Top Banner
ISSN 0856 - 3861 Na. 1028 SHAABAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu ‘Karume mpya’ acharuka Ataka Zanzibar iwe na Polisi, sarafu yake Awambia vijana wasiogope wakati ni huu Ampasha Vuai, asema Zanzibar sio ya CCM Hakuna adhabu atakaegoma kuhesabiwa Na Bakari Mwakangwale Waziri William Lukuvi ajiuzulu Amesababisha watu kufa kwa ‘Babu’ Sema: kweli imefika, batili imetoweka Hatimae Dr. Haji Mponda aibuka shujaa HAKUNA atakayeadhibiwa kwa kukataa kuhesabiwa katika sensa ya idadi ya watu na makazi. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Asema Mkurugenzi wa Takwimu Dr. Chuwa Ateta na Masheikh wanaowakilisha Waislam Kipengele cha dini kikiwekwa sensa iahirishwe Takwimu, Dkt. Abina Chuwa. Dr. Chuwa alikuwa akifafanua taarifa iliyokuwa imetolewa awali kuwa atakae kataa kuhesabiwa atakamatwa na kufungwa jela au kupigwa faini. Akitoa ufafanuzi huo mbele ya Wanazuoni wa Kiislamu, Mkurugenzi huyo amesema kuwa sheria itamchukulia hatua mtu ambaye ataharibu vitendea kazi vya maofisa wa Sensa. LEO hii tunaona dini moja tu inayohodhi kila kitu hadi kufikia nyimbo za dini kupigwa katika ofisi za Serikali bila ya woga wowote. Picha za kiongozi wa dini kubandikwa kwenye maofisi ya Serikali. Hakuna haki wala uwiano wa asili (fair play and natural justice). Ukanda wa kikabila na udini vimechangia kutufikisha hapa tulipo leo. Kanda na dini moja kuhodhi sehemu zote nyeti. Hili halina Tujuane ili watu wa dini moja wasihodhi kila kitu kificho tena. Nenda TRA, Wizara ya Fedha, CRDB, NBC, idara zinazohusu pesa na maamuzi ziko mikononi mwao. Ukiuliza utaambiwa wao wamesoma!! Hivi ni chuo kipi kinasomesha kabila au dini moja tu au kozi zipi zinasomesha kabila au dini moja tu!!! “Sababu kubwa hakuna “fair play na natural justice” hata mashuleni”!!! (Soma makala Uk. 8) RC Arusha azidi kukoroga Sensa Atisha Masheikh. Apashwa ukweli mchungu Adai msimamo wao utamwongezea dhambi Kiroja: Shehe Bakwata ashangiliwa na maaskofu Inaendelea Uk. 2 MZEE Hassan Nassoro Moyo WAZIRI William Lukuvi akipata 'kikombe' kwa 'Babu'.
16

Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

Nov 02, 2019

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

ISSN 0856 - 3861 Na. 1028 SHAABAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamu

‘Karume mpya’ acharukaAtaka Zanzibar iwe na Polisi, sarafu yakeAwambia vijana wasiogope wakati ni huuAmpasha Vuai, asema Zanzibar sio ya CCM

Hakuna adhabu atakaegoma kuhesabiwaNa Bakari Mwakangwale

Waziri William Lukuvi ajiuzulu

Amesababisha watu kufa kwa ‘Babu’Sema: kweli imefika, batili imetowekaHatimae Dr. Haji Mponda aibuka shujaa

HAKUNA atakayeadhibiwa kwa kukataa kuhesabiwa katika sensa ya idadi ya watu na makazi.

H a y o y a m e e l e z w a na Mkurugenzi Mkuu wa

Asema Mkurugenzi wa Takwimu Dr. ChuwaAteta na Masheikh wanaowakilisha WaislamKipengele cha dini kikiwekwa sensa iahirishwe

Ta k w i m u , D k t . A b i n a Chuwa.

D r. C h u w a a l i k u w a akifafanua taarifa iliyokuwa imetolewa awali kuwa atakae kataa kuhesabiwa atakamatwa na kufungwa jela au kupigwa faini.

Akitoa ufafanuzi huo mbele ya Wanazuoni wa Kiislamu, Mkurugenzi huyo amesema kuwa sheria itamchukulia hatua mtu ambaye ataharibu vitendea kazi vya maofisa wa Sensa.

LEO hi i tunaona dini moja tu inayohodhi kila kitu hadi kufikia nyimbo za dini kupigwa katika ofisi za Serikali bila ya woga wowote.

Picha za kiongozi wa dini kubandikwa kwenye maofisi ya Serikali. Hakuna haki wala uwiano wa asili (fair play and natural justice).

Ukanda wa kikabila na udini vimechangia kutufikisha hapa tulipo leo.

Kanda na dini moja kuhodhi sehemu zote nyeti. Hili halina

Tujuane ili watu wa dini moja wasihodhi kila kitu

kificho tena. Nenda TRA, Wizara ya Fedha, CRDB, NBC, idara zinazohusu pesa na maamuzi ziko mikononi mwao.

Ukiuliza utaambiwa wao wamesoma!! Hivi ni chuo kipi kinasomesha kabila au dini moja tu au kozi zipi zinasomesha kabila au dini moja tu!!!

“Sababu kubwa hakuna “fair play na natural justice” hata mashuleni”!!! (Soma makala Uk. 8)

RC Arusha azidi kukoroga Sensa

Atisha Masheikh. Apashwa ukweli mchunguAdai msimamo wao utamwongezea dhambiKiroja: Shehe Bakwata ashangiliwa na maaskofu

Inaendelea Uk. 2

MZEE Hassan Nassoro Moyo

WAZIRI William Lukuvi akipata 'kikombe' kwa 'Babu'.

Page 2: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

2 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0652 849227, 0713 110148, DSM. www.ipctz.org E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House (Jengo dogo), barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAONI YETU

Tahariri

Hakuna adhabu atakaegoma kuhesabiwaInatoka Uk. 1

“Hakuna atakayefungwa kwa kukataa kuhesabiwa, ila anatakiwa aelimishwe isipokuwa sheria itachukuliwa kwa mtu ambaye atachana karatasi (dodoso) lakini atakae kataa inabidi aelimishwe lakini sio kumweka mahabusu, kama ilivyoelezwa.”

Alisema Dk. Chuwa katika kikao kilichowakutanisha yeye, Kamaishana wa Sensa na Masheikh wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu wakiongozwa na Mwenyekiti wao Sheikh Suleiman Amran Kilemile, katika ofisi zao Kariakoo, Jijini Dar es Salaam, Jumatatu wiki hii.

Dkt. Chuwa, aliwataka Wanazuoni hao kuangalia uzalendo zaidi wa Taifa, na gharama ambazo Serikali tayari imeingia mpaka sasa, kwani dunia nzima inajua hali ilivyo sasa nchini na kuwataka wawashawishi Waislamu kushiriki katika Sensa.

Ama kuhusu kuzagaa kwa Takwimu zisizo rasmi ambazo zinalalamikiwa na Waislamu, Dkt. Chuwa, alisema Takwimu ambazo wanazijua za idadi ya Waislamu na Wakristo ni ile ya mwaka 1957 na si vinginevyo.

Kwa kauli hiyo ya Mkuu wa Takwimu ni kuwa, serikali imezitupilia kwa mbali zile takwimu za 1967 ambazo zilichakachuliwa na kudai kuwa Wakristo ni wengi.

Katika sensa ya mwaka 1957 Waislamu walikuwa wengi kuliko Wakristo kwa uwiano wa 3:2 lakini ilipofika 1967 ikadaiwa kuwa Wakristo ni asilimia 32, Waislamu 30% na wenye kufuata dini za asili 37%.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya serikali, Jumuiya ya Kimataifa ilihoji ikitaka kujua nini kimetokea kwa Waislamu.

Je, kumetokea mauwaji ya Kimbari (genocide), njaa iliyouwa Waislamu pekee au Waislamu wote wamegoma kuzaa ikawa wanakufa tu bila kuzaana.

Ni kutokana na kukosekana na majibu ya maswali hayo, nyaraka za sensa za ya 1967 leo ukizitafuta huzipati, imebaki tu ile namba ya jumla inayotaja idadi ya Watanzania mwaka huo.

Na ndio maana leo Mkuu wa Takwimu anasema kuwa takwimu pekee halali na za kuaminika zilizopo serikalini z inazoonesha idad i ya Waislamu na Wakristo ni ile ya sensa mwaka 1957.

Kutokana na rekodi hii, hakuna namna ambayo sensa itaaminika kipengele cha dini kikiwekwa kama hakun a utaratibu mpya utakaowekwa kuhakikisha kuwa kila hatua ya watu kuhesabiwa watu wa dini zote wapo wanahakiki idadi inayotolewa kwa kila kijiji/kitongoji/ mtaa mpaka kujumlisha na kutangaza matokeo ya mwisho.

Ni kwa sababu hii kama hoja ya Waislamu itakubalika, i tabidi sensa iahirishwe taratibu zipangwe upya.

Kwa upande mwingine, Dr. Chuwa amekiri kuwa takwimu nyingine zinazozagaa mitaani si sahihi na zinaweza kuleta machafuko ndani ya nchi, huku akidai kwamba tatizo hilo limechangiwa na kutokana na sheria iliyopo sasa kuwanyima mamlaka ya kukemea hali hiyo.

“Hizi Takwimu zilizopo sheria ingekuwa inaturuhusu tungewashitaki kwani hii ni kuleta vita kubwa ndani ya nchi. Hatuwezi kukaa na takwimu za namna hii, sheria iliyopo haiana meno ndio maana haya yote yanatokea.” Alisema Dkt. Chuwa.

Katika kikao hicho, Maalim Ally Bassaleh alisema kuwa japo Tume imefanya hambo la msingi kuwaona Masheikh hao wawakilishi halali wa Waislamu, na wanaotambuliwa

na kusikilizwa na Waislamu, lakini wafahamu kuwa nyuma yao kuna umma wa Kiislamu wanaosubiri serikali inasema nini juu ya madai yao.

Alisema, haoni kama kuna ugumu wa kuingizwa kipengele cha Dini, ili hali hata Umoja wa Mataifa unaruhusu na kutambua kipengele cha Dini.

“Mimi naomba maana hata Umoja wa Mataifa unaruhusu kipengele cha Dini kuwemo katika Sensa, kiingizwe, itasaidia kusahihisha zile hesabu zisizo sahihi ambazo zimezagaa, ombi letu wekeni k i amba tan i sho , i k ib id i sensa isogezwe mbele ili kurekebisha suala hili, hapo hapatakuwa na ugomvi na Waislamu.” Alisema Maalim Bassaleh.

Maalim Bassaleh, alisema suala la kutishana kwamba watu watafungwa kwa sababu hawatahesabiwa, aliwataka maafisa hao kuliangalia kwa kina na si kucheza na imani za watu.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Sheikh Suleiman Amrani Kilemile, akichangia kwa upande wake alieleza kuwa Waislamu hawakuwa na nia ya kususia Sensa hiyo kwani wanaelewa umuhimu wake, bali kilichopelekea

MAALIM Ally Bassaleh

Inaendelea Uk. 4

WAKATI Wais lamu sehemu mbal imbal i n c h i n i n a d u n i a n i kwa ujumla wakiwa wamefikisha nusu ya funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, ni muda muafaka kwao kuanza kujiandaa kwa ajili ya kutoa Zakat Fitri.

S a d a k a a m b a y o hutolewa na kila Muislamu m w e n y e u w e z o w a kukidhi mahitaji yake ya msingi kwa ajili ya kuwawezesha wasiokuwa na uwezo kusherehekea sikukuu ya Eid el Fitri kama wanavyosherehekea wale wenye uwezo.

Kwa kawaida Zakat Fitr hutolewa na kila Muislamu mwenye uwezo wa kutoa zaka hiyo. Katika familia, kwa maana ya mke, mume na watoto, basi wazazi kwa maana ya baba au mama analazimika kuwalipia watoto wote alio nao. Hata kama kuna yeyote ambaye anaishi katika familia kwa kutegemea huduma ya baba au mama, basi huyo mzazi au mlezi mweye famil ia analazimikia kumlipia zakat Fitr.

Kila kichwa hulazimika kutoa au kutolewa Zakat Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa eneo husika anakoishi mpokeaji au mtoaji.

Kutokana na hali halisi ya maisha, ni vyema mtoa Zakat Fitr akaanza kujiandaa na mapema hususan kwa wale wenye familia zinazowategemea au ndugu jamaa ambao ni tegemezi kwake.

Kwa sehemu kubwa

Waislam jiandaeni kutoa Zakatul Fitri

ya Tanzania, chakula kinachopendwa sana na Waislamu walio wengi katika sikukuu ya Eid el Fitr ni wali, pilao, chapati na mboga inayotegemewa ni nyama, samaki, kuku na maharagwe kwa kiasi.

Kilo moja ya Mchele safi hivi sasa ni shilingi 2,000, pishi moja ni shilinghi 5000. Kulingana na hali ya vipato vya watu wa nchi yetu, Kama mtoa Zakat Fitr, hususan yule mwenye watu wanaomtegemea iwapo hatajiandaa mapema kuanzia sasa, basi ni wazi kwamba zoezi zima la kutekeleza ibada hii ya Zakat Fitr litakuwa gumu kwake na kuna hatari ya funga yake kuingia dosari.

Hatari ya kuingia dosari inakuja kwa kuzingatia kwamba kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu na hadithi, Z a k a t F i t r n d i y o inayokamilisha utimilifu wa funga ya Ramadhani kwa mfungaji. Inaelezwa kwamba iwapo mfungaji hatatowa Zakat Fitr hatatoa Zaka hii, basi funga yake itakuwa inaning’inia kati ya mbingu na ardhi.

U k i a c h a Z a k a t Fitr, bado Waislamu wana utara t ibu wa kuwanunulia wapendwa wao mavazi mapya. Hii ni kutokana na mafundisho yetu kwamba ni sunna kwao kuvaa nguo mpya siku ya Eid.

Hivyo kwa kuzingatia hayo, ndio maana leo tunawakumbusha na mapema Waislamu kwamba wajiandae na mapema kutekeleza ibada hii muhimu ili kuleta wepesi kwao mara baada ya kuondoka Ramadhani.

Page 3: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

3 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Habari

‘Karume mpya’ acharukaMZEE Hassan Nassoro Moyo, maarufu kwa sasa ‘Karume Mpya’, amesema wakati ni huu wa kudai hadhi na mamlaka kamili ya Zanzibar kama dola.

K a t i k a k u t o a w i t o huo, akawataka vijana kupigania Zanzibar yao wala wasiogope bali hiyo iwe ‘Jihad’ yao kama yeye ambapo amejiwekea msimamo wa kuipigania Zanzibar hata kama hiyo itamgharibu kufukuzwa CCM.

“Leo vijana nakwambieni kwamba muda umeshafika na muda huu ndio wakati wake wa kuyasema haya msiogope.”

A m e s e m a , k w a k e Zanzibar kwanza kwani CCM imekuja baada ya nchi na muungano.

Akitoa historia ndefu ya nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar Mzee Moyo alisema kwamba viongozi na waasisi wa muungano walikuwa wamekubaliana baadhi ya mambo katika muungano mwaka 1970 baada ya viongozi wa Baraza la Mapinduzi kuhoji uendeshaji wa shughuli za Muungano na kutangaza hatua kadhaa ikiwemo ya kutaka Rais wa Zanzibar kujulishwa juu ya hali ya hatari inapotokea Tanzania.

A k i z i t a j a h a t u a nyengine zilizokubalika, Moyo alisema Baraza la Mapinduzi lilitaka kila upande wa Muungano ujitegemee kwa kila upande kuwa na jeshi lake la polisi, kuwa na mamlaka kamili juu ya masuala ya uhusiano wa kimataifa na pia pande hizo kila moja kuwa na sarafu yake.

Al i sema , baada ya v i o n g o z i w a B a r a z a la Mapinduzi wakiwa wamefuatana na Mzee Karume kutoa hoja hiyo mbele ya Mwalimu Nyerere, wakaambiwa muda wa suala hilo haujafika.

Akasema ikiwa wakati ule muda ulikuwa haujafika, basi sasa ni wakati wake.

“Alipoambiwa Mwalimu Nyerere basi akasema

Na Alghaithiyyah Zanzibar

muda haujafika, lakini leo vijana nakwambieni kwamba muda umeshafika na muda huu ndio wakati wake wa kuyasema haya msiogope”, aliwaambia vijana ambao walioalikwa katika mkutano huo wa waandishi wa habari.

Muasisi huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema yuko tayar i kurejesha kadi ya chama chake iwapo atalazimika k u f a n y a h i v y o h u k u akisisitiza kuunga mkono Muungano wa Mkataba.

A k i z u n g u m z a n a waandishi wa habari Mjini Zanzibar juzi Jumatano, amesema ataendelea kutetea msimamo wake wa kutaka Muungano wa mkataba kwa kuwa muungano uliopo kwa miaka 48 sasa umeshindwa kutatua kero zilizopo na kuleta matumaini kwa Wazanzibari.

“Jambo kubwa ni nchi, chama lilikuwa jambo la pili na kama viongozi wetu wa chama wanataka kutupeleka huko tukaeleze ms imamo wa chama, mimi nasema muungano umekuja kwanza na hivyo ndio ninavyojua mimi na huo ndio msimamo wangu lakini ikiwa wanatwambia ture jesha kadi , mimi nitakuwa tayari lakini siwezi kuacha nchi yangu ...nchi ilikuwa jambo la mwanzo”, alisiitiza Mzee Moyo.

