Top Banner
1 ROCE PUBLISHER P.O. Box 7812, Dar es Salaam, Tanzania Kimeandikwa na Profesa Dr Detschko Svilenov,Dr. Sci. Academy of Science of Bulgaria, Sofia Je, Biblia Inasemaje kuhusu Wakati Uliopita, Uliopo na Ujao wa Mwanadamu?
32

J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

Feb 20, 2018

Download

Documents

TrầnLiên
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

1

ROCE PUBLISHERP.O. Box 7812,

Dar es Salaam, Tanzania

Kimeandikwa na

Profesa Dr Detschko Svilenov,Dr. Sci.Academy of Science of Bulgaria, Sofia

J e , B i b l i a I n a s e m a j e k u h u s uW a k a t i U l i o p i t a ,

U l i o p o n a U j a o w a M w a n a d a m u ?

Page 2: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

2

Je, Biblia Inasemaje kuhusu Wakati Uliopita,Uliopo na Ujao wa Mwanadamu?

Kile ambacho kila mtu anatakiwa kufahamu kuhusumwisho wa dunia

Published byROCE PUBLISHERS,Dar es Salaam, Tanzania

© Nehemiah Mission

Toleo la kwanza 2009ISBN............

Kwa mawasiliano:Nehemiah Mission,P.O.Box 4939,Dar es Salaam, Tanzania

Tafsiri na uhariri wa mwisho:Askofu Rodrick MbwamboJuni, 2009

Kimepigwa chapa na Business Printers Ltd,Lugoda St., Dar es Salaam, Tanzania

Page 3: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

3

Yaliyomo

UTANGULIZI 4

1. Kristo na Mafundisho yake 7

2. Biblia inaweza kuaminiwa na kutegemewa 9

3. Biblia na Sayansi 12

4. Unabii katika Biblia 16

5. Mafundisho ya Biblia Kuhusu Mwisho wa Dunia 26

6. Mwisho wa Hotuba 29

7. Uamuzi wenye Busara 30

Page 4: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

4

Kitabu hiki kinahusu hotuba iliyotolewa mbele ya wabunge, maprofesawa vyuo vikuu, waandishi wa habari na wafanyabiashara, kwenyebunge la Bulgaria. Baadaye maelezoya hotuba hii yalichapishwa katika gazeti kubwa la kila siku la Bulgarialiitwalo ‘TRUD’, la tarehe 3 Marchi, 2001. Nakala laki tatu arobainielfu za gazeti hili zilichapishwa siku hiyo. Katika hotuba hii Profesa.Dr. Detschko Svilenov anaonyesha msimamo wa Biblia kuhusu Wakatiuliopita, uliopo na ule ujao wa wanadamu.

Mtoaji wa hotuba hii pamoja na marafiki wake, wameamuakuichapisha hotuba hii kwa lugha mbalimbali kutokana na kuelewaumuhimu wa kila mtu kujua mambo yaliyozungumziwa katika madahii likiwemo lile la mwisho ya dunia. Hebu sasa fuatana na profesa Dr.Detschko Svilenov katika hotuba yake aliyoitoa mwezi Julai mwaka2000.Ndugu waheshimiwa Mabibi na Mabwana,

Mwaka 2000 mamilioni ya watu walikusanyika duniani kote,kumkumbuka mtu mashuhuri aliyebadilisha maisha ya watu wengikutokana na kujitoa kwake. Katika kumbukumbu hiyo, watuwaliimimina mioyo yao kumshukuru mtu huyo kutokana nakusababisha mabadiliko makubwa katika maisha yao. Niwe wazi zaidikusema kuwa, ujio wa Yesu Kristo duniani ndilo tukio kubwa kulikomatukio mengine yote yaliyowahi kutokea katika historia yamwanadamu. Ni uumbaji wa mwanadamu peke yake ndio unaoweza

UTANGULIZI

Page 5: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

5

kulinganishwa na tukio hili. Miaka elfu mbili iliyopita, mtu huyumashuhuri alizaliwa kwa njia isiyo ya kawaida. Kuzaliwa kwakekulitabiriwa na manabii miaka maelfu huko nyuma, na ulimwenguulikuwa unamngojea kwa hamu kubwa. Baada ya kuzaliwa aliishimaisha ya kawaida, akifanya kazi kwa uaminifu na jamaa zakewalikuwa watu wa kawaida.

Ingawa mtu huyu hakuwahi kukuandika kitabu cho chote, vitabuvilivyoandikwa juu yake ni vingi kuliko vile vilivyoandikwa kuwahusuwatu wengine mashuhuri katika historia ya mwanadamu. Hotuba zakezimehifadhiwa kwa karne nyingi kama urithi mkamilifu kwawanadamu. Maneno yake ni uzima, yanafanya kazi na yametafsiriwana kuenezwa ulimwenguni kote katika lugha na ndimi zaidi ya elfunne. Kama hili halitoshi, zaidi ya watu bilioni moja wamejiweka chiniya uanafunzi wake licha ya kuwa katika kuishi kwake, hakuwahikuanzisha chuo cho chote. Yesu Kristo hakuwa mkandarasi wamajengo, lakini majengo mengi makubwa na ya kuvutia yamejengwakwa ajili yake. Amewavutia wanamuziki mashuhuri duniani kutungakutengeneza muziki unaohusu tabia, mwenendo na nguvu ya manenoyake, licha ya kuwa yeye mwenyewe hakuwa mwanamuziki.

Mtu huyu alikuwa sio daktari, lakini aliponya na anaendelea kuponyawatu walio na magonjwa ya kila aina. Hali kadhalika, ulimwenguumejaa kazi za kuvutia za kisanii zinazohusisha maisha yake na kazizake, licha ya kuwa hakuwa msanii. Yesu Kristo hakuwa ‘Jenerali’,lakini ana majeshi mamilioni kwa mamilioni katika kila nchi duniani.Sambamba na mabadiliko haya yaliyotokana na ujio wake, historia yawanadamu nayo imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo nimaisha kabla ya Kristo (K.K), na maisha baada ya Kristo (B.K).Shuhuda hizi kuhusu ukuu wake zinaonyesha upekee usio na mipakawa udhihirisho wa nguvu na mamlaka yake.

Kutokana na mabadiliko yaliyosababishwa na maisha ya mtu huyu,watu wengine katika miaka tuliyo nayo wanamwangalia kama mletamabadiliko na maendeleo katika jamii. Ukiangalia jinsi wanadamuwalivyoishi kabla ya Kristo, utakubaliana na ukweli huu kwa asilimiamia moja. Maisha ya wanadamu na ustaarabu wake yanawiwa nayekutokana na mafundisho yake kuwa sababisho la kukomeshwa kwabiashara ya utumwa, pamoja na kurejesha hadhi na heshima yawanawake. Kabla ya ujio wake dini na jamii nyingi zilikuwazinamchukulia mwanamke kama chombo cha kuzaa na kutumiwatu. Lakini Yeye alipokuja alisema; “…Hakuna mwanamume walamwanamke, maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika

Page 6: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

6

Kristo Yesu” (Wagalatia 3:28).Pasipo shaka yoyote, maadili ya Kikristo yamesababisha mtizamo

wa jamii kuhusu mwanamke kubadilika na kuwa bora zaidi. Kutokanana mabadiliko ya kidemokrasia yanayoendelea katika mataifambalimbali, maendeleo na usitawi katika kila nchi yanapimwa kwakuangalia nafasi za wanawake kiutawala katika nchi au jamii husika.

