Top Banner
ISSN 0856 - 3861 Na. 1214 RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA , JAN 29-FEB. 4, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] Soma Uk. 13 Aungana na Salmin ‘Barzakh’ Safari ni nzito! Kwako Dk. Ndalichako… Tatizo ni ‘majipu’ ya Kamati ya Kutunuku “Naamini maandishi yangu yatawaathiri wengi pamoja na mimi mwenyewe kwa kila hali kiafya, na hata kisaikolojia. Lakini ni tafakari isiyofikirika kutokea katika nchi ambayo inajivunia kuwa na asilimia 99% ya Waislamu ambao ni ndugu.” Aliepusha balaa la Aus na Khazraj Dua zetu, Shein atuvushe salama Yale ya Micheweni 2001 yasirejee Karume Shujaa DK. Aman Abeid Karume DK. Ali Mohamed Shein. MAALIM Seif Sharif Hamad. CHAMA cha Wananchi, CUF, kimesema hakitashiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, 2016. CUF imesema, haitashiriki kwa sababu uchaguzi huo sio halali kwa vile uchaguzi halali ulishafanyika. CUF “inatoa CUF haitashiriki Uchaguzi Machi wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali.” (Soma Tamko la CUF uk.5)
20

ANNUUR_1214

Apr 14, 2016

Download

Documents

zanzibariyetu
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: ANNUUR_1214

ISSN 0856 - 3861 Na. 1214 RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA , JAN 29-FEB. 4, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected]

Soma Uk. 13

Aungana na Salmin ‘Barzakh’Safari ni nzito!

Kwako Dk. Ndalichako…

Tatizo ni ‘majipu’ ya Kamati ya Kutunuku

“Naamini maandishi yangu yatawaathiri wengi pamoja na mimi mwenyewe kwa kila hali kiafya, na hata kisaikolojia.

Lakini ni tafakari isiyofikirika kutokea katika nchi ambayo inajivunia kuwa na asilimia 99% ya Waislamu ambao ni ndugu.”

Aliepusha balaa la Aus na Khazraj Dua zetu, Shein atuvushe salamaYale ya Micheweni 2001 yasirejee

Karume ShujaaDK. Aman Abeid Karume

DK. Ali Mohamed Shein. MAALIM Seif Sharif Hamad.

CHAMA cha Wananchi, CUF, kimesema hakitashiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Machi 20, 2016.

CUF imesema, haitashiriki kwa sababu uchaguzi huo sio halali kwa vile uchaguzi halali ulishafanyika.

CUF “inatoa

CUF haitashiriki Uchaguzi Machi

wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali.” (Soma Tamko la CUF uk.5)

Page 2: ANNUUR_1214

2 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Fethullah-Gulen

Jee Unajua?

MASUALA1.Sayari ipi ilio na baridki kali kabisa? Jawabu: Neptune2.Sayari ipi ilio na uzito mkubwa kuliko zote? Jawabu: Jupiter3.Jua lina asilimia ngapi ya Hydrogen na Helium? Jawabu: 25, 354.Umri wa Jua miaka mingapi? Jawabu: 4.57 bilioni 5.Masafa ya kutoka duniani hadi mwezini. Jawabu: 384,400km6.Kwenye Mwezi kuna maisha? Ndio, Sio. Jawabu: Sio7.Mwezi wa Kiislamu hufwata mzunguko wa …………………………… Jawabu: Mwezi8.Mwezi wa Kizungu hufwata mzunguko wa……………………………… Jawabu: Jua9.Matumaini ya maji kupatikana yapo katika Sayari ipi? Jawabu: Mars10.Jua likitoka Magharibi itakuwa nini? Jawabu: Mwisho wa dunia.

