TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA DAR ES SALAAM KOZI: SHAHADA YA ELIMU YA WATU WAZIMA NA MAFUNZO ENDELEVU MWAKA WA MASOMO: 2013/2014 MWAKA WA PILI MODULI: KUCHAMBUA NADHARIA ZA UHAKIKI MSIMBO WA MODULI: KIU 07431 MWEZESHAJI: MWALIMU KILEO AINA YA KAZI: KAZI YA KIKUNDI NAMBA TATU WASHIRIKI KATIKA KAZI:- 1. SADI ISSA 2. TESHA ANTUSA 3. MLINGWA AGNESS 4. MASIMBA SHABANI R.A. 5. HABIBU ABASSI
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
TAASISI YA ELIMU YA WATU
WAZIMA
DAR ES SALAAMKOZI: SHAHADA YA ELIMU YA WATU WAZIMA NA
MAFUNZO
ENDELEVU
MWAKA WA MASOMO: 2013/2014 MWAKA WA PILI
MODULI: KUCHAMBUA NADHARIA ZA UHAKIKI
MSIMBO WA MODULI: KIU 07431
MWEZESHAJI: MWALIMU KILEO
AINA YA KAZI: KAZI YA KIKUNDI NAMBA TATU
WASHIRIKI KATIKA KAZI:-
1. SADI ISSA
2. TESHA ANTUSA
3. MLINGWA AGNESS
4. MASIMBA SHABANI R.A.
5. HABIBU ABASSI
6. MSHANA EMELINE
7. KISHIMBWE HALIMA
8. GODFREY RENATUSI
9. HAMISI SHABANI
SWALI:
Uhakika wa Fani katika Kitabu CHA KILIO CHA HAKI.
UTANGULIZI
“KILIO CHA HAKI” ni Tamthilia iliyoandikwa na Alamin Mazrui(1981). Tamthilia hii inaelezea mapambano baina ya wafanyakazi naudhalimu wa makaburu. Tamthilia hii ina sawiri mapambano ya nchinyingi za kiafrika kutaka kujikomba kutoka kwa watawala wakikoloni.
Katika tamthilia hii mwandishi amemchora mwanamke jasiri
aliyejikomboa kimawazo na ndiye aliyekua kiongozi wa mapambano na
anadhihirisha udhalimu wa jamii yake unaowapata wafanyakazi kwa
Mwanamke huyu.Alifaulu katika kuwazindua wafanyakazi wenzake ili
wapambane na udhalimu na watetee haki zao. Mapambano haya
yanaleta mwamko wa kisiasa ambao ndio mwanzo wa matayarisho ya
vita vilivyoikomboa nchi nzima kutoka na ukoloni.
UHAKIKI WA TAMTHILIA KILIO CHA HAKI
FANI
Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001).Introduction to the study
of literature.
“Fani ni ufundi wa mwanafasihi anaoutumia katika uandishi wa kazi
yake, ili aweze kufikisha ujumbe wake kwa wasomaji wake. Katika
uchambuzi wa tamlithiliya hii vipengele vilivyo chambuliwa ni
Ninyi ndio washenzi mnao…..mnao….Uk 12 (alisema Zari)
Aaaa….rafiki zangu…..kusena kweli...kwa hakika….sifahamu kwa
nini(Delamon Uk 13)
SITIARI
Sitiari hulinganisha vitu au watu bila kutumia viunganishi.Hulinganisha vitu kama vinafanana kabisa.
Katika riwaya hii mwandishi ameweza kuipamba kazi yake kwakutumia sitiari mbalimbali.
Mfano:“Mimi ndiye simba” Uk 32 hapa baba yake lanina alikuwa namaana ya kuwa yeye ndiye mkuu wa familia akiomgea kitu hakuna wakumpinga.
Mfano “Huyu ni punda tu asiyejua fadhila Uk 38 hapa tumemuonababa Lanina alikuwa akimwambia mwanawe Lanina. Akimaanishamwanawe hana shukrani maana shukrani ya punda ni mateke.
Mfano “Siasa ni mchezo mchafu”Uk 76.Hapa mwandishi amelinganishasiasa na mchezo mchafu, kama vile kufungwa gerezani na kuaibishwambele za watu.
TASHIHISI
Ni kuvipa vitu uwezo wa kufanya jambo anbalo halina uwezo au sifa
ya kufanya jambo tofauti na uwezo wa kibinadamu.
