Top Banner
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 1 BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 Juni, 2017 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, Katibu. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018. MHE. CATHERINE V. MAGIGE (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI): Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
334

MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

May 09, 2023

Download

Documents

Khang Minh
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

1

BUNGE LA TANZANIA____________

MAJADILIANO YA BUNGE___________

MKUTANO WA SABA

Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 Juni, 2017

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:-

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:

Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yaWizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE (K.n.y. MWENYEKITI WAKAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI):

Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini kuhusuutekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini kwamwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamatijuu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwamwaka wa fedha 2017/2018.

Page 2: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

2

MHE. ESTHER N. MATIKO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WAKAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI):

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusuWizara ya Nishati na Madini juu ya Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI:

MASWALI KWA WAZIRI MKUU

NAIBU SPIKA: Maswali kwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu tutaanza na MheshimiwaDevotha Mathew Minja.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa ni sera ya Serikalikuboresha kilimo hapa nchini, ikizingatiwa kwamba kilimokinatoa ajira kwa Watanzania kwa zaidi ya asilimia 80 nakilimo kimekuwa kikihudumia Watanzania kwa maana yakujitosheleza kwa chakula, lakini kwa kuwa pia ni sera Serikaliiliamua kuja na mikakati ya kuboresha sekta ya kilimo ikiwani pamoja na kutoa majukumu kwa mawakala wapembejeo hapa nchini ili waweze kutoa huduma hizo zapembejeo kwa wakulima wetu hapa nchini.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, mawakala wa pembejeowamefanya kazi yao kwa uadilifu mkubwa toka mwaka2014/2015; 2015/2016 lakini mpaka sasa hivi mawakala haohawajalipwa fedha zao.

Je, Mheshimiwa Waziri Mkuu ni sera ya Serikalikuwarusha mawakala ambao wamefanya kazi yao vizuri?

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaanzakujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, naomba nitumie nafasihii kutoa pole kwa Watanzania, pia kwa Kambi ya Upinzani

Page 3: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

3

inayoongozwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani,Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe, kwa kifo cha kiongoziwetu wa kisiasa toka Kambi ya Upinzani toka Chama chaCHADEMA Mheshimiwa Philemon Ndesamburo ambaye janaalitangulia mbele za haki, nitoe pole pia kwa mke na watotowa marehemu, nitoe pole pia kwa Wabunge wenzangu kwasababu Mheshimiwa Marehemu Ndesamburo tulikuwa nayehapa ndani ya Bunge. Nitoe pole pia kwa Watanzania wotekwa sababu tumempoteza kiongozi ambaye alioneshauwezo mkubwa wa kulitetea Taifa, alionesha uwezomkubwa wa kusemea Watanzania kwa ujumla wake. Sotekwa pamoja tumuombe marehemu Mzee wetu Ndesamburoili Mwenyezi Mungu aweze kuiweka roho yake mahala pema.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nianze kujibu swali laMheshimiwa Devotha Minja, Mbunge wa Morogoro kamaifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba sera yaSerikali, moja kati ya mambo muhimu ni kuboresha kilimona Serikali za awamu zote zimeendelea kufanya vizuri kwenyeeneo hili kwa kusisitiza kilimo na Serikali tunatambua kwaasilimia zaidi ya 80 ya Watanzania tunategemea kilimo. Hatampango wetu wa sasa wa Tanzania ya viwanda na uchumiwa viwanda unategemea kilimo zaidi ili kuendesha viwandavyetu. Nikiri kile ambacho umesema Mheshimiwa Mbungekwamba tunapata msaada sana na Watanzania ambaowanajitoa katika kuunga mkono jitihada za Serikali kwausambazaji wa pembejeo, kufanya kazi mbalimbali za kilimona namna ambavyo wanajitahidi kuwa wavumilivu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakiri kwamba ni kweliwanatudai, lakini katika hili nataka niseme ukweli kwambatulipoanza mfumo wa utoaji wa pembejeo kwa njia yavocha na kuwatumia hawa mawakala kutupelekeapembejeo hizi kwa wakulima kule vijijini, zipo dosari kadhaaambazo tumeziona. Moja ya dosari kubwa ambayotumeiona ni kwamba baadhi ya mawakala, wachachewamekuwa siyo waaminifu sana. Kwamba walikuwawanashirikiana na watendaji wetu wa vijiji kule katika

Page 4: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

4

kuorodhesha majina ya wakulima ambao si wakulima nahawapo, wamewapa mbolea, madawa na kudai fedhanyingi sana ambazo hazipo na tukajikuta tuna deni ya zaidiya shilingi bilioni 65. Ninazo kumbukumbu kwa sababu haomawakala wote nimekutana nao, tumekaa nao hapatumejadili namna nzuri lakini tuliwaambia dosari hii kwawachache wao na kwamba tumewahakikishia Serikaliitawalipa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nataka tufanye jambomoja lazima tujiridhishe tuende kwenye vijiji kupitia watendajiambao ni waaminifu kufanya uhakiki wa kama kwelipembejeo hizi ziliwafikia wakulima ili tueze kujua deni halisi.Nataka nikuhakikishie baada ya kuwa tumeanza uhakiki huomaana yake tumeshafanya uhakiki awamu ya kwanza. Katiya shilingi bilioni 35 zilizoonekana kwenye orodha ya madeniya awali tulipata shilingi bilioni sita tu ambazo Serikaliinadaiwa. Lakini bado tuna shilingi bilioni 30 nyingine ambazosasa na kwa mujibu wa mazungumzo yangu na mawakalawote ambao walikuja hapa wiki mbili zi l izopitatumekubaliana. Kimsingi kwanza, tumewasihi waendeleekuwa wavumilivu pia tumeshukuru kwamba wamekuwawavumilivu kwa kiasi hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni muhimu tufanye huouhakiki ili tujue Serikali hasa inadaiwa kiasi gani ili tuwezekuwalipa. Nataka nikuhakikishie kwamba kazi hiyoinaendelea na tuko kwenye hatua za mwisho na tutawalipamadeni yote. Kila aliyefanya kazi vizuri kwa uaminifu, denilake atalipwa kwa sababu hiyo ni stahili yake na kweliumefanya kazi nzuri ya kufikisha pembejeo kwa wakulimana tunatambua mchango wao na tutaendelea kuheshimumchango wao. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, umekiri kwamba ni kweliSerikali inadaiwa, lakini umesema kwamba kuna dosariambazo zimejitokeza katika uhakiki wa zoezi hilo na toka

Page 5: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

5

mwaka 2014/2015 – 2015/2016 ni muda mrefu. Serikali kwanini haiwezi kuona kwamba kuna haja sasa ya kuharakishazoezi hilo kama watu wanastahiki zao wakalipwa kwamaana hivi sasa ninavyozungumza ziko taarifa kwamba kunabaadhi ya mawakala hivi sasa wameuziwa nyumba zao, kunabaadhi ambao hivi sasa wanashindwa kusomesha watotowao shule na kuna baadhi ya mawakala ambao wamefarikikwa mshituko baada ya kuona nyumba zao zinauzwa namabenki. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri Mkuu, kazi hii kama hawa watummewatambua na wamefanya kazi yao kwa uadilifi. Serikalikwenye hii Kamati ya kuandaa mawakala ilijumuisha Serikaliwakiwemo wa TAKUKURU, Polisi, Wakurugenzi, Wakuu waWilaya. Sioni ni kwa nini uhakiki wa namna hii naucheleweshaji wa namna hii kwa hawa watu ambaowamefanya kazi yao kwa uadilifu. Mheshimiwa Waziri Mkuuumetoa commitment kwa mawakala hawa kwa siku….

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Devotha Minja muda wakounakwisha naomba uulize swali sasa ili uweze kujibiwa.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Waziri Mkuuulitoa siku 25 kwamba zoezi hili la uhakiki liwe limefanyikaTanzania nzima kwa mawakala zaidi ya 940. Ni kwa ninimpaka sasa kwa miaka hiyo toka mwaka 2014 watu hawaSerikali haitaki kuwalipa haki yao ya msingi? (Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwelikupitia mazungumzo yetu kwa pamoja na mawakala wotetulitoa muda ambao tumejipanga kufanya uhakiki wamadeni yaliyobaki ili tuweke utaratibu wa kulipa na tarehehiyo imeishia jana tarehe 31. Kwa hiyo, sasa nasubiri taarifakutoka Halmashauri za Wilaya zote zitakazokusanywa kwenyengazi ya Mikoa na Mikoa itatuletea takwimu na baada yakupeleka Wizara ya Kilimo ikishapitia watapeleka Wizara yaFedha na malipo hayo yatalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba baadhi yamawakala kwa mujibu wa mazungumzo yetu walieleza adha

Page 6: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

6

hiyo ambayo wanaipata, lakini kupitia kauli hii wanasikiapia hata wale wadai kwamba, wale wote ambaowatakuwa na madeni sahihi baada ya kuhakikiwa ni watuwema na ndio ambao pia tunajua tunatakiwa tuwalipe.Kwa hiyo, hakuna umuhimu wa kuharakisha kunyang’anyanyumba, na kufanya vitu vingine ni jambo la kuona kwambataratibu hizi tunazozitumia ni taratibu ambazo zinaleta tijakwa Watanzania, zinaleta tija kwa Serikali kwa sababutungeweza kupoteza mabilioni ya fedha ambayo yangewezapia kusaidia kwenye miundombinu nyingine, lakini sasatumebaini kwamba hayakuwa ya ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natumia nafasi hii kutoawito kwa watumishi wa Serikali wote ambao wamehusikakatika hili ambao pia tutawabaini kwamba wao walihusikakwenye wizi, ubadhirifu na udanganyifu huo wotetutawachukulia hatua kali, hilo moja.

Pili, wale wote ambao wameshiriki katika hili, nirudietena kuwahakikishia kwamba madeni hayoyakishathibitishwa kwamba fulani anadai kiasi fulanitutawalipa kama ambavyo tumetangaza, ahsante sana.(Makofi)

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika,nashukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali kwaWaziri Mkuu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, baadhi ya walimu wenyeulemavu kutegemeana na ulemavu walionao wanahitajivifaa maalum vya kujifunzia na kufundishia katika utekelezajiwa majukumu yao ya kila siku. Vifaa hivyo ni pamoja namashine za maandishi ya nukta nundu, shime sekio pamojana vifaa vingine. Natambua kazi nzuri iliyofanywa ofisi yakopia Wizara ya Elimu kwa kutoa vifaa kwa wanafunzi wenyemahitaji maalum. Bado tatizo lipo kwa walimu hasa kwakuzingatia kwamba sio walimu wote wenye ulemavuwanaopangiwa kwenye shule zenye mahitaji maalumambazo shule hizo zina vifaa hivi.

Page 7: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

7

Je, wewe kama Baba na hasa kwa kuzingatiamasuala haya ya watu wenye ulemavu yako chini ya ofisiyako, nini kauli yako ili kuhakikisha kwamba walimu hawawanatekelezewa mahitaji yao na kutimiza majukumu yaopasipo matatizo yoyote? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri Mkuu majibu.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inauratibu mzuri sana wa kuhahakisha kwamba Watanzaniawenzetu wenye mahitaji maalum wanapata huduma stahikiili waweze kukamilisha shughuli zao za siku katika nyanjambalimbali. Moja kati ya ushahidi kwamba jambo hililimeratibiwa vizuri Serikali zote zilizopita pamoja na hii yaAwamu ya Tano tumeweza kutenga Wizara inayoshughulikiaWatanzania wenzetu ambao wana mahitaji maalum. Ofisiya Waziri Mkuu ambayo mimi mwenyewe nipo, ndio hasaWizara ambayo inashughulikia kwa ujumla wake, lakini tunaWizara ya Elimu na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) zote hizi zinaratibukwa namna ambavyo tumepanga utaratibu wa kufikishahuduma hii mahali hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia hawa wote ambaowana mahitaji maalum, tunatambua kwamba wakati wotewanahitaji kujielimisha, kupitia taasisi na shule mbalimbalina kule wako waelimishaji ambao wanafanya kazi hiyo kilasiku. Sisi tuna utaratibu kwenye maeneo haya ya vyuo, taasisina shule mpango wa kwanza tumepeleka fedha zakuwahudumia pale ambapo wanahitaji huduma kulinganana mahitaji yake. Wako wale ambao hawana usikivu mzuri,uono hafifu, ulemavu wa viungo, wote hawatumewaandalia utaratibu kwa kupeleka fedha kwenyeHalmashauri ili waweze kuhudumiwa. Pia walimu ambaowanatoa elimu hii nao pia tumeweza kuwawezesha kwakuwapa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kulingana na ainaya mahitaji ambayo tunayo.

Pia walimu hawa tunawapeleka semina mara nyingikuhakikisha kwamba na wao pia wanapata elimu ya kisasazaidi ili kuweza kuwahudumia vizuri hawa wote.

Page 8: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

8

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni l ini Serikaliitajiimarisha katika kutoa huduma hii ni kwamba Serikaliimeandaa kituo cha Msimbazi Center kuwa ni eneo lakukusanyia vifaa ambavyo tunavisambaza kwenye shule nataasisi zote ili viweze kutumika katika kufundishia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikuhakikishie piaJumanne wiki ijayo napokea vifaa vingi sana vya elimu kuleDar es Salaam ambavyo vimeletwa kwa ajili ya kupelekakwenye shule zetu za msingi. Miongoni mwa vifaa ambavyopia tutakabidhiwa siku ya Jumanne ni pamoja na vifaa vyaWatanzania wenzetu walioko vyuoni, kwenye shule ambaowana mahitaji maalum.

Kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Amina Mollel natunajua jitihada zako za kusemea sana eneo hili kwambaSerikali iko pamoja, Serikali inaendelea kuratibu vizuri naniendelee kukuhakikishia kwamba Serikali itaendelea kuratibuna kuhakikisha kwamba vifaa vya kujifunzia na kufundishiavitapatikana na hawa waelimishaji wanapata elimu ya marakwa mara ili waweze kuwasaidia hawa wenzetu ambaowana mahitaji maalum. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana, vilevile naishukuru sana Serikali yanguinayoongozwa na Chama cha Mapinduzi, nakushukuru sanaMheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri yenye kutiamoyo na faraja kwa watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali dogo la nyongezana swali hili ni kwa mujibu wa Mwongozo wa Huduma kwaWatumishi wa Umma Wenye Ulemavu ambao katika kifungucha 3 (12) chenye vipengele vya (a), (b), (c) na (d)vinatambua na vinasisitiza na kusema kwamba, nitanukuukidogo; “kutambua kuwa ni haki ya watumishi wenyeulemavu kupatiwa mahitaji yao muhimu kama vile vifaa vyakuwaongezea uwezo, fedha kwa ajili ya matibabu naukarabati wa afya zao (rehabilitation), nyenzo na vifaa hivivitolewe na waajiri.

Page 9: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

9

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ninataka kupata kauliyako Mheshimiwa Waziri Mkuu, baadhi ya waajirihawatekelezi majukumu haya kwa watumishi wa ummawenye ulemavu. Kama baba mwenye dhamana, nini kauliyako kwa waajiri wasiotimiza wajibu wao kama Mwongozowa Utumishi wa Umma unavyowataka kutekeleza mahitajihayo kwa watumishi wa umma wenye ulemavu? Ahsante.

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, kamaambavyo ameeleza kwamba, uko mwongozo wa Serikalijuu ya Watumishi wa Umma wanaofanya kazi kwenye taasisizetu za Serikali, lakini pia sio Serikali tu, hata taasisi zisizokuwaza kiserikali, unawataka waajiri wote wanapowaajiriwenzetu ambao wana mahitaji maalum lazimawatekelezewe mahitaji yao ili kuwawezesha kufanya kazi yaovizuri. Kwa maana hiyo, kwa upande wa Serikali Wizara zoteziko hapa, Mawaziri wako hapa, Makatibu Wakuu wanaisikiakauli hii na kwamba lazima sasa watekeleze mahitaji namatakwa ya Serikali ya kuwahudumia hawa watumishiwenye mahitaji maalum kulingana na sekta zao. Kama yeyeyuko upande wa ukarani, basi wahakikishe ana vifaa vyakutosha kumwezesha kufanya kazi hiyo vizuri na hivyo kilasekta lazima apate huduma hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatoa wito kwa sektabinafsi kutoa nafasi zaidi za ajira kama ambavyo Serikalitunawaajiri wenye mahitaji maalum. Hakuna sababu yakukwepa kuwaajiri ati kwa sababu unatakiwakuwahudumia. Wote ni Watanzania na wote wana uwezona tumethibitisha uwezo wao, pia hata Mheshimiwa Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli, kuthibitisha kwamba sera hii ni yetu ndani ya Serikaliametoa ajira, ameteuwa watumishi ambao wana mahitajimaalum na hawa wote mahali pao pa kazi wanawezeshwakwa vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikuhakikishietutaendelea kuajiri ndani ya Serikali na ninatoa wito kwa sektabinafsi ziajiri Watanzania wenzetu wenye mahitaji maalumwote ambao tunaajiri, wenye mamlaka ya kuajiri, na

Page 10: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

10

Mwenyekiti wa Tume ya Ajira yuko hapa wa Chama chaWaajiri yuko hapa, asikie ili awaelekeze wenzake kwamba,ni wajibu wa kila muajiri kuwawezesha wenye mahitajimaalum kufanya kazi zao baada tu ya kuajiri, kamaambavyo Sera ya Serikali inahitaji kufanya hivyo. Ahsante.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Emanuel AdamsonMwakasaka.

MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza swali la papo kwapapo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Naomba kwanza kabla sijauliza swali languniipongeze Serikali chini ya Dkt. John Pombe Magufuli kwajinsi ilivyoshughulikia suala zima la vyeti fake pamoja nawatumishi hewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba niulize swalikwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni Serikali ilifanyamaamuzi ya kuzuia kusafirisha mchanga wa dhahabu nje yanchi, katika kufanya hivyo Serikali itakuwa imepoteza dirakatika demokrasia ya kiuchumi duniani, lakini si hivyo tuitakuwa pia imeleta mahusiano ambayo si mazuri na nchimbalimbali duniani. Nini tamko la Serikali kuhusu jambo hili?(Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli sasatuko kwenye matarajio ya kupata taarifa iliyo kamili kwenyesakata la mchanga na nataka nizungumzie eneo ambaloumehitaji zaidi la nini Serikali inatamka juu ya hili i l ikuwaondolea hofu wawekezaji wetu wale waliowekezakwenye maeneo ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni Watanzaniawenyewe walionesha hofu kubwa kwa kipindi kirefu, hataWaheshimiwa Wabunge katika michango yenu mbalimbali

Page 11: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

11

kwa miaka iliyopita, hata pia katika kipindi hiki cha Serikalihii ya Awamu ya Tano mmeendelea kuitaka Serikali ichukuehatua thabiti na kutaka kufanya uchunguzi wa kina juu yamchanga unaotoka nchini kupeleka nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais wetu Dkt.John Pombe Magufuli amelitekeleza hilo pale ambapoalinituma mimi mwenyewe kwenda Kahama, kwenda kuonazoezi la ufungashaji wamchanga na kuuona mchanga huo,lakini nilipomletea taarifa akaamua kuunda Tume na aliundatume mbili, moja ya kwenda kuukagua mchanga wenyewena kujua ndani kuna nini, lakini ya pili, ni ile Tume ambayoinahakiki, itatoa taarifa ya madhara ya kiuchumi, lakini piamadhara ya kisiasa kwa ujumla na mahusiano kwa ujumlawake. Mpaka sasa tumepata taarifa moja na bado tunasubiritaarifa ya pili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hili nataka nitumienafasi hii kuwasihi wawekezaji wote, kwanza wasiwe namashaka kwa sababu, lengo la Serikali ni kujiridhisha tukwamba, je, mchanga huu unaosafirishwa kwenda nje unanini? Na wala hatubughudhi uzalishaji wao. Baada ya kuwatumepata taarifa ya kwanza, bado hatua kamilihazijachukuliwa, tunasubiri taarifa ya kamati ya pili, baadaya hapo sasa Serikali itakaa chini na kutafakari kwa kupataushauri kutoka sekta mbalimbali za kisheria, za kiuchumi namaeneo mengine hatua gani tuchukue. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niendeleekuwatoa hofu wawekezaji wale walioko kwenye sekta ile yamadini wawe watulivu. Hatuna jambo ambalo tumelifanyiakazi dhidi ya hatua ambazo tumechukua ndani ya nchi kwawatu wetu ambao tunao ambao tuliwapa dhamana yakusimamia hilo, lakini wawekezaji wote waendelee nashughuli zao za uwekezaji kama ambavyo tumekubaliana,wale ambao wako kwenye mchanga kwa sababu juziwameambiwa watulie, watulie, hakuna jambo ambalolitafanywa ambalo halitatumia haki, ama litaenda nje yahaki au stahili ya mwekezaji huyo na kila kitu kitakuwa wazi.(Makofi)

Page 12: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

12

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pia nitoe pia raihata kwa Watanzania wawe watulivu. Tumeona watuwanatoa matamko wakidhani labda kuna uonevu, hapana!Watu watulie wasubiri majibu ya Serikali ambayo yatalindahaki ya kila mwekezaji, lakini na sisi pia Watanzania ambaotunaona tuna rasilimali zetu, hatuhitaji hizi rasilimali zipoteehovyo, lazima tuwe na uhakiki. Katika hili naomba mtuungemkono Serikali kwa sababu kazi tunayoifanya ni kwa manufaaya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uhakiki huu ni kwa manufaayetu Watanzania, ili tuwe na uhakika wa matumizi sahihi yarasilimali zetu nchini. Kwa kufanya hilo tutakuwa tunajuatunapata nini na pia tujue tunaratibu matumizi yake na sisiWabunge nadhani ndio hasa wahusika kama wawakilishiwa wananchi, twende tukawatulize wananchi waachekutoa matamko wasubiri Kamati zile. Pia tuzungumze nawawekezaji wetu ili nao pia wawe watulivu, bado Kamatiya pili haijatoa taarifa, baada ya hiyo maamuzi yatafanyika.Ahsante sana. (Makofi)

MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongezakwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Kwa kuwa tatizo hili la upimaji wa mchanga linaanziakule ambako ndiko kuna machimbo yenyewe. Ni nini mkakatiwa Serikali kuhakikisha kule origin source kunawekwa mashineambazo sasa tatizo hili halitajirudia tena?(Makofi)

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati yamikakati ambayo tunayo ni kupokea wawekezaji natumeanza kuona wawekezaji kadhaa wakija kuonesha niaya kuwekeza kwenye eneo hili. Awali kulikuwa na usirimkubwa wa namna ya kuwakaribisha wawekezaji hawakuwekeza kujenga mitambo hii na ndio kwa sababu Serikaliimeanza kuchukua hatua za awali kwa vile tunajuakwamba, kuna maeneo ambayo yalikuwa hayaoneshwiwazi ikiwemo na eneo la kuwakaribisha wawekezaji wakujenga mitambo hii hapa nchini.

Page 13: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

13

Baada ya muda mfupi kama ambavyo mamboyameanza kujitokeza tutaamua kuwekeza, kujenga mashinezetu hapa hapa nchini au kuwakaribisha wawekezaji aukuona uwezo wa Serikali kama tunaweza ili sasa tuwezekutatua tatizo ambalo linatukabili sasa la kupotezamchanga ambao tunautoa hapa na kupeleka nje kwa ajiliya uyeyushaji na kupata aina mbalimbali za madini. Ahsante.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuumekwisha. Mheshimiwa Waziri Mkuu tunakushukuru sanakwa majibu, ahsante sana. Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:

MASWALI NA MAJIBU

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tutaendeleana maswali ya kawaida, tunaanza na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini,sasa aulize swali lake.

Na. 317

Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji KulipwaMishahara au Posho

MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza:-

Serikali ina mpango gani wa kuwalipa posho aumishahara Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji ilikurahisisha ufanisi wa shughuli zao?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini,kama ifuatavyo:-

Page 14: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

14

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inathamini nakutambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Wenyevitiwa Vijiji na Mitaa katika maendeleo ya Taifa. Serikaliimezingatia na kuweka utaratibu wa kushirikisha viongozihawa wanaolipwa posho maalum kwa motisha kupitiaasilimia 20 ya mapato yanayorejeshwa na Halmashaurikwenye vijiji. Asilimia 17 ya fedha hizo zinatakiwa kutumikakwa shughuli za utawala, ikiwemo kulipa posho ya Wenyevitiwa Vijiji na Mitaa na asilimia tatu kwa shughuli za maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepangakuboresha utaratibu huu kwa kuingiza katika mapendekezoya marekebisho ya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa ilikuweka utaratibu mzuri wa urejeshaji wa asilimia 20 kwenyevijiji na kuwanufaisha walengwa. Aidha, tumeimarishamfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashaurizote ili kujenga uwezo wa kutenga asilimia 20 kwenda kilakijiji.

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante.

Kwa kuwa Serikali imekiri kwamba Wenyeviti wa Vijijina Vitongoji wanafanya kazi nzuri na imekuwaikiwategemea kwenye kazi zote na hata kualika mikutanoyote ya Wabunge, Madiwani na kufanya kazi kubwa, asilimia20 ambayo Mheshimiwa Waziri ameitaja katika majibu yakeya msingi haijawahi kupelekwa hata siku moja.

Je, kwa nini sasa Serikali isilete namna nzuri yakuwalipa moja kwa moja hawa Wenyeviti kwa sababu, niviongozi ili pasiwe na utaratibu huu wa asilimia ambayohaijawahi kupelekwa tangu wameanza kazi hizi mpakasasa? (Makofi)

Swali la pili, kwenye swali langu la msingi nilielezahabari ya Madiwani. Madiwani kimsingi wanapata poshondogo ya shilingi 300,000 na kitu kama sikosei. Je, ni lini sasamnaongeza posho hizi ili walau basi wafanye kazi nzuri katikachini ya Halmashauri zetu huko Wilayani? (Makofi)

Page 15: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

15

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwelinafahamu concern ya Mheshimiwa Flatei, lakini jambo hilisio la Mheshimiwa Massay peke yake, naamini Wabungewengi sana wanaguswa na jambo hili. Na ndio maanaunaona Mheshimiwa Massay alivyosimama hapa watu wengisana, kila mtu alismama kutaka kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu naombaniseme ni kweli, kuna baadhi ya Halmashauri hizi poshohazirudi, lakini Halmashauri nyingine zinafanya vizuri katikaurejeshaji wa posho hii ya asilimia 20. Ndiyo maana sasatumesema katika mpango wetu wa kufanya marekebishoya Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura Namba 290,tumeweka kifungu maalum ambacho kinampa Wazirimwenye dhamana na jambo hilo kuweka suala zima laregulation maalum ya kulilazimisha suala hili sasa liwe sualala kisheria sio suala la kihiyari.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombanikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge ni kwamba utaratibuwetu katika jambo hili mimi ninaamini si muda mrefu sheriahiyo ya fedha itakuja hapa, tutaifanyia marekebisho, sasaitakuwa ni muarobaini na katika hili naomba niwasihi kwahali ya sasa hasa Wakurugenzi wetu wote kwamba asilimia20 kupeleka kila kijiji sio jambo la hiyari ni jambo la lazimasasa tulipeleke ili wananchi wetu kule chini waweze kufanyakazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ajenda ya posho yaMadiwani, ninakumbuka kwamba tulikuwa na Tume Maalumhapa ilikuwa maarufu kama Tume ya Lubeleje ambayo ilipitiamaeneo mbalimbali na bahati nzuri Mheshimiwa MzeeLubeleje amerudi tena Bungeni kama Senior MP, ilipendekezamapendekezo mbalimbali, ndio maana tumesema kwanyakati mbalimbali kwamba, Serikali inaangalia jambo hilina jinsi gani utaratibu wetu wa mapato utakuwa vizuri basitutafanya marekebisho kwa kadri itakavyowezekana.(Makofi)

Page 16: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

16

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Na mimi niseme tu kwamba mimi nimiongoni mwa Wenyeviti wa Tanzania wa Serikali ya Mtaawa Vodacom Kata ya Chanji kwa hiyo, ninaloliuliza ninalijuana changamoto zake.

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi ya Serikaliinayotengwa watekelezaji wa kwanza ni Wenyeviti waSerikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji, kauli hii ya kwambawataanza kulipwa posho sio mara ya kwanza ndani ya Bungehili.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba time frame nilini sheria italetwa hapa ili Wenyeviti waanze kulipwa poshokwa sababu sio hisani wanafanya kazi kubwa? (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibuswali la Dada yangu, Mheshimiwa Aida, Mbunge wa VitiMaalum, lakini Mwenyekiti wa Serikali ya Kiji j i, kamawalivyokuwa Wenyeviti wengine wa Jimbo la Ukonga kulenikifahamu hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama nilivyosemahapa kwamba kwanza kulikuwa na uzembe. Naombaniseme kwamba hata ile asilimia 20 kama kungekuwa nacommitment ya kurudi vizuri katika Halmashauri zetu, maanasasa hivi tunapozungumza kuna Halmashauri nyinginezinafanya vizuri katika hilo. Tuna baadhi ya ushahidi kunaHalmashauri nyingine Wenyeviti wake wa vijiji wanalipwavizuri kutokana na kwamba wameweka commitment yaasilimia 20 lazima irudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala zima la timeframe ni kwa sababu ni suala la sheria ni suala la kimchakatona taratibu zote sheria hii imeshapitia hivi sasa inaendanadhani katika Baraza la Mawaziri kupitia katika vifungumbalimbali, ikishakamilika itakuja humu Bungeni. Sasaniwaombe Waheshimiwa Wabunge sheria ikija humutunawaomba tushiriki wote kwa pamoja vizuri kwa sababu,

Page 17: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

17

ina vifungu vingi sana vinazungumzia suala la mapato katikaSerikali za Mitaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni imani yangu kwambatutajadili kwa kina tuje kuangalia jinsi gani tutafanyamarekebisho mazuri ambayo yataenda kuwagusa Wenyevitiwetu wa Serikali za Vijiji kuweza kupata ile posho yao kwakadiri inavyostahiki. (Makofi)

MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kuwa na sheria nizuri kwa upande mmoja, lakini kwa upande wa pil iHalmashauri zetu zinakabiliwa na matatizo makubwa yakiuchumi. Sasa Serikali inatoa tamko gani kuhusu kuziwezeshaHalmashauri zetu hizi kuweza kukusanya pesa za kutosha iliziweze kuwalipa watu hawa ambao ni muhimu sana kwenyemaendeleo ya vijiji vyetu?(Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, katika sualazima la ukusanyaji wa mapato la Halmashauri kuwa katikahali ngumu ya uchumi, kwanza ni commitment yetu woteWabunge na Madiwani kuhakikisha kwamba Halmashaurizetu zikusanye vizuri. Kwa sababu, miongoni mwa kigezokimojawapo cha existence ya Halmashauri lazima iwezekukusanya mapato ndiyo maana imepewa ridhaa kuwaHalmashauri kamili. Katika hili sasa ndiyo maana katika kipindihiki kilichopita tumetoa maelekezo mbalimbali katika sualazima la ukusanyaji wa mapato, hasa kutumia mifumo yaelectronic.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niwahakikishieWaheshimiwa Wabunge, katika maeneo mbalimbali tuna-success story kwamba leo hii kwa kutumia mifumo yaelectronics tumepata mafanikio makubwa. Sasa maelekezoyangu nadhani twende katika compliance vizuri katikamatumizi mazuri ya hii mifumo, kuna mahali pengine mifumoipo, lakini haitumiki vizuri, watu wana-divert kutoka katika

Page 18: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

18

mifumo ya ukusanyaji wa mapato hivi, mifumo ile sasainajukana ipo, lakini wengine hawapati manufaa katika hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwasihi sana Wakurugenziwote katika Halmashauri zote twende kuhakikisha kwambakatika idara zetu za fedha tunazisimamia vizuri. Lengo kubwani kwamba, mapato yaliyopangwa kupitia Mabaraza yaMadiwani yaende kukusanya vizuri ili tukuze mapato katikaHalmashauri zetu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendelea.Mheshimiwa Juma Selemani Nkamia, swali lake litaulizwa naMheshimiwa Moshi Selemani Kakoso

Na. 318

Wilaya ya Chemba Kutokuwa na Hospitali

MHE. MOSHI S. KAKOSO (K.n.y. MHE. JUMA S. NKAMIA)aliuliza:-

Wilaya ya Chemba haina hospitali jambolinalowalazimu wananchi wake zaidi ya laki tatu kwendakupata huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.

Je, Serikali ina mkakati gani wa haraka wakuhakikisha Wilaya hiyo inapata hospitali?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri waNchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali laMheshimiwa Juma Selemani Nkamia, Mbunge wa Chemba,kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya yaChemba imetenga kwa kupima eneo la ekari 23.7 kwa ajiliya kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya. Katika mwaka wafedha 2017/2018 Halmashauri imeomba maombi maalum ya

Page 19: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

19

shilingi bilioni mbili ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo. Aidha,upo mpango wa kukopa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima yaAfya ili kufanikisha ujenzi wa hospitali hiyo kwa awamu. Ofisiya Rais - TAMISEMI itashirikiana na Halmashauri ya Chemba ilikuhakikisha mipango ya ujenzi wa hospitali hiyo unafanikiwa.(Makofi)

NAIBU WAZIRI: Mheshimiwa Moshi Kakoso, swali lanyongeza.

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika,nishukuru sana kwa majibu ya Serikali ambayo yanamatumaini ya ujenzi ya Hospitali ya Wilaya.

Swali la kwanza, kwa kuwa Serikali iliahidi na mipangoyake inachukua muda mrefu, je, Serikali ina mpango ganiwakati inajipanga kuweza kukiboresha kituo cha afya chaHamai il i kiweze kutoa huduma nzuri sambamba nakuchimba kisima ambacho ni tatizo kwenye eneo la kituohicho cha afya?

Swali la pili, kwa kuwa matatizo ya Halmashauri yaWilaya ya Chemba ni sawa na tatizo lililoko kwenye Wilayaya Tanganyika na Naibu Waziri analifahamu hili. Serikali iliahidikujenga kituo cha afya Majalila. Je, ni lini Serikali itaanzautekelezaji wa kujenga kituo hicho cha Majalila?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi Rais -TAMISEMI, majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katikaHalmashauri ya Chemba tunao huu mpango wa kuhakikishatunajenga Hospitali ya Wilaya. Kwa vile changamoto yaJimbo la Chemba ni kubwa ndiyo maana Serikali katikampango wake wa kuboresha vile vituo vya afya 100, kituocha afya cha Hamai ni miongoni mwa vituo vya afyaambacho tunaenda kukiwekea ufanisi mkubwa wa ujenziwa miundombinu ambapo imani yangu ni kwamba si mudamrefu mchakato huo utaanza.

Page 20: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

20

Kwa hiyo, naomba nikuhakikishie kwamba kwawananchi wa Chemba na hili tumeshaongea na MheshimiwaNkamia kwamba tutafanya kila liwezekanalo katika kipindikifupi kijacho tutaenda kukiboresha kile kituo cha afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika suala zima la Wilayaya Tanganyika Mheshimiwa Mbunge unafahamu tulikuwawote Tanganyika nilivyokuja Jimboni kwako. TulitembeleaMakao Makuu yako na Wilaya yako ya Tanganyika ambayoni mpya, ndiyo maana tumepanga katika mpango wakuboresha Wilaya hii katika eneo la Majalila kile kituo chaafya ambacho kinasuasua sana tutamekiingiza katikampango wa vituo vya afya 100.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge naomba nikuhakikishekwamba wananchi wa Tanganyika wawe na imani kwambaSerikali inaenda kufanya investment kubwa eneo lile iliwananchi wa Tanganyika wapate huduma nzuri za afya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Hadji Mponda swalila nyongeza.

MHE. DKT. HADJI H. MPONDA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru, kwa kuniona.

Matatizo yanayowakabili wananchi wa WilayaChemba kwa kukosa huduma za Hospitali za Wilayayanalingana kabisa na ya Wilaya ya Malinyi ambapowananchi hawana Hospitali ya Wilaya. Halmashauri ya Malinyiimeweka utaratibu kuomba TAMISEMI kuifanya Hospitali yaLugala ambayo inamilikiwa na taasisi ya kidini kuwa Hospitaliya Wilaya, lakini ombi hilo na utaratibu huu TAMISEMIwamesimamisha.

Je, Serikali ina utaratibu gani wa haraka wakuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Malinyi kupata hospitaliya Wilaya?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya RaisTAMISEMI majibu.

Page 21: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

21

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweliukiangalia Ulanga, Malinyi wana changamoto kubwa yasekta ya afya. Katika mpango wa haraka MheshimiwaMponda, naomba nikuhakikishie kwamba kuna kituo chaafya cha Mtimila ambacho tumekiwekea kipaumbeletunakuja kukiwekea miundombinu muda si mrefu, kuanziahuu mwezi wa sita kwenda mwezi wa saba inawezekanamchakato huo utaanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwahakikishe wananchi waMalinyi kwamba Serikali imewaona, tutaenda kufanya kazikubwa pale ambayo mtakuja kuona ikifika mwezi wa nanehapo Mungu akijalia, inawezekana hali ikawa ni tofautiwananchi watakwenda kupata huduma nzuri sawa sawana kituo cha afya cha Lupilo katika Jimbo la Ulanga (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Sware Semesi swali lanyengeza.

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kuwa hii hospitali ya Wilaya ya Kondoainahudumia Halmashauri tatu; na kwa kuwa imepata ufinyumdogo sana wa bajeti na kuleta changamoto katikamadawa na vifaa tiba. Sasa Serikali inaona lini wakatiinafikiria kuwapatia watu wa Chemba hospitali yao, hospitalihii ikaongezewa bajeti ili kuweza kuhudumia vyema Wilayahizi tatu? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya RaisTAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Kondoachangamoto ni kubwa na ndiyo maana ukiangalia kunaMajimbo matatu tofauti ambayo ni Chemba, Kondoa Vijijinina Kondoa Mjini lakini hospitali inayotumika sasa hivi niHospitali ile ya Kondoa na ukiangalia population mpaka watuwengine kutoka katika wilaya especially kama Wilaya yaHanang’ walioko mpakani wengine wanakuja hapa Kondoa.

Page 22: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

22

Kwa hiyo, jambo hili ni kubwa na tumeliona ndiyomaana katika mpango wetu wa bajeti wa mwaka huu sasahasa ukiangalia basket fund tumebadilisha utaratibu wabasket fund tumeongeza bajeti katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo letu ni kuangalia nijinsi gani tutafanya ili wananchi wapate huduma. Hata hivyotumetoa maelekezo maeneo mbalimbali, kwa mfano tunaHalmashauri ya Kondoa Mji na Halmashauri ya Kondoa Vijijinilakini hospitali ni moja. Nimewahitaji Wakurugenzi wamaeneo yale waangalie katika suala zima la basket fundkatika Halmashauri ambapo ile hospitali iko na jinsi ganikufanya kwa kuweka utaratibu wa kusaidia ile hospitaliangalau kwa hali ya sasa iweze kufanya vizuri kwa sababuwananchi wote wanaohudumiwa ni watu kutoka maeneohayo ambapo ni hospitali yetu lazima tutakuja kuweka nguvuwananchi wapate huduma nzuri. Kwa hiyo, nikushukuru sanaSerikali inaifanyia kazi jambo hili.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Afya Maendeleoya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,

WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA,WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuruMheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini natakakuongeza kwenye swali la Mheshimiwa Sware.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kugawanya fedhakwa ajili ya dawa, vifaa na vifaa tiba tunazingatia vigezovikuu vitatu. Kigezo cha kwanza ni idadi ya walengwawanaopewa huduma katika hospitali hiyo (service population)ambapo inachukua asilimia 70, kigezo cha pili ni hali yaumaskini katika eneo husika ambacho kinabeba asilimia 15na kigezo cha tatu ni hali ya vifo vya watoto chini ya miakamitano. Kwa hiyo, nilikuwa namuomba Mheshimiwa SwareHalmashauri hizi tatu ambazo zinatumia Hospitali ya Wilayaya Kondoa wakae pamoja watuletee mapendekezo yaoWizara ya Afya kwamba hospitali hii inahudumia Halmashauritatu na sisi tutazingatia katika kuwaongezea bajeti ya dawa.Ninakushukuru sana. (Makofi)

Page 23: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

23

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Martha Mlata.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika,asante kwa kuwa swali la msingi linafanana kabisa na Wilayampya za Mkalama pamoja na Ikungi na wanatimiza vigezovyote ambavyo Waziri amevitaja hapa.

Je, Serikali ni lini sasa italeta huduma za hospitali zaWilaya katika Wilaya hizo za Mkalama na Ikungi? Ahsante.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweliMkalama ni Halmashauri mpya na imegawanyika kutokaHalmashauri ya Iramba, tunaenda kuhakikisha tunaboreshakile kituo cha afya cha Inimbila kwa sasa lengo kubwa nikwamba kiweze kuwa na suala zima la upasuaji kuondoahaya mambo ya referral system, ambapo tunajua kwambajambo hili tukilifanya litasaidia sana wananchi wa Jimbo laMkalama kuweza kupata huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, hali kadhalika katika kituocha afya cha Ikungi tunaenda kuweka uboreshaji mkubwawa miundombinu ya afya ambayo kwa wananchi wa eneolile wataweza kupata huduma mzuri hivi sasa ambapo kamanilivyosema awali tumeingiza katika mpango ule wa vituovya afya 100 ambao Serikali iko katika hatua za mwisho kwasababu kila kitu kimeshakamilika, tegemeeni WaheshimwaWabunge katika maeneo hayo Serikali imewasikia naitafanya mambo hayo kwa kadri iwezekanavyo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Gekul swali fupi.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika,ninakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Waziri ulifika Babati ukaonahospitali yetu ya Mrara na tukakueleza kwamba tunapata

Page 24: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

24

wagonjwa kutoka Kondoa ambalo ndiyo swali la msingi sikuya leo. RCC tulishakaa kwamba hospitali yetu ipandishwehadhi kutoka kituo cha afya kwenda hospitali ya Wilayanaomba nifahamu Mheshimiwa Naibu Waziri ni l inipendekezo letu hilo la RCC mtalifanyia kazi maana hospitaliya Mrara ina hali mbaya na wagonjwa ni wengi tunashindwakuwahudumia?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,TAMISEMI majibu kwa kifupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli nimefikana Mheshimiwa Mbunge tuliambatana pamoja siku iletukitembea. Ni kweli wanachangamoto kubwa sana ni kwavile utaratibu wa upandishaji wa vituo uko kwa mujibu washeria na utaratibu ambao ninyi mmeshakamilisha jambo hilolote na hivi sasa liko Wizara ya Afya katika final stages,nadhani Wizara ya Afya itakapokamilisha hilo jambomtapata mrejesho, kwa sababu dhamira ya Serikali nikuwahudumia wananchi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, kama mambo yotekatika Mkoa yamekamilika naamini Wizara ya Afya ita-finalizes hilo jambo lengo kubwa ni kuwasaidia wananchiwa Babati waweze kupata huduma vizuri. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaingiaWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, MheshimiwaSaumu Heri Sakala Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swalilake.

Na. 319

Kurasimisha Bandari Bubu-Tanga

MHE. SAUMU H. SAKALA aliuliza:-

Kando kando mwa Bahari ya Hindi Mkoani Tanga,pameibuka bandari bubu ambazo nyingine zinakuwa kubwa

Page 25: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

25

na kuhudumia watu wengi zaidi na askari wasio waaminifuhufanya bandari bubu hizo kuwa vyanzo vyao vya mapatokwa kuchukua rushwa kwa watu wanaopitisha mizigo yaokatika bandari hizo.

Je, ni lini Serikali itazirasimisha bandari hizo na kuzifanyazitambulike ili wafanyabiashara wanaozitumia wawe huru?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali laMheshimiwa Saumu Heri Sakala, Mbunge wa Viti Maalum,swali lake kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina taarifa ya uwepowa bandari bubu katika mwambao wa Pwani ikiwa nipamoja na maeneo ya Tanga. Aidha, kuibuka kwa bandarihizi bubu kumeleta changamoto za kiusalama, kiulinzi nakiuchumi. Hivyo, ili kudhibiti matumizi ya maeneo hayamamkala zinazohusika za pande zote mbili za Serikali yaMuungano zinashirikiana na kudhibiti hali hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na mikakati yapamoja na vikao vya kiutendaji ambavyo vimekuwavikifanyika kwa kuwahusisha Wakuu wa Mikoa yote yamwambao na visiwani, Wizara zinazohusika kutoka Bara naVisiwani, Mamlaka ya Usafiri Baharini ya Zanzibar (ZMA)Mamlaka ya Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Shirika laBandari la Zanzibar (ZPC), Mamkala ya Usimamizi wa BahariTanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Uhamiaji,Halmashauri na vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini.Mikakati ya pamoja iliyowekwa ni pamoja na:-

(i) Kutambua bandari zenye umuhimu kwa wananchikiuchumi na kijamii ili kuzirasimisha kwa kuziweka chini yauangalizi wa vijiji vilivyo kwenye maeneo husika;

(ii) Kuimarisha ushirikiano na Serikali za Mitaa kwakutumia Kamati za Ulinzi na Usalama ili zihusike katika

Page 26: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

26

kudhibiti matumizi mabaya ya bandari bubu katika maeneoambayo mamlaka husika hazina uwakilishi wa moja kwamoja;

(iii) Kuwa na kaguzi za mapoja kwa lengo la kuongezaufanisi katika matumizi ya vifaa kama vile boti za ukaguzina kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na umuhimu wasuala hili, Serikali kupitia mamlaka nilizokwishazitaja,inasimamia kuhakikisha mikakati hii iliyowekwa inatekelezwakwa wakati ili bandari bubu hizi zikiwemo za mwambao waMkoa wa Tanga zirasimishwe na kuwekwa chini ya uangaliziwa mamlaka husika.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Saumu Sakala swali lanyongeza.

MHE. SAUMU H. SAKALA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Pamoja na majibu marefu ya MheshimiwaNaibu Waziri lakini nina maswali mawili madogo yanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati ambayo NaibuWaziri ameielezea inaonyesha kabisa nia ya muda mrefu nabado iko ndani, lakini tatizo hili huku nje bado linaendeleakuwa kubwa yaani watu bado wanaendelea kuathirika sanana bandari hizi bubu.

Swali la kwanza, je, Serikali haioni kwamba kwakuendelea kuweka mikakati hiyo mirefu ndani wananchiwanaathirika na pengine sasa ingefika wakati ikachukuamkakati wa kudhibiti angalau wakati ile mikakati ya mudamrefu ikiwa inaendelea?

Swali la pili, bandari bubu hizi ziko katika viji j ivinavyozunguka mwambao wote wa pwani. Kwa kufanyamikutano na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Bandari na watuwengine haoni kama anawatenga wale wanakijiji au waleambao wanazitumia zile bandari na ambao wanaishi karibu

Page 27: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

27

na zile bandari na sasa pengine ingekuwa ni vizuri Serikaliikaenda kwa wahusika moja kwa moja kuzungumza naoikaangalia? Kuna athari pia za mazingira uchafuzi wamazingira ni mkubwa sana katika bandari hizi bubu. Ahsantesana.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, hii mikakati siyomirefu sana nimejaribu tu kuisoma kwa kirefu lakini siyo mirefusana. Ni mikakati mitatu tu maalum isipokuwa nimeileza kwaundani ndiyo maana inaonekana kama ni mikakati mirefuau ya muda mrefu.

Hata hivyo nadhani kitu cha kufahamu hapa nikwamba bandari bubu inaanzishwa katika maeneo ambayomaeneo ya karibu tu kuna bandari ambayo ni rasmi. Kwahiyo ni tabia ya watu kukimbia bandari rasmi na kujianzishiabandari bubu pembeni.

Kwa hiyo suala la kuahusisha walioanzisha bandaribubu tutalifanya katika maana ya kudhibiti, lakini siyo kwamaana ya kumshirika wakati yeye aliyeanzisha hiyo bandaribubu huku akijua kwamba anafanya makosa na anatafutafedha kwa njia ambayo siyo sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili, ni kweliwanaohudumia hizo bandari bubu kama nilivyosema niwatu ambao wamejianzishia uratatibu wao nje ya utaratibuwa Serikali na tutafanya kila njia kuhakikisha kwambatunawashirikisha katika kudhibiti lakini wakati wa kurasimishahata vile vijiji tunavyowapa mamlaka wanawatumia waleambao wana uzoefu wa kuendesha hizi bandari na hivyotukifanya hivyo masuala ya usafi na mazingira wa bandarihizo yatashughulikiwa kikamilifu.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Musukuma swali lanyongeza.

Page 28: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

28

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kuwa matatizo yaliyopo kwenyemwambao wa Pwani hayana tofauti sana na matatizoyaliyoko kule Geita. Mkoa wa Geita unayo bandari bubuinaitwa Nungwe ambayo inatumiwa na Mgodi wa GGMkushusha shehena kubwa.

Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari baada ya kumalizashughuli za Bunge afuatane na Wabunge wa Geita akalionelile eneo ili Serikali iweze kuipitisha kuwa bandari halali nawatumiaji wengine waweze kupita pale? (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano majibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru kwahiyo taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Musukuma kuhusu hiyobandari bubu ya Nungwe na niko tayari kufuatana naepamoja na Wabunge wengine wa Geita ili tukaiangalie hiyokwa undani na tuone kama ipo katika orodha ambayoinashughulikiwa na viongozi wa Mikoa wa Ziwa Victoriakatika kushughulikia suala la kudhibiti bandari bubu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Masoud swali la nyongeza.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru taarifa ya Serikali inaeleza kwamba katiya Dar es Salaam na Bagamoyo kuna bandari bubu 32. Serikalimuda wote imekuwa ikisema kwamba iko katika mikakatiya kuhakikisha kwamba bandari bubu hizi zinawezakudhibitiwa, lakini tatizo linaloendelea la kuingia kwenyenyaya za umeme, matairi ya magari fake pamoja na maziwaya watoto fake yanaendelea kuadhiri afya za binadamu namatukio mengine ya hapa na pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Wazirianaweza akawaambia nini Watanzania juu ya mkakati waziada kuhakikisha kwamba matairi ya magari fake, nyaya zaumeme, maziwa ya watoto fake yanadhibitiwa katika

Page 29: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

29

bandari bubu kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo? Naombamajibu ya haraka. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Unaomba majibu ya haraka au majibuya uhakika? (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZINAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli katikabandari bubu zilizoko katika mwambao wa Pwani kuanziaTanga hadi Bagamoyo na Kunduchi tuna kazi kubwa sanatunaifanya pale ya intelijensia pamoja na kazi ya kuhakikishakwamba chochote kinachotoka pale hakingii katika sokokabla hakijakamatwa na Serikali. Nadhani unakumbuka nimara nyingi tu tumeshika bidhaa mbalimbali zinazotokaupande wa pili kuingia upande huu mwingine wa nchi kwamaana inatoka Zanzibar kuingia huku kupitia hizi bandaribubu tumefanyakazi kubwa sana ya kuhakikisha kwambazinasimamiwa haziathiri soko la nchi yetu na pili, hawaletibidhaa ambazo ni fake kama ambavyo Mheshimiwa Mbungeamesema.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafanya kazi hiyo na kwakweli nichukue nafasi hii kuwapongeza sana vyombo vyaulinzi na usalama vya maeneo hayo kwa kazi kubwawanayofanya.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ajali Akbar.

MHE. AJALI R. AKBAR: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa matatizoyanayoikumba Tanga pamoja na Bagamoyo ya bandari bubuyanafanana sana na mpaka kati ya Newala na Msumbijiambapo wananchi wa Msumbiji wanakuja kutibiwa paleNewala. Ni lini sasa Wizara ya Ujenzi itakuja kufanya iwe rasmibadala ya kuwaachia polisi wale wananchi wanaokujakutoka Msumbiji wanakimbizana nao. Kwa nini sasa Wizaraikaja na ikarasimisha na ikawa ni rasmi? Naomba jibu lakoMheshimiwa Waziri.

Page 30: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

30

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukuefursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge ambayeametoa taarifa hii. Alitupa taarifa mapema na nimpe tutaarifa kwamba suala hili tumeanza kulifanyia kazi kwanguvu zote na matokeo yatakapokuwa tayari tutakujatumfahamishe.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Yosepherswali fupi.

MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante, tatizo la ongezeko la bandari bubu katika Mkoawa Tanga ni kutokana na uwezo mdogo wa Bandari ya Mkoawa Tanga. Je, Waziri anatuambia nini kuhusu kuboreshaBandari ya Tanga kwa maana ya kina na miundombinu iliongezeko hili la bandari bubu liweze kupungua? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, naombanimthibitishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tuna mradiambao sasa hivi unaendelea, unatarajiwa kukamilikakaribuni wa kuongeza kina katika lile eneo ambalo sasa hivitunalitumia. Vilevile unafahamu kwamba tuna nia pia yakuanzisha bandari kubwa zaidi ya Mwambani na kamasehemu ya mradi ule mkubwa wa kuhakikisha mizigo yakutoka Uganda inapita katika reli ile ya kutoka Tanga –Musoma na Bandari ya Mwambani. Mipango hii ya Serikali nithabiti na tumeanza kuitekeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hilo la kuongeza kinani karibuni tu mwezi ujao kazi hiyo itakuwa imekamilika.

Na. 320

Bodi ya Kusajili Makandarasi (CRB)

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA aliuliza:-

Serikali iliunda Bodi ya Kusajili Wakandarasi (CRB)

Page 31: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

31

ambayo ina jukumu la kusajili, kuratibu na kusimamiamwenendo wa makandarasi nchini.

(a) Je, tangu kuanzishwa kwa CRB ni wakandarasiwangapi Watanzania wamesajiliwa na taasisi hiyo?

(b) Je, Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya zinatumiavigezo gani kutoa kazi kwa wakandarasi?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ka niaba ya Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano napenda kujibu swali laMheshimiwa Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala, Mbungewa Nkenge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Bodi ya Usaji l i waMakandarasi tangu ilipoanzishwa mwaka 1997 imesajili jumlaya makandarasi wa Kitanzania 13,523. Kati ya makandarasihao, makandarasi 8,935 usajili wao uko hai na makandarasi4,578 wamefutiwa usajili kutokana na sababu mbalimbalizikiwemo kushindwa kulipia ada ya mwaka na kukiukataratibu nyingine zinazoongoza shughuli za ukandarasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vigezo vinavyotumiwa naSerikali katika utoaji wa zabuni kwa makandarasivinazaingatia matakwa ya Sheria ya Ununuzi wa Umma yamwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013. Vigezo hivyo nipamoja na kampuni kusajil iwa na Bodi ya Usajil i waMakandarasi, ukomo wa ukubwa wa kazi kulingana nadaraja la usajili, mahitaji maalum ya mradi husika, wataalam,vitendea kazi, uzoefu wa utekelezaji wa miradi ya aina hiyona uwezo wa ampuni kifedha wa kutekeleza mradi husika.(Makofi)

MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: MheshimiwaNaibu Spika, ahsante sana. Pamoja na ukweli kwambawakandarasi 13,000 ni kidogo sana ukilinganisha na idadi yaWatanzania, ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Page 32: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

32

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa kigezo kimojawapo kinachotumika kutoa kazi wanaangalia uzoefu wakufanya kazi hiyo hiyo kwa yule anayeomba na kwa kuwatumekuwa tukisisitiza kutoa ajira kwa vijana wetu, graduateswanapo-graduate tunawaambia waanzishe makampuni.

Swali la kwanza, je, vijana hawa wanapo-graduatekwenye vyuo vikuu wakaanzisha kampuni, wakiomba kaziwataweza kupata kazi kwa utaratibu huu? (Makofi)

Swali la pili, ukiangalia sifa mojawapo inayotumikakazi ni kwamba uwezo wa kifedha wa Mkandarasi lakiniuzoefu unaonyesha uwezo wa kifedha wa wakandarasi wetuni mdogo, wengine wanafutiwa hata kwa kushindwa kulipaada na wengine wanashindwa hata ku-access mabenki kwasababu ya utaratibu mbovu wa mabenki tulionao.

Je, Serikali haioni wakati umefika wa kuanzisha Benkiya Wakandarasi na kuboresha taratibu ili kuwezeshaWakandarasi wetu waweze kujikomboa na kupambana naumaskini. (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasatunawahamasisha graduates wa fani ya uhandisi pamojana ubunifu wa majenzi waanzishe kampuni na Serikali inawindow maalum. Tumeweka window maalum ya kuhakikishahawa watu tunawapa training, nadhani mfano utagunduapale Daraja la Mbutu tulifanya hivyo, hatukuzingatia uzoefubali tulifanya pale ya majaribio, vilevile barabara ya kuleBunda kwenda Serengeti nayo vilevile kuna kilometa 50tuliziweka kwa hawa Mbutu Joint Venture, tunaona kwambakumbe hilo linawezekana na ndani yao ameshajitokezamkandarasi mmoja sasa amepata uwezo mkubwa zaidi,Kampuni ya Mayanga ambayo sasa inajenga uwanja wandege wa Geita.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutalifanya hilona tutaendelea kulifanya lakini lazima tuzingatie sheria kwasababu tukienda kinyume cha sheria tutakwenda kinyume

Page 33: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

33

na kile ambacho tulikubaliana humu Bungeni. Tutatafuta kilaaina ya mwanya kujaribu suala hili za uzoefu lisitukwamishesana kuhamasisha wakandarasi wa kizalendo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala la uwezo wakifedha ni suala la wakandarasi wenyewe na nadhaniMheshimiwa Balozi Buberwa Kamala unafahamu kwambawakandarasi wana mpango huo wa kuanzisha benki yaona Serikali tutaendelea kuhamasisha mpango huo ukamilike.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cecilia Paresso swali lanyongeza.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa ni ukweli kwamba wakandarasi hapanchini pamoja na wazabuni mbalimbali ambao wamekuwawakitoa huduma kwa Serikali, wamekuwa wakiidai Serikalifedha nyingi na Serikali imekuwa hailipi kwa wakati.

Je, ni l ini sasa Serikali itahakikisha kwambawakandarasi hao wakimaliza kazi na wazabuni wakimalizahuduma wanazotoa waweze kulipwa kwa wakati bilakuhatarisha kazi ambazo wanafanya?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli wakatitunaingia tulirithi deni la shilingi trilioni 1.215 la makandarasi.Nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais pamojana Wizara ya Fedha wametuwezesha kati ya hizotumeshalipa shilingi bilioni zaidi ya 790, sasa hivi tumebakizadeni dogo sana katika yale madeni ya nyuma makubwa.Ingawa kwa kulipa madeni hayo, makandarasiwameendeleza kuongeza nguvu ya kuongeza kazi nawameongeza tena madeni mengine, lakini hayo madenimengine walau sasa hivi yanashughulikiwa kwa namnaambayo hayazalishi tena idle time ambayo ni fedha ambazotunalazimika kuzilipa wakati kazi haifanyiki kwa sababu tuya kuchelewa kulipa.

Page 34: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

34

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru kwamba sasasuala hilo halipo tena na kwa kweli tunaishukuru sana Serikaliya Awamu ya Tano kwa kazi hii, naomba mtupongeze natutaendelea kukamilisha deni l i l i lobakia il i hatimayewakandarasi hawa wasiwe tena na madeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine miradi yoteya wakandarasi wazalendo tumekuwa tukilipa kikamilifukabisa, huwa haichelewi kwa sababu tunajua uwezo waoni mdogo na kwa kulipa mara deni linapo-accrue lengo nikuwawezesha hawa wakandarasi wa kizalendo wawezekukua zaidi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Daniel Mtuka swali lanyongeza.

MHE. DANIEL E. MTUKA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo lanyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na tatizo kubwasana katika nchi hii hasa katika utekelezaji wa miradimikubwa, mkandarasi kupewa Mikoa zaidi ya miwili amamitatu. Jambo hili limekuwa likiifanya miradi kuchukua mudamrefu, kwa mfano miradi ya REA.

Je, hatuna wakandarasi wa kutosha kwa mfanokatika miradi ya REA ili kila mkoa uwe na mkandarasi mmojakuokoa muda? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa miradi ya REAkuna sababu maalum ya kufanya hivyo na imetokana nauzoefu wa nyuma. Lakini kimsingi katika miradi ya masualaya ujenzi iwe majengo, barabara au reli tunafuataqualificatio/sifa ambazo huyu mkandarasi amefuata na kwamujibu wa Sheria ya Manunuzi inavyotuongoza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tufuate hivyo,inawezekana kabisa mkandarasi wa Mkoa mwingine

Page 35: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

35

akapata kazi mkoa mwingine ni kitu cha kawaida kabisakama ilivyo mkandarasi wa nje ya nchi anapopata ndani yanchi yetu ni kitu cha kawaida kinachoangaliwa ni sifa yamkandarasi aliyeomba hiyo kazi na kwa mujibu wa taratibuza zabuni.

MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo lanyongeza.

Kwa kuwa swali la msingi limeongelea vigezo na kwakuwa Rais aliyepo madarakani wakati akiwa Waziri wa Ujenzi,aliweka kigezo kwamba kazi zinapotangazwa walaukampuni moja ya mwanamke ipate kazi ili kuwainuawanawake na jambo hilo kwa sasa linafifia.

Je, Mheshimiwa Naibu Waziri anaweza kutuambiaana mkakati gani wa kutoa walau waraka TANROADS naHalmashauri kwamba wanawake wanapopata kazi wame-qualify wapewe kazi hizo ili kuwainua wanawake? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru sanaMheshimiwa Munde kwa swali hili la nyongeza kwa sababuananipa fursa ya kuelezea nini Wizara yangu inafanya katikakuwainua wakandarasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nafahamu tuna mradimaalum wa kuhakikisha kwamba wakandarasi wanawakekwanza wanapatikana kwa sababu ili wapatikane kwanzalazima wajisajili na Bodi ya Usajili wa Wahandisi. Ndani yaBodi ya Usajili wa Wahandisi tuna programu maalum kwaajili ya wanawake tu na nashukuru wenzetu wa NORADwanatusaidia fedha kwa ajili ya kuhakikisha hawa wahandisiwanawake wanasajiliwa, wakishasajiliwa wanaanzishakampuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kawaida kampuni hizozinazoanzishwa na akina mama tunazilea kama nilivyosema,kila wanapopata kazi na wamekuwa wakipata kazi

Page 36: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

36

mbalimbali ingawa kwa sasa bado ni kampuni chachezilizoanzishwa kupitia njia hiyo na tutaendelea kuzihamasishanyingi zaidi zianzishwe. Kila wanapopata kazi wanalipwamalipo yao yote wanayostahili ili waweze kuendelea kukua,huwa hatuwaachii deni la aina yoyote katika wakandarasihawa wazalendo na hasa hawa wakandarasi akina mama.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaendelea,tutamalizia swali letu la mwisho Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa DevothaMathew Minja, Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swali lake.

Na. 321

Changamoto Zinazokabili Kazi za Wasanii

MHE. DEVOTHA M. MINJA aliuliza:-

Mchango wa kazi za wasanii umeonekana katikakutoa ajira lakini bado wasanii wanakabiliwa nachangamoto mbalimbali za kuhujumiwa kazi zao ambapoMheshimiwa Rais ametoa maagizo mbalimbali yakushughulikia watu wanaohujumu kazi za wasanii.

Je, mpaka sasa ni hatua gani zimechukuliwa?

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijajibu swali laMheshimiwa Devotha naomba kwa ruhusa yako nichukuenafasi hii kutoa taarifa fupi ya mafanikio ya mrembo AishaMabula ambaye tulimuona hapa hivi karibuni Bungeni,aliewezeshwa na Waheshimiwa Wabunge kushirikimashindano ya ulimbwende ya Miss World Super Model nchiniChina.

Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya washiriki walikuwa52 kutoka nchi mbalimbali duniani lakini kutoka Afrika ni

Page 37: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

37

wawili ambapo mmoja wao ni huyo Bi. Aisha Mabula naAisha Mabula alifanikiwa kuingia 14 bora kama fainali nakatika fainali hiyo alishika nafasi ya tisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hiikumpongeza Bi. Aisha kwa kuiwakilisha vizuri nchi yetu yaTanzania pamoja na Bara la Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekeekabisa niwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wenzangukwa moyo wenu wa ukarimu ambapo mlimchangia nakumuwezesha kushiriki katika mashindano hayo ya kiduniaambayo naamini kabisa mafanikio haya yatamuwezeshakupata ajira na kuendelea kuitangaza nchi yetu Kimataifana hasa katika sekta ya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya utangulizi huumfupi naomba sasa kwa niaba ya Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo napenda kujibu swali laMheshimiwa Devotha Mathew Minja, Mbunge wa VitiMaalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu kupitiaKamati ya Urasimishaji wa Kazi za Filamu na Muziki nchiniinayojumuisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Barazala Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) naChama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) hutoa miongozombalimbali kuhusiana na masuala ya ulinzi na kazi za sanaa.

Aidha, kwa kushirikiana na COSOTA Wizara kupitiaBASATA na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) hutoa copyrightclearance certificate kwa mmiliki wa kazi yoyote ya sanaakabla ya kupewa stempu ya kodi ya TRA. Lengo la stempuhizo ni kurasimisha sekta ya filamu na muziki katika uuzaji waCD, DVD, kanda na kadhalika na hivyo kukabiliana na hujumakatika kazi za wasanii.

Mheshimiwa Naibu Spika, pale ambapo sheria nataratibu za forodha na za kulinda hakimiliki zinakiukwa nahivyo kuathiri maslahi ya wasanii, Serikali huendesha

Page 38: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

38

operesheni za kukamata kazi hizo za sanaa zenye utata. Hadikufikia Machi 2017, Wizara ilifanya operesheni kubwa mbilina za kawaida sita dhidi ya filamu zinazoingia sokoni bilakufuata utaratibu ambapo jumla ya kazi 2,394,059zilikamatwa zikiwemo kazi za nje ya nchi 2,393,529 zenyethamani ya zaidi ya shilingi 3,590,293,500 na za ndani 530 zenyethamani ya shilingi 1,590,000.

Aidha, mitambo ya kufyatua kazi za fi lamu(duplicators) 19, printers za CD/DVD nane, DVD writers 31,kompyuta tatu na UPS saba zilikamatwa katika opereshenihizo.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyoeleza NaibuWaziri, kazi za wasanii ni kuburudisha, kuelimisha, kuonya nakukosoa, wasanii wamekuwa wakifanya kazi hizi hata wakatiwa kampeni tulishuhudia wasanii walivyofanya kazi yao vizurina wakati mwingine waliimba nyimbo za kuponda upinzanina mlikuwa mkishangilia. Jambo la kushangaza hivi sasawasanii wakiimba nyimbo za kukosoa Serikaliwanashughulikiwa na mfano mzuri ni Ney wa Mitego pamojana Roma Mkatoliki.

Swali la kwanza, je, ni wakati gani sasa kazi hizi zawasanii zinathaminika?

Swali la pili, kwa bahati mbaya sana Rais ametoamaagizo ya wale ambao wamehujumu kazi za wasanii nakuacha kabisa kuwawajibisha Serikali yake ambayoimeshindwa kabisa kuthamini kazi nzuri iliyofanywa naMarehemu Mzee Francis Ngosha ambaye amekufa akiwamaskini wa kutupwa.

Je, Serikali inataka kukamata kazi za wasanii wakatininyi wenyewe mmemuhujumu Mzee Francis Ngosha ambayempaka sasa hivi hana lolote, amekufa na hakuacha alamayoyote katika familia yake? (Makofi)

Page 39: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

39

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Devotha, naamini kwambasaa ya Mwongozo hutaomba Mwongozo kwamba maswaliyako hayajajibiwa kikamilifu, kwa sababu hakuna swali hatamoja kati ya hayo mawili linalotokana na swali lako la msingi.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, majibu.

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli maswali yakeyako nje kidogo na swali la msingi, lakini kwa sababu tu yakumbukumbu tulizonazo, swali lake la kwanza linaloulizakwamba ni wakati gani kazi za wasanii zinathaminiwa?Kama alivyosema mwenyewe, kwamba kazi ya sanaa nikuburudisha, kuelimisha, kuonya, kukosoa na kadhalika,niseme tu kwamba kazi za wasanii tunazithamini wakati wotehasa wakati zinapoelimisha, zinapoburudisha na kufanya kazizile ambazo zinalijenga Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kusemakwamba wasanii huwa wanashughulikiwa wakiikosoaSerikali, nimfahamishe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba kazihizi za sanaa zinasimamiwa na sheria. Tunayo Sheria ya BASATANamba 23 ya mwaka 1984, tuna Sheria nyingine Namba 4 yaBodi ya Filamu ya mwaka 1976 na tuna Sheria ya Hakimilikina Hakishiriki Namba 7 ya mwaka 1999. Kwa hiyo,tunachohitaji ili tuweze kuzithamini kazi hizi ni kwambawasanii wazingatie sheria, wafuate sheria na taratibu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa wasaniiambao tunaona kwamba wameenda kinyume, hatua huwazinachukuliwa na hatua zenyewe, kwa mfano kuna msaniimmoja anaitwa Nikki Mbishi ambaye alipewa tu onyokutokana na kuweka picha ya Rais Mstaafu wa Awamu yaNne katika wimbo wake I am sorry JK. Hizo ni hatua tuambazo huwa tunazichukua ili wasanii hawa wafuate sheria.Sheria ya BASATA inahitaji wasanii hawa wapitishe nyimbozao BASATA ili ziweze kukaguliwa kabla hazijatolewa.

Page 40: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

40

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wakiwawamepitia kule ina maana kwamba watatoa kitu ambachokinazingatia sheria na kinafuata maadili, sasa huu ni ukiukwajiwa maadili.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwingine ambayeameshawahi kupewa onyo ni Diamond kupitia kwa Menejawake, ambaye alitumia majina ya viongozi bila kufuatautaratibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Ney wa Mitego, huyualiimba wimbo wake wa Wapo ambapo ulifungiwa naBASATA kwa muda, lakini baadaye ulifunguliwa baada yakuwa na makubaliano ya jinsi ya kuuboresha huo wimbo.Huyo mwingine Roma, hakuna hatua ambayo imechukuliwana Serikali kwa mwaka huu kuhusu msanii huyo na ninadhanininyi ni mashahidi kwamba alijieleza yeye mwenyewe kwavyombo vya habari na Mheshimiwa Waziri pia alikuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili ambalolinamhusu Marehemu Francis Ngosha na MheshimiwaDevotha anadai kwamba Serikali imemhujumu, hii siyo kweli,hakuna hujuma. Kimsingi yapo majina mezani mpaka sasakama matatu hivi yanayohusiana na ubunifu wa nembotunayoitumia, ambayo ni nembo ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mpaka sasa badohaijajulikana ni nani hasa ambaye ni mbunifu wa nembo hii.Kwa sababu kwa mfano, yupo Marehemu ambayealishatangulia mbele za haki muda mrefu anayeitwa AbdallahFarhan wa Zanzibar, yeye vielelezo tayari vimeshakutwakatika kumbukumbu zake jinsi alivyokuwa akibuni nemboyetu ya Taifa, nembo ya Kenya pamoja na nembo ya OAUkipindi hicho alipokuwa akisoma Makerere University. Kwahiyo, yapo majina ambayo yanadaiwa kwamba yalishirikikatika kutengeneza nembo hii. Ninaomba sana… (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Susan Lyimo, tafadhali.Mheshimiwa Waziri, malizia majibu.

Page 41: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

41

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana wataalamwafanye kazi ya kutambua ni nani hasa ambaye alishirikikubuni. Kwa sababu Marehemu Francis yeye anajulikanakama ni mchoraji, lakini siyo mbunifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, labda niseme tu kwambalabda swali la Mheshimiwa Devotha Minja ni ishara ya wazikwamba kuna uhitaji mkubwa sana wa kuwa na orodha yawasanii na kazi ambazo wamezifanya na ni kitu ambachosasa hivi Wizara tumeanza kukifanya ili kusudi tuwe na orodhaya wasanii wote katika nchi yetu na kazi ambazowanazifanya ili mwisho wa siku utata kama huu usiwezekutokea tena. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Joseph Haule.

MHE. JOSEPH L. HAULE: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuuliza swalidogo la nyongeza.

Moja kati ya changamoto kubwa za wasanii waTanzania ni kuibiwa kazi zao, lakini pia kutonufaika na kazizao kwa sababu ya kazi hizo kutolindwa ipasavyo. Tunaonakuna upungufu mkubwa sana kwenye Sheria Namba 7 yamwaka 1999, Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Je, Serikali haioni kwamba huu sasa ni muda muafakawa kuileta sheria hii kwenye Bunge lako Tukufu tuwezekuibadilisha na kuirekebisha ili iweze kusaidia wasanii waTanzania waweze kupata haki zao, kwa sababu wengiwanakufa masikini, wanaibiwa kazi zao mtaani lakiniwanaowaibia tunawajua?

NAIBU SPIKA: Umeshaeleweka Mheshimiwa ProfesaJay, Mheshimiwa Naibu Waziri majibu. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NAMICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Hili sualatayari COSOTA imeshaliona, hii ni Sheria ya Hakimiliki na

Page 42: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

42

Hakishiriki. Kwa kuanzia imeanza kufanya utaratibu wakubadilisha kifungu namba 46. Kwa hiyo, mchakato huuunaendelea, tuwe na subira ili marekebisho yaweze kufanyikaikiwa ni pamoja na kanuni zake. Ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tumefikamwisho wa kipindi chetu cha maswali na majibu kwa sikuya leo. Matangazo yaliyopo mezani yanahusu wageni.

Tutaanza na wageni waliopo Jukwaa la Spika nahawa ni wageni 75 wa Wizara ya Nishati na Madini ambaoni Profesa James Mdoe ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu, tunayepia Engineer Dkt. Julian Pallangyo ambaye ni Naibu KatibuMkuu - Nishati, yupo pia Engineer Benjamin Mchwampakaambaye ni Kamishna wa Madini, yupo pia Engineer InnocentLuoga ambaye ni Kaimu Kamishna wa Nishati na Masualaya Petroli. (Makofi)

Pia wapo Wenyeviti wa Bodi kutoka taasisi zilizo chiniya Wizara hiyo, yupo Dkt. Alexander Kyaruzi ambaye niMwenyekiti wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), yupopia Profesa Sufian Bukurula ambaye ni Mwenyekiti wa Shirikala Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), yupo pia Dkt. GideonKaunda ambaye ni Mwenyekiti wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) na Dkt. Adelardus Kilangi ambaye ni Mwenyekiti waMamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA).(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, pia yupo vilevile BaloziAlexander Muganda ambaye ni Mwenyekiti wa Shirika laMadini la Taifa (STAMICO), yupo Profesa William Mwegohaambaye ni Mwenyekiti Chuo cha Madini, Profesa ShukraniManya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakala wa JiolojiaTanzania (GST), Dkt. Stephen Mdachi ambaye ni MwenyekitiWakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), yupopia Profesa Jamidu Katima ambaye ni Mwenyekiti waMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),yupo pia Ndugu Beatus Segeja ambaye ni Mwenyekiti waKampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) nahawa wameambatana na Wakuu wa Idara, Vitengo na

Page 43: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

43

Taasisi pamoja na Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini.(Makofi)

Wapo pia wageni wa Waheshimiwa Wabunge,wageni 31 wa Mheshimiwa Pauline Gekul ambao niWaheshimiwa Madiwani, Wajumbe wa Kamati ya Utendajiya Jimbo kutoka Babati Mjini, Mkoa wa Manyara, karibunisana. (Makofi)

Tunao pia wageni 66 wa Mheshimiwa Joseph Hauleambao ni wanafunzi 60 na walimu sita wa Shule ya MsingiKantui kutoka Ruaha, Mikumi Mkoani Morogoro. Karibunisana. (Makofi)

Tunao pia wageni waliotembelea Bunge kwa ajili yamafunzo ambao ni wanafunzi 21 kutoka Chuo Kikuu chaMzumbe, Tawi la Dar es Salaam. Karibuni sana wageni wetuBungeni. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, baada ya tangazo hilo,tutaendelea na shughuli zilizo mbele yetu. Katibu.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mwongozo wa Spika.

MWONGOZO WA SPIKA

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kasheku Musukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Nasimama kwa Kanuni ya 68(7) kwaruhusa yako. Kuna suala linaloendelea, nataka kupataMwongozo wako.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa Bungeni tumekuwatukipiga marufuku sana tabia za uhamasishaji hasa kwamasuala yanayohusiana na watoto, mambo ya mimba zautotoni na mambo mengine, lakini kuna tangazolinaendelea kwenye vyombo vya habari linasema jaza ujazwena katika li le tangazo amechorwa mtoto wa shule

Page 44: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

44

amewekwa pale juu ana mimba halafu hapa chiniyanaendelea matangazo yanasema jaza ujazwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili sisi tunaotoka kulevijijini hatujui vizuri Kiswahili cha Pwani, tunalitafsiri vibaya;na imekuwa lugha hata kwa watoto wa shule sasa kulemitaani wanasema nijaze nikujaze. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba Mwongozowako, kwa nini Serikali isipige marufuku maneno haya ya jazaujazwe? Hayaendani na utamaduni wa Kitanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, naombaMwongozo wako.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mussa Mbarouk.

MHE. MUSSA B. MBAROUK: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. Na mimi nimesimama kwa Kanuni ya 68(7) kwajambo lililotokea mapema hapa Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Naibu Waziri waHabari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akimjibu MheshimiwaDevotha Minja, lilizungumzwa suala la Marehemu MzeeNgosha aliyefariki katika Hospitali ya Muhimbili tarehe 28 Mei.Sasa naomba Mwongozo wako kujua, pamoja na kwambahadi leo kwanza kwa masikitiko makubwa, Serikali haijuimpaka leo aliyetuchorea nembo ya Taifa ni nani na piampaka leo hii sisi Tanzania hatuna Vazi Rasmi la Taifa, naombaMwongozo wako. Je, Serikali ina mpango gani wa kuisaidiaau kuifanyia nini familia ya Mzee Ngosha ili ibaki kamakielelezo kwa kuwa inasadikika kwa maelezo yakemwenyewe yule Mzee Ngosha alisema alianza kubuni nemboya Taifa mwaka 1957 akiwa katika mashamba ya MkongeMkoani Tanga?

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, vilevile Serikali imejifunzanini katika kuwaenzi watu maarufu na mashuhuri hapaTanzania ili yasije yakajitokeza matatizo na kasoro kamakwenye suala la Mzee Ngosha? Ahsante.

Page 45: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

45

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waitara.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mwongozo wa Spika.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Ninasimama kwa Kanuni ya 68(7).

Mheshimiwa Naibu Spika, nina jambo ambalo natakaunisaidie kunipa Mwongozo wako kwa sababu inawezaikatugombanisha na sisi hasa upande wa Upinzani hapa;inaonesha kwenye kumbukumbu zenu kutoka kwenye Kitichako hapo kwamba mimi kwenye hili Bunge nimechangiamara tatu.

Mimi nimechangia mara mbili, siyo mara tatu nakitendo cha kuongeza siku ya kuchangia kinanifanya kwenyeWizara kama ya leo muhimu sana ambayo nimejipangamwezi mzima kuchangia, sitapata nafasi kwa sababutunaangalia umechangia mara ngapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, i l i kuepukakutugombanisha, sisi na viongozi wetu wa Kambi ya Upinzanihapa, ni muhimu nipate Mwongozo wako. Miminimechangia dakika kumi kwenye Wizara ya Elimu na dakikatano ambazo niliomba heshima ya Kiti nikachangia Wizaraya Ardhi. Sikuchangia tena, ila kama niliomba Mwongozoukabadilishwa kwamba nil ichangia, ndiyo naombaMwongozo wako ili uweze kunisaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, yangu ni hayo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mtolea na wa mwishoatakuwa Mheshimiwa Catherine Magige.

MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kuniona. Nasimama kwa Kanuni hiyo hiyoya 68(7).

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Orodha ya Shughuliza Bunge za Leo kwenye Hoja za Serikali, leo tutajadili hotuba

Page 46: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

46

ya Wizara ya Nishati na Madini na ukirudi kwenye ratiba mpyakabisa iliyotolewa tarehe 24 Mei, 2017, inaonesha kwambasiku ya Alhamisi tarehe 1 Juni yaani leo mpaka Ijumaa ndiyoutakuwa huo mjadala wa Nishati na Madini unaendelea.Ukishuka chini ya hii ratiba imeandikwa pia siku ya Ijumaa,tarehe 2 Juni Ijumaa hiyo hiyo ambayo ipo kwenye Nishatina Madini inarudiwa tena kwamba mpaka JumatanoKamati ya Bajeti itakuwa inakaa na Serikali kujadili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hii ratiba iko sahihi,naomba Mwongozo wako kwamba je, huu mjadala waWizara ya Nishati na Madini utakuwa ni wa siku mbili au wasiku moja na nusu? Kwa sababu tunapanga wachangiajikutokana na uwiano ule wa vyama, kwa hiyo, tunafahamukama mjadala ni wa siku moja sisi hapa tunakuwa na dakika10, lakini kama ni wa siku mbili maana yake tunakuwa nadakika 40.

Sasa kama siku ya Ijumaa ina majukumu mawilitofauti, maana yake itatuvuruga pia katika kupangawachangiaji. Vilevile shughuli ya Kamati ya Bajeti kukaa naSerikali ni takwa la Sheria ya Bajeti ambayo inataka ni lazimaziwe siku sita. Sasa ukiitoa hiyo Ijumaa maana yake zile sikusita hazitimii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naombaMwongozo wako hapa, hii ratiba ikoje ili tuweze kujipangavizuri? Nakushukuru.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Catherine Magige.

MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba Mwongozo wako. Wiki i l iyopita kunaMwongozo ulitolewa hapa Bungeni na Mwenyekiti,Mheshimiwa Zungu ndiye alikuwepo hapo kwenye Kiti naakasema kuwa Mwongozo huo utatolewa maamuzi na Kiticha Spika, lakini hadi sasa hivi ni kimya. Mwongozo huounahusu Shule ya Butwa iliyopo Geita ambapo tulipotezawatoto watatu, boti ilizama. Mpaka sasa hivi ni wiki ya piliwatoto hawaendi shule wala hawajui hatma yao ni nini?

Page 47: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

47

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama wazazi, naombaWaheshimiwa Wabunge, nimeulizia boti ni shilingi milioni 15tu, ikiwezekana, hata tukatwe kwa siku shilingi 30,000 kilaMbunge ili watoto wale waweze kununuliwa boti ile. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mwongozo wako.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nimeombwaMwongozo na Mheshimiwa Joseph Kasheku Musukumakuhusu tangazo ambalo limesikika ama kuonekana katikavyombo vya habari na kwa maelezo ya MheshimiwaMusukuma anaomba Mwongozo kwa Kanuni ya 68(7) naametoa maelezo ambayo sina haja ya kuyarudia juu yamaneno yanayotumika katika tangazo la simu amamatangazo ya simu ama makamupuni ya simu. Wakatiakimalizia kuomba Mwongozo wake, amesema kwa niniSerikali isipige marufuku tangazo kama hilo?

Waheshimiwa Wabunge wote tunaelewa zipochangamoto mbalimbali, kimsingi hili jambo kwa mujibu waKanuni aliyotumia Mheshimiwa Musukuma siyo jambolinaloweza kuombewa mwongozo Bungeni kwa sababuhalijatokea hapa ndani. Hata hivyo kwa sababu hilotanganzo pengine lipo kwa wale walioliona ama kulisikia,ziko namna mbalimbali ambazo matangazo menginehutolewa pengine siyo na kampuni husika, lakini ni kwa ajiliya uchafuzi. Sasa Bunge lisije likaingizwa katika mazingiraambayo tangazo linahusishwa na kampuni fulani ikaonekanakampuni hiyo ndiyo iliyotengeneza tangazo. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, yapo mazingira mbalimbalinanyi ni mashahidi, makampuni yanayogombana amayanayokuwa mahasimu hasa kwenye eneo la dawa,wanatoa matangazo kwamba dawa hii ina madhara hayakwa sababu dawa hiyo inatoka kiwanda fulani naMheshimiwa Waziri wa Afya amekuwa akiwasiliana na TFDAkila wakati kutoa ufafanuzi.

Kwa hiyo, hata hili aliloomba Mheshimiwa Musukumatuwe makini katika kuyaangalia haya mambo, lakini hata

Page 48: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

48

hivyo TCRA iwe inatazama haya mambo kwa haraka. KamaKampuni haijatoa hilo tangazo, yule aliyelianzisha achukuliwehatua ili kuzuia matangazo kama hayo ya kuchafulianabiashara, kwa sababu wote tunajua katika biashara yakomambo mengi.

Kwa hiyo, upande wa Serikali, TCRA iliangalie jambohilo kama ni kweli na limeleta taabu katika jamii lifanyiwekazi kwa haraka ili lisilete mkanganyiko uliopo.

Vile vile nimeombwa pia mwongozo wa pili naMheshimiwa Mussa Mbarouk kwa mujibu wa Kanuni ya 68(7).Mheshimiwa Mbarouk wakati akieleza ametoa maelezokuhusu swali la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa DevothaMinja kuhusu Marehemu Ngosha na kwamba anasikitikaSerikali haimjui mtengeneza nembo na pia akauliza hapomaswali mawili kwamba Serikali ina mpango gani wakutunza familia ya Marehemu Ngosha na pia Serikaliimejifunza nini katika kutunza kumbukumbu?