Mtu yeyote mwenye mashaka anatakiwa kutambua kuwa sayansi,mahakama, dini, sanaa, historia, falsafa pamoja na mambo mengineyanayohusu ustaarabu wa mwanadamu, vinashuhudia upekee wauwezo na mvuto wa Yesu Kristo katika jamii. Kama vile Mungu asivyona mwanzo wala mwisho, ukuu wa Yesu Kristo nao hauna mwisho.Mashirika mbalimbali vya kijamii duniani yanathibitisha kuwa rehemana udugu wa kipekee katika kuhudumiana kwa kiwango kikubwa nimatunda ya Ukristo. Pasipo shaka yoyote waanzilishi wa shirika kubwaduniani linalotoa misaada ya kibinadamu la Msalaba Mwekundu,waliongozwa na Roho Mtakatifu na mafundisho ya Yesu Kristo,kuchagua alama ya Kikristo kuwa ni nembo ya shirika lao. Yesualitupatia kanuni ya msingi kuhusu maisha ya kuhudumiana palealiposema, “Yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyiwatendeeni vivyo hivyo” (Mathayo 7:12). Hali kadhalika katikawaraka wa Warumi tunakutana na maneno yasemayo, “Adui yakoakiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe” (Warumi12:20).

Page 7: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

7

Je, Yesu Kristo pamoja na mafundisho yake anatuhusu vipi katikanchi yetu? Je, taifa letu linawiwa nini na Ukristo? Ingawa ulimwenguleo una orodha ndefu ya watu mashuhuri wanaokumbukwa kutokanana kazi walizozifanya, bado Yesu Kristo ndiye aliye na mvuto mkubwakuliko wote. Miongoni mwa viongozi mashuhuri wa kidini tusiowezakuwalinganisha na Yesu ni pamoja na Ndugu Kirilos na Methodios,Mt. Klementi wa Okrid, shemasi Wasili Levski pamoja na watu wenginekatika nchi yetu waliotumia vipawa vyao kuijenga nchi yetu. Je, kwanini Yesu Kristo peke yake awe ndiye ufunguo wa historia yamwanadamu? Yesu alilijibu swali hili katika Injili ya Yohana Yesukwa kusema: “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima” (Yohana14:6). Andiko hili limebeba ukweli wa kipekee kuhusu asili yake,mafundisho aliyoyatoa, umishenari wake na kazi ya ukombozialiyoifanya kama Mwana wa Mungu aliye Hai. Asili peke yake pamojana habari zote za kweli zinazomhusu, ndiyo ni Biblia.

Mpaka sasa katika hotuba yangu nimesisitiza juu ya mambomakubwa matatu ambayo ni, Yesu Kristo, Biblia na mwanadamu.Ninachotaka ukione hapa ni kuwa, ingawa katika hotuba yangunitazungumzia ukumbusho wa kuzaliwa kwa Kristo kamaunavyoonekana katika Biblia, nitakazia zaidi habari zinazomhusu YesuKristo, Biblia na mwanadamu kama zilivyoandikwa katika Biblia. Kaziya ukombozi iliyofanywa na Yesu Kristo, ndiyo mhimili mkubwa wamaisha ya wanadamu na maana ya injili ya Kristo. Ujumbe ulio

KRISTO NAMAFUNDISHO YAKE

Page 8: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

8

muhimu kuliko jumbe zote zinazoweza kumvutia kila mtu ni kuwaKristo alikuja, Kristo yupo na Kristo atarudi.

Sambamba na ukweli huu, upekee na umaarufu wa Biblia unazaamaswali yafuatayo: Je, ujumbe wa Mungu kwa wanadamu yaaniBiblia, unastahili kuwa msingi wa kweli? Je, tunaweza kuziamini nakuzitegemea habari zote ambazo Biblia inatupatia? Kutokana na madayetu tutalazimika kuamua msimamo wa kuchukua katika maisha yetu.

Page 9: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

9

Kimsingi mwanadamu anaweza kumfikiria Mungu kwa njia kuu mbili:Njia ya kwanza ni ile ya kuongozwa na mawazo yake mwenyewe naya pili, ni ile ya kuongozwa na ufunuo kutoka kwa Mungu. Kujaribukumfahamu Mungu kupitia njia ya kwanza kwa kiwango kikubwandiko kulikochangia kuzaliwa kwa dini nyingi pamoja na vikundimbalimbali vya imani za uongo. Dini na imani zote hizi zilianza najuhudi za wanadamu kutaka kumjua na kumfikia Mungu kwa nguvuna akili za kibindamu. Hata hivyo kumfikia Mungu kupitia ufunuokutoka kwa Mungu, ndiyo njia ya pekee iliyo sahihi katika kumjua nakumfikia Mungu. Ukweli huu ndio unaoifanya imani ya Kikristokutofautiana na dini zingine zilizopo duniani.

Kujaribu kumfikia Mungu kwa kutumia nguvu na akili zakibinadamu kunatukumbusha vitabu viwili vilivyoandikwa namwanafalsafa mashuhuri wa zamani wa Kiyunani aliyejulikana kamaAristotele. Kimoja kati ya vitabu hivyo alikiandika kwa ajili ya watuwa kawaida na kile cha pili alikiandika kwa wasomi waliofundishwakupambanua mambo. Hivi ndivyo kazi ya Mungu ilivyo, mwanadamuanaweza kuchagua kumfahamu Mungu kwa kutumia akili na piaanaweza kumfahamu kwa njia ya ufunuo unaopatikana katika Biblia.Watu wanaomtafuta Mungu kwa njia hii ya pili, ndio wanaofanikiwakumwona na kumwamini.

Kitabu hiki cha zamani ni chenye mvuto wa kushangaza. Kilichukuatakribani miaka 1600 kuandikwa hivyo kukifanya kuwa kitabu pekee

BIBLIAinaweza kuaminiwana kutegemewa

Page 10: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

10

kilichokuwa muda mrefu kuandikwa kuliko vitabu vyote vilivyopochini ya jua. Kimeundwa na vitabu 66, vilivyoandikwa na zaidi yawaandishi hamsini. Waandishi hawa waliokuwa wanatofautiana katikaumri, kazi, vyeo, hadhi na elimu. Wengi katika waandishi hawawalikuwa hawajuani, walitoka katika nchi tofauti na kuzungumzalugha tofauti. Mawazo ya waandishi hawa yanaweza kuelezewa kwakutumia wazo kuu moja ambalo ni, “mpango wa Mungu kuhusuukombozi wa wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo pekee ambaye piani Bwana wetu.”

Pasipo shaka yoyote kitabu hiki kimebeba sifa za kipekeezinazokifanya kisifananishwe na kitabu kingine chochote. Kimetafsiriwakwa lugha na lahaja zaidi ya 4000 zikijumuisha lugha ya ‘breli’inayotumiwa na vipofu. Kila mwaka nakala milioni 60 za Biblia ausehemu ya Biblia zinachapishwa duniani kote, hivyo kukifanya kuwakitabu kinachoongoza kimauzo. Sambamba na kuongoza kiuchapishaji,kinaongoza duniani kwa kuenea ambapo kimefikia zaidi ya nusu wawanadamu duniani.

Takwimu za usambazaji wa vitabu zinaonyesha kuwa miongonimwa vitabu vinavyochapishwa na kusambazwa, asilimia tano tu yavitabu hivyo ndivyo vinavyouzwa baada ya miaka saba. Hakika Bibliani Neno la Mungu linalodumu na lisilotikiswa na chochote. Biblia nimsingi wa utamaduni wa kibinadamu na haipingani na sayansi kamabaadhi ya watu wanavyofikiria. Ni kitabu kinachogeuza maadili yajamii kutokana na ukweli kuwa, kinambadilisha mwanadamu.

Wakati uliopita mtu mmoja asiyeamini kuwepo kwa Mungualitembelea visiwa vya Fiji na kumwambia kiongozi mmoja wa kijadimaneno yafuatayo: “Wewe ni ‘chifu’ mkubwa, ila nimesika kuona kuwawewe na watu wako mmekubali kubadilishwa na wamishenari kuwaWakristo.” Baada ya kusikia maneno ya mtu huyu, kiongozi huyu wajamii moja huko Fiji alimwonyesha jiwe kubwa na kumwambia, “Kablaya kuja kwa wamishenari waliotuletea Biblia, tulitoa kafara zawanadamu kwa miungu kwa kubamiza vichwa vyao hadi kufa juu yajiwe hili. Walipokufa tulibanika minofu yao juu ya moto na kuila. KamaBiblia isingetufikia na kuondoa ushenzi wetu, wewe usingerudinyumbani kwako. Kama Injili isingetufikia, ambayo wewe unaidharauna kuikebehi, tungekukata vipande na kuila nyama yako. Biblia ni silahayenye nguvu dhidi ya maovu ya aina zote.”