Mfano: mzee alisema:
“Kwa nini ewe bara la Afrika
Ewe nchi uliyepambwa kwa weusi
Ewe roho wa kizazi chetu
Tukutilieje mbolea siku baada ya siku
Kwa kutaraji utatuzalia
RIDAA.
Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema ridaa ni misemo
ambayo kuonyeshwa kushangazwa kwa jambo fulani. Misemo hii
huambatana na matumizi ya alama za mshangao katika kukubali
jambo, kuchukia au kuonyesha heshima maalumu.
Mfano:
Na malalamiko yatapungua!” Uk 15 alisema shindo
“Tafadhali usinifanyie uhuni huo!” alisema Lanina Uk 25
“Mimi si Malaya” alisema Lanina Uk 25
“Aaa! Ni hilo tu Lanina” Uk 25 (alisema kachero)
“Lanina! Tereki!” (alisema kachero) Uk 26
“Ewe twende tukalale mama eh!” alisema Lanina Uk 30
WAHUSIKA
Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema mwandishi Alamin
Mazrui wa tamthilia ya KILIO CHA HAKI amewatumia wahusika kwa
kuwagawa katika makundi mbalimbali ambayo ni wahusika wakuu,
wahusika wasaidizi na wahusika mviringo.
MHUSIKA MKUU
Mhusika nkuu katika tamthilia yaKILIO CHA HAKIni Lanina. Alamini
Mazrui alimtumia Lanina kwa kutumia nadharia ya ufeministi.
Lanina amekuwa mwanamke aliyepigania haki na ukombozi wa mwanamke
pamoja na kutetea maslahi ya wafanyakazi wenzake. Hivyo alisimama
kidete bila kukata tamaa katika kupigania haki pamoja na kuwa
alipata mateso na manyanyaso mbalimbali hadi kufikia hatua ya
kuwekwa kizuizini.
Mfano
Katika ukurasa wa 14 anasema
“Lakini sisi tunajaribu kutetea haki zetu……”
Askari anampiga kofi na kusema wacha upuuzi wako huo. Haki! Haki
unapigania kitu hata hujui ukipewa utafanyia nini?
Pia Lanina ni mama wa watoto wawili yaani Dida na Badi.
Hii inadhihirika pale ambapo Lanina alipokuwa akimpapasa mwanawe
Dida
“Pole Dida mwanangu.
Nimesharudi sasa hivi.uk 30
Wasifu mwingine wa Lanina ni mke wa Mwengo. Hii inadhihirika pale
ampapo Mwengo alipokuwa akiongea na Lanina.
Mimi ni mume wako ala!Umesahau? Kwa nini hunijibu? Kwa nini
umenipuuza namna hii?
DELAMON
Huyu ni mhusika mkuu pia kwani ameonekana tangu mwanzo wa matukio
katika tamthiliya hii hadi mwisho. Hapa mwandishi ametumia
nadharia ya ubada (ukoloni) akiwakilisha jinsi wakoloni walivyo
wagandamiza wafanyakazi wa kiafrika kiuchimi.
Hii imejitokeza katika ukurasa wa 13 pale ambapo Lanina anamjibu
Delamon kwa hasira “….. nyingi hamkuja hapa kwa manufaa/faida
yetu…… mmekuja kwa maslahi yenu wenyewe………… uk 13.
Pia Delamon ni mmiliki wa shamba kwa maana nyingine ni mnyonyaji,
Hii inajidhihirisha katika onyesho la 6
“Katika shamba la Delamon wakati wa mapunziko. Tereki, matuvu,
Dewe, Mussa na mfanyakazi mwingine wanatokeza wamevaa nguo za
kazi. Uk 43.
WAHUSIKA WASAIDIZI
Mwandishi amewagawa wahusika wasidizi katika makundi mawili,
ambayo ni wale wenye msimamo wa nadharia ya Ki-Marx na wale
wasaliti. Nadharia hii ya kimary huonyesha wahusika wa
kimaendeleo, pia huonyesha matumaini ya juu ya kizazi cha
binadamu (tabaka fulani lina kandamizwa lakini linaonyesha
matumaini)
Wahusika aliowatumia kwa nadharia ya Ki-Marx ni Mussa na Dewe
ambao walishirikiana na Lanina katika harakati za kuwakomboa
wafanyakazi ili kupata maslai yao ya kazi. (katika ukurasa wa
2).
“Mussa (kwa hasira) “wasikilize wapumbavu hawa! Ati Lanina
amechochea mgomo
Lanina hata hakuwepo siku ya mgomo.
