-
Mwongozo wa choo cha VetivaVile mtu yeyote anaweza unda na
kutumia choo chake wakati wowote kwa kutumia
nayasi ya vetiva.
Matumizi ya nyasi ya vetiva yachukuliwa pahala pa utumiaji wa
choo cha kuchimbiwa,huleta ufaraga/ficha siri na kuifanya choo cha
watu/usaha kuumbuka kwa haraka.Nyasi kwa jina jiji vilivile
zinaweza tumiwa katika mahali penye baridi au ukali wa mazingira
ambapo vetiva hazikui.
Utafsiri wa hivi punde wa mwongozo huu unaweza patikana
kwa:http://www.healthy-mind-body.com/humanitarian/vetiver_latrine.html
1
http://www.healthy-mind-body.com/humanitarian/vetiver_latrine.html
-
Umuhimu: Sio ghali kama vyoo vya kawaida (ni dola 25-50)
ishirini na tano hadi hamsini badala ya (dola
mia tano (500). Hupatikana kirahisi kuliko choo cha
miinuko,mwangaza na ufaraga unaweza ongezwa
kulingana na mahitaji. Huweza kujengwa kwa urahizi hata katika
mashinani. Mizizi ya nyazi ya vetiva huongezea nguvu ukuta wa choo
Mzingi wake wa saruji huweza kubebwa na kutumiwa pahali pengine
ikiwa choo kimejaa. Nyazi za vetiva huleta mandhari ya siri maluum
na vilevile vinaweza katwa kwa matumizi
mengine kama(Kuwakisha moto,chakula cha mifugo,kuunda
mbolea,kuunda vikapu,kuezeka nyumba,kutumiwa kwenye ujenzi wa
kuta…nakadhalika).
Mizizi ya vetiva hunyonya na kusaidia kwenye uozo wa taka za
choo hivyo kupunguza uchafufuzi wa mazingira.
Hujengwa kwa urahizi kwa hivyo yeyote mwenye mahitaji hayo
anaweza jijengea. Hujisafisha na kujikarabati yenyewe,msingi wake
hukubalia maji ya mvua kuingia kwa shimo
hivyo basi kuosha na vile vile kurutubisha mizizi ya nyasi kuota
tena.
Udhaifu Wake: Nyasi hizi zinamahitaji ambazo ni lazima
zitimizwe: 1)Unyunyizaji wa maji ikiwa nyasi
zimepandwa wakati wa kiangazi; 2)Mahali amabapo haina jua sana;
3)Kuzuia wanyama wasiharibu hadi zitakapokuwa timamu.
Vetiva huchukua takribani msimu 1-2 (Mmoja hadi miwili) ya
upanzi kukomaa na kutumiwa vilivyo.
Sheria ya usafi wa uma zinaweza zuia utumiaji wa choo cha
vetva.
Nyasi ya vetiva huzuia mmomonyoko hata katikahali mbaya.Picha
hii huonyesha jinsi nyasi hii
inavyoshika udongo kwa nguvu wakati wammonyoko na kando yake
ambapo hapana nyasi
hizi humomonyoka na kusombwa.
Mzizi ya vetiva huwa na mashiko yanguvu mchangani kwa vile
huenda futi 4-5
(nne hadi tano) chini ya ardhi.Picha hiihuonyesha kiwambo cha
vetiva (matawi na
kati ishakatwa) baada ya kungolewa nawatu watatu kwa kutumia
jembe na mbao
kuinulia.
2
-
Pahali Pa UjenziVipengele vinne muhimu kizingatiwa wakati wa
ujenzi wa choo cha vetiva.
1. Jua: Vetiva hupenda jua kwa kipimo kila siku.Ikiwa eneo hilo
lina kichaka basi muhimu kufweka/kukata matawi mengineyo.
2. Uchafuzi: Ni vyema uchafu wa choo kubaki salama kwenye
shimo.Uangalifu hutakakikana ili uchafu huo usipate upenyu na
kuingia katika maji masafi ya kunywa au kwenye mito.Vyoo hivi
vinafaavijengewe upande wa chini wa bonde mbali na miito na
chemichemi za maji.Vyoo unafaa view mita 30kutoka kwenye vianzo vya
maji.Vyoo vile vile vinafaa view mita 2 kutoka ardhini kuinuka
juu.Hii inazuia upenyu wa uchafu majini wakati wa mvua
nyingi/gharika.
