yamean-dikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo), watu ambao utambulisho wao kamili unajulikana kwa Mungu peke yake tu. (Kwa hali hiyo, wakati washirika wote wa kanisa ulimwenguni wanapaswa kuwa washirika wa kanisa la mahali, si washiriki wote wa kanisa la mahali walio washiriki wa kanisa la ulimwengu.)

C.2. Kanisa la Mahali

Kanisa la mahali, ambalo mara nyingi huitwa tu kanisa, ni kielelezi imara cha kanisa ulimwenguni kwa nyakati zote, zilizopo na zijazo na mahali pote, hii ina maana ya ju-muiya ya waumini inayoonekana katika mahali maalum na kipindi maalum. Ni kweli pia,

65

Page 74: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

kwamba pale kanisa la mahali linapoondoka chini ya utawala wa Kristo, ambaye ndiye kichwa, licha ya kuendelea kuitwa kanisa, halitaendelea kuwa sehemu ya Kanisa ulim-wenguni (Ufu 2:5).

Kanisa la ulimwenguni na kanisa la mahali ndizo maana mbili pekee za neno “ecclesia (eklesia)” katika Maandiko. Biblia kamwe huwa haiongelei dhehebu, utaifa, yahusuyo ukoo au makanisa mengine. Kila kitu tulichokisema juu ya utambulisho na wito wa Kanisa kimeangalia hali ya ujumla wake na kinalihusu kanisa la ulimwenguni. Makanisa ya mahali yaweza kujichagulia mfumo, maono n.k. na sehemu ya mwisho ya mafunzo haya itatumika kutambulisha uongozi wa kichwa, ada ya moyo (uchaguzi wa thamani), na tumaini (au maono) ya kanisa hili.

D. Wewe na Kanisa

Tunaanza kwa kuuliza:

• Kanisa ni nini na wito wake ni nini?

• Ni kwa nini kanisa ni sehemu muhimu ya maisha ya muumini? Kwa kujibu swali la kwanza tunakuwa tumelijibu tayari swali la pili kwa sehemu kubwa. Kila muumini wa kweli anakuwa moja kwa moja sehemu ya kanisa la ulimwenguni wakati anapozaliwa mara ya pili. Lakini kama ilivyo kwamba kanisa la ulimwengu linatakiwa lifanywe kuonekana katika kipindi na mahali husika ili liweze kuleta mabadiliko na kuwa na maana ya kuwepo kwake, vivyo hivyo muumini binafsi anapaswa kuwa sehemu ya kanisa la mahali ili kuwe na uhalisi wa ukiri wake na imani. Siyo tu kwamba ni jambo lisi-lowezekana kusalimika na kukua kama Mkristo katika hali ya kujitenga, wazo kama hilo ni geni kabisa katika Maandiko. Hakuna mwongofu aliyekuwa mfuasi wa “Mungu-Yahweh” katika Agano la Kale pasipo kuwa mshirika wa Israeli; neno “mtakatifu” halitajwi kabisa katika umoja ndani ya Agano Jipya lakini mara zote linatajwa katika wingi. Kum-penda Mungu na kuwa mali yake ni kuwapenda watu wake na kuwa mali yao.

Mkristo analihitaji kanisa la mahali kwa yote atakayoweza kuyapokea (maelekezo, kuchungwa na ushirika) na kwa kile atakachokitoa (vipawa na huduma): kukua ni jambo lisilowezekana kama hivyo vyote havipatikani. Kila taswira ya Kanisa tuliyoiangalia ina-sisitiza juu ya mahali na nafasi maalum kwa muumini ndani ya kanisa. Wajibu wa kila raia kwa ajili ya ustawi wa taifa; kila mwanafamilia ana sehemu na majukumu yanayom-husu katika kusaidia ndugu zake; kila jiwe lina sehemu katika jengo la hekalu; kila muumini ni kuhani anayemhudumia Mungu na wengine; kila kiungo cha mwili lazima ki-fanye kazi yake kwa ajili ya afya na utendaji mzuri wa mwili mzima; askari asiyefanya kazi anahatarisha usalama wa jeshi lote. Kwa hiyo tafuta kanisa la mahali pale unapo-sikia Mungu kukwita, mahali utakapojiweka chini ya uongozi, maono na kadhalika, na jitoe kabisa, jihusishe na ukue!

66

Page 75: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

E. Mnyororo wa Kanisa

1Tim 3:14-15Efe 1:22-23Efe 2:19-22Ufu 1:5-6Rum 12:5Efe 5:25-272Kor 10:3-5Efe 3:10

67

Page 76: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kumi na Moja: Kuwekewa Mikono

“Uichochee karama ya Mungu, iliyo ndaniyako kwa kuwekewa mikono yangu.”(2 Tim 1:6)

Ni nini kinachoweza kueleweka kutokana na kauli hii, “kuwekewa mikono”?

“Kuwekewa mikono” ni kitendo cha mtu mmoja kuweka mikono juu ya kichwa cha mwingine kwa madhumuni maalumu ya kiroho. Kwa kawaida tendo hili huandamana na sala au tamko la kiunabii au vyote viwili.

Tendo la mtu kumwekea mikono mtu mwingine si tendo liendalo kinyume na tabia za kawaida za kibinadamu. Kwa mfano, mtoto anapolalamika kuumwa na kichwa au homa, ni jambo la kawaida ambalo mama wa mtoto hulifanya hata bila kufikiria yaani kumwe-kea mkono mtoto kichwani kama namna ya kumpunguzia mtoto maumivu. Ndani ya kanisa, tendo la kuweka mikono laweza kuchukuliwa kama mwendelezo wa tabia ya kib-inadamu. Hata hivyo, tunayo mamlaka ya Maandiko yenyewe yanayoliweka tendo hili katika ya mafundisho makuu ya msingi katika Ukristo.

A. Kutoa Baraka, Mamlaka na Uponyaji

Kuwekewa mikono kwa kawaida huwa na uwezekano wa moja kati ya mambo matatu yafuatayo.

1. Mtu anayeweka mikono juu ya mwingine anaweza kuwa anatoa baraka ya kiroho au mamlaka juu ya yule anayemwekea mikono.

2. Mtu anayeweka mikono anaweza kuwa anaonyesha mbele ya watu wote baraka fu-lani ya kiroho au mamlaka fulani ambayo yule anayewekewa mikono ameyapokea tayari kutoka kwa Mungu.

3. Mtu anayeweka mikono, anaweza kuwa anamuweka mtu mikononi mwa Mungu mbele ya watu wote, kwa ajili ya jukumu maalumu au huduma yule anayewekewa mik-ono.

Mara nyingine, makusudi yote haya matatu yaweza kujumlishwa katika tendo moja hili la kuwekewa mikono.

Tendo la kuwekewa mikono limewekwa kumbukumbu katika Agano la Kale kama tara-tibu iliyokubalika katikati ya watu wa Mungu. Mfano wa jambo kama hilo unaweza kuwa ule wa Yusufu akiwaleta wana wake wawili Efraemu na Manase kwa baba yake Yakobo, ili awabariki. Kwa njia ya Yakobo kuwawekea mikono, baraka ingeingizwa ndani ya wa-nae hao wawili.

Mfano mwingine unaoonyesha matumizi ya kuwekewa mikono katika Agano la Kale ni pale Bwana alipomwambia Musa: “Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu mwenye roho ndani yake, ukamwekee mkono wako, kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; ukampe mausia mbele ya macho yao. Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili mkutano wote wa wana wa Israeli wapate kutii. Kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama Bwana alivyosema kwa mkono wa Musa.” (Hes 27:18-20, 23).

68

Page 77: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Tendo hili la Musa kumwekea mikono Yoshua lilikuwa la muhimu sana kwa Yoshua na pia kwa kusanyiko lote la Israeli. Kwa tendo hili lililoagizwa na Mungu, Musa aliweza ku-hamisha kwa Yoshua kiwango cha hekima ya kiroho na heshima ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameipokea toka kwa Mungu. Yoshua aliweza kutambuliwa mbele ya hadhara ya jamii yote ya Israeli, kama kiongozi aliyeteuliwa na Mungu kumrithi Musa.

Katika Agano Jipya huduma ya uponyaji wa magonjwa inaonekana kuwa sababu inay-opelekea mtu awekewe mikono. Yesu alitoa kibali cha tendo hili katika utume wake wa mwisho kwa wanafunzi. “Kwa jina langu … wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.” (Mk 16:17-18).

Baadaye katika Agano Jipya kanuni nyingine ambayo ni ya tofauti kidogo inateuliwa kuwa njia ya uponywaji wa magonjwa ya mwili. “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana. Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa. ” (Yak 5:14-15). Kanuni iliyoteuliwa hapa ni ile ya kumpaka mafuta mgonjwa katika jina la Bwana.

Lakini kanuni hizi zinatenda kazi kipee kupitia imani katika Jina la Bwana; yaani jina la Yesu.

Tena, unapowapaka mafuta watu ambao ni wagonjwa, kwa kawaida tendo hili huam-batana na kitendo cha kuwekewa mikono kwa wakati huo huo. Kwa njia hii, maagizo ya kanuni hizo mbili huambatanishwa na kuwa kanuni ambayo ni moja . Hata hivyo, jambo hili si lazima liwe hivyo. Ni kanuni iliyo ya kimaandiko kabisa kuwawekea mikono wagonjwa pasipo kuwapaka mafuta au kuwapaka mafuta wagonjwa pasipo kuwawekea mikono.

Mazingira ambamo maagizo haya mawili yanaonekana katika Maandiko yanaelekea kuashiria kwamba zinakuwepo nyakati ambapo inafaa zaidi kutumia agizo moja kuliko jingine. Ni hali inayostahili kila agizo la kuwawekea watu mikono linapoandamana na huduma ya Uhubiri wa Injili. Hata hivyo, kupakwa mafuta huwa ni tendo linalokusudiwa lifanyike kwa wale ambao ni watu walioamini tayari na kushiriki katika kanisa fulani la Kikristo.

Ni jambo lililo kinyume kabisa kwa mtu anayekiri kuwa ni Mkristo aliye mgonjwa kutafuta msaada wa matabibu wa kibinadamu kabla ya kuanza kwanza kutafuta msaada kutoka kwa Mungu mwenyewe, kupitia kwa viongozi wa kanisa waliosimikwa.

Wakati mwingine uponyaji hupatikana mara moja, mara tu mikono inapowekwa juu ya mtu aliye mgonjwa. Hata hivyo, mara nyingine msaada huja polepole. Mara nyingine nguvu za Mungu za uponyaji hutokea mtu anayewekewa mikono akazihisi zinapoingia ndani yake. Hata hivyo, nyakati nyingine, huwa hakuna kabisa msisimko unaotokana na nguvu hiyo. Vyovyote iwavyo, kama anayetafuta uponyaji atakuwa na imani halisi, ni la-zima uponyaji utatokea hata kama hakuna hisia ya ghafla inayosisimua au tukio la muu-jiza.

B. Kupokea Roho Mtakatifu na Vipawa vya Kiroho

B.1. Kuwawezesha wengine kumpokea Roho Mtakatifu

69

Page 78: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kusudi la pili la kuwawekea watu mikono, kama lilivyofanywa katika Agano Jipya, li-likuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia wale waliokuwa wakitafuta ubatizo wa Roho Mtakatifu.

Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaonyesha matukio matano ambayo ndani yake watu walipokea ubatizo wa Roho Mtakatifu. Katika matukio matatu kati ya hayo matano, wale waliotafuta ubatizo wa Roho Mtakatifu walihudumiwa na waumini wengine kwa njia ya kuwekewa mikono.

1. Mjini Samaria mitume Petro na Yohana waliweka mikono yao juu ya waumini wapya na kisha wakawaombea. Baada ya hapo ikadhihirika kwamba “watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono” (Mdo 8:18).

2. Mjini Dameski mwanafunzi Anania aliweka mikono juu ya Sauli wa Tarso ili akimwom-bea aweze kuona tena na pia aweze kujazwa na Roho Mtakatifu. Katika tukio hili vyote viwili yaani uponyaji wa mwili na pia ubatizo katika Roho Mtakatifu vilitokea kwa Sauli, kupitia katika agizo ka kuwawekea watu mikono. (Mdo 9:17).

3. Katika mji wa Efeso wanafunzi ambao Paulo aliwahudumia wanampokea Roho Mtakatifu mara baada ya Paulo kuwawekea mikono. (Mdo 19:1-6).

Hakika, hii si njia pekee ambayo kwa hiyo watu wanaweza kupokea ubatizo katika Roho Mtakatifu. Watu walioketi ndani ya chumba ghorofani nyumbani mwa Kornelio walipokea kipawa hicho moja kwa moja, pasipo mtu yeyote kuwawekea mikono. Hata hivyo, tunaweza kusema kwamba ni jambo la kawaida na la kimaandiko kwa wale wanaohitaji ubatizo wa Roho Mtakatifu kuhudumiwa na waamini wengine kwa njia ya kuwekewa mikono.

