Top Banner
1 1 COVER PAGE
12

COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

Mar 10, 2021

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

11

COVER PAGE

Page 2: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

22

Mwanzoni kwa mwezi October mwaka 2019 uongozi wa Jatu ulianza utafiti wa kili-mo cha matunda kama sehemu muhimu ya maandalizi ya kuanza kuzalisha bidhaa zitokanazo na matunda. Uongozi unapendekeza ifikapo mwaka 2024 kampuni iwe na uwezo mkubwa wa kuzalisha matunda pamoja na vinywaji vya aina mbali mbali vitokanavyo na matunda.

Katika kufikia dhana hii ilipendekezwa kwa kuanza tuanzie mkoa wa Tanga ambako matunda huzalishwa kwa wingi zaidi, hata hivyo tunapendekeza kuanza na matunda ya Aina nne kama ifuatavyo;

Utafiti wetu ulilenga kujua yafuatayo;

1. Aina za matunda yanayolimwa eneo la Muheza2. Teknolojia wanayotumia3. Mbegu zinazotumika 4. Masoko wanayouza mazao5. Upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo cha matunda

Mkoa wa Tanga ni mkoa wenye rotuba nzuri na hali ya hewa inayoruhusu Aina mbali mbali za mazao. Machungwa ikiwa zao kuu la biashara katika mkoa huu. Tulichagua kuanza utafiti wetu katika wilaya ya Muheza ambapo tuliweza kukutana na uongozi wa wilaya na wakatupa ushirikiano mzuri katika kufanya utafiti wetu ambao ulifanyika takribani kata 11 zenye wakulima wa matunda zaidi ya 10,000 kwa muda wiki mbili.

UTANGULIZI

MACHUNGWA MAEMBE PARACHICHI NANASI

Page 3: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

33

6. Kiwango cha uzalishaji wa matunda kwa sasa7. Changamoto za kilimo cha matunda kwa ujumla8. Fursa ambazo Jatu inaweza kuzitumia kwa faida ya wanachama wake.

Utafiti wetu uliongozwa na mkuu wa idara ya Utafiti ya jatu plc Ndugu paul Kapalata Msabila, ambaye aliambatana na wataalamu wa wataalamu wa udongo na mimea, uchumi, maji na Umwagiliaji.

Pia timu ya Utafiti ilipata ushirikiano kutoka halmashauri ya Muheza ambapo iliunga-na na Afisa kilimo wilaya Ndugu, Hoyange Mbwambo pamoja na maafisa kilimo wa kata zote tulizotembelea. Pia tulipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wakulima na wafanyabiashara wa matunda katika wilaya ya Muheza.

Njia zilizotumika kufanya utafiti:

Njia kuu tulizotumia ni kama vile;1. Kuona kwa macho (observation)2. Kujaza Dodoso 3. Mahojiano na mijadala baina ya wadau.4. kusoma nyaraka na report mbali mbali

TIMU YA WATAFITI

Page 4: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

44

MATOKEO YA UTAFITI

1. Aina za Matunda.Katika mkoa wa Tanga mazao Aina mbali mbali yanakubali ikiwa ni pamoja na ma-hindi, muhogo, viungo na katani. Hata hivyo kwa upande wa matunda, matunda Aina ya Nanasi, Nazi, Fenesi na machungwa ndo yaliyozoeleka Zaidi. Ili kujiridhisha, timu yetu ya watalaamu ilichukua udongo kwa ajili ya kwenda kupima ili kujua kama Aina nyingine za matunda zinaweza kukubali kama vile parachichi na maembe. Bado tunaendelea na vipimo, tukikamilisha tutawapa majibu. Hata hivyo zao la mchungwa lilithibitishwa kama zao linalo kubali sana ukanda wa Tanga kwa wilaya ya handeni, korogwe na muheza.

2. Aina za Mbegu zinazotumikaTuligundua kwamba wakazi wa Tanga kwa sehemu kubwa wanatumia mbegu za kienyeji katika zao la machungwa. Wengi wanalima chungwa Aina ya Valencia na msasa.

Page 5: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

55

3. Teknolojia WanayotumiaTuligundua kwamba teknolojia inayotumika katika kilimo hichi cha matunda ni dhaifu na iliyopitwa na wakati, watu wanalima kwa mazoea sana. Ni zao ambalo wengi waki-panda wanasahau kama wamewekeza na hivyo huduma za shamba ni hafifu, mkuli-ma husubiri tu msimu ufike avune na kuuza matunda wakati hajahudumia kitaalamu shamba lake. Hali hii inasababisha mazao yasiyo na ubora.