3. Utumiaji Wa Karibu: Choo lazima kiwe karibu na makao ya
familia ili hata mtu mgonjwa aweze kukifikia hata kama ni
usiku,lakini mbali kidogo ili nzi wasiweze kusafirisha uchafu
nyumbani.Kiuweka choo mita sita (6) mabli na nyumba ni masafa
unaokubalika kikamilifu.
4. Ushawazishaji: Ushawazishaji wa msingi wa choo hutakikana
timamu.
3
-
UsafiMagonjwa mengine husabishiwa na viini vinavyoishi kwenya
kinyaa na huweza kusambazwa kupitia midomoni.Njia za kawaida za
usambazaji,nzi,mikononi na chakula.Mseto wa utumiaji wa safi,vyoo
vilivyojengwa vizuri na kunvya mikono vizuri huweza kuzuia
uambukizaji na kundeleza afya nzuri.
Ujenzi Wa Choo Cha Kuchimbwa
Pahali: Chimbe choo chako kwenye sehemu thabiti huku pande zake
mbili ziwe umbo la mstatili ili ipunguze uwezekano wa
kuporomoka.Umbo lake kwenda chini na upande huweza
tofautiana.Jedwali la hapo chini linaweza kutuonyesha jinsi uteuzi
muhimu hutekelezwa.Ikiwa msingi wa choo utasafirishwa kutoka mahali
moja hadi nyingine basi msingi huo uwe wa mdwara utafaa zaidi.Ikiwa
choo hicho kitadumu mahala pake hapo,basi mtindo wa mraba
utatumiwa/unafaa zaidi.Msingi hiyo miwili husaidianyasi ya vetiva
kua vyema na kuongezea nguvu choo chake.
4
-
Round Square
Umuhimu:1) Choo chenye udwara huwa na kuta zenye
nguvu tele. Vitu2) Vifaa vichache tu vitahitajika kuunda
slabi
yake.3) Slabi hiyo vilevile huwa rahisi kuhamisha
kwani huweza kubingirishwa kwa haraka.
Umuhimu:1) Choo kama hiki huwa na maisha marefu ya
utumizi kuliko cha mstatitili.2) Na pia slabi yake huwa rahizi
kujenga.
Udhaifu Wake:1) Slabi ya mraba huwa ngumu kutengeza.2) Slabi
dwari ni nypesi kushinda ya mraba.
Udhaifu Wake:1) Slabi ya mraba huwa ngumu kuhamisha
kwani zingine huwa na uzito wa kilo 200.2) Vifaa vingi hutumika
katika ujenzi wake na
kwa hivyo ni ghali.3) Choo cha mraba pia haidumu sana.
Urefu na upana was shimo huweza badilishwa kulingana na
mahitaji.Shimo yenye upana wa mita 1 na mita 2.3 kwa kina huweza
kutumiwa na familia ya watu sita kwa muda wa miaka mitano.Ikiwa
upana wa shimo itabadilishwa,lazima kiwango cha msingi wake
kubatilishwa pia.Sakafu yake yapasa kuwa sentimita 20 pana kuliko
shimo yenyewe. Usajili huu hutumiwa kwa ongezeko la ½(nusu mita) ya
shimo ambalo hujazwa kwa mchanga ukimalizwa.Hii hufanywa ili kuzuia
uchafuzi wa mchanga.Ili kujua vyema urefu wa matumizi ya choo
chako,kadiria matumizi hivi kwamba kila mja/mtu hutumia kiwango
upana wa kiubika 0.6 kila mwaka.Hilo litaongezeka mpaka kubiki 0.1
ikiwa watumizi wa choo hizo watajisafisha kwa kutumia bidhaa ghusi
kama mabaki ya mahindi na mawe.Hesabu hii ni ya choo cha
kawaida.Hata hivyo choo cha vetiva kinaweza dumu zaidi kwani mizizi
yake huozesha chemichemi hizo.Utafiti unaonyesha kuwa choo chenyw
kimo cha 1.2 huweza kudumu kwa muda wa karibu mwaka.
