Top Banner
Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu? Ripoti ya Utafiti wa Hali na Upatikanaji wa Elimu kwa watoto wenye Ulemavu Tanzania. Desemba 2008
40

Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

Oct 04, 2019

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?Ripoti ya Utafiti wa Hali na Upatikanaji wa Elimu kwa

watoto wenye Ulemavu Tanzania.

Desemba 2008

Page 2: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

��

ShukraniUchunguzi huu wa Kitafiti uliandaliwa na wafanyakazi wa HakiElimu wakishirikiana na Kitila Mkumbo, Mhadhiri Idara ya Saikolojia ya Elimu Chuo kikuu cha Dar es Salaam. Dkt Kitila Mkumbo aliwapa wafanyakazi mafunzo ya taratibu za ukusanyaji wa data/taarifa na kusimamia zoezi zima la utafiti.Wafanyakazi wafuatao wa HakiElimu walishiriki kwenye zoezi kama watafiti na hivyo kusafiri wilayani na kukusanya data: Gervas Zombwe, Richard Lucas, Rajab Kondo, Annastazia Mdimi and Moses Gasana.

Ripoti hii iliandaliwa na Kitila Mkumbo. Uhariri, mrejesho, na ushauri ulitolewa na Elizabeth Missokia, Samuel Saiguran, Robert Mihayo, Gervas Zombwe, and Annastazia Rugaba.

Shukrani nyingi kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kuruhusu zoezi hili kufanyika katika shule mbalimbali wilayani.

Tunawashukuru pia watoto, wazazi, kamati za shule walimu, na maafisa Wilayani tuliohojiana nao na kupata taarifa mbalimbali zilizosaidia kukamilisha zoezi hili. Bila ushiriki wao wa dhati zoezi hili lisingekamilika. Tunawashukuru sana kwa michango na utayari wao kufanya kazi nasi.

© HakiElimu, 2008 ISBN 9987-423-76-0

HakiElimu, PO Box 79401, Dar es Salaam, Tanzania

Simu: (255 22) 2151852/3, Faksi: (255 22) 2152449

Sehemu yeyote katika kitabu hiki inaweza kutolewa kwa namna nyingine yeyote kwa madhumuni ya kielimu na yasiyo ya kibiashara, kwa kuzingatia kuwa chanzo kitatajwa na nakala mbili zitapelekwa HakiElimu.

Page 3: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

���

YaliyomoMuhtasari ivFinyazo viMajedwali na chati viiSehemu 1: Utangulizi wa utafiti, Malengo na mbinu 1 1.1 Utangulizi 2 1.3 Malengo ya utafiti 3 1.4 Muundo na mbinu za utafiti 3 1.4.2 Washiriki na eneo la utafiti 4Sehemu 2: Matokeo ya utafiti 6 2.1 Upatikanaji wa Elimu kwa watoto wenye ulemavu 7 2.1.2 Uandikishaji wa watoto wenye ulemavu shule za Tanzania 7 2.1.3 Uwiano wa uandikishaji kati ya watoto wenye ulemavu na watoto wasio na ulemavu: Kisa mkasa cha wilaya tatu 8 2.2 Matokeo juu ya uzoefu, maoni na mitazamo ya juu watoto wenye ulemavu 11 2.2.3 Maoni ya walimu juu ya uelimishaji wa watoto wenye ulemavu na elimu jumuishi:Matokeo ya majadiliano katika vikundi mjadala 13 2.2.4 Uzoefu na maoni ya watoto wenye ulemavu kuhusu ufundishaji na mazingira ya kujifunzia shuleni kwao 13 2.3 Support for inclusive education among teachers 17 2.3.1 Utangulizi 17 2.3.2 Mitazamo ya walimu kuhusu elimu jumuishi 18 2.4 Mitazamo ya watoto wasio na ulemavu kuhusu watoto wenzao wenye ulemavu 20 2.4.1 Utangulizi 20 2.4.2 Maoni na mtazamo wa watoto wasio na ulemavu juu ya kujifunza pamoja na wenzao wenye ulemavu 20Sehemu 3: Mjadala, Hitimisho na Mapendekezo 23 3.1 Majadiliano 24 3.3 Mapendekezo 25 3.3.1 Kwa uamuzi wa ki-sera 26Marejeo: 27Viambatisho 28 Kiambatisho 1 28 Kiambatisho 2 30 Kiambatisho 3 31

Page 4: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

iv

MuhtasariKwa kutumia mbinu za kinadharia na vitendo, utafiti huu umechambua changamoto na fursa za kielimu zilizopo kwa watoto wenye ulemavu.Utafiti huu umetathmini kwa kina vikwazo vya kielimu ambavyo watoto wenye ulemavu katika shule za Tanzania wanakumbana navyo. Kuna vikwazo vitano ambavyo vimeainishwa navyo ni:

Moja, Mpango mbovu katika ujenzi wa majengo ya shule, ambayo hayawapi fursa watoto wenye ulemavu kuweza kuyatumia, hasa wale wenye ulemavu wa macho na viungo.

Pili, Uelewa mdogo na kutothamini mambo yanayowahusu watu wenye ulemavu miongoni mwa walimu, viongozi wa shule na jamii kwa ujumla. Mambo yote haya yana madhara pindi linapokuja suala la kutambua na kuthamini mahitaji ya kielimu kwa watoto wenye ulemavu.

Tatu, Wazazi walio wengi hawako tayari kuwaandikisha watoto wenye ulemavu katika shule. Hii ni kutokana na mila na desturi ambazo zina wabagua watoto wenye ulemavu. Matokeo yake kiwango cha uandikishaji katika shule kwa watoto wenye ulemavu kimebakia kuwa cha chini.

Nne, Kutokana na ukosefu wa mafunzo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu na elimu jumuishi,walimu wengi hawako tayari kufundisha darasa lenye watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu. Hali hii imechangiwa na kutotekelezwa kwa vitendo sera ya serikali inayohusu elimu jumuishi, ambayo ingetoa fursa zaidi za kielimu kwa watoto wenye ulemavu.

Tano, Shule nyingi hazina sifa za kufundisha watoto wenye ulemavu kutokana na ukosefu wa vifaa muhimu na matini yanayofaa kufanikisha tendo la ujifunzaji kwa watoto wenye ulemavu.

Pengine kikwazo zaidi cha kielimu kwa watoto wenye ulemavu ambacho kinaweza kujumuisha vikwazo vyote ni kwamba hakuna juhudi za makusudi zilizochukuliwa kuondoa vikwazo hivi. Kwa hiyo, kuna haja kwa wadau wote wa elimu pamoja na wapenda elimu na maendeleo hapa nchini kuzindua kampeni zitakazolenga kuwainua katika elimu watu waliotengwa, hasa watoto wenye ulemavu. Kushindwa kutoa fursa za kielimu kwa watoto wenye ulemavu ni kudidimiza, “malengo”, mafanikio na “matarajio” ya MMEM ambao unasisitiza “elimu kwa wote”.

Kwa kuzingatia kuwa Tanzania ni mwanachama wa jumuiya nyingi za kimataifa ambazo zinatambua na kuhimiza falsafa ya elimu kwa wote, likiwemo Tamko la Salamanka na namna ya kulitekeleza (UNESCO, 1994), kuna haja ya kuondoa vikwazo vinavyozuia upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye ulemavu. Ripoti imependekeza hatua nyingi za kisera ili kuondoa vikwazo vya elimu kwa watoto wenye ulemavu, ambazo zinajumuisha:

Kuanzisha mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu yenye lengo la kupatia walimu mafunzo, mbinu na maarifa ya namna ya kufundisha watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na elimu jumuishi.

Kuwepo na haja ya kurekebisha majengo ya shule ili kuyafanya yaweze kufikiwa na watoto wenye ulemavu. Pia, kuna haja ya kupitisha sheria ambayo itaamuru kurekebishwa kwa majengo ya shule ili kuyawezesha kutumiwa na watoto wote, hasa wale wenye ulemavu.

Ni muhimu kuwepo na uhamasishaji nchi nzima kuhusu hatima ya watoto wenye ulemavu pamoja na umuhimu wa elimu kwa watoto wenye ulemavu. Uhamasishaji huu inabidi uwe chachu katika kuongeza

Page 5: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

v

mahitaji ya elimu kwa watoto wenye ulemavu. Ni muhimu ieleweke wazi kuwa malengo ya MMEM yenye kuhakikisha kuwa watoto wote wamepewa fursa katika elimu hayataweza kufikiwa kama watoto wote wenye ulemavu hawataandikishwa katika shule na kupewa elimu bora sawa na watoto wengine.

Ripoti hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza inajumuisha utangulizi, malengo na mbinu za utafiti. Sehemu ya pili inaelezea matokeo ya utafiti na kutoa hitimisho pamoja na mapendekezo kutokana na utafiti uliofanyika. Tunawasihi kuungana nasi kutetea elimu ya watoto wenye ulemavu!

Page 6: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

vi

Finyazo BBEST Takwimu za Elimu ya Msingi Tanzania

CWDs watoto wenye Ulemavu

DEO Afisa Elimu wa Wilaya

MOEVT Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

PCA Uchambuzi Mkuu wa Takwimu

PEDP Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi

REO Afisa Elimu wa Mkoa

UNESCO Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni

URT Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Page 7: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

vii

Majedwali na ChatiTables

Jedwali ukurasa

1Uandikishaji wa watoto wenye ulemavu katika shule za msingi Tanzania: Takwimu za kitaifa 2008

10

2 Uwiano wa watoto wenye ulemavu wenye umri wa kwenda shule na wale walioko shule katika wilaya D1 kufikia 2008

11

3Uwiano wa watoto wenye walemavu wenye umri wa kwenda shule na wale waliopo Shuleni katika wilaya ya D2 kufikia 2008

12

4Uzoefu na pamoja na sifa za walimu waliojibu maswali yaliyohusu mtazamo wao kuhusu watoto wenye ulemavu

25

Figures

chati ukurasa

1 % ya watoto wenye ulemavu wenye umri wa kwenda shule walioandikishwa katika shule za msingi kuendana na aina ya ulemavu: Takwimu za kitaifa 2008

10

2 % ya watoto wenye ulemavu wenye umri wa kwenda shule walioandikishwa katika shule za msingi wilaya D1 na D2.

13

3 Uwiano wa sasa katika uandikishaji miongoni mwa watoto wenye ulemavu katika wilaya D1 na D2

13

4 % ya walimu waliopewa mafunzo kuhusu watoto wenye mahitaji maalumu na elimu jumuishi katika shule zilizotembelewa katika wilaya husika

16

5 % ya walimu waliokubaliana na wale walioikataa hoja kwamba elimu jumuishi inaweza kuwasaidia watoto wenye ulemavu kujifunza kikamilifu

26

6 % ya walimu waliokubaliana na wale walioikataa hoja kwamba:elimu jumuishi ni muhimu na ni bora kuiunga mkono

28

7 % ya watoto waliokubaliana ama kuikataa hoja kwamba inawezekana kushirikiana kitaaluma, kujenga urafiki na kuishi pamoja na watoto wenye ulemavu kama walivyo watoto wengine wasio na ulemavu

32

8 % ya watoto waliokubaliana waziwazi ama kuikataa katakata hoja kwamba inawezeka-na kushirikiana kitaaluma, kujenga urafiki na kuishi pamoja na watoto wenye ulemavu kama walivyo watoto wengine wasio na ulemavu

32

Page 8: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

1

SeHeMU 1

UtangUlizi, Malengo na MbinU za UtaFiti

Page 9: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

2

1.1 UTangUliziMiongoni mwa malengo muhimu ya elimu Tanzania ni kuendeleza na kukuza mahitaji vya mtu kwa ajili ya maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla, ambapo mtu ni sehemu ya jamii. Ili kutimiza malengo ya elimu nchini, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imeanzimia kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapatiwa fursa ya elimu ( Jamhuri ya muungano wa Tanzania [URT], 2001a). Wizara imeazimia kuhakikisha kuwa watoto wote wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo wenye ulemavu wanapewa fursa ya elimu (ibid). Ili kutimiza malengo ya elimu, Tanzania imejiwekea malengo, miongoni mwayo ni kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapewa fursa ya elimu ifikapo mwaka 2010 kwa 100%(ibid., p.7). Ili kufikia malengo na matarajio ya elimu kwa wote,watoto wenye ulemavu wanapaswa kuandikishwa na kumaliza elimu ya msingi na kuendelea.

