DPC KANISA LETU KARIBU Dar es Salaam Pentecostal Church Kinondoni Rd (Mkabala na TX Market) SLP 7931, Dar es Salaam Email yetu: [email protected] www.dpctz.org Dar es Salaam Pentecostal Church Ibada ya Kiingereza - Jumapili Saa 2.00 Asubuhi Ibada ya Kiswahili - Jumapili Saa 4.30 Asubuhi DPC 1. Mungu anakupenda na alikuumba ili umjue yeye Upendo wa Mungu “ Kwa Maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee, ili kila amwaminie asipotee bali awe na Uzima wa milele ” Yohana 3:16 . Mpango wa Mungu "Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfah amu Yesu Kristo ambaye umemtuma." (Yohana 17:3 ). Je ni kitu gani kinazuia sisi tusimjue Mungu? 2. Mwanadamu ni Mwenye dhambi na amejitenga na Mungu, Hivyo hawezi kumjua Mungu au kuujua upendo wa Mungu. Mwanadamu ni Mwenye dhambi "kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Mwanadamu aliumbwa ili awe na mahusiano na Mungu, ila kutokana na usumbufu wake akaamua kwenda njia yake na uhusiano na Mungu ukavunjika. Uwezo wa kuamua wa mwanadamu ukaleta tabia ya uasi au kutofautiana na Mungu na hichi ndicho Biblia inasema kuwa ni dhambi. Mwanadamu Ajitenga "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu (Warumi 6:23). "... (Wale ambao hawamjui) Atawahukumu wale wasiomjua Mungu, wasioitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. 9 Wataadhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake." (2 wathesalonike 1:8,9) K aribu 3.Yesu Kristo ni Msaada wa Mungu kwa Wanadamu wenye dhambi. Kupitia yeye, tunaweza kumjua Mungu binafsi na kujua upendo wake. Alikufa kwa ajili yetu "Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu." (Warumi 5:8). Alifufuka kutoka katika wafu "Kwa maana niliyopokea ndio niliyowapa ninyi, nayo ni muhimu sana: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama ilivy oandikwa katika Maandiko. 4 Na kwamba alizikwa na kufufuka siku ya tatu, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. 5 Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili. 6 Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja, na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa." (1 Wakorinth 15:3-6). Ni njia pekee ya Kumfikia Mungu "Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.'" (Yohana 14:6). 4.Tunatakiwa kumpokea Yesu awe Bwana Na Mwokozi wa Maisha Yetu,Ndipo tuweze kumjua Mungu na Kuujua Upendo wake. "Bali wote waliompokea na kumwamini aliwapa haki ya kufanywa watoto wa Mungu" (John 1:12) Tunampokea Yesu kwa Imani "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. 9 Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote asije akajisifu juu ya wokovu wake.t" (Waefeso 2:8,9). Tunapompokea Yesu Kristo, Tunazaliwa Upya (Yohana 3:1-8.) Tunampokea Yesu Kristo kwa Mwaliko wa Mtu Binafsi [Yesu anasema] "Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami." (Ufunuo 3:20). Kumpokea Yesu kunahusisha kumwangalia Mungu kwa toba na Kumwamini Kristo kuja kwenye maisha yako na kusemehe dhambi na kukufanya uwe vile anataka. Inakupsa ukubali kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu na kwamba alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Tunampokea kwa imani na kwa tendo la hiari.