[Type text] Page 1 UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARA KWA KUONGEZA PATO LA FAMILIA MUZEZA DISTRICT COUNCIL KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI KIBIASHARA
[Type text] Page 1
UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI NA CHOTARA
KWA KUONGEZA PATO LA FAMILIA
MUZEZA DISTRICT COUNCIL
KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI KIBIASHARA
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 2
UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI
1. Utangulizi
2. Banda bora la kuku
3. Njia za ufugaji wa kuku chotara
4. Utunzaji wa kuku chotara
5. Utunzaji wa vifaranga
6. Utengenezaji wa chakula cha kuku
7. Magonjwa ya kuku
8. Masoko
UTANGULIZI
Asilimia 75% ya Watanzania ni wafugaji wa kuku wa asili. Kila mtanzania
anaweza kufuga kuku bila kujali hali ya kipato kwa kuwa kuku wa asili
wanavumilia magonjwa na wanakubali mazingira yote ya ufugaji. Kuku wa asili
wamekuwa wakifugwa holela bila kuzingatia kanuni bora za ufugaji wa kuku
hivyo kupelekea mazao duni na hata kupungua kwa idadi ya kuku wa asili.
Hivyo ipo haja ya kuboresha mazingira na kufuata kanuni za ufugaji bora.
Lengo ni kuongeza uzalishaji wa mayai kutoka mayai 60 hadi mayai 100 kwa
kuku kwa mwaka na kuongeza uzalishaji wa nyama ya kuku kutoka kilo 1 hadi
kilo 2.5 kwa kuku kwa kipindi cha miezi sita.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 3
SURA YA KWANZA.
BANDA LA KUKU
Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Banda bora la
kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
Lijengwe kwenye sehemu ambayo inaweza kufikika kwa urahisi.
Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa
hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na
wanyama hatari, Zingatia kanuni za ufugaji bora ili kujihakikishia usalama
wa chakula na
kujiongezea kipato.
Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika
kwa urahisi.
Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali
na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala
Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu
ya kulelea vifaranga
Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo
vya chakula na maji
Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa
wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 4
Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa
na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.
Sehemu nzuri ya kujenga banda ni:
Ile inayofikika kwa urahisi
Ile yenye mwanga wa kutosha
Isiyo na upepo mkali
Isiyoruhusu maji kusimama au kuingia ndani.
Sifa za banda
1. Sakafu – inaweza kuwa ya saruji, mbao au iliyosiribwa kwa udogo
2. Isipitishe unyevu, isiwe na nyufa na iwe rahisi kusafishwa
Ukuta
Ukuta lazima uwe imara ili kuweza kushikilia paa,
Ukuta unaofaa uwe wa matofali ya saruji au matofali ya kuchoma , pia
kuna uweaekano wa kutumia miti, fito, mabanzi na mabati. Kama
ukitumia mabanzi au fito ni vyema kuondoa magamba na kupaka dawa
kwa ajili ya kuzuia mchwa.
Katika sehemu za joto, ukuta ujengwe mita moja kutoka chini kwenda juu
na sehemu iliyobaki izibwe kwa kutumia wavu ili kuingiza hewa na kuzuia
wanyama wakali, sehemu za baridi ukuta ujengwe kutoka chini hadi juu
ilimradi kuwe na madirisha ya kutosha kupitisha hewa
Ni muhimu kusiriba ukuta ili kuzuia nyufa vile vile inarahisisha kusafisha
nakunyunyiza dawa za kuzuia wadudu
Paa:
Liwe imara na lisilovuja
Liezekwe kwa kutumia mabati , nyasi, madebe, makuti au vigae
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 5
Vipimo vya banda
Kuku wanahitaji nafasi tofauti kutegemea na umri aina na njia za ufugaji
Kwa muda wa majuma manne ya mwanzo eneo la mita mraba1 au eneo la
hatua moja linatosheleza vifaranga 16. Banda lenye eneo la mita mraba 16
linaweza kulea vifaranga 320 hadi majuma 4. Baada majuma manne ya umri
nafasi iongezwe.