Lanina, Dewe na Mussa walikuwa watu wenye msimamo, hawakukata
tamaana waliendelea na mapambo hadi mwisho katika uk 62 pale
Lanina alivyokuwa anaonge na Mussa na Dewe.
“Ndugu zangu, ari yetu ndiyo mwokozi wetu, ari yetu lazima
tuisujudie
Isitoshe walipenda maendeleo kwa sababu walikuwa wanapinga
kunyanyaswa na kuonana na makaburu uk 14.
“Lakini sis tunajaribu kutetea haki zetu tu kama….”
Mhusika mwingine ni baba Lanina, amechorwa na mwandishi kama
mfuasi wa mfumo dume na kuona kuwa mwanamke hawezi kutetea haki
wala kufanya mapinduzi, ukurasa wa 38.
Baba akionyesha yenye ndiye msemaji wa mwisho.
“Mimi ndiye simba wa nyumba hii ningurumapo sitaki kuzisikia
sauti zenu za kijinga hapa (Akimgeukia Lanina)
Na wewe binti ya shetani?
Mimi si wale wanaume wengine unaochezeachezea. Mimi si kina
Mwengo mimi ni dume kweli kweli umesikia hivyo!
Mtu katili
Hafai kuigwa katika jamii
JUKWAA
Onyesho la Kwanza (uk 1-14)
Mussa na Dewe wanasoma taarifa tokea gazetini zinaeleza kuwa
kamishina Hunderson amemkamata Lanina wa Muyake kwa tuhuma ya
mauaji ya watu watatu wenye shamba la bwana Delamon.
Onyesho la Pili (uk 15-20)
Lanina anawajibu makachero kuwa Delamon na wenzake hawakuja
kutunufaisha bali kunyonya nchi zetu.
Onyesho la Nne (uk 29-36)
Lanina karudi nyumbani lakini amekutana na lawama za mume wake
Bwana Mwengo kwa kumuachia familia kwa muda mrefu. Hata hivyo
walisamehana na kutaka waendelee kushirikiana.
Onyesho la Tano (uk 37-42)
Lanina anakutana na wazazi wake kijijini, baba yake anamlaani na
hata kupigwa yeye na mama yake kwa sababu Lanina hafuati mila na
desturi za kwao na mama yake ndiye aliyepewa kumfunza.
Onyesho la Sita (uk 43-48)
Hapa wasaliti Matovu, Tereki naPelekha wanajifariji na kuwaona
akina Mussa na Dewe na Lanina kuwa ni wajinga, kwa kukataa ofay a
Bw. Delamon.
Onyesho la Saba (uk 49-55)
Wasaliti hawa wana wanamshawishi Lanina arudi kazini kwa vile
wamemhusiwa kuendesha shughuli za siasa na mshahara unapanda juu
kidogo. Lanina anakataa na kuwa fukuza nyumbani kwake.
Onyesho la Nane (uk 56-65)
Lanina yupo kwenye kioski cha mzee Engeli. Mussa, Dewe na Lanina
wanakutana kupeana taarifa kuwa eti Delamon ameruhusu kuendesha
shughuli za kisiasa na kuendeleza mapambano ya kudai haki zao
kazini.
Onyesho la Tisa (uk 66-72)
Katika ofisi ya Bwana Delamon wamesikia Sauti za wafanyakazi
walipoamua kuimba nyimbo za kimapinduzi.
Onyesho la Kumi (uk 73-77)
Hapa Lanina akiawa gerezani anakutana na Askari malaya,ambaye
alimtongoza Lanina lakini Lanina anamkatalia na kumpiga teke
sehemu zake za siri, pia Lanina anaitwa na jaji ili kutoa utetezi
wake katika(uk 77).
MANDHARI
Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema mandhari ni
sehemu au mahali ambapo kazi ya fasihi hutendeka. Katika
tamthiliya ya KILIO CHA HAKI mwandishi ametumia mandhari tofauti
tofauti kama vile shambani (kwa bwana Delamon) uk 43 mahamamani,
kijijini (kwa baba na mama wa Lanina) mtunzi ametumia mandhari
hayo ili kuonyesha matendo mbalimbali ambayo yalitumika kuibua
dhamira mbalimbali.
MALEBA NA VIFAA
Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasemamaleba ni mavazi
anayotumia msanii katika Sanaa yake. Kalika kumpamba mhusika.
Mavazi yaliyotumika katika tamthiliya hii ni pamoja na:-
Matambara uk 5 na uk 77. Matambara ni nguo zilizochanika
zinazoonyesha suala la umaskini, hapa alivaa mzee ambaye hali
yake ya maisha ilikuwa duni.
