Top Banner
Mwongozo wa Bajeti kwa Wananchi
12

Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

Mar 01, 2020

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

Mwongozo wa Bajeti kwa Wananchi

Page 2: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

2

Shukrani

Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi kutoka Serikalini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango (MoFP), Asasi za Kiraia ambazo ni wanachama wa Policy Forum pamoja na Sekretarieti ya Policy Forum waliotoa michango iliyosaidia kuliboresha rasimu hii.

Ahsanteni sana!

Irenei Kiria

Mkurugenzi Mtendaji

Page 3: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

3

Tanzania ni miongoni mwa nchi za kidemokrasia ulimwenguni. Wananchi wake wamepewa haki na wajibu kisheria wa kushiriki kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali kama vile; kiuchumi, kisiasa na kijamii kwa ujumla. Katika suala la uchumi hususani uandaaji wa bajeti ya serikali, wananchi wana mchango na nafasi kubwa katika upatikanaji na ugawaji wa rasilimali za taifa. Michango yao kupitia kodi na michango mbalimbali ndiyo inayoiwezesha serikali kutekeleza mipango ya maendeleo. Nafasi yao katika kushiriki uandaaji wa bajeti ya Serikali huimarisha usimamizi na uwajibikaji.

na mojawapo ya sababu ni uelewa mdogo juu ya faida na jinsi ya kushiriki katika mchakato huo.

Mwongozo huu umeandaliwa na Sikika ili kumwezesha mwananchi kuelewa nafasi na haki yake ya kushiriki katika mchakato wa uandaaji na utekelezaji wa bajeti. Dhumuni lingine ni kumfahamisha mwananchi umuhimu wa kutoa mchango wake wa mawazo, kulipa kodi na tozo mbalimbali na namna zinavyoweza kuleta manufaa kwa jamii na nchi kwa ujumla; pia kushiriki katika ufuatiliaji wa bajeti husika.

Mwongozo huu umegawanywa katika sehemu kuu tatu zinazomuonesha msomaji dhana nzima ya bajeti, mchakato wa bajeti na fursa za mwananchi kushiriki katika mchakato huo.

Page 4: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

4

Sehemu A: Dhana ya Bajeti

Bajeti ni nini?Bajeti ni makadirio ya mapato na jinsi mapato hayo yatakavyotumika katika kipindi fulani. Makadirio ya matumizi ya mapato yanatokana na malengo yanayopangwa na mhusika wa bajeti, ambaye anaweza kuwa mtu binafsi, familia, kijiji, taasisi au Serikali.

Bajeti ya Serikali ni nini? Bajeti ya Serikali ni makadirio ya namna ambavyo Serikali imepanga kukusanya na kutumia fedha katika kipindi cha mwaka mmoja. Lengo ni kuiwezesha Serikali kutoa huduma kwa jamii kwa kuzingatia mahitaji ambayo huainishwa na wananchi na kupewa kipaumbele kulingana na umuhimu. Orodha ya mahitaji kulingana na kipaumbele hupelekwa katika mamlaka husika kwa ajili ya majumuisho. Mamlaka hizo ni kama vile Vijiji/Mtaa, Kata, Wilaya na Wizara mbalimbali. Vipaumbele katika ngazi hizi huibuliwa na wananchi kupitia mikutano shirikishi kati ya wananchi na viongozi katika ngazi hizo. Vipaumbele hivyo huwekwa katika mpango na kupangiwa gharama katika kipindi cha mwaka mmoja mmoja, ambao huitwa mwaka wa fedha na huanzia mwezi Julai kila mwaka hadi mwezi Juni mwaka utakaofuata.

Kwa nini bajeti ni muhimu? Bajeti ni muhimu kwa sababu hutoa muongozo wa matumizi na husaidia katika udhibiti wa fedha kuanzia mtu binafsi hadi taifa kwa ujumla. Bajeti humwezesha mwananchi kutambua ni kiasi gani cha fedha kilichopangwa, kiasi kinachokusudiwa kukusanywa kama mapato na kiasi kitakacho tumika kutekeleza shughuli mbalimbali hivyo kuweza kufanya maamuzi sahihi juu ya matumizi ya fedha. Bajeti pia inasaidia kuleta usawa wa maendeleo kulingana na mahitaji.

Bajeti ya Serikali huwaonesha wananchi namna Serikali inavyopanga kukusanya fedha na kuzitumia katika kuhudumia jamii ikizingatia majumuisho ya vipaumbele vilivyowekwa na jamii.

Fedha za bajeti ya Serikali zinatoka wapi?Serikali hukusanya fedha kwa idhini ya Bunge kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi kama ifuatavyo;

Vyanzo vya ndaniSerikali hukusanya mapato ya ndani kupitia taasisi zake mbalimbali kama vile Mamlaka ya Mapato (TRA), mashirika na taasisi za Serikali na Halmashauri. Mapato hayo yamegawanyika katika sehemu kuu

Page 5: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

5

mbili, yaani mapato yanayotokana na kodi na mapato yasiyotokana na kodi.

1. Mapato yatokanayo na kodi

Mapato haya yamegawanyika katika sehemu mbili;

(i) Kodi ya moja kwa moja yaani hulipwa moja kwa moja na mtu binafsi, kampuni ama shirika, mfano; kodi ya mapato, kodi ya ardhi, kodi ya majengo n.k.

(ii) Kodi isiyo ya moja kwa moja; hii hulipwa na mtu anayetumia huduma au kununua bidhaa mfano; kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ambayo mtumiaji huilipia baada ya kupata huduma au kununa bidhaa. Kwa lugha rahisi ni kwamba mtoa huduma ama muuza bidhaa huijumuisha kodi hii katika gharama za mauzo, hivyo mnunuaji wa bidhaa au mtumiaji huduma kupitia malipo ndio huilipa kodi hii. Mfano manunuzi ya vyakula, mavazi, vifaa vya ujenzi, au

kwa kulipia huduma kama

2. Mapato yasiyo ya kodi (tozo)

Mapato haya ni kama vile faini kwa kukiuka sheria, ada za vibali, ada ya leseni, michango na gawio kutoka kwa mashirika ya umma na mashirika ya kisheria, mapato kutokana na mauzo ya mali za Serikali, ada za vibali na leseni, ada za watumiaji wa miundombinu ya umma na mchango wa hiari, n.k.

Vyanzo vya njeKadhalika, Serikali hupata fedha kutoka nje ya nchi kupitia vyanzo mbalimbali kama mikopo, misaada na michango mbalimbali. Kwa mfano Serikali huomba mkopo au hupata misaada ili kujenga miundombinu, vituo vya afya na vilevile kuboresha huduma za afya. Pia Serikali kupitia wahisani mbalimbali hupata misaada isiyo fedha kama vile vifaa, vifaa tiba na vipimo vya maabara. Fedha hizi hutolewa na wadau wa maendeleo kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, Benki ya Dunia, na nchi zilizoendelea.

Page 6: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

6

Bajeti ya Serikali hupangwa katika kipindi cha mwaka mmoja wa fedha ambao hugawanywa katika hatua nne zinazotengeneza mzunguko wa bajeti ambazo ni; Mipango, Uidhinishaji, Utekelezaji na Ufuatiliaji.

1. Mipango

Hatua hii huanzia katika ngazi ya jamii. Ngazi hii ya msingi huwahusisha wananchi na viongozi wa vijiji/mitaa na kata kuainisha mahitaji na kuyapa vipaumbele kupitia mikutano ya jamii. Kwa pamoja hujadili na kisha viongozi huiwasilisha mipango hii katika ngazi ya wilaya/halmashauri kwa ajili ya majumuisho kwa idara mbalimbali na uidhinishaji wa Baraza la Madiwani. Mipango na bajeti iliyoidhinishwa na baraza huwasilishwa katika ngazi ya Mkoa kupitia Sekretarieti ya Mkoa na hatimaye Sekretarieti inapitia na kuiunganisha mipango yote kisha inawasilishwa Serikali Kuu (Wizara-TAMISEMI) ambapo Serikali kupitia Baraza la Mawaziri hupeleka

mapendekezo hayo Bungeni ili kujadiliwa. Mpango huu wa awali huitwa‘ mapendekezo ya bajeti’.

2. Uidhinishaji

Hatua hii ni muhimu inatoa mustakabali wa Taifa wa bajeti kujadiliwa na kuidhinishwa na Bunge kisheria. Baada ya mapendekezo ya bajeti kuwasilishwa Bungeni hujadiliwa na kuidhinishwa na Bunge pamoja na sheria ya fedha. Sheria ya fedha hutoa muongozo wa namna Serikali inavyopaswa kukusanya mapato. Ushiriki katika hatua hii muhimu huhusisha Wabunge tu ambao huwakilisha wananchi kutoka katika majimbo yao husika.

3. Utekelezaji

Baada ya bajeti na sheria ya fedha kuidhinishwa Bungeni, Serikali huanza utekelezaji wa mpango wa bajeti kwa kukusanya mapato na kufanya matumizi kwa kutoa huduma mbalimbali kwa jamii. Utekelezaji huu umegawanyika katika ngazi mbalimbali za Serikali kulingana na majukumu ya ngazi hizo. Mfano, utekelezaji wa mpango wa afya unaanzia katika ngazi ya Sekta ya Afya yaani Wizara ya Afya na taasisi zake, ngazi ya mkoa, wilaya, kata, kijiji/mtaa na vituo vya kutolea huduma. Mara nyingi utekelezaji hufanyika baada ya kupokea fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kulingana na bajeti iliyopitishwa.

Sehemu B: Mchakato wa Bajeti

Page 7: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

7

Hatua za mchakato wa bajeti za Serikali za MitaaMfumo wa uaandaaji wa bajeti kuanzia ngazi za Serikali za mitaa/vijiji mpaka serikali kuu

Chanzo:http://www.trustafrica.org/annualreport2012/pdf/Flier.pdf. Retrieved on September 27, 2019.

*Wananchi wanashiriki/shwa katika hatua ya tatu kupitia mikutano ili kufahamu mipango ya Mtaa/Kijiji.

4. Ufuatiliaji

Katika hatua ya ufuatiliaji, Serikali kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (au CAG) ambaye kapewa mamlaka kikatiba kukagua

katika ngazi zote za Serikali Kuu na Serikali za Mitaa hufanya shughuli hii, kisha kupitia taarifa zake kwa umma huonesha mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza katika utekelezaji wa bajeti iliyopitishwa. Kazi hii kubwa na muhimu hufanywa ili kuhakikisha;

1. Taarifa zote za kifedha ni za kweli

2. Wananchi wananufaika na huduma zitolewazo kwa kuzingatia mgao wa matumizi ya kodi wanazolipa.

Baada ya mwaka wa fedha kukamilishwa na hatua hii ya ufuatiliaji mwaka mwingine wa fedha huanza kwa kupanga bajeti mpya. Utaratibu huu hurudiwa kila mwaka na ndiyo maana huitwa ‘mzunguko wa bajeti’.

kuandaa muongozo wa bajeti

Nove - Dec1 Januari2

Kuwasilisha mipango kwenye kamati za maendeleo ya kata

FebruariMipango ya kijiji inaandaliwa kwa kuzingatia uainishwaji wa fursa na vikwazo vya maendeleo(O&OD)

Machi

Mipango ya kijiji inajumuishwakatika mipango ya kata

Machi/Aprili 5

Mipango ya kata inaunganishwa na kuandaa mpango na bajetiya mamlaka za serikali za mitaa (LGA)

Aprili6

Mipango na bajeti za mamlaka za selikali za mitaa zinapitiwa na halimashaurina kujadiliwa na kuidhinishwa na baraza la madiwani7

Mipango ya seriali za mitaa (LGA)inapitiwa na kuunganishwa nasekretarieti ya mkoa

Mei8Mipango na bajeti za mamlaka za serikali za mitaazinaunganishwa kuwa mpango mmojawa OWM-TAMISEMI

Juni/Julai9

Mipango na bajetiya OWM-TAMISEMIinajadiliwa katika bunge na kupitishwa

Agosti10Serikali za mitaa zinapokeabajeti ya mwishoiliyoidhinishwa na ulipaji wa pesa unaanza

Septemba....11

Zoezi la utekelezajimiradi unaanza

MCHAKATO

WA

BAJETI

4

3

Page 8: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

8

Sehemu C: Ushiriki wa Wananchi

Wananchi ni sehemu muhimu katika mzunguko wa bajeti. Ushiriki wao katika mchakato wa bajeti (mipango, utekelezaji, usimamiaji na ufuatiliaji) unasaidia katika kutoa maamuzi sahihi yanayolenga kuleta mabadiliko na kuboresha utoaji na upatikanaji wa huduma katika jamii hususani huduma za afya. Hii ni kwa sababu, wananchi ndio wanufaika wa huduma zitolewazo na Serikali na wanakutana na changamoto zitokanazo na huduma hizo.