Mtu mmoja alimzawadia mtoto wake Biblia na kuandika ndani yakemaneno yafuatayo: “Mwanangu, ama Kitabu hiki kitakuzuia kutendadhambi, au dhambi itakuzuia kukisoma.” Nguvu ya kubadilisha

Page 11: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

11

inayopatikana katika kitabu hiki ndiyo inayokifanya kipingwe nakupigwa vita kupita vitabu vyote na wakati huo huo kuongoza kwakupendwa duniani. Kwa maneno mengine, kitabu hiki kinashambuliwana wakati huo huo kusifiwa. Biblia ndicho kitabu kipekee kitokachokwa Mungu, chenye mafundisho yaliyo hai na yasiyo na makosa.Uwezo wake unadhihirisha usahihi wa maudhui yake.

Ndani ya Biblia kuna kweli zinazoeleweka kirahisi, na pia ziko kwelizingine ambazo wanadamu kutokana na ubinadamu wao,wanashindwa kuzielewa. Wakati fulani mpinzani mmoja wa Bibliaalimweleza mwandishi mmoja wa habari ndugu Mark Twain kuwa,anasumbuka kutokana na kutoelewa mambo mengi yaliyoandikwakatika Biblia. Ndugu Mark Twain naye akamjibu kwa kusema, “nduguyangu, mimi ninasumbuliwa na mambo ambayo nimekutana nayokatika Biblia na kuyaelewa!”

Page 12: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

12

Siku hizi tunaishi katika enzi za sayansi, teknolojia na maendeleomakubwa ya kompyuta. Ni wakati ambao sayansi inaenea kupita kiasikatika pande zote. Katika kipindi tulicho nacho mwanadamu anawezakuchambua muundo na umbile la ‘molekuli’ na kufanya utafiti kuhusuasili yake. Kupitia njia ya teknolojia ya vinasaba mwanadamu anawezakuchagua aina ya mnyama au mmea anaotaka kuukuza. Maendeleohaya ya kisayansi yanatufanya tujiulize ikiwa uvumbuzi huuunapingana na ukweli wa Biblia au ikiwa sayansi inakanusha Biblia.Ukweli ni kuwa tunaweza kuiamini sayansi, kuitegemea na kuitumiakuthibitisha kweli zinazopatikana katika Biblia. Mara nyingi watu wasiona elimu ya kutosha na wanaoegemea upande mmoja ndiowanaofikiria kuwa Biblia na sayansi ni vitu viwili vinavyopingana.Misimamo inayofuatwa na baadhi ya watu ya kuwa na imaniinayokataa kufikiri na kufikiri kunakokataa imani, ni misimamo hatariisiyotupeleka kwenye ukweli.

Ili tupate jibu kuhusu swali letu lililohoji ikiwa maelezo yaliyokondani ya Biblia ni ya kuaminika yakilinganishwa na maelezo ya sayansi,inatubidi kulinganisha maelezo ya pande mbili. Kwa kuwa hatunamuda wa kutosha kujibu swali hili kwa undani, nitazungumzia mifanomichache tu inayohusu tafiti na chunguzi za kisayansi zinazohusu elimuya mambo ya kale, elimu ya sayansi ya mazingira, historia, jiografia,fizikia ya uchunguzi wa miamba, sayansi ya kompyuta na sayansi yautabibu. Hata maelezo yanayotokana na sayansi ya fizikia na elimu

BIBLIAn aSayansi

Page 13: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

13

ya uchunguzi wa miamba kuhusu mwenendo na umbile la duniayanapatana kabisa na maelezo ya Biblia. Mifano ya maelezo haya nipamoja na yale yanayohusu gharika, utumwa katika nchi ya Misri,kushambuliwa kwa mji wa Yerusalemu, ustaarabu wa miji ya kalekama vile Babeli, Tiro, Sodoma na Gomora. Habari zilizoandikwa katikaBiblia kuhusu mifano hii zinaweza kuhakikishwa kwa ushahidiulioandikwa.

Kwa kuwa matokeo ya tafiti za kisayansi yanathibitisha habarizinazopatikana katika Biblia, inaonyesha wazi kuwa sayansi,inathibitisha kuwa habari zinazopatikana katika Biblia ni za kweli.Ukweli huu unatupa kuamini habari zote tunazokutana nazo katikaBiblia. Tunapotafakari upekee wa Biblia, tunaweza kuelewa sababuzinazowafanya watu mashuhuri kuiheshimu na kuipenda, kuliko vitabuvingine vilivyoko chini ya jua. Yafuatayo ni maelezo mafupi ya mtualiyeipenda Biblia licha umashuhuri aliokuwa nao katika ulimwenguwa sayansi.

“Siku moja mwaka 1890, wanaume wawili walikuwa wakisafiri kwatreni kutoka mji wa Lyon kwenda Paris. Mmoja alikuwa mzee mwenyendevu nyingi na mvi anayekadriwa kuwa na umri wa miaka 65. Msafiriwa pili alikuwa kijana aliyejulikana kwa jina la Gaston Leroux, mwenyeumri wa miaka 25 hivi. Kijana huyu alikuwa anakwenda kuhudhuriasemina katika asasi ya Profesa mashuhuri nchini Ufaransa ndugu LouisPasteur.

Katika kusafiri kwao walijikuta katika mazungumzo yaliyokuwa nashabaha ya kufahamiana. Baada ya yule kijana kueleza dhumuni lasafari yake, yule mzee alimjibu na kusema. “Ndugu nimefurahi kusikiakuwa unataka kuendeleza kiwango chako cha elimu, sayansiunayotaka kujifunza ni muhimu kutokana na ukweli kuwa itakusaidiakuthibitishia ukuu wa kipekee unaohusu uumbaji. Bila shaka wewe nimwamini.”

Yule kijana alimwangalia yule mzee kwa macho ya dharau nakusema, “kuamini maana yake ni nini? Ninachojua ni kuwa sayansiinaweza kujitegemea bila huyo Mungu mwenye upendounayemzungumzia.” Yule mzee kwa heshima na unyenyekevu hukuakiwa ameshikwa na butwaa, alimjibu kwa kusema: “Ndugu yanguhuo ni mtizamo wako na baadhi ya wasomi wana mtizamounaofanana huo ila ukweli ni kuwa, sayansi ya kweli ….” Kufikia hapoyule kijana aliingilia kati huku akiwa amekasirika na kusema, “ninafikiritofauti kabisa na vile unavyofikiri; sayansi unayoizungumzia ni yazamani na haifanyi kazi katika siku tulizo nazo. Sayansi ya leo ni ya

Page 14: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

14

tofauti kabisa na imepiga hatua kiasi cha kutomhitaji Mungu walausaidizi wowote kutoka kwake.”

Baada ya kuelewa msimamo wa huyu kijana, mzee yule alitambuakuwa kuendelea kuzungumza na yule kijana hakutaweza kuzaamatunda yoyote yaliyo mazuri. Akiwa katika hali ya kuhuzunika, alitoaBiblia ndani ya begi lake, akaomba na kuanza kuisoma. Kabla yakuachana baada ya kufika mwisho wa safari yao, yule mzee alimpatiayule kijana kikadi chenye jina na anuani yake na kusema, “utakapofikakwenye semina usiache kunitafuta licha ya kutofautiana kwetukimtizamo, huenda nikakusaidia kwa namna moja au nyingine.” Yulekijana alipoiangalia ile kadi alikutana na majina yafuatayo, ProfesaLouis Pasteur!

