SIWA LA KISWAHILI ni kijarida ambacho kinachapishwa na Idara ya Kiswahili, Chuo Ki- kuu cha Nairobi. Hili ndilo toleo la pili. Karibuni ili mpate kufahamu habari za hivi punde kabisa kutoka katika Idara ya Kiswahili. Toleo hili pia linaangazia maswala mbali mbali yanayohusiana na shughuli za Idara, wahadhiri, wanafunzi na wafanyikazi wengine idarani. Wa- hadhiri kadhaa wamechapisha vitabu vipya, wengine wao wamehudhuria na kuwasilisha makala katika makongamano mbali mbali ya humu nchini na katika nchi za kimataifa. Vile vile toleo hili lina habari kuhusu shughuli za kufundisha Kiswahili ikiwa ni pamoja na mi- hadhara, safari na tafiti za nyanjani, uwasilishaji wa mapendekezo na matokeo ya utafiti unao- fanywa na wanafunzi wa kiwango cha uzamili, miongoni mwa mambo mengine. KARIBUNI! DIBAJI CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI DIbaji………………………….1 mkuu wa idara…………... TAhariri……………………. Machapisho………………. Makongamano………….. Ufundishaji………………. Mahafala…………………. Wahadhiri………………... Wanafunzi……………….. USHIRIKIANO……………. KIJARIDA CHA IDARA YA KISWAHILI JANUARI - MEI 2016 SALAMU ZA MKUU WA IDARA YALIYOMO Karibuni katika Idara ya Kiswahili. Nina furaha kubwa ku- waalika kusoma SIWA ambayo ndiyo mbiu yetu. Toleo hili linaonyesha shughuli mbali mbali zinazofanywa na wa- hadhiri na wanafunzi wa Idara ya Kiswahili. Mathalani uta- julishwa kuhusu vitabu na machapisho ya hivi karibuni kabisa yaliyoandikwa na wasomi wetu wa Kiswahili, ushirikiano tulio nao na vyuo vingine ulimwenguni, makon- gamano yalioyoandaliwa ama kuhudhuriwa na wahadhiri wetu, pamoja na shughuli zao za utafiti. Vile vile, utasoma kuhusu shughuli za wanafunzi wetu wa Kiswahili. Singependa kukuondolea utamu wa mambo utakayofurahia utakaposoma taharasha hii tukufu. Karibuni! Prof. John Habwe Mkuu wa Idara
6
Embed
CHUO KIKUU CHA NAIROBI SIWA LA KISWAHILI - Latest …kiswahili.uonbi.ac.ke/sites/default/files/chss/arts/linguistics... · Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya ...
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
SIWA LA KISWAHILI ni kijarida ambacho
kinachapishwa na Idara ya Kiswahili, Chuo Ki-
kuu cha Nairobi. Hili ndilo toleo la pili.
Karibuni ili mpate kufahamu habari za hivi
punde kabisa kutoka katika Idara ya Kiswahili.
Toleo hili pia linaangazia maswala mbali mbali
yanayohusiana na shughuli za Idara, wahadhiri,
wanafunzi na wafanyikazi wengine idarani. Wa-
hadhiri kadhaa wamechapisha vitabu vipya,
wengine wao wamehudhuria na kuwasilisha
makala katika makongamano mbali mbali ya
humu nchini na katika nchi za kimataifa.
Vile vile toleo hili lina habari kuhusu shughuli
za kufundisha Kiswahili ikiwa ni pamoja na mi-
hadhara, safari na tafiti za nyanjani, uwasilishaji
wa mapendekezo na matokeo ya utafiti unao-
fanywa na wanafunzi wa kiwango cha uzamili,
miongoni mwa mambo mengine.
KARIBUNI!
DIBAJI
CHUO KIKUU CHA NAIROBI
SIWA LA KISWAHILI
DIbaji………………………….1
mkuu wa idara…………...
TAhariri…………………….
Machapisho……………….
Makongamano…………..
Ufundishaji……………….
Mahafala………………….
Wahadhiri………………...
Wanafunzi………………..
USHIRIKIANO…………….
