Top Banner
JOHARI YA TIBA ASILIA Suweid s suweid
40
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: tibb

JOHARI

YA

TIBA ASILIA

Suweid s

suweid

Page 2: tibb
Page 3: tibb

September 2011

Page 4: tibb

DIBAJI

1. UTANGULIZI.................................................ERROR! BOOKMARK NOT DEFINED.

2. AINA YA TIBA ASILIA.....................................ERROR! BOOKMARK NOT DEFINED.

3. TAALUMA....................................................ERROR! BOOKMARK NOT DEFINED.

4. NASAHA......................................................ERROR! BOOKMARK NOT DEFINED.

4.1 Existing conditions.....................................................Error! Bookmark not defined.

4.2 Type of soil.................................................................Error! Bookmark not defined.

4.3 Maximal stress with reconstructed deck and SATCC loading.....Error! Bookmark not

defined.

4.3.1 Abutments................................................................Error! Bookmark not defined.

4.3.2 Piers.........................................................................Error! Bookmark not defined.

4.4 Conclusion..................................................................Error! Bookmark not defined.

5. RESULTS OF THE STRUCTURAL ANALYSIS – DETERMINING LOAD CASES

ERROR! BOOKMARK NOT DEFINED.

5.1 Calculation of support reactions.................................Error! Bookmark not defined.

Page 5: tibb

UTANGULIZI

الرحيم الرحمن الله بسم

Amesema ALLAH S.W katika kitabu chake kitukufu Q 17:18; “Na tukaiteremsha Qur’an

kuwa ni ponyo na ni rehma kwa wale wanao amini.”" شفاء هو ما القران من وننزل

للمؤمين "ورحمة

Nae mtume S.A.W “amesema “kila ugonjwa una dawa yake”. " دواء داء "لكل

Basi ni wajibu wetu kustafiti na kupata tiba halali kwa magonjwa yanaotupata sisi

wanaadamu.

Alhamdulillah namshukuru ALLAH S.W. kwa neema zake na uwezo wake yeye alo tukuka

kuliko kiumbe chochote.mfano wake hamna hakuzaa wala hakuzaliwa.Na

maombi na sala pamoja na salam zi muendee Bw. Wetu MUHAMMAD S.A.W

pamoja na swahaba zake.Na rehma ziwashukie walimu na maulamaa pamoja na

mawalii wa ALLAH S.W. Amiin ya rabbal alamiin

Namshukuru ALLAH S.W kwa kunipa fursa hii ya kuandaa yaliomo katika tiba

asilia.Nimeweza kugundua kwamba tiba za kiasili ni aula au bora kuliko tiba za

kisasa ambazo ni mchanganyiko wa kemikali (Chemicals) Kwani:

Utumiaji wake ni salama hazina madhara baada ya utumizi wake (“side effect”) mfano

Thalidomine na penicillin n.k.

Dawa za kiasili zina uwezo wa kutibu ugonjwa zaidi ya moja mfano asali.

Dawa za kiasili sio ghali kama za kisasa

Nchi kama China, India na South Africa zipo mstari wa mbele kuendeleza na kustafiti njia

bora za matumizi ya tiba za asili ambapo wameweza kufungua vyuo vya tiba asilia mfano:

Chinese Medical institute (China) na Ibn Sina intitute of Tibb (South Africa).

AINA YA TIBA ZA ASILIKuna aina nyingi za tiba asilia nitaelezea baadhi kwa kifupi.

Page 6: tibb

Tiba ijulikanayo kama tibb (Greeco-Arabic medical therapy) asili yake ni Arabuni nayo

pia hutumika sehemu za Uswahilini kama vile pwani ya Afrika Mashariki. Tiba hii asili

yake haswa ilitumika sehemu ya Arabuni na hata mashariki ya bara uropa na ilikuwa

katika enzi za utawala wa Bw. Mtume S.A.W., enzi za Ummaya (Ummayads) Abbasiya

(Abbasids), Fatmiya (Fatmids), Uthmaniya (Ottomans). Tiba hii ina jumuisha matabibu wa

kiyunani(Greeks) kama Hippocrates na Aristotle’s ambao ni wana falsafa wakubwa

pamoja na matabibu wakubwa wa kiislamu kama vile Ibn SINA(Avicenna) na Ibn RUSHDI

na wengine wengi walioweza kufanya maajabu ya tiba asili kwa wakati huo . Tukiongezea

juu ya tiba hii pia kuna TIBB NABAWI ambao ilitumika wakati wa mtume wetu

MUHAMMAD S.A.W. Hii ni tiba ambayo inahusu sana zinguo. Kuzinguliwa ni ile hali ya

kusomewa Qur’an tukufu kwa ajili ya kupata unafuu au kupona kutumia aya tukufu au

kujisomea na kujizingua kutumia aya tukufu au;

“ISMULLAHUL 3’ADHAM. األضم الله ”اسم

" للمؤمين ورحمة شفاء هو ما القران من "وننزل

Q 17:18; “Na tukaiteremsha Qur’an kuwa ni ponyo nani rahma kwa wale wanao

amini.”

Qur’an ni pozo la la maradhi. Bw. MtumeS.A.W. Asema:

“Bora ya dawa ni Qur’an”

“ القران الدواء ”خير

Fani hii ya tiba ilikuwa ni elimu iliotangaa mno miongoni mwa waarabu na ilikuwa na watu

maalumu katika zama tofauti. Mtume (S.A.W) alimteua Al-Harith bin kaldah (R.A) kumtibu Sa’3ad

bin Abiwaqas(R.A.)

Tiba lishe (dieto therapy) tiba hii inakusanya lishe ambazo tunatumiakwa ajili ya afya

ya binadamu. Nayo ni vigawanyo miongoni maboga, matunda, nyama n.k. Mtume asema:

“ : القرا بشفاءين والعسل نعليكم ”

Shikamaneni na dawa mbili :Qur’an na asali.

Tiba tabii (nature-therapy) tiba hii inatumia uwezo wa kitabii(nature) kama vile nishati

ya jua(sun energy) kutumia udongo(clay) maji(water) n.k. ALLAH S.W asema katika

Qur’an tukufu

“ يؤمنون افأل حي شيء كل الماء من ”وجعلنا

“na tukajaaliya maji ni uhai wa kila kitu jee hamuamini ?”

Tiba ya sumaku (magneto-therapy) tiba hii nayo ina tumia nishati ya sumaku kuponya

maradhi yanao sumbua pia hata maradhi sugu ambayo yamewashinda madaktari bingwa.

Tiba hii ni salaama ana poza 100%.

Tiba ya kubonyeza na za kutoboa (acupressure and acupuncture) na tiba nyingi

ambazo ni zenye faida na wala hazina madhara kama tiba za kisasa zinazo jumuisha

upasuaji na uchunguzi wenye gharama nyingi kama vile kupembuliwa (medical scanning)

ambazo zinatumia mionzi mikali (radiation) pia kuna na X-RAY (inayotumia mionzi ya

infra-red n.k) zote hizi huweza kumsababishia anaetibiwa kupata ugonjwa wa saratani

Page 7: tibb

(cancer) aidha wa ngozi za mwili au kichwa na kadhalika. Hivyo basi tiba asilia ndio njia

bora na yenye natija ya pozo 100%.

Tiba ya mkojo (Auto urine therapy) hii nayo ni tiba inayo tumia mkojo. Tiba hii

hutumika sana Hindi na China. Uhindini tiba hii ina julikana sana na inaitwa SAVIMBI.

Hivyo kuifanya ni tiba rahisi zaidi juu ya upatikanaji wake wa mkojo. Pia unaweza

ukatumia pamoja na sumaku kujitibia. Tiba hii kwa muislamu inakuwa ni haramu kwa

sababu mkojo ni najisi. Lakini endapo kutakosekana namna ya ponyo basi inajuzu

kuitumia mpaka upatapo unafuu au kama huduma ya kwanza ili au mpaka ipatikane tiba

mbadala ilio halali ili kupona.

Tiba inayotumia tembe zilizo hakikiwa kisasa zitokanazo na mitishamba (Homoeopathy).

