-
UFUNUO 1• Picha za Hukumu na Tumaini
• Mtu akigeukia kitabu cha Ufunuo kando ya vitabu vingine vyote
vya Agano Jipya, ataona kama anaingia kwenye nchi ya kigeni. Badala
ya masimulizi na nyaraka zenye maelezo ya wazi ya mambo halisi na
maagizo, anaona kitabu kilichojaa malaika, baragumu, matetemeko ya
nchi, wanyama, majoka, na mashimo ya kuzimu
• Yapo yanayoeleweka kwa urahisi, mf Yohana anapotambulisha
kitabu 1:9
• Maelezo mengine yanaweza yakawa rahisi, 6:12-17 na mengine
magumu 11:1-10, kuelewa.
• Ni kitabu kunachogawa wakristo katika makundi ya ”ufafanuzi” •
Vipo vitabu vingi vya ufafanuzi wa siri za Ufunuo, • Katika somo
hii tutazingatia Exegeses, • Tunataka kufahamu yanayofahamika •
Tutatoa ashauri ya jinsi ya kusoma kitabu hiki bila kupotea….
-
UFUNUO 2
• Muundo wa kitabu cha Ufunuo • Waraka, barua = Yohana
anawaandikia makanisa • Unabii = Inasema juu ya mambo yatakayokuja,
na pia
yaliyokuwepo kwa wakati wake. Rejea zinazotumika ni za wakati
ule.
• Ufunuo [apokalypsis] = kufunua siri, lakini pia kutokana na
yanayoeezwa imepata maana ya ”mambo ya mwisho pia”
• Ni muhimu sna kutambua na kufahamu aina hii ya maandiko kama
tutaweza kufaidi kitabu cha Ufunuo.
-
UFUNUO 3• Ufunuo kama andiko ya mambo yajayo [apocalypsis] 1
• Ni moja kati ya maandiko ya ”ki-apocalyptic” inayofahamika na
iliyoandikwa kati ya mwaka 200kK hadi 200 bK. Ingawa yalikuwa ya
namna nyingi pia yapo kadhaa yanayofanana nayo ni;
• 1. Misingi yake tunaipata katika AK na hasa kwenye vitabu kama
vya; Ezekieli, Danieli Zekaria na sehemu ya Isaya. Yanahusu mambo
ya mwisho na jinsi Mungu atakavyotenda katika ushindi kwa kukomesha
uovu.
• 2. Mwandishi ameambiwa aandike (1:9) si kama vitabu vya
kiunabii ambavyo hasa ni rejea ya utabiri ya nabii fulani.
• 3. Lugha ni ya maono, ndoto, siri mafumbo a mifano. waandishi
mara nyingi walitumia jina la bandia ya mtu maarufu wa zamani, na
kitabu kilidai kuwa sasa muda wa kufunuliwa imeingia ndiy o maana
linaandikwa. Hao wazee waliyaona hayo zamani lakini hawakuruhusiwa
kuyafunua hadi wakati wake, wakati ambayo ulikuwa umeingia.
-
UFUNUO 4• Ufunuo kama andiko ya mambo yajayo [apocalypsis] 2
• 4. Lugha ya mifano tumezoea sana tunaposoma Biblia na Yesu
mwenyewe alitumia mifano sana, lakin mifano yake yalihusu
yanayoeleweka. Mt 5:13, Lk 17:37, Hos 7:11, Hos 7:8. Lakini picha
na mifano ya Ufunuo ni tofauti. Ingawa tunatambua kwa mfano simba,
akini hapa anaunganika na kiumbe kingine na matokeo yake ni mambo
ya ajabu.Uf 13:1, Uf 12:1, Uf 9:10.
• 5. Kwa vile viliandikwa moja kwa moja, viliandikwa kwa muundo
wa makusudi. Walipanga maandiko yao katika vikundi . Walikuwa na
”michezo ya mahesabu”. Utakuta kazi ilipendeza sana. Mara kwa mara
makundi haya yanapowekwa pamoja, huonyesha kitu (k.m., hukumu) bila
kulazimika kupendekeza kuwa kila picha iliyojitenga huifuata ya
awali.
