JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA 4 MWAKA 2010 Dar Es Salaam Juni, 2011 www.JamiiForums.com
137
Embed
Rasimu Ya 2 Ya Taarifa Ya Utafititi-Ufaulu K4 2010[1]
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI NA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA YA UTAFITI
KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO
CHA 4 MWAKA 2010
Dar Es SalaamJuni, 2011
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
i
SHUKRANI
Utafiti huu umehusisha wataalamu mbalimbali katika hatua za kubuni, kutayarisha,
kukusanya, kuchambua takwimu na kuandika ripoti. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
kwa pamoja zinawashukuru wataalamu wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine
katika hatua mbalimbali za utafiti huu. Pia tunawashukuru wadau wote wa elimu
waliohusika katika kutoa taarifa za utafiti. Aidha shukrani za pekee ziiendee Wizara ya
Fedha kwa kufanikisha mchakato mzima wa utafiti.
Shukrani pia zimwendee Bwana Jumanne Abdallah Sagini, Naibu Katibu Mkuu -
TAMISEMI kwa kuwa msimamizi mkuu wa kazi hii. Aidha, shukrani za dhati ziwaendee
wajumbe wa kikundi kazi kilichohusika katika utafiti huu kuanzia hatua za awali hadi
mwisho. Wajumbe hao ni:
JINA TAASISI WADHIFA
1. Francis M. Liboy OWM-TAMISEMI - Mwenyekiti
2. Lawrence John Sanga WEMU - Katibu
3. Fred Davidson Sichizya WEMU - Mjumbe
4. Abdallah Shaban Ngodu WEMU - Mjumbe
5. Hadija Mchatta Maggid WEMU - Mjumbe
6. Paulina Jackson Mkoma WEMU - Mjumbe
7. Elia Kalonzo Kibga WEMU - Mjumbe
8. Paulina Mbena Nkwama OWM-TAMISEMI - Mjumbe
9. Makoye J.N. Wangeleja TET - Mjumbe
10.Edward Simon Haule NECTA - Mjumbe
Aidha shukrani zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa TET kwa kugharamia vikao vya kikundi
kazi kupitia huduma ya ukumbi na chakula wakati kikiwa Dar-es-salaam.
Prof. Hamisi O. DihengaKatibu Mkuu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
ii
DIBAJIRipoti hii ya utafiti inahusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato
cha 4 mwaka 2010. Utafiti huu umefanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Waziri Mkuu-
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi (WEMU) ikihusisha Taasisi ya Elimu Tanzania na Baraza la Mitihani la
Tanzania.
Utafiti huu ulilenga kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa
Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010. Pamoja na baadhi ya sababu hizo kuwa dhahiri kwa
wadau wa elimu Serikali iliamua kufanya utafiti ili kuweza kubaini chanzo na ukubwa wa
tatizo. Utafiti huu unatoa mapendekezo kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu na ubora wa
elimu ya sekondari.
Ripoti hii inaonesha kwamba yapo masuala ya kimfumo, mfano mapungufu katika
usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini ambayo yanaweza kutatuliwa na serikali moja
kwa moja. Aidha, yapo masuala yanayohusu kujenga uwezo kwa wasimamizi na
watekelezaji wa mitaala, kuhakikisha upatikanaji wa vifaa bora na vya kutosha vya
kufundishia na kujifunzia na uboreshaji wa majengo na miundombinu ambayo
yanahitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali na wabia wake.
Matokeo ya utafiti huu ni muhimu kwa serikali, washirika wa maendeleo na wadau
mbalimbali wa elimu kwani inaonesha chanzo na ukubwa wa matatizo na changamoto
zinazojitokeza na inatoa mapendekezo ya namna ya kuyatatua na kukabiliana na
changamoto za kielimu. Hivyo sote kwa pamoja yatupasa tujipange na kuelekeza nguvu
zetu kupitia mipango yetu ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ili tuweze
kuyamaliza matatizo haya na kuinua ubora wa elimu nchini.
Ninawaomba wadau wa elimu nchini kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ili kuweza
kupiga hatua katika utekelezaji wa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Serikali inayo
nia ya dhati ya kutekeleza mapendekezo haya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu
ya sekondari nchini.
Mh. Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB)Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
iii
YALIYOMO
SHUKRANI............................................................................................................................................. i
DIBAJI.................................................................................................................................................... ii
VIFUPISHO............................................................................................................................................ v
MUHTASARI PEMBUZI ..................................................................................................................... vi
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI................................................................................................ 15
1.1. Usuli ....................................................................................................................................... 151.2. Hoja ya Kufanya Utafiti ....................................................................................................... 181.3. Malengo ya Utafiti................................................................................................................ 191.4. Maswali ya Utafiti................................................................................................................. 191.5. Muundo wa Ripoti ................................................................................................................ 20
SURA YA PILI: MAPITIO YA MAANDIKO.................................................................................... 21
2.1 Sera na Mipango ya Elimu.................................................................................................. 212.2 Mipango na Mikakati ya Elimu ........................................................................................... 222.3 Uongozi katika Elimu ........................................................................................................... 232.4 Usimamizi na Uendeshaji.................................................................................................... 242.5 Ugharamiaji wa Elimu ......................................................................................................... 252.6 Ufuatiliaji na Tathimini ya Elimu........................................................................................ 27
SURA YA TATU: MWONGOZO WA UTAFITI............................................................................... 55
3.1. Utangulizi .............................................................................................................................. 553.2. Mbinu ya Utafiti .................................................................................................................... 553.3. Eneo la Utafiti ....................................................................................................................... 563.4. Uchaguzi wa Sampuli .......................................................................................................... 563.5. Zana za Utafiti ...................................................................................................................... 573.6. Utaratibu Uliotumika Kufanya Utafiti ................................................................................ 58
3.6.1. Kukusanya Taarifa Kutoka Ngazi ya Taifa ................................................................ 583.6.2. Kukusanya Taarifa Kutoka katika Kanda, Mkoa na Halmashauri .......................... 583.6.3. Kukusanya Taarifa Kutoka Shuleni na katika Jamii ................................................. 59
3.7. Uchambuzi wa Data............................................................................................................. 593.8. Maadili ya Kufanya Utafiti ................................................................................................... 59
SURA YA NNE: MATOKEO YA UTAFITI NA UCHAMBUZI WA DATA................................... 61
4.1. Utangulizi .............................................................................................................................. 614.2. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu .................................................................................. 63
4.2.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu katika Ngazi Mbalimbali................................. 634.2.2. Mmomonyoko wa Maadili Katika Jamii...................................................................... 684.2.3. Mwamko Duni wa Jamii Katika Elimu ........................................................................ 694.2.4. Siasa Kuingilia Masuala ya Kitaalam ya Kielimu....................................................... 694.2.5. Ufinyu wa Bajeti ya Elimu ........................................................................................... 704.2.6. Maoni Kuhusu Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................. 714.2.7. Mapendekezo kwa Walioshindwa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 Mwaka 2010 75
4.3. Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala ............................................................................. 764.3.1. Utayarishaji wa Mitaala................................................................................................ 76
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
iv
4.3.2. Uwepo wa Mihtasari Shuleni na Vyuoni .................................................................... 774.3.3. Utekelezaji wa Mtaala .................................................................................................. 784.3.4. Mafunzo Kabilishi kwa Ajili ya Mtaala Ulioboreshwa ............................................... 794.3.5. Maoni Kuhusu Utekelezaji wa Mtaala ........................................................................ 79
4.4. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa........................................................................... 804.4.1. Utungaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 ....................................................... 804.4.2. Usambazaji na Usimamizi wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4.......................... 824.4.3. Usahihishaji wa Mtihani ya Taifa wa Kidato cha 4 .................................................. 834.4.4. Mchango wa Alama za Mazoezi Endelezi (Continuous Assessment-CA) Katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4................................................................................ 854.4.5. Upangaji wa Madaraja Unaofanywa na NECTA ....................................................... 864.4.6. Matumizi ya Miongozo na Nyaraka Mitihani ............................................................. 884.4.7. Athari za Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2............................................................ 884.4.8. Maoni Kuhusu Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa ......................................... 90
4.5. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ................................................... 934.6. Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu............................................................... 97
4.6.1. Mfumo wa Utayarishaji wa Walimu............................................................................... 974.6.2. Ajira na Upangaji wa Walimu ..................................................................................... 984.6.3. Uwepo wa Walimu katika Shule .................................................................................. 1004.6.4. Maoni ya Kuimarisha Ubora na Uwepo wa Walimu .............................................. 106
4.7. Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia ........................................................ 108
SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO .................................................................. 115
5.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu ................................................................................ 1155.2. Utekelezaji wa mitaala ...................................................................................................... 1185.3. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa......................................................................... 1195.4. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu ................................................. 1215.5. Mfumo wa utayarishaji wa walimu.................................................................................. 1215.6. Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia .......................................................................... 124
Kiambatisho Na. 3.1: Maeneo Yaliyohusika katika Utafiti ...................................................... 130Kiambatisho 3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa ........................................... 132Kiambatisho 4.1 – Takwimu za ukaguzi wa shule ( 2007–2010) katika Halmashauri zilizofanyiwa utafiti....................................................................................................................... 133
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
v
VIFUPISHOBEST Basic Education Statistics in Tanzania CA Continuous Assessment (Mazoezi Endelezi) CG Capitation Grant CDTI Community Development Training InstituteCWT Chama cha Walimu Tanzania EFA Education for All EMAC Educational Materials Approval Committee ETP Education and Training Policy FDC Folk Development CollegeFTC Full Technician Certificate GBS General Budget Support GDP Gross Domestic Product GER Gross Enrolment Rate MKUKUTA Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania MMES Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari MEMK-WSM Mkakati wa Elimu ya Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Shule za Msingi MMEM Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi MMEMWA Mkakati wa Menejimenti na Maendeleo ya Walimu MoEVT Ministry of Education and Vocational Training MWAKEM Mafunzo ya Walimu Kazini Elimu ya Msingi MTEF Medium Term Expenditure Framework MDGs Milemium Development Goals (Malengo ya Maendeleo ya Milenia) MUCE Mkwawa University College of Education NCDF National Curriculum Development Framework NECTA National Examinations Council of Tanzania OC Other Charges OUT Open University of Tanzania OWM-TAMISEMI Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa PETS Public Expenditure Tracking System SEDP Secondary Education Development Programme TAMONGSCO Tanzania Association of Managers of Non Government Schools and Colleges TEHAMA Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TET Taasisi ya Elimu Tanzania TEN/MET Tanzania Education Network/Mtandao wa Elimu Tanzania TES Tanzania Elimu Supplies TIE Tanzania Institute of Education TSD Teachers Service Department (Idara ya Huduma kwa Walimu) UKIMWI Ukosefu wa Kinga Mwilini URT United Republic of Tanzania TRC Teachers Resource Centre UPE Universal Primary Education (Elimu ya Msingi kwa Wote) WEMU Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
vi
MUHTASARI PEMBUZI
Utoaji wa elimu nchini Tanzania unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo (ETP) ya
mwaka 1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya
Taifa 2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya
Maendeleo ya Milenia (MDGs).
Katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu
ilianzishwa. Aidha, Programu za Mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na
Sekondari (MMES) zilianzishwa kutekeleza program ya sekta. Mafanikio ya MMEM
yameongeza mahitaji ya upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango wa
Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu la
kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-
2014) imeweka kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari.
Kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka kila
mwaka kwa mfululizo wa miaka minne 2007 (90.3%), 2008 (83.6%), 2009 (72.5%) na
2010 (50.4%). Kutokana na hali hiyo, Serikali iliamua kufanya utafiti ili kubaini sababu
za kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na tatizo
hilo.
Utafiti huu ulifanyika katika mikoa 11, ikiwa ni mmoja kwa kila Kanda ya Elimu. Aidha,
jumla ya Halmashauri 22 zilihusishwa, mbili kutoka kila mkoa ikiwa moja iliyofanya
vizuri na nyingine iliyofanya vibaya katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4. Kwa kila
Halmashauri jumla ya shule sita zikiwemo nne za serikali na mbili zisizo za serikali
zilihusika katika utafiti huu. Jumla ya shule 132 ambapo 88 ni za Serikali na 44 ni
shule zisizo za Serikali zilihusishwa. Pia, ofisi za elimu na ukaguzi wa shule, Taasisi ya
Elimu Tanzania (TET), Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), pamoja na baadhi ya
asasi za serikali na zisizo za serikali zilihusishwa. Jumla ya wajibuji 3,894 walilengwa
katika utafiti ambapo washiriki 3,037 sawa na asilimia 80.0% walifikiwa.
Taarifa na takwimu za utafiti zilikusanywa kwa kutumia Madodoso, Majadiliano ya
Pamoja, Hojaji, maandiko na makala mbalimbali. Uchambuzi wa takwimu umefanyika
kwa kuwasilisha hoja za wajibuji katika namba (asilimia), majedwali na chati ili kuleta
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
vii
taarifa zenye mantiki kulingana na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti kuhusu
kushuka kwa kiwango cha ufaulu cha Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 2010
yamewasilishwa kama ifuatavyo:-
a) Usimamizi na Uendeshaji wa Elimu
Utafiti umedhihirisha kuwa matatizo yanayohusu usimamizi na uendeshaji
yameathiri ufanisi katika utoaji wa elimu bora nchini. Baadhi ya viongozi wa
elimu huteuliwa bila kuzingatia utaalamu, taaluma, uwajibikaji, uwezo na
uadilifu. Aidha, maamuzi ya kitaalamu kuhusu uendeshaji wa elimu hufanyika
kisiasa bila kuzingatia utaalamu na tafiti. Vile vile ufinyu wa bajeti ya Wizara ya
Elimu na TAMISEMI (Elimu) unafanya usimamizi na uendeshaji wa elimu
kutokuwa fanisi.
Utekelezaji wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada na ziada umekuwa na
changamoto ambazo zimeathiri uchapishaji, usambazaji na upatikanaji wa vitabu
vyenye ithibati katika shule na vyuo. Aidha, kuna uelewa mdogo kwa wanafunzi
na walimu katika matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia na kujifunzia
katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu.
Utafiti umebaini kuwa, mmomonyoko wa maadili kama vile matumizi ya lugha
mbaya; matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),
kutozingatia mafundisho ya dini, matumizi ya dawa za kulevya na kujiingiza
katika masuala ya mapenzi ni masuala yaliyobainishwa kuchangia kumeathiri
maendeleo ya taaluma shuleni.
b) Utayarishaji na Utekelezaji wa Mitaala
Utafiti umeonesha kuwepo kwa changamoto za utayarishaji na utekelezaji wa
mtaala kwa miaka mitano iliyopita. Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005
umetekelezwa bila kufanyiwa majaribio (piloting). Aidha, utafiti umebaini kuwa
kwa miaka mitatu iliyopita (2008 hadi 2010), jumla ya walimu 588 (1.5%)
walipata mafunzo kabilishi. Taarifa hii inaonesha kuwa walimu wengi hawana
maarifa na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari uliboreshwa.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
viii
Ni muhimu watekelezaji mitaala kupatiwa mafunzo kabilishi ili kuimarisha
utendaji kazi wao na kuwawezesha kupata fursa ya mabadiliko ya mtaala, dhana
na nadharia za ufundishaji na ujifunzaji.
Pia, utafiti umebaini upungufu wa mihtasari ya mtaala ulioboreshwa katika shule
za sekondari. Katika shule zilizofanyiwa utafiti, takwimu zinaonesha kuwa kuna
upungufu wa mihtasari kwa wastani wa asilimia 45.4 ambapo masomo ya
Mathematics na Geography yameongoza kwa kuwa na upungufu wa zaidi ya
asilimia 50. Vilevile, kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka
TET kwenda shuleni.
c) Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimu
Utafiti huu ulilenga Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya
utoaji wa elimu, utekelezaji wa mtaala na ukaguzi wa shule.
Utafiti ulibaini kuwa asilimia 49 ya wakuu wa shule hawafuatilii kikamilifu utoaji
wa taaluma shuleni, hali hii inapunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji.
Hivyo inapaswa wakuu wa shule wasimamie kikamilifu majukumu yao kama
ilivyoainishwa katika Mwongozo wa Usimamizi wa Shule.
Aidha, ilibainika kuwa hakuna ufuatiliaji wala tathmini iliyofanyika tangu mtaala
wa elimu ya sekondari ulioboreshwa uanze kutumika mwaka 2005 na kwamba
mitaala hiyo haikufanyiwa majaribio kabla ya utekelezaji wake. Kutofanya
tathmini kwa wakati kuhusu utekelezaji wa mtaala hakutoi fursa kwa serikali na
wadau wa elimu kubaini matatizo na changamoto za utoaji elimu na kuyapatia
ufumbuzi kwa wakati na hivyo kupunguza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji
Pia utafiti umebaini kuwa, katika shule 132 zilizotembelewa, shule 18 (13.53%)
zilikaguliwa mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010. Hali kadhalika
shule 6 (51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na shule 46 (34.59%)
hazikukaguliwa kabisa. Aidha, taarifa za ukaguzi wa shule hazifanyiwi kazi
ipasavyo. Kutokaguliwa kwa shule hizo za sekondari kumepunguza ufanisi wa
usimamizi na utoaji wa elimu bora.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
ix
d) Mfumo wa Utayarishaji na Uwepo wa Walimu
Ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya Taifa huchangiwa na sababu mbalimbali.
Uwepo wa walimu wenye sifa stahiki shuleni ni moja ya sababu muhimu.
Utafiti umebaini kuwa, sifa za udahili kwa walimu tarajali wa stashahada ni za
ufaulu wa kiwango cha chini (1Principal na 1Subsdiary) katika masomo ya
kufundishia na baadhi yao hawana wito wa kazi ya ualimu. Aidha utafiti umebaini
kuwa kuna changamoto katika matayarisho ya walimu tarajali unaosababishwa
na upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Aidha, matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu
kimasomo hususani katika masomo ya sayansi na Mathematics unaosababishwa
pia na upangaji usiozingatia mahitaji hususan katika sehemu zenye mazingira
magumu. Katika shule zilizofanyiwa utafiti imebainika kuwa somo la
Mathematics, lina mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo
kuna upungufu wa walimu 264 sawa na asilimia 60.6. Tatizo la upungufu wa
walimu ni changamoto katika utoaji wa elimu.
e) Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
Matokeo mbalimbali yahusuyo mfumo wa mitihani yamebainishwa ikiwa ni
pamoja na muundo wa maswali yatolewayo shuleni kutokidhi viwango
vinavyotumika na NECTA.
Aidha, Miundo ya mitihani ya Taifa haiwafikii baadhi ya walimu na wanafunzi na
hivyo kutoielewa. Hii inaonesha jinsi ambavyo baadhi ya walimu na wanafunzi
hawapati fursa ya kuiona na kuitumia miundo ya mitihani na miongozo katika
shule za sekondari. Uwepo wa Nyaraka na miongozo mbalimbali ya mitihani
katika shule ni muhimu katika kumwandaa mtahiniwa hivyo, wadau wote
wanapaswa kupata na kutumia machapisho hayo.
Utafiti umebaini kuwa, uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule haufanywi
kwa makini. Aidha, utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts’
walizosahihisha badala ya posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
x
kwa siku ni baadhi ya masuala yanaweza kuchangia kupungua kwa umakini wa
usahihishaji.
Aidha utafiti umebaini kuwa, mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45%
majaribio na mazoezi na 5% projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au
mchakato wake katika matokeo ya mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu.
Hata hivyo NECTA wanatumia vigezo vingine vya ulinganifu sanifu ambavyo
mchakato wake wa kuvitumia haueleweki kwa wadau. Aidha utafiti umebaini
kuwa, gredi zinazotumika shuleni kwa uzoefu wa miaka mingi ni A (81-100), B
(61-80), C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa
alama za gredi zinazotumika kwa Mtihani wa Taifa wa K4 huamuliwa na Kamati
ya Kutunuku ambapo gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si chini ya alama
70. Hali hii ya kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu baina ya shule
na NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama za gredi. Vilevile, kuna
mapungufu ya kuadhibu watahiniwa kwa kuteremshwa daraja la I au la II kuwa
la III kutokana na kufeli baadhi ya masomo ya msingi na ya mchepuo.
f) Mazingira na Vifaa vya Kufundishia na Kujifunzia
Utafiti umebaini kuwa katika shule 132 zilizofanyiwa utafiti, kuna upungufu mkubwa
wa miundombinu, samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni ikijumuisha
maabara ya Chemistry (79.6%), Biology (66%) na Physics (65.2%) nyumba za
walimu (72%), na maktaba (80.6%). Aidha, baadhi ya shule zimepata usajili bila
kutimiza vigezo na nyingine kujengwa mbali na makazi ya jamii husika. Vilevile
utafiti umebaini upungufu wa vifaa vya kufundishia ikiwa ni pamoja na vitabu vya
kiada na ziada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa kwa baadhi ya masomo
kwa wastani wa 75.5% katika shule zilizofanyiwa utafiti.
Matokeo ya utafiti pia yamebaini kutokuwepo kwa chakula cha mchana kwa
wanafunzi katika shule za kutwa, na hivyo kuathiri mahudhurio na umakini wa
wanafunzi katika ujifunzaji.
Hali hii ya upungufu wa miundombinu, upatikanaji wa vitabu vinavyoendana na
mihtasari iliyoboreshwa na kutokuwepo kwa chakula cha mchana ni changamoto
ambazo zinaathiri utekelezaji wa mitaala shuleni.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
xi
Mapendekezo
Kutokana na taarifa za utafiti kuna mapungufu na changamoto mbalimbali zilizoathiri
kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa Kidato cha 4 mwaka 2010. Mapendekezo
muhimu yametolewa ambayo yanaweza kutekelezwa kwa muda mfupi, kati na mrefu.
1. Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,
uadilifu na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na
zisikaimishwe kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;
2. Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,
tathmini na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya
utoaji wa elimu;
3. Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili kutatua
changamoto zilizopo;
4. Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)
kianzishwe kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji
na haki za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa
inakidhi malengo yaliyokusudiwa; Utaratibu wa motisha kwa walimu
unaoendana na uzito wa kazi, wadhifa na ugumu wa mazingira anapofanyia kazi
uandaliwe na utekelezwe ipasavyo;
5. Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya
mitihani ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate sifa za kujiendeleza
kitaaluma na kitaalamu;
6. Vyuo vya ufundi stadi kama vile VETA vipanuliwe ili kuwawezesha wahitimu wa
kidato cha 4 wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na
stadi za kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri;
7. Walimu wenye sifa wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji katika shule
zote. Pia, Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule
ziandaliwe;
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
xii
8. Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji yaimarishwe.
9. Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo
vinavyotakiwa;
10.Walimu wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia
pia alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kama
ilivyoelekezwa katika mwongozo wa mazoezi endelezi;
11.Utungaji na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala
inayotekelezwa
12.Adhabu katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III
baada ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila
mtahiniwa apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake;
13.Hadhi ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja
wanafunzi. Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada
(Remedial)
14.Mfumo rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika
kwa wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki
kwa watahiniwa;
15.Wasahihishaji wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu kwa sababu ni
haki ya mwajiriwa wa serikali;
16.Mafunzo kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa kwa walimu na wakaguzi wote. Aidha Mafunzo maalumu kuhusu
dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na kutekelezwa kwa maafisa
mitaala na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo;
17.Mihtasari ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft
copy) ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi;
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
xiii
18.Jukumu la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili
kubaini dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki;
19.Taratibu za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya
utafiti, tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake.
20.Fedha za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo. Vilevile, Hosteli/mabweni na
nyumba za walimu zijengwe kwenye shule za sekondari zilizo mbali na makazi
ya watu, na wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha
mchana;
21.Sifa za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada
zipandishwe kuwa Principal mbili za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha
mwalimu kuwa mahiri kitaaluma;
22.Vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa
miundombinu ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na
ongezo la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa. Wakufunzi na wahadhiri
wapewe mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi (Competence Based
Curriculum);
23.Maabara ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na
kuimarishwa katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali
watatumia kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na
kuandika. Pia Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa
walimu wa masomo yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za
sekondari;
24.Utaratibu maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post
Graduate Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili
kukabiliana na tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi;
25.Ukaguzi wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa
kupatiwa nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia;
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
xiv
26.Ufuatialiaji wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada
pamoja na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe;
27.Sheria ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo
na ithibati katika shule nchini.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
15
SURA YA KWANZA: UTANGULIZI1.1. Usuli
Utoaji wa elimu nchini Tanzania unaongozwa na Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka
1995. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo unaenda sambamba na Dira ya Taifa
2025, MKUKUTA, kutimiza malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo ya
Maendeleo ya Milenia (MDGs). Aidha, utekelezaji wa será hiyo unaenda sambamba na
utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama ya Mapinduzi ya mwaka 2010.
Katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo, Programu ya Maendeleo ya Sekta ya
Elimu ilianzishwa 1997 na kuhuhishwa 2001 na 2008. Aidha, Programu za Mipango ya
Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Sekondari (MMES) zilianzishwa kutekeleza
program ya sekta. Mafanikio ya MMEM (2002-2006) na MMEM II (2007-2011)
yameongeza mahitaji ya upanuzi wa Elimu ya Sekondari, ambapo Mpango wa
Maendeleo ya Elimu ya Sekondari – MMES I (2004-2009) ulitekelezwa kwa lengo kuu
la kuongeza uandikishaji wa wanafunzi katika shule za sekondari na MMES II (2010-
2014) imeweka kipaumbele katika kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari. Mafanikio
hayo yalihitaji dhamira kubwa ya uwekezaji katika elimu ambapo Serikali imetoa
mgawo mkubwa wa fedha za umma. Aidha, wazazi, jamii, na wahisani wana mchango
mkubwa katika utoaji wa elimu nchini na kuifanya Tanzania iwe mbele ya muda wa
kuyatekeleza na kuyafikia malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yanayohusu
upatikanaji wa elimu kwa usawa wa kijinsia.
Mantiki ya elimu ni kumsaidia kila mtoto kukuza maarifa, stadi na mielekeo ili aweze
kuishi maisha yenye ustawi duniani kwa kumsaidia kuanza kujua kusoma na kufanya
hesabu na stadi ambazo zinaweka msingi wa uwezo wa kudadisi, kufikiri, kusikiliza,
kuuliza maswali, kuchambua, kupambanua na kuwasiliana kwa kujiamini (UWEZO,
2010). Stadi hizi na maendeleo ya mwanafunzi yanapimwa wakati wa mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji wa somo husika ambapo mazoezi na mitihani anuai hutolewa
na walimu. Wakati mwingine, upimaji hufanyika baada ya mchakato wa ufundishaji na
ujifunzaji nje ya darasa.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
16
Mitihani ni nyenzo mojawapo inayotumika katika upimaji ambayo hufanyika kwa
nyakati mbalimbali kama vile robo, nusu au mwisho wa muhula na wakati wa kuhitimu
ngazi ya elimu husika. Mitihani ya ndani katika ngazi ya Elimu ya Msingi, Sekondari na
Vyuo vya ualimu hutolewa na taasisi husika. Aidha ipo mitihani ya kitaifa ambayo ni
Mitihani ya Darasa la IV na VII (Msingi), Mitihani ya Kidato cha 2, 4 na 6 (Sekondari)
na Mitihani ya Cheti na Stashahada (Vyuo vya Ualimu). Mitihani ya Darasa la IV
huendeshwa na Idara ya Elimu ya Msingi ya WEMU na ya kidato cha 2 huendeshwa
na Idara ya Ukaguzi wa Shule. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) inahusika na
uendeshaji wa Mitihani ya Darasa la VII (Msingi), Kidato cha 4 na 6 (Sekondari) na
Mitihani ya ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada.
Mtihani wa Taifa wa Darasa la IV ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya mwanafunzi
katika kupima ufahamu na kumudu stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Mtihani huu hutumiwa kutathmini maendeleo ya mwanafunzi kwa kipindi cha miaka
minne ya kwanza ya Elimu ya Msingi. Aidha, Mtihani wa Darasa la VII hutumika
kuthibitisha kuhitimu kwa mwanafunzi katika ngazi ya Elimu ya Msingi na hutumiwa
kufanya maamuzi ya uchaguzi wa mwanafunzi kuendelea na Elimu ya Sekondari na
mafunzo ya fani mbalimbali.
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya
mwanafunzi. Mtihani huu hutumiwa kutathimini maendeleo ya mwanafunzi kwa
kipindi cha miaka miwili ya mwanzo ya elimu ya sekondari. Aidha, mtihani huu ni
sehemu ya mazoezi endelezi (Continuous Assessment-CA), hivyo huchangia katika
matokeo ya mwanafunzi katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 (Waraka wa Elimu
Na. 5, 1999).
Mitihani ya Taifa ya Kidato cha 4 na 6 inathibitisha kuhitimu kwa mwanafunzi katika
ngazi za elimu ya sekondari ya kawaida (Ordinary Level) na juu (Advanced Level).
Matokeo ya mitihani hii hutumiwa kufanya maamuzi ya uchaguzi wa wanafunzi
kuendelea na mfumo rasmi wa elimu kwa ngazi inayofuata, mafunzo ya fani
mbalimbali na ajira. Mitihani hii inalenga katika kupima ubora wa elimu itolewayo na
matokeo yake ni kiashiria cha ubora huo.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
17
Mwaka 2005 na 2007 mtaala wa elimu ya sekondari uliboreshwa kutoka mtaala
unaozingatia maudhui (Content Based Curriculum) na kuwa mtaala unaozingatia ujuzi
(Competence Based Curriculum). Tofauti na mtaala unaozingatia maudhui, mtaala
unaozingatia ujuzi upimaji wake ni wenye kumjali mwanafunzi kwa kuzingatia usawia
katika maeneo makuu matatu ambayo ni maarifa (knowledge), mwelekeo (attitudes)
na stadi (skills). Aidha, upimaji huu pia huzingatia uelewa wa wanafunzi katika dhana
(nadharia), vitendo na mtazamo.
Zana zinazotumika wakati wa upimaji ni pamoja na mazoezi ya darasani, majaribio,
mitihani, vitendo (practicals) na projekti. Mwongozo wa NECTA wa Mazoezi Endelezi
(NECTA: 1990) unafafanua kuwa ufaulu wa mwanafunzi utapimwa kwa kutumia
alama za mazoezi endelezi na alama za Projekti ambazo zitajumuishwa kuchangia
asilimia 50 kwenye alama ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4.
Kiwango cha ufaulu kwa Mitihani ya Taifa ya Darasa la VII, Kidato cha 2 na 4
kinaonesha kuendelea kushuka katika ngazi za Elimu ya Msingi na Sekondari tangu
mwaka 2007 toka asilimia 70.48 mwaka 2006 hadi 53.55 mwaka 2010 kwa ngazi ya
elimu ya msingi, asilimia 91.9 mwaka 2007 hadi asilimia 61.8 mwaka 2010 kwa
Mtihani wa Kidato cha 2 na asilimia 90.3 mwaka 2007 hadi asilimia 50.4 mwaka 2010
Mtihani wa Kidato cha 4 kama inavyooneshwa katika Jedwali Na.1.1.
Jedwali Na. 1.1 Kiwango cha Ufaulu Mitihani wa Darasa la VII, Kidato cha 2 na Kidato cha 4 (%) Mwaka 2006 – 2010
Mtihani 2006 2007 2008 2009 2010
Darasa la VII 70.48 54.18 52.73 49.41 53.55
Kidato cha 2 76.2 91.9 73.5 65.3 61.8
Kidato cha 4 89.12 90.3 83.6 72.5 50.4
Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results Statistics 2007-2010, WEMU, 2010.
Pamoja na kushuka kwa ufaulu wa jumla katika Mtihani wa Taifa ya Kidato cha 4, vile
vile ufaulu umeshuka katika baadhi ya masomo kama vile Mathematics na English
Language kama inavyooneshwa katika Jedwali Na. 1.2.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
18
Jedwali Na. 1.2: Kiwango cha Ufaulu (%) Kidato cha 4 kwa Masomo ya Mathematics na English Language 2006 – 2010
Somo 2006 2007 2008 2009 2010
Mathematics 23.67 31.32 24.33 17.78 16.09
English 80.98 75.54 63.23 60.03 30.33
Chanzo: The National Examinations Council of Tanzania, Examinations Results Statistics 2007-2010
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 yameonesha kuwa
kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia 39.9 toka mwaka 2007. Matokeo hayo
pia yanaonesha idadi ya watahiniwa ambao hawakufaulu ni asilimia 49.60.
1.2. Hoja ya Kufanya Utafiti
Kitaalamu, mitihani ni nyenzo itumikayo kupima kiwango cha ujuzi ambacho
mwanafunzi amekipata. Mtihani unalenga katika kupima uelewa wa wanafunzi kwa
elimu itolewayo na matokeo yake ni kiashiria cha ubora huo. Kiwango cha ufaulu wa
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 kimeendelea kushuka mfululizo kwa miaka minne
tangu 2007 (Jedwali Na.1.1). Hali hii imejitokeza pia kwa matokeo ya mitihani ya
Darasa la IV, Kumaliza Elimu ya Msingi (Darasa la VII) na ile ya Elimu ya Sekondari ya
Kidato cha 2. Athari ya matokeo mabaya katika mitihani ya kuhitimu ni kuwa na jamii
ambayo haina elimu ya kiwango kilichokusudiwa kitaifa.
Kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2010 kumekuwa
tofauti na matarajio ya Serikali na wadau wengine wa elimu na hivyo kuibua hoja
mbalimbali juu ya sababu zilizochangia hali hiyo. Jamii ya Watanzania kwa ujumla
ingependa kujua hali halisi kuhusu kushuka kwa ufaulu. Hivyo, Serikali kwa kupitia
WEMU na OWM-TAMISEMI ikaona ni muhimu kufanya utafiti wa kisayansi ili kubaini
kiini cha tatizo.
