Top Banner
TANZANIA PORTS AUTHORITY www.ports.go.tz | Bendera Tatu S.L.P. 9184 Dar es Salaam | Email: [email protected] | Namba za Bure: 0800110032 / 0800110047 TOLEO NO: 01 NOV 13 - NOV 25 2017 TPA KUTUMIA MFUMO WA VITAMBULISHO VYA KIELELTRONIKI 11 15 10 DAR PORT MABINGWA INTER-PORTS GAMES 2017 WASHAURI BALOZI ZITUMIKE KUITANGAZA TPA KIBIASHARA 05 TOZO ZIPUNGUZWE ILI KUVUTIA WATEJA. M amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetenga jumla ya Shs. Milioni 75 kusaidia huduma za Afya, Elimu na huduma za jamii kama vile maji safi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko alipokuwa akikabidhi msaada wa madawati 90 katika shule ya msingi Lushamba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Buchosha, Sengerema. NDANI Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandishi Deusdedit Kakoko akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Rwagati, Wilayani Bukoba. Inaendelea UK 2 >> @tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @ tanzaniaports TPAHQ TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 01 Na Leonard Magomba na Beatrice Jairo Eng. Kakoko amesema kwamba TPA imejikita zaidi kusaidia elimu na huduma za afya kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya taifa lolote lile duniani. “Unapozungumzia maendeleo ya nchi, elimu ndio ya kwanza kabisa kwa sababu hapo ndipo watapatikana wabunifu wa mipango ya maendeleo,” amesema, Eng. Kakoko. Amesema kwamba hata matukio ya kushambulia vikongwe yanayotokea mikoa mingi ya Kanda ya Ziwa ni kwasababu ya uhaba wa Elimu. “Hawa watoto wakielemika basi umeelimisha Taifa, kesho na keshokutwa wakimuona kikongwe ana macho mekundu TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, AFYA KANDA YA ZIWA
16

TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

Oct 23, 2021

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TANZANIA PORTS AUTHORITY

www.ports.go.tz | Bendera Tatu S.L.P. 9184 Dar es Salaam | Email: [email protected] | Namba za Bure: 0800110032 / 0800110047 TOLE

O N

O: 0

1 N

OV

13 -

NO

V 25

201

7

TPA KUTUMIA MFUMO WA VITAMBULISHO

VYA KIELELTRONIKI

11

15

10

DAR PORT MABINGWA INTER-PORTSGAMES 2017

WASHAURI BALOZI ZITUMIKE KUITANGAZA

TPA KIBIASHARA

05

TOZO ZIPUNGUZWE ILI

KUVUTIA WATEJA. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetenga jumla ya Shs. Milioni 75 kusaidia huduma za Afya, Elimu na huduma za jamii kama vile maji safi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu

wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko alipokuwa akikabidhi msaada wa madawati 90 katika shule ya msingi Lushamba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Buchosha, Sengerema.

NDANI

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandishi Deusdedit Kakoko akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa kijiji cha Rwagati, Wilayani Bukoba.

Inaendelea UK 2 >>

@tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @ tanzaniaports TPAHQ TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 01

Na Leonard Magomba na Beatrice Jairo

Eng. Kakoko amesema kwamba TPA imejikita zaidi kusaidia elimu na huduma za afya kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya taifa lolote lile duniani.

“Unapozungumzia maendeleo ya nchi, elimu ndio ya kwanza kabisa kwa sababu hapo ndipo watapatikana wabunifu wa mipango ya maendeleo,” amesema, Eng. Kakoko.Amesema kwamba hata matukio

ya kushambulia vikongwe yanayotokea mikoa mingi ya Kanda ya Ziwa ni kwasababu ya uhaba wa Elimu. “Hawa watoto wakielemika basi umeelimisha Taifa, kesho na keshokutwa wakimuona kikongwe ana macho mekundu

TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, AFYA KANDA YA ZIWA

Page 2: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

2 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Jamii

watampeleka hospitali badala ya kumshambulia wakidhani ni mchawi,” amesema. Ametolea mfano mataifa kama ya China, Vietnam, Malaysia yamepiga hatua zaidi kimaendeleo ndani ya kipindi kifupi kuliko Tanzania sababu ya kuwa na watu wenye afya njema na walioelimika. Kakoko amesema kwamba msaada huo utasaidia miji na vijiji vilivyo karibu na Bandari kama vile Musoma, Nansio, Ukerewe, Lushamba, Nyamirembe, Kemondo, Mwanza North na South. Mkurugenzi Mkuu amesema kwamba madawati hayo

yametengezwa Tanzania na SUMA JKT ambayo ipo chini ya jeshi letu la kujenga Taifa, kwa lengo la kuiunga mkono Taasisi hiyo, huku TPA nayo ikitoa mchango wake. Ukiondoa elimu, sekta nyingine iliyo katika vipaumbele vya TPA ni afya na ndio maana kwa upande huo pia Mamlaka imechangia vitu mbalimbali kama vitanda, magodoro, mashuka na vyandarua. Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosha, Bw. Leonard Chacha aliishukuru TPA kwa kuwaunga mkono katika shughuli za maendeleo. Bw. Chacha amesema kwamba

ni jukumu letu sote kuhakikisha kwamba madawati hayo yanatunzwa ili yatumike kwa muda mrefu.“Napenda kuchukua fursa hii kuwataka Mwenyekiti pamoja na walimu wote wa shule hii ya Lushamba kuhakikisha kuwa rasilimali hii tunaitunza vizuri ili itumike kwa muda mrefu,” amesisitiza. ‘‘Tumeshuhudia na kuona sote kuwa ni madawati imara na yana uwezo wa kukaliwa na watu wazima wanne. Hivyo tuyatumie vizuri.’’ Shule ya Msingi ya Lushamba ilianzishwa mwaka 1972 ikiwa na wanafunzi 32 na walimu watatu, kwa sasa shule hii ina wavulana 686 na wasichana 643. Mpaka sasa TPA imeshatoa misaada katika Halmashauri za Musoma, Ukerewe na Chato zilizopo Kanda na Ziwa.