• Ufunuo wa Yohana unafuata taratibu hizo isipokua kwa sehemu
moja. Anayeandika anatajwa nahatumii jina la bandia.
Anajitambulisha kwa wasomji. (Sura ya 2-3), halafu aliambiwa
kuandika na aliambiwa asifiche maandishi haya sababu mda unakaribia
(22:10)
-
UFUNUO 5• Ufunuo kama unabii
• Sababu moja yake ya kuacha kutumia jina la mtu mwingine
inaweza kua kwamba aliishi katika ”tayari ila bado”. Anafahamu
kwamba siku za mwisho zimeanza kupitia kazi ya Yesu. Kitu ambayo
ilithibitisha kuwa aliishi katika karne mpya ilikua kwamba Roho wa
Bwana alikua amemiminwa juu ya watu. Wengine waliokuwa wameandika
vitabu kama vyake walikuwa wakiishi katik enzi ya ‘‘Roho
aliyezimishwa’’ . Yeye alikuwa ”katika Roho” wakati alipopewa
ufunuo huo (1:10-11)
• Anazungumzia kitabu chake kama unabii huo (1:3; 22:18-19)
anasema kuwa yeye na kanisa linaloteswa kwa ajili ya ushuhuda wa
Yesu (1:9; 20:4) ambao ushuhuda huo ni ”Roho wa unabii” (19:10)
Bila shaka hiyo ilithibitisha kua Roho wa unabii alikua
ameshawasili.
• Ufunuo inatumia lugha isiyoeleweka kwa urahisi, lakini pia
lugha ambayo inaeleweka bila matatizo, lugha ambayo tumezoea kuiona
katika maandiko ya manabi katika Agano la Kale. (Na pia katika siku
zetu)
-
UFUNUO 6
• Ufunuo kama Waraka / Barua • Kitabu kimeandikwa kwa sababu ya
hali fulani, imeandikwa kwa
makanisa waliyo na mahitaji ya kusikia ujumbe huo na wanaishi
katika mazingira fulani. Anawasalimu kama vile tulivyozoea katika
barua zingine ya Biblia. (1:4-7; 22:21)
• Kwa hiyo ni muhimu kujua mazingira na historia ya wakati ule,
kusudi tufahamu hali iliyokuwepo na kwa jinsi hii tuelewe ujumbe wa
maandishi.
-
UFUNUO 7• Umuhimu wa exegeses 1 • Tunarudia mafundisho ambayo
tumeshayapitia lakini tunalenga
katika kitabu chetu cha sasa. Kanuni chache cha *exegeses. • 1.
Kazi ya kwanza ni kujaribu kugundua kusudi ya mwandishi,
pamoja na Roho Mtakatifu. Kusudi la kuandika kitabu cha ufunuo.
Kuna ujumbe gani ambao anapenda kuwapatia makanisa ya Asia ndogo ?
Lazima tutegemee kwamba wao waliweza kufahamu barua waliyoipata !
Inawezekana kwao haikuwa kazi sana maana waliishi wakati ule na pia
walikua wamezoea lugha ya namna ile.
• 2. Ufunuo nikitabu kinacho tabiri, kwa hiyo inaweza ikawa na
maana ”ya pili” ambayo imepewa na Roho Mtakatifu, ambayo siyo
rahisi sana kuuelewa, hata Yohana na yalemakanisa inawezekan
yalipata shida na machache ya kitabu hiki. Lakini *exegeses
haihusiki na ujumbe uliyofichika, inahusika na yale yanayoeleweka
kabisa. Hermeneutics inahusika na yale ya mafumbo.
