-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
1
BUNGE LA TANZANIA
________
BUNGE LA KUMI NA MBILI
_________
MAJADILIANO YA BUNGE
MKUTANO WA KWANZA
Kikao cha Nne – Tarehe 13 Novemba, 2020
(Bunge Lilianza Saa 3:00 Asubuhi)
(Saa 3.06 Asubuhi Viongozi wa Kitaifa Walianza
KuingiaUkumbini)
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (Mhe. Zubier AliMaulid)
na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) (Mhe.
Martin Ngoga) Waliingia Ukumbini
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe.Prof. Ibrahim
Hamis Juma) na Jaji Mkuu wa Serikali yaMapinduzi Zanzibar (Mhe.
Omar Othman Makungu)
Waliingia Ukumbini
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti waBaraza la
Mapinduzi (Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi) na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (Mhe. HemedSuleiman Abdullah)
Waliingia Ukumbini
(Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)
Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mhe.
Kassim Majaliwa Majaliwa) Aliingia Ukumbini
(Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Mhe. Samia
Suluhu Hassan) akiongozana na Naibu Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe. Dkt.Tulia
Ackson) Waliingia Ukumbini
(Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)
(Saa 3:51 Asubuhi Bunge Lilisitishwa kwa muda)
(Saa 4.15 Asubuhi Bunge lilirudia)
(Hapa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mhe.Dkt. John P.
J. Magufuli) akiongozana na Spika wa Bunge laJamhuri ya Muungano wa
Tanzania (Mhe. Job Y. Ndugai)
Waliingia Ukumbini
(Hapa Wabunge Walipiga Makofi na Vigelegele)
D U A
Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua
SPIKA: Ahsanteni Waheshimiwa Wabunge, mnawezakukaa.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania - Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, MheshimiwaMakamu wa Rais - Mama Samia
Suluhu, Mheshimiwa Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi - Dkt. HusseinAli Mwinyi ambaye amekuwa Mbunge mwenzetu
kwa miaka20 mfululizo humu ndani, Mheshimiwa Makamu wa Pili waRais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa NaibuSpika,
Mheshimiwa Jaji Mkuu, Mheshimiwa Jaji Mkuu Zanzibar,Mheshimiwa
Spika Zubeir Ali Maulid kutoka Baraza laWawakilishi na Mheshimiwa
Spika Martin Ngoga kutokaBunge la Afrika ya Mashariki
ninawakaribisha sana kwa niabaya Waheshimiwa Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Rais, tuna wageni wengi sana kamautakavyoona
galleries zetu hizo zimejaa, nitawatambulisha
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
3
mwishoni baada ya hotuba yako, lakini pia kumbi nyingineza Bunge
pia nazo zimejaa wageni nje ya ukumbi huu ambaonao wanafuatilia
kila kinachoendelea hapa live.
Nichukue nafasi hii kabla sijatoa taarifa yangu rasmi,niseme
kwamba Mheshimiwa Rais jumla ya WaheshimiwaWabunge Kikatiba wa
Bunge hili kuwa wanakuwa ni 393 jumlawote, waliopo hivi sasa ni
359. Bado tunasubiri Wabungewatano kutoka Baraza la Wawakilishi na
Mheshimiwa Spikaupo hapa, bado tunasubiri Wabunge watano hapa.
Halafutunasubiri Mheshimiwa Rais wateule wa kwako kumi;wanawake
watano, wanaume watano, pia tunasubiri walewa Viti Maalum kutoka
vyama vingine kwa kadriwatakavyokuja. (Makofi)
Kwa hiyo, jumla yetu tutakuwa 393 pale tunapokuwatupo kamili
kabisa full house, kwa sasa ni 359. Katika hao 359tuna Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Wabunge wa CUFwatatu, tunapaswa kuwa na Wabunge
wa ACT Wazalendowanne, tuna Mbunge wa CHADEMA mpaka sasa hivi
nimmoja na tuna Wabunge wa Chama cha Mapinduzi 256.
Mheshimiwa Rais kati ya hao, Wabunge wa VitiMaalum ni 94, lakini
wanawake kwa ujumla wanakuwa 94kujumlisha 24. Ningeomba Wabunge
wanawake wote palemlipo hebu msimame angalau Mheshimiwa Rais apate
pichaya uwakilishi wa akina mama Bungeni, kila Mbungemwanamke
asimame, wengine bado wamekaa naombaWabunge Wanawake wote msimame.
(Makofi/Vigelegele)
Kwa hiyo, Watanzania wanaweza wakaona uwakilishiwa akina mama
ulivyo kwa kweli ni mkubwa kabisa,hongereni sana wote, ni moja ya
nchi chache zenye uwakilishimkubwa kiasi hiki wa wakina mama katika
Ukanda wetu waAfrika. (Makofi)
Mheshimiwa Rais, pia ningependa niseme kwambakatika Wabunge hawa
tulionao hadi hivi sasa, Wabungewapya kati ya 259 ni 206. Naomba
Wabunge wapyamsimame pale mlipo, wapya wote. Waandishi wa
Habari
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
4
picha hii ni muhimu sana ya Wabunge wapya, inatoa pichaya
demokrasia ya nchi yetu jinsi ambavyo mabadiliko kwawakati mmoja wa
miaka mitano huwa ni makubwa sana.Safari hii mpaka sasa hivi
Mheshimiwa Rais ni asilimia 61.1mpaka sasa ya Wabunge wapya.
Ahsanteni sana mnawezakukaa. (Makofi/Kicheko)
Waheshimiwa Wabunge, hiyo inatoa picha kwambakukaa hapa ni
shughuli, kuendelea kuwepo hapa siyomasihara. Inabidi mumsikilize
Mheshimiwa Rais na mzingatieatakayoyaeleza hapa unaweza ukarudi,
ahsante sana.(Kicheko)
Mheshimiwa Rais na Waheshimiwa Wabunge, kwamujibu wa Ibara ya
91(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania na Kanuni za
Bunge Kanuni ya 32 ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la Juni, 2020
ningependa kuwajulishakwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli yupo pamojanasi
leo hii ili kulihutubia na kulifungua rasmi Bunge jipya laKumi na
Mbili ambalo limekaa katika Mkutano wake waKwanza ulioanza tarehe
10 Novemba na tumefanya kazi yakuwaapisha Wabunge wote 359 hadi
hivi sasa, tumefanyakazi ya uchaguzi wa kumpata Spika, tumefanya
kazi yakumpata Naibu Spika na tumefanya kazi ya kupiga
kurakuthibitisha pendekezo la uteuzi wa Waziri Mkuu
MheshimiwaKassim Majaliwa Majaliwa. Hizo ndizo kazi zilizopangwa
kwaajili ya Bunge hili la mwanzo na zote
tumeshazikamilisha,imebakia sasa hotuba yako Mheshimiwa Rais
ambayoukiimaliza tutakuwa tunaahairisha Bunge hili hadi wakatiambao
nitautaja pale mwishoni. (Makofi)
Mheshimiwa Rais, kwa heshima na taadhima sasaningeliomba
nikukaribishe uhutubie Bunge hili na kupitiakuhutubia Bunge hili
basi uhutubie Taifa na Taifa zima kwakweli limejipanga kukusikiliza
huko walipo Watanzania nadunia nzima kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Rais, nakukaribisha sana. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
5
MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI - RAIS WAJAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA: Mheshimiwa Spika,mara ya mwisho nilipoingia
kwenye ukumbi huu kulifungaBunge la Kumi na Moja tulibahatika kuwa
na Marais wetuwastaafu watatu, lakini kama mnavyokumbuka mmoja
waMarais wetu Wastaafu wa Awamu ya Tatu ametanguliambele ya haki
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa. Pianakumbuka wapo pia baadhi ya
Wabunge katika Bungelililotangulia na watumishi wengine wa Bunge
waliotanguliambele ya haki, basi kwa heshima yao kabla ya kuanza
hotubayangu, ninawasihi sote tusimame tumkumbuke MheshimiwaMkapa
pamoja na Wabunge wote waliofariki dunia tangukufungwa kwa Bunge la
Kumi na Moja.
(Hapa Wabunge na Wageni Waalikwa Walisimamakuwaombea watu wote
walifariki dunia)
MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI - RAIS WAJAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA: Mwenyezi Munguaiweke roho ya Marehemu Mzee
Mkapa pamoja namarehemu wetu wote mahali pema peponi, amina.
Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, napendaniseme kwamba
Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania Ibara ya 91(1) imempa
dhamana Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania kulifungua rasmi
Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania, ni kwa sababu hiyo
nimekujahapa leo kulihutubia Bunge hili kwa lengo la kutimiza
mashartihayo ya Katiba.
Napenda nianze kwa kumshukuru sana MwenyeziMungu aliyetujaalia
neema ya uhai na kutuwezesha kuionasiku ya leo. Aidha, nakupongeza
wewe Mheshimiwa SpikaJob Ndugai, Mbunge wa Jimbo la Kongwa kwa
kuchaguliwakwa mara nyingine kuliongoza Bunge hili ukiwa
Spika,hongera sana. (Makofi)
Nampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kwakuchaguliwa tena
kwa mara nyingine kuwa Naibu Spika tenamara hii akiwa Mbunge wa
kuchaguliwa kutoka Jimbo la
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
6
Mbeya Mjini, hongera sana Mheshimiwa Dkt. Tulia, huu
niuthibitisho kwamba nchi yetu kupitia Serikali inayoongozwana
Chama cha Mapinduzi inawaamini sana wanawake.Kama mnavyofahamu
Makamu wetu wa Rais MheshimiwaSamia Suluhu Hassan naye ni
mwanamama. (Makofi/Vigelegele)
Aidha, Bunge hili la Kumi na Mbili nalo lina Wabungewengi
wanawake kama ulivyotaja. Kwa msingi huo, napendanitumie fursa hii
kuwaahidi kuwa Serikali ninayoiongozaitaendelea kuwaamini wanawake
katika kushika nafasimbalimbali za uongozi. Wanawake na akina mama
oyee.(Makofi)
WABUNGE WANAWAKE: Oyee.
MHE. DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI - RAIS WAJAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA: Mheshimiwa Spika,napenda pia kuwapongeza
Waheshimiwa Wabunge wotekwa kuchaguliwa kwenu kuwa Wabunge wa Bunge
hili laKumi na Mbili. Mmechaguliwa kwa vile wananchi wana imanikuwa
mna uwezo wa kuwawakilisha vizuri. Nafahamumichakato ilivyokuwa,
Wajumbe na kadhalika. Hivyo,nawasihi sana Waheshimiwa Wabunge
msiwaangushewananchi waliowachagua, Watanzania wana imani kubwasana
na Bunge hili la Kumi na Mbili. (Makofi/Kicheko)
Nitumie fursa hii pia kuwashukuru WaheshimiwaWabunge kwa
kuridhia na kumpitisha Mheshimiwa KassimMajaliwa kuwa Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, ahsanteni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimekuja kulizindua Bunge hilibaada ya nchi
yetu kufanikiwa kumaliza Uchaguzi Mkuuuliofanyika tarehe 28 Oktoba,
2020 kwa uwazi, amani nautulivu mkubwa. Kwa msingi huo, napenda
nirudiekuipongeza Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi kwa
kusimamiavizuri zoezi la Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu
kuanziauandikishaji wapiga kura, uchukuaji na urejeshaji fomu
zawagombea, usimamizi wa kampeni na pia zoezi la kupiga
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
7
kura na utoaji wa matokeo mapema. Kwa hakika,tumethibitisha
uwezo mkubwa katika kusimamia uchaguzibila kutegemea misaada kutoka
nje. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Tumeya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage,Makamu Mwenyekiti wa Tume
Jaji Mstaafu HamidMahamoud, Makamishna wa Tume, Mkurugenzi wa
UchaguziDkt. Wilson Mahera pamoja na watendaji wote wa
Tume,hongereni sana kwa kazi nzuri mliyofanya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekeenawapongeza kwa jinsi
tulivyotumia vizuri fedhamlizotengewa, kama inavyofahamika uchaguzi
wa mwakahuu uligharamiwa na Serikali kwa asilimia 100 ambapo
kiasicha shilingi bilioni 331 kilitengwa. Hata hivyo mpaka
uchaguziumekamilika, Tume imetumia shilingi bilioni 262 tu. Hii ni
isharanzuri ya uadilifu mkubwa walionao viongozi na watendaji
waTume ya Taifa ya Uchaguzi, hongereni sana. Natoa rai kwataasisi
nyingine kuiga mfano mzuri wa Tume hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa moyo wa dhati kabisanarudia kuwashukuru
viongozi wetu wa dini kwa kutuongozavyema kwa sala na dua katika
kipindi chote cha uchaguzina hatimaye tumeweza kumaliza uchaguzi
wetu salama.Nawasihi waendelee kuliombea Taifa letu ili libaki
katikamikono ya Mwenyezi Mungu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, narudia pia kuvishukuru vyombovyetu vya ulinzi
na usalama kwa kusimamia vizuri amani nautulivu wa nchi yetu na
mipaka yetu wakati wote wauchaguzi. Hii ni ishara kuwa vyombo vyetu
vya ulinzi nausalama ni imara na vinafanya kazi kwa weledi
mkubwa,hongereni sana vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisanatoa shukrani nyingi
kwa Watanzania wenzangu wote kwakushiriki vizuri na kuonesha
utulivu mkubwa kwenye uchaguziuliopita kuanzia kwenye zoezi la
uandikishaji wapiga kura,wakati wa kampeni, upigaji kura na kupokea
matokeo.