Tiba hii pia hutumika sana bara la asia nayo imefanyiwa utafiti wa kina ambao ni

wakisasa kabisa unaoendana na tiba za kisasa wa kutumia tembe mf. Aconite 30 inayo

tibu magonjwa kama maumivu ya mgongo au maumivu ya jointi za mwili n.k. Mazoea ya

matumizi ya madawa ya kisasa husabisha uleweshaji kama mabugizi (tranquilizer)

ambazo ni dawa zinazotumika hospitalini.

Tiba ya Ayurveda. Hii ni aina ya tiba ambayo ilitumika sana Uchinani na Uhindini kwa hiyo

utakuta tiba hizi zimetiliwa mkazo nchi mbili hizi. Tiba ya yoga ni tiba nzuri tu yenye uwezo wa

kuponya. Mgonjwa una takiwa kuwa mvumilivu na kufata maagizo kama yanavyo elekezwa.

Msisitizo wa tiba hii ni kupasha mazoezi kulinda afya yako. Huu ni uwazi kwani ufanyapo

mazoezi hua unajijenga kiafya na kujikinga na maradhi madogo madogo kama homa n.k.

Tiba za jadi (traditional medicine) aina ya tiba hii ilitumiwa sana na babu zetu katika

bara la Afrika.Tiba hii ilihusisha sana utumizi wa mizizi ya mitishamba au miti yenyewe

hata majani. Pengine kwa kunusa au kutafuna au hata kumeza na mtu ukapona. Wengi

tunazidharau au kuziogopa tiba hizi kwa kuzifikiria tu kwamba hazitibu au kuponya mtu

kwa vile niza kizamani au zimepitwa na wakati. Hizo ni fikra tu lakini ukweli ni kwamba

mababu na mabibi waliweza kudumu na dawa hizi kutoka jadi na jadi na waliweza kuishi

maisha marefu tofauti na sisi wa leo . Ondoa fikra hizi kwani dawa za jadi ni tiba na

inaponya amini usiamini. Kuna tafauti ya utabibu wa jadi ambao unajulikana kama

utabibu na kuna uchawi ambao ni ushirikina na haramu kwa sababu urogi wa aina yoyote

ule ni matendo ya kinyume cha maadili ya jamii kidini na kitikadi za kidunia kwani

mchawi anaporoga mtu basi humdhuru. Na waganga feki ambao hudanganya watu

kwamba wanauwezo wakuwaondoshea shida zao na tabu zao. Usiamini kwani ni waongo

na wazandiki wakuu wasio na uwezo waina yoyote. Bali mtegemezi wako ewe muislamu

awe ni ALLAH S.W. Amesema Mwenye ezi Mungu S.W. katika surat (3araf:24)

( ينصرون والانفسهم نصركم اليستطعون دونه من تدعون (ولدين

Page 8: tibb

TAALUMAKuna msemo usemao “kinga ni bora kuliko tiba” (prevention is better than curation).

“ العالج خيرمن ”الوقية

Binadamu kwa hakika ameumbwa na umbile dhaifu sana hivyo basi anapopatikana na

dhiki ya maradhi basi huwa ni mdhaifu zaidi ya utakavyomfikiria wakati akiwa ana uzima.

Mfano mzuri; mathalan: anapodungwa na mwiba mdogo tu basi huhangaika sana hadi

mwiba ule uondolewe. Huu ni uthibitisho wa wazi zaidi kama alivyothibitisha ALLAH S.W.

katika QUR’AN tukufu. Kwa hiyo binadamu ana takiwa kuwa makini zaidi juu ya siha

yake. Kuna taratibu ambazo zina mpasa binadamu kuzifuatilia kwa umakini ili uweze

kujikinga na magonjwa mengi. Ili tuweze kujifahamu tunatakiwa kujua lishe inayo mpasa

mtu kupata.

LISHE

Chakula ni muhimu kwa maisha ya mtu. Mtu alie hai huitaji vyakula vya aina mbalimbali

kwa kazi mbalimbali mwilini. Mahitaji ya chakulakwa mmea na hayatofautiani sana.

Mimea ina uwezo wa kusanisi chakula chao lakini wanyama na binadamu hutegemea

mimea. Vyakula vimegawanyika kama ifuatavyo;

Wanga (carbohydrate), mafuta na samli (fats & lipids), protini (protein), vitamini (vitamin),

madini (minerals).

MLO KAMILI

Mlo kamili ni mlo ulo na protini, wanga, mafuta na samli, madini na vitamin.

Tunahitaji chakula kulingana na umri, kazitunazozifanya, mwili wa mtu, afya ya mtu,

ujauzito na kunyonyesha.

Mahitaji ya wanga ni 80%.

Mahitaji ya protini ni 10%.

Mahitaji ya vitamin, madini, mafuta na samli pamoja na maji ni 10%.

MMENG’ENYO WA CHAKULA (DIGESTIVE SYSTEM)

Ili chakula kitumike mwilini kwa ajili ya afya yako, kina hitaji kivunjwevunjwe na

kusagwasagwa kiweze kuwa katika hali rahisi ya kuweza kusharabiwa. Kazi hiyo

hufanywa na mfumo wa mmeng’enyeko (digestive system). HIchi ni kitendo cha kubadili

chakula kutoka hali tata isoweza kusharabiwa kuwa katika hali rahisi inayoweza

kusharabiwa na mwili. Chakula kinaposafiri katika njia yake hufanyiwa mabadiliko ya

kiumbo na kikemikali. Kila sehemu ya mmeng’enyo wa chakula ina kazi maalumu.

Zifuatazo ni kazi za kila sehemu.

KINYWA

Sehemu ya mwanzo ipokeao chakula.chakula kiwepo mdomoni hutafunwa na

kusagwasagwa na meno. Mate husaidia kukilainisha. Ulimi husaidia kukigeuzageuza na

kukiviringisha kuwa tonge. Kwa msaada wa ulimi, tonge hilo husukumwa kuelekea

Page 9: tibb

kwenye umio. Napo husukumwa kuelekea kwenye mfuko wa tumbo. Hapa basi vyakula

rojorojo hupita kwa urahisi kuliko vile vizito.

MFUKO WA TUMBO

Hapa chakula kinahifadhiwa kwa masaa tatu hadi nne. Mfuko huu unauwezo wa

kupanuka ukiwa na chakula na kusinyaa au kujirudi ukiwa hauna chakula. Chakula

huchanganywachanganwa kwa muda wote kinapokuwa kwenye mfuko huu pamoja na

misukumo iliopo husababisha chuzi lijulikanalo kama tuitumbo.

INI

Hii ndio ogani kubwa kuliko zote katika kiwiliwili cha binadamu Ini huweka akiba ya

chakula Kama wanga iitwayo glaikojeni, pia vitamin na madini. Ini hutengeneza nyongo

ambayo husaidia katika mmng’enyo wa mafuta na samli.

UTUMBO MWEMBAMBA

Utumbo huu ni mwembamba na mrefu zaidi kuliko ogani nyingine yeyote ya njia ya

chakula. Chakula huwa ndani hapa kwa muda mrefu zaidi. Chakula hukutana na

misukumo yenye vinyeng’enya vitokavyo kwenye kongosho na utumbo mwembamba,

vinavyo saidia katika uyeyushaji na kusharabiwa kwa sehemu kubwa ya chakula.

Mchuziko huu uloyeyushika ulo na virutibisho husambazwa kwenye mwili wote na ndio

mwili ukapata afya na nguvu mtu akaweza kutembea na kufanya kazi.

UTUMBO MPANA

Chakula ambacho hakikusharabiwa wala kumeng’enywa huelekea kwenye utumbo

mpana, sehemu ndogo ya chakula hiki husharabiwa na kumeng’enywa hapa. Sehemu

kubwa ya maji yaliotokana na mmeng’enyo wa chakula husharabiwa na utumbo

mpana.Sehemu iliobaki ya chakula huelekea kwenye puru (ujiko) na kutolewa nje ya

mwili kupitia hajakubwa kama kinyesi.

