Top Banner
AL-KASHIF AL-KASHIF SWAHILI - JUZUU YA PILI
247

Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Mar 07, 2016

Download

Documents

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambo mengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwa wafasiri wengine.
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

AL-KASHIFAL-KASHIFSWAHILI - JUZUU YA PILI

Page 2: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 9987 665 34 - 9

Kimeandikwa na:Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya

Kimetafsiriwa na:Sheikh Hasan Mwalupa

P.O. Box 1017, Dar es Salaam/Tanzania.Email:[email protected]

Kimehaririwa na: Dr.M.S. Kanju.

S.L.P 1017, Dar es Salaam.Email: [email protected]: www.dartabligh.org

Kupangwa katika kompyuta na:Ukhti Pili Rajabu.

Toleo la kwanza: Februari 2004Nakala:5000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

P.O. Box 1017Dar es Salaam, TanzaniaSimu:+255 22 2110640Fax: +255 22 2126757

Email: [email protected]: www.alitrah.org

Page 3: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

YALIYOMO

AL- BAQARAH –(Sura ya pili)

Aya 142: Nini kilichowageuza kutoka Qibla chao . . . . . . . . . . .2

Kwa nini kuswali upande maalum . . . . . . . . . . . . . . .2

Aya 143: Tumewafanya kuwa ni Umma wa wastani . . . . . . . . .4

Ukamilifu na uwiano katika Uislamu . . . . . . . . . . . . .6

Aya 144-145: Hakika tunakuona unavyogeuza uso wako................10

Ni wakati gani unapasa kuelekea Qibla......................14

Watu wa Qibla.............................................................14

Uislamu na watu wenye upendeleo na dini zao 16

Aya 146-147: Wanamjua kama wanavyowajua watoto wao . . . . . . . .

18

Mimi na Mhubiri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

18

Aya 148-152: Kila Umma ulikuwa na Qibla chake . . . . . . . . . . . . . .

20

Katiba ya Uislamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

24

Page 4: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Kumshukuru Mneemeshaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

26

Aya 153-157: Jisaidieni kwa Subira . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

26

Thamani ya Pepo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

30

Aina ya malipo ya wanaosubiri . . . . . . . . . . . . . . . . .

32

Aya 158: Swafa na Marwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

34

Aya 159-162: Wanaoficha yaliyoteremshwa . . . . . . . . . . . . . . . . . .

36

Ubaya wa adhabu bila ya ubainifu . . . . . . . . . . . . . . .

38

Hukumu ya laana katika sharia . . . . . . . . . . . . . . . .

40

Aya 163-164: Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja . . . . . . . . . . . . . . .

42

Mbingu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

42

Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Page 5: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

42

Kuwapo Mungu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

44

Upi uliotangulia Usiku au Mchana . . . . . . . . . . . . . . .

46

Aya 165-167: Wanafanya waungu asiyekuwa

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

46

Taqlid na Maimamu Wanne . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

50

Aya 168-170: Kuleni vilivyomo katika Ardhi . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

50

Kufuata na msingi wa itikadi . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

54

Aya 171: Mfano wa anayeita asiyesikia . . . . . . . . . . . . . . . . . .

58

Aya 172-173: Kuleni Vizuri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

60

Mwenye dharura na hukumu yake . . . . . . . . . . . . . .

62

Aya 174-176: Wafichao aliyoyateremsha

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Page 6: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

62

Mvutano kati ya Haki na Batili . . . . . . . . . . . . . . . . . .

66

Aya 177: Anatoa mali akiwa aipenda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

68

Wema katika ufahamu wa Ki-Qur’an . . . . . . . . . . . . .

74

Aya 178-179: Kisasi cha waliouawa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

74

Aya 180-182: Wasia kwa wazazi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

80

Kuwausia warithi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

82

Aya 183-185: Mmelazimishwa kufunga . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

84

Aya 186: Naitikia maombi ya mwombaji . . . . . . . . . . . . . . . . . .

88

Aya 187: Mmehalalishiwa Usiku wa Saumu . . . . . . . . . . . . . .

90

Aya 188: Kula mali kwa Batili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

92 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Hukumu ya kadhi fasiki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Page 7: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu.

UTANGULIZI WA MCHAPISHAJI

Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako hivi sasa ni juhudi ya miaka mingisana ya watu waliojitolea kuona kazi hii imefanikiwa bila ya kumsahauMarhum Abu Muhammad wa London.

Kama lilivyo jina la Tafsiri yenyewe ndivyo ilivyo Tafsiri yenyewe ambayomwanachuoni huyu mahiri kabisa aliyeifafanua ni mtu aliyebobea katikafani zote ambazo mfasiri (Mfafanuzi) anatakiwa awe nazo.

Sheikh Muhammad Jawad Mughniyya ameonesha cheche zake katikavitabu vingi alivyoviandika katika maudhui mbali mbalimbali na hivyokujipatia wasomaji wengi sana.

Msomi huyu, mwenye fikra huru na anayetetea kile anachokiamini, nimtu mwenye mawazo mapana na kuyaangalia mambo kwa undanisana, kipaumbele chake ni katika maslahi ya umma huu na amejaribusana kwenda na wakati.

Sifa kubwa pekee ya mwanachuoni huyu ni kuwa yeye hakujihusishasana na kung’ang’ania madhehebu fulani tu, labda hii yatokana na wad-hifa wake wa ukadhi aliokuwa nao katika nchi ya Lebanon ambayo inamadhehebu mengi, ambapo sula la madhehebu ni nyeti nchini humo,hata hivyo yeye aliweza kuamua matatizo ya watu kwenye ofisi yakekulingana na madhehebu yao pale walipomwendea, hiyo ilimsaidia sana

i

Page 8: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

hata kuweza kutoa kitabu kitwacho ‘Al-Fiqh a’laa madhaahabil-khamsah’(Fikhi ya madhehebu matano) yaani ya Hanafi, Maaliki, Shafi, Hambali naShia (ambacho twataraji kitatoka hivi karibuni Inshaallah).

Jambo lililotupa msukumo wa kukifasiri kitabu hiki kwa lugha yaKiswahili ni zile faida nyingi atakazozipata msomaji na kujua mambomengi na ya ajabu yaliyo mapya kwake ambayo si rahisi kuyapata kwawafasiri wengine.Msomaji atapata faida katika fani za Sayansi, Siasa, Historia, Mashairi,visa vizuri, na Saikolojia miongoni mwa mengine; ndiyo maana msoma-ji atashangaa kidogo anapoisoma Tafsiri hii atakapoona mwandishiamewataja na kuwanukuu watu kama kina Mfalme Edward, wanasyan-si kama kina Enstein, Charlie Champlin (Mchekeshaji maarufu), nawengineo, hali inayoifanya tafsiri hii kuwa ni ya kipekee kabisa.

Mtindo alioutumia mwandishi ni sahali uliokusudiwa watu wa tabakambalimbali, wanavyuoni na watu wa kawaida.

Nia yetu ni kukigawanya kitabu hiki bure lakini tumelazimika kukiuzakwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji.

Mwisho: Shukrani kubwa iwaendee bila ya kuwataja watu waliojitoleausiku na mchana, jopo la wafasiri, wahariri, wachapaji, waliotupa moyona kutoa maoni yao na walioisimamia ili kuhakikisha kwamba kitabukimemfikia msomaji.

Mchapishaji.

ii

Page 9: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Makosa ya Chapa.

Sikumbuki kama nimewahi kusoma kitabu kilichotoka kupigwa chapa, chazamani au cha sasa, bila ya kukuta makosa ya chapa. Nafikiri sitasomakitabu kisichokuwa hivyo. Nimejaribu sana kuliepuka hilo katika tungozangu, lakini sikufanikiwa.

Nilikuwa sifikirii kama ninaweza kuona makosa haya katika maandishi yaMsahafu Mtukufu, kama yale yaliyo katika baadhi ya chapa; kwa mfanoneno yabswatu kwa swad, badala ya yabsutu kwa sin, na katika chapa yaTafsir Arrazi ya Misr ya mwaka 1935, Sura ya (2:146). Imeandikwa LaYa’alamuun, (hawajui) badala ya Ya’alamuun (wanajua). Mfano wamakosa haya hausameheki.

Katika Tafsir Al-Manar, chapa ya Pili, sura (5:212), imeandikwa“Fawqahum ila yawmil qiyama badala ya Fawqahum yawamal qiyama”.Hatuwezi kusema kosa hili ni kubwa zaidi kuliko lile.

Lakini mkosaji atatuletea udhuru kwa msemo mashuhuri huko kwetu jabalamail ‘Makosa ya chapa.’

Katika Tafsiri Majmau chapa ya Urfan, Sura (46:15), imeandikwa: “ Hattaidaha balagha arbai’ na sanah badala ya: Hattaidaha balagha ashuddahuarbai ‘ na sanah”

Kusema hivi sio kama ninajitetea kutokana na makosa ya chapa atakay-oyakuta msomaji katika kitabu hiki, ijapokuwa naomba msamaha kamalitatokea hili, lakini makusudio yangu hasa ni kumwambia yule atakayefun-gua macho yake kwenye makosa ya matamko na kuufungia macho uzuriwa maana. Vilevile ninamwambia yule ambaye siku moja aliniambia:“Vitabu vyako vimejaa makosa ya chapa, kama kwamba hakuna kitu cho-chote katika vitabu hivyo isipokuwa makosa ya chapa tu. Wote haoninawaambia: Mungu awasamehe na aniongoze mimi na nyinyi.

Vyovyote iwavyo, mimi ninaomba msamaha kutokana na makosa yakifikra na ya chapa. Anasema Amirul Muminiin (a.s): “Watu wote ni wapun-gufu wenye kuchanganyikiwa, isipokuwa yule aliyehifadhiwa na MwenyeziMungu.” Na Mwenyezi Mungu (s.w.t) ndiye mwenye jukumu la kunikubaliayale niliyoyapatia na kunisamehe niliyakosea, kwa jaha ya Mtume na kizazichake, ziwashukie rehema na amani (Amin).

MUHAMMAD JAWAD MUGHNIYYAH

iii

Page 10: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

iv

Page 11: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

142. Watasema wapumbavumiongoni mwa watu: Ninikilichowageuza na kibla chaowalichokuwa nacho? Sema:Mashariki na Magharibi niya Mwenyezi Mungu.Humwongoza amtakayekwenye njia iliyonyooka.

NINI KILICHOWAGEUZA NA KIBLA CHAO?

Aya 142:

LUGHAAmesema Ibnul Arabi katika Tafsiri yake: “Kila asiyejua hakika ya dini yaKiislamu, huyo ni mpumbavu kwa sababu yeye ana akili hafifu. Nenokibla limechukuliwa kutoka katika neno isitqbal (kuelekea); yaani kilaupande anaouelekea mtu.

MAANA

Watasema wapumbavu miongoni mwa watu: Nini kilichowageuza nakibla chao walichokuwa nacho?

Mitume waliotangulia walikuwa wakiswali kuelekea Baitul Maqdis. NaMtume s.a.w.w, kwa amri ya Mwenyezi Mungu, aliswali akielekea hukokwa muda usio mfupi. Lakini alikuwa akitamani lau kibla kingegeuzwakuwa Al-Kaaba; na Mwenyezi Mungu alikathibitisha matamanio yake,kama itakavyoelezwa.

Makusudio ya wapumbavu hapa ni Mayahudi, kwa sababu ndio waliowalau-mu Waislamu kuacha kwao kuelekea Baitu Maqdis.Tamko sayaqulu (watasema) kwa dhahiri linafahamisha kuwa MwenyeziMungu alimfahamisha Mtume Wake Mtukufu kauli ya wajinga kabla yakutokea. Ama yule anayesema kuwa neno sayaqulu, ingawaje kwa dhahirilinafahamisha siku za usoni, lakini makusudio yake ni muda uliopita; nakwamba Mwenyezi Mungu alimwambia Mtume Wake baada ya kusema

Page 12: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

2

wajinga, sio kabla ya kusema. Neno hilo limekuja kwa muda ujao, kwa vileyaliyosemwa yalikuwa yamekwisha kadiriwa. Ama kwa hakika kauli hii nikujaribu kutoa tafsiri nyingine (taawil) bila ya dharura yoyote, na bila yadalili yoyote inayofahamisha hilo.

Kwa vyovyote ilivyo ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrishaMtume Wake Mtukufu Muhammad (s.a.w.w), kuwajibu wajinga hawa kwam-ba:

Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Humwongozaamtakaye kwenye njia iliyonyooka.

Yaani pande zote ni za Mwenyezi Mungu;

na kwamba Al-Kaaba na Baitul Maqdis kwake ni sawa tu. Lakini kwahekima na masilahi mara nyingine humwongoza anayemtaka kwenyeBaitul Maqdis, na mara nyingine kwenye Al-Kaaba.

KWA NINI KUSWALI UPANDE MAALUM?

Hapa pana swali wanaloliuliza watu wengi; nalo ni: Kwa nini swala niwajibu kwa kuelekea upande maalum, na haiswihi isipokuwa upande huo,Na pamoja na kujua kuwa Yeye (s..w.t) yuko kila mahali? amekwishasema waziwazi:

“ ....basi mahala popote muelekeapo ndipo kwenye uelekeo wa MwenyeziMungu (2:115).

Jibu: Kwanza Mwenyezi Mungu s.w.t. amesema:

“...Na elekeza uso wako upande wa msikiti Mtakatifu (Al-Kaaba); napopote mlipo zielekezeni nyuso zenu upande huo...” (2:144).

Page 13: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

3

Aya hii ni ubainifu na tafsiri ya Aya 115; na makusudio yake ni kuwakuelekea upande wowote katika swala ni katika swala ya sunna wakati wakwenda au kuwa juu ya chombo, na katika swala ya asiyejua kibla kikowapi.

Makusudio ya Aya 144 ni kuelekea (Al-Kaaba) katika swala ya wajibu.Ufafanuzi wa hilo umekwishatangulia katika Aya 115.

Pili, usahihi wa swala unategemea amri ya Mwenyezi Mungu. Kutokana naasili hii hapana budi tuangalie: Je amri ni tuswali upande wowote tunaouta-ka sisi au upande maalum. Ikiwa kauli ya kwanza ndiyo sawa, basi itakuwayaswihi swal akwa kuelekea upande wowote tutakaa. Ikiwa ni kauli ya pili,basi itakuwa haiswihi swala isipokuwa upande ulioamrishwa tu; ni sawaiwe ni Al-Kaaba au Baitul Maqdis, au mahali pengine.

kwa neno zima, kufuata amri ni jambo mbali na kuweko Mwenyezi Mungukila upande ni jambo jengine.

Ibada ni katika mambo yanayongoja ubainifu wa Mwenyezi Mungu kupitiakwa Mtume Wake, wala hakuna nafasi ya dhana na uwezekano; isipokuwakwa nassi sahihi iliyo wazi. Na Mwenyezi Mungu aliamrisha Waislamukuswali kuelekea Baitul Maqdis kwanza. Lau wangeliswali kwa kuelekeaAl-Kaaba isingekubaliwa swala yao. Kisha akawaamrisha kugeukia Al-Kaaba. Lau wangelielekea BaitulMaqdisi baada ya amri hiyo, basiisingekubaliwa swala yao; pamoja na kuwa pande zote mbili ni zaMwenyezi Mungu. Hilo ni kwa sababu ya kuwa kipimo cha kusihi swalani kuafikiana na sharti zote, kama vile ambavyo kuharibika kwake ni kuhal-ifu amri.

Page 14: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

4

UMMA WA WASTANI

Aya ya 143

LUGHA

Neno wast lina maana ya ‘kati kati’; na neno wasat lina maana ya ‘ubora’.Mtume anasema: Bora ya mambo ni wastani. Linakuja neno wasata kwamaana ya ‘kulingana sawa’ (wastani). Neno wastani na ubora yanakuru-biana.

Makusudio ya wasat hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameijaaliadini ya Waislamu ni ya wastani; yaani ni ya kati na kati katika itikadi namaadili. Kwa upande wa itikadi, hakuna ushirikina wala ulahidi, bali nitawhidi tu. Na kwa upande wa maadili, sio ya kimaada wala kiroho, bali nipande zote mbili kwa sharti ya kulingana sawa na kukamilika.

143. Na kama hivyo hivyo tume-wafanya kuwa umma wawastani, ili muwe mashahidijuu ya watu wote, na Mtumeawe shahidi juu yenu. Nahatukukifanya kibla uli-chokuwa nacho ila tupatekumjua yule anayemfuataMtume na yule atakayegeukaakarudi nyuma . Na kwahakika lilikuwa ni gumuisipokuwa kwa wale ambaoMwenyezi Mungu aliowaon-goza. Na hakuwa MwenyeziMungu ni Mwenyekuwapotezea imani yenu.Hakika Mwenyezi Mungu,kwa watu, ni Mpole, Mwenyekurehemu.

Page 15: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

5

Neno ‘kurudi nyuma’ ni istiara ya kueleza mtu anayemkufuru MwenyeziMungu na Mtume Wake, kwa sababu mwenye kuacha imani yake yukokatika daraja ya asiyeendelea mbele.MAANA

Na kama hivyo hivyo tumewafanya kuwa umma wa wastani

Jumla hii ni ubainifu wa kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Na Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.” (2:213).

Hilo ni kubainisha kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaneemeshawafuasi wa Muhammad (s.a.w.w) kwa uongofu. Linalodhihirisha zaidiuongofu huu ni kuwa Yeye amewajaalia wao kuwa katikati; yaanihawakuzidisha, kama vile kuzidisha waungu, wala hawakupunguza, kamavile ulahidi (kumkana Mungu). Hayo ni upande wa kiitikadi. Ama upandewa kimaadili, wastani wake ni kwa kuwa amewachanganyia mambo yakiroho na ya kimwili katika mafunzo yake na maelekezo yake - sio ubahiliwa kiroho wala ubadhirifu wa kimaada, bali kuna uwiano kati yao.

Baadhi wameifanya kauli hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. “Tumewafanyakuwa umma wa wastani”, kuwa ni dalili ya hoja ya ijmai. Lakini hiyo nikutoa dalili mahali pasipokuwa pake, kwa sababu haikuja kubainisha kuwaijmai, ni hoja au sio hoja.

Wengine wamesema kwamba kauli hii ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) inafa-hamisha kuwa kila Mwislamu ni mwadilifu kwa tabia. Hii pia nayo nibatili kabisa, kwa sababu uadilifu hauthibiti isipokuwa kwa kujua au kwaushahidi.

UKAMILIFU NA UWIANO KATIKA UISLAMU

Binadamu ni mwili uliotokana na mchanga unaokwisha, na ni roho inay-odumu inayotokana na siri ya Mwenyezi Mungu, kama alivyosema: “Nawanakuuliza kuhusu roho. Sema: Roho inatokana na amri ya Mola

Page 16: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

6

wangu.” (17:85). Kwa vile vitu viwili hivyo (mwili na roho) vina mahita-ji na matakwa ndipo ikaletwa sharia ya Kiislamu kwa ajili ya kutoamaelekezo ya msingi na nidhamu ili visizidiane. Kwa maneno menginebinadamu ni sehemu mbili. Kuipuuza mojawapo ni kupuuza dhati yabinadamu mwenyewe.

Uislamu umekataza utawa na kuitesa nafsi kwa kuiepusha na maumbile yakawaida,kama ulivyoharamisha matamanio ya kupita mipaka na umeha-lalisha starehe za maisha, kama kula, kuvaa vizuri n.k. Kwa hivyo,atakayeziangalia Aya za Qur’ani atakuta kwamba dunia yote imeumbwakwa ajili ya uhai wa mtu wenye kuridhisha kwa namna inayokubalika kwawote, na kwamba kuipupia, ni kuifanyia hiyana kama ambavyo kuwazuiawatu wengine na hiyo dunia ni ufisadi na hatari kwa usalama wa jamii. Nariziki bora kabisa katika Uislamu ni ile iliyotolewa jasho.

Anas anasema: Siku moja tulikuwa na Mtume (s.a.w.w.). safarini wenginewakawa wamefunga, na wengine hawakufunga. Tukashuka sehemu fulaniwakati wa joto. Wale waliofunga wakaanguka wote, ikawa wanahudumi-wa waliokula. Mtume (s.a.w.w) akasema.: Wasiofunga leo wamechukuamalipo yote.

Huu ndio msingi wa uwiano katika Uislamu. Sio ibada itakayozuiakuhangaikia maisha wala sio ulafi utakaozuia kumwabudu MwenyeziMungu.

Ili muwe mashahidi juu ya watu wote, na Mtume awe shahidi juuyenu

Maana ya matamko haya yako wazi; na maana ya kiujumla pia yako wazi.Lakini tatizo liko kwenye kuelezea sisi Waislamu ni mashahidi juu yaakina nani? Mtume (s.a.w.w) atakuwa shahidi Kesho dhidi ya yule aliye-halifu miongoni mwetu, kwa kutoufata Uislamu na hukumu zake. Je sisitutakuwa mashahidi dhidi ya wasiokuwa Waislamu kwa kuwa wamehali-fu Kitabu na Sunna?

Page 17: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

7

Kauli za wafasiri zimekuwa nyingi na za kugongana juu ya hilo; namisikupata ya kunituliza. Nionavyo mimi ni kwamba ulama wa Kiislamuwana wajibu wa kuufikisha ujumbe wa Muhammad (s.a.w.w) kwa watu,wawe ni Waislamu wasiojuwa au Waislamu wasio. Mwenye kutekelezawajibu huu mtukufu, basi atakuwa shahidi dhidi ya yule aliyemfikishiakuwa hakuyatumia mafunzo. Na atakayeupuuza wajibu huu, na asiufik-ishe, basi Muhammad (s.a.w.w) atakuwa shahidi dhidi yake Kesho mbeleya Mwenyezi Mungu kwamba yeye amefanya hiyana.

Kwa ufafanuzi zaidi tupige mfano huu: Mtu ana mali na mtoto mdogo.Alipohisi kifo chake kiko karibu alimuusia jirani yake anayemtegemeakwa dini yake mtoto wake aitumie mali hiyo kumlelea na kumwelimishia..Akitekeleza yule aliyeusiwa, na mtoto akafaulu, basi ni sawa. Lakini yulealiyeusiwa akimshughulikia yule mtoto, bali mtoto akafanya uasi nakukataa mafunzo, basi aliyeusiwa atakuwa shahidi dhidi ya mtoto. Kamaaliyeusiwa ndiye aliyezembea, basi mzazi atakuwa shahidi dhidi yaaliyeusiwa kwa kuwa aliyeusiwa ana jukumu mbele ya Mwenyezi Munguna yule mzazi.

Vile vile na sisi ulamaa tuna majukumu makubwa mbele ya MwenyeziMungu ya kufikisha mwito wa Uislamu kwa watu wa dini mbali mbali kwahekima na mawaidha mazuri, na kuwafunza hukumu zake wale wasiozijuamiongoni mwa Waislamu. Yeyote atakayezembea wajibu huu Keshoatashuhudiwa na bwana wa viumbe mbele ya Mola Mwenye nguvu. Hii niikiwa amepuuza na hakutangaza, sikwambiidini na ikiwa yeye ndiye sababuya kupatikana shaka katika watu wake.

Na hatukukifanya Kibla ulichokuwa nacho ila tupate kumjua yuleanayemfuata Mtume na yule atakayegeuka akarudi nyuma.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t) kumwamrisha Mtume Wake kugeuzaKibla huku, baadhi ya walitia shaka na kusema: Mara huku wafuasi waMtume s.a.w.w. na Mayahudi nao wakachukua fursa ya kuwatia shaka wajin-ga kuhusu Mtume. Hao Mayahudi walikuwa, na bado wangalia na wataen-

Page 18: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

8

delea kuwa ni watu wa fitina na ufisadi wenye vitimbi na hadaha kwa maum-bile yao. Hutengeneza matatizo na kumwekea vikwazo kila mwenye Iiikhlasina hujaribu kuzigeuza jamii kuzipeleka kwenye janga. Ndio tabia na maum-bile yao.

Na hivyo ndivyo ilivyo kwa maadui wa haki; daima, na katika zama zote,watumia hudhaifu wa akili na kuwafanya ni chombo cha kufanyia vitim-bi, uharibifu na vurugu.

Imam Ali amewaelezea watu hao kwa ufasaha zaidi aliposema: “Ni wanya-ma wasiokuwa na mchungaji. Wanamfuata kila atakayewapigia kelele. Ni(bendera) wanafuata upepo. Hawakupata mwanga wa elimu, walahawakutegemea nguzo imara.”

Mwenyezi Mungu alimpa habari Mtume Wake mtukufu kwamba walewaliotia shaka si waumini bali imani yao ni ya hivi hivi tu, haina msingi;na tumewapatia mtihani huu ili ufichuke ukweli kwako na kwa wengine.

Na kwa hakika lilikuwa ni gumu, ispokuwa kwa wale ambaoMwenyezi Mungu aliowaongoza.

Nao ni wale wenye imani halisi, sio imani ya kuazima.

Unaweza kuuliza: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anajua kila kitu kabla yakutokea. Sasa kuna wajihi gani basi kusema: ili tupate kumjua yuleanayemfuata Mtume?

Jibu: Lengo hapa ni kumdhihirisha mtiifu na asi ili libainike hilo mbele zawatu, ajulikanae kila mmoja vile alivyo.

Wafasiri wengi wamesema kwamba ujuzi wa Mwenyezi Mungu kuhusumatukio, ni aina mbili: ya kujua kitu kabla ya kuwa kukijua ambayo ni elimuya ghaibu na baada ya kuwa, ambayo ni elimu ya ushahidi; na huo ndio ndioujuzi uliokusudiwa katika Aya hii. Yaani Mwenyezi Mungu ametaka kujuabaada ya kuwa, kama alivyo jua kabla ya kuwa. Na huku ni kucheza na

Page 19: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

9

maneno tu. Elimu ya Mwenyezi Mungu ni moja. Elimu ya ghaibu ndiyo hiyohiyo elimu ya ushahidi .

Na hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwapotezea imani yenu.Hakika Mwenyezi Mungu, kwa watu, ni Mpole, Mwenye kurehemu

Hii ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wale wenye uthabiti kati-ka imani yao kwa Mtume (s.a.w.w) kwa shida na raha, wasiokuwa na shakana amri Zake wala makatazoYake.

Wafasiri wengi wamesema kuwa sababu ya kushuka Aya hii ni kwambabaadhi ya masahaba waliswali na Mtume kwa kibla cha kwanza, nawakafa kabla ya kugeuzwa kibla cha pili. Akaulizwa Mtume kuhusu swalayao, ndipo Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hiyo.

Sisi hatutegemei mapokezi ya sababu za kushuka Aya isipokuwamachache tuliyo na yakini nayo, kwa sababu ulamaa hawakujishughulishasana na usahihi wake, kama walivyofanya kwa mapokezi ya Hadithi zahukumu za sharia..

Page 20: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

10

144. Kwa hakika tunakuonaunavyogeuza geuza uso wakombinguni; nasitutakuelekeza Kibla ukipen-dacho. Basi elekeza usowako upande wa MsikitiMtukufu (Al-Kaaba). Napopote mlipo, geuzeni nyusozenu upande huo. Na hakikawale waliopewa Kitabuwanajua kwamba hiyo ndiyohaki itokayo kwa Mola wao;na Mwenyezi Mungu siMwenye kughafilika na yalewanayoyatenda.

145. Na hao waliopewa Kitabuhata ukawaletea hoja za kilanamna, hawatafuata Kiblachako; wala wewe si mwenyekufuata Kibla chao, walabaadhi yao si wenye kufuataKibla cha wengine. Na kamautafuata matamanio yaobaada ya elimu iliyofikia,basi utakuwa miongoni mwamadhalimu.

Page 21: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

11

HAKIKA TUNAKUONA UNAVYOGEUZA GEUZA USO WAKO

Aya 144-145

MAANA

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: “Imepokewa kwa Imam Jafar Sadiq(a.s.) kwamba: Kiligeuka Kibla Al-Kaaba baada ya kuswali Mtume(s.a.w.w), Makka kwa muda wa miaka 13 akielekea Baitul Maqdis. Nabaada ya kuhamia Madina, aliswali miezi saba, kisha Mwenyezi Munguakamwelekeza Al Kaaba.

“Sababu hiyo ni kwamba Mayahudi walikuwa wakimkejeli Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa kumwambia: “Wewe unatufuata sisi,unaswali kwenye Qibla chetu.” Mtume akaingiwa na majonzi makubwa, aka-toka usiku akawaana angalia pambizoni mwa mbingu, akingojea amri yaMwenyezi Mungu kuhusu jambo hilo. Kulipokucha akaswali swala yaAdhuhuri katika msikiti wa Bani Salim. Alipomaliza rakaa mbili alishukiwana Jibril akamshika na kumgeuza upande wa Al-Kaaba, akamteremshia Ayahii: “Kwa hakika tunakuona unavyogeuza geuza uso wako mbingu-ni,”Mtume akaswali rakaa mbili kuelekea Baitul Maqdis, na rakaa mbilikuelekea Al- Ka’aba.

Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu (Al Kaaba).

Ameusifu Msikiti huo kwa utukufu, ambapo ni wajibu kuutakasa na niharamu kuuvunjia heshima. Al-Kaaba ni sehemu ya Masjidul Haram(Msikiti Mtukufu) nao ni sehemu ya Haram ambayo inakusanya Makka namipaka yake, kama ilivyoelezwa katika vitabu vya Fiqhi, katika Mlangowa Hijja, katika masuala ya ihram na kuwinda katika Haram.

Yanayojulikana katika Qur’ani ni kwamba kila amri ya wajibu wa kishariainayoelekezwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu huingia waliokalifisha(mukallafin) wote, mfano:

Page 22: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

12

“Na simamisha Swala katika ncha mbili za mchana na mwanzo wa usiku.”(11:114).

Haiwezekani kuwa amri ya wajib inahusika na yeye Mtume tu, ila kamakuna kitu kinachofahamisha hilo; kama Aya hii:

“Na katika usiku swali tahajjud.*1 Hiyo ni sunna kwa ajili yako...”(17:79).

Neno ‘kwa ajili yako’ linafahamisha kwamba taklifa hii haimhusu mtumwingine isipokuwa yeye.

Vile vile njia ya Qur’ani ni kwamba taklifa zenye kuelekezwa kwa watu naMuhammad (s.a.w.w) pia huwamo, bila ya kuwako tofauti hata ndogo yamwelekezo huo kati yake na mwingine. Kwa hivyo umma unaingia kati-ka kauli yake Mwenyezi Mungu: Basi elekeza uso wako upande waMsikiti Mtukufu (Al-Ka’aba).

Na popote mlipo, geuzeni nyuso zenu upande huo

Yaani popote mnapokuwa - baharini au bara, kwenye tambarare au maja-balini, Mashariki au Magharibi - ni juu yenu kuelekea Msikiti Mtukufukwa sehemu ya mbele ya mwili, wala haijuzu kuupa mgongo katika swala,au kuuelekea kwa upande wa kuume au kushoto, n.k.

Kutokana na hali hiyo, Kibla huhitalifiana kwa kuhitalifiana miji. Huendaikawa, kwa watu wa mji mmoja, ni Magharibi, na kwa wengine niMashariki kwa ajili hii Waislamu wamejishughulisha sana na suala laKibla na wakaweka elimu mahsusi kwa jina la “Elimu ya Qibla”, kinyumena Wakristo ambao wanalazimiana na upande wa Mashariki daima, naMayahudi nao; wao ni upande wa Magharibi popote walipo, hata kama

* 1 Swala za sunna za usiku wa manane.

Page 23: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

13

hilo litalazimisha kuipa mgongo Baitul Maqdis.

Unaweza kuuliza: Ikiwa umma unaingia katika msemo unaoelekezwa kwaMtume, na msemo unaolekezwa kwa umma unamchanganya na Mtume; basikwa nini kuikusanya misemo inayoelekea sehemu mbili katika Aya moja namaudhui moja tena bila ya kuwako kitenganisho? Yaani Mwenyezi Munguanasema: Elekeza uso wako- ewe Muhammad - upande wa Msikiti Mtakatifu,na popote mtakapokuwa - enyi Waislamu - geuzeni nyuso zenu upande huo.

Jibu: Kugeuka Kibla ni tukio kubwa katika Uislamu, na kulikuja kutokanana raghba ya Mtume (s.a.w.w). Kwa hivyo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ali-taka kulinabihisha hilo, na kulitilia mkazo kwa kulikariri.

Zaidi ya hayo ni kuwa, kwa asili, taklifa hiyo ni ya Muhammad (s.a.w.w),kwa sababu imekuja kwa raghba yake na, kwa kufuatilia, umma wake.

LINI NI WAJIBU KUELEKEA KIBLA?

Al Kaaba ni Kibla kwa aliye ndani ya Msikiti Mtukufu ambamo Al Kaabaimo ndani yake, Msikiti ni Kibla kwa watu wa Haram; yaani watu waMakka na pembeni mwake. Na Haram, au upande ambao imo, ni Kiblakwa watu wa Mashariki na Magharibi.

Ni wajibu kuelekea Kibla katika swala za kila siku, rakaa za ihitiyat,mafungu yaliyosahauliwa katika swala, na sijda mbili za kusahau. Vilevile ni wajibu kuelekea Kibla kwa ajili ya Swala yoyote ya wajibu, ikiwe-mo Swala ya tawafu, na Swala ya maiti. Pia ni wajibu kumwelekeza Kiblamtu aliye katika hali ya kukata roho na wakati wa kumzika, na wakati wakumchinja mnyama.

Ama katika swala za sunna ni wajibu kuelekea Kibla katika hali ya utulivutu, na wala sio wajibu katika hali ya kutembea na kupanda chombo chakusafiria.

Page 24: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

14

WATU WA KIBLA

Watu wa Kibla, watu wa Qur’ani, watu wa shahada mbili na Waislamu,yote hayo ni misamiati yenye maana moja. Ama lile jina la ‘wafuasi waMuhammad’ (Mohammedan), ni jina tulilobandikwa na maadui waUislamu, wakiwa na maana kwamba sisi ni wafuasi wa mtu na wala sio wadini ya Mwenyezi Mungu; kama Mabudha ambao ni wafuasi wa Budha naWazoroasteri ambao ni wafuasi wa Zoroaster.

Kwa vyovyote vile, lengo la kifungu hiki ni kuzindua kwamba umma waKiislamu - pamoja na kutofautiana miji yake, rangi na lugha, zake - unaku-sanywa na kuunganishwa na misingi ya aina moja, ambayo ni ghali nayenye thamani zaidi kuliko uhai wake, kwa sababu Waislamu wotewanadharau maisha kwa ajili ya misingi hiyo, wala hawawezi kuidharaumisingi hiyo kwa ajili ya maisha. Na misingi hiyo ni pamoja nakumwamini Mwenyezi Mungu na Kitabu Chake, kumwamini Muhammad(s.a.w.w) na sera yake na kuswali kwa kuelekea Kibla. Basi mwenyekumkufurisha anaye swali kwa kuelekea Kibla, na akamtoa katika idadi yaWaislamu, atakuwa ameidhoofisha nguvu ya Uislamu, na atakuwaamelichana jina la Waislamu, na kusaidia maadui wa dini, atake asitake.

Na hakika wale waliopewa Kitabu wanajua kwamba hiyo ndiyo hakiitokayo kwa Mola wao.

Makusudio ya Mayahudi na Wakristo, na wala sio Mayahudi peke yao,kama ilivyosemwa, kwa sababu neno lenyewe ni la kuenea, linaenea, nawala hakuna dalili kuwa ni mahsusi.

Wafasiri wametofautiana kuhusu dhamiri ya annahul-haqq kwamba je nihuo Msikiti au ni huyo Mtume? Sababu ya kutofautiana ni kwamba ime-shatangulia kutajwa Mtume kwa kusemwa: “Kwa hakika tunakuonaunavyogeuza geuza uso wako,” imetangulia kutajwa vile vile MsikitiMtukufu.

Sisi tunamili upande wa wanaosema kuwa dhamiri hiyo inarudia Msikitikwa sababu ndilo tamko la karibu zaidi, na dhamiri hurudia tamko lakaribu zaidi. Kwa hivyo maana yanakuwa, Waliopewa Kitabu wanajua kabisa

Page 25: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

15

kwamba Ibrahim (a.s.), baba wa Mitume na mkubwa wao ndiye ambayealiyeijenga Nyumba Tukufu (Al Kaaba), lakini wao wameikataa si kwa sababuyoyote, isipokuwa isipokuwa kwamba imo mikononi mwa Waarabu ambaowanaitumikia na kuihami. Lau isingelikuwa mikononi mwa Waarabu,Mayahudi wangelikuwa, wa kwanza kuitukuza, na wangeliiheshimu sana.

Na hao waliopewa Kitabu hata ukiwaletea hoja za kila namna,hawatafuata Kibla chako

Yaani hawafuati mila yako, sembuse kufuata Kibla chao. Nao hawana hojayoyote isipokuwa ujinga na ukaidi.

Na wala wewe si mwenye kufuata Kibla chao

Huenda baadhi ya watu wa Kitabu walitaraji kuwa Mtume (s.a.w.w) ataru-dia Kibla alichokielekea kwanza, ndipo Mwenyezi Mungu akawakatishatamaa kabisa kwa kauli yake hiyo; kama alivyomkatisha tamaaMuhammad (s.a.w.w) kuwa wao “hawatafuata Kibla chako.”

Wala baadhi yao si wenye kufuata Kibla cha wengine

Mayahudi wanaswali kwa kuelekea Magharibi, na Wakristo wanaelekeaMashariki, wala kundi moja haliwezi kuacha walilonalo na kulifuata kundijingine. Basi vipi wataweza kufuata Kibla chako, ewe Muhammad? Balimigawanyiko ilioko baina ya Mayahudi wao kwa wao,. Mauaji yaliy-otokea kati ya Wakatoliki na Waprotestanti na baina ya makundi yaKikristo vile vile, ni mingi kuliko iliyoko baina yao na Waislamu, hayanamfano wa fedheha yake katika zama zote.

Na kama utafuata matamanio yao baada ya elimu iliyokufikia, basiutakuwa miongoni mwa madhalimu.

Ni muhali kufuata Mtume matamanio yao, kwa sababu yeye ni maasum(mwenye kuhifadhiwa na madhambi). Lakini lengo la makatazo haya nikumpa nguvu Mtume katika kuamiliana kwake na Mayahudi, na kusima-ma nao imara, kwani hakuna kheri yoyote ya kupatana nao, wala haku-na,tumaini lolote kwao. Haliwezi kufaa jaribio lolote la kuwazuia navitimbi na ufisadi wao, kwa sababu wao wana maumbile ya shari, kupin-ga haki na kumfanyia uovu anayewafanyia wema. Yamekwishaelezwa

Page 26: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

16

hayo katika kuifasiri Aya ya 120.

UISLAMU NA WATU WENYE UPENDELEO WA DINI ZAO

Ni jambo lenye kuingia akilini kwamba wataalamu wa kila aina wanawezakuhitilafiana katika masuala yasiyokuwa ya kidini. Lakini baada yakukumbushana na kudurusi, waafikiana katika lile walilohitilafiana. Hilolimekwishatokea.

Ama wakihitalifiana ya dini mbalimbali katika masuala ya kidini, basikuafikiana kwao ni muhali, hata kama zitakuwepo dalili elfu. Imethibitikwa wataalamu wa elimu ya saikolojia, kwamba watu kubadili tabia yao nirahisi zaidi tena sana kuliko kubadili dini yao. Hilo ni kwamba watu wengihupendelea dini za mababa na mababu zao. Hata hivyo,hakuna dini iliyo-julikana kukataza kufuata mababu isipokuwa Uislamu ambao umetegemeaakili peke yake katika kuthibitishia misingi yake. Mwenye kuangalia Ayaza Qur’ani na Hadith za Mtume ataziona zimetilia umuhimu kufuatiliaakili kwa kiasi kile kile zinavyotilia umuhimu wa kumwamini MwenyeziMungu. Kwa sababu imani hiyo haiepukani kabisa na nuru ya akili tima-mu katika kuongoka kwake.

146. Wale tuliowapa Kitabuwanamjua yeye kamawanavyowajua watoto wao.Na hakika kundi katika waowanaificha haki na haliwanaijua.

147. Haki ni iliyotoka kwa Molawako. Basi usiwe miongonimwa wanaofanya shaka.

Page 27: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

17

WANAMJUA KAMA WANAVYOWAJUA WATOTO WAO

Aya 146-147

MAANA

Wale tuliowapa Kitabu wanamjua kama wanavyowajua watoto wao.

Yaani wanavyuoni wengi wa Kiyahudi na wa Kikristo wanajua kwa usahi-hi na uwazi Utume wa Muhammad (s.a.w.w) kama wanavyowajua watotowao, kwa namna isiyokuwa na shaka yoyote, kwa sababu Tawrati na Injilizimetoa bishara ya kuja kwake, na zikamtaja kwa sifa zake na alama zakeambazo hazikupatikana kwa mwingine yeyote. Mwenyezi Mungu anase-ma:

“...Wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurati na Injili...” (7:157).

“Na aliposema Isa bin Maryam: Enyi wana wa Israili! Mimi ni Mtumewa Mwenyezi Mungu kwenu, nisadikishaye yaliyokuwa kabla yangu katikaTawrati na kutoa bishara ya Mtume atakayekuja baada yangu ambaye jinalake ni Ahmad. Lakini alipowajia kwa hoja zilizo wazi, walisema: Huu niuchawi ulio wazi.” (61:6).

Abdallah bin Salam alikuwa ni mmoja wa maulamaa wa Kiyahudi; kishaakasilimu. Miongoni mwa maneno aliyoyasema ni: “Mimi ninaujua zaidi

Page 28: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

18

Utume wa Muhammad kuliko ninavyomjua mwanangu.” Alipoulizwa kwanini, alisema: “Mimi sitii shaka kwamba Muhammad ni Mtume, lakini mtotowangu, pengine mama yake amefanya hiyana.”

Na hakika kundi katika wao wanaificha haki na hali wanaijua.

Ndio! Wanaficha, hata kama wangeliona jina la Muhammad katika LauhulMahfudh, kwa sababu ya kupupia uongozi wa duniani na maslahi ya kibi-nafsi. Inadi hii ya kuficha haki haihusiki na Mayahudi na Wakristo tu,Kwani sababu ya kuficha haki ni ya kijumla. Tumekwisha waona baadhiya mashekhe wanakana sifa za wenzao kwa sababu ya chuki na hasadi tu.

Haki ni iliyotoka kwa Mola wako. Basi usiwe miongoni mwa wanao-fanya shaka.

Mtume (s.a.w.w) shaka ya yale yaliyotoka kwa Mola wake, na ni muhalikuyatilia shaka; na Mwenyezi Mungu anajua kuwa Mtume wake Mtukufuhawezi kutia shaka. Lengo la Aya hii ni kubainisha kwamba aliy-omteremshia Muhammad hayana shaka wala matatizo yoyote kabisa. Mtuakiyakanusha na kuyapinga, basi atakuwa anafanya hivyo kwa inadi naukaidi tu.

MIMI NA MHUBIRI

Tarehe 15-7-1963 alinitembelea mtaalamu wa mambo ya nchi za mashari-ki, Mkristo, kutoka Italia ambaye alikuwa akizungumza lugha ya Kiarabuvizuri. Basi tukawa na mjadala kwa mdomo na kwa maandishi. Miongonimwa aliyosema ni: “Qur’ani inaitambua wazi wazi Injili. Basi kwa niniWaislamu wanaikana?” Nikamjibu kuwa Qur’ani inakiri Injili iliyobashiriUtume wa Muhammad (s.a.w.w); kama ilivyosema:

“...Na mwenye kutoa bishara ya Mtume atakayekuja baada yangu ambayejina lake ni Ahmad...” (61:6).

Page 29: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

19

“...Wanamuona ameandikwa kwao katika Tawrati na Injili...” (7:157).

Kisha Qur’ani inaendelea kusema:

“Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam;alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: ‘Kuwa’, basi akawa.” (3:59).

Na Injili yenu inasema kuwa Isa ni Mungu! Sasa vipi mnatutaka tuiamini,na wakati huo huo tuiamini Qur’ani?

Ikiwa Wakristo wanakataa kupingana na kukosana kwa hukumu ya akilitu, na kukubali kuwa akili inaweza kupingana na kutoafikiana katika dinina itikadi, basi Waislamu wanaliona hilo ni muhali; haliwezekani kiakili nakidini na katika kila kitu, kwa sababu misingi ya dini kwao inakuwa ndaniya akili tu.

148. Na kila mmoja anamwelekeo anaouelekea.Basi shindaneni kufanyamema. Popote mtakapo-kuwa, Mwenyezi Munguatawaleta nyote pamoja.Hakika Mwenyezi Mungu niMweza wa kila kitu.

Page 30: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

20

149. Na popote uendapo utakakoelekeza uso wako upande waMsikiti Mtukufu; na hiyondiyo haki itokayo kwa Molawako. Na Mwenyezi Mungusi Mwenye kughafilika nayale mnayoyatenda.

150. Na popote uendapo elekezauso wako upande wa MsikitiMtukufu, na popote mlipoelekezeni nyuso zenu upandehuo ili watu wasiwe na hojajuu yenu, isipokuwa walewaliodhulumu miongonimwao. Basi msiwaogope,niogopeni Mimi, ili niwa-timizie neema Zangu na ilimpate kuongoka.

151. Kama tulivyomleta Mtumekwenu anayetokana nanyinyi, anayewasomea AyaZetu na kuwatakasa nakuwafundisha Kitabu naHekima na kuwafundishamliyokuwa hamyajui.

Page 31: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

21

152. Basi nikumbukeninitawakumbuka, nanishukuruni wala msinikufu-ru.

KILA UMMA ULIKUWA NA KIBLA CHAKE

Aya ya 148-152

MAANA

Na kila mmoja ana mwelekeo anaoulekea

Mwenyezi Mungu alipotaja kibla ambacho amewaamrisha Waislamukukielekea, nacho ni Al Kaaba, na akataja kuendelea kwa Mayahudi naManaswara kuelekea mielekeo yao, alibainisha kuwa siri ya kung’ang’aniahuku ni kwamba kila umma ulikuwa na kibla chake ulichojichaguliakuelekea, na wala haukiachi hata kama ubaya wa mwelekeo wenyewe ukowazi kama jua. Kwa hivyo kauli Yake hii inafanana na kauli Yake:

“...Kila kikundi kinafurahia kilicho nacho” (30:32).

Hayo ndiyo niliyoyafahamu kutokana na dhahiri ya tamko hilo. Wafasirinao wameleta kauli nyingi katika Aya hii; mwenye Majmau ametaja nne.

Basi shindaneni kufanya mema. Popote mtakapokuwa MwenyeziMungu atawaleta nyote pamoja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwezawa kila kitu

Page 32: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

22

Yaani achaneni na watu wa Kitabu na washirikina walio wakaidi, namielekeo yao na kung’ang’ana kwao na upotofu, mfanye amali njema.Kwani marejeo yenu Kesho ni Kwake Mwenyezi Mungu, ambapo atalipwathawabu mwenye haki na mwenye kufanya wema, na kuadhibiwa mwenyebatili mtenda maovu. Kama wanavyosema wafasiri maana ya: “Popotemtakapokuwa Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja” ni ahadi yathawabu kwa watiifu, na kiaga cha adhabu kwa waasi. Ama kusema Kwake:“Hakika Mwenyezi Mungu ni Mweza wa kila kitu” ni dalili na sababu yakuwezekana kufufuliwa viumbe baada ya mauti.

Na popote uendapo elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtukufu.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu hapa amekariri kuelekeaMsikiti Mtukufu mara tatu, na katika Aya ya 149 mara mbili; yaaniamekariri mara tano mfululizo?

Jibu: Mwenye Majmaul Bayan ametaja kauli tatu, na Razi ameleta tano.Miongoni mwa kauli hizo ni lile jibu lililozoeleka na kurithiwa ambalo nikukaririwa huko ni kwa ajili ya kutilia mkazo na umuhimu. Lakini nafsiyangu haikutulia kabisa kwa kauli hizo, wala sina chochote cha kusemaisipokuwa kwamba huenda kukariri huku hapa ni kutokana na jambolililohusu wakati huo ambalo hatulijui. Kuna mambo mangapi ambayohayaingii katika udhibiti na hisab!.

Inajulikana wazi kuwa mapokezi ya Aya na sababu zake yako ya kiujumlana mahsusi, na haifai kwa yeyote kutafsiri au kuleta taawili, kwa kutege-mea dhana bila ya kupata asili yake yoyote.

Ili watu wasiwe na hoja juu yenu

Wafasiri wengi wamesema kuwa Mtume (s.a.w.w) alipokuwa akiswalikuelekea Baitil Maqdis, washirikina na Waarabu walisema: “VipiMuhammad anadai kwamba yeye yuko kwenye dini ya Ibrahim,hali haswalikuelekea Al Kaaba aliyokuwa akiielekea Ibrahim na Ismail?” Na waliopewaKitabu wakasema “Yaliyo katika Vitabu vyetu ni kwamba Mtume , sio Baitul

Page 33: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

23

Maqdis. Sasa vipi tunaweza kuukubali Utume wa Muhammad? Kwa hivyowote, washirikina na waliopewa Kitabu,wakaifanya hiyo, kuwa hoja,wanayoitumia kwa dhana yao. Mwenyezi Mungu akambadilishia Kiblakuelekea Al Kaaba, na akaifanya ndio Kibla cha kudumu kwa Mtume naWaislamu wote mpaka Siku ya Malipo, ili hawa na wengine wasibakiwe nahoja yoyote.

Dhahiri ya jumla (Aya) inafahamisha kwamba kuswali kuelekea Al Kaabakunavunja hoja ya wapinzani. Ama kuwa ni kina nani hao wapinzani, Ayahaikubainisha. Inawezekana kuwa njia ya kukata hoja ya wapinzani ni kuwaAl Kaaba imejengwa na Ibrahim (a.s.) na akaswali hapo. Hilo ni lenyekuafikiwa na wote; na Muhammad atafuata mwendo wa Ibrahim

Isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao

Yaani hakuna hoja yoyote juu yako ukiswali, isipokuwa kwa mpinzani asiyena haki ambaye hategemei dalili za kiakili katika upinzani, wake wala uon-gozi wa kidini, isipokuwa kung’ang’ania, na ukaidi.

Basi msiwaogope, niogopeni Mimi

Yaani msiogope lawama katika haki, Mimi pekee ndiye ninayewamilikiamanufaa na madhara.

Ibnul Arabi, katika Tafsiri yake, anasema: Maana ya niogopeni ni, jueniUtukufu Wangu ili makafiri wasijifanye watukufu kwenu.

Amirul Muminin (a.s.) naye anasema: “Amekuwa mkubwa Muumbajikatika nafsi zao, akawa mdogo asiyekuwa Yeye katika macho yao.”

Ili niwatimizie neema Zangu na ili mpate kuongoka.

Yaani nimewaneemesha kwa Uislamu, na nimewatimizia neema kwakuwapa Kibla chenu kilichowafanyia moja neno lenu na kuwakusanya, nakinachoelekewa na watu wa mataifa mbali mbali wa pembe zote za dunia,wa rangi na lugha mbali mbali.

Page 34: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

24

KATIBA YA UISLAMU

Mtaalamu mmoja anasema kuwa katiba ya Uislamu ina vipengele vitatuMwenyezi Mungu Mmoja, Kitabu kimoja na Kibla kimoja. Waislamuhukusanyika kutoka pembe zote za dunia kila mwaka ili wamwabuduMwenyezi Mungu Mmoja kwa sharia hiyo moja, kwenye nchi Mmoja,nchi ya mji wa kiroho. Hivi ndivyo ulivyokuwa umoja wa itikadi, umojawa sharia na umoja wa mji, ili wakumbuke Waislamu kwamba wao, hatawakitofautiana miji, lugha, rangi na nasaba, lakini wanakuwa wamoja kwadini, wanaabudu Mwenyezi Mungu Mmoja na ni wananchi wa nchimmoja.

Kama tulivyomleta Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anayewa-somea Aya Zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na Hekimana kuwafundisha mliyokuwa hamyajui.

Wanavyuoni wana maneno mengi na marefu kuhusu maana ya nenoHekima. Tunavyofahamu sisi ni kuwa kila kinachowekwa mahali pakepanapostahili, kiwe ni kitendo au kauli, basi ni hekima.

Hali yoyote iwayo, maana ya jumla ya Aya hii ni kwamba MwenyeziMungu (s.w.t.) amewaneemesha Waarabu kwa Kibla; kama alivyowa-neemesha kabla kwa Muhammad (s.a.w.w) ambaye ni katika wao na ana-tokana na wao. Amewapa umbo jipya; akawatwaharisha na uchafu wa shir-ki na tabia mbaya. Kwa hivyo, kwa fadhila zake, wakawa ni watu wa dinina sharia ya Mwenyezi Mungu ambayo misingi yake ni uadilifu na usawa,kama ambavyo wamekuwa na dola iliyopanuka, mpaka lugha yao ikawakubwa na ikaenea kwa sababu ya Qur’ani na fasaha yake.