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
8
Hakuna shaka, uchaguzi wa mwaka huu kwa mara
nyingineumethibitisha ulimwengu kuwa sisi watanzania ni
wapendaamani, tunajitambua, hatudanganyiki na
tumekomaakidemokrasia, ahsanteni sana Watanzania
wenzangu.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, masuala yote muhimutuliyoyapanga kuyatekeleza
kwenye miaka mitano ijayotumeyaweka kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM
ya mwaka2020 hadi 2025 ambayo ina kurasa 303, kwa bahati
nzuriWaheshimiwa Wabunge wengi wa Bunge hili wanaifahamuvizuri
Ilani hiyo kwa vile wameitumia katika kuomba kura kwawananchi
kwenye Uchaguzi Mkuu uliomalizika. Lakinisambamba na masuala hayo
yaliyopo kwenye Ilani yetu yaUchaguzi wa mwaka 2020/2025
tunaendelea pia kutekelezana kusimamia mambo yote niliyoyaeleza
wakati nikizunduaBunge la Kumi na Moja tarehe 20 Novemba, 2015.
Mheshimiwa Spika, kama mtakavyokumbuka kwenyehotuba hiyo ya
kuzindua Bunge la Kumi na Moja nilielezamambo mengi sana ambayo
kimsingi yaliyotoa falsafa bilana vipaumbele vya Serikali ya Awamu
ya Tano baadhitumeyatekeleza vizuri yapo ambayo hatujayatekeleza
kwaukamilifu na mengine yapo kwenye hatua mbalimbali zautekelezaji.
Kwa hiyo, kwenye miaka mitano ijayotutaendelea kusimamia na
kutekeleza mambo yoteniliyoyaeleza kwenye hotuba ya kuzindua Bunge
la Kumi naMoja, hii ndiyo sababu nimeamua kuigawa tena hotubayangu
ya uzinduzi wa Bunge la Kumi na Moja kwenuWaheshimiwa Wabunge il i
mkaisome na hatimayeikawaongoze katika kutekeleza majukumu yenu
vizuri.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo yote naombaMheshimiwa Spika
uniruhusu nitaje baadhi ya mambomuhimu tunayoyapa kipaumbele
kikubwa katika kipindi chamiaka mitano ijayo.
Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza na muhimututakalolipa
kipaumbele kikubwa kwenye miaka mitano ijayo
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
9
ni kuendelea kulinda na kudumisha tunu za Taifa letu yaaniamani,
umoja na mshikamano, uhuru wa nchi yetu,Muungano na Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar. Katika hilonaahidi kushirikiana kwa karibu
sana na Rais mpya waZanzibar Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi.
Kamwehatutakuwa na mzaha na yeyote mwenye kutakakuhatarisha amani
ya nchi yetu, mwenye nia ya kuvurugaumoja na mshikamano wetu na pia
mwenye kutaka kutishiauhuru wetu, Muungano pamoja na Mapinduzi
Matukufu yaZanzibar. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napenda pia kutumia fursa hiikumuahidi
Mheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi kwambakwenye miaka mitano ijayo
Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania itatoa ushirikiano
mkubwa wa kufanya kazi kwakaribu na Serikali ya Zanzibar.
(Makofi)
Kwa kifupi naweza kusema tutafanya kazi kwapamoja kwa lengo la
kuleta maendeleo kwa pande zetuzote mbili za Muungano. Katika hilo
nampongeza sanaMheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi kwa hotuba
nzurialiyoitoa wakati wa kuzindua Baraza la Wawakilishi,
kwenyehotuba yake alitoa dira, mwelekeo na kutaja vipaumbelevya
Serikali ya Awamu ya Nane ya Zanzibar, hongera sanakwa Mheshimiwa
Rais Dkt. Mwinyi kwa hotuba nzuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kupitia Bunge hili napendanimuahidi Mheshimiwa
Rais Dkt. Hussein Mwinyi kuwa nitampaushirikiano wa kutosha katika
kutekeleza yote aliyoyaahidiwakati wa uzinduzi rasmi la Baraza la
Wawakilishi. (Makofi/Vigelegele)
Mheshimiwa Spika, sambamba na kulinda nakudumisha tunu za nchi
yetu, kwenye miaka mitano ijayotutaendelea kuimarisha utawala bora
hususani kwakusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma pamoja
nakuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, wizi, ufisadi naubadhirifu
wa mali za umma. Katika miaka mitano iliyopitatuliwachukulia hatua
za kinidhamu watumishi 32,555 nakuiwezesha nchi yetu kushika nafasi
ya kwanza kati ya nchi
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
10
35 za Afrika kwa kupambana na rushwa kwa mujibu waTransparency
International na pia kushika nafasi ya 28 katiya nchi 136 duniani
kwa matumizi mazuri ya fedha za ummakwa mujibu wa utafiti wa Jukwaa
la Uchumi la Dunia yaaniWorld Economic Forum wa mwaka 2019.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata hivyo watumishi wazembebado wapo, wala
rushwa bado wapo na pia wezi nawabadhirifu wa mali za umma bado
wapo, kwa hiyo, katikamiaka mitano ijayo tutaendelea kushughulikia
matatizo hayo,kwa kifupi niseme utumbuaji majipu utaendelea.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata hivyo kwa upande mwinginetutaendelea
kuboresha mazingira ya kazi pamoja na maslahiya watumishi wetu wote
ili yaendane na hali halisi ya maishaya Watanzania, tutaangalia
maslahi yao, kwa hiyo watumishiwasiwe na wasiwasi, wachape kazi.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo piatumejipanga
kuendeleza jitihada za kukuza uchumi, kamaunavyofahamu katika
kipindi cha miaka mitano iliyopitatulijitahidi kusimamia vizuri
uchumi wetu ambapo ulikua kwawastani wa asilimia saba kwa mwaka.
Aidha, pato ghafi laTaifa limeongezeka kutoka shilingi trilioni
94.349 mwaka 2015hadi kufikia shilingi trilioni 139.9 mwaka 2019.
Tulidhibitimfumuko wa bei kutoka asilimia 6.1 mwaka 2015 hadi
kufikiawastani wa asilimia 4.4 na kuongeza akiba ya fedha za
kigenikutoka Dola za Marekani bilioni 4.4 hadi kufikia dola
zaMarekani bilioni 5.2 mwezi Julai, 2020 ambazo
zinatuwezeshakununua bidhaa na huduma kwa miezi sita. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo kwenye miakamitano iliyopita
tuliongeza mauzo yetu ya nje kutoka Dola zaMarekani bilioni 8.9
mwaka 2015 hadi Dola za Marekani bilioni9.7 mwaka 2019, pia kuvutia
uwekezaji wenye thamani yaDola za Marekani bilioni 14.6 sawa na
zaidi ya shilingi trilioni30. Aidha, tulifanikiwa kupunguza
umaskini wa kipato hadikufikia asilimia 26.4 kwa takwimu za mwaka
2017/2018.Mafanikio haya bila shaka ndiyo yamewezesha mwezi
Julai,2020 nchi yetu kutangazwa kuingia katika kundi la nchi za
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
11
uchumi wa kati kutoka kundi la nchi maskini. Hongereni
sanaWatanzania, hongereni sana Waheshimiwa Wabunge.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa mafanikio hayoyamepatikana miaka mitano
kabla ya muda uliopangwayaani mwaka 2025, kwa hiyo kwenye miaka
mitano ijayotunakusudia kuendeleza mafanikio ya
kiuchumiyaliyopatikana na tutahakikisha ukuaji wa
uchumiunawanufaisha wananchi hususani kwa kuinua vipato
vyao,kupunguza umaskini na tatizo la ajira. Katika hilo
tunalengakukuza uchumi wetu kwa wastani angalau asilimia nane
kwamwaka na pia kutengeneza ajira mpya zipatazo milioni
nane.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, tutaendelea pia kuboresha serazetu za uchumi
jumla na sera za fedha (microeconomics andmonitory policies) pia
kuhakikisha viashiria vyote vya uchumiikiwemo thamani ya sarafu
yetu, mfumuko wa bei pamojana viwango vya riba vinabaki kwenye hali
ya utulivu, piatutaongeza jitihada za kuwawezesha wananchi
wetukiuchumi kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba ama yenyeriba nafuu
ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwaHalmashauri zetu.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, pia kupitia mifuko na programumbalimbali
zilizoanzishwa na Serikali ambayo kwa idadi zipo18 baadhi ya mifuko
hiyo ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana(YDF), Mfuko wa Maendeleo ya
Wanawake (WDF), Mfuko waTaifa wa Kuendeleza Wajasiriamali (NEDF),
Mfuko wa KutoaMikopo kwa Wajasiriamali Wadogo (SELF-Microfinance
Fund),Mfuko wa Kuthamini Mikopo ya Mauzo ya Nje, Mfuko waKilimo
Kwanza na kadhalika. Tutaimarisha usimamizi wamifuko hii na
kuhakikisha Watanzania wanaifahamu, najuamifuko hii ni mingi ipo
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo basinakuagiza Mheshimiwa
Waziri Mkuu hii ikawe kazi yako yakwanza kushughulikia. Ikiwezekana
muangalie uwezekanowa kuiunganisha baadhi ya mifuko ili ifanye kazi
kwa tija zaidina kupunguza gharama za uendeshaji. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
12
Nataka mifuko hii ikawasaidie wananchi wa kawaidawakiwemo
wamachinga, akina baba na akina mama lishepamoja na wajasiriamali
wengine wadogo wadogo, kwa hiyokazi yako Mheshimiwa Waziri Mkuu
ukaanze na hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sambamba na kutoa mikopotutaendelea pia
kutekeleza programu mbalimbali za kukuzaujuzi na maarifa ikiwemo
maarifa ya ujasiriamali ili kuwapaujuzi na uzoefu wananchi wetu
utakaowawezesha kujiajiriama kuajirika ndani na nje ya nchi,
tutaendelea piakutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Awamu
yaTatu Mzunguko wa Pili tuliouzindua mwezi Februari, 2020ambao
utagharimu takribani shilingi trilioni 2.032. Tutahakikishafedha
hizo zinawafikia walengwa ambao ni wananchimaskini.
Mheshimiwa Spika, muhumu zaidi ni kwamba katikakipindi cha miaka
mitano ijayo sekta binafsi pia itapewaumuhimu wa pekee sana.
Tunataka mtu yeyote atakayetakakuwekeza asisumbuliwe kwa kuwekewa
vikwazo vya ainayoyote. Watanzania ni matajiri, lakini baadhi yao
wanasitakuwekeza hapa nchini kwa kuogopa kusumbuliwa namaswali
yasiyo na msingi, tunahitaji kuwa na mabilioneawengi wa Kitanzania.
(Makofi)
Tunahitaji mabilionea wengi wa Kitanzania wakiwemoWaheshimiwa
Wabunge. Nataka Watanzania wote washirikikikamilifu katika kujenga
uchumi wa nchi yao sambamba nakuwekeza, Watanzania wahamasishwe
kuweka fedhakwenye benki za hapa nchini ili kusaidia benki zetu
kufanyabiashara na kuimarisha mzunguko wa fedha na kupunguzariba
kwa wakopaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge naWatanzania
mnaonisikiliza, wakati wa kufanya mambo bilawoga nataka niwaambie
Waheshimiwa Wabunge ni sasa,tumechelewa sana! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo piatutafungua
milango wa sekta binafsi kufanya majadiliano na
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
13
Serikali ili kutafuta muafaka wa migogoro ya kibiashara(business
disputes) iliyopo kwa faida ya pande zote mbili.Lengo letu ni kuona
Tanzania inakuwa mahali pazuri pakufanya biashara
duniani.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika miaka mitano iliyopitatumefuta tozo 168
ambapo tozo 114 zilihusu kilimo, mifugona uvuvi na tozo nyingine 54
zilihusu biashara. Tutaendeleana utaratibu huo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mbali na hatua hizo kwa lengo lakukuza uchumi
kupambana na umaskini na pia kukabilianana tatizo la ukosefu wa
ajira, tunakusudia kwenye miakamitano ijayo kuweka mkazo mkubwa
katika kukuza sekta zetukuu za uchumi na utazlishaji hususani
kilimo, ufugaji, uvuvi,viwanda, madini, biashara na utalii. Sekta
hizi ndizo zenyekuajiri Watanzania wengi, kwa hiyo, ni wazi
tukifanikiwakuzikuza uchumi wetu utakua kwa kasi na hivyo
kupunguzamatatizo ya umaskini na ukosefu wa ajira nchini.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo kwenye kilimo kwamfano,
tunakusudia kuongeza tija na kukifanya kilimo chetukuwa ni kilimo
cha kibiashara, lengo ni kujihakikishia usalamawa chakula,
upatikanaji wa malighafi za viwandani na piakupata ziada ya kuuza
nje. Ili kufanikisha hayo tutahakikishapembejeo na zana bora za
kilimo ikiwemo mbegu, mbolea,viuatilifu, dawa na matrekta
vinapatikana kwa uhakika nakwa gharama nafuu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tutaongeza pia eneo laumwagiliaji kutoka hekta
561,383 hadi hekta milioni 1.2mwaka 2025, hii itasaidia kupunguza
utegemezi kwenyemvua. Tataimarisha mifumo ya upatikanaji wa mitaji
kwawakulima wadogo na wawekezaji kwa kushirikiana na taasisiza
fedha ikiwemo Benki yetu ya Maendeleo ya Kilimo pamojana benki
nyingine. Tutashughulikia pia tatizo la upotevu wamazao (post
harvesting loss) ikiwemo kwa kukamilisha ujenziwa vihenge na
maghala maeneo mbalimbali nchini ambayoyataongeza uwezo wetu wa
kuhifadhi mazao kutoka tani190,000 za sasa hadi tani 501,000.