Maandiko yanatuonya kwamba agizo hili la kuwawekea waumini mikono lisichukuliwa kwa wepesi au kufanywa pasipo uangalifu. Kwa kuwa Paulo anamuagizaTimotheo ak-isema, “Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi..”(1 Tim 5:22).

Ikiwa kama kuwekewa mikono kutazaa matokeo halisi ya kiroho, basi itapasa kuwepo mahusiano ya kiroho ya moja kwa moja kati ya waumini wawili. Katika mahusiano haya ya kiroho ya moja kwa moja kati ya watu hao wawili, upo uwezekano wa kutokea mad-hara ya kiroho kwa mmoja au waumini wote wawili. Endapo kama roho ya mmojawapo wa hao wawili haitakuwa safi, kuna uwezekano kwamba roho ya mwenzake itaam-bukizwa kutokana kwa kugusana huko kunakotia unajisi. Ukweli kwamba hili ni jambo la hatari unathibitishwa na maonyo mawili ya Paulo anapoonya, “usizishiriki dhambi za watu wengine” na “Ujilinde nafsi yako uwe safi”.

Kwa kuwa huduma ya kuwekewa mikono imepewa kibali katika Maandiko, tunawezaje kujilinda na hatari za kiroho zinazohusiana na huduma hii? Jibu ni kwamba kuna njia nne za muumini kujilinda na hatari hizo.

1. Huduma hii haitakiwi ifanywe kirahisi-rahisi au pasipo uangalifu bali mara zote ifanywe katika roho ya maombi na unyenyekevu.

2. Uongozi wa Roho Mtakatifu ni sharti utafutwe katika kila hatua: tuombe pamoja na nani, tuombe wakati gani, tuombeje?.

3. Muumini anayewawekea wengine mikono hana budi ajue jinsi ya kujiombea mwenyewe utakaso endelevu kwa roho yake na ulinzi upatikanao katika damu ya Kristo.

70

Page 79: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

4. Muumini anayewawekea wengine mikono lazima yeye mwenyewe awezeshwe na Roho Mtakatifu ili kuzishinda nguvu za kiroho za adui zinazojaribu kufanya kazi ndani au kupitia ndani ya yule aliyewekewa mikono.

B.2. Kutoa au Kugawanya Vipawa vya Kiroho

Toka katika sehemu ya Maandiko ambamo tendo hili hutajwa, ingeonekana kwamba tendo la kuwekewa mikono linahusishwa na utendaji wa kipawa au karama ya unabii.

Utoaji au ugawaji wa vipawa au karama za kiroho ni njia ya kimaandiko kwa ajili ya ku-wathibitisha au kuwaimarisha waumini katika maisha yao ya imani na uzoefu wa kiroho. Paulo anawaandikia Wakristo walioko Roma akielezea hamu yake ya kutaka “kuwapa karama ya rohoni, ili mfanywe imara”. (Angalia Rum 1:11-12).

Kulingana na mtazamo wa Agano Jipya, vipawa vya kimungu vya kiroho ni sehemu na kiungo muhimu katika mpango kamili wa Mungu kwa ajili ya kanisa. Pasipo vipawa hivi, kanisa haliwezi kutenda na kuenenda katika kiwango cha nguvu na ufanisi kadri Mungu alivyokusudia lienende.

Fikiria yote anayofundisha Paulo vile afikirivyo kwamba vifaa vya kiroho vyafaa vitolewe au kugawanywa. Mtu ambaye Paulo anamuhusisha katika jambo hili ni mtenda kazi mwenzi wake katika huduma, aitwaye Timotheo.

“Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwe-kewa mikono ya wazee..” (1 Tim 4:14).

“Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu..‚ (2 Tim 1:6).

“Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.” (1 Tim 1:18).

Kutoka ndani ya Maandiko tunajifunza kwamba:

1. Timotheo alipokea baadhi ya vipawa vilivyotambulika.

2. Vipawa au karama za kiroho zilitolewa kwa Timotheo kupitia njia ya kuwekewa mik-ono.

3. Kugawiwa kwa kipawa au karama ya kiroho kwa njia ya kuwekewa mikono kulihu-sishwa pia na baadhi ya matamshi ya kiunabii.

Kuwekewa mikono kulikuwa ni njia ambayo mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa kwa Timotheo yaliachiliwa kufanya kazi katika uzoefu wake. Agizo la kuwekewa mikono katika uzoefu wa Timotheo, liliunganishwa na karama ya unabii, ili kwa njia hiyo aweze kuongozwa, kutiwa moyo na kuwezeshwa kutimiza huduma yake aliyopewa na Mungu.

C. Watumishi Kuwekwa WakfuKusudi linalofuata la watu kuwawekea mikono linahusishwa na tendo la kuwatuma mi-tume kwenda katika huduma nje ya kanisa la mahali.

Kanisa la mahali llililokuwa Antiokia ndilo linalotoa mfano ulio wazi katika jambo hili (an-galia Mdo 13:1-4).

71

Page 80: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

“Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao..” (Mdo 13:2).

Tendo la kuwawekea mikono liliwakilisha tukio la hadhara na la wazi la viongozi wa kanisa kutoa tamko kwamba Mungu amewachagua Paulo na Barnaba kwa ajili ya huduma mahsusi. Kwa tendo hilo la kuwawekea mikono viongozi wengine wa kanisa waliowawekea mikono waliomba hekima maalum ya kiroho, neema, na nguvu ambayo wangeihitaji kwa ajili ya kulitimiza kusudi waliloitiwa na Mungu.

C.1. Uteuzi wa Mashemasi na Wazee

Mfumo wa lazima wa uongozi ndani ya kanisa ni mfumo ulio rahisi kabisa. Unakamil-ishwa na ngazi mbili – na hizo ndizo ngazi pekee za kiuongozi au utawala ndani ya kanisa. Ngazi hizi mbili ni zile za wazee na mashemasi.

Sifa zinazohitajika kwa ajili ya ngazi hizi za uongozi zimeainishwa katika sehemu za Maandiko zifuatazo: Mdo 6:3, 1Tim 3 na Tito 1:5-9. Kwa msingi wa sehemu hizo za Maandiko, twaweza kuhitimisha kwamba tabia kuu za nafasi hizi za uongozi ni kama zi-fuatavyo: Jukumu la msingi la wazee ni kutoa uelekeo wa kiroho kwa kanisa na maele-kezo kwa kanisa. “Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.” (1Tim 5:17).

Kwa upande mwingine, neno shemasi katika maana yake ya asili ilikuwa ni “mtumishi”.Katika Matendo 6:2 kazi ya msingi ya shemasi ni kutumika. Kwa wao kutumika kwa jinsi hii, waliwapa uhuru wazee ili wawe na muda kwa ajili ya kazi yao mahususi ya maombi na huduma ya Neno la Mungu.

Mfumo wa Agano Jipya wa wazee kuwekwa wakfu kwa jukumu waliloitiwa na Mungu ni kupitia tendo la hao kuwekewa mikono na timu ya kitume. Mashemasi huwekwa wakfu kupitia tendo la kuwekewa mikono na wazee. (angalia Mdo 6:1-6, 1Tim 5:17-22).

Kwa kuhitimisha, makusudi makuu matano ya kuwekewa mikono yaliyoainishwa katika Agano Jipya ni: 1) kutoa huduma ya uponyaji kwa walio wagonjwa, 2) kuwasaidia wale wanaotafuta ubatizo katika Roho Mtakatifu, 3) kuwasaidia watu kupokea vipawa vya ki-roho, 4) kutuma mitume waende katika huduma za nje na 5) kuwaweka wakfu mashe-masi na wazee katika kanisa la mahali.

D. Mnyororo wa Kuwekewa Mikono

D.1. Agano la Kale

Hesabu 8:9 – kuwaweka wakfu makuhani.Hesabu 27:22 – kuwasimika watu katika ngazi za uongozi katika Israeli.Kumbukumbu 34:9 – kupokea roho ya hekima.

D.2. Wagonjwa kupokea uponyaji

Mat 19:13Mk 8:25Lk 4:40Lk 13:13Mdo 28:7-8

72

Page 81: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

D.3. Kuwasaidia wanaotafuta ubatizo katika Roho Mtakatifu

Mdo 8:16-17Mdo 9:17Mdo 19:1-6

D.4. Kuwasaidia watu wapokee vipawa vya kiroho

1 Tim 4:132 Tim 1:61 Tim 5:22

D.5. Kuwatuma mitume katika huduma za njeMdo 6:5

D.6. Kuwatenga viongozi kwa ajili ya utumishi katika kanisa la mahali

Mdo 13:1-4

73

Page 82: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kumi na Mbili: Unabii

Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wa-nadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtaka-tifu. (2 Pet 1:21)

A. Maandiko na Roho ya Unabii

“Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.” (Ufu 19:10e )

A.1. Unamhusu Yesu

Andiko hili linafafanua ushuhuda wa Yesu kuwa na maana iliyo sawa, au kiini chake kwamba hiki ndicho kiini cha roho ya unabii. Maneno haya siyo tu kwamba yanatoa ufa-fanuzi wa kuwapo Maandiko; yanafafanua pia matamshi yote yanayoambatanisha hoja ya kuwa ni unabii wa kweli. Yesu Kristo atakuwa ndiye kiini cha unabii wote, kama jinsi alivyo kiini cha Biblia yote.

A.2. Unabii na Biblia

Kuna hali ya kuzidiana kwa ukuu wa ngazi za uvuvio, na hivyo ile hali ya kutoweza ku-kosea na mamlaka na thamani kati ya neno la Mungu lililoandikwa (Biblia) na “maneno” ya unabii ndani ya Kanisa. Kuwepo kwa maneno ya unabii ni kitu kinachotamanika (1Kor 14:1) na kunasaidia (1Kor 14:3-5), lakini Maandiko yamevuviwa na yana ukamilifu wa kutoweza kukosea na ndiyo maana Maandiko ni mamlaka yetu ya mwisho. Maandiko ni yenye kutamanika sana zaidi ya dhahabu safi (Zab 19:7-11).

Maneno ya unabii yatolewayo na vyombo vya kibinadamu ambavyo vina walakini au ka-soro lazima yathibitishwe kwa kuyachunguza na kuyalinganisha na Neno la Mungu, yaani Biblia. Mungu hawezi kuchanganyikiwa. Hatasema kitu kimoja ndani ya Neno lake kisha akupe neno la unabii linalopingana na neno lake.

B. Unabii Kwa Watu Binafsi

“Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.’ ”

“Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusa-lemu. Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu. Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke.” (Mdo 21:10-14)

“Unabii kwa watu binafsi” unahusu unabii unaohusisha masuala ya kibinafsi ambayo Roho Mtakatifu humsukuma mtu mmoja ampe mwingine. Biblia kwa wazi kabisa ina-

74

Page 83: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

ruhusu kuwepo kwa unabii kwa watu binafsi. Nathan alimletea Daudi “neno” kutoka kwa Mungu la kumkabili katika dhambi yake (2 Sam 12:13). Agabo alimuonya Paulo juu ya matatizo yaliyomsubiri akifika Yerusalemu. Sehemu ya Maandiko hapo juu, inatufunulia pia mipaka ya kiusalama au vizuizi vya kusaidia kulinda, kusiweko na matumizi yasiyo-faa ya unabii kwa watu binafsi na hivyo kuturuhusu kulitumia tendo hili la kibiblia kwa hali ifaayo.

• Neno litakalonenwa kwa kawaida halitakuwa jipya kwa mtu aliyetajwa lakini litathi-bitisha jambo ambalo Mungu atakuwa tayari amekwisha sema naye. Kutoka Matendo 20:22-24 tunajua kwamba Paulo alikuwa tayari anafahamu juu ya masuala yaliyotajwa na Agabo.

• Mwenendo wa mtu aliletaye neno huhitajika upimwe. Kibali cha Agabo hakikupimwa kwa usemi wake kwamba alikuwa na neno la unabii bali kwa vile alivyokumbukwa kwamba alikuwa mtu wa Mungu mwaminifu aliyetumiwa mara nyingi katika utendaji wa kipawa hiki (Mdo 11:28, Mdo 21:10).

• Maisha ya Kikristo kamwe hayafanani na maisha katika dini za uongo, kwa maana ya kutawaliwa na matamshi kama ya waganga/wachawi au mashauri ya watu maarufu kama maguru kama waitwavyo wataalam wa mambo ya kiroho katika dini za Kihindu. Paulo hakubadilisha mipango yake kwa sababu ya unabii wa Agabo, au kwa sababu ya msisitizo wa watu wengine. Alilipokea neno lao kwa hali ya kulikubali lakini hata hivyo hakubadilisha mipango yake.