Katika kuwakumbuka watu mashuhuri waliounufaisha ulimwengukwa kazi zao, wako wanasayansi na watu wengi waliopita na waliopowalio na msimamo kama wa Profesa Louis Pasteur wa kulipenda Nenola Mungu. Ningekuwa na muda wa kutosha ningetaja majina mengiya wale wote ambao kwa ujuzi na hekima yao, walisaidia kuelezeakazi kuu za Mungu za ufufuo kuhusu uumbaji kama unavyoelezewakatika Biblia. Kwa unyenyekevu mkubwa watu hawa waliipenda Bibliana kuisoma kila wakati katika maisha yao. Wakati wote watu hawawalimpenda na kumheshimu Mungu kama Muumbaji. Miongoni mwawanasayansi hawa ni baba wa fizikia ya atomu Albert Einstein,mtaalamu wa elimu ya sayansi maisha ya viumbe hai (physiology)Iwan P. Pawlow, mwanzilishi wa nadharia ya kwanta Max Planck namtaalamu katika kazi ya uchunguzi wa miali ulimwengu ndugu RobertMillikan.

Watu hawa walimwamini Muumbaji wao wakitambua kuwa,“Sayansi ni juhudi zinazolenga kuuelewa uumbaji. Kila mara sayansiya kweli hutafuta jibu la swali kuhusu jinsi mifumo ya sayari ilivyotokeawakati ambao imani yenyewe ni kipawa cha Mungu kinachotuwezeshakumfahamu Mungu na sifa yake. Ni muumbaji peke yake ndiyeanayeweza kutoa jibu kuhusiana na sayari na mifumo yake”.Wataalamu wa maendeleo wana uhakika kwamba imani na sayansini pande mbili zisizotenganishika na zinazohitajika katika maisha yawanadamu.

Mwisho naomba nimalize maelezo yangu na manenoyaliyozungumzwa na mwanasayansi bingwa wa zamani aliyejulikanakwa jina la Peter Bamm. Mtu huyu alisema kuwa, “Biblia inafundishakwamba mwanadamu huishi wakati unaoanzia na uumbaji nakumalizikia na hukumu ya mwisho. Kuamini ukweli huu ni faraja

Page 15: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

15

kubwa kwa wanadamu na kuzaa matumaini yasiyo na mwisho. Lakinisiku hizi wako baadhi ya wanasayansi wanaofikiri kwamba wanadamuwanaishi katika kipindi kilichoanza na nyani na kikomo chaokitasababishwa na vita vya silaha za atomu. Kutokana uzushi huuwatu wengi hujikuta katika mashaka makubwa na kukata tamaa.Maneno haya tunaweza kuyaunganisha na maneno ya mtungamashairi wa Kijerumani Johann Wolfgang von Goethe, aliyesemakuwa uwezo na uchangamfu katika jamii au taifa vinategemea nafasiya Biblia katika jamii au taifa husika. Hadi kufikia hapa nadhaninimetoa maelezo yanayotosha kujibu swali lililouliza ikiwa maelezoyanayopatikana ndani ya Biblia yanaweza kuaminika au la. Hata hivyo,ziko hoja nyingine nyingi katika Biblia zinazoweza kuondoa mashakakuhusu yale yaliyoandikwa ndani yake.

Page 16: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

16

Taarifa za kinabii zilizoandikwa katika Biblia ni kitu cha ajabukisichoweza kulinganishwa na maandishi ya dini nyingine zilizopoduniani. Hata kama mtu ni mpinzani mkubwa kiasi gani wa Biblia,kweli zinazohusu nabii hizi zina uwezo wa kunyamazisha upinzaniwake. Mambo yaliyotabiriwa na watu wa Mungu karne nyingi namiaka maelfu iliyopita, yalitimizwa kwa wakati uliopangwa. Katikahali ya kushangaza historia inathibitisha mambo yaliyoandikwa mudamrefu kabla ya kutokea kwake. Uthibitisho wa jinsi hii unaopatikanakatika Biblia peke yake, unaweza tu kuelezewa kama ufunuo kutokakwa Mungu. Mungu peke yake ndiye Muumbaji wa nyakati, ingawaYeye mwenyewe hafungwi na muda. Yeye anapanga, anatawala nakila kitu kinachohusu wakati ujao, kiko wazi mbele zake.

Unabii wa Biblia mara zote unahusu sehemu maalum, watu na halimaalum. Kutokana na maelezo ya kisayansi na elimu ya kawaida yakibinadamu kukubali kuhusu kutimia kwa nabii hizi, ni wazi nabiinyingine za kibiblia zilizosalia kuhusu wakati ujao wa wanadamu, nazozitatimizwa pale muda wake utakapowadia. Ufunuo tunaoupata katikaBiblia ndio msingi pekee unaotakiwa kuongoza maswala yote yawanadamu yanayohusu wakati uliopita, uliopo na ule ujao. Kwakuangalia kutimia kwa nabii hizi, tunatambua wazi kuwa neno laMungu ni kweli na linajipigania lenyewe.

Ili kutoa mwanga zaidi kuhusu nabii za kibiblia ambazo kutimiakwake kumethibitishwa na maelezo ya historia pamoja na uvumbuzi

UNABIIkatikaBiblia

Page 17: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

17

wa kisayansi nitataja baadhi ya nabii hizo. Biblia inasema wazi kuwamaswala yote yanayohusu ulimwengu, uhai na mwanadamu yakomikononi mwa Muumbaji. Vitu vyote vimeumbwa katika hali yaukamilifu na kuwepo kwake kunaongozwa na utaratibuunavyoendana na jinsi vilivyoumbwa pamoja na makusudiyaliyosababisha uumbaji huo.

Uumbaji ni tendo lililokamilika na baada ya hayo mabadilikoyanayoweza kutokea ni yale ya kiwango cha chini (microevolution)na sayansi inathibitisha ukweli huu. Kisayansi ukweli huu unawezakuonekana kwa kuangalia kanuni za kuhifadhi vitu, nishati,mwendojoto, kanuni ya asili na ya matokeo, sayansi ya taarifa na yampangilio, kanuni za sayansi ya mawasiliano na mipango. Kinyumechake nadharia ya ‘evolution’ pamoja na ile ya uumbaji wa vitukujiumbwa vyenyewe kutoka umbo moja kwenda lingine, zinapinganana kanuni za asili zinazohusu sayansi ya viumbe.

Katika Biblia tunasoma kuhusu janga kubwa lililotokea katika historiaya mwanadamu na kusababisha kutenganishwa kwa mwanadamuna Muumbaji wake. Mbali ya kusababisha kifo kwa waasisi wa jangahili, tukio hili la kutisha liliwaletea wanadamu wote mauti. Leo hiibaada ya maelfu ya miaka kupita tangia kutokea kwa janga hili, badoathari ya mwanadamu kutenganishwa na Mungu zinaendelea kuitikisadunia. Kutokana na wanadamu wawili wa kwanza kutomtii Mungu,chuki, uhalifu, ukatili, vurugu, ugaidi, vita, matatizo ya wakimbizi,uzinzi, uasi na mambo mengi yanayofanana na haya, yaliwezakutokea. Mzizi wa maovu haya uko katika sura ya tatu ya kitabu chaMwanzo.

Biblia inatangaza kuja kwa mtu maalum atakayemtengenezeamwanadamu njia ya kuirudia paradisho aliyokuwa ameipoteza. Mungumwenyewe ndiye aliyetoa tangazo la kuja kwa mtu huyo, ambaye piani mwanawe mpendwa Yesu Kristo na ikawa hivyo. Kama zilivyo nabiizingine habari za kutokea kwa mtu huyu zilitabiriwa miaka maelfukabla ya kuja kwake na zikaandikwa katika Biblia. Kwa mfano, mwaka710 K.K nabii Mika alitabiri kuwa Yesu Kristo atazaliwa katika mji waBethlehemu, naye nabii Isaya mwaka 730 K.K alitabiri kuwa YesuKristo atazaliwa na bikira. Katika kitabu cha Zaburi na Isaya kunasura mbili za unabii wa ajabu unaoelezea mateso ya Bwana Yesu, kufakwake msalabani na kufufuka kwake. Mfalme Daudi ndiye aliyetabirimaelezo yanayopatikana katika Zaburi ya ishirini na mbili, miaka 1000K.K. Unabii mwingine ni ule uliotabiriwa na nabii Isaya na kuandikwakatika kitabu cha Isaya sura ya 53.

