Top Banner
FATIMA Al-ZAHRA Kimeandikwa na: Sayyid Muhammad al-Husaini al-Shirazi Kimetajumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui P.O. Box 19701, Dar es Salaam. Tanzania. Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page A
46

Fatima al-Zahra

Mar 22, 2016

Download

Documents

Cha kuzingatia ni kwamba kumjua mtukufu huyu ambaye ni Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) ni wajibu kwa Waislamu wote, kwani ameshasema (a.s): “Jueni kwamba mimi ni Fatima al-Zahra.” Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini. Bibi Fatima (a.s.) ni maasumu wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake na kumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha Amirul Muuminina Ali (a.s) na watoto wake walio maasumu (a.s).
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Fatima al-Zahra

FATIMA Al-ZAHRA

Kimeandikwa na:Sayyid Muhammad al-Husaini al-Shirazi

Kimetajumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui

P.O. Box 19701, Dar es Salaam. Tanzania.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page A

Page 2: Fatima al-Zahra

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL-ITRAH FOUNDATION

ISBN: 978 - 9987 - 512 -21 -8

Kimeandikwa na:Sayyid Muhammad al-Husaini al-Shirazi

Kimetajumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui

P.O. Box 19701, Dar es Salaam/Tanzania.

Kimehaririwa na: Septemba,2008 Dr. M. S. Kanju

Email: [email protected]. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania

Simu: +255 22 2110640

Kupangwa katika Kompyuta na:Hajat Pili Rajab.

Toleo la kwanza: Septemba,2008Nakala:1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah Foundation

P.O. Box 19701Dar es Salaam, TanzaniaSimu:+255 22 2110640Fax: +255 22 211310

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page B

Page 3: Fatima al-Zahra

YALIOMO

1. Neno la mchapishaji………………………………................................2

2. Al-Hadith al–Qudsi………………………………….….........................5

3. Ushahidi wa kihistoria………………………………….......................15

4. Njama zaendelea........…………………………………………............16

5. Utukufu wa Zahra............................................………….…….............17

6. Zahra (a.s) ni Nuru ya Mwenyezi Mungu.............................................17

6. Bibi wa wanawake wa ulimwenguni………………………….............19

7. Kigezo na mfano mwema…………………………………..................20

8.Maisha ya ndoa.......................................................................................21

9. Ukarimu wake…………………………………………………............22

10. Miongoni mwa Ibada zake………………………………..................23

11. Katika elimu ya Az - Zahraa…..…………………………..................24

12. Hotuba yake Msikitini.........................................................................25

13. Shahada na uchungu...........................................................................25

14. Fatwa kuhusu Bi. Fatma-Zahra (a.s) ………………….......................29

15. Bibliografia..........................................................................................34

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page C

Page 4: Fatima al-Zahra

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabukiitwacho, Fatimah al-Zahra. Sisi pia tumekiita, Fatima al-Zahra.

Kijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatima Zahra (a.s), bintiwa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kati ya mihadhara ya thamani ya mare-hemu Imam Muhammad al-Husaini al-Shirazi (Mwenyezi Mungu amrehe-mu).

Ni kitabu cha aina yake katika lugha ya Kiswahili kinachoelezea maisha yaBibi huyu mtukufu mwenye nuru. Cha kuzingatia ni kwamba kumjuamtukufu huyu ambaye ni Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) niwajibu kwa Waislamu wote, kwani ameshasema: “Jueni kwamba mimi niFatima al-Zahra.” Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini. BibiFatima (a.s.) ni maasumu wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake nakumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha AmirulMuuminina Ali (a.s) na watoto wake walio maasumu (a.s).

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wamaendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, nganoza kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tenakatika akili za watu.

Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamuakukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyaleya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page D

Page 5: Fatima al-Zahra

Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukubali juku-mu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wotewalioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwakwake.

Mchapishaji:Al-Itrah FoundationS. L. P. 19701Dar-es-Salaam, Tanzania

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page E

Page 6: Fatima al-Zahra

F

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page F

Page 7: Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 1

Page 8: Fatima al-Zahra

2

Fatima al-Zahra

NENO LA MCHAPISHAJI (KIARABU)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

“Lau kama si wewe basi nisingeumba ulimwengu……”

Hadithil-Qudusi tukufu…… kwayo zimetaabika akili na kupumbaa, nakwayo fahamu zimetahayari lakini nyoyo safi zimeipenda…… ikaathiri,ikaangaza na nuru yake ikawaangazia walio mbinguni kama nyota zinavy-owaangazia walio ardhini.

Amesema Al-Imam Swadiq (a.s): “Mwenyezi Mungu hafanyi mamboisipokuwa kwa kupitia sababu1 (zake)”. Kwa kanuni hii Mwenyezi Munguameumba ulimwengu, nayo ni kanuni ya ‘sababu na kisababishwa’ au‘chanzo na matokeo’ (Al-I’lalu wal-Ma’aluulaat) kulingana na walivyose-ma wanafalsafa, na wote wanaafikiana kwamba chanzo kikuu au mwanzil-ishi wa vitu ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Mwenyezi Mungu anase-ma: “Lau kama si wewe basi nisingeumba ulimwengu…..”,anamwambia Mtume wake Mtukufu na kipenzi chake, Muhammad binAbdullah (s.a.w.w), yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu amemfanyaMtume (s.a.w.w) ndio sababu ya lengo la kuumba, kwa maana kwambalau kama si Muhammad na kizazi chake, na wajibu wa kuwajua, kuwapen-da na kuwatii (a.s) basi Mwenyezi Mungu asingeumba ulimwengu huu…

Na katika Hadithi nyingine anasema (s.w.t): “Mja wangu nimeumba vitukwa ajili yako na nimekuumba wewe kwa ajili yangu, nimekupa duniakwa ihsani na nimekupa akhera kwa imani”2. Wa mwanzo kuambiwana mkusudiwa ni Mtume wa wanadamu Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul–bait wake (a.s).

1Baswairud-Darajaat uk: 6, na rejea Ghawaaliy liaaliy J: 3 uk: 286.2 Kalmatullahi uk: 169

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 2

Page 9: Fatima al-Zahra

3

Fatima al-Zahra

Hadithi hii na nyingine nyingi kati ya Hadithi tukufu za Qudsi, za Mtumena Maimam zilizopokelewa kuhusu jambo hili huenda kuna ugumu kwabaadhi kuzielewa au kuzistahamili, na ameshasema ImamAmirul’Muuminina Ali (a.s): “Jambo letu ni gumu mno halistahamiliisipokuwa Malaika mkuruba au Nabii mursali au mja ambaye MwenyeziMungu ameujaza moyo wake imani”3. Jambo hili linahitaji moyo uliojaaimani na uchamungu na viwiliwili vinavyoenda mbio kwa kufanya ibadana kutii, usiku na mchana bila ya taabu, uchovu n.k.

Kijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatma Zahra (a.s) ni katiya mihadhara ya thamani ya Al-Imam Muhammad Al-Husein As-Shirazi(Mwenyezi Mungu amrehemu) - ambayo ameitoa kabla ya miaka 25,yaani 17 Jumadul-Ulaa 1400 A.H. ikawa imesambazwa na kupataumashuhuri tangu wakati huo kwa nguvu ya mvuto wake, uzuri wake, nakwa maana yake nzuri, hadi ikawa ndugu na jamaa wanapokezana kandazake… kisha baadae ikatolewa katika njia ya maandishi, na hatimaye Al-Imam as-Shirazi akayarejea na akaongeza baadhi ya nukta muhimu nakutoa ufafanuzi uliohitajika…, ni kitabu kizuri kilioje, na ni haja iliojekwa wakati huu ambao mazungumzo yamekuwa ni mengi kuhusu Bibi wawanawake wa ulimwenguni (a.s), mijadala na midahalo imezidi juu yashakhisiya yake tukufu na nafasi yake katika umma.

Cha kuzingatia ni kwamba kumjua Bibi wa wanawake wa ulimwenguni(a.s) ni wajibu kwa waislamu kwani ameshasema (a.s): “Jueni kwambamimi ni Fatma-Zahra.”4 Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini… yeye ni maasum wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake nakumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha Amirul-Muuminina Ali (a.s) na watoto wake maasumu (a.s).

3 Al-Khiswali uk. 624.4 Kwa maelezo zaidi rejea (Min fiqihiz-Zahraa juz. 3, Khutba yake msikitini.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 3

Page 10: Fatima al-Zahra

4

Fatima al-Zahra

Na sisi katika taasisi yetu iitwayo Muasasatul-Kalmati litahqiyqi wanashirtumesimamia kuchapisha na kusambaza kijitabu hiki kwa kutaraji kuwakutokana na nafasi yake tukufu awe ni kati ya waombezi wetu siku yamalipo. Amani na shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi waviumbe vyote.

Muasastul-Kalmat litahaqiyqi wanashir P.O Box 6080 – Shauran - Beirut – Lebanon.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 4

Page 11: Fatima al-Zahra

5

Fatima al-Zahra

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, salana salamu zimwendee Mtume Muhammad (s.a.w.w) na aali zake wemawaliotoharika (a.s), na laana daima ziwashukie maadui zao hadi Siku yaMalipo.