• Unabii wowote huja kwa sehemu (1 Kor 13:9 inaeleza, “Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza neno la Mungu si kamili”) hii ikiwa na maana kwamba kwa kadiri unabii unavyoweza kuwa kweli bado hauonyeshi sura ya mambo kwa ukamilifu. Neno la Agabus lilikuwa la kweli na Paulo alifungwa Yerusalemu. Lakini kifungo hiki hatimaye kilimpa Paulo nafasi ya pekee kuhudumu katika mji wa Roma (Mdo 23:11).

Tunapaswa kuwa katika hali ya sala tunapofikiria unabii tunaopewa, kama Mariamu alivyofanya alipotafakari taarifa iliyoletwa na wachungaji (Lk 2:19). Muitikio wa haraka haraka huwa kitu kisichotakiwa sana; kwa lugha rahisi, ni vyema kusubiri ukitarajia kuona kile Mungu atakachofanya. Unabii kwako binafsi hauna hatari ikiwa utachukuliwa sambamba na neno la Biblia, lakini pia neno la unabii kwetu binafsi halitakiwi ligeuke kuwa njia itakayoamua uelekeo wa maisha yetu. Mungu anaweka wazi ndani ya Biblia kwamba sisi ni watoto wake (Yn 1:12) na kwamba Yeye anazungumza moja kwa moja nasi (hasa kupitia katika Biblia, angalia 2 Tim 3:16). Katika Yohana 10:27 Yesu anasema, “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.” Pia ni jambo lililo wazi kwamba ikiwa Mungu anaweza kuzungumza na mtu juu ya mtu mwingine pia anaweza kuzungumza na mtu yule Yeye mwenyewe.

C. Hamu ya Kuwa na Huduma ya Kinabii

Tunapaswa kutamani kuwa watu wanaosikia kutoka kwa Mungu na kulitangaza neno lake. Isaya 42:9 inatuambia kwamba kabla Mungu hajafanya chochote, Yeye kwanza hutujulisha sisi. Mungu amechagua kufanya kazi kupitia kwa wanadamu, na sisi kama watu wake, tunawajibika kulitangaza neno la Mungu (yaani Neno lake katika hali ya maandishi na pia kunena mambo mapya anayotaka sisi tuyaseme) kwa ulimwengu. Ka-tika 1Wakorintho 14:1 na 39 tunaambiwa kutamani kipawa cha kiunabii.

Tunaona kutokana na Maandiko hayo hapo juu kwamba ni juu yetu sisi wenyewe kuona kwamba tunatamani na kutafuta kuisikia sauti ya Mungu. Kwa jumla, Mungu hainui mtu

75

Page 84: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

hivihivi tu au kutuma sauti inayounguruma kutoka mbinguni hadi alipo mtu huyo. Badala yake, ni wale wanaomtafuta Mungu kwa bidii wanaomsikia anaponena. (Mungu an-aweza na husema kwa sauti inayosikika katika nyakati fulani, kama katika 1Samweli 3:10-11, japo namna hii hutokea mara chache tu.)

Muulize Mungu maswali. Katika Yer 33:3 Mungu anaahidi kutujibu kwa kutuonyesha mambo makuu ambayo hayachunguziki. Twaweza kumuuliza Mungu, tukiwa katika hali ya moyo safi, atuambie ni kwa nini hatuoni miujiza mingi ya uponyaji na kwa nini hatukui na kuongozeka kiimani kama inavyotupasa. (Mungu haogopi maswali.) Mungu ataon-goza na kutuelekeza tunapotekeleza azma ya kuutafuta ufalme wake (Mat 6:33). Tuna-paswa kutamani kusikia kutoka kwa Mungu ili tuweze kuwasaidia wenzetu na sisi wenyewe binafsi.

Zaidi ya hapo, tunahitaji tuweze kumsikia Mungu akinena nasi kila siku. Tunaambiwa kwamba Yesu alifanya tu kile alichomuona Baba akikifanya (Yn 5:19). Vivyo hivyo, sisi nasi tunatakiwa kutamani kufanya kile tu ambacho Baba anataka tukifanye. Tunatakiwa tukae karibu yake ili tuweze kujua kile anachotaka hasa sisi tukifanye (katika mambo madogo na pia mambo makubwa yanayohusu uelekeo wa maisha yetu).

D. Je, Hivi Twaweza Kutarajia Kumsikia Mungu Akinena?

Katika Yohana 10:3-5 tunamuona Yesu kama mchungaji mwema. Anatamani kutuon-goza na anataka sisi tuweze kuisikia sauti yake. Wakati tunapoijua sauti yake tutaweza kupambanua kati ya yale yaliyo kweli na yasiyo ya kweli (kwa sababu Yesu ni Kweli, Yn 14:6) na tunajua kwamba ni hamu ya Mungu kutuona tukiongozwa na kuingizwa katika kweli yote (Yn 14:16-17, Yn 14:26, Yn 16:13). Kuna mifano mingi ndani ya Biblia ya wa-nadamu walioisikia sauti ya Mungu (siyo lazima kwamba ilikuwa sauti iliyosikika kwa masikio yetu ya nyama au mwili). Mfano mmoja ni Yeremia (Yer 1:2a, Yer 1:4-5, Yer 1:11-14, Yer 2:1, Yer 2:4-5). 1 Wakorintho 2:12 inatuambia kwamba Mungu anataka sasa tukielewe kile ambacho ametukirimia na Waefeso 5:17 yatuambia sisi tuweze kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Hatuwezi kuanza kukielewa kitu ambacho hata hatujak-isikia. (Hii kwa hakika inahusu nia yake katika Neno lake lililoandikwa na pia mapenzi yake kwa ajili ya maisha yetu binafsi.)

E. Kuitambua Sauti ya Mungu

Kwa kawaida tunaweza kuzitambua sauti za wanadamu. Twaweza kujua ni nani anaye-sema nazo kwa kutumia masikio yetu na kusikiliza kwa kuipambanua sauti fulani. Hata hivyo, tunapotaka kuitambua sauti ya Mungu, inatupasa kutumia kigezo kingine tofauti.

Kama vile kwa sauti za wanadamu, kadiri tunavyoendelea kuisikia sauti ya Mungu, ndivyo tunavyojifunza kuitambua. Sisi tuna sauti nyingi (mfano kama mawazo, falsafa, utamaduni, kanuni na mila) zinazosema nasi kila siku na tunatakiwa kupambanua ili ku-jua sauti ipi ni ipi (1Yoh 4:1). Kwa kusoma Biblia yetu kila mara tunapata uwezo wa kui-sikia sauti ya Mungu. Biblia imejaribiwa na kuthibitishwa kwamba ni neno la Mungu mara na mara tena katika kipindi chote cha miaka 2,000 iliyopita. Ikiwa kama tunaisoma Biblia yetu mara kwa mara tutaweza kuwa kama watu “waliotega” kusikia neno la Mungu.

Kigezo kingine, kwa kawaida ni hiki: je ujumbe unaleta uzima, tumaini na kutia moyo (1Kor 14:3), pengine hata wito wa kuingia katika toba, au je, ni ujumbe unaowashusha

76

Page 85: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

moyo na kuwaharibu watu? Tunamtumikia Mungu wa upendo naye hutoa jumbe za amani na upendo ili kuwajenga watu na kuwavuta wamkaribie.

Chanzo kingine kizuri cha sauti ya Mungu hupatikana katika mikutano ya Kikristo (kama ibada za kanisa au vikundi vya nyumbani, na hata tunapokuwa na muda wa kukaa pa-moja na marafiki Wakristo). Tunapolisikia neno la Mungu likihubiriwa, tunaliona neno la Mungu likiwa katika vitendo na tunaposikia juu ya njia zake sisi pia tunapata uzoefu wa kuitambua sauti yake. Angalia Zab 1:1-2 na Zab 119:9-16.

Tunapokuwa tunajaribu kuisikia sauti ya Mungu, tunatakiwa tujihadhari na “kusikia” vitu ambavyo tungependa kuvisikia badala ya kusikiliza ili tusikie kile ambacho kwa hakika Mungu anakisema. 2Timotheo 4:3 inazungumzia “mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.” Hatupaswi kuwaambia wengine mambo yale wanayotaka kuyasikia kwa kujibunia mambo ya kusema na hatupaswi kuwasikiliza wale wanaotuambia mambo mazuri yanayotupendeza. Tunahitaji kuwa na kiasi yaani uwezo wa kutawala hisia na misisimko yetu kwa kuwa hili ni eneo lililo rahisi kupelekea kufanya makosa. Mara nyingi mtu kuwa na mtu kama rafiki au kiongozi wa kanisa ambaye unawajibika kwake laweza kuwa jambo linalosaidia. Ikiwa hutaki kukiweka katika mikono ya wengine kile “ulichok-isikia” unaweza kuwa unajidanganya pasipo wewe mwenyewe kujua.

F. Wakati Gani Mungu Anasema Nasi na Kwa Njia Gani?

Hapa chini kuna njia ambazo Mungu anazitumia kusema nasi:

• Mungu anaweza kusema nasi mara nyingi kwa kadiri sisi wenyewe tunavyotaka kum-sikia akisema nasi, kwa njia ya Biblia (2 Tim 3:16). Tunapaswa kuisoma Biblia na kusali kila siku (Lk 11:3, Yn 6:48-51).

• Kama ilivyokuwa kwa Yesu (Yn 5:19), Mungu hutuongoza katika hali zinazojitokeza kila siku. Si lazima tutumie masaa mengi tukiwa katika sala na kufunga kabla Mungu ha-jaweza kusema nasi.

• Mungu anasema nasi tunapomhitaji na pale tunapomwita (Zab 86:7).

• Wakati wengine wanapohitaji kusikia sauti yake, Mungu husema nasi na hututaka tu-wafikishie ujumbe wake. Hii inaweza kuwa kwa sababu wale wengine hawamsikilizi Mungu (Yer 1-2) au pengine kwa sababu Mungu anakuwa amechagua kuupitishia ujumbe huo kwako. Angalia 1 Wafalme 11:31 wakati Ahija anaposema na Yeroboamu. Ni kweli kwamba Paulo alimwandikia Timotheo akimpa maelekezo na mashauri ya kimungu. Mungu husema pia na wengine wanaoweza kutuletea ujumbe wake—waweza kuwa ujumbe wa kiujumla (kama vile ukweli wa kijumla kutoka katika Maandiko) au ujumbe maalum (neno la unabii). “Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, ninyi mliusikia, mkaupokea, si kama vile ujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.” (1The 2:13)

• Tunaweza pia kujitengea nyakati za sala, nyakati ambazo tunaweza kuwa katika sala na kumpa nafasi Mungu ili atuhudumie. Yesu alilifanya hili mara nyingi, kama katika Marko 6:46.

• Katika nyakati maalum za maombi na kufunga, kama katika Matendo 13:2, Mungu husema nasi.

• Mungu husema nasi kwa njia nyingi, kwa mfano, kupitia malaika zake

77

Page 86: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

(Lk 1:11), au kwa njia ya maono (Mdo 9:10, 16:9-10) na njozi au ndoto (Mwa 31:11), au maneno ya maarifa au hekima (1 Kor 12:8). Mungu pia hutumia dhamira zetu (Rum 2:15) au utambuzi (Flp 1:10), na pia atatumia hata matukio fulani fulani (Mdo 18:3).

G. Tunafanya Nini na Neno la Mungu?

Mara unapotamani kumsikia Mungu na kumtafuta katika ukamilifu wa moyo wako, Yeye atasema na wewe. Kama unajihisi kuwa na ujumbe kutoka kwa Mungu, yafuatayo ni maelekezo ya hatua unazotakiwa kuzichukua.

G.1. Hakikisha na Ujue kuwa ni Neno Kutoka Kwa Mungu

Kwanza kabisa, hakikisha na ujue kwa hakika kwamba ni neno toka kwa Mungu. Je, neno lenyewe linapingana na Biblia? Kama hivyo ni kweli, basi ni hakika neno hilo halikutoka kwa Mungu. Kamwe Mungu hawezi kupingana na neno lake. Kama jambo hilo ni lenye umuhimu, na wewe unaona kwamba huijui Biblia vizuri, lijadili jambo hilo na mtu anayeijua Biblia vya kutosha, na pia anayemjua Mungu kuliko hatua uliyo nayo wewe mwenyewe.

