Top Banner
HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN C. MINJA KWA WATUMISHI WA JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA WAKATI WA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2015 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2016 MAKAOMAKUU YA MAGEREZA TAREHE 31 DESEMBA. 2015 Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana leo hii tukiwa na afya njema na matumaini makubwa ya kuuona mwaka mpya 2016. Nashukuru pia kupata fursa hii ya kukutana nanyi katika Baraza hili Maalum la Watumishi wa Makao Makuu la kufunga mwaka huu 2015, na kupitia Baraza hili naongea na watumishi wote wa Jeshi la Magereza nchini. Kama ilivyo kawaida katika mabaraza ya kufunga mwaka nitafanya tathmini ya yale yaliyojiri katika Jeshi kwa kipindi cha mwaka 2015 ambapo nitazungumzia mafanikio na changamoto zilizojitokeza na pia kutazama mwelekeo na matarajio yetu kwa mwaka 2016. Napenda niwapongeze na kuwashukuru watumishi wote kwa ujumla kwa ushirikiano mliouonesha katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali tuliyokabidhiwa na Serikali yetu na kuweza kuyafanikisha kwa kiwango cha kuridhisha, pamoja na kuwa na mazingira yenye changamoto kadhaa. Jeshi la Magereza limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kwa kiasi fulani zimeathiri utekelezaji wa majukumu yake. Changamoto hizo ni pamoja na ufinyu wa bajeti, makazi duni ya Maafisa na Askari, Uhaba wa vitendea kazi, Uhaba na uchakavu wa vyombo vya usafiri na mawasiliano, ukosefu wa zana na pembejeo, mabadiliko ya hali ya hewa kiasi cha kuathiri uzalishaji, tatizo la miundombinu ya magereza n.k. Pamoja na changamoto hizo na nyinginezo, kila mmoja wetu katika sehemu yake ya kazi amefanya jitihada kiasi kuwezesha Jeshi kutekeleza majukumu yake kwa kiwango cha kuridhisha licha ya kukabiliwa na changamoto hizo. Katika kukabiliana na changamoto hizo na nyinginezo, Jeshi la Magereza limekuwa likifanya jitihada mbalimbali na za makusudi kufanya maboresho katika maeneo kadhaa Hi kuongeza tija na ufanisi katika
7

HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

Feb 05, 2020

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN C. MINJAKWA WATUMISHI WA JESHI LA MAGEREZA TANZANIA BARA WAKATIWA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA 2015 NA KUUKARIBISHA MWAKA

2016 MAKAOMAKUU YA MAGEREZA TAREHE 31 DESEMBA. 2015Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana leohii tukiwa na afya njema na matumaini makubwa ya kuuona mwaka mpya2016. Nashukuru pia kupata fursa hii ya kukutana nanyi katika Baraza hiliMaalum la Watumishi wa Makao Makuu la kufunga mwaka huu 2015, nakupitia Baraza hili naongea na watumishi wote wa Jeshi la Magerezanchini.

Kama ilivyo kawaida katika mabaraza ya kufunga mwaka nitafanyatathmini ya yale yaliyojiri katika Jeshi kwa kipindi cha mwaka 2015ambapo nitazungumzia mafanikio na changamoto zilizojitokeza na piakutazama mwelekeo na matarajio yetu kwa mwaka 2016.

Napenda niwapongeze na kuwashukuru watumishi wote kwa ujumla kwaushirikiano mliouonesha katika utekelezaji wa majukumu mbalimbalituliyokabidhiwa na Serikali yetu na kuweza kuyafanikisha kwa kiwangocha kuridhisha, pamoja na kuwa na mazingira yenye changamoto kadhaa.

Jeshi la Magereza limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbaliambazo kwa kiasi fulani zimeathiri utekelezaji wa majukumu yake.Changamoto hizo ni pamoja na ufinyu wa bajeti, makazi duni ya Maafisana Askari, Uhaba wa vitendea kazi, Uhaba na uchakavu wa vyombo vyausafiri na mawasiliano, ukosefu wa zana na pembejeo, mabadiliko ya haliya hewa kiasi cha kuathiri uzalishaji, tatizo la miundombinu ya magerezan.k.

