Volume 1, Issue 1 Business Name WARSHA YA WADAU WA KILIMO NA MKUTANO MKUU WA MWAKA 1. Dkt Sinare Sinare - Mwenyekiti 7. Bibi. Jackline Mkindi– Mjumbe 2. Professa Andrew Temu - M/ Mwenyekiti 8. Bibi. Helen Ainea Usiri– Mjumbe 3. Dr. Salum Diwani - Mwekahazina 9. Bw. Sebastian Sambuo– Mjumbe 4. Bw. Salum Shamte– Mjumbe 10. Bw. Felix Mosha– Mjumbe 5. Bw. Abdul Mwilima– Mjumbe 11. Mhe. Jitu Soni– Mjumbe 6. Bw. Willigis Mbogoro– Mjumbe YALIYOMO Jarida la Agricultural Council of Tanzania Jarida la Agricultural Council of Tanzania We unite, we dialogue, we advocate Toleo Na. 16. Oktoba – Disemba 2013 KILIMO KWANZA– AGRICULTURE FIRST WARSHA YA WADAU WA KILIMO NA MKUTANO MKUU WA MWAKA WAJUMBE WA BODI WA ACT KUPEANA TAARIFA NA KUZITUMIA KUENDELEZA VYAMA MAFUNZO YA KILIMO– BIASHARA KWA WARATIBU WA TAP KUBADILISHANA UZOEFU KUHUSU UTUNGAJI WA SERA ZA KILIMO KUFUFUA ZAO LA KOROSHO Tarehe 2 na 3 Desemba 2013, ACT ilifanikisha matukio muhimu mawili. Siku ya kwanza ilikutanisha wataalamu wa nyanja mbalimbali wapatao 80 kujadili masuala matatu: Ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji, Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya kilimo na ufugaji, Athari za kodi kwenye sekta ya kilimo. Siku ya pili ulifanyika Mkutano Mkuu wa Mwaka. Wanachama walipokea na kujadili mada ambazo ni za kawaida katika tukio la aina hii. Miongoni mwake ni: Kupokea na kujadili Taarifa ya Mwenyekiti na Hesabu za ACT, na kuchagua Wakaguzi wa Hesabu. Wakati huohuo, ACT inaandaa mkutano wa wadau utakaofanyika Januari 2014, ambao utajadili suala la Kilimo cha Kibiashara katika nchi za Afrika Mashariki. Pia, Bodi ya ACT ilipata viongozi wapya. Viongozi hao ni; Dkt. Sinare Y. Sinare kama Mwenyekiti, Profesa Andrew Temu, kutoka SUA, Morogoro kama Makamu Mwenyekiti, na Bw. Abdul Mwilima, kutoka Agricomat, Kigoma, kama Mjumbe. WAJUMBE WA BODI YA ACT
4
Embed
Jarida la Agricultural Council of Tanzania Toleo Na. …actanzania.or.tz/wp-content/uploads/2016/08/ACT...yaliyofanyiwa utafiti na kuhakikiwa, ambavyo yanaathiri sekya ya Kilimo. 2.
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
2. Professa Andrew Temu - M/ Mwenyekiti 8. Bibi. Helen Ainea Usiri– Mjumbe
3. Dr. Salum Diwani - Mwekahazina 9. Bw. Sebastian Sambuo– Mjumbe
4. Bw. Salum Shamte– Mjumbe 10. Bw. Felix Mosha– Mjumbe
5. Bw. Abdul Mwilima– Mjumbe 11. Mhe. Jitu Soni– Mjumbe
6. Bw. Willigis Mbogoro– Mjumbe
YALIYOMO
Jarida la Agricultural Council of Tanzania
Jarida la Agricultural Council of Tanzania
We unite, we dialogue, we advocate
Toleo Na. 16. Oktoba – Disemba 2013
KILIMO KWANZA– AGRICULTURE FIRST
WARSHA YA
WADAU WA
KILIMO NA
MKUTANO MKUU
WA MWAKA
WAJUMBE WA
BODI WA ACT
KUPEANA
TAARIFA NA
KUZITUMIA
KUENDELEZA
VYAMA
MAFUNZO YA
KILIMO–
BIASHARA KWA
WARATIBU WA
TAP
KUBADILISHANA
UZOEFU KUHUSU
UTUNGAJI WA
SERA ZA KILIMO
KUFUFUA ZAO LA
KOROSHO
Tarehe 2 na 3 Desemba 2013, ACT ilifanikisha
matukio muhimu mawili. Siku ya kwanza
ilikutanisha wataalamu wa nyanja mbalimbali
wapatao 80 kujadili masuala matatu:
Ardhi kwa ajili ya kilimo na ufugaji,
Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya kilimo na
ufugaji,
Athari za kodi kwenye sekta ya kilimo.