<< Inatoka UK 1

TPA yatenga milioni 75 kusaidia Elimu, Afya Kanda ya Ziwa

‘‘Bw. Chacha amesema kwamba ni jukumu letu sote kuhakikisha kwamba madawati hayo tunayatunza ili yatumike kwa muda mrefu.’’

Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Deusdedit Kakoko akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva, Mashuka kwa ajili ya matumizi ya Hospitali za Manispaa ya Temeke.

Page 3: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 3

Biashara

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Munir Bashir ameyasema hayo katika barua yake ya shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko ambapo pamoja na mambo mengine alielezea jinsi Bandari ya Dar es Salaam ilivyo na ufanisi mkubwa. “Tunashukuru sana menejimenti ya TPA na wafanyakazi kwa utendaji wenu mzuri na wa hali ya juu uliowezesha kuhudumia shehena yetu iliyoletwa na meli ya MV Loving,” ilisema sehemu ya barua hiyo. Sehemu ya barua ya Mkurugenzi wa MINOLACS iliongeza, “…

Ahadi hiyo imetimizwa mapema baada ya Kampuni hiyo kupakua tani 12,000 za ngano mapema mwezi wa Oktoba na kuahidi kuendelea kuleta shehena kubwa zaidi. MINOLACS ni Kampuni binafsi inayojishughulisha na biashara ya nafaka, kwa ajili ya chakula yenye uwezo wa mauzo ya kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 6.8 kwa mwaka. Tayari TPA imefungua huduma zake katika nchi ya Burundi, mji wa Bujumbura ili kusogeza huduma zake karibu na wateja. Pia ina ofisi zake mjini Lusaka- Zambia, Kigali-Rwanda na Lubumbashi – Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo na wakala wa Masoko mjini Kampala, Uganda.

“TUNASHUKURU SANA MENEJIMENTI YA TPA NA WAFANYAKAZI KWA UTENDAJI WENU MZURI NA WA HALI YA JUU ULIOWEZESHA KUHUDUMIA SHEHENA YETU ILIYOLETWA NA MELI YA MV LOVING...”

KAMPUNI YA BURUNDI YAAHIDI KUITUMIABANDARI YA DAR ES SALAAM

Na Levina Msia

Kampuni ya MINOLACS ya Burundi imeahidi kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya kuridhika na ufanisi wa hali ya juu wa kuhudumia shehena ya ngano tani 12,000 za kampuni hiyo hivi karibuni.

tunawashukuru sana na tunaaahidi kuongeza shehena kufikia tani 16,000 za ngano tutazopitisha Bandari ya Dar es Salaam.”

Mkurugenzi

Mkuu wa TPA,

Mhandisi Deusdedit

Kakoko akikabidhi

zawadi kwa

Balozi wa

Rwanda hapa

nchini, Mhe.

Eugene Kayihura

wakati Balozi huyo

alipomtembelea

ofisini kwake Makao

Makuu hivi karibuni.

Page 4: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

4 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Korosho

BANDARI YA MTWARA YAJIZATITI KUHUDUMIA SHEHENA YA KOROSHO

Na Fassie Obadia

Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw Nelson Mlali amesema Bandari ya Mtwara imefanya maboresho makubwa ili kuhudumia shehena ya korosho katika msimu huu wa mwaka 2017/2018.

Mkuu huyo wa Bandari amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya usafirishaji wa Korosho mwaka 2016/2017 na mipango ya kuhudumia shehena kwa mwaka 2017/2018 katika kikao cha wadau na watumiaji wa Bandari ya Mtwara kilichofanyika Bandarini hapo hivi karibuni Bw. Mlali alisema kwa msimu wa mwaka 2016/2017 jumla ya tani 215,852 za shehena ya korosho zilisafirishwa kupitia Bandari ya Mtwara ikiwa ni ongezeko la asilimia 85.6 ikilinganishwa na tani 116,289 zilizosafirishwa msimu wa mwaka 2015/2016. Aidha, aliwaeleza wadau kwamba

Bandari ya Mtwara imejipanga vizuri kuhudumia shehena ya korosho msimu huu ambapo maboresho mbalimbali tayari yamefanyika. “Tumeongeza maeneo ya kufanyia stuffing, vifaa, na tunatoa huduma saa 24 siku saba za wiki,” alisema. Alisema Bandari hiyo pia imeongeza eneo la kuhifadhia makasha matupu na kuendelea kuimarisha ulinzi wa Bandari na mali za Wateja wakati wote. Wadau hao walielezea kufurahishwa na hatua zilizochukuliwa na Mamlaka ili kutatua changamoto zilizojitokeza katika msimu wa mwaka 2016/2017 hususani ufinyu wa eneo la kufanyia

(stuffing) na upungufu wa vitendea kazi. Wadau hao wameahidi kushirikiana na Mamlaka ili kuhakikisha kwamba usafirishaji wa korosho kwa mwaka 2017/2018 unafanyika kwa mafanikio makubwa.