Kuna njia tatu ambazo zinaweza kutumiwa ili kuendeleza pamoja na kutoa fursa zaidi za elimu mahususi kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo wenye ulemavu, njia hizo ni: Shule maalumu, shule zenye watoto mchanganyiko na elimu jumuishi. Shule maalumu mara nyingi hutoa huduma kwa ajili ya watoto wenye ulemavu tofauti na shule za kawaida. Shule mchanganyiko hutoa mafunzo kwa watoto wenye ulemavu sambamba na wale wasio na ulemavu, hata hivyo, muda wa ziada hutengwa kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu. Elimu jumuishi huwawezesha watoto wote kusoma katika shule moja na katika mazingira ya aina moja(kama vile darasa moja) bila ya kuwabagua watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na wenye ulemavu.

Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ikitilia mkazo elimu ya watu wenye walemavu kupitia elimu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu. Bila shaka, elimu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu imekuwa ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali, elimu ya msingi, elimu ya watu wazima, elimu ya sekondari, na elimu ya ualimu (URT, 2001b). Elimu kwa wale wenye mahitaji maalumu ni ile inayotolewa kwa watoto wenye ulemavu. Kimsingi aina saba za ulemavu zimeweza kutambuliwa nazo ni ulemavu wa macho, ulemavu wa kusikia, ulemavu wa ngozi ulemavu wa akili, ulemavu wa viungo, ububu na ukiziwi (URT, 2001b, uk. 11).

Elimu jumuishi katika siku za karibuni ndiyo imepewa kipaumbele zaidi kuliko aina nyingine, na inachukuliwa kama njia bora zaidi katika kufanikisha malengo ya elimu kwa wote. Kimsingi, Tanzania imeridhia matamko mbalimbali ya kimataifa ambayo yamelenga kuinua elimu jumuishi mashuleni, miongoni mwa matamko hayo ni tamko la Haki za watoto, 1386/1959, tamko la Haki za Watu wasiojiweza, 3447/1975 na Tamko la Salamanka na Hatua za utekelezaji wake (UNESCO, 1947). Tamko la Salamanka na Hatua za utekelezaji wake (UNESCO, 1947), kwa mfano, limeridhia haki za elimu kwa kila mtu kama lilivyoelezwa katika tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, 1948, na kuboreshwa katika mkutano wa Dunia wa Elimu wa mwaka 1990 ambao ulitilia mkazo elimu kwa wote kwa msingi wa haki za binadamu bila kujali tofauti baina ya watu (uk. Vii).

Misingi ya Tamko la Salamanka na namna ya kuitekeleza ni kuhakikisha kuwa shule zote zijenge mazingira mazuri ya kusomea kwa watoto wote bila kujali tofauti ya viungo, uwezo wa akili, jamii atokayo mtoto, lugha pamoja na mambo mengine; yakiwemo watoto wasiojiweza pamoja na wale wenye uwezo wa juu kiakili bila kuwasahau wale wanaotoka katika maeneo yaliyotengwa kielimu na yale makundi ya watu waliosahauliwa (uk.6).

Page 10: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

3

Pia Tanzania imeridhia Azimio la Elimu kwa Wote (EFA). Elimu kwa wote huendana na kutoa fursa katika elimu ya msingi kwa watoto wote, ni elimu endelevu, huzingatia ubora wa elimu pamoja na kuwahusisha watoto wote, wakiwemo wenye ulemavu (UNESCO, 2000). Hii ina maana kwamba bila kuendeleza sera za elimu jumuishi katika elimu na kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapatiwa fursa ya elimu bila kujali tofauti baina ya watoto, malengo ya Elimu kwa wote yanaweza yasifikiwe.

1.2 ElimU jUmUishi ni nini?Dhana ya elimu jumuishi imekuwa ikibadilika kulingana na wakati. Mwanzoni elimu jumuishi ilimaanisha kitendo cha kuwajumuisha watoto wenye mahitaji maalumu katika madarasa yenye watoto wasio na ulemavu. Wanazuoni wa siku hizi wamekuwa wakitumia elimu jumuishi kumaanisha dhana pana zaidi, ambayo mbali na kuwahusisha watoto wenye mahitaji maalumu(wenye ulemavu), dhana hii sasa inatumika kumaanisha pia watoto wanaoishi katika mazingira magumu (Beyers & Hay, 2007). Kwa hiyo waandishi wengi wamekuwa wakitumia dhana ya elimu jumuishi kumaanisha watoto wenye aina mbalimbali za uwezo na wale wenye ulemavu (Salend, 2001; 1996; Roach, 1995). Kwa hali hiyo elimu jumuishi ni aina ya elimu inayowaweka pamoja watoto wenye mahitaji maalumu, wale wenye uwezo wa juu kiakili na wale wenye ulemavu (Lloyd, 2008). Dhana ya elimu jumuishi imejengeka katika falsafa kwamba watoto wote, bila kujali aina ya ulemavu pamoja na uwezo wao kiakili, wanapaswa kuelimishwa katika madarasa ya kawaida ambapo watasoma pamoja na watoto wenzao wenye umri unaofanana (Crawford, 1994).

Japokuwa serikali ya Tanzania imeridhia falsafa ya elimu kwa wote, bado haieleweki ni kwa namna gani mahitaji ya watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na wale wenye matatizo mbalimbali yatashughulikiwa. Kwa hiyo, kuna haja ya kushughulikia kwa makini kuhusu fursa na umuhimu wa elimu jumuishi nchini Tanzania. Kuna haja hasa ya kutathmini fursa ya watoto wenye ulemavu katika elimu hapa Tanzania. Ni katika mantiki na msingi huu utafiti huu umefanyika.

1.3 malEngo ya UTaFiTiUtafiti huu unalenga kubainisha fursa pamoja na changamoto mbalimbali za kielimu ambazo watoto wenye ulemavu wanakabiliana nazo katika shule za Tanzania. Kimsingi utafiti huu umejikita katika malengo,manne, ambayo ni:

i) Assess Kutathmini kiwango cha fursa katika elimu ambayo watoto wenye ulemavu wanapata.

ii) Kutambua mambo yanayokwamisha fursa katika elimu pamoja na yale yanayotoa fursa katika elimu kwa watoto wenye ulemavu.

iii) Kutathmini maandalizi ya shule, utayari pamoja na mazingira ya kufundishia kwa ujumla, pamoja na kuendeleza elimu jumuishi na kutathmini na kutambua mahitaji ya shule katika kufundisha watoto wenye ulemavu

1.4 mUUndo na mbinU za UTaFiTi1.4.1 muundo/mbinu

Kutokana na malengo ya utafiti huu kuwa mapana na yenye sura tofautitofauti, imelazimu kutumia mbinu za maelezo/viwango na takwimu. Njia ya takwimu kwa upande mmoja ilitumika ili kupata maoni na mtizamo

Page 11: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

4

wa wadau wa elimu ( walimu, watoto na watunga sera) kuhusu uendeshaji wa elimu jumuishi kwa ujumla, pamoja na changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu katika shule za Tanzania kuhusiana hasa na fursa ya elimu.

Kwa upande mwingine njia ya maelezo ilitumika katika kubainisha uzoefu na changamoto zilizopo katika ufundishaji na ujifunzaji wa watoto wenye ulemavu. Kwa hiyo, kama alivyopata kuandika Richardson (2003), Thomas (2005) na Byman (2006), njia ya maelezo/viwango ilitumika kufafanua takwimu.

1.4.2 WashirikinamaeneoyautafitiUtafiti ulifanyika katika kanda sita, ukihusisha wilaya saba. Ili kutunza siri, Wilaya zilijulikana kama: D1, D2, D3, D4, D5, D6 na D7. Wilaya zilichaguliwa kwa kuzingatia watoto wenye ulemavu, yaani wilaya zenye watoto wengi zaidi wenye ulemavu na zile zenye watoto wachache zaidi. Katika kila wilaya, shule mbili zilichaguliwa, shule moja ya msingi na shule moja ya sekondari. Wadau wa elimu waliochaguliwa walikuwemo walimu, watoto wa shule, wakuu wa shule na Maofisa Elimu wa Wilaya.

1.4.3 ZanazautafitiZana kuu saba za utafiti zilitumika. Zana hizi zinaelezwa kwa ufupi hapa chini:

i) Dodoso kuhusu mtazamo wa walimu: Walimu walijaza dodoso yenye sehemu mbili. Katika sehemu ya kwanza walimu walitakiwa kutoa taarifa za jumla kama vile umri, jinsia, uzoefu na sifa katika elimu pamoja na mafunzo kuhusu elimu jumuishi. Katika sehemu ya pili, walimu walipatiwa orodha ya maelezo 20, yaliyolenga kutathmini mambo mbalimbali yakiwemo mtazamo wa walimu juu ya elimu jumuishi, pamoja na kuonesha kiwango cha kukubali au kukataa mambo mbalimbali yaliyozungumziwa katika dodoso hiyo. Kwa hiyo walimu walipaswa kuonesha ama hawakubaliani hata kidogo (1) au wanakubaliana katika kiwango cha juu (5).

ii) Dodoso kuhusu mtazamo wa watoto: Kama ilivyokuwa kwa walimu, watoto pia walilazimika kujaza dodoso yenye sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza iliuliza maswali ya jumla na sehemu ya pili ilikuwa na maswali yaliyolenga kutathmini mtazamo wao juu ya kusoma pamoja na watoto wenzao wenye ulemavu. Ili kutathmini mtazamo wao kuhusu kusoma na watoto wenzao wenye ulemavu, watoto wasio na ulemavu walipewa orodha yenye maswali 28, ambayo yalikuwa yakipima mambo mbalimbali kuhusu mtazamo wao juu ya watu wasiojiweza/wenye ulemavu na pia walitakiwa kuonesha ni kwa kiwango gani wanakubaliana au hawakubaliani, ambapo walipaswa kusema ama hawakubaliani hata kidogo (1) ama wanakubaliana kwa kiwango cha juu (5).

iii) Makundi mjadala na walimu: Haya yalitumiwa ili kupata taarifa zaidi pamoja na kuweka sawa mambo ambayo hayakujibiwa kikamilifu katika dodoso ya awali.

iv) Mahojiano/usaili na watoto wenye ulemavu:Haya yalitumiwa kufanya tathmini kuhusu maoni na uzoefu wa watoto wenye ulemavu kuhusu mchakato wa kujifunza. Maswali haya yalijumuisha mambo mengi, ikiwamo hisia zao kuhusu namna watoto wenzao wasio na ulemavu walivyowachukulia, changamoto wanazokumbana nazo katika masomo yao wakiwa pamoja na watoto wasio na ulemavu pamoja na mazingira ya shule kwa ujumla.

Page 12: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

5

v) Mahojiano/usaili kwa Wakuu wa shule na maafisa Elimu wa Wilaya: Hawa walifanikisha upatikanaji wa taarifa pamoja na takwimu kuhusu watoto wenye ulemavu katika shule na wilaya zao ambazo tulizitembelea. Pia walifanikisha upatikanaji wa takwimu kuhusu vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa ajili ya watoto wenye ulemavu pamoja na maoni yao kuhusu elimu jumuishi.

vi) Ushiriki wa moja kwa moja(kuangalia mazingira): Njia hii ilitumika kuona ni kwa jinsi gani mazingira ya shule yalitoa fursa ya kufundisha na kujifunza kulingana na mahitaji ya watoto wenye ulemavu.

vii) Takwimu za Wilaya zinazoonesha uandikishaji kwa watoto wenye ulemavu. Njia hii ilitumika kukusanya takwimu za uandikishaji wa watoto wenye ulemavu kwa miaka mitatu ya nyuma kiwilaya. Ni fomu maalumu waliopewa kila ofisi ya Afisa elimu wa wilaya kujaza taarifa hizo. Mbinu hii ilisaidia sana kupata taarifa nyingi zilizotakiwa.

Page 13: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

6

SeHeMU 2

Matokeo Ya UtaFiti

Page 14: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

7

2.1. UpaTiKanaji Wa ElimU KWa WaToTo WEnyE UlEmavU2.1.2 Uandikishaji wa watoto wenye ulemavu katika shule za Tanzania.

Tangu mwaka 2001, Tanzania imekuwa ikitekeleza mpango maalumu wa Elimu ya Msingi (MMEM) wenye malengo ya kutoa elimu bora na endelevu kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule. Mafanikio ya MMEM yako wazi, hasa kutokana na ukweli kuwa, kupitia mpango huu idadi ya uandikishaji katika shule za msingi imeongezeka. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (MOEVT), wastani wa jumla wa uandikishaji umepanda kutoka 78% mwaka 2000 hadi 114% mwaka 2007. Pia uwiano halisi wa uandikishaji umepanda kutoka 59% mwaka 2000 hadi kufikia 97.3% mwaka 2007: idadi ya watoto wa shule za msingi wanaoandikishwa imeongezeka kutoka 7, 083,063 mwaka 2004 hadi kufikia 8,316,925 mwaka 2007 (URT, 2007).

