Top Banner

of 16

Jarida Jan Apr 2016.pdf

Jul 05, 2018

Download

Documents

khalfan said
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    1/16

     HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

     J A R I D A JANUARI-APRILI, 2016

    H A L I U Z W I

    Jengo la wazazi namba mbili ambalo kwa sasa lina uwezo wa kulaza akina mama wajawazito 91. Hudumanyingine zinazopatikana katika jengo hili ni pamoja na kliniki ya wajawazito, kliniki pamoja na chanjo kwa

    watoto chini ya umri wa miaka mitano na huduma ya uzazi wa mpango.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    2/16

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    Y A L  

    I   Y  OM

     O

    Jarida hili limeandaliwa na

     Ami niel A li gaesha Mkuu w a Kit engo cha Mawasi lian o

    Neema Mwangomo Afis a Habari

    John Stephen Afisa Habari

    [email protected] +255 755 648 636

      Jina Cheo Barua pepe Simu ya kiganjani

    [email protected]

    [email protected] +255 743 182 106

     joh n.mass [email protected] z +255 743 145 392

    Mtaa wa Kalenga barabara ya Malik, Kitalu Na. 1048

    S.L.P. 65000, Dar es Salaam, Tanzania.

    Simu +255 22 2151367-9 / Nukushi: +255 22 2150234

    Barua pepe: [email protected] / Tovuti: www.mnh.or.tz.

    1 M uhimbil i yapongezwa ujenzi wa ICU

    3 Muhimbil i kupandikiza f igo

    4 M uhimbil i yaboresha huduma za wagonjwa wa nje

    5 Huduma ya usikivu kwa watoto kuimarishwa Muhimbil i

    6 Kamat i ya Bunge huduma za Jamii

    8 Mapato yaongezeka kwa asil imia 41 ndani ya miezi mit atu

    8 Dawa Muhimbil i sasa ni asi l imia 95

    9 Naibu Waziri Afya aagiza M uhimbili kuboresha huduma

    10 Muhimbil i haijasit isha huduma ya Selimundu

    11 M h. Ummy aridhishwa na ukarabat i wa jengo la wazazi namba mbili

    12 Muhimbil i yapokea msaada wa mashini ya kusaidia watoto kupumua

    12 Muhimbil i haijasit isha huduma ya Selimundu

    13 Idara magonjw a ya Urolojia yaendelea kuim arika

    7 Posho za Wafanyakazi M uhimbil i kuboreshwa

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    3/16

    1

    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangwallaameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaujenzi wa chumba maalumu cha kulaza wagonjwawanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) chenye uwezowa kulaza wagonjwa 15 kwa wakati mmoja.

    Hayo aliyasema mapema mwaka huu wakatiakizindua chumba hicho kilichopo jengo la Mwaiselaambapo sasa Hospitali imeongeza uwezo wa kulazawagonjwa hao kutoka vitanda vinane vya awali hadikufikia vitanda 25.

    Alisema Hospitali iendelee kuongeza uwezo wavitanda hivyo hadi kufikia viwango vya kimataifakama vilivyoainishwa na shirika la afya ulimwenguni(WHO) linalotaka kuwa asilimia 10 ya jumla yavitanda vya kulaza wagonjwa katika Hospitali kuwavya ICU. Uzinduzi huo wa huduma bora, umetajwakuwa ni njia ya kuelekea kuondokana na kupeleka

    wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Hospitaliya Taifa Muhimbili ina vitanda 1,500 hivyo inahitajivitanda vya ICU 150.

    Dkt. Kigwangalla alisema ndani ya mwaka mmojakuanzia sasa, Serikali itaondoa huduma ya kupelekawagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu na ndiyomaana inaendelea kuboresha huduma za matibabukatika hospitali za umma hapa nchini.

    Alisema huduma hiyo itatolewa kwa gharama nafuukuliko ilivyokuwa hapo awali. Alisema wizara

    inaangalia vizuri jinsi ya kuondoa utaratibu huo wakupeleka wagonjwa nje na kuitaka Muhimbilikuendelea kujipanga kukidhi mahitaji ya wagonjwawaliokuwa wanapelekwa nje.

    “Endapo kutakuwepo na mgonjwa anayetakakwenda nje idara husika ndiyo itampeleka baada yakujiridhisha kuwa wao wameshindwa kumtibu. Hapakazi tu haya ndiyo mabadiliko ya kweli ya serikali yaawamu ya tano tunayoyaleta” alisema Dkt.Kigwangalla.

    Akitoa taarifa yake wakati wa uzinduzi huo, KaimuMkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa MuhimbiliProf. Lawrence Museru, alisema Uongozi waHospitali umesimamia uboreshaji wa huduma ya

    M uhim bili yapongezwa ujenzi wa ICU

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    Yaongeza vitanda vya ICU kutoka 8 hadi 25 

    Naibu Waziri wa Afya na M aendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watot o, Dkt. Hamisi Kigwangal la akikata utepe ikiwa ni i shara ya kuzindua ICU hiyo.

     Inaendelea Ukurasa wa 2 ...

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    4/16

    2

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    tiba ya wagonjwa mahututi kwa upanuzi nauwekezaji wa vifaa vya kisasa katika wodi hiimaalumu kama vile mashine za kupumulia, vifaa vyauchunguzi wa kihadubini kwa magonjwa ya tumbona mapafu, Ultrasound ya kisasa inayochunguza piamishipa ya damu, vitanda vya kisasa kwa matumiziya wagonjwa mahututi ikiwa ni pamoja na utoaji wamafunzo ya kitaalam ya ubingwa kwa madaktari nawauguzi watakaohusika na utoaji wa huduma hii.