G.2. Mtii Mungu

Mara unapokuwa umethibitisha kwamba ujumbe huo umetoka kwa Mungu, utii ujumbe huo (Ebr 3:7, Zab 95:7). Katika Kut 34:1-4 tunaona kwamba Musa alitii maelekezo ya Mungu mara moja pasipo kuchelewa. Ikiwa hatumtii Mungu, mioyo yetu huzidi kuwa migumu, na kwa kadiri tunavyoendelea kuifanya migumu ndivyo tunavyopoteza uwezo wa kusikia na kutiii maagizo yake. Uwezo wetu wa kumsikia Mungu hupungua na ku-pungua, hii ikitutengenezea njia tunayoifuata tukididimia na kuelekea maangamivu. Kama ukikuta kwamba ujumbe ule hautoki kwa Mungu, utupilie mbali na ujaribu kuji-funza kutoka katika uzoefu huo kwa kuwa sisi wote hukosea. Nyakati chache za kwanza utakapomsikia Mungu hutakuwa na hakika kama kweli unasikia kutoka kwa Mungu au la—lakini kwa kadiri muda utakavyoendelea ndivyo unavyozoea kuisikia sauti yake, uta-kuwa na uwezo wa kujua mara moja pasipo kuchelewa kwamba ni ujumbe kutoka kwa Mungu na utaweza kutii kirahisi mara Mungu anaposema nawe. Jione salama na thabiti mara unaposikia ujumbe kutoka kwa Mungu.

Ujumbe Mungu anaokupa waweza kuwa kwa ajili ya mtu unayemjua, au pengine kwa ajili ya kanisa lako la mahali. Ujumbe waweza kuwa kwa ajili yako mwenyewe. Una-takiwa ujue utafanya nini na ule ujumbe Mungu anaokupatia. Je, ni lazima umwambie mtu yule ambaye Mungu amesema juu yake, au uwe kimya tu juu ya jambo Mungu alili-lokufunulia huku ukiendelea kuliombea? Je, utautumia ujumbe huo katika maisha yako mwenyewe au uwashirikishe wazee wa kanisa lako la mahali? Aina hii ya maswali yana-takiwa yajibiwe kila wakati ili uweze kulitendea kazi neno la Mungu katika njia bora kabisa kadiri iwezekanavyo.

Yawezekana kabisa usiuelewe ujumbe anaokupa Mungu. Hii ilitokea kwa Danieli kama vile ilivyowekwa katika kumbukumbu katika Danieli 12:8a. Inavyozidi kutokea hivyo, uta-jikuta upo katika hitaji la kumsubiri Mungu hadi akupe ufahamu ulio bora zaidi au un-aweza kuhitajika uzungumze na rafiki au mzee ndani ya kanisa lako juu ya suala hilo.

G.3. Lihifadhi Neno Katika Hali ya Usalama

78

Page 87: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kama ilivyo kwa kila habari yenye thamani, tunatakiwa kuweka kumbukumbu ya ma-neno Mungu anayotupatia. Hii inatusaidia kwa kadiri inavyotupa kumbukumbu ya ma-tukio na kuturuhusu tuwe waaminifu kwa maneno hayo. Pia kufanya hivi kunatuongezea uwezo wa kusikia mambo mengine zaidi kutoka kwa Mungu kama tukiwa na bidii ya kuandika yote tunayosikia kutoka kwa Mungu. Tafuta mfumo unaofanya kazi vizuri zaidi kwako, kama kutumia jarida au kijitabu kidogo. Vipande vidogovidogo vya karatasi hupo-tea kwa urahisi na havisaidii sana pale unapotaka kujikumbusha mambo ya nyuma.

H. Hitimisho

Mungu anatamani kusema na watu wake. Sisi nasi tunahitaji kutamani kusikia kutoka kwake. Tunapoendelea kumtafuta Yeye atakuwa karibu na atakutana nasi. Mungu ana-taka kuwasiliana nasi – kama ingekuwa siyo hivyo asingemtuma Yesu kufa kwa ajili yetu. Tunapaswa kujiweka tayari kuwa wajumbe wa Mungu, tukilichukua neno lake lililo-andikwa na kulinena kwa watu wanaotuzunguka na pia kulipeleka hadi kwa mataifa ya ulimwengu.

I. Mnyororo wa UnabiiMwa 49:11Kor 14:1-5Yn 10:3-52Tim 3:16-171The 2:131Yoh 4:1Ebr 3:7-8

79

Page 88: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kumi na Tatu: Uinjilishaji

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwa-fundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” (Mat 28:19-20)

A. Njia Ngumu Ya Mashaka Kuelekea Uinjilishaji

Ni jambo linalokubaliwa na wote kwamba ulimwengu unapitia kile wanatheolojia wana-chokiita “upeo kuelekea kipindi cha hatari katika uinjilishaji.” Wakristo wanajikuta katika hali ya kusongwa na ulimwengu uliojaa falsafa zisizo na chochote cha maana unaowataka watoe majibu, na hivyo wao kujikuta wakirudi nyuma na kujitengea mahali pa siri wanakoweza kuishi maisha yao ya uadilifu huku wakiogopa kuingia katika mida-halo ambayo itayaweka nje yale wanayoyaamini ili wayapiganie.

Kinyume na jambo hili, huu ni wakati ambapo Kanisa haliwezi kushindwa kutoa mchango utakaoonekana ni wenye manufaa. Mwanatheolojia mmoja aitwaye Lapide, anamwita Yesu, “Muasi wa Pendo” naye anaizungumzia huduma yake kama yenye “kuvunja mipaka.” Yesu huyo huyo bado yupo hapa akifanya kazi katika Kanisa lake na kupitia kwa Kanisa lake, kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hamu ya Mungu ni kuona Kanisa likisimama na kuwa shahidi anayeng’ariza wema wake, neema na upendo kwa ulim-wengu uliopotea kabisa katika giza nene. Anatutaka “ tung'ae kama nyota zinavyolian-gaza anga” kwa kadiri tunavyoendelea kushika imara “neno la uzima” (Flp 2:15b-16a). Je, hivi kweli tunaweza kupingana na changamoto yake inayotutaka tuinuke na kui-ruhusu nuru ya Kristo iangaze?

Katika hotuba yake maarufu ya Mlimani, Yesu anasema:

“Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” (Mat 5:14-16)

B. Tabia Tatu za Uinjilishaji

Tutazichunguza tabia tatu za uinjilishaji. Hata hivyo Orodha hii haina maana kwamba itakuwa imeeleza kila kinachotakiwa kuelezwa.

B.1. Wito na Utume

“Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.” (2 Pet 1:10)

“Nawasihi….mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa.” (Efe 4:1b)

Kusudi la dondoo zifuatazo ni kutaka kuonyesha umuhimu wa wito wetu – ambao ni wito kwa wote:

80

Page 89: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

• Kunahitajika kuwe na “uhakika juu ya wito”: Ni muhimu kabisa kuwe na wito ulio wazi ndani ya kila mmoja wao. Chris Wienand aliwahi kusema, “Ikiwa kutakuwa na uhakika wa wito ndani yako, wewe utaongoza na wengine watakufuata.”

• Kutimiza utume mkuu si jambo la hiari, wala si suala la kuwa na wakati au la, bali ni jambo linalotakiwa litokane na kuamini juu ya umuhimu wa kuutimiza pasipo kuchelewa.

“Umahiri” ni neno linaloelezewa kumaanisha “utendaji kazi kwa uangalifu ulio kamili pa-sipo upungufu.” Wayne Meyers anasema kwamba wengine wanahitaji “kupigwa teke takatifu,” kwamba tunahitaji kuirudisha “U” (‘u’ kubwa) kwa sababu tulichobakiza sasa badala ya utume mkuu ni “ondosho kuu”), kwamba hatuwezi kutembea kwa kasi tuli-yokwenda nayo mwaka uliopita, tunapaswa kuongeza hatua na kwamba kuja kwa Yesu mara ya pili kunategemea hatua tulizoanza nazo. Mungu hajamtoa yeyote asishughulike na utume mkuu (Mat 28). Mungu huwapitisha, Shetani huwaondoa. Yesu alikuwa na haya ya kusema katika Mathayo 12:30, “Yeyote asiyejiunga nami, ananipinga; na yeyote asiyekusanya pamoja nami, hutawanya.”

• Tukiwa katikati ya tendo la ibada (Isa 6, Mdo 13:2) ndani ya uwepo wake, ana-tupa maelekezo kwa ajili ya utumishi na sisi tunajitoa kwake tukiwa na utayari. Mifano ya kuangalia ni pamoja na ule wa Eliya, Paulo, Barnaba, Isaya.

• Kuuelewa utume wako kutaweka hamu ndani yako kwa ajili ya kuwa na maisha yaliyo safi, kutakupa moyo wa kujitoa kwa ajili ya watu na pia ufahamu huo uta-kuandaa wewe kuweza kuilipa gharama yoyote itakayohitajika. Tunatakiwa ku-muomba Mungu atupe roho itafutayo kuwavuta watu wengine.

B.2. Gharama na Changamoto

Dondoo zifuatazo zinakusudiwa kutoa changamoto kwetu ili tutoke katika hali ya kuhesabu tu gharama za wito wetu kwa Mungu, na kuingia katika hatua za kulipa gharama na kuashiria kuingia kwa utawala wa Mungu tukifanya hivyo kwa hiari na kwa uaminifu:

• Mungu yupo katika hatua ya kukusanya “kikosi cha jeshi la dharura” kilicho tayari kulipa gharama. Watu “wenye mtazamo wa ki-Pollyanna” (alivyosema David Bosch) hawatakuwa na utayari wa kuchimba mahandaki ya vita wakiwa wame-piga magoti kwa kuogopa risasi zinazovuma zikipita juu kidogo ya vichwa vyao. Je, sisi tutaondoka pia katika hatua ya kuhesabu gharama na kuingia katika ha-tua inayofuata ya kulipa gharama? “Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka ku-jenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.’”(Lk 14:28-30) Wayne Meyers alisema kwamba Mungu anatafuta kuwa na jeshi, na sio umati wa wasikilizaji, jeshi litakaloacha nyayo kubwa ndani ya vitabu vya historia.

• Mungu huwatumia watu wa kawaida walio tayari na kuwageuza kuwa watu wasio wa kawaida lakini watiifu. Huchagua mambo mapumbavu ya ulimwengu huu ili kuwaaibisha wenye hekima ili asiwepo wa kujivuna mbele yake. (Angalia 1 Kor 1:27-31).

Anainua watu kutoka katika walio “wapumbavu” wenye imani katika yale yasiyoonekana, wanaobeba kila siku ushuhuda wa matendo makuu na ya ajabu ya Mungu—wakiamini kiasi kinachozidi yale yawezayo kuaminika, kwamba “kwa Mungu mambo yote hu-

81

Page 90: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

wezekana.” (Mat 19:26, Ebr 11). C. T. Studd alisema, “Wengine wataishi katika kivuli cha kengele ya kanisa lakini acha mimi niishi hatua moja toka mahali jehanamu ilipo.”

• Tunahitaji watu wasiotishwa na changamoto yoyote iliyo ndani yao. Alipoulizwa ni nini iliyokuwa siri ya mafanikio yake, William Duma alijibu, “Kujifanya rahisi kwa wengine na mtu mgumu kwa nafsi yangu mwenyewe.” Ujasiri au ushupavu ume-fafanuliwa na Ernest Hemmingway kama “neema katika hali ya shida.” Kama Paul Yonggi Cho asingetoa kauli hii ya kiutume, “Kama si mimi basi nani, kama si hapa basi wapi, kama si sasa basi lini?” kungekuwa na shimo kubwa wana-loenda watu wasioamini katika nchi ya Korea ya Kusini ambako sasa kuna ma-milioni ya waumini.

B.3. Mwenendo na Uwezo

Tusipokuwa na “mwenendo” hatutaweza kuwa na uwezo wa kukabiliana na wito wa “kuenenda na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi.” Yafuatayo, hata hivyo, yanawakil-isha machache kati ya mambo yote ya lazima yanayotakiwa kwa ajili ya mwenendo unaotakiwa na kanuni:

• Mashahidi, watenda kazi, wavunaji na wale wapandao hufanywa, na sio kwamba wanazaliwa wakiwa hivyo. Hatuzaliwi tukiwa na upendo na huruma.Kama hali ya kuwa na shauku, Gordon Macdonald anasema, vitu hivi huja kwa njia moja tu, utii (1Yoh 4).

• Hatuzaliwi tukiwa na hamu ya kupanda na kuhubiri injili au Ufalme: “Hapo aka-waambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.” (Mat 9:37-38). Lakini Mungu yumo katika biashara ya kubadilisha watu. Anawa-badilisha makahaba na wahuni kuwafanya wawe wana wake wa kike na kiume wacha Mungu, watu dhaifu wanabadilishwa na kufanywa kuwa watu wenye nguvu.

• Tunatakiwa kuwa watu wenye mioyo laini-iliyo rahisi kuelekezwa, yenye kuweza kuwa na huruma kuwaelekea waliopotea, wasiofikiwa bado na wale waliosahau-liwa.