Kauli hiyo ya Moyo imekuja siku chache baada ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai kuwataka wafuasi wote wa chama hicho kuheshimu sera ya chama ambayo ni serikali mbili kama ilivyo hivi sasa na kuwaonya wale wote ambao watakwenda kinyume na chama hicho.

Mbali ya kauli ya Vuai, Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mjini kilipitisha azimio la kuwataka baadhi ya Wabunge, Wawakilishi, M u w e k a H a z i n a w a Chama hicho Mansoor Yussuf Himid na Makamo Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar Amani Abeid Karume kuacha tabia ya kuhubiri sera za vyama vyengine.

Azimio hilo lililopitishwa

RAIS mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume

na wajumbe 400 lilisema viongozi hao wamekuwa na tabia ya kuunga mkono ms imamo wa ku taka mabad i l iko ndan i ya muungano msimamo ambao unakwenda kinyume na msimamo wa chama chao ambapo sera za chama cha CCM ni serikali mbili zenye mfumo uliopo ambapo masuala la muungano ni kushughulikiwa na sio kubadili mfumo.

Akitoa historia refu ya harakati zake za ukombozi mbele ya waandishi wa habari, Mzee Moyo alisema anashangazwa na kauli ya kuwanyamazisha wananchi wasitoe maoni yao kwa kisingizio cha kwenda kinyume na sera za CCM wakati suala la Muungano ni muhimu zaidi kuliko chama.

“Chama kimekuja baadae kwanza ilianza nchi na ukaja muungano, sasa

msiwazuwie watu kutoa maoni yao kwa kutwambia chama kinasema hivi au vile”, alisema Mzee Moyo huku akionesha uso wa kukasirika.

Mzee Moyo, aliyewahi kuwa waziri na kushika nyadhifa mbali mbali k a t i k a S e r i k a l i y a Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano alisema aliwataka vijana kuendelea kutoa maoni yao bila ya woga kwani kufanya hivyo ni kuendeleza kazi aliyokuwa akiifanya Mzee Karume kutetea nchi yake.

A idha Mzee Moyo ambaye ni miongoni mwa waasisi wa Mapinduzi na Muungano alisema chanzo cha Zanzibar kuibua madai hayo, yalitolewa baada ya Mwalimu Nyerere kuamuru kikosi cha jeshi kutoka Zanzibar kwenda katika shughuli za vita vya ukombozi wa Msumbiji

bila kumwarifu Rais wa Zanzibar jambo ambalo halikumfurahisha Mzee Karume.

Mzee Moyo atakuwa ni mwana CCM wa kwanza kukariri hadharani maneno ya Mzee Karume aliyosema dhidi ya Muungano juu ya mambo iwapo yatakwenda kombo.

“Mzee Karume alisema wazi muungano kama koti likikukera unalivua lakini pia Mzee Karume aliufananisha huu muungano na kanzu ambapo alisema unaweza kuivua”, alisisitiza Mzee Moyo ambaye alisema kutoa maoni ni moja ya uhuru na sera za chama chake.

A idha Mzee Moyo alikumbushia yaliomkuta Rais wa awamu ya pili ya serikali ya Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi pia hakufanya makosa aliotaka Muungano unaoendeshwa bila kuingil ia mambo ya Zanzibar na serikali nyingine inayoshughulikia masuala ya Tanganyika yasiyokuwa ya Muungano lakini akasema bahati mbaya nia hiyo ilikuwa amekwenda nayo peke yake bila ya kuwashauri wenzake.

“Sisi tulikaa kimya kwa sababu yeye kama kiongozi mkuu wa nchi akaona aende nayo peke yake kwa hivyo Moyo akaa kimya hakusema kitu lakini angetwambia sisi tungemuunga mkono”, alikumbushia.

Akitoa nasaha zake Mzee Moyo alisema huu sio wakati tena wa Chama Cha Mapinduzi kuwazuwia watu wasitoe maoni yao bali wanatakiwa kuwaachia watoa maoni yao kwa uhuru na uwazi ili kuunda muungano unaokubalika na wenye maslahi kwa nchi zote mbili Tanyanyika na Zanzibar.

Hata hivyo Mzee Moyo aliwakemea sana viongozi wenye mawazo yao na kukataa kupokea mawazo ya wenziwao na kusema kwamba nchi hii sio ya CCM na kila mmoja awe huru kutoa maoni yao na kuwataka viongozi wa CCM wavumilie juu ya

Inaendelea Uk. 4

Page 4: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

4 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Habari

‘Karume mpya’ acharukaInatoka Uk. 3maoni yanayotolewa.

“Mimi nasema suala la Muungano haliwezi ku geu zw a l a Chama , ….chama kumetoa mchango kwa kuunga mkono uamuzi wa serikali mbili –Tangayika na Zanzibar kuungana, sasa mnapotwambia tunakiuka sera za chama ...chama gani? Alaa mnataka kuwaziba watu midomo bwana”, alisema Moyo.

Aliwaambia viongozi wa CCM wasioweza kutoa kasoro ndani ya muungano na kukataa kutoa muundo wa muungano wajue kuwa wanajidanganya wenyewe na kuwadanganya wenziwao.

Mzee Moyo alisema huwezi kuendesha Nchi kwa sera ya Chama fulani na kudai kwamba Muungano huu hawendi kwa sera za Chama cha Mapinduzi.

Mzee Moyo alifahamisha kuwa Watanganyika walifika pahala na wao wakadai serikali yao lakini chama cha Mapinduzi kiliwazuia.

“Lak in i na wambia Watanganyika kuwa muda wao ndio huu umefika na wao wadai taifa lao”, alisema Mzee Moyo.

Sambamba na hilo Mzee Moyo alitumia fursa hiyo kwa kujibu mapigo kwa wale wote ambo walimwambia yeye amekuwa msaliti wa Chama cha mapinduzi.

Mzee Moyo alisema anachokifanya yeye ni kukubali mabadiliko katika taifa ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima kwa vizazi vipya.

Alisema kuna viongozi w e n g i w a n a u c h o y o na kudai kwamba yeye anachokiangalia ni Hadhi ya Zanzibar Kitaifa na kimataifa.

Akijibu hoja za baadhi ya wana CCM waliosema kwamba yeye sio mwana mapinduzi, Mzee Moyo a l i s e m a “ K u n a w a t u ambao wanajifanya ni wana Mapinduzi wajue wanachokizungumza na waelewe mimi ni nani katika Kupigania uhuru wa Nchi hii, kuna watu wanadhani mapinduzi yalitayarishwa na watu wa kumi nne hamna lile lilikuwa ni kundi la mapambano lakini

lilitayarishwa na Wazanzibar wote”, aliongeza.

“Kuna Mtu anaitwa Ali Ameir mwambieni asema anapozungumza kwa wewe ul ipindua elewa kuwa haya yote yalitayarishwa kwa muda usiseme jambo usilolijua”, aliongeza Mzee Moyo.

Alisema Mzee Karume alimuamini sana na sehemu nyingi alikuwa akimsogeza yeye na kutaka ushauri kwake na kuhoji kwani wakati huo hakukuwa na vijana ambao angeweza kumsaidia Mzee Karume.

“Mimi nikawa championi wa ASP hapa Zanzibar baada ya hapo nikaenda Urusi ambapo vyama vilikwenda kuzungumzia uhuru wa Zanzibar na huko nikapigiwa simu niende London mimi ni l ikuwa observer wa Kwanza na hayo yote ni Mzee Karume alitaka iwe hivyo sasa wajiulize why mimi wasiwe wengine”, alihoji Mzee Moyo.

Hakuna adhabu atakaegoma kuhesabiwaInatoka Uk. 2

msimamo huo ni kutokan na kuzagaa kwa takwimu zisizo rasmi.

“Sasa hali hii tukaona Waislamu tuiombe Serikali iweke k ipengele cha Dini katika Sensa hii, ili ukweli ujulikane. Sensa ya mwisho ilionyesha wazi, hapakutokea vita kubwa ya Waisalamu kwa Waislamu tukapungua, l e o t u m e p u n g u a j e , tunataka kipengele cha dini kirejeshwe.” Alisema Sheikh Kilemile.

Kwa upande wake B w. N a s s o r o , a l i y e mwanasheria wa Umoja wa wanazuoni hao, alisema, Waislamu wasilazimishwe kuhesabiwa kwa kutishiwa sheria.

A l i s e m a , i k i w a itategemewa sheria ili kuwaingiza Waislamu k a t i k a S e n s a , u p o uwezekano mkubwa zaidi wa kupata takwimu zisizo sahihi kwa sababu wapo watu ambao watakuwa tayari kufungwa kuliko kuhesabiwa kwa nguvu.

“Mkipuuza haya ya

Waislamu hata kama ni wachache, je matokeo hayo mtakayo tangaza yatakuwa sahihi? Mkitoa majibu mfano Tanzania kuna watu milioni 50, lakini watu elfu kumi hawakuhesabiwa hiyo itakuwa sensa ya namna gani.” Alisema na kuhoji.

Wa k a t i h u o h u o , Kamishna wa Sensa Hajjat Amina Mrisho, amesema madai ya Waislamu ya kuingiza kipengele cha Dini katika Dodoso za Sensa atayafikisha kwa Rais Jakaya Kikwete, ili kuangalia uwezekano wa kuwepo suala hilo.

Maamuzi hayo ya Tume ya Taifa ya Takwimu, y a m e k u j a b a a d a y a kukutana na Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, na kujadiliana kwa kina juu ya suala la Waislamu kushiriki katika zoezi la Sensa.

“Hayo yote tumeyasikia ninachoweza kusema, sisi hapa hatuna mamlaka nayo tutayapeleka nitayapeleka kwa Mh. Rais (Kikwete) ili

ajue nini kinachoendelea.” Alisema Hajjat Mrisho.

A l i s e m a , w a z o l a M a s h e k h k u t a k a kuchapishwa karatasi, m a a l u m i l i i w e kama k iamba tan i sho kinachohusu Dini za watu, atalibeba kama hoja na kulifikisha katika ngazi za juu, kama ambavyo w a n a p o k e a m o n i mengine.

“Kuweka kipande cha karatasi kama mlivyoshauri siwezi kuamua mimi, hayo ni lazima tuyapeleke k w a w a n a o h u s i k a , kama ambavyo mengi tumekutana nayo na hili pia tutalipeleka.” Alisema.

Alisema, endapo wakuu wao watataka ufafanuzi zaidi atawataarifu Masheikh hao ili waweze kukutana nao, huku akiwatoa hofu kwamba kuyafikisha ni wajibu wake.

Kwa upande wake Kamishna wa Sensa kutoka Zanzibar, Bw. Ameir, alisema Wanazuoni wamewapa hoja za msingi ambazo watazifanyia kazi ambapo kutokana na kuwa hawana maamuzi ya mwisho, watayafikisha

katika ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi.

Alisema, hoja hizo wataz i f ik isha haraka katika kikao chao Agosti 4, katika kikao chao cha kamati kuu ya Sensa, kama walivyozipokea kwa uzito wake.

“Sidhani kama watakuwa wakaidi kiasi hicho cha kush indwa kue l ewa , mmetupa na kujenga hoja muhimu ambazo tumezikubali. Lakini sisi hatuna maamuzi nayo itabidi tuyapeleke juu na bahati nzuri Tarehe 4, tutakuwa na kikao cha kamati kuu ya Sensa, hili swala tutakwenda k u l i z u n g u m z a k a m a tulivyoyapokea tutajenga hoja nao wenzetu waione ho ja h iyo” . Al i sema Kamishna Amir.

Akielezea msimamo wa Waislamu Zanzibar, juu ya Sensa ijayo alisema, w a n a u n g a m k o n o msimamo wa Waislamu wa Bara, kutaka kipengele cha Dini kutiwa katika Sensa, pamoja na kuwa wao hawana shaka na Takwimu za kidini Zanzibar.

MZEE Hassan Nassoro Moyo

Page 5: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

5 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Kimataifa

UMOJA wa Ulaya EU umekataa pendekezo la Israel la kutaka Hizbullah kuorodheshwa katika orodha ya makundi ya kigaidi.

Umoja huo umekataa wito wa Waziri wa Mambo y a N j e w a U t a w a l a hasimu wa Israel Avidgor Lieberman, a l iyetaka Wanaharakati wa Hizbullah ya Lebanon waorodheshwe

EU wakataa kuorodheshwa Hizbullah kama kundi la kigaidi

katika orodha ya vikundi vya ugaidi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus Erato Kozakou-Marcoullis, ambaye nchi yake inashikilia uenyekiti wa mzunguko wa EU amesema, hakuna muafaka miongoni mwa nchi zote za Ulaya kuhusu kuiweka Hezbollah katika orodha ya mashirika ya kigaidi.

Kozakou-Marcoullis

amesema Hizbullah ni shirika lenye mrengo wa kijeshi na ambalo pia linashiriki kikamilifu katika siasa za Lebanon.

Utawala dhalimu wa Israel umekuwa ukieneza tuhuma zisizo na msingi d h i d i y a H i z b u l l a h . Propaganda hizo za Israel zinatokana na hali halisi kwamba, utawala huo umekuwa ukipata pigo

mara kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa Hizbullah a m b a o w a m e k u w a kikwazo kikubwa katika harakati zake za kidhalimu mashariki ya kati.

P i g o k u b w a z a i d i u l i l ipa ta u tawala wa Kizayuni wa Israel kutoka Hizbullah ni katika vita vya siku 33 vya Israel dhidi ya Lebanon mwaka 2006.

C H I N A i m e z i d i s h a kiwango cha kunununua mafuta kutoka Iran kwa asilimia 17 hivyo kufikia tani milioni 2.6 katika kipindi cha mwezi Juni mwaka huu, licha ya kuwepo vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi kuzuia ununuzi wa mafuta ghafi kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Idara kuu ya forodha ya China imetangaza kuwa nchi hiyo ambayo inahesabiwa kuwa ni ya pili kwa ustawi wa uchumi duniani mwezi Juni mwaka huu, kwa siku ilinunua mapipa ya mafuta yasiyopungua 635,000 kutoka Iran.

C h i n a a m b a y o n i mnunuzi namba moja wa mafuta ya Iran imepinga vikwazo vya Marekani dhidi ya Tehran na kueleza kuwa ununuzi wake wa mafuta ghafi kutoka Iran ni halali kikamilifu.

Marekani na Umoja wa Ulaya zimeidhinisha vikwazo vipya dhidi ya sekta za mafuta na fedha ili kuzizuia nchi nyingine duniani kununua mafuta ya Iran au kujihusisha na miamala ya kifedha na benki kuu ya Iran.

NAIROBIS e r i k a l i y a K e n y a imeidhinisha sheria mpya inayosema kuwa shule za Kiislamu zitaingizwa katika mfumo rasmi wa masomo nchini Kenya.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation toleo la Julai 24, mfumo wa shule za Kiislamu ujulikanao kama Duksi utaingizwa katika masomo rasmi ya shule katika maeneo yenye Waislamu wengi nchini humo.

M f u m o w a D u k s i u m e k u w a u k i t u m i w a na jamii ya Wakenya wenye asili ya Somalia na unajumuisha kuhifadhi Q u r ’ a n i n a m a s o m o mengine ya Kiislamu.

Katibu wa Kudumu katika Wizara ya Elimu Profesa Geroge Godia, alisema shule hizo za Kiislamu zitapata msaada rasmi wa

Serikali ya Kenya kugharamia madrasa za Qur’ani

kifedha kutoka mfuko wa serikali.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa muswada wa sheria kuhusu Elimu ya Msingi Mwaka 2012, ni jukumu la serikali kuwalipia karo wanafunzi wa madrasa za Kiislamu na pia kuwapa chakula wakiwa katika madrasa.

Waziri wa Elimu wa Kenya Mutula Kilonzo, amesema uamuzi huo wa serikali unaenda sambamba na katiba mpya pamoja na mpango wa miaka 20 wa maendeleo nchini Kenya.

Wanazuoni wa Kiislamu wakiongozwa na Sheikh Mohammad Khalifa wa Baraza la Maimamu na Wahubiri, ameipongeza hatua hiyo ya serikali.

Aidha ametoa wito kwa serikali kuidhinisha rasmi sheria ya kuwapa haki wasichana wa Kiislamu kuvaa hijabu. RAILA Odinga, Waziri Mkuu wa Kenya.

Baraza la EU lapinga sheria zinazowalenga WaislamuKAMISHNA wa Haki za Binadamu katika Baraza la Ulaya Nils Muižnieks amezitaka serikali za nchi za Ulaya kufuta sheria zote na hatua zinazowalenga Waislamu kama sheria inayopiga marufuku vazi la hijabu nchini Ufaransa.

N i l s M u i ž n i e k s

amesema kuwa serikali za Ulaya zinapaswa kufuta sher ia na hatua zote zinazowalenga Waislamu na kup iga marufuku ubaguzi unaolenga dini au itikadi za watu katika nyanja zote.

Amesisitiza kuwa vyama vikubwa katika nchi za Ulaya vimetumia hisia za

khofu zilizoenezwa dhidi ya Waislamu kuunga mkono sher ia z inazowabana wafuasi wa dini hiyo.

