Top Banner

of 104

Hotuba Ya Kuagana Na Kuvunja Bunge La Kumi, 2015

Nov 04, 2015

Download

Documents

HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA KUAGANA NA KUVUNJA BUNGE LA KUMI, 2015.
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
  • 1

    HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO

    KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA

    TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA

    KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YA

    MUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE,

    DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015

    Mheshimiwa Spika;

    Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu

    mwingi wa rehma kwa kutujalia uzima na kutuwezesha

    kuishuhudia siku hii adhimu katika historia ya Bunge letu

    na nchi yetu. Hatimaye siku ya kuvunja Bunge la Kumi

    imewadia ili kuwezesha hatua husika za mchakato wa

    Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ziweze kutekelezwa.

    Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia

    nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu ili niweze

    kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini,

    shukrani zangu kubwa ni kwa uongozi wako mahiri na

    shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi

    rahisi. Penye wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari

  • 2

    mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama

    salmini. Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari

    hodari, uliyethibitisha uhodari na umakini wako katika

    uwanja wa medani. Wewe ndiwe mwanamke wa kwanza

    kushika wadhifa huu wa juu kabisa katika mhimili huu wa

    kutunga sheria na umeidhihirishia dunia kuwa wanawake

    wakipewa nafasi wanaweza.

    Mheshimiwa Spika;

    Niruhusu pia nitoe shukrani na pongezi zangu za dhati

    kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kazi kubwa na nzuri

    mliyoifanya. Mmetimiza ipasavyo wajibu wao wa Kikatiba

    wa Kutunga Sheria na kusimamia Serikali. Nawashukuru

    kwa ushirikiano wenu na msaada wenu. Ni ukweli ulio

    wazi kuwa bila ya ninyi Wabunge wetu na Bunge hili,

    tusingeweza kupata mafaniko na maendeleo tuliyoyapata.

    Mmejijengea, nyinyi wenyewe na Bunge letu heshima

    kubwa mbele ya wananchi. Mmeitendea haki demokrasia

  • 3

    ya Tanzania na kuliletea heshima kubwa Bunge letu nchini,

    kikanda na kimataifa.

    Mheshimiwa Spika;

    Tarehe 30 Desemba 2005 nilipozindua Bunge la Tisa

    nilielezea mtazamo wangu kuhusu nchi yetu na kutaja

    majukumu ya msingi na vipaumbele vya Serikali ya Awamu

    ya Nne. Nilisema tutatekeleza wajibu wetu na vipaumbele

    hivyo kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Tarehe 16

    Julai, 2010 wakati wa kuvunja Bunge hilo nilielezea

    mafanikio tuliyopata na changamoto zilizotukabili katika

    kipindi hicho. Tarehe 28 Novemba, 2010 wakati wa

    kuzindua Bunge hili la Kumi niliainisha vipaumbele vya

    Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika kipindi changu cha

    pili cha uongozi wa nchi yetu na kuahidi kuvitekeleza kwa

    ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi. Kama ilivyo ada, leo

    tunafikia mwisho wa uhai wa Bunge la Kumi, naomba

    kutumia fursa hii kutoa mrejesho wa utekelezaji wa

  • 4

    majukumu ya Serikali na yale mambo ambayo tuliahidi na

    kupanga kufanya.

    Umoja, Amani na Usalama

    Mheshimiwa Spika;

    Niliahidi kuwa katika kipindi cha uongozi wangu

    nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa Tanzania

    inaendelea kuwa nchi moja na watu wake wanaendelea

    kuwa wamoja, wanaopendana na kushirikiana licha ya

    tofauti zao za rangi, dini, makabila, mahali watokako, na

    ufuasi wa vyama vya siasa. Pia, kwamba nchi yetu

    itaendelea kuwa yenye amani, usalama na utulivu.

    Leo tunapoagana, ninyi na mimi, ni mashuhuda kuwa

    Tanzania na Watanzania tumebakia kuwa wamoja. Hata

    hivyo, katika kipindi hiki kumekuwepo na matukio ya hapa

    na pale madogo na makubwa, yaliyotishia umoja wa nchi

    yetu na watu wake. Yapo mambo yaliyopandikizwa kuleta

    chuki baina ya Tanzania Bara na Zanzibar, baina ya

  • 5

    Wakristo na Waislamu na baina ya maeneo fulani ya nchi na

    wengine.

    Bahati nzuri, msimamo thabiti wa viongozi wakuu wa

    Serikali zetu mbili wakisaidiwa na viongozi wengine pamoja

    na ushirikiano na viongozi wa dini na wa jamii na uelewa

    wa wananchi, vimeliwezesha taifa letu kushinda

    changamoto hizo na matishio yote hayo. Changamoto hizi

    zimethibitisha ubora wa mazungumzo. Ni kweli kabisa

    kwamba wanaozungumza hawagombani na

    wanaozungumza humaliza tofauti zao bila kugombana.

    Mheshimiwa Spika;

    Niruhusuni, nitumie nafasi hii kuwashukuru kwa mara

    nyingine viongozi wakuu wenzangu, Makamu wa Rais, Rais

    wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu

    wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais

    Zanzibar, viongozi wa dini, viongozi wa jamii na wananchi

    wote kwa ushindi tulioupata katika kudumisha umoja wetu.

    Hata hivyo, tahadhari kubwa lazima iendelee kuchukuliwa

  • 6

    kwani watu wenye nia mbaya kwa nchi yetu au na umoja

    wetu hawajaisha na hawajafurahi kwamba hawajafaulu.

    Huenda wakajaribu tena. Tunachotakiwa kufanya ni

    kuendelea kushikamana ili hata wakijaribu tena washindwe.

    Muungano Wetu Umeimarika Zaidi

    Mheshimiwa Spika;

    Nafurahi kwamba namaliza kipindi changu cha

    uongozi tukiwa tumeweza kudumisha na kuuimarisha

    Muungano wetu adhimu na adimu Barani Afrika.

    Mtakumbuka kuwa katika hotuba yangu ya kufungua

    Bunge la Tisa nilisisitiza umuhimu wa viongozi wa pande

    zetu mbili kukutana mara kwa mara kuzungumzia ustawi

    wa Muungano wetu. Nafurahi kwamba jambo hili

    limefanyika chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais,

    akisaidiwa na Waziri Mkuu kwa upande wa Tanzania Bara

    na kwa upande wa Zanzibar, Waziri Kiongozi katika awamu

    yangu ya kwanza na Makamu wa Pili wa Rais katika

    awamu hii.

  • 7

    Mafanikio yaliyopatikana ni makubwa. Masuala

    mbalimbali ya zamani na mapya yamezungumzwa,

    yameshughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi. Kwa mfano,

    hadi mwaka 2005 zilikuwa zimebakia kero 13 za Muungano

    zilizoainishwa na Tume ya Shelukindo, hivi sasa zimebaki

    kero nne. Tayari ufumbuzi wa kero moja unakamilishwa

    kiutawala na tatu zimeshughulikiwa kwa ukamilifu katika

    Katiba Inayopendekezwa. Kama kura ya maoni ingekuwa

    imefanyika na Katiba hiyo kupitishwa kungekuwa hakuna

    kiporo cha kero za Tume ya Shelukindo. Lakini kwa vile

    kura ya maoni haijafanyika ndiyo maana tunaendelea

    kuzitaja. Hata hivyo, Serikali zetu mbili zimezungumza na

    kukubaliana tutafute njia ya kumaliza suala la rasilimali ya

    mafuta na gesi. Ndiyo maana katika Muswada wa Petroli

    hoja ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ya kusimamia

    uchimbaji wa mafuta na kumiliki mapato yake ilijumuishwa.

    Natoa shukrani nyingi kwa Bunge lako tukufu kwa

  • 8

    kupitisha Muswada huo. Moja ya kero kubwa katika

    Muungano tumeimaliza.

    Mpasuko wa Kisiasa Zanzibar

    Mheshimiwa Spika;

    Mtakumbuka kuwa nilizungumzia kusononeshwa

    kwangu na mpasuko wa kisiasa uliokuwepo Zanzibar

    wakati ule na kuelezea utayari wangu wa kusaidia

    kuuondoa. Kama mjuavyo mazungumzo yalifanyika ndani

    ya CCM na CUF na baina ya vyama hivyo na muafaka

    ukapatikana. Serikali ya Umoja wa Kitaifa ikaundwa na

    mpasuko wa kisiasa ukawa umepatiwa tiba. Matokeo ya

    yote hayo ni kuwa mazingira ya kisiasa na kijamii

    yamekuwa bora zaidi siku hizi kuliko ilivyokuwa kabla ya

    hapo.

    Ni matumaini yangu kuwa ndugu zetu wa Zanzibar

    watayadumisha mafanikio haya ili waendelee kuishi kwa

  • 9

    amani, upendo na udugu. Natambua kuwepo kwa

    changamoto za hapa na pale katika uendeshaji wa Serikali

    hiyo. Jambo linalonipa faraja ni kuwa matatizo yenyewe

    hayahusu muundo wa Serikali bali yanaletwa na watu

    kupishana kauli au kutofautiana katika uendeshaji wa

    baadhi ya mambo. Mimi naamini hayo ni mambo

    yanayoweza kumalizwa kwa wadau kukaa kitako na

    kuzungumza kama ilivyokuwa kabla ya muafaka.

    Amani na Usalama

    Mheshimiwa Spika;

    Nchi yetu iko salama, mipaka iko salama kwa sababu

    Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea

    kutimiza ipasavyo jukumu lake la kulinda uhuru na mipaka

    ya nchi yetu. Katika kipindi hiki tumewekeza sana katika

    kuliimarisha Jeshi letu kwa vifaa na zana za kisasa za kivita

    na mafunzo. Tumeimarisha Kamandi za Nchi Kavu, Anga

    na Majini. Utayari kivita wa jeshi letu ni mzuri tena wa hali

    ya juu. Weledi na nidhamu ya Wanajeshi wetu ni ya hali ya

  • 10

    juu. Tumeboresha maslahi na makazi ya wanajeshi kwa

    kujenga nyumba mpya za kuishi. Utekelezaji wa mpango wa

    kuwajengea nyumba 10,000 unaendelea vizuri. Hadi hivi

    sasa nyumba 6,064 zinaendelea kujengwa nchi nzima na kati

    yake nyumba 3,096 zimekamilika. Namaliza kipindi changu

    cha kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na

    Usalama kwa kujiamini kwamba Tupo vizuri. Pamoja na

    hayo kazi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka 15 wa

    kuimarisha JWTZ lazima iendelezwe ili kulifikisha Jeshi letu

    pale tulipopakusudia.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka 10 hii tumefanya jitihada kubwa ya

    kupambana na uhalifu ili kulinda usalama wa maisha na

    mali za watu waishio Tanzania. Mtakumbuka kuwa mwaka

    2005 na mwanzoni mwa 2006 kulikuwa na matukio mengi

    ya ujambazi. Niliahidi wakati wa kampeni na katika hotuba

    yangu Bungeni kwamba hatutawaacha majambazi

    waendelee kutamba. Hali ile imedhibitiwa. Ingawaje

  • 11

    matukio ya ujambazi hayajaisha, lakini hayako kama

    ilivyokuwa wakati ule.

    Hali kadhalika, matukio ya uhalifu wa kuwania mali

    yamepungua kutoka 53,268 mwaka 2005 hadi 43,808 mwaka

    2014. Natoa pongezi nyingi kwa Jeshi la Polisi kwa kazi

    kubwa na nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kufanya.

    Jambo ambalo bado hatujafanikiwa vya kutosha ni ajali za

    barabarani. Lazima tuendelee kuzitafutia muarobaini wake.

    Niruhusuni niwatambue na kuwashukuru Inspekta Jenerali

    (mstaafu) Omari Mahita, Inspekta Jenerali (mstaafu) Said

    Mwema na Inspekta Jenerali Ernest Mangu aliyepo sasa kwa

    uongozi wao mzuri.

    Mafanikio haya ni matokeo ya uwekezaji wa Serikali

    katika utakelezaji wa mpango wa maboresho ya Jeshi la

    Polisi uliobuniwa wakati wa uongozi wa Ndugu Saidi

    Mwema, IGP mstaafu. Jeshi la Polisi linaendelea

    kuwezeshwa kwa zana, vifaa na mafunzo. Taratibu

  • 12

    zimekamilika za kulipatia Jeshi hilo magari ya kutosha ili

    kuongeza ufanisi.

    Pia, tumeendelea kuboresha maslahi na mazingira ya

    kuishi Maafisa na Askari. Kwa ajili hiyo tumekarabati

    baadhi ya nyumba zilizopo, tumejenga nyumba kadhaa

    mpya za ghorofa, za kawaida na mabweni. Mipango

    imekamilika ya kuwezesha ujenzi wa nyumba 10,000

    ambazo zitapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la uhaba wa

    nyumba za kuishi katika Jeshi la Polisi.

    Mheshimiwa Spika;

    Jeshi letu la Magereza nalo limeendelea kutekeleza

    vizuri majukumu yake ya kulinda wafungwa na

    kurekebisha tabia zao. Aidha, huduma za malazi, mavazi,

    chakula na usafiri kwa wafungwa zimeendelea kuboreshwa.