Waheshimiwa Wabunge, haya ni maswali ambayoMheshimiwa Mussa Mbarouk ana uwezo wake yeye kuiulizaSerikali ili imjibu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbarouk hayo nimaswali ambayo unapaswa kuiuliza Serikali na siyo Kiti ili kitoemwongozo. Ni Serikali ndiyo inayopaswa kujibu na weweunajua utaratibu wa namna ya kuiuliza Serikali. Aidha,unapeleka swali lako la msingi ili upate nafasi ya kuliulizakikamilifu ama swali la namna hiyo likitokea, basi utaliulizakama nyongeza ili Serikali ikupe majibu na siyo Kiti ndiyokikupe mwongozo.

MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN: (Hapa hakutumia kipazasauti).

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Yussuf, tafadhali!

Waheshimiwa Wabunge, pia nimeombwamwongozo na Mheshimiwa Mwita Waitara akizungumzakuhusu michango ya leo na kwamba yeye katika karatasiambayo imetayarishwa na upande wa Ofisi ya Bunge

Page 49: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

49

inaonesha kwamba amechangia mara tatu, lakini yeyekachangia mara mbili tu na ana hofu kwamba anawezaasipate nafasi katika chama chake kwa sababukumbukumbu zinaonesha amechangia mara tatu badalaya kuonesha amechangia mara mbili ili apewe fursa yakuchangia leo.

Waheshimiwa Wabunge, kwanza ujumbe huoMheshimiwa Waitara alishaniletea, na mimi nimeshapelekaili Ofisi iweze kuangalia ameshachangia mara ngapi, maanawakati mwingine hata sisi wenyewe Wabunge tunasahautumechangia mara ngapi ikiwa ni pamoja na hata maswalihuwa tunasahau kwamba tumeshauliza mara ngapi?

Kwa hiyo, Ofisi itaniletea hapa majibu nami nitatoataarifa ka chama chake kwamba amechangia mara ngapi.Lakini na vyama navyo viangalie namna nzuri ya kuwekawachangiaji kwa sababu Waheshimiwa Wabunge wavyama vyote vilivyoko humu Bungeni wanayo malalamiko.

Kwa hiyo, ma-Chief Whip wa vyama hivi waangalienamna nzuri ya kuweka wachangiaji ili kusiwe na hayamalalamiko yanayotokea kwamba wengine wanachangiana wengine hawachangii. Kwa hiyo, Chama cha CHADEMAkitapokea taarifa nikishapata kutoka ofisini, sasa mtaamuakama mtampa nafasi ama hamumpi nafasi.

Mwongozo mwingine nilioombwa ni kutoka kwaMheshimiwa Abdallah Mtolea ambaye ameomba kuhusuorodha ya shughuli za leo ambapo ratiba aliyonayoinaonesha shughuli inayoanza leo yaani mjadala wa Wizaraya Nishati na Madini utakuwa leo na kesho naye anaulizakwamba ikiwa ni leo na kesho kwa mujibu wa ratibaambayo ilikwishatolewa mapema, basi siku sita ambazo nimatakwa ya kisheria ya bajeti, Kamati ya Bajeti itashindwakufanya kazi yake kisheria, kwa maana ya kwamba itafanyakazi pungufu ya siku sita ikiwa haitaanza kesho na kwa kuwakesho ratiba inaonesha kwamba tutaendelea na Wizara yaNishati na Madini, basi yeye ana wasiwasi huo.

Page 50: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

50

Sasa kwa kuwa ameomba mwongozo wa Kiti,Mheshimiwa Mtolea usiwe na wasiwasi juu ya hilo, Bunge hililinapenda kufuata sheria, kwa hiyo, siku ya kesho itapangwakwa namna ambayo Sheria ya Bajeti haitapungukiwamatakwa yake na kwa hiyo, tutaianglia hiyo orodha yakesho itaonesha namna nzuri ambayo tutalifanya hilo sualaambalo linatakiwa kisheria la kuwa la siku sita ambazozitaanza kuhesabiwa kuanzia kesho. Kwa hiyo, orodha yamatukio mtaiona kwenye orodha ambayo ni ya kesho sasana siyo ya leo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mtolea usiwe nawasiwasi, Bunge halina mpango wa kuvunja Sheria ya Bajeti.

Waheshimiwa Wabunge, pia nimeombwamwongozo wa mwisho na Mheshimiwa Catherine Magigeambaye ameeleza kuhusu watoto watatu waliozama waShule ya Butwa na kwamba mpaka sasa watoto hawawaliobaki sasa wanashindwa kwenda shule kwa sababu botiwaliyokuwa wakisafiria inaonekana haiko salama kwa ajiliya kuvusha watoto kwenda shule na kuwarudisha na wakatiakiendelea kuomba mwongozo huo ametoa maelezokwamba leo siyo siku ya kwanza kuomba mwongozo huu,ulishaombwa wiki iliyopita na maelezo yakatolewa kwambaMheshimiwa Spika atatoa mwongozo juu ya jambo hilolifanywe vipi.

Mheshimiwa Catherine Magige ameendelea na kutoamapendekezo kwamba Waheshimiwa Wabunge tukatweshilingi 30,000 ili boti ambayo kwa taarifa aliyoitoa inayouzwashilingi milioni 15 iweze kununuliwa na watoto hawa wawezekwenda shule. Pamoja na mambo mengine, imekuwepomiguno mingi sana humu ndani baada ya kusikia pendekezohili la kukatwa shilingi 30,000.

Waheshimiwa Wabunge, kwa kuwa mwongozoulishatolewa na Mheshimiwa Zungu kwamba MheshimiwaSpika atatoa maelezo, basi mwongozo huu ulioombwa naMheshimiwa Catherine Magige ni wa kukumbusha Kiti kuhusumwongozo unaosubiriwa aliokuwa ameahidi MheshimiwaZungu. Kwa hiyo, utafanyiwa kazi na majibu yataletwa.(Makofi)

Page 51: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

51

Waheshimiwa Wabunge, baada ya hayotunaendelea, Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishatina Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa niaba ya Waziri wa Nishati naMadini. (Makofi)

WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI -K.n.y. WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Mheshimiwa NaibuSpika, kwanza naomba ruhusa yako kulingana na ukubwawa kitabu hiki basi hotuba yetu yote kama ilivyo kwenyekitabu iingie kwenye Kumbukumbu Rasmi za Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ombi lingine naombauniruhusu nichukue fursa hii kuwatakia funga nzuri, yenyerehema ndugu zangu wote waislamu waliofunga Tanzaniana duniani kote na hasa Jimbo la Muleba ya Kaskazini.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia taarifailiyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, naomba kutoahoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadilina kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha wa2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema sisi WaheshimiwaWabunge wote na hivyo kutuwezesha kuendelea nautekelezaji wa majukumu yetu ya Kitaifa ndani na nje yaBunge.

Page 52: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

52

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii kwa dhatikuwapongeza viongozi wetu wote wa Kitaifa kwa jinsiwanavyojituma katika kutatua matatizo na changamotombalimbali za Taifa letu na hatimaye kuwaletea wananchimaendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya kipekeenitumie fursa hii kumshukuru na kumpongeza MheshimiwaDkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Serikali yake kwa jinsianavyochukua hatua za kusimamia na kulinda rasilimali zaTaifa hasa Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba pia kumpongezaMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kazi yake nzurianayoendelea kuifanya tangu alipoteuliwa. Aidha,nampongeza Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim MajaliwaMajaliwa kwa jinsi anavyoendelea kusimamia shughuli zaSerikali kwa nguvu zake zote. Tuwaombee wote MwenyeziMungu ili waendelee na kasi hiyo na hatimaye nchi yetu iwezekupiga hatua za kimaendeleo kwa kasi kubwa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakupongeza wewe binafsi,Mheshimiwa Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wote waKamati mbalimbali za Kudumu za Bunge lako Tukufu pamojana watendaji wa Ofisi ya Bunge kwa jinsi mnavyoliendeshaBunge letu Tukufu kwa ufanisi mkubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe shukurani za kipekeepia kwa Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko, Mwenyekiti waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini; naMheshimiwa Deogratias Francis Ngalawa, MakamuMwenyekiti wa Kamati hiyo. Aidha, nawashukuru Wajumbewote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madinikwa maoni na ushauri wao waliokuwa wakiutoa katikautekelezaji wa shughuli za Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hiikuwapongeza Waheshimiwa wote walioteuliwa katika

Page 53: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

53

kipindi hiki na kupata Ubunge. Kwa namna ya kipekeenimpongeze Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudikwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Sheria na Katiba.Nawapongeza pia Waheshimiwa Wabunge wotewaliochaguliwa kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la AfrikaMashariki na ni matarajio yetu kuwa watatuwakilisha kwaufanisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakupa pole wewe binafsi,Mheshimiwa Spika na Bunge lako Tukufu kwa kumpotezamwenzetu, Marehemu Samuel Sitta aliyekuwa MbungeMstaafu wa Jimbo la Urambo Magharibi, Spika Mstaafu waBunge la Tisa na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Vilevile nitoepole kwa Bunge lako Tukufu kwa kuwapoteza MheshimiwaHafidh Ali Tahir, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani -Zanzibar pamoja na Mheshimiwa Elly Marko Macha, Mbungewa Viti Maalum wa CHADEMA. Pia natoa pole nyingi kwawazazi, walezi, ndugu na familia za wanafunzi waliopataajali kule Arusha. Naungana na Waheshimiwa Wabungewote wenzangu kutoa pole kwa familia za Marehemu nakumwomba Mwenyezi Mungu azilaze roho za Marehemumahali pema peponi. Amen.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayoya awali, naomba sasa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji washughuli za Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedhawa 2016/2017 pamoja na makadirio ya mapato na matumizikwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa shughuli kwamwaka 2016/2017 pamoja na mpango wa bajeti wa2017/2018. Maeneo yaliyopewa Kipaumbele kwa mwaka wafedha wa 2016/2017 katika sekta ya nishati ni pamoja nakuimarisha uzalishaji, usafirishaji na kuongeza kasi yausambazaji wa umeme nchini, kuendelea na utekelezaji wampango wa kuboresha sekta ndogo ya umeme, kuendelezanishati jadidifu, kuvutia uwekezaji katika sekta ya nishatihususan kwenye uzalishaji wa umeme na katika utafiti wamafuta na gesi asilia. Aidha, Wizara ilifanya mapitio (updates)ya PSMP 2016 kwa lengo la kutumia vyanzo vya nishati

Page 54: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

54

vilivyopo nchini ambapo gesi asilia itachangia asilimia 40,makaa ya mawe yamepangwa kuchangia asilimia 35,umeme wa maji tunalenga kuchangia asilimia 20 na vyanzovingine asilimia tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Wizara ilitoakipaumbele katika ukusanyaji wa mapato ya Serikaliyatokanayo na rasil imali za madini, kuwaendelezawachimbaji wadogo na wa kati wa madini, kuhamasishashughuli za uongezaji thamani za madini, kuendelea nautafutaji wa graphite na madini mengineyo yanayohitajikakatika teknolojia za kisasa na kuimarisha ufuatiliaji na ukaguziwa afya, usalama, mazingira na uzalishaji wa madini katikamigodi midogo, ya kati na mikubwa. Sambamba na hayo,Wizara iliweka msisitizo katika kuwajengea uwezo watumishikatika fani mbalimbali na pia kusimamia, kufuatilia nakuboresha sera, sheria, kanuni, mipango na miongozombalimbali ili kuboresha ufanisi na tija katika sekta ya nishatina madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedhawa 2017/2018 Wizara itaendelea kutekeleza maeneo yavipaumbele mbalimbali yakiwemo kuimarisha uzalishaji,usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini; kuimarishaukusanyaji wa na mapato ya Serikali yatokanayo na rasilimaliza gesi asilia na madini; kusimamia uingizaji, utunzaji nausambazaji wa mafuta nchini; kuwezesha uwekaji wamtandao wa usambazaji wa gesi asilia viwandani namajumbani pamoja na uendelezaji wa mradi wa kusindikagesi asilia (LNG).

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Wizara piaitatekeleza maeneo mengine mapya ambayo ni pamoja nakuendeleza utekelezaji wa mradi mkubwa wa ujenzi wabomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga,Tanzania; ujenzi wa bomba la mafuta safi kutoka Dar esSalaam, Tanzania hadi Ndola, Zambia; kukamilishamazungumzo kuhusu ujenzi na upatikanaji wa gesi asiliakwenye viwanda vya mbolea vinavyotarajiwa kujengwakatika maeneo ya Kilwa Masoko, Lindi na Mtwara na

Page 55: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

55

kuendelea na utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhamiaDodoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Nishati na Madinikatika mwaka wa fedha wa 2016/2017 ilipanga kukusanyajumla ya shilingi bilioni 330.68. Hadi kufikia mwisho wa mweziMachi, 2017 Wizara ilikusanya jumla ya shilingi bilioni 266.21sawa na asilimia 72. Katika mwaka wa fedha 2017/2018,Wizara inatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 727.50sawa na ongezeko la asilimia 96.3 ikilinganishwa na mwaka2016/2017. Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwamapato yatokanayo na mauzo ya gesi asilia ambayo mwaka2017/2018 yanakadiriwa kufikia shilingi bilioni 477.36ikilinganishwa na shilingi bilioni 115.13 kwa mwaka 2016/2017.Hii ni kutokana na kukamilika kwa bomba la gesi ambapoviwanda vingi vinatarajia kuunganishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti iliyopitishwa kwa ajiliya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka 2016/2017 ni jumla yashilingi trilioni 1.122 ambayo inajumuisha fedha za miradi yamaendeleo shilingi trilioni 1.056, sawa na asilimia 94 ya bajetiyote. Bajeti ya Matumizi ya Kawaida ilikuwa shilingi bilioni66.23 sawa na asilimia sita. Hadi kufikia tarehe 25 Mei, 2017Wizara ilishapokea jumla ya shilingi bilioni 591.39 sawa naasilimia 52.71.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Wakalawa Nishati Vijijini (REA) hadi kufikia tarehe 25 Mei, 2017ulikuwa umepokea jumla ya shilingi bilioni 448.87 sawa naasilimia 76.39 ya bajeti yake kwa mwaka 2016/2017.Sambamba na hatua hiyo, Wizara imeendelea kusimamiakwa umakini mkubwa matumizi ya fedha za umma nakulingana na ukaguzi uliofanywa na PPRA katika kipindi chamwaka 2015/2016 Wizara ya Nishati na Madini imekuwamiongoni mwa Wizara tatu bora kwa kupata alama yaasilimia 88.85. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa 2016/2017Wizara ilitekeleza mipango na shughuli mbalimbali kamaifuatavyo:-

Page 56: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

56

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni mpangokabambe wa uendelezaji wa sekta ndogo ya umeme namatumizi ya gesi asilia. Mwezi Desemba, 2016 Serikaliilikamilisha mapitio ya mpango kabambe wa uendelezaji wasekta ndogo ya umeme. Mpango huo umebainishautekelezaji wa miradi ya uzalishaji na usafirishaji wa umemekatika kipindi cha muda mfupi, kati na mrefu. Mpango huoumezingatia ukuaji wa mahitaji ya umeme nchini, gharamanafuu ya uwekezaji na uchangiaji wa vyanzo mbalimbali vyanishati (energy mix).

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara pia imeandaa rasimuya mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia (NaturalGas Utilization Master Plan) chini ya ufadhili wa Shirika laMaendeleo la Kimataifa la Japan (JICA). Mpango huuunatoa mwongozo kuhusu matumizi bora ya gesi asiliapamoja na uboreshaji wa miundombinu ya gesi asilia. Aidha,mpango huu unatekelezwa kwa kipindi cha miaka 30 kuanzia2017 hadi 2046 ambapo jumla ya futi za ujazo trilioni 18.7 zagesi asilia zimepangwa kutumika kwa ajili ya matumizi yasoko la ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea najitihada za makusudi za kuongeza Idadi ya wananchiwanaopata huduma ya umeme nchini. Hadi kufikia Machi,2017 idadi ya wananchi waliofikiwa na huduma ya umeme(overall electricity access level) imefikia asilimia 67.5kulinganisha na asilimia 40 iliyofikiwa mwezi Aprili, 2016.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, idadi ya wananchiwanaopata huduma ya umeme (urban electricity accesslevel) imefikia asilimia 97.3 ikilinganishwa na asilimia 63.4iliyofikiwa mwaka 2014/2015, wakati wanaopata hudumaya umeme vijijini (rural electricity access level) imefikia asilimia49.5 ikilinganishwa na asilimia 21 ya mwaka 2014/2015.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Machi,2017 idadi ya wananchi waliounganishiwa umeme (overallelectricity connection level) imefikia asilimia 32.8 ikilinganishwana asilimia 30 ya mwaka 2015/2016. Aidha, idadi ya wananchi

Page 57: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

57

waliounganishiwa umeme mijini (urban electricity connectionlevel) imefikia asilimia 65.3 wakati waliounganishiwa umemevijijini (Rural electricity connection level) imefikia asilimia 16.9

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mipango yakuongeza uzalishaji wa umeme nchini, Wizara imeendeleana utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo Kinyerezi Imegawatts 240, Kinyerezi I extension megawatts 185 na Mradiwa Rusumo megawatts 80.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi huu wa Rusumo waMW 80, Tanzania itapata MW 26.6. Katika kuendelea nautekelezaji wake, wakandarasi walisaini mkataba tarehe 9Novemba, 2016. Aidha, malipo ya awali kwa Wakandarasi,kiasi cha dola za Marekani milioni 16.3 sawa na takribanishilingi bilioni 37.67 yamefanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, uzinduzi rasmi wa kuanzaujenzi huo (ground breaking ceremony) ulifanywa na Mawaziriwanaosimamia masuala ya nishati wa nchi za Tanzania,Rwanda, Burundi, pamoja, Maafisa kutoka Benki ya Duniana Benki ya Afrika walihudhuria shughuli hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na miradi hiyo,Serikali pia ipo katika hatua mbalimbali za maandalizi yautekelezaji wa miradi mingine ya uzalishaji umeme ikiwemoMradi wa Malagarasi MW 45, Mradi wa Kakono (Kagera)MW 87, Mradi wa Somanga Fungu (Lindi) MW 300, Kinyerezi IIIMW 600 na Kinyerezi IV MW 330, Mradi wa Mtwara MW 300,Mradi wa Kiwira MW 200 na Miradi ya uzalishaji ya sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wamiundombinu ya usafirishaji umeme, Serikali imeendelea nautekelezaji wa miradi ya kimkakati ambayo ni pamoja naMradi wa Msongo wa KV 400 kutoka Iringa hadi Shinyangaambao ulikamilika mwezi Desemba, 2016. Mradi wa Msongowa KV 220, kutoka Makambako hadi Songea, Mradi wa Njiaya Umeme ya Msongo wa KV 400 wa Singida, Arusha,Namanga.

Page 58: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

58

Aidha, miradi mingine ya usafirishaji umemeitakayoendelea kutekelezwa kwa mwaka 2017/2018 nipamoja North - West kutoka Mbeya – Sumbawanga –Mpanda – Kigoma – Nyakanazi wa KV 400; Mradi wa North -East kutoka Kinyerezi hadi Arusha kupitia Chalinze na Segerawa KV 400, Somanga Fungu hadi Kinyerezi KV 400, Rusumohadi Nyakanazi KV 220 pamoja Bulyanhulu hadi Geita KV 420.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendeleakutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini awamu ya pilina kuanza awamu ya tatu ya miradi hiyo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako, hapondiyo niwaombe Waheshimiwa Wabunge mnapochangia,kumbuka kuandika vijiji vyenu ambavyo havijapata umemekusudi kwa mamlaka niliyonayo leo niweze kuwakumbuka.(Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi Kabambe waKusambaza Umeme Vijijini awamu ya pili (REA Turnkey PhaseII); katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Serikali kupitia REAimekamilisha kazi ya ujenzi wa vituo sita vya kuongeza nguvuya umeme kutoka msongo KV 11 hadi KV 33 katika miji yaKasulu, Kibondo, Kigoma, Mbinga, Ngara na Tunduru; ujenziwa kusambaza umeme wa msongo wa KV 33 zenye urefuwa kilometa 17,740; ujenzi wa vituo vidogo vya kupoozeana kusambaza umeme 4,100 na ujenzi wa njia ndogo yausambazaji umeme zenye urefu wa kilomita 10,970.

Hadi kufikia mwezi Machi, 2017, wateja wa awali153,821 waliunganishiwa umeme sawa na asilimia 62 ya lengola kuwaunganishia wateja 250,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kazi ya kuunganishiaumeme kwenye Makao Makuu ya Wilaya 13 za Busega,Buhigwe, Chemba, Itilima, Kakonko, Kalambo, Kyerwa,Mkalama, Mlele, Momba, Nanyumbu, Nyasa na Uvinzazimekamilika na kufanya jumla ya Makao Makuu ya Wilayazinazopata umeme kupitia REA kufikia 25.

Page 59: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

59

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi kabambe waKusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu na hapo ndiyopa kushika kalamu hapo!

Mheshimiwa Naibu Spika, maandalizi ya mradi wakusambaza umeme vijijini awamu ya tatu yamekamilika nautekelezaji unaanza. Mradi huu ni wa miaka mitano kuanzia2016/2017 hadi 2020/2021. Mradi unahusisha kuongeza wigowa usambazaji umeme kwenye maeneo yaliyofikiwa namiundombinu ya umeme (densification); kufikisha umeme wagridi kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa na umeme (gridextension); na miradi ya umeme ya nje ya gridi (off-grid)utokanao na nishati jadidifu, hasa umeme jua (solar power).

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zilizofikiwa kwa sasani pamoja na kusainiwa mikataba na kuanza utekelezaji waawamu ya kwanza ya mradi wa densification mweziDesemba, 2016 na pia kukamilika taratibu za ununuzi naupatikanaji wa wakandarasi na kusambaza umeme kwenyevijiji vilivyo kwenye mkuza wa njia ya kusafirisha umeme wakutoka Iringa hadi Shinyanga.

Aidha, uchambuzi wa maoni maombi 300 yakusambaza umeme wa nishati jadidifu kwa vijiji vilivyo njeya gridi ya Taifa umekamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na miradi hiyoya REA, Serikali imeendelea kutekeleza miradi mingine yausambazaji nchini. Miradi hiyo ni pamoja na mradi wakuboresha mfumo wa huduma za umeme pamoja na njiaya usambazaji umeme kwenye Mikoa ya Arusha, Dar esSalaam, Kilimanjaro na pia katika Miji ya Ngara, Biharamulona Mpanda na katika maeneo mengine nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nilihakikishie Bungelako Tukufu kuwa Wizara yangu itaendelea kusimamia kwaweledi na ufanisi miradi yote ya uzalishaji, usafirishaji nausambazaji wa umeme ili kufikia azma ya Tanzania kuwanchi ya viwanda.

Page 60: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

60

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirudie sentensihiyo. Naomba nilihakikishie Bunge lako Tukufu kuwa Wizarayangu itaendelea kusimamia kwa weledi na ufanisi miradiyote ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme ilikufikia azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Neno nchiya viwanda iko bolded.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi hiki Serikaliimeendelea kuendeleza rasilimali za mafuta na gesi asiliakatika maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, utafutaji wa mafuta na gesiasilia; kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/2017 utafitiwa mafuta na gesi asilia umeendelea kufanyika katikamaeneo ya baharini na nchi kavu ambapo hadi kufikia sasakiasi cha futi za ujazo TCF tril ioni 57.25 za gesi asiliazimeshagundulika nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuongeza matumizi yagesi asilia nchini, jumla ya viwanda 42 tayari vimeunganishwana miundombinu ya gesi asilia. Katika mwaka 2016/2017,Serikali imeendelea kutafuta wateja wapya na kuendelezaujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia. Majadilianokati ya TPDC na Dangote Cement Tanzania Limited ya Mtwarayamekamilika kwa ajili ya kupata gesi asilia.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Kiwanda chaGoodwill Ceramic Tanzania kil ichopo Mkurangakimeunganishwa tayari na kuanza kutumia gesi asilia.Majadiliano yanaendelea kati TPDC na viwanda vya BakhressaFood Factory, Knauf Gypsum na Lodhia Steel vilivyopoMkuranga Mkoani Pwani ili navyo kupatiwa gesi asilia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea nausimamizi wa uagizaji mafuta kwa pamoja kupitia wakalawake (Petroleum Bulk Procurement Agency). Pamoja namanufaa mengine, mfumo huu umesaidia kupunguzagharama za meli kusubiri kupakua mafuta (demurrage costs).Hivi sasa gharama hizo ni kati ya dola 1.6 mpaka 3.5 kwa

Page 61: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

61

tani moja ya mafuta, tofauti na dola na 45 hadi 50 kwa tanimoja iliyokuwa ikitumika kabla ya mfumo huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichomekee,Tanzania tunaagiza takriban tani za mafuta milioni 2.5 zidishana demurrage ya 50 tuliyokuwa tuna-suffer, leo tuna-sufferdemurrage moja, utajua umuhimu wa mfumo huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kushuka kwa gharamaya manunuzi (premium) kutoka wastani wa dola za Marekani50 kwa tani, kabla ya utaratibu huu mpaka wastani watakriban dola 20 kwa tani na uhakika wa usalama waupatikanaji wa mafuta nchini ni manufaa mengine ya mfumohuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedhawa 2017/2018 Serikali itaanzisha mpango wa kuongezaupakuaji wa mafuta kwa kutumia Bandari ya Tangayatakayokuwa yanasambazwa Mikoa ya Kaskazini na piakuanzisha Mfumo huu Bandari ya Mtwara kwa ajili ya mikoaya kusini na na nchi jirani. Vilevile kuanzisha uingizaji wabidhaa za Liquefied Petroleum Gas kwa kutumia mfumo wauagizaji wa pamoja.

Mheshimiwa Naibu Spika , katika mwaka wa2016/2017 taarifa ya tathmini ya athari za mazingira na kijamiiimekamilika. Pamoja na taarifa hiyo, Mpango wa kuwapatiamaeneo mbadala wananchi waishio katika eneolitakalojengwa mitambo ya LNG la Likong’o Mkoani Lindi(resettlement action plan) umekamilika. Vilevile, kazi zakuingiza michoro ya eneo la Mradi wa LNG kwenye ramaniya Mipango Miji imekamilika. Majadiliano yanaendelea kufikiamakubaliano ya utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajikuchukua muda wa takriban miaka nane hadi 10 kufikiauzalishaji kamili wa LNG.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kushirikikatika Miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu yakusafirisha mafuta kwa ajili ya manufaa zaidi kwa Taifa letu.Miradi hiyo ni ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la

Page 62: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

62

Afrika Mashariki kutoka Hoima Kabaale (Uganda) hadiBandari ya Dar es Salaam (Tanzania) ambapo kazizilizofanyika hadi mwezi Machi, 2017 ni pamoja na kusainiwakwa Mkataba wa Makubaliano ya Awali (MoU); kufanyatathmini ya njia ya bomba (survey); tathmini ya mahitaji yanjia ya bomba (infrastructure requirements) na tathmini yaathari ya mazingira kijamii na kusainiwa kwa Inter-Governmental Agreement tarehe 26 Mei, 2017 KampalaUganda.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi mwingine ni wa ujenziwa bomba la kusafirisha mafuta safi (White PetroleumProducts) kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola(Zambia) ambao pia utahusisha ujenzi wa mabomba yamatoleo ya mafuta (take-off points) katika maeneo yaMorogoro, Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe. Mambo yakusafirisha mafuta kwa malori utakwisha, watu wa Mikoa yaKusini mtakuwa mnatumia bomba.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika juhudi za kupanuawigo wa vyanzo vya umeme nchini, Serikali imeendeleakusimamia utekelezaji wa miradi ya nishati jadidifu ambayoni pamoja na nishati ya jua, nishati ya upepo, miradi yatungamotaka, umeme wa maporomoko madogo ya maji,usambazaji wa umeme kwa mfumo wa gridi ndogo nauendelezaji wa matumizi ya biogas.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Kampuni yaUendelezaji wa Jotoardhi (Tanzania GeothermalDevelopment Company Limited) ambayo ni kampuni tanzuya TANESCO, imekamilisha utafiti wa kina (detail surface study)wa uendelezaji nishati ya jotoardhi katika maeneo ya ZiwaNgozi kule Mbeya. Utafiti umewezesha kuainisha sehemu tatuza kuchoronga visima vya majaribio katika eneo la ZiwaNgozi ili kutathmini kiasi cha hifadhi ya rasilimali ya jotoardhina uwezo wake wa kuzalisha umeme.

Vilevile Serikali ipo katika hatua za mwisho zakukamilisha utafiti wa kina katika maeneo ya Mbaka-Kiejo,Mkoani Mbeya na Luhoi Mkoani Pwani.

Page 63: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

63

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa sekta yamadini katika mwaka 2016/2017 na mpango kwa mwaka2017/2018; Serikali imeendelea kuchukua hatua na kuwekamipango mbalimbali ya kuendeleza utafutaji na ugunduziwa gesi ya Helium ambayo ni adimu duniani. Katika mwakawa fedha wa 2016/2017, Kampuni ya Helium One Limitedimeendelea kufanya utafiti wa gesi hiyo kupitia kampuni zaketanzu za Gogota (TZ) Limited, Njozi (TZ) Limited na Stahamili(TZ) Limited kwenye Mikoa ya Rukwa na Manyara. Utafitiuliofanyika umewezesha kugundulika kwa Helium ya wingiwa takriban futi za ujazo bilioni 54 kutokana na sampuli zamavujia (gas seeps) zilizochukuliwa katika maeneo matanoyaliyopo Ziwa Rukwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi za kuchoronga visimavya utafiti katika maeneo hayo zinatarajiwa kuanza mwaka2018 ili kuhakiki kiasi halisi cha gesi ya Helium kilichopo katikamaeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wa sekta yamadini katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka 4% mwaka2015 kutoka asilimia 3.7 ya mwaka 2014 katika kipindi chakuanzia Machi - Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara ilikusanyamrabaha wa jumla ya dola za Marekani milioni 56.77 sawana shilingi bilioni 130.90 kutoka kwenye migodi mikubwa yaBulyanhulu, Buzwagi, Geita, New Luika, North Mara,STAMIGOLD, Tanzanite One, Mwadui, Ngaka na Dangote.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kiasi cha mrabaha washilingi bilioni 4.23 kilikusanywa kutokana na mauzo yadhahabu iliyozalishwa kwa kuchenjua “vat leaching.” Aidha,shilingi bilioni 4.45 ulikusanywa kutokana na uzalishaji wamadini ya ujenzi na viwandani. Vilevile kiasi cha shilingi milioni14.52 kutokana na ada za leseni na vibali mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Wizara ilikusanyamrabaha wa dola za Marekani milioni 2.40 sawa na shilingibilioni 5.55 kutokana na mauzo ya Almasi na dola za Marekani906,347 sawa na shilingi bilioni 2.09 kutokana na mauzo yavito ghafi na vilivyokatwa. Katika kipindi hicho, Serikali pia

Page 64: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

64

ilikusanya Kodi ya Mapato (Corporate Tax) ya jumla ya shilingibilioni 79.26 kutoka kwa Kampuni ya Geita Gold MiningLimited na North Mara Gold Mine Limited.

Mheshimia Naibu Spika, katika kipindi hiki Kampuniza uchimbaji mkubwa wa madini zimeendelea kulipa ushuruwa huduma (service levy) kwa Halmashauri mbalimbaliambapo Jumla ya shilingi bilioni 11.27 zimelipwa. Katikamwaka wa fedha wa 2017/2018, Wizara itaendelea kuzipatiaHalmashauri husika takwimu sahihi za mauzo ya madini ilikuwezesha ukusanyaji ushuru wa huduma kutokana nauchimbaji wa madini ndani ya Halmashauri zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kipindi cha kuanziamwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 jumla ya wakia milioni1.05za dhahabu, wakia 414,128 za fedha na ratili milioni 10.4 zashaba, zenye jumla ya thamani ya dola za Kimarekani bilioni1.36 sawa na shilingi trilioni 3.14 zilizalishwa na kusafirishwanje ya nchi kutoka migodi ya STAMIGOLD, Bulyanhulu, Buzwagi,Geita, New Luika na North Mara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimuwa wawekezaji wakubwa. Naomba nirudie, Serikaliinatambua umuhimu wa wawekezaji wakubwa wa nje nawa ndani katika uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha2017/2018 Serikali inadhamiria kushirikiana na wadau kupitiasera, sheria na mikataba ya uendelezaji wa sekta hii ilikuhakikisha uwekezaji katika sekta unaendelea na kushamiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imeendelea najitihada za kuendeleza uchimbaji mdogo wa ikiwa ni pamojana kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo,kutenga fedha zaidi za ruzuku na kuimarisha shughuli zaugani.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika kipindi hikiSerikali kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali zaMadini wa Benki ya Dunia Awamu ya Pili inaendelea na

Page 65: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

65

hatua za uanzishwaji wa Vituo vya Mfano saba vyakuchenjua madini katika maeneo ya Buhemba (Mara), D-Reefna Kapanda (Mpanda), Itumbi (Chunya), Katente (Geita),Kyerwa (Kagera) na Maweni (Tanga).

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedhawa 2017/2018 Wizara itaendelea kutoa huduma za ugani kwawachimbaji wadogo nchini. Aidha, kwa kupitia STAMICO naGST, imepanga kutoa mafunzo ya nadharia na vitendo kwawachimbaji wadogo 4,000 katika Kanda za Kusini, ZiwaNyasa, Kati na Kusini Magharibi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha kuanziamwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017, jumla ya maombi ya leseni8,942 ya utafutaji na uchimbaji wa madini yalipokelewa naWizara kwa njia ya mtandao. Il i kuhakikisha lesenizinazotolewa zinafanyiwa kazi, Wizara imeendelea kufuatiliawamiliki wa leseni na waliobainika kutotekeleza mashartihusika ya leseni hizo walifutiwa leseni zao. Katika kutekelezaazma hiyo, jumla ya leseni 2,153 zilifutwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naendelea kutoa wito kwawadau wa sekta ya madini kujisajili kwa njia ya mtandao ilikurahisisha huduma za utoaji leseni na kuongeza uwazi hivyokupunguza malalamiko ya kuwepo kwa upendeleo katikautoaji wa Leseni za Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha kuanziamwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 jumla ya migodi 1,115ilikaguliwa na kuhakikisha kuwa salama, afya na utunzajiwake ulikuwa vizuri. Pia usalama na mazingira ya migodiunazingatiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na juhudi hizo zaWizara katika ukaguzi wa migodi, ajali zimeendelea kutokeahususan kwenye migodi ya wachimbaji wadogo. Katikakipindi cha hiki jumla ya ajali 17 zilitokea katika migodi hiyona kusababisha vifo vya wachimbaji 30. Aidha, katika ajalihizo, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya madiniwalifanikiwa kuokoa wachimbaji 42 wakiwa hai.

Page 66: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

66

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na kuongezekakwa ajali katika migodi, Wizara yangu katika mwaka wafedha wa 2017/2018 itaimarisha ukaguzi wa Migodi hiyo nchinzima na kuwa na taarifa za kila mwezi. Migodi yote ambayoitabainika kutokidhi vigezo vya kiusalama kwa mujibu yaKanuni za Afya na Usalama Migodini za mwaka 2010itafungwa mara moja hadi marekebisho stahiki ya kiusalamayatakapofanyika na kuridhiwa na Mkaguzi wa Migodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imeendeleakuhamasisha na kuwezesha Kampuni za Madini kuendeleana miradi mikubwa ya madini. Miradi hiyo ni pamoja nagraphite (Kinywe) iliyopo Nachu, Namangale na ChilaloWilayani Ruangwa; Chidya na Chiwata Wilayani Masasi naEpanko, Mahenge Wilayani Ulanga. Madini ya graphiteyanatumika kwenye kutengeneza vilainishi (lubricants), betrina vifaa vya kwenye injini za magari. Uwekezaji katika miradihiyo upo katika hatua mbalimbali za kukamilisha tathminiya athari za mazingira na ulipaji wa fidia. Aidha, Miradi yaRare Earth Elements (REE) na Niobium iliyopo katika Wilayaya Songwe ipo katika hatua za juu za utafiti na uanzishwajiwa migodi sawia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendeleakuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi wanaozungukamigodi kuhusu fursa zilizopo katika migodi inayowazunguka.Kwa hali ilivyo sasa, ushiriki wa Watanzania katika kutoahuduma na kuuza bidhaa kwenye Migodi umefikia takribanasilimia 50. Vilevile, Wizara inaendelea kuhamasisha migodikutoa zabuni kwa Wananchi wanaozunguka migodi naKampuni za Wakandarasi wa Kitanzania ili kutoa fursakwa Watanzania kuuza huduma na bidhaa kwenye migodihiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuongeza ushiriki waWatanzania katika migodi mikubwa, Serikali imetunga sheriana kanuni za kuzitaka kampuni za madini zenye leseni kubwaza uchimbaji kuandikisha asilimia 30 ya hisa katika Soko laHisa la Dar es Salaam. Natoa wito kwa wananchi kujiandaaili Kampuni za madini zikisajiliwa kwenye Soko la Hisa la Dar

Page 67: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

67

es Salaam, Watanzania wajitokeze kwa wingi kununua hisana hivyo kushiriki kwenye umiliki wa rasilimali zao za madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018 Wizara itaendelea kuchukua hatua za makusudikuelimisha umma kuhusu manufaa na fursa zilizopo katikasekta ya madini na kushirikiana na taasisi nyingine zaSerikali, kujenga uwezo wa Watanzania kushiriki katika sektahiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi hiki Wizaraimefanikiwa kufanya minada miwili ya Madini ya TanzaniteMkoa wa Arusha ambapo mnada wa kwanza ulifanyikamwezi Agosti, 2016 na mnada wa pili ulifanyika mwezi Machi,2017. Katika mnada wa Kwanza madini yenye thamani yadola za Marekani milioni 3.45 yaliuzwa na kuiwezesha Serikalikukusanya mrabaha wa thamani ya dola za Marekani 150,491sawa na shilingi milioni 347.78.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mnada wa pili,madini yenye thamani ya dola za Marekani milioni 4.20yaliuzwa na kuiwezesha Serikali kukusanya mrabaha wa dolaza Marekani 210,114.36 sawa na shilingi milioni 485.57. Aidha,Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ilikusanya ushuru wahuduma kiasi cha shilingi milioni 27.99.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na faida nyingine,minada hii husaidia kupunguza utoroshaji wa madini nje yanchi na kuitangaza Tanzania katika medani ya Kimataifakuhusu fursa za madini zilizopo hapa nchini. Aidha, Wizarailifanya Maonesho ya Kimataifa ya Vito na Usonara, Arushakuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei, 2017.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa UsimamiziEndelevu wa Rasilimali za Madini umeanza ujenzi wa Kituocha Mafunzo kwa wachimbaji wadogo cha Rwamgasa,Geita. Kituo hiki kinajengwa kwa ushirikiano baina ya Wizara,Mgodi wa Geita na Ushirika wa Wachimbaji Wadogo waRwamgasa.

Page 68: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

68

Mheshimiwa Naibu Spika, shughuli nyinginezilizofanyika ni kukamilisha utaratibu wa ununuzi kwa ajili yaukarabati wa Ofisi za Madini za Bariadi, Bukoba, Chunya,Kigoma, Mpanda, Musoma, Songea, Ofisi za STAMICO naChuo cha Madini Dodoma. Aidha, ununuzi wa vifaambalimbali vya kutoa huduma za ugani kwa wachimbajiwadogo kupitia STAMICO, GST na Ofisi za Madini za Kandaumekamilika. Katika mwaka wa fedha 2017/2018 Wizarakupitia mradi wa SMMRP unatarajia kuanza ukarabati naupanunzi wa Ofisi za Madini za Bariadi, Bukoba, Chunya,Kigoma, Mpanda, Musoma, Songea, ofisi za STAMICO naChuo cha Madini Dodoma. Lengo la ni kuboresha mazingiraya kazi ya ofisi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala wa Jiolojia Tanzaniakwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walifanyautafiti wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera tarehe10 Septemba, 2016 na kuaandaa taarifa za utafiti. Piawataalamu kutoka Wakala, Chuo cha Ardhi na Chuo chana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walitoa elimu kwa Ummana kwa wahanga wa tetemeko hilo. Aidha, wakalauliendelea kukusanya takwimu kutoka vituo nane vyakudumu vilivyoko nchini vya kupimia matetemeko ya ardhi,kuchakata takwimu, kuchora ramani na kuhifadhia kwenyekanzidata kisha kuzitolea taarifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha2017/2018 wakala utaendelea kuratibu majanga asilia yakijiolojia ikiwemo pamoja na matetemeko ya ardhi, milipukoya volkano, maporomoko ya ardhi ili kubaini maeneo yenyehatari ya kupata maporomoko ya ardhi na kutoa ushaurikwa wananchi waishio katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali mwaka 2009ilianzisha wakala maalum kwa ajili ya ukaguzi wa shughuliza uwekezaji katika sekta ya madini, kazi kubwa ikiwa nipamoja na kukagua gharama za uwekezaji wa makampunimakubwa, mapato yatokanayo na uwekezaji huo, kodipamoja na mrahaba. TMAA hufanya kazi hizi kwa kushirikianana Ofisi za Madini za Kanda, TRA pamoja na Wizara ya Mambo

Page 69: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

69

ya Ndani. Utendaji wa taasisi hii uliendelea kuonyeshamapungufu katika sekta kwa kubaini mianya ya upotevu wamapato ya Serikali. Pamoja na utendaji huo, wadaumbalimbali wakiwemo wananchi wa kawaida waliendeleakupaza sauti wakidai Taifa linaibiwa kupitia miradi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia maoni na ushauriwa wadau wakiwemo Waheshimiwa Wabunge, Serikaliimekuwa ikichukua hatua kadhaa kulinda maslahi ya Taifa.Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuweka wataalamu wakukagua uzalishaji wa madini katika baadhi ya migodimipakani, viwanja vya ndege na katika bandari. Kutokanana jitihada hizo, kwa mwaka wa 2016/2017 wakala uliwezakukamata madini jumla ya thamani ya dola za Kimarekani119,906.45 sawa na shilingi milioni 277.10 katika viwanja vyandege vya Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza naSongwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua nyingineiliyochukuliwa na Serikali ni kuifanyia marekebisho Sheria yaMadini Namba 18 ya mwaka 2010 kupitisha Sheria ya Uwazina Uwajibakaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesiasilia, TEITI Act Na. 23 ya mwaka 2015 ili kuruhusu kuwekwauwazi taarifa za ustawishaji, gharama za uwekezaji nauendeshaji pamoja na mapato yatokanayo na madini ilikuongeza uwajibikaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedhawa 2016/2017 wakala ulifanya ukaguzi na kuwezesha Serikalikukusanya mrabaha wenye thamani ya shilingi bilioni 4.45ikilinganishwa na jumla ya shilingi bilioni 6.27 zilizokusanywakwa kipindi cha 2015/2016. Kiwango kidogo cha mrabahauliopatikana, kushuka kwa mrabaha kwa mwaka 2016/2017na vilio vya wananchi viliipelekea Serikali kuchua hatuambalimbali ili kuhakikisha mapato ya Serikali yanapatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka fedha2017/2018, Serikali itaimarisha Wakala wa Ukaguzi wa Madinikwa kuzingatia maoni na ushauri wa wadau mbalimbalipamoja na ushauri wa Kamati za kudumu za Bunge.

Page 70: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

70

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile maoni na ushauriMaalum iliyoundwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, kuchunguza mchanga uliomokatika makontena ya makinikia ya dhahabu utazingatiwa.Lengo la jitihada hizi ni kuhakikisha kwamba Taifa linanufaikaipasavyo na rasilimali za madini. (Makofi)

Aidha, tuna matumaini makubwa kuwa maoni,ushauri na maelekezo yatakayotolewa na Kamati Maalumiliyoundwa na Mheshimiwa Rais kupitia mfumo wa kisera,kisheria na kimuundo kuhusu uendeshaji wa shughuli za Wizarahii katika masuala ya rasilimali ya madini tutatekeleza.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, STAMICO imeendeleakutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wakununua madini ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogowalioko Kyerwa Mkoani Kagera. Hadi kufikia Machi, 2017tani 18.08 za madini hayo ziliuzwa na kulipatia Taifa jumla yashilingi 325.49 ambazo Serikali ilipata mrahaba wa shilingimilioni 13.02 na shilingi 976,471 zimelipwa katika Halmashaurikama ushuru.

Vile vile ili kukidhi mahitaji ya makaa ya mawe nchini,STAMICO imeaanza rasmi uchimbaji wa makaa hayo katikakilima cha Kabulo Kiwira kuanzia mwezi Aprili, 2017. Jumlaya tani 107,078 zinakadiriwa kuchimbwa kwa mwaka. Lengola mradi huu ni kuviuzia viwanda makaa ya mawe kwa ajiliya utengenezaji wa saruji na marumaru.

Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo cha Madini Dodomakimedahili jumla ya wanafunzi 527 katika fani za Jiolojia naUtafutaji Madini, Uhandisi Migodi, Uhandisi Uchenjuaji Madini,Sayansi za Mafuta Uhandisi na Usimamizi wa MazingiraMigodini. Pia chuo kimeandaa mtaala mpya wa upimaji ardhina migodi ambao umewasilishwa NACTE kwa ajili ya usajili.

Aidha, chuo kimefanya upanuzi na ukarabati wa ofisina madarasa, ujenzi wa ukumbi wa mihadhara pamoja naviwanja vya michezo katika mwaka wa fedha 2017/2018

Page 71: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

71

chuo kitaendelea kupanua wigo wake kwa kutoa mafunzo,kuanzisha programu mbalimbali za upimaji ardhi migodini.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutambuamchango wa taasisi mbalimbali za Serikali na washirika wamaendeleo ambao wamekuwa mstari wa mbele kuungamkono juhudi za Serikali za kuleta maendeleo kupitiamisaada yao mbalimbali kwenye Sekta za Nishati na Madini.

Kwa niaba ya Serikali napenda kutoa shukrani za dhatikwa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Maendeleo yaAfrika Kusini, Benki ya Dunia, Benki ya Exim China, Benki yaUshirikiano wa Kimataifa Japan, Benki ya Maendeleo yaKiarabu, Benki ya Unicredit Austria, Climate Investment Fund,Economic Development Cooperation Fund, OPEC Fund forInternational Development, Mfuko wa Uendelezaji Jotoardhipamoja na Taasisi na Mashirika ya AFD (France), Shirika laMazingira la Umoja wa Mataifa ICEIDA, CIDA, DfID, IDA, Benkiya Dunia, JICA, KfW (Germany), GIZ (Germany), NORAD(Norway), NDF (nchi za Nordic), SIDA (Sweden), Umoja waUlaya, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) TheNertherlands (DRIVE), USAID na nchi za Brazil, Denmark,Finland, Iceland, Norway na Korea ya Kusini kwa kutakjabaadhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha mwakawa fedha wa 2017/2018 Serikali kupitia Wizara hii itaendelezaushirikiano wa shirika hawa kwa maendeleo na menginekwa ujumla. Hiyo ndiyo inataitwa economic diplomacy.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe shukrani.Naomba nimalizie kwa kumshukuru kwa dhati MheshimiwaDkt. Merdad Matogolo Chananja Kalemani, Mbunge waChato, Naibu Waziri wa Nishati na Madini kwa mchangowake katika kusimamia sekta hii. Nakiri wazi kuwa mchangowake umekuwa msaada mkubwa katika kuendeleza sektahii. Naomba nichomekee kidogo, napenda kusema kwambaMheshimiwa Kalemani amevivaa kikamilifu viatu vyamtangulizi wake. (Makofi)

Page 72: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

72

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vilevile nitumienafasi hii kuwashukuru Naibu Makatibu Wakuu Profesa JamesEpiphan Mdoe pamoja na Mhandisi Juliana LeonardPallangyo, Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara naVitengo pamoja na watumishi wote wa Wizara kwamichango yao na utendaji mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua fursa hii yakipekee kuwashukuru Wakuu wote wa Taasisi, Wenyeviti waBodi na Wajumbe wa Bodi za Taasisi pamoja na watumishimbalimbali wa taasisi zilizo chini ya Wizara kwa mchangowao katika kutekeleza majukumu ya Wizara hii. Mtawaonanje, hata mvao wao inaonekana kwamba wanatokakwenye nishati na madini. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee napendakumshukuru tena, Mheshimiwa Rais kwa jinsi anavyojitoakusimamia rasilimali za nchi hii na kulinda maslahi mapanaya wananchi wa Taifa letu. Nawashukuru wananchi kwanamna ya kipekee wanaojitokeza kumuunga mkonoMheshimiwa Rais na kumwombea kila anapochukua hatuaili kuwaletea maendeleo Watanzania. Hakika kiongozi wetumkuu anastahili maombi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hitimisho, bajeti ya Wizaraya Nishati na Madini kwa mwaka 2017/2018 pamoja nakutumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali, imelengakatika kutekeleza miradi mikubwa ya nishati ili kuchocheasekta za kiuchumi na hivyo kukuza uchumi wa Taifa letu namaendeleo ya Watanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara pia katika kipindihiki itaendelea na utekelezaji wa maelekezo ya Serikali yaAwamu ya Tano ya upatikanaji wa nishati ya uhakika ilikuwezesha kufikiwa kwa lengo la Taifa ya kuwa nchi yaviwanda. Katika kutekeleza azma hiyo, fedha za miradi yamaendeleo ambazo ni shilingi bilioni 756.76 sawa na asilimia80.6 ya fedha zote za maendeleo zimeelekezwa katikakutekeleza miradi ya kimkakati ya nishati.

Page 73: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

73

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Bunge lako Tukufulikubali kupitisha Makadirio ya fedha jumla ya shilingi998,337,759,500 kwa mwaka wa 2017/2018. Mchanganuo wabajeti hiyo ni kama ifuatavyo:-

(i) Shilingi 938,632,006,000 sawa na asilimia 94.1, bajetiyote ni kwa ajili ya kutekeza miradi ya maendeleo. Asilimia94.1 ya bajeti hii ni kwa ajili ya maendeleo. Kati ya fedha hizoshilingi 763,304,679,000, sawa na asilimia 81 ya fedha zote zamaendeleo ni fedha za ndani na shilingi 175,327,327,000, sawana asilimia 19 ni fedha za kutoka nje.

(ii) Shilingi 59,705,753,500 sawa na asilimia 5.9 ya bajetiyote kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo yaWizara Katiya fedha hizo, shilingi 28,833,681,500 sawa naasilimia 48.3 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi30,872,072,000 sawa na asilimia 51.7 zitatumika kulipamishahara ya watumishi wa Wizara hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tena nitoe shukranizangu za dhati kwako wewe Mheshimiwa Naibu Spika,Mheshimiwa Spika na kwa Waheshimiwa Wabunge wote kwakunisikiliza. Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizarakwa anwani ya www.mem.go.tz vilevile hotuba hii inavielelezo mbalimbali kama mlivyoviona kwa ajili ya ufafanuziwa masuala muhimu yanayohusu sekta ya nishati na madini.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuota hoja.(Makofi)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe)

NAIBU SPIKA: Hoja imeungwa mkono.

Page 74: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

74

HOTUBA YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUHUSUMAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA

FEDHA 2017/2018 – KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

A. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifailiyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, naomba kutoahoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadilina kupitisha mpango na makadirio ya Mapato na Matumiziya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha wa2017/18.

2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema sisiWaheshimiwa Wabunge wote na hivyo kutuwezeshakuendelea na utekelezaji wa majukumu yetu ya kitaifa ndanina nje ya Bunge. Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, Bungelimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kikatiba likiwemola kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

3. Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwapongezakwa dhati viongozi wetu wa kitaifa kwa jinsi wanavyojitumakatika kutatua matatizo na changamoto mbalimbali za Taifaletu na hatimaye kuwaletea wananchi maendeleo. Viongozihao wameendelea kutoa miongozo ambayo kila maraimekuwa ikilenga kuwaondolea wananchi kero mbalimbalikatika maeneo yao. Dhamira hii imedhihirika wazi kwa jinsiSerikali ya Awamu ya Tano inavyoshughulikia masuala yenyemaslahi ya kitaifa yakiwemo ya vita dhidi ya rushwa,madawa ya kulevya, ubadhirifu wa mali za Umma, malipohewa pamoja na kurudisha uwajibikaji Serikalini.

4. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nitumiefursa hii kumshukuru na kumpongeza Dkt. John Pombe JosephMagufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naSerikali yake jinsi anavyochukua hatua za kusimamia nakulinda rasilimali za Taifa hasa madini.

Page 75: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

75

5. Mheshimiwa Spika, naomba pia kumpongezaMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi yake nzuri anayoendeleakuifanya tangu alipoteuliwa. Aidha, nampongeza WaziriMkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwa jinsianavyoendelea kusimamia kwa karibu shughuli za Serikalitangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani.Ni wazi kuwa Viongozi wetu hao wa kitaifa kwa kipindi kifupiwalichokaa madarakani wamefanya kazi nzuri na kubwakwa kutoa na kutekeleza miongozo makini ya kulisaidia Taifaletu. Tuwaombee wote kwa Mwenyezi Mungu ili waendeleena kasi hiyo ambayo imekuwa ni chachu ya mabadilikokatika nyanja mbalimbali na hatimaye nchi yetu iweze kupigahatua za kimaendeleo kwa kasi kubwa zaidi.

6. Mheshimiwa Spika, nikupongeze wewe binafsi,Mheshimiwa Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wotewa Kamati mbalimbali za Kudumu za Bunge lako Tukufupamoja na Watendaji wa Ofisi ya Bunge kwa jinsimnavyoliendesha Bunge letu Tukufu kwa ufanisi mkubwa.Nitoe Shukrani za kipekee pia kwa Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb.), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishatina Madini na Mhe. Deogratias Francis Ngalawa (Mb.),Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo. Aidha, nawashukuruWajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishatina Madini. Kwa kweli, nikiri kuwa Kamati hii imekuwa msaadamkubwa katika usimamizi na uendelezaji wa Sekta za Nishatina Madini nchini kutokana na maoni na ushauri waowanaoutoa kwa Serikali kupitia Wizara yangu.

7. Mheshimiwa Spika, naomba kuungana piana Waheshimiwa Wabunge wenzangu kuwapongezaWaheshimiwa Wabunge wapya walioteuliwa hivi karibunina Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaambao ni: Mheshimiwa Salma Rashid Kikwete; MheshimiwaAbdallah Majura Bulembo; Mheshimiwa Anne KillangoMalecela; na Mheshimiwa Prof. Palamagamba John AidanMwaluko Kabudi. Aidha, nimpongeze Mheshimiwa MchungajiDkt. Getrude Rwakatare, kwa kuteuliwa kuwa Mbunge waViti Maalum kupitia CCM.

Page 76: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

76

Pia, nampongeza Mheshimiwa Juma Ali Juma,Mbunge wa Jimbo la Dimani kwa heshima kubwa aliyopewana wananchi wa Jimbo la Dimani ili awawakilishe kwenyeBunge hili la kumi na moja (11). Vilevile, nimpongezeMheshimiwa Catherine Nyakao Ruge kwa kuteuliwa kuwaMbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA. Niwapongezepia Waheshimiwa Wabunge wote waliochaguliwakuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la Afrika Mashariki na nimatarajio yetu kuwa Wabunge hao wenzetuwatatuwakilisha kwa ufanisi na umakini mkubwa kwenyeBunge la Afrika Mashariki.

8. Mheshimiwa Spika, nikupe pole wewe binafsina Bunge lako Tukufu kwa kumpoteza mwenzetu tuliyekaanaye humu kwa muda mrefu, marehemu Samwel Sittaaliyekuwa Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo Magharibi,Spika Mstaafu wa Bunge la T isa (2005 – 2010) na Mwenyekitiwa Bunge la Katiba. Wote tunakiri kuwa Kiongozi huyoalikuwa mchapakazi, hodari na mwenye msimamo katikamasuala yenye tija kwa Taifa. Vilevile, nitoe pole kwa Bungelako Tukufu kwa kuwapoteza Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir,aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar; pamojana Mheshimiwa Dkt. Elly Marko Macha, Mbunge wa VitiMaalum wa CHADEMA. Naungana na Wabunge wenzangukutoa pole kwa familia za marehemu. Pia, natoa pole nyingikwa wazazi, walezi, ndugu na familia za wanafunzi wa Shuleya Msingi Lucky Vicent waliopoteza maisha katika ajali yagari iliyotokea Wilayani Karatu hivi karibuni. Msiba ni sualagumu, lakini hatuna la kufanya zaidi ya kumwombaMwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pemapeponi, Amen.

9. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo yaawali, naomba sasa kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji washughuli za Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka waFedha wa 2016/17 pamoja na Mpango na Bajeti kwa Mwakawa Fedha wa 2017/18.

Page 77: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

77

B. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZAWIZARA YA NISHATI NA MADINI KWA MWAKA 2016/17PAMOJA NA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

10. Mheshimiwa Spika, Maeneo ya Kipaumbele kwaMwaka wa Fedha wa 2016/17 katika Sekta ya Nishati nipamoja na: kuimarisha uzalishaji, u s a f i r i s h a j i nakuongeza kasi ya usambazaji wa umeme nchini;Kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha SektaNdogo ya Umeme (Electricity Supply Industry Reform Strategyand Roadmap); Kuendeleza Nishati Jadidifu (RenewableEnergies) kama vile umeme jua, upepo, maporomokomadogo ya maji, jotoardhi na tungamotaka; na kuvutiauwekezaji katika Sekta ya Nishati, hususan kwenye uzalishajiwa umeme na katika utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia.

11. Mheshimiwa Spika, pamoja na maeneo hayo yaNishati, Wizara pia ilitoa kipaumbele katika Sekta ya Madinihususan katika: Kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Serikaliyatokanayo na rasilimali za madini kwa kuziwezesha Ofisiza Madini za Kanda, Ofisi za Afisa Madini Wakazi, Kitengocha Leseni cha Wizara pamoja na Wakala wa Ukaguzi waMadini Tanzania (TMAA); Kuwaendeleza Wachimbaji Wadogona wa Kati wa madini; Kuhamasisha shughuli za uongezajithamani wa madini; Kuendelea na utafutaji wa graphitena madini mengine yanayohitajika kwenye teknolojia yakisasa (Rare Earth Elements-REE); na Kuimarisha ufuatiliaji naukaguzi wa afya, usalama, mazingira na uzalishaji wa madinikatika migodi midogo, ya kati na mikubwa.

12. Mheshimiwa Spika, sambamba na maeneo hayoya ki-Sekta, Wizara vilevile iliweka msisitizo katika maeneomengine yakiwemo: kuwajengea uwezo Watumishi waWizara katika fani za Umeme, Mafuta, Gesi Asilia, Jiolojia,Jemolojia, Uhandisi Migodi na Uthaminishaji wa Vito naAlmasi; kuelimisha umma na kuboresha mawasiliano kati yaWizara na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya Nishati naMadini; kuboresha mazingira ya Ofisi na vitendea kazi kwaWatumishi ili kuongeza ufanisi na ubora katika utoaji wahuduma zinazohusu Nishati na Madini; na kusimamia,

Page 78: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

78

kufuatilia na kuboresha Sera, Sheria, Kanuni, Mipango naMiongozo mbalimbali ili kuboresha ufanisi na tija katika Sektaza Nishati na Madini.

13. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2017/18, Wizara ya Nishati na Madini itaendelea kutekelezamaeneo ya vipaumbele mbalimbali yakiwemo: kuimarishauzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini;kuimarisha ufuatiliaji na ukaguzi wa afya, usalama, mazingirana uzalishaji wa madini katika migodi midogo, ya kati namikubwa; kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Serikaliyatokanayo na rasilimali za Gesi Asilia na Madini; kusimamiauingizaji, utunzaji na usambazaji wa mafuta nchini; nakuwezesha uwekaji wa mtandao wa usambazaji wa GesiAsilia viwandani na majumbani pamoja na uendelezaji waMradi wa Kusindika Gesi Asilia (Liquefied Natural Gas - LNG).Aidha, Wizara pia itatekeleza maeneo mengine mapyaambayo ni pamoja na: kuendelea na utekelezaji wa MradiMkubwa wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutokaKabaale (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Ujenzi wa Bombala Mafuta Safi kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola(Zambia); Kukamilisha mazungumzo kuhusu ujenzi naupatikanaji wa Gesi Asilia kwenye Viwanda vya Mboleavinavyotarajiwa kujengwa katika maeneo ya Kilwa Masoko(Lindi) na Mtwara; Kuendelea na ujenzi wa Mradi wa kuzalishaumeme wa Rusumo, MW 80; na Kuendelea na utekelezajiwa Agizo la Serikali la kuhamia Dodoma.

Ukusanyaji wa Maduhuli yaSerikali kwa Mwaka 2016/17

14. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madinikatika Mwaka wa Fedha wa 2016/17 ilipanga kukusanyaJumla ya Shilingi bilioni 370.68 ikilinganishwa na Shilingibilioni 286.66 kwa Mwaka 2015/16. Mapato hayoyanatokana na vyanzo mbalimbali vikiwemo: Ada zakijiolojia; Mrabaha; Ada za Mwaka za Leseni; Mauzo yaNyaraka za Zabuni; Mauzo ya Gesi Asilia; Tozo ya mauzo yaumeme; na Shughuli za utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia. Hadikufikia mwishoni mwa Mwezi Machi, 2017 Wizara ilikuwaimekusanya Jumla ya Shilingi bilioni 266.21 sawa na asilimia

Page 79: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

79

72 ya lengo lililokusudiwa. Wizara itaendelea na juhudi zakukusanya ili kufikia lengo lililowekwa katika kipindi chaMwaka wa Fedha wa 2016/17.

15. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2017/18, Wizara inatarajia kukusanya Jumla ya Shilingi bilioni727.50 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 370.68 kwa Mwakawa Fedha wa 2016/17 kutokana na vyanzo vyake vyamapato, sawa na ongezeko la asilimia 96.3. Ongezeko hilola makisio ya makusanyo limetokana na kuongezeka kwamchango wa mapato yatokanayo na mauzo ya Gesi Asiliaambayo kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17 yalikadiriwaShilingi bilioni 115.13 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 477.36kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18. Kuongezeka kwamauzo ya Gesi Asilia kutatokana na kuanza kutumika kwaGesi Asilia katika viwanda vipya vikubwa. Viwanda hivyo nipamoja na: GOODWILL, Bakhresa Food Products na LodhiaGroup vilivyopo Mkuranga - Pwani; Dangote kilichopoMtwara; pamoja na Coca - Cola na Bidco vilivyopoKinondoni - Dar es Salaam.

Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini Kwa Mwaka2016/17

16. Mheshimiwa Spika, Bajeti iliyopitishwa kwa ajiliya Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi zake kwaMwaka wa Fedha wa 2016/17 ni Jumla ya Shilingi trilioni1.122. Bajeti hiyo inajumuisha Fedha za Miradi ya MaendeleoShilingi trilioni 1.056, sawa na asilimia 94 ya Bajeti yote yaWizara. Kati ya fedha hizo za Maendeleo, Shilingi bilioni724.84 sawa na asilimia 68.6 ni fedha za Ndani na Shilingibilioni 331.51 sawa na asilimia 31.4 ni fedha za Nje. Kwaupande wa Bajeti ya Matumizi ya Kawaida, Wizara na Taasisizake ilitengewa Jumla ya Shilingi bilioni 66.23, sawa naasilimia 6 ya Bajeti yote kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17. Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 38.87, sawa na asilimia58.7 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (O.C.) na Shilingibilioni 27.36, sawa na asilimia 41.3 ni Mishahara kwa ajili yaIdara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya Wizara. Fedhazilizopokelewa hadi Mwezi Mei, 2017

Page 80: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

80

17. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 25Mei, 2017 Wizara ilikuwa imepokea Jumla ya Shilingi bilioni591.39, sawa na asilimia 52.71 ya Bajeti yote iliyotengwa kwaMwaka wa Fedha wa 2016/17 ambayo ni Shilingi trilioni 1.122.Kati ya fedha hizo zilizopokelewa, Shilingi bilioni 51.64 ni fedhaza Matumizi ya Kawaida ambapo Matumizi Mengineyo (O.C.)ni Shilingi bilioni 28.48 na Mishahara (P.E.) kwa Wizara naTaasisi zake ni Shilingi bilioni 23.16. Kiasi kilichopokelewa nisawa na asilimia 77.97 ya fedha zote za Matumizi ya Kawaidazilizotengwa ambazo Jumla yake ni Shilingi bilioni 66.23.

18. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho Jumlaya Shilingi bilioni 654.06 ambazo ni fedha za Miradi yaMaendeleo zilipokelewa ambapo fedha za Ndani ni Shilingibilioni 522.96 na fedha za Nje ni Shilingi bilioni 131.1. Fedhahizo ni sawa na asilimia 61.93 ya Bajeti yote ya Miradi yaMaendeleo kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17 ambayo niShilingi trilioni 1.056. Fedha hizo zilizopatikana zilielekezwakatika Miradi ya kupeleka umeme vijijini kupitia Wakala waNishati Vijijini (REA); Mradi wa Kinyerezi I Extension (MW 185);ulipaji wa deni la Mradi wa Kinyerezi I (MW 150); Mradi waUjenzi wa Njia ya Kusafirisha Umeme ya Makambako – Songea(kV 220); malipo ya madeni ya TANESCO na Mradi waUendelezaji wa Rasilimali za Madini (SMMRP). Aidha, kwaupande wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) hadi kufikiatarehe 25 Mei, 2017 ulikuwa umepokea Jumla ya Shilingibilioni 448.87 sawa na asilimia 76.39 ya Bajeti yake kwaMwaka wa Fedha wa 2016/17.

Ufanisi wa Wizara katika Masuala ya Manunuzi

19. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakusimamia matumizi ya fedha za Umma kwa umakinimkubwa kwa kuhakikisha kuwa masuala ya ununuziyanafanyika kwa ufanisi mkubwa. Katika ukaguzi wa ununuzi(Procurement Audit) uliofanywa na PPRA katika kipindi chaMwaka 2015/16, Wizara ya Nishati na Madini imekuwamiongoni mwa Wizara tatu bora kwa kupata alama yaasilimia 88.85. Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18, Wizaraitaendelea kusimamia manunuzi kwa ufanisi zaidi katika

Page 81: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

81

kuhakikisha kuwa fedha za Umma zinatumika ipasavyo kwamaslahi ya maendeleo ya Taifa letu.

SEKTA YA NISHATI

SERA, MIPANGO NA SHERIA KATIKA SEKTA YA NISHATI

Mpango Kabambe wa Uendelezaji wa Sekta Ndogo yaUmeme (PSMP) na Matumizi ya Gesi Asilia (NGUMP)

20. Mheshimiwa Spika, Serikali katika kipindi chaMwaka wa Fedha wa 2016/17 imekamilisha mapitio yaMpango Kabambe wa Uendelezaji wa Sekta Ndogo yaUmeme (Power System Master Plan - PSMP 2016 Update)ambayo ilikamilika Mwezi Desemba, 2016. Mpango huoumebainisha utekelezaji wa Miradi ya uzalishaji na usafirishajiwa umeme katika kipindi kifupi (2016 – 2020), kati (2021 - 2025)na kirefu (2026 - 2040). Katika kipindi kifupi, kiasi cha MW 4,193zinahitajika, kipindi cha kati MW 1,280 na kirefu MW 14,646zinahitajika kuongezwa ili kuweza kukidhi mahitaji ya umemenchini.

21. Mheshimiwa Spika, Mpango huo wa PSMPumezingatia ukuaji wa mahitaji ya umeme nchini, gharamanafuu ya uwekezaji na uchangiaji wa vyanzo mbalimbali vyanishati (energy mix) ambapo umeme utazalishwa kutokanana Gesi Asilia, maporomoko ya maji, makaa ya mawe, jua,upepo, jotoardhi na tungamotaka. Mapitio hayo yalifanyikakwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo: Wizara naTaasisi za Serikali; Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan(JICA); na Sekta Binafsi.

22. Mheshimiwa Spika, sambamba na mapitio yaPSMP, Wizara pia imeandaa Rasimu ya Mpango Kabambewa Matumizi ya Gesi Asilia (Natural Gas Utilization Master Plan– NGUMP) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo laKimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikisha Taasisi mbalimbaliza Serikali, Sekta Binafsi na Wataalam kutoka nchi za Japanpamoja na Trinidad and Tobago. Mpango huu unatoamwongozo kuhusu matumizi bora ya Gesi Asilia, uboreshaji

Page 82: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

82

wa miundombinu ya Gesi Asilia pamoja na kuweka misingiya kuhakikisha Sekta zote za uchumi zinahusishwa.Mpango huu utatekelezwa kwa kipindi cha Miaka thelathini(30) kuanzia 2017 hadi 2046, ambapo Jumla ya Futi za UjazoTrilioni 18.7 za Gesi Asilia zimepangwa kutumika kwa ajili yamatumizi ya Soko la Ndani. Aidha, Gesi Asilia kwa ajili yauzalishaji umeme ndio kipaumbele cha kwanza cha Mpangohuu ambapo kiasi cha Gesi Asilia kilichotengwa ni Futi zaUjazo Trilioni 8.3, sawa na asilimia 44.4 ya Gesi Asiliailiyotengwa kwa ajili ya Soko la Ndani.

Kanuni za Maboresho na Ushindani katika Sekta Ndogo yaUmeme, Upangaji wa Bei ya Gesi Asilia na Ushirikishwaji waWatanzania katika Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia

23. Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha Kanuni zaMaboresho na Ushindani katika Sekta Ndogo ya Umeme zaMwaka 2016 (The Electricity (Market Re- Organization andPromotion of Competition) Regulations, 2016) na kutangazwakwenye Gazeti la Serikali, Na. 229 la tarehe 21 Oktoba,2016. Kanuni hizo, pamoja na mambo mengine, zinatoamwongozo wa jinsi ya kuchochea ushindani kwenyeshughuli za uzalishaji umeme na kuratibu shughuli hizo kupitiaKamati Maalumu (Electricity Infrastructure ProcurementCoordinator - EIPC).

24. Mheshimiwa Spika, Mwezi Oktoba, 2016 Serikaliilikamilisha Kanuni za upangaji wa bei ya Gesi Asilia kwa ajiliya matumizi mbalimbali na kutangazwa katika Gazeti laSerikali Na. 285. Aidha, kwa kutumia Kanuni hizo ukokotoajiwa bei za Gesi Asilia kwa ajili ya viwanda vya kimkakativinavyojumuisha Viwanda vya Mbolea na Saruji ulikamilikaMwezi Januari, 2017. Lengo la upangaji wa bei hizo nikuhamasisha uwekezaji katika Viwanda vya Mbolea ilikufanikisha upatikanaji wa mbolea ya bei nafuu nchini mwetu.

25. Mheshimiwa Spika, kufuatia mafanikioyaliyopatikana katika utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia,Serikali imeona upo umuhimu wa kuhakikisha Watanzaniawanashiriki katika Tasnia hiyo ipasavyo. Ili kufanikisha azma

Page 83: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

83

hiyo, Serikali imeandaa Kanuni Mahsusi zitakazoongozaKampuni za Mafuta na Gesi Asilia jinsi zitakavyowezakuwashirikisha Watanzania katika Tasnia ya Mafuta na GesiAsil ia (Local Content Regulations). Kanuni husikazimeandaliwa kwa kushirikisha Wadau mbalimbaliwakiwemo Taasisi za Umma, Kampuni za Mafuta na Gesi Asiliana Asasi za Kiraia. Kanuni hizo zimekamilika na zimetangazwakatika Gazeti la Serikali Na. 197 la tarehe 5 Mei, 2017.

26. Mheshimiwa Spika katika kuhakikisha hudumaza udhibiti wa Nishati zinaendelea kufanyika kwa uwazi,ubora na ufanisi kwa lengo la kukuza Uwekezaji na kuboreshaUstawi wa Kijamii na Kiuchumi kwa Jamii ya WatanzaniaMamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) iliandaaKanuni (Rules) mbalimbali. Kanuni hizo ni pamoja na: Kanuniza Uendelezaji na Usimamizi wa Miradi Midogo ya Umeme(The Electricity (Development of Small Power Projects) Rules,2016, GN No. 217 of 2016); Kanuni za Tozo na Ada za Leseni zaUmeme (The Electricity (Licensing Fees) Rules, 2016, GN No.287 of 2016); Kanuni za Usimamizi wa Mifumo ya Umeme (TheElectricity (System Operation Services) Rules, 2016, GN No. 324of 2016); Kanuni za Usimamizi wa Soko la Biashara ya Umeme(The Electricity (Market Operation Services) Rules, 2016, GN No.325 of 2016); Kanuni za kusimamia Uuzaji umeme (The Electricity(Supply Services) Rules, 2017, GN No. 4 of 2017); na Usimamiziwa Biashara ya Rejareja ya Petroli Vijijini na kwenye Miji Midogo(The Petroleum (Retail Operations in Townships and Villages)Rules, 2017, GN No. 14 of 2017).

SEKTA NDOGO YA UMEME

Hali ya Upatikanaji wa Umeme Nchini

27. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2016/17 Serikali imeendelea kuboresha Sekta Ndogo yaUmeme kwa kuimarisha hali ya uzalishaji, usafirishaji pamojana kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme nchini. Umemeuliozalishwa kwa Mwaka 2016 na kuingizwa katika Gridi yaTaifa uliongezeka na kufikia GWh 7,092 ukilinganisha na GWh6,227 zilizozalishwa Mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia

Page 84: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

84

12.20. Aidha, mahitaji ya juu ya umeme kwa Mwaka wa Fedhawa 2016/17 yameongezeka hadi kufikia MW 1,051.27 iliyofikiwatarehe 14 Februari, 2017 ukilinganisha na MW 1,026.02 katikaMwaka 2015/16. Katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17mitambo yetu ina uwezo wa kuzalisha umeme wa kiasi chaMW 1,450.

28. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na jitihadaza makusudi za kuongeza Idadi ya Wananchi wanaopatahuduma ya umeme kwa lengo la kushamirisha shughuli zakiuchumi na kijamii. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2017 Idadi yaWananchi waliofikiwa na huduma ya umeme (overallelectricity access level) imefikia asilimia 67.5 kulinganishana asilimia 40 iliyokuwa imefikiwa Mwezi Aprili, 2016. Aidha,Idadi ya Wananchi wanaopata huduma ya umeme mijini(urban electricity access level) imefikia asilimia 97.3ikilinganishwa na asilimia 63.4 iliyofikiwa Mwaka 2014/15;wakati wanaopata huduma ya umeme vijijini (rural electricityaccess level) imefikia asilimia 49.5 ikilinganishwa na asilimia21 iliyofikiwa Mwaka 2014/15.

29. Mheshimiwa Spika, kutokana na uhakiki ambaoulifanywa na Shirika la Takwimu la Taifa (National Bureau ofStatistics-NBS), hadi kufikia Mwezi Machi, 2017 imebainikakuwa Idadi ya Wananchi waliounganishiwa umeme (overallelectricity connection level) imefikia asilimia 32.8ikilinganishwa na asilimia 30 Mwaka 2015/16. Aidha, Idadiya Wananchi waliounganishiwa umeme mijini (urbanelectricity connection level) imefikia asilimia 65.3 wakatiwaliounganishiwa umeme vijijini (rural electricity connectionlevel) imefikia asilimia 16.9.

Kuongeza Uzalishaji wa Umeme

Mradi wa Kinyerezi II – MW 240

30. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mradi waKinyerezi II unaendelea vizuri. Gharama zote za utekelezajiwa Mradi huu zimeshalipwa. Kazi zifuatazo zimeshafanyikaau zinaendelea kufanyika: Mkandarasi SUMITOMO kutoka

Page 85: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

85

Japan anaendelea na ujenzi wa miundombinu na misingi(foundations and concrete beams) kwa ajili ya kusimikaMitambo sita (6); ujenzi wa Jengo la Ofisi umekamilika nakwa sasa linatumiwa na Wataalam wa SUMITOMO, TOSHIBAna TANESCO; na utengenezaji wa mitambo (manufacturing)unaendelea nchini Japan, Korea Kusini na Singapore. Aidha,transfoma nne (4) kati ya nane (8) na Mitambo mitatu (3)kati ya sita (6) iliwasili nchini Mwezi Februari, 2017 ambapokazi ya kufunga Mitambo imeanza Mwezi Aprili, 2017.

31. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha wa 2017/18 utengenezaji wa Mitambo ya Mradiwa Kinyerezi II viwandani utakamilishwa na kazi ya ufungajiwa Mitambo itaendelea. Aidha, Mtambo wa kwanza wakuzalisha umeme wa MW 30 unategemewa kukamilikaifikapo Mwezi Desemba, 2017 na Mradi mzima unatarajiwakukamilika Mwezi Desemba, 2018.

Mradi wa Kinyerezi I Extension – MW 185

32. Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu Mradiwa Kinyerezi I MW 150 ulikamilika na kuanza kuzalisha umemerasmi Mwezi Machi, 2016. Baada ya Mradi huo kukamilika,Serikali kupitia TANESCO iliingia Makubaliano na Kampuni yaJacobsen Elektro AS ya Norway ili kupanua Mradi huo kwakuongeza Mitambo mingine ya MW 185 (Kinyerezi I Extension)na hivyo kufanya uwezo wa Kituo hicho kuwa na Jumla yaMW 335. Makubaliano hayo yalitokana na azma ya Serikaliya kuondoa upungufu wa nishati ya umeme kwa kutumiaGesi Asilia inayopatikana nchini mwetu.

33. Mheshimiwa Spika, kazi zilizofanyika kwa Mradiwa Kinyerezi I Extension ni kukamilisha malipo ya Mkandarasiwa Ufundi, Kampuni ya Citec kwa asilimia 90 na Kampuniya General Electric ya Marekani imekamilisha matengenezoya Mitambo kwa asilimia 100 na Mitambo ipo tayarikusafirishwa kuja nchini. Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18, Mkandarasi ataendelea na kazi ya ufungaji wa Mitamboambapo Shilingi bilioni 60, fedha za Ndani zimetengwa kwa

Page 86: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

86

ajili ya kazi hiyo. Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapomwishoni mwa Mwaka 2019.

Mradi wa Mto Malagarasi - MW 45

34. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusisha ujenziwa Mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 45 kwa kutumiamaji ya Mto Malagarasi uliopo Mkoani Kigoma naunatekelezwa na TANESCO. Aidha, Benki ya Maendeleo yaAfrika (AfDB) imeonesha nia ya kufadhili Mradi huu. Taratibuza kumpata Mshauri Mwelekezi wa Mradi zinaendeleaambapo kwa sasa uchambuzi wa zabuni unafanyika naunatarajiwa kukamilika Mwezi Mei, 2017. Gharama zautekelezaji wa Mradi huu ni Dola za Marekani milioni 149.5,sawa na takriban Shilingi bilioni 345.49 na unatarajiwakukamilika Mwaka 2020. Katika Mwaka wa Fedha 2017/18,Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 2.8 kwa ajili yakuanza kugharamia utekelezaji wa Mradi huu.

Mradi wa Kakono - MW 87

35. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusu ujenzi waMtambo wa kuzalisha umeme wa MW 87 kwa kutumia majiya Mto Kagera uliopo Mkoani Kagera na unateke- lezwa naTANESCO. Serikali imewasilisha maombi ya Mkopo kwa Benkiya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Mwezi Julai, 2016 kwa ajiliya kutekeleza Mradi huu ambapo AfDB wameonesha nia yakuufadhili. Mshauri Mwelekezi Kampuni ya SP StudioPietrangeli ya Italia amepatikana kwa ajili ya usimamizi waMradi.

36. Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha taratibuza kubadilisha umiliki wa eneo la Mradi wa Kakono lenyeukubwa wa Hekta 1,100 kutoka kwa Wamiliki wa sasa(NARCO na Kagera Sugar) kwenda TANESCO. Maombiyamewasilishwa kwa Mamlaka husika za Wilaya za Misenyina Karagwe ili kupima na kutambua mipaka ya eneo la Mradi.Gharama za ujenzi wa Mtambo na njia ya usafirishaji umemeni Dola za Marekani milioni 379.4, sawa na takriban Shilingibilioni 876.79 na Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo

Page 87: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

87

Mwaka 2021. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza Mradihuo kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ni Shilingi bilioni 2.05ambazo ni fedha za Nje.

Mradi wa Rusumo - MW 80

37. Mheshimiwa Spika, Mradi huu wa Rusumo waMW 80, Tanzania itapata MW 26.6. Katika kipindi cha Mwakawa Fedha wa 2016/17 Wakandarasi wa kujenga Kituo chakufua umeme, COCO Group Jingal Water (China) andHydropower Construction Company (Canada), walisainiMkataba tarehe 9 Novemba, 2016. Wakandarasi haowatahusika na kazi za “Civil and Hydro- mechanical”.Pamoja nao watakuwepo Andritz Hydro GmbH andAndritz Hydro PVT Ltd kutoka nchi ya Austria watakaohusikana kazi za Electro-mechanical. Aidha, malipo ya awali kwaWakandarasi kiasi cha Dola za Marekani milioni 16.3 sawana takriban Shilingi bilioni 37.67 yamefanyika na utekelezajiwa Mradi unaendelea.

38. Mheshimiwa Spika, uzinduzi rasmi wa kuanzaujenzi (Ground breaking ceremony) wa Kituo cha kufuaumeme cha Rusumo ulifanywa na Mawaziri wanaosimamiamasuala ya Nishati wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi,pamoja na Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo yaAfrika (AfDB) tarehe 30 Machi, 2017. Gharama za ujenzi waMtambo wa kufua umeme ni Dola za Marekani milioni 340sawa na takriban Shilingi bilioni 785.74. Mchango wa Serikalini Dola za Marekani milioni 113 ambao ni Mkopo kutokaBenki ya Dunia (WB). Kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18,kiasi cha Shilingi bilioni 2.8 kimetengwa kugharamiashughuli za ujenzi wa Kituo hicho na Mradi unatarajiwakukamilika Mwaka 2020.

Mradi wa Somanga Fungu (Lindi) - MW 300

39. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza kiwango chauzalishaji wa umeme nchini, Serikali imepanga kuongezaMitambo ya kuzalisha umeme ya MW 300 kwa kutumia GesiAsilia katika eneo la Somanga Fungu Wilaya ya Kilwa, Mkoani

Page 88: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

88

Lindi. Upembuzi Yakinifu wa Mradi ulikamilika Mwezi Oktoba,2016 kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia. Hatua inayofuata nikutangazwa kwa Mradi ili kupata Mtekelezaji (EPC &Financing) atakayeshirikiana na Serikali kutekeleza Mradiunaokadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 423, sawana takriban Shilingi bilioni 977.55 na unatarajiwa kukamilikaMwaka 2020.

Mradi wa Somanga Fungu - MW 240.

40. Mheshimiwa Spika, ili kuendelea kuongezakiwango cha uzalishaji wa umeme nchini, Serikali kupitiaTANESCO imepanga kutekeleza mradi wa MW 240 kwakutumia gesi asilia. Mradi huu utatekelezwa katika eneo laSomanga Fungu, Kilwa kwa utaratibu wa EPC with financingkupitia Kampuni ya Sumitomo ya Japan. Gharama zakutekeleza mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za MarekaniMilioni 300 ambapo asilimia 85 itatolewa na Benki ya Japan(Japan Bank for International Cooporation - JBIC) na asilimia15 ya fedha hizo itatolewa na Serikali ya Jamhuri yaMuungano ya Tanzania.

41. Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu wamradi huu inaendelea na inatarajiwa kukamilika baada yamiezi mitatu (3). Kazi yote ya ujenzi inatarajiwa kufanyikandani ya miaka miwili (2) na mradi unatarajiwa kukamilikaMwaka 2020. Mradi huu utamilikiwa na Serikali.

Mradi wa Kufua Umeme Mtwara - MW 300

42. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO ilianzamajadiliano na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake laUshirikiano wa Kimataifa (JICA) kuhusu utekelezaji wa Mradiwa Kuzalisha Umeme kwa kutumia Gesi Asilia wa MW 300.Mradi huu utahusisha ujenzi wa Mitambo ya kufua umemena njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 400 kutokaMtwara hadi Somanga Fungu.

43. Mheshimiwa Spika, Kazi zinazoendelea kwasasa ni upembuzi yakinifu na baada ya hapo TANESCO

Page 89: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

89

itafanya majadiliano ya kiufundi na kifedha. Utekelezaji wamradi huo utaimarisha upatikanaji wa umeme katika Mikoaya Lindi na Mtwara pamoja na kuingiza Mikoa hiyo katikaGridi ya Taifa. Aidha, ujenzi huo utawezesha kuuza umemewa ziada nchi za jirani ikiwemo Msumbiji. Mradi huuunatarajiwa kukamilika Mwaka 2020 na utamilikiwa naSerikali.

Mradi wa Umeme wa Makaa ya Mawe Kiwira - MW 200

44. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia STAMICOimeanza majadiliano na Serikali ya Urusi ambayo imeoneshania ya kufadhili utekelezaji wa Mradi wa Kiwira kwa ajili yakuzalisha umeme wa MW 200 kwa kutumia Makaa ya Mawepamoja na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongowa kV 400 kutoka Kiwira hadi Kituo cha Mwakibete (Mbeya)na kuingizwa katika Gridi ya Taifa. Kazi zitakazofanyikaMwaka 2017/18 ni pamoja na kukamilisha majadiliano naMwekezaji na kuendelea kuchimba makaa ya mawe.Gharama ya Mradi wote inakaridiwa kuwa Dola za Marekanimilioni 440.