Page 18: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

18

Ukweli kuhusu ujio wa Mwokozi ulimwenguni, shuhuda za historiaya maisha yake na kazi alizofanya, unaungwa mkono na nabii karibumia tatu nyingine zilizotolewa kabla ya kuja kwake. Katika Biblia zikopia nabii zinazohusu kuangamizwa kwa miji mikubwa ya kale,kuangamizwa kwa mataifa yaliyokuwa na nguvu na kuhusu ustaarabuuliotokea katika mataifa mbalimbali. Ifuatayo ni baadhi ya mifanoinayohusu nabii hizi.Kuangamizwa kwa mji wa Ninawi

Habari za kuangamizwa kwa mji wa Ninawi ni miongoni mwa nabiiza kushangaza ambazo maelezo yake yanapatikana katika Biblia.Habari hizi zilitabiriwa na Nabii Nahumu mwaka 700 K.K. Katikautabiri wake alitabiri kuwa mji mkubwa huu, utaangamizwa kabisana hautajengwa tena. Unabii huu ulitimizwa mwaka 606 K.K, wakatiWamedi walipouharibu na kuuteketeza. Sawasawa na maneno ya NabiiNahumu, mji huu haujawahi kujengwa.Kuangamizwa kwa Babeli

Kufuatana na unabii uliotolewa na Nabii Isaya mwaka 730 K.K. naule uliotolewa na Nabii Yeremia mwaka 650 K.K, ilitabiriwa kuwa mjiwa Babeli utaharibiwa, hautajengwa na watu hawatakaa tena ndaniyake. Badala yake utageuka kuwa kifusi tu. Karne moja baada ya unabiihuu kutolewa, Wamedi walishirikiana na Waajemi kuungamiza mjihuu na hadi leo, bado haujajengwa. Siku hizi limebakia kuwa bwawalisilo na kitu.Kuangamizwa kwa Yerusalemu

Katika injili ya Mathayo Yesu Kristo alitoa unabii ufuatao juu yakuangamizwa kwa mji huu. “Amini, nawaambieni, Halitasaliahapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa” (Mathayo24:2). Mnamo mwaka 70 B.K. unabii huu ulitimia pale Titoalipoyaongoza majeshi ya dola ya Kirumi kuuangamiza. Sawasawana unabii wa Yesu mawe ya hekalu yalibomolewa na wanajeshi wakatiwa kutoa dhahabu iliyoyeyuka na kunasa katikati ya mawe ya kuta zahekalu. Hii ni baadhi tu ya mifano ya miji ya zamani ambayo habariza kuangamizwa kwake zilitabiriwa katika Biblia na kuthibitishwa nahistoria. Mifano mingine inayotajwa katika Biblia ni ile inayohusu mijiya Nofu (Memphis), Ashkeloni, Gaza, Betheli, Samaria, Yeriko,Kapernaumu, Sodoma, Gomora na kadhalika.Tabiri kuhusu kuanguka kwa mataifa maarufu ya zamanikatika Biblia

Sambamba na Biblia kutabiri juu ya kuangamizwa kwa mijimikubwa ya zamani, imetabiri pia juu ya kuangamizwa kwa mataifa

Page 19: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

19

makubwa ya kale yaliyokuwa na nguvu. Mataifa yanayohusika katikanabii hizi ni pamoja na haya yafuatayo:Taifa la Waedomu

Hili ni taifa lenye nguvu ambalo mji wake mkuu ulikuwa Petra.Nabii Ezekieli na Yeremia kwa wakati tofauti walitabiri juu yakuanguka kwa taifa hili. Siku hizi wachunguzi wa historia wanakubalikuwa unabii huu ulitimizwa baada ya karne nyingi kupita. Sawasawana unabii uliotolewa, taifa la Edomu lilisambaratika na kufutika kabisausoni pa nchi.Taifa la Wafilisti

Kuangamizwa kwa taifa hili nako kulitabiriwa na nabii Sefania naAmosi. Leo hii eneo lao, ni sehemu ya nchi ya Israeli.Historia ya ulimwengu katika kitabu cha Danieli

Kitabu cha Nabii Danieli nacho kinaelezea unabii wa ajabu wenyeukweli wa kushangaza. Maelezo ya unabii huu yanahusu historianzima ya ulimwengu kuanzia mwaka 2600 K.K wakati wa utawalawa Babeli chini ya Mfalme Nebukadreza, hadi mwisho wa nyakati.Maelezo ya unabii huu yanapatikana katika kitabu cha Danieli suraza 2, 7, 8 na 11. Katika Biblia kuna maelezo na dodoso nyingi zinazohusumaendeleo ya miji ya Babeli, Umedi na Uajemi, Byzanzitine, Misri,Ashuru na Rumi. Mtu yeyote anayefahamu historia kamwe hapinganana kweli wa nabii hizi. Kutokana na usahihi wa maelezo ya nabii hizi,wataalamu waliohusika kuzihakiki walidhania kuwa nabii hiziziliandikwa baada ya matukio yenyewe kutokea!

Sayansi imethibitisha ukweli wa maelezo ya kitabu cha Nabii Danielikuanzia kwa mwandishi mwenyewe na tarehe ya uandishi. Baadayenitazungumzia jinsi unabii wa Danieli unavyohusiana na matukioyanayotokea katika ulimwengu tulio nao na ule ujao. Katika hili ukoukweli kuwa miongoni mwa mataifa ya kale yaliyopo duniani, taifa laWayahudi lina nafasi ya kipekee katika nabii za kibiblia. Ni jambo lakustajabisha kuona kuwa Biblia ilitangulia kutabiri zamani mamboyaliyotokea na yanayoendelea kutokea katika taifa hili. Musa alitabirimambo haya pamoja na nabii Ezekieli katika sura ya 36. Hali kadhalikakatika sura ya 21 ya injili ya Luka tunakutana na maelezo ya unabiiuliotolewa na Yesu Yesu kuhusu taifa hili.

Maelezo ya Biblia katika nabii hizi yalieleza wazi wazi kuwa taifahili litakuwa tajiri na litateswa mara kwa mara. Hali kadhalikazimeelezea juu ya kutubu kwake na mwisho kutekwa kwake na jinsiwatakavyotawanyika katika ulimwengu mzima. Katika kitabu chaYeremia tunasoma kuwa, “Naam, nitawatoa watupwe huko na

Page 20: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

20

huko katika falme zote za dunia, wapate mabaya; wawe kitucha kulaumiwa, na mithali, na dhihaka, na laana katika mahalipote nitakapowafukuza” (Yeremia 24,9). Hivi ndivyo Mungualivyomwambia Yeremia aandike juu ya taifa la Israeli miaka 670hivi kabla kabla ya kufukuzwa kwao. Kwa njia hii taifa hili lilijihukumulenyewe pale waliposema: “Damu yake na iwe juu yetu, na juu yawatoto wetu” (Mathayo 27:25).

Mtu yeyote aliyeona filamu “Schindlers Liste” anaweza kuona kuwaunabii huu ulitimia pale Wayahudi milioni sita walipouawa wakati wavita kuu ya pili ya dunia. Yako maeneo mengi pia katika maandikoMatakatifu yanayozungumzia unabii kuhusu kuanzishwa upya kwataifa la Kiyahudi na kurudi kwao katika nchi yao. Nabii hizizinapatikana katika sura ya tatu ya kitabu cha Hosea, sura ya pili yakitabu cha Yoeli, Zekaria sura ya nane. Hali kadhalika katika Ezekieli36:24 na Ezekieli sura ya 37, tunapata maelezo ya kina kuhusu unabiihuu. Watu waliotawanyika ulimwenguni kote kwa amri ya Mungukwa miaka karibu elfu mbili, waliochukiwa, kuteswa na kudhihakiwa,wamerejea tena mahali pa urithi wao na kuwa taifa kamili mwaka1948.