Idadi ya kuku katika eneo la mita za mraba.
Aina ya kuku
Njia za ufugaji Kuku wa mayai Kuku wa nyama
Sakafu ya matandazo 3 - 4 6 - 8
Ufugaji wa kwenye
vichanja maalumu vya
chuma
8 - 12 15 - 25
Vifaa vinavyohitajika katika banda la kuku:
Vyombo vya maji – maalumu vya plastiki au bati vya kuweka maji kwa ajili
ya kuku, unaweza kutumia sahani na kopo jaza maji kwenye kopo kisha
lifunike na sahani na ligeuze hii ni kwa ajili ya vifaranga, kwa ajili ya kuku
wakubwa unaweza kutumia sufuria, vungu, madebe au karai.
Vyombo vya chakula- kwa ajili ya vifaranga ni chano za mayai, makasha
yaliyobebea vifaranga na vyombo maalumu vya bati au plasitiki. Kwa
kuku wakubwa ni vile vyombo maalumu vilivyotengenzwa kwa mbao au
bati.
Viota – kuna aina mbili za viota ambavyo vinatumika kwa ajili ya kutagia
mayai
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 6
1. aina ya kwanza ni kiota cha kuku mmoja mmoja , kila kiota
kinaweza kutumiwa na kuku watano kwa zamu. Vipimo vya
kila kiota viwe SM 30 upana, SM 30 urefu na SM 35 kina,
upande wa mbele uwe wazi lakini SM 10 za kwanza kutoka
chini zizibwe kwa mbao
2. Aina ya pili ya kiota cha jumla, kinaweza kutumiwa na kuku
watano hadi sita kwa wakati mmoja vipiomo view SM 30
upana , SM150 urefu na SM55 kina.
Sifa za kiota
Kiwe na giza kiasi, giza hupunguza tabia ya kuku kula
mayai na kudonoana
Kiwe kimewekwa mahali ambapo ni rahisi kwa kuku
kuingia na kutoka.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 7
SURA YA PILI
NJIA MBALIMBALI ZA UFUGAJI WA KUKU
Kuku huweza kufugwa kwa kutumia njia mbalimbali kutegemea ukubwa wa
eneo na uwezo wa mfugaji, kuna njia tatu za ufugaji wa kuku nazo ni :
Ufugaji huria- kuku huachwa wenyewe wajitafutie chakula na maji ,
ufugaji huu hutumika sana kwa kuku wa asili na hakuna utaratibu wowote
wa kuwapatia chakula cha ziada
Faida-
haina gharama kubwa
Kuku wanapata mzoezi yakutosha
Hasara-
Huharibu mazingira, hula mazao hasa nafaka
Ni rahisi kuku kuathriwa na wezi, wanyama wakali au hali
mbaya ya hewa.
Ni rahisi kuambukizwa na kusambaza magonjwa
Wanaweza kutaga mayai vichakani
Ukuaji wake ni hafifu
Kuna uwezo wa kuhamia nyumba nyingine.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 8
Ufugaji ndani ya uzio- huu ni ufugaji unaofanyika katika sehemu
iliyozungushiwa uzio . Kuku hujitafutia chakula chao wenyewe na kuna
utaratibu wa kuwapaokatia maji na chakula cha ziada. Ndani ya uzio
kuna banda ambalo kuku wanaweza kulala, kuingia na kutoka wakati wa
mchana. Ufugaji huu unatumika kwa kuku chotara na kuku wa kisasa.