KIJARIDA CHA IDARA YA KISWAHILI JANUARI - MEI 2016
SALAMU ZA MKUU WA IDARA
YALIYOMO
Karibuni katika Idara ya Kiswahili. Nina furaha kubwa ku-waalika kusoma SIWA ambayo ndiyo mbiu yetu. Toleo hili linaonyesha shughuli mbali mbali zinazofanywa na wa-hadhiri na wanafunzi wa Idara ya Kiswahili. Mathalani uta-julishwa kuhusu vitabu na machapisho ya hivi karibuni kabisa yaliyoandikwa na wasomi wetu wa Kiswahili, ushirikiano tulio nao na vyuo vingine ulimwenguni, makon-gamano yalioyoandaliwa ama kuhudhuriwa na wahadhiri wetu, pamoja na shughuli zao za utafiti. Vile vile, utasoma kuhusu shughuli za wanafunzi wetu wa Kiswahili. Singependa kukuondolea utamu wa mambo utakayofurahia utakaposoma taharasha hii tukufu. Karibuni!
Prof. John Habwe
Mkuu wa Idara
TAHARIRI
MACHAPISHO
Wapenzi wa lugha teule ya Kiswahili ninawa-
karibisha katika toleo hili la SIWA. Hili ni
toleo la pili la kijarida hiki kinachochapishwa
na Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nai-
robi.
Ndani ya toleo hili, mtapata habari mbali mbali zinazohusu Idara ya Kiswahili. Habari hizi ni pamoja na shughuli za ufundishaji, utafiti na uchapishaji zinazofanywa na wa-taalamu wa lugha na fasihi ya Kiswahili waliomo katika Idara. Kumbuka kwamba
Idara hii ina wataalamu waliobobea katika nyanja mbali mbali za lugha na fasihi ya Kiswahili. Nina matumaini kwamba utafurahia kujisomea toleo hili la hivi karibuni kabisa la SIWA. Maoni yenu yanakaribishwa; yatume kwa [email protected]. Karibuni!
UKURASA 2 SIWA LA KISWAHILI
IDARA YA
KISWAHILI INA
WATAALAMU
WALIOBOBEA
KATIKA NYANJA
ANUWAI ZA
LUGHA NA
FASIHI YA
KISWAHILI
Dkt. Nyachae Michira Mhariri Mkuu
Tangu toleo la mwisho la SIWA, wataalamu kutoka Idara ya Kiswahili wameweza kuchap-isha kazi mbali mbali kama ifuatavyo. Prof. John H. Habwe akishirikana na wa-taalamu wengine ametoa kamusi ya kisasa ya lugha ya Kiswahili. Kamusi hii inajulikana kama KAMUSI ELEZI YA KISWAHILI (2016). Kamusi ni ya kisasa na imeandikwa kwa ufundi wa kipekee na ina maelezo mufti ya vidahizo. Miongoni mwa sifa kuu za KAMUSI ELEZI YA KISWAHILI ni kwamba ina: Vidahizo zaidi ya 45,000 Maneno yapatayo 1,000 mapya Matamshi ya kifonetiki ya vidahizo Ufafanuzi wa methali, semi na nahau Mifano mwafaka Michoro na picha maridhawa Upeo wa kimataifa
“KAMUSI ELEZI YA
KISWAHILI NI KA-
MUSI YA KISASA
ILIYOANDIKWA
KWA UFUNDI WA
KIPEKEE NA ILIYO
NA MAELEZO
MUFTI YA VIDA-
HIZO...ITAWAFAA
WATAALAMU,
WANAFUNZI NA
WATUMIZI WEN-
GINE WA LUGHA
YA KISWAHILI”
MACHAPISHO
UKURASA 3 JANUARI - MEI 2016
Miali ya ushairi ni diwani ya mashairi ya kisasa ya
Kiswahili ambayo yametungwa na washairi mbali
mbali na kuhaririwa na Dkt. Iribe Mwangi na
wenzake. Diwani hii ilichapishwa na EAEP
mnamo mwaka wa 2015.
Pendo la Karaha ni riwaya iliyoandikwa na Prof.
John H. Habwe. Riwaya hii ina hadithi ya
kusisimua kuhusu changamoto ambazo vijana
wanapitia wanapokimbilia katika nchi za kigeni
wakitoroka umaskini kwao.
Kaza Macho ni diwani ya mashairi yaliyotungwa na
Prof. Wadi Wamitila. Diwani hii inasheheni
mashairi yenye ubunifu mkubwa pamoja na yana-
tathmini maswala mbali mbali yanayomkumba
mwanadamu. Diwani hii ilichapishwa na Vide
Muwa Publishers.
Ukuzaji wa Kiswahili: Dhima na Majukumu ya Asasi
Mbali Mbali ni kitabu kinacholeta pamoja makala
na tahakiki za wasomi mbali mbali kuhusu
maendeleo na ukuaji wa Kiswahili. Wasomi hao
wametathmini majukumu ya asasi kama vile elimu,
vyombo vya habari na mawasiliano, bunge, wizara
na vyuo vikuu katika maendeleo ya Kiswahili.