KUSHARABIWA KWA CHAKULA

Baada ya chakula kumeng’enywa inafikia hatua ya kusharabiwa na vinywelea vilivyo

katika utumbo mwembamba.Vinywelea hivi vijulikavyo kama vilasi huchuja protein,

wanga na madini zilizosharabiwa na kugeuzwa aminotindikali(aminoacid), sukari nyepesi

(glucose),tindikali za mafuta na shahamutindikali(fattyacid) na chumvi husafirishwa

kwenye mishipa ya vena hadi kwenye ini. Mchuziko huu husafirishwa na damu hadi

kwenye moyo.Damu hiyo nayo husambaza chakula hicho mwili mzima kwa matumizi

mbalimbali ya kiafya. Hapa sukari na amino huhifadhiwa kama glaikojeni na pia

hupatikana yurea ambayo ni tindikali (uricacid). Ile ambayo haitajiki mwilini huchujwa na

kusafirishwa kwa kibofu cha mkojo nayo huchanganyikana na maji ambayo

hayakusharabiwa nao hutolewa nje ya mwili kama mkojo kupitia haja ndogo.

AFYA Ni hali inayotokamana na kuwa mzima wa umbile (physical), akili (mental) na

uchangamfu (social) na kuwa huru kutokana na maradhi na udhaifu unaosababishwa na

maradhi. Unatakiwa kuzingatia mambo ambayo yanaweza kukupa tiba kwani Imam

Ghazali asema “tiba ya mgonjwa anayo mwenye kuugua ugonjwa” hivyo basi mgonjwa

Page 10: tibb

anajuwa ni ugonjwa gani unaomsibu hivyo kutoa njia na namna atakavyotibiwa.

Binadamu anatakiwa ajiangalie na kujilinda ili malengo ya kuwa na siha yawepo. Umbile

lake limeumbwa na seli zinazo ungana kama alivyosema ALLAH S.W. (Q. 76:2)

“ نطفةامشاج من خلقنااالنسان ”ان

Kuna mambo kadhaa yanayo pelekea kuwa katika afya bora nayo ni:

I. Mazingira (environment).

Unapopumua na kupata hewa safi (oxygen) unakuwa ni mwenye siha kiukamilifu kwani

hewa nzuri iko huru na madhara na magonjwa yanayo sababishwa na hewa chafu au

mbovu. Hewa ya joto huleta magonjwa lakini pia hutibu magonjwa yaletwayo na hewa

baridi. Hewa baridi husaidia kwenye mmeng’enyeko wa vyaakula n.k. Ibn Sina ametuarifu

kwamba “hewa ndio kiini cha maisha”. Hewa in poza na kudhibiti halijoto ya mwili. Pia

ina safisha hewa ambazo hazifai kuwa mwilini kama kabondayoksaid. Maumivu ya

kichwa na hata uchovu wa mwili husababishwa na upugufu wa hewa ya oksijeni mwilini.

Hasira na woga pia vinaweza unamudu upatapo hewa safi na kamili. Fanya zoezi la

kupumua kila siku utaepukana na maradhi mengi duniani.

Zoezi la kupumua hewa safi.

Unafanya zoezi hili kila alfajiri kwa sababu oksijeni haijachafuka (polluted) ni safi. Njia za

kupumua ni kuvuta hewa safi ndani kwa utaratibu huku ukisikilizia mlio wa “aah” na

kuzizuia kwa muda wa kama dakika tano au kumi na ukizoea ishirini, halafu toa pumzi

zote kwa pamoja ukisikilizia mlio wa “hu”.hivyo kulirudia zoezi kila mara ukiwa umetulia.

Kwa kufanya zoezi hili unaepukana na hisia za hasira, woga, na pia unapata usingizi

mzuri unapolala usiku. Niajabu lakini ni kweli pia.

Pia dawa zinazo mfaa mgonjwa ni zile zinazotoka pale aishipo mgonjwa. Mazingira ya

mgonjwa na dawa ni mamoja,

II. Chakula (food) na vinywaji (drinks).

Vyakula tulavyo ni muhimu sana katika kuhakikisha mtu anakuwa na afya bora ili

kuhifadhi nguvu za mwili kufanya kazi tofauti za kimwli na zisizo za kimwili. Baadhi ya

vyakula huathiri na kuleta matatizo yanayo sababisha upungufu wa mwili kufanya kazi

itakikanavyo au hata kusababisha magonjwa na maradhi mengi. Vyakula vyenye mafuta

mengi sio vizuri kwani huharakisha mishipa ya damu kukakamaa na hivyo kupunguza

uwezo wa damu kuzunguka mwilini hivyo basi huleta upungufu wa nguvu mwilini au hata

kuwa na udhwaifu wa kufanya tendo la ndoa. Vinywaji kama kahawa huharibu mishipa ya

damu na kusababisha shinikizo la damu. Pombe aina zote sio salama. Pombe ina sumu

ambayo huathiri mishipa ya fahamu pole pole bila mnywaji kujitambua. Pombe pia

huharibu mishipa ya damu na kuathiri utendaji kazi wa ini ambalo husaidia kutoa sumu

mbalimbali mwilini. Ama katika vinywaji bora ni maji.

“Msinywe kinacholewesha kwani kileweshaji ni kilevi na kilevi ni haram.”

" حرام مسكر وكل حمر مسكر "كل

Vyakula vya joto husababisha joto mwilini na kinyume ya vyakula vya ubaridi.

Mwanafalsafa Hippocrates anatuarifu katika nadharia ya chakula na vinywaji kwamba:

Page 11: tibb

“kama ugonjwa tiba yake ni chakula basi achana na madawa” tiba inaongozwa na lishe

ya binadamu hivyo basi kipengele kikubwa cha sha bora ni lishe. Madhara mengi

yanaletwa dharau juu ya lishe. Nimeelezea namna gani chakula kinameng’elwa na

kusharabiwa ndani ya kiwiliwili cha mwanadamu. Mwisho wa kusharabiwa linapatikana

joto. Joto nalo ni muhimu linatakiwa lisizidi au kupungua wakati wa mmeng’enyeko.

Elimu ya viumbe hai pamoja na kemia ina tegemea sana aina ya chakula kilichotumika.

Chaguo la chakula linategemea mambo mawili nayo ni:

Tabia na mwenendo wa mtu kutokana na umri, msimu wa majira na hali ya hewa.

Mizani ya kusharabiwa. Vyakula na vinywaji viko katika mzunguko wa aina moja.

Kutafunwa na kukimeza kisha kimeng’enywe kwenye utumbo kisha kusharabiwa halafu

kusambazwa mwilini kama chuzi kupitia mishipa ya damu kwa kazi mbalimbali za kimwili.

Ulaji wa lishe bora.

Ili uboreshe afya yako katika awamu mbalimbali za maishaunahitaji ulaji wa aina tofauti.

Mtoto mdogo anahitaji virutubishiili kusaidia ukuaji wa mwili, kijana nae

anhitajikuboresha afya yake ili kuwa na kujengeka kimwili na kisaikolojia katika ukuaji

wake,vilevile mtu mzima nae anhitaji lishe bora kumwezesha kuwa na afya bora

kuendesha maisha yake na familia yake. Vilevile kina mama wajawazito na

wanyonyeshao wanahitaji lishe bora nao ili waweze kuwalelea viumbe ambavyo ni

tegemezi juu ya lishe wanayoitumia.

III. Mwendo (movement) na mapumziko (rest).

Maisha ni harakati, hivyo maisha ni mwendo na mwendo ni maisha. Katika mfumo

mzima wa maisha ya binadamu mpaka wakati anapokufa tunaona yupo katika mwendo

wa harakati za kimaisha. Huu ni mfumo wa kawaida kabisa na wa kiasili. Kuna harakati

aina mbili katika mfumo mzima wa mwanaadmu nazo ni:

I) Mwendo hiari (voluntary Movement), hii ni mienendo ambayo inatokamana

na umbile la nje lenye muonekano asilia nayo ni kwa utumizi wa miguu,

mikono, vidole, mdomo n.k. mienende ya viungo hivi tuna vidhibiti na

kuviongoza.

II) Mwendo usio wa hiari (involuntary movement) ni mienendo ambayo hatuna

uwezon wa kuvidhibiti na kuviongoza mfano mapigo ya moyo, upumuaji,

pafu, utumbo, n.k.

