-
Waliomeremeta
Toleo la 84, September-Oktoba, 2010
Kukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari na kuhakikishaviwango vya juu
kabisa vya weledi na uwajibikaji
Jarida la Baraza la Habari TanzaniaToleo la 156, Agosti,
2020ISSN 0856-874X
TBC yatimuliwa mkutano wa Chadema
TEF yahimiza waandishi walindwe
EJAT kuwa Tanga
Uk 7 Uk 11Uk 9
Kuripoti uchaguziClouds yawa majeruhi wa kwanza
Kuripoti uchaguzi:Clouds yawa majeruhi wa kwanza
-
Waliomeremeta
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
BODI YA UHARIRI:Kajubi Mukajanga Katibu Mtendaji – MCTDavid
Mbulumi Meneja ProgramuHamis Mzee Mhariri
MAWASILIANOKwa Maoni na Malalamiko:Katibu MtendajiBaraza la
Habari Tanzani (MCT)S.L.P. 10160, Dar es SalaamSimu: +255 22
27775728, 22 2771947Simu ya Kiganjani: +255 784 314880Fax: + +255
22 2700370Baruapepe: [email protected]: www.mct.or.tzFacebook:-
www.facebook.com/mediacounciltanzania Twiter:-
www.twitter.com/mctanzania
2
TAHARIRIJarida la Baraza la Habari Tanzania
Usimamishaji vyombo vya habari wakati wa uchaguzi uachweKampeni
za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 zimeanza kwa matatizo. Baada ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutahadharisha vyombo vya habari
kuwa waangalifu katika kuripoti uchaguzi, chombo kimoja kikubwa cha
habari kimekuwa muathirika wa kwanza.
Bila shaka kwa kufuatilia onyo lililotolewa na NEC, Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) imeifungia kwa wiki moja Clouds kwa
kukiuka kanuni kwa kutangaza Wabunge waliopita bila kupingwa.
Kosa la Clouds ni kukiuka kanuni ya Sheria ya utangazaji ya
vyama vya siasa ya mwaka 2015 katika vipindi vyao vya 360 na Power
na kwamba uamuzi wa TCRA umetolewa baada ya Redio na Runinga ya
Clouds kutangaza matokeo ya mchakato wa uteuzi katika baadhi ya
majimbo bila kuidhinishwa na NEC.
Ingawa vilikuwepo vyombo vingine hasa magazeti yaliyochapisha
habari hiyo kabla kukubaliwa na NEC, havikuonywa na mamlaka ya
udhibiti.
Wakati Clouds wakitekeleza amri hiyo, NEC imetangaza siku moja
baadaye majina ya wabunge waliopita bila kupingwa.
Tukubali kwamba Clouds Media walikosea, lakini kukifungia kituo
kwa wiki bila kujali athari za kiuchumi na kijamii sio sahihi na
haki.
Ni muhimu izingatiwe kuwa kituo hicho licha kuwa na mikataba ya
utangazaji, wananchi wengi wanaokipenda wamekoseshwa kupata habari,
elimu na burudani kufuatia hatua hiyo ya kukifungia.
Pia kabla hatua kali kama hiyo kuchukuliwa, wenye mamlaka lazima
wafikirie suala la kuishi kwa maana ya kipato cha watu
wanaofanyakazi kwenye kituo hicho.
Kwa hiyo ni muhimu kwa mamlaka za udhibiti kutambua kuwa katika
kipindi cha uchaguzi kwa kuwa wananchi wanategemewa kufanya maamuzi
makini, majukwaa mengi ya taarifa kwa maana ya vyombo vya habari
yanahitajika.
Kwa kupunguza vyombo vya habari, ni ushahidi wa wazi kwamba
mamlaka za udhibiti hazioni umuhimu wa kuwa na vyombo vingi
vikifanyakazi.
Ni muhimu badala ya kuamuru ufungaji mamlaka za udhibiti lazima
zizingatie kuchukua hatua ambazo zitahimiza uboreshaji wa mwenendo
na utendaji wa vyombo vya habari. Kufungia kuwe mambo yaliyopitwa
na historia.
MCT, MSHINDI WA TUZO YA IPI 2003
FREE MEDIA PIONEER
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
-
Waliomeremeta
Toleo la 84, September-Oktoba, 2010
Na Mwandishi wa Barazani
Katika siku ya pili ya kuanza kampeni za ucha-guzi mkuu wa mwaka
huu Agosti 27, 2020, kituo cha runinga na radio cha Clouds Media
kimeamriwa
Amri hiyo inafuatia onyo lililotolewa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutangaza na
kuchapisha wagombea waliopita bila kupingwa.
Wagombea zaidi ya 15 akiwemo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walisemekana wameshinda katika
majimbo yao kwa staili hiyo.
Ripoti hizo kuhusu walioshinda bila kupingwa zimetokea wakati
kuna madai kutoka wagombea wa upinzani ambao wanadai walizuiwa na
wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo kuwa fomu zao zina
makosa.
Kumekuwepo taarifa kwamba walionyimwa haki yao ya kuwa wagombea
wamepinga maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi na kukata rufani
NEC.
Kwa vyombo vya habari vimetumia mazoea na uzoefu kwamba
inapotokea kuwa wagombea wengine wanapokosa sifa, mgombea aliyebaki
anakuwa amepita bila kupingwa.
Safari hii NEC inaviambia vyombo vya habari kwamba yenyewe ndiyo
inayohusika
3
Habari
Toleo la 156, Agosti, 2020
Clouds marejuhi wa kwanza wa kuripoti uchaguzi
Endelea Ukurasa wa 4
Wananchi wakiwe kwenye mkutano wa hadhara.
kusitisha matangazo kwa kuki-uka kanuni.
-
Waliomeremeta
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
4
Habari
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
kutangaza taarifa za washindi. Hata hivyo Clouds
inaadhibiwa wakati vyombo vingine kama gazeti la chama Uhuru na
moja ya magazeti ya kimkakati Jamvi la habari zilichapisha habari
hiyo katika kurasa zao za kwanza hali inayoonyesha kutumika viwango
tofauti katika kuadhibu.
Akitangaza adhabu kwa Clouds kutoka Agosti 28 had Septemba 3,
2020, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano
Tanzankia (TCRA) ,James Kilaba alizungumzia ukiukwaji wa kanuni za
utangazaji.
Agosti 26 , 2020, alisema , Clouds ilitangaza taarifa kuhusu
wagombea walioshinda katika kipindi cha runinga 360 na Power
Breakfast cha redio.
Wenye uzoefu na shughuli za vyombo vya habari wameeleza wasiwasi
kwamba ikiwa katika siku ya kwanza ya mchakato wa uchaguzi hatua
kali zinachukuliwa dhidi ya vyombo vya habari, vyombo vingapi
vitafungiwa ifikapo siku ya kupiga kura Oktoba 28, 2020?
