-
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio
mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya
Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22
2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya
Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]
HABARI ZA NISHATI &MADINI
Toleo No. 76 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Julai 17
- 23, 2015
BulletinNews
Ofisi ya Mawasiliano Serikalini inapokea habari za matukio
mbalimbali kwa ajili ya News Bullettin hii na Jarida la Wizara ya
Nishati na Madini
Wasiliana nasi Kitengo cha Mawasiliano kwa simu Namba +255 22
2110490 Fax 2110389 Mob: +255 732 999263 au Fika Ofisi ya
Mawasiliano Ghorofa ya Tano (MEM) Barua pepe: [email protected]
http://www.mem.go.tz
HABARI ZA NISHATI &MADINI
Toleo No. 51 Limesambazwa kwa Taasisi na Idara zote MEM Tarehe -
23-29 Januari , 2015
JWTZ wapongezwa kunusuru mtambo wa Msimbati-Uk4
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini
Stephen Masele
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati,
Charles Kitwanga
Mkurugenzi Mtend-aji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba
Mkurugenzi Mkuu wa REA, Dk. Lutengano Mwakahesya
Wabunge Soma habari Uk. 2
Waimwagia sifa MEM, TANESCO, REA
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA RASMI BODI YA TANESCO
-Uk2Mradi gesi asilia wafikia asilimia 98
Soma habari
Uk. 2
Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati
Kituo cha kupokelea gesi eneo la Somanga kikiwa kimekamilika
Mitambo ya kupokelea gesi ya Kinyerezi iliyokamilika
kufungwa
Mitambo ya kusafisha gesi na nyumba za wafanyakazi
Madimba, Mtwara
Uk. 2
-
2 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Asteria Muhozya na Teresia Mhagama
Imeelezwa kuwa, utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa mitambo ya
kusafisha gesi asilia ya Madimba na Songongo, Kilwa, pamoja na
bomba la kusafirisha gesi hiyo
kutoka Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam kupitia Somanga
Fungu itakamilika hivi karibuni.
Hayo yameelezwa katika taarifa ya mwezi Juni mwaka huu,
iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Kusambaza Gesi
(GASCO) ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba
Akielezea hatua zilizofikiwa katika miradi hiyo, Musomba
alieleza kuwa, kwa ujumla mradi huo umefikia asilimia
98 za ujenzi na kukamilika kwake kutaunganisha maeneo
yanayozalisha gesi asilia hususan Mnazi Bay- Mtwara, Songosongo,
Kiliwani, Mkuranga, Ntorya na gesi iliyogunduliwa katika eneo la
bahari ya kina kirefu.
Akifafanua zaidi alisema kuwa, Bomba limekamilika kwa asilimia
99.6 kwa ujumla, mitambo ya kusafisha gesi asilimia 97.5. Manunuzi
ya vifaa vya ujenzi wa mradi yamekamilika kwa asilimia 100, na
mradi mzima umekamilika kwa asilimia 98.
Musomba alisema kuwa, hatua
hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDC kuhakikisha kuwa,
Tanzania inazalisha umeme wa kutosha kupitia rasilimali hiyo na
wananchi wake wananufaika na rasilimali ya gesi asilia.
Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa, gesi inatumika katika
kuzalisha umeme ambao kwa sasa unazalishwa kwa kutumia nishati ya
mafuta ambayo huagizwa kutoka nchi za nje na hivyo kuligharimu
taifa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni, alieleza Musomba.
Kuhusu mitambo ya kuchakata gesi asilia, alisema kuwa, ujenzi wa
eneo la
kusimika mitambo, jengo la kuendesha mitambo pamoja na barabara
za ndani katika eneo la Madimba Mtwara umekamilika kwa asilimia 98,
wakati ule wa Songosongo umekamilika kwa asilimia 100 na usimikaji
mitambo umekamilika kwa asilimia 98.
Akizungumzia suala la ajira katika mradi huo, alisema kuwa,
kumekuwepo na wafanyakazi wapatao 1,427 wenye mchanganyiko wa
wageni pamoja na watanzania kwa ngazi zote hadi taarifa hii
inatolewa.
Aidha, kuhusu ajira kwa upande wa TPDC, alieleza kuwa, shirika
hilo tayari limeajiri wafanyakazi wapya wapatao 92 kwa upande wa
mitambo ya kusafisha gesi na 42 kwa upande wa bomba la kusafirisha
gesi, ambao tayari wanashiriki katika usimamizi wa shughuli za
ujenzi.
Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa, mradi unatekelezwa kwa
kutumia fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Jamhuri
ya watu wa China. Jumla ya gharama za ujenzi wa mradi huo ni Dola
za Marekani zipatazo bilioni 1.255, ambapo asilimia 95 ni mkopo na
asilimia 5 ni mchango wa Serikali.
Vilevile taarifa inaeleza kuwa gharama nyingine nyingi ambazo
serikali imeendelea kuzibeba nje ya asilimia 5 zinazotajwa ni
pamoja na gharama za upatikanaji wa mkuza wa Bomba la gesi kutoka
Mtwara hadi Somanga Fungu na kuongezeka kwa upana maeneo mengine
mengi ya mkuza tokea Somanga Fungu kuja Dar es Salaam hadi Tegeta.
Hadi sasa zimefikia kiasi cha pesa za ki-Tanzania zipatazo shilingi
Bilioni 200.
Katika hatua nyingine, akizungumza wakati akifunga rasmi Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwishoni mwa wiki, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
alieleza kuwa, serikali imejipanga kuhakikisha kuwa, hadi ifikapo
mwaka 2020 uzalishaji umeme unafikia kiasi cha megawati 3000
kutokana na matumizi ya gesi asilia.
