MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 1 MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI WA ARDHINI (Na 3 YA 2019) ________ KANUNI _______ MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (KANUNI ZA TOZO), 2019 SEHEMU YA KWANZA VIFUNGU VYA AWALI 1. Jina. 2. Matumizi. 3. Tafsiri. SEHEMU YA PILI HUDUMA ZINAZODHIBITIWA 4. Huduma zilizo chini ya kanuni za tozo. SEHEMU YA TATU KIBALI CHA TOZO KWA NJIA YA USHINDANI 5. Tozo kwa njia y ushindani. 6. Kibali ha tozo kwa njia ya ushindani. 7. ukomo. SEHEMU YA NNE MAOMBI NA MAPITIO YA TOZO 8. Maombi ya tozo. 9. Maombi ya mapitio ya tozo. 10. Uwasilishaji wa mlaji. 11. Kutoa Maombi. 12. Uwajibikaji. 13. Mamlaka kuanzisha mapitio ya tozo. SEHEMU YA TANO MAAMUZI JUU YA TOZO 14. Muongozo wa maamuzi ya tozo. 15. Uamuzi wa tozo. SEHEMU YA SITA MAKOSA NA ADHABU 16. Makosa. 17. Vifungu vya ujumla. 18. Nguvu ya kufifisha adhabu. SEHEMU YA SABA VIFUNGU VYA UJUMLA 19. Taarifa juu ya tozo. 20. Chapisho la tozo zilizoidhinishwa. 21. Onyesho la tozo zilizoidhinishwa. 22. Kitabu cha tozo na majedwali ya viwango. 23. Utolewaji wa risiti kwa huduma iliyotolewa.
14
Embed
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI...MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO) 3 katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au kupotea (iliyofikiwa
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
1
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI WA ARDHINI
(Na 3 YA 2019)
________
KANUNI
_______
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (KANUNI ZA TOZO), 2019
SEHEMU YA KWANZA
VIFUNGU VYA AWALI 1. Jina.
2. Matumizi.
3. Tafsiri.
SEHEMU YA PILI
HUDUMA ZINAZODHIBITIWA 4. Huduma zilizo chini ya kanuni za tozo.
SEHEMU YA TATU
KIBALI CHA TOZO KWA NJIA YA USHINDANI
5. Tozo kwa njia y ushindani.
6. Kibali ha tozo kwa njia ya ushindani.
7. ukomo.
SEHEMU YA NNE
MAOMBI NA MAPITIO YA TOZO 8. Maombi ya tozo.
9. Maombi ya mapitio ya tozo.
10. Uwasilishaji wa mlaji.
11. Kutoa Maombi.
12. Uwajibikaji.
13. Mamlaka kuanzisha mapitio ya tozo.
SEHEMU YA TANO
MAAMUZI JUU YA TOZO 14. Muongozo wa maamuzi ya tozo.
15. Uamuzi wa tozo.
SEHEMU YA SITA
MAKOSA NA ADHABU 16. Makosa.
17. Vifungu vya ujumla.
18. Nguvu ya kufifisha adhabu.
SEHEMU YA SABA
VIFUNGU VYA UJUMLA
19. Taarifa juu ya tozo.
20. Chapisho la tozo zilizoidhinishwa.
21. Onyesho la tozo zilizoidhinishwa.
22. Kitabu cha tozo na majedwali ya viwango.
23. Utolewaji wa risiti kwa huduma iliyotolewa.
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
2
24. Mpango wa punguzo la tozo.
25. Uzuizi wa tozo.
26. Mapitio ya maamuzi ya Mamlaka.
27. rufaa.
28. [imefutwa]
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI
(Na. 3 YA MWAKA 2019)
________
KANUNI
_______
(Zimetengenezwa chini ya kifungu cha 45)
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (KANUNI ZA TOZO), 2019
PART I
PRELIMINARY PROVISIONS Jina 1. kanuni hii itaitwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (kanuni
za Tozo) , 2019.
