-
za mwambao wa Bahari ya Hindi na za kwenye Maziwa Makuu ya
Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Mbali na hilo TPA ilikabidhiwa majukumu zaidi ya kumiliki na
kuendeleza Bandari zilizokuwa zinaendeshwa na Kampuni ya Huduma za
Meli (Marine Services Company Limited – MSCL) katika Maziwa
Makuu.
Majukumu mengine iliyokasimiwa ni pamoja na kuendeleza shughuli
za Bandari, kutangaza huduma za Bandari, kushirikisha na kusimamia
sekta binafsi katika uendelezaji, uboreshaji na uendelezaji wa
Bandari za
TANZANIA PORTS AUTHORITY
www.ports.go.tz | Bendera Tatu S.L.P. 9184 Dar es Salaam |
Email: [email protected] | Namba za Bure: 0800110032 / 0800110047
TOLE
O N
O:
07
MEI
14
- M
EI 2
7 20
18
@tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq @ tanzaniaportshq TPAHQ TPA
GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 01
05
WAFANYAKAZI WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA
KUPIMA AFYA
TPA YATOA MSAADA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA
MUHIMBILI
03
NDANI
amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeadhimisha miaka
13 tangu kuanzishwa kwake Aprili, 2005. TPA ilianzishwa kwa mujibu
wa Sheria ya Bandari Na. 17 ya mwaka 2004 ambapo awali ilikuwa
ikiitwa Mamlaka ya Bandari Tanzania – THA ambayo ilianzishwa mwaka
1977 mara baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki.
Mwandishi Wetu
Jumuiya hiyo ilikuwa inaendesha Bandari kupitia Shirika la
Bandari la Afrika Mashariki lililoanzishwa mwaka 1967. Historia
inaonesha kwamba THA ilikuwa na kazi ya kusimamia na kuendesha
Bandari za mwambao wa bahari tu ambazo ni Dar es Salaam, Tanga,
Mtwara, Bagamoyo, Mafia, Pangani, Lindi na Kilwa. TPA ambayo
ilianza rasmi kufanya kazi tarehe 15 Aprili, 2015 ilikasimiwa kazi
ya kuendeleza na kusimamia Bandari zote
TPA YAADHIMISHA MIAKA 13 YA MAFANIKIO
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta
Nditiye akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi,
Menejimenti, Wafanyakazi wa TPA pamoja na baadhi ya Wadau wa
TPA.
Mmwambao wa bahari na za kwenye Maziwa Makuu nchini.
Katika kipindi cha miaka 13 sasa tangu ilipoanzishwa, TPA
imeendelea kuhudumia wateja wake katika Bandari zake kwa kuwapatia
huduma bora. Huduma hizo ni pamoja na za kuhudumia meli ambapo TPA
imeendelea kuboresha miundombinu ya magati na kuwa na marubani
wa
13
BANDARI TANGA YATOA MSAADA WA VITANDA 10
VYA KUJIFUNGULIAPANGANI!
07
WIKI YA KUADHIMISHA MIAKA 13 YA UTOAJI
HUDUMA TPAYAHITIMISHWA KWA
BONANZA..
-
2 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Maadhimisho
TPA yaadhimisha miaka 13 yenye mafanikio lukukikuongoza meli
wenye ujuzi na uzoefu mkubwa.
Pia kuwajengea uwezo wafanyakazi wengine wanaohusika na
uhudumiaji wa meli wakati wa kuingia na kutoka Bandarini. Pia TPA
imefanikiwa kupunguza muda wa kukaa meli Bandarini kwa kuongeza
ufanisi kwa kushirikiana na wadau wa Bandari kama vile idara za
Uhamiaji na Afya.
Kwa upande wa kuhudumia mizigo ya wateja TPA imeboresha kwa
kuwajengea uwezo wafanyakazi wake ili waweze kuhudumia wateja kwa
kuwapatia huduma bora. TPA imeweza kuzinunulia Bandari zake vifaa
bora na vya kisasa vya kuhudumia meli na mizigo ya wateja. TPA kwa
kushirikiana na wadau wake imefanikiwa kutoa huduma kwa wateja wake
kuchukua mizigo yao Bandarini kwa muda wa saa 24 kwa siku 7 za
wiki. TPA imefanikiwa kuwawezesha wateja kulipia tozo za Bandari
kwa kutumia mfumo wa E-payament.