Kuwepo kwa taifa la Israeli leo ni mfano ulio wazi na kithibitishocha kipekee katika historia kuhusu ukweli usiopingika wa nabii za bibliaunaotokana na kutimia kwake! Nitanataja zaidi nabii zinazohusumambo yajayo kuhusu kifo, hukumu na matukio yajayo ( ‘eskatalojia’),kwa sababu taifa hili limechaguliwa na Mungu na kupewa nafasimaalum kalenda ya historia ya wanadamu. Matukio yanayolitokeataifa hili ndiyo kalenda maalum inayoupeleka ulimwengu katika tukiokubwa la kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Page 21: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

21

Kurudi kwa Yesu Kristo duniani ni sehemu ya mpango wa Mungukuhusu wokovu wa wanadamu na pia ni swala linalozungumziwa sanakatika vizazi mbalimbali. Hata mtume Petro alimuuliza Yesu Kristoswali hili miaka elfu mbili iliyopita. “Tuambie, mambo hayoyatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwishowa dunia” (Mathayo 24:3). Katika kulijibu swali hili, Yesu hakutajamwaka, siku wala saa, badala yake alielezea dalili zitakazotokea kablaya siku hii kuu ya kurudi kwake.

Mtume Petro, Paulo na mwinjilisti Luka waliandika kwa kina kuhusudalili hizi. Hata Yohana katika kitabu chake cha ufunuo wameandikakwa mapana kuhusu dalili hizi. Kwa kuelezea dalili hizi, Biblia imewatoawanadamu katika giza la kutotambua majira ya kurudi kwa Yesu Kristo.Kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka kitabu cha Ufunuo wa Yohanayako maelezo mengi kuhusu nyakati za mwisho na kurudi kwa YesuKristo. Maandiko haya yanaonyesha wazi kuwa habari za kurudi kwaYesu ndicho kiini cha mpango wa Mungu wa wokovu kwa wanadamuWasomi wa Biblia wamegundua kwamba katika kila aya thelathinikatika Biblia takatifu, aya moja inazungumzia juu ya kurudi kwa Yesu.Kinachoonekana hapa ni kuwa kurudi kwake kumeelezewa maranyingi zaidi kuliko kuja kwake kwa mara ya kwanza.

Katika Agano la Kale kurudi kwa Bwana kunatajwa mara kwa marakatika vitabu vya manabii, na katika Agano Jipya ziko sura maalumzinazozungumzia swala hili. Kutajwa huku kunaonyesha jinsi kuzaliwa

MATUKIOYanayoelezaKurudi kwa YesuKristo

Page 22: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

22

kwa Kristo na kazi yake ya ukombozi, kulivyotabiriwa maelfu ya miakakabla ya kutokea. Tunachojifunza kutokana na ukweli huu ni kuwa,yote yaliyotabiriwa katika Biblia kuhusu kurudi kwa Mwana wa Munguna mwisho wa dunia kutatokea bila shaka yoyote. Katika Bibliatunasoma haya: “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenukwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwonaakienda zake mbinguni” (Matendo ya Mitume 1:11).

Unabii huu ndio ujumbe mkubwa katika nabii za Mungu, na niukweli unaogusa mioyo ya wanadamu wote na kuwaletea matumainiwakati wa mashaka, na kukosa raha. Swali kubwa tunaloweza kujiulizakuhusiana na unabii huu wa kurudi kwa Yesu, ni hili la ni lini tukiohili litakapotokea? Mkristo wa kweli anayefahamu Neno la Munguhatathubutu kubashiri saa, siku au mwaka ambao mwisho wa duniana hukumu ya mwisho vitatokea. Ufunuo pekee tulio nao ni manenoyaliyotamkwa na Yesu pale aliposema kuwa, “Si kazi yenu kujuanyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yakemwenyewe” (Matendo ya Mitume 1:7). Hata hivyo kutokana naumuhimu wa mambo haya kwa kila wanadamu, Yesu Kristohakuwaacha wanafunzi wake katika giza kuhusu siku hii ya hukumuna ya kurudi kwake. Katika Biblia tunasoma juu ya hali na matukiombalimbali yatakayotokea duniani yanayojulikana katika Biblia kamadalili za siku mwisho.1. Kutokea kwa nyakati za dhiki

Miongoni mwa dalili za siku za mwisho ni pamoja na vita,kuongezeka kwa maasi, magonjwa, njaa, matetemeko ya ardhi,ukatili,chuki, kuporomoka kwa maadili, uzushi, uongo, kutawaliwa na pesa,ukaidi, kuharibu mimba, kutowajali wengine, ugaidi, tawala mbayana maovu mengine yanayofanana na haya. Katika miaka tuliyo nayomambo haya yameenea kama mafuriko ukilinganisha na ilivyokuwahuko nyuma. Kutokana na mafuriko haya ya maovu na majanga,walimwengu wanayaona mambo haya kama kitu cha kawaida.2. Dalili kupotoka kwa wanadamu kiroho

Yesu alitabiri pia kuhusu mafundisho ya uongo pamoja na walimuwatakaopotosha mafundisho ya kweli ya Yesu Kristo. Wakati huo huoalitabiri kuhusu kuongezeka kwa chuki dhidi ya wanafunzi wa kweliwa Yesu Kristo. Biblia imeeleza bayana kuwa wakristo watateswakatika nchi mbalimbali. Siku hizi tunashuhudia jinsi watuwanavyopotoshwa kiroho kwa njia mbalimbali. Leo hii kuna dinizinazoshughulikia imani za siri zinazomkataa Mungu huku kukiwana ongezeko kubwa la watu wanaojihusisha katika mambo ya uchawi,

Page 23: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

23

nyota, mizimu, kuangalia nyakati mbaya na mafundisho ya dini zaMashariki ambayo kwa kiwango kikubwa huwanasa vijana. Kama hayahayatoshi, kuna ongezeko kubwa la viongozi wa kiroho wanaojiwekawenyewe badala ya kuitwa na Mungu.

Mambo haya yanapingana na maagizo Mungu yanayopatikanakatika kitabu cha Kumbukumbu la torati yanayosema kuwa:“Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yakekati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtuatazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, walamsihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtuapandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kishani kwa sababu ya hayo BWANA, Mungu wako, anawafukuzambele yako. Uwe mkamilifu kwa BWANA, Mungu wako”(Kumbukumbu la Torati 18:10-13). Ukengeufu tulioutajaumeenea kama donda ndugu kila mahali katika mataifa yaliyoendeleana yale yanayoendelea.3. Kuanzishwa upya kwa taifa la Israeli

Tayari tumeonyesha umuhimu wa taifa la Israeli katika usitawi namaendeleo ya wanadamu wote. Kuanzishwa tena kwa taifa la hilihakukuwa tu kwa maana kwa taifa la Israeli, bali ilikuwa pia ni isharaya kuvutia inayoashiria kukaribia kwa siku ya kurudi kwa Yesu na yahukumu ya mwisho. Zaidi ya miaka 2,500 Mungu alimpa nabii Ezekieliujumbe ufuatao; “Tazama, nitawatwaa wana wa Israeli toka katiya mataifa walikokwenda, nami nitawakusanya pande zote,na kuwaleta katika nchi yao wenyewe; … Katika miaka yamwisho, utaingia nchi … juu ya milima ya Israeli, iliyokuwaukiwa wa daima; … Itakuwa katika siku za mwisho, nitakuletaupigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue” (Ezekieli 37:21;38:8.16).

