Top Banner
MAFUNDISHO KITABU CHA MWONGOZO
30

Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

Dec 21, 2016

Download

Documents

dangminh
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

MAFUNDISHO

K I TA B U C H A M W O N G O Z O

Page 2: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

MAFUNDISHO

K I TA B U C H A M W O N G O Z O

Kimechapiswa naKanisa la Yesu Kristo la Warakatifu wa Siku Za Mwisho

Salt Lake City, Utah

Page 3: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

© 1999 by Intellectual Reserse, Inc.Haki zote Zimehifadhiwa

Kimepigwa chapa katika United States of America

Kiingereza Kimeidhinishwa: 5/99Tafsiri Imeidhinishwa: 5/99

Translation of Teaching GuidebookSwahili

Page 4: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

Utangulizi iv

Jitayarishe Mwenyewe Kiroho 1

Fundisha Vile Yesu Alivyofundisha 3

Tumia Njia Mbali Mbali za Kufundisha 8

Tayarisha Somo Lako 12

Elewa Wale Unao Fundisha 15

Mafanikio Ya Kufundisha 17

Muhtasari Juu ya Mafunzo ya Injili 19

Contents

iii

Page 5: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

Kitabu hiki cha MaongozoKimeundwa Kutumiwa na wazazi,viongozi, na walimu. KinawezaKutumika kama sehemu ya jitihadaza kibinafsi za kuimarika kamamwalimu. Pasipo na Teaching, NoGreater Call (Kufundisha, MwitoUsiyo na Kipimo) inaweza kutumikakama msingi wa mafundisho ya Injilina kuboresha mikutano ya mwalimuona ukurasa wa 18.

Bwana Amefundisha:

“Na nawapeni amri kwambamtafundishana maagizo ya ufalme.

“Fundisheni enyi kwa dhati naneema yangu itakuwa nanyi,kwamba mtafundishwa kikamilifuzaidi kwa mafafanusi ya akili, katikamwenendo mzuri, katika kanuni,katika mafundisho, katika sheria yainjili, na katika mambo yote yanayohusu ufalme wa Mungu, ambavyomtahitaji ili muelewe” (D&C88:77–78) (ona M&M 88:77–78).

Yapasa nyumbani kuwa mahali pamsingi ambako haya hutendeka.Mafundisho na elimu ya nyumbanihusaidiwa na yale yanayopewakanisani. Sisi sote kama walimu huwana wajibu katika hali hizi zilizotajwakwa jirani na wale tunaoshirikiananao katika maisha ya kila siku.Tunafundisha kama wazazi, wana,mabinti, waume, mabibi, ndugu nadada. Tunafundisha kama viongoziwa kanisa, walimu darasani, walimu

wa nyumbani na walimu wakutembeleana. Tunafundisha piakama wafanyi kazi wenzetu, jirani na marafiki. Wakati mwinginetunafundisha kwa yale mambotunayosema na ushuhuda tunaotoa,na hata mara nyingi tunafundishakwa mfano.

Ukingoni mwa bahari la Galilaya,Bwana aliyefufuka alimwambiaPetro “Lisha wana-kondoo wangu”(Yohana 21:16–17). Mwito wakufundisha huhitaji kwamba tulishenafsi za wengine kwa ukweli wainjili na ambayo huwaelekeza kwamwokozi (ona Moroni 6:4). Fikiriajuu ya wajibu wa mafundisho yainjili kwa wokovu wa watoto waBaba aliye Mbinguni. Unawezakuwazia wajibu uliyo na cheo autukufu zaidi?

Ukiwa mzazi au mwalimu mwenyemwito mpya, unaweza kuwasazaidijuu ya huu wajibu. Kumbukenikwamba Mungu yu tayarikukusaidia. Ameahidi kwambatukiwa wanyenyekevu na wenyeimani, atayafanya yaliyo dhaifu yaweyenye nguvu kwetu (ona Ether12:27). Katika jitihada zetu kusitawikama mwalimu, tunaweza kujengauzoefu wetu tulio upata awali naujuzi wetu katika maisha. Uwezowetu utaongezeka tunavyo tayarishakwa makini, tunapowatilia nguvuwale tunafundisha, natunapotumainia Bwana.

Utangulizi

iv

Page 6: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

Unapofanya yale uwezayo kuhudumukatika mwito wako wa kufundisha,Bwana atakuongezea maarifa iliushawishi wengine kwa mema.Atakupanulia hata zaidi ya vipawa na uwezo wako wakati unaohitajika.

Tafuteni Mwongozo wa RohoMtakatifuTafuteni Roho Mtakatifuunapofundisha. Anaweza kukusaidia kufahamu mahitaji ya wale unaowafundisha nakutayarisha masomo yanayofaa.Atakupoesha moyo na kutayarishaakili yako ili upokee nyongeza yaufunuo na maongozi.

Unapojitayarisha kiroho, Roho auRoho Mtakatifu, atakuongoza nakukusaidia katika mafundisho yako.Roho Mtakatifu ni wa maana kwakufundisha kanuni na ukweli wainjili. Bwana amesema, kwambaRoho atapewa kwetu kwa maombiya imani, na kwamba tusipopokeaRoho, tusifundishe (ona D&C 42:14).Madokezo yafuatayo yatakusaidiakufundisha kwa uongozi wa RohoMtakatifu.

KuteuzwaUnapoitwa kufundisha, unapaswauteuzwe na hupewe baraka mahususina viongozi wako wa ukuhani. Barakahii itakusaidia kutimiza mwito wako.

Jitayarishe Mwenyewe Kiroho

1

Page 7: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

yako. Watafundishwa kutokana namfano wa maisha yako.

Mwalimu mmoja alipata wakatimgumu kuhisi uongozi, wa RohoMtakatifu alivyokuwa akitayarishamasomo yake Alipokua akitoa sala la usaidizi, akakumbukakwamba amekasirikia jirani wakealiyemwonyesha ukali. Kwaunyenyekevu, akamwomba Bwanakumsameha. Siku ifuataya,akamwendea Jirani wake na kuombamsamaha kwa ugumu wa roho yakekwake. Yeye na jirani yake wakawamarafiki na akaweza tena kufurahiauongozi wa Roho Mtakatifu.

Kuwa MnyenyekevuUnyenyekevu unaweza kukusaidiakuepukana na ushawishi wa kujitakiamaelekezo yako mwenyewe auukitumainia elimu na akili yakozaidi. Unaweza kuonyeshaunyenyekevu kwa kufuata ushaurikutoka Mithali 3:5–6: “MtumainiBwana kwa moyo wako wote; walausizitegemee akili zako mwenyewe.Katika njia zako zote mkiri yeye,naye atayanyosha mapito yako.”Bwana amefundisha kwamba tukiwawanyenyekevu, Bwana aliye Munguwetu atakuongoza kwa mkono, nakukupatia majibu kwa maombi yako”(M&M 112:10).

Toa Maombi Mara kwa MaraToa maombi mara kwa mara nauulize Bwana kukubariki unaposomana kujitayarisha. Wakati mwingineunaweza kuongeza mfungo kwamaombi. Omba ili uwaelewe nakuwapenda kwa kibinafsi waleunaowafundisha. Jifunze kutambuana kufuata maonyo ya RohoMtakatifu atakayekujia.

Soma Maandiko MatakatifuKwa maombi soma maandikomatakatifu. Unapofanya hivyo,utajifunza kuhusu Mwokozi na kukuakatika elimu ya kweli. Roho Mtakatifuatakusaidia kuelewa maandikomatakatifu na kuona jinsi yanahusikakwa mahitaji ya washiriki darasani au kwa jamii. Kuongeza maombi na mfungo kwa masomo yako yamaandiko matakatifu, utaongezewanguvu na uongozi wa Roho Mtakatifukatika mafundisho yako.

Fuata InjiliFuata mafundisho ya Injili kabisa vileiwezekanavyo. Tubu vishawishi vyaawali. Unapofanya haya, utapokeaufahamu na nguvu. Imani na furahautakayohisii kutokana na jitihadazako za kufuata injili yatakuwa wazikwa wengine. Watahisi uwazi waushuhuda wako na nguvu ya ahadi

.

2

Page 8: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

mafundisho kila wiki. Inamaanishapia kujali washiriki wa darasa lako.Fanya bidii kuwajua kila mmoja waokibinafsi. Itakusaidia kuwafundishakwa kusudiwa zaidi. Wanawezakuhitaji usaidizi wako wakatiwanapata shida, au wakati wakikosakuhudhuria mikutano, au ikiwa niwalemavu. Kumbuka ya Mwokozijuu ya kondoo wake mmojaaliyepotea (ona Luka 15:3–6).

Mwalimu mmoja wa mtotoaliyekuwa anakosa kuhudhuriamafundisho ya darasa aligunduakwamba kila wakati alipoongea na jamii ya huyo mtoto, mtotoalihudhuria kanisa Jumapili ifuatayo.Alijaribu kuongea na wazazi wake

Wapende Wale UnaofundishaWakati wa maisha yake duniani,Mwokozi alionyesha upendo mkuu na uelewano kwa kila mtu.Aliwafundisha walio maskini,matajiri, fukara na wenye dhambi.Alitufundisha kupenda kila mmojana kusaidiana. Alisema, “Amri mpyanawapa, Mpendane, Kama vilenilivyowapenda ninyi, nanyimpendane vivyo hivyo” (Yohana13:34). Tukiwaonyesha upendo waletunafundisha, wanatambua zaidiustahilivu wao wa maisha ya milele,wanaongeza shauku yao kwamafunzo, na wanapokea Roho zaidi.

Maana ya kuwa mwalimu wa injilihuwa na maana zaidi ya kutoa

Fundisha Vile Yesu Alivyofundisha

3

Page 9: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

wazi na iliyoeleweka, hadithi, namifano kutoka kwa maisha yakawaida ya kila siku. Masomo yakeyalikuwemo pamoja na uzoefumwingi wa kawaida ambao watuwengi walielewa. Aliongea juu yakondoo aliyepotea, utafutaji wa pesa,na sherehe juu ya kurudi kwa mwanampotevu (ona Luka 15).

Wakati mwingi, Mwokozi aliyatajamaandiko matakatifu akifundisha.Elekeza wale unaowafundisha kwa kutumia maandiko matakatifumara kwa mara wakati wa somo.Waelezee waelewa kwamba walewatu wanaotajwa katika maandikomatakatifu waliishi kwa hakika nawalipata majaribio na furaha katikajuhudi zao za kuhudumia Bwana.Uliza maswali yanayohitaji kupekuakatika maandiko matakatifu ili wale unaowafunza wapate majibu.Wahimize kusoma nyumbani kwakibinafsi. Wafundishe jinsi ya kutumiausaidizi wa kusoma katika maandikomatakatifu. Wafundishe jinsi yakutumia mafunzo ya usaidizi katikamaandiko matakalifu. Peana kaziinayowalazimisha kupekua maandikomatakatifu na katika maneno yamanabii wa siku za mwisho.

Fundisha kwa RohoWalimu wanapaswa kujitahidi wawena Roho wa Bwana wanapofundisha.Mtu anaweza kufundisha ukweli wakindani, na washiriki wanawezakujihusisha katika majadiliano

mara kwa mara na kutamka juu yaupendo wake kwa huyo mtoto. Hataalijitolea kumchukua huyo mtotoshuleni wakati wazazi wakewalikuwa kazini kumwezeshakuhuduria shughuli za darasa.

Kama mwalimu, unaweza piakufanya mengi kuwashirikishawashiriki na kuwasaidia kubakiwaongofu kwa injili. Hii ni yamuhimu mahususi kwa washirikiwapya na wale wasioshirikikikamilifu. Wasaidie kila marakujihisi wamekaribishwa. Pata njia ya kuwawezesha kushiriki darasani.Jitayarishe kufundisha injili kwaRoho na kwa upendo.

Fundisha Ukweli wa InjiliMwokozi alifundisha juu ya ukweliwa injili. Alizihimiza kanuni namaagizo za kwanza. . . . Imani, toba, ubatizo, na kupokea RohoMtakatifu. Alitufundisha kupendanana kuhudumiana. Alifundisha juu ya ukuhani, maagano, na maagizo,na juu ya yote yatupasavyo kujua ili turejee kwake. Tunapaswa piakufundisha injili vile imefunuliwakatika maandiko matakatifu namaneno ya manabii wa siku zamwisho. Mambo ya ulimwengu, yakibinafsi, maono yetu, na mambo yakubahatisha au yaliyo na mabishanohayaruhusiwi kufundishwa.

Mwokozi alifundisha ukweli wa injilikwa njia rahisi. Alitumia lugha iliyo

4

Page 10: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

Alika Kusoma Kwa BidiiBwana alisema, “tafuteni maneno ya hekima kutoka kwa vitabu vizurizaidi; Anatwambia pia kutafuta elimu,ata kwa kusoma na kwa imani (onaD&C 88:118). Kila mshiriki ana wajibuwa kupata elimu ya ukweli kwa bidiizake. Wajibu wa mwalimu ni kuamshatamaa ya kusoma katika wengine, wakuelewa, na kufuata injili. Ili kutimizawajibu huu, unaweza kutilia mkazokwa mambo matatu:

1. Amsha na ushikilie usikivu wao. Funguo wa kutekeleza hiihutegemea shauku yako kwakusoma injili. Mwingine hutegemeanjia yako ya kufundisha ambayoitafanya mafundisho yako yawewazi, yenye kuvutia, na rahisikukumbuka (ona ukurasa wa 8–11).Kuamsha shauku huwa mahususizaidi hapo mwanzoni wa fundisho.Ukipanga mafundisho yako, tafutanjia ya kualika Roho, kupata kilammoja kuwa msikivu mwanzonina kutilia mkazo katika agizo aukanuni ipasayo kufundishwa.

2. Endeleza ushirikiano. Panga njia za kushirikisha kila mmoja katikamasomo yako. Unaweza kuombammoja wao kusoma dondoo aumaandiko matakatifu au kuhadithia.Unaweza kuwaalika kujibu maswalina kutoa maoni yao juu ya mafunzobila wasi wasi. Unaweza kuulizammoja au wengi wao kuimbawimbo au kucheza ngoma. Katika

yanayovutia, lakini ikiwa hayupoRoho, mambo haya hayatasisitizwakwa nguvu katika roho zao. Rohoakiwepo, wote watatiliwa nguvukatika upendo wao kwa Baba aliyembinguni na Yesu Kristo, katikaupendo wao mmoja kwa mwingine,na katika jitihada zao za kufuatainjili. Mambo yafuatayo unawezakuyafanya ili kuvutia Roho katikaMafundisho yako.

• Anza kwa Maombi.

• Fundisha kutoka kwa maandikomatakatifu na maneno ya manabiiwa siku za mwisho.

• Toa ushuhuda wako.

• Shirikiana kwa uzoefu wako nauwaalike wengine kufanya hivyo.

• Tumia muziki (ona ukurasa wa (9).

• Onyesha upendo wako kwa Bwanana wengine.

Kama utayitayarisha mwenyewe,Roho Mtakatifu atakuangazia na kukuongozo unapofundisha.Unaweza kupata mvutio juu ya wale unaofundisha na yale mambounayopaswa kutilia mkazo kwakuwafundisha. Unaweza kupokeamaono na hisia kuhusu jinsi unawezakufundisha kwa njia inayofaa zaidi. Uwezo wako wa kufundishautaongezeka kadiri kwa unyenyekevuunatii minong’onong’o ya Roho.Utawezesha wale unaofundisha piakutambua ushawishi wa Roho.

5

Page 11: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

wanaoshirikiana wanatendewakwa heshima na uungwana.

3. Wasaidie kuyahusisha yale mambowanasoma. Inakupasa kuwasaidiawasomi pia kuyahusisha yalewamefundishwa na maisha yao ya kawaida mbali mbali. Hiiinaweza kuwa pamoja nakuwagawanyia kazi na kuwapahimizo ambazo huwasaidia kupatauzoefu wa mafunzo yaliyo naukweli. Kumbuka kwambakusoma injili bila kuiambatanishana maisha yako uwa haina maana.

Kuza Hali ya KusomaHali inayofaa zaidi kwa kusomainjili ni ile ambayo kila mmojadarasani anajali hali ya kusoma ya wengine. Utashi wa kusomahuongezeka wakati walimu nawasomi hupendana na husaidianakuelewa na kufuata mafundisho ya injili. Wakati wewe na waleunaowafunza huhusika katika halihio inayofaa, mafatizo hayatatokea.Inakupasa ufanye yote uwezayokukuza hali ifaayo na kuwasaidiawale unafundisha jinsi ya kuikuzahali hiyo.

Yafuatayo ni mambo ungefanyakukusaidia kukuza hali ifaayo yakusoma.

• Fika kwa saa ukiwa na vifaa vyotevya kufundisha.

• Hakikisha kwamba darasa lipo safi,kumepangwa vizuri, kuna hali

maombi, unaweza kuchagua yeyotekutoa ushuhuda au kuhadithia juu ya uzoefu wa kibinafsi unaoambatana na somo. Wakatimwingine inakuwa muhimukuwaomba huu ushirikiano awali ili wapate nafasi ya kujitayarisha na ili washiriki bila hofu.

Thumuni kubwa la mwalimummoja katika somo lake lilikuwakuhimiza umuhimu wa kusomakitabu cha Mormoni. Aliwaalikavijana katika darasa lake kufikiriajuu ya andiko takatifu ambalolimebadilisha maisha yao. Halafuakawaalika watatu au wanne waokusimama na kushirikiana mistariyao ya maandiko matakatifudarasani lote na kueleza jinsimaandiko hayo yamebadilimaisha yao. Kadiri kila mmojawao aliposhirikiana kuhusunguvu za kitabu cha Mormoni,washiriki wa darasa Wakatiliwautashi wa kusoma na kutafakarimaandiko matakatifu kila siku.

Watu wengine wanasitasita kwakushirikiana. Usiwaombe baadhiyao kama kibinafsi kusoma kwasauti na kuomba hadi uhakikishekwamba wanahisia vizuri kufanyahivyo. Ikiwa una shaka juu yautayari wa mshiriki kushirikiana,uliza wenye kujitoa badala yawale wanaositasita. Wanafunziwengi watajifunza pole polekuhisi vizuri wakishirikianawakiona kwamba wale

6

Page 12: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

• Mabishano yakitokea, nyamazahadi kila mmoja anakupa usikivu.Alafu endelea na somo.

• Ikiwa wengine wao huongeleshanawakati wa mafundisho, ongea naobaadaye ukiuliza ushauri waokuhusu njia ya kufaulu wakati wa mafundisho.

• Ikiwa mmoja wao anashikiliakauli wakati wa majadiliano,elekeza maswali yako kwawashiriki wengine au eleza kwaupole kwamba ungependa walehawajashiriki kufanya hivyo.

• Ikiwa washiriki darasani wametoamapendekezo yanayovutia darasambali na mafundisho, washukurulakini elekeza mafundisho iweilikichwa cha Somo hilo.

Tabia hiyo ya mabishano itapungukavile unavyopata njia za kuenezaupendo, ukubaliano na ushirikiunaofaa katika kikundi hicho.

njema, na bila mafalizo vileunavyoweza.

• Anza na ufunge kwa saa.

• Salimia na ukaribishe kila mshirikidarasani kibinafsi, ikiwezekana.

• Fanya yale mambo yanayoalikaRoho na kusitawisha heshima nauungwana.

• Wapende washiriki na kuwasaidiawapende kuhusika.

• Uliza maswali ambayo huelekezawashiriki kwa uangalifu.

• Tia moyo katika washiriki darasanikusikizana kwa heshima nauelewano.

• Jihadharishe na majadilianoyanayoweza kuharibu au kulegezashuhuda au kufukuza Roho.

Hata baada ya kutenda yoteuwezayo kusitawiwisha hali yakusoma, unaweza bado kupatachangamoto, yafuatayo yawezakukusaidia kuyakomesha baadhi yachangamoto na shida za kawaida:

7

Page 13: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

watasikiliza zaidi ukihadithia katikamaneno yako, badala ya kuyasoma.Watoto wadogo pia hupenda kuigahadithi.

Mwalimu mmoja alianzisha somolake na hadithi kutoka maandikomatakatifu. Kwa mfano, wakati somo lake lilikuwa juu ya rehema,aliwaambia juu ya msamaria mwema.Watoto wangefikiria akilini juu ya ile picha ya mtu aliyeangukiwa nawanyang’anyi na juu ya wale waumewaliopitia kando na kuenda zaowalipomwona. Walistaajabu juu ya rehema na uungwana wa yule msamaria aliyemtunza yulealijeruhiwa. Watoto walitazamia hizihadithi. Mwalimu alijifunza kutumia

Kunayo mambo mengi ambayoungefanya ili somo lako lifaulu,lifurahishe na kusaidia washirikikujifunza ukweli wa injili. Tumiamaono yafuatayo:

Tumia Hadithi na MifanoHadithi na mifano huamsha nakuvutia mawazo za watu nahuonyesha jinsi kanuni za injilihutumika katika maisha ya kawaida.

Utapata hadithi zinazovutia kutokamaandiko matakatifu na kutokakitabu cha mwalimu. Kabla yakufundisha somo lako, soma kilahadithi unayopanga kutumia. Fanyamazoezi ya kuhadithia kutumiamaneno yako. Darasa lako

Tumia Njia Mbali Mbali za Kufundisha

8

Page 14: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

ngano akikichanganya na magugu.Akaonyesha hiki kifurushi wakatiwote alivyokuwa akifundisha.

Mwalimu mwingine akawaulizawashiriki wa darasa kufikiri juu ya kitu ambacho wangefananisha na toba. Mshiriki mmoja akaelezakwamba toba ni kama sabuni, maanayake, inaweza kutusafisha kutokakwa dhambi.

Tumia NyimboUtumiaji wa nyimbo ni njia mojahalisi ya kualika Roho wa Bwanakatika somo lako. NyimbounatuSaidia kuonyesha viletunavyohisi kwa urahisi kuliko kwakunena.

Nyimbo za kanisa hufundisha kanuninyingi za injili na zinaweza kutumikakatika somo lo lote. Unaweza kualikamtu kibinafsi, kikundi au familianzima au darasa kuimba wimbounaohusikana na somo lile na hukumwingine anacheza piano ingine.Ama unaweza kucheza wimboulioimbwa na kurekodiwa.

Mwalimu mmoja alitayarisha somojuu ya huduma. Akachagua wimboulio ambatana na madhumuni yake.Wakati wa somo, akaalika dadammoja kusoma maneno ya ulewimbo na huyu dada mwingineakauimba kwa sauti iliyo nyororoAkawauliza darasani kwa upolekwaza juu ya maneno yaliyokuwa

sauti yake na uso kuvutia watotokwa masomo. Washiriki wa darasawakayajua na kuyapenda maandikomatakatifu zaidi.

Tumia Picha na VifaaMara kwa mara Mwokozi alitumiavifaa vilivyo rahisi alipokuwaakifundisha. Alitumia mifano yangano, mchanga, mawe, na vituvinginevyo vilivyosaidia watukuelewa yale aliyokuwa anafundisha.Kwa mfano, Alifananisha ufalme waMungu kwa hazina iliyo kubwa sanahata mtu lazima auze yote aliyonayoili akaipate.

Angalia pahali ulipo. Ni vitu ganivya kawaida unavyoweza kutumiakusaidia washiriki darasani kuelewakanuni za injili zaidi.

Ungependa kutumia picha namichoro iliyo ya kawaida kuongezakufahamu kanuni za injii. Onyeshapicha kutoka kwa zana ya michoroya picha za Injili kutoka MaandikoMatakatifu. Chora picha zilizo rahisiubaoni au kwa karatasi kusaidiakuchangamsha hadithi yako.

Mwalimu mmoja alipeana somo juu ya mfano wa ngano na magugu.Washiriki wa hilo darasa walikaakatika eneo la ulimaji. kwa hivyomwalimu alijua wataelewa kwambamimea ya ngano inaweza kuharibiwana magugu yakitolewa mapema.Akatayarisha kifurushi wa bengu ya

9

Page 15: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

“Ni msingi gani isipokuwamwamba wa Kristo ambao watu hujenga maisha yao wakatimwingine?”

“Jinsi gani umebarikiwa vileulivyojenga maisha yako katikamwamba wa Kristo?”

• Uliza maswali yanayo sitawishaushirikiano wa maono na uzoefuwa kibinafsi kati ya washiriki. Kwa mfano:

“Kwa nini Bwana anatuhimizakuomba kila wakati?”

“Jinsi gani amejibu maombi yako?”

• Uliza maswali yanayosaidiawashiriki kutumia kanuni za injilikatika maisha yao. Kwa mfano:

“Tunawezaje kujitayarishawenyewe vyema ili kupokeamajibu kwa maombi yetu?”

“Unawezaje kuja kujua kwambaYesu Kristo ndiye Mwokozi waulimwengu?”

“Unawezaje kutilia nguvuushuhuda wako kwamba JosephSmith ni nabii wa Mungu?”

Ukiulizwa swali ambalo huwezikujibu, uliza washiriki wa darasakukusaidia kujibu, au mwambiealiyeuliza kwamba utampa jibuwakati ufuatayo.

Usijishugulishe kama washirikihunyamaza kwa muda mchache

yakisomwa. Huu wimbo ulisaidiawashiriki kuhisi juu ya umuhimu wa huduma zaidi.

Uliza Maswali Yanayoalika KutoaMaoni na Kukuza MajadilianoKuuliza maswali yanayofaahusitawisha kutafakari katikamafunzo na majadiliano ya somolako. Maswali na majadilianohusaidia katika njia nyingi. Husaidiawashiriki kuwa wasikivu wakati wa somo. Unaweza kuangalia kamawashiriki wa darasa wanaelewasomo. Wanaweza kufundishanawanapojibu na kujadiliana juu yamaswali. Wanaweza kujifunza jinsiya kuendesha maisha yao kulinganana kanuni za injili.

Unavyotayarisha masomo, azimu juuya yale maswali ya kuuliza. Maoniyafuatayo yanaweza kukusaidia.

• Uliza maswali yanayosaidiawashiriki kufikiri juu ya kanuni lainjili na jinsi ya kulitumia maishanimwake. Maswali yanayositawishafikira huanza na “Kwa nini?” Au“Jinsi gani?” Ujiepushe na kuulizamaswali yanayojibiwa na “ndio”au “la” au neno moja moja.

Kwa mfano, katika mafundisho juu ya kutazamia Mwokozi kamaMkuu katika maisha yetu, unawezakuuliza maswali kama yafuatayo.

“Ni maana gani kujenga maishayetu juu ya mwamba wa Kristo”.

10

Page 16: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

wa tawi kabla ya kualika mgenianayeishi nje ya kata au tawi lako.

Kwa mfano raisi wa jamii ya wazeemmoja alialika mshiriki mwinginekuja na kuwaelezea wazee juu ya njia za kuvutia za kufundisha masomoya nyumbani kwa watoto waliokuwawakiwatembelea. Wazee hawakupatatu ufahamu upya juu ya umuhimu wawatoto kushiriki katika majadilianowakati ule wa mafundisho nyumbani,Lakini vilevile walipokea maonomengi juu ya jinsi ya kuwasaidiakushiriki.

Tumia ShughuliShughuli zilizo rahisi na kuhusika na somo husaidia washiriki, zaidiwatoto na vijana kusoma kanuni zainjili. Shughuli zinazofaa kama hizihusitawisha masomo ya injili. Vitabuvingi vya mafundisho vya Kanisahupeana ushauri juu ya hizishughuli.

baada ya kuwauliza swali. Wakatimwingine wanahitaji wakati wa kufikiri juu ya jibu. Lakini,ikionekana kama hawajui jibu,unaweza kuuliza kwa njia nyingine.Ukiuliza mtu swali, Inafaa kumuitakwa jina lake la kwanza na halafukuuliza swala.

Mwishowe usijaribu kuyakomeshamajadiliano mazuri juu ya somoshauri uharakishe kufikisha somo lilemwisho. Ya muhimu zaidi ni kuhisiushawishi wa Roho, Kusitawishakuelewa kwao kwa injili katika maishayao, na kuwahimiza kufuata injili.

Alika Wageni MaalumWakati mwingine ungependa kualikawageni maalum katika darasa lako.Unaweza kuuliza mshiriki wa Kanisaanayestahili kupeana ripoti, kushirikina hadithi, au kushuhudia. Mjulishemapema huyu mtu, kipimo chawakati anaweza kutumia. Pataruhusa kutoka kwa Askofu au raisi

11

Page 17: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

• Nakili za maandiko matakatifu zakutumika na washiriki wa darasa.

• Magazeti ya Kanisa yaliyo namafundisho ya manabii wa siku za mwisho.

• Vifaa vya mafunzo ya maandikomatakatifu katika lugha yako.

• Picha za namna moja ambazohuitwa zana za Michoro ya Pichaza Injili, inayopaswa kupatikanakatika maktaba ya nyumba yamikutano.

Chunguza vifaa vinavyopatikana iliutayarishe jinsi ya kuvitumia katikamasomo yako. Sio lazima uwe navifaa vilivyo bora ili ufundishevifaavyo. Kristo alifundisha masomo

Yakubidi kutayarisha masomo yakufundisha kwa makini ili uwezekufundisha kanuni za injili kwa njia ifaayo. Modokezo yafuatayoyatakusaidia kujitayarisha.

Tambua Mahali Pa Kutoa MafunzoKanisa limetayarisha, kwa makinivifaa vya masomo vilivyo idhiniwavya kuambatana na maandikomatakatifu, na mafundisho yamanabii wa siku za mwisho. Ulizakiongozi wa kuhani au wa usaidiziwa tawi kama vifaa vituatavyo vimoili vitumiwe.

• Kitabu cha mwalimu kilichobainishwa na Kanisa kutumikadarasani.

Tayarisha Somo Lako

12

Page 18: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

yao?” Masomo mengi katika vitabuvilivyotolewa na Kanisa huwapamoja na sentensi ya madhumuni.Sentensi hizi zitaweza kukusaidiakuamua jinsi kila fundisholitawavutia wale utafundisha.

Amua ya KufundishaBaada ya kuamua ni nini madhumuni la somo, amua kanuni ambazoutafundisha ili kuthibitishamadhumuni yako. Vitabu vingi vyamasomo huwa pamoja na maandikomatakatifu, hadithi, na habarinyingine za kukusaidia ufundishesomo. Mara nyingi somo lina habarinyingi kushinda wakati uliopewakuyafundisha kwa mara nyingi.Chagua vifaa ambavyo vinakuwa nausaidizi kwa wale utakawafunza.Jiulize, ni maagizo na kanuni ganikatika somo hili zitafaa zaidi kwakufundisha washiriki ili kuwawezeshakushindana na changamoto zinazo-wakumba wakati huu?”

Ukihitaji kutumia mafundisho zaidi yayale yanayopatikana katika kitabu chamafundisho na maandiko matakatifu,wazia kutumia hadithi na matamko ya uraisi wa kwanza, mafundisho yamwalimu wa kutembelea, na magazetiya Kanisa, haswa mafundisho yamkutano kuu wa kanisa.

Unavyo wasia wa kufundisha:

• Kwa maombi, soma yaliyomokatika lile somo.

mengi katika hali ya unyenyekevu.Kilicho chenye kukushawishi katika mafundisho yako ni Roho.Unapotumia vifaa vya kufundishakwa njia ifaayo na kuongezwa naRoho ndipo utakapo faulu zaidikatika mafundisho yako.

Tayarisha MapemaTayarisha masomo yako mapema.Wakati mwingine inafaa zaidiukianza kutayarisha masomo yakowiki kadhaa kabla ya kuyafundisha.Hii inakupatia nafasi ya kufikiri nakuomba kuhusu vichwa vya masomona kujitayarisha vya kutosha.

Tia Mkazo Katika Madhumuni la SomoKila somo unalofundisha lazima liwe na madhumuni. Kwa mfano,madhumuni la somo juu ya kufungalinaweza kusaidia washiriki darasanikuelewa baraka za kufunga auumuhimu wa kufunga kwa kusudimaalum siku ya Jumapili ya kufunga.Maana ya kufundisha na majadilianolazima yatilie mkazo hilomadhumuni.

Kwa kuamua juu ya madhumuni lasomo soma maandishi ya kitabu chakufundisha na maandiko matakatifuyanayombatana. Omba Bwanaakusaidie uelewe habari iliyomuhimu zaidi katika somo hili kwa manufaa ya wale unafundisha.Jiulize, “Somo hili litafaidisha vipiwale ninafundisha katika maisha

13

Page 19: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

kubadilisha tabia zake. Mshiriki wadarasa ile alisaidiwa sana kurekebishamaisha yake alipoisikia hadithi hii.

Kwa taarifa zaidi kuhusu njia yamafunzo yatakayokusaidiakufundisha somo hili, o na ukurasawa (pages 8–11) ya kitabu hiki chamwongozo.

Panga MwishoMara nyingi Mwokozi alieleza kwa kifupi yale aliyofundisha na kuwahimiza kuyatumia yalemafunzo maishani mwao (onamsemo wa Msamaria Mwema Luka10:30–37). Unapomaliza somo, lazimauyarudie masomo hayo kwa kifupi.Utawashauri jinsi ya kutumia hayamaagizo au kanuni maishani nakuwaalika kutoa maoni juu ya njiazingine. Wape shauri kujaribu njiamoja ya hayo wiki ijayo. Katikamasomo yafuatayo, waulize kuelezayale wamejifunza kutokana na bidii zao.

Mwalimu katika darasa mojaaliwaalika wanafunzi wakekuhudumia kwa kisiri kila siku kwa wiki. Mwanzoni wa kila somo,mwalimu aliwauliza kueleza jinsiilivyokuwa kwa kifupi. Washirikiwengi katika darasa hilowakashirikiana kwa shauku nafuraha juu ya yale yaliyotokea nakusema furaha iliyowapata walipohudumu. Shauku hii ikawatiawengine wao moyo wa kuhudumiawengine zaidi kwa kipekee.

• Orodhesha mafundisho na kanuniyaliyo muhimu katika somo lile.

• Wakati wo wote, kumbuka mahitajina mazigira ya wote unaofundisha.

• Fuata uongozi wa Roho.

Ni vizuri sana kuweka mkazo katikakanuni moja au mbili tu.

Amua Jinsi UtafundishaUkiamua juu ya yale utakayofundisha,lazima uamue jinsi ya kuyafundisha.Somo kwa dhati mafundisho hayo na kwa maombi tafakari juu ya njiainayofaa zaidi kuyafundisha. Njia za kutumia yapasa kusaidia wasomikuelewa na kuyatumia yaleunafundisha.

Kwa uangalifu soma maandikomatakatifu, hadithi na maandikomengine yaliyotajwa katika masomona maandiko yoyote matakatifu yale yatakusaidia kufundisha agizo au kanuni. Tayarisha Kuwasaidiawashiriki darasani kuelewa jinsimaandiko yatawasaidia maishanimwao (ona 1 Nefi 19:23).

Pia fikiria juu ya uwezekano wakutumia hadithi na mifano kutokamaishani mwako na yale ya washirikidarasani mwako. Kwa mfano, kijanammoja aliacha kuvuta sigara baada ya fundisho la ukuhani kuhusu Nenola Hekima ambako mwalimu alielezajinsi ndugu yake alishinda mwenendohuu. Kwani mfano huu ulionyeshakwamba mvutaji sigara anaweza

14

Page 20: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

Watoto hasa wanajifunza ushirikiano,wema, na uvumilivu. Wasaidiekutokushindwa katika eneo hizi kwakuwakumbusha mfano wa Yesu nakuwahimiza kumfuata.

Watoto wanatumaini kwa wanaamini.Wataamini yale utawafundisha. Piawatakutazama na kufuata mfanowako.

VijanaKile kipindi kati ya utoto na uzimawakati mwingine huwa wenye shidana changamoto. Washiriki wa darasawanaweza kuwa na wajibu mwingikatika familia zao, shuleni, na kazini.

Ni kwa umuhimu kuelewa waleunaowafundisha. Fikiri juu ya uzimana uzoefu wa washiriki darasanimwako. Watu wenye miaka tofautiwanamahitaji tofauti na husoma kwanjia tofauti.

WatotoWatoto wanakua kwa kimwili, kijamii,kimaoni na kiroho. Unapotayarishasomo lako, kumbuka talauta, uwezona mahitaji ya kila mtoto.

Watoto wanafurahia wingi. Tumiahadith fupii, michezo iliyo rahisi,picha, vifaa vinavyoonekana, nanyimbo yanayoendeleza shauku yao.

Elewa Wale Unaofudisha

15

Page 21: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

katika somo na mjadiliane juu yamaoni yenu.

Watu WazimaWatu wazima darasaniwanatofautiana kwa miaka, kwamaisha yao ya awali na kwa uzoefu.Tumia hizi tofauti kusitawisha darasalako. Tia washiriki hawa moyo wakushirikiana kwa hekima inayotokakwa uzoefu wao. Tumia ujuzi waomwingi.

Fundisha ukweli wa injili kwa njiarahisi. Roho Mtakatifu atawasaidiawashiriki kuelewa na kutumia ukwelihuo maishani mwao kibinafsi.

Mawaidha yafuatayo yanawezakutusaidia na kuwashawishi vijanakwa wema.

Tayarisha kila somo lihusikalo halisina maisha yao. Wasaidie kuona jinsiinjili inaweza kujibu maswali yao nakuwasaidia kuchagua vyema.

Vijana wanaweza kuhisi upweke nakutokudhaminiwa. Saidi kila mmojawao kuwa mwenye manufaa katikadarasa lako. Kuwa mmoja wa wenyekikundi kinacho tambua nguzo yainjili huwapa vijana nguvu ya Kirohona huwawezesha kuweka maishayao safi.

Onyesha kwamba unaheshimumaoni yao. Washawishi kushiriki

16

Page 22: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

bwana yake ameamua kukusanyafamilia yake pamoja kila siku kwamaombi ya jamii kwa sababu yaRoho aliyomshawishi wakati wamafundisho yake. Ameamua piakuwapeleka familia yake kwahekalu kufungwa pamoja. Kwaupendo huyu mama alimshukurumwalimu kwa jitihada alizofanyakualika Roho katika darasa lao.Hapo ndipo moyo wa mwalimuukajawa na unyenyekevu, naakaelewa ukweli wa lengo namafanikio ya kufundisha.

Unapofundisha, utabarikiwa pia nawanafunzi wako. Elimu yako juu ya injili na ushuhuda wa Mwokozi

Kama mwalimu, unaweza kupatafuraha ile inayopatikana kutokana nakusaidia wengine kukua katika elimuyao ya injili. Udhati, na uaminifuwako kwa kufundisha yatasaidiakuimarisha ushuhuda wa wenginekatika Mwokozi na kuwaimarishakwa kufuata amri.

Mwalimu mmoja katika darasa lamafundsiho ya Jumapili alihofiakwamba kulikuwa na wengidarasani walio hitimu kuliko yeye.Aliwasa kama mafundisho yakeyangetoa mabadiliko. HalafuJumapili moja, mshiriki wa hiyodarasa akamchukua mwalimukando. Akamwambia kwamba

17

Mafanikio ya Kufundisha

Page 23: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

unavyonyenyekea na kujaribukufuata yale unayofundisha kwabidii. Maisha yako yatajaziwa kwasababu ya huruma wako kamamwalimu.

utaongezeka vile unavyosoma,kutayarisha na kufundisha masomoya injili. Utahisi upendo mwingi kwawengine. Utahisi Roho mwingi zaidiakimiminika katika maisha yako

18

Page 24: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

mafunzo ya kinyumbani na ya darasaambako mwalimu anafunza masomozaidi.

Maoni juu ya kila somo yameandikwakatika kitabu hiki cha mwongozo.Vile mkufunzi anavyotayarisha kilasomo, anapaswa kufafanua maoniyaliyo sehemu ya kichwa “Tumia Njia Mbali Mbali ya kufundisha”.Mwishoni wa kila somo, inapasamkufunzi kutilia moyo washirikikutokea yale wamesoma siku ilemaishani mwao kama katika mafunzoya darasa Kanisani au katika mafunzoya familia nyumbani. Mwenendo huu utasitawisha walimu. Ila vileilivyotajwa, inapaswa masomo hayaya mukhtasari kufundishwa kadiri ya

Mukhtasari kwa mafundisho ya Injilihuwapa washiriki wa Kanisa nafasiya kusoma na jinsi ya kuwa walimuwazuri zaidi. Mkufunzi waMukhtasari ndiye mwalimu wakuimarisha masomo au yule yuko nauzoefu zaidi ya walimu wengineambaye huitwa na askofu au raisi watawi. Muhtasari huu wawezakufundishwa wakati wa mafunzo yaJumapili au wakati mwingine ufaao.Ikiwa Mukhtasari huu hupangiwakufunzwa kwa viongozi na walimukutoka tawi fulani, unawezakufundishwa kama sehemu yamafunzo ya kawaida ya uongozi. Paleambapo watu hukaa mbali au vifaavya kawaida havitoshi mafunzo kamahaya kuendelea, ingefaa kuunganisha

Mukhtasari Juu ya Mafunzo ya Injili

19

Page 25: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

Wiki 3Tia mkazo zaidi juu ya “Fundishaukweli wa Injili,” inayopatikanakatika sehemu ya kichwa “FundishaVile Yesu Alifundisha,” himizaumuhimu wa kufundisha injili katikaimani, wazi, nauraisi, ukitumiamaandiko matakatifu, na imarishampango wa kusoma injili kwakibinafsi.

Wiki ya 4Tia mkazo kwa “Fundisha kwaRoho” inayopatikana katika sehemuya kichwa “fundisha Vile Yesualivyofundisha.” Hakikisha walimukwamba wanaweza kuwa na Rohowanapofundisha. Wasaidie kutambuana kufuata Roho.

Wiki ya 5Tia mkazo kwa “Alika kusomakwenye Bidii” inayopatikana katikasehemu yenye kichwa “Fundisha VileYesu Alivyofundisha.” Himiza njiadhahiri ambazo walimu wanawezakutumia kusaidia wale wanaofundishakubali wajibu wa kujifunza injili nakutii amri yake kikamilifu.

Wiki ya 6Tia mkazo kwa “Kuza Hali yaKusoma,” inayopatikana katikasehemu yenye kichwa “FundishaVile Yesu Alivyofundisha.” Wasaidie

wiki nane kulingana na hati ifuatayo.(Maandiko ya muhtasasi ya wikikumi na mbili yapatikana katikakitabu cha Teaching, No Greater Callkufundisha, mwito usiyo kusaida, naitumike inapopotikana.) Madokezohaya yanahusika na mkufunzi.

Wiki ya KwanzaPatia kila mshiriki wa darasamwandiko sawa wa hiki kitabu chamwongozo, na mkaangalieyaliyomo. Tia mkazo kwenyeutangulizi na sehemu yenye kichwa“Jitayarishe Mwenyewe Kiroho.”Himiza umuhimu wa kuteuliwa nakutii injili ili uweze kuwa na Roho.

Wiki ya 2Tia mkazo kwa “Penda waleunaowafundisha” inayopatikanakatika sehemu yenye kichwa“Fundisha Vile Yesu Alivyofundisha.”Angalia pia tabia za rika ukurasa wa(pages 15–16) wa kitabu hiki chamwongozo. Uliza washiriki darasanikushirikishana juu ya hali njemailiyotokea walivyo jaribu kwa upendokuwaelewa au kuwasaidia jamii yaoau washiriki wengine darasani.Mnaweza pia kujadiliana jinsi walimuwanaweza kuwafikia na kulisha kilammoja kulingana na mahitaji yao,hasa waongofu wapya, wasioshughulika kamili, na washirikiwalemavu.

20

Page 26: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho

kutilia mkazo milango fulani katikasehemu yenye kichwa “Mafanikio yakufundisha.” Uliza washiriki darasanikushirikiana kwa maoni kuhusu njiaambazo waalimu wamebariki maishayao na njia ambazo nao kama waalimuwameweza kusaidia wengine.

Baada ya mwisho wa fundisho,wahimize washiriki kuendeleakujiboresha kama waalimu. Ikiwa niwalimu wapya ambao wameitwa,kiongozi wao wa kuhani au msaidiziwa uraisi anapaswa kukutana nao nakuwakabilisha kwa kifupi kuhusulile darasa na washiriki wake.Baadaye, inawapasa kupeana ripotikwa huyu kiongozi kila mara iliwajadiliane kuhusu mahitaji nachangamoto yao. Wanaweza kualika kiongozi kwa darasa lao-Kuwasaidia iwezekanavyo.Mkufunzi anayehusika na kuboreshakwa waalimu anaendelea kufanyahivyo kwa wale waalimu ambaowameitwa kufunza kwa madarasa nawale wanao fundisha familia zao hawana wajibu wa kuongoza.

washiriki kuelewa jinsi ya kusaidiakukuza hali ambayo kila mtuanashiriki na wana hamu yakusoma.

Wiki ya 7Tia mkazo kwa sehemu yenyekichwa “Tumia Njia Mbali Mbali yakufundisha.” Kutunga somolinalofaulu huhitaji kutafakari nakuvumbua, na mafunzo kutokasehemu hii yaweza kusaidia sana.Uliza washiriki darasani kuonyeshaau kushirikiana kwa uzoefu walionaoau waliopata kutokana na mafunzoya kufundisha yaliyo jadiliwa katikasehemu hii.

Wiki ya 8Tia mkazo sehemu yenye kichwa“Tayarisha somo Lako.” Saidiawashiriki darasani kuelewaumuhimu wa kuanzisha matayarishoya somo mapema, na jadiliana jinsiya kutunga na kufundisha masomoyanayofaa.

Wakati ufaao mafundisho haya yamuhktasari yakiendelea, unaweza

21

Page 27: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho
Page 28: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho
Page 29: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho
Page 30: Kitabu cha mwongozo – Mafundisho