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 36

CHEMSHA BONGO: 37Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

MASUALA

1.Asili ya mto Amazon unatokea wapi? Peru, Brazil Kenya.2.Mto gani unaigawa Urusi na China? Amur, Missisipi.3.Azerbhajan mji mkuu wake ni Baku ipo katika sehemu ya ziwa gani? Lake Balghash, Caspian Sea, Zambezi4.Ziwa gani kubwa nchini Ulaya? 5.Nchi gani ya Afrika ina jina la ziwa na ndio jina la nchi? Zambia, Tanzania, Malawi6.Muislamu yupi nchini Marekani akijinasibisha na Utume?7.Muislamu gani nchini Marekani aliopinga watu kujinasibisha rangi yao na Uislamu?8.Jina la asili la mwanzo la Msumbiji lilikuwa ni :9.Nchi ya Ureno ikijulikana awali kama :10.Kisiwa cha Comoro kinajulikana kwa jina gani kwa Kiarabu?:

1.Ujerumani ndio nchi yenye watu wake wenye kuzaa kwa idadi ndogo, katika kila watu 1,000 huzaliwa watoto 8.2: http://www.bbc.com/news/world-europe-329299622.Nchi za Kiafrika zinaongoza kwa uzazi nchi ya Niger katika kila watu 1,000 huzaliwa watoto 45, Mali 44, Uganda 43, Zambia 42, Burundi na Malawi 42, Somali 40: https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/rankorder/2054rank.html3.Nchi ya Lesotho inaongoza kwa watu kufariki kwa idadi kubwa, katika kila watu 1,000 hufariki watu 14: https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/rankorder/2066rank.html4.Kati ya nchi zenye wanawake wengi kuliko wanaume ni Estonia, Latvia, Russia, Ukraine, Belarus, Armania, Lithuania: http://www.aneki.com/women_men.html5.Nchi zinaongoza miji yake kuwa na usafi wa hali ya juu ni Finland ikifwatiwa na Norway, Sweden, Iceland, Canada, Switzerland: http://www.aneki.com/cleanest.html?&order=desc&orderby=table_cleanest.value&number=10&cntdn=asc6.Kati ya nchi zinazozalisha nishati mbadala kwa wingi ni Zambia, Nepal, Congo DRC, Albania, Tajiksatn, Norway: http://www.aneki.com/highest_renewable_electricity.html7.Miji ilio na maisha magumu na matumizi ya chini ni: Brazzaville iliopo Congo, Bangui Afrika ya Kati, Baghdad huko Iraq : http://www.aneki.com/worst_cities.html8.Kati ya nchi ambayo Matetemeko ya ardhi ndio kwao ni Afghanistan, Algeria: http://www.aneki.com/list_countries.php?t=Earthquake_Prone_Countries&slide=39.Nchi zinaongoza viogozi wao kula rushwa ni Indonesia, Philippines, Congo DRC, Nigeria, Serbia na Montenegro, Haiti, Peru, Ukraine: http://www.aneki.com/corruption_leaders.html10.Nchi ya Sweden inaongoza katika usawa wa jinsia ikifwatiwa na Norway, Iceland, Denmark, Finland, New Zealand, Denmark: http://www.aneki.com/best_gender_equality.html

“ENYI wale ambao mmeamini msile mali zenu kati yenu kwa batili, isipokuwa zitakapokuwa ni biashara yenye kutokana na maridhiano kati yenu na msiziuwe nafsi zenu hakika Mwenyezi Mungu hakuacha kuwa kwenu ni mwenye huruma sana”. [AN-NISAA 29]

Wakati Qur’an inaposema: Msile mali zenu kati yenu kwa batili” inatumia msemo wenye kukusanya. Qur’an inayaelekeza macho kwenye uharamu wa kula mali za umma ubavuni mwa mali za jamaa na wenye udugu au kutumia vitu vyao, pasi na radhi yao, kama unavyoingia katika maelezo hayo, uporaji, na wizi na matumizi mabaya na ujinga katika kutumia mali na kupata mali kwa njia

An nisaa: 29zisizokubaliwa na sheria.

Ama faida yenye kupatikana kutokana na kubadilishana mali kutokana na kuridhiana pande zote zinazohusika, na faida yenye kutokana na biashara (hiyo sio kosa) na – Ndiyo iliyotajwa hapa, kwa sababu biashara ni njia muhimu na nyenzo ya kupata faida. Hiyo ni faida inayotosha kwa ajili ya maisha, hakuna haja wala ulazima wa kutumbukia katika njia za haramu, wala kwenye njia ambazo uhalali wake na uharamu wake hauko bayana.