Kitabu hiki kimehaririwa na Dkt. Nyachae Mi-
chira na wenzake na kuchapishwa na Focus Books.
Idara ya Kiswahili ina muafaka wa kubadil-
ishana wanafunzi na vyuo vikuu vingine vya
kimataifa. Kwa mfano, tuna mwanafunzi wa
Kiswahili anaysomea shahada yake katika
Chuo Kikuu cha Humboldt kule Ujeru-
mani. Mwanafunzi huyo anaitwa Shadrack
Kirimi (kulia).
Mpango huu wa ubadilishanaji wanafunzi
umewafaidi wanafunzi kutoka Idara ya
Kiswahili. Vile vile, Idara huwa inawapokea
wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya kigeni.
USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Wanafunzi katika Nchi za Kigeni
Idara ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Nai-
robi ina muafaka na Chuo Kikuu cha
Masomo ya Kigeni cha Hankuk, Korea ya
Kusini ambapo msomi wa Kiswahili
anakwenda kufundisha Kiswahili katika
chuo hicho kwa muda wa miaka miwili.
Kwa hivi sasa, Dkt. Tom Olali anaelekea
kukamilisha kipindi chake cha miaka mi-
wili katika chuo kikuu hicho cha Hankuk.
Chuo hicho cha Hankuk, kupitia kwa
Idara ya Kiswahili, kimemteua Dkt. Nya-
chae Michira kuchukua nafasi hiyo kwa
miaka miwili kuanzia mwezi wa Agosti,
2016. Dkt. Michira anafundisha fasihi ya
Kiswahili na vile vile ni mtalaamu wa
maswala ya mitalaa.
Idara ya Kiswahili inampongeza Dkt. Mi-
chira kwa uteuzi huo na inamtakia kila la
kheri atakaposafiri kwenda Korea Kusini.
UKURASA 4 SIWA LA KISWAHILI
Idara ya
Kiswahili ina
muafaka na
chuo kikuu
cha masomo
ya kigeni cha
hankuk, kule
korea ya
kusini ambako
dkt. Michira
atakwenda
kuchukua
nafasi ya dkt.
Olali
Dkt. Tom Olali
Dkt. Nyachae Michira
IDARA INA
MPANGO WA KU-
BADILISHANA
WANAFUNZI NA
VYUO VIKUU VYA
KIGENI KWA
MANUFAA YA
WANAFUNZI
WETU
Wataalamu wa Kiswahili Prof. RayyaTimammy na Dr. Iribe Mwangi
walihudhuria Kongamano la 29 la Swahili kule Bayreuth, Ujerumani kutoka
tarehe 6 hadi 8 Mei, 2016. Wasomi hao waliwasilisha makala yanayohusu
mada mahususi katika nyanja zao.
Prof. Timammy ni mtaalamu wa fasihi huku Dkt. Iribe ni mwanaisimu.
Wote wawili wamechapisha kazi nyingi kuhusu maswala mbali mbali ya
Kiswahili.
Prof. Timammy aliwasilisha makala juu ya “Tamathali za usemi na taswira
katika Utenzi wa Ukimwi ni Zimwi”.
Dkt. Iribe naye akazungumza kuhusu maswala ya fonolojia ya Kiswahili katika makala aliyoiita “Analytical Problems in Standard Kiswahili Pho-nology”.
Katika kongamano hilo, kulikuwepo waandishi watajika wa Kiswahili kama vile Prof. Abdilatif Abdalla mtunzi wa diwani maarufu ya Sauti ya Dhiki.
KONGAMANO LA 29 KISWAHILI LA BAYREUTH
Page 5 VOLUME 1, ISSUE 1
KONGAMANO LA
BAYREUTH
LILIWALETA
PAMOJA
WATAALAMU NA
WAANDISHI
WATAJIKA WA
LUGHA YA
KISWAHILI KAMA
VILE PROF.
ABDILATIF
ABDALLA, PROF.
RAYYA TIMAMMY,
DKT. IRIBE
MWANGI, NA
WENGINE WENGI
Dkt. Iribe (kulia) na Prof. Abdilatiff Abdalla, Mohamed Kellef na Gikambi wakiwa Bayreuth
Prof. Timammy (ameketi kulia) akiwa na washiriki wengine katika kongamano la Bayreuth