    Changamoto kubwa ni msongamano wa wafungwa

    Magerezani. Naamini mipango ya kujenga magereza mapya

    na kupanua yaliyopo ikitekelezwa tatizo litaisha. Aidha,

    mpango wa maboresho ya Jeshi la Magereza ukikamilika na

  • 13

    kutekelezwa, utaboresha mazingira ya kufanyia kazi na

    kuishi maafisa na askari, hivyo kupandisha morali wao na

    kuongeza ufanisi.

    Jeshi la Kujenga Taifa

    Mheshimiwa Spika;

    Ahadi yangu ya kuanzisha upya utaratibu wa

    kuchukua vijana wa mujibu wa Sheria katika Jeshi la

    Kujenga Taifa imetimia. Mpaka hivi sasa vijana 38,200

    wamekwisha hitimu mafunzo hayo wakiwemo

    Waheshimiwa Wabunge. Nawapongeza sana Waheshimiwa

    Wabunge walioshiriki kwa kuongoza kwa mfano. Imesaidia

    sana utaratibu huo kuanza upya bila vipingamizi. Ni

    matumaini yangu kuwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Ulinzi

    na Jeshi la Kujenga Taifa watakaa pamoja kujadili namna ya

    kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zilizopo. Naamini

    zinaweza kumalizwa, vijana wetu wakashiriki mafunzo bila

    matatizo yoyote.

  • 14

    Utawala Bora

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi cha miaka kumi hii tumetekeleza

    dhamira yetu ya kujenga na kuimarisha utawala bora kwa

    sera, sheria, mifumo, taasisi na kwa rasilimali watu.

    Tumefanya hivyo katika maeneo yote muhimu yakiwemo

    yale yahusuyo haki za binadamu, demokrasia, mapambano

    dhidi ya rushwa, maadili ya viongozi, ukusanyaji wa

    mapato na nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na

    mgawano wa madaraka hati ya mihimili.

    Bunge la Jamhuri ya Muungano

    Mheshimiwa Spika;

    Serikali imetimiza ipasavyo wajibu wake kwa mhimili

    mkuu wa dola wa Kutunga Sheria. Tulianzisha Mfuko wa

    Bunge na kuongeza fedha katika bajeti ya Bunge toka

    shilingi bilioni 30.58 mwaka 2005/06 hadi shilingi bilioni

    173.76 mwaka 2015/16. Pia tumeanzisha Mfuko wa Jimbo ili

  • 15

    kuwawezesheni Wabunge kuchangia katika kutatua

    changamoto za maendeleo zinazowakabili wananchi wa

    majimbo yao. Bunge letu limetekeleza ipasavyo majukumu

    yake kupitia Kamati zake za kudumu na pale ilipolazimu

    Kamati teule zilizoundwa.

    Katika kipindi hiki miswada 163 imepitishwa, maswali

    ya msingi 7,544 na ya nyongeza 22,632 yameulizwa na

    kujibiwa. Kamati teule 2 ziliundwa. Haya ni mafanikio

    makubwa kwa Bunge letu. Bunge hili limefanya kazi kubwa

    na kazi ya kutukuka. Michango na ushauri wake umekuwa

    chachu ya baadhi ya hatua na mabadiliko ya kisera, kisheria

    na kiutendaji yaliyofanywa na Serikali. Kwa kweli

    mnastahili pongezi nyingi. Huwezi kutaja mafanikio ya

    Serikali ya Awamu ya Nne bila kutambua mchango wa

    Bunge hili.

    Mchakato wa Katiba

    Mheshimiwa Spika;

  • 16

    Kama sote tujuavyo, kupitia Sheria iliyotungwa na

    Bunge hili, mwaka 2013 tulianzisha mchakato wa

    Mabadiliko ya Katiba kwa lengo la kuipatia nchi yetu Katiba

    mpya iliyo bora zaidi kuliko iliyopo sasa. Nafurahi kwamba

    mchakato huo ulituwezesha kupata Katiba

    Inayopendekezwa ambayo imekidhi matarajio hayo.

    Narudia kutoa pongezi za dhati kwa Tume ya Mabadiliko

    ya Katiba na Bunge Maalum la Katiba kwa kazi kubwa na

    nzuri waliyofanya. Hatua iliyobaki ni Kura ya Maoni

    ambapo sote tunasubiri maelekezo ya Tume ya Uchaguzi.

    Mimi naamini iwapo itapitishwa, Katiba Inayopendekezwa

    itaimarisha zaidi taifa letu.

    Vyama vya Siasa

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumeshuhudia vyama vya siasa

    vikiendelea kuimarika na kujijenga nchini. Idadi ya vyama

    vya siasa imeongezeka kutoka 18 hadi 24. Vyama vya siasa

    vimefanya shughuli zake kwa uhuru. Viongozi na

  • 17

    wanachama wao wamefanya mikutano mingi na hata

    maandamano kote nchini. Baraza la Vyama vya Siasa na

    TCD vimekuwa vyombo muhimu vilivyofanya kazi nzuri ya

    kujenga ushirikiano miongoni mwa vyama vya siasa.

    Yamekuwa majukwaa muhimu ya mashauriano baina ya

    vyama vya siasa kwa masuala mbalimbali. Matatizo na

    changamoto nyingi zimeweza kupatiwa ufumbuzi. Ni

    matumaini yangu kuwa vyombo hivi viwili vitaendelezwa

    na kuimarishwa miaka ijayo.

    Huu ni mwaka wa Uchaguzi, na vyama vya siasa ndiyo

    wahusika wakuu. Ni matumaini yangu kuwa vyama vya

    siasa vitaheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi. Hii

    itasaidia kuwepo kwa utulivu na amani katika mchakato wa

    uchaguzi.

    Uchaguzi Mkuu

    Mheshimiwa Spika;

    Habari kubwa hapa nchini sasa ni uchaguzi mkuu.

    Tayari Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na ile ya Zanzibar

  • 18

    (ZEC) zimekwisha tangaza tarehe 25 Oktoba, 2015 kuwa ni

    siku ya kufanyika uchaguzi mkuu. Maandalizi ya uchaguzi

    huo yanaendelea vizuri. Tume ya Taifa ya Uchaguzi

    inaendelea na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwa

    mfumo mpya wa teknolojia ya Biometric Voters Register

    (BVR). Hadi sasa zoezi la uandikishaji limekamilika katika

    mikoa 13 na linaendelea katika mikoa 11 na katika mkoa wa

    Dar es Salaam na Zanzibar uandikishaji unategemea kuanza

    mwezi huu. Kwa taarifa za Tume ya Uchaguzi, tayari

    wamekwisha andikisha hadi sasa wapiga kura milioni 11

    kati ya lengo la kuandikisha wapiga kura kati ya milioni 21

    hadi 23.

    Sisi katika Serikali tutaendelea kutimiza wajibu wetu

    wa kuiwezesha Tume kutimiza wajibu wake. Napenda

    kuwahakikishia kuwa kila Mtanzania mwenye haki ya

    kupiga kura atapata fursa ya kuandikishwa. Shime

    tuhimize watu wajitokeze kujiandikisha ili wasikose haki

    yao hiyo.

  • 19

    Uhuru wa Habari

    Mheshimiwa Spika;

    Mtakubaliana nami kuwa katika kipindi hiki uhuru wa

    habari na uhuru wa watu kutoa maoni yao umepanuka

    sana. Tanzania kuna magazeti ya kila siku 16 na kati ya hayo

    ya Serikali ni 2 (Daily News, Habari Leo). Pia magazeti ya

    kila wiki yapo 62. Aidha, kuna vituo vya redio 115 na vya

    televisheni 29. Serikali haifanyi uhakiki wa habari kabla ya

    kuchapishwa au kuandikwa. Tumeamua hivyo kwa imani

    yangu kwamba ustawi wa demokrasia hutegemea sana

    uhuru wa vyombo vya habari. Pili, kwa vile tunatambua

    manufaa ya vyombo vya habari kuelimisha jamii,

    kupambana na maovu na kuhimiza uwajibikaji.

    Pamoja na hayo, hatukusita wala kuchelea kuchukua

    hatua pale uhuru huo ulipotumiwa vibaya na kutishia

    kuvuruga amani, umoja na usalama wa jamii au taifa. Au,

  • 20

    pale ambapo Sheria za nchi zimekiukwa. Huo ni wajibu

    wetu wa kikatiba ambao mimi na wenzangu tuliapa

    kuutimiza.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kuongeza uwazi na mawasiliano na wananchi

    mwaka 2007 tulianzisha tovuti ya wananchi. Tovuti hiyo

    imeshapokea hoja 117,243 na kati ya hizo zilizohusu Serikali

    zilikuwa 78,258 na zote zimeshughulikiwa.

    Katika kuboresha mfumo wa mawasiliano, Tanzania

    imeshahama kutoka mfumo wa analogia na kuingia kwenye

    mfumo wa digitali. Hii ni hatua kubwa muhimu kwa

    maendeleo ya tasnia ya habari nchini. Jambo ambalo

    nasikitika kuwa hatukuweza kulikamilisha ni utungaji wa

    Sheria ya Haki ya Upatikanaji wa Habari na Sheria ya

    Vyombo vya Habari. Miswada imekamilika na kusomwa

    mara ya kwanza hapa Bungeni lakini mchakato wake

    haukuweza kufika mwisho. Tunawaachia wenzetu wajao

    washughulike nayo katika Bunge la 11.

  • 21

    Vita dhidi ya Rushwa

    Mheshimiwa Spika;

    Vita dhidi ya rushwa ni eneo jingine ambalo tulilivalia

    njuga katika Awamu ya Nne. Tumepata mafanikio ya kutia

    moyo katika mapambano dhidi ya rushwa ingawaje kazi

    bado ni kubwa. Tumefanya mambo matatu. Kwanza,

    tumetunga Sheria Na. 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na

    Kupambana na Rushwa ambayo imeongeza nguvu ya

    mapambano dhidi ya uovu huu. Idadi ya makosa ya rushwa

    iliongezwa kutoka 4 mpaka 24 na wigo wa wakosaji pia,

    kwa kuhusisha watu katika sekta binafsi. Mifumo ya

    upelelezi na uendeshaji mashitaka nayo imeimarishwa.

    Tumeunda chombo kipya TAKUKURU badala ya

    TAKURU ambacho kimepewa majukumu ya kuzuia na

    kupambana na rushwa badala ya kuzuia peke yake.

    TAKUKURU imepewa mamlaka zaidi katika kuongoza

    mapambano haya. Taasisi imeendelea kuimarishwa kwa

  • 22

    kuipatia zana na vifaa vya kufanyia kazi pamoja na

    rasilimali watu na mahitaji mengine. Tumeiwezesha

    TAKUKURU kufungua ofisi katika Mikoa na Wilaya zote.

    Mheshimiwa Spika;

    Maboresho haya yamewezesha idadi ya kesi za tuhuma

    za rushwa zinazofikishwa mahakamani kuongezeka kutoka

    kesi 50 mwaka 2005 hadi 1,900 mwaka 2014. Jumla ya

    shilingi bilioni 87.8 ziliokolewa. Watumishi wa Serikali 97

    wameachishwa kazi kwa tuhuma za rushwa na matumizi

    mabaya ya ofisi zao baada ya ushahidi wa kijinai

    kukosekana. Kwa upande wa kupambana na rushwa

    kwenye shughuli za uchaguzi, tumetunga Sheria ya

    Kudhibiti Gharama za Uchaguzi Na. 6 ya mwaka 2010 ili

    kutoa majibu ya kilio cha siku nyingi dhidi ya watu

    wanaotumia fedha kununua kura.

    Mapato na Matumizi ya Fedha na Mali za Serikali

    Mheshimiwa Spika;

  • 23

    Nilieleza katika hotuba yangu ya Kuzindua Bunge la

    Tisa tarehe 30 Desemba, 2005 kuwa tutatoa kipaumbele cha

    juu kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali na nidhamu ya

    matumizi ya Serikali. Leo miaka kumi baadae ninaona

    fahari tumepata mafanikio makubwa. Mapato ya Serikali

    yameongezeka kutoka shilingi bilioni 177.1 mwaka 2005

    kwa mwezi hadi takriban shilingi bilioni 850. Hii

    imewezesha bajeti ya Serikali kukua kutoka trilioni 4.13

    mwaka 2005/2006 hadi trilioni 22.49 mwaka 2015/2016.

    Isitoshe imetuwezesha kupunguza misaada na mikopo ya

    washirika wa maendeleo kutoka asilimia 42 ya Bajeti ya

    Serikali mwaka 2005 hadi asilimia 15 mwaka 2014/2015 na

    tumejipa lengo la kushusha zaidi hadi asilimia 8 mwaka

    huu wa fedha wa 2015/2016.

    Mheshimiwa Spika;

    Mafanikio haya yametokana hasa na kazi kubwa

    tuliyoifanya ya kuimarisha Mamlaka ya Mapato ambao

    wanastahili pongezi zetu nyingi. Bado naamini tunaweza

  • 24

    kufanya vizuri zaidi ya hivi, kama tukiongeza udhibiti kwa

    mianya ya kupoteza mapato na kuimarisha zaidi TRA na

    mamlaka nyingine za ukusanyaji mapato ya Serikali. Bado

    ukusanyaji wa mapato yasiyokuwa ya kodi katika

    Halmashauri za Wilaya na Miji na katika Wizara, Idara

    zinazojitegemea na Wakala wa Serikali uko chini ya lengo.

    Huku kuendelee kufanyiwa kazi.