Hakuna takwimu zinazoonyesha uwiano wa uandikishaji kwa watoto wenye ulemavu ama wale wenye mahitaji maalumu hapa nchini. Katika utafiti huu, juhudi zimefanyika ili kupata takwimu sahihi kupitia maswali ya dodoso pamoja na taarifa mbalimbali zilizopatikana kupitia kwa Maafisa Elimu wa Wilaya na shule husika. Pia takwimu za kitaifa zimetumika katika utafiti huu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (MOEVT), hadi kufikia mwaka 2007, kulikuwa na watoto 24,003 wenye ulemavu walioandikishwa katika shule za msingi Tanzania ambao ni sawa na asililimia chini ya moja (URT, 2007).

Hakika, takwimu za serikali zinaonyesha kwamba ni asilimia moja tu (1%) ya watoto wenye ulemavu ndiyo wamepata fursa ya elimu hapa nchini (URT, 2001b).

Jedwali 1 na chati 1 zinaonesha uwiano katika uandikishaji wa watoto wenye ulemavu hadi kufikia Juni 2008. Takwimu zinaonesha kwamba hadi kufikia Juni 2008, kulikuwa na watoto wenye ulemavu wanaokaribia 34,661, wavulana 19,998 na 14,663 ni wasichana walioandikishwa katika shule za msingi hapa nchini. Chati 1 inaonesha kuwa wengi wa watoto walioandikishwa katika shule za msingi (40%) walikuwa ni wale wenye ulemavu wa viungo, (21%) ni wale wenye ulemavu wa akili na (17%) walikuwa wenye ulemavu wa kusikia.

Vilevile takwimu zinaonesha kwamba kati ya watoto walioandikishwa wavulana walikuwa asilimia hamsini (57%) na wasichana walikuwa asilimia arobaini na mbili nukta tatu (42.3%) (chati 1). Hii ni kinyume kabisa na mwelekeo wa uandikishaji katika shule za msingi ambao unaonesha kuwa idadi ya wasichana na wavulana ni karibu sawa. Kwa mfano, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na MOEVT, uandikishaji wa wasichana katika shule za msingi mwaka 2008 ulikuwa 49.6% (URT, 2008). Hali hii inaibua maswali mengi kuhusu tofauti kubwa ya wastani wa uandikishaji kati ya wasichana na wavulana wenye ulemavu hapa nchini. Inawezekana tofauti hii imechangiwa na jamii yenyewe ambayo ina mtazamo wa kuwapendelea zaidi watoto wa kiume wenye ulemavu badala ya watoto wa kike. Hata hivyo takwimu hizi hazitoi picha halisi kuhusu uwiano halisi uliopo kati ya watoto wa kike wenye ulemavu na wale wa kiume walioandikishwa katika shule na wale watoto wenye ulemavu wenye umri wa kwenda shule lakini hawakupata fursa hiyo.

Page 15: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

8

jedwali 1: Uandikishaji wa watoto wenye ulemavu shule za msingi:Takwimu za kitaifa 2008

aina ya ulemavu

Wavulana Wasichana jumla %Wasichana %Wavulana

Albino 1713 1394 3107 44.9 55.1

kusikia 3180 2532 5712 44.3 55.7

viungo 8068 5783 13851 41.8 58.2

akili 4296 2945 7241 40.7 59.3

ububu 296 231 527 43.8 56.2

Aina nyingi 435 280 715 39.2 60.8

mwingineo 2010 1498 3508 42.7 57.3

Jumla Kuu 19998 14663 34661 42.3 57.7

Chanzo:URT,2008,uk.36-37(Takwimukatikaasilimiazimewekwanamwandishi)

Ulemavu wa kuona/Albino, 9%

Kusikia, 17%

viungo, 40%

Akili, 21%

Ububu, 2%

mchanganyiko, 2%

Mwingine, 10%

Chati1:Asilimiayawatotowenyeulemavuwalioandikishwakatikashulezamsingikulingananaainayaulemavuwalionao:takwimuzakitaifa2008

Kutokana na kukosekana na takwimu sahihi kuhusu uandikishaji wa watoto wenye ulemavu wenye umri wa kwenda shule, watafiti waliamua kutafuta taarifa kutoka kwa Maafisa Elimu wa wilaya pamoja na wakuu wa shule katika wilaya husika. Ni wilaya mbili tu, D1 na D2 ndizo angalau zilikuwa na takwimu sahihi kuhusu watoto wenye ulemavu katika wilaya zao. Hata hivyo, taarifa hizo zilikuwa hazioneshi idadi halisi ya watoto wenye ulemavu wenye umri wa kwenda shule walioko shuleni na walioko nyumbani. Taarifa hizi zimefafanuliwa zaidi sehemu zinazofuata.

2.1.3 Uwiano uliopo wa watoto wenye ulemavu waliopo shuleni ukilinganisha na watoto wasio na ulemavu:Utafitikutokakwenyewilayatatu.

Kati ya wilaya saba zilizotembelewa, ni wilaya mbili tu D1 na D2, ndizo zilikuwa na takwimu zinazoonesha idadi kamili ya watoto wenye ulemavu waliopo shuleni, hii ilisaidia kukokotoa uwiano wa watoto walemavu

Page 16: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

9

katika wilaya hizo. Taarifa za watoto wenye ulemavu waliopo shuleni zilipatikana kutoka kwenye ofisi za Elimu za wilaya. Idadi ya jumla ya watoto wenye ulemavu waliopo katika wilaya mbili ilipatikana kutoka kwenye Takwimu za Elimu za Taifa (BEST) zilizokusanywa kati ya mwaka 2007 na 2008. Takwimu hizi zimewasilishwa katika jedwali namba 2 na 3 na katika chati namba 3, 4 na 5.

Kama ilivyoonyeshwa katika jedwali namba 2, katika wilaya D1 kulikuwa na jumla ya watoto 923 wenye ulemavu walioandikishwa katika shule mbalimbali, kati yao wavulana walikuwa 537 na wasichana walikuwa 386. Kati ya watoto hawa, 615 (66.6%) walikuwa na ulemavu ufuatao: ulemavu wa kuona/albino (4.8%), ulemavu wa kusikia (14.6%), ulemavu wa viungo (28.8%), na ulemavu wa akili (17.4%). Kwa ujumla, watoto wenye ulemavu mkubwa wa macho kati yao wasichana walikuwa (63.6%) na wavulana walikuwa (36.4%), hata hivyo kulikuwa na wavulana wengi wenye ulemavu ambao walikuwa wameandikishwa shule ambapo idadi yao ilikuwa (58%) ukilinganisha na wasichana ambao walikuwa asilimia 42 (42%).

jedwali 2: Uwiano wa watoto wenye ulemavu wenye umri wa kwenda shule walioandikishwa shuleni katikawilayaD1hadikufikia2008.

Aina ya ulemavu

Watoto wenye ule-mavu katika wilaya

Watoto wenye ulemavu mashuleni

%wale-mavu

mashu-leni (wa-sichana)

%wale-mavu

mashu-leni (wa-vulana)

%wale-mavu

mashuleni (ki- ujumla)

wa-vu-lana

wasi-chana

Jum-la

wa-vu-lana

wasi-chana Jumla

kuona/ Albino 46 45 91 16 28 44 63.6 36.4 4.8

Kusikia 89 85 174 68 67 135 49.6 50.4 14.6

Viungo 306 177 483 181 94 275 34.2 65.8 29.8

Akili 96 79 175 92 69 161 42.9 57.1 17.4

Jumla 537 386 923 357 258 615 42.0 58.0 66.6

Chanzo: Taarifa kutoka kwenye eneo la utafiti kama zilivyokokotolewa na mwandishi

Tanbihi:CWD=watotowenyeulemavu

Katika wilaya D2, katika chati 3 kulikuwa na watoto 427 wenye ulemavu walioandikishwa katika shule, kati yao wenye ulemavu wa macho walikuwa 31 ambayo ni sawa na (7.3%), watoto 76 ni wenye ulemavu wa kusikia ambayo ni asilimia (17.8%), watoto 236 walikuwa na ulemavu wa viungo ambayo ni sawa na asilimia (55.3%) na 84 ambayo ni sawa na asilimia (19.7%) walikuwa na ulemavu wa akili. Kwa ujumla katika wilaya D1 wavulana wenye ulemavu walikuwa asilimia 60 na wasichana walikuwa asilimia 40 katika wilaya ya pili.

Page 17: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

10

jedwali 3: Uwiano wa watoto wenye ulemavu katika wilaya d1 dhidi ya wale walioandikishwa mwaka 2008

Aina ya Ulemavu

CWD wilayani CWD mashuleni

%CWD mashuleni (wasicha-

na)

%CWD mashuleni (wavulana)

%CWD (kiujum-

la)

Wav Was Jumla Wav Was Jumla

kuona/ Al-bino

50 37 87 19 12 31 38.7 61.3 1.8

Kusikia 259 205 464 44 32 76 42.1 57.9 4.4

Viungo 408 240 648 145 91 236 38.6 61.4 13.5

Akili 314 231 545 48 36 84 42.9 57.1 4.8

Jumla 1031 713 1744 256 171 427 40.0 60.0 24.5

Chanzo: Taarifa kutoka kwenye eneo la utafiti kama zilivyokokotolewa na mwandishi

Tanbihi:CWD=watotowenyeulemavu

Kwa ujumla, asilimia 66 ya watoto wenye ulemavu katika wilaya D1 walikuwa wamefikia umri wa kwenda shule, hata hivyo ni asilimia 24.5 tu ndiyo walikuwa wameandikishwa shule (Tazama chati namba tatu). Japokuwa serikati imeongeza uandikishaji wa watoto waliofikia umri wa kwenda shule, kupitia mpango maalumu wa MMEM, bado watoto wenye ulemavu hawajapewa kipaumbele. Kwa mfano, wakati uandikishaji wa watoto wenye umri wa kwenda shule katika wilaya D1 ni asilimia 66.6 na asilimia 24.5 katika wilaya D2; uwiano wa watoto wenye umri wa kwenda shule katika walioandikishwa katika mikoa ya Kagera na Mwanza ambapo wilaya mbili zilizofanyiwa utafiti zipo ni asilimia 99 (Tazama chati namba 4).

Ingawa uwiano wa watoto wenye ulemavu katika wilaya hizi mbili uko chini ukilinganisha na uwiano wa uandikishaji wa watoto wote kwa ujumla, bado uwiano huu ni mkubwa ukilinganishwa na ule uliotolewa na BEST ambacho ni kitabu cha Takwimu za Elimu Tanzania ambacho kinaonesha kuwa wastani wa watoto wenye ulemavu walioandikishwa katika shule mbalimbali Tanzania ni chini ya asilimia moja. Hali hii inaibua maswali kuhusu usahihi wa takwimu kati ya zile zilizotolewa katika ngazi za wilaya.

! !

!

!

!

Kuona

1020

3040

50607080

90100

0

2% 5% 4%

15% 14%

29%

5%

25%

67%

17%

!Albino

Kusikia viungo Akili Ki-ujumla

Aina ya ulemavu

D2

D1

Chati2:AsilimiayawatotowenyeulemavuwenyeumriwakwendashulewalioandikishwakatikaWilayaD1naD2

Page 18: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

11

Chati3:uwianowauandikishajiwasasawawatotowenyeulemavunawalewakawaidakatikawilayaD1naD2

Tanbihi:CWD=watotowenyeulemavu.

2.2 maToKEo ya UTaFiTi KUhUsU UzoEFU, maoni na mTazamo Wa

WalimU KUhUsU ElimU KWa WaToTo WEnyE WalEmavU: 2.2.1 je, shule zinakumbana na vikwazo au matatizo gani katika kufundisha watoto wenye ulemavu?

Uchambuzi wa taarifa kutoka kwenye maswali ya dodoso uligundua matatizo makuu manne ambayo shule zinakumbana nayo katika kufundisha watoto wenye ulemavu. Matatizo hayo ni miundombinu duni, ukosefu wa mafunzo kuhusu elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu miongoni mwa walimu na ukosefu wa vifaa vya kufundishia watoto wenye ulemavu. Matatizo haya yameelezewa kwa ufupi hapa chini:-

2.2.1 (a) Miundombinu duni. Miundombinu ni miongoni mwa matatizo yanayokwamisha ufundishaji na ujifunzaji kwa watoto wenye ulemavu. Matatizo haya yalibainishwa na wakuu wengi wa shule ambazo zilitembelewa wakati wa utafiti. Wakuu wengi walibainisha kuwa majengo mengi ya shule na hata yale yaliyojengwa chini ya MMEM hayakuzingatia mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Matokeo yake, watoto walio wengi hasa wale wenye ulemavu wa macho na viungo hupata shida sana kutembea kutoka eneo moja kwenda jingine wanapokuwa shuleni.