Kukadiria Utumishi Wa Choo
Matarajio ya matumizi: watu watu 6*0.06 kiubiki mita *miaka
5=1.8 kubiki mita
Matumizi ya choo: Mita 1*mita 1*1.8 mita (2.3 mita-0.5 mita)=1.8
kubiki mita
Ikiwa upana wa choo itabadilishwa,huna budi pia kubadilisha
kiwango cha slabi na nguzo zake.Slabi iwe sentimita 20 kuzidi upand
wa shimo,na nguzo za choo pia ziwe sentimita 70 zaidi ya shimo.
Sakafu Ya Choo:Sakafu ya choo huweza kuundwa kwa: Mchanga vipimo
vitatu,kokoto vipimo vitatu,saruji mfuko moja.Bidhaa hivi vinaweza
kupatikana mashinani.Kokoto iwe saisi ndogo,mchanga isiwe na uchafu
na mawe.Aina ya waya ya meshi hutumika kutenganisha mchanga na
uchafu.Mkorogo huu huweza kubadilishwa kulingana na maeneo na pia
uwepo wa bidhaa hizi mashinani.Kwa mfano unaweza kuwa na mkorogo wa
mchanga vipimo viwili,kokoto vipimo vine na saruji moja.Pia
unakubaliwa vipimo vine vya mchanga, vipimo viwili vya kokoto na
mfuko moja wa saruji.Mikorogo
5
-
kama huu huongezewa maji kulingana na matumizi.Kadiria ndoo tatu
za maji na vile vile katika usafishaji wa vyombo vya kazi.Slabi hii
na nguzo zinaweza undwa kwa umbo mbalimbali kwa kutumia miti
iliyowekwa sakafuni.Kazaslabi hii kwa kutumia nguzo 3/8 vile
ilivyochorwa kwenye mchoro wa picha.Ukimaliza nguzo hizo za nyaya
hukunjwa vyema ndani ya slabi ili pasiwe na chuma/waya yoyote
nje.Kabla ya kuumwaga mkorogo wa saruji,mawe ndogo ndogo zinaweza
kutumiwa katika kuinua nguzo yenyewe pahali pake.Shimo ya choo
utengenezwa kwa kuta na kuubana kwa jiwe ama chombo cha
plastiki.Shimo lenyewe isiwekubwa wa sentimita 25 pande zote.Kipimo
hiki huhakikishia hata motto mdogo usalama wake.Ondoa kifuniko cha
sakafu baada ya masaa matatu,hata hivyo unaweza kutandazia maganda
ya miti,mchanga,karatasi ya plastiki juu ili kuufanya saruji ukauke
polepole.Ijapokuwa wajenzi wengine hutumia sakafu hii baada ya siku
6,slabi dhabiti huachwa hadi siku 21.Baada ya udhabiti wa
slabi,unaweza hamishwa kufunikia shimo ya choo na kuekeza mawe
kando kando kote ili choo chako kisiporomoke chini.Ikiwa unahitaji
kiti cha choo,basi unaweza tumia saruji pamoja na tafali au
mti.Hakikisha kuwa shimo ya choo imefunikwa kila wakati kuzuia nzi
wasiingie.Kifuniko cha choo kinaseza tengenezwa kwa kutumia mbao
lakini mtindo huu haidumu kama ya saruji.Ni muhimu kifuniko hiki
kifungwe na kufunguliwa kwa kutumia mguu,hii huzuia uasambazaji na
uchafuzi wa mikono.Miti isiyooza kwa haraka ama bamboo inaweza
tumika kutengeneza slabi.Miti hii huchongwa sambamba halafu mkorogo
wa saruji kutandazwa juu yake.Mbinu hii si ghali kutengeneza lakini
haidumu kuliko saruji na vilevile haiwezi kuhamishwa kwingine kwa
matumizi.