Mwendo au kuwa katika harakati huleta joto mwilini. Na unapopumzika basi mwili hupata

ubaridi unazubaa. Nishati ni lazima kwa ajili ya mienendo yetu. Ikiwa harakati za kimwili

zataongezeka basi joto nalo lina ongezeka hivyo vuguvugu kupungua, viungo

vinapochoka huitaji mapumziko ili kupunguza joto na kutia uvuguvugu kwani ukizidisha

harakati za mwili basi inamadhara hivyo mapumziko yakuwa ni wajibu. Kulala ndio aina

kubwa ya kujipumzisha ukizidisha kulala pia ina madhara yake. Kwa kawaida binadamu

anatakiwa kujipumzisha masaa sit akizidisha masaa nane. Lakini sio zaidi ya hayo kwani

mshairi atuambia:

" حب علي شب انتهمله كالطفل والنفس النهم شهوة يقوي الطعم ءن

ينفطم تفطمه وءن "الرضاع

" يصم او يصم ماتولي الهواي ءن توليه ان وحاذر هواها "فاصرف

Page 12: tibb

Hakika chakula ni chenye huzidisha matamanio na nafsi ni kama mtoto mchanga

anyonyweshwapo hupenda kunyonyeshwa na unapomzuia basi nae huacha.

IV. Hisia/Jazba (emotion).

Hisia humwongoza mtu kwa yale atakayo yafanya. Mfano hasira, furaha n.k. mwili wa

binadamu unathiriwa na jazba na hisia. Hisia ni kuwa na: hasira, furaha, karaha, huzuni

na aibu. Hasira inachemsha mwili na kukausha mwili. Mtume S.A.W. ametuasa juu ya

hasira kama muislamu unatakiwa kuzuia hasira kutokana na mafunzo ya dini ya kiislamu.

Na katika Qur’an 3:34 imezungumzia kuhusu hasira. Kuhusu furaha imeruhusiwa kwa

muumin kama alivyo taja ALLAH S.W. katika Qur’an tukufu 10:58

“ فليفرحوا فبذالك برحمته و الله بفضل ”قل

“Sema kutokana na fadhla za mola wako na rehema zake zinazo wafanya

kufurahikia”

“ بضله من بماsاتاهمالله ”فرحين

“Ya furahikieni ambayo ALLAH S.W. alowapa na kuwaneemesheni” (Q. 3:170).

Huzuni pia ni hisia na kaizungumzia sana bw. Mtume S.A.W. na ukiona umekuandama

sana basi sema “lahaula wala quwata illa billah”

Hiki ni kipengele kikuu katika tiba, ina hakiki uwezo wa mgonjwa kupona au kutokupona

au hata kufariki. Hii ina tokana na mgonjwa kuathirika kisaikolojia hivyo kutaalamu

kwanza anatakiwa atibiwe kisaikolojia. Jazba na hisia zinamadhara makuu kwa

mwanadamu husababisha ‘shock’ au shinikizo la moyo na kadhalika. Zifuatazo ni tabia

zinazoletwa na jazba au hisia:

Hamaki (anger), wasiwasi (worry), huzuni (grief), woga (fear), udhwaifu (depression),

msisimko (excitement). Uwezo wa kumbukumbu au kudhamiria ndio kipengele muhimu

katika hisia zenye jazba na kuleta madhara au kuwa sawa kisaikolojia. Kisayansi huitwa

psychoneuroimmunology ambayo inatokana na ubongo kushirikiana na mishipa ya

fahamu na kinga za mwili inayoipa uwezo wa kupambana na sumu zisababishazo

magonjwa na maradhi, ili mwili kuwa na afya njema. Na jambo la msingi kwa taaluma hii

ni akili kuwa katika hali bora yenye uwezo wa ufahamu thabiti.

V. Ulalaji (sleep) na uamkaji (wake).

Unapo lala basi viungo vyote vina pumzika na uwamkapo viungo vinakuwa katika

harakati.kila kiumbe anahitaji kulala ili kupumzisha akili na mwili. Mtu anapotoka jasho

usingizini ina maana kwamba maji pamoja na kioevu (fluid) zisizohitajika zimeondolewa

mwilini. Kutokana na mapumziko hayo ndipo zimeweza kuondolewa ndani ya mwili

kupitia utando wa juu wa mwili ambao ni ngozi. Unatakiwa kula chakula cha jioni masaa

matatu kabla ya kulala na utembee kwa muda wa dakika kumi na tano au ishirini. Masaa

bora kulala ni masaa nane na ianze saa nne hadi saa kumi na moja. Lala kuegemea

upande wa kulia kwani unakirahisishia chakula mwenendo wake kwenda kwenye utumbo

na pia inapunguza presha ya moyo ambao upo kushoto, pamoja na hayo pia kongosho

na ini zina fanya kazi vizuri. Unapolala kuegemea kushoto unasababisha presha kwa

moyo kutokana na chakula kuwa juu ya utumbo. Pia kulala sana au kulala kutokulala kwa

Page 13: tibb

muda unaotakiwa kunasababisha madhara kama uchovu, kudumaa akili,kuleta usumbufu

wa mmeng’enyeko wa chakula na kadhalika.

VI. Ufutaji (elimination) and Uzuiaji (retention).

Zikiwa katika mizani basi huwa inadumisha afya bora.

Mambo haya ndio Afya na ndio uhai wako. Linda afya yako kwa ajili ya uhai wako. Na

ujitakase kwa mola wako ili uwe ni miongoni mwa watu wema.Jambo muhimu kwa

mwanaadamu kuweza kulinda afya yake ni tumbo lake. Amesema mbora wa viumbe bw.

Mtume S.A.W.

“ النشبع أكلنا واsذا نجوع حتي نأكل ال قوم ”نحن

“Sisi ni Uma ambao hatuli ila tuwe na njaa na tulapo huwa hatushibi.”

Hizi ni miongoni mwa tabia za mtume alizo tufundisha ili kudumisha afya bora.kula sana

kuna madhara au hata kula hovyohovyo nako kuna madhara yake. Amesema tena mtume

S.A.W. katika hadith kutoka kwa imam Tirmidhy

“ فكانماحيزت يوما قوت عنده جسده في معافا سربه في امنا منكم اصبح من

فيرها ب بحذا الدنياى ”له

‘Aamkae asubuhi na akawa ni mwenye afya kimwili na kiroho nikama mwenye kumiliki

dunia nzima.’

MAJI

Page 14: tibb

MAJI NI UHAI.

“ يؤمنون افأل حي شيء كل الماء من ”وجعلنا

“na tukajaaliya maji ni uhai wa Kila kitu jee hamuamini?

Maji ni muhimu kwa viumbe hai hivyo basi tilia maanani sifa kamili ya maji yanayo mfaa

binadamu. Sifa zifuatazo ni muhimu sana kwa maji kuwa mazuri kwa matumizi yake nayo

ni:

1. Rangi ya maji iwe safi na angavu (transparent).

2. Yasiwe na harufu ya aina yoyote.

3. Yenye ladha ya kitabii (natural taste).

4. Yenye uzito hafifu yasiwe mazito sana.

Basi almuhimu ni kwamba asilimia 70 ya umbile la mwana adamu linahitaji maji.

Kutokana na hikma ya bwana mtume s.a.w kutoka kwa Anas bin Malik (R.A.) asema:

“ انه ويقول ثلث اشراب في متنفس وسلم عليه الله صلي الله رسول كان

وامرء وابرء ”اروي

“Mtume S.A.W hunywa kinywaji kwa matama matatu na kila tama husema hii

imetosheleza na yenye afya na yenye kukata kiu.”

Wala musinywe kwa kusimama.

" قائما يشرب ان نهيآ "انه

Ama katika vinywaji bora ni maji.

Msinywe kinacholewesha kwani kileweshaji ni kilevi na kilevi ni haram.

" حرام مسكر وكل خمر مسكر "كل

Aina za maji:

Maji ya mvua, maji ya kisima, maji ya bahari, maji ya ziwa, maji ya mto, maji ya umande,

maji ya mvuke na maji ya barafu.