-
UFUNUO 8• Umuhimu wa exegeses 2
• 3. Kuweka Ufunuo katika *analojia na vitabu vingine vya agano
jipya siyo vizuri kwa sababu hatuelewi kama Yohana alikuanavyo
wakati alipoandika Ufunuo. Tunaweza kutambua lugha inayotumika
katika Ufunuo tukisoma baadhi ya maandiko ya Agano la Kale, lakini
haitusaidii katika utafsiri inatufanya tu tutambue aina ya lugha
inayotumika. Lazima tutafute ndani ya kitabu chenyewe kama tunataka
kupata ”ufunguo wa ufumbuzi” wa kitabu cha Ufunuo.
• 4. Mifano au picha zinazotolewa ni tatizo nyingine pia.
Inawezekana mawazo mengine ameyapata katika Agano la Kale, lakini
pia katika vitabu vigine ambavyo vilipatikana wakati ule. (Kumbuka
tunaongelea lugha tu siyo ujumbe) Kwa mfano: Ukimwandikia mchumba,
au ukiandika barua ya kiofisi utakuta lugha inayotumika ni tofauti
sana) Hata kama ametoa picha zingine katika maandiko mengine
haileti uhakika kwamba anakusudia kuipatia maana ile ile.
Inawezekana kwamba yeye na Roho Mtakatifu wameweza kubadili maana
kidogo.
-
UFUNUO 9• Umuhimu wa exegeses 3.
• Picha / mifano mengine ni kama tunayatambua kutoka AK, na pia
inaonekana kwamba tafsiri yake ni sawa sawa na AK. Kwa mfano ;
”Mnyama anayetoka baharini” maana yake ni kwamba utakuja utawala
fulani, siyo mtu ni nchi. Lakini mifano mengine yanapishana, Simba
wa Yuda anageuka kua mwana kondoo (5:5-6) Mwanamke wa sura ya 12
anasimamia kitu kizuri lakini wa 17 ni mbaya.
Baadhi ya mifano
tunapewa tafsiri yake katika maandishi yenyewe. ”Vinara vya taa
saba” (1:12- 20) ni kanisa, Joka wa sura ya 12 ni Ibilisi. Yohana
anapotupatia tafsiri ya picha fulani hiyo inakua msingi wetu katika
kuelewa analolisema. (1:17-18; 1:20: 12:9; 17:9; 17:18)
Ni muhimu
koelewa hizo picha kama ujumla fulani, siyo kuchambua picha moja
moja kwa njia ya *kialegoria. Kidogo ni kama mifano ya kwenye
Injili, ni muhimukuelewa point iko wapi. Mifano na picha zinatumika
kwa kuongeza ujumbe tuweze kuipata sawa sawa
• 5. Ufunuo siyo kitabu ambayo inaeleza jinsi itakavyokua siku
za mwisho kwa mpango wa ”A mpaka Z”. Inayokusudi nyingine. Ujumbe
wake hasa ni kutufahamisha kwamba Mungu anaye ”control” katika
historia na katika yatakayokuja na wakati tuliyonao. Ataokoa
waliyowake na atahukumu dunia.
-
UFUNUO 10
• Mazingira ya kihistoria • Tuko pale tena...tufanyeje ???? •
Anza kwa kusoma kitabu chote mpaka unapoanza kukipatapata. • Rudia
tena chukua notes na referenses ambayo yanaweza kuwa ya
maana (Kazi hii tutaipitia zaidi wakati wa kusoma ufunuo wa
Yohana)
• Mazingira ya maandishi • Lazima kuangalia maandiko yote katika
ujumla,ni hatari kuchambua
fungo fulani halafu kuipatia tafsiri ya peke yake.. • Kila fungo
ni ”block” katika jengo nzima. Kuondosha ”block” moja
hapa na nyingine pale na kuamini ndipo tafsiri kamili
itapatikana. Lazima kuangali lote.