• Tunatakiwa tuwe watu wanaoruka na kutoka ndani yetu wenyewe kwenda nje kwa wengine. Smith Wigglesworth alisema kwamba kuna vitu viwili vitakavyo-tusababisha sisi turuke na kutoka nje ya maisha yetu wenyewe:Usafi wa moyo na imani. Alisema pia, “Mungu hana nafasi kwa mtu anayeangalia nyuma, anayefikiri ya nyuma au kutenda kama bado yuko nyuma” (nukuu toka katika kitabu kiitwacho “The Secret of His Power”. Katika Luka 9:62 Yesu al-isema, “Yeyote anayeshika jembe tayari kulima na huku anaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.”

• Hatuwezi kuwa watu ambao maisha yetu yote tunaangalia mambo ya kibinafsi, lakini badala yake ni heri sisi tuwe watu wanyenyekevu. Ed Silvoso anaandika, “Kila unapolenga katika mambo yako binafsi na kazi yako binafsi, hata kama ni kazi kwa ajili ya Mungu, unafanya iwe rahisi sana kwa adui yako kukufanya ulenge katika mengi yenye upungufu na yaliyo mbali na ukamilifu ili akuharibie sherehe ya ushindi wako.” Imetaarifiwa kwamba Mungu alinena na Smith Wig-glesworth mara moja akisema, “Wigglesworth, Ninakwenda kukuunguza hadi uungue kabisa na kwisha, hadi kutakapokuwa hakuna tena Wigglesworth, bali Yesu peke yake.”

82

Page 91: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

C. Kanuni Zinazofaa Kwa Ajili ya Uinjilishaji

Hapa kuna mambo machache ya kukumbuka:

• Tumeitwa ili kuwafanya watu wawe wanafunzi wa Kristo na siyo kukusanya maamuzi ya watu kwa ajili ya Kristo. Tunafanya kazi siyo tu kuwaleta watu kwa Yesu bali pia kuwaleta wakiwa wamekomaa ndani yake, waking’ariza mfano wake kwa utukufu ulio wa wazi.

• Tumeitwa kuwa mashahidi—hii ina maana kwamba mtindo wetu wa maisha na pia maneno yetu sharti yang’arize wema wa Mungu, neema yake na upendo.

• Tunatakiwa tuwafanye watu kuwa wanafunzi wa Kristo, na si wanafunzi wetu.

• Kumbuka kwamba maisha ya Yesu yanahusu uwepo wake na nguvu zake.

• Uishinde hofu, ulegevu na mchoko. Ni John Wimber aliyewahi kusema,“Miujiza iliyo mingi hutokea wakati ambapo karibu kila mmoja anakuwa amekata tamaa na kurudi nyumbani.”

• Alf Cooper anasema kwamba kuna funguo mbili kwa ajili ya uinjilishaji: hali ya kuwajali watu na moyo unaowaka (upendo wenye wivu) kwa ajili ya Bwana.

D. Dondoo Zinazoweza Kusaidia Kwa Uinjilishaji

• Ufunguo kwa ajili ya kila eneo si lazima iwe “njia ya kufuata” bali njia inayofuatwa itegemee na mlengwa au walengwa.

• Njia inayofuatwa lazima itimize hitaji. Kila mlango una ufunguo: utafute.

• Fanyeni kazi katika mtindo wa timu au vikundi.

• Waambie watu wewe/ninyi ni akina nani na mnafanya nini (njia ya kawaida ya kuonyesha uungwana).

• Usiuze Ukristo wako mfano wa wafanya biashara za mkononi (angalia 2 Kor 2:17).

• Uliza maswali. Kama huna hakika, usitoe majibu ya kubuni.

• Fuatilia.

83

Page 92: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

E. Mnyororo wa Uinjilishaji

Rum 3:10-12Rum 3:21-24Rum 10:11-15Isa 6:8Yn 20:21Mat 28:19-20Mdo 1:8Mat 5:14-16

84

Page 93: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kumi na Nne: Vita Vya Kiroho

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mam-laka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. (Efe 6:12)

A. UtanguliziUhalisi wa vita vya kiroho unashuhudiwa na Maandiko kwa upande mmoja na pia katika shuhuda za maisha ya watu wengi. Maandiko yananena juu ya “mema” na “mabaya” (Mat 5:45, Yn 3:20) juu ya “falme” mbili zinazopingana (Mk 4:26-30, Lk 11:18) na habari za mawakala wa mema na mabaya, “wakipambana” kila mmoja dhidi ya mwingine: hii ina maana, Mungu na Shetani (Ayubu 1-2), malaika na mapepo (Ufu 12:7, Dan 10) na pia “wana wa ufalme” na “wana wa yule mwovu” (Mat 13:38, 1 Yoh 3:2; 3:7-10). Bilbia imejaa lugha ya vita, maneno kama mapigano, pigana, shindana, jitahidi, pingana, shambulia, adui, silaha, maaskari, songa mbele, pinga na kabiliana. Vita iliyopo ni vita halisi. Hata hivyo, si vita inayoonekana kwa macho ya kimwili bali ni ya kiroho: majeshi ya uovu na falsafa za uovu.

“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” (Efe 6:12)

“Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome.” (2 Kor 10:4)

Maneno ya Yesu na pia uzoefu wa maisha yake pia unashuhudia juu ya uhalisi wa ku-wako kwa vita vya kiroho. Mara nyingi alizungumzia vita hiyo na mwenyewe alihusika na vita hiyo kwa kuishiriki na pia kupigana. Alishawishiwa na Shetani (Mat 4, Mk 1:12, Lk 4), Alipingwa na watu waovu (Herode na mamlaka za dola ya Kiroma) na aliukabili ufalme wa giza kwa kutoa mapepo, kuwaponya wagonjwa na kufufua wafu. Mkabala wake mkuu dhidi ya nguvu za giza, hata hivyo, ulikuwa ni pale msalabani na ushindi wake mkuu kabisa dhidi ya majeshi ya uovu ulidhihirishwa na kufufuka kwake.

Watu walio wengi, waumini na wasioamini, wale wenye mapepo, waliokombolewa na wanaojihusisha na huduma ya ukombozi, wanashuhudia juu ya uhalisi wa nguvu za ki-roho, ziwe za wema au uovu. Na ni jambo la kweli, kwamba njaa ya kutamani uhalisi wa nguvu za kiroho ndiyo iwavutayo watu wajiingize katika mambo ya kichawi.

Asili ya vita vya kiroho ilitokana na anguko la Shetani. Shetani aliumbwa na Mungu kama malaika aliyekuwa na mamlaka ya kulinda kiti cha enzi cha Mwenyezi Mungu, na-fasi iliyompa umaarufu na heshima kubwa. Kutoka katika Ezekieli 28 na Isaya 14 tuna-ona kwamba Shetani alikuwa na uzuri au urembo mkuu, alikuwa ni mwenye utukufu na alijaa hekima. Hata hivyo, alianguka kutoka mahali pake pa heshima kwa sababu ya dhambi ya kiburi na kutafuta makuu. Akishindwa kuridhika na hali ya kuinuliwa kwa jinsi hiyo, alitaka awe hata juu ya Mungu na kwa sababu hiyo akatupwa chini kutoka huko mbinguni (Eze 28:17, Isa 14:13-14) akifuatana na takriban theluthi moja ya malaika (Ufu 12:7-9).

85

Page 94: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Katika hali ya kunyenyekezwa kwa jinsi hiyo, Shetani aligeuka kuwa mwenye kujaa ha-sira, chuki, uchungu na mwenye kunia madhara (Ufu 12:12c). lengo lake, toka wakati ule hadi sasa, ni kujilipiza kisasi juu ya Mungu kwa:

• Kushambulia na kuharibu kazi ya Mungu ya uumbaji (mwanadamu na ulim-wengu) na kazi yake ya ukombozi (Israeli, Kristo na Kanisa).

• Kwa kufanya uwepo mfumo mbadala wa kiulimwengu ambao yeye mwenyewe ndiye kiongozi wake.

• Kujipatia utukufu na ibada kwa ajili yake mwenyewe. Anaanza kisasi chake kwa kuwashawishi Adamu na Hawa wafanye dhambi yake ileile ya kiburi cha kujitakia makuu (“mtakuwa kama Mungu,” angalia Mwa 3:1-6). Kwa kutenda dhambi, mwanadamu alipoteza nafasi yake katika bustani ya Edeni na kujikuta akishiriki-ana na Shetani katika kuitawala nchi aliyokuwa amepokea kama urithi kutoka kwa Mungu (Mwa 1:28, Lk 4:5-6). Kwa hali hii, tunaweza kuona jinsi uovu ulivy-oletwa duniani na Shetani akishirikiana na mwanadamu.

Jibu la Mungu la haraka dhidi ya tendo hili la kwanza la kisasi lilikuwa ni kumtangazia Shetani hatima ya maangamivu yake (Mwa 3:15) na kuanzisha bila kuchelewa mpango wake mkuu wa ukombozi, kwanza kwa kupitia kwa Israeli, kisha kupitia Yesu na Kanisa.

Kabla ya kuiangalia vita inayolikabili Kanisa jinsi ilivyo, ni muhimu kuelewa kiwango chake na mipaka yake na kujua kwamba adui yetu ana mipaka ya wakati, nafasi anay-oweza kuwepo, vitendo vyake na uwezo wake. Shetani na mapepo yake wana mipaka ya muda kwa sababu hatima ya kuwepo kwao (kushindwa kwao kwa jumla) ni jambo la hakika. Yesu atakaporudi, hukumu iliyonenwa na Mungu katika kitabu cha Mwanzo itakamilishwa (Mat 8:29, Ufu 12:10-12; 20:10; 21:4-8; 22:15). Nguvu za kishetani zina mipaka ya nafasi ziwezayo kukalia. Wao ni viumbe tu, siyo kama Mungu alivyo, na kwa hivyo hawawezi kuwepo kila mahali kwa wakati mmoja.

Wana mipaka katika yale wawezayo kufanya. Katika kitabu cha Ayubu tunamwona Mungu akiweka mipaka juu ya kile ambacho Shetani angeweza kumfanyia mtumishi wake (Ayubu 1:12, Ayubu 2:6). Uwezo wao una mipaka:

• Shetani halingani na Mungu.

• Malaika walioanguka wanazidiwa kwa wingi na malaika watiifu wa Mungu (ni the-luthi moja pekee walioanguka pamoja na Shetani).

• Nguvu ya adui ilipunguzwa kwa sehemu kubwa na tendo la Kristo kuja na kuwa mwanadamu na pia ufufuko wake (“walitupwa nje,” “walifungwa” na “aliwapoko-nya madaraka” kulingana na Mat 4:23-24, Lk 4:38-41, Kol 2:15, 1 Yoh 3:8b, na Ufu 1:18).

• Yesu huwapa waumini nguvu na mamlaka wafanye hivyo alivyofanya.

• Yesu, kupitia kifo na ufufuko wake, amemfunga yule aliyekuwa mwenye nguvu na sasa sisi twaweza kuingia na kuzitwaa mali alizozimiliki (Mk 3:27, Mat 12:29). Tunachojihusisha nacho kwa sasa ni “operesheni za kupiga deki –yaani kusafisha.” (Angalia Mk 6:7-13, Lk 10:17-19, Mk 16:17-20, Rum 16:20 na 1Yoh 4:4).

Uone kwamba kitabu cha ufunuo kiko wazi: Mungu hayuko katika tendo la “kupigana.” Hii si kazi inayomfanya Mungu ajitahidi, lakini ni mkakati wa wokovu kuelekea lengo la uhuru kamili wa kuondokana na dhambi na visababishi vya dhambi (vishawishi).

86

Page 95: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Shetani anakusanya majeshi yake yote kwa ajili ya vita, na kabla ya sekunde kupita Mungu anamhukumu na kufutilia mbali yale makusudi yake yote mabaya.

B. VitaAdui atafanya kila kitu katika uwezo wake ili aliharibu Kanisa. Anajaribu kuitimiza azma hii kwa njia mbili.

B.1. Yeye Mwenyewe Huwaharibu Waumini

Shetani hutuharibu kwa kutuiba. “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima - kisha wawe nao tele.” (Yn 10:10) Hii inajumlisha, kifo (vita, utoaji mimba, vitendo vya jinai, maafa na tawala za viongozi waovu) na uharibifu (mali, fedha, mahusiano na familia).