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa nidhamu ya matumizi ya fedha na

    mali za Serikali tulielekeza nguvu zetu katika kuimarisha

    utaratibu wa manunuzi Serikalini na ukaguzi wa hesabu za

    Serikali. Kwa upande wa ununuzi wa bidhaa na huduma,

    tumeendelea kuimarisha Sheria na Mamlaka ya Ununuzi wa

    Umma ili iweze kuhakikisha kuwa kuna usimamizi thabiti

    wa sheria hiyo na kanuni zake. Kama mjuavyo sehemu,

    kubwa ya fedha za Serikali hutumiwa katika ununuzi wa

    bidhaa na huduma, hivyo kuwepo usimamizi mzuri ni

    jambo jema. Ukikosekana, wizi na rushwa hutawala.

  • 25

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa ukaguzi wa hesabu za Serikali,

    tumechukua hatua za makusudi za kuimarisha Ofisi ya

    Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

    Tumetunga Sheria mpya inayoipa nguvu na uhuru zaidi

    Ofisi hiyo. Aidha, tumewaongezea bajeti, vitendea kazi na

    rasilimali watu. Ofisi 8 za Mikoa zimejengwa na 2

    zinaendelea kujengwa.

    Nafurahi kwamba maagizo yangu kwa viongozi na

    watendaji katika Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kuhusu

    Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za

    Serikali kupewa uzito linazingatiwa. Taarifa hizo sasa

    zinasomwa, zinajadiliwa na hatua kuchukuliwa kwa kasoro

    zilizoonekana. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali

    imefanya kazi nzuri. Wezi na wabadhirifu wanaobainika

    kuchukuliwa hatua za kisheria mara makosa

  • 26

    yanapogundulika. Kitaifa taarifa hiyo hujadiliwa Bungeni

    kwa muda wa kutosha.

    Mheshimiwa Spika;

    Niliamua pia kuanzisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa

    Ndani wa Serikali na kuwaweka Wakaguzi wa Ndani wote

    wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa chini ya Mamlaka yake

    na kuwajibika kwake. Ofisi hii imesaidia kuhakikisha sheria

    na kanuni za matumizi ya fedha na mali ya umma

    zinaheshimiwa. Pia, katika ufuatiliaji na utekelezaji wa

    mapendekezo ya CAG. Uimarishaji wa ukaguzi wa ndani na

    ule wa CAG umesaidia kuboresha hesabu za Serikali kuwa

    nzuri zaidi siku hizi. Hati safi zimeongezeka na hati chafu

    zinazidi kupungua Serikalini. Kwa mfano katika

    Halmashauri za Wilaya na Miji, hati safi zimeongezeka

    kutoka 56 mwaka 2006 hadi 150 mwaka 2014. Hati zenye

    mashaka ni 13 na hakuna Hati isiyoridhisha. Kazi ya

    kuimarisha ukaguzi na nidhamu ya matumizi lazima

    iendelezwe.

  • 27

    Maadili ya Viongozi wa Umma

    Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka 10 hii tumeimarisha mfumo wa

    kusimamia maadili ya viongozi. Tumefanya hivyo kwa

    kutambua kuwa maadili mema ni sifa ya msingi ya kiongozi

    na huiletea heshima Serikali. Tumeendeleza Kamati ya

    Maadili na kuunda Baraza la Maadili kwa mujibu wa Sheria

    ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya 1995.

    Tumepanua wigo na kwamba sasa mali za viongozi na

    familia zao hutolewa taarifa na kiongozi katika Tamko la

    Mali la kila mwaka. Hii inasaidia kuondoa uwezekano wa

    kiongozi kuficha mali kwa mgongo wa mwenza wake au

    mtoto.

    Mheshimiwa Spika;

    Kamati ya Maadili sasa si tu inapokea fomu na

    kuzihifadhi, bali inafanya ukaguzi wa mali za viongozi na

  • 28

    kuzifuatilia. Kikwazo chao ni kupata rasilimali fedha. Hili

    litazamwe zaidi. Pale inapoonekana kuna makosa ya

    kimaadili wahusika hufikishwa kwenye Baraza la Maadili.

    Sote tumeshuhudia kazi nzuri iliyofanywa na Baraza hilo

    wakati wa sakata la Escrow. Bado kazi ya kuimarisha

    Kamati ya Maadili kwa rasilimali fedha, vitendea kazi,

    majengo ya ofisi na rasilimali watu haina budi kuendelezwa.

    Muhimili wa Mahakama

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi cha miaka 10 hii tumefanya jitihada

    kubwa za kuimarisha mhimili wa Mahakama. Miongoni

    mwa mambo mengine, tumefanya mambo muhimu kwa

    madhumuni ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa

    jukumu lake la msingi la utoaji haki.

    Kwanza, tumetenganisha shughuli za kutoa haki na za

    utawala. Tumeunda Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama

    ya kushughulikia mambo ya fedha na utawala. Hivyo basi,

    Wasajili wa Mahakama wanabaki na jukumu la kutoa haki.

  • 29

    Mpaka sasa mabadiliko haya yamekuwa ya manufaa

    makubwa kwa Mahakama kwani yameboresha utekelezaji

    wa majukumu katika Mahakama. Pili, tumeanzisha Mfuko

    wa Mahakama ambao unaipa Mahakama uhuru katika

    kuendesha shughuli zake. Sambamba na hilo tumeongeza

    bajeti ya Mahakama kutoka shilingi bilioni 36.6 mwaka

    2006/07 hadi shilingi bilioni 87.6 mwaka 2014/15. Jambo

    linalohitaji kuboreshwa ni Hazina kutoa fedha kwa wakati

    ili shughuli zifanyike kama ilivyopangwa.

    Mheshimiwa Spika;

    Jambo la tatu, ni kwamba tumeongeza idadi ya Majaji

    wa Rufani, Majaji wa Mahakama Kuu, Mahakimu Wakazi

    na Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo. Lengo letu ni

    kuongeza nguvukazi ya kusikiliza na kuamua mashauri.

    Kwa upande wa Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo

    wameanza kuteuliwa watu wenye Shahada ya Sheria. Hivi

    sasa itawawezesha watu wenye mashauri katika Mahakama

    hizo kupata utetezi wa Mawakili. Kati ya mwaka 2005 na

  • 30

    2015 tumeongeza Majaji wa Rufani kutoka 8 mwaka 2005

    hadi 16, na Majaji wa Mahakama Kuu kutoka 37 hadi 81

    katika kipindi hicho. Hali kadhalika, tumeongeza idadi ya

    Majaji wanawake. Katika Mahakama ya Rufani wapo 5 na

    katika Mahakama Kuu wapo 32 na kufanya jumla yao kuwa

    37. Hivi sasa tunao jumla ya Mahakimu Wakazi 1,266 katika

    ngazi zote za Mahakama. Kati ya hao 534 sawa na asilimia

    35 ni wanawake. Idadi ya Majaji na Mahakimu wanawake

    hivi sasa ni kubwa kuliko wakati wowote uliopita.

    Mheshimiwa Spika;

    Kutokana na mipango mizuri iliyowekwa na Jaji Mkuu

    Mohamed Chande Othman Mahakama zimepiga hatua

    kubwa katika kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani.

    Majaji wamejiwekea malengo kwa kila Jaji asikilize na

    kuamua mashauri yasiyopungua 220 kwa mwaka na kila

    Hakimu Mkazi mashauri 250 na wale wa Mahakama ya

    Mwanzo mashauri 260 kwa mwaka. Kwa sababu hiyo,

    kuanzia Julai, 2014 hadi kufikia mwezi Machi mwaka 2015

  • 31

    yalifunguliwa mashauri 177,586 na Mahakama ilisikiliza na

    kuamua mashauri 179,962. Maana yake ni kuwa

    zimesikilizwa zote na nyingine zilizobakia miaka ya nyuma.

    Bila shaka kwa kasi hii sasa mrundikano wa kesi utabakia

    kuwa historia katika kipindi kifupi kijacho. Nawapongeza

    sana Majaji na Mahakimu kwa kazi nzuri waifanyayo.

    Kwa upande wa ujenzi wa majengo ya Mahakama

    Kuu, wamekamilisha ujenzi wa jengo la Mahakama Kuu za

    Divisheni ya Kazi pamoja na majengo ya Mahakama Kuu

    Mikoa ya Shinyanga na Kagera. Aidha, majengo mawili ya

    Mahakama za Wilaya na 12 ya Mahakama za Mwanzo nayo

    yamekamilika. Hivi sasa, ujenzi unaendelea wa majengo ya

    Mahakama Kuu 9 za mikoa iliyosalia, Mahakama za Wilaya

    9 na za mwanzo 25.

    Maboresho ya Mfumo wa Utoaji Haki

    Mheshimiwa Spika;

    Jambo lingine ambalo tumefanya katika nia ya

    kuongeza uwajibikaji, ufanisi, na kupunguza malalamiko ya

  • 32

    wananchi na ucheleweshaji wa mashauri ni kutenganisha

    kazi ya upelelezi wa makosa ya jinai na uendeshaji wa

    mashtaka hayo Mahakamani. Polisi waliokuwa wanafanya

    yote sasa watashughulikia upelelezi na ofisi ya Mkurugenzi

    wa Mashtaka ndiyo inayoendesha mashauri. Tayari Ofisi za

    Mkurugenzi wa Mashtaka zimekwishafunguliwa katika kila

    Mkoa na sasa tunaenda wilayani. Aidha, tumeboresha Ofisi

    ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa rasilimali watu,

    vitendea kazi na fedha ili kuongeza ufanisi katika utendaji

    wa ofisi hiyo muhimu sana. Kuna haja ya kuendelea

    kuongezea rasilimali fedha na vitendea kazi ili ufanisi

    uongezeke zaidi.

    Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki, tumeimarisha Tume ya Haki za

    Binadamu na Utawala Bora kwa kuiwezesha kwa nyenzo,

    rasilimali fedha na watu. Tume sasa inafanya kazi katika

    eneo lote la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kutokana na

  • 33

    utumiaji wa mfumo wa elektroniki malalamiko ya wananchi

    mengi zaidi yanafikishwa kwenye Tume na mengi

    yanapatiwa ufumbuzi. Kwa mfano, idadi ya malalamiko

    yaliyowasilishwa Tume yameongezeka kutoka 9,455

    mwaka 2006 hadi 25,921 mwaka 2014 na uwezo wa Tume

    kushughulikia malalamiko kwa mwaka umeongezeka

    kutoka malalamiko 3,021 mwaka 2005 hadi malalamiko

    18,501 mwaka 2014.

    Utendaji Serikalini

    Maeneo ya Utawala

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa nia ya kusogeza huduma, mwaka 2010 tulianzisha

    mikoa mipya 4 ya Geita, Simiyu, Njombe na Katavi na

    wilaya mpya 19. Pia, tulianzisha Halmashauri 45, kata 1,432,

    vijiji 1,949, Mitaa 1,379 na vitongoji 8,777. Nimeamua

    kuanzisha mkoa mpya wa Songwe kutoka mkoa wa Mbeya

    na Wilaya sita kama ifuatavyo: Tanganyika mkoani Katavi,

    Kigamboni na Ubungo mkoani Dar es Salaam, Songwe

  • 34

    mkoani Mbeya, Kibiti mkoani Pwani na Malinyi mkoani

    Morogoro. Najua tulikuwa na maombi mengi lakini kwa

    sasa tufanye haya.

    Maslahi ya Wafanyakazi

    Mheshimiwa Spika;

    Serikali ya Awamu ya Nne imelipa umuhimu wa juu

    suala la kuboresha maslahi ya watumishi wa Serikali. Karibu

    kila mwaka tumekuwa tunaongeza kima cha chini cha

    mshahara. Kwa sababu hiyo, kima cha chini cha mshahara

    kimeongezeka kutoka shilingi 65,000 mwaka 2005 hadi

    shilingi 265,000 mwaka wa jana. Mwaka huu tumefikia

    shilingi 300,000. Najua bado hakikidhi mahitaji lakini

    ukilinganisha na tulikokuwa kipindi hiki tumeongeza sana

    mishahara ya wafanyakazi. Vile vile, tumeendelea

    kupunguza kodi ya mapato kwa mfululizo kutoka asilimia

    18 mwaka 2005 hadi asilimia 11 mwaka huu. Dhamira yetu

    ni kutaka kutoa nafuu zaidi kwa wafanyakazi. Vile vile,

    tumewapandisha vyeo watumishi 233,876 na kulipa

  • 35

    malimbikizo ya watumishi 422,348 ya kiasi cha shilingi

    bilioni 384.8.

    Mheshimiwa Spika;

    Tumetekeleza sera ya ugatuaji wa madaraka kwa

    wilaya jambo ambalo limelazimu kuongeza rasilimali fedha

    na watu kwa Halmashauri za Wilaya na Miji. Kwa ajili hiyo

    ruzuku kwa Halmashauri zetu imeongezeka kutoka shilingi

    bilioni 780 mwaka 2005/2006 hadi shillingi trilioni 4.69

    mwaka 2015/2016. Aidha, tumeimarisha utumishi katika

    Halmashauri kwa kuajiri watumishi wengi wa kada

    mbalimbali.