Takwimu zinaonesha kuwa
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
14
kila mwaka nchi yetu inapoteza wastani wa kati ya asilimia30 na
asilimia 40 ya mavuno yake kwa sababu mbalimbaliikiwemo kukosekana
kwa miundombinu ya kuhifadhi mazaoyetu. Zaidi ya hapo tunakusudia
kuanzisha bidhaa mbalimbaliza huduma za bima ya kilimo na pia
kuingia makubaliano yakibiashara na nchi walaji na wanunuzi wa
mazao ili kupatasoko la uhakika zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mazao ya kimkakati tunayolengakuyapa
kiupaumbele kikubwa katika miaka mitano ijayo nipamba, korosho,
chai, kahawa, tumbaku, mkonge,michikichi, cocoa, alizeti pamoja na
miwa, lakini pia mazaoya chakula. Nchi yetu kwa mwaka inaagiza tani
zipatazo800,000 za ngano na kwa ujumla tunatumia wastani wa
shilingitrilioni 1.3 kuagiza chakula kutoka nje, hii ni aibu kwa
nchikama Tanzania! Hivyo, basi ni lazima tutafute majawabu yasuala
hili na hii ndio ikawe kazi ya kwanza ya Waziri wa
Kilimonitakayemteua. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo tutaweka mkazomkubwa kwenye
kilimo cha mazao ya bustani yaanimatunda, mbogamboga, maua na
viungo ambachokinakua kwa kasi kubwa nchini, hivi sasa nchi yetu
inashikanafasi ya 20 kwa kuzalisha wa wingi mazao hayo duniani
namauzo yetu ya nje yameongezeka kutoka Dola za Kimarekanimilioni
412 mwaka 2015 hadi kufikia Dola za Kimarekani milioni779 mwaka
2019. Hii ndiyo sababu hatuna budi kukiendelezakilimo cha mazao
hayo na katika hilo napenda kuliarifu Bungehili kuwa kwenye miaka
mitano ijayo tunakusudia kununuandege moja ya mizigo ili
kurahisisha usafirishaji wa mazao yabustani, lakini pia minofu ya
samaki pamoja na nyama.Wakulima wetu ni lazima watajir ike na
shughuliwanazozifanya. Hivyo basi, Mawaziri wa Kilimo,
Biashara,Mambo ya Nje na Mabalozi wajipange vizuri katika
hili.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mifugo; kamamnavyofahamu nchi
yetu inashika nafasi ya pili kwa mifugomingi Barani Afrika. Tuna
ng’ombe milioni 33.4, mbuzi milioni21.3, kondoo milioni 5.65, punda
657,389 lakini pia tuna idadi
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
15
kubwa ya kuku, bata, kanga na kadhalika. Hata hivyo, niukweli
usiopingika kwamba sekta hii bado haijanufaisha vyakutosha. Kwa
kuzingatia hilo, kwenye miaka mitano ijayotunakusudia kuikuza sekta
ya mifugo ili ichangie ukuaji wauchumi na kupunguza matatizo ya
umaskini na ukosefu waajira nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumepanga kuongeza maeneoya ufugaji kutoka
hekta 2,788,901 za sasa hadi hekta milionisita. Tunataka wafugaji
wetu wasiteswe na mifugo yao,mifugo ni utajiri. Sambamba na hayo,
tutahamasisha ufugajiwa kisasa, tutaongeza vituo vya kuzalisha
mbegu bora napia kuongeza uzalishaji wa chakula cha mifugo
viwandanikutoka tani 900,000 hadi tani milioni nane. Zaidi ya
hapotutakamilisha ujenzi wa machinjio saba unaoendeleamaeneo
mbalimbali nchini ambapo kwa pamoja yatakuwana uwezo wa kuchinja
ng’ombe 6,700 na mbuzi 11,000 kwasiku. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa machinjio hayo siyo tuutasaidia
kupatikana kwa nyama bora inayouzwa hadikwenye masoko ya kimataifa,
bali pia utawezeshaupatikanaji wa ngozi bora kwa ajili ya
kutengeneza bidhaaza ngozi. Takwimu zinaonyesha kuwa takribani
asilimia 90 yangozi inayozalishwa nchini kwa sasa haina ubora
unaohitajikakimataifa na kwa sababu hiyo mojawapo ni uchinjaji
wawanyama kienyeji. Kwa hiyo, machinjio yanayojengwayatapunguza
tatizo hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuikaribisha sektabinafsi
kuwekeza kwenye viwanda vya kutengeneza bidhaaza mifugo yaani
nyama, ngozi, maziwa, kwato na kadhalikana katika hilo tunaahidi
kutoa vivutio maalum kwawatakaoweza kuanzisha viwanda vya aina hiyo
na viwandahivyo vitasaidia kuinua vipato vya wafugaji wetu na
piakuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. Na hapa natakaniweke
bayana kuwa watendaji wataokwamisha ujenzi waviwanda hivyo
tutawashughulikia, kwa sababu saa nyinginetunakuwa na mipango
mizuri, Watendaji wa chini
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
16
wanakwamisha. Ilani ya Uchaguzi sitaki icheleweshwe na
mtuyeyote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nchi yetu pia imebarikiwa kuwana maeneo mengi
yanayofaa kwa shughuli za uvuvi ikiwemoUkanda wa Pwani, Maziwa,
Mito na Mabwawa. Hali hiiinaifanya sekta hii kuwa na nafasi ya
kutoa mchangomkubwa kwenye kukuza Pato la Taifa na pia kupambana
naumaskini na tatizo la ajira. Hata hivyo, kwa sasa mchangowake
bado ni mdogo sana. Hivyo basi, kwenye miaka mitanoijayo
tunakusudia kuikuza sekta hii ya uvuvi ikiwemokuimarisha shughuli
za uvuvi kwenye Bahari Kuu ambakotumekuwa tukipoteza mapato
mengi.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa report ya Kamatiya Bunge kuhusu
shughuli za uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka2018; shughuli za uvuvi
kwenye Bahari Kuu zinaweza kuiingiziaSerikali mapato ya moja kwa
moja ya takribani shilingi bilioni352.1 kwa mwaka endapo mifumo,
usimamizi na udhibitiingekuwa imara. Samaki wangechakatwa hapa
nchini hatahivyo mapato yaliyokuwa yamekusanywa kwa kipindi
chamiaka tisa yaani kuanzia 2009 hadi 2017 yalikuwa shilingi
bilioni29.79 tu sawa na shilingi bilioni 3.3 kwa mwaka. Kiwango
hikicha mapato hakikubaliki. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hii ndiyo sababu tunataka kwenyemiaka mitano
ijayo kuisimamia vizuri shughuli ya uvuvi waBahari Kuu ili Taifa
letu linufaike na rasilimali zake kwa kuhusishasekta binafsi. Kwa
bahari nzuri, tayari mwaka huu 2020tumetunga sheria mpya ya
kusimamia na kuendeleza uvuviwa Bahari Kuu. Aidha, tumepanga
kununua meli nane zauvuvi kwa kusihirikiana na Shirika la IFAD.
Meli hizo nane, nnezitakuwa upande wa Zanzibar na nne zitakuwa
upande waTanzania Bara. Meli hizi zitashiriki katika uvuvi wa
Bahari Kuu.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama mnavyofahamu suala lauvuvi wa Bahari Kuu
ni la Muungano, tunakusudia pia kujengabandari kubwa ya uvuvi
itakayotoa ajira zipatazo 30,000 na
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
17
tutaendelea kuihamasisha sekta binafsi kujenga viwanda
vyakuchakata samaki.
Sambamba na kusimamia Bahari Kuu, tutakuzashughuli za uvuvi
kwenye Maziwa yetu Makuu yaani Victoria,Ziwa Tanganyika na Ziwa
Nyasa pamoja na Mito yetumikubwa, tutahamasisha wavuvi wetu wadogo
kujiungakwenye vikundi ili tuweze kuwapatia mitaji, ujuzi, vifaa na
zanaza uvuvi, na hali kadhalika tutapitia upya tozo za
maeneombalimbali ili kuwapunguzia wavuvi kero na kuvutia
uwekezajikwa wavuvi wetu. Tutahamasisha pia watu binafsi
kujengamabwawa na kufuga kisasa kwa kutumia vizimba. Sekta yauvuvi
ni lazima itoe mchango mkubwa kwenye uchumi wanchi yetu. Wateule
wote wa sekta hii ni lazima walisimamiehili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ni ndoto kufikiria kwambatutaweza kukuza
uchumi au kupambana na umaskini pamojana tatizo la ukosefu wa ajira
bila kuendeleza nguvu katikakukuza sekta ya viwanda. Duniani kote
sekta ya viwandandiyo muhimili mkuu wa kukuza uchumi, kupambana
naumaskini pamoja na matatizo ya ajira. Kwenye miaka
mitanoiliyopita tulifanikiwa kujenga viwanda vipya takribani
8,477ambavyo vilitengeneza ajira zipatazo 480,000 ambapo Mkoawa
Pwani uliongoza kwa kujenga viwanda vingi.Nawapongeza sana uongozi
wa Mkoa wa Pwani. (Makofi)
Hivyo basi, kwenye miaka mitano ijayo tutaendelezajitihada za
kukuza sekta hiyo. Mkazo mkubwa tutauwekakwenye viwanda vyenye
kutumia malighafi zinazopatikanakwa wingi hapa nchini yaani mazao
ya kilimo, mifugo na uvuvivyenye kuajiri watu wengi na ambavyo
bidhaa zakezinatumika kwa wingi hapa nchini kama vile nguo,
bidhaaza ngozi, mafuta ya kula, sukari, saruji na kadhalika.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, ili kuvutia uwekezaji kwenye sektaya viwanda
tutaendelea kuboresha mazingira ya biasharana uwekezaji ikiwemo
kuangalia masuala ya kodi na kuondoavikwazo na urasimu. Pamekuwepo
na urasimu nyingi nakusumbuliwa kwa wawekezaji kwa kuzungushwa
zungushwa
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
18
na hivyo kuwafanya wakate tamaa. Mimi nataka mwekezajimwenye
fedha zake akija apate kibali ndani ya siku 14.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, na kwa sababu hiyo nimeamuasuala la uwekezaji
ikiwa ni pamoja na Kituo cha UwekezajiTanzania (TIC) kulihamishia
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuukwenda Ofisi ya Rais ili hao
wanaokwamisha nikapambanenao mwenyewe. Lakini zaidi ya hapo,
tumepanga kujengaUkanda na Kongani yaani clusters za viwanda kila
mkoakulingana na mazao na maliasili zinazopatikana
huko.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano iliyopitatumepata mafankio
makubwa kwenye sekta ya madini.Mapato yameongezeka kutoka shilingi
bilioni 168 mwaka2014/2015 hadi shilingi bilioni 527 mwaka
2019/2010. Mchangowa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa
umeongezekakutoka asilimia 3.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2
mwaka2019. Zaidi ya hapo kwa mara ya kwanza katika historia yanchi
yetu, mwaka 2019 sekta ya madini iliongoza kwakutuingizia fedha
nyingi za kigeni Dola za Marekani bilioni 2.7.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kulipongeza sanaBunge la
Kumi na Moja kwa kutoa mchango mkubwa katikakupatikana kwa
mafanikio haya ikiwa ni pamoja na kutungasheria humu Bungeni.
Ahsanteni sana WaheshimiwaWabunge. (Makofi)
Nina imani kuwa, Bunge hili la Kumi na Mbili litafuatanyayo za
Bunge la Kumi na Moja na katika hili napendaniliarifu Bunge hili
tukufu kuwa kwenye miaka mitano ijayotutaendelea kuimarisha ulinzi
na usimamizi wa madini yetukama tulivyofanya kwa kujenga ukuta wa
Mirerani kwakuimarisha Sheria zetu ili madini yetu yasitoroshwe na
Serikalikukoseshwa mapato. Aidha, tunakusudia kuendelea
kufanyamajadiliano na wawekezaji wakubwa kwa kuzingatia mfanowa
makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
19
Barrick yaliyowezesha kuundwa kwa Kampuni ya TwigaMinerals
Corporation.
Mheshimiwa Spika, nchi yetu imebarikiwa kuwa namadini mbalimbali
ikiwemo dhahabu, almasi, Tanzanite,chuma, bati, nickel, copper na
kadhalika. Lakini aidha tunagesi za aina mbalimbali kama vile
ethane, methane pamojana helium. Kwa taarifa tulizonazo kwa mfano
kwenye gesi yahelium ambayo inapatikana kule Rukwa ni tani nyingi
sanazilizoko kule za ujazo zikichimbwa zinatosha ku-supply
dunianzima kwa miaka 20. (Makofi)
Kwa hiyo, kama zinaweza zikahudumia dunia kwamiaka 20 huu ni
utajiri mwingine tulionao sisi Watanzania. Hiindiyo sababu kila
siku nimekuwa nikisema sisi siyo maskini, sisini matajiri, nchi
yetu ni tajiri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu madini, pia kwenyemiaka mitano
ijayo tutaendelea kuimarisha Shirika letu la Taifala Madini yaani
STAMICO ili lishiriki kikamilifu kwenye shughuliza madini
kuwawezesha wachimbaji wetu wadogo wadogoikiwa ni pamojha na
kuwatengea maeneo ya uchimbaji,kuwapatia mafunzo mikopo pamoja na
vifaa na katika hilinatambua kuwa wapo baadhi ya watu wamepewa
leseniza utafiti na uchimbaji, lakini hawajazifanyia kazi.