Siku ya pili ulifanyika Mkutano Mkuu wa
Mwaka. Wanachama walipokea na kujadili
mada ambazo ni za kawaida katika tukio la
aina hii.
Miongoni mwake ni: Kupokea na kujadili
Taarifa ya Mwenyekiti na Hesabu za ACT, na
kuchagua Wakaguzi wa Hesabu. Wakati
huohuo, ACT inaandaa mkutano wa wadau
utakaofanyika Januari 2014, ambao utajadili
suala la Kilimo cha Kibiashara katika nchi za
Afrika Mashariki.
Pia, Bodi ya ACT ilipata viongozi wapya.
Viongozi hao ni; Dkt. Sinare Y. Sinare kama
Mwenyekiti, Profesa Andrew Temu, kutoka
SUA, Morogoro kama Makamu Mwenyekiti,
na Bw. Abdul Mwilima, kutoka Agricomat,
Kigoma, kama Mjumbe.
WAJUMBE WA BODI YA ACT
KUPEANA TAARIFA NA KUZITUMIA KUENDELEZA VYAMA
Tarehe 22 hadi 25 Oktoba 2013, watumishi
wawili wa ACT, Bw. Cleophas Rwechungura na
Khalid Ngassa, walikuwa Bujumbura, Burundi,
ambako walishiriki katika mafunzo kuhusu
utaalamu wa kupeana habari / taarifa kwa lengo
la kuendeleza vyama vya wakulima. Mafunzo
hayo yalifadhiliwa na IFAD na kusimamiwa na
Muungano wa Vyama vya Wakulima Afrika
Mashariki– EAFF.
Mafunzo hayo yalishirikisha baadhi ya vyama vya
wakulima kutoka Kenya, Burundi na Tanzania.
Washiriki walifundishwa jinsi ya kuimarisha
vyama vya wakulima kwa kuelimisha watendaji
pamoja na wanachama, na mbinu za kupeana
taarifa na kwa lengo la kujiendeleza. Hii ni
pamoja na: “Kuimarisha upashanaij wa habari
na utamaduni wa kubadilishana maarifa na
ujuzi”.
MAFUNZO YA KILIMO– BIASHARA KWA WARATIBU WA TAP
Ubia wa Kilimo Tanzania - TAP kwa sasa unao waratibu
wa shughuli zake katika wilaya 25. Katika jitihada za
kufanya kilimo kiendeshwe kibiashara, TAP iliomba msaada
wa kifedha na kitaalamu ili kuelimisha Waratibu wake
ustadi wa kilimo cha kibiashara na kanuni za kilimo cha
mkataba.
Mafunzo haya yamekuwa yakifanyika kwa awamu. Zoezi
la karibuni lilifanyika katikati ya Novemba 2013, jijini Dar
es Salaam. FAO kupitia Programu ya Kuendeleza
Mifumo ya Uzalishaji wa Chakula, Nyanda za Juu- SHFSP,
ilifanikisha mafunzo kwa Waratibu wa TAP, ambao
baadae watatoa elimu hiyo kwa wakulima, na kwa wadau
wengine kwenye mlolongo wa thamani.
Utaalamu huu ni muhimu sana, hasa tukizingatia
kwamba TAP II itaanza karibuni, ambayo mkazo wake ni:
“Kukuza kilimo kwakuchochea uwekezaji na
kukiendesha kibiashara”.
Page 2 Jarida la Agricultural Council of Tanzania ACT NEWS
2 Jarida la ACT– Toleo Na. 16
Awamu ya kwanza ilikuwa ya miaka mitatu
2008– 2011 na ilihusisha wilaya 25. Matarajio ni
kwamba awamu ya pili itapanuka kwa
kujumuisha wilaya nyingine 25.