    Usawa wa kijinsia

    Mheshimiwa Spika;

    Mwaka 2005 niliahidi wakati wa kampeni na wakati wa

    kuzindua Bunge la Tisa, kuwa tutaongeza ushiriki wa

    wanawake katika shughuli na nyanja mbalimbali za maisha

    ya watu wa nchi yetu ikiwemo nafasi za maamuzi. Ninyi na

    mimi ni mashahidi kwamba tumetimiza ahadi hiyo. Idadi

  • 36

    ya Wabunge wanawake imeongezeka kutoka 62 mwaka

    2005 hadi 127. Hivi sasa hamsini kwa hamsini ni rasmi

    katika Katiba Inayopendekezwa. Kwa mara ya kwanza

    katika historia ya nchi yetu na Bunge letu tumepata Spika

    mwanamke Mheshimiwa Anne Semamba Makinda.

    Wanawake wameongezeka katika ngazi zote kuu za

    uamuzi. Kwa mfano, tunao Mawaziri wanawake 10, Naibu

    Mawaziri wanawake 5, Majaji wanawake 37 na Wakuu wa

    Wilaya wanawake wako 53. Kwa upande wa Makatibu

    Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa,

    Wakurugenzi Watendaji n.k. pia wameongezeka. Katika

    elimu nako tuna usawa wa kijinsia kwa upande wa idadi ya

    wanafunzi wa kike na wa kiume katika shule za msingi na

    sekondari. Katika vyuo vya elimu ya juu, idadi ya

    wanafunzi wa kike imeongezeka kwa kasi kutoka 10,039

    mwaka 2005 hadi 78,800 mwaka 2014.

  • 37

    Hali ya Uchumi

    Mheshimiwa Spika;

    Wakati ninaingia madarakani mwaka 2005 niliwaahidi

    Watanzania wenzangu kuwa tutafanya kila tuwezalo

    kujenga uchumi ulio imara na shirikishi. Hususan, nilisema

    nitaendeleza sera za mageuzi ya kiuchumi na kuweka

    misingi madhubuti ya kukuza uchumi, kuongeza ajira,

    kuongeza Pato la Taifa na kupunguza umaskini. Katika

    miaka kumi iliyopita tumeendelea kusimamia kwa kiwango

    kizuri sera za uchumi jumla na sera za uchumi katika ngazi

    ya chini zinazogusa wananchi wa kawaida.

    Jitihada zetu hizo zimezaa matunda ya kutia moyo.

    Katika kipindi hiki, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa

    takriban asilimia 7. Nchi yetu ni miongoni mwa mataifa 10

    ya Afrika na 20 duniani ambayo uchumi wake unakua kwa

    kasi kubwa. Pato ghafi la Taifa limeongezeka zaidi ya mara

    tatu kutoka shilingi trilioni 14.1 mwaka 2005 hadi kufikia

    trilioni 79.4 mwaka 2014. Hivyo basi, pato la wastani la

  • 38

    Mtanzania nalo limeongezeka kutoka shilingi 441,030

    mwaka 2005 hadi shilingi 1,724,416 mwaka 2014.

    Mheshimiwa Spika;

    Mauzo yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola za

    Marekani bilioni 1.67 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani

    bilioni 8.76 mwaka 2014 na kutunisha akiba yetu ya fedha

    za kigeni na kutuwezesha kuagiza bidhaa na mahitaji ya

    nchi kutoka nje kwa kipindi cha miezi 4.1 kama

    tulivyopanga. Mfumuko wa bei ni asilimia 6.1.

    Mheshimiwa Spika;

    Kama mjuavyo, mwaka 2000 nchi yetu ilijiwekea Dira

    ya Taifa ya Maendeleo ya hadi mwaka 2025. Mwaka 2010

    tulitengeneza Mpango wa Muda Mrefu (Long Term

    Perspective Plan) wa (2010 2025) wa kuongoza utekelezaji

    wa Dira kwa miaka 15 iliyobaki. Tuligawa utekelezaji wake

    katika Mipango mitatu ya Maendeleo ya Miaka Mitano kila

    mmoja. Tuko katika hatua za mwisho za utekelezaji wa

  • 39

    Mpango wa Kwanza, (2011/12 2015/16) na kuandaa

    mpango wa pili (2016/17 2021/22).

    Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa madhumuni ya kuboresha utendaji wa Serikali

    nilianzisha Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).

    Huu ni mfumo mpya wa kupanga, kufuatilia na kusimamia

    utekelezaji wa malengo na shughuli za Serikali kwa nia ya

    kuhakikisha kuwa kilichokusudiwa kinafanyika, tena kwa

    wakati. Tuliamua kuanza na sekta sita za Elimu, Nishati,

    Kilimo, Uchukuzi, Maji na Mapato ya Serikali. Baadae

    sekta ya afya na uboreshaji mazingira ya uwekezaji

    ziliongezwa.

    Katika kipindi hiki kifupi Mpango umethibitisha kuwa

    wenye manufaa. Mambo katika sekta zilizojumuishwa

    katika BRN yameanza kwenda vizuri. Changamoto yetu

    kubwa imekuwa ni upatikanaji wa fedha zinazohitajika kwa

  • 40

    wakati kutoka Hazina. Kama changamoto hiyo

    isingekuwepo mambo yangekuwa mazuri zaidi.

    Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa kutambua umuhimu wa uwekezaji katika kukuza

    uchumi, kuzalisha ajira, kuongeza mapato na kupunguza

    umaskini, Serikali yetu imekuwa inachukua hatua thabiti za

    kutengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji

    wa ndani na nje kuchagua Tanzania kuwa nchi inayofaa

    kuwekeza.

    Mwaka 2010 tumetengeneza Sera na kutunga Sheria ya

    Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (Public

    Private PartnershipPPP). Lengo letu ni kuweka mazingira

    mazuri kwa sekta binafsi kuvutika kushirikiana na Serikali

    katika shughuli za kiuchumi na maendeleo. Faida kubwa ya

    utaratibu huu ni kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwekeza

    katika baadhi ya shughuli ambazo sekta binafsi inaweza

    kubeba sehemu ya gharama. Hii siyo tu inaongeza kasi ya

  • 41

    maendeleo, bali kuiwezesha Serikali kuokoa fedha ambazo

    inaweza kuzitumia kwa shughuli nyingine.

    Juhudi zetu za kuboresha mazingira ya uwekezaji

    zinaendelea kuzaa matunda mema. Kati ya 2005 na 2014,

    Kituo chetu cha Uwekezaji (TIC) kimesajili miradi 7,159

    yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 154.274. Kati ya

    miradi hiyo asilimia 49.38 ni ya wawekezaji wa ndani,

    asilimia 23.41 ni wawekezaji wa kutoka nje na asilimia 27.18

    ni miradi ya ubia baina ya Watanzania na wawekezaji wa

    kigeni. Ajira 16,000 zilipatikana. Ukuaji huu wa uwekezaji

    umeongeza mapato ya Serikali.

    Kwa mujibu wa taarifa ya uwekezaji iliyotolewa na

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda na Biashara

    Duniani (UNCTAD) ya mwaka 2015, Tanzania inaongoza

    Afrika Mashariki kwa kuvutia uwekezaji. Ilipata Dola za

    Marekani bilioni 2.142 sawa na asilimia 31.5 ya uwekezaji

    wote katika Jumuiya yetu.

  • 42

    Sekta za Uzalishaji

    Sekta ya Kilimo

    Mheshimiwa Spika;

    Kuendeleza kilimo ilikuwa ni moja ya mambo

    tuliyoyapa kipaumbele cha juu. Shabaha yetu kuu ni kutaka

    kuongeza tija ili uzalishaji uongezeke, wakulima wapate

    mavuno mengi, masoko ya uhakika yawepo na bei iwe nzuri

    ili mapato yao yaongezeke na umasikini uwapungukie. Vile

    vile wao na taifa lijitosheleze kwa chakula.

    Kwa ajili hiyo mwaka 2006 tuliasisi Programu ya miaka

    7 ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (Agricultural Sector

    Development ProgrammeASDP). Katika Programu hiyo,

    matatizo yanayofanya tija na uzalishaji katika kilimo kuwa

    mdogo yalitambuliwa na kutengenezewa mpango wa

    kuyatatua. Serikali pia ilianzisha mikakati, programu na

    mipango mingine ya kuongeza msukumo katika kuleta

    mageuzi ya kilimo. Miongoni mwa hiyo ni mkakati wa

    Kilimo Kwanza, Mpango wa Kuendeleza Kilimo katika

  • 43

    Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Mpango wa

    Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo (TAFSIP), Sera ya

    Umwagiliaji tuliyoitunga mwaka 2010 na Programu ya

    Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika.

    Mheshimiwa Spika;

    Pamoja na hayo, tumeongeza pia bajeti ya sekta ya

    kilimo kutoka shilingi bilioni 233.3 mwaka 2005/06 hadi

    shilingi bilioni 1,084.7 mwaka 2014/15. Kuongezwa kwa

    bajeti kumewezesha fedha za ruzuku ya mbolea na

    pembejeo kuongezeka kutoka shilingi bilioni 7.5 mwaka

    2005/06 hadi shilingi bilioni 299.3 mwaka 2013/14. Matrekta

    makubwa na madogo yameongezeka kutoka 7,491 mwaka

    2005 hadi 16,412 mwaka 2014. Kwa sababu hiyo matumizi

    ya jembe la mkono yamepungua kutoka asilimia 70 hadi

    asilimia 62. Tumeongeza maafisa ugani kutoka 3,379 mwaka

    2005 hadi 7,974 mwaka 2014.

    Vituo vya utafiti wa kilimo tumeviongezea rasilimali

    fedha, watu na vitendea kazi. Aidha, tumeanza safari ya

  • 44

    kufufua mashamba ya mbegu ya Serikali na kuhusisha sekta

    binafsi, Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa katika

    kuzalisha mbegu. Aidha, tumeimarisha Wakala wa Mbegu

    (Agricultural Seed Agency ASA) na kuongeza uzalishaji

    wa mbegu bora kutoka tani 10,477.17 mwaka 2005 hadi tani

    32,340 mwaka 2014.

    Mheshimiwa Spika;

    Juhudi za Serikali kuendeleza kilimo zimezaa matunda

    mazuri. Tija katika uzalishaji wa mazao ya biashara na

    chakula imeongezeka. Kwa upande wa mazao ya chakula

    uzalishaji umeongezeka kutoka tani milioni 9.66 mwaka

    2005 hadi tani milioni 16.01 mwaka 2014. Ongezeko hili

    limeliwezesha taifa letu kujitosheleza kwa chakula kwa

    asilimia 125 mwaka 2014 ikilinganishwa na asilimia 95

    mwaka 2005. Uzalishaji wa mazao ya asili ya biashara

    umeongezeka toka tani 427,738 mwaka 2005 hadi tani

    569,054 mwaka 2014 na uzalishaji wa mbegu za mafuta

    umeongezeka karibu ya mara 4 toka tani 1,389.9 mwaka

  • 45

    2005 hadi tani 5,545.6 mwaka 2014. Aidha, uzalishaji wa

    matunda nao umeongezeka toka tani milioni 1.2 mwaka

    2005 hadi tani milioni 4.4 mwaka 2014 na maua toka tani

    5,862 hadi tani 10,790.

    Mheshimiwa Spika;

    Upatikanaji wa masoko ya uhakika na bei nzuri kwa

    mazao ya wakulima bado ni changamoto. Pia kuna tatizo la

    upungufu wa maghala ya kuhifadhi mazao. Jitihada

    zinaendelea kupata mkopo au wabia wa kujenga maghala

    ya kisasa nchi nzima. Programu ya Mageuzi na

    Modenaizesheni ya Ushiriki ilianzishwa ili kutatua tatizo la

    masoko. Aidha, tumeanza maandalizi ya kuanzisha soko la

    bidhaa (Commodity Market Exchange) kwa nia hiyo hiyo.

    Naamini misingi mizuri tuliyoijenga pamoja na kuenea kwa

    SACCOS na kuanza kwa Benki ya Kilimo ikiendelezwa

    itatoa mchango mkubwa katika kuongeza kasi ya

    mapinduzi ya kilimo.

  • 46

    Mifugo

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa mifugo, dhamira yetu ilikuwa kuanza

    safari ya kuleta mageuzi katika sekta hii. Safari hiyo

    tumeianza kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya

    Mifugo. Changamoto zinazochangia maendeleo duni ya

    sekta hii zimeainishwa na kutengenezewa mkakati wa

    utekelezaji. Katika kipindi hiki malambo 1,008, majosho

    2,364 na maabara 104 za mifugo zimejengwa. Visima virefu

    101 vimechimbwa, malambo 370 na majosho 499

    yamekarabatiwa katika kipindi hiki cha miaka 10.

    Ukarabati na ujenzi wa majosho umeongeza idadi

    kutoka 2,177 mwaka 2006 hadi 3,637 mwaka 2015.

    Tumeongeza Maofisa Ugani kutoka 2,270 mwaka 2005 hadi

    6,041 mwaka 2014. Kuhusu uhamilishaji, tumeongeza vituo

    kutoka kituo 1 mwaka 2005 hadi vituo 8 mwaka 2015 na

    kuwezesha ngombe 955,360 kuhamilishwa katika miaka 10

    hii.

  • 47

    Mheshimiwa Spika;

    Mazingira mazuri ya uwekezaji kwa sekta binafsi

    tuliyoyajenga yamewezesha viwanda vya kusindika nyama,

    maziwa na vyakula vya mifugo kuongezeka. Viwanda vya

    kusindika maziwa vimeongezeka kutoka 22 mwaka 2005

    hadi 74 mwaka 2015. Viwanda vya kuzalisha vyakula vya

    mifugo vimeongezeka kutoka viwanda 6 mwaka 2005 hadi

    80 mwaka 2015 vikiwa na uwezo wa kusindika tani milioni

    1.4 za vyakula hivyo kwa mwaka. Aidha viwanda na

    machinjio ya kisasa 9 vimejengwa katika kipindi hiki.