    Prof. Museru alisema hatua hii imefanikishakuongeza vitanda vya wagonjwa mahututi kutokavinane hadi 25 ikiwa ni ongezeko la asilimia miambili kutoka uwezo wa awali, na kwamba Hospitaliinaamini kuwa juhudi hizi zitapunguza kwa kiasi

    kikubwa msongamano wa wangojwa wodini auwale wanaopokelewa moja kwa moja wenyemahitaji ya tiba hii muhimu na hivyo kupunguzaongezeko la idadi ya vifo visivyo vya lazima

    Ujenzi na uwekaji wa vifaa umegharimu kiasi chashilingi milioni 930 ambapo Hospitali ilichangia kiasicha shilingi milioni 230 na taasisi isiyo ya kiserikaliya Gastrenterology Foundation ya Ujerumani imetoamsaada wa vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingimilioni 700.

    Katika hatua nyingine Dkt. Kigwangalla alimshukuruRais wa taasisi hiyo ya Ujerumani Prof. MeinhardClassen kwa moyo wake wa upendo wa kuisadiaHospitali katika ujenzi wa ICU hii pamoja na mchangomkubwa walioutoa katika ujenzi na uwekaji wa vifaatiba mbalimbali katika kituo cha tiba na mafunzo yamagonjwa ya matumbo, ini na saratani ukanda waAfrika Mashariki kilichopo Hospitalini hapa.

    . . . ujenzi wa ICU

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    5/16

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    M uhimbil i kupandik iza f igoHospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kuanzakutoa huduma ya kupandikiza figo nchini ifikapo

    Disemba mwaka 2016 ili kupunguza idadi yawagonjwa wanaokwenda nje ya nchi kupata hudumahii.

    Katika kutekeleza azima hii, tayari Hospitali imeombaSerikalini fedha kuwezesha ujenzi wa miundombinuna ununuzi wa vifaa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.Aidha Hospitali tayari imeanza maandalizi yakupeleka watalaam wake kwenda kupata mafunzowakiwemo madaktari, wauguzi, watalaam wa usingizina fani nyingine muhimu katika kutoa huduma yaupandikizaji wa figo.

    Akitoa mchanganuo wa watalaam hao Mkurugenzi waHuduma za Tiba Dkt. Hedwiga Swai alisema kwakuanza Hospitali itapeleka madaktari bingwa watatukujifunza namna ya kupandikiza figo, madaktaribingwa wa figo wawili, wauguzi wawili kwa ajili yachumba cha upasuaji na upandikizaji wa figo, wauguziwawili kwa ajili ya uangalizi maalumu wa wagonjwawalioko vyumba vya upasuaji na upandikizaji wa figo,watalaam wa usomaji na uchunguzi wa vinyama vyafigo ili kugundua chanzo cha ugonjwa wa figo kwawagonjwa hao, pamoja na mtalaam wa radiolojia.

    Kupeleka watalaam nje kuongeza ujuzi 

    “Tumeanza kufanya maandalizi ya vyumba vyaupasuaji ili kuhakikisha ifikapo Disemba mwaka huu

    au mapema Januari 2017 kazi hii ya upandikizajiwafigo inaanza mara moja Hospitalini hapa” alisemaDkt. Swai.

    Hospitali pia inakusudia kupeleka timu ya watalaamwake wa figo kutembelea nchi mbalimbali dunianiambazo zimeendeleea katika kutoa huduma yaupandikizaji figo ili kujifunza namna bora ya kufanyahivyo pamoja na kuanzisha ushirikiano baina yaHospitali hizo na Hospitali ya Taifa Muhimbili.Hospitali zilizofanikiwa duniani ni zile zinazofanyakazi zake kwa kushirikiana na watalaam kutokamataifa mbalimbali yaliyoendelea.

    Hospitali kwa sasa inahudumia wagonjwa takribani100 wanaokuja kusafisha damu angalau mara tatuk w a j u m a . A i d h a k u n a w a g o n j w a 2 0 0waliopandikizwa figo wanaohudhuria kliniki za figoHospitalini hapa wakiwemo watoto.

    Hospitali inaona wagonjwa wapatao 40 hadi 50 kila jumatano ya wiki ambao wana matatizo ya figo lakinihawajafikia hatua ya kusafishwa damu amakupandikizwa figo nyingine. Pia watoto 6 hadi 10wenye matatizo ya figo huonwa kila wiki.

    Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. Hedwiga Swai akizungumzia nia ya hospitali hiyo kut oa huduma za kupandikiza figo kuanzia Desemba mw aka huu.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    6/16

    4

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    M uhimbili yaboresha huduma za wagonjwa wa nje

    Hospitali  ya Taifa Muhimbili imeboreshahuduma za afya kwa wagonjwa wa nje ili wapatemuda zaidi wa kutibiwa na kupata ushauri wa daktarikatika kliniki mbalimbali. Uanzishwaji huu unalengakupunguza msongamano wa wagonjwa, na

    kuwapunguzia muda wa kusubiri kupata huduma.Hii inatoa fursa kwa watu ambao hawana nafasimuda wa asubuhi na wangependa kupata matibabumuda wa jioni.