Miradi ya Kinyerezi III - MW 600 na Kinyerezi IV - MW 330

45. Mheshimiwa Spika, Miradi hii imepangwakutekelezwa chini ya Mpango wa ubia kati ya Serikali na SektaBinafsi (PPP). Aidha, Majadiliano ya utekelezaji wa Miradiyamechukua muda mrefu kutokana na sababu mbalimbaliikiwemo Wabia kuhitaji dhamana ya Serikali (GovermentGuarantee); Mwekezaji kutaka Serikali iingie Makubaliano yamoja kwa moja na Wakopeshaji (Direct Agreement withLenders); Mfumo wa utekelezaji miradi kati ya Build Own andOperate (BOO) na Build Own Operate and Transfer (BOOT)kwa miradi ya IPP, na Bei ya umeme (tariff) zinazopendekezwana Wawekezaji kuwa za juu kuliko bei elekezi zinazotolewana EWURA.

46. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kusisitiza kuwaMfumo wa utekelezaji miradi utumike wa Build Own andOperate (BOO) au EPC & Financing ambapo hakutakuwa

Page 90: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

90

na Government Guarantee, Capacity Charge wala MinimumOff - Take. Aidha, CAPEX (Investment cost) isiwe sehemu yaformula itakayotumika kupata bei ya umeme (tariff) naTANESCO italipia gharama za energy component (variableOperation and Maintenance cost - O&M).

Miradi ya Uzalishaji Umeme ya Sekta Binafsi

47. Mheshimiwa Spika, upande wa Miradi yaUzalishaji Umeme inayotekelezwa na Sekta Binafsi (IPP)ikiwemo Mradi wa Somanga Fungu MW 320 wa Kilwa Energy;Mradi wa Mchuchuma MW 600; na Ngaka MW 400 chini yaShirika la Maendeleo la Taifa (NDC) bado ipo katika hatuambalimbali za majadiliano.

Upanuzi na Uboreshaji wa Njia za Usafirishaji wa Umeme

Mradi wa Msongo wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadiShinyanga (Backbone Transmission Investment Project - BTIP)

48. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa njia ya umemewa Msongo wa kilovolti 400 na upanuzi wa Vituo vyakupozea umeme kutoka Iringa – Dodoma – Singida – Tabora- Shinyanga ulikamilika Mwezi Desemba, 2016 kwa asilimia100. Kwa sasa umeme unasafirishwa kwa kutumia njia hiyona kupelekea kuboresha upatikanaji wa umeme katikamaeneo ya Mikoa hiyo na kwenye Gridi ya Taifa kwa ujumla.Uzinduzi rasmi wa Mradi huu utafanywa na Mheshimiwa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mradi wa Msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadiSongea na Usambazaji wa Umeme Vijijini kwa Mikoa yaNjombe na Ruvuma

49. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusu ujenziwa njia ya kusafirisha umeme wa Msongo wa kV 220 kutokaMakambako hadi Songea yenye urefu wa kilomita 250, ujenziwa Vituo Vipya vya kupozea umeme eneo la Madaba na

Page 91: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

91

Songea, umeme wa Msongo wa kV 220/33 na upanuzi waKituo cha kupozea umeme cha Makambako. Kwa upandewa njia ya kusafirisha umeme kV 220 Makambako – Songea,Mkandarasi amekamilisha manunuzi ya vifaa vya Mradi nausimikaji wa nguzo umeanza Mwezi Machi, 2017.

50. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa ujenziwa Vituo vitatu (3) vya kupoza umeme vyenye uwezo wa kV220/33 katika maeneo ya Makambako, Madaba na Songea,Wakandarasi Kampuni za Shandong Taikai na NorinoInternational za China zinaendelea kupima sampuli zaudongo na kusawazisha maeneo ya kujenga Vituo hivyo naujenzi utaanza Mwezi Mei, 2017. Aidha, kwa upande wa kaziya usambazaji umeme, Mkandarasi Kampuni ya IsoluxIngenieria S.A ya Hispania inaendelea na kazi ya kusimikanguzo na kuvuta nyaya ambapo hadi kufikia Mwezi Aprili,2017 amekamilisha umbali wa kilomita 365 kati ya 580, sawana asilimia 62.9 katika maeneo ya Mkoa wa Ruvuma. Kwaupande wa Makambako hadi Njombe usimikaji wa nguzona kuvuta nyaya umefikia kilomita 118 kati ya kilomita 393,sawa na asilimia 30. Aidha, Kituo kidogo cha kupozeaumeme cha Songea kV 33/11 kimekamilika kwa asilimia 52.

51. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka waFedha wa 2017/18 Wakandarasi Shandong Taikai na NorinoInternational za China wataendelea na kazi za kukamilishaujenzi wa Vituo vya kupoza umeme na Kampuni ya KalpataruPower Transmission Ltd ya India itaendelea na ujenzi wa njiaya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.Aidha, Kampuni ya Isolux ya Hispania itaendelea na ujenziwa njia ya usambazaji umeme na kuunganisha vijiji vilivyopokati ya Makambako hadi Songea kwenye Mkuza wa njia yausafirishaji umeme. Kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 Mradiumetengewa Shilingi bilioni 3 fedha za Ndani ikiwa nimchango wa Serikali na Shilingi bilioni 8 ikiwa ni fedha zaNje kutoka Serikali ya Sweden kupitia Shirika lake la Maendeleola Kimataifa (Sida). Utekelezaji wa Mradi huu unatarajiwakukamilika Mwezi Agosti, 2018.

Page 92: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

92

Mradi wa Njia ya Umeme ya Msongo wa kilovolti 400 waSingida – Arusha – Namanga

52. Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Miradi yaushirikiano wa ki- Kanda ikiwemo Mradi wa njia ya kusafirishaumeme Singida – Arusha – Namanga kV 400. Kazizilizofanyika katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17 ni pamojana: TANESCO kusaini Mkataba na Kampuni ya KalpataruPower Transmission Ltd kutoka nchini India kwa ajili ya ujenziwa njia ya umeme kutoka Singida hadi Babati (km 150),Kampuni ya Bouygues Energy & Services ya Ufaransa kwa ajiliya ujenzi wa njia ya umeme kutoka Babati hadi Arusha (km150) na Kampuni ya Ubia kati ya Energoinvest ya Yugoslaviana EMC ya India kwa ajili ya ujenzi wa njia ya umeme kutokaArusha hadi Namanga (km 114); na kukamilika kwa tathminiya athari za mazingira na mali za Wananchi watakaopishaujenzi wa njia ya kusafirisha umeme.

53. Mheshimiwa Spika, taratibu za kupataMkandarasi wa ujenzi wa Kituo kipya cha Arusha cha Msongowa kV 400/220 na upanuzi wa Kituo cha Singida zimekamilika.TANESCO inatarajia kusaini Mkataba na Kampuni ya Ubiakati ya Energoinvest ya Yugoslavia na EMC ya India ambayoimeshinda zabuni Mwezi Aprili, 2017. Aidha uchambuzi wazabuni za Wakandarasi wa usambazaji umeme vijijiniumeanza. Gharama za Mradi huu ni Dola za Marekani milioni258.82, sawa na takriban Shilingi bilioni 598.13. Fedha hizizinatolewa na AfDB, JICA na Serikali ya Tanzania ambayoitachangia Dola za Marekani milioni 43.89, sawa na takribanShilingi bilioni 101.43.

54. Mheshimiwa Spika, kazi zilizofanyika katika Mwakawa Fedha wa 2016/17 ni pamoja na kukamilisha taratibu zamalipo ya fidia na kuanza kutekeleza Mradi kwa awamu.Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18, Serikali imetengafedha za Ndani Shilingi bilioni 48 kwa ajili ya ulipaji wa fidia.Aidha, utekelezaji wa Mradi utaanza baada ya ulipaji wafidia kukamilika na Wakandarasi kulipwa malipo ya awali.Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi Desemba, 2019.

Page 93: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

93

Mradi wa North - West wa kilovolti 400 kutoka Mbeya –Sumbawanga – Mpanda – Kigoma – Nyakanazi

55. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2016/17 kazi ambazo zimefanyika ni pamoja na: kudurusuUpembuzi Yakinifu wa Mradi kutoka Msongo wa kV 220 nakuwa kV 400 kwa eneo la Mbeya hadi Nyakanazi lenye urefuwa kilomita 1,080; utafiti wa athari za mazingira kwa Awamuya Pili kutoka Nyakanazi – Kigoma - Mpanda, kilomita 568ambao umekamilika Mwezi Februari, 2017; na kuanzaMajadiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania, Serikali ya Korea ya Kusini kupitia Shirika lake laMaendeleo (EDCF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)kwa ajili ya kupata fedha za utekelezaji wa Mradi. Hatuailiyofikiwa ni kwamba tayari Serikali kupitia Wizara ya Fedhana Mipango imewasilisha maombi rasmi kwa Taasisi hizo yaDola za Marekani milioni 428 sawa na takriban Shilingi bilioni989.11.

56. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa2017/18 kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kukamilishataratibu za upatikanaji wa fedha za kutekeleza sehemu yaMradi huo kutoka Nyakanazi hadi Kigoma kwa ufadhili waEDCF ya Korea Kusini ambayo imeonesha nia ya kutoaMkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 50,sawa na takriban Shilingi bilioni 115.55; kukamilisha utafitiwa athari za mazingira kutoka Mpanda hadi Sumbawanga;na kulipa fidia Wananchi kutoka Nyakanazi hadi Kigomaambapo Shilingi bilioni 12.3 zimetengwa katika Mwakawa Fedha wa 2017/18.

Mradi wa North - East wa kilovolti 400 kutoka Kinyerezi hadiArusha kupitia Chalinze na Segera

57. Mheshimiwa Spika, Mradi huu una lengo lakusafirisha umeme kutoka Kituo cha Kinyerezi, Dar es Salaamhadi Arusha kwa lengo la kukidhi mahitaji ya umeme kwenyeGridi ya Taifa hususan katika Mikoa ya Pwani, Tanga,Kilimanjaro na Arusha. Gharama ya Mradi huu ni takribanDola za Marekani milioni 692.7, sawa na takriban Shilingi

Page 94: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

94

trilioni 1.6 ambapo Benki ya Exim ya China itatoa Mkopowa asilimia 85 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania itatoa asilimia 15 ya gharama za Mradi.

58. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2016/17 kazi zilizofanyika kwenye Mradi huu ni pamoja na:kusainiwa kwa Mkataba wa Mkopo na pande husika MweziAgosti, 2016; kusainiwa kwa Mkataba kati ya TANESCO naMtaalamu Mshauri Kampuni ya TBEA kutoka China kwa ajiliya usimamizi wa Mradi Mwezi Januari, 2017; na kukamilikakwa tathmini ya mali kwa maeneo ya kujenga Vituo vyakupoza umeme vya Segera na Tanga pamoja na eneo lanjia ya umeme kutoka Kinyerezi hadi Kiluvya, Dar es Salaam.

59. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2017/18 kazi zilizopangwa kufanyika kwenye Mradi huu nikukamilisha tathmini ya mali za Wananchi watakaopishasehemu ya Mradi, pamoja na kulipa fidia kwa Awamu yaKwanza kutoka Kinyerezi hadi Chalinze. Serikali imetengafedha za Ndani kiasi cha Shilingi bilioni 19.80 kwa ajili yakulipa fidia kwa Waathirika pamoja na mchango wa sehemuya asilimia 15 ya gharama ya Mradi.

Mradi wa njia ya umeme ya Msongo wa kilovolti 400 kutokaSomanga Fungu hadi Kinyerezi

60. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusu ujenzi wanjia ya kusafirisha umeme kutoka eneo la Somanga FunguMkoani Lindi hadi Kinyerezi Mkoani Dar es Salaaam pamojana ujenzi wa Kituo cha kupoza umeme eneo la SomangaFungu. Njia hii itatumika kusafirisha umeme utakaozalishwana Mitambo yenye uwezo wa kufua takriban MW 620inayotarajiwa kujengwa eneo la Somanga Fungu KilwaMkoani Lindi. Katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17 TANESCOimesaini Mkataba na Mtaalam Mshauri Kampuni ya ByucksanPower Ltd ya Korea Kusini ili kudurusu Upembuzi Yakinifu nakusimamia ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme; na kulipafidia kwa Wananchi wanaopisha ujenzi wa njia hiyo. Hadikufikia Mwezi Machi, 2017 ulipaji wa fidia kwa mali zaWaathirika wa Mradi ulikuwa umefanyika kwa Waathirika

Page 95: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

95

2,305 kati ya 3,901 (sawa na asilimia 59.1) kwa kiasi cha Shilingibilioni 46.29.

Mradi wa njia ya Umeme wa Msongo wa kilovolti 220kutoka Kituo cha Kufua Umeme wa Maji cha Rusumo hadiNyakanazi

61. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Rusumo wa MW 80unahusisha ujenzi wa njia za kusafirisha umeme kutokaRusumo, Mto Kagera hadi kwenye Gridi ya nchi za Burundi,Rwanda na Tanzania. Kwa upande wa Tanzania, Mradi huuunahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Kituocha kuzalisha umeme cha Rusumo hadi Nyakanazi yenye urefuwa kilomita 98 kwenye Msongo wa kV 220. Mradi huuutasaidia kuunganisha Mikoa ya Kagera, Kigoma, Rukwa naKatavi kwenye Mfumo wa Gridi ya Taifa na kuipatia umememwingi zaidi na wa uhakika.

62. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha wa 2016/17 kazi zilizofanyika kwenye Mradi huu nipamoja na: kusainiwa kwa Mkataba Mwezi Desemba, 2016kati ya TANESCO na Mtaalam Mshauri, Kampuni za WSPCanada Inc. na GOPA International Energy Consultant GmbHya Ujerumani kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa Mradi;upimaji wa njia na kufanya tathmini ya fidia ya mali zaWananchi watakaopisha eneo la Mradi. Aidha, Serikaliimewasilisha taarifa ya Upembuzi Yakinifu Benki ya Maendeleoya Afrika (AfDB) Mwezi Februari, 2017 kwa ajili ya ujenzi waKituo cha kupoza umeme eneo la Benaco lililopo WilayaniNgara, Mkoani Kagera.

63. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 kazi zitakazofanyika kwenye Mradi huu ni:kukamilisha ulipaji wa fidia kwa Waathirika wa Mradi nakuwapata Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa njia yakusafirisha umeme pamoja na Kituo cha kupoza umeme chaBenaco Wilayani Ngara, Mkoani Kagera. Serikali imetengakiasi cha Shilingi bilioni 5.2 fedha za Ndani kwa ajili ya kulipafidia.

Page 96: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

96

Mradi wa Njia ya umeme ya Msongo wa kilovolti 220 kutokaBulyanhulu hadi Geita

64. Mheshimiwa Spika, Mradi utahusisha ujenzi wanjia ya umeme wa Msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita55 pamoja na usambazaji umeme katika vijiji vinavyopitiwana Mradi Wilayani Geita. Mradi huu unatekelezwa kwaMkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Kiarabu (Arab Bankfor Economic Development in Africa - BADEA), OPEC Fund forInternational Development (OFID) na Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania. Kazi zilizofanyika kwa Mwaka waFedha wa 2016/17 ni kukamilisha uchambuzi wa zabuni zakuwapata Wakandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirishaumeme Mwezi Februari, 2017 na tathmini ya mali za Wananchiwatakaopisha eneo la Mradi.

65. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa2017/18 kazi zitakazofanyika kwenye Mradi huu ni kulipa fidiakwa Wananchi watakaopisha eneo la Mradi na pia kuanzaujenzi. Fedha za Nje zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza Mradihuu ni Shilingi bilioni 7 na fedha za Ndani ni Shilingi bilioni 1kwa ajili ya kulipa fidia.

Mradi wa Njia ya umeme ya Msongo wa kilovolti 220kutoka Geita hadi Nyakanazi

66. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusisha ujenziwa njia ya kusafirisha umeme wa Msongo wa kV 220 yenyeurefu wa kilomita 133, Kituo cha kupoza umeme chaNyakanazi na kusambaza umeme kwenye vijiji vinavyopitiwana Mradi. Aidha, Mradi huu utagharimu takriban Euro milioni45 sawa na Shilingi bilioni 95.67 kwa ufadhili wa KfW yaUjerumani, AFD ya Ufaransa, Jumuiya ya Ulaya (EU) na Serikaliya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

67. Mheshimiwa Spika, kazi zilizofanyika kwenye Mradihuu kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17 ni pamoja na: upimajiwa njia kuu ya usafirishaji umeme kutoka Geita hadiNyakanazi;tathmini ya gharama ya fidia kwa mali za

Page 97: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

97

Wananchi watakaoathirika; tathmini ya athari ya kijamii namazingira; pamoja na usanifu wa Mradi.

68. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa2017/18 kazi zitakazofanyika kwenye Mradi huu ni pamojana kukamilisha ulipaji wa fidia kwa Wananchi watakao-athirika pamoja na kuanza utekelezaji wa Mradi. Fedha zaNje zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza Mradi huu ni Jumlaya Shilingi bilioni 9.1 ambapo Shilingi bilioni 1.6 ni fedha zaNje na fedha za Ndani ni Shilingi bilioni 7.5 kwa ajili ya kulipafidia.

Miradi ya Usambazaji wa Umeme

Mradi wa kuboresha Mfumo wa usamba- zaji umeme katikaJiji la Dar es Salaam chini ya Ufadhili wa JICA

69. Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulihusisha kazizifuatazo: ukarabati wa Kituo cha Ilala kV 132/33/11; ujenziwa Jengo Jipya la “Control Center” la Ilala; ufungaji wa njiaya pili ya usafirishaji umeme wa Msongo wa kV 132 kutokaUbungo hadi Ilala; kupanua Kituo cha kupoza umeme chaMsasani kV 33/11; ujenzi wa Vituo Vipya vinne (4) vya kupozaumeme wa kV 33/11 vya Jangwani Beach, Mwananyamala,Msasani na Muhimbili; ujenzi wa njia mpya za Msongo wa kV33 kutoka Vituo vya kupoza umeme vya Makumbusho, CityCentre na Tegeta kwenda Vituo Vipya vya Mwananyamala,Muhimbili, Jangwani na Msasani.

70. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mradi huuulifadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake laMaendeleo la JICA kwa gharama ya Dola za Marekanimilioni 38, sawa na takriban Shilingi bilioni 87.82 nautekelezaji wake umekamilika kwa asilimia 100 Mwezi Machi,2017. Mradi huu unasubiri kuzinduliwa rasmi na Viongozi waKitaifa.

Page 98: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

98

Mradi wa Kuboresha Mfumo wa Usambazaji Umeme katikaManispaa ya Dodoma chini ya Ufadhili wa JICA

71. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCOipo katika majadiliano na Serikali ya Japan kupitia Shirikalake la Ushirikiano la Kimataifa (JICA) katika utekelezaji waMradi wa kuboresha mfumo wa Usambazaji Umeme katikaManispaa ya Dodoma. Mradi huu utahusisha ujenzi wa njiaya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 132 yenye urefu wakilometa 135 kutoka Zuzu kwenda Msalato na Kikombo naujenzi wa Vituo viwili (2) vya kupoza umeme vyenye uwezowa MVA 90 kila kimoja katika maeneo ya Msalato naKikombo. Kazi nyingine itakuwa ni ujenzi wa njia zakusambaza umeme za msongo wa kV 33 zenye urefu wakilometa 71 katika Manispaa ya Dodoma.

72. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mradi huuutaimarisha upatikanaji wa umeme katika Manispaa yaDodoma na vitongoji vyake na pia kukidhi mahitaji yaumeme yatakayoongezeka kutokanaa na Dodoma kuwaMakao Makuu ya nchi. Aidha, Mradi huu unatarajiwakuanza Mwaka wa fedha 2018/19 na utagharimu Dola zaMarekani milioni 38 sawa na takriban Shilingi bilioni 76.Mradi wa TEDAP wa Kuboresha Njia za Usambazaji Umeme(Distribution) Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam na Kilimanjarochini ya Ufadhili wa Benki ya Dunia

73. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusisha upanuzina ujenzi wa Vituo Vipya 19 vya kupoza umeme waMsongo wa kV 33/11 pamoja na ujenzi wa njia za usambazajiumeme kwa Msongo wa kV 33 na kV 11 zenye urefu wakilomita 107 na kilomita 34.01 sawia katika Mikoa ya Arusha,Dar es Salaam na Kilimanjaro kwa gharama ya Dola zaMarekani milioni 43, sawa na takriban Shilingi bilioni 99.37.Fedha hizi zimetolewa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wakewa TEDAP.

74. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Mradi huu upokatika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo hadi kufikiaMwezi Aprili, 2017 asilimia 85 ya kazi zote zilizopangwa

Page 99: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

99

zilikamilika na matarajio ni kukamilisha Mradi huo ifikapoMwezi Juni, 2017.

Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme Jijini Dar esSalaam chini ya Ufadhili wa Finland

75. Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulihusishauboreshaji wa miundombinu ya umeme katika Jiji la Dar esSalaam kwa kufanya yafuatayo: kujenga Kituo kipya chakupoza umeme cha Msongo wa kV 132/33; kufungaKangavuke mbili (2) zenye uwezo wa MVA 50 kila mojakwenye Kituo cha City Centre; kujenga njia ya umeme waMsongo wa kV 132 chini ya ardhi kutoka Kituo cha Ilalahadi Kituo kipya cha City Centre; kujenga njia ya mzungukowa umeme (ring circuit) chini ya ardhi wa Msongo wa kV 33kutoka Kituo cha kupoza umeme cha City Centre kwendaSokoine – Railway – Kariakoo na kurudi tena City Centre;pamoja na kuanzisha Kituo cha kuongozea Mifumo yaUsambazaji umeme katika Msongo wa kV 33 na kV 11(Distribution SCADA) katika eneo la Mikocheni.

76. Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulifadhiliwa naSerikali ya Finland kwa gharama ya Euro milioni 21.8 na Dolaza Marekani milioni 1.5 sawa na takriban Shilingi bilioni 3.47.Kituo cha kuongozea Mifumo ya Usambazaji umeme katikaMsongo wa kV 33 na kV 11 (Distribution SCADA) kilichopoMikocheni kilizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri waMuungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(Mb.) tarehe 16 Novemba, 2016. Mradi huo ulikamilika MweziFebruari, 2017.

Mradi wa ORIO kwa Miji ya Ngara, Biharamulo na Mpanda

77. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusisha ufungajiwa Mitambo ya kufua umeme yenye uwezo MW 2.5 kwakila Wilaya za Biharamulo, Mpanda na Ngara na kupanuanjia za usambazaji umeme kwa lengo la kuyapatia maeneohusika umeme wa uhakika. Gharama ya Mradi ni Euro milioni33.5 sawa na Shilingi bilioni 71.22 kupitia ufadhili wa Serikali

Page 100: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

100

ya Uholanzi iliyotoa asilimia 50 na Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania iliyotoa asilimia 50.

78. Mheshimiwa Spika, Mradi huu umekamilika kwaWilaya ya Biharamulo Mwezi Septemba, 2016 na Wilayaya Ngara Mwezi Desemba, 2016. Mafunzo ya Wajasiriamalikatika maeneo ya Mradi na mafunzo ya afya na usalamakazini kwa Wafanyakazi wa TANESCO katika Vituo hivi vyaumeme vya Biharamulo, Mpanda na Ngara yamefanyikaMwezi Machi, 2017. Kazi inayoendelea kwa sasa ni ufungajiwa Mitambo ya kufua umeme na ujenzi wa miundombinuya kusambaza umeme katika Wilaya ya Mpanda ambapounatarajia kukamilika Mwezi Juni, 2017.

Mradi wa TANESCO wa Urban Electrification

79. Mheshimiwa Spika, Mradi huu unahusu usambazajiumeme kwa Wateja ambao hawajaunganishwana umememaeneo ya mijini (urban electrification programme). Aidha,Mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya Msongo wa kilovolti132 kutoka Morogoro hadi Mtibwa umeingizwa kamasehemu ya utekelezaji wa Mradi huu. Benki ya Maendeleo yaAfrika (AfDB) imeonesha nia ya kufadhili Mradi huu kwagharama ya Dola za Marekani milioni 222.62 sawa natakriban Shilingi bilioni 514.47.

80. Mheshimiwa Spika, kazi zitakazofanyikakwenye Mradi huu kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 nipamoja na: TANESCO kuboresha Upembuzi Yakinifu (feasibilitystudy) ikihusisha Mradi wa Morogoro – Mtibwa wa kV 132;Serikali kusaini Mkataba wa Ufadhili na AfDB; na baadaekuanza utekelezaji wa Mradi.

Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini kupitia Wakala waNishati Vijijini (REA)(i) Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA Turnkey Phase II)

81. Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha azma yaSerikali ya kuhakikisha kuwa Wananchi wengi zaidi wanapata

Page 101: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

101

huduma za umeme, Serikali ilitekeleza Mradi Kabambe waAwamu ya Pili (REA Turnkey Phase II) wa Kusambaza UmemeVijijini katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. Katika kipindi chaMwaka wa Fedha wa 2016/17 Wakala ulikamilisha kazizifuatazo: ujenzi wa Vituo sita (6) vya kuongeza nguvu yaumeme kutoka Msongo wa kV 11 hadi 33 katika Miji ya Kasulu,Kibondo, Kigoma, Mbinga, Ngara na Tunduru; ujenzi wa njiaza kusambaza umeme za Msongo wa kV 33 zenye urefu wakilomita 17,740; ujenzi wa Vituo Vidogo vya kupoza nakusambaza umeme 4,100; na ujenzi wa njia ndogo yausambazaji umeme zenye urefu wa kilomita 10,970. Hadikufikia Mwezi Machi, 2017, Wateja wa awali 153,821 sawa naasilimia 62 walikuwa wameunganishiwa umeme kati yaWateja 250,000 waliopangwa kuunganishwa.

Aidha, kazi za kuunganisha umeme kwenye MakaoMakuu ya Wilaya 13 za Busega, Buhigwe, Chemba, Itilima,Kakonko, Kalambo, Kyerwa, Mkalama, Mlele, Momba,Nanyumbu, Nyasa, na Uvinza zimekamilika na kufanya Jumlaya Makao Makuu ya Wilaya zilizopelekewa umeme kupitiaMiradi ya REA kufikia 25. Gharama za Mradi wa huu ni Shilingibilioni 900.15 zote zikiwa ni fedha za Ndani.

(ii) Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamuya Tatu (REA Turnkey Phase III)

82. Mheshimiwa Spika, hadi Mwezi Agosti, 2016 Vijiji4,395 vilikuwa vimefikiwa na umeme sawa na asilimia 36 yavijiji 12,268 vilivyopo Tanzania Bara. Lengo la Serikali ni kufikiaVijiji 7,873 vilivyosalia ifikapo Mwaka 2020/21. Kwa Mwakawa Fedha wa 2016/17 maandalizi ya Mradi wa KusambazaUmeme Vijijini Awamu ya Tatu yamekamilika na utekelezajiumeanza. Mradi huu ni wa miaka mitano (5) kuanzia 2016/17 hadi 2020/21 na unalenga kufikisha huduma ya umemekwenye vijiji vyote nchini ambavyo bado havijafikiwa naumeme. Mradi unahusisha: kuongeza wigo wa usambazajiumeme kwenye maeneo yaliyofikiwa na miundombinu yaumeme (Densification); kufikisha umeme wa Gridi kwenye vijijiambavyo havijafikiwa na umeme (Grid extension); na Miradiya umeme ya nje ya Gridi (off-grid) utokanao na NishatiJadidifu, hasa Umeme Jua (Solar power).

Page 102: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

102

83. Mheshimiwa Spika, hatua zilizofikiwa katikamaandalizi na utekelezaji ni pamoja na kukamilika kwauandaaji wa orodha ya vijiji ambavyo havijapatiwa umeme;kusainiwa Mikataba na kuanza utekekelezaji wa Awamuya Kwanza ya Mradi wa Densification Mwezi Desemba,2016 unaohusisha Mikoa ya Arusha, Iringa, Mara, Mbeya,Pwani na Tanga kwa ufadhili wa Serikali ya Norway kwa kiasicha Shilingi bilioni 28.62. Aidha, taratibu za upatikanaji waWakandarasi wa kusambaza umeme kwenye vijiji vilivyokwenye Mkuza wa njia ya kusafirisha umeme wa BackborneTransmission Investment Project (BTIP) kutoka Iringa hadiShinyanga umekamilika na Mradi umeanza kutekelezwaMwezi Januari, 2017. Vilevile, uchambuzi wa maombi 300 yakusambaza umeme wa Nishati Jadidifu kwa vijiji vilivyo njeya Gridi ya Taifa umekamilika na utekelezaji wake utaanzaMwezi Julai, 2017.

84. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa2017/18 Serikali itaendelea na utekelezaji kwa kufikishaumeme katika vijiji 3,559 ambavyo tayari Wakandarasiwalishaanza kazi. Aidha, Serikali kupitia REA itakamilishataratibu za ununuzi wa Wakandarasi kwa ajili ya kufikishaumeme kwenye vij i j i 4,314 vil ivyosalia ambavyovinajumuisha vijiji ambavyo vitapatiwa umeme wa nje yaGridi (off-grid). Aidha, Serikali itaendelea na kusambazaumeme kwenye vijiji vilivyo pembezoni mwa Mkuza wa njiaya kusafirisha umeme wa Backborne Transmission InvestmentProject (BTIP) kutoka Iringa hadi Shinyanga.

85. Mheshimiwa Spika, Fedha zinazohitajikakutekeleza Mradi huu kwa Miaka Mitano ni takriban Shilingitrilioni 7. Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18 Serikaliimetenga kiasi cha Shilingi bilioni 469.09 fedha za Ndani naShilingi bilioni 30 fedha za Nje.

(iii) Mradi wa Mfano wa Kupunguza Gharama zaMiundombinu ya Usambazaji Umeme Vijijini (Low Cost DesignStandards for Rural Electrification)

86. Mheshimiwa Spika, katika kupunguza gharamaza ujenzi wa miundombinu ya usambazaji umeme vijijini,

Page 103: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

103

Serikali ilipata ruzuku kutoka Benki ya Dunia ya kufanya utafitikuhusu gharama hizi na kutekeleza Mradi wa Mfano. Utafitihuo ulifanyika katika Wilaya za Kilombero na Mbozi ambapoulibaini kuwa gharama zinaweza kupungua kwa kati yaasilimia 30 hadi 40 iwapo Miradi itatekelezwa kwa kutumiateknolojia ya gharama nafuu. Katika Mwaka wa Fedha wa2016/17 kwenye Mradi huu kazi ya ujenzi wa miundombinuiliendelea na hadi kufikia Mwezi Desemba, 2016 kazi zilikuwazimekamilika kwa asilimia 96 (Mbozi) na asilimia 94(Kilombero). Mradi huu unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni,2017.

(iv) Utekelezaji wa Programu ya Awamu ya Pili ya Mradi waSustainable Solar Market Package (SSMP – II)

87. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Programu yaAwamu ya Pili ya Mradi wa Sustainable Solar Market Package(SSMP – II) unahusu ujenzi wa Mifumo ya Umeme Juakatika Wilaya nane (8) za Biharamulo, Bukombe, Chato,Kasulu, Kibondo, Namtumbo, Sikonge na Tunduru. Hadikufikia Mwezi Desemba, 2016, Jumla ya Mifumo Midogo yaUmeme 4,620 yenye uwezo wa kWp 115 ilifungwa. Gharamaza Mradi ni Dola za Marekani milioni 18 sawa na Shilingibilioni 41.60 ambazo ni Mkopo kutoka Benki ya Dunia.

(v) Mradi wa Kuhamasisha Upelekaji na Matumizi ya UmemeVijijini (Lighting Rural Tanzania) 2014

88. Mheshimiwa Spika, Mradi huu ulihusishakusambaza umeme unaotokana na Mifumo ya NishatiJadidifu (renewable energies) kwa kujenga Gridi NdogoNdogo zinazojitegemea kwenye maeneo yaliyo mbali naGridi ya Taifa na maeneo ya Visiwani. Mradi huu ulitekelezwana Waendelezaji 18 kwa ujumla katika maeneo mbalimbalinchini. Mradi huu unatekelezwa katika maeneo ya vijijinikatika Mikoa ya Arusha, Iringa, Kigoma, Lindi, Manyara, Mara,Mbeya, Morogoro, Mwanza, Njombe, Pwani, Ruvuma naSingida. Hadi kufikia Mwezi Desemba, 2016 Mradi ulikuwaumefikia asilimia 72 na gharama za Mradi ni Shilingi bilioni

Page 104: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

104

4. Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania.

SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI ASILIA

Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia

89. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Mwaka waFedha wa 2016/17 utafiti wa Mafuta na Gesi Asil iaumeendelea kufanyika katika maeneo ya baharini na nchikavu. Aidha, kushuka kwa bei za Mafuta na Gesi Asilia katikaSoko la Dunia, kumeathiri kasi ya shughuli za utafutaji Mafutana Gesi Asilia nchini. Pamoja na changamoto hizo, Jumlaya visima vitatu (3) vilichorongwa. Visima viwili (Kitatange-1na Bunju-1) vilichorongwa na Kampuni ya Shell/BG katikaVitalu namba 1 na 4 vilivyopo kwenye kina kirefu cha maji yaBahari ya Hindi ambapo vyote havikuwa na mashapo yaGesi Asilia kama ilivyotarajiwa. Kisima cha tatu (Ntorya -2)kilichorogwa na Kampuni ya Ndovu Resources katika Kitalucha Mtwara kuhakiki Gesi Asilia iliyogunduliwa katika Kisimacha Ntorya –1 na kazi ya kutathmini kiasi kilichopo inaendelea.Kwa sasa kiasi cha Gesi Asilia kilichogunduliwa nchini ni Jumlaya Futi za Ujazo (TCF) Trilioni 57.25 ambapo Gesi Asiliailiyogunduliwa Nchi Kavu ni TCF Trilioni 10.12 na kina kirefucha Bahari ya Hindi TCF Trilioni 47.13. Hata hivyo, ugunduzihuu mpya uliofanywa katika Kisima cha Ntorya - 2 utaongezakiasi cha Gesi Asilia iliyogunduliwa nchini baada ya tathminikukamilika.

Matumizi ya Gesi Asilia Viwandani

90. Mheshimiwa Spika, Jumla ya Viwanda 42 tayarivimeunganishwa na miundombinu ya Gesi Asilia. KatikaMwaka wa Fedha wa 2016/17, Serikali kupitia TPDCimeendelea kutafuta Wateja wapya na kuendeleza ujenziwa miundombinu ya kusambaza Gesi Asilia. Majadiliano katiya TPDC na Dangote Cement Tanzania Limited – Mtwarayamekamilika na majadiliano yanaendelea kati yake naBakhressa Food Factory, Knauf Gypsum na Lodhia Steelvilivyopo Mkuranga Mkoani Pwani. Aidha, Kiwanda cha

Page 105: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

105

Goodwill Ceramic Tanzania Limited tayari kimeunganishwana kuanza kutumia Gesi Asilia ambapo kitatumia Jumla yaFuti za Ujazo milioni saba kwa siku (7 mmscfd).

91. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TPDCitakamilisha mazungumzo na Kiwanda cha kuzalisha Mboleacha Kilwa Masoko ambacho TPDC ni Mbia pamoja naKampuni ya Ferrostaal Industry Project GmbH ya Ujerumanina Wabia wake Holdor Topsoe A/S na Fauji Fertiliser CompanyLimited. Kiwanda hiki hadi kukamilika kitagharimu kiasi chaDola za Marekani bilioni 1.92 sawa na takriban Shilingi trilioni4.44. Mahitaji ya Gesi Asilia yanatarajiwa kuwa Futi za Ujazomilioni 104 kwa siku (104 mmscfd) na kitazalisha mbolea ainaya amonia tani 2,200 kwa siku pamoja na aina ya urea tani3,850 kwa siku.

92. Mheshimiwa Spika, vilevile, mawasiliano naMajadiliano kuhusu upatikanaji wa Gesi Asilia kwa Kiwandacha kuzalisha Mbolea cha Mtwara chini ya Kampuni ya Helmya Ujerumani na Wabia wake ambao ni Halmashauri zaMkoa wa Mtwara yanaendelea. Kiwanda hiki hadi kukamilikakitagharimu kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 sawa natakriban Shilingi tril ioni 2.77. Mahitaji ya Gesi Asil iayanatarajiwa kuwa Futi za Ujazo milioni 80 kwa siku (80mmscfd) na kitazalisha mbolea tani 3,700 kwa siku.

Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (Bulk ProcurementSystem)

93. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea nausimamizi wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja kupitia Wakalawake (Petroleum Bulk Procurement Agency – PBPA). Taratibuza uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja zimeainishwa katikaSheria ya Petroli (The Petroleum Act, No. 21) ya Mwaka 2015pamoja na Kanuni za Uagizaji wa Bidhaa za Petrolikwa Pamoja - (The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations,2017, GN No. 198 of 2017). Mfumo huu unaweka utaratibu wamafuta yote kuagizwa kwa pamoja kwa kutumia utaratibumaalum unaowekwa ili pia kupata manufaa ya kiuchumi(economies of scale) na mafuta yanayokidhi ubora. Aidha,

Page 106: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

106

Mfumo huu umelenga kuhakikisha usalama wa upatikanajiwa mafuta (security of supply of petroleum products) nchinikwa wakati wote.

94. Mheshimiwa Spika, Mfumo wa zabuni ndioumekuwa unatumika katika kupata Kampuni zitakazoagizana kuleta mafuta nchini. Kampuni za mafuta huwasilishakwa Wakala kiasi cha mafuta ya petroli, dizeli, mafuta yandege na mafuta ya taa wanachohitaji kuuza kwa Mwezimzima. Baada ya kupata kiasi cha mafuta kutoka kwaKampuni hizo, Wakala huandaa nyaraka za zabuni nabaadaye kutoa taarifa ya zabuni hiyo kwa Kampuni zotezilizoidhinishwa (pre- qualified) kushiriki katika zabuni za kuletamafuta. Mafuta yanayotakiwa kutumika hapa nchini nilazima yaagizwe kwa kutumia Mfumo huu (mandatory forlocally used fuel), lakini mafuta yanayopitia hapa nchini(transit) si lazima kuagizwa kwa kupitia Mfumo huu (it isoptional).

95. Mheshimiwa Spika, Mfumo huu umeletamafanikio makubwa katika Sekta Ndogo ya Mafuta na Taifakwa ujumla. Baadhi ya mafanikio hayo ni kushuka kwagharama ya manunuzi (Premium) kutoka wastani wa Dolaza Marekani 50 kwa tani kabla ya utaratibu huu mpakawastani wa takriban Dola za Marekani 20 kwa tani na uhakikawa usalama wa upatikanaji wa mafuta nchini. Hii ni kutokanana ukweli kwamba zabuni za mafuta ya Mwezi hutolewazaidi ya Mwezi mmoja kabla ya muda husika, pamoja nauhakika wa usahihi wa takwimu za mafuta yaliyoagizwa nakuingia hapa nchini. Kutokana na takwimu hizi vyombombalimbali vinaweza kupanga mipango yake kwa ufanisizaidi ikiwemo Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi zamafuta na kiasi cha fedha zinazoweza kupatikana kwaMwezi kutokana na mafuta kwa ajili ya Mfuko wa NishatiVijijini, Mfuko wa Barabara, n.k.

96. Mheshimiwa Spika, Mfumo huu pia umesaidiakupunguza gharama za meli kusubiri kupakua mafuta(Demurrage costs). Hivi sasa gharama hizo ni kati ya Dola zaMarekani 1.6 na 3.5 kwa tani moja ya uzito tofauti na Dola

Page 107: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

107

za Marekani 45 hadi 50 kwa tani moja ya uzito iliyokuwakabla ya Mfumo huu kuanza kutumiwa. Kupungua kwagharama hizi kunatokana na upangaji mzuri wa meliunaofanywa na PBPA na kuongezeka kwa sehemu zakupakulia mafuta. Jitihada za TPA kujenga sehemu ya SPMambapo meli kubwa za dizeli zinaweza kupakua mafuta navilevile kuanza kutumika kwa Bandari ya Tanga kumepunguzasana msongamano wa meli katika sehemu ya Kurasini OilJet One (KOJ 1).

97. Mheshimiwa Spika, vilevile, Mfumo huuumewezesha EWURA kupanga bei elekezi kwa kutumiatakwimu sahihi za bei ya Mafuta katika Soko la Dunia nagharama za kusafirisha mafuta hadi hapa nchini. Aidha,Mfumo huu umepunguza gharama za meli kusubiri kabla yakupakua mafuta (demurrage) na umewezesha kudhibitiubora wa mafuta yanayoagizwa nchini.

98. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha MweziJanuari hadi Desemba, 2016 Jumla ya lita bilioni 4.97 zamafuta ziliingizwa nchini ambapo lita bilioni 4.73 ziliingizwakupitia Bandari ya Dar es Salaam na lita milioni 237.85ziliingizwa kupitia Bandari ya Tanga. Kati ya mafuta hayo,lita bilioni 2.34 sawa na asilimia 47.11 yalikuwa kwa ajili yamatumizi ya ndani na lita bilioni 2.65 sawa na asilimia 52.89yalikuwa kwa ajili ya Nchi Jirani.

99. Mheshimiwa Spika, mafuta kwa ajili ya matumiziya ndani yameongezeka kwa asilimia 2.23 kutoka lita bilioni2.29 Mwaka 2015 hadi lita bilioni 2.34 Mwaka 2016. Aidha,mafuta yaliyoagizwa kwa ajili ya Nchi Jirani (Burundi, DRC,Rwanda, Uganda na Zambia) yameongezeka kwa asilimia3.02 kutoka lita bilioni 2.57 Mwaka 2015 hadi lita bilioni 2.65Mwaka 2016. Ongezeko hilo linatokana na kukua kwamahitaji ya mafuta ndani ya nchi hizo pamoja na nchi jiranikuongeza uagizaji wa mafuta kupitia Bandari ya Dar esSalaam.

100. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2017/18 Serikali itaanzisha Mpango wa kuongeza upakuaji

Page 108: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

108

wa mafuta kwa kutumia Bandari ya Tanga yatakayokuwayanasambazwa Mikoa ya Kaskazini mwa nchi na piakuanzisha Mfumo huu kwa Bandari ya Mtwara kwakusambaza katika Mikoa ya Kusini mwa nchi na Nchi Jirani.Vilevile, kuanzisha uingizaji wa bidhaa za Liquified PetroleumGas (LPG) kwa kutumia Mfumo kama huu ili kuweza kupatafaida zinazopatikana kwa Mfumo wa uagizaji kwa pamoja.

101. Mheshimiwa Spika, uagizaji wa mafutakwa pamoja umeendana na uboreshaji wa viwango vyamafuta anayonunua mlaji wa mwisho katika kituo. Ili kudhibitiubora wa mafuta, Serikali ilifanya uamuzi wa kupunguzatofauti kati ya bei ya Mafuta ya Taa na bei ya mafuta yaPetroli na Dizeli. Kuimarisha udhibiti wa ubora wa mafuta,vinasaba vimekuwa vikitumika kubaini uchanganyaji wamafuta unaoathiri ubora. Hata hivyo, utaratibu wa matumiziya vinasaba umekuwa ukilalamikiwa na baadhi ya wadauhali iliyosukuma Wizara yetu kuangalia kwa makini mfumohuu mwaka wa fedha ujao.

Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG Project)

102. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2016/17 taarifa ya tathmini ya athari za mazingira na kijamiiimekamilika. Pamoja na taarifa hiyo, Mpango wa kuwapatiamaeneo mbadala Wananchi waishio katika eneolitakalojengwa Mitambo ya LNG la Likong’o Mkoani Lindi(Ressettlement Action Plan) umekamilika. Vilevile, kazi zakuingiza Michoro ya eneo la Mradi wa LNG kwenye Ramaniya Mipango Miji imekamilika. Aidha, utaratibu wa uvunajiGesi Asilia kutoka kina kirefu cha maji ya Bahari ya Hindi hadieneo la nchi kavu (Concept selection) kwa Kitalu Na.1 naKitalu Na.2 umekamilika na kwa Kitalu Na.4 unatarajiwakukamilika katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

103. Mheshimiwa Spika, Majadiliano ya kufikiaMakubaliano ya utekelezaji wa Mradi (Host GovernmentAgreement - HGA) kati ya Kikosi Kazi cha Wataalam waSerikali (Government Negotiation Team) na Kampuni zaUtafutaji Mafuta na Gesi Asilia (IOCs) yalianza rasmi Mwezi

Page 109: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

109

Septemba, 2016. Mradi huu utachukua muda wa takribaniMiaka nane (8) hadi kumi (10) kufikia uzalishaji na utagharimutakriban Dola za Marekani bilioni 30, sawa na takribanShilingi trilioni 69.33. Kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18Shilingi bilioni 13 zimetengwa kwa ajili ya malipo ya fidia,upatikanaji wa ardhi pamoja na shughuli nyingine za Mradihuu.

Miradi ya Usafirishaji wa Mafuta na Gesi Asilia

Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la AfrikaMashariki (EACOP) kutoka Kabaale (Uganda) hadi Bandariya Tanga (Tanzania)

104. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kushirikikwa karibu katika matayarisho ya ujenzi wa Bomba lakusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Kabaale (Uganda) hadiTanga (Tanzania), kilomita 1,445. Kazi zilizofanyika hadi MweziMachi, 2017 ni pamoja na: kusainiwa kwa Mkataba waMakubaliano ya Awali (MoU); kutolewa kwa Vivutio vyaKodi; kufanya tathmini ya njia ya Bomba (survey); tathmini yamahitaji ya njia ya Bomba (infrastructure requirements); naTathmini ya Athari ya Mazingira Kijamii (Environmental andSocial Impact Assesment) na kusainiwa kwa Inter-Governmental Agreement (IGA) tarehe 26 Mei, 2017.Gharama za Mradi huu ni Dola za Marekani bilioni 3.5 sawana takriban Shilingi trilioni 8.09. Wadau Wakuu katika Mradihuu ni Kampuni ya TOTAL (Ufaransa), CNOOC (China) naTULLOW (Uingereza) pamoja na Serikali za Tanzania naUganda.

105. Mheshimiwa Spika, kazi zitakazotekelezwa katikaMwaka wa Fedha wa 2017/18 ni pamoja na Mabunge yanchi husika (Tanzania na Uganda) kuridhia Mkataba huo;kuanza Mazungumzo ya Mkataba baina ya Serikali husikana Kampuni ya Bomba (Host Government Agreement -HGA); kuanza Mazungumzo ya Mkataba wa Wanahisa(Shareholders Agreement); kuanza Mazungumzo ya Mkatababaina ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na Kampuni ya Bomba;Mwekezaji kukamilisha usanifu wa Mradi (Front End

Page 110: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

110

Engineering Design - FEED), upimaji (survey) wa eneo lakujenga ghala katika Bandari ya Tanga; utafiti katika Mkuzawa Bomba na katika eneo la Bahari karibu na Bandari yaTanga (mateocean and geophysical technical studies).

Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Safi (WhitePetroleum Products) kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadiNdola (Zambia)

106. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ujenzi wa Bombala Kusafirisha Mafuta Safi (White Petroleum Products)kutoka Dar es Salaam (Tanzania) hadi Ndola (Zambia)unahusisha ujenzi wa Bomba lenye urefu wa takribankilomita 1,710 litakalojengwa sambamba na Bomba laTAZAMA linalosafirisha Mafuta Ghafi (Crude Oil) kutoka Dar esSalaam hadi Ndola. Bomba Jipya litakuwa na uwezo wakusafirisha tani milioni nne (4) za mafuta kwa Mwaka. Mradihuu pia utahusisha ujenzi wa Mabomba ya Matoleo yamafuta (take-off points) katika maeneo ya Morogoro, Iringa,Njombe, Mbeya na Songwe. Gharama za Mradi huuzinakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 1.5 sawa naShilingi trilioni 3.47.

107. Mheshimiwa Spika, Makubaliano ya kuanza ujenziwa Bomba la Kusafirisha Mafuta Safi yalitokana na ziara yaRais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu,aliyoifanya nchini Tanzania tarehe 29 Novemba, 2016 nakukutana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi huu nikuunda Kamati Ndogo (sub - committees) chini ya MakatibuWakuu wanaoshughulikia masuala ya Nishati zitakazojadilimasuala ya Sheria (Legal and Institutional framework), Fedha(Fiscal and Financing Options) na Utaalam (Technical Issues);kuandaa Andiko la Mradi (Project Concept Paper);kutengeneza Hadidu za Rejea (Terms of Reference) kwa ajiliya kufanya Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study) utakaooneshagharama za Mradi na namna bora ya kutekeleza Mradi.

Page 111: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

111

Kazi nyingine inayoendelea ni kupitia Mikataba iliyopo yaKisheria na ya Kifedha ya TAZAMA (TAZAMA Convention, 1968,Article of Association of TAZAMA).

108. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Bomba hiliutafanywa kwa ushirikiano wa nchi mbili za Tanzania naZambia na utaleta manufaa makubwa kwa nchi zote.Kwa upande wa Tanzania manufaa yatakayopatikana nipamoja na uhakika wa upatikanaji wa mafuta nchinihususan Mikoa ya Dodoma, Iringa, Katavi, Mbeya, Morogoro,Njombe, Ruvuma, Shinyanga, Singida, Songwe, Rukwa naTabora; ufanisi, usalama na bei nafuu katika kusafirishamafuta ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya maloriya mafuta ambayo yamekuwa yakiharibu miundombinu yabarabara. Utekelezaji wa Mradi huu unatarajiwa kuanzaMwaka 2018 na kukamilika Mwaka 2021.

Miradi ya Usambazaji Gesi Asilia Mikoa ya Dar es Salaam,Lindi, Mtwara na Pwani

109. Mheshimiwa Spika, Mwezi Desemba, 2016 Shirikala Maendeleo ya Petroli (TPDC) lilitangaza zabuni ya kumpataMshauri Mwelekezi ili kuhuisha taarifa ya Upembuzi Yakinifuna usanifu wa kina wa michoro ya Mradi wa KusambazaGesi Asilia Mkoani Dar es Salaam. Utaratibu wa kukamilishazoezi la kumpata Mshauri linatarajiwa kukamilika mwishonimwa Mwezi Juni, 2017. Taarifa ya Mshauri itakayopatikanaitatumika kushawishi Taasisi za Fedha zilizoonesha nia yakufadhili Mradi huu zikiwemo, Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB) na Benki ya Exim ya China. Katika Mwaka wa Fedha2017/18 Serikali imetenga Shilingi bilioni 1 kwa ajili ya uhuishajiwa taarifa ya Upembuzi Yakinifu. Aidha, kwa upande waMikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, Serikali kupitia TPDCimeendelea na juhudi za kutafuta fedha za Mikopo ya ribanafuu kwa ajili ya utekelezaji wa usambazaji Gesi Asilia kwaajili ya matumizi ya viwandani, majumbani na Taasisimbalimbali kwenye Mikoa hiyo.

Page 112: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

112

SEKTA NDOGO YA NISHATI JADIDIFU (i) Nishati ya Jua (SolarEnergy)

110. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka waFedha wa 2016/17, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsiilifanikisha kupatikana kwa MW 1 katika maeneo ambayoyako nje ya Gridi ya Taifa kwenye Kisiwa Cha Bwisya kilichopoZiwa Viktoria na maeneo mengine katika Wilaya za SimanjiroMkoani Manyara na Lumuli Mkoani Iringa. Aidha, kupitiaMfumo wa Usambazaji wa Umeme wa Jua Majumbani nakwenye Taasisi za Afya na Elimu (Solar Home Systems), kiasicha MW 2 kilipatikana katika maeneo mbalimbali nchini nakufanya upatikanaji wa umeme kwa kupitia Mfumo huukufikia takriban MW 9.

111. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Serikali itakamilisha uandaaji wa Ramani yamaeneo yenye fursa za uwekezaji wa uzalishaji wa umemewa Jua ikijumuisha uainishaji wa miundombinu husika kwalengo la kuvutia uwekezaji katika Sekta Ndogo hii. Aidha,Serikali kupitia TANESCO itaanza kufanya Upembuzi Yakinifukatika Maeneo ya Kishapu na Visiwa vya Mafia kwa ajili yauzalishaji umeme wa Jua kwa kati ya MW 50 hadi 300.

Serikali pia kwa kushirikiana na Sekta Binafsiitahakikisha kuwa Visiwa zaidi vya Ziwa Victoria vikiwemovya Bukerebe, Bulubi, Bushengele, Bwiro, Izinga, Kamasi, KweruKuu, Kweru Mto, Sizu na Zeru vinapatiwa umeme kupitia GridiNdogo za Umeme wa Jua. Aidha, Serikali itaendelea kuwekamazingira wezeshi kwa Wasambazaji wa vifaa na Mifumoya Umeme Jua ili maeneo mengine yaliyo pembezoni yapateumeme kwa njia hii.

(ii) Nishati ya Upepo (Wind Energy)

112. Mheshimiwa Spika, uwekezaji katika Nishati yaUpepo kwa kiasi kikubwa unaathiriwa na upatikanaji waardhi. Katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17, Serikali kwakushirikana na Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe naHalmashauri ya Mji wa Makambako ilifanya utatuzi wa

Page 113: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

113

mgogoro wa ardhi kati ya Mwekezaji (Kampuni ya Sino-Tan)na Halmashauri husika. Kazi inayoendelea ni kupitia upyatathmini ya fidia kwa wananchi watakaopisha utekelezajiwa Mradi.

Aidha, Kampuni ya Windlab ya Afrika Kusini ilianzautafiti wa takwimu za Upepo ili kuwekeza katika eneo laMakambako. Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18 Serikaliitafanya tathmini ya kina na ufuatiliaji wa Miradi ya Umemewa Upepo na kuwabaini Waendelezaji wanaohodhimaeneo kwa muda mrefu bila kuyaendeleza ili maeneohayo yaweze kushindanishwa na kupewa Waendelezajiwenye uwezo wa kuyaendeleza. Kiasi cha Shilingi bilioni 1.3ambazo ni fedha za Nje kimetengwa kwa ajili ya uendelezajiwa Miradi ya Nishati ya Jua na Upepo.

(iii) Miradi ya Tungamotaka (Bio- Energies)

113. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2016/17 uzalishaji wa umeme kwa kutumiaTungamotaka (Biomass) zitokanazo na mabaki ya miwakatika Viwanda vya Sukari, mazao ya misitu na mkongeumefikia MW 38 ambapo MW 10.5 zimeunganishwa kwenyeGridi ya Taifa na MW 27.5 zinatumika kwa ajili ya shughuli zaViwanda husika. Viwanda hivyo ni Tanganyika PlantingCompany (TPC) cha Mkoani Kilimanjaro MW 10; KilomberoSugar Company Limited cha Mkoani Morogoro MW 9; MtibwaSugar cha Mkoani Morogoro MW 5; Kagera Sugar cha MkoaniKagera MW 5; Tanzania Wattle Company (TANWAT) chaMkoani Iringa MW 2.5; Ngombeni Biomass Project cha MafiaMW 1 na Mkonge Energy cha Mkoani Tanga MW 1. KatikaMwaka wa Fedha wa 2017/18 Wizara itaendelea nauhamasishaji wa Sekta Binafsi ili kuongeza uzalishaji waumeme utokanao na Tungamotaka. Hatua hii itaongezamchango wa Tungamotaka katika upatikanaji wa umemenchini kwa takriban MW 2 ambazo zitaongezwa kwenye Gridiya Taifa na kiasi kingine zaidi kutumika kwa ajili ya Viwandahusika.

Page 114: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

114

(iv) Miradi ya Jotoardhi (Geothermal)

114. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Kampuni yaUendelezaji wa Jotoardhi (Tanzania GeothermalDevelopment Company Limited - TGDC), ambayo ni KampuniTanzu ya TANESCO, imekamilisha utafiti wa kina (detail surfacestudy) wa uendelezaji Nishati ya Jotordhi katika maeneo yaZiwa Ngozi (Mbeya) mnamo Mwezi Septemba, 2016, chini yaufadhili wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP)na Shirika la Maendeleo la Iceland (ICEIDA). Aidha, utafitiumeweza kuainisha sehemu tatu (3) za kuchoronga Visimavya Majaribio (Slim Wells) katika eneo la Ziwa Ngozi ilikutathmini kiasi cha hifadhi ya rasilimali ya Jotoardhi na uwezowake wa kuzalisha umeme. Vilevile, Serikali kupitia MshauriMwelekezi ambaye ni Electro- consult ya nchini Italia chiniya ufadhili wa Serikali ya Iceland kupitia Shirika laMaendeleo la Iceland (ICEIDA) yupo katika hatua za mwishoza kukamilisha utafiti wa kina (detail surface studies) katikamaeneo ya Mbaka-Kiejo, Mkoani Mbeya na Luhoi MkoaniPwani.

115. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18, Serikali kupitia TGDC imejipanga kutekeleza Mradiwa uchorongaji Visima Vitatu (3) vya utafiti katika eneo laZiwa Ngozi. Gharama za Mradi ni Dola za Marekanimilioni 12 sawa na Shilingi bilioni 27.73. Mradi huuutafadhiliwa na Serikali kwa kushirikana na Mfuko waUendelezaji Jotoardhi (Geothermal Risk Mitigation Facility -GRMF) ulio chini ya Kamisheni ya Afrika (AUC). Serikaliitagharamia kiasi cha Dola za Marekani milioni 8.78 sawana Shilingi bilioni 20.29 na kiasi kilichobakia cha Dola zaMarekani milioni 3.33 sawa na Shilingi bilioni 7.70 kitatolewana GRMF kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

116. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18, Serikali kupitia TGDC inategemea kufanyautafiti wa kina (detail surface study) katika eneo la Kisaki,Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na GRMF. Gharama zaMradi huu ni kiasi cha Dola za Marekani milioni 1.32 sawa naShilingi bilioni 3.05. Serikali itachangia kiasi cha Dola za

Page 115: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

115

Marekani 165,210 sawa na Shilingi milioni 381.80 na GRMFitachangia kiasi cha Dola za Marekani milioni 1.16 sawa naShilingi bilioni 2.68.

117. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TGDCinaendelea kutathmini uendelezaji wa rasilimali ya Jotoardhikwa ajili ya matumizi ya moja kwa moja (direct heat uses).Matumizi hayo ni pamoja na kutengeneza mabwawa yakuogelea ya maji moto pamoja na uboreshaji wa sehemuhizo za asili ambazo huvutia utalii. Matumizi mengine nipamoja na uzalishaji wa mazao ya kilimo cha maua namboga mboga, ukaushaji wa nafaka, ufugaji wa samaki nashughuli za viwandani (industrial processes). Miongoni mwasehemu ambazo zinaweza kuendelezwa kwa matumizi hayoni Ibadakuli iliyoko Mkoani Shinyanga na Songwe katikaMkoa wa Songwe.

118. Mheshimiwa Spika, ili kuwa na uendelezajiendelevu wa Nishati ya Jotoardhi nchini, Serikali inaendeleana uandaaji wa Mpango Mkakati wa Uendelezaji waJotoardhi na Sheria ya kuendeleza Jotoardhi nchini. Mpangowa kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kazi hii utakamilikaMwezi Agosti, 2017. Utekelezaji wa kazi hizi unafadhiliwa naClimate Investment Funds (CIF) kupitia Mpango wa ScalingUp Renewable Energy Programme(SREP) kupitia Benki yaMaendeleo ya Afrika (AfDB) kwa gharama ya Dola zaMarekani 450,000, sawa na takriban Shilingi milioni 1.04.

(v) Umeme wa Maporomoko Madogo ya Maji (Mini-Hydro)

119. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendeleakuhamasisha uendelezaji wa Miradi ya MaporomokoMadogo ya Maji ili kuhakikisha inatoa mchango katikakuwafikishia umeme Wananchi na hasa wa vijijini. KatikaMwaka wa Fedha wa 2016/17 kiasi cha MW 36.99 kutokaMaporomoko Madogo ya Maji kilizalishwa ambapo MW 6.11zimeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na kiasi cha MW 30.88kinatumika katika Gridi Ndogo Ndogo na Taasisi. Baadhi yamaeneo hayo yenye Maporomoko Madogo ya Maji ni Andoya

Page 116: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

116

(Mbinga), Darakuta (Manyara), Ikondo (Njombe), Kiliflower(Arusha), Mwenga (Mufindi), Tulila (Songea) na Yovi (Kilosa).

120. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2017/18 Serikali itaendelea kuhamasisha uendelezaji waMiradi ya Maporomoko Madogo ya Maji ili kuhakikisha inatoamchango wa upatikanaji wa umeme wa bei nafuu nchini.

(vi) Usambazaji Umeme kwa Mfumo wa Gridi Ndogo (Mini-Grids)

121. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2016/17 Serikali ilifanya ukaguzi na uhakiki wa Mifumoya Gridi Ndogo ili kubaini changamoto zinazowakabiliWaendelezaji. Katika kutatua changamoto hizo, Serikaliiliandaa Viwango na Kanuni za usimamizi wa Gridi Ndogozinazotoa Mwongozo wa uendeshaji wake hususan paleeneo husika linapofikiwa na Gridi ya Taifa. Katika Mwakawa Fedha wa 2017/18 Serikali itaendelea kuweka mazingirabora ya uendelezaji wa Gridi Ndogo za Umeme ili kuwezeshaWananchi kupata umeme hasa maeneo ya Visiwa na yaleyaliyo pembezoni. Aidha, kupitia REA III, Mradi huuumetengewa Shilingi bilioni 50 ambazo ni fedha za Njekutoka Serikali za Uingereza na Sweden ambapo Jumla yaMW 26.9 zinatarajiwa kuzalishwa.

(vii) Uendelezaji wa Matumizi ya Bayogesi (Biogas)

122. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2016/17, Serikali kwa kushirikiana na Kituo cha Usambazajina Uendelezaji wa Teknolojia ya Kilimo Vijijini (Center forAgricultural Mechanization and Rural Technology - CAMARTEC) imewezesha ujenzi wa Mitambo 1,980 na kufanya Jumlaya idadi ya Mitambo iliyojengwa kufikia 15,980 tanguProgramu ianze Mwaka 2009. Wananchi 95,880 katika Mikoayote ya Tanzania Bara walinufaika na programu hii kwakuweza kumiliki Mitambo na kutumia Bayogesi kwa ajili yakupikia na kuwasha taa. Aidha, Makampuni Binafsi yaujenzi wa Mitambo ya Bayogesi yapatayo 100 yalianzishwana kutoa ajira kwa Watanzania takriban 1,000. Ili kuongeza

Page 117: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

117

msukumo wa ujenzi wa Mitambo mingi ya Bayogesi nchini,Mwaka 2016 Serikali kupitia Mfuko wa Nishati Vijijini ilianzakutoa ruzuku kwa ajili ya ujenzi wa Mitambo 10,000 nchini.Gharama ya Utekelezaji wa Progamu nzima hadi kufikiaMwaka 2019 ni Dola za Marekani milioni 10.7 sawa natakriban Shilingi bilioni 24.73. Katika Mwaka wa Fedha wa2017/18 Jumla ya Shilingi bilioni 1.5 zimetengwa kwa ajili yakutekeleza Mradi huu.

123. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Serikali itaendelea kutoa ruzuku kupitia Mfukowa Nishati Vijijini ili kuhamasisha Kampuni za uzalishajimkonge, korosho pamoja na Halmashauri za Miji kutumiateknolojia ya Bayogesi katika uzalishaji wa umeme kwa lengola kuongeza thamani ya mazao na utunzaji wa mazingirakwa kutumia Mabaki ya Mazao na Taka za Mijini. KupitiaMpango huu, REA imetenga Jumla ya Shilingi bilioni 50 kwaajili ya kutekeleza Miradi mbalimbali ya Nishati Jadidifuikiwemo teknolojia ya Bayogesi.

(viii) Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Upatikanaji wa NishatiEndelevu kwa Wote (Sustainable Energy for All initiative -SE4ALL)

124. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni moja ya nchizinazotekeleza Mpango wa Umoja wa Mataifa wa NishatiEndelevu unaojulikana kama Sustainable Energy for All(SE4ALL). Mpango huu una lengo la kuwapatia nishati borawatu wote Duniani ifikapo Mwaka 2030. Katika Mwaka waFedha wa 2016/17 Wizara ilikamilisha maandalizi ya “ActionAgenda” na “Investment Prospectus” ambazo ni Miongozomuhimu katika utekelezaji wa malengo ya SE4All. Aidha,Serikali kupitia ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)ilianza maandalizi ya kuandaa utaratibu wa utekelezaji wamiongozo hii. Vilevile, kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleola Umoja wa Mataifa (UNDP), Wizara ilikamilisha maandaliziya Programu ya Miaka Mitano (5) ambayo itasaidia kuanzakwa utekelelezaji wa Mpango wa SE4ALL.

Page 118: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

118

125. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua mchangowa Tanzania katika jitihada zake za utekelezaji wa SE4ALL,Mwaka wa Fedha wa 2016/17 Umoja wa Mataifa uliichaguaTanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa SE4ALL kwa nchiza Afrika zinazoendelea uliofanyika tarehe 5 hadi 6 Desemba,2016. Mkutano huo uliandaliwa kwa ushirikiano na Ofisi yaUmoja wa Mataifa (UN) inayoshughulikia nchi zinazoendelea(Office of the High Representative for LCDS) pamoja na Shirikala Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

126. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Serikali kwa kushirikiana na UNDP, AfDB na Wadauwengine wakiwemo Umoja wa Ulaya na Benki ya Duniaitaendelea na utekelezaji wa SE4ALL ikiwa ni pamoja nauhamasishaji wa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezajiwa Miradi iliyobainishwa katika Mpango wa Uwekezaji waSE4ALL (Investment Prospectus) na uratibu wa shughuli zaProgramu hii.

(ix) Mpango wa Matumizi Bora ya Nishati (Energy Efficiency)

127. Mheshimiwa Spika, Matumizi Bora ya Nishati(Energy Efficiency) ni suala linalotakiwa kupewa kipaumbeleili kupunguza upotevu wa nishati kuanzia uzalishaji, usafirishaji,usambazaji hadi mtumiaji wa mwisho. Kutokana na juhudimbalimbali zilizofanywa na Serikali pamoja na TANESCOzikiwemo za kukarabati na kuwekeza katika njia za usafirishajina usambazaji wa umeme, upotevu wa umeme umepunguakutoka asimilia 21 ya Mwaka wa Fedha wa 2015/16 hadiasilimia 17 kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17. Kwa Mwakawa Fedha wa 2017/18 Serikali itaendelea na uwekezaji wakuboresha njia za usafirishaji na usambazaji umeme ilikuhakikisha kwamba upotevu wa umeme unashuka hadikufikia asilimia 16.

128. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Watumiajiwa mwisho (demand side), katika Mwaka wa Fedha wa2016/17 Serikali kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU)imeandaa Mpango Mkakati wa Matumizi Bora ya Nishatiulioweka mipango na Miradi mbalimbali ya kuzuia upotevu

Page 119: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

119

wa nishati katika nyumba za makazi, majengo ya biashara,viwanda na Taasisi. Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18Serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemoUmoja wa Ulaya (EU), Sida, NORAD na GIZ itaendeleakutekeleza Mradi huu.

129. Mheshimiwa Spika, Gharama za Nishati hususanumeme zinachukua sehemu kubwa ya gharama za uzalishajikatika viwanda. Ili kuongeza ushindani wa viwanda vyetuni muhimu kupunguza gharama za uendeshaji kwakudhibiti upotevu wa nishati na matumizi yasiyo ya lazima.Katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17 Serikali kwa kushirikianana Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) imeandaaMpango Kazi wa Matumizi Bora ya Nishati kwa WatumiajiWakubwa (Energy Efficiency Action Plan for DesignatedConsumers) na itatekeleza Mpango huo kwa kushirikianana GIZ katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18. Mradi huuunakadiriwa kugharimu kiasi cha Euro milioni 10 sawa naShilingi bilioni 21.3 na utatekelezwa katika kipindi chaMwaka wa Fedha wa 2017/18 hadi 2020/21.

SEKTA YA MADINI

Utafutaji na Ugunduzi Nchini wa Gesi ya Helium

130. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendeleakuchukua hatua na kuweka mipango mbalimbali yakuendeleza utafutaji na ugunduzi wa Gesi ya Helium ambayoni adimu Duniani. Katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17,Kampuni ya Helium One Limited imeendelea kufanya utafitiwa Gesi hiyo kupitia Kampuni zake Tanzu za Gogota (TZ)Limited, Njozi (TZ) Limited na Stahamili (TZ) Limited zenyeleseni za utafutaji katika maeneo mbalimbali ya Mikoa yaRukwa na Manyara (Ziwa Eyasi na Balangida). Katikakutekeleza kazi hizo, Kampuni hiyo ilitoa Kandarasi kwa VyuoVikuu vya Oxford na Durham vya nchini Uingereza kufanyautafiti katika leseni zake zil izopo Ziwa Rukwa. Utafitiuliofanywa na Vyuo hivyo umewezesha kugundulika kwaHelium ya wingi wa takriban Futi za Ujazo bilioni 54 kutokanana sampuli za mavujia (gas seeps) zilizochukuliwa na

Page 120: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

120

kufanyiwa uchunguzi katika maeneo matano (5) yaliyopoeneo la Ziwa Rukwa. Kiasi hicho kinakadiriwa kuwa kikubwazaidi ya mara sita (6) ya mahitaji ya Dunia kwa sasa.

131. Mheshimiwa Spika, Kazi ya uchorongaji waVisima vya Utafiti katika maeneo hayo zinatarajiwa kuanzaMwaka 2018. Kazi hiyo itawezesha kuhakiki kiasi halisi chaGesi ya Helium kilichopo katika maeneo ilipogunduliwa.Aidha, uchimbaji wa Gesi ya Helium utaanza mara baadaya kukamilika kwa kazi ya utafiti wa kina, Upembuzi Yakinifuna Tathmini ya Athari za Mazingira na pia leseni yauchimbaji wa Gesi hiyo kutolewa. Kwa sasa shughuli zakukusanya taarifa zaidi za kijiolojia, kijiofizikia, na 2D Seismicsurvey zinaendelea ili zitumike kwa ajili ya uchorongaji waVisima vya Utafiti (Exploration wells). Gesi ya Helium, pamojana matumizi mengine hutumika kupooza mashine za MRIScanners na vinu vya nuclear na pia hutumika katika floatingballoons.Serikali imeunda Kikosi Kazi chake ambachokitafanya kazi na Wataalam Wazoefu kutoka nchi zenyeuzoefu mkubwa wa Gesi ya Helium.

Ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na Shughuli za UchimbajiMadini Nchini

132. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara ilikusanyaMrabaha wa Jumla ya Dola za Marekani milioni 56.77sawa na takriban Shilingi bilioni 131.20 kutoka kwenyeMigodi Mikubwa ya Bulyanhulu,Buzwagi, Geita,NewLuika,North Mara, STAMIGOLD, TanzaniteOne, Mwadui, Ngaka naDangote. Pia, kiasi cha Mrabaha wa Shilingi bilioni 4.23kilikusanywa kutokana na mauzo ya dhahabu iliyozalishwakwa kuchenjua marudio kwa teknolojia ya “vat leaching”.Aidha, Mrabaha wa Shilingi bilioni 4.45 ulikusanywa kutokanana uzalishaji wa madini ya ujenzi na viwandani kutoka kwaWachimbaji Wadogo. Makusanyo hayo yametokana na kaziya ukaguzi na uhakiki wa madini yaliyozalishwa katika Migodihiyo inayofanyika kwa ushirikiano baina ya Ofisi za Madini zaKanda na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA).

Page 121: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

121

Vilevile, Wizara imekusanya kiasi cha Shilingi milioni14.52 kutokana na ada za Leseni na Vibali mbalimbali.

133. Mheshimiwa Spika, vilevile katika kipindi chakuanzia Mwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara ilikusanyaMrabaha wa Dola za Marekani milioni 2.40 sawa na Shilingibilioni 5.55 kutokana na mauzo ya Almasi na Dola zaMarekani 906,347 sawa na Shilingi bilioni 2.09 kutokana namauzo ya vito ghafi na vilivyokatwa mathalan Tanzanite,Garnet, Moonstones, Ruby, Spinel, Tourmaline, Garnet,Sapphire, Amethyst, Tsavorite na Zircon. Malipo hayayalitokana na kazi ya uthamini iliyofanywa na TanzaniaDiamond Sorting Unit- TANSORT.

134. Mheshimiwa Spika, pamoja kupungua kwashughuli za uwekezaji katika Sekta ya Madini katika miakahivi karibuni kulikotokana na kushuka kwa bei ya madinikatika soko la dunia, mchango wa Sekta ya Madini katikaPato la Taifa umeongezeka kufikia Asilimia 4 Mwaka 2015kutoka Asilimia 3.7 Mwaka 2014/15.

135. Mheshimiwa Spika, aidha, Ajira za moja kwamoja (direct employment) kwa Watanzania kwenye migodimikubwa nchini imepungua kutoka 7,335 Mwaka 2015 nakufikia 6,207 mwaka 2016 ikiwa ni punguzo la Asilimia 15.Punguzo hilo l imesababishwa na migodi kupunguzawafanyakazi hususan wa ajira za muda na mikatabakutokana na kushuka kwa bei ya dhahabu. Aidha, idadi yawataalam toka nje ya nchi (expatriates) imepungua kutoka333 mwaka 2015 na kuwa 294 mwaka 2016 ikiwa ni punguzola Asilimia 12.

136. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho hicho,Wizara kupitia TMAA ilifanya ukaguzi wa hesabu za Fedhaza Migodi Mikubwa na ya kati kwa kushirikiana na Mamlakaya Mapato Tanzania (TRA) na kuiwezesha Serikali kukusanyaKodi ya Mapato (Corporate Tax) ya Jumla ya Shilingi bilioni79.26 kutoka kwa Kampuni za uchimbaji mkubwa wadhahabu nchini. Kati ya malipo hayo, Shilingi bilioni 45.76zimelipwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited na

Page 122: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

122

Shilingi bilioni 33.50 zimelipwa na Kampuni ya North MaraGold Mine Limited. Kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18, Wizarakupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) itaendeleakufanya ukaguzi ili kuhakikisha malipo stahiki, hususan Kodiya Mapato (Corporate Income Tax) yanalipwa Serikalini.

137. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Serikali inalenga kukusanya Jumla ya Shilingibilioni 194.4 katika Sekta ya Madini ikilinganishwa na Shilingibilioni 215.96 zilizokadiriwa kukusanywa kwa Mwaka waFedha wa 2016/17. Kiasi hicho ni sawa na upungufu waasilimia 9.98. Upungufu huo unatokana na kushuka kwa beiya Dhahabu kwenye Soko la Dunia na kupungua kwashughuli za utafutaji wa Madini nchini. Wizara itaendeleakuimarisha ukaguzi na usimamizi wa shughuli za madini ikiwani pamoja na kuweka mkazo katika ukusanyaji wa ada naMrabaha kutoka kwa Wachimbaji wa aina (kada) zote naWafanyabiashara wa madini nchini ili kufikia lengo laukusanyaji maduhuli kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18.

Ushuru wa Huduma (Service Levy)

138. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi 2017, Kampuni za uchimbajimkubwa wa madini zimeendelea kulipa Ushuru wa Huduma(Service Levy) kwa Halmashauri mbalimbali ambapo Jumlaya Shilingi bilioni 11.27 zimelipwa. Kati ya Fedha hizo, Mgodiwa Geita umelipa kiasi cha Shilingi bilioni 3.92 kwaHalmashauri ya Mji wa Geita; Mgodi wa Bulyanhulu Shilingimilioni 760.57 kwa Halmashauriya WilayayaMsalala na Shilingimilioni 374.61 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale;Mgodi wa North Mara Shilingi bilioni 3.10 kwa Halmashauriya Wilaya ya Tarime; Mgodi wa Buzwagi Shilingi bilioni 1.48kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama; Mgodi wa New LuikaShilingi milioni 697.77 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya;na Mgodi wa STAMIGOLD Shilingi milioni 167 kwa Halmashauriya Wilaya ya Biharamulo. Mgodi wa TanzaniteOne umelipaShilingi milioni 66 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro;na Mgodi wa Wiliamson Shilingi milioni 516.87 kwaHalmashauri ya Wilaya ya Mwadui. Aidha, Kampuni ya

Page 123: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

123

Dangote Tanzania Limited imelipa Shilingi milioni 187.92 kwaHalmashauri ya Wilaya ya Mtwara. Katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18, Wizara itaendelea kuzipatia Halmashauri husikatakwimu sahihi za mauzo ya madini ili kuwezesha ukusanyajiwa ushuru wa HudumakutokakwaKampuni zinazoendeshauchimbaji ndani ya Halmashauri zao.

Uzalishaji na Mauzo ya Madini Nje ya Nchi

139. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017Jumla ya wakiamilioni1.05zaDhahabu, wakia 414,128 za Fedha na ratilimilioni 10.4 za Shaba zilizalishwa na kusafirishwa nje ya nchikutoka Migodi Mikubwa ya STAMIGOLD, Bulyanhulu, Buzwagi,Geita, New Luika na North Mara. Thamani ya Madiniyaliyosafirishwa kwa kila Mgodi ni kama ifuatavyo: Mgodiwa STAMIGOLD Dola za Marekani milioni 15.09, Mgodi waBulyanhulu Dola za Marekani milioni 245.60, Mgodi waBuzwagi Dola za Marekani milioni 174.35, Mgodi wa GeitaDola za Marekani milioni 465.76, Mgodi wa New Luika Dolaza Marekani milioni 76.15 na Mgodi wa North Mara Dola zaMarekani milioni 381.02 ambapo Jumla ya thamani ya madinihayo ni Dola za Marekani bilioni 1.36 sawa na Shilingi trilioni3.14.

140. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Jumlaya karati 163,748 za Almasi na kilogram 2,872.79 za Tanzanite(Grade A – I) zil izalishwa na Migodi ya Mwadui naTanzaniteOne, sawia. Katika Mwaka wa Fedha wa 2017/18,Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa shughuli zauzalishaji na biashara ya madini na kuwavutia WawekezajiWapya hususan kwenye madini ya graphite (kinywe), lithiumna madini mengine yanayohitajika kwenye teknolojia yakisasa (Rare Earth Elements- REE) ili kuongeza mchango waSekta ya Madini katika maendeleo makubwa ya uchumi waTaifa letu.

141. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambuaumuhimu wa wawekezaji wakubwa wa nje na wa ndanikatika uwekezaji kwenye Sekta ya Madini. Kwa Mwaka wa

Page 124: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

124

Fedha 2017/18, Serikali inadhamiria kwa kushirikiana nawadau kupitia Sera, Sheria na mikataba ya uendelezajiwa sekta hii ili kuhakikisha uwekezaji katika sekta unaendeleana kushimiri.

Kuendeleza Shughuli za Uchimbaji Mdogo wa Madini

142. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea najitihada za kuendeleza uchimbaji mdogo wa madini nchini.Jitihada hizo ni pamoja na kutenga maeneo zaidi kwa ajiliya Wachimbaji Wadogo, kutenga Fedha zaidi za ruzuku nakuimarisha Shughuli za Ugani.

143. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara imetenga maeneo11 kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo wa madini yaliyopoMsasa na Matabe Mkoani Geita, Biharamulo na KyerwaMkoani Kagera, Itigi Mkoani Singida, D-Reef, Ibindi naKapanda Mkoani Katavi, Ngapa Mkoani Ruvuma, NzegaMkoani Tabora na Kitowelo Mkoani Lindi. Maeneo hayo yanaukubwa wa takriban Hekta 38,951.7. Aidha, Wizara kupitiaShirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Wakala wa JiolojiaTanzania (GST) inaendelea kufanya tathmini ya kina katikamaeneo hayo ili kubaini uwepo wa mashapo ya madini zaidikwa lengo la kuongeza tija kwa Wachimbaji Wadogo.

144. Mheshimiwa Spika, katika kuwawezeshaWachimbaji Wadogo wa madini kupata vifaa, Serikaliilitenga kiasi cha Shilingi bilioni 7.48 kwa ajili ya kutoaRuzuku Awamu ya III kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevuwa Rasilimali za Madini (Sustainable Management of MineralResources Project – SMMRP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.Maombi ya Ruzuku Awamu ya III yaliyowasil ishwayamefanyiwa uchambuzi wa kina na taratibu kwa ajili yakutolewa ruzuku hiyo zinakamilishwa. Hata hivyo, utoaji waRuzuku hiyo umechelewa kutokana na baadhi ya Wanufaikawa Ruzuku Awamu ya II kutumia fedha hizo kinyume naMakubaliano ya Mikataba baina yao na Serikali.

Page 125: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

125

145. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana natatizo hilo, Wizara imewaandikia barua Wanufaika wa Ruzukukwa kuwajulisha mapungufu ya utumiaji wa Ruzuku hiyo iliwafanye marekebisho na kwa wale watakaoshindwawarudishe fedha. Utoaji wa Ruzuku Awamu ya III utaendeleabaada ya kujiridhisha na utekelezaji wa zoezi hili.

146. Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa Wanufaikawote wa Ruzuku kuhakikisha kuwa wanatumia fedha hizokuendeleza Miradi ya uchimbaji na uchenjuaji madini kwamujibu wa Mikataba yao. Wale wote watakaothibitikakutumia Fedha za Ruzuku vibaya hatua za kisheriazitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

147. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mradi waUsimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP) wa Benkiya Dunia Awamu ya II inaendelea na hatua za uanzishwajiwa Vituo vya Mfano saba (7) vya kuchenjulia madini katikamaeneo ya Buhemba – Mara, D-Reef na Kapanda – Mpanda,Itumbi – Chunya, Katente - Geita, Kyerwa - Kagera na MaweniMkoani Tanga. Uanzishwaji wa Vituo hivi utagharimu Jumlaya Dola za Marekani milioni 8.4 sawa na Shilingi bilioni 19.41.Vituo hivyo vitatumiwa na Wachimbaji Wadogo kuchenjuamadini na kujifunza namna bora na endelevu ya kuendeshaMigodi yao kitaalam na kwa tija zaidi. Kazi iliyofanyika hadisasa ni utafiti wa kina ambapo uchorongaji wa miambaumefanyika katika maeneo hayo ili kubaini uwepo wamashapo ya kutosha ya madini husika. Kituo cha saba (7)kitakuwa eneo la Masakasa/Mkwenyule-Wilayani Kilwaambacho ni Kituo cha uongezaji thamani madini ya chumvi.Tayari eneo la Kituo hiki limekaguliwa na linafaa kwamatumizi yaliyokusudiwa.

148. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara imetoa mafunzokwa Wachimbaji Wadogo 6,000 katika Kanda ya Kati,Kanda ya Kati Magharibi, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Kusini,Kanda ya Kusini Magharibi, Kanda ya Mashariki, Kanda yaZiwa Nyasa, Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi na Kanda yaZiwa Viktoria Mashariki. Mafunzo hayo yalihusu masuala ya

Page 126: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

126

uchimbaji madini, uchenjuaji, afya na usalama Migodini,ujasiriamali na utunzaji wa mazingira na yalitekelezwa naMaafisa Madini wa Kanda na Mikoa. Zoezi hilo lilifanyika ikiwani sehemu ya kazi za kawaida za kupitia Bajeti za Ofisi zaKanda za Matumizi ya Kawaida.

149. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2017/18 Wizara itaendelea kutoa Huduma za Ugani kwaWachimbaji Wadogo nchini. Aidha, kwa kupitia STAMICO naGST, Wizara imepanga kutoa mafunzo ya nadharia navitendo kwa Wachimbaji Wadogo 4,000 katika Kanda zaKusini, Ziwa Nyasa, Kati na Kusini Magharibi. Pia, Wizaraitaendelea kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Mfano nakuendelea kufanya utafiti wa kina kwenye maeneoyaliyotengwa kwa ajili ya Wachimbaji Wadogo. Shughuli hizozimetengewa Jumla ya Dola za Marekani milioni 5.6 sawana takriban Shilingi bilioni 12.94 na zitagharamiwa na Mradiwa SMMRP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia

Uboreshaji wa Utoaji na Usimamizi wa Leseni za Madini

150. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendeleakuboresha huduma za utoaji na usimamizi wa Leseni zamadini kwa kuwezesha malipo ya ada za Leseni za madinikufanyika kwa njia ya Mtandao (online payments). Katikakipindi cha kuanzia Mwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017, Jumlaya maombi ya Leseni 8,942 ya utafutaji na uchimbaji wamadini yalipokelewa na Wizara kwa njia ya Mtandao (OnlineMining Cadastre Transactional Portal). Kati ya hayo, maombi585 ni ya utafutaji mkubwa, maombi 17 ni ya uchimbaji wakati na maombi 8,340 ni ya uchimbaji mdogo. Baada yauchambuzi wa maombi hayo, Jumla ya Leseni 3,467zilitolewa. Kati ya hizo, Leseni 296 ni za utafutaji mkubwa,10 za uchimbaji wa kati na 3,161 za uchimbaji mdogo. Wizaraitaendelea kusimamia kwa karibu utoaji wa Leseni ili kukuzamchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa.

151. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa Lesenizinazotolewa zinafanyiwa kazi, Wizara iliendelea kufuatiliaWamiliki wa Leseni na waliobainika kutotekeleza masharti

Page 127: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

127

husika ya Leseni hizo walifutiwa Leseni zao. Katika kutekelezaazma hiyo, Jumla ya Leseni 2,153 zilifutwa, kati ya hizo, Leseni72 zilikuwa ni za utafutaji madini na 2,081 ni za uchimbajimdogo wa madini. Aidha, hati za makosa (default notices)243 zilitolewa kwa Wamiliki wa Leseni za utafutaji madini, 13kwa Wamiliki wa Leseni za uchimbaji wa kati na 2,186 kwaWamiliki wa Leseni za uchimbaji mdogo. Naendelea kutoawito kwa Wadau wa Sekta ya Madini kujisajili kwa njia yaMtandao ili kurahisisha huduma za utoaji Leseni na kuongezauwazi hivyo kupunguza malalamiko ya kuwepo kwaupendeleo katika utoaji wa Leseni za madini.

152. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa2017/18, Wizara itaendelea kuboresha Mfumo wa utoaji waLeseni na kutoa mafunzo kwa Watendaji; kuhamasishaWadau wa madini ambao hawajasajiliwa ili wawezekutumia Mfumo huu; kufanya ukaguzi wa Leseni; na kufutaLeseni ambazo hazifanyiwi kazi.

Kuimarisha Usimamizi wa Migodi Nchini

153. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Jumla ya Migodi 1,115ilikaguliwa ili kuhakikisha kuwa Kanuni za Usalama, Afyana Utunzaji wa Mazingira Migodini zinazingatiwa. Kati yaMigodi hiyo, Migodi Mikubwa minne (4), Migodi ya Kati 52 naMigodi Midogo 1,059 ilikaguliwa. Ukaguzi huo umesaidiakuimarisha hali ya Afya, Usalama na Utunzaji wa Mazingirakwa Wachimbaji wa Migodi husika.

154. Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi za Wizarakatika ukaguzi wa Migodi, ajali zinaendelea kutokea hususan,kwenye Migodi ya Wachimbaji Wadogo kutokana nakutofuata Sheria na Kanuni za uchimbaji madini. Maeneoambako ajali zimetokea kwa wingi ni maeneo yenyemifumuko ya madini (mineral rush areas) ambayoyanavamiwa na kuchimbwa bila leseni hususan kwenyemaeneo ya hifadhi za misitu ambako Wizara ya Nishati naMadini haina uwezo wa kutoa leseni bila ridhaa ya Mamlakahusika. Katika kipindi cha Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Jumla

Page 128: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

128

ya ajali 17 zilitokea katika Migodi hiyo na kusababisha vifovya Wachimbaji 30. Aidha, katika ajali hizo, Serikali kwakushirikiana na Wadau wa Sekta ya Madini walifanikiwakuokoa Wachimbaji 42 wakiwa hai. Wizara inatoa shukraniza dhati kwa Viongozi wa Serikali, Kampuni za Madini,Taasisi mbalimbali, Wachimbaji Wadogo na Wadau wotewalioshiriki kwa namna moja ama nyingine kuokoa maishaya wahanga wa ajali Migodini.

155. Mheshimiwa Spika, kutokana na kuongezekakwa ajali katika Migodi ya Wachimbaji Wadogo, Wizarakatika Mwaka wa Fedha wa 2017/18 itaimarisha ukaguzi waMigodi hiyo nchi nzima na kuwa na taarifa za kila Mwezi zaMigodi yote inayofanya kazi. Migodi yote ambayo itabainikakutokidhi vigezo vya kiusalama kwa mujibu ya Kanuni zaAfya na Usalama Migodini za Mwaka 2010 itafungwamara moja hadi marekebisho stahiki ya kiusalamayatakapofanyika na kuridhiwa na Mkaguzi wa Migodi.Aidha, Wizara itaendelea kuwajengea uwezo Wakaguzi waMigodi kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali ndani na njeya nchi ili waweze kukagua Migodi kwa umakini zaidi nakupunguza matukio ya ajali.

156. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia utunzajiwa mazingira Migodini, Kampuni ya ACACIA inayomilikiMigodi ya Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara imeweka HatiFungani (Rehabilitation Bond) ya kiasi cha Dola za Marekanimilioni 41.10 sawa na takriban Shilingi bilioni94.98 kwaajili ya kurekebisha mazingira. Mkataba wa Makubalianohayo umepitishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali nakusainiwa na pande zote mbili tarehe 14 Desemba, 2016.Aidha, Hati Fungani kwa ajili ya Kampuni ya WilliamsonDiamonds Limited inayomiliki Mgodi wa Almasi wa Mwaduiinapitiwa na Wataalam wa Wizara na itawasilishwa Ofisiya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya ushauri wakekabla ya kusainiwa. Pia, Kampuni za Geita Gold MiningLimited, Shanta Mining Co. Limited (New Luika Gold Mine),STAMIGOLD Mine na Dangote Industries Tanzania Ltdzimewasilisha Mipango yao ya ufungaji Migodi yao kulinganana Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Kamati ya Kitaifa ya

Page 129: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

129

Ufungaji wa Migodi imeshaanza kupitia Mipango hiyo.Wamiliki wa Mgodi wa TanzaniteOne wameelekezwakutayarisha Mpango wa Ufungaji Mgodi huo na kuwasilishaWizarani mapema iwezekanavyo. Migodi ya Kati na Mikubwayote nchini inafuata utaratibu huo kwa mujibu wa Sheria yaMadini ya Mwaka 2010. Pia, Wizara itaendelea kutoa elimukwa Wachimbaji Wadogo kuhusu kuandaa Mpango waUtunzaji Mazingira (EPP) kwa kuzingatia Sheria ya Madini yaMwaka 2010.

157. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18, Wizara itakamilisha Mkataba baina yake naKampuni ya Williamson Diamonds Limited kwa ajili ya kuwekaHati Fungani na kupitia na kukamilisha Mipango ya UfungajiMigodi (Mines Closure Plans) kwa Migodi iliyobaki. Pia, Wizarakupitia National Mine Closure Committee itapitia nakukamilisha Mpango wa Ufungaji wa Hati Fungani kwa Migodiya TanzaniteOne, Dangote, Geita Gold Mine, New Luika GoldMine na STAMIGOLD.

Usimamizi wa Masuala ya Baruti Nchini

158. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Jumla ya tani 31,092 zaBaruti na Vipande 3,878,607 vya Fataki viliingizwa nchini kwaajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa madini,utafutaji wa Mafuta na Gesi Asil ia na ujenzi wamiundombinu. Aidha, Wizara ilitoa vibali 135 vya kuingizaBaruti nchini, vibali 280 vya kulipulia Baruti na Leseni 31 zamaghala ya kuhifadhia Baruti. Maghala hayo yana uwezowa kuhifadhi Jumla ya tani 553 za Baruti (fractured explosives)na Vipande milioni 5.5 vya Viwashio (detonators).

159. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwakawa Fedha wa 2017/18, Wizara itaendelea kuimarishausimamizi wa masuala ya Baruti nchini ikiwa ni pamoja nakutoa elimu na mafunzo ya matumizi bora na salama yaBaruti kwa Wachimbaji Wadogo wa madini na Wadauwengine kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali; kukaguamaghala ya kuhifadhia Baruti; kusimamia matumizi sahihi ya

Page 130: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

130

Baruti kulingana na Sheria zilizopo sambamba na kuwasilishaBungeni Muswada Mpya wa Sheria ya Baruti ya Mwaka 2017kwa kuwa Sheria iliyopo ina mapungufu ya udhibiti wamatumizi mabaya ya Baruti.

Kuhamasisha Shughuli za Uongezaji Thamani Madini

160. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi 2017, Wizara ilitoa Jumla yaLeseni 40 za uchenjuaji wa marudio ya madini ya dhahabu.Aidha, ongezeko la leseni hizo limewezesha Serikali kuongezamapato yatokanayo na shughuli za uchenjuaji dhahabuambapo Jumla ya Mrabaha wa Shilingi bilioni 4.23umekusanywa. Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2016/17 Kituo cha Jimolojia Tanzania (Tanzania Gemological Centre– TGC) kilichopo Arusha kimeendelea kutoa mafunzo ya mudamfupi (Miezi 6) ya usanifu wa madini ya Vito (lapidary)ambapo wanafunzi 18 walidahiliwa Mwezi Machi, 2016 nakumaliza Septemba, 2016. Pia, wanafunzi wengine 18walidahiliwa kuanzia Mwezi Oktoba, 2016 na wanatarajiwakumaliza masomo yao mwishoni mwa Mwezi Mei, 2017na hivyo kufanya Jumla ya Wahitimu wa Kituo hicho kufikia65 tangu kuanzishwa kwa mafunzo hayo Mwezi Novemba,2014. Mafunzo hayo yanaendelea kudhaminiwa na Mfuko waKuwaendeleza na Kuwajengea Uwezo Wanawake (ArushaGem Fair Women Foundation Fund) ulioanzishwa kupitiaMaonesho ya Vito ya Arusha.

161. Mheshimiwa Spika, Wizara ilianzisha taratibuza usajili wa Kituo hicho kwenye Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE) katika Mwaka 2015/16. Hata hivyo, usajili waKituo hiki haujakamilika hadi sasa baada ya NACTE kusitishakwa muda usajili wa vyuo nchini kwa lengo la kufanya uhakikiwa ubora wa vyuo vilivyopo. Mara NACTE watakapoanzatena zoezi la kusajili vyuo, Wizara itahakikisha kuwa usajiliwa TGC unakamilishwa haraka. Usajili ukikamilika, Kituokinakusudia kutoa mafunzo ya Diploma ya Gem & JewelleryTechnology ambapo mhitimu katika Mwaka wa Kwanzaatapata Cheti cha Basic Technician Certificate in Gem &Jewellery Technology (NTA Level 4), Mwaka wa Pili Technician

Page 131: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

131

Certificate in Gem & Jewellery Technology (NTA Level 5) naMwaka wa Tatu Ordinary Diploma in Gem & JewelleryTechnology (NTA Level 6). Pia, Kituo kinatarajia kutoa mafunzoya muda mfupi kwa kozi mbalimbali za uongezaji thamanimadini.

162. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kukijengeauwezo Kituo cha TGC, Wizara inawatumia WakufunziWaelekezi kutoka nje ya nchi na wakati huo huo inajengauwezo wa Wakufunzi wa Kitanzania. Wizara imepelekaWatumishi watatu (3) katika nchi za Sri Lanka, India naThailand kusomea fani za usonara (Jewelly design & making),ukataji na uchongaji (lapidary) na jimolojia (gemology).Wataalam hao wamehitimu mafunzo hayo na wameanzakazi kwenye Kituo cha TGC.

163. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Wizara imepanga kupeleka Watumishi wenginesaba (7) kusomea fani mbalimbali za uongezaji thamanimadini kupitia Mradi wa SMMRP unaofadhiliwa na Benki yaDunia. Jumla ya Shilingi milioni 694.76 zinakadiriwa kutumikakwa ajili ya kugharamia mafunzo hayo. Aidha, ili kukiongezeaufanisi, Kituo kimepewa sub-vote itakayoanza kutumikaMwaka wa Fedha wa 2017/18.

Uchambuzi na Uthaminishaji wa Madini ya Vito

164. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara kupitia TANSOR Timeendelea kusimamia uthamini wa madini ya Almasi naVito ambapo kiasi cha karati 174,700 za Almasi zenyethamani ya Dola za Marekani milioni 47.95 sawa na Shilingibilioni 110.81 zilithaminishwa na kusafirishwa nje ya nchi.Vilevile, Wizara ilifanya uthamini wa madini ya Vito ambapoil ithaminisha tani 604.39 za madini ya mapambo(Ornamental stones), gramu milioni 3.30 za vito ghafi na karati177,339 za madini ya vito yaliyosanifiwa kwa thamani ya Dolaza Marekani milioni 23.46 sawa na Shilingi bilioni 54.22.Kutokana na shughuli hizo, Serikali imekusanya Mrabaha waDola za Marekani milioni 3.31 sawa na Shilingi bilioni 7.65.

Page 132: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

132

165. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha wa2017/18 Wizara itaendelea kusimamia kwa umakini zaidishughuli ya uthaminishaji wa madini ya Almasi na Vito vingineili kuhakikisha Serikali inapata mapato stahiki. Aidha, Wizaraitaanzisha na kusimamia masoko (magulio) ya ndani yamadini ya Vito kwa kushirikiana na Ofisi za Madini za Kandana itatoa huduma za kijimolojia kwa Wachimbaji Wadogona wa Kati.

166. Mheshimiwa Spika, uanzishwaji wa masoko(magulio) ya ndani ya madini ya Vito unalenga kuwaendelezaWachimbaji Wadogo kwa kuwapatia soko la uhakika nabei za ushindani karibu na maeneo ya Morogoro (Mkuyuni),Merelani, Tanga na Tunduru na kupata madini yenye uboraunaohitajika katika Maonesho ya Kimataifa ya Vito ya Arusha(Arusha Gem Fair - AGF) ambayo hufanyika mara moja auzaidi kwa mwaka.

Miradi Mikubwa ya Madini

167. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendeleakuhamasisha na kuwezesha Kampuni za madini katikauendelezaji wa Miradi Mikubwa ya madini. Miradi hiyo nipamoja na Miradi ya graphite (kinywe) iliyopo Nachu,Namangale na Chilalo Wilayani Ruangwa; Chidya naChiwata Wilayani Masasi na Epanko, Mahenge WilayaniUlanga. Madini ya graphite yanatumika kwenye kutengenezavilainishi (lubricants), betri na vifaa vya kwenye injini za magari.Uwekezaji katika Miradi hiyo upo katika hatua mbalimbaliza kukamilisha tathmini ya athari za mazingira na ulipaji wafidia. Hata hivyo, Mradi wa Epanko umekumbwa na tatizola baadhi ya Wananchi kukataa kupisha maeneo yao kwaajili ya kuanzishwa kwa Mradi huo. Wizara kwa kushirikianana Uongozi wa Mkoa wa Morogoro inaendelea kutoa elimukwa Wananchi juu ya umuhimu wa Mradi huo.

168. Mheshimiwa Spika, Miradi mingine ambayo ipokatika hatua ya uendelezaji ni pamoja na Mradi wa Uraniambao upo eneo la Mto Mkuju katika Wilaya ya Namtumbo.Mradi huo unaendelezwa na Kampuni ya Mantra Tanzania

Page 133: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

133

Limited. Hata hivyo kutokana na kushuka kwa bei ya madiniya urani katika Soko la Dunia, Mradi huo umechelewa kuanzakwa kuwa uchimbaji ukifanyika sasa Serikali na Mwekezajihawataweza kupata manufaa stahiki.

169. Mheshimiwa Spika, Miradi ya Rare Earth Elements(REE) na niobium iliyopo katika Wilaya ya Songwe ipo katikahatua za juu za utafiti na uanzishwaji wa Mgodi, sawia.Kukamilika na kuanzishwa kwa uchimbaji wa madini katikaMiradi hii kutasaidia nchi kupata Mapato kutoka kwenyemadini mengine zaidi ya dhahabu ambayo Migodi yake mingiinaendelea kufungwa kutokana na kuisha kwa mashapokatika maeneo husika.

Utatuzi wa Migogoro

170. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017, Wizara imeendelea najuhudi za kutatua migogoro mbalimbali katika Sekta yaMadini. Katika kipindi hicho Wizara kupitia Kamati Maalumya Wataalam wa Serikali imefanya uhakiki kwa Wananchiwa Kitongoji cha Nyamichele Kij i j i cha Nyakunguruwanaozunguka eneo la Mgodi wa Dhahabu wa North Maraambao walifyekewa mazao yao wakati wa zoezi la kufanyatathmini ya mali na ardhi Mwaka 2013. Jumla ya Wananchi2,742 walifanyiwa uhakiki wa maeneo yao ili kupisha shughuliza Mgodi. Lengo la uhakiki huo lilikuwa ni kubaini Wamilikihalali wa maeneo hayo il i walipwe fidia ya mazaoyaliyofyekwa pamoja na gharama za usumbufu.

171. Mheshimiwa Spika, kati ya Wananchi 2,742waliohakikiwa, Wananchi 1,586 wamebainika kutokuwa nakasoro za umiliki wa maeneo yao na Kamati ilipende- kezawalipwe fidia ya mazao yao yaliyofyekwa pamoja nagharama za usumbufu. Wananchi wenye umiliki wa maeneo(parcels) 1,016 wamebainika kuwa na kasoro mbalimbali zaumiliki wa ardhi, Kamati ilipendekeza majina ya wamiliki wamaeneo hayo yachunguzwe na TAKUKURU na Vyombo vinginevya Dola ili haki itendeke.

Page 134: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

134

172. Mheshimiwa Spika, pamoja na kutoa mudawa kutosha kwa ajili ya uhakiki huo, Wananchi wanaomilikimaeneo (parcels) 139 hawakujitokeza kwa ajili ya kuhakikiwa,hivyo Kamati ilipendekeza kuwa Wananchi hao wasilipwechochote na kama wataona hawakutendewa hakiwanaweza kudai haki hiyo kupitia Vyombo vya Sheria. Aidha,pamoja na malipo hayo, Wananchi wataendelea kumilikimaeneo yao kwa kuwa Mgodi umeazimia kuendelezauchimbaji kwa njia ya chini kwa chini (Underground Mining).

173. Mheshimiwa Spika, Pamoja na kushughulikiamalalamiko ya fidia za Wananchi wa Kijiji cha Nyakunguru,Kamati pia ilitoa maelekezo kwa Mgodi wa North Marakuwalipa fidia stahiki na kuwahamisha Wananchi wote waliondani ya eneo hai laMgodi (Mita 200) ili kupisha shughuli zaMgodi. Maeneo hayo ni yale yaliyomo katika Vijiji vyaMatongo, Nyangoto, Nyabichune, Mjini Kati, Nyakunguru,Komarera na Kijiji cha Kewanja.

174. Mheshimiwa Spika, Serikali imefanikiwa kutatuamgogoro wa Wananchi wa eneo la Magambazi WilayaniHandeni waliokuwa wamevamia eneo la Leseni yauchimbaji la Kampuni ya Canaco. Wananchi haowameondolewa katika eneo hilo na Kampuni hiyo imekubalikutoa sehemu ya eneo ndani ya Leseni kwa ajili ya kuendeshashughuli za uchimbaji kwa Wananchi hao. Aidha, Wananchiwameelekezwa kuunda vikundi na kuvisajili kabla ya kupewaLeseni za uchimbaji. Hadi sasa vikundi saba (7) vimeundwana kusajiliwa, kikundi kimoja kimeshapewa Leseni nakimeanza shughuli za uchimbaji na vikundi vingine sita (6)viko katika utaratibu wa kupatiwa Leseni za uchimbajimdogo. Kampuni ya Canaco imeahidi kuvipatia baadhi yavifaa vya uchimbaji vikundi vitakavyopatiwa Leseni katikamaeneo hayo.

Ushiriki wa Watanzania Katika Shughuli za Madini (LocalContent)

175. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendeleakuhamasisha na kutoa elimu kwa Wananchi wanaozunguka

Page 135: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

135

Migodi kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo katika Migodiinayowazunguka. Kwa hali ilivyo sasa, ushiriki wa Watanzaniakatika kutoa huduma na kuuza bidhaa kwenye Migodiumefikia takriban asilimia 50. Vilevile, Wizara inaendeleakuhamasisha Migodi kutoa zabuni kwa Wananchiwanaozunguka Migodi na Kampuni za Wakandarasi waKitanzania ili kutoa fursa kwa Watanzania kuuza hudumana bidhaa kwenye Migodi hiyo.

176. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendeleakuhamasisha Wamiliki wa Viwanda kutumia malighafi zamadini yanayopatikana hapa nchini ili kukuza Viwanda vyaNdani. Katika kutekeleza hilo, Wizara imeweka zuio kwaViwanda vya Saruji kuingiza malighafi (Makaa ya Mawe naMadini ya Jasi) kutoka Nje ya Nchi. Ili kuhakikisha Wamilikiwa Viwanda vya Saruji wanapata malighafi zinazotakiwana kwa muda muafaka, Serikali imewaelekeza kuingiaMikataba na Wachimbaji wa madini ya Jasi na Makaa yaMawe.

177. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza uwazi na ushirikiwa Watanzania katika Migodi Mikubwa, Serikali kupitia Gazetila Serikali Na. 286 la tarehe 07 Oktoba, 2016, imetunga Kanuniza Usajili wa Hisa kwa Kampuni za Madini (The Mining(Minimum Shareholding and Public Offering) Regulations,2016). Kanuni hizi zinazitaka Kampuni zenye Leseni kubwa zaUchimbaji wa Madini (Special Mining Licence) kuandikishaasilimia 30 ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (Dares Salaam Stock Exchange – DSE). Kanuni zinazitaka Kampunizilizopata leseni kabla ya kutangazwa kwa Kanuni kusajiliasilimia 30 ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam ndaniya kipindi cha miaka miwili tangu kutangazwa kwa Kanunihizi. Aidha, Kampuni ambazo zitapata leseni baada yakutangazwa kwa Kanuni hizi zinatakiwa kutekeleza mashartiya Kanuni hizi ndani ya mwaka mmoja kutoka tarehe yakupewa Leseni.

178. Mheshimiwa Spika, kupitia Gazeti la SerikaliNa. 44 la tarehe 24 Februari, 2017 (The Mining (MinimumShareholding and Public Offering) (Amendment) Regulations,

Page 136: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

136

2016), Serikali imefanya Marekebisho ya Kanuni hizi kwakuzitaka Kampuni ambazo zinamiliki Leseni za UchimbajiMkubwa zilizotolewa kabla ya kutangazwa kwa Kanuni hizikutekeleza masharti ya Kanuni hizi ndani ya kipindi cha miezisita (6) tangu tarehe ya kutangazwa kwa mabadiliko yaKanuni hizo. Pia, Kampuni ambazo zitapata leseni baada yakutangazwa kwa Kanuni hizi sasa zinatakiwa kusajili asilimia30 ya Hisa katika Soko la Hisa mara baada ya kuanza shughuliza uchimbaji.

179. Mheshimiwa Spika, kwa sasa kuna Jumla yaKampuni 12 zinazomiliki Leseni 14 za uchimbaji mkubwazinazohitajika kusajiliwa kwenye Soko la Hisa. Kampuni hizoni Bulyanhulu Gold Mine Limited, Pangea Minerals Limited,Geita Gold Mining Limited, North Mara Gold Mine Limited(2), STAMIGOLD Company Limited, Williamson DiamondsLimited, Mantra Tanzania Limited, El-Hilal Minerals Limited,Kiwira Coal Mines Limited, Tanzania China InternationalMineral Resources Limited (2), Uranex Tanzania Limited naDangote Industries Limited. Wizara imeagiza Kampuni hizozijisajili kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

180. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Mwaka waFedha wa 2017/18 Wizara itaendelea kuchukua hatua zamakusudi kuelimisha umma kuhusu manufaa na fursa zilizopokatika Sekta ya Madini na kushirikiana na Taasisi nyingine zaSerikali kujenga uwezo wa Watanzania kushiriki katika Sektahiyo. Natoa wito kwa Wananchi kujiandaa ili Kampuni zamadini zikisajiliwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam,Watanzania wajitokeze kwa wingi kununua Hisa na hivyokushiriki kwenye umiliki wa rasilimali zao za madini.

Kuvutia Uwekezaji Katika Sekta ya Madini

181. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara imeendeleakuhamasisha na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezajikatika Sekta ya Madini nchini kupitia Balozi za nchimbalimbali zilizopo ndani ya nchi na Balozi zetu zilizopo njeya nchi zikiwemo Afrika Kusini na Canada. Aidha, Wizara

Page 137: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

137

imefanikiwa kushiriki kwenye Mkutano Mkubwa wa kuvutiawawekezaji Afrika unaojulikana kama Mining Indaba –Afrika ya Kusini ambapo Serikali imetoa taarifa mbalimbalikuhusu mazingira ya uwekezaji katika Sekta ya Madini. Pia,Wizara imeshiriki katika Mikutano ya Kimberly ProcessCertificate System (KPCS) katika Nchi ya Umoja wa Falme zaKiarabu (UAE) na International Conference on Great LakesRegion (ICGLR) katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia yaKongo (DRC).

182. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Wizara imefanikiwakufanya Minada Miwili ya Madini ya Tanzanite Mkoani Arushaambapo Mnada wa Kwanza ulifanyika Mwezi Agosti, 2016na Mnada wa Pili ulifanyika Mwezi Machi, 2017. Katika Mnadawa Kwanza madini yenye thamani ya Dola za Marekanimilioni 3.45 yaliuzwa na kuiwezesha Serikali kukusanyaMrabaha wa thamani ya Dola za Marekani 150,491 sawa naShilingi milioni 347.78. Katika Mnada wa Pili madini yenyethamani ya Dola za Marekani milioni 4.20 yaliuzwa nakuiwezesha Serikali kukusanya Mrabaha wa kiasi cha Dola zaMarekani 210,114.36 sawa na Shilingi milioni 485.57. Aidha,Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ilikusanya Ushuru waHuduma kiasi cha Shilingi milioni 27.99.

183. Mheshimiwa Spika, lengo kuu la Minada hii nikuwakutanisha moja kwa moja Wazalishaji wa Madini yaTanzanite, Wafanyabiashara na wenye Viwanda vyakuongeza thamani madini ili kuwezesha Wafanyabiasharakuuza madini yao kwa bei ya ushindani na Serikali kukusanyaMapato stahiki. Aidha, Minada hii husaidia kupunguzautoroshaji wa madini nje ya nchi na kuitangaza Tanzaniakatika medani ya Kimataifa kuhusu fursa za madiniyanayopatikana nchini. Pia, Wizara ilifanya Maonesho yaKimataifa ya Vito na Usonara, Arusha kuanzia tarehe 03 hadi05 Mei, 2017.

184. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka waFedha wa 2017/18, Wizara itaendelea kushiriki katikaMaonesho na Makongamano ya Kitaifa na Kimataifa ili

Page 138: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

138

kutangaza fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini hapanchini. Pia, kuandaa Maonesho ya Kimataifa na Minada yaMadini ya Vito itakayohusisha Wanunuzi wa Ndani na Nje.

Katika Minada ya madini ya Tanzanite Serikaliitahakikisha Wauzaji wanajumuisha Tanzanite iliyokatwa ilikukuza Viwanda vya ndani vya kukata Madini ya Vito. Natoawito kwa Wadau wa madini ya Vito waendelee kushirikianana Wizara ili kufanikisha Maonesho na Minada hiyo kwalengo la kukuza Masoko ya Ndani na kuhamasisha shughuliza uongezaji thamani madini nchini.

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP)wa Benki ya Dunia

185. Mheshimiwa Spika, Mradi wa Usimamizi Endelevuwa Rasilimali za Madini (Sustainable Management of MineralResource Project – SMMRP) Awamu ya II unaofadhiliwa naBenki ya Dunia umeanza ujenzi wa Kituo cha mafunzo kwaWachimbaji Wadogo cha Rwamgasa - Geita. Kituo hikikinajengwa kwa ushirikiano baina ya Wizara, Mgodi wa Geitana Ushirika wa Wachimbaji Wadogo wa Rwamgasa. Ujenziwa Kituo hicho utagharimu kiasi cha Dola za Marekani500,000 sawa na Shilingi bilioni 1.16 ambao unatarajiwakukamilika ifikapo Mwezi Julai, 2017.

186. Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine za Mradihuu zilizofanyika ni pamoja na kukamilika kwa taratibu zaununuzi za kuwapata Washauri Waelekezi (Consultants)kwaajiliyakusanifunakusimamiaukarabatiwa Ofisi za Madiniza Bariadi; Bukoba; Chunya; Kigoma; Mpanda; Musoma;Songea; Ofisi za STAMICO; na Chuo cha Madini Dodoma.Kwa sasa Mradi unaendelea na utaratibu wa kuwapataWakandarasi i l i ukarabati huo uanze. Aidha, Mradiumekamilisha ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kutoaHuduma za Ugani kwa Wachimbaji Wadogo kupitiaSTAMICO, GST na Ofisi za Madini za Kanda. Shughuli hizozimegharimu takriban Dola za Marekani milioni 5.68 sawana Shilingi bilioni 13.13 na zimefadhiliwa na Benki ya Dunia.

Page 139: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

139

187. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mradi waSMMRP imewezesha GST na STAMICO kufanya utafiti wakijiolojia katika maeneo yanayokusudiwa kuanzishwa VituoBora vya Mfano na maeneo mengine ya uchimbaji mdogo.Fedha zilizotumika kwa ajili ya kazi hii ni Dola za Marekanimilioni 3.7 sawa na Shilingi bilioni 8.55 ambazo zimetolewana Benki ya Dunia. Kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 kupitiaMradi wa SMMRP, Wizara inatarajia kuanza ukarabati naupanuzi wa Ofisi za Madini za Bariadi; Bukoba; Chunya;Kigoma; Mpanda; Musoma; Songea; Ofisi za STAMICO; naChuo cha Madini Dodoma. Lengo la ukarabati ni kuboreshamazingira ya kazi ya Ofisi hizo ikiwa ni pamoja na kuongezavyumba vya mikutano na madarasa vitakavyotumikakufundishia Wachimbaji Wadogo (Centres of Excellence).Vilevile, Wizara itaanza ujenzi wa Vituo vya Mafunzo(Demonstrating Centres) vitatu (3) katika Awamu ya Kwanzakwenye maeneo ya Itumbi (Chunya), Katente (Bukombe) naMkwanyule (Kilwa).

Wakala wa Jiolojia Tanzania (Geological Survey of Tanzania -GST)

188. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017, Serikali kupitia Wakalawa Jiolojia Tanzania (GST) iliendelea kukusanya taarifa zaJiosayansi na kuchora Ramani kwa ajili ya kuvutia uwekezajikatika Sekta ya Madini. GST kwa kushirikiana na GeologicalSurvey of China wamefanya na kukamilisha utafiti waJiokemia katika Mikoa ya Mbeya na Songwe ambaoulifadhiliwa na Serikali ya China.

Pia, GST kwa kushirikiana na Geological Survey ofFinland na Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) imetengenezaRamani za Jiokemia za nchi nzima (Country Wide Multi-Element Geochemical Maps) zinazoainisha wingi wa madiniya aina mbalimbali za metali (kama dhahabu, shaba,chuma, nikeli, bati n.k.) katika sehemu mbalimbali za nchi.Mradi huu umefadhiliwa na Serikali ya Finland kwa kiasi chaEuro 750,000 sawa na takriban Shilingi bilioni 1.59.

Page 140: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

140

189. Mheshimiwa Spika, Wakala unaendelea na kaziya utafiti wa uchenjuaji ili kuongeza thamani ya madini yaNikeli kwa Wachimbaji Wadogo wa Milima ya MwahanzaHaneti Dodoma. Wakala umekamilisha utafiti wa uchenjuajiwa madini ya Shaba katika Wilaya za Mpwapwa na Kilosakwa lengo la kuongeza thamani ya madini ya Shaba. Pia,Wakala uliendelea kutoa Huduma za Maabara zauchunguzi na upimaji wa sampuli za Jiotekinolojia kwa ajiliya ujenzi wa miundombinu kwa Wateja mbalimbaliwakiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma na Mgodi wa Almasiwa Mwadui.

190. Mheshimiwa Spika, Wakala kwa kushirikiana naChuo Kikuu cha Dar es Salaam walifanya utafiti wa Tetemekola Ardhi lililotokea Mkoani Kagera tarehe 10/9/2016 nakuandaa taarifa za utafiti. Pia, Wataalam kutoka Wakala,Chuo Kikuu cha Ardhi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaamwalitoa elimu kwa umma na kwa wahanga wa Tetemekohilo. Aidha, Wakala uliendelea kukusanya takwimu kutokaVituo nane (8) vya kudumu vilivyoko nchini vya kupimiaMatetemeko ya Ardhi, kuchakata takwimu, kuchora Ramanina kuzihifadhi kwenye kanzidata (database) kisha kuzitoleataarifa.

191. Mheshimiwa Spika, Wakala kwa kushirikiana naGeological Survey of Finland (GTK), umechapisha Ramani zaJiolojia za block ya Nachingwea-Masasi/Tunduru na taarifa(Explanatory Notes) zake baada ya kupata matokeo kutokaMaabara za GST, SUA pamoja na GTK-Finland. Vilevile, Wakalaumekusanya takwimu katika maeneo ya Wilaya za Kondoana Singida unaolenga kupata vyanzo vya nishati ya Jotoardhikwa ajili ya uzalishaji umeme na umefadhiliwa na USAID kwathamani ya Shilingi milioni 33.44. Utafiti huu unafanyika chiniya Mradi wa “Partnership for Enhanced Engagement inResearch Project (PEERP)”, unaofadhiliwa na Serikali yaMarekani.

192. Mheshimiwa Spika, Wakala umeanzisha Mfumowa kuuza na kusambaza Ramani mbalimbali za Jiolojia naJiofizikia, taarifa na takwimu kwa Wadau mbalimbali kwa

Page 141: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

141

njia ya Mtandao (data sales portal) na inaendelea kuimarishana kuboresha Mfumo wa kuchakata, kutunza nakusambaza takwimu na taarifa za Jiosayansi kwa Wadau(Geological and Mineral Information System – GMIS).

193. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Wakala umepanga kuendeleza tafiti nakukusanya taarifa za Jiosayansi kwa ajili ya kuchora Ramaninne (4) za Jiolojia za Mfumo wa QDS kwa skeli ya 1:100,000(QDSs 264, 275, 276 na 277) na Ramani nyingine mbili zaJiokemia za Mfumo wa QDS (QDS 264 na 275) kwenye maeneoyaliyopo katika Wilaya za Songea Vijijini, Ludewa na Madaba.Pia, Wakala umejipanga kufanya uhakiki maalum (fieldchecks) wa Jiolojia, Jiokemia na kuboresha Ramani za QDS49, 64 na 65 na kukusanya na kuhakiki taarifa za uwepo wamadini nchini na kuboresha kanzidata yake.

194. Mheshimiwa Spika, Wakala utaendelea kuratibumajanga asilia ya Kijiolojia ikiwa ni pamoja na Matetemekoya Ardhi, Milipuko ya Volkano, Maporomoko ya Ardhi(uchunguzi wa Jiomofolojia) ili kubaini maeneo yenye hatariya kupata Maporomoko ya Ardhi na kutoa ushauri kwaWananchi waishio katika maeneo hayo. Aidha, Wizaraitaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa Wakala kwakununua vifaa vya utafiti wa Kijiolojia na Maabara. Wakalawa Jiolojia ulichakata takwimu na taarifa mbalimbali zaMatetemeko ya Ardhi zilizokusanywa kuanzia Mwaka 1900kuhusu mahali yalipowahi kutokea pamoja na ukubwa wakekatika Mji wa Dodoma. Hii itawezesha kuainisha maeneoyenye Mipasuko chini ya Ardhi ambayo yana uwezekanomkubwa wa kutokea Matetemeko. Ramani zinazooneshataarifa hizi zinaweza kutumika katika upangaji bora waMji wa Dodoma, hivyo nachukua fursa hii kuwashauriHalmashauri ya Manispaa ya Dodoma na Wadau wenginekushirikiana na GST katika kupanga matumizi bora ya Ardhi.

Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA)

195. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2009 Serikali ilianzishaWakala maalum kwa ajili ya Ukaguzi wa Shughuli za

Page 142: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

142

Uwekezaji katika Sekta ya Madini (TMAA). Kazi kubwa ikiwani pamoja na kukagua gharama za uwekezaji wamakampuni makubwa, mapato yatokanayo na uwekezajihuo, kodi pamoja na mrabaha unaolipwa Serikalini. TMAAhufanya kazi kwa kushirikiana na Ofisi za Madini za Kandahusika, TRA, pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani. Utendajiwa Taasisi hiyo uliendelea kuonesha mapungufu katika Sektakwa kubaini mianya ya upotezaji wa mapato ya Serikali.Pamoja na utendaji huo, wadau mbalimbali wakiwemoWananchi wa kawaida waliendelea kupaza sauti wakidaiTaifa linaibiwa kupitia miradi ya madini.

196. Mheshimiwa Spika, kufuatia maoni na ushauriwa wadau, Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ilikulinda maslahi ya Taifa. Serikali imeandaa na kuwaongezeauwezo watendaji, imepanga watendaji wenye ujuzi katikamaeneo ya migodini, mipakani, viwanja vya ndege nakwenye bandari zilizopo nchini. Kutokana na jitihada hizo,kwa Mwaka 2016/17, Wakala uliweza kukamata madini yenyejumla ya thamani ya Dola za Marekani 119,906.45 sawa naShilingi milioni 277.10 katika viwanja vya ndege vyaArusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Songwe.

197. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2016/17, Wakala ulifanya ukaguzi na kuwezesha Serikalikukusanya mrabaha wenye thamani ya Shilingi bilioni 4.45ikilinganishwa na jumla ya Shilingi bilioni 6.27 zilizokusanywakwa kipindi cha Mwaka 2015/16. Kupatikana kwa kiwangokidogo cha mrabaha, kushuka kwa mrabaha uliokusanywakwa Mwaka 2016/17 na vilio vya wananchi kulipelekea Serikalikuchua hatua mbalimbali ili kuhakikisha Serikali inapatamapato stahiki na kukuza Pato la Taifa.

198. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2017/18,Serikali itaimarisha Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) kwakuzingatia maoni na ushauri wa wadau mbalimbali. Ushauriuliotolewa na Kamati Maalum za Bunge pamoja na KamatiMaalum ya Wataalam iliyoundwa rasmi na Mheshimiwa Raiskuchunguza mchanga uliomo katika makontena yamakinikia ya dhahabu utazingatiwa. Lengo la jitihada hizi ni

Page 143: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

143

kuhakikisha kwamba Taifa linanufaika kikamilifu kutokanana rasilimali za madini.

Shirika la Madini la Taifa (State Mining Corporation – STAMICO)

199. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017, STAMICO kupitia Kampuniyake Tanzu ya STAMIGOLD imezalisha Jumla ya wakia 12,092za Dhahabu na wakia 1,659 za madini ya Fedha (silver) nakuiingizia Kampuni Shilingi bilioni 36.88. Kampuni pia ililipaSerikalini Mrabaha wa Shilingi bilioni 1.48.

200. Mheshimiwa Spika, kupitia uchimbajiunaofanyika kwa ubia kati ya STAMICO na Kampuni yaTanzaniteOne Mining Limited (TML), Jumla ya kilo 2,872.79 zaTanzanite zilizalishwa na kuuzwa kwa kipindi cha Mwezi Julai,2016 hadi Machi, 2017 ambapo Jumla ya Shilingi bilioni16.93 zilipatikana na Shilingi milioni 846.5 zililipwa Serikalinikama Mrabaha.

201. Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizo,STAMICO pia inaendelea kutekeleza Mradi wa ununuzi wamadini ya Bati kutoka kwa Wachimbaji Wadogo waliokoKyerwa Mkoani Kagera ambapo hadi kufikia Machi, 2017tani 18.08 za madini hayo ziliuzwa na kulipatia Shirika Jumlaya Shilingi milioni 325.49 ambazo zimewezesha ulipaji waMrabaha kwa Serikali wa kiasi cha Shilingi milioni 13.02 naShilingi 976,471 zimelipwa kama ushuru wa Huduma kwaHalmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Aidha, katika kipindi chakuanzia Mwezi Januari hadi Machi, 2017 Jumla ya kilo 1,205za madini ghafi ya Bati zimenunuliwa kwa Jumla ya Shilingimilioni 22.90.

202. Mheshimiwa Spika, ili kukidhi mahitaji ya Makaaya Mawe nchini, STAMICO imeanza rasmi uchimbaji waMakaa hayo katika Kilima cha Kabulo - Kiwira kuanzia MweziAprili, 2017 ambapo Jumla ya tani 107,078 zinakadiriwakuchimbwa kwa Mwaka na Mradi huu utagharimu kiasi chaShilingi bilioni 2.39. Lengo la Mradi huu ni kuwauzia Makaaya Mawe Viwanda vya Saruji na watumiaji wengine.

Page 144: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

144

203. Mheshimiwa Spika, Shirika limefanikiwa kufanyakazi ya ukadiriaji na uthaminishaji wa mashapo ya madiniyaliyopo kwenye Mradi wake wa dhahabu wa Buhembaambapo kiasi cha wakia 441,772 za dhahabu (indicatedresources) zimekadiriwa kuwepo katika mashapo hayo.Aidha, Mwezi Juni, 2017 kazi za ukadiriaji na uthamini wamashapo zitafanyika katika mashimo ya Buhemba Mainna Mwizi na kazi hizo zitakapokamilika zitawezeshaongezeko la mashapo yanayokadiriwa kufikia wakia 600,000.Mpango uliopo ni kutafuta Mwekezaji wa kuingia naye Ubia.

204. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 Shirika limeendeleakufanya tathmini za uwepo wa mashapo katika Leseni zakeza madini inazozimiliki. Leseni zilizofanyiwa utafiti ni Leseni yadhahabu iliyopo Busanda – Mkoani Geita na Madini ya RareEarth Elements - REE iliyopo Sengeri Mkoani Songwe. Pia,Shirika limepata Leseni 20 za uchimbaji madini mdogo (PML)wa kokoto katika maeneo ya Chigongwe Dodoma na UbenaZomozi Pwani ambazo zitawezesha uanzishaji wa Mradi wakokoto katika maeneo hayo. Katika Mwaka wa Fedha wa2017/18 jumla ya Shilingi bilioni 2.64 zimetengwa kwa ajili yakutekeleza Mradi huu.

205. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017, STAMICO imeendeleakutoa huduma za kitaalam kwa Wachimbaji Wadogo nchini.Jumla ya Wachimbaji Wadogo 15 wamefanyiwa utafiti waKijiolojia katika maeneo ya Lwamgasa - Geita (Blue Reef),Bukandwe - Mbogwe, Nyampalahala – Bukombe (Paso Mine),Mpinga-Bahi, Mkalama na Mandawa-Rwanga (MkalamaCopper Gold Project), Kazikazi – Itigi, Kiteto, Wami - Pangani(Jiwe Project), Kerezia na Ng’anzo – Bukombe, Nsagali GoldMine na Makangaga – Kilanjelanje - Kilwa (MishanguInternational). Tafiti hizo zimewezesha Wachimbaji haokupata taarifa za uwepo wa madini katika maeneo yaoambazo wanaweza kuzitumia kupata mikopo kutoka Taasisiza Fedha. Wachimbaji waliofaidika na taarifa hizo za utafitina waliofanikiwa kupata mikopo kutoka Benki ya Uwekezaji

Page 145: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

145

Nchini - TIB ni Nsagali Gold Mine na Makangaga- Kilanjelanje- Kilwa (Mishangu International).

206. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017 STAMICO kwa kushirikianana GST chini ya Mradi wa SMMRP unaofadhiliwa na Benki yaDunia imefanya utafiti wa Kij iosayansi unaohusishauchorongaji wa miamba na ukadiriaji wa mashapo ya madinikatika maeneo yanayotarajiwa kuanzisha Vituo vya Mfanovya uchenjuaji wa madini kwa Wachimbaji Wadogo katikamaeneo ya Itumbi (Chunya), Katente (Bukombe) naKapanda (Mpanda). Katika kipindi hiki Jumla ya mita 4,138za Reverse Circulation (RC) na mita 5,201 za Diamond Drilling(DD) zilichorongwa kwenye maeneo hayo. Aidha, STAMICOitaendelea kuboresha taarifa zinazohusu WachimbajiWadogo pamoja na upatikanaji wa masoko ya madini nchinikupitia Tovuti ya Wachimbaji Wadogo ya STAMICO (SmallScale Mining Portal – www. ssm-stamico.co.tz) na Mfumo wautoaji wa taarifa hizo kupitia simu za kiganjani.

207. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18, Shirika litaendelea kufanya tafiti katika maeneoyake ya Busanda (Dhahabu), Sengeri Southern Extension(Rare Earth Elements) na Mingoyo Lindi (Graphite) pamojana kutoa Huduma za kibiashara za ushauri wa kitaalam(Consultancy) katika Sekta ya Madini.

208. Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Shirika pia limepanga kuendelea kuchimbaMakaa ya Mawe katika Leseni yake ya Kilima cha Kabulo –Kiwira ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 10 kimetengwa naSerikali kwa ajili ya kuendeleza Mradi huo. Aidha, Shirikalinaendelea kukamilisha ukadiriaji wa mashapo ya dhahabupamoja na usanifu wa Mgodi katika Mradi wa Buhembapamoja na kutafuta Mbia mwenye uwezo ili kuendelezaMradi huo. Pia, Shirika litaendelea kusimamia Miradi yakeya STAMIGOLD pamoja na Miradi ya Ubia ikiwemoTanzaniteOne ili kuongeza ufanisi na Mapato ya Serikali.

Page 146: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

146

Asasi ya Uwazi Katika Rasilimali za Madini na Gesi Asilia(Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative – TEITI)

209. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai 2016 hadi Machi, 2017 TEITI imeandaa Mpango-Kazi (Road Map) wa kuanzisha Rejista ya Majina na taarifaza Watu Wanaomiliki Hisa katika Leseni na Mikataba yaMadini, Mafuta na Gesi Asilia kama ilivyoahidiwa na Mhe.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) alipomwakilishaMheshimiwa Rais katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi kuhusuKudhibiti Rushwa (London, Anti-corruption Summit, 2016)uliofanyika Nchini Uingereza, tarehe 12 Mei, 2016. Aidha, TEITIimefanya mapitio ya Sheria (Legal Review Study) kwa ajili yamaandalizi ya uanzishaji wa Rejista hiyo. Lengo ni kubainikama kuna vipengele katika Sheria zilizopo vinavyokatazauwekaji wazi wa majina ya watu wanaomiliki hisa katikaLeseni na Mikataba ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia, hasaSheria ya Kampuni ya Mwaka 2002 (Companies Act, 2002)kwa ajili ya kuvifanyia marekebisho.

210. Mheshimiwa Spika, maandalizi kwa ajili yaukusanyaji wa Takwimu za Kodi zilizolipwa na Kampuni zaMadini, Mafuta na Gesi Asilia katika Mwaka wa Fedha wa2014/15 na 2015/16 yamekamilika. Maandalizi hayoyamezingatia maelekezo ya Waheshimiwa Wabunge waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini yaliyotolewaMwezi Oktoba, 2016 kwa kukusanya na kuweka wazitakwimu za misamaha ya kodi, matumizi ya mafuta namishahara ya Wafanyakazi wa Kigeni. Ripoti zitatolewa kwaumma kuanzia Mwezi Juni, 2017.

211. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza matakwaya Sheria ya TEITI ya Mwaka 2015 Kifungu 16 (1)(a)kinachomtaka Waziri kuweka wazi Mikataba ya Madini,Mafuta na Gesi Asilia, Mwezi Desemba, 2016 Wizara ilizitaarifuKampuni zenye Mikataba ya Madini na Gesi Asilia (MDAs naPSAs) kwamba inakusudia kuweka wazi Mikataba hiyo.Kampuni hizo zinatakiwa kuifahamisha TEITI kwa mujibu waKifungu 27 (2) kama kuna sehemu ndani ya Mikataba hiyoambayo kibiashara ni muhimu kutowekwa wazi. Kati ya

Page 147: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

147

Kampuni 24, Kampuni nne (4) za madini na 20 za Mafuta naGesi Asilia, Kampuni mbili (2) zimewasilisha maombi TEITIambayo hivi sasa yanafanyiwa kazi. Aidha, maandaliziyanafanyika ili kuweka wazi Mikataba ya Kampuni hizokwenye Tovuti za Wizara.

212. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa2017/18 TEITI itakamilisha na kutoa kwa Umma Ripoti ya Malipoya Kodi yanayofanywa na Kampuni za Madini, Mafuta naGesi Asilia kwa Serikali kwa kipindi cha Mwaka wa Fedha wa2016/17. Aidha, TEITI itaendelea kuelimisha Umma juu yamatumizi ya takwimu zinazotolewa katika Ripoti zake iliwaweze kutumia takwimu hizo katika kuhoji uwajibikaji waSerikali.

Chuo cha Madini Dodoma (Mineral Resources Institute –MRI)

213. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanziaMwezi Julai, 2016 hadi Machi, 2017, Chuo kimedahili Jumlaya wanafunzi 527 katika fani za Jiolojia na Utafutaji Madini;Uhandisi Migodi; Uhandisi Uchenjuaji Madini; Sayansi za Mafutana Gesi Asilia; na Uhandisi na Usimamizi wa MazingiraMigodini. Pia, Chuo kimeandaa Mtaala mpya wa UpimajiArdhi na Migodi (Curriculum for Land and Mine Surveying)ambao umewasilishwa NACTE kwa ajili ya usajili. Aidha, Chuokimefanya upanuzi na ukarabati wa Ofisi na madarasa, ujenziwa ukumbi wa mihadhara pamoja na viwanja vya michezokupitia Mradi wa SMMRP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.Pia, Wizara imetoa Jumla ya Shilingi milioni 148.03 kwa ajiliya ufadhili kwa vijana 71 wanaosoma fani mbalimbali zamadini, Mafuta na Gesi Asilia katika Chuo hiki.

214. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18 Chuo kitaendelea kupanua wigo wake wa kutoamafunzo kwa kuanzisha programu mpya ya Upimaji Ardhina Migodi. Pia, Chuo kimekusudia kuandaa Mtaala waWachimbaji Wadogo kwa ajili ya Watendaji wa kada ya katiwatakaoweza kujiajiri kama Wachimbaji Wadogo wenyeujuzi au kufanya kazi moja kwa moja na Wachimbaji Wadogo

Page 148: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

148

wengine kote nchini. Aidha, Chuo kitaendelea kuwajengeauwezo Watumishi wake na pia kuendelea kuimarishamiundombinu yake muhimu.

C. AJIRA NA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU

215. Mheshimiwa Spika, ili Watumishi wa Wizarawaweze kufanya kazi kwa weledi na ufanisi zaidi ikilengakuinua mchango wa Sekta za Nishati na Madini kwenye Patola Taifa, katika Mwaka wa Fedha wa 2016/17, Wizara iliandaaMpango wake wa mafunzo kwa kipindi husika. KupitiaMpango huo, Wizara ilipanga kupeleka Watumishi 87 katikamafunzo ya muda mrefu na Watumishi 166 katika mafunzoya muda mfupi. Mpango huo unaendelea kutekelezwaambapo hadi kufikia mwishoni mwa Mwezi Machi, 2017,Watumishi 67 wamehudhuria mafunzo ya muda mrefu ndanina nje ya nchi. Kati ya hao 2 wanasomea Shahada yaUzamivu, 43 Shahada ya Uzamili, 16 shahada ya kwanza na6 Stashahada. Aidha, katika kipindi hicho Wizara ilipelekaWatumishi28 katika mafunzo ya muda mfupi ndani na nje yanchi. Mafunzo hayo yalitolewa katika fani mbalimbalizikiwemo: Uthaminishaji, Ukataji na Utafiti wa Vito; UhandisiMigodi; Jiolojia; Fedha, Uhasibu na Usimamizi katika masualaya Mafuta na Gesi Asilia; Usimamizi wa Mazingira; Uchumi naSera za Umma; Sheria hususan katika Mafuta na Gesi Asilia;Petroli; na masuala ya Jiosayansi kwa ujumla. Pamoja namafunzo haya kufanyika nchini, Watumishi walihudhuriamafunzo nje ya nchi zikiwemo: Australia, Brazil, China, India,Norway, Sri Lanka, Thailand na Uingereza. Mafunzo hayo yamuda mrefu na muda mfupi kwa ujumla yaligharimu Jumlaya Shilingi bilioni 1.41 zikiwa ni fedha za Ndani na Njezilizotengwa na Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/17.

216. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafunzo hayo,Wizara pia iliendelea kushirikiana kwa karibu na Washirikawa Maendeleo il i kupata ufadhili wa masomo kwaWatanzania wanaokidhi vigezo katika nchi mbalimbalikwenye mafunzo ya Shahada za Uzamili na Uzamivu. KatikaMwaka wa Fedha wa 2016/17 Watanzania 16 walipataufadhili wa kusomeshwa nchini China Shahada ya Uzamili

Page 149: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

149

na wawili (2) Shahada ya Uzamivu kutoka Serikali ya Jamhuriya Watu wa China katika masuala ya Mafuta na Gesi Asilia.

217. Mheshimiwa Spika, i l i kuendelea kuwapaWatumishi ujuzi mbalimbali kwa ajili ya kuinua utendaji wao,Wizara kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 imepangakuwapeleka Jumla ya Watumishi 227 katika mafunzo ya fanimbalimbali zikiwemo: Usimamizi wa Rasilimali za Mafuta naGesi Asilia; Sheria; Uchumi; Jiolojia; Jemolojia; pamoja naFedha na Uhasibu katika masuala ya Mafuta na Gesi Asilia.Kati ya Watumishi hao, 77 watahudhuria mafunzo ya mudamrefu na Watumishi 150 mafunzo ya muda mfupi. Katikakipindi hiki Wizara imetenga Jumla ya Shilingi milioni 679.73kwa ajili ya kuwezesha mafunzo hayo.

218. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha ustawi naafya za Watumishi wanaoishi na virusi vya UKIMWIwaliojitokeza, Wizara imeendelea kuwawezesha Watumishi10 kwa kuwapa huduma ya lishe na dawa kwa kuzingatiaWaraka wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa Mwaka 2006. KatikaMwaka wa Fedha wa 2017/18, Wizara itaendelea kutoa elimumahali pa kazi i l i kuzuia maambukizi mapya nakuwahudumia waathirika wa UKIMWI kadriwatakavyojitokeza na Jumla ya Shilingi milioni 12zimetengwa kwa ajili hiyo. Sambamba na jitihada hizo,Wizara pia itaendelea kuhamasisha Watumishi kupima afyazao mara kwa mara ili kujua kama wana Magonjwa SuguYasiyoambukiza (MSY) kama vile magonjwa ya shinikizo ladamu, kisukari na saratani ili waweze kuchukua hatua stahikimapema. Aidha, Wizara itaendelea kuwahamasishaWatumishi juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuimarishaafya zao kwa ajili ya kuendelea kulitumikia Taifa letu ipasavyona kwa ufanisi zaidi.

219. Mheshimiwa Spika, katika kuwapa motisha nakuongeza tija kwenye utendaji kazi kwa Watumishi wake,Wizara imeendelea kubuni njia mbalimbali ikiwemo yakuwapandisha vyeo Watumishi wake. Katika kutekelezadhana hii, kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 Wizarainatarajia kuwapandisha vyeo Jumla ya Watumishi 360

Page 150: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

150

ambao wamepata sifa za kitaaluma na wenye utendajimzuri wa kazi kulingana na Sera ya Menejimenti na Ajira katikaUtumishi wa Umma ya Mwaka 1999.

D. WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUHAMIA DODOMA

220. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madiniinaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tanoiliyoamua kwa dhati kutekeleza maamuzi ya Mwasisi wa Taifaletu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya Mwaka1973 ya kuufanya Mji wa Dodoma kuwa Makao Makuu yaNchi yetu ambapo pia maamuzi hayo yamesisitizwa kwenyeIlani ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 katika Ibara ya 151 kuhusukuhamishia Makao Makuu Dodoma. Katika kutekelezaMaamuzi hayo, Wizara imeanza kutekeleza Mpango waKitaifa wa zoezi hilo ambalo linatekelezwa kwa awamu.Katika Awamu ya kwanza, tarehe 10 Februari, 2017 Wizarailihamisha Watumishi 47. Awamu hii ilihusisha Watumishi wangazi mbalimbali wakiwemo Waziri, Naibu Waziri, KatibuMkuu, Naibu Makatibu Wakuu, Makamishna, Wakurugenzi naMaafisa. Kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18, Wizaraitaendelea kutekeleza Maamuzi hayo ambapo katika kipindihicho Watumishi 107 wanatarajiwa kuhamishwa kuanziaMwezi Agosti, 2017.

E. UIMARISHAJI WA MAWASILIANO KATI YA WIZARA NA JAMII

221. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea naMpango wake wa utoaji taarifa mbalimbali kuhusuutekelezaji wa shughuli zake kupitia Kitengo chake chaMawasiliano Serikalini. Katika Mpango huo, Wizara imeandaana kuchapisha Matoleo ya Majarida 40 kuhusu habari za kilaWiki za Wizara na Taasisi zake. Majarida yamesambazwa kwaWananchi, Balozi za Tanzania nje ya nchi, mitandao ya kijamii,makundi ya WhatsApp, Tovuti ya Wizara, vyombo vya habarina Maafisa Habari wa Taasisi mbalimbali. Kupitia Mpangohuu zaidi ya wadau 7,500 wamepata taarifa hizo. Katikakipindi hiki pia, Wizara iliwahabarisha Wananchi na Wadaumbalimbali kuhusu masuala yanayoendelea katika Sekta za

Page 151: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

151

Nishati na Madini kupitia vyombo mbalimbali vya habarivikiwemo radio, magazeti, tovuti na televisheni.

222. Mheshimiwa Spika, Wizara pia imeendeleakutoa elimu kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali kwakutumia gari lake la matangazo ambalo kimsingi limekuwachachu ya kuzitangaza shughuli muhimu zinazotekelezwa naWizara katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu yakiwemoya uchimbaji mdogo wa madini. Katika Mwaka wa Fedhawa 2017/18, Wizara itaendeleza juhudi hizo kwa kutoa elimukwa Wananchi wengi zaidi.

F. USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

223. Mheshimiwa Spika, napenda kutambuamichango ya Washirika wa Maendeleo ambao wamekuwamstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali za kuletamaendeleo kwa kupitia misaada yao mbalimbali kwenyeUtekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Sekta za Nishatina Madini. Kwa niaba ya Serikali, napenda kutoa shukrani zadhati kwa: Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Benki yaMaendeleo ya Afrika Kusini (DBSA), Benki ya Dunia (WB), Benkiya Exim ya China, Benki ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan(JBIC), Benki ya Maendeleo ya Kiarabu (BADEA), Benki yaUnicredit Austria, Climate Investment Fund (CIF), EconomicDevelopment Cooperation Fund (EDCF), OPEC Fund forInternational Development (OFID), Mfuko wa UendelezajiJotoardhi (GRMF) pamoja na Taasisi na Mashirika ya: AFD(France), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP),ICEIDA (Iceland), CIDA (Canada), DfID (UK), IDA (Benki yaDunia), JICA (Japan), KfW (Germany), GIZ (Germany), NORAD(Norway), NDF (Nchi za Nordic), Sida (Sweden), Umoja waUlaya (EU), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),The Nertherlands (DRIVE) na USAID (United States ofAmerica); na nchi za Brazil, Denmark, Finland, Germany,Iceland, Norway na Korea ya Kusini. Katika kipindi cha Mwakawa Fedha wa 2017/18, Serikali kupitia Wizara ya Nishati naMadini itaendeleza ushirikiano na Washirika hawa na wenginewa Maendeleo ili kuendeleza miradi mbalimbali.

Page 152: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

152

G. SHUKRANI

224. Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwakumshukuru kwa dhati Mhe. Dkt. Medard Matogolo ChananjaKalemani, Mbunge wa Chato, Naibu Waziri wa Nishati naMadini kwa ushirikiano anaonipatia katika kusimamia Sektaza Nishati na Madini. Nakiri wazi kuwa michango yakeimekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wamajukumu yangu ya kila siku ya Wizara na kitaifa kwa ujumla.

225. Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa mafanikioyote ya Wizara yanategemea ushirikiano wa WatendajiWakuu na Wataalam mbalimbali. Hivyo, naomba nitumienafasi hii kuwashukuru Naibu Makatibu Wakuu Prof. JamesEpiphan Mdoe pamoja na Dkt. Mhandisi Juliana LeonardPallangyo, Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara naVitengo pamoja na Watumishi wote wa Wizara. Watendajihao wa Wizara wamekuwa makini katika kunipa ushauri naufafanuzi katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji, haliambayo imenisaidia katika kuiongoza Wizara kwa ufanisi nahatimaye kuleta mafanikio makubwa.

226. Mheshimiwa Spika, nichukue pia fursa ya kipekeekuwashukuru Wakuu wote wa Taasisi, Wenyeviti wa Bodi naWajumbe wa Bodi za Taasisi pamoja na Watumishimbalimbali wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yetu kwaushirikiano wao wanaonipatia katika kutekeleza majukumutuliyopewa. Ni matumaini yangu kuwa ushirikiano huu utazidikuendelezwa siku zijazo kwa lengo la kuinua mchango waSekta za Nishati na Madini katika Pato la Taifa.

227. Mheshimiwa Spika, kipekee napendakumshukuru tena Mheshimiwa Rais kwa jinsi anavyojitoakusimamia rasilimali za nchi hii kwa maslahi mapana yawananchi na Taifa letu. Ninawashukuru wananchiwanaojitokeza kumuunga mkono Mheshiwa Rais nakumuombea kila anapochukua hatua il i kuwaleteamaendeleo Watanzania. Hakika kiongozi wetu mkuuanastahili maombi.

Page 153: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

153

H. HITIMISHO

228. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Wizara ya Nishati naMadini kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 pamoja nakutumika katika kutekeleza shughuli mbalimbali, imelengakatika kutekeleza Miradi Mikubwa ya Nishati ili kuchocheaSekta nyingine za kiuchumi na hivyo kukuza uchumi wa Taifaletu na maendeleo ya Watanzania kwa ujumla. Wizara piakatika kipindi hiki itaendelea kwa kasi na utekelezaji wamaelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya upatikanaji waNishati ya uhakika ili kuwezesha kufikiwa kwa lengo laTanzania kuwa Nchi ya Viwanda. Katika kutekeleza azmahiyo, sehemu kubwa ya Fedha za Miradi ya Maendeleoambazo ni Shilingi bilioni 756.76, sawa na asilimia 80.6 yaFedha zote za Maendeleo zimeelekezwa katika kutekelezaMiradi ya kimkakati ya Nishati.

229. Mheshimiwa Spika, naomba Bunge lako Tukufulikubali kupitisha Makadirio ya Jumla ya Shilingi998,337,759,500 kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18.Mchanganuo wa Bajeti hiyo ni kama ifuatavyo:

(i) Shilingi 938,632,006,000, sawa na asilimia 94ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi yaMaendeleo. Kati ya Fedha hizo Shilingi763,304,679,000 ,sawanaasilimia81 ya fedha zote zaMaendeleo ni Fedha za Ndani na Shilingi 175,327,327,000,sawa na asilimia 19 ni Fedha za Nje.

(ii) Shilingi 59,705,753,500, sawa na asilimia 6 yaBajeti yote ya Wizara ni kwaajiliyaMatumiziyaKawaida.Katiyafedha hizo, Shilingi 28,833,681,500, sawa na asilimia 48.3 yafedha zote za Matumizi ya Kawaida ni kwa ajili ya MatumiziMengineyo (Other Charges – O.C.) na Shilingi 30,872,072,000,sawa na asilimia 51.7 zitatumika kulipa Mishahara yaWatumishi (Personnel Emolument – P.E) wa Wizara na Taasisizake.

230. Mheshimiwa Spika, naomba tena nitoe shukranizangu za dhati kwako na kwa Waheshimiwa Wabunge wote

Page 154: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

154

kwa kunisikiliza. Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti yaWizara kwa anuani ya www. mem.go.tz. Vilevile, Hotuba hiiina vielelezo mbalimbali kwa ajili ya ufafanuzi wa masualamuhimu yanayohusu Sekta za Nishati na Madini.

231. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

NAIBU SPIKA: Tutaendelea na Mwenyekiti wa Kamatiya Nishati na Madini. (Makofi)

MHE. DOTO M. BITEKO - MWENYEKITI WA KAMATI YAKUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: MheshimiwaNaibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99(9) na Kanuni ya117 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari mwaka2016, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati ya Kudumu yaBunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa majukumuya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu makadirio,mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilifanya vikaokadhaa kwa lengo la kupokea na kuchambua taarifa yautekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha2016/2017 na kuchambua makadirio na mapato na matumizikwa mwaka 2017/2018 sambamba na utekelezaji wa shughuliza Wizara hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati pia ilifanya mambomambo yafuatayo; ukaguzi wa baadhi ya miradi yamaendeleo iliyoidhinishwa fedha kwa mwaka wa fedha2016/2017; kupokea taarifa ya utekelezaji wa Bajeti pamojana maoni na ushauri wa Kamati kwa mwaka wa fedha2016/2017; uchambuzi wa makadirio ya mapato na matumiziya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa hii inaoneshamatokeo ya shughuli hizi pamoja na maoni na ushauri waKamati. Katika Mkoa wa Tanga Miradi ya Umeme Vijijini (REA)katika Awamu ya Kwanza na Awamu ya Pili imetekelezwakatika Wilaya nane za Mkoa huo. Miradi hiyo yenye ukubwa

Page 155: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

155

wa Kv 33 imetekelezwa na Wakandarasi wawili ambao niSDG International Service na Sengerema Engineering GroupLtd.

Mheshimiwa Naibu Spika, jumla ya vijiji 218 vya Mkoawa Tanga vimenufaika na ukamilishaji wa miradi ya REAkatika awamu ya pili. Ziara ya ukaguzi na utekelezaji wamiradi hiyo ilifanyika katika Kijiji cha Tongoni katika Wilayaya Tanga Vijijini ambacho ni kijiji cha mfano miongoni mwavijiji vilivyopatiwa umeme wa REA Awamu ya Pili.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mradi huu, Kamatiyako ilibaini kuwepo na malengo ya mradi awamu ya pilihayakukamilika kwa asilimia 100. Miradi ililenga kuvipatiaumeme vijiji au kaya 138, hata hivyo ni kaya 90 peke yakendizo zilizopatiwa umeme sawa na asilima 65.0.

Kwa upande mwingine Kamati ilibaini pia kuwa elimukuhusu mradi wa umeme wa densification kwa wananchihaijaeleweka vizuri na pia miradi husika haijaanza rasmikatika vijiji vyote ambavyo vihavijaunganishwa na umemekatika awamu zilizotangulia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Geita unanufaikana mradi wa umeme vijijini katika awamu ya pili ambapozaidi ya vijiji 101 vilikuwa kwenye tathmini ya awali yakuunganishiwa umeme. Mkandarasi anayeshughulika nauunganishaji wa umeme kwenye mkoa huu ni NakuroiInvestment Company Limited. Kamati ilifanya ukaguzi wautekelezaji wa miradi hiyo katika vij i j i vya Nyakato,Buzilayombo kama vijiji vya mfano miongoni mwa vijiji vingivinavyopatiwa umeme kwenye awamu hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mahojiano nawananchi wa vijiji hivyo, Kamati ilibaini kuwa malengo yamradi katika awamu ya pili ilikuwa ni kuzipatia kaya 165umeme katika vijiji hivyo, lakini mpaka Kamati inakwendakwenye vijiji hivyo kaya 127 ndizo zilikuwa zimeshapatiwaumeme. Hata hivyo, kati hizo kaya 130 ambazo ni sawa naasilimia 78.0 zilikuwa zimeshapata umeme. Katika kijiji cha

Page 156: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

156

Buzilayambo kaya 32 sawa na asil imia 25 zil ikuwazimeshapatiwa umeme na katika kijiji cha Nyakato.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilibaini kwambachangamoto kubwa katika miradi ya REA inayotekelezwakatika Mkoa wa Geita ni uunganishwaji mdogo wa wananchikatika huduma ya umeme na hivyo kutokufikiwa kwamalengo ya utekelezaji wa mradi huo katika maeneo hayo.Aidha, Kamati ilibaini kuwa mashine Humba iliyofungwayenye uwezo wa Kv 200 ambayo ni kubwa ikilinganishwa namahitaji ya eneo hilo ilifungwa kwenye kijiji hicho ilhali mahitajiya umeme kwenye kijiji hicho siyo makubwa kwa kiasi hicho.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa umeme waKinyerezi unatekelezwa na Shirika la Umeme la Tanzania(TANESCO) kwa lengo la kuzalisha Megawati 185 zaidi yaumeme katika mradi huu wa umeme wa gesi wa KinyereziOne ambao tayari unazalisha Megawati 150; unakadiriwakukamilika na dola za Kimarekani 188 zimeshalipwa na Serikalikwa asilimia 100 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Junimwaka 2018. Kwa upande wa mwaka wa fedha 2016/2017shilingi bilioni 110 zilitengwa na hadi wakati Kamati inakaguamradi huu, kiasi cha shilingi bilioni 88 sawa na asilimia 80kilikuwa kimeshatolewa katika utekelezaji wa mradi huu.Kamati inaipongeza sana Serikali kwa jitihada zake zakupeleka fedha kwenye mradi huu muhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mafanikio hayo,Kamati ilibaini changamoto kadhaa zilizokuwa zinakabiliutekelezaji huu ikiwa ni pamoja na tozo mbalimbalizinazotozwa na TANROADS kutoka TANROADS na VATzinazotokana na ukubwa na uzito wa mizigo usio wakawaida wa mitambo inayotumika katika kutekeleza mradihuu. Tozo hizi zinachangia kuongezeka kwa gharama zamiradi hivyo kuchelewesha utekelezaji wa mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na changamotozinazoukabili mradi huu, bado dhamira ya dhati ya Serikaliya kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme wauhakika katika nchi hii kinazidi kudhihirika, ambapo katika

Page 157: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

157

mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 90 kutokakatika vyanzo vya ndani zimetengwa kwa ajili ya kutekelezana kukamilisha mradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati kupitia Bunge lakoTukufu linaitaka Serikali kupeleka fedha zote za miradi yaumeme zilizobaki yaani bakaa kwa mwaka wa fedha2016/2017 ili kukamilisha miradi hiyo muhimu kwa ajili yakuwasaidia Watanzania kupata umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa Kinyerezi IImegawati 240, unatekelezwa vilevile na Shirika la UmemeTanzania (TANESCO) kwa lengo la kuzalisha megawati 240kwa mfumo wa kisasa zaidi unaoitwa Combined Cycle PowerPlant. Gharama za mradi huo ni dola za Kimarekani 344ambapo ni asilimia 85 ya gharama hizo italipwa na JapanExport Trading Financing na asilimia 15 pekee iliyobakiimelipwa na Serikali ya Tanzania mwezi Februari, 2016. Ujenziwa mradi huu umeshaanza na unatekelezwa kwa kasiambapo tayari misingi ya majengo imewekwa na baadhiya mitambo kufungwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, pamoja naujenzi huo kuanza kwa kasi, bado kuna changamotombalimbali za tozo kama vile forodha kama vile CustomLevies, Custom Processing Fees pamoja na Custom Dutiesambazo zinatakiwa kulipwa na TANESCO. Tozo hizi zimekuwazikichangia ongezeko la gharama katika utekelezaji wa mradihuu na kufanya mradi huu kuto kutotelezwa kwa kasiinayokusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati ilitaarifiwa kwambamaombi ya TANESCO kwenda kwa TANROADS ambayoyalihusu kupatiwa msamaha wa kodi na tozo hizozinazotokana na ukubwa wa uzito wa mitambo usio kuwawa kawaida (out of gouge heavy roads charges) yalikataliwa.Aidha, ucheleweshaji wa malipo hayo unaweza kusababishamitambo hiyo kuchelewa kufika eneo husika la mradi nahivyo kuchelewesha utekelezaji wa mradi husika.

Page 158: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

158

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati vilevile ilitembeleamradi wa Bulyanhulu Geita Kv 220. Mradi huu unahusisha ujenziwa kituo kidogo cha kupoozea umeme cha Geita chamsongo wa Kilovoti 220 pamoja na usambazaji wa umemekatika vijiji 10 vilivyopo ndani ya eneo la utekelezaji ambapogharama yote kwa ujumla ni dola za Kimarekani milioni 23ambazo ni mkopo kutoka katika Benki ya BADEA na tayarigharama na fidia nyingine zote zimeshalipwa kwa wananchiwote waliopisha eneo la mradi huo kama inavyostahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kukamilika kwaulipaji wa fidia wananchi waliopisha eneo la mradi badomradi huu umeshindwa kuanza kutokana na kuchelewakupatikana kwa Mhandisi Mshauri wa mradi. Mradi huuutakapoanza utasaidia kuongeza hali ya upatikanaji waumeme wa uhakika katika Mkoa wa Geita. Aidha, mradihuu utaunganisha wateja zaidi ya 1,500 ikiwemo Mgodi waGGM ambao unahitaji MW zaidi ya 11 kwa ajili ya shughulizake za mgodi na kusaidia migodi mingine ya wachimbajiwadogo wadogo iendeshwe vizuri kutokana na kupatikanakwa nishati ya umeme. Kamati inaishauri Serikali kutatuachangamoto hizo haraka iwezekavyo ili mradi huo uwewenye tija kwa Mkoa wa Geita na maeneo jirani na uwezekuwanufaisha wananchi pamoja na wawekezaji wanaohitajiumeme kwa ajili ya shughuli zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mgodi wa Dhahabu waBuckleef wenye leseni za uchimbaji mkubwa (Special MiningLicence) katika Mkoa wa Geita unamilikiwa na mkatabawa ubia ulioingiwa mwaka 2011 kati ya Serikali ya Tanzaniakupitia Shirika lake la STAMICO na Kampuni ya TANZAM 2000.Kupitia mkataba huo, STAMICO inamiliki asilimia 45 naTANZAM inamiliki asilimia 55 ya hisa.

Kwa mujibu wa mkataba huo (Joint VentureAgreement) TANZAM ina jukumu la kutafuta fedha zakuendesha mgodi huo wakati huo jukumu la STAMICOlilikuwa kuhamisha leseni zake 12 kwa kampuni hiyo. Hadiwakati wa ziara katika mgodi huu, Kamati ilibaini kwambalicha ya leseni zote za uchimbaji kukabidhiwa kwa mbia huyo,

Page 159: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

159

hakuna kazi yoyote iliyokwisha kufanyika katika kuendelezamgodi huo toka kampuni hiyo iingie mkataba na STAMICO.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kampuni kuripotikuwa imekamilisha ufungaji wa mtambo mpya wakuchenjulia dhahabu, Kamati inasikitishwa na kitendo chambia kutokuzingatia ushauri wa STAMICO kuhusu aina yamtambo unaofaa kutumika katika eneo hilo, hatua ambayoimesababisha Serikali kupata hasara. Kamati inaishauri Serikalikuwa makini inapoingia ubia katika sekta ya madini ilikuepuka wabia wa aina hii ambao hawazingatii ushauri wambia mwenza yaani STAMICO jambo linalosababisha hasarazisizo kuwa za msingi. Kamati haikuona jitihada zozote zambia huyo za kuendeleza mgodi huo kama walivyokubalianakwenye mkabata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Kamati imesikitishwana usimamizi mbovu wa STAMICO katika mgodi huo licha yakuwa na mashapo (reverses) yenye uhakika wa kuzalishadhahabu yameishafanyiwa utafiti na kubainika. Hatua stahikizinashauriwa kuchukuliwa ili kurekebisha kasoro hizo ambazozimebainika kwa mbia huyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu wachimbaji wa kati,Kamati ilifanya ziara ya ukaguzi wa migodi ya Busolwa Miningna Nyarugusu Processing Plant, iliyopo Mkoa wa Geita. Lengola ziara il ikuwa ni kujifunza jinsi wachimbaji wa katiwanavyoendesha shughuli zao na kubainisha mchangowalionao katika pato la Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Busolwa Mining ni mgodiunaomilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100 na Kamatiilijionea unavyoendesha shughuli zake kwa kutekeleza sheriana kanuni mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulipa kodi zotestahiki za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, tangu mgodi huo uanzemwaka 2014, umeshalipa kodi ya thamani shilingi bilioni 120,mrabaha shilingi bilioni 562, kodi ya zuio kwa mwaka 2017shilingi milioni 20 na service levy shilingi milioni 48.

Page 160: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

160

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto kubwainayoukabili mgodi huu ni ufinyu wa eneo la kutupia mabakiyanayotokana na shughuli za mgodi (TSF). Hivyo nimapendekezo ya Kamati kuwa maombi ya mgodi huokupatiwa eneo lingine yashughulikiwe mapema ili kusaidiakuongeza uhai wa mgodi huo ambao umeajiri zaidi yaWatanzania 500.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu madini ya vito yaTanzanite, Kamati yako imeendelea kusikitishwa na jitihadandogo zinazofanywa na Wizara ya Nishati na Madini kuokoamapato yatokanayo na madini ya vito Tanzanite na Almasinchini. Hata hivyo, hakuna mikakati madhubuti ya kuokoarasimali hizi kutokana na usimamizi usioridhisha wa migodihiyo. Pamoja na changamoto nyingi za mikataba baina yaSTAMICO na Tanzanite One ambapo mgodi huo pekee ndiounaozalisha madini haya adimu duniani, Kampuni yaTanzanite One amekuwa akitoa taarifa zisizokuwa sahihi kwambia mwenza yaani STAMICO toka alivyoanza kuzalishaTanzanite hapa nchini. Kwa mfano, kuanzia Juni, 2013 hadiMachi, 2016, STAMICO ameripoti mauzo ya jumla ya dola zaKimarekani milioni 16.7 na Tanzanite One katika kipindi hichohicho aliuza madini yenye thamani ya dola za KimarekaniMilioni 17.9 ambapo kuna tofauti ya dola milioni 1.3hazikuripotiwa na kampuni hiyo na hivyo Serikali kukosa kodiyake. Hivyo, kutokana na tofauti hiyo STAMICO wamepotezajumla ya dola za Kimarekani 182,855.19. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kampuni hiyo yaTanzanite One imekuwa hailipi kodi ya mapato na tozo zagharama mbalimbali kwa STAMICO kama vile gharama yauangalizi na usimamizi (monitoring and evaluation unit cost)ambapo jumla ya milioni 131.7 zinadaiwa na STAMICO. Piakukosekana kwa akaunti ya pamoja kati ya wabia hawa,kunasababisha mambo mengi hasa ya kifedhakutokufahamika kwa mbia mwenzake yaani STAMICO kamainavyotakiwa na mkataba (joint venture). Kwa namnamkataba huo unavyoendeshwa kwa pande hizi mbili,umekuwa hauna manufaa kwa Serikali ya moja kwa moja,kwa kuwa kampuni hiyo imekuwa haitekelezi kwa kiasi

Page 161: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

161

kikubwa matakwa ya mkataba huo pamoja na maagizombalimbali ya Serikali ambayo imekuwa ikipewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 3 Mei, 2017, Kamatiyako ilihudhuria maonesho ya madini ya vito jijini Arusha nakujionea jinsi maonesho haya yanavyoweza kuisaidia sektahii ya madini ya vito hapa nchini. Pamoja na mafanikio yakuanzisha mnada na maonesho hayo ya vito hapa nchini,bado changamoto ni nyingi zinazokabili sekta hii ya madiniya vito hasa madini ya Tanzanite. Changamoto kubwa niutoroshaji wa madini haya nje ya nchi ambayo ndiyoinayoendelea kutuumiza kama Taifa kwa kuwa Tanzaniandiyo nchi pekee inayozalisha madini haya ya Tanzanite lakiniTanzania hiyo hiyo siyo muuzaji wa kwanza wa madini yaTanzanite duniani. Hata hivyo, uanzishwaji wa maoneshohaya kwa kiasi kikubwa bado haujaweza kusaidia kutatuachangamoto zinazokabili sekta hii ya madini ya vito hapanchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hasara kubwatunayopata kama Taifa kwenye madini haya pekee nchini,Kamati inashauri Bunge lako Tukufu kwa mara nyingine tenakama tulivyokwishashauri siku za nyuma suala la mkatababaina ya TML pamoja na STAMICO liweze kuangaliwa upyana kuangaliwa kwa namna bora zaidi litakayoweza kuletatija. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu madini ya dhahabu,sekta ya madini nchini inaendelea kukabiliwa nachangamoto nyingi hasa katika suala la ukusanyaji wa kodiza Serikali. Sekta hii imechangia kwa asilimia nne katika Patola Taifa mchango ambao bado ni kidogo sanaukilinganishwa na ongezeko la uzalishaji wa madini hayakatika sekta hiyo. Kwa mfano, katika mwaka 2016 nchi yetuilizalisha jumla ya wakia milioni 1.42 za madini ya dhahabuikilinganishwa na wakia milioni 1.36 zilizozalishwa mwaka2015. Ongezeko hilo la uzalishaji ambalo ni sawa na asilimia4.4, lilitakiwa kwenda sambamba na ongezeko la ukusanyajiwa mapato ya kodi hapa nchini.

Page 162: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

162

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inasikitishwa naulipaji hafifu wa kodi za mapato unaofanywa na wawekezajikatika migodi mikubwa hapa nchini. Kwa mfano, mwaka2016 ni migodi miwili peke yake ndiyo iliyolipa kodi ya mapatoyaani North Mara na Geita Gold Mine. Kamati inaitaka Serikalikuchukua hatua madhubuti kufuatilia jambo hili ili migodihii iweze kulipa kodi hizi kama inavyostahiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na malalamikomengi kutoka kwa wawekezaji nchini hasa kwenye sekta yamadini wakidai Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT returns)ambayo kiutaratibu inapaswa kulipwa baada ya migodikukamilisha hesabu zao na kuwasilisha TRA, Serikali imekuwahaijalipa hizo fedha kwa migodi hiyo kwa madai ya kuwakuna changamoto kadhaa ambazo Serikali ilikuwa inazipitiaili kuhakiki madeni hayo. Kamati inaishauri Serikali kuhakikiharaka madeni haya na kuwalipa wawekezaji hawa ilikutokuathiri uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inamiliki mgodimmoja tu kwa asilimia 100 ambao ni Mgodi wa Stamigoldkupitia Shirika la STAMICO. Mgodi huu licha ya kuajiriWatanzania zaidi ya 700, bado kumekuwa na jitihada ndogoza Serikali katika kuusaidia mgodi huu katika masuala yamsingi ya kuuendeleza kama ifuatavyo:-

(i) Kutokuusaidia mgodi huu kupata fedha za kufanyautafiti katika leseni zinazozunguka eneo hili ili kuongeza uhaiwa mgodi;

(ii) Mgodi haujasaidiwa kupata msamaha wa kodiya mafuta na vipuli kama ilivyo kwa migodi minginemikubwa;

(iii) Ukosefu wa Mining Development Agreement kwamuda mrefu unakwamisha mgodi huu kujiendesha kibiasharakama ilivyokuwa kwa migodi mingine; na

(iv) Mgodi huu unakabiliwa na deni kubwa kutokakwa wazabuni mbalimbali wanaotoa huduma katika mgodi

Page 163: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

163

huo. Kamati inaitaka na kuishauri Serikali kuingilia kati denihili ili kuepusha shughuli za mgodi huo kusimama nakusababisha hasara kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati hairidhishwi najitihada zilizofanywa na Wizara ya Nishati na Madini katikakuusaidia Mgodi huu wa Stami Gold. Changamoto hizizikitatuliwa kikamilifu, zitaongeza uzalishaji wa mgodi huuna kuongeza uhai wa mgodi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na malalamikoya muda mrefu kwa sasa kutoka kwa wananchiwanaozunguka Mgodi wa North Mara katika maeneo yaNyamichele katika vijiji vya Nyakunguru, Murwambe,Matongo na Nyamongo. Pamoja na tathimini ya ardhikukamilika toka Aprili, 2013 na Kamati kutoka Wizara ya Nishatina Madini kukamilisha kazi yake ya tathimini na utatuzi wachangamoto hizi hasa za mauaji mpaka sasa wananchi badohawajalipwa fidia zao.

Kamati inashangazwa na hatua ya malipo yawananchi hao kucheleweshwa kwa takribani miaka minnesasa licha ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madinikuunda na kutuma Kamati za Uhakiki nne kati ya mwaka2014 na 2017. Kamati inaishauri Serikali kuingilia kati suala hiliili wananchi hao ambao wameteseka kwa muda mrefuwaweze kupata stahiki zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati inampongeza sanaMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli na kuunga mkono jitihada zake katikakuendelea kufuatilia kwa karibu sekta ya madini nchini ikiwani pamoja na kuunda Kamati Maalum ya Wataalamuiliyochunguza mchanga uliyoko katika makontena wa madini(makinikia) yaliyopo katika maeneo mbalimbali nchini.Kamati iliweza kubaini uwepo wa viwango vingi vyadhahabu, shaba, silva, salfa na chuma katika makinikia hayoyanayosafirishwa nje. Pia uchunguzi huo umeonesha kuwepokwa madini ya kimkakati yaani strategic metals ambayoyalitajwa kwenye Kamati hiyo. Madini hayo kwa sasa

Page 164: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

164

yanahitajika sana duniani na yana thamani kubwasambamba na madini ya dhahabu ambayo taarifa zakezilikuwa hazitolewi na wawekezaji. Hata hivyo, Kamatiinaendelea kusubiri taarifa nyingine ya Kamati Maalumiliyoundwa na Mheshimiwa Rais itakayoendelea na uchunguziambao utabainisha masuala ya kiuchumi na kisheria ili sasakama Taifa tuweze kunufaika na rasilimali za madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ndogo ya gesi. Tangukugundulika kwa gesi asilia mwaka 1974 katika eneo la SongoSongo mwaka 1982 katika eneo la Mnazi Bay pamoja naeneo la Bahari ya Kina kirefu mwaka 2010/12, uzalishaji wagesi katika miradi iliyogundulika hapa nchini ulianza miakaya 2004 hadi 2006. Kamati inaipongeza sana Serikali kupitiaShirika lake la TPDC kwa kuandaa Mpango Kabambe waMatumizi na Usambazaji wa Gesi Asilia ya nchi mwaka 2016-2045 yaani Natural Gas Utilization Master Plan. Mpango huuutasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa dira ya matumizi bora yagesi asil ia kwa kuzingatia vipaumbele mbalimbalivilivyowekwa ili rasirimali hii iwafikie Watanzania walio wengizaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jitihada hizozinazofanywa na TPDC, bado TPDC inakabiliwa na madenimakubwa yaliyokwamisha shirika hili kuendelea kwa miradiyake. Madeni hayo yanasababishwa na hatua ya Serikalikutenga fedha kidogo kwa miradi hiyo muhimu, hivyokukwamisha shirika hili kutekeleza miradi hiyo. Tangukugundulika kwa gesi hiyo hapa nchini, jumla ya viwanda 41na taasisi mbili zimekwisha kuunganishwa katika mtandaowa matumizi ya gesi asilia.