Matumizi 2. Kanuni hizi zitatumika kwa watoa huduma wa huduma
zinazodhibitiwa.
Tafsiri 3. katika kanuni hizi isipokuwa muktadha unapoonyesha
vinginevyo: Act No. 3 of 2019 “Sheria” maana yake “sheria ya udhibiti wa usafiri ardhini”; “Mamlaka” maana yake “ Mamlaka ya udhibiti usafiri wa Ardhini
iliyoanzishwa na Sheria ya udhibiti usafiri wa Ardhini; “Mlaji” maana yeke ni “mtu mtumiaji wa huduma za usafiria ardhini”; “Mpango wa punguzo” maana yake punguzo ya tozo kwa kufuata
mfumo; “mtoaji mkubwa wa huduma” maana yake ni mtoa huduma ambaye
anafanya peke yake mwenye kuweza kuleta faida au kupunguza
ushindani katika soko katika kipindi husika na mwenye umiliki wa hisa
zinazozidi asilimia 35 “watoa huduma watarajiwa” maana yake ni mtu au kampuni yenye nia ya
kutoa huduma zinazodhibitiwa “mwanafunzi” maana yake ni mwanafunzi wa shule ya Awali, msingi au
sekondari akiwa amevalia sare ya shule au kabeba kadi ya utambulisho
ya shule; “Mlaji aliesajiliwa” inajumuisha baraza la Ushauri la Mlaji la au Mlaji
aliesajiwa na baraza na walaji; “jedwali la viwango” maana yake ni ratiba ya tozo zilizoidhinishwa
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
3
katika muundo wa jedwali “viwango vya marejesho” maana yake uwiano wa fedha iliyoingizwa au
kupotea (iliyofikiwa au isiyofikiwa) katika uwekezaji, dhidi ya kiasi cha
pesa kilichowekezwa katika muda; “huduma zinazodhibitiwa” maana yake huduma zozote zinazotolewa
ukijumuisha huduma zote ambazo Mamlaka imezidhihirisha kuwa ni
huduma chini ya Sheria hii; “sekta inayodhibitiwa” maana yake usafiri wa ardhi, usafiri reli, usafiri
wa umma kwa njia ya barabara, biashara chini ya ardhi and usafirishaji
wa njia ya kebo; “mtoa huduma” maana yake mtu au chombo kilichosajiliwa na kupewa
leseni ya kutoa au kujihusisha na huduma zinazodhibitiwa; “usafiri nchi kavu” unajumuisha usafiri wa reli, barabara na usafiri kwa
njia ya waya; “tozo” maana yake malipo yanayotozwa na mtoa huduma kwa hudum
anazozitoa “kitabu cha tozo” maana yake kitabu kilichoandaliwa na mtoaji wa
huduma akionyesha tozo zilizoidhinishwa; “Kitengo cha usafirishaji” maana yake ni behewa la abiria na gari, basi,
lori, pikipiki ya magurudumu mawili au matatu.
SEHEMU YA PILI
HUDUMA ZINAZODHIBITIWA Huduma zilizo
chini ya kanuni
hizi za tozo
4.-(1) mtoa huduma hatatakiwa kuweka au kudai tozo ambazo
hazikuidhinishwa na Mamlaka .
(2) Mamlaka itadhibiti tozo katika huduma zifuatazo: (a) Usafirishaji wa abiria kwa njia ya Reli;
(b) Usafirishajiwa mizigo kwa njia ya Reli;
(c) Usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara;
(d) Usafirishajiwa mizigo kwa njia ya Barabara na;
(e) Huduma yoyote itakayotangazwa na Mamlaka kuwa ni Huduma
inayodhibitiwa.
(3) Bila ya kuathiri vifungu (1) na (2) vya kanuni ya nne,
Mamlaka haitadhibiti tozo pale itakapodhihirika uwepo wa wa ushindani
katika huduma zinazodhibitiwa.