Kunawezekana kulifahamu angalizo la maneno haya “na msiziue nafsi zenu” angalizo ambalo limekuja katika aya hii juu ya maana mbili:

1. Hakika yule ambaye anatenda madhambi ya kuteleza katika riba au kamari au rushwa na kadhalika katika njia za haramu, hakika mtu huyo kwa kufanya hivyo, atakuwa ameiua nafsi yake kihali na ameimaliza.

2. Hakika watu watakapoingia katika muamala wowote katika miamala iliyoharamishwa na iliyobatili na yenye dhulma katika kuchuma mali na kuzitoa, na kila matumizi yoyote yaliyo katika namna hii, na kuukubali msingi wowote wenye kutegemea kwenye utaratibu huo

kama ubepari au uhuru wenye kuvuka mpaka na kadhalika, kufanya hivyo kutapelekea kwenye kudhihiri mifumo mingine, kama majibu ya kitendo hicho kama vile, ukomonisti. Na ehee ni kama hivyo mtaufungua mlango mbele ya wauaji na wamwagaji damu na kwenye matendo ya kuwakimbiza watu na kuwatoa katika maeneo yao.

Ndiyo, mtakapoingia tokea mwanzo katika mfano wa mifumo hii matokeo ni kwamba nyinyi mtaingia katika kuwaua baadhi yenu baadhi. Kwa sababu hiyo, msiuache Uislamu na mkaupuuza, matokeo yake mtaingia katika njia zenye kupotea zenye kutofautiana. Yatakuwa matokeo yake ni kwamba baadhi yenu watawaua baadhi nyingine. Ndiyo kwa hakika hali ya dunia ambayo unafanyika ndani yake utekelezaji wa mifumo hii hali ya kuonekana mbele ya macho yetu hali hiyo inaunga mkono na inaisadikisha aya hii.

3. Uwazi wa aya hii unakubaliana kikamilifu pamoja na maana ya kukataza kujiua, maana, kusimama mtu na kujiua yeye mwenyewe, isipokuwa ni kwamba, zinapatikana baadhi ya sehemu nyingine za aya hii. Kwa mfano, kuharibu uwiano uliopo kati ya matabaka na makundi linaivuta jamii hiyo kwenye matatizo misuguano ya ndani, kama ambavyo kusimama baadhi ya wajinga ukichimbuka kutokana kuelewa kwao kwa makosa kuhusu Zuhdi – kwa kuacha njia zilizo kubaliwa na sheria, kwa ajili ya kuchuma na kuchagua ufukara na uduni wa maisha, hilo linapelekea kwenye unyonge wa umma na kuangamia, kama ambavyo kutawalia mmoja wao juu ya mali za watu wengine kwa njia ambazo hazikubaliani na sheria au kuwashakiza watu wengine juu ya unyang’anyi huu na kutawalia kusikokuwa kwa kisheria kunamfanya mtu huyo astahili kuuliwa na hizi ni baadhi ya nukta zenye kufahamika kutokana na aya.

Na inadhihirika rehma ya Mwenyezi Mungu iliyo pana na yenye kuenea, kusimama kwake kwa kuongoza kwenye njia ya salama zaidi na hili ndilo jambo linalongojewa kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na neema ndogo ndogo.

B J N E P T U N E M W J S 384,400 Km

I C A R T O O N P A O U O 980,00Km

L H E L I U M N U R R A L 111,111,000Km

O R O M E S P A I S L A A 788

N F M W E Z I W O S D N R 88,888

I L O L T O S F Y K G K S 12,345,679

4.5 R O I T E R S A W E E Y 4.57 bilioni

M W I S H O W A D U N I A 888,999 Km

A L A S K G J U P I T E R 25

N E P T U N E Z S I O D 75 35

A S A E B M L E B T U J M B

N U U L A U A L A A T U A A

D D T A L S D I L N U Z L L

B A R M G S O J A Z R U C G

R N A B H A G A D A U L O H

A S I E A M A M B N K K L A

Z O S D S B D O U I I A M S

I U A U H E A H R A S M X H

L U K U S I R A T K O A T S

A M U R K D M U E M R A C

S U N S T A U E K N A U I N

M A L A W I F D A Y L S W D

R O M E R Y F T L A I A A A

Page 3: ANNUUR_1214

3 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Habari

Bismillahir Rahmanir Rahim. “NA KUMBUKENI neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu. (Zamani) mlikuwa maadui, Naye akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo, kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto (wa Jahannam), Naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni aya zake ili mpate kuongoka.” (3:103)