Kwa ujumla utafiti huu unakubaliana na kile ambacho wakuu wa shule walikiona katika maeneo yao. Kwa ujumla mazingira ya shule yaliyotembelewa katika utafiti huu hayazingatii mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Majengo mengi ya shule yana ngazi ndefu ambazo watoto wenye ulemavu hasa wale wanaotumia baiskeli maalumu za kutembelea hawawezi kuyafikia. Miundombinu duni katika shule nyingi pengine inasababishwa na ukosefu wa fedha au fungu maalumu la kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu hasa wale wenye ulemavu. Lakini pia miundombinu duni inasababishwa na uelewa mdogo wa jamii kuhusu mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Baadhi ya wakuu wa shule walisema kwamba ukosefu wa fungu au mfuko maalumu wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu mashuleni hasa katika shule za bweni imesababisha ugumu wa kuwatunza watoto hao kutokana na kwamba gharama za kuwatunza ziko juu sana. Kutokana na tatizo hili, watoto wenye ulemavu kwa mujibu wa wakuu wa shule wanakabiliwa na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa chakula, mavazi na usafiri hasa pindi wanapougua.

Page 19: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

12

Hata hivyo, baadhi ya shule zimekuwa zikisaidiwa na mashirika yasiyo ya kiserikali kama vile World Vision na zimefanikiwa kuboresha mazingira ya shule na kuyafanya kuwa bora kwa mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Kwa mfano, kuna shule moja yenye watoto 32 wenye ulemavu mbalimbali kama vile ulemavu wa macho, hosteli za watoto na baadhi ya madarasa ambayo kwa sasa yanafikiwa hata na watoto wenye ulemavu ulemavu wa kusikia na ulemavu wa viungo. Shule hiyo imefanikiwa kurekebisha ngazi za kuingilia bwaloni, mabwenini na katika baadhui ya madarasa ili watoto wenye ulemavu wayatumie kiurahisi.

2.2.1 (b) Ukosefu wa mafunzo ya elimu maalumu kwa walimu.Mafunzo kuhusu elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu au elimu jumuishi, ni vigezo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa mpango wa elimu jumuishi kwa ujumla na katika kuwezesha tendo la kufundisha na kujifunza miongoni mwa watoto wenye ulemavu. Katika utafiti huu iligundulika kuwa walimu walio wengi hawana mafunzo kuhusu ufundishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ama elimu jumuishi. Matatizo haya yanakwamisha ufanisi katika kufundisha watoto wenye mahitaji maalumu.

Kwa hakika, taarifa kuhusu ukosefu wa mafunzo miongoni wa walimu kuhusu elimu maalumu na jumuishi zilipatikana baada ya uchambuzi wa taarifa katika shule kuhusu sifa za walimu. Isipokuwa katika wilaya D4 ambapo kati ya walimu 21 walikuwepo shuleni, asilimia 33.3 walikuwa angalau na mafunzo kuhusu elimu maalumu au elimu jumuishi. Katika wilaya zingine ni chini ya asilimia 15 (15%) ya walimu ndiyo waliokuwa na mafunzo kuhusu elimu maalumu au elimu jumuishi. Vilevile, katika shule zilizotembelewa katika wilaya D2, D5 na D6 hazikuwa na walimu waliopewa mafunzo kuhusu elimu maalumu au elimu jumuishi (Tazama chati 5). Hali hii inatisha, kutokana na ukweli kuwa katika wilaya D2 na D6 zilikuwa na karibu idadi sawa ya watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu. Kwa mfano kulikuwa na wanafunzi 14 wenye ulemavu waliotembelewa katika wilaya D2 na 34 katika wilaya D6.

Chati4:Asilimiayawalimuwenyemafunzokuhusuelimumaalumuauelimujumuishikatikawilayazilizotembelewa.

2.2.1 (c)Ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu. Wakuu wa shule walibainisha kuwa ukosefu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa watoto wenye mahitaji maalumu ni miongoni mwa matatizo yanayokwamisha ufanisi katika ufundishaji. Maoni ya wakuu wa shule kuhusu upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu yalifanana katika uchambuzi

Page 20: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

13

wa nyaraka za data zilizogundulika. Katika shule 14 tulizotembelea kwenye wilaya shiriki, ni wilaya mbili tu za D4 na D7 zilizokuwa na vifaa vya watoto wenye ulemavu. Kwa mfano, shule moja katika wilaya D4 ilikuwa na mashine za breille 6, viti vya kutembelea 15, na mashine za kuandikia 6. Shule nyingine katika wilaya D7 ilikuwa na mashine za Breile 8 na mashine za kuandikia za breile 4.

2.2.1 (d)Utashi mdogo wa kisiasa miongoni mwa watunga sera na viongozi, kutoa maamuzi ya kivitendo kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kuwasaidia watoto wenye ulemavu. Wadau wengi wa elimu waliohojiwa walishangazwa na juhudi za serikali kujenga madarasa mengi yasiyo rafiki kwa walemavu ilihali wakijua kuwa walemavu wapo. Istoshe wadau wengi hawakuona mantiki ya kudai vifaa vya walemavu ni aghali, maana watu wenye ulemavu ni wachache sana ukilinganisha na walio wazima. Kama alivyonukuliwa Afisa elimu wa wilaya moja iliyotembelewa, alisema;

“Nikitukisichoelewekakutoamanenomenginanyarakanyingizakiseranaprogrammbalimbalizihusuzoelimukwawatuwenyeulemavuwakatihakunaniayakwelikivitendokuwasaidiawalemavu.Kamaserikaliitakuwananiadhabitiinaweza kuwasaidia, maana sio wengi”.(Afisa Elimu Wilaya D1)

2.2.2 mchango wa wazazi na jamii katika kuwaelimisha watoto wenye ulemavu

Wakuu wa shule waliombwa kutoa maoni yao kuhusu msaada wanaopewa na jamii pamoja na wazazi kuhusu kuwaelimisha watoto wenye ulemavu. Katika shule zilizotembelewa wakati wa kufanya utafiti huu, iligundulika kuwa msaada unaotolewa na wazazi pamoja na jamii kuhusu kuwaelimisha watoto wenye ulemavu ni mdogo mno. Baadhi ya wakuu wa shule walifikia hatua ya kusema baadhi ya wazazi wamekuwa vikwazo katika kuwaelimisha watoto wenye ulemavu kwa kuwa wazazi hao huwatelekeza watoto wao mara tu wanapoandikishwa shule; Kwa mfano, mkuu mmoja wa shule alilalamika kwamba:

“ Wazazi hawatoi msaada wowote. Kwa hakika wao ndiyo kikwazo; wanawatelekeza watoto wao mara tu wanapoandikishwa shuleni”(Mkuu wa shule ya msingi katika wilaya D6)

Mkuu mwingine wa shule anabainisha kwamba:

“Jamiihaitoimsaadawowotekatikakuwaelimishawatotowenyeulemavu.Wazazihawatoiushirikianowowote;maratuwatotowaowanapoandikishwashulewaohuwatelekezamojakwamojanahuwahawatakikupewataarifayoyote!”(Mkuu wa shule ya msingi katika wilaya D7)

Pia baadhi ya washiriki walibainisha kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa hawapewi kipaumbele katika baadhi ya wilaya ukilinganisha na makundi mengine yaliyotengwa kama watoto yatima, kwa mfano, mkuu wa shule katika wilaya D5 alibainisha :

“Katikawilayayetuulemavusiyosualamuhimusanaukilinganishanamakundimengineyaliyolengwakamavilewatotoyatima.Kunamashirikamengiyanayosaidiawatotoyatimakatikawilayayetulakinihakunaaliyejitoakusaidiawatotowenyeulemavu.”

2.2.3 maoni ya walimu kuhusu kuwaelimisha watoto wenye ulemavu pamoja na elimu jumuishi: matokeo kutoka majadiliano katika vikundi mjadala

Katika shule zilizotembelewa wakati wa kufanya utafiti huu, majadiliano katika makundi mjadala ya walimu ilifanyika ili kusikia maoni yao kuhusu kuwafundisha watoto wenye ulemavu pamoja na elimu jumuishi. Katika kila shule, kundi maalumu lenye washiriki kati ya watoto 5 na tisa lilichaguliwa kwa kuzingatia jinsia,

Page 21: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

14

uzoefu na sifa tofautitofauti. Kwa ujumla majadiliano katika makundi mjadala 9 (tisa) yalifanyika katika shule 14 zilizotembelewa. Masuala manne yaliibuka wakati wa kuchambua taarifa kutokana na uzoefu wao, maoni na mtizamo wao kuhusu kuwafundisha watoto wenye ulemavu pamoja na dhana ya elimu jumuishi katika shule zao. Masuala hayo yanachambuliwa kwa ufupi hapa chini:-

2.2.4 Uelewa wa walimu kuhusu elimu jumuishi

Walimu walionesha uelewa tofautitofauti kuhusu elimu jumuishi. Kwa ujumla walimu wengi walionesha kuelewa kuhusu dhana ya elimu jumuishi. Walimu wengi walioshiriki katika mjadala kuhusu elimu jumuishi, walieleza kuwa elimu jumuishi ni aina ya elimu ambapo watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu kwa pamoja hutumia madarasa yale yale ambayo hutumiwa na watoto wasio na ulemavu. Baadhi ya maoni ya walimu kuhusu elimu jumuishi yanaelezwa hapa chini:

“Elimu jumuishi ni aina ya elimu ambapo watoto wenye ulemavu huchangamana na watoto wenzao wasio na ulemavu (mwalimu wa shule ya msingi katika wilaya D7 mwenye jinsia ya kiume)

“Elimu jumuishi huwaweka pamoja watoto wa aina tofautitofauti, wenye jinsia tofauti, wasiojiweza, wenye kujiweza, masikini,matajiri;hujumuishaainazotezawatoto”

“[Elimu jumuishi] ni aina ya elimu ambapo watoto wenye ulemavu hujifunza pamoja na wenzano ambao hawana ulemavukatikadarasamoja”(Mwalimu katika shule ya sekondari msingi katika wilaya D4).

Kwa ujumla, uelewa wa walimu kuhusu elimu jumuishi ulizingatia zaidi kuwaweka watoto wenye ulemavu katika madarasa ya kawaida na haukuzingatia watoto wenye matatizo mengine. Kitaalamu zaidi, elimu jumuishi hulenga kuwaweka pamoja watoto wote waliotengwa na wale wasiopatiwa huduma bora kama vile watoto wanaotoka katika familia duni ama yatima.

2.2.5 Uelewa wa walimu kuhusu “ulemavu” au “mtu asiyejiweza”.

Walimu pia waliulizwa waeleze wanavyoelewa kuhusu dhana ya “kutojiweza ama mtu asiyejiweza” Walimu walio wengi walielewa dhana ya kutojiweza kama ukosefu wa uwezo ambao humfanya mtu ashindwe kuhimili maisha yake kikamilifu na kwa kujitegemea. Kwa mfano, walimu walibainisha kwamba:

[mtu asiyejiweza] ni “yule mwenye mahitaji maalumu”

[mtu asiyejiweza] ni “ yule mwenye mapungufu katika kiungo kimoja au zaidi”

Hata hivyo walimu wengi hawakuwa na uhakika sana kuhusu dhana ya kutojiweza. Kwa mfano, katika majadiliano ya kikundi kimoja, walimu walitumia muda mrefu kujadili iwapo m watoto aliyepoteza uwezo wa kuongea kutokana na matatizo kwenye uti wa mgongo kama anaweza kuchukuliwa kama mwenye ulemavu au la. Hii inathibitishwa na maoni hapa chini.

“Kunamwatotommojaaliyepatautiwamgongonamatokeoyakeamepotezauwezowakuongeanakwasasanibubunasinauhakikakamaanawezakusikia.Je,tunawezakumchukuliahuyukamamtuasiyejiwezawakatihakuzaliwahivyo;nahalihiiimetokeahivikaribunitukutokananaugonjwa?”

Kwa mujibu ya maoni yaliyotolewa na walimu na kunukuliwa hapo juu, inaonekana kwamba mtu mwenye ulemavu ni yule aliyezaliwa nao na wala si yule aliyepata ulemavu baadaye. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani dhana ya ulemavu ilivyo ngumu kueleweka kwa baadhi ya watu.

Page 22: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

15

Pia kutokana na takwimu zilizokusanywa kutoka baadhi ya wilaya, inaonesha kuwa ulemavu unahusishwa vilevile na magonjwa sugu kama vile pumu, anemia, VVU na UKIMWI. Hata hivyo kitaaluma watoto wenye magonjwa haya hawawezi kuhusishwa na ulemavu ijapokuwa kutokana na magonjwa hayo wanaweza kuwa na matatizo katika tendo la kujifunza.