AL–HADITH AL-QUDSI

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi Al-Qudsikumwambia Mtume wake Mtukufu (s.a.w.w): “Ewe Muhammad lau kamasi wewe basi nisingeumba ulimwengu, na lau kama si Ali basi nisingeku-umba na lau si Fatmah basi nisingewaumba nyinyi.”5

Kuna tofauti gani baina ya Hadith Al-Qudsi na Aya za Qur’ani Tukufu?Tofauti baina yake ni katika mambo mengi, kati ya hayo ni: -Changa moto: Kwani Qur’ani Tukufu ni muujiza kutoka kwa MwenyeziMungu, inabeba ndani yake mwongozo kamili kwa ajili ya maisha memaduniani na akhera na humo kuna muujiza na changamoto katika nyanjazote:Kielimukifasihikijamiikiuchumikisiasa na katika mambo ya ghaibu5 Rejea Kaashif liaaliy cha Al-Arandasi kama alivyonukuu As-Sayid Mir Jihaaniykatika Janatul-aswimah na Allamah Al-Mrandi katika Multaqaal Bahrain uk. 14na Mustadraku Safinatil-Bihari Juz. 3, uk. 334 na ameinukuu Awaalimul-Ulumiuk. 26 kutoka katika Majmaun-Nurain na katika Fiqiuhiz -Zahraa Juz. 19.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 5

Page 12: Fatima al-Zahra

6

Fatima al-Zahra

Kisha changamoto haiko katika Qur’ani tu bali na kwa yule aliyeteremshi-wa Qur’ani pia, naye ni Nabii Mtukufu (s.a.w.w). Amesema MwenyeziMungu Mtukufu:

“Sema kama watakusanyika wanadamu na majini ili walete mfano waQur’ani basi wasingeweza kuleta mfano wake hata kama watasaidi-ana baadhi yao kwa baadhi” (Sura Al-Israi: 88)

Na katika Aya nyingine amesema (s.w.t):

“Au wanasema ameizua, sema leteni Sura kumi mfano wa Qur’anizilizozuliwa kama nyinyi ni wakweli”. (Sura Hud: 13)

Na katika Aya ya tatu anasema (s.w.t):

“Kama nyinyi mnashaka kwa yale tuliyoyateremsha kwa mja wetubasi leteni Sura moja mfano wa Qur’ani na waiteni mashahidi wenuwasiokuwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wakweli.” (Sura Al-Baqarah: 23)

Hapa unadhihiri muujiza wa Qur’ani na changamoto ya Qur’ani Tukufuambapo tangu iliposhuka hadi leo hii watu wameshindwa kuleta hata sura

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 6

Page 13: Fatima al-Zahra

7

Fatima al-Zahra

moja angalau mfano wa Suratul–Kauthar. Qur’ani Tukufu inaendelea kuwana sifa hii hadi siku ya Kiyama, na changamoto hii ipo na itaendelea kuba-ki milele.

Na Hadith Al-Qudsi ni ile ambayo imetoka kwa Mwenyezi MunguMtukufu lakini sio mahsusi kwa Mtume Muhamad tu, bali inawahusuManabii wengine wa Mwenyezi Mungu na wala haina sifa ya changamotona muujiza. Baadhi ya maulamaa wamekusanya kiasi kikubwa cha HadithiAl- Qudsi katika vitabu vyao mfano:-

Al–Allammah Al–Majlisiy (r.a) katika kitabu chake Al-Biharul-Anwaar nakatika baadhi ya vitabu vyake vingine

Ndugu yangu As-Shahdi6 katika kitabu chake Kalmatu llahi.

Ama neno Qudsi- lina maana ya tukufu - yaani isiyo na dosari au upungu-fu. Al-Hadithi Al-Qudsi ni Hadithi tukufu ambayo imeepukana na kasorona upungufu.

Hadithi Al-Qudsi ziko aina mbili:

1. Zenye njia imara ya upokezi - yaani zilizopokewa kutoka kwa Mtumewa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) kwa sanadi sahihi naambazo wamezipokea kutoka kwao wapokezi waaminifu.

2. Mursal sanad – yaani sanadi zake hazikuungana na mursal yakeinakuwa ni dhaifu.

Hivyo ambayo iko katika aina ya kwanza ndio yenye kukubaliwa nakutegemewa na Maulamaa. Ama aina ya pili, kama humo kutakuwa na

6 Ayatullah As-Shahidi As-Sayyid Hasani As-Shiraz mwasisi wa Hauzatuz-Zainabiyah –Syria.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 7

Page 14: Fatima al-Zahra

8

Fatima al-Zahra

hekima, mawaidha na mwongozo ambao una manufaa kwa mwanadamuau hukumu isiyo ya lazima, basi itakuwa inaingia katika kanuni ya “tasaa-muhu” katika hoja za Sunnah7 nk… hivyo inakubaliwa pia.

Tukiongezea ni kwamba nyingi kati yake maulamaa mashuhuriwamezikubali, kuzikubali kwao na kuzifanyia kazi kunalazimu kuzitumia.Kama ilivyobainishwa katika Usul, hususan inapokuwa haizalishi huku-mu ya kisheria, ambapo Hadith Al-Qudsi aghalabu zinakuja katika upandewa maadili, adabu, hekima, desturi za kijamii na mwongozo katika baadhiya maslahi na kuhadharisha baadhi ya ufisadi wa kilimwengu, kijamii,kitabia n.k.

Tukirejea mwanzo, hakika Hadithi ambayo tumeitungia kijitabu ni daliliiliyo wazi juu ya utukufu wa Ahlul–bait (a.s) na daraja zao, hususan asiliya mti wao mtukufu naye ni Fatma, baba yake, mume wake na watotowake (a.s).

MAANA YA HADITHI

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anamhutubia Mtume wake mtukufu(s.a.w.w) kwa kumwambia: “Ewe Muhammad lau kama si wewe basinisingeumba ulimwengu”. Hivyo yeye ndio lengo la kuumba.

Na “Lau kama si Ali basi nisingekuumba wewe”, na “Lau kama si FatmahZahra basi nisingewaumba nyinyi.” Katika sharti hili la mwisho inadhi-hirika kwetu thamani ya Fatma Zahra (a.s) na utukufu wake kwaMwenyezi Mungu Mtukufu, kwa Mtume wake na kwa Maimamu (a.s),fadhila kubwa aliyonayo na athari ya kisheria na kimaumbile katikakuumbwa ulimwengu na viumbe wote…

7 Rejea kitabu Risaalatu Tasaamuh fiy adilatis–Sunnah (cha mtunzi huyu) ndaniya kitabu al-Waswaailu ilaa rasaaili J: 6 cha Imam As-Shirazi.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 8

Page 15: Fatima al-Zahra

9

Fatima al-Zahra

Tumezungumzia Hadithi hii ya Al-Qudsi hasa kwa ajili ya kupata utukufuwa kutaja baadhi ya fadhila za Bibi huyu mtukufu ambaye Mtume waMwenyezi Mungu amesema juu yake: “Binti yangu Fatma Zahra ni Bibiwa wanawake wa ulimwenguni.” 8

Huenda yatakuja maswali mawili katika akili za baadhi ya watu: Swali la kwanza: Je, Mwenyezi Mungu ni bakhili - Mungu atulinde nahilo – kiasi kwamba lau si Mtume (s.a.w.w) asingeumba ulimwengu,sayari, jua, mwezi na nyota? Kama si hivyo basi nini maana ya “Lau siwewe nisingeumba ulimwengu?”

Katika swali hili tunauliza: Kwanza: Je, Mwenyezi Mungu ana madhumuni na lengo katika kuumbaulimwengu au hana?Jawabu: Ndio, anayo madhumuni na lengo.

Pili: Lengo hilo ni lipi?Jawabu: Ni kumfikisha mwanadamu kwenye ukamilifu wa kiroho wa haliya juu kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Sikuwaumbamajini na watu isipokuwa waniabudu.”3

Tatu: Je ukamilifu ni jambo linalofahamika wazi kwa watu wote? Yaanikatika hisia za dhahiri au zilizofichikana?

Jawabu: Hakika hauko wazi kwa watu wote.

Nne: Je, kuna uwezekano wa kuufikia ukweli huu au hapana?Jawabu: Kwa kawaida hakuna uwezekano wa mwanadamu kuufikia ilakwa wasila wa dalili na kiongozi.

Tano: Dalili ni ipi na kiongozi ni nani?Jawabu: Dalili ni Qur’ani Tukufu na kiongozi ni Nabii (s.a.w.w), FatmaZahra na Maimamu (a.s). 8 Amaalis-Suduqu uk. 298 Majlis No. 49 Hadith ya 12.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 9

Page 16: Fatima al-Zahra

10

Fatima al-Zahra

Kama hivyo ndivyo basi mwenye kukamilisha lengo la kuumbwa niMtume, Fatmah na Maimamu (a.s), hivyo kama sio wao kungekuwa naupungufu katika kuumba ulimwengu, na Mwenyezi Mungu Mtukufuhaumbi kiumbe chenye upungufu, kwa ajili hiyo amesema (s.w.t): “Lau siwewe nisingeumba ulimwengu…”

Ama ikiwa Mwenyezi Mungu anamuumba mwanadamu bila ya kuumbadalili pamoja naye basi lengo la kuumba kwake halitatimia, na hiyo ita-maanisha upungufu wa Muumbaji na kushindwa kwake – tunajilinda kwaMwenyezi Mungu kwa hayo – na kuumbwa mwandamu kutakuwa ni upu-uzi, na Mwenyezi Mungu ametakasika kutokana na upuuzi.9 Kwa msingihuu, kuumbwa Nabii Mtukufu kunakuwa ndio sababu ya kuumbwaulimwengu huu, na kwamba cha mwanzo alichoumba Mwenyezi Mungu ninuru ya Nabii (s.a.w.w) na Ahlul Bait wake (a.s)10 na kisha akaumbaulimwengu huu wote kutokana na nuru yao. Hivyo wao ndio sababu yalengo la kimaumbile kama wanavyosema watu wa falsafa.