Ametolea mfano nchi za Ubelgiji na Ufaransa ambako sheria za nchi hizo zinawatoza faini wanawake wa Kiislamu wanaovaa nikabu katika maeneo ya

umma. Kamishna wa Haki za

Binadamu wa Baraza la Ulaya anasema Waislamu barani humo wanakabiliana na aina mbalimbali ya ubaguzi na ukatili.

Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na Wakala wa Umoja wa Ulaya wa

Haki za Binadamu pia ulibaini kuwa thuluthi moja ya Waislamu barani humo wamekumbana na vitendo vya kibaguzi katika miezi 12 iliyopita na kwamba robo ya Waislamu waliohusishwa katika uchunguzi huo wametiwa nguvuni na vyombo vya usalama mwaka uliopita.

China yazidisha ununuzi wa mafuta ya Iran

Page 6: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

6 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala/Tangazo

S H U K U R A N I z o t e anastahiki Mwenyezi Mungu na zikatosha na amani z iwaf ik ie w a j a w a k e a m b a o waliochujwa kisha baada ya utanguliza huu kwa hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaumba w a t u t o f a u t i , n a akawauumbia kila mmoja akil i akafikiria kwa akili hiyo. Na akampa mapendekezo ambayo anapata maamuzi ndani ya akampa uwazo wa kuyamiliki matakwa tofauti.

K w a m i s i n g i h i y o huchagua watu wenyewe wanayoyataka na lau kama angetaka Mwenyezi Mungu kuwaumba watu wote wawe waumini, basi angewaumba hivyo katika tauhidi (Mungu Mmoja) na imani kama alivyowaumba malaika. Ambao hawakiuki a m r i z a M w e n y e z i Mungu na wanafanya wanayaamr i shwa tu . Lakini Mwenyezi Mungu ameviumba viumbe vyake na kuvitofautisha kwa matakwa yake na kuchagua yeye mwenyewe. Yeye ndiye anayepitisha marejeo ya nafsi yake.

Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu mwenye kuongoka amejiongoa y e y e m w e n y e w e n a a t a k a y e j i p o t e z a amejipoteza mwenyewe) Surat Israi. Amesema tena anayetaka na Aamini na anayetaka na Akafuru) Surat Al-kahfi.

M w e n y e z i M u n g u a m e m p a b i n a d a m u m a t a k w a i l i a p a t e maamuzi maalum ya namna ya binadamu huyu

Kutofautiana dini kwa watu hakuzui kuishi vizuri na kusaidiana kwa manufaa

Na SHEIKH ABUBAKAR SULEIMANI

ndio mtu lau angetaka kuwalazimisha juu ya dini moja katika kuiamini bali ame acha uhuru. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu (Lau angetaka Mola wako basi angefanya uma wote ni mmoja na hawaachi kuwatofautisha isipokuwa yule atakaye mrehemu Mola wako na hivyo ndivyo alivyo waumba. Surat Huud.

Amesema tena “Lau kama angetaka Mola wako wangeamini watu wote duniani hivi wewe unawachukia watu hadi wawe waumini.” Surat Yunus. Na kwa kuwa M w e n y e z i M u n g u mtukufu amewaumba watu katika dini tofauti, basi hapana budi waendeane wao kwa wao ni wajibu kwa Waislamu kuishi na wanaotofautiana nao dini. haifai kuwalazimisha wafuate dini yetu.

Na kama ilivyokuwa h a i f a i k w a y e y o t e kutulazimisha mmoja sisi katika kuacha dini yetu au kuzuia katika kumuabudu Mola wetu. Hii ni kuonyesha wingi wa dini huu ndio unaokiri na kuukubali Uislamu na anatakiwa na Muislamu aishi vizuri na wenziwe hata kama kuna tofauti kati yao kidini kwani haya yanapatikana kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu maamuzi yake na kwa hivyo basi amewaamrisha Mwenyezi Mungu waumini wawafanyie mema wale wasio Waislamu kwa sharti tu kuwa hawawa dhulumu.

Amesema Mwenyezi M u n g u M t u k u f u (hawakatazini Mwenyezi Mungu juu ya wale ambao hawakupigeni vita katika dini na wala hawakutoeni m a j u m b a n i m w e n u

kuwafanyia wema na usawa kwao hakika Mwenyezi M u n g u a n a w a p e n d a wafanyao usawa) Sura Mumtahinah.

Na vile vile yamepatikana maendeleo ya Kiislamu na yakakua kwa njia ya kusaidiana pamoja na wasio wais lamu kwa kupata faida kwa heri zao na kubadilishana manufaa yao. Na kuna dini nyingine ambazo zimepanuliwa na Uislamu na zikaishi karne nyingi chini ya kivuli cha Uislamu wao ndio watawala wa Ulimwengu wao ndio wenye nguvu za mwanzo katika dunia walikuwa na uwezo wa kulazimisha dini lakini haikufanya hivyo kamwe.

Na wakaishi na wale wasio Waislamu watu wa mikataba ya kujikomboa na wao walikuwa na mambo yao na Waislamu walikuwa na mambo yao kwani wao

walikuwa na makanisa yao na misalaba yao na kengele zao na mavazi yao maalumu (Fumu zao) kwani kila binadamu ana uchuguzi wake kwa kuwa umemuachia dini yake na ni haki yake kuishi na dini yake na ainue alama zake na atekeleze wajibu wake.

H a k i k a m i o n g o n i mwa ajabu ya msamaha wa Uis lamu kwamba h a u m l a z i m i s h i m t u y e y o t e k u a c h a k i t u k i l i c h o r u s h u s i w a i l i k u w a p e n d e z e s h a Waislamu.

Uis lamu umepanda imani na uelewa na fikra z inazomfanya aweze kuishi kwa kusamehe kwa kukata mitazamo ya wasio Waislamu. Kwani yeye Muslamu anaishi na watu wote kwa kuwa ni viumbe ambavyo amevitukuza Mwenyezi Mungu naye

ni hivyo hivyo akiamini kuwa hesabu ya watu wote ni huko akhera (kiama) a m e s e m a M w e n y e z i Mungu Mtukufu (Na kwa hivyo lingania na uwe na msimamo kama ulivyo amrishwa na wala usifuate anasa zao na sema nimeamini kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika kitabu, Mwenyezi Mungu ni Mola (Mola) wetu na Mola wenu tuna sisi matendo yetu na nyinyi mna matendo yenu hakuna hoja kati yetu na kati yenu. Mwenyezi Mungu atatukusanya kati yetu sote na kwake yeye tu ndio marejeo (Marudio)

Mwenyezi Mungu ndiye muwezeshaji Mwenyezi Mungu mpe rehema mtume (S.A.W) na shukrani zote anastahiki mwenye Mungu Mola wa viumbe wote.

TAMPRO JOB CENTRE

SEMINA YA MAFUNZO YA AJIRA Jumuiya ya Wataalamu wa Kiislam Tanzania (TAMPRO) kupitia Kituo chake cha Kazi na Ajira

kinawatangazia Semina ya Mafunzo ya Ajira na Ujasirimali ili kutoa ujuzi, miongozo na kuwajengea uzowefu na uwezo katika soko la ajira, kwa kuzingatia mambo halisi yahusuyo ajira na kazi kwa kutumia wabobezi wa wanaoshughulikia masuala hayo.

Walengwa: Wahitimu na wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya Juu na wenye kuhitaji.Siku: Jumapili terehe 12/08/2012Muda: Saa 3:00 asubuhi - 10:00 jioniMahala: Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam

Mada: 1. Mbinu za kutafuta na kupata ajira: CV, Utafutaji, Uombaji na Usaili2. Changamoto kwa waajiriwa wapya: Kuchelewa kuajiriwa, Kushindwa kazi, Kupoteza ajira3. Fursa za Asasi za Fedha za Kiislam katika Kujiajiri: Benki na SACCOS, Jinsi ya kuanzisha

Mradi ukiwa huna kitu. (AMANA bank, KCB Bank, Stanbic Bank, TAMPRO SACCOS, Kutaibah SACCOS na Hajj Trust SACCOS watakuwepo)

Ushiriki: Shilingi 10,000/= kwa mtu mmoja (Kwa ajali ya mafunzo na cheti).Muhimu: Washiriki watapatiwa vyeti. Taarifa za washiriki zitahifadhiwa kwa ajili ya kuunganishwa na waajiriKujisajili: Ili kujisajili piga 0716776226, 071352114 au fika TAMPRO Makao Makuu, Magomeni

Usalama, jirani na Halmshauri ya Kinondoni. Wahi kuijiandikisha kwani nafasi ni chache.Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0716776226, 0778776226, 0713521147 au info@tampro.

org

Sharif M. H.MRATIBU MAFUNZO

P.O. BOX 72045, Dar es Salaam, TANZANIA. TEL+255 0655 654900, +255 713 731300, +255 754261600. Email: [email protected],

Web: www.tampro.org

Page 7: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

7 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Habari

RC Arusha azidi kukoroga SensaMKUU wa Mkoa hamiliki uhai na mauti wala Pepo na Jahannamu kwa hiyo asitishe watu.

Hayo ni maoni ya baadhi ya Masheikh mashuhuri jijini Arusha kufuatia kitisho kilichotolewa na Mkuu wa Mkoa huo Bwana Magessa Mulongo.

Mkuu huyo wa Mkoa a l i t oa k i t i s ho h i cho b a a d a y a M a s h e i k h w a n a o k u b a l i k a k w a Waislamu na kuheshimiwa na Waislamu jijini hapo kwamba ndio viongozi wao wanaowasikiliza kusema kuwa, hakuna Muislamu atakayehesabiwa mpaka m a d a i y a Wa i s l a m u yasikilizwe.

Hiyo ilikuwa katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Julai 31, 2012 ambapo mgeni rasmi na mzungumzaji mkuu alikuwa Mkuu huyo wa Mkoa. Kikao kilihusisha Masheikh na Maaskofu.

A l i p o k a r i b i s h w a kuongea, Mkuu huyo wa Mkoa alieleza umuhimu wa sensa ya watu na makazi ambapo alitaka pia kupata kama maoni ya viongozi wa dini.

Alikuwa Sheikh wa B A K WATA S h e i k h Shaabani Juma aliyeanza kuongea akisema kuwa anaunga mkono sensa kufanyika.

Kauli yake ikapigiwa makofi mengi kwa furaha n a s h a n g w e k u b w a kutoka kwa Maaskofu hali iliyowafanya hata viongozi wa serikali mkoa wal iokuwepo kubak i wakistaajabu.

Hata hivyo, shangwe hiyo ilizimwa na Mwakilishi wa Shura ya Maimamu Mkoa wa Arusha Sheikh Mustafa Kiago aliyesema kuwa pamoja na uzuri wa sensa, lakini sensa ya mwaka huu Tanzania haitafanikiwa iwapo madai ya Waislamu ya kuwepo kipengele cha dini hayatasikilizwa.

A k a s e m a , k i t e n d o cha Television ya Taifa ( TBC1 ), kalenda za serikali zilizotolewa katika ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania kutoa takwimu z inazoonyesha kuwa Wakristo ni wengi kuliko Waislamu, inadhihirisha kwamba ipo haja ya sensa

ya watu na makazi kuwa na kipengele cha dini ili kuondoa utata uliopo.

Pia Sheikh Mustafa aliongeza kuwa kwenye sheria ya mwaka 2002 kipengele cha 15,17 na 32 kipengele cha dini kinaruhusiwa kuingizwa kwenye dodoso la sensa.

Baada ya maoni hayo mkuu wa mkoa alijibu kuwa sheria hiyo ya 2002 bado haijaanza kutumika.

Katika kukazia hoja yake, Sheikh Mustafa alisema kuwa kuna sheria ya Umoja wa Mataifa inayoruhusu watu kuhesabiwa kwa mujibu wa dini zao.

Mkuu huyo wa mkoa akajibu kuwa Tanzania haifanyii kazi sheria ya Umoja wa Mataifa.

Baada ya maoni hayo Mkuu huyo wa mkoa a l iwaambia v iongozi wa dini kuwa kuna watu wanataka kumsababishia apate madhambi.

Akiwataja watu hao alisema kuwa ni Imamu wa Msikiti wa Ngarenaro, Sheikh Mahamudu, Imamu wa Msikiti Mkuu, Sheikh

Hambali na Imamu Msikiti wa Quba, Sheikh Jafari Lema.

“Wapelekeeni salamu zangu kuwa mimi ninayo madhambi mengi sana, kwa n in i wanatafu ta kuniongezea mengine?”

Alisema Mkuu huyo wa Mkoa bila kufafanua na haikuweza kufahamika n i kwa n in i a l iamua kutowaalika Masheikh na Maimamu hao i l i a z u n g u m z e h o j a n a shutuma zake wenyewe wakiwepo.

K u t o k a n a n a mtafaruku ul io tokea , kikao kilimalizika bila muafaka huku Sheikh wa Bakwata akiibuka shujaa kwa kushangil iwa na Maaskofu japo mwisho wa yote serikali haikupata ilichotarajia.

Akitoa maoni yake, Sheikh Hambali amesema kuwa anashangazwa na kauli ya Mkuu wa Mkoa na ni vyema Mkuu huyo akafafanua anakusudia kuwafanyia uovu gani

Masheikh wa Arusha hali itakayomwongezea madhambi.

“Ni vizuri Mkuu huyo wa Mkoa akafafanua kauli yake hiyo kwani sisi tayari tumeona ni vitisho dhidi yetu. Hivi mtu akikuambia wewe una t aka mimi nipate madhambi tafasiri yake hasa ni nini? Tena anakutumia salamu.”

S h e i k h a m e s e m a kuwa yeye katika haki hamuogopi kiumbe yeyote, bali anamuogopa Yule ambaye ameshikilia uhai wake, uhai wa mwenye kututisha, na uhai wa kiumbe chochote duniani ambaye ni ALLAH.

Adha anamuuliza Mkuu huyo wa Mkoa kwamba kama angesikia Askofu Pengo anadai kipengele cha dini kiwekwe katika dodoso la sensa angemtolea kauli za vitisho?

“Tunamwambia sisi hatumuogopi hata kidogo kwa mfano wa chembe ya hardali na sisi tunatuma sa l amu kwake kuwa

Muislamu kumuogopa kiumbe ni dhambi kubwa kuliko dhambi zote. Ni shirki.”

I m a m u H a m b a l i anaifananisha kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa na ile ya Waziri Steven Wasira aliyoitoa huko Dodoma kwa kuwaambia Waislamu kama hawaelewi , maaskofu wao wanamwelewa. Jambo ambalo ni dharau kubwa, basi serikali ikafanye sensa na hao wenye kuelewa, i s ihanga ike na wa tu wasiotaka kuelewa hata wakifahamishwa.

Katika kuhitimisha maoni yake, Imamu Hambali amewaasa Waislamu nchini wasimame imara kutetea haki yao bila kumuogopa yeyote kwani amani ya nchi hii ilipiganiwa na Waislamu mpaka uhuru ukapatikana.

Kwa upande wake S h e i k h M a h a m u d u Nyambwa amesema kuwa suala la kutishana halipo kwani kinachodaiwa hapa ni haki. “Siogopi vitisho vyake”, alisema Sheikh Mahamudu.

S he ikh M ahamudu amesema yeye kama Sheikh wa Wilaya ya Arusha , ameshaweka msimamo kwa Waislamu kama kiongozi wao kuwa hakuna kuhesabiwa mpaka pawepo na kipengele cha dini katika dodoso la sensa.

Kuhusu suala la Kadhi, Sheikh Mahamudu alisema mpaka sasa Waislamu hawajapata Kadhi hivyo w a t a e n d e l e a k u d a i Mahkama ya Kadhi ambayo itatambulika katika Sheria za nchi na kuwezeshwa uendeshwaji wake na utekelezaji wa hukumu na maamuzi yake.

K i l i c h o f a n y w a n a Mufti wa Bakwata ni kichekesho kwani Kadhi hawezi kupatikana kabla ya Mahkama yenyewe kuwepo.

Akasema, wala serikali i s i j i d a n g a n y e k u w a imej ivua dh ima kwa ku i tumia BAKWATA kama muhuri wa kuzima madai ya Waislamu kuhusu Mahkama ya Kadhi.

Na Mwandishi Wetu, Arusha

JOPO la Maulamaa. Safu ya mbele ktoka kushoto Maalim Bassaleh, Sheikh Mohamed Issa na Sheikh Imran Kilemile.

Page 8: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

8 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala

PAMOJA na kwamba S e r i k a l i k a m a v i l e inaonekana kutia pamba masikio huku ikijaribu kui tumia BAKWATA, kama njia ya kuwalainisha Wa i s l a m u k u s h i r i k i katika Sensa ya Watu na Makazi, lakini ukweli ni kuwa hali mitaani ni tete na Waislamu wanasisitiza kuwa hawatoshiriki zoezi hilo.

Je, wadau katika kitengo hicho cha Taifa cha Takwimu wanasemaje juu ya hatua ya Serikali kufumbia macho msimamo huo na wana mtazamo gan i ku fa t i a msimamo wa Waislamu na je ni kweli hakuna umuhimu wa kuingizwa kipengele cha Dini katika Sensa, na kwa nini iliondoshwa.

An nuur, ilipata fursa ya kuongea na Meneja wa Idara ya Mazingira na Uchambuzi wa Takwimu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, aliyejitambulisha kwa Majina ya Sango Abas Simba, aliye bobea katika taaluma ya Takwimu, watu na maendeleo, kwa ujumla ali toa maoni yake kwa kina na uwazi na jinsi gani anavyoliangalia suala hili.