Nimeanza na kumtanguliza Mwenyeenzi Mungu kwa kuwa ninachokiandika ni kitu kizito na hakijawahi kuandikwa popote kwa ukamilifu wake zaidi ya kwenye kitabu kile kilichotayarishwa na Chama Cha Wananchi (CUF) na kwenye ripoti za Shirika la Human Rights Watch ya mwaka 2012.

Ni mambo ambayo yanahitaji mazingatio makubwa kwetu sote kama wananchi kwa kila mmoja na nafsi yake kuwa ana dhima kubwa ya kuhakikisha usalama wake na usalama wa mwenzake. Lakini pia kwa viongozi ambao nao wamebeba dhima na jukumu kubwa zaidi mbele ya Mwenyeenzi Mungu na wanaowaongoza.

Naamini maandishi yangu yatawaathiri wengi pamoja na mimi mwenyewe kwa kila hali kiusalama, kiafya, na hata kisaikolojia. Ni kwa sababu najaribu kuvuta hisia za miaka 15 iliyopita ambapo makubwa yalitokea katika nchi yetu ya majonzi na huzuni ya unyama uliokithiri. Ni maumivu yasiopona. Ni uonevu usiosahaulika. Na ukatili usiosameheka. Lakini tafakari isiyofikirika kutokea katika nchi ambayo inajivunia kuwa na asilimia 99% ya Waislamu ambao ni ndugu.

Nimekuwa nikitumia mfano mmoja kila mara panapotokea masuala ya kuzungumzia umuhimu wa kudumisha amani na maelezo haya ninayoyandika leo ni kama hadithi au simulizi lakini ni simulizi ya ukweli ambao imetokea Januari 27 mwaka 2001 wakati ambao nchi iligubikwa na harufu ya damu ya Wazanzibari iliyomwagika. Maumivu makali yaliokosa tiba. Majonzi na masikitiko makubwa yaliojaa ndani ya nyoyo za wengi. Nchi iligubikwa kiza kinene ambayo yaliokuwa hayajawahi kushuhudiwa yakashuhudiwa. Yaliokuwa hayajaonekana na kusikika, yakaonekana na kusikika katika aridhi hii ya Tanzania kwenye Visiwa vya Zanzibar.

Karume Shujaa

Salma Said, Zanzibar

Yalianza Januari 26 ambapo Imamu wa Msikiti wa Mbuyuni Sheikh Juma Mohammed akiwa juu ya vespa yake akielekea nyumbani kwake maeneo ya Mtendeni, alipigwa risasi na kufariki hapo hapo wakati akitokea kusali sala ya Ijumaa. Na siku ya Januari 27 ndio watu wapatao 62 walifariki na wengine kadhaa kujeruhiwa na kuacha vilema, wajane na mayatima. Wengine wakaingia kuishi porini na kwa mara ya kwanza, Tanzania ikatoa wakimbizi waliokimbilia eneo la Shimoni, Mombasa Nchini Kenya na wengine Somalia.

Sababu ya kutokea hayo ilikuwa ni maandamano yalioandaliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) yaliokuwa yakipinga matokeo ya uchaguzi yaliomuweka madarakani Rais Amani Abeid Karume katika kipindi cha Awamu ya Kwanza ya utawala wake, huku Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.

Sio mambo ya kukumbushwa kila wakati kwa sababu sio mambo mazuri na sio mambo ya kuigwa wala ya kutolewa mifano kwa kuwa ni mambo ambayo yameshapita, lakini hayawezi kuondoka katika nyoyo za watu kwa sababu waliotenda na waliotendewa bado wapo katika nchi hii ambao wengi wao wahai na wanatembea kama kawaida. Lakini kubwa na la kutisha na kusikitisha pia, viashiria vya kurejea haya vinaonekana waziwazi.