Faida-
Gharama yake ni nafuu
Ni rahisi kuelewa kiwango cha utagaji na utotoaji
wao
Si rahisi kuku kuathiriwa na wezi, wanyama wakali au
hali mbaya ya hewa
Si rahisi kuambukizwa magonjwa mbali mbali
Hasara-
Gharama za ujenzi wa uzio na vifaa kwa ajili ya
chakula na maji
Njia hii inahitaji eneo kubwa
Ufugaji ndani ya Banda – kuku hufugwa ndani ya banda wakati wote na
hupatiwa maji na chakula. Njia hii hutumika zaidi kwa ufugaji wa
kibiashara
Faida
Kuku wengi huweza kufugwa katika eneo dogo
Nirahisi kuwahudumia
Sio rahisi kuambukizwa magonjwa kutoka nje
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 9
Wanakuwa na usalama wa uhakika
Hasara Gharama za mwanzo zinahitaji mtaji mkubwa
Ugonjwa unapotokea ni rahisi kuambukizana
Ufugaji huu unahitaji utaalamu wa kutosha
SURA YA TATU
UTUNZAJI WA KUKU WA ASILI/CHOTARA
KUCHAGUA KUKU BORA JIKE WA ASILI WA KUFUGA.
Aina za kuku wa asili wanaopatikana hapa nchini ni pamoja na Kuchi (Kuza),
Poni (Kishingo), Njachama, Kinyavu, Mbuni na Tongwe (Msumbiji). Mfugaji
anaweza kuongeza uzalishaji kwa kuchagua kuku mwenye sifa zifuatazo:-
Uwezo wa kutaga mayai mengi (kati ya 15-20) katika mzunguko mmoja
wa utagaji (Jedwali Na 10),
Uwezo wa kuatamia na kuangua vifaranga wengi,
Uwezo wa kustahimili magonjwa,
Anayetoka maeneo yasiyo na magonjwa; na
Umbo kubwa na kukua haraka.
MASUALA YA KUZINGATIA WAKATI WA KUMCHAGUA KUKU MTAGAJI WA
KIENYEJI.
Viungo vya mwili (Sifa)
Macho
- Maangavu, yenye wekundu kwa mbali na makubwa yamejaa kwenye soketi
za macho.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 10
Mdomo
- Wenye rangi ya njano kwa mbali Kisunzu/upanga
- Chekundu, laini, kimelala kidogo upande na kinang’aa Shingo
- Iliyosimama Umbali kati ya kidari na nyonga
- Upana wa vidole 3-4 vya mpimaji Upana wa nyonga
- Upana wa vidole 3 vya mpimaji
KUCHAGUA KUKU BORA WA KISASA.
Kuku bora wa kisasa kwa ajili ya mayai au nyama ni mwenye sifa zifuatazo:-
Uwezo wa kuanza kutaga wakiwa na umri mdogo (miezi 5 - 6)
kutegemeana na koo,
Umbo kubwa na anayekua haraka (kilo 1.5-2.0 kwa kipindi cha wiki 8-12)
kutegemea na koo kwa kuku wa nyama,
Anayetaga mayai mengi (250 au zaidi) kwa kuku wa mayai kwa mwaka;
na
Awe na uwezo wa kutaga katika umri wa miezi 6 - 8.
KUCHAGUA JOGOO BORA WA MBEGU.
Jogoo wa mbegu anatakiwa awe na sifa zifuatazo:
Achaguliwe kutoka kwenye koo zenye sifa ya kutaga mayai mengi,
Mrefu, umbo kubwa, miguu imara na yenye nguvu,
Awe machachari, ushawishi kwa mitetea na ari ya kupanda; na
Uwezo wa kupanda akiwa na umri wa miezi 7 – 10.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 11
MAYAI KWA AJILI YA KUTOTOA VIFARANGA.
Uchaguzi wa Mayai
Mayai kwa ajili ya kutotoa vifaranga yawe na sifa zifuatazo:-
Yaliyorutubishwa na jogoo,
Yasiwe na nyufa,
Yasiwe na maganda tepetepe,
Yasiwe na kiini kilichovunjika,
Yawe na ukubwa wa wastani; na
Yasiwe yamekaa zaidi ya wiki 2 baada ya kutagwa.
Wastani wa jogoo mmoja kwa majike kumi (10).
KUCHAGUA MAYAI YA KUANGULIWA.
Mayai yanayofaa kuanguliwa yawe na ukubwa wa wastani, yasiwe na nyufa,
yasiwe ya mviringo kama mpira, yasiwe na uchafu, mayai mazuri ni yale
yaliyotagwa na kuku aliyepandwa na jogoo.