Tutazifutaleseni zao na maeneo hayo tutawagawia wachimbajiwadogo
wadogo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wadogo nimuhimu sana katika
kukuza sekta ya madini. Tutaendeleapia kuimarisha masoko ya madini
pamoja na kuhamasishaujenzi wa viwanda vya uchenjuaji, uyeyushaji,
usafirishaji nautengenezaji wa bidhaa za madini. Tunataka
madiniyachimbwe hapa Tanzania, yachenjuliwe hapa
Tanzania,yayeyushwe hapa Tanzania kisha bidhaa za
madinizitengenezwe hapa Tanzania na ndipo ziuzwe nje ama watukutoka
nje waje kununua bidhaa za madini hapa nchini.Tutakuwa
tumetengeneza uchumi wa kutosha lakini piatutatengeneza ajira za
kutosha kwa Watanzania. Ni imaniyetu kuwa kutokana na hatua
tulizopanga kuzichukua, sekta
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
20
ya madini itaweza kuchangia angalau asilimia 10 ya Pato laTaifa
ifikapo mwaka 2025. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, utalii ni sekta nyingine ambayotutaipa mkazo
mkubwa kwenye miaka mitano ijayo; sektahii imeajiri takribani watu
milioni nne. Kwenye miaka mitanoiliyopita ilikuwa ikitoa mchango
mkubwa ambao ulikuwaunaridhisha ambapo idadi ya watalii
waliotembelea nchiiliongezeka kutoka watalii 1,137,182 mwaka 2015
hadi watalii1,510,151 mwaka 2019. Mapato nayo yaliongezeka
kutokaDola za Marekani bilioni 1.9 mwaka 2015 hadi kufikia Dola
zaMarekani bilioni 2.6 mwaka 2019. Nitumie fursa hii
kuipongezaHifadhi yetu ya Taifa ya Serengeti kwa kuchaguliwa
kuwahifadhi bora Barani Afrika kwa mwaka 2020. Kwenye miakamitano
ijayo tumejipanga kuongeza iddai ya watalii hadikufikia milioni
tano mwaka 2025 na mapato kutoka Dola zaMarekani bilioni 2.6 za
sasa hadi Dola za Marekani bilioni sita.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, hatua tutakazochukua ni pamojana kupanua wigo
wa vivutio vya utalii ikiwemo kukuza utaliiwa mikutano na uwindaji
wa wanyamapori, kuimarisha utaliiwa fukwe, kujenga miundombinu ya
kuwezesha meli za utaliikuzuru nchini na kuongeza kasi ya
utangazaji wa vivutio vyetu.Vilevile tutazihamaisha taasisi za watu
binafsi kuanzisharanchi, mashamba na bustani za wanyama
kamainavyofanyika nchi zingine ili kuzuia ujangili na kukuza
utalii,lakini pia kuongeza vipato na fursa za ajira kwa
Watanzania.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika hilo, napenda kuwaarifuWatanzania
kupitia Bunge hili tukufu kuwa tumepunguza beikwa ajili ya kupata
wanyama wa mbegu kutoka porini.Mathalani, bei ya nyati wa mbegu
imepungua kutoka Dolaza Marekani 1,900 hadi kufikia shilingi
200,000, pofu kutokaDola za Marekani 1,700 hadi shilingi 310,000,
swala kutokaDola za Marekani 150 hadi shilingi 90,000; hivyo basi,
nawasihiWatanzania hata ninyi Waheshimiwa Wabunge popotewalipo
changamkieni fursa hii ya kuanza kufuga wanyamawalioko porini.
(Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
21
Mheshimiwa Spika, hii ni fursa pekee, kuna nchimbalimbali
zimekuwa zikifanya hivyo, mojawapo ni nchi kamaAfrika ya Kusini na
kadhalika. Hii itatufanya Watanzania wotetufaidike na biashara ya
wanyamapori, lakini pia watuwataanzisha butcher za wanyamapori na
wataanza kuwalabadala ya kula nyama ya pori kuonekana ni adui.
Zaidi yahapo, tutaendelea kupitia upya kodi na tozo mbalimbali
ilikuzifuta ama kupunguza kodi zenye kero. Kwenye miakamitano
iliyopita, tulipunguza ada za leseni za biashara ya utaliikwa
Wakala wa Kusafirisha Watalii yenye idadi ya magarichini ya manne
kutoka Dola za Kimarekani 2,000 hadi Dolaza Marekani 500 na matokeo
yake idadi ya kampuni zaKitanzania zimeongezeka kutoka 643 mwaka
2015 hadikampuni 1,687 mwaka 2020. Tutaendelea na hatua
hizo.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, tuna imani, hatua hizi
nilizoelezazitatuwezesha kufikia malengo tuliyojiwekea ya
kukuzauchumi kwa angalau asilimia nane kwa mwaka na kuinuavipato
vya Watanzania, kupunguza umaskini na kutengenezaajira mpya milioni
nane. Hata hivyo, najua ili kufikia malengohaya tunategemea sana
kupata ushirikiano kutoka sektabinafsi. Kama mnavyofahamu, sekta
binafsi ndiyo engine yakujenga uchumi wa kisasa. Hivyo basi,
narudia kuikaribishasekta binafsi ya hapa nchini na kutoka nje
kuwekeza katikasekta nilizozitaja na ambazo sikuzitaja.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, napenda kuwahakikishia watu wasekta binafsi
kuwa Tanzania ni mahali pazuri na sahihi pakuwekeza. Nchi yetu ina
amani na utulivu, tumebarikiwa kuwana fursa nyingi za uwekezaji,
nchi yetu ipo kwenye eneo lakimkatati, sisi pia ni wanachama wa
East Africa Communityna SADC ambazo zina soko la watu takriban
milioni 500. Kwahiyo narudia, kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza
hapa nchini.Kwa bahati nzuri, tangu mwaka jana tumeanza
kutetekelezaMpango wetu wa Kuboresha Mazingira ya Biashara
(Blueprintfor Regulatory Reforms to Improve the Business
Environmentin Tanzania). Hivyo basi, mazingira ya biashara na
uwekezaji,kwenye miaka mitano ijayo yanatarajiwa kuwa bora
zaidikuliko miaka mingine yote. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
22
Mheshimiwa Spika, ili kukuza uchumi pamoja na sektaya uzalishaji
ni lazima tuimarishe miundombinu, hususan yausafiri na nishati ya
umeme. Kamwe huwezi kukuza sekta yakilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda,
uchimbaji madini na utalii bilakuimarisha miundombinu na huduma za
usafiri pamoja naupatikanaji wa huduma za umeme. Kwa hiyo,
kamailivyokuwa kwenye miaka mitano iliyopita, tutaendeleakuweka
mkazo mkubwa kwenye ujenzi wa miundombinu yausafiri na kuboresha
huduma za usafirishaji. Tutakamilishamiradi tuliyoianzisha na
kuanza kutekeleza miradi mipya nakatika hilo tumepanga kwenye miaka
mitano ijayo,kukamilisha ujenzi wa kilometa 2,500 za barabara za
lami nakuanza ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa
kilometa6,006. (Makofi)
Najua Wabunge wengi mmetoa ahadi za barabarakwenye maeneo yenu,
ili hatimaye tuweze kufikia lengo letula kuunganisha mikoa na
wilaya zote kwa barabara za lami.Barabara hizo zimetajwa kwenye
Ilani yetu ya Uchaguzi nazingine zinatokana na ahadi tulizotoa
katika kipindi chakampeni. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumepanga pia kukamilisha ujenziwa madaraja
saba na kuanza madaraja mengine 14likiwemo Daraja la Kigongo –
Busisi, Wami na Pangani. Zaidiya hapo, tutaendelea kushughulikia
tatizo la msongamanowa magari kwenye miji na majiji yetu, hususan
Arusha, Dar esSalaam, Mbeya, Mwanza na hapa Dodoma ambakotumepanga
kujenga barabara ya mzunguko ya njia nneyenye urefu wa kilometa 110
ambapo makandarasi wawilitayari wamekwishapatikana na ujenzi
utaanza hivi karibuni.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa usafiri wa reli,tumepanga
kuendelea kuimarisha usafiri wa Reli ya Kati naTAZARA. Aidha,
tutakamilisha ujenzi wa reli ya kisasa kutokaDar es Salaam -
Morogoro hadi Dodoma na kuanza ujenziwa vipande vya reli ya Mwanza
– Isaka; Makutopora – Tabora;Tabora – Isaka hadi Tabora – Kigoma na
Kaliua – Mpandahadi Kalema. Zaidi ya hapo, tutanunua vichwa vya
treni ya
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
23
njia kuu 39 na kukarabati 31; tutanunua mabehewa ya mizigo800 na
kukarabati 690 na pia tutanunua mabehewa 37 yaabiria na kukarabati
mabehewa 60. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu usafiri wa majini,tumepanga kukamilisha
upanuzi wa bandari zetu kuu yaaniDar es Salaam, Bandari ya Tanga na
Bandari ya Mtwarapamoja na zilizopo kwenye Maziwa yetu Makuu
yaaniVictoria, Tanganyika na Nyasa. Tumepanga pia kununua melimpya
ya mizigo kwa ajili ya kutoa huduma katika Bahari yaHindi.
Tutakamilisha ujenzi wa meli mpya, kukarabati meli yaMV Butiama na
kuanza ujenzi wa meli ya kubeba mabehewa(ferry wagon) Ziwa
Victoria. Tutaikarabati MV Liemba na MTSangara pamoja na kuanza
ujenzi wa meli mpya ya kubebaabiria 600 na mizigo tani 400 na
nyingine kubwa ya kubebamizigo tani 4,000 kwenye Ziwa Tanganyika.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu usafiri wa anga, tutajengakiwanja kipya
cha Msalato, kikubwa; tutafanya upanuzi naukarabati wa viwanja vya
ndege kumi na moja, vikiwepo vyaKigoma, Shinyanga, Sumbawanga,
Tabora, Mtwara naSongea pia kujenga kwa kiwango cha lami njia za
kutua nakuruka ndege kwenye viwanja vya Iringa, Lake Manyara,Tanga,
Musoma, Lindi, Kilwa Masoko, Njombe, Singida Simiyuna kadhalika.
Zaidi ya hapo, tutanunua ndege mpya tano,ambapo kama nilivyosema,
moja itakuwa ya mizigo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa miundombinu hii yausafiri pamoja na
uboreshaji wa huduma za usafirishaji sio tuutachochea shughuli za
uchumi na uzalishaji, lakini piaitakuwa ni hatua nzuri ya kuelekea
kufikia malengo yetu yakuifanya nchi yetu kuwa lango kuu la
biashara kwenyeukanda huu; hivyo kuweza kunufaika na nafasi ya
kijiografia.Nchi yetu imezungukwa na nchi takribani nane.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu sekta ya nishati,tutaendelea kuimarisha
miundombinu ya nishati na piakuboresha upatikanaji wa huduma za
umeme. Katika hilo,tunakusudia kukamilisha ujenzi wa Bwawa la Kufua
Umemela Nyerere litakalozalisha megawati 2,115 na kuanza ujenzi
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
24
wa miradi mingine mipya ya umeme wa maji katika eneo laRuhudji
megawati 358; Rumakali megawati 222; Kikongemegawati 300 na pia
umeme wa gesi asilia Mtwaramegawati 300; Somanga Fungu megawati
330, Kinyerezi IIImegawati 600, Kinyerezi IV megawati 300; pamoja
na miradimingine midogo midogo. Aidha, tunakusudia kuzalishaumeme
megawati 1,100 kwa kutumia nishati jadidifu yaanijua, upepo, na
jotoardhi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumepanga pia kukamilisha miradiya kusafirisha
umeme wa Msongo wa kilovoti 400 wa Singida– Arusha hadi Namanga na
Iringa – Mbeya hadi Tundumaambayo itaunganisha nchi yetu na jirani
zetu za Kenya naZambia. Tutatekeleza mingine ya kuunganisha
maeneomuhimu ya nchini kwenye Gridi ya Taifa ikiwemo Kigoma.Kwenye
miaka mitano iliyopita, tulitekeleza miradi mingi yakusafirisha
umeme na hivyo kupunguza matumizi ya umemewa mafuta; na tukaweza
kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 719kwa mwaka. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuhusu umeme pia kwenye miakamitano ijayo,
tumepanga kufikisha umeme kwenye vijiji vyoteambavyo bado
havijafikishiwa umeme, ambapo idadi yakehaizidi vijiji 2,384. Kwa
sababu kwenye miaka mitano iliyopita,kwa takwimu za hadi jana
tumefikisha umeme kwenye vijiji9,884 kutoka vijiji 2,018 mwaka
2016. Nchi yetu ina vijiji 12,280.Miradi hii yote ya umeme
itakapokamilika sio tu itatuwezeshatuwe na umeme wa kutosha na
kufikisha umeme kwenyemaeneo yote nchini, bali pia itatufanya tuwe
na ziada yakuweza kuuza nje, pia itatusaidia kupunguza gharama
zaumeme kuliko gharama za sasa hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sambamba na hayo, kuhusunishati, kwenye miaka
mitano ijayo, tutaanza utekelezaji wamiradi ya kielelezo yaani
flagship projects ya bomba lamafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tangalenye urefu wa kilometa 1,445. Mradi huu ni mkubwa
na niwa kwanza kuwa mkubwa duniani kwa kusafirisha mafutaambayo
yako heated kwenye distance kubwa ya kilometa1,444 na kilometa zote
1,115 ni Tanzania, kilometa zingine 300
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
25
na kitu zitakuwa nchini Uganda. Mradi wa Kusindika GesiAsilia
(LNG) Mkoani Lindi, nao tutahakikisha unaanza kufanyakazi. Zaidi ya
hapo, tutaendelea kuhamasisha matumizi yagesi asilia na gesi ya
mitungi majumbani, kwenye taasisi naviwanda na magari ili kupunguza
uharibifu wa mazingira naathari za mabadiliko ya tabianchi.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, dunia hivi sasa ipo kwenyeMapinduzi ya Nne ya
Viwanda yaani The Fourth IndustrialRevoulution) ambayo yanaongozwa
na Sekta yaMawasiliano (ICT). Shughuli nyingi duniani, kwa
sasazinafanyika kwa kutumia TEHAMA. Hivyo basi, na sisi hatunabudi
kuendana na kasi hiyo ya kukua kwa sekta yamawasiliano. Kwa msingi
huo, tumepanga, kwenye miakamitano ijayo, pamoja na masuala
mengine, kufikishamiundombinu ya Mkongo wa Taifa kwenye maeneo
mengiya nchi yetu, hususan wilayani. Tutaongeza wigo wa matumiziya
mawasiliano ya kasi yaani broadband kutoka asilimia 45ya sasa hadi
asilimia 80 mwaka 2025. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, aidha, tumepanga kuongezawatumiaji wa internet
kutoka asilimia 43 ya sasa hadi asimilia80 mwaka 2025 na pia
kuboresha matumizi ya simu zamkononi ili kupatikana nchi nzima.