Mwaka 1948 ulimwengu kwa mara ya kwanza ulishuhudia kurudikwa Wayahudi kwa wingi kutoka katika pande zote za dunia, nakuingia katika nchi yao iliyofufuka tena. Baada ya kuingia katika nchiyao ilichukua miaka isiyozidi ishirini, kwa Israeli kuwa taifa mashuhurilenye nguvu katika maswala ya kisiasa,kijeshi na kiuchumi katika eneola Mashariki ya Kati. Sawasawa na maneno ya manabii katika Biblia,taifa hili liligeuza eneo la jangwa kuwa mashamba yenye wingi wamazao.4. Kuinuka kwa taifa la Urusi kijeshi

Unabii mwingine unaohusu siku za mwisho uliotimia ni ule

Page 24: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

24

ulioandikwa katika sura ya 38 ya kitabu cha Ezekieli. Maendeleoyaliyofikiwa na taifa la Urusi na umaarufu wake kijeshi, vinalinganana unabii huu. Mpaka sasa mataifa ya bara la Ulaya Magharibi naAsia yanamwangalia “Dubu wa Siberia” kwa tahadhari kubwa. Hii nikwa sababu, kufuatana na unabii katika kitabu cha Ezekieli, katikasiku siku za mwisho dubu huyu atatoka katika pango lake, ilikushindana na Simba aliye wa kabila la Yuda.5. Kuongezeka kwa maarifa

Kuongezeka kwa maarifa ni jambo lingine tunalokutana nalo katikaunabii wa Danieli unaohusu siku za mwisho. Katika kitabu cha Danielitunasoma maneno yafuatayo; “Lakini wewe, Ee Danieli, yafungemaneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho;wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka”(Danieli 12:4)

Inavyoonekana siku hizi, maarifa ya wanadamu na elimuvimeongezeka kwa namna ya kushangaza. Kamwe hatutakosea paletutakapoziita siku zetu kwa ni ni za sayansi na tekinolojia. Katika karnechache zilizopita mwanadamu alijishughulisha katika uvumbuziuliozaa vitu kama ndege, roketi, simu, televisheni, tovuti, kompyuta,na utandawazi. Ujuzi na elimu vimeongezeka kiasi cha kuufanyaulimwengu uchanganyikiwe. Haijawahi kutokea wakati wowote katikahistoria ya wanadamu ambapo kumekuwa na ubunifu na uvumbuziunaoenea kwa kasi kama ilivyotokea katika siku tulizo nazo.6. Bomu la Atomu na silaha za Nyuklia

“Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hizombingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asilivitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndaniyake zitateketea. Basi, kwa kuwa vitu vyote hivi vitafumuliwahivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katikamwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ileya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbinguzitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea nakuyeyuka?” (2 Petro 3:10-12). Unabii huu wa mtume Petro wasiku za mwisho na kuja kwa Bwana unahusishwa na kipindi cha bomula atomu na silaha za nyuklia. Kwa ujumla kama mtu yeyote atatafakarikwa kumaanisha maneno yanayopatikana katika Biblia takatifu,mashaka na kejeli zake dhidi ya Biblia vitageuka kuwa heshima kuu.7. Kununua na kuuza kwa kutumia namba

“Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajirikwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa

Page 25: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

25

katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;tena kwamba mtu awaye yote asiweze kuuza wala kununua,isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabuya jina lake” (Ufunuo 13:16-17). Maandiko ya aya hizi yanahusuunabii unaohusu kipindi kitakachokuwepo kabla ya siku ya Mwisho.Kulingana na maandiko haya, unabii huu unazungumzia kuanzishwakwa utaratibu kufanya biashara kwa kutumia njia za kielectronikibadala ya pesa taslimu. Kulingana na mfumo huu, kila mtu atapewenamba inayomhusu yeye binafsi, inayoendana na jina lake naasipokuwa na namba hiyo hataweza kununua, wala kuuza kituchochote. Siku hizi karibu asilimia themanini hivi za shughuli za kifedha(transactions) hufanywa kwa njia hizi za kielektronic zinazohusishamatumizi ya kadi.8. Kurejea kwa dola ya Rumi

Katika kitabu cha Danieli sura ya 7 na pia katika kitabu cha Yohana,tunakutana na unabii mwingine unaohusu kuanzishwa tena kwa dolaya Rumi kabla ya kuwadia kwa Siku ya Mwisho. Wanatheolojiawanahusisha unabii huu na Jumuiya ya uchumi ya Ulaya,iliyoanzishwa na mataifa machache ya Ulaya katika mkataba uliotiwasahihi katika mji wa Rumi. Kuondolewa kwa mipaka na kuwepo kwasarafu moja katika mataifa ya jumuiya hii, ni ishara nyingineinayolenga kuwadia kwa mwisho wa nyakati.9. Kuanzishwa kwa umoja wa mataifa

Katika kitabu cha mwisho cha Biblia tunasoma juu ya kuanzishwakwa utawala wa dunia nzima, utakaotokea wakati wa siku za mwisho.“Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwajeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yoteikamstajabia mnyama yule. Wakamsujudia yule joka kwasababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudiayule mnyama, wakasema, Ni nani afananaye na mnyamahuyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye? Naye akapewakinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewauwezo kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua

Page 26: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

26

kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, namaskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanyavita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kilakabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juuya uso wa nchi watamsujudia, kila mtu ambaye jina lakehalikuandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana-Kondoo,aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia” ( Ufunuo 13:3-8). Kuanzishwa kwa umoja wa mataifa (UNO) pamoja na miundoyake ya kijeshi, uchumi, na shirika la fedha duniani, ni moja ya daliliya wazi ya kukaribia kwa siku ya mwisho.

10. Kasi ya kuhubiriwa kwa injili ya UfalmeYesu Kristo anasema: “Habari Njema ya ufalme itahubiriwa

katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote;hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” (Mathayo 24:14; Luka24:47; Matendo 1:8). Kuhusiana na dalili hii ni wazi kuwa kukuakwa sayansi na tekinolojia pamoja na kuenea kwa Ukristo, vimechangiakuleta mabadiliko yaliyoupata ulimwengu katika karine zilizopita.Kuwepo kwa njia za kisasa za mawasiliano kwa kiwango kikubwakumechangia kufikiwa kwa maendeleo haya ya Umisheni wa imaniya Kikristo. Kuenea huku kwa injili ya ufalme wa Mungu dalili ya waziinayoonyesha kukaribia kwa siku ya kurudi kwa Yesu.

Page 27: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

27

Mpaka kufikia hapa tumeangalia matokeo machache yaliyotabiriwakatika Biblia, kama ishara za siku za mwisho. Kutokea kwa dalili hizikunatuwezesha kuelewa kukaribia kwa siku Kristo atakaporudi duniani.Jambo la kuzingatia hapa ni kuwa dalili tlizoziongelea sizo zinazoitwasiku za mwisho. Kile tunachojifunza ni kuwa dalili hizi, ni mwanzo tuwa uchungu na maumivu kwa wote waliokataa kuziamini habarinjema ya Yesu Kristo (Mathayo 24:8). Hali kadhalika, dalili hizizinaashiria mwanzo wa furaha kwa wale wote wanaomwamini YesuKristo, atakayerudi kuwachukua. Ili kukuza ufahamu wetu kuhusukile kitakachotokea siku za mwisho, naona ni vema tuangalie kwaundani jinsi Biblia inavyotufundisha kuhusu mfuatano wa matukiohaya ya siku za mwisho.1. Kunyakuliwa kwa kanisa

Baada ya kukamilika kwa ishara za siku za mwisho tulizokwishakuziangalia, Yesu Kristo atarudi duniani. Kulingana na maelezo yaagano jipya kuja kwake kutatokea katika awamu kuu mbili. Awamuya kwanza ni tunayoiongelea iliyotajwa katika Biblia kama Unyakuowa kanisa.

Mtume Paulo katika waraka wake kwa Wathesalonike ametumiamaneno yafuatayo kulielezea tukio hili: “Kwa sababu Bwanamwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, nasauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; naowaliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio

MAFUNDISHOya BibliaKuhusuMwisho wa Dunia

Page 28: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

28

hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ilitumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwanamilele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo” (1 Wathesalonike4:16-18).