UANGUAJI WA VIFARANGA WA ASILI.
Kwa kawaida kuku mmoja anaweza kuatamia mayai 12 hadi 15 kwa mara
moja, kuku awekewe mayai ya kuatamia wakati wa kuatamia unapofika,
inashauriw a kumwekea kuku mayai ya kuatamia wakati wa usiku kwani
akiwekewa mchana anaweza kuyaacha.
Kutayarisha kuku wa kuatamia:- kuku wanaotazamiwa kuatamia lazima
wachaguliwe kwa makini siku mbili kabla ya kuatamia ili kuhakikisha kwamba
hawana chawa, utititri au viroboto. Kuwepo kwa wadudu hao husababisha
kuku wasitulie kwani huwakosesha raha hali hii husababisha kuanguliwa kwa
vifaranga vichache.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 12
SURA YA NNE
UTUNZAJI WA VIFARANGA.
Kuku chotara wanahitaji matunzo bor a. endapo unahitaji kupata kuku wengi
nakuongeza kipato au kuboresha lishe ya familia, basi inakubidi uwatunze
vifaranga vizuri kwa kuhakikisha hawafi ovyo.
Vifaa kwa ajili ya kuwapatia joto vifaranga – joto ni la muhimu katika uhai wa
vifaranga , katika juma la kwanza joto linalostahili katika sehemu ya kulea ni
350C joto hili lipunguzwe kwa 20C kila baada ya juma moja hadi kufikia 270C
katika juma la tano. vifaranga wanaweza kupatiwa joto kwa kutumia vyombo
mbalimbali vya umeme, taa za chemli au jiko la mkaa
UFUATILIAJI WA VIFARANGA KUANZIA WIKI 1 – 4.
WIKI YA KWANZA
Siku ya kwanza hadi ya tano (1 – 7) vifaranga wapewe
Chick formula (dawa ya vitamini ya vifaranga) kwenye maji kwa muda
wa siku 5
Chakula cha vifaranga cha kuanzia
Chanjo ya mdondo angalau kati ya siku ya 5 hadi 7.
Vifaranga wawekwe kwenye banda safi lililowekwa maranda (yasiwe
mepesi yenye vumbi kwani yatawaletea vifaranga mafua
Vifaranga wakae na mama yao ili awapatie joto (kuwatamia) au
wawekwe kwenye chumba maalumu chenye joto.
WIKI YA PILI
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 13
Siku ya 8 – 14
Vifaranga waendelee na chakula cha vifaranga
Siku ya 12 hadi 14 wapewe dawa ya kinga ya kuvaa makoti (kuhara
damu)
WIKI YA TATU
Siku ya 15 – 21
Chakula cha vifaranga kiendelee
Vifaranga warudie kupewa dawa/vitamin ya vifaranga (chick formula )
kwa muda wa siku tano
Siku ya 20 – 21 wapewe dawa ya minyoo ya kuku. Dawa ya minyoo
inatakiwa uwape kuku wote ulio nao bila ya kujali kundi. Baada ya miezi
mitatu kuku wote wanatakiwa kupewa dawa ya minyoo tena.
Banda la kuku (vifaranga) lifagiliwe na kuwekwa tena maranda safi
Kama uliwapa chanjo ya kuchanganya na maji inabidi urudie siku ya 25.
WIKI YA NNE : Rudia dawa ya kuvaa makoti (Esb3)
Vifaranga waendelee na chakula
Vifaranga wapewe dawa za kinga ya magonjwa mbalimbali kulingana
na ushauri wa mtaalamu
Madawa hayo ni kama
Antibiotic zilizochanganywa na vitamini (OTC Plus)
Madawa aina ya salfa- Trisulmycine, S-Dime, Fluquine
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 14
SURA YA TANO
UTENGENEZAJI CHAKULA CHA KUKU
Chakula cha kuku lazima kiwe na viini lishe muhimu kama vile:-
Protein.
Wanga.
Madini.
Vitamini.