Khanga uk 39, mama alipojifuta machozi kwa kutumia khanga. Khanga
katika tamthiliya hii ya kilio chetu inawakilisha utamaduni
wamavazi ya mwanamke wa Kitanzania.
VIFAA
Vifaa ni zana zinazotumiwa na wahusika wa kazi ya fasihi ili
kuweka uhalisia.
Mfano wa kiko kilichotumiwa na bwana Delamon inaashiria tabia za
wakoloni kuvuta kwa kutumia kiko, (ukurasa wa 10).
Sigara ni kifaa kilichotumiwa na Lanina kuonyesha tabia ya
mwanamke huyu jasiri kuwa ni mvutaji sigara. Pingu nabundiki ni
silahazilizotumiwa na wakoloni ili kuwatisha na kuwagandamiza
waafrika ili wawanyonye kwa urahisi (ukurasa wa 14).
TASWIRA NA ISHARA
I. ISHARA
Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). AnasemaTaswira na
Isharani maelezo yanayoeleza jambo kwa njia ya kufichika ili
msomaji afikiri na kugundua mwenyewe.
Kutikisa kichwa, katika ishara hii tunaona Lanina akimkatalia
Mwengo juu ya mawazo yake potofu juu ya mkewake Lanina hii
inapatikana uk 34. Pia mama yake Lanina alitikisa kichwa
kuonyesha kukubaliana na mumewe. Ishara hizi zinaonyesha matumizi
mbalimbali ya viungo vya mwili vya wahusika wake.
II. TASWIRA
Paneli la Kiswahili (2009-2014) wanasema taswira ni matumizi ya
lugha inayotumia maneno yanayojenga picha au fumbo fulani kwa
msomaji.
KILIO CHA HAKI, inaonyesha mifadhaiko na manung’uniko
yawafanyakazi wakidai haki zao kama vile, mshara ndogo, mazingira
mabovu ya kazi, na vifaa duni vya utendaji kazi.
Makaburu; hii ni taswira iliyotumika kuonyesha wanyonyaji ambao
walikuwa wakiwanyonya na kuwanyanyasa wafanyakazi wao kwa
kuwalipa ujira mdogo na hata kufanya kazi kwa muda mrefu.
Lanina; alikuwa akiwakilisha kundi la wapenda maendeleo, pia
anawakilisha wanawake wanaojitambua na wanaoelewa matatizo
yanayowakumba wananchi wa maeneo wanayoishi.
Shamba la bwana Delamon. Hii ni taswira inayowakilisha mandhari
yaliyokuwa yakitumika kunyonya na kudhurumu haki ya wanyonge
mfano; Lanina na wenzake.
Wanfanyakazi hii ni taswira iliyokuwa ikiwakilisha umma ulio kuwa
ukionewa na kunyanyaswa na bwana Delamon.
Picha ya jalada la KILIO CHA HAKIni ishara ya mwanamke
anayedondosha machozi kwa kulia kutokana na dhuluma na
unyanyasaji anaofanyiwa na jamii yake.
KUFAULU KWA MWANDISHI WA RIWAYA YA KILIO CHA HAKI
Mwandishi ametumia lugha rahisi inayoeleweka yenye lugha ya
kishairi, nyimbo na matumizi mazuri ya wahusika waliobeba dhamira
mbalimbali, hivyo kufanya kazi imvutie msomaji na kuchangamsha
hadhira. Kuna mfano wa shairi (uk 62).
Ari yetu ndio mwokozi wetu
Ari yetu lazima tuisujudie, Ari hii ya mwaka tuliyoivumbika, Iliyojaa joto lisiloburudika
Ije ituongoze mpaka mwisho kufika,
Na kutuzimia kiza cha mwaka
JINA LA KITABU
Jina la kitabu linasadifu yaliyomo. KILIO CHA HAKI, kitaswira
linaangalia matatizo na manung’uniko yaliyokuwa yakiwakumba
wafanyakazi katika shamba la bwana Delamon.
Matatizo hayo ni kama vile, ujira mdogo, kufanya kazi kwa muda
mrefu, mazingira mabovu ya kazi pamoja na vifaa hafifu vya
utendaji kazi, pia ukosefu wa demokrasia.
Matatizo na manung’uniko hayo ni vilio vya haki ambayo
viliwapelekea wawe na vilio kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo au
waweze kujikomboa kutoka kwenye mikono ya makaburu.