4. MasokoMasoko yanayotumika katika zao la machungwa ni masoko ya kienyeji kupitia kwa walanguzi Yaani madalali. Hakuna kiwanda hata kimoja katika wilaya ya Muheza am-bako tulifanya utafiti, ukizingatia kwamba ndo wilaya inayozalisha matunda kwa wingi katika mkoa wa Tanga. Kwa sasa bei ya chungwa moja inakadiriwa kua kati ya shs. 40-100, hii inategemea na aina ya mbegu na wingi wa mavuno pamoja na upatikanaji wa soko.

Ardhi hii kupatikana inategemea na ukubwa unaohitajika, kwa mfano; shamba kubwa kuanzia ekari 500 unaweza kupata pori, lakini ukitaka shamba ambalo lipo tayari si rahisi kupata zaidi ya ekari 50 kwa pamoja kutoka kwa wananchi, labda kama serikali itakuwa nalo.

5. Upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kulima machungwa.Katika wilaya ya Muheza unaweza kupata shamba la machungwa kwa njia kuu 3;

1. Unaweza kununua shamba ambalo tayari linamatunda, yaani limeshapandwa na kuhudumiwa michungwa ambapo kwa ekari moja wanauzwa kati ya tshs. Milion 15-75 (inategemea na sehemu au ukubwa wa mimea Lakini pia Aina ya mbegu na ubora wa shamba)

2. Shamba ambalo Bado halijapandwa mazao Yaani lililo wazi lakini safi kwa ajili ya kupanda, ni kati ya shiling laki 7 hadi milion moja na nusu (1,500,000/-)

3. Shamba pori, yaani shamba ambalo halijasaifishwa kabisa, ambapo ukihitaji kuliti-mia lazima uanze kukata miti, kung’oa visiki na kusafisha. Hili unaweza kulipata kuan-zia tshs. 200,000 -500,000/-.

Page 6: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

66

6. Kiwango cha Uzalishaji wa Machungwa kwa sasa.Ni zaidi ya wakulima 10,000 wanalima Hekta 8400 za machungwa katika wilaya ya Muheza, uzalishaji sio mzuri sana na machungwa mengi hayana kiwango cha kushin-dana katika soko la dunia, Kwani yanalimwa kienyeji na huduma sio nzuri. Hata hivyo kwa ajili ya kulisha kiwanda cha kati kampuni itahitajika kuanza kilimo cha matunda ili kuboresha ubora wa matunda Lakini pia kuongeza tija katika uzalishaji.

8. Fursa ambazo jatu inaweza kuzitumia.Jatu kama kampuni inayolenga kuunganisha wakulima maeneo mbalimbali Tanzania inaweza kutumia fursa hii kufanya yafuatayo;

a. Kuanzisha mashamba ya kisasa ya kilimo cha machungwa b. Kuanzisha soko la kudumu la machungwa c. Kuanzisha kiwanda maalumu ya kusindika machungwa na kutengeneza juice pamoja na kuuza machungwa ghafi kwa ajili ya kula binadamu.d. Kiwanda cha mazao yatokanayo na machungwa kinaweza kuongeza bei na thamani ya zao la chungwa kwa mkulima na hivyo kusaidia katika kujenga afya na kutokomeza umaskini kuanzia kwa mkulima hadi mlaji.

7. Changamoto za Kilimo cha Matunda.Changamoto kubwa katika zao hili ni; Magonjwa, mbegu hafifu, soko na technoloJia.

Page 7: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

77

Kwa shamba ambalo tayari ni safi; na kwamba mkulima atahitaji kulinunua kutoka kwa bei ya sasa, mchanganuo ni kama ifuatavyo;

Gharama hizi kwa mwaka wa pili zitajumuisha palizi, dawa na kuhudumia kama ilivyo ainishwa hapo juu.

9. MCHANGANUO WA GHARAMA ZA AWALI ZA KULIMA CHUNGWA.

HATUA ZA KILIMO MSIMU 1 GHARAMA

SHAMBA

KULIMA EKARI 1

KUPANDA MACHUNGWA

KUHUDUMIA MCHE 1

DAWA

JUMLA KUU

MSIMU WA PILI JUMLA KUU

1,000,000/-

500,000/-

500,000/-

600,000/-

200,000/-

500,000/-

3,400,000/-

1,300,000/-

60,000/-

40,000/-

Kununa Shamba

Kulima na kuandaa shamba kwa ajili ya kupanda

Kuchimba mashimo na kuweka mbolea ya samadi: 5,000/- kila shi-mo ambapo kwa ekari moja ni sawa na mashimo 100.