SEHEMU YA TATU
IDHINI YATOZO KUPITIA NJIA YA USHINDANI Tozo kupitia njia
ya ushindani 5.-(1) Tozo itakayopatikana kwa njia ya ushindani baina pande
nyingine tofauti na Mamlaka, katika huduma inayodhibitiwa, itahesabiwa
kama tozo iliyopitishwa na Mamlaka kwa ajili ya mkataba wa Huduma (2) Kwa kuzingatia kanuni ndogo (1), tozo itakubalika kuwa ni
tozo iliyopatikana kwa njia ya ushindani kama;-
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
4
(a) Upande wenye nia ya kujihusisha na utoaji huduma, utatakiwa
kuwalisisha kwa Mamlaka nyaraka za zabuni kwa ajili ya kupata
idhini kabla ya kualika wazabuni;
(b) kabla ya kukabidhi zabuni iliyofanikiwa, chombo cha ununuzi
kinawasilisha mkataba uliopendekezwa kwa mtoaji wa huduma
anayetarajiwa kwa Mamlaka kwa lengo la kujiridhisha kama
muongozo wa Mamlaka ulifuatwa ipasavyo
(c) mkataba wa mtoa huduma mtarajiwa utatakiwa kuonyesha;-
(i) mchakato wa udhibiti wa mapitio ya tozo kama
ulivyoonyeshwa katika kanuni hizi itakapotokea
mabadiliko ya tozo katika kipindi cha mkataba wa
utoaji huduma;
(ii) vigezo vya utendaji ambavyo vinaendana na tozo
iliyopendekezwa; na
(iii)Haja ya mtoa huduma kufuata mahitaji mengine ya
kisheria.
Idhini ya tozo
iliyopatikana kwa
njia ya ushindani
6.-(1) Pale ambapo Mamlaka itaona njia ya ushindani ndio bora
zaidi katika kupata mtoa huduma wahuduma zinazodhibitiwa, Mamlaka
itamtaka Wakala kuanzisha hatua za zabuni na bei ya zabuni iliyoshinda
itahesabika kama tozo iliyoidhinishwa. (2) mtoa huduma mtarajiwa atatakiwa kufuata - (a) Mchakato wa udhibiti wa mapitio ya tozo inapotokea
mabadiliko katika kipindi cha mkataba wa huduma; (b) vigezo vya utendaji ambavyo vinaendana na tozo
iliyopendekezwa; na (c) Mahitaji mengine yoyote ya kisheria.
Limitations 7. Tozo iliyoidhinishwa chini ya kanuni ya 5 na 6 cha kanuni hizi,
itatumika kwa mkataba husika pekee.
SEHEMU YA NNE
MAOMBI NA MAPITIO YA TOZO Maombi ya
Tozo 8.-(1) Mtu yeyote mwenye nia ya kutoa huduma zinazodhibitiwa
atatakiwa kuwasilisha maombi kwa mamlaka kwa ajili ya kufanyiwa
Tathmini na kutolewa vibali. (2)Maombi y tozo yatafanyika kwa kujaza fomu kama
iliyoonyeshwa kwenye jedwali la kwanza la kanuni hizi na
itaambatishwa na nyaraka zifuzatazo- (a) Leseni halali ya mwendeshaji au udhibitisho wa
maombi ya; (b) Taarifa za karibuni za kibiashara za benki
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
5
(c) Mpango wa biashara;
(d) Tozo inayopendekezwa; (e) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo
iliyopendekezwa;
(f) Tozo maalum inayopendekezwa kwa wanafunzi; na (g) Nyaraka nyingine yoyote itayohitajika na Mamlaka
kuambatanishwa.