“Hali ni mbaya na hakuna hata chombo kimoja cha habari kiko
salama”, amesema mmoja wa watu hao akiongeza kuwa vyombo vya habari
sasa vinapita katika
ncha kali ya kisu. Mzoefu mwingine alisema
kuwa vyombo vya habari vimegeuzwa kuwa gunia la mazoezi la
mabondia, vikipigwa kuwa upande.
Wakati Clouds imesimamishwa kwa wiki, Runinga ya mtandaoni ya
Kwanza imesimamishwa kwa miezi 11 kwa kutangaza taarifa kuhusu
virusi vya corona ambayo wenye mamlaka hawakupendezwa nayo. Gazeti
la Tanzania Daima limefutiwa leseni yake na jaribio la kutaka
kupata leseni nyingine inasuasua huku wafanyakazi wake wakiishi
bila kipato.
Clouds marejuhi wa kwanza wa kuripoti uchaguziInatoka Ukurasa wa
3
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania James
Kilaba.
-
Waliomeremeta
Toleo la 84, September-Oktoba, 2010
Na Mwandishi wa Barazani
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limeorodhesha maswali kadhaa
yanayohusu ushiriki wa waandishi wa habari katika uchaguzi katika
siasa za ushindani.
Hii inafuatia kauli ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari,
Kajubi Mukajanga, kuwa wanahabari watakaoshiriki katika uchaguzi
mkuu wasirejee kwenye vyumba vya habari.
Taarifa hiyo ilipokewa kwa mawazo mchanganyiko huku baadhi ya
waandishi na wadau wakisema kuwa hiyo ni kukiuka haki ya kikatiba
ya watu.
Baraza pamoja na maswali hayo limetoa majibu kuhusu nafasi ya
wanahabari katika uchaguzi hasa uchaguzi wa vyama vingi.
Maelezo kamili katika orodha hiyo ya
maswali na majibu kuhusu wanahabari kushiriki katika uchaguzi ni
kama ifuatavyo.
Mwaka huu 2020 ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania. Waandishi wa
habari wana nafasi muhimu sana katika zoezi hili la kidemokrasia.
Wao ni kati ya “watumishi wa umma” walio mstari wa mbele, bila
kujali wameajiriwa katika chombo binafsi, cha serikali, chama, au
hata cha dini.
Ni jukumu lao kuwapasha habari sahihi na za kina Watanzania ili
kuwasaidia katika kufanya maamuzi wanayoona ni sahihi wakati wa
kupiga kura.Wanahabari wanapaswa kufanya kazi kwa uaminifu na
kuaminiwa na wasomaji, watazamaji na wasikilizaji wao. Kwa sababu
hiyo, wanapaswa kuzingatia maadili ya taaluma, lakini pia miiko
inayowakataza kufanya lolote linaloweza kuwaondolea kuaminika na
jamii.
Kwa sababu hiyo, Baraza la Habari Tanzania (MCT) lilichapisha
Mwongozo wa Kuandika Habari za Uchaguzi Tanzania toleo la Pili
lililotolewa Machi 2015.
Hivi karibuni kumekuwa na mjadala katika vyombo vya habari
kuhusu nafasi ya mwandishi na vyombo vya habari wakati wa
uchaguzi.
Mjadala umejikita katika haki za mwanahabari kama raia, lakini
hasa katika urari wa uhuru wa mwanahabari kugombea na kuendelea
kuwa mwanahabari. Pamoja na Mwongozo wa 2015, tunatoa maelezo na
ushauri ufuatao ili kuwasaidia wanahabari na wasimamizi wa vyombo
vya habari wanapokabiliwa na mtanziko unaohitaji kufanyiwa
uamuzi.
Maelezo haya yanatolewa kwa utaratibu wa kujibu maswali ambayo
yamekuwa yakiulizwa zaidi (Frequently Asked Questions – FAQ) mwaka
huu kuhusu wanahabari na vyombo vya habari wakati wa uchaguzi.
Swali: Je ni sahihi kwa mwandishi wa habari kujihusisha na
siasa?Jibu: Siasa ni mfumo unaoongoza maamuzi katika jamii
tunayoishi na siasa inamwathiri kila mtu. Kamusi Kuu ya Kiswahili
iliyo-tolewa na Baraza la Kiswahili la Taifa (2017) inaelezea siasa
kama: a) mfumo wa kiitikadi unaotumiwa na kikundi cha watu au jamii
fulani kuwaendeshea serikali pamoja na shu-ghuli za jamii hiyo;
b) shughuli zinazofanywa na serikali ya nchi fulani;
ch) shughuli zinazolenga kuboresha hadhi ya mtu au kuongeza
uwezo wa kimadaraka ndani ya asasi fulani.
Kwa hiyo sote tunahusika na siasa hata kama hatuko ndani ya
vyama vya siasa
5
Habari
Toleo la 156, Agosti, 2020
Endelea Ukurasa wa 6
Wanahabari na uchaguzi: Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Wanahabari wakiwa kwenye mojawapo ya matukio ya habari.
-
Waliomeremeta
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
6
Habari
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
kuendesha siasa za kishindani ili kutafuta madaraka ya dola. Ni
sahihi na ni haki ya mwanahabari kwa kuwa hii ni haki ya kiraia na
kikatiba. Ni haki yao ya msingi kama walivyo raia wengine hapa
nchini.
Swali: Ikiwa ni hivyo, ina maana gani kusema waandishi wa habari
wanaoji-husisha katika siasa za ushindani wa-ondoke kwenye vyumba
vya habari?
Jibu: Kwanza, ieleweke kuwa mwandishi wa habari kama sehemu ya
jamii ana haki ya kikatiba kuwa mpiga kura na pia ana haki ya
kupigiwa kura. Lakini kwa asili ya kazi yake, anapaswa kuondoka
katika chumba cha habari kwa wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa
kuwa akiamua kuwa mgombea, tayari amechukua upande katika ushindani
wa kisiasa. Ikumbukwe kuwa hivi sasa nchi yetu iko katika mfumo wa
vyama vingi, ambapo vyama mbalimbali vinashindana katika uchaguzi.
Haitaswihi kwa mwandishi asubuhi kupanda jukwaani kupiga salamu za
chama na jioni kuwa katika chumba cha habari kuandika au kuhariri
habari za uchaguzi, au katika studio. Na uchaguzi ndiyo habari
inayotawala katika kipindi hicho chote. Kwa hiyo anapaswa kukaa
kando.
Ni kanuni ile ile inayozuia watumishi wa umma kuwa ofisini
wanapoingia katika uchaguzi. Ni kuepuka mgongano wa maslahi
(conflict of interest). Ni kuhakikisha kuwa habari zinaandikwa na
kuchakatwa bila upendeleo (impartiality).
Swali: Lakini mwandishi mwadilifu anaweza kuhakikisha kuwa
anafanya kazi yake kwa kufuata maadili (ethi-cal) na kutopendelea
(impartial). Kwa nini asiruhusiwe?