Kupiga halo au kuchabanga ili kulainisha udongo

Kuandaa, kuhudumia na kupanda miche hadi kuota, 5,000/- kila mche kwa ekari moja sawa na miche 100

Kuhudumia mche mmoja kwa mwe-zi 500 ( kwa mwaka mzima ni sawa na 500 x 100 x12 (kupiga dawa, kupogolea na kufanya uangalizi wa jumla)

Palizi kwa mwaka inatakiwa anga-lau palizi 4 na palizi moja ni tshs. 50,000/- (50,000 x 4)

Kununua dawa kwa mwaka.(Makadi-rio)

Page 8: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

88

Kwa mwaka wa tatu ambao tunategemea kuanza kuvuna msimu wa kwanza gharama zifuatazo zitaongezeka;

HATUA ZA KILIMO MSIMU 3 GHARAMA

KUHUDUMIA MCHE 1

DAWA

KUVUNA

USAFIRI NA KODI

JUMLA KUU

600,000/-

200,000/-

500,000/-

500,000/-

1,800,000/-

Kuhudumia mche mmoja kwa mwe-zi 500 ( kwa mwaka mzima ni sawa na 500 x 100 x12 (kupiga dawa, kupogolea na kufanya uangalizi wa jumla)

Palizi kwa mwaka inatakiwa anga-lau palizi 4 na palizi moja ni tshs. 50,000/- (50,000 x 4)

Kuvuna kwa kila chungwa moja ni tshs, 5 na inakadiriwa kwa msimu wa kwanza kwa mbegu bora unaweza kupata kati ya chungwa 400-600 (wastani 500) hivyo kuvuna ni sawa na 250,000 kwa msimu mmoja am-bapo kwa mwaka ni laki tano maa-na kuna misimu miwili (hii ni kwa ku-tumia nguvu kazi watu kwa kutumia mashine inawezakupungua)

Kununua dawa kwa mwaka.(Makadi-rio)

Usafiri na kodi za serikali itategemea-na na umbali wa kiwanda au soko.

Hivyo basi jumla ya gharma za kuhudumia ekari moja ya chungwa kuanzia kununua shamba hadi kuvuna ni sawa na; 3,400,000/- + 1,300,000 + 1,800,000 = 6,500,000.

TAHADHARI: LAKI TANO (500,000/-)

Page 9: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

99

9. FAIDA TARAJIWA.Kwa ekari moja mkulima anategemea kupata wastani wa machungwa 500, kampuni ya jatu itaweza kutoa soko la uhakika kwa mkulima kaunzia tshs 100 kwa chungwa, hivyo kwa mche mmoja ambao unazalisha chungwa 500 na kila chungwa linauzwa tshs. 100, jumla ya tshs. 50,000 zitapatikana kwa mche mmoja, kwa miche 100 am-bayo ndo ipo katika ekari moja, mkulima anategemea kupata tshs. 5,000,000/= (mil-lion tano).

Ikimbukwe kwamba kwa Tanga kuna misimu miwili ya mavuno ya machungwa, hivyo mkulima atapata faida hii mara mbili kwa mawaka ambayo ni sawa na tshs. Million kumi. (10,000,000) hivyo basi ili kupata faida halisi; kwa awamu ya kwanza ya uwekeza-ji, mkulima anatagemea kupata jumla ya tshs. 10,000,000 – 7,000,000 = 3,000,000/- hii ni faida kwa mwaka.

Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara-ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka miwili ya mwanzo; kwa mfano;

Katika mwaka wa nne mkulima atatumia kadirio la tshs. 1,800,000 – 2,000,000/- ku-hudumia shamba na mavuno yanategemea kua Zaidi ya chungwa 500 kwa mche. Hivyo, tukiendelea kubaki na mauzo yetu ya awali ya tshs. Million kumi, mkulima atapata faida ifuatayo; 10,000,000 – 2,000,000 = 8,000,000/- hii ni faida ya kudumu kwa si chini ya miaka 20 ambayo mkulima ataendelea kuchuma machungwa kwa ekari moja.