Page 15: tibb

JOTO (HEAT) NA UNYEVUNYEVU

(MOISTURE)

Joto ni muhimu katika mwili wa binadamu. Kutokana na michakato (process) mingi

yanayofanyika mwilini, wakati wa mmeng’enyeko na kusharabiwa chakula, mwili huitaji

joto kwa ajili ya michakato ya mmeng’enyeko kufanikiwa kukamilika. Endapo joto

litapungua au kukosekana kabisa basi mmengenyeko hautakamilika au hata kufanyika

hivyo kusababisha kuenea na kupatikana kwa toksin ambayo ni aina ya kemikali yenye

sumu inayotolewa na bakteria ndani ya mwili yenye uwezo wa kudhuru seli za mwili. Hii

ina maana kwamba kwa mchakato wa aina yoyote ndani ya mwili wa binadamu kugemka

(transpire) lazima kuwe na uhamishaji na utumikaji wa joto. Wanasayansi wametafsiri

mchakato huu kama mwendojoto (thermodynamic: sayansi ya uhusiano wa joto na aina

nyingine za nishati). Mfano utafunapo tunda tufaa mwili unachemka kutoa nishati joto

(heat energy). Ili kuifadhi joto mwilini tunahitaji lishe bora ambayo itazalisha nishati kutia

joto mwilini. Pia ujiepushe na hisia, msongo (stress), mazingira na maradhi. Onyo:

kumbuka kwamba badiliko lolote hata kama ni dogo kiasi gani lina weza kukudhuru

auhata kukusababishia kifo. Kumbuka kwamba joto muhimu kuwepo kwa kila mchakato

unaofanyika mwilini lakini uvuguvugu ni hali halisi ya uhai wake. Pamoja na yote hayo

kumbuka 60% ya mwili umeumbwa kwa maji. Kila seli iliyo mwilini ina hitaji maji kuishi.

Ukosekanaji wa maji mwilini kuna ua haraka zaidi ya ukosekanaji wa chakula. Maji

yanadhibiti halijoto ya mwili na inabatilisha ain azote za toksin (sumu).

Joto na uvuguvugu ni asili halisi ya kiwiliwili cha binadamu. Hivyo kujenga tabia na hata

umbile lenyewe.

Kuna sifa za kimsingi ambazo ni lazima ziambatanishwe na joto pamoja na vuguvugu

nazo ni:

1. MOTO - Una sifa ya joto, kavu, hafifu na kakamavu.

2. HEWA - Ina sifa ya joto, vuguvugu, hafifu na kakamavu.

3. MAJI - Yana sifa ya baridi, vuguvugu, nzito na isiyo na hisia.

4. ARDHI - Ina sifa ya baridi, kavu, nzito naisiyo na hisia.

Kutokana na sifa hizo basi hata tabia na mwenendo wa binadamu unajulikana kutokana

na asili ya mambo yaliotajwa hapo juu. Ili kuwa na uchangamfu Hippocrates

amelizungumzia kinadharia na kuligawanya vigawanyo vinne. Navyo ni:

a). Damu (blood).

b). Balaghamu (phlegm).

c).Nyongo njano (yellow bile).

d). Nyongo nyeusi (black bile).

Hippocrates anasisitiza kwamba “umuhimu ni kujua sifa na tabia za mtu zinazomhusu ili

uweze kumtibu kuliko kufahamu maradhi gani aliyonayo mtu”

Page 16: tibb

Hivyo basi silka ya mtu kutokana na tabia yake, mwenendo wake ndio itakayo mwezesha

kuishi maisha bora. Hebu tuangalie kwa kifupi hizi tabia na sifa kutokana wajihi (physical

appearances), mustakbali (tendancy) na sifa bainishi (personality traits).

1. SIFA YA JOTO NA VUGUVUGU.

WAJIHI: Umbile la wastani, amejengeka kimisuli na si mnene.

MUSTAKBALI: Wanahamu ya kula na hupenda vinywaji baridi. Wanapendelea

halihewa (weather) baridi nay a ukavu. Ni wakakamavu wa wastani.

SIFA BAINISHI: Ni wachangamfu na mwenye bashasha, muwazi, mzungumzaji na

mshawishaji.

2. SIFA YA BARIDI NA VUGUVUGU:

WAJIHI: Umbo wastani na zaidi, ana mafuta mengi kwenye mwili zaidi misuli.

Mishipa ya vena si rahisi kuonekana. Ngozi iliyo pauka.

MUSTAKBALI: wanapendelea vyakula na vinywaji vya joto. Wanapendelea pia

halihewa ya joto na hawapendelei halihewa ya ubaridi. Miili yao ni rahisi

kunenepeka na mara nyingi hupatwa na magonjwa yanaohusiana na

mabalaghamu. Mara nyingi huwa ni wenye kuburudika ki maisha.

SIFA BAINISHI: kwa kawaida ni watulivu, wakarimu, wavumilivu na wasikivu.

3. SIFA YA UBARIDI NA UKAVU:

WAJIHI: Umbo ni mwembamba. Ngozi iliyo pauka na kavu ulo komaa. macho

makali.

MUSTAKBALI: wanapendelea vyakula na vinywaji vya joto na vuguvugu.

Wanapendelea pia halihewa ya joto na hawapendelei halihewa ya ubaridi. Hupata

magonjwa ya gesi na wavivu wanaopenda kulala.

SIFA BAINISHI: kwa kawaida ni wabunifu, waerevu, wasomi na.

4. SIFA YA JOTO NA UKAVU:

WAJIHI: Umbo wastani na zaidi, ana mafuta mengi kwenye mwili zaidi misuli.

Mishipa ya vena inaonekana kwa urahisi. Ngozi iliyonzuri na laini yenye mng’ao.

MUSTAKBALI: wanapendelea vyakula na vinywaji vya baridi na vuguvugu.

Hawapendelei halihewa ya joto hupendelea halihewa ya ubaridi. Ni wakakamavu.

SIFA BAINISHI: kwa kawaida ni wanajiweza, wepesi wa hamaki, wanapenda sifa.

5. Pia kuna elimu iliotumika katika karne za nyuma wakati wa mfalme NAPOLEON.

Sanaa hii ilijulikana kama “physiognomy” yaani hii ni sanaa ya kumjua mtu kwa

kumtalii wajihi wa uso wake. Unaanzia kusoma bapa la uso, macho, pua, mdomo,

lips, masikio, kidevu, na sauti.

Page 17: tibb

LADHA Vigawanyo vya ladha ni sita nazo ni:

1. Chachu (sour). Sifa za vyakula vichachu vinaongeza ubaridi na ukavua ambao

utumiaji wake unaathiri mfumo mzima wa mmeng’enyeko na mfumo mzima wa

mshipa fahamu (nervous systeme: mshipa wa fahamu ndio ambao hukamilisha

mawasiliano baina ya mfumo neva na sehemu za mwili kutumia kodineva ambalo

ni tita kubwa za neva zipitazo ndani ya uti wa mgongo ikishirikiana na mkusanyiko

wa seli ambazo huunda tishu za neva ziitwazo nyuroni). Pia zina ifanya damu

kuwa nzito kuliko ya kawaida hivyo kuathiri mfumo mzima wa mzunguko wa damu

mwilini. Ngozi ya mwili inageuka kuwa kavu na kukunyaza (wrinkle).

2. Chungu (bitter). Utumiaji wa vyakula vichungu kupita kiasi husababisha ukavu na

kuleta joto mwilini. Hii ina athiri pafu na kupasua mshipa ya ateri hivyo kuvujisha

damu. Ngozi ya mwili inakuwa na ukavu sana.

3. Ukali (pungent).kizidisho cha vyakula vikali hutia joto na ukavu mwilini.huathiri ini

na hudhoofisha misuli ya mwili.

4. Chumvichumvi (salty). Kizidisho cha vyakula vyenye chumvi nyingi huzidisha joto

na kutia uvuguvugu mwilini. Ina zidisha mapigo na kuathiri moyo na kusababisha

shinikizo la damu (blood pressure).

5. Tamu (sweet). Kizidisho cha vyakula vitamu hutia joto na kutia vuguvugu

kiwiliwili. Ina athiri wengu (spleen), kongosho (pancreas) na figo (kidney).