Na katika Hadithil-Kisaa: “Hakika Mimi sikuumba mbingu na ardhi walamwezi na jua, sayari hazizunguki, bahari haiendi wala meli hazitembeiisipokuwa kwa ajili ya mapenzi ya hawa watano.”11

8 Amaalis-Suduqu uk. 298 Majlis No. 49 Hadith ya 12.9 Kwa ufafanuzi rejea Qaulu sadid fiy sharhit tajiriyd katika kusudio la nne kati-ka unabii na uimamu cha mtunzi wa kitabu hiki.10 Yanabiul Mawadah Juz. 1 uk. 118, Shawahidut-Tanzil Juz. 1 uk. 414, NahjulHaq cha Allamah al-Hilliy uk. 190, Tafsir Burhan cha Baharan Juz. 3 uk. 170,Nurul-Abswar, Tafsir Tha’alab katika tafsiri ya Aya ya 54 Suratul Furqan.Yanabiul Mawadah Juz. 1 Babul Awal uk. 14 pia Juz. 1 10-11, TadhkiratulKhawaas cha Ibn Jawzi uk. 46, Kashiful Ghumah Juz. 2 uk. 84, Dalailun-Nubuwah Juz. 2 uk. 148 nk. 11 Duau waziyarah: Hadithul kisaa pia tazama mujaladi wa 1 (min fiqihiz-Zahraa).

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 10

Page 17: Fatima al-Zahra

11

Fatima al-Zahra

Na amesema Al-Imamu Al–Mahdi (a.s): “Sisi tumeumbwa kwa ajili yaMola wetu na viumbe wameumbwa kwa ajili yetu.”12

Na imekuja katika Biharul-Anwar ya Allammah Al–Majilisi amenukuukutoka kwenye kitabu Al-Hidayah cha Sheikh Tusiy amesema: “Ni wajibutuitakidi kuwa unabii ni wa kweli kama ambavyo tunaitakidi kuwa tawhidni ya kweli na kwamba manabii ambao amewatuma Mwenyezi Mungu ni124,000, wamekuja kwa haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwambakauli yao ni kauli ya Mwenyezi Mungu na jambo lao ni jambo laMwenyezi Mungu na kuwatii wao ni kumtii Mwenyezi Mungu na kuwaasiwao ni kumwasi Mwenyezi Mungu; na kwamba wao hawakutamkaisipokuwa yatokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutoka katikawahyi wake na kwamba mabwana wa Manabii ni watano na wao ndio borazaidi, wao ndio walipewa sheria na wao ni ulul-azmi nao ni: Nuhu,Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad (a.s).

Na kwamba Muhammad ndio Bwana wao na mbora wao na kwamba aliku-ja kwa haki na ameisadikisha Mitume, na kwamba wale ambaowamemwamini wakamwadhimisha, wakamnusuru na wakafuata ile nuruiliyoteremshwa pamoja naye hao ndio wenye kufaulu, na ni wajibu tuitaki-di kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuumba kiumbe bora na kituku-fu zaidi Kwake kuliko Muhammad (s.a.w.w), na baada yake ni Maimamu(a.s.), na wao ndio viumbe vipenzi zaidi kwa Mwenyezi Mungu na wamwanzo wao kumkubali Mwenyezi Mungu, pale Mwenyezi Mungualipochukua ahadi kwa Manabii katika ulimwengu wa kiroho naakawashuhudisha juu ya nafsi zao kwa kuwauliza: Je, yeye si ndio Molawao? Wakasema: Ndio wewe ni Mola wetu.

Na kwamba Mwenyezi Mungu alimtuma Nabii wake (s.a.w.w) kwaManabii katika ulimwengu wa kiroho; na kwamba Mwenyezi Mungualimpa kila Nabii aliyompa kwa kadri ya kumjua kwake Nabii wetu

12 Al-ghaibatu cha Tuusiy uk. 285 Hadith ya 7 na al-Ihtijaaj uk. 467.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 11

Page 18: Fatima al-Zahra

12

Fatima al-Zahra

(s.a.w.w) na kwa kutangulia kwake katika kumkubali. Na tunaitakidikwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba vitu vyote kwa ajili yakena Ahlul–Bait wake, na kwamba lau kama si wao basi Mwenyezi Munguasingeumba mbingu, ardhi, Pepo na Moto wala Adam, Hawa, Malaikawala chochote katika vilivyoumbwa”13 mwisho wa kunukuu.

Maneno haya yaliyonukuliwa kutoka kwa As-Suduq ni muhtasari waHadithi na riwayah nyingi zilizokuja kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s) zina-zotueleza kwamba wao ndio msingi wa kuumbwa ulimwengu, naMwenyezi Mungu amewajaalia kuwa ni wasila wa kuumbwa ulimwenguna sababu ya lengo lake, kama ambavyo wao (a.s) ndio sababu ya hurumaya Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa ulimwengu na wao ndio sababuya kuendelea kuwepo kwa ulimwengu… Na zinaeleza hayo wazi dalilimbali mbali… kama sio wao basi ardhi ingedidimia.14

SWALI LA PILI:

Nini maana ya ‘Lau kama si Ali basi nisingekuumba?’ Wakati Mtume(s.a.w.w) ana shakhsiya tukufu zaidi, kwa nini kuumbwa kwake kuambat-ane na kuumbwa kwa Ali Amirul-Muuminina (a.s) na nini uhusiano uliopobaina yao?

Jawabu la hilo ni kwamba: Uimamu ambao unapatikana kwaAmirul–muuminina ni mwendelezo wa kawaida wa kazi ya unabii, nakwamba mnyororo wa uhusiano baina ya unabii na uimamu umemfanyaAmirul-Muuminina (a.s) awe ndio mwenye kukamilisha lengo la kuumb-wa Mtume (s.a.w.w) kwa sababu Nabii (s.a.w.w) alikuja ili kuongaza watuna kuwafikisha katika ukamilifu unaotakikana. Lakini umri wa Nabii(s.a.w.w) ni mfupi na hakuna budi apatikane baada yake atakayeendeleakuongoza njia, tukiongezea kwamba watu wengi hawafikii kwenye

13 Biharul Anwar Juz. 16, uk. 372 Fadhail Nabii (s.a.w.w) wakhaswaiswihi.14 Rejea al-Kaafiy Juz. 1, uk. 179, Hadith ya 10.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 12

Page 19: Fatima al-Zahra

13

Fatima al-Zahra

ukamilifu mara moja bali hatua kwa hatua. Hivyo ilikuwa hakuna budi yakupatikana mtu mwingine kwa ajili ya kukamilisha na kuendeleza baada yakufariki Nabii (s.a.w.w) ambaye ndio wasii wa Mtume na Imamu baadayake Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (a.s).

Tukiongezea kwamba watu walifanya njama katika dini ya Mtume waMwenyezi Mungu na wakapotosha Uislamu, na kama si Ali (a.s) basiisingebainika haki na batili….. kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungualimuumba Ali (a.s) ili asimame dhidi ya upotovu, mfarakano na ikhitila-fu ambazo zitapatikana katika umma baada ya kuondoka Mtume Mtukufu(s.a.w.w). Kama sio kuwepo Amirul-Muuminina (a.s) basi juhudi yote aliy-oifanya Mtume katika kueneza ujumbe wa Uislam ingepotea na watuwangerudi kwenye ujahili wa kikafiri kwa mara nyingine, na huenda upo-tovu na itikadi zilizo kama vile Mungu kuwa na kiwiliwili, kutezwa nguvu,taf’widh n.k, zingeenea katika ulimwengu wa Kiislamu, fikra ambazoalikujanazo Muawiya na mfano wake baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w)ili kubomoa juhudi na kazi ya Nabii (s.a.w.w) ya kueneza dini tukufu yaKiislamu, na badala yake kufuata nyendo za Muawiya na kutekelezamisingi yake, hiyo ni sawa iwe katika hukumu za kisheria au za kuamilianapamoja na watu wengine, serikali na wananchi… hivyo isingepatikanafaida inayotakikana ya kuwepo dini ya Kiislamu, na kutumwa kwa Nabiiambako hakujafikia lengo kamili, na hapo kusingekuwa na faida yeyote.

Hapa inadhihirika dharura ya kuwepo Imam Ali (a.s) ambapo ilishuka Ayaya kukamilika dini kwa ajili yake siku ya Ghadir pale Mtume waMwenyezi Mungu alipomtawaza Ali (a.s) kuwa Khalifa baada yake kwaamri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu akisema (s.w.t):

“Leo nimewakamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema yanguna nimekuridhirieni Uislam kuwa dini yenu.” (Sura Al-Maidah: 3)

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 13

Page 20: Fatima al-Zahra

14

Fatima al-Zahra

Imam Ali alikuwa amesimama msimamo sambamba na neno la ujumbe waMwenyezi Mungu kwa ajili ya kuuhami na kuulinda kutokana na hila zawanafiki… Amesema (s.w.t):

“Na hakuwa Muhammad isipokuwa Mtume walishapita kabla yakeMitume, je akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu.”(Sura Ali Imran: 144)

Mwenyezi Mungu kwa Aya hii tukufu amekusudia kuwa haijuzu kuachamambo ya dini ya Mwenyezi Mungu kwa watu bila ya kiongozi, sawa aweMtume yupo au hayupo.15

Kweli Imam Ali Amirul –muuminina (a.s) alikuwa na jukumu kubwa na lamsingi katika kusimama dhidi ya nia za wanafiki, makafiri na wapotosha-ji, na kuuhifadhi Uislamu kutokana na upotovu na uovu. Imepokewa kuto-ka kwa Imam Ali (a.s) kwamba amesema: “Mimi nimeng’oa mzizi wa fiti-na na hakuthubutu yeyote asiyekuwa mimi kufanya hivyo.” 16