Zaidi ya hapo, tutatoavipaumbele kwenye masuala ya utafiti na
ubunifu kwenyeTEHAMA, tutawatambua na kuwasajili wataalam wote
waTEHAMA; na tunakusudia kuweka anuani za makazi (postalcode)
maeneo mbalimbali nchini. Tutaimarisha pia usalamakwenye masuala ya
mawasiliano. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sambamba na kukuza huduma zamawasiliano,
tunakusudia kuendelea kuboresha huduma zajamii, hususan afya, elimu
na maji. Kuhusu afya, kamamnavyofahamu Waheshimiwa Wabunge, kwenye
miakamitano iliyopita tumepata mafanikio makubwa sana ,ikiwemo
kujenga vituo vya kutolea huduma za afya zaidi ya1,887; Zahanati
1,198; Vituo vya Afya 487; Hospitali za Wilaya99; Hospitali za
Rufaa Mikoa 10; na Hospitali za Rufaa zaKanda tatu. Vilevile,
tumepunguza vifo vya akinamamawajawazito kutoka wastani wa vifo
11,000 kwa mwaka
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
26
mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa vifo 3,000 kwa mwakahivi sasa
na tunataka vipungue zaidi. Halikadhalika rufaa yakupeleka wagonjwa
nje zimepungua kwa asilimia 90 baadaya kuimarisha huduma za
kibingwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo kwenye miakamitano ijayo
tunakusudia kuendeleza ujenzi wa miundombinuya kutolea huduma za
afya, hususan zahanati, vituo vya afyana Hospitali za Wilaya kwenye
maeneo ambako hazipo.Tutaimarisha pia upatikanaji wa dawa, vifaa na
vitendanishina kuongeza watumishi wa afya pamoja na
kuimarishaMifuko yetu ya Bima ya Afya ili kufikia lengo la
kuwawezeshawananchi wote kupata Bima ya Afya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wakati wa ugonjwa wa corona,mbali na
kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu, tiba za asiliau tiba mbadala
nazo zimesaidia sana. Hivyo basi, kwenyemiaka mitano ijayo,
tumekusudia kuimarisha Kitengo chaUtafiti wa Tiba Mbadala. Sisi
Watanzania hatupaswi kamwekudharau dawa zetu za asili ama tiba
mbadala na kwasababu hiyo, matibabu na maduka rasmi ya dawa
asiliyataruhusiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, zaidi ya hapo, tutaimarishahuduma za matibabu
ya kibingwa na ubingwa bobezi ilikufikia viwango vya kimataifa.
Tunataka huduma zote za afyazipatikane hapa hapa nchini, akitaka
matibabu ya dawambadala au za asili atibiwe hapa hapa, akitaka za
hospitalIatibiwe hapa hapa ili watu waje watibiwe na
ikiwezekanawatu kutoka nje waje kutibiwa hapa nchini. Kimsingi,
tayariwameanza kuja kutibiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye elimu, tutaendelea kutoaelimu ya msingi
na sekondari bila malipo; tutaongeza bajetiya mikopo kwa wanafunzi
wa elimu ya juu ili kuongeza idadiya wanufaika. Aidha, tutaendelea
kujenga na kukarabatimiundombinu ya elimu, ikiwemo shule, madarasa,
mabweni,maabara, maktaba, ofisi na nyumba za walimu, hostelipamoja
na kumbi za mihadhara. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
27
Tutahakikisha tunaendelea kuboresha elimuinayotolewa ili iweze
kutoa maarifa na ujuzi wa kutosha kwawahitimu wetu. Tutahimiza
ufundishaji wa masomo ya sayansina hisabati, hususan kwa wanafunzi
wa kike ambaotunakusudia kujenga shule moja ya sekondari kwenye
kilamkoa kwa ajili ya kufundisha masomo ya sayansi kwawasichana.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, tutaweka pia mkazo mkubwakwenye elimu ya
ufundi na katika hilo, tunalenga kuanzishavituo mahiri vya mafunzo
kwa taasisi za elimu ili kuzalishavijana wenye uwezo unaohitajika
kitaifa, kikanda nakimataifa ambapo kiasi cha Dola za Marekani
milioni 75kimepangwa kutumika. Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaamitabobea katika TEHAMA; Taasisi ya Teknolojia Mwanzaitabobea
kwenye masuala ya ngozi; Chuo cha Taifa chaUsafirishaji
kitakachobobea katika taaluma za usafiri wa angana Chuo cha Ufundi
Arusha kitabobea katika nishati jadidifu.
Kuhusu maji; mafanikio makubwa sana yamepatikanakwenye miaka
mitano iliyopita. Tumetekeleza miradi ipatayo1,422 yenye thamani ya
takribani shilingi trilioni 2.2. Hiiimefanya upatikanaji wa maji
safi na salama kuongezekakutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi kufikia
asilimia 70.1mwaka 2020 kwa vijijini na kwa mijini kutoka asilimia
74 mwaka2015 hadi asilimia 84 mwaka 2020. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata hivyo napenda nikiri kwambanilipokuwa
kwenye kampeni, moja ya changamoto kubwaniliyoelezwa na wananchi,
ilikuwa shida ya maji hususanmaeneo ya vijijini. Kwa msingi huo,
kwenye miaka mitano ijayotutajitahidi kuelekeza nguvu zaidi katika
kushughulikia sualala maji ikiwemo kuhakikisha kuwa fedha
zinazopelekwa vijijinikutekeleza miradi ya maji zinatumika vizuri.
Kwa sababu nikweli fedha nyingine zilizokuwa zinapelekwa vijijini
zilikuwahazitumiki vizuri na miradi ilikuwa haikamiliki. Nataka
kuonamiradi ya maji inayojengwa inakamilika kwa wakati na
piawatendaji wawe wabunifu na kuacha kufanya kazi kwamazoea. Mito
na maziwa yetu yatumike kikamilifu katikakuwafikishia maji wananchi
wa maeneo husika. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
28
Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo, piatutaimarisha
Mfuko wa Taifa wa Maji ili kuuongezea uwezowa kifedha wa kutekeleza
miradi ya maji. Tutakamilisha piamiradi mikubwa ikiwemo ya miji 28
itakayogharimu shilingitrilioni 1.2. Upo mradi wa maji wa kutoa
maji Ziwa Victoriaunaogharimu takribani shilingi bilioni 600 na
mradi mkubwawa maji wa Arusha wenye thamani ya shilingi bilioni
520.
Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwasihiWatanzania
kulinda vyanzo vya maji na miundombinuinayojengwa. Nitoe wito pia
kwa viongozi wote mkiwemoWaheshimiwa Wabunge, kulifanya suala la
kutunza vyanzovya maji na miundombinu yake kuwa ajenda muhimu
katikashughuli zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayotumejipanga pia
kuendelea kuimarisha na kukuza uhusianowetu na nchi mbalimbali kwa
kuzingatia sera yetu ya mamboya nje inayoweka msisitizo wa
diplomasia ya kiuchumi.Tutakuza urafiki na ujirani mwema na pia
tutashiriki kikamilifukwenye shughuli za kikanda, kibara na
kimataifa hususankwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na nimefurahi
kumwonaMbunge anayewakilisha Bunge letu la Afrika Mashariki na
piaJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja waAfrika na
Umoja wa Mataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tutaendelea pia kushirikianakwenye shughuli za
kulinda amani. Halikadhalika kwenyemiaka mitano ijayo tutaendeleza
jitihada za kukuza nakuimarisha demokrasia, kulinda uhuru na haki
ya wananchina vyombo vya habari. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata hivyo napenda kukumbushakuwa lengo la
demokrasia ni kuleta maendeleo na siyo fujo.Hakuna demokrasia isiyo
na mipaka. Aidha, uhuru na hakivinakwenda sambamba na wajibu na
hakuna uhuru au hakiisiyo na wajibu. Vyote vinakwenda sambamba.
Najuanimeeleweka vizuri. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
29
Mheshimiwa Spika, kama nilivyoahidi wakati wakipindi cha kampeni
kwenye miaka mitano ijayo tutaendeleakuboresha mazingira ya kufanya
biashara kwa wajasiriamaliwadogo yaani machinga, mama lishe,
babalishe,waendesha bodaboda, bajaji na kadhalika. Kamamnavyofahamu
kwenye miaka mitano iliyopita tulianzishautaratibu wa kutoa
vitambulisho maalum kwa wajasiriamaliwetu wadogo. Kwenye miaka
mitano ijayo tunakusudiakuviboresha vitambulisho hivyo ikiwemo
kuweka picha nataarifa nyingine muhimu, kama ilivyo kwenye
Vitambulishovya Taifa au passport. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hii itawawezeshawafanyabiashara watakaotumia
vitambulisho hivyokutambulika, ikiwemo kwenye benki na hivyo,
kupata mikopokwa ajili ya kukuza biashara zao. Hii pia
itawawezeshawafanyabiashara wetu wadogo wadogo kukua na
kutajirika.Hilo ndiyo lengo letu. Tunataka wafanyabiashara
wetuwadogo wadogo wawe wanakua na kutajirika na siyo sikuzote
wabaki kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano ijayo piatutakuza sekta ya
sanaa, michezo na utamaduni ambayoinakua kwa kasi kubwa hivi sasa.
Kama nilivyoahidi wakatiwa kampeni, tutaikuza zaidi sekta hii,
hususan kwa kuimarishausimamizi wa masuala ya hatimiliki ili
wasanii wawezekunufaika na kazi zao. Ninafarijika kuona kuna
wasanii ambaoni Wabunge miongoni mwetu humu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tutahuisha pia Mfuko waUtamaduni wa Sanaa ili
kuwasaidia wasanii wetu ikiwemokupata mafunzo na mikopo. Tutaanza
pia kutenga fedhakidogo kidogo kwa ajili ya kuziandaa timu zetu za
Taifa. Katikahilo, napenda kutumia fursa hii kuitakia heri timu
yetu ya TaifaStars kwenye mechi yao dhidi ya Tunisia baadaye leo,
pamojana mwana masumbwi wetu Hassan Mwakinyo ambaye nayeana pambano
leo. Watanzania tunataka ushindi, tumechokakushindwa shindwa.
(Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
30
Mheshimiwa Spika, kwenye miaka mitano iliyopitatumefanikiwa
kuhamishia Makao Makuu ya Serikali hapaDodoma. Viongozi, Wabunge na
watumishi wote wa Serikaliwenye kustahili kuhamia Dodoma tayari
wameshahamiaDodoma. Kwenye miaka mitano ijayo tutakamilisha ujenzi
waofisi na pia kuendelea na ujenzi wa makazi ya watumishi. Zaidiya
hapo, tutaendelea kutekeleza miradi ya miundombinuambayo tayari
nimeitaja, barabara ya njia nne, uwanja wandege wa Msalato na
kadhalika. Tutashughulikia suala laupatikanaji wa maji katika Jij i
la Dodoma. Natakaniwahakikishie Wana-Dodoma wote mkiwepo ninyi
Wabungena sisi wote na Watanzania, suala la maji tutalitatua
harakasana Dodoma. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, masuala mengine ambayotutayapa kipaumbele ni
kama ifuatavyo:-
(i) Tutafanya uendelezaji na uboreshaji wa makazi yawananchi
ambapo tutahakikisha vifaa vya ujenzivinapatikana kwa gharama nafuu
na mikopo ya ujenziinapatikana kwa riba nafuu; (Makofi)
(ii) Tutashughulikia pia masuala la mabadiliko yatabianchi;
(iii) Tutashughulikia masuala ya watu na makundimaalum wakiwemo
wazee na watu wenye ulemavu; (Makofi)
(iv) Tutaendeleza vita dhidi ya biashara haramu yadawa za
kulevya. (Makofi)
(v) Tutaimarisha sekta ya misitu na nyuki, ikiwemo kwakuanzisha
viwanda vya mazao ya nyuki ili sekta hiyo itoemchango mkubwa kwenye
uchumi wa nchi yetu.Tutahamasisha pia wafugaji wa nyuki.
(Makofi)
(vi) Tutahakikisha wamiliki wa magari wanatoamikataba kwa
madereva ili kuipa hadhi inayostahili kazi hiyona kuchochea
shughuli za huduma za usafirishaji. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
31
Mheshimiwa Spika, nilifurahi jana uliwatambulishahapa madereva
akina mama wanaoendesha malori. Nimatumaini yangu na wewe
Mheshimiwa Spika utatoa mfanosasa, utaanza kuendeshwa na dereva
mwanamke pamojana Naibu Spika. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, katika hilo suala la maderevainawezekana hata
katika Bunge hili ikatungwa sheriamahususi ya kuwalinda madereva
wetu wa nchi hii, kwasababu tutashughulikia pia kero mbalimbali za
wananchiikiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, na kadhalika.
Kwenyehili nitawaomba sana Waheshimiwa Wabunge mtusaidiesana katika
maeneo yenu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hili napenda pia kuwaagizaviongozi wa Serikali
kuanzia ngazi za vijiji, kata, tarafa, wilayana mikoa, kuhakikisha
wanatenga siku maalum ya kukutanana wananchi kwenye maeneo yao ili
kusikiliza kero zao nakuzipatia ufumbuzi. Kero nyingine ni nyepesi
sana ambazozinaweza zikatatuliwa hata katika level ya vijiji,
lakini wakatimwingine zinasubiri mpaka viongozi wa kitaifa
wanapopita.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa ujumla mambotuliyoyapanga kuyatekeleza ni
mengi sana, kweli ni mengisana, baadhi nimeyaeleza na yapo mengine
mengi ambayoyameelezwa vizuri kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM
yenyekurasa 303, lakini kwa sababu ya muda sitaweza kuyaelezayote.