Hakikisha chakula unachotengeneza kinakuwa na mchanganyiko wa
vyakula vifuatavyo
Vyakula vya kujenga mwili kama vile ya kunde, samaki, mashudu ya
ufuta, pamba na alizeti.
Vyakula vya kulinda mwili na kukinga mwili usipate maradhi kam
kabichi, michicha, majani ya mapapai na nyasi mbichi.
Vyakula vinavyojenga mifupa kama vile aina ya madini, chokaa,
mifupa iliyosagwa, chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama
kalisiamu na Fosforasi husababisha matege, kukunjamana kwa vidole,
kufyatuka kwa misuli ya goti na kupofuka macho.
Mambo ya kuzingatia kabla ya kutengeneza chakula cha kuku
Jinsi ya kupata vyakula vya aina mbalimbali
Kiasi cha viini lishe vinavyohitajika kulingana na umri wa kuku kwa mfano
vifanga wanahitaji protein asilimia 18 hadi 22, kuku wanaokuwa
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 15
wanahitaji asilimia 17 hadi 19, kuku wa mayai wanahitaji asilimia 15 hadi
17
Viwango vya uchanganyaji wa aina za vyakula mbalimbali
Mchanganyiko wa chakula cha kuku chotara Kg 30
1. Pumba za mahindi debe - 2
2. Mashudu ya pamba/alizeti kg - 4
3. Dagaa zilizosagwa kg 1
4. Mifupa iliyosagwa kg 1
5. Chokaa ya mifugo kg 1
6. Damu iliyosagwa kg 1
7. Lukina iliyokaushwa debe ½
8. Chumvi ya kawaida vijiko vikubwa 2
9. Madini premix kg 1/8
10. DCP vijiko 3
Mfano wa chakula cha vifaranga kuanzia siku ya kwanza hadi majuma manne:
VYAKULA KIASI (KG)
Mahindi 30
Pumba za mahindi 20
Soya 18
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 16
Mashudu ya alizeti 20.5
Dagaa zikaangwe kuua wadudu 5
Mifupa iliyosagwa 3
Damu iliyosagwa 1
Chumvi 0.5
Vitamini 2
Mfano wa chakula cha kukuzia kuanzia juma la nne.
VYAKULA KIASI (KG)
Mahindi 45
Pumba za mahindi 20
Soya 20
Mashudu ya pamba 5
Dagaa zikaangwe kuua wadudu 2.5
Mifupa iliyosagwa 4
Damu iliyosagwa 1
Chumvi 0.5
Vitamini 2
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 17
Mfano wa chakula cha kuku mayai kuanzia juma la nne hadi ishirini
VYAKULA KIASI (KG)
Mahindi 45
Pumba za mahindi 25
Soya 5
Mashudu ya alizeti 12.5
Dagaa zikaangwe kuua wadudu 4
Chokaa 3
Damu iliyosagwa 3
Chumvi 0.5
Vitamini 2
Mfano wa chakula cha kuku wa mayai kuanzia juma la ishirini na kuendelea
VYAKULA KIASI (KG)
Mahindi 50
Pumba za mahindi 15.5
Soya 18
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 18
Mashudu ya pamba 5
Dagaa zikaangwe kuua wadudu 4
Mifupa iliyosagwa 3
chokaa 2
Chumvi 0.5
Vitamini 2
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 19
SURA YA SITA
MAGONJWA YA KUKU
Magonjwa husababishwa na virusi, bacteria, vimelea, minyoo, viroboto,
chawa, utitiri, lishe duni na uchafu
KUWATENGA WAGONJWA- kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku
wagonjwa ili ugonjwa usisambae kwa kuku wote
Kuku huweza kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo
husababisha hasara kubwa kubwa kwa mfugaji . hasara hiyo ni kama vile
Gharama ya matibabu
Kudumaa kwa kuku
Vifo vya kuku
Upungufu wa mayai
JINSI YA KUZUIA MAGONJWA (KANUNI)
USAFI – ni muhimu sana kwa ajili ya kuzuia magonjwa
CHANJO- kuku wapatiwe chanjo dhidi ya ugonjwa wa kideri (Mdondo)
KUNYWESHA DAWA ZA MINYOO – kuku wapatiwe dawa za minyoo kila
baada ya miezi mitatu
Magonjwa yanayosababishwa na virusi
Mdondo – new castle
Dalili za ugonjwa
Kuku kukohoa
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 20
Kuhema kwa shida
Hutokwa na ute mdomoni na pua
Hupatwa kizunguzungu
Kuharisha mharo wa kijani na njano
Hatimaye kuku hufa gafla
Vifo huweza kufikia asilimia 90
Kinga na tiba
Usafi wa banda na vyombo
Usafi wa mazingira na kuchoma mizoga inayoweza kuletwa na
ndege
Usiruhusu watu kuingia kwenye banda ovyo
Kuku wapewe kinga wakiwa na umri wa siku 5-7
hakuna tiba dhidi ya ugonjwa huu Ndui ya kuku
kuku hupatwa na vipele vya mviringo kwenye upanga, masikio,
miguu na sehemu zisizo na manyoya.