Akieleza kuhusu miswada ya Sheria za Petroli na TEITI iliyosomwa
Bungeni hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene, Rais Kikwete alisema yuko tayari kuisaini miswada
hiyo wakati wowote itakapomfikia.
Mradi gesi asilia wafikia asilimia 98
Wakandaras i wa miradi ya k u b o r e s h a miundombinu ya
umeme
kwenye vituo vya kupoozea umeme jijini Dar es Salaam wametakiwa
kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo ndani ya muda uliopangwa.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Kamishna Msaidizi wa Umeme,
Mhandisi Innocent Luoga wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa
Mradi wa Kusambaza Umeme ujulikanao kwa jina la Electricity V
unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambao
unahusisha ujenzi na ukarabati wa vituo vya kupoozea umeme vya
Sokoine, Ilala na Njiro.
Aidha, ziara hiyo pia ilihusisha ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi na
Ukarabati wa Vituo vya Ilala na New City Centre pamoja na ujenzi wa
vituo vipya vya Ilala na Muhimbili ambao unafadhiliwa na
Serikali
ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na
vilevile Mradi wa Mfumo wa Kusimamia na Kudhibiti Usambazaji wa
Umeme Dar es Salaam ujulikanao kama Distribution SCADA System
uliopo Mikocheni unaofadhiliwa na Serikali ya Finland.
Mhandisi Luoga alielezea lengo la ziara hiyo kuwa ni kujionea
hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo
Hatua hiyo itaiwezesha Serikali kupitia TPDC kuhakikisha kuwa,
Tanzania inazalisha umeme wa kutosha kupitia rasilimali hiyo na
wananchi wake wananufaika na rasilimali ya gesi asilia
Mitambo ya kusafisha gesi ya Madimba
Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati
>>Inaendelea Uk. 3
Mradi wa Electricity V- Ilala: Transfoma mpya iliyofungwa kwenye
kituo cha kupooza umeme cha Ilala mara baada ya majaribio ya
awali.
-
3BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
TahaririMEM
Na Badra Masoud
FIVE PILLARS OF REFORMS
KWA HABARI PIGA SIMU KITENGO CHA MAWASILIANO
BODI YA UHARIRI MHARIRI MKUU: Badra Masoud
MSANIFU: Essy OgundeWAANDISHI: Veronica Simba, Asteria Muhozya,
Greyson Mwase Teresia Mhagama, Mohamed Saif, Rhoda James
na Nuru Mwasampeta
INCREASE EFFICIENCYQUALITY DELIVERY
OF GOODS/SERVICESATISFACTION OF
THE CLIENTSATISFACTION OF
BUSINESS PARTNERS
SATISFACTION OF SHAREHOLDERS
TEL-2110490FAX-2110389
MOB-0732999263
Hongera Simbachawene kwa mkakati wa kuisuka
Upya TIPER
TEL-2110490FAX-2110389
MOB-0732999263
Kamishna Msaidizi wa Umeme, Mhandisi Innocent Luoga (wa pili
kushoto) akimsikiliza Meneja Mradi wa Electricity V, Mhandisi
Florence Gwangombe (wa pili kulia) wakati wa ziara yake kwenye
kituo cha kupoozea umeme cha Ilala.
Luoga aagiza miradi ya Umeme Dar ikamilike kwa wakati
ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zinazokabili utekelezaji
wa miradi husika.
Katika taarifa yake ya utekelezaji wa Mradi wa Electricity V,
Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Florence Gwangombe alisema kutokana
na sababu mbalimbali huenda mradi huo ukachelewa kukamilika tofauti
na makubaliano ya awali kitendo ambacho kilimkera Mhandisi Luoga na
hivyo kumuagiza Meneja huyo kukaa na wakandarasi wa Mradi na
kurejea makubaliano ya awali.
Mhandisi Florence alisema moja ya sababu inayopelekea
Mradi huo kuwa na kasi ndogo ni wakandarasi kushindwa kuajiri
wafanyakazi wa kutosha.
Mhandisi Luoga aliwaagiza wakandarasi hao ambao ni kampuni ya
National Contracting Company Ltd (NCC) ya India na ELTEL Group
kutoka Finland kuhakikisha wanaajiri wafanyakazi wa kutosha na pia
kuandaa ratiba ya shughuli zinazotakiwa kufanywa ili kuepuka
kuchelewa kukamilika kwa miradi husika.
Aidha, Mhandisi Luoga aliwaagiza Mameneja Miradi wa Shirika la
Umeme Nchini (TANESCO) kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi
madhubuti wa miradi iliyo chini yao ili kuleta matokeo
yanayotarajiwa.Alisema lengo la Serikali ni
kuhakikisha taifa linakuwa na umeme wa uhakika kwa ajili ya
kukuza uchumi hivyo aliwaasa mameneja hao kuhakikisha azma hiyo
inatimia.
Ninawasisitiza muhakikishe kunakuwepo na ufatiliaji makini wa
miradi mnayoisimamia na sio kuwaachia wakandarasi wafanye kila kitu
bila usimamizi wenu, aliagiza Mhandisi Luoga.
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya NCC Ltd, Sadeesh John
alimuahidi Mhandisi Luoga kuwa atahakikisha kasi ya utekelezaji
inaongezeka na kutimiza maagizo husika ili kuhakikisha mradi
unakamilika ndani ya muda uliopangwa.
>>Inatoka Uk. 2
Mapema wiki hii Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
alikutana na Uongozi wa Shirika la kuhifadhi mafuta ya TIPER ambayo
serikali ni mbia kwa asilimia 50.
Katika kikao hicho alisisitiza kuhusu dhamira ya Serikali
kuboresha na kulisuka upya shirika hilo la kuhifadhi mafuta ili
liweze kutoa huduma ya kupokea mafuta kwa kampuni zote kwa haki na
usawa.