Utafiti huu umefanyika kwa matarajio ya kuibua mambo yaliyosababisha kushuka kwa
ufaulu ikiwa ni pamoja na kubaini uzito na upeo wa matatizo yaliyojitokeza. Matokeo
ya utafiti huu yatatumiwa na Serikali na wadau wa elimu katika kufanya maamuzi na
kuchukua hatua stahiki za kuinua kiwango cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
19
Kidato cha 4. Utafiti huu unatoa mwelekeo sahihi kwa Serikali ili kupata ufumbuzi wa
changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu.
1.3. Malengo ya Utafiti
1.3.1.Lengo Kuu
Lengo kuu la utafiti huu lilikuwa kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu ili
kuchukua hatua sahihi za kukabiliana na tatizo la kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa
Kidato cha 4 na hatimaye kuinua ubora wa Elimu ya Sekondari nchini.
1.3.2. Malengo Mahsusi
Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa:
(i). Kufanya uchambuzi wa kiwango cha ufaulu wa watahiniwa wa Mtihani wa Taifa
wa Kidato cha 4 mwaka 2010;
(ii). Kubaini utoshelevu wa walimu katika shule za sekondari;
(iii). Kuchunguza hali ya mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji;
(iv). Kukusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu wa
Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4;
(v). Kuchunguza ufanisi wa mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu;
(vi). Kuchambua mfumo wa uendeshaji wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4;
(vii). Kubaini michango ya wadau wa elimu katika usimamizi na uendeshaji wa Elimu
ya Sekondari; na
(viii). Kuchambua mfumo wa utayarishaji wa walimu wa sekondari.
1.4. Maswali ya Utafiti
a) Nini sababu za kushuka kwa ufaulu wa watahiniwa wa Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 mwaka 2010?
b) Je shule zina walimu wenye sifa na wa kutosha katika kutekeleza mtaala?
c) Hali halisi ya mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ikoje?
d) Nini maoni ya wadau wa elimu kuhusu kuinua kiwango cha ufaulu wa Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha 4?
e) Nini kifanyike kwa wahitimu waliofeli Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka
2011?
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
20
f) Mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu ni wa namna gani?
g) Mfumo wa uendeshaji (utungaji, usambazaji, usimamizi, usahihishaji na
upangaji wa madaraja) Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 ukoje?
h) Alama za mazoezi endelezi (CA) zina mchango gani katika Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4?
i) Wadau wa elimu wana mchango gani katika usimamizi na uendeshaji wa Elimu
ya Sekondari?
j) Walimu katika Shule za Sekondari wanaandaliwaje?
1.5. Muundo wa Ripoti
Ripoti ya utafiti kuhusu kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4 mwaka 2010, ina sura tano ambazo zimepangiliwa katika mtiririko
unaoanza na tatizo la utafiti mpaka hitimisho. Kila sura imebeba dhima moja ili
kujenga mtiririko wenye mantiki katika kujibu hoja na maswali ya utafiti.
Sura ya kwanza ya ripoti, imebeba utangulizi wa tatizo la utafiti ambapo usuli wa
tatizo, hoja ya kufanya utafiti, malengo na maswali ya utafiti yameainishwa. Sura ya
pili imeeleza mapitio ya maandiko kuhusu Sera na Mipango ya Elimu, usimamizi na
uendeshaji, ufuatiliaji na tathmini ya elimu, mitaala na utekelezaji, mitihani,
upatikanaji na usambazaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia, mazingira ya
kufundishia na kujifunzia na uandaaji na upatikanaji wa walimu.
Mwongozo wa utafiti (Methodolojia) umetolewa katika sura ya tatu na unajumuisha
eneo la utafiti, walengwa wa utafiti, uchaguzi wa sampuli, zana za utafiti, utaratibu wa
kufanya utafiti na uchambuzi wa takwimu. Matokeo ya utafiti na uchambuzi wa
takwimu kulingana na malengo na maswali ya utafiti yamejadiliwa katika sura ya nne.
Taarifa ya utafiti imehitimishwa katika sura ya tano ambapo hitimisho na
mapendekezo muhimu kutokana na matokeo ya utafiti yameainishwa.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
21
SURA YA PILI: MAPITIO YA MAANDIKO
2.1 Sera na Mipango ya Elimu
Kama ilivyo kwa mataifa yote, Tanzania ina mfumo wake wa elimu tangu ilipopata
uhuru mwaka 1961. Mfumo huo umepitia katika mabadiliko anuai ikiwa ni pamoja na
utoaji wa elimu, mitaala na tathmini na upimaji. Serikali ilifuta Sheria ya Elimu ya
mwaka 1927 na kupitisha Sheria ya Elimu ya mwaka 1962 ili kurekebisha utoaji wa
elimu kwa kuleta usawa na kutoa ubaguzi wa rangi na dini uliokuwepo wakati wa
ukoloni (Sera ya Elimu na Mafunzo, 1995).
Mwaka 1967, falsafa ya Elimu ya Kujitegemea (Education for Self Reliance) ilianzishwa
ambapo msisitizo mkubwa uliwekwa kwenye ujenzi wa maarifa, ujuzi na mwelekeo
unaotakiwa katika kujenga jamii inayojitegemea (Nyerere, 1967). Pamoja na mambo
mengine falsafa hiyo ilisisitiza utoaji wa elimu utakaowasaidia wahitimu kushiriki
ipasavyo katika kujenga na kuiletea maendeleo jamii ya Watanzania juu ya masuala
yahusuyo ujenzi wa ari, udadisi na kufanya uchunguzi wa kisayansi, ubunifu, uwezo
wa kutatua matatizo ya kijamii na uwezo wa kujiamini na ushirikiano. Mitaala ya
Tanzania huandaliwa kwa kuzingatia dhana ya falsafa ya elimu ya kujitegemea.
Kati ya mwaka 1967 na 1978, Serikali ilichukua hatua kadhaa na ilitunga sheria
mbalimbali ili kuhalalisha hatua zilizochukuliwa wakati wa azimio la Arusha na Elimu
ya Kujitegemea. Sheria na hatua hizi zilijumuishwa na sheria za elimu za 1969 na
1978; Mpango wa Madaraka Mikoani wa 1972; Sheria ya Baraza la Mitihani la Taifa
Na. 21 ya 1973; Elimu ya Msingi kwa Wote (UPE) na Azimio la Musoma la mwaka
1974; Sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Na. 12 ya 1975 na Sheria ya Taasisi
ya Elimu Tanzania Na. 13 ya 1975.
Mwaka 1981, Tume ya Rais ya Elimu iliundwa ili kuchunguza mfumo wa elimu
uliokuwepo na kutoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya lazima yaliyohitajiwa
kufanyika nchini ifikapo mwaka 2000. Mapendekezo mengi yaliyowasilishwa na Tume
mwaka 1982 yalitekelezwa na Serikali ikiwemo upanuzi wa elimu ya sekondari.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
22
Mwaka 1990, Serikali iliunda Tume Maalumu ya Elimu kuangalia upya mfumo wa
elimu kwa ajili ya Karne ya 21. Mwaka 1992 Tume hii iliwasilisha taarifa serikalini
ambapo mapendekezo yake yalizingatiwa katika kuunda Sera ya Elimu na Mafunzo,
1995.
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ambayo ipo katika mchakato wa kuhuishwa
ndiyo inayotumika katika utoaji wa elimu nchini. Sera hiyo inatekelezwa na Wizara
zote lakini zilizo muhimu kwa elimu rasmi na elimu ya nje ya mfumo rasmi ni Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU), Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto. Utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo pia unaenda sambamba na Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2025, MKUKUTA, Malengo ya Elimu kwa Wote (EFA) na Malengo
ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) ambapo Serikali imeridhia Mikataba hiyo (SEDP II,
2010).
Elimu ya Sekondari ni kiungo muhimu kati ya Elimu ya Msingi na Elimu ya Juu. Moja
ya malengo ya elimu ya sekondari ni kumwandaa mwanafunzi kwa ajili ya elimu ya
kati, ya juu, ya ufundi na ufundi stadi na kujiunga na ulimwengu wa kazi (Sera ya
Elimu na Mafunzo, 1995).
2.2 Mipango na Mikakati ya Elimu
Serikali ilianzisha Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu mwaka 1997 na
kuifanyia marekebisho mwaka 2001 na 2008 ili kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo
nchini. Ili kufanikisha utekelezaji wa programu hiyo, ilianzishwa mipango na mikakati
mbalimbali kama vile Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM, 2002-2006)
na awamu ya pili ya MMEM (2007-2011). MMEM ilianzishwa ili kuboresha elimu ya
msingi na kutoa fursa sawa ya elimu kwa watoto wote.
Mafanikio ya MMEM yamesababisha upanuzi wa elimu ya sekondari, ambapo Mpango
wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari - MMES awamu ya kwanza, 2004-2009 na
awamu ya pili (2010-2014) unatekelezwa ili kuongeza uandikishaji wa wanafunzi
katika shule za sekondari kwa kuzingatia fursa na usawa. Aidha, MMES II imetoa
kipaumbele katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari, ambapo mpango huu
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
23
umeharakisha utekelezaji wa ibara ya 5.4.2 ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka
1995 inayosisitiza kujenga na angalau shule moja ya sekondari kwa kila Kata nchini.
Idadi ya shule za sekondari (za serikali na zisizo za serikali) imefikia 4,266 mwaka
2010 ukilinganisha na shule 1,745 zilizokuwepo mwaka 2005, ongezeko hili ni sawa
na asilimia 144.5. Mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi
(Kidato cha 1-4) walioandikishwa katika shule za sekondari za kawaida kutoka
wanafunzi 489,942 mwaka 2005 hadi kufikia 1,566,685 mwaka 2010. Vilevile,
kumeimarika kwa vigezo vya kupimia maendeleo ya Elimu kama Gross Enrolment
Ratio (GER) na Net Enrolment Ratio (NER) kutoka asilimia 15.9 na 10.3 mwaka 2005
kufikia asilimia 47.3 na 30.8 mwaka 2010. Mafanikio haya makubwa yamepatikana
kutokana na ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, Serikali, Wafadhili pamoja na
wadau wengine mbalimbali wa elimu.
Katika kuinua ubora wa elimu ya sekondari, MMES awamu ya kwanza ilikuwa na lengo
la kuboresha mtaala ili uendane na mahitaji ya soko la ajira. Maboresho ya mtaala
yalifanyika katika ngazi ya Elimu ya Msingi, sekondari na mafunzo ya ualimu mwaka
2005 na 2007. MMES pia ilikuwa na lengo la kuongeza ubora wa elimu ya sekondari
kwa kutatua tatizo la upungufu wa walimu na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya
ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia (Updated SEDP, 2007 ).
2.3 Uongozi katika Elimu
Mfumo wowote wa elimu unategemea uongozi na utawala bora ili kufikia malengo
yaliyowekwa. Mbinu nzuri za uongozi ni muhimu kwa ufanisi wa mfumo wa elimu na
mafunzo na asasi zake. Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inabainisha kuwa uongozi
wa Elimu na mafunzo unafanywa na Wizara kadhaa, mashirika ya Umma na mashirika
yasiyo ya kiserikali.
