-
MAONESHO YA KWANZA (1) YA
KIMATAIFA YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA
Taarifa ya Maonesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya
Mwafrika Tarehe 16 23 Novemba 2014, Viwanja vya
Mnazi mmoja Dar es Salaam, Tanzania Afrika Mashariki
JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA LTD
Imeandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Ltd
S.L.P 90447
Dar es Salaam, Tanzania.
Simu ya Mkononi: + 255756147487
Barua pepe: [email protected]
-
1
Yaliyomo.
uk
1.0 UTANGULIZI
.................................................................................................................................
2
2.0 MALENGO MAKUU YA MAONESHO
.....................................................................................
4
3.0 MAANDALIZI YA MAONESHO
......................................................................................................
6
3.1 Uhamasishaji wa Ushiriki
...................................................................................................................
7
3.2 Uchapishaji wa Majarida na Mabango ya Kunadi Maonesho
.......................................................... 8
3.3 Uundwaji wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi
..................................................................................
8
4.0 UDHAMINI WA MAONESHO
....................................................................................................
9
5.0 WASHIRIKI WA MAONESHO
.................................................................................................
10
6.0 ULINZI NA USALAMA WAKATI WA MAONESHO
............................................................ 10
6.1 VIONGOZI NA WAGENI MASHUHURI WALIOTEMBELEA MAONESHO
........................................... 10
7.0 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE
...............................................................................
11
8.0 WALIOCHANGIA MAFANIKIO YA MAONESHO
..............................................................
12
9.0 KUFUNGA
....................................................................................................................................
13
10.0 HITIMISHO
..................................................................................................................................
14
Kiambata:....Ripoti ya fedha
-
2
JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA LIMITED
RIPOTI YA MAONESHO YA KWANZA YA KIMATAIFA YA
TIBA ASILI YA MWAFRIKA, 2014
1.0 UTANGULIZI
Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika
yalifanyika
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, vilivyopo kwenye Manispaa ya
Ilala
Mkoani Dar es Salaam, Tanzania kuanzia tarehe 16 23 Novemba,
2014.
Lengo lilikuwa ni kuimarisha ushirikiano wa huduma ya Tiba Asali
na Tiba
ya kisasa katika kuimarisha huduma ya Afya ili kuleta Maendeleo
endelevu
na kutengeneza mtandao wa huduma ya Tiba Asili, Kutoa Elimu kwa
Umma
kuhusu Tiba Asili, Utafiti na uboreshaji wa dawa Asili kwa
kuzingatia sera,
Sheria, kanuni na miongozo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala na
kuyafanya
Maonesho haya kuwa ya Kimataifa na kufanyika kila mwaka.
Maonesho yalifunguliwa rasmi tarehe 17 Novemba, 2014 na
Mheshimiwa
Dkt Seif Seleman Rashid (Mb), Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii
akiwakilishwa na Ndugu Dunford Makala, Kamishna wa Ustawi wa
Jamii
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii. Pamoja naye alikuwepo Dr
Liggyle
Vumilia, Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii.
Wageni wengine walioambatana na Mgeni Rasmi walikuwa kama
ifuatavyo:
Bi Lucy Samweli, Mfamasia wa Idara ya Tiba, sehemu ya Tiba Asili
na Tiba
Mbadala Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi Gertrude
Ngweshemi,
Afisa Mwandamizi Ukuzaji Masoko na Huduma za Ukuzaji Biashara
toka
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na
wageni
wengine waalikwa. Mgeni Rasmi alipata fursa ya kutembelea
mabanda ya
-
3
washiriki wa Maonesho na kupata maelezo kuhusu dawa, bidhaa,
huduma na
matibabu mbalimbali yanayotolewa na Washiriki wa Maonesho
hayo.