Ili kuweza kuhakikisha TPA inaendelea kutoa huduma bora katika
Bandari zake, iliamua kuwekeza katika miradi mikubwa ya kuboresha
na kuendeleza Bandari zake kukabiliana na changamoto ya ongezeko la
shehena na kuweza kuingiza meli kubwa katika Bandari zake.
Kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam, TPA imeweza kukamilisha
miradi mingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Boya la Mafuta (Single
Point Mooring – SPM) kuhudumia meli kubwa za mafuta zenye uwezo wa
kuchukua mafua hadi tani 150,000. Ujenzi wa Kituo Kimoja cha Huduma
(One Stop Centre), Mradi wa kisasa wa ulinzi (Integrated Security
System), ujenzi wa barabara za kuingia lango namba 4 na 8 na ujenzi
wa karakana ya meli (Dock Yard).
Mradi mkubwa unaotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam ni
Dar es Salaam Maritime Gateway Project ambao ni mradi wa uboreshaji
na uongezaji wa kina katika gati namba 1 hadi 7, kuongeza kina cha
mlango wa Bandari na mzunguko wa kugeuza meli pamoja na kujenga
gati namba 13 na 14.
Katika Bandari ya Mtwara, TPA imeongeza gati namba 2 kuipanua
Bandari hiyo kuwa ya kisasa kwa lengo la kuiwezesha kuhudumia meli
kubwa na shehena kubwa zaidi. Mradi huo una lengo la kutoa mchango
mkubwa katika kukuza uchumi wa mikoa ya Mtwara, Lindi and
Ruvuma.
Pia taifa kwa ujumla litanufaika kwa kuwapatia fursa wateja
kuteremshia mizigo yao katika Bandari hiyo. Mradi huo uliwekwa jiwe
la msingi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. John Pombe Magufuli Machi, 2017.
Pia katika Bandari ya Tanga Serikali ya Tanzania imeingia
makubaliano na Serikali ya Uganda kujenga bomba kubwa la mafuta la
kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda kupitia Bandari ya
Tanga. Mradi huu upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na
unakwenda sambasamba na mradi mwingine wa ujenzi wa Bandari mpya ya
Mwambani Tanga.
Aidha, TPA inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya Bandari
zilizoko katika Maziwa Makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Bandari hizo zimejengewa na zinaendelea kujengewa uwezo kuhudumia
meli, abiria na mizigo ya wateja.
Pia ili kuhudumia mizigo ya wateja vizuri TPA inatekeleza mradi
wa Bandari Kavu ya Kwala, Ruvu, ambapo imenunua maeneo ya Katosho
Kigoma kwa ajili
ya mizigo ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na eneo
la Fela, Misungwi kwa ajili ya mizigo ya Uganda.
Ili kusogeza huduma za Bandari karibu na wateja wake, TPA
imefungua ofisi zake; Lubumbashi katika nchi ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Lusaka nchini Zambia, Kigali nchini Rwanda
na Bujumbura nchini Burundi. Pia, TPA ina mawakala Goma nchini DRC,
Kampala nchini Uganda na iko mbioni pia kumpata wakala nchini
Malawi.
Kwa muda wa miaka 13, TPA imepata mafanikio mengi ya kujivunia
katika Bandari zake ambayo yamechangia maendeleo makubwa ya
kiuchumi na kijamii kwa Tanzania na nchi jirani zinazotumia Bandari
za TPA.
Aidha TPA kwa kushirikiana na wadau wake itaendelea kuboresha
utoaji huduma kwa wateja wake kwa kuwajengea uwezo wafanyakazi
wake, kuboresha miundombinu pamoja na vifaa, kuendelea kutoa huduma
bora kwa haraka na gharama nafuu kwa kutumia mifumo ya kisasa
kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
TPA kwa kumjali mteja ina kituo cha huduma kwa mteja ambacho
kina simu ambazo mteja anaweza kupiga au kutuma ujumbe mfupi wa
maandishi bure kuuliza swali lolote au kupata
‘‘Kwa upande wa Bandari ya Dar es Salaam, TPA imeweza
kukamilisha miradi mingi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Boya la
Mafuta (Single Point Mooring – SPM) kuhudumia meli kubwa za mafuta
zenye uwezo wa kuchukua mafua hadi tani 150,000. Ujenzi wa Kituo
Kimoja cha Huduma (One Stop Centre), Mradi wa kisasa wa ulinzi
(Integrated Security System), ujenzi wa barabara za kuingia lango
namba 4 na 8 na ujenzi wa karakana ya meli (Dock Yard).’’