Maombi ya
mapitio ya Tozo 9.-(1) mtoa huduma anayeomba mapitio ya tozo, atawasilisha
maombi yake kwa Mamlaka na atajaza fomu inayopatikana katika
jedwali la pili katika kanuni hizi ikiambatanishwa na;- (a) Leseni halali ya mwendeshaji;
(b) Maendekezo ya tozo; (c) Sababu na haki ya kufanya mapitio ya tozo pamoja na
faida kwa mlaji baada ya mapitio hayo;
(d) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo
iliyopendekezwa; (e) hesabu zilizokaguliwa kwa miaka tatu mfululizo au
pungufu kulingana na umri wa taasisi; (f) ripoti ya utendaji ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa
kina wa kiufundi na uchambuzi wa kifedha kwa miaka
mitano iliyopita au pungufu kulingana na umri wa
taasisi hicho; na; (g) nyaraka nyingine yoyote itakayohitajika na Mamlaka. (2) Mtoa huduma atatakiwa kuwasilisha maombi ya marejeo ya
tozo si pungufu ya miaka mitatu tangu mapitio ya mwisho kufanyika. (3) Bila ya kuathiri kifungu kidogo cha pili, mapitio ya huduma
za usafirishaji wa abiria yatafanyika kila mwaka kwa kuzingatia mapato
ya uwekezaji yanaposhuka zaidi ya asilimia 10% au kuongezeka zaidi ya
asilimia 25%; (4) Bila kuathiri maombi vifungu 8 na 9 vya kanuni, mtoa
huduma ataweza kuwasilisha maombi ya tozo kwa niaba ya watoa
huduma wengine wanaofanana.
Wasilisho la
mlaji 10.-(1) mlaji aliesajiliwa ataweza kuwasilisha maombi ya mapitio
kwa Mamlaka. (2) bila ya kuathiri kifungu kidogo (1), mlaji wa huduma
zinazodhibitiwa ataweza kuanzisha mapitio ya tozo kwa kufanya
wasilisho kwa Mamlaka. (3) wasilisho lilitengenezwa kwa kufuata vifungu vidogo (1) na
(2) vya kanuni, vitatakiwa kuambatishwa na; (a) tozo inayopendekezwa;
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
6
(b) sababu na haki za mapitio na namna mlaji atanufaika
na mapitio;
(c) (d) Karatasi ya mahesabu yaliyotolewa kufikia tozo
iliyopendekezwa; na (d) Nyaraka nyingine yoyote itakayohitajika na mamlaka.
(4)Mara baaada ya kupokea risiti ya wasilisho, Mamlaka itafanyia
uchunguzi wasilisho ili kutambua uhitaji wa kufanya mapitio ya tozo.. (5) pale ambapo wasilisho lililowasilishwa halionyeshi haki ya
mapitio ya tozo, Mamlaka itatakiwa ndani ya siku 14 tangu kupokea kwa
wasilisho, kumtaarifu mlaji ipasavyo huku ikionyesha sababu za kwanini
mchakato wa mapitio ya tozo haujaendelea. Kuondoa
Maombi 11. Muombaji wa tozo au mapitio ya tozo ataweza kuondoa
Maombi yake wakati wowowte kabla ya Maamuzi ya tozo hayajafanyika. Uwajibikaji 12. Mtoa huduma atatakiwa kuheshimu maamuzi yaliyotolewa na
Mamlaka juu ya pendekezo la tozo. Uanzilishi wa
Mamlaka kwenye
mapitio ya tozo
13.- (1) Mamlaka itaweza kwa kuamua yenyewe, kufanya
uchunguzi wa mapitio ya tozo kwa mtoa huduma yoyote itakapotokea -
(a) Kuna mabadiliko katika mazingira yanayohitaji marekebisho
ya tozo; (b) Tozo inayodaiwa na mtoa huduma haikuidhinishwa na
Mamlaka; (c) Makadirio yaliyotumika kufanya mahesabu ya tozo
yamebadilika kwa kiasi kikubwa; (d) Mtoa huduma kashindwa kuwasilisha maombi ya maitio ya
tozo ndani ya muda ulioelekezwa. (2) Mamlaka katika kutumia nguvu yake ya kufanya mapitio,
itaweza kumtaka mtoa huduma kuwasilisha taarifa fulani na kwa muda
elekezi. (4) ikiwa mtoa huduma ameshindwa, bila sababu za msingi,
kuwasilisha taarifa zilizohitajika ndani ya muda ulioainishwa, Mamlaka
itasitisha mchakato wa mapitio ya tozo.