Baada ya hapo ndugu Boniventura Mwalongo Mwenyekiti wa Kamati
ya
Maandalizi alisoma Ujumbe wa Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya
Tiba
Asili ya Mwafrika. Katika ujumbe wake Mwenyekiti alimkaribisha
Mgeni
rasmi, wageni waalikwa na washiriki wa Maonesho katika maonesho
haya
muhimu ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika ambayo yalifanyika
kwa
mara ya kwanza hapa nchini.Nakufanya kuwa tukio la kihistoria
katika nchi
yetu, Pia aliwashukuru wadau mbalimbali waliofanikisha kufanyika
kwa
Maonesho hayo.Kisha akamkaribisha Mgeni rasimi, kwa hotuba ya
ufunguzi,
Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwanza alitoashukrani kwa
kuwa
mgeni rasmi wa kwanza wa Maonesho haya Makubwa ya Biashara
ya
Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika ambayo yamefanyika kwa mara
ya
kwanza hapa nchini kwetu. Katika hotuba yake alipongeza Jukwaa
la Tiba
Asilia Tanzania kwa kuanzisha Maonesho ya Tiba Asili ambayo
yataleta
Manufaa makubwa kwenye sekta ya Afya ikizingatiwa kuwa Tiba
Asilia
husaidia wananchi wengi Mijini na Vijijini, alitoa rai kwa
Jukwaa la Tiba
Asilia Tanzania kuyaendeleza Maonesho haya kufikia kiwango cha
Kimatifa
na kuyafanya Maonesho hayo kila Mwaka.Na aliwataka washiriki
kutumia
fursa nzuri waliyoipata kubadilishana uzoefu kutoka kwa
washiriki wanje ya
nchi na Aliwaambia wananchi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya
na
Ustawi wa Jamii inaitambua huduma ya Tiba Asili na Tiba
Mbadala.
Pia alitoa pongezi kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania,(TanTrade) kwa kutambua umuhimu wa Tiba Asili na Tiba
Mbadala
hapa nchini na kutoa ushirikiano wa hali ya juu katika
kuhakikisha maonesho
haya ya Kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika
yanafanyika katika
-
4
ngazi za Kimataifa kwa kutumia utaalam walionao. Pia aliahidi
kuwa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii iko tayari kutoa ushirikiano thabiti
ili
maonesho haya yafanyike sambamba na maadhimisho ya siku ya Tiba
Asili
ya Mwafrika na kushirikisha wadau wengine.
Aidha aligusia changamoto zilizopo katika Tiba Asili,na kwamba
Serikali
inasisitiza waganga na watoa huduma wote wa Tiba Asili na Tiba
Mbadala
kufuata sheria Na. 23 ya mwaka 2002 kama usajili wa waganga na
vituo
vyao, kutojihusisha na Uzuzaji, Uchawi, ushirikina na upigaji wa
ramli, vile
vile na matangazo ya kwenye redio, Televisheni na magazeti
pamoja na
uwekaji wa mabango barabarani.
Kauli Mbiu ya Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya
mwafrika
Mwaka 2014 ilikuwa Kuimarisha Ushirikiano wa Tiba Asili na Tiba
ya
Kisasa katika Kuimarisha Huduma ya Afya Afrika, Kauli Mbiu
hii
ilichaguliwa Mahsusi ili kuhamasisha uboreshaji wa huduma ya
Tiba Asili na
kuziingiza Dawa za Asili kwenye utoaji wa huduma za Afya ili
kuleta
maendeleo endelevu katika sekta ya Afya nchini Tanzania.
2.0 MALENGO MAKUU YA MAONESHO
Lengo kuu la Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asilia
ya
Mwafrika ni kuhamasisha uboreshaji na uendelezaji wa utoaji
huduma ya
Tiba Asili katika Sekta ya Afya kwa kuzitangaza, kuboresha na
kuziingiza
dawa za asili kwenye mfumo wa kisasa wa utoaji huduma za Afya na
kutoa
Elimu kwa umma kuhusu Tiba Asili na Utafiti kwa kuzingatia Sera,
Sheria,
Kanuni na Miongozo ili kuleta maendeleo endelevu katika Sekta ya
Afya
nchini, Afrika na duniani kwa ujumla.