Kunyakuliwa kwa kanisa litakuwa ni tukio la kufumba na kufumbuana si watu wote duniani watakaoliona au kuelewa kwa kina kuhusukutokea kwake. Unyakuo utawatenga waamini dhidi ya wasioaminina kasha kutatokea mateso duniani ambayo hayajawahi tangia duniakuumbwa. Kitakachotokea katika utenganisho huu ni kuwa, walewatakaokutwa duniani wakiwa hai, watabadilishwa na kuchukuliwakwenda mbinguni pamoja na wenzao watakaofufuliwa wakatiparapanda ya mwisho itakapolia. Tukio hili litauacha ulimwenguukiwa na wale tu waliokataa kumwamini Yesu Kristo.2. Kipindi cha dhiki kuu

Baada ya kunyakuliwa kwa wanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo,kitaanza kipindi cha dhiki kuu kitakachoambatana na kuanzishwa kwautawala wa mfumo wa kifalme. Utawala huu utakaotambulika kwaalama ya namba 666, na utaongozwa na mpinga kristo. Kulingana naunabii unaomhusu mtu huyu unaopatikana katika kitabu cha Ufunuowa Yohana, mpinga Kristo ataitawala dunia kwa ukatili usio na kifanikwa kipindi cha miaka saba.3. Vita vya Har magedoni

Kulingana na unabii wa Yesu katika injili ya Mathayo, wakati wadhiki kuu, dunia itapigwa kwa mapigo mbalimbali ya kutisha hadipale Kristo atakapokuja duniani kwa nguvu, na utukufu mwingi, akiwapamoja na watu wake. “Lakini mara, baada ya dhiki ya sikuzile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, nanyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbingu zitatikisika”(Mathayo 24:29).

Baada ya kipindi hiki cha dhiki kuu, Yesu atarudi tena duniani akiwapamoja na watakatifu walioungana naye wakati wa unyakuo. Kurejeakwake kutafuatiwa na vita kubwa kati ya majeshi ya mataifambalimbali, dhidi ya Kristo na jeshi lake. Kulingana na unabii katikakitabu cha Ufunuo wa Yohana Vita hii ambayo Kristo atakuwamshindi, itapiganwa mahali paitwapo Harmagedoni.4. Utawala wa Kristo wa milenia

Baada ya ushindi wa Yesu katika vita ambayo wataalamu wa Bibliawanaiita vita kuu ya tatu ya dunia, ufalme wa Kristo na watakatifuwake utaanza hapa duniani. Biblia inauita utawala huu, utawala wamilenia yaani, utawala wa Kristo wa miaka elfu duniani.

Page 29: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

29

5. Ufufuo wa wasioaminiMwishoni mwa utawala wa Yesu, utafuatia ufufuo wa wale wote

waliokataa kumwamini Yesu Kristo wakati wa uahi wao. Watu hawawatasimama mbele ya Kiti cha Enzi Cheupe, na kuhukumiwa na kashakutenganishwa na Muumbaji wao milele. Watu hawa watapelekwaziwa la moto, ziwa ambalo Biblia inaliita Jehanamu, hiyo ndiyomaskani ya milele ya Shetani na mauti.6. Kubadilishwa kwa mbingu na dunia ya sasa

Baada ya kukamilika kwa matukio yote niliyotangulia kuyaelezea,mbingu na dunia zitapitishwa katika moto na kasha, Mungu ataumbambingu mpya na dunia mpya mahali ambapo kweli na amanizitakapotawala milele. Mahali hapa palipo na raha isiyo na kikomondipo yatakapokuwa maskani ya milele ya wale wote watakaomkubaliYesu Kristo kuwa ni Mwana wa Mungu na kumpokea maishani mwaokama Bwana na Mwokozi wao.

Page 30: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

30

Ndugu wapendwa,Wakati wa kuingia mwaka 2000, watu wengi walidhania kuwa huo

ndio utakapokuwa wakati wa kutukia kwa matukio haya ya siku yamwisho. Walishangaa pale mwaka huo ulipopita bila mambo hayakutokea. Katika hili tunatakiwa kujihadhari na watu wa jinsi hii, tukijuakuwa hakuna mahali popote katika Biblia palipotaja siku, mwezi aumwaka wa kurudi kwa Yesu Kristo. Biblia imezungumza tu bila kuficha,kuwa siku hiyo itakuja ila hatujui kuwa ni lini. Huenda tumebakiwana mwaka mmoja, miaka kumi, karne moja na inawezekana kwambatunayo nafasi ya mwezi mmoja au siku moja tu. Kwa kuwa hatujuisiku wala saa, ni vema tuishi huku tukitambua kuwa Yesu Kristo pekeyake ndiye anayeshika majaliwa ya maisha yetu mikononi mwake.Tena kuna kitabu kimoja pekee kinachofaa kuongoza maisha yetupamoja na kutupeleka kwa Mungu. Kitabu hiki ni Biblia Takatifu.Mungu akubariki kwa kuisoma hotuba hii.

MWISHOwa hotuba

Page 31: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

31

Mpendwa ambaye umesoma kitabu hiki, napenda ufahamu kuwaMungu hana upendeleo. Mbele zake wanadamu wote wako sawa. Yeyeanaokoa wote wanaomjia bila kujali hali zao kiuchumi, elimu, rangi,kabla, dini, mila au utamaduni. Kitu pekee kinachoangaliwa nakuheshimiwa na Mungu ni hiari ya mtu katika kuamua mustakabaliwa umilele wa maisha yake. Hii ndiyo sababu iliyomfanya amuumbewanadamu na uhuru wa kuchagua aina ya maisha anayotaka kuyaishi.Kwa kinywa cha Yoshua aliwaambia wana wa Israeli manenoyafuatayo; “…Chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba nimiungu ile ambayo baba yenu waliitumikia…lakini mimi nanyumba yangu tutamtumikia BWANA…” (Yoshua 24:20). Yesualipokuja alizungumza maneno yanayofanana na haya pale aliposema:“Tazama nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sautiyangu, na kufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakulapamoja naye, yeye pamoja nami” (Ufunuo 3:20).

Mpenda, umepata nafasi ya kusoma mambo yanayoungojeaulimwengu tulio nao, yatakayowapata wanadamu wote weweukiwa mmoja wao. Neno la Mungu limetuonya kuhusu mambohayo kwa kupitia maneno yafuatayo: “Basi kwa kuwa vituvyote hivi vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watuwa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu na kuihimiza; ambayokatika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya

UAMUZIwenyebusara

Page 32: J e , Bib lia I n a s e m a je k u h u s u Wa k a t i U ...biblia-inasemaje.mwokozi.com/biblia_inasemaje.pdf · Wa k a t i U lio p it a , U lio p o n a U ja o w a M w a n a d a m

32

asili vitateketea na kuyeyuka?” (2 Petro 3:11-12).Neno la Mungu linasema leo hii kama utaisikia sauti ya Mungu

usifanye moyo wako kuwa mgumu. Hima ikimbie ghadhabu ya Mungukwa kumkubali Yesu Kristo ambaye ni dhabihu ya Mungu iliyotolewakwa ajili ya dhambi zako. Yesu Kristo ni mwana-Kondoo aichukuayedhambi ya ulimwengu na leo ndiyo saa yako ya wokovu. Mpe Yesumaisha yake kwa kuamini maneno yafuatayo moyoni mwako nakuyakiri kwa kinywa chako:

“Mungu mwenyezi, mimi ni mwenye dhambi na sina uwezowa kuziondoa, wala dini yangu haina uwezo wa kuziondoa.Naamini juu ya dhabihu uliyoitoa yaani Yesu Kristo mwanawako mpendwa. Kwa hiari yangu namkubali awe Bwana namwokozi wangu binafsi. Natubu dhambi zangu zote leo hii naninayatoa maisha yangu ili yatawaliwe na wewe. AsanteMungu kwa kunisikia, kunikubali, kunipokea na kuniokoakatika jina la Yesu mwanao” Ameni.