Sheria mbalimbali zilizowezesha wizara na taasisi kubeba wajibu wa elimu na mafunzo
zina uhusiano mdogo na sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978. (Ripoti ya Tume ya
Rais ya Elimu, 1982) Sheria hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 1995 ili kujumuisha
maeneo mengine ya elimu na mafunzo, pamoja na uongozi, utawala na fedha.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
24
Ibara ya 4.3 katika Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa madaraka na
utoaji uamuzi katika uongozi na utawala wa elimu na mafunzo vimebaki kwenye ngazi
ya wizara. Mwaka, 2009 usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari ulihamishiwa
katika serikali za Mitaa. (Waraka wa Elimu Na. 13 wa Mwaka 2009). Usimamizi huu
unaendana na Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) kwamba
‘Wizara zinazo wajibika na elimu na mafunzo zitakasimu madaraka yao ya uongozi na
utawala wa elimu na mafunzo kwa vyombo vya chini vya jamii’.
Viongozi na watawala wa elimu kwenye ngazi za taifa, Mkoa, Halmashauri na asasi
wawe na uzoefu na sifa za juu kitaaluma na kitaalamu na wawe na ujuzi katika
uongozi na utawala wa kielimu. Katika kuimarisha usimamizi na uongozi katika elimu,
utoaji wa mafunzo ya kujenga uwezo umetiliwa mkazo kwa kila ngazi ya elimu
(Updated SEDP, 2007).
2.4 Usimamizi na Uendeshaji
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inashughulika na masuala ya uandaaji wa sera,
mitaala, kuweka viwango, usimamizi wa ubora wa elimu, itolewayo na kufanya
ufuatiliaji na tathmini. Serikali iliamua kugatua majukumu ya usimamizi na uendeshaji
wa shule za sekondari kwenda katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na utekelezaji
wake ulianza rasmi tarehe 1 Julai, 2009. Lengo la mabadiliko hayo ni kuboresha
huduma ya utoaji wa elimu na kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na wananchi.
Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) imeeleza katika ibara ya 4.3.6 kuwa
‘Bodi na Kamati za asasi za elimu na mafunzo zitawajibika katika uendeshaji, kupanga
maendeleo, nidhamu na fedha za asasi zilizochini ya mamlaka yao’.
Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari (1997) kinaeleza kuwa ‘Bodi ya shule ni
chombo muhimu ambacho kila shule inapaswa kuwa nacho ili kufanikisha lengo la
elimu ya Sekondari nchini. Kwa mujibu wa sheria ya Elimu Na 25 ya mwaka 1978 na
rekebisho lake Na.10 la mwaka 1995. Bodi ya Shule imepewa mamlaka ya kusimamia
uongozi na uendeshaji wa mipango yote ya maendeleo ya shule; kusimamia nidhamu
ya walimu, wanafunzi na masuala ya fedha za shule.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
25
Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari (1997) kinaelekeza kuwa uongozi na
utawala unaopaswa kuwepo katika kila shule ya sekondari ni Mkuu wa shule, Makamu
Mkuu wa Shule na Mwalimu Mwandamizi Taaluma. Chini ya Mwalimu mwandamizi
Taaluma watakuwepo viongozi wafuatao: Mwalimu Mshauri Mafunzo na Kazi, Wakuu
wa idara za Masomo, Walimu wa Masomo Walimu wa Madarasa na Mwalimu
Mwandamizi Malezi na Utamaduni. Aidha, chini ya Mwalimu Mwandamizi Malezi na
Utamaduni watakuwepo viongozi wafuatao: Mwalimu Mlezi wa nyumba/Hosteli,
Mratibu wa Michezo. Pia shule zitakuwa na Mwalimu Mwandamizi Uzalishaji Mali na
Mwalimu wa Zamu
2.5 Ugharamiaji wa Elimu
Ugharamiaji wa Elimu na Mafunzo nchini kwa ujumla ni jukumu la Serikali. Aidha,
jamii, wazazi/walezi, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wengine wa elimu
huhusishwa katika kugharamia elimu. Serikali pia inapata fedha za nje kwa Washirika
wa Maendeleo kwa ajili ya kugharamia elimu kupitia njia tatu zifuatazo; misaada ya
bajeti (General Budget Support- GBS), Mifuko ya pamoja (Basket funds) na Misaada
ya miradi ya Maendeleo (Direct Project Funds) (Andiko la MMES, 2004). Kwa ajili ya
kupima ufanisi na athari kutokana na rasilimali na matumizi ya fedha za umma,
serikali inatumia mfumo wa matumizi wa muda wa kati (Medium – Term Expenditure
Framework -MTEF).
Ugharamiaji wa elimu umeendelea kuwa mojawapo ya vipaumbele vya serikali.
Asilimia ya Bajeti ya sekta ya elimu kutoka kwenye bajeti kuu ya Taifa imeendelea
kupanda na kushuka kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, 2000/01 hadi 2010/11 kama
ilivyobainishwa katika Jedwali Na. 2.1
Jedwali Na 2.1 Mgawo wa Bajeti ya Sekta ya Elimu 2000/01 -2010/11Mwaka wa Fedha
Kielelezo Na. 4.9: Asilimia ya Upungufu wa Miundombinu katika Shule Zilizofanyiwa Utafiti
Chanzo: Takwimu za Utafiti, 2011
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
111
Aidha, walimu katika hojaji walibainisha kuwepo kwa mlundikano wa wanafunzi katika
vyumba vya madarasa, maktaba na maabara hali inayothibitisha upungufu wa
miundombinu hivyo kuathiri ufundishaji na ujifunzaji. Vilevile, wanafunzi katika
mahojiano ya pamoja walibainisha athari ya ukosefu wa hosteli/mabweni shuleni
hupelekea wanafunzi kulazimika kutembea umbali mrefu kati ya shule na makazi yao.
Matokeo haya kwa ujumla yanaonesha hali isiyoridhisha katika suala la miundombinu
ya shule tofauti na ilivyoelekezwa na Sera ya Elimu na Mafunzo, 1995 na Mwongozo
wa Samani wa Wizara ya Elimu (2001).
4.6.2.3 Uwepo wa Vitabu vya Kiada na ZiadaUtafiti umebaini kuwa kuna upungufu wa vitabu vya kiada vinavyoendana na mtaala
ulioboreshwa kama inavyooneshwa katika Kielelezo Na 4.10. Aidha, utekelezaji wa Sera ya
upatikanaji na usambazaji wa vitabu ya Mwaka 1992 imekuwa na changamoto ingawa
serikali imeendelea kukasimu majukumu ya kununua vitabu shuleni.
Kielelezo Na. 4.10: Asilimia ya Upungufu wa Vitabu katika Shule
Zilizofanyiwa Utafiti
Chanzo: Data za Utafiti, 2011
Kielelezo Na. 4.10 kinaonesha kuwa upungufu wa vitabu vya kiada na ziada kwa
wastani wa asilimia 75.5 kwa shule zote zilizofanyiwa utafiti. Aidha, wajibuji
walionesha kuwa ununuzi wa vitabu huathiriwa na wanafunzi kutolipa ada na bei
kubwa ya vitabu.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
112
Wakuza mitaala waliohojiwa walieleza changamoto za ucheleweshaji wa uhakiki wa
vitabu na utoaji ithibati inayofanywa na Kamati ya kuhakiki ubora wa machapisho ya
kielimu (EMAC). Walimu wakuu walitoa changamoto ya upungufu wa vifaa vya
kufundishia pamoja na vitabu vya kiada vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa
kwa baadhi ya masomo, na kuwepo baadhi ya mada katika vitabu vya kiada
vilivyopewa ithibati na EMAC kutoendana na mahitaji ya mihtasari iliyoboreshwa.
Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa pamoja na shule nyingi kuwa na vitabu vichache,
baadhi ya vitabu hivyo haviendani na mtaala ulioboreshwa. Aidha, kukosekana kwa
mamlaka rasmi ya kusambaza vitabu katika ngazi ya Halmashauri pia ilibainishwa
kuwa chanzo cha ukosefu wa vitabu vinavyoendana na mtaala. Pia, mahojiano ya
pamoja ya wanafunzi na walimu yameonesha kuwa shule nyingi hazina utaratibu
mzuri wa matumizi ya vitabu hata vile vichache vilivyopo. Kwa ujumla, utafiti
unaonesha upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada katika shule nchini na
matatizo katika upatikanaji, usambazaji na matumizi yake katika shule. Hali hii ina
athari kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa taaluma shuleni.
4.6.3 Maoni ya Kuboresha Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia
Kati ya wakuu wa shule 132 wa shule za sekondari waliohojiwa, asilimia 61
wameeleza kuwa mazingira mazuri ya kazi ni fursa inayowafanya walimu waendelee
kubaki kwenye vituo vyao. Aidha, asilimia 57 (12) ya Maafisaelimu sekondari wa
Halmashauri waliohojiwa wameeleza kuwa mazingira mazuri yenye huduma za kijamii
kama maji, afya, usafiri, umeme, teknolojia ya habari na mawasiliano ni fursa
inayowafanya walimu kuwepo shuleni. Uwepo wa mazingira mazuri ya kazi kwa
walimu ni motisha itakayowafanya walimu kubaki katika vituo vyao na kutimiza
majukumu yao ya kufundisha kwa ukamilifu.
Wajibuji wamependekeza kuwepo na vitabu vya kutosha shuleni ambavyo
vimeidhinishwa na utaratibu wa kupitia vitabu. Aidha, Kitengo cha Kamati ya
Kutathimini Machapisho ya Kielimu (EMAC) kiimarishwe ili kiwe na watendaji wenye
ujuzi. Serikali irudishe utaratibu wa kuwa na aina moja ya vitabu vya kiada
vitakavyotumika nchi nzima kwa kila somo (visiwe zaidi ya viwili). Wizara inunue na
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
113
kusambaza vitabu hivyo ili kuwezesha kuwepo kwa vitabu vya kutosha shuleni. Hali
kadhalika, matumizi ya TEHAMA shuleni yatiliwe mkazo ili kuwezesha wanafunzi
kupata maarifa kwa njia ya mtandao. Vilevile, imeshauriwa kuwa Serikali ithibiti
matumizi holela ya vitabu vya kugushi vya kufundishia na kujifunzia shuleni. Pia vifaa
vya maabara viongezwe katika kila shule na shule zilizo na maabara ziwezeshwe ili
shule za karibu zisizo na maabara zitumie maabara za shule hizo teule.
Kuhusu posho kwa walimu, ilipendekezwa kuwepo na posho maalum ya kufundishia
ambayo ni asilimia 50 ya mshahara, posho ya mazingira magumu, kupandishwa
madaraja, mafunzo kazini, kuboresha huduma za jamii kama vile umeme, maji,
usafiri na nyumba bora ili kutoa motisha kwa walimu. Vilevile serikali ianzishe mfuko
wa kuwakopesha walimu ili kuwavutia wadumu kufundisha katika mazingira magumu.
Serikali ilishauriwa kuhamasisha wadau mbalimbali wa elimu kuimarisha miundombinu
shuleni kwa kuziwezesha shule kuwa na maktaba, maabara na vifaa vyake ili mitihani
ya “alternative to practical” iondolewe, kuwepo kwa mabweni na vyumba vya kutosha
hasa kwenye shule zilizojengwa kwenye mazingira magumu. Pia, ilipendekezwa kuwa
shule zijengewe uzio ili kuimarisha ulinzi. Sambamba na hilo wadau walipendekeza
kuwe na utaratibu wa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wa shule za kutwa
ili wanafunzi hao waweze kujifunza kwa ufanisi zaidi.
Aidha, ilipendekezwa kuwe na ziara za mafunzo na kuimarisha vyama vya kimasomo
ili kuwajengea wanafunzi na walimu utamaduni wa kusoma vitabu ili kuwapatia na
uwezo wa kujitafutia maarifa wenyewe kwa mfumo wa kujitegemea.