Jibu: Bahati mbaya, kanuni ya kuepusha mgongano wa maslahi na
impartiality haitegemei kabisa dhamira njema ya muhusika. Mizania
yake inaegemea kwenye: wenzio watakuonaje (how will your peers
perceive you) na watu watakuonaje (how will the general public
perceive you). Kwa hiyo kama kuna mazingira yoyote yanayoleta
mashaka au kuweza kuleta mashaka, muhusika anapaswa kukaa pembeni.
Mahakimu na majaji wanapojitoa kusikiliza kesi kwa
kuwa kuna shutuma kwamba watapendelea upande fulani, wanajitoa
si kwa kuwa hawana maadili au weledi, au hawajiamini kuwa wanaweza
kufanya kazi yao bila upendeleo. Wanajitoa kwa sababu ya kanuni
hiyo. Kwa hivyo kama kuna mazingira ya kufanya mwandishi atiliwe
shaka kwa kuwa ameshaonyesha yuko upande fulani katika mchakato wa
ushindani wa kisiasa, basi anakaa pembeni ili ashiriki vizuri bila
kumkwaza yeyote.
Swali: Je, suala hili la waandishi kuto-jihusisha na siasa za
ushindani wakiwa ndani ya vyumba vya habari liko kishe-ria?
Jibu: Hapana; sheria zetu za habari
haziongelei suala hili. Kuna makatazo ya kimaadili ambayo pia ni
makatazo ya kisheria, na mengine sio ya kisheria. Makatazo kama
hayo husimamiwa na wasimamizi wa vyombo vya habari wenyewe na/au
vyombo vya kitaaluma, sio sheria au mahakama.
Swali: Ni sababu zipi zinazosababisha mwanahabari akiingia
kwenye siasa za ushindani ajitenge na taaluma, ukilin-
ganisha na taaluma nyingine?Jibu: Ni kwa asili na mahitaji ya
kazi
yake kama ilivyoelezwa hapo juu. Mwanahabari anatoa habari,
uchambuzi, maoni na kuvisambaza kwa jamii. Kukiwa kuna suala
linalohusu mgongano wa maslahi ama uwezekano wa upendeleo anakaa
pembeni. Katika hilo, mhasibu, mhandisi, daktari na wengine wana
mazingira tofauti, japo nao wana mambo yao ambayo yanaweza
kuwasababishia mgongano wa maslahi. Lakini pia utumishi wa umma
unazuia kuingia katika mchakato wa uchaguzi ukiwa ofisini. Jambo
kubwa hapa ni conflict of interest na
impartiality.
Swali: Mbona kuna waandishi wa michezo ambao ni mashabiki wa
timu fulani au waandishi wa bu-rudani ambao ni wapenzi wa wasanii
fulani? Unasemaje kuhusu hao?
Jibu: Kitakuwa kichekesho kulinganisha mapenzi kwa timu ya mpira
au bondia fulani au mwanamuziki fulani na uchaguzi wa viongozi wa
kisiasa. Kila mtu ana kitu fulani anachokipenda, lakini hayo ni
mambo binafsi. Kupigania nafasi ya uongozi wa kisiasa sio jambo
binafsi. Muhimu ni kuzingatia suala la maadili na mgongano wa
maslahi.
Swali: Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanza-nia (MCT),
alikuwa mbunge wa Bunge la Ka-tiba, je hii siyo siasa?
Jibu: Bila shaka ni siasa, tena siasa ya hali ya juu! Mgongano
wa maslahi uko wapi katika kushiriki katika mchakato jumuishi na wa
pamoja wa kuandika katiba kwa ajili ya nchi?
Suala si siasa; na anayesema siasa hazimhusu haelewi sana
asemalo. Siasa zinaathiri maisha ya kila mmoja. Katika ushindani wa
vyama ni muhimu wanaoripoti ushindani huo waonekane kazi yao
inafanywa kwa haki. Lakini pia tukumbuke kuwa siasa ya Bunge la
Katiba haikuwa siasa ya ushindani, ni tofauti sana na hii ya sasa
ya kugombea nafasi mbali mbali ndani ya vyama vya siasa, Katibu
alikwenda kwenye Bunge la Katiba kama mmoja wa wawakilishi wa
tasnia ya habari
Maswali yanayoulizwa mara kwa maraInatoka Ukurasa wa 5
i
WANAHABARI NA
UCHAGUZI – MASWALI
YANAYOULIZWA ZAIDI
Agosti 2020
Endelea Ukurasa wa 8
-
Waliomeremeta
Toleo la 84, September-Oktoba, 2010
Na Mwandishi wa Barazani
Shirika la Utangazaji la Tanza-nia (TBC) liliamriwa kuondoka
kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema . Chadema ilikuwa ikifanya
mkutano
wake wa kwanza wa kampeni uliokuwa ukihutubiwa na mgombea wa
urais kwa tiketi ya chama hicho, Tundu Lissu, Mbagala Jijini Dar es
Salaam na inaelekea TBC ilikuwa ikitoa matangazo yake kwa namna
ambayo haikupendeza chama hicho.
Kulikuwa na madai kuwa badala ya kuonyesha umati wa watu
waliohudhuria mkutano huo, kamera ya TBC ilikuwa ikionyesha watu
wachache waliokuwa wakifika katika eneo la mkutano kabla ya hata
mkutano kuanza.
Pia ilidaiwa shirika hilo la utangazaji halikuwa likimuonyesha
mgombea huyo urais wakati akihutubia katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alizungumzia mgogoro huo
na TBC na kusisitiza kuwa katika mkutano huo waliwataka
waondoke.
Mbowe alisema kuwa uamuzi wa chama hicho ulipokewa vizuri na
wapenda habari kutangazwa kwa haki.
Alisema chama chake kinaamini katika uhuru wa habari na inaafiki
na kuukubali uandishi wa weledi lakini kinapinga muandishi wa
upendeleo.
“ Tunakaribisha chombo chochote cha ambacho kinataka kutangaza
shughuli zetu lakini matangazo yao yawe ya haki na yasiyo na
upendeleo.’
Mbowe alisema TBC inaweza kusamehewa na kukaribishwa Chadema
kama itabadili mwenendo wa kutangaza habari za chama hicho.
7
Habari
Toleo la 156, Agosti, 2020
…TBC yatimuliwa kwenye mkutano wa Chadema
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa
kampeni.
-
Waliomeremeta
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
katika mchakato wa Katiba na si mwanachama wa chama fulani. Ndio
maana hukumuona akipanda jukwaani kunadi sera za chama fulani wala
kuvaa gwanda.
Swali: Kuna vyombo ambavyo vinamilikiwa na vyama vya siasa, hili
limekaaje? Je, vyombo vya habari vinaruhusiwa kuunga mkono
vyama?
Jibu: Ieleweke kwamba si kosa kwa chama cha siasa kuwa na chombo
cha habari. Historia inatuonyesha kuwa mwanzo wa magazeti barani
Ulaya yalianzishwa yakiwa yanashadadia vyama na mielekeo ya
kiitikadi. Kwa hiyo chombo hiki cha habari kiliunga mkono mrengo wa
kushoto, hiki mrengo wa kulia, na kadhalika. Lakini hata chombo cha
habari kisichomilikiwa na chama cha siasa kinaweza kuamua kuunga
mkono sera za chama kimojawapo. Na kwa hakika, chombo cha habari
kinategemewa kutetea maslahi ya jamii kwa jinsi kinavyoona, na
wakati wa uchaguzi jambo hili hujitokeza wazi katika kuunga mkono
sera zinazonadiwa na washindani.