-
5
Maonesho ya Kimataifa ya Tiba Asili yalilenga kutoa fursa
zifuatazo:-
i. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kuwa Jukwaa la kuwawezesha
Washiriki wa maonesho ya kwanza kuimarisha ushirikiano wa
Tiba
Asili na Tiba ya kisasa, na Watowa huduma wa Tiba Asili,
Watafiti
wa dawa Asili, Wavumbuzi, Wasindikaji wa Dawa Asilia
kuonesha
bidhaa na huduma wanazotoa kwa jamii.
ii. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Kuwa jukwaa la kuunganisha
pamoja
Asasi, Taasisi, Kampuni, na Watu kutoka nchi mbalimbali
kukutana
na kufahamiana kwa lengo la kutengeneza mitandao ya
Kibiashara,
kujifunza, kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya
kimaendeleo
katika Tiba Asilia kwa lengo la kuboresha huduma ya afya.
iii. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kuwa jukwaa la Kutoa taarifa
sahihi
kuhusu umuhimu wa TIBA ASILI NA TIBA MBADALAili
kubadilisha mtazamo wenye kasumba potofu uliotokana na
kutawaliwa na wakoloni na ukoloni mamboleo ambao umesinyaza
Tiba Asili na kuhusishwa na Imani za kichawi na Ushirikina
hivyo
kupelekea kudharauliwa kwa watabibu wa Tiba Asili. hivyo
maonesho yanatusaidia kubadilisha na kupanua wigo wa ufahamu
katika taaluma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala
iv. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Kuwa Jukwaa la kukutanisha
watoa na
wapokea huduma , wauzaji na wanunuzi wa bidhaa za Asili
jambo
litakalowezesha Washiriki wa Maonesho kupata mrejesho wa
moja
kwa moja kutoka kwa watumiaji huduma na bidhaa (wahitaji)
wao
kuhusu maoni na mtazamo wao kutokana na huduma na bidhaa
wanazozitoa. Jambo hili litamsaidia mzalishaji au mtoa huduma
kujua
-
6
ni wapi panahitaji marekebisho na maboresho katika kutoa huduma
au
bidhaa zake kwa Jamii.
v. Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Kuwa Jukwaa la Kujenga mtandao
wa
ushirikiano na kupeana ujuzi mbalimbali kwa kuwa kila mmoja
ana
ujuzi wa pekee ambapo kwa pamoja yatapatikana matokeo yenye
ufanisi na Kuchochea fursa za Utafiti wa maendeleo.
3.0 MAANDALIZI YA MAONESHO Maandalizi ya Maonesho yalifanyika
chini ya uratibu wa Jukwaa la Tiba
Asilia Tanzania ambapo Vikao vinne (4) vya Maandalizi
vilifanyika. Vikao
hivyo ni:
Kikao cha Kwanza
Kikao cha Mkutano Mkuu chenye wajumbe 56 kutoka katika vyama 12
vya
Watabibu wa Tiba Asili. Kikao hiki kilijadili masuala ya
kuandikisha
Jukwaa la Tiba Asili kisheria, na kuweka bayana maandalizi ya
Maonesho
ya Tiba Asilia ya Mwafrika.
Kikao cha Pili
Kikao cha pili kilikuwa cha wajumbe 20, katika vyama 12 vya Tiba
asili kila
chama kilitoa mjumbe mmoja na wajumbe 8 kutoka Kamati Kuu. Kikao
hiki
kiliazimia kupanga utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano Mkuu,
Kikao cha Tatu
Kikao cha tatu kilikuwa na wajumbe 11 kikiwa na dhumuni la
kufuatilia na
kufanikisha maazimio ya vikao vyote vya juu na kutekeleza
maazimio hayo.
Kikao cha Nne
Kikao cha nne kilikuwa cha ushirikiano wa wataalam kutoka Jukwaa
la Tiba
Asili Tanzania, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na
Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambacho pamoja na
maazimio
-
7
mengine kiliwachagua viongozi wa kamati ya wataalam kwa
maandalizi ya
Maonesho ambapo Boniventura Mwalongo aliyekuwa Mratibu Jukwaa
la
Tiba Asili Tanzania alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati
ya
Maandalizi ya Maonesho, Bi Lucy Samweli Mfamasia wa Idara ya
Tiba,
sehemu ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii
alichaguliwa kuwa Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho na
Bi
Gertrude Ngweshemi Afisa Mwandamizi, Ukuzaji Masoko, na Huduma
za
Ukuzaji Biashara toka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania
(TANTRADE) alichaguliwa kuwa Mhazini wa kamati ya Maandalizi
ya
Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika.