Katika mahojiano haya, Bw. Simba, awali ya yote a l i anza ku toa pongez i kwa viongozi wa Dini ya Kiis lamu wal iochagiza Serikali kutaka kipengele cha DINI kiwemo katika dodoso la kuhesabia Sensa ya Watu na Makazi, japokuwa haungi mkono msimamo wa kususia uandikishaji wake kwa sababu ambazo atakazo zianisha katika ujumla wa maoni yake.

Anasema, amefarijika kupata fursa hii aliyoiita kama ‘malumbano ya hoja’ ambayo ilianzishwa na viongozi wa dini ya Kiislamu baada ya TBC (Televisheni) kutangaza idadi ya watu kwa kuzingatia dini zao. Alidai, ataeleza kwa kina kitaalamu suala hili baada ya wachangiaji wengi wanaopinga suala la dini kuwemo kwenye dodoso la sensa ya watu na makazi, waelewe umuhimu wake.

K a u l i y a R a i s J a k a y a Kikwete juu ya Sensa

Bw. Sango anasema, kauli ya Mheshimiwa Rais Kikwete, al iyoitoa Ji j ini Mbeya, imetonesha donda la umakini wa watendaji wake kutiliwa shaka kwani inamkumbusha sakata la gari la wagonjwa la Loliondo kutaka kupelekwa Ngorongoro.

“ W a s h a u r i w a k e wamempotosha Rais wetu kwa kuwa upo ushahidi wa kimaandishi pamoja na

Tujuane tusidhulumiane

vitabu vya Sensa ya watu vilivyoainisha Watanzania kwa kufanya uchambuzi wa kina si tu kwa kuangalia Dini kwa ujumla bali kwa kuainisha dini kutokana na madhehebu yao kama vile Wakatoliki, Waanglikana, Walutheri, Shia, Suni, na wasio na Dini”. Alisema.

Mbali na dini, Bw. Sango anasema, maswali yaliyohusu kabila na rangi au utaifa yalikuwepo kwenye Sensa hadi kufikia mwaka 1967 (Rejea Ripoti ya Sensa ya watu na makazi mwaka 1967).

Bw. Sango mwenye Digrii ya elimu ya watu (M. A. Demography) anahoji, “Hivi ni lini Watanzania wataacha kuwa na majibu mepesi katika kuyaendea maisha ya Watanzania?”

Anasema, inasikitisha kuona wanasiasa wetu na wasomi wakubwa wa mambo ya Uchumi/Mipango na Elimu ya Watu (Demography) kukaa kimya katika suala muhimu kama hili kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu.

Anaain isha kwamba, haiingii akilini kuwa viongozi wetu na wasomi hawa hawajui suala la Utamaduni – “ C u l t u r e ” a m b a m o ndani yake kuna kipengele cha Imani, miiko, lugha, nakadhalika (beliefs, ethics, language, etc) hivi ni moja ya viashiria vya watu chenye kupewa umuhimu mkubwa

katika kupanga mipango ya maendeleo na kutoa maamuzi ya kisera au kiutendaji.

Ukimya huo wa wasomi wa fani hiyo anauelezea kuwa unaleta maswali mia na pengine ndiyo chimbuko la mgawanyo mbaya wa mapato ya Serikali, ajira na huduma za jamii na hata baina ya makundi ya watu hapa nchini. Kwani haitoshi kusema hivi tu, bali wanafikia kumdanganya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, eti hatujawahi kuwa na swali la Dini katika Sensa zilizopita!!

A n a s e m a , y e y e n i miongoni mwa Watanzania wa l iobaha t ika kusoma masuala ya Takwimu na Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadae kusoma masuala ya Watu na Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Botswana kabla ya kusoma elimu ya watu (M. A. Demography) degree ya pili. Katika mafunzo hayo walifundishwa mfumo (new Concept) mpya wa kupanga mipango kwa kushirikisha viashiria vya watu (Integrating Population Variables into Development Plans). Aidha, mafunzo hayo yaliwakumbusha mifumo mbalimbali itumiwayo na nchi zenye kufuata sera ya Ujamaa na Ubepari.

S a b a b u z a k u o n d o a kipengele cha Dini

Kwa kifupi alifafanua kwamba, mfumo wa Ujamaa

ndiyo ulipelekea kuondoa kipengele cha utamaduni katika kupanga mipango na kutoa maamuzi ya kisera na kiutendaji. Uliaminisha wananchi kuwa watu wote ni sawa wenye utamaduni mmoja, miiko aina moja na lugha moja. Kwao wao mtawanyo wa wananchi kwa kufuata utamaduni (Dini) uliondolewa (rejea Lenin na Mao ideologies). Hali ilikuwa tofauti katika mfumo wa Kibepari, utambuzi na uzingatiaji wa Utamaduni uliendelea kuwepo katika utendaji wa Serikali zao.

Kwa maana hiyo Bw. Sango, alisema katika mfumo wa Kibepar i , mipango ya Maendeleo, utoaji wa maamuzi ya k i se ra na kiutendaji ulizingatia pamoja na viashiria vingine vya watu, suala la utamaduni kwa maana ya dini, miiko na lugha vilipewa nafasi kubwa.

Al i to lea mfano nchi kama Uingereza kwamba, wametoa fursa ya kisheria kwa Waislamu kuwa na Mahakama za kidini, sheria za ruhusa ya uanzishaji wa shule zinazofuata miiko ya dini zinaruhusiwa. Hali iko hivi hata Italia na ushahidi ni kukataliwa kupingwa marufuku vazi la Hijabu na Waziri wa Utamaduni wa nchi hiyo.

“Nichukue fu r sa h i i kuwakumbusha wasomaji na Watanzania kwa jumla kuwa mifumo yote hii tumekwisha itumia hapa Tanzania Bara kabla na baada ya Uhuru, mfumo wa Kibepari ulitumika

kabla ya Uhuru na baada ya uhuru hadi mwaka 1967”.

Ni katika kipindi hiki ana th ib i t i sha kwamba, mipango ya maendeleo na maamuzi yalifuata pamoja na mambo mengine, utamaduni kwa maana ya dini, mila na rangi za wananchi. Hivyo taarifa juu ya dini, kabila na rangi za watu zilizingatiwa (Rejea Taarifa za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 1948, 1958 na 1967).

Anaweka wazi kwamba, Mabadil iko ya Sera ya Maendeleo kutoka Ubepari na kufuata Sera ya Ujamaa na Kujitegemea iliyofanyika mwaka 1967 ilileta dhana ya UMOJA kwa lengo la kuyaunganisha makundi ya watu kuwa kundi kubwa moja la “WATANZANIA” wenye utamaduni mmoja yaani Ujamaa na Kujitegemea wakiwa na lengo la kujenga Utaifa badala ya makundi mbalimbali yenye mila, dini na rangi tofauti. Kuanzia hapo suala la utamaduni l ikaondolewa, mipango y a m a e n d e l e o i k a w a inawajumuisha Watanzania wote, zikaandaliwa sera za kijumla na kutoa maamuzi ya kijumla tu.

M k a k a t i w a w a k a t i huo ukawa kuinua hali ya maisha kwa kufanikisha ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira, kujenga usawa wa kiuchumi na kuwapatia wananchi mahitaji ya msingi (UN, 1986). Kwa mujibu wa Bw. Sango, anasema wazo la msingi lilikuwa kwamba endapo ukuaji wa uchumi utaongezeka kwa kasi utasaidia kuondoa au kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira, tofauti ya kipato na umasikini miongoni mwa Watanzania!

Kat ika mtazamo huo anasema, mkazo mkubwa uliwekwa katika viashiria viwili tu vya watu yaani wingi wa watu na ongezeko lao (Population size and its growth) ambayo viliwezesha kukokotoa viashiria vya pato la Mwaka la nchi na wastani wa pato la kila Mwananchi (GDP and per Capita GDP). Hata hivyo anasema, mfumo huu haukukidhi malengo yaliyokusudiwa kutokana na makosa ya kupanga mipango ya maendeleo bila kujali viashiria vya makundi ya watu pamoja na “Utamaduni”!

Hali hiyo imepelekea matumizi ya viashiria vya watu katika kupanga mipango na kutoa maamuzi ya kisera na kiutendaji yaliendelea k u t u m i k a k a t i k a n c h i zilizofata sera za Kibepari. Taarifa za dini, rangi au Utaifa na kabila ziliendelea kukusanywa katika Sensa za Watu na Makazi pamoja na

Si sahihi watu wa dini moja kuhodhi mamlakaUjumbe umefika, tushiriki sensa nchi itawalike

Na Bakari Mwakangwale

Inaendelea Uk. 13

Page 9: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

9 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala

Waziri William Lukuvi ajiuzulu NAJIULIZA ila sijapata j ibu . Kama Babu wa S a m u n g e a m e w e z a ‘ k u t a p e l i ’ M a w a z i r i w a S e r i k a l i m p a k a wakamwona kuwa n i mwokozi wao na kumpa kila huduma ya upendeleo, hali inakuwa vipi mawaziri hawa wanapokutana na wenye ‘brifu kesi’ na tai zao kutoka 1600 Pennsylvania Avenue, NW Washington, DC 20500.

Kama Babu Mwaisapila a l iweza kuwapumbaza watendaji wandamizi wa serikali na sera zake za ndoto na hekaya za kuongea na Mungu, akapewa magari na kuwekewa ulinzi mkali, ni kwa kiasi gani wanachuma na kuvuna Symbion, Barrick Gold Corporation, AngloGold Ashanti na wale “Economic Hit Men?”

Kama mchungaji mstaafu A m b i l i k i l e a m e w e z a kuwapumbaza watu kiasi hiki na kikombe chake ‘ c h a k i t a p e l i ’ m p a k a baadhi ya watu serikalini wakaona ‘mwokozi’ ndie yeye; ikawasahau walimu, madaktari muhimbili; wa maana akaonekana Babu apelekewe barabara, umeme na kujengewa baabara maalum, mangapi ya hovyo yatakuwa yanafanywa kwa kupumbazwa na waliomzidi maarifa na wadhifa wa kikanisa Mwaisapila?

Kilichofanyika Samunge, ni utapeli, wizi na mauwaji; nani anawajibika? Watu waliokufa pale Samunge wakisubiri kikombe ni mamia. Wapo mamia pia waliokufa baada ya kupata kikombe kwa sababu waliambiwa waachane na dawa zao za awali za hospitali. Watu wa kisukar i na presha wakawa wanakula vyakula walivyokuwa wamezuiwa na madaktari wao. Presha na kisukari kilipotibuka, hawakupona. Yamewakuta haya kutokana na uhamasishaji uliofanywa na Mawaziri walioacha kawaida yao ya kwenda London na Mumbai kut ibiwa wakakimbil ia Loliondo. Walihamasishwa pia na kauli za Waheshimiwa sana Mawaziri (baadhi) na Maaskofu ambazo zilipambwa sana na vyombo vya habari. Nani anabeba dhima hii? Kwa nini waliohamasisha jinai hii wasiwajibishwe? Tumejifunza nini katika kadhia hii? Je, yaishe tu kwa kauli ya Waziri wa Afya kwamba dawa ya Babu ni feki?

Kilichowafanya Mawaziri kumiminika kwa Babu Loliondo kupata kikombe na hivyo kuwahamasisha watu wa kawaida kukimbilia

Na Omar Msangi huko, ilikuwa udini, shida ya maradhi iliyoleta kukata tamaa na kukosa subra au ndio uwezo wa akili zetu umeishia hapo? Kwa wale waliokuwa wagonjwa mahutut i na ndugu zao wa l iokuwa wakiwauguza, wanaweza kusameheka . Ugon jwa una mtihani mkubwa. Hao tunaweza kusema, shida ya ugonjwa na tamaa ya kupata nafuu ilifunika uwezo wao wa kufikiri wakaamini kuwa kweli mchungaji Ambilikile Mwaisapila anaongea na Mungu na kaletewa ‘kikombe’ c h a k u p o n y a u k i m w i , kisukari, kifafa na presha. Vipi na hawa waheshimiwa wetu John Pombe Magufuli, Steven Wassira na William Lukuvi?

Awali ngoma ya Samunge ilipoanza kuvuma, aliyekuwa Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda alitoa msimamo wa serikali kwamba dawa ya Babu haijathibitishwa kitaalamu kwamba inatibu ukimwi, kisukari na presha kama ilivyokuwa ikidaiwa. Na kutokana na jinsi watu walivyokuwa wakijazana kijijini hapo ikilinganishwa n a h u d u m a z a k i a f y a zilizokuwepo, Waziri Haji a l i zu iya wa tu kwenda mpaka uchunguzi kamili utakapofanyika kubaini ukweli juu ya dawa hiyo au hapo serikali itakapo hakikisha kuwa kuna huduma za kibinadamu za kukidhi haja.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Waziri Haji ilizua balaa. Mawaziri wenzake ndani ya serikali wakawa wa kwanza kumpinga. Kesho yake tu Waziri Will iam Lukuvi akahamasisha watu kwenda akisema kuwa ser ika l i haijapiga marufuku. Yeye alikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kupiga kikombe cha Babu, dawa iliyotokana na ndoto ya sadiki ukipenda. Kilichofuatia ni kauli kali za maaskofu wakitangaza kupambana na Dr. Haji na yeyote atakayezuiya watu kwenda kuonja utamu na Baraka za dawa ya mchungaji anayedai kuongea na Mungu. Mungu ambaye humpangia hata bei ya kuuzia kikombe kwamba isizidi shilingi 500.

Walipodaka Maaskofu, hapo tena waandishi wa habari wakapata sherehe. Kila kukicha ni Loliondo habari mpya mpya za kuhimiza watu kwenda zinaibuka.

“Sumaye atinga Loliondo”, “Wassira, Mkono nao watua kwa Babu”, “Maguful i apata kikombe”, “Magufuli apeleka shilingi bilioni moja Lo l iondo” , “Ole wake atakayemgusa Babu wa Loliondo, Kanisa laapa kupambana kumlinda”, “Serikali yanywea kwa Mchungaji Loliondo, yabariki

aendelee na tiba, kumpa ushirikiano”, “Tiba Loliondo: Serikali yasalimu amri. Yampelekea Babu gari.”

Kila aliyesikia kwamba M a w a z i , Wa b u n g e n a wakubwa wengine, badala ya hukimbilia London, Afrika ya Kusini na India kama kawaida yao, sasa wanapigana vikumbo kwenda kupata uzima kwa Babu, aliona huko ndio pa kwenda. Vyombo vya habari vikaendelea kukoleza kwa vichwa vya habari: “Maajabu: Dawa ya Babu yathibitishwa kutibu ukimwi.” “Mchungaji aongea na Mungu aambiwa hata wa kisukari na presha watapona.” Wachawi waliotaka kumjaribu Babu wanaswa.” “Maelfu wapata kikombe.” “Waliokunywa watoa ushuhuda, wasema wamepona kabisa.”

Almuradi i l ikuwa ni hamasa juu ya hamasa vyombo vya habari vikijitahidi kuhamasisha watu kwenda.

Tuliobahatika kuliona jambo hili toka awali kwa jicho la wasiwasi na kujaribu kutoa tahadhari, ilikuwa kama sauti ya nyikani isiyosikika. Baada ya mamia kwa maelfu ya watu kufa, leo ndio serikali inazinduka na kusema kuwa dawa ile ilikuwa feki.

Gaze t i moja ambalo lilishabikia sana likisema: “Maajabu: Dawa ya Babu yathibitishwa. Ni kazi ya wataalamu wawili.” Juzi hapa baada ya kauli ya Waziri Bungeni likaamka na kichwa cha habari. Dawa ya Babu

Feki!Labda niulize, wakati ule

serikali ikimwekea ulinzi m c h u n g a j i A m b i l i k i l e Mwaisapila na kuona kuwa huduma aliyokuwa akitoa ni muhimu sana kuliko hata madakitari mabingwa Muhimbili na Bugando, ilitumia vigezo gani?

Gazeti la Mwananchi la Mei 3, 2011 likiarifu juu ya uamuzi wa ser ikal i kumuwekea ulinzi Babu wa kikombe lilisema:

“Msaidizi wa mchungaji Mwaisapi la ambaye ni Ofisa wa Serikali, Frederick Nisajile alitangaza kuwa sasa ni marufuku kumsalimia mchungaji bila idhini (ya maofisa wa usalama na walinzi wake) kwa sababu za kiusalama.”

Juzi hapa wakati serikali inatoa kauli kwa vyombo vya habari ni kwa nini baadhi ya malipo ya walimu yalichelewa ilisema kuwa hiyo ni kutokana na sababu kuwa ilikuwa ni lazima serikali ifanye uchunguzi kubaini iwapo madai ya walimu yalikuwa ya kweli. Sasa kama huo ndio mtindo na utaratibu wa ufanyaji kazi serikalini, hawa mawaziri na watumishi wa serikali walioharakisha kupeleka barabara, umeme na kumuwekea ulinzi mchungaji m s t a a f u M w a i s a p i l a , uchunguzi gani walifanya hata kujiridhisha kuwa madai yake ni ya kweli?

Walithibitisha vipi kwamba

ndoto zake za kuongea na Mungu ni za kweli? Je, serikali iliwahi kumshuhudia Babu akiongea na mungu na kupata maagizo ya kutibu watu kwa kikombe? Au kwa vile yalikuwa madai ya mchungaji, hayahitaji uchunguzi wala kuhoji? Je, serikali ilihofia kitisho cha Askofu Laizer kwamba kanisa litambana na yeyote atakayebeza ndoto za Babu?