Baadhi ya washiriki kwenye mafunzo wakisikiliza kwa makini mtoa mada.
ACT hufanya shughuli zake kwa kushirikiana na sekta binafsi na ya umma. Huduma zake zinalenga wadau wote, wa ngazi zote kulingana na mahitaji yao halisi.
KUFUFUA ZAO LA KOROSHO
Mwanzoni mwa Oktoba 2013, Bw. Renatus
Mbamilo kutoka ACT alikuwa miongoni mwa
washiriki kwenye warsha iliyojadili uzoefu wa
Vyama vya Wakulima katika michakato ya
kuimarisha hali ya chakula katika ngazi ya taifa na
kanda. Warsha hiyo ilifanyika jijini Nairobi.
Madhumuni ya jumla, ni kuimarisha ushiriki wa
Shirikisho la Vyama vya Wakulima, Afrika
Mashariki - EAFF kwenye mchakato huu.
Washiriki walipanuliwa ufahamu wao kuhusu
utaratibu wa mchakato. Kumewekwa mfumo
wa kupima, kufuatilia na kutathmini athari za sera
za kilimo kwa wazalishaji.
Mfumo huu unatekelezwa na FAO kwa
kushirikiana na wabia wengine kwa lengo kukuza
utendaji katika vyama, na hivyo kuimarisha
ukuaji wa kilimo.
Page 3 Volume 1, Issue 1 ACT NEWS
3 Jarida la ACT– Toleo Na. 16
Tarehe 4 na 5 Novemba 2013, ANSAF na ACT kwa
pamoja waliandaa warsha ya kujadili changamoto
zinazokabili zao la korosho nchini Tanzania.
Wabia wengine kwenye shughuli hii ni; Bodi ya
Korosho Tanzania, Kituo cha Uwekezaji Tanzania,
Taasisi za Kifedha, Wahisani, na wawakilishi wa
wakulima wa korosho. Lengo la warsha lilikuwa
kutafakari jinsi ya kufufua zao la korosho ili tunufaika
nalo.
Hali ya korosho siyo nzuri, kiwango cha uzalishaji wa
korosho na ubora wake, uko chini sana, isitoshe, ni
asilimia 20 tu ndiyo inayosindikwa hapa Tanzania, kiasi
kinachobakia husafirishwa hadi India kubanguliwa.
Katika hali hii, washiriki wa warsha walikubaliana:
Kusaidia wakulima katika jitihada zao za kupata
mazao makubwa yenye ubora wa juu.
Kuhakikisha kwamba korosho zote zinabanguliwa
hapahapa Tanzania, kusudi bei yake iongezeke, pia
wananchi wapate ajira.
KUBADILISHANA UZOEFU KUHUSU UTUNGAJI WA SERA ZA KILIMO
Baadhi ya wawakilisha wa taasisi
zilizoandaa warsha hii.
Zabibu ni zao linaloweza kutajirisha Wakulima.
Soko lake ni kubwa.
ACT NEWS
Ubia wa Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Partnership– TAP. Ni muungano wa hiari
baina ya taasisi za umma na binafsi zinazofanya kazi kwa pamoja katika masuala ya kilimo.
Wabia wanochangia katika ushirikiano huu ni pamoja na CNFA/TAGMARK, AGRA, FIPS,
RUDI. Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, NMB na MS-Tanzania. Pamoja na makampuni
ya mbolea na mbegu na mbegu kama Yara, minjingu Mines & Fertilizer Co. Bytrade, Pannar,
Mosanto, Seedco na Kibo Seed. Hadi sasa shughuli za TAP zimeenea kwenye wilaya 25.
Malengo ya TAP
Lengo kuu la Ubia wa Kilimo Tanzania ni kuchangia kupunguza umasikini vijijini. Na lengo
mahususi ni kutoa pembejeo sahihi za kilimo kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na kuboresha
masoko ya mazao kwa kutumia mlolongo wa thamani wenye tija ukisaidiwa na sekta ya
umma na binafsi.
Programu inalenga katika:
Upatikanaji nafuu wa pembejeo
Masoko bora ya bidhaa za wazalishaji
Ongezeko la uzalishaji katika kilimo
Uwekezaji kwenye sekta binafsi ya Kilimo
Mbinu za kufanikisha shughuli za maendeleo na biashara