Lakini lazima chombo cha habari kiweke wazi msimamo wake, na
ueleweke wazi bila kificho (declare interest). Lazima
wanaokisikiliza, kukisoma au kukitazama waujue msimamo huu. Hii
itawasaidia kuwa na faida ya ziada wakati wanapotafakari
waliyoyapata toka chombo hicho. Ndiyo maana, mathalani, tunajua
kuwa CNN inaegemea Democratic Party wakati Fox tunajua iko upande
wa Rais Donald Trump na chama chake. Tunajua hili hata pale
tunapochukua remote na kuchagua channel fulani.
Hata hivyo, vyombo vyote vya habari vinahusika kufuata utaratibu
na maadili ya uandishi wa habari. Hata kama mwanahabari yuko kwenye
chombo cha habari cha chama fulani, anatakiwa kutopendelea,
kutompaka mwingine matope lakini pia kufanya uandishi na sio
propaganda au uzushi, ilimradi anufaishe upande huu na kukandamiza
mwingine. Na ni lazima kutenganisha maoni na habari.
Swali: Mwandishi au waandishi ambao wamelikiuka hili wana adhabu
gani?
Jibu: Hili ni suala la mjadala, haliko kwenye sheria. Kama
mlivyosikia kuna Padre wa Kanisa Katoliki amesimamishwa kutokana na
kujihusisha kwake na siasa za ushindani; wao inawezekana wana
sheria za dini zinazowazuia, lakini sisi hatuna sheria. Na hapo
ndipo linakuja suala la vyombo vya habari vyenyewe kujiwekea
utaratibu wa ndani.
Swali: Majuzi MCT mlinukuliwa mkisema wamiliki wa vyombo vya
habari wanapaswa kulitolea miongozo iliyo wazi ndani ya vyumba vya
habari, ni miongozo gani mlikuwa mnailenga hapa?
Jibu: Katika tasnia ya habari, mbali ya Kanuni za Maadili (Code
of Ethics), kuna miongozo inayotuongoza katika utendaji wa kila
siku ndani ya vyombo vya habari. Kuna miongozo ya namna ya kuvaa
(dress code), namna ya kuandika habari zetu (stylebooks), miongozo
inayotuongoza katika shughuli za kila siku za ukusanyaji habari
ikiwamo mambo kama ununuaji wa habari na picha, utafutaji wa habari
kwa kificho, na kadhalika (Internal codes of conduct). Kuna sera za
uhariri (editorial policies), kuna mhariri wa jamii (Ombudsman,
Public Editor). Hii ndiyo miongozo ambayo inaweza kuwekwa madhubuti
kwa ajili ya kuwaongoza waandishi wa habari katika kila wanalotaka
kulifanya.
Katika suala hili, ni bora kila chombo cha habari kilitafakari
na kuona kinalitolea maamuzi gani. Liwekwe wazi katika sera ya
uhariri ili mwandishi au mhariri anapoingia katika chombo hicho
aelewe tangu mwanzo. Baraza la Habari limeshasaidia vyombo kadhaa
kuandaa miongozo yake ya ndani kwa maombi ya vyombo hivyo.
Swali: Je, baada ya uchaguzi, mwandi-shi aliyeondoka kwa ajili
ya kugombea na hakufanikiwa anaruhusiwa kurudi?
Jibu: Hilo nalo ni suala la miongozo katika vyombo vya habari.
Sera ya chombo iseme wazi. Kwa mfano, kuna vyombo vya kimataifa
ambavyo ukitaka kugombea nafasi yako inakuwa wazi na kutangazwa.
Ukitaka kurudi, kama nafasi utaikuta bado wazi, unashindana na
wenzio na ukipata, unajaza fomu ya kueleza mgongano wa maslahi
(declaration of conflict) ili hilo lizingatiwe katika namna
utakavyopangiwa kazi. Wengine, kama Nation Media Group ya Kenya na
Standard, ukishakwenda kwenye siasa huruhusiwi kurudi. Hata
ukibainika kuwa kada wa chama unaambiwa uchague uandishi au ukada.
Baraza la Habari la Kenya ambalo husajili wanahabari mwaka 2016
lilitoa taarifa kuwataka wanahabari wote waliokuwa na malengo ya
kugombea mwaka 2017 kujiuzulu mara moja na kutoa tahadhari ya
kuwafutia usajili wote ambao wangejaribu kuingia katika uchaguzi
wakiwa ndani ya vyumba vya habari. Bodi ya Uhariri ya gazeti la New
York Times inapiga marufuku jaribio lolote la kutafuta
nafasi ya kisiasa ukiwa bado mwandishi wao. Ni miongozo ya ndani
ambayo wameona itawasaidia kuepusha migongano ya maslahi na
upendeleo. Ni hatua walizochukua kuhakikisha kuwa heshima ya vyombo
hivyo haitiliwi shaka.
Lakini pia miongozo hii itaeleza, ikiwa chombo kitampokea
mwandishi anayerudi baada ya kuwa mwanasiasa, atafanya kazi ipi?
Labda atakuwa mwanasafu (columnist), au labda kitamtumia katika
majopo ya mijadala huku historia na mrengo wake vikiwekwa bayana,
na kadhalika. Jambo la msingi ni kuilinda taaluma dhidi ya
mwonekano wa kutozingatia misingi yake ya kutenda haki na kutoa
ukweli kwa usahihi.
Swali: Mwandishi wa habari kuwa mwanasafu kunamtofautisha vipi
na uana siasa wake? Maana kuna wana-safu ambao ni wanasiasa.
Jibu: Ukiwa mwanasafu, huwi katika nafasi ya kuamua habari gani
itoke au isitoke, lakini pia, hupati nafasi ya kuhariri habari na
kuifanya uonavyo. Ni muhimu pia mwishoni mwa safu vyombo vya habari
vitoe maelezo mafupi kuhusu wanasafu wake, ili watu wawaelewe.
Swali: Kuna mwandishi mahiri sana, mwalimu na aliwahi kuwa
mwanasiasa mpaka kuwa mbunge, mpaka mwezi uliopita alikuwa Mhariri
wa Jamii (Public Editor) kwenye kampuni moja kubwa ya habari
nchini. Hili likoje hasa kiutendaji kazi?
Jibu: Hii ni kazi mojawapo ambayo mtu kama huyo anaweza kufanya.
Jukumu la Mhariri wa Jamii ni kuhakikisha taaluma na maadili ndani
ya chombo husika yanazingatiwa ili kulinda maslahi ya mlaji (jamii)
na kutunza heshima ya chombo. Yeye hahusiki na maamuzi ya kiuhariri
kabla ya habari au makala kuchapishwa. Lakini anatoa ushauri wa
kitaalamu kuhusu maudhui yaliyochapishwa. Lakini pia Mhariri wa
Jamii hushughulikia malalalamiko kutoka kwa wasomaji pale
yanapoletwa, kwa lengo la kuyasuluhisha ili kuzinufaisha pande
zote, ule wa chombo cha habari na wa mlalamikaji.