Kamati inaipongeza sana Serikali kwa kuendelezamiradi hiyo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia.Miradi hiyo mikubwa inatarajia kukamilika ifikapo Juni, 2018ambapo inatarajia kuongeza zaidi ya megawati 425 katikaGridi ya Taifa, hivyo kupunguza tatizo la umeme nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, maoni ya jumla kuhusuutekelezaji wa miradi ya maendeleo; kutokana na ziara ya

Page 165: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

165

ukaguzi wa miradi ya maendeleo, Kamati inatoa maoniyafuatayo:-

(i) Utekelezaji wa bajeti kwa Wizara ya Nishati naMadini haukuwa wa kuridhisha kwa kuwa fedha zilizotolewahadi kufikia Machi, 2017 ni asilimia 36 peke yake. (Makofi)

(ii) Miradi mingi haikutekelezeka kama ilivyopangwakwa kuwa fedha zilizotengwa hazikutolewa na kupelekwakwa wakati kama ilivyotakiwa.

(i) Miradi mingi ya REA katika Awamu ya Pil ihaikukamilika kutokana na kasoro mbalimbali kama vileuainishaji wa maeneo bila kuzingatia vijiji na vitongojiambavyo tayari vina wananchi wengi na ufungaji wamashine humba nyingi kutokidhi mahitaji ya eneo husika.(Makofi)

(ii) Serikali iangalie upya namna bora ya kuwasaidiawachimbaji wa kati kwa kuwapatia maeneo ya kutosha kwakuwa wameonesha nia ya dhati ya kuendeleza sekta yamadini.

(iii)Ruzuku iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madinikwa wachimbaji wadogo haikusimamiwa vizuri na hivyokushindwa kuleta tija kwa waliokusudiwa.

(iv) Pamoja na Mipango mizuri ya TPDC katikakuendeleza sekta ya gesi nchini, ni lazima Serikali iwekezefedha za kutosha katika miradi ya gesi ili kuharakisha azmaya nchi yetu kuingia katika uchumi wa viwanda.

(v) Serikali itenge fedha za kutosha na kuzipeleka kwawakati kwenye miradi ya kimikakati kama vile Mgodi waMakaa ya Mawe wa Kiwira.

(vi) Uwekezaji katika sekta ya madini unahitajikuangaliwa na kusimamiwa upya ili uweze kuleta faida kwaTaifa.

Page 166: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

166

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi wa taarifa nautekelezaji wa bajeti na uzingatiaji wa maoni ya Kamatimwaka 2016/2017; Kamati ilifanya uchambuzi wa bajeti kwakuzingatia mambo makuu matatu ambayo ni makusanyoya maduhuli kwa mwaka wa fedha 2016/2017; hali yaupatikanaji wa fedha kutoka Hazina na uzingatiaji wa maonina ushauri uliotolewa na Kamati ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ilipanga kukusanyamaduhuli yenye jumla ya shilingi bilioni 370.68 ikilinganishwana shilingi bilioni 286.66 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Taarifa ya utekelezaji inaonesha kuwa hadi kufikia tarehe 28Februari, 2017 Wizara ilikuwa imekusanya jumla ya shilingibilioni 239.38 sawa na asilimia 64.5 ya lengo. Makusanyo hayoyaliweza kufikia lengo kutokana usimamizi mzuri uliokuwaumewekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, uchambuzi wa Kamatiumebaini kuwa makadirio ya mchango wa Idara ya Madinikwa mwaka fedha 2017/2018 yameshuka kwa asilimia 4.5ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2016/2017. Aidha,Makadirio ya mchango wa Idara ya Madini, yameongezekakwa asil imia 4.5 kwa mwaka wa fedha 2017/2018ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2016/2017. Ufafanuzi zaidiumeoneshwa kwenye kielelezo kilichoambatishwa pamojana hotuba hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, upatikanaji wa fedhakutoka Hazina; kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Wizara yaNishati na Madini iliidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 1.12kwa ajili ya kutekeleza malengo yake. Hadi kufika tarehe 13Machi Wizara ilikuwa imepokea shilingi bilioni 404, sawa naasilimia 36 kama nilivyoeleza hapo nyuma. Bajeti ya miradiya maendeleo na yenyewe ilikuwa imepangiwa shilingi trilioni1.1 sawa na asilimia 94 ya bajeti yote ya Wizara.

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia Machi, 2017shilingi bilioni 372 zilikuwa zimekwisha kupokelewa sawa naasilimia 35. Kwa upande wa fedha za Matumizi Mengineiliidhinishiwa shilingi bilioni 64.22 hadi kufikia Machi, 2017

Page 167: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

167

Wizara ilikuwa imepokea shilingi bilioni 31.24 sawa na asilimia47 ya fedha zilizoidhinishwa. Ni maoni ya Kamati kwambafedha hizi ziweze kupelekwa kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika uchambuzi wa bajetiwa mwaka 2016/2017, Kamati ilitoa maoni, ushauri namapendekezo kwa Wizara kwa kuzingatia matakwa yaKikanuni. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa baadhiya ushauri uliotolewa na Kamati umezingatiwa vizuri na Wizaraya Nishati na Madini na kufanyiwa kazi. Bado kuna tatizo lausimamizi usioridhisha katika miradi ya Umeme Vijijini katikamaeneo mengi hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika ziara ambazozimefanywa na Kamati kuna maeneo mengi ambayousimamizi haukuwa wa kuridhisha. Mfano, ufungaji wamashine humba zilizokuwa chini ya kiwango katika maeneomengi umesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinuya umeme il iyokwisha kutayarishwa katika maeneombalimbali. Fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya mkakatini kidogo sana ukilinganisha na mahitaji halisi ya fedhazinazohitajika kwa ajili ya kuendeleza miradi hiyo. Kamatiinaiomba Serikali ione sasa umuhimu wa kuipatia miradi hiyohasa Mradi wa Jotoardhi fedha za kutosha ili uwezekutekelezwa kwa sababu una potential kubwa ya kupatiaumeme nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda,naomba hotuba yote iingie kwenye Hansard, sasa nitasomamaoni ya Kamati.

Baada ya Kamati kutekeleza majukumu ya Kikanuniambayo ni ukaguzi wa miradi ya maendeleo, uchambuzi wataarifa ya utekelezaji wa Wizara, kwa mwaka wa fedha2016/2017 na makadirio ya matumizi ya Wizara kwa mwakawa fedha 2017/2018, Kamati ina maoni na ushauri ufuatao:-

(i) Kwa kuwa utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijinikatika awamu mbili zilizotangulia umekuwa na changamotonyingi hasa katika Mikoa ya Tanga na Geita ambako Kamati

Page 168: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

168

ilitembelea na kukagua; Kamati inashauri kuwa changamotozilizobainika ikiwa ni pamoja na baadhi ya maeneoyaliyorukwa zipatiwe ufumbuzi haraka kabla ya kuendeleana Awamu ya Tatu ya REA. (Makofi)

(ii) Kamati inaishauri Serikali ikamilishe taratibu nachangomoto zilizojitokeza katika kuchelewesha VAT returnskwa wawekezaji ili kutokuathiri uwekezaji nchini.

(iii) Pamoja na juhudi mbalimbali zilizofanywa naWizara katika usimamizi wa madini ya Tanzanite, Kamatiinashauri Serikali iangalie upya mikataba hiyo iliyoingiwa naSTAMICO na wabia mwenzake kama ina tija kwa Taifa.

(iv) Ruzuku kwa wachimbaji wadogo iliyotolewa naSerikali kwa awamu zote mbili kwa kiasi kikubwa imeshindwakutimiza malengo na kukosa usimamizi mzuri. Aidha, ni vemaSerikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ikaangalia namnabora ya kusimamia fedha hizi ikiwa ni pamoja na kuwapatiamafunzo wachimbaji wadogo wadogo ili kufuatilia kwakaribu wachimbaji hao.

(v) Sekta ya uchimbaji wa kati imeendelea kukua kwakiasi hapa nchini kwa kiwango cha kuridhisha. Hivyo ni vyemaSerikali ikaangalia upya jinsi ya kuisaidia kupata baadhi yamisamaha ya kodi kama vile mafuta na vipuli ili kuwanufaishawachimbaji hawa wa nchini.

(vi) Leseni zote ambazo zinakiuka Sheria ya Madiniikiwa ni pamoja na kushindwa kuendelezwa kwa muda mrefuzifutwe na kupewa wachimbaji wadogo wadogo na wa katikwa kuwa wameonesha nia ya dhati ya kuendeleza sektahiyo. (Makofi)

(vii) Pamoja na Serikali kuandaa Mpango Kambambewa Matumizi ya Gesi Asilia nchini, ni vyema ukafanyika utafitina upembuzi yakinifu kuhusu miradi yote mikubwa yausambazaji wa gesi katika maeneo mbalimbali ili kuwezakujua kama ina manufaa ya kiuchumi kwa Taifa letu. Hatua

Page 169: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

169

hii itasaidia kuepusha nchi yetu kuingia kwenye mikopoambayo ni mzigo kwa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nichukue fursa hiikumpongeza sana Mheshimiwa Spika pamoja na wewebinafsi, Wenyeviti wote wa Bunge kwa kazi nzuri mnayoifanyaya kuliongoza Bunge letu. Mungu awajalie afya njema,hekima na busara katika kutekeleza wajibu wenu mkubwatuliowakabidhi.

Napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwaniaba ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu kwa MheshimiwaProf. Sospeter Muhongo aliyekuwa Waziri wa Nishati naMadini na Mheshimiwa Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziriwa Nishati na Madini pamoja na watendaji wote wa Wizarahii wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu, Profesa James Mdoena Dkt. Juliana Pallangyo kwa ushirikiano waowanaoendelea kutupatia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee,naomba nimshukuru sana mtoa hoja Mheshimiwa Mwijagealiyesoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini,kwa kweli amesoma vizuri sana na ameeleza vizuri sanamambo yote yaliyokuwa kwenye hotuba ile.

Kwa namna ya pekee naomba vilevile niwashukurusana wWajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishatina Madini kwa michango yao muhimu katika shughuli zoteza Kamati katika kipindi hiki cha uchambuzi wa bajeti. Nidhahiri kuwa bila weledi na ushirikiano walionipa Kamati hiiisingeweza kufikia hatua hii ya mafanikio.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, kwa namnaya pekee naomba nimshukuru Katibu wa Bunge Dkt. ThomasKashililah, Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge, NduguAthuman Hussein, Mkurugenzi Msaidizi, Ndugu MichaelChikokoto, Makatibu wa Kamati Ndugu MwanahamisiMkunda na Ndugu Felister Mgonja pamoja na Msaidizi waKamati Ndugu Kokuwaisa Gondo kwa uratibu mzuri washughuli zote za Kamati na hatimaye kukamilisha taarifa hii.

Page 170: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

170

Mheshimiwa Naibu Spika, niwashukuru sana wananchiwa Bukombe ambao wamenituma kuja kwenye Bunge hilikuwawakilisha na naomba niwatie moyo kwamba kaziwaliyonituma tunaifanya kwa nguvu zote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa Bunge lakoTukufu likubali kuidhinisha Makadirio na Mapato na Matumiziya Fungu 58 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ambayo nishilingi 998,337,759,500.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja nanaomba kuwasilisha. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mwenyekiti wa Kamati yaNishati na Madini.

TAARIFA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NAMADINI KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA YA

NISHATI NA MADINI KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017PAMOJA NA MAONI YA KAMATIKUHUSU MAKADIRIO YA

MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

________________________

1.0 UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 99 (9)na Kanuni ya 117(11) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleola Januari, 2016, naomba kuwasilisha Taarifa ya Kamati yaKudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Kuhusu Utekelezajiwa Majukumu ya Wizara ya Nishati na Madini, kwa Mwakawa Fedha 2016/2017, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusuMakadirio ya Mapato na Matumizi, kwa Mwaka wa Fedha2017 /2018.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya vikao kadhaakwa lengo la kupokea na kuchambua Taarifa ya utekelezajiwa Bajeti ya Wizara, kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 nakuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi, kwa Mwaka

Page 171: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

171

wa Fedha 2017/2018. Sambamba na utekelezaji wa shughulihiyo, Kamati pia ilifanya mambo yafuatayo:-

i) Ukaguzi wa baadhi ya Miradi ya Maendeleoiliyoidhinishiwa Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017;

ii) Kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Bajetipamoja na Maoni na Ushauri wa Kamati kwa Mwaka waFedha 2016/2017;

iii) Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato naMatumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Mheshimiwa Spika, Taarifa hii inaonesha matokeo yashughuli hizo pamoja na Maoni na Ushauri wa Kamati.

2.0 UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEOILIYOTENGEWA FEDHA KWA MWAKA 2016/2017

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia masharti ya Kanuniya 98(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari,2016, Kamati ilifanya ziara za ukaguzi wa Miradi ya Maendeleoinayotekelezwa chini ya Wizara ya Nishati na Madini, katikaMikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Geita. Lengo la ziara hizolilikuwa ni kujionea utekelezaji wa Bajeti ya Maendeleoiliyoidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja nachangamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wake.

Aidha, Kamati ilikagua Miradi iliyotengewa fedha naambayo haikutengewa fedha katika Bajeti ya Maendeleoya Mwaka 2016/2017 na miradi ambayo inatekelezwa katikaSekta ya Madini. Miradi iliyokaguliwa ni hii ifuatayo:-

i) Miradi ya Umeme Vijijini, Wilaya ya TangaVijijini;

ii) Miradi ya Umeme Vijijini, Wilaya ya Geita Vijijini;

iii) Mradi wa Umeme wa Gesi Kinyerezi I Extension(MW 185);

Page 172: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

172

iv) Mradi wa Umeme wa Gesi Kinyerezi II (MW 240);

v) Ukarabati wa Kituo cha Kufua Umeme, Hale;

vi) Mradi wa Umeme Bulyanhulu-Geita KV 220;

vii) Mgodi wa Dhahabu wa Backleef;

viii) Migodi ya Wachimbaji Wadogo waliopataRuzuku ya Serikali; na

ix) Migodi ya Wachimbaji wa Kati.

2.1 Maelezo na Matokeo ya Ukaguzi wa Miradiya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017

2.1.1 Miradi ya Sekta ya Nishati iliyokaguliwa naKamati

2.1.1.1 Miradi ya REA katika Mkoa wa Tanga

Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Tanga miradi yaumeme vijijini (REA) katika awamu ya kwanza na awamu yapili, imetekelezwa katika wilaya nane (8) za mkoa huo. Miradihiyo yenye ukubwa wa KV 33 imetekelezwa na wakandarasiwawili ambao ni STEG International Services Ltd naSengerema Engineering Group Ltd. Jumla ya vijiji 218 vyamkoa wa Tanga vimenufaika na ukamilishwaji wa miradi yaREA katika awamu ya pili.

Mheshimiwa Spika, ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wamiradi hiyo ilifanyika katika Kijiji cha Tongoni, katika Wilayaya Tanga Vijijini, ambacho ni kama kijiji cha mfano miongonimwa vijiji vilivyopata umeme wa REA Awamu ya Pili.

Katika mradi huu Kamati yako ilibaini kuwa malengoya mradi katika awamu ya pili, hayakukamilika kwa asilimiamia moja. Mradi ulilenga kuzipatia umeme kaya 138, hatahivyo, ni kaya 90 tu kati ya hizo ndizo zimepata umeme,ambazo ni sawa na asilimia 65% tu.

Page 173: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

173

Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine,changamoto kubwa iliyobainika katika miradi ya REA katikaMkoa wa Tanga, ni pamoja na uunganishwaji mdogo waWananchi katika huduma hii ya nishati, Mashine Humba(Transformer) kuharibika mara kwa mara na kushindwa kukidhimahitaji ya eneo husika.

Pia Kamati ilibaini kuwa, baadhi ya vitongoji na vijijihavijaunganishwa na huduma ya umeme katika awamu mbilizilizokwisha kamilika. Kwa maoni ya Wananchi ambao Kamatiilipata fursa ya kuzungumza nao waliieleza Kamati kuwa, tafiti(survey) zilizofanyika mwaka 2015 katika maeneo ya mradihazikuwa za kimkakati (not strategic)kwa kuwa mchoro wamradi husika ulisababisha nguzo za umeme kuwekwa katikamaeneo ambayo wananchi walio wengi hawanufaiki.

Kwa upande mwingine, Kamati ilibaini kuwa, elimukuhusu mradi wa densification kwa wananchi haikuelewekavizuri na pia mradi husika haujaanza rasmi katika vijiji vyoteambavyo havikuunganishwa katika awamuzilizokwishakamilika.

Mheshimiwa Spika, napenda kulijulisha Bunge lakotukufu kwamba, kufuatia ziara ya Kamati katika Kijiji chaTongoni, mashine Humba iliyokuwa na tatizo imebadilishwa,na Kamati inaipongeza sana Serikali kwa kuchukua hatuamapema.

2.1.1.2 Miradi ya REA katika Mkoa wa Geita

Mheshimiwa Spika, Mkoa Geita umenufaika na Mradiwa Umeme Vijijini katika awamu ya pili, ambapo zaidi ya vijiji101 vilivyokuwa kwenye tathmini ya awali vimeunganishwa.Mkandarasi aliyeshughulika na uunganishaji wa umemekatika Mkoa huu ni M/s Nakuroi Investment Co Ltd. Kamatiilifanya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi hiyo katika vijiji vyaNyakato na Buzilayombo, kama vijiji vya mfano miongonimwa vijiji vilivyopata umeme wa REA awamu ya pili.

Page 174: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

174

Katika mahojiano na wananchi wa vijiji hivyo, Kamatiilibaini kuwa malengo ya mradi katika awamu ya pili ilikuwani kuzipatia umeme kaya 165 katika kijiji cha Buzilayombo nakaya 127 katika kijiji cha Nyakato. Hata hivyo, kati ya hizo, nikaya 130 sawa na asilimia 78% zilikuwa zimepata umemekatika kijiji cha Buzilayombo na kaya 32 sawa na asilimia25% tu katika kijiji cha Nyakato.

Mheshimiwa Spika, Kamati i l ibaini kwamba,changamoto kubwa katika miradi ya REA inayotekelezwakatika Mkoa wa Geita ni uunganishwaji mdogo wa Wananchikatika huduma ya umeme na hivyo kutokufikiwa kwamalengo ya utekelezaji wa mradi huu katika maeneo hayo.

Aidha, Kamati i l ibaini kuwa Mashine Humbailiyofungwa ina uwezo wa KV 200, ambao ni mkubwaikilinganishwa na mahitaji ya eneo husika ambalo halinawatumiaji wengi. Yapo maeneo mengine ambayo Kamatiilibaini kuwa yanahitaji Mashine Humba zenye uwezomkubwa lakini zimefungiwa Mashine Humba zenye uwezomdogo na hivyo kusababisha uharibikaji wa mara kwa mara.

2.1.1.3 Mradi wa Umeme wa Gesi Kinyerezi IExtension (MW 185) na Mradi wa Umeme wa Gesi waKinyerezi II (MW 240)

Mheshimiwa Spika, mradi huu unatekelezwa na Shirikala Umeme Tanzania (TANESCO) kwa lengo la kuzalisha MW185 zaidi za umeme katika Mradi wa Umeme wa Gesi KinyereziI ambao tayari unazalisha MW 150. Mradi unakadiriwakugharimu dola za kimarekani milioni 188 ambazo zimelipwana Serikali kwa asilimia mia moja (100%) na unatarajiwakukamilika mwezi Juni, 2018.

Katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, shilingi bilioni 110zilitengwa na hadi wakati Kamati inakagua mradi huu, kiasicha shilingi bilioni 88 sawa na asilimia 80% kilikuwakimeishatolewa katika utekelezaji wa mradi huo. Kamatiinapongeza jitihada za Serikali kwa kupeleka fedha mapemakatika mradi huo muhimu.

Page 175: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

175

Pamoja na mafanikio hayo, Kamati i l ibainichangamoto kadhaa zinazokabili utekelezaji wa mradi huu,ikiwa ni pamoja na tozo mbalimbali (surcharges) kutokaTANROADS na VAT zinazotokana na ukubwa na uzito usio wakawaida wa mitambo inayotumika katika mradi huu (out ofgauge heavy loads charges). Tozo hizo zinachangiakuongezeka kwa gharama za mradi na hivyo kucheleweshautekelezaji wake.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na changamotozinazoukabili mradi huu, bado dhamira ya dhati ya Serikaliya kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme wauhakika nchini kinazidi kudhihirika ambapo katika mwakawa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi bilioni 90 kutoka vyanzovya ndani zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza nakukamilisha mradi huu.

Mheshimiwa Spika, Kamati kupitia Bunge lakoinaitaka Serikali kupeleka fedha zote za miradi ya umemezilizobaki (Bakaa) kwa Mwaka wa fedha 2016/2017 ilikukamilisha miradi hiyo muhimu kwa wakati kamailivyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kinyerezi II MW 240unatekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwalengo la kuzalisha Megawati 240 kwa mfumo wa kisasa zaidiunaoitwa Combined Cycle Power Plant. Gharama ya mradihuu ni dola za kimarekani milioni 344 ambapo asilimiathemanini na tano (85%) ya gharama hizo italipwa na JapanExport Trading Financing na asilimia kumi na tano (15%)iliyobaki tayari imelipwa na Serikali ya Tanzania mweziFebruari, 2016.

Ujenzi wa Mradi huu umeishaanza na unatekelezwakwa kasi, ambapo tayari misingi ya majengo imewekwa nabaadhi ya mitambo kufungwa. Hata hivyo, pamoja na ujenzihuo kuanza kwa kasi, bado kuna changamoto mbalimbaliza tozo kama vile forodha (customs levies), railway levies,custom processing fees pamoja na custom duties, ambazozinatakiwa kulipwa na TANESCO. Tozo hizo zimekuwa

Page 176: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

176

zikichangia ongezeko la gharama katika utekelezaji wa mradihuu.

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitaarifiwa kwamba,maombi ya TANESCO kwa TANROADS, ambayo yalihusukupatiwa msamaha wa kodi na tozo hizo zitokanazo naukubwa na uzito wa mitambo usio wa kawaida (out of gaugeheavy loads charges) yalikataliwa. Aidha, ucheleweshaji wamalipo hayo unaweza ukasababisha mitambo kuchelewakufika eneo husika la mradi na hivyo kuchelewesha utekelezajiwa mradi.

2.1.1.4 Mradi wa Ukarabati wa Kituo cha KufuaUmeme Hale

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya ziara ya ukaguzikatika Kituo cha Hale ambacho kilizinduliwa mwaka 1964.Kituo hiki ni moja ya vituo vitatu vinavyotumia nguvu ya majikuzalisha umeme nchini, na kina mitambo miwili (2) yenyeuwezo wa kuzalisha MW 10.5 kila mmoja. Mwaka 1986mtambo mmoja ulipata hitilafu kwenye msuko wa MashineHumba(stator winding)na ulifanyiwa marekebisho makubwa,hata hivyo, mtambo huo uliharibika tena mwaka 2004.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kufanyaukarabati mkubwa wa mitambo yote miwili kwa ufadhili waSerikali ya Sweden, ambayo ilikubali kutoa Kroner Milioni 200kupitia Shirika lake la misaada la SIDA. Asilimia 60 ya fedhahizo ni ufadhili na asilimia 40 ni Mkopo wa kibiashara.Makubaliano ya ufadhili wa mradi huu yalifanyika tarehe 11Julai, 2013 baada ya upembuzi yakinifu kukamilika, hata hivyoukarabati wa mitambo hiyo bado haujaanza kwa kuwa badohajapatikana mkandarasi atakaye tekeleza mradi huo.

Kamati inaona kwamba, kuchelewa kuanza kwaukarabati wa Mitambo hiyo kunaendelea kupunguza zaidiMegawati 10 kwenye Gridi ya Taifa, hivyo Kamati inaishauriWizara iharakishe taratibu hizo ili ukarabati uanze mapemakama ilivyokusudiwa.

Page 177: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

177

2.1.1.5 Mradi wa Bulyanhulu- Geita KV 220

Mheshimiwa Spika, Kamati ilitembelea mradi huuambao unahusisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme chaGeita (msongo wa 220/33kv) pamoja na usambazaji waumeme katika vijiji kumi (10) vilivyopo ndani ya eneo lautekelezaji wa mradi. Gharama za Mradi ni dola za kimarekanimilioni 23 ambazo ni mkopo kutoka benki ya BADEA, na tayarigharama na fidia nyingine zote zimekwisha kukamilika nawananchi wote waliopisha eneo la mradi wameshalipwafidia wanazostahili.

Pamoja na kukamilika kwa ulipaji fidia Wananchiwaliopisha eneo la mradi, bado Mradi huu umeshindwakuanza kwa wakati kutokana na kuchelewa kupatikana kwaMhandisi Mshauri wa Mradi.

Mheshimiwa Spika, Mradi huu utakapoanza utasaidiakuongeza hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika katikaMkoa wa Geita. Aidha, Mradi huu utaunganisha wateja zaidiya 1500 ukiwemo Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) ambaounahitaji zaidi ya MW 11 kwa ajili ya shughuli za Mgodi, nakusaidia Migodi mingine ya Wachimbaji wadogo ambayohaiendeshwi vizuri kutokana na kukosekana kwa umeme wauhakika.

Kamati inaishauri Serikali kutatua changamoto hizoharaka iwezekavyo ili Mradi huo wenye tija kwa Mkoa waGeita, uweze kuwanufaisha wananchi pamoja nawawekezaji wanaohitaji umeme mkubwa kwa ajili yakuendesha shughuli zao.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Serikalikupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa kukamilisha mradimuhimu wa Rusumo Hydropower unaoziunganisha nchi tatuza Tanzania, Rwanda na Uganda, mradi huu umeongeza MW26 kwenye Gridi ya Taifa. Mradi huu utasaidia upatikanajiwa umeme kwa mikoa ya Kagera na Kigoma na hivyokupunguza matumizi ya umeme wa mafuta ambao ni ghaliukilinganisha na umeme wa maji.

Page 178: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

178

2.1.2 Miradi ya Sekta ya Madini iliyokaguliwa naKamati

2.1.2.1 Mgodi wa Dhahabu wa Buckleef

Mheshimiwa Spika, Mgodi wa Dhahabu wa Buckleefwenye leseni ya Uchimbaji Mkubwa(Special Mining License)SML Na. 04/92 uko katika Mkoa wa Geita na unamilikiwa kwamkataba wa ubia ulioingiwa mwaka 2011 kati ya Serikalikupitia STAMICO na Kampuni ya TANZAM 2000.

Mheshimiwa Spika, kupitia mkataba huo, STAMICOinamiliki asilimia 45 na TANZAM 2000 inamilki asilimia 55 yahisa. Kwa mujibu wa mkataba (Joint Venture Agreement) huoTANZAM 2000 ina jukumu la kutafuta fedha za kuendeshaMgodi (Operator) wakati jukumu la STAMICO lilikuwakuhamishia Leseni zake 12 kwa Kampuni hiyo.

Hadi wakati wa ziara katika mgodi huu, Kamati ilibainikwamba, licha ya Leseni zote za uchimbaji na utafitikukabidhiwa kwa Kampuni hiyo, hakuna kazi yeyoteiliyokwishafanyika katika kuendeleza Mgodi huo tanguKampuni hiyo iingie Mkataba na STAMICO.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Kampuni kuripoti kuwaimekamilisha ufungaji wa Mtambo mpya wa kuchenjuliadhahabu, Kamati inasikitishwa na kitendo cha mbia huyokutozingatia ushauri wa STAMICO kuhusu aina ya Mtambounaofaa kutumika katika eneo hilo, hatua ambayoinaisababishia Serikali hasara. Kamati inaishauri Serikali kuwamakini inapoingia ubia katika Sekta ya madini ili kuepukawabia wa aina hii ambao hawazingatii ushauri wa Mbiamwenza, (STAMICO) jambo linalosababisha hasara zisizo zamsingi.

Mheshimiwa Spika, Kamati haikuona jitihada zozoteza Mbia huyo za kuendeleza Mgodi kama walivyokubalianakwenye Mkabata. Aidha, Kamati imesikitishwa na usimamizimbovu wa STAMICO katika Mgodi huo licha ya kuwa naMashapo (Reverse) yenye uhakika wa kuzalisha Dhahabu na

Page 179: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

179

kuliingizia Taifa mapato. Aidha, hatua stahiki zichukuliwe ilikurekebisha kasoro ambazo zimebainika katika ubia huo.

2.1.2.2 Migodi ya Wachimbaji Wadogo waliopataRuzuku ya Serikali-Geita (Blueleef Mining na Mgusu Mining)

Mheshimiwa Spika, katika awamu zote mbili zamalipo, jumla ya Shilingi Bilioni 8,071,000,000/= zimetolewana Serikali kwa kuratibiwa na Wizara ya Nishati na Madini, najumla ya Wachimbaji Wadogo 115 wamenufaika kwa kupataruzuku hizo katika mikoa mbalimbali. Katika awamu yakwanza ya malipo, kiwango cha juu kwa kila mnufaikakilikuwa ni Dola za Kimarekani 50,000 na awamu ya pilikiwango cha juu cha mnufaika kilikuwa ni Dola za Marekani100,000. Kwa maoni ya Kamati, viwango hivyo vya fedha nivikubwa ikilinganishwa na usimamizi mdogo unaotolewa naWizara ya Nishati na Madini.

Katika Mkoa wa Geita jumla ya Wachimbaji WadogoWadogo Saba (7 ) wamenufaika na ruzuku ya Serikali,vikiwemo Vikundi vya Wajasiriamali wanaoshughulika katikamaeneo ya wachimbaji wadogo. Katika ziara ya ukaguzi waMigodi ya wachimbaji wadogo waliopata ruzuku, Kamatiiliridhishwa na utendaji wa wachimbaji wadogo watatu (3)tu kati ya Saba (7) waliopata ruzuku ambao wameendelezashughuli zao za uchimbaji katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio hayo kwabaadhi ya wanufaika, Kamati ilibaini changamoto kubwa yausimamzi wa fedha usioridhisha kwa Wachimbaji Wadogo.Aidha, Wanufaika hao wa ruzuku kwa namna moja amanyingine hawakutumia fedha hizo kwa malengoyaliyokusudiwa na Serikali.

Kwa kuwa, awamu zote mbili za utoaji wa ruzukukwa Wachimbaji Wadogo kumekuwa na kasoro mbalimbalikwenye matumizi na usimamizi wa ruzuku hizo, Kamatiinaishauri Serikali kufanya tathmini (evaluation) ya fedha hizokabla haijaanza awamu nyingine ili kuhakiki na kutatuachangamoto nyingi ambazo zipo kwa sasa.

Page 180: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

180

2.1.2.3 Migodi ya Wachimbaji wa Kati

(Busolwa Mining na Nyarugusu Processing Plant)

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya ziara ya ukaguziwa Migodi ya Busolwa Mining na Nyarugusu Processing Plant,iliyopo Mkoa wa Geita. Lengo la ziara lilikuwa ni kujifunza jinsiWachimbaji wa Kati wanavyoendesha shughuli zao nakubaini mchango wao katika mapato ya Serikali.

Busolwa Mining ni Mgodi unaomilikiwa na Mtanzania,yaani mzawa kwa aslimia mia moja, na Kamati ilijionea jinsiunavyoendesha shughuli zake kwa kutekeleza Sheria naKanuni mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kulipa kodi zote zaSerikali. Tangu Mgodi huo uanze kazi mwaka 2014,umeshalipa kodi za thamani ya shilingi bilioni 120, Mrabahashilingi Bilioni 562, kodi ya zuio kwa mwaka 2017 shilingi Milioni20 na Service Levy shilingi Milioni 48.

Mheshimiwa Spika,changamoto kubwa inayoukabiliMgodi huu ni ufinyu wa eneo hasa la kutupia mabakiyatokanayo na shughuli za Mgodi yaani (TSF). Hivyo nimapendekezo ya Kamati kuwa, maombi ya Mgodi huokupatiwa eneo lingine yashughulikiwe mapema ili kusaidiakuongeza uhai wa Mgodi huo ambao umeajiri zaidi yaWatanzania 300.

3.0 SEKTA YA MADINI

3.1 Madini ya Vito ya Tanzanite

Mheshimiwa Spika, Kamati yako imeendeleakusikitishwa na jitihada ndogo zinazofanywa na Wizara yaNishati na Madini za kuokoa mapato yatokanayo na Madiniya Vito yaani Tanzanite na Almasi nchini. Hata hivyo hakunamikakati madhubuti ya kuokoa Rasimali hizi kutokana nausimamizi usioridhisha wa Migodi hiyo, pamoja nachangamoto nyingi za Mikataba baina ya Stamico naTanzanite One Mining Limited (TML), ambao ndiyo Mgodipekee unaozalisha Madini haya Duniani.

Page 181: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

181

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Tanzanite One MiningLimited (TML) amekuwa akitoa Taarifa za uongo kwa mbiamwenza yaani STAMICO toka alivyoanza uzalishaji waTanzanite hapa nchini, kwa mfano kuanzia Juni, 2013 hadiMachi, 2016 STAMICO ameripoti mauzo ya jumla ya Dola zakimarekani Milioni 16,671,167 na TML katika kipindi hicho hichoaliuza Tanzanite yenye thamani ya Dola za kimarekani Milioni17,930,653 ambapo tofauti ya Dola Milioni 1,259,483hazikuripotiwa na Kampuni hiyo na hivyo hazikuripiwa kodiya Serikali. Hivyo, kutokana na tofauti hiyo Stamicowamepoteza jumla ya Dola za kimarekani 182,855.19.

Mheshimiwa Spika, pia kampuni hii ya Tanzanite OneMining Limited (TML) imekuwa hailipi kodi ya Mapato na tozo/gharama mbalimbali kwa Stamico kama vile Gharama yaUangalizi na usimamizi (Monitoring and Evaluation Unit Cost)ambapo jumla ya shilingi milioni 131,695,626 zinadaiwa naSTAMICO, pia kukosekana kwa akaunti ya pamoja kati yawabia hawa kuna sababisha mambo mengi hasa ya kifedhakutokufahamika kwa STAMICO kama inavyotakiwa naMkataba (Joint Venture) huo.

Mheshimiwa Spika, kwa namna Mkataba huounavyoendeshwa kwa pande hizi mbili (Joint Venture)umekuwa hauna manufaa kwa upande wa Serikali, kwakuwa Kampuni hiyo imekuwa haitekelezi kwa kiasi kikubwamatakwa ya Mkataba huo pamoja na maagizo mbalimbaliya Serikali inayokuwa ikipewa hasa wakati Kampuni hiyoilipofukuza Wafanyakazi zaidi ya 201 bila kufuata Sheria nautaratibu za nchi.

Mheshimiwa Spika, Tarehe 3 Mei, 2017, Kamati yakoilihudhuria maonesho ya madini ya Vito jijini Arusha, nakujionea jinsi maonesho haya yanavyoweza kuisaidia sektahii ya Madini ya Vito hapa nchini. Pamoja na mafanikio yakuanzisha Mnada na Maonesho hayo ya Vito hapa nchini,bado kuna changamoto nyingi zinazoikabili Sekta hii yaMadini ya Vito hasa kwa madini ya Tanzanite.

Page 182: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

182

Changamoto kubwa ni utoroshawaji wa madinihayo nje ya nchi. Changamoto hiyo ndiyo inayoendeleakuliumiza Taifa letu kwa kuwa ndiyo nchi pekee Duniani yenyeneema hiyo, nakuifanya Tanzania kuwa siyo nchi ya kwanzakwa uuzaji wa Madini hayo ya Vito duniani. Hata hivyo,uanzishwaji wa maonesho hayo kwa kiasi kikubwa badohaujaweza kusaidia kutatua changamoto zinazokabili sektahii ya Madini ya vito hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hasara kubwatunayopata kama Taifa kwenye Madini haya pekee nchini,Kamati inalishauri Bunge lako tukufu kwa mara nyingine tenalifuatilie kwa kina changamoto za Mkataba huo baina yaTML na STAMICO ili Bunge tuweze kuishauri Serikali namnabora ya kukabiliana na Mikataba isiyokuwa na maslahi kwaTaifa.

Madini ya DhahabuMheshimiwa Spika, Sekta ya Madini nchini

imeendelea kukabiliwa na changamoto nyingi hasa katikasuala la ukusanyaji wa Kodi za Serikali. Sekta hii imekuwaikichangia asilimia 4% tu katika pato la Taifa, mchangoambao ni kidogo sana ikilinganishwa na ongezeko lauzalishaji katika Sekta hiyo.

Kwa mfano; katika mwaka 2016 nchi yetu ilizalishajumla ya Wakia milioni 1.42 za Madini ya Dhahabuikilinganishwa na Wakia milioni 1.36 zilizozalishwa katikamwaka 2015. Ongezeko hilo la uzalishaji ambalo ni sawa naasilimia 4.4%, lilitakiwa kwenda sambamba na ongezeko laukusanyaji wa Kodi za Mapato nchini.

Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa na ulipajihafifu wa kodi za Mapato unaofanywa na Wawekezaji katikaMigodi mikubwa hapa nchini.Kwa mfano; Mwaka 2016 niMigodi miwili tu nchini ndiyo iliyolipa Kodi ya Mapato ambayoni North Mara Gold Mine na Geita Gold Mine. Kamati inaitakaSerikali kuchukua hatua madhubuti juu ya Wawekezajiambao hawalipi kodi ili kuhakikisha Kodi zote muhimuzinalipwa kwa wakati.

Page 183: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

183

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko mengikutoka kwa Wawekezaji nchini hasa kwenye sekta ya Madini,wakiidai Serikali Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT returns)ambayo kiutaratibu inapaswa kulipwa baada ya Migodikukamilisha hesabu zao na kuwasilisha TRA. Serikali haijalipafedha hizo kwa Migodi hiyo kwa madai ya kuwepochangamoto kadhaa ambazo Serikali ilikuwa inazifuatilia ilikujiridhisha kabla ya kuzilipa. Kamati inaishauri Serikalikutatua changamoto hizo ili Migodi hiyo iweze kulipwa fedhahizo.

Mheshimiwa Spika, Serikali inamiliki mgodi mmoja tukwa asilimia mia ambao ni Mgodi wa Stamigold kupitia Shirikala STAMICO. Mgodi huu licha ya kuajiri Watanzania zaidi yamia saba (700), bado kumekuwa na jitihada ndogo za Serikalikatika kuusaidia Mgodi huo katika masuala ya msingi yakuuendeleza kama vile;

1. Serikali kutousaidia Mgodi kupata fedha zakufanya utafiti katika leseni zinazozunguka eneo hili ilikuongeza uhai wa mgodi;

2. Mgodi haujasaidiwa kupata msamaha wakodi ya mafuta na vipuli vya uendeshaji kama ilivyo kwamigodi mingine ya wawekezaji nchini;

3. Ukosefu wa Mining Development Agreement(MDA) kwa muda mrefu unaukwamisha Mgodi kujiendeshakibiashara kama ilivyo kwa Migodi mingine nchini;

4. Mgodi huu unakabiliwa na deni kubwa kutokakwa Wazabuni mbalimbali wanaotoa huduma katika Mgodihuo. Kamati inaitaka Serikali kuingilia kati deni hilo ili kuepushashughuli za Mgodi huo kusimama na kusababisha hasarakubwa.

Kamati hairidhishwi na jitihada zilizofanywa na Serikalikupitia Wizara ya Nishati na Madini katika kuusaidia Mgodihuo wa Stamigold. Changamoto hizo zikitatuliwa kikamilifu,

Page 184: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

184

uzalishaji wa Madini ya Dhahabu unaweza kuongezeka katikaMgodi huo.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na malalamiko yamuda mrefu sasa kutoka kwa Wananchi wanaozungukaMgodi wa North Mara hasa maeneo ya Nyamichele katikavijiji vya Nyakunguru, Murwambe, Matongo na Nyamongo.Pamoja na tathimini ya ardhi kukamilika toka mwezi Aprili,2013 na Kamati kutoka Wizara ya Nishati na Madini,kukamilisha kazi yake ya tathmini na utatuzi wa changamotohasa zile za mauaji katika eneo hilo,mpaka sasa Wananchihao bado hawajalipwa fidia zao.

Kamati inashangazwa na hatua ya malipo yaWananchi hao kucheleweshwa kwa takribani miaka minnesasa, licha ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini,kuunda na kutuma Kamati za Uhakiki nne (4) kati ya mwaka2014 hadi 2017.

Kamati inaishauri Serikali kuingilia kati suala hili, iliWananchi hao ambao wameteseka kwa muda mrefu sasawaweze kupata stahiki zao.

Mheshimiwa Spika, Kamati inampongeza Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John PombeMagufuli na kuunga mkono jitihada zake katika kuendeleakufuatilia kwa karibu zaidi Sekta hii ya Madini nchini, ikiwa nipamoja na kuunda Kamati maalum ya Wataalamuiliyochunguza mchanga uliyo katika makontena ya mchangawa madini (Makinikia)yaliyopo katika maeneo mbalimbalihapa nchini. Kamati hii iliweza kubaini uwepo wa viwangovingi vya madini ya dhahabu, shaba, silva, salfa, na chumakatika makinikia hayo yanayosafirishwa nje ya nchi.

Pia uchunguzi huo umeonesha kuwepo kwa madiniya kimkakati yaani (Strategic metals) ambayo niIridium,Rhodium, Ytterium, Beryllium, Tantalum na Lithium, madinihaya kwa sasa yanahitajika sana Duniani na yana thamanikubwa sambamba na madini ya dhahabuambayo Taarifazake zilikuwa hazitolewi na wawekezaji.

Page 185: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

185

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, Kamati inaendeleakusubiri taarifa nyingine ya Kamati Maalum ya Waatalamuiliyoundwa na Mhe. Rais, inayoendelea na uchunguzi ambaoutabainisha masuala ya Kiuchumi na Kisheria ili sasa kamaTaifa tuweze kunufaika na Rasilimali zetu za Madini.

Mheshimiwa Spika, kwa dhati kabisa Kamatiinakupongeza wewe binafsi kwa kuamua kufuatilia jambohili kwa ukaribu, na kutoa uamuzi kuwa utaunda Kamatimaalumu ya kufuatilia masuala ya Madini, ili Bunge lakotukufu nalo litekeleze kikamilifu jukumu lake la kikatiba lakuisimamia na kuishauri Serikali.

4.0 SEKTA NDOGO YA GESI.

Mheshimiwa Spika,tangu kugundulika kwa Gesi Asilinchini mwaka 1974 katika eneo la Songo Songo, mwaka 1982katika eneo la Mnazi Bay pamoja na eneo la Bahari ya Kinakirefu mwaka 2010/12, uzalishaji wa gesi katika miradi yoteiliyogundulika hapa nchini ulianza miaka ya 2004 hadi 2006.

Kamati inaipongeza Serikali kupitia Shirika la TPDC kwakuandaa Mpango Kabambe wa Matumizi na Usambazaji waGesi Asilia nchini wa mwaka 2016-2045 (Natural Gas UtilisationMaster Plan). Mpango huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kutoaDira ya Matumizi bora ya Gesi Asilia kwa kuzingatiavipaumbele mbalimbali vilivyowekwa ili Rasirimali hii iwafikiena kuwanufaisha Wananchi wengi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada mbalimbalizinazofanywa na TPDC, bado kuna changamoto kubwa yaMadeni yanayolikwamisha Shirika hili katika uendelezaji wamiradi yake. Madeni hayo yanasababishwa na hatua yaSerikali kutenga fedha kidogo kwenye miradi hiyo muhimuna hivyo kukwamisha Shirika kutekeleza miradi hiyo kwawakati.

Mheshimiwa Spika, tangu kugundulika kwa Gesi hiyohapa nchini, jumla ya Viwanda 41 na Taasisi 2 vimekwishaunganishwa katika mtandao wa matumizi ya Gesi Asilia.

Page 186: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

186

Aidha, Kamati inaipongeza Serikali kwa kuendeleza miradiya kuzalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia. Miradi hiyomikubwa inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2018 ambapoinatarajiwa kuongeza zaidi ya Megawati 425 kwenye Gridiya Taifa, na hivyo kupunguza tatizo la umeme nchini.

2.3 Maoni ya Jumla kuhusu Utekelezaji wa Miradiya Maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, kutokana na ziara ya ukaguzi wamiradi ya maendeleo Kamati inatoa maoni yafuatayo:-

(i) Utekelezaji wa Bajeti kwa Wizara ya Nishati naMadini, haukuwa wa kuridhisha kwa kuwa fedha iliyotolewahadi Machi, 2017 ni asilimia 36 tu;

(ii) Miradi mingi haikutekelezeka kamailivyopangwa kwa kuwa fedha zilizotengwa hazikutolewa nakupelekwa kwa wakati kama ilivyotakiwa;

(iii) Miradi mingi ya REA katika Awamu ya Pilihaikukamilika kutokana na kasoro mbalimbali kama vileuainishaji wa maeneo bila kuzingatia vijiji na vitongojiambavyo tayari vina wananchi wengi, na ufungaji waMashine Humba nyingi kutokidhi mahitaji ya eneo husika;

(iv) Serikali iangalie upya namna bora yakuwasaidia Wachimbaji wa Kati kwa kuwapatia maeneo yakutosha kwa kuwa wameonesha nia ya dhati ya kuendelezaSekta ya Madini;

(v) Ruzuku iliyotolewa na Serikali kupitia Wizaraya Nishati na Madini kwa Wachimbaji Wadogo Wadogo,haikusimamiwa vizuri na hivyo kushindwa kuleta tija kwaWananchi waliokusudiwa;

(vi) Pamoja na Mipango mizuri ya TPDC katikakuendeleza Sekta ya Gesi nchini, ni lazima Serikali iwekezefedha za kutosha katika miradi ya Gesi ili kuharakisha azmaya nchi yetu kuingia katika uchumi wa viwanda;

Page 187: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

187

(vii) Serikali itenge fedha za kutosha na kuzipelekakwa wakati kwenye miradi ya kimkakati kama vile Mgodi wamakaa ya Mawe wa Kiwira; na

(viii) Uwekezaji katika sekta ya madini unahitajikuangaliwa upya hasa katika uwekezaji wa Migodi mikubwa.

3.0 UCHAMBUZI WA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WABAJETI NA UZINGATIAJI WA MAONI YA KAMATI KWA MWAKAWA FEDHA 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Kamati ilifanya uchambuzi waBajeti kwa kuzingatia mambo makuu matatu ambayo ni:-Makusanyo ya Maduhuli kwa mwaka wa fedha 2016/2017,Hali ya upatikanaji wa fedha kutoka Hazina na Uzingatiajiwa maoni na ushauri uliotolewa na Kamati ya Nishati naMadini wakati huo.

3.1 Uchambuzi wa Taarifa kuhusu Ukusanyajiwa Maduhuli kwa mwaka wa fedha 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Wizara ilipanga kukusanyamaduhuli yenye jumla ya Shilingi bilioni 370.68 ikilinganishwana Shilingi bilioni 286.66 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.Taarifa ya utekelezaji inaonesha kuwa, hadi kufikia 28 Februari,2017, Wizara ilikuwa imekusanya jumla ya Shilingi bilioni239.38 sawa na asilimia 64.5 ya lengo. Makusanyo hayoyanaweza kufikia lengo lililowekwa kama Wizara itaongezajuhudi katika kipindi kilichobaki.

Uchambuzi wa Kamati umebaini kuwa Makadirio yamchango wa Idara ya Madini kwa mwaka fedha 2017/18yameshuka kwa asilimia 4.5% ikilinganishwa na mwaka wafedha 2016/17. Aidha, Makadirio ya mchango wa Idara yaNishati, yameongezeka kwa asilimia 4.5% katika mwaka wafedha 2017/18 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2016/17.Ufafanuzi zaidi umeoneshwa kupitia Kielelezo Na. 01 chaTaarifa hii.

Page 188: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

188

Kielelezo Na. 01

Aidha Kamati ilielezwa sababu zilizosababishakuongezeka kwa makusanyo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 kama ifuatavyo:-

i) Usimamizi bora wa mapato kutoka vyanzovya ndani;

ii) Kuanzishwa kwa Minada ya Madini ya Vitonchini;

iii) Kuongezeka kwa Mauzo ya Gesi Asilia kwawatumiaji wapya hasa baada ya viwanda vipya zaidi ya 41kuunganishwa kwenye mtandao wa matumizi ya Gesi;

3.2 Upatikanaji wa Fedha kutoka Hazina

Mheshimiwa Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017Wizara ya Nishati na Madini iliidhinishiwa jumla ya Shilingi

0

50,000,000,000

100,000,000,000

150,000,000,000

200,000,000,000

250,000,000,000

KIASI ASILIMIA KIASI ASILIMIA

2016/2017 2017/2018IDARA YA MADINI 215,962,385,000 58.3 194,397,889,999 53.8

IDARA YA NISHATI 154,377,501,000 41.6 166,326,844,600 46.1

IDARA NA VITENGO VINGINE 344,003,000 0.1 266,403,000 0.1

HALI YA UKUSANYAJI WA MADUHULI

Page 189: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

189

trilioni 1.12 kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake. Hadi kufikiatarehe 13 Machi, 2017 Wizara ilikuwa imepokea jumla yaShilingi Bilioni 404.12, sawa na asilimia 36 ya Bajeti yoteiliyoidhinishwa na Bunge lako tukufu.

Bajeti ya Miradi ya Maendeleo iliyoidhinishwa naBunge lako ilikuwa ni Shilingi Trilioni 1.06, sawa na asilimia 94ya bajeti yote ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2016/17. Hadikufikia Machi, 2017 Shilingi Bilioni 372.88 zilikuwa zimetolewa,sawa na asilimia 35 tu ya fedha za Maendeleo.

Kwa upande wa fedha za Matumizi Mengineyo (OC),fedha iliyoidhinishwa ilikuwa Shilingi bilioni 66.22 na hadikufikia Machi, 2017 Wizara ilikuwa imepokea kiasi cha ShilingiBilioni 31.24, sawa na asilimia 47% ya fedha zilizoidhinishwa.Mwenendo huu wautolewaji wa fedha za matumizimengineyo unakwamisha usimamizi bora wa fedha za miradiya maendeleo, kwani Watendaji wanashindwa kusimamiamiradi hiyo kwa kukosa fedha.

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya fedha za maendeleokutoka nje kwa mwaka wa fedha 2016/17 ilikuwa ni ShilingiBilioni 331.51. Hadi kufikia Machi, 2017jumla ya Shilingi Bilioni38.57, sawa na asilimia 12% tu zilipokelewa na kupelekwakatika miradi mitatu ambayo ni Miradi ya Umeme Vijijini, Mradiwa Hale Hydropower na Mradi wa Makambako- Songea.Upatikanaji huu mdogo wa fedha za nje kwenye miradi yaMaendeleo, umekwamisha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wamiradi mingi iliyotengewa kiasi kikubwa cha fedha za nje.

Mheshimiwa Spika, Kamati inaipongeza Wizara yaNishati na Madini kwa kubaini namna utegemezi wa fedhaza nje za maendeleo unavyoathiri utekelezaji wa miradi hiyo,na hivyo kuamua katika Bajeti ya Mwaka wa fedha 2017/18kutenga fedha za maendeleo kutoka vyanzo vya ndani tu.Uamuzi huu utasaidia miradi mingi kutekelezwa bilakutegemea fedha za Wahisani ambao wamekuwahawatekelezi kikamilifu ahadi zao.

Page 190: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

190

Ufafanuzi zaidi kuhusu uwiano kati ya Bajetiiliyoidhinishwa na fedha zilizopatikana hadi Machi, 2017 nikama unavyoonekana kupitia Kielelezo No.2 katika taarifahii.

Kielelezo Na. 2

CHANZO: Taarifa ya Wizara ya Nishati na Madini Fungu58 kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Mheshimiwa Spika, Kamati inasikitishwa na utolewajiwa fedha za miradi ya maendeleo usioridhisha, hivyokusababisha miradi mingi kushindwa kukamilika kamailivyopangwa katika mwaka wa fedha 2016/17. Kamatiinaona ni vyema kuwa na miradi michache ya kipaumbeleambayo itaweza kupelekewa fedha kuliko kuwa na miradimingi ambayo haitaweza kutekelezwa kwa mwaka husikakwa kukosa fedha.

3.3 Mapitio ya Utekelezaji wa Ushauri waKamati

Mheshimiwa Spika, katika uchambuzi wa Bajeti yaMwaka 2016/17, Kamati i l itoa Maoni, Ushauri naMapendekezo, kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 7(1)ya Nyongeza ya Nane ya Toleo la Januari, 2016 iliyoelezeamajukumu ya Kamati ya kusimamia na kufuatilia utendaji kaziwa shughuli za Wizara katika Sekta za Madini na Nishati.

BAJETI ILIYOIDHINISHWA 2016/2017 FEDHA ILIYOPATIKANA HADI MACHI,2017

UFAFANUZI KIASI ASILIMIA

KIASI ASILIMIA

JUMLA KUU Tri 1.12 100 Bil 404.12 36

FEDHA ZA MAENDELEO

Tri 1.06 94 Bil 372.88 35

MATUMIZI YA KAWAIDA

Bil 66.22 6 Bil 31.24 47

Page 191: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

191

Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kuwa, baadhi ya ushauriuliotolewa na Kamati umezingatiwa na baadhi badohaujafanyiwa kazi na Serikali kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, bado kuna tatizo la usimamiziusioridhisha katika miradi ya Umeme Vijijini, katika maeneomengi hapa nchini. Katika ziara ya ukaguzi wa miradi yamaendeleo, Kamati ilibaini changamoto mbalimbali katikamaeneo mengi zilizoathiri utekelezaji wa miradi. Mfano;ufungaji wa Mashine Humba zilizochini ya kiwango katikamaeneo mengi umesababisha kuharibika mara kwa marana hivyo wananchi waliopata miradi ya umeme vijijinikutokupata faida ya Nishati hiyo hata baada ya kukamilikakwa miradi hiyo.

Fedha zilizotengwa kwa ajili ya baadhi ya miradi yakimkakati ni kidogo sana ukilinganisha na mahitaji halisi yafedha zinazohitajika katika kuendeleza miradi hiyo. Kamatihaioni dhamira ya dhati ya Serikali ya kuendeleza miradi hiyo,hasa ile ya Joto Ardhi ambayo utekelezaji wake haujaanzalicha ya upembuzi yakinifu kukamilika muda mrefu uliopita.

Mheshimiwa Spika, kuhusu jitihada zinazofanywa naSerikali za kulipa madeni ya TANESCO, Kamati haioni mikakatiya dhati ya Serikali ya kumaliza madeni hayo kwa wakati.Aidha, mwenendo hafifu wa ulipaji wa madeni hayounakwamisha kwa kiasi kikubwa shughuli za utendaji waShirika hilo.

4.0 UCHAMBUZI WA MPANGO NA MAKADIRIO YAMAPATO NA MATUMIZI KWA (FUNGU 58) MWAKA WA FEDHA2017/2018

4.1 Mapitio ya Malengo ya Wizara kwa Mwakawa Fedha 2017/2018

Mheshimiwa Spika, wakati wa kufanya uchambuziwa Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2017/18,Kamati imebaini kuwa Wizara imekuwa ikisimamia nakutekeleza malengo hayo zaidi ya miaka mitano sasa. Hii

Page 192: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

192

inatokana na umuhimu wake kwa kuzingatia majukumuyaliyoainishwa kwa mujibu wa Sheria ya Utekelezaji waMajukumu ya Wizara ya Nishati na Madini, Sura 299, TheMinisters (Discharge of the Ministerial Functions) Act.

Mheshimiwa Spika, Mwaka wa Fedha 2017/18 Wizaraitatekeleza na kusimamia Malengo Makuu Matano (5)yafuatayo:-

i) Kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa Sektaya Nishati kwa Maendeleo endelevu ya Taifa;

ii) Kuboresha uendelezaji na usimamizi endelevuwa rasilimali za madini kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi;

iii) Kuimarisha utoaji wa huduma kwa wadaukatika Sekta za Nishati na Madini;

iv) Kuboresha utoaji wa huduma kwa watumishiwaathirika wa VVU na UKIMWI ili kupunguza maambukizi; na

v) Kuondoa vitendo vya rushwa katika sekta yaNishati na Madini.

Mheshimiwa Spika, malengo haya yakitekelezwavizuri yatatimiza azma ya Wizara ya kuendeleza sektainazozisimamia hasa Sekta ya Madini ambayo inatarajiwakuongeza pato la Taifa, na Sekta ya Nishati inayotegemewakutekeleza azma ya Taifa kufikia Uchumi wa Viwandaunaotarajiwa na Wananchi wetu.

4.2 Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato

Mheshimiwa Spika, Mwaka wa Fedha 2017/18 Makisioya makusanyo ya Maduhuli yanakadiriwa kuwa jumla yaShilingi bilioni 360.99 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 370.68kwa mwaka wa fedha 2016/17. Kati ya makusanyo hayoShilingi bilioni 194.39 sawa na asilimia 53.8 zitakusanywa naIdara ya Madini, Shilingi bilioni 166.33 sawa na asilimia 46.6%

Page 193: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

193

zitakusanywa na Idara ya Nishati na Shilingi bilioni 266.40sawa na asilimia 0.1% zitakusanywa na Idara na Vitengovingine katika Wizara.

Makadirio ya makusanyo ya mapato yameshuka kwaasilimia 2.6% ikilinganishwa na makadirio ya makusanyo yamwaka wa fedha 2016/17. Aidha Makusanyo ya maduhulikwa Idara ya Madini yameshuka kwa asilimia 9.98%ikilinganishwa na makusanyo ya Mwaka wa fedha 2016/17.

Kamati inataka kufahamu ni kwa sababu ganiMakusanyo ya Maduhuli kwa Idara ya Madini yanatarajiwakushuka ilhali kama nchi tunatamani Sekta ya Madiniiendelee kutoa mchango mkubwa kwenye pato la Taifa.

4.3 Uchambuzi wa Makadirio ya Matumizi

Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Bajetiya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ni jumla ya Shilingi Bilioni 998,337,759,500 ikilinganishwana Shilingi Trilioni 1,122,845,741,000 zilizoidhinishwa na Bungekwa mwaka 2016/2017. Bajeti hii ya Matumizi imepungua kwaasilimia 11.1%.

Kamati ilitaka ufafanuzi ni kwanini Bajeti hii imeshukakwa kiwango hicho, wakati nchi inatarajia kuendeleza miradimikubwa ya Nishati ambayo inategemewa katika uchumiwa Viwanda. Wizara ilifafanua kuwa Bajeti hii imeshukakutokana na kupungua kwa fedha za nje hasa kwenye Miradiya Maendeleo.

Kamati inaishauri Wizara kuacha kutegemea sanafedha za nje, kwa kuwa zimekuwa hazitolewi kwa wakati nahivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa Miradi yaMaendeleo kwa mwaka husika. Kwa mfano; Bajeti ya nje kwamwaka wa fedha 2016/17 ilikuwa Shilingi Bilioni 331.51. Hadikufikia Machi, 2017 Wizara ilikuwa imepokea Shilingi Bilioni38.57 sawa na asilimia 12% ya Bajeti yote iliyotegemewakatika miradi ya maendeleo.

Page 194: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

194

Fedha za ndani kwa ajili ya REA zimepungua kutokaShilingi Bilioni 534,400,000,000 mwaka 2016/17 hadi ShilingiBilioni 469,090,426,000 kwa mwaka 2017/18, upungufu ambaoni sawa na asilimia 12.2%. Aidha, bajeti hii itatoka kwenyetozo mbalimbali, ambapo tozo za mafuta ni Shilingi354,950,000,000 na tozo ya Umeme ni Shilingi 41,514,000,000na Bajeti ya Serikali ni Shilingi 72,626,426,000.

Mheshimiwa Spika, kupungua kwa Bajeti ya Miradi yaMaendeleo pamoja na mwenendo wa upatikanaji wa fedhaza Miradi ya maendeleo usioridhisha, kama ilivyoshuhudiwakwa mwaka wa fedha 2016/17, kunaweza kusababishamiradi mingi ya kimkakati kushindwa kutekelezwa kamailivyokusudiwa.

Aidha, bajeti ya matumizi ya kawaida kwa mwakawa fedha 2017/18 ni Shilingi Bilioni 59,705,753,500. Bajeti hiiimepungua kwa asilimia 10.2% ikilinganishwa na bajeti yamwaka wa fedha 2016/17 ambayo ilikuwa Shilingi Bilioni66,481,072,000. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 28,833,681,500ni kwa ajili ya matumizi mengineyo (OC), ambazo piazimepungua ikilinganishwa na shilingi Bilioni 38,654,138,000zilizotengwa mwaka 2016/17.

Kuendelea kupungua huku kwa bajeti ya Matumiziya Kawaida kunaweza kupunguza ufanisi katika kusimamiaBajeti ya Miradi ya Maendeleo iliyotengwa kwa Watumishikukosa fedha za kwenda kusimamia Wakandarasiwanaotekeleza miradi hasa ile ya Umeme Vijijini.

Mheshimiwa Spika, Kamati yako hairidhishwi nautekelezaji wa Bajeti ya Wizara inayoidhinishwa na Bunge lakotukufu, kutokana na kiasi cha fedha kinachotolewa kuwakidogo. Kwa mfano; kwa upande wa bajeti ya maendeleo,fedha zinazoidhishwa na Bunge, na kiasi ambacho kimekuwakikitolewa ni chini ya asilimia 50.

Mwenendo huo wa Bajeti hauwezi kuleta tija kwenyeutekelezaji wa miradi inayokusudiwa katika kipindi husika.Ni vyema Serikali ikatenga Bajeti inayotekelezeka kwa

Page 195: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

195

kuanisha miradi michache na kuhakikisha fedha za utekelezajiwake zinapelekwa kikamilifu.

5.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI

Mheshimiwa Spika, baada ya Kamati kutekelezamajukumu yake ya kikanuni ambayo ni ukaguzi wa miradi yamaendeleo, uchambuzi wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajetiya Wizara, kwa mwaka wa fedha 2016/17 na makadirio namatumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2017/18, Kamatiina maoni na ushauri ufuatao:-

5.1 Kwa kuwa, utekelezaji wa Miradi ya Umemeviji j ini katika awamu mbili zi l izokamilika ulikuwa nachangamoto nyingi hasa katika Mikoa ya Tanga naGeita,ambako Kamati ilitembelea na kukagua; Kamatiinashauri kuwa,changamoto zilizobainika ikiwa ni pamoja nabaadhi ya maeneo kurukwa, zipatiwe ufumbuzi wa harakakabla ya kuendelea kwa Mradi wa Umeme vijijini,Awamuya Tatu (REA III) .

5.2 Kamati inaishauri Serikali ikamilishe taratibu zakumaliza changomoto zilizojitokeza na kuchelewesha malipoya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT returns) kwawawekezaji wa sekta ya Madini ili kuendelea kuboresha haliya uwekezaji hapa nchini.

5.3 Pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywana Wizara katika usimamizi wa Madini ya Tanzanite, Kamatiinashauri Serikali kuwa, iangalie upya Mikataba yoteiliyoingiwa na STAMICO na mbia mwenza kama ina tija kwaTaifa.

5.4 Ruzuku kwa Wachimbaji Wadogo iliyotolewana Serikali katika awamu zote mbili kwa kiasi kikubwaimeshindwa kutimiza malengo kwa kukosa usimamizi mzuri.Aidha, ni vema Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madiniikaangalia namna bora ya kusimamia fedha hizi ikiwa nipamoja na kuwapatia mafunzo Wachimbaji na kufuatiliakwa karibu shughuli za Wachimbaji hao.

Page 196: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

196

5.5 Sekta ya Uchimbaji wa Kati imeendelea kukuakwa kiasi cha kuridhisha, hivyo ni vyema Serikali ikaangaliaupya jinsi ya kuisaidia kupata baadhi ya misamaha ya kodikwenye Mafuta na Vipuli vinavyotumika katika shughuli zauchimbaji nchini.

5.6 Leseni zote ambazo zinakiuka Sheria ya Madiniikiwa ni pamoja na kushindwa kuendelezwa kwa muda mrefu,zifutwe na kupewa Wachimbaji Wadogo na wa Kati, kwakuwa wameonesha nia ya dhati ya kuendeleza Sekta hiyonchini.

5.7 Pamoja na Serikali kuandaa MpangoKambambe wa Matumizi ya Gesi Asilia nchini, ni vyemaukafanyika utafiti na upembuzi yakinifu kuhusu miradi yotemikubwa ya usambazaji wa Gesi katika maeneo mbalimbali,ili kuweza kujua kama ina manufaa ya kiuchumi (EconomicValue)kwa Taifa. Hatua hii itasaidia kuepusha nchi kujiingizakwenye mikopo ambayo ni mzigo kwa Taifa.

6.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kukupongezawewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge, kwakazi nzuri mnayoifanya ya kuliongoza Bunge. Mungu awajalieafya njema, hekima na busara, katika kutekeleza wajibu huumkubwa tuliowakabidhi.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa niabaya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini,kwa Mhe. Prof. Sospeter Mhongo, (Mb) - aliyekuwa Waziriwa Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani, (Mb)-Naibu Waziri wa Nishati na Madini, pamoja na Watendajiwote wa Wizara hiyo wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu,Prof. James Mdoe, kwa ushirikiano wao mkubwa kwa Kamatiyetu wakati wote.

Kwa namna ya pekee nawashukuru Wajumbe waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kwamchango wao adhimu katika shughuli za Kamati, katika

Page 197: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

197

kipindi hiki cha uchambuzi wa Bajeti kwa Fungu 58. Ni dhahirishahiri kuwa, bila weledi na ushirikiano walionipa, Kamatiisingeweza kufikia hatua hii ya mafaniko.

Kwa heshima kubwa naomba majina yao katikaorodha ifuatayo yaingizwe kwenye Hansard:-

1.Mhe. Doto Mashaka Biteko, Mb - Mwenyekiti2. Mhe. Deogratius Ngalawa, Mb - M/Mwenyekiti3. Mhe. Mohamed Juma Khatib, Mb - Mjumbe4. Mhe. Ally Mohamed Keissy, Mb - “5. Mhe. Yussuf Kaiza Makame, Mb - “6. Mhe. Zainabu Mussa Bakar, Mb - “7. Mhe. Haroon Mulla Pirmohamed, Mb - “8. Mhe. Mwantakaje Haji Juma, Mb - “9. Mhe. Daimu lddi Mpakate, Mb - “10. Mhe. Catherine Valentine Magige, Mb - “11. Mhe. Oscar Rwegasira Mukasa, Mb - “12. Mhe. Stella Ikupa Alex, Mb - “13. Mhe. Joyce Bitta Sokombi, Mb - “14. Mhe. Bahati Ali Abeid, Mb - “15. Mhe. Mauled Said Abdalah Mtulia, Mb - “16. Mhe. Desderius John Mipata, Mb - “17. Mhe. Katani Ahmad Katani, Mb - “18. Mhe. Susan Limbweni Kiwanga,Mb - “19. Mhe. Vedastus Mathayo Manyinyi, Mb - “20. Mhe. Bupe Nelson Mwakang’ata, Mb - “21. Mhe. Maryam Salum Msabaha, Mb - “22. Mhe. Innocent Lugha Bashungwa,Mb - “23. Mhe. Wilfred Muganyizi Lwakatare, Mb - “24. Mhe. Dunstan Luka Kitandula, Mb - “25. Mhe. John Wegesa Heche, Mb - “26.Mhe. Anne Kilango Malecela, Mb - “

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee napendakumshukuru Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Didimu Kashilillah,Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge, Ndg. AthumanHussein, Mkurugenzi Msaidizi, Ndg. Michael Chikokoto,Makatibu wa Kamati Ndg. Mwanahamisi Munkunda na Ndg.Felister Mgonja, pamoja na Msaidizi wa Kamati, ndg.

Page 198: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

198

Kokuwaisa Gondo, kwa uratibu mzuri wa shughuli zote zaKamati na hatimaye kukamilisha Taarifa hii kwa wakati.

Naomba sasa Bunge lako Tukufu, likubali kuidhinishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Fungu 58 kwa Mwakawa Fedha 2017/2018 ambayo ni Shilingi 998,337,759,500.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na naombakuwasilisha.

Dotto Mashaka Biteko, (Mb)MWENYEKITI

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI01Juni, 2017

NAIBU SPIKA: Sasa tutamsikia Msemaji Mkuu wa Kambiya Upinzani kuhusu Wizara ya Nishati na Madini. (Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA – MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI:Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Hotuba hiiimegawanyika katika sehemu 11 kuanzia (a)mpaka (k) nazimezungumzia kuhusu mchakato wa Katiba Mpya namustakabali wa madini; mapitio ya utekelezaji wa bajeti;sekta ya nishati; sekta ya gesi; nishati jadidifu na teknolojiaya upepo na jua; sekta ya madini; utekelezaji wa Maazimioya Bunge na mwenendo usioridhisha wa mpango wa uwazina uwajibikaji katika tasnia ya uziduaji. Kwa sababu maeneohaya ni mengi na muda ni mfupi, naomba hotuba yote kwaukamilifu wake iingie kwenye Kumbukumbu za Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuna rekebisho katikaukurasa wa tano kwenye aya ya mwisho, maneno “asilimia30 ya dhahabu inayozalishwa” yasomeke “asilimia 30 yamadini yanayozalishwa” kwa sababu dhahabu ni 5% na 25%ni fedha, shaba na madini mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote niungane nawote wenye mapenzi mema katika kuomba ulinzi wa

Page 199: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

199

Mwenyezi Mungu wakati wa kutimiza wajibu wa Kibunge kwamujibu wa Ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, kuishauri na kuisimamia Serikali kwa Wizara yaNishati na Madini juu ya bejeti ya mwaka 2016/2017 naMakadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha2017/2018. Aidha, nitumie fursa hii kuwatakiwa waislamuwote mfungo mwema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitambue mchangoMheshimiwa John Heche, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara yaNishati na Madini alioutoa katika maandalizi ya hotuba hii.Aidha, tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu awezekupona na kurejea katika utekelezaji wa majukumu yake.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie fursa hiikutoa pole kwa familia ya marehemu Mzee PhilemonNdesamburo, wanachama wa CHADEMA kote nchini,wananchi wa Moshi Mjini na Kilimanjaro, Wabunge naWatanzania wote walioguswa na msiba huu. Marehemuatakumbukwa kwa mchango wake kama mmoja wa waasisiwa chama chetu, Mbunge mstaafu na mfanyabiasharamashuhuri, Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema.

Mheshimiwa Naibu Spika, mchakato wa Katiba Mpyana mustakabali wa madini na gesi asilia. Novemba 4, 2016Mheshimiwa Rais alipokuwa akizungumza na Watanzaniakupitia vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es salaam, alinukuliwaakisema hakuwahi kuzungumzia Katiba Mpya wakati wakampeni zake, kwa hiyo si kipaumbele chake na kwambakipaumbele chake ni kuinyoosha nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Serikali hii ya Awamuya Tano ikisema swala la Katiba Mpya sio kipaumbele chake,Watanzania walitoa mapendekezo ya kuwepo kwa vifungukwenye Katiba Mpya vinavyohusika na madini, mafuta nagesi asilia ili kuondoa migogoro inayohusu rasilimali nakuwezesha mali ya nchi na wananchi kunufaika na maliasiliambazo Mwenyezi Mungu amelijalia Taifa letu. Mapendekezo

Page 200: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

200

na matakwa ya wananchi kuhitaji Katiba Mpya kuwa navifungu vinavyohusika na madini, mafuta na gesi asiliayalitokana na ukweli kwamba Katiba ya sasa ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania hususan Ibara ya 27 haijawekamisingi bora ya umiliki, usimamizi na ushughulikiaji wa masualaya rasilimali za nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uzoefu wa nchi nyinginekuhusu Katiba na mustakabali wa madini, mafuta na gesiasilia; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kutoamifano michache juu ya uzoefu wa nchi nyingine ili kuioneshaSerikali hii ni nini hasa kilitokea kwa wenzetu ambao piawalikuwa na tatizo kama la kwetu. Nchini Norway uchimbajiwa mafuta na gesi asilia ulianza mwaka 1971 na kwa sasaNorway ni mojawapo ya nchi zilizofanikiwa kwa kiwangokikubwa katika kuboresha uchumi na maisha ya wananchikutokana na sekta ya mafuta na gesi asilia. Mafanikio yaNorway yalipatikana baada ya kubadili sera zilizokuwazinatoa upendeleo kwa makampuni binafsi na kuweka serazilizokuwa zinatoa kipaumbele kwa maslahi ya nchi nawananchi. Pamaja na hayo Norway iliweka mafuta na gesiasilia katika Katiba yake Ibara ya 110 na msimamo huoukafafanuliwa zaidi na Sheria ya Mafuta. Huu ni mfano waKatiba na sheria kuwekwa kipaumbele na kutumika kamanyenzo ya kunyoosha nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi ya Bolivia ni mfano wapili ambao Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendakuutoa kwa nia na malengo yaleyale. Nchi hii ni miongonimwa nchi ambazo zimejaliwa kuwa na utajiri mkubwa wamafuta na gesi. Pamoja na utajiri huo, wananchi wa Boliviakwa kipindi kirefu walikuwa na malalamiko kuwa mafuta nagesi asili haziwanufaishi. Bolivia ilifanya mabadiliko ya serazake lakini tofauti na Norway, mabadiliko ya Boliviayalisababishwa na malalamiko na vurugu za wananchiwaliokuwa wanataka mabadiliko.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzia miaka ya 2000, nchiya Bolivia i l ishuhudia vurugu na maandamanozilizosababishwa na kile kilichoitwa vita ya maji kutokana

Page 201: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

201

na kupinga kubinafsishwa kwa maji na baadaye vurugu hizizilihamia katika gesi asilia na mafuta.

Aidha, mwaka 2003 vurugu na maandamanomakubwa dhidi ya sera mbovu zilisababisha aliyekuwa Raiswa Bolivia Gonzalo Sanchez de Lozada maarufu kama Gonikujiuzulu na kukimbilia Marekani. Hata hivyo, alirithiwa naMakamu wa Rais ambaye naye alilazimishwa kujiuzulumwaka 2005 kwa maandamano kama mtangulizi wake.Mwaka 2006 Evo Morales alichaguliwa kuwa Rais wa nchihiyo na aliongoza nchi hiyo kupata Katiba Mpya mwaka 2009ambayo pamoja na mambo mengine ilihakikisha kuwamafuta na gesi yananufaisha wananchi wa Bolivia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania pia inayo madini,mafuta na gesi asilia kama zilivyo nchi ambazo mifano yakeimeelezwa, ikumbukwe kwamba mwaka 2013, Tanzaniailishuhudia vurugu na umwagaji wa damu kwa wananchiwasiokuwa na hatia Mkoani Mtwara zilizosababishwa namgogoro wa gesi ambao kiini chake ni madai ya wananchikutonufaika na rasilimali. Mchakato wa mabadiliko ya Katibaulibeba matumaini ya Watanzania kwamba pamoja namambo mengine nchi ingeweka misingi ya wananchikunufaika na rasilimali ikiwemo madini, mafuta na gesi asilia.Hata hivyo, mchakato huo ulikwama na kupunguzamatumaini kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hii inayoongozwana CCM inataka mpaka wananchi waanzishe migomo namaandamano ndiyo itambue kwamba Katiba Mpya nikipaumbele cha wananchi katika masuala ya msingi ikiwemorasilimali za nchi. Hivi ni lini Rais atatambua kwamba Katibana sheria ndio zana muhimu za kunyoosha nchi?

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Wizara yaNishati na Madini kuwa mstari wa mbele kwa kushirikianana Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikisha mchakato wamabadiliko ya Katiba unaendelezwa na masuala ya madinina mafuta yanapewa kipaumbele katika Katiba Mpya.(Makofi)

Page 202: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

202

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wa kufanya katikakipindi hiki ambacho Katiba Mpya haijapatikana. Kwa kuwaTanzania tunakabiliwa na changamoto kubwa katika sektaza madini, mafuta na gesi asilia, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni, inapendekeza kwamba Serikali ilete mbele ya Bungelako Tukufu marekebisho ya sheria ambayo yataweka misingiifuatayo:-

(i) Serikali isimamie shughuli za uvunaji wa madinikatika mfululizo wake wote (entire chain) kuanzia kwenyeuchimbaji ili kuhakikisha kuwa madini yanatoa mchangokatika maendeleo ya kiuchumi ya Taifa.

(ii) Kuwepo na utaratibu wa kutoa leseni kwa njia yazabuni ya wazi badala ya utaratibu wa mikataba kati yaSerikali na mwekezaji. (Makofi)

(iii) Serikali iwe na makampuni ya kutosha yanayowezakuingia katika ubia na makampuni au taasisi zingine aumjumuiko wa makampuni katika shughuli za uvunaji wamadini, mafuta na gesi asili. Serikali pia imiliki hisa kutokanana thamani ya rasilimali za madini yetu. (Makofi)

(iv) Ili kupunguza mianya ya rushwa na kuongezauwajibikaji katika mikataba, iwepo sheria inayotaka Bungekuridhia mikataba yote ya utafutaji na uvunaji wa madini,mafuta na gesi asilia. (Makofi)

(v) Serikali ihakikishe kuwa kwa niaba ya wananchi,Tanzania inanufaika na uvunaji wa madini, mafuta na gesiasilia na usiwepo mkataba wowote unaokiuka misingi hii.

(vi) Uvunaji wa madini, mafuta na gesi asilia uhakikisheunachangia kuboresha maisha ya jamii, ajira na kulindamazingira, kuhakikisha pia maslahi ya Serikali kuu,Halmashauri za Wilaya, vijiji na waathirika wa uwekezajimkubwa wananufaika na miradi hiyo.

(vii) Wananchi ambako uwekezaji unafanyikawashirikishwe kuhusu maamuzi yote yanayohusu utafutaji na

Page 203: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

203

uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia na Halmashaurizao zihusike katika umiliki kupitia hisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, makinikia ama mchangawa dhahabu na hatma ya sekta ya madini nchini. Tarehe 24Mei, 2017 Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alipokea Ripotiya Kamati ya Kwanza ya Rais juu ya kusafirishwa nje kwamakinikia ya dhahabu ama shaba maarufu kama mchangawa dhahabu. Aidha, wakati wa tukio la kukabidhi ripoti hiyo,Mwenyekiti wa Kamati tajwa Profesa Abdulkarim Mrumaalieleza muhuktasari wa matokeo ya ripoti hiyo na Rais alitoakauli mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni vyema ikafahamikakwamba makinikia haya yanahusu migodi miwili yaBulyankulu na Buzwagi chini ya kampuni moja ya Acacia.Makinikia haya yanahusu takribani 30% ya madini, 5% ikiwadhahabu, 25% ikiwa shaba, fedha na madini mengineambayo kwa sheria mbovu na mikataba mibovu ni mali yamwekezaji huku stahili ya nchi ikiwa ni mrabaha wa 4% tu.Ripoti hiyo ya makinikia ama mchanga wa dhahabu haihusumapato ya Taifa na maslahi ya nchi katika 70% ya dhahabuinayopatikana katika mgodi wa Bulyankulu na Buzwagi walahaihusu 100% ya dhahabu na madini mengineyanayopatikana katika migodi mingine nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais makini kabla ya kufikiriamakinikia angefikiria kuhusu madini yanayochimbwa nakuchenjuliwa kwa ukamilifu hapa nchini lakini nchi haipatimapato yanayostahili. Hivyo, taarifa ya Kamati ya ProfesaMruma na kauli za Rais zimeiingiza nchi na wananchi katikamjadala mdogo wa makinikia ama mchanga badala yamjadala mkubwa wa madini na matatizo makubwayaliyopo katika mfumo wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika muktadha huo, kablaya kutoa maoni kuhusu makinikia ama mchanga wadhahabu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa mwitokwa Bunge na wananchi kujadili matatizo makuu ya sektaya madini katika Taifa letu. Matatizo makubwa katika sekta

Page 204: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

204

ya madini katika nchi yetu yamesababishwa na sera na sheriambovu zilizotungwa chini ya Serikali inayoongozwa na CCMna mikataba mibovu iliyoingiwa katika awamu mbalimbali.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapojadili mathalanikukosa mapato kutoka Mgodi wa Bulyankulu ni vyematukakumbuka kuwa katika kipindi cha mwisho cha Rais AliHassan Mwinyi makampuni ya kigeni yaliongezeka kuingiakatika nchi yetu. Kati ya makampuni hayo ni pamoja naSutton Resources ya Vancouver, Canada, iliyopatiwa lesenikwa ajili ya eneo la Bulyanhulu au Butobela mwaka 1994.Leseni hiyo ilitolewa na Mheshimiwa Jakaya Kikwetealipokuwa Waziri wa Maji, Nishati na Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mara baada ya RaisBenjamin Mkapa kuapishwa mwaka 1995 iliandikwa faxbaada ya Rais kuapishwa iliyokuwa na maneno “our manhas been sworn into office, now Bulyankulu file will move.” Nakweli mwaka 1996 wachimbaji wadogo wadogowalihamishwa kwa nguvu na wengine wakidaiwa kufukiwakatika mashimo na Kampuni ya Sutton Resourceswakakabidhiwa eneo hilo. Yaliyofanywa Bulyanhulu pia kwanamna nyingine yamefanyika katika maeneo mengine kwanyakati tofauti ikiwemo Nyamongo, Mererani, Geita naBuzwagi na mengineyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuyawekea makampunihayo mazingira halali ya kisheria ya kunyonya rasilimali zanchi mwaka 1997, Bunge la Jamhuri ya Muunganolilitengeneza matatizo makubwa kwa kutunga sheria mbilimbovu kwa siku moja chini ya hati ya dharura. Kati ya sheriahizo ni Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya Sheriaya Fedha (Financial Laws Miscellaneous Act) ya mwaka 1997ambayo ilifanya marekebisho makubwa katika sheriambalimbali za kodi ambayo yalifuta kwa kiasi kikubwa kodi,tozo na ushuru mbalimbali kwa kampuni za madini. Matokeoya sheria hii ni miaka mingi ya kukosa mapato ya kutoshakatika madini. Sheria nyingine ni ile Sheria ya UwekezajiTanzania (Tanzania Investment Act, 1997) ambayo iliyapa

Page 205: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

205

makampuni ya nje kinga za kisheria za mambo ambayomengine yanalalamikiwa kuhusu makampuni hayo mpakasasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, udhaifu katika mfumomzima wa madini katika nchi yetu ukataasisishwa mwaka1998 kwa Bunge kutunga Sheria ya Madini (Mining Act, 1998).Sheria hii kimsingi i l iweka bayana kwamba madiniyanayopatikana na fedha za mauzo yake ni mali ya mwenyeleseni. Sheria iliruhusu makinikia ama mchanga kusafirishwanje ya nchi kwa ajili ya usafishaji. Nchi yetu kupitia sheria hiiilipaswa kulipwa mrabaha wa asilimia tatu, sheria ya mwaka2010 ilichofanya ni kuongeza tu kiwango mpaka asilimia nnetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwinginesheria zetu zinatoa wajibu kwa makampuni kulipa kodi yamapato ya 30%. Hata hivyo, ni baada ya kupata mapatoyenye kutozwa kodi (taxable income) yaani baada ya kupatafaida. Sheria hizi mbovu zimeruhusu kwa muda mrefumakampuni ya madini kuondoa gharama zote za uzalishajikabla ya kutangaza mapato ya kikodi. Makampuni hayoyametumia mianya hiyo na udhaifu wa taasisi za nchi yetumathalani TMAA na TRA kuweka gharama zisizostahili na hivyokutangaza kupata hasara na kutolipa kodi au kutangazakupata faida kidogo na kulipa kodi kiduchu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais makini alipaswa kablaya kuzuia makinikia ama mchanga kudhibiti mianya kamahii ya upotevu mkubwa wa mapato katika madini. Mfumohuu wa kuepuka kodi ama tax avoidance na kupanga kodiama tax planning ambao umeikosesha nchi mapato kwamuda mrefu umehalalishwa na sheria mbovu za nchi yetu.Rais makini alipaswa kuanza na sheria mbovu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, matokeo ya kuwa na serabomu na sheria mbovu ni mikataba mibovu ambapo kwaupande wa mikataba ya uendelezaji wa madini kati yaSerikali na makampuni makubwa MDAs, mikataba hiyoimeweka misamaha ya kodi na kuachia pia mianya ya

Page 206: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

206

uepukaji wa kodi. Mikataba hiyo mibovu imetoa misamahaambayo mingine hata haipo katika sheria tajwa kwa mfano,Halmashauri zi l izo na migodi ya madini makampuniyameruhusiwa kutoa kiwango cha jumla cha dola laki mbilikwa ajili ya tozo za huduma badala ya kati ya 0.14% na 0.3%ya mapato ya mwaka ya kampuni (annual turn over) ambayoyangekuwa malipo makubwa zaidi kwa Halmashauri zetu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nyakati mbalimbali,tumeomba mikataba hiyo iletwe Bungeni ili ijadiliwe nakupitiwa upya, hata hivyo Serikali hii inayoongozwa na CCMimekuwa ikigoma. Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikalikuileta mikataba hiyo Bungeni na kuwezesha majadiliano yamarekebisho (renegotiation) kati ya Serikali na wawekezaji ilinchi na wananchi waweze kunufaika ipasavyo na rasilimaliambazo Mwenyezi Mungu amelijalia Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala hayahayakuzungumzwa na Mwenyekiti wa Kamati ya MakinikiaProfesa Mruma wala Mheshimiwa Rais wakati akipokea ripotiya mchanga. Badala yake ilitolewa taarifa yenye kuoneshakuwa katika makontena 267 yaliyopo bandari ya Dar esSalaam kiwango cha dhahabu katika makontena yoteambacho ni cha mwezi mmoja tu wa uzalishaji kimetajwakuwa tani 7.8 au wakia 250,000. Kwa mahesabu rahisi tu yakuzidisha kiwango hicho kwa kufanya makadirio ya mwakana kujumlisha na uzalishaji mwingine wa migodi hiyo yaBulyanhulu na Buzwagi tu kunaifanya Tanzania kuwamzalishaji namba tatu wa dhahabu duniani. Hapa kunamwelekeo wa udanganyifu wa kitakwimu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, taswira hasi imeanzakujengeka kimataifa ambapo tarehe 25 Mei, 2017 jarida laMining Journal lilichapisha makala “Trouble in Tanzania”ambayo ilimalizia kwa mwito wa kufanyika kwa “World RiskSurvey” ambayo takwimu za sasa nchi yetu inatarajiwakuporomoka. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaSerikali kuwasilisha Bungeni taarifa kamili ya Kamati hiyoikiwemo metholojia iliyotumika kutathmini sampuli ili ijadiliwe

Page 207: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

207

na Bunge liweze kuazimia kufanya uchunguzi huru kuhusujambo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ikumbukwe kuwa Serikaliiliwahi kuunda Tume ambayo ilijulikana kama Tume yaMheshimiwa Jaji Mark Bomani ambayo ilipewa kazi yakuishauri Serikali kuhusu usimamizi wa sekta ya madini. Aidha,Tume hiyo iligusia kipengele cha uchenjuaji na usafishaji wamadini. Katika ukurasa wa 157 wa Taarifa ya Kamati ya Raisya kuishauri Serikali kuhusu usimamizi wa sekta ya madini yamwaka 2008 Kamati i l isema na ninanukuu; “Kamatiimechambua hali halisi ya shughuli za uchenjuaji na usafishaji(smelting and refinery) wa madini hapa nchini na kuona kuwashughuli hizi hazifanyiki katika kiwango cha kuridhisha. Aidha,hakuna miundombinu hasa umeme na reli ya kuwezeshakuanzishwa kwa shughuli hizo. Hali hii imetokana nakutokuwepo kwa mkakati wa kisera wa kuhamasishauwekezaji katika uchenjuaji na usafishaji wa madini hapanchini.”