-
TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 3
Msaada
‘‘Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi
Mkuu wakati wa kutoa msaada huo, Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru
Mhando amesema kuwa TPA inawajibika kuiangalia jamii kwa kuisaidia
mambo mbalimbali na kwamba Mamlaka imeamua kuwafariji watoto hao
kwa kukabidhi msaada wa “wheelchairs” 20 na “thermometers” 40 kwa
wodi ya watoto ya hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa kwake.’’
BI. MTAWA AMEIOMBA JAMII KWA UJUMLA KUWASAIDIA WATOTO HAO KWA
VITU MBALIMBALI MBALI NA VIFAA TIBA NA KWAMBA MSAADA ULIOUTOLEWA NA
TPA UMEPOKELEWA NA UONGOZI PAMOJA NA WAZAZI WA WATOTO KWA MOYO
MKUNJUFU NA UTAWASAIDIA KWA KIWANGO KIKUBWA.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu
wakati wa kutoa msaada huo, Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando
amesema kuwa TPA inawajibika kuiangalia jamii kwa kuisaidia mambo
mbalimbali na kwamba Mamlaka imeamua kuwafariji watoto hao kwa
kukabidhi msaada wa “wheelchairs” 20 na “thermometers” 40 kwa wodi
ya watoto ya hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni sehemu ya
kuadhimisha miaka 13 tangu kuanzishwa kwake.
Tarehe 15 Aprili, 2018 TPA imetimiza miaka 13 tangu kuanzishwa
kwake tarehe 15 Aprili 2005. TPA ilianzishwa kupitia Sheria ya
Bandari Na. 17 ya 2004” ikiwa na jukumu la kusimamia, kuendeleza na
kuendesha Bandari
amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa
vitu mbalimbali kwenye wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 13 ya TPA ambapo
kilele chake ilikuwa ni Jumapili, Aprili 15, 2018.
Focus Mauki
TPA YATOA MSAADA WODI YA WATOTO HOSPITALI YA MUHIMBILI
Mzilizopo katika bahari na maziwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa
Hospitali ya Taifa Muhimmbili, Bi. Agnes Mtawa ambaye alimwakilisha
Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili, amewashukuru sana TPA kwa kuwakumbuka
watoto hao na kuiomba Mamlaka na watanzania wote kutowasahau na
kuwatembelea wodini mara kwa mara ili kuwafariji watoto hao.
Bi. Mtawa ameiomba jamii kwa ujumla kuwasaidia watoto hao kwa
vitu mbalimbali mbali na vifaa tiba na kwamba msaada ulitolewa na
TPA umepokelewa na uongozi pamoja na wazazi wa watoto kwa moyo
mkunjufu na utawasaidia kwa kiwango kikubwa.
Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando akikabidhi msaada kwa wodi
ya watoto Muhimbili kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.
-
4 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Ukaguzi/Mafunzo
WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI YA TPA (BOARD OF SURVEY)
WAKIKAGUA MALI CHAKAVU ZILIZOPO BANDARI YA DAR ES SALAAM.
BAADHI YA VIONGOZI WA MENEJIMENTI YA TPA WAKIWA KATIKA PICHA YA
PAMOJA NA WAKUFUNZI WA PSPTB MARA BAADA YA KUKAMILIKA KWAMAFUNZO YA
UNUNUZI NA UGAVI YALIYOFANYIKA BANDARI YADAR ES SALAAM HIVI
KARIBUNI.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru
Mhando akizindua zoezi la kupima afya kwa kupima afya yake katika
wiki ya maadhimisho ya miaka 13 ya TPA.
-
TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 5
Afya/HQ/Dar
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando
wakati alipomwakilisha Mkurugenzi Mkuu kwenye zoezi la kupima afya
na uchangiaji damu lililofanyika katika eneo la idara ya zimamoto,
Bandari ya Dar es Salaam.
“Kwanza kabisa napenda kuwashukuru wale wote ambao wamejitokeza
leo kuchangia damu kwa wenye uhitaji pamoja na kupima afya zao,
natoa wito kwa wafanyakazi wote kuwa na ari na moyo wa kusaidia
wenye shida na damu na pia wapime afya zao mara kwa mara, hata mimi
leo nitapima afya yangu na kuchangia damu ili kutoa hamasa,”
amesema Bi. Mhando.
Zoezi hilo kwa Wafanyakazi la kuchangia damu lilikuwa ni
muendelezo wa maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa TPA
mwaka 2005.
Kwa upande wake akizungumza kuhusu zoezi hilo, Mwenyekiti wa
Chama cha Wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam (DOWUTA), Bw.