Maazimio
mengine yalikuwa kuandaa bajeti ya maonesho, Mawasiliano pamoja
na
kutoa Utaalamu katika kufanikisha Maonesho ya Kwanza ya
kimataifa ya
Tiba Asili ya Mwafrika, kuyasajiri na kuyaingiza katika kalenda
ya
Maonesho nchini.
KATIKA MAANDALIZI, MAMBO YAFUATAYO YALIFANYIKA;
3.1 Uhamasishaji wa Ushiriki Maandalizi yalianza kwa
uhamasishaji wa Serikali na Taasisi zake,
Taasisi za Kimataifa, Asasi za Kijamii na Kimataifa, pamoja na
wadau
kushiriki katika Maonesho hayo. Mbinu zilizotumika kuhamasisha
ni
pamoja na kufanya kampeni ya mlango kwa mlango (door to door)
kwa
kuyatembelea makampuni mbali mbali, Jumuiya zao na Balozi za
nchi
za nje zilizopo Tanzania, kuwasiliana na Balozi za Tanzania
zilizo nchi
za nje, kutuma barua pepe na barua za kawaida za mialiko pamoja
na
kutumia vyombo vya habari. Hata hivyo, matokeo ya
uhamasishaji
-
8
hayakuwa na matunda tarajiwa kwakuwa maandalizi yamefanyika
katika
muda mfupi sana.
Aidha, iliandaliwa kampeni ya matangazo kupitia mitandao ya
Kijamii
na vyombo mbalimbali vya habari kwa kushirikiana na
makampuni
mengine yaliyoshiriki katika Maonesho. Wawakilishi
mbalimbali
walikwenda kwenye vituo vya televisheni na redio na kutoa
taarifa na
maelezo kuhusiana na Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba
asili
na Tiba mbadala.
3.2 Uchapishaji wa Majarida na Mabango ya Kunadi Maonesho Ili
kuimarisha utoaji taarifa za Maonesho hayo kwa umma majarida,
vipeperushi na mabango (Promotional Material) ya kunadi
Maonesho
yaliandaliwa na kuchapishwa.
3.3 Uundwaji wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi Kamati ya
Kitaifa iliundwa ikijumuisha Mjumbe kutoka Jukwaa la Tiba
Asili Tanzania, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na
TanTrade
ambapo Boniventura Mwalongo Mratibu Jukwaa la Tiba Asili
Tanzania
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
Maonesho,
Bi Lucy Samweli Mfamasia wa Idara ya Tiba, sehemu ya Tiba Asili
na
Tiba Mbadala Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii alichaguliwa
kuwa
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Maonesho na Bi Gertrude
Ngweshemi Afisa Mwandamizi, Ukuzaji Masoko, na Huduma za
Ukuzaji Biashara toka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania
(TANTRADE) alichaguliwa kuwa Mhazini wa kamati ya Maandalizi
ya
Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika kwa
ajili
ya zoezi zima la kuratibu, kusimamia na kuandaa taratibu zote
za
Maonesho ili kuhakikisha kuwa maandalizi yanakwenda ipasavyo
na
-
9
yanakuwa shirikishi. Kamati hii ilifanya kazi kutokana na
maazimio
yaliyotolewa na Mkutano Mkuu pamoja na Kamati Kuu.
4.0 UDHAMINI WA MAONESHO
Wadhamini na Wafadhili mbalimbali walijitokeza kuunga mkono
Maonesho
ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika, udhamini huo
ulichangia
kwa kiasi kikubwa kufanikisha Maonesho hayo. Ufadhili huu
ulitolewa na
Wadau wafutao: - (Wilfred Jumanne Mwazini) kutoka Kituo cha
Huduma ya
Uponyaji, JKBRS International, Boresa Traditional Medicine
Company
Limited, Adulkharim Mambo Saleh na Cocacola Kwanza Limited.