Na kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Nilimwona Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w) siku ya Fatih Makka amegandamana na pazia la Al-Ka’aba naye anasema: “Ee Mwenyezi Mungu niletee msaidizi miongonimwa watoto wa ami yangu atakayeniongezea nguvu.” Jibrilu akateremkakwake akasema: “Ewe Muhammad je, Mwenyezi Mungu hajakuungamkono kwa upanga kati ya panga za Mwenyezi Mungu ulioelekezwa kwamaadui wa Mwenyezi Mungu? Anamkusudia kwa hilo Ali bin AbuTwalib.”17

15 Rejea Majmaul Bayan cha Tabarisi Juz. 1, uk. 512-514.16 Nahjul Balagha Khutba na. 93.17 Biharul Anwar Juz. 1, uk. 61 mlango wa Babu 106 Hadith ya 1.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 14

Page 21: Fatima al-Zahra

15

Fatima al-Zahra

USHAHIDI WA KIHISTORIA

Muawiya bin Abu Sufian alikusanya pembezoni mwake kundi kati ya waleambao hawamchi Mwenyezi Mungu na walikuwa ni wapenda dunia… basiakatengeneza kwao Uislamu mahsusi na mfumo mbaya zaidi kuliko wakijahilia, kutokana na Uislam huu wa ki-Banii Umayyah watu wakawawanauwana baadhi yao kwa baadhi kwa jina la dini, na katika aliyoyafanyaMuawiya ni kwamba alichoma moto Waislamu arobaini elfu huko Yemenikwa jina la dini. Na kama sio kusimama kidete Amirul-Muumina mbele yaMuawiya basi dini ya Kiislamu ingekuwa ni wasila wa kufanyia dhulma,ufedhuli, udikteta na kupora haki za wengine.

Hakika akili na mantiki inaunga mkono Hadithi hii ya Al-Qudusi iliyotan-gulia ambapo kama sio kuja kwa Amirul- muumina na Maimam maasum(a.s) baada ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w) watu wasingejua Uislamu wakweli, na wangedhani kuwa Uislamu ndio ule upotovu wa Banu Umayya,kiasi kwamba Bani Umayya waliufanya Uislamu kuwa ni wasila wakutu-mikia maslahi yao ya kidunia na kushibisha matamanio yao na shahawazao.

Na kama sio Ahlul-Bait (a.s) basi mafunzo sahihi ya dini yangefutwa nakuzimika nuru yake na zingetawala katika jamii ya Kiislamu itikadiambazo zinamaanisha kuwa dini ndio hii dhulma ujeuri na upotovu wa ki-Bani Umayya, hiyo ni kwa sababu watu walioishi katika utawala wa BaniUmayya hawakuona mwendo mzuri alioufundisha Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w) katika kujenga jamii ya Kiislamu.

Je, uovu wa Muawiya na mfano wake ulikuwa ni mwendo wa Mtume waMwenyezi Mungu? Hapana. Hakika wao walikuwa wanatangaza ufisadina upotovu na kuwa mbali na hukumu za dini, walikuwa wanakunywapombe, wanauwa watu wema bila ya hatia, wanavunja heshima za watu,yote hayo kwa jina la ukhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 15

Page 22: Fatima al-Zahra

16

Fatima al-Zahra

hawakutosheka na hilo bali walikuwa wanadai kuwa wao ni wawakilishiwa Mwenyezi Mungu duniani na kwamba vitendo vyao vyote ni sahihi navinafuata sheria… imenukuliwa kutoka kwa Muawiya kwamba siku mojaalimwambia Mughira bin Shuubah: “Humru wamezidi na nimefikiriakuuwa theluthi yao.”18

NJAMA ZAENDELEA

Lakini Imam Amirul-Muuminina (a.s) alisimama imara dhidi ya mbinu yaMuawiya na kuuhifadhi Uislamu kutokana na upotovu. Ama baada yaAmirul-Muuminina kufa shahidi, ni nani atakayesimama kwa muda wotewa historia dhidi ya watawala ambao wanachezea mali za umma kwa jinala Uislamu mfano wa Bani Umayya na Bani Abbas?

Kwa sababu hii kulikuwa na haja sana kuwepo Maimamu watukufuMaasum (a.s) na kama sio wao dini yote ingefutwa na kazi ya Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Amirul-Muuminina ingepotea kabisa…Hapa linabainika kwetu jukumu la Fatma Zahra (a.s) kuwa ni ukweli mkuuna ni dharura mno katika hekima ya Mwenyezi Mungu katika kuumba,nayo ni ambayo inafasiriwa na kipande cha tatu katika Hadithi Al–Qudsi:“Na lau kama sio Fatma basi nisingewaumba nyinyi.”

Hii ni pamoja na kuongezea kwamba Az-Zahra (a.s) alikuwa na jukumu lamsingi katika kuwafedhehesha wale waliotawala kwa jina la Uislamu, nakama sio msimamo wake imara basi waislamu wa kawaidawangechanganyikiwa… hivyo yeye alikuwa kati ya waliohifadhi dini yaMtume wa Mwenyezi Mungu punde tu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w).

18 Humru –Yaani Humraau: Hao ni walioingia katika Uislamu baada ya kutekwa,na katika kamusi imeandikwa: al-Mawaaliy na al-Humrau ni yeyote asiye kuwaMwarabu.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 16

Page 23: Fatima al-Zahra

17

Fatima al-Zahra

UTUKUFU WA ZAHRA (AS)

Fatmatuz-Zahraa (a.s) ana jukumu kubwa katika kujenga na kuipa nguvumisingi ya dini ya Kiislamu na kuimarisha nguzo zake, ambapo anasemaMwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi Al–Qudsi: “Na lau kama siFatma nisingewaumba nyinyi”, hivyo Fatma Zahra ni zawadi yaMwenyezi Mungu na tuzo la uchamungu kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w)19

na neema nyingi, naye ndio siri ya Uimamu na kitovu cha kuumbwaMaimamu maasum (a.s) ambapo yeye ndio ameupa uhai, nuru na amesi-mamisha dini ya haki kupitia kwa watoto wake na misimamo yake yakihistoria… hadi leo hii unaona Uislamu umehifadhika kwa fadhila zakupatikana kwake na kwa kuwepo Imam Al-Mahdi (a.s), yeye ni barakakatika baraka za Fatma (a.s).

Kuna Hadithi nyingi mutawatir zinazoelezea nafasi ya Zahra (a.s) na zime-pokewa na pande mbili katika vitabu vyao mbalimbali. Kama ambavyokutukuza cheo chake Zahra (a.s) ni kutukuza hadhi ya unabii na diniambayo ameiteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

ZAHRA (A.S) NI NURU YAMWENYEZI MUNGU

Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Mwenyezi Mungu ali-umba nuru ya Fatma (a.s) kabla ya kuumba mbingu na ardhi” (Maelezoyake yameshepita hapo juu).

Baadhi ya watu wakasema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, je yeye si

19 Hii nikuashiria kauli yake (s.w.t): “Hakika sisi tumekupa kheri nyingi”Suratul Kauthar:1.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:27 PM Page 17

Page 24: Fatima al-Zahra

18

Fatima al-Zahra

mwanadamu?” Akasema: “Fatma ni Hurul’aini wa kibinadamu.”Wakasema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, vipi yeye ni Hurul’aini wakibinadamu?” Akasema: “Mwenyezi Mungu amemuumba kutokana nanuru yake kabla ya kumuumba Adam ambapo alikuwa ni roho, MwenyeziMungu alipomuumba Adam akamuonyesha kwake.” Wakasema: “EweNabii wa Mwenyezi Mungu Fatima alikuwa wapi?” Akasema: “Alikuwachini ya Arshi.”

Wakasema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, chakula chake kilikuwanini?” Akasema: “Tasibihi, tahalili na tahamid, Mwenyezi Mungu alipo-muumba Adam na akanitoa katika mgongo wake Mwenyezi Munguakapendelea kumtoa yeye katika mgongo wangu, akamjaalia kuwa tufahakatika pepo, na Jibrilu (a.s) aliniletea akaniambia: ‘As-salam alaika warah-matullahi wabarakatuhu ewe Muhammad.’ Nikasema, waalaika salamuwarahmatullahi wabarakatuhu ewe kipenzi changu Jibril. Akasema: ‘EweMuhammad hakika Mola wako anakusalimia.’ Nikasema: Amani inatokakwake na kwake inarejea. Akasema: ‘Mwenyezi Mungu amekupa zawadiya tunda hili kutoka peponi.’ Nikalichukua na nikalikumbatia kifuanimwangu. Akasema: ‘Ewe Muhammad, Mwenyezi Mungu anasema ulile.

Basi nikalipasua nikaona nuru angavu nikaogopa kwayo. Akasema: ‘EweMuhammad una nini mbona huli? Lile na wala usiogope kwani hiyo ninuru ya Mansurah mbinguni, na katika ardhi ni Fatmah.’ Nikasema kipen-zi changu Jibril kwa nini ameitwa Mansurah mbinguni na ardhini akaitwaFatma? Akasema: ‘Ameitwa Fatma ardhini kwa sababu wafuasi wakewataepushwa na moto, na maadui zake wamenyimwa mapenzi yake. Nakatika mbingu ni Mansurah nayo ni kauli yake (s.w.t):

“Katika miaka michache. Amri ya Mwenyezi Mungu kabla yake na

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 18

Page 25: Fatima al-Zahra

19

Fatima al-Zahra

baada yake. Na siku hiyo watafurahi waumini kwa nusura yaMwenyezi Mungu, anamnusuru amtakaye naye ni mwenye nguvu,mwingi wa rehema” (Sura Rum: 4 -5)

Yaani nusura ya Fatma kwa wanaompenda.’”20

Na marehemu baba yangu21 alitunga kaswida nzuri na ndefu katika uzaowake mtukufu na hizi ni baadhi ya beti zake: Johari imechomoza kwa uzuri wa nuru yake,Dunia ikaangaza kwa nuru yake,Ulimwengu umeangaza kwa nuru ya miali yake,Kwa nuru ya miali yake imeangaza sehemu zake,Mwanga mzuri ulioje, ukatoa nuru na nuru yake,Imeongoa wanadamu kwa uongofu wake.