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa hiyo iliendeleakusema kuwa; “Kamati ilibaini kuwa kukosekana kwashughuli hizi hapa nchini kunazifanya kampuni kama vileBulyanhulu Gold Mine Limited kusafirisha mchanga (copperconcetrate) kwenda Japan na China ili kuchenjuliwa. Halihii isiporekebishwa, italazimisha mgodi wa Kabanga Nickelunaotarajiwa kuanzishwa kupeleka mchanga nje ya nchikwa ajili ya kuchenjuliwa. Hii itaifanya Serikali kutokuwa nauhakika wa kiasi na aina ya madini yaliyomo katika mchangahuo na inaweza kuathiri mapato ya Serikali.”

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati katikamapendekezo yake kwa Serikali kuhusu kipengele hiki,ilipendekeza; “Serikali iweke mikakati katika Sera ya Madinina kutunga au kurekebisha Sheria ya Madini ili kuingizavipengele vitakavyowezesha uanzishwaji na uimarishwaji waviwanda vya uchenjuaji na usafishaji wa madini hapa nchini.”

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais Magufuli alikuwaMjumbe wa Baraza la Mawiziri wakati taarifa hii inawasilishwa

Page 208: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

208

kwa Rais Jakaya Kikwete. Aidha, Rais Magufuli alikuwa namuda toka alipoingia madarakani kuweza kushughulikiajambo hili katika hali yenye kuepusha migogoro isiyo yalazima. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa mwito kwaBunge kuingilia kuishauri na kuisimamia Serikali kwamustakabali mwema wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niongelee mapitio yautekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2016/2017. Kwa mwaka wafedha 2016/2017 Wizara ya Nishati na Madini iliidhinishiwajumla ya shilingi 1,122,583,517,000 na kati ya fedha hizo shilingi1,056,354,669,000 zilikuwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Aidha, hadi kufikia tarehe 13 Machi, 2017 fedhazilizokuwa zimetolewa na Hazina kwa ajili ya kutekelezamiradi ya maendeleo ni shilingi 372,877,980,724 tu sawa naasilimia 35 ya fedha zote za maendeleo zilizotengwa kwamwaka 2016/2017. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia takwimuzil izooneshwa hapo juu utabaini kwamba miradi yamaendeleo ilitekelezwa kwa kiwango cha asilimia 35 tu.Miradi iliyokwama ni pamoja na miradi ya umeme vijijini.Aidha, miradi hii inatekelezwa kwa kiwango hicho pamojana sababu nyingine ni kutokana na Taifa kukosa fedha zawafadhili kwa miradi ya umeme ikiwemo miradi ambayoingepata ufadhili wa MCC . Kwa maneno mengine,Watanzania wameshindwa kunufaika na miradi yamaendeleo kutoka kwa wafadhili kutokana na kukosekanakwa utawala bora, kuvurugwa kwa uchaguzi Zanzibar nauvunjifu wa haki za binadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali hiiiliwaaminisha Watanzania kuwa miradi itatekelezwa kwagharama za fedha za ndani katika kipindi cha bajeti chamwaka wa fedha 2016/2017, Kambi Rasmi ya UpinzaniBungeni inataka kupata majibu ya kina kuhusu sababuzilizopelekea Serikali kushindwa kutekeleza bajeti yake hukuikijinadi ndani ya Bunge hili Tukufu kwamba fedha za MCChazina madhara na Taifa litatekeleza miradi kwa fedha zake.

Page 209: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

209

Je, kwa mwendo huu ni l ini Taifa l itafikia malengotuliyojiwekea kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo yaTaifa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa Maazimioya Bunge. Bunge hili limekuwa likitoa Maazimio mbalimbaliyanayohitaji utekelezaji wa Serikali lakini kwa bahati mbayasana Bunge limekuwa halipatiwi mrejesho wa utekelezwajiwa Maazimio hayo. Tafsiri ya jambo hili ni dharau au nikutokana na ukweli kwamba Bunge hili halina meno. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge la Kumi lilipitishaMaazimio baada ya Kamati ya PAC kupitia Taarifa ya Mdhibitina Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusiana na fedhaza capacity charge ambazo TANESCO ilikuwa inatakiwakuilipa IPTL lakini kukawepo na kesi ya kupinga kiwango hichocha malipo na kulazimu fedha hizo kuwekwa Benki Kuu kwakufungua akaunti iliyoitwa Tegeta Escrow Account.

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 28 Novemba, 2014,Bunge lilipitisha Maazimio nane kuhusiana na uporwaji wamabilioni ya fedha za Serikali zilizowekwa Benki Kuu. Azimiomoja lililokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na utendajiwa TANESCO ni Azimio namba saba, nanukuu; “Bungelinaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununuamitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwaTANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo.”

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa Bunge halijapewataarifa ya utekelezaji wa Azimio hilo na hadi sasa TANESCObado inalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3 kila mwezi kwa IPTL.Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ni kwa nini Serikaliimeshindwa kutekeleza Azimio hilo na inaendelea kumlipamtu aliyeinunua IPTL katika mazingira yenye ufisadi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Spika Anne Makinda aliundaKamati Maalum ya Bunge kwenda kuzungumza na wananchiwa Mtwara kuhusu sakata la ujengwaji wa bomba la gesiasilia kutoka mkoani humo mpaka Dar es Salaam, kufuatiakuzuka kwa vurugu za tarehe 22 Mei 2013. Kamati hiyo ya

Page 210: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

210

Mheshimiwa Spika Makinda ilikuwa chini ya Mbunge waMuleba Kaskazini, Charles Mwijage ambaye leo amesomahotuba kwa niaba ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati hii ya Bunge ilitumiafedha za walipa kodi na ilifanya kazi hiyo na kuiwasilisha kwaMheshimiwa Spika tarehe 20 Desemba, 2013. Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inamtaka Spika kuwezesha taarifa hiyokuwasilishwa Bungeni ili mapendekezo ya Kamati hiyoyajadiliwe na Bunge na kuwa maazimo rasmi ya Bungekuweza kutekelezwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, yamekuwepo piamaazimio mengine ya Bunge juu ya uchunguzi kuhusiana namapato na ufisadi kwenye gesi asilia hususani juu ya Kampuniya Pan African Energy Tanzania (PAT) ambayo nayo Serikalihaijawasilisha taarifa ya kuhitimisha utekelezaji mpaka hivisasa. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikalikuwasilisha Bungeni taarifa maalum juu ya utekelezaji waMaazimio yote ya Bunge yanayohusu Wizara ya Nishati naMadini ambayo hayajatekelezwa mpaka hivi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, makadirio ya mapato namatumizi kwa mwaka wa fedha 2017/ 2018; katika mwakawa fedha 2017/2018 Wizara ya Nishati na Madini inakadiriakutumia jumla ya shilingi 998,337,759,500 ikilinganishwa nashilingi 1,122,583,517,000 zilizoidhinishwa na Bunge mwaka2016/2017 sawa na upungufu wa asilimia 11. Sababuzinazotolewa na Serikali za kupungua kwa bajeti ni kupunguakwa makadirio ya fedha za nje kutoka shilingi 331,513,169,000mwaka 2016/ 2017 hadi shilingi 175,327,327,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, madhara ya kukosekanakwa fedha za nje…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, kengele ya pil iimeshagonga, una dakika moja, malizia.

Page 211: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

211

MHE. JOHN J. MNYIKA - MSEMAJI MKUU WA KAMBIRASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI:Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinapenda kusisitiza kama ambavyo imekuwa ikifanya katikahotuba zilizowahi kutangulia kwamba, sehemu kubwa yamatatizo ya Wizara ya Nishati na Madini yamechangiwa nayanaendelea kuchangiwa na sababu za kibinadamuikiwemo ukosefu wa utashi wa kisiasa huku masuala muhimuyakiachwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Taifa bado linahitajimabadiliko ya kimfumo ili kuwezesha hatua za haraka zakusimamia sera sahihi, uongozi makini na taasisi thabiti katikasekta ya nishati na madini pamoja na kuchukua hatua stahikiili kuziwezesha sekta hizi za nishati na madini kuongeza patola Taifa na kupelekea wananchi kuzifaidi rasilimali zao kulikomatamko hewa yanayolenga kupata umaarufu wa kisiasa,huku hatua zinazopaswa kuchukuliwa zikiachwa miakanenda rudi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mnyika.

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANIBUNGENI WIZARA YA NISHATI NA MADINI MHESHIMIWA

JOHN JOHN MNYIKA (MB), KUHUSU UTEKELEZAJI WA BAJETIYA WIZARA KWA MWAKA 2016/2017 NA MAKADIRIO YA

MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA2017/ 2018 KAMA ILIVYOWASILISHWA MEZANI

(Inatolewa chini ya 99(9) ya kanuni za Bunge,Toleo la Mwaka, 2016)

A. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika, Awali ya yote niungane na wenyemapenzi mema katika kuomba ulinzi wa mwenyezi Munguwakati wa kutimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa Ibaraya 63 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kuishauri na kuisimamia Serikali kwa Wizara ya Nishati naMadini juu ya bajeti ya mwaka 2016/2017 na makadirio ya

Page 212: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

212

mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/2018.Aidha, nitumie fursa hii kuwatakia waislamu wote mfungomwema katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mheshimiwa Spika, Nitambue mchango MheshimiwaJohn Heche, Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati naMadini alioutoa katika maandalizi ya hotuba hii. Aidhatuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kuponana kurejea katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kutoapole kwa familia ya marehemu Mzee Philemon Ndesamburo,wanachama wa CHADEMA kote nchini, wananchi wa MoshiMjini, wabunge na watanzania wote walioguswa na msibahuu. Marehemu atakumbukwa kwa mchango wake kamammoja wa waasisi wa chama chetu, Mbunge wa Mstaafuna Mfanyabiashara Mashuhuri. Mwenyezi Mungu amlazemahali pema.

B. MCHAKATO WA KATIBA MPYA NAMUSTAKABALI WA MADINI, MAFUTA NA GESI ASILIA

Mheshimiwa Spika, Novemba 4, 2016 MheshimiwaRais alipokuwa akizungumza na watanzania kupitia vyombovya habari, ikulu jijini Dar es salaam alinukuliwa akisemahakuwahi kuzungumzia katiba mpya wakati wa kampenizake, kwa hiyo siyo kipaumbele chake na kwambaanachotaka kwanza ni kunyoosha nchi.

Mheshimiwa Spika, wakati Serikali hii ya awamu yatano ikisema swala la katiba mpya kama siyo kipaumbelechake, watanzania walitoa mapendekezo ya kuwepo kwavifungu kwenye katiba mpya vinavyohusika na madini,mafuta na gesi asilia il i kuondoa migogoro ambayoinayohusu rasilimali na kuwezesha nchi na wananchi kunufaikana maliasili ambazo Mwenyezi Mungu amelijalia taifa letu.

Mheshimiwa Spika, mapendekezo na matakwa yawananchi kuhitaji katiba mpya kuwa na vifunguvinavyohusika na madini, mafuta na gesi asilia, yalitokana

Page 213: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

213

na ukweli kwamba katiba ya sasa ya Jamhuri ya muunganowa Tanzania hususan ibara ya 27 haijaweka misingi bora yaumiliki, usimamizi na ushughulikiaji wa masuala yanayohusurasilimali za nchi.

1. Uzoefu wa nchi nyingine kuhusu katiba namustakabali wa madini, mafuta na gesi asilia

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinapenda kutoa mifano michache juu ya uzoefu wa nchinyingine ili kuionesha Serikali ni nini hasa kilitokea kwawenzetu, ambao nao pia walikuwa na tatizo kama la kwetu.Nchi ya Norway ilianza uchimbaji wa mafuta na gesi asiliamwaka 1971 na kwa sasa Norway ni mojawapo ya nchizilizofanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuboresha uchumina maisha ya wananchi wake kutokana na sekta ya mafutana gesi asilia. Mafanikio ya Norway yalipatikana baada yakubadili sera zilizokuwa zinatoa upendeleo kwa makampunibinafsi na kuweka sera zilizokuwa zinatoa kipaumbele kwamaslahi ya nchi na wananchi. Pamaja na hayo, Norwayiliweka mafuta na gesi asilia katika katiba yake, ibara ya110b na msimamo huo ukafafanuliwa zaidi na sheria yamafuta. Huu ni mfano wa katiba na sheria kuwekwakipaumbele na kutumika kama nyenzo ya kunyoosha nchi.

Mheshimiwa Spika, Nchi ya Bolivia ni mfano wa piliambao Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia inapendakuutoa kwa nia na malengo yaleyale. Nchi hiyo ni miongonimwa nchi ambazo zimejaliwa kuwa na utajiri mkubwa wamafuta na gesi. Pamoja na utajiri huo, wananchi wa Boliviakwa kipindi kirefu walikuwa na malalamiko kuwa mafutana gesi asilia haziwanufaishi. Bolivia ilifanya mabadiliko yasera zake lakini tofauti na Norway, mabadiliko ya Boliviayalisababishwa na malalamiko na vurugu za wananchiwaliokuwa wanataka mabadiliko.

Mheshimiwa Spika, kuanzia miaka ya 2000, nchi yaBolivia ilishuhudia vurugu na maandamano zilizosababishwa

Page 214: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

214

na kile kilichoitwa vita vya maji kutokana na kupingakubinafisishwa kwa maji na baadaye vurugu hizo zilihamiakatika gesi asilia na mafuta. Aidha mwaka 2003 vurugu namaandamano makubwa dhidi ya sera mbovu zilisababishaaliyekuwa Rais wa Bolivia Gonzalo Sanchez de Lozada“Goni” kujiuzulu na kukimbilia Marekani. Hata hivyo alirithiwana makamu wa Rais ambaye pia alilazimishwa kujiuzulumwaka 2005 kwa maandamano kama mtangulizi wake.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2006 Evo Moralesalichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo na aliongoza nchi hiyokupata katiba mpya mwaka 2009 ambayo pamoja namambo mengine ilihakikisha kuwa mafuta na gesi asiliayananufaisha wananchi wa Bolivia.

Mheshimiwa Spika, Tanzania pia inayo madini,mafuta na gesi asilia kama zilivyo nchi ambazo mifano yakeimeelezwa hapo juu. Ikumbukwe kwamba mwaka 2013Tanzania ilishuhudia vurugu na umwagaji wa damu kwawananchi wasiokuwa na hatia mkoani Mtwarazilisababishwa na mgogoro wa gesi ambao kiini chake nimadai ya wananchi kutokunufaika na rasilimali. Mchakatowa mabadiliko ya katiba ulibeba matumaini ya watanzaniakwamba pamoja na mambo mengine nchi ingeweka misingiya wananchi kunufaika na rasilimali ikiwemo madini, mafutana gesi asili. Hata hivyo mchakato huo ulikwama nakupunguza matumaini ya wananchi. Serikali hiiinayoongozwa na CCM inataka mpaka wananchiwaanzishe migomo na maandamano ndio itambuekwamba katiba mpya ni kipaumbele cha wananchi katikamasuala mengi ikiwemo juu ya rasilimali za nchi? Hivi ni liniRais atatambua kwamba katiba na sheria ni zana muhimuza kunyoosha nchi? Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitakaWizara ya Nishati na Madini kuwa mstari wa mbelekushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kuhakikishamchakato wa mabadiliko ya katiba unaendelezwa namasuala ya madini, mafuta na gesi yanapewa kipaumbelekatika katiba mpya.

Page 215: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

215

2. Ushauri wa kufanya katika kipindi hikiambacho katiba mpya haijapatikana

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Tanzania tunakabiliwana changamoto katika sekta ya madini, mafuta na gesiasilia, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inapendekezakwamba, Serikali i lete mbele ya Bunge lako tukufumarekebisho ya sheria ambayo yataweka misingi ifuatayo;

• Serikali isimamie shughuli za uvunaji wa madinikatika mfululizo wake wote (entire production chain) kuanziakwenye uchimbaji ili kuhakikisha kuwa madini yanatoamchango katika maendeleo ya kiuchumi ya Taifa.

• Kuwepo kwa utaratibu wa kutoa leseni kwanjia ya zabuni ya wazi badala ya utaratibu wa mikatabakati ya Serikali na mwekezaji.

• Serikali iwe na makampuni yake yanayowezakuingia katika ubia na makampuni au taasisi zingine aumjumuiko wa kampuni katika shughuli za uvunaji wa madini,mafuta na gesi asili Tanzania. Serikali pia imiliki hisa kutokanana thamani ya rasilimali zetu.

• I l i kupunguza mianya ya rushwa nakuongezeka kwa uwajibikaji katika mikataba, iwepo sheriainayotaka bunge kuridhia mikataba yote utafutaji na uvunajiwa Madini, Mafuta na gesi asilia.

• Serikali ihakikishe kwa niaba ya wananchi,Tanzania inanufaika na uvunaji wa madini, mafuta na gesiasilia, na usiwepo mkataba wowote unaokiuka misingi hii.

• Uvunaji wa madini, mafuta na gesi asiliauhakikishe unachangia kuboresha maisha ya jamii, ajira nakulinda mazingira, kuhakikisha pia maslahi ya Serikali kuu,halmashauri za wilaya, vijiji na waathirika wa uwekezajimkubwa wananufaika na miradi iliyopo.

Page 216: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

216

• Wananchi ambako uwekezaji utafanyikawashirikishwe kuhusu maamuzi yeyote yanayohusu utafutaji,na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia na halmashaurizao zihusike katika umiliki kupitia hisa.

3. Makinikia ama “Mchanga wa Dhahabu” naHatma ya Sekta ya Madini Nchini

Mheshimiwa Spika, Tarehe 24 Mei 2017 MheshimiwaRais Dr John Magufuli alipokea ripoti ya Kamati ya Kwanzaya Rais juu ya kusafirishwa nje kwa makinikia ya dhahabu/shaba. (Maarufu kama “Mchanga wa Dhahabu”). Aidha,wakati wa tukio la kukabidhi ripoti hiyo Mwenyekiti wa Kamatitajwa Prof Abdulkarim Mruma alieleza muhuktasari wamatokeo ya ripoti hiyo na Rais alitoa kauli mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, Ni vyema ikafahamika kwambamakinikia haya yanahusu migodi miwili ya Bulyankulu naBuzwagi chini ya kampuni moja ya Acacia. Makinikia hayayanahusu takribani asilimia 30 ya dhahabu inayozalishwakatika migodi hiyo ambayo kwa sheria mbovu na mikatabamibovu ni mali ya mwekezaji. Huku stahili ya nchi ikiwamrabaha wa asilimia nne (4%) tu. Ripoti hiyo ya makinikiaama ‘mchanga wa dhahabu’ haihusu mapato ya taifa namaslahi ya nchi katika asilimia 70 ya dhahabu inayopatikanakatika migodi ya Bulyankulu na Buzwagi wala haihusu asilimia100 ya dhahabu na madini mengine yanayopatikana katikamigodi mingine nchini.

Mheshimiwa Spika, Rais makini kabla ya kufikiriamakinikia angefikiria kuhusu madini yanayochimbwa nakuchenjuliwa kwa ukamilifu hapa nchini lakini nchi haipatimapato yanayostahili. Hivyo, taarifa ya kamati ya Prof Mrumana kauli za Rais zimeiingiza nchi na wananchi katika mjadalamdogo wa makinikia ama mchanga badala ya mjadalamkubwa madini na matatizo makubwa yaliyopo katikamfumo wetu.

Mheshimiwa Spika, katika muktadha kabla ya kutoamaoni kuhusu makinikia ama mchanga Kambi Rasmi ya

Page 217: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

217

Upinzani inatoa mwito kwa Bunge na wananchi kujadilimatatizo makuu ya sekta ya madini katika taifa letu. Matatizomakubwa katika sekta ya madini katika nchi yetuyamesababishwa na sera na sheria mbovu zilizotungwa chiniya Serikali inayoongozwa na CCM na mikataba mibovuiliyoingiwa katika awamu mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, tunapojadili mathalani kukosamapato kutoka mgodi wa Bulyankulu ni vyema tukakumbukakuwa katika kipindi cha mwisho cha Rais Ali Hassan Mwinyimakampuni ya kigeni yaliongezeka kuingia katika nchi yetu.Kati ya makampuni hayo ni pamoja Kampuni ya SuttonResources ya Vancouver, Canada, iliyopatiwa leseni kwa ajiliya eneo la Bulyanhulu/Butobela mwaka 1994. Leseni hiyoilitolewa na Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipokuwa Waziriwa Maji, Nishati na Madini. Mara baada ya Rais BenjaminMkapa kuapishwa mwaka 1995 iliandikwa fax baada ya Raiskuapishwa iliyokuwa na maneno “our man has been sworninto office, now Bulyankulu file will move”. Na kweli Mwaka1996, wachimbaji wadogo wadogo walihamishwa kwanguvu huku mengine wakidaiwa kufukiwa katika mashimona kampuni ya Sutton Resources wakakabidhiwa eneo hilo.Yaliyofanywa Bulyankulu yalifanywa pia kwa namna nyinginekatika maeneo mengine kwa nyakati tofauti tofauti ikiwemoNyamongo, Mererani, Geita na Buzwagi.

Mheshimiwa Spika, ili kuyawekea makampuni hayomazingira halali ya kisheria ya ‘kunyonya rasilimali nchi’Mwaka 1997, Bunge la Jamhuri ya Muungano lilitengenezamatatizo kwa kutunga sheria mbili mbovu kwa siku mojachini ya hati ya dharura. Kati ya sheria hizo ni Sheria yaMarekebisho mbali mbali ya Sheria za Fedha (Financial LawsMiscellaneous Amendments Act, 1997) ambayo ilifanyamarekebisho makubwa katika sheria mbali mbali za kodiambayo yalifuta kwa kiasi kikubwa kodi, tozo na ushuru mbalimbali kwa makampuni ya madini. Matokeo ya sheria hii nimiaka mingi ya kukosa mapato ya kutosha katika madini.Sheria nyingine ni ile ya Uwekezaji Tanzania (TanzaniaInvestment Act, 1997) ambayo iliyapa makampuni ya nje kinga

Page 218: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

218

za kisheria za mambo ambayo mengine yanalalamikiwakuhusu makampuni hayo mpaka sasa.

Mheshimiwa Spika, udhaifu katika mfumo mzima wamadini katika nchi yetu ukataasisishwa mwaka 1998 kwaBunge kutunga Sheria ya Madini (Mining Act, 1998). Sheria hiikimsingi iliweka bayana kwamba madini yanayopatikana nafedha za mauzo yake ni mali ya mwenye leseni. Sheria iliruhusumakinikia ama mchanga kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili yausafishaji. Nchi yetu kupitia Sheria hii ilipaswa kulipwamrabaha wa asilimia 3, sheria ya mwaka 2010 imeongeza tukiwango kuwa asilimia 4.

Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine sheria zetuzinatoa wajibu wa makampuni hayo kulipa kodi ya mapatoya asilimia 30, hata hivyo ni baada ya kupata ‘mapato yenyekuweza kutozwa kodi’ (taxable income); yaani baada yakupata faida. Sheria hizo mbovu zimeyaruhusu kwa mudamrefu makampuni ya madini kuondoa gharama zote zauzalishaji kabla ya kutangaza mapato ya kikodi. Makampunihayo yametumia mianya hiyo na udhaifu wa taasisi za nchiyetu mathalani TMAA na TRA kuweka gharama zisizostahilina hivyo kutangaza kupata hasara na kutolipa kodi aukutangaza faida ndogo na kulipa kodi kiduchu. Rais makinialipaswa kabla ya kuzuia makinikia ama mchanga kudhibitimianya kama hii ya upotevu mkubwa wa mapato katikamadini. Mfumo huu wa ‘kuepuka kodi’ (tax avoidance) na‘kupanga kodi’ (tax planning) ambao umeikosesha nchimapato kwa muda mrefu umehalalishwa na sheria mbovuza nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, matokeo ya kuwa na sera bomuna sheria mbovu ni mikataba mibovu ambapo kwa upandewa Mikataba ya Uendelezaji wa Madini (MDAs) kati ya Serikalina makampuni makubwa, mikataba hiyo imewekamisamaha ya kodi na kuachia pia mianya ya uepukaji wakodi. Mikataba hiyo mibovu imetoa misamaha ambayomingine hata haipo katika sheria tajwa kwa mfano kwahalmashauri zi l izo na migodi ya madini makampuniyameruhusiwa kutoa kiwango cha ujumla cha dola laki mbili

Page 219: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

219

kwa ajili ya tozo ya huduma badala ya asilimia kati ya 0.14na 0.3 ya mapato ya mwaka ya kampuni (annual turn over)ambayo yangekuwa malipo makubwa zaidi. Kwa nyakatimbalimbali tumeomba mikataba iletwe Bungeni ili ijadiliwena kupitiwa upya hata hivyo Serikali imekuwa ikigoma. KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuileta mikataba hiyoBungeni na kuwezesha majadiliano ya marekebisho(renegotiation) kati ya Serikali na wawekezaji ili nchi nawananchi waweze kunufaika ipasavyo na rasilimali ambazoMwenyezi Mungu amelijalia taifa letu.

Mheshimiwa Spika, masuala haya hayakuzungumzwana Mwenyekiti wa ‘kamati ya makinikia’ wala MheshimiwaRais wakati akipokea ‘ripoti ya mchanga’. Badala yakeilitolewa taarifa yenye kuonyesha kuwa katika makontena277 yaliyopo bandari ya Dar Es Salaam kiwango chadhahabu katika makontena yote ambacho ni cha mwezimmoja tu wa uzalishaji kimetajwa kuwa tani 7.8 (au wakia250,000). Kwa mahesabu rahisi tu ya kuzidisha kiwango hichokwa kufanya makadirio ya mwaka na kujumlisha na uzalishajimwingine wa migodi hiyo miwili ya Bulyankulu na Buzwagi tukunaifanya Tanzania kuwa mzalishaji namba tatu wadhahabu duniani!.

Mheshimiwa Spika, hapa kuna mwelekeo waudanganyifu wa kitakwimu. Taswira hasi imeanza kujengekakimataifa ambapo tarehe 25 May 2017 jarida la Mining Journallilichapisha makala “Trouble in Tanzania” ambayo ilimaliziakwa mwito wa kufanyika kwa ‘World Risk Survey’. KambiRasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kuwasilisha Bungeni taarifakamili ya kamati hiyo ikiwemo metholojia iliyotumikakutathmini sampuli ijadiliwe na Bunge liweze kuazimiauchunguzi huru uweze kufanyika.

Mheshimiwa Spika, Ikumbukwe kuwa Serikali iliwahikuunda tume ambayo ilijulikana kama, tume ya MheshimiwaJaji Mark Bomani, ambayo ilipewa kazi ya kuishauri Serikalikuhusu usimamizi wa sekta ya madini. Aidha tume hiyo iligusiakipengele cha uchenjuaji na usafishaji wa Madini. Katikaukurasa 157 wa taarifa ya kamati ya Rais ya kuishauri Serikali

Page 220: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

220

kuhusu usimamizi wa sekta ya Madini ya mwaka 2008 kamatiilisema na nina nukuu “Kamati imechambua hali halisi yashughuli za uchenjuaji na usafishaji (smelting and refinery) wamadini hapa nchini…na kuona kuwa shughuli hizi hazifanyikikatika kiwango cha kuridhisha. Aidha hakuna miundombinuhasa umeme na reli ya kuwezesha kuanzishwa kwa shughulihizo. Hali hii imetokana na kutokuwepo kwa mkakati wa kiserawa kuhamasisha uwekezaji katika uchenjuaji na usafishaji wamadini hapa nchini”

Mheshimiwa Spika, Taarifa hiyo inaendelea kuwa“kamati ilibaini kuwa kukosekana kwa shughuli hizi hapanchini kunazifanya kampuni kama vile Bulyankulu Gold MineLimited kusafirisha mchanga (Copper Concetrate) kwendaJapan na China ili kuchenjuliwa. Hali hii isiporekebishwa,italazimisha mgodi wa Kabanga Nickel unaotarajiwakuanzishwa kupeleka mchanga nje ya nchi kwa ajili yakuchenjuliwa. Hii itaifanya Serikali kutokuwa na uhakika wakiasi na aina ya madini yaliyomo katika mchango huo nainaweza kuathiri mapato ya Serikali”. Kamati katikamapendekezo yake kwa Serikali, kuhusu kipengele hiki,ilipendekeza “Serikali iweke mikakati katika sera ya madinina kutunga au kurekebisha sheria ya madini ili kuingizavipengele vitakavyowezesha uanzishwaji na uimarishwaji waviwanda vya uchenjuaji na usafishaji wa madini hapa nchini”.Rais Magufuli alikuwa mjumbe wa baraza la mawiziri wakatitaarifa hii inawasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete. Aidha, RaisMagufuli alikuwa na muda toka alipoingia madarakanikuweza kushughulikia jambo hili katika hali yenye kuepushamigogoro isiyo ya lazima. Kambi Rasmi ya Upinzani inatoamwito kwa Bunge kuingilia kuishauri na kuisimamia Serikalikwa mustakabali mwema wa sekta ya madini nchini.

C. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI KWAMWAKA 2016/2017

Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2016/2017Wizara ya Nishati na Madini iliidhinishiwa jumla ya shilingi1,122,583,517,000 na kati fedha hizo, shilingi 1,056,354,669,000zilikuwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Aidha hadi kufikia

Page 221: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

221

tarehe 13 Machi, 2017 fedha zilizokuwa zimetolewa na hazinakwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ni shilingi372,877,980,724 tu sawa na 35% ya fedha zote za maendeleozilizotengwa kwa mwaka 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia takwimu zilizooneshwahapo utabaini kwamba, miradi ya maendeleo ilitekelezwakwa 35% tu. Miradi iliyokwama ni pamoja na ya umeme vijijini.Aidha Miradi hii inatekelezwa kwa kiwango hicho pamojana sababu nyingine ni kutokana na Taifa hili kukosa fedha zawafadhili kwenye miradi ya umeme ikiwemo miradi ambayoingepata ufadhili wa MCC. Kwa maneno menginewatanzania wameshindwa kunufaika na miradi yamaendeleo kutoka kwa wafadhili kutokana na kukosekanakwa utawala bora, kuvurugwa kwa uchaguzi wa Zanzibarna uvinjifu wa haki za Binadamu.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuwa Serikali iliwaaminishawatanzania kuwa miradi itatekelezwa kwa gharama zafedha za ndani katika kipindi cha Bajeti cha mwaka wa fedha2016/2017. Kambi Rasmi ya Upinzani inataka kupata majibuya kina, kuhusu sababu zilizopelekea Serikali kushindwakutekeleza bajeti yake, huku ikijinadi ndani ya Bunge hili tukufukwamba fedha za MCC hazina madhara na Taifa litatekelezamiradi kwa fedha zake! Je, kwa mwendo huu ni lini Taifalitafikia malengo tuliyojiwekea kwa mujibu wa Mpango waMaendeleo ya Taifa?

D. SEKTA YA NISHATI

1. Shirika la umeme Tanzania – TANESCO

i. Usimamizi wa kampuni Binafsi za uzalishajiumeme na gharama za kuiuzia TANESCO

Mheshimiwa Spika, Shirika la umeme Tanzania,TANESCO katika jitihada za kuhakikisha kunakuwa naupatikanaji wa uhakika wa umeme nchini, shirika liliingiamikataba na makampuni binafsi yanayozalisha umeme kwalengo la kuiuzia TANESCO. Aidha taarifa ambazo kambi Rasmi

Page 222: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

222

ya Upinzani Bungeni inazo ni kwamba, TANESCO inanunuaumeme kwa bei ya wastani wa shilingi 544.65 kwa kila “unit”na kuuza kwa shilingi 279.35 na hivyo kulifanya shirika kupatahasara ya shilingi 265.3 kwa kila unit.

Mheshimiwa Spika, kabla ya kusitishwa kwa mkatabana kampuni ya Symbion, TANESCO ilikuwa inalipa jumla yadola za Marekani milioni 16.36 kama capacity charge kwamakampuni yanayozalisha umeme wa dharura. Taarifaambazo Kambi Rasmi ya Bunge lako Tukufu inazo zinaoneshakwamba Kwa sasa, Shirika linatumia Dola za Marekani milioni9.75 kwa mwezi kununua umeme kutoka Aggreko, Songasna IPTL na gharama za umeme zinazolipwa na TANESCO kwamwezi ni Dola za Marekani milioni 9.75.

Mheshimiwa Spika, Bei za nishati ya umemeinayotozwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)zinadhibitiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji(EWURA) kila robo mwaka baada ya mapitio ya gharamahalisi za uzalishaji. Aidha kwa mujibu wa tarifa ambazo KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inazo ni kuwa mapitio ya kila robomwaka ya bei ya nishati ya umeme hayahusishi madeniyaliyojitokeza kabla ya kuanzishwa kwa utaratibu wa mapitioya bei ya umeme ya robo mwaka. Hivyo, utaratibu huuMheshimiwa Spika, hauiwezeshi TANESCO kulipa madeni yoteinayodaiwa.

Mheshimiwa Spika, bei ya umeme inayopitishwa naEWURA haionyeshi gharama halisi zilizotumiwa na TANESCOjambo linaloathiri uwezo wa TANESCO katika kulipa madeniyanayolikabili Shirika. Kambi Rasmi ya Bunge lako Tukufuinaishauri Serikali kupitia EWURA kuzipitia kwa umakinigharama za umeme ili kuhakikisha kuwa gharama zote zauzalishaji wa umeme zinahusishwa, ili hatimaye, kusaidiaupatikanaji wa faida baada ya uwekezaji wenye lengo lakuboresha huduma na kuongeza matokeo chanya kwaTANESCO.

Mheshimiwa Spika, shughuli za TANESCO zinahusishapia utekelezaji wa mikataba mbalimbali ikiwemo iliyoridhiwa

Page 223: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

223

kipindi cha Serikali za awamu zilizotangulia. Miongoni mwamikataba hiyo ni ile iliyopigiwa kelele na watanzania kuwaina harufu ya ufisadi na baadhi ikidaiwa kutokuwa na maslahikwa Taifa. Mikataba hii inayohusu ununuzi wa umeme ni ghalikwa unit kiasi cha kuipa wakati mgumu TANESCO kupatafedha za kujiendesha na wakati huo huo kuwauzia umemewatanzania kwa bei juu, hivyo inapaswa kupitiwa upya.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinataka Serikali kulieleza Bunge hili tukufu pamoja nawatanzania, ni lini TANESCO itapitia mikataba yote mibovuya shirika hilo na ikibidi TANESCO kuachana na mikataba ileinayoongeza mzigo na gharama za uendeshaji wa shirikahilo?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Bunge lako Tukufuinaishauri Serikali mambo ya nyongeza yafuatayo:

i. Bei za umeme zinazopitishwa na EWURAzizingatie gharama halisi zinazotumiwa na TANESCO kuzalishaumeme au kununua toka kwa makampuni binafsi ya uzalishajiumeme kuliko hali i l ivyo kwa sasa kwa kuwa shirikalinaonekana kuendeshwa kwa kuficha ukweli kuliko uhalisiaambao hauwekwi wazi.

ii. Kwa kuwa miongoni mwa majukumu yashirika hili ni pamoja na kufua na kuimarisha mitambo yaumeme ya shirika, kununua kutoka kwa wazalishaji binafsina nchi za jirani, basi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali kuhakikisha manunuzi ya umeme tokakwenye makampuni binafsi ya uzalishaji umeme yanafanyikakwa uwazi na ushindani kama inavyotakiwa na sheria yamanunuzi ili kuiweesha TANESCO kununua umeme kwa beinafuu.

iii. Ili kuhakikisha shirika linatimiza jukumu lake lakuwekeza kwenye miradi mipya ya uzalishaji, usafirishaji,usambazaji na kufanya tafiti za vyanzo mbalimbali vya nishatiya umeme kama vile nguvu za maji (hydropower), gesi asilia,makaa ya mawe (coal), jua na upepo; Serikali iliwezeshe

Page 224: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

224

shirika la umeme nchini (TANESCO) ili iweze kuwekeza kwenyeuzalishaji umeme wa bei nafuu hivyo kusaidia kuepukanana utaratibu wa kununua toka vyanzo vya gharama kubwa.

ii. TANESCO kushindwa Kukusanya Madeni

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni Mheshimiwa Raisalikaririwa akisema TANESCO wanapaswa kukusanya madeniwanayodai na akaenda mbali zaidi na kusema hata kamaIkulu inadaiwa TANESCO ikate tu umeme. Aidha katika haliya kawaida kauli hiyo ilitarajiwa iende sambamba na vitendokwa Serikali pamoja na taasisi zake kulipa madeni ya shirikahilo kwa ukamilifu.

Mheshimiwa Spika, Kwa taarifa ambazo Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inazo ni kuwa TANESCO inadai fedhanyingi ambazo hazijakusanywa na hadi kufikia tarehe 30 Juni,2016 jumla ya deni la umeme kwa Serikali na taasisi zake zilifikaShilingi bilioni 144.854, sawa na asilimia 67.4 ya deni lote laumeme. Deni lililobaki kwa wateja binafsi ni Shilingi bilioni70.063 sawa na asilimia 33. Ni wazi kuwa, kutokulipwa kwamadeni ya umeme na taasisi za umma na binafsi kunaathiriuwezo wa TANESCO kujiendesha kwa ufanisi na kulipa madenikwa wadaiwa wake.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali kupitia Wizara hii, kuliambia Taifa ni lini Serikaliilitoa maelekezo kwa taasisi zake kulipa madeni ya umemekwa wakati na ni lini hasa deni hili la shilingi bilioni 144.8litalipwa kwa TANESCO ili kauli ya Rais ionekene ni ya uhalisiana siyo matamko ya kufurahisha tu?

iii. Wizara ya Nishati na Madini Kutolipa Deni laKodi ya Pango kwa TANESCO

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaelewa kwamba Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madiniiliingia makubaliano na TANESCO ya kupanga jengo kwamuda wa miaka 10 kwa ajili ya matumizi ya ofisi kwenyejengo la TANESCO lililopo barabara ya Samora, jijini Dar es

Page 225: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

225

Salaam. Aidha muda rasmi wa kuanza makubaliano hayoilikuwa tarehe 1 Januari, 2013 kwa kodi ya Shilingi milioni 26.60kwa mwezi. Hata hivyo, Kwa taarifa zilizopo Wizara haijalipakiasi chochote tangu mkataba uliposainiwa, kiasi ambachohakijalipwa kimefikia Shilingi bilioni 1.12. Kambi Rasmi yaUpinzani inauliza ni lini Serikali itailipa Tanesco fedha hizo zapango?

Mheshimiwa Spika, Wizara imetenga fedha hizikwenye fungu lipi kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 kwaajili ya kulipia deni la shilingi bilioni 1.12? Kambi Rasmi yaUpinzani inauliza, Serikali inapata wapi uthubutu wa kuiagizaTANESCO kuwakatia umeme wateja wake inaowadai wakatiWizara mama yake inadaiwa na TANESCO fedha nyingi kamahizo?

iv. Miradi ya kuzalisha umeme kwa njia ya Majina Jotoardhi

Mheshimiwa Spika, miradi ya kufua umeme wa majiinakadiriwa kuwa miongoni mwa miradi ambayo umemewake ni wa bei ya chini ikilinganishwa na uzalishaji wa umemekwa kutumia mitambo inayozalisha umeme kwa kutumianishati ya Mafuta. Pamoja na miradi ya kufua umeme yaKakono- MW 87, mradi wa Malagarasi MW 45 na Mradi waRusumo – MW 80, lakini bado kuna miradi mingi ambayoSerikali haionyeshi jitihada zozote za kuikamilisha kwa wakatipamoja na kwamba miradi hiyo ilishatumia fedha za walipakodi katika hatua za awali za utekelezaji wake.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Mpango wa piliwa Maendeleo wa Miaka mitano ni kwamba Serikaliilitarajiwa kuendeleza mradi wa kuzalisha 200MW waGeothermal wa Ngozi- Mbeya. Takwimu zinaonesha kuwagharama za mradi huo ni shilingi bilioni 204.72 na kila mwakahadi 2020/21 zilitakiwa kutengwa shilingi bilioni 40.94.

Mheshimiwa Spika, kama inavyojulikana kuwamipango bila kuwa na bajeti ya utekelezaji ni sawa nahadithi tu. Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Waziri alieleze

Page 226: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

226

Bunge, je kuna umuhimu kwa waheshimiwa wabungekuendelea kurejea miradi ya umeme kama ilivyoorodheshwakwenye kitabu cha Mpango wa awamu ya pil i wamaendeleo ya miaka mitano huku Serikali ikiwa haitengifedha kwa ajili ya utekelezaji?

v. Ununuzi wa Transfoma kutoka nje ya Nchi

Mheshimiwa Spika, TANESCO kwa kipindi kirefuwamekuwa wakinunua transfoma kutoka nje ya nchi wakatihapa nchini kuna kiwanda cha TANALEC kinachotengenezatransfoma hizo. Kwa mujibu wa Mkurungenzi wa kiwanda,Transfoma zao zina ubora wa Kimataifa na kwa sasa na wanamatarajio ya kutengeneza Transforma ambazo hazitumiimafuta ili kuepukana na wizi wa mafuta kwenye Transformawa mara kwa mara. Aidha aliyekuwa Waziri wa Nishati naMadini, Profesa Sospeter Muhongo alikaririwa akiliagiza Shirikala Umeme Tanzania TANESCO kuacha kununua Transfomerkutoka nje ya nchi na badala yake wanunuezinazotengenezwa nchini.

Mheshimiwa Spika, Katika ziara yake kwenye kiwandacha utengenezaji transfoma cha TANALEC mkoani ArushaWaziri alionesha kushangazwa na kauli ya watendaji waTANESCO kuwa transfoma zinazotumika nchini ni kutoka njeya nchi. Aidha TANESCO kupitia kwa Meneja mauzo namasoko Kanda ya Kaskazini ilikiri kuwepo kwa changamotohiyo na kwamba hali hiyo inasababishwa na sheria ya ununuzikuwabana.

Mheshimiwa Spika, wakati TANESCO wakilalamikiasheria ya ununuzi kuwabana, aliyekuwa Waziri wa Nishati naMadini alipotembelea kiwanda cha Kutengeneza Transformacha TANALEC alipingana vikali na kauli ya watendaji waTANESCO kuwa sheria ya manunuzi ndio inawakatazakununua Transiforma hizo. Aidha Waziri aliagiza TANESCOkununua Transforma hizo ambazo wao wana hisa na kuhususheria za manunuzi kukataza kununua bidhaa zaowenyewe ni mbinu na rushwa zilizojaa katika zabuni zamanunuzi.

Page 227: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

227

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Bunge lakotukufu, inashangazwa na kitendo cha Serikali kwa kupitiaWizara ya Nishati na Madini kupingana na TANESCO kuhususheria ya manunuzi, wakati TANESCO wakisemakinachowafanya kununua transfoma kutoka nje ya nchi nisheria ya ununuzi, Serikali kwa upande wao wanasema hizoni mbinu za rushwa zilizojaa katika zabuni za manunuzi. Kwakuwa Serikali inakiri kuwepo kwa mbinu za rushwa katikazabuni za manunuzi, na kwa kuwa Serikali hii inasema niSerikali ya viwanda lakini, Serikali yenyewe ikiwa hainunuibidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ya nchi; je ni liniSerikali itaacha maigizo haya na kuja na suluhisho la tatizohili kwa kuchukua hatua dhidi ya watendaji iliosemawanaendekeza mbinu hizo za rushwa?

2. Wakala wa nishati vijijini- (REA)

Mheshimiwa Spika, lengo la uanzishwaji wa REAlilikiwa ni kuwapatia wananchi waishio vijijini nishati bora.Pamoja na umuhimu wa wakala huyu bado Serikalihaijaonesha kwa vitendo kuwa ina nia ya kusaidia wakalahuyu ili aweze kuimiza majukumu yake kikamilifu na hasalinapokuja suala la kuupatia fedha kama zinavyoombwa nazinavyopitishwa na Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Spika, takwimu zinaonesha kuwa Serikaliimekuwa haitimizi wajibu wake wa kuipatia REA fedha kamazinavyotengwa na kuidhinishwa na Bunge hili, kwa mfanomwaka 2008/2009 zilipitishwa shilingi bilioni 20.00 lakini fedhazilizotolewa ni shilingi bilioni 12.06 sawa na 60%. Mwaka 2009/2010, fedha zilizopitishwa ni shilingi bilioni 39.55 na kiwangocha fedha zilizotolewa ni shilingi bilioni 22.14 sawa na 56%.Mwaka 2010/2011 kiasi cha fedha kilichotengwa ni shilingibilioni 58.883 na kiasi cha fedha kilichotolewa ni shilingi bilioni14.652 sawa na 25%, mwaka 2011/2012 kiasi kilichotengwa nishilingi bilioni 71.044 na kiasi cha fedha kilichotolewa ni shilingibilioni 56.748 sawa na 80%, mwaka 2012/2013 kiasi cha fedhakilichotengwa ni shilingi bilioni 53.158 na kiasi cha fedhakilichotolewa ni shilingi bilioni 6.757 sawa na 13%.

Page 228: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

228

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniimeamua kutoa takwimu hizo ili kuonesha kwamba tatizola Serikali kutopeleka fedha kwa Wakala huyu pamoja nakwamba sasa fedha hizi zinatokana na fedha za wananchikupitia ongezeko la shilingi 100 kwenye kila lita moja yamafuta ya petroli kwa ajili ya nishati vijijini lakini bado fedhahazipelekwi kwenye miradi hiyo. Ni vyema sasa Serikaliiwaambie watanzania sababu zinazosababisha kushindwakupelekwa kwa fedha hizi kwa wakala huyu wakati wananchiwameshatoa fedha kwa ajili ya lengo hilo.

Mheshimiwa Spika, uzoefu kutoka kwenye awamumbili zilizotangulia zinaonesha kwamba, Serikali imekuwaikishindwa kupeleka fedha kwa ajili ya miradi ya REA kwawakati na pale ambapo imekuwa ikipelekwa basi fedha hizozimekuwa ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji ya mradi husika,hali inayosababisha miradi kushindwa kukamilika kwawakati.

Mheshimiwa Spika, kucheleweshwa kupelekwa kwafedha za miradi kunasababisha miradi pia kuchelewakukamilika na kuchelewa kukamilika kwa miradi kwa wakatikunasababisha kuongezeka kwa gharama za miradihusika.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya wakala iliyotolewaJanuari, 2017 takwimu zake zinaonyesha kuwa jumla ya miradi13 inayoendelea kutekelezwa yenye thamani ya shilingi1,210,050,878,902 kama mikataba yake ilivyosainiwa, hadisasa fedha zil izotolewa na Serikali ni shil ingi1,019,957,110,048.20 na kiasi kil icho baki ni shil ingi190,093,768,854. Hiki ni kiasi kikubwa cha fedha, na ni miradiiliyoingiwa mikataba tu, lakini REA ina miradi mingi kwakulingana na bajeti zilizopitishwa na Bunge pamoja naMpango wa Maendeleo wa Taifa.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha kuorodhesha miradikumi na tatu tu inayoendelea kutekelezwa, maana yake nikutaka kupimwa kwa kigezo kidogo na sehemu kubwainayolingana na bajeti inayotengwa na miradi iliyopangwa

Page 229: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

229

katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa isipimwe kwakiwango cha fedha kilichotakiwa kutengwa.

i . Mapungufu katika utekelezaji wa miradi yaumeme vijijini kwa awamu ya pili:

Mheshimiwa Spika , kuna malalamiko ambayoyamekuwa yakijitokeza kutokana na utekelezaji wa miradiya umeme vijijini katika awamu ya pili ambayo Serikaliimeeleza kuwa imekamilika. Baadhi ya mifano ya mapungufukutoka maeneo mblimbali ni pamoja na mkoani Mara,mkandarasi kuweka transfoma zenye 50 kVA na ufungajiwake kutokamilika, badala ya transfoma yenye 100 kVA;Mkoani Morogoro kulikuwa na utekelezaji mdogo wa mradiambapo ni 15.6% ya wateja wa umeme wa njia tatuwaliunganishiwa umeme, huku kwa wateja wa njia mojawaliounganishiwa umeme ni 29%. Aidha wakati utendaji wamkandarasi huyu ukiwa hivi, mkandarasi inadaiwa alikuwaameshalipwa karibia 69.6% ya fedha zote. Mapungufumengine ni pamoja na kuongezwa kwa wigo kazi namkandarasi bila idhini ya wakala wa umeme vijijini, transfoma21 badala ya transfoma 10 ziliwekwa ambayo ni kinyume namkataba.

Mheshimiwa Spika, Huko Babati baadhi ya vijijivilikosa umeme kutokana na TANESCO kushindwa kuidhinishaombi la kutumika kwa nguzo zake za umeme; kasoro zakiufundi huko Arumeru; mgogoro wilaya ya Hai mkoaniKilimanjaro unaohusu ardhi inayodaiwa kuwa mali yamamlaka ya viwanja vya ndege na hivyo kuathiri upatikanajiwa umeme kwa baadhi ya vijiji.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Serikali, kutoa kauli juu ya hatua ilizochukua ilikurekebisha kasoro ambazo zilijitokeza katika utekelezaji waREA awamu ya pili.

Page 230: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

230

ii. Utekelezaji wa REA awamu ya Tatu

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni wakala wa umemevijijini REA umezindua mradi wa kusambaza umeme vijijiniawamu ya tatu, baada ya kukamilika kwa awamu mbilizilizotangulia, taarifa iliyotolewa kwa umma inaoneshakwamba mradi huu utajumuisha vijiji 7,873 katika mikoa yotena wilaya za Tanzania bara kwa utekelezaji wa kipindi chamiaka mitano.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewana REA kupitia tovuti yake, wakala wa Nishati vijijini REA,ulikamilisha taratibu za zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa mradikabambe wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu. REAkupitia taarifa hiyo uliwajulisha wakandarasi walioshindakwamba hatua iliyokuwa inafuata ni kuwapatia barua za tuzo(Award Letters) na kusaini mikataba.

Mheshimiwa Spika, zabuni hizo zilihusu mradi wa REAawamu ya tatu, zinalenga kufikisha umeme wa gridi kwenyevijijini 3559 katika mikoa 25 ya Tanzania bara, kwa thamaniya zaidi ya Bilioni 900.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na kwamba mradi huuunagharimu fedha nyingi za walipa kodi, takribani bilioni 900lakini tayari kuna madhaifu mengi yameshajitokeza katikamichakato ya dhabuni hizo. Taarifa ambazo kambi Rasmiya Upinzani Bungeni imezipata kuhusu mapungufu katikamchakato wa zabuni za tenda ni pamoja na baadhi yakampuni kupewa zabuni wakati hazijasajiliwa katika bodi yausajili wa makandarasi; kampuni ambazo hazikusajiliwa nabodi ya wakandarasi lakini wakashirikiana na wabia ambaoni wa madaraja ya chini na hawakustahili kupewa zabunikubwa; baadhi ya makampuni yenye sifa sawa namakampuni yaliyopata zabuni kukosa zabuni hizo; baadhiya makampuni kupewa zabuni wakati makampuni hayohayana sifa za kupewa zabuni hizo na baadhi ya makampunikupewa zabuni wakati makampuni hayo yalikosa sifa zauzoefu katika kazi hizo.

Page 231: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

231

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa zabunizilizotangazwa makampuni yenye sifa za moja kwa mojakwenye zabuni hizi ni makampuni yenye sifa za daraja lakwanza. Makampuni yenye sifa za daraja la kwanza hayanaukomo wa kiasi cha fedha zinazopaswa kulipwa kwenye kilakifungu. Daraja la pili kikomo cha fedha ni shilingi bilioni 2,daraja la tatu, shilingi bilioni 1.2, daraja la IV shilingi milioni600, Daraja la V shilingi milioni 300 na Daraja la VI shilingi milioni150.

Mheshimiwa Spika, Taarifa ambazo Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni imepata zinaonesha kwamba, yapomakampuni yanayodaiwa kupatiwa zabuni katika mazingirayenye utata na hivyo, Kambi Rasmi ya Bunge lako tukufuinaitaka Serikali kufanya uchunguzi juu ya makampuni hayoili kuhakikisha fedha hizi za mradi wa REA III hazitumiki kwamakampuni yasiyo na uwezo wa kutekeleza miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Radi Service Limitedambayo iliingia ubia na kampuni za Njarita Contractor Ltdpamoja na kampuni ya Agwila Electrical Contractors Ltd, nawalipata mafungu ya zabuni ya dola 991,971 za kimarekanina shilingi bilioni 7.393. Aidha wabia hao pia walishinda lotnyingine yenye thamani ya dola milioni 3.787 na shilingi bilioni25.61. Pamoja na ushindi wa kampuni hizi, zenye ubia, taarifaza Bodi ya Usajili wa wakandarasi (CRB) zinaonesha kwamba,kampuni ya Radi ni ya daraja la II na III, kampuni ya Agwilakwa mujibu wa taarifa za CRB ni ya daraja la V, na kampuniya Njarita Contractor, usajili wake ni wa daraja la V. Paleinapotokea kampuni zote wabia ikawa hakuna kampuniyenye daraja la I, lakini zikawa zimeungana, zinaruhusiwakuandika barua CRB ili zipatiwe kibali kabla ya kuombazabuni. Kampuni zote hizi, pamoja na kuwa wabiahazikuwahi kuandika barua na kupewa kibali. Lakini piapamoja na kwamba, kampuni hizi hazikusajiliwa kwa darajala I, walipewa kazi ya mabilioni ya shilingi kwenye lots zotembili zilizooneshwa hapo juu, kinyume na taratibu.

Mheshimiwa Spika, Kampuni nyingine ya whitecityInternational Contractor Limited iliingia ubia na kampuni ya

Page 232: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

232

Guangdong Jianneng Electric Power Engerneering nakupewa zabuni ya lot yenye thamani ya dola milioni 2.9 zaMarekani na shilingi bilioni 22. Wakati wabia hawa wakishindazabuni hiyo, taarifa za Bodi ya Usajili wa Makandarasizinaonesha kwamba, kampuni ya Whitecity InternationalContractor Limited imesajiliwa kwa kazi umeme daraja laIV, Majengo daraja la II, Civil daraja la IV na civil specialistdaraja la II. Mbia mwenza, kampuni ya Guangdong JiannengElectrical Power Engineering, kwa taarifa zilizopo hana usajiliwowote kutoka bodi ya usajili wa makandarasi.

Mheshimiwa Spika, Zabuni nyingine yenye utata,ilitolewa kwa kampuni ya MF Electrical Engineering Limitedambayo iliingia ubia na kampuni ya GESAP EngineeringGroup Limited. Kampuni hizi kwenye lot ya kwanza wanalipwadola milioni 5 pamoja na bilioni 23.748, lot ya pili walishindazabuni yenye thamani ya dola milioni 3.852 za marekani napia bilioni 19.899. Aidha taarifa kutoka bodi ya usajili wamakandarasi zinaonesha kwamba MF Electrical EngineeringLimited usajili wake ni wa daraja la V,na kampuni ya GESAPEngineering Group Limited usajili wake kwenye maswala yaumeme ni wa daraja la II.

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Joe’s Electrical Ltdiliingia ubia na kampuni ya AT & C Pty na L’S Solution Ltd,kampuni zote hizi hadi zinakabidhiwa barua za kusudio lakuwapa zabuni hazikuwa na usajili kutoka bodi ya usajili wamakandarasi, lakini pamoja na upungufu huo, REA waliwezakuwapatia lots mbili, lot ya kwanza ina thamani ya dola zakimarekani milioni 1.5 na shilingi bilioni 15.695 na huku lot yapili ikiwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 1.915pamoja na shilingi bilioni 17.958. Ikumbukwe kwamba, ikiwakampuni ya kigeni kama hii ya Joe’s hata kama ina darajala I, lakini akishakuwa na mbia mtanzania ambaye hanausajili, basi wanakosa sifa ya kupewa zabuni lakini, kamaambavyo inaonekana hapa, kampuni hii ilipewa zabuni yaushindi wa lots mbili.

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Nipo Group Limitedinausajili bodi ya usajili wa wakandarasi wa Daraja la V,

Page 233: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

233

kampuni hii haina mbia lakini ilipewa zabuni yenye thamaniya dola za kimarekani milioni 2.011 na kiasi kingine cha shbilioni 15.545. Kampuni hii ilipewa zabuni hii ikiwa ni marayake ya kwanza kufanya kazi za kiwango cha gridi na hivyokama zilivyo kampuni nyingine pia uwezo wake unatiliwamashaka.

Mheshimiwa Spika, ni vyema ikaeleweka kwambaKambi Rasmi ya Upinzani haipingi wazawa wala wagenikupewa zabuni za ujenzi, tunachotaka kuona ni taratibu zotezinazingatiwa. Hivyo, kutokana na uchunguzi huo makampuniyakayobainika kuwa yalipewa zabuni bila viwango ni vyemavigogo wote walio nyuma ya makampuni hayo wakajulikanana hatua zaidi zikachukuliwa.

E. SEKTA YA GESI- NCHINI:

1. Bomba la Gesi kutoka Mtwara hadi Dar esSalaam

Mheshimiwa Spika, Bomba la kusafirisha Gesi asiliakutoka Mtwara hadi Dar es Salaam lilijengwa na Kampuni yaChina Petroleum and Technology Development Company(CPTDC) kwa gharama ya takriban Dola za Kimarekanitakriban bilioni 1.283 ambapo kati ya hizo, dola za Kimarekanibilioni 1.225 zilipatikana kama mkopo wa masharti nafuukutoka Benki ya Exim ya China. Marejesho ya mkopo huoyalitegemea kupatikana kwenye mauzo ya gesi asilia baadaya kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa bomba na kuanzakutumika kibiashara.

Mheshimiwa Spika, kuna taarifa kwamba bomba lagesi lilijengwa kabla ya kutafuta wateja na kusainianamkataba wa mauziano ya gesi asilia kati ya Shirika laMaendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na wateja lengwa wagesi asilia. Aidha mapungufu haya kwa vyovyote ile yanaathirimalipo ya mkopo kwa vile mauzo halisi ya gesi asilia yatakuwachini ya kiwango cha makadirio ya awali cha futi za ujazomilioni 138.8 kwa siku (mmscfd).

Page 234: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

234

Mheshimwa Spika, taarifa ambazo Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni imepata zinaonyesha kwamba, kwa sasaShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ndilo mteja mkuu wagesi asilia; ambapo anatumia wastani wa futi za ujazo milioni46.61 kwa siku, sawa na asilimia sita (6%) tu ya ujazo wabomba; ambapo, kiasi hicho ni pungufu futi za ujazo milioni737.39 kwa siku ili kujaza bomba. Matumizi haya ni tofauti namakubaliano ya awali ambayo ilikua TANESCO liweze kutumiatakribani futi za ujazo milioni 80 kwa siku kama ilivyokuwakwenye makubaliano ya mkataba wa mauziano ya gesi asilia(GA).

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Bunge lako tukufuinapenda kupata ufafanuzi kutoka Serikali kuhusu jitihadaambazo Serikali imechukua ili kuhakikisha wateja zaidi wa gesiasilia wanapatikana ili mkopo uweze kulipwa kabla yamarekebisho ya ulipaji ambayo yataongeza gharama kubwakwa Serikali.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinafahamu kwamba mkataba wa mauziano ya gesi asilia katiya TPDC na TANESCO uko wazi kwamba TANESCO itatumiagesi asilia kwenye mitambo yake sita (6) ya kuzalisha umemeya Kinyerezi I, Kinyerezi II, Ubungo I, Ubungo II, Tegeta naSymbion kwa kima cha chini cha matumizi cha futi za ujazomilioni 80 kwa siku na futi za ujazo milioni 138.8 kwa siku kamakiwango cha juu. Hata hivyo, hadi sasa mtambo wa kuzalishaumeme wa Kinyerezi I ndio pekee unaotumia gesi asiliakuzalisha umeme; na unatumia kiwango asilimia thelathinina nne (34%) ya kiasi cha gesi yote iliyolengwa kutumiwa naTANESCO.

Mheshimiwa Spika, Mitambo mingine mitanoiliyokuwa imekadiriwa kutumia kiasi cha (66%) bado haijaanzakutumika; na haijulikani ni lini mitambo hiyo itaanza kutumiagesi asilia. Hata hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinafahamu kwamba, TANESCO bado ina mikataba ya mudamrefu na wazalishaji wakubwa wa umeme ambao nikampuni ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL) na Songas;ambapo mikataba yao inaisha mwaka 2022 kwa ule wa IPTL

Page 235: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

235

na mwaka 2023 kwa Songas. Hii inaiongezea TPDC naTANESCO ugumu kwenye kutimiza vifungu walivyokubalianakwenye mkataba wa mauziano gesi asilia (GA).

Mheshimiwa Spika, ni ushauri wa Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni kwamba, mikataba ya makampuniyaliyotajwa hapo juu haina maslahi kwa taifa na hivyo, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inazitaka TPDC, TANESCO naWizara ya Nishati na Madini wajadiliane ni kwa namna ganimitambo ya uzalishaji umeme ya TANESCO itaweza kumalizikakwa haraka ili bomba la gesi litumike kwa ufanisi na kuwezakulipa mkopo wa bomba la gesi kutoka Benki ya Exim yaChina kwa wakati.

Pia, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikalikuliambia Bunge lako tukufu, Ni jitihada gani Serikali imefanyakutafuta wateja zaidi wa gesi asilia ili kuongeza mapato yagesi na kuiwezesha TPDC kutimiza wajibu wa kulipa madeni?

2. TANESCO kudaiwa na TPDC Ankara za Mauzokiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 61.35

Mheshimiwa Spika, taarifa ambazo Kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inazo ni kwamba mnamo tarehe 31 Oktoba2013, TPDC na TANESCO walisainiana mkataba wa TPDCkuiuzia gesi asilia TANESCO. Katika mkataba huo pia, kulikuwana makubaliano kwamba Serikali iweke dhamana benki kiasikinachoweza kulipa mauzo ya gesi kwa miezi mitatu au zaidikwa ajili ya TPDC huku dhamana hiyo ikitakiwa kuwapo hadipale madeni yote ya TANESCO yanayohusiana na kuuzianagesi asilia yatakapolipwa.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ambazo KambiRasmi ya Upinzani Bungeni haijafahamu, Serikali haikuwekadhamana hiyo kinyume na makubaliano hayo. Aidha, hadikufikia mwezi Desemba 2016, jumla ya deni la mauzo ya gesiasilia kiasi cha dola za kimarekani milioni 61.35, sawa nashilingi za Kitanzania bilioni 133.4, kimelimbikizwa bila kulipwana TANESCO.

Page 236: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

236

Mheshimiwa Spika,hali ya TANESCO kuchelewa kuilipaTPDC, inasababisha TPDC kuchelewa kuyalipa makampuniyanazouza gesi. Na hivyo kuongeza hali ya sintofahamukwenye ulipaji wa mkopo kutoka benki ya Exim ya China.Kuchelewa huku kwa malipo kunaweza kusababishagharama zaidi za riba ambayo itatakiwa kulipwa na TPDCkwa wadai wake.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kufahamunini mpango wa Serikali kupitia TPDC wa kuhakikisha inalipamadeni kutoka kwa wauzaji wa gesi na mkopo kutoka Benkiya Exim ya China ili kuepuka kulipa riba kubwa hapobaadaye.

3. Kuzuiliwa kuingia kwa Gesi ya Tanzanianchini Kenya

Mheshimiwa Spika, Hivi karibuni, Serikali ya Kenyaimepiga marufuku uingizwaji nchini humo wa gesi ya kupikiakutoka Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na KatibuMkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya, Kenya ilipiga marufukuuingizwaji wa gesi kutoka Tanzania ndani ya siku saba kuanziatarehe 24 Apri, 2017. Uamuzi wa Kenya ni kinyume na misingiya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapoTanzania na Kenya ni wanachama. Aidha kwa mujibu waitifaki ya soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki, bidhaakutoka nchi wanachama zinaruhusiwa kusambaa ndani yanchi wanachama wa Jumuiya hii.

Mheshimiwa Spika, Uamuzi wa Kenya kuzuia Gesikutoka Tanzania ni uamuzi ambao kwa vyovyote vileunalenga kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika masharikina kuwazuia watanzania wanaofanya bishara hii nchiniKenya, Kambi Rasmi ya Bunge lako tukufu, inaitaka Serikalikutoa ufafanuzi ndani ya Bunge lako tukufu kuhusu

i. Hatua ambazo imechukua kwa kuhusishaWizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Jumuiya ya AfrikaMashariki pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara ilikuwanusuru watanzania wanaofanya biashara hii nchini

Page 237: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

237

Kenya na kuhakikisha mkataba wa Jumuiya ya AfrikaMashariki na pamoja na itifaki ya Masoko ya pamojahavivunjwi?

ii. Ikiwa Kenya inafanya hivyo kwa kulindaBandari yao ya Mombasa, bidhaa zake za ndani pamoja nawafanya biashara wake, na kwa kuwa kwa kufanya hivyoKenya imevunja mkataba na itifaki za soko la pamoja, jeSerikali inachukua hatua gani za kisheria dhidi ya kitendo chaKenya kuzuia bidhaa kutoka Tanzania na nini hatma yabidhaa za Kenya zilizo kwenye soko la Tanzania?

F. KIGUGUMIZI CHA WIZARA YA NISHATI NAMADINI KURUHUSU UWEKEZAJI KATIKA UZALISHAJI WA UMEMEKWA KUTUMIA NISHATI JADIDIFU (RENEWABLE ENERGY) KATIKATEKNOLOJIA ZA UPEPO NA JUA (WIND &SOLAR ENERGY)

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo kubwa la uwekezajikatika uzalishaji wa nishati jadidifu kwa kutumia teknolojia yajua na upepo, licha ya nchi yetu kuwa na rasilimali jua naupepo wa kutosha. Kutokana na uwepo wa rasilimali hizo,wapo wawekezaji ambao wameonyesha nia ya kutakakuwekeza katika uzalishaji wa nishati hiyo, lakini Wizara yaNishati na Madini imekuwa haitoi ushirikiano kwa wawekezajihao, jambo ambalo linairudisha nyuma sekta ya nishati nchini.

Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa umeme kwa kutumiateknolojia ya jua na upepo, unaweza kutoa mchangomkubwa wa umeme katika gridi ya taifa kwani tunazorasilimali jua na upepo za kutosha kuliko hata majirani zetu.Nchi yetu inayo sera na sheria za kuendesha teknolojia hizi,lakini tunajiuliza kwa nini Wizara inazuia sekta hii kuendelea?

Mheshimiwa Spika, EWURA wamefanya kaziiliyogharimu taifa ya kutengeneza kanuni za uzalishaji wanishati jadidifu kwa wazalishaji wadogo (Small PowerProducers – SPP Regulations) ambazo zilizokwisha kukamilikatangu July, 2016. Kanuni hizo zinaitwa “the Second GenerationSmall Power Producers Regulations” Regulation hizi

Page 238: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

238

zimeainisha uzalishaji wa umeme katika teknolojia za upepona jua katika makundi makuu matatu:

i. Kiwango cha 0 – mpaka Mega Watt 1 (0 –1MW)

ii. Kiwango cha kuanzia Mega Watt 1 – mpakaMegawatt 10 (1 – 10 MW)

iii. Kiwango cha kuanzia MegaWatt 10 nakuendelea.

Mheshimiwa Spika, hizi kanuni za Second GenerationSmall Power Producers’ zil iyofanyiwa kazi na EWURAzinaelekeza makundi yote matatu yaliyotajwa hapo juukuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia hizi na kuuzakwenye grid ya taifa kwa taratibu zilizoelekezwa kwenyesheria ya Umeme Sura 131 kama ifuatavyo:

Kundi la 1: (0 – 1 MW) litatumia “Feed-in Tarrifinayopangwa na EWURA kwa kuzingatia ukokotoajiuliozingatia gharama za uzalishaji kwa teknolojia hizi ambazoni chini kuliko teknolojia zingine zinazotumiwa na TANESCOkwa sasa isipokuwa teknolojia ya maji (hydro) ambayoimeathiriwa sana na hali ya “ tabianchi”(climate change).Kwa kiasi kikubwa aina hii haina matatizo mengi kwa sababuinashughulikiwa na EWURA na TANESCO bila kulazimishaurasimu wa Wizara.

Kundi la 2: (1 MW – 10 MW) ambayo ndioinategemewa kuwa na mchango mkubwa katika kuongezarenewable energy kwenye grid ya taifa, sheria hii inaelekezakufuata utaratibu wa “Competetive bidding”). Sheria hii itaipaSerikali/Tanesco kuchagua kwa kupitia zabuni za wazi,mwekezaji mwenye uwezo kiteknolojia, kifedha na mwenyekuahidi kuuza umeme kwenye gridi ya taifa kwa bei yenyemaslahi kwa taifa kupitia SPPA (Small Power PurchasingAgreement).

Page 239: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

239

Mheshimiwa Spika, Utaratibu huu ulishatangazwa naEWURA kwa wawekezaji wa teknolojia hizi wa ndani na njekwa takribani Zaidi ya mwaka mzima sasa. Wawekezaji hawahadi sasa wamekwisha kutumia gharama nyingi za kufanyamaandalizi yaliyoelekezwa na EWURA kujiandaa kwa zabunihizi; ikiwa ni pamoja na kufanya makubaliano ya Ardhi kubwainayohitajika kwa miradi ya aina hii, na gharama nyinginenyingi zinazoambatana na uwekezaji wa miradi ya aina hii.

Mheshimiwa Spika, EWURA/na TANESCOwamekamilisha kazi yao na kukabidhi shughuli hii kwa Wizaraya Nishati na Madini ambayo kila wawekezaji wakiwafuatakuulizia kinachoendelea wanajibiwa wasubiri. Hali hiiinawakatisha tamaa wawekezaji wa teknolojia hizi, ambazotunaamini zitaongeza umeme ulio rafiki kwa mazingira yetukwenye gridi ya taifa, na umeme ulio na gharama nafuuukilinganisha na wa kutumia mafuta. Miradi hii ndio inawezakuwa upgraded kwa jinsi grid yetu ya taifa inavyokua nahatimae kufikia Megawatt 50 – 100 na kuendelea.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinashangazwa na kitendo cha Serikali kuweka mkazo pekeekwenye miradi mikubwa ya upepo ya Singida naMakambako ambayo kiuhalisia haitakamilika hivi karibuni.Tafiti zinaonyesha kuwa hata wenzetu waliobobea katikateknolojia hizi walianza na miradi midogo midogo mingi ya10 MW na ikawa upgraded taratibu hadi kufikia giant windfarms and solar farms.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinaitaka Wizara ya Nishati na Madini iharakishe zabuni yaushindani( Competetive bidding process) ya teknolojia hizikama sheria ya EWURA inavyoelekeza il i kuwezeshakupatikana kwa teknolojia hizi tunazozihitaji kwa ukomboziwa wananchi wetu kwenye sekta hii ya umeme usioharibumazingira.

Kundi la 3: Kwa mujibu wa sheria ya EWURA, EWURAhaina udhibiti mkubwa. Mwekezaji ameachiwa uhuru wakufanya majadiliano na TANESCO kuhusu PPA (Power

Page 240: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

240

Purchasing Agreement).Lakini sheria inawatakawakishakubaliana wakasajili PPA hiyo EWURA. Uzoefuunaonyesha miradi hii itatuchukua nchi hii miaka mingikufanikiwa. Na mfano rahisi ni miradi mikubwa ya umemewa upepo ya Singida na Makambako ambayo imegubikwana migogoro mikubwa ya ardhi.

Mheshimiwa Spia, kwa kuzingatia taratibu za uzalishajikatika makundi yote matatu, wataalamu wengi wanashaurikuwa kipaumbele cha nishati jadidifu katika gridi yetu ya taifakwa kutumia upepo na jua ni katika Kundi la 2, ambalolinaruhusu wawekezaji kuomba kufanya uzalishaji kwakutumia zabuni za wazi – competitive bidding.

G. SEKTA YA MADINI

Mheshimiwa Spika, sekta ya madini inahusu utafutajina uchimbaji wa madini. Nchi ya Tanzania imebarikiwa kuwana utajiri mkubwa wa madini, lakini mchango wa sektakwenye uchumi hauridhishi. Pamoja na maoni ambayoKambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tumeyatoa kupitia hotubahii kwenye kipengele kuhusu makinikia ama ‘mchanga wadhahabu’ yapo masuala ya ziada ambayo ni vyema Wizaraya Nishati na Madini ikayatolea majibu kama ifuatavyo.

1. Mapungufu katika Mikataba ya uchimbajiMadini

Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi kirefu yamekuwepomalalamiko yanayohusu mikataba ya uchimbaji madiniambayo Serikali iliingia na wawekezaji wa makampuni yauchimbaji wa madini. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinafahamu kwamba baadhi ya mikataba ya madiniiliyoingiwa kati ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano yaTanzania na makampuni ya madini ni pamoja na mikatabakati ya kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) inayoendeshamgodi wa dhahabu wa Geita, na Kampuni ya ACACIAinayoendesha migodi ya Buzwagi, Bulyanhulu na MaraKaskazini.

Page 241: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

241

Mheshimiwa Spika, kwa taarifa ambazo Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inazo ni kwamba, mikataba ya madinimingi ina vifungu visivyolinda maslahi ya umma, vifungu hivyoni pamoja na vile vinavyoweka masharti yasiyoridhisha katikakuongeza mikataba, vifungu vinavyozuia mabadiliko yasheria kuathiri mikataba husika, sera zisizoridhisha kwenyefedha za kigeni na forodha, motisha za kodi zilizozidi, kwenyetaratibu za kihasibu katika kutambua na kukokotoa matumiziya mitaji.

Mheshimiwa Spika, Kutokana na mapungufu hayoyaliyoko kwenye mikataba ya uchimbaji wa madini, KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali;

i. Kuacha kulalamika na badala yake itumiekifungu kinachoruhusu kurejewa kwa mikatabakinachopatikana kwenye mikataba mingi ya madini ili kurejeamakubaliano yaliyoafikiwa na kuhakikisha kuwa Serikaliinajiepusha na kutoa matamko ya potofu ambayo yanaendakinyume na matakwa ya mikataba husika.

ii. Aidha ili kuhakikisha maslahi ya Taifa namaslahi hayaathiriki ni maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzanikuwa Serikali iyaite makampuni ya wawekezaji kwenye madinina kujadiliana nayo jinsi ya kufanya marekebishoyanayohitajika.

iii. Serikali iboreshe usimamizi kwa makampunibinafsi yanayofanya kazi za kutafuta na kuvumbua miambayenye madini ili kuiwezesha Serikali kuwa na taarifa sahihi naza ziada zitakazoisaidia kwenye majadiliano na kufanyamaamuzi.

2. Madhaifu ya sheria za kukusanya mapatokwenye sekta ya Madini

Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi kirefu Taifa hili linakosamapato yanayotokana na rasilimali za Taifa kutokana nasababu mbali mbali, ambazo miongoni mwake ni sababuzinazotokana na madhaifu ya sheria zetu. Aidha miongoni

Page 242: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

242

mwa sheria ambazo zinachangia Taifa kukosa mapatokwenye sekta ya Madini ni pamoja na Sheria ya Kodi yaOngezeko la Thamani (VAT). Kwa mujibu wa sheria hii, kifungucha 55(1) cha sheria hii, kinatoa mwanya kwa migodi yauchimbaji wa madini kupewa marejesho ya Kodi ya VAT.Sheria hii, sawa na sheria za zamani kwa pamoja zinaruhusutozo ya kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango cha sifurikwa bidhaa zinazosafirishwa kuuzwa nje ya nchi.

Mheshmiwa Spika, Ni wazi kwamba soko kubwa laMadini liko nje ya nchi na kwa sababu hiyo madini yoteyanayopatikana yanauzwa nje ya nchi. Hii inapelekea kodiinayotokana na manunuzi ya bidhaa za mtaji, mafuta nagharama nyingine yanayofanywa na makampuni ya migodindani ya nchi kuzidi ile inayotokana na mauzo (Output Tax).Hivyo, migodi hiyo kustahili marejesho ya kiasi kilichozidikutokana na kifungu cha 83(2) cha sheria ya Kodi yaongezeko la Thamani.

Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali kutoza kodi yaongezekeo la thamani kwa kiwango cha sifuri kwenye bidhaazote zinazosafirishwa kuuzwa nje ya nchi ilikuwa ni kukuzaviwanda vya ndani. Taarifa ambazo Kambi Rasmi ya Upinzaniya Bunge lako tukufu inazo zinaonesha kwamba migodimikubwa minne (4) ya dhahabu Geita, Bulyanhulu, MaraKaskazini, Pangea na mmoja wa Almasi wa Williamson kwakipindi cha miaka minne mfululizo kuanzia Mwaka 2012ilirejeshewa marejesho makubwa ya kodi ya Ongezeko laThamani kwa kiasi cha shilingi bilioni 1,144.

Mapungufu yanayoonekana ni kwa Sheria hiyokutokuweka makundi ili kuonyesha ni bidhaa zipi zinazostahilimotisha hiyo na hivyo kusababisha madini ambayo kwanamna yoyote lazima yauzwe nje ya nchi nayo pia kunufaikana motisha hiyo kama vile ambavyo bidhaa za kilimo naviwandani zinavyonufaika. Kambi Rasmi ya Bunge lako Tukufuinaitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu;

i. Ni lini hasa Serikali italeta ndani ya Bunge lakotukufu Mabadiliko ya sheria ya Ongezeko la thamani VAT ili

Page 243: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

243

kuondoa tozo ya kiwango cha sifuri kwenye mauzo ya madinina vito nje ya nchi kwa kuweka makundi yanaoonesha nibidhaa zipi zinazostahili motisha ya tozo ya kiwango chasifuri na kuziacha bidhaa za kilimo na Viwanda zikiendeleakunufaika?

ii. Kwa kuwa mabadiliko ya sheria hii, yataathirimikataba iliyopo kati ya Serikali na makampuni ya UchimbajiJe, Ni lini Serikali itaanzisha majadiliano na makampuni yauchimbaji madini kuhusu matokeo ya mabadiliko hayokwenye Mikataba yao (MDAs)?

3. Utofauti wa Kodi kwenye sekta ya Madini.

Mheshimiwa Spika, Sote tunafahamu kwambamikataba ya uchimbaji madini kati ya Serikali na makampuniya uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Mara Kaskazini,Geita, Buzwagi na Bulyanhulu ilisainiwa kabla Sheria ya Kodiya Mapato ya mwaka 2004 haijatungwa, isipokuwa mkatabawa uchimbaji wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliosainiwa2007. Kwa muktadha huo viwango vya tozo za kodi katikamikataba hiyo vilitokana na sheria ya kodi ya mapato yamwaka 1973 na havijabadilishwa kuendana na sheria mpyakutokana na kuwapo kwa kifungu kinachozuia mabadilikoya viwango vya tozo za kodi kwenye mikataba hiyo.

Mheshimiwa Spika, Ifuatayo hapa chini ni baadhi yamifano inayotokana na baadhi ya maudhui ya mikatabahiyo;

i. Mikataba hiyo inaainisha viwango vya zuio lakodi katika ada ya usimamizi pamoja na huduma za kiufundikati ya asilimia 3 mpaka 5. Hali hii ni tofauti na matakwa yaSheria ya Kodi ya Mapato ambayo inataka viwango vya zuiola kodi katika ada ya usimamizi pamoja na huduma zakiufundi kuwa asilimia 15.

ii. Mikataba hiyo pia inataka ushuru wahalmashauri ulipwe kwa kiwango kisichozidi Dola zaKimarekani 200,000 kwa mwaka. Takwa hili pia ni kinyume

Page 244: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

244

na kifungu cha 6 (1) (u) cha sheria ya Serikali za Mitaa yamwaka 1982 inayotaka ushuru wa ndani ulipwe kwa kiwangocha asilimia 0.3 ya mauzo ya mwaka.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mifano tajwa hapojuu ni ushauri wa Kambi Rasmi ya Upinzani kuwa Serikaliinapaswa kujadiliana na makampuni ya uchimbaji madinikupitia kifungu cha utakaso wa mkataba kinachopatikanakwenye mikataba takribani yote ili kurekebisha viwango vyatozo za kodi kwa kuzingatia vigezo vya kiuchumivinavyobadilika kufuatana na muda tangu kusainiwa kwamikataba hiyo na hivyo kuliwezesha Taifa kupata mapatoyanayostahili kulingana na rasilimali hii.

4. Misamaha ya tozo na Ushuru, sekta ya Madini.

Mheshimiwa Spika, Misamaha kwenye tozo na ushuruwa mafuta il itolewa kwa makampuni ya madini i l ikuyapunguzia gharama za uzalishaji umeme kwa ajili yakuendeshea mitambo. Kifungu cha 8 cha Sheria ya Tozo zaUshuru wa Mafuta na Barabara ya mwaka 1985 kinampaWaziri wa Fedha mamlaka ya kutoa msamaha wa tozo yaushuru wa mafuta kwa kutangaza kwenye gazeti la Serikali.Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inafahamu kwambaSerikali, kupitia gazeti la Serikali Namba 190 lililochapishwatarehe 15 Julai 2011, ilitoa msamaha wa tozo ya ushuru wamafuta kwenye mafuta yanayoagizwa au kununuliwa namakampuni makubwa ya madini yanoyojihusisha nauchimbaji wa dhahabu nchini.

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa toleo hilo, Serikalipia ilibatilisha matoleo yote yaliyowahi kutolewa awali kuhusumisamaha ya kodi; na tangazo hilo likaweka utaratibu wakutumiwa na makampuni husika ili kuweza kupata msamahahuo. Taarifa ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazoni kwamba migodi mikubwa minne ya Geita Gold Mine,Bulyanhulu, Buzwagi na Mara Kaskazini inayojihusisha nauchimbaji wa dhahabu nchini imesamehewa tozo za ushuruwa ndani na mafuta kiasi cha shilingi bilioni 126.7 kwa mwaka2015 na 2016.

Page 245: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

245

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinarudia ushauri iliotoa kwenye mgodi uliochini ya STAMICOkwamba, Serikali, kupitia Wizara ya Nishati na Madini na Shirikala Umeme Tanzania TANESCO, kuhakisha inapeleka umemekwenye migodi mikubwa nchini ili kuiondolea Serikali sababuza kusamehe kodi kwenye mafuta. Kitendo cha kuipelekeamigodi umeme, kitasaidia kuongeza mapato kwenye Serikaliyatayotokana na kuuza umeme kwenye makampuni hayo.

5. Misamaha ya kodi za Mafuta yanayonunuliwa njekwa matumizi ya uchimbaji wa madini: 1URAYA Ta yaN

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Tangazo la SerikaliNa. 190 na 191 la mwaka 2011 na jedwali la tatu la sheria yakodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 1997 limetoamsamaha wa malipo ya ushuru wa bidhaa, ushuru wamafuta, na kodi ya ongezeko la thamani kwenye mafutayanayoingia kwa lengo la kutumika katika migodi kwa ajiliya uchimbaji wa madini.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinazo taarifa zinazoeleza kwamba mafuta yamekuwayakisafirishwa kutoka bandari ya Dar es Salaam kuelekeakunakodaiwa kuwa ni kwenye migodi ya uchimbaji wamadini lakini hakuna uthibitisho unaoonesha kwambamafuta hayo yalifika katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu.Aidha Sehemu ya 2(g) ya jedwali la Tangazo la Serikali namba190 na 191 la mwaka 2011 inasema kwamba tofauti yoyoteinayosababishwa na kutokupokea mafuta yaliyotoka katikamakampuni ya masoko ya mafuta, ukaguzi, matumizi yamafuta kwa mtu mwingine zaidi ya makampuni ya migodiau matumizi yoyote yasiyokusudiwa yanatakiwa kutozwa kodiitakayokatwa kutoka kwenye akaunti ya escrow. KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inapenda kufahamu hatuaambazo Serikali inachukua ili kuthibiti tabia hii ambayoinasababisha ukosefu wa mapato yanayotokana nakutolipiwa ushuru wa forodha.