Hapana shaka kwamba lau si Muhammad na kizazi cha Muhammad,Waarabu wasingelikuwa na historia wala turathi zozote; wasingekuwa nachochote zaidi ya kuabudu masanamu, ujinga na kuwazika watoto wa kikewakiwa hai, ili kuepuka gharama za kuwalisha. Bali Muhammad (s.a.w.w),Mwarabu, ni neema kubwa juu ya watu wote. Kwa sababu yake, watu

Page 35: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

25

wamepiga hatua za haraka katika nyanja za elimu na maendeleo. Uhakikahuu wameukiri na kuusajili wataalamu wa Kimagharibi wenye insafi;, natumeyanakili baadhi ya haya katika kitabu Al-Islam Wal Aql (Uislamu naAkili).

Kwa ajili ya neema hiyo aliyowaneemesha Waarabu, ndio MwenyeziMungu akawataka wamkumbuke na kumshukuru, na akahadharisha wasi-je wakaikufuru neema hiyo na hisani, kwa kusema:

Basi nikumbukeni nitawakumbuka, na nishukuruni wala msinikufuru

Yaani nikumbukeni kwa kunitii, nami nitawakumbuka kwa malipo nathawabu; na mnishukuru kwa neema ya Uislamu na Utume wa Muhammadambaye anatokana na nyinyi, wala msikufuru kumhalifu Mwenyezi Mungu naMtume Wake. Mahali pengine Mwenyezi Mungu anasema:

“... Mkishukuru nitawazidishia, na mkikufuru basi adhabu Yangu ni kalisana.” (14:7).

Amirul Muminin Ali (a.s.) alisema: “Mwenyezi Mungu hawezi kufunguamlango wa shukrani na akawafungia wa malipo.” Anaendelea kusema:“Mkumbukeni sana Mwenyezi Mungu, kwani huo ndio ukumbusho mzuri,na kuweni na raghba ya aliyowaahidi wanaomcha Mwenyezi Mungu,kwani ahadi Yake ni ya kweli sana.”

KUMSHUKURU MNEEMESHAJI

Moja kwa moja akili inafahamu kuwa kumshukuru Mwenyezi Mungu niwajibu kwa kila aliye baleghe mwenye akili, hata kama isingeshuka Ayayoyote au kuja Hadith yoyote ya kuwajibisha hilo, kwani Yeye Mtukufundiye Muumbaji Mwenye kuruzuku.

Page 36: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

26

Maana ya kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.), baada ya kuitakidikwamba Yeye ndiye Mwanzilishi na Mrudishaji, na kwamba Yeye nimweza wa kila kitu, ni kutii amri Zake na makatazo Yake, na kutegemezamambo Kwake peke Yake.

Hayo ni kwa upande wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Ama mtu akimfanyiawema mtu kama yeye, je inapasa, yule aliyefanyiwa wema, kumshukurualiyemfanyia wema, kiasi ambacho kama hakumshukuru kwa namna fulaniatakuwa ni asi mwenye kustahili adhabu?

Hapana kutojuzu kuacha kushukuru, shaka kwamba kumshukuru aliyeku-tendea wema ni jambo zuri, bali hiyo ni alama ya watu wema. Ama kuwani wajibu au la, hakuna dalili juu yake. Kwa hivyo kila habari iliyokujakuhusu kumshukuru mwenye kuneemesha asiyekuwa Mwenyezi Mungu,Mtume au Ahlul Bait wake, ni pendekezo tu ya kuwa ni vizuri; kamaalivyosema Ali (a.s.): “Ukiwa una uwezo juu ya adui yako, basi ufanyemsamaha ndio shukrani ya uwezo ulionao juu yake.”

Kumsamehe aliyekufanyia ubaya sio wajibu, lakini ni sunna kwa ijmai. Amamsemo unaosemwa sana: “Asiyeshukuru kiumbe, hamshukuru Muumba”,hiyo ni hukumu ya kimaadili tu, siyo ya lazima.

Hata hivyo, kukanusha neema na kumwambia aliyekufanyia wema:“Hukufanya wema” ni haramu, kwa sababu ni uwongo; na kumfanyia uovundio haramu kabisa, kwa sababu uovu ni haramu kwa dhati yake, hata kwaasiyekufanyia wema. Lakini pamoja na hayo, wajibu wa kushukuru nijambo moja na uharamu wa uwongo na kutenda uovu ni jambo jingine.

Page 37: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

27

153. Enyi mlioamini! Jisaidienikwa subira na swala; hakikaMwenyezi Mungu yukopamoja na wanaosubiri.

154. Wala msiseme kwamba walewanaouawa katika njia yaMwenyezi Mungu ni wafu,bali wa hai lakini nyinyihamtambui.

155. Na hakika tutawajaribu kwachembe ya hofu na njaa naupungufu wa mali na wanafsi na wa matunda. Nawape bishara wanaosubiri.

156. Ambao ukiwapata msiba,husema: Hakika sisi ni waMwenyezi Mungu, na KwakeYeye tutarejea.

157. Hao juu yao zitakuwa barakazitokazo kwa Mola wao, narehema, na hao ndio wenyekuongoka.

Page 38: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

28

TAKENI MSAADA KWA SUBIRA

Aya 153-157

SUBIRA

Enyi mlioamini! Jisaidieni kwa subira na swala; hakika MwenyeziMungu yuko pamoja na wanaosubiri.

Mwenye Tafsiri ya Al-Manar anasema: Subira (uvumilivu) katika Qur’aniimetajwa mara sabini; hiyo inafahamisha umuhimu wake. Na MwenyeziMungu ameijaalia ni kitu cha kuusiana katika Sura Al Asr kwa kuikutanishana haki, kwani mwenye kuilingania haki hana budi kuwa nayo.”

Mwenye Bahrul Muhit ameiweka mbali sana aliposema: “Subira na swalani nguzo mbili za Uislamu” Ameghafilika na Hadith inayosema:“Umejengwa Uislamu juu ya mambo matano: Kushuhudia kuwa hakunaMola isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa MwenyeziMungu, kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga mwezi wa Ramadhan nakuhiji Makka kwa mwenye kuweza njia ya kuendea.” Subira haimo katikanguzo hizo. Pia ameghafilika kuwa kuna taklifa za lazima ambazo mukallafanatakiwa kuzifanya na ataadhibiwa kwa kuziacha; kama, swala, kulipadeni, n.k.

Na kuna taklifa nyingine ambazo ni za kimwongozo; zimekuja kinasaha nazinafanana na amri, lakini mukallaf hawezi kuadhibiwa kwa kuziacha;kama usafi, kuosha mikono kabla ya kula, kukatazwa kushiba sana, n.k. Naamri ya kusubiri ni aina hiyo. Sasa yako wapi haya na nguzo za dini,ambazo mwenye kuziacha anakuwa ametoka katika dini?

Kisha subira haisifiwi hiyo yenyewe hasa, isipokuwa inasifiwa ikiwa ninyenzo ya kufikilia jambo kuu: kama subira katika jihadi takatifu, subirajuu ya ufukara na uhitaji, subira kwa ajili ya kuipata elimu na subira juuya matatizo ya familia na kulea watoto.

Page 39: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

29

Vile vile subira juu ya kumwokoa mwenye kudhulumiwa, subira juu yakauli ya mtu mpumbavu kwa kukinga shari, au kufanya subira kwakumkosa mpenzi asiyesahaulika. Kwani kuendelea kufazaika ni kuzidishamsiba; kama alivyosema Amirul Muminin Ali (a.s.): “Mwenye kuyakuzamasaibu madogo, Mwenyezi Mungu humwingiza kwenye makubwa.”

Bazar Jamhar aliulizwa: “Kwa nini, ewe mfalme mwenye hekima, husik-itiki kwa yaliyokupita wala hufurahi kwa yaliyopo?” Akasema:“Yaliyopita hayawezi kufutika kwa majonzi, wala yaliyopo hayawezikudumu kwa furaha.” Mwingine alisema: “Siwezi kukiambia kitu kili-chokwisha kuwa natamani kisingekuwa, au ambacho hakikuwa natamanikingekuwa.”

Mara nyingine subira huenda ikawa mbaya kama kusubiria njaa na uwezowa kufanya kazi upo, na kusubiri juu ya ukandamizwaji. Katika hali hiisubira nzuri ni kumkabili dhalimu.

Unaweza kuuliza: Kuna uhusiano gani kati ya swala na subira mpakazikakutanishwa pamoja katika Aya?

Jibu: Maana ya subira ni kutulizana moyo ingawaje una machungu. Hiyoinahitajia kuwa na imani kubwa na Mwenyezi Mungu, na kuamini kuwaYeye “yu pamoja na wenye kusubiri”. Hakuna mwenye shaka kwambaswala inatilia mkazo mategemeo haya na ni hakikisho la imani hii kwakuongezea kwamba, ni kumwomba Mwenyezi Mungu kunapunguzamachungu ya masaibu.

Wala msiseme kwamba wale wanaouawa katika njia ya MwenyeziMungu ni wafu, bali wa hai lakini nyinyi hamtambui.Mfano wa Aya hii ni kama nyingine isemayo:

“Wala usiwadhanie wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwani wafu, bali wa hai wanaruzukiwa kwa Mola wao.” (3:169).

Page 40: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

30

Inajulikana kuwa kila anayefariki hurejea kwa Mola wake, awe mwema aumwovu, shahidi au asiyekuwa shahidi; isipokuwa kwamba mwema anaon-doka kwenye maisha ya chini kwenda kwenye maisha ya juu na mwovuinakuwa kinyume chake.

Hapa imehusishwa kutajwa shahidi; ama ni kwa kueleza cheo chake mbeleza Mwenyezi Mungu kwa kuhimiza ushahidi, au ni kwa kutokana na yaliy-onakiliwa kutoka kwa Ibn Abbas: kwamba Aya hii ilishuka kwa sababu yawaliouliwa katika Vita vya Badr, ambao ni muhajirin kumi na nne na ansarwanane; ikasemwa ameuawa fulani na fulani; ndipo ikashuka Aya hii. Nahaya hayako mbali, kwani kauli ya Mwenyezi Mungu: Msiwaite wafu,inafahamiisha hilo.

Vyovyote iwavyo, ambalo tunapaswa kuamini ni kwamba mwenye kufashahidi kwa kuupigania Uislamu au kitu chochote kinachofungamana nahaki, uadilifu na utu, atakuwa anahama kutoka ulimwengu unaoonekanakwenda kwenye ulimwengu usioonekana na huko atakuwa na maishamema; na kwamba yeye anatofautiana na aliyekufa kifo cha kawaida.Amirul Muminin anasema: “Naapa kwa yule ambaye nafsi ya mtoto waAbu Twalib iko mikononi mwake! Kupigwa mapigo elfu ya panga ni borakwangu kuliko kufa kitandani.”

Ama hakika ya maisha ya shahidi baada ya mauti, na kuhusu riziki anay-oneemeshwa, ni jambo tusilolijua na wala hatuna haja ya kulifanyia utafi-ti kwa sababu hatujakalifishwa kulijua.

THAMANI YA PEPO

Na hakika tutawajaribu kwa chembe ya hofu na njaa na upungufu wamali na wa nafsi na wa matunda. Na wapashe habari njema wanao-subiri

Yeyote anayefuata haki ni lazima aigharimie kwa nafsi yake, watu wake aumali yake: Na kila haki inavyokuwa kubwa, ndivyo gharama inavyokuwakubwa; lau kama si hivyo wanaopigania haki wasingelikuwa na fadhila

Page 41: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

31

yoyote, na watu wote wasingelifuata haki. Kwa hali hiyo ndiyo tunapatatafsiri ya Hadith hii tukufu: “Misukosuko amepewa muumini . . . nakwamba wenye misukosuko mikubwa zaidi ni Mitume; kisha wanaowafu-atia.” Vile vile misukosuko ya Mitume inakuja kwa kadiri ya daraja zao.Mtume mtukufu (s.a.w.w.) amesema: “Hakuudhiwa Mtume yeyote kamanilivyoudhiwa mimi.” Amirul Muminin naye amesema: “Hakika haki ninzito lakini nzuri, na batili ni hafifu lakini mbaya.” Inatosha kuwa niushahidi kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, na hali hamjajiwa na mfano wa walewaliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara. . .” (2:214).

Aya hii inafahamisha kuwa Pepo haipati isipokuwa mwenye kujitoleamhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na kujitolea mhanga hakuwikatika uwanja wa vita vya jihadi na watu wa shirki na makafiri peke yake,bali machukivu yoyote anayoyavumilia mtu kwa ajili ya kuipigania haki nauadilifu ni kujitoa mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na ni thamaniya Pepo; hata kama kupigania kwenyewe ni kwa neno la kumjibu dhalimuna kumsaidia mwenye haki.

Baada ya kuingilia kuandika tafsiri, nimekuwa na yakini isiyo na shaka yoy-ote kwamba hataingia Peponi isipokuwa yule aliyeudhiwa akawa na subira,ijapoku, ni ukandamizwaji na balaa, katika njia ya haki na uadilifu. Kwauchache , kuifunga nafsi yake na yaliyoharamishwa, au kufanya juhudi kwaajili ya mwingine, hata kama ni mzazi au mtoto. Kipimo cha Pepo ni kuvu-milia mashaka kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu. Ama kuingia Peponi,kwa “anayekaa uraha mustarehe,” ni jambo lililo mbali sana.

Ambao ukiwapata msiba, husema: ‘Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu, na Kwake Yeye tutarejea

Page 42: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

32

Maana ya hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu ni kukiri kuwa yeye niMfalme na wa kuabudiwa; na maana ya Kwake Yeye tutarejea ni kukubaliufufuo baada ya mauti.

Kisha kujaribiwa kwa misukosuko ni mtihani ambao unadhihirisha hakikaya mtu. Muumini mwenye akili haachi dini yake kwa kushukiwa na mis-iba; wala hapayuki payuki kwa maneno ya ukafiri na ufasiki na ujinga, balianakuwa na subira; wala misukosuko haiwezi kumwondolea akili yake naimani yake.

Ama mwenye akili na imani dhaifu hutawaliwa na shetani, akaenda nayekila mwenendo wa ukafiri na shutuma, na hushuka chini kwenye udhalili.Kauli nzuri kuhusu haya ni ile ya bwana wa mashahidi, Hussein bin Ali,siku ya msiba wa Karbala, “Watu ni watumwa wa ulimwengu, na dini ikokwenye ndimi zao, wanaipeleka kule kwenye maisha yao, Wakijaribiwakwa misukosuko, huwa wachache wenye dini.”

Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao, na rehema.

Baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni takrima na ni cheo cha juu; narehema Yake kwa waja Wake ni huruma Yake kwao na kuwaongozakwenye kheri na kuwaneemesha.

Katika Hadith moja imeelezwa: “Hakuna Mwislamu aliyepatwa namasaibu, akakimbilia amri ya Mwenyezi Mungu kwa kusema: ‘Hakikasisi ni wa Mwenyezi Mungu na Kwake Yeye tutarejea. Ewe Mola wangu!Wewe ndiwe unayeyatoshea masaibu yangu, basi nilipe katika masaibuhayo na unipe badali bora.’ isipokuwa Mwenyezi Mungu humlipa nahumpa badali bora.”

AINA YA MALIPO YA WANAOSUBIRI

Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewapawenye kusubiri aina nane za malipo na utukufu:

1. Mapenzi. Mwenyezi Mungu anasema:

Page 43: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

33

“...Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaosubiri.” (3:146).

2. Ushindi. Mwenyezi Mungu anasema:

“...Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wanaosubiri.” (2:153).

3. Ghorofa za Peponi. Mwenyezi Mungu anasema:

“Hao ndio watakaolipwa ghorofa kwa kuwa walisubiri.” (25:75).

4. Malipo mengi. Mwenyezi Mungu anasema:

“Hakika wanaosubiri watapewa ujira wao pasipo hisabu...” (39:10).

5. Bishara. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wape bishara wanaosubiri.” (2:155).

Page 44: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

34

6 na 7. Baraka na rehema. Mwenyezi Mungu anasema:

“Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao, na rehema.”(2:157).8. Uongofu. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na hao ndio wenye kuongoka.” (2:157).

158. Hakika Swafaa na Mar-wa nikatika alama za MwenyeziMungu. Basi anayeikusudiaNyumba hiyo au akafanyaUmra, si kosa kwake kuzizun-guuka. Na anayefanya kheri,basi Mwenyezi Mungu niMwenye shukrani (na) Mjuzi.

SWAFAA NA MAR -WA

Aya 158

LUGHA

Swafaa na Mar-wa ni vilima viwili vilivyoko Makka karibu na Al Kaaba.Mahujaji na wanaofanya umra huenda saa’y baina ya vilima hivyo.

Page 45: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

35

MAANA

Hakika Swafaa na Mar-wa ni katika alama za Mwenyezi Mungu

Ibada ziko namna mbali mbali na wakati mbali mbali. Kwa kuangaliawakati, kuna zile za kila siku ambazo ni swala, na nyingine ni za kilamwaka ambazo ni kufunga Ramadhani, na pia iko ya mara moja tu katikaumri, nayo ni kuhiji kwa mwenye kuweza.

Hijja ni moja ya nguzo tano zilizojengewa Uislamu, ambazo ni: shahadambili, kusimamisha swala, kutoa zaka, kufunga Ramadhani na kuhiji Al -Kaaba.

Umrah, ni kwa kawaida kama hijja, lakini katika umra hakuna kwenda Arafa,wala kulala Muzdalifa au kutupa mawe Mina. Utakuja ufafanuzi wakeinshaallah katika Aya ya 196 na sura nyingine zinazozungumzia hilo.

Kwa ujumla ni kwamba aina zote za ibada, ikiwemo hijja, hazina nafasi yakufanyiwa ijtihadi wala kuelezwa sababu yoyote; isipokuwa inatosha nassi(nukuu) ya Qur’ani na Hadith tu; na kila ambalo litazidi hayo, Mungu(s.w.t.) hajaliridhia.

Linalooneshwa na Aya hii ni kwamba Swafaa na Mar-wa ni sehemu zakufanyiwa ibada kwa kuzizunguka, kama inavyooneshwa kwa kauli Yake:

Basi anayeikusudia Nyumba hiyo au kufanya umra, si kosa kwakekuzizunguka

Kuzunguka huku ndiko kunakojulikana kwa jina la Saa’y baina ya Swafaana Mar-wa. Ama namna ya kufanya saa’y na idadi ya mizunguko yake nakuanzia Swafaa, yatakuja maelelzo yake mahali pake inshaallah.

Unaweza kuuliza: Kufanya saa’y kati ya Swafaa na Mar-wa katika hijja niwajibu kwa ijmai pamoja na kuwa ibara ya “Si kosa” inafahamisha kufaajambo hilo, na wala sio lazima, na kwamba hakuna dhambi kuliacha.

Page 46: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

36

Jibu: Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Si kosa” haikuja kubainisha hukumuya saa’y kuwa ni wajibu au la, isipokuwa imekuja kubainisha kuwa Saa’yni sharia, na Uislamu unaikubali na kuithibisha. Ama kujua hukumu yakena je, ni faradhi au ni sunna, hayo yanafahamishwa na dalili nyingine

Zimekuja Hadith mutawatir za Mtume, na wamekongamana Waislamu, juuya wajibu wa kufanya saa’y katika hijja ya Kiislamu. Katika Majmaul-Bayananasema kuwa Imam Jaffar Sadiq amesema: “Waislamu walikuwa wakionakwamba Swafaa na Marwa ni mambo yaliyozushwa wakati wa Jahiliya.Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akateremsha Aya hizi”. Yaani anaziondoa dhanahizi na kubainisha kwamba Swafaa na Mar-wa zinatokana na Uislamu tanguasili; washirikina wakizizunguukia huwa wanajikurubisha kwa masanamu,lakini Waislamu huwa wanazizunguka kwa kumtii Mwenyezi Mungu na kufu-ata amri Zake.

Na anayefanya kheri, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye shukrani (na)Mjuzi.

Yaani anayefanya wema, kwa kufanya saa’y kati ya Swafaa na Mar-wabaada ya kutekeleza wajibu alionao, basi Mwenyezi Mungu atamlipawema kwa wema wake. Shaakir (mwenye shukrani) ni katika sifa zaMwenyezi Mungu; na maana ya Mwenyezi Mungu kumshukuru mja wakemtiifu, ni kuwa Yeye yuko radhi naye na kumpa thawabu kutokana nashukrani yake na utiifu wake.

Page 47: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

37

159. Hakika wale wanaoficha tuliy-oyateremsha, katika ubainifuna uwongofu, baada ya Sisikuyabainisha kwa watuKitabuni, hao anawalaaniMwenyezi Mungu, nawanawalaani wanaolaani.

160. Ila wale waliotubu nakujirekebisha na wakabain-isha, basi hao nitawataka-balia toba yao, na Mimi niMwingi wa kutakabali toba,Mwenye kurehemu.

161. Hakika wale waliokufuru, nawakafa hali ni makafiri, haowana laana ya MwenyeziMungu na ya Malaika na yawatu wote.

162. Humo watadumu, hawata-punguziwa adhabu walahawatapewa muda.

Page 48: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

38

WANAOFICHA TULIYOYATEREMSHAAya 159-162

MAANA

Hakika wale wanaoficha tuliyoyateremsha, katika hoja na uwongofu,baada ya Sisi kuyabainisha kwa watu Kitabuni, hao anawalaaniMwenyezi Mungu, na wanawalaani wanaolaani

Dhahiri ya Aya hii ni kwamba inaanzia habari nyingine isiyofungamana nayaliyo kabla yake. Makusudio ni kuwa kila mwenye kujua hukumu katikahukumu za dini, ambazo ubainifu wake umekuja katika Kitabu chaMwenyezi Mungu au katika Hadith za Mtume wa Mwenyezi Mungu aukatika hukumu ya akili, na akaificha, basi yeye amelaaniwa mbele yaMwenyezi Mungu, na pi ameloloaaniwa na watu wa mbinguni na ardhini.Mwenyezi Mungu ameashiria hukumu ya akili kwa kutaja “uwongofu”.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: “Hoja ni dalili za kisharia, na uwon-gofu ni dalili za kiakili...”

Laana haiko kwa watu wa Kitabu tu, bali inamhusu kila mwenye kufichahaki kwa vile:

1. Tamko la Aya halikufungwa na jambo lolote.

2. Lau tutakadiria kuwa Aya hii imeshuka kutokana na waliyoyafanyawatu wa Kitabu, ya kupotoa Tawrati na Injili, basi tutasema: mashukiohayafanyi hukumu iliyoshuka kuwa mahsusi, kama wasemavyo wanafi-ki, ambao wanakusudia kusema kuwa: tukio mahsusi haliwezi kufanyatamko la kiujumla kuwa mahasusi.

3. Imethibiti katika elimu ya Usul kwamba kufungamana hukumu juu yasifa kunafahamisha kuwa sifa ni sababu. Na hapa laana inafungamanana kuficha kwenyewe. Kwa hivyo inakuwa laana inaenea kwa kilachenye kufichwa.

4. Imekuja Hadith inayosema: “Mwenye kuulizwa elimu anayoijua, aka-ficha, atafungwa lijamu ya moto Siku ya Kiyama.

Wameafikiana mafakihi kwa tamko moja kwamba kumfundisha asiye juahukumu za dini yake ni dharura ya wajibu kifaya (wajibu wa kutosheana)

Page 49: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

39

kwa kila mwenye kuijua; wakiitekeleza baadhi basi jukumu limewaon-dokea wote; na wakiiacha wote, basi watastahili adhabu wote.

Maana ya laana Mwenyezi Mungu, ni kumtoa mwenye kulaaniwa katikarehema Yake, na maana ya laana ya Malaika na watu ni dua ya kutakamwenye kulaaniwa atolewe katika rehema ya Mwenyezi Mungu.

UBAYA WA ADHABU BILA YA UBAINIFU

Jukumu la, na lizibainisha ikiwa hazijamfikia Mukallaf aliyebaleghe namwenye akili timamu, mbele ya Mwenyezi Mungu hupimwa kwa kum-fikia taklifa zenyewe na kuzijua, wala sio kupatikana taklifa. Kwa sababukuacha kumfikia ni sawa na kutokuwepo.

Hata hivyo ni wajibu kwa kila mwenye kukalifiwa na sharia (mukallaf) ata-fute na kufanya utafiti wa ubainifu na dalili za hukumu katika sehemuzinakopatikana, na kuwaulizia wanaohusika katika dini na sharia, walahaifai kwake kufanya uzembe na kupuuza, kisha aje atoe udhuru kuwahajui. Kwa sababu mwenye kuzembea ni sawa na mwenye kufanyamakusudi, bali huo uzembe hasa ni makusudi, kwa vile mzembe anakuwaamekusudia kuacha kutafuta na kusoma. Kama akifanya bidii na asipatelolote, basi atakuwa hana jukumu, hata kama ubainifu uko.

Hakika huu ni msingi ulio wazi kiakili; ni akili gani inayoweza kumlaumumwingine, ambaye hakufanya uzembe, kwa jambo asilolijua?Wanavyuoni wa Fiqhi wamesema kwa pamoja kuhusu msingi huu, naumethibitishwa na sharia katika Aya kadhaa; kama Aya hii tunay-oizungumzia: “Baada ya Sisi kuzibainisha kwa watu.” Pia Aya inayosema:

“...Na sisi si wenye kuwadhibu mpaka tumpeleke Mtume.” (17:15).

Katika Hadith za Mtume iko inayosema: “Umeondolewa umma wanguyale wasioyoyajua.” Tutayarudia maudhui haya kila tutakapofikiliakwenye Aya inayoyagusia inshaallah.

Page 50: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

40

Ila wale waliotubu na kujirekebisha na wakabainisha

Yaani wale wanaoificha haki ni wenye kulaaniwa, isipokuwa wale walio-tubu na kujuta kwa ikhlasi katika toba yao kwa kuazimia kutorudiamakosa; kisha wakayabainisha wazi wazi yale waliyokuwa wameyafichamwanzo; kwani kutubia kwa mwizi tu hakutoshi maadamu hajarudishahaki ya wenyewe.

Basi hao nitawatakabalia toba yao,na Mimi ni Mwingi wa kutakabalitoba, Mwenye kurehemu

Neno tawwab (mwingi wa kukubali toba) ni katika sifa za MwenyeziMungu (s.w.t.). Ameiandamiza rehema na kukubali toba, kwa kukumbushakuwa sababu ya Yeye kukubali kwake toba kwa aliyemfanyia uovu, nirehema Yake kwa waja Wake.

Hakika wale waliokufuru, na wakafa hali ni makafiri, hao wana laanaya Mwenyezi Mungu na ya Malaika na ya watu wote.Hata mwenye kumkufuru Mwenyezi Mungu na kumkanusha, MwenyeziMungu huikubali toba yake, akitubia, na humsamehe na kumrehem, walahatamwadhibu isipokuwa yule atakayekufa na huku ameng’ang’ania ukafirina maasia, kwa sababu yeye katika hali hiyo anastahili laana ya watu wambinguni na wa ardhini.

Unaweza kuuliza: Kwa nini Mwenyezi Mungu anasema: “Na ya watuwote” na inajulikana kuwa katika watu kuna wasiomlaani kafiri, hasa walemakafiri?

Jibu: Makusudio ya kauli Yake Mwenyezi Mungu; “Na ya Malaika wotena ya watu wote” ni kwamba huyo anayekufa hali ya kafiri anasthili laanaya watu wa mbinguni na wa ardhini, iwe wamemlaani au hawakumlaani;hata kama ni makafiri kama yeye huwa astahili laana yao.

Katika Qur’ani inaelezwa kwamba makafiri Kesho watalaaniana wenyewekwa wenyewe.

Page 51: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

41

“...Kisha siku ya Kiyama baadhi yenu watawakufurisha wengine na baad-hi yenu watawalaani wengine...” (29:25).Humo watadumu, hawatapunguziwa adhabu wala hawatapewa mudahumu, ni humo mwenye laana.

Maana ya kudumu katika laana ni kukaa milele katika athari ya hiyo laanaambayo ni Moto. Razi anasema: “Maana ya ‘hawatapewa muda’ nikwamba wakiomba muda hawatapewa na wakilia kutaka kuokolewahawataokolewa, na wataambiwa: ‘Nyamazeni wala msiseme’. MwenyeziMungu apishie mbali.”

HUKUMU YA LAANA KATIKA SHARIA

Kumlaani mtu ni haramu, na ni katika madhambi makubwa kwa sababu niuadui sawa na kuingilia mali ya mtu; katika Hadith inaelezwa “Hakikalaana ikitoka kwa mtu, huzunguka. Ikimkosa humrudia mwenyewe.”

Hata hivyo ziko laana zilizoruhusiwa na sharia ambazo ni:-1. Kafiri. Aya ni nyingi sana kuhusu kafiri, kama hii tunayoizungumzia.

Ama Hadith zimepetuka kuwa mutawatir. Miongoni mwazo ni ile iliyokatika kitabu Ahkamul Qur’an cha Kadhi Abu Bakr Al-Muafiri. Ametajawakati wa kutafsiri (2:161), kwamba Mtume alisema:(s.a.w.w.) “EweMwenyezi Mungu! Hakika Amr bin Al-Aas amenikebehi, na anajuakuwa mimi si mshairi. Basi mlaani.”

2. Dhalimu. Awe Mwislamu au si Mwislamu, kutokana na kauli YakeMwenyezi Mungu “Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalimu”(7 : 44)

3. Mwenye kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.Amesema Mwenyezi Mungu:

“Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule amzuliaye uwongo MwenyeziMungu? Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao, na mashahidi watase-

Page 52: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

42

ma: Hawa ndio waliomzulia uwongo Mola wao. Tambueni! Laana yaMwenyezi Mungu juu ya madhalimu.” (11:18)4. Mwenye kufanya ufisadi.5. Mwenye kufitini na kusababisha zogo.Ama laana ya wasiokuwa hao waliotajwa, kuna mushkeli na yahitajiwakuangaliwa vizuri. Ndio, ni kweli kwamba mwenye kudhihirisha maasiabila ya kujali, inajuzu kumsengenya. Lakini kujuzu kusengenya ni kitukingine, na laana ni kitu kingine. Ama wanavyotumia watu kuwalaaniwanyama, n.k., ni upuuzi, unaofaa kutupiliwa mbali.163. Na Mungu wenu ni Mungu

Mmoja, hakuna munguisipokuwa Yeye, Mwingi warehema, Mwenye kurehemu.

164. Hakika katika kuumbwambingu na ardhi, na kuhital-ifiana usiku na mchana, navyombo ambavyo hupitakatika bahari pamoja naviwafaavyo watu, na majialiyoyateremsha MwenyeziMungu kutoka mawinguni,na kwa maji hayo akaihuishaardhi baada ya kufa kwake,na akaeneza humo kila ainaya wanyama, na mabadilishoya pepo, na mawinguyanayoamrishwa kupitabaina ya mbingu na ardhi, niishara kwa watu wenye akili.

Page 53: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

43

NA MUNGU WENU NI MUNGU MMOJA

Aya 163-164

MAANA

Na Mungu wenu ni Mungu Mmoja, hakuna mungu isipokuwa Yeye.Amirul Muminin, katika kumuusia mwanawe, Hassan (a.s.), alisema:“Ewe mwanangu! Jua kwaamba lau Mola wako angelikuwa na mwenza-ke, basi wangelikujua Mitume Wake na ungeliona athari za Ufalme naUsultani Wake, na ungelijua vitendo Vyake na sifa Zake.”

Maelezo ya kukanusha mshirika yatakuja katika kufafanua Aya ya (17:42)(21:22) na (23:91).

MBINGU

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi.

Katika mbingu kuna nyota zinazozidi chembe za mchanga kwa idadi;nyota iliyo ndogo zaidi miongoni mwazo, ni ile ambayo ni kubwa kulikoardhi ya mara milioni. Kila kundi la nyota linakuwa katika mkusanyikomkubwa unaoitwa ‘galaxy’ unaokusanya zaidi ya nyota milioni mia moja.Idadi ya mikusanyiko hiyo ni zaidi ya milioni mbili. Kila mkusanyiko ukombali na mwingine kwa masafa ya simu ya upepo ambayo umbali wakekufikiwa ni miaka milioni tatu. Yaani mikusanyiko hiyo yote katika angailiyo wazi ni sawa na nzi anayepotea katika dunia. Nyota zote hizo nagalaxies zake zinakwenda kwa kipimo na utaratibu mzuri.

Huu ni mfano mmoja wa mamilioni kwa mamilioni ya uweza waMwenyezi Mungu na ukubwa Wake uliovumbuliwa na Sayansi za leo. NaQur’ani Tukufu bado inawaambia wavumbuzi hao:

“...Nanyi hamkupewa elimu ila kidogo tu.” (17:85).

Page 54: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

44

ARDHI

Ardhi ni tufe lililo angani. Inazunguuka mara moja kwa masaa ishirini nanne, mchana ukafuatana na usiku. Inaelea kulizunguka jua mara mojakwa mwaka ambapo hufuatana misimu minne kwa mwaka. Ardhi inazun-gukwa na mfuniko wa gesi wenye gesi zote muhimu kwa uhai. mfunikohuo unahifadhi gesi za kiwango cha nyuzi joto kinachowiana na uhai.Vile vile unachukua mvuke wa maji kutoka baharini na kuupeleka masafaya mbali juu, na hatimaye yanaanguka nakuwa mvua.

Lau kama upana wa ardhi ungelikuwa mdogo kuliko ulivyo sasa, ingel-ishindwa kuhifadhi uzani; na joto lingepanda kufikia hadi ya kuuai; nakama ungelikuwa ni mkubwa zaidi ya ulivyo ingelizidi mvutano wake, naziada hiyo ingeliathiri maisha kupita kiasi.

Vile vile, lau kama umbali wa ardhi na jua ungelizidi kuliko ulivyo hivisasa, kiasi cha joto kingelipungua. Na kama ardhi ingelikurubia zaidi juakuliko ilivyo hivi sasa, basi joto lingezidi. Katika hali zote mbili maishayangelikuwa magumu juu ya ardhi.

Kwa hivyo mduara wa ardhi, na kipimo cha sehemu wazi zinazoizunguka,mzunguko wake kulizunguka jua, kuzungukwa kwake na mfuniko waanga, kuwa mahali maalum na kuwa upana wake ni kiasi maalum, yotehayo yanamwandalia mtu sababu za kupata uhai juu ya ardhi. Lauingekosekana moja ya sifa hizi - kwa mfano, upana wake kuwa mdogo aumkubwa, au kuwa mbali au karibu na jua au kukosa mfuniko wa gesi, inge-likuwa vigumu mtu kuwa ni wa duniani, kwa ushahidi wa wataalamu.

Ni jambo lisiloingia akilini kuwa utaratibu huu uwe umepatikana kwasadfa tu. Bali yote hayo ni kwa hekima ya Mwenye hekima na mpangiliowa Mwenye kupanga.

KUWAKO MUNGU

Katika kufasiri Aya ya 21 na 22 za sura hii, tumetaja dalili za kuwakoMpangaji mambo, Mwenye hekima. Miongoni mwa dalili hizo ni dalili yakufikia kikomo, na kwamba mpangilio wa ndani uliofanywa kwa hekima

Page 55: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

45

kati ya mbingu na ardhi haiwezekani kuwa umepatikana kwa sadfa (kiba-hati) tu!

Wala hakuna tafsiri yenye kukinaisha isipokuwa ile ya kuwako Mweza,Mwenye hekima. Na Qur’ani imetegemea dalili hii na ukionesha katikaAya nyingi, kama vile Aya hii tuliyonayo.

Kwa mnasaba wake, tunarudia kutoa dalili ya kuwako Mwenyezi Mungu,lakini kwa mbinu isiyokuwa ile tuliyoitumia wakati wa kufasiri Aya ya 21.Lakini kabla ya kitu chochote, tunatanguliza haya yafuatayo:

Wamaada wameamua kuwa sababu ya elimu na maarifa ni kuona nakujaribu tu. Kila linaloaminika kupitia majaribio ni elimu, na kilalinaloitakidiwa kwa njia hiyo, isiyokuwa basi hawaliiti kuwa ni elimu balini itikadi. Kwa hivyo elimu na itakidi - katika istilahi yao -ni vitu viwilitofauti katika machimbuko yake. Mtu akipata msaada wa majaribio kwakusihi yale anayoyaitakidi, basi yanakuwa yale yanayoitakidiwa ni elimu.

Kwa hivyo, kwa msingi wao huo, inakuwa kuamini kuwako MwenyeziMungu yuko ni itikadi si elimu. Nasi tunawaambia: Lakini vile vilekuamini kutokuwako Mungu ni itikadi si elimu, kwa sababu hakutegemeimajaribio. Kwa hivyo itikadi zimekutana. Kwa maneno mengine, nikwamba kila yanayoambatana na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) - ikiwa nikukubali au kupinga, - ni katika mambo ya ghaibu (yaliyojificha). Ikiwamwenye kuamini kuwako Mungu anaamini ghaibu bila ya majaribio, vilevile mwenye kukanusha hategemei majaribio, bali hutegemea ghaibu.Kwa hivyo wote ni sawa.

Baada ya utangulizi huu tutaonyesha kauli ya wamaada wakanushaji nakauli ya wenye kuamini Mungu kisha tumwachie hiyari msomaji.

Wakanushaji wanasema: Kuwako ulimwengu na yaliyomo ndani yake -nidhamu, mtu pamoja na hisia zake na akili yake, yote hayo hayategemeiudhibiti wowote wala mantiki, isipokuwa yamepatikana kibahati (sadfa)tu. Kwa hivyo ulimwengu ulipatikana kibahati, kisha ukapatikana utarati-ratibu na mpango kibahati; na kila kitu kimechukua mahali pake pana-postahiki kibahati tu; na maada ndiyo iliyoleta uhai na akili, kusikia na

Page 56: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

46

kuona. Kwa maneno mengine, ni kwamba maada iliyo pofu ndiyo munguinayoweza kila kitu. Lakini imepata uwezo, hekima na upangilio wamambo kwa sadfa.

Ama wanaoamini kuwako Mwenyezi Mungu wanasema: Ulimwengu nanidhamu yake, umepatikana kwa makusudio na kwa hekima, na mpangiliowa Mola Mweza na Mwenye hekima.

Sasa, msomaji ewe, jiulize swali hili: Ni nini chanzo cha ulimwengu,utaratibu na walahidi? Au ni kwa makusudio na mipangilio, kama wase-mavyo waumini?

Jiulize swali hili, kisha ujijibu kwa akili yako. Ama Voltaire mashuhuriamelijibu swali hili kwa kusema: “Fikra ya kuwako Mwenyezi Mungu nidharura, kwa sababu fikra ya kupinga ni upumbavu.”

UPI ULIOTANGULIA: USIKU AU MCHANA?

Wataalamu wamehitilafiana kuwa mwangaza umetangulia giza au giza, ndilolililotangulia mwangaza katika kupatikana? Wengine wanasema mchana ndiouliotangulia usiku; kwa hivyo usiku wa siku ni ule unaokuja baada yamchana. Wengine wamesema usiku ndio uliotangulia mchana;kwa hivyousiku unakuwa ni usiku wa mchana utakaokuja. Watu wa kwanza walipende-lea kauli hii. Kwa hivyo usiku wa Ijumaa kwao ni ule usiku unaokuwa kablaya alfajiri ya Ijumaa; na hivyo hivyo nyusiko nyingine zote. Na katika waliy-oyatolea dalili ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na usiku ni ishara kwao; tunauvua humo mchana...” (36:37).

Page 57: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

47

165. Na katika watu kuna wanao-fanya waungu wasiokuwaMwenyezi Mungu,wanawapenda kama kumpen-da Mwenyezi Mungu. Lakiniwale walioamini wanampendaMwenyezi Mungu sana. Nalau waliodhulumu (nafsi zao)wangelijua watakapoionaadhabu kwamba nguvu zote niza Mwenyezi Mungu, nakwamba Mwenyezi Mungu niMkali wa kuadhibu.

166. Pindi waliofuatwa watakapo-wakataa wale waliowafuata,na hali ya kuwa wamekwishaiona adhabu na kuwakatikiamafungamano.

167. Watasema wale waliofuata:‘Lau kama tungeweza kurudinasi tukawakataa kamawalivyotukataa. Hivi ndivyoMwenyezi Mungu atakavy-owaonesha vitendo vyao kuwamajuto juu yao; walahawatakuwa wenye kutokaMotoni.

Page 58: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

48

WANAFANYA WAUNGU ASIYEKUWA MWENYEZI MUNGU

Aya 165-167

MAANA

Na katika watu kuna wanaofanya waungu wasiokuwa MwenyeziMungu, wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu

Yaani kuna baadhi ya watu wanamshirikisha Mwenyezi Mungu kwasababu wamemfanya kuwa na wenziwe katika baadhi ya mambo anay-ohusikana nayo Yeye; kama vile kunufaisha na kudhuru. Imam Baqir (a.s.)amesema: “Waungu ambao wamewafanya na kuwapenda kama kumpen-da Mwenyezi Mungu ni maimamu wa dhuluma na wafuasi wao.”

Imesemwa kuwa maana ya kumpenda Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni kupen-da ukamilifu, kwa sababu Yeye ni ukamilifu mtupu. Imesemwa pia: Nikujua utukufu Wake, uweza Wake na hekima Yake. Na imesemwa: Nikuamini kuwa Yeye ndiye mwanzilishi na Mwenye kurejesha, na kwambakila kitu kiko chini ya mamlaka yake.

Sisi tuko kwenye njia ambayo tunakwenda nayo: ya kuchagua maanayenye kuafikiana ambayo yako wazi na yaliyo rahisi kufahamika. Kwamsingi huu basi tunasema: Anayempenda Mwenyezi Mungu ni yule asiye-fuata matamanio yake mtii Mola wake; kama alivyosema Imam Sadiq(a.s.) katika kumwelezea ambaye dini ichukuliwe kwake. Kwa manenomengine, kumpenda kwako Mwenyezi Mungu ni kuacha unayoyatakawewe na kufanya anayoyataka Yeye; kama ambavyo maana ya kumpendaMtume (s.a.w.w) ni kufanya jambo kulingana na sunna yake.

Ama Mwenyezi Mungu kumpenda mja Wake, ni kumlipa thawabu.Imekuja Hadith inayosema: “Nitampa bendera kesho mtu anayempendaMwenyezi Mungu na Mtume Wake, na anayependwa na Mwenyezi Munguna Mtume Wake.” Makusudio ya mtu hapa ni Ali bin Abi Twalib. YaaniAli anamtii Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atamlipa thawabu na

Page 59: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

49

Mtume anamtukuza na kumtanguliza.

Kwa hivyo basi, kila anayemtii kiumbe, akaacha kumtii Muumba, huyoamefanya waungu wasiokuwa Mwenyezi Mungu, atake asitake.

Lakini wale walioamini wanampenda Mwenyezi Mungu sana

Kwa sababu wao hawamshirikishi na yeyote katika twaa, kumwamini nakumtegemea. Ama wale wasioamini wanawategema waungu wengi nahumshirikikisha Mwenyezi Mungu na wao katika twaa, kutaka kheri nakujikinga na shari.

Na lau waliodhulumu (nafsi zao) wangelijua watakapoiona adhabukwamba nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu

Yaani lau washirikina ambao wamezidhulumu nafsi zao wangelijua kwam-ba hakuna mwenye usultani, katika siku ya haki na ya kupambanuliwahukumu, isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Yeye peke Yake ndiyeMwenye mamlaka ya kuwaadhibu waasi na kuwalipa mema watiifu - lauwangelijua hivyo, basi wangelikuwa na yakini kwamba atakayekuwa pekeYake kesho katika kuendesha mambo ya Akhera ndiye huyo huyo aliyepangaulimwengu huu. Kwa hivyo jawabu ya lau limeondolewa, linafahamikakutokana na mpangilio wa maneno.

Pindi waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali yakuwa wamekwishaiona adhabu na kuwakatikia mafungamano

Maneno bado yanaendelea kwa wale wanaofanya waungu wasiokuwaMwenyezi Mungu: nao ni wale wanaoongozwa na wafuasi; na waungu: naoni wale viongozi. Kesho pazia litakapofunguka, kiongozi atamkataamfuasi wake kwa ajili ya shida ya adhabu itakayotokea, na uhusiano waoutakatika. Mwenye Majmaul-Bayan anasema: “Zitaondoka zile sababuzote zinazomkinika kushikana nazo mapenzi, udugu, cheo, mikataba yaumoja, n.k. walizokuwa wakinufaika nazo hapa duniani. Na hilo nimwisho wa kukata tamaa.”

Page 60: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

50

Aya hii inafanana na Aya inayosema:

“...Kila umma utakapoingia, utawalaani wenza; mpaka watakapokusanyi-ka wote humo, wa nyuma wao watasema kuhusu wa kwanza wao: Molawetu! Hawa ndio waliotupoteza; basi wape adhabu ya Moto maradufu!Atasema: ‘(mtaadhibiwa) nyote maradufu, lakini nyinyi hamjui.”(7:38).

Watasema wale waliofuata: Lau kama tungeweza kurudi nasitukawakataa kama walivyotukataa.

Kesho kila asi atatamani arudi duniani kutengeneza yale aliyokuwa ameya-haribu, hasa wafuasi wa watu wapotevu. Na hakuna kitu kilicho mbali mnona matamanio haya, zaidi ya hilo, bali ni majuto yanayoichoma nafsi, sawana moto unavyochoma mwili. Majuto hayo ni matunda ya kufuata mata-manio na kupetuka mipaka.

Dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba inahusika na makafiri, lakini kwamujibu wa sababu ya hukumu, inamhusu kila anayefaata na kusaidia mad-halimu na mafisadi, na kila mwenye kuitakidi kwamba asiyekuwaMwenyezi Mungu anaweza kunufaisha na kudhuru mwenye kuchukua diniyake kutoka kwa wasio jua na wapotevu.

Kwa hakika Aya hii inawahusu hao wote; hata mwenye kutamka shahadambili, akaswali na kutoa zaka; isipokuwa asiyejua ambaye ameshindwakujua hakika ya mambo yale na kujua yanayoweza kujulikana na akiliyoyote iliyo timamu.

Page 61: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

51

TAKLIDI NA MAIMAMU WANNE

Yamekuja maelezo katika Tafsiri ya Al-Manar kwa kunakiliwa kutoka kwaSheikh Muhammad Abduh kwamba maimamu wanne: Abu Hanifa, Malik,Shafi na Bin Hambali wamekataza kufuatwa na kuchukuliwa kauli zao, nakwamba wao wanaamrisha ziachwe kauli zao na kifuatwe Kitabu chaMwenyezi Mungu na Sunna za Mtume Wake. Baada ya kunakili kauli yakila Imamu katika hilo, akasema: “Lakini Karkhi - mmoja wa mafakihi waKihanafi- anasema wazi kwamba asili ni kauli ya Abu Hanifa. KamaKitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna za Mtume Wake zitaafikiana nakauli ya Hanafi ni sawa; na kama si hivyo, basi ni lazima kauli yaMwenyezi Mungu au Hadith ifanyiwe taawili ili iweze kuafikiana na kauliya Abu Hanifa.”

Maana ya maneno haya ni kuwa kauli ya Abu Hanifa ndiyo inayohukumuna kuitangulia Qur’ani na Hadith. Kauli hii kwa dhati yake ni kufuru.Kuna kufuru gani kubwa zaidi ya ile ya kuiacha kauli ya Mwenyezi Munguna Mtume Wake kwa sababu ya kauli ya Abu Hanifa na wafuasi wake? Je,kuna tofauti gani kati ya mwenye kusema haya na wale waliotajwa naMwenyezi Mungu aliposema:

“Na wanapoambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu; huse-ma “Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu...” (2:170).

Tutafafanua kwa upana zaidi suala la taklidi katika kufasiri Aya ya 170 yasura hii inshaallah.

Kwa hivyo kufanya amali kwa kutegemea kauli za maimamu wane nikufanya amali bila ya ijitihadi wala taklidi, kwa sababu hao wannewamekataza kufuatwa.

Page 62: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

52

168. Enyi watu! Kuleni vilivyomoardhini halali zuri, wala msi-fuate nyayo za Shetani.Hakika yeye kwenu ni aduialiye dhahiri.

169. Hakika yeye anawaamrishamachafu tu na maovu, nakumzulia Mwenyezi Mungumsiyoyajua.

170. Na wanapoambiwa: Fuatenialiyoyateremsha MwenyeziMungu; husema: Bali tutafu-ata yale tuliyowakuta nayobaba zetu.’ Je, hata kamababa zao walikuwa hawafa-hamu chochote walahawakuongoka?

KULENI VILIVYOMO KATIKA ARDHI

Aya 168-170

LUGHA

Halali ni kila ambalo halikuthibiti kukatazwa katika sharia; na haramu nilile lililothibiti kukatazwa. Makusudio ya uzuri hapa ni lile ambalolinapendelewa na nafsi na kuburudika nalo, kwa sharti ya kutokuwa ni

Page 63: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

53

lenye kukatazwa. Na ni lile ambalo mwisho wake ni uovu.

Enyi watu! Kuleni vilivyomo ardhini halali na vizuri.

Maneno haya yanawahusu watu wote; ni sawa awe ya mtu aliyeji-haramishia mwenyewe baadhi ya vyakula au asiyejiharamisha; ni sawaawe ni muumini au kafiri; kwa sababu kafiri atazuiliwa neema za Akheratu, sio starehe za dunia. Kuna Hadith Qudsi isemayo: “Mimi ninaumba,na anaabudiwa mwingine; na ninaruzuku, na anashukuriwa mwingine.”

Katika vyakula kuna vya halali na haramu. Mwenyezi Mungu ameviha-lalisha vya kwanza, sio vya pili. Na kila hakikukatazwa na sharia ni halali.Hadith inasema: “Hakika Mwenyezi Mungu amenyamazia vitu, sio kwakusahau. Kwa hivyo msijikalifishe navyo; ni rehema kwenu kutoka kwaMwenyezi Mungu.” Mara nyingine uharamu, wa kitu hutokana na sababuiliyokizukia; kama vile mali iliyochukuliwa kwa riba, utapeli, rushwa auwizi.

Wala msifuate nyao za Shetani. Hakika yeye kwenu ni adui aliyedhahiri

Baada ya Mwenyezi Mungu kuhalalishia watu halali anawahadharishakuifanya haramu. Ibara ya tahadhari hii ameileta kwa kukataza kumfuataShetani na tashwishi zake ambazo zinampambia mtu yale yasiyokuwahalali kwake na kila ambalo linamhadaa, ili afanye mambo ya haramu;kama vile kunywa pombe, zinaa, uwongo na ria. Au kumhadharishakufanya wajibu; kama vile kumtia mtu hofu ya ufakiri ikiwa atatekelezahaki iliyojuu yake kwa kutoa mali, au madhara ikiwa atafanya jihadi aukusema haki. Yote hayo ni katika mawazo ya Shetani. Mwenyezi Munguameuelezea usemi wa Shetani aliposema:

“Na kwa hakika nitawapoteza na nitawatia tamaa...” (4:119).

Page 64: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

54

“...Basi nitawavizia (waja Wako) katika njia Yako iliyonyooka. Kishanitawajia kwa mbele yao na nyuma yao na kuumeni kwao na kushotonikwao; hutawakuta wengi katika wao ni wenye kushukuru.”(7:16-17).

Hakika yeye anawaamrisha maovu na machafu tu, na kumzuliaMwenyezi Mungu msiyoyajua

Huu ni ubainifu wa athari na natija za kuitika mwito na nyayo za Shetani,nazo ni tatu: Kwanza ubaya ni ambao ni kila kitendo ambacho mwishowake ni mbaya. Pili ni uchafu, aina mbaya ya maasia ambao ndio. Tatu nikumsingizia Mwenyezi Mungu msiyoyajua: kwamba Yeye ana washirikana watoto, kuhalalisha haramu, na kuharamisha halali. Vile vile kufanyaamali kwa kukisia na kupendelea, katika kutoa hukumu ya sharia.

Na wanapoambiwa! Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu;husema: Bali tutafuata yale tuliyowakuta nayo baba zetu

Dhamiri ya wanapoambiwa inamrudia kila anayefuata mwingine bila yahoja wala dalili, na kuacha kauli ya Mwenyezi Mungu na Mtume kwa yakauli ya mababa. Makusudio ya aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ni kilayale yaliyo na dalili na hoja na yakaaminiwa na akili zilizo timamu.

Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote walahawakuongoka?

Yaani wanafuata baba zao hali hawafahamu chochote katika mambo yadini?

Makusudio ya hawafahamu chochote sio kuwakanushia kufahamu kila

Page 65: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

55

kitu, ijapokuwa kwa dhahiri Aya hii inaonesha hivyo; bali makusudio nikuwakanushia kufahamu, kwa vile maneno ya dini tu yanahusianayenyewe na mambo ya kidini.

Tutaonesha katika kifungu kifuatacho kwamba Aya hii inafahamisha ubayawa kufuata mambo ya upotevu. Ama kufuata ya uongofu, hilo ni ufuasimzuri.