6. Iso ladha (no taste/insipid) vyakula aina hii hutia ubaridi na uvuguvugu mwilini.

Zinaathiri tezi (glands) mchakato wa mmeng’enyeko na hupunguza idadi ya

chembechembe nyekundu katika seli za damu ambayo husafirisha oksijeni

ambapo inasababisha ugonjwa wa upungufu wa damu uitwao safura (anaemia).

Pia husababisha nywele kung’oka na kuleta kiara.

Page 18: tibb

NASAHA, HEKIMA NA FALSAFA ZA

TIBA ASILIA.

Maradhi yamegawanyika migawanyo miwili nazo ni

1. Maradhi ya nyoyo; hii ni aina ya maradhi ambayo haina kipimo cha aina yoyote

kutibika kwake ni kazi. haya maradhi ya moyo nayo ni aina mbili :

a) Shubhatu na mashaka; yaani kuwa na shauku juu ya dini yako na mola wako,

mtume, qur’an n.k.

b) Matamanio (hawa nafsi).

2. Maradhi ya kiwiliwili. Kitaaluma kiwiliwili huwa katika hali kuu tatu nazo:

a) Hali ya kitabia; kuwa katika hali ya kawaida bila kuwa na maradhi ya aina

yoyote yaani kuwa ni mwenye afya bora.

b) Hali ya kuwa mgonjwa na kukosa afya bora.

c) Kuwa baina ya hali mbili zilizo tajwa hapo juu, yaani kuwa si mgonjwa wala si

mzima.

Baadhi ya nasaha na falsafa za tiba asilia:

a) Kula na kunywa bali usizidishe kupita kiasi. amesema subhana hu wata3ala:

“ والتسرفوا وشربوا ”كلوا

“Kuleni na kunyweni na wala msizidishe ikawa ni isirafu.”

b) Usile vyakula na vinywaji vibaya.

c) Kunywa maji kwa kituo usinywe kwa mkupuo mmoja kama alivyo tufunza nabiaallah

S.A.W.

d) Usinywe maji au kula kwa kusimama kama alivyo tufunza nabiaallah S.A.W

aliposema kutoka kwa Anas bin Malik (R.A.):" قائما يشرب ان نهيآ hakika "انه

tumekatazwa kunywa kwa kusimama. Mambo manne hudhuru kiwiliwili chako:

jimai baada ya kushiba chakula, jimai na vizee, kuoga ukiwa umeshiba chakula na

kula nyama ilokaushwa na jua.

e) Jipumzishe kidogo baada ya kula chakula cha mchana. Na hakikisha umetembea

hatua hata mia mbili kwa uchache baada ya kula.

f) Usilale bila kwenda haja.

g) Jihadhari na kuoga baada ya kushiba.

h) Usile mayai ukachanganya na maziwa.

i) Usile samaki pamoja na mayai.

j) Usile samaki pamoja na maziwa. Kwani unaweza ukapata magonjwa kama ukoma na

kupooza mwili au kufura mwili na kadhalika.

k) Ukila samaki usioge kwa maji baridi wakati umal; izapo kula subiri baada ya jisaa

ndipo uoge.

Page 19: tibb

l) Ulapo matunda basi hakikisha hunywi maji baridi.

m) Usinywe maji uwamkapo usiku.

n) Usipooze chakula kwa kupulizia pumzi za mdomo. Pia usirudishie pumzi ndani ya

chombo unachokitumia unywapo maji n.k.

o) Usinywe maji baridi baada ya kula chakula cha moto.

p) Usijizoeshe kula nyama hasa nyama nyekundu kam ng’ombe, mbuzi n.k.

q) Usinywe maziwa uumwapo na kichwa na ugojwa wa ini. Unywapo maziwa na

kumaliza sukutua mdomo au piga mswaki kuepukana na meno kuoza.

r) Usile vyakula au vinywali vyenye harufu mbaya.

s) Baada ya kula chakula usimamapo usiji nyooshe kwani kufanya hivyo

unakichanganya chakula cha amani na kipya hivyo kuharibu mmeng’enyeko wa

chakula kipya.

t) Usile wala kunywa damu ya kiumbe chochote. Damu hubeba maradhi mengi.

u) Usile chakula kibichi ambacho hakija pikwa au tunda bichi.

v) Usile matunda mabovu.

w) Usile vyakula vichachu.

x) Usile vyakula vikali.

y) Usile vyenye mapilipili makali.

z) Usile vyakula ambavyo havijapikika au hakijaiva sawa.

aa) Usile vinavyotoa harufu mbaya.

bb)Usile au kunywa ukiwa umejilaza au umesimama kaa na usiegemee sehemu.

MLO SUMU (FOOD POISONING)Mshairi atuambia:

" حب علي شب انتهمله كالطفل والنفس النهم شهوة يقوي الطعم ءن

ينفطم تفطمه وءن "الرضاع

" يصم او يصم ماتولي الهواي توليه" ءن ان وحاذر هواها فاصرف

“Hakika chakula ni chenye huzidisha matamanio na nafsi ni kama mtoto mchanga

anyonyweshwapo hupenda kunyonyeshwa na unapomzuia basi nae huacha”.

Mlo ambao umeathrika na kuchafuliwa na bakteria au vimelea vya maradhi huleta

maumivu makali na kusababisha maradhi kama kuharisha na kutapika. Sio mlo pekee pia

vinywaji kama maji, juisi, maziwa n.k. hata hivyo mlo sumu pia ina weza sababishwa na

virusi au kemikali zilizomo ndani ya mimmea na vyakula au hata samaki au nyama

iliyooza au kuwa na sumu ndani yake bila kujulikana. Uchafuzi wa vyakula pia

husababishwa na mazingira machafu au mazingira yenye vumbi n.k.

Mtu anapo harisha au kutapika husaidia mwili kuondoa mada za sumu au atharikatika

mfumo wa mmeng’enyeko wa chakula (digestive tract) na hivyo kuzizuia sumu na vidudu

maradhi (germs) kuingia katika mfumo wa damu.

Page 20: tibb

Vyakula vinavyo tokana na wanyama, vyakula vibichi na vyakula vya jamii ya mboga

ambazo hazioshwi kwa umakini vizuri, maji yasiochemswa au kinywaji

kilichotengenezwa na maji ambayo hayana sifa kamili ya maji,maziwa n.k. vinaweza kuwa

na vijidudu maradhi (germs) kama vile salmonela na listeria na kusababisha mlo sumu au

food poisoning. Ili kuepukana na mlo sumu :

a.) Osha mikono kwa utaratibu na umakini unapo tayarisha na kuandaa chakula.

b.) Safisha chombo ,sehemu zote utakazo tumia kwa maandalizi ya chakula, spoji na

leso za kupangusia.

c.) Pika na kuchemsha vyakula kama nyama na kadhalika.

d.) Funika chombo chenye kuhifadhi chakula.

e.) Chemsha maziwa, maji na pasha moto vyakula vilivyo poa.

f.) Angalia vyakula vya mikebe na makopo au vya madukani au hata sabuni,dawa za

meno n.k. matumizi yake yanakwisha lini.

Kwa machache inajuzu kwa muisilamu kuwa na umakini na kuwa muangalifu ili kueza

kuepukana na madhara yasababishwayo na mlo sumu.

Page 21: tibb

ASILI YA TIBA ASILIA NA LISHE.Kuna msemo wa kichina usemao “tiba asilia na lishe inaoana tangu jadi na jadi” ni

kwamba tiba na chakula asili yao ni moja lakini yenye matumizi tofauti.kuna baadhi ya

tulavyo havitajiki kama ni chakula au ni dawa mfano tende, kitunguu thaumu au maji,

siki, mayai, simsim, au hata mchele na kadhalika, katika zama tofauti vilitumika kama

dawa au tiba kwa mgonjwa. Pia kuna vyakula vingi vyenye sifa ya tiba.

AINA YA VYAKULA TIBA

Uji aidha unatokana na mchele, mahindi, mtama, soya n.k wachina walipendelea

kuchemsha mchele mpaka ukawa uji kisha kunywa. Hii ilitibu magonjwa yanaotoka

tumboni na kongosho.wachina wanamini kwamba uji huu ni bora kuliko uji wa wimbi,

mtama na mahindi.

