Utafiti wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania (THMIS) wa mwaka 2011-12, ulitathmini mikakati ya kuzuia malaria, tiba ya malaria, kiwango cha malaria na upungufu wa damu mwilini. Katika kaya zote nchini Tanzania, 91% zinamiliki angalau chandarua kimoja kilichotiwa dawa. Umiliki wa chandarua chenye dawa ni mdogo zaidi Mkoa wa Mjini Magharibi (67%) na ni mkubwa zaidi katika Mkoa wa Lindi (96%). Kwa nchi nzima, 14% tu ya kaya ndizo zilizokuwa zimepulizia dawa ndani ya nyumba miezi 12 kabla ya utafiti, lakini 87% ya kaya Zanzibar zilikuwa zimepuliziwa dawa miezi 12 kabla ya utafiti. Upungufu wa damu ni dalili kubwa ya malaria. Nchini Tanzania, 6% ya watoto chini ya miaka mitano wana upungufu wa damu kiasi hadi upungufu mkubwa wa damu, ambao ni chini ya haemoglobin 8.0/dl. Kwa ujumla, kiwango cha upungufu wa damu wa wastani hadi mkubwa kinapungua sambamba na kuongezeka kwa umri. Watoto na wajawazito ndio waathirika wakubwa wa malaria. Mwaka 2011-12, 72% ya watoto chini ya miaka mitano na 75% ya wajawazito walilala kwenye chandarua chenye dawa usiku wa kuamkia siku ya utafiti. Matumizi ya chandarua kwa wanakaya, watoto chini ya miaka mitano na wajawazito yameongezeka kwa kiasi kikubwa tangu mwaka 2004-05. Kaya 9 kati ya 10 zina angalau chandarua kimoja kilichowekwa dawa. Robo-tatu ya wakazi katika kaya wangeweza kulala kwenye chandarua chenye dawa ikiwa kila chandarua kimoja chenye dawa katika kaya kingetumiwa na watu wawili. Kwa ujumla, 68% ya watu katika kaya walilala katika chandarua chenye dawa usiku wa kuamkia siku ya utafiti. Nchini Tanzania, 9% ya watoto chini ya miaka mitano walikutwa na malaria walipofanyiwa kipimo cha papo kwa hapo (Rapid Diagnostic Test - RDT). Maambukizi ya malaria yanaongezeka kadri umri unavyoongezeka. Umiliki, Upatikanaji na Utumiaji wa Chandarua chenye Dawa 75 Wenye angalau chandarua 1 chenye dawa Waliokuwa wamelala katika chandarua chenye dawa 91 Asilimia ya: 56 68 Wenye vyandarua vyenye dawa vya kutosha kwa kaya nzima* Wanaotumia chandarua chenye dawa katika kaya* *Kwa makadirio ya chandarua kimoja kwa watu 2 Kaya Wanakaya Umiliki wa Chandarua Kilichotiwa Dawa na Upuliziaji Dawa 92 14 91 Kaya zenye angalau chandarua kimoja chenye dawa Kaya zilizopulizia dawa ndani angalau miezi 12 iliyopita Kaya zenye angalau chandarua 1 chenye dawa na/au zilizopuliziwa dawa angalau miezi 12 iliyopita Asilimia ya: Kiwango cha Upungufu wa Wastani hadi Mkubwa wa Damu kwa Watoto 9 7 9 7 6 Umri kwa miezi Asilimia ya watoto wa umri wa miezi 6-59 wenye upungufu wa damu mwilini wa kiwango cha wastani hadi wa kiwango cha juu (haemoglobin <8.0 g/dl) 6-8 9-11 12-17 18-23 24-35 36-47 48-59 4 3 Jumla 6-59 6 Zaidi ya 90% ya wanawake na wanaume wa miaka 15- 49 wanafahamu kwamba kuna njia za kujikinga dhidi ya malaria. Njia iliyotajwa na watu wengi ya kuepuka malaria ni kulala kwenye chandarua. Mwenendo wa Utumiaji wa Chandarua Chenye Dawa 15 20 16 27 Wanakaya wote Asilimia ya waliolala kwenye chandarua chenye dawa usiku wa kuamkia siku ya utafiti 45 68 57 75 Watoto chini ya miaka 5 2010 TDHS 2011-12 THMIS 2007-08 THMIS 2004-05 TDHS Wajawazito 15-49 16 26 64 72 Malaria kwa Watoto 4 5 6 9 10 Umri kwa miezi Asilimia ya watoto wenye miezi 6-59 waliopimwa na kukutwa na malaria kwa kipimo cha papo kwa hapo (RDT) 6-8 9-11 12-17 18-23 24-35 36-47 48-59 11 12 Jumla 6-59 9 Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania 2011-2012 Malaria kwa Watoto (kwa Mikoa) Asilimia ya watoto wenye miezi 6-59 walioonekana kuwa na malaria baada ya kufanyiwa kipimo cha papo kwa hapo (RDT). Tanzania 9% Unguja <1% Kagera 8% Mara 25% Simiyu 3% Mwanza 19% Geita 32% Shinyanga 7% Tabora 9% Kigoma 26% Katavi 5% Rukwa 5% Mbeya 1% Singida <1% Dodoma 3% Manyara 1% Arusha <1% Kilimanjaro <1% Tanga 6% Morogoro 13% Pwani 10% Iringa <1% Njombe 2% Lindi 26% Ruvuma 12% Mtwara 17% Dar es Salaam 4% Pemba <1% Kiwango cha malaria kinatofautiana sana baina ya mikoa. Kiwango cha malaria kiko juu zaidi katika mikoa ya Geita, Kigoma na Lindi.