‘‘ALISEMA Bandari HIYO IMEONGEZA ENEO LA KUHIFADHIA MAKASHA MATUPU NA KUENDELEA KUIMARISHA ULINZI WA Bandari NA MALI ZA WATEJA WAKATI WOTE.’’

Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali akizungumza na Wadau wa zao la Korosho hivi karibuni.

Page 5: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 5

Ziara

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh. Hawa Ghasia (Mb.) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtwara vijijini wakati Kamati yake ilipotembelea Bandari ya Mtwara ili kukagua miundombinu ya Bandari pamoja na miradi ya maendeleo. “Mamlaka iangalie uwezekano wa kupunguza tozo zake mbalimbali kwa Kampuni ya Dangote ili Kampuni iweze kusafirisha saruji yake kupitia Bandari ya Mtwara, si mteja huyu tu, bali hata wateja wengine,” alisema Mhe. Ghasia. Akijibu hoja hiyo Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Karim Mattaka aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu aliwashukuru wabunge kwa ushauri wao na kuelezea kuwa tayari kuna ‘tariff concessions’ ambayo hutolea kulingana na kiasi cha mzigo anaosafirisha mteja na namna anavyotumia Bandari. Ziara ya Kamati hiyo pia ililenga kujifunza na kujionea changamoto za Bandari ya Mtwara na kufahamu imejipanga vipi kuhudumia shehena itakayochochewa na uchumi wa viwanda. Kamati hiyo ilipokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Prof. Ignas Rubaratuka, Manaibu Wakurugenzi Wakuu, Mhandisi Karim Mattaka, na Bw. Lazaro Twange, pamoja na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi (DOWUTA). Menejimenti ya TPA pia iliwasilisha taarifa ya utendaji ya Bandari hiyo, kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2012/2013 hadi 2016/2017 na Kamati ilitoa ushauri mbalimbali. Kamati ilishauri vitendea kazi viongezwe Bandari ya Mtwara hasa wakati wa msimu wa korosho

“Mamlaka ikamilishe taratibu zake ili Bandari ya Mtwara iweze kutumika katika upokeaji wa Mafuta,’’ alisema Mwenyekitiwa Kamati.

KAMATI YA BUNGE: TOZO ZIPUNGUZWE ILI KUVUTIA WATEJA

Na Fassie Obadia

Kamati ya Kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania imeishauri Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kuangalia uwezekano wa kupunguza tozo zake ili kuvutia wateja wengi zaidi.

na mradi wa ujenzi wa Gati Na 2 usimamiwe na kukamilika kwa wakati. “Mamlaka ikamilishe taratibu zake ili Bandari ya Mtwara iweze kutumika katika upokeaji wa mafuta, “ alisema Mwenyekiti. Mh. Ghasia alishauri Mamlaka kutafuta wateja zaidi kwa kuongeza kampuni zaidi za meli, na kuhakikisha mradi wa upanuzi wa Bandari ya Mtwara unakamilika kwa kushirikisha wadau wengine kama TRL na TANROADS ili kasi ya upanuzi wa Bandari iendane na maboresho ya miundombinu mingine kama barabara na reli.

Naibu Kaimu Mkurugenzi Mkuu (Miundombinu), Mhandisi Karim Mattaka (kushoto) akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Mhe. Hawa Ghasia (kulia) wakati Kamati yake ilipofanya ziara Bandari ya Mtwara.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA aliishukuru Kamati hiyo kwa kufanya ziara Bandari ya Mtwara na akaahidi kufanyia kazi ushauri wao kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Page 6: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

6 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Habari Picha

Wajumbe wa Baraza Kuu la Majadiliano la TPA wakiwa katika Kikao cha 42 cha Baraza hilo kilichofanyika katika Bandani ya Mtwara.

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Uendeshaji), Bw. Lazaro Twange akikabidhi msaada wa vitanda kwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dr. Vincent Naano.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (wa pili kulia) akifurahia jambo na wanafunzi mara baada ya kukabidhi madawati 90 kwa Shule ya Msingi Lushamba.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji-Zanzibar, Mhe. Balozi Ali Karume akimsikiliza Mkuu wa Bandari ya Kigoma, Bw. Moris Mchindiuza wakati alipotembelea banda la TPA katika maonesho ya Siku ya Bahari Duniani.

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Huduma), Bi. Fransisca Muindi akiwa kwenye Kongamano la Kimataifa la Biashara nchini Burundi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya (TPA), Prof. Ignas Rubaratuka na Wajumbe wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko wakikagua Gati ya Ntama iliyopo Buchosa katika Wilaya ya Sengerema wakati wa ziara ya Bodi kukagua Miradi.

Page 7: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 7

Habari Picha

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Lazaro Twange (kushoto) akikabidhi zawadi kwa kiongozi wa msafara wa Wafanyabiashara kutoka Zambia, Bw. Michael Nyirenda.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPA, Dk. Francis Michael akizungumza na Wafanyakazi wakati wa uzinduzi wa michezo ya Bandari.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Fredy Liundi akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wakishuhundia kufika kwa Mitambo ya Ujenzi wa Gati jipya Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akishiri kazi ya ujenzi wa ‘scanner’ wakati wa ziara yake katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni.