Ni hisia zilizo kali unazipata unapoyakumbuka madhila yaliowafika ndugu na jamaa ambao waliathirika na matukio yale, ingawa sikuwepo nchini siku ya tukio lenyewe, lakini mwaka 2002 nilibahatika kuwa miongoni mwa wanaharakati wachache kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) waliokwenda kufanya tafiti za tukio lile kwa kuangalia athari walizopata akina mama na watoto wakati wa matukio hayo. Mbali ya kufanya tafiti, pia tulitumia fursa hiyo kuwatoa khofu wanawake hao wajitokeze kwa wingi kwenye Tume iliyoundwa na Serikali iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake, Hashim Mbita kwa ajili ya kukusanya maoni na ushuhuda wa yaliowafika waathirika wa matukio hayo ya Januari 27, 2001.

Shirika moja la kimataifa liitwalo Urgent Action Fund ndilo lililotupeleka Kisiwani Pemba kufanya utafiti huo ambao katika utafiti ule kuna mambo mengi tuliyaona, sio ya kujifunza tu, bali tuligundua kuna watu bado wameathiriwa vibaya sana na matukio yale kiafya na kisaikolojia, na ndio maana khofu na woga ulitawala zaidi miongoni mwa wanawake wengi ambao tulifanya nao mazungumzo.

Wanaharakati hao wote wakitokea Tanzania Bara isipokuwa kwa upande wa Zanzibar nilikuwa mimi na Ally Saleh na kwa hakika

sisi ndio tuliandika mapendekezo hayo na kuwashauri wanaharakati wenzetu kuja kufanya kazi pamoja ambapo katika kazi hiyo kulikuwa na wanaume wawili tu, Ally Saleh (BBC) wakati huo na Khamis Suleiman (Chanel Ten).

Nimetoa picha hiyo ili muone namna mazingira ambayo tuliofanyia kazi wakati huo ni sisi wanawake ambao tulikuwa tukiwakabili na kuwauliza masuali wale waathirika waliokumbwa na matatizo wakati huo lakini licha ya kuwa wanaharakati waliokwenda kufanya utafiti walikuwa ni wanawake pekee, lakini haikuwa kazi nyepesi kuwadadisi na kuweza kupata maelezo yao.

Mambo mengi tulijifunza kutojiamini, woga, khofu, aibu na haya ndio vilivyokuwa vikitawala katika mahojiano yetu. Wanawake wakituogopa wakiona kama kwamba tumekwenda kuhoji ili tuwazamishe zaidi badala ya kuwasaidia na kuwapa faraja. Pamoja na kuwa tulipofika tulifuatana na wenyeji na tulijigawa kwa makundi katika kufanya usaili huo, lakini baadhi ya waathirika wakiogopa sana kuongea na sisi baadhi yao wakisogea upande wangu wakionesha kuniamini zaidi kuliko wale wenzangu, wakati huo mimi ni mgeni sana Kisiwani Pemba. Kumbe wameona peke yangu niliyevaa Hijaab.

Nikajiuliza ni kitu gani kilichowapa imani wanifuate mimi zaidi? Lakini baadae nikagundua kuwa kumbe ni khofu tu walikuwa wakiamini wale waliokuja ni watu waliotumwa kutoka Bara kufuatilia mambo yao. Baadhi ya watu wakinifuata nje na kuniuliza “Eti wale wenzako ulokuja nao sio usalama wa taifa, maana isije kuwa tunatoa maelezo yetu baadaye tukajiwa usiku kufuatwa majumbani kupigwa tena?” Masikini walikuwa wakionesha khofu zao.

Kwa kuona hisia waliokuwa nazo,

ikabidi nitumie taaluma yangu na kuwaeleza kuwa hapana sote tupo sawa na sote tunafanya kazi pamoja na lengo letu sio kuwaongezea matatizo waliyopata, bali kuja kuwasaidia namna gani ya kuweza kujiondoa katika mawazo mazito waliyonayo. Baada ya hapo jioni tunapomaliza kazi hujumuika nikawaeleza wenzangu suala hilo kwamba kuna baadhi ya watu wanaogopa na hawatuamini kwa hivyo tukatumia mbinu mpya ya kuweza kuwavuta wengi na kuwahoji.

Tulijigawa mafungu na tukaitisha