Tunaambiwa kuwa kabla ya Babu kutoa dawa alikuwa kitoa maombi “kwa jina la Yesu.”

Je, kwa vile Kikombe kilikuwa kikitolewa kwa jina la Yesu, ndio ilisababisha s e r i k a l i k u h a m a s i s h a watu kwenda na yenyewe kugharamia ufanisi wa utapeli huo?

Lengo nini hasa lilikuwa? Kuuwa watu au kuupa nguvu Ukristo? Kama lengo lilikuwa ndio hilo, pengine ambacho walisahau akina Lukuvi ni kuwa batili haidumu hata uipambe vipi. Batili ni yenye kuondoka tu.

Naam, kwa kauli hii ya serikali Bungeni, sasa ni zamu ya Dr. Haji Mponda kumgeukia Mheshimiwa sana William Lukuvi na kumsomea kipande hiki cha maneno matukufu yasemayo:

“Na sema: Ukweli umefika na uwongo umetoweka. Uwongo (mwishowe) huwa nd io wenye ku toweka (kuondoka).” (17:81).

WAZIRI William Lukuvi akipata 'kikombe' kwa 'Babu'.

Page 10: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

10 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala

KWA mara nyingine tena mwezi mtukufu wa Ramadhan umetufikia. W a i s l a m u w o t e duniani, kama mwili mmoja, tunaitikia wito wa Mwenyezi Mungu kufunga, i l i kupata radhi zake. Waislamu tunaonyesha kwa vitendo umoja wetu kama umma, na jinsi muongozo wetu Qur’an Tukufu, ulivyo na nguvu ya ajabu katika kuuhamasisha ummah wetu, kutekeleza amri na maagizo ya Mwenyezi Mungu:

“ E n y i M l i o a m i n i ! M m e l a z i m i s h w a kufunga (Swaumu) kama w a l i v y o l a z i m i s h w a waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu” Qur(2:183).

Ni mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao kila mmoja wetu atafanya juhudi kubwa za kutafuta radhi na msamaha wa Mwenyezi Mungu kupitia mwezi huu.

Huu pia ni mwezi wa kutafakari kwa kina na kutathmini hali ya ummah wetu, ambao unafunga Swaumu ya Ramadhan duniani kote. Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, ummah wa Ki i s l amu duniani umekumbwa na mitihani mizito. Katika eneo la Mashariki ya K a t i , t u m e s h u h u d i a mageuzi makubwa ya kisiasa, ambapo watawala madikteta waliotawala n c h i z a Wa i s l a m u k i b a b e k w a m i o n g o kadhaa wameng’olewa madarakani.

Katika mageuzi hayo ya kisiasa, yaliyojulikana kama ‘Arab Spr ing’ , maelfu ya watu, wakiwemo wanawake, watoto na vikongwe, wameshuhudia risasi, vifaru, makombora na madege ya kivita yakiua ndugu zao na wengine k u t i w a u l e m a v u w a kudumu. Waislamu wa Afghanistan na Pakistan w a m e e n d e l e a k u i s h i kwenye mateso makubwa yanayotokana na vita vya Marekani katika ukanda wa Asia ya Kati. Mashambulizi ya Drones na mabomu mazito yamesababisha vifo na uharibifu mkubwa wa mali katika nchi hizo za Waislamu. Wakati matukio hayo yakijaza ‘Channels’

Tutekeleze Qur’an kwa vitendo! Na Said Rajab

za habari dunia nzima, Waislamu wa Palestina wanaendelea kuteseka kutokana na kukaliwa kimabavu na Mazayuni. Somalia nako hal i s i shwari.

Tukirudi hapa nyumbani, ummah wa Kiislamu bado upo katika ukandamizaji mkubwa wa Mfumo Kristo. Kila Waislamu wakitaka kujikomboa kutoka kwenye ukandamizaji huu au kutaka kuishi kwa maelekezo ya dini yao, mkono mrefu wa Mfumo Kristo unaibuka na kuzima jitihada hizo. Watoto wetu wanafelishwa makusudi na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ili wakose nafasi za kuendelea na elimu ya juu. Wengine wanafukuzwa shule kwa sababu ya kuomba eneo la kufanyia ibada!

Hoja ya Waislamu kudai Mahakama ya Kadhi, ili mashauri yao kuhusu ndoa, talaka, mirathi na waqfu yaendeshwe kwa mujibu wa maelekezo ya dini yao imezimwa kiana. Waislamu wanadai Mahakama ya Kadhi, na kimsingi hakuna tatizo lolote isipokuwa roho mbaya tu ya Mfumo Kristo. Suala la kujiunga na OIC pia limezimwa na Mfumo Kristo bila sababu za msingi. Hoja za Waislamu kuhusu Sensa zinapuuzwa na Serikali ingawa zina mantiki. Ufupi wa maneno, Waislamu wa Tanzania wamebanwa kila upande na hawapumui.

Ka t ika mfungo wa Ramadhan hii, Waislamu tutafakari kuhusu matukio haya na tujiulize kwanini U m m a h w e t u n d i y o unaoteseka duniani kote, licha ya Mwenyezi Mungu kutupa muongozo wa Qur’an na Sunna za Mtume wake? Mwenyezi Mungu ameueleza mwezi mtukufu wa Ramadhan kama mwezi ambao Qur’an imeshuka:

( “ M w e z i h u o mlioambiwa mfunge) ni Mwezi wa Ramadhan ambao imeteremshwa hii Qur’an ili iwe uongozi kwa watu na hoja zilizo w a z i z a u o n g o z i n a upambanuzi” Qur (2:185). Qur’an hii imeteremshwa kama ‘Huda’ (uongozi) na ‘Furqaan’ (kipambanuzi) kwa watu wote. Misikiti

yetu yote bila shaka itajaa visomo vya Qur’an Tukufu, na Waislamu watasoma Qur’an kwa wingi sana katika mwezi huu mtukufu kama ilivyo desturi yetu.

Lak in i swa l i bado l i n a b a k i , k w a n i n i tumeshindwa kuichukua Qur’an kama ‘Huda’ na ‘Furqaan’ katika masuala yanayohusu ummah wetu? Kwa miongo kadhaa sasa, sheria, kanuni na taratibu z inazotawala mambo yetu kwenye nchi zetu hazitoki ndani ya Qur’an. Tunatawaliwa na mafisadi ambao ajenda yao kuu ni kuangamiza dini yetu. Sawa, tunaweza kusoma Qur’an kwa wingi kwenye misikiti yetu, lakini maisha yetu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanaendeshwa na sheria zinazompinga Mungu.

Tumefanywa tuamini kwamba ufumbuzi wa matatizo yetu ya kisiasa, k iuchumi na k i jami i kama ummah, hauwezi kupatikana kutoka kwenye

Qur’an, ambayo ndiyo imani, itikadi, utamaduni na urithi wetu. Qur’an il ipoondolewa kutoka kwenye maisha yetu ya kila siku na kubaki kama muongozo tu kwenye Swala, Zaka na Funga, m a d h i l a y e t u n a y o yakaanza. Leo hii Ummah wa Kiislamu duniani kote uko njia panda, na hauwezi kuvuka hapo mpaka wenyewe ubadilike kwanza. Mwenyezi Mungu anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao” Qur(13:11)

Hali yetu kama Ummah ha i t abad i l i ka mpaka tuifanye Qur’an kuwa kiongozi na kipambanuzi chetu baina ya haki na batili. Lazima tuijenge jamii yetu katika misingi ya kufahamu Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, na haushii kwenye kufunga na kuswali tu. Kufunga kwetu mwezi mtukufu wa Ramadhan

kuwakilishe dhamira yetu ya kumuabudu Mwenyezi Mungu. Lakini kumuabudu huku Mwenyezi Mungu kuwe na maana ya kufanya juhudi za kusimamisha dini yake katika ardhi. Mwenyezi Mungu mtukufu azikubali Funga na Swala zetu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na alete mageuzi katika ummah wa Kiislamu dunia nzima!

“Mwenyezi Mungu a m e w a a h i d i w a l e walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri kuwa atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale waliokuwepo kabla y a o , n a k w a y a k i n i atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani b a a d a y a h o f u y a o . Wawe wanan i abudu , h a w a n i s h i r i k i s h i n a c h o c h o t e . N a watakaokufuru baada ya hayo, basi hao ndiyo wavunjao amri ze t i” Qur(24:55).

Ramadhan Karim!

Madrasat Baytul Ulumi Mbezi Luis kwa Yusufu kwa kushirikiana na Ustadh pamoja na viongozi wa Madrasa wanaomba msaada kwa Waislamu wenye moyo wa huruma kusaidia ili kufanikisha mashindano ya Kuhifadhi Qur'an yaliyoandaliwa chuoni hapo. Mashindano hayo ni ya kuanzia kuhifadhi juzuu mbili, tatu na kuhifadhi Hadithi. Mashindano yatafanyika tarehe 24/08/2012. Tunaomba Waislamu wasaidie fedha kwa ajili ya kununua zawadi za kuwapa motisha vijana wa Madrasa. Kwa Pesa ambayo ni Tshs 850,000/ (Laki nane na nusu tu).

Amesema Mwenyezi Mungu "Mwenye Kutoa Kwa ajili ya kuendeleza Qur'an Malipo yake ni makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama".

Wabillah Tawfiiq

KWA MAWASILIANO ZAIDI: 0717 649313, 0685 351590, 0718 354364

Madrasat Baytul Uhumi

BAADHI ya wanafunzi wa Madrasat Ulumi

Page 11: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

11 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala

V I J A N A w a U m o j a wa Kitai fa Zanzibar t u m e s h t u s h w a s a n a kufuatia matamshi/kauli na misimamo ya baadhi ya viongozi na wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yenye shabaha ya kutumia vitisho na mabavu katika kuzizima hoja za baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wake wenye mawazo mbadala/tofauti.

Hapa tunawakusudia viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mjini na Afisi Kuu, Kisiwandui pamoja na baadhi ya viongozi wastaafu wa CCM ambao wanawatisha na kuwashinikiza viongozi katika chama chao hususan Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Wananchi wa Zanzibar waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar wakiwa na wajibu wa kuwatetea wananchi wa Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wakilindwa na kinga kwa mujibu na kanuni za Baraza na Sheria za nchi.

Hao wenye kutoa vitisho na kuweka sh in ik i zo wajue kuwa vitendo vyao hivyo ni kupora uhuru wa wananchi na kuondosha uhalali wa zoezi zima la marekebisho ya katiba. Vitendo vyao hivyo ni sawa na kuwapangia wananchi nini cha kusema na vitendo kama hivyo ni uvunjifu wa katiba na sharia za nchi na ni uporaji wa haki za msingi kabisa za wananchi wote na ni fedheha na aibu kubwa kwa CCM.

Ifahamike wazi kuwa kupatikana kwa aina ya mfumo wa muungano tunaoutaka utapatikana pale tu ambapo wananchi wote bila ya kujali vyama vyao watakuwa na uhuru usio na masharti ili waweze kutoa maoni yao vinginevyo zoezi hili lote litapoteza maana na uhalali wake na hivyo kuwa batili.

Katika hali kama hii tunamuomba Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein waingilie kati ili kulinda uhuru wa wanachama na sisi wananchi kwa ujumla wetu. Halikadhalika tunamuomba Mwenyekiti wa Tume ya Pamoja ya Marekebisho ya Katiba, Mheshimiwa Jaji

Tamko la Indhari!Na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

PANDU Amir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi

Joseph Warioba pamoja na Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutoa tamko juu ya kauli hizi za kushtusha za baadhi ya viongozi hawa wa CCM ili wananchi turidhike juu ya uhuru wetu na uhalali wetu wa kutoa maoni bila ya shinikizo la aina yoyote kutoka chama chochote.

Kauli na misimamo hiyo inaonekana sio tu kwenda kinyume na Azimio la Haki za Binaadamu zinazothamini uhuru na uwezo wa kila raia kuwa na mawazo na maamuzi tofauti. Misimamo n a m a t a m s h i h a y o yanapingana hata na kauli ya Rais Jakaya Kikwete, Rais Ali Mohammed Shein na Jaji Warioba ambao kwa pamoja walisema wazi kuwa wananchi wako huru kuwa na maoni tofauti juu ya mchakato wa katiba na wawe huru katika kuyatoa mawazo yao. Aidha, Rais Kikwete alisema na tunamnukuu: “Kwa upande wa mchakato wa kupata katiba mpya, n a w a s i h i Wa t a n z a n i a tujiandae kwa maoni ya kutoa. Tutofautiane bila kupigana”. Hata anayeitwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

aliwahi kusema katika hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa Uganda People’s Congress (UPC), tarehe 7 Juni, 1968: “Chama kina uwezo kuiambia Serikali nini matilaba ya watu, na kwamba ni muhimu kuweko wanachama ndani ya chama wanaoweza kuhakikisha kwamba Serikali na watu wanashirikiana kutekeleza matilaba ya watu”.

Tunatanabahisha kuwa tutofautiane katika fikra bila ya kubezana, kutishana wala kupigana. Aidha, tunatanabahisha kuwa kauli kama hizi zilizoanza k u t o l e w a z i n a z o b e b a agenda ya vitisho na kuiviza demokrasia hazitavumiliwa. Ni busara kusoma alama za nyakati.

Nchi hizi mbili za Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimetokana na asili ya utawala wa chama kimoja cha siasa baada ya mapinduzi ya Zanzibar na uhuru wa Tanganyika, na hatimaye kuwepo kwa chama kimoja tu kwa nchi zote mbili. Siasa ya vyama vingi imeanza katika uchaguzi mkuu wa 1995, kiasi cha miaka kumi na saba iliyopita, tofauti na utawala wa chama kimoja wa miaka

zaidi ya thelathini.Kwa miaka hiyo thelathini

na kitu, hakukuwa na tafauti kubwa baina ya Chama na Serikali. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa alikuwa Katibu wa Mkoa wa Chama, viongozi wa Chama walikuwa na hadhi ya viongozi wa Serikali kama vile kusafiria pasi za kibalozi. Katika kila Wizara, Idara na Mashirika, kulikuwa na ofisi za Chama cha Mapinduzi, na Mwenyekiti wake, na bendera ya chama ndio ilokuwa ikipepea. Hii inaonesha wazi tutokapo na jinsi mfumo wa fikra za watu (mindsets) ulivyojengeka.

Kutokana na hali hii sera za Chama na Serikali hazikuweza kuwa na tafauti yoyote. Sera zote za chama ndio zilikuwa sera za serikali. Kwa maana hiyo sera ya kuwa na Muungano wa Serikali mbili iliyopo ndani ya Katiba ya Muungano ndiyo ya Chama tawala cha wakati huo na ndio maana bado kuna baadhi ya viongozi (wahafidhina) w a n a o l a l a m i k a l e o juu ya haya mabadiliko tunayoyatarajia, na ndio maana vilevile tunashuhudia wakikaripia na hata kupinga juu ya mabadiliko ya sera hizo.

Wakati umebadilika na nchi zetu zina vyama vingi vya siasa, vyenye sera zao na wanachama wao ambao wote ni wananchi wenye haki sawa juu ya maamuzi mazito ya nchi kama katiba zinavyoeleza. Zaidi ya Chama tawala, hakuna hata chama kimoja chenye sera yake ya muundo wa nchi, kwa sababu vinafahamu kwamba sera hii haiwezi kuwa ukiritimba wa chama kimoja, bali ni ridhaa ya wananchi wote, hata wale ambao siyo wanachama au wafuasi wa chama chochote cha siasa.

Kwa hivyo huu utaratibu wa kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi ni wa kupongezwa. Hata hivyo, indhari ichukuliwe ya kuhakikisha kwamba ukweli na uadilifu unatawala katika zoezi hili, na kwamba kila mwananchi apewe fursa ya kutoa maoni huru bila ya shinikizo la kuimba nyimbo ya sera za Chama chake. Hii itakuwa kinyume kabisa na wanavyofanya baadhi ya

viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutaka kuwatisha na kuwanyanyapaa baadhi ya wanachama wake wenye fikra tofauti zinazokwenda kwa mujibu wa hali ya siasa zilivyo hivi leo. Huu ni wakati wa wananchi kupingana bila ya kupigana na hii ndio demokrasia itakayotuletea amani na usalama. Hapa elimu ya uraia ndipo inapohitajika.

Tu n a s i s i t i z a k u w a matokeo ya zoezi hi l i yaheshimiwe na wote. T u n a j u a k w a m b a Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni kiongozi mwandamizi wa Chama chake. Tunamuomba kwamba asiyumbishwe na sera za Chama chake katika zoezi hili. Tume ni suala linalojitegemea na maslahi ya nchi na watu wake ni makubwa kuliko sera za vyama. Huu ni wakati wa kusonga mbele si wakati tena wa kutazama nyuma. Wakati na mawimbi hayamsubiri mtu.

Tufanye kazi kat ika m a a d i l i y a s h a b a h a yanayoheshimu mawazo, maoni na maamuzi ya wananchi. Tuna wajibu wa kusimama juu ya ukweli kama tunavyouona bila ya kujali misingi na mirengo ya vyama. Sote kwa ujumla wetu kuanzia vyama, Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Serikali zote mbili ni watumishi wa watu.