    Akizungumza na Jarida hili, Mkuu wa Idara yawagonjwa wa Nje Dkt. Raymond Mwenesano,alisema utaratibu huu mpya utahusu wagonjwawanaokuja kutibiwa na kuondoka, hasa wanaolipafedha taslimu, wanachama wa Mfuko wa Taifa waBima ya Afya, bima mbalimbali za afya na watumishiambao kampuni zao zina mikataba na hospitali.

      “Katika kliniki ambazo zimeshaanza kufanya kazi,madaktari bingwa pekee ndio watakaoonawagonjwa na si vinginevyo. Huduma hizi kwa sasazinatolewa kila siku kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa12:00 jioni. Kwa siku za Jumamosi huduma hutolewakuanzia saa 3:00 hadi saa 8:00 mchana,” alisema Dkt.Mwenesano.

    “Huduma za kliniki zilikuwa hazitolewi kwa kiwangocha kuridhisha kutokana na kukosekana muda wakutosha wa kuhudumia wagonjwa hivyo uboreshwajihuu, tunapenda kuwajulisha wananchi hasawagonjwa wanaotumia bima za afya wafike kwa ajiliya kupata huduma za afya” alisema Dkt. Mwenesano.

    Kiliniki hizi zinaendelea kufanyika katika jengo lawagonjwa wa nje linalotazamana na jengo la wazazina jengo la wagonjwa wa NHIF lililo karibu na eneo la

    Makuti. Wagonjwa wanaopata rufaa kuja Muhimbiliwanaendelea na utaratibu wa kawaida wakuwasilisha barua za rufaa ili wapatiwe huduma.

    Wagonjwa kuonwa hadi saa 12 jioni na Jumamosi 

    Mkuu wa Idara ya Huduma za Wagonjwa wa Nje Dkt. Raymond Mwenesano akizungumzia uboreshaji wa huduma kwa wagonjw a wa nje baada ya

    kukutana na waandishi wa habari.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    7/16

    5

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    Huduma ya usik ivu kwa watoto k uimarishwaMuhimbi l iHuduma ya watoto wenye matatizo ya usikivuinatarajiwa kuanza kutolewa kwa kiwango cha

    ubingwa wa juu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikuwawezesha watoto wengi wenye matatizo hayokupata huduma hiyo kwa wakati.

    Mikakati hiyo imeelezwa na Kaimu MkurugenziMtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof.Lawrence Museru wakati akizungumza nawazazi/walezi ambao walifika Hospitalini hapa kwaajili ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao ambaowana matatizo ya usikivu sanjari na kupata maonimbalimbali kutoka kwa wazazi hao.

    Prof. Museru alisema kimsingi mahitaji ya matibabuhayo ni makubwa na upasuaji huo haufanyiki hapanchini hivyo wagonjwa wengi wenye kuhitajihuduma hii hutegemea matibabu hayo nje ya nchi naambayo ni gharama kubwa.

    “Mpango uliopo sasa ni kuhakikisha huduma hiiinaanzishwa ili wagonjwa wenye matatizo hayawaweze kutibiwa hapa nchini kwa sababu kunawataalam wa kutosha na naamini hatua hiyoitawasaidaia wananchi wengi kupata matibabu hayo”alisema Prof. Museru.

    Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Magonjwa yaMasikio, Pua na Koo, Dkt. Edwin Liyombo alisematayari Hospitali imepeleka andiko la kuiomba serikalikuanzisha programu maalum itakayowasaidia

    madaktari kupata mafunzo pamoja na kupata vifaatiba ili upasuaji huo uweze kufanyika hapa nchini.

    Dkt. Liyombo alisema mgonjwa mmoja akipelekwanchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huuhugharimu kati ya shilingi milioni 85 hadi Milioni 100lakini endapo matibabu hayo yatafanyika hapa nchinigharama itapungua kwa kiasi kikubwa.

    Akizungumzia kuhusu utaratibu wa kukutana nawazazi ambao watoto wao wana matatizo ya usikivuDkt. Liyombo alisema utaratibu huo ni endelevukwani una lenga kufuatilia maendeleo ya mtoto nakumuwezesha mzazi kupata ushauri wa kitaalam.

    Kaimu M kurugenzi wa M NH Profesa Museru ( katikati ) akiwa na M kuu

    wa Idara ya M asikio , Pua na Koo Dkt. Edwin Liyombo (kushoto) na

    Fayaz Jaf fer .

    aimu M kurugenzi wa (MNH )Prof. Lawrence Museru pamoja na mt aalam wa masikio Fayaz Jaffer w akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wat oto ambao

    wal iofanyiwa upasuaji na kuwekewa kifaa maalum cha kuwasaidia kusikia ili kuweza kuwasiliana.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    8/16

    6

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    Kamati ya Bunge huduma za Jamiiyaipongeza Muhimbili kwa Utendaji

    Kamati ya Bunge ya KudumuHuduma za Maendeleo ya Jamiiimeipongeza Hospitali ya Taifa yaMuhimbili pamoja na taasisizilizopo katika Hospitali hiyo nakujionea mambo mbalimbali yakiutendaji pamoja na kubainishakero mbalimbali zinazoikumbasekta ya Afya hapa nchini.

    Kamati hiyo inaongozwa naMwenyekiti wake, Mh. Peter

    Serukamba (Mbunge) pamoja nawajumbe mbalimbali wa kamati,walitembelea Hospitali hii nakupata fursa ya kutembezwa katikawodi na majengo kadhaa yaHospitali hiyo na kupata maelezonamna ya uendeshaji na utoaji wahuduma unavyofanyika.