    Usindikaji wa ngozi pia umeongezeka kutoka vipande

    790,000 mwaka 2005 hadi vipande milioni 3.78 mwaka 2014.

    Hivi sasa kwa mfano, uzalishaji wa malisho ya mifugo (hei)

    umefikia marobota 957,860 ikilinganishwa na marobota

    178,100 mwaka 2005.

    Safari yetu ya kuanza kuondoka kwenye uchungaji

    kwenda kwenye ufugaji imeanza. Vijiji vingi vimeandaa

    mipango ya matumizi bora ya ardhi na hivyo vimetenga

  • 48

    maeneo ya kilimo na ya ufugaji. Tuendelee kuhimiza vijiji

    vyetu kutekeleza mipango hiyo ili wafugaji wapate maeneo

    ya malisho mbali na mazao ya wakulima. Pia, tuhimize

    uhamilishaji kama mlango wa kuingilia kwenye kuboresha

    kosafu za mifugo yetu.

    Uvuvi

    Mheshimiwa Spika;

    Wakati nazindua Bunge la Tisa tarehe 30 Desemba 2005

    nilisema kuwa Serikali ya Awamu ya Nne itatoa kipaumbele

    kwenye kuendeleza sekta ya uvuvi. Katika kutekeleza hayo

    tumefanya yafuatayo. Kwanza, nimeunda Wizara mpya ya

    Mifugo na Uvuvi. Pili, tulifuta kodi ya zana za uvuvi ili

    kuwawezesha wavuvi kupata zana bora na za kisasa kwa

    bei nafuu zaidi. Tatu, tumeimarisha vyuo vya uvuvi na hivi

    sasa vina uwezo wa kudahili wanafunzi 1,215

    ikilinganishwa na wanafunzi 127 mwaka 2005. Hii

    imetuwezesha kuongeza wagani wa uvuvi kutoka 103

    mwaka 2005 hadi 540 mwaka 2014. Nne, tumeongeza sana

  • 49

    juhudi za kupambana na uvuvi haramu ili kutunza

    mazingira, mazalia ya samaki na kuzuia kuvuliwa au

    kuuawa kwa samaki wadogo.

    Tumeimarisha maabara ya Taifa ya Samaki pale

    Nyegezi kwa vifaa vya kisasa na wataalamu ili iende na

    wakati. Tano, tumeongeza msukumo wa kuhimiza ufugaji

    wa samaki na kuwezesha mashamba ya samaki kuongezeka

    kutoka 13, 011 mwaka 2005 hadi 20, 325 mwaka 2014.

    Uvuvi haramu unapungua. Mapato ya sekta ya uvuvi

    yameongezeka kutoka shilingi bilioni 351.6 mwaka 2005

    hadi shilingi trilioni 1.8 mwaka 2013. Bado tuna kazi kubwa

    ya kufanya katika sekta hii ili kuongeza tija na mapato ya

    wavuvi na taifa.

    Utalii

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa utalii, tumeendelea na jitihada za

    kuiendeleza sekta hii muhimu. Tumeongeza kutangaza

    vivutio vya utalii vya nchi yetu katika masoko makubwa

  • 50

    duniani. Sekta ya utalii imekua kwa wastani wa asilimia 7.1

    na imechangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.

    Idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii 612, 754 mwaka

    2005 hadi watalii 1,140,156 mwaka 2014. Idadi ya vitanda

    katika mahoteli imeongezeka kutoka 15,828 hadi 21,929.

    Mapato pia yameongezeka kutoka Dola za Marekani

    milioni 823.05 mwaka 2005 hadi Dola za Marekani bilioni 2

    mwaka 2014. Ajira za moja kwa moja zimeongezeka kutoka

    32,673 hadi 686,130 na zisizokuwa za moja kwa moja kutoka

    165,883 hadi 1,318,109. Haya ni mafanikio makubwa na ya

    kujivunia.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumekabiliana na tukio kubwa la

    ujangili wa wanyamapori hasa wa ndovu kutokana na

    kushamiri kwa biashara ya meno ya ndovu na bei kuwa

    kubwa katika nchi za Mashariki ya Mbali. Vuguvugu la

    ujangili lilifikia kiwango cha kutishia kumaliza ndovu

    nchini na dunia nzima. Tukaamua kuchukua hatua za

  • 51

    kuidhibiti hali hiyo. Tumefanya operesheni tatu kukabiliana

    na tishio hili. Ya kwanza, iliendeshwa na Idara ya

    Wanyamapori na Misitu wakishirikiana na TANAPA na

    Ngorongoro Conservation Area. Hii hasa ilihusu

    kupambana na ujangili katika hifadhi na mapori ya

    Kaskazini mwa Tanzania. Mafanikio makubwa yalipatikana.

    Mheshimiwa Spika;

    Operesheni ya pili ni ile iliyohusisha Jeshi la Polisi

    katika hifadhi na sehemu nyingine za Tanzania. Operesheni

    Kipepeo kama ilivyoitwa nayo ilipata mafanikio. Na ya tatu,

    Operesheni Tokomeza iliyohusisha vyombo vyote vya ulinzi

    na usalama. Pamoja na changamoto zake operesheni hizi

    zimesaidia sana kupunguza kasi ya ujangili nchini. Matokeo

    yake katika sensa ya ndovu iliyofanyika mara ya mwisho,

    ukiacha Ruaha, hali katika hifadhi na mapori mengine ina

    muelekeo mzuri.

    Kuundwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA)

    yenye mamlaka makubwa zaidi ya kusimamia sekta ya

  • 52

    wanyamapori nako kutaimarisha uhifadhi na mapambano

    ya ujangili. Kwa mipango na program zilizopo Wizarani,

    naamini mambo yatakuwa mazuri zaidi muda si mrefu.

    Viwanda

    Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka kumi hii, sekta ya viwanda imeendelea

    kukua kwa kasi nzuri ya kutia moyo. Viwanda vikubwa,

    vya kati na vidogo vimeongezeka kutoka 11, 544 mwaka

    2005 hadi viwanda 51,224 mwaka 2015. Kati ya mwaka 2005

    na 2014 na miradi 751 imepewa leseni za kudumu na BRELA

    ya kuanzisha viwanda. Mchango wa sekta ya viwanda

    katika Pato la Taifa umefikia asilimia 7.3 mwaka 2014

    kutoka asilimia 6.8 mwaka 2005. Mchango wa viwanda

    kwenye mauzo ya nje umeongezeka kutoka asilimia 9.3

    mwaka 2005 hadi asilimia 23.3 mwaka 2014.

    Tunategemea ukuaji mkubwa wa viwanda katika

    Mpango wa Pili wa maendeleo wa miaka 5 kutokana na

    misingi imara tuliyoijenga katika Mpango wa Kwanza.

  • 53

    Ujenzi wa kiwanda cha chuma kule Liganga na makaa ya

    mawe cha Mchuchuma, unatarajiwa kuanza mwaka huu na

    kiwanda cha kuchakata gesi pale Lindi unatarajiwa kuanza

    baada ya taratibu za kuwapatia ardhi zitakapokamilika.

    Hivi ni viwanda vya msingi na mama ambavyo vitachochea

    kasi ya ukuaji wa viwanda nchini na uchumi kwa jumla.

    Madini

    Mheshimiwa Spika;

    Sekta ya Madini ndiyo ya pili baada ya utalii kwa

    kuingiza fedha nyingi za kigeni. Kama nilivyoahidi, tulipitia

    upya sera, sheria na mikataba ya madini iliyokuwepo na

    kutengeneza sera na sheria mpya. Halikadhalika,

    tulianzisha mazungumzo na baadhi ya makampuni ambayo

    hatimaye yalizaa marekebisho ya mikataba yao na hivyo

    kuboresha maslahi ya taifa.

    Kufuatia marekebisho hayo, makampuni husika ya

    madini yanalipa kodi ya mapato. Bila ya hivyo huenda

    mpaka leo yangekuwa hayajaanza kulipa kodi. Kutumika

  • 54

    kwa Sheria mpya ya Madini, viwango vipya vya mrahaba na

    kupunguzwa kwa misamaha ya kodi vimeongeza mapato ya

    Serikali. Aidha, tuliunda Wakala wa Ukaguzi wa Madini

    Tanzania (TMAA) ambao umewezesha kukagua mahesabu

    ya migodi kuhusu uwekezaji na mauzo ya madini na

    kuwawezesha TRA kutoza kodi stahiki kutoka kwa

    makampuni hayo.

    Mheshimiwa Spika;

    Mabadiliko haya pamoja na kuongezeka kwa

    uwekezaji katika sekta hii yamewezesha mchango wa sekta

    ya madini katika Pato la Taifa kuongezeka kutoka asilimia

    2.9 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 3.5 mwaka 2014.

    Thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi pia imeongezeka

    kutoka Dola za Marekani milioni 655.5 mwaka 2005 hadi

    kufikia Dola za Marekani bilioni 1.794 mwezi Desemba

    2014. Mambo yangekuwa mazuri zaidi kama bei ya dhahabu

    isingeshuka katika kipindi hiki.

  • 55

    Mheshimiwa Spika;

    Serikali ilifanya uamuzi wa kulifufua na kuliwezesha

    Shirika letu la Madini (STAMICO) kuanza tena kazi ya

    utafutaji na uchimbaji wa madini kupitia kampuni zake

    tanzu. STAMICO kwa kupitia kampuni yake ya

    STAMIGOLD imeanza kuzalisha dhahabu na kuuza nje.

    Vilevile, tumejiunga na Mpango wa Uwazi wa Uvunaji wa

    Maliasili (EITI) ambao umesaidia sana katika kuongeza

    uwazi katika biashara ya madini na kusaidia katika

    ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye makampuni ya

    madini.

    Katika kipindi hiki, migodi mitatu mipya ilianzishwa

    nayo ni Migodi ya dhahabu wa Buzwagi (Shinyanga) na

    New Luika (Mbeya) na mgodi wa makaa ya mawe wa

    Ngaka (Ruvuma). Aidha, miradi mikubwa mingine 8

    imeendelezwa na kufikia hatua ya kuanzisha mgodi

    ukiwemo Mradi wa Urani wa Mkuju (Ruvuma), Mradi wa

    Chuma Liganga na Mradi wa Makaa ya Mawe wa

  • 56

    Mchuchuma (Njombe). Pia, ajira rasmi kwenye migodi

    mikubwa nchini imeongezeka kutoka waajiriwa 3,517

    mwaka 2005 hadi waajiriwa 15,000 mwaka 2014. Hali

    kadhalika, makampuni ya madini yameongeza unununzi

    wa bidhaa na huduma hapa nchini (local procurement)

    kutoka Dola za Marekani milioni 230.41 mwaka 2005 hadi

    Dola za Marekani milioni 536.56 mwaka 2014.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki pia, tumetenga maeneo 8 kwa ajili

    ya wachimbaji wadogowadogo. Maeneo haya yamewezesha

    wachimbaji wadogo kuchimba madini bila bughudha.

    Aidha, Wizara imenunua mitambo miwili kwa ajili ya

    uchorongaji wa miamba kusaidia utafiti wa madini kwa ajili

    ya wachimbaji wadogo. Tumeanzisha mfuko wa

    kuwakopesha wachimbaji wadogo pale Wizarani ili kutoa

    fursa kwa wachimbaji wadogo kupata mikopo ya

    kuendeleza shughuli zao.

  • 57

    Nishati

    Mheshimiwa Spika;

    Wakati naanza kazi ya uongozi wa nchi yetu, Tanzania

    ilikuwa inakabiliwa na ukame mkubwa uliosababisha

    upungufu mkubwa wa chakula. Pia kulikuwa na upungufu

    mkubwa wa umeme kwa sababu ya mabwawa ya kuzalisha

    umeme kukosa maji ya kutosha. Serikali ililazimika kulisha

    watu zaidi ya milioni 3,776,000 na kukodisha mitambo ya

    kuzalisha umeme. Kwa siku za usoni tuliamua kuchukua

    hatua thabiti ya kuongeza uzalishaji wa umeme kwa

    kutumia gesi asilia na vyanzo vingine kama vile makaa ya

    mawe, mionzi ya jua na upepo.

    Ujenzi umekamilika wa bomba la kusafirisha gesi

    kutoka Mtwara na Songo Songo litakaloongeza kiasi cha gesi

    kuja Dar es Salaam na kuwezesha uzalishaji wa megawati

    3000 za umeme. Wakati huo huo kazi ya kujenga vituo vya

    kufua umeme inaendelea pale Kinyerezi, Dar es Salaam.

  • 58

    Umeme huo utakidhi mahitaji ya umeme sasa na miaka

    kadhaa ijayo.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tuliunda Wakala wa Umeme

    Vijijini (REA) ambao wamefanya kazi kubwa na nzuri ya

    kusambaza umeme kwa vijiji 5,336 kati ya vijiji 12,423

    nchini. Kazi kubwa iliyofanyika vijijini inapochanganywa

    na ile ya mijini imeongeza idadi ya Watanzania wanaopata

    umeme kutoka asilimia 10 hadi asilimia 40 mwaka 2015.

    Uamuzi uliofanywa katika Bajeti ya mwaka huu wa

    kukusanya fedha kwa ajili ya umeme vijijini kupitia mafuta

    ya petroli, utasaidia sana kuongeza kasi ya kusambaza

    umeme vijijini.