TanTrade
pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zilitoa ufadhili wa
utaalam
(technical assistance).
Picha za matukio mbalimbali
zikionyesha sehemu ya ufungaji wa
maonesho. Ndugu Simba A . Simba
muwakilishi wa mgeni rasmi katika
kufunga maonesho ya Kwanza ya
Kimataifa ya Tiba Asili ya mwafrika
akiwa na Viongozi mbalimbali wa
jukwaa la Tiba Asili Tanzania.
-
10
5.0 WASHIRIKI WA MAONESHO
Jumla ya washiriki 58 walishiriki katika Maonesho ya Tiba Asili
ya
Mwafrika hii ikiwa ni pungufu kulinganisha na matarajio ya
kamati ya
maandalizi ambapo kamati ilitarajia kuwa na washiriki wapatao
100.
Upungufu huu ulitokana muda mfupi wa maandalizi ingawa juhudi za
ziada
za kuhamasisha zilizofanyika. Washiriki walikuwa ni pamoja na
Watabibu
wa Tiba Asili, watengenezaji wa Dawa Asili,Wakunga wa Tiba
Asili,
Kampuni za Dawa Asili na Vipodozi vya Dawa Asili, Wasambazaji
wa
Vifaa Tiba Asili na Tiba Mbadala, Watengenezaji wa Vyakula
Asili, Kliniki
za Tiba Asili na Tiba Mbadala pamoja na kazi za
mikono(sanaa).
6.0 ULINZI NA USALAMA WAKATI WA MAONESHO
Masuala ya Ulinzi, Usalama yalisimamiwa na Jeshi la Polisi
kwa
kushirikiana na Walinzi wa MG Manispaa ya Ilala ambao walilipwa
malipo
kwa siku.
6.1 VIONGOZI NA WAGENI MASHUHURI WALIOTEMBELEA
MAONESHO.
Baadhi ya Viongozi na Wageni Mashuhuri waliotembelea Maonesho
ni
kama wafuatao: -
i. Nd. Dunford Makala Kamishna wa Ustawi wa Jamii Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye alimwakilisha Mgeni Rasmi
Mhe.
Dkt Seif Seleman Rashidi (Mb) Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii
katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho.
ii. Dr Liggyle Vumilia, Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, Wizara ya Afya
na
Ustawi wa Jamii.
-
11
iii. Nd. Masalida Zephania, Afisa Maendeleo ya vijana kutoka
Ofisi ya
mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam.
iv. Mhe. Kingunge Ngombale Mwiru, aliyekuwa Mjumbe wa Bunge
Maalum la Katiba aliwakilisha Tiba Asili na Mlezi wa Tiba
Asili.
v. Nd Josephat Rweyemam Mwenyekiti wa CISO Afrika Mashariki.
vi. Eng. Armin Zedlitschka kutoka Ujerumani na
vii. Eng. Siliwat Jodelist kutoka Ujerumani.
viii. Ndugu Simba Abdulrahman Simba Tabibu Asili
aliyemuwakilisha
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Abdallah O. Kigoda
(Mb)
katika kufunga Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili
ya
Mwafrika.
7.0 CHANGAMOTO NA UFUMBUZI WAKE
Yafuatayo ni mapungufu yaliyojitokeza katika maandalizi na
usimamizi wa
Maonesho ya kwanza ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika na
hatua za
ufumbuzi wake;
7.1 Kulikuwa na mwitikio mdogo wa washiriki hivyo kupelekea
Maonesho
kuhudhuriwa na washiriki wachache sana kinyume cha
matarajio.
Washiriki hawakuwa na uelewa wa umuhimu wa kushiriki
Maonesho
kwa ajili ya kutangaza bidhaa na huduma zao. Hii inatokana na
ukweli
kuwa, maandalizi ya Maonesho yalifanyika kwa muda mfupi sana,
hivyo
mawasiliano hayakuwafikia walengwa wengi katika muda
muafaka.