Hivyo, basi nawaagiza Mawaziri nitakaowateua,pamoja na watendaji,
kuisoma vizuri ilani yetu, kuielewa nakuitafasiri vizuri ilani hiyo
katika sera na mipango kazi yautekelezaji kwenye Wizara au Taasisi
wanazoziongoza iliitakapofika mwaka 2025 tuweze kuitekeleza
kikamilifu ilanihiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, najua pia ili kuweza kutekelezavizuri ilani
yetu tutahitaji sana kupata ushirikiano kutokakwenye Bunge hili.
Kama mnavyofahamu, Bunge ni kiungomuhimu kati ya Serikali na
wananchi. Kwa hiyo, nina uhakikaendapo tutashirikiana vizuri miaka
mitano ijayo itakuwa ya
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
32
maajabu na mafanikio makubwa kwa nchi yetu. Binafsi sinashaka
kwamba Bunge hili litatoa ushirikiano wa kutosha kwaSerikali.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, napenda niwekebayana kuwa
ninaposema tunaomba ushirikiano,haimaanishi kwamba tunataka muunge
mkono kila kitu, lahasha! Penye kukosoa kosoeni, lakini kwa hoja na
kutoamapendekezo ya namna ya kushughulikia. Tunahitajiconstructive
criticism na siyo kukosoa kwa lengo la kukosoatu. Katika hilo, kwa
upande wetu Serikali tunaahidi kutoaushirikiano wa kutosha kwa
Bunge hili ili kuliwezesha kutimizamajukumu yake ipasavyo.
(Makofi)
Mheshimiwa Spika, tutatoa pia ushirikiano kwa mhimiliwa Mahakama
na nimeshukuru sana Mheshimiwa Jaji Mkuuna Majaji wengine wa
Mahakama pamoja na Jaji Mkuu waupande wa Zanzibar wote wako hapa
ili nao wawezekutimiza majukumu yao ya kusimamia haki nchini.
Kamamnavyofahamu Mahakama ni muhimu sana katika kuongozaSerikali,
ni muhimu katika kujenga maelewano katika jamii,kudumisha amani na
usalama, pia kuchochea shughuli zakiuchumi. (Makofi)
Kwa mujibu wa Katiba yetu, mimi ni sehemu ya Bungehili. Hivyo,
basi, kabla sijahitimisha hotuba yangu, napendakutumia fursa hii
kuwashukuru wageni wetu wotewalioungana nasi kwenye tukio hili. Ni
vigumu kuwataja wote,lakini pia nataka niwahakikishie Waheshimiwa
Wabunge,mimi niko pamoja nanyi na kamwe sitawaacha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, kwaunyenyekevu mkubwa,
baada ya kusema hayo, sasanatamka kwamba nimelifungua rasmi Bunge
la Kumi na Mbilila Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mungu libariki Bunge letu, Mungu abariki Wabungewote, Mungu
ibariki Tanzania.
Mheshimiwa Spika, ahsanteni sana. (Makofi)
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
33
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA, MHESHIMIWA
JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI,WAKATI WA KUFUNGUA RASMI BUNGE LA 12 LA
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA DODOMA,13 NOVEMBA, 2020 -
KAMAILIVYOWASILISHWA MEZANI
_____________
Mheshimiwa Spika;Mara ya mwisho nilipoingia kwenye Ukumbi huu
KulifungaBunge la 11, tulibahatika kuwa na Marais wetu
Wastaafuwatatu. Lakini leo, wapo wawili. Mmoja, MheshimiwaBenjamin
William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,ametangulia mbele za
haki. Hivyo basi, kabla ya kuanzahotuba yangu, nawasihi sote
tusimame tumkumbuke pamojana wabunge wote waliofariki dunia tangu
kufungwa kwaBunge la 11. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya MarehemuMzee
Mkapa pamoja na marehemu wetu wote mahali pemapeponi. Amina.
Mheshimiwa Spika;Baada ya utangulizi huo, napende niseme kwamba,
Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 91 Ibarandogo ya
kwanza imempa dhamana Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania
kulifungua rasmi Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania. Ni kwa
sababu hiyo, nimekujahapa leo kulihutubia Bunge hili kwa lengo la
kutimiza mashartihayo ya Kikatiba.
Napenda nianze kwa kumshukuru sana Mwenyezi Mungualiyetujalia
neema ya uhai na kutuwezesha kuiona siku yaleo. Aidha, nakupongeza
wewe, Mheshimiwa Job Ndugai,Mbunge wa Jimbo la Kongwa kwa
kuchaguliwa, kwa maranyingine, kuliongoza Bunge hili ukiwa Spika.
Hongera sana.Nampongeza pia Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson
kwakuchaguliwa kwa mara nyingine kuwa Naibu Spika; tenamara hii
akiwa Mbunge wa kuchaguliwa kutoka Jimbo laMbeya Mjini. Hongera
sana Mheshimiwa Dkt. Tulia. Huu niuthibitisho kwamba, nchi yetu,
kupitia Serikali inayoongozwana Chama Cha Mapinduzi, inawaamini
sana wanawake.
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
34
Kama mnavyofahamu, Makamu wetu wa Rais, MheshimiwaSamia Suluhu
Hassan, naye ni mwanamama. Aidha, Bungehili la 12 nalo lina Wabunge
wengi wanawake. Kwa msingihuo, napenda nitumie fursa hii kuahidi
kuwa, Serikalininayoingoza, itaendelea kuwaamini wanawake
katikakushika nafasi mbalimbali za uongozi. Wanawake naakinamama
Oyee!!!
Napenda pia kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wotekwa kuchaguliwa
kwenu kuwa Wabunge wa Bunge hili la12. Mmechaguliwa kwa vile
wananchi wana imani kuwa mnauwezo wa kuwawakilisha vizuri. Hivyo
basi, nawasihimsiwaangushe wananchi waliowachagua. Watanzaniawana
imani kubwa sana na Bunge hili.
Nitumie fursa hii pia kuwashukuru Waheshimiwa Wabungekwa
kuridhia na kumpitisha Mheshimiwa Kassim Majaliwakuwa Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ahsanteni sana.
Mheshimiwa Spika;Nimekuja kulizindua Bunge hili baada ya nchi
yetu kufanikiwakumaliza Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba,
2020kwa uwazi amani na utulivu mkubwa. Kwa msingi huo,napenda
nirudie kuipongeza Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzikwa kusimamia
vizuri zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu;kuanzia kwenye
uandikishaji wapiga kura; uchukuaji naurejeshaji fomu za wagombea;
usimamizi wa kampeni na piazoezi la kupiga kura na utoaji matokeo
mapema. Kwa hakika,Tume imedhihirisha uwezo mkubwa katika
kusimamiaUchaguzi bila kutegemea misaada kutoka nje.
MheshimiwaMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji
MstaafuSemistocles Kaijage; Makamu Mwenyekiti wa Tume, JajiMstaafu
Hamid Mahmoud Hamid; Makamishna wa Tume;Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Dkt. Wilson Mahera pamoja naWatendaji wote wa Tume; hongereni sana
kwa kazi nzuri.
Lakini, kwa namna ya pekee, nawapongeza kwa namnamlivyotumia
vizuri fedha mlizotengewa. Kamainavyofahamika, Uchaguzi wa Mwaka
huu uligharamiwa na
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
35
Serikali kwa asilimia 100, ambapo kiasi cha shilingi bilioni
331kilitengwa. Hata hivyo, mpaka Uchaguzi umekamilika, Tumeimetumia
shilingi bilioni 262 tu. Hii ni ishara ya uadilifu mkubwawalionao
Viongozi na Watendaji wa Tume ya Taifa yaUchaguzi. Hongereni sana.
Natoa rai kwa Taasisi nyinginekuiga mfano mzuri wa Tume hii.
Kwa moyo wa dhati kabisa, narudia kuwashukuru Viongoziwetu wa
Dini kwa kutuongoza vyema kwa sala na dua katikakipindi chote cha
Uchaguzi; na hatimaye tumeweza kumalizaUchaguzi wetu salama.
Nawasihi waendelee kuliombea Taifaletu ili libaki katika mikono ya
Mwenyezi Mungu.
Narudia pia kuvishukuru vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalamakwa
kusimamia vizuri amani na utulivu wa nchi yetu namipaka yake wakati
wote wa Uchaguzi. Hii ni ishara kuwavyombo vyetu vya ulinzi na
usalama ni imara na vinafanyakazi kwa ueledi mkubwa. Hongera sana
kwa vyombo vyetuvya ulinzi na usalama.
Kwa namna ya pekee kabisa, natoa shukrani nyingi kwaWatanzania
wenzangu wote kwa kushiriki vizuri na kuoneshautulivu mkubwa kwenye
Uchaguzi uliopita; kuanzia kwenyezoezi la uandikishaji wapiga kura,
wakati wa kampeni, upigajikura na kupokea matokeo. Hakuna shaka,
Uchaguzi waMwaka huu, kwa mara nyingine, umeuthibitishia
ulimwengukuwa sisi Watanzania ni wapenda amani,
tunajitambua,hatudanganyiki na tumekomaa kidemokrasia.
Ahsantenisana Watanzania wenzangu.
Mheshimiwa Spika;Masuala yote muhimu tuliyopanga kutekeleza
kwenye miakamitano ijayo, tumeyaweka kwenye Ilani ya Uchaguzi ya
CCMya Mwaka 2020 – 2025 ambayo ina kurasa 303. Kwa bahatinzuri,
Waheshimiwa Wabunge wengi wa Bunge hil iwanaifahamu vizuri Ilani
hiyo kwa vile wameitumia katikakuomba kura kwa wananchi kwenye
Uchaguzi Mkuuuliomalizika.
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
36
Lakini, sambamba na masuala hayo yaliyomo kwenye Ilaniyetu ya
Uchaguzi wa mwaka 2020 - 2025, tutaendelea piakutekeleza na
kusimamia mambo yote niliyoeleza wakatinikizindua Bunge la 11,
tarehe 20 Novemba, 2015.
Kama mtakavyokumbuka, kwenye Hotuba hiyo ya kuzinduaBunge la 11
nilieleza mambo mengi sana, ambayo, kimsingi,yalitoa falsafa, dira
na vipaumbele vya Serikali ya Awamuya Tano. Baadhi tumeyatekeleza
vizuri; yapo ambayohatujayatekeleza kwa ukamilifu na mengine yapo
kwenyehatua mbalimbali za utekelezaji. Kwa hiyo, kwenye miakamitano
ijayo, tutaendelea kusimamia na kutekeleza mamboyote niliyoyaeleza
kwenye Hotuba ya Kuzindua Bunge la 11.Hii ndiyo sababu nimeamua
kuigawa tena Hotuba yangu yaUzinduzi wa Bunge la 11 kwenu
Waheshimiwa Wabunge ilimkaisome na hatimaye ikawaongoze katika
kutekelezamajukumu yenu vizuri.
Hata hivyo, pamoja na hayo yote, naomba MheshimiwaSpika
uniruhusu nitaje baadhi ya mambo muhimututakayoyapa kipaumbele
kikubwa katika kipindi cha miakamitano ijayo.
Mheshimiwa Spika;Jambo la kwanza na muhimu tutakalolipa
kipaumbelekikubwa kwenye miaka mitano ijayo ni kuendelea kulindana
kudumisha tunu za Taifa letu, yaani Amani, Umoja naMshikamano,
Uhuru wa Nchi yetu, Muungano na MapinduziMatukufu ya Zanzibar. Na
katika hilo, naahidi kushirikiana kwakaribu sana na Rais mpya wa
Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Hussein Mwinyi. Kamwe, hatutakuwa na mzaha
na yeyotemwenye kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu; mwenyenia ya
kuvuruga umoja na mshikamano wetu; na pia mwenyekutaka kutishia
Uhuru wetu, Muungano pamoja na MapinduziMatukufu ya Zanzibar.
Napenda pia kutumia fursa hii kumwahidi Mheshimiwa RaisDkt.
Hussein Mwinyi kwamba, kwenye miaka mitano ijayo,Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoaushirikiano mkubwa na kufanya
kazi kwa karibu na Serikali ya
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
37
Zanzibar. Kwa kifupi, naweza kusema, tutafanya kazi kwapamoja
kwa lengo la kuleta maendeleo kwa pande zetuzote mbili za Muungano.
Na katika hilo, nampongeza sanaMheshimiwa Rais Dkt. Hussein Mwinyi
kwa hotuba nzurialiyoitoa wakati wa kuzindua Baraza la Wawakilishi.
Kwenyehotuba yake alitoa dira, mwelekeo na kutaja vipaumbelevya
Serikali ya Awamu ya Nane ya Zanzibar. Hongera sanakwa Mheshimiwa
Rais Dkt. Mwinyi kwa hotuba nzuri. KupitiaBunge hili, napenda
nimwahidi Mheshimiwa Rais Dkt. HusseinMwinyi kuwa, nitampa
ushirikiano wa kutosha katikakutekeleza yote aliyoahidi wakati wa
Uzinduzi Rasmi waBaraza la Wawakilishi.
Mheshimiwa Spika;Sambamba na kulinda na kudumisha tunu za nchi
yetu,kwenye miaka mitano ijayo, tutaendelea kuimarisha utawalabora,
hususan kwa kusimamia nidhamu kwenye utumishi waumma pamoja na
kuzidisha mapambana dhidi ya rushwa,wizi, ufisadi na ubadhirifu wa
mali za umma. Kwenye miakamitano iliyopita, tuliwachukulia hatua za
kinidhamu watumishi32,555 na kuiwezesha nchi yetu kushika nafasi ya
kwanza katiya nchi 35 za Afrika kwa kupambana na rushwa, kwa
mujibuwa Transparency International; na pia kushika nafasi ya
28kati ya nchi 136 duniani kwa matumizi mazuri ya fedha zaumma kwa
mujibu wa Utafiti Jukwaa la Dunia (WorldEconomic Forum) wa mwaka
2019.
Hata hivyo, watumishi wazembe bado wapo; wala rushwabado wapo;
na pia wezi na wabadhirifu wa mali ya ummabado wapo. Kwa hiyo,
kwenye miaka mitano ijayo,tutaendelea kushughulikia matatizo hayo.