Pamoja na changamoto hizo na nyinginezo, kila mmoja wetu katikasehemu yake ya kazi amefanya jitihada kiasi kuwezesha Jeshi kutekelezamajukumu yake kwa kiwango cha kuridhisha licha ya kukabiliwa nachangamoto hizo.

Katika kukabiliana na changamoto hizo na nyinginezo, Jeshi la Magerezalimekuwa likifanya jitihada mbalimbali na za makusudi kufanyamaboresho katika maeneo kadhaa Hi kuongeza tija na ufanisi katika

Page 2: HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

f LJt<utekelezaji wa majukumu yake. Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwamwaka 2015 kutokana na jitihada hizo ni kama ifuatavyo;-

• Sera ya Taifa ya Magereza sasa iko tayari, kinachosubiriwa niMamlaka zinazohusika na ukamilishaji wake zikamilishe. Kukamilikakwa Sera hii kutawezesha Jeshi la Magereza kutekeleza Mpangowake wa Maboresho katika maeneo mbalimbali.

• Katika kushughulikia kero ya makazi, hivi karibuni Jeshi la Magerezakupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesaini Mkataba naKampuni ya Poly Technologies Inc ya Nchini China kwa ajili yakujengewa nyumba elfu tisa na mia tano (9,500) za makazi yaMaafisa na Askari katika maeneo mbalimbali ambayo kwa kipindikirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi.

• Katika kushughulikia kero ya usafiri Jeshi la Magereza pia limesainiMkataba na Kampuni za Ashok Leyland na Jeep ambapo magari miatisa na tano (905) yanategemewa kupokelewa mapema mwakani.

• Kwa upande wa Vyuo vyetu vya Magereza, Chuo chetu cha MaafisaMagereza Ukonga kimefanikiwa kupata usajili wa kudumu kutokaBaraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for TechnicalEducation - NACTE) na sasa ni Chuo cha Taaluma ya Urekebishajiambacho kina mamlaka kamili ya kujiendesha (-Autonomous).Kupatikana kwa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji kutasaidia kutoaelimu stahili ya Urekebishaji itakayotambulika ndani na nje ya Nchi.Elimu hii itaongeza weledi wa askari wetu watakaopitia kwenyeChuo hiki. Udahili wa wanafunzi unategemea kuanza mapemamwakani.

• Watumishi 494 wamepewa vibali vya kusoma fani mbalimbali katikavyuo vya nje ya Jeshi kwa ngazi tofauti kama ifuatavyo: Phd (04),Shahada ya Uzamili 7, Postgraduate Diploma 9, Shahada/Stashahada ya juu 123, Stashahada 141 na Astashahada 210.

• Kimataifa, kwa upande wa ulinzi wa amani Jeshi la Magerezalimeendelea kupeleka Maafisa kwenye Nchi mbalimbali. Kwa mwaka

Page 3: HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

2015 maafisa wawili (02) Congo DRC mmoja (01) Liberia na mmojaSouth Sudan vile vile Maafisa wawili (02) Nchini Namibia kamaWakufunzi.

• Kuhusu Kilimo, Mashamba ya Jeshi la Magereza yanaendeleakutumika kama mashamba darasa katika maeneo mbalimbali nchini.Sambamba na hilo, mashamba hayo yameendelea kutumika nawanafunzi wa Vyuo Vikuu kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Aidha,Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Wakala wa Mbegu za Kilimoliliendelea kuzalisha mbegu bora za Kilimo. Msimu wa 2014/2015kwa mfano ekari 214 zililimwa na kuzalishwa mbegu zenye uzito waKilogram 27,000 (tani 27) za mbegu za Mahindi, Nyanya, Alizeti naUfuta. Uzalishaji huu bado haujakidhi mahitaji makubwa ya mbeguyaliyopo. Juhudi zinaendelea kufanywa ili kuzalisha mbegu bora kwawingi.

• Kwa upande wa Mifugo ambayo ni ng'ombe, mbuzi, kondoo nanguruwe wameongezeka kutoka 16,986 mwezi Januari, 2015 hadi23,413 mwezi Desemba, 2015 sawa na ongezeko la asilimia 37.8%.Pia tumefufua mradi wa ufugaji wa kuku wa kisasa Gereza Ukongana KPF Morogoro na ufugaji wa Samaki Gereza Kwamgumi, Korogwena KMKGM.