Mashaka Karume amesema zoezi hilo ni sehemu
afanyakazi wameaswa kujenga utamaduni wa kupima afya kila wakati
pamoja na kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye
uhitaji waliopo katika mahospitali mbalimbali nchini.
Focus Mauki
WAFANYAKAZI WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA
W
ya mambo ambayo walipanga kwa pamoja kama Chama na Menejimenti
ili kuadhimisha miaka 13 ya TPA.
“Damu ambayo tunachangia itatumika katika hospitali mbalimbali
kwa wagonjwa wenye uhitaji, jambo hili tunajivunia kwamba
tunasaidia kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu,” amesema
Mashaka.
Bw. Mashaka amefafanua zaidi kwamba, “Ni wajibu wa Wafanyakazi
kuchangia damu kwa sababu Taifa linahitaji damu
ya kutosha na wanaohitaji kutumia damu ni Watanzania wenzetu,
kwa hiyo tunalolifanya sisi ni jambo jema kwa maslahi ya familia
zetu na Taifa kwa ujumla.”
Zoezi hilo la uchangiaji damu ambalo liliratibiwa vizuri kwa
kushirikiana na Zahanati ya Mamlaka chini ya Mganga Mkuu Dkt.
Mkunde Mlay lilikuwa la mafanikio makubwa huku wafanyakazi wengi
wakitoa maoni kuwa liwe ni endelevu.
Mkurugenzi wa Fedha, Bi. Nuru Mhando akizindua zoezi la kupima
afya kwa kupima afya yake katika wiki ya maadhimisho ya miaka 13 ya
TPA.
Wafanyakazi wa TPA wakishiriki zoezi la kuchangia damu kwa ajili
ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika hospitali
mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
-
6 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Afya/Tanga
WAFANYAKAZI BANDARI YA TANGA WACHANGIA LITA 100 ZA DAMU
Zoezi hilo la kuchangia damu lilianza Aprili 10 na likaendelea
Aprili 11, 2018 likiwahusisha Wafanyakazi wa Bandari pamoja na
baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga.
Katika kipindi cha siku moja, takribani lita 35 za damu
zilikusanywa huku lengo likiwa ni kukusanya lita 100 za damu.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo hospitali ya rufaa ya Bombo peke
yake inatumia takribani lita 3 hadi 5 kwa siku katika kuhudumia
wagonjwa mbalimbali wenye kuhitaji damu kuokoa maisha yao.
atika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 13 ya TPA,
Wafanyakazi wa Bandari ya Tanga na baadhi ya Wananchi wa Mkoa Tanga
wameshirikiana kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu.
Moni Jarufu
K
‘‘Kwa mujibu wa takwimu zilizopo hospitali ya rufaa ya Bombo
peke yake inatumia takribani lita 3 hadi 5 kwa siku katika
kuhudumia wagonjwa mbalimbali wenye kuhitaji damu kuokoa maisha
yao.’’
Wafanyakazi wa TPA wakishiriki zoezi la kuchangia damu kwa ajili
ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika hospitali
mbalimbali Jijini Tanga.
Wafanyakazi wa TPA wakishiriki zoezi la kuchangia damu kwa ajili
ya kusaidia wagonjwa wenye uhitaji waliopo katika hospitali
mbalimbali Jijini Tanga.
-
TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 7
Michezo/Mtwara
Maadhimisho hayo yaliitimishwa kwa kupambwa na Bonanza kabambe
lililohusisha mazoezi ya viungo (aerobic) kwa wafanyakazi wote,
Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu, kukimbiza kuku, kuvuta kamba,
mchezo wa bao na Mpira wa Pete kwa timu za Menejimenti na
Wafanyakazi.
Akifungua bonanza hilo Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson
Mlali aliwasisitiza wafanyakazi kuwa na tabia ya kushiriki kwenye
mazoezi mbalimbali ya mwili kwa ajili ya kujenga Afya njema pia
kuepuka magonjwa mbalimbali ili kuleta ufanisi mzuri katika
Utendaji kazi.
Bonanza hilo lilimalizika kwa timu za wafanyakazi kuibuka
washindi kwenye michezo yote na kujishindia zawadi mbalimbali
zikiwemo kuku na fedha taslimu.