KUFUATA NA MISINGI YA ITIKADI

Kufuata (taklidi), kulivyo hasa, si kuzuri wala si kubaya kwa ujumla, balikunatofautiana kwa aina zake zifuatazo:

1. Kufuata mkumbo, ambako kwa binadamu na wanyama ni sawa sawa;kama vile kuwika kwa jogoo anapomsikia mwenzake amewika, na kuliakwa punda anapomsikia mwenzake amelia. Hali kadhalika kwa upandewa binadamu; mmoja anaweza kupiga kofi kwa ajili ya hotuba, nawengine wote wakaigiza bila ya kutambua, hata kama hawakufahamukitu katika yaliyosemwa. Au mtu anaweza kuangalia upande fulani,ikawa kila anayemuona naye huangalia huko, bila ya kukusudia. Hukundiko kufuata ambako si kuzuri wala si kubaya, kwa sababu kuko njeya hisia na matakwa.

2. Kufuata mitindo na desturi fulani ya jamii; kama vile namna ya mavazina mengineyo katika mambo ya jamii ambayo yamefanywa na wakub-wa na wadogo, na wajuzi na wasiokuwa wajuzi. Hii ni katika aina yakufuata ambako kunaweza kuwa kuzuri au kubaya kulingana namtazamo wa watu.

3. Asiyejua kumfuata mtaalamu katika mambo ya kidunia; kama vileutabibu, uhandisi, kilimo, ufundi, n.k. Huku ni kufuata kuzuri bali nimuhimu sana katika ustawi wa jamii. Lau kama si hivyo, basi utaratibuungeharibika na kazi zingelisimama. Kwani mtu hawezi kujua kila kituna kupata kila anayoyahitajia peke yake. Mtu alikuwa, na ataendeleakuwa, na haja ya kusaidiana na kubadilishana huduma.

Page 66: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

56

4. Mujtahid kumfuata mujtahid mwenzake katika mambo ya kidini.Huku kunakataliwa na akili, na ni haramu kisharia; kwa sababu, aliy-oyajua ni hukumu ya Mwenyezi Mungu katika haki yake, haijuzukuyaacha kwa sababu ya kauli ya mtu mwingine. Ni mtu gani mwenyeakili ya sawa sawa, anayethibitikiwa na hoja, akaikataa kwa hoja yamwingine? Na ni alim gani anayeacha kauli ya Mwenyezi Mungu naMtume wake aliye mausumu na kutegemea kauli ya anayeweza kupa-ta na kukosa?

5. Asiye na elimu kumfuata mujtahid mwadilifu katika masuala tanzu yakidini, kama vile hukumu za ibada, halali na haramu, twahara, najisi nakusihi miamala, n.k. Kufuata huku ni wajibu kisharia, kwa sababu nikumfuata aliyechukua ujuzi wake kutokana na hoja na dalili; sawa namgonjwa, asiye na ujuzi wa ugonjwa wake na dawa yake, kumfuatadaktari. Asiyejua anakalifiwa na hukumu, na hakuna njia ya kuzifuataisipokuwa kumrudia mjuzi.

“...Basi waulizeni wenye kumbukumbu (wajuzi) ikiwa nyinyi hamjui.”

(16:43).

Hata hivyo, asiyejua akiswali na kufunga kwa kufuata baba zake namfano wao, sio kwa kufuata mujtahid mwadilifu, na ibada zakezikaafikiana na fat-wa za mujtahid, hizo zitakuwa sahihi na kukubaliwa;kwa sababu kufuata (taklidi) si sehemu wala sharti la yanayoamrishwa,isipokuwa ni nyenzo tu ya kufikilia kwenye amri. Hata inaweza kusihimaamiliano yake kama yakiwa ni sawa sawa.

Kuhusu kauli ya anayesema kuwa ibada inahitajia nia ya kujikurubishakwa Mwenyezi Mungu, na kwamba nia hiyo haithibiti ila itokane namujtahid au mwenye kumfuata, kauli hiyo ni madai tu, kwa sababumaana ya nia ya kujikurubisha ni kutekeleza yaliyoamriwa kwa nia safiyenye kutakata na kila uchafu wa kidunia. Hapana mwenye kutia shaka

Page 67: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

57

kwamba hayo yanaweza kupatikana bila ya mujtahid. Kauli yakeMwenyezi Mungu (s.w.t.):“...Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote walahawakuongoka?”inafahamisha kuwa ikiwa baba alikuwa kwenye uon-gofu, na akafuatwa na mtoto, itasihi.

6. Kufuata katika misingi (itikadi) ya dini, kama kumjua MwenyeziMungu na sifa Zake, Utume wa Muhammad na isma yake, na ufufuo.Wanavyuoni wengi wa Kisunni na Kishia wameikataza aina hii ya kufu-ata, nakusema wakasema kuwa haijuzu (haifai), kwa sababu taklidi nikufuata kitu bila ya dalili. Na huo ndio ujinga hasa; yaani mwenye kuse-ma kuwa Mwenyezi Mungu yuko, kwa kufuata tu, ni sawa na mwenyekusema yuko, hayuko.

Wanavyuoni hawa wamesema: “Tumejuzisha taklidi katika matawi ya dinina masuala ya kuamiliana, lakini sio katika misingi ya kiitikadi; kwa sababulinalotakiwa katika matawi ni amali tu kwa kufuata kauli ya mujtahid, jamboambalo linawezekan; lakini kwa misingi ya kiitikadi, linalotakikana ni elimuna itikadi.”

Wahakiki katika Sunni na Shia wamesema kuwa taklidi ikiafikiana nauhakika ulivyo, ni sahihi; sio kwa sababu hilo ndilo linalotakikana; naijtahidi sio sharti wala fungu la imani na kusadikisha, isipokuwa ni njia tu;sio ukomo.

Hii ni kweli kabisa, kwa sababu linalozingatiwa katika misingi ya itikadini imani sahihi yenye kuafiki. Kwa ajili hii ndio Mtume (s.a.w.w)akakubali Uislamu wa kila aliyeuamini na ikatulia nafsi yake kwa ukweliwake na Utume wake, bila ya kufanya ijtahidi na kuangalia. Ama Aya zili-zokuja kukemea wanaofuata mababa, mfumo wake unafahamisha kuwamakusudio ni kufuata batili na upotevu, sio haki na uongofu. Na hakika hiiinadhihiri kwa kila mwenye kufikiria kwa undani maana ya kauli yaMwenyezi Mungu:

Page 68: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

58

“Hata kama nawaletea yenye mwongozo bora kuliko mliyowakuta nayobaba zenu.?” (43:24).

“Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote walahawakuongoka?” (2:170).

Ufahamisho wa Aya zote hizi ni kwamba, kama baba zao wangelikuwa nadesturi yenye uongofu ambao umeteremshwa na Mwenyezi Mungu kwaMtume, basi ingelifaaa kuwafuata mababa hao, kwa sababu linalotakiwa nikufuata aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu. Wakiyafuata, basi watakuwawamefuata amri na wametii, na hawataulizwa kitu kingine baada ya twaa.

Kwa ufupi ni kwamba kila anyefuata kauli ya Mwenyezi Mungu naMtume, atakuwa amefuata haki yenye kuthibiti kwa dalili, ni sawa aweamejua dalili hiyo au la. Inatosha kujua kwa jumla kwamba kuna dalilisahihi waliyoifuata wahusika wanaofanya ijtihadi. Bali mwenye kufuatahaki bila ya kuijua kwamba hiyo ni haki, hataadhibiwa kwa kuacha kuji-fundisha hata kama hastahiki thawabu na kusifiwa. Hayo yanafahamikakutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

“Na (wazazi wako) wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna elimunayo, usiwatii ...” (31:15).

Page 69: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

59

Hiyo vile vile inafahamisha kuwa wakikushurutisha kumwamini MwenyeziMungu na ukawatii bila ya kuwa na elimu nayo, basi hapana ubaya kwako.

Tumefafanua kuhusu kuwakalidi maimamu wanne katika kufasiri Aya ya 167ya sura hii. Mwenye kutaka narudie.

171. Na mfano wa wale walioku-furu, ni kama mfano waanayempigia kelele asiyesikiaila wito na sauti tu. Ni viziwi,mabubu, vipofu; kwa hivyohawafahamu.

MFANO WA ANAYEITA ASIYESIKIA.

Aya 171

MAANA

Mwenyezi Mungu katika Aya hii anawapigia mfano makafiri ambaowameng’ang’ana na dini ya baba zao. Akawafananisha na wanyama, naakamfananisha na mchungaji, yule anayewalingania kwenye haki. Kamaambavyo wanyama hawafahamu chochote katika maneno ya mchungajiisipokuwa sauti wanayoizowea baada ya kuzoweshwa, vile vile makafirihawafahamu haki wala manufaa ambayo wanalinganiwa. Kwa hakika waoni kama viziwi japo wanasikia; ni kama mabubu japo wanasema, na ni kamavipofu japo wanaona.

katika Qur’ani mna Aya nyingi ambazo hazimtofautishi kiziwi asiyewezakusikia kabisa na yule anayeisikia haki lakini asiitumie; kama vile Aya hiituliyo nayo:

Page 70: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

60

Asiyesikia ila wito na sauti tu

Na kauli nyingine:

“Wanaokubali ni wale wanaosikia ...” (6:36).

Na kauli nyingine:

“Wala msiwe kama wale wanaosema: Tumesikia, na kumbe hawasikii.”(8:21)

Unaweza kuuliza kuwa dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa MwenyeziMungu (s.w.t) amewafananisha makafiri na mchungaji wanyama, siowanyama, kwa sababu amesema: Na mfano wa wale waliokufuru nikamamfano wa yule anayemwita asiyesikia. Lililowazi ni kuwa anayeita nimchungaji, na asiyesikia ni mnyama. Kwa hivyo makafiri wanakuwa nikama mchungaji anayepigia kelele wanyama, sio kama wanyama, kamaulivyosema katika tafsiri ya Aya. Sasa imekuwaje?

Jibu: Hapa kuna kukadiriwa maneno ambao yanaeleweka kutokana na fuolake; nayo ni: Hakika mfano wa wanaowalingania makafiri kwenye haki nikama mfano wa anayemwita asiyesikia.”

Page 71: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

61

172. Enyi mlioamini! Kuleni vizuritulivyowaruzuku, namumshukuru MwenyeziMungu ikiwa mnamwabuduYeye tu.

173. Hakika amewaharamishiamzoga, tu na damu, na nyamaya nguruwe, na kilichochinji-wa asiyekuwa MwenyeziMungu tu. Basi aliyefikwa nadharura (akala) bila kutamaniwala kupita kiasi, yeye hanadhambi. Hakika MwenyeziMungu ni Mwenye maghufira,Mwenye kurehemu.

KULENI VIZURIAya 172-173

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu kuwaambia watu wote kwa kauli Yake: “Enyiwatu! kuleni vilivyomo ardhini,” amerudia kusema tena, lakini akiwahu-sisha waumini:

Enyi mlioamini! Kuleni vizuri tulivyowaruzuku

ili awabainishie kwamba imani sahihi sio kujizuia na vitu vizuri, kamawanavyofanya baadhi ya watawa, makasisi na wengineo; kwa sababuMwenyezi Mungu (s.w.t.) ametuhalalishia kustarehe na maisha na neemaza kimwili na akatuamrisha kuzishukuru; na maana ya kuzishukuru ni kuz-

Page 72: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

62

itumia katika njia inayotakikana.

Amirul Muminin Ali (a.s.) anasema: “Uchache wa yanayowalazimu kwaMwenyezi Mungu ni kutozitumia neema Zake kwa kumwasia.” Huendawale wenye jaha na utajiri, wakaidhika kwa hekima hii iliyo na fasaha,wasiitumie katika anasa iliyoharamishwa na kuwa na kiburi na kupetukamipaka.

Hakika amewaharamishia mzoga, na damu tu na nyama ya nguruwena kilichochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu

Hakuna mwenye shaka kwamba makusudio ya uharamu hapa ni uharamuwa kitendo, ambacho ni kula, sio uharamu wa kitu chenyewe. Kwani kituhakiwezi kutajwa kwa uhalali na uharamu.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja , katika Aya iliyotangulia, uhalali wavinavyoliwa, hapa anatupa aina nne ya vilivyo haramu kuliwa:

1. Mfu. Ni kila mnyama aliyekufa bila ya kuchinjwa kisharia.2. Damu. Makusudio ni damu iliyotengeka na nyama, kwa sababu iliyo

pamoja na nyama inasamehewa.3. Nguruwe. Nyama yake, shahamu yake na mwili wake wote, kinyume

na anavyosema Daud Dhahiri aliposema: “Ni haramu nyama ya ngu-ruwe tu, sio mafuta yake,” kwa kuchukulia dhahiri ya tamko, eti Ayaimetaja nyama tu. Ilivyo ni kwamba imetajwa nyama kwa sababu ndioinayotumika zaidi.

4. Kilichochinjiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Yaani yule aliyetajiwa jinala asiyekuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), wakati wa kuchinjwa; ni sawakuchinjwa kwenyewe kuwe ni kwa ajili ya masanamu, matambiko,mazindiko au vitu vingine.

Hekima ya kuharamishwa aina tatu za kwanza ni kiafya ambayo matabibuwanaijua. Ama hekima ya kuzuia kile kilichotajiwa aisyekuwa MwenyeziMungu, ni ya kidini yenye lengo la kuchunga tawhid kuwa na mshirika nakumwepusha Mwenyezi Mungu na Unaweza kuuliza; Dhahiri ya Aya inafahamisha kwamba hakukuharamish-wa isipokuwa aina hizi nne tu za vyakula, kwa sababu neno tu linafaa-

Page 73: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

63

hamisha mambo mawili:

Kwanza, kuthibitisha yale yanayoelezwa, ambayo hapa ni kuharamishwavitu vinne.Pili, kuthibitisha kukanusha ambako hapa ni kutoharamishwa vitu vingineispokuwa vitu hivi vinne tu; hali kuna vyakula vingine vilivyoharamishwa:kama mbwa, wanyama wanoshambulia, wadudu, baadhi ya samaki. n.k.

Ufafanuzi zaidi unaweza kuupata katika vitabu vyetu vya Fiqhi; kama vilekitabu chetu cha Fiqhi Al- Imam Jafar Sadiq ( a.s.)

Jibu: Ndio dhahiri ya Aya inafahamisha hivyo, lakini halitumiwi hilo baadaya kongamano la wanavyuoni na kuthibiti Hadith za Mtume. Wala hii siyoAya yapekee ambayo dhahiri yake imeachwa na kongamano la wanavyuonikutokana na Hadith.

Kwa ujumla ni kuwa ni wajibu kumtaja Mwenyezi Mungu (s.w.t.) wakatiwa kuchinja. Mwenye kuacha kufanya hivyo kwa makusudi, basi alicho-kichinja ni haramu, ni sawa iwe aliacha kwa kujua au kutojua. Ama aki-acha kwa kusahau, basi haiwi haramu. Inatosha kutaja Allahu Akbar au Al-hamdulillah au Bismillah au Lailaha illa Ilahu, n.k.

MWENYE DHARURA NA HUKUMU YAKE

Basi aliyefikwa na dharura bila kutamani wala kupita kiasi, yeye hanadhambi.

Mwenye dharura ni yule ambaye anahofia nafsi yake kufa ikiwa hatakulakitu cha haramu, au anahofia kuzuka maradhi au kuzidi maradhi, anahofiamadhara na adha juu ya nafsi nyingine yenye kuheshimiwa; kama vilemwenye mimba kuiogopea mimba yake au mwenye kunyonyesha kumhofiamwanawe, au mwenye kulazimishwa kwa nguvu kula au kunywa kitu chaharamu, kwa namna ambayo, kama hakufanya hivyo, atapata adha ya nafsiyake au mali yake au utu wake.

Yote haya, na mifano yake, ni katika mambo yaliyosamehewa katika kutu-mia kitu cha haramu, lakini kwa kiasi kile tu kinachoweza kuondoa mad-hara. Kuanzia hapo ukawa mashuhuri ule msemo wa mafakihi: “Dharurahupimwa kwa kiasi chake”. Hilo linafamishwa na kauli yake Mwenyezi

Page 74: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

64

Mungu: “Basi aliyefikwa na dharura bila kutamani wala kupita kiasi, yeyehana dhambi.” Mwenye kutamani ni yule anayefanya haramu bila yadharura, na mwenye kupitisha kiasi ni yule anayepitisha kiasi cha haja.

174. Hakika wale wafichao aliyoy-ateremsha Mwenyezi Mungukatika Kitabu na wakanunuakwacho thamani ndogo, haohawali matumboni mwaoisipokuwa Moto: walaMwenyezi Munguhatawasemesha Siku yaKiyama, wala hatawatakasa;na wao wana adhabu chungu.

175. Hao ndio walionunua upotevukwa uwongofu, na adhabukwa maghufira. Basi ni ujasiriulioje wa kuvumilia Moto?

176. Hayo ni kwa sababuMwenyezi Mungu ame-teremsha Kitabu kwa haki, nawale waliohitilafiana katikaKitabu (hiki) wamo katikaupinzani ulio mbali.

Page 75: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

65

WAFICHAO ALIYOYATERMSHA MWENYEZI MUNGU

Aya 174-176

MAANA

Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katikaKitabu na wakanunua kwacho thamani ndogo

Inasemekana kuwa Aya hii imewashukia watu wa Kitabu walioficha sifa zaMuhammad (s.a.w.w) na Utume wake.

Kwa vyovyote itakavyokuwa sababu ya kushuka Aya, makusudio hapa nikwa kila anayeijua haki akaficha kwa kuitolea na kuipotoa kwa manufaa yakebinafsi; awe ni Yahudi, Mkristo au Mwislamu; kwa sababu tamko lililotumi-wa hapa lililotumiwa hapa ni la kuenea na ‘linalozingatiwa ni kuenea tamko,si kuhusika sababu za kushuka kwake.’

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtisha mpotevu huyu katika Aya nyingi;miongoni mwazo ni zile zilizotangulia (Aya ya 146 na 159) na zitakazofu-atia katika Sura Al-Imran, Nisaa, Maidah na Aya hii tuliyonayo. Zote hizoni hasira za Mwenyezi Mungu na kiaga kikali cha adhabu na mateso kwasababu ni wajibu haki itukuzwe na kutangazwa kwa kila njia, na kuondoamikanganyo yote ya kutofahamika. Vile vile ni wajibu kumpiga vitamwenye kuipinga, kwa nguvu zote, na kujitoa mhanga kwayo-kwani haisi-mami dini kujitoa mhanga. Wala nidhamu au uhai isipokuwa kwa haki.

Hao hawali matumboni mwao isipokuwa Moto

Yaani wanachokula ni kile kitakachostahilisha wao kutiwa Motoni. Hiyo nikatika kuelezea kinachosababishwa, ambacho ni Moto, na kinachos-ababisha, ambacho ni kula haramu.

Yametajwa matumbo hapa, ingawaje inajulikana kuwa hakuliwi isipokuwakwa ajili ya tumbo, ili kuonyesha kuwa linalowashughulisha wao nikujaza matumbo yao tu.

Page 76: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

66

Wala Mwenyezi Mungu hatawasemesha siku ya Kiyama.

Ni kinaya cha kuachana nao na kuwakasirikia.

Wala hatawatakasa yaani: wala hatawatakasa na madhambi kwakuwasamehe.

Hao ndio walionunua upotevu kwa uwongofu

Upotevu ni kufuata matamanio, na uwongofu ni kufuata Kitabu chaMwenyezi Mungu. Na kununua upotevu kwa uwongofu ni kuathirika nabatili kuliko haki.

Basi ni ujasiri ulioje wa kuvumilia Moto?

Huku sio kuelezea ujasiri wao kwa Moto; wala sio kuustaajabia. Maana kiten-do cha kustaajabu hutokana na kutojua sababu ya jamb; na hilo muhali kwaMwenyezi Mungu (s.w.t.), kwani Yeye anajua kila kitu. Makusudio hasa hapani kuonyesha namna ya kujitia ujasiri kwao kwa Mwenyezi Mungu, kwakuacha hukumu Zake na mipaka Yake, na kufuata upotevu na batili.

Kwa hivyo makusudio ni kuleta picha ya hali yao hiyo na kupiga mfano wamarejeo yao ambayo haiwezekani kuyafanyia ujasiri kwa vyovyote. Razianasema: “Walipojiingiza kwenye lile linalowajibisha Moto, wamekuwakama wenye kuridhia adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwa majasiri waadhabu hiyo; sawa na kumwambia yule anayejiingiza kwenye lile linalokasirisha serikali: Ni ujasiri ulioje wako kufungwa jela?

Unaweza kuuliza: Tumejua hiyo ndiyo hali ya yule anayeijua haki akai-ficha. Sasa ni ipi hali ya asiyejua chochote katika yaliyoteremshwa naMwenyezi Mungu, lakini pamoja na hayo anasema: Hii ni haramu, na hiyoni halali, na wala hana chochote cha kutegemea isipokuwa dhana nakuwazia tu?

Jibu: Huyu ana hali mbaya zaidi kuliko yule anayeijua haki na akaificha,kwa sababu yeye amejiweka daraja ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kuji-fanya ndio msingi wa sharia, wa kuhalalisha na kuharamisha.

Page 77: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

67

MVUTANO KATI YA HAKI NA BATILI

Mwenye Tafsir ya Al-Manar amemnakili Sheikh Muhammad Abduhkwamba amesema katika kuifasiri Aya hii:

“Katika Waislamu kuna wanaoficha yaliyoteremshwa na MwenyeziMungu kwa kupotoa na kuleta taawili, kama wanavyofanya Mayahudikuficha sifa za Mtume. Waislamu hao wanatambua mivutano miwili inay-opingana: mvutano wa haki waliyoijua, na mvutano wa batili waliy-oizoweya. Hayo huwatingisha na kuwaathiri, na haya huwapa kiburi nachuki. Akili zao zikashinda yale waliyoyajua na nyoyo zao zimeshindayale waliyoyazowea. Wakathibiti kwenye yale waliyoyapotoa; wakawawamo katika vita kati ya akili na dhamiri. Wakifikiria Kesho (Akhera),starehe za sasa (duniani) zinawatokea puani, lakini wanapoonja utamu wawanayoyafanya husahau yatakayokuja. Je, huku kuhisi kuitweza haki nakuinusuru batili sio moto unaowaka mbavuni mwao? Je thamani ya hakiwanayoila si miti ya miba ambayo hainenepeshi wala kuondoa njaa?”

Hayo ni sahihi kwa upande wa baadhi ya wale wanaojitilia shaka katikadhamiri zao na kujilaumu, wakiwa wanafanya dhambi. Lakini wenginewamezoweya batili mpaka ikawa ni tabia yao, na kuliona adui kila lenyeharufu ya haki na utu.

Na sasa, ninapoandika maneno haya, ni mwezi wa Juni 1967. Katikamwezi huu ulio na shari, Israel imevamia baadhi ya sehemu za miji yaWaarabu kwa msaada wa Uingereza na Marekani, na wamewatoa watumajumbani mwao, wakawafukuza zaidi ya watu laki mbili na nusu(250,000), wakawachoma wake kwa waume, na watoto, kwa mabomu yanapalm.

Wengi wameiunga mkono fedheha hii na kuichezea ngoma; wanatamani lauIsrael ingeendelea na uovu wake. Mapenzi ya nafsi kwao yamezidi akili nadhamiri zao mpaka zikaisha zote bila ya kubaki athari yoyote, wakawa sawana wanyama. Ndipo Mwenyezi Mungu akawaita kuwa ni watu wasio naakili, wasiofahamu na kwamba wao ni wanyama, bali ni wapotevu zaidi

Page 78: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

68

kuliko wanyama.

Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki

Hayo ni ishara ya adhabu itakayowashukia wale wanaoficha haki. Na,kauli Yake Mwenyezi Mungu: “Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ame-teremsha Kitabu”, ni kubainishwa sababu za adhabu hiyo, ambazo nikuthubutu kwao kuwa wajasiri wa kuihalifu haki iliyokuja katika Kitabucha Mwenyezi Mungu.

Na wale waliohitilafiana katika kitabu wamo katika upinzani uliombali.

Wafasiri wamehitalifiana kuhusu makusudio ya kauli hii: waliohitilafina kati-ka Kitabu. Wafasiri wengi, akiwemo mwenye Majmaul - Bayan, wamesemani makafiri; na kuhitilafiana kwao ni kwamba kuna waliosema kuwa Qur’anini uchawi; wengine wakasema ni utenzi, na wengine wakasema ni vigano vyawatu wa kale.

Baadhi ya wafasiri wamesema makusudio ya waliohitilafiana ni Waislamu;kwamba wao, baada ya kuafikiana kuwa Qur’ani inatoka kwa MwenyeziMungu, wamehitilafiana katika kuifasiri na kuiletea taawili; waka-gawanyika kwenye vikundi. Ilitakiwa wao wawe na tamko moja kwa vileQur’ani ni moja.

Inawezekana pia kuwa makusudio ni makafiri, lakini sio kwa kuwawengine walisema kuwa Qur’ani ni uchawi; na wengine wakasema kuwani utenzi au vigano, bali ni kwamba wao ndio sababu ya pekee ya kuhiti-lafiana, kupigana na kuacha kuafikiana na tamko la haki kati yao na walewalioiamini Qur’ani.

Page 79: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

69

177. Sio wema kuelekeza nyuso

zenu upande wa mashariki na

magharibi tu, lakini wema ni

wa anayemwamini Mwenyezi

Mungu, na Siku ya Mwisho, na

Malaika, na Kitabu na

Manabii; na akawapa mali,

pamoja na kuipenda, ,jamaa

na mayatima na masikini na

mwananjia, na waombao, na

katika ukombozi wa

watumwa; na akasimamisha

swala na akatoa zaka; na

watekelezao ahadi zao

wanapoahidi, na wanaokuwa

na subira katika shida na

dhara na katika wakati wa

vita. Hao ndio waliosadikisha

na ndio wanaomcha

(Mwenyezi Mungu).

Page 80: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

70

ANATOA MALI PAMOJA NA KUIPENDA

Aya 177

LUGHA

Kila amali ya Kheri ni wema. Mwananjia ni msafiri asiyesafiri kwa maa-sia, akaishiwa na mali asiweze kurudi kwake. Madhara ni kila linalomd-huru mtu, iwe ni maradhi au kumkosa mpenzi, n.k.

MAANA

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameyataja mambo aliyoyazingatiakuwa ni nguzo ya wema, uchaji Mungu na imani ya kweli. Katika mambohayo, kuna yanayofungamana na itikadi, yanayofungamana na kutoa mali,yanayofungamana na ibada na yale yanayofungamana na akhlaq (tabianjema). Kabla ya kufafanua kila moja ya mambo hayo, ameanza kwa kuse-ma:

Sio wema kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi tu

Maneno haya waanaambiwa watu wote, ijapokuwa sababu ya kushuka nimahsusi, kwa sababu la kuzingatiwa ni uenezi wa neno, sio sababu zakushuka kwa Aya.

Makusudio ya Aya ni kuwaambia waumini na wanaoswali, kwambakuswali tu upande maalum, sio kheri ya dini iliyokusudiwa; kwa sababuswala imewekwa ili anayeswali amwelekee Mwenyezi Mungu peke Yakena kuachana na wengine.

Baada ya utangulizi huu, ameingilia kubainisha misingi ya itikadi ambayondiyo nguzo ya wema, na ameikusanya katika mambo matano ambayoyamekusanywa na kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Page 81: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

71

Lakini wema ni wa anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku yaMwisho na Malaika na Kitabu na Manabii

Kumwamini Mwenyezi Mungu ndio msingi wa amali njema inayo -sababisha kumtii Mwenyezi Mungu katika yote aliyoyaamrisha nakuyakataza. Kuamini Malaika ni kuamini wahyi ulioteremshwa kwaMitume; na kuwakana Malaika ni kuukana wahyi na Utumwa. MwenyeziMungu anasema:

“Ameiteremsha Roho mwaminifu juu ya moyo wako, ili uwe miongoni mwawaonyaji.” (26: 193-194).

Kuamini Kitabu ni kuamini Qur’ani; na kuamini Manabii ni kuamini shariazao.

Mambo yote haya matano yanarejea kwenye mambo matatu; KuaminiMwenyezi Mungu , Utume na Siku ya Mwisho. Kwa sababu kuaminiUtume kunachanganya kuamini Malaika na Kitabu.

Baada ya hayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaashiria taklifa za kimali kwakauli Yake:

Na akawapa mali akiwa aipenda

Imesemekana kuwa dhamiri katika kuipenda inamrudia Mwenyezi Mungu,kwa vile jina Lake limetangulia katika kauli Yake: “Mwenye kumwami-ni Mwenyezi Mungu” Na imesemekana kuwa dhamiri hiyo inarudia mali,na inakuwa kama kauli Yake Mwenyezi Mungu:

“Hamtapata wema mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda...”(3:92).

Page 82: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

72

Vile vile kauliYake:

“Pamoja na kukipenda.....” (76:8).

Kauli hii ndiyo iliyo dhahiri zaidi, kwa sababu dhamiri hurudia kilichokaribu zaidi, sio cha mbali. Kisha makusudio ya kutoa mali hapa sio zakaya wajibu, kwa sababu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameunganisha hilo nakutoa zaka, na kuunganisha kunamaanisha kutofautika vilivyoungwa.

Aya imetaja aina sita za wale ambao inatakikana wapewa mali: 1. Jamaa; nao niwatu wa karibu wa mwenye mali, kwa sababu wao ndio

wenye haki zaidi ya kutendewa wema. Mwenyezi Mungu anasema:

“Na wale, katika nyinyi, wenye fadhila na wasaa wasiape kutowapa akra-ba” (24:22).

Ni wajibu aliye karibu kumlisha akraba, ikiwa ni wazazi na watoto,kama wanashindwa kujilisha. Ama wasiokuwa hao, kuwapa ni sunna,sio wajibu, kama wanavyosema mafakihi.*

* Hanafi wanasema : Ni wajibu mtu kuwalisha jamaa zake wa karibu asioweza kuwaoa.Hambali wamesema: Ni sharti mlishaji awe ni mrithi wa anayelishwa.Maliki wanasema:Si wajibu kulisha isipokuwa baba, mama na watoto wa kuwazaa tu, sio ndugu wengine.Shia Imamiya na Shafii wanasema: Ni wajibu kuwalisha wazazi, mababu na kuendelea juu,na watoto, wajukuu na kuendelea chini.

Page 83: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

73

2. Mayatima; ambao hawana mali wala mlezi wa kuwatunza. Kwa hivyoitakuwa ni wajibu kwa wenye uweza kuwalea, ikiwa hakuna hazina yaWaislamu (Baitul-maal).

3. Maskini; wale wenye haja ambao hawawanyoshei watu mkono waudhalili (hawaombi).

4. Mwananjia; yule ambaye ameishiwa safarini asiyeweza kurudi kwaobila ya msaada.

5. Wenye kuomba; wale ambao wanawanyoshea watu mikono ya udhalili.Jambo hilo limeharamishwa kisharia, isipokuwa kwa dharura ya hali yajuu; sawa na dharura ya kula mfu, kwa rai yetu. Dalili tosha ya uhara-mu wake ni kwamba ni udhalili na utwevu. Na udhalili, huo wenyewe,ni haramu; uwe umetokana na mtu mwengine au na yeye mwenyewe.

Kuna Hadith inayosema: “Si halali kupewa sadaka tajiri, na mwenyenguvu aliye mzima wa mwili.” Makusudio hapa ni: mwenye uweza wakujichumia

6. Watumwa; yaani kununua watumwa na kuwaacha huru kwa kuwakom-boa na utumwa. Lakini maudhui haya hayapo siku hizi, kutokana nakutokuwepo utumwa.

Kwa ujumla aina sita hizi alizozitaja Mwenyezi Mungu ni kwa njia yamfano, sio kwamba hizo ndio zote. Yako mambo mengi ambayo ni vizurikuyatolea mali; kama kujenga shule, vituo vya mayatima, mahospitali,kuilinda dini na nchi, na mengineyo yanayohusu umma kwa ujumla.

Ikiwa heshima ya mtu itavunjika isipokuwa kwa kutoa mali, basi ni wajibukuitoa kwa mwenye kuweza, kwa sababu kuihifadhi nafsi hiyo ni wajibuna lolote ambalo wajibu fulani hauwezi kutekelezeka isipokuwa kwakufanya jambo hilo, basi ni wajibu kulifanya.

Mwenyezi Mungu ameashiria nguzo ya kutenda wema ya kiibada kwakauli Yake:

Page 84: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

74

Na akasimamisha Swala na akatoa Zaka.

Swala ni ya kutakasa nafsi, Saumu ni ya kutakasa mwili, na zaka ni yakutakasa mali.

Akaashiria kwenye nguzo ya maadili kwa kusema:

Na watekelezao ahadi zao wanapoahidi.

Ahadi inayopaswa kutekelezwa iko namna mbili. Ya kwanza ni ile inayokuwakati ya mja na Mola wake; mfano yamini nadhiri na ahadi, kwa sharti zilizo-tajwa katika vitabu vya Fiqhi. Hayo tumeyafafanua katika Juzuu ya Tano yakitabu Fiqhul-Imam Jafar Sadiq .

Ya pili, ni aina ya ahadi ya muamala unaopita kati ya watu, kama vilebei,ajira, deni n.k, ambayo ni wajibu kuitekeleza.

Muumini mwema anatekeleza mambo yote yanayomlazimu; hata kamahakuna uthibitisho wa kuumlazimisha kutekeleza. Ama kutekeleza kiagasio wajibu kisharia, bali ni sunna kwa mafakihi.

Miongoni mwa tabia nzuri zenye kusifiwa, katika nguzo za wema, ni subi-ra (uvumilivu) ambayo inaoneshwa na kauli Yake Mwenyezi Mungu:

Na wanaokuwa na subira katika shida na dhara na wakati wa vita

Shida ni ufukara, na dhara ni maradhi, n.k. Makusudio ya kuvumiliaufukara na maradhi sio kuyaridhia, kwani Uislamu umewajibishakuhangaika na kufanya juhudi kwa kadri iwezekanavyo ili kujitoa katikaukata, maradhi, ujinga, na kila linalorudisha nyuma maendeleo.

Makusudio yake hasa ni kutosalimu amri kabisa katika shida, na kuwa namshikamano na kufanya kazi kwa uthabiti na bidii ili kujikwamua na yaliy-owapata. Baadhi ya wafasiri wanasema: “Mwenyezi Mungu amehusishakutaja uvumilivu katika mambo matatu: (ufukara, maradhi na vita), pamo-ja na kuwa uvumilivu unatakiwa katika hali zote, kwa sababu hali hizo tatuni miongoni mwa balaa na mitihani mikubwa. Mwenye kuvumilia hayo,

Page 85: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

75

basi anaweza kuvumilia mengine.

Hao ndio waliosadikisha na ndio wanaomcha (Mwenyezi Mungu).

Hao ni ishara ya wale ambao wamekusanya mambo yote haya yaliyotajwa- misingi ya itikadi, kutoa mali, kutekeleza ibada kwa ajili ya MwenyeziMungu na tabia nzuri. Hakika hao ni wakweli katika imani yao, wenyekuogopa ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake.

Ama wale wanaosema kwa vinywa vyao tu, kuwa: ‘Tumeamini’ walahawatoi wanayoyapenda wala kutekeleza yanayowalazimu na kuvumiliakatika shida; wote hao wako mbali na wema.

WEMA KATIKA UFAHAMU WA KIQUR’ANI

Aya hii imeonesha mambo matano: misingi ya itikadi, taklifa za kimali,ibada, kutekeleza ahadi na kuvumilia shida. Haya mambo mawili yamwisho ni katika mambo ya kimaadili.

Kwa dhahiri ni kwamba ibada, kama swala na saumu ni athari ya imani nani alama yake isiyoepukika nayo; kwa sababu asiyeamini kuwako Mungu,hawezi kumwabudu.

Ama kutoa mali, kutekeleza ahadi na kuvumilia shida, hayo yanapatikanakwa anayemwamini Mwenyezi Mungu na anayemkanusha. Kwani wengiwa wanaomwamini Mungu wanasema wasiyoyatenda, ni wabahili; hatakwenye nafsi zao, na wanasalimu amri mbele ya shida. Lakini maranyingine mkanushaji Mungu huweza kujitolea mhanga katika kupiganiauadilifu na utu, anakuwa imara katika shida na kutekeleza anayoyasema.

Kwa hivyo, kidhahiri, inaonyesha kuwa imani hailazimiani na tabia njema,wala kufuru hailazimiani na tabia mbaya. . . lakini ilivyo hasa ni kuwahakuna imani bila ucha Mungu.

Lakini Aya hii (Sio wema ...). Imezingatia imani kuwa pamoja na tabia njemabila ya kutengana, kwa maana yakuwa sio kumwamini Mungu pekee ndiko

Page 86: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

76

kutakakomfanya mtu kuwa mwema; wala tabia nzuri bila ya imani haiwezikumfanya mtu awe mwema, bali hapana budi kumwamini Mwenyezi Mungu,kuwa na tabia njema na kumwabudu. . . Kwa hivyo basi ‘mwema’ anavy-oelezwa katika Qur’ani ni muumini mwenye kufanya ibada, mtekelezajiahadi, karimu na mvumilivu.

178. Enyimlioamini! Mmeandiki-wa kisasi kwa wenye kuuliwa;muungwana kwa muung-wana, na mtumwa kwamtumwa, na mwanamke kwamwanamke. Na anayesame-hewa na ndugu yake cho-chote, basi ni kufuatana kwawema na kulipa kwa ihsani.Hiyo ni tahafifu itokayo kwaMola wenu na rehema. Naatakeyeruka mipaka baada yahayo, basi ana adhabu iumiza-yo.

179. Mna uhai katika kisasi, enyiwenye akili, ili msalimike.

Page 87: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

77

KISASI CHA WALIOUAWA

Aya 178 - 179

MAANA

Wanavyuoni wa sharia ya Kiislamu wamepanga namna tatu za adhabu:

1. Haddi; kama kukata mkono wa mwizi, kupigwa mawe hadi kufa kwamzinifu aliye na mume au mke, kupigwa viboko kwa mnywaji pombe,n.k. Utakuja ufafanuzi mahali pake inshallah.

2. Diya (Fidia); Hiyo ni adhabu ya kimali.

3. Kisasi; kufanyiwa yule aliyefanya jinai kwa makusudi sawa na vilealivyomfanyia yule aliyemuua, au aliyemkata kiungo au aliyemjeruhi.Ama kupiga, hakuna kisasi. Mafakihi wameweka maelezo maalum kwakila namna ya adhabu hizo tatu, na Aya hii inaingia katika kisasi.

Enyi mlioamini! mmeandikiwa kisasi kwa wenye kuuliwa.

Wakati wa ujahiliya (kabla ya Uislamu) watu walikuwa hawana sheriayenye mpango; walikuwa wakiuana kidhuluma na kiuadui, na kulipizanakisasi kwa watu wasiokuwa na hatia, wala sio kwa yule aliyekosa. Mtu wakawaida akiuawa, basi watu wake wataua idadi kubwa ya watu wa muua-ji. Na, kama mwanamke akimuua mwanamke mwenzake, basi mahalipake patachukuliwa na mwanamume wa ukoo wake au kabila yake;wanaweza kuua hata watu kumi kwa mmoja tu.

Dhuluma hii ilisababisha vita vya kikabila; watoto na wajukuu wakarithiuadui na chuki. Ndipo Mwenyezi Mungu akaweka sharia hii ya kisasi,ambayo inafahamisha usawa, na kisasi kiwe kwa yule aliyefanya jinai kwahali yoyote awayo na wala sio watu wasiokuwa na makosa, na pia kusi-weko na ziada au upungufu, kinyume na ilivyokuwa kwa watu waujahiliya., Na kwa sharti ya kuwa kuua kwenyewe kuwe ni kwa kukusu-

Page 88: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

78

dia sio kwa kukosea au bila kukusudia.* 2

Katika maana ya Aya hii ni kauli Yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.):

“...Nafsi kwa nafsi...” (5:45).

“...Lakini asipite kiasi katika kuua...”(17:33).

“Na malipo ya ubaya ni ubaya ...” (42:40).

“...Basi anayewataadia mtaadieni kwa kadri alivyowataadia nyinyi...”(2:194).

Muungwana kwa muungwana, na mtumwa kwa mtumwa, namwanamke kwa mwanamke

Maana yake yako wazi, hayahitaji ufafanuzi. Hiyo ni ibara ya kuletausawa katika kisasi kati ya muuaji na muuliwa katika uhuru, utumwa nauke.*2 Kuua kwa makusudi ni kukusudia kitendo na kuua; kama mtu kumchoma kisumwengine kwa kukusudia kumchoma na kumuua, au kakusudia kitendo cha kuua tu, kamakukusudia kumchoma katika moyo wake lakini bila ya kukusida kuua. Hayo ni mauaji yakukusudia. Ama kuua kwa makosa, ni kukosea katika kusudio lake na kitendo chake; kamamwenye kukusudia kumfuma mnyama akampata mtu. Hapo mtu huyo siye aliyekusudiwakufumwa wala kuuliwa. Kuua bila ya kukusudia ni kukusudia kitendo, lakini sio kuua;kama anayempiga mtoto kumtia adabu, akafa. Hapo tendo la kupiga limekusudiwa, lakinimauti hayakukusudiwa. Katika hali hizi mbili (Kuua kwa makosa na kuu bila ya kukusu-dia) hakuna kisasi isipokuwa fidia tu.

Page 89: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

79

Pengine utauliza: Linaloeleweka kwa utungo wa maneno ya Aya hii nikuwa muungwana hauawi kwa kumuua mtumwa, na kuwa mwanamumehauawi kwa hilo; na mwanamume akiwa mwanamke, nae pia hauawi kwahilo. Je haya ni mambo yaliyoafikiwa na mafakihi?

Jibu: Aya hii imeelezea hali tatu tu; nazo ni: muungwana kumuua muung-wana , na mtumwa kumuua mtumwa, na mwanamke kumuua mwanamke.Haikuelezea hali zilizobaki; nazo ni nne: ya muungwana,kumuuaMtumwa, na mtumwa kumuua muungwana, na mwanamume kumuuamwanamke, na mwanamke kumuua mwanamume.

Aya hii imeonesha, kwa maneno yake, kwamba kisasi kimewekewa shariakatika hali tatu za kwanza. Na hilo limeafikiwa na mafakihi wote, kwasababu hakuna anayepinga kuwa Qur’ani imesema hivyo wazi wazi.Lakini Aya hii, vile vile, haikatai wala haithibitishi kisasi katika hizo halinne nyengine - si kwa kutamka wala kwa kufahamika. Ka ajili hii itabidikurejelea dalili nyengine: za sunna au ijmai (kongamano)

Mafakihi wamehitilafiana katika hili. Malik, Shafi na Ibn Hambal wame-sema kwamba muungwana hauawi kwa kumuua mtumwa.Lakini AbuHanifa amesema:Muungwana atauawa kwa kumuua mtumwa asiyekuwawake, lakini hauawi kwa kumuua mtumwa wake mwenyewe. Kisha wotemaimamu wanne hao wameafikiana kuwa mwanamume atauawa kwakumuua mwanamke, na kimyume chake pia.

Shia Imamiya, kwa upande wao, wanasema: Muungwana akiua mtumwa,hauawi isipokuwa atapigwa kipigo kikali na kutozwa diya ya mtumwa. Namwanamke akimuua mwanamume kwa makusudi, walii wa huyo mwana-mume aliyeuawa atakuwa na hiyari baina ya kuchukua diya (fidia) kwamwanamke huyo, kama mwanamke huyo ataridhia, na baina ya kumuua.Akiamua kumuua, watu wa mwanamke huyo hawatalipishwa kitu.Mwanamume naye akimuua mwanamke , walii wa huyo mwanamkeatakuwa na hiyari baina ya kuchukua diya, kama muuaji ataridhia, na bainaya kumuua na kuwalipa warithi wa muuaji nusu ya diya ya mwanamume,dinari 500.

Page 90: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya pili 2. Sura Al-Baqarah

80

Na anayesamehewa na ndugu yake chochote, basi ni kufuatana kwawema na kulipa kwa ihsani.

Neno “chochote” linafahamisha kwamba walii wa aliyeuawa, akisamehechochote kinachofungamana na muuaji, kama kusamehe kumuua na kuridhiakuchukua fidia, basi inatakikana muuaji aukubali msamaha huu kwa wema.Imesemekana pia kuwa neno chochote linafahamisha kuwa, kama warithiwakiwa wengi, na mmoja wao akamsamehe muuaji, basi hakuna kisasi, hatakama waliobakia watang’ang’ania kutaka kisasi.

Vyovyote iwavyo, hakika Mwenyezi Mungu amemwekea kwa walii wa damuiliyomwagwa haki ya kisasi kutoka kwa aliyeua kwa makusudi. Wala hanahaki ya kumlazimisha muuaji atoe fidia ikiwa mwenyewe muuaji anatakakuuliwa, kama ambavyo muuaji naye hawezi kumlazimisha walii waaliyeuawa kuchukua fidia ikiwa mwenyewe anataka kulipiza kisasi cha kuua.

Lakini wote wawili wanaruhusiwa kuafikiana na kufanyiana suluhu kwa kiasicha mali ya fidia, kiwe kichache au kingi, ili kiwe ni badala ya kisasi.Maafikiano hayo yakitimia, basi itakuwa ni lazima kutekelezwa na wala hai-wezekani kubadilisha.

Ni juu ya walii wa aliyeuawa kumtaka muuaji badala ya kisasi kwa wema, bilaya kumtilia mkazo wala kumdhikisha au kuomba zaidi ya haki yake. Na ni juuya muuaji kutoa mali kwa wema, bila ya kuchelewesha, kupunguza aukufanya hadaa yoyote.

Hiyo ni tahafifu itakayo kwa Mola wenu na rehema

Yaani hekima ya kuwekwa fidia badala ya kisasi ni tahfifu na rehemakwenu.

Na atakayeruka mipaka baada ya hayo, basi ana adhabu iumizayo

Walikuwa baadhi ya watu wakati wa ujahiliya, wanaposamehe nakuchukua fidia, kisha wakampata muuaji baadaye, wakimuua Hapo

Page 91: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

81

Mwenyezi Mungu akakataza kupetuka mipaka huku, na akamwahidiadhabu iumizayo mwenye kuyafanya hayo.

Baadhi ya wafasiri wanasema: namlazimu hakimu ahukumu kuuliwa yulealiyemuua muuaji baada ya msamaha; hata kama atatoa fidia na kuridhiawalii wa aliyeuliwa. Lakini kauli hii ni ya kuonelea uzuri hivyo tu, lakiniAya haifahamishi hilo, kwa karibu wala kwa mbali.

Mna uhai katika kisasi enyi wenye akili

Hii ni sababu ya kuwekwa sharia ya kisasi na kubainisha hekima yale, nakwamba katika hukumu hiyo mna kuwalinda watu wasifanyiane uadui.Kwani mwenye kujua kwamba yeye atauliwa baada ya kuua, ataogopa.Ama kutoa mali sio kuzuia kuua, kwani watu wengi wangeliweza kutoamali kwa sababu ya kuwakomoa maadui zao.

Wafasiri wamerefusha maneno katika kubainisha ufasaha wa Aya hii nakuilinganisha na msemo unaosema; “Kuua ni kinga ya kuua.” Baadhi yaowametaja njia sita za ubora wa Aya hii. Alusi, katika Tafsiri yake, ame-ongeza mpaka kufikia kumi na tatu; na waliokuja baada ya Alusi naowakaongeza zao. Njia zote hizo zinarudia kwenye utafiti wa matamshi tu.

Page 92: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

82

180. Mmeandikiwa mmoja wenuanapofikwa na mauti, kamaakiacha mali, kuwausia kituwazazi wawili na akraba kwanamna nzuri (inayokubalika).Ni haki haya kwa wenye kum-cha Mungu.

181. Na atakayeubadilisha (wasiahuo) baada ya kuusikia, basidhambi yake ni juu ya walewatakaoubadilisha. HakikaMwenyezi Mungu ni Mwenyekusikia, Mjuzi.

182. Mwenye kuhofia mwusiajikwenda kombo au (kufanya)dhambi, akasuluhisha bainayao, basi hatakuwa na dhambi.Hakika Mwenyezi Mungu niMwenye maghufira, Mwenyekurehemu.

WASIA KWA WAZAZI

Aya 180-182

LUGHA

Neno Khayri lina maana ya kinyume cha shari, na makusudio yake hapa ni‘mali’. Inasemekana kuwa kila linapokuja neno khayr katika Qur’anilinakuwa makusudio yake ni mali; kama ilivyo katika Sura (11:84) (24:33),

Page 93: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

83

(100:8), , n.k.* 3

MAANA

Mmeandikiwa mmoja wenu anapofikwa na mauti, kama akiacha mali,kuwausia wazazi wawili na akraba kwa namna nzuri. Ni haki hayakwa wenye kumcha Mungu. Inayokubalika.

Aya hii ni miongoni mwa Aya za hukumu, na inaingia katika mlango wawasia. Kauli za mafakihi na wafasiri zimekuwa nyingi na kugonganakuhusu Aya hii Miongoni mwa kauli hizo ni kama zifuatazo:-

• Ikiwa mtu ana mali na akaona dalili za mauti, basi ni wajibu kwake kuu-sia kitu katika mali yake kwa wazazi wawili na ndugu wa karibu, hatakama wao ndio watakaoirithi; atawakusanyia urithi na wasia.

• Wasia ni wajibu kwa jamaa zake wakiwa sio warithi.• Wasia kwa akraba ni sunna tu, si wajibu.

• Kuwausia warithi haki yao na viwango vyao vya kurithi. Kwa hivyo Ayaitakuwa inapita mapito ya Aya inayosema:

“Mwenyezi Mungu anawausia juu ya watoto wenu; fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili.” (4:11).• Wasia utakuwa ni wajibu kwa jamaa ikiwa mali ni nyingi.• Aya ni mansukh (haitumiki hukumu yake) kwa Aya ya urithi; na

mengineyo zaidi ambayo hayana msingi.

KUWAUSIA WARITHISunni na Shia wametofautiana katika kuswihi wasia kwa warithi.* 3 Kauli hii nimeikuta katika baadhi ya vitabu vya tafsiri nilivyonavyo, lakini inaping-wa na Aya inayosema:“Aya yoyote tunayoifuta au kuisahauliza tunaleta iliyo bora kulikohiyo au iliyo mfano wake ...”(2 : 106) ambapo hapa kuna neno khayr lililotumiwa kwamaana ya Aya iliyo bora, sio mali.

Page 94: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

84

Madhebu manne yameafikiana kuwa hauswihi, wakitegemea Hadith ise-mayo: “Hakuna wasiya kwa warithi”.

Shia Imamiya wameafikiana juu ya kuswihi wasia kwa warithi na wengi-neo, kwa kutothibiti Hadith hiyo kwao, na kwamba dalili ya kuswihi wasiainachanganywa kwa ujumla na wasia kwa warithi; mbali riwaya mahsusikutoka kwa ahlul bait (a.s.). Dalili yenye nguvu kuliko zote, ya kuswihiwasia kwa warithi, ni Aya hii tuliyo nayo. Allama Hilli katika kitabu AtTadhkira anasema:

“Wasia kwa warithi unafaa kwa kauli za wanavyuoni wetu wote, ni sawawarithi wamekubali au la. Hilo ni kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu( s.w.t.) kwenye Aya hizi tulizo nazo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu ame-wajibisha kuwausia wazazi wawili, ambao wao ndio akraba (jamaa wakaribu) mno wa maiti, kisha akasema kutilia mkazo wajibu huo: Ni hakihaya kwa wenye kumcha Mungu. Yaani anamwambia yule ambayehayaitakidi haya kuwa si katika wamchao Mungu. Tena akatilia mkazokwa mara ya pili kwa kauli yake: Na atakayeubadilisha (wasia huo)baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha.Mwisho akaitilia mkazo jumla hii kwa kusema: Hakika Mwenyezi Munguni Mwenye kusikia, Mjuzi.

Unaweza kuuliza: Shia wamesema inajuzu kuusia, na wala hawakusema nilazima, pamoja na kuwa Aya imeweka wazi kuwa ni wajibu, maana nenokutiba (imeandikwa) lina maana ya kufaridhiwa (kuwajibishiwa). Kwahivyo basi, Shia wameihalifu dhahiri ya Aya kama walivyoihalifu Sunni,kwa kusema kuwa hauswihi wasia kwa warithi?

Jibu: Wameafikiana Waislamu wote kwamba kutoa hukumu ya sharia kati-ka Qur’ani, hakufai ila baada ya kuangalia Hadith za Mtume, na baada yakufanya utafiti wa ijmai vile vile. Kama hakuna Hadith wala ijmai katikamaudhui ya Aya, basi inajuzu kutegemea dhahiri ya Aya.

Imethibiti katika Hadith na ijmai kwamba wasia kwa akraba sio wajibu,Kwa hivyo hapana budi kuichukulia Aya kuwa ni sunna katika wasia nawala sio wajibu, na yanakuwa maana ya: Ni haki kwa wenye kumchaMungu, ni kwamba: Sunna hii ni imethibiti kwa haki, kwa sababu maana

Page 95: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

85

ya neno haki ( kwa Kiarabu)ni ‘kuthibiti’.