Yawezekana kabisa Wakristo wakakaliwa na mapepo, hii ina maana, ya kupingwa na kutumiwa na nguvu za kipepo hadi wanapopata ukombozi kwa kuwekwa huru kutoka katika nguvu hizo. Adui hupata njia ya kuingia ndani ya maisha yetu kwa mojawapo ya njia hizi tatu:

• Sisi wenyewe tunapompa njia ya kupitia (mahali pa kuwekea mguu akipapata hupageuza kuwa ngome kubwa). Hii inawezekana ikatokana na dhambi ya mara kwa mara ambayo hatuifanyii toba (ni pamoja na kila aina ya ufisadi na dhambi ya zinaa, ulevi wa kuangalia picha chafu, kucheza kamari, ulevi, hasira, kutoku-samehe, uchungu, vitendo vya hila, tamaa ya kuwa juu ya wengine na kupenda fedha). Tunaweza pia kumpa adui njia ya kuingilia maishani mwetu kwa kujihu-sisha na vitu vinavyohusiana na uchawi (ni pamoja na kupiga bao au ramli, karata za kubashiri bahati, kuagua, madawa yatolewayo na waganga wa jadi wanaotumia mapepo (majini) n.k), michezo ya kujihami kama karate, kungfu, yoga, imani za uongo, dini zenye asili ya Bara Hindi na Uchina, ibada za ma-babu, ramli/falaki, imani za mizimu, uchawi wa watu weusi na weupe na ibada za kishetani). Angalia Mdo 5:3, Efe 4:27 na Yak 4:1-10 ambamo hali inayompa shetani mlango inatokana na kuufuata mwili na kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu.

• Kupitia laana zilizokuwa juu ya vizazi vilivyopita: ngome za mapepo zinaweza kurithishwa hadi kizazi cha pili na cha tatu. (uzoefu wetu unaonyesha kwamba kufuata imani mbaya ya ki-Freemason kwaweza kuwasababishia wanawake matatizo ya viungo vya uzazi na mengine kama vipindi vyao vya kike kuwa vy-enye maumivu makubwa, uzazi wa shida au utasa.) Mifano inajumlisha pia ulevi, kukosa uadilifu katika mahusiano ya kimwili, ndoa kuvunjika, hila, nia ya kujiny-onga, kunyanyasa kimwili na kijinsia. Angalia Kut 20:5 na Kut 34:7. Angalia pia Hos 4:12-13 Maandiko yanapozungumzia “Nia (roho) ya kufanya uzinzi” na “Kwa hiyo binti zenu hufanya uzinzi.”

• Kupitia vitendo visababishavyo mshituko wa kiakili, mfano kama kukataliwa, ku-tarikiwa, mauaji, kubakwa, kudhalilishwa kihisia, kimwili, na kijinsia. Angalia Yn 10:10 na 1 Pet 5:8-9.

Njia ya kukabiliana na mambo haya kwa kawaida huwa ni ukombozi. Hata hivyo, jihad-hari na hali ya kuwa na mtazamo unaokuwa kama ugonjwa wa hisia za kuona maisha yamejaa magonjwa na shida mbalimbali: sababu yaweza isiwe kukaliwa na mapepo na badala yake kumbe ni hali ya uchanga, udhaifu wa mwenendo wa mtu, hali ya dhambi

87

Page 96: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

au mawazo ambayo bado hayajabadilishwa. Kama shida itakuwa inasababishwa na mapepo basi bila shaka hali hiyo itadhihirika kwa wengine.

Vitendo vifuatavyo vitatosheleza kumuweka mtu mbali na kukaliwa na nguvu za mapepo:

• Tubu (ungama, geuka kabisa na kuziacha dhambi na kisha enenda katika uele-keo ulio tofauti na ule ulioufuata kwanza). Angalia Yak 4:1-10.

• Kana, geuka uwe kinyume na vitu vyenye asili ya kishetani (hii inahusisha ku-haribu vitu vyovyote vinavyohusiana na dhambi, vitendo vya kichawi, laana au tukio lililosababisha mshituko wa kiakili). Angalia Mdo 19:17-20.

• Mpokee Roho Mtakatifu (kwa ajili ya uponyaji kamili, kufanywa upya na kukamil-ishwa). Angalia Yn 4:4.

• Mpinge Shetani. “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkar-ibieni Mungu, naye atawakaribia ninyi.” (Yak 4:7-8a)

• Endelea kutembea katika uhuru na uadilifu.

B.2. Hutufanya Tujiangamize Wenyewe

• Vishawishi: Katika Luka 4 tunaweza kutambulisha angalau njia tatu ambazo adui huzitumia kutujaribu. Kwanza, kumjaribu Mungu, hii ina maana, kiburi (Lk 4:9-12), pili, tamaa ya mwili (Lk 4:3-4, Mwa 3:6) na tatu, kupotosha njia ya kupata tuyatakayo (Lk 4:5-8) (kwa mfano, kujipatia fedha kwa udanganyifu, kumfanya mke au mume wako afanye unavyotaka kwa kumhadaa kwa njia ya hila au kwa njia za kumkandamiza, kujipatia mafanikio kwa kutumia njia za mkato au kwa kutumia udanganyifu, kujipatia cheo kwa njia ya kujipandisha mwenyewe au kugombania madaraka badala ya kutumika na kusubiri hadi Mungu mwenyewe atakapokuinua). Njia tunazozitumia kupinga vishawishi ni kwa kuitawala nafsi (Gal 5:22-23, 2 Pet 1:5-7, 1 Kor 7:5) na kuwa tayari hata kuonewa ukitegemea msaada wa Mungu pekee. Ni maeneo yaliyofichika ya maisha yetu yatuwekayo katika utumwa. Silaha inayotulinda dhidi ya mashambulizi ya adui ni dirii ya haki (Efe 6:14): tunatangazwa kuwa huru kwa njia ya imani katika kifo cha upatanisho pale msalabani na tunafanywa kuwa watakatifu kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani yetu (1 Kor 1:2, Kol 1:22, Rum 12:1). Pia, tunapokuwa katika hali ya kupin-gana na majaribu hatutakiwi kukata tamaa “Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu ali-yeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuliana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.” (Ebr 4:15-16).

• Mashitaka (Ufu 12:10, Zak 3:1): “Shetani” katika lugha ya Kiebrania ina maana ya “mshitaki.” Shetani huleta mashitaka ya uongo (uongo, angalia Yn 8:44) au huja na kutushutumu juu ya dhambi tulizofanya zamani. Njia tunayoitumia kuka-taa mashitaka haya ni kwa njia ya Neno la Mungu, hii ikiwa na maana ya, Maan-diko na unabii (1 Tim 1:18-19). Silaha inayotusaidia hapa ni mkanda wa kweli (Efe 6:14).

• Udanganyifu (2 Kor 4:4, Mwa 3:4-13, Gal 3:1): Sisi tunaushinda udanganyifu ndani ya wasioamini kwa kuwahubiri injili na kuwaombea wapokee ufunuo (2 Kor 10:4-5). Tunazuia udanganyifu ndani ya waumini kwa njia ya kuendelea kupokea mafundisho ya imani na ushirika (Mdo 2:42, 1 Tim 4:13-16). Silaha yetu dhidi ya udanganyifu ni upanga wa Roho, ambao ni Neno la Mungu (Efe 6:17).

88

Page 97: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

• Mashaka (Mwa 3:1, Mk 4:15, Yak 1:6-8): Sisi hupinga mashaka kwa njia ya imani (Yn 20:27-29, Mat 17:20, Mk 11:22, 1Kor 16:13, 2Kor 16:13; 5:7). Imani yetu ya-hitajika kuongezeka (2Kor 10:15, 2The 1:3) Inawezaje kukua? “Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.” (Rum 10:17) Silaha yetu dhidi ya mashaka ni ngao ya imani (Efe 6:16). Ngao huwa haifai kitu isi-pokuwa tu pale inapoinuliwa na kuwekwa katika nafasi inayofaa kwa ulinzi: imani yetu haina budi iwekwe katika utendaji.

• Kukatishwa tamaa: Kukata tamaa mara nyingi hufuatia shambulio la kushutu-miwa, mashaka na matatizo yasiyopatiwa utatuzi (Zab 42:3; 42:9-10, Zab 77:7-9, Omb 3:19-20). Tunalishinda shambulio hili kwa sifa. Tunamwabudu Mungu, tu-nayaondoa macho yetu yasiangalie matatizo na kuyafanya yaungalie ukuu wa Mungu na uaminifu wake, tunajizuia tusisikilize mashutumu na kugagaa katika tope la mashaka na kuanza kujikumbusha maneno ya Mungu, yaani, kuitafakari Kweli (Zab 42:5-6; 77:10-15, Omb 3:21-24, Isa 61:3). Tunapojivika sifa sisi wenyewe hujipatia uwezo wa kushinda hali ya kukata tamaa. Njia nyingine ya kuishinda hali ya kukata tamaa ni kwa njia ya unabii (1Kor 14:3): Neno la Mungu hutia moyo! Kwa hiyo, silaha yetu dhidi ya shambulio hili, ni mkanda wa kweli (sifa huturudisha katika kweli juu ya Mungu na ahadi zake) na upanga wa Roho ambao ni Neno la Mungu (Efe 6:14,17)

• Uasi: Uasi ni kuishi kinyume na kanuni za Mungu au kutokuwa chini ya utawala wa Mungu: kufanya mambo tupendavyo badala ya apendavyo Mungu, kukataa kuliamini au kulitii Neno la Mungu, kupingana na mfumo wa Mungu (angalia, kwa mfano, habari ya uasi wa Sauli katika 1Sam 15, na hasa 1Sam 15:22-23). Kwa kweli kujiweka huru mbali na Mungu, ni kuwa shirika na Shetani (1Sam 15:23, Kumb 18:10) aliyekuwa muasi wa kwanza na ambaye anataka kupanda mbegu za uasi ndani ya waumini na wasioamini pia. Tunapigana dhidi ya uasi kwa ku-tumia silaha ya unyenyekevu (kujijua na kukubali hali zetu vyovyote vile tulivyo, angalia Fil 2:3-8 na Isa 14:14: Nia ya Shetani) na Utii kwa utawala wa Kristo, an-galia Ebr 12:9 na Yak 4:6-7). Pia tunahitaji kujitiisha kila mmoja chini ya mwen-zake, na hasa chini ya wale ambao Mungu amewaweka katika mamlaka juu yetu (Rum 13:1-5, Ebr 13:17, 1 Pet 2:18, Efe 5:21, Kol 3:18, 1 Pet 5:5-6).

C. Maombi (Sala) na KufungaHata hivyo, kuna vita nyingine tunayopigana. Hii inafanana na kutuma jeshi la anga li-ende na kuharibu maeneo yenye mizinga inayolinda anga lake mara tunapoanza ku-songa kuendea eneo la adui. Hii ni vita ya maombi au sala na kufunga. Angalia Dan 10:2-14 na Dan 10:20.

Tunapoomba na kumtaka Mungu apeleke malaika zake waende na kufanya vita katika ulimwengu wa roho dhidi ya falme za kipepo na mamlaka za giza, uwezo wetu wa ku-songa katika eneo la adui tukiwa tumelindwa na kupata upenyo vinakuwa ni ushindi wa hakika. Ni muhimu kukumbuka kwamba lengo letu ni kuiteka nchi. Haifai kitu kuomba tu kwamba ufalme wa Mungu uendelezwe huku tukikaa pasipo kufanya kitu chochote.

“Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya wataka-tifu, kutoka mkononi mwa malaika. Na huyo malaika akakitwaa kile chetezo, akakijaza

89

Page 98: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

moto wa madhabahu, akautupa juu ya nchi, kukawa radi na sauti na umeme na tete-meko la nchi.” (Ufu 8:4-5)

D. HitimishoAgizo kuu la Kanisa ni kuupanua ufalme wa Mungu. Hili tunalifanya kwa kuwafanya mataifa wawe wanafunzi, kuihubiri injili, kuwaganga waliovunjika mioyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, kuwalisha na kuwavika maskini, kuwapenda maadui zetu, kuwa watu wafanyao amani na kuwatetea wanaokandamizwa. Katika kuyafanya haya tutap-ingwa na adui na hivyo sisi lazima tufanye vita vya kiroho dhidi yake.

Kwa kutumia maneno mengine, sisi ni jeshi la Mungu ambalo limepewa mamlaka na kuwezeshwa kwa kupewa silaha na Mungu mwenyewe ili kuitwaa ardhi inayokaliwa na adui. Ili tuweze kulitimiza kusudi hili tunatakiwa kuwa askari walio na afya njema ya ki-roho, hali inayotuwezesha kujihusisha katika vita kama hiyo iliyotajwa hapo juu.

Mwishowe, tunapoendelea kupigana vita vya kiroho tunahitaji kukumbuka jinsi Mungu alivyo mkuu, uwezo wake mkuu, ukamilifu wa nguvu zake, mamlaka yake yasiyo na kikomo, na tunahitaji kukumbuka usemi wa Yesu kwamba milango ya kuzimu haitaweza kulishinda Kanisa (Mat 16:18). Kwa hali hii, tunaweza kupigana vita tukiwa na ujasiri na uhakika wa ushindi.