Kwahiyo dhana ya ulemavu ni ngumu kueleweka kwa baadhi ya walimu na hivyo inakuwa vigumu sana kuwatambua watoto wenye ulemavu shuleni kwao. Kutokana na dhana finyu kuhusu ulemavu miongoni mwa walimu, watoto wasio na ulemavu wanaweza kuchukuliwa kama wenye ulemavu n.k.

2.2.6 maoni ya walimu kuhusu elimu jumuishi

Walimu waliombwa watoe maoni yao kuhusu kutumia mbinu ya elimu jumuishi kama njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wenye ulemavu na wale wenye mahitaji maalumu. Kulikuwa na mgawanyiko miongoni mwa walimu kuhusu umuhimu wa elimu jumuishi. Baadhi ya walimu waliunga mkono mbinu ya elimu jumuishi na waliiona ni mbinu bora kwa watoto kwa kuwa watoto wote watakuwa na uwezo wa kutimiza ndoto zao katika elimu. Baadhi ya walimu walikuwa na maoni kwamba kuwaweka watoto wenye ulemavu katika madarasa ya kawaida italeta usumbufu katika ufundishaji. Baadhi ya maoni ya walimu yaliyokuwa yakikosoa mfumo wa elimu jumuishi yameelezewa hapo chini:

“watotowenyeulemavuwanahitajiuangaliziwahaliyajuu;kuwachanganyanawatotowasionaulemavuitasababishausumbufudarasani.Piaitachukuamudamrefusanakatikakufundishadarasalanamnahiyo.” (Mwalimu wa shule ya msingi Wilaya D2 wa jinsia ya kiume). Wengine pia walisema.

“ sipendi elimu jumuishi.Kuwachanganya watotowenyeulemavunawasionaulemavu itasababisha kitendo chakujifunzakiwechapolepolemnonahiinisawanakuwarudishawatotonyuma”(Mwalimu wa shule ya msingi mwenye jinsia ya kike katika wilaya D7).

“[Wazo la elimu jumuishi siyo zuri] watoto wenye ulemavu watakuwa wakikatishwa tamaa na wale wasio na ulemavu” (Mwalimu wa shule ya msingi mwenye jinsia ya kiume katika wilaya D6).

“ Elimu jumuishi inawafaa watoto wasio na ulemavu mkubwa lakini ni ngumu kwa watoto wenye ulemavu mkubwa. Ikiwautawachanganyawatotowenyeulemavunawasionaulemavuutasababishawatotowenyeulemavukunyanyasikadarasani”(Mwalimu wa shule ya sekondari mwenye jinsia ya kike katika wilaya D7).

Baadhi ya walimu walibainisha kuwa kufundisha darasa lenye watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu ni changamoto kubwa hasa pale panapokuwa na ukosefu wa vifaa bora vya kufundishia na kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu na wale wenye mahitaji maalumu. Pia baadhi ya walimu walikuwa na mtazamo hasi kuhusu watoto wenye ulemavu. Kwa mfano mwalimu mmoja alisema kuwa watoto wenye ulemavu hawana uwezo wa kujifunza kama watoto wasio na ulemavu, kwahiyo wasichanganywe na wengine wasio na ulemavu. Mwalimu huyo allinukuliwa akisema:

“watotowenyeulemavuniwazitosanalinapokujasualalakujifunza.Hawawezikufanyachochote.Wakatimwingineunapowapatiamtihaniwaohunakiliswalikamalilivyobadalayakulijibu.watotowenyeulemavuhawawezikujifunzachochotechamaana!”(Mwalimu wa shule ya sekondari mwenye jinsia ya kiume katika wilaya D6).

Hata hivyo, katika majadiliano walimu waliunga mkono suala la elimu jumuishi. Walibainisha kuwa elimu jumuishi itawapa moyo wa kujifunza watoto wenye ulemavu kama wajifunzavyo watoto wengine. Pia elimu jumuishi itapunguza unyanyapaa. Mwalimu mmoja alitoa maoni yafuatayo:

Page 23: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

16

“ Elimu jumuishi itasaidia kupunguza tatizo la unyanyapaa. Kama watoto wenye ulemavu watasoma pamoja na watotowenzaowasionaulemavuhaliyaoyakujiaminiitaongezekanawatakuwakamawatotowengine.Kuwabaguaamakuwatengawatotowenyeulemavuitasababishawajionewanyongenawasionathamanikatikajamii”(Mwalimu wa kiume wa shule ya sekondari katika wilaya D4).

Baadhi ya walimu hawakukubaliana na maoni kuwa watoto wenye ulemavu ni wazito sana katika akili zao na kwamba hawawezi kujifunza wala kufanya chochote. Kwa mfano, mwalimu mmoja katika wilaya D7 alitoa maoni kwamba watoto wenye ulemavu wana uwezo mkubwa wa kujifunza kama watapatiwa fursa na vilevile kama watasaidiwa. Walitoa mifano inayoonesha mafanikio ya watoto wenye ulemavu katika mitihani ya taifa ambayo watoto wenye ulemavu wameonesha kufanya vizuri kama watoto wengine. Kwa mfano, katika wilaya D7, kulikuwa na watoto watatu waliokuwa na ulemavu wa macho; watoto hao walifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na wote walifaulu. Hii ilikuwa mwaka 2006. Pia mwaka 2007, watoto wanne wenye ulemavu, wawili wakiwa na ulemavu wa viungo na wawili wakiwa na ulemavu wa macho walifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na wote walifaulu.

Kwa ujumla nukuu zilizotolewa hapo juu zikionesha kupinga suala la elimu jumuishi, pia zinaonesha udhaifu na uelewa mdogo miongoni mwa walimu kuhusu namna ya kushughulikia masuala ya watoto wenye ulemavu. Walimu wengi walioshiriki majadiliano wakati wa utafiti walielezea ugumu wanaoupata katika kuwasiliana na watoto wenye ulemavu wa macho na masikio na pia jinsi ya kutatua migogoro ya watoto. Kwa mfano mwalimu mkuu alibainisha kuwa:

“Walimuwaliowengiwanapatamatatizokatikakuwahudumiawatotowenyematatizomakubwayakusikianakuona.Wakatimwinginetunalazimikakutowaandikishawatotowenyeulemavumkubwa.Kwamfano,mwakahuutulilazimikakumrudisha nyumbani mtoto mmoja baada ya kugundua kuwa alikuwa hana uwezo wa kusikia wala kuongea. Je,utamfundishajemtotowanamnahiyo?”

Mwalimu mwingine alilalamika:

“ Nafundisha jiografia, darasani kwangu nina watoto wawili wenye ulemavu wa macho. Wakati ninapofundisha usomajiwaramani,huwaninahangaikasanamaanahuwasijuinifanyeninihasakwawatotowasioona!”

2.2.7 Uzoefu na maoni ya watoto wenye ulemavu kuhusu mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni kwao.

Maoni ya watoto wenye ulemavu kuhusu mazingira ya ufundishaji shuleni kwao yalipatikana kupitia njia ya maswali dodoso pamoja na majadiliano. Kuna mambo mawili yaliyoibuka kutokana na maswali ya dodoso pamoja na majadiliano. Mambo haya yanahusu changamoto ambazo watoto wenye ulemavu wanazipata wakati wanaendelea na tendo la kujifunza. Mambo hayo yameelezewa na kufafanuliwa hapa chini.

matatizo ambayo watoto wenye ulemavu huyapata wakiwa shuleni

• Matatizo ya usafiri,Kwa kupitia maswali ya dodoso pamoja na majadiliano, ilibainika kwamba watoto wenye ulemavu hukumbwa na vikwazo vingi sana katika mazingira yao ya kujifunza/elimu. Kwa mfano, watoto wengi wenye ulemavu walioshiriki katika mahojiano na kujaza dodoso walieleza kuwa hawana uhakika wa usafiri wa kuwapeleka shule pamoja na kuwarudisha nyumbani. Kutokana na tatizo hili, wengi walikuwa wakifika shuleni wamechelewa kutokana na muda mwingi uliopotelea njiani. Wengi walielezea kwamba wanategemea usafiri wa marafiki zao ambao hutumia baiskeli zao

Page 24: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

17

kuwapatia huduma za usafiri. Kwa mfano m watoto mmoja katika shule moja iliyopo wilaya D7 alibainisha kuwa:

“Usafiri ni tatizo kubwa linalotukabili hapa. Mimi nategemea usafiri wa baiskeli ya rafiki yangu ambao hauaminiki sana. Mara kwa mara mimi huchelewa kufika shuleni na matokeo yake huwa nakosa vipindi vingi.”

• Ukosefu wa vifaa vya kujifunzia, watoto wenye ulemavu pia walielezea ukosefu wa vifaa vya kujifunzia kuwa ni tatizo jingine linalokwamisha maendeleo yao darasani. Kwa mfano watoto wenye ulemavu wa macho walielezea kuwa hakuna vitabu vinavyofaa kwa ajili yao. Kwa mfano m watoto mmoja wa darasa la sita mwenye ulemavu wa macho alibainisha kuwa:

“Maisha ni magumu sana hapa maana inaniwia ugumu jinsi ya kufika shuleni na kurudi nyumbani. Kila kitu ni kigumu.Hakunavitabu.Kwamfano,mimi sinauwezowa kuona lakini shuleni kwetuhakunavitabu kwaajili yawatotowenyeulemavuwamacho.Tangunimekujahapasijawahikuonakitabu.”

Walipotakiwa kuelezea ni kwa jinsi gani wanakabiliana na tatizo la ukosefu wa vitabu shuleni kwao m watoto mmoja alielezea kuwa watoto wenzao wasio na ulemavu huwasomea na wao husikiliza kile kinachosemwa. Alibainisha kuwa:

“Rafiki yangu ambaye hana ulemavu wa macho hunisomea. Hata hivyo, si kila mara anakuwa na mimi kwa sababu ana mambomenginepiaanayotakiwakuyafanya.Halazimikikuwanamimimudawote!”

• Kujisikia kupuuzwa na kutoridhishwa na walimu, watoto walio wengi hawakufurahishwa na elimu wanayopewa shuleni hapo. Walibainisha kuwa elimu wanayopata shuleni kwao haina ubora unaotakiwa. Kwa hiyo, hawaichukulii kama elimu inayowafaa! Baadhi ya watoto walielezea kuwa baadhi ya walimu wao wamekuwa hawatoi msaada wowote kwao bali wamekuwa wakipata msaada toka kwa watoto wenzao. Miongoni mwa watoto aliyeshiriki majadiliano alibainisha:

“Wengi wetu sisi[watoto wenye ulemavu] hupata elimu duni. Kwa hakika hatupati elimu yoyote kutoka kwa walimu wetu.Wanaotusaidiazaidiniwatotowenzetu.Kwamfano,mwalimuwaHisabatiakiingiadarasanikwetuyeyehuwajalizaidiwatotowasionaulemavu.KwasisiwatotowenyeulemavusomolaHisabatihatufaidikinalokwasababuhatunamwalimuambayeanawezakutusaidiailitujifunzekikamilifu.”

• Unyanyapaa, Tatizo lingine ambalo watoto wenye ulemavu hukumbana nalo ni unyanyapaa na kudhalilishwa kunakofanywa na watoto wasio na ulemavu ambao huwacheka watoto wenye ulemavu na kuwapachika majina. M watoto mmoja alibainisha kuwa:

“Baadhiyawatotohuwawananichekakwasababunijichomojatuambalokwanguhuwezakuona.Huwawananiitababunawakiniitahivyomimihujisikiahuzunisana!”

M watoto mwingine alikuwa na mawazo yanayofanana naya wa kwanza na alibainisha kuwa:

“Tatizo kubwa linalonikabili ni kuwa baadhi ya watoto wana tabia ya kunicheka. Wao huniambia kuwa ninavutamarijuanakwakuwamachoyangunimekundu.PindininapovaamiwaniyanguwaohuniitabwanaTozi!”