Mhariri wa Jamii pia huandika maoni na makala kuhusu mwenendo wa
taaluma, lakini pia huandika kuelimisha jamii kuhusu ufanyaji kazi
wa vyombo vya habari na dhima ya vyombo hivyo. Hutoa elimu, yaani
media literacy. Kazi mahsusi hutegemea mkataba wake lakini kwa
ujumla hayo ndiyo majukumu yake. Uwezekano wa mgongano wa maslahi
ni mdogo sana katika kazi ya Mhariri wa Jamii.
8
Habari
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
Maswali yanayoulizwa mara kwa maraInatoka Ukurasa wa 6
-
Waliomeremeta
Toleo la 84, September-Oktoba, 2010
9
Toleo la 156, Agosti, 2020
Habari
Na Mwandishi wa Barazani
Kaimu Mwenyekitti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus
Balile amehimiza wahariri kuwalinda wanahabari wao watakaokuwa
wakiripoti uchaguzi.
Alisema uchaguzi umewadia, tusikubali kusukumwa na
wanasiasa.
Alikuwa akizungumza katika mkutano wa mwaka wa TEF mjini
Dodoma.
Uchaguzi Mlkuu wa kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika
Oktoba 28, 2020.
Wakili mashuhuri , Jebra Kambole akiwakilisha Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu aliwasilisha mada kuhusu sheria za vyombo vya
habari zinazohusu uchaguzi akielezea mambo muhimu ya sheria hizo na
vikwazo.
Wawakilishi wa Mfuko wa Wanawake (WFT) pia walizungumzia
uchaguzi na vyombo vya habari.
Taasisi zingine zilizowasilisha mada kwenye mkutano huo
uliofanyika Agosti 21 na 22 ni pamoja na Benki ya NMB, Umoja wa
Mataifa, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Jii, Bodi ya Manunuzi ya Umma,
RITA, Wakfu wa Habari Tanzania na Mfuko wa
Fidia ya Wafanyakazi. Wazungumzaji wa taasisi hizo
waliwaelimisha wahariri kuhusu majukumu ya taasisi zao na jinsi
ya kushirikiana na vyombo vya habari.
Taasisi hizo mbalimbali siyo tu ziliwasiloisha mada kwenye
mkutano huo, bali pia zilifadhali.
Masuala muhimu ya TEF yalizungumzwa katika mkutano huo
ni juhudi za kuwezesha kupatikana kwa usajili wa jukwaa
hilo.
Mkutano ulifahamishwa kuwa hatua iliyofikiwa ni kuchukua nafasi
ya jukwaa moja la zamani lililojulikana kwa jina la EFOTA. Chini ya
mchakato unaoendelea EFOTA iliyokuwa na malengo mapana itafutwa na
mahala pake patajazwa na TEF mpya.
TEF yahimiza waandishi kulindwa wakati wa uchaguzi
Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) , Deodatus
Balile akizungumza katika mkutano mkuu wa jukwaa hilo. Kulia ni
Katibu wa TEF, Neville Meena.
Wahariri waliohudhuria mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF) mjini Dodoma.
-
Waliomeremeta
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
10
Fursa
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
RAINFOREST JOURNALISM FUND CALL FOR PROPOSALS—INTERNATIONAL
PROJECTS
The Pulitzer Center is inviting proposals for grants to
journalists reporting for wide-reaching major news media outlets on
tropical rainforests in any part of the world.
Thematic AreasThe supported international journalism projects
will focus on the following themes:• Tropical forests' role in the
overall climate
equation and weather patterns globally, regionally and locally,
and the consequences for human life and living conditions caused by
deforestation
• Deforestation drivers• Solutions to halt deforestation
Funding Information• The Pulitzer Center will fund
international
travel costs associated with reporting projects on tropical
rainforests, with an emphasis on issues that have gone unreported
or under-reported in the mainstream American media.
• The amount of individual travel grants will depend on the
specific project and detailed budget planning. Most awards fall in
the range of $5,000 to $15,000 but depending on project specifics
may be higher.
• On approved projects, half of the grant amount is generally
paid just before travel and the remainder on submission of the
principal material for publication or broadcast. Specific grant
terms are negotiated during the application process.
Eligibility CriteriaGrants are open to all journalists, writers,
photographers, radio producers or filmmakers; staff journalists as
well as free-lancers of any nationality are eligible to apply.
Applications Process• Applications must be received in English.•
Applications must include the following: o A description of the
proposed project,
including distribution plan, in no more than 250 words
o A preliminary budget estimate, including a basic breakdown of
costs. Travel grants cover hard costs associated with the
reporting; please do not include stipends for the applicants.
Fixer/translator/driver fees are acceptable
o Three samples of published work, either print or
broadcast.
o Three professional references. These can be either contact
information, or letters of recommendation. The latter is encouraged
when letters from interested producers or editors are
available.
o A copy of your curriculum vitae. o Applications may also
include a more
detailed description of project but this will be considered as
optional supplement only. The most important part of the submission
is the 250-word summary.
For more information, visit Pulitzer Center.
Highlights Important Dates
Post Date - 24-Jul-2020
Deadline Date – Ongoing
Donor NamePulitzer Center
Grant Size$10,000 to $100,000
CategoryGrant
Reference URLhttps://pulitzercenter.org/rainforest-
journalism-fund-call-proposals-international-projects
Focus Areas of Interest Environment
Media
-
Waliomeremeta
Toleo la 84, September-Oktoba, 2010
11
Habari
Toleo la 156, Agosti, 2020
Na Mwandishi wa Barazani
Kanuni mpya za maudhui mtandaoni zinabinya na haziendani na
viwango vinavyokubalika vya kimataifa.
Uchambuzi kuhusu kanuni hizo, unaeleza kuwa zinabana na hasi kwa
uhuru wa uhariri, uhuru wa habari. uandishi wa habari na uhuru wa
kujieleza kwa jumla.
Uchambuzi huo uliagizwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT)
kupitia kanuni hizo ambazo zinafuta zile za mwaka 2018.
Imeelezwa kuwa katika uchambuzi huo kanuni hizo siyo tu zina
orodha ndefu ya kanuni zinazozuiliwa, pia zimeingiza taratibu ngumu
za leseni.
Kanuni zinakiuka viwango vya kimataifa vya uhuru wa kujieleza,
vifungu 6(d) na 7(2) vya mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya
Afrika Mashariki wa mwaka 1999, kifungu cha 18 cha Katiba ya
jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya mwaka 1977 na Sera ya Taifa ya
Utangazaji ya mwaka 2003.
Kanuni hizo zinaimarisha kashfa kuwa uhalifu zinazuia vyanzo vya
habari kutotajwa, zinatoa faini kubwa kwa ukiukaji na kuipa
madaraka makubwa ya kuondoa maudhui Mamalaka ya Udhitibi
Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Wakati kanuni za mwaka 2018 zinazofutwa zilielekeza maudhui
yanayokataliwa yaondolewa katika saa 12, kanuni za sasa zinatoa saa
mbili tu kufanya hivyo.
Kanuni hizo zimegawa leseni katika makundi manne - habari na
matukio, burudani,
elimu/ dini na kutangaza moja kwa moja katika vyombo mbalimbali
–redio na runinga.
Kuanzishwa kwa lenseni za makundi, uchambuzi unaeleza ni jaribio
la kubana upeo wa chombo kwa maana ya maudhui na maeneo ya
kijiografia.
“Kwa mfano, iwapo chombo ni kikubwa, vingine vyote vinatakiwa
ama kushughulikia habari na matukio tu, burudani au masuala ya dini
ama kuwa na leseni zaidi ya moja.
Kwa ujumla hakuna hata chombo kinachoweza kutoa habari ama
taaarifa kwa umma bila kuwa na leseni, jambo linalokiuka haki ya
kikatiba inayotolewa na kifungu cha 18 kinachotoa uhuru kwa kila
mtu kutafuta, kukusanya, kuchakata na kusambaza habari bila kujali
mipaka ya nchi.
Uchambuzi huo unaeleza na pia kuongeza kuwa kanuni hizo pia
zinabinya uandishi wa habari za uchunguzi kwa kuwa zinazuia
uchapishaji wa mawasiliano rasmi ya siri.
Kuhusu chanzo kutotambulishwa ambalo ni jambo muhimu katika
uhuru wa kujieleza, kanuni zinazuia.
Uchambuzi huo umeonyesha kuwa kutojitambuliwa kunatoa mwanya
mpana wa siri kwa mtu kuwa na maoni na kuwa na uhuru wa kujieleza
bila kuingiliwa.
Ukizungumzia msimamo wa msimamizi wa Umoja wa Mataiafa wa Uhuru
wa Kujieleza, uchambuzi huo unaeleza kuwa njia bora ni kutumia
vyanzo bila kujitaja ama vifaa vya kitaalamu ili kukuza na kulinda
uhuru wa kujieleza mtandaoni badala ya kuukwaza kwa kuzuia
utaratibu wa kutojitambulisha.
Kuhusu Sera ya Utangazaji ya 2003, imeelezwa na uchambuzi huo
kuwa kanuni hizo haziendani kabisa na matakwa ya sera hiyo ya
utangazaji katika njia mbalimbali kama: • Kanuni hizi hazitoi
mazingira wezeshi kwa vyombo vya habari kufanyakazi kwa ufanisi
na uhuru wa habari kama ilivyo katika Sera ya utangazaji ya 2003.
Ingawa sera inataka kuwepo mazingira wezeshi, kanuni zinakwaza
uhuru wa habari kwa kuwa na taratibu za kubinya habari na kufanya
kashfa kuwa uhalifu.
• Wakati sera ya Habari na Utangazaji ya 2003, inahimiza
serikali kuondoa vikwazo kwa wananchi kupata taarifa, kanuni
zinaweka vikwazo hivyo.
• Kwa kanuni hizi kusisitiza kuwa na leseni na hatua zingine na
kubinya maudhui haki ya raia ya kupata habari inaathirika. Hii ni
kutokana na vizingiti vikali vinaathiri uhuru wa kujieleza ambavyo
vinaaathiri pia kupata taarifa.
Kanuni za mtandaoni za mwaka 2018 zilipotolewa na serikali, MCT
kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na
Umoja wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC) walifungua shauri
Mahakama Kuu.
Kufuatiwa kupitishwa kwa kanuni hizi mpya, kesi hiyo haipo
tena.
Uchambuzi kamili wa kanuni hizi mpya unapatikana katia tovuti ya
MCT www.mct.or.tz
Kanuni mpya za mtandaoni zabana uhuru
wa habari, kujieleza
-
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
12
Balozi mstaafu Ferdinand Kamuntu Ruhinda amekuwa mwandishi wa
habari, mhariri, mtumishi wa serikali mwandamizi, mwanadiplomasia,
mwanastrategia wa kisiasa na mfanyabiashara. Alikuwa rafiki wa
karibu wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, hayati Benjamin William
Mkapa, aliyefariki dunia Julai 23, mwaka huu baada ya kuugua.
Balozi Ruhinda alikutana na Mkapa kwa mara ya kwanza mwaka 1966
kwenye chumba cha habari cha iliyokuwa Tanganyika Broadcasting
Corportion (TBC) wakati Ruhinda akiwa ameajiriwa kuwa Mwandishi wa
Habari na Mkapa msoma habari wa kujitegemea.
Tangu hapo walianzisha urafiki usiomithilika wa kitaaluma na
kijamii ambao umedumu kwa zaidi ya nusu karne. Mwaka 1967,
walifanya kazi pamoja kwenye Magazeti ya Chama ya Uhuru, la
Kiswahili na la Kiingereza, The Nationalist, ambako Mkapa alikuwa
Mhariri Mtendaji na Ruhinda Mhariri Msanifu na baadaye Mhariri wa
Habari.
Mwaka 1972 wakati Mkapa aliopoteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji wa
Magazeti ya Serikali, The Daily News, Ruhinda akachukua nafasi ya
Mkapa kwenye Magazeti hayo ya Chama. Mwaka 1974 Mkapa aliteuliwa
kuwa Mwandishi wa Habari wa Rais Nyerere na mwaka 1976 akahamishwa
na kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) ambapo
mwaka huo huo Ruhinda naye akachukua nafasi ya Mhariri Mtendaji wa
The Daily News.
Baadaye Mkapa akaingia katika shughuli za diplomasia na baadaye
siasa akiwa Mbunge na Waziri hadi kufikia nafasi ya juu kabisa ya
kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1995.
Ruhinda hakuingia kwenye Siasa hasa bali alijiunga na shughuli
za Diplomasia pia, kwanza akiwa Naibu
Balozi wa Tanzania nchini Sweden na baadaye Balozi kamili Canada
na China kabla ya kustaafu utumishi wa umma, mwaka 1993.
Ni watu wa umri mmoja, miaka 82.Akielezea kuhusu wapi, vipi na
lini
hasa mlikutana kwa mara ya kwanza na Mkapa, Balozi Ruhinda
alisema alikutana na Ben Mkapa kwa mara ya kwanza, mwaka 1966,
miaka 54 iliyopita, tukiwa bado vijana. Tokea wakati huo, wamekuwa
marafiki. Tuliaminiana sana. Nadhani sitakosea kusema kuwa tokea
nijuane naye, haikupata kupita wiki mbili bila kukutana naye, ana
kwa ana, ama kuzungumza naye kwa simu, ama kwa mawasiliano ya aina
nyingine. “Na msinielewe vibaya, Ben alikuwa na marafiki wengi, na
wa karibu, siyo mimi peke yangu”
anasema.Alisema walikutana katika
mazingira ya kazi. Wakati huo yeye akiwa ameajiriwa kama
Mwandishi wa Habari katika Chumba cha Habari cha Tanganyika
Broadcasting Corporation (TBC), wakati huo yeye, Ben alikuwa Msoma
Habari za Kiingereza wa kujitegemea, anayekuja wakati wa muda wake
nje ya kazi.