BIBI MBORA WA WANAWAKE WAULIMWENGUNI

Zahra (a.s) katika mwanzo wa kujenga jamii ya Kislamu Madina alikuwani mdogo kwa umri, bado hajafikia miaka minane ila alikuwa na fahamuna utambuzi wa elimu ya kiuchamungu, ya kidini na umaasumu kamili,kiasi kwamba alitekeleza jukumu muhimu katika ukuaji wa jamii mpya yaKiislamu, alisifika kwa ikhilasi yake, kufuatilia kwake matukio na uelewawake wa ujumbe wa mbinguni, pamoja na kuwepo wanawake wenginekatika nyumba ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w), lakini yeye alipata cheo chajuu kitukufu kwa Mwenyezi Mungu na katika jamii ya Kiislamu. Hiyo nikutokana na kuteuliwa kwake na Mwenyezi Mungu, ikhilasi yake, ibadayake, ukarimu wake, jihadi yake, zuhudi yake, subira yake na uvumilivuwake katika njia ya Mwenyezi Mungu.

20 Ma’anil –Akhibar uk. 396 na 397.21 Ni Ayatullahi Al-Udhnaa Mirzaa Mahdi As-Shirazi.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 19

Page 26: Fatima al-Zahra

20

Fatima al-Zahra

Alitekeleza majukumu aliyokuwa nayo kwa njia nzuri mno, hivyo akas-tahiki kuwa ni Bibi mbora wa wanawake wa ulimwengu kwa wa mwanzona wa mwisho. Katika Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Fadhili alisema:Nilimwambia Abu Abdillahi (a.s) nieleze juu ya kauli ya Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuwa yeye ni Bibi mbora wa wanawake, je niwa ulimwengu wake tu? Akasema: “Huyo ni Mariam, yeye alikuwa ni Bibimbora wa wanawake wa ulimwengu wake tu. Lakini Fatma ni bibi mborawa wanawake wa ulimwengu kwa waliotangulia na wajao.”.22

Hivyo Fatma Zahra (a.s) amestahiki kuwa kuwepo kwake ni sharti lakupatikana Mtume (s.a.w.w) na Amirul-Muuminina Ali (a.s) kamailivyokuja katika Hadithi Al–Qudsi, ambapo yeye alikuwa na jukumu lakukamilisha na kutimiza katika kujenga jamii ya Kiislamu, na kutimizalengo la kuumbwa wanadamu na Mtume Mtukufu, ambapo lau si FatmaMaimamu wasingeumbwa kutoka katika kizazi cha Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w) katika ulimwengu huu. Na kukosekana Maimamu inamaana ya kubatilika kuwepo kwa Nabii, na kubatilika kuwepo kwaUislamu kwa pamoja, na haya mawili kwa umuhimu wake yanasababishakubatilika kuwepo wanadamu vile vile… hivyo basi kama sio Fatma (a.s)kusingepatikana mwendelezo wa (kazi) ya Nabii na kuifanya idumu, hivyoyeye (a.s) ndio siri ya Uimamu tukiongezea yaliyotangulia katika kusima-ma kwake dhidi ya njama ambazo zilitokea baada ya Nabii (s.a.w.w).

KIGEZO NA MFANO MWEMA

Hakika anayefuatilia maisha ya Bibi Fatma Zahra (a.s) anakuta kuwa yeyeni chuo kamili katika nyanja mbalimbali za maisha… hivyo anapasa kuwani kigezo chema kwa wanawake wote, bali hata kwa wanaume pia. Yeyendiye aliyesimama pamoja na baba yake katika kutangaza Uislamu, ame-vumilia adha za washirikina wa kikuraishi pamoja na kundi dogo la wau-

22 Ma’anil- Akhibar uk. 107.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 20

Page 27: Fatima al-Zahra

21

Fatima al-Zahra

mini katika shi’ab (bonde) la Abu–Talib, amevumilia mateso ya kuhamatoka Makka kwenda Madina… pia amesimama kidete pamoja na Amirul–Muuminina (a.s) ambaye aliimarisha misingi ya Uislamu… hivyo alikuwani kati ya waliohama na kupigana jihadi.

Vilevile amevumilia uchungu na ugumu wa nyakati ngumu kwa kuipakwake kisogo dunia na kuchagua akhera, kama ambavyo aliolewa naAmirul–Muuminina ili kushirikiana naye katika kuimarisha ujumbe pamo-ja na Uimamu, kuimarisha nguzo za jamii ya Kiislamu na kutangazaujumbe wa Mwenyezi Mungu sambamba na baba yake na mume wakeambaye alitoa nafsi yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu… na huu ni mfanomwema watakaouiga wanawake wa ulimwenguni.

MAISHA YA NDOA

Yeye pia aligawana majukumu ya maisha ya ndoa na Imam Ali (a.s),majukumu ya ndani ya nyumba yalikuwa ni juu yake na ya nje yalikuwajuu ya mume wake. Kutoka kwa Abu Jaafar (a.s) amesema: “Hakika Fatmaalichukua dhamana kwa Ali ya kazi za nyumbani, kukanda unga, kuokamikate na kusafisha nyumba, na Ali akachukua dhamana kwake kwayaliyo nje ya nyumba kuleta kuni na chakula.

Siku moja Ali alimwambia: “Ewe Fatma je, unachochote?” Akasema: “Hapana… naapa kwa aliye tukuza haki yako hatukuwa na cho-chote tangu siku tatu tunachoweza kukukirimu kwacho.”

Akasema: “Kwa nini hukuniambia?” Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alinikataza kukuomba chochote.Aliniambia usimuulize mtoto wa ami yangu chochote, akikuletea chochotepokea vinginevyo usimuulize.”’

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 21

Page 28: Fatima al-Zahra

22

Fatima al-Zahra

Abu Jaafar (a.s) akasema: Imam Alitoka akakutana na mtu akamkopadinari kisha akarejea nayo na wakati wa jioni umeshaingia, akakutana naMiqdad bin al-Aswad akamwambia Miqidad: “Nini kimekutoa katikawakati huu? Akasema: “Njaa, naapa kwa aliye tukuza haki yako eweAmirul-muuminina.” Mpokezi amesema: “Nilimuuliza Abu Jaafar Mtumewa Mwenyezi Mungu alikuwa hai?” Akasema: “Mtume wa MwenyeziMungu alikuwa hai. Imam Ali akamwambia Miqdad: “Mimi pia njaaimenitoa nimekopa dinari na nitakupa, akampa akarejea akamkuta Mtumewa Mwenyezi Mungu amekaa na Fatma (a.s) anaswali na baina yao kunakitu kimefunikwa, alipomaliza akaleta kile kitu wakakuta vipande vyamikate na nyama. Akasema: “Ewe Fatma hivi umevitoa wapi?” Akasema:“Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anamruzukuamtakaye bila ya hisabu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambianikueleze aliye mfano wako na aliye mfano wake?” Akasema: Nieleze.Akasema: Mfano wako ni mfano wa Zakaria alipoingia kwa Mariam kati-ka mihrabu akamkuta ana chakula, akasema: “Ewe Mariam umekitoawapi? Akasema: ‘Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu hakika MwenyeziMungu anamruzuku amtakaye bila ya hisabu. 23 Wakala (chakula hicho)kwa muda wa mwezi mmoja, nacho ni chakula anachokula Al-Mahdi (a.s)nacho kipo kwetu.24

UKARIMU WAKE

Kati ya sifa zingine alizokuwanazo Fatma Zahra (a.s) na ambazo zinapasaziwe ni funzo katika jamii na umma wowote unaotaka kuendelea ni zuhu-di, ukarimu, kutoa kwa wingi, subira na tabia nzuri iliyotukuka. Kisa chakulisha chakula ambacho kimepokewa katika Qur’ani tukufu katikaSuratud-Dahri ni ushahidi mzuri juu ya hilo ambapo walitoa chakula chaopekee na ambacho ni vipande vya mikate tu kwa watu watatu, kwa muda

23 Hii ni ishara ya kauli yake (s.w.t) katika Suratul Al-Imran: 37.24 Tafsirul Ayashi Juz. 171 na 172.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 22

Page 29: Fatima al-Zahra

wa siku tatu mfululizo wakabaki na njaa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nahiyo ni baada ya kuweka nadhiri ya kufunga kwa ajili ya Mwenyezi Munguwakipona Hasan na Husein (a.s) kutokana na maradhi waliyougua,walipokaa tayari kwa kufuturu mlango uligongwa na maskini, wakatoavipande vya mikate yao kwa maskini na wakalala njaa, vivyo hivyo wali-fanya siku ya pili kumfanyia yatima na katika siku ya tatu mambo yali-jirudia kwa mateka. Hivyo Mwenyezi Mungu aliteremsha sura kamili kwaajili yao nayo ni Suratud–Dahri, na miongoni mwayo ni Aya hizi:

“Na wanawalisha chakula maskini, yatima na mateka hali ya kuwawao wanakihitaji.” (Surat Insaan: 8.)