    M i o n g o n i m w a s e h e m uwalizotembelea ni pamoja na WodiMaalum ya wagonjwa wa afya yaak i l i , chumba maa lum cha

    wagonjwa mahututi (ICU) kilichopoMwaisela, Idara ya magonjwa yadharura, jengo la wazazi nambambili, pamoja na Taasisi yaMagonjwa ya Moyo ya JakayaKikwete.

    Akitoa majumuisho baada yakutembelea maeneo ya HospitaliMwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba alisema kuna kazikubwa inafanyika Muhimbili na

    kwamba wafanyakazi na uongoziwanastahili pongezi kutokana namazingira wanayofanyia kazi naidadi kubwa ya wagonjwa na kerombalimbali zikiwemo za kisera namiundo mbinu.

    Mh. Serukamba aliahidi kuwaKamati yake itafanya kila iwezavyokuhakikisha Hospitali ya TaifaMuhimbili inapewa kipaumbelekwa kuongezewa bajeti ya kutoshakutekeleza majukumu yake

    kikamilifu. Fuatilia habari katikapicha.

    Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, Dkt. Frank Masao akitoa 

    ufafanuzi kwa kamat i ilipot embelea Idara yake.

    Kaimu M kuu wa Idara ya M agonjwa ya Dharura, Dkt. Upendo George

    akitoa ufafanuzi kwa kamati i lipotembelea Idara hiyo.

    Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla akit oa 

    ufafanuzi kwa kamat i kuhusiana na matumizi ya mashini ya CT Scan 

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    9/16

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    Hospitali ya Taifa Muhimbili inakusudiakuboresha posho zote wa wafanyakazi wanazopatasasa hivi na kuongeza nyingine mpya ifikapo Julai,Mosi mwaka huu.

    Akizungumza na jarida hili, Kaimu MkurugenziMtendaji wa Hospitali hii Prof. Lawrence Muserualisema kumekuwa na hali ya kutoridhika ya mudamrefu kwa wafanyakazi kuhusiana na kanuni naviwango vya posho vinavyolipwa kwa makundimbalimbali ya wafanyakazi hususani poshozinazolipwa kutokana na mchango wa mfanyakazikatika kumhudumia mgonjwa moja kwa moja.

    Prof. Museru alisema hali hii ya kutoridhikailisababisha kutokukua kwa mapato ya Hospitalikama ambavyo inategemewa kwa kuwa wafanyakaziwenye taaluma ya udaktari na huduma zinazomgusamgonjwa moja kwa moja wanaona ni vyema kutumiamuda wao wa ziada kwenda kuwahudumiawagonjwa kwenye hospitali nyingine, haliinayopunguza idadi ya wagonjwa wanaolipiahuduma kuja Muhimbili.

    Alisema wafanyakazi wengine walio katika idarasaidizi ambao hawamgusi mgonjwa moja kwa moja

    nao wamekuwa hawaridhiki na posho wanazopatana hivyo kusababisha kufanya kazi chini ya kiwango.“Kutokana na changamoto nilizoeleza hapo juu,Menejimenti iliunda kamati maalumu ya kupitiaposho zinazolipwa sasa na kutoa mapendekezo yakuboresha posho hizo kulingana na kiwango cha

    Posho za Wafanyakazi M uhim bilikuboreshwa

    mapato ya ndani ya Hospitali ili kuchochea motisha

    kwa wafanyakazi na kuongeza tija katika huduma namapato ya Hospitali' alisema Prof. Museru.

    Alisema Kamati imeshauri kuwa Menejimenti yaHospitali ieendelee kubuni na kutekeleza mikakatimbali mbali ya kuongeza mapato ya Hospitali nakuchukua hatua madhubuti za kupunguza gharamaza uendeshaji.

    Prof. Museru alisema kwa kuzingatia wastani wamapato ya Hospitali kwa sasa na matarajio ya mpakaMwezi Juni 2016, Kamati imependekeza kuongezekakwa viwango vya posho zilizopo na kuweka poshompya kabisa ifikapo Julai Mosi mwaka 2016.

    Kwa sasa Hospitali imefanikiwa kulipa malimbikizoya madeni yote ya wafanyakazi hadi kufikia Februari2016 ambayo walikuwa wakiidai kwa kipindi kirefuambayo ni posho ya kuitwa (on-call allowance),posho ya usiku ya wauguzi, malipo ya poshombalimbali ikiwemo malipo ya nauli ya likizo kwaw a f a n y a k a z i w o t e n a w a t a l a a m w o t ewanaoshughulika moja kwa moja na wagonjwa,alisema Prof. Museru.

    Aliongeza kuwa kutolipwa kwa malipo hayokulishusha morali ya wafanyakazi kwa kiwangokikubwa na kupunguza kasi ya ufanyaji kazi na hivyokusababisha kukosekana tija katika utoaji wahuduma. Taarifa zaidi zitawajia katika toleo lijalo la

     jarida hili.

    Kaimu M kurugenzi M tendaji w a MNH Prof. Lawrence Mseru Wa nane kutoka kushoto kat ika picha ya pamoja na baadhi ya w ajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    10/16

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    8

    M apato yaongezekakwa asil imia 41 ndani yamiezi mit atu

    Ukusanyaji  wa mapato ya ndani katika

    Hospitali ya Taifa Muhimbili umeongezeka kwaasilimia 41 katika kipindi cha miezi mitatu kutokaDisemba 2015 hadi kufikia Februari 2016ukilinganisha na mapato yaliyokusanywa katikakipindi cha miezi mitano ya mwanzo wa mwaka wafedha 2015/2016 kuanzia Julai hadi Novemba.