Vifaa vya ujenzi wa slabi-vifaa vya kutumiwa tena
Miti 4,sentita 5*sentimita 10(2*4s) kila moja mita 1.2 ambao
hutumiwa kujengea slabi ya saruji.Glasi moja nyepesi wa sentimita
6.3,urefu wake 377 sentimita kwa utunzi wa slabi.Miti mitatu(3),
sentimita 5*10(2*4s) kila mita 1.8 kusaidia kwenye nguzo.Mbao nne
za vipimo 5 kwa 10 sentimita (2*4) kwa 40*30 sentimitaGlasi ndogo
moja ya kipimo cha 6.3 sentimita kuwekewa slabi.Mbao moja
kilichokatwa kwa mfano wa kitumbuo cha ufunguo kwa slabi.Ikiwa
hakipatikani basin doo ndogo cha kipimo cha sentimita 25 huweza
kutika.Kijiko cha saruji na shepeo hutumiwa kwa saruji.Vifaa vya
usafishaji kama vile plastiki wa kuzuia uchafu kwenye
saruji.Msumeno wa kukata vyuma.Jembe ndogo,shepeo na vyuma vya
uchimbajiVisikiki kama msumari,nyundo na kisebusebu hutajika
Orodha ya vifaa- vinavyotumika mara moja tu
Nyasi za vetiva hamsini ( vetiva vidogovidogo)Vyuma/ vidhibiti
viwili vya vipimo vya 9.5 milimitaSaruji mfuko moja wa uzani wa
kilo 50Ndoo tatu za maji (kutumiwa kukoroga na usafishaji wa
vyombo)Ndoo tatu za mchangaNdoo tatu za kokoto
6
-
Choo nzuri chenye ukuta sambamba. Tumia mguu wala sio mkono kwa
kuufungwakifuniko cha choo.
Utengenezaji wa slabi kwa kutumia vindoo na mbao.Ndoo hii ni
kubwa sana,ni kama sentimita 30badala ya sentimita 25.
7
-
8
-
9
-
10
-
Jinsi Ya Kupanda Vetiva
Panda nyasi hii sentimeta 10-15 kwenye mistari tatu
zinazofuatana kuzunguka choo chako.Mistari hiyoiwe sentimeta 30-40
kutoka moja hadi nyingine.Acha sehemu ndoo cha kuingia/kama
mlango.Kutoka katika ukuta wa choo ,acha sentimeta 30 kabla ya
kupanda nyasi hii,kwani kufanya hivyo itafanya mizizi yake kushika
chini vizuri.Panga ununuzi wa vetva 50 ikiwa utafwata muundo huu.Ni
vizuri kupanda wakati wa vua ili kuepuka unyunyuzaji maji.Maji taka
za nyumba huweza kutumiwa katika shnguli hii.Tumia mbolea kwenye
upanzi wako.Ikiwa kuna kiangazi unaweza ongezea nyasi
zingine,matawi maganda na mbao kuwa vizuizi vya jua.Pia unafaa
kuchunga wanyama wasiharibu vetva wakati huo hadi labda baada ya
miezi (4-6).
Vetiver latrine with newly planted slips, notice that the slips
are planted right next to the slab and will not interfere with the
slab as the roots grow down vertically and not horizontally.
Utunzi Wa VetivaKwa msimu wa mwaka moja vetiva zitakua kwa
pamoja na kuunda kichaka .Nyasi hizi zinaweza katwakwa matumizi
mbalimbali.Wakati wa kukatwa hakikisha umeacha sehemu ya kama
sentimita 30 kutoka ardhini.Nyasi hii hutumiwa kulisha wanyama moja
kwa moja au kama sileji.Pia huweza kuwa kukarabitiwa na kutumiwa
kama kuni kwenye upishi na hautoi moshi,hutumiwa kutengneza
vyombo,wezekaji wa nyumba.