Wafanyakazi waliishukuru Mamlaka kwa kuwapa nafasi ya kujumuika
pamoja katika kusherekea maadhimisho ya miaka 13 ya utoaji huduma
kwa TPA na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza
Tija.
amlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeadhimisha
Kumbukumbu ya Miaka 13 Ya utendaji kazi kuanzia tarehe 09 hadi 15
Aprili, 2018 Kupitia Bandari zake zote za Tanzania ikiwemo Bandari
ya Mtwara. Katika kuadhimisha wiki hiyo Mamlaka iliandaa shughuli
mbalimbali za kijamii ikiwemo ‘Press Conference’, Kutembelea na
kutoa misaada kwa Jamii, Wanajamii Kutembelea Bandari kujifunza
vitu tofauti na kumalizika na Bonanza lililohusisha michezo
mbalimbali.
Fassie Obadia
WIKI YA KUADHIMISHA MIKA 13 YA UTOAJI HUDUMA TPA YAHITIMISHWA
KWA BONANZA KABAMBE BANDARI YA MTWARA
M
Wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara wakijumuika pamoja katika
kufanya mazoezi ya pamoja ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 13
ya TPA.
Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson Mlali, akimkabidhi zawadi
kocha wa timu ya mpira wa pete Bi. Mariam Said.
-
8 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Michezo/HQ/Dar
Michezo hiyo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za kutimiza Miaka
13 ya TPA tangu kuanzishwa kwake Aprili 2005, ilijaa burudani hasa
katika michezo ya kufukuza kuku na kukimbia na magunia.
Shindano la mpira wa miguu lilikuwa kati ya timu ya iliyokuwa
THA na TPA. Mpaka kipenga cha mwisho matokeo yalikuwa sare ya
1-1.
Kwa upande wa Mpira wa Pete matokeo yalikuwa vijana TPA vikapu
4-10 THA. Mchezo wa kukimbiza kuku (wanaume) ambao ulikuwa na
burudani ya aina yake ushindi ulienda kwa Ibrahimu Mbatto huku
mchezo wa kukimbia na gunia (wanawake), Bi. Modesta Kaunda akiibuka
kidedea na Bw. Jonas Bwoma akiibuka kidedea kwa upande wa
wanaume.
Mwaka huu TPA inaadhimisha miaka 13 tangu ilipoanzishwa mwaka
2005 ambapo awali ilikuwa ikitambulika kama THA.
atika kusherekea Maadhimisho ya Wiki ya TPA, Wafanyakazi wa
Makao Makuu na Bandari ya Dar es Salaam, wameshiriki katika michezo
mbalimbali ikiwemo Kandanda, mpira wa pete, kukimbiza kuku na Gunia
michezo iliyochezwa katika viwanja vya klabu ya Bandari
Kurasini.
Innocent Mhando
WAFANYAKAZI WASHIRIKI MICHEZO KUADHIMISHA MIAKA 13
K
Wanamichezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakati
waliposhiriki michezo ya kuadhimisha miaka 13 ya TPA.
Wanamichezo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakati
waliposhiriki michezo ya kuadhimisha miaka 13 ya TPA.
-
TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 9
Msaada/Mwanza
Msaada huo umetolewa hivi karibuni na aliyekuwa Mkuu wa Bandari
hiyo, Bw. Daniel Sira ambaye aliongozana na Wafanyakazi mbalimbali
wa Bandari hiyo. Msaada huo ulikuwa ni muendelezo wa kusherehekea
miaka 13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake mnamo Aprili
15, 2005.
ongozi wa Bandari ya Mwanza umetoa msaada wa mchele, sabuni,
mafuta ya kupikia na unga wa sembe kwa kituo cha kutunza wazee cha
Bukumbi jijini Mwanza.
Mwandishi Wetu
BANDARI MWANZA YASAIDIA WAZEE WASIOJIWEZA BUKUMBI!
U
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bandari ya Mwanza wakiwa katika picha
ya pamoja na wazee wa kituo cha Bukumbi mara baada ya kuwakabidhi
misaada mbalimbali.
‘‘Uongozi wa Bandari ya Mwanza umetoa msaada wa mchele, sabuni,
mafuta ya kupika na unga wa sembe kwa kituo cha kutunza wazee cha
Bukumbi jijini Mwanza.’’
Aliyekuwa Mkuu wa Bandari ya Mwanza, Bw. Daniel Sira akikabidhi
msaada kwa wazee wa kituo cha Bukumbi.
-
10 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Ziara/Mtwara
Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake kwenye
Bandari ya Mtwara ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kuadhimisha
miaka 13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake Aprili 15,
2005.