Sehemu ya mtambo utakaotumika kwa ajili ya ujenzi wa Gati jipya Bandari ya Dar es Salaam ukiwasili Bandarini hapo hivi karibuni.

Page 8: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

8 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Mradi

Na Moni Jarufu

BANDARI TANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA BOMBA

LA MAFUTA GHAFI

Mradi wa Bomba la Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Mh Yoweri Museveni hivi karibuni utatoa ajira 30,000 katika kipindi cha ujenzi wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga eneo la Chongoleani nje kidogo ya Jiji la Tanga.

Akizungumza katika jukwaa la biashara lililofanyika Jijini Tanga hivi karibuni, Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga Bw. Percival Salama alisema pamoja na ajira hizo, idadi ya mizigo na vifaa vitakavyotumika katika mradi huo vitahitaji zaidi ya magari 25,000 kutoka Bandarini hadi katika eneo la mradi. Tafsiri ya hili ni ukuaji wa ajira katika maeneo yote unakopita mradi huu. ‘… yatahitajika zaidi ya magari 25,000 makubwa ya kubeba mizigo (project cargo) kutoka Bandarini hadi kwenye eneo la mradi, hivyo kuna haja kubwa ya kuwekeza na kuandaa rasilimali watu ya kutosha.’’ alisema Bw. Salama na kuongeza kuwa Mamlaka ya Bandari(TPA) imejipanga kuhakikisha

wanahudumia kwa ufanisi mkubwavifaa vya mradi yote vitakavyopitia Bandari ya Tanga ili kuharakisha ujenzi wa mradi huo unamalizika kwa wakati, ikiwa ni pamoja na kuongeza vifaa vya kisasa vya kupakia na kupakuamizigo Bandarini. Bw. Salama aliwahimiza wakazi wa Tanga kutumia fursa vizuri katika kipindi chote cha ujenzi wa mradi huo kwani ajira mbalimbali zitazalishwa huku Wafanyabiasharana Wajasiriamali mbalimbali wakinufaika na fursa katika sekta ya vyakula, sekta ya mahoteli, sekta ya shule na pamoja na sekta ya mawasiliano. Aidha, Bw. Salama amesema Serikali itahakikisha inajenga Bandari kubwa

na za kisasa (hub port) ili kuongeza pato kubwa la Taifa, kwani Bandarikubwa (hub port) itasaidia kupokeamizigo ya nchi jirani ambazo hazinaBandari, na pia Tanzania itaondokanana kuwa Bandari zinazolisha ambazo zinalipunguzia Taifamapato. Kupitia viwanda na miradi mbalimbali inayokuja katika Mkoa wa Tanga, Bandari ya Tanga inatarajia kupokea na kusafirisha mizigo maratano (5) zaidi ya kiwango cha sasa. Wakati huohuo Kiwanda kikubwa cha Saruji Afrika Hengya kinatarajiwa kujengwa mkoani Tanga ambapo zaidi ya makasha elfu moja (1,000) yanatarajiwa kupakuliwa katikaBandari ya Tanga kwa ajili ya ujenziwa kiwanda hicho.

Page 9: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 9

Afya

Waraka wa Wizara kwa TPA umebainisha kuwa ugonjwa wa tauni ni mojawapo kati ya magonjwa hatari yanayofuatiliwa kwa karibu kwa kuzingatia kanuni za afya za Kimataifa za Shirika la Afya Duniani. Kufuatia waraka huo, Mkurugenzi Mkuu amewataka watumishi wote wa Mamlaka kuzingatia tahadhari iliyotolewa na Wizara kutokana na uwezekano uliopo wa kupokea mizigo inayotoka nchini Madagascar yenye vimelea vya maambukizi. Ugonjwa wa tauni husambaa kwa kasi kwa kuenezwa na bakteria wanaoishi kwenye viroboto vinavyoishi kwa kuwategemea wanyama hususani panya wa porini. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa huu mara tu atakapoumwa na kiroboto mwenye bakteria au kwa kuvuta hewa kutoka kwa mgonjwa

SERIKALI YATAHADHARISHA JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA TAUNI

• YAAGIZA MIZIGO YOTE KUTOKA MADAGASCAR IKAGULIWE • WAFANYAKAZI WASHAURIWA KUCHUKUA TAHADHARI

Na Focus Mauki

Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa taarifa ya kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa tauni nchini Madagascar ambapo mpaka kufikia Septemba 2017, tayari watu 20 wameripotiwa kufariki nchini huko huku idadi ya wagonjwa ikiwa ni 104.

aliyepata maambukizi. Kutokana na urahisi wa kupata maambukizi ya ugonjwa huu, Mamlaka imeona ni vyema Wafanyakazi wote wakaanza kuchukua tahadhari mapema kutokana na uwezekano wa mwingiliano wa vyombo vya usafiri kutoka mataifa ya nje hususani Madagascar katika maeneo ya Bandari. Ili kujikinga na kuchukua tahadhari

Menejimenti imeshauri ni vyema tahadhari mbalimbali zikaanza kuchukuliwa mapema hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha maeneo yote kwenye umbali wa mita 400 kuzunguka maeneo ya shughuli za Bandari yanakuwa salama dhidi ya wadudu na wanyama hususani panya. Aidha Mamlaka inafanya tathmini ya uwepo wa mazalio ya wadudu na panya na kuyaaribu, kudhibiti na kuondoa taka ngumu, kusafisha maeneo ya kazi wakati wote, kutoa taarifa ya vifo vingi vya wanyama wanaokufa katika maeneo ya Bandari kwa wakati mmoja hususani panya na kushirikiana na ofisi ya afya Bandarini kufanya ukaguzi wa mizigo yote inayotoka katika nchi zenye maambukizi kama vile Madagascar.