Makusudio ya (Namna nzuri inayokubalika) ni kuwa kitu chenye kuusiwakinanasibiana na hali ya mwenye kuusia na mwenye kuusiwa; kisiwekichache cha kudharaulika, wala kisiwe zaidi kikawadhuru warithi. Yaaanikisizidi thuluthi ya mali itakayoachwa na marehemu. Kuna Hadithinayosema: “Hakika Mwenyezi Mungu amewapa thuluthi ya mali yenuwakati wa kufa kwenu.”

Na atakayeubadilisha (wasia huo) baada ya kuusikia

Yaani atakayebadilisha wasia huo na kuugeuza na hali anajua.

Basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoubadilisha

Yaani dhambi ya kubadilisha itamwangukia yule mwenye kubadilisha,awe ni mrithi, walii, hakimu, wasii au shahidi. Hii ni dalili kwambamwenye kufanya dhambi huwa ni juu yake mwenyewe peke yake. Ikiwamarehemu alimuusia mtu ambaye alimwamini kuwa atamtekelezea haki yaMwenyezi Mungu au ya watu aliyonayo, halafu aliyeusiwa akafanyauzembe au hiyana, basi maiti hana dhambi yoyote isipokuwa dhambi ikojuu ya yule aliyeusiwa.

Razi anasema: “Wanavyuoni wameitolea dalili Aya hii, kwamba mtotomdogo hawezi kuadhibiwa kwa ukafiri wa baba yake. Na haya ni katikamambo yaliyo wazi kiakili ambayo Qur’ani imeyathibitisha kwa mifumombali mbali; kama Aya inayosema:

“Wala hatabeba mbebaji mzigo wa mtu mwingine.” (35:18).

Mwenye kuhofia muusiaji kwenda kombo au (kufanya) dhambi, aka-suluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi.

Kufanya dhambi hapa kuna maana ya ‘kukusudia dhuluma’. Aya hiiinaivua hukumu ya Aya iliyotangulia; yaani mwenye kubadilisha wasiaatakuwa na dhambi, isipokuwa kama muusiaji amekosea katika wasiawake. Hapo itajuzu kwa wasii au walii au hakimu kubadilisha wasia kuto-

Page 96: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

86

ka kwenye batili na kuuweka kwenye haki. Lililoharamishwa ni kubadil-isha haki kuiweka kwenye batili, si kuibadilisha batili kuiweka kwenyehaki.

Hayo ndiyo waliyoyataja wafasiri kuhusu maana ya Aya; nayo ni sahihihayo yenyewe. Lakini yale tunayoyafahamu kutokana na mfumo mzimawa Aya, na kuthibitishwa na mwenye Majmaul-Bayan, ni kwamba mtuakitokewa na dalili za mauti, na akausia mambo ambayo ndani yake mnadhuluma - kama kuwapa wengine na kuwanyima wengine - na katika wasiahuo wakahudhuria watu wenye akili na waumini, basi itakuwa hakunadhambi kwa yule aliyehudhuria kumwonesha haki muusiaji, na kusu-luhisha kati yake na warithi wake, ili wote waafikiane na kuridhiana, walausizuke baina yao ugomvi na migongano baada ya kufa muusiaji.

183. Enyi mlioamini!Mmeandikiwa kufungakama walivyoandikiwawaliokuwa kabla yenu, ilimpate kumcha Mungu.

184. Siku maalum za kuhisabika.Na atakayekuwa mgonjwakatika nyinyi, au yuko safarini,basi atimize idadi katika sikunyingine. Na wale wanaoiwezakwa shida, watoe fidia kwakumlisha maskini. Naatakayefanya kheri kwa kuji-tolea, basi ni bora kwake. Nakufunga ni bora kwenu, ikiwamnajua.

Page 97: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

87

185. Ni mwezi wa Ramadhaniambao imeteremshwa katika(mwezi) huo Qur’ani, kuwamwongozo kwa watu naupambanuzi. Basiatakayekuwa mjini katikamwezi huu naaufunge; namwenye kuwa mgonjwa ausafarini, basi atimize hisabukatika siku nyingine.Mwenyezi Mungu anawatakiawepesi wala hawatakii uzito,na mkamilishe hisabu hiyo, namumtukuze Mwenyezi Mungukwa kuwa amewaongoza, na ilimpate kushukuru.

MMELAZIMISHWA KUFUNGA

Aya 183 -185

MAANA

Enyi mlioamini! Mmeandikiwa kufunga kama walivyoandikiwawaliokuwa kabla yenu.

Saumu ni miongoni mwa ibada muhimu, na ni katika dharura za dini, kamailivyo wajibu swala na zaka. Katika Hadith imesemwa: “Uislamu ume-jengwa juu ya mambo matano: kushuhudia kuwa hapana molaanayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwam-

Page 98: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

88

ba Muhammad ni Mtume Wake (shahada), kusimamisha swala, kutoa zaka,kufunga mwezi wa Ramadhani na kuhiji Makka kwa anayeweza.

Mafakihi na wametoa fatwa kwamba yeyote anayekana wajibu wa saumu,basi ni murtadi (si Mwislamu tena), na ni wajibu kumuua. Na mwenyekuamini kuwa saumu ni wajibu, lakini akaiacha kwa kupuuza, ataaziriwakutokana na vile anavyoona hakimu wa sharia. Kama akirudia ataaziriwamara ya pili. Akirudia tena atauawa. Wengine wamesema atauawa mara yanne.

Saumu ni ibada ya zamani aliyoifaradhisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwawatu waliotangulia, kwa namna inayotofautiana na yetu sisi Waislamu,kwa kiasi chake namna yake na wakati wake. Kufananishwa hapa kumeku-ja kwa uwajibu tu, bila ya kuangalia sifa, idadi ya siku na wakati wake. Nakufananisha kitu sio lazima kiwe sawa kwa njia zote.

Ili mpate kumcha Mungu.

Wafasiri wengi wamesema kuwa jumla hii inaonesha hekima ya saumuambayo ni mazoezi ya mwenye kufunga kuweza kudhibiti nafsi, kuachamatamanio ya haramu na kuwa na subira (uvumilivu). Hadith inasema:“Saumu ni nusu ya subira.” Imam Amirul Muminin (a.s.) anasema: “Kilakitu kina zaka (utakaso), na zaka ya mwili ni kufunga.” Amesema tena:“Mwenyezi Mungu amefaradhisha saumu kwa majaribio ya ikhlasi yaviumbe...”

Kimsingi ni kwamba kila maamrisho ya Mwenyezi Mungu na makatazoYake ni majaribio ya ikhlasi ya viumbe, lakini saumu ina taklifa kubwazaidi, kwa sababu ina kushindana na kupambana na nafsi, kuweza kuid-hibiti na mambo inayoyapendelea ambayo ni chakula, kinywaji na mata-manio ya kimwili.

Siku (maalum) za kuhisabika

Hizo ni siku za Ramadhani, kwa sababu Mwenyezi Mungui hakutufarad-hishia zaidi ya Ramadhani.

Page 99: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

89

Na mwenye kuwa mgonjwa, au safarini, basi atimize hisabu katikasiku nyingine. Na wale wanaoiweza kwa shida, watoe fidia kwa kum-lisha maskini

Mwenyezi Mungu ametaja katika Aya hii mambo matatu ya kuruhusiwakufungua Ramadhani ambayo ni: maradhi, safari na uzee.

Maradhi anayoruhusiwa mtu kufungua ni kuwa ni mgonjwa ambaye,kama atafunga, maradhi yake yatazidi, au zitazidi siku zake za ugonjwa.Au pengine ni mzima, lakini anaogopa kuwa, kama atafunga, atazukiwana maradhi mapya. Ama udhaifu tu, hauwezi kumruhusu mtu kufungua,maadamu anaweza kustahmili na mwili wake uko salama. Ikiwa mgonjwaatang’ang’ania kufunga, pamoja na kuthibitika madhara, basi saumu yakeitakuwa batili na ni wajibu kwake kulipa, sawa na aliyefungua bila udhu-ru.

Imethibiti, kwa upande wa Sunni na Shia, kwamba Mtume (s.a.w.w) ame-sema ; “Si wema kufunga safarini.” Katika Tafsir Al-Manar imekujaHadith mashuhuri iliyopokewa kwa Mtume mtukufu: “Mwenye kufungasafarini ni kama mwenye kufungua akiwa nyumbani.” Na katika waliotajaHadith hii ni Ibn Maja na Tabari.

Razi naye amesema: “Wanavyuoni wa kisahaba wamesema kuwa niwajibu mgonjwa na msafiri waungue, kisha wafunge siku nyingine (idadiya siku walizofungua). Na hiyo ndiyo kauli ya Ibn Abbas na Ibn Umar.Vile vile Daud bin Ali Al-Asfahani.

Kutokana na hali hiyo, kufungua safarini ni wajibu na wala sio ruhusa tu.Yaani haifai msafiri kufunga kwa hali yoyote ile kutokana na kutokuwepoamri ya kufunga. Na dalilli yenye nguvu kuliko zote, juu ya hilo, ni kwam-ba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewajibisha kulipa kwa safari kwa namnaile ile aliyowajibisha kwa maradhi, pale aliposema: Na mwenye kuwamgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyingine; na walahakusema ‘...au safarini, akafungua, basi atimieze hisabu...’. Na kukadirianeno akafungua ni kinyume na dhahiri; wala hakuna haja ya kukadiria

Page 100: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

90

maneno mengine ikiwa maana yanasimama bila ya kukadiria.

Ama ruhusa ya tatu ya kufungua, ni uzee. Mwenyezi Mungu ameoneshahilo kwa kauli Yake: Na wale wanaoiweza kwa shida, watoe fidia kwakumlisha maskini.

Hukumu hii inamhusu mzee aliye dhaifu kwa sababu ya ukongwe, awemume au mke. Kuweza kwa shida ni kufanya kitu kwa shida na mashakasana. Huyu ndiye anayehiyarishwa kati ya kufunga na kufungua pamojana kutoa fidia ambayo ni kuwalisha maskini. Kuna Hadith sahihi kuhusuhilo kutoka kwa Ahlul Bait (a.s.)

Na atakayefanya kheri kwa kujitolea, basi ni bora kwake

Yaani mwenye kuzidisha kulisha zaidi ya maskini mmoja, au kumlishamaskini mmoja zaidi ya kiasi cha wajibu, basi ni bora kwake. Anayo hiyariya kumwita maskini muhitaji amlishe mpaka ashibe, au ampe chakula chaunga au nafaka anachokula, kiasi kisichopungua gramu mia nane (800gm).Na inaruhusiwa kumpa pesa zenye thamani ya chakula kwa sharti yakumwambia: “Ifanye ni thamani ya chakula chako.”

Na kufunga ni bora kwenu

Yaani mzee, mume na mke, walio wakongwe, ingawaje wanahiyarishwakati ya kufungua na kufunga lakini wakihiyari kufunga: ni bora mbele yaMwenyezi Mungu kuliko kufungua na kutoa fidia.

Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huoQur’ani.

Mwenye Majmaul-Bayan anasema: Mwenyezi Mungu alipohusisha kufun-ga katika mwezi wa Ramadhani, amebainisha kwamba hekima katika hilini kuwa Qur’ani, ambayo juu yake ndio kuna mzunguuko wa dini naimani, iliteremshwa katika mwezi huo.

Page 101: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

91

Kisha akanakili mwenye Majmaul-Bayan kutoka kwa Mtume (s.a.w.w), kwanjia ya Sunni na Shia, kwamba: Sahifa za Ibrahim (a.s.) ziliteremshwa sikuya tatu ya mwezi wa Ramadhani, Tawrati ya Musa (a.s.) siku ya sita, Injili yaIsa (a.s.) siku ya kumi na tatu , Zaburi ya Daud (a.s.) siku ya kumi na nane,na Qur’ani ilimshukia Muhammad (s.a.w.w) siku ya ishirini na nne.

Unaweza kuuliza: Hakika kauli Yake Mwenyezi Mungu. “Ni mwezi waRamadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo Qur’ani” kwa dhahiriinafahamisha kuwa Qur’ani imeteremshwa yote katika mwezi wa Ramadhanina inavyojulikana ni kuwa Qur’ani iliteremshwa kwa vipindi katika mudawote wa Mtume ambao ni miaka ishirini na tatu. Ni vipi?

Jibu: Makusudio ni kwamba kushuka kwake kulianza katika mwezi waRamadhani, sio kwamba imeteremshwa yote katika mwezi huo. Na usikuambao ilishuka Qur’ani unaitwa Laylatul-Qadr, yaani, usiku wa cheo.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:

“Hakika sisi tumeiteremsha (Qur’ani) katika usiku uliobarikiwa ...”(44:3).

Zaidi ya hayo ni kwamba msahafu unaitwa Qur’ani, na sehemu yake piainaitwa Qur’ani.

Ama kauli ya anayesema kwamba Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur’anikutoka Lawhi Mahfudh, iliyoko juu mbingu saba, na kuileta katika mbin-gu ya dunia kwa mkupuo mmoja katika usiku wa Laylatul Qadr, kishaakaiteremsha kwa Muhammad (s.a.w.w) kwa vipindi, kauli hii haina daliliyoyote.

Kuwa mwongozo kwa watu na upambanuzi

Upambanuzi ni kinachopambanua kati ya haki na batili baina na baina yakheri na shari. Tumekwishaeleza maana ya uongozi katika kufasiri Aya ya

Page 102: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

92

pili, na kwamba Qur’ani si kitabu cha Falsafa, Historia au elimu za maum-bile, isipokuwa ni ufumbuzi, uongozi na rehema. Na kauli Yake MwenyeziMungu kuwa ni mwongozo kwa watu inafahamisha kuwa mawaidha, heki-ma na viaga na yote ambayo yamo katika Qur’ani,watu wote wanayafa-hamu, wala hahusiki na mujtahid au watu mahsusi.

Basi atakayekuwa mjini katika mwezi huu naaufunge

Yaani mtu ambaye yuko mjini kwao, hayuko safarini katika mwezi huu, niwajibu kwake kuufunga, wala haifai kwake kufungua bila ya udhuruwowote. Linalofahamisha kuwa makusudio ya neno shahida ni kuwamjini, ni kauli Yake Mwenyezi Mungu inayofuatia isemayo:

Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katikasiku nyingine.

Amerudia kutaja ugonjwa na safari kwa kutilia mkazo kwamba katikamwezi wa Ramadhani kunajuzu kufungua katika hali maalum, ili kuwajibuwale wanaoshikilia kwamba kufungua hakujuzu kwa hali yoyote.

Mwenyezi Mungu anawatakia wepesi wala hawatakii uzito.

Kwa dhahiri ya mfumo wa maneno ulivyo, ni kwamba jumla hii ni sababuya kujuzu kufungua katika hali ya ugonjwa, safari na uzee. Lakini kwauhakika, ni sababu ya hukumu zote. Imekuja Hadith isemayo:“Wafanyieni wepesi (watu), wala msiwafanyie uzito; na wapeni habari zafuraha, wala msiwafukuze.”

Anayesema kuwa kufungua Safarini ni amri, sio ruhusa atakuwa amefasirikauli Yake Mwenyezi Mungu: Anawatakia wepesi, kwamba MwenyeziMungu anawataka mfungue katika safari, hataki mfunge. Na anayesemakuwa kufungua ni ruhusa, sio amri atakuwa amefasiri kwamba MwenyeziMungu (s.w.t.) anataka muwe na wasaa katika mambo yenu na kuchagualile ambalo ni jepesi kwenu. Ikiwa kufungua ndio wepesi kwenu, sawa; naikiwa kufunga ndio kwepesi, sawa. Ikiwa yule ambaye inakuwa wepesi

Page 103: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

93

kwake kufunga katika mwezi wa Ramadhani na kuona uzito kulipa, basikufunga ni bora. Hakuna anayetia shaka kwamba kuzingatia dhahiri yatamko la Aya kunatilia nguvu zaidi maana haya kuliko ya kwanza. Laukwamba si Hadith sahihi kutoka kwa Ahlul Bait kutokana na babu yao(s.a.w.w.), tungelisema kwamba kufungua katika safari ni ruhusa, sio amri.

Na mkamilishe hisabu hiyo

Hii ni sababu ya kulipa alikowajibisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kauliYake: Basi atimize hisabu katika siku nyingine. Yaani ni juu yenu kulipasaumu kwa idadi ya siku mlizofungua katika mwezi wa Ramadhani, kwasababu ya maradhi na safari, ili itimie idadi ya siku za mwezi kamili ambazomara huwa thelathini na mara huwa ishirini na tisa.

Na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amewaongoza na ilimpate kushukuru.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametubainishia hukumu za dini Yake, ilitumtukuze na tumshukuru. Mwenye Majmaul-Bayan anasema:“Makusudio ya kumtukuza Mwenyezi Mungu, ni takbira za Idd baada yaswala ya magharibi ya usiku wa Idd, Isha na Asubuhi, na vile vile baada yaswala ya Idd kwa mujibu wa madhehebu yetu; yaani takbira inayokaririwabaada ya swala ya Idd ambayo husomwa hivi:

“Allahu Akbar, Allahu Akbar, Lailaha illa llaahu Wallahu Akbar, AllahuAkbar wa lillaahilhamd; Allahu Akbar alaama hadaana.”

Maana yake ni: Mwenyezi Mungu ni Mkubwa zaidi, Mwenyezi Mungu niMkubwa zaidi, hapana mwengine isipokuwa Mwenyezi Mungu, naMwenyezi Mungu ni Mkubwa, zaidi na sifa njema zote ni za MwenyeziMungu; Mwenyezi Mungu ni Mkubwa zaidi kwa aliyotuongoza.

Page 104: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

94

186. Na waja Wangu watakapoku-

uliza habari Yangu, Mimi niko

karibu. Naitikia maombi ya

mwombaji anaponiomba.

Basi nawaniitikie Mimi na

waniamini Mimi ili wapate

kuongoka.

NAITIKIA MAOMBI YA MWOMBAJI

Aya ya 186:

MAANA

Na waja wangu watakapokuuliza habari yangu, mimi niko karibu.naitikia maombi ya mwombaji anaponiomba.

Inasemekana kuwa bedui mmoja alimwendea Mtume na kumuuliza:“Mola wetu yuko karibu ili tumnog’oneze? Au yuko mbali tumpigiekelele?” Ndipo ikateremshwa Aya hii kuwa ni jawabu ya bedui huyo.

Kama ni sawa kauli hii, au sio sawa, inanasibiana na maudhui.

Dua ni katika ibada bora na imehimizwa sana katika Qur’ani na Hadithkwa sababu ni dhihirisho la utumwa wa mtu kwa Mwenyezi Mungu nakumhitajia kwake Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Hayo tumeyazungumzia kwaurefu katika kitabu Bainallah Wal Insan.

Unaweza kuuliza: Kauli Yake Mwenyezi Mungu: anaponiomba baada yakauli yake: naitikia maombi ya mwombaji ni jaribio la kupata ambachotayari kipo, kwa sababu inafanana na kauli ya mwenye kusema:“Mwangalie mkaaji akiwa amekaa, na msikilize msemaji akiwa anasema?”

Jibu: Makusudio ya anaponiomba, ni dua inayotoka katika moyo wa

Page 105: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

95

mwenye ikhlasi na mkweli katika maombi yake, sio dua ya ulimi tu. Hiyoinafanana zaidi na kauli ya mwenye kusema: “Mtukuze mwanachuoniakiwa ni mwanachuoni”, akimaanisha mwanachuoni wa kikweli kweli, siomwenye jina tu la wanachuoni.

Swali la pili ambalo ni maarufu na mashuri ni: Dhahiri ya kauli yakeMwenyezi Mungu Mtukufu naitikia maombi ya mwombaji, na kauli Yake;niombeni nitawaitikia ni kwamba Mwenyezi Mungu anamwitikia kilaanayemwomba; wakati ambapo mtu anaweza kuomba sana na kun-yenyekea, lakini haitikiwi maombi yake. Ni vipi?

Wafasiri wamelijibu swali hilo kwa majibu mbali mbali, baadhi yaowakafikia majibu sita. Wote wameafikiana kwamba muumini, mtiifu kwaMwenyezi Mungu, huitikiwa maombi yake, kinyume na mwingine. Lakinikauli hii inabatilika kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliitika maombi ya Ibilisi

“Akasema: Nipe muda mpaka Siku watapofufuliwa (viumbe), Akasema(Mwenyezi Mungu): Utakuwa miongoni mwa waliopewa muda.” (7: 14- 15)

Vyovyo iwavyo, jibu la swali hilo linahitaji ufafanuzi kwa njia zifuatazo:

1. Mja kumwomba Mola wake mambo yanayopingana na desturi, kamavile kutaka riziki bila ya mihangaiko yoyote, elimu bila ya kujifundishana mengineyo ambayo ni ya kutaka masababisho bila ya sababu, nakuingia nyumba kwa ukutani wala sio mlangoni. Hiyo siyo dua, au nidua ya asiyemjua Mwenyezi Mungu na hekima Zake na desturi Yake.Kwani Mwenyezi Mungu ana desturi kwa viumbe Vyake.

“... Wala hutapata mabadiliko katika mpango wa Mwenyezi Mungu.”

Page 106: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

96

(48:23).

2. Kutaka tawfiki na uongofu katika hukumu za dini kwa kufanya amaliza kheri, kutekeleza wajibu na kuacha maasia na mambo ya haramu,

“Tuongoze njia iliyonyooka” (1:6)

Vile vile dua ya kuomba kujiepusha na shari na maafa:

“ Sema najilinda kwa Mola wa asubuhi. Na shari ya alichokiumba”(113:1 - 2)

Pia kuna dua ya kumwomba Mwenyezi Mungu sababu za kufaulu katikariziki, elimu na afya:

“Ewe Mola wangu! Nikunjue kifua changu. Na unifanyie nyepesi kaziyangu.” (20:25-26)

Hayo yote ni kwa sharti ya kuwa mwombaji awe na ikhlasi na kumtege-mea Mwenyezi Mungu peke Yake. Hayo ndiyo maombi ya Mitume nawatu wema, na ndio makusudio ya dua zao.

3. Kabla ya yote inatakikana kwanza tuzinduke, wala tusiipuuze hakika hiitunayoiona na kuishuhudia kwa macho; nayo ni kwamba: MwenyeziMungu (s.w.t.) humpa anayemwomba na asiyemwomba, kwa rehema naukarimu kutoka kwake; na kwamba humpa ufalme anayemtaka, nahumzuilia humdhalilisha anayemtaka, na humwinua anayemtaka; na

Page 107: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

97

humpa nguvu anayemtaka bila ya dua.

Kwa hivyo basi kauli Yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): Naitikia maombiya mwombaji anaponiomba, haina maana kwamba Yeye hatoi isipokuwakwa dua. Wala kauli Yake:

“Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wanaofanya wema.”(7:56)

Kuwa rehema ya Mwenyezi Mungu iko mbali na waovu. Hapana si hiyo!Hakika rehema Yake imeenea kila kitu.

“... Na kutoa kwa Mola wako hakukuzuiwa.” (17:20)

Ni vizuri kueleza kuwa zimekuja baadhi ya riwaya za dua ya maumivu yatumbo, nyingine za maumivu ya mgongo, ya jicho, ya meno, n.k. Hadithhizo, ama zitakuwa ni za kuzuliwa tu, kwa sababu haziendi na hali halisiwala hazifai chochote; au pengine makusudio ni kujibidiisha kufanya mat-ibabu pamoja na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Inasemekana kwamba Amirul Muminin (a.s.) alimpitia bedui aliyekuwa nangamia mwenye ukurutu karibu yake. imam akamwuliza bedui: “Kwa ninihumfanyii dawa?” Akajibu: “Kwa nini ewe Amirul Muminin!Ninamfanyia” Imam akauliza: “Dawa gani?”Bedui akajibu: “Dua”Imamakasema: “Pamoja na dua, tumia dawa ya utomvu.”

Basi nawaniitikie Mimi na waniaminiRazi katika Tafsiri yake anasema: “Mwenyezi Mungu (s.w.t.)anamwambia mja Wake: Mimi ninaitikia maombi yako pamoja na kwam-

Page 108: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

98

ba Mimi sikuhitajii kabisa. Basi nawe vile vile uwe ni mwenye kuitikiamaombi yangu pamoja na kwamba wewe ni mwenye kunihitajia kwa kilahali. Ni ukubwa ulioje wa ukarimu huu!”

187. Mmehalalishwa usiku wasaumu kuwaingilia wakezenu. Wao ni vazi lenu nanyinyi ni vazi lao. MwenyeziMungu anajua kuwa mlikuwamkizihini nafsi zenu, kwahivyo amewatakabalia tobayenu na amewasamehe. Basisasa ingilianeni nao na takenialiyowaandikia MwenyeziMungu. Na kuleni na kuny-weni mpaka uwabainikieweupe wa Alfajiri katika weusiwa usiku wakati wa asubuhi.Kisha timizeni saumu mpakausiku. Na wala msiingiliane-nao na hali mko katika itikafumsikitini. Hiyo ni mipaka yaMwenyezi Mungu, msiikari-bie. Namna hii MwenyeziMungu anabainisha isharaZake kwa watu ili wapatekumcha.

Page 109: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

99

MMEHALALISHIWA USIKU WA SAUMU

Aya 187

LUGHA

Usiku wa saumu ni ule anaoamkia mtu akiwa amefunga. Kwa asili nenorafath lina mana ya uchafu. Makusudio yake hapa ni kumwingilia mke.Vazi ni nguo ya kuvaa, lakini makusudio katika Aya hii ni kuchanganyi-ka.

Mmehalalishiwa usiku wa saumu kuingiliana na wake zenu

Yaani inafaa kwa mwenye kufunga kumwingilia mkewe katika usiku wakufunga. Usiku wa kufunga unakusanya siku zote za Ramadhani na walahauhusiki na usiku fulani, au sehemu fulani tu ya usiku.! Hilo limefa-hamika kutokana na kuachiwa neno bila ya kufungwa na kitu kingine.

Mwenyezi Mungu amefumba kujamii (kuingilia) kwa neno rafath (ucha-fu) kwa ajili ya kuitakasa ibara; kama vile ambavyo amefumba katikaAya nyingine kwa maneno kama: kugusa, kuingiliana na kukurubiana. IbnAbbas anasema: "Mwenyezi Mungu ni mwenye staha; hufumbia ana-chotaka."

Wao ni vazi lenu na nyinyi ni vazi laoBaadhi ya wafasiri wanasema: Vazi hapa ni fumbo la ‘kukumbatiana’. Razianasema: “Rabii amesema kuwa wao ni tandiko kwenu, na nyinyi ni shukakwao”. Haya ni sawa na tafsiri ya mustashriqina wanaosema: “Wao nisuruali kwenu, na nyinyi ni suruali kwao”. Ilivyo hasa ni kuwa neno libasni matokeo ya neno laabasa kwa maana ya ‘kuchanganyika’ na ‘kuvaana’.

Makusudio kwa ujumla ni kubainisha hukumu ya kuruhusiwa kuingilianana wanawake usiku wa saumu; kwani mke na mume wakiwa pamoja nakutangamana, basi inakuwa uzito sana kwa mume kuvumilia.

Mwenyezi Mungu anajua kuwa mlikuwa mkizihini nafsi zenu, kwahivyo amewatakabalia toba yenu na amewasamehe.

Msemo hapa unawaelekea baadhi na wala sio wote. Hilo tunalifahamukutokana na neno hiyana, kutakabali toba na msamaha; kuwa baadhi yao

Page 110: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

100

walimwasi Mwenyezi Mungu. Na maasia yenyewe tunayafahamukutokana na neno la Mwenyezi Mungu: Basi sasa ingilianeni nao. Hapainaeleweka kwamba, kutokea sasa, amewahalalishia kuingiliana na wakezenu. Kwa hivyo ni lazima iwe, kabla ya sasa, kulikuwa ni haramu kishakukawa ni halali.

Wafasiri wengi wamesema kwamba Mwenyezi Mungu alimhalalishiamfungaji, tangu mwanzo wa sharia, kula na kunywa na kujamiiana namkewe usiku wa saumu kwa sharti la kutolala, au kuswali, swala ya Isha. Akilala usiku, au kuswali Isha, basi ni haramu juu yake kula, kunywa nakujamii mpaka uingie usiku unaofuatia. Na kwamba sahaba mmoja haku-jifunga kwa sharti hili; hivyo alimjamii mkewe baada ya kuamka, kishaakajuta sana na akakiri makosa yake kwa Mtume (s.a.w.w.). Ndipo ikashu-ka Aya hii.

Vyoyote iwavyo, ni kwamba nafsi ina mambo ambayo inakuwa vigumumtu kujizuwiya nayo. Kwa hivyo huishibisha kwa kujificha, au kwa kuasidini ya Mwenyezi Mungu. Basi lililo bora ni kuhalalisha lile linalopen-delewa ikiwa kuna njia yoyote ya kuhalalisha, ili mtu asivutwe kwenyemaasi mara kwa mara, hatimaye akawa ni mwenye kudharau na kutojalidini na hukumu za Mwenyezi Mungu.

Na takeni aliyowaandikia Mwenyezi Mungu

Ambayo ni kustarehe na wake zenu wakati wa usiku wa saumu: jamboambalo, hapo mwanzo, lilikuwa haramu.

Na kuleni na kunyweni mpaka uwabainikie weupe wa asubuhi kati-ka weusi wa usiku wa kati wa alfajiri

Yaani mmehalalishiwa kula na kunywa kama mlivyohalalishiwa kujami-iana, kuanzia mwanzo wa usiku mpaka machimbuko ya alfajiri.

Imepokewa Hadith ya Mtume (s.a.w.w.): "Alfajiri ni mbili. Ama ileambayo iko kama mkia wa mbwa mwitu, hiyo haihalalishi kitu wala hai-haramishi. Ama iliyo katika umbo mstatili ambayo inaenea pambizoni,hiyo ni halali kuswali ndani yake na ni haramu chakula”.

Page 111: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

101

Kisha timizeni saumu mpaka usiku

Mwanzo wa saumu ni kuanzia alfajiri, na mwisho wake ni unapoanzausiku. Usiku unaingia kwa kutua jua, lakini kutua kwake hakuwezi kuju-likana kwa kufichika machoni tu, bali hujulikana kwa kutoweka wekun-du upande wa mashariki kwa sababu mashariki ndiyo inayochomozamagharibi. Kwa hivyo wekundu wa mashariki unakuwa ni akisi ya mwan-ga wa jua; na kila linavyozidi kujificha zaidi jua, ndipo akisi hii inavy-opotea

Ama yale wanayotuhumiwa Shia kwamba wao wanachelewesha swala yaMagharibi na futari ya Ramadhani mpaka zitokeze nyota, huo ni uwongona uzushi. Imam Sadiq (a.s.) aliambiwa kuwa watu wa Iraq wanachelewe-sha swala ya Magharibi mpaka zitokeze nyota. Akasema. "Hiyo ni kazi yaadui wa Mwenyezi Mungu, Abul Khattwaab."

Na wala msiingiliane nao na hali mko katika itikafu msikitini

Katika vitabu vya Fiqhi kuna mlango mahsusi unaoitwa Mlango wa Itikafu.Aghlabu mafakihi huutaja baada ya Mlango wa Saumu. Maana ya itikafukatika sharia ni ‘mtu kukaa katika msikiti wa jamaa sio chini ya siku tatu,kwa masiku mawili, kwa mwenye kufunga; na kwamba asitoke msikitiniisipokuwa kwa haja muhimu, na kurudi mara moja anapomaliza’.

Ni haramu kwa mwenye kukaa itikafu kuingiliana na mwanamke usiku aumchana; hata kubusu na kugusa kwa matamanio. Kukatazwa hapa kuna-fungamana na kuvaana na mwanamke kwa hali yoyote; iwe ni ndani yamsikiti au nje. Mwenye kukaa itikafu akitoka msikitini na akajamiiana namwanamke usiku, hata kama atakoga na kurudi msikitini, atakuwa ame-fanya haramu; na itamlazimu kutoa kafara ya mwenye kufungua makusu-di katika mwezi wa Ramadhani - kumwacha huru mtumwa, au kufungamiezi miwili mfululizo, au kulisha maskini sitini.

Page 112: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

102

188. Wala msile mali zenu baina

yenu kwa batili na ku-

zipeleka kwa mahakimu ili

mpate kula sehemu ya mali

ya watu kwa dhambi na hali

mnajua.

KULA MALI KWA BATILI

Aya 188

MAANA

Wala msile mali zenu baina yenu kwa batili

Msemo unaelekezwa kwa wote wenye kulazimiwa na sharia.

Maana ya msile mali zenu, ni sawa na kauli Yake: Mwenyezi Mungu;Msijiue yaani msiuane. Hiyo inafahamisha umoja wa utu, na kwamba utuni kama kiwiliwili kimoja na watu ni viungo vyake, lililopata kiungo kimo-ja linafikia kiungo kingine.

Makusudio ya kula, ni kutumia mali iliyopatikana kwa njia isiyo halali.Neno kati yenu katika Aya linahusisha mali iliyopatikana kwa miamala yaharamu, kama riba; au mali iliyosimama kwa haramu, kama pombe, ngu-ruwe, hadaa au utapeli ambayo sharia hayakubali. Mfano wa hayo ni kauliYake Mwenyezi Mungu:

"... Msile mali zenu baina yenu kwa batili, isipokuwa iwe biashara kwakuridhiana...."(4:29)

Page 113: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

103

Ama uharamu wa mali iliyochukuliwa kwa unyang'anyi, wizi, kiapo chauwongo, n.k., hayo yanafahamika kwa dalili nyingine. Kwa ajili hii, ndipomafakihi wakatoa dalili kwa Aya mbili hizo juu ya kubatilika kila muamala(mapatano) aliouharamisha Mwenyezi Mungu.

Aya hii inafahamisha wazi wazi kwamba Uislamu unakubali mtu kumilikichake (mali ya mtu binafsi).

Na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watukwa dhambi

Haya yanaungana na kula. Makusudio ya dhambi hapa ni ‘rushwa’, kwakuangalia mfumo wa maneno ulivyo. Maana yaliyokusudiwa ni kukatazakutoa rushwa kwa mahakimu kwa ajili ya kula mali za watu.

Na hali mnajua

Yaani msifanye dhambi hii na hali mnajua ubaya wake. Hakuna mwenyekutia shaka kwamba kufanya jambo ovu na huku mtu anajua, ni uovu zaidikuliko kufanya na shaka shaka. Kuna Hadith isemayo: "Kujizuia na shakashaka ni bora kuliko kujitia katika maangamizo." Basi ni bora zaidikujizuia ikiwa mtu anajua uharamu.

Rushwa ni katika mambo makubwa yaliyoharamishwa, hata katika huku-mu ya haki. Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wameilaani rushwa namwenye kuitoa, mwenye kuipokea na mwenye kuwaunganisha wawilihao. Imepokewa Hadith inayofahamisha kuwa rushwa ni kumkufuruMwenyezi Mungu (s.w.t.); na riwaya nyingine inasema ni shirki.

HUKUMU YA KADHI FASIKI

Mahanafi wanasema kuwa hukumu ya kadhi fasiki inafaa. Hayoyameelezwa katika kitabu maarufu kiitwacho Ibn Abidin chapa ya mwaka1325 hijriya., Mlango wa Hukumu. Ninamnuukuu: "Fasiki ni mtu wakutoa ushahidi, kwa hivyo anaweza kuwa kadhi."

Page 114: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

104

Na katika kitabu Fat-hul Qadir J5 uk. 454. Mlango wa Hukumu, amese-ma; "Ilivyo ni kuwa hukumu ya kila mtawala inafaa, hata kama ni mjingatena fasiki, na hayo ndiyo yaliyo wazi katika madhehebu yetu."

Shia Imamiya wamesema kwa kauli moja kwamba fasiki hawezi kuhuku-mu, na hukumu yake haifai kutekelezwa, hata awe na elimu kiasi gani.

Wamelitilia mkazo hilo kundi la mafakihi wa Kiimamiya waliposemakuwa mwenye haki haijuzu kupeleka madai yake kwa kadhi asiye mwadil-ifu, hata kama hawezi kuipata haki yake isipokuwa kwake, kwa kuwa lausi kadhi huyo, basi haki yake itapotea.

Akihalifu mwenye haki yake, akaenda kwa kadhi asiye mwadilifu, naakamhukumia haki, basi haijuzu kuchukua chochote kilichohukumiwahata kama ni haki; kwa kufuata kauli ya Imam Jafar As Sadiq (a.s.):"Anachokichukua ni haramu, ijapokuwa ni haki yake iliyomthibitikia."

Mafakihi wengi wa Kiimamiya wamesema kwamba mwenye hakianaweza kumtaka msaada asiyekuwa mwadilifu ili kupata haki yake ikibi-di, ikiwa hawezi kupata njia nyingine, bila ya kutofautisha kuwa hakiyenyewe ni deni au mali. Kwa sababu kuzuia madhara ya nafsi kunajuzu,bali mara nyingine huwa ni wajibu, ikiwa hakutimii isipokuwa kwa kum-rudia asiyekuwa mwadilifu. Ama dhambi na haramu iko juu ya mwenyekuzuia kuitoa haki, sio mwenye kuchukua haki yake.

HUKUMU YA KADHI HAIBADILISHI UHAKIKA WA MAMBO

Hakimu mwadilifu akiwahukumu watu wawili na akampa haki asiyekuwa nahaki, kwa mwenye haki kushindwa kutoa ushahidi, basi haijuzu kuchukua ali-chohukumiwa, kwa sababu hukumu ya hakimu haigeuzi uhakika. Mtume(s.a.w.w.) anasema: "Mimi ni mtu kama nyinyi isipokuwa napewa wahyi tu,na nyinyi huja kutaka hukumu kwangu. Huenda mwingine wenu akawa fasa-ha zaidi kwa hoja kuliko mwenzake, nami nikahukumu kwa mujibu wa niliy-oyasikia. Basi ninayemhukumia kitu katika haki ya nduguye, (ajue)nimemhukumia kipande cha Moto."

Page 115: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

105

Lakini Abu Hanifa amesema kinyume cha hivyo. Mwenye Tafsir Al- Manar,katika kuelezea Aya hii, amemnukuu Abu Hanifa kuwa amesema: "Kadhiakihukumu kuvunjika ndoa kati ya mume na mke kwa ushahidi wa uwon-go, itakuwa haramu kwao kuishi maisha ya ndoa. Na kama shahidi akitoaushahidi wa uwongo kwamba fulani amemuoa fulani, na hakimu akahuku-mu kuwa ni sawa, basi ni halali kwa mwanamume kumwingilia bila ya ndoa,kwa kutosheka na hukumu ya kadhi ambayo anajua kuwa sio haki."

189. Wanakuuliza kuhusu miezi.Sema: 'Hiyo ni vipimo vyanyakati kwa ajili ya watu naHijja. Wala si wema kuingiamajumba kwa nyuma yake,bali wema ni anaye mchaMungu. Na ingieni majumbakwa milangoni mwake, namcheni Mwenyezi Mungu ilimpate kufaulu.

WANAKUULIZA KUHUSU MIEZIAya 189

MAANA

Wanakuuliza kuhusu miezi.

Swali hili linawezekana kuwa na pande mbili, ikiwa tutaliangalia mbali najibu lake linalofuatia: Kwanza, ni kuwa ni swali la kutaka kujua sababuza kisayansi za kutokana na tofauti inayoonekana - kuanzia mwezi mwan-damo, kisha mwezi mkamilifu, tena unarudi kama ulivyokuwa. Pili, kuwani kuuliza hekima yake, sio sababu za kisayansi.

Page 116: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

106

Tukiliangalia swali pamoja na jibu lake: Sema: Hiyo ni vipimo vyanyakati kwa ajili ya watu, litakuwa ni swali la hekima tu, na wala sio lasababu za kisayansi. Hili ndilo lenye nguvu zaidi.

Ama kauli ya anayesema kuwa wao waliuliza kuhusu sababu za kisayan-si, na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.). akamwamrisha Mtume Wakekuwajibu kwa kubainisha hekima kuonyesha kuwa swali lao haliko mahalipake, kwa sababu wao wameshindwa kuzitambua sababu za kisayansiambazo zinahitaji darasa ndefu na za undani, na utangulizi mwingi wakielimu; na lililobora kwao ni waulize hekima na faida ya kutofautianamiezi, jambo ambalo wao wanaweza kulifahamu. Ama kauli hiyo haitege-mei dalili yoyote isipokuwa kuonelea kuwa ni vizuri hivyo tu.

Unaweza kusema kuwa dalili iko; nayo ni kauli Yake Mwenyezi Mungu(s.w.t.): “Wala si wema kuingia majumbani kwa nyuma yake”. Kwambakuuliza kwenu sababu za kisayansi, ni sawa na kutaka kuiingia nyumba kwanyuma; lakini kuuliza kwenu hekima yake, ni kama anayetaka kuingianyumba kwa mlango wake.

Jibu: Kwanza hiyo ni ijtihadi ya kuleta taawili ya tamko, wala siotafsiri ya dhahiri ya tamko hilo.

Pili, imethibiti kuwa jumla hii imeshuka kutokana na waliyokuwawakiyafanya watu wa jahiliya, ya kuingia nyumba kwa nyuma. Na ufafanuzini kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume Wake kuwajibu kuwa heki-ma ya kutofautiana miezi ni kuyawekea wakati maslahi yao na mambo yaoya kidunia: kama vile madeni na nyujira, na mambo yao ya kidini: kama vilehijja na saumu. Kwa maneno mengine, ni jibu linapitia katika kauli YakeMwenyezi Mungu (s.w.t):

“: ...Ili mjue idadi ya miaka na hisabu..." (10:5)

Bali wema ni anayemcha Mungu.Na ingieni majumba kupitia milangoni mwake

Page 117: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

107

Wafasiri wengi wasema: watu wa jahiliya, ilikuwa mtu anapohirimia hijja,hutoboa tundu ya kuingilia au hutengeneza ngazi ya kupandia sakafuni; naakiwa ni katika mabedui hutoka kwa nyuma ya kibanda.

Baadhi ya Waislamu nao walikuwa wakifanya hivyo hapo mwanzomwanzo, ndipo ikashuka Aya kuwabainishia kwamba wema ni kum-wogopa Mwenyezi Mungu, kufanya amali za kheri na kujiepusha na maa-sia na machafu, sio kuingia majumba kwa sakafuni na mengineyo ambayohayaingii akilini wala hayana lengo la dini na imani.

190. Na piganeni katika njia yaMwenyezi Mungu na walewanaowapiga, wala msi-chokoze. Hakika MwenyeziMungu hawapendi .

191. Na wauweni popote muwapa-tapo, na watoeni popotewalipowatoa; na fitina nimbaya zaidi kuliko kuua. Walamsipigane nao karibu naMsikiti Mtukufu mpaka wapi-gane na nyinyi huko.Wakipigana na nyinyi, basiwaueni. Namna hivi ndivyoyalivyo malipo ya makafiri.

192. Lakini wakikoma, basi haki-ka Mwenyezi Mungu niMwenye maghufira, Mwenyekurehemu.

Page 118: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

108

193. Na piganeni nao mpakakusiwe na fitina, na dini iweya Mwenyezi Mungu pekeYake. Na wakikoma, basi usi-weko uadui ila kwa madhal-imu.

NA PIGANENI KATIKA NJIA YA MWENYEZI MUNGU

Aya 190 -193

LUGHA

Neno fitna lina maana ya balaa na misukosuko, na makusudio yake hapani ‘ukafiri’, yaani kuwaharibu watu na dini ya Mwenyezi Mungu. Hiyo nikutokana na kuliandamiza na neno: "Na dini iwe ya Mwenyezi Mungupeke Yake."

MAANA

Katika Majmaul Bayan imepokewa kwa Ibn Abbas kwamba Mtume(s.a.w.w.) alipotoka, yeye na sahaba zake, katika mwaka ambao walitakakufanya umra wakiwa watu elfu moja na mia nne (1400), walipofikaHudaybiya, washirikina waliwazuia wasiingie Al-Kaaba. Wakachinjawanyama wao hapo Hudaybiya;* 4 kisha wakafanya suluhu na washirikinakurudi, na waje mwaka ujao.

Mwaka ulipofika Waislamu walijiandaa tena kufanya umra, lakini wakao-gopa kupigwa vita na washirikina. Mtume (s.a.w.w.) na sahaba zakewakachukia kupigana na washirikina katika mwezi mtukufu tena ndani yaHaram (sehemu takatifu ya Makka).

*4 Hayo yalikuwa mwezi wa Dhul-qaada (mfunguo pili) mwaka wa sita wa Hijriya. NaHudaybiya siku hizo ilikuwa na maji mengi na miti. Lakini leo imegeuka na kuwa jangwakama nilivyoiona mwaka 1964 B.K

Page 119: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

109

Ndipo Mwenyezi Mungu alipoteremsha Aya hii, na kuidhinisha kupi-gana. Baadhi ya jamaa wamesema kuwa hiyo ndiyo Aya ya kwanzakushuka kuhusu vita.

UISLAMU UNAPIGA VITA DHULUMA NA UFISADI

Baadhi ya ambao wana ghera na Uislamu, na kujaribu kuugombea kwakila njia, hata kama itapingana na misingi ya Qur'ani, wamesema kuwaUislamu hauruhusu kupigana na yeyote isipokuwa mchokozi; na vita vyaKiislamu, katika zama za Mtume, vilikuwa ni vya kujikinga, sio huju-ma; na walitoa dalili kwa Aya kadhaa miongoni mwazo ni Aya hii tuliy-onayo sasa, na Aya nyingine inayosema:

"...Na piganeni na makafiri nyote kama wao wanavyopigana nanyi wote "(9:36)

Lililowafanya kuugombea Uislamu hivyo, ni madai ya maadui waUislamu kwamba Uislamu ni dini ya vita, sio dini ya amani, kwa kisin-gizio cha vita vya Mtume (s.a.w.w.).

Ukweli hasa ni kuwa Uislamu umeruhusu kupigana kwa sababu mbalimbali, k.m. kujikinga nafsi, na kupigana na madhalimu

Mwenyezi Mungu amesema:

“Na makundi mawili ya waumini yakipigana, basi yapatanisheni. Moja yahayo likidhulumu jengine, basi lipigeni lile linalodhulumu mpaka lirudikwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." (49:9)

Page 120: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

110

Na vile vile amesema, katika kuumaliza ukafiri wa wanaomkufuru:

"Piganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho,wala hawaharimishi alivyoviharimisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wakewala hawafuati dini ya haki miongoni mwa waliopewa Kitabu, (piganeninao) mpaka watoe kodi kwa hiari yao, hali wametii." (9:29)

Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Nimeamrishwa kupigana na watu mpakawaseme hapana mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kama wakisemahivyo, basi imehifadhika nami damu yao na mali zao."Lakini kupigana kwa aina hii hakuruhusiwi isipokuwa kwa idhini yaMaasum au naibu wake, ili kuepuka vurugu.

Kujuzu kupigana kwa kujikinga, hakuna maana kuwa hakuna idhini yakupigana kwa malengo mengine, kama vile kumaliza dhuluma naukafiri. Uislamu umeruhusu kupigana kwa ajili ya kupatikana dini ya hakina uadilifu, kwa sababu ukafiri, woo wenyewe ni uadui kwa jinsi unavy-oeleweka katika Uislamu. Lakini Uislamu umeharamisha kupigana kwaajili ya kutawala watu na kuwapokonya uweza wao na kutawala uchumiwao.Uislamu umejuzisha kutumia nguvu ili kumaliza maovu na madhambi,na kupigania haki za binadamu, uhuru wake na heshima yake. Wakoloniwalianzisha vita, wakaleta machafuko na kumwaga damu, wakatumiaelimu (Sayansi) kwa ajili ya kuvunja miji na kuangamiza watu, kuua nakunyonya, na kuiweka juu dhuluma na uadui * 5

* 5 Katika mwaka 1957 kilitolewa kitabu huko Amerika, kinachohusu mustakabali wanguvu za nuklia cha Tryto. Imeelezwa humo kwamba maendeleo ya Sayansi yame-teremsha bei ya kumuua mtu. Kabla bomu la atomic ilikuwa ikigarimu pauni nyingikumuua tu. Baadaye ikagharimu pauni moja; na baada ya bomu la haidrojeni ikawainagharimu shilingi moja tu.

Page 121: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

111

Hiyo ndiyo jawabu sahihi ya wale wanaojaribu kuutweza Uislamu naNabii wake, kwamba Uislamu ni dini ya vita na upanga.

Uislamu ni dini iliyokamilika. Inampiga vita kila asiyefuata haki nauadilifu, na anayeleta uharibifu na ufisadi katika ardhi. Na kumkufuruMwenyezi Mungu ni dhuluma na ufisadi katika dini ya Kiislamu nasharia yake.

Kulingana na suala hili hatuna budi kudokeza kuwa mafakihi wa mad-hehebu zote za Kiislamu wameafikiana kwa kauli moja kwamba yeyoteanayevunja miko ya Mwenyezi Mungu kwa kuihalalisha na kwa kumwagadamu, na kunyakua mali, basi yeye na anayemkufuru Mwenyezi Munguni sawa; hata akiswali na kufunga na kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungutukufu. Bali huyu ni mwovu zaidi kuliko yule mwenye kukufuru, lakiniakazuia umwagaji damu na kunyakua mali, na akijizuia kuwaudhi watu.

Ndio! Wote wawili ni makafiri; hilo halina shaka. Lakini mmoja ni kafirialiyewakinga waja wa Mwenyezi Mungu na shari yake n aduhia wake; namwingine ni mwovu kwa Mwenyezi Mungu na kwa waja. Mtume waMwenyezi Mungu ( s.a.w.w.) amesema: "Bora ya watu ni yule mwenyekuwanufaisha zaidi watu, na mwovu zaidi wa watu ni yule ambaye watuwanahofia shari yake."

Tunasema tena! kila mwenye kukanusha hukumu ya kisharia iliyothibiti kwadhahiri ya dini na Waislamu wote, basi huyo ni kafiri hata kama amezaliwa nawazazi Waislamu na akatamka shahada mbili.

Wala msichokoze

Yaani, msipigane kwa ajili ya manufaa ya kibinafsi,, bali piganeni kwalengo la kiutu lenye heshima, na kwa lengo la kuihami dini na haki, walamsiwaue watoto, wazee na wagonjwa. Vile vile msiharibu majengo na kuka-ta miti. Mafunzo yote haya na mengineyo yamekuja katika sunna zaMtume.

Page 122: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

112

Na waueni popote muwapatapo

Yaani waueni makafiri wakati wowote na mahali popote walipoisipokuwa kwenye Msikiti Mtukufu, kwa sababu kupigana hapo ni hara-mu isipokuwa wakianza wao humo.

Unaweza kuuliza: Katika Aya ya mwanzo kumeamrishwa kupigana naanayepigana na Waislamu. Lakini kwenye Aya hii kumeamrishwa kupi-gana tu, bila ya kufungamanishwa na kitu kingine. Je, Aya hii imefuta ile,kama inavyosemwa?

Jibu: Hapana kufutwa hukmu. Hivi punde tumeonesha kwamba kujuzukupigania nafsi hakufahamishi kuwa hakuna ruhusa ya kupigana kwalengo jengine; kama vile kumaliza ukafiri na dhuluma. Kamaukimwambia mtu: 'Wewe ni mtu mzuri' haina maana kuwa mwingine simtu mzuri.

Basi ni hivyo hivyo kauli ya Mwenyezi Mungu: 'Piganeni na wanaowapi-ga' haina maana msipigane na wasiowapiga. Ndio! Kama angelisema:Msipigane isipokuwa na wanaowapiga, hilo lingefahamisha kufunga: kwausipigane na yeyote mwengine ila yule aliyekupiga. kukanusha.

Na watoeni popote walipowatoa

Washirikina wa Makka walimtoa Mtume (s.a.w.w.) na sahaba zakehapo Makka, si kwa lolote isipokuwa tu masahaba hao wamemwaminiMwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kwa hivyo Mwenyezi Munguakamwamrisha Mtume Wake na Waislamu, wakirudi Makka wakiwawashindi, wamtoe hapo kila asiyemwamini Mwenyezi Mungu na MtumeWake; sawa na vile walivyofanywa wao na washirikina, 'malipo yenye kulin-gana.' Inasemekana kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliwatoa washirikina, ulipoku-ja msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi, kwa kuchukulia Aya hii.

Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua

Page 123: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

113

Hii ni sababu ya kujuzu kuwaua washirikina. Makusudio ya fitina hapani ushirikina. Maana ya kuwa mmeruhusiwa kuwaua washirikina, nikuwa dhambi ya shirki ni mbaya zaidi kuliko dhambi ya kuua.

Baadhi ya tafsiri zinasema Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekusudia katikakauli yake hiyo, kuwa washirikina wa Makka, hapo mwanzo wa mwito waUislamu, walikuwa wakimfitini mwenye kusilimu kwa kumuudhi,kumwadhibu na kumtoa mjini kwake. Na hiyo ni fitina mbaya zaidikuliko kuua. Kwa ajili hii ndio kukaruhusiwa kuwaua na kuwatoa mijinimwao.

Vyovyote iwavyo, makusudio ya neno fitna katika Qur'ani sio ya kufanyaumbeya na udaku kama wanavyofikiria wengi.