SEHEMU YA TANO
MAAMUZI YA TOZO Mchakato wa
maamuzi juu ya
tozo
14. Chini ya kifungu cha 19 cha Sheria, pamoja na mambo
mengine yoyote ambayo Mamlaka itaona yanafaa, mamlaka itatakiwa
ndani ya siku 90 tangu kupokelewa kwa maombi ya tozo, kupitia au
kuwasilisha, kufanya mapitio na kutoa Uamuzi juu ya tozo. (1) Mamlaka itatakiwa kutoa taarifa kwa umma juu ya maombi ya
tozo kupitia kwenye gazeti linalosomwa sana kuita uwasilisho wa wadau
kwa njia ya maandishi, ndani ya siku 14 tangu kutolewa kwa taarifa. (2) Mamlaka itakapojiridhisha kwamba taarifa husika
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
7
zimetolewa, itatakiwa- (a) Kuidhinisha au kutofautiana maombi ya tozo na
kuambatishwa masharti ndani yake; au (b) Kukataa maombi ya tozo na kutoa Sababu ya kukataa maombi
hayo. Uamuzi wa tozo 15. Mamlaka itatakiwa kufanya maamuzi ya tozo kwa kuzingatia
yafuatayo; (a) Gharama za ufanisi katika utengenezaji, uzalishaji na utoaji
huduma,; (b) Matamanio ya kuchochea viwango vya ushindani na kuvutia
soko; (c) Viwango vyovyote husika, pamoja na vile vya kimataifa vya
bei,gharama, na faida kwenye mali katika sekta
zinazolinganishwa, (d) Athari za kiuchumi za maamuzi; (e) Maslahi ya walaji na wawekezaji; (f) Marejesho ya mali katika sekta zinazodhibitiwa; (g) Uhitaji wa kuongeza ufanisi katika matumizi ya sekta
zinazodhibitiwa; (h) Uhitaji wa kua na bei isiyobadilika badilika; (i) Sababu nyingine yoyote Mamlaka itaona inafaa.
SEHEMU YA SITA
MAKOSA NA ADHABU Makosa 16.-(1) Mtu yeyote ambaye - (a) Atashindwa kutoa tiketi au risiti kwa huduma husika; (b) Atatumia tozo ambazo hazikupitishwa na Mamlaka; (c) Atashindwa kuonyesha tozo kwa namna ambavyo Mamlaka
imeelekeza; (d) Atashindwa kuwasilisha kitabu cha tozo, jedwali la viwango
kwa Mamlaka; (e) Atawasilisha kwa Mamlaka nyaraka, taarifa, maelezo ambayo
ni ya uongo au si sahihi; au; (f) Atamzuia au weka vizuizi kwa afisa wa Mamlaka au Inspekta
katika kufanya majukumu yaliyo chini ya kanuni hizi; Atakua ametenda kosa na atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi za
kitanzania Milioni moja na isiyozidi shilingi milioni tatu, au kifungo
kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.,
Isipokuwa,kosa litakalofanywa na kampuni, litawajibika kulipa
faini isiyozidi shilingi Milioni Tano. (2) mtu yeyote atakayeshindwa kutoa taarifa pale atakapohitajika na
Mamlaka kutoa taarifa, atakua ametenda kosa na mara baada ya kukutwa
na hatia, atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi za kitanzania Laki tatu
au kifungo kisichozidi kipindi cha miezi kumi na tano au vyote viwili
kwa pamoja,
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
8
isipokuwa, kosa litakapofanywa na kampuni, adhabu yake ni faini
isiyozidi kiasi cha shilingi laki tano Adhabu z