Bandari ya Dar es Salaam

‘‘Ugonjwa wa Tauni husambaa kwa kasi kwa kuenezwa na bakteria

wanaoishi kwenye viroboto vinavyoishi kwa kuwategemea wanyama

hususani panya wa porini.’’

Page 10: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

10 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Uhusiano

WASHAURI BALOZI ZITUMIKE KUITANGAZA TPA KIBIASHARA

Na Levina Msia

Wanadiplomasia kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Chuo cha Diplomasia wakiwa Bandari ya Dar es Salaam.

Maofisa Mambo ya Nje wameishauri TPA kutumia Balozi za Tanzania zilizopo nchi mbalimbali kujitangaza kibiashara na kukabiliana na upotoshaji wa taarifa za TPA.

Ushauri huo ulitolewa na Maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Chuo cha Diplomasia walipofanya ziara ya mafunzo katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. Baada ya kupata maelezo mafupi kuhusu shughuli za Bandari hiyo pamoja na kuangalia Makala ya Bandari (Corporate Documentary), maafisa hao waliipongeza Menejimenti kwa ufanisi mzuri. “Documentary ya TPA ni nzuri sana , napendekeza zitolewe CDs nyingi zisambazwe Balozi zetu zote ili maofisa ubalozi wazisambaze kwenye taasisi na Kampuni kubwa za kibiashara kwa ajili ya kuwezesha

taasisi hizo kuifahamu TPA zaidi na kukabiliana na taarifa za upotoshaji juu ya utendaji wa Bandari za Tanzania, “ alisema ofisa mmoja. Ili kujiimarisha kibiashara, maofisa hao walipendekeza kuwa TPA iendeleze ushirikiano wa karibu na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kupanua wigo wa wateja nje ya nchi. Akitoa shukrani kwa Meneja wa Bandari kwa niaba ya maofisa hao Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Idara ya Diplomasia ya Uchumi Bi Desderia Sabuni alisema TPA inafanya kazi ngumu sana na ya muhimu kwa Taifa hivyo wanastahili pongezi.

“Jukumu kubwa walilo nalo TPA ni kuiendeleza Diplomasia ya Uchumi ya Tanzania, kwa upande wa uchukuzi, ambalo sisi ndio tunalipigania, nawapongeza sana,“ alisema mwanadiplomasia huyo. Aidha alisema wao kama maafisa mambo ya nje watakuwa mabalozi wazuri wa Mamlaka ya Bandari Tanzania. Maofisa hao wapatao 25 pamoja na wahadhiri wao pia walitembelea vitengo mbali mbali ili kujifunza jinsi vinavyotekeleza shughuli zake.

Page 11: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 11

Teknolojia

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Bw. William Kapela katika mazungumzo na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni. Alisema kuwa mpango huu ni awamu ya pili ya Utekelezaji wa Mradi wa “ Intergrated Security System Phase II” ambapo utahusisha matumizi ya Biometric IDs ambazo zimewekewa kifaa maalum “chip” itakayogusishwa katika kifaa maalum kingine ili kumtambua mhusika na wakati huo huo kupeleka taarifa moja kwa moja katika mifumo mingine ya idara ya Utumishi na Fedha kwa utekelezaji mwingine. “Vitambulisho vya kieletroniki vitaondoa matumizi ya vitabu vya kawaida vya mahudhurio, ambacho kitatumika pia kama kibali cha mfanyakazi kuingia Bandarini,“ alisema Bw. Kapela Vitambulisho hivyo pia vitatumika kufungua milango ya kuzunguka “Turn Style” baada ya ukaguzi, kufungua mageti kwa ajili ya kuingia au kutoka kazini na milango ya majengo mbalimbali ambapo taarifa zitapelekwa kwa Mkuu wake wa Idara, Idara ya Utumishi na Fedha,” aliongeza Kapela. Mradi huo utakapokamilika, kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Ulinzi utadhibiti tabia za baadhi ya wafanyakazi kupoteza muda wa kazi kwa kwenda eneo tofauti na mahali alipoagizwa, kupunguza utoro, kuimarisha usalama pamoja na kumfanya Mfanyakazi kufika kwa wakati sehemu za kazi au eneo alipoagizwa. “Vitambulisho hivi vitaondoa uhuru wa Mfanyakazi kutoka au kuingia eneo husika kwani taarifa

WAFANYAKAZI KUTUMIA MFUMO WA VITAMBULISHO VYA KIELELTRONIKI

Na Innocent Mhando

Mamlaka inaandaa mfumo wa vitambulisho vya kieletroniki “Biometric ID’s” kwa ajili ya wafanyakazi kutoka au kuingia Bandarini ili kuachana na mfumo wa kutumia daftari cha mahundurio.