Simbachawene alisema lengo la kulisuka upya Shirika hilo ni
kuliboresha na kuhakikisha kuwa linatoa huduma ya kuhifadhi na
kupitisha mafuta yote yanayoletwa nchini, na kuhakikisha gharama za
kuhifadhi mafuta hapa nchini zinakuwa nafuu.
Kwa mara nyingine tunapenda kupongeza jitihada zinazofanywa na
Serikali katika kuhakikisha kwamba Sekta ya mafuta nchini
inalinufaisha taifa ikiwemo kuleta unafuu wa nishati hiyo.
Hakika katika hili la kuisuka upya TIPER ni mikakati madhubuti
ambayo inatarajia kuleta mabadiliko makubwa katika Shirika hivyo,
wadau wa TIPER na Watanzania tuunge mkono juhudi hizi za Serikali
kwani kauli hii ya sasa inadhihirisha dhamira ya dhati ya Waziri
Simbachawene juu ya kulisuka upya Shirika hilo ambapo alisisitiza
umuhimu TIPER katika sekta ya mafuta nchini, na kuleza kwamba hivi
sasa shirika hilo linahitajika kuliko wakati mwingine wowote.
-
4 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
JK ajivunia mchango Sekta ya Madini
Na Asteria Muhozya,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amesifu jitihada zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Nne
katika
kuimarisha Sekta ya Madini nchini na kuitaja kuwa ni ya pili kwa
kuingiza fedha za kigeni baada ya Sekta ya Maliasili.
Rais Kikwete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akihutubia
wananchi kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mjini
Dodoma na kuyataja mafanikio kadhaa katika Sekta hiyo, ikiwemo ya
migodi ya madini kuanza kulipa ushuru wa huduma.
Hotuba ya Rais Kikwete inarejea taarifa ya awali iliyotolewa na
Wizara ya Nishati na Madini ikieleza kuwa, mgodi wa dhahabu wa
Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya
Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya
Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha
asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika.
Tayari migodi inalipa kodi ambazo zinachangia katika pato la
Taifa. Pia tuna Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 haya yote yamesaidi
kuweza kunufaika zaidi kupitia rasilimali hii, alisisitiza
Rais.
Aidha, Rais Kikwete alieleza mafanikio
yaliyopatikana baada ya serikali kulifufua upya Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO), ambapo alisema kuwa, mafanikio hayo
yamechangia shirika hilo kumiliki mgodi wake wa dhahabu wa
STAMIGOLD uliopo Biharamulo, ambao tayari umeanza kutoa mikuo ya
dhahabu.
Vilevile, katika hotuba yake, Rais Kikwete alieleza namna
Serikali ilivyofanya jitihada za kuwawezesha wachimbaji wadogo
kupewa ruzuku, lengo likiwa ni kuwawezesha kutoka katika uchimbaji
mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati.
Katika taarifa yake wakati akizindua Kamati inayoshughulikia
maombi ya ruzuku Awamu ya Pili hivi karibuni, Kamishna wa Madini
Tanzania, Mhandisi Paul Masanja alisema kuwa, kiwango cha fedha
katika awamu hii kimeongezwa kufikia Dola za Kimarekani milioni na
tatu na shilingi za Kitanzania bilioni 1.7 kutoka Dola za Marekani
Laki tano (500,000) zilizotolewa Awamu ya Kwanza.
Lakini pia tumetenga maeneo 8 kwa ajili ya wachimbaji wadogo.
Tumefanya hivi ili wasisumbuliwe na wachimbaji wakubwa, alisema
Kikwete.
Vilevile, Rais Kikwete alisema kuwa, mikataba imerekebishwa ili
kulinda na kulinufaisha taifa ambapo pia baadhi ya mafanikio ya
marekebisho hayo yamewezesha Kampuni za madini kuongeza huduma ya
bidhaa zinatolewa nchini tofauti na ilivyokuwa awali.
Katika hotuba yake pia aliitaja migodi mipya 3 ikiwemo ya Makaa
ya Mawe ya Ngaka na Liganga na Chuma Mkuju, ambayo ilianzishwa
katika kipindi cha miaka 10 na kueleza kuwa, sekta hiyo imeongeza
kiwango cha ajira kutoka 3,500 hadi kufikia 15,000.
>> Aitaja ya pili kuingiza fedha za Kigeni baada ya
Maliasili>> Ajira zaongezeka kutoka 3,500 hadi 15,000.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete
Ujumbe kutoka Malawi watembelea Tanzania kujifunza sheria ya
Madini, CADASTRE.Na Rhoda James
Ujumbe kutoka Serikali ya Malawi umetembelea Wizara ya Nishati
na Madini mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo la kujifunza masuala
mbali mbali ikiwemo Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Mfumo mpya wa
kusajili leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online mining
Cadastre Transactional Portal)
Ziara hiyo ya Malawi imekuja kufuatia nchi hiyo kuwa katika
mchakato wa kutunga Sheria mpya ya Madini. Ujumbe huo pia
umetembelea Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA),Ofisi ya
Madini Kanda ya Mashariki, Kampuni ya Madini ya Acacia, pamoja na
kitengo cha Leseni na TEHAMA katika Wizara ya Nishati na
Madini.
Ujumbe huo kutoka Malawi umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa
kazi nzuri wanayoifanya katika kuendeleza sekta ya Madini na
kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya Serikali hizo
mbili.
Ujumbe kutoka Malawi ukiwa katika Wizara ya Nishati na Madini
wakati ulipofika Wizarani hapo kujifunza masuala ya Madini.
Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya
Nishati, Mrimia Mchomvu na kushoto kwake ni Kamishna Msaidizi wa
Madini kitengo cha Leseni, John Nayopa.
Kulia ni kiongozi wa Msafara wa Ujumbe kutoka Malawi Katibu
Mwandamizi, Ben Botolo akielezea jambo katika kikao hicho.