Wala msipigane nao karibu na Msikiti Mtukufu mpaka wapigane nanyinyi huko.

Hili ni sharti la kujuzu kupigana katika Haram tukufu, ambayo ame-haramisha Mwenyezi Mungu kupigana ndani yake, isipokuwa kamaikivunjiwa heshima kwa kupigana.Wakipigana nyinyi, basi waueni.Kwa sababu wao wameanza na wakauvunjia heshima Msikiti Mtakatifu. Namwenye kuanza hakudhulumiwa, isipokuwa yeye ndiye dhalimu.

Lakini wakikoma, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira,Mwenye kurehemu.

Kulingana na mfumo wa maneno ulivyo, unahukumia kuwa maana yakeni: Wakijizuia kupigana nanyi katika Msikiti Mtukufu, basi nanyi jizuieni namuwasamehe, kwa vile sababu iliyolazimisha kupigana nao ni kuanza kwaovita; wakijizuia basi sababu imeondoka.Wafasiri wengi wamesema kuwa maana yake ni: Wakitubia kutokana naukafiri, na wakamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Kwa sababukafiri hawezi kusamehewa na Mwenyezi Mungu kwa kuacha kupigana tu,bali husamehewa kwa kuacha kufuru. Lakini huku ni kumhukumiaMwenyezi Mungu(s.w.t.) kwa sababu Yeye anaweza kumsamehe anayemta-ka, hata kama ni kafiri. Naam! Ni kweli kuwa Mwenyezi Mungu hawezi

Page 124: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

114

kumwadhibu mwema kabisa, sababu Yeye ni Mwadilifu, lakini anawezakumsamehe mkosaji kwa namna yoyote ya uovu itakavyokuwa, kwa sababuYeye ni Karimu, Mwenye huruma.Na piganeni nao mpaka kusiwe na fitina, na dini iwe ya MwenyeziMungu (s.w.t) peke yake.

Yaani Jihadi ni kwa ajili ya kumwamini Mwenyezi Mungu. Na kuumalizaukanushaji (wa kumkanusha Mwenyezi Mungu) ni wajibu maadam duni-ani kuna athari ya shirki na ulahidi. Kama yakiondoka haya, na watu wotewakaamini, basi wajibu wa jihadi utakuwa umeondoka.

Kwa ujumla, ni kwamba wajibu wa jihadi kwa ajili ya kuuenezaUislamu, una sharti ya kupatikana idhini ya Imam mwadilifu, na walahaijuzu kwa hali yoyote bila ya amri yake. Ama jihadi ya kuihami dini nanafsi, wajibu wake umeachwa bila ya kuwekewa sharti lolote.Na wakikoma, basi usiweko uadui ila kwa madhalimu.

Yaani kama wakiacha ukafiri na wakasilimu, basi si halali kuwauaisipokuwa kwa sababu zinazowajibisha kuua, ambazo ni moja kati yamambo matatu: kukufuru baada ya kuamini, kuzini baada ya kuwa na mkeau mume,na kuua mtu bila ya haki yoyote.

194. Mwezi Mtukufu kwa mweziMtukufu na vitu vyenyekutukuzwa vina kisasi. Basianayewataadia, nanyi mtaa-dieni kwa kadiri ya alivy-owataadia. Na mcheniMwenyezi Mungu na (jueni)kwamba Mwenyezi Munguyuko pamoja na wanaomcha.

Page 125: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

115

195. Na toeni katika njia yaMwenyezi Mungu walamsijitie, kwa mikono yenu,katika maangamivu, nafanyeni wema. HakikaMwenyezi Munguhuwapenda wafanyao wema.

MIEZI MITUKUFU

Aya 194 - 195

MAANA

Mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu.

Miezi mitukufu ni minne; mitatu inafuatana, nayo ni Dhul-Qaada, DhulHijja na Muharram (Mfunguo pili, mfunguo tatu na mfunguo nne). Namwezi mmoja uko pekee; nao ni mitukufu Rajab. Miezi hii imeitwa kwasababu ya kuharamishwa kuuana ndani ya miezi hiyo. Katika wakati waujahiliya na wa Uislamu, ilikuwa mtu anaweza kukutana na mtu aliye-muua baba yake katika miezi hiyo, na asimfanye chochote.

Yameshatangulia maelezo kwamba Mtume na sahaba zake walitakakufanya umra katika mwezi wa Dhul-qaada (Mfunguo pili) mwaka wasita (6 Hijriya), wakazuiwa na washirikina na wakatupiwa mishale namawe; kisha wakafanyiana suluhu kuwa Waislamu warudi mwaka utakao-futia. Lakini Waislamu wakaogopa washirikina wasije wakaanza kupi-gana katika mwezi mtukufu; ndipo Mwenyezi Mungu akawapa idhini yakupigana na washirikina, na akabainisha kuwa lenye kukatazwa ni kuan-za uadui wa kupigana, na sio kujikinga.

Kwa hivyo maana ya mwezi mtukufu kwa mwezi mtukufu ni kwambamwenye kuihalalisha damu yenu, enyi Waislamu, katika mwezi huu, basinanyi ihalalisheni damu yake katika mwezi huo huo.

Page 126: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

116

Na vitu vyenye kutukuzwa vina kisasi.

Yaani mwenye kuvunja heshima ya Mwenyezi Mungu atalipizwa kisasi,na atafanywa kama alivyofanya. Hiyo ndiyo asili kwa ujumla inayoondoakila udhuru wa mwenye kuvunja heshima. Mwenye kuhalalilisha damu zawatu, mali zao na heshima zao, naye atahalalishiwa kwa kiasi kile ali-chowahalalishia wao. Heshima ya mtu inatokana na heshima yaMwenyezi Mungu isipokuwa akiivunja heshima ya mwingine. Hapo ndipoitakapokuja haki ambayo daima iko juu, wala haitukukiwi. Hapa ndipotunapata tafsiri ya:

Anayewataadia nanyi mtaadieni kwa kadiri alivyo wataadia.

Sharti la kulipiza ni kuwa kuwe sawa na kosa la aliyeanza, bila yakuzidisha au kupunguza. Hicho ndio kisasi hasa kilivyo.

Unaweza kuuliza: Anayeanza kuchokoza , yeye ni mchokozi bila ya wasi-wasi wowote. Lakini mwenye kumlipiza kisasi mchokozi, kwa mfanowa alivyofanyiwa, hawi mchokozi. Kwa hivyo kuna wajihi gani kwaMwenyezi Mungu kusema: Mtaadini (mchokozeni)?

Jibu: Makusudio ya kuwafanyia uchokozi, sio uchokozi hasa kwa maanayake, isipokuwa makusudio ni malipo ya uchokozi uliofanywa kwa kipimochake bila ya kudhulumu. Hayo ni mfano wa kauli Yake MwenyeziMungu(s.w.t.):

"Na malipo ya ubaya ni ubaya ulio sawa na (ubaya) huo..." (42:40)Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu.

Kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu kunakuwa ni kwa masilahi yaumma; kama vile shule, hospitali na nyumba za kulea mayatima. Vile vilejihadi, sadaka kwa mafukara na maskini, na kuwalisha watu wa nyum-bani. Bora zaidi ya kutoa ni kule kunakohusika na kutia nguvu nakuieneza dini, kuthibitisha haki na kuibatilisha batili.

Wala msijitie, kwa mikono yenu, katika maangamivu

Page 127: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

117

Mwenyezi Mungu ametumia neno mikono kwa maana ya nafsi (mtu kuji-ingiza mwenyewe). Tukiangalia jumla hii peke yake, bila ya kuangaliamfumo mzima wa maneno, ingelikuwa maana yake ni kuwa: haijuzukwa mtu kufanya lolote ambalo lina madhara, na bila ya kuwako man-ufaa kwa ujumla. Lakini tukichunga mfumo wa maneno, na kuja kauliYake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): wala msijitie, kwa mikono yenu, katikamaangamivu baada ya kusema: Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu,basi maana yanakuwa: Toeni katika mali zenu, sio kwa ubahili walaubadhirifu, kwa sababu yote hayo mawili yanaleta uangamivu. Kwa hivyoAya, kwa maana haya, inakuwa kama ile Aya isemayo:

"Na wale ambao wanapotoa hawafanyi ubadhirifu wala ubahili, baliwanakuwa katikati ya hayo."(25:67)

Inasemekana pia kwamba maana yake ni: Msijitie, kwa mikono yenu,kwenye maangamivu kwa kuacha kupigana jihadi na maadui wa dini nakutoa mali kwa ajili ya kuwaandaa wapiganao jihadi, kwa sababu hilolitawaogopesha na kumpa nguvu adui; muangamie na mdhalilike.

Haya ndiyo yaliyothibitishwa na uzoevu walioupitia Waislamu. Wamekosauhuru wao na heshima yao tangu walipoacha jihadi na kutoa mali kwa ajiliya kuinusuru haki na uadilifu. Hivyo akapata tamaa kila mnyang'anyaji namnyakuzi; hata Wazayuni, vibaraka wa ukoloni, nao waliivamia Palestinamnamo 1948. Baada ya Waarabu kunyamaza na wasifanye jihadi, kwamiaka ishirini, wakaiteka Sinai na ukanda wa Gaza Magharibi mwa mtoJordan; wakazikalia sehemu hizo kwa msaada wa Amerika, Uingereza naUjerumani Magharibi. Wakawaua wanaume na kuwafukuza wanawake nawatoto. Lau Waislamu wangelipigana nao jihadi kabla yake, wangeliokokana maangamivu haya na udhalili huu, na wala dola ya Israel isingekuwepokabisa.

Na fanyeni wema

Kwa jihadi na kujitolea mali katika njia ya Mwenyezi Mungu, na katikakila njia inayomridhisha Mungu, na yenye sifa nzuri.

Page 128: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

118

196. Na timizeni hijja na umra kwaajili ya Mwenyezi Mungu. Nakama mkizuiliwa, basi (chin-jeni) wanyama walio wepesikupatikana. Wala msinyoevichwa vyenu mpaka wanya-ma hao wafike machinjionimwao. Na atakayekuwamgonjwa katika nyinyi, auana adha kichwani mwake,basi atoe fidia kwa kufungaau sadaka au kuchinja mnya-ma. Na mtakapokuwa sala-ma, basi mwenye kujistarehe-sha kwa kufanya umra, kishaakahiji, achinje mnyama aliyemwepesi kumpata. Naasiyepata, ni kufunga sikutatu katika hijja na siku sabamtakaporudi; hizo ni sikukumi kamili. Hayo ni kwayule ambaye watu wakehawako karibu na Msikitimtukufu. Na mcheniMwenyezi Mungu na juenikwamba Mwenyezi Mungu niMkali wa kuadhibu.

Page 129: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

119

197. Hijja ni miezi maalum. Naanayejilazimisha kufanyahijja katika miezi hiyo, basihakuna kuingiliana nawanawake wala kutoka kati-ka mipaka wala mabishanokatika hijja. Na kheri yoyotemnayoifanya MwenyeziMungu anaijua. Na chukuenimasurufu, na hakika masu-rufu bora ni ucha Mungu; nanicheni Mimi, enyi wenyeakili.

198. Si vibaya kwenu kutafuta rizi-ki ya Mola wenu. Namtakapomiminika kutokaArafa, mtajeni MwenyeziMungu katika Mash'aril-Haram: Na mkumbukenikama alivyowaongoza,ijapokuwa zamani mlikuwamiongoni mwa waliopotea.

199. Kisha miminikeni kutokamahali wanapomiminika watu(wote), na mumwombeMwenyezi Mungu maghufira;hakika Mwenyezi Mungu niMwenye kughufiria, Mwenyekurehemu.

Page 130: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

120

200. Na mmalizapo kuzitimizaibada zenu, basi mtajeniMwenyezi Mungu kamamlivyokuwa mkiwataja babazenu; bali mtajeni zaidi. Nakuna baadhi ya watu wase-mao: Mola wetu! Tupe(mema) hapa duniani; naokatika Akhera, hawanafungu lolote.

201. Na miongoni mwao kuna ase-maye; Mola wetu! Tupemema duniani na (tupe)mema Akhera, na utukingena adhabu ya Moto.

202. Hao ndio wenye fungu kati-ka waliyoyachuma, naMwenyezi Mungu niMwepesi wa kuhisabu.

Page 131: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

121

203. Na mtajeni MwenyeziMungu katika siku zinazo-hisabiwa. Na mwenyekufanya haraka katika sikumbili, basi si dhambi juuyake; na mwenye kukawiapia si dhambi juu yake, kwamwenye kumcha(Mwenyezi Mungu). Namcheni Mwenyezi Mungu,na jueni kwamba nyinyimtakusanywa Kwake.

TIMIZENI HIJJA NA UMRA

Aya 196 - 203

MAANA

Aya hizi zimeonesha baadhi ya hukumu za hijja. Mafakihi wamewekavitabu maalum vinavyohusu hijja, nami nimetunga kitabu kwa jina Al-Hajjaala Madhahibil-Khamsa; kisha nikakiunganisha katika kitabu Al-Fiqhala Madhahabil Khamsa wakati kiliporudiwa kuchapishwa kwa mara yatatu. Vile vile nimeizungumza kwa urefu katika Juzuu ya Pili ya kitabuFiqhul Imam Jafar Sadiq (a.s.)

Hijja imekuwa ikijulikana tangu zama za Nabii Ibrahim na Ismail (a.s.), nailiendelea katika zama za ujahiliya; na Uislamu ukaithibitisha baada yakuisafisha na mambo machafu, na kuongeza baadhi ya ibada.

Na timizeni hijja na umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu

Maana ya hijja kilugha, ni ‘kukusudia’, na kisharia ni ‘ibada maalum kati-ka mahali na wakati maalum’. Umra kilugha ni ‘ziara yoyote’; na kisharia

Page 132: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

122

ni ‘ziara katika Al-Ka’aba kwa namna maalum’.

Hijja ni wajibu katika Qur’ani, Hadith na ijami. Bali wajibu wakeumethubutu kwa dhahiri ya dini. Na mwenye kuikanusha sio Mwislamu,sawa sawa na aliyekanusha wajibu wa saumu na swala Ama umra, ShiaImamiyya na Shafi wamesema ni wajibu, Hanafi na Maliki wamesema nisunna.

Kusema kwake Mwenyezi Mungu: Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kuna-maanisha: Hijini na fanyeni umra kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke Yake,na sio kwa makusudio ya kidunia. Kwani Waarabu walikuwa wakikusudiakuhiji kwa ajili ya kukutana, kujifaharisha, kutafuta mahitaji na kuhudhuriasoko. Ndipo Mwenyezi Mungu akaamrisha hijja iwe ni kwa makusudioYake Yeye kwa ibada safi yenye kutakasika na makusudio yoyote mengine.

Na kama mkizuiliwa, basi (chinjeni) wanyama walio wepesikupatikana

Yaani ikiwa mmehirimia hijja, kisha mkazuilika kukamilisha ibada kwa njiayake ya kisharia; kutokana na maradhi au adui na mengineyo, basi ni juuyenu kuchinja mnyama atakayepatikana kwa urahisi. Kwa uchache awe nimbuzi, wastani ni ng’ombe, na wa juu zaidi ni ngamia.

Wala msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama hao wafike machinjionimwao

Maneno haya yanaelekezwa kwa wale waliozuilika, ambao hawakuwezakutimiza hijja au umra. Wao hawatakuwa wametoka katika ihramu yao(miko ya hijja) mpaka wajue kwamba mnyama amefika mahali pake pakuchinjwa. Na mahali pa kuchinja ni Mina, ikiwa ni hijja; na kama ni umra,basi ni Makka. Hayo ni itakapokuwa kizuizi ni maradhi. Ama ikiwa kizuizini adui, basi mahali pa kuchinja ni pale mahali palipotokea kizuizi; kwasababu Mtume (s.a.w.w.) alichinja mnyama wake Hudaybiya, alipozuiliwana washirikina kuzuru Nyumba tukufu (Al Kaaba) ya Mwenyezi Mungu

Page 133: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

123

Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi, au ana adha kichwanimwake, basi atoe fidia kwa kufunga au sadaka au kuchinja mnyama.

Yaani ikiwa mwenye kuhirimia atanyoa kichwa chake kwa dharura, basi nijuu yake kutoa kafara kwa kuwa na hiyari baina ya kufunga siku tatu,kuwalisha maskini sitini au kuchinja mnyama; kwa uchache awe ni mbuzi.

Na mtakapokuwa salama, basi mwenye kujistarehesha kwa kufanyaumra, kisha akahiji, achinje mnyama aliyewepesi kumpatia.

Yaani mtu asiyekuwa na kizuizi, akafanya umra kisha akahiji baadae kati-ka mwaka huo huo, basi ni juu yake kuchinja mnyama. Hii ndiyo aina yahijja inayojulikana kwa jina la Haj Tamattui (hijja ya starehe) ambayo niwajibu kwa wasiokuwa watu wa Makka. Imeitwa hijja ya starehe, kwasababu mwenye kuhiji baada ya kumaliza amali za umra anatoka kwenyemiko ya umra mpaka aje ahirimie hijja.

Na asiyepata, ni kufunga siku tatu katika hijja na siku saba mtakaporudi;hizo ni siku kumi kamili.

Imam Jafar Sadiq (a.s.) amesema: Mwenye kufanya Hajj Tamattu, asipopatamnyama, atafunga siku tatu katika hijja - siku ya saba, ya nane na ya tisa kati-ka Dhul-Hijja (Mfungo tatu) wala hakuna sharti la iqama, na siku saba atafun-ga atakaporudi kwa watu wake. Hizo ni siku kumi kamili za kutosheleza mnya-ma.

Hayo ni kwa yule ambaye watu wake hawako karibu na msikitimtakatifu.

Mwenye Majmaul - Bayan amesema kuwa hayo yaliyotangulia kutajwa katikatamattui ya umra kisha hijja, sio kwa watu wa Makka na walio karibu yake,bali ni kwa ambaye hayuko Makka: yule ambaye yuko mbali na Makka kwazaidi ya maili kumi na mbili (12) kwa kila upande.

Mafakihi wa Kishia Imamiyya wamesema: hajj tamattui ni wajibu kwawalio mbali na Makka, wala haimjuzii yeye kuhiji hijja qiran na ifrad,kwani hizo ni wajibu kwa watu wa Makka na wa kando kando yake. Na

Page 134: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

124

wao haijuzu kwao kuhiji hajj tamattui. Kwa ufafanuzi zaidi angalia vitabuvya Fiqhi.

Hijja ni miezi maalum.

Nayo ni kuanzia Shawwal, Dhul-qaad na kumi la mwanzo la Dhul-Hijja.(Mfunguo mosi, Mfunguo pili na Mfunguo tatu) Mwenye kuhirimia kablayake, hijja yake haitaswihi; na mwenye kuhirimia ndani ya miezi hiyo,itaswihi na ataleta amali zilizobakia.

Na anayejilazimisha kufanya hijja katika miezi hiyo, basi hakunakuingiliana na wanawake wala kutoka katika mipaka wala mabis-hano katika hijja.

Makusudio ya kuingiliana na wanawake hapa ni kujamii. Mtu akimjamiimkewe na huku amehirimia hijja, basi hijja yake imeharibika, sawa sawana aliyejamii au kula huku akiwa amefunga. Kwa hivyo atakamilisha hijjayake, kisha aje alipe mwaka ujao; kama ilivyo kwa mwenye kuiharibuSaumu yake Ramadhani.

Makusudio ya kutoka katika mipaka (ufuska), ni uwongo na kutukana.

Ama kuhusu mabishano, riwaya za Ahlul Bait zinasema, kwamba hilo ni mtukusema: “Hapana wallahi” au “Kwa nini, wallahi” n.k.

Si vibaya kwenu kutafuta riziki ya Mola wenu

Kwa vile wakati wa ujahiliya watu walikuwa wakifanya biashara nakuchuma siku za hijja, kulidhaniwa kuwa ni haramu. Ndipo MwenyeziMungu (s.w.t.), akaondoa tuhuma, hii na akabainisha kwamba kuchumahakupingani na ikhlasi katika amali za hijja.

Na mtakapomiminika kutoka Arafa, mtajeni Mwenyezi Mungu katikaMash’aril - Haram

Page 135: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

125

Arafa ni mahali maalum. Kumiminika kutoka Arafa ni kuondoka,Mash’aril-Haram ndipo pale panajulikana kama Muzdalifa; na kutua haponi wajibu, kama ilivyo kwa Arafa.

Kisha miminikeni kutoka mahali wamiminikapo watu (wote)

Inasemekana kuwa Makureshi walikuwa hawatui Arafa pamoja na watuwengine kwa kiburi tu; ndipo Mwenyezi Mungu akamwamrisha MtumeWake kutua hapo, na kutoka pamoja na watu, ili abatilishe waliyokuwawakiyafanya Makureshi.

Na mmalizapo kuzitimiza ibada zenu, basi mtajeni Mwenyezi Mungukama mlivyokuwa mkiwataja baba zenu; bali mtajeni zaidi.

Imepokuwa kutoka kwa Imam Baqir baba wa Imam Sadiq (a.s.) kwambawatu walikuwa wanapomaliza Hijja wanakusanyika huko na kuwatajawazazi wao kwa fahari, ndipo Mwenyezi Mungu akawaamrisha kuliachahilo na badala yake wamtaje Mwenyezi Mungu na jinsi alivyowaneeme-sha. Kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuwaneemesha wao na mababa zao.

Na kuna baadhi ya watu wasemao: Mola wetu! Tupe (mema) hapaduniani; nao katika Akhera hawana fungu lolote. Na miongoni mwaokuna asemaye: Mola wetu! Tupe mema duniani na (tupe) memaAkhera, na utukinge na adhabu ya moto. Hao ndio wenye fungu kati-ka waliyoyachuma, na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.

Watu katika hijja zao wako aina mbili. Aina ya kwanza ni ile ya asiyetakalolote isipokuwa starehe ya dunia, na hana hamu yoyote isipokuwa duniatu, na anapomwabudu Mwenyezi Mungu humwabudu kwa ajili ya dunia.Aina hii ndio wenye kunyimwa neema ya Akhera. Ama aina ya pili ni yuleya anayetaka kheri ya dunia na akhera, na anaifanyia amali dunia yake naAkhera yake. Huyu ndiye mwenye radhi mbele ya Mwenyezi MunguKesho kwa kulipwa amali zake njema.

Page 136: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

126

Mwenye Tafsir Rawhul - Bayan amenukuu kutoka kwa Imam Ali bin AbiTwalib (a.s.) kwamba wema katika dunia ni ‘mwanamke mwema’ na kati-ka Akhera ni ‘hurulain’. Ama adhabu ya Moto ‘makusudio yake nimwanamke muovu’.

Iwe ni sahihi Hadith hiyo au la, lakini mimi najua kuna watu wanaohisi, ndaniya nyoyo zao kwamba lau wao wangekuwa katika Jahanam, kisha wakahi-yarishwa kutoka katika Jahanam na warudi kwa wake zao waliokuwa naoduniani au wabaki Jahannam, basi wangelichagua kubaki katika Jahannamkuliko kuishi tena na wake zao hao, ambao Mwenyezi Mungu , badala yao,amewapa walio wazuri kuliko wao.

Na mtajeni Mwenyezi Mungu katika siku zinazohisabiwa

Makusudio yake ni siku tatu za tashriq; nazo ni: tarehe kumi na moja,kumi na mbili na kumi na tatu katika mwezi wa Dhul-Hijja (Mfunguotatu).

Si wajibu kwa mwenye kuhiji kulala Mina usiku wa kumi na tatu, lakinikwa sharti ya kuwa atoke Mina siku ya kumi na mbili baada ya kupindukajua, na kabla ya magharibi, na awe hakuvunja miko ya kuwinda au kujamii.Kwa hali hiyo ndipo tunapopata tafsiri ya kauli Yake Mwenyezi Mungu:

Na mwenye kufanya haraka katika siku mbili, basi si dhambi juuyake; na mwenye kukawia pia si dhambi juu yake, kwa mwenye kum-cha (Mwenyezi Mungu).

Yaani mwenye kuacha kuwinda na mwenye kuacha wanawake katika ihra-mu yake.

Ikiwa amevunja miko kwa kulala na mke au kuwinda, au alichwelewa najua siku ya kumi na mbili akiwa yuko Mina, basi itakuwa wajibu kwakekulala usiku wa kumi na tatu na kutupia mawe vikuta vitatu (shetani) asub-uhi yake.

Page 137: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

127

204. Na katika watu kunaambaye kauli yake inaku-pendeza katika maisha yaduniani, nayehumshuhudiza MwenyeziMungu kwa yaliyo moyonimwake, na hali ni hasimumkubwa kabisa.

205. Na anapotawala hufanyabidii katika ardhi kufanyaufisadi, na huangamizamimea na viumbe, naMwenyezi Mungu hapendiufisadi.

206. Na anapoambiwa: McheMwenyezi Mungu, hupand-wa na mori wa kufanyadhambi. Basi Jahannaminamtosha, nayo ni makaomabaya mno .

207. Na katika watu yuko auzayenafsi yake kwa kutaka radhiya Mwenyezi Mungu, naMwenyezi Mungu ni Mpolekwa waja.

Page 138: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

128

KAULI ZAO ZINAKUPENDEZA

Aya 204 - 207

MAANA

Baadhi ya wafasiri wapya wamejaza kurasa kwa maneno matamu katikakufasiri Aya hizi, lakini hawakuzidisha chochote zaidi ya kuwagawanyawatu kwenye wema na uovu. Kwa dhahiri, haya yanajulikana na wote;hayahitaji ubainifu wowote, sikwambii tafsiri ndefu tena.

Unaweza: kuuliza; Ikiwa kugawanyika watu kunajulikana na wote, basikubainisha kunakuwa ni maelezo ambayo tayari yameshaelezwa, nakufafanua lililofafanuliwa, na yapasa kuyachukulia maneno ya MwenyeziMungu (s.w.t.) vizuri?

Jibu: Inawezekana kuwa makusudio ni kuongoza na kuelekeza, kwambamwenye akili anatakikana kutohadaiwa na dhahiri ya mambo, walaasimwamini mwenye kutengeneza maneno matamu. Kwa sababu wafisadi nimabingwa wa kazi hiyo na kazi ya ria. Kwa hivyo ni juu yetu kutomtege-mea yeyote isipokuwa baada ya kufanya majaribio na kupatikana dalili yaukweli wake na usafi wake.

Hiyo ndiyo asili ya ujumla inayoenea katika hukumu nyingi za dini na zakidunia; kama kuchagua hakimu, kadhi, naibu, au mufti na kila anayesi-mamia masilahi ya umma.

Ajabu ya maajabu ni kutakiwa shahada za elimu tu kwa mwenye kujitokezakwa kazi muhimu ya mji au nchi, na inayogusa maisha ya watu. Lakinihaulizwi uaminifu wake na tabia yake, pamoja na kuwa hayo ndio msingi.Wengi wenye shahada wanazitumia kuwa ni zana za kuibia.

Na katika watu kuna ambaye kauli yake inakupendeza katika maishaya duniani, naye humshuhudiza Mwenyezi Mungu kwa yaliyo moyonimwake, na hali ni hasimu mkubwa kabisa.

Page 139: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

129

Yaani wanadhihihirisha mapenzi na kheri, na hali wao ndio maadui zaidiwa kheri na watu wa kheri.

Na anapotawala hufanya bidii katika ardhi kufanya ufisadi

Wamehitilafiana wafasiri kuhusu neno tawalla. Je makusudio ni ‘kuon-doka’ ambapo maana yake itakuwa ni: anapoondoka kwa yule aliyemdan-ganya, ‘huhangaika katika ardhi kwa ufisadi? Au kwamba makusudio ni‘kutawala na usultani’ambapo,itakuwa: maana yake, ‘Na atakapokuwamtawala, atafanya wanayoyafanya watawala waovu ya kuangamiza mimeana viumbe’?

Mwenye Tafsir Al - Manar amenakili kutoka kwa ustadhi wake, SheikhMuhammad Abduh, kwamba ameyapa nguvu maana ya utawala kwakuunganisha na kauli Yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "Na anapoambiwa:Mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wa kufanya dhambi;" kwamaana ya kuwa mtawala mkaidi anakuwa na kiburi kuongozwa kwenyemaslahi, au kupewa tahadhari ya mambo ya ufisadi. Yeye hujiona yuko juuya haki, kama vile alivyo juu ya watu wake anaowatawala, basiitawezekanaje kwa mtu kumwambia amwogope Mwenyezi Mungu?

Na huangamiza mimea na viumbe

Mimea ni kilimo na viumbe ni wanyama. Makusudio ni maslahi yote yakiuchumi katika kilimo, viwanda na ufugaji, mali ghafi, na mengineyoyanayohusika na uhai wa watu na maisha yao. Mwenyezi Mungu amehu-sisha kutaja kilimo na ufugaji kwa vile viwanda wakati huo havikuwa naumuhimu wowote kama ilivyo sasa.

Uharamu wa mambo hayo, kwa mtazamo wa Uislamu, ni sawa na uhara-mu wa kumwaga damu; na mwenye kukusudia ubaya katika vitu hivyo,ndio amekusudia ubaya wa utu hasa, hata kama vitu hivyo ni milki ya aduianayepiga vita Waislamu. Mtume (s.a.w.w.) amekataza kukata miti,kuharibu mimea na majengo, na kutia sumu miji ya washirikina siku zavita, n.k. Lau tunailinganisha sharia ya Kiislamu na mambo yanayofanywa

Page 140: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

130

leo na dola za kikoloni, na vita vyao vya silaha za kemikali kwenyemimea, watu na wanyama, na kuitia sumu anga kwa mabomu ya atomikina kuyatupa kwa wanawake na watoto - lau hayo yote tunayalinganisha naUislamu, basi tutajua huruma, uadilifu na utu wa Uislamu na unyama wadola za Magharibi na jinsi zilivyopetuka mipaka katika dhuluma naunyang'anyi.

Na Mwenyezi Mungu hapendi ufisadi.

Hakuna ufisadi mkubwa zaidi ya kuzusha vita na kutumia silaha zenyekubomoa ili kuwatawala watu, na kuwanyang'anya chakula na matundaya jasho lao.

Na anapoambiwa: Mche Mwenyezi Mungu, hupandwa na mori wakufanya dhambi

Mtu mwema mwenye ikhlasi hukubali masahihisho na nasaha; bali huz-itafuta na kuzikaribisha, kwa sababu yeye hana lengo jengine zaidi yahaki, wala hatafuti sifa, kwa sababu amali yake ni kwa ajili yaMwenyezi Mungu (s.w.t.), sio umashuhuri. Imam Amirul Muminin (a.s.)anasema katika maneno anayowasifia wanaomcha Mwenyezi Mungu:

"Hawaridhiki na amali zao chache, wala hawakioni kingi kilicho kingi.Wao hujituhumu nafsi zao, na ni wanyenyekevu katika amali zao."

Katika hotuba yake siku za Ukhalifa wake alisema:

"Mtu, hata kama ana cheo kikubwa vipi katika haki, na fadhila kubwa vipikatika dini, hawezi kuwa hahitajii kusaidiwa katika haki zake alizobebeshwana Mwenyezi Mungu; wala mtu, hata kama nafsi zinamfanya mdogo vipi nakudharauliwa na macho vipi, sio kuwa hawezi kusaidia au kusaidiwa...Wala msinidhanie kuwa mimi ni mzito katika haki nitakayoambiwa, wala nimwenye kutaka kujitukuza, kwani mwenye kuifanya nzito haki atakayoam-biwa au uadilifu atakaooneshwa, basi kwake kuitumia haki na uadilifu nikuzito zaidi."

Page 141: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

131

Hivyo ndivyo anavyotakikana mwanachuoni mwenye ikhlasi ya kwelikuwa. Ama mnafiki mwenye hiana,neno la haki huwa zito kwake kwasababu litamfedhehesha; na hununua sifa za uwongo kwa thamani kubwaili azibe upungufu wake na uovu wake.”

Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi yaMwenyezi Mungu

Yaani baadhi ya waumini wanaikabili jihadi, na wanapenda mauti kwa ajiliya Mwenyezi Mungu, kama wale wengine wanavyopenda uhai. Hawanalengo jengine isipokuwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na thawabuZake.

Razi, katika kutafsiri Aya hii, anasema kuhusu sababu za kushuka kwakekuwa kuna riwaya tatu: mojawayo ni kwamba Aya hii imeshuka kwasababu ya Ali bin Abi Twalib (a.s.) alipolala kwenye kitanda cha Mtumewakati wa Hijra, akasimama Jibril kichwani kwake, Mikail miguunimwake na huku Jibril ananadi: Pongezi! Pongezi! ewe Ali! MwenyeziMungu anajionea fahari kwako, mbele ya Malalika. * 6

* 6 Sheikh Mudhaffar katika kitabu Dalailu Swidq J2 anasema; “Wale ambao wamenakilikuwa Aya hii imeshuka kwa haki ya Ali, ni Razi, Thaalabi na mwenye Yanabiul Mawadda, AbuSa’adaat katika Fadhail Itrati Twahira, Ghazali katika Ihyai, Hakim katika Mustadrak naAhmad bin Hambal katika Musnad yake. mbali riwaya nyingine zilizopokewa kwa upande waShia.

Page 142: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

132

208. Enyi mlioamini! Ingienikatika usalama nyote,wala msifuate nyayo zaShetani. Kwa hakika yeyekwenu ni adui aliye wazi.

209. Na kama mkiteleza baada yakuwafikia ubainifu, basi juenikwamba Mwenyezi Mungu niMwenye nguvu, Mwenyehekima.

210. Hawangoji ila kuwafikia(adhabu ya) MwenyeziMungu katika vivuli vyamawingu na Malaika, nahali mambo yamekwisha; namambo yote hurudishwakwa Mwenyezi Mungu.

Page 143: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

133

INGIENI KATIKA USALAMA NYOTE

Aya 208 - 210

MAANA

Enyi mlioamini! Ingieni katika usalama nyote

Imesemekana kuwa makusudio ya neno silmi hapa ni Uislamu, na kwambamaneno haya wanaambiwa wanafiki ambao wameificha kufuru na kudhi-hirisha Uislamu. Na imesemekana pia kuwa wanaambiwa wenye kumwami-ni Mwenyezi Mungu katika waliopewa Kitabu ambao hawakusilimu. Naimesemekana kuwa wanaambiwa Waislamu wote. Kwa hivyo maana yakeyanakuwa ni kumtii Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea katika hukumuZake zote, sio baadhi tu. Na pia imesemekana kuwa maana yake ni suluhukwa maana ya kuwa: Ingieni katika suluhu nyote.

Tuonavyo sisi ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemwamrishamwenye kumwamini Mwenyezi Mungu imani iliyo sahihi kuingia katikalile ambalo mna salama yake ya dunia na Akhera. Na njia ya usalama ina-julikana na wote, nayo ni kusaidiana, kuungana, na kuacha vita nauhasama. Vile vile kuyashinda matamanio na hawaa, na hawaa, na kuwana ikhlasi katika kauli na vitendo.

Makusudio ya maana hayo yanatiliwa nguvu na kauli Yake MwenyeziMungu:Wala msifuate nyayo za shetani. Kwa hakika yeye kwenu niadui, aliye wazi: aliyoileta mara tu, baada ya kusema Ingieni katikausalama nyote.

Hapo Mwenyezi Mungu amezingatia kuwa nyayo za Shetani kinyumechake ni usalama; na amemweka mtu mbele ya mambo mawili tu, haku-na la tatu: ama kuingia katika usalama, au kufuata nyayo za Shetaniambazo ndio dhati ya uovu, ugomvi, shari na ufisadi.

Page 144: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

134

Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu, basi jueni yakwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kuingia katika usalama nakukataza kufuatwa nyayo za Shetani, amemhadharisha na kumtisha yuleatakayehalifu amri Yake na makatazo Yake kwa kusema: Basi jueni kwam-ba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.Mwenye nguvu,hashindwi katika amri yake, wala hakimzuwii chochote kwa alilokusudiakulifanya. Na Mwenye hekima humlipa mema mtiifu na humwadhibu asi.

Razi anasema: "Huo ndio ukomo wa kiaga kwa sababu ni kuhofisha bilaya kutaja adhabu. Huenda mzazi akamwambia mtoto wake: "Ukiniasi basiwewe wanijua, na wajua, uweza wangu kwako. Maneno hayo yakawa nimakemeo ya ufasaha zaidi kuliko kutaja kipigo na mengineyo.”

Hawangoji ila kuwafikia (adhabu ya) Mwenyezi Mungu katika vivulivya mawingu na Malaika.

Maana kwa ujumla ni kwamba wale wenye kukadhibisha na kuasi wataji-wa na adhabu kwa ghafla, wala hawataokoka.

Aya iko katika mwelekeo wa Aya inayosema:

"Na hawangoji ila Saa (ya Kiyama) iwajie kwa ghafla...?" (47:18).

Na hali mabo yamekwisha; na mambo yote hurudishwa kwaMwenyezi Mungu.

Mauti, ambayo hayana budi kuja, yakija, na Kiyama kikaja, kila kitu kitako-ma kimekwisha na hapatabakia, wala mbele ya wenye makosa, isipokuwahesabu na mateso.

Page 145: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

135

SIRI NA MATUKIO YA GHAFLA

Hakuna yeyote ajuaye yatakayomtokea mbele na siri ya wakati, heri aushari. Hawezi kuyajua hayo vyovyote atakavyokuwa na elimu au imani:

"Na nafsi yoyote haijui itachuma nini kesho." (31:34)

Mara nyingi mtu hujiwa na heri kwa ghafla wakati yeye anatazamia kupa-ta shari; na hujiwa ghafla na shari wakati anapotazamia heri. Hakuna kitukinachotia uchungu kama hicho cha kupata shari wakati wa kutazamiaheri; kama vile ambavyo hakuna kitu kitamu kama kupata heri wakati wakutazamia shari.

Mwenye akili hawezi kughurika na alivyo navyo, bali hufikiria mzun-guko wa zama; kama vile ambavyo hakati tamaa na lolote linalompata;kwani dunia inageuka milele; ndio maana ikasemwa; "Kudumu hali nimuhali na faraja inakuja kutokana na dhiki." Imam Ali (a.s.) anasema:"Baada ya dhiki ni faraja.

Anaendelea kusema Imam:"Hakika Musa bin Imran alitoka kuwatafutia watu wake moto

akasemeshwa na Mwenyezi Mungu na akarudi akiwa Mtume.

"Mwenyezi Mungu anasema:

"...Hawakati tamaa: “...ya rehema ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watumakafiri." (12:87).

Page 146: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

136

Na amesema tena: ... Hawajiaminishi na mipango ya Mwenyezi Munguila watu wenye hasara." (7:99).

Imeelezwa katika vitabu vya Historia na Sera kwamba Ibn Ziyat alikuwawaziri na Wathiq’s Mu'tasim; naye alikuwa ni katika mataghuti wa haliya juu na dhalimu mkubwa. Alitengeneza tanuri la chuma alilolijaza mis-umari yenye ncha pambizoni mwake.Alipokuwa akimkasirikia mtu,alikuwa akimtupa humo; kila alivyojitingisha ndivyo misumari ilivy-omwingia mwilini mwake.

Mutawakkil alipotawala, alimshika Ibn Ziyat na akamfunga kwa chumamikononi mwake na miguuni mwake, kisha akamtupa katika tanuri hilo, nabaadaye akafa. Kabla ya kufa alisikika akiimba shairi hili:Sifazake tulia, hebu nenda pole pole, Kigeugeu dunia, huenda nyuma na mbele.

211. Waulize wana wa Israili niishara ngapi zilizo wazi tulizo-wapa? Na anayezibadilishaneema za Mwenyezi Mungubaada ya kumfikia, basihakika Mwenyezi Mungu niMkali wa kuadhibu.

212. Wamepambiwa makafirimaisha ya duniani, nawanawafanyia maskharawale walioamini. Na walewanaomcha (MwenyeziMungu) watakuwa juu yaoSiku ya Kiyama. NaMwenyezi Mungu hum-ruzuku amtakaye bilahesabu.

Page 147: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

137

WAULIZE WANA WA ISRAILI

Aya 211 - 212

MAANA

Waulize wana wa Israili, ni ishara ngapi zilizo wazi tulizowapa?

Makusudio ya waulize hapa sio swali hasa, kwa sababu Mtume (s.a.w.)anajua hali zao; wala makusudio sio kuelezea hali waliyokuwa nayo,kama ilivyo katika Aya ya 49 na inayofuatia. Makusudio hasa ni kuwaWaislamu wazingatie na wawaidhike kwa hali ya Waisraili.

Njia ya kuwaidhika ni kuwa Waisraili walijiwa na Mtume Musa (a.s). kwamiujiza na ishara ambazo ni mkono kuwa mweupe, fimbo kugeukanyoka, na kupasuka bahari. Vile vile kufunikwa na wingu, kuteremshiwamanna na salwa, na jabali kutoka maji. Pamoja na hayo yote waliasi nakukhalifu! Ndipo Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa madhila na utwe-vu katika dunia, na adhabu iumizayo huko Akhera.

Waislamu nao wamejiwa na Muhammad (s.a.w.w.) kwa miujiza na hojazinazofahamisha ukweli wa Utume wake, ishara na kuswihi sharia yake.Naye akawafikilizia habari kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa waingiekatika Uislamu wote, kwani humo watapata kheri na utengeneo wao.Kama wakiasi, kama walivyofanya Waisraili, basi yatawapata yaliy-owapata Waisraili.

Na anayezibadilisha neema za Mwenyezi Mungu baada ya kumfikia,basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.

Makusudio ya neema hapa ni dalili za haki, kwani hizo ni katika neemakubwa kwa sababu ndani yake mna uongofu, na kuokoka na kuhiliki naupotevu.

Makusudio ya kuzibadilisha ni kuziasi na kuziharibu. Kwa hiyo kauli yakeMwenyezi Mungu (s.w.t.): Na anayezibadilisha neema za MwenyeziMungu baada ya kumfikia” ni sawa na kauli Yake:

Page 148: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

138

"Na kama mkiteleza baada ya kuwafikia ubainifu..." (2:209).

Vile vile kusema Kwake:Basi hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu ni sawa na kusema:

“Kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye hekima." (2:209)

Maana ni moja na lengo ni moja.

HAPANA IMANI BILA (UCHA MUNGU)

Wamepambiwa makafiri maisha ya duniani

Hapana tofauti kabisa kati ya mwenye kukanusha kuwako MwenyeziMungu na yule mwenye kuamini kinadharia tu, akawa anaifadhili duniayake kuliko Akhera yake. Hapana tofauti abadan kati ya wawili hao, kwasababu kila mmoja wao amefitinika na dunia na vipambo vyake, naameathirika na kitu cha sasa hivi kuliko cha muda ujao; kheri na fadhilaamezipima kwa kipimo cha manufaa yake binafsi, wala hakuyapa na mamboaliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu wala misimamo ya kitu.

Mimi kila ninavyozidi kuzama katika tafsiri ya Qur'ani, na kuangalia kwaundani Aya zake, huzidi yakini kwamba imani bila ya ucha Mungu hainamaana yoyote; na kwamba kila anayeiangalia dunia kuwa ndio makusudioyake yote, basi atakuwa ameiweka mbali sharia ya haki na dini, atake asitake.

Na matokeo yasiyoepukika, ya tangulizi mbili hizi ni kwamba mwenyekumkanusha Mungu na mwenye kumwamini ni sawa maadamu huyo‘muumini’ anaifadhili dunia yake kuliko dini yake, wala haiipi uzito wowotekwa maneno yake na vitendo vyake.

Page 149: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

139

Imekuja Hadith mutawatir kutoka kwa Mtume mtukufu (s.a.w.w.) akisema:"Dunia na Akhera zina madhara." Yaani zinadhuriana; kuihujumu moja yao nikuiacha nyingine. * 8

Imam Ali (a.s.) anasema: "Hakika dunia na Akhera ni maadui wawiliwanaotofautiana, na ni njia mbili tofauti. Mwenye kuipenda dunia naakaitawalisha, ataichukia Akhera na kuwa adui yake. Zote mbili ni kamaMashariki na Magharibi; mwenye kutembea kati yazo huwa mbali nanyingine kila anapokaribia mojawapo."

Na wanawafanyia maskhara wale walioamini

Ni kawaida wale wanaozichezea hoja za Mwenyezi Mungu na hukumuZake, wakahalalisha damu na mali ya haramu - ni kawaida hao kuwadha-rau na kuwachezea wale wanaojilinda na maharamisho na kuvumilia tabuna mashaka kwa ajili ya kumridhisha Mwenyezi Mungu. Ni kawaida kwayule asiyeshughulikia isipokuwa maisha haya, kumdharau yuleanayeyashughulikia haya na ya baada ya kufa.

Na wale wanaomcha (Mwenyezi Mungu) watakuwa juu yao Siku yaKiyama

Amesema wale wanaomcha wala hakusema wale walioamini, kwa sababuimani bila ucha Mungu si lolote, kama tulivyobainisha.

Maana hapa yako wazi, ni kuwa makafiri wakiwadharau waumini hivisasa, basi mambo yatabadilika Kesho. Mwenyezi Mungu anasema:

"... Hakika fedheha na adhabu leo itawafika makafiri." (16:27).

* 8 Kuna Hadith nyingine inayosema: “Si mbora wenu yule mwenye kuacha dunia kwa Akhera,wala Akhera kwa dunia, lakini mbora wenu ni yule atakayechukua hii na hii . Mumini mwenyenguvu ni bora na anapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko Muumini dhaifu.”.

Page 150: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

140

"Basi leo wale ambao wameamini wanawacheka makafiri."(83:34)

Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.

Riziki ni mbili: riziki ya duniani na riziki ya Akhera. Riziki ya dunia ina-julikana, na riziki ya Akhera, ni ‘neema isiyokatika, na isiyokuwa nachembe ya huzuni au hofu; hataipata yeyote isipokuwa kwa imani na amalinjema. Anasema Mwenyezi Mungu:

"Na wale walioamini wakatenda mema, hao ndio watu wa Peponi. Humowatakaa milele." (2:82).

Ama riziki huipata duniani, na kafiri na Muumini, mwema au mwovu, naanayehangaika au asiyehangaika; kama vile urithi, zawadi, wasiya, n.k.Vile vile inaweza kupatikana kwa njia ya halali,na ni ya haramu, kamavile kunyang'anya, kughushi na utapeli.

Mwenye Tafsir Al-Manar amenakili kutoka kwa mwalimu wake SheikhMuhammad Abduh, kwamba amesema wakati wa kutafsiri Aya hii,kwamba riziki bila ya kuhangaika inaweza ikapatikana kwa baadhi yawatu. Ama kwa umma; ni muhali kujitosheleza isipokuwa kwa kuhangai-ka na kufanya kazi. Huo ni ukweli ulio wazi kabisa.

Page 151: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

141

213. Watu wote walikuwa milamoja. Basi MwenyeziMungu akapeleka Manabiiwatoa - bishara na waonyaji.Na pamoja nao akawa-teremshia kitabu kina-choshikamana na haki ilikihukumu baina ya watukatika yale waliyohitilafiana.Na hawakuhitilafiana katikahayo ila wale waliopewaKitabu, baada ya kuwafikiaubainifu, kwa sababu ya uha-sidi baina yao. NdipoMwenyezi Mungu akawa-ongoza walioamini haki waliy-ohitilafiana kwa idhini Yake.Na Mwenyezi Mungu hum-wongoza amtakaye kwenyenjia iliyonyooka.

WATU WOTE WALIKUWA MILA MOJA

Aya 213

LUGHA

Mwenyezi Mungu amelitumia tamko umma katika Kitabu Chake kwamaana nyingi. Miongoni mwake ni mila Mwenyezi Mungu anasema:

Page 152: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

142

"Hakika mila yenu hii ni mila moja." (21:92)

Au kwa maana ya kundi. Mwenyezi Mungu anasema:

"Na katika wale tuliowaumba wako watu wanaoongoza kwa haki tu...(7:181).

Pia limekuja kwa maana ya muda; kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu(s.w.t.):

"Na kama tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda uliokwisha hisabi-wa..." (11:8).

Vile vile kwa maana ya Imam anayefuatwa - Mwenyezi Mungu anase-ma:

"Hakika Ibrahim alikuwa mfano (wa kufuatwa) mnyenyekevu kwaMwenyezi Mungu..." (16:120).

Ama makusudio ya neno umma katika Aya hii tunayoifasiri, ni ‘mila’.

Page 153: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

143

MAANA

Kauli za wafasiri zimegongana katika kuelezea maana ya Aya hii. Raziameifafanua kwa kiasi cha kurasa saba. Ama mwenye Tafsir Al - Manar ,yeye ameifafanua kwa kurasa ishirini na mbili na kumwacha msomaji wakawaida patupu, bila ya kuambua chochote. Na sisi, kama kawaida yetu,tumo katika njia yetu ya kumfanyia wepesi yule msomaji wa kawaida,kwa kiasi kile kitakachoafikiana naye. Kwa hivyo ufafanuzi wake ni kwauwazi na ufupi, ili aweze kuangalia vizuri Aya za Mwenyezi Mungu kwawepesi na kuathirika nafsi yake. Kama kutakuwa na maudhui muhimu,basi tutayaeleza katika kifungu cha peke yake.

Watu wote walikuwa mila moja.

Yaani walikuwa wa umbile ambalo Mwenyezi Mungu amewaumbia watu,na ambalo Mtume (s.a.w.w.) ameliashiria kwa kusema: "Kila anayezali-wa huzaliwa kwenye fitra (umbile la usawa)." Mwenye Majmaul - Bayananasema: "Masahaba wetu wamepokea kutoka kwa Imam Abu Jafar alBaqir, kwamba, kabla ya Nuh, * 8 watu walikuwa mila moja ya umbilealilowaumba Mwenyezi Mungu - si wenye kuongoka walakupotea;.Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume. Kwa haya maanayake itakuwa kwamba wao walikuwa ni wenye kuabudu kulingana na akilizao, bila ya uongofu wa Mitume wala sharia."

Kisha wakajiliwa na mawazo na fikra ambazo ziliwapeleka katika tofautiya itikadi na rai, hatimaye kwenye uadui wa wao kwa wao. Kwa hivyowakagawanyika vikundi vikundi baada ya kuwa ni wa mila moja.Mwenyezi Mungu akawapelekea Mitume na Vitabu vinavysema kweli navinavyohukumu mizozo yao. Haya ndiyo maana yaliyo wazi ya kauliYake Mwenyezi Mungu:

Basi Mwenyezi Mungu akapeleka Manabii watoa - bishara nawaonyaji. * 8 Imeelezwa katika Tafsir Rawhul-bayan kwamba baina ya Adam na kupewa utume Nuh kunakiasi cha miaka themanini (80)

Page 154: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

144

Na pamoja nao akawateremshia Kitabu kilichoshikamana na haki ilikihukumu baina ya watu katika yale waliyohitilafiana.”

Hapa inatubainikia kwamba katika maneno kuna jumla iliyokadiriwaambayo ni : "Watu wote walikuwa mila moja kisha wakahitilafiana”

Linalofahamisha hilo ni kauli inayosema: "Ili kihukumu baina ya watukatika yale waliyohitilafiana." Na hilo linatiliwa nguvu na kauli hii:

"Na watu hawakuwa isipokuwa mila moja; kisha wakahitilafi-ana..."(10:19).

Na hawakuhitilafiana katika hayo ila waliopewa Kitabu, baada yakuwafikia ubainifu, kwa sababu ya uhasidi baina yao

Yaani: Watu ambao walikuwa ni mila moja, kisha wakahitilafiana na Mwen-yezi Mungu akawapelekea Mitume, watu hao pia walihitilafiana Mitumehao; wengine waliamini na kusadiki, na wengine wakakufuru na kukad-hibisha baada ya kuthubutu hoja na dalili wazi za mkato. Hakuna sababu yoy-ote ya kukadhibisha huku isipokuwa uhasidi na kuhofia manufaa yao ya kib-inafsi na uadui.

Ndipo Mwenyezi Mungu akawaongoza alioamini katika hakiwaliyohitilafiana kwa idhini Yake.

Yaani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewafikisha wenye nia njema kwenyeimani ya haki aliyokuja nayo Mtume; na imani hiyo ni kwa amri YakeMwenyezi Mungu (s.w.t.) Kwa hivyo makusudio ya idhini ni ‘amri.’

Na Mwenyezi Mungu humwongoza amtakaye kwenye njia iliy-onyooka

Page 155: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

145

Katika kufasiri Aya ya 26 ya sura hii, kifungu cha ‘Uongofu na Upotevu’,tumetaja maana ya uongofu ambayo miongoni mwake ni: mtu kukubali mtunasaha na kuzitumia; na hayo ndiyo makusudio yake hapa. MwenyeziMungu (s.w.t.) huwaafikisha watu wema kukubali nasaha na kufanyavitendo vya haki na kheri.