zitapelekwa mara tu anapopitisha kitambulisho chake katika vifaa hivyo pia ataruhusiwa kutoka au kungia mahali na ruhusa ya kuingia eneo hilo mfano kutoka Makao Makuu kwenda Bandari ya Dar es Salaam, “General Cargo” kwenda Kurasini Oil Jetty (KOJ). Aidha mradi huo utatekelezwa sambamba na utaratibu wa utambuzi wa namba za magari, ambapo magari yote ya watumishi wa Mamlaka yatawekwa katika mfumo na magari hayo yatapita katika geti husika pale ruhusa au kibali kitakapokuwepo. Mradi wa Intergrated Security System (ISS) una lengo la kuboresha ulinzi na usalama katika Bandari ya Dar es Salaam na baadaye katika Bandari zingine ambapo mpaka

sasa katika Bandari ya Dar es Salaam tayari zimefungwa “Closed-Circuit Television (CCTV)” kamera 463 na vizuizi vya mageti “Gate Barrier” ,. Mradi huo umehusisha ufungaji wa vitambuzi vya vitambulisho vya kieletroniki na namba za magari, vifaa vya ukaguzi kama scanner kwa ajili ya mizigo midogo, Mfanyakazi, abiria, pamoja na vipaza sauti kwa ajili ya upashanaji habari na matangazo, na milio ya dharula, X-ray machines, Gate houses, Metal detectors, Radioactive Portal Monitors, Perimeters Intruder Detection System na Main Control Room ambapo camera zote zinaonekana kupitia screen zilizowekwa katika chumba hicho.

Askari wa Bandari akionyesha jinsi vitambulisho vya kielektoniki (Biometric IDs) vitakavyotumika kuingia na kutoka Bandarini.

Page 12: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

12 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Tovuti

Tovuti hiyo ambayo itakuwa ikipatikana kwa urahisi kupitia kikowa cha www.ports.go.tz itawezesha wateja watakaoitembelea kuwasiliana moja kwa moja mubashara (live) na dawati la watoa huduma (customer service desk) mbalimbali za Bandari pamoja na Wakuu wa Bandari. Mbali na huduma hizo, katika tovuti hiyo pia kutakuwa na sehemu maalumu ambayo mteja anaweza kutuma swali lake moja kwa moja kwa mtoa huduma ambaye nae ataweza kuwasiliana na mteja au kuweka kumbukumbu ya hoja au swali na kulipatia majibu yatakayomridhisha mteja. Huduma nyingine ambazo zitakuwa zikipatikana katika tovuti hii mpya ni pamoja na taarifa mbalimbali kuhusiana na ratiba za kila siku za meli, huduma za kulipia mizigo Bandarini, huduma za kupata taarifa za ankara (invoice) na taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na majarida ya Mamlaka. Tovuti hii pia itatumika kutangaza

TOVUTI YA MAMLAKA YENYEMUONEKANO MPYA YAZINDULIWA

Na Focus Mauki

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imezindua tovuti (website) yake mpya ambayo itarahisisha mawasiliano baina ya Bandari , wateja, wadau na jamii kwa ujumla.

mifumo mbalimbali ya Mamlaka inayohusiana na utoaji wa mizigo Bandarini kama vile mfumo wa malipo wa kisasa wa ‘e-payment’ ambao mtu yoyote (sio lazima wakala wa kutoa mzigo) mwenye mzigo Bandarini anaweza kuona nakala ya ankara yake ya malipo. Uwezekano wa kuona ankara ya malipo utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la wateja kupewa ankara ya malipo ya kughushi na mawakala wasio waaminifu kwa lengo la kujinufaisha au kutapeli wateja. Huduma zitakazotolewa na tovuti hii zitazingatia mahitaji mbalimbali ya wadau wote ambapo kwa wadau wasio wateja wa Mamlaka pia wataweza kuona taratibu (import and export procedures) za kuzingatia pale anapoagiza (import) au anaposafirisha (export) mzigo wake. Ili kuweza kukidhi mahitaji ya lugha za wadau wa Bandari tovuti hii pia itakuwa ikipatikana katika lugha tatu (3) hii ni pamoja na Kiswahili,

Kiingereza na Kifaransa na kwa kuanzia katika awamu hii ya kwanza tovuti hii itaanza kupatikana katika lugha ya Kiingereza. Tovuti hii pia inatarajiwa kuwa kiiunganishi cha wadau mbalimbali wa Mamlaka ambapo wadau watakoitembelea wataweza kuona na kupata huduma kwenye tovuti nyingine za wadau mbalimbali ambao wanafanya kazi na TPA hii ikiwa ni pamoja na Wakala wa Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Wizara ya Kilimo na Chakula, Wizara ya Uvuvi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Mionzi Tanzania (TAEC), Chama cha Mawakala wa Ushuru na Forodha (TFFA) na Chama cha Mawakala wa Meli (TASAA) na wadau wengine wote wanaofanya kazi na TPA.

Muonekano wa Tovuti mpya ya TPA inayopatikana kupitia www.ports.go.tz

‘‘Tovuti hii pia itatumika kutangaza mifumo mbalimbali ya Mamlaka inayohusiana na utoaji wa mizigo Bandarini’’

Page 13: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 13

Jamii

VIFAA TIBA, MADAWATI, VYANDARUA, NA MABATI VYAKABIDHIWA KUSAIDIA JAMII

Na Focus Mauki

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Huduma), Bi. Fransisca Muindi akikabidhi msaada wa madawati kwa Shule ya Msingi Bangwe, Kigoma.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendelea na mkakati wake wa kuchangia huduma za jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali kwenye jamii zilizopo katika maeneo yenye Bandari hapa nchini.