Katika Maonesho ya mwaka huu 2015 Kamati ya Maandalizi
inashauriwa kuanza maandalizi mapema na taarifa itolewe kwa
washiriki
kuhusu umuhimu wa kushiriki katika Maonesho kama njia muhimu
ya
kutangaza bidhaa na huduma zao pamoja na manufaa mengine.
-
12
7.2 Mahudhurio ya watembeleaji hayakuwa yakuridhisha kutokana
na
Maonesho kutofanyiwa matangazo mapema. Matangazo
yaliyofanyika
yalifanyika katika muda mfupi na hiyo haikutosha kuwafikia
watembeleaji wa kutosha. Maonesho yajayo Kamati ya
Maandalizi
inashauriwa ihakikishe matangazo yanafanyika mapema ili
kuwafikia
wananchi wengi.
7.3 Jukwaa la Tiba Asili Tanzania liweke nguvu katika
kujitangaza, kuwa na
machapisho yanayoelimisha na kuendana na wakati na yenye ubora
wa
kuvutia matumizi bora na salama ya Tiba Asili na Dawa Asili.
Mikakati
ifanyike ya kutoa elimu kwa wananchi na wadau Tanzania
kuhusu
shughuli za Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa kupitia machapisho,
radio,
television, magazeti na midahalo mbalimbali. Watanzania na
Ulimwengu
wanahitaji kupata uelewa kwa kuwa kwa sasa wanaichukulia Tiba
Asili
ni ushirikina, ulamari, na uchawi na hivyo imesababisha baadhi
ya watu
waichukie na kutoipa kipaumbele.
8.0 WALIOCHANGIA MAFANIKIO YA MAONESHO
Jukwaa la Tiba Asili Tanzania Limited tunatoa shukrani za dhati
kwa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wizara ya Viwanda na
Biashara,
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ofisi ya
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi
mbalimbali, Vyombo vya Habari, Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Idara ya
Habari Maelezo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Bunge la
Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, pamoja
na
Taasisi kutoka sekta ya Umma na sekta binafsi zilizochangia
kufanikisha
Maonesho haya.
-
13
Vilevile, kwa namna ya pekee Jukwaa linapenda kutambua
mchango
mkubwa wa Nd Wilfreid Jumanne Mwazini wa Kituo cha Huduma ya
Uponyaji, JKBRS International, Boresa Traditional Medicine
Company
Limited, Tabibu Abdulkarim Mambo Saleh Tiba Asili za kisunah,
Coca-
Cola Kwanza Ltd waliodhamini shughuli mbalimbali za
Maonesho.
9.0 KUFUNGA
Maonesho yalifungwa saa 11:30 jioni na Waziri wa Viwanda na
Biashara
Dkt. Abdallah O. Kigoda (MB) ambaye kutokana na sababu zilizo
nje ya
uwezo wake.Aliwakilishwa na Ndg. Simba Abdulrahman Simba
Tabibu
Asili na Mjumbe wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania, ambapo
alipofika katika
viwanja vya Maonesho alipokelewa na Uongozi wa Jukwaa na Mafisa
wa
Serikali kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka
ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na kisha
alitembelea
Ngoma ya Asili ya Wamakonde ya kikundi cha Mchabwede, na Mabanda
ya
washiriki, alipomaliza alikaribishwa Jukwaa kuu akapokea risala
ya
washiriki,Ujumbe wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Tiba Asili Tanzania
na
Arafa ya Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Maonesho. Kwanza
alitoa
shukrani na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata fursa ya
kipekee ya
kumuwakilisha Mgeni rasmi kufunga Maonesho ya kwanza ya
Kimataifa ya
Tiba Asili ya Mwafrika, pili akawashukuru Viongozi wa Jukwaa la
Tiba
Asili Tanzania na Kumtakia kheri Mhe. Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa
Tanzania Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa akipata matibabu
nchini
Marekani ili apone haraka na kuendelea katika ujenzi wa Taifa,
pia
aliwataka washiriki wote kwenda kuboresha huduma na vituo vyao
ili
kuendelea kuiletea heshima huduma ya Tiba Asili na kuziingiza
Dawa Asili
kwenye utoaji wa huduma za Afya ili kuleta Maendeleo endelevu
katika
huduma za Afya nchini. Alitoapongezi kwa kuandaa Jukwaa la Tiba
Asili
Tanzania pia alitoapongezi kwa wadau waliohusika kwa maandalizi
na
ushiriki wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Mamlaka ya
Maendeleo ya
Biashara Tanzania (TANTRADE) kwaniaba ya Waziri wa Viwanda
na
Biashara. Aidha alisema kwamba ni matarajio yake kwamba Maonesho
haya
ambayo niyakwanza kufanyika nchini yatasajiliwa rasmi ili
yaweze
kufanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya siku ya Tiba
Asili ya
Mwafrika inayoadhimishwa 31 agosti kila mwaka katika nchi 46
barani
-
14
Afrika. Kwani yataleta tija kwa Watanzania hususani wadau wa
Tiba Asili
na Tiba Mbadala ambao wamekuwa na shahuku yakuona wanakuwa
na
maonesho kama haya na kuonesha bidhaa na huduma zao za
Asili.