TOFAUTI KATI YA WATU

Kulipatikana kutofautiana kati ya watu tangu Qabil alipomuua nduguye,Habil; kukaendelea hadi leo, na kutabaki hadi Siku ya Mwisho.Kutofautiana hakuhusiki na watu wa dini tu, kama wanavyodai wasio-jua hakika ya mambo. Ttunaona pia kutofautiana kusikokuwa kwa dinikumefikia hadi ya maneno kugeuka na kuwa vita vya kumalizana.Ugomvi kati ya dola za kibepari kumepelekea vita vya atomiki. Bomulilitupwa Hiroshima, kwa wanawake na watoto, na dola ya kibepari dhidiya dola nyingine ya kiberi pia. Na kugawanyika mwelekeo kwa dola zakiujamaa kunaeleweka. Vile vile dola za Kiafrika na Kiasia zinatofautianakulingana na upande wa wanyonyaji wanaozinyonya. Ama kutofautianakwa dola za Kiarabu, matokeo yake ni kupatikana Israel ndani ya nchiyao, na hatimaye kusalimu amri mnamo tarehe 5 Juni, 1967.

Hali yoyote iwayo, kutofautiana kuna sababu nyingi. Kati yazo ni: kuto-fautiana katika malezi na maendeleo, katika tabia na akili, na kutofautianakunakotokana na mgongano wa masilahi na manufaa ya kiutu.

Tofauti inayotokana na maendeleo, akili na tabia inaweza kurekebishwakwa kufanya yale yanayoafiki misingi iliyothibitishwa na elimu namajaribio. Lakini tofauti zinazotokana na kugongana kwa manufaa yakiutu hazina dawa isipokuwa kumzuwia adui kwa nguvu.

Maelezo yetu haya, ni kukamilisha tuliyoyasema katika kufasiri Aya ya113, kifungu cha "Kila mmoja anavutia dini yake."

Page 156: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

146

214. Au mnadhani kuwa mtaingiaPeponi na hali hamjajiwa namfano wa wale waliopitakabla yenu? Yaliwapatamashaka na madhara, nawakasukwasukwa hata akase-ma Mtume na wali-oaminipamoja naye: Nusura yaMwenyezi Mungu itafika lini?Jueni kuwa nusura yaMwenyezi Mungu iko karibu.

KUINGIA PEPONI

Aya 214

MAANA

Au mnadhani kuwa mtaingia Peponi na hali hamjajiwa na mfanowa wale waliopita kabla yenu? Yaliwapata mashaka na madhara

Hakika Aya hii tukufu inamwelekea kila mwenye kuamini haki, akaitu-mia na akailingania. Inamwambia waziwazi kwamba desturi yaMwenyezi Mungu kwa wanaoinusuru haki, ni kuitolea thamani yake waowenyewe, watu wao na hata mali zao. Vile vile wavumilie adha na kuwana subira juu ya masaibu na shida. Waliokuwa kabla yenu walipambanana aina kwa aina za maudhi wakasubiri. Je, nanyi mtasubiri kamawalivyosubiri? Au nyinyi mnataka kuingia Peponi bila ya kuilipiathamani? Mwenye Pepo hiyo amekataa isipokuwa thamani yake iwe niimani, ikhlasi na kuvumilia hofu, njaa na upungufu wa mali na nafsi!

Page 157: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

147

Yamekuja maelezo katika khutba mojawapo ya Nahjul Balagha:"Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akisema:‘Hakika Pepo imezungukwa na machukivu, na Moto umezungukwa naanasa. Na jueni kuwa hakuna kitu katika twaa ya Mwenyezi Munguisipokuwa huwa mna machukivu, na hakuna kitu katika maasia yaMwenyezi Mungu isipokuwa huwa mna anasa.’"

Kwa faida zaidi ni vizuri msomaji arudie tuliyoyataja katika kufasiri Ayaya 155, kifungu cha'Thamani ya Pepo.'

Na wakasukwasukwa hata akasema Mtume na walioamini pamojanaye: Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini?

Nusura ya Mwenyezi Mungu itafika lini, ni swali kutoka kwa Mtume nawaumini, linaloleta picha ya misukosuko na shida walizozipata kutokakwa maadui wa haki na makundi ya batili

Maana kwa ujumla ni kwamba wanusuru - haki waliotangulia walipatwa nashida na wakaingia katika misukosuko mpaka wakadhani kwamba nusuraimechelewa; hivyo wakaitaka ije haraka kwa kusema: Nusura ya MwenyeziMungu itafika lini? Mwenyezi Mungu naye akawajibu kwa kusema:

Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu iko karibu

Aya hii iko katika mwelekeo wa Aya isemayo:

"Hata Mitume walipokata tamaa, wakadhani ya kwamba wamekadhibish-wa, msaada wetu uliwajia..." (12:110)

Page 158: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarahah

148

215. Wanakuuliza watoe nini?Sema: Kheri yoyotemtakayotoa ni kwa ajili yawazazi wawili na akraba namayatima na maskini namwananjia. Na kheri yoyotemnayoifanya MwenyeziMungu anaijua.

WATOE NINI?Aya 215

MAANA

Wanakuuliza watoe nini?

Maneno haya anaambiwa Mtume (s.a.w.w.).

Sema: Kheri yoyote mtakayotoa ni kwa ajili ya wazazi wawili na akra-ba na mayatima na maskini na mwananjia.

Makusudio ya neno kheri hapa ni mali. Wazazi wawili ni baba mama, babuna bibi, kwa sababu wao wanaingia katika jina la wazazi wawili. Akrabani ndugu wa karibu wa mtoaji. Yatima ni kila asiyekuwa na baba namwana njia ni yule aliyeishiwa njiani na kushindwa kufika kwa watuwake, na wala hana chakula.

Unaweza kuuliza kuwa dhahiri ya Aya inaonesha kuwa watu waliulizaaina ya kitakachotolewa sio nani wa kumpa. Na jibu ni la matumizi, siola aina. Sasa je, imekuwaje?

Wafasiri wengi wamesema kuwa makusudio ya jawabu ni kumzinduamuulizaji kwamba yeye anatakikana kuuliza nani wa kumpa, sio nini

Page 159: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

149

atoe. Razi amemnakili Qafafal kwa jibu jingine; nalo nikuwa hata kamaswali liko kwa tamko la maa (nini) lakini kilichoulizwa ni nani wakumpa, sio cha kutoa, kwa sababu cha kutoa kinajulikana.

Sheikh Muhammad Abduh ameyatilia mkazo hayo kwa kauli yake:"Wasomi wa fani ya Mantiki ndio waliosema kuwa swali la maalinahusika na aina na jinsi..." Lakini Waarabu wanaitumia kwa nini naaina. Qur'ani haiendi kimfumo wa Aristotle na mantiki yake, isipokuwaiko katika mfumo wa lugha ya Kiarabu ulio wazi. Jibu hili lina nguvukuliko la kwanza ijapokuwa natija ni moja.

Swali la pili: Je kuwapa waliotajwa katika Aya hii, ni wajibu au sunna?

Jibu: Ni wajibu kwa wazazi kuwalisha watoto, na watoto kuwalishawazazi ikiwa upande mmoja una uwezo na mwengine hauna uwezo wakujilisha wenyewe. Kitolewacho hiki hakihesabiwi kuwa ni zaka. Kwasababu kuwapa wazazi na watoto ni wajibu mbali na wajibu wa zaka. Amamayatima na wasafiri na wananjia, inajuzu kuwapa kutokana na zaka yawajibu, kama vile ambavyo inajuzu kuwapa wote sadaka ya sunna.

Na sadaka ya suna hupewa kila mhitajia, awe Mwislamu au siMwislamu, kwa sababu kuna malipo katika kumnywesha kila mwenyeini la joto (kiu), kama ilivyoelezwa katika Hadith.

Page 160: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

150

216. Mmeandikiwa kupigana(vita) nalo ni (jambo) lakuchukiza kwenu. Na huen-da mkachukia kitu nacho nikheri kwenu, na huendamkapenda kitu nacho nishari kwenu. Na MwenyeziMungu anajua na nyinyihamjui.

217. Wanakuuliza juu ya kupi-gana (vita) katika mweziMtukufu. Sema: Kupiganavita katika (miezi) hiyo ni(dhambi) kubwa. Nakuzuilia watu na njia yaMwenyezi Mungu nakumkufuru na (kuwazuilia)Msikiti Mtukufu, na kuwa-toa wenyewe humo nikukubwa zaidi mbele yaMwenyezi Mungu. Na fitinani kubwa zaidi kuliko kuua.Wala hawataacha kupiganananyi mpaka wawatoe kati-ka dini yenu, kama waki-weza. Na yeyote katikanyinyi atakayertadi, kishaakafa hali ya kuwa kafiri,basi hao zimepomoka amalizao duniani na Akhera. Nahao ndio watu wa Motoni,humo watakaa milele.

Page 161: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

151

218. Hakika wale walioamini nawale waliohama na wakapi-gana jihadi katika njia yaMwenyezi Mungu, hao ndiowenye kutaraji rehema yaMwenyezi Mungu, naMwenyezi Mungu niMwenye kughufiria, Mwenyekurehemu.

MMEANDIKIWA KUPIGANA VITA

Aya 216 - 218

MAANA

Mmeandikiwa kupigana vita.

Mmeandikiwa hapa ni kwa maana ya ‘mmewajibishiwa.’

Mwenyezi Mungu amewajibisha vita kwa Waislamu si kwa kuwa vitavinapendeza au vinatakiwa mara kwa mara. Pia si kwa ajili ya kupanuanchi na kutawala au kunyonya mataifa mengine, isipokuwa ni kwa ajili yakuinusuru na kuitetea haki.

Haki, kama ilivyo, ni fikra na nadharia tu. Ama kuifuatilia na kulazimiananayo kunahitaji kazi ngumu ambayo, kwanza, ni kuilingania kwa heki-ma na kwa njia iliyozoeleka. Kama haikuwezekana, basi ni wajibukuitekeleza haki kwa nguvu. Nadharia yoyote isiyotegemea nguvu zakiutekelezaji, basi kuwepo kwake na kutokuwepo ni sawa.

Kwa ajili hii ndio Mwenyezi Mungu akawajibisha, katika Aya hii nanyinginezo, kupigana jihadi na kila adui wa haki, ikiwa hakuna faidakwake kumwamrisha mema na kumpa mawaidha mazuri. Lau si nguvu za

Page 162: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

152

kiutekelezaji, basi nguvu za kisharia zingekuwa ni maneno tuyanayosemwa mdomoni na kuandikwa.

Nalo ni (jambo) la kuchukiza kwenu. Na huenda mkachukia kitunacho ni kheri kwenu, na huenda mkapenda kitu nacho ni sharikwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamujui.

Wafasiri wamesema: Masahaba wa Mtume walichukia vita, kwa sababu nitabia ya mwanaadamu kuona uzito kujiingiza katika jambolitakalomwangamiza. Lakini, wakati huo huo, wanaitikia amri yaMwenyezi Mungu kwa kutaka radhi Yake; sawa na mgonjwa anayekun-ywa dawa kwa kutaka kupona. Na Mwenyezi Mungu amewazindua kwakuwambia: Huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu kwa kuwamatunda ya vita na jihadi yanawarudia wenyewe, na sio Mwenyezi Mungu.Huu ndio ufupi wa waliyoyasema wafasiri, na dhahiri ya matamshi inak-ubaliana nayo.

Lakini tukiwaangalia masahaba wenye ikhlasi na ushujaa katika jihadi,kujitolea kwao kwa ajili ya dini na jinsi dini ilivyotawala hisia zao. Vilevile tukiangalia jinsi walivyopuuza uhai kwa kutaka kufa mashahidi,mpaka ikawa anayeokoka vitani na kurudi salama anajiona ni mwovuasiye na maana - tukiangalia yote haya na kuyatia akilini mwetu, wakatitunaifasiri Aya hii, tutaona kuwa haielekei kwa masahaba, kamawalivyosema wafasiri hao, kuchukia vita, na kwamba hapana budikuifasiri Aya hii kwa maana nyingine itakayosaidia mazingatio, naitakayochukuana na matamko.

Kwa ufupi, maana yake ni kuwa masahaba walikuwa wakiogopa kuwaUislamu utamalizwa na washirikina kutokana na idadi yao kuwa kubwa naya Waislamu kuwa ndogo; kwamba wao, lau watapingana na makafiri kwanguvu, wataangamia kusibakie atakayeunusuru Uislamu, na mwito waKiislamu uende bure.

Kwa hivyo walichukia vita kwa kuhofia Uislamu, sio nafsi zao. NdipoMwenyezi Mungu akawabainishia kuwa vita wanavyoitiwa na

Page 163: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

153

kuvichukia ni bora kwao na kwa Uislamu, na kwamba kukaa tukutapelekea kumalizwa wao na Uislamu; na wao hawajui hakika hii,lakini Mwenyezi Mungu anajua, kwa sababu Kwake halijifichi lolote.

Aya hii inashabihiana sana na kauli Yake Mwenyezi Mungu:

"Ewe Mtume! Wahimize walioamini waende vitani. Wakipatikana kwenuwatu ishirini wanaosubiri watawashinda mia mbili. Na kama wakiwawatu mia moja kwenu watawashinda elfu moja ya wale waliokufuru,maana wao ni watu wasiofahamu." (8:65)

Wanakuuliza juu ya kupigana (vita) katika mwezi mtukufu. Sema:Kupigana (vita) katika (miezi) hiyo ni (dhambi) kubwa.

Yamekwishapita maelezo katika kufasiri Aya ya 192 na inayofuatia hiyo.

Na kuzuilia watu na njia ya Mwenyezi Mungu na kumkufuru na(kuwazuilia) Msikiti Mtukufu, na kuwatoa wenyewe humo ni kukub-wa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu

Waarabu walikuwa wakijizuilia kupigana katika miezi mitukufu ambayoni Dhul-Qaada, Dhul-Hijja, Muharram na Rajab (Mfunguo pili, Mfunguotatu, Mfunguo nne na Mfunguo kumi). Mtume naye akaithibitisha ada hii,kwa sababu inapunguza shari na umwagikaji wa damu. Kwa ujumlaUislamu umethibitisha kila ada nzuri au isiyokuwa mbaya iliyokuwawakati wa Jahiliya.

Lakini Waarabu, waliokuwa wakiitukuza na kuitakasa miezi hii, walivun-ja miko yake na wakatangaza vita na Mtume katika mwaka wa sitaHijriya; wakamzuwia pamoja na masahaba wake kuzuru

Page 164: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

154

Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu na kumfitini mwenye kusilimu;

wakawa wanamwadhibu kwa aina aina ya adhabu kwa muda wa miakakumi na tatu; kama walivyofanya kwa Bilal, Suhaib, Khabbab na Ammarbin Yasir pamoja na baba yake na mama yake.

Lakini Waislamu walipotaka kujikinga au kulipiza kisasi kwa washirikina,washirikina walianza kupiga mayowe kwa propaganda za upotevu,kwamba Waislamu wamevunja miko. Ndipo Mwenyezi Mungu (s.w.t.)akawabainishia kuwa makosa waliyoyafanya wao kwa Waislamu nimakubwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko kupigana katika miezimitukufu. Na kwa ajili hii Waislamu wamehalalishiwa kupigana nawashirikina mahali popote na wakati wowote watakapowapata kwakuchukua kisasi.

Na fitina ni kubwa zaidi kuliko kuua

Yaani kuwafitini Waislamu na dini yao, mara nyingine kwa kuwaadhibuna mara nyingine kwa kujaribu kuwatia shaka katika nyoyo zao, ni kubayazaidi kuliko kupigana katika miezi mitukufu.

Wala hawataacha kupigana nanyi mpaka wawatoe katika dini yenu,kama wakiweza.

Lengo la washirikina ni kutobakia athari yoyote ya Uislamu duniani. Nakwa ajili hii tu, ndio wanapigana na Waislamu, na wanaendelea kupigananao. Basi kama Waislamu watachukia kupigana na washirikina, lengo lamaadui litatimia.

Roho hii ya kikafiri ya kiadui, inaendelea mpaka leo popote pale penyeharufu ya Uislamu; inaendelea katika nafsi za wengi katika Mashariki naMagharibi. Sababu ya kwanza ya uadui kwa Uislamu ni utu wake, uadili-fu wake na kuzuia kwake dhulma na ufisadi. Kwa sababu hiyo ndiowanawakusudia kila shari na kuwapiga vita kwa nyenzo mbalimbali. Vilevile kuwafitini kulingana na hali ilivyo. Kwa hivyo ni juu yetu kuzindukana maadui hawa, na kuwapiga vita kwa silaha ile ile wanayotupiga nayo.

Page 165: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

155

Na yeyote katika nyinyi atakayeritadi, kisha akafa hali ya kuwakafiri, basi hao zimepomoka amali zao duniani na Akhera . Na haondio watu wa Motoni, humo watakaa milele.

Hii ni hadhari na tishio kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwamwenye kuwaitikia maadui wa dini na kutoka katika dini yake. kwa hilo,mtu huyo atapata hasara ya duniani na Akhera, na mwisho wake niJahannam ambayo ni marejeo mabaya.

Na kauli Yake Mwenyezi Mungu: Kisha akafa hali ya kuwa kafiri, inafa-hamisha wazi wazi kwamba mwenye kuritadi (kutoka katika dini), aki-tubia kabla ya kufa, Mwenyezi Mungu huikubali toba yake na huondoke-wa na adhabu; na akili inakubaliana na hilo. Lakini mafakihi wa Kishiawamesema: Ikiwa aliyeritadi ni mwanamume, na kutoka kwake kukawakunatokana na kuzaliwa; kisha akatubia, basi ataondokewa na adhabu yaAkhera tu. Ama ya duniani, ambayo ni kuuliwa, itakuwapo. Kama kuri-tadi kwake kunatokana na mila, basi hatauawa.* 9 Katika ufafanuzi huuwametegemea riwaya za Ahlul Bait (a.s.).

Maana ya kupomoka amali zao duniani ni kuwa wao watafanyiwa mua-mala wa kikafiri kuongezea kustahili kuuawa. Ama kupomoka amali zaohuko Akhera, ni adhabu na mateso.

Hakika wale walioamini na wale waliohama na wakapigana jihadi kati-ka njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wenye kutaraji rehema yaMwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria,Mwenye kurehemu.

Baada ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutaja hali ya washirikina nawaliotoka katika Uislamu, na kutaja adhabu yao, amefuatishia kutajawaumini na malipo yao.

* 9 Aliyeritadi kwa kuzaliwa ni kuwa; wazazi wake au mmoja wao ni Mwislamu, na murtadiwa mila ni kuwa wazazi wake ni makafiri, kisha yeye akasilimu baadaye akatoka kwenyeUislamu.

Page 166: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

156

Waliohama (muhajirina) ni wale waliohama kutoka Makka kwendaMadina pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na waliopi-gana jihadi ni wale waliofanya juhudi zao kuunusuru Uislamu na kupi-gana na maadui zake.

IBADA YA MWENYE KUTUBIA BAADA YA KURITADI (KUTOKAKATIKA UISLAMU)

Mwenye kutoka katika Uislamu (murtadi) akitubia na akarudi katikaUislamu kabla ya kufa, Mwenyezi Mungu humkubalia toba yake kwa huku-mu ya kiakili na kwa dhahiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): Kishaakafa hali ya kuwa kafiri alipounganisha kupomoka amali na kufa katikahali ya ukafiri.

Hapo basi yanakuja maswali mawili:

Swali la kwanza: Je, ibada zake kama vile swala, hijja, saumu na zaka,zitaswihi baada ya kurudi kwenye Uislamu au la?

Mafakihi wa Kisunni wameafikiana kuwa zinasihi na kukubaliwa.Mafakihi wa Kishia wameafikiana kwamba zinazokubaliwa ni za yulewa mila, na wamehitilafiana kuhusu za wa kuzaliwa. Wengi wao wame-sema haziswihi kwa hali yoyote, na kwamba Uislamu wake, baada ya kuu-toka, haumfai chochote duniani, bali atatendewa muamala anaofanyiwakafiri; isipokuwa Uislamu wake utamfaa Akhera tu, kwa kuondokewa naadhabu. Lakini wahakiki wa mambo katika wao, na sisi tu pamoja nao,wamesema: Bali zinaswihi ibada zake, na utamfaa Uislamu wake naatafanyiwa muamala wa Mwislam duniani na Akhera.

Swali la Pili: Je, Murtadi akirudi katika Uislam atalazimika kulipa ibadazake alizozifanya wakati alipokuwa Mwislamu kabla ya kurtadi. Laualikuwa ameswali na kuhiji, alipokuwa Mwislamu, kisha akaritadi, kishaakatubia, je ataswali tena na kuhiji baada ya kurudi Uislamuni?

Hanafi na Maliki wamesema kwamba atalazimika kulipa. Na Shafiiamesema kwamba hatalazimika.

Page 167: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

157

Ama mafakihi wa Kishia, walisema kuwa zinaswihi ibada za mwenyekutubia baada ya kuritadi, wao wanasema kuwa mtu hatalipa ibada yoy-ote aliyoifanya wakati ni Mwislamu, na kabla ya kuritadi; isipokuwa atal-ipa yaliyompita wakati wa kuwa ameritadi tu.

KUPOMOKA

Muutazila wamesema kuwa thawabu za muumini mtiifu zilizotanguliazinaanguka zote kwa maasia yatakayofuatia. Hata aliyeabudu umri wakewote, kisha akanywa tama moja tu la pombe, huwa ni kama ambayehakumwabudu Mwenyezi Mungu kabisa. Vile vile twaa inayofuatia inaon-doa madhambi yaliyotangulia; na hayo ndiyo maana ya kupomoka amali.

Shia Imamiya na Ash’ari wameafikiana kuwa hakuna kupomoka.Wamesema kuwa kila amali ina hesabu yake inayoihusu; wala twaa hai-fungamani na maasia, wala maasia na twaa, bali atakayefanya wema (hata)uzani wa sisimizi atauona, na atakayefanya shari uzani wa sisimizi piaatauona, Mwenye kufanya uovu na wema, akiwa muumini, MwenyeziMungu ataupima wema wake na uovu wake. Ikiwa uovu utazidi, atakuwakama ambaye hakufanya wema; na ikiwa wema utazidi, atakuwa kama hak-ufanya uovu, kwa sababu wingi unafuta uchache. Ikiwa yote ni sawa, basiatakuwa kama ambaye hakutokewa na lolote.

Kupomoka kuko mbali sana na maana haya. Maana yake ni ya sawamwenye kufa: akiwa kafiri baada ya kuwa Mwislamu, ukafiri wake huuutakuwa unafichua kwamba amali zake alizokuwa akizifanya wakati niMwislamu, hazikuwa katika njia inayotakikana kisharia, wala kustahikichochote tangu mwanzo; sio kwamba alistahiki thawabu kisha zikafutwa,bali hili ni katika upande wa kuzuwia sio kuondoa; yaani thawabuhazikuwepo.

Page 168: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

158

219. Wanakuuliza kuhusu ulevina kamari. Sema: Katikahivyo mna madhara makub-wa na manufaa kwa watuNa madhara yake ni makub-wa zaidi kuliko manufaayake. Na wanakuuliza watoenini? Sema: Vilivyowazidia.Namna hii Mwenyezi Munguanawabainishia Aya mpatekufikiri.

220. Duniani na Akhera. Nawanakuuliza kuhusu maya-tima. Sema:Kuwatengenezea ndiyokheri. Na kamamkichanganyika nao, basi nindugu zenu. Na MwenyeziMungu anamjua fisadi namtengenezaji. Na kamaangelitaka MwenyeziMungu, angeliwatia katikadhiki. Hakika MwenyeziMungu ni Mwenyenguvu,Mwenye hekima.

Page 169: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

159

ULEVI NA KAMARI

Aya 219 - 220

LUGHA

Limetumiwa neno khamr, lenye maana ya kufunika, kwa maana ya ulevi,kwa sababu ulevi unafunika akili. Na limetumiwa neno maysir, lenyemaana ya wepesi, kwa maana ya kamari, kwa sababu chumo la kamarilinakuwa jepesi bila ya jasho.

MAANA

Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari

Waliuliza baadhi ya Waislamu kuhusu hukumu ya ulevi na kamari katikaMadina; yaani zaidi ya miaka 13 tangu ulipoanza mwito wa Kiislamu. Hiyoinafahamisha kuwa hukumu Yake ilikuwa imenyamaziwa muda mrefu,kama zilivyonyamaziwa baadhi ya hukumu za haramu mpaka wakatiwake maalum, kulingana na masilahi. Mara nyingine kubainisha hukumukunataka hekima ya kuchukulia mambo pole pole.

Inasemekana kuwa ubainifu wa hukumu ya pombe ulikuwa hivi, kwasababu Waislamu walikuwa wameizoweya wakati wa Ujahiliya (kabla yakuja Uislamu); lau wangelizuiliwa mara moja tu, ingelikuwa uzito kwao.Bali Mwenyezi Mungu aliwakumbusha Waislamu walipokuwa Makkakwamba katika jumla ya neema Zake ni kwamba wao wanafanya ulevi nakupata riziki kutokana na tende na zabibu. Anasema Mwenyezi Mungu:

"Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi nariziki nzuri..." (16:67)

Page 170: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

160

Baadhi ya waislamu waliuliza kuhusu hukumu ya pombe na kamari,Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume Wake kuwajibu:

Katika hivyo mna madhara makubwa na manufaa kwa watu. Na mad-hara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake.

Jawabu hili peke yake halitoshi kuwa ni dalili ya wazi wazi ya uharamuwa ulevi, kwa sababu hakusema kuwa ulevi ni haramu. Linafahamisha tukawaida ya kujikinga na madhara ni bora kuliko kutengeneza maslahi, namuhimu inatanguliwa na muhimu zaidi.

Lakini tukiangalia Aya isemayo:

"Sema: Mola wangu ameharimisha mambo maovu yaliyodhihiri na yaliy-ofichika, na madhara na uasi pasipo haki..." (7:33)

tukaiunganisha na hii tunayoizungumzia, tutapata dalili ya kuharimishwaulevi waziwazi na kwa mkato, kwa sababu natija inayopatikana ni kuwa:ulevi ni madhara; na kila madhara ni haramu. Kwa hivyo ulevi ni haramu.Hiyo ni pamoja na kuongezea Aya inayosema:

"Enyi mlioamini! Hakika ulevi na kamari na masanamu na mishale ya kuti-zamia (ramli) ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo ilimpate kufaulu. Hakika Shetani anataka kuwatilia uadui na bughudhabaina yenu kwa ulevi na kamari, na kuwazuilia kumkumbuka MwenyeziMungu na kuswali. Basi je, mtaacha?" (5:90 - 91)

Page 171: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

161

Kwa hivyo kusema jiepusheni navyo ni amri ya kujiepusha, na amri inafa-hamisha wajibu. Na kusema basi je mtaacha? ni kukataza, na kukatazakunafahamisha uharamu. Ndipo Waislamu waliposikia Aya hii wakasema:"Tumeacha.

"Ama ile Aya inayosema:

"Enyi mlioamini! Msiikurubie swala hali mmelewa..."(4:43)

ilishuka kabla ya Aya (5:90-91), ambazo ni kali na zenye uzito mkubwazaidi, na tumeeleza kwamba huenda ilikuwa ni hekima ya kuchukulia mambopole pole katika kubainisha uharamu, kwa vile kutoikurubia swala halimmelewa haina dalili yoyote ya kuonyesha uhalali wa pombe nje ya.Tutayafafanua hayo nje ya inshaallah tutakapofikia Aya hizo.

Zaidi ya hayo, Waislamu wote- tangu mwanzo hadi hivi leo - wamekonga-mana kwa kauli moja tu kuwa ulevi ni katika madhambi makubwa, nakwamba mwenye kuuhalalisha siye Mwislamu. Na mwenye kuinywakwa kupuuza ni fasiki, na atapigwa (haddi) viboko thamanini.

Imekuja Hadith mutawatir kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwambaamemlaani mwenye kupanda mti wa (hiyo pombe), mwenye kuigema,anayeiuza, anayeinunua, anayewahudumia wanywaji, na mnywaji. Naimeelezwa katika baadhi ya Hadith kwamba hakuna sharia yoyote yambinguni ila imekataza ulevi.

Tumeyaeleza kwa ufafanuzi zaidi maudhui haya katika Juzuu ya Nne yakitabu Fiqhul Imam Jafar Sadiq katika Mlango wa Vyakula na Vinywaji.

Na madhara yake ni makubwa zaidi kuliko manufaa yake

Makusudio ya ithm hapa ni madhara. Na madhara ya pombe hudhihiri katikamwili, akili na mali; na vile vile katika kuacha kumkumbuka MwenyeziMungu, kugombana na kufanya mambo yaliyoharamishwa.Wanahistoria

Page 172: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

162

wanasema kwamba baadhi ya walevi walizini na mabinti zao!

Abbas bin Mirdas, alikuwa kiongozi wa watu wake katika zama zaJahiliya (kabla ya Uislamu). Alijiharimishia pombe yeye mwenye tu kwamaumbile yake. Alipoulizwa sababu, alisema: "Siwezi kuchukua ujingakwa mikono yangu niutie mwenyewe tumboni mwangu, wala siko radhiasubuhi niwe bwana wa watu na jioni niwe safihi wao."

Daktari mmoja mashuhuri wa Kijerumani alisema: "Fungeni nusu yamabaa na mimi ninawadhaminia kuwa hamtahitajia nusu ya zahanati namahospitali na majela."

Ama kamari, hii huleta uadui na chuki, na kuzuia kutajwa MwenyeziMungu; kama ilivyoonyesha Aya tukufu. Vile vile inaharibu tabia kwakuzoeya uvivu na kutafuta riziki kwa ndoto tu! Pia inavunja majumba nainamtia mtu kwenye umaskini ghafla, ndani ya saa moja tu. Inatoshakamari kuwa haramu, kwa kule kuchukua mali bure bure tu.

Na wanakuuliza watoe nini? Sema: Vilivyowazidia

Yaani: Toeni vilivyozidi haja zenu na za familia yenu.

Amri ya kutoa hapa ni ya sunna, sio ya wajibu, isipokuwa inakuwa wajibukutoa zinathibiti sharti za khumsi na zaka. Tutaelezea kwa ufafanuzi,inshaallah.

Iwe itakavyokuwa, hii Aya hii ni kama isemayo:

"Wala usifanye mkono wako ni wenye kufungwa shingoni mwako, walausiukunjue ovyo ovyo usije ukawa ni mwenye kulaumiwa, mwenye kufil-isika." (17:29)

Page 173: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

163

Imeelezwa katika Hadith kwamba mtu mmoja alikwenda kwa Mtume(s.a.w.w.) na kibonge cha dhahabu kama yai, akamwambia Mtume: "EweMtume wa Mwenyezi Mungu! Chukua hii ni sadaka; wallahi sina cho-chote zaidi ya hiyo." Mtume hakumtia maanani. Kisha akamfuata tenana kurudia kumwambia. akamwambia kwa hasira: Ilete!” Mtume.Akakichukua. Kisha akamrudishia mwenyewe akisema: "Mtu ananijia namali yake naye hana kitu kingine chochote; kisha aombe watu! Hakikasadaka inatokana na kujitosha. Chukua mwenyewe! Hatuna haja nayo."

Iko Hadith pia kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiiwekea familiayake matumizi ya mwaka mzima.

Namna hii Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya mpate kufikiriduniani na Akhera

Yaani Mwenyezi Mungu anatubainishia hukumu Yake katika pombe nakamari, na hukumu Yake katika vile ambavyo tunatakikana kuvitoa sada-ka katika mali zetu, kwa maslahi yetu. Yeye haamrishi isipokuwa lileambalo lina maslahi ya kidunia na kiakhera, na wala hakatazi isipokuwalile lenye uharibifu.

Yatupasa kuuzingatia na kuuchunga uhakika huu. Tusimwasi MwenyeziMungu katika yoyote ya maamrisho Yake na makatazoYake. Kwa hivyomakusudio ya kauli Yake Mwenyezi Mungu: Mpate kufikiri duniani naAkhera" ni kwamba tufanye amali kwa ajili ya zote mbili (dunia na akhera);tusishike moja tukaacha nyengine.

Na wanakuuliza kuhusu mayatima

Wakati wa Ujahiliya (kabla ya Uislamu), watu walizowea sana kunufaikana mali za mayatima. Pengine mtu aliweza kumwoa yatima, au kumwozamtoto wake, kwa tamaa ya mali ya yatima huyo tu. Ulipokuja Uislamu,Mwenyezi Mungu akamteremshia Mtume Wake Aya hizi:

Page 174: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

164

"Hakika wale ambao mali ya mayatima kwa dhuluma, wanakula Motomatumboni mwao..." (4:10)

"Wala msikurubie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya wemakabisa..."(6:152)

Basi ziliposhuka Aya hizo waliacha kuchanganyika na kuwasimamiamayatima. Hapo maslahi yao yakaharibika, na maisha yao yakawamabaya. Ndipo baadhi ya Waislamu wakauliza kuhusu hali hiyo. Likajajawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu:

Sema: Kuwatengenezea ndio kheri.

Maana yake: Msijizuilie na kuchanganyika na mayatima na kuzikurubiamali zao, kama mnataka kuwatengenezea uzuri katika malezi yao, adabuzao na kusimamia mali zao. Bali hilo lina malipo kwenu na thawabu.Linaloharamishwa ni kuzifuja na kuzila mali zao kwa batili tu.

Na kama mkichanganyika nao, basi ni ndugu zenu

Kundi la wafasiri limesema: "Hii ni idhini kutoka kwa Mwenyezi Mungukwa anayesimamia yatima, kumshirikisha pamoja na familia yake katika kulana kunywa, ikiwa hilo ni sahali kwa msimamizi, na achukue kutoka katikamali ya yatima kiasi kile cha malezi

Na Mwenyezi Mungu anamjua fisadi na mtengezaji.

Page 175: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

165

Fisadi ni yule anayesimamia yatima ili afuje mali zake; na mtengezaji niyule anayesimamia mali ya yatima kwa maslahi ya yatima kwa dhati. Kwahivyo kauli Yake hiyo Mwenyezi Mungu ni kemeo kwa mwenye kutakakufuja na kufanya ufisadi.

Na kama angelitaka Mwenyezi Mungu angeliwatia katika dhiki

Makusudio hapa ni kwamba Mwenyezi Mungu amehalalishakuchanganyika yatima na familia ya msimamizi, na kuchukua katika maliya yatima thamani ya kile alichompatia posho, ili huyo msimamizi asiwena mashaka wala uzito, kwa sababu Mwenyezi Mungu anawatakia watuwepesi, hawatakii uzito.

Hapa inaonesha kuwa si lazima kuwe na usawa wa kutopungua kitu hatakidogo, kati ya kile alichokula yatima pamoja na familia ya msimamizi, nakile atakachochukua badali kutoka katika mali ya yatima; kwaniMwenyezi Mungu (s.w.t.) husamehe tofauti ndogo isiyoepukika. Bali msi-mamizi anaweza hata kula katika mali ya yatima kwa wema, akiwa fukara.Hayo ni kwa kauli Yake Mwenyezi Mungu:

"...Na aliye tajiri basi ajiepushe, na atakayekuwa mhitaji basi ale kwakadri ya ada.” (4:6)

Page 176: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

166

221. Wala msiwaoe wanawakewashirikina mpaka waamini.Na mjakazi muumini ni borakuliko mshirikina, hata aki-wapendeza. Wala msiwaozewanaume washirikina mpakawaamini. Na mtumwamuumini ni bora kulikomshirikina, hata akiwapen-deza. Hao wanavutiakwenye Moto, na MwenyeziMungu anavutia kwenyePepo na maghufira, kwa idhi-ni Yake. Naye hubainisha AyaZake kwa watu ili wapatekukumbuka.

MSIWAOE WANAOMSHIRIKISHA MWENYEZI MUNGUAya 221MAANA

Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazimuumini ni bora kuliko mshirikina, hata akiwapendeza. Wala msi-waoze wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa muuminini bora kuliko mshirikina, hata akiwapendeza.

Aya hizi ni miongoni mwa Aya za hukumu, na zinaingia katika Mlangowa Ndoa.

Kabla ya kuingilia madhumuni ya Aya, kwanza tutajaribu kufasiri neno.nikah, mushrikin, amah,na abd.Neno nikah lina maana mbili: kufunga ndoa na kumwingilia mwanamke.

Page 177: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

167

Neno mushrikin (washirikina) imesemekana kuwa ni kila asiyeaminiUtume wa Muhammad (s.a.w.w.). Kwa kauli hii watakuwa wanaingiawatu wa Kitabu,ambao ni Mayahudi na Wakristo. Na inasemekana kuwaQur'ani haikusudii watu wa Kitabu, kwa tamko la Mushrikin japo wanase-ma kuwa Isa ni Mwana wa Mungu, na kwamba wanaamini Utatu waMungu. Waliosema haya wametoa dalili kwa Aya hizi:

"Hawapendi waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu wala washiriki-na..."(2:105)

"Hawakuwa wale ambao wamekufuru katika watu wa Kitabu nawashiririkina..." (98:1) Katika Aya hizo kuna viunganishi kati ya watu wa Kitabu na washirikina,na, kiunganishi kinafahamisha tofauti, kwa kawaida; kwa sababu kitu haki-wezi kuunganishwa na chenyewe.

Neno amah (mjakazi) na abd linatumiwa kwa mtumwa, na hata kwaaliyehuru. Unaweza kumwambia aliye huru: Ewe mjakazi wa MwenyeziMungu, Vile vile mtumwa; kwa sababu binadamu wote ni watumwa waMwenyezi Mungu.Maana ya Aya hii, kwa hivyo, ni kuwa: Enyi Waislamu! Msimuoemwanamke mshirikina maadamu yuko katika shirki, bali oeni mwanamkeanayetokana nanyi, hata kama ni duni ya mshirikina kwa umbo na tabia.Wala msimwoze mshirikina maadamu yumo katika shirki, bali mwozenimwanamume katika nyinyi, hata kama ni duni ya mshirikina kwa jaha namali.

Hao wanavutia kwenye moto

Yaani hekima ya kukataza kuoana hao washikina. ni hiyo ya kuvutiaMotoni, na kwamba muungano wa kindoa na wao unapelekea uharibifu waitikadi na dini. Kwa uchache unapelekea ufasiki na kupuuza hukumu za

Page 178: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

168

Mwenyezi Mungu.

Tunayoyashuhudia hivi leo ni kwamba vijana wetu -wa kike na wakiumewengi wako katika hali mbaya kuliko makafiri na washirikina, kutokanana kudharau kwao, kuipuuza dini na kujivua kabisa katika athari za dini.Wanawalea watoto wao malezi yasiyokuwa ya dini wala ya tabia njema.Lau kama si shahada zao kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja naMuhammad ni Mtume Wake, tungeliwajibika kuwafanyia muamala wawalahidi na washirikina.

Lakini kwa sababu ya tamko hili tu (la shahada), ndiyo damu yao na maliyao imehifadhika, ni kuswihi kuoana na kurithiana, nao hata kama sha-hada hiyo ni ya kitaklidi na kurithi.* 10

Na Mwenyezi Mungu anavutia kwenye Pepo na maghufira

Hapa kuna vivutio viwili:

• Kivutio cha kwanza, ni cha washirikina, cha kufanya yale yanayotiawatu Motoni na kwenye ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

• Kivutio cha pili. ni cha Mwenyezi Mungu cha kufanya yanayoletamaghufira na kuingia Peponi. Miongoni mwa hayo ni kuoa mwenyekuamini mshirikina, sio na kuolewa na muumini, sio mshirikina.

Hapana mwenye shaka kwamba waumini ndio wanaoitika mwito waMwenyezi Mungu na watakaopata maghufira Yake na hatimae kuingiaPepo Yake kwa idhini Yake; yaani kwa uongofu na tawfiki Yake.

KUOA MWENYE KITABU (AHLUL-KITAB)

Wameafikiana Waislamu kwamba haijuzu kwa Mwislamu kuoa au kuolewana asiyekuwa na kitabu; kama vile kuoa wale wanaoabudu masanamu, jua namoto, n.k. kwa ufasaha zaidi yule asiyeamini.

* 10 Ndoa na mirathi zinakuwa kwa dhahiri ya Uislamu, sio kwa Uislamu halisi. Hayotumeyafanyia utafiti katika kitabu Usulul Ithbat sehemu ya ‘Madai na Kuhalifu Sharia’.

Page 179: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

169

Vile vile haijuzu kumuoa au kuolewa na Majusi, hata kama imesemwaMajusi ni shabihi ya wenye kitabu.

Wameafikiana madhehebu manne ya Ahli Sunna juu ya kusihi kumuoamwenye kitabu, na wamehitalifiana Mafaqihi wa Kishia. Wengi waowamesema kuwa haijuzu kwa Mwislamu kumuoa Yahudi au Mkristo. Nawengine wamesema inajuzu. Miongoni mwa Ulamaa wakubwa waliose-ma hivyo ni Sheikh Muhammad Hassan katika Jawahir, shahidi wa Pilikatika Masalik na Sayyid Abul Hassan katika Wasilah, wamesema ina-juzu. Na sisi tuko pamoja na rai hii kwa dalili hizi:

1. Dalili zinazohalalisha ndoa zimemtoa Mwislamu mwanamume kumwoaMshirikina, na Mwislamu mwanamke kuolewa na mshirikina namwenye kitabu. Kwa hivyo inafahamisha kuwa wasiokuwa hao ina-juzukuoa.

2 Kauli yake Mwenyezi Mungu:

"Leo mmehalalishiwa kula vilivyo vizuri na chakula cha wale waliopewaKitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao; na wanawakewasafi waumini na wanawake wasafi katika wale waliopewa Kitabu kablayenu..." (5:5)

Kuhusu kauli Yake Mwenyezi Mungu (60-10): Wala msiwaweke wanawakemakafiri katika kifungo cha ndoa (zenu),” makusudio ya makafiri hapo niwashirikina, sio waliopewa Kitab. kwa sababu Aya hiyo iliwashukiawanawake waliosilimu na kuhama na Mtume, wakiwaacha waume zaowashirikina; na mfumo mzima wa Aya unafahamisha hivyo. Aya yenyewe nihii:

Page 180: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

170

Kuhusu neno lake Mwenyezi Mungu lililomo katika Aya hii, la kuzuiaWaislamu kuoa wanawake washirikina, tumeshatangulia kusema kuwa hilo nimaalum kwa wanawake washirikina tu, nao sio wanawake. waliopewa Kitabu.

"Enyi mlioamini! Watakapowajia wanawake walioamini wanaohama,basi wafanyieni mtihani Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi imani yao.Mkiwajua ni waumini, basi msiwarudishe kwa makafiri. Hawa si halalikwao wanaume makafiri wala wao wanaume makafiri si halali kwao. Nawarudishieni (waume zao mahari) waliyotoa. Wala kwenu si vibaya kuwaoaikiwa mtawapa mahari yao (hao wanawake). Wala msiwaweke katika kifun-go cha makafiri..."(60:10)

Pia ziko Hadith sahihi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul Bait wakekatika kuswihi Mwislamu kumuoa mwanamke katika waliopewa Kitabu.Na haya tumeyafafanua zaidi katika Juzuu ya Tano ya kitabu. Fiqhul ImamJafar Sadiq. Mlango wa Yaliyo haramishwa kifungu cha Kutofautiana Dini

Page 181: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

171

222. Wanakuuliza kuhusu hedh.Waambie: Ni udhia. Basijiten-geni na wanawakewakati wa hedhi, wala msi-wakurubie mpaka wat-wahirike. Wakisha toharikabasi waendeni palealipowaamrisha MwenyeziMungu. Hakika MwenyeziMungu huwapenda wanao-tubia na huwapenda wa-naojitwahirisha.

223. Wake zenu ni mashambayenu. Basi yaendeenimashamba yenu mpendavyo,na tangulizieni nafsi zenu; namcheni Mwenyezi Mungu najueni kwamba mtakutananaye, na wape habari njemawenye kuamini.

HEDHI

Aya 222 - 223

MAANA

Baada ya kumuuliza Mtume mtukufu (s.a.w.w.) kuhusu mwezi mtukufu,ulevi, kamari watakachotoa na mayatima; kisha walimuuliza kuhusu hedhi.Amesema Razi: "Imepokewa habari kuwa Mayahudi na Majusi walikuwawakikaa mbali sana na wanawake wakati wa hedhi; Wakristo nao walikuwawakiwaingilia bila ya kujali hedhi. Na watu wa zama za Jahiliya (kabla ya

Page 182: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

172

Uislamu) walikuwa hawali, hawanywi, hawakai kitanda kimoja wala hawakainyumba moja na mwanamke mwenye hedhi, kama walivyokuwa wakifanyaMajusi na Mayahudi.Wanakuuliza kuhusu hedhi. Waambie: Ni udhia. Basi jitengeni nawanawake wakati wa hedhi

Swali lilitokea kuhusu kuchanganyika na wanawake wakati wa hedhi; ndipoMwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume Wake mtukufu kuwajibu wauliza-ji kwamba wajitenge na wanawake siku za hedhi; yaani wasiwaingilie.Imekuja Hadith inayosema; "Fanyeni kila kitu isipokuwa kuwaingilia tu."

Neno adha (udhia) ni ‘chochote kinachochukiza. Na makusudio yake hapani madhara kwa kuwa ni uchafu na najisi.

Wala msiwakurubie mpaka watwahirike

Wamehitalifiana juu ya makusudio ya kutwahirika kuwa: je, ni kukatikadamu tu; na ikikatika, inajuzu kumwingilia hata kama hajaoga, makusudioni kuoga baada ya damu kukatika; kwa hivyo haijuzu kumwingilia mpakabaada ya damu kukatika na kuoga?

Wamesema Shia: Inajuzu kumwingilia. mjaradi wa damu kukatika, hatakama hajaoga, kwa sababu hivi ndivyo linavyofahamika neno tuhr (twa-hara) Ama kujitwahirisha hiyo ni kazi ya wanawake ambayo inakuwabaada ya twahara (kwisha damu).

Amesema Malik na Shafii: Haijuzu kumwingilia ila baada ya kuoga.

Na wanasema Mahanafi: Ikiendelea damu kwa muda wa siku kumi, ina-juzu kumkurubia kabla ya kuoga. Lakini ikakatika damu kabla ya siku,kumi haijuzu kumwingilia mpaka aoge. Mwenye tafsiri ya Al Manarameelezea juu ya ufafanuzi huu kwa kusema: "Huu ni ufafanuzi wakushangaza." Wakisha twahirika, basi waendeeni pale alipowaamrisha MwenyeziMunguNeno haythu (pale) ni uhakika wa mahali. Kwa maana hivyo inakuwa:Waendeeni tupu ya mbele, kama inavyofahamika. Masuala ya hedhina hukumu zake tumeyazungumzia kwa tafsiri zaidi katika kitabu Fiqhul

Page 183: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

173

Imam Jafar Sadiq na kitabu Al Fiqhu Alal Madhahibil Khamsa.Wake zenu ni mashamba yenu. Basi yaendeeni mashamba yenumpendavyoNeno annaa kulingana na sarufi (nahau ya Kiarabu) lina maana ya vyovyote,wakati wowote au popote. Zimekuja kauli nyingi kuhusu maana ya nenohilo annaa katika Aya hii. Kuna mwenye kusema: Ni kwa maana ya wakatiwowote; yaani muwaendee (muwaingilie) wakati wowote, usiku au mchana.Wengine wakasema ni kwa maana ya popote; yaani mna hiyari yakuwaingilia popote, tupu ya mbele au nyuma. Vile vile kuna mwenye kusemani kwa maana ya vyovyote; yaani kwa hali yoyote, kukaa au kulala, n.k.

Limesema kundi la wafasiri, miongoni mwao akiwa ni mwenye tafsiriya Al Manar ambaye ni miongoni mwa wanavyuoni wa Kisunni, namwenye Tafsiri ya Bayanu Ssada ambaye ni miongoni mwa wanachuoniwa Kishia, kwamba Neno shamba linafungamana na mazao na ni tupuya mbele tu ndiyo ambayo inaweza kuoteshwa mazao (mtoto ) mbalikuwa kuiendea tupu ya nyuma ni udhia.Sisi tunaiunga mkono rai hii kwa sababu mbili: kwanza ni kuwa mazaohayapatikani isipokuwa kwa kupitia tupu ya mbele tu, kama walivyotajawafasiri hao. Pili, kauli Yake Mwenyezi Mungu: Waendeni palealipowaamrisha Mwenyezi Mungu inaonyesha makusudio ni mbele, baadaya kufasiri haythu kwa maana ya mahali.Kuna baadhi ya mafakihi wa Kishia wanaojuzisha kumwendea mkenyuma, lakini kwa makuruhu makubwa sana. Wengine wamedai kuwa ati hayo ni ya Shia peke yao na kwamba hakunayeyote kati ya waislamu anayeafikiana nao kwa hilo, hali inajulikanakuwa Razi mwanachuoni wa Kisunni amenakili, katika kuifasiri Aya hii,kwamba Ibn Umar na Malik walikuwa wakisema: "Makusudio ya Aya nikujuzisha kuwaendea wanawake nyuma." Na Al-Hafidh Abu Bakr Al-Andalusi wa madhehebu ya Kimalii (Sunni) - aliyekufa mwaka 542Hijriya - katika Juzuu ya Kwanza ya kitabu Ahkamul Qur'ani uk 73, chapaya mwaka 1331 A.H. alisema hivi (ninamnukuu): “Wamehitilafianawanavyuoni katika kujuzu kumwendea mke nyuma Wengi wamejuzisha."Ameyaeleza hayo Ibn Shaban katika Jimau Nis-waan wa Ahkamul Qur'ani

Page 184: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

174

na akategemeza, kwa kujuzu kwake kundi la masahaba watukufu, na tabiinana kwa Malik, kwa riwaya nyingi. Na Bukhari ametaja kutoka kwa Ibn Aun,kutoka kwa Nafi kwamba Ibn Umar alikuwa akisoma Sura ya Al- Baqarahmpaka alipoifikia anna shiitu alisema: Je unajua imeteremka kuhusu nini?Nikasema: La. Akasema: Imeshuka kuhusu kadha na kadha; yaani tupu zanyuma za wanawake”

224. Wala msimfanye MwenyeziMungu ni pondokeo laviapo vyenu, (ili) mfanyemema na mumche(Mwenyezi Mungu) na kusu-luhisha kati ya watu. NaMwenyezi Mungu niMwenye kusikia, Mjuzi.

225. Mwenyezi Mungu hata-patiliza kwa sababu yakuapa kwenu kwa upuuziupuuzi, lakini huwapatilizakwa yaliyokusudiwa nanyoyo zenu. Na MwenyeziMungu ni Mwingi wamaghufira, Mpole .

226. Kwa wale ambao wanaapakujitenga na wake zao niwa kungojea miezi minne.Na kama wakirejea basiMwenyezi Mungu niMwingi maghufira,Mwenye kurehemu.

227. Na wakiazimia talaka, basiMwenyezi Mungu niMwenye kusikia, Mjuzi.

Page 185: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

175

YAMINI

Aya 224 - 227

Wala msimfanye Mwenyezi Mungu ni pondokeo la viapo vyenu

Mwenyezi Mungu amekataza kutangulizwa katika kila jambo kwa kuapasana, kwa sababu mwenye kukitaja kitu sana huwa amekifanya ni pondokeolake. Mwenyezi Mungu amekushutumu kuapa sana kwa kauli Yake:

“Wala usimtii kila mwenye kuapa sana, aliye dhalili." (68:10)

Mwenye kuapa sana haiba yake hupungua, dhambi zake zikazidi naakatuhumiwa uwongo.

(Ili) mfanye mema na mumche (Mwenyezi Mungu) na kusuluhishakati ya watu

Hili ndio sababu ya kukatazwa kuapa; maana yake ni kwamba MwenyeziMungu anawakataza kuapa bila ya dharura, ili muwe wema wanaomchaMungu, wenye kufanya wema duniani, sio ufisadi.

Mwenyezi Mungu hatawapatiliza kwa sababu ya kuapa kwenu kwaupuuzi upuuzi

Baada ya Mwenyezi Mungu kukataza kuapa bila ya dharura, amebainishakwamba mengi yanayowapitia watu katika ndimi zao mfano Wallahi vile'auSio hivyo Wallahi, n.k.; siyo viapo vya uhakika isipokuwa ni mchezo tuunaokuja kwenye ulimi bila ya kukusudia, wala hayana athari yoyote; ndiyoikawa Mwenyezi Mungu hakuwajibisha kafara katika dunia wala hakunaadhabu Akhera.

Page 186: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

176

Lakini atawashika katika yaliyokusudiwa na nyoyo zenu.

Kwa sababu Mwenyezi Mungu Ambaye umetukuka utukufu wake, haan-galii sura na kauli, bali huangalia nia na vitendo, kama anavyosema:

"Mwenyezi Mungu hatawapatiliza kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakiniatawapatiliza kwa viapo mlivyoapa kwa nia mliyoifunga (barabara). Basikafara yake ni kuwalisha maskini kumi kwa chakula cha wastani mna-chowalisha watu wa majumbani mwenu au kuwavisha, au kumwacha hurumtumwa. Asiyeweza kupata hayo, basi afunge siku tatu. Hiyo ndiyokafara ya viapo vyenu mnapoapa...." (5:89)

Mtu aliyebaleghe, mwenye akili timamu, mwenye kukusudia, na aliye nahiyari, akiapa na akakhalifu, basi itampasa kutoa kafara ya kumwacha hurumtumwa au kuwalisha au kuwavisha maskini kumi. Akishindwa hayo, ata-funga siku tatu. Tumezungumzia zaidi kuhusu kiapo, sharti zake na hukumuzake katika Juzuu ya Tano ya Fiqhul Imam Jafar Sadiq.