• Kuhusu uwekezaji, tumeingia ubia na Kampuni ya TARBIM tokaUturuki kuingia ubia na Jeshi la Magereza. Tayari ekari 1,500zimeshalimwa ambapo miundo mbinu ya umwagiliaji inatarajiwakujengwa. Katika uwekezaji huu Jeshi la Magereza linachangia ardhiambapo Kampuni ya TARBIM inatoa utaalamu, mtaji na nguvukazi.Kwa ujumla katika mradi huu Jeshi la Magereza linamiliki hisa 30(30%) na Kampuni ya TARBIM hisa 70 (70%).

• Sambamba na mradi wa Bagamoyo, tunao mradi wa umwagiliajiGereza Idete ambapo Mkandarasi anaendelea na ukamilishaji wamiundo mbinu. Hadi sasa sehemu ya banio imekamilika kwa asilimia95 na mfereji mkuu umekamilika kwa asilimia 70. Kazi ambazo

Page 4: HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

hazijafanywa ni pamoja na kujenga mifereji midogo ya umwagiliaji(Secondary Canals).

• Tumeingia Mkataba na Kampuni ya kutengeneza Saruji ya TwigaCement kwa utaratibu wa ubia Hi kushirikiana kwenye uchimbaji wamadini ya chokaa ambayo ni mali ghafi muhimu katika utengenezajiwa Saruji huko Gereza la Wazo Hill. Kazi ya uchimbaji chokaainatarajia kuanza muda wowote kuanzia sasa. Katika kutekelezawajibu wake kwa jamii, Kampuni hiyo imetoa Saruji na fedha zakuanza kujenga nyumba za askari. Faida kubwa ambayo Jeshi laMagereza litaipata kutokana na ubia huo ni malipo ya fedha taslimuyatakayotokana na mavuno ya chokaa hiyo.

• Ujenzi wa maduka makubwa (Shopping Malls) pia unatarajia kuanzakatika Gereza Karanga (Moshi) na Kihonda (Morogoro) kwa ubia naMfuko wa Mafao ya Wastaafu wa GEPF. Mshauri Mtaalam wa mradihuu tayari ameshakamilisha kazi na ujenzi utaanza hivi karibuni.

• Jeshi la Magereza limefanikiwa kuandaa Andiko la Jeshikujitosheleza kwa chakula ambalo limeshawasilishwa Serikalini.Katika andiko hilo jumla ya mashamba kumi na moja yameainishwakwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nafaka, nyama na mafuta yakupikia. Mashamba hayo yako kwenye Magereza ya Kitengule,Arusha, Mollo, Ubena, Mugumu, Kitai, Songea, Kwitanga na Kimbiji.Kiasi cha Tshs. 13.6 bilioni zinaombwa ili kufanikisha mradi huu.Hata hivyo Serikali imeonesha nia nzuri ya kuunga mkono mpangohuu.

• Jeshi vile vile limefanikiwa kuandaa Andiko lenye kuhusisha miradinane (Quick Win Projects) ambayo miradi hiyo ikiwezeshwainaweza kuongeza thamani za mali zetu tunazozalisha. Andiko hiloliko mamlaka za juu zinazohusika,kwa mapitio na maamuzi. Miradihiyo ni Kokoto (Msalato), Samani (Ukonga), Viatu (Karanga),Ushonaji (Ukonga), Umwagiliaji (Idete), Mifugo (Ubena 8t Mbigiri) naAlizeti (Ushora), Msalato, Kongwa na Warm kuu.

Page 5: HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

• Kwenye suala la michezo timu zetu zimeshiriki kikamilifu kwenyemashindano mbalimbali na kupata ushindi, katika nafasi tofauti.Timu hizo ni za Mpira wa Wavu, (Volleyball), Mpira wa magongo(Hockey), Mpira wa Mikono (Handball) na kwa upande wa timu yetuya Mpira wa Miguu inaendelea kufanya vizuri kulinganisha na misimumiwili iliyopita. Aidha baadhi ya wachezaji wetu wa Mpira waMagongo walishiriki mashindano ya kimataifa Afrika Kusini kwa ajiliya kufuzu mashindano ya Olimpiki. Kwa upande wa Riadha, askariwetu wawili walishika nafasi za kwanza katika mashindano yakimataifa.