Na kwa kifupi,niseme, utumbuaji majipu utaendelea. Hata hivyo,
kwaupande mwingine, tutaendelea kuboresha mazingira ya kazipamoja
na maslahi ya watumishi wetu wote ili yaendane nahali halisi ya
maisha ya Watanzania. Kwa hiyo, watumishiwasiwe na wasiwasi.
Waendelee kuchapa kazi.
Mheshimiwa Spika;Kwenye miaka mitano ijayo pia, tumejipanga
kuendelezajitihada za kukuza uchumi. Kama unavyofahamu, katika
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
38
kipindi cha miaka mitano iliyopita, tulijitahidi kusimamia
vizuriuchumi wetu, ambapo ulikua kwa wastani wa asilimia 7
kwamwaka. Aidha, Pato ghafi la Taifa limeongezeka kutokashilingi
trilioni 94.349 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi trilioni139.9
mwaka 2019; tulidhibiti mfumuko wa bei, kutoka asilimia6.1 mwaka
2015 hadi kufikia wastani wa asilimia 4.4 nakuongeza akiba ya fedha
ya kigeni kutoka Dola za Marekanibilioni 4.4 hadi kufikia Dola za
Marekani bilioni 5.2 mwezi Julai,2020 ambazo zinatuwezesha kununua
bidhaa na hudumakwa miezi 6.
Zaidi ya hapo, kwenye miaka mitano iliyopita, tuliongezamauzo
yetu ya nje kutoka Dola za Marekani bilioni 8.9 mwaka2015 hadi Dola
za Marekani bilioni 9.7 mwaka 2019; na piakuvutia uwekezaji wenye
thamani ya Dola za Marekani bilioni14.6, sawa na zaidi ya shilingi
trilioni 30. Aidha, tulifanikiwakupunguza umasikini wa kipato hadi
kufikia asilimia 26.4 kwatakwimu za mwaka 2017/2018. Mafanikio
haya, bila shaka,ndiyo yamewezesha, mwezi Julai 2020, nchi yetu
kutangazwakuingia kundi la nchi za uchumi wa kati kutoka kundi la
nchimasikini. Na mafanikio hayo yamepatikana miaka mitanokabla ya
muda uliopangwa, yaani mwaka 2025.
Kwa hiyo, kwenye miaka mitano ijayo tunakusudiakuendeleza
mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana natutahakikisha ukuaji uchumi
unawanufaisha wananchi,hususan kwa kuinua vipato vyao, kupunguza
umasikini natatizo la ajira. Na katika hilo, tunalenga kukuza
uchumi wetukwa wastani wa angalau asilimia 8 kwa mwaka na
piakutengeneza ajira mpya zipatazo milioni 8. Tutaendelea
piakuboresha sera zetu za uchumi jumla na sera za fedha
(yaanimacroeconomic and monetary policies), na pia
kuhakikishaviashiria vyote vya uchumi; ikiwemo thamani ya sarafu
yetu,mfumko wa bei pamoja na viwango vya riba; vinabakikwenye hali
ya utulivu.
Tutaongeza pia jitihada za kuwawezesha wananchi wetukiuchumi kwa
kuwapatia mikopo isiyo na riba ama yenyeriba nafuu, ikiwemo mikopo
ya asilimia 10 inayotolewa naHalmashauri zetu; na pia kupitia
Mifuko na Programu
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
39
mbalimbali zilizoanzishwa na Serikali, ambayo kwa idadi zipo18.
Baadhi ya Mifuko hiyo ni Mfuko wa Maendeleo ya Vijana(YDF); Mfuko
wa Maendeleo ya Wanawake (WDF); Mfuko waTaifa wa Kuendeleza
Wajasiriamali (NEDF); Mfuko wa KutoaMikopo kwa Wajasiriamali Wadogo
(SELF Microfinance Fund),Mfuko wa Kudhamini Mikopo ya Mauzo ya Nje;
Mfuko waKilimo Kwanza. n.k. Tutaimarisha usimamizi wa Mifuko hii
nakuhakikisha Watanzania wanaifahamu.
Najua Mifuko hii mingi ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu;
hivyobasi, nakuagiza Mheshimiwa Waziri Mkuu, hii ikawe kazi yakoya
kwanza kuishughulikia; ikiwezekana, mwangalieuwezekano wa
kuiunganisha baadhi ya mifuko ili ifanye kazikwa tija zaidi na
kupunguza gharama za uendeshaji. NatakaMifuko hii ikiwasaidie
wananchi wa kawaida, wakiwemomachinga, akina baba na mama lishe
pamoja nawajasiriamali wengine wadogo.
Sambamba na kutoa mikopo, tutaendelea kutekelezaProgram
mbalimbali za kukuza ujuzi na maarifa, ikiwemomaarifa ya
ujasiriamali, ili kuwapa ujuzi na uzoefu wananchiwetu
utakaowawezesha kujiajiri ama kuajirika ndani na njeya nchi.
Tutaendelea pia kutekeleza Mpango wa KunusuruKaya Masikini Awamu ya
Tatu Mzunguko wa Pili tuliouzinduamwezi Februari 2020, ambao
utagharimu takriban shilingitrilioni 2.032. Tutahakikisha fedha
hizo zinawafikia walengwa,ambao ni wananchi masikini.
Muhimu zaidi ni kwamba, katika kipindi cha miaka mitanoijayo,
sekta binafsi itapewa umuhimu wa pekee sana.Tunataka mtu yeyote
atakayetaka kuwekeza asisumbuliwekwa kuwekewa vikwazo vya aina
yoyote. Watanzania nimatajiri lakini baadhi yao wanasita kuwekeza
hapa nchinikwa kuogopa kusumbuliwa na maswali yasiyo na
msingi.Tunahitaji kuwa na Mabilionea wengi wa Kitanzania.
NatakaWatanzania wote washiriki kikamilifu katika kujenga uchumiwa
nchi yao.
Sambamba na kuwekeza, Watanzania wahamasishwekuweka fedha kwenye
Benki za hapa nchini ili kusaidia benki
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
40
zetu kufanya biashara na kuimarisha mzunguko wa fedhana
kupunguza riba kwa wakopaji. Waheshimiwa Wabungena Watanzania
mnaonisikiliza, wakati wa kufanya mambobila woga ni sasa. Kwenye
miaka mitano ijayo pia tutafunguamilango kwa sekta binafsi kufanya
majadiliano na Serikali ilikutafuta mwafaka ya migogoro ya biashara
(businessdisputes) iliyopo kwa faida ya pande zote mbili. Lengo
letu nikuona Tanzania inakuwa mahali pazuri pa kufanya
biasharaduniani. Kwenye miaka mitano iliyopita, tumefuta tozo
168,ambapo 114 zilihusu kilimo, mifugo na uvuvi na tozo nyingine54
za biashara. Tutaendelea na hatua hizo.
Mheshimiwa Spika;Mbali na hatua hizo; kwa lengo la kukuza
uchumi,kupambana na umasikini, na pia kukabiliana na tatizo
laukosefu wa ajira, tunakusudia, kwenye miaka mitano ijayo,kuweka
mkazo mkubwa katika kukuza sekta zetu kuu zauchumi na uzalishaji,
hususan kilimo, ufugaji, uvuvi, viwanda,madini, biashara na utalii.
Sekta hizi ndizo zenye kuajiriWatanzania wengi. Kwa hiyo, ni wazi,
tukifanikiwa kuzikuza,uchumi wetu utakua kwa kasi na hivyo
kupunguza matatizoya umasikini na ukosefu wa ajira nchini.
Kwa msingi huo, kwenye KILIMO, mathalan, tunakusudiakuongeza
tija na kukifanya kilimo chetu kuwa cha kibiashara.Lengo ni
kujihakikishia usalama wa chakula, upatikanaji wamalighafi za
viwandani na pia kupata ziada ya kuuza nje. Ilikufanikisha hayo,
tutahakikisha pembejeo na zana bora zakilimo, ikiwemo mbegu,
mbolea, viatilifu/dawa na matrekta,vinapatikana kwa uhakika na kwa
gharama nafuu.Tutaongeza pia eneo la umwagiliaji kutoka hekta
561,383 hadihekta milioni 1.2 mwaka 2025 ili kupunguza utegemezi
kwenyemvua.
Tutaimarisha mifumo ya upatikanaji wa mitaji kwa wakulimawadogo
na wawekezaji kwa kushirikisha taasisi za fedha,ikiwemo Benki yetu
ya Maendeleo ya Kilimo pamoja na benkinyingine. Tutashughulikia pia
tatizo la upotevu wa mazao(yaani post harvest loss), ikiwemo kwa
kukamilisha ujenzi wavihenge na maghala maeneo mbalimabli nchini
ambayo
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
41
yataongeza uwezo wetu wa kuhifadhi mazao kutoka tani190,000 za
sasa hadi tani 501,000. Takwimu zinaonesha kuwa,kila mwaka, nchi
yetu inapoteza wastani wa kati ya asilimia30 - 40 ya mavuno yake
kwa sababu mbalimbali, ikiwemokukosekana kwa miundombinu ya
kuhifadhi. Zaidi ya hapo,tunakusudia kuanzisha bidhaa mbalimbali za
huduma yaBima ya Kilimo na pia kuingia makubaliano ya kibiashara
nanchi walaji na wanunuzi wa mazao ili kupata soko la uhakika.
Mazao ya kimkakati tunayolenga kuyapa kipaumbelekikubwa ni
pamba, korosho, chai, kahawa, tumbaku,mkonge, michikichi, cocoa,
alizeti na miwa; lakini pia mazaoya chakula. Nchi yetu kila mwaka
inaagiza tani 800,000 zangano na kwa ujumla, tunatumia wastani wa
shilingi trilioni1.3 kuagiza chakula kutoka nje. Hii ni aibu kwa
nchi kamaTanzania. Hivyo basi, ni lazima tutafute majawabu ya
sualahili. Na hii ndiyo ikawe kazi ya kwanza ya Waziri wa
Kilimonitakayemteua.
Lakini, zaidi ya hapo, tutaweka mkazo mkubwa kwenye kilimocha
mazao ya bustani (matunda, mbogamboga, maua naviungo), ambacho
kinakua kwa kasi kubwa nchini. Hivi sasanchi yetu inashika nafasi
ya 20 kwa kuzalisha kwa wingi mazaohayo duniani na mauzo yetu ya
nje yameongezeka kutokaDola za Marekani milioni 412 mwaka 2015 hadi
kufikia Dolaza Marekani milioni 779 mwaka 2018/2019. Hii ndiyo
sababu,hatuna budi kukiendeleza kilimo cha mazao hayo. Na
katikahilo, napenda kuriafu Bunge hili Tukufu kuwa, kwenye
miakamitano ijayo, tunakusudia kununua ndege moja ya mizigo
ilikurahisisha uzafirishaji wa mazao ya bustani, lakini pia
minofuya samaki pamoja na nyama. Wakulima wetu ni lazimawatajirike
na shughuli wanazozifanya; hivyo basi, Mawaziriwa Kilimo, Biashara,
Mambo ya Nje na Mabalozi wajipangevizuri katika hili.
Kwa upande wa MIFUGO, kama mnavyofahamu, nchi yetuinashika
nafasi ya pili kwa wingi wa mifugo Barani Afrika. Tunang’ombe
milioni 33.4; mbuzi milioni 21.3; kondoo milioni 5.65;punda
657,389; lakini pia tuna idadi kubwa ya kuku, bata,
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
42
kanga, n.k. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, sekta hii
badohaijatunufaisha vya kutosha.
Kwa kuzingatia hilo, kwenye miaka mitano ijayo,
tunakusudiakuikuza sekta ya mifugo ili ichangie ukuaji uchumi
nakupunguza matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira
nchini.Tutaongeza maeneo ya ufugaji kutoka hekta 2,788,901 zasasa
hadi hekta 6,000,000. Tunataka wafugaji wasiteswe namifugo yao.
Mifugo ni utajir i. Sambamba na hayo,tutahamasisha ufugaji wa
kisasa; tutaongeza vituo vyakuzalisha mbegu bora na pia kuongeza
uzalishaji wa chakulacha mifugo viwandani kutoka tani 900,000 hadi
tani milioni 8.
Zaidi ya hapo, tutakamilisha ujenzi wa machinjio sabaunaoendelea
maeneo mbalimbali nchini, ambapo, kwapamoja, zitakuwa na uwezo wa
kuchinja ng’ombe 6700 nambuzi 11,000 kwa siku. Ujenzi wa machinjio
hizo sio tu utasaidiakupatikana kwa nyama bora itakayouzwa hadi
kwenyemasoko ya kimataifa bali pia utawezesha upatikanaji wangozi
bora kwa ajili ya kutengeneza bidhaa za ngozi. Takwimuzinaonesha
kuwa, takriban asilimia 90 ya ngozi inayozalishwanchini kwa sasa
haina ubora unaohitajika; na sababumojawapo ni uchinjaji wanyama
kienyeji. Kwa hiyo, machinjioyanayojengwa yatapunguza tatizo
hilo.
Nitumie fursa hii, kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza
kwenyeviwanda vya kutengeneza bidhaa za mifugo (nyama,
ngozi,maziwa, kwato, n.k.). Na katika hilo, tunaahidi kutoa
vivutiomaalum kwa watakaowekeza kwenye viwanda hivyoambavyo
vitasaidia kuinua vipato vya wafugaji wetu na piakuongeza fursa za
ajira kwa Watanzania. Na hapa, natakaniweke bayana kuwa, watendaji
watakaokwamisha ujenziwa viwanda hivyo tutawashughulikia.
Mheshimiwa Spika;Nchi yetu pia imebarikiwa kuwa na maeneo
mengiyanayofaa kwa shughuli za uvuvi, ikiwemo Ukanda wa
Pwani,Maziwa, mito na mabwawa. Hali hii inafanya sekta hii kuwana
nafasi ya kutoa mchango mkubwa kwenye kukuza Patola Taifa na pia
kupambana na umasikini na tatizo la ajira.