Na watumishi hawana haki wala mamlaka wala n g u v u z i n a z o w a z i d i mabwana zao ambao ni wananchi kama Katiba zote mbili zinavyolithamini hilo. Tunawajibika katika hili kutoa huduma ya kizalendo n a k w a s a b a b u h i y o itakuwa huduma ya kweli na isiyosimamia misingi ya vyama.

Sisi Vijana wa Umoja wa Kitaifa ni waumini wenye kuheshimu uhuru wa mawazo ya kila mwananchi; lakini pia tunabeba kauli mbiu (motto) isemayo: “Maslahi ya wananchi ni makubwa zaidi kuliko yale ya vyama vya siasa.” Historia itakuja kutuhukumu.

Nakala:- Mheshimiwa Jaji Joseph

Warioba, Mwenyekiti wa Tume ya Pamoja ya Marekebisho ya Katiba.

Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar

Page 12: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

Je! Una maoni, barua au Mashairi? Tuandikie:Mhariri AN-NUUR,

S.L.P. 55105, Dar es Salaam au tutumie kwa Barua pepe

E-mail: [email protected]

12 AN-NUURMashairi/Barua RAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012

Ala ala ndugu zangu, enyi nyote Islamu,Zisomeni beti zangu, zenye usia muhimu,Ninenayo siyo yangu, bali ya uislamu,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

Aloyamrisha Mungu, yote twapaswa pupia,Na alokataza Mungu, shuruti kuyakimbia,FUNGA amri ya Mungu, hata nayo SWALA pia,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

Ndugu yangu islamu, usiwe kama YAHUDI,Ebu dumisha NIDHAMU, kwa amrize WAHIDI,Vyote SWALA na SWAUMU, kafaradhisha WADUDI,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

SWAUMU watekeleza, SWALA waitelekeza,FAJR unaibeza, NAUMU waendekeza,Shukalo wajigubiza, kisa baridi na kiza,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

DHUHRI huna habari, u ‘BIZE’ na shughulizo, Adhanaye ‘napojiri, huwa kwako ni chukizo,Ndo kwanza unang’ang’ana, na mamboyo mzomzo,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

LAASWR wajivuta, fulifuli kijiweni,‘POOL’ hapo na KARATA, wacheza hadi jioni, DARSA ‘ we kuzifwata, muhali msikitini,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI. MAGHRIBI waikwepa, eti wawahi futari,Kisha badaye walipa, kwa muda wa kukhitari,Huko ni kutapatapa, u mwenyewe wajighuri,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

ISHAI wahudhuria, kwajili ya manuizo,Hilo likishatimia, wakimbilia pumbazo,DHUNNA na ‘KOMEDI’ pia, vyatosha kuwa VIGEZO,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

TARAWEHE waikacha, ‘si SUNNA tu’ wanena,RUNINGA usiku kucha, ‘PONOGRAFI’ kuona,‘Mefanya hilo ni ‘KACHA’, adhimu na ya maana,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

Hupaswi SWAUMU tenda, na SWALA kuifariki,IBADA zote ZAENDA, SAMBAMBA si kwa fariki,‘Takuwa kombo ‘meenda, falau ‘tazifariki,SWAUMU pasi na SWALA, LENGO kutimu MUHALI.

ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

Nabtadi kuangaza, SUNNAH hii kwa kaumu,Si sawia kuibeza, kwani ni SUNNAH adhimu,Si nyingine nadokeza, TARAWEHE ya msimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza.

“Si sunnah” twajisemeza, kupunguza umuhimu,Kathiri twaikengeza, kwa aini la rajimu,Ya kwake twayatukuza, yenye khasara kuzimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza.

Twadunisha yenye ‘izza’, twaadhimisha ya ghamu, Yatotunyima mwangaza, kwa la kaburi dhwalamu,Akhera nako ni kiza, na mzomzo nadamu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza.

Nini tutamueleza, HAKIMU wa mahakimu ,Hilo ‘kija ‘tuuliza, siku hiyo ya hukumu,Yu nani wa kumjuza, amama atakadamu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Yalo LAGHWU twatukuza, ya KHERI hatuna hamu,KARATA kutwa twacheza, pasipo kukosa hamu,Na nikahi twachombeza, bayana kwa maharimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza.

Kwa ‘POOL’ twajitokeza, lilosheheni haramu, Kamari linoikuza, kwa kufilisi kaumu,ALLAH alotukataza, twapokezana kwa zamu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza.

Kucheza BAO twaweza, mchana kutwa twadumuWasaa twaupoteza, kwenye DHUMNA kukumu,Na RUNINGA zatumeza, kama joka la mdimu, Sunnah hii ya msimu, kwanini twaipuuza. Thamaniya ‘metimiza, RISALA yangu ‘metimu,Kwa Mola kujisogeza, si kwa FARADHI kutimu,Bali kujinyenyekeza, kwa SUNNAH kujilazimu, Sunnah hii ya msimu, si vyema kuipuuza.

ABUU NYAMKOMOGI MWANZA.

TARAWEHE, SI SUNNAH TU !!!

M WA L I M U N y e r e r e al iunda siasa za nchi akapanga Maaskofu wa kusimamia na kuendesha s iasa zake . Akaweka mawakala wakali wa kanisa ndani ya dola kusimamia siasa zake. Haikutosha, akaweka na vibaraka wa kuhami siasa zake.

Kwa bahati mbaya, tofauti na matarajio walikuwa nayo wazee wetu wakati wa kudai uhuru, Uislamu na Waislamu ndio wakawa walengwa wakuu wa siasa za Nyerere. Hii ina maana Waislamu hawakutakiwa kupewa fursa ya kuendea. Ushahidi upo tele. Muhimu ni kuwa Nyerere alidhibiti elimu isiende kwa Waislamu. Kwa mpango huu, Nyerere

Siasa za Nyerere zinaendelea kuwatafuna Waislamu Tanzania

Angalia “ Kazi” wa Bakwata alivyopatikana na suala la Kadhi lilivyopinduliwa .

Hii ni kwa sababu siasa za Nyerere tangu mwazo hazikuwa na heri na Uislamu. Aliusambaratisha kila kona. Nyerere aliwahi kusema heri zichezewe jumuiya za chama chake lakini si Bakwata. Hii maana yake ni kumba alijuwa wapinzani wa Siasa zake lazima watakuwa Waislamu na hivyo akabuni DUDE Bakwata kuzuia umoja na sauti ya pamoja ya Waislamu nchini Sasa tumebaini mchezo wenyewe.

Amesema msomi mmoja wa Cho Kikuu, hakuna uchaguzi unaosimamiwa na dola kwa umakini mkubwa wa kutisha kama wa Mufti

hizo siasa za Nyerere. Hii ni licha ya kuwa marais Waislamu huja na neema na mabadiliko chanya kwa nchi. Ndugu zetu wa Zanzibar wanatafunwa na siasa za huyu huyu “ mtakatifu” Mtarajiwa.

Mapenzi ya chama na dola kwa nyie Bakwata yako wapi kwa miaka yote hii? Wenzenu makanisa wana mahospitali makubwa, ya mikoa na wilaya, wana vyuo vikuu, si nchi ya 15. Tv nyingi na maredio lukuki Bakwata hawana ha ta kimoja katika hivyo! Fahari ya kujidai ndiyo viongozi wa Waislamu ni nini hasa? Au ni hii kutangaza mwezi tu, na kuonyeshwa katika TV za ITV na TBC kama inavyofanyika sasa kupitia sheikh wao wa Mkoa wa Dar es Salaam? Wanatia uchungu sana Bakwata. Hivi hawa Bakwata ni Waislam kweli? Hawaoni? H a w a s i k i i ? H a w a n a Nyoyo? Bila kuondoa siasa ya Nyerere inavyotutafuna Waislamu tangu 1954 mpaka sasa, tutarajie makubwa zaidi. Waislamu ni watu wa mabadiliko na wenye utambuzi a mambo. Kwa juhudi za kila Muislamu, vyovyote alivyo na alipo, tunakaribia kujikomboa. Tulipambana na Wareno na Wajerumani na tukamtoa Mwing i reza . S iasa za Nyerere nazo tutaziondoa nchini mwetu. Allah tulindie nchi yetu nzuri Tanzania.

Mohamed MohamedDar es salaam.

alifanikiwa kujaza Wakristo ndani ya utumishi na uongozi wa Dola mpaka sasa.

Jambo la kuzingatiwa na Wai s l amu wote n i kuwa, muda ambapo siasa chafu alizoasisi Mwalimu Nyerere dhidi ya Uislamu na Waislamu zitaendelea kutawala nchini mwetu. Tujue bila shaka yoyote, uonevu, kuupuuzwa na kudharauliwa hav i t aondoka kamwe .

wa Bakwata! Hata uchaguzi wa Rais ni cha mtoto. Hapa lipo jambo kubwa na ndiyo maana juhudi zote za Waislamu kuingiza wasomi, waadilifu ndani ya Bakwata hukumbana na mkono wa chuma wa siasa za Nyerere ndani ya Chama na dola. Hata marais Waislamu kuandamwa na kuchafuliwa mara kwa mara na matumbo ya maaskofu ni katika hizo

SWAUMU BILA YA SWALA

KATIKA makala ya Ramadhani wiki iliyopita, kulikuwa na kipengele k inachosema kuwa: “Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano; ya kwanza ikiwa ni kushuhudia ya kwamba hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah (Sw) na kwamba Muhammad (s.a.w) ni Mtume wa Allah (Sw). Ya pili ni kutoa Zakah na ya tatu ikiwa ni kuhiji katika nyumba tukufu ya al-Kaaba na ya tano ni kufunga mwezi wa

Shukran msomajiRamadhani.”

Utaona kuwa nguzo ya swala iliachwa na hivyo kufanya ile ya Zakka kutajwa kuwa ndiyo nguzo ya pili. Ilivyo sawa ni kuwa nguzo ya pili ni swala, ya tatu zakka, nne saumu na tano kuhiji.

Lakini pia kulikuwa na msomaji aliyekuwa na wasiwasi kutokana na habari iliyosema:

“kuwa imepokewa hadithi kutoka kwa Mama `Aishah na Ummu Salamah ( ra) kwamba Mtume (s.a.w) alikuwa akiamka

na janaba kutokana na kukutana kimwili na wake zake, kisha anaoga na kufunga (Al Bukhariy na Muslim).”

Msomaji mmoja alitaka kujua kuwa iwapo kauli hiyo ni sahihi. Tunasema ni sahihi. Na usahihi uliokusudiwa hapa ni kuonyesha kuwa ‘kuamka na janaba’ hakufungui swaumu.

Tu n a t o a s h u k r a n i kwa wasomaj i we tu waliotupigia simu kutoa maoni yao na kukosoa.

Mhariri.

Page 13: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

13 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala

tafiti zinginezo (rejea ripoti za Sensa za Watu na Makazi South Africa, USA, Sweden, n.k.).

Aidha, anasema nadharia ya kutumia viashiria vya w a t u k a t i k a k u p a n g a mipango ya maendeleo na utoaji maamuzi ya kisera na kiutendaji ulikubalika na kuanza kutumika katika baadhi ya nchi zinazoendelea baada ya mkutano wa kidunia wa watu mjini Bucharest mwaka 1974 (1974 World Population Conference at Bucharest) na kusisitizwa mwaka 1984 katika mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya Watu nchini Mexico.

“ M a k u b a l i a n o h a y a yakapelekea kuanzishwa kwa kozi ya Watu na Maendeleo iliyodhaminiwa na shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu (UNFP A) na vyuo viwili vya ukanda wa Afrika vikapewa jukumu hili la kutoa elimu hii. Kanda ya Kusini mwa jangwa la Sahara kilikuwa Chuo Kikuu Cha Botswana (Botswana University) na nchi za kaskazini mwa jangwa la Sahara kilikuwa nchini Misri.”

Bw. Simba, anasema anapenda kutumia fursa hii pia kulikumbusha Taifa kuwa suala la dini hapa nchini lilijumuishwa katika dodoso la Sensa ya watu na makazi kabla na baada ya uhuru (rejea ripoti za Sensa ya watu miaka ya 1948, 1958 na 1967). Kama alivyotangulia kusema hapo awali, swali hili liliondolewa kwenye Sensa ya mwaka 1978, hii ilitokana na ile dhana ya “watu wote ni sawa”.

Anaa in i sha madhara yaliyotokana na dhana hii katika kupanga mipango ya maendeleo na maamuzi ya kisera na kiutendaji u l iyofany ika , kuwa n i kusahaulika kwa baadhi ya makundi ya jamii wakati wa ujenzi wa majengo ya Serikali, walemavu hawakuzingatiwa na wachoraji wa majengo ya huduma za jamii, na hata ofisi za Serikali na uwiano baina ya wanaume na wanawake katika masomo, ajira na uongozi haukuzingatiwa.

M g a w a n y o w a a j i r a kwa makundi ya jamii haukufuatwa hal i h iyo inadhihirisha upungufu wa ajira kwa vijana ukilinganisha na wazee, na hata makundi mengine hususani ya dini. Hali hii imetokea kwa sababu Watanzania wote waliwekwa katika chungu kimoja.

Bw. Sango anasema, Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa baada ya kuona kuwa umoja wetu wa kinadharia hauendi kama unavyotakiwa kwa sababu ambazo aidha zinafahamika au zilizofichika, kukaibuka vikundi vya kikanda na kidini ambavyo v ing ine v i l i t ambu l iwa kisheria na vingine vipovipo tu.

Tujuane tusidhulumiane Inatoka Uk. 8

Anasema, sote ni mashahidi kwani tunasoma matangazo magazetini na kusikiliza radioni taarifa za wito “watu kutoka Mkoa fulani, Wilaya fulani na hata kata fulani tukutane sehemu fulani saa fulani na mgeni wa heshima a t a k u w a M h e s h i m i w a Mbunge ambae ni Waziri wa Wizara fulani, na pengine akwa ni wa mkoa husika.”.

Yanayozungumzwa katika vikao hivyo ndio chimbuko la kuwepo kwa mgawanyo mbovu wa elimu, kazi, mafungu ya fedha za Serikali na mgawanyo wa maeneo ya kiutawala. Leo hii tunaona dini moja tu inayohodhi kila kitu hadi kufikia nyimbo za dini kupigwa katika ofisi za Serikali bila ya woga wowote, picha za kiongozi wa dini kubandikwa kwenye maofisi ya Serikali na kadha wa kadha.

Bw. Sango anasema, hivi sasa hakuna haki wala uwiano wa asili (fair play and natural justice). Ukanda wa kikabila na udini vimechangia kutufikisha hapa tulipo leo, kanda na dini moja kuhodhi sehemu zote nyeti. Hili halina kificho tena. Nenda TRA, Wizara ya Fedha, CRDB, NBC, idara zinazohusu pesa na maamuzi ziko mikononi mwao. Ukiuliza utaambiwa wao wamesoma!! Kufatia hali hiyo anahoji, kwamba hivi ni chuo kipi kinasomesha kabila au dini moja tu au kozi zipi zinasomesha kabila au dini moja tu!!! “Sababu kubwa hatujuani hivyo hakuna “fair play na natural justice” hata mashuleni”!!

“Kama nilivyosema hapo juu, upangaji mipango na utoaji wa maamuzi yanapaswa kuzingatia mtawanyiko wa makundi ya watu. Viashiria

vya watu kama vile watoto, wanawake, wanaume, wazee, walemavu, imani, jinsia na utamaduni vinapaswa kukusanywa kwa kutumia sensa ya watu na makazi kwa kuwa inamuhusisha kila mtu (Complete Enumeration).”

Hapa msomi huyo wa Watu na Maendeleo, anasema hakuna namna nyingine ambayo Serikali itaweza kutumia kupata taarifa ya dini na lugha kwa maana ya kabila na miiko yao, hivyo kukataa kuweka swali la dini ni kuwanyima Watanzania haki yao ya msingi katika kuhudumiwa na Serikali.

Kwa nini Swali la Dini ni Muhimu

A n a s e m a , Wa k o l o n i waliliona tatizo la utamaduni na hasa dini kuwa ni nyeti katika kupanga mipango ya maendeleo na kutoa maamuzi ya k i se ra na kiutendaji. Hivyo Waislamu wa l i ruhus iwa k i she r i a kutumia sheri zao za ndoa na mirathi kwa kuanzishiwa Mahakama za Kidini na w a k a t e u l i w a M a k a d h i wa Majimbo na Wilaya. Maamuzi yao juu ya ndoa na Mirathi yaliheshimika katika Mahakama za Kiserikali, lakini pia walipiga marufuku ufugaji wa nguruwe na mabucha yake katika maeneo waishio Waislamu kwa wingi, baa na vilabu vya pombe viliwekwa nje ya maeneo waishio raia, wakulima hawakuchanganywa na wafugaji, wafugaji walipewa maneo ya kufugia mbali na mashamba ya wakulima, shule zilitawanywa kwa uwiano wa idadi ya watu, hapakutokea sehemu moja kuwa na shule nyingi za Serikali huku wakiwa na idadi ndogo ya wakazi.

Athari ya kutokuwepo vishiria v ya Watu (Dini/Kabila)

Anasema, Kutofuatwa kwa upangaji wa mipango na u toa j i wa maamuzi kwa kutumia v iash i r ia vya watu baada ya 1967 kulisababisha migongano ya kijamii wakiwemo Wasonjo n a Wa m a s a i Wi l a y a n i Ngorongoro, Wakulima na Wafugaji Wilayani Kilosa na Rufiji. Ugomvi baina ya Waislamu na Wakristo Manzese, Mwanza, Geita, na kwingineko.