2.3 KUUnga mKono ElimU jUmUishi miongoni mWa WalimU2.3.1 Utangulizi

Ili kujua kwa kiwango gani walimu walikuwa wanaunga mkono suala la elimu jumuishi, maswali ya dodoso

Page 25: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

18

yaliandaliwa kwa walimu, na walimu waliotarajiwa kushiriki katika majadiliano walichukuliwa bila vigezo maalumu. Maswali ya dodoso yalikuwa na sehemu kubwa mbili, kuchunguza mambo yanayohusiana na umri, jinsia pamoja na uzoefu katika kufundisha bila kusahau sifa husika za walimu. Sehemu ya pili ilihusisha uchunguzi kuhusu mtazamo wa walimu kuhusu elimu jumuishi. Walimu mia moja na tatu(103)waliweza kujaza maswali ya dodoso ambao asilimia 53.9 walikuwa wanaume. Wastani wa umri wa washiriki ulikuwa miaka 36.9. Zaidi ya asilimia 40 ya washiriki walikuwa na uzoefu kuhusu taaluma ya ualimu kwa zaidi ya miaka 10 na asilimia 51.6 ya washiriki walikuwa wenye kiwango cha stashahada ya ualimu na wengi wa washiriki walikuwa ni walimu wa shule za sekondari (Tazama chati 4).

jedwali 4: sifa na uzoefu wa walimu waliojaza maswali ya dodoso yaliyohusu mtazamo wao kuhusu elimu jumuishi

Wanaume Wanawake Jumla

N % N % N %

Uzoefu wa kufundisha

Chini ya miaka 5 28 50.9 7 16.7 35 36.1

Miaka 5-10 11 20.0 10 23.8 21 21.6

Zaidi ya miaka10 16 29.1 25 59.5 41 42.3

Sifa za kiualimu

Cheti daraja A 14 26.9 30 69.8 44 46.3

Cheti daraja B 1 1.9 1 2.3 2 2.1

Diploma au zaidi 37 71.2 12 27.9 49 51.6

Ngazi ya kufundisha

Shule za msingi

Shule za sekondari

2.3.2 mitazamo wa walimu kuhusu elimu jumuishi

Jedwali 5 linatoa ufupisho kuhusu mtazamo wa walimu kuhusu elimu jumuishi. Kwa wastani walimu wengi (44%) waliojibu maswali ya dodoso walikuwa hawana uhakika iwapo kama walikubaliana au kutokubaliana na wazo la elimu jumuishi (namba ya kati=3, wastani=3.34, chini=0.72) ikimaanisha kuwa walimu wengi hawakujua umuhimu wa elimu jumuishi na jinsi inavyowasaidia watoto wenye ulemavu ama wale wenye mahitaji maalumu. Hata hivyo, kwa wastani asilimia 44 ya walimu ama walikubaliana moja kwa moja (2.2%) ama walikubaliana wakiwa na maoni kwamba elimu jumuishi ni muhimu katika kufanikisha kitendo cha ujifunzaji kwa watoto wenye ulemavu au wale waliotoka kwenye makundi yaliyotengwa (Tazama chati 5)

Page 26: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

19

0

12

44 42

20

102030405060708090

100

SikubaliKabisa

Sikubali Sina uhakika Nakubali Nakubai kabisa

Chati5:Asilimiayawalimuwaliokubalianaamakukataawazokuwaelimujumuishiinawezakuletaufanisikatikaufundishajiwawatotowenyeulemavu

Kiambatanisho 1 kinaelezea kwa ufupi mawazo mbalimbali yaliyotolewa na walimu kuhusu elimu jumuishi. Kama inavyoonekana katika jedwali, uungwaji mkono wa elimu jumuishi miongoni mwa walimu ulikuwa mdogo, ambao wastani wake ulikuwa ya asilimia 50 ya washiriki ambao waliunga mkono elimu jumuishi (Tazama chati).

Kwa hakika walimu wengi ambao ni asilimia 61.2 waliunga mkono wazo kuwa elimu jumuishi inasababisha matatizo katika ufundishaji kuliko faida zake hasa kwa walimu kwa kuwa huwaongezea walimu mzigo mwingine. Asilimia 28.8 ya walimu walikubaliana moja kwa moja, na asilimia 32.4 walikubaliana huku wakisisitiza kuwa “elimu jumuishi husababisha matatizo mengi kuliko kuwatenganisha. Vilevile asilimia 50.5 ya walimu ama walikubaliana moja kwa moja (19.4%) au walikubaliana (31.1%) na maelezo kuwa “elimu jumuishi husababisha mwalimu kuwa na kazi nyingi za ziada.”

Bila shaka walimu walio wengi hawaungi mkono elimu jumuishi kutokana na ukweli kuwa wengi wao hawana taaluma na uwezo wa kufundisha watoto wa aina tofautitofauti na mahitaji tofautitofauti kama walivyo watoto wenye ulemavu. Hali hii inathibitishwa na maelezo ya walimu ambao walikuwa wanahitaji wapewe mafunzo maalumu ya namna ya kufundisha katika darasa lenye watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu. Kwa mfano, asilimia 98.3 ya walimu ama walikubaliana moja kwa moja (77.7%) au walikubaliana (20.6%) na wazo kuwa “walimu wanahitaji kupewa mafunzo maalumu kuhusu elimu jumuishi.” Pia ni asilimia 10.7 tu ya walimu waliokuwa wakijibu swali ama walikubaliana (2.9%) moja kwa moja au walikubali (7.8) maelezo kuwa “walimu pamoja na wafanyakazi wengine walikuwa na uwezo wa kufundisha katika madarasa yenye watoto wenye ulemavu na wasio na ulemavu.”

Wakati wa uchambuzi wa takwimu kuna mambo mawili yaliyoibuka ambayo kimsingi yanahusiana na elimu jumuishi. Mambo hayo yanaweza kugawanywa katika makundi makuu mawili (Tazama kiambatanisho 2); kundi la kwanza lilitathmini maoni ya walimu kuhusina na elimu jumuishi na jinsi elimu jumuishi inavyoweza kuwasaidia watoto wenye ulemavu pamoja na makundi mengine yaliyotengwa katika jamii. Kundi la pili lilitathmini mtazamo na utayari wa walimu katika kuunga mkono elimu jumuishi. Makundi haya yalifafanuliwa kwa undani ili kuona ni kwa kiwango gani walimu waliunga mkono.

Page 27: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

20

Uchambuzi wa takwimu ulionyesha kuwa karibu kila kundi lilikuwa likiungwa mkono kwa kiwango sawa na walimu, ikimaanisha kuwa ni 40% tu ya walimu waliamini kuwa elimu jumuishi ilikuwa ni muhimu na kwamba iliungwa mkono vilevile na wadau wengine wakiwamo watunga sera, uongozi wa shule pamoja na watoto (Tazama chati 6).

15%21%

45%

33% 35%31%

40% 39%

5% 8%

0102030405060708090

%

%%%%%%%%

%%100

wanakubali elimujumuishi

Elimu jumuishi ni muhimu

Nakubalikabisa

Nakubalikabisa+nakubali

NakubaliSinauhakika

SikubaliSikubalikabisa

6%0%

Chati6:Asilimiayawalimuwaliokubaliaukutokubaliananamaelezokuwa:elimujumuishinivyemaiungwemkononakwambaelimujumuishinimuhimu.

2.4 miTazamo Wa WaToTo Wasio na UlEmavU KUhUsU WEnzao

WEnyE UlEmavU2.4.1 Utangulizi

Mtazamo wa watoto wasio na ulemavu kuhusu wenzao wenye ulemavu ni suala la muhimu sana kwa kuwa linatusaidia kuelewa utayari wao kuhusu kusoma na wenzao wenye ulemavu, na pia linatusaidia kupima ni kwa kiwango gani watoto wasio na ulemavu wanaunga mkono suala la elimu jumuishi. Kwa hivyo, jambo la msingi kuzingatia wakati wa kuandaa program za elimu jumuishi ni kupata kwanza mtazamo wa watoto wasio na ulemavu kuhusu wenzao wenye ulemavu.

Katika utafiti huu, watoto 1103 wa shule za msingi ambao walikuwa asilimia 19.1 na wale wa sekondari ambao walikuwa asilimia 80.1 walijaza maswali ya dodoso yaliyokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya maswali ya dodoso ilihusu mambo ya jumla na sehemu ya pili ilijumuisha mambo 26 ambayo yalikuwa ya kipima mtazamo wao kuhusu watoto wenye ulemavu.

Kati ya watoto 1103 waliojaza maswali ya dodoso, 51% walikuwa ni wavulana na 49% walikuwa wasichana. Wastani wa umri wa washiriki ilikuwa miaka 16.5. kati ya watoto hao ni asilimia 24.5 tu walitoa taarifa kuwa walikuwa na mtu mwenye ulemavu katika familia yao na 37.2% tu walikuwa na rafiki mwenye ulemavu wakati 41.6% walisema kuwa walishawahi kukutana na mtu mwenye ulemavu wiki mbili kabla ya kujaza maswali ya dodoso.

2.4.2 maoni ya watoto wasio na ulemavu kuhusu kujifunza pamoja na wenzao wenye ulemavu

Kiambatanisho namba 3 kinaeleza kwa ufupi kuhusu maoni ya watoto wasio na ulemavu kuhusu kujifunza pamoja na kuchangamana na wenzao wasio na ulemavu.

Kwa ujumla, kama kiambatanisho 3 kinavyoonesha, watoto wasio na ulemavu walionesha kuunga mkono

Page 28: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

21

suala la kusoma pamoja na wenzao wenye ulemavu. Wastani wa kati ulionesha kiwango cha 4.2 ya watoto ambao walikubaliana na maelezo yaliyozungumziwa iwapo walikuwa tayari kuchangamana pamoja na kusoma pamoja na wenzao wenye ulemavu.

Kuhusu mambo ya uhusiano kwa mfano 79.7% ya watoto walisema walifurahia kuwa na rafiki mwenye ulemavu, hii ikimaanisha kuwa 54.5% walikubaliana moja kwa moja na 25.2% wakikubalina na maelezo kuwa: “ Ningefurahia kuwa na rafiki mwenye ulemavu.” Pia 91.3% ya watoto walieleza kufurahia iwapo mtoto mwenye ulemavu angewaalika nyumbani kwao, hii ina maana kuwa 60.5% walikubaliana moja kwa moja na 27.7% walikubaliana na maelezo kuwa: “Ningefurahia kama m watoto mwenye ulemavu angenialika nyumbani kwao.” Vilevile 90.5% ya watoto walielezea utayari wao wa kucheza pamoja na watoto wenzao wenye ulemavu, hii ilimaanisha kuwa 58% walikubaliana moja kwa moja na 32.5% walikubaliana na maelezo kuwa: “ningependa kucheza na watoto wenye ulemavu nyumbani kwao.”

watoto wasio na ulemavu vilevile walikuwa na mtazamo chanya kuhusu kushirikiana kitaaluma na wenzao wenye ulemavu. Kwa mfano, 83.3% ya watoto walieleza kuwa hawaogopi kukaa na wenzao wenye ulemavu darasani, hii ikiwa na maana kuwa 58.3% walikubaliana moja kwa moja na 25% walikubaliana na maelezo kuwa: “ Nisingeogopa kama m watoto mwenye ulemavu angekaa karibu yangu darasani.” Pia 86% ya watoto walielezea kuwa wangefurahia kufanya kazi pamoja na wenzao wenye ulemavu, hii ikimaanisha kuwa 60% ya watoto walikubaliana moja kwa moja na 26% walikubaliana na maelezo kuwa: “Ningefurahia kufanya kazi pamoja na mtoto mwenzangu mwenye ulemavu.”

Hata hivyo watoto wengi wasio na ulemavu walikuwa na fikra kuwa watoto wenzao wenye ulemavu hawakuwa wenye furaha na pengine walikuwa hawajimudu kitaaluma kama watoto wasio na ulemavu. watoto wengi vilevile waliwahurumia sana wenzao wenye ulemavu. Kwa mfano, ni 26.1% tu ya watoto wasio na ulemavu walidhani wenzao wenye ulemavu wanafurahia maisha, hii ikimaaanisha kuwa ni 7.7% tu ya watoto walikubali moja kwa moja na 5.8% ya watoto walikubaliana na maelezo kuwa: “ watoto wenye ulemavu wanafurahia maisha kama watoto wengine.”

Vilevile ni 42.9% tu ya watoto walijibu kuwa watoto wenye ulemavu walikuwa na furaha kama watoto wengine, hii ikimaanisha kuwa, 27.2% ya watoto walikubaliana moja kwa moja na 15.7% ya watoto walikubaliana na maelezo kuwa: “ watoto wenye ulemavu wanafurahia maisha kama watoto wengine.”