Mheshimiwa Spika, kuna taarifa pia zinazohusumapungufu yaliyojitokeza katika uondoshaji wa mafuta ya

Page 246: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

246

migodini kwa kutumia maghala yanayohifadhi bidhaazinazosubiri kulipiwa kodi. Ikumbukwe kwamba, Kifungu 74-75 cha Kanuni ya Ushuru wa Forodha Afrika Mashariki yamwaka 2010 inahitaji mlipa kodi kupata leseni na kutimizamasharti yote yaliyoainishwa katika kifungu 74(1-4) na 75(1-2) ili kuweza kuendesha ghala linalohifadhi bidhaa zinazosubirikulipiwa kodi. Zaidi ya hayo, kifungu 76 kinahitaji mmiliki leseniwa ghala linalohifadhi bidhaa zinazosubiri kulipiwa kodikutekeleza dhamana kwa bidhaa zinazohifadhiwa katikaghala linalohifadhi bidhaa zinazosubiri kulipiwa kodi

Mheshimiwa Spika, taarifa zaidi zinasema kwambalita 3,500,000 za mafuta ya petroli yaliyonunuliwa na kampuniya mafuta ya Oryx na yaliondoshwa kupitia TANSAD yenyekumbukumbu namba TZSR-14-1171746 ya tarehe 10/12/2014.Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka ufafanuzi kuhusumaswala yafutayo:

i. Kama Serikali inaouhakika na ushahidikwamba M/S Oryx Oil Company Limited ilikuwa na leseni yakuendesha ghala linalohifadhi bidhaa zinazosubiri kulipiwakodi;

ii. Serikali inasema nini kuhusu mizigoiliyookolewa chini ya usimamizi wa ghala linalohifadhi bidhaazinazosubiri kulipiwa kodi bila dhamana kinyume na kifungu76 cha Kanuni ya ushuru wa forodha Afrika Mashariki yamwaka 2010;

iii. Serikali inao uhakika na ushahidi kama lita49,046 za mafuta ya petrol zilihamishwa kwenda kampuni yamigodi (North Mara) na kampuni ya mafuta ya Oryx; na kamasivyo, inachukua hatua gani kwenye jambo hili.

iv. Kwa kuwa taarifa zinasema kwamba Oryxndiye muingizaji wa mafuta; na siyo North Mara ambayealifuzu kupata msamaha wa kodi, Serikali imechukua hatuagani dhidi ya Oryx?

Page 247: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

247

6. Kampuni ya STAMICO na mgodi kutopatiwaumeme na TANESCO.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia STAMICO, ilichukuamgodi wa dhahabu wa Tulawaka kutoka kampuni ya AfrikanBarrick Gold (ABG). Mkataba wa kuhamisha umiliki ulifikiwatarehe 15 Novemba, 2013 na jina la mgodi likabadilika tokamgodi wa Tulawaka kwenda mgodi wa Biharamulo. Hatahivyo ili kuendesha mgodi, STAMICO iliunda kampuni mpyakwa jina la STAMIGOLD.

Mheshimiwa Spika, Kwa taarifa zilizopo kuhusu ufanisiwa mgodi chini ya usimamizi wa kampuni ya STAMIGOLD nikwamba, Wizara ya Nishati na Madini imechelewesha ruhusaya Leseni Kubwa ya Uchimbaji Madini kwenda STAMIGOLD.Kwa mujibu wa Kifungu cha 9(2) cha Sheria ya Madini ya2010 kunahitaji kuwepo kwa kibali cha maandishi kutokaWizara ya Nishati na Madini kabla umilikishwaji wa lesenikubwa ya kuchimba madini haijaamishwa kutoka kwakampuni moja kwenda nyingine. Taarifa zinaonesha kuwabaada ya STAMIGOLD kuchukua mgodi walihitaji pia kurithimkataba uliokuwepo awali kati ya Afrikan Barrick Gold (ABG)na Serikali ili nao waweze kupata faida na motisha alizokuwaanapata muendeshaji wa awali.

Mheshimiwa Spika, kuchelewesha kutoa kibali chakuhamisha leseni ni kuwanyima haki STAMIGOLD kutumia fursakama vile misamaha ya kodi zinazopatikana kwenyemkataba waliorithi kutoka African Barrick Ltd kuna athari zakiutendaji kwa Kampuni hii ya Umma ukilinganisha namanufaa wanayopata makampuni binafsi kwa mfanomsamaha wa kodi ya mafuta (Fuel levy & excise duty)

7. Mgodi kutopatiwa umeme na TANESCO

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na hitaji la mudamrefu la mgodi kuunganishwa na umeme wa gridi ya Taifana au kupatiwa umeme kutoka shirika la umeme nchiniTANESCO bila mafanikio. Aidha kwa sasa mgodi unatumiaumeme unaozalishwa kwa kutumia majenereta. Taarifa ya

Page 248: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

248

kila mwezi ya uendeshaji mgodi inaonyesha kuwa mahitajiya umeme kwa mwezi mgodini ni takriban kilowati milioni1.1 ambazo zinazalishwa na lita 300,000 za mafuta ya dizeliambayo inagharimu takriban shilingi milioni 670. KwaUchambuzi uliofanywa na STAMIGOLD unaonyesha kuwa hizokilowati zinazohitajika kama zikipatikana kutoka TANESCO,gharama zake ni takribani shilingi milioni 273.79 (gharamaikihusisha tozo zote zilizopo kwenye umeme kama VAT (18%)REA (3%) na EWURA (1%)

Mheshimiwa Spika, Kwa kutumia umeme waTANESCO, STAMIGOLD itaokoa karibia nusu ya gharamainazoingia sasa kuzalisha umeme wa mafuta.

Kambi Rasmi ya Bunge lako tukufu inapenda kupataufafanuzi kutoka Serikalini kuhusu mgodi huu kama ifuatavyo:

i. Ni lini Serikali kupitia Wizara ya Nishati naMadini itakamilisha mchakato wa kuipatia STAMIGOLD kibalicha kutumia mkataba wa kuchimba madini aliokuwaanautumia Afrikan Barrick Gold (ABG).

ii. Kwa kuwa mgodi huu ukiunganishwa kwenyegridi ya Taifa, kutasaidia kupungua kwa gharama hizi nakupelekea mchango chanya kwenye faida ya kampuni namapato kwa taifa. Je, Serikali kupitia Wizara ya Nishati naMadini, itaunganisha lini mgodi wa STAMIGOLD kwenye gridiya taifa ili kuupunguzia gharama za kujiendesha; na hivyo,kuuongezea fursa ya kupata faida kwa mgodi huu?

iii. Kwa kuwa migodi mingine mikubwa na ya katiinapata msamaha wa kodi ya mafuta (fuel levy & excise duty)Je, Serikali itatoa lini msamaha huo ili mgodi huu upatemsamaha sawa na migodi mingine?

8. Mgodi wa MMG Gold Ltd

Mheshimiwa Spika, kuna Mgodi unaoitwa MMG GoldLtd, upo kwenye kijiji cha Seka, Jimbo la Musoma Vijijinikilometa zipatazo 42 kutoka Bunda mjini, ukiwa unaelekea

Page 249: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

249

upande wa Ziwa Victoria. Kimsingi, mgodi upo karibu sanana Ziwa, hata maji ya kufanyia shughuli zake wanavutakutoka ziwani. MMG Gold Ltd ni Kampuni Tanzu ya Kampuniya MUTUS LIBER INTERNATIONAL LTD (MLI) yenye makao yakemakuu Dubai –Falme za Kiarabu na inafanya kazi zake nchiniGhana, Djibouti, Kenya, Madascar na Oman.

Mheshimiwa Spika, uendeshaji wa mgodi huo badounaendeshwa kama vile ni mgodi wa wachimbaji wadogowadogo, kwa maana kwamba watumishi/wafanyakazi waohawapo kwenye mfumo wa hifadhi za jamii, hawakatwi kodiya mshahara na hivyo Serikali kupoteza mapato yake. Nambaya zaidi ni kwamba “Gold Pregnant Carbon” zinaendakuchomwa Mwanza kinyemela na hivyo kutokuwemokwenye mfumo rasmi wa ukaguzi wa Wakala wa Madini(TMAA).

Mheshimiwa Spika, Mgodi huu bado ni mpya nakama taasisi zetu za ukaguzi na uthibiti utashindwakufanyakazi kama inavyotakiwa ni dhahiri kabisa, tutakuwatunaambiwa kwamba mgodi unazalisha hasara na hivyowanashindwa kulipa kodi ya makampuni. Kambi Rasmi yaUpinzani inaamini kabisa kwamba yale yote yanayoendeleakatika Mgodi yanafahamika na Wizara hivyo tunaitaka Serikaliilieleze Bunge hadi sasa utendaji wa mgodi huo ukoje nakodi ya wafanyakazi (PAYE) inalipwa kwa kiwango gani?

9. Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira:

Mheshimiwa Spika, Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwirakwa sasa unamilikiwa na Serikali kupitia STAMICO. Kabla yamwaka 2005, mgodi huu ulikuwa chini ya usimamizi waSTAMICO. Lakini kufuatia sera ya ubinafsishaji ya Chama ChaMapinduzi, mwaka 2005, 70% za umiliki wa mgodi huuzilihamishiwa kampuni iitwayo ‘Tan Power Resources Ltd’.Mwaka 2008 hisa zikachukuliwa na Serikali kupitia Msajili waHazina na umiliki wa mgodi huu ukarudishwa chini yaSTAMICO mwaka 2014. Kwa taarifa ambazo kambi Rasmi yaUpinzani Bungeni inazo ni kwamba Mgodi wa Makaa ya

Page 250: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

250

Mawe Kiwira haujaanza tena kuchimba makaa ya mawetokea ulipochukuliwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, taarifa mbalimbali zinaoneshakuwa mgodi wa Kiwira unakumbana na vikwazo vya Kisheria,kwa mfano ipo changamoto inayohusu cheti cha hisa chaMgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira (KCML) ambacho badohakijahamishiwa STAMICO; na hivyo cheti hicho badokinasomeka kwa jina la Tan power Resources Ltd. Kwa taarifaambazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo ni kwamba,hali hii imesababishwa na kitendo cha Mamlaka ya MapatoTanzania kutotoa hati ya kuthibitisha ulipaji wa kodi (taxclearance certificate) kwa kampuni ya Tan power Resources.

Mheshimiwa Spika, madhara ya kutobadilishwa kwajina hilo, kulipelekea Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira(NEMC), kwa mujibu wa kifungu 18(2)(b) cha Kanuni zaUkaguzi na Tathmini ya Athari za Mazingira (the EnvironmentalImpact Assessment and Audit Regulations) 2005, kuikataataarifa ya Tathmini ya Athari za Mazinigra ya STAMICO(Environmental Impact Assessment (EIA) report) kwa sababuhati ya hisa za kampuni hii ilikuwa bado inasomeka kwa jinaTan Power Resources Ltd.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kukosekana kwa hatiya umiliki yenye jina la STAMICO inakwamisha juhudi za shirikakuendeleza mgodi na pia inawia vigumu shirika kuingia ubiana wawekezaji wengine, Je Serikali, kupitia ofisi ya Msajili waHazina na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inafanyajuhudi gani kuhakikisha hati ya kutodaiwa inapatikana nahati hiyo ya hisa inatolewa kwa jina la STAMICO.

Mheshimiwa Spika, changamoto za kiutendajizinazoukabili mgodi wa makaa ya mawe ya Kiwira ni pamojana ukweli kwamba toka mgodi huu uhamishwe STAMICOmwaka 2014, hakuna fedha za maendeleo zimewahikupelekwa. Suala hili limesababisha kushindwa kuanzakuzalisha.

Page 251: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

251

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Bunge lako tukufuinataka kufahamu ni lini Serikali itapeleka fedha katika mgodihuu kama ambavyo zimekuwa zikipangwa lakini hazipelekwihuko? Pia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka majibukujua ni lini Kiwira italipa shirila la umeme TANESCO deni lamuda mrefu la kiasi cha shilingi bilioni 1.8.?

10. Mgodi wa Cata Mining Company

Mheshimiwa Spika, kuna kampuni ya uchimbajimadini inayoitwa CATA MINING COMPANY LTD yenye MiningLicense Na. 483/2013, inayofanya shughuli zake katika eneola Kiabakari, Wilaya ya Musoma Vijijini. Kampuni hiyo iliyokuwana leseni 16 za uchimbaji mdogo (Primary Mining License-PML) zilizokuwa zinamilikiwa na Ndugu MAHUZA MUMANGINYAKIRANG’ANI.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa vijiji vya Kiabakarina Nyamisisye wanalalamika kuhusiana na uharibifu wanyumba zao takriban mia saba (700) uliotokana na milipukoya baruti za kupasua miamba na hivyo kupata hasara kubwasana. Aidha,wananchi hao wanatuhumu pia kwambasehemu ya uchimbaji huo unafanyika ndani ya Kambi ya Jeshila Wananchi Tanzania. Kwa mujibu wa ramani ambayoKambi Rasmi ya Upinzani inayo nakala eneo la uchimbajilinaonekana kuwa ni kijiji cha Kyawazaru/Katario na Kitongojicha Kyarano na si eneo la jeshi lililoko kijiji cha Nyamisisye.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inazotaarifa kwamba Wizara ya Nishati na Madini ilishapewamalalamiko hayo lakini hajayapatia ufumbuzi unaostahili.Hivyo, Waziri atoe maelezo Bungeni ni kwanini ameshindwakumaliza mgogoro huo mpaka sasa?

11. Wachimbaji wadogo wadogo

Mheshimiwa Spika, Miongoni mwa changamotozil izoko katika sekta hii ni pamoja na changamotozinazowahusu wachimbaji wadogo wadogo. Pamoja namaelezo ya Serikali kuhusu hatua ambazo Serikali imekuwa

Page 252: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

252

ikichukua dhidi ya kundi hili lakini bado uchimbaji mdogowa madini umekuwa ukiendelea kwa kutumia nyenzo nateknolojia duni ya uchimbaji na kukosa taarifa sahihi zamashapo katika maeneo wanayochimba. Pamoja nakutengwa kwa maeneo machache ya wachimbaji, kupewaleseni za uchimbaji lakini bado wachimbaji wadogo wadogowanapewa maeneo ya kuchimba bila kuwa na uhakika wauwepo wa madini kwenye eneo husika.

Mheshimiwa Spika, baadhi ya wachimbaji wadogowadogo wamekuwa wakipata mikopo kidogo kwa ajili yakuendeshea shughuli za uchimbaji na kwa kuwa Serikaliimekuwa ikiwatengea maeneo machache ya kufanyauchimbaji huo lakini baada ya muda wachimbajiwanalazimika kuhama maeneo hayo kwa kile wanachodaimaeneo hayo hayana madini.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinataka kupata maelezo ya Serikali ni lini sasa Serikali itasaidiakufanya utafiti wa awali kwenye maeneo ili wanapokujakuwagawia wachimbaji wadogo wadogo hawa, uwepouhakika kwa wachimbaji wadogo wadogo hao kupatamadini kipindi wakipewa maeneo husika?

12. Ukaguzi wa Mazingira Migodini

Mheshimiwa Spika, uchafuzi wa mazingira migodinini tatizo ambalo linaikumba migodi mingi iliyopo hapa nchini.Wakati swala la mazingira lipo chini ya Ofisi ya Makamu waRais, Wizara ya Nishati na Madini pia inahusika na madharaya mazingira yanayotokana na shughuli za uchimbaji wamadini kwa wachimbaji wadogo wadogo, wachimbaji wakati pamoja na wachimbaji wakubwa.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Nishati na Madini,kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini (Tanzania Mineral AuditAgency) zilisaini hati za makubaliano na baraza la taifa lamazingira NEMC ili kuwawezesha TMAA kufanya ukaguzi wauchafuzi wa mazingira migodini. Hata hivyo taarifa inaoneshakwamba mara nyingi migodi inapokuwa inafanya uchafuzi

Page 253: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

253

wa mazingira hutozwa faini kulingana na uchafuzi ulifanywana kutakiwa kumaliza tatizo hilo.

Mheshimiwa Spika, mgodi wa Tulawaka Gold MinesProject uliwahi kukutwa na tatizo la kutiririsha kemikali namgodi huo ulipaswa kulipa faini ya shilingi milioni 25 na mgodiulilipa faini hiyo, aidha tatizo siyo ulipaji wa faini hiyo ila tatizolinaonekana kuwepo kwenye kutokusitisha uchafuzi huo wamazingira. Mgodi wa Kilimanjaro Mine ltd ulitozwa faini yashilingi milioni 6 lakini zililipwa mil 2 pamoja na kwambakiwanda kiliomba NEMC kuwapunguzia adhabu. Migodiambayo imewahi kutembelewa na kubainika matatizo yauchafuzi wa mazingira ni pamoja na Golden Pride Ltduliotozwa faini ya milioni 60 kutokana na kosa la kutiririshauchafu wenye madhara, mgodi wa Bulyanhulu –kutiririshauchafu hatarishi, mgodi wa North mara, Geita Gold Minesna mgodi wa Williamson Mines Ltd.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinatoa rai kwa Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini-TMAA kwa kushirikiana na NEMC kuhakikisha inafanya ukaguzikwa lengo la kuangalia ni kwa kiasi gani, matatizoyaliyopelekea migodi hiyo kutozwa faini yaliwezakuhitimishwa.

H. UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGEMheshimiwa Spika, Bunge hili limekuwa likitoa

maazimio mbalimbali yanayohitaji utekelezaji wa Serikali,lakini kwa bahati mbaya sana, Bunge limekuwa halipatiwimrejesho wa utekelezwaji wa maazimio hayo. Tafsiri ya jambohili ni dharau au ni kutokana na ukweli kwamba Bunge hilihalina meno.

Mheshimiwa Spika, Bunge la 10 lilipitisha maazimiobaada ya Kamati ya PAC kupitia taarifa ya mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kuhusiana na fedha zaCapacity Charge ambazo TANESCO ilikuwa inatakiwa kuilipaIPTL lakini kukawepo na kesi ya kupinga kiwango hicho chamalipo na kulazimu fedha hizo ziwekwa Benki Kuu kwakufungua akaunti iliyoitwa “Tegeta Escrow Account”.

Page 254: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

254

Mheshimiwa Spika, tarehe 28 Novemba, 2014 Bungelilipitisha maazimio nane (8) kuhusiana na uporwaji wamabilioni ya fedha za Serikali zilizokuwa zimewekwa Benki Kuu.Lakini azimio moja lilikuwa na uhusiano wa moja kwa mojana utendaji wa TANESCO kwa kupunguza nguvu ya shirikanalo ni Azimio Namba 7- lililosema kwamba nanukuu “Bungelinaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununuamitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwaTANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo”.

Mheshimiwa Spika, hadi sasa Bunge halipewa taarifaya utekelezaji wa azimio hilo na hadi sasa TANESCO badoinalipa kiasi cha shilingi bilioni 4.3 kila mwezi. Kambi Rasmi yaUpinzani inataka maelezo ni kwanini Serikali imeshindwakutekeleza azimio hilo na kuendelea kumlipa mtu aliyeinunuaIPTL katika mazingira yenye ufisadi?

Mheshimiwa Spika, Spika Anne Makinda aliundaKamati Maalumu ya Bunge kwenda kuzungumza nawananchi wa Mtwara kuhusu sakata la ujengwaji wa bombala gesi asilia kutoka mkoani humo hadi Dar es Salaam, kufuatiakuzuka kwa vurugu tarehe 22 Mei 2013. Kamati hiyo yaMheshimiwa Spika Makinda ilikuwa chini ya Mbunge waMuleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM).

Mheshimiwa Spika, Kamati hii ya Bunge ilitumia fedhaza walipa kodi na il ifanya kazi na kuiwakil isha kwaMheshimiwa Spik tarehe 20 Desemba, 2013. Kambi Rasmi yaUpinzani inaitaka Spika kuwezesha taarifa hiyo kuwasilishwaBungeni ili mapendekezo ya kamati hiyo yajadiliwe na Bungena kuwa maazimo rasmi ya Bunge na kuweza kutekelezwana Serikali.

Mheshimiwa Spika, aidha yamekuwepo pia maazimiomengine ya Bunge juu ya uchunguzi kuhusiana na mapatokwenye gesi asilia hususani juu ya Kampuni ya Pan AfricanEnergy Tanzania (PAT) ambayo nayo Serikali haijawasilishaBungeni taarifa ya kuhitimisha utekelezaji. Hivyo, Kambi Rasmiya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuwasilisha taarifa

Page 255: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

255

maalum Bungeni juu ya utekelezaji wa maazimio yote yaBunge yanayohusu Wizara ya Nishati na Madini ambayohayajatekelezwa mpaka sasa.

I. MWENENDO USIORIDHISHA WA MPANGO WAUWAZI NA UWAJIBIKAJI KATIKA TASNIA YA UZIDUAJITANZANIA-TEITI

Mheshimiwa Spika, Mpango wa Uwazi na Uwajibikajikatika Tasnia ya Uziduaji(EITI) ni wa kimataifa ulioanzishwamwaka 2003 kwa utiwaji saini kanuni 12 za uwazi katikamalipo na mapato ya sekta ya uziduaji ili kuongeza uwazikatika uendeshaji wa tasnia ya uziduaji. Mpango huu ni umojawenye uwakilishi sawa baina ya Serikali, Makampuni na Asasiza kiraia.

Mheshimiwa Spika , Kimataifa, mpango huuunasimamiwa na Bodi ya Kimataifa yenye uwakilishi waSerikali zinazotekeleza mpango huu, makampuni na asasi zakiraia zinazounga mkono uwazi na uwajibikaji katika tasniaya uziduaji. Baada ya kusainiwa kwa kanuni hizo, mpangohuu umeungwa mkono na asasi za kiraia, wawekezajiwakubwa karibia wote na mataifa 52 Tanzania ikiwemo.Tanzania ilijiunga na mpango huu tarehe 16 mwezi wa pilimwaka 2009 kwa tamko la Rais.

Mheshimiwa Spika, toka Tanzania ianze kutekelezampango huu, wananchi wamepata fursa ya kupata baadhiya taarifa za mapato yanayotokana na madini na gesi asilia,tofauti kati ya malipo yaliyofanywa na makapuni na mapatoyaliyopokelewa na Serikali. Pia taarifa juu ya makampunigani yanalipa kodi kwa kiasi gani na yapi hayalipi tozo nakodi mbalimbali stahiki zimetolewa.

Mheshimiwa Spika, hii imesaidia ukuaji wa mapatokutoka kwenye sekta ya uziduaji kwani uwazi na uwajibikajiumeongezeka kiasi. Tanzania imekwisha toa ripoti 6 zamlinganisho wa malipo na mapato ya tozo na kodimbalimbali ambazo zilifichua upungufu wa takriban TZS63,748,566,888.00 ambazo ni fedha za tozo na kodi zilizolipwa

Page 256: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

256

Serikalini kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2014 kamaifuatavyo:

* Ripoti ya tatu imeondolewa kwenye mitandao yotekwa shinikizo la makampuni

Mheshimiwa Spika, toka mpango huu uanze, fedhazilizoripotiwa kupotea zimekuwa zikipungua kila mwakakama ilivyooneshwa hapo juu na mapato yaliyoripotiwakupatikana yamekuwa yakipanda kama ifuatavyo; ripoti yakwanza Bil. 128, ripoti ya pili Bil. 435, ripoti ya tatu takribaniBil.500, ripoti ya nne takribani Bil.700, ripoti ya tano Bil. Takribani900 na ripoti ya sita takribani Tril.1.2 fedha za kitanzania.

Mheshimiwa Spika, Mwaka 2015 mpango huuulipewa nguvu ya kisheria kwani baadhi ya Taasisi namakampuni yalikuwa hayatoi ushirikiano ipasavyo. Pamojana mapungufu yaliyopo kwenye Sheria, sheria imeundaKamati ya kutekeleza mpango huo iitwayo Kamati ya TEITIchini ya kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Uwazi na UwajibikajiKatika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia TanzaniaNa. 23 ya 2015. Chini ya Sheria hii, Kamati hiyo inapaswa kuwana Mwenyekiti anayeteuliwa na Rais wa Jamhuri ya

2008/9 23,738,542,000.00

2009/10

5,002,169,000.00

2010/11* 11,000,000,000

2011/12

2,148,537,891.00

2012/13 12,920,549,420.00

2013/14

8,938,768,577.00

Total

63,748,566,888.00

Page 257: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

257

Muungano wa Tanzania na wajumbe wengine wasiopunguakumi na tano wakiwemo watano wanaoteuliwa na Waziriwa Nishati na Madini (Serikali), watano kutoka kampuni zauziduaji na watano kutoka asasi za kiraia zinazojihusisha namasuala ya utawala bora katika tasnia ya uziduaji.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa kanuni zakimataifa za mpango huu na kifungu cha 8 cha Sheria hii,Kamati ya TEITA inapaswa kuwa madarakani kwa kipindi chamiaka mitatu na wajumbe wanaweza kuteuliwa tena kwakipindi kingine kimoja tu. Kutokana na ukweli kuwa kamati hiiilianza kabla ya sheria kuanza, Kamati iliundwa mara yakwanza mwaka 2009 na kumaliza muda wake mwaka 2012,uchaguzi na uteuzi wa wajumbe na mwenyekiti ulifanyika,japo baadhi ya wajumbe walirudi kwani kanuni ziliruhusu.Wajumbe hao wa mwaka 2012 walimaliza muda waomnamo mwaka 2015 na uchaguzi na uteuzi wa wajumbewengine ulifanyika mwaka 2016 kwa mujibu wa sharia ya TEITI.Mchakato huu uliingia doa kubwa la kisheria.

Mheshimiwa Spika, kinyume na matakwa ya Sheria,hususan kifungu cha 5(1) kinachompa mamlaka Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua Mwenyekiti,aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongoakiwa anafahamu hana mamlaka alimteua KaimuMwenyekiti wa Kamati hiyo nafasi ambayo haipo kisheria.Kaimu huyu ameendelea kuwepo na anaendesha shughuliza Kamati huku akiwa hana mamlaka kisheria na hivyo yoteyanayofanyika chini yake ni batil i l icha ya fedhazinazoendelea kutumika kuyafanya hayo wakati wakitambuakuwa si halali mbele ya sheria.

Mheshimiwa Spika, tunafahamu kuwa Kamati yaUteuzi ya Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI inayoundwa chiniya kifungu cha 6(1) iliitoa tangazo la wananchi kupelekamaombi ya kujaza nafasi hiyo ya Mwenyekiti. Kinachoibuamaswali ni kuwa Kamati hii ya Uteuzi baada ya kufanya usailina wananchi walioomba kujaza nafasi hiyo ilitoka na majibukuwa wote walioomba hawana uwezo wa kuijaza nafasihiyo.

Page 258: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

258

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu waKamati ya TEITI tulitarajia, Kamati ya uteuzi ingelirudia zoezihilo mara moja au kutumia njia nyingine bora ili ipendekezemajina kwa Rais kwaajili ya uteuzi. Hadi leo, ni mwakaumekwisha pita na hakuna lililofanyika. Inashangaza zaidihata Kamati ya TEITI iliyoko madarakani inayoongozwa naKaimu Mwenyekiti ilipoomba kupata majina ya walioombakujaza nafasi hiyo, mpaka leo haijawahi kupewa majina hayoili ijiridhishe kuwa ni kweli hawana sifa, japo uchunguzi wasuala hil i unaonesha kuwa CAG Mstaafu Utuoh nimmojawapo wa watanzania walioomba kujaza nafasi hiyo.

Mheshimiwa Spika, Katika mazingira hayo, KambiRasmi ya Upinzani inaona kuwa ni dhahiri kuwa Serikali hainautashi wa dhati wa kushiriki mpango huu wa uwazi nauwajibikaji? Na hata kama hakuna utashi wa kisiasa, je nihalali kuvunja sheria halali iliyotungwa na Bunge la Jamhuriya Muungano wa Tanzania kwa makusudi?

Mheshimiwa Spika, ni muhimu pia ikafahamika kuwakatika kifungu cha 10(2) cha Sheria ya Uwazi na Uwajibikajikatika Tasnia ya Uziduaji ya Mwaka 2015, Kamati ya TEITIimepewa majukumu makubwa na muhimu, baadhiyakiwemo ni kufanya uchunguzi wa jambo lolote linalohusuuziduaji ikiwemo viwango vya uzalishaji wa makampuni yauziduaji.

Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi, Waziri bilakuwa na mamlaka na kinyume cha sheria hususan kifungucha 5(4) cha sheria hiyo Na. 23 ya 2015 hakutangaza mjumbemmoja aliyechaguliwa kihalali na asasi za kiraia kamainavyotakiwa kisheria. Ifahamike kuwa, wajumbe watanotoka asasi za kiraia wanapaswa kuchaguliwa na asasi zakiraia kwa utaratibu wao na kupelekwa kwa Waziri iliwatangazwe kama walivyo na sio vinginevyo.

Mheshimiwa Spika, bila kuwa na mamlaka na hukuakivunja sheria, Waziri aliacha kutangaza jina moja lamwakilishi wa asasi za kiraia kutoka kwenye majina matanoyaliyowasil ishwa kwake bila kutoa sababu zozote.

Page 259: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

259

Tunafahamu kuwa yapo malalamiko ambayo yalipelekwakwa Waziri juu ya mchakato wa kuwapata wawakilishi haowatano ila hata baada ya juhudi za Waziri kueleweshwa juuya kutokuwepo kwa uhalali wa malalamiko hayo kulikofanywa na muungano wa asasi za kiraia zinazojishughulishana masuala ya uziduaji uitwao HAKIRASILIMALI, bado Wazirihakulifanyia kazi jambo hilo ambalo tarehe 30/05/2017lilikamilisha mwaka. Pia ni vyema ikafahamika chini ya Sheriahiyo Namba 23 ya 2015, Waziri hana mamlaka kupokea rufaaza uteuzi wa wawakilishi wa asasi za kiraia wala wale wakampuni za uziduaji.

Mheshimiwa Spika, ukiacha uvunjaji huo wa sheriaya uwazi, Sekretariat ya TEITI imekumbwa na kashfa yakimataifa ya wizi wa kimtandao ambayo inalichafua jina laTaifa letu kitaifa na kimataifa. Sekretariat ya TEITI iliingiamkataba na asasi ya Ujerumani-Open Oil, ikiwapa kazi yakutoa mafunzo juu ya uwazi wa mikataba ya sekta yauziduaji. Katika makubaliano yao, TEITI ilipaswa kuilipa OpenOil baada ya kutoa mafunzo.

Mheshimiwa Spika, Open Oil walimaliza kazi yao nakudai malipo ambayo inasemekana yalilipwa kwa njia yamtandao kutoka Benki Kuu ya Tanzania kwenda kwenyeakaunti namba 26110562 iliyopo benki ya Llyods ya mjiniLondon, Uingereza inayosemekana ni ya Open Oil UG baadaya mazungumzo na mwakilishi wa Open Oil. Hata hivyo,baada ya muda sio mrefu, OpenOil walidai malipo yao nakuambiwa kuwa yalishalipwa. Baada ya uchunguzi wa awaliwa Serikali, iligundulika kuwa domain name ya Open Oililikuwa imedukuliwa na hivyo malipo hayakwenda kwamlengwa Open Oil. Serikali ilianzisha uchunguzi wa udukuzihuo kupitia Interpol lakini uchunguzi huo haujakamilikampaka sasa toka mwaka 2016 ulipoanza huku kukiwepo nataswira ya udanganyifu kwa upande wa taasisi za Tanzania.

Mheshimiwa Spika, Uvunjwaji huu wa sheria katikauteuzi wa Kaimu Mwenyekiti na kutokutangaza Mjumbe watano aliyechaguliwa kihalali na asasi za kiraia na kutokufuatiliaipasavyo upotevu wa malipo ya Open Oil umelitia doa taifa

Page 260: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

260

letu na Serikali ya Awamu ya Tano kitaifa na kimataifa kiasikwamba, Tanzania iko mbioni kuondolewa kwenyeutekelezaji wa Mpango huu wa Uwazi na Uwajibikaji waKimataifa.

Maswali ya msingi kwa Wizara ya Nishati na Madini nikama ifuatavyo;

i. Je, Serikali inaelewa umuhimu wa kutatuamatatizo haya mapema kwani ikichelewa Tanzaniaitaondolewa kwenye ushiriki wa mpango huu?

ii. Je, Serikali inaweza kulihakikishia Bunge hilikuwa bado inathamini uwazi na uwajibikaji na hivyo badoinaunga mkono mpango huu.

iii. Je, Serikali inaweza kulihakikishia Bunge hili nilini itayatatua matatizo haya ikiwemo ni pamoja nakumtangaza mwakilishi wa tano wa asasi za kiraia, Raiskumteua mwenyekiti mahsusi wa Kamati hii nyeti nakukamilisha uchunguzi wa malipo ya Open Oil na kuchukuahatua?

iv. Je, Wizara inamelezo gani kuhusu kuondolewamtandaoni kwa taarifa ya tatu ya TEITI (2011/12)?

J. MKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWAMWAKA 2017/ 2018

Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2017/2018, Wizara ya Nishati na Madini inakadiria kutumia jumlaya shil ingi 998,337,759,500 iki l inganishwa na shil ingi1,122,583,517,000 zilizoidhinishwa na Bunge mwaka 2016/2017,sawa na upungufu wa 11%. Sababu zinazotolewa na Serikaliza kupungua kwa Bajeti ni kupungua kwa makadirio ya fedhaza nje kutoka shilingi 331,513,169,000 mwaka 2016/ 2017 hadishilingi 175,327,327,000.

Mheshimiwa Spika, madhara ya kukosekana kwafedha za nje, yanaonekana kuendelea kuiathiri Bajeti ya

Page 261: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

261

Serikali hii kwa kuwa, kwa mujibu wa makadirio ya Bajeti yaMaendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini, Wizara imetengakiasi cha shilingi 938,632,006,000 ikilinganishwa na shilingi1,056,354,669,000 zilizotengwa mwaka 2016/17, sawa naupungufu wa 11.1%. Aidha wakati mwaka huu 2017/2018bajeti ya Wizara hii ikipunguzwa asilimia 11.1%, bajeti ya 2016/2017 Wizara ya Nishati na madini i l ipewa na hazina404,120,668,889.00 sawa na 36% ya fedha zote za bajeti yaWizara hii iliyopitishwa 2016/2017.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Bunge lako tukufuinaona haya ni madhara ya Serikali kutopenda ushauri nakuona haipangiwi cha kufanya. Kwa muktadha huo KambiRasmi ya Upinzani Bungeni inataka majibu kutoka Serikalinikuhusu mambo yafuatayo:

i . Ni sababu zipi za msingi zinazopelekeakupungua kwa fedha za nje kwenye Bajeti ya Wizara.

ii. Miongoni mwa vyanzo vya fedha kutokachanzo cha nje kilikuwa ni fedha kutoka Millenium ChallengeCorporation, na MCC ilisitisha msaada wake kwa Tanzaniakutokana na kukosekana kwa utawala bora, kufutwa kwauchaguzi wa Zanzibar na kuvunjwa kwa Haki za Binadamu,Je Serikali inachukua hatua gani za kuondoa sababuzilizopelekea wadau wa maendeleo kusitisha misaada yakekwa Tanzania likiwemo shirika la misaada la Marekani MCC

K. HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeniinapenda kusisitiza kama ambavyo imekuwa ikifanya katikahotuba zilizowahi kutangulia kwamba, sehemu kubwa yamatatizo ya Wizara ya Nishati na Madini yamechangiwa nayanaendelea kuchangiwa na sababu za kibinadamuikiwemo ukosefu wa utashi wa kisiasa huku maswala muhimuyakiachwa.

Page 262: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

262

Mheshimiwa Spika, Taifa lilihitaji na bado linahitajimabadiliko ya kimfumo ili kuwezesha hatua za haraka zakusimamia sera sahihi, uongozi makini na taasisi thabiti katikasekta nyeti za Nishati na Madini, pamoja na kuchukua hatuastahiki ili kuziwezesha sekta hizi za Nishati na Madini kuongezapato la Taifa na kupelekea wananchi kuzifaidi rasilimali zao,kuliko matamko hewa ambayo yanalenga kupata umaarufuwa kisiasa, huku hatua zinazopaswa kuchukuliwa zikiachwamiaka nenda miaka rudi.

Mheshimiwa Spika, nimalize kwa kuwashukuruwananchi wa jimbo la Kibamba na Wilaya mpya ya Ubungokwa kukikataa Chama Cha Mapinduzi, nawashukuru kwakunipatia ushirikiano wao katika kazi za kuwawakilishakwenye vyombo vya maamuzi na kuhamasisha maendeleojimboni kwetu. Kwa namna ya pekee Nitambue mchangowa Meya wetu wa Ubungo, Mheshimiwa Boniface Jacobpamoja na madiwani wote ambao hufanya kazi kwa niabayangu jimboni ninapokuwa kwenye majukumu mengine yakitaifa. Nawashukuru Viongozi mbalimbali kwa ushirikianowao, viongozi wa kidini na kiroho na wanafamilia yaMarehemu Mzee wetu John Michael Dalali kwa ushauri waona kunipatia ujasiri wa kuendeleza uadilifu katika kusimamiaukweli, haki na ustawi wa jamii ya watanzania.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hao, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni naombakuwasilisha!

……………………John John Mnyika (Mb)

Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya UpinzaniWizara ya Nishati na Madini

01/06/2017

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mnyika.(Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea na uchangiajibaada ya kusikia hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini,

Page 263: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

263

hotuba ya Mwenyekiti na pia Msemaji wa Kambi Rasmi yaUpinzani. Tutaanza na wachangiaji walioko hapa mbele, kilachama kimeleta majina. Tutaanza na Mheshimiwa NajmaGiga, atafuatiwa na Mheshimiwa Sixtus Mapunda naMheshimiwa Balozi Adadi Rajab ajiandae.

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa NaibuSpika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kwanza. Kwanzasina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezeshakufika mwezi huu wa Ramadhani tukiwa wazima nakutekeleza majukumu yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwanza kabisa kwakuunga mkono hotuba ambayo imetolewa na Wizara hii yaNishati na Madini. Kwa kweli Serikali kwa upande wa Wizarahii imejitahidi. Vyovyote tutakavyofanya na kusema hatunabudi kuishukuru Serikali kwa jitihada inazochukua katika sualala sekta hii ya nishati na madini hasa tukizingatia usimamiziimara uliopo katika Awamu hii ya Tano ya Serikali yetu chiniya uongozi makini kabisa wa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. JohnPombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia sina budikumshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza laMapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kwa namna ambavyoamepokea wito wa uungwana kabisa na busara kulipokeadeni ambalo ZECO inadaiwa na TANESCO na kuahidi kulilipa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vile dawa ya deni nikulipa, Mheshimiwa Rais amechukua hekima na busarakuweza kukubali na mpaka hivi sasa deni la shilingi bilioni11.8 limeshalipwa ambapo shilingi bilioni 10 zimelipwa naSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na shilingi bilioni 1.8zimelipwa kupitia ZECO. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli hatuna budikuipongeza Serikali kupitia TANESCO, tusipoipongezatutakuwa hatuna shukrani. Pamoja na upungufu yoteambayo TANESCO inayo lakini kazi inayofanywa lazimatuishukuru na kuithamini. (Makofi)

Page 264: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

264

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona kwenye kitabuhumu miradi mbalimbali imeshatekelezwa ikiwemo KinyereziI na II ambazo zinaendelea lakini pia tuna REA, usambazajiwa umeme vijijini, kazi inafanywa kubwa kwa mazingiramagumu. Tukipita sisi wengine tunaona juu ya milima kunanguzo huko, tunashangaa zimetandazwaje, chini yamabonde huko tunakuta nguzo tunashangaazimetandazwaje, lazima tuwe wenye kushukuru na lazimatuwapongeze. Naamini kwamba Serikali kupitia TANESCOitatatua changamoto hatua kwa hatua ili tuweze kwendavizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mchango wangu utaelekeahuko huko kwenye nishati ya umeme na hapa nitazungumziamfumo uliopo baina ya Shirika la TANESCO na ZECO. Nisemewazi kwamba kutokana na mfumo uliokuwepo siku za nyumana pengine huu uliopo sasa hivi, ndiyo umepelekea ZECOkuwa na deni kubwa kwa TANESCO. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nielezee yaleambayo yamepeleka mfumo huu kuonekana kamaunaendelea kuipa deni ZECO. Kwanza ni tozo ya KVA. Hiinikizungumza wataalam wanaelewa, ni tozo ya watumiajiwakubwa wa umeme kwa mfano viwanda na kadhalika.ZECO tunachukua kilovoti 132 kwa bei ya shilingi 16,550 lakiniwatumiaji hawa wa kilovoti 33 ambao wanachukua kwaTanzania Bara wanatozwa shilingi 13,200 kwa kilovott moja.Kwa hiyo, utaona difference iliyopo ya mfumo katikauendeshaji na kuipelekea ZECO kuweza kulimbikiza deni.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wawekezaji ambaowana tamaa ya kuwekeza Zanzibar wanashindwa kuwekezakwa ajili ya tozo hii, hivyo naomba sana Serikali ilizingatie.Kwa mfano, mwaka 2011 utaona pia mtiririko wa mabadilikoya tozo unavyobadilika, naweza kutoa mfano mwaka 2011ZECO iliongezewa tozo ya asilimia 81.1 wakati Tanzania Barailiongezwa tozo ya asilimia 19.4 tu, ni difference kubwa sana.Kwa hiyo, naomba Serikali izingatie sana kupitia Shirika hili laUmeme. (Makofi)

Page 265: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

265

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukitoa mfano pia mwaka2013 TANESCO na ZECO walikubaliana kupitia Wizara yaNishati na Madini kwamba sasa umefika wakati hizi kilowattsper hour Zanzibar ipunguziwe kwa asilimia 31. Matokeo yake,TANESCO iliendelea kuingiza hiyo asilimia 31 hatimaye denihili likatajwa mwisho wake kuwa ni shilingi bilioni 121.9 ambayoround figure ni shilingi bilioni 122 wakati ZECO wanaendeleakuhesabu kwamba wameshatolewa punguzo la asilimia 31na kulikubali deni hilo kuwa ni shilingi bilioni 65.5. Kwa hiyo,tunaweza kuona difference hizo na naomba sanaMheshimiwa Waziri husika na timu yake waweze kuangaliakwa upande huu wa TANESCO. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni suala la ZECO kuwaend user, nikizungumza end user anakuwa kama mtumiajiwa kawaida wa Tanzania Bara. Kwa nini nasema hivyo? Kwasababu mtumiaji wa kawaida wa Tanzania Baraanapelekewa umeme kupitia miundombinu ya TANESCOlakini ZECO tunaletewa umeme kwa bei ambayo mtumiajiwa Tanzania Bara anapewa with operational costs za ZECO,miundombinu na gharama zote ni za ZECO. Kwa hiyo,tuangalie hali inavyokwenda tuone mfumo uko vipi, niayangu ni kueleza mfumo huu tuweze kuusahihisha ili tuwezekwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kutokana na hilitunasema kwamba ZECO na TANESCO ni mashirika ya Serikali,moja kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano na linginekupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. ZECO yenyeweinakuwa na madeni ambayo inadai Taasisi za Serikaliikiwemo na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru MheshimiwaHussein Mwinyi, Wizara yake imeweza kupunguza shilingimilioni 400 deni ambalo tulikuwa tunawadai na sisi ndiyotumeweza kurudisha TANESCO. Kwa hiyo, tuangalie hayamambo ili sisi tuweze kulipa deni na Serikali taasisi zake iwezekulipa. (Makofi)

Page 266: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

266

MBUNGE FULANI: Sawa sawa.

MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Kwa hiyo, hilo ni mojaambalo nilipenda nizungumzie kwa upande huo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna huduma nyingineza jamii ambazo zinaigusa jamii moja kwa moja. Kwa mfano,ZAWA ambayo inashughulika na masuala ya kusambaza majiZanzibar, tunaidai zaidi ya shilingi bilioni 20. Tunashindwakuwafungia umeme kwa sababu Watanzania wanaoishiZanzibar watakosa maji. Kwa hiyo, inabidi shirika hili tuonemfumo gani ambao utaweza kuwa bora na mzuri ili tusijetukaingia kwenye migogoro ambayo mimi sipendi kuiita kero,nasema bado ni challenge, tuzirekebishe hizi challenge iliWatanzania wote wanaoishi Tanzania Bara na wale waliokoZanzibar ambao wote ni wa Jamhuri ya Muungano yaTanzania waweze kunufaika na huduma hii bila matatizoyoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hili Shirika la ZECOlinafanya kazi kubwa kuikusanyia mapato TANESCO. Mbalina hayo madeni ambayo yametokana na hizo sababunilizozitaja, tunatumia umeme kuanzia shilingi milioni 400 hadishilingi milioni 500 kwa mwezi na bahati nzuri kuanzia mwaka2015 Desemba tunalipa current bill kwa maana kwambaankara kamili ya kila mwezi. Kwa hiyo, ili kuweka sawamambo haya, tuonekane na sisi ZECO kule kwambatunaifanyia biashara TANESCO ambayo ni taasisi ya Jamhuriyetu ya Muungano Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mfano mwingine,tumeweza kuikusanyia shilingi bilioni 41.8 katika kipindi chamiezi tisa kuanzia 2016 hadi kufikia Machi, 2017. Kwa hiyo,sasa nachoshauri mbali na kuwekwa huyu MtaalamMwelekezi nitaomba ushauri wake ufuatwe ili twende sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho ni kwamba sisiZECO basi angalau tupewe fursa ya kuwa agent wa TANESCOili tuweze kulipwa na kuweza kugharamia operation cost ilitusiweze kuleta migogoro katika Muungano. (Makofi)

Page 267: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

267

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipanafasi, pamoja na kuunga mkono hotuba hii naomba sanaushauri huu uweze kuzingatiwa ili tuweze kuimarishaMuungano wetu. Ahsanteni sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwenyekitiwetu. Nadhani Serikali imesikia yale ambayo yatawezakujibiwa hapa sawa yatajibiwa hapa, yale ambayohayatahusiana moja kwa moja na shughuli za Bunge hili,tafadhali myashughulikie huko kwa namna ya ofisi ili Bungelisije likajikuta linajadili mambo ambayo halina mamlakanayo.

Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea naMheshimiwa Sixtus Mapunda atafuatiwa na MheshimiwaBalozi Adadi Rajab.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa na mimi nafasi ya kuchangiakwenye hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, naombanichukue fursa hii kuipongeza Wizara kwa hotuba nzuriambayo kwa kweli ukiitizama kwa kina inatoa matumainiya Taifa letu kwenda kwenye nchi ya viwanda hasaukizingatia msingi mkuu wa Taifa la viwanda unatokana naWizara hii ya Nishati na Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2015 kipindi chakampeni, Rais wetu mpendwa wakati anajinadi alipofikiakuongelea suala la sekta ya madini ali j ipambanuapasipokuwa na kificho kwenye changamoto kubwa tanozinazoikabili Wizara ya Nishati na Madini au katika ujumlawake sekta ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais wetu mpendwaalizunguka nchi nzima akasema, toka tumeingia ubia nawabinafsishaji na hawa wenzetu, tukawapa migodiwakashirikiana na sisi tumepita kwenye changamoto kubwazifuatazo:-

Page 268: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

268

(i) Kunyanyaswa kwa wachimbaji wadogo,sambamba na kulipwa fidia ndogo wawekezajiwanapotwaa maeneo. (Makofi)

(ii) Sekta ya madini ina usimamizi mbovu unaopelekeaSerikali kukosa mapato. (Makofi)

(iii) Sekta ya madini inakutana na changamoto yakutoroshwa kwa madini kwa njia mbalimbalikunakoipotezea Serikali mapato. (Makofi)

(iv) Sekta ya madini inakutana na changamoto yamikataba mibovu inayoipunja Serikali mapato. (Makofi)

(v) Sekta ya madini inakutana na tatizo la matumizimabaya ya misamaha ya kodi ambayo wawekezajiwamepewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais akamaliziakwa kusema mkinipa ridhaa ya kuongoza nchi hii,nitahakikisha haya mambo matano nakwenda kuyafanyiakazi. Watanzania wakamuamini wakampatia Urais, akaingiaofisini toka siku kwanza kipindi cha hotuba yake hapa Bungeniakasema nchi yetu tajiri, nchi yetu ina rasilimali nyingi,tukizitumia rasilimali zetu vizuri nchi yetu itakuwa donorcountry. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina uhakika aliyasemahaya kwa sababu alikuwa anaijua Tanzania vizuri. Akajipamuda wa kutosha, akai-study hiyo sekta ya madini akajakugundua kuna makinikia yanatoweka nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo yote niliyoyasema yapokwenye changamoto namba tatu niliyosema sekta ya madiniinakutana na utoroshwaji wa madini, kwa namna yoyote ileiwe hoja ya kisheria, iwe hoja ya mahusiano, hoja yakutoroshwa kwa madini yetu Watanzania Raisalikwishaisema na akafanyia kazi. Leo hii namshangaaMtanzania yeyote yule anayehoji modality au namna Rais

Page 269: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

269

alivyoitengeneza Tume ya kwenda kuyakamata nakuyachunguza yale makontena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mtu mmoja anaitwaEdmund Burke na baadaye Abraham Lincoln na Martin Lutherthe King waliwahi kusema, evils will prevail if good peopledo nothing. Changamoto zote za madini tunazozionazitaendelea kuwepo kama watu wazuri hawatafanya kitu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, alichokifanya Rais wetu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ile segment ya watuwazuri wanapofanya jambo ambapo kuna uovu.Kinachonishangaza mnataka uovu tuutengenezee modality?Unavyokwenda kumkamata mwizi unataka umtaarifu mwizikesho nitakuja kukukamata, ujiandae pamoja na mtu wakukuwekea dhamana ili ukifika Mahakamani tukutoe, jamani!Hivi kweli sisi ni wazalendo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachonikwaza zaidi siohili...

MBUNGE FULANI: Sema baba.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,kinachonikwaza zaidi hii ajenda kwa muda mrefu pioneerswalikuwa wale pale. Pioneers wa ajenda hii kwa muda mrefuwalikuwa wale pale, tutawataja kwa majina …

MBUNGE FULANI: Ndiyo. (Makofi)

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,waliosema hizi changamoto tano wale kule, MheshimiwaMnyika umewahi kusema, Mheshimiwa Mwita Waitaraumewahi kusema, Mheshimiwa Tundu Lissu amewahi kusema,hawa ndiyo waliosema hayo mambo matano. Tenawakasema mnakaa na hii mikataba ya nini si vunjeni,hawakusema wale. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Walisema.

Page 270: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

270

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,kilichowafanya leo wabadili gia angani ni nini? Hawa watuwana tatizo la uzalendo, niwaombe ndugu zangu tuwewazalendo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu yeyote anayeona shakaambapo kuna evils and good people they are doingsomething halafu akawatilia mashaka, kwa kweli napatashida sana kuwaelewa. Nilichotarajia kutoka kwao, kwanzawangesema tunakushukuru Rais, tumesema kwa miaka mingihakuna aliyewahi kutusikiliza wewe umetusikiliza halafu ndiyotwende yale mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mnyikaamekuja hapa ana hoja ya mikataba it is true, mikataba nitatizo hakuna mtu anayepinga na Rais alishasema mikatabani tatizo. Nil ichotegemea waseme makinikia ndiyofoundation ya mjadala ya mikataba.

MBUNGE FULANI: Aaa wapi.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,utakwenda kwenye kujadili mkataba ukiwa na evidencetunaibiwa kwa kiasi gani, ninyi wawekezaji rekebisheni hapakwa sababu tumethibitisha pasipokuwa na shaka lolotemnatuibia. Sasa mnataka twende tujadili terms za mikatabahatuna kitu mikononi? (Makofi)

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika,Taarifa, Taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sixtus kuna taarifa yakupokea, endelea Mheshimiwa Bashe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika,nataka nimpe taarifa ndugu yangu Mheshimiwa Sixtuskwamba Nzega kuna Kampuni ilikuwa inaitwa Resoluteimeondoka na ten billion ya Halmashauri ya Nzega ya servicelevy, nil itaka nimuongezee tu madhara. Pia nil itakanimuongezee kwamba ikimpendeza kwenye hotuba

Page 271: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

271

amshauri Rais na Serikali GGM bado wanaendelea ku-processdhahabu kwa hiyo zikakaguliwe na zile ili tujue tunakoelekea.(Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sixtus Mapunda, unaipokeataarifa hiyo?

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Ahsante sana MheshimiwaBashe, kwanza naipokea taarifa yako kwa mikono miwili.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna siku hapa niliwahikusema story ya jongoo na mwana jongoo…

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,Taarifa.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Katika misingi ileile ya habariya jongoo na mwanajongoo, unapotaka kutatua tatizo lawizi wa watu….

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,Taarifa.

WABUNGE FULANI: Endelea.

NAIBU SPIKA: Subiri uitwe Mheshimiwa Waitara.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Unapotaka kutatuamatatizo katika sekta hii ya madini lazima uwe na sehemuya kuanzia. Hivi mnataka tuanzie wapi kwenye hili?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sixtus taarifa nyingine,Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mnyika taarifa inatolewana mtu aliyepewa nafasi ya kuzungumza. MheshimiwaWaitara mpe taarifa Mheshimiwa Mapunda.

Page 272: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

272

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,naomba nimpe taarifa ndugu yangu Mheshimiwa SixtusMapunda kwamba ni kweli wapinzani walisema, tulisemana uliowataja walisema na ni kweli kwamba mikataba hiiyote na kama alivyosema evils nadhani ni wao wao ndiyowalitengeneza mikataba mibovu na sasa tunaendeleakusema kwamba hata mikataba hiyo pia hatuwezi kuionaleo hapa hata mpaka kesho. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa nyingine ni kwambabado …

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waitara, nadhaniunaelewa maana ya taarifa, sasa unachotoa hapo nimchango ambapo jina lako umeshaomba chama chakokilete kwa hiyo utapewa nafasi ya kuchangia. Mpe taarifakatika anayozungumza yale ambayo hayapo sawa amaunamuongeza siyo unachangia. Hiyo siyo taarifa ni mchango,mpe taarifa. (Makofi)

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakuelewa na nakushukuru. Naomba nimpe taarifa kwambayote yaliyofanywa wamefanya wao yaani Serikali na chamachake, waliotenda leo ni wao na yaliyopo na madhambimengine ni wao.

MBUNGE FULANI: Wao wao.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,hiyo ndiyo taarifa yangu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Sixtus Mapunda unaipokeataarifa hiyo?

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza naomba unilindie muda wangu wameuchezea sana.Hii taarifa ngoja niipe maelezo mazuri i l i iwe taarifailiyokamilika kwa sababu haijakamilika. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Sawa sawa.

Page 273: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

273

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,mfumo wowote wa kisheria kuna mhimili unaitwa mhimili waBunge ndiyo unaotunga sheria na mfumo wowote wakuongoza nchi katika namna yoyote ile chimbuko lake niBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Upungufuwowote unaoonekana ninyi mlikuwepo na sisi tulikuwepo.

WABUNGE FULANI: Aah.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Ajenda ya sheria zotezilizopitishwa humu ndani ninyi mlikuwepo sisi tulikuwepo.

WABUNGE FULANI: Aah.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,my concern is not about the past, my concern ni sasatunapoanza kupiga hatua. Tumeliona tatizo, tunatatuatatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napata shida sanakuwaelewa watu wa aina kama ya akina MheshimiwaMwita. (Makofi)

MHE. CECILIA D. PARESSO: Taarifa.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,napata shida sana, kwanza naomba nilindie muda wangu,nina dakika zangu tatu zimekuwa disturbed…

MHE. CECILIA D. PARESSO: Taarifa.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Naomba nipewe mudawangu nimalize vizuri.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba wotemkae amalizie mchango wake, Mheshimiwa Sixtus Mapundadakika moja. (Makofi)

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,hakuna kichekesho cha mwaka kama kile ambapo mtu

Page 274: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

274

umeliona kosa, unalirekebisha halafu mtu anatokeaanakuambia kwa nini ulikosea si uendawazimu huo? Yaanimimi napata shida kuelewa, kosa limetokea unalirekebisha,katika process ya kulitatua tatizo unasema eti kwa niniulikosea, ni akili za chizi tu zenye uwezo wa kufanya mambokama haya. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mapunda,muda wako umekwisha.

MHE. SIXTUS R. MAPUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Balozi AdadiRajab. (Makofi)

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa NaibuSpika, na mimi nashukuru sana kupata nafasi ya kuchangiaWizara hii ambayo ni muhimu sana ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sanaMheshimiwa Rais kwa kitendo chake cha kuzuia yalemakontena pale bandarini na nampongeza sana kwakuunda ile Tume ya kuanza kuangalia kiini hasa cha utoroshajiwa madini hapa nchini. Ripoti ya Tume inabidi WaheshimiwaWabunge tuipongeze sana kwa sababu pale ndiyo mwanzowa kuanzia, madini ya nchi hii yamekuwa yakitoroshwa kwamuda mrefu sana na kwa kiwango kikubwa.Tumeshuhudiabaadhi ya migodi hapa nchini inatengeneza mpaka viwanjavya ndege ndani ya mgodi. Tumeshuhudia baadhi ya migodihapa nchini inaweka kampuni za ulinzi kutoka nje kwenyemigodi ya hapa nchini, maana yake ni nini hiyo? Maana yakeni utoroshaji kwamba wanatayarisha viwanja vya ndege,wanatayarisha ulinzi kutoka nje ili sisi tusiweze kuona nabaadaye madini hayo yanaondoka kwa kiwango kikubwa.Sasa hii ripoti inadhihirisha kwamba tumeibiwa muda mrefusana.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, taarifa.

Page 275: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

275

WABUNGE FULANI: Aah.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Balozi kuna taarifa,Mheshimiwa Msigwa.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, hili ni Bunge na tunapenda tupate taarifa sahihi.Mchangiaji anasema hawa wageni wanatayarisha viwanjavya ndege bila utaratibu, hii nchi ina vyombo vya ulinzi naUsalama, taarifa hizi za kusema wanatayarisha bila utaratibuna hii ni nchi yetu ni kulipotosha Taifa. Naomba tuongee vituambavyo ni kweli na yeye mwenyewe amekuwa…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa hiyo siyo taarifa,wewe unazijua Kanuni na unajua Kanuni gani utumie ili uletehiyo hoja yako. Hiyo siyo taarifa ya kumpa Mheshimiwa Balozi,Mheshimiwa Balozi malizia mchango wako. (Makofi)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Imprest, imprest hizo.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana …

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Ana-retire imprest.

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana. Mimi mwenyewe nimeviona hivyoviwanja na nimeona hizo kampuni kwenye migodi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja hapa WaheshimiwaWabunge lazima tushikamane, hii ni hoja ya Serikali, sasa hizihoja za kupinga ambazo zinatolewa aidha, madini hayo nimengi au siyo mengi lakini kuna dalili za utoroshaji jamani,lazima tushikamane. Sasa tunapotoa hoja hapa oohtutashtakiwa, ngoja twende tukashtakiwe, kwani tunaogopakwenda International court, tunaogopa kwenda kwenyearbitration, twendeni tukashtakiwe na tutatoa arguments,tuna ushahidi ambao umeonekana na Kamati imedhihirisha.Waheshimiwa Wabunge hiki ni kipindi ambacho tunatakiwatushikamane kwa sababu tutakapofanikiwa kudhibiti madini

Page 276: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

276

yetu maendeleo yatakuwa kwa kasi sana, kwa hiyo,nawaomba tushikamane. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti hii sijaonaMheshimiwa Waziri akizungumzia suala la ujenzi wa Kiwandacha Kusafisha Madini. Namuomba aipangue bajeti yake naahakikishe kwamba anaweka huo msimamo wa kuwekahela za Kiwanda cha Kusafisha Madini. Wakati masuala hayayanaendelea kushughulikiwa ngoja tuanze mchakato wakujenga kiwanda chetu hapa kama tukishindwa basi tuingieubia na watu binafsi kwa maslahi yetu lakini lazimatuhakikishe kwamba kiwanda hicho tuna ki-manage sisi tusijekufanya makosa tena na kuibiwa. Namshangaa nduguyangu Mheshimiwa Lissu juzi wakati anaongea alipokuwaana-criticize ya kuongelea case ya Bulyanhulu, naifahamucase hiyo nimeishughulikia na wakati huo Mheshimiwa Lissualikuwa anatetea sana wachimbaji wadogo na namnamakampuni makubwa ambavyo yanataka kuwadhulumuwachimbaji wadogo mali zao. Jana akawageuka tenaanaponda mimi nimeshangaa sana. Kwa hiyo, nasematushikamane ili tuondoe hili tatizo ili tuweze kupata hela nyingiza kuweza kuleta maendeleo hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nizungumzie REA III, REAwamefanya kazi nzuri sana ila katika kipindi hiki hawakufanyakazi nzuri ukilinganisha na kipindi cha nyuma. Sasa sijui ni kwasababu gani lakini mipango ambayo wameiweka kwenyeREA III tunategemea waanze kutekeleza vizuri. Pale Muhezakwenye Jimbo langu Mheshimiwa Waziri unajua umenipa REAIII vijiji 44, list ya mkandarasi ambayo umenikabidhi ina vijiji37, nakuomba urudishe vile vijiji vyangu saba ili wananchiwa kule ambao wameanza kufunga nyaya waweze kupataumeme. Vijiji hivyo ni vya Kwakope, Kibaoni, Magoda,Mbambala, Kitopeni, Masimbani, Msowelo vyote hivyowananchi wameshajitayarisha na wako tayari kwa ajili yakufungiwa umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho napendakupongeza sana juhudi ambazo zinafanyika kwa ajili yabomba la mafuta la kutoka kule Hoima Uganda mpaka

Page 277: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

277

Tanga. Tunaamini hii ni chachu na wananchi wa Tangawanategemea sana kwamba bomba hilo litawaleteamaendeleo makubwa ya viwanda na vitu vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,naunga mkono hoja na nakushukuru sana kwa kunipa nafasihii. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, muda wetuumemalizika kwa kipindi cha kwanza cha leo, nitataja majinamachache tutakayoanza nayo mchana nao ni MheshimiwaSelemani Zedi, Mheshimiwa Hasna Mwilima, MheshimiwaAlmas Maige, Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, MheshimiwaPeter Msigwa, Mheshimiwa Jesca Kishoa, Mheshimiwa JamesMillya, Mheshimiwa Maulid Mtulia, Mheshimiwa Yussuf KaizaMakame na Mheshimiwa Mohammed Juma Khatib. Hayondiyo majina tutakayoanza nayo lakini yapo majina zaidi yahayo.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,nasitisha shughuli za Bunge mpaka saa 10.00 jioni.

(Saa 7.00 Mchana Bunge lilisitishwa hadi Saa 10.00 Jioni)

(Saa 10.00 Jioni Bunge lilirudia)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu.

NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI:

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishatina Madini kwa mwaka wa fedha 2017/2018

(Majadiliano yanaendelea)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendeleana majadiliano ya hoja ya Wizara ya Nishati na Madini,tutaanza na Mheshimiwa Selemani Zedi atafuatiwa na

Page 278: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

278

Mheshimiwa Hasna Mwilima na Mheshimiwa Almas Maigeajiandae.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ili na mimi kwa niaba yawananchi wa Jimbo la Bukene niweze kuchangia hotuba hiiya Wizara muhimu sana, Wizara ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, kwa dhatiya moyo wangu, nichukue nafasi hii kumpongezaMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwajitihada zake za dhati za kuzuia wizi kwenye rasilimali za nchiyetu na hasa rasilimali katika sekta ya madini. Jambo ambalotunatakiwa wote tuwe clear ni kwamba hakuna anayepingaau anayekataa uwekezaji. Mheshimiwa Rais hapingi walahakatai uwekezaji na siku zote Mheshimiwa Rais amekuwaakihimiza wawekezaji wa ndani na wa nje waje kwa wingikadri iwezekanavyo. Mheshimiwa Rais anachochukia ni wiziwa rasilimali zetu na ambao tukiuacha uendelee utaturudishanyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Bashe asubuhiwakati anatoa taarifa kwa Mheshimiwa Sixtus aligusia kidogo,sisi Halmashauri ya Wilaya ya Nzega ni wahanga wakudhulumiwa na haya makampuni ambayo wakatimwingine hayafuati taratibu na sheria zinazotakiwa. ResoluteTanzania Limited wamechimba dhahabu pale Nzega tangumwaka 1999 na sasa hivi wamesimamisha uchimbaji lakininavyoongea sasa hivi Resolute wameondoka na service levyzaidi ya shilingi bilioni kumi ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.Mara zote tukifuatilia wanatoa visingizio vya kisheria, by-lawslakini kimsingi wanapaswa watulipe fedha hizi. Nina imanikubwa Serikali hii ya Awamu ya Tano itaingilia kati kutusaidiaili Halmashauri ya Wilaya ya Nzega tusiweze kudhulumiwashilingi bilioni kumi zetu za service levy ambazo kimsingi nihaki yetu tulipaswa tupate kama sehemu ya ushuru wahuduma kutoka kwa Kampuni hii ya Resolute. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu kampuni hiiimesimamisha uzaliashaji na haina mfanyakazi hata mmoja

Page 279: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

279

lakini tunajua ma-directors wapo na tunajua director mmojani Mtanzania na wengine wa nje. Tunajua bado wapo wanaissue zao zingine za kikodi na mambo mengine wanaendeleaku-sort out lakini kampuni ipo. Kwa hiyo, bado kuna uhalaliwa sisi kuendelea kudai na wao kutulipa stahili yetu kamaambavyo inastahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalonapenda kushauri ni kwamba Mheshimiwa Rais ameoneshamfano kwenye eneo la madini lakini naomba jitihada hizo zaMheshimiwa Rais ziende sasa mpaka kwenye rasilimali ya gesi.Bahati nzuri gesi ambayo tumeigundua kwa kiwangokikubwa hatujaanza kuichimba nako huku kuna dalilikwamba tusipokuwa makini pia kuna uwezekano mkubwawa wawekezaji kwa maeneo haya wakaendelea kutunyonyaau kutudanganya na hatimaye tukajikuta kwamba hatupatistahili zetu kama ambavyo tunatakiwa. Kwa hiyo, jitihadahizi ziende hata kwenye eneo la gesi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie eneo lawachimbaji wadogo. Napongeza jitihada za Wizara,Mheshimiwa Naibu Waziri, Mheshimiwa Kalemani tumekuwatukiwasiliana lakini na watendaji wake wa madini, Ofisi yaTabora na ya Kanda nipongeze kwa jitihada ambazo sasahivi wanazifanya katika kuhakikisha kwamba wachimbajiwadogowadogo maeneo ya Nzega na yanayozungukawanapata leseni na shughuli zao zinarasimishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Wilaya ya Nzegakuna maeneo mengi tu ambayo leseni zi l izokuwazinamilikiwa na hii Kampuni ya Resolute ambayo imeondokana kimsingi walisha-surrender leseni zao. Wananchi wengiambao sasa wameamua kuondokana na umaskini kwakufanya shughuli hizi za uchimbaji mdogo mdogowamekuwa wakiomba leseni ili waweze kuchimba kihalalilakini kutokana na mfumo wa kuomba leseni, mfumo badounaonesha leseni hizi zinamilikiwa na hawa Resolute, kwahiyo wananchi kila wakiomba mfumo unawakatalia lakinimaeneo hayo yako wazi, Resolute walishaondoka hawafanyichochote. Kwa hiyo, naomba Wizara ifanye utaratibu ili

Page 280: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

280

maeneo haya sasa ndani ya mfumo yafunguliwe ili wananchina vikundi ambavyo vimejihamasisha, vimeji-organize,wameamua kuondokana na umaskini kwa kuanzisha ajirakatika shughuli za uchimbaji mdogomdogo mfumo uwezekuwakubaliana kuomba leseni hizi na kuweza kupatahatimaye wafanye shughuli zao kihalali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo hayayamezunguka eneo lililokuwa la Mgodi wa Resolute lakinihata maeneo ya Mwangoye ambayo yako ndani ya Jimbola Bukene pia yanakabiliwa na tatizo hili. Nina imani kubwasana na Naibu Waziri, Mheshimiwa Kalemani na wafanyakaziwa Ofisi ya Madini Tabora na Kanda, nina uhakika jambo hililiko ndani ya uwezo wao na watalifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalonapenda kuzungumzia ni bomba la kutoa mafuta Ugandampaka Tanga. Jimbo langu la Bukene na Wilaya ya Nzega nimoja ya maeneo ambayo yatanufaika na kupitiwa nabomba hili. Juzi Jumatatu nilikuwa Jimboni na kuna Kampuniya GSB ambayo ndiyo wamepewa kazi ya kufanya tathminiya mazingira na athari za kijamii, walituita pale ili kutu-sensitizekuhusu bomba hili. Niseme kwamba wananchi wa Jimbo laBukene na Wilaya ya Nzega wako tayari, wanalisubiri bombakwa mikono miwili na habari njema tulizopata ni kwambamaeneo yote ambayo bomba litapita kutakuwa na fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ushauri wangu nikwamba yule mkandarasi mkuu wa bomba ahakikishe kazizile ndogo ndogo ana-subcontract kwa makampuni yawazawa ili na wenyewe waweze kufaidi. Pia kazi za vibaruazisizohitaji utaalamu wa juu basi wapewe vibarua ambaowanatoka katika maeneo ya vijiji husika ambapo bombalitapita. Nimeambiwa kwangu pale katika Kata ya Igusulendipo kutakuwa na kituo kikubwa ambacho kutakuwa nawafanyakazi zaidi ya 1,000. Kwa hiyo, sisi tunalichukulia hilikama ni fursa ya ajira, kupata uzoefu na kuinua hali ya maishaya wananchi wetu wa Jimbo la Bukene. Kwa hiyo, wananchiwa Igusule, Mwamala, Kasela, Mwangoe na Lusu wako tayariwanalisubiri bomba hili kwa mikono miwili. (Makofi)

Page 281: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

281

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu umemewa REA Awamu ya Tatu. Nichukue fursa kwa dhati kabisaniipongeze Wizara na hasa Naibu Waziri MheshimiwaKalemani ambaye alikuja Jimboni kwangu na kuhamasishaumaliziaji wa umeme wa REA Awamu ya Pili. Sasa hivi maeneoyote ambayo umeme umeweza kufanikiwa kumetokeamabadiliko makubwa kabisa kwa hali za maisha na hali zakiuchumi za wananchi. Kwa hiyo, Jimbo langu la Bukene nimfano wa namna ambavyo nishati ya umeme inawezakubadilisha maisha ya mahali fulani. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Selemani Zedi, muda wakoumeisha.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja asilimia mia moja na nawapongezasana watendaji wote wa Wizara hii, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Tunaendelea naMheshimiwa Hasna Mwilima atafuatiwa na MheshimiwaLolesia Bukwimba na Mheshimiwa Peter Msigwa ajiandae.

MHE. HASNA S. MWILIMA: Mheshimiwa Naibu Spika,na mimi kwa niaba ya wananchi wangu wa Jimbo laKigoma Kusini nishukuru kwa kunapata nafasi ya kuchangiaWizara hii nyeti, Wizara ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze sana kwanza kwakumpongeza Waziri aliyewasilisha makadario ya bajeti yaWizara hii kwa kushirikiana na Mheshimiwa Naibu Waziri.Natambua kwamba uwezo wanao na wanaweza kufanyakazi vizuri katika Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaanza kuzungumziasuala la Jimboni kwangu, naomba nimpongeze sana Raiswetu Dkt. John Pombe Magufuli, kwa hatua nzuri aliyochukuaya kuunda Tume. Leo tumesikia hapa taarifa ya upande wa

Page 282: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

282

pili unaonesha masikitiko kwamba Rais ameanza kwa kazindogo walitaka aanze na mikataba lakini tarehe 29/03/2017sote tunatambua kwamba Mheshimiwa Rais aliunda Tumena ikafanya kazi yake chini ya Profesa Mruma.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania wote nimashahidi, Mheshimiwa Rais alitumia uwazi, akaitoa iletaarifa kwa uwazi kwenye vyombo vya habari, wananchiwalioko vijijini, wanaotumia redio walisikia, wenye kuonaluninga waliona na akasoma taarifa. Kwa mfano kwenyeyale makontena 277 kwa taarifa aliyoitoa Mheshimiwa Raiswetu il ionyesha kwamba Watanzania kupitia hayomakontena 277 tunapoteza takribani bilioni 676. Halafu leotunasema hii ni kitu kidogo wakati pesa hizi zinazopoteatungezipeleka kwenye majimbo yetu, Serikali ingeelekezakwenye kujenga hospitali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo kwenyemakontena hayo wakati Mheshimiwa Rais anatoa taarifaimeonekana pia tuna upotevu wa copper na sulphur. Kwamfano, nilikuwa naangalia kwenye taarifa ya copperinaonesha kwamba kwenye kila kontena tuna tani 20 zacopper zinazopotea. Ukijumlisha yale makontena yote 277unapata tani 1440.4 zenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni17.9. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachonishangaza sisi wotetunafahamu wakati sisi wageni hatujaingia Bungeni siku zanyuma tulikuwa tukiangalia Bunge tunawasikia wapinzaniwanaisema Serikali ya Chama cha Mapinduzi inakumbatiamafisadi na wanasema Serikali ya Chama cha Mapinduziinaachia rasilimali za nchi zinaibiwa. Leo Mheshimiwa Raisamewasikia kwamba wapinzani walikuwa na vidonda sasaanajaribu kuona ni jinsi gani anaponyesha vile vidondawalivyokuwa navyo siku za nyuma. Raha ya donda, ukiwana kidonda chochote lazima kipate dawa, iwe ni dawa yakizungu, iwe ni dawa ya kienyeji lakini lazima kipate dawa.Mheshimiwa Rais analeta dawa kwa kuanza na hayamakontena 277 lakini tunasema kwamba angeanza namikataba, angeanza na mikataba wapinzani hao hao

Page 283: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

283

wangesema Rais kakurupuka, anaanzaje na mikataba kablaya kufanya uchunguzi. Sasa ameanzia makontena nduguzangu ili kubaini hivi kweli huu mchanga unapopelekwa njetunaibiwa au hatuibiwi? Kamati imetueleza kuwa tunaibiwana Mheshimiwa Rais ametuambia anajiandaa kutoa taarifaya pili kwa nini jamani tusimpe muda tukaisikiliza na ile taarifaya pili ili tuweze kuona inatuletea nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakumbuka siku za nyumawakati wa makelele ya ufisadi, tunaibiwa rasilimali zetu, BabaAskofu, Mwadhama Kadinali Pengo wa Jimbo la Dar esSalaam Katoliki aliwahi kuhoji, hivi hawa wanaopiga kelelekwamba Watanzania wanaibiwa rasil imali zaozinatoroshwa, wanaongea kwa uchungu wa dhati auwanaongea kwa sababu wamekosa fursa na wao ya kuiba?Mimi nilifikiri kwenye suala hili tusimame kama Watanzania,tusimame kama nchi, tuache itikadi zetu, tumpe moyo Rais.Kama hatumpi moyo atafikia wapi kuwaza kuichambua namikataba, kutoa fursa ili Bunge nalo tuletewe hiyo mikatabatuipitie na tumsaidie Rais kubadilisha yale ambayo tunaonani upungufu?

Kwa hiyo, naomba sana tuwe na subira ndugu zangu,mambo mazuri hayahitaji haraka. Tume imetoa taarifa yakwanza tusubiri taarifa ya pili na nina imani Mheshimiwa Dkt.John Pombe Magufuli ni mtu makini na atatupa taarifa yapili na kwa taarifa zilizoko huko nje ni kwamba Watanzaniawamefurahi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siku ile Rais anatoa taarifakaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu hapa alihojiwa nawaandishi wa habari akasema wao kama Upinzaniwamekuwa wanapiga kelele siku nyingi sana lakini Serikalihaichukui hatua, leo Serikali inachukua hatua tunasema ninisasa, si tuipongeze? Halafu jamani ndugu zangu tujengeutamaduni wa kupongeza au kukosoa Serikali pale ambapoinapostahili, sio kila kitu tupinge. Hata nyumbani kwakoinawezekana kabisa ukirudi mke unamnunia lakini sikuakikupikia chakula kizuri si ni lazima umsifie, umwambiekwamba leo mke wangu umenipikia chakula kizuri ili kesho

Page 284: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

284

apate nafasi ya kwenda kununua zaidi na aweze kukupikiazaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kumpongeza Raisna hiyo jitihada aliyofanya, naomba sasa niende kwenyeJimbo langu. Jimbo langu lina vijiji 61 tuna umeme kwenyevijiji kumi tu.

MBUNGE FULANI: Eheee.

MHE. HASNA S. MWILIMA: Kwenye REA Awamu ya Pilitulipata vijiji kumi vya Kandaga, Mlela, Kazuramimba,Kalenge, Uvinza na Mwamila lakini kwenye Awamu hii ya Tatuya REA pia tumepangiwa vijiji kama 11. Rai yangu, naombaWaziri ambaye amewasilisha hapa waweze kushirikiana naNaibu Waziri na Mkurugenzi wa REA Tanzania Ndugu Msofewaone ni jinsi gani wanatusaidia wananchi wa Uvinza ili basituweze kuongezewa vijiji. Ni jambo la aibu kuona tanguuhuru vijiji 61 tuna umeme kwenye vijiji kumi tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawapongezakwanza wametufikiria kwa mara ya kwanza tunapata umemempaka Kijiji cha Malagarasi kwenye Kata ya Mganza. Najuahuu ni mwanzo mwema ndiyo hatua sasa ya kupeleka umemekwenye Tarafa yangu ya Nguruka. Kwa maana utoke paleMalagarasi uende Mlyabibi, Bweru mpaka Nguruka. Ninaimani kwa sababu Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzini sikivu itayapokea haya na kuyafanyia kazi. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wamzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Hasna, mudawako umekwisha.

MHE. HASNA S. MWILIMA: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Anafuata Mheshimiwa AlmasMaige, Mheshimiwa Lolesia Bukwimba na Mheshimiwa PeterMsigwa ajiandae.

Page 285: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

285

MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana kwa kuniruhusu niongee au nichangiekatika Wizara hii ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianzekuwapongeza sana Wizara hii ya Nishati na Madini naniwakumbushe wananchi na Wabunge wenzangu humu jinsigani tulikuwa miaka mitatu, mitano, sita iliyopita wakatiambapo tulikuwa na mgawo, siku mbili au siku tatu hakunaumeme na hatukulalamika; leo mgawo umekuwa historiahakuna mtu anayepongeza? Si tuwapongeze hawa wenzetukwamba, wamefanya kazi kubwa sana? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia, nyuma yamafanikio yote haya yupo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri yaMuungano ambaye amekuwa anatoa miongozo ya kulipahela chungu nzima kwa mfano Kinyerezi Phase II ilisimamakwa sababu haikuwa na hela. Hela nyingi zimeingizwa paleili mradi ule uanze, haya ni mafanikio makubwa sana. Vilevile iko miradi ya Rusumo huko, miradi mingine ya gesiinayoleta umeme ambao tunautumia majumbani naviwandani; haya ni mafanikio ambayo Wizara hii inatakiwaipongezwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia, niseme ukwelikwamba mwenzangu, rafiki yangu Mheshimiwa ProfesaMuhongo amepata ajali ya kisiasa na amemwacha hapaMheshimiwa Engineer Merdad. Bado Wizara hii imewasilishwavizuri na mwenzangu Mheshimiwa Mwijage hapa leo,tumefurahi kwa yote aliyoyasema na kama alivyosema yeyeMheshimiwa Mwijage, Mheshimiwa Merdad ameziba pengo,amevaa viatu vya Mheshimiwa Profesa Muhongo.Naipongeza Wizara hii kwa mambo hayo makubwailiyoyafanya, lakini hasa kusimamia miradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuongea kwangu leonitaongelea pia, suala la REA ambao ni mradi mkubwaunaoendelea, lakini vile vile ningependa nichukue nafasi hii

Page 286: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

286

kuongelea mambo ambayo yametokea hivi karibuni ingawayameongelewa pia, lakini suala la makinikia haliwezi kupitwabila kusemewa kwa undani na kwa ukweli wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunapenda ku-quote aukunukuu maneno katika lugha nyingine, mimi ningependakunukuu leo maneno kutoka lugha yetu ya Kinyamwezi namaneno hayo ni kwamba, “Mradi Kuyile” yaani mraditunakwenda, “Nabhagemanyile” nilikuwa najua na kudharauyani “Kubyeda”.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo fulani akifanyakiongozi wa nje ya nchi, hasa kutoka kwa wakubwa hawa,kama container hili moja lingekamatwa kule Malaysia auSingapore au Marekani, basi watu hapo wangeandika nakusifia sana. Tumekamata makontena 277 watu wanaonabusiness as usual, mradi kuyile, mradi tunakwenda,haiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, madini haya yaliyokuwemokatika mchanga huu wa makinikia umetia hasara sawasawana bajeti ya nchi hii kwa miaka mitano. Si chini ya miakamitano, makontena haya kwa miaka 17, tungeweza kupatamali iliyotoka mle ndani tungeweza kuendesha nchi hii kwamiaka mitano, bajeti ya nchi nzima. Sasa Mheshimiwa Raisamefanya juhudi kubwa sana, ametimiza wajibu wake wakukamata makontena haya, lakini bado naona tayarikunakuwa na watu ambao wameanza kudharau suala hili,jambo hili si sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua kuna juhudi kubwasana ya waliokamatwa sasa kujaribu kufunika jambo hili nakuna watu wanasema tutashitakiwa, mimi nashindwakuelewa! Umuibie mtu na ushahidi upo halafu ukamshtaki!Sielewi kama kutakuwa na sheria, au sijui watatumia njiagani ya kutushitaki sisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, napata tabu sananinapoona wenzetu wanaanza kuongelea, kwamba nitatizo la mikataba, kwa hiyo mikataba hii ingeanza kwanza

Page 287: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

287

kuchanganuliwa kabla ya kushughulikia makontena. Hatahivyo, ijulikane kwamba ili uuchambue upya mkataba lazimamkataba uwe na makosa, sasa makosa yameonekana,kumbe katika mkataba huu watu wanaiba, sasa huu wizindio ushahidi wa kuweza kuchambua mikataba.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwakumbusheWaheshimiwa Wabunge wote humu ndani kwamba, sisi wotehumu ndani ya Bunge hili tunao wajibu wa kutetea maslahiya watu waliotuleta humu ndani, nao ni wananchi, iliwananchi hawa wasiibiwe, lakini vile vile wananchi hawawasidhulumiwe na wananchi hawa wajione wako salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilinukuu maneno yaKinyamwezi, lakini sasa ninukuu maneno ya Kiyunani,“Delegatus Non Protest Delegae”; mtu aliyepewa jukumu,wajibu wa dhamana hana haki ya kumkabidhi mtumwingine tena wajibu huo aliokabidhiwa. Wajibu wetu sotehumu ndani ni kuungana kwa pamoja kutetea wananchiwaliotuleta humu ndani; leo inakuwaje sisi Wabungetunaanza kubadilika na kutetea mambo ambayo hayanaukweli ndani yake? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais ameundaTume ya Wataalam, wamechambua mchanga ule na kutoamajibu; je, hatuaminiani? Wabunge humu ndani wanaanzakuongelea kwamba, inawezekana ule mchanga ni hadithiambayo wanaicheza ngoma ya walioibiwa. Ukweli nikwamba kuhusu mchanga ule tufuate maelekezo na taarifailiyotolewa na wataalam wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niende kwenye miradiya REA. Pamoja na mafanikio makubwa katika awamu yakwanza na ya pili ya REA kumekuwa na udhaifu mdogomdogo uliotokana na utendaji, hasa uwajibikaji wa watufulani katika mradi ule, wameruka vijiji fulani. Kwa mfanojimboni kwangu vijiji vikubwa ambavyo vina shule, vinazahanati, vina vituo vya afya vimerukwa! Bahati nzurinilimwona Mheshimiwa Muhongo kabla hajaacha kuwaWaziri na tukakutana pia na mkandarasi huyu, nina imani

Page 288: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

288

tuliyoongea yatakuwa sahihi kwamba, watafanya varianceya mabadiliko kidogo ya mkataba kwa aslimia 15 ambapoVijiji vya Majengo, Ikongolo, Kanyenye, Nzubuka na Kituo chaUpuge vitapata umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka Mheshimiwa Waziriatakapokuja hapa anithibitishie kwamba, waliyoniambiaviongozi wa REA kwamba, maeneo haya yatapata umeme,yapate umeme. Maana itakuwa jambo la ajabu bahati nzuriau mbaya katika vijiji hivyo ndiko mimi natoka, sasa watuwamekuwa wanasema ahaa, Mbunge huyu mnaona hafai,hata umeme kwake hakuna! Hayumo kwenye REA Phase Twona Phase Three.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili jambo litaleta matatizomakubwa sana ya kisiasa, nawaombeni sana MheshimiwaWaziri atakapokuja kujumuisha awe ameongea na watu waREA ili waingize Vijiji vya Upuge kwenye kituo kimoja cha afyakiko pekee, Vijiji vya Majengo, Kanyenye, Ikongolo, Nzubukana Kiwembe.