Baada ya kueleza mafanikio yaliyopatikana napenda kuwapatia maagizoyaliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Tano kama ifuatavyo;-

(i) Kubana matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima na kuwa nanidhamu katika matumizi ya fedha za Serikali na mali zaumma.

(ii) Kuzingatia utendaji wa kazi wenye tija na kuachana na ule wakufanya kazi kwa mazoea (business as usual).

(iii) Kupiga vita rushwa na ufisadi.

(iv) Watumishi wote wa Umma wahudhurie na wabaki kazini kwamuda wote uliopangwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zaUtumishi wa Umma.

(v) Watumishi wote kuwahi kazini na kutumia kitabu chamahudhurio (Attendance Register).

(vi) Kuhakikisha kuwa watumishi wanawajibika kwenye maeneoyao ya kazi na kutumia rasilimali za ofisi kama vile 'computer'kwa shughuli za ofisi tu.

(vii) Kuwahudumia wananchi kwa haraka, weledi, umahiri nanidhamu ya hali ya juu.

Page 6: HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

(viii) Kuweka utaratibu wa Watumishi wa Umma kuvaa beji zenyemajina yao Hi wananchi wanaohudumiwa wawatambue.

(ix) Kuweka Dawati la Msaada (help desk) kwenye ofisi ya ummakwa ajili ya wananchi wanaofuata huduma kwenye ofisi hiyo.

(x) Taasisi za Umma ziweke utaratibu wa kupata mrejesho(feedback) kwa huduma zinazotolewa na ofisi hizo ziimarishemawasiliano kwa umma kwa ujumla.

(xi) Kuhakikisha kuwa Watumishi wa Umma wanatunza siri zaSerikali.

(xii) Kuwa na Mkataba wa Huduma kwa Mteja unaotekelezwa.

Kufuatia maagizo hayo nachukua nafasi hii kuagiza utekelezaji wakeufanyike haraka na kutoa mrejesho. Aidha utendaji wetu wa kazi kila sikuuende sambamba na maagizo hayo.

Katika mwaka 2016 maeneo yatakayopewa kipaumbele ni kamaifuatavyo;-

• Kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kama ufugaji waKuku wa kienyeji na Samaki.

» • Kuongeza uzalishaji wa bidhaa kutoka kwenye Viwanda vyetu

• Kuanzisha kilimo cha mazao ya kibiashara yenye thamani kama vilemaua, mbegu za mafuta, mboga za aina mbalimbali na matunda

• Ujenzi wa Rest House katika Mikoa.

• Ujenzi wa nyumba za askari.

• Kuendeleza ujenzi na ukamilishaji wa miradi ya umwagiliaji

• Kuanzisha Ofisi za Wakuu wa Magereza (M) kwenye mikoa mipya yaKatavi, Simiyu, Njombe na Geita.

• Kuakikisha Chuo cha Taaluma ya Urekebisha kinaanza rasmi.

Page 7: HOTUBA YA KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA …magereza.go.tz/docs/Hotuba_ya_CGP_mwaka_mpya.pdfkirefu yamekuwa yakikabiliwa na ukosefu wa nyumba za makazi. • Katika kushughulikia kero

• Kuendeleza mikakati ya kupunguza msongamano magerezani kwakuimarisha ushirikiano wa vyombo vya Haki Jinai, kuhamasishamatumizi ya adhabu mbadala n.k.

Nimalizie hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwakampya 2016 kwa kuwataka nyote kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na Taratibu zinazotawala uendeshaji wa Jeshi la Magereza. Aidhakatika utekelezaji wenu wa kazi za kila siku uende sambamba na kasi yaSerikali ya Awamu ya Tano Hi tuweze kufikia ufanisi unaotarajiwa.

Niwatakie nyote pamoja na familia zenu afya njema na mafanikio katikamwaka mpya 2016

J. C. MinjaKAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA