www.inclusion-international.org Sauti Yangu Isikilizwe! Kuwasaidia watu wenye ulemavu wa akili kushiriki katika masuala ya kijamii na harakati za kisiasa. Warsha kwa ajili ya Watetezi Binafsi (Watu Wenye Ulemavu wa Akili) na Familia zao Tarehe 31 Julai 2015, Zanzibar
40
Embed
Sauti Yangu Isikilizwe! Kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ... · –Tuna haki ya kutoa maoni juu ya shughuli za serikali na jinsi jamii zetu zinavyoendeshwa. • Nina maoni kuhusu
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
www.inclusion-international.org
Sauti Yangu Isikilizwe!
Kuwasaidia watu wenye ulemavu wa akili
kushiriki katika masuala ya kijamii na harakati
za kisiasa.
Warsha kwa ajili ya Watetezi Binafsi (Watu
Wenye Ulemavu wa Akili) na Familia zao
Tarehe 31 Julai 2015, Zanzibar
Utaratibu wa Uwasilishaji
• Utangulizi
• Madhumuni, Malengo na Matarajia ya Mradi
• Ukweli juu ya WWUA duniani
• Ushirikishwaji wa WWUA katika Siasa
• Wajibu wa Serikali
• Uchaguzi Jumuishi
• Mambo yanayopelekea Ujumuishi
• Vikwazo na Vihunzi – Tulichojifunzo
• Tathmini ya Warsha
“Piga kura na mimi nipige
Kama mimi sistahiki kupiga kura na wewe
pia hustahiki, Amua!!!”
Kwa nini tupo hapa? Kuhamasisha ushiriki wa watu wenye ulemavu wa akilikatika harakati za kisiasa.
Warsha hii inalenga :
Kutoa elimu kuhusu namna ya kushiriki katika harakati zakijamii kwa familia, watetezi binafsi na jumuiya za familia zawatetezi binafsi
Kuweka mikakati ya kuongeza ushiriki wa watu wenye ulemavuwa akili katika harakati za kisiasa
We gratefully acknowledge the UN Democracy Fund for its support of this project, Accessing the Ballot Box.
Makaribisho na Utangulizi
– Je! Wewe ni NANI?
– Utanufaika vipi nawarsha hii?
Mradi II: Nje ya kisandukucha kupigia kura
• Warsha hii ni sehemu ya mradi wa kuhamasisha ushiriki katikaharakati za kisiasa kwa watu wenye ulemavu wa akili: Kukifikiakisanduku cha kupigia kura
• Madhumuni ya mradi huu ni: – Kujenga msingi wa ushriki wa watu wenye ulemavu wa akili kwenye
harakati za siasa katika nchi za Kenya, Lebanon na Zanzibar.
– Kuongeza uelewa wa watu wenye ulemavu wa akili, familia na jumuiyazao pamoja na taasisi za serikali juu ya haki ya watu wenye ulemavu waakili kushiriki katika harakati za siasa
– kupeana nyenzo (mbinu) ili kuleta mabadiliko chanya
Mradi II: Matarajio
• Kuongeza uelewa juu ya ushiriki wa watu wenye ulemavu waakili katika harakati za siasa katika nchi 3 teule.
• Watu wenye ulemavu wa akili, familia na Jumuiya zao katikanchi hizo wana uwezo wa kutatua baadhi ya vikwazovinavyowakabili watu wenye ulemavu wa akili kuhusiana naushiriki wao katika harakati za kisiasa.
• Kuongeza uelewa miongoni mwa Maafisa wa Tume ya Uchaguzina wanajamii juu ya jinsi ya kuwasaidia watu wenye ulemavuwa akili kutekeleza haki yao ya kushiriki katika harakati zakisiasa
Pamoja:
• Tutajifunza kuhusu ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu waakili katika harakati za kisiasa
– Nini maana ya ushirikishwaji wa kisiasa na una umuhimu gani
• Tutafahamu kwa nini sauti zetu hazisikilizwi– Vikwazo vinavyotuzuia kushirikishwa
• Tutajifunza jinsi ya kuishawishi jamii itushirikishe
– Namna ya kupaza sauti zetu na kusikilizwa
• Tutasaidiana fikra za jinsi ya kuchukua HATUA
Tunamaanisha Nini Tunaposema “Ushirikishwaji wa Harakati za Kisiasa”
Unamaanisha pia:
• Kupiga kura na kushirikishwa katika utungaji waSera na Sheria zinazotuhusu.
– Pia unajulikana kama ushirikishwaji katikamasuala ya kiraia .
• Uwezo wa kusema kile ninachokiona muhimukwangu na kuamua mustakabali wa nchi yangu
– Hii inajumuisha haki yangu ya kupiga kura nakutoa maoni juu ya Sera na Sheria ambazozinanigusa.
Ushirikishwaji katika harakati za kisiasa unamaanisha kuishawishi Serikali yakoikusikilize.
Tunachokijua kuhusu Ushirikishwaji katika harakati za kisiasa duniani ?
• Familia nyingi za watu wenye ulemavu wa akili na Jumuiya zao hazilipi umuhimu suala la ushiriki wao katika harakati za siasa.
• Kuna unyanyapaa wa kimfumo dhidi ya watu wenye ulemavuwa akili hususan wanawake ambao hawashirikishwi katikamasuala ya siasa.
• Watu wenye ulemavu wa akili wananyimwa haki ya kupiga kurana kushiriki katika mchakato wa kisiasa.
LAKINIWatu wenye ulemavu wa akili wana hamu ya kupatiwa fursa ya kushirikikatika harakati za ujenzi wa jamii zao ili na wao watambuliwe nakuthaminiwa kama sehemu ya jamii.
Kufanikisha hilo:
• Watu wenye ulemavu wa akili na familia zao hapana budi wapewe fursasawa ya kushiriki katika harakati za siasa kikamilifu kama raia wengine.
• Watu wenye ulemavu wa akili, familia na Jumuiya zao lazima wapewefursa za kutoa maoni yao kuhusu programu zinazogusa maisha yao, sanjarina maamuzi yanayoathiri ustawi wao na jamii zao.
• Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa CRPD ni fursa muhimu kwa sababuunatambua haki ya watu wenye ulemavu wa akili kushiriki katika harakatiza siasa (Ibara 29).
Ibara ya 29 ya CRPD
Serikali zitabeba dhamana ya kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavuwanapata haki zao za kisiasa na fursa za kufurahia haki hizo katika hali yausawa kama raia wengine, na kwamba:
a) Zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanashiriki vilivyo katikaharakati za kisiasa na kijamii katika hali ya usawa kama raia wengine, waowenyewe au kupitia wawakilishi waliowachagua pasi na shinikizo,zikiwemo haki na fursa za kushiriki katika kuchagua na kuchaguliwa,ikiwemo:
i. Kuhakikisha utaratibu wa kupiga kura, vifaa na nyenzo zilizopo nimuafaka, zinapatikana na ni rahisi kufahamika na kutumiwa;
ii. Kulinda haki za watu wenye ulemavu kwa kupiga kura ya siri, nakushiriki katika kura za maoni bila vitisho, na kugombea nyadhifambali mbali, kushika nyadhifa za uongozi na kutekeleza majukumuyote katika ngazi zote za serikali, na kurahisisha matumizi ya vifaa nateknolojia saidizi kila inapowezekana;
Ibara 29 ya CRPD
iii. Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanakuwa huru katika kutoa maoni yao na kueleza dhamira zao kama wapiga kura, na pale itapolazimu, kwa utashi wao wenyewe, kuruhusu usaidizi kutoka kwa mtu waliomteuwa wenyewe;
a) Kujenga kwa makusudi mazingira ambayo yataruhusu watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika harakati za maendeleo ya nchi yao, ikiwemo:
i. Kushiriki katika jumuiya zisizo za kiserikali na vyama vinavyojihusisha na masuala ya umma na siasa katika nchi, na katika harakati na uongozi wa vyama vya siasa;
ii. Kuunda na kujiunga na jumuiya za watu wenye ulemavu ili kuwawakilisha katika medani za kimataifa, kitaifa, kimkoa na hata mtaa.
CRPD katika lugha rahisiIbara ya 29: Jinsi ya kushirikishwa katika harakati za siasa
Watu wenye ulemavu wana haki ya kushiriki kama
katika harakati za siasa kama watu wengine
Watu wenye ulemavu wana haki ya kupiga
kura kwa kuwahakikishia kuwa:
• Mchakato wa upigaji kura ni rahisi na
wenye kufahamika
• Upigaji kura ni siri
CRPD katika lugha rahisi Ibara ya 29: Jinsi ya kushirikishwa katika harakati za siasa
• Kuruhusu usaidizi ili kuwawezesha watu wenye
ulemavu kupiga kura katika namna wanayoitaka, na
inapohitajika.
• Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu
wanashirikishwa katika jumuiya zisizo za kiserikali
na vyama vya siasa.
• Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wana fursa
ya kujiunga na jumuiya za watu wenye ulemavu.
Hii inamaanisha nini?
• Fomu za kupigia kura zinapatikana, vituo na taratibu za upigaji kura zimerahisishwa kwa ajili yangu
• Naweza kupiga kura katika hali ya faragha siku ya uchaguzi
• Nasaidiwa kupata kitambulisho na cheti cha kuzaliwa ili nisajiliwe katika daftari la mpiga kura
• Taarifa za upigaji kura kama vile maeneo ya vituo vya kupigia kura na wagombea zinapatikana katika namna iliyorahisishwa – hii ni pamoja na matumizi ya lugha iliyo rahisi kufahamika na picha pia
• Nina uhuru wa kumteua mtu wa kunisaidia kupiga kura. Hii inajulikana pia kama usaidizi wa kupiga kura
• Naweza kuchaguliwa kuiongoza taasisi ya serikali
• Naweza kushiriki katika jumuiya za kiraia zinazojihusisha na masuala ya kijamii na kisiasa na uongozi katika vyama vya kisiasa
• Naweza kuunda au kujiunga na jumuiya zinazowakilisha watu wenye ulemavu wa akili kuanzia ngazi ya mtaa, mkoa, taifa na kimataifa
Kwa nini hatusikilizwi?
• Sheria inatamka kuwa haturuhusiwi kupiga kura au kushiriki katika shughuli za kiserikali.
• Jamii haiamini kuwa tunaweza kuwa na mchango wa maana
• Hatujui Sera na Sheria zinazungumzia nini na jamii haioni umuhimu wa sisi kujua
• Sijui jinsi ya kuifanya jamii inisikilize au jinsi ya kuleta mabadiliko
• Sijawahi kupewa fursa ya kushirikishwa katika jamii yangu. Na mimi nahitaji kupata elimu na nahitaji kufanya kazi.
• Familia zetu hazioni umuhimu wa sisi kupiga kura au kutoa maoni yetu kuhusu Sera na Sheria.
• Jamii haituthamini.
Vikwazo Vikuu
1. Kunyimwa uwezo wa kisheria
2. Sera na Sheria zinazotubagua
3. Changamoto za kufikiwa
4. Desturi za kijamii na kiutamaduni
5. Ukosefu wa elimu juu ya Haki za Watu Wenye Ulemavu wa Akili
6. Ukosefu wa miundo mbinu au nyenzo sahihi za kushughulikia Haki za kushirikikatika harakati za kisiasa na kiraia
7. Harakati za kisiasa na kiraia hazipewi kipa umbele kinachostahiki na familia zetu
8. Kutengwa na kunyanyapaliwa.
Kwa nini nisikilizwe?
• Maamuzi yanayofanywa na serikali yananigusa kwahivyo lazima inisikilize.
– Tuna haki ya kutoa maoni juu ya shughuli za serikali najinsi jamii zetu zinavyoendeshwa.
• Nina maoni kuhusu yale mambo ninayohisi ni muhimukwangu.
• Jamii yangu inapaswa kujua kilicho muhimu kwangu namsaada ninaouhitaji ili nikubalike na kushirikishwakatika jamii yangu.
– Ushiriki wangu unaweza kusaidia kujenga jamiishirikishi ambayo inajali mahitaji ya watu wenyeulemavu wa akili.
Kwa nini nisikilizwe?
• Kusikilizwa ndiko kunakonifanya niwe raia sawa na wengine. Sitaki kutengwa!
• Nikisikilizwa najua kuwa makundi YOTE yanasikilizwa. Hii inaifanya jamii yetu iwe rafiki kwa KILA MTU.
• Serikali yangu itakapotambua mahitaji yangu itatunga sera na sheria ambazo zinatilia maanani mahitaji ya kila mmoja wetu.
Ushirikishwaji katika harakati za kisiasa
KABLA YA UPIGAJI KURA
Kupitia na kushinikiza mikutano ya vyama; mipango yaserikali/vipaumbele
WAKATI WA UPIGAJI KURA
Kupiga kura; ufikiwaji wa mchakato mzima wa uchaguzi
BAADA YA UPIGAJI KURA
Kushiriki katika utungaji wa sera za umma na kusimamiataasisi za serikali kwa kufanya ukaguzi na mbinunyengine
KABLA ya uchaguzi
Mtu mmoja mmoja
• JIANDIKISHE
– Unaweza kuhitajikitambulisho cha uraia ilikujiandikisha
• Kutana na kiongozi wako mteule
– Serikali na viongozi wanahitajikujua masuala ya watu wenyeulemavu ili kuyaingiza katikavipa umbele vyao
– Waelezee hali yako ya maisha, matumaini yako na yaleambayo ungependawakufanyie.
Makundi
• Waite wagombea na waelezematatizo ya watu wenye ulemavukwa ufasaha
• Kutana na wawakilishi wa serikali
• Shinikiza mabadiliko
– Je! Kuna sheria zinazowazuiawatu wenye ulemavu kupigakura?
• Uchambuzi wa Sera jumuishi
– Utekelezaji wa mkataba waCRPD
– Sera, bajeti, mchanganuo waprogramu
Wakati wa uchaguzi
Mtu mmoja mmoja
• Elezea kile unachokiona muhimukwako na kile ambachoungependa serikali ikufanyie ilikufikia lengo la ujumuishi
• Piga simu katika vipindi vya rediona runinga na uulize maswalikuhusu watu wenye ulemavu
• Fuatilia midahalo na jinsi ganiwananchi wanaweza kushiriki
• Wagombea wanaweza kuhitajimaoni yako
– Waite na uzungumze nao, waulize watawafanyia niniwatu wenye ulemavu
Jumuiya
• Wapeni wanachama wenu taarifaza kiuchambuzi kuhusiana namikutano yote ya kisiasa
• Andikeni “waraka” mtaowapawagombea ambao unaainishamasuala ya msingi na“waombeni” wayatekeleze
• Andaeni au shirikini katikamidahalo yote inayozungumziamasuala ya watu wenye ulemavu
• Fanyeni kampeni za kuhamasishawatu juu ya haki ya kupiga kura
• Kwa kutumia mfano wafundisheniwatu wenye ulemavu jinsi yakupiga kura
Siku ya UchaguziMtu mmoja mmoja
• Jua kilipo kituo chako cha kupigiakura
– Hwenda ukahitaji kituomaalum cha kupigia kura
• Piga kura
Jumuiya• Ziwasaidie watu wenye ulemavu
kuvifikia vituo vya kupigia kura
• Ziwasaidie watu wenye ulemavukupiga kura
Baada ya UchaguziMtu mmoja mmoja• Fuatilia kwa viongozi wako
wateule
– Mahusiano yanapaswa kuwaendelevu na sio wakati wauchaguzi pekee
• Shiriki katika midahalo
• Hadithia maisha yako/uzoefuwako kwa ajili ya ripoti n.k
• Jihusishe!