    Gesi Asilia

    Mheshimiwa Spika;

    Tumepata mafanikio katika utafutaji wa mafuta na gesi

    asilia. Kuanzia mwaka 2010 nchi yetu imepata bahati ya

    ugunduzi wa kiasi kikubwa cha gesi bahari kuu. Mpaka sasa

  • 59

    zimegundulika futi za ujazo trilioni 47.08. Ukijumlisha na

    futi za ujazo trilioni 8 zilizogunduliwa takriban miaka 40

    iliyopita kule Songo Songo na Msimbati jumla ya rasilimali

    ya gesi asilia nchini ni futi za ujazo trilioni 55.08. Kazi ya

    utafutaji inaendelea na wataalamu wanasema kuwa

    Tanzania inaweza kuwa na akiba ya futi za ujazo trilioni

    200. Kiasi cha gesi kilichogunduliwa mpaka sasa ni

    kikubwa na kufanya Tanzania kuwa mahala papya pa

    kuipatia dunia nishati hii.

    Gesi asilia tuliyonayo ikisimamiwa na kutumiwa vizuri

    itaiwezesha nchi yetu na watu wake kupata maendeleo

    makubwa na kuondokana na umaskini. Ni fursa ya aina

    yake ya kuipatia Serikali mapato makubwa na kuiwezesha

    kutimiza kwa uhakika majukumu yake na mipango yake.

    Lakini, ili hayo yaweze kufanyika hapana budi pawepo

    usimamizi mzuri wa hatua zote muhimu za mnyororo wa

    thamani: yaani utafutaji, uchimbaji, usafirishaji, uuzaji wa

    gesi asilia na matumizi yake nchini kama nishati na mali

  • 60

    ghafi ya viwanda upande mmoja. Upande mwingine

    inategemea sana matumizi mazuri ya mapato yatokanayo na

    rasilimali hiyo.

    Mheshimiwa Spika;

    Ni kutokana na kutaka kuhakikisha kwamba mambo

    yanakuwa hivyo ndiyo maana tumetunga Sera ya Gesi

    Asilia na kuwasilisha katika Bunge hili ile Miswada miwili

    yaani wa Sheria ya Petroli na ule wa Matumizi ya Mapato ya

    Mafuta na Gesi. Nawashukuru Waheshimiwa Wabunge

    kwa kuipitisha Miswada hii nami nitaitia saini mara

    nitakapoletewa.

    Usafirishaji na Uchukuzi

    Barabara

    Mheshimiwa Spika;

    Serikali ya Awamu ya Nne, imetoa kipaumbele cha juu

    kwa uendelezaji wa miundombinu ya usafirishaji na

    uchukuzi nchini. Hii ni pamoja na barabara, reli, bandari,

    usafiri wa majini na usafiri wa angani. Tumeendeleza kazi

  • 61

    ya kuongeza mtandao wa barabara za lami nchini kwa

    mafanikio makubwa. Karibu barabara kuu zote nchini na

    zile zinazounganisha mikoa zimekamilika kujengwa au kazi

    ya ujenzi inaendelea. Kwa sababu hiyo hivi leo kutokea po

    pote nchini kwenda Dar es salaam unafika siku hiyo hiyo,

    tofauti na ilivyokuwa zamani watu walichukua zaidi ya siku

    moja. Adha ya kupita Kenya na Uganda kwa watu wa

    Mikoa ya Ziwa tumeimaliza.

    Katika mkakati wetu wa kupanua mtandao wa

    barabara za lami nchini, tulitambua barabara za urefu wa

    kilomita 11,474 za kujengwa kwa kiwango cha lami. Baadae

    tuliongeza barabara nyingine na kufikisha kilomita 17,742

    katika mpango huo. Utekelezaji wake upo katika hatua

    mbalimbali. Tayari ujenzi wa kilomita 5,568 kwa upande

    wa barabara kuu na kilomita 535 kwa barabara za mijini

    umekamilika. Ujenzi wa kilomita 3,873 unaendelea.

    Upembuzi yakinifu na usanifu umekamilika kwa barabara

    za urefu wa kilometa 4,965 kinachosubiriwa ni kupatikana

  • 62

    fedha ujenzi uanze. Baadhi ya barabara hizo zimo katika

    bajeti ya mwaka huu wa fedha. Barabara za urefu wa

    kilometa 3,336 zinafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu

    wa kina.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki pia, madaraja madogo 7,200 na

    makubwa 12 yamejengwa na mengine 16 yapo katika hatua

    mbalimbali za ujenzi. Miongoni mwa madaraja makubwa

    yaliyokamilika ni daraja la Mto Malagalasi na yanayojengwa

    ni daraja la Kigamboni na lile la Mto Kilombero. Madaraja

    haya yalikuwa miongoni mwa matano yaliyopangwa

    kujengwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa

    Miaka Mitano mara baada ya uhuru. Madaraja mawili yaani

    la Kirumi lilijengwa mwaka 1985 na la Rufiji mwaka 2003.

    Kwa upande wa vivuko, tumeongeza vipya 15 na kufikisha

    idadi ya 28 kote nchini mwaka 2014.

  • 63

    Mheshimiwa Spika;

    Tumeongeza sana fedha katika mfuko wa barabara

    kutoka shilingi bilioni 73.08 mwaka 2005/06 hadi shilingi

    bilioni 866.63 mwaka 2015/16. Hii itasaidia katika

    matengenezo ya barabara za lami tulizojenga na kujenga

    nyingine mijini. Hali kadhalika itatumika kuimarisha

    barabara za udongo na changarawe wilayani na vijijini

    ziweze kupitika wakati wote. Katika kipindi hiki barabara

    za changarawe zimeongezeka kutoka kilometa 9,424 hadi

    kilometa 22,089.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika miaka kumi hii idadi ya vyombo vya moto yaani

    magari, bajaji na pikipiki imeongezeka kutoka 1,696,088

    mwaka 2005 hadi 3,313,254 hivi sasa. Ongezeko hili

    linalotokana na hali ya kiuchumi ya watu wengi kuwa nzuri

    limezua tatizo la msongamano wa magari katika miji mingi

    nchini. Katika jiji la Dar es Salaam ambako tatizo ni kubwa

    zaidi na Serikali imekuwa inachukua hatua mbalimbali

  • 64

    kupunguza ukali wake. Tunapanua ukubwa wa baadhi ya

    barabara, kujenga barabara za mzunguko (ring roads) na

    sasa tunaanza ujenzi wa barabara za juu ya nyingine

    (flyovers). Tulianzisha matumizi ya treni katika reli za

    TAZARA na TRC kusafirisha abiria. Hivi sasa reli hizo

    zinasafirisha abiria milioni 2,804,269 kwa mwaka ambao

    wangehitaji daladala 253 kwa siku. Mpango mkubwa wa

    kuendeleza matumizi ya reli, Dar es Salaam umeandaliwa

    na tumeanza kuutafutia fedha.

    Usafiri wa Reli

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumetumia muda mwingi kutafuta

    ufumbuzi wa matatizo yanayozikabili reli zetu za TAZARA

    na TRC. Kimsingi reli hizo zimekuwa zinakabiliwa na

    matatizo ya uchakavu wa miundombinu na uongozi na

    uendeshaji usioridhisha. Kwa sababu ya matatizo hayo reli

    hizi ambazo kila moja inaweza kusafirisha tani milioni 5

    kwa mwaka zinasafirisha kati ya tani 200,000 na 300,000 tu.

  • 65

    Hivyo basi, mizigo mingi husafirishwa kwa barabara na

    kutishia uhai wa barabara ambazo tumezijenga kwa

    gharama kubwa.

    Kwa upande wa reli ya kati, uboreshaji wa reli kati ya

    Dar es Salaam na Tabora unakaribia kukamilika na

    utaendelea mpaka Kigoma na Mwanza. Wakati huo huo

    mchakato wa ujenzi wa reli mpya ya upana wa kimataifa

    (standard gauge) unaendelea. Ujenzi unaweza kuanza

    mwaka huu kutegemea kukamilika kwa majadiliano na

    mabenki yaliyoonyesha utayari wa kutukopesha pesa za

    ujenzi.

    Mheshimiwa Spika;

    Azma yetu ya kufufua reli ya TAZARA nayo

    tumeiwekea mkakati. Sisi na Zambia tumekubaliana

    kushirikiana kwa karibu katika kutafuta ufumbuzi wa

    matatizo yanayoikabili reli yetu hiyo. Bahati nzuri marafiki

    zetu wa China nao wamekubali kutusaidia katika mipango

    yetu hiyo. Ni matumaini yangu kuwa safari hii tutapata

  • 66

    ufumbuzi wa kudumu kwa matatizo yanayoathiri ufanisi

    wa reli hii yenye umuhimu wa aina yake kwa uhai na

    ustawi wa uchumi wa nchi zetu na watu wake.

    Bandari

    Mheshimiwa Spika;

    Tumeboresha na kuimarisha huduma katika bandari ya

    Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa. Mwaka 2014

    bandari yetu ilihudumia tani milioni 14.4 ukilinganisha na

    tani milioni 6.7 mwaka 2005. Mwaka huu inaweza kufikia

    tani milioni 18. Siku hizi huduma hutolewa kwa saa 24 na

    kasi ya kupakua, kupakia na kutoa mizigo imeongezeka

    sana na wizi umepungua sana. Hata wale walioacha

    kuitumia bandari yetu wameanza kurudi.

    Mheshimiwa Spika;

    Kuanza kutumika kwa mfumo wa Single Customs

    Territory unaorahisisha upakuaji na upakiaji mizigo ya nchi

    za Jumuiya ya Afrika Mashariki kumeongeza zaidi ufanisi.

  • 67

    Tuko katika majadiliano na DRC na Zambia ambao nao

    wameonyesha nia ya kuingia katika mfumo huu.

    Kuongezeka kwa usafirishaji wa mizigo inayopita

    nchini kuna faida kwani sekta ya usafirishaji inachangia

    zaidi ya asilimia 15 ya pato la taifa. Hali kadhalika, ujenzi

    wa gati za 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam

    unaotegemewa kuanza mwezi huu utawezesha huduma ya

    makasha kuongezeka kutoka makasha 600,000 hadi

    makasha 1,200,000. Mipango ya kuboresha bandari za

    Mtwara, Tanga na zile zilizo kwenye Maziwa yetu makuu

    na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo zitaiwezesha Tanzania

    kunufaika na fursa ya jiografia yake.

    Usafiri wa Anga

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki tumefanya jitihada kubwa ya

    kuwekeza kwenye ukarabati, upanuzi na ujenzi wa viwanja

    vya ndege nchini. Tumekarabati Uwanja wa Ndege wa

    Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao umeongeza uwezo

  • 68

    wa kuhudumia kutoka ndege 7 hadi 30 hivi sasa. Aidha

    tunajenga jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo lenye

    uwezo wa kuhudumia abiria milioni 3.5. Ujenzi huo

    unategemewa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu.

    Kukamilika kwake kutauwezesha uwanja wa Kimataifa wa

    Julius Nyerere kuhudumia abiria milioni 6 na ndege nyingi

    zikiwemo ndege kubwa za kisasa za Airbus 380.

    Mheshimiwa Spika;

    Vile vile, tumeufanyia ukarabati na upanuzi Uwanja

    wa Kimataifa wa Kilimanjaro ambao ni muhimu sana kwa

    sekta ya utalii ya ukanda wa kaskazini. Uwanja mpya wa

    ndege wa Songwe kule Mbeya umekamilika na hivi sasa

    unatumika. Hali kadhalika, tumeviboresha upya viwanja

    vya ndege vya Arusha, Mafia, Mpanda, Kigoma, Tabora,

    Mwanza na Bukoba.

    Ujenzi, upanuzi na ukarabati huu tulioufanya,

    umechangia sana katika ongezeko kubwa la safari za ndege

    na abiria nchini. Safari za ndege kuja nchini zimeongezeka

  • 69

    toka safari 78 mwaka 2005 zilizokuwa zinatolewa na

    kampuni 29 za usafiri wa ndege hadi safari 175 zinazotolewa

    na kampuni 55 mwaka 2014. Aidha, abiria wanaoondoka na

    kuwasili katika viwanja vya ndege wameongezeka kutoka

    2,172,519 mwaka 2005 hadi abiria 4,670,380 mwaka 2013.

    Siku hizi Watanzania wanaopanda ndege wanaongezeka

    kwa kasi kubwa.

    Mheshimiwa Spika;

    Jambo ambalo hatukuweza kufanikiwa ni lile la

    kufufua Shirika letu la Ndege. Tumefanikiwa kulifanya lisife

    lakini hatukuweza kulihuisha lirejee hata kwenye ile hali

    yake ya zamani. Hata hivyo, fikra na mawazo kuhusu

    mkakati wa kulijenga upya shirika hilo yapo. Kwa sasa

    Menejimenti imepewa jukumu la kuandaa mpango wa

    biashara unaoeleweka na unaokopesheka, kisha Serikali

    itaona namna ya kulisaidia shirika.

  • 70

    Utabiri wa Hali ya Hewa

    Mheshimiwa Spika;

    Sambamba na hayo, tumeboresha huduma za utabiri

    wa hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa imepatiwa vifaa

    vipya ambavyo vimeongeza ufanisi na usahihi wa utabiri

    unaotolewa. Mwezi Februari 2014 Mamlaka hiyo ilipata

    cheti cha utoaji wa huduma bora cha ISO na hivyo kuufanya

    taarifa zake kutambuliwa kimataifa.