Vifo vichache kwa kuku wa kubwa, wadogo hufa nusu ya kundi
Kinga na tiba
Kuku wapewe chanjo wakiwa na umri wa miezi 2
Wapewe vitamin na antibiotic
Usafi wa banda na mazingira
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 21
Hakuna tiba
Mafua makali ya ndege
Dalili
Kupumua kwa shida
Kukohoa na kupiga chafya
Kutokwa na machozi
Kuku kupinda shingo na kuanza kuzunguka
Kuvimba kichwa
Kuharisha kinyesi chenye majimaji , rangi ya kijani na baadaye
kinyesi cheupe
Kinga na tiba
Ukiona dalili hizo toa taarifa kwa Daktari/mtaalamu aliye karibu
nawe
Ugonjwa huu hauna tiba Homa ya matumbo
Dalili
Kuku huharisha mharo wa kijani
Vilemba na upanga hupauka kutokana na upungufu wa damu
Manyoya husimama
Vifo huweza kufikia asilimia 50
Kinga na tiba
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 22
Usafi wa banda
Tibu kwa kutumia dawa zinazoshauriwa na wataalamu kama
vile Esb3
Kipindupindu
Dalili
Kuku huhara mharo wa njano
Husinzia na kulegea
Hulala kichwa kikining’inia kwenye mabawa
Magoya husimama
Hushindwa kusimama hatimaye hufa
Vifo huweza kufikia asilimia 50
Kinga na tiba
Usafi wa banda, vyombo na mazingira yake
Tumia dawa ya chanjo kwa kufuata ushauri wa mtengenezaji
wa chanjo
Ugonjwa huweza kutibika kwa dawa aina ya sulfa
Mafua ya kuku Coryza
Dalili
Kuvimba uso na macho
Kamasi hutiririka toka puani na mdomoni
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 23
Hukohoa
Huhema kwa shida na kukoroma
Mayai hupungua asilimia 10 - 40
Kinga na tiba
Usafi wa b anda na mazingira yake
Kuku wagonjwa watengwe na ikibidi wachinjwe
Wapewe dawa ya chanjo siku 2 kabla ya kuanzwa
CTC 30%
MINYOO.
Ni wa wadudu wanaoleta madhara kwa kuku na hata kwa wanyama
wengine. Kuku hupata minyoo kwa kula vyakula vyenye kinyesi chenye wadudu
waha
Dalili
Kuku hudumaa
Manyoya huwa hafifu
Damu hupungua
Kupungua uzito na kukonda
Utagaji wa mayai hupungua
Minyoo huweza kuonekana kwenye kinyesi
Kinga
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 24
Safisha banda kwa dawa ya kuuwa wadudu
Badilisha matandazo
Safisha vyombo vya chakula na maji
Tenganisha kuku wakubwa na wadogo
Kuku wapewe dawa za kuzuia minyoo kila baada ya miezi
mitatu
Kwa ushauri zaidi Muone mtaalamu wa mifugo.