Kutokana na maoni hayo imeonekana kuna upungufu wa vifaa vya kufundishia na
kujifunzia, miundombinu ya kutosha, ziara za mafunzo na vyama vya masomo. Aidha,
ukosefu wa fedha, ubovu wa miundombinu, uchapaji na usambazaji mbaya wa vitabu
vinavyoendana na mihtasari iliyoboreshwa, na uelewa mdogo wa lugha ya Kiingereza
kwa walimu na wanafunzi, ni changamoto ambazo zinaathiri utekelezaji wa mitaala
shuleni.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
114
Pamoja na juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia
kama ilivyobainishwa katika MMES I na II, bado kuna changamoto za uwepo wa vifaa
vya kutosha. Aidha, zinahitajika juhudi za makusudi kuhamasisha wanafunzi
kupenda masomo ya Sayansi na Mathematics kwa kuhakikisha kuwepo kwa vifaa
toshelevu vya kufundishia na kujifunzia kwa sababu Taifa linahitaji wataalam ili
kuhimili ushindani wa kisayansi na kiteknolojia.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
115
SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
Sura hii inaainisha hitimisho la matokeo ya utafiti kwa kuzingatia masuala
yanayoendana na malengo mahsusi na maswali ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu
yameonesha sababu mbalimbali za kushuka kwa ufaulu zilizobainishwa na kujadiliwa
katika sura ya nne. Sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu zimegawanyika katika
sehemu mbili ambazo ni chanzo (cause) cha tatizo na athari (effects). Matokeo ya
utafiti yameonesha kuwa usimamizi na uendeshaji wa elimu katika ngazi zote ni
chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
mwaka 2010. Usimamizi na uendeshaji wenye mapungufu umeathiri utayarishaji na
utekelezaji wa mitaala, mfumo wa utayarishaji na uwepo wa walimu, mfumo na
taratibu za mitihani ya taifa, mazingira na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na
mfumo wa ufuatiliaji na tathmini ya utoaji wa elimu.
Aidha, mapendekezo yamewasilishwa kwa kila suala na kubainishwa kwa kuzingatia
muda wa utekelezaji ambao ni mfupi, wa kati na mrefu. Muda mfupi (MF) ni kipindi
chini ya mwaka mmoja, muda wa kati (MK) ni mwaka mmoja hadi mitatu na muda
mrefu (MR) ni zaidi ya miaka mitatu.
5.1. Usimamizi na Uendeshaji wa Elimui) Baadhi ya viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali wanateuliwa bila kuzingatia
vigezo vya utaalamu, uzoefu na uadilifu. Hali hii imepelekea kuwa na usimamizi na
uendeshaji usioridhisha na kuwepo na uwajibikaji mdogo katika ngazi mbalimbali
za kielimu;
ii) Maamuzi ya kitaalamu yahusuyo elimu pamoja na uendeshaji wake hufanyika
kisiasa na hivyo kuleta athari katika utekelezaji wa mipango ya utoaji wa elimu
bora nchini;
iii) Kuna ufinyu wa bajeti ya Wizara ya Elimu, TAMISEMI na Halmashauri, hivyo
usimamiaji na uendeshaji wa elimu kutokuwa na ufanisi unaotakiwa kulingana na
malengo ya elimu;
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
116
iv) Utekelezaji wa Sera ya matumizi ya vitabu vingi vya kiada hauendani na
upatikanaji wa vitabu vyenye ithibati na hivyo kusababisha kuwepo kwa vitabu vya
kughushi na kupenyezwa kwa vitabu visivyo na ubora; na
v) Kuna matatizo makubwa katika matumizi ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia
na kujifunzia katika elimu ya sekondari, na hivyo kuathiri ufundishaji na ujifunzaji.
vi) Kutokuwepo kwa uadilifu katika usimamizi na matumizi ya fedha zilizotengwa licha
ya ufinyu wa bajeti hali inayokwamisha kufikia malengo ya utoaji wa elimu bora;
na
vii) Kumekuwepo na ongezeko kubwa la wahitimu waliofeli katika mtihani wa Taifa wa
Kidato cha 4, hivyo kuwanyima fursa ya kuendelea na masomo ya juu na fani
mbalimbali.
Mapendekezo
a) Uendeshaji, usimamizi, mawasiliano na mahusiano baina ya asasi za kielimu,
Taasisi, ofisi za elimu mikoa, Halmashauri, na mashirika yasiyo ya kiserikali
uimarishwe katika utoaji wa elimu kwa ngazi zote; (MF)
b) Uadilifu katika usimamizi na matumizi ya fedha zilizotengwa uimarishwe; (MF)
c) Mchakato wa kutoa ithibati ufanyike kwa ukamilifu ili kupata vitabu vyenye ubora
unaotakiwa; (MF)
d) Ufuatialiaji wa usambazaji, upatikaji na utumiaji wa vitabu vya kiada na ziada
pamoja na vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia uimarishwe; (MF)
e) Ufundishaji na ujifunzaji wa somo la English kwa shule za Awali, Msingi na
Sekondari uimarishwe; (MF)
f) Uteuzi wa viongozi mbalimbali wa kielimu uzingatie uzoefu, utaalamu, uwezo,
uadilifu na uwajibikaji. Aidha, nafasi za uongozi zilizoachwa wazi zijazwe na
zisikaimishwe kwa muda mrefu ili kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa elimu;
(MK)
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
117
g) Klabu za masomo kama vile “English, Mathematics, Science na Geography clubs”
vianzishwe na kuimarishwa; (MF)
h) Mfumo wa kuandaa viongozi katika kuachiana madaraka (succession plan)
uanzishwe/kuimarishwa na kutumika; (MK)
i) Maamuzi yanayohusu masuala ya elimu yafanywe kwa kuzingatia utaalam,
tathmini na tafiti za kisayansi ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya
utoaji wa elimu; (MF)
j) Bajeti ya elimu iongezwe na izingatie vipaumbele katika sekta ya elimu ili kutatua
changamoto zilizopo; (MK)
k) Chombo cha Kusimamia Taaluma ya Ualimu (Teachers Professional Board)
kianzishwe kwa lengo la kushughulikia viwango vya taaluma, maadili, utendaji na
haki za walimu ili kulinda hadhi ya kazi ya ualimu na kuhakikisha kuwa inakidhi
malengo yaliyokusudiwa; (MK)
l) Utaratibu wa motisha kwa walimu unaoendana na uzito wa kazi, wadhifa na
ugumu wa mazingira anapofanyia kazi uandaliwe na utekelezwe ipasavyo; (MK)
m) Wanafunzi wanaofeli katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 wahimizwe kufanya
mitihani ya marudio kama watahiniwa binafsi ili wapate sifa za kujiendeleza
kitaaluma na kitaalamu; (MK)
n) Programu maalumu ya mafunzo ya lugha ya kiingereza kwa walimu wa masomo
yote ianzishwe na itekelezwe katika shule zote za sekondari; (MK) na
o) Sheria ya vitabu itungwe ili kudhibiti usambazaji na matumizi ya vitabu visivyo na
ithibati katika shule nchini. (MR) na
p) Vyuo vya ufundi stadi kama vile VETA, Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC),
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (CDTI) vipanuliwe ili kuwawezesha wanafunzi
wanaopenda kujiunga na vyuo hivyo kujiunga na kupata ujuzi na stadi za
kuwawezesha kuajiriwa na kujiajiri. (MR)
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
118
5.2. Utekelezaji wa mitaala
i) Mafunzo kabilishi juu ya mtaala ulioboreshwa mwaka 2005 na 2007 ambao
unazingatia ujuzi yametolewa kwa kiwango kidogo kwa walimu, wakaguzi na
Maafisa Mitihani na hivyo kutotekeleza mtaala ipasavyo;
ii) Dhana ya mtaala unaozingatia ujuzi (competence Based Curriculum) haieleweki
kwa wadau wengi wakiwemo maafisa mitaala, maafisa mitihani, wakaguzi wa
shule na walimu;
iii) Upungufu wa mihtasari ya masomo na vitabu vya kiada na ziada vinavyoendana
na mtaala ulioboreshwa katika shule na vyuo vya ualimu umeathiri mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji;
iv) Mitaala inatayarishwa bila kufanyiwa majaribio (piloting). Kutojaribisha mitaala
wakati wa utayarishaji wake kunasababisha kutekeleza mitaala yenye mapungufu
na isiyokidhi mahitaji ya jamii; na
v) Kuna tatizo la mfumo wa usambazaji wa mihtasari kutoka TET kwenda shuleni,
aidha TET huuza mihtasari na kusababisha upungufu shuleni.
Mapendekezo
a) Mafunzo maalumu kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa kwa maafisa mitaala na maafisa mitihani ili kuwajengea uwezo; (MF)
b) Mafunzo kabilishi kuhusu dhana ya mitaala inayozingatia ujuzi yaandaliwe na
kutekelezwa kwa walimu na wakaguzi wote; (MF)
c) Mihtasari ya kutosha isambazwe shuleni na isiuzwe. Aidha nakala laini (soft copy)
ya mihtasari iwekwe kwenye mtandao (website) ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi na TET ili wadau waweze kuipata kiurahisi; (MF)
d) Ithibati ya vitabu vyenye kukidhi mahitaji ya mtaala iharakishwe. Aidha mafunzo
elekezi yatolewe kwa waandishi na wachapishaji ili wachapishe vitabu
vinavyoendana na mtaala ulioboreshwa; (MK) na
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
119
e) Taratibu za utayarishaji wa mitaala zizingatiwe ikiwa ni pamoja na kufanya utafiti,
tathmini na kujaribisha mitaala kabla ya utekelezaji wake. (MR)
5.3. Mfumo na Taratibu za Mitihani ya Taifa
i) Muundo na aina ya maswali yanayotolewa na walimu katika ngazi ya shule kwa
kiasi kikubwa haufanani na ule wa mitihani ya Taifa. Hivyo upimaji wa wanafunzi
shuleni kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa katika mitihani ya Taifa;
ii) Wanafunzi wana uelewa mdogo wa lugha ya kufundishia (Kiingereza) na hivyo
kushindwa kujibu maswali ya mitihani ipasavyo;
iii) Kuna mianya ya uvujaji wa mitihani unaotokana na kutokuwa na vyumba vya
kuhifadhia mitihani (strong room) katika ngazi ya Halmashauri na shule;
iv) Uteuzi wa wasahihishaji unafanyika kwa upendeleo na hivyo kupoteza umakini
katika usahihishaji;
v) Wasahihishaji wa mitihani ya Taifa hulipwa kwa kiwango kidogo cha pesa na
kufanya kazi kwa muda mrefu kwa siku, na hivyo kushusha ari na kupoteza
umakini katika usahihishaji;
vi) Miongozo ya usahihishaji (marking scheme) ya baadhi ya masomo yenye
mapungufu na makosa katika baadhi ya maswali hutumika wakati wa usahihishaji
wa mitihani ya taifa, hivyo kuwanyima haki watahiniwa;
vii) Muundo wa mitihani (Format) kutowafikia baadhi ya walimu na hivyo kutopata
fursa ya kuutumia katika kuwaandaa wanafunzi;
viii) Mwongozo kuhusu mchango wa CA wa 50% (45% majaribio na mazoezi na 5%
projekti) katika mtihani wa Taifa hautumiki au mchakato wake katika matokeo ya
mwisho haufahamiki kwa wadau wa elimu. Hii inatoa matokeo ambayo siyo
halisia, pia ni kinyume na mwongozo wa mazoezi endelezi (CA) wa NECTA;
ix) Baadhi ya shule huwasilisha NECTA alama za CA zisizo na uhalisia na hivyo
kusababisha NECTA kukosa imani na alama hizo;
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
120
x) Ufaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 una athari katika ufaulu wa Mtihani
wa Taifa wa Kidato cha 4;
xi) Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 2 ni sehemu ya mazoezi endelezi (CA) na
hautumiki kuchuja wanafunzi kuendelea na Kidato cha 3. Hali hii imepunguza ari
ya ufundishaji na ujifunzaji;
xii) Utoaji wa adhabu ya kumshusha mtahiniwa daraja kutokana na kufeli kwa baadhi
ya masomo ya msingi na ya mchepuo hakuleti usawa katika ufaulu pia ni kinyume
na alama za madaraja husika; na
xiii) Kuna tofauti ya taratibu zinazotumika kupata gredi katika mitihani ya Taifa na
zile zinazotumika kupata gredi hizo katika mitihani ya shule. Hali hii inasababisha
watahiniwa kutopata gredi stahiki, hivyo kuathiri ufaulu.