A i d h a , v i b a l i v y a kuanzisha Baa na vilabu vya usiku vinatolewa hata katika maeneo waishio watu, ufugaji wa wanyama wakubwa na wadogo katika maeneo ya makazi. Unafuga Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo katikati ya jiji la Dar re Salaam bila kuzingatia sheria zilizopo!!.

H a k u n a u w i a n o w a makundi ya kijamii katika masomo, ajira na utawala. Hata tukifuata takwimu zilizotolewa na TBC bado mambo yaliyoanishwa hapo juu hayajazingatiwa! Hivyo basi Bw. Sango anasema, kuingizwa swali la utamaduni kwa maana pana ya dini na kabila kungeweza kutathmini mgawanyo wa mambo aliyoyaanisha hapo juu kwa kufuata haki bila “Religious and tribalism influences”!

Je! Waislamu wagomee Sensa?

“Mimi nasema hapana tunahi ta j i subra kat ika kuliendea jambo hili ili wasije ingizwa kwenye mtego unaoratibiwa na watu wa chama fulani cha Siasa na baadhi ya wanaharakati

wakisaidiwa na baadhi ya viongozi wengine wa dini wenye dhamira ya kuifanya nchi hii isitawalike. Pia naungana na Sheikh Bassaleh, alivyotuasa katika suala la uteuzi wa Kadhi na mfumo ulioruhusiwa na Serikali kuwa waangalifu na wenye kufanya subra ili wasije kufarakana. Mimi naamini kuwa mwanadamu hupitia hatua tatu katika kukabiliana na tatizo au changamoto inayomkabili.”

Alianisha hatua hizo kuwa, hatua ya kwanza iliyofanywa na Masheikh ni kuitambua changamoto. Hivyo basi, Mashekh wamekwisha onesha changamoto ambazo zinakwaza katika kufikia k i w a n g o c h a j u u c h a maendeleo ya nchi yao. Changamoto hizo ni pamoja na:- mgawanyo mbaya wa huduma za jamii kama vile elimu, afya na maji; mgawanyo mbaya wa ajira na mapato; na mgawanyo mbaya wa uongozi na fedha za Serikali.

Hatua ya pili ni kuzisema changamoto hadharani! Masheikh wamekwisha shuhudia kwa Mwenyezi Mungu hali ilivyo kwa sasa na kutabiri kutokea uvunjifu wa amani kwa siku zijazo kutokana na changamoto hizi. Ushahidi huu utawafanya kuwa salama juu ya waumini wao kwa yale yatakayojiri baadae p ind i uvun j i fu wa amani utakapotokea. Wamesema. Wametimiza wajibu wao.

M w i s h o a n a s e m a Masheikh, wametoa nasaha ya ufumbuzi wa changamoto hizi ili kudumisha amani ya kweli nchini. Jukumu l i lobakia mbele yao ni kuendelea kuikumbusha Serikali kuwa kiongozi bora ni yule anayetawala nyoyo za watu na sio kutawala miili ya watu. Kwani mwenye kutawala nyoyo za watu hutumia rasilimali za Taifa kidogo kushawishi wananchi wake juu ya maendeleo yao.

Aidha, mwenye kutawala mi i l i ya watu hutumia gharama kubwa kulazimisha nyoyo za watu kufuata maamuzi yatolewayo na viongozi wao!!

“Nukta yangu ni kuwa Waislamu wajiandikishe kwa sababu ile ile ya kuendelea kuwa wamoja katika dini, kuepuka kuingizwa katika j ambo l i s i lowahusu la kuifanya nchi isitawalike k a m a w a l i v y o k u s u d i a waanzilishi wa jambo hili na mwisho madai haya mazuri yalichelewa kuwasilishwa katika hatua za awali za mchakato wa sensa kwani hivi sasa Serikali imekwisha ingia gharama kubwa ya kuchapisha madodoso na vifaa vinginevyo.”

Wabillah TawfiiqSango Abas Simba

(Simu 0754 992 506)

Page 14: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

14 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala/Tangazo

Inawatangazia Waislamu wote kuwa imeandaa safari ya Hijja na Umra mwaka 2012 kwa dola (US) $ 3375 tu.Mambo yatakayogharamiwa.Semina za Hijja, Huduma za Afya, Airport charge na Tiketi za ndege, Nyumba za kulala Makka na Madina, Ihram na Kuchinja kwa ajili ya Tamaa-tuu, Chakula wakati wote, Usafiri na ziara Makka na Madina, Mahema Mina na Arafa. KUHIJIWA ni DOLA US $ 1450.Fomu zinapatikana.1 Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam- Magomeni Mtaa wa Dosi na Mkadini Nyumba namba 26 Mkabala na Show Room ya Magari Tel: 0713 730 444 au 0773 804101 au 0785 930 444 au 0773 930 444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar RahaLeo Tel: 0777 484982, 0777 413987.3. Abubakar Maulana wa Markaz Kiwalani Dar Es salaam Tel: 0784 453838.4. Abdallah Salehe Mazrui ( Hoko) Dar es salaam Tell. 0715 72 4444.5. Salim Is-haq Dar es Salaam Tell: 0754 286010, 0774 786101.6. Dukani kwa Mohamed Hafidh Mazrui Wete Pemba Tel: 0777 482665.7. Sheikh Daudi Khamis Sheha Tel: 07776 79692.8. Maalim Seif Humoud Hamed Kijichi Zanzibar Tel: 0777 417736.

Wahi mapema kulipia ili ushughulikiwe mapema, kama utalipia kwa Account No 048101000030 NBC piga simu kwanza 0774 412975.Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa ni cha Bei nafuu zaidi na huduma zake ni bora zaidi ya vikundi vingine.

Ahlul Daawa Hajj and Travel Agency

Inatoka Uk. 16

NI jambo la kawaida kwa Waislamu kutoa sadaka za futari au kufuturisha watu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Lakini zaidi ni kwamba Waislamu wale wenye uwezo, wamekuwa wakielekeza futari zao kwa wahitaji zaidi, ambao ni kundi la watu wasiokuwa na uwezo au wasiomudu au wasiokuwa na uhakika wa kujipatia mlo wa futari japo wanafunga, masikini na yatima.

Waislamu kipindi hiki kwa kutambua kuwa Ramadhani ni nguzo na ni mwezi wa kuchuma kutoka kwa Mwenyezi Mungu, huwatendea wema na kuwakirimu yatima, ili nao wamudu kutekeleza nguzo hii muhimu katika Uislamu. Pia watu wanatoa sadaka za futari na nyinginezo kipindi hiki cha Ramadhani kwa kutambua kuwa suala hilo ni moja kati ya maamrisho ya dini ya Kiislamu.

Futari inapoandaliwa kwa wakwasi badala ya Yatima Na Shaaban Rajab Qur ’an i Tukufu ka t ika

aya mbali mbali imebainisha jukumu la watu hususan ya Kiislamu kuhusu kuwasaidia na kuwakirimu mayatima.

Allah (sw) katika Sura Al Baqara aya ya 83 anasema: “...Na tulipofunga agano na Wana wa Israili: Hamtamuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu; na muwafanyie wema wazazi na jamaa na mayatima na masikini... “

Qur’an Tukufu imewaenzi yatima na wasiojiweza kwa kiwango cha hali ya juu na kuhimiza suala la kuwahudumia katika mahitaji yao kibinafsi na kijamii.

K u w a h u d u m i a y a t i m a , maskini na wasiojiweza ni katika majukumu ya Waislamu. Lakini pia kuzembea au kupuuza jukumu hilo ni tendo baya hapa duniani na hata kesho Akhera.

Mtume Muhammad (SAW) anasema: ‘Nyumba bora zaidi ni ile ambayo ndani yake mayatima wanakirimiwa na nyumba mbaya zaidi ni ile ambayo mayatima wanatendewa maovu.’ (Abul Fadhl Ali bin Hassan Tabrasi

Uk. 167). P a m o j a n a Wa i s l a m u

kufahamu hili, inasikitisha na kushangaza kuwa baadhi ya Masheikh wetu wakitumia fursa hii ya kuwasaidia wasiojiweza kufuturu, wao wamejihimu na kutumia masurufu yao kufuturisha wanaojiweza na wakwasi.

Ingekuwa afadhali kama wangealika wakwasi hao, ambao wengi wao wakiwa si wafungaji kwa ajili ya kujumuika na Sheikh muandazi katika futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wahitaji. Hapa mtu anaweza akajiuliza Sheikh kuandaa futari kumfuturisha mkwasi ambaye hana hakika kama kafunga,

alikusudia kutekeleza ibada au alikuwa amelenga kupata maslahi yake binafsi kutoka kwa mualikwa?

Kama sivyo, basi ifahamike kuwa futari ni kwa aliyefunga na ina adabu zake. Vinginevyo itaitwa mlo wa jioni kama si wa usiku.

Kuitetea Zanzibar katika Muunganokuirejea historia hiyo. Katika demokrasia, wengi wape kutokana na wingi wa kura, na tusipofanya jaribio la makusudi na la dharura kuwapata viongozi wa safu za juu kutoka sehemu zote za Muungano wetu, basi wengi watatoka sehemu moja na kuendelea kujenga hisia kwamba sehemu moja ya Muungano imeelemewa. Ndio maana kuna wengine wanajihisi wamesakamwa na wanaomba waachiwe wapumuwe.

Tunapopata fursa ya kuchagua viongozi wa juu, kama vile Rais wa Jamhuri ya Muungano, ni vyema wale wanaodai kuitetea Zanzibar wawe mstari wa mbele katika kumpata mgombea bora kutoka Zanzibar na kumsaidia ili ateuliwe. Hili ni muhimu kufanyika, hasa baada ya uongozi wa ngazi ya juu kabisa kukamatwa na viongozi kutoka sehemu moja ya Muungano kwa muda mrefu. Mwenye kuitetea Zanzibar kikweli kwenye hi lo , hawezi kudai kwamba hakuna Mzanzibari anofaa kwenye wadhifa huo. Anayechukua msimamo huo, anachangia Zanzibar kusakamwa na kukosa pumzi. “Tuacheni

tupumuwe” aambiwe na yeye pia. Mzanzibari anayewakataa wagombea wote kutoka Zanzibar na kumuunga mkono mgombea kutoka bara kwa hali na mali aendelee kutawala, asidai kwamba anaitetea Zanzibar na kudai “Tuacheni tupumuwe”. K w a n i k w e n y e kusakamwa na Bara, na yeye si alichangia? Ya yeye alichangia katika k u t u k o s e s h a p u m z i , ilimradi yeye apumuwe vizuri zaidi baada ya kutuuza. “We were sold down the river to the highest bidder by our own kith and kin”. Kikulacho kinguoni mwako.

U m e f i k a w a k a t i Watanzania tuwe makini sana. Tutetee haki zetu kwenye Muungano wetu, na tujizatiti katika kuepusha “Dhana” ya aina yoyote ya kwamba upande mmoja wa Muungano we tu , umeelemewa. Tuunde Katiba mpya itoondowa dhana ya kutawaliwa na tutoe fursa kwa pande zote ziachwe zipumuwe. Tukishindwa kwenye hilo, tutajitakia maradhi. Na wahenga walisema “Maradhi ya kujitakia; Mtu hapewi pole”.

Balozi Karume.

ADMISSION INTO CERTIFICATE AND DIPLOMA PROGRAMES FOR THE ACADEMIC YEAR 2012/2013

AL- MAKTOUM COLLEGE OF ENGINEERING AND TECHNOLOGY (AMCET)

AL- MAKTOUM COLLEGE OF ENGINEERING AND TECHNOLOGY (AMCET) is a Technician level Institute accredited by the National Council for Technical Education (NACTE). The College is situated in Mbezi Beach area, about 1 km from Tangi bovu bus stop and 5 km from Mwenge bus station along Ali Hassan Mwinyi Road to Bagamoyo.

AMCET invite applications from all qualified Tanzanians and foreign to pursue various Diploma and Certificate Programs for the 2012/2013 academic year. Deadline for submission of filled application forms is 13th August 2012. Application forms are available at the college building along Bagamoyo Road. Forms can also be down loaded from the website (www.al-maktoumcollege.com)

Courses offered are as follows:• INFORMATION TECHNOLOGY;• ELECTRONIC ENGINEERING; • ELECTRICAL ENGINEERING;• SHORT COURSES ARE ALSO AVAILABLE.Commencement: our courses will commence on August, 21st 2012.Duration:• The program runs as follows: - 1 Year for Basic Technician Certificate (NTA Level 4) and 3

Years for Ordinary Diploma (NTA Level 4-6).• 2 Years Diploma Courses (NTA Level 5-6) are also available for A-level students with

appropriate qualifications.Minimum Entry Requirements:A) Ordinary Diploma (NTA Level 4-6). The applicant should possess a Certificate of Ordinary Secondary School with a minimum pass “D”

grade in Mathematics and English. A pass in Physics will be added advantage.OR The applicant should possess at least Division IV in the Certificate of Ordinary Secondary School

with (NVTA II) in a relevant field from a recognized VETA Institution.B) Diploma Courses (NTA Level 5-6)Applicants are required to have acquired a Technician Certificate (OR) Equivalent qualification

in Advanced level Certificate of Secondary Education with a minimum pass at a Principal Level in Mathematics or Physics and a Subsidiary pass in any other relevant subject.

If less than minimum qualifications, you can qualify through College Bridge Up Course.AMCET offers highly competitive fees structure for Certificate and Diploma courses. Limited

scholarships are available for highly qualified students. Free accommodation will be available for the first 75 students. Application fees: 10,000 (non- refundable)

All inquiries should be addressed to: The Principal, Al-Maktoum College of Engineering and TechnologyP.O.BOX 7206 Dar es SalaamFor further information please contact us at: Tel: 22 2617703/4 Mobile: 0713 423 405 OR 0713 220 304

Page 15: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

15 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012Makala

Kwa mahitaji ya viroba bora vipya kabisa kwa matumizi mbalimbali sasa unaweza kupata kwa bei ya jumla na rejareja kwa saizi zote kwa bei nafuu zaidi, kwa BANDO.

Tupo mtaa wa Likoma na Pemba Kariakoo, Dar es Salaam (nyuma ya Msikiti wa Idrisa).

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana kwa simu: 0657 800999/0683 800999.

VIROBA MURUA

WIKI iliyopita kuna kituko cha aina yake kimetokea ndani ya Chama cha Mapinduzi upande wa Zanzibar kwa wanachama wachache wa Chama hicho Wilaya ya Mjini kuasi dhidi ya mamlaka halali ya CCM. Ni kisa. Kituko kinachoweza kuvunja mbavu pale baadhi ya Wana CCM walipotoa tamko la kuwatuma viongozi wao wa Wilaya kuwataka Makamu M w e m y e k i t i w a C C M Zanzibar na Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kunyang’anywa kadi kwa madai wamekwenda kinyume na msimamo wa CCM juu ya Muungano.

Viongozi wale waliobariki uasi ndani ya CCM nawafanisha na aliyekuwa Rais wa Umoja wa Vijana wa African National Congress(ANC) Julius Malema. Katika mkutano huo ambao mbali ya kutaka Makamu Mwenyekiti wao Karume afukuzwe CCM, lakini pia walitaka wanachama wengine kama Mweka Hazina wa Chama hicho Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid nae kunyanganywa kadi!

Kisa na mkasa; ni msimamo wa Hamza Hassan Juma, Mshimba Mbarouk, Thuwayba Edington Kisasi, Omar Yussuf Mzee, Mahmoud Mohammed Mussa, Haroun Ali Suleiman, Asha Bakar Makame, Salmin Awadh Salmin, Othman Masoud Othman, Nassor Salim, Mansoor Yussuf Himid katika muundo wa Muungano wakiukosoa hadharani kuwa hauna tija kwa kuwa umeshindwa kufikia kile Wazanzibari walichokuwa wakikitaka baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na matumaini yao kat ika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwa Karume wanamtuhumu kuunga mkono mabadiliko ya muundo wa Muungano, ingawa Karume hajapata kusema aina gani ya mfumo wa muundo wa Muungano anaupendelea.

W a n a c h a m a w a l e wanamvumish ia Makamu Mwenyekiti wao jambo ambalo hakulisema. Uvumi wao ni sawa na abrakadabra inayotaka kuzuka ndani ya CCM. Mambo ya uzushi, fitna na pengine kutaka kukigawa Chama chao kikongwe katika Bara la Afrika.

Kuwepo kwa mawazo tofauti ndani ya CCM au kwenye jamii sio kosa kwani muda mfupi baada ya NEC ya CCM kukutana Dodoma mwezi Mei mwaka huu ilitoa taarifa ya kuelezea msimamo wake kuhusu muundo wa Muungano kuendelea na mfumo wa sasa.

H a t a h i v y o , M a k a m u Mwenyekiti Bara, Pius Msekwa a k i h o j i w a n a S h i r i k a l a Utangazaji la Ujerumani idhaa ya Kiswahili alisema pamoja na msimamo huo wa CCM wanachama wake hawajafungika kuwa na mawazo au kutoa fikra tofauti na ule wa Chama chao kwenye kutoa maoni katika Tume ya Mabadiliko ya katiba.