E. Mnyororo wa Vita vya KirohoEfe 6:122Kor 10:4Yn 10:10Yak 4:7-10Mat 4:10-11Kol 2:15Efe 4:271Pet 5:8-9

90

Page 99: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Sura ya Kumi na TanoMaono, Thamani na Vyombo

A. UtanguliziMisingi ya kitume na Kinabii (Efe 2:20) ni ya lazima kwa mtu mmoja mmoja, kwa familia, kanisa la mahali na labda tupendekeze, hata kwa ajili ya jamii yote. Yesu alisema katika Mat 7:24, “Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.” Swali linalohitajika lijibiwe ni hili:

Misingi hii ndani ya maisha ya mtu binafsi ni ipi?

Misingi hii ndani ya maisha ya kanisa la mahali fulani ni ipi?

Na zaidi ya hapo, mtu anahitajika kuifanyia kazi misingi hii ili kujihakikishia uthabiti, usa-lama, na wepesi wa kufanya kila linalotakiwa.

KICHWA(Mamlaka)

MOYO TUMAINI(Moyo wa Huduma) (Maono)

B. Kichwa (Mamlaka/Uongozi)Ni jambo lenye umuhimu kabisa kwamba sisi kama waumini tutauelewa mfumo wa mamlaka katika maisha yetu kama vile ilivyo kwa kanisa. Japokuwa mambo haya yanashughulikiwa ipasavyo katika semina za uongozi, maeneo yafuatayo ni muhimu sana uweze kuyaelewa.

B.1. Mungu na Neno Lake

Ni lazima tuwe chini ya mamlaka ya Mungu na neno lake. Ni jambo lenye maana kabisa kwamba Maandiko yawe ndiyo mipaka ya mazingira ambayo ndani yake kila kipengele cha maisha katika kanisa, iwe maisha ya mtu binafsi au ya wengi, kinapimwa: kwa hali ya mvinyo (uhai, uwezo na nguvu ya kanisa) kama ilivyo kwa viriba au vyombo unamo-kaa mvinyo (mfumo, mwelekeo). Ni lazima tuwe na hakika inayotupa ujasiri kwamba vy-ote hivi vinalingana vizuri na kile kinachotakiwa na kweli ya Biblia. Tumejaribu kuenenda hivi katika kila hatua ilivyowezekana. Ni wazi kwamba sisi wanadamu huyasoma na kuyaangalia Maandiko kupitia miwani yenye rangi kadhaa tofauti. Rangi hizi ni lazima zifutwe na kuondolewa, ili maana halisi ya Maandiko iweze kutuletea uzima wa kweli utokao kwa Mungu. Mara nyingi tunasoma Maandiko kupitia miwani ya mwenendo na tabia, utamaduni wetu na uzoefu wetu wa kidini. Kuyaangalia Maandiko kupitia miwani kama hiyo kutatuzuia tusiweze kufikia uelewa wa kibiblia unaotakiwa. Hata hivyo, tuna-pokuwa wenye kuijua kweli, hiyo kweli itatuweka huru. Kubwa tunalolitafuta ni kujiweka chini ya Mungu na neno lake, bila kuwa na sababu yoyote ya kujuta, au kuwa na vizuizi vinavyopunguza maana kwa kujitengenezea mfumo unaobagua kati ya vitu unavyovi-taka na vile usivyovitaka, kutoka katika mafundisho ya Biblia.

91

Page 100: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

B.2. Uongozi wa Kanisa la Mahali

Biblia iko wazi katika suala la uongozi ndani ya Kanisa kwamba wazee ndiyo mamlaka iliyo ya juu zaidi katika Kanisa la mahali. Matendo 20 na 1Pet 5 ndizo sehemu mbili zilizo wazi zaidi zinazoweza kutusaidia kuelewa na kutambua nafasi ya wazee ndani ya kanisa la mahali. Majukumu yao yanajumuisha:

• Serikali ya kimungu na uongozi.

• Kusimamia na kuendelea kuyaweka makusudi ya msingi mbele ya kanisa zima

• Kuongoza na kushauri.

• Kuchunga na kulisha.

Wazee hawachaguliwi kidemokrasia lakini wanatambuliwa kutokana na kile wanachoki-fanya ndani ya kanisa la mahali na kuwekwa wakfu kwa kufuata mfumo wa huduma ya mitume. Wazee ni watu ambao, pamoja na wake zao, wameonyesha hali fulani ya sifa katika mwenendo wao, kwa wao binafsi, familia zao, ndani ya kanisa na ulimwenguni. Kwa nyongeza juu ya sifa ya mwenendo wa maisha yao, wana uelewa ulio wazi wa ma-fundisho ya Maandiko na wanavyo vipawa vinavyosaidia na vilivyo vya lazima kwa ajili ya utendaji wa majukumu yao kwa mafanikio. Kilicho cha lazima ni kwamba kunahitajika kuwe na wito ulio wazi kutoka kwa Mungu.

Katika baadhi ya madhehebu baraza la mashemasi ndio ngazi iliyo ya juu ya uongozi wa kanisa la mahali. Katika mikondo mingine ya kidhehebu mashemasi wanakuwepo kwa ajili ya kufanya shughuli ndogondogo ambazo zimefichwa ndani ya kipengele cha huduma au utumishi. Kwa hakika, uelewa wa utume wa kibiblia kwa mashemasi unaipa ngazi yao heshima inayostahili. Katika Matendo 6 mitume wa kwanza waliwatambua na wakawaweka wakfu mashemasi kwa ajili ya huduma yao. Majukumu yao ni pamoja na:

• Kuwatumikia na kuwasaidia wazee.

• Kuwapokea wazee baadhi ya majukumu ili wao waweze kutumia muda katika maombi na kujifunza neno la Mungu.

• Kujishughulisha na yote yahusuyo kukua na kupanuka kwa huduma ya kanisa la mahali.

• Kutafuta kutatua mizozo inayotokea katika mahusiano ya waumini.

• Kujishughulisha na changamoto zinazotokea kutokana na tamaduni tofauti.

• Kupanua na kuchunguza vipawa vyao wenyewe.

• Kuliruhusu neno la Mungu lifanikiwe.

Katika makanisa yetu ya siku hizi, watu hawa wanaweza kuwa pamoja na wale wa-naoongoza vikundi vya nyumbani na wale waongozao vikundi vya uinjilishaji, vikundi vi-navyoongoza ibada na vingine vifananavyo na hivyo.

B.3. Vikundi vya Kitume, Kinabii

Kwetu sisi, kati ya mambo yanayotusikitisha miongoni mwa mashtaka juu ya Kanisa ni kule kutangatanga na kwenda mbali na mfumo wa Kanisa kama ulivyo ndani ya Maan-diko. Kanisa linaonekana kubweteka likiendelea kuzungumzia makardinali, maaskofu wakuu, wasimamizi na kadhalika, kuliko lilivyo katika kuzungumzia mitume na manabii.

92

Page 101: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Maandiko yasingeziweka ngazi hizo kama zingekuwa hazina umuhimu ndani ya kanisa la mahali. Vikundi au timu za kitume, kinabii ni vya lazima kwa ajili ya kulileta kanisa la mahali katika:

• Umoja.

• Kukomaa.

• Uthabiti.

• Kujengwa.

“Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjil-isti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutaka-poufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mka-milifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo.

Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila ki-ungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.” (Efe 4:11-16)

Siyo tu kwamba huduma hizi hufanya kuwe na umoja, kukomaa, uthabiti na kujengeka kwa makanisa ya mahali, pia wenye huduma hizi huyatia nguvu makanisa ya mahali wanayoyatumikia, kwa kuyasaidia na kuyaongoza, hata kuyaingiza katika ushiriki mkubwa wa jukumu la kuwafanya mataifa wawe wanafunzi. Dudley Daniel anasema kwamba vikundi vya kitume vinaweka mfumo wa kiutawala wenye mazingira yanayofaa kwa ajili ya ufalme wa Mungu, kwa:

• Kuinua vikundi au timu za kitume.

• Kuanzisha makanisa na kuyaingiza makanisa katika hali ya kukomaa.

• Kuendeleza makanisa yenye utamaduni wa kitume/kiunabii.

• Kujenga mitandao na vikundi au timu nyingine za kitume na kinabii kwa ajili ya kuyagusa mataifa ya ulimwengu kwa namna ambayo itayabadilisha.

• Kuwafanya mataifa wawe wanafunzi kwa kuanzisha makanisa ya Agano Jipya ambayo nayo yataleta mabadiliko ndani ya jamii yanamoanzishwa.

Ni heshima iliyoje kwetu sisi kuwa washiriki wa maono ambayo yameenea kila pembe ya dunia yanayotafuta kuleta mabadiliko katika kila utamaduni na tamaduni ndogo zilizo ndani ya tamaduni kubwa ili kuharakisha kurudi kwa Bwana.

C. Moyo Wetu (Kiini Au Roho ya Utamaduni Wetu)

Kama vile mama anavyokuwa kioo cha maisha katika familia, vivyo hivyo, kila kanisa la mahali lina kiini au roho ya utamaduni wake ambao ni wa Kikristo katika hali ya ujumla wake lakini pia maalum kwa kanisa la mahali, hivyo kulipa kanisa hilo ladha ya kipekee na mapigo yake ya moyo. Kwa kadiri tunavyotafuta kuyaonyesha yale ambayo Mungu ametuita tuyafanye, tutakuwa:

93

Page 102: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

• Wenye msimamo usiotetereka.

• Wenye kufaa kwa mahitaji yaliyopo.

• Walio halisi.

• Wenye mahusiano.

Ukijifunza kuyajua Maandiko kwa uaminifu kutoka kitabu cha Mwanzo hadi ufunuo, uta-ona kwamba Mungu ni mwenye msimamo usiotetereka na pia mwenye kuhusiana. Kwa maneno mengine anafananishwa na mwanadamu mwenye upendo apendaye sana ku-jenga mahusiano ya upendo. Ukianzia na uhusiano wake na Adamu hadi kujitoa kwake na upendo wake kwa taifa la Israeli, toka kwa Abrahamu, Musa na Yoshua hadi manabii, kwa Kristo aliyechukua mwili wa kibinadamu, mahusiano ndani ya Kanisa yanatoa ufun-guo wa kuyaelewa maisha ya kanisa. Kwa hakika, sisi sio shirika, kampuni ya biashara au taasisi. Kwa kadiri uhalisi wa mahusiano ulivyo, sisi ni familia inayotafuta kuishi moyo au kiini hiki katika njia za kawaida, katika mtazamo ulio wa wazi na wa kweli wa imani yetu. Mambo haya tunayoyathamini yanaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

Kulipenda na kuliruhusu Neno la Mungu litawale kila eneo la maisha na mwenendo.

Maombi au sala ni ya lazima kwa kila jambo tufanyalo. Vielelezo vyote vya kibiblia juu ya maombi au sala ni vya muhimu, kwa kadiri tunavyouona uso wa Mungu katika yote tu-fanyayo.

Kuwa na mtindo wa maisha ya ibada. Tunadhihirisha ibada itokayo ndani ya mioyo yetu kwa njia za ubunifu na zinazotosheleza mahitaji ya nyakati tunazoishi, tukidhamiria ku-muweka Kristo awe sababu ya kila tufanyacho.

Urafiki kabla ya utendaji. Kujenga mahusiano yenye nguvu yanayofanya kuwe na uwa-jibikaji kati yetu ni muhimu sana kwetu, tukiudhihirisha upendo wetu kupitia hali ya kuwa wakarimu.

Familia ni muhimu kwa ajili ya yote tuyafanyayo. Tunajitahidi kwa ajili ya watu wenye kila rika, rangi na utamaduni wajumuishwe ndani ya familia ya Mungu, kwa kuwa jumla kama hiyo ndiyo ufalme wa Mungu halisi.

Kuzivuta roho. Uinjilishaji kwa njia ya kujiingiza ndani ya jamii yetu, taifa letu na mataifa ya ulimwengu kwa kuwapelekea Injili.

Kazi ya kuwatunza na kuwafanya watu wawe wanafunzi. Kuwasaidia watu binafsi waweze kukua ndani ya Kristo na kuwaingiza katika ukamilifu walioitiwa kama sehemu muhimu ya ukuhani wa waumini.

Ukarimu. Tunalenga kuwezesha kila ngazi ya huduma kwa kutumia fedha zetu, muda, vipawa na watu. Pia tunalenga kuwafikisha watu wote katika hali ya uhuru wa kifedha na uwajibikaji kifedha.