Baadhi ya misaada hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko, huku mingine ikitolewa na Manaibu Kaimu Wakurugenzi Wakuu Bi. Fransisca Muindi na Bw. Lazaro Twange. Kwa upande wa misaada iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Deusdedit Kakoko ni pamoja na visima vitatu vya maji ambavyo amevikabidhi kwa wakazi wa Kata ya Kemondo kijiji cha Rwagati. Visima hivyo vitatu vya maji safi vipo katika vijiji vya Mashule na Burogo vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Vijijini. Misaada mingine iliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu ni pamoja na msaada wa madawati tisini (90) yenye thamani ya Shilingi Milioni 9.9 ambayo aliyakabidhi kwa Shule ya Msingi Lushamba iliyopo katika

Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Sengerema. Msaada mwingine uliokabidhiwa na Mhandisi Kakoko ni mashuka 900 yenye thamani ya Shilingi Milioni 10 ambayo yamekabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaviva kwa ajili ya hospitali tatu (3) za Manispaa ya Temeke. Mbali na msaada huo Mamlaka pia imetoa msaada wa vifaa tiba vikiwa ni vitanda saba (7) vya kujifungulia wajawazito pamoja na vyandarua mia tatu (300) vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15. Vifaa tiba hivyo vilikabidhiwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Uendeshaji), Bw. Lazaro Twange kwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe. Dk. Vincent Naano ambaye alisema vitatumika kupunguza uhaba

kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa ya Musoma pamoja na kwenye vituo vingine vya afya vya Bweri, Nyasho, Mwangi na Nyamatare. Kwa upande wake Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Huduma), Bi. Fransisca Muindi alikabidhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu msaada wa mabati 625 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kalinzi pamoja na madawati 130 kwa ajili ya Shule ya Msingi Bangwe Mkoani Kigoma. Mbali na misaada hiyo Mamlaka pia tayari imekabidhi msaada wa mashuka 300 kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Wilayani Chato. Mpaka sasa tayari Mamlaka imekwishachangia misaada ya aina mbalimbali kwa jamii yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 75.

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu (Uendeshaji), Bw. Lazaro Twange akikabidhi madawati kwa Shule za Kanda ya Ziwa

‘‘Mbali na msaada huo Mamlaka pia imetoa msaada wa vifaa tiba vikiwa ni vitanda saba (7) vya kujifungulia wajawazito pamoja na vyandarua mia tatu (300) vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15.’’

Page 14: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

14 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Michezo

Prof. Rubaratuka ametoa nasaha hizo hivi karibuni wakati alipozungumza na Wafanyakazi kwenye uzinduzi wa michezo ya Bandari (Inter-Ports) 2017 iliyomalizika jijini Mwanza hivi karibuni. “Bodi ya TPA inatambua na kuthamini michezo kwani inajenga afya, ukakamavu na kudumisha ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuongeza tija ndani ya Mamlaka, hivyo itumieni michezo hii kuongeza tija kwenye maeneo yenu ya kazi,” amesema Prof. Rubaratuka. Mbali na kusisitiza jambo hilo, Prof. Rubaratuka pia ameipongeza Menejimenti pamoja na DOWUTA kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika maeneo mbalimbali ya Bandari huku kwa mwaka huu yakifanyika jijini Mwanza. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko amewataka Wafanyakazi kutumia fursa waliyoipata kushiriki

Michezo ya Bandari ambayo imekuwa maarufu inashirikisha michezo ya aina mbalimbali kama vile mpira wa miguu (soccer), mpira wa pete (netball), riadha, kurusha mkuki, kuvuta kamba na mchezo wa kikapu (basketball). Michezo hii kila mwaka huzishirikisha timu mbalimbali ambapo kila kituo hutoa timu shindani. Bandari na vituo vinavyoshiriki michezo hii kila mwaka ni pamoja na Makao Makuu, Bandari ya Tanga, Bandari ya Mtwara, Bandari ya Kigoma, Bandari ya Mwanza, Bandari ya Kyela pamoja na Bandari ya Dar es Salaam.

“Bodi ya TPA inatambua na kuthamini michezo kwani inajenga afya, ukakamavu na kudumisha ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuongeza tija ndani ya Mamlaka, hivyo itumieni michezo hii kuongeza tija kwenye maeneo yenu ya kazi,”-Prof. Rubaratuka

Na Focus Mauki

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka

ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Prof. Ignas Rubaratuka amewaasa Wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na kuongeza tija katika maeneo yao ya kazi.

michezo kwa kubadilishana uzoefu miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kudumisha ushirikiano baina ya Wafanyakazi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPA, Prof. Ignas Rubaratuka akizungumza na

Wafanyakazi (hawapo pichani), Jijini Mwanza hivi karibuni.