-
5BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Serikali kuisuka upya TIPERNa Mwandishi Wetu
Serikali imedhamiria kuboresha na kulisuka upya shirika la
kuhifadhi mafuta TIPER ili iweze kutoa huduma ya kupokea mafuta kwa
kampuni zote kwa haki na usawa.
Waziri mwenye dhama na Wizara ya Nishati na Madini George
Simbachawene amebainisha hayo wiki hii alipozungumza na Uongozi wa
shirika hilo huku akisisitiza kwamba lengo la Serikali kuboresha
shirika hilo ni kuhakikisha inatoa huduma ya kuhifadhi na kupitisha
mafuta yote yanayoletwa nchini.
Simbachewene aliongeza kusema kwamba hadi ifikapo mwishoni mwa
mwaka huu kampuni hiyo itakuwa na uwezo wa kuhifadhi mafuta kiasi
cha lita 300,000.
Kwa dhati kabisa tumeamua kuiboresha kampuni hiyo na tunapanga
ifikapo Septemba mwaka huu uwezo wa TIPER wa kuhifadhi mafuta
utaongezeka kutoka lita 147,000 hadi kufikia 210,000 na itakapofika
Desemba watakuwa na uwezo wa kuhifadhi mafuta lita 300,000,
alisisitiza George Simbachawene.
Waziri Simbachawene aliongeza kwamba lengo la Serikali kuchukua
hatua ya kuiboresha TIPER ni kuhakikisha gharama za kuhifadhi
mafuta hapa nchini zinakuwa nafuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TIPER, Daniel Belair ( Wa
kwanza kulia) akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene (kushoto) na ujumbe wake walipotembelea shirika lake
hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Bodi ya TIPER Prof. Abdulkarim Mruma akieleza
jambo katika moja ya vikao na Waziri
Wanafunzi waliopata ufadhili wa China waaswaNa Greyson Mwase,
Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu,
Wizara ya Nishati na Madini, Mrimia Mchomvu amewataka
wanafunzi wanaosomea masuala ya gesi na mafuta nchini China
kutumia utaalam na uzoefu wao katika kuleta mabadiliko kwenye sekta
ya gesi na mafuta nchini.
Mchomvu aliyasema hayo ofisini kwake, alipotembelewa na
wanafunzi waliofadhiliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili
ya mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika masuala ya gesi na mafuta
katika Chuo Kikuu cha Jiosayansi Wuhan kilichopo nchini China.
Wanafunzi hao ambao ni miongoni mwa wanafunzi nane
waliofadhiliwa na Wizara kusomea masuala ya gesi na mafuta kwa
mwaka 2013, walifanya ziara hiyo kwa lengo la kuishukuru Wizara
pamoja na kuelezea mikakati yao katika kutumia elimu na uzoefu
walioupata kuinua sekta za gesi na mafuta.
Alisema lengo la Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini la
kupeleka wanafunzi hao lilikuwa ni kuzalisha wataalam kwa ajili ya
kufanya kazi katika Wizara, makampuni ya utafiti na uchimbaji wa
mafuta na gesi
nchini. Kutokana na kukua kwa shughuli za
utafutaji wa gesi na mafuta nchini kama Serikali tulipanga
mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wazawa kushiriki
katika shughuli hizo kwa kuwapeleka kusomea masuala ya gesi na
mafuta ili waweze kufanya kazi na mashirika ya umma na makampuni
yaliyowekeza katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na
mafuta nchini, alisema Mchomvu.
Mchomvu aliendelea kusema kuwa wataalam hao wanaweza kutumia
elimu na uzoefu walioupata kutoka China kufanya kazi kwenye
mashirika ya umma, taasisi na makampuni binafsi yanayojishughulisha
na shughuli za uchimbaji na utafutaji wa gesi na mafuta.
Alisisitiza kuwa serikali pekee, haiwezi kuajiri wahitimu wote
wanaomaliza mafunzo ya gesi na mafuta bali kazi yake kuu ni
kuwapatia elimu itakayowawezesha kushiriki katika fursa mbalimbali
zinazojitokeza katika setka ya gesi na mafuta.
Sekta ya gesi na mafuta inakua kwa kasi kwa sasa, fursa ni
nyingi hivyo ni jukumu lenu kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira
zinazojitokeza katika makampuni ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta
na gesi. Kuna Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) ambalo
lina kampuni
tanzu, makampuni ya utafutaji wa gesi na mafuta ya Statoil na BG
ambayo yanahitaji wataalam, alisisitiza Mchomvu.
Wakielezea uzoefu walioupata katika chuo hicho, wanafunzi hao
walisema wamejifunza kwa kina hatua za utafutaji, uchimbaji na
usafirishaji wa mafuta na gesi kwa kutumia vifaa vya kisasa hali
iliyowapa uwezo wa kufanya kazi na kampuni za kimataifa.
Bishanga Januarius ambaye ni mwanafunzi wa mwaka pili katika
chuo hicho alisema kuwa utaalam na uzoefu alioupata katika chuo
hicho utamwezesha kufanya kazi katika kampuni yoyote ya utafiti na
uchimbaji wa madini na kuwa na mchango mkubwa kwa taifa.
Alisema kuwa elimu ya vitendo waliyoipata katika makampuni ya
mafuta na gesi nchini China imewapa mwanga mkubwa katika shughuli
zote za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi.
Aliishauri Serikali kuendelea kutoa ufadhili katika fani za
mafuta na gesi pamoja na masuala ya mazingira kwani shughuli za
utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta ni lazima ziende sambamba na
utunzaji wa mazingira.