9

Page 10: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

10

Utafiti na mrajesho huu ni mwanzao wa mradi mkubwa wa jatu katika matunda na vi-wanda, hata hivyo ili kukamilisha mradinwetu huu, tutapitia katika hatua kuu zifuatzo;

MKAKATI WA JATU

1. UTAFITI

2. KILIMO

Utafiti wetu bado unaendelea na tumeugawa katika sehemu kuu mbili, sehemu ya kwanza tunatafiti na kuanza kutekeleza zao ambalo limezoeleka yaani machungwa. Hatua ya pili tunapima udongo ili kujiridhisha kama tunaweza kulima matunda aina zingine katika eneo hili. Lakini tukishindwa kulima matunda mengine tanga kama tu-livyo ainisha hapo juu, tutuaendelea na utafiti katika mikoa mingine kama vile Iringa, njombe na Mbeya, lengo ni kuwa na matunda aina ambali mbali na hata kuwa na viwnada vingi Zaidi kila eneo.

Kwa kuwa tayari tumejiridhisha kwamba jamii husika inahitaji huduma za jatu kati-ka elimu, Teknolojia na Masoko, tumeridhia kuanza kutekeleza mradi wa kilimo cha matunda katika mkoa wa Tanga, na hapa tutaweza kulima katika wilaya ya muheza, hendeni na korogwe maana kote hali ya hewa inaruhusu. Hivyo basi tutawashirikisha wanajatu ambao walio mbali na maeneo waweze kununua mashamba na kuanza ku-jiandaa na zao hili. Lakini pia tutaanza kuhudumia wakulima waliopo tayari ili kuweza kuboresha mazao yaliyopo kwa sasa na kukuza uzalishaji na kipato.

Page 11: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

11

3. VIWANDA

4. UZALISHAJI

5. BIDHAA

Ili kutoa suruhisho la kudumu kwa wenyeji na pia kwa wanachama watakao lima na jatu, soko la uhakika lazima lianzishwe. Ni mkakati wa jatu kuanza kujiandaa kujenga kiwanda cha kati na cha kisasa kwa ajili kuchakata matunda haya na pia kuandaa ma-chungwa na kuyauza katika soko kubwa la ndani na nje ikiwezekana.

Baada ya kuanza uzalishashi kwa yale mazao ambayo tumechagua tunandelea ku-panua wigo wa mashamba na kiwanda ili kukidhi mahitaji ya wakulima na walaji wa bidhaa za jatu ambao wanaongezeka kila siku.

Tunategemea kuwa na bidhaa aina mbali mbali zitokanazo na mali ghafi ya matunda haya, mfano wa bidhaa hizo ni; juice fresh, juice iliyoboreshwa (flavored juice), uji na matunda fresh.

11

Page 12: COVER PAGE - WordPress.com · 2021. 1. 20. · Mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa mwaka wa pili wa mavuno kwani ghara - ma za uendeshaji ni ndogo sana ukilinganisha na miaka

12

HITIMISHOIdara ya miradi inashukuru uongozi wa jatu plc kwa kuendelea kutoa sapoti ya ku-hakikisha utafiti huu unafanyika kwa weledi, tunaishukuru na kuipongeza serikali hasa halmshauri ya wilaya ya muheza kwa ushirikiano na msaada waliotoa kukamilisha zo-ezi hili kwa hatua hii, lakini pia tunawashukuru wanachama wetu ambao mko tayari kuwekeza katika miradi hii. Tuwahimize tu kwamba; kilimo kinalipa endapo kitafany-ika kwa tija na kwa kuzingatia kanuni sahihi za kilimo, JATU kwa nafasi tuliyo nayo katika jamii, tunajipambanua vyema kabisa ni kwa namna gani swali hili linawezekana tukianza na utafiti ambao tumejitoa kuifanya kwa weledi na moyo. Tunatoa rai, kama kuna mwanachama atapata wazo la kilimo cha zao lolote na kwamba anaweza kusaid-ia kwa namna moja ama nyingine timu ya utafiti kufika eneo husika, awasiliane nasi ofisi ya utafiti kwa mawasiliano yafuatayo;

Jatu Public limited companyMkuu wa idara ya utafiti,S.L.P 42,155Dar es salaam cc.Ofisi maalumu ya utafiti, DODOMASimu: 0653104160Tovuti: www.jatukilimo.comBarua pepe: [email protected]