Na kisa hiki kimepokelewa pia na Masuni.25

MIONGONI MWA IBADA ZAKE

Vilevile Fatma Zahra alikuwa anamcha Mwenyezi Mungu kwa ikhilasi naimani ya juu ambapo moyo wake ulikuwa ni chemchemu yenye kububuji-ka kwa kumjua Mwenyezi Mungu na kufungamana Naye. Amesema ImamHasan (a.s): “Nilimuona mama yangu hali akiwa amesimama kwenyemswala wake usiku wa Ijumaa basi aliendelea kurukuu na kusujudu hadiyakakaribia mapambazuko ya asubuhi, na nilimsikia anawaombea waumi-ni kwa kuwataja majina yao na kuwaombea dua kwa wingi na walahaiombei nafsi yake chochote…Nikamwambia: “Ewe mama yangu kwanini huiombei nafsi yako kama unavyowaombea wengine?” Akasema:“Ewe mwanangu jirani kwanza kisha nyumbani.” 26

23

Fatima al-Zahra

25 Rejea Fatumatuz-Zahraa (a.s) fiyl Qur’an uk. 313 kwa kunukuliwa kutokakatika tafsirur Ruhulmaan Juz. 92 na uk. 157.26 I’lalus-Sharau uk, 181.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 23

Page 30: Fatima al-Zahra

24

Fatima al-Zahra

KATIKA ELIMU YA ZAHRA (AS)

Na kati ya sifa zingine alizojipamba nazo Bibi wa wanawake wa ulimwen-guni (a.s) ambazo ni wajibu kwa waislamu waume kwa wake wachukuekigezo kwake, nayo ni elimu… Ambapo alikuwa ni mjuzi, kwani alikuwaanapata elimu kutoka katika mji wa elimu naye ni Mtume (s.a.w.w) nakutoka katika mlango wa mji wa elimu naye ni Ali (a.s).27 Hivyo yeyeanamjua Mwenyezi Mungu na anajua uhakika wa ulimwengu na falsafa yamaisha kama ambavyo kuwa kwake karibu na msikiti wa Nabii kulimpafursa ya kufuatilia sheria za Mwenyezi Mungu na kusoma Aya zakeTukufu, hii ni pamoja na kwamba yeye alikuwa na elimu ya tabia njema.

Nafasi yake tukufu na elimu yake nyingi imemuwezesha kulea, kufundishana kuelekeza wanawake wa ulimwengu katika kila mji na kila zama, husu-san wanawake wa ulimwengu wake ambao walikuwa wakikusanyikakwake na kuchukua elimu ya Kiislamu na walikuwa wanamuuliza kilakitu. Zahra alikuwa mwalimu na mlezi hata kwa wanaume kwa kupitiakwa wanawake.

Kutoka kwa Imamu Hasan Al-Askari (a.s) amesema: “Mwanaumealimwambia mke wake: “Nenda kwa Fatma Binti Rasulillah muulize juuyangu, kuwa mimi ni katika wafuasi wao au sio katika wafuasi wao?”Akamuuliza. Akasema (a.s): “Mwambie kama anafanya tuliyomwamuruna anaacha tuliyomkataza basi yeye ni katika wafuasi wetu vinginevyohapana.” Akarejea na akampa habari. Akasema: “Ole wangu nani atan-iokoa kutokana na dhambi na makosa? Hivyo mimi nitakaa motoni milele,kwani asiyekuwa katika wafuasi wao atakaa motoni milele.” Mke wakeakarejea na akamwambia aliyoyasema mume wake. Fatma (a.s) akasema:

27 Ni kuashiria Hadith isemayo “Mimi ni mji wa elimu na Ali ni mlango wakeanayetaka elimu basi aeindee kupitia katika mlango wake.” Uyunul-Akhbar uk:233.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 24

Page 31: Fatima al-Zahra

“Mwambie sivyo, wafuasi wetu ni kati ya watu bora mno peponi na kilaanayetupenda na mwenye kuwapenda wanaotupenda na mwenyekuwachukia maadui zetu na mwenye kujisalimisha kwa moyo wake naulimi wake kwetu sio katika wafuasi wetu kama watakhalifu maamrishoyetu na makatazo yetu katika madhambi mengine, wao pamoja na hayolakini wataingia peponi, lakini ni baada ya kutakaswa kutokana na mad-hambi yao kwa balaa na misiba au kwa adhabu ya Kiyama kwa aina zamateso yake, au katika tabaka la juu la moto wa Jahannam na adhabu zake,hadi tutakapowaokoa kwa mapenzi yetu kutoka kwayo na kuwaletakwetu.”

HOTUBA YAKE MSIKITINI

Kati ya mambo muhimu yaliyobakia kwetu kutoka kwa Bibi Fatma Zahra(a.s) ni hotuba yake aliyoitoa msikitini ambayo ni mchanganyiko wa elimumbalimbali na maarifa mengi, na hotuba hiyo inahitaji mijaladi mingi ilikuielezea. Kama ambavyo kupitia hotuba yake na misimamo yake alitoamwongozo sahihi kwa vizazi vijavyo hadi Siku ya Kiyama.

SHAHADA NA UCHUNGU

Baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) Fatma alikuwaanaishi pamoja na mume wake Imam Amirul -Muuminina Ali (a.s) katikadaraja la juu kabisa la jihadi kwa ajili ya kuhifadhi dini ya Kiislamu naujumbe wa Mwenyezi Mungu, ambao Mtume wa mwisho na Mbora waviumbe, ameutangaza na kuimarisha misingi yake, hivyo majukumu yao nimakubwa zaidi na muhimu baada ya kuondoka Mtume wa MwenyeziMungu (s.a.w.w). Fatma hakutazama matukio kama ni kitu cha kupita tu,bali alikuwa anasimama dhidi ya udikteta na ukandamizaji, na alikuwaanazingatia msimamo wa watu kuwa ni hatua au mwanzo wa kurudinyuma na kuuhesabu kuwa ni kuzima maendeleo ya Kiislamu yenye

25

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 25

Page 32: Fatima al-Zahra

kukua, msimamo wake huu ulikuwa ndio mwanzo wa jihadi na kufa shahi-di ambao uliendelea hadi kwa watoto wake na kizazi chake, jihadi ya ImamHusein Bwana wa Mashahidi (a.s) kule Karbala na kufa kwake shahidi nimlolongo wa msimamo wa Fatma wenye kuendelea dhidi ya kupotoshaUislamu.

Misimamo hii ya kishujaa iliathiri sana afya yake hadi alipata majerahamengi baada ya maadui kuvamia nyumba yake na kilichofuatia baada yahapo ni kuvunjwa ubavu wake na kuharibika kwa mimba ya MuhsinShahidi. Hiyo ilikuwa ndio sababu ya kufa kwake shahidi naye akiwa naumri wa miaka kumi na nane.

Imekuja katika riwaya kuwa, Fatma–Zahraa aliugua sana kwa muda wasiku arobaini hadi alipofariki (a.s). Alipohisi dalili ya kufa kwake alimwi-ta Ummu Amina na Asma binti Umais na akamtuma kwa Ali na akamleta,akasema (a.s): “Ewe mtoto wa ami yangu, hakika mimi naona dalili zakuondoka na mimi sioni kwa niliyonayo isipokuwa ni mwenye kumfuatababa yangu baada ya punde kidogo, na mimi nakuusia mambo ambayoyapo katika moyo wangu…”28

Imam baada ya kusikiliza wosia wake na miongoni mwayo ni kumuoaUmaamah baada yake, na amtengenezee jeneza, na asishuhudie yeyotejeneza lake ambaye amemdhulumu na kupora haki yake, azikwe usiku nakwa siri… Naye akamwambia, kama ilivyo katika riwaya; “Ewe binti waMtume wa Mwenyezi Mungu, umeitoa wapi habari hii na wahyi ume-shakatika kwetu?” Akasema: “Ewe Abul-Hassan nilikuwa nimelilala, maranikamuona kipenzi changu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kati-ka kasri ya durr nyeupe, aliponiona akasema: “Njoo kwangu ewe bintiyangu kwani mimi ninahamu kukutana na wewe.” Nikasema: “Wallahimimi ninahamu ya kukutana na wewe zaidi kuliko wewe. “Akasema weweutakuwa kwangu usiku wa leo, naye ni mkweli kwa aliyoyaahidi na ni

26

Fatima al-Zahra

28 Tafsirul-Imam Hasan al-Askari (a.s) uk. 308.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 26

Page 33: Fatima al-Zahra

mwenye kutekeleza aliyoyaahidi.”29

Fatma Zahra alikufa shahidi usiku wa Jumapili hali akiwa kadhulumiwa,baada ya kupita siku tatu za Jamadil-Aakhar mwaka wa kumi na mojahijiria akiwa na umri wa miaka kumi na nane na miezi saba, yaani baadaya kufariki baba yake kwa miezi mitatu… hivi ndivyo ilivyokuja katikabaadhi ya riwaya… na katika riwaya zingine ni kwamba alifariki tarehe 13Jamadil-Awwal.

Pamoja na kwamba alifariki dunia katika umri mdogo lakini amebakia hadileo hii kuwa ni chuo kwa vizazi vijavyo na taa yenye nuru, anaangaza upo-tovu, udikteta na anang’oa madiketa dhalimu na anasimama dhidi ya kilaanayetaka kuzima mafunzo ya dini hii tukufu. Umma unapata somo namazingatio kutokana na misimamo yake na ushujaa wake kama ambavyounajifunza somo na mazingatio kutokana na misimamo ya watoto wakema’asum, kwa ushujaa wao na kubeba kwao majukumu ya Uislamuambapo wameutetea kwa upeo bora wa kuutetea.