11
-
Usafisaji Na Utunzi Wa Choo
Ni vyema kuhakikisha usafi wa sakafu ya choo chako kwa kutumia
sabuni na maji pekee wala sio didha za klorini..Hii ni muhimu kwa
kuwa kitatunza mizizi ya vetiva.Ikiwa sakafu hii haina paa,basi
maji ya mvua itasaidia katika usafishaji kwani maji yataingia moja
kwa moja kutoka kwa slabi hadi kwenye shimo la choo.Ukarabati wa
kila mara ni buhimu kuzuia uporomokaji wa choo.Katika nchi ya
Haiti,takribani vyoo 365 za vetiva zilizojengwa mashinani,ni mbili
(2) ambayo ni asilimia 0.5 peke zilizobomoka kulinganana utafiti
uliofanywa miaka miwili unusu(2.5) iliyopita.Njia moja nyeti ya
kuzuia vyoo kuporomoka kando na kuvijenga kwenye pahala thabiti ni
upanzi wa vetiva na kuiacha ishikamane.Njia ya pili ni kukagua
dalili za awali za mmomonyoko.Dalili za kuonyesha kuwa choo
kitaporomoka huonekana mapema hivyo basi inaweza zuiliwa.Ikiwa
nyufa zimeonekana,ziba kwa mchanga/au maganda ya miti halafu pandia
vetiva juu yake.Mzizi ya vetiva hudhibiti mashimo na kuzuia
uporomokaji.Ikiwa nyufa ni kubwa sana basi shimo nyingine ni lazima
ichimbwe na slabi kuhamishwa huko.
Choo cha vetiva kilichokomaa na chenye useri auufaraga.
Choo chenye upenyu wa mwangaza napaipu ya kutoa harufu.
Urudiaji wa matumizi:
Wakati shimo la choo kimejaa,sakafu yake ya saruji/slabi pia na
nyasi ya vetiva huhamishiwa pahala pengine.Chimba chini kando yam
mea wa vetiva,zitoe zikiwa zimeshikana,chonga mizizi na uache
sentimita kumi na tano (15) matawi uyachonge kwa sentimita (15-20)
na pia uzigawe kwenye vitatu vitatu hadi vitano(3-5) kwa kutumia
upanga au vyombo kama jembe shoka.Rudia upansi wake vile ulivyo
fanya katika choo cha mwanzo.Choo cha kwanza kifunikwe kwa mchanga
nusi mita(1/2) mahala hapo panaweza limwa baada ya miaka miwili au
mti wa matunda inaweza pandwa hapo mara moja.
12
-
Vetiva zilizopandwa kwa mstari Vetiva zilizopandwa chini
mno.
Ukarabati
Utunzi:
kuibadilisha/kukarabati,uhamazisho itakuwa muhimu ili wazo hili
la choo kama hiki kikubaliwa na jamii wenye itikadi na imani
mbalimbali.Kijumba kinaweza jengwa juu ya slabi kuleta upekee
Fulani.Pia kifaa kama kiti cha choo kinaweza jengwa juu ya shimo ya
kukalia.Shimo ya inchi 4 inaweza achwa ili kuleta mwangaza.Ikiwa
kumejengwa nyumba hii,bomba ya kuputisha harufu mbaya huwekwa na
kupitishwa kwa paa.Ni vyema nyaya itumiwe kwenye bomba hizi kuzuia
nzi na wadudu wengine kuingia chooni.Kwa mawaidha ya ziada juu ya
ujenzi wa vyoo hivi na vile vinapambwa wasiliana na mtandao wa:
http://www.clean-water-for-laymen.com/privy-privacy-shelter.html.
Nyasi ya jiji:
Kwenye mahali pasipopatikana nyasi ya vetiva,choo hiki kinaweza
jengwa kwa kutumia nyasi ya jiji.Vetiva hukua vyema kwenye maeneo
ya joto na hukua katika tropiki pekee.Nyasi ya jiji hata hivyo
huweza vumulia baridi/joto na pia udongo wenye chumvi.Mzizi yake
huzagaa kote na kama vetiva hudhibiti udongo.Kwa hivyo nyasi ya
jiji huwa mbadala nzuri ya vetiva ikitakikana.Nyasi hii pia huzuia
mmomonyoko wa ardhi/udongo kama vile vetiva.
13
http://www.clean-water-for-laymen.com/privy-privacy-shelter.html
-
Mzizi ya nyasi ya jiji vilivile huzuia mmmonyoko kama vile
vetiva
Udwara Wa Ndizi:
Ukarabati mwingine muhimu ni uongezaji wa miche ya ndizi kwenye
udwara/mzunguko wa choo cha vetiva.Jamii hukubali kukitunza choo
cha cha vetiva ikiwa ina mimea ya matunda yanayowakidhi.Panda miche
mitano ya ndizi kwa safu na kuacha nafasi inayootakikana kando ya
vetiva.Mti wa papai pia huweza pandwa katkati ya ndizi na kuacha
nafasi ya kuingia chooni.Mimea hiihunyunyiziwa maji hadi itakapokua
vyema hasa wakati wa kiangazi.Ijapokuwa sio hatari kula matunda
kutoka kwa miti hii,hata hivyo si salama kupanda mboga karibu na
choo kwa sababu ya uasambazaji wa uchafu.