Supu nzito ya nyama, mayai na samaki nitiba asili na hakuna pingamizi kwa hili.kwa supu

hii una changanya na mdalasini au tangawizi na vitunguu, pilipilimanga, au soya n.k.

Page 22: tibb

TIBA ZA MAGONJWABAADHI YA MADAWA ZA TIBA ASILIA KWA KISWAHILI, KIINGEREZA NA KWA

KIARABU.

Dawa nyingi katika hizi hazina majina ya Kiswahili basi hutumia majina ya kiarabu.

Kiswahili kiingereza kiarabu

Anisuni Aniseed انسيون

Kitunguu maji onion بصل

Mrujuani/bunsaji Violet بنفسج

Ukwaju Tamarind / حمر هند تمر

Kitunguu thaum Garlic /فوم ثوم

Hina Heena حنا

Hardali Mustard حردل

Mafuta yam bono Castor oil خر

Hash-hash/mpopi Poppy خاش خش

Mdalasini Cinnamon سين دار

Mahindi Corn درة

Ruwandi Rhubard رواند

Kudhumani/mkoma manga Pomegranate رمان

Rehani Basil /حبق ريحان

Zatari Thym زعتر

Zafarani Saffron زعفران

Tangawizi Ginger زنجبيل

Ufuta Sesame سمسم

Sanamaki Senna سنمكي

Hawajiguzrati Dill/Anet شبت

Subili Aloe صبر

Arkisusi Liquorice السوس عرق

Afsi Galinut عفص

Fijili Reddish فجل

Karafuu Clove قرنفيل

Kafiuri Camphoreكافور

Kuzbara Corianderكزبرة

Bizari Cuminكمون

Lozi Almondلوز

Nanaa Mintنعناع

Page 23: tibb

Tumbaku ya wazuka Dandelionهند

Iliki Cardamon هيل

Asmini Jasmin ياسمين

Kungumanga Natmeg fruitجوزبو

Mustaka Lentisk مصطكي

Uvumbani mdogo Wild thym (creeping)نمام

Mnuka uvundo Skirret سنسبان

Mazumai Common lettuceشنجار

Tini Figrool تين

Zabibu Grape زبيب

Koto Coctus قسط

Nduna قفر

Magadi Borax بورق

Majani ya mpera Pears Leaves كمثري رق

Zaiti Olive زيتون

Asali Honeyعصل

Shimari (Habalhalawa) حلوا حبة

Helf/Habbahamra (sufu) حمرا حبة

Basbas jawza

Halilinji

Sakabanji

Darfilfil

Hamdhwa

Giligilani

Maji ya wardi Rose water الورد الماء

Manimani (murra fatwir)

Bakal hadi

Habbat sawda Blackseed

Manjano صفراء

Harmali

Habbat-thufaa

Uwatu Fenugreek الحلبة

Ammonia Ammonia نشادر

Gubiti/sukari guru Barley sugar نبات سكر

Fustuki Pistacchio فستق

Saladi Lettuce الخس

Mwaloni Oak البلوط

Page 24: tibb

Kiwawi Neetle

Kotimiri Parsley البقدونس

Kanganga Fern السرخس

Page 25: tibb

SIFA ZA BAADHI YA DAWA

1. ASALI العسل

Allah s.w amesema katika Qur’an tukufu :( 16:68-69)

" : كلي ثم يعرشون الشجرومما بيوتاومن الجبال من أنتخذي انحل الي ربك وأوحي

فيه الوانه مختلف شراب بطونها من يخرج ذلال ربك سبل فسلكي الثمرات كل من

يتفكرون لقوم ألية ذالكل في ءن للناس "شفاء

“Na akamfahamisha mola wako nyuki namna ya kujenga nta katika majabali na miti na

katika majumba ya wanaadamu.kisha kuleni katika miti na matunda ya kila namna na

urudi katika mola wako alizozifanyia wepesi njia zao: kinatoka katika matumbo yao

(nyuki) kinywaji chenye rangi tofauti(mbalimbali);ndani yake muna ponyo (pozo)kwa

wanaadamu,hakika katika hayo muna mazingatio kwa wenye kutafakari”.

Ufafanuzi wa aya hii ni kwamba nyuki ni kiumbe ambacho Allah s.w amempa uwezo wa

kutoa asali ambayo kwa mwanaadamu ni dawa asilia. Nyuki hukusanya mbochi za

mauwa huyameza na ndani ya tumbo lake, ikajitengeneza kwa mchanganyiko wa kemikali

zilizomo tumboni mwake na kuitoa kupitia mdomo wake na kuitandua katika kapu la nta

kama asali. Imethibiti kisayansi kwamba hakuna kirusi wala bakteria kinachoweza kuishi

ndani ya asali. Ndani ya asali kuna kiini cha potashi/shura ambacho humnyima bakteria

uvuguvugu ambao ndio asili ya uhai wake. Kwa hali ilivyo ni kwamba madaktari bingwa

wa mrengo wa kushoto (wa tiba za kileo au za kimagharibi) wamethibitsha hayo yalio

tajwa na kuelezwa katika Qur’an tukufu. Hivyo maneno ya Allah s.w ni ya ukweli na sahihi

kabisa na ni zingatio kwa wanaadaamu. Inakuwa ni wajibu wa kila Muisilamu kuzingatia

na kumfuata Allah s.w ili apate uongofu hapa duniani na kesho akhera. Hii ni dawa

ipatikanayo katika klinik ya Allah s.w.

Ndani ya asali hupatikana aina nyingi za sukari, pia hupatikana vitamin zote, aina zote za

madini, pia hupatikana vinyeng’enya (enzyme) na aina nyigi za tindikali pia hupatikana

homoni zinazoongeza nguvu na nishati ya mwili.pia hupatikana kiuavijasumu (antibiotic)

vinavyopambana na bakteria na aina nyingine za vijidudu na sumu zenye madhara na

kumpa kinga mwanaadamu. Wanasayansi wamegundua kuwa asali ina haidrojini inayo

zuia saratani. Katika karne hii kulipatikaniwa mtoto wa kifarao katika haram aliezikwa

kwenye sanduku akiwa ndani ya asali kwa muda wa zaidi ya miaka 4500 iliopita bila ya

kuoza wala kunuka, muujiza huu unapatikana ndani ya asali.

KEMIKALI ZILIZOMO

Vitamins A, B1, B2, B3, B5, B6, D, E, H, K, W, n.k

Protein, na madini yafuatayo; chuma(iron), chokaa(calcium),

fosforasi/simetali(phosphorus), kibiriti(sulphur), magnesi(magnesium),shaba(copper),

risasi(lead), bati(tin) n.k.

Page 26: tibb

Sukari aina ya glukos (glucose), fraktos (fructose), maltos (maltose), dekistirin (dextrin),

laktos (lactose), oksidez (oxidase), n.k.

UTENDAJI

1. Lishe yenye kila kitu kinacho hitajika mwilini.

2. Inaongeza vuguvugu ndani ya tumbo.

3. Ina mchango mkubwa katika mmeng’enyeko wa chakula.

4. Ina dhibiti na kurekebisha michakato baina ya wengu na tumbo.

5. Ina dhibiti presha ya damu.

6. Ina ongeza nishati ndani ya mwili.

7. Ina dhibiti magonjwa yanayo patikana kwenye mishipa ya damu ipokeayo damu

safi/shinikizo la damu “arterio-sclerosis”

8. Ina dhibiti na kupambana na bakteria na vidudu ndani ya mwili ina viuasumu

ndani yake.

9. Ina dhibiti saratani.

10. Ina antiseptic inayozuia bakteria kuzaliana kweye jeraha au ngozi.

11. Inatia nguvu misuli ya moyo.

2. HABBAT SAWDA السوداء الحبة

Ina majina mengi. Pia huitwa habbatul baraka au kamunil aswad. Wairani huiita shuniz,

wahindi huiita kalongee. Huku afrika mashariki huitwa habasoda au yai leusi au zinyeu.