ujumla 17. Mtu yeyote atakayekiuka vifungu vya kanuni hizi kwa
makosa ambayo adhabu zake hazijafafanuliwa, ataadhibiwa kwa kulipa
faini isiyozidi kiasi cha shilingi laki tano au faini kama zilivyoelekezwa
katika sheria za sekta husika au sheria nyingine, yenye adhabu kubwa
zaidi. Nguvu ya
kufifisha
Adhabu
18.-(1) bila ya kuathiri vifungu vya kanuni hii vinavyohusiana na
adhabu, pale mtu atakapotenda kosa chini ya kanuni hizi, Mamlaka
itakua na uwezo muda wowote kabla ya kuanza kusikilizwa kwa hili
shauri, wa kufifisha adhabu na kuagiza mtu huyo kulipa kiasi cha pesa si
pungufu ya nusu ya kiwango halisi cha faini ya kosa lenyewe ambacho
mtu huyu angetakiwa kulipa kama angekutwa na hatia ya kosa: Mamlaka itakua na nguvu ya kufifisha adhabu pale tu ambapo
mtu alietenda kosa, amekubali na kuomba kwa maandishi kosa lake
kufifishwa. (2) pale ambapo Mamlaka imefifisha adhabu katika kanuni hizi,
agizo lililotajwa katika kanuni (1): (a) Litatakiwa kuwekwa katika maandishi na litatakiwa
kuambatishwa na maandishi ya kukiri kwa kosa pamoja na
ombi kufifishiwa adhabu kulingana na kifungu cha kanuni
husika na, nakala ya amri hiyo atapatiwa mtenda kosa kama
akihitaji; (b) itabainisha kosa lililofanywa, jumla ya pesa iliyoamuru
kulipwa na tarehe ambayo malipo yatafanyika; na (c) Inaweza kutekelezwa kama amri ya Mahakama kwa malipo
ya kiasi kilichoainishwa katika agizo.
SEHEMU YA SABA
VIFUNGU VYA UJUMLA Taarifa kuhusu
Tozo 19. mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa sahihi na ya
kujitosheleza juu ya tozo zilizoidhinishwa kwa walaji. Uchapishaji wa
tozo
zilizoidhinishwa
20. mtoa huduma kabla ya kuanza kutumia tozo zilizopitishwa na
mamlaka atatakiwa, kutoa notisi ya siku 14 kwa umma juu ya tozo mpya
kupitia taarifa itakayotakiwa sambazwa kwa sehemu pana kupitia
magazeti, redio na televisheni. Onyesho la tozo
iliyoidhinishwa 21.(1) mtoa huduma atatakiwa kuweka tozo katika sehemu
zinazooneka kama ilivyo orodheshwa katika kanuni. - (a) Katika hatua ya mauzo; (b) Katika vituo vya huduma kwa walaji; (c) Vitengo husika vya usafirishaji; na (d) Kwenye bodi za matangazo za mtoa huduma au tovuti
MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (TOZO)
9
inayopatikana. Vitabu vya tozo
na jedwali la
viwango
22.-(1) mtoa huduma atatakiwa kuandaa kitabu cha mapitio ya
tozo au jedwali la viwango kutegemea na kesi iliyopo wakati huo,
kujumuisha tozo iliyoidhinishwa na kuwasilisha nakala kwa mamlaka. (2) mtoa huduma atatakiwa kuwasilisha andalio au mapitio ya
kitabu cha tozo au jedwali la viwango, kulingana na hali ya wakati
huo,kwa Mamlaka ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe ya kutolewa kwa
idhini ya tozo ya Mamlaka. Utoaji wa tiketi
kwa huduma
iliyotolewa
23.-(1) mtoa huduma atatakiwa kutoa risiti kwa Mlaji kama
ushahidi wa malipo yaliyofanyika kwa huduma iliyotolewa.