14
-
15
-
Mbegu Za Paipai Kama Kizuizi Na Pia Tiba:
Wadudu/viini vya utumbo ni jambo la kawaida kote hata katika
nchini zilizoendelea. Kando na kuonyesha dalili mbalimbali tumboni
kama upungufu wa uzani,pia zinweza fanya mtu kupoteza fikra ama
kuwa na kiarusi.Ikiwa miti hii itapandwa karibu ,basi mbegu zake
zitatumika kama dawa za minyoo.Kumeza vijiko vine ndogo vya mbegu
mbichi au vijiko viwili vya mbegu vilivyokauka kutoa tiba kamili
kwa watu wazima na watoto.Mbegu hizi zinauchacha Fulani kwa
wengine.Wale wanaoweza kumeza mzima bila kuzisiaga mdomoni ndio
njia rahisi.Kwa watoto au wasioweza kuzimeza ,basi mbegu hizi
hukaushwa, husiagwa na kuchanganywa na sukari au asali,ama
siagi.Mbinu hii huzuia uakali wake.Dawa hii huweza tumiwa mara moja
kwa mwezi na huzuia minyoo tumboni.Lakini mkorogo huu usitumiwe
sana/nyinyi kwani husababisha udhaifu wa mbegu mwilini.Kwa watoto
au wasioweza kuzimeza mzima ,basi mbegu hizi hukaushwa,husiagwa na
kuchanganywa na sukari au asali,ama siagi.Mbinu hii huzuia ukali
wake.Dawa hii huweza tumiwa mara moja kwa mwezi na huzuia minyoo
tumboni.Lakini mkorogo huu usitumiwe sana/nyingi kwani husababisha
udhaifu wa mbegu mwilini.Kwa maeneo ambayo paipai hukuzwa na
vyakula hupeanwa shuleni kwa watoto,njia hii ya tiba huwezajaribiwa
ili kiimarisha afywa na masomo ya wanafunzi kwa gharama ndogo
sana.
Papaya ukwa huu hutoa mavuno 3 ya matibabu ya antiparastic
16
-
Marejeleo:
1. Okeniyi J, Ogunlesi T, Oyelami O, Adeyemi L; 2007;
Effectiveness of dried Carica papaya seeds against human intestinal
parasitosis; Journal of Medicinal Food; 10(1): 194-196.
Mapokeshi:
1) Owen Lee (www.vetiverlatrine.org); Mhasisi wa mwongoza wa
vyoo vya vetiva pamoja na picha zao.
2) TVNI (The Vetiver Network International, www.vetiver.com);
Mhasisi wa vetiva pamoja na jiji na picha zao.
3) Dale Rachmeler, PhD ([email protected]); Mhariri wa
mwongozo.
4) Roger Gietzen, MD (www.healthy-mind-body.com &
[email protected]); Mhasisi pamoja na wahariri wote
katika kazi hii na picha zao.
5) Kwa ruhusa ya uchapishaji wa mwnogozo huutafadhali wasiliana
na; Mr Daniel O Simba @ [email protected],ama ;
www.imanigroupkenya.org.
Hatimiliki:
© 2016 Roger Gietzen, MD. Haki zote zimehifadhiwa.Uchapishaji
huu uwe huru kwa yeyote ulimwenguni mzima.Usambaji mahali popote
unaruhusiwa na kwa njia yoyote ile hata ya mtandao ni bora tu iwe
ni bure/bila malipo.Shughuli hii isiwe ya kibiashara au kipata
faida Roger Gietzen, MD ([email protected]).
17
mailto:[email protected]:[email protected],amamailto:[email protected]://www.healthy-mind-body.com/mailto:[email protected]://www.vetiver.com/http://www.vetiverlatrine.org/