    Mawasiliano

    Mheshimiwa Spika;

    Tumepiga hatua kubwa katika sekta ya teknolojia ya

    habari na mawasiliano. Tumejenga Mkongo wa Taifa wa

    Mawasiliano wenye urefu wa kilometa 7,560

    unaounganisha miji mikuu ya mikoa yote ya Tanzania Bara

    isipokuwa mkoa mpya wa Simiyu. Kwa Mikoa ya Unguja na

    Pemba, ujenzi wake utakamilika mwezi ujao. Katika Awamu

    ya Pili, Mkoa wa Simiyu na wilaya zote nchini

    zitaunganishwa.

  • 71

    Ujenzi wa mkongo huu umechangia katika kuongeza

    ubora na kasi ya mawasiliano, na kushusha gharama za

    mawasiliano. Kwa mfano, gharama za kupiga simu

    zimeshuka kutoka shilingi 115 kwa dakika mwaka 2005

    hadi shilingi 34.92 mwaka 2014 na gharama za intaneti

    zimeshuka kutoka wastani wa shilingi 36,000 kwa Gigabyte

    moja mwaka 2005 hadi wastani wa shilingi 9,000 kwa

    Gigabyte moja (GB 1) mwaka 2014. Hii imeshusha pia

    gharama za biashara kwa kurahisisha mawasiliano na

    malipo kati ya mabenki na kwa njia ya mtandao na simu.

    Kwa upande wa laini za simu, zimeongezeka kutoka

    laini milioni 2.96 mwaka 2005 hadi milioni 28 mwaka 2014.

    Watu wanaotumia intaneti wameongezeka toka milioni 1.6

    hadi milioni 9.3 mwaka 2014. Kukua kwa mawasilino ya

    simu kumewezesha watumiaji milioni 12.3 kupata huduma

    ya fedha kupitia simu za mkononi. Kati ya Julai 2013 na

    Aprili 2014 jumla ya miamala milioni 972.6 ilifanyika yenye

    thamani ya shilingi trilioni 28. Huu ni wastani wa zaidi ya

  • 72

    shilingi trilioni 2 kwa mwezi na kufanya Tanzania

    kuongoza duniani kwa huduma hii.

    Mheshimiwa Spika;

    Tulitambua kuwa makampuni binafsi ya simu

    hayapendi kuwekeza vijijini ambako biashara si kubwa

    kama mijini. Kwa kutambua umuhimu wa huduma ya

    mawasiliano kwa maendeleo, Serikali iliamua ibebe mzigo

    huo. Kwa sababu hiyo tumeanzisha Mfuko wa Mawasiliano

    kwa Wote (UCSAF) ambao utawezesha kata na vijiji vyote

    nchini kufikiwa na huduma za mawasiliano. Mfuko huo

    umekwisha wezesha jumla ya kata 52 na vijiji 314 kufikiwa

    na huduma hizo. Upelekaji wa huduma za mawasiliano

    kupitia Mfuko huo zinaendelea kwa kata nyingine 163 zenye

    vijiji 922, ambapo wananchi milioni 1.2 watanufaika.

    Mheshimiwa Spika;

    Tumechukua hatua ya kuhakikisha kuwa mianya ya

    kodi inazibwa na kwamba makampuni yanalipa kodi stahiki

    kwa kununua na kufunga mtambo wa Kusimamia

  • 73

    Mawasiliano ya simu nchini. Mtambo huo unaowezesha

    Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kukusanya takwimu

    halisi za mawasiliano yanayofanywa. Tangu kuanza

    kutumika kwa mtambo huo, mwaka jana Serikali imeweza

    kukusanya shilingi bilioni 24.6 ambazo vinginevyo

    zisingepatikana. Aidha, tumekuwa nchi ya kwanza Afrika

    ya Mashariki kuhama kutoka mfumo wa analojia kwenda

    digitali. Karibu tutakamilisha kwa mikoa yote. Tunazipokea

    nchi kadhaa zinazokuja kujifunza kwetu juu ya uendeshaji

    wa zoezi hili.

    Ardhi na Makazi

    Mheshimiwa Spika;

    Maisha bora kwa kila Mtanzania ni pamoja na

    kuboresha makazi ya watu. Sote tunafahamu kuwa makazi

    ni hitajio la msingi la binadamu. Lengo letu la kuboresha

    huduma za ardhi, nyumba na makazi limepata mafanikio

    makubwa. Tumepeleka huduma za utawala wa ardhi karibu

    zaidi na wananchi kwa kuanzisha Kanda nane za

  • 74

    kusimamia upangaji, upimaji na utoaji hatimiliki. Uamuzi

    huu umepunguza lile tatizo la watu kuchelewa kupata hati

    miliki. Toka 2006 hadi sasa jumla ya hati 164,275

    zimetolewa, vijiji 10,500 vimepimwa na kati yake vijiji 10,341

    vimepatiwa hatimiliki.

    Mheshimiwa Spika;

    Tumetunga Sheria kwa ajili ya kuwezesha upatatikanaji

    wa mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba. Sheria hizo ni

    pamoja na Sheria ya Mikopo ya Nyumba (Mortage Finance)

    na Sheria ya Kutambua Milki ya Sehemu ya jengo haswa

    kwenye maghorofa (Unit Tittles Act) ya mwaka 2008. Sheria

    hizi kwa ujumla wake zimewezesha watu wengi zaidi

    kupata mikopo ya kujenga au kukarabati nyumba zao na

    kuwawezesha watu kupata umiliki wa sehemu ya jengo.

    Mabadiliko hayo pia yamewezesha sekta ya nyumba

    kukua kwa kasi kubwa na majengo na nyumba za kisasa

    kujengwa katika kipindi cha miaka 10 hii. Dar es Salaam ya

    leo na ile ya 2005 ni tofauti kabisa. Shirika la Nyumba la

  • 75

    Taifa, Wakala wa Nyumba za Serikali, Mifuko ya Hifadhi ya

    Jamii nayo imefanya uwekezaji mkubwa sana katika ujenzi

    wa nyumba katika kipindi hiki.

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa upande wa watumishi wa serikali kuwa na

    nyumba mwaka 2008 tulianzisha Mfuko wa Mkopo kwa

    watumishi wa umma ambao hadi sasa umetoa mikopo ya

    shilingi bilioni 5.4 kwa watumishi 1,169. Pia, tumeanzisha

    Kampuni ya Mikopo ya Nyumba kwa ajili ya watumishi wa

    umma ambayo tayari imeanza kazi.

    Mheshimiwa Spika;

    Ninayo furaha kueleza kuwa makazi ya wananchi pia

    yameendelea kuwa bora. Takwimu za Sensa ya Watu na

    Makazi ya Mwaka 2012, inaonyesha kuwa idadi ya nyumba

    zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutoka asilimia 46

    mwaka 2002 hadi asilimia 65 mwaka 2012. Kwa lugha

    nyingine nyumba zilizoezekwa makuti na nyasi zimezidi

  • 76

    kupungua. Haya ni mafanikio makubwa ya kutia moyo na

    hatua muhimu katika kuboresha maisha ya Watanzania.

    Utafiti

    Mheshimiwa Spika;

    Jambo lingine ambalo tumeliwekea msingi mzuri ni

    eneo la utafiti. Hili ndilo eneo ambalo ilitalivusha taifa letu

    kwenda katika maendeleo makubwa zaidi. Niliamua

    Serikali ichukue hatua za makusudi za kufufua shughuli za

    utafiti ambazo zilikuwa zinapita katika kipindi kigumu.

    Niliamua kuwa Serikali ianze safari ya kutenga fedha za

    kutosha kwa ajili ya utafiti. Tulianza na shilingi bilioni 10

    na kuendelea kuongeza mwaka hadi mwaka na kufika

    shilingi bilioni 60 mwaka 2014, katika kipindi cha kujitahidi

    kufikia asilimia 1 ya bajeti ya Serikali na hatimaye asilimia 1

    ya pato la Taifa kwa ajili ya shughuli za utafiti.

    Mheshimiwa Spika;

    Kwa kutumia kiasi hiki kidogo kilichopo wanasayansi

    wetu 344 wamepata ufadhili wa masomo ya shahada ya

  • 77

    Uzamili na 173 wa shahada ya Uzamivu. Miradi 70 ya

    utafiti imefadhiliwa, kati ya hiyo 22 ni ya kilimo. Fedha hizi

    pia zimewezesha Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia

    kuanzisha viatamizi vya teknohama ambavyo vimewezesha

    vijana wetu kubuni na kuvumbua teknolojia zenye manufaa

    kwa maendeleo ya jamii na taifa. Wamezalisha ajira na

    kunufaisha watu wengi. Kampuni ya Max Malipo ni mfano

    mmojawapo mzuri wa matokeo mazuri ya viatamizi hivi.

    Huduma za Jamii

    Elimu

    Mheshimiwa Spika;

    Katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge la Tisa

    mwaka 2005 nilisema kuwa, Hakuna Taifa lililopata

    maendeleo bila kuendeleza elimu. Hivyo kuendeleza elimu

    nchini itakuwa agenda muhimu ya Serikali ya Awamu ya

    Nne. Tumetimiza ahadi. Katika kipindi chote cha miaka

    kumi bajeti ya sekta ya elimu ndiyo iliyokuwa kubwa kuliko

    za sekta nyingine zote. Mwaka huu 2015 bajeti ya elimu

  • 78

    imefikia shilingi trilioni 3.4 ikilinganishwa na shilingi

    bilioni 669.5 za mwaka 2005.

    Mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu ndani

    ya miaka 10 hii ni ya kutia moyo. Tumeongeza shule za

    msingi kutoka 14,257 mwaka 2005 hadi 16,538 mwaka 2015

    na wanafunzi wameongezeka kutoka 7,541,208 hadi

    8,202,892. Upanuzi huu umewezesha asilimia 98 ya watoto

    wanostahili kupata elimu ya msingi sasa kuandikishwa.

    Kwa kushirikiana na wananchi na sekta binafsi

    tumeongeza Shule za Sekondari kutoka Shule 1,745 mwaka

    2005 hadi Shule 4,753 mwaka 2015. Idadi ya wanafunzi

    imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,804,056

    mwaka 2015. Katika kipindi hiki pia vyuo vya Ufundi

    vimeongezeka kutoka 184 mwaka 2005 hadi 744 mwaka

    2015 na wanafunzi katika vyuo hivyo wameongezeka

    kutoka 40,059 hadi 145,511 mwaka 2015. Haya ni mafanikio

    makubwa sana.

  • 79

    Kwa nia ya kuongeza ubora wa elimu, tumechukua

    hatua thabiti za kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu,

    vitabu, maabara za sayansi na vifaa vya kujifunzia na

    kufundishia. Tumepanua mafunzo ya ualimu wa Cheti,

    Stashahada na Shahada. Hii imetuwezesha kuongeza idadi

    ya walimu wa Shule za Msingi kutoka 135,013 mwaka 2005

    hadi 202,752 mwaka 2015, na walimu wa Shule za Sekondari

    kutoka 18,754 mwaka 2005 hadi 88,908 mwaka 2015. Uhaba

    wa walimu wa masomo ya sanaa si tatizo tena, tunao wa

    kutosha. Tuna upungufu wa walimu 20,141 wa masomo wa

    sayansi na hisabati. Ninaamini, hata hivyo, kwa programu

    za kusomesha walimu wa sayansi vyuoni zilizopo, katika

    miaka michache ijayo tatizo hili nalo tutalipatia ufumbuzi.

    Kwa mfano, Chuo Kikuu cha Dodoma, mwaka 2014

    kimeanza kudahili wanafunzi 5,000 wa ualimu wa masomo

    ya sayansi.

    Mheshimiwa Spika;

  • 80

    Kwa upande wa maabara za sayansi, katika shule za

    sekondari za kata tayari maabara 5,979 zimejengwa na

    nyingine 4,410 ziko katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.

    Hivi sasa tunashughulikia upatikanaji na usambazaji wa

    vifaa kwa matumizi ya maabara hizo. Kwa upande wa

    vitabu tumeweza kuboresha upatikanaji wake kwa

    mwanafunzi wa Shule za Msingi kutoka uwiano wa 1:5

    mwaka 2005 hadi 1:3 mwaka 2015. Katika shule za sekondari

    uwiano ni 1:2 ukilinganisha na 1:8 mwaka 2005.

    Mheshimiwa Spika;

    Katika kipindi hiki pia tumeshuhudia upanuzi

    mkubwa wa elimu ya juu nchini. Idadi ya vyuo vikuu

    imeongezeka kutoka vyuo 26 mwaka 2005 hadi 52 mwaka

    2015. Miongoni mwa vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha

    Dodoma na cha Nelson Mandela cha Arusha ambavyo

    vimejengwa na Serikali ya Awamu ya Nne. Tumeanza

    mchakato wa kujenga Chuo Kikuu cha Julius Nyerere cha

    Kilimo kule Butiama. Vyuo hivi ni fahari ya nchi yetu kwani

  • 81

    tumevijenga kwa fedha zetu wenyewe bila msaada kutoka

    kwa wafadhili. Ongezeko la vyuo vikuu limefanya idadi ya

    wanafunzi kuongezeka kutoka wanafunzi 40,719 mwaka

    2005 hadi 218,959 mwaka 2014. Idadi ya wanafunzi

    wanaonufaika na mikopo nayo imeongezeka kutoka

    wanafunzi 16,345 mwaka 2005 hadi wanafunzi 99,590

    mwaka huu.