Kwa wale ambao wanaapa kujitenga na wake zao ni wa kungojeamiezi minne. Na kama wakirejea basi Mwenyezi Mungu ni Mwingiwa maghufira, Mwenye kurehemu. Na wakiazimia talaka, basiMwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mjuzi.

Kuapa kujitenga katika sharia ni mtu kuapa kuwa hatamwingilia mkewe.Mafakihi wa Kishia wameshartiza kuwa, ili kiwe ni kiapo, mke aweameingiliwa; kama si hivyo hakitakuwa kiapo; na kuwe ni kuapa mume

Page 187: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

177

kuacha kumwingilia mkewe umri wake au muda unaozidi miezi minne,kwa sababu mke anayo haki ya kuingiliwa angalau mara moja kila mieziminne, kwa uchache.

Wamesema: Kama atamwingilia kabla ya miezi minne, atatoa kafara, nakizuizi kitaondoka, kama kwamba hakukuwa kitu; na ikipita zaidi yamiezi minne na asimwingilie, basi mke akisubiri na akaridhia, hiyo ni juuyake wala haifai kwa yeyote kumpinga. Na kama akishindwa kusubiri nakuridhia atamshtaki mume kwa hakimu wa sharia. Baada ya kupita mieziminne atalazimishwa kumrudia au kumwacha Akikataa. atafungwa mpakaachague mojawapo ya mambo mawili; wala si haki kwa hakimukumwachisha kwa nguvu. Kama mume ataamua kurudi, basi atatoa kafarailiyotajwa.

228. Na wanawake waliopewatalaka watangoja twaharatatu. Wala si halali kwaokuficha alichokiumbaMwenyezi Mungu katikamatumbo yao, ikiwawanamwamini MwenyeziMungu na Siku ya Mwisho.Na waume zao wana hakizaidi ya kuwarudia katikamuda huo, kama wakitakakufanya suluhu. Nao(wanawake) wanayo hakisawa na ile iliyo juu yao kwasharia. Na wanaume wanadaraja juu yao. MwenyeziMungu ana nguvu, Mwenyehekima.

Page 188: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

178

WALIOTALIKIWA

Aya 228:

MAANA

Na wanawake waliopewa talaka wangoje tohara tatu.

Tamko la waliopewa talaka kwa dhahiri ni lenye kuenea kwa yeyote yulealiyepewa talaka, awe anatoka hedhi au amekoma, muungwana au kijakazimwenye mimba au asiyekuwa nayo, mkubwa au mdogo asiyetimiza miakatisa. Lakini dhahiri hiyo siyo makusudio yake. Kwa sababu baadhi yawanaotalikiwa hawana eda, kwa tamko la Qur'an;

"Enyi mlioamini Mtakapowaoa wanawake wenye kuamini kisha mkawa-pa talaka kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayaoihis-abu..."(33:49)

Pia aliyekoma. Mafakihi kwa Kishia wanasema kwamba hana eda hatakama ameingiliwa na mume. Vile vile mtoto mdogo chini ya miaka tisa.

Na kuna wanawake wanaokaa eda kwa twahara mbili, kama mjakazi.Wengine wanakaa miezi mitatu, sio kwa twahara tatu; huyo ni yule ambayeyuko katika rika la kutokwa na hedhi, lakini hatokwi; kama ambavyomwenye mimba, muda wake wa kukaa eda unaisha wakati atakapozaa.Mwenyezi Mungu anasema;

"...Na wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa..." (65:4)

Page 189: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

179

Kwa hivyo basi, makusudio ya waliopewa talaka katika Aya hii, ni yulealiyeingiliwa akiwa na umri wa zaidi ya miaka tisa, asiye na mimba naanayeendelea kupata hedhi.

Shia, Malik, na Shafii wamefasiri neno Qurui kwa maana ya twahara, namakusudio yake ni siku za kuwa twahara baina ya hedhi mbili. Kama aki-achwa wakati wa mwisho mwisho wa twahara yake, itahisabiwa pia nikatika eda, na atakamilisha twahara mbili baada yake. Ama Hanafi naHambali wamefasiri neno qurui kwa maana ya hedhi tatu.

Wala si halali kwao kuficha alichokiumba Mwenyezi Mungu katikamatumbo yao

Ili kufahamu hakika ya jumla hii itabidi kuanza kueleza haya yafuatayo:

Mafakihi wa Kisunni wameigawa talaka mafungu mawili: ya sunna nabid'a (uzushi). Hebu tuwaachie wenyewe tafsiri ya ‘talaka ya sunna’ nabid’a talaka ya ( uzushi).

Katika kitabu Al-Mughni cha Ibn Qudama Juzuu 7 uk. 98, chapa ya tatu,anasema: "Maana ya talaka ya sunna ni talaka ambayo inaafiki amri yaMwenyezi Mungu na amri ya Mtume wake, nayo ni talaka katika hali yatohara asiyomwingilia." Na katika kitabu hicho, hicho uk. 99, amesema:"Hakika talaka ya bid'a ni kumwacha akiwa bado yumo katika hedhi, aukatika hali ya twahara aliyomwingilia."Amesema Razi katika tafsiri ya Ayaya 1 katika Sura ya 86; "Talaka katika twahara ni lazima. Vyinginevyohaitakuwa ya sunna."

Kwa hali hiyo basi, mke kupewa talaka katika hedhi, au katika twaharaaliyeingiliwa, siyo talaka ya kisharia, bali ni bid'a (uzushi); na kila uzushini upotevu na kila upotevu, ni Motoni.

Ama kumtaliki mke katika twahara asiyoingiliwa na mumewe, inakuwandiyo talaka iliyofuata sharia ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Hapondipo inapofafanuka siri ya kauli Yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): "wala

Page 190: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

180

sihalali kwao kuficha alichokiumba Mwenyezi Mungu katika matumboyao." Kwa sababu kuweza kujua kuwa talaka imetoka kisunna au kibid’akunategemea kuijua hali ya mwenye kuachwa; akiwa twahara au akiwa nahedhi?

Kimsingi njia ya kujua sifa mbili hizi (twahara na hedhi) inamtegemeamwanamke mwenyewe. Kwa hivyo itabidi aaminiwe maadamu hajulikanakuwa ni mwongo. Imam Jafar Sadiq amesema: Mwenyezi Munguamewachia wanawake mambo matatu: twahara, hedhi na mimba." Katikariwaya ya pili imeongezwa eda.

Shia wanaafikiana na Sunni kwamba talaka, ikiwa katika hedhi au katikatwahara aliyoingiliwa, inakuwa ya uzushi; na ikiwa ni katika twaharaambayo hakuingiliwa inakuwa ni ya sharia ya Mtume (s.a.w.w.). Lakini Shiawamesema talaka ya uzushi sio talaka kabisa; yaani si sahihi. Talaka sahihi,inayomtenganisha mume na mke, ni talaka ya sunna; yaani inayotokea kati-ka twahara asiyoingiliwa. Sunni wanasema: Hapana! Talaka ya uzushi nisahihi na inahusika na athari zote za talaka, isipokuwa tu kuwa yule mwenyekuacha atapata dhambi.

Hiyo ni kusema kuwa Sunni hawatofautishi baina ya talaka ya kawaidana ya uzushi katika kuswihi kwake; wanalotofautisha ni katika kupatamadhambi na uasi tu. Ama Shia wametofautisha kati ya hizo mbili, kwaupande wa usahihi, na si upande wa dhambi.

Ikiwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.

Hii ni kuogopesha na kuweka utisho kwa wenye kuficha yaliyo tumboni nawala sio sharti la kuwajibisha kusadiki, kwa sababu maana yake ni kwambaimani inazuiwa uwongo; kama vile kumwambia mtu: "Ikiwa unamuogopaMwenyezi Mungu usiseme uwongo."

Tumetangulia kueleza kuwa mwenye kutalikiwa ndiye atakayeamini-wa katika twahara, hedhi na mimba. Maana yake ni kuwa itakayotege-mewa ni kauli yake katika kubaki eda na kwisha kwake. Ilivyo ni kwam-ba haki ya mume katika kurejea, itategemea kutokwisha kwa eda kamaambavyo muungano (wa nasaba ya mtoto) unaambatana na twahara na

Page 191: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

181

hedhi. Vile vile kuswihi na kutoswihi talaka kwa upande wa mafakihi waKishia. Akiwa na hedhi, na akasema kuwa ni tohara, basi talaka haitakuwa,na atabaki ni mke wa mtu; kama akisema eda yake imekwisha kwa tohara nakumbe bado, haki ya mume ya kurejea itafutika. Lakini akiolewa katika halihiyo atakuwa mzinifu. Kwa sababu hii na nyinginezo, ndio MwenyeziMungu akawakataza wanawake kuficha vilivyo katika matumbo yao naakawakemea kwa hilo.

Na waume zao wana haki zaidi ya kuwarudia katika muda huo,kama wakitaka kufanya suluhu

Kauli yake Mwenyezi Mungu "katika muda huo" ni ule muda wa kungo-jea (muda wa eda). Maana yanayopatikana hapa ni kwamba MwenyeziMungu, (s.w.t.) baada ya kubainisha wajibu wa eda, ametaja haki yamwenye kutaliki kumrejea mtalaka wake katika muda wa eda, ikiwa nitalaka rejea.

Haki hiyo ni ya mume, mke aridhie asiridhie. Wala kurejea mke hakuhita-ji kufunga ndoa tena na mahari, kama vile ambavyo hakuhitajii mashahi-di kwa mafakihi wa Kishia. Utakuja ubainifu wake pamoja na dalili zaokwenye Sura ya Talaka (65).

Makusudio ya kauli Yake Mwenyezi Mungu "kama wakitaka kufanyasuluhu" ni suluhu kati ya mume na mke bila ya kukusudia madhara katikakurejea.

Unaweza kuuliza: Kama mume akimrejea mtalaka wake ndani ya eda kwakukusudia madhara sio suluhu, je kurejea kutakuwa sahihi au la?

Jibu: Kutaswihi kurejea, lakini mume atapata dhambi, kwa sababukukusudia suluhu ni sharti ya hukumu ya taklifa, ambayo ni kuhalalishakurejea, wala sio sharti ya maudhui yenyewe ya kurejea na kuswihikwake.

Nao (wanawake) wanayo haki sawa na ile iliyo juu yao kwa sharia

Makusudio ya kufanana haki hapa sio ya kufanana kijinsia, kwambayanayostahiki kwa mume, kama vile mahari na posho, basi na mke pianaye atoe, la; isipokuwa makusudio hapa ni kuwa sawa wajibu na

Page 192: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

182

yanayostahiki. Mafakihi wanasema kwamba haki ya mume kwa mkeweni kutiiwa kitandani; na haki ya mke kwa mume ni kulishwa na kuvish-wa. Mwenye tafsiri ya Al Manar anasema haki ya mume kwa mke na hakiya mke kwa mume ni ile ada ya mambo ya watu, isipokuwa yale yaliy-oharamishwa katika sharia. Linaloonekana kwa ada kuwa ni haki kwa mkena mume, basi litakuwa ni sawa mbele za Mwenyezi Mungu.

Yanayodhihirika, hapa kutokana na mfumo wa Aya hapa, ni kwamba hakiiliyo kwa mke ni eda, ukweli katika kuitolea habari eda na kuacha kupin-ga kurejea kulikokamilisha masharti. Na haki iliyo juu ya mume ni kukusu-dia suluhu katika kurejea na usuhuba mzuri, wala sio madhara. Ama hakinyingine za mume na mke ziko mbali na Aya hii.

Na wanaume wana daraja juu yao.

Wamehitilafiana wanavyuoni na wafasiri kuhusu makusudio ya daraja hiiinayomtofautisha mwanamume na mwanamke. Ikasemwa kuwa ni akili nadini; ikasemwa kuwa kuwa ni mirathi, na pia ikasemwa kuwa ni ubwana;yaani inampasa mke kumtii mume na kumsikiliza.

La kushangaza ni kwamba wengine wamefasiri daraja ya juu hapa kwamaana ya ndevu; kama ilivyoelezwa katika kitabu Ahkamul Qur'an cha Abubakr Al-Andalusi.

Sio mbali na maana kuwa makusudio ya daraja hapa ni kuiweka talaka nakurejea mikononi mwa mume, sio mwa mke.

MWANAMUME NA MWANAMKE KATIKA SHARIA YA KIISLA-MU

Uislamu umezitangulia sharia na kanuni zote katika kumkomboamwanamke na kuzithibitisha haki zake, baada ya kuwa mwanamume alim-tumia mwanamke kama bidhaa tu, akamfanya kama mnyama, ambapompaka hivi karibuni Ulaya na Marekani walikuwa wakifanya hivyo.

Uislamu unapomtofautisha mwanamke na mwanamume unamtofautishakwa tofauti za kimaumbile au maslahi ya jamii. Ni jambo lisiloingia akili-ni wala uadilifu kufanya usawa katika kila kitu kati ya yule mwenye

Page 193: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

183

kujishughulisha zaidi na magauni, mitindo ya mavazi, kuchana nywele,n.k.; na yule anayehisi majukumu ya mwenzake (mkewe) na watoto nakustahamili mashaka kwa ajili yake (mke) na kwa ajili yao wote.

Iwe itakavyokuwa, mafakihi wa Kiislamu wamezitaja tofauti kati ya mwana-mume na mwanamke katika hukumu za kisharia kama ifuatavyo:

1. Fidia ya kuuliwa mwanamke ni nusu ya mwanamume.2. Kutoa talaka na kurejea kuko mikononi mwa mume, sio mke.3. Haijuzu kwa mke kusafiri, na kutoka nyumbani kwake, isipokuwa kwa

kukubali mume lakini mume anaweza kufanya hivyo.4. Si wajibu kwa mwanamke kuswali Ijumaa, hata yakitimia masharti.5. Haijuzu mwanamke kutawalia jambo wala kuwa Kadhi, isipokuwa kwa

Abu Hanifa. Yeye anasema inafaa katika haki za watu, lakini sio zaMungu.

6. Hawezi kuwa imamu wa swala ya wanaume, lakini mwanamume anawezakuwa imamu wa wanawake.

7. Ushahidi wake haukubaliwi kabisa katika mambo yasiyohusiana na mali,hata akiwa pamoja na waume, isipokuwa katika maswala ya uzazi.Lakini unakubaliwa akiwa pamoja na wanaume kwa sharti ya kuwaushahidi wa wanawake wawili ni sawa na wa mwanamume mmoja.

8. Katika mirathi mtoto wa kike anapata nusu ya fungu la mtoto wakiume.

9. Ni lazima ajifunike mwili wake wote - hata nywele - mbele za waumewasio maharimu, lakini kwa mwanamume mbele za wanawake wajibuwake ni kustiri tupu mbili tu.

10. Hapigani jihadi wala hatoi kodi wala hauliwi vitani, iwapo hajapigana.11. Mama hashirikiani na baba katika usimamizi (uwalii) wa mtoto wao

mdogo katika ndoa, au katika matumizi ya mali yake (mtoto). Haki yayote hayo ni ya baba.

12. Haifai kushindana mashindano ya farasi na kulenga shabaha.13. Mafakihi wametoa fatwa kuwa fidia ya aliyeuawa kimakosa

inachukuliwa na ndugu zake wa karibu kwa upande wa baba tu;kama vile kaka, ami na watoto wao, lakini sio wa kike.

14. Mwanamke akimuua mwanamume, atauliwa bila ya kutoa fidia;lakini mwanamume akimuua mwanamke, basi hawezi kuuliwa mpaka

Page 194: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

184

walii wa mwanamke atoe nusu ya fidia kwa warithi wa muuaji.

229. Talaka ni mara mbili; basi nikushikamana kwa wema aukuachana kwa ihsani. Wala sihalali kwenu kuchukua cho-chote katika mlichowapa,isipokuwa wakiogopa (wotewawili) kwamba hawatawezakusimamisha mipaka yaMwenyezi Mungu. Basi mkio-gopa kwamba hawatawezakusimamisha mipaka yaMwenyezi Mungu, itakuwahapana ubaya kwao kupokeaajikomboleacho mke. Hiindiyo mipaka ya MwenyeziMungu; basi msiipetuke. Nawatakaoipetuka mipaka yaMwenyezi Mungu, basi haondio madhalimu.

230. Na kama amempa talaka ( yatatu) basi si halali kwakebaada ya hapo mpaka aolewena mume mwingine. Na(mume wa pili) akimwacha,basi hapo si vibaya kwaokurejeana wakiona kuwawatasimamisha mipaka yaMwenyezi Mungu. Na hii nimipaka ya Mwenyezi Munguanayoibainisha kwa watuwajuao.

Page 195: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

185

TALAKA NI MARA MBILI

Aya 229 - 230

MAANA

Talaka ni mara mbili.

Waarabu katika zama za Ujahiliya (kabla ya Uislamu) walikuwa na talaka,eda na kurejeana katikati ya eda. Lakini talaka haikuwa na idadi maalum.Mtu akiweza kumwacha mkewe mara mia na kumrudia. Kwa hivyomwanamke akawa ni kitu cha kuchezewa mikononi mwa mwanamume.

Kuna riwaya inayoeleza kuwa mtu mmoja alimwambia mkewe:"Sitakukurubia milele, na pamoja na hivyo utabaki kwangu tu, hutawezakuolewa na mwingine." Mke akauliza: "Itakuwaje hivyo?" Mume aka-jibu: "Nitakuacha mpaka ukikaribia muda wa kwisha eda nikurudie, hala-fu nikuache tena, n.k." Mwanamke akamshtakia Mtume (s.a.w.w.).Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii: "Talaka ni mara mbili;"yaani talaka ambayo mnaruhusiwa kurejea ni talaka ya kwanza na ya pilitu! Ama ya tatu si halali kurejea, mpaka mke aolewe na mume mwingine;kama alivyosema Mwenyezi Mungu: "Na kama amempa talaka ( ya tatu)si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine."

Basi ni kushikamana kwa wema au kuachana kwa ihsani

Mume akimwacha mkewe mara ya pili ana hiyari kati ya mambo mawiliakiwa yumo katika eda. Jambo la kwanza ni kumrejea kwa kukusudiakupatana na kutangamana. Huku ndiko kushikamana kwa wema. Jambo lapili, ni kumwacha mpaka ishe eda yake, amtekelezee haki yake, asimtajekwa ubaya baada ya kutengana wala asimkatishe anayetaka kumwoa baadayake. Huko ndiko kuachana kwa ihisani.

Unaweza kuuliza: Wafasiri wengi wamefasiri kuachana kwa ihisani ni tala-ka ya tatu, na wakatoa ushahidi wa Hadith ya Mtume (s.a.w.w.). Sasaimekuwaje wewe kuipinga kauli yao hii na kufasiri ‘kuachana’, kuwa ni

Page 196: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

186

kupuuza na kuacha kumrejea katika muda wa eda?

Jibu: Neno kumwacha, kwa dhati yake, linawezekana kuwa ni talaka yatatu, na linawezekana kuwa ni kumnyamazia mtalaka na kuwacha kumrejea.Lakini kwa kuchunga mfumo ulivyo, maana ya neno inarudia maana ya pili;yaani kuacha kurejea, kwa sababu kauli yake Mwenyezi Mungu "Kamaamempa talaka (ya tatu) basi (mwanamke huyo) si halali kwake baada yahapo," inatokana na kumweka. Maana yake yanakuwa ni: akimwacha baadaya kumweka, na akamrejea katikati ya talaka ya pili, itakuwa talaka ni ya tatuwala si halali kwa mwenye kuacha kumwoa, mpaka aolewe na mumemwingine. Kwa hivyo haiwezekani kuwa imetokana na kumweka kwamaana ya talaka ya tatu, kwa sababu maana itakuwa alimwacha mara ya nnebaada ya kumwacha mara ya tatu. Na ilivyo ni kwamba hakuna talaka yanne katika Uislamu. Ama Hadith iliyofasiri kumweka kwa maana ya talakaya tatu, si thabiti.

TALAKA TATU

Madhehebu manne ya Kisunni yameafikiana kuwa atakaye mwambiamkewe: Nimekuacha talaka tatu, au akisema: Nimekuacha! Nimekuacha!nimekuacha, basi itakuwa ni talaka tatu, na itakuwa haramu kukaa nayempaka aolewe na mume mwingine. Shia wamesema itakuwa ni talaka mojatu, na ni halali kumrejea, maadamu yuko katika eda.

Katika tafsiri ya Al Manar imepokewa kutoka kwa Ahmad bin Hambalkatika Musnad yake, na Muslim katika Sahih yake, kwamba talaka tatuzilikuwa moja katika zama za Mtume (s.a.w.w.), za Abu Bakar na baad-hi ya miaka ya Ukhalifa wa Umar. Lakini Umar ikamdhihirikia fikranyingine akasema: "Hakika watu wamefanya haraka katika jambolililokuwa na upole kwao; laiti tungeliwapitishia."Basi akapitisha (kuwakusema talaka tatu ni tatu).

Kisha amenakili mwenye tafsiri Al Manar, kutoka kwa Ibn Al Qayyim,kwamba masahaba wote walikuwa wakikubali kwamba talaka tatu haziku-tokea kwa pamoja tangu mwanzo wa Uislamu mpaka miaka mitatu ya

Page 197: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

187

Ukhalifa wa Umar. Vile vile walifutu hivyo jamaa katika masahaba, tabi-ina (waliokuwapo baada ya masahaba) na waliokuja baada ya hao tabiina(tabii-tabiina), na kwamba fatwa juu ya hilo inaendelea kila wakati; hatakatika baadhi ya wafuasi wa maimamu wanne wako waliofutu hivyo.Wala si halali kwenu kuchukua chochote katika mlichowapa

Katika mlichowapa hapa ina maana kiwe kingi au kichache; yaani ikiwamume ndiye asiyemtaka mke, na akapendelea kumpa talaka, basi si hakikwake kuchukua vile alivyompa zawadi au mahari. Mwenyezi Munguanasema:

"Na kama mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja waommempa, rundo mali, basi msichukue chochote katika hiyo. Je,mnachukua kwa dhuluma na kwa dhambi iliyo wazi" (4:20)

Hiyo ni ikiwa mume ndiye asiyemtaka mke. Ama ikiwa mke ndiye asiyem-taka mume, basi hapana kizuwizi cha mke kumpa mume kile kinachom-ridhia ili amwache, ni sawa chenye kutolewa kiwe ni kiasi cha mahari aukichache au zaidi ya mahari. Talaka hii inaitwa khul'u (kujivua); na mumekatika talaka hii hana haki ya kumrejea katika eda maadamu anaendeleakulipwa. Isipokuwa kama huyo mke atabadilisha katikati ya eda.

Kuhusu talaka hii ya khul'u, Mwenyezi Mungu anasema:

Isipokuwa wakiogopa (wote wawili) kwamba hawataweza kusi-mamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kwambahawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, itakuwahapana ubaya kwao kupokea ajikomboleacho mke.

Hii ni kuelezea uwezekano wa kuchukua kitu kutoka kwa mke. Mipakaya Mwenyezi Mungu ni haki na wajibu wa kila mmoja kwa mwenzake(mke na mume). Maana yake: Enyi waume! Msichukue kitu kutoka kwa

Page 198: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

188

watalaka wenu kwa sababu yoyote ile, isipokuwa sababu moja tu, ambayoni ikiwa mke ndiye anayemchukia mume, wala hawezi kuishi naye, kiasiambacho hali itapelekea kumwasi Mwenyezi Mungu katika kutia dosarihaki za unyumba; na huenda mume naye akaogopa kumkabili mke kwauovu. Katika hali hii, itafaa kwa mke kudai talaka kwa mume na kum-lipa ridhaa; kama vile ambavyo inajuzu kwa mume kuichukua ridhaahiyo.

Imekuja Hadith kwamba Thabit bin Qays alikuwa amemuoa bint wa Abdullabin Ubayy. Naye alikuwa akimpenda, lakini mke hampendi mume. Naalikuwa amempatia shamba. Mke akenda kwa Mtume (s.a.w.w.) akasema:"Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Mimi na Thabit kichwa changuhakipatani na chake." Thabit akasaili: "Na lile shamba?" Mtumeakamwambia bint Abdulla: "Unasemaje?" Akasema: "Ndio, tena na ziadanitampa." Mtume akasema: "Hapana! Shamba tu," Basi wakafanyiana khul'u.

Linakuja swali katika aya hii: Kwa nini ikaja dhamiri ya wawili katika"Isipokuwa wakiogopa (wote wawili) ya kwamba hawataweza kusimamishamipaka ya Mwenyezi Mungu." Kisha ikaja dhamiri ya wengi kwa kusema:"Na kama mkiogopa". Kwa nini dhamiri zisiafikiane katika jumla mbili?

Jibu: Dhamiri ya wote wawili ni ya mke na mume, na dhamiri ya 'mkio-gopa' ni ya mahakimu na wasuluhishi. Yaani wakiogopa mume na mke,mahakimu na wasuluhishi kushindwa kusimamishwa mipaka ya MwenyeziMungu. Makusudio hasa ni kuondoa hofu ya kutoa na kuchukua kwa wote.

Swali la pili: Kwa nini ikaja dhamiri ya wawili katika: Si dhambi juu yao(mume na mke), na tunajua kuwa anayepokea ni mume tu.

Jibu: Hapa pametumiwa dhamiri ya wawili kuonesha kwamba hapanaubaya kwa alichotoa mke na kwa alichochukua mume; kwa kufahamukuwa kujuzu kutoa kunalazimisha kujuzu kupokea.

Swali la tatu: Ikiwa mke na mume wameridhiana kufanya khul'u, mkeakatoa mali ili aachwe; lakini uhusiano wao ni mzuri. Je, itaswihi khul'una itafaa mume achukue fidia?

Page 199: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

189

Madhehebu zote nne zimesema khul'u itafaa, na itafungamana na atharizote za khul'u.

Shia Imamiyya wamesema haiswihi hiyo khul'u, wala mtaliki hawezikumiliki fidia. Lakini talaka itaswihi, na itakuwa ni talaka rejea kwa shar-ti zake. Wametoa dalili ya kuharibika khul'u na kutojuzu kuchukua fidiakwamba Aya imeshartisha kujuzu hilo kwa kuogopa kuingia katika maa-sia, kama ndoa ikiendelea. Ama Aya inayosema:

"Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni hidaya; lakini waki-watunikia kitu katika hayo mahari kwa ridhaa ya nafsi zao, basi kulenikiwashuke kwa raha." (4:4)

makusudio yake ni kwamba anachotoa mke hapo ni zawadi tu, sio badaliya talaka. Hivyo Aya hiyo iko mbali na khul'u.

Swali la nne: Kama mume akifanya makusudi ubaya ili apate mali kuto-ka kwa mke, na mke naye akatoa mali na ikatolewa talaka kwa misingi hii;je, khul'u itakuwa halali? Na je, ni halali kuchukua mali?

Jibu: Abu Hanifa anasema: "Khul'u ni sahihi, mali ni lazima itolewe, namume ana dhambi."

Shafi na Malik wamesema: "Khul'u ni batili, na mali irudishwe kwamke kwa sababu ya kauli Yake Mwenyezi Mungu:

"... Wala msiwataabishe ili mpate kuwanyang'anya baadhi ya vile mlivy-owapa..." (4:19)

Page 200: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

190

Hayo yamo katika kitabu Al- Mughni, cha Ibn Qud dama,Juz 7, uk 55, chapaya 3.

Shia Imamiyya wamesema: "Haiswihi khul'u, ni haramu kuchukua mali,lakini itakuwa ni talaka rejea kwa kukamilika sharti zake."

Ama sisi tuko katika fikra ya kuwa talaka hiyo ni upuuzi tu, lakiniimekuwa; sio khul'u wala talaka rejea, kwa sababu kinachojengeka kwauharibifu ndio kimeharibika chote. Hayo tumeyafafanua zaidi katikakitabu Fiqhul Imam Jafar Sadiq, Juz 6, Mlango wa Khul'u, kifungu chaHukumu za khul'u.

Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hapompaka aolewe na mume mwingine. Na (mume wa pili) akimwacha,basi hapo hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watasi-mamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu.

Maana ni kuwa mwenye kumwacha mkewe mara tatu, basi si halali kwakekumwoa tena mpaka aolewe na mume mwingine kwa ndoa sahihi, tenaamwingilie. Imekuja Hadith inayosema: "Si halali kwa mume wa kwan-za mpaka wa pili amwonje (amwingilie)."

Huyu mume wa pili ndiye anayeitwa muhallil (mhalalishaji); Ni lazimaawe ni baleghe, na ndoa iwe ya daima sio ya mut'a. Zikitimia sharti; kishamume wa pili akatalikiana naye kwa mauti au talaka, na ikaisha eda, basiitafaa kwa mume wa kwanza kufunga ndoa naye tena.

Page 201: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

191

231. Na mtakapowapawanawake talaka, wakafikiamuda wao, basi washikenikwa wema au waacheni kwawema. Wala msiwawekekwa kudhuriana mkafanyauadui. Na atakayefanyah i v y o , a m e j i d h u l u m umwenyewe. Wala msiz-ifanyie mzaha Aya zaMwenyezi Mungu. Na kum-bukeni neema ya MwenyeziMungu juu yenu, na Kitabualichowateremshia na heki-ma, kwa kuwaonya. Namcheni Mwenyezi Mungu,na jueni kwamba MwenyeziMungu ni Mjuzi wa kilakitu.

232. Na mtakapowapawanawake talaka nawakafikia muda wao, msi-wazuie kuolewa na waumezao, ikiwa wamepatana kwawema. Hayo anaonywa nayoyule, miongoni mwenu,anayemwamini MwenyeziMungu na Siku ya Mwisho.Hayo ni mazuri mno kwenuna safi kabisa. Na MwenyeziMungu anajua, na nyinyihamjui.

Page 202: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

192

MNAPOWAPA TALAKA WANAWAKE

Aya 231 - 232

MAANA

Na mtakapowapa wanawake talaka, wakafikia muda wao, basiwashikeni kwa wema au waacheni kwa wema.

Msemo huu unaelekezwa kwa waumini wote au kwa watu wote; ni kamavile Mwenyezi Mungu ametaka kusema: Enyi waumini! Atakapompa tala-ka mmoja wenu mkewe.

Baada ya Mwenyezi Mungu kubainisha kwamba mwenye kupewa talakani lazima akae eda, kwamba anaweza kurudiwa na mumewe zikikamili-ka sharti, kwamba ni haramu baada ya talaka ya tatu mpaka aolewe namume mwingine, na kwamba si halali kuchukua kitu kwa mke kwa ajiliya talaka, isipokuwa ikiwa mke ndiye asiyemtaka mume baada yakuyabainisha yote hayo, Mwenyezi Mungu anatubainishia vile tunavy-otakiwa kuchunga haki ya anayekaa eda.

Kuchunga haki kutathibitika kwa mwenye kuacha kuazimia moja kati yamawili: kumrejea mtalaka wake wakati inapokaribia kumalizika eda, kwakukusudia usuluhishi na utangamano mzuri. Na huku ndiko kurejea kwawema. Au kumwacha bila ya kumtaaradhi kwa ubaya pamoja nakumtekelezea kila analostahiki. Na huku ndiko kumwacha kwa wema.

Kwa hivyo inatubainikia kuwa makusudio ya Aya iliyotangulia siyomakusudio ya Aya hii tuliyonayo. Aya ile iliyotangulia inabainisha kuwakurejeana ni talaka ya kwanza na ya pili na siyo ya tatu. Na hii inabain-isha vile tunavyotakiwa kuwafanyia waliopewa talaka; kama ambavyomakusudio ya kufikilia muda wao ni kukurubia, sio kufika hasa.

Wala msiwaweke kwa kudhuriana mkafanya uadui.

Page 203: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

193

Yaani msiwarudie kwa kukusudia kuwaudhi au kuwafanyia ubaya; muware-jee tu kwa makusudio ya kutekeleza haki za unyumba na kusaidiana yaleyaliyo na maslahi kwa wote.

Unaweza kuuliza: Kwa nini imesemwa kudhuriana, ambapo makusudioni kuepusha madhara ya mume kwa mke?

Jibu: Kumdhuru mke kunasababisha kudhurika kwa mume pia, kwasababu ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu juu yake, shutuma za watukwake, na mke kulipiza kisasi. Hapo ndio unyumba unageuka kuwaJahannam kwa mume na mke na huenda moto ukaenea kwa jamaa nandugu. Ndio maana Mwenyezi Mungu anasema: Na atakayefanya hivyo,amejidhulumu mwenyewe. Yaani si kumdhulumu mke peke yake.

Wala msizifanyie mzaha Aya za Mwenyezi Mungu.

Hiki ni kiaga na kemeo kwa yule mwenye kukiuka mipaka ya MwenyeziMungu katika haki za unyumba. Njia ya kuzifanyia mzaha Aya zaMwenyezi Mungu, ambaye limetukuka neno lake, ni kwamba kila mwenyekudai kumwamini Mwenyezi Mungu na hakufuata dini kwa sharia zake,halafu akapuuza hukumu zake, halali yake na haramu yake, basi atakuwaamefanya mzaha, atake asitake. Sawa na anayem-uahidi mtu kitu hali akiwana niya ya kutotekeleza. Baadhi ya wahenga wamesema: "Mwenye kutubudhambi na huku anaendelea nayo ni kama mwenye kumcheza shere Muumbawake."(Mungu apishie mbali!)

Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu.

Miongoni mwa hizo ni kuwa Mwenyezi Mungu ametuumbia wanawake ilitupate utulivu kwao na tusaidiane nao katika yale yenye utengeneo wa famil-ia. Ikiwa tunamwamini Mwenyezi Mungu na tunafuata amri zake kweli, basini juu yetu kufanya lile litakaloleta lengo hili na kujie-pusha na kila linalole-ta uovu katika familia na kuchafua usafi wa maisha ya ndoa.

Na mtapowapa talaka wanawake na wakafikia muda wao, msiwazuie

Page 204: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

194

kuolewa na waume zao.Makusudio ya kufikia muda katika Aya iliyotangulia ni kukaribia kwishaeda na makusudio yake hapa ni kwisha kabisa hiyo eda.

Katika Aya hii kuna mielekezo miwili ya misemo (mnapowapa talaka, namsiwazuie) ambayo wafasiri wamehitilafiana; kwamba, je yoteinaelekezwa upande mmoja au pande tofauti?

Kuna wenye kusema kuwa unaelekezwa kwa upande mmoja tu wawaume; na maana yake ni: Enyi waume, mnapowapa talaka wanawake naeda yao ikaisha, basi msiwazuwie kuolewa na waume wenginewanaowaridhia. Kwa sababu mwanamume alikuwa akimhukumu mtalakawake na kumzuia, kuolewa na mume mwingine baada yake.

Wengine wanasema: Msemo wa kwanza Mtakapowapa talaka, unaelekezwakwa waume, na wapili msiwazuie, unaelekezwa kwa mawalii; kwa maanaya: Enyi waume, mnapowapa talaka wanawake, basi nyinyi mawalii msi-wazuwie watoto wenu kurudiana na waume zao wa kwanza, ikiwa eda imek-wisha. Wanaosema hivi wametoa ushahidi wa Hadith ya Mu'ukil binYasir.* 12

Inaeleweka kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: "Mtakapowapa talakawanawake na wakafikia muda wao msiwazuwie" ni jumla ya pamoja iliyona sharti, na jawabu lake ni msiwazuie.

Ikiwa sharti ya mwenye kumwambia ni mwingine na jawabu liwe kwamwingine na maana yawe ni: Enyi waume mtakapowapa talaka wanawakebasi nyinyi mawalii msiwazuie, hapa kutakuwa na mkorogano ambao hau-paswi kuwapo katika maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.)

Usahihi hasa ni misemo miwili (sharti na jawabu lake) inaelekezwa

* 12 Imepokewa kutoka kwa Mu’ukil bin Yasir kwamba yeye amesema: “Nilikuwa na dadaaliyeolewa na binamu yake kisha akampa talaka wala asimrejee mpaka ikaisha eda, wakatakakurudiana nikamzuia; ndipo ikashuka Aya hii.”

Page 205: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

195

kumoja tu kwa waumini wote; sio waume peke yao wala mawalii tu, wala pia sio kwa wote, bali ni kwawaumini. Hali hii inakuja mara nyingi katika maneno yake MwenyeziMungu (s.w.t.), na maana yanakuwa: Enyi mlioamini mmoja wenu akim-pa talaka mkewe, eda ikaisha na akataka kuolewa na mume mwingine aukurudiwa na mumewe wa kwanza, basi msimzuie kama wakipatana kwawema; yaani wakiazimia kuoana.

Na kauli yake Mwenyezi Mungu: Ikiwa wamepatana kwa wema inafa-hamisha kuwa mke anaweza kujioza yule anayemridhia, bila ya kumngojawalii.

Unaweza kusema: hakika Aya imeuondoa uwalii (usimamizi) kwa wanawakewalioachwa tu, na wala haikuutaaradhi usimamizi kwa wengineo. Kwahivyo kuuondoa usimamizi kwa wanawali kunahitajia dalili.

Jibu: Kuthibitisha usimamizi ndiko kunakohitajia dalili; ama kuondoa, daliliyake ni ya asili kwamba kila aliyebaleghe mwenye akili mume au mke nihuru katika mambo yake wala hatawaliwi na yeyote, kwa vyovyoteatakavyokuwa isipokuwa tu kama atakiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu(s.w.t.)

Hayo anawaonywa nayo yule, miongoni mwenu, anayemwaminiMwenyezi Mungu na siku ya mwisho.

Hayo ni ishara ya hayo aliyoyataja Mwenyezi Mungu katika hukumu zake.Anaonywa nayo, yaani wanaonyeka nayo wenye imani sahihi. Ama wengi-neo katika wenye imani mbovu, masikioni mwao mna vizuwizi, hawasikiimawaidha ya Mwenyezi Mungu na hukumu Zake wala uongozi Wake.

Aya hii ni dalili ya wazi kwamba hakuna imani bila ya ucha Mungu na imanisahihi haiepukani na mawaidha, na asiye waidhika wala kunufaika na amri zaMwenyezi Mungu hana hata chembe ya imani.

Page 206: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

196

Hayo ni mazuri mno kwenu na safi kabisa.

Hayo ni ishara ya mawaidha na kutumia hukumu ya Mwenye-zi Mungu kati-ka maisha ya ndoa kwa ujumla na hasa katika waliopewa talaka. Hakunamwenye shaka kwamba ndoa yenye lengo la utu na kusaidiana katika heri,inaleta ongezeko na usafi katika riziki, usafi wa tabia, heshima na ufanisi kwawatoto. Ama makusudio yakiwa mabaya, basi mwisho wake ni ukafiri,uharibifu, balaa na mashaka katika maisha ya wazazi na watoto.

Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.

Makusudio sio kutupa habari kuwa Yeye ni mjuzi au mjuzi zaidi, hapana.Hilo liko wazi halihiitaji mafunzo wala ufafanuzi. Makusudio hasa ni kutiliamkazo na kuhimiza kutekeleza hukumu Zake Mwenyezi Mungu; hata kamahaikutubainikia njia ya manufaa yapatikanayo katika hukumu hiyo. Kwasababu Mwenyezi Mungu ambaye imetukuka hekima yake, haamrishiisipokuwa lenye heri na maslahi na wala si lazima tuijue heri hiyo kwaufafanuzi; bali inatosha tu kujua kuwa Mwenye kuamrisha na Mwenyekukataza, ni Mjuzi Mwenye hekima, halijifichi lolote Kwake liwe ardhini aumbinguni.

Kwa ujumla ni kuwa kuna tofauti kati ya mumin na asiyekuwa mumin.Mumin anaabudu kulingana na kauli ya Mwenyezi Mungu na anafanyaamali katika hali ya kuyakinisha kupatikana manufaa, hata kama atashind-wa kuyafahamu kwa ufafanuzi.

Ama asiyekuwa mumin hafanyi kitu mpaka ajue au adhani kuwa kunamanufaa anayoyajua yeye mwenyewe kwa akili yake au aongozwe nakiumbe kama yeye, ambapo mara nyingi anaruka patupu na kubainikiwana kinyume, lakini mumin anakuwa katika amani ya Mwenyezi Mungu nahifadhi Yake.

Page 207: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

233. Na wazazi wa kikewawanyonyeshe watoto waomiaka miwili kamili, kwaanayetaka kukamilisha kun-yonyesha; na ni juu yaaliyezaliwa mtoto huyo(baba) chakula chao na nguozao kulingana na desturi.Wala haikalifishwi nafsiyoyote ila kwa uweza wake.Mzazi (Mama) asitiwetaabuni kwa ajili yamwanawe, wala aliyezaliwamtoto (baba) kwa ajili yamwanawe. Na juu ya mrithini mfano wa hivyo. Nakama wote wawili wakitakakumwachisha (kunyonya)kwa kuridhiana na kushau-riana, basi si kosa juu yao.Na kama mkitaka kuwapa-tia watoto wenu Mama(wengine) wa kuwanyoye-sha, basi haitakuwa vibayajuu yenu kama mkitoa mli-chowaahidi, kwa desturi. Namcheni Mwenyezi Munguna jueni kwamba MwenyeziMungu anayaona mnayoya-tenda.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

197

Page 208: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

MAMA WANYONYESHEAya 233

MAANA

Na wazazi wa kike wawanyonyeshe watoto wao.

Wafasiri wamehitilafiana katika makusudio ya tamko la wazazi wa kike. Je, ni waliopewa talaka tu, au ni walio kwa waume zao tu, au wote pamo-ja? Wengi wanasema kwamba tamko hilo linawakusanya wote kwa kuan-galia kidhahiri; wala hakuna dalili ya kuhusisha upande mmoja tu. Nasisi tunaelekea upande huu. Kwa sababu kunyonyesha kunamtegemeamama kwa hali yoyote awayo, sio kwa kuwa na mume wala kwa kuwa nimtalikiwa.

Wawanyonyeshe watoto wao: ni amri ya mapendekezo tu, sio lazima;kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

"... Na kama mkiona uzito kati yenu, basi amnyonyeshee (mwanamke)mwingine." (65:6)

Maana yake ni kuwa akina mama wanayo haki ya kuwanyonyesha wato-to wao kuliko watu wengine.

Unaweza kuuliza kwamba kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na ni juu yababa chakula chao na nguo zao" inatilia nguvu kuwa makusudio yaWazazi watakao nyonyesha ni wanawake walioolewa au walio katikatalaka rejea tu; na wala sio walioachwa ambao imekwisha eda yao. Kwasababu mtalikiwa, chake ni malipo ya kunyonyesha tu sio chakula; kwa hiyo Aya haiwahusishi waliopewa talaka.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

198

Page 209: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Jibu: Hapana kizuizi kwa tamko moja kuenea kihukumu kwa upandemmoja na kuhusika upande mwingine pamoja na kupatikana dalili. Ikohadithi na wamekongamana wanavyuoni kuwa mwenye kupewa talakahana posho isipokuwa malipo ya kunyonyesha; kwa hiyo hakuna daliliiliyohusisha upande fulani, basi tunafuata kuenea kwa wote.(aliye katikandoa na mtalikiwa)

MIAKA MIWILI KAMILI.

Hapa kuna maswali mawili: Kwanza: Je, inafaa mama kunyonyeshamtoto zaidi ya miaka miwili?

Jibu: Ndio, hasa ikiwa mtoto anahitajia ziada. Kuwekwa kiwango chamiaka miwili kuna faida tatu:

1. Mama asidai malipo zaidi ya miaka miwili.

2. Ukitokea mzozano kati ya baba na mama kuhusu muda wa kunyonyeshamtoto, basi hukumu itakuwa ya Mwenyezi Mungu: 'Miaka miwilikamili.'

3. Kunyonyeshwa mtoto baada ya miaka miwili na mtu kandohakuwezi kusababisha uharamu kati ya mnyonyeshaji na mtoto: Hivyondivyo walivyosema Shia na Shafii. Ama Abu Hanifa yeye amesemahiyo ni mpaka baada ya miezi thelathini.

Swali la pili: Je, inafaa kupunguza muda wa miaka miwili?

Jibu: Inafaa kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Kwa anayetakakukamilisha kunyonyesha.

Na pia kauli yake: Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwakur-idhiana na kushauriana, basi si kosa juu yao

Je, tutarudia sharia katika kiwango cha chini cha muda wa kunyonyesha,au tutaangalia hali ya afya ya mtoto?

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

199

Page 210: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Mafaqihi wengi wamesema uchache wa muda wa kunyonyesha ni miezi21 kwa kauli yake Mwenyezi Mungu:

"... Na kubeba mimba kwake na kumwachisha ziwa ni miezi thelathini..."(46:15)

Tukitoa miezi tisa ambayo aghlabu inakuwa ya mimba, inabakia mieziishirini na moja.

Kwa vyovyote ilivyo, umuhimu ni kuchunga afya ya mtoto na maslahiyake ambayo yanatofautiana kwa kutofautiana miili. Na utafiti huuulikuwa na umuhimu hapo zamani ambapo hakukuwa na lishe yakutosha. Ama hivi leo ambapo lishe zimejaa tele, suala hili halinamaudhui tena.

Na ni juu ya aliyezaliwa mtoto huyo (baba) chakula chao na nguo zaokulingana na desturi.

Kwa dhahiri ulazima wa kulea uliotajwa hapa ni kwa mke na aliye katikaeda ya talaka rejea. Kimetajwa chakula na mavazi kwa sababu yaumuhimu wake.

Makusudio ya desturi ni kuangalia hali ya matumizi ya mke katika jamiiyake. Ama kuangalia hali ya mume kimali, Mwenyezi Mungu anasema:

Haikalifishwi nafsi yoyote ila kwa uweza wake.

Tafsir wazi ya jumla hii tunaweza kuipata katika kauli yake MwenyeziMungu:

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

200

Page 211: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

"Mwenye uwezo atoe kadiri ya uwezo wake; na yule ambaye amepun-gukiwa riziki yake, atoe katika kile alichopewa na Mwenyezi Mungu;Mwenyezi Mungu hamkalifishi mtu yoyote ila kwa kadiri ya alichom-pa..."(65:7)

Imam Jaffar Sadiq (a.s.) alikuwa na marafiki wengi, mara nyinginewalikuwa wakichelewa kuondoka nyumbani kwake mpaka unafika wakatiwa chakula, basi huwaletea chakula; mara huwaletea mkate na siki na maranyingine huwaletea chakula kizuri kabisa. Mmoja akamuuliza sababu yakufanya hivyo. Imam akamjibu: "Tukiwa na nafasi tunawapa cha nafasi natukiwa na dhiki tunawapa cha dhiki."

Mzazi (Mama) asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala mwenyekuzaliwa mtoto (baba) kwa ajili ya mwanawe.

Inapasa kuangalia vizuri Aya hii, kwa sababu makadhi hivi sasa wanatoaushahidi sana kwa Aya hii katika hukumu zao na kuifasiri kuwa baba asimd-huru mama kwa sababu ya mtoto. Ama watu wa tafsiri wanakurubiakuafikiana kwa pamoja kwamba maana yake ni kinyume na hivyo; kwambamama asikatae kumnyonyesha mtoto wake na kumdhuru kwa kutakakumkasirisha baba yake kwa hilo.

Mwenye Majmaul Bayan anasema: "Mama asiache kumnyonyesha mtotowake kwa ajili ya kumuudhi baba yake." Sasa haya yako wapi na ushahidi wamakadhi kwamba baba asimdhuru mama kwa sababu ya mtoto?

Na sisi tunasema, baada ya kuitia akilini Aya bila ya kutegemea zaidimaneno ya mafaqihi na wafasiri, kwamba mara nyingi kunapotokeakutengana kati ya mtu na mkewe, humfanya mtoto ndio chombo chakukasirishana, na matokeo yake mtoto hudhurika kwa kumfanya mtotondio kafara la ugomvi wao.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

201

Page 212: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Mfano mama anaweza kukataa kumnyonyesha mtoto, hata kama iko haja,ili amuudhi baba. Au baba anaweza kumnyang'anya mama mtoto nakumpatia mtu mwingine amnyonyeshe, hata kama mamake anataka kum-nyonyesha.

Mwenyezi Mungu amekataza kudhuriana kwa namna yoyote ile, iwe kwamtoto, baba au mama kwa sababu ya mtoto. Haya ndiyo yanayokuja harakakwenye fahamu katika kauli yake Mwenyezi Mungu. Wala hayapingani nakauli ya wafasiri, isipokuwa yanayopingana ni kutolea ushahidi makadhi;ingawaje kauli yao yenyewe ni sahihi, lakini makosa yako katika kutoleaushahidi.

Na juu ya mrithi ni mfano wa hivyo .

Wamehitalifiana kuhusu makusudio ya mrithi, je ni mrithi wa baba aumrithi wa mtoto?

Mfumo wa maneno unatilia nguvu kwamba ni mrithi wa mwenye mtoto(baba), lakini maana hayasimami sawa. Kwa sababu mtoto na mama ni kati-ka jumla ya warithi wa baba na kwamba kauli yake Mwenyezi Mungumfano wa hivyo inaonyesha ni wajibu kwa mrithi wa baba kutoa posho ileiliyo wajibu kwa baba.

Kwa hivyo inamaanisha posho ya mama ni wajibu kwa mama, kwa mtotowake na kwa warithi wengine wakiwepo. Inavyo-julikana ni kuwa posho yamama si wajibu kwa yeyote ikiwa huyo mama anauwezo; ni sawa uwezo huouwe umetokana na kumrithi mume, au la. Kwa hivyo basi hakuna maanakusema kuwa ni wajibu kujilisha kutokana na mali yake.

Kama tukifasiri mrithi kwa maana ya mrithi wa mtoto, basi itakuwa tunahi-talifiana na dhahiri kwa upande mmoja; pia tutakuwa tunahitilifiana na haliilivyo kwa upande mwingine. Kwa sababu posho ya mama si wajibu kwaanaye mrithi mtoto. Ni kweli kuwa Mama anaweza kuchukua ujira wa kun-yonyesha kutoka katika mali ya mtoto wake (anaye mnyonyesha), ikiwaanayo mali, lakini ujira wa kunyonyesha ni kitu kingine na posho ni kitukingine kwa maana yake sahihi.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

202

Page 213: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Ilivyo hasa ni kwamba Aya hii ni miongoni mwa Aya za mifano zenye kuta-tiza ndio maana Malik akasema kuwa ni Mansukh (iliyoachwa hukumuyake) kama alivyonakili Abu bakr Al-maliki katika kitabu cha AhkamulQur'an. Baadhi ya wafasiri wameiruka na wengine wameinakilia kauli zisizokuwa na nguvu.

Kutatiza kwake kama tulivyobainisha ni ikiwa itabaki dhahiri ilivyo, maanahayatasimama sawa; yaani tukifasiri mrithi kwa maana ya mrithi wa baba nakufasiri mfano wa hivyo kwa maana ya posho ya mama. Na kama tukifasirimrithi kwa maana ya mrithi wa mtoto na mfano wa hivyo kwa maana yamalipo ya kunyonyesha, maana yatakuwa sawa lakini tutakuwa tunahitalifi-ana na dhahiri ya matamko mawili (mrithi na mfano wa hivyo). lakinihakuna njia nyingine zaidi ya kuhitalifiana na dhahiri ya tamko na kulifasirikimaana (taawili). Sio mbali kuwa Hadith zenye kupokewa katika kuny-onyesha na malipo yake, ni mfano wa dalili ya kuswihi taawili hii.

Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha (kunyonya) kwakuridhiana na kushauriana, basi si kosa juu yao.

Yaani baba na mama kwa kushauriana wanaweza kumwachisha mtotokabla ya miaka miwili au baada yake kwa maslahi ya mtoto; bali inajuzukwa baba kumpa mnyonyeshaji mwingine; Mwenyezi Mungu ame-lionyesha hilo kwa kusema:

Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu Mama (wengine) wa kuwany-onyesha, basi haitakuwa vibaya juu yenu kama mkitoa mlichowaahidi kwadesturi.

Msemo 'mkitoa mlichowaahidi,' unaele-kezwa kwa akina baba. Maana yakeni enyi akina baba! Hakika mama ana haki zaidi ya kumyonyeshamwanawe kuliko mtu wa kando; naye mama anastahiki malipo ya kawaida.Ikiwa mumempa haki hii na mkamdhamiria kumpa malipo ya kunyonyeshaya kawaida, lakini akataka zaidi, basi si vibaya hapo kuwapatia watotowenu wanyonyeshaji wengine. Imesemwa kuwa maana yake ni mkiwapatiawanyonyeshaji wa nje malipo ya kawaida si vibaya kwenu.Vyovyote iwavyo, ni juu ya baba kumpatia haki (malipo) yake kila mmoja,awe mama au mama wa kunyonyesha tu.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

203

Page 214: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

204

234. Na wale wanaokufa miongo-ni mwenu na kuacha wake(hao wake) wangoje mieziminne na siku kumi. Nawanapofikilia muda wao,vibaya kwenu kwa yalewanayojifanyia, yanayoafikiada. Na Mwenyezi Munguana habari za mnayoyaten-da.