Alisema hivyo kwa sababu pamoja na huduma ya Tiba Asili
katika
maonesho haya, pia kuna kazi za mikono ambazo zinawakilisha
bidhaa asili
za hapa nchini. Fursa nzuri na ya kipekee kabisa hivyo msisite
kuitumia
endapo itatokea tena hapo mwakani. Aliahidi , Wizara ya Viwanda
na
Biashara ipo tayari kutoa mchango wa hali na mali kuona Sekta
hii inakuwa
na kuboreshwa ipasavyo na hivyo kuhudumia soko la ndani, la
kikanda na
hata la kimataifa. Na aliwasilisha shukrani za Mhe Dkt. Abdallah
O. kigoda
(MB) kupata taarifa mapema kabisa na kuahidi Wizara
itashirikiana na
Jukwaa la Tiba Asili Tanzania ipasavyo hapo mwakani. Aidha
amekubali
ombi la kuwa Barozi wa Tiba Asili Tanzania, nakuomba kukutana
na
uongozi wa Jukwaa la Tiba Asili kupata ufafanuzi juu ya
majukumu
yanayoendana na Ubarozi wa Tiba Asili.
Aidha alisema anatambua umuhimu wa Tiba Asili na changamoto
zinazo
ikabili Tiba Asili nchini. Na kuhimiza utoaji wa elimu endelevu
kwa Umma
kupitia machapisho, vyombo vya Habari, semina na Makongamano.
Pia
alilitaka Jukwaa la Tiba Asili kuitangaza Tanzania kimataifa kwa
Tiba Asili
nzuri tulizonazo.
Kuhusu Viwanda vya kusindika dawa za Tiba Asili nchini vyenye
kiwango
cha kimataifa alisema nitawaomba viongozi wa Jukwaa watembelee
Ofisini
kwake ilikuongea zaidi juu ya maombi yote haya ikiwa nipamoja
na
kuchochea uwepo wa viwanda kwajili ya dawa Asili nchini.
MWISHO
Ndg Simba Ablahman Simba alifunga rasmi Maonesho ya kwanza
ya
kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika na aliahidi kufikisha
risala,Arafa na
Hotuba kwa Mhe. Dkt Abdallah O. Kigoda Waziri wa Viwanda na
Biashara.
10.0 HITIMISHO Tunaomba kuwasilisha ripoti ya Maonesho ya kwanza
ya Kimataifa ya Tiba
Asili ya Mwafrika yaliyofanyika tarehe 16-23 Novemba 2014
Kiambata Ripoti ya Fedha
-
15
Picha ya Pamoja ya baadhi ya washiriki na viongozi wakati wa
kufunga maonesho ya kwanza ya kimataifa yaTiba Asili ya
mwafrika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam, tanzania
Bonivetura Ferdinandi Mwalongo
MWENYEKITI JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA LIMITED.
Februari, 2015