• Kumbuka Ufunuo ni barua pia yenye mtiririko wa habari. Tofauti
na vitabu vya manabii wa AK
-
UFUNUO 11• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 1 • Kazi ya
kwanza haina tofauti na vitabu vingine vya Biblia, ni lazima
tuelewe ujumbe wa wapokeaji
wa barua wakati ule. Kitabu cha Ufunuo ni kitabu cha kiunabii
kwa hiyo pia tunaelewa kwamba ili husu siku zao za mbele.
• Mara nyingi inahusu ”siku za mbeke za karibu” hiyo kwetu
itakua ni historia. (Kama vile Yeremia alivyotabiri kweli Yuda
wakawa mateka, na pia kama vile Yohana alivyonena pia Warumi
walipewa hukumu ya mda)
• Tunapoona matokeo ya maneno waliyonena, na yanapothibitishwa
katika maandiko ya kihistoria inakua ni rahisi kuelewa
alichokitabiri. Tunaweza kuangalia sababu za hukumu na kujihadhali
tusije tukahukumiwa kwa sababu hizo. Yanatufundisha kwamba Mungu
anahukumu dhambi, na kwamba atahukumu kila nchi inayowafanyia
wakristo ,watu wake, mabaya.
• Pia tunajifunza kwamba ufuasi siyo kitu rahisi lazima tukubali
msalaba wakati tunapomfuata Yesu wetu. Hatujaahidiwa ushindi juu ya
kifo na mateso baali tumeahidiwa ushindi kupitia kifo na
mateso.
• Hiyo inafanya Ufunuo kua kitabu ambacho inawapa moyo wakristo
wanaoishi katika mateso mbali mbali kwa ajili ya imnai yao. Inawapa
ahadi kwamba Mungu anayo ”control” juu ya mambo yote. Ameyaona
anajua la kufanya.
• Mafundisho hayo ni muhimu kurudia mara kwa mara mana ni lazima
kanisa liwe linaishi ndani ya ukweli wa namna hii, ukishindwa
kugundua ujumbe huo katika Ufunuo, hakika umeshindwa kupata ujumbe
wowote.
• Lakini pia kuna mengine......na hiyo bila shaka ni tatizo pia.
Mengi yanayohusu wakati ule pia inahusu wakati wa mwisho. Lakini
kuyachambu vizuri siyo rahisi mana yanasukwa pamoja katika
mchanganyiko usiyo chambuliwa. Msaada kidogo tunaweza kupata
tukitumia taratibu zifuatazo:
-
UFUNUO 12• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 2
• 1. Lazima tuelewe kwamba mifano na picha ni mifano na picha
siyo hali halisi. Zinapenda kutuonyesha hali fulani lakini siyo
hali hii katika ukamilifu. Pia inawezekana kua baadhi ya mambo
hayatakiwi kuchukuliwa katika utafsiri zipo tu kama chumwi kidogo.
Kwa hiyo parapanda zile nne zinapolia na kuwakilisha taabu
zitakazokuja. Inawakiloisha taabu ila inaweza ikawa tofauti na
jinsi inavyoelezwa katika kitabu.
• 2. Pia kuna picha zinazo eleza juu au hukumu ambayo itakuja,
na ulazima wakuja kwa hukumu hiyo, lakini haina maana kwamba
itatokea sasa hivi au katika mda wa karibu. Wakati shetani
alipotupwa chini kutoka mbinguni (sura 12), kwa sababu ya kufa na
kufufuka kwa Yesu, alianza vita yake na kanisa. Alifahamu kwamba
mda wake ni mfupi na kwamba una mipaka, lakin haisemi urefu wa mda
wake wala hata yeye hawezi kujua. Sisi tunaelewa kwamba ipo siku
yake ya kufungwa na haachiwi tena, ila hatujui siku wala saa..