Jumuiya• Fuatilia utekelezaji wa ahadi za
vyama/viongozi wa serikali
• Shinikiza mabadiliko
– Kuna sheria zinazowazuiawatu kupiga kura?
• Tathmini ya sera jumuishi
– Hii inapaswa kuwa endelevukabla na baada ya uchaguzi
– Utekelezaji wa mkataba wa CRPD
– Sera, bajeti, uchanganuzi watathmini ya programu
• Fuatilia na tathmini athari/matokeoya juhudi za serikali
– Ripoti serikalini, ripoti kwamashirika ya kimataifa
Mfano: PANAMA
Juhudi zinazofanywa kabla ya uchaguzi ilikuongeza ushiriki wa raia, ni pamoja na kuandaamikutano ya kutoa elimu kwa umma na kuandaamidahalo na wagombea wa kiti cha urais.
Kuchukua ahadi ya utekelezaji wa sera ambazozitaboresha ushiriki wa watu wenye ulemavu nafamilia zao katika nyanja zote za maisha
Kuanzisha Sekretarieti ya kitaifa kwa ajili yaushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katikajamii (SENADIS).
Pata taarifa
• Ziombe familia zetu, marafiki na watu wa kuaminika/jumuiya ili wakupatietaarifa hizo
• Fanya utafiti iwapo sheria kwenye nchi zetu zinatuzuia tusipige kura
– Shirikiana na jumuiya zetu kwa kutumia vigezo maalum tathmini iwaponchi zetu zinatekeleza mkataba wa CRPD. Vigezo hivyo vinapatikanakatika ripoti kuu.
• Tafuta jumuiya katika nchi zetu ambazo zinajihusisha na mahitaji yetu.
Tufanye tusikilizwe
• Zungumza na viongozi wetu wateule au wawakilishi. Wawakilishi wetu wapo kwa ajili ya maslahi yetu. Wanawajibu wa kusikiliza maoni yetu kuhusu mambo yenyemaslahi kwetu.
“Sisi (familia zilizoathiriwa na ulemavu) hatuonekani kama makundi yawatu wengine…….sababu hakuna watu wengi wenye ulemavu katika maeneno yetu
tunayoishi kama walivyo wakulima na wafanya biashara. Kuna mengi tuwezayokuyafanya lakini uwezo duni wa kifedha unatukwaza. Lakini siku tulipotembelewa
[na kiongozi wetu tuliomchagua] tulibaini kuwa iwapo kila mwanasiasa angejipangiautaratibu wa kututembelea kama hivi ingesaidia kuongeza uelewa,”
• Wasilisha ripoti mbadala kwa mashirika ya Umoja waMataifa kuhusu juhudi ambazo nchi yako inachukua kutatuachangamoto za watu wenye ulemavu.
ShirikianaHatuwezi kufanya haya peke yetu
• Shirikiana na wataalamu mbali mbali ili tuweze kuongeza uelewa wao juu ya masuala ya watu wenye ulemavu
• Anzisha jumuiya zinazohamasisha haki za watu wenye ulemavu na ushiriki wao kisiasa.
Jifunze kupitia wengine
• MENCAP – Makundi yote ya Wanachama; Kampeni ya Pata kura yangu
• Holland – midahalo ya siasa
– Andaa midahalo ili kujadili mambo ambayo ni muhimu kwako/kundi lako
• Lebanon – Shirikisho la Watu wenye Ulemavu
– Kufanya kazi pamoja na kushirikiana na wadau wengine
• Canada – candidate pledge cards; inaandaa midahalo yote na wagombea
• Germany/Japan/Peru – strategic litigation – inapigania kufuta sheria inayowazuia watu walio chini ya uangalizi (kulelewa) kupiga kura
• Kenya/Zanzibar – viti maalum vya uwakilishi bungeni na Baraza la Wawakilishi