Mapendekezo
a) Walimu wawapime wanafunzi kwa kuwapa mazoezi endelezi (CA) yenye uhalisia
(authentic) pia alama za CA zitumike katika Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4
kama ilivyoelekezwa katika mwongozo wa mazoezi endelezi; (MF)
b) Uteuzi wa wasahihishaji uzingatie sifa na usawa kutoka shule za kitaifa, jamii na
zisizo za serikali; (MF)
c) Utungaji na uhakiki wa mitihani ya taifa uboreshwe na uzingatie mitaala
inayotekelezwa; (MF)
d) Adhabu katika upangaji wa madaraja inayomshusha mtahiniwa hadi daraja la III
baada ya kufeli mojawapo ya masomo ya msingi au mchepuo iondolewe ili kila
mtahiniwa apate daraja linalolingana na kiwango cha ufaulu wake; (MF)
e) Fomati ya mitihani ya Taifa isambazwe katika shule zote na ufuatiliaji ufanyike
kuhakikisha kwamba kila mwalimu anaitumia; (MF)
f) Utaratibu wa kuweka kwenye mtandao (website) taarifa muhimu zinazohusu
taratibu na maelekezo mbalimbali ya uendeshaji wa mitihani ya Taifa na utoaji
matokeo uimarishwe. Kwa mfano ziwekwe fomati za mitihani, ripoti za tathmini za
mitihani, taratibu za mitihani; (MF)
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
121
g) Hadhi ya Mtihani wa taifa wa Kidato cha 2 irudishwe ili utumike kuchuja
wanafunzi. Aidha, wanafunzi wasiokuwa na uwezo wapatiwe masomo ya ziada
(Remedial); (MF)
h) Mfumo rasmi wa kupata gredi katika mitihani ya shule na Taifa unaofahamika
kwa wadau wote wa elimu utayarishwe na kutumika kikamilifu ili kuleta haki kwa
watahiniwa; (MF) na
i) Wasahihishaji wa mitihani ya taifa walipwe posho ya kujikimu (perdiem) kwa
sababu ni haki ya mwajiriwa wa serikali. (MK)
5.4. Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Utoaji wa Elimui) Mfumo wa ukaguzi wa shule za sekondari kuwa katika ya ngazi ya kanda hauleti
ufanisi katika ufuatiliaji na tathmini ya elimu; na
ii) Ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mtaala umefanyika kwa kiwango kidogo
hivyo kutobainika kwa dosari za utekelezaji wake;
Mapendekezo
a) Ukaguzi wa shule, utafiti wa elimu, ufuatiliaji na tathmini uimarishwe kwa kupatiwa
nyenzo na wataalamu wa kutosha ili kutoa maamuzi yenye uhalisia; (MF)
b) Viongozi wa elimu wafanye ziara za mara kwa mara na za kushtukiza shuleni ili
kufuatilia uendeshaji wa elimu; (MF)
c) Jukumu la kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mtaala litekeleze kikamilifu ili
kubaini dosari za kiutekelezaji na hivyo kufanya marekebisho stahiki; (MF) na
d) Ukaguzi wa shule ngazi ya elimu ya sekondari uwe katika ngazi ya Mkoa na
Halmashauri ili kusogeza huduma karibu na walengwa na kuimarisha usimamizi na
uendeshaji; (MK)
5.5. Mfumo wa utayarishaji wa walimu
i) Sifa za udahili wa mwalimu tarajali anayeandaliwa kufundisha elimu ya sekondari
ngazi ya stashahada (1 Principal, and 1 Subsidiary passes) hazitoshelezi kumfanya
mwalimu anayeandaliwa kuwa mahiri;
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
122
ii) Baadhi ya wadahiliwa katika vyuo vya ualimu kutokuwa na wito wa kazi ya ualimu
hivyo kusababisha walimu hao kutokuwa na maadili ya kazi ya ualimu na
kutodumu katika ajira;
iii) Matayarisho hafifu ya walimu tarajali yanatokana na wingi wa wanachuo darasani,
upungufu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kutotumika
kwa mbinu shirikishi. Hali hii inasababisha kutopata walimu mahiri wa kutekeleza
mtaala ulioboreshwa;
iv) Baadhi ya wanachuo wanaomaliza shahada ya elimu huajiriwa kuwa wakufunzi
katika vyuo vya ualimu moja kwa moja, utaratibu ambao unawafanya wanachuo
watayarishwe na wakufunzi wasio na uzoefu wa kufundisha; na
v) Wanachuo wengi wana tatizo la kutumia lugha ya kiingereza katika kuandika na
kujieleza, hivyo wanapohitimu hushindwa kutumia lugha hiyo katika kufundisha
katika shule za sekondari.
i) Kuna upungufu mkubwa wa walimu pamoja na usambazaji wa walimu usiofuata
uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi kati ya shule na shule, mijini na vijijini. Hali hii
inasababisha wanafunzi kutofundishwa ipasavyo;
ii) Kuna walimu wasio na sifa kufundisha sekondari ambao wapo katika shule za
sekondari wakifundisha bila utaalamu wa ualimu;
iii) Kuna upungufu mkubwa wa walimu unaosababishwa na walimu wa shule moja
kwenda masomoni kwa wakati mmoja hususan wa leseni, na hivyo kuathiri
ufundishaji na ujifunzaji shuleni; na
vi) Baadhi ya shule huwatumia wahitimu wa kidato cha 6 na 4 na wasiokuwa na
taaluma na maadili ya ualimu. Hii inasababisha wanafunzi kutopata fursa ya elimu
na malezi bora.
Mapendekezo
a) Walimu wasambazwe kwa usawa kwa kuzingatia mahitaji (ikama) katika shule
zote; (MF)
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
123
b) Programu za mafunzo zisizoathiri ikama ya walimu katika kila shule ziandaliwe;
(MF)
c) Uanzishwe utaratibu wa kuwatumia walimu kufundisha shule zaidi ya moja kwa
masomo yenye ukosefu au upungufu wa walimu; (MF)
d) Sifa za udahili wa kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya stashahada
zipandishwe kuwa Principal 2 za masomo atakayofundisha, ili kumwezesha
mwalimu kuwa mahiri kitaaluma; (MK)
e) Vifaa vya kufundishia na kujifunzia vya kutosha vipatikane na upanuzi wa
miundombinu ufanyike katika vyuo vya ualimu na vyuo vikuu ili kuendana na
ongezo la udahili na kufikia viwango vilivyowekwa; (MK)
f) Wakufunzi na wahadhiri wapewe mafunzo kazini juu ya mtaala unaozingatia ujuzi
(Competence Based Curriculum) ; (MK)
g) Wakufunzi mahiri na wenye uzoefu wa kufundisha katika shule za sekondari
waajiriwe. Aidha wahitimu wa vyuo vikuu wanaoajiriwa moja kwa moja waanzie
kazi katika shule za sekondari za mazoezi; (MK)
h) Uhamasishaji ufanyike kwa wahitimu wa kidato cha 6 na vyuo vikuu kuelewa fursa
za kazi ya ualimu ili waweze kuijiunga na kuifanya kazi hiyo; (MK)
i) Maabara ya lugha ya kiingereza (language laboratory) zianzishwe na kuimarishwa
katika Vyuo vya ualimu na Vyuo vikuu ambapo walimu tarajali watatumia
kujifunzia lugha ya kiingereza ili kuongeza stadi za kuongea na kuandika; (MR)
j) Udahili wa walimu tarajali uzingatie mahitaji ya walimu kimasomo ili kukabiliana na
upungufu walimu katika baadhi ya masomo; (MK)
k) Udahili wa walimu tarajali ngazi ya stashahada ufanyike kwa wahitimu wa Kidato
cha 4 waliojaza “Sel Form” na mafunzo yawe miaka mitatu yakijumuisha masomo
ya taaluma (Kidato cha 5-6) na ualimu ili kupata walimu mahiri na wenye wito;
(MK)
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
124
l) Utaratibu maalumu uanzishwe kwa kuwapatia mafunzo ya Ualimu (Post Graduate
Diploma in Education) wahitimu wa shahada zisizo za ualimu ili kukabiliana na
tatizo la upungufu wa walimu kwa muda mfupi; (MK)
m) Utaratibu wa kutumia/kuajiri watu ambao sio walimu kufundishaji katika shule za
sekondari uachwe; (MK)
n) Utaratibu uandaliwe wa kuwaendeleza walimu wanaofundisha katika shule za
sekondari ambao hawana utaalam wa ualimu ili kuwajengea uwezo walimu hao;
(MK)
o) Utaratibu uanzishwe wa kuwatumia Walimu na Maafisa wa Elimu wastaafu ili kutumia
uzoefu wao katika kufanikisha shughuli mbalimbali za elimu; (MK)
p) Wahitimu wa kidato cha 6, 4 na vyuo vikuu wanaofundisha katika shule za
sekondari wajiendeleze kwa kusomea taaluma ya ualimu; (MK) na
q) Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji yaimarishwe. (MK)
5.6. Mazingira ya Kufundishia na Kujifunzia
i) Kuna upungufu mkubwa wa samani na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Hali hii inasababisha wanafunzi kutoshiriki kikamilifu katika mchakato wa
ufundishaji na ujifunzaji;
ii) Baadhi ya shule zimepata usajili bila kutimiza vigezo vinavyohitajika kama vile
maabara za Sayansi, maktaba, ofisi na nyumba za walimu na hivyo shule hizo
kuendeshwa kwa mapungufu;
iii) Baadhi ya shule zimejengwa mbali na makazi ya wanafunzi na walimu. Hali hii
inawasababisha walimu na wanafunzi kutumia muda mrefu wa kwenda na kurudi
shuleni na hivyo kupunguza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji; na
iv) Kutokuwepo kwa chakula cha mchana katika shule za kutwa, hivyo kuathiri
mahudhurio na umakini wa wanafunzi katika ujifunzaji.