Balozi Ruhinda anasema Ben aliipenda kazi yangu na urafiki wetu
ulianzia hapo.
“Nimemfahamu kwa muda mrefu sana, zaidi ya miaka 50. Kwa kweli,
uhusiano wetu ulikuwa zaidi ya urafiki. Tulikuwa ndugu. Tulikuwa
watu tofauti sana mwanzoni”, anasema na kuongeza kuwa“sote
Mkapa kama mwandishi wa habari - Ruhinda
Endelea Ukurasa wa 14
Katika mahojiano maalum na waandishi watatu waandamizi nchini,
Balozi Ferdinand Ruhinda ametoa ushuhuda na shukrani kuhusu rafiki
na ndugu yake hayati Benjamin Mkapa. Saidi Nguba, mmoja wa
waandishi hao anaelezea jinsi Balozi Ruhinda anavyomzungumzia Mkapa
kama Mwandishi wa Habari.
Balozi Ferdinard Ruhinda akisalimiana na Rais Benjamin Mkapa
katika mojawapo ya matukio ya kijamii na kifamilia.
Wasifu
-
Waliomeremeta
Toleo la 84, September-Oktoba, 2010
13
Toleo la 156, Agosti, 2020
Habari
Na Mwandishi wa Barazani
Amri ya Serikali ya Zanzibar kumsimamisha mwandishi wa habari
kwa miezi sita imeondolewa. Talib Ussi Hamad, ambaye
anaandikia gazeti la Tanzania Daima sasa yuko huru kufanyakazi
tena na alipoulizwa kuhusu uamuzi huo wa serikali alisema
amefurahishwa kwamba sasa anaweza kufanyakazi tena.
Barua ya kuondoa amri hiyo ilitiwa saini na Mkurugenzi wa Idara
ya Habari Zanzibar, Dk.Juma Mohamed Salum.
Barua hiyo ya Agosti 3, 2020 ilieleza“umeruhusiwa kuendelea na
kazi ya uandishi kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti , Machapisho na
Wakala Na 5 ya 1988 na marekebisho yake Na 8 ya 1997.”
“Kwa barua hii, idara inafuta uamuzi wake wa awali uliotolewa
kupitia barua kumbukumbu namba IHM/WH32/1/VOL.IV/40 ya
20/4/2020”,barua hiyo imeeleza.
Hamad alisimamishwa kwa kile wenye mamlaka serikalini kudai
alikiuka maadili ya taaluma.
Anadaiwa kuwa alitoa habari kuhusu mgonjwa wa COVID-19 bila
ridhaa yake kinyume na maadili ya kitabibu.
Hamad alisema alibanwa ili aombe radhi baada ya kuripoti habari
yake hiyo lakni alikataa kwa maelezo kuwa habari hiyo ilikuwa na
umuhimu kwa umma.
Pia alisema alifungua kesi katika Mahakama Kuu Zanzibar Julai 3
kupinga kwa kutopewa nafasi ya kujibu kabla ya kusimamishwa.
Serikali ya Zanzibar ilitarajiwa kupeleka majibu Mahakamani
Agosti 4, lakini badala yake akapokea barua ya kumruhusu kuendelea
na uandishi wa habari.
Aliposimamishwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Kamati ya
Kutetea Waandishi (CPJ) zilihimiza aachiwe ili afanye kazi
yake.
Amri ya kumsimamisha Hamad imeondolewa wakati gazeti alilokuwa
akiandikia– Tanzania Daima, halisamabazwi tena kwa sababu leseni
yake ilifutwa na Msajili wa Magazeti wa Idara ya
Habari Tanzania Bara kwa madai ya kukiuka maadili.
Hamad ameeleza matumaini kwamba gazeti hilo huenda likaruhusiwa
kuchapishwa tena kabla ya uchaguzi mkuu.
Mwandishi aruhusiwa kufanyakazi tena Z’bar
Mwandish Talib Ussi Hamada.
-
Waliomeremeta
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
14
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
tukitokea pande mbili tofauti kabisa za nchi… pembezoni mwa
nchi. Mmoja akitokea Kaskazini Magharibi kabisa na mwingine Kusini
kabisa mwa nchi yetu. Mmoja anatokea karibu na Mto Ruvuma na
mwingine akitokea Mto Kagera. Tuliunganishwa hasa na haiba zetu za
kikazi, kimaisha na kisiasa.”
Mwaka mmoja tu, baada ya kujuana naye, Balozi Ruhinda anasema
aljiunga na Magazeti ya Chama cha TANU ya The Nationalist
(Kiingereza) na Uhuru (Kiswahili), ambako Mkapa alikuwa Mhariri
Mtendaji.
“Nikafanya kazi chini yake, kwanza nikiwa Msanifu Habari
(Sub-Editor), na baadaye Mhariri wa Habari (News Editor). Utaona
kuwa urafiki wetu ulianzia kwenye shughuli za uandishi wa habari.
Urafiki wetu pia ulikuwa wa kisiasa. Kama mnavyojua nyie, uandishi
wa habari hauna tofauti kubwa na siasa. Baadaye, mwenzangu akaingia
moja kwa moja kwenye siasa.
Mimi nikabakia kwenye uandishi wa habari, lakini urafiki wetu
ukabakia pale pale na kuzidi kukomaa.” Kuhusu tuhuma kuwa Mkapa
amekuwa alikuwa zaidi mdhibiti na mzuia habari na siyo Mwandishi wa
Habari aliyebobea baada ya kupikwa vizuri na kuiva na kuzuia mawazo
huru, utoaji habari bila ya vikwazo na mijadala ya wazi, alisema
hakubaliani hata kidogo na Mkapa kupachikwa tuhuma hizo.
“Angalia, wakati najiunga na The Nationalist, na nyinyi wenyewe
mmefanyakazi katika vyombo vya habari na mnajua utaratibu huu,
tulikuwa tunafanya mkutano wa tathmini na kuchambua magazeti kila
siku asubuhi na yeye ndiye aliyekuwa mwenyekiti.
Tulijadiliana kwa uwazi, kwa urafiki na uhuru kamili kama
wanataaluma. Tulikubaliana na tulihitilafiana. Lakini hatimaye,
yeye kama Mhariri ndiye alitoa msimamo wa mwisho.