Kujenga timu au vikundi katika kila ngazi ya huduma. Kupitia mahusiano ya kirafiki tu-natenda yote tuwezayo tukiwa na nia ya kumuwezesha na kumshirikisha kila mmoja ali-tumikie kusudi la Mungu katika kizazi chetu.

Kujenga viongozi wacha Mungu, walio wazi na wanaowajibika. Viongozi wacha Mungu ni viongozi watumishi waongozao wengine kwa kuonyesha mfano.

94

Page 103: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kuwa na moyo wa kiutume na kiunabii. Kuwa wanafunzi “wanaoona” na “kuenenda” kwa kuutii utume mkuu.

Mambo haya, kwa kadiri yanavyoelezwa wazi, yanawakilisha nia yetu ya kuishi kama jamii ya Kikristo ya Agano Jipya. Linakuwa jambo lenye manufaa makubwa kwetu kuta-futa utelekelezaji wa imani yetu katika mipaka ya mambo haya ya thamani. Yanaleta hali ya ukweli na uwazi katika mfumo wetu wa uongozi, na kutusaidia tugundue furaha na utoshelevu wa maisha ya kweli katika jamii ya Kikristo.

D. Tumaini (Maono)“Pasipo maono, watu huacha kujizuia; bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.” (‘watu huangamia’ KJV) Mith 29:18

Hatutakiwi kushangazwa na ukweli kwamba kila muumini binafsi, kila familia, kila kanisa la mahali, kila timu ya kiutume na kinabii tunayohusiana nayo na Kanisa la ulimwengu, wote hawa ni sehemu ya urithi ambao Mungu ametupatia.“Umenipimia sehemu nzuri sana; naam, urithi wangu ni wa kupendeza.” (Zab 16:6 BHN)

Ni heshima na faida iliyo kuu mno kujua kwamba tunao urithi ulio na pande tofauti za upeo. Katika baadhi ya madhehebu ya Kikristo urithi huu unaonekana kama ni wao peke yao. Mtazamo huu ni tofauti na mtazamo unaofundishwa na Biblia. Maandiko yanatupa urithi unaovuka mbali na mtu binafsi na hisia zao za baraka, ustawi na furaha. Tuna-poutambua ukweli huu, ukweli wenyewe huanza kutuingiza katika furaha, utoshelevu, faida na ndani ya majukumu ya kanisa la mahali na timu za kiutume kwa mataifa.

D.1. Kiutume

“Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako.” Zab 2:8 (Angalia pia Mdo 1:8; Mat 28:19-20)

Kwa kiutume tuna maana ya kuwa na mapigo ya moyo wa Mungu kwa ajili ya kwenda na kuwatafuta mataifa ya ulimwengu hata kuwaona wakiguswa na nguvu ya injili.Tunafanya kazi ya kuona makanisa yakianzishwa mahali mahali na kuimarika, na kwa njia ya makanisa yale ya mahali mataifa wanafanywa kuwa wanafunzi. Tunataka kuona mataifa wanafikiwa na kubadilishwa.

Tunataka kuona kila kabila na kila taifa likipata kufaidi faida za injili na kuwaacha wenyewe wafanye uamuzi wa kumkubali au kumkataa Kristo.

D.2. Kiunabii

“Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii”. Ufu 19:10Tunataka kuwa na huduma ya kinabii kwa Kanisa na pia kwa ulimwengu. Kwa Kanisa jukumu letu la kinabii ni kuangusha na kung’oa kila kitu kilicho nje ya duara ya mfumo wa Mungu wa kibiblia na uweza wake. Kwa ulimwengu tunataka kuwa na huduma ya kinabii, kurudisha mfumo wa Mungu katika kila eneo la maisha ndani ya jamii. Tunaamini kwamba injili ipo kwa ajili ya kugusa maisha ya kisiasa, kibunge, kielimu, kiuchumi, kija-mii, kimichezo, kibiashara na katika nyanja za sanaa. Kama Yohana Mbatizaji alivyompa mfalme changamoto, tunaamini kwamba watu wa Mungu wenye huduma ya kinabii wataupa ulimwengu changamoto. Iwe katika masuala ya utoaji mimba au picha chafu, matumizi au mifumo ya kifedha isiyo halali au mamlaka za kisiasa zinazotumiwa kwa faida za wenye uchu, ni jukumu la Kanisa kuinuka na kuchukua msimamo.

95

Page 104: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

D.3. Uinjilishaji

Mtu fulani aliwahi kusema kwamba kanisa ndicho chombo pekee kinachokuwepo kwa ajili ya wale wasio wanachama au washiriki wake. Hii inaelezea kwa usahihi moyo wa upendo kwa waliopotea, na lengo kuu la kanisa linavyowalenga wao. Tunaliona hili kwa uwazi katika huduma ya Bwana Yesu.

‘Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.” Lk 19:10

Ni jukumu letu kuona kwamba injili inasonga mbele. Tunaamini kwamba Yesu ni njia pe-kee ya kwenda kwa Baba. Hakuna njia nyingine ya wokovu inayoweza kuwepo isi-pokuwa kupitia kwake. Tunaamini kwamba Kanisa ni gari la Mungu kwa ajili ya kuuletea ulimwengu unaokufa, chumvi na nuru. Tukitumia njia zote zinazowezekana tunataka tuuguse ulimwengu kwa kutumia nguvu ya injili na kisha tutembee kwa ujasiri wa Maan-diko hata tuweze kuona maisha yao yakiguswa na kubadilishwa.

D.4. Kuchunga, Kufundisha na Mafunzo

“Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu”. Heb 6:1

“Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.” 2Tim 2:2

Maono yetu ni kuwaona wanaume na wanawake wakiingia katika ukamilifu wa maisha ya imani. Pia ni nia yetu, kumchukua kila muumini binafsi, chini ya uongozi wa Roho na kwa njia ya mafundisho na mafunuo ya Maandiko, na kuwaendeleza kutoka katika utoto wa kiroho hadi kukomaa na kuwa watu wazima. Tunataka kumwona kila muumini akitembea toka katika utukufu hadi utukufu, toka katika uhuru hadi uhuru, Kutoka katika hali ya madhaifu hadi ukamilifu, kutoka imani hadi imani na kutoka nguvu hadi nguvu. Huo ndio wajibu wa uwakili wetu kama viongozi, nasi tumejitoa kwa mioyo yetu kwa ajili ya jukumu hilo. Tunaamini kwamba wanaume na wanawake wanaletwa kwetu kwa ajili ya majira ya mafunzo na uwezeshwaji ili wainuliwe na kisha waachiliwe kuingia katika utimilifu wa wito wao. Maono haya ambayo ni kama kiungo cha mkono wa kanisa la ma-hali yana umuhimu mkubwa sana. Siyo tu kwamba tunataka kuwachukua watu kuvuka uelewa juu ya kweli za msingi zinazokutikana katika Waebrania 6, na kuwaingiza katika kina cha mafundisho na uelewa wa kibiblia, lakini pia tunatamani kuyashughulikia masu-ala yanayojitokeza kwa wakati huu ili kuleta utatuzi wa kibiblia juu ya kila suala lililopo. Tunaamini pia kwamba Maandiko yanaendelea kufanya kazi bila kukoma katika kuleta mabadiliko ndani ya maeneo makuu ya maisha yetu. Kwa kadiri tunavyokomaa katika uhusiano wetu na Mungu, ndivyo tunavyochukua majukumu makubwa zaidi ulimwen-guni, tuna hali ya kuonekana kiutendaji katika maisha ya kanisa na mipaka ya mahusi-ano yetu inapanuka, na hivyo kuhitaji hali ya kuendelea kuimarika katika misingi yetu kunakoletwa na kuyajua zaidi Maandiko. Kufundisha kunatuwezesha kuonyesha kwa nje mazingira ya imani yetu jambo linaloongeza kasi yetu ya kukua, kupewa ufunuo na ue-lewa.

E. Vyombo vya Kusafirishia Maono, Thamani“Magari” au “vyombo” vyetu ni njia zile tunazozitumia kutimiza maono yetu na yale am-bayo tumeyaona kuwa ya thamani.

96

Page 105: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

Kila muumini ni lazima ahudhurie ibada katika kusanyiko la kanisa na pia ibada za nyumba kwa nyumba. (Mdo 2:42-47; Ebr 10:25).

Pia, kila mmoja anapaswa kuyapenda na kujitoa kwa mafundisho ya ‘mitume’ kwa ushirika, na “kuishi pamoja kindugu, kumega mkate na kusali.” Mdo 2:42. Kwa hali hii,Makanisa yatakusanyika katika ushirika na pia yatakuwa na ibada za nyumbani kwa misisitizo tofauti katika siku za juma.

Kisha, kila kanisa litaweka kipaumbele kuhudhuria mikutano inayoandaliwa na timu au vikundi vya huduma ya New Covenant Ministries (Huduma za Agano Jipya). Mikutano hii huandaliwa nyumbani na pia kimataifa.

Mikutano hii yaweza kuchukua sura ya sherehe zinazofanyika katika maeneo yaliyocha-guliwa ndani ya miji, warsha za mafunzo ya uongozi na nafasi za huduma ndani ya taifa au mataifa.

F. Muhtasari na HitimishoTukiwa tumejitahidi kuelezea kwa njia nyingi na zilizo tofauti, huu ndio muhtasari wa ma-ono yetu, yale tunayoyathamini na magari au vyombo vyetu. Tunataka tumalizie kwa ku-leta mtazamo wetu mkuu kuelekea utume wetu kwa mataifa. Katika Mat 28:18-20 Yesu anasema wazi, hali akiwa amefikia saa ya kuwaacha wanafunzi wake, kwamba utume wetu wa msingi ni kwenda na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi. Zaidi ya kumfanya mtu mmoja mmoja awe mwanafunzi, kwa hali ya wazi kabisa Kristo anakabidhi fimbo ya mbio za kupokezana za kuwapelekea mataifa injili.

Katika Luka 19:10 tunaambiwa kwamba Mwana wa Mtu alikuja kwa kusudi moja, nalo ni kutafuta na kuwaokoa waliopotea. Kusudi lake la msingi lilikuwa ni kuwatafuta mithili ya kuwanusa ili awagundue walipo na kuwaleta kwake wote waliovunjika mioyo, walio-chubuliwa na watu wenye dhambi wa dunia hii, hao ni wewe na mimi, ili atuingize katika uhusiano na Mungu, atupatanishe sisi na nafsi zetu, sisi na wanadamu wenzetu na pia sisi na mazingira yetu. Kwa sababu hii, utume wetu wa kuwafanya mataifa wawe wana-funzi hauna budi kuwa unaoongezeka nguvu, na sio wenye kupungua. Katika Matendo 1:8 Yesu anasimama juu ya Mlima wa Mizeituni na kuurudia tena wito huu mkuu. Ana-zungumza akimaanisha kwamba hatuna budi tuichukue injili kutoka katika maeneo ya-liyo jirani na sisi na hata kuifikisha katika mataifa yaliyo mbali.

Hili linatakiwa kuwa jambo linalogusa moyo wa kila muumini kwa uzito sana na pia kila kanisa. Kwa kadiri tunavyoendelea kujihusisha na kazi zetu za kikuhani, ndani ya nyumba zetu, makanisa yetu na maeneo yaliyo jirani na sisi, vivyo hivyo tunatakiwa kuu-kumbatia wito wetu wa kikuhani kwa kueneza injili kwa wale ambao bado hawajafikiwa (Rum 15:16). Tunahitimisha kwa kukupa orodha ya Maandiko yanayoionyesha mada hii kila mahali kutoka katika kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Wewe kuwa sehemu ya yale tuyafanyayo siyo tu kwamba ni kujiweka chini ya mamlaka ya Maandiko na katika yale tunayoamini kuwa na thamani ya kweli yanayotokana na ufunuo wa Biblia, lakini pia ni kujitoa, kutokana na hamasa ya kiufunuo, ili kuipeleka injili kwa mataifa ya ulimwengu. Tunaomba Mungu akufungamanishe na kukufanya wewe kuwa sehemu muhimu na moja ya jino katika gurudumu kubwa litakaloweza kuutimiza wito wa utume huu mkuu.

“Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, na miisho ya dunia kuwa milki yako.” (Zab 2:8)

“Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.” (Isa 6:8)

97

Page 106: KUJENGA MISINGI YA IMANI - NCMI Global - · PDF fileKuweka Misingi ya Imani Kadiri tunavyoendelea kukua na kukomaa katika imani yetu ndani ya Yesu ... Sura ya Nane: Biblia 44 A. Kile

“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” (Mat 28:19-20)

“Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.’ ” (Mk 16:15)

“Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” (Mdo 1:8)

“Kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha ku-tajwa.” (Rum 15:20a)

“Ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,” (Ufu 5:9d)

“Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.” (Ufu 22:2b-c)

98