Akiwa Bandarini hapo Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea
Bandari ya Mtwara kujionea shughuli mbalimbali za Bandari ambapo
amejionea jinsi ambavyo “Patrol Boat” inavyofanya kazi ya
kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya Bandari na Bahari kwa
Ujumla.
kuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa ameipongeza TPA
kwa jitihada inazozifanya za kuimarisha ulinzi katika Bandari zake
hususani Bandari ya Mtwara.
Fassie Obadia
MKUU WA MKOA MTWARA AIPONGEZA TPA KWA KUTIMIZA MIAKA 13!
M
Akiwa Bandarini hapo Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea
Bandari ya Mtwara kujionea shughuli mbalimbali za Bandari ambapo
amejionea jinsi ambavyo “Patrol Boat” inavyofanya kazi ya
kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya Bandari na Bahari kwa
Ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa (kushoto) akiwa
na Mwenyeji wake Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali
(katikati).
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa (kulia) na Mkuu
wa Bandari ya Mtwara, Bw. Nelson Mlali (kushoto) wakiwa ndani ya
boti ya ulinzi.
-
TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 11
Msaada/Mtwara
Akipokea vifaa hivyo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Ligula Dkt. Dickson Sahini aliishukuru Mamlaka kwa msaada walioutoa
kwa kuwa Hospitali hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa
ukosefu wa mashuka ambapo walikuwa na upungufu wa mashuka 992 ya
kulalia wagonjwa jambo ambalo limekuwa ni usumbufu kwa wagonjwa
wanaolazwa hospitalini hapo.
Akiwa Bandarini hapo Mkuu wa Mkoa alipata fursa ya kutembelea
Bandari ya Mtwara kujionea shughuli mbalimbali za kiBandari ambapo
amejionea jinsi ambavyo “Patrol Boat” inavyofanya kazi ya
kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo ya Bandari na Bahari kwa
Ujumla.
Mashuka hayo yenye thamani ya Tshs. 1,335,000/= yalikabidhiwa na
Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson Mlali. Akikabidhi mashuka hayo
Bw. Mlali alisema kwamba TPA inaadhimisha miaka 13 ya Utoaji huduma
toka ilipoanzishwa mwaka 2005.
Hivyo Mamlaka imeona ni vyema kuishukuru Jamii kwa kuipa
ushirikiano toka ilipoanzishwa kwa kutoa kile kidogo ambacho
imepata kwa kipindi chote hicho ikiwa ni shukrani kwa jamii
atika wiki ya kuadhimisha miaka 13 ya utoaji huduma kwa TPA toka
ianzishwe Bandari ya Mtwara imetoa msaada wa mashuka mia moja (100)
katika hospitali ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula.
Fassie Obadia
HOSPITALI YA LIGULA YANUFAIKA NA MASHUKA 100 KUTOKA BANDARI YA
MTWARA
kwa kuunga mkono kazi mbalimbali za Mamlaka. Vilevile Mamlaka
inaunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kuboresha
utoaji huduma katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na
ustawi wa Jamii.
Akipokea vifaa hivyo Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Ligula Dkt. Dickson Sahini aliishukuru Mamlaka kwa msaada walioutoa
kwakuwa Hospitali hiyo ilikuwa inakabiliwa na uhaba mkubwa wa
ukosefu wa mashuka ambapo walikuwa na upungufu wa mashuka 992 ya
kulalia wagonjwa jambo ambalo limekuwa ni usumbufu kwa wagonjwa
wanaolazwa hospitalini hapo.
Vile vile alitoa rai kwa Taasisi na Mashirika mengine kuiga
mfano wa Mamlaka kwa kusaidia Hospitali hiyo kutatua changamoto
mbalimbali zikiwemo ukosefu wa ‘Sunction Machine’, ‘Wheel Chairs’,
‘Autoclaves’ nk.
K
Mkuu wa Bandari ya Mtwara Bw. Nelson Mlali akikabidhi msaada wa
shuka kwa Kaimu Daktari Mfawidhi hospitali ya Mkoa wa Ligula Dkt.
Dickson Sahini
-
12 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Wadau/Masoko
Mkutano huo ambao umewakutanisha wateja na wadau wa TPA ulikuwa
na lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja namna
wanavyoweza kushiriki kwa pamoja katika kuboresha huduma za
Bandari.
Mkutano huo umefanyika kwa siku moja katika ukumbi wa mikutano
wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
aibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta
Nditiye ameiagiza TPA kuongeza shehena ya mzigo katika Bandari zake
hususani Bandari za maziwa. Ametoa agizo hilo wakati alipofungua
rasmi mkutano wa wadau wa TPA ambao ulifanyika Jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.