MASOKO:
Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa
ya msingi yatakayomsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya
juu katika biashara anayoifanya:
Kwanza kabisa ajiulize kama bidhaa anayozalisha ina soko? Na kama soko lipo:
• Lipo wapi na hali ya miundombinu za kulifikia iko vipi ( ili afahamu gharama ya
kufika sokoni kama utaamua kuuzia sokoni).
• Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani na wakati gani sokoni
• Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi ( ubora n.k. ili uzalishe sawa na matakwa
ya soko n.k)
• Kama wanunuzi watakuwa na utayari kununulia unakozalishia, je unao uwezo
wa kutosheleza mahitaji yao (ili uweze kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza
uzalishaji au kwa kuungana na wazalishaji wengine).
• Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo
na faida zaidi kwako baada ya kuondoa gharama za kufuata soko) Ila ukiamua
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 25
kuuzia sokoni hakikisha unao uwezo wa kushindana na wauzaji wengine huko
sokoni.
Majibu ya maswali haya ndiyo yatakayokupa msingi wa kujipanga kiuzalishaji ili
hatimaye upate faida. Hivyo hata kabla hujaanza kuzalisha fahamu haya
yaliyotajwa hapa juu.
(a) Kutafuta na kutumia taarifa za masoko ya sehemu tofauti:
Kwa kadri utakavyokuwa unaendelea kuzalisha, mabadiliko mbali mbali
yatatokea kuhusiana na uzalishaji wako na hata kuhusiana na soko la bidhaa
unayozalisha kwa maana ya kuku.
Ili uendane na mabadiliko yanayotokea ni muhimu mzalishaji upate taarifa za
hali ya soko mara kwa mara. Taarifa hizi zitakusaidia kufanya maamuzi
yatakayokuwezesha kuendelea kupata faida.
Taarifa za masoko zinaweza kupatikana kwa wazalishaji kadhaa kuungana na
kuunda umoja wao. Katika umoja huo wawakilishi wachache wanakuwa na
jukumu la kutafuta taarifa za masoko ya kuku sehemu mbali mbali ambako
kunaweza kuwapa wazalishaji tija zaidi.
Walio katika umoja huo watatumia taarifa hizo kufanya maamuzi ya kuuza kwa
faida zaidi kwa pamoja au kwa mmojammoja kutegemeana na hali halisi.
Watoa taarifa pia watafanya mawasiliano ya kuwajulisha wanunuzi juu ya
upatikanaji wa kuku kwenye maeneo wanakozalishiwa.
(b) Mbinu zaidi ya kupata masoko mazuri:
(i) Umoja wa kuzalisha na kuuza;
Kwa kawaida kama bidhaa ina soko, wateja hupatikana kwa urahisi pale
wanapohakikishiwa upatikanaji wa bidhaa kwa wingi katika sehemu moja.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 26
Katika hali hii, wanunuzi huwa tayari hata kununua kwa bei ya juu zaidi kwa
sababu ya kupunguza muda na gharama ya kutafuta bidhaa ya kutosha
kupeleka sokoni.
Kwa upande wa kuku jambo hili linawezekana kama mfugaji atafuga kuku
wengi wa umri usiopishana sana kwa wakati mmoja. Watakapofikia kimo
kinachofaa kuuza utawauza wengi kwa wakati mmoja na kwa faida zaidi.
Mahali ambapo mfugaji mmoja mmoja hawezi kukidhi wingi wa hitaji la
wanunuzi, wafugaji kadhaa wanaweza kuunda umoja wao wa kuzalisha (kila
mmoja kwake ) na kuuza kwa kipindi kimoja na kupata faida zilizotajwa hapa
juu.
Faida nyingine ya kuuza katika umoja ni kuongezeka kwa uwezo wenu wa
kupanga na kusimamia bei mnayotaka kuuzia. Sauti na uamuzi wenu wa
pamoja utawapa nguvu ya kusimamia bei yenu mnayoipanga dhidi ya bei za
chini wanazotaka wanunuzi. Uwezo wako wa kusimamia bei unayoitaka ni
mdogo ukiuza peke yako.