Na wanadamu bado wangali wanangojea kudhihiri kwa Swahib Zaman Al-Imam Al-Mahdi (a.s) ili kuwaokoa kutoka katika makucha ya wakan-damizaji na madikteta, udhalimu na uadui ili aeneze uadilifu wa Kiislamupembe zote za ulimwengu na kukamilisha lengo ambalo kwa ajili yakeameumbwa Nabii (s.a.w.w), Amirul-Muumina (a.s) kwa kueneza uadilifu,amani na uongofu katika sehemu zote za ardhi. Na katika yaliyotanguliazinadhihiri baadhi ya dalili za kauli za Mwenyezi Mungu Mtukufu katikaHadithi Al–Qudsi: “Ewe Ahmad lau kama si wewe basi nisingeumbaulimwengu na lau kama si Ali basi nisingekuumba wewe na lau kama siFatma basi nisingewaumba nyinyi.”

Kama sio Fatma basi asingepatikana Al-Hujjah (Al-Imam Al-Mahdi) naMaimamu wengine (a.s)… na kama sio wao basi kusingekuwa na uadilifu,

27

Fatima al-Zahra

29 Rejea Min fiqihiz Zahraa Juz. 2 na Juz. 3 na Juz. 4, katika hotuba ya Zahraa(a.s).

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 27

Page 34: Fatima al-Zahra

amani wala dini.

Rehema na amani ziwe juu yako ewe Fatma; na ziwe juu ya baba yako, mume wako na watoto wako wema.

Amani iwe juu yako ewe Bibi wa wanawake wa ulimwenguni.Amani iwe juu yako ewe mama wa Maimam wa watu wote.Amani iwe juu yako ewe uliyedhulumiwa haki yako.

Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu mja wako binti wa Nabii wako. Mke wa wasii wa Nabii wako, amani itakayomnyanyua daraja, Daraja juu ya daraja ya waja wako wema, Miongoni mwa watu wa duniani na mbinguni.”30

Huu ndio mwisho wa tuliyokusudia kuyabainisha katika kitabu hiki, tuna-muomba Mwenyezi Mungu ayakubali kwani yeye ni mwenye kusikiamaombi. Ametakasika Mola wako, Mola Mwenye enzi na yale wanay-omsifu, rehema na amani iwashukie Mitume, na kila sifa njema ni yaMwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, na rehema na amani zimshukieMuhammad na aali zake wema.31

Qum tukufuMuhammad As- Shirazi.

28

Fatima al-Zahra

30 Biharul Anwar Juz. 43, Uk. 191 hadith ya 20 chapa ya Beiruti.31 Biharul Anwar Juz. 43, Uk. 179 hadith ya 15, chapa ya Beiruti.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 28

Page 35: Fatima al-Zahra

FATWA KUHUSU FATMA ZAHRA (AS)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

Kwa Ayatullahi Al-Udhuma As-Sayid Muhammad Al–Husein As-Shirazi

Assalam alaikum.Tafadhali tunaomba utupe fatwa ya mas’ala yafuatayo ambayo huwayanaulizwa sana siku hizi katika baadhi ya jamii na Mwenyezi Munguawape malipo mema.

Swali la 1: Je Nabii (s.a.w.w), binti yake Fatma Zahra (as ) na Maimamukumi na wawili (a.s) ni ma’asum? Je, uma’asumu wao niupi? Ni kwa maasi tu, au hata katika kukosea na kusahau, auni kwa hayo pamoja na kulala usingizi mzito unaoshindausikivu hadi kupitwa na Swala?

Jawabu: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenyekurehemu.

Assalamu alaikum warahamatullah wabarakatuhNabii Mtukufu, binti yake Fatma Zahra, Amirul-Muumina na Maimamukumi na moja wanaotokana na kizazi chake wote ni ma’asum wamehifad-hiwa kutokana na maasi ya aina zote, kusahau na kutokana na usingiziunaoshinda usikivu hadi wakati wa Swala upite. 32 Bali wao ni ma’asumhata katika kuacha mambo ambayo sio wajibu lakini yana fadhila, natumezungumza katika dalili za kiakili na za kunukuu kuhusu uma’asumhuu katika sehemu mbalimbali za vitabu vyetu katika misingi ya akida nafiqih.

29

Fatima al-Zahra

32 Mafatihul jinaan na ziara ya Zahraa.

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 29

Page 36: Fatima al-Zahra

Swali la 2: Daraja ya uma’asum kwa ma’asumu kumi na nne ni sawa auinatofautiana?

Jawabu: Daraja ya uma’asumu wao ni moja na inalingana.

Swali la 3: Mmetaja katika kitabu chenu Min fiqihiz-Zahraa zaidi yamara moja kwamba Zahra ana daraja kubwa je, ni upi mpakawa daraja lake, je linapita daraja la Maimam wote au baadhiyao au ni Maimam wanaompita kwa daraja?

Jawabu: Ndio Fatma ana daraja la juu lakini liko chini ya daraja la babayake Mtume wa Mwenyezi Mungu na linalingana na daraja lamume wake Amirul-Muuminina Ali (a.s) na liko juu ya darajala watoto wake kumi na moja (a.s).

Swali la 4: Vile vile mmetaja katika kitabu chenu baadhi ya matukioambayo yalitokea baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w) je, niupi mtazamo wenu humo?

Jawabu: Qur’ani Tukufu imeeleza hayo ambapo imesema: “Je, akifaau akiuliwa mtarejea nyuma kwa visigino vyenu?” (SuratAali Imran: 144).

Swali la 5: Je, Fatma Zahraa (a.s) ni shahidi? Kwani mmetaja katikakitabu chenu kuwa alikufa shahidi.

Jawabu: Ndio yamepokewa hayo katika riwaya sahihi na pia imetajwakatika vitabu vya historia.

Swali la 6: Je, yeye alikuwa ni Swidiqah? Kama Qur’ani ilivyosema juuya Mariam binti Imran kwamba yeye alikuwa Swidiqah,

Jawabu: Ndio imepokewa katika athari zinazozingatiwa kwamba yeyealikuwa Swidiqah na ndio maana alioshwa na

30

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 30

Page 37: Fatima al-Zahra

Amirul–muuminina Ali ibn Abu Talib ambaye anafanana nayekatika daraja licha ya kuwepo mwanamke ambaye angewezakumuosha, kwani As-Swidiqah hawezi kuoshwa isipokuwa naAs –Swidiq, na yeye ni bora kuliko Mariam kama zilivyoelezawazi hayo riwayah ambazo ni mutawatiri.

Swali la 7: Nini maoni yenu katika historia zilizotaja kupigwa kwaFatma Zahraa, kuporwa Fadak yake, kubanwa kwake bainaya mlango na ukuta na kuharibiwa mimba ya Muhsin n.k ?

Jawabu: Hayo yote yamethibiti na ni sahihi.

Swali la 8: Nini mtazamo wenu juu ya uongozi wa kimaumbile na kish-eria wa ma’asum kumi na nne kwa ujumla, na hususan kwaFatma Zahra, na mmeshaeleza hayo katika kitabu chenu Minfiqihz- Zahraa (a.s) ?

Jawabu: Dalili nyingi zinazozingatiwa zimeunga mkono hayo kwam-ba Fatma Zahra na ma’asum wengine wote (a.s) wana uon-gozi wa kimaumbile na kisheria, na imekuja katika ziara yaImam Al-Husein (a.s) ambayo amesema kwayo Sheikh As-Suduq kwamba ni ziara sahihi zaidi katika mapokezi yafu-atayo: “Matakwa ya Mola katika makadirio ya mambo yakeyanateremka kwenu na yanatoka katika nyumba zenu na niyenye kutokana na yale yaliyohukumiwa kwa waja.”

Swali la 9: Nini mtazamo wenu kuhusu Raja’ah, asili yake, nasaba yakena ni kwa nani kati ya ma’asum?

Jawabu: Raja’ah imethibiti kwa dalili zinazozingatiwa na asili yake nikatika Qur’ani Tukufu na nasaba yake ni kwa Ma’asum wotekumi na nne (a.s), na itaanza baada ya kudhihiri Imam wakumi na mbili Al-Mahdi (a.s).

31

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 31

Page 38: Fatima al-Zahra

Swali la 10: Je, dalili juu ya Imam Mahdi inatofautiana na dalili yaMaimam wengine?

Jawabu: Hapana … haitofautiani, kuna dalili zinazofanana katikaUimam wa Maimam kumi na mbili (a.s), nazo ni makumi yaAya za Qur’ani ambazo zimefanyiwa taawili kulingana nariwaya mutawatir, dalili za kiakili kuhusu Maimam kumi nambili, na kuna dalili mahususi za kunukuu juu ya uimamuwa kila mmoja kati ya Maimam kumi na wawili (a.s), navilevile Imam Mahdi kwani zimepokewa riwaya maelfukatika mamia ya vitabu, zaidi ya hapo ni dalili za kiakili juuya uimam wake.

Swali la 11: Hadithi tukufu iliyopokewa kutoka kwa Mtume waMwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Maimam baada yangu nikumi na wawili” ni mutawatiri kwenu? Je, kuna shaka yey-ote juu ya kuzaliwa Imam wa kumi na mbili ambaye niImam Al–Mahdi (a.s)?

Jawabu: Hadith hii ni mutawatir na wala hakuna shaka katika kuzali-wa kwa Imam wa kumi na mbili, na dalili juu ya hilo ni nyin-gi kwani kama sio kuwepo kwa Al-Hujjah basi ardhiingeteketea pamoja na watu wake na kwamba kamakungekuwa na watu wawili wanaoishi ardhini basi mmojawao angekuwa ndio Al-Hujjah kulingana na ilivyopokewajuu ya hilo riwaya mbalimbali ambazo ni mutawatir.