Ni vema wananchi wakaelewa kuwa mamlaka yote ya Serikali na viongozi

wa umma hutoka kwao, na wao ndio wamiliki wa bajeti na viongozi ni wasimamizi na watekelezaji wa matakwa ya wananchi. Hivyo basi, wananchi wanaweza kushiriki katika mchakato wa bajeti kupitia hatua zifuatazo;

Hatua ya mipango: wananchi na viongozi wa vijiji/mitaa kupitia mikutano ya vijiji/mitaa, hushirikiana kujadili mipango ya kijiji na kubaini mahitaji yao kisha kuweka vipaumbele ili kuboresha mipango iliyopo katika jamii.

Page 9: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

9

Hatua ya utekelezaji wa bajeti: Wananchi kupitia mikutano ya vijiji, hukutana na kuelezwa miradi iliyopangwa kutekelezwa katika vijiji/mitaa yao ili waweze kuijua na kushirikiana na viongozi wao katika kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo.

Hatua ya usimamizi: wananchi wanao wajibu wa kuisimamia na kuwasimamia viongozi wao katika kutekeleza majukumu na miradi ya maendeleo katika jamii yao na kutoa mrejesho kwa wananchi juu ya utendaji kazi, mafanikio na changamoto wanazopitia ili kuweza kujadili kwa pamoja. Shughuli hii ya usimamizi huweza kufanywa kupitia

mikutano ya vijiji/mitaa au kamati husika (mfano kupitia kamati za kusimamia huduma za afya za vituo).

Katika kuhakikisha wananchi wanafahamu na kupata taarifa zinazohusu bajeti na kuweza kushiriki kuanzia hatua ya uandaaji hadi kufuatilia utekelezaji wake, Halmashauri zote nchini zinawajibika kurahisisha upatikanaji wa taarifa za bajeti kwa umma kwa kuchapisha taarifa hizo na kuzitangaza kwa uwazi kupitia njia mbalimbali kama

yaliyopo katika maeneo yao ya Wilaya, kata, vijiji na mitaa, mbao

za kata, vijiji, mitaa na pia kwenye

Page 10: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

10

zahanati na tovuti ya halmashauri husika. Hii ni kwa mujibu wa kifungu namba 90 (i-ii) cha Memoranda ya Fedha ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1997. Lakini, ili wananchi washiriki vyema katika masuala ya kijamii, wanahitaji kupata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu mikakati na maendeleo ya jamii yao, rasilimali zilizopo na uhalisia wa utoaji huduma.

Taarifa za bajeti zinazotakiwa kuchapishwa ni kama zifuatazo:

• Taarifa ya mapato na matumizi(muhtasari wa hesabu) na

• Ripoti yoyote iliyotiwa saini na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Aidha,ili kuboresha utolewaji na upatikanaji wa huduma nzuri za afya,wananchi wana haki ya kujua taarifa za mapato na matumizi ya fedha za vituo vya kutolea huduma za afya na kutoa maoni na vipaumbele vyao ili kuongeza uwajibikaji, uwazi na utekelezaji wa vipaumbele.

Page 11: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

11

Hitimisho

Ni matarajio yetu kuwa, mara baada ya mwananchi kusoma mwongozo huu na kuuelewa, atatambua haki na nafasi yake ya kushiriki katika mchakato wa bajeti na hata kuchukua hatua ya kufuatilia taarifa za bajeti katika sehemu husika, hatimaye kushiriki kikamilifu katika zoezi hili lenye mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya Taifa.

Page 12: Sikika - Mwongozo wa Bajeti Kwa Wananchi BRIEF - Mwongozo wa Bajeti... · Natoa shukrani za dhati kwa wanachama wa Kikundi kazi cha Uchambuzi wa Bajeti (BWG) kilichojumuisha uwakilishi

Sikika inafanya kazi ya kuhimiza uboreshaji wa mifumo ya afya na

usimamizi wa fedha kupitia uwajibikaji jamii na uraghibishi

katika ngazi zote za serikali

Nyumba Na. 69Ada Estate, Kinondoni Barabara ya Tunisia Mtaa wa Waverley StreetS.L.P 12183Dar es Salaam, Tanzania.Simu: +255 22 26 663 55/57

Nyumba Na. 340 Mtaa wa KilimaniS.L.P 1970 Dodoma, Tanzania. Simu: 0262321307 Nukushi: 0262321316

Ujumbe mfupi: 0688 493 882 Nukushi: +255 22 26 680 15Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.sikika.or.tzTwitter: @sikika1Facebook: Sikika1Instagram: Sikika1