Ni mbegu nyeusi huwezakusagwa ikawa unga na pia kuikamua ikawa katika muundo wa

mafuta. Ni kavu na ina joto. Ni jamii ya “nigella sataiva” ni mmea wenye urefu wa milimita

tatu. Huwa na maua meupe, na katikati huwa na fumbuza (capsule) linapopevuka

hupasuka na kutoa mbegu ambazo zikutanapo na hewa katika anga hewa hubadilika na

kuwa nyeusi na ndio asli yake kuitwa habasoda au mbegu nyeusi.

“ : عليك وسلم عليه الله صلي الله رسول فيها مقال فان السوداء الحبة بهذه

السام اال داء لكل ”شفاء

Amesema Mtume s.a.w: “shikamaneni na hii habasoda, hakika muna shifaa/pozo ya kila

ugonjwa isipokuwa mauti” (Bukhari)

KEMIKALI ZILIZOMO

Vitamins A, B1, B2, B3, B5, B6, D, E, H, K, W, n.k

Protein, na madini yafuatayo; chuma(iron), fosfeti, fosforasi/simetali(phosphorus),

kibiriti(sulphur), magnesi(magnesium),shaba(copper), risasi(lead), bati(tin) n.k.

Sukari aina ya fraktos (fructose), maltos (maltose), dekistirin (dextrin), laktos (lactose), oksidez

(oxidase), n.k.

Ina kiuavijasumu (antibiotic),pia ina karotini yenye uwezo wakudhibiti saratani,ina homoni zenye

kuihisha nguvu za kiume na kuongeza manii,ina vimeng’enya(enzyme), ina

kizimatindikali(antacid), antijeni zinapatikana ndani yake ambazo husisimua utengenezaji wa

fingo.

UTENDAJI

1. Lishe yenye kila kitu kinacho hitajika mwilini.

Page 27: tibb

2. Inaongeza vuguvugu ndani ya tumbo.

3. Ina mchango mkubwa katika mmeng’enyeko wa chakula.

4. Ina dhibiti na kurekebisha michakato ndani ya mwili.

5. Ina dhibiti mvilio wa damu (contusion) na shinikizo la damu ugojwa wa moyo.

6. Ina ongeza nishati ndani ya mwili.

7. Ina dhibiti uvimbe wa figo na huvunjavunja mawe tumboni na kwenye nyongo.

8. Ina dhibiti na kupambana na bakteria na vidudu ndani ya mwili ina kijiuasumu

ndani yake.

9. Inadhibiti magonjwa ya ngozi, muasho na pele.

10. Inaondosha uchovu na kutoa nishati

11. Inadhibiti saratani.

3. KITUNGUU THAWM الثوم

Kitunguu thaumu au saumu ni katika jamii ya yungiyungi (lilliacea family). Matumizi ya kitunguu

thawm yalianza tangu zamani wakati wa dola za mafarao (pharoes dynasty). Kitunguu thawm

kimetajwa katika Qur’an kama fuum, kama alivyo sema Allah s.w (Q: 2:62):

“ وقثانها بقلها من األرض تنبت مما لنا يخرج ربك لنا فادع واحد طعام علي نصبر لن موسي يا قلتم واذ

وبصلها وعدسها ”وفومها

“Na (kumbukeni waliposema kumwambi Musa): Ewe Musa hatuwezi kusubiria kwa chakula cha

namna moja tu, basi tuombee kwa mola wako atutolee vioteshwavyo katika ardhi kama maboga

yake, matango yake, vitunguu thawmu zake, dengu zake, na vitunguu maji vyake.”

Katika zama za mafarao vitunguu walipewa wejenzi wa haram (pyramid)ili wapate nguvu na

nishati ya kufanya kazi. Wanafilosofia wengi wamekielezea kitunguu thawm au maji kwamba ni

tiba asili yenye uwezo mkubwa kuponyesha. Wapigana miereka wa kirumi wakati wa tawala za

kirumi (Roman empire) walikuwa wakila thawm kuwapa nishati na nguvu pamoja na wepesi

katika mashindano ya miereka. Kina weza kuliwa kama kilivyo au kikafanywa juisi. Kidole

kimoja ni dozi nzuri kila siku kuitumia. Kinapo pikwa tiba hupotea.

KEMIKALI ZILIZOMO

Vitamins A, B1, B2, na C.

Protein 49%, na madini: Chuma(iron),Chokaa (calcium) na fosfora (phosphorus). Ina kiuavijasumu

(antibiotic), pia ina karotini yenye uwezo wakudhibiti saratani, ina antiseptiki. Ina aina ya mafuta

allicin. Mafuta ya sulfa 25%

UTENDAJI

1. Inaongeza vuguvugu ndani ya tumbo.

2. Ina mchango mkubwa katika mmeng’enyeko wa chakula.

3. Ina dhibiti na kurekebisha michakato ndani ya mwili.

4. Ina dhibiti michango na minyoo.

5. Ina ongeza nishati ndani ya mwili.

Page 28: tibb

6. Ina kolestro inayosafisha damu.

7. Ina viuavijasumu (antibiotics).

8. Inadhibiti sumu ya nyoka, nge nk.

9. Inaondosha gesi, huponya vidonda katika ngozi na kudhibiti mshipa wa nyonga

(sciatica).

10. Huponya kikohozi nani dawa nzuri ya meno.

11. Hudhibiti shinikizo la damu.

12. Ina madhara ya kuumisha kichwa, hutia kiu na utumiaji kwa wigi inasababisha

kupungua nuru ya macho.

4. KITUNGUU MAJI البصل

Kitunguu maji ni katika jamii ya yungiyungi (lilliacea family). Matumizi ya kitunguu maji nayo pia

yalianza tangu zamani wakati wa dola za mafarao (pharoes dynasty). Kitunguu maji nacho pia

kimetajwa katika Qur’an kama bassal, kama alivyo sema Allah s.w (Q: 2:62):

“ وقثانها بقلها من األرض تنبت مما لنا يخرج ربك لنا فادع واحد طعام علي نصبر لن موسي يا قلتم واذ

وبصلها وعدسها ”وفومها

“Na (kumbukeni waliposema kumwambi Musa): Ewe Musa hatuwezi kusubiria kwa chakula cha

namna moja tu, basi tuombee kwa mola wako atutolee vioteshwavyo katika ardhi kama maboga

yake, matango yake, vitunguu thawmu zake, dengu zake, na vitunguu maji vyake.”

Katika zama za mafarao vitunguu walipewa wejenzi wa haram (pyramid)ili wapate nguvu na

nishati ya kufanya kazi. Wanafilosofia wengi wamekielezea kitunguu thawm au maji kwamba ni

tiba asili yenye uwezo mkubwa kuponyesha. Kina weza kuliwa kama kilivyo au kikafanywa juisi.

Kinatakiwa kitumiwe kikiwa bado ni kibichi, kikikaa kwa muda hufanya oksaidi ambayo inakuwa

ni sumu. Inatengezwa juisi ambayo huua vijidudu vya kinamasi na vya kifua kikuu (TB).

KEMIKALI ZILIZOMO

Vitamins: B1, B2, na C.

Protein, na madini: Chuma(iron), Chokaa (calcium), magnesi(magnesium) na fosfora. Ina

kiuavijasumu (antibiotic), pia ina karotini yenye uwezo wakudhibiti saratani, ina antiseptiki. Ina

aina ya mafuta allicin. Mafuta ya sulfa 25%,

UTENDAJI

1. Inaongeza vuguvugu ndani ya tumbo.

2. Ina mchango mkubwa katika mmeng’enyeko wa chakula.

3. Ina dhibiti na kurekebisha michakato ndani ya mwili.

4. Ina dhibiti michango na minyoo.

5. Ina ongeza nishati ndani ya mwili.

6. Ina kolestro inayosafisha damu.

7. Ina viuavijasumu (antibiotics).

8. Inadhibiti sumu ya nyoka, nge nk.

9. Inaondosha gesi, huponya vidonda katika ngozi na kudhibiti mshipa wa nyonga

(sciatica).

Page 29: tibb

10. Huponya kikohozi nani dawa nzuri ya meno.

11. Hudhibiti shinikizo la damu.