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
125
Mapendekezo
j) Jamii na wadau wengine wa elimu wahamasishwe kugharamia elimu nchini; (MF)
k) Usajili wa vyuo na shule za Serikali na zisizo za Serikali uzingatie vigezo
vinavyotakiwa; (MF)
l) Fedha za kutosha kwa ajili ya kununua samani na vifaa vya kufundishia na
kujifunzia shuleni zitengwe na kutumika ipasavyo; (MK)
m) Utaratibu wa usafiri wa wanafunzi na walimu kwenda na kurudi shuleni uandaliwe
kwa shule ambazo ziko mbali na makazi ya walimu na wanafunzi; (MK)
n) Hosteli/mabweni na nyumba za walimu zijengwe kwenye shule zilizo mbali na
makazi ya wanafunzi na ya walimu; (MR) na
o) Wanafunzi katika shule zote za kutwa wapatiwe chakula cha mchana ili kuimarisha
ufundishaji na ujifunzaji. (MR)
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
126
REJEA1.0 Lissu H. S (2008). Public Perception On The Use Of Continuous Assessment
Marks In Grading O-Level Secondary, M.Ed. (Science Education) Dissertation(Unpublished), Faculty of Education, University of Dar es Salaam.
2.0 Natinal Examinations Council of Tanzania: Examinations Processing, Dar es Salaam, July, 1986
3.0 National Examinations Council of Tanzania: NECTA WEBSITE, Dar es Salaam, May 2001
4.0 National Examinations Council of Tanzania: The Examinations Regulations, Dar es Salaam, 2006.
5.0 NECTA, 2004. Thirty Years of National Examinations Council of Tanzania (1973-2003). Dar es Salaam.
6.0 National Examinations Council of Tanzania: Certificate of Secondary Eeducation Examination, Paper on Literature in English, Dar es Salaam, Oktober, 2010
7.0 National Examinations Council of Tanzania: Certificate of secondary Education Examination Format, Dar es Salaam, February, 2008
8.0 National Examinations Counci of Tanzania: Guidelines on the Conduct and Administration of Continuous assessment in Secondary Schools and teacher Training Colleges, Dar es Salaam,
9.0 United Republic of Tanzania: Education and Traininng Poplicy, Ministry of Education, Dar es Salaam, 1995.
10.0 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi: Waraka wa Elimu Na. 1 wa Mwaka 2006, WEMU, 2006
11.0 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi: Waraka wa Elimu Na. 5 wa Mwaka 1999, Mtihani wa kidato cha Pili katika Shule za Sekondari, WEMU, 1999.
12.0 Babyegeya E (2006) Teacher Education in Tanzania: developments and prospects, Journal of Issues and practice in Education (pg.32-46).
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
127
13.0 TIE (1991) A Summary Report on baseline Survey on primary, secondary and Teacher Education Curriculum Reform in Tanzania Mainland, MOEVT, Dsm.
14.0 Meena W.E. (2009) Curriculum Innovation in Teacher Education. Abo Academy University Press.
15.0 Osaki K.M. (1996) “Changing Forms of Curriculum in Tanzania” in Papers in Education and Development No. 17, DSM.
16.0 IBE/UNESCO (Dec 2000) Capacity Building for Curriculum Specialists in East & South East Asia and The Pacific, Bangkok, Thailand.
17.0 WEU (1995) Sera ya Elimu na Mafunzo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dar es Salaam.
18.0 TIE (2003) National Curriculum Development Framework (NCDF), TIE, Dar es Salaam.
19.0 TIE, (2008) Secondary Education Curriculum for Tanzania Mainland. Dar es Salaam.
20.0 TET ( Februari 2011) Taarifa ya Utekelezaji wa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Elimu na Walimu kwa miaka 2005-2010, TET Dar es Salaam.
21.0 WEU (Juni 2005) Marekebisho ya Mtaala wa sekondari na Kuunganishwa kwa Masomo, Wizara ya Elimu na Utamaduni, Dar es Salaam.
22.0 MOEVT (2007) Teacher Development Management Strategy (TDMS), Ministry of Education & Vocational Training, Dar es Salaam.
23.0 MoEVT (2001) Practices and Possibilities in Teacher Education in Tanzania, edited by Mhando et al., Ministry of Education and Vocational Training , Dsm
24.0 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Februari 1982), Mfumo wa Elimu ya Tanzania 1981-2000:Ripoti na Mapendekezo ya Tume ya Rais ya Elimu, Juzuu la Kwanza, JMT, Dsm.
25.0 MoEVT (May 2004) A Deliberate Support to Licensed Teachers-Facilitator and Mentor’s Guide, Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
26.0 WEMU (2006), Kiongozi cha Mkaguzi wa shule. Dar es Salaam
27.0 WEMU (2009), Hotuba ya bajeti ya WEMU 2009/2010 p.43). Dar es Salaam
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
128
28.0 Ngodu, A. S . (2007), Licensed Teachers’ Professional Develepment and the Fate of Teaching Science and Mathematics in Secondary Schools. M.Ed. (Science Education) Dissertation. (Published), Faculty of Education, University of Dar es Salaam.
29.0 WEMU (2009), Mihtasari ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada iliyorekebishwa, na Utaratibu wa Kutahini (Barua ya Kamshina), Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm
30.0 MoEVT (2010) Basic Education Statistics in Tanzania, 2006 – 2010, Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
31.0 WEMU (2010) Moduli ya Ujuzi wa Kufundisha kwa Umahiri, MWAKEM, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, DSM
32.0 MoEVT (2005) Facts About Basic Education in Tanzania, Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
33.0 MoEVT (2001), Construction of Secondary Schools, Guidelines for Buildings and Furniture., Ministry of Education and Vocational Training , Dsm
34.0 WEMU (2007), Utaratibu wa kuzingatia katika kuanzisha Shule za Serikali za kutwa zinazojengwa kwa nguvu za wananchi (Barua ya Kamshina), wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm
35.0 WEMU (2005), Nyaraka za Elimu za mwaka 1998 – 2005, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dsm
36.0 MoEVT( 2008), Education Sector Development Program(EDSP) (2008 – 17), Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
37.0 MoEVT (2004), Secondary Education Development Program(SEDP) (2004 –2009), Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
38.0 MoEVT (2010), Education Sector Review Aide Memoire. Ministry of Education and Vocational Training, Dsm
39.0 MoEVT, The Teacher Management Development Strategy 2008 – 2013
40.0 Wizara ya elimu na Utamaduni (1997 ) Kiongozi cha Mkuu wa shule ya Sekondari . Dar es Salaam
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
129
41.0 MOEVT (2010), Secondary Education Development Program II (SEDP II) 2010 – 2014, MOEVT, Dsm
42.0 Nyerere (1967), Education for Self Reliance ……………………………………………
43.0 MOEVT (2002), Primary Education Development Program I (PEDP I) 2002 -2006, MOEVT, Dsm
44.0 MOEVT (2017), Updated Secondary Education Development Program I (SEDP I) 2007, MOEVT, Dsm
45.0 MOEVT (2007), Primary Education Development Program I (PEDP I) 2002 -2006, MOEVT, Dsm
46.0 WEMU (2009), Waraka wa Elimu Na.13 wa mwaka 2009, WEMU, Dsm
47.0 MOEVT (2010), Public Expenditure Tracking Survey, MOEVT, Dsm
48.0 OWM-TAMISEMI (2011), Taarifa ya OWM-TAMISEMI……………………………
Na. Eneo la Utafiti Ngazi1 Taasisi ya Elimu Tanzania Taifa2 Baraza la Mitihani la taifa Taifa3 Vyuo Vikuu Mkoa/Taifa4 Vyuo vya Ualimu Mkoa5 Uk aguzi wa Shule Kanda Kanda6 Ukaguzi wa Shule Wilaya Wilaya7 Elimu Mkoa Mkoa8 Elimu – Halmashauri(M) na (S) Wilaya9 Tume ya Utumishi wa Umma (TSD) Wilaya10 Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Wilaya11 Madhehebu ya Dini Wilaya12 Mashirika yasiyo ya Kiserikali Wilaya13 TAMONGSCO Taifa14 TEN/MET Taifa15 Ofisi ya Mh. Mbunge Wilaya16 Ofisi ya Mh. Diwani Kata
www.JamiiF
orums.com
Rasimu 2
132
Kiambatisho 3.5: Zana na Idadi ya Wajibuji Kitaifa na Kimkoa
Na AINA YA ZANA WAJIBUJI
MALENGO IDADI YA WAJIBUJI WALIOPATIKANA KITAIFA NA KIMKOA
JUMLA
KIM
KO
A
KIT
AIF
A
KIT
AIF
A
RU
VU
MA
RU
KW
A
SH
INY
AN
GA
SIN
GID
A
DS
M
PW
AN
I
KA
GE
RA
MA
RA
LIN
DI
MA
NY
AR
A
TA
NG
A
1 Dodoso A Wakaguzi wa Shule Kanda 4 44 4 4 4 4 4 4 1 4 4 4 4 412 Dodoso B Mkuu wa Shule 12 132 12 12 12 12 12 12 12 12 13 12 12 1323 Dodoso C Wakurugenzi TET 4 4 44 Dodoso D Wakuu wa Idara za Mitihani NECTA 5 4 45 Hojaji A Wahadhiri - Vyuo Vikuu 2 4 46 Hojaji A Wanachuo- vyuo Vikuu vya Elimu 2 4 47 Hojaji A Wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu 2 22 2 2 2 4 2 2 8 2 2 2 288 Hojaji A Wanachuo- vyuo vya Ualimu 4 44 4 4 4 8 4 4 6 4 4 2 449 Hojaji B Afisa Elimu Mkoa 1 11 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1 1110 Hojaji B Wakurugenzi Halmashauri 2 22 2 1 2 2 2 1 2 1 2 1511 Hojaji B Afisa Elimu Halmashauri (S) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 1 2 2 2 2112 Hojaji C Afisa Elimu Halmashauri (M) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 1 2 2 2 2113 Hojaji C Mkaguzi Mkuu wa Shule(W) 2 22 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2 2214 Hojaji D Maafisa Tume ya Utumishi wa
Umma TSD (W)2 22 2
2 2 2 2 2 2 2 2 2 222
15 Hojaji E Afisa CWT (W) 2 22 2 2 3 2 2 2 2 2 2 2 2 2316 Hojaji E Viongozi wa Dini 4 22 4 4 2 4 4 4 4 2 4 4 4 4017 Hojaji E Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 2 22 2 1 2 2 2 1 1 2 2 2 1718 Hojaji F Wabunge 2 22 1 2 2 2 2 1 3 1 2 1 1719 Hojaji F Madiwani 2 22 2 2 5 11 2 2 2 11 2 2 2 4320 Hojaji F Wazazi/Walezi 4 44 4 4 35 21 4 4 4 5 4 6 4 9521 Hojaji G Wajumbe wa Bodi ya Shule 4 44 4 4 18 17 4 4 4 16 4 3 4 8222 Hojaji H Wahitimu wa Kidato cha 4 - 2010 60 660 39 48 23 30 24 60 15 73 17 12 60 40123 Mahojiano ya Pamoja A Wakuza Mitaala 5 10 1024 Mahojiano ya Pamoja B Maafisa Mitihani (NECTA) 5 8 825 Mahojiano ya Pamoja C TAMONGSCO 5 6 626 Mahojiano ya Pamoja C TENMET 5 6 627 Mahojiano ya Pamoja D Walimu 60 660 43 67 67 43 72 60 50 48 51 52 60 61328 Mahojiano ya Pamoja E Walimu Wasahihishaji Mitihani
Kidato cha 460 660 8
4 9 7 30 24 5 4 3 8 60 162
29 Mahojiano ya Pamoja F Wanafunzi Kidato cha 3-4 120 1320 108 109 106 115 120 116 100 112 130 4 120 1140