Na kwa kweli hiyo ndiyo kazi ya Mhariri kutoa msimamo na
mwelekeo wa gazeti. Kwa maana hiyo, Mhariri yeyote ni Mdhibiti wa
gazeti lake,
aliongeza Balozi Ruhinda na kwamba Mkapa aliwazuia waandishi
kuandika walivyotaka kulingana na sera ya gazeti, ama alizima
mawazo yao… hapana, siyo kweli alisema. “Nakumbuka wakati wetu
kwenye The Nationalist tulikuwa na waandishi kutoka hadi Ghana na
Biafra (Nigeria) na kila mtu alikuwa huru kutoa fikra na mawazo
yake. Isipokuwa, ni dhahiri kuwa uamuzi wa mwisho ulikuwa wa kwake,
akiwa Mhariri. Na hii ndiyo desturi ya utendaji kazi wa vyombo vya
vya habari duniani kote na kutoa uamuzi ni wajibu muhimu na mahsusi
wa Mhariri,” aliongeza
Kuhusu Mkapa alikopata mafunzo ya taaluma ya Uandishi wa Habari
Balozi Ruhinda alisema alipata
mafunzo ya Uandishi wa Habari kabla ya kuteuliwa kuyaongoza
Magazeti ya Chama. Alipelekwa kwenye Gazeti moja mashuhuri la
Uingereza, (Daily) Mirror, na kupata stadi na uzoefu wa Uandishi wa
Habari na Uhariri. Lakini hata kabla ya kupelekwa huko, Mkapa
alikuwa na uwezo wa kuandika vizuri, akiwa hodari kwa lugha za
kufanyia kazi hiyo za Kiingereza na Kiswahili.
Alisema kwa maoni yake, Mkapa alikuwa Mwandishi wa Habari bora
na Mhariri makini kuliko wengi wale wanaomlaumu.
•Mwandishi anapatikana kwa Simu ya Mkononi/WhatsApp: 0754-388418
na Barua-pepe: [email protected]
Mkapa kama mwandishi wa habari - RuhindaInatoka Ukurasa wa
12
Benjamin Mkapa alipokuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya
Nationalist na Uhuru.
Wasifu
-
Na Mwandishi wa Barazani
Mkutano Mkuu wa Baraza la Habari Tanzania utafanyika Tanga
Septemba 28, 2020.
Zaidi ya wawakilishi 100 wa vyombo mbalimbali vya habari
wanategemewa kuhudhuria mkutano huo.
Agenda za kawaida za mkutano huo ni kwamba utapokea ripoti ya
Katibu Mtendaji wa Baraza, Taarifa ya Fedha ya mwaka 2019 na uteuzi
wa Mkaguzi wa Hesabu za Baraza kwa mwaka 2020.
Mkutano huo pia utapitisha Kanuni za maadili ya habari
zilizopitiwa upya.
Kanuni hizo za maadili hupitiwa kila baada ya miaka mitatu
kuhakikisha zitazingatia mabadiliko ya tasnia.
Aidha mkutano huo utawachagua wajumbe wapya wa Bodi ya Baraza
kwa kuwa muda wa iliyopo sasa.
Rais mpya wa bodi atachaguliwa lakini kutokana na hitaji la
katiba , theluthi mmoja
ya wajumbe wa Bodi wa sasa lazima wabakie kwa lengo la kuweka
muendelezo na theluthi moja ya wajumbe watakaochaguliwa lazima wawe
wanawake.
Rais wa Baraza ni Jaji mstaafu Thomas Mihayo, Makamu wa Rais
ni Hassan Mitawi.Wajumbe wengine wa Bodi ni
Jaji mstaafu,Juxon Mlay, Edda Sanga, Anna Henga, Dk. Edmund
Mndolwa, Dinnah Chahali, Bakari Machumu na Wallace Mauggo.
Bodi hiyo ilifanya mkutano wake wa mwisho Agosti 28, 2020.
15
Toleo la 156, Agosti, 2020
Habari
Mkutano Mkuu MCT kufanyika Tanga
Rwehabura Rugamba, Mhariri wa EATV na EA Radio akipokea cheti
kutoka kwa Makamu Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Hassan
Mitawi katika Mkutano Mkuu wa Baraza wa mwaka 2019. Kulia ni Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania, Kajubi Mukajanga.
Wajumbe kutoka taasisi mbalimbali za habari wanachama wa MCT
wakiwa kwenye mkutano wa mwaka wa 2019.
-
Na Mwandishi wa Barazani
Baada ya kufanyika kwa mafanikio Jijini Dar es Salaam tangu
kuanzishwa kwake mwaka 2009, kilele cha Tuzo za Umahiri za Uandishi
wa Habari Tanzania (EJAT) zitafanyika nje ya jiji hilo.
Kajubi Mukajanga, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT
amesema kuwa safari hii kilele cha tuzo hizo za kuwatambua
wanahabari waliofanya vizuri kitafanyika Tanga.
Septemba 28, 2020 ndiyo tarehe ya kilele cha tuzo hizo sherehe
ambazo zitajumisha wanahabari kutoka sehemu mbalimabli nchini.
Hii ni mara ya 11 kwa Tuzo hizo ambazo hushindaniwa kila mwaka
na wanahabari 11 wameibuka kuwa washindi wa jumla.
Katika miaka mitatu ya mwisho wanawake wameibuka washindi wa
jumla.
Mwanamke wa kwanza kufungua pazia kwa ushindi wa jumla kwa
wanawake ni Florence Majani ambaye alikuwa akiandikia gazeti la
Mwananchi 2016, akifuatiwa na Vivian Pyuza wa CG FM mwaka 2017 na
Salome Kitomari wa Nipashe mwaka 2018.
EJAT imekuwa tukio la kujuimisha wanahabari wa nchi yote kwa
kuwa washindi wanaibuka kutika sehemu mbalimbali kuanzia redio za
jamii na hata vyombo vikuu vya habari.
Jumla ya kazi 450 zimepokewa kwa tuzo za mwaka huu ambazo
zilizinduliwa rasmi Oktoba 11, 2019.
Mwaka huu kuna makundi 21 ambapo matatu ni mapya.
Makundi mapya ni Ubunifu kwa maendeleo ya Binadamu, Hedhi salama
na Athari za Afya na mazingira kutokana na matumizi ya
kemikali.
Makundi mengine ni Fedha na Biashara, Kilimo na Biashara ya
Kilimo, Elimu, Utalii na Uhifadhi, Uandishi wa Data, Haki za
Binadamu na Utawala Bora, Mpiga picha bora, Mchora vibonzo bora,
Mpiga picha bora wa video, uandishi wa jinsia, Mafuta, gesi na
Usimamizi wa madini, Usalama wa Barabara, Kundi la wazi, Uandishiwa
habari za watoto, jinsina afya ya uzazi, na habari za wazee.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha kazi za kushindanisha ilikuwa
januari 31, 2020.
Washirika wa EJAT ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Wakfu wa
Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la
Tanzania (MISA-Tan),Chama cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), HakiElimu, AMREF,
SIKIKA, Agriculture Non-State Actors Forum (ANSAF), Chama cha
Wamiliki wa vyombo vya Habari Tanzania (MOAT na Umoja wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
16
Jarida la Baraza la Habari Tanzania
Kilele EJAT kufanyika nje ya Dar Habari
Salome Kitomari mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe
akiibuka kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi wa jumla wa Tuzo za
Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2018.