Swali la 12: Mmetaja katika kitabu chenu Min fiqihz-Zahraa kuwaFatmatuz-Zahraa (a.s) alijali sana na kutetea uongozi wamume wake, Imam Amirul-Muuminina Ali (a.s) na watotowake kumi na mmoja, je ni upi mpaka wa hilo? Je, hayo niwajibu kwetu katika wakati huu?

Jawabu: Fatma Zahra (a.s) alikuwa mtetezi wa mwanzo baada ya

32

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 32

Page 39: Fatima al-Zahra

baba yake Nabii (s.a.w.w) wa Uimam wa Amirul-muumini-na Ali bin Abi Talib (a.s) na katika njia hii amejitolea yeyebinafsi pamoja na mwanae Muhsin na hakuacha fursa yeyoteambayo kwayo angeweza kunusuru uimamu wa Amirul-Muuminina na kuthibitisha haki yake isipokuwa aliitumia,na ni wajibu kwa waumini kuiga mfano kwake (a.s) na hiyoni kulingana na zama na sehemu na kulingana na mashartiyaliyotajwa katika vitabu vya fiqihi, kwani kila kitendo,kauli na ridhaa yake ni hoja ya kisheria.

Swali la 13: Mmetaja katika kitabu chenu kuwa ni Sunna kusimulia hotu-ba yake ya Fadak kutokana na kupokelewa kwake kwa wingikatika riwaya za Ma’asum (as ), je ni Sunna kutaja kila kina-chohusiana na Fatma Zahra (a.s) kati ya yaliyotokea juuyake baada ya baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w)?

Jawabu: Ndio yote hayo ni Sunna, na hayaepukani ima kuwa ni kauliyake au kitendo chake au ridhaa yake, na yote ni hoja kamatulivyotaja, na ambayo yako nje na hayo ambayo yanaambat-ana na fadhila zake na sifa zake (a.s), basi hakuna mushikelikatika Sunna kwa kuyataja, kuyanukuu na kuyaeneza baliinaweza kuwa ni wajibu kama yatakuwa yanahusiana nawajibu katika kuamrisha mema, kulingania kheri na kuenezadini tukufu.

Swali la 12: Mmetaja katika juzuu ya kwanza ya Min fiqihiz–Zahrakwamba yeye ni kati ya ambao Mwenyezi Mungu amefarad-hisha kutiiwa na viumbe wote, na mmetoa ushahidi wa baad-hi ya riwaya, je hizi riwaya kwa mtazamo wenu ni zenyekuzingatiwa? Kwa ihsani yenu tunaomba majibu na Allahswt. awalipe kila la kheri.

Jawabu: Ndio hakika hizi riwaya zinazingatiwa na tumetia mkazo kati-

33

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 33

Page 40: Fatima al-Zahra

ka kuzingatiwa kwake katika kitabu kilichotajwa, na vileviletumetaja dalili zingine kama ambavyo tumeeleza ufafanuzi wabaadhi ya yaliyotajwa katika kitabu chetu Fiqihul–Ba’iu) nakatika vitabu vyetu vingine vingi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie kuwa ni katika kundilinaloshikamana na Fatma Zahra, baba yake, mume wake na watoto wake(a.s), na tuwe kati ya waliojitenga na maadui zao, na atujaalie kuwa kati yawanaotaja fadhila zao, kueneza Sunna zao na kutangaza hazina ya elimuyao, na tuwe ni wenye kufaulu kwa kuwapenda wao duniani na akherahakika Mwenyezi Mungu yuko karibu na ni Mwenye kujibu maombi.

Wasalaam alaikum warahmatu-llahi wabarakatuh.

Muhammad As-Shirazi.

34

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 34

Page 41: Fatima al-Zahra

BIBLIOGRAFIAAl – Qur’ani.Nahjul-Balagha.Al-aamaal cha Sheikh As Suduq.Al-Ihtijaaj cha Twabarsi.Al-Jannatul asim cha Mir Jihaan.Al-Khisal cha Sheikh Suduq.Ad Duau wa Ziyaarah cha Imam As-Shirazi.Al–Ghaibah cha Sheikh Suduq.Al-Qaulu Sadid fiy sharh At Tajirid cha Imam As Shirazi.Al–Kaafi cha Sheikh Kulain.Al–Wasail ilaa Rasail cha Imam Shirazi.Biharul–Anwar cha Allammah Al – Majilsi.Baswairu Darajaat cha Safarul-Qummi.Tafsirul - Imam Al–Hasan Al -Askari.Tafsirul–Ayyashi cha Ayyashi.Risaalatut Tasamuh fiy Adilati s Sunan cha Imam As Shirazi.Ilalus Sharaiu cha Sheikh Suduq.Awalimul – Ulumi cha Bahran.Uyunul–Akhbar Ar–Ridhaa (as ) cha Sheikh As Suduq.Ghawali layali cha Ibn Jamhur Al–Ahsai.Fatmatuz-Zahraa (a.s) fiyl–Qur’ani cha Ayatullah Al-Udhmaa As SayyidAs-Swadiq As Shirazi.Kashful –Alii cha Al-Arandasi.Kalmatullah cha Ayatullah As Shahid As Sayid Hasan As Shirazi.Lisanul–Arab cha Ibn Mandhur.Majma’ul–Bayan cha Twabrsi. Majmau Nurain cha Sabzawari. Mustadrakus-Safinatul-Bihar cha Namaazi.Ma’anil – Akhbar cha Sheikh As Suduq.Mafatihul Jinan cha Al–Muhadith Al–QummiMultaqaal–Bahrain cha Al – MarandiMin fiqihiz–Zahra cha Imam As Shirazi

35

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 35

Page 42: Fatima al-Zahra

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NAAL - ITRAH FOUNDATION:

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na Moja

2. Uharamisho wa Riba3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili5. Hekaya za Bahlul6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)8. Hijab vazi Bora9. Ukweli wa Shia Ithnaashari10. Madhambi Makuu11. Mbingu imenikirimu12. Abdallah Ibn Saba13. Khadijatul Kubra14. Utumwa15. Umakini katika Swala16. Misingi ya Maarifa17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia18. Bilal wa Afrika19. Abudharr20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu21. Salman Farsi22. Ammar Yasir23. Qur'an na Hadithi24. Elimu ya Nafsi

36

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 36

Page 43: Fatima al-Zahra

25. Yajue Madhehebu ya Shia26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu27. Al-Wahda28. Ponyo kutoka katika Qur'an. 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii30. Mashukio ya Akhera31. Al Amali32. Dua Indal Ahlul Bayt33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.34. Haki za wanawake katika Uislamu35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake36. Amateka Na Aba'Khalifa37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)38. Adhana.39 Upendo katika Ukristo na Uislamu40. Nyuma yaho naje kuyoboka41. Amavu n’amavuko by’ubushiya42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya46. Kusujudu juu ya udongo47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)48. Tarawehe49. Malumbano baina ya Sunni na Shia50. Kupunguza Swala safarini51. Kufungua safarini52. Umaasumu wa Manabii53. Qur’an inatoa changamoto

37

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 37

Page 44: Fatima al-Zahra

54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm55. Uadilifu wa Masahaba 56. Dua e Kumayl57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s)61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili63. Kuzuru Makaburi64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu67. Tujifunze Misingi Ya Dini68. Sala ni Nguzo ya Dini69. Mikesha Ya Peshawar70. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu71. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy

onyooka72. Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje?73. Liqaa-u-llaah74. Muhammad (s) Mtume wa Allah75. Amani na Jihadi Katika Uislamu 76. Uislamu Ulienea Vipi?77. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) 78. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) 79. Nahjul Balagha Sehemu ya Kwanza80. Nahjul Balagha Sehemu ya Pili.81. Amali za Ramadhani

38

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 38

Page 45: Fatima al-Zahra

82. Mariam, Yesu na Ukristo kwa Mtazamo wa Kiislamu83. Ujumbe sehemu ya kwanza84. Ujumbe sehemu ya pili

39

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 39

Page 46: Fatima al-Zahra

BACK COVERKijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatima Zahra (a.s), bintiwa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kati ya mihadhara ya thamani ya mare-hemu Imam Muhammad al-Husaini al-Shirazi (Mwenyezi Mungu amrehe-mu).

Ni kitabu cha aina yake katika lugha ya Kiswahili kinachoelezea maisha yaBibi huyu mtukufu mwenye nuru.

Ni kitabu kizuri kilioje, na ni haja ilioje kwa wakati huu ambaomazungumzo yamekuwa ni mengi kuhusu Bibi wa wanawake waulimwenguni (a.s), mijadala na midahalo imezidi juu ya shakhsia yaketukufu na nafasi yake katika Umma.

Cha kuzingatia ni kwamba kumjua mtukufu huyu ambaye ni Bibi wawanawake wa ulimwenguni (a.s) ni wajibu kwa Waislamu wote, kwaniameshasema (a.s): “Jueni kwamba mimi ni Fatima al-Zahra.” Yaani kuni-jua mimi ni wajibu kwa kila muumini. Bibi Fatima (a.s.) ni maasumu wapekee katika jinsia yake, kumpenda kwake na kumtawalisha kwake nisawa na kumpenda na kumtawalisha Amirul Muuminina Ali (a.s) na wato-to wake walio maasumu (a.s).

Kimetolewa na kuchapishwa na:Alitrah FoundationS.L.P. – 19701,Daressalaam. TanzaniaSimu: +255 22 2110640Simu/Nukushi: +255 22 2127555Tovuti: www.alitrah.orgKatika mtandao: www.alitrah.info

40

Fatima al-Zahra

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd 7/1/2011 3:28 PM Page 40