Top Banner
HakiElimu •Mtaa wa Mathuradas Na. 739 • SLP 79401 Dar es Salaam, Tanzania • Simu: +255 22 2152449 • Barua pepe: info@hakielimu.org • Tovuti: www.hakielimu.org Toleo la 28, 2011 | ISSN 1821 5076 Na Robert Mihayo, Dar Es Salaam Katiba, ni msingi wa sheria na sera zote za nchi husika. Hivyo ni nadra kubadilika mara kwa mara. Lakini huweza kubadilishwa pale jamii inapoona umuhimu wa kufanya hivyo kwa nia ya kuiboresha. Sasa hivi watanzania tunajadili mchakato utakaotumika katika kuibadili katiba ya nchi yetu. Wananchi wamekuwa wakihamasishwa kuitumia fursa hii vizuri ili muda wa kutoa mapendekezo ya katiba mpya utakapofika, waweze kuleta mapendekezo yatakayoboresha maisha yao kutokana na kuwa na katiba bora. Ni dhahiri kuwa kuna maeneo mengi yanayohitaji kuboreshwa. Moja ya maeneo hayo ni sekta ya elimu ambayo ndiyo nguzo mama ya sekta nyingine zote zikiwemo uchumi, afya, kilimo, sheria, jamii na kadhalika. Elimu ndiyo njia pekee inayowezesha nchi kujenga raslimali watu ili kupambana na adui umasikini, kuboresha afya na katika kujenga nchi yenye uchumi imara Kupitia mipango ya Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na wa Sekondari (MMES), mnamo mwaka 2010, idadi ya shule za msingi ilipanda kutoka 11,873 mnamo mwaka 2001 hadi 15,816 wakati idadi ya watoto walioandikishwa iliongezeka takribani mara mbili kutoka 4,875,185 mwaka 2001 to 8,419,305 mwaka jana, 2010. Idadi ya shule za sekondari pia imepanda sana kutoka shule za sekondari 937 mwaka 2001 hadi shule 4,266 mwaka 2010; ikiwa ni ongezeko la 355%! Kila kata ina walau shule moja ya sekondari! Wakati idadi ya wanafunzi 638,699 walioandikishwa katika shule za sekondari mwaka 2010, mwaka 2001 ni wanafunzi 289,699 tu ndio walioandikishwa. Kwa hakika haya siyo mafanikio ya kubeza kwani hakuna nchi ambayo imeweza kupiga hatua za maendeleo kwa kuendelea kutotoa vijana wanaoelea katika bahari ya ujinga! Tatizo ni kuwa upanuzi huu wa elimu ya msingi na sekondari hauendi sambamba na malengo yanayobainishwa katika Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ambayo ni pamoja na kuwaandaa wanafunzi kujiunga na ulimwengu wa kazi, kumwezesha kila mtoto kupata mbinu za kupata njia za kutatua matatizo, kujenga uwezo wa kujifunza, uwezo wa kujiamini na kujiendeleza katika masuala ya sayansi na teknolojia n.k. Utafiti uliofanywa na HakiElimu mwaka 2008 ulionesha kuwa, “Ingawa shule nyingi zimejengwa na walimu wengi zaidi kuajiriwa, na wanafunzi wengi kuandikishwa …ubora wa elimu haujaimarika sana.” Pia Shirika la Uwezo, limebaini kuwa kati ya wanafunzi 10 wanaomaliza darasa la saba, wanafunzi watatu hawawezi kufanya hesabu za darasa la pili. Aidha, takribani mhitimu mmoja wa elimu ya msingi kati ya wahitimu watano, hawezi kusoma hata Kiswahili cha darasa la pili. Kwa kifupi ni kuwa uwezo wa wanafunzi kusoma, kuhesabu, kuandika, kuongea, kujenga hoja, kujiamini, kuwa wabunifu umezidi kupungua kadri siku zinavyopita. Matokeo ya mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2010 yalionesha kuwa ni asilimia 12 tu ya watahiniwa waliofanya mtihani huo ndio waliofaulu kwa kiwango cha Divisheni 1 hadi 3! Karibu nusu ya watahiniwa walipata divisheni 0; na asilimia 88% walipata divisheni 4 na 0. Shule zilizoongoza kwa kufanya vibaya ni shule za kata ambako ndiko watoto wa walalahoi wamesheheni. Ni dhahiri kuwa kuna kasoro kubwa katika mfumo wa elimu yetu. Enzi za Mwalimu, kulikuwa na Sera ya Ujamaa na Kujitegemea. Katiba ya mwaka 1977, ilitamka wazi kwamba kila mtu alikuwa ana haki ya kuelimishwa na kila mtu alikuwa na uhuru wa kutafuta elimu katika fani aipendayo kwa uwezo na upeo wake. Hivyo mtoto wa mkulima masikini aliweza kusoma darasa moja na mtoto wa Hakimu wa Tarafa hiyo; na kama angechaguliwa kwenda shule ya sekondari angeweza kusoma darasa moja na mtoto wa Mkuu wa mkoa, Waziri au hata wa Rais na kushirikiana nao katika hali ya usawa kabisa! Wakati huo, Serikali iligharamia elimu kwa kutumia kodi za wananchi. Elimu ilikuwa ni mojawapo ya huduma za jamii. Mwalimu Nyerere alipenda kila mtoto apate elimu bora itakayomwezesha kukabiliana na changamoto atakazokumbana nazo katika maisha yake na ya jamii yake. Lakini baada ya kuingia masoko huria, sera zilibadilika na kuwataka watu “wachangie” katika uendeshaji wa elimu, kile kifungu cha katiba kilibadilishwa na kusomeka; “Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, …” Yaani watu walipe kodi, lakini watumie kipato chao kidogo, kulipia huduma za jamii, hii ni sawa na kulipa kodi mara mbili! Katiba mpya inayokuja lazima ifute sera hii, kwa kuwa inaligawa taifa. Tofauti na enzi za Mwalimu ambapo watoto wote walikuwa na haki ya kupata elimu bora itakayowasaidia katika maisha yao na jamii zao, sasa elimu bora inatolewa kwa watoto wa matajiri, watoto wa walalahoi hawana fursa hiyo tena. Hii imejenga matabaka ya walio nacho na wasionacho. Kwa mfano shule zenye vifaa muhimu vya kufundishia na walimu wa kutosha ni za gharama kubwa; hivyo wanaoweza kusomesha watoto wao huko ni matajiri tu. Shule za serikali na kata ambazo zinatoa elimu kwa gharama nafuu ambako ndiko watoto wa masikini wamerundikana, hazina vifaa kama maabara, maktaba, vitabu wala walimu bora au wa kutosha, madarasa yamefurika. Idadi kubwa ya watoto waliofanya vibaya katika mtihani wa Kidato cha 4 ni wale waliokuwa wakisoma katika shule za kata ambazo ni viota vya kutotoa watoto wanaopata elimu ambayo haitawasaidia lolote maishani mwao wala ya jamii zao. Wakati umasikini unazidi kuwaelemea watanzania wengi, shule zinazotoa elimu bora zinazidi kuwa za gharama kubwa! Tofauti na enzi za Mwalimu, elimu sasa si huduma ya jamii bali ipo kibiashara zaidi. Mathalani, ada ya kumusomesha mtoto kwa mwaka mmoja katika baadhi ya shule hizi ni zaidi ya ada anayolipa mwanafunzi anayesomea shahada ya uzamili pale Mlimani! Sera za kibaguzi za aina hii zinaligawa taifa. Katiba ijayo ifute ubaguzi wa aina hii. Katiba irekebishwe ili kuondoa matabaka kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho katika elimu. Katiba Ijayo Ifute Ubaguzi Katika Elimu Tunahitaji katiba itakayomwezesha mtoto wa mkulima masikini kusoma darasa moja na mtoto wa Mkuu wa mkoa, Waziri au hata wa Rais kama Ibara ya 11 ibara ndogo ya (2) isomeke“kila mtu ana haki ya kuelimishwa na kila mtu ana uhuru wa kutafuta elimu katika fani aipendayo kwa uwezo na upeo wake” na ibara ndogo ya (3) vile vile isomeke Serikali itakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.
4

Katiba Ijayo Ifute Ubaguzi Katika Elimuhakielimu.org/files/publications/SautiElimu 28 6-9-11.pdfkatiba ya nchi ni kitu gani. Pia ni vizuri wananchi wajue historia ya katiba tulizowahi

Jan 08, 2020

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Katiba Ijayo Ifute Ubaguzi Katika Elimuhakielimu.org/files/publications/SautiElimu 28 6-9-11.pdfkatiba ya nchi ni kitu gani. Pia ni vizuri wananchi wajue historia ya katiba tulizowahi

HakiElimu •Mtaa wa Mathuradas Na. 739 • SLP 79401 Dar es Salaam, Tanzania • Simu: +255 22 2152449 • Barua pepe: [email protected] • Tovuti: www.hakielimu.org

Toleo la 28, 2011 | ISSN 1821 5076

Na Robert Mihayo, Dar Es Salaam

Katiba, ni msingi wa sheria na sera zote

za nchi husika. Hivyo ni nadra kubadilika

mara kwa mara. Lakini huweza

kubadilishwa pale jamii inapoona

umuhimu wa kufanya hivyo kwa nia ya

kuiboresha.

Sasa hivi watanzania tunajadili mchakato

utakaotumika katika kuibadili katiba ya

nchi yetu. Wananchi wamekuwa

wakihamasishwa kuitumia fursa hii vizuri

ili muda wa kutoa mapendekezo ya katiba

mpya utakapofika, waweze kuleta

mapendekezo yatakayoboresha maisha

yao kutokana na kuwa na katiba bora.

Ni dhahiri kuwa kuna maeneo mengi

yanayohitaji kuboreshwa. Moja ya

maeneo hayo ni sekta ya elimu ambayo

ndiyo nguzo mama ya sekta nyingine zote

zikiwemo uchumi, afya, kilimo, sheria,

jamii na kadhalika.

Elimu ndiyo njia pekee inayowezesha

nchi kujenga raslimali watu ili kupambana

na adui umasikini, kuboresha afya na

katika kujenga nchi yenye uchumi imara

Kupitia mipango ya Maendeleo ya Elimu

ya Msingi (MMEM) na wa Sekondari

(MMES), mnamo mwaka 2010, idadi ya

shule za msingi ilipanda kutoka 11,873

mnamo mwaka 2001 hadi 15,816 wakati

idadi ya watoto walioandikishwa

iliongezeka takribani mara mbili kutoka

4,875,185 mwaka 2001 to 8,419,305

mwaka jana, 2010.

Idadi ya shule za sekondari pia imepanda

sana kutoka shule za sekondari 937

mwaka 2001 hadi shule 4,266 mwaka

2010; ikiwa ni ongezeko la 355%! Kila

kata ina walau shule moja ya sekondari!

Wakati idadi ya wanafunzi 638,699

walioandikishwa katika shule za

sekondari mwaka 2010, mwaka 2001 ni

wa n a f u n z i 2 8 9 , 6 9 9 t u n d io

walioandikishwa. Kwa hakika haya siyo

mafanikio ya kubeza kwani hakuna nchi

ambayo imeweza kupiga hatua za

maendeleo kwa kuendelea kutotoa vijana

wanaoelea katika bahari ya ujinga!

Tatizo ni kuwa upanuzi huu wa elimu ya

msingi na sekondari hauendi sambamba

na malengo yanayobainishwa katika Sera

ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995

ambayo ni pamoja na kuwaandaa

wanafunzi kujiunga na ulimwengu wa

kazi, kumwezesha kila mtoto kupata

mbinu za kupata njia za kutatua matatizo,

kujenga uwezo wa kujifunza, uwezo wa

kujiamini na kujiendeleza katika masuala

ya sayansi na teknolojia n.k.

Utafiti uliofanywa na HakiElimu mwaka

2008 ulionesha kuwa, “Ingawa shule

nyingi zimejengwa na walimu wengi zaidi

kuajiriwa, na wanafunzi wengi

kuandikishwa …ubora wa elimu

haujaimarika sana.” Pia Shirika la Uwezo,

limebaini kuwa kati ya wanafunzi 10

wanaomaliza darasa la saba, wanafunzi

watatu hawawezi kufanya hesabu za

darasa la pili. Aidha, takribani mhitimu

mmoja wa elimu ya msingi kati ya

wahitimu watano, hawezi kusoma hata

Kiswahili cha darasa la pili.

Kwa kifupi ni kuwa uwezo wa wanafunzi

kusoma, kuhesabu, kuandika, kuongea,

kujenga hoja, kujiamini, kuwa wabunifu

umezidi kupungua kadri siku zinavyopita.

Matokeo ya mtihani wa Kidato cha nne

mwaka 2010 yalionesha kuwa ni asilimia

12 tu ya watahiniwa waliofanya mtihani

huo ndio waliofaulu kwa kiwango cha

Divisheni 1 hadi 3! Karibu nusu ya

watahiniwa walipata divisheni 0; na

asilimia 88% walipata divisheni 4 na 0.

Shule zilizoongoza kwa kufanya vibaya ni

shule za kata ambako ndiko watoto wa

walalahoi wamesheheni. Ni dhahiri kuwa

kuna kasoro kubwa katika mfumo wa

elimu yetu.

Enzi za Mwalimu, kulikuwa na Sera ya

Ujamaa na Kujitegemea. Katiba ya

mwaka 1977, ilitamka wazi kwamba kila

mtu alikuwa ana haki ya kuelimishwa na

kila mtu alikuwa na uhuru wa kutafuta

elimu katika fani aipendayo kwa uwezo

na upeo wake.

Hivyo mtoto wa mkulima masikini

aliweza kusoma darasa moja na mtoto wa

Hakimu wa Tarafa hiyo; na kama

angechaguliwa kwenda shule ya

sekondari angeweza kusoma darasa moja

na mtoto wa Mkuu wa mkoa, Waziri au

hata wa Rais na kushirikiana nao katika

hali ya usawa kabisa!

Wakati huo, Serikali iligharamia elimu

kwa kutumia kodi za wananchi. Elimu

ilikuwa ni mojawapo ya huduma za jamii.

Mwalimu Nyerere alipenda kila mtoto

apate elimu bora itakayomwezesha

k u k a b i l i a n a n a c h a n g a m o t o

atakazokumbana nazo katika maisha yake

na ya jamii yake.

Lakini baada ya kuingia masoko huria,

sera zilibadilika na kuwataka watu

“wachangie” katika uendeshaji wa elimu,

kile kifungu cha katiba kilibadilishwa na

kusomeka; “Kila mtu anayo haki ya

kujielimisha, …” Yaani watu walipe kodi,

lakini watumie kipato chao kidogo,

kulipia huduma za jamii, hii ni sawa na

kulipa kodi mara mbili! Katiba mpya

inayokuja lazima ifute sera hii, kwa kuwa

inaligawa taifa.

Tofauti na enzi za Mwalimu ambapo

watoto wote walikuwa na haki ya kupata

elimu bora itakayowasaidia katika maisha

yao na jamii zao, sasa elimu bora

inatolewa kwa watoto wa matajiri, watoto

wa walalahoi hawana fursa hiyo tena. Hii

imejenga matabaka ya walio nacho na

wasionacho.

Kwa mfano shule zenye vifaa muhimu

vya kufundishia na walimu wa kutosha ni

za gharama kubwa; hivyo wanaoweza

kusomesha watoto wao huko ni matajiri

tu. Shule za serikali na kata ambazo

zinatoa elimu kwa gharama nafuu

ambako ndiko watoto wa masikini

wamerundikana, hazina vifaa kama

maabara, maktaba, vitabu wala walimu

bora au wa kutosha, madarasa

yamefurika. Idadi kubwa ya watoto

waliofanya vibaya katika mtihani wa

Kidato cha 4 ni wale waliokuwa

wakisoma katika shule za kata ambazo ni

viota vya kutotoa watoto wanaopata

elimu ambayo haitawasaidia lolote

maishani mwao wala ya jamii zao.

Wakati umasikini unazidi kuwaelemea

watanzania wengi, shule zinazotoa elimu

bora zinazidi kuwa za gharama kubwa!

Tofauti na enzi za Mwalimu, elimu sasa si

huduma ya jamii bali ipo kibiashara zaidi.

Mathalani, ada ya kumusomesha mtoto

kwa mwaka mmoja katika baadhi ya shule

hizi ni zaidi ya ada anayolipa mwanafunzi

anayesomea shahada ya uzamili pale

Mlimani! Sera za kibaguzi za aina hii

zinaligawa taifa. Katiba ijayo ifute

ubaguzi wa aina hii.

Katiba irekebishwe ili kuondoa matabaka kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho katika elimu.

Katiba Ijayo Ifute Ubaguzi Katika Elimu

Tunahitaji katiba itakayomwezesha mtoto wa mkulima masikini kusoma darasa moja na mtoto wa Mkuu wa mkoa, Waziri au hata wa Rais kama Ibara ya 11 ibara ndogo ya (2) isomeke“kila mtu ana haki ya kuelimishwa na kila mtu ana uhuru wa kutafuta elimu katika fani aipendayo kwa uwezo na upeo wake” na ibara ndogo ya (3) vile vile isomeke “ Serikali itakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.

Page 2: Katiba Ijayo Ifute Ubaguzi Katika Elimuhakielimu.org/files/publications/SautiElimu 28 6-9-11.pdfkatiba ya nchi ni kitu gani. Pia ni vizuri wananchi wajue historia ya katiba tulizowahi

Na, Mchungaji Dr. Lechion Peter Kimilike Katiba iliyopo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ninaielewa vizuri pamoja na marekebisho yake. Hii ni kwa sababu mabadiliko yake yamechangia sana hali za maisha ya watu wengi walio katika rika langu kielimu, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kipengele cha msingi ambacho ningependa kizingatiwe kwa umakini zaidi katika kuboresha maisha, ni nafasi ya ujenzi wa dhamira ya utaifa au uzalendo. Jambo hili ni nguzo ya maendeleo na kwa kipindi kirefu limepuuzwa na matokeo yake ni kuongezeka kwa kasi ya mmomonyoko wa maadili. Ni kweli kwamba Katiba iliyopo inasema Tanzania haina dini ila Watanzania wanazo dini zao. Kwa kipengele hicho Serikali imeacha suala la dini liwe huria wakati dini pekee ndiyo yenye uwezo wa kujenga utamaduni, mila na desturi. Matokeo ya mfumo huu

huria ni hii hali iliyopo sasa ambayo mambo yanakwenda kinyume na utaifa au uzalendo. Hivi sasa watoto na vijana wengi wa kitanzania hawalelewi katika utu stahiki unaolenga mstakbali wa Taifa lao. Kawaida dini zinahusishwa na ardhi ambapo thamani ya utu na uhuru ndipo hujikita. Kwa sasa kizazi cha baada ya uhuru kimeendelea kuondolewa kutoka katika ardhi na hivyo kujenga Taifa la wakimbizi au watumwa wasiokuwa na kwao. Kwa mfano wale waliokuwa wanaishi kwa ufugaji wamenyang’anywa ardhi na sasa wanatangatanga nchi nzima. Aidha, idadi kubwa ya watu sasa hawamiliki ardhi bali wanaishi kwa kupanga nyumba na mashamba. Kwa namna fulani historia inafutika katika maisha ya watu na hivyo si rahisi kuendelea na mema ya wahenga. Ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu kuunda katiba mpya unapaswa

kuzingatia ulinganifu wa watu wa kada mbalimbali katika maeneo ya kijiografia na fursa mbalimbali za kimaisha. Kwa maana hiyo ukusanyaji maoni utoe fursa sawa kwa wananchi wote. Serikali isiogope gharama kwa kuwa suala la kubadilisha katiba limegusa hisia ya umma na wawe tayari kubeba majukumu hayo kwa kuwa ni kazi yao kuhudumia wananchi kwa maslahi ya Taifa. Aidha, Serikali itoe muda wa kutosha kuanzia katika kuandaa muswada, kutoa maoni, kushirikishwa kwa wananchi. Serikali haipaswi wala kwenda haraka, kwani inaweza kuwafanya wananchi wahisi kuwa kuna ajenda ya siri nyuma yake pengine ya kukidhi matakwa ya wachache. Mwisho Serikali ijitahidi kudhibiti siasa isitawale zaidi kwenye mchakato wa Katiba bali kuwepo na ulinganifu wa kutosheleza fani zingine za uchumi, kijamii na dini.

Wananchi Wote Wapewe Fursa Kutoa Maoni Kuhusu Katiba

Na Mussa Msengi Gunda Katika ulimwengu hakuna maendeleo endelevu yanayoweza kufikiwa bila ya kuwashirikisha kikamilifu wananchi katika shughuli za maendeleo ya kijamii na kitaifa kwa ujumla. Maendeleo haya hutokea pale wananchi wanaposhiriki katika kuchangia jambo husika kwa matumaini kuwa ipo siku hali itaboreka kuliko ilivyo sasa. Ushiriki wa wananchi ni pamoja na kupewa fursa za kutambua na kuelewa vizuri kile wanachotakiwa kushiriki ili waweze kukipa msukumo zaidi. Kwa bahati mbaya katika nchi yetu mambo mengi yamekuwa yakifanyika bila hata kuwashirikisha wananchi kwa kiasi kikubwa na hata kama watashirikishwa basi mawazo yao yatakuwa “yanatengwa” tu. Mathalani, watajiuliza je, mawazo yaliyopendekezwa na wananchi yanafanana na ya viongozi? Inapokuja katika suala la utekelezaji panakuwepo na mkanganyiko katika baadhi ya majukumu kwa wananchi, huwafanya kuona jambo fulani haliwahusu na kama linawahusu basi halitafanyika kwa moyo wa dhati. Matokeo yake ni kuwepo kwa ubadhirifu, hujuma na hata kutokamilika kwa miradi husika. Leo hii Tanzania tuko katika mjadala wa uandikaji wa “Katiba Mpya”. Mambo mengi yananichanganya na huenda yanawachanganya wananchi walio wengi hususani tunaoishi vijijini. Swali la kujiuliza ni je: huu mjadala ni kwa wasomi na wanasiasa tu? Jambo hili liko wazi kwamba wananchi tulio wengi hatuelewi Katiba inasema nini kuhusu masuala mbalimbali ya nchi ikiwemo hili la ushiriki wa wananchi katika kuibadili hii katiba yenyewe. Wananchi walio wengi wanajiuliza washiriki vipi, wapi na kwa njia ipi katika

kutoa maoni ya kuandika katiba mpya ya nchi. Wananchi wengi wanafuata malumbano ya wanasiasa na wasomi kwa kusikiliza misimamo yao bila kujali na kujua yeye mwananchi ana nafasi pia ya kutoa maoni yake katika kuandaa katiba mpya. Kumekuwepo na mijadala kuhusu kuandaa katiba mpya, ni vizuri tukatambua kuwa katiba si ya mtu mmoja au ya watu fulani bali ni ya watanzania wote; mimi na wewe. Aidha, wananchi wengi hawafahamu haki, wajibu na majukumu yao kwa nchi yao. Kwa hiyo ni lazima ufanyike utaratibu mapema wa namna ya kuwaelimisha watanzania wote katika kuandaa katiba mpya na jinsi wananchi watakavyoshiriki

kikamilifu katika zoezi zima. Nahitimisha kwa kuwaomba wale wote kwa namna moja au nyingine wanaosimamia suala la kupata maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba wawasaidie wananchi kwanza kuielewa katiba iliyopo. Aidha, wanapaswa kuwafahamisha wananchi hao kuhusu umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa kuibadili katiba ili kuhakikisha kuwa rasilimali nyingi za taifa zinatumika vizuri na kuwafikia wananchi bila kumilikiwa na wachache. Tanzania yenye demokrasia na utawala bora inawezekana kama wananchi watashirikishwa kutoa mawazo yao na yakazingatiwa kwa kile wanachohitaji.

Wananchi wahamasishwe kushiriki kuandaa katiba mpya

Na, Birolele Ramadhani , Biharamulo Napenda kupendekeza hatua za msingi zinazopaswa kufuatwa katika kuandaa katiba mpya ili kuhakikisha kunakuwa na mustakabali mzuri kwa maisha yetu na taifa kwa ujumla. Kwa maoni yangu kitu cha kwanza kabisa kinachopaswa kufanywa ni kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuandaa katiba mpya kuanzia ngazi ya vitongoji na vijiji. Suala la kuwaelimisha wananchi litawasaidia kutambua na kufahamu katiba ya nchi ni kitu gani. Pia ni vizuri wananchi wajue historia ya katiba tulizowahi kuwa nazo zilikuwa zinaundwaje, na akina nani walishiriki katika kuunda katiba hizo. Hili linapasa kuhusisha katiba zote kuanzia Katiba ya Uhuru mwaka 1961, Katiba ya Jamhuri 1962, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya 1964, Katiba ya muda ya Tanzania 1965 na Katiba ya kudumu ya 1977 pamoja na marekebisho yake. Hatua nyingine ni wananchi kufahamu na kutambua katiba ya Tanzania ina mapungufu gani na iliundwa kwa kuzingatia vipengele gani na mapungufu yaliyomo ndani ya katiba hii.

Wananchi pia wanapaswa kufahamu muswada wa serikali wa marekebisho ya katiba ambao kwa maoni yangu una vipengele viwili; kipengele cha kwanza ni maana halisi ya muswada wa marekebisho ya katiba, na cha pili, muswada wa serikali wa marekebisho ya katiba kama njia ya kuunda katiba mpya. Ikumbukwe kuwa muswada huo ulipelekwa Bungeni kwa hati ya dharura, lakini baadae wananchi, wanasiasa, mashirika ya kiraia na wanaharakati walipaza sauti zao na kutamka kuwa muswada huu haukushirikisha wananchi na pia ulikuwa na makosa mengi ambayo yangehatarisha kupata katiba yenye taswira ya kuwalinda watu wachache. Baada ya wadau kupinga ndipo Bunge likatoa tamko la kurudisha muswada huo kwa wananchi ili uanze kujadiliwa upya kuanzia ngazi ya kijiji, kata, vitongoji, tarafa , wilaya, mkoa mpaka kitaifa. Ni vizuri pia kuwepo na utaratibu ambao utatupatia katiba mpya yenye taswira ya ushiriki wa wananchi, kwa maoni yangu napendekeza kuwepo na Mkutano wa katiba, Tume ya katiba, Bunge la katiba na kura za maoni.

Baada ya hapo ndio ufuate utaratibu wa uwekaji wa misingi muhimu ya uundaji wa katiba ambayo ni uhalali, ujumuisho, pamoja na uimarishaji wa jamii za kiraia. Pia itabidi pawepo ukweli na uwazi, pawepo uwezo wa matakwa ya wananchi na tathmini ya mahitaji. Aidha inapaswa pawepo uwajibikaji, na jukumu la vyama vya siasa, jumuiya za kiraia, na wanataaluma.

H a t u a Z i p i

Zifuatwe Ili Kupata

Katiba Bora?

Na Deogratious Mfuko, Gonja Maore-Same Wananchi wengi wa sasa hawana tabia ya kusoma taarifa mbalimbali zitolewazo na Serikali au hata zile zinazopatikana kwenye magazeti. Hii ni kutokana na kutojali au ni matokeo ya misingi tuliyojengewa toka katika ngazi ya familia zetu. Tabia hii inaweza kutuletea madhara makubwa hasa wakati huu wa mchakato wa kupata katiba mpya. Nimekuwa nikijiuliza swali muhimu. Je, ni watanzania wangapi wamesoma katiba ya sasa? Je, tunao wasomi wangapi ambao wanaweza kusimama na kusema wameisoma katiba vizuri na kugundua ni wapi ina makosa? Au ndio tumejenga tabia ya kusikia baadhi ya wanasiasa wakisema nasi tunaunga mkono bila hata kuchambua? Je, tunajua ni nini kimeandikwa kwenye katiba ya zamani au tunashabikia tu?

Ukweli ni huu, tusipojenga tabia ya kusoma, ni wazi kuwa katiba mpya nayo itachakachuliwa na wachache. Nionavyo mimi, bado watanzania tuna nafasi ya kusoma machapisho mbalimbali, ingawaje pia ipo changamoto ya upatikanaji wake hasa sehemu za vijijini. Hivyo kama hatuna utaratibu wa kwenda hata kwa jirani na kumuomba gazeti tusome, tutawezaje kuikosoa katiba?

Tusipojenga Tabia ya Kusoma, Katiba Itachakachuliwa

Page 3: Katiba Ijayo Ifute Ubaguzi Katika Elimuhakielimu.org/files/publications/SautiElimu 28 6-9-11.pdfkatiba ya nchi ni kitu gani. Pia ni vizuri wananchi wajue historia ya katiba tulizowahi

Na, Maxmillian J. Chuhila. Dar Es Salaam Nashukuru sana kwa SautiElimu kunipa nafasi ya kutoa maoni yangu kuhusiana na mchakato mzima wa maandalizi ya katiba mpya ambayo itakidhi matakwa ya watanzania wote. Ni tegemeo langu kwamba SautiElimu imewapa wadau wengi zaidi fursa hii ya kutoa maoni yao kuhusu suala hili. Katiba ndiyo msingi wa sheria zote zilizopo na zinazoendelea kutungwa katika nchi yetu. Hivyo ni vema kuwashirikisha wananchi katika mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba ili kukidhi matakwa ya wananchi. Kwa mtazamo wangu mchakato wa kuelekea kwenye kuandaa katiba mpya haujalenga maslahi ya watanzania walio wengi. Walengwa ni makundi fulani ya watanzania ambao wanaonekana kama ni

watanzania zaidi ya wengine. Ishara zinajionesha wazi kuwa mchakato wa kukusanya maoni umekuwa ni finyu mno kiasi ambacho hauwezi kuakisi matakwa ya wengi. Ikiwa Tanzania tuna mikoa zaidi ya ishirini na sita na raia wapatao milioni 40, inakuwaje vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kukusanya maoni ya watanzania hao wote viwe chini ya ishirini? Hivi kweli vituo hivi tunategemea vitatoa picha halisi ya maoni ya watanzania zaidi ya milioni arobaini? Maoni yatakayopatikana kwa njia hii hayawezi kutoa picha sahihi ya watanzania wanataka nini. Suala la pili la kuangalia ni je, ni kwa kiasi gani wananchi wamepewa elimu ya kutosha kuhusu namna watakavyotoa maoni yao? Je, wananchi wanaijua hiyo katiba ya zamani wanayotakiwa kuibadilisha? Wanajua ina mapungufu yapi? Kwa bahati mbaya sana, asilimia

kubwa ya wasomi, wakulima na wafanyakazi wamekuwa washabiki wa kitu wasichokijua. Vyombo mbalimabli vya habari vimesharipoti kwamba watanzania hawaifahamu katiba. Na wangelipenda kuisoma kwanza kabla ya kutoa maoni yao. Kama hali ni hiyo kwa nini basi tunafanya haraka kubadilisha katiba ambayo wananchi hata hawaifahamu? Katiba zenyewe upatikanaji wake ni mgumu sana. Katika hali ya kushangaza mpaka duka kuu la serikali ambalo lilitakiwa kuwa na nyaraka hiyo bado katiba haikupatikana. Ni mwezi wa nne 2011 ndipo nimepata toleo lenye marekebisho ya mwaka 2005 baada ya miaka sita ya kuitafuta. Hali hii inaonesha jinsi ilivyo vigumu kupata katiba. Kama mimi nimesumbuka

hivi kuipata katiba je, hali ikoje kwa watanzania walioko vijijini ambao wanaunda sehemu kubwa ya idadi yetu? Nahitimisha kwa kusema ni vizuri tukiwa na katiba mpya. Pia yatupasa kuipata katiba mpya kwa utaratibu mzuri, ulio wazi na wenye manufaa kwa kila mwananchi na si watu wachache kujinufaisha kwa mgongo wa kundi jingine.

Matukio katika picha

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu naye alikuwa mmoja wa wachangiaji. Alikuwa na haya ya kusema „Katiba Mpya ya Zanzibar inasema Zanzibar ni nchi na mipaka yake ni visiwa vya Unguja na Pemba na visiwa vidogo na eneo lake la maji ya bahari…Mipaka ya Zanzibar ni tofauti na Mipaka ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.‟ Je katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasemaje?

“Kuna umuhimu wa kuwa na Tume huru ya uchaguzi…” haya yalikuwa ni maneno ya Mwanasheria mkongwe Bw. Mabere Marando alipokuwa akichangia hoja katika kongamano la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Kongamano la Uchambuzi wa Katiba UDSM:

Na Mahmoud Akilimali, Dar es Salaam Napenda kutumia fursa hii adhimu, ya kutoa maoni yangu kuhusu umuhimu wa wananchi kujielimisha juu ya haki zetu kikatiba. Katiba ndiyo dira la utawala wa nchi. Hii inaonyesha jinsi nchi yetu ilivyokomaa kisiasa. Lakini kila kitu kina mapungufu yake. Kwanza wananchi wengi wa vijijini, ambao ni takribani asilimia 75% ya wananchi wa Tanzania hawaielewi Katiba yetu ilivyo. Hivyo ni muhimu mchakato huu wa marekebisho ukaendana na

mafunzo hata kwa kuanzia viongozi wa Kata. Huwezi, kuchangia jambo bila kuwa na hata theluthi ya uelewa! Katiba niliyoapata kuiona ni ile ya mwaka 1977, chapisho la Kiingereza. Mungu bariki naelewa Kiingereza kidogo, angalau cha kuombea maji. Ipo katiba ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili lakini imeandikwa kitaalam. Je, mkulima Masanja wa Mwanza na Kalimanzila wa Kigoma wataelewa kilichoandikwa? Tusipojielimisha au kuwaelimisha

wananchi ni dhahiri kwamba wasomi na wanasiasa watachangia vyema mchakato wa katiba na kuuteka kwa manufaa yao na siyo Taifa. Kumekuwa na manung’uniko hasa kutoka kwa ndugu zetu wa visiwani Zanzibar, hususani kuhusu suala la Muungano. Wengi wameonekana wakitaka kuwe na muungano wa serikali tatu; ya visiwani Zanzibar kama nchi, ya Tanganyika, na ile ya Muungano. Hii ni kero ya msingi, isikilizwe na kufanyiwa kazi. Lakini kuuvunja umoja si jambo la msingi. Maamuzi magumu yafanywe,

lakini na busara itumike. Kuna njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika pia ili kuwaelimisha wananchi kuhusu kuandika katiba mpya. Mathalani itasaidia kama vitakuwepo vipindi maalumu kwa njia ya redio na runinga. Labda viitwe: ''Mwananchi Ijue Katiba Yako.'' Vipindi hivyo vitakuwa muhimu kwa wananchi wengi kupata taarifa zitakazowasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Tujielimishe kuhusu haki zetu za kikatiba

M c h a k a t o wa K u b a d i l i K a t i b a Wa h i t a j i U m a k i n i

Na Wambura Wasira, Dar es Salaam

Katiba ya kudumu ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania ilitungwa mwaka

1977. Ndani ya miaka 34, Katiba hii ya

kudumu ilishafanyiwa marekebisho mara

14.

Mabadiliko ya kwanza ya katiba

yaliyopitishwa na kusainiwa mnano

Tarehe 9 Agosti Mwaka 1979 na Rais wa

kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage

Nyerere, yalilenga zaidi sura ya tano ya

katiba ya sasa inayohusu sheria

zinazoongoza shughuli za Mahakama.

Mabadi l iko makubwa ni ya le

yaliyopitishwa na kusainiwa na Rais wa

wakati huo mnamo Tarehe 16 Februari

Mwaka 1984 ikiwemo ya kuongeza

Sehemu ya Tatu ya Haki na Wajibu

Muhimu katika Sura ya Kwanza.

Ukurasa wa pili wa nakala ya sheria hii

iliyopewa jina la Sheria ya Marekebisho ya

Tano katika Katiba ya Nchi, ya Mwaka

1984, uliandika maneno yafuatayo

“Kufuta sehemu ya kwanza na ya pili

ya sura ya kwanza na kuweka

nyingine badala yake”. Mabadiliko

haya yanaonekana katika ibara ya 5 na ya

6 ya sheria hii ya marekebisho ya tano.

Moja ya sheria iliyoandikwa upya ni hii ya

Ibara 11 ibara ndogo ya (2) inayosomeka

“Kila mtu anayo haki ya kujielimisha,

na kila raia atakuwa huru kutafuta

elimu katika fani anayopenda hadi

kufikia upeo wowote kulingana na

stahili na uwezo wake”. Je, kama

mwananchi ana uwezo na upeo lakini

fedha hana hii sheria inamsaidia nini?

Kipengele kinachofuata cha (3) kinasema

“Serikali itafanya jitihada kuhakikisha

kwamba watu wote wanapata fursa

sawa na za kutosha kuwawezesha

kupata elimu na mafunzo ya ufundi

katika ngazi zote za shule na vyuo

vinginevyo vya mafunzo”.

Kipengele hiki kinawapa watendaji wa

Serikali, nafasi ya kuendelea kufanya

jitihada na siyo kuwajibika kuhakikisha

inatoa elimu bora kuanzia ngazi ya msingi

hadi chuo kikuu. Hapa Serikali

inapaswa iwajibike kuhakikisha

watoto wetu wanapata fursa sawa

katika elimu.

Matokeo yake ndiyo tunayaona sasa,

watoto wetu wanasoma katika shule

ambazo zina upungufu mkubwa wa vifaa

vya kujifunzia, kufundishia pamoja na

walimu. Pamoja na haki hiyo ya

kujisomesha waliyo nayo, je uwezo wa

kujisomesha wautoe wapi?

Kama kweli Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya

Mrisho Kikwete alitamka wazi kuwa

hakuna mtoto wa Kitanzania

atakayefukuzwa shule kwa sababu ya

kukosa ada kwa nini sasa isiwekwe

bayana katika Katiba ya Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania ili Serikali

iwajibike katika kuhakikisha mtoto wa

k i t a n z a n i a a n a p a t a e l i m u

itakayomuwezesha kupata maisha bora na

kuisaidia familia yake hapo baadaye?

Kama Hayati Baba wa Taifa alilijali taifa

hili mpaka kuwawezesha viongozi wetu

kufika hapo walipo, inakuwaje wao

wanashindwa kuona mbele na kujua kuwa

wanaendelea kuzalisha kizazi ambacho

kitaendelea kuishi katika dimbwi kubwa la

umasikini?

Katiba mpya izingatie hili; mtoto wa

kitanzania awe na haki ya kusomeshwa.

Aidha, haki hiyo ya kusomeshwa iwe ni

pamoja na haki ya kupewa vifaa muhimu

vikiwemo vitabu vya kiada na ziada,

madawati, madarasa bora, na walimu wa

kutosha, ili watoto wetu ambao ni taifa la

kesho waweze kupata elimu bora na siyo

bora elimu.

K a t i b a M p y a I t o e K i p a u m b e l e K a t i k a E l i m u

Page 4: Katiba Ijayo Ifute Ubaguzi Katika Elimuhakielimu.org/files/publications/SautiElimu 28 6-9-11.pdfkatiba ya nchi ni kitu gani. Pia ni vizuri wananchi wajue historia ya katiba tulizowahi

Na, Maxmillian J. Chuhila Mjadala unaoendelea hivi sasa kuhusu katiba upo zaidi kwa maslahi ya vyama vya siasa kuliko mustakabali wa taifa. Vyama vya siasa vinajinadi kuwa ndio waanzilishi wa mchakato huo. Ni kweli, kwani wangefanya nini kingine? Lakini inapofikia hatua tuliyopo kwa sasa mchakato hautakiwi uwe ni kwa maslahi ya chama fulani cha siasa bali ni wa kila mtanzania. Mchakato wa katiba unaonekana kumilikiwa na wanasiasa kuliko wananchi wenyewe. Ni sahihi kwamba wanasiasa ndiyo chachu ya kuongelea mambo yanayowahusu wananchi. Wanasiasa ni wawakilishi wa wananchi. Tujiulize hapa, mchakato wa katiba ni kwa manufaa ya nani? Je, ni kwa nini

basi vyama vya siasa vinalazimisha umiliki wa mchakato huo? Hisia za uvyama katika mchakato huu zinajitokeza sana katika midahalo na mijadala ambapo kila anayechangia maoni yake ni lazima aendane na upepo fulani wa kiitikadi ili akubaliwe na ashangiliwe na washiriki. Hii ni hatari sana, kwani inamnyima huyo mchangiaji hata haki yake ya kikatiba ya kutoa maoni yake kwani anaanza kuzomewa kabla hata hajamaliza maoni yake. Wengine wamekuwa wakishindwa kujieleza kama walivyotaka. Hali hii haifai. Kama ingekuwa ni lazima watu wote waongee lugha moja katika mchakato basi hakungekuwa na haja ya kushirikisha watanzania wengi.

Wanasiasa wamemiliki mchakato si kwa maslahi ya watanzania wote bali ni kwa maslahi yao wenyewe. Ukiangalia na kusikiliza kilio cha wanasiasa wetu hawa utasikia wanataka katiba ibadilishwe ili pawe na tume huru ya uchaguzi. Kwa haraka hili linamnufaisha mwanasiasa anayeona tume iliyopo haimsaidii kufikia malengo yake, pamoja na kwamba mwananchi wa kawaida anaweza kufaidika kwa kuona thamani ya kura yake aliyompigia kiongozi atakayetangazwa kihalali kushinda uchaguzi, na si lazima iwe kwa kishindo. Kipengele kingine kinacholalamikiwa na wanasiasa ni Ibara ya 39 kifungu (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, kinachomlazimisha mgombea wa nafasi ya urais kuwa mwanachama wa chama cha siasa na mteule wa chama chake kugombea nafasi hiyo. Hiki kinalalamikiwa kuwa kiachwe huru kisimlazimishe mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Ibara 41 Ibara ndogo (7) inayosema; Iwapo mgombea [Urais] ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake. Lakini pia Ibara ya 67 Ibara ndogo (1) kifungu (b) inamlazimisha mgombea ubunge kuwa mwanachama aliyependekezwa na chama chake kuwania nafasi hiyo. Hizi ndizo sehemu za haraka ambazo wanasiasa wanatamani zirekebishwe haraka iwezekavyo. Haitashangaza endapo tutasikia vipengele hivyo vimekubaliwa kurekebishwa na mchakato mzima wa katiba ukawa umeishia hapo na wanasiasa wakanyamaza kimya. Je, hayo ndiyo pekee watanzania wanataka yabadilishwe? Tujiulize ni wanasiasa wangapi wanaoongelea katiba mpya iweke ukomo wa ubunge kama kwa rais? Mtu

mmoja asiwe mbunge wakati huo huo mkurugenzi wa shirika fulani la umma, mkuu wa mkoa na kadhalika. Hawasemi haya kwa sababu yanagusa maslahi yao. Wito wangu ni kwamba muda mwingi utumike katika kuwapa elimu ya uraia watanzania walio wengi ili waijue katiba iliyopo kabla ya kuanza mchakato wa kuandaa katiba mpya. Hatari ninayoiona hapa ni ile ile inayolalamikiwa leo kuwa katiba iliyopo haikuakisi maoni ya wengi. Bila kuchukua hatua haraka hii nayo itakuwa hivyo au itaakisi maoni ya wengi wasiojua wanatoa maoni kwa ajili ya nini. Ni jukumu la vyama vya siasa, asasi za kiraia, mashirika ya dini, wanaharakati na makundi mabalimbali ya kijamii kama watanzania kusaidia kueneza elimu ya uraia kwa wenzetu ili kurahisiha mchakato wa kuandaa katiba mpya. Wanasiasa hawapaswi kuwatumia wananchi kujijengea uhalali wa kuonekana ni wanamapinduzi, na hivyo kujikusanyia umaarufu wenye faida katika chaguzi kuu zijazo. Watende wanachohubiri bungeni kwa maslahi ya taifa kwanza, ya vyama baadaye.

Tusiwaachie Wanasiasa Wateke Mjadala wa Katiba Mpya

Na Fatuma Mpanga, Mkuranga-Pwani

Sasa hivi kuna taarifa kuwa kuna mjadala kuhusu mabadiliko ya Katiba. Ukweli ni kuwa haya mabadiliko mimi binafsi siyafahamu kwa sababu kama kuna katiba ya sasa basi iko kwa Mkuu wa Wilaya na pengine kwa Mkurugenzi wa halmashauri tu.

Hivyo kwa sisi wanajamii hususani huku vijijini kuielewa katiba ya nchi si

rahisi. Kama kuna wananchi wanaoielewa basi ni wachache mno. Ndiyo maana sasa katika hali hii, kuikosoa au kusema tuifanye

marekebisho inatuwia vigumu.

Ingekuwa inachapishwa na kupatikana kirahisi kama zilivyo katiba za vyama ningeitolea maamuzi. Lakini kama sijui

kilichoandikwa ndani ya hii katiba kweli itakuwa ni vigumu kwa sasa.

Inakuwa ni sawa na kumuuliza mlemavu

wa macho kama amemuona mtu fulani akipita. Je, yeye anaona?

Hali hii ndiyo inayotukabili wananchi wengi:

katiba ya sasa bado: hatuielewi!

Ndio sawa

n a s i s i

wanajamii, hatuelewi!

Wananchi wengi hatuielewi Katiba

PATA MACHAPISHO MAPYA!

HakiElimu ni shirika la hiari linalolenga kufikia usawa, haki na demokrasia katika elimu na jamii kwa ujumla. Tunafanya hivyo kwa kuwezesha jamii kupata habari, kubadili shule na mfumo wa uundaji wa sera; kuchochea ubunifu wa mijadala ya umma; kufanya utafiti yakinifu, uchambuzi wa sera na utetezi na kushirikiana na wadau ili kuendeleza manufaa ya pamoja na kuzingatia haki za jamii. Je una kero, kisa au mafanikio kuhusu elimu, demokrasia na haki za binadamu katika eneo lako na ungependa maoni yako yachapishwe kwenye Toleo lijalo la Jarida hili la SautiElimu? Tutafurahi kupata maoni. Tuandikie makala nasi tutaichapisha kwenye toleo lijalo. Tuma makala kupitia anuani ifuatayo: HakiElimu SautiElimu S. L. P 79401 Dar es Salaam Tanzania Simu: (022) 2151852 au 3 Faksi: (022) 2152449 Barua Pepe: [email protected] Tovuti: www.hakielimu.org Shukrani kwa wachangiaji, wapiga picha, wachoraji na kwa wote walioandaa habari zilizochapishwa katika jarida hili. Unaruhusiwa kunakili sehemu yoyote ya jarida hili kwa minajili isiyo ya kibiashara. Unachotakiwa kufanya no kunukuu chanzo cha sehemu iliyonakiliwa na kutuma nakala mbili kwa HakiElimu.

Wahariri Elizabeth Missokia Robert Mihayo Mtayarishaji Wambura Wasira

Wachangiaji Agnes Mangweha Benedicta Mrema Edwin Mashasi Honoratus Swai

Picha HakiElimu Michoro Jacob mwasumbi

© HakiElimu 2011

Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe. John Mnyika alisema, „Ibara ya 98 inasema kwamba Bunge ndilo lenye mamlaka ya masuala ya Katiba. Hakuna kipengele kina-chozungumzia kura ya maoni wala mkutano mkuu wa Taifa wa Katiba…‟ Je, wananchi wanaingia wapi kwenye sheria hii?