“WAFANYAKAZI ONGEZENI TIJA”-PROF. RUBARATUKA

Page 15: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017 | 15

Michezo

Bandari ya Dar es Salaam imeibuka kidedea na kuendelea kuweka historia baada ya mwaka jana Bandari ya Tanga kutawazwa washindi lakini kwa mwaka huu kushindwa kuutetea ubingwa wao. Bandari ya Dar es Salaam iliibuka washindi wa kwanza katika michezo yote ikiwemo Kandanda, Bao, Pete, Kamba, Mkuki (wanaume) huku Bandari ya Tanga wakiambulia ushindi wa kwanza katika Mchezo wa Kikapu, Kurusha tufe (wanaume) na Mkuki (wanaume/wanawake). Michezo hiyo ilizinduliwa rasmi tarehe 15 Oktoba 2017 na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Profesa Ignas Rubaratuka na kufungwa tarehe 20 Oktoba 2017 na Mkuu wa Bandari ya Mwanza Bw. Daniel Sira kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko. Awali, akizindua Michezo hiyo, Prof. Ignas Rubaratuka aliwaasa Wafanyakazi wa TPA kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza tija. “Bodi ya TPA inatambua na

BANDARI YA DAR ES SALAAM KINARA “INTER-PORTS GAMES 2017’’

Na Innocent Mhando

Bandari ya Dar es Salaam imeibuka mshindi wa jumla katika Michezo ya 10 ya Bandari “Interports Games Season 10 2017” iliyofanyika Jijini Mwanza katika viwanja vya CCM Kirumba.

kuthamini michezo kwani hujenga afya, ukakamavu na inadumisha ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuongeza tija ndani ya Mamlaka,” amesema Prof. Rubaratuka, na kuipongeza Menejimenti ya DOWUTA kwa kuandaa mashindano hayo. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko amewakata Wafanyakazi kutumia fursa waliyopata kushiriki michezo kubadilishana uzoefu miongoni mwao na kudumisha ushirikiano. Wakati akifunga michezo hiyo Mkuu wa Bandari ya Mwanza Bw. Daniel Sira akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alitoa pongezi kwa Menejimenti kwa kudumisha na kuendeleza michezo hiyo kwa kuwa inawakutanisha Wafanyakazi na kuboresha afya zao. “Michezo hii inatuunganisha, inaboresha afya za wafanyakazi na ndio maana inaendelea, hivyo naipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari

Timu ya kuvuta kamba Bandari ya Tanga ikiwa katika mashindano ya Michezo ya Bandari ambayo yamefanyika Jijini Mwanza hivi karibuni.

na Wafanyakazi wote” alisema Sira.Pia alipongeza Kamati ya michezo kwa maandalizi mazuri na wafanyakazi kwa ujumla waliojitokeza kushiriki katika michezo mbalimbali na kuwakilisha vyema vituo vyao pamoja na nidhamu waliyoionesha kipindi chote cha michezo hiyo mapaka kufikia tamati. Wachezaji bora kwa mwaka huu na aina ya Mchezo na Kituo chake katika mabano ni Bw. Joel Maganga (Kandanda, Tanga), Bi Angela Kapaya (Pete, Tanga), Bw. Omary Said ( Bao, Dar es Salaam), Shagi Benjamini (Riadha wanaume, Tanga) Bi. Fadhila Yusufu (Riadha wanawake, Dar es Salaam). Katika mchezo wa Kamba wanaume mshindi ni Fred Katembo wa Bandari ya Maziwa na kwa wanawake Bi. Pricilla Mkaka wa Makao Makuu

Inaendelea UK 16 >>

Page 16: TPA YATENGA MILIONI 75 KUSAIDIA ELIMU, NDANI AFYA …

16 | TPA GAZETI NOV 13 - NOV 25 2017

Michezo

(Hq) aliibuka kidedea.Muhstasari wa washindi wa Michezo mbalimbali na vituo vyao ni kama ilivyoonyeshwa hapo chini kwenye Jedwali:

Michezo ya Bandari “Inteports Games” hushirikisha timu kutoka Bandari ya Dar es Salaam, Maziwa, Tanga , Mtwara katika michezo mbalimbali ikiwemo Kamba, Kandanda, Mpira wa Pete, Riadha Bao na Kurusha tufe na Mkuki.

JEDWALI (1)1 2 3 4 5

MCHEZO KANDANDA MPIRA WA PETE

MPIRA WA KIKAPU

KAMBA RIADHA (Overall)

MSHINDI DSM PORT (1) DSM PORT (1) TANGA (Wanaume ) (1) DSM PORT

DSM PORT(Pts 102)

MAKAO MAKUU (2) TANGA (2) DSM PORT 2) TANGA TANGA PORT(Pts 99)

(3) MAKAO MAKUU

(3) MAZIWA (3) MAKAO MAKUU

MTWARA (Pts 51)

(Wanawake) (1)DSM PORT

(2) MAKAO MAKUU

(3) TANGA

JEDWALI (2)1 2 3

MCHEZO BAO MKUKI (Wanaume) TUFE (Wanaume)

MSHINDI (1) DSM PORT (Pts. 14) (1) DSM PORT(Siraji Yusuph)

(1) TANGAMohamed Fazal

(2) TANGA (Pts 12) (2) MAZIWA(Fredy Katembo)

(2) DAR PORTAlly Mnubi

(3) HQ NA MTWARA (Pts. 10)

(3) TANGA(Abdallah Waziri)

(3) Siraji Yusuph

MCHEZO MKUKI (Wanawake) TUFE (Wanawake)

MSHINDI (1) TANGAAmina Kubo

(1) TANGAAmina Kubu

(2) TANGA Gladness Mwandigha

2) DAR ES SALAAMHawa Senkoro

(3) DAR PORTModesta Kaunda

(3) MTWARALetician Njunju

<< Inatoka UK 15