235. Wala si vibaya kwenukuonyesha ishara ya kuwa-posa wanawake, au kutiaazma katika nyoyo zenu.Mwenyezi Mungu anajuakwamba nyinyi mtawakum-buka. Lakini msifanye naoahadi kwa siri; isipokuwamseme maneno yaliy-oruhusiwa na sharia. Walamsiazimie kufunga ndoampaka muda uliofaradhiwaufike. Na jueni ya kwambaMwenyezi Mungu anayajuayaliomo katika nafsi zenu,basi tahadharini naye. Najueni kwamba MwenyeziMungu ni Mwenye maghufi-ra, mpole.

Page 215: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

EDA YA KUFIWA

Aya 234 - 235:

MAANA

Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake; wangoje mieziminne na siku kumi.

Mafaqihi wote wameafikiana kwamba eda ya mwenye kufiwa na mume nimiezi minne na siku kumi. Awe mkubwa au mdogo; mwenye kutoka hedhiau aliyekoma, mwenye kuingiliwa au la. wamelitolea dalili hilo kwa Ayahii.

Ama akiwa na mimba, madhehebu manne ya kisunni yamesema: Eda yakeitakwisha kwa kuzaa; hata kama ni muda mchache tu, baada ya kufamumewe, kiasi ambacho anaweza kuolewa hata kabla ya kuzikwa mumewe,kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu:

"... Na wanawake wenye mimba eda yao ni mpaka watakapo-zaa..." (65:4)

Mafaqihi wa Kishia wamesema: Eda yake ni ule muda utakaorefuka zaidi;yaani ikipita miezi minne na siku kumi kabla ya kuzaa atangojea mpakaazae; au akizaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi, atakaa eda yamiezi minne na siku kumi. Wametoa dalili juu ya hilo kwa ulazima wakukusanya Aya mbili; "Wangoje miezi minne na siku kumi" na "Eda yaoni mpaka watakapozaa."

Aya ya kwanza imejaalia eda kuwa ni miezi minne na siku kumi, nayoinakusanya mwenye mimba na asiye na mimba; na Aya ya pili imeifanyaeda ya mwenye mimba ni kuzaa, nayo inakusanya mwenye kuachwa namwenye kufiwa na mumewe. Kwa hivyo kutakuwa na mgongano kati yadhahiri ya Aya mbili kwa mwanamke mwenye mimba ambaye atazaa kabla

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

205

Page 216: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

ya miezi minne na siku kumi: Kwa mujibu wa Aya ya pili itakuwa edaimekwisha na kwa mujibu wa Aya ya kwanza itakuwa bado haijaisha kwasababu miezi minne na siku kumi haikutimia.

Vile vile utapatikana mgongano ikipita miezi minne na siku kumi, akiwabado hajazaa; kwa mujibu wa Aya ya kwanza eda itakuwa imekwisha kwasababu muda wa miezi minne na siku kumi umekwisha; na kwa mujibu waAya ya pili itakuwa eda bado haijaisha kwa sababu hajazaa. Na manenoya Qur'an ni mamoja ni lazima yaafikiane.

Kwa hivyo tukiziunganisha Aya mbili na kuzikusanya katika jumla moja,zikawa hivi; "Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake; wan-goje miezi minne na siku kumi. Na wanawake wenye mimba eda yao nimpaka watakapozaa."Tukizikusanya hivi, maana yake yatakuwa ni: Eda yamwenye kufiwa na mumewe ni miezi minne na siku kumi, kwa asiyekuwa namimba; na mwenye mimba ambaye atazaa kabla ya kupita miezi minne nasiku kumi. Na itakuwa eda ya mwenye kufiwa, mwenye mimba ambayeatazaa baada ya kupita miezi minne na siku kumi, ni kuzaa. Kama akiulizamwulizaji: Vipi Shia wamefanya eda ya mwenye mimba, aliyefiwa namume, ni muda utakaorefuka pamoja na kwamba Aya "Na wanawake wenyemimba eda yao ni mpaka watakapozaa", iko wazi kwamba eda inaisha kwakuzaa?

Shia naye anaweza kujibu kwa kusema: "Vipi madhehebu manne yaSunni yakasema kuwa eda ya mjane mwenye mimba inaweza kuwa hatamiaka miwili kama ikiendelea mimba pamoja na kuwa Aya "Na walewanaokufa miongoni mwenu na kuwaacha wake, (nao wake) wakae wan-goje miezi minne na siku kumi" iko wazi kwamba eda ni miezi minne nasiku kumi?"

Kwa hiyo hakuna jengine lolote la kuchukulia Aya mbili isipokuwa kuchuku-lia kauli ya muda utakaorefuka zaidi.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

206

Page 217: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Na wanapofikia muda wao, basi si vibaya kwenu kwa yale wanayoji-fanyia, yanayoafiki ada Mwenyezi Mungu anazo habari mnayoyaten-da.

Yaani kama ukisha muda wa eda ya mjane, basi hapana dhambi kwenu enyiWaislamu kwa mwanamke kufanya yale aliyozuiliwa wakati wa eda; kamakujipamba na kuonekana, na wanaotaka kuwaoa kwa njia ile iliyo maarufukisheria. Hapa Mwenyezi Mungu anawaambia Waislamu wanaume, kwasababu ni juu yao kuwazuia wanawake wanapopetuka mipaka ya kisheria.Wameafikiana mafaqihi kwa kauli moja kuwa mjane aliyefiwa na mumewakati wa eda ni wajibu kwake kujiepusha na kila linalomfanyakuonekana mrembo wa kutamanika.

Wala si vibaya kwenu kuonyesha ishara ya kuwaposa wanawake.

Mwenyezi Mungu ameharamisha ndoa katikati ya eda ya namna yoyote,bali ni haramu pia kwa mwanamume kumposa mwanamke akiwa katikaeda yake, iwe ni eda ya kufiwa na mume au ya talaka bain, lakiniMwenyezi Mungu anahalalisha kufanya ishara ya posa bila ya kudhi-hirisha, katika isiyokuwa eda ya talaka rejea. Kwani mtalaka katika edahiyo bado yuko mikononi mwa mumewe.

Au kutia azma katika nyoyo zenu.

Kila linalopita akilini na kuazimiwa na moyo halina ubaya kwa Mungu, kwasababu liko nje ya uwezo wa mtu; lililo kwenye uwezo wa mtu ni zile athari.Kwa hivyo mtu akiazimia kuoa mke aliye edani, sio dhambi. Lakini akiidhi-hirisha azma yake hii akamposa, basi atakuwa ni mwenye dhambi. Kwasababu kuazimia kuko nje ya uwezo na kudhihirisha kuko ndani ya uwezo wamtu. Iko Hadith inayosema: "Ukiwa na donge moyoni usilitekeleze." Hapoamekataza kufanya, ambako ni athari ya hilo donge, lakini hakukataza kuwa nadonge kwa sababu hakuzuiliki.

Mwenyezi Mungu anajua kwamba nyinyi mtawakumbuka.Kwa hivyo ndio akawahalalishia kuonyesha ishara, lau angeliwazuia basimngeliona mashaka.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

207

Page 218: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Lakini msifanye nao ahadi kwa siri.

Hiyo ishara ya kuoa pia haifai kuionyesha kwa siri wakati wa eda katikafaragha. Kwa sababu faragha kati ya mwanamume na mwanamke inale-ta mambo asiyoyaridhia Mwenyezi Mungu. Iko Hadith inayosema:

"Hakai faragha mwanamume na mwanamke isipokuwa shetani huwawatatu wao." Hasa ikiwa mume anamtamani aliyekaa naye faragha,isipokuwa ikiwa mume ana yakini kwamba faragha haitaleta haramu kati-ka maneno wala vitendo, hapo ndipo itajuzu kusema naye yale ambayo simabaya, hata kusema kwa dhahiri. Ndio Mwenyezi Mungu akalegeza kido-go kwa kusema; "Isipokuwa mseme maneno yaliyoruhusiwa na sharia."

Wala msiazimie kufunga ndoa mpaka muda uliofaradhiwa ufike.

Yaani msifunge ndoa ndani ya eda mpaka ishe.

NDOA KATIKA EDA

Baada ya kuafikiana Waislamu wote kwamba kufunga ndoa na kuposawazi wazi katikati ya eda, ni katika mambo ya haramu, na kwamba ndoaitakuwa batili baada ya kuafikiana hivi, wakahitalifiana juu ya uharamuwa waliofunga ndoa ndani ya eda. Je mwanamke atakuwa haramu mileleau inawezekana kufunga ndoa tena baada ya kwisha eda?

Hanafi na Shafi wamesema hakuna kizuizi cha kumwoa mara ya pili. Hayoyamo katika kitabu Bidayatul Mujtahid.

Shia wamesema: Akifunga naye ndoa na hali anajua kuwa yuko katikaeda, basi atakuwa haramu kwake daima, iwe amemwingilia auhakumwingila. Na akifunga naye ndoa bila ya kujua kuwa yuko kwenyeeda, basi hatakuwa haramu, isipokuwa kama amemwingilia, na anawezakumwoa tena baada ya eda kama hakumwingilia.

Hii ndio hukumu ya kufunga ndoa katikati ya eda. Ama kuposa hakunaathari yoyote isipokuwa dhambi tu.

Maajabu niliyoyasoma katika suala hili ni yale yaliyo katika kitabu AhkamulQur'an cha Abu Bakr Al Andalusi wa madhehebu ya Malik, pale aliposema:

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

208

Page 219: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

“Akimposa katikati ya eda, kisha akafunga naye ndoa baada ya eda, basini lazima amwache talaka moja, kisha aanze upya kumchumbia na kufungandoa.”

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

209

236. Si vibaya kwenu kamamkiwapa wake talakaambao hamjawagusa aukuwabainishia mahari. Nawapeni cha kuwali-waza,mwenye wasaa kadiri aweza-vyo na mwenye dhiki kadiriawezavyo. Kiasi cha kuwali-waza, cha kawaida. Ndiohaki kwa wafanyao mema.

237. Na kama mkiwapa talakakabla ya kuwagusa nammekwisha wakadiriamahari, basi ni nusu ya hayomahari mliyokadiria.Isipokuwa (wanawakewenyewe) wasamehe auasamehe ambaye kifungocha ndoa kiko mikononimwake, na kusamehe ndikokuliko karibu zaidi natakua. Wala msisahau fad-hila baina yenu; hakikaMwenyezi Mungu anayaonamnayoyafanya.

Page 220: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

TALAKA KABLA YA KUINGILIA

Aya 236 -237

MAANA

Si vibaya kwenu kama mkiwapa wake talaka ambao hamjawagusaau kuwabainishia mahari

Yaani hamlazimiwi na mahari. Kwa ujumla maana yake ni kwamba mwenyekufunga ndoa na mwanamke wala asimtajie mahari katika ndoa, kishaakamwacha kabla ya kumwingila, basi hana ulazima wa kutoa mahari;isipokuwa mwanamke anastahiki kupewa kiasi cha kumliwaza tu. Kiasihicho ataangalia mume uwezo wake; kwa mfano tajiri anaweza kutoa mkufuwa thamani ya shs. 1000, mtu wa kawaida akitoa bangili ya Shs. 500 namasikini akatoa nguo ya Shs. 20. Katika haya Mwenyezi Mungu anasema:

Na wapeni cha kuwaliwaza mwenye wasaa kadiri awezavyo, namwenye dhiki kadiri awezavyo. Kiasi cha kuwaliwaza, cha kawaida.Ndio Haki kwa wafanyao mema.

Wale ambao wanazifanyia wema nafsi zao kwa kumtii Mwenyezi Mungu(s.w.t.)

Na kama mkiwapa talaka kabla ya kuwagusa na mmekwishawakadiria mahari, basi ni nusu ya hayo mahari mliyokadiria.

Ikiwa amefunga ndoa akataja mahari kisha akamwacha kabla yakumwingilia, basi anastahiki nusu ya mahari.

Isipokuwa (wanawake wenyewe) wasamehe.

Yaani haifai kumzuilia mwanamke nusu ya mahari au kitu chochote,isipokuwa kama akisamehe mwenyewe kwa radhi yake.

Au asamehe ambaye kifungo cha ndoa kiko mikononi mwake.

Mume ndiye ambaye kifungo cha ndoa kiko mikononi mwake. Makusudioni kwamba mwenye kupewa talaka kabla ya kuingiliwa hastahiki zaidi

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

210

Page 221: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

ya nusu ya mahari yaliyotajwa isipokuwa kama mume atampa yote aukumpa zaidi ya nusu.

Na kusamehe ndiko kuliko karibu zaidi na takua.

Msemo unaelekezwa kwa wote, mume na mke, kuwahimiza kusameheana.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

211

238. Angalieni sana swala, na ileswala ya katikati. Na sima-meni kwa unyenyekevu kwaajili ya Mwenyezi Mungu.

239. Na kama mkiwa na hofu,basi ni hali ya kuwamnakwenda kwa miguu aummepanda. Namtakapokuwa katika amani,basi mkumbukeni MwenyeziMungu kama alivyowafunzayale mliyokuwa hamyajui.

SWALA YA KATIKATI

Aya 238 - 239:

Angalieni sana Swala na ile Swala ya katikati

Kuziangalia sana ni kuzitekeleza kwa nyakati zake na njia zake. MwenyeziMungu ameihusisha hii kwa kuipa uzito na umuhimu; kama umuhimu waJibril na Mikail katika Malaika alipowahusu wao, baada ya kuwakusanya naMalaika wen-gine katika kauli yake:

Page 222: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Ambaye ni adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wakena Jibril na Mikail..." (2:98)

Wamehitalifiana kuhusu swala ya katikati, mpaka kufikia kauli kumi na nane;kama ilivyonakiliwa katika kitabu Naylul Awtwar. Kauli iliyo mashuhuri zaidini ile inayosema kuwa ni swala ya Alasiri, na kuna riwaya katika hilo.Imesemwa kwamba imeitwa swala ya katikati kwa sababu iko baina ya swalambili za (Maghribi na Isha) na swala mbili (Asubuhi na Adhuhuri). Amasababu ya kutajwa kwake ni kwamba inakuwa wakati ambao aghlab watuwanashughulika.

Mwenye tafsir ya Al Manar amenakili kutoka kwa Ustadh wake, SheikhMuhammad Abduh, kwamba yeye amesema: Lau si kuwako kongamano juuya tafsiri ya Wusta kuwa ni moja ya swala tano na wala sio tano zote, basiyeye angeliifasiri kwa swala bora; na Mwenyezi Mungu amehimiza na kutil-ia mkazo swala bora nayo ni ile ambayo moyo unakuwapo ndani ya hiyoswala, nafsi kuwa na mwelekeo wa kuwa na ikhlas kwa Mwenyezi Munguna kuzingatia maneno Yake. Sio swala ya kujionyesha au ya mwili tu, lakinimoyo haupo.

Haya ndiyo maelezo mazuri zaidi niliyosoma katika tafsiri ya Aya hii,nayo yanatiliwa nguvu na kauli yake Mwenyezi Mungu:

Wamefuzu waumini ambao katika swala zao huwa ni wanyenyeke-vu."(23:1-2)

Na simameni kwa unyenyekevu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Yaani mumuombe Mwenyezi Mungu katika swala zenu kwa unyenyeke-vu wa kuhisi ukubwa na utukufu wake, hali ya kuachana na mamboyanayoushughulisha moyo.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

212

Page 223: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Na kama mkiwa na hofu basi ni hali ya kuwa mnakwenda kwamiguu au mmepanda.

Swala haisamehewi kwa hali yoyote ile. Mtu akiwa anashindwa kufanyabaadhi ya vitendo vyake, basi atatekeleza vile atakavyoweza. Akishindwakufanya vitendo vyote, basi ataswali kwa kutamka na kuashiria. Ikiwahivyo pia atashindwa, basi ataleta picha ya swala moyoni.

Hapa anaashiria Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwamba mtu anaweza kufiki-wa na wakati wa Swala naye yuko vitani akiwa amekabiliana na adui, n.k.basi ataswali kadiri atakavyoweza, kwa kwenda au akiwa amepanda kitu;kwa kuelekea Qibla au bila ya kuelekea.

Mwenye Majmaul Bayan anasema: “Swala ya kuhofia adui ni rakaa mbiliiwe ni safirini au nyumbani, isipokuwa Maghrib tu, hiyo ni rakaa tatu.

Imepokewa Hadith kwamba Imam Ali (a.s.) katika usiku wa vita vya Hariraliswali kwa kuashiria na ikasemwa ni kwa takbir, na kwamba Mtume(s.a.w.w.) siku ya vita vya Ahzab aliswali kwa kuashiria.

Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Mwenyezi Mungukama alivyowafunza yale mliyokuwa hamyajui.

Yaani hofu ikiondoka basi swalini swala ya kawaida ile mliyofundishwamwanzo.

KUACHA SWALA KUNAPELEKEA UKAFIRI

Tumezungumzia swala katika kufasiri Aya iliyotangulia na sasa tunaun-ganisha kifungu hicho na haya yafuatayo:

Majaribio yamethibitisha kwamba kuacha swala mara nyingi kunapele-ka ukafiri na athari zake. Hiyo ni kwamba kafiri hajali kufanya haramu,basi hivyo hivyo mwenye kuacha swala anafanya mambo ya haramu bilaya kujali. Popote penye ukafiri pana uovu na uchafu. Hali hiyo inaletwana kuacha swala.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

213

Page 224: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Dalili kubwa zaidi inayoonyesha hakika hii ni ufisadi katika zama zetuhizi. Haya mabaa, madanguro na ma casino katika miji yetu. Na pia hukukutembea nusu-uchi kwa mabinti zenu na tabia mbaya za watoto wetu(kuiga wazungu), yote hayo ni natija ya kuacha swala; kwa dalili ya kuwahaya yote hayakuwako wakati wa swala ilipokuwa imezoeleka kwa wato-to wetu wa kiume na wa kike. Hiyo ndiyo tafsir ya Hadith tukufu inayose-ma:

"Tofauti kati yetu sisi na nyinyi (makafiri) ni swala; mwenye kuiachaamekufuru."

Haitamtosha mtu kusema: Mimi ni Mwislamu au kutamka shahada mbili(kushahadia) tu, maadamu amali zake ni za kikafiri na kilahidi.

Hakika mlahidi haoni haya wala kigegezi chochote kuacha swala, nahafichi hilo, bali hutangaza hasa, kwa sababu hafuati dini. Basi hivyohivyo vijana wetu wa kileo wanaona fahari kujulikana kuwa hawaswali,bali wanamdharau mwenye kuswali na swala yenyewe. Kwa hivyo haku-na tofauti kati yao na walahidi.

Si vibaya kama tukinukuu mawaidha mazuri kutoka katika kitabu Al-IslamKhawatir wa Sawanih cha Mfaransa, Comte Henry Descarte kilichofasiri-wa kwa Kiarabu anasema:

"Nilisafiri katika jangwa la jimbo la Hawaran nikiwa na wapanda farasi the-lathini, wote wakinihudumia mimi. Wakati tukiendelea na msafara, mara sautiikanadi kwamba wakati wa swala ya Alasiri umefika. Wapanda farasi wotewakashuka haraka; mara wakajipanga safu za swala ya jamaa, nikawaninawasikia wakilikariri neno Allahu Akbar kwa sauti ya juu. Likawa jinahilo la Mungu linaniingia akilini zaidi kuliko nilivyoingiwa akilini na somola elimu ya Mungu. Nikahisi kukosa raha kuliko sababishwa na haya nakuhisi kwamba hao wapanda farasi ambao walikuwa wakinitukuza mudamchache uliopita, hivi sasa wakiwa katika swala yao, wanahisi kwamba wakokatika makao ya juu zaidi na wenye nafsi tukufu zaidi kuliko mimi. Launingeitii nafsi yangu ningeliwapigia kelele kwa kusema: Mimi pianinamkubali Mungu na ninajua Swala.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

214

Page 225: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Ni uzuri ulioje wa mandhari ya watu hao katika swala yao na huku farasi waowako pembeni mwao wakiwa wametulia kimya kamba zao zikiwa chini,kama kwamba wao nao wanainyenyekea swala; farasi aliyekuwa akipendwana Mtume kwa mapenzi ambayo yalimpelekea Mtume kuifuta pua yake kwashuka yake.

Nilisimama pembeni nikiwaangalia wan-aoswali na kujikuta mimi nikopweke kabisa nikionyesha alama ya kukosa imani, kana kwamba mimi nimbwa tu, aliye mbele ya wale wanaomkariria Swala Mola wao kwaunyenyekevu unaotoka katika nyoyo zilizojaa ukweli na imani.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

215

Page 226: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

240. Na wale wanaokufa miongo-ni mwenu na wakaachawake, wausie kwa ajili yawake zao kupata matumiziya mwaka mmoja bila yakutolewa. Wakiondoka, basisi vibaya kwenu kwa yalewaliyojifanyia wenyewe,yanayofuata desturi. NaMwenyezi Mungu niMwenye nguvu, Mwenyehekima.

241. Na wanawake waliopewatalaka wapewe cha kuwali-waza kulingana na desturi;hiyo ni haki kwa wenyetakua.

242. Namna hiyo MwenyeziMungu anawabainishia AyaZake ili mpate kufahamu.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

216

Page 227: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

NA WALE WANAOKUFA

Aya 240 - 242

MAANA

Ilikuwa ni ada ya Waarabu kabla ya Uislamu kwamba mtu akifa, mkewehapati urithi wowote isipokuwa posho yake ya mwaka mmoja tu; kwasharti akae eda katika nyumba ya mumewe. Akitoka kabla ya mwaka, basihana posho. Aya hii ni uthibitisho wa hayo, na yalikuwapo katika mwan-zo wa Uislamu.

Wafasiri na mafaqihi wote wameafikiana kwa kauli moja kwamba Aya hiini Mansukh hukumu yake (haitumiki tena) na imenasikhwa na Aya mbili:

1. "Na wale wanaokufa miongoni mwenu na kuacha wake, wangoje mieziminne na siku kumi..."(2:234)

2. "...Nao (wake zenu) watapata robo ya mlivyoacha, ikiwa hamnamtoto, lakini ikiwa mnaye mtoto basi wao (wanawake) watapata thu-muni..." (4:12)

Kwa maana kuwa atajilisha mwenyewe kutokana na fungu lake.

Pamoja na kwamba Aya hii haitumiki kabisa hukumu yake katika sharia,lakini tutaifasiri kama walivyofanya wafasiri.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

217

Page 228: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Na wale wanaokufa miongoni mwenu na wakaacha wake, wausie kwaajili ya wake zao kupata matumizi ya mwaka mmoja.

Ilikuwa kabla ya kutotumika Aya hii ni wajibu kwa wale ambao wanadhi-hirikiwa na alama za mauti kuusia kwa ajili ya wake zao wazuiliwemajumbani kwa kupewa posho.

Bila ya kutolewa.

Yaani posho itakuwa wajibu kama wakitaka kukaa katika nyumba ya bwanaaliyefariki. Ama wakitoka, basi si wajibu. Kwa hivyo ndio akaashiriaMwenyezi Mungu kwa kusema:

Wakiondoka basi si vibaya kwenu.

Yaani hamna jukumu kuwapa posho. Kwa maneno mengine posho niwajibu kwa kubaki nyumbani, wakitoka hakuna posho.

Kwa yale waliyojifanyia wenyewe, yanayofuata desturi.

Mwanamke akitoka nyumbani kwa mumewe aliyefariki, anaweza kuji-pamba na kuposwa katika mipaka ya sharia; yaani mwanamke aliyefiwa namumewe ana hiyari kubaki nyumbani kwa mume kwa muda wa mwakammoja na kupewa posho au kutoka asipewe posho.

Na wanawake waliopewa talaka wapewe cha kuwaliwaza kulinganana desturi; hiyo ni haki kwa wenye takua.

Kutoa ni lazima kuangalia hali ya mtoaji; kama ilivyokwishaelezwa kati-ka Aya ya 236. Tamko la wenye kupewa talaka linawakusanya wataliki-wa wote ambao wanagawanyika sehemu nne.

1. Mwenye kupewa talaka akiwa amekwishaingiliwa na amekwisha bainishi-wa mahari, huyu atapata mahari yote, kama ilivyobainishwa katika Aya ya229.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

218

Page 229: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

2. Mwenye kupewa talaka bila ya kuingiliwa na amekwisha bainishwamahari; yeye atapata nusu ya mahari; kama ilivyoelezwa katika Aya ya 237.

3. Mwenye kupewa talaka akiwa ameingiliwa, lakini hakubainishiwamahari; yeye atapata mahari kiasi cha makisio ya desturi yao. Hilowameafikiana Waislamu wote.

4. Mwenye kupewa talaka, bila ya kuingiliwa na bila ya kubainishiwamahari. Huyu hana mahari, isipokuwa atapewa cha kumliwaza tu; kamailivyoelezwa katika Aya ya 236.

Kwa ufupi ni kwamba cha kuliwaza hupewa yule mwenye kupewa talakabila ya kuingiliwa na bila ya kubainishiwa mahari wakati wa ndoa. Amawengine hakuna ulazima wa kuwapa bali ataachiwa mwenyewe aliyetoatalaka akitaka atampatia cha kuliwaza, asipotaka ni basi. imesemwa kuwani sunna kumpatia.

Namna hiyo Mwenyezi Mungu anawabainishia Aya zake ili mpatekufahamu.

Yaani mpate kujua. Kwa sababu ambaye haonyeki na kuacha kutumiahukumu za Mwenyezi Mungu, basi yuko katika daraja ya wasiokuwa naakili.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

219

Page 230: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

243. Je, hukuwaona wale

waliotoka majumbani mwao

nao walikuwa maelfu wakio-

gopa mauti? Mwenyezi

Mungu akawaambia:

Kufeni; kisha akawafufua.

Kwa hakika Mwenyezi

Mungu ni Mwenye fadhila

juu ya watu, lakini watu

wengi hawashukuru.

244. Na piganeni katika njia yaMwenyezi Mungu, na juenikwamba Mwenyezi Munguni Msikizi, Mjuzi.

KUOGOPA MAUTI

Aya 243 - 244

MAANA

Wafasiri wamerefusha maneno kuhusu Aya hii, wengi wao wameonyeshakuwa ni kisa cha kihistoria na kuchafua kurasa katika kukielezea kisa hiki.Baadhi yao wamesema hivi:

Watu katika Waisrail waliamrishwa kupigana jihadi dhidi ya adui zao.Wakaogopa kupigana ili wasife, wakayakimbia majumba yao kwa kuogopakufa. Mwenyezi Mungu akawaua ili kuwafahamisha kwamba hakuna kitu

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

220

Page 231: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

chochote kinachoweza kukinga mauti; kisha akawafufua ili wazingatie nawamalize umri wao uliobakia.

Ya kushangaza zaidi niliyoyasema katika tafsiri ya Aya hii ni kwambammoja wa wafasiri anasema: "Mauti ni namna mbili: Mauti ya mateso,nayo ni yale ya ambayo mtu huhuishwa baada ya kufa hapa hapa duniani.Na mauti ya ajali ambayo mtu atafufuliwa akhera."

Wengine wamesema walikimbia maradhi ya Tauni, lakini sio kwa kupiganajihadi.

Muhyiddin bin Arabi ameifasiri Aya hii kwa tafsiri yake ya Kisufi kwakusema: "Mwenyezi Mungu aliwaua kwa ujinga akawafufua kwa elimu naakili."

Sheikh Muhammad Abduh ameichukulia Aya hii ni tamthiliya ya mazinga-tio na maonyo na wala sio tukio la kweli, na kwamba lengo la ishara hii nikubainisha desturi ya Mwenyezi Mungu katika umma mbali mbali, na kwam-ba umma ambao unapigana jihadi na kulinda haki yake, utakuwa na maishamema; na umma ambao una woga na kusalimu amri kwenye dhulma, utaishimaisha ya udhalili.

Kwa hivyo kauli yake Mwenyezi Mungu kufeni ina maana ishini kwakutawaliwa na kukandamizwa kwa ajili ya woga wenu, kwa sababu mfanowa maisha kama hayo ni mauti sio uhai. Na kauli yake akawahuyisha; inamaana aliwahuyisha kwa maisha ya uhuru na utukufu kwa sababu ya jiha-di yao na kupigania haki yao.

Huu ni muhtasar mfupi sana wa rai ya Sheikh Muhammad Abduh ambayoameifafanua kwa urefu sana. Na rai hiyo, kama unavyoiona, ni yakimwamko lakini haitokani na dalili ya tamko la Aya. Rai yake yenyeweni sahihi bila ya shaka lakini iko mbali na dalili ya tamko. Huenda ikad-haniwa kwamba ni ya karibu kuliko zile kauli nyingine za wafasiri kwaupande huu. Kwa sababu kauli zao zinategemea riwaya za Kiisrail nangano tu. Na kauli ya Sheikh ina lengo la kuhamasisha, kupinga dhulma na

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

221

Page 232: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

kujitoa mhanga kwa ajili ya uhuru na heshima ya mtu, jambo ambalo linamwelekeo.

Vyovyote iwavyo Aya hii inawezekana kuwa na maana mbali mbali, ndiomaana kauli zikawa nyingi; wala hakuna kitu katika tamko la Aya kina-chofahamisha kuswihi kauli kwa dhati.

Hata hivyo, kauli ya Sheikh Abduh ndio yenye nguvu zaidi ya kauli zote kwakuangalia mwelekeo, kama tulivyokwisha eleza. Pia inasaidiwa na mpangiliowa maneno, pale alipofuatishia Mwenyezi Mungu moja kwa moja na Ayainayosema: "Na piganeni katika njia ya Mwenyezi Mungu na jueni kwam-ba Mwenyezi Mungu ni msikizi, mjuzi."

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

222

245. Ni nani atakayemkopeshaMwenyezi Mungu mkopomzuri, ili amzidishie ziadanyingi? Mwenyezi Mungundiye anayezuia na hukunjana hukunjua na kwakemtarejezwa.

NI NANI ATAKAYEMKOPESHA MWENYEZI MUNGU

Aya 245

MAANA

Baada ya Mwenyezi Mungu kuamrisha kupigania haki katika Aya iliy-otangulia, katika Aya hii anahimiza kutoa mali ya kuwaandaa wapiganaji.Kwa sababu vita, kama vile vinavyohitajia watu, pia vinahitajia mali.

Mwenye kusoma bajeti ya vita, ya madola makubwa hivi sasa, hana budikupotewa na tarakimu. Baadhi ya Dola za kimagharibi zimefikia zaidi yaelfu mia nne milioni. Lakini bajeti yote hii inahusika na kufanya uadui,

Page 233: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

kutaka ukubwa kutawala kimabavu, kuwakandamiza watu na kuwatawalakatika mambo yao yote. Ama jihadi aliyoihimiza Mwenyezi Mungu katikakitabu chake ni jihadi kwa ajili ya kupigania haki na kujikinga na maadui.

Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri.

Ilivyo hii ni amri ya kujitolea. Imekuja kwa njia ya swali ili kuilainishamioyo ya waumini, waweze kuona wepesi kujitolea kwa kutaka radhi yaMwenyezi Mungu.

Na kauli yake Mwenyezi Mungu mkopo mzuri ni kuonyesha kuwa maliitakayotolewa ni lazima iwe ya halali sio ya haram na kujitolea kwa radhi nakukusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu. Atimize sharti hizo, iliMwenyezi Mungu amzidishie ziada nyingi.

Imam Jaffar Sadiq (as) anasema: Iliposhuka Aya hii:

“Atakayefanya wema atapata jaza bora kuliko huo ...” (28:84).

Mtume alisema:“Ewe Mola wangu nizidishie”, Mwenyezi Munguakateremsha Aya hii:

“... Atakayefanya wema, atalipwa mfano wake mara kumi ...” (6:160)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mola wangunizidishie” basi Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii “IliMwenyeziMungu amzidishie ziada nyingi.” Na wingi mbele ya Mwenyezi Munguhauna idadi.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

223

Page 234: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Na Mwenyezi Mungu hukunja na kukunjua.

Yaani hudhikisha na kufanya wasaa, kwa maana kuwa Mwenyezi Mungu(s.w.t.) hakuwahimiza waja wake kutoa kwa kuwa ana haja; hapana, Yeyeni mkwasi, na wao ni wahitaji. Lengo hasa ni kuwaongoza kwenye amaliya heri.

Na Kwake mtarejezwa.

Ili mwema alipwe kwa wema wake na mwovu kwa wovu wake.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

224

246. Je, Hukuona wakubwa wawana wa Israil baada yaMusa walipomwambia Nabiiwao: Tuwekee mfalme ilitupigane katika njia yaMwenyezi Mungu. (Mtumewao) akasema: Je, haielekeikuwa hamtapiganamtakapoandikiwa kupi-gana? Wakasema:Itakuwaje tusipigane katikanjia ya Mwenyezi Mungu nahali tumetolewa nje yamajumba yetu na watotowetu? Walipoandikiwakupigana, wakageukaisipokuwa wachache mion-goni mwao. Na MwenyeziMungu anawajua madhal-imu.

Page 235: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

247. Na Nabii wao akawaambia:Hakika Mwenyezi Munguamewachagulia Talut kuwamfalme. Wakasema: Vipiatakuwa na ufalme juuyetu, na hali sisi tunastahikizaidi ufalme kuliko yeye,naye hakupewa wasaa wamali? Akasema: HakikaMwenyezi Mungu amem-teua juu yenu naamemzidishia ukunjufu waelimu na kiwiliwili. NaMwenyezi Mungu humpaufalme Wake amtakaye. NaMwenyezi Mungu niMwenye wasaa, Mjuzi.

248. Na Nabii wao akawaambia:Hakika alama ya ufalmewake ni kuwajia lile san-duku ambalo ndani mnakitulizo na mabaki ya yalewaliyoyaacha watu waMusa na wa Harun, wak-ilibeba Malaika. Hakikakatika hayo mna dalilikwenu ikiwa nyinyi niwenye kuamini.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

225

Page 236: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

249. Basi Talut alipoondoka najeshi, alisema: MwenyeziMungu atawafanyia mtihanikwa mto. Basi atakayekuny-wa humo si pamoja nami naasiyekunywa atakuwa pamo-ja nami; ila atakayetekafumba kwa mkono wake.Wakanywa humo isipokuwawachache miongoni mwao.Basi walipovuka, yeye nawale walioamini pamojanaye walisema: Leohatumwezi Jalut, na Jeshilake. Na wenye yakini yakukutana na Mola waowalisema: Makundi man-gapi madogo yameshindamakundi makubwa kwaidhini ya Mwenyezi Mungu.Na Mwenyezi Mungu yupamoja na wafanyao subira.

250. Na walipotoka kupambanana Jalut na jeshi lake walise-ma: Mola wetu, tumiminiesubira na uisimamisheimara miguu yetu na utasai-die tuwashinde watumakafiri.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

226

Page 237: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

251. Basi wakawashinda kwaidhini ya Mwenyezi Mungu;na Daud akamuua Jalut, naMwenyezi Mungu akampaufalme na hekima na akam-fundisha aliyoyataka. Nakama Mwenyezi Munguasingeliwazuia watu, baadhiyao kwa wengine, ingeli-haribika ardhi; lakiniMwenyezi Mungu niMwenye fadhila juu yaviumbe vyote.

252. Hizo ni Aya za MwenyeziMungu, tunakusomea kwahaki; na hakika wewe nimiongoni mwa Mitume.`

KISA CHA TALUT

Aya 246 - 252:

Tumekwishaeleza katika tafsiri ya Aya ya 2 kwamba Qur'an ni kitabu chamwongozo na dini, na ni kitabu cha kueleza tabia njema na sharia; sio kitabucha visa na Historia au Filosofia na Sayansi, Mwenyezi Mungu (s.w.t.)akielezea tukio la Kihistoria hulieleza kwa ajili ya mawaidha na kuwatakawatu wazingatie; na wala haileti kisa chote kwa upambanuzi katika pandezake zote. Hilo limeelezewa katika Aya kadhaa; kama vile:

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

227

Page 238: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

"Kwa hakika katika visa vyao, kuna fundisho kwa wenye akili ..." (12:111)

"Zimepita desturi kabla yenu, basi tembeeni katika nchi na muoneulikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha." (3: 137)

Sheikh Muhammad Abduh anasema; "Kujaribu kuifanya Qur'an kuwa nikitabu cha Historia ni kuhalifu desturi ya Qur'an na ni kuziepusha nyoyo namawaidha yake, na pia ni kulipoteza lengo lake na hekima yake. Lililowajibu kwetu ni kufahamu yaliyomo ndani yake na kuzitumia fikra zetu kati-ka kutoa mafundisho, tujivue na yale yanayoitusi na kuikebehi Qur'an, natujipambe na yale yanayoisifu Qur'an na kuiweka vizuri.

Mwenyezi Mungu amekidokeza kisa cha Talut katika Aya hizi (246-252),Nasi tutakitaja kama vile yanavyofahamisha matamko ya Aya hizi; kishatutaidokeza sehemu za mafundisho na mawaidha.

Baada ya kufa Musa (a.s.) walikuwako makhalifa wake katika Manabiiwaliokuwa wakiendeleza amri za Mwenyezi Mungu katika Waisrail.Miongoni mwa makhalifa ni Mtume aliyeelezwa katika Qur'an bila ya kuta-jwa jina lake, isipokuwa alikuwa wakati wa Nabii Daud (a.s.), kama zinavy-ofahamisha Aya. Wafasiri wengi wanasema alikuwa akiitwa Samuel.

Siku moja kikundi cha Waisrail kilimwendea na kumwambia" "Tuwekeemkuu wa jeshi ambaye tutafuata rai yake katika kupanga vita, na tupiganepamoja naye katika njia ya Mwenyezi Mungu,"

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

228

Page 239: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Mtume wao akawaambia - na alikuwa amekwisha watahini - "Mimi naonamtamwacha kama vita vikianza na mkiitwa kwenye jihad,"

Wakasema: "Tutamwachaje ikiwa adui ametutoa katika majumba yetu; nakutuweka mbali na watoto wetu?"

Basi Nabii wao akamtaka shauri Mwenyezi Mungu kwa yule atakayefaakuongoza vita, Mwenyezi Mungu akampelekea wahyi kwa kusema kuwa"Mimi nimewachagulia wao Talut kuwa mfalme," Inasemekana - aliitwaTalut kwa sababu ya urefu wake; kutokana na neno la Kiarabu Tul (urefu),.

Mtume alipowapa habari hiyo kwamba Mwenyezi Mungu amemchaguaTalut walisema: "Atakuwaje mfalme wetu na wala hatokani na ukoowowote mtukufu tena ni maskini?" Mtume akasema: "Kiongozi hahitajiukoo isipokuwa awe na ushujaa na maarifa ya kuendesha mambo. NaMwenyezi Mungu (s.w.t.) amempa Talut uwezo wa kielimu na ki-umbo nanyenzo nyingine za kiongozi,"

Wakasema: "Basi tunataka alama itakayofahamisha uwezo wake."

Akasema:"Alama ni kurudishiwa kasha; litaletwa na Malaika kwa amriya Mwenyezi Mungu," Inasemekana kasha hilo lilikuwa na mabaki ya mbaoza Musa, fimbo yake, nguo zake na baadhi ya sehemu ya Taurat. Na walikuwawamenyang'anywa na Wapalestina katika vita fulani. Pia imesemwa kwam-ba Mwenyezi Mungu aliliinua kulipeleka mbinguni baada ya kufa Musa.Lilipowajia kasha kutoka kwa Mwenyezi Mungu waliamini uongozi waTalut.

Talut akawaongoza kwenda kupigana na adui yao; akawafahamisha kuwawatapitia kwenye mto ambako watatahiniwa kuangaliwa ikhlasi yao.Ambaye atakuwa na subira hatakunywa isipokuwa kiasi cha kitanga chakecha mkono. Atakayefuata ndiye msafi mwenye kutegemewa. Ama ambayeatakunywa mpaka amalize kiu, sio wa kutegemewa katika vita na jihadi.Walipopitia kwenye mto waliasi kama kawaida yao, wakanywa isipokuwakikundi kidogo tu, kilithibiti kwenye ukweli na uaminifu.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

229

Page 240: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Yalipokutana makundi mawili, Waisiralil wakiongozwa na Talut (Sauli) naWapalestina wakiongozwa na Jalut (Goliat), Waisrail wengi waliogopa nakumwambia Talut; "Hatumuwezi Jalut na jeshi lake," Waumini wachacheambao hawakunywa maji wakasema : Makundi mangapi madogo yameshin-da makundi makubwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu," Wakam-wombaMwenyezi Mungu awape subira uthabiti na ushindi. Mwenyezi Munguakawatakabalia dua yao baada ya kujua nia yao, azma yao na ukweli katikania. Daud akamuua Jalut na maadui wakahsindwa vibaya sana. Daud akawamaarufu mwenye kusikika sana baada ya kumuua Jalut. Baada ya hapoMwenyezi Mungu akampa Utume, akamtremshia Zabur na akamfundishakutengeneza deraya na elimu ya dini na upambanuzi wa maneno; kamaalivyosema Mwenyezi Mungu: Mwenyezi Mungu akampa ufalme na heki-ma."

Huu ndio muhtasari wa zinavyofahamisha Aya tukufu. Ama Daud kum-woa binti ya Talut na kujaribu kufanya vitimbi vya kumuua kwa kumuozabinti yake, teo ya Daud na mawe yake, na kisa cha Daud na wanyamawakali mwituni, na mfano wa hayo yaliyomo katika vitabu vya Tafsir,vyote hivi ni visa ambavyo havina tegemeo lolote la mapokezi isipokuwamapokezi ya Kiisrail.

Ama somo la kisa hiki ni anayefaa kuongoza ni yule mwenye uwezo wakielimu na kiumbo na wala sio yule mwenye nasaba na fahari au mwenyejaha na mali; na kwamba ushindi utakuwa pamoja na subira na imani nawala sio kwa wingi wa watu; na njia ya kumjua mwema na mwovu ni kwamajaribio na mitihani.

Baada ya kuelezea muhtasari wa kisa na somo lake, sasa tunaingiliakufasiri jumla za maneno.

MAANA

Je, hukuona wakubwa wa wana wa Israil baada ya Musa.

Kwa dhahiri msemo unaelekezwa kwa Mtume, na katika maana unaelekezwakwa wasikilizaji wote; na tamko linaelekezwa kwa mwenye kukijua kisa naasiyekijua pia. Unaweza kumwambia mtu; "Je hujui fulani amefanya nini,"

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

230

Page 241: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

wakati huo unataka kumfahamisha aliyoyafanya.

Walipomwambia Nabii wao; Tuwekee mfalme ili tupigane katika njiaya Mwenyezi Mungu.

Inasemekana Nabii waliyemwambia hayo ni Samuel.

(Mtume wao) akasema; Je, haielekei kuwa hamtapigana mtakapoandikiwa kupigana!

Yaani; je mambo yako kama ninavyoona kuwa miongoni mwenu kunawatakaojitoa na kuacha kupigana kama mkifaradhiwa vita?

Wakasema: Itakuwaje tusipigane katika njia ya Mwenyezi Mungu nahali tumetolewa nje ya majumba yetu na watoto wetu?

Walikanusha kuwa na chochote kitakacho wafanya waache jihadi; na wak-abainisha sababu itakayowafanya wapigane ambayo ni kutolewa majum-bani mwao na kutenganishwa na watoto wao.

Walipoandikiwa kupigana waligeuka, isipokuwa wachache miongonimwao.

Watu wengi wana sifa hii; wanathibitisha na wanaazimia kufanya mambo,lakini wakati ukifika wanajificha mvunguni. Ufasaha zaidi wa yaliyosemwakuhusu mambo hayo ni kauli ya Bwana wa mashahidi Hussein bin Ali (a.s.);"Watu ni watumwa wa dunia na dini wameilamba kwa ndimi zao tu,inachukulika yanapokuwa mazuri maisha yao. Wapatwapo na misukosuko,wenye dini wanakuwa wachache.

Na Mtume wao akawaambia; Hakika Mwenyezi Mungu amewachag-ulia Talut kuwa mfalme. Wakasema: Vipi atakuwa na ufalme juuyetu, na hali sisi tunastahiki zaidi ufalme kuliko yeye, naye hakupewawasaa wa mali?

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

231

Page 242: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Mantiki hii haiwahusu Waisrail tu, bali watu wengi walikuwa na wanaen-delea kuwa na mawazo kwamba cheo ni cha mwenye mali na jaha.Mwenyezi Mungu anasema:

"Na wanapokuona hawakufanyi ila ni mzaha tu (wanasema); 'Ati huyundiye Mwenyezi Mungu aliyemtuma kuwa Mtume?' "(25:41)

Akasema: Hakika Mwenyezi Mungu amemteua juu yenu naamemzidishia ukunjufu wa elimu na kiwiliwili.

Yaani uongozi haui kwa sababu ya mali na nasaba, bali ni kwa elimu naikhlasi. Makusudio ya ukunjufu wa kiwiliwili ni kutokuwa na maradhi, kwasababu maradhi yanamzuwia kiongozi kutekeleza wajibu wake.

Inasemekana kuwa Talut alikuwa mrefu zaidi kuliko mtu wa kawaida kwakiasi cha dhiraa moja ya mkono.

MATAKWA YA MWENYEZI MUNGU NA KIONGOZI MWOVU

Na Mwenyezi Mungu humpa ufalme wake amtakaye.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni Mfalme wa wafalme, humpa ufalmeamtakaye na humvua amtakaye; humtukuza amtakaye na humdhalilishaamtakaye; heri imo mikononi mwake na Yeye ni muweza juu ya kila kitu.Hapana shaka katika hilo; lakini, Yeye ambaye hekima yake imetuku-ka, ni Mwadilifu, hamdhulumu yeyote na hafanyi mambo kiholela. Vipiisiwe hivyo na hali Yeye amesema:

"Na kila kitu kwake ni kwa kipimo."(13:8)

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

232

Page 243: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Yaani kwa nidhamu na sababu, sio kwa sadfa au kiholela; hata mali yaharamu na utawala wa dhulma una sababu zake za kijamii.

Unaweza kuuliza: Je utawala mwovu na utajiri wa unyanga'nyi unatege-mea matakwa ya Mwenyezi Mungu?

Jibu: Hapana, Mwenyezi Mungu ameharamisha dhulma na unyanga'nyi.Na Yeye hajiingizi katika mambo ya kijamii kwa njia ya Kun fayakun (kuwaikawa). Mwenyezi Mungu hamzuwii kwa nguvu dhalimu kutokana na dhul-ma yake isipokuwa anamkataza kwa kisheria na kimwongozo na anamuhad-harisha na kumtolea viaga. Atakapohalifu atamwadhibu siku ya malipo iliyokubwa. Kama angelitaka kumzuwia angelifanya, lakini anaacha mamboyapite kwa sababu zake na desturi zake.

Huenda ikawa huu ndio mwelekeo wa kumnasibishia Mwenyezi Munguufalme kwa jumla. Kwa hivyo yanakuwa maana. "humpa ufalme wakeamtakaye" ni kwamba Mwenyezi Mungu lau angelitaka kuuzuwia kwanguvu ufalme kwa asiyeustahiki, angelizuwia na wala asingelifikia kwenyeufalme mtu dhalimu pamoja na kuwepo sababu zake za kikawaida.

Vyovyote iwavyo utajiri wa mtu na ufalme wake unakuja kutokana na natijayakijamii anayoishi. Ama kuunasibisha na matakwa ya Mwenyezi Mungumoja kwa moja bila ya sababu yoyote ni makosa kabisa.

Na Mtume wao akawaambia: Hakika alama ya ufalme wake ni kuwa-jia lile sanduku.

Sanduku hilo lilikuwa la Musa alilokuwa akiwekea Taurat. MwenyeziMungu alikuwa amelipaza mbinguni baada ya kufa Musa kwakuwakasirikia Mayahudi kama ilivyosemwa.

Ambalo mna ndani kitulizo.

Yaani kitulizo cha nyoyo zenu ambapo sanduku lilikuwa na jambo tuku-fu la kidini kwa Wana wa Israil.

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

233

Page 244: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Na mabaki ya yale waliyoyaacha watu wa Musa na wa Harun.

Mwenyezi Mungu hakubainisha ni mabaki gani hayo. Watu wa Musa na waHarun ni Mitume ambao walilirithi sanduku hilo.

Wakilibeba Malaika.Yaani kwa miujiza. Basi Talut alipoondoka na jeshi,alisema: Mwenyezi Mungu atawafanyia mtihani kwa mto, basiatakayekunywa humo si pamoja nami, na asiyekunywa atakuwa pamo-ja nami; ila atakayeteka fumba kwa mkono wake.

Imepokewa kwamba Talut aliwaambia Waisrail: "Asitoke na mimi kwenyejihadi mzee, mgonjwa, aliyejenga jengo ambalo hajalimaliza, mwenyekushughulishwa na biashara, au mume aliyeoa mke ambayehajamwingilia." wakakusanyika jamaa wenye sifa zinazotakiwa, naulikuwa ni wakati wa kiangazi na joto kali, wakafuata njia isiyokuwa namaji. Walipolalamikia kiu, Talut aliwaambia: "Mwenyezi Mungu atawapamtihani katika utii na uasi kwa mto mtakaoupitia. Atakaye kunywa katikamto huo si katika wafuasi wangu waumini, isipokuwa akinywa kidogokiasi cha kiganja.

Wakanywa humo isipokuwa wachache miongoni mwao.

Inasemekana idadi ya waumini ilikuwa ni 313 kama idadi ya watu wa vitavya Badr. Hakika wema walikuwa na wanaendelea kuwa ni nadra sanakupatikana.

Basi alipovuka yeye na wale walioamini pamoja naye walisema: Leohatumwezi Jalut na jeshi lake.

Aliendelea mbele Talut pamoja na wale waliomtii baada ya kuvuka mtompaka wakakutana na Jalut na jeshi lake. Walipoona wingi wa adui yao,waligawanyika makundi mawili; kundi lilisema hatumwezi Jalut na kundilikasema:

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

234

Page 245: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makubwa kwa idhiniya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wafanyaosubira.

Ambao wamejizatiti kwa kupigana jihadi na kujitoa mhanga kwa ajili yamaisha mema yaliyo bora ambayo ni kuishi huru katika nchi iliyo huru nakujitosheleza kwa chakula na wataalamu katika nchi iliyoendelea. Ama kuvu-milia udhalili na umasik-ini ni uchafu katika kazi ya shetani.

Na walipotoka kupambana na Jalut na jeshi lake walisema: Molawetu, tumiminie subira na uithubutishe miguu yetu, na utusaidie juu yawatu makafiri.

Waumini walipojiona ni wachache na maadui zao ni wengi walikimbiliakwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kuomba na kunyenyekea kwa ikhlas;na Mola wao akawatakabalia dua.

Na Daud akamuua Jalut. Na Mwenyezi Mungu akawapa ushindi waumi-ni dhidi ya makafiri. Ikathibitika, kwa fadhila Zake na rehema Zake, dhanaya waliosema: "Makundi mangapi madogo yameshinda makundi makub-wa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu."

Na Mwenyezi Mungu akampa ufalme na hekima na akamfundishaaliyoyataka. Yaani Mwenyezi Mungu alimtawalisha Daud mahali pa Talutbaada ya kufa kwake. Hekima ni ishara ya Zabur. Mwenyezi Mungu anase-ma:

"...Na tukampa Daud Zabur." (4:163)

Na akamfundisha kutengeneza deraya (mavazi ya vita), Mwenyezi Munguanasema:

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

235

Page 246: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

"Na tukamfundisha (Daud) kutengeneza mavazi kwa ajili yenu ili yawahi-fadhi katika mapigano yenu ..." (21:80)

Na kama Mwenyezi Mungu asingeliwazuia watu baadhi yao kwawengine ingaliharibika ardhi. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenyefadhila juu ya viumbe vyote.

Yaani jamii yoyote ambayo ndani yake hamna utawala (serikali) basiitakuwa na vurugu. Na kwamba akili na sharia bila ya nguvu ya utekeleza-ji haiwezi kuleta amani na nidhamu. Imam Ali (a.s.) anasema "Mfalme nimsaidizi wa Mwenyezi Mungu katika ardhi yake... "Lakini mara ngapiwafalme wameiharibu ardhi na watu wake. Pamoja na hivyo, lakini hawa-tengenei watu wasiokuwa na mwendeshaji.

Hizo ni Aya ya Mwenyezi Mungu, tunakusomea kwa haki; na hakikawewe ni miongoni mwa Mitume.

Mwenyezi Mungu alimsomea Mtume wake Aya zake na Mtume akatu-somea ili tuzingatie hakika yake na tuzifanye ndizo desturi za vitendovyetu vyote ili tuwe na maisha mema yenye utulivu.

"Sema mimi nawaonya kwa wahyi na viziwi hawasikii mwito wanapoony-wa." (21:45)

MWISHO WA JUZUU YA PILI

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

236

Page 247: Qurani Tukufu - Al Kashif Juzuu No - 2

Tafsir Al-Kashif: Juzuu ya Pili 2. Sura Al-Baqarah

237