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
43
Hata hivyo, kwa sasa, mchango wake bado ni mdogo. Hivyobasi,
kwenye miaka mitano ijayo tunakusudia kuikuza sektahii, ikiwemo
kuimarisha shughuli za uvuvi kwenye Bahari Kuu,ambako tumekuwa
tukipoteza mapato mengi.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Kamati ya Bunge kuhusu Shughuliza Uvuvi
wa Bahari Kuu ya Mwaka 2018; shughuli za uvuvikwenye Bahari Kuu
zinaweza kuingizia Serikali mapato yamoja kwa moja ya takriban
shilingi bilioni 352.1 kwa mwakaendapo mifumo ya usimamizi na
udhibiti ingekuwa imara nasamaki wangechakatwa hapa nchini. Hata
hivyo, mapatoyaliyokuwa yamekusanywa kwa kipindi cha miaka tisa
(2009hadi 2017) yalikuwa shilingi bilioni 29.79, sawa na shilingi
bilioni3.3 kwa mwaka. Kiwango hiki cha mapato hakikubaliki.
Hii ndiyo sababu, tunataka, kwenye miaka mitano ijayo,kuisimamia
vizuri shughuli za uvuvi wa Bahari Kuu ili Taifa letulinufaike na
rasilimali zake, kwa kuhusisha sekta binafsi. Kwabahati nzuri,
tayari, mwaka huu (2020) tumetunga SheriaMpya ya Kusimamia na
Kuendeleza ya Uvuvi wa Bahari Kuu.Aidha, tumepanga kununua Meli 8
za Uvuvi kwa kushirikianana Shirika IFAD (4 upande wa Zanzibar na 4
upande waTanzania Bara) ili zishiriki katika uvuvi wa Bahari Kuu.
Kamamnavyofahamu, suala la uvuvi wa bahari kuu ni la
Muungano.Tunakusudia pia kujenga Bandari kubwa ya Uvuvi
itakayotoaajira zipatazo 30,000; na tutaendelea kuihamasisha
sektabinafsi kujenga viwanda vya kuchakata samaki.
Sambamba na kusimamia Bahari Kuu, tutakuza shughuli zauvuvi
kwenye Maziwa yetu Makuu (Victoria, Tanganyika naNyasa) pamoja na
Mito yetu mikubwa. Tutahamasisha wavuviwetu wadogo kujiunga kwenye
vikundi ili tuweze kuwapatiamitaji, ujuzi, vifaa na zana za uvuvi;
na halikadhalika tutapitiaupya tozo na maeneo mbalimbali ili
kuwapunguzia wavuvikero na kuvutia uwekezaji. Tutahamasisha pia
watu binafsikujenga mabwawa na kufuga kisasa kwa kutumia
vizimba.Sekta ya uvuvi ni lazima itoe mchango mkubwa kwenyeuchumi
wa nchi yetu. Wateule wote wa sekta hii ni lazimawalisimamie
hili.
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
44
Mheshimiwa Spika;Ni ndoto kufikiria kwamba utaweza kukuza uchumi
aukupambana na umasikini pamoja na tatizo la ukosefu waajira bila
kuelekeza nguvu katika kukuza sekta ya viwanda.Duniani kote, sekta
ya viwanda ndiyo mhimili mkuu wa kukuzauchumi, kupambana na
umasikini pamoja na matatizo yaajira. Kwenye miaka mitano
iliyopita, tulifanikiwa kujengaviwanda vipya takriban 8,477 ambavyo
vilitengeneza ajirazipatazo 480,000, ambapo Mkoa wa Pwani uliongoza
kwakujenga viwanda vingi. Naupongeza sana uongozi wa Mkoawa
Pwani.
Hivyo basi, kwenye miaka mitano ijayo, tutaendeleza jitihadaza
kukuza sekta hiyo. Mkazo mkubwa tutauweka kwenyeviwanda vyenye
kutumia malighafi zinazopatikana kwa wingihapa nchini (mazao ya
kilimo, mifugo na uvuvi); vyenye kuajiriwatu wengi; na ambavyo
bidhaa zake zinatumika kwa wingihapa nchini (nguo, bidhaa za ngozi,
mafuta ya kula, sukari,saruji, n.k.).
Ili kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya viwanda,
tutaendeleakuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji,
ikiwemokuangalia masuala ya kodi na kuondoa vikwazo na
urasimu.Pamekuwepo na urasimu mwingi na kusumbuliwa kwawawekezaji
kwa kuzungushwa zungushwa na hivyokuwafanya wakate tamaa. Mimi
nataka mwekezaji mwenyefedha akija apate kibali ndani ya siku 14.
Kwa sababu hiyo,nimeamua suala la uwekezaji ikiwa ni pamoja na
Kituo chaUwekezaji Tanzania (TIC) kulihamisha kutoka Ofisi ya
WaziriMkuu kwenda Ofisi ya Rais i l i hao wanaokwamishanikapambane
nao mimi mwenyewe. Lakini, zaidi ya hapo,tumepanga kujenga Ukanda
na Kongani (clusters) zaviwanda kila mkoa kulingana na mazao na
maliasilizinazopatikana.
Mheshimiwa Spika;Kwenye miaka mitano il iyopita tumepata
mafanikiomakubwa kwenye sekta ya madini. Mapato yameongezekakutoka
shilingi bilioni 168 mwaka 2014/2015 hadi shilingi bilioni527 mwaka
2019/2020. Mchango wa sekta ya madini kwenye
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
45
Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3.4 mwaka 2015hadi
kufikia asilimia 5.2 mwaka 2019. Zaidi ya hapo, kwa maraya kwanza,
katika historia ya nchi yetu, mwaka 2019, sektaya madini iliongoza
kwa kutuingizia fedha nyingi za kigeni,Dola za Marekani bilioni
2.7. Nitumie fursa hii kulipongezaBunge la 11 kwa kutoa mchango
mkubwa katika kupatikanakwa mafanikio haya.
Nina imani kuwa Bunge hili la 12 litafuata nyayo za Bunge la11.
Na katika hili, napenda niliarifu Bunge hili Tukufu kuwa,kwenye
miaka mitano ijayo, tutaendelea kuimarisha ulinzi nausimamizi wa
madini yetu, (kama tulivyofanya kwa kujengaUkuta Mirerani) kwa
kuimarisha Sheria zetu ili madini yetuyasitoroshwe na Serikali
kukoseshwa mapato. Aidha,tunakusudia kuendelea kufanya majadiliano
na wawekezajiwakubwa kwa kuzingatia mfano wa
Makubalianoyaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya
Barrickyaliyowezesha kuundwa kwa Kampuni ya Twiga
MineralsCorporation.
Nchi yetu imebarikiwa kuwa na madini mbalimbali, ikiwemodhahabu,
almasi, Tanzanite, chuma, bati, nickel, copper, n.k.Aidha, tuna
gesi aina mbalimbali, kama vile ethane, helium,ambayo hivi karibuni
zimepatikana futi za ujazo bilioni 138kwenye Ziwa Rukwa, ambazo
zinaweza kuhudumia duniakwa miaka 20. Hii ndiyo sababu, kila siku
nimekuwa nikisema,sisi sio masikini; sisi ni matajiri. Nchi yetu ni
tajiri sana.
Lakini, kuhusu madini pia, kwenye miaka mitano ijayo
piatutaendelea kuliimarisha Shirika letu la Taifa la
Madini(STAMICO) ili lishiriki kikamilifu kwenye shughuli za
madini;kuwawezesha wachimbaji wetu wadogo, ikiwa ni pamojana
kuwatengea maeneo ya uchimbaji, kuwapatia mafunzo,mikopo pamoja na
vifaa. Na katika natambua kuwa, wapobaadhi ya watu wamepewa leseni
za utafiti na uchimbajilakini hawajazifanyia kazi; tutazifuta
leseni zao, na maeneohayo kuyagawa kwa wachimbaji wengine,
hususanwachimbaji wadogo. Wachimbaji wadogo ni muhimu sanakatika
kukuza sekta ya madini.
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
46
Tutaendelea pia kuimarisha masoko ya madini pamoja nakuhamasisha
ujenzi wa viwanda vya uchenjuaji, uyeyushaji,usafishaji na
utengenezaji wa bidhaa za madini. Tunatakamadini yachimbwe hapa
Tanzania, yachenjuliwe,yayeyushwe na kisha bidhaa za bidhaa za
madinizitengenezwe hapa hapa Tanzania; na ndipo ziuzwe nje amawatu
kutoka nje waje kununua bidhaa za madini hapa nchini.Ni imani yetu
kuwa, kutokana na hatua tulizopangakuzichukua sekta ya madini
itaweza kuchangia angalauasilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka
2025.
Mheshimiwa Spika;Utalii ni sekta nyingine ambayo tutaipa mkazo
mkubwakwenye miaka mitano ijayo. Sekta hii imeajiri takriban
watumilioni 4. Kwenye miaka mitano iliyopita, ilikua kwa kiwangocha
kuridhisha, ambapo idadi ya watalii waliotembeleanchini iliongezeka
kutoka watalii 1,137,182 mwaka 2015 hadiwatalii 1,510,151 mwaka
2019. Mapato nayo yaliongezekakutoka Dola za Marekani bilioni 1.9
mwaka 2015 hadi kufikiaDola za Marekani bilioni 2.6 mwaka 2019.
Nitumie fursa hiikuipongeza Hifadhi yetu ya Taifa ya Serengeti
kwakuchaguliwa kuwa Hifadhi Bora Barani Afrika kwa mwaka2020.
Kwenye miaka mitano ijayo, tumejipanga kuongeza idadi yawatalii
hadi kufikia milioni 5 mwaka 2025 na mapato kutokaDola za Marekani
bilioni 2.6 za sasa hadi Dola za Marekanibilioni 6. Hatua
tutakazochukua ni pamoja na kupanua wigowa vivutio vya utalii,
ikiwemo kukuza utalii wa mikutano nauwindaji wanyamapori;
kuimarisha utalii wa fukwe; kujengamiundombinu ya kuwezesha meli za
utalii kuzuru nchini nakuongeza kasi ya utangazaji wa vivutio
vyetu.
Vilevile, tutazihamaisha taasisi na watu binafsi
kuanzisharanchi, mashamba na bustani za wanyama, kamainavyofanyika
nchi nyingine; ili kuzuia ujangili na kukuza utalii;lakini pia
kuongeza vipato na fursa za ajira kwa Watanzania.Na katika hilo,
napenda kuwaarifu Watanzania, kupitia Bungehili Tukufu kuwa,
tumepunguza bei kwa ajili ya kupatawanyama wa mbegu. Mathalan, bei
ya nyati wa mbegu
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
47
imepungua kutoka Dola za Marekani 1,900 hadi kufikia
shilingilaki mbili; Pofu kutoka Dola za Marekani 1,700 hadi
shilingi310,000 na Swala kutoka Dola za Marekani 150 hadi
shilingi90,000. Hivyo basi, nawasihi Watanzania wenzangu,
popotewalipo, kuchangamkia fursa hiyo; ambayo itachochea
piauanzishaji wa butcher za wanyama pori.
Zaidi ya hapo, tutaendelea kupitia upya kodi na tozombalimbali
ili kuzifuta ama kupunguza kodi zenye kero.Kwenye miaka mitano
iliyopita, tulipunguza ada ya leseni yabiashara ya utalii kwa
wakala wa kusafirisha watalii yenyeidadi ya magari chini ya manne
kutoka Dola za Kimarekani2,000 hadi Dola za Marekani 500 na matokeo
yake idadi yakampuni za Kitanzania zimeongezeka kutoka 643 mwaka
2015hadi 1,687 mwaka 2020.
Mheshimiwa Spika;Tuna imani, hatua hizi nilizoeleza
zitatuwezesha kufikiamalengo tuliyojiwekea ya kukuza uchumi kwa
angalauasilimia 8 kwa mwaka, kuinua vipato vya Watanzania,kupunguza
umasikini na kutengeneza ajira mpya milioni 8.Hata hivyo, najua,
ili kufikia malengo haya, tunategemeasana kupata ushirikiano kutoka
sekta binafsi. Kamamnavyofahamu, sekta binafsi ndiyo injini ya
kujenga uchumiwa kisasa.
Hivyo basi, narudia kuikaribisha sekta binafsi ya hapa nchinina
kutoka nje kuwekeza katika sekta nilizozitaja; na ambazosikuzitaja.
Na napenda niwahakikishie watu wa sekta binafsikuwa, Tanzania ni
mahali pazuri na sahihi pa kuwekeza. Nchiyetu ina amani na utulivu;
tumebarikiwa kuwa na fursa nyingiza uwekezaji; nchi yetu ipo kwenye
eneo la kimkatati; sisi piani Wanachama wa jumuiya mbili, EAC na
SADC, ambazo zinasoko la watu takriban milioni 500.
Kwa hiyo narudia, kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza
hapanchini. Na kwa bahati nzuri, tangu mwaka jana,
tumeanzakutetekeleza Mpango wetu wa Kuboresha Mazingira yaBiashara
nchini (yaani Blueprint for Regulatory Reforms toImprove the
Business Environment in Tanzania). Hivyo basi,
-
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)
48
mazingira ya biashara na uwekezaji, kwenye miaka mitanoijayo,
yanatarajiwa kuwa bora zaidi.
Mheshimiwa Spika;Ili kukuza uchumi pamoja na sekta za uzalishaji
ni lazimatuimarishe miundombinu, hususan ya usafiri na nishati
yaumeme. Kamwe, huwezi kukuza sekta za kilimo, ufugaji,
uvuvi,viwanda, uchimbaji madini na utali i bila
kuimarishamiundombinu na huduma za usafiri pamoja na upatikanajiwa
huduma za umeme. Kwa hiyo, kama ilivyokuwa kwenyemiak