-
UFUNUO 13• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 3
• 3. Mifano ambayo inakua na hali ya sasa lakini pia yanakaribia
mambo ya baadaye ni lazima tuweze kuvichambua katika miwili, hata
kama waliyoisoma mara ya kwanza walitegemea kwamba yote yatatokea
kwa wakati wao. Picha hizo zinasimulia hukumu na wokovu utakaokuja
na pia zinakua na hali ya ”sasa ila baado” ndani yake. Lakini
hakuna kanuni zakufuata katika kuelewa vizuri ipi ni ipi, hatuwezi
kusema kwa uhakika hiyo ni siku ya mwisho au hiyo itatokea wakati
tungali hapa.
• Kitu muhimu ni kujaribu kujihadhali sana tusije tukakwama
katika kujaribu kuelewa nini itatokea sasa na nini ni la baadaye.
Kitabu hiki haikuhusika na vita vya Ruanda, Burundi na Zaire. Wala
haikutaja ukommunisti, uislamu na sijui nini ambayo sisi tunaweza
kuliiingiza katika kufafanua kwetu. Wala haituletei ratiba ya siku
za mwisho....
-
UFUNUO 14• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 4
• 4. Ingawa kuna sehemu katika Ufunuo ambayo mpaka leo
haijatokea wala kufafanuliwa kihakika, hatuja pewa vifaa vya
kutumia tunaposoma juu ya mambo haya. Hapo AJ inaonyesha wasi wasi
kidogo au kuyumba. Mpinga Kristo ni mfano mmoja ambao inatupa
shida. Paulo anapomsema anaonekana ni mtu binafsi (2Thess 2:3-4) na
katika Ufunuo 13-14 anajitokeza kama kaisari wa Roma. Katika mifano
yote hio miwilini kama atajitokeza kwa siku za mbele. Lakini katika
1Yoh ni kama inaletwa tafsiri nyingine, inaweza kua mtu yeyote yule
ambaye anaharibu kazi ya kanisa kwa ndani. Sasa tumweleweje huyo
Mpinga Kristo.
• Katika historia yetu watawala wengi wametajwa kama wao ndio
mpinga kristo; Hitler, Idi Amin na wengi wengine. Na kwa kweli wote
hao wanaweza wakawa tafsiri mojawapo ya Mpinga Kristo, na inaweza
kua tafsiri juu ya neno kwamba wapinga kristo wengi watajitokeza
(1Yoh 2:18).
• Lakini je! atakua mtawala wa ulimwengu wote ambaye ataongoza
mambo yote ya dunia katika siku za mwisho, je, ni hivyo
tutakavyoelewa Ufunuo 13-14? Siyo lazima ! Lakini pia inawezekana.
Kwa vile A.J. halina msimamo kamili itabaki makisio to hakuna
uhakika...
-
UFUNUO 15
• Maswali ya kihermeneutics (Ufafanuzi) 5 • 5. Mifano na picha
ambazo ni za siku za mwisho kabisa, lazima
tuziruhusu kubaki pale pale kwa mfano: 11:15-19, na 19:1-22:21,
zinahusika na wakati wa mwisho kabisa. Sehemu hizo ni lazima
ziangaliwe kama kipindi ambacho baado halijatufikia katika hali
yoyote.
• Kama vile sura za kwanza katika Biblia zinahusu Mungu na
uumbaji kitabu cha mwisho inahusika na mwisho wa kila kitu hapa
duniani. Tunaona kwamba Mungu atayamaliza yote kama vile
alivyokusudia kila kitu kwa mda wake na mpango wake. Kuelewa hiivyo
inatupa moyo wa kuvumilia katika yote tunayoyapata, kama vile
ilivyowafariji waliyosoma Ufunuo wakati ule.
• Mpaka hapo tutaishi katika ”sasa ila baado” ambapo ”sasa yetu”
ni kwamba tunasoma maneno yake Mungu na kuyafuata, pamoja nakupokea
yale yote anayotupatia. Lakini tunategemea kwamba kutakuja siku
moja ambayo mambo mengi yatakua tofauti ”Hawatakua na haja ya
kufundishana....maana watanijua” (Jeremia 31:33)