Focus Mauki
NAIBU WAZIRI AZINDUA KONGAMANO LA WADAU
N
Mkutano huo ambao umewakutanisha wateja na wadau wa TPA ulikuwa
na lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja namna
wanavyoweza kushiriki kwa pamoja katika kuboresha huduma za
Bandari.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta
Nditiye akizungumza na wadau wa TPA kwenye mkutano uliofanyika
Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wadau mbalimbali wa TPA wakifuatilia mada zilizowasilishwa
kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 13 ya TPA.
-
TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 13
Msaada/Tanga
Mkuu huyo wa Bandari amekabidhi msaada huo kwa naibu waziri wa
maji na umwagiliaji na mbunge wa pangani, mhe. Jumaa aweso na mkuu
wa wilaya ya pangani, mhe. Zainab abdallah.
Msaada huo uliotolewa na TPA ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake aprili 15, 2005.
‘‘Msaada huo uliotolewa na TPA ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
13 ya TPA tangu ilipoanza rasmi majukumu yake aprili 15,
2005.’’
Mkuu wa Bandari ya Tanga, Bw. Percival Salama akikabidhi msaada
wa vitanda vya kujifungulia kwa Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe.
Zainab Abdallah. Kushoto ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji na Mbunge
wa Pangani, Mhe. Jumaa Aweso.
Baadhi ya vitanda vilivyotolewa msaada na TPA kwa Wilaya ya
Pangani.
BANDARI TANGA YATOA MSAADA WA VITANDA 10 VYA KUJIFUNGULIA
PANGANI!
kuu wa Bandari ya Tanga, Bw. Percival Salama amekabidhi msaada
wa vitanda 10 vya kujifungulia kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya
Pangani.
Moni Jarufu
M
-
14 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Wanafunzi/Mtwara
Wakiwa Bandarini hapo wanafunzi hao pia walipata fursa ya
kujifunza kuhusiana na utendaji kazi wa Bandari ikiwa ni pamoja na
namna Bandari ilivyojizatiti kikamilifu kukabiliana na majanga
mbalimbali ikiwemo ya moto. Mbali na elimu ya nadharia Wanafunzi
hao pia wamepata fursa ya kujifunza kwa vitendo namna ya uzimaji wa
moto wa aina mbalimbali kwa kutumia chombo maalumu cha kuzimia moto
‘Fire Extingusher’.
anafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari wa Mkoa wa
Mtwara wamepata fursa ya kupata elimu kuhusiana na shughuli za
Bandari hususani elimu ya zimamoto ikiwa ni sehemu ya maadhimisho
ya Miaka 13 ya TPA.
Fassie Obadia
MAADHISHO YA MIAKA 13WANAFUNZI MTWARA WANUFAIKA NA ELIMU YA
BANDARI!
W
‘‘Mbali na elimu ya nadharia Wanafunzi hao pia wamepata fursa ya
kujifunza kwa vitendo namna ya uzimaji wa moto wa aina mbalimbali
kwa kutumia chombo maalumu cha kuzimia moto ‘Fire
Extingusher’.’’
Wataalamu wa zimamoto na usalama wa Bandari ya Mtwara wakitoa
elimu kuhusiana na vifaa vinavyotumika wakati wa kuzima moto.
Mtaalamu wa zimamoto na usalama wa Bandari ya Mtwara akitoa
elimu kwa wanafunzi kuhusiana na vifaa vinavyotumika wakati wa
kuzima moto.
-
TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018 | 15
Tamasha/Dar
“Michezo hii ilianzishwa mahsusi ili kujenga, kuimarisha
Muungano na undugu bila kusahau kuboresha afya za Wafanyakazi wa
pande zote za Bara na Visiwani,” amefafanua Eng. Kakoko na kuongeza
kuwa michezo hii itaendelea kufanyika kila mwaka kwa lengo la
kuwaenzi Waasisi wa Muungano wa Tanzania.
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit
Kakoko wakati akifunga michezo ya Tamasha la Pasaka ambayo kwa
mwaka huu imefanyika katika vwanja vya Klabu ya Bandari Kurasini
jijini Dar es Salaam.
“Michezo hii ilianzishwa mahsusi ili kujenga, kuimarisha
Muungano na undugu bila kusahau kuboresha afya za Wafanyakazi wa
pande zote za Bara na Visiwani,” amefafanua Eng. Kakoko na kuongeza
kuwa michezo hii itaendelea kufanyika kila mwaka kwa lengo la
kuwaenzi Waasisi wa Muungano wa Tanzania.