    Afya

    Mheshimiwa Spika;

    Tumepata mafanikio ya kutia moyo kwa upande wa

    kuboresha na kupanua huduma ya afya nchini. Tuliazimia

    kusogeza huduma ya afya karibu na wanapoishi watu kwa

    kujenga vituo vya kutoa huduma ya afya vipya na

    kuimarisha vilivyopo. Kati ya mwaka 2005 na 2014 vituo vya

    kutolea huduma za afya 2,175 vimejengwa. Kati yake

    hospitali 19, vituo vya afya 168 na zahanati 1,883

    zimejengwa.

  • 82

    Tumeimarisha hospitali ya Taifa ya Muhimbili,

    Hospitali za Rufaa za Kanda, Mikoa na Wilaya kwa

    kuzipatia vifaa vya tiba na uchunguzi (MRI, CT Scan, X ray,

    Ultra Sounds, Maabara n.k). Tumejenga maabara ya Taifa ya

    Afya ya Jamii ambayo inatumika kama maabara ya

    Kimataifa ya Rufaa kwa nchi za SADC. Tumeimarisha

    maabara za mikoa kwa majengo na vifaa vya kisasa vya

    uchunguzi wa magonjwa. Maabara yetu ya Mbeya sasa ina

    uwezo wa kubaini virusi vya Ebola jambo ambalo miezi

    michache iliyopita tulikuwa tunapeleka sampuli Nairobi.

    Hivi sasa hospitali za wilaya zinaweza kufanya uchunguzi

    wa mwenendo wa figo na ini.

    Mheshimiwa Spika;

    Tumeboresha huduma ya Afya ya Kinywa katika

    Hospitali ya Muhimbili kwa kufunga mashine 26 za kisasa

    za tiba ya meno na maabara ya kisasa ya kutengeneza meno

    bandia. Pia tumeimarisha huduma ya afya ya kinywa kwa

    kuweka vifaa vya tiba ya meno kwenye Halmashuri 91. Hivi

  • 83

    sasa hospitali 136, vituo vya afya 63 na zahanati 3 zinatoa

    huduma hiyo nchini.

    Tumeanza kupata mafanikio katika dhamira yetu ya

    kujenga uwezo wetu wa ndani wa kuchunguza na kutibu

    maradhi ya figo, moyo, saratani na mishipa ya fahamu

    ambayo tumekuwa tunapeleka wagonjwa wengi nje. Kwa

    mfano, tangu Taasisi ya Moyo ianze kutoa huduma pale

    Muhimbili wagonjwa 71,963 wamepatiwa matibabu

    wakiwemo 692 waliofanyiwa upasuaji. Watu hao

    wangepelekwa nje taifa lingelipa pesa nyingi. Uwezo wetu

    utaongezeka sana hospitali ya Mloganzila itakapokamilika.

    Mheshimiwa Spika;

    Tumebadilisha utaratibu wa kusambaza dawa kutoka

    Bohari ya Dawa. Tumeongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba

    kutoka shilingi bilioni 40.6 mwaka 2005 hadi shilingi

    bilioni 147 mwaka 2014. Idadi ya watu wanaonufaika na

    Mfuko wa Afya ya Jamii na Mfuko wa Bima ya Afya

  • 84

    wameongezeka kutoka asilimia 3 mwaka 2005 hadi asilimia

    19 mwaka 2014.

    Katika kipindi hiki tumetoa msukumo mkubwa katika

    kupambana na maradhi makubwa ya kuambukiza

    yanayosababisha vifo vya watu wengi. Tumeendesha

    kampeni ya kupambana na malaria nchi nzima kwa

    kubadilisha dawa ya kutibu malaria na kugawa vyandarua

    26,371329 kwa watoto chini ya miaka mitano, kwa akina

    mama wajawazito na katika kila kaya. Aidha, tumepulizia

    dawa ya kuua mbu ndani ya nyumba katika mikoa ya kanda

    ya ziwa. Matokeo ya jitihada hizo ni kupungua kwa

    maambukizi ya malaria kwa asilimia 51 na vifo kwa

    asilimia 71. Baada ya kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua

    viluwiluwi vya mbu pale Kibaha kuanza uzalishaji, safari ya

    kutokomeza malaria hapa nchini ni ya uhakika.

    Mheshimiwa Spika;

    Juhudi zetu katika kupambana na ukimwi

    zimewezesha kushuka kwa maambukizi ya ukimwi kutoka

  • 85

    asilimia 7.7 mwaka 2005 hadi asilimia 5.1 mwaka 2012.

    Idadi ya watu waliopima virusi vya ukimwi imeongezeka

    kutoka 365,189 mwaka 2005 hadi 25,468,564 mwaka 2014.

    Aidha, tumewezesha vituo 5,244 na asilimia 97 ya vituo

    vyote vinavyotoa huduma ya uzazi kutoa huduma ya kuzia

    maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

    Mheshimiwa Spika;

    Kati ya mwaka 2005 na 2014 tumeongeza udahili wa

    wanafunzi katika vyuo vya afya kutoka 3,025 mwaka 2005

    hadi 11,807 mwaka 2014. Katika kipindi hicho wataalamu

    wa afya 55,608 wameajiriwa. Aidha, tumeongeza ajira ya

    kada mbalimbali za afya. Kwa sababu hiyo idadi ya

    madaktari imeongezeka kutoka madaktari 1,048 mwaka

    2006 hadi madaktari 2,325 mwaka 2014. Halikadhalika,

    madaktari wasaidizi wameongezeka kutoka 1,223 hadi

    1,914, wauguzi kutoka 15,961 hadi 22,942 wataalamu wa

    Maabara kutoka 1,277 hadi 2,378 mwaka 2014. Hivi sasa

    uwiano wa Daktari kwa wagonjwa ni 1:6,666 ikilinganishwa

  • 86

    na 1:35,714 mwaka 2005. Na, uwiano wa Muuguzi kwa

    wagonjwa umeshuka kutoka 1:2,347 mwaka 2005 hadi

    1:2,008 mwaka huu.

    Mheshimiwa Spika;

    Tumeendesha kampeni ya kuboresha lishe nchini na

    kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Lishe (2011-2016). Kwa ajili

    hiyo mwaka 2013 tulizindua Programu ya Uongezaji wa

    Virutubishi. Matokeo ya jitihada zetu hizo yameanza

    kuonekana. Udumavu umepungua toka asilimia 44 mwaka

    2005 hadi asilimia 35 mwaka 2014 na uzito pungufu toka

    asilimia 17 hadi asilimia 13.

    Kwa jumla juhudi zetu za kuboresha huduma ya afya

    zimezaa matunda ya kuridhisha. Wastani wa umri wa

    kuishi wa Mtanzania umeongezeka toka miaka 49 mwaka

    2005 hadi miaka 62 hivi sasa. Vifo vya watoto wachanga

    vimepungua toka vifo 68 kwa kila vizazi hai 1000 hadi vifo

    21 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2014. Vifo vya watoto

    chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 112 kwa kila

  • 87

    vizazi hai 1000 mwaka 2005 hadi vifo 54 kwa kila vizazi hai

    1000 mwaka 2014, na vifo vya akinamama wajawazito

    vimepungua toka vifo 578 kwa vizazi hai 100,000 hadi vifo

    432 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2012. Haya ni mafanikio

    ya kutia moyo ingawaje bado tunatakiwa kuendeleza juhudi

    zaidi mara dufu ili vifo vipungue zaidi na zaidi.

    Maji

    Mheshimiwa Spika;

    Serikali ya Awamu ya Nne imefanya juhudi kubwa

    katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na

    salama na usafi wa mazingira katika kipindi hiki.

    Tumekamilisha miradi ya maji katika miji mikuu ya mikoa

    8, Wilaya 6 na Miji midogo 2. Aidha, miradi katika miji

    mingine 13 ya mikoa, 27 ya Wilaya na Miji midogo

    inaendelea kutekelezwa. Utekelezaji wa miradi hii

    umewezesha kiwango cha upatikanaji maji mijini kufikia

    wastani wa asilimia 86 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia

    73 mwaka 2005. Na kwa Vijijini imefikia asilimia 67.6

  • 88

    Mwaka 2014 ukilinganisha na asilimia 53 mwaka 2005.

    Tumevuka lengo letu la kuwapatia maji asilimia 65 ya

    wakazi wa vijijini.

    Aidha, miradi inayoendelea kutekelezwa hivi sasa

    itakapokamilika katika mwaka huu wa fedha upatikanaji wa

    maji mijini utafikia asilimia 90 ambalo ndilo lengo la Ilani ya

    uchaguzi ya CCM. Vijijini inaweza kufikia asilimia 70

    ambayo ni juu ya lengo la asilimia 65.

    Aidha, tumeboresha huduma za uondoaji wa maji taka

    katika miji ya Tanga, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa,

    Songea, Tabora na Morogoro. Uboreshaji huu wa huduma

    za utoaji wa maji taka ni mwanzo mzuri katika kuhakikisha

    kwamba tunakuwa na mipango mizuri ya maji taka mijini.

    Uwezeshaji wa Wananchi

    Mheshimiwa Spika;

    Uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ilikuwa ni moja ya

    dhima kuu ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005.

    Katika kutekeleza dhamira hii, Serikali imeendeleza kwa

  • 89

    mafanikio makubwa mifuko ya kutoa mikopo kwa vijana,

    wanawake, wajasiriamali wadogo na kuanzisha fursa

    nyingine mpya. Watu wengi wamenufaika na wao wenyewe

    kuwa chachu ya kuzalisha ajira, kupunguza umasikini na

    kuinua hali za maisha ya watu walioguswa na fursa

    zilizopatikana.

    Tumeiwezesha Benki ya Wanawake kuanza na

    kuendelea kutoa huduma. Kama mjuavyo niliamua Serikali

    ichangie mtaji wa mwanzo na inaendelea kuchangia mtaji

    huo. Tayari Benki hiyo imeshakopesha watu 125,000 na kati

    yao wanawake ni asilimia 82. Hali kadhalika, nilifanya

    uamuzi wa makusudi wa kuifufua Benki ya Rasilimali (TIB).

    Dhamira yangu ni kutaka iwepo Benki ya maendeleo

    itakayotoa mikopo ya muda mrefu na wa kati kwa

    wawekezaji wazawa. Hii itawezesha kuanzisha na

    kuendesha shughuli za viwanda, madini, utalii na biashara

    kwa urahisi.

  • 90

    Tumeiwezesha Benki ya Rasilimali kwa mtaji, rasilimali

    watu na vitendea kazi na kuifanya iwe moja ya benki ya

    kutumainiwa nchini. TIB imeshatoa mikopo kwa

    makampuni 365 yenye thamani ya shilingi bilioni 512.

    Aidha, imetoa mikopo kwa miradi 201 yenye thamani ya

    shilingi bilioni 156 kupitia dirisha dogo la kilimo. Natoa

    pongezi maalum kwa viongozi na watumishi wa Benki ya

    Rasilimali kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya katika

    kipindi hiki kifupi. Naomba waendelee na moyo huo kwa

    maslahi ya nchi yetu.

    Mheshimiwa Spika;

    Tumetimiza ahadi yetu ya kuimarisha ushirika nchini

    kama nguzo kuu ya kuunganisha nguvu za wanyonge

    kujiletea maendeleo. Katika kipindi hiki, idadi ya Vyama

    vya Ushirika vya aina mbalimbali nchini imeongezeka

    kutoka 5,832 mwaka 2005 hadi 9,604 mwaka 2015.

    Kwa upande mwingine, Vyama vya Akiba na Mikopo

    (SACCOS), vimeongezeka zaidi ya mara tatu kutoka vyama

  • 91

    1,875 mwaka 2005 hadi 5,559 mwaka 2014. Akiba, hisa na

    amana za wanachama zimeongezeka kwa zaidi ya mara

    tano kutoka Shilingi bilioni 85.6 mwaka 2005/2016 hadi

    Shilingi 463 bilioni mwaka 2014 na mikopo kwa

    wanachama imekua mara 13 toka shilingi bilioni 65.7 hadi

    shilingi bilioni 893 mwaka huu. Kwa hakika haya ni

    mafanikio makubwa ya kujivunia. Watu wengi

    wamewezeshwa kupunguza umasikini wao na wengine

    kuondoka katika lindi la umasikini.

    Sanaa na Michezo

    Mheshimiwa Spika;

    Niliahidi kusaidia kukuza michezo na sanaa nchini.

    Kwa upande wa michezo niliahidi kuwa Serikali italipia

    makocha. Nilitimiza ahadi yangu kwa michezo ya soka,

    netiboli na ngumi. Kwa upande wa riadha tuliwapeleka

    wanariadha wetu China, Ethiopia na New Zealand kwa

    maandalizi ya mashindano ya kimataifa. Timu yetu ya taifa

    ya soka haijafanya vizuri sana. Kwa upande wa soka

  • 92

    tulianza kupata matumaini lakini baadae yakafifia. Timu

    yetu ya taifa ya soka haijafanya vizuri sana pamoja na

    kubadili makocha. Hata vilabu vyetu pia havifanyi vizuri.

    Kwa kweli lazima Watanzania tukae chini na kujiuliza kwa

    nini hatufa