Baada ya maswali 26 yaliyokuwa yakipima mtazamo wa watoto wasio na ulemavu yalipochambuliwa kwa kina, kuna maswala matatu makuu yalijitokeza ambayo ni: “Imani kwamba inawezekana kushirikiana kitaaluma na watoto wenye ulemavu (CWD), imani kwamba inawezekana kuwa na rafiki na mwenye ulemavu (CWD) na imani kuwa watoto wenye ulemavu wana uwezo na akili kama watoto wengine na wako kawaida.” Masuala haya yalipochambuliwa, iligundulika kwamba watoto walio wengi waliamini kuwa inawezekana kushirikiana kitaaluma na watoto wenye ulemavu na inawezekana kuishi na wenzao wenye ulemavu. Hata hivyo, watoto walio wengi walikuwa hawana imani kuwa watoto wenye ulemavu walikuwa na uwezo sawa na watoto wengine. Kwa mfano, katika chati 7 na 8 inaonesha kuwa ni 7% tu ya watoto walikubaliana na maelezo kuwa watoto wenye ulemavu wanao uwezo sawa kama walivyo watoto wengine.

Page 29: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

22

0

10

20

30

40

50

60

70

80

90

100 %

%

%

%

%

%

%

%

%

%

%SikubaliKabisa

Sikubali Sinauhakika

Nakubali NakubaliKabisa

Wanaweza kushirikiana Na wenye ulemavu

Wanaweza kuwa marafikiNa kuishi na wenye ulemavu

Walemavu wanauwezo Na wako kawaida

Chati 7: Asilimia ya watoto wenye ulemavu wanaokubaliana au kutokubaliana kuwa inawezekana kushirikiana kitaaluma, kuwa na rafiki mwenye ulemavu pamoja

nakuishinawenzaowenyeulemavunakwambawatotowenyeulemavunisawanawatotowengine.

89 % 90 %

7 %

0%

102030405060708090

100

Wanawezakushirikiana

Na walemavu

Wanaweza kuwa marafiki

Walemavu wana uwezo

Chati 8: Asilimia ya watoto waliokubaliana moja kwa moja ama kukubali maelezo kuwa inawezekana kushirikiana kitaaluma, kuwa na rafiki ama kuishi pamoja na

kwambawatotowenyeulemavunisawanawatotowengine.

Page 30: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

23

SeHeMU 3

Majadiliano, HitiMiSHo na Mapendekezo

Page 31: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

24

3.1 majadilianoUtafiti huu ulilenga kutathmini fursa ya elimu kwa watoto wenye ulemavu pamoja na changamoto zinazowakabili watoto wenye ulemavu katika shule za Tanzania. Mambo mengi yameibuka. Kwanza, utafiti umegundua kuwa ni watoto wachache sana wenye umri wa kwenda shule ambao wameandikishwa kwenye shule mbalimbali hapa nchini: kwa mfano takwimu za serikali zinaonesha kuwa ni asilimia moja tu(1%) ya watoto wenye ulemavu hapa nchini ambao wamepatiwa fursa katika elimu ya msingi. Vilevile utafiti huu umeonesha kuwa ni chini ya asilimia moja (1%) ya watoto wenye ulemavu ndio walioandikishwa katika shule mbalimbali. Hali hii inakwenda kinyume na malengo ya serikali ya kuhakikisha kuwa elimu inatolewa kwa wote. Hakika, kama watoto walemavu hawatapewa fursa katika elimu, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi hapa nchini yaani MMEM hautafanikiwa, maana baadhi ya malengo yake yatakuwa hayajafikiwa.

Hata hivyo, mafanikio yaliyofikiwa katika MMEM ambapo uandikishaji wa watoto katika shule za msingi hapa nchini wa zaidi ya 80% hauwalengi watoto wenye ulemavu. Waliopatiwa fursa ya elimu ni wachache mno ukilinganisha na idadi kamili ya watoto wote.

Pili, ingawa serikali imekuwa ikiendeleza falsafa ya elimu jumuishi kama njia mojawapo ya kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wenye ulemavu, bado kuna shule chache sana hapa nchini ambazo zinatumia mfumo huu. Kwa hakika, watoto wengi wenye ulemavu bado wanasoma katika shule maalumu au kwenye madarasa ya pamoja ambayo hayajengi dhana halisi ya elimu jumuishi.

Mambo ambayo yanaonekana kama kikwazo kwa elimu jumuishi ni mengi. Mambo haya yanajumuisha kwa mfano, mtazamo hasi miongoni mwa walimu kuhusu elimu jumuishi. Kwa mfano katika utafiti huu ni chini ya 50% ya walimu ndio waliunga mkono mfumo wa elimu jumuishi. Hata hivyo, uchambuzi wa kina ulipofanyika ilibainika kuwa elimu jumuishi haiungwi mkono zaidi kutokana na uelewa mdogo pamoja na ukosefu wa taaluma inayohusu watoto wenye mahitaji maalumu na jinsi ya kufundisha madarasa yenye watoto wenye ulemavu na wale wasio na ulemavu.

Suala hili limechangiwa na ukosefu wa mafunzo miongoni mwa walimu yanayohusu watoto wenye mahitaji maalumu na jinsi ya kushughulikia watoto wenye ulemavu. Kwa kweli katika kipindi hiki ambapo kuna walimu wachache wenye taaluma kuhusu elimu maalumu ni vyema kuziendeleza shule maalumu pamoja na madarasa mchanganyiko badala ya kusisitiza elimu jumuishi ambayo kimsingi inaweza kufanikiwa tu pale panapokuwa na walimu wa kutosha wenye mafunzo kuhusu elimu kwa ajili ya wenye mahitaji maalumu na walemavu wakiwemo.

Tatu, utafiti huu umegundua kuwa kati ya watoto walioandikishwa shule, wengi wao ni wale wenye ulemavu wa viungo na ni wachache sana wenye ulemavu kama vile ulemavu wa akili, macho na kusikia. Haijulikani kama hali hii inatoa taswira ya mambo yalivyo katika jamii kwamba watoto wenye ulemavu wa viungo wamepewa upendeleo wa pekee kuliko watoto wenye ulemavu wa aina mwingine. Vilevile inawezekana kuwa shule huwa zinaona unafuu katika kushughulikia matatizo ya watoto wenye ulemavu wa viungo badala ya watoto wengine; na kwa hiyo huwa ziko radhi kuwapokea. Hili ni eneo linalopaswa kufanyiwa utafiti hapo baadae.

Nne, matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa kuna mambo mengi yanayokwamisha fursa ya elimu kwa watoto wenye ulemavu. Kwanza, karibu shule zote zilizotembelewa zilionekana kuwa na mazingira yasiyofaa kwa watoto wenye ulemavu, hasa ulemavu wa viungo na macho. Pili, walimu wengi pamoja na wakuu wa

Page 32: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

25

shule walionesha uelewa mdogo kuhusu masuala yanayohusu watu wenye ulemavu. Hali hii ni kikwazo kikubwa katika kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu na wale wenye ulemavu. Hii inamaanisha kuwa baadhi ya watoto wenye ulemavu wanaweza wasitambuliwe na hivyo mahitaji yao kutobainishwa ama pengine watoto wasio na ulemavu kuchukuliwa kama wenye ulemavu. Hali hii inaweza kuleta madhara ya kisaikolojia katika masomo yao. Ukizingatia mtazamo hasi miongoni mwa walimu kuhusu watoto wenye ulemavu na kuhusu elimu jumuishi, hali hii vilevile inadhihirisha ni kwa jinsi gani shule hazijaandaliwa vizuri na hazina vifaa ambavyo vinaweza kutumika kufundishia watoto wenye ulemavu.

Pengine kikwazo kikubwa kabisa katika elimu kwa watoto wenye ulemavu ni kwamba hakuna juhudi za makusudi za kitaasisi ambazo zimechukuliwa ili kuondoa vikwazo hivi. Masuala ya watoto wenye ulemavu yametajwa kidogo katika MMEM pamoja na kwenye sera zingine za elimu; pia masuala ya watoto wenye ulemavu hayazungumziwi katika katiba za mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini.

3.2 hiTimishoWakati juhudi za serikali katika kuboresha upatikanaji pamoja na ubora wa elimu hapa nchini zikiwa wazi na zenye kutia moyo, hali ni tofauti kabisa kwa upande wa watoto wenye ulemavu. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa juhudi za hivi karibuni za kuboresha upatikanaji wa elimu ya msingi kwa wote hazijazingatia mahitaji ya watoto wenye ulemavu. Kwa hali hiyo, watoto wenye ulemavu hawajanufaika na matunda ya MMEM na MMES pamoja na program nyingine za mabadiliko ya elimu hapa nchini.

Utafiti huu umegundua mambo mengi yanayokwamisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wenye ulemavu hapa nchini. Mambo yanayokwamisha upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye ulemavu ni pamoja na kwanza, vikwazo vya kimitizamo na kimazingira katika elimu ambapo mazingira ya shule hayakujengwa kwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu.

Pili, walimu hawajaandaliwa kufundisha watoto wenye ulemavu, hivyo kazi ya kuwachanganya watoto wa kawaida na wale wenye maghitaji maalumu imeonekana kuwa nzito sana kwako.

Tatu, walimu wakuu walio wengi pamoja na walimu wa kawaida wana uelewa mdogo kuhusu masuala yanayohusu watu wenye ulemavu. Hali hii ni kikwazo kikubwa katika kuwatambua watoto wenye mahitaji maalumu na wale wenye ulemavu.

Nne, si wazazi wengi wenye watoto wenye ulemavu wako tayari kuwapeleka watoto wao shuleni, wengi hawawajali kikamilifu. Matokeo yake watoto wengi wenye ulemavu wamekuwa wakibaki nyumbani pamoja na kwamba wamefikia umri wa kwenda shule kutokana na kutotambuliwa.

Tano, pamoja na wazazi kutowapeleka watoto wao shule, jamii pia haina mwamko mkubwa kuhusu masuala ya watoto wenye ulemavu. Bado haijathamini na kutambua elimu kwa watoto wenye ulemavu. Haioni kuwa watoto wenye ulemavu wanaweza kupata maarifa muhimu ambayo yatawafanya waweze kuendesha maisha yao pamoja na kujitegemea katika maisha.

3.3 mapEndEKEzoKuna mambo mawili ambayo yameibuka katika utafiti huu na ambayo yanahitaji maamuzi ya kisera pamoja na kufanyiwa utafiti zaidi.

Kwanza, utafiti huu umegundua kuwa kuna vikwazo vya kimtizamo pamoja na kimazingira ambavyo

Page 33: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

26

vinazuia upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye ulemavu na kwamba tunapaswa kuviondoa ili kuondoa matatizo ya kielimu yanayowakabili watoto hawa.

Pili, utafiti huu umebainisha pengo la kitaalumu kuhusu mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu. Hakuna takwimu za kitaifa zinazohusiana na upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye ulemavu na hivyo utafiti wa kina unahitajika ili kupata picha halisi kuhusu hatima ya kielimu ya watoto wenye ulemavu hapa nchini.

Kutokana na maelezo yaliyopo hapa juu, mapendekezo yafuatayo yametolewa kwa ajili ya utekelezaji wa kisera pamoja na utafiti zaidi:

3.3.1 Kwa ajili ya uamuzi wa kisera • Walimu wengi walioshiriki katika utafiti huu walionesha uelewa mdogo kuhusu masuala

yanayowahusu watu wenye ulemavu. Hali hii ilitokea kutokana na ukweli kuwa walimu walikuwa hawana mafunzo yanayohusu watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na elimu jumuishi. Kwa hakika ni walimu wachache sana ambao wamepewa mafunzo kuhusu elimu maalumu. Kuna haja ya kuwa na mipango ya muda mrefu inayolenga kuwapatia walimu mafunzo kuhusu namna ya kufundisha watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na elimu jumuishi. Katika mpango wa muda mfupi, inafaa serikali pamoja na wadau wengine wa elimu kuanzisha mafunzo kwa njia ya semina na warsha katika wilaya na mikoa mbalimbali. Kama mpango wa muda mrefu, kuna haja ya kuingiza katika mtaala wa elimu ya ualimu, mafunzo yanayohusu watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na elimu jumuishi. Na kupeleka walimu wengi zaidi kwenye chuo cha elimu maalumu ili wapate mafunzo yatakayo wasiadia kufundisha kwa tija watoto wenye ulemavu pamoja na wale wenye mahitaji maalumu.

• Karibu shule zote zilizotembelewa wakati wa kufanya utafiti huu ziligundulika kujengwa katika hali ambayo watoto wenye ulemavu hasa wa macho na viungo hawawezi kutumia mazingira hayo. Hii ina maanisha kuwa majengo mengi hata yale yaliyojengwa kupitia MMEM hayakuzingatia mahitaji pamoja na hali za watoto wenye ulemavu. Kwa hiyo, kuna haja katika awamu ya pili ya MMEM kuyarekebisha majengo katika shule ili yafae vilevile kutumiwa na watoto wenye ulemavu.

• Na ni vyema kujenga utamaduni na utashi wa kimaamuzi kwa kuweka mikakati inayoshikika kama vile kujenga majengo muda wote yanayokidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu, na pia kutenga pesa ya kutosha kwa ajili ya vifaa vya watu wenye ulemavu. Kuna haja ya kupitisha sheria itakayolazimisha ujenzi wa majengo kuzingatia pia mahitaji ya watoto wenye ulemavu.

• Utafiti huu umegundua kuwa mahitaji ya watoto wenye ulemavu hayatambuliwi wala kuthaminiwa na wadau wa elimu pamoja na jamii kwa ujumla. Kuna haja ya kutoa elimu kwa jamii pamoja na kuongeza uhamasishaji juu ya umuhimu na hatima ya kielimu kwa watoto wenye ulemavu nchi nzima. Uhamasishaji huu uendane na uboreshaji wa mahitaji ya kiuchumi kwa watoto wenye ulemavu pamoja na wale wenye mahitaji maalumu. Ni muhimu ieleweke kuwa malengo ya MMEM ya kuhakikisha kuwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa hatajafikiwa kama watoto wenye ulemavu hawatapewa fursa ya kupata elimu kama wale wasio na ulemavu. ni utashi tu na uamuzi kivitendo watu wenye ulemavu watafurahia haki yao ya kupata elimu.Tuwajibike kwa pamoja!

Page 34: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

27

marEjEo beyers, C. & hay, j. (2007). Can inclusive education in South (ern) Africa survive the HIV and AIDS

pandemic? International Journal of Inclusive Education, 4, 387-399.

bryman, a. (2006). Integrating quantitative and qualitative research: how is it done? QualitativeResearch, 6, 97-113.

Crawford, C.b. (1994). Full inclusion: One reason for opposition. Retrieved on June 14, 2008 from http://my.execpc.com/~presswis/inclus.html.

richardson, j.T.E.(Ed.) (2003). Handbook of Qualitative research methods for psychology and the socialsciences. UK: BPS Blackwell.

roach, v. (1995). Supporting inclusion: Beyond the rhetoric. PhiDeltaKappan, 77, 295- 2999.

salend, s.j. (2001). Creating inclusive classrooms: Effective and reflective practices (4th ed.). Upper Saddle River, NJ: Merrill.

Thomas, r.m. (2005). Blending qualitative & quantitative research methods in theses and dissertations.Thousands Oaks, California: Corwin Press.

UnEsCo (2000). Inclusion in Education. The participation of disabled learners. Paris, France

UnitedNationsEducational,ScientificandCulturalOrganization(UNESCO)[1994].TheSalamancaStatementandFrameworkforActiononspecialneedseducation. Paris: UNESCO.

UnitedRepublicofTanzania[URT)(2001a).The education and training development programme document. Final Report. Dar es Salaam: Ministry of Education and Culture.

UrT (2001b). Education in a global era: Challenges to equity, opportunity for diversity. Dar es Salaam: Ministry of Education and Culture.

UrT (2007). Basic education statistics in Tanzania: National data, 2007.

UrT (2008). Basic education statistics in Tanzania: National data, 2008.

Page 35: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

28

viambaTishoKiambatanisho 1:

% ya washiriki

Namba ya

katikatiKukataa kabisa

kukubaliBila

maonikuku-bali

Ku-kubali kabisa

Jumla (kukubali kabisa na kukubali

1. Katika elimu jumuishi mahi-taji ya watoto hufikiwa

4 15.5 22.4 9.3 33.6 17.8 51.4

2. Elimu jumuishi haisababishi tatizo lolote ka-tika ufundishaji

4 6.9 23.4 9.3 34.6 20.6 55.2

3. Naamini wa-zazi wanaunga mkono elimu jumuishi

3 5.0 4.0 28.0 32.0 14.0 46.0

4. Bodi ya shule inaunga mkono elimu jumuishi

4 5.8 14.6 28.2 36.9 14.6 51.5

5. Naamini mwalimu wenzangu wa-naunga mkono elimu jumuishi

4 14.7 18.4 18.4 34.0 17.5 51.5

6. Mchanganyiko darasani hu-boresha mazin-gira ya kujifun-zia darasani

4 10.7 14.6 7.8 42.7 24.3 67.0

7. Msaada wa uongozi ni muhimu

4 5.9 9.8 10.8 47.1 26.5 73.6

8. Wizara ya elimu inaunga mkono elimu jumuishi

3 7.9 10.9 34.7 29.7 16.8 46.5

9. Elimu jumuishi haisababishi matatizo katika ufundishaji

2 28.8 32.4 5.9 23.5 9.8 33.3

Page 36: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

29

% ya washiriki

Namba ya

katikatiKukataa kabisa

kukubaliBila

maonikuku-bali

Ku-kubali kabisa

Jumla (kukubali kabisa na kukubali

10. Wafanyakazi wa shule wa-naunga mkono elimu jumuishi

3 10.9 18.8 23.8 27.7 18.8 46.5

11. Elimu maalu-mu na elimu ya kawaida huunga mkono elimu jumuishi

3 6.0 20.0 28.0 31.0 15.0 46.0

12. Walimu wa-nahitaji ku-pewa mafunzo kuhusu elimu jumuishi

5 1.0 1.0 0.0 20.6 77.7 98.3

13. Walimu na wafanyakazi wengine wako tayari kwa ajili ya elimu jumui-shi

2 39.2 37.3 12.7 7.8 2.9 10.7

14. Elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu si muhimu

3 22.5 24.5 7.8 30.4 14.7 45.1

15. watoto wenye ulemavu wako tayari kusoma na wenzao wa-sio na ulemavu

4 3.9 9.7 30.1 36.9 19.4 56.3

16. Elimu jumuishi haimwongezei kazi ya ziada mwalimu

2 19.4 31.1 9.7 32.0 7.8 39.8

17. Wazazi wamer-idhishwa na elimu jumuishi

3 5.9 14.9 42.6 22.8 13.9 36.7

Page 37: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

30

% ya washiriki

Namba ya

katikatiKukataa kabisa

kukubaliBila

maonikuku-bali

Ku-kubali kabisa

Jumla (kukubali kabisa na kukubali

18. Walimu wanao-fundisha shule maalumu na wale wa elimu shirikishi wote hushirikiana

3 11.7 25.2 27.2 24.3 11.7 36.0

19. Mwalimu mkuu huratibu shu-ghuli za elimu jumuishi

3 18.4 31.1 25.2 19.4 5.8 25.2

Kiambatanisho 2: matokeo kutokana na mchanganuo wa masuala 19

Umuhimu wa elimu jumuishi Utayari na uungwaji mkono shuleni

1. Mazingira tofauti darasani

huimarisha tendo la kujifunza

2. Elimu jumuishi ni njia bora ya

kufikia mahitaji ya watoto

3. Elimu jumuishi kwa watoto

walemavu siyo muhimu

4. Elimu jumuishi haitasababisha

matatizo yoyote katika

ufundishaji

5. Elimu jumuishi haisababishi

matatizo yoyote katika

ufundishaji

6. Mwalimu mkuu huratibu

shughuli za elimu jumuishi

7. Walimu na wafanyakazi wengine wako tayari kwa elimu

jumuishi

8. Mwalimu mkuu katika shule huratibu shughuli za elimu

jumuishi

9. Walimu wa shule maalumu na wale wa shule za kawaida

hushirikiana

10. Walimu wa shule maalumu na wale wa shule za kawaida

wanaunga mkono elimu jumuishi

11. Naamini wazazi wanaunga mkono elimu jumuishi watoto

wasio na ulemavu wako tayari kusoma na wenzao wenye

ulemavu

12. Bodi ya shule inaunga mkono elimu jumuishi

13. Wafanyakazi wa shule wanaunga mkono elimu jumuishi

14. Wizara ya elimu inaunga mkono elimu jumuishi

15. Uongozi unaunga mkono elimu jumuishi

16. Naamini walimu wenzangu wanaunga mkono elimu

jumuishi

Page 38: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

31

Kiambatanisho3:Asilimiayawatotowalioshirikikatikautafitinakukubalianaamakutokubaliananamaelezo kuhusu watoto wenye ulemavu

% ya Washiriki

Namba ya kati-kati

Kukataa kabisa

kukataa katikati kukubaliKu-

kubali kabisa

Jumla (kukubali kabisa na kukubali

1. Ningefurahi kuwa na rafiki mwenye ulemavu

5.0 7.8 5.2 7.3 25.2 54.5 79.7

2. Siwahurumii watu wenye ulemavu

1.0 68.3 24.0 2.2 1.5 4.0 5.5

3. Ningefurahi kama mtoto mwenye ulemavu angeni-karibisha kwao

5.0 1.9 1.9 5.0 30.7 60.5 91.2

4. Ningefurahia kumkaribisha mtoto mwenye ulemavu nyum-bani kwetu

5.0 1.7 1.1 2.8 27.7 66.6 94.3

5. Ningependa ku-cheza na mtoto mwenye ulemavu nyumbani kwao

5.0 1.6 2.7 5.1 32.5 58.0 90.5

6. Ningependa kum-karibisha mtoto mwenye ulemavu katika sherehe yangu

5.0 1.5 0.6 3.1 29.3 65.4 94.7

7. Ningeahirisha likizo yangu ili kumsindikiza mtoto mwenye ulemavu

4.0 5.8 9.0 20.6 27.2 37.5 64.7

8. Ningejisikia vibaya iwapo mtoto mwenye ulemavu angenikaribisha katika sherehe ya siku yake ya kuza-liwa

5.0 14.9 9.0 5.5 15.3 55.3 70.6

9. Ningefurahia kuishi pamoja na mtoto mwenye ulemavu

5.0 2.7 1.3 3.6 26.7 65.7 92.4

Page 39: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

32

% ya Washiriki

Namba ya kati-kati

Kukataa kabisa

kukataa katikati kukubaliKu-

kubali kabisa

Jumla (kukubali kabisa na kukubali

10. Ningempenda rafiki mwenye ulemavu kama walivyo marafiki wengine

5.0 10.9 6.6 6.5 16.0 60.0 76.0

11. Nisingemkimbia mtoto mwenye ulemavu

5.0 4.9 3.7 3.3 21.3 66.8 88.1

12. Ningependa kuishi na mtoto mwenye ulemavu jirani yangu darasani

5.0 3.6 2.3 5.1 33.2 53.9 87.1

13. Ningetoa taarifa zangu za siri kwa mtoto mwenye ulemavu

4.0 4.5 4.9 16.3 27.7 46.5 74.2

14. Nisingeogopa iwa-po mtoto mwenye ulemavu angekaa jirani yangu

5.0 7.9 3.8 5.1 25.0 58.3 83.3

15. Ningejisikia vizuri kufanya kazi za darasa na mtoto mwenye ulemavu

5.0 6.1 3.5 4.4 26.0 60.0 86.0

16. Nitamfariji mtoto mwenye ulemavu anayetaniwa da-rasani

5.0 3.0 1.6 1.5 25.6 68.3 93.9

17. Ningemtambuli-sha mtoto mwe-nye ulemavu kwa marafiki zangu

5.0 8.0 6.0 4.9 17.6 63.4 81.0

18. Watoto wenye ulemavu wanahi-taji furaha kama watoto wengine

3.0 25.5 19.7 33.2 10.0 11.6 21.6

19. watoto wenye ule-mavu wanajihuru-mia kutokana na hali yao

2.0 30.7 21.6 34.2 5.8 7.7 13.5

Page 40: Watoto wenye Ulemavu wana Fursa ya Kupata Elimu?hakielimu.org/files/publications/document132Watoto_ulemavu.pdf · ikipewa kipaumbele katika sekta ya elimu, sambamba na elimu ya awali,

33

% ya Washiriki

Namba ya kati-kati

Kukataa kabisa

kukataa katikati kukubaliKu-

kubali kabisa

Jumla (kukubali kabisa na kukubali

20. watoto wenye ulemavu wana fu-raha kama watoto wengine

3.0 15.4 12.6 29.1 15.7 27.2 42.9

21. watoto wenye ule-mavu hawahitaji msaada

1.0 74.2 20.5 2.5 1.3 1.6 2.9

22. watoto wenye ule-mavu hawahitaji mafunzo toka kwa watu wazima

1.0 61.9 24.6 8.1 3.3 2.2 5.5

23. Siwahurumii watoto wenye ule-mavu

5.0 17.3 12.6 4.1 14.8 51.3 66.1

24. sijisikii vibaya pale ninapomwona mtoto mwenye ulemavu

5.0 3.7 3.1 3.7 24.3 65.2 89.5

25. siogopi kukaa karibu na mtoto mwenye ulemavu

5.0 4.0 3.1 5.9 21.6 65.4 87.0

26. nitajua cha kum-wambia mtoto mwenye ulemavu

5.0 5.2 4.0 14.1 20.7 56.1 76.8