Mheshimiwa Naibu Spika, yako mambo menginekatika Wizara hii ambayo ni mazuri sana, lakini mambomadogomadogo haya yanaipaka matope Wizara naionekane kama haifanyi kazi. La sivyo, Wizara hii imefanyakazi kubwa sana kutafuta gesi, kusimamia upatikanaji wagesi, kusimamia uunganishaji wa bomba kutoka Uganda kujaTanga, kusimamia mambo mengi, gesi kutoka kule Mtwarakuja Dar-es-Salaam na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema sana, naombaniwaachie na wenzangu. Naunga mkono hoja moja kwamoja. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa LolesiaBukwimba, atafuatiwa na Mheshimiwa Peter Msigwa naMheshimiwa Jesca Kishoa ajiandae.

Page 289: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

289

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana kwa kunipa nafasi, ili na mimi niweze kuchangiaWizara ya Nishati na Madini. Kwanza nianze kwakumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwauwasilishaji mzuri wa bajeti ya Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru sanaMheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwajinsi ambavyo amechukua hatua za makusudi kuwezakutetea na kuangalia changamoto mbalimbali zinazogusawachimbaji wadogo wa madini Tanzania. Mwanzonikulikuwa na unyanyasaji mkubwa sana wa wachimbaji wamadini, lakini tumemwona Mheshimiwa Rais akiwa Ikuluakiona wachimbaji wakinyanyaswa anatoa maagizo namaelekezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nitumie fursa hiikwa niaba ya Wachimbaji wadogo wa Tanzania kumshukuruna kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwaanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kuhusiana na sualala ile Tume iliyochunguza mchanga unaosafirishwa nje ya nchi.Mimi binafsi natoka sehemu ambako madini yako kwa wingiya dhahabu. Kweli, nitumie fursa hii kumshukuru sanaMheshimiwa Rais na kumpongeza kwa hatua aliyochukua,kwa kweli, imetupa moyo sisi pamoja na wananchi kwaniilikuwa ni kero kubwa sana, hasa kwa sisi ambao tunatokeamaeneo haya ya wawekezaji wakubwa wa dhahabu.Wananchi walikuwa kila wakati wakiuliza, inakuwajemchanga unasafirishwa, walisema sisi hatuoni hata faidayoyote ya kuwa karibu na wawekezaji hawa wakubwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa hatua ambayoMheshimiwa Rais ameichukua mimi binafsi nimefarijika nawananchi wamefurahi sana; na tunamwambia MheshimiwaRais aendelee na kasi hii na mikataba iangaliwe upya ilikuona jinsi ambavyo wananchi tunaweza kunufaika zaidikutokana na madini ambayo Mwenyezi Mungu ametupatia.(Makofi)

Page 290: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

290

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya pongezi hizo,binafsi napenda kuzungumzia kwenye madini. Jimbo laBusanda ni jimbo ambalo limebarikiwa na Mwenyezi Mungu,siku zote huwa nasimama hapa nasema tunayo madini yakutosha. Nilipokuwa nikiangalia bajeti ya Mheshimiwa Wazirisijaona chochote kuhusiana na Jimbo la Busanda kwa kweli,japokuwa ndiko ambako madini mengi yanatokea, hasawachimbaji wadogo wako wengi sana kule.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda MheshimiwaWaziri atakapo-wind up aniambie maeneo ya Nyarugusu,hajazungumzia maeneo ya Rwamgasa, pamoja na Mgusuna sehemu mbalimbali za wachimbaji. Naomba azungumzieatakapo-wind up kwa sababu kwenye bajeti sijaonachochote kuhusiana na maeneo hayo niliyoyataja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo kunaeneo la STAMICO ambalo limekuwa ni kilio cha muda mrefusana kwa wananchi wa Nyarugusu na Mheshimiwa Wazirimwaka uliopita alisema kwenye bajeti kwambaanalishughulikia na ataweza kulitafutia ufumbuzi suala hili,lakini mpaka sasa hata kwenye bajeti sijona akizungumziahata kidogo. Kwa hiyo, naomba atakapo-wind up aniambiena wananchi waweze kusikia kwa sababu wanasikiliza nahata hivyo wako kwenye TV wanaangalia ili kuona kwamba,je, suala hili limeweza kushughulikiwa? Kwa hiyo, naombaMheshimiwa Waziri aliangalie suala hili na aweze kulifuatilia.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo paleRwamgasa mwaka 2015, paliteuliwa kuwa sehemu maalumkwa ajili ya uanzishwaji wa eneo la uchenjuaji wa dhahabuwa mfano. Hata hivyo nimesikitika kwamba kwenye Kitabucha Bajeti, ukurasa wa 103, kati ya vituo saba vya mfanovya kuchenjua dhahabu Rwamgasa haijatajwa tena; sasanapenda kuuliza, je, imeondolewa kwenye huo utaratibu?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2015, Benki ya Duniailikuja kuzindua rasmi mradi huo pale Rwamgasa na hataleo hakuna chochote kinachoendelea na wananchi

Page 291: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

291

wanaendelea kuulizia juu ya suala hili. Kwa hiyo, naombaMheshimiwa Waziri atueleze, wawaeleze wananchi waRwamgasa kuhusiana na suala hili, kwa sababu Serikali nikwa muda mrefu imeteua Rwamgasa kuwa Kituo Maalumkwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu lakini leo hii Rwamgasahaipo kwenye bajeti kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile maeneo ya Buckreefni maeneo ambapo Serikali pamoja na TANZAM wamefanyauwekezaji, lakini sisi wananchi hatuoni faida yoyote kutokanana huo mgodi. Kwa nini Serikali isiangalie upya mkataba huoili ikiwezekana wapewe wananchi maeneo hayo wawezekuchimba na kunufaika na rasilimali za Taifa zilizopo katikanchi ya Tanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile TANZAMwamechukua eneo Rwamgasa, wakulimawamenyang’anywa maeneo na mpaka sasa hawajapewafidia yoyote. Naomba Mheshimiwa Waziri aniambie, kwasababu maeneo hayo wananchi hawaruhusiwi kulima walakufanya kazi yoyote pale, lakini hawajapewa fidia yoyote.Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri wazungumzie sualahili, ili wananchi waweze kujua hatma yao kuhusiana na sualahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi binafsi napendakuishauri Serikali kwamba Mkataba huu wa Buckreef naTANZAM uangaliwe upya na ikiwezekana eneo hili wapewewananchi ili waendelee kuchimba dhahabu na kuwekamchango wao kwenye pato la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kwa upande waumeme; nichukue nafasi hii kuishukuru Serikali japokuwatunaona Serikali inaendelea kupeleka umeme hasa katikaMiji mbalimbali. Kwa mfano Katoro mpaka sasa hiviwanasambaza kwa kasi umeme, lakini bado jitihadazinahitajika zaidi kwa sababu wananchi wanahitaji umeme.Kati ya Kata zangu 22 ni kata 10 tu ndizo zilizofikiwa. Kwahiyo, niombe Serikali iwekeze nguvu zaidi, ikiwezekana REA

Page 292: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

292

iongezewe fedha zaidi ili wananchi hasa walio wengi waliokovijijini waendelee kupata umeme wa uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayoniangalie kwa habari ya mafuta. Kuna vinasaba ambavyovimekuwa vikilipiwa dola 14 kwa lita 1,000. Hivi vinasabakwa nchi ya Tanzania kwa kweli, vinaongeza gharama yamafuta. Naiomba Serikali iondoe hii gharama, ifute kabisavinasaba hivi kwa sababu sasa hivi bei ya mafuta ya dizelina bei ya mafuta ya petroli na mafuta ya taa karibuzinalingana, kwa hiyo uchakachuaji haupo tena umepunguakabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba kwakuwa, katika nchi nyingine za Afrika Mashariki kama Kenyavinasaba hivi gharama yake ni dola tatu mpaka nne, lakinisisi ni dola 14, kwa nini inakuwa hivyo sisi katika nchi yaTanzania? Ndio maana sasa mafuta yanakuwa na bei yajuu zaidi kuliko nchi nyingine wakati sisi tuna bandari hapahapa Tanzania. Kwa nini bei ya mafuta iwe juu ukilinganishana nchi nyingine wakati sisi tumebarikiwa pia kuwa nabandari katika nchi ya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo sasanichukue nafasi hii kuiomba sasa Serikali iangalie kiundanihabari ya wachimbaji wadogo wadogo ambaonimewazungumzia kwa miaka mingi, iangalie namna yakutatua changamoto zao sasa, kwa sababu imekuwa nikipindi kirefu wananchi wanahangaika, wanalia, wanahitajikupewa maeneo ya uchimbaji. Hatuwezi kufikia uchumi wakati bila ya kuwawezesha hawa wachimbaji wadogo wamadini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo wakatiule ambapo Mheshimiwa Profesa Muhongo alikuwa Wazirialikuja Geita akatoa maelekezo kwamba ziangaliwe zileleseni ambazo hazifanyi kazi waweze kupewa wananchi.Mkoa wa Geita tu tuna zaidi ya leseni 1,700 ambazo ni zautafiti pamoja na wachimbaji wadogo wadogo na wa kati.Hata hivyo, kati ya leseni hizo zinazofanya kazi ni leseni 30 tu,

Page 293: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

293

kwa hiyo leseni nyingi hazifanyi kazi. Nitumie fursa hii kuiombaWizara iangalie namna ya kuwapatia wananchi leseni hiziambazo hazifanyi kazi, hasa vikundi vya wachimbajiwadogo ambao wanafanya shughuli mbalimbali zauchimbaji. Kwa hiyo...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bukwimba, muda wakoumekwisha.

MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika,naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Peter Msigwa,atafuatiwa na Mheshimiwa Jesca Kishoa na Mheshimiwa Ole-Millya ajiandae.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi siwapongezi Wizarahii kwa sababu kwanza wanatimiza majukumu yao na pesawanazozitumia ni kodi ya wananchi. Ila ninachoweza kusemaJimbo langu limekaa vizuri kwenye miundombinu ya maji naumeme tuko vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kusemakinachofanyika humu ndani ya Bunge ni sawa na babaambaye anaenda sebuleni anajisaidia halafu watoto namama wanamchachamalia kwamba atoe uchafualiojisaidia sebuleni, halafu anapoutoa anasemamnishangilie nimefanya kazi kubwa. Hiki ndio kinachofanyikana nyie Wabunge wa Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka jana, Bunge laKumi…

Page 294: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

294

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika,Kuhusu Utaratibu!

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa naomba ukae;Kuhusu Utaratibu, Kanuni?

KUHUSU UTARATIBU

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Naibu Spika,Kanuni hiyo hiyo!

Mheshimiwa Naibu Spika…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

MHE. MARTHA M. MLATA: Mzungumzaji anayeongeaanatumia lugha ya kuudhi humu ndani na hali yeye niMchungaji. Amejisaidia yeye?

MBUNGE FULANI: Unatumia Kanuni gani?

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa, endelea nauchangiaji. (Makofi)

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, Bunge la 10 wakati wa saga la Escrow tulikaa katikaBunge hili mpaka saa sita za usiku na Waheshimiwa Wabungewote tulikubaliana kuhakikisha Mheshimiwa Profesa Muhongona watu wengine waondolewe. Pamoja na MheshimiwaKigwangalla wote mnajua kwenye kumbukumbu alisemahajawahi kuona Profesa muongo kama MheshimiwaMuhongo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wa CCM na sisihapa kwa wingi wetu wote mkapiga makofi mkashangiliaMheshimiwa Profesa Muhongo aondoke na kwa sababu,

Page 295: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

295

Mheshimiwa JK alikuwa anaheshimu maamuzi ya Bunge,Mheshimiwa Profesa Muhongo na wenzake waliondoka.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, alivyokuja MheshimiwaMagufuli, alivyoanza kuteuwa Baraza la Mawaziri hakujalikwamba Bunge liliona nini, lilifanya nini, akasema hapa kazi,mnamuonea wivu, namchagua Mheshimiwa Muhongo;mkapiga makofi mkasema jembeee! Huko ng’ambo huko,kwa sababu ya wingi wenu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, juzi baada ya huu mchangaamemtumbua, tena mnashangilia mnasema jembee! Ninyi,ninyi! Hebu tufike mahali tuone wajibu wetu wa Bunge ninini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumza MheshimiwaTundu Lissu ambaye walau katika Bunge hili ana historia yamigodi na jinsi ambavyo watu wameonewa, amefungwampaka ndani na mikataba iliyowekwa. Kweli, amekuwaakitetea na hajaacha kutetea wachimbaji wadogo, lakinileo tunaanza kujitoa ufahamu! Wataalam wanasema…

MBUNGE FULANI: Taarifa!

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: …when you are lostspeed is useless; ukipotea spidi haina maana! Ukipoteaunarudi unasoma ramani…

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa kuna taarifa kutokakwa Mheshimiwa Oscar Mukasa.

MHE. OSCAR R. MUKASA: Mheshimiwa Naibu Spika,nataka kutoa taarifa kwamba maisha siyo static,hayasimami, ni dynamic, ndiyo maana hata Lowassa aliitwafisadi mkubwa lakini baadaye akageuka kuwa... (Makofi)

Page 296: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

296

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, Mukasa taarifaanayopewa mchangiaji inapaswa kuwa weweunamwongeza yale aliyochangia, kama hayako sawasawaunarekebisha, ndiyo taarifa. Mheshimiwa Msigwa endeleakumalizia mchango wako.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, this is just a joke, tunazungumza Bunge hatuzungumzimambo ya Lowassa hapa. Tunazungumza Bunge na wajibuwa Bunge, na tunaowazungumzia humu ndani ni walewaliopewa madaraka ya kuongoza nchi hii. Leo mnajitoaufahamu mnashangilia Magufuli utadhania ni Columbusanagundua kisiwa cha Australia huko bara la Australia.Anachokifanya Magufuli si kitu cha kwanza. Subirini …

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE WALEMAVU): MheshimiwaNaibu Spika, kuhusu mwongozo

M W O N G O Z O

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa naomba ukae,kuhusu utaratibu. Mheshimiwa Msigwa uwe na utulivuumepewa nafasi ya kuchangia, mimi ndiye ninayeamua kwahiyo usitake kujibizana na mimi, ni kama nilivyokupa nafasindivyo ninavyompa mtu mwingine, kwa hiyo usitakekujibizana saa hizi. Mheshimiwa Chief whip.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE,KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE WALEMAVU: MheshimiwaNaibu Spika, Mheshimiwa Msigwa anaelewa ni Mbungemzoefu na anajua utaratibu wa kikanuni. Sasa ninachotakakusema, taratibu zinazotumika humu ndani katikakuchangia, kanuni ya 64 ukiangalia kanuni ya (g) kwanzainasema mchangiaji yeyote lazima atumie lugha ambayo niya staha, haidhalilishi watu wengine na si lugha ya kuudhi.

Mheshimiwa Naibu Spikia, vile vile katika kuwa nastaha unapomtaja Rais wa nchi hii ni lazima useme

Page 297: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

297

Mheshimiwa Rais na umtaje jina lake. Hata hivyo sidhani hatakwa utamaduni wetu tu Mbunge anaweza akasimama hapaakasema Magufuli! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamheshimu MchungajiMsigwa lazima atumie lugha ya staha. Mheshimiwa Rais wanchi hii anaitwa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.Kwa hiyo naomba sana Wabunge wazingatie kanuni ya 64halafu Mbunge aseme kwa kujenga hoja zake, lakiniakizingatia utaratibu wa Kikanuni. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, MheshimiwaWaziri ameomba utaratibu na anataja kanuni ya 64(1)kifungu cha (g) kinasema;

“bila ya kuadhiri masharti ya ibara ya 100 ya katibayanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadilanokatika Bunge, Mbunge hatatumia lugha ya kuhudhi auinayodhalilisha watu wengine.”

Waheshimiwa Wabunge hii kanuni ya 64 fasili (1) inamaeneo mengi tu ambayo yamekatazwa Bungeni, naukiisoma utagundua haya ni mambo yasiyoruhusiwa,yametakwa mambo mengi hapa. Naomba tutumie mudawetu vizuri kwa kuchangia kwa kufuata masharti ya kanunihii, yale mambo yasiyoruhusiwa tujiepushe nayo maana kilawakati tutakuwa tukipotezeana muda katika mamboambayo tuna uwezo wa kutumia vinywa vyetu sisi kamaviongozi kwa kuzungumza na kufikisha hoja inavyotakiwa.Mheshimiwa Msigwa naomba uzingatie masharti ya kanuniya 64.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa NaibuSpika, naomba unitunzie muda wangu. Ninachokisemaalichokifanya Mtukufu Mheshimiwa Rais Dkt. John PombeMagufuli si kipya, maana mnashangilia hapa utadhania niColumbus amugundua Bara la Australia. Tume ya akina Maigehapa wapo akina Zito. Haya mambo waliyazungumza.Alipoingia Ikulu tulitegemea angeona mafaili, kitu ganikifanyike kuhusiana na matatizo ya tasnia hii na kwenye

Page 298: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

298

Baraza la Mawaziri naye alikuwepo. Sasa hapa mnabebangoma mnashangilia kama tumevumbua bara lingine wakatini mambo yenu wenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ninyi CCM niwaungwana mngewaomba radhi Watanzania, kwambatumechafua sebule. Sebule tumeiweka katika hali mbaya yahewa tunawaomba radhi tumewakosea. Sasa mnazungukahapa kwa mlango wa nyuma kama vile sisi wote ni watoto.Eti tumpongeze Mheshimiwa Rais, hii nchi ni ya wote. Sikuzote mnasema hapa ndiyo!, iweje nchi ya wote hapa kwenyemambo yasiyokuwa na maana? Tunajitoa ufahamu, ndiyo.Tume ya akina Maige hawa walienda walizunguka nchi nyingiduniani na walilipwa hela nyingi sana Tume…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msigwa umetokakukumbushwa yule ni Mheshimiwa Mbunge kwa hiyo anaitwaMheshimiwa Maige tafadhali, hizi kanuni tusisipungukietumetunga wenyewe. Wewe unaitwa Mheshimiwa mwite nayeye Mheshimiwa ili tusiwe tunarudia rudia haya mambo .Ahsante sana.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA… na wenzakewalizunguka dunia mzima, sasa leo mnakuja hapatumpongeza Mheshimiwa Rais na nataka niwaambieWatanzania, hizi lugha tunazozungumza hapa kuhusuinvestors unajua kuna mtu mwingine anadhani investors hawawa madini wana–invest kama kibanda chako unachouzamkaa huko nyumbani.

Mheshimiwa Naibu Spika, wengi hapa mnazungumzakwa sababu hamjaenda kwenye migodi mkaona heavyinvestments walizoziweka kule ndani. Kwa hiyo si kitu chadakika moja; unadhani kwamba unaweza ukawaambiatoka leo ingia leo? It is a heavy, ni hela nyingi. Muwaulizewenzenu waliotangulia tulifanya nini kwenye Dowanstulivyojaribu kutaka kuwapeleka mahakamani. Mnasimamatu hapa mnasema tuwapeleke mahakamani, sawa tutaenda

Page 299: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

299

lakini hiki tunachocheza nacho hapa si kitu kidogo; nakuwapoteza investors si kitu kidogo. Hakuna mtu wa upinzanianayetaka tuibiwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunachozungumza ni juuya method iliyotumika na namna ya kufanya haya mambo.Tumezungumza miaka mingi tangu wakati wa MheshimiwaRais Ally Hassan Mwinyi; kwamba watu wanaingia vibayamkabisha na ndiyo tabia yenu. Tulivyokuja na suala la Katiba,likiwa linatoka kwetu mkalivamia mkashindwa kulimaliza;tulipokuja na suala elimu bure mkashindwa kulimaliza;tuliwaambia haya madini nayo mnakosea, narudia, narudiatena, When you are lost speed is useless; ukipotea huongeziaccelerator, hukanyagi mafuta bali unasoma ramani naramani pekee ambayo mngechukua ni ile ya Tume ya Bomani,soma anasema nini, ndicho ambacho tungetakiwa kukifanyandugu zangu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawatukana wawezekajikama vile invaders kama vile wametuvamia. Hawa watutukiwaambia kesho tu wanaondoka. Leo tunawaambia wezihii mikataba tumefanya wenyewe, Sheria tumetungawenyewe, leo tunawaita wezi eti tumekamata makontenamia saba, kwani yameanza kusafiri leo? Vyombo vya usalamahavikuwepo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunachokisema sisi kamaWatanzania mbinu mnayotumia si sahihi. Njia mnayotumiasi sahihi kwa sababu inatuingiza chaka zaidi. Niwaombekama Bunge, tunachotakiwa kufanya hapa ni kuiombaSerikali i-engage, tuingie kwenye majadiliano badala yakufikia kwenda mahakamani. Kwa sababu nawa- guarantee,kama wakitupeleka Mahakamani we are going to lose bigtime, whether you like or not. Cha msingi Bunge tungetoaushauri badala ya kuwafukuza investor na kuwatuna. Ma-investors wale wanaweka heavy money…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

WABUNGE FULANI: Mmehongwa hela,

Page 300: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

300

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Kama tumehongwahela nyie

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tuwe nautulivu.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: … Mikataba mliingiawenyewe na mmeifanya hii nchi ya trial and error halafuleo…

MBUNGE FULANI: Sumaye alikuwepo.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Leo mnasema eti tuwewazalendo. Katika Bunge liloisha kuna mikataba mingi Sherianyingi zimetungwa kwa hati ya dharura na hizi Sheria nyingitumekuwa tukizipinga…

MBUNGE FULANI: Morena.

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA…tukijaribu kuwashaurilakini huwa hamsikii. Niwaombe Waheshimiwa Wabungehebu tuache kujitoa ufahamu. Wengi wenu hapa mnapigakelele hata hiyo Sheria ya Madini hamjasoma, hamjui hatahiyo migodi, mmekuwa washangiliaji tu kama MheshimiwaTundu Lissu anavyosema… (Kelele)

MBUNGE FULANI: Dolla dolla dollaa

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA …mmekuwawashangiliaji hamjasoma hata Sheria unakuja hapa hufanyiresearch huwezi kuuliza maswali, wewe walichosema tuunashangilia shangilia tu hapa, hili ni Bunge la aina gani?Hebu tuache kujitoa ufahamu turudi kwenye nafasi, tuachekujitoa ufahamu; na wengi wenu mnapiga kelele tu kwenyemajimbo yenu hakuna lami, maji, umeme mnatetea mamboya ovyo tu. Tunachozungumza hapa tunazungumzamustabali wa Taifa letu siyo ushabiki. Siyo ushabiki wa kupigapiga makofi hujaletwa kupiga piga makofi hapa. KasomeSheria za madini chimba visima hakikisha unatetea maslahiya nchi yako.

Page 301: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

301

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani hii dozi inatoshanitarudi kidogo kwenye ufahamu.

MBUNGE FULANI: Morena! Morena!

MBUNGE FULANI: Dolla! Dolla hizo!

MBUNGE FULANI: Msigwa Morena hiyo!

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tusikilizane,twende kwa utulivu. Mheshimiwa Msigwa yeye ameshasemajimbo lake halina shida yoyote, sasa Mbunge mwinginemwenye shida zako ukisahau kutaja mambo ya jimboutakuwa hatarini. Mheshimiwa Jesca Kishoa, atafuatiwa naMheshimiwa atafuatiwa na Mheshimiwa James MillyaMheshimiwa Maulid Said Abdallah Mtulia ajiandae.

MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nitazungumzia sualazima la gesi na baadaye nitajielekeza kwenye suala laumeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muda mrefu katikataifa letu wananchi wa Tanzania wemekuwa na matumainimakubwa sana kuhusiana na suala la gesi ya Mtwara.Matumaini haya yametokana na sababu nyingi mbalimbaliikiwa ni pamoja na sababu ya miradi miwili mikubwa. Mradinamba moja ni mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwarakwenda Dar es Salaam ambalo limechukua takriban shilingitrilioni 2.5 katika utekelezaji wake na mradi wa pili ni mradiwa LNG (Liquefied Natural Gase) ambayo kama ingekuwaimetekelezeka kwa sasa ingekuwa imetumia Dola zaKimarekani bilioni 30.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa muda mrefu sanaSerikali hii ya Chama cha Mapinduzi imekuwa ikitumia akilindogo sana kupanga mipango na kutekeleza miradimikubwa na mambo makubwa. Bomba la gesi la Mtwarakwenda Dar es Salaam limetumia pesa nyingi sana, lakinikwenye ripoti ya CAG anaonesha bomba hili la gesi lina uwezo

Page 302: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

302

wa kufanya kazi kwa asilimia sita tu. Tafsiri yake ni kwambahata hilo deni ambalo tumelikopa China la trilioni 2.5hatuwezi kulilipa kwa sababu bomba hili halifanyi kazi vizuri;matokeo yake tutaanza kuchukua fedha kutoka kwenyemadawa; tutaanza kuwabana wafanyabiashara kwa ajiliya kulipa deni hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tatizo lingine ambaloni kubwa sana. Naomba Mheshimiwa Waziri husikaatakapokuja kuhitimisha atoe majibu ni ni kwa niniwanakuwa wana poor project plan ambayo inapelekeamiradi mikubwa kama hii inashindwa kutekelezeka kwaufanisi?

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa LNG (LiquefiedNatural Gas) haijawahi kutokea katika Taifa hili kuwa namradi mkubwa kama huu. Huu ni mradi wa kihistoria, lakinicha kushangaza mradi huu umeshindwa kutekelezaka kwasababu Serikali mmeshindwa ku-deal na investors.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa kwenye meza yangunina taarifa kutoka kwenye jarida kubwa kabisa la kimataifala Reuters la Uingereza ambalo nimem-quote meneja waStatoil anaeleza kwamba mradi huu umeshindwakutekelezeka kwa sababu ya kusuasua kwa Serikali ya Chamacha Mapinduzi. Kama utahitaji taarifa hii naomba umtumemhudumu aje aichukue copy yako nimekutolea. (Makofi,)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziriatakapokuja kuhitimisha aseme tatizo ni nini? Nimesikiakwenye hotuba asubuhi anasema kwamba majadiliano badoyanaendelea. Wawekezaji wanalalamika, tatizo ni nini? Nihivi, hawa investors ambao anawapiga danadanawamehamisha mradi huu wa LNG wameupeleka Msumbiji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu kupelekwaMsumbiji tafsiri yake ni kwamba kufikia mwaka 2021 ambapomradi huu unakwenda kutekelezeka maana yake ni kwambaMsumbiji watateka soko la gesi katika Afrika Masharikipamoja na Kusini mwa Afrika.

Page 303: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

303

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri labdasijui ni kutofahamu, mimi nashindwa kuelewa!Unapozungumzia uwekezaji wa takriban dola za Kimarekanibilioni 60, bilioni 30 unakuwa unazungumzia uchumi waUganda. Uchumi wa Uganda ni takrban dola la Kimarekanibilioni 60. Unapozungumzia investment ya dola za Kimarekanibilioni 30 unazungumzia robo tatu ya uchumi wa Tanzaniaambao ni dola za Kimarekani bilioni 45. Unapokuwaunazunguzia uwekezaji wa takriban dola bilioni 30 unakuwaunazungumzia mara kumi ya uchumi wa Rwanda. Uwekezajihuu ni mkubwa sana. Namwomba sana Mheshimiwa Waziriatakapokuja kuhitimisha atupe sababu kwa nini mradi huuunashindwa kutekelezeka kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu suala zima laumeme. Taifa hili lina vyanzo vingi vya umeme. Tunamaporomoko ya mito, tuna upepo, kwa mfano mimi mkoawangu wa Singida kuna upepo wa kumwaga. Pia tunamakaa ya mawe ukienda kule Liganga na Mchuchumatakrban tani milioni 480 zimejaa kule, lakini bado umeme niwa kusuasua.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimepitia mpango wamiaka mitano uliotolewa na Waziri wa mwaka 2016 - 2021ukurasa wa 12 unaonyesha kwamba mwaka 2011 Serikaliilidhamiria kuongeza megawatt kutoka 900 mpaka 2,700kufikia mwaka 2011, lakini cha kusikitisha mpaka inafikamwaka 2016 megawatt zilizoongezeka 1,246 na kwa bahatimbaya sana nimemsikia na Mheshimiwa Waziri asubuhikwenye hotuba yake na nimeipitia kumbe zimeshuka tenamwaka huu zimekuwa Megawatt 1,051.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kama kuna Waziriyeyote hapa asimame aniambie kama kuna nchi yoyoteimewahi kufanya mapinduzi ya viwanda kwa megawatt2,000. Mnampa Mheshimiwa Rais mizuka ya uchumi waviwanda na wakati mmeshindwa na mnajua haiwezekani.(Makofi)

Page 304: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

304

Mheshimiwa Naibu Spika, mnapowaita wawekezajiwaje kuweze katika taifa letu na wakati umeme uliopo niwa kukatika…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jesca Kishoa naona kunaWaziri amesimama. Naibu Waziri Mheshimiwa StellaManyanya.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa sababu alitaka kujuakama kuna Waziri anaweza akampa taarifa natakanimwambie kwamba viwanda vinatumia umeme kwacapacity tofauti tofauti, si viwanda vyote lazima vitumiemegawatt 2000. Hata sasa hivi tulivyo kuna viwanda tenavikubwa vinatumia KVA 500 tu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kishoa, unaikubali taarifahiyo?

MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Naibu Spika,naanzaje kupokea taarifa tena ya kijinga namna hii? (Makofi/Kicheko)(Maneno Haya Si Sehemu ya Taarifa Rasmi zaBunge)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee naunilindie muda wangu…

MBUNGE FULANI: Acha kutukana bwana.

MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Naibu Spika,yaani katika taifa letu ikitokea mvua hata ya saa moja tu,umeme unakatika.

Mheshimiwa Naibu Spika, mnapowaita wawekezajiwaje kuwekeza na wakati umeme wenu ni wa kukatika nakuwaka, mnataka kuwaharibia mitambo yao? (Makofi)

T A A R I F A

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

Page 305: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

305

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jesca Kishoa kuna taarifanyingine, Mheshimiwa Deo Sanga

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika,nimesimama kwa Kanuni ya 68(7). Kwa mzungumzajianayezungumza sasa hivi; ni lazima tuwe na nidhamu nakauli ndani ya Bunge. Afute kauli yake ya kumwambiaMheshimiwa Mbunge mwenzake na ni Waziri mjinga, lazimatukubaliane hilo.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jesca Kishoa ilikuwa atoetaarifa lakini anakuomba ufute hayo maneno ya kumuitaMheshimiwa Naibu Waziri mjinga.

MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Naibu Spika,sijamwita Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba ni mjinga,nilichosema ni kwamba taarifa aliyotoa ndio ya namna hiyo.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika …

NAIBU SPIKA: Sasa Mheshimiwa Kishoa kwa sababuhiyo taarifa kuna aliyeitoa, naomba ili tuweze kwenda vizuriwewe ondoa hilo neno la “taarifa ya kijinga”, sema tuhuikubali taarifa tusonge mbele.

MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Naibu Spika,sawa, kwa kulinda muda wangu naomba niondoe manenohaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Serikaliinayojipambanua kwamba ni Serikali ya viwanda kunamambo ambayo yalipaswa kupewa kipaumbele. Mimibinafsi nimeunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais zakununua ndege pamoja na kujenga reli ya standard gauge,lakini katika Serikali inayojipambanua kwamba yenyewe niya viwanda hii haikuwa kipaumbele. Kipaumbele nambamoja kilipaswa kuwa ni umeme, kilimo na mambo mengine

Page 306: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

306

lakini kukimbilia kufanya mengine ndiyo maana mamboyanakuwa hayaendi. Niwashauri Waheshimiwa Mawaziriwamsaidie Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nijielekeze kwenyeskendo (scandal) kubwa sana ambayo nimewahikuizungumza humu ndani na leo nairudia na nitairudia kwaufupi tu. Nataka nijue kauli ya mwisho ya Serikali kuhusianana capital gain tax ambayo haijalipwa kwenye transfer ofshares kutoka kampuni ya BG kwenda kanuni ya Shell. Hii nchisi shamba la bibi, hii nchi ina wananchi na hii nchi ni yawananchi. Nataka kauli ya mwisho kutoka Serikalini, hizifedha ambazo mpaka dakika hii hazijalipwa. Tatizo ni nini?Akina nani walihusika? Ni nani alivunja sheria hii naamechukuliwa hatua gani? Mheshimiwa Waziri na Naibuwake naomba majibu hapa kesho atakapohitimisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Jesca Kishoa.Mheshimiwa James Milly atafuatiwa na Mheshimiwa MaulidMtulia na Mheshimiwa Yussuf Kaiza Makame ajiandae.

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Naibu Spika, lakwanza nianze kuwapongeza rika langu, ndugu zangu wote,ma-korianga popote walipo nchini kwa kufikia hatua yamuhimu ya maisha yao, tunakwenda kukabidhi madaraka.Hata hivyo, niwatakie heri wenzetu wale wa Kimnyak,Irkimayana kwa namna ambavyo wanapokea madarakakutoka kwetu kwa mila za kimasaii.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo,nimshukuru kipekee Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kufikajimboni kwangu na kuniahidi jambo moja, kwamba VAT yaasilimia 18 inayotozwa kwa mnunuzi wa tanzanite kwenyesoko huria itaondolewa. Nina imani kwamba Wazirianapokuja kuhitimisha hii VAT ataiongelea. Ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nisikitike pia kuhusuruzuku, hamjatoa kwa wachimbaji wadogo wadogo wa

Page 307: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

307

Mererani hususani akinamama ambao na wenyewe wanawawakilishi wao kila mahali wanajaribu kujipambanuakatika suala la kiuchumi lakini wamefanya application naWizara yenu haijatoa hata ruzuku moja kwao.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayonaomba niingie kwenye suala la tanzanite. Sheria ya Madiniya mwaka 2010 ambayo na wewe unaifahamu imewekabayana kwamba madini ya vito yatachimbwa na wazawalakini leseni yoyote itakayotoka haitazidi square kilometamoja. Kwenye application iliyofanyika 2013 application yaleseni HQP26116 ya Tanzanite One iliiomba Wizara kutoa leseniya madini, wao wenyewe wamempa square kilometa 7.6kinyume na sheria. Kuna majadiliano makubwa ya kisheriakati ya Wizara yako na watumishi, wengine wakikataa lakinikulikuwepo na shinikizo mwaka 2013 na ushahidi huo uponaomba niulete acheni kufisidi nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabungewenzangu mmemwelewa Mheshimiwa Tundu Lissu vibaya.Ninyi mnafahamu kesi ya Dowans tumepoteza kama nchina kesi ya Richmond tumepoteza kama nchi. MheshimiwaRais, Wabunge wa Upinzani hawakatai kwamba kunamadudu nchi hii kuhusu mikataba lakini nendeni kwa styleambayo nchi haitapata hasara kwa baadaye. Eleweni hivyoWabunge wenzangu wa CCM. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu Tanzanite Oneilipewa leseni kinyume na masharti ya sheria na aliyehusikakatika hilo, aliyesaini leseni hiyo ni ndugu Engineer Ally Samajena anajulikana yupo, naomba Serikali ifuatil ie.Walichokifanya ndugu zangu, kwa sababu sheria ya 2010inaruhusu yeyote anayechimba mable na graphite aruhusiwekupewa takribani square kilometa 10; wakasema kwenyeleseni yao hiyo wana–apply mable na graphite na si tanzanite.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo ukienda kwenyedocumentation zote Kampuni ya Tanzanite One haijawahihata siku moja kusafirisha nje mable na graphite. Ujanja huuulitumika na ninyi mnatakiwa mwelewe nchi yetu

Page 308: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

308

inavyoibiwa. Mtu anaomba leseni ya kitu kingine lakinianachimba kitu kingine, ipo kwenye documentation.Anaomba leseni ya mable na graphite lakini anakwendakuchimba tanzanite. Niwaambie Waheshimiwa Wabungewenzangu, nchi yetu inamalizwa; tusiposimama kamawananchi wanaoipenda nchi hii, tutaimaliza nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge,kampuni iliyoingia mkataba na Serikali 2013/2014 inaitwa SkyAssociate, sasa huyo Sky Associate ni nani? Ni kampuniiliyosajiliwa mahali panaitwa Virgin Island ambayo inafanyakazi zake Hong Kong. Kampuni hii haipo Tanzania nahaijasajiliwa Tanzania. Mheshimiwa Ngonyani anafahamukwa sababu taarifa aliyotoa kwa umma wakati yupoWizarani pale; Mheshimiwa Ngonyani aliwaambia watukwamba ndugu Faisal Juma Shabash ambaye ni Mtanzaniaanamiliki asilimia 25, alisema Hussein Gonga anamiliki asilimia35, Ridhiwan Urah, si huyu Ridhiwan anamiliki asilimia 40.Hakuna popote, si TIC, sio kwenye usajili wetu wa makampuniTanzania, watu hawa wanaonekana. Hii kampuni ni yakitapeli na Serikali inawalinda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndugu zangu lingine, hawajamaa wanafanya minada. Kampuni hii ya Tanzanite Oneimeuzwa kwenda Sky Associate kwa dola milioni tano yakulipana kwa mafungu. Minada miwili waliyofanya Agostina Februari wameuza takribani dola milioni saba…

MHE.HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bashe, taarifa.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika,nataka kumpa tarifa ndugu yangu James Millya, kwambakwa kuwa yeye katika maelezo yake anakiri Tanzanite Onemchezo unaoendelea ni wizi. Ningemwomba katika hotuba

Page 309: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

309

yake tu atumie fursa hii vile vile kumwomba Mheshimiwa Raisatoe Executive Order mgodi ule usimamishe uzalishaji nautaratibu wa kisheria ufuatwe. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa James Ole Millya,unaipokea taarifa hiyo?

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Naibu Spika,naipokea kwa mikono miwili, nimwombe Mheshimiwa Raisatumie mamlaka yake leo asimamishe uzalishaji wa kampunihiyo, lakini na Mheshimiwa Ngonyani pia ashughulikiwe. Pianiombe STAMICO inayohusika kufisadi nchi yetu, wewe tulia…(Makofi)

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. HALIMA J. MDEE: Halafu declare interest.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Ngonyani, taarifa

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: Mheshimiwa Naibu Spika, msemajianayesema sasa hivi analipotosha Bunge. Kampuni ya SkyAssociate si ya Tanzania, Kampuni ya Sky Associate ni kamaalivyosema ni ya Virgin Islands. Pili Kampuni ya Sky Associateshaikuwahi kununua hisa za kampuni ya Tanzania, Kampuniya Sky Associates ilinunua hisa za kampuni ya Uingerezakwenye soko la hisa la Uingereza ambalo Tanzania hatunacontrol nalo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kampuni ambayo ilikuwainamiliki hisa hizo ambazo zilinunuliwa na Sky Associate nikampuni ya Richland Resources. Kampuni ya RichlandResources ndiyo iliyokuwa inamiliki kwa asilimia 100 kupitiakampuni ya South Africa, Kampuni ya Mererani MiningLimited. Kwa hiyo, namwomba sana…

Page 310: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

310

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika,kuhusu utaratibu.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NAMAWASILIANO: … ni vizuri akaangalia jinsi kampuni hizizilivyoingia nchini na jinsi transaction hiyo ilivyofanyika badalaya kulipoteza Bunge hapa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa James Ole Millya unaipokeataarifa hiyo?

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Naibu Spika,kwanza niombe tu kwa heshima kwamba sipokei taarifa hiyo,lakini kwa sababu nimeomba Tume ya Rais iundwe na hayayote anayoyasema yataonekana kwa sababu kwa kawaidana yeye atahojiwa; haya yote atakuja kuyaeleza kwamba,je, kampuni hii ni ya Kitanzania au sio ya Kitanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naongea kitukimoja, akanushe mtu yeyote hisa hizo zimeuzwa kwa dolamilioni tano tu, lakini kwa masoko ya Agosti 2016 na Februariwatu hawa wameuza madini kwa milioni saba, tayari almostbilioni 16 na capital gain hawalipi, ndugu zangu nchi yetuinaibiwa sana. Hata hivyo, Kampuni ya Tanzanite One Limitedimekuwa ikitoa taarifa za uongo kwa mbia mwenza, yaaniSTAMICO tangu alivyoanza uzalishaji wa tanzanite hapanchini. Kwa mfano, kuanzia Julai 13 hadi Julai 16, STAMICOameripoti mauzo ya jumla ya dola za kimarekani milioni 16wakati kiukweli ni milioni 17, tayari kuna dola almost kati yamilioni moja mpaka laki kadhaa zinaibiwa, ndiyo maanatunasema watu hawa wanaiba.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini hilo halitoshi, minadainayoandaliwa yote, nilimwandikia barua Kamishna Msaidiziwa Madini pale Arusha, ndugu Ali Adam, tarehe 20 mweziwa pili 2017, kwamba ninaomba uniambie tenda ya kwanzana tenda ya pili waliyouziwa madini yetu kwenye tenda niakina nani? Alichonijibu officially, tarehe 24 Februari, ipokwenye documentation na barua imegongwa; wameuziwaGemoro Company Limited, kampuni ya India, Viber Global

Page 311: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

311

Limited Kampuni ya India, Kala Jewels Kampuni ya India, ShreeNarayan Gems ya India, hiyo ni tenda ya kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tenda ya pili ameuziwa ArwiInternational ya India, Shree Narayan ya India na ndugu zanguWaheshimiwa Wabunge watu hawa wote wana mahusianoya karibu na kampuni ambayo imesajiliwa Virgin Islandinayofanya kazi zake Hong Kong. Waheshimiwa Wabungenchi yetu inaibiwa, ni muda muafaka madini haya yatanzanite wengi wenu hamyafahamu, ni madini ambayoyangeweza kubadilisha maisha ya watu wa Simanjiro lakiniyangeweza kubadilisha maisha ya watanzania wengi.Ninaomba kwa ukubwa wetu tuingilie jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa James muda wakoumeisha, zilishagonga zote mbili, hawa hapa ndio watunzamuda, ahsante sana.

Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na MheshimiwaMaulid Said Mtulia atafuatiwa na Mheshimiwa Yussuf KaizaMakame ambaye atachangia kwa dakika tano naMheshimiwa Mohamed Juma Khatib atakayechangia pia kwadakika tano.

MHE. MAULID S. A. MTULIA: Mheshimiwa Naibu Spika,awali ya yote nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungumwingi wa rehema kwa kunijalia kuwa na afya njema nakupata fursa hii ya kuchangia katika mjadala huu muhimusana. Pili, nitoe mkono wa Baraka na kuwatakia RamadhanMubarak Waislam wote na hasa wa Jimbo la Kinondoni naTanzania kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hili la Ramadhan vilevile niseme kwamba katika kupeana mkono wa baraka,ndugu zetu, kwa taarifa nilizonazo Zanzibar na hasa Pemba

Page 312: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

312

kuna uhaba mkubwa wa nafaka, kwa maana ya viazimbatata pamoja na mihogo. Mheshimiwa Mwijage kwasababu ni Waziri wa Biashara anasikia hili achukue fursakuwahakikishia wafanyabiashara wetu wa bara wanajitahidikupeleka vyakula haraka iwezekanavyo ili kupunguza ugumuhuu na Ramadhan iwe nyepesi kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze MheshimiwaMwijage kwa usomaji mzuri wa taarifa ya bajeti na niombemzee wa uchumi wa diplomasia kama wakati mwingineakiwa anamu-opt anaweza akafanya mambo yakawamepesi sana, ameisoma vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mwenyekiti waKamati yangu, Mheshimiwa Dotto Biteko, kiongozi kijana,kamati yake iko makini na amesoma ripoti nzuri sana ambayohata wachangiaji imewasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nataka nizungumze,mimi mbunge wa Mjini na sina tatizo sana na REA I, II na IIIlakini mimi nina tatizo kubwa sana la bei ya umeme, tunatatizo umeme ni bei juu sana. Bei juu ya umeme inatokanana gharama ya uzalishaji ambayo TANESCO wanaipata bilakusahau gharama za usambazaji. Hata hivyo, tuna umemewa maji ambao gharama yake ni shilingi 36 tofauti na umemewa gesi ambao ni shilingi 147na umeme wa mafutatunaambiwa shilingi 368.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna taarifa ya Kambi Rasmiya Upinzani ya Wizara ya Fedha, Waziri Kivuli alisema kwambaumeme unanunuliwa kwa shilingi 500 na TANESCO wanauuzakwa shilingi 280.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia gharama hizi zauzalishaji kama tungetumia umeme wa maji na umeme wagesi, gharama zetu za umeme zingeshuka kwa chini yaasilimia 50 ya sasa. Umeme wetu unakwenda juu sana, nikwa sababu ya haya makampuni yanayozalisha umeme kwanjia ya dharura tuliyoingia mikataba, umeme wa mafuta, nimakampuni ambayo yananyonya sana nchi yetu.

Page 313: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

313

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna makampuni hayayanajulikana Songas, Dowans, Pan African; ni makampuniambayo yanazalisha umeme kwa gharama kubwa na leonimepata nafasi ya kuwauliza watendaji wetu, je, tukiachakutumia umeme wa mafuta tukitumia umeme wa maji nagesi na njia nyingine hatuwezi ku-survive? Wanasematunaweza, lakini tuna kikwazo kikubwa cha mikataba,mikataba tuliyoingia na makampuni ya uzalishaji umeme niya ajabu sana, ni mikataba ambayo mimi nashindwa,mikataba gani tunaingia, wataalam wetu wanaingiajekwenye mikataba ambayo haina room ya kutoka? Hii nindoa ya aina gani? Au ndiyo ile ndoa wanayosema yaKikatoliki?

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunatamani na tunafikiriawataalam wetu wanapoingia kwenye mikataba wawekena mlango wa dharura wa kutoka, lakini leo mikataba yetuhii ukiingia, ukitoka, unapelekwa mahakamani. Nina habarikwamba Dowans wamesimamishiwa mkataba na wakombio wanakwenda mahakamani na kuna hataritukalipishwa pesa nyingi. Sasa kwa utaratibu huu nafikiri tatizoliko kwa watendaji na wataalam wetu. Inakuwaje mikatabatukiingia hatuwezi kutoka? Nafikiri hili jambo si sawa na kwakweli umeme umekuwa ghali lakini sababu kubwa ni huuumeme wa mafuta ambao hatuwezi kujitoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo Songas tungewezakuachana nao, hatuwezi kwa sababu ya mikataba. LeoDowans mnataka tuachane nao, hatuwezi kwa sababu yamikataba. Leo Pan African tunataka kuachana nao hatuwezikwa sababu ya mikataba. Hivi hii ni mikataba gani ambayohawa wataalam wanaingiaje mikataba ambayo hatunaroom ya kutoka? Napata taabu sana mimi hapa na kwakweli kwa utaratibu huu nchi hii tutakuwa tunasokota kambanyuma inaungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, TANESCO ina deni kubwalinalofikia kiasi cha bilioni 800, inadaiwa. Kama TANESCOinadaiwa zaidi ya bilioni mia nane, lazima umeme upandena ili ushuke lazima tutoke kwenye mikataba hii. Kwa hiyo

Page 314: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

314

Mheshimiwa Waziri aje kutueleza ni namna gani tutatokakwenye hii mikataba ya kinyonyaji, mikataba ambayoinapandisha bei ya umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo,nimuunge mkono dada yangu, Mheshimiwa Najma leoamezungumza jambo zuri sana kuhusu Zanzibar. TANESCOinawa-treat ile Kampuni ya Umeme Zanzibar kana kwambani mtumiaji wa kawaida, wanamuuzia umeme kanakwamba wanamuuza Mr. Juma, Mr. Ali, hawazingatiikwamba yule naye anakwenda kufanya biashara.Wanamtozea mpaka Kodi ya VAT wakati na yeye alipaswaatengeneze aweze kuuza aweke na kodi yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono, ni vizuriwakapewa huo u-agency, au kama itashindikana wao wanauwezo wa kununua umeme wenyewe, wanunue kutokakatika makampuni yanayozalisha umeme wafanye transferkwenda kwao Zanzibar ili na wao liwe ni shirika ambalolinaweza kujinunulia umeme kwa watengenezaji umeme nabadala yake lisiwe shirika ambalo linapitisha umeme halafulinatozwa bei ya mtumiaji wa kawaida, hii siyo fair. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili ambalonataka nilizungumze, tulikuwa katika bajeti ya maji,wachangiaji wengi hapa walivyochangia walioneshakwamba ili bajeti yetu ya maji ipate pesa nyingi tuongezetozo kwenye mafuta, shilingi hamsini na mimi nilisemakuongeza tozo ya shilingi hamsini kwenye mafuta tafsiri yakehatumsaidii mwananchi wa kawaida, kwa sababu yeyeatakwenda kuilipia hii kwenye upatikanaji wa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nikapendekezakwamba, tuna hawa jamaa zetu wa EWURA, waowanasimamia vinasaba na juzi tu hapa kulikuwa namchakato wa kumpata mzabuni wa vinasaba. Tendaimefanywa, makampuni yamejitokeza, makampuni matatuyaka-qualify kwa kutumia vigezo walivyoviweka EWURA naMakampuni yaliyo-qualify ilikuwa ni SICPA, SGS na kampuninyingine ambayo jina lake sikulipata.

Page 315: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

315

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa haya makampuniukiangalia tenda waliyoweka hii kampuni ambayoinaonekana imeshinda tenda bei yake ni kubwa.Nilipendekeza hapa, ni vizuri sasa watu wa EWURAwakaisaidia nchi kutafuta mkandarasi ambaye ame-tenderkwa gharama ya chini ili… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha MheshimiwaMtulia.

MHE. MAULID S. A. MTULIA: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante. (Makofi)

MHE. YUSSUF KAIZA MAKAME: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina ajenda tatu tu zakuzungumza, ajenda ya kwanza ni huu mchanga wadhahabu ambao kila mmoja anauzungumza. Ajenda ya pilini ile sheria ambayo ilipitishwa na Bunge hili mwaka 2015inayohusu mafuta na gesi na ajenda ya tatu ni hili deni laZECO kwa TANESCO.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mchanga; hapahatuhitaji kunyoosheana vidole tena kama Bunge, hatuhitajikunyoosheana vidole, hatuhitaji kuonesheana mchangaulichukuliwa vipi au dhahabu iliibiwa vipi. Kinachohitajikasasa ni kuwa wamoja, hatuhitaji tena kukaa tofauti,kinachotakiwa tumeona kwamba tunaibiwa ni lazima Bungeliwe kitu kimoja, hatuhitaji kitu kingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababuMheshimiwa Profesa Muhongo kabeba wizi wote au uhangawa miaka au nusu karne, miaka 50 tumekuwa tukiibiwamhanga leo katolewa Mheshimiwa Profesa Sospeter

Page 316: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

316

Muhongo, kaondoka. Mbuzi wa kafara kashaondoka natulishajua nini tulichoibiwa, tujitahidi tukae pamoja kwa ajiliya Taifa na manufaa ya watoto wetu wanaofuata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri kwa Serikali; kwangumimi na muono wangu, hii ni sehemu nzuri kabisa ya kuanzia.Haiwezekani unakuwa unaibiwa baadaye ukasema kwanzausizuie mali iliyoibiwa utafute namna ulivyotayarisha kuibiwa.Kwanza ukamate mali, baadaye u…, haya, ila mkubalimakofi haya myakubali kwamba ninyi ndio mliotuingizakatika wizi wa miaka 50 na hili mpige makofi. Kamamlivyoleta ndege, mkubali kwamba ninyi CCM au Serikali yaCCM ndio mliotupeleka kwenye wizi huu wa miaka 50; namkisimama mjisifu na mkubali udhaifu wenu, hilo ni moja.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili, nashaurimikataba, sheria na zile sera zote tuzilete Bungeni na zilezinazotakiwa kwenda kwenye mamlaka ya utendajizifanyiwe marekebisho ili mambo haya yasijitokeze tena. Hatahivyo, tujenge refinery zetu wenyewe, kwa nini tunashindwa?Wameamua kuhamia Dodoma bila bajeti wameweza, kwanini wanashindwa kujenga viwanda vya kuchakatiadhahabu yetu hapa? Kwa nini wanashindwa hil i?Wamewalipa wafanyakazi wa Wizara ya Fedha milioni 10,15, 20 wengine kuhamia Dodoma, wanashindwa ku-maintainhii mali yetu tuliyonayo? Hii ni natural resources, ikiondokahakuna tena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine, nashauri, kwa nchiza wenzetu wenye maono ya mbali wanajenga, kwa sababuhizi zikiondoka hazirudi tena, baada ya miaka 50, 55 hatunatena hiki kitu. Kwa hiyo, tusije tukawaonesha wenzetu historiaya mashimo, tuwaoneshe kwamba tulikuwa na dhahabu,tulikuwa na tanzanite, tulikuwa na whatever, kwa hiyo hivivyote vinatakiwa vifanyike.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichangie pia Sheria ya Gesi;Waheshimiwa Wabunge, Sheria ile ya Mafuta waliiingiza

Page 317: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

317

mkenge Zanzibar na lazima wakubali na walivunja Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 102(1), Ibaraya 105(2), Ibara ya 106(3), zote walizivunja…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha MheshimiwaMakame. Mheshimiwa Mohammed Juma Khatib, dakikatano, atafuatiwa na Mheshimiwa Phillipo Mulugo.

MHE. MOHAMMED JUMA KHATIB: Mheshimiwa NaibuSpika, nashukuru kwa kupata nafasi. Niseme mapema tukwamba leo nina saumu, kwa hiyo ule wasiwasi na mashakakwamba kila atakayesimama hapa ataangusha nondo, miminina saumu, kwa hiyo nitazungumza kwa upole kabisa.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niseme kwambanampongeza sana Mheshimiwa gwiji wa siasa, waliokuwahawamfahamu Maalim Seif niwaambie kwamba yule ni gwijiwa siasa, pale chuo kikuu tena rekodi yake mpaka leohaijavunjwa, alifanya Degree ya Political Science pamoja naInternational Relations. Sasa wakati tunakuja Bungeni; natakaniwaondoe wasiwasi; alituita sisi akatufunda vizuriakatuambia kwamba mnakwenda huko lakini tunatakamuwe Wabunge wastaarabu. Serikali inapofanya vizuriipongezeni na inapofanya vibaya isemeni, ikosoeni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hilo halitoshitulipokuwa katika kikao cha UKAWA, Mheshimiwa Mboweakarudia maneno hayo hayo. Kwa hiyo niwaambie kwambasisi Wapinzani tutasifu pale ambapo litafanyika jambo zuri,pale ambapo mtavurunda, msitegemee sisi tutawasifu.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mawaziri wameapa, tenakiapo cha Kikatiba kabisa cha kumshauri Mheshimiwa Rais,naomba hiyo kazi waifanye kwa ufanisi mkubwa. Wao kamaCabinet wana collective responsibil ity, wanatakiwa

Page 318: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

318

wayaendee mambo ya kitaifa kwa pamoja, wanatakiwawamshauri Mheshimiwa Rais kwa pamoja na kwa hekima.Isitokee wanakaa na Mheshimiwa Rais muda wote mpakaanaondoka madarakani halafu mmoja anakuja kusemakwamba mtu anatumia muda mwingi zaidi kwenda safariza nje kuliko kwenda kumsalimia mama yake. Hivi huu mudawote waliokuwa pamoja kama aliona kwamba hilo lakwenda safari za nje ni baya zaidi kuliko kwenda kumsalimiamama yake kwa nini hakusema mapema? Hilo ni la pili(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu, niwape polewananchi wa Tanzania hasa Tanzania Bara ambao Serikali,niseme kwa nia safi kabisa, walitegemea kuwaondoleamatatizo mengi likiwemo la kukosa umeme katika maeneoyao. Kwa sababu nchi hii kabla ya Mradi wa REA ilikuwaimekatika mapande; pande la mijini pamoja na vijijini,huduma ya umeme ilikuwa iko mjini tu lakini vijijini kotekulikuwa giza tupu.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili la kuanzisha Mradihuu wa REA ni suala zuri sana, lakini nalo limekumbwa namatatizo na moja kati ya matatizo hayo ni pale wakubwawetu wanapotuambia kwamba wataulinda Muungano huukwa gharama zote. Wananchi wa vij i j ini walikuwawanategemea mradi wa REA, na mradi wa REA ulikuwaunategemea msaada mkubwa wa MCC.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa huu msaada wa MCCumekosekana kwa sababu demokrasia hakuna, demokrasiahaiheshimiwi, anayeingia kwenye uchaguzi akashinda siyeanayepewa. Kwa hiyo, hili limewakwaza sana WatanzaniaBara kwa ajili ya kupata umeme huu wa MCC, hilo ni lakwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzungumzaji)

Page 319: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

319

NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha MheshimiwaKhatib, ahsante sana. Mheshimiwa Phil l ipo Mulogo,atafuatiwa na Mheshimiwa Constantine Kanyasu,Mheshimiwa Joseph Musukuma ajiandae. (Makofi)

MHE. PHILLIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Naibu Spika,nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ili kuweza kuchangiakatika Wizara hii ya Nishati na Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda tu kumpongezaMheshimiwa Rais kwa hatua zote alizozichukua kuhusumasuala ya mchanga. Nakubaliana naye kabisa kwaasilimia 100 na tunasubiria hiyo Kamati nyingine ambayoinashughulika na masuala ya kiuchumi na sheria tuje tuonena yenyewe itasema nini, halafu baada ya hapo twendembele. Hata hivyo, kwa hatua mpaka hivi sasa tunavyosemanakubali kwa asilimia 100 kwamba Mheshimiwa Rais nimzalendo sana katika nchi hii na anavaa kabisa uzalendokatika nchi hii kwa ajili ya kulitumikia Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nirudi kwenyemasuala ya Jimbo langu la Songwe. Daima nikiwanachangia hapa huwa nasema miaka yote, kwamba; sasasijui nitumie neno Serikali kwa ujumla ama niseme tu Wizarahii; Wizara ya Nishati na Madini Jimbo la Songwe naona kamavile inapendelea. Mheshimiwa Mwijage utakumbukaulipokuwa Naibu Waziri wa Wizara hii alifika jimboni kwangu,Kata ya Kanga na aliniahidi kunipa umeme na hivinimwambie Kata ya Kanga umeme unawake kwa initiativeszako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini Jimbo la Songwe linakata 18 na hivi ninavyosema kata sita angalau zina umemena kata 12 hazina umeme. Hata hivyo, WaheshimiwaMawaziri hawa wanasahau kwamba tulikuwa Mkoa waMbeya zamani, sasa tuko Mkoa wa Songwe. Kule kwaMheshimiwa Mwambalaswa vijiji vingi vina umeme, kuleMbozi vijiji vingi vina umeme, kule Momba kwa MheshimiwaSilinde vijiji vingi vina umeme, kasoro Jimbo la Songwe, kunanini? Mheshimiwa Dkt. Kalemani, nimekwenda mara nyingi

Page 320: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

320

sana ofisini kwake, nimekwenda kwenye dawati lakekumlalamikia, kwa nini Jimbo la Songwe hawatuleteiumeme? Tumekosa nini mbele za Mungu?

Mheshimiwa Naibu Spika, wiki iliyopita nilichangiahapa kwenye Wizara ya Elimu, nikasema kwamba wenzetukule, sisi wilaya mpya hatuna chochote, hatuna majengo yawilaya, hatuna nyumba za watumishi, hatuna barabara yalami, hatuna VETA, hatuna maji makao makuu ya wilaya,yaani kila kitu hatuna, hata umeme vijijini hatuna, yaani hataumeme tu tukose? Kwa kweli kesho nitakuwa mkali sanakwenye kushika shilingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sijawahi kuwa mkali kwenyehilo, lakini kesho, Mheshimiwa Mwijage, nitashika shilingi yake,kwa sababu yeye ameshawahi kufika kwenye jimbo langu,anawafahamu wananchi wangu na tulimpa na ng’ombena mbuzi siku ile Mheshimiwa Mwijage, tukamweka akawaMtemi kwa sababu alifanya jambo zuri sana na alichangiana maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo Kata za Gua, Udinde,Kapalala, Mbangala, Manda, Namkukwe na Mpona na vijijizaidi ya 30, hatuna umeme. Nimekwenda pale REA MakaoMakuu kulalamika lakini mpaka leo umeme hakuna, kunanini Songwe na ni mkoa mpya na ni wilaya mpya? Jamaninaomba na sisi watufikirie tuweze kula keki ya Taifa na sisi,wanatunyanyasa mno, hatuna chochote, nalalamika kilasiku hapa. Mwenzenu sina barabara, nimesema hapa, sinachochote, basi hata umeme wa REA. Naomba, MheshimiwaDkt. Kalemani, nimemlalamikia sana kila siku nikija anasemaatanipa mkandarasi, siwaoni hao wakandarasi wa Songwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mtu wamemwekakule Mbeya anayesimamia masuala ya nishati ya umemeMkoa wa Songwe, hapatikani na Mheshimiwa Naibu Waziri,nimemlalamikia huyo mtu kwa nini wasimuwajibishe. Hatakikushirikiana na Wabunge wa Songwe masuala ya umeme

Page 321: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

321

na anamfahamu na nilimpa na namba zake za simu, please,naombeni umeme. Safari hii na mimi sasa nitakuwa mkali,nimekuwa mpole mno, nitakuwa mkali sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Shanta Gold Miningambao kule kwetu wanajiita New Luika Gold Mining; kwakweli watu wa madini hawa; ndiyo maana nimempongezana Mheshimiwa Rais; watu hawa ni waongo sana. Mwakawa jana amekuja Mheshimiwa Profesa Muhongo kwenyejimbo langu, tumekwenda kwenye Kij i j i cha Saza,tumekubaliana na Mheshimiwa Dkt. Kalemani anajua, watuwa Kijiji cha Saza wamelalamika, kuna eneo la wachimbajiwadogo wadogo lakini watu wa Shanta wameliingilia eneolile mpaka kwenye nyumba za wananchi, makaburi,miembe, miti, kila kitu kimekwenda Shanta, kwa nini.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kumlalamikiaMheshimiwa Profesa Muhongo, wamekuja na MheshimiwaKandoro aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mwaka janawamefika pale, tumekaa vikao siku sita, tumehukumu kesina watu wa Shanta wakashindwa mbele ya wanakijiji, mbeleya mkutano wa hadhara na TBC walionesha na miminilikuwepo pale. Hata hivyo, Mheshimiwa Waziri alitoa rulingpale pale, kwamba eneo hili tuwape wananchi, lakinimpaka leo sina barua inayowaonesha wananchi kwambawamepata lile eneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Dkt. Kalemanina yeye nakumbuka nilimwambia, naomba kesho aniambie,baada ya Waziri kutamka kwamba lile eneo ni la wananchina wamuulize Mheshimiwa Profesa Muhongo popote hukoalipo aseme baada ya pale nini kilichoendelea, nakwendaofisini kila siku anasema subiri. Hawa watu wa Shanta wananini? Wametoa nini huko?

Mheshimiwa Naibu Spika, haya, juzi nilikuwa Jimboni,nimeuliza swali jana hapa kwa Mheshimiwa Waziri wa Maji,nasema hivi; hawa watu wa Shanta hawa tena wamefungatayari mto. Mto unatoka Rwika unakwenda Mbangala mpakaMaleza wamefunga kwa ajili ya wananchi wasipate maji,

Page 322: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

322

kwa nini wanatuonea hivi jamani? Vijana wa Mbangalampaka wakataka kufanya fujo lakini Polisi wakawawekandani, tunawaonea wananchi bure. Hawa watu wa madinini waongo sana na mimi ndio maana sielewani nao kwasababu ya hiyo toka mwaka jana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu nilipomwambiaMheshimiwa Profesa Muhongo amekuja pale sasa na hiloeneo tumewanyang’anya, basi leo ni chuki ya Mbunge nawananchi hatuelewani kule Songwe. Naomba tafadhalisana, maji yafunguliwe la sivyo mimi nitakwenda jimbonikuwachukua watu wa Saza na kuwachukua watu waMbangala tukashirikiane tuchukue majembe na shokatukatoboe lile bwawa ili na mimi mje mnipige, mnifunge,haiwezekani kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mikataba wameweka nakijiji lakini ni mikataba feki; na wamesema wao wenyewekwamba; mikataba tumeweka, hamuwezi kutufanyachochote kwa sababu sisi Serikali inatulinda. Tafadhali sanaMheshimiwa Mwijage, Mheshimiwa Dkt. Kalemani,nawaomba suala hili walitamkie kesho watu wa Ashantiwatoboe lile bwawa na wananchi wangu waweze kupatamaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayowala siwezi kuchangia mambo mengi sana, naombatupate...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwamuda wa mzunguzaji)

NAIBU SPIKA: Muda umekwisha Mheshimiwa Mulugo.

MHE. PHILIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Naibu Spika,ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Lakini usiende kuwakusanya haowananchi tafadhali, kwa sababu ni kosa Kisheria.

Page 323: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

323

Waheshimiwa Wabunge, tutaendelea hawaWabunge waliosalia kwa muda tulionao watachangiadakika tano tano. Mheshimiwa Costantine Kanyasuatafuatiwa na Mheshimiwa Musukuma na Mheshimiwa HawaAbdulrahman Ghasia ajiandae

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana. Naomba kuanza kwa kumpongezaMheshimiwa Rais kwa ujasiri mkubwa na hasa kwa sababumimi na Mheshimiwa Rais mwenyewe tunatoka kwenye mkoaambao hawa wachimbaji wa dhahabu kwa kweliwanatuachia mashimo matupu na watu wanaendelea kuwamaskini. Kwa hiyo, hizi jitihada za Mheshimiwa Rais tunaziungamkono, tunampongeza sana na wananchi wa Mkoa waGeita kimsingi ambao wameshuhudia miaka 19 dhahabuinachimbwa lakini Makao Makuu ya Mji wa Geita hakunabarabara, Makao Makuu ya Mji wa Geita hakuna maji,hospitalini hakuna wodi, shule watoto wanakaa chinikilometa moja kutoka kwenye mgodi pale watu ni maskinisana; wanaona juhudi hizi za Mheshimiwa Rais zinatakiwakuungwa mkono.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nawashangaa sanawenzangu hawa ambao wanapinga kwa sababu kamawalivyosema wenzangu huko nyuma, walikuwa kila sikuwanalalamika wanasema kwamba nchi hii inaibiwa…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: …lakini natakakusema kwamba Mheshimiwa Rais aendelee…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,taarifa.

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: …na ikiwezekana naaangalie pia katika maeneo mengine ambapo MheshimiwaRais aangalie machimbo…

Page 324: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

324

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mnyika bahati mbayamuda wetu umekwisha sana, kwa hiyo, hakutakuwa nataarifa isipokuwa kuhusu utaratibu. Mheshimiwa Kanyasu.

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa NaibuSpika, nakushukuru sana. Kwanza nataka nimkumbusheMheshimiwa Mnyika katika ukurasa wake wa sabaamezungumzia kwamba Serikali iliingia mkataba wa loyaltywa four percent. Hii ni four percent siyo ya force declaration.Unapofanya force declaration, four percent yeyote hainamaana yoyote ile kwa sababu unazungumzia four percentya value gani? Hawa watu wanafanya four percent ya uongohalafu wanakuja kuwatetea hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine la pili; nilikuwanamshangaa sana Mheshimiwa Mnyika kwenye ukurasa wakewa tisa anasema kwamba taswira ya Tanzania kwenye jaridamoja huko la Mining journal inasema trouble in Tanzania kwasababu Rais ameanza kufuatilia wizi, so what? Trouble, yeskuna wizi unagundulika, unataka Rais asigundue wizi? Lazimaili hii…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu utaratibu

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: …lazima MheshimiwaRais afuatilie kwa sababu unaposema trouble in Tanzania,kama kuna wizi umegundulika lazima Rais afuatilie sasa miminakushangaa unapo…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kanyasu, MheshimiwaMnyika utaratibu kikanuni.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,msemaji anayezungumza hasemi ukweli. Yeyeanazungumzia…

WABUNGE FULANI: Kanuni!!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mnataka Kanuni?

Page 325: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

325

WABUNGE FULANI: Ndiyo!!

MHE. JOHN J. MNYIKA: Hivi unaniuliza mimi kuhusuKanuni? Kanuni ya 63 na Kanuni ya 64 sawa sawa?

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mnyika zungumza na Kitimuda wetu umekwisha kama nilivyokwambia ulivyosimamamwanzo, kwa hiyo zungumza na kiti ili tusipoteze muda.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,msemaji anazungumzia mgodi wa Geita, mgodi wa GGM.Mgodi wa GGM hausafirishi makinikia ya dhahabu nje ya nchi.Kwa hiyo, wizi anaousema kwamba Rais ameufuatiliahauhusu kabisa yaani anasema uongo hauhusu kabisa mgodiwa GGM na ndiyo maana sisi wengine tunasema mgodi waGGM…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mnyika umesemamwenyewe kwamba kanuni unazifahamu vizuri. Kanuniinayohusu yeye kuzungumza uongo wewe unajua unapaswakulileta kwangu ili mimi niamue namna gani. Sasa hichounachosema hapo huoneshi namna gani yeyeanavyodanganya na ni Kanuni gani nitajie ili mimi sasaniweze kutoa rulling kwenye huo utaratibu unaouomba,sekunde moja.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Nimekwisha kwambia niKanuni ya 63 na 64 juu ya kusema uongo Bungeni. Kanuni ya63…

NAIBU SPIKA: Naomba ukae Mheshimiwa Mnyika .Naomba ukae, kaa chini nimeshasimama, kaa. Naombauzime hiyo microphone yako Mheshimiwa Mnyika.

Waheshimiwa Wabunge, nilishawahi kusema hapanarudia tena; ukitumia kanuni ya 63 kwamba mtuanazungumza uongo maana yake wewe uoneshe kwanza;wewe ndiyo unayetakiwa kuonesha namnaanavyozungumza uongo. Waheshimiwa Wabungetusikilizane, mimi niko hapa wala sijasinzia kama Wabunge

Page 326: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

326

wengine, Mheshimiwa alipokuwa anachangia ametaja Mkoawa Geita hajataja neno uchimbaji wa madini kwenye mgodiwa Geita Gold Mine hajataja kitu kama hicho.

Mheshimiwa Mnyika naomba utulie; nitampa nafasiMheshimiwa Kanyasu aendelee na mchango wake kwasababu hayo maneno Mheshimiwa Mnyika unayosemaamezungumza uongo Mheshimiwa Kanyasu hajasema,kasema Mkoa wa Geita na ameendelea na mchango wakehajautaja mgodi wa Geita. Mheshimiwa Kanyasu maliziamchango wako.

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa NaibuSpika...

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,ungenipa nafasi ya kueleza uongo.

MHE. COSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa NaibuSpika, ulichosema ni sahihi na namshangaa sana nduguyangu hapa mimi nazungumzia issue katika general yake yeyeanajaribu kwenda katika eneo dogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwa sababu ya muda,kuna mzungumzaji pia mmoja amezungumzia kwambauzalishaji wa umeme umepungua, nilitaka aende kwenyeukurasa wa 21 ataona mahitaji ya umeme ndiyoyaliyoongezeka kutoka megawats 1,026 kwenda megawats1,051, lakini uzalishaji wetu ni megawats 1,450.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii kuishukurusana Wizara hii. Geita tulikuwa tuna matatizo makubwa sanaya umeme, unakatika kila siku; hivi ninavyozungumza sasahivi umeme wa Geita haukatiki, umeme wa Geita uko imarana ninachowaomba tu sasa hivi ni kuhakikisha sasa umemehuu kama ahadi ambavyo ilikuwa kwamba vijiji ambavyovilikuwa havijapata umeme wa REA vinapata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ambalo natakakusema hapa ni kwamba pamoja na umeme wa Geita

Page 327: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

327

kutokatika, lipo tatizo ambalo nilimwambia MheshmiwaNaibu Waziri kwamba TANESCO hawana vifaa. Kwa hiyowatu wanapoomba umeme wanachukua muda mrefu sanakupata connection ya umeme; hivyo nadhani pamoja najuhudi za REA TANESCO wakae upya wafikirie namnaambavyo wanaweza kuongeza mtaji. Kama TANESCOwameshindwa kuwa na vifaa vya kutosha kwenye store, nivizuri wakaruhusu vendors wengine wakawa na vitu hivikwenye maduka na wao wa-control quality kuliko ilivyo sasa,mteja ameomba umeme leo anafungiwa mwezi wa 10 kwasababu wewe huna meter, kwa sababu wewe huna wayawakati soko hili ni soko huria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huo ndiyo ushauri wangu.Nakushukuru sana kunipa nafasi. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa JosephMusukuma.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana, dakika tano ni kidogo, ningemwombadada yangu Hawa Ghasia akaniachia sijui kama atakubali.

WABUNGE FULANI: Amekubali.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Amekubali, kwa hiyodakika 10, nakushukuru sana dada yangu (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwakunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza nimpongeze sanaMheshimiwa Rais kwa ujasiri aliouonesha kwenye makinikiahayo yaliyoshikwa huko bandarini. Pia nimpongeze kwa ujasirina kwa bahati mbaya leo Profesa Muhongo hayupo hapa,nilitaka nimkaribishe darasa la saba huwa tunakaa huku ilituwe tunamfundisha hali halisi ya Watanzania tunayoina kulemajimboni, tukaachana na ule u-profesa.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wengi humuwanaopiga kelele wamekaa na wawekezaji na wengine

Page 328: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

328

hata dhahabu hawaijui. Wanasema hatujaisoma Sheria yaMadini lakini yeye hajawahi hata kuona madini, anamilikinyanya, kwa hiyo hivi vitu bora akakaa ili tuzungumze watutulio na uchungu. Iringa na dhahabu wapi na wapi? Huyumtu anamiliki nyanya, kuku na mbwa halafu anakuja kuanzakujadili vitu vya msingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimwambie rafikiyangu msomi kabisa tuachane suala la mchanga;anifafanulie na aelewe wizi ambao uko kwenye migodi hiimikubwa. Ukienda kwenye uhalisia…

MBUNGE FULANI: Taarifa

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: …kwenye hii migodi yaNorth Mara ukienda Buzwagi, ukienda Kahama Mining kotekuliko na migodi hii kuna kanembo kadogo kameandikwaACACIA; na ACACIA ana hisa asilimia 21 kila mgodi naameziuza kule Uingereza amepata Dola bilioni 275 na Serikaliyetu TRA wakaenda kudai kodi, akawaambia mimi sina filekwenu, tumeshinda kesi amekata rufaa. Sasa alichokiuza kuleUingereza ameuza nini? si ameuza North Mara ya Mara,ameuza ACACIA, ameuza Buzwagi ya Kahama, ameuzaKakola? Sasa hawa watu wana kesi nyingi na ndiyo maanaMheshimiwa Rais amesema tuwachunguze. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu kingine, suala hili siyola Bunge, ni Mbunge gani aliyegundua kama tunaibiwa ulemchanga pale? Ni Mheshimiwa Rais na jitihada zake, acheniakamilishe Tume atuletee humu ndani. Tunaachakushughulika na mambo ambayo tumelipwa poshokuzunguka kama Kamati tukayaibua sisi wenyewe, mtukaibua mwenyewe, hajakamilisha uchunguzi wake, ninyimnaanza kusema anafukuza wawekezaji, anawafukuzawapi? Hii ni mifano tu, hili Bunge siyo lile mlilozoea kwambamnakaa kule nyie wenye midomo, mnapewa hela kujakutupigisha makofi, mtazirudisha time hii.

Page 329: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

329

Mheshimiwa Naibu Spika, hata wenzangu hawaupinzani wengine humu ndani mnapiga makofi burewenzenu wamekula hela Morena pale mnataka tuwataje?Acheni watu wafanye uchunguzi…

MBUNGE FULANI: Taja

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: …….tufike mahali Raisatoe mwelekeo. Rais ndiyo ameshika makontena walahayakushikwa na Tundu Lissu. Nawashangaa Wanasheriamimi siyo Mwanasheria huyu ndiyo Rais. Dira ya Wanasheriawetu inayoongozwa na Rais Tundu Lissu ndiyo hiyo yakupingana na sisi tunaibiwa? Naomba sana hawa vijanawatulie Mheshimiwa Rais afanye kazi, kile ni kichwa achakishike na mtashikwa na mengine zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama kweli huu mchangawanavyosema wenzetu kwamba ukipelekwa kule Japanwao wanatoa madini ya aina tatu; wanatoa dhahabu,copper na silver. Sasa uchunguzi tu wala hatuhitaji Maprofesawaliohangaika na wanaoendelea kupiga maneno humundani, watupeleke kule Japan wakatuoneshe ule mchangabaada ya kutoa yale madini matatu ule mchanga unamadini 32 ule unaobaki una nini? Kama una mali tuuze basikule Japan hata kama wameyafyatua matofali si tutavunjatu hivi, tunapima, tunapata yale madini yetu? Tunapigahesabu kubwa ambazo hawa hawaelewi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi natokea kwenye hiyomigodi mikubwa, nataka niwaambie ambao hawaijui hatadhahabu. Tunanunua mfuko mmoja wakati hawajaanzakusafirisha na bunduki, vijana walikuwa wanazunguka nawale madereva ukiuziwa kamfuko kamoja karambo ka-Azam kale Sh.800,000 unapata Sh.16,000,000 na tulikuwatunaiba kweli na watu wamepata hela. Sasa kama hakunadhahabu kwa nini wanasindikiza na Mapolisi mbele na nyumana makontena yale yanalindwa hata yakiwa bandarini?

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambieWatanzania wajue na kama ingekuwa Mheshimiwa Rais

Page 330: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

330

anaweza kupokea ushauri wangu; hawa wanaobwabwajahuku tukawaruhusu wakafanye mikutano kule Kanda yaZiwa, hamtarudi ninyi, hamjui shida tulizonazo. Tumeibiwavya kutosha, tumuache Mheshimiwa Rais afanye kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Ole Milyakwa sababu yeye anajua maana ya Tanzanite, anajuatunavyohaingaika, ameunga mkono, achana na hao watu,mtu wa Dar es Salaam na dhahabu wapi na wapi? Mnyikaanamiliki mtambo wa kujengea nyumba, hakuna kitu, hawawanatusumbua…

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,kuhusu utaratibu.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Watuache,tumemwamini Mheshimiwa Rais afanye kazi

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa WaziriMuhongo...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Musukuma, MheshimiwaWaitara kuhusu utaratibu kanuni?

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru natumia Kanuni ya 68(7) lakini pia isomwepamoja na Kanuni ya…

NAIBU SPIKA: Kanuni ya 68(7) inahusu Mwongozo,umeomba Kuhusu Utaratibu, taja Kanuni.

MHE. MWITA M. WAITARA: Kanuni ya 64(1)(a)

(Hapa baadhi ya Wabunge waliongea bila mpangilio)

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru sana. Kaa chini!

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,64(1) (a).

Page 331: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

331

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mnyika wewe ambayeunazijua sana Kanuni, Mbunge mwenzio ametajwa jinaanazungumza kuhusu utaratibu na wewe unasimama kuhusuutaratibu, sasa unampa utaratibu yule ama yule? Sasa kamaunataka kumwambia yeye kakosea Kanuni subiri nimalizanenaye mimi kwa sababu yeye anazungumza na mimi.Mheshimiwa Waitara.

MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru, Kanuni ya 68(1) isomwe sambamba na Kanuniya 64(1) (a) kuhusu utaratibu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwamba MheshimiwaMusukuma amesema hapa kwamba kuna watu wamepokeafedha kule Morena na wanapiga kelele inaangukia kwenyeKanuni ya 64(1) (a) hayo maneno aliyoyasema kama ni ukweliathibitishe na kama si kweli ayafute maana hizo ni tuhuma.Anachafua Bunge hili kwamba kuna watu wamepokearushwa kuja kubadilisha maneno humu ndani.

MBUNGE FULANI: Ataje majina! Taja!

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tusikilizane.Mheshimiwa Waitara amesimama kuhusu utaratibu kwamujibu wa Kanuni ya 68(1) akisema kwamba kanuni ya 64(1)(a) ndiyo anayotumia, kwamba:-

“Mbunge hatatoa ndani ya Bunge taarifa ambazohazina ukweli”

Kanuni ya 64(a) inamtaka Mheshimiwa huyu kwasababu maana yake ni kwamba hizi taarifa hazina ukweli,Mheshimiwa Waitara ungetupeleka kwenye Kanuni ya 63inayohusu kutosema uongo Bungeni. Baada ya kutupelekaKanuni ya 63 ungetimiza masharti yaliyoko hapo ili sasa Kitikiweze kutoa maamuzi. Kwa sababu hiyo Kanuni uliyoisoma,kwamba Mbunge hatasema uongo Bungeni, Kanuni ya 63inataka wewe kwanza ndiye uanze.

Page 332: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

332

Nayasema haya kila wakati wewe ndiyo uoneshe yeyeanadanganya vipi i l i Kiti kitoe maamuzi. Kwa hiyo,Waheshimiwa Wabunge Kanuni hizi tunavyozisoma tuzisomezote kwa pamoja.

Baada ya kusema hayo, tutamalizia na MheshimiwaMusukuma muda wetu unakwisha watu wanakwendakufuturu.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Naibu Spika,nakushukuru. Mheshimiwa Waitara asifikiri mimi ni mwogawa kupokea taarifa, kwa vile umefafanua nilikuwa right tukuwataja, lakini nitawavumilia. Nimwambie tu kwamba,kwa vile yeye ameona nimesema uongo, anawezaakasimama yeye akatuambia kule African dream aliyelipaposho ni nani kwenye kile kikao kilichofanyika? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunaotoka kwenyemachimbo tunaiomba Wizara ya Nishati na Madini, maeneomengi yamemilikiwa na watu wanakaa Dar es Salaam walahawayachimbi. Sisi tunapata shida kila mwaka kuombaWabunge wa Geita na Mungu katupa neema hii.Mheshimiwa Waziri alikuja akatuambia mwezi wa Saba nawa Tisa kuna maeneo yanarudishwa kwa wananchitunayasubiria.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo natakaniwaambie wako wawekezaji wazawa wadogo tuwamewekeza zaidi ya bilioni 30 migodi kama ya GGM kwanini Serikali na Wizara yake isiwakuze watu kama hawa? Ukomgodi wa Busolwa Mining, uko mgodi huko Bunda, kwa ninitusijaribu kuwakuza hawa tukaachana na hawa Wazunguwababaishaji? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Geita siku moja ilikuja ilehelicoptor kuchukua dhahabu. Ilipofika pale wakazidishiatofauti na mkataba ulivyo, akakataa kurusha helicoptor, lakiniTMAA hawa walikuwa wamegonga dhahabu iende kwakiwango kile kile. Kwa hiyo, hawa wanaopiga kelelehawaelewi jamani nchi inaibiwa wajaribu kuja kututembelea

Page 333: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

333

wenzenu tunaachiwa mahandaki. Naliomba Bungetumuachie Rais kazi hii aimalize, potelea mbali hata kamatunashtakiwa kwani Sheria ni ruler au ni glass kwambaikidondoka itavunjika? Tukishtakiwa…

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu utaratibu.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: …Kwani Tundu Lissuasiposhtakiwa ana kazi gani? Wanasheria wetu watafanyakazi tuiachie Serikali na tumuachie Rais, sisi kama Bungetumuunge mkono.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Kuhusu utaratibu.

MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: …na mimi binafsi sijawahikuona Rais wa ajabu kama Tundu Lissu, huyu ndiyo wakwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika,Mheshimiwa Rais hajawahi kuzuia helicoptor, makinikiahayana uhusiano kabisa na ile helicoptor

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabungehamnyanyaswi, kasomeni tu hizi Kanuni, halafu msipendesana kuropoka humu ndani, wananchi wanajua ninyi niviongozi wakubwa sana ndiyo maana mnaitwaWaheshimiwa. Msipende kuropoka na usipende kusema kituambacho huna uhakika nacho, kwa hiyo someni hizi Kanunivizuri ili twende vizuri humu ndani maana tuko wengi sana.

Waheshimiwa Wabunge, baada ya kusema hayo,tumefika mwisho wa michango yetu ya leo. Kuna majina yaWabunge wa CCM.

Mheshimiwa Kubenea; Waheshimiwa WabungeKanuni hizi zinataka kwanza; Kiti kikisimama weweunanyamaza kimya ndiyo Kanuni zetu tulizojitungia hilo ni

Page 334: MKUTANO WA SABA Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 1 ...

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT)

334

moja. La pili; usizungumze wakati mtu aliyeitwa Spika naKanuni hizi, Spika maana yale you speak so you don’t speakwhen I am speaking, alright? (Makofi)

Ndiyo Kanuni zetu tulizozitunga ndivyo zinavyosemakwa hiyo tuzifuate, maana tumejiwekea utaratibu kamatunataka kuzibadilisha tutumie utaratibu wa kawaidatubadilishe. Tuwe tu na heshima ya kawaida kabisa, sisi wotehumu ndani ni viongozi.

Kwa upande wa CCM majina yaliyokuwa yameletwayalikuwa mengi, lakini kwa uwiano tumemaliza vizuri. Kwahiyo, majina watakaochangia kwa upande wa CCM keshoni Mheshimiwa Bahati Ali Abeid, Mheshimiwa VenanceMwamoto, Mheshimiwa Ajali Akbar, Mheshimiwa Dkt. FaustineNdugulile, Mheshimiwa Livingstone Lusinde, MheshimiwaGoodluck Mlinga, Mheshimiwa Hawa Abdulrahman Ghasiana mengine yatakayoongezeka kwa mujibu wa uwiano wauchangiaji wa kesho.

Baada ya kusema hayo Waheshimiwa Wabungenaahirisha shughuli za Bunge mpaka kesho terehe 2Juni, 2017asubuhi saa tatu kamili.

(Saa 12.00 Jioni Bunge liliahirishwa mpaka Siku yaIjumaa Tarehe 2 Juni, 2017, Saa Tatu Asubuhi)