    Akizungumza na Jarida hili Kaimu MkurugenziMtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof.Lawrence Museru alisema wastani wa mapatoyaliyokusanywa katika kipindi cha miezi mitatu tokaDisemba 2015 hadi kufikia Februari 2016 ilikuwa

    shilingi bilioni 3.2 kutoka wastani wa shilingi bilioni2.3. Hospitali ilizalisha kiasi cha shilingi bilioni 3.3kutoka wastani wa shilingi bilioni 2.3 ilizokuwaikizalisha kwa kipindi cha miezi mitano kabla (yaaniJulai 2015 hadi Novemba 2015).

    Alisema mwenendo wa mapato unaonesha kuwamapato ya Hospitali yanaongezeka katika kila mwezikutoka shilingi bilioni 3.1 mwezi Januari 2016 hadikufikia shilingi bilioni 3.7 mwezi Februari 2016.Mapato haya yanatarajiwa kufikia Shilingi bilioni 4.5ifikapo mwezi Juni 2016.

    Alisema usimamizi thabiti wa wafanyakazi katikakutekeleza majukumu yao kila mmoja kwa nafasiyake na pia kupunguza kero za wafanyakazi ndikokulikochochea uzalishaji wenye tija kwa kiwangokikubwa sana na hivyo kuleta matokeo yenye tijakatika ukusanyi wa mapato.

    “Haya ni mafanikio makubwa sana kwa upande wamapato kuwahi kupatikana katika kipindi hicho,

    tumeona Hospitali ina fursa kiasi gani ya kuzalishakiasi kingi cha fedha na hivyo kuweza kujitoshelezakwa kiwango fulani katika uendeshaji wa shughulizake kutokana na mwelekeo wa mapato yalivyo”alisema Prof. Museru.

    Baadhi ya wagonjwa wakilipia gharama za matibabu katika Hospitaliya Taifa Muhimbili .

    Dawa M uhimbil i sasani asi l im ia 95

    Kiwango  cha upatikanaji wa dawa kwawagonjwa Hospitalini hapa kimeongezeka kutokachini ya asilimia 50 hadi kufikia asilimia 95 katikakipindi cha mwenzi Januari hadi Aprili 2016.

    Hospitali ya Taifa Muhimbili inatekeleza agizo la Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakuhakikisha kila mgonjwa anayekuja kutibiwa hapaanapata dawa na huduma nyingine kwa gharamanafuu ndani ya Hospitali.

    Akiongea na Jarida hili, Kaimu Mkurugenzi Mtendajiwa Hospitali Prof. Lawrence Museru alisemaupatikanaji wa dawa kwa kiwango hicho umetokanana mwitikio wa wananchi kuchangia huduma zote zaafya kwa lengo la kuhakikisha mgonjwa anapatahuduma kwa gharama nafuu hususani wagonjwa wa

    kuchangia gharama za matibabu.

    “Kiwango cha upatikanaji wa dawa Hospitalini hapani zaidi ya 95% na ikitokea mgonjwa amekosa dawaHospitali inalazimika kununua dawa hiyo nakumletea mgonjwa ili kumuondolea usumbufu”alisema Prof Museru.

    Kuhusu wagonjwa wasio na uwezo wa kuchangia,Prof. Museru alisema ikitokea kuna mgonjwa hanauwezo wa kuchangia huduma, utaratibu wakumuombea msamaha utatumika na mgonjwa huyoatapata huduma bila malipo.

    Alisema ni muhimu sana Watanzania kuchangiahuduma za matibabu ili kusudi Hospitali ya TaifaMuhimbili iendelee kupata fedha kidogo zakuhakikisha wagonjwa wanapokuja hapa wanapatadawa na vifaa vingine vya kuwahudumia.

    Mfamasia akitoa maelezo kwa wat eja namna ya kutumia dawa husika 

    Jitahidiufuatemaelekezo

     ya dawahii

    Nitajitahidi

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    11/16

    9

    Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangallaameiagiza Hospitali ya Taifa Muhimbili kuboreshahuduma zote ikiwemo huduma za kulipia kiwangocha daraja la kwanza ili kuongeza mapato yaHospitali na mgonjwa kuona thamani ya fedhaaliyolipia.

    Dkt. Kigwangalla aliyasema hayo mara tualipotembelea Hospitaini hapa kuona viwango vyahuduma katika idara ya magonjwa ya dharurapamoja na idara ya mionzi

    Akiwa Idara ya Magonjwa ya Dharura alisemaHospitali inao madaktari bingwa na wauguziwaliobobea katika eneo la dharura hivyo ni muhimuwakaendelea kuonesha viwango vya juu vya utoajihuduma kila mtu kwa nafasi yake mahali pake pa kazi.“Mkiendelea kufanya hivyo, mtaongeza sanathamani ya kazi yenu na mtaendelea kuaminika nawananchi kutokana na nia yenu ya kuwahudumiawahitaji” alisema Dkt. Kigwangala.

    Kuhusu huduma za mionzi Dkt. Kigwangalla alisema

    Naibu Waziri Afya aagiza M uhim bili k uboreshahuduma

    Hospitali ya TaifaM u h i m b i l i n iHospitali kubwa naya kwanza kwa ummakuwa na vifaa vyauchunguzi kupitiai d a r a h i i h i v y okuwataka watalaamkutumia weledi walionao kutoa huduma yakiwango cha juuku l i ko Ho sp i t a l iyeyote hapa nchini.