Naye Yazid Idd ambaye ni mhitimu katika chuo hicho aliishukuru
Wizara kwa ufadhili huo na kuishauri Wizara kupeleka wanafunzi
kwenye vyuo vingine vinavyotoa
mafunzo ya mafuta na gesi katika nchi nyingine zilizopiga hatua
katika sekta hizo.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya
Nishati na Madini Mrimia Mchomvu, ( wa pili kutoka kushoto)
Mkurugenzi Msaidizi Utumishi, Wizara ya Nishati na Madini Lucius
Mwenda ( wa pili kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wanafunzi waliowahi kufadhiliwa na Wizara kwa ajili ya
kusomea Shahada ya Uzamili katika musuala ya gesi katika vyuo vya
China.
-
6 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Na Jacqueline MattowoSTAMIGOLD
Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO) imetimiza mwaka mmoja wa
uchimbaji dhahabu katika mgodi wake wa Biharamulo uliopo
wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera ambapo kiasi cha wakia 16,388 za
dhahabu zimekwisha zalishwa tangu uchimbaji dhahabu ulipoanza rasmi
mnamo mwezi Julai mwaka 2014 na jumla ya wakia 12,923 za dhahabu
zenye thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 15.6 zimeuzwa kwenye
soko la kimataifa.
Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikana katika maeneo ya West Zone
na Mojamoja takribani kilomita tatu na nusu kutoka uzio wa mgodi
ambapo uchimbaji wa dhahabu bado unaendelea. Maeneo hayo mapya
yalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodi wa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa
na kampuni ya African Barrick Gold sasa ACACIA mwishoni mwa mwaka
2013.
Akizungumza katika hafla ya kusherehekea mwaka mmoja tangu
kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu iliyofanyika mwishoni
mwa juma katika mgodi wa Biharamulo, Meneja Mkuu wa mgodi wa
Biharamulo, Mhandisi Dennis Sebugwao alieleza kuwa matarajio ya
mgodi ni kutafuta namna
ya kuhakikisha uzalishaji wa dhahabu unaendelea kwa kiwango
kikubwa na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na
kuongeza nafasi za ajira kwa Watanzania kwa ajili ya maslahi ya
Taifa zima.
Siwezi kuficha furaha yangu, siku ya leo ni siku ya muhimu kwetu
sote katika historia ya Mgodi huu kwani tunathibitisha kwa Serikali
na Watanzania
wenzetu kuwa, Watanzania wasomi na wenye taaluma mbalimbali
katika sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu wameendelea
kuonyesha uwezo wao kwa kuhakikisha uzalishaji unaendelea kufanyika
katika mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bila kuwepo wataalam wa kigeni
kama ilivyokuwa ikiaminiwa. alieleza Sebugwao.
Mhandisi Sebugwao pia alielezea mafanikio yaliyofikiwa na mgodi
ndani ya mwaka mmoja ambayo ni pamoja na mgodi kuendeshwa kwa
kufuata taratibu za usalama na afya kazini, ulinzi imara ndani na
nje ya mgodi, kupunguza gharama za uendeshaji wa mgodi, kulipa
ushuru wa huduma wa 0.3% ya mauzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya
Biharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9 mpaka June 2015,
kuajiri wafanyakazi wa Kitanzania 340 wa fani mbalimbali za
kitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwa wakazi wa vijiji vilivyo
jirani na mgodi na wakandarasi wa Kitanzania 281.
Aliongeza kuwa mgodi umekuwa ukizisaidia jamii zilizo jirani na
mgodi kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni
pamoja na kugawa madawati 1500 kwa shule zenye upungufu katika
Wilaya za Biharamulo, Muleba na Ngara, ujenzi wa choo cha wanafunzi
Shule ya Msingi Mavota, ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa manne
Shule ya Msingi Mpago, ukarabati
wa miundo mbinu pamoja kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia
vikundi vitatu vya ujasiriamali kwa kununua vyakula vya asili,
mbogamboga na matunda wanayozalisha.
Kwa upande mwingine, katika kusherehekea siku hiyo shamrashamra
mbalimbali zilifanyika ikiwemo mpira wa miguu na mpira wa kikapu
ambapo timu ya mgodi ya mpira wa miguu ilicheza mechi ya kirafiki
na timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vijiji vya Mavota na Mkunkwa
na timu ya mgodi kuibuka kidedea kwa bao 2-0. Baada ya michezo
kumalizika timu zote za mpira wa miguu zilikabidhiwa zawadi na
Meneja Mkuu wa mgodi.
Katika kuhitimisha sherehe hizo zilitolewa zawadi na vyeti kwa
wafanyakazi 10 ambao walifanya vizuri katika Idara zao kwa kipindi
cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambao pia walipatiwa heshima ya
kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodi kukata keki ya kutimiza mwaka
mmoja wa uzalishaji.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka
STAMICO Deusdedith Magala, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika hilo Mhandisi Edwin Ngonyani, aliupongeza uongozi na
wafanyakazi wa mgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika na
kusema kuwa mafanikio yanayopatikana ni sifa kwa Shirika na Taifa
kwa ujumla kwani tayari mgodi umethibitisha uwezo wa Watanzania
kuzalisha dhahabu bila kuongozwa na wataalam wa kigeni.
Nimefurahishwa sana na mafanikio mliyofikia pamoja na namna
wafanyakazi wanavyojituma baada ya kutembelea maeneo mbalimbali
hapa mgodini na kujionea kazi zinavyofanyika naomba muendelee na
bidii hiyo na vile vile mjitahidi kuongeza zaidi njia za
mawasiliano za kutangaza mafanikio ya mgodi huu mfano misaada
inayotolewa katika jamii ili dunia na taifa kwa ujumla kufahamu
kuwa ipo kampuni ya Kitanzania inayochimba dhahabu kwa manufaa ya
Taifa zima la Tanzania alifafanua Magala.
Mbali na mafanikio hayo mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bado
unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kuyumba
kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia, ufinyu wa mtaji wa
kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi pamoja na uhaba wa maji
kutokana na vyanzo vilivyopo kutegemea msimu wa mvua.
Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo ilizalisha dhahabu yake ya
kwanza mnamo mwezi Agosti 2014 na mpaka sasa imeendelea kuweka
historia kwa kuwa kampuni pekee hapa nchini inayozalisha dhahabu
kwa kusimamiwa na kuendeshwa na wataalam wa Kitanzania pekee.
Stamigold yatimiza mwaka mmoja wa uchimbaji dhahabu.
Mratibu wa kitengo cha Tehama na Mawasiliano, Belatrix Kasuga
akipokea cheti cha mfanyakazi bora kutoka kwa Meneja mkuu wa mgodi
Mhandisi Dennis Sebugwao (kulia) wakati wa maadhimisho ya mgodi
kutimiza mwaka mmoja wa uzalishaji. Pembeni ni Meneja Uchimbaji,
Mhandisi Abdallah Kwassa aliyeshikilia zawadi tayari kwa
kumkabidhi.
Pichani Keki ya mfano wa mawe ya dhahabu iliyoandaliwa katika
hafla ya mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo kutimiza mwaka mmoja wa
uzalishaji.
-
7BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Na Veronica Simba
Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) imetoa taarifa yake ya
utendaji kwa kipindi cha Serikali ya Awamu
ya Nne (2005-2015), ambayo pamoja na mambo mengine imeainisha
mafanikio yaliyopatikana katika nyanja mbalimbali.
Taarifa hiyo iliyotolewa hivi karibuni, imeainisha mafanikio ya
Wakala huo kwa kipindi husika katika makundi matatu ambayo ni
utekelezaji wa kazi za jiosayansi, kuboresha rasilimali watu,
vitendea kazi, miundombinu na mazingira yake pamoja na kazi na
tafiti zilizokamilika na zinazoendelea kutekelezwa.
Kwa upande wa utekelezaji wa kazi za jiosayansi, Taarifa ya GST
imeeleza kuwa Ramani mpya 60 za jiolojia zimekamilika na
kuchapishwa. Ramani hizi ni muhimu kwani huwezesha kubainisha uwepo
wa madini katika eneo husika.
Pia, taarifa ilibainisha kuwa ukusanyaji wa takwimu za
jiofizikia kwa kutumia ndege umefanyika katika Wilaya 35 ambayo ni
asilimia 15 ya eneo la nchi. Wilaya hizo ni Dodoma, Bahi, Kongwa,
Mpwapwa, Nchemba, Kondoa, Chamwino, Iramba, Manyoni, Ikungi,
Mkarama na Singida.
Wilaya nyingine ni pamoja na Igunga, Babati, Kiteto, Hanang,
Simanjiro, Mbulu, Moshi, Same, Monduli, Korogwe, Handeni, Kilindi,
Bagamoyo, Mvomero, Kilosa, Gairo,
Mbarali, Chunya, Bukombe, Kahama, Ushirombo, Biharamulo na
Mpanda.
Takwimu hizi zimeainisha maeneo yenye viashiria mbalimbali vya
uwepo wa madini, kwa mfano eneo la Misaki, Mpambaa, Sambaru na
Londoni ambapo ufahamu wa uwepo wa madini ya dhahabu umeongezeka,
taarifa imeeleza na kuongeza kuwa, takwimu hizi zimeonesha ongezeko
la uwepo wa madini ya graphite huko Merelani mkoani Manyara na
katika wilaya za Kilindi na Handeni.
Imeelezwa kuwa, pamoja na kubaini ongezeko la madini mbalimbali,
pia taarifa hizi hubaini mipasuko kwenye ardhi hivyo kusaidia
kuratibu matetemeko na majanga mengine ya asili.
Vilevile, uchunguzi wa sampuli kwenye maabara umeongezeka kutoka
sampuli 650 (mwaka 2005) kwa mwaka na kufikia jumla ya sampuli 4500
hadi 5600 kwa mwaka kwa hivi sasa. Imeelezwa kuwa ongezeko hili la
sampuli limetokana na kuboreshwa kwa vitendea kazi, majibu sahihi
ya uchunguzi na wafanyakazi kupatiwa elimu na motisha.
Kuhusu kuboresha rasilimali watu, vitendea kazi, miundombinu na
mazingira yake, taarifa ya GST inaonyesha kwamba watumishi wapya
wapatao 100 wameajiriwa na mafunzo mbalimbali ya muda mfupi na
mrefu yameendelea kutolewa ndani na nje ya nchi. Vilevile, Wakala
umeboresha vitendea kazi vya maabara, ugani, jiofizikia, uchoraji
ramani, ofisi na samani.
Aidha, taarifa imeeleza kuwa kwa upande wa kazi zilizofanyika ni
pamoja na kukamilika kwa jumla ya tafiti 27. Tafiti hizo zilihusu
utafutaji wa madini ya metali/vito, madini ya viwanda, nishati
ya jotoardhi, matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkano,
mmomonyoko wa ardhi, upatikanaji wa magadi, uchenjuaji wa madini,
ushauri wa namna bora ya utafutaji na uchimbaji wa madini kwa
wachimbaji wadogo na uhifadhi wa mazingira.
Wakala wa Jiolojia Tanzania ulianzishwa kama Wakala wa Serikali
chini ya Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2005 na kupewa jukumu la
kubainisha maeneo yenye kupatikana madini mbalimbali nchini ili
kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya madini kwa lengo la kukuza
uchumi wa Taifa.
Pia, GST imepewa jukumu la kuratibu majanga asili ya jiolojia
(matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkano, mionzi ya asili kutoka
kwenye miamba, kemikali za sumu zitokazo kwenye miamba na udongo,
maporomoko ya ardhi) na kutoa ushauri wa namna ya kujikinga na
kupunguza athari za majanga hayo.
Dhima ya GST ni kutoa takwimu na taarifa za jiosayansi za
kiwango bora kwa gharama stahiki kwa wadau ili kuongeza ufahamu wa
rasilimali za madini, hivyo kuchangia katika lengo la Taifa la
kupunguza umaskini, kuongeza ufahamu wa majanga ya asili na jinsi
ya kupunguza athari zake, utunzaji wa mazingira, kuboresha usalama
wa watu na mali zao.
GST yaeleza mafanikio katika Serikali ya Awamu ya Nne
Takwimu hizi zimeainisha maeneo yenye viashiria mbalimbali vya
uwepo wa madini, kwa mfano eneo la Misaki, Mpambaa, Sambaru na
Londoni ambapo ufahamu wa uwepo wa madini ya dhahabu
umeongezeka
Watalaam wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakifanya utafiti
wa Jiolojia katika ukanda wa Dhahabu wa Lupa(Lupa Gold Field),
wilayani Chunya mkoani Mbeya
-
8 BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
Elimu ya OMCTP kuanza kutolewa kwa kutumia gari la matangazo
Na Zuena Msuya
Wizara ya Nishati na Madini imeanzisha mfumo mpya wa usajili wa
wateja kwa kutumia
njia ya mtandao ijulikanayo kama Online Mining Cadastre
Transactinal Portal( OMCTP) utakaowawezesha waombaji na wamiliki wa
leseni za madini kujisajili kwa njia ya mtandao ili kufahamu na
kuhakiki taarifa zao kwa urahisi.
Kamishna Msaidizi wa Madini anayeshughulikia leseni, John Nayopa
amesema utaratibu huo umeanzishwa ili kutekeleza agizo la Serikali
la kutaka Wizara na Taasisi za Serikali kurahisha upatikanaji wa
huduma bora karibu na wananchi, kupokea malipo ya Serikali kwa njia
za kielektroniki ili kudhibiti mapato tofauti na ilivyokuwa
hapo
awali.Mwaka 2000, kitengo cha utoaji
leseni kilikuwa Dodoma Wakati huo mamlaka ya utoaji leseni
ilikuwa Dar-es-Salaam hali iliyosababisha ucheleweshaji wa kutolewa
leseni na pia mfumo wa utoaji na kuchambua
leseni ilifanyika kwa mkono, alisema Nayopa.
Aliongeza kuwa mfumo huo unafanana na ule unaotumiwa na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) katika malipo ya leseni za magari au mfumo
wa kununua luku ambao utawapunguzia wananchi ugumu wa kupata
huduma.
Nayopa alisema mfumo wa OMCTP utaongeza uwazi na kasi ya utoaji
wa leseni za madini,wateja wataingiza maombi ya leseni wao wenyewe,
hivyo kupunguza tatizo la mlundikano wa maombi katika ofisi za
madini.
Vile vile alisema kuwa wateja watapata taarifa za leseni zao
kila wakati na kujua wanapotakiwa kufanya malipo ya leseni au
watakapotakiwa kutuma taarifa za utendaji kazi pia kurahisisha
mawasiliano kati ya Wizara na wamiliki wa leseni.
Awali waombaji wa leseni walilazimika kwenda katika ofisi za
madini kujaza fomu za maombi, kufyeka mipaka ya eneo wanaloomba na
kuweka vibao; kisha kumleta Afisa madini ili kukagua eneo
linaloombwa na hatimaye kwenda kufanya malipo ya maombi hayo kwenye
ofisi ya Madini,alisema Nayopa
Aliongeza kuwa wateja na Serikali watakuwa na uhakika na maombi
yote yatakayowasilishwa (yakiwamo maombi ya sihia (transfer),
kuhuisha leseni n.k.); na pia kuwa na uhakika na malipo yote
yatakayofanywa kupitia mfumo wa OMCTP
Aidha aliongeza kuwa ili kutoa elimu kwa wadau wote wa madini
Wizara itatoa mafunzo kuanzia tarehe 19 Julai hadi pale
itakapomaliza wadau wote kwa kuanzia mikoa ya Kanda ya Mashariki,
Kanda ya Kati,Magharibi na Kanda ya Kusini.
-
9BulletinNewshttp://www.mem.go.tzHABARI ZA NISHATI/MADINI
STAMIGOLD YATIMIZA MWAKA MMOJA WA UCHIMBAJI DHAHABU
Kwa wadau wa sekta za Nishati na Madini, tembelea kurasa mpya za
Wizara kwenye Mitandao ya Kijamii ya Twitter na Facebook kwa anuani
ya Nishati na Madini Karibu tuhabarishane na
tujadili kuhusu sekta za Nishati na Madini kwa maendeleo ya
Watanzania wote.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Kampuni ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO) imetimiza mwaka mmoja wa uchimbaji
dhahabu katika mgodi wake wa Biharamulo uliopo wilayani Biharamulo
Mkoa wa Kagera ambapo uchimbaji ulianza rasmi mnamo mwezi Julai,
2014. Ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uchimbaji (Julai 2014
Juni 2015), kiasi cha wakia 16,388 za dhahabu zimekwishazalishwa na
jumla ya wakia 12,923 za dhahabu zenye thamani ya Dola za
Kimarekani Milioni 15.6 zimekwishauzwa kwenye soko la
kimataifa.
Kiasi hicho cha dhahabu kilipatikana katika maeneo ya West Zone
na Mojamoja takribani kilomita tatu na nusu kutoka uzio wa mgodi
ambapo uchimbaji wa dhahabu bado unaendelea. Maeneo hayo mapya
yalikabidhiwa STAMICO kutoka mgodi wa Tulawaka uliokuwa ukimilikiwa
na kampuni ya African Barrick Gold sasa ACACIA mwishoni mwa mwaka
2013.
Akizungumza katika hafla ya kusherehekea mwaka mmoja tangu
kuanza kwa shughuli za uchimbaji wa dhahabu iliyofanyika katika
mgodi wa Biharamulo, Meneja Mkuu wa mgodi wa Biharamulo, Mhandisi
Dennis Sebugwao alieleza kuwa matarajio ya mgodi ni kutafuta namna
ya kuhakikisha uzalishaji wa dhahabu unaendelea kwa kiwango kikubwa
na gharama nafuu ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza
nafasi za ajira kwa Watanzania kwa ajili ya maslahi ya Taifa
zima.
Siwezi kuficha furaha yangu, siku ya leo ni siku ya muhimu kwetu
sote katika historia ya Mgodi huu kwani tunathibitisha kwa Serikali
na Watanzania wenzetu kuwa, Watanzania wasomi na wenye taaluma
mbalimbali katika sekta ya uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu
wameendelea kuonyesha uwezo wao kwa kuhakikisha uzalishaji
unaendelea kufanyika katika mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bila
kuwepo wataalam wa kigeni kama ilivyokuwa ikiaminiwa. alieleza
Sebugwao.
Mhandisi Sebugwao pia alielezea mafanikio yaliyofikiwa na mgodi
ndani ya mwaka mmoja ambayo ni pamoja na mgodi kuendeshwa kwa
kufuata taratibu za usalama na afya kazini, ulinzi imara ndani na
nje ya mgodi, kupunguza gharama za uendeshaji wa mgodi, kulipa
ushuru wa huduma wa 0.3% ya mauzo kwa Halmashauri ya Wilaya ya
Biharamulo kiasi cha Shillingi milioni 40.9 mpaka June 2015,
kuajiri wafanyakazi wa Kitanzania 340 wa fani mbalimbali za
kitaalamu, ajira za muda mfupi 43 kwa wakazi wa vijiji vilivyo
jirani na mgodi na wakandarasi wa Kitanzania 281.
Aliongeza kuwa mgodi umekuwa ukizisaidia jamii zilizo jirani na
mgodi kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni
pamoja na kugawa madawati 1500 kwa shule zenye upungufu katika
Wilaya za Biharamulo, Muleba na Ngara, ujenzi wa choo cha wanafunzi
Shule ya Msingi Mavota, ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa manne
Shule ya Msingi Mpago, ukarabati wa miundo mbinu pamoja kuwawezesha
wananchi kiuchumi kupitia vikundi vitatu vya ujasiriamali kwa
kununua vyakula vya asili, mbogamboga na matunda wanayozalisha.
Kwa upande mwingine, katika kusherekea siku hiyo shamrashamra
mbalimbali zilifanyika ikiwemo mechi ya mpira wa miguu ambapo timu
ya mgodi ilicheza mechi ya kirafiki na timu iliyoundwa na wachezaji
kutoka vijiji vya Mavota na Mkunkwa na timu ya mgodi kuibuka
kidedea kwa bao 2-0. Baada ya michezo kumalizika timu zote za mpira
wa miguu zilikabidhiwa zawadi na Meneja Mkuu wa mgodi.
Katika kuhitimisha sherehe hizo zilitolewa zawadi na vyeti kwa
wafanyakazi 10 ambao walifanya vizuri katika Idara zao kwa kipindi
cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambao pia walipatiwa heshima ya
kushiriki na Meneja Mkuu wa mgodi kukata keki ya kutimiza mwaka
mmoja wa uzalishaji.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka
STAMICO Deusdedith Magala, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika hilo Mhandisi Edwin Ngonyani, aliupongeza uongozi na
wafanyakazi wa mgodi kwa kazi nzuri ambayo inaendelea kufanyika na
kusema kuwa mafanikio yanayopatikana ni sifa kwa Shirika na Taifa
kwa ujumla kwani tayari mgodi umethibitisha uwezo wa Watanzania
kuzalisha dhahabu bila kuongozwa na wataalam wa kigeni.
Nimefurahishwa sana na mafanikio mliyofikia pamoja na namna
wafanyakazi wanavyojituma baada ya kutembelea maeneo mbalimbali
hapa mgodini na kujionea kazi zinavyofanyika. Naomba muendelee na
bidii hiyo na vile vile mjitahidi kuongeza zaidi njia za
mawasiliano za kutangaza mafanikio ya mgodi huu mfano misaada
inayotolewa katika jamii ili dunia na taifa kwa ujumla kufahamu
kuwa ipo kampuni ya Kitanzania inayochimba dhahabu kwa manufaa ya
Taifa zima la Tanzania alifafanua Magala.
Mbali na mafanikio hayo mgodi wa STAMIGOLD Biharamulo bado
unakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kuyumba
kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia, ufinyu wa mtaji wa
kuendesha shughuli mbalimbali za mgodi pamoja na uhaba wa maji
kutokana na vyanzo vilivyopo kutegemea msimu wa mvua.
Kampuni ya STAMIGOLD Biharamulo ilizalisha dhahabu yake ya
kwanza mnamo mwezi Agosti 2014 na mpaka sasa imeendelea kuweka
historia kwa kuwa kampuni pekee hapa nchini inayozalisha dhahabu
kwa kusimamiwa na kuendeshwa na wataalam wa Kitanzania pekee.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano
STAMIGOLD Biharamulo Plot. No. 417/418
UN Road S.L.P 78508
Dar es Salaam. Email: [email protected] Website:
www.staigold.co.tz
KAMPUNI YA STAMIGOLDMGODI WA BIHARAMULO
TAARIFA KWA UMMA