R a i s J a k a y a K i k w e t e akizindua Tume ya Jaji Warioba nae aliweka mkazo haki ya kutoa maoni na kila mtu kuheshimu mawazo ya mwengine. Ibara ya 18(a) ya katiba ya Jamhuri

CCM maslahi na vitisho vya Chui wa karatasiya Muungano wa Tanzania inasema; kila mtu anao uhuru wa maoni na kueleza fikra zake.

Msimamo huo unatiliwa mkazo na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein alipowahakikishia Wazanzibari kwamba wako huru kutoa maoni wayatakayo, hakuna atakayeingilia.

K i t abu cha Cyc l e s o f American kilichotungwa na Arthum Schelesinger Jr anasema kutokufungwa na mawazo ya kale kat ika mazingira yanayobadi l ika kunampa kiongozi wa kidemokrasia nafasi ya kutengeneza maonjo matamu ili apendwe na kufurahiwa na wengi.

Je, viongozi wale wa CCM Wilaya ya Mjini wanadhani watapendwa kwa kukandamiza uhuru wa maon i , ku i sh i maz ing i ra ya k i s i a sa ya kibabaishaji ambayo kwanza hayakisaidii Chama hicho, lakini pia kinaweza kukimbiwa na wanachama kwani mfumo wa vyama vingi sera na uwazi ndani ya vyama ndio kigezo cha watu kujiunga na Chama husika.

Sheria inampa mtu kuwa mwenye haki mbele ya mtu mwingine na papo hapo kuwa mwenye haki mbele ya jamii kwa ujumla hivyo, wanachama wa CCM na hasa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanayo haki ya kijamii Social justice katika suala zima la mustakabali wa mfumo wa muundo wa Muungano wanaouona unafaa.

Mara nyingi haki ya kijamii ndio kilele cha demokrasia ambapo maamuzi ya nchi yapo mikononi mwa wananchi wenyewe na yafaa kutambua kuwa pasipo haki hakuna amani, Tulitegemea wakati huu ambapo Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaendelea kukusanya maoni kungekuwa na uhamasishaji wa CCM Mjini kuwahimiza wanachama wao kwenda kutoa maoni.

Kama kosa la akina Hamza H a s s a n J u m a , M s h i m b a Mbarouk, Thuwayba Edington Kisasi, Omar Yussuf Mzee, Mahmoud Mohammed Mussa, Haroun Ali Suleiman, Asha Bakar Makame, Mohamed Raza Daramsi, Salmin Awadh Salmin, Othman Masoud Othman, Nassor Salim, Mansoor Yussuf Himid, na wengineo ambao wanawajibika kuitetea Zanzibar ni kosa na dhambi kwa CCM Wilaya Mjini basi historia itawahukumu kwa uzalendo wao, vyenginevyo, CCM maslahi watalia na kusaga meno kwa vigae.

CCM maslahi wanataka kuwapitisha Wazanzibari katika njia yenye miba, kiza kinene iliyokuwa na mashaka mengi huku tope za Uhafidhina zikiwanasa miguuni na kuchelewesha safari katika kufikia Muungano wenye maslahi kwa kila upande, Tanganyika na Zanzibar.

Kwa kutaka kuwanasua Wa z a n z i b a r i n a t o p e l a Muhafidhina, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman akitoa mada

katika semina kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuhusu katiba mpya, aliukosoa Muungano kwa k iwango a m b a c h o k i l i w a r i d h i s h a Wawakilishi.

Katika kuthibitisha udhaifu wa muundo wa Muungano, Mwanasheria Mkuu anauliza mambo kadhaa ik iwemo uhalali wa Rais wa Muungano kuchaguliwa kwa wingi wa kura kwa kuzingatia tofauti ya idadi ya watu baina ya Zanzibar na Tanzania Bara; Uhalali wa Rais wa Zanzibar kuwa Mjumbe tu wa Baraza la Mawaziri na sio Mwakilishi wa Zanzibar ndani ya Baraza la Mawaziri ili kuepuka kubanwa na Kanuni ya Baraza la Mawaziri ya Uwajibikaji wa pamoja.

Nini wajibu wa kikatiba wa Makamu wa Rais katika uendeshaji wa Serikali, Makamu wa Rais ni Msaidizi Mkuu wa Rais wa Muungano kuhusiana na Zanzibar kama ilivyokusudiwa na Mapatano ya Muungano? Jee ni Msaidizi Mkuu wa Rais wa Muungano kwa Mambo ya Muungano au Msaidizi Mkuu ni Waziri Mkuu? Hoja nyengine aliyowahi kuieleza Mwanasheria Mkuu ni pamoja na Makamu wa Rais hana urithi akimaanisha katika Serikali ya Muungano hana Mamlaka wala haiwakilishi Zanzibar na kwa mujibu wa katiba na sheria Rais wa Jamhuri ya Muungano anaweza akitaka tu,halazimiki.

Jee Mawaziri wanaotoka Zanzibar wal iomo kat ika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Muungano wanaiwakilisha Zanzibar au ni watumishi wa Rais wa Muungano kama walivyo Mawaziri wengine?

Jee kuna chombo chochote cha Kikat iba au kisher ia kinacholazimisha Serikali mbili za Jamhuri ya Muungano kukutana, kushauriana na kufanya maamuzi ya pamoja kama Mamlaka mbili za kuendesha Jamhuri ya Muungano?

Katika mfumo wa sasa wa Serikali mbili upo uwezekano wa Serikali mbili zinazoongozwa na vyama viwili tofauti kufanya kazi kwa maelewano, Jee kipo chombo cha kutatua mizozo inayoweza kujitokeza baina ya Serikali mbili?

Maswali haya sio yangu, ni ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar katika mada yake kwa Wawakil ishi ambayo yanatuthibi t ishia haja ya mabadiliko ya muundo wa Muungano ingawa wapo watu wengine kwa ulevi wa madaraka wanayafumbia macho kwa tama ya vyeo na pesa.

M s a n i i m a a r u f u k u l e Msumbiji , Marcelino Dos Santos katika moja ya tungo zake alisema ”We Must Plant”. Tafsiri ya haraka haraka ni kwamba tuna lazima ya kupanda, kupanda nini, mawazo ya mabadiliko katika muundo wa Muungano ambao wengi wanataka uwe wa Serikali mbili, lakini wa mkataba sio wa kikatiba.

W a z a n z i b a r i w e n g i

wanaotumikia Serikali ya Muungano aghalab wamekuwa wakisahau kule walikotoka, wakifika Tanganyika wanageuka na kuwaona Wazanzibar i wakorofi na baadhi ya wakati hata kuwabeza.

Tumeshangazwa na matamshi ya Waziri wa Ulinzi, Shamsi Vuai Nahodha katika michango yake katika semina ile akionekana kutetea sana mfumo huu mbovu na dhaifu wa muundo wa Muungano.

N a h o d h a a n a e l e z a namna kero za Muungano zinavyoshughulikiwa katika Kamati isiyokuwa na meno ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais, tumuulize Nahodha, miaka 48 kipi kimesababisha kushindwa kutatuliwa kwa kero hizo na sababu za kuzuka kwake?

Alipokuwa Waziri Kiongozi, Nahodha al iandika barua kumwandikia Waziri Mkuu juu ya maamuzi ya Baraza la Wawakilishi kuliondoa suala la mafuta na gesi asilia katika mambo ya Muungano, barua hiyo hadi hivi leo yeye anakuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Waziri Mkuu hajaijibu, tuseme haijafika pale Magogoni, imepotea Posta, au ndio wapo mbioni kuijibu?

Ndipo mwasisi wa Muungano, Hassan Nassor Moyo alipohoji kama kuna dhamira ya dhati ya kutatua kero hizo maana ni kipindi kirefu kimepita na pia alitoa angalizo kwamba wao enzi zao walifanya makosa, lakini makosa hayo lazima yasawazishwe na kizazi hichi.

Mwanafalsafa wa Ugiriki Socrates aliyeishi baina ya mwaka 469 BC – 399 BC siku moja aliwashangaza Wagiriki alipokwenda sokoni mkononi ameshika tochi akimulika mulika, wachuuzi walianza kumdadisi, imekuwaje leo? Akawaambia “kwenye nuru hii, kuna walio gizani.”

Kweli kuna walio gizani na ndio maana wameanza kutoa vitisho kwa wengine wakiwatishia kuwafukuza katika CCM. Hapa nataka kukumbusha jambo moja, wakati fulani, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema “CCM sio baba yake wala mama yake” akafafanua “ikiwa kitapoteza sera na mwelekeo sina sababu ya kubaki ndani ya Chama hicho”

Sitaki kuamini kwamba CCM imepoteza sera, bali kuna watu ndani ya Chama hicho husasan Zanzibar hawana dira, hawana sera, wala hawana mwelekeo

wanaishi kwa fitna, chuki na hawatumii bidii yao kukigeuza Chama hicho kuwa kimbilio la wengi, hawa ni ‘mufilisi’ kisiasa.

Mfumo wa muundo wa Muungano wa sasa hauwezi kusafishika kwa maji taka, lazima tutumie maj i saf i l a sa l ama na wa la wa le wanaojidanganya kuwa vitisho vinasaidia kulinda Muungano wanaota ndoto ya mchana sawa na ‘Mfalme aliyetembea uchi’ huku watu wake wakijipanga barabarani kusifia vazi jipya la mfalme wao na wakijifanya hawaoni ubovu wa vazi jipya la Mfalme lililomweka nusu uchi kweupeni.

Tunashukuru Mungu wapo watetezi wa kweli wa Zanzibar kama Mwanasheria Mkuu anayetoa kasoro za Muungano bila woga, kama pale alipoelezea kizungumkuti cha kukosekana mfumo rasmi wa lila Mamlaka kuitambua Mamlaka Nyengine.

Othman anasema Hiyo ni kasoro kubwa sana katika Muungano na ambayo kwa bahati mbaya imejificha. Miongoni mwa athari zake ni Kwanza, ingawa Rais wa Jamhuri ya Muungano ana mamlaka kwa mambo ya Muungano ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar, masuala kama vile ya Sheria za jinai si suala la Muungano na hivyo kinga aliyonayo ya kutoshtakiwa ndani ya Katiba ya Muungano haiwezi kutumika Zanzibar kwa vile Zanzibar ina mamlaka na sheria zake za jinai.

Mwanasheria Mkuu anauliza Suala muhimu hapa ni jee Rais wa Muungano anaweza kushtakiwa kwa kosa la jinai ndani ya Zanzibar? .Suala hili kwa hali ya sasa linaweza kuonekana la kituko, lakini ni la muhimu sana” Anasema.

Hakuishia kwa Rais wa Muungano,pia aliuliza kwa Rais wa Zanzibar anapokwenda Tanzania Bara. “Pili, suala kama hili ni muhimu kujiuliza kwa Rais wa Zanzibar anapokuwa ndani ya Tanzania Bara. Tatu, Katiba haijaweka bayana masuala ya mashirikiano ya kimahkama hasa katika utekelezaji wa amri za Mahakama za pande mbili. Jambo pekee lililoelezwa ni upelekaji hati za Mahakama”

K w a m a s w a l i h a y o yasiyokuwa na majibu ndipo pale haja na ulazima wa kuwa na mfumo wa muundo wa Mungano wa mkataba unaposhika nafasi kwani kwa mazingira yalivyo njia pekee na bora ya kuweka sawa nyumba yetu ni kufanya mabadiliko ya muundo. (Makala hii tumeitoa kwa hisani ya Na Abdallah Vuai.)

Page 16: Sauti ya Waislamu · Fitr iliyo kamili kiasi cha vibaba viwili na nusu au pishi moja au kilo mbili na nusu. Kinachotolewa Zakat Fitr lazima kiwe ni chakula kinachopendwa na watu wa

16 AN-NUURRAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Limited, S.L.P. 78495 Dar es Salaam.

AN-NUUR Gazeti la An-nuur na watendaji wake wanawatakia Waislamu

wote Ramadhani Kareem, Ramadhani Mubaraka.16 RAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012

MTU yoyote ambae anadai kuitetea Zanzibar k a t i k a M u u n g a n o , h a w e z i w a k a t i h u o huo kudai Muungano u v u n j i k e . I w a p o Muungano utavunjika, hiyo Zanzibar utaiteteaje katika Muungano ambao umeshavunjika? Lazima kuitetea Zanzibar katika mfumo wa Muungano ambao unatoa haki sawa kwa nchi mbili ambazo zimeungana. Mwanzo wa haki hizo ni katika kuongoza Muungano kwenye safu zote za Serikali ya Muungano, kuanzia ngazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CHUO Kikuu Cha Waislamu Morogoro (MUM) kimepata pigo baada ya kufiwa na wanafunzi wake 14, katika ajali ya Meli ya Mv Skagit, iliyotokea hivi karibuni ikitoka Jijini Dar es Salaam ikielekea Zanzibar.

Wanafunzi hao kwa pamoja walifikwa na mauti baada ya kuwa safarini katika Meli hiyo wakitoka Chuoni kwao (Morogoro) wakielekea makwao katika likizo fupi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Chuo hicho, Bw. Saddy Ally, alisema wanasikitika kupoteza wanafunzi 14, kati ya hao wanawake 5 na wanaume 9, ambao wote walikuwa ni wanachuo wa mwaka wa kwanza chuoni hapo, wakichukua Shada ya Ualimu.

Alisema, wanafunzi h a o w a l i k u w a w a m w a n z o k u m a l i z a m i t i h a n i y a o n a kulazimika kuondoka

Msiba mkubwa MUMNa Bakari Mwakangwale kwa ajili ya kwenda makwao kwa ajili ya mapumziko, ambapo ka t ika t imu nz ima katika safari yao ni wanafunzi watau tu ndio walinusuruika katika ajali hiyo.

Alisema, walichelewa kutoa taarifa mapema kutokana na kufatilia kwa karibu taarifa hizo, ambapo iliwalazimu kutuma wawakilishi Zanzibar kujiridhisha na kukuta ni kweli hali hiyo baada ya kuonana na family husika.

A l i s e m a , c h u o kimepata msiba mkubwa kwa kupoteza wanafunzi 14, kwa mpigo, chuo kimetoa rambirambi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema, marehemu hao walikuwa ni wenyeji wa Pemba na Unguja, chuo kinawaomba ndugu na jamaa kwa ujumla kuwa na subira katika kipindi hiki cha majonzi pamoja na kuwa na subra kwa msiba huo.

Innalilah wainailaihr Rajiun

Abdallah Sudi Mohamed Asha Juma Abdallah Hassan Fakh Seif Khadija A. Seif

Khamis Ali Suleiman Mangi Haji Haji Mgeni Mwinyi Omar Patima Makame Simai

Rashid Fadhil Saleh Rashid Mohd Juma Said Salim Khatib Said Simai Iddi

Kuitetea Zanzibar katika MuunganoNchi mbili zikiungana

huwa zinasaka “Equity” kwenye huo Muungano. Uwiano wa haki huleta usawa kwa pande zote mbili na kuchelea upande mmoja kujihisi wametawaliwa au wamemezwa. Kujihisi au kuwa na hisia ya kutawaliwa huleta unyonge wa kuhisi kuna ukosefu wa utetezi; maana kwenye utetezi kamili, hakuna kupunjwa, kunyanyaswa, au kuonewa. “In politics, perception is everything”. Kwenye siasa, kila kitu hutokana na hisia. Ukihisi unadhulumiwa, huwachi kulalamika.

Kwenye nchi zinoungana kisiasa, tatizo la kwanza ni

kupanga safu ya uongozi utoridhisha sehemu zote za Muungano. Mara nyingi, katika kuepuka vurugu za kuchagua Rais mpya wa Muungano, mapendekezo ni kwamba Rais wa nchi moja ndie awe Rais mpya wa huo Muungano. Hii humaan i sha kwamba Rais wa ile nchi nyengine awe Makamo wa Rais, ili wale Marais wawili kab la ya Muungano , waongoze serikali ya Muungano kwenye safu ya Rais na Makamo wake. Pia, humaanisha kwamba baada ya kipindi au vipindi muafaka, na yule Makamo au kiongozi mwengine kutoka nchi yake, aweze

kuongoza kwenye safu ya Urais wa Muungano. Na upande wa pili wa Muungano utowe Makamo wa Rais.

K a t i b a a m b a y o tumepania kuibadi l i , imetamka wazi kwenye h i l o , n a w a t e t e z i w a Z a n z i b a r h i l o wamelifurahia. Katika Katiba mpya, bora hilo libaki, na katika kutilia mkazo “Equity” na uwiano utaochelea migogoro na malalamiko ya kuelemewa, ni bora Katiba itamke wazi juu ya suala la kupishana na kuwepo zamu kwenye Urais na vyeo vyengine vya juu.

Kila Katiba huwa na

Yaloagizwa, Yaloelezwa, n a Ya n o t e g e m e w a kutokana na i t ikadi . “Tradi t ions” n i k i tu muhimu katika uteuzi wa viongozi, na katika Muungano ni lazima kujenga itikadi ya kuteua viongozi kutoka pande zote mbili. Watetezi wa nchi zao ni lazima kusimamia hilo. Lazima kuwe na “Deliberate at tempt” Jaribio la makusudi na la dharura kutoa zamu kwenye uongozi, ilimradi watoteuliwa wakidhi sifa z inotegemewa. Hayo yamefanyika katika historia ya Muungano wetu, na sioni kwanini iwe mwiko

Inaendelea Uk. 14