Chama cha akiba na mikopo ni kikundi cha watu waliojiunga kwa hari yao
kufanya ushirika wa kuweka akiba zao kwa pamoja na kutoa mikopo kwa
urahisi kutokana na akiba zao.
Kwa wafugaji wa kuku kibiashara wanashauriwa kuwa na chombo cha namna
hii kitakachokuwa na utaratibu wa wanachama kuweka na pia wanachama
hawa kuwa na fursa ya kukopa kwa lengo kubwa la kuendeleza ufugaji wao
wa kuku kibiashara.Ufugaji wa kibiashara ungehitaji kuongeza mtaji mara kwa
mara kulingana na mahitaji ya soko husika. Mfumo wa kuweka na kukopa
utakuwa chanzo kizuri na cha kuaminika kukidhi haja ya mtaji endelevu kwa
wafugaji wa kuku.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 27
Michango kwa ajili ya akiba inaweza kutokana na makato ya mapato
yanayotokana na mauzo ya bidhaa za kuku ( vifaranga,mayai, kuku n.k. ). Au
kiwango maalum kwa wakati maalum kinaweza kuwekwa na wanachama ili
kitolewe kwa utaratibi wanaokubaliana.
Wanachama wanaweza kukopa kutoka kwenye chama chao kwa ajili ya
ununuzi wa mahitaji, mbalimbali ya kuku kama:
• Madawa
• Vyakula
• Ukarabati au ujenzi wa mabanda ya kuku n.k
(ii) Faida za chama kama hiki ni:
• Wanachama watapata sehemu ya kuhifadhi pesa yao kwa usalama kwa ajili
ya matumizi ya baadaye.
• Masharti ya kukopa ni nafuu kuliko vyombo vingine vya kifedha.
• Wanachama hujifunza misingi ya kushirikiana, mahusiano na kusaidiana.
• Wanachama hupata maarifa ya ziada kuhusu maswala ya kifedha.
Chama cha namna hii, lazima kiwe na kanuni za kukiongoza ambazo hutungwa
na wanachama wenyewe.
Kanuni hizi zilenge kulinda malengo ya chama na kila mwanachama
anawajibika kuzizingatia.
(iii) Mambo makuu ya kuzingatia katika katiba ni:
• Malengo ya chama
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 28
• Haki, wajibu na malengo ya wanachama
• Viwango vya viingilio
• Hisa na michango
• Uongozi na majukumu
• Vikao na mikutano
• Utunzaji wa kumbukumbu
• Mikopo na riba
• Taratibu za kutoa mikopo
• Migawanyo ya faida
(iv) Mambo ya msingi ya kusimamia na kuendesha chama cha Akiba na
Kukopa ni pamoja na:
Uhiari wa wanachama
Uongozi uwe wa kidemokrasia
Kusiwe na urasimu
Chama lazima kiwe na vitabu vitakavyotumika kuweka kumbukumbu ya
hifadhi za fedha za wanachama
Uwekaji wa akiba uwe wa mara kwa mara
Mkopo ulipwe kwa muda uliopangwa
Fedha za chama ziwekwe benki au kwenye masanduku maalum ya
kutunzia kwa utaratibu uliopendekezwa Mahesabu ya chama yafanyiwe
ukaguzi mara kwa mara.
Muheza – Idara -Mifugo na uvuvi.
[KANUNI ZA UFUGAJI BORA WA KUKU WA ASILI ] Page 29
Kikundi kama hiki kinaunganisha nguvu pamoja na kupunguza tatizo la kupata
huduma ya kifedha hasa katika maeneo ya vijijini.Hata hivyo jambo la msingi la
kufanikisha malengo ya vyombo hivi ni kuzingatia kanuni zilizowekwa na
wahusika. Vilevile utaalam wa kutosha wa kuendesha na kusimamia chombo
vya namna hii ni muhimu uwepo.
(Kwa ushauri zaidi wanachama wamuone Afisa Ushirika aliyepo karibu yao).