Kwa upande mwingine Eng. Kakoko ameridhia timu za Shirika la
Bandari ya Zanzibar (ZPC) na Shirika la Meli Zanzibar (SHIPCO)
kushiriki katika michezo ya “Bandari Interports” ambayo kwa mwaka
huu 2018 imepangwa kufanyika Makao Makuu ya Nchi Mkoani Dodoma.
amasha la Pasaka ambalo huwakutanisha Wafanyakazi wa Bandari za
Tanzania Bara na Visiwani litaendelea kufanyika kila mwaka kwa
lengo la kuenzi Waasisi wa Muungano wa Tanzania.
Innocent Mhando
TAMASHA LA PASAKA LA BANDARI KUTUMIKA KUENZI WAASISI WA
MUUNGANO!
TKwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Bandari ya
Dar es Salaam (DOWUTA), Bw. Mashaka Karume amepongeza ushirikiano
na upendo uliopo baina ya Wafanyakazi wa pande zote mbili hususani
katika kufanikisha michezo ya Bonanza la Pasaka.
Nae Bw. Hassan Ahmed akiongea kwa niaba ya uongozi wa Klabu ya
Bandari na Wanamichezo kutoka TPA ameishukuru Menejimenti ya TPA
kwa kutoa idhini na hatimaye kufanikisha Tamasha hilo na kuahidi
kwamba Wafanyakazi watafanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu
wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuuenzi Muungano kwa
vitendo.
Katika mchezo wa soka timu ya Makao Makuu waliibuka kidedea kwa
3-1 dhidi ya Shirika la Meli Zanzibar na kwa upande wa Bandari ya
Dar es Salaam walishindwa kufurukuta mbele
ya Shirika la Bandari Zanzibar kwa kuchapwa bao 2-0.
Katika mchezo wa kuvuta kamba Makao Makuu Wanaume na Wanawake
waliwavuta Shirika la Meli Zanzibar kwa seti zote mbili huku katika
mchezo wa Kamba Bandari ya Dar es Salaam waliwagalagaza wavuta
kamba wa Shirika la Bandari Zanzibar kwa seti zote mbili.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bandari ya Dar ea
Salaam walipata alama 32 -20 dhidi ya timu ya Shirika la Bandari
Zanzibar na kwa upande wa Makao Makuu mpira wa pete walishindwa
kufurukuta mbele ya Wanzibari kwa kufungwa kwa alama 11 -19 na
Shirika la Meli Zanzibar.
Wafanyakazi wa TPA, Shirika la Bandari ya Zanzibar (ZPC) na
Shirika la Meli Zanzibar (SHIPCO) wakiserebuka kwenye tamasha la
Pasaka ambalo linafanyika mara moja kwa mwaka kwa lengo la kujenga
mahusino mema ya kazi.
-
16 | TPA GAZETI MEI 14 - MEI 27 2018
Geti GetiMasoko
Akiongea na Waandishi wa Habari wa nchini Uganda, Kakoko amesema
kufunguka kwa kipande hicho kutafungua fursa nyingi za kibiashara
na kurahisisha usafirishaji wa shehena kati ya Tanzania na
Uganda.
Pichani Mkurugenzi Mkuu huyo anaonekana akiwa anakagua ukarabati
wa reli hiyo ambapo pia walikutana na Uongozi wa URC kwenye Kikao
Kazi.
kurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko amekutana na
Uongozi wa Shirika la Reli Uganda (URC) na Wafanyabiashara wa
Uganda ili kupanga mkakati madhubuti wa matumizi ya kipande cha
reli cha Kilomita 9 kati ya Port Bell na Kampala ambacho
kinafanyiwa ukarabati mkubwa ili kuanza kutumika kwa ajili ya
kupitishia shehena ya Uganda kutokea Bandari ya Mwanza.
Mwandishi Wetu
TPA YAKUTANA NA URC NAWAFANYABIASHARA WA UGANDA
M
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Deusdedit Kakoko (wa tano kushoto)
akiwa katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Uganda
(URC), Eng. Charles Kateeba (katikati). Wengine katika picha ni
Menejimenti ya TPA na URC.
‘‘Akiongea na Waandishi wa Habari wa nchini Uganda, Kakoko
amesema kufunguka kwa kipande hicho kutafungua fursa nyingi za
kibiashara na kurahisisha usafirishaji wa shehena kati ya Tanzania
na Uganda.’’