    “Ningependa kuonamatumizi makubwaya mashini hii ya CT-S c a n m p y amliyonunua na MRI iliwagonjwa wawezekuona thamani yamaj ibu hal is i yavipimo vinavyotokahapa” alisema Dkt.Kigwangalla.

    A l i o n g e z a k u w a

    Hospitali ya TaifaM u h i m b i l i i n amadaktari bingwawengi na wenye

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    uwezo mkubwa wa kutoa huduma na wengine niwataalamu wa magonjwa mbalimbali ikiwamomoyo na figo hivyo naamini wanaweza kufanyamabadiliko makubwa.

    Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dkt. Flora Lwakatarealisema mashini mpya ya CT Scan ambayoimenunuliwa na Hospitali inaendelea kutoa hudumabora kwa wagonjwa kutokana na kuwa na teknolojiaya hali ya juu. “Mashini hii ya CT Scan ni ya kisasa nainafanya kazi haraka na kwa ubora wa hali ya juu namajibu yanapatikana kwa wakati” alisisitiza Dkt.Lwakatare.

    Akizungumzia mashine za CT-Scan na MRI, Prof.Museru amesema kwamba Serikali ya awamu ya tanoinayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli iliagizaHospitali kununua mashini mpya ya CT-Scan yenyeuwezo wa 126 slices ili kukidhi mahitaji na viwangovya wateja.

    “Uwapo wa mashine hii mpya umeongeza uwezo kwakiwango kikubwa wa kupima wagonjwa wengi kwawakati mmoja. Sasa tunaweza kumpima mgonjwammoja tumbo na kifua kwa sekunde sita. Awali

    tulikuwa tunapima wastani wa wagonjwa 20, lakinisasa tunapima wagonjwa wastani wa 50 ndani ya saa24”alisema Prof. Museru.

    Aliongeza kuwa kuwapo kwa mashine hizi mbili zaCT-Scan, Hospitali haitegemei tena kukosekana kwavipimo vinavyohitaji mashine hizi. Aidha mashine hiimpya ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye nguvukubwa imewezesha kufanya vipimo vya kiutalaamuzaidi hasa kwa upande wa viungo vya ndani kamamoyo, utumbo, ubongo na hivyo kupata majibusahihi ya chunguzi na uhakika zaidi

    Mkuu wa Idara ya M ionzi, Dkt . Flora Lwakatare akit oa maelezo kuhusiana mashini ya CT Scan 

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    12/16

      J e n g o  l a w a z a z  i  n a m  b a m o  j a  l e n y e v  i  t a n  d a  3  2  6 a m p a p o  k a  t  i  y a  h  i v  i   1  4  0 n  i  v  i  t a n  d a v y a w a  t o  t o w a  l  i o z a  l  i w a  k a  b  l a y a w

     a  k a  t  i  n a v  i  t a n  d a  2  1 n  i   k w a a  j  i  l  i   k  i n a

     m a m a  k u  j  i  f u n g u  l  i a .

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    13/16

    11

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    M h. Ummy aridhishwa na uk arabat i wa jengo la wazazi namba mbil i

    Waziri  wa Afya Maendeleo ya Jamii, JinsiaWazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (MB)ameridhishwa na ukarabati uliofanywa naHospitali ya Taifa Muhimbili kwenye jengo lawazazi namba mbili ambalo kwa sasa linalazawagonjwa wapato 63.

    Akizungumza mara baada ya kutembelea jengohilo Mh.Ummy alisema anaridhishwa na zoezi hilola ukarabati na kuonyesha furaha yake kuwa kwasasa hakuna mama mjamzito anayelala chini.

    “Kuwepo kwa jengo hili ni faraja kwa kina mamanafurahi kuona ukarabati unaendelea vizuri na upokatika hatua nzuri kwakweli mnastahili pongezikwani mnafanya kazi nzuri” alisema Mh. Ummy.

    Jengo la wazazi namba mbili lilikabidhiwa kwaHospitali ya Taifa Muhimbili mapema mweziFebruari mwaka huu baada ya Mh. Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Dkt. John JosephPombe Magufuli kutembelea Hospitali hii nakukuta akina mama wengi wamelala chinikutokana na kukosa nafasi ya kulala vitandanikatika jengo la wazazi namba moja. Mpaka sasa

     jengo hilo lina jumla ya vitanda 63 ambavyovinatumika na wakina mama wanaendeleakupatiwa huduma.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    14/16

    12

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    Taasisi  isiyo ya kiserikali ya Human Walfare Trust imetoa msaada wa mashini moja ya kusaidia watotokupumua yenye thamani ya shilingi milioni 17 ili kusaidia jitihada za idara ya magonjwa ya dharura kuongezanguvu na vitendea kazi wakati wa kuwahudumia watoto.

    Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya shirika hilo Bw. Dipak Vassa alisema lengo ni kuendelea kusaidia sekta yaafya na kwamba shirika lake linatarajia kuendelea kushirikiana zaidi na idara ya magonjwa ya dharura na maeneomengine ya Hospitali ili kuimarisha huduma bora za afya.

    Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura Dkt. Juma Mfinanga alisema mashini hiyo imekuja wakati muafakaambapo idara inajiimarisha katika nyaja mbalimbali za kutoa huduma za dharura kwa makundi yote ya wahitaji.

    M uhimbili yapokea msaada wa mashini yakusaidia watoto k upumua

    Hospitali ya Taifa Muhimbili imesisitiza kuwahaijasitisha utoaji wa huduma za matibabu zaugonjwa Selimundu (Sickle Cell) na wala haitasitishautoaji wa huduma hiyo na kwamba watuwanaoeneza uvumi kuwa huduma hiyo imesitishwawana maslahi yao binafsi kuhusu tiba ya wagonjw ahao.

    Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendajiwa Hospitali Prof. Lawrence Museru wakatiakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni

    kuhusu utoaji huduma kwa wagonjwa hao nakuutaka umma kuelewa kwamba huduma hiyohaijasitishwa.

    M uhimbil i hai jasit isha huduma ya Selimundu

    Prof. Museru alisema ni kweli kwamba takribanimiaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhilimatibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa waselimundu ambao muda wake umeisha Machi 31mwaka huu.

    “Mradi huu kwasababu ya utafiti ulihitaji wagonjwawote wa selimundu kuja Muhimbili kwa ajili ya utafitina tiba, hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwawengi hata wasiohitaji huduma ya selimundu kujaMuhimbili licha ya kwamba mahitaji yao hayakuhitajiwataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili“alisemaProf. Museru.

    Alisema hata kabla ya mradi huo kuanza, Hospitaliilikuwa inatibu wagonjwa wa selimundu waliokuwa

    Kaimu M kurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Museru

    akipokea msaada wa mashini za kuwasaidia wat oto wadogo kupumua.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    15/16

    13

    Huduma ya matatizo ya njia ya haja ndogo urolojiaimechukua sura mpya baada ya kuanzishwa kwaIdara inayoshughulikia matatizo hayo. Idara yaUrolojia ilianzishwa Julai mwaka 2015 ili kuimarishahuduma hizo ambazo zina wagonjwa wengiukilinganisha na idara nyingine za Hospitali ya TaifaMuhimbili.Mkuu wa Idara hiyo Dkt. Ryuba Nyamsogoro alisemalengo lingine ni kuanzisha vitengo vipya ndani yaIdara ya Urolojia vitakavyobobea kwenye maeneo yaupasuaji wa njia za mkojo kwa kutumia hadubini(endourology)Alisema idara itaanzisha pia kitengo cha Urolojia kwawatoto (Paediatric Urology) na kujikita katika kutibusaratani ya njia za mkojo (Uro-oncology).Dkt. Nyamsogoro alisema idara hiyo itaimarishahuduma hizo na vile vile itakuwa ikitoa huduma kwa

    wagonjwa wa fistula na makovu kwenye njia zamkojo (reconstructive urology&uro-gynaecology)na kwamba idara hiyo itabobea pia katika shughuli yaupandikizaji wa figo kwa wagonjwa wenye tatizokwani matatizo ya figo na mfumo wa urolojia

    vinaenda pamoja.Tutaendelea kushirikiana na idara nyingine za kitaifana kimataifa katika tiba, mafunzo na utafiti ili kukuzana kuongeza uwezo na weledi katika tiba hii, alisema

    Dkt. Nyamsogoro.Alisema kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwemoupungufu wa vyumba vya upasuaji tatizo ambalosasa Menejimenti ya Hospitali inalifanyi kazi kwaharaka kwa kuongez aidadi ya vyumba vya upasuajiili kukidhi mahitaji ya idara hii katika kutoa hudumayake.Idara hii inakabiliwa na uchache wa wataalamu waurolojia waliobobea zaidi kwenye urolojia kwaupande wa watoto na katika upasuaji wa njia zahadubini na upasuaji wa figo. Jitihada kubwa badozinahitajika kukidhi mahitaji ya watalaam katika eneohili ili kuendana na mahitaji makubwa ya wagonjwa.

    Idara hii inaona wagonjwa wa nje karibu 190 kwa juma na jumla ya wagonjwa kati ya takribani 30wanafanyiwa upasuaji kwa juma sawa na wagonjwa120 kwa mwezi.

     JA NU A R I-A PR ILI , 2016

     J ARIDA LA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

    Idara magonjwa ya Urolojia yaendeleakuimarika

    Wagonjwa 190 wanaonwa kliniki kwa juma pia 30 hufanyiwa upasuaji kwa juma 

    Mkuu wa Idara ya Idara ya Urolojia, Dkt. Ryuba Nyamsogoro akifaf anua jambo kuhusiana na kuanzishwa kwa i dara hiyo

    kwenye Hospital i hapa.

  • 8/15/2019 Jarida Jan Apr 2016.pdf

    16/16

     

    HAKI NA WAJIBU WA MTOA HUDUMAHAKI

    a. Haki ya kuheshimiwa na mteja

     b. Haki ya kutokutoa huduma kwa mteja/mgonjwa endapo mgonjwa ana wasiwasi naye

    au anahisi jambo lolote lisilo la kawaida

    c. Kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na mteja au ndugu wa mteja/mgonjwad. Kujadiliana na jopo la watalaam wenzake kitaaluma kuhusu mgonjwa/mteja bila

    kuingilia au kutoa siri za mteja/mgonjwa

    e. Kutumia mgonjwa/mteja kuelekeza watalaam walioko katika mafunzo kwa vitendo

    f. Kufanya utafiti baada ya kupata kibali na kusambaza taarifa za ufatifi huo kitaaluma

     bila kuingilia siri za mgonjwa

    g. Kutokuwajibishwa kutokana na huduma aliyotoa kumpa madhara mteja/mgonjwa

    endapo huduma hiyo itakuwa imetolewa kufuatana na utaratibu na miongozo husika

    WAJIBU

    Uadilifu

    Hospitali ina wajibu wa kutoa huduma bora za afya kwa kuzingatia kanuni, maadili,

    uadilifu na umakini, bila upendeleo.

    Heshima

    Kuwa na mazingira yanayomjali mgonjwa zaidi na kuwapa heshima wateja wetu,

    kuwaonyesha utu, uaminifu na mawasiliano mazuri kwa kufanya kazi kwa pamoja kama

    timu ili kutoa huduma bora.

    Uwajibikaji

    Hospitali pamoja na wafanyakazi wote watahakikisha wanapata maoni ya jamiiwanayoihudumia kuhusu uwajibikaji wake kwa kutoa taarifa mbalimbali kwa jinsi

    itakavyotakiwa.

    Ubora

    Hospitali itatekeleza majukumu yake kwa kutumia rasilimali zote zilizopo ili kutoa

    huduma bora na za kibingwa kwa wagonjwa na wadau wake.

    Usalama

    Hospitali itashirikiana bega kwa bega na wagonjwa, wafanyakazi na walinzi wa hospitali

    ili kuimarisha ulinzi thabiti wa wagonjwa, wafanyakazi na taarifa za wagonjwa.

     

    MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

     

    1

     

    HAKI NA WAJIBU WA MTEJAHAKI WAJIBU

    Haki ya kupata matibabu yahospitali:a. Kupata ushauri wa kitabibu na

    matibabu yanayokidhi kikamilifu

    viwango vya uboravinavyokubalika.

    Haki ya kupata habari:a. Kupata habari kwa lugha rahisi

    kuhusu huduma gani za afyazinazopatikana, na gharama yahuduma hizo.

     b. Kumjua mtoa huduma kwa jina nawadhifa wake.

    c. Kupewa taarifa na maelezo sahihiya hali yako ya afya yakijumuisha

    utambuaji wa ugonjwa, mwelekeowa maendeleo ya ugonjwa kutokana

    na dalili za ugonjwa huo namatibabu yanayopendekezwa

    yanayojumuisha madhara yakawaida na hatua mbadala zilizosahihi.

     

    d.

     

    Kujua tiba unayostahili kupata na jinsi tiba inavyofanya kazi mwilini

    na madhara yanayoweza kutokeakutokana na tiba hiyo kwa lugha

    rahisi.

     

    Utaratibu na Uadilifua. Fuata kwa hiari yako mipango na

    maelekezo yaliyokubaliwa na kutolewakwako na watoa huduma

     b. Timiza ahadi yoyote utakayoweka, auijulishe hospitali au kliniki mapema

    inavyowezekana kama hutaweza kufanyahivyo.

    c. Usitoe malipo yoyote yasiyo halali kwa

    mfanyakazi wa Hospitali ya TaifaMuhimbili.d. Lipia gharama za huduma utakazopewa na

    hakikisha umepewa risitie. Mpe mtoa huduma wako wa afya maelezo

    ya kutosha kadiri iwezekanavyo kuhusuafya yako ya sasa, maradhi yako yaliyopita,

    kikwazo chochote cha kutotumia ainafulani ya dawa (aleji) na taarifa nyingine

    muhimu.f.

     

    Jali haki za wagonjwa wengine na watoa

    huduma za afya kwa kufuata taratibu zahospitali kuhusiana na mwenendo wako iliusiathiri wengine au huduma nyingine.

    g.

     

    Usimtake mhudumu yeyote afya kutoahabari, risiti au vyeti visivyo halali.

    h.

     

    Usiharibu raslimali za hospitalii.

     

    Kutunza kumbukumbu za taarifa za

    matibabu alizonazo mteja

    Haki ya kuchagua:

     

    a.

     

    Kukubali au kukataa tiba, uchunguzi

    au matibabu yoyote na kuelezwakuhusu matokeo yanayoweza

    kutokea kwa kufanya hivyo. b.

     

    Kutoa mawazo na kuchagua aidha

    kushiriki au kutoshiriki kwenye programu za uchunguzi wa tiba.

     

    Ulinzi na Usalamaa.

     

    Usiingie na silaha yeyoye ndani ya

    Hospitali hususani panga, virungu, visu, bunduki, bastola, misumari n.k 

     b.

     

    Usiingie na vilevi ndani ya Hospitaliikiwemo pombe na dawa za kulevya

    c.

     

    Usifanye fujo ndani ya Hospitalid.

     

     Ni wajibu wako kutunza mali zako kama

    simu, mkoba n.k 

     

    Haki ya kupewa faragha:

     

    a.

     

    Kupewa faragha, heshima na fursa

    ya kufuata imani za kidini na za

    kiutamaduni bila ya kunyanyaswa ilimradi imani hizo haziingiliani na

    taratibu za matibabu. b.

     

    Kusitiriwa kwa habari

    zinazohusiana na hali yako ya afya.

     

    c.

     Kuitwa kwa jina lako

     na siyo kwa

    tatizo alilonalo mgonjwa au rangi,kabila au Taifa lake.  

    Nidhamu/Heshimaa.

     

    Usitoe lugha za matusi au kejeli kwa mtoa

    huduma

    Usafia.

     

    Usitupe taka hovyo ndani na nje ya eneo laHospitali

     

    Haki ya kutoa malalamiko na kutoa

    maoni:

     a.

     

    Kutoa maoni kwa lengo lakuboresha huduma.

     b. Kulalamika kupitia mamlakazilizoidhinishwa na Hospitali kwa

    madhumuni hayo,