Top Banner
mbegu bora za soya Uzalishaji wa Kwa maelezo zaidi, wasiliana na: Maruku Agricultural Research Institute, S.L.P. 127, Bukoba, Tanzania Simu/Fax +255 732 983258; Barua pepe: [email protected]
8

Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

Dec 28, 2019

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

1

mbegu bora za soyaUzalishaji wa

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:Maruku Agricultural Research Institute, S.L.P. 127, Bukoba, TanzaniaSimu/Fax +255 732 983258;Barua pepe: [email protected]

Page 2: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

2

1. Kuchagua mbegu

Chagua mbegu bora zinazoshauriwa kitaalamu (k.m. Uyole soya 1 na Uyole soya 2).

Fahamu uotaji wa mbegu kwa kupanda mbegu 30. Iwapo mbegu 25 au zaidi zitaota, mbegu hizo zinafaa kupandwa.

Page 3: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

3

2. Kutayarisha eneo

Ondoa majani na magugu yote.

Tifua eneo kwa kina kirefu.

Sawazisha eneo vizuri ili kulaininisha udongo.

Eneo liwe na udongo wenye kima kirefu na usiotuwamisha maji.

Page 4: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

4

4. Kuweka vichochezi vya rutuba

Changanya mbegu na vichochezi vya rutuba ya udongo kulingana na maelezo yaliyoko kwenye pakiti ya vichochezi vya rutuba ya udongo.

Tandaza mbegu zilizochanganywa na vichochezi vya rutuba ya udongo kwenye turubai au karatasi safi la nailoni kwenye kivuli kwa muda wa dakika 20 hadi 30.

Unashauriwa kupanda mbegu zote zilizochanganywa na vichochezi vya rutuba ya udongo siku moja.

Page 5: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

5

4. Kupanda

Panda mapema mara tu mvua inaponyesha.

Tumia mfuko mmoja wa DAP ya kilo 50 kwa kila ekari (nusu kizibo cha soda kwa kila shimo).

Tia DAP kwenye shimo la kupandia halafu changanya na udongo ili kuondoa athari za mbolea kwenye uotaji wa mbegu.

Page 6: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

6

5. Kutunza shamba

Punguza mimea ibaki 2 kama iliyoota ni zaidi ya mimea 2.

Ng’oa mimea yote ambayo haifanani na mbegu zilizopandwa.

Tumia Folicur ili kuzuia ugonjwa wa kutu ya majani.

Madawa aina ya Cypermethrin au Lambda (Karate) huzuia wadudu wanaoshambilia majani ya mimea (leaf rollers na leaf eaters).

Page 7: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

7

6. Kuvuna

Vuna mimea mara tu mifuko ya maharage ya soya yanapogeuka kuwa ya rangi ya kahawia.

Weka mimea iliyovunwa kwenye jua kwa siku 3-5 kutegemea kiasi cha jua.

Ondoa mbegu kwenye mimea kwa kupiga mimea kwenye turubai safi lililotandazwa chini. Pepeta kuondoa uchafu kisha chambua mbegu ili kuondoa mbegu zilizoharibika na zenye magonjwa.

Page 8: Uzalishaji wa mbegu bora za soya - Home | Cabi ASHCafricasoilhealth.cabi.org/wpcms/wp-content/uploads/2014/05/207-ARI-Maruku-Soybean...Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora

8

Kwa kufuata kanuni bora za uzalishaji mbegu bora za soya utapata mavuno kiasi cha tani 2 hadi 3 kwenye hektari 1 (ekari 2½ )

7. Kuvuna na kuhifadhi

Kausha mbegu kwa kufikia kiwango cha unyevu wa 11-12%. Kiasi hiki cha unyevu itafikiwa iwapo ukiuma mbegu kwa meno zitakuwa ngumu na kutoa sauti.

Weka mbegu za soya kwenye mifuko ya nailoni (mifuko ya salifeti) inayopitisha mwanga.

Hifadhi magunia ya mbegu za soya juu ya chanja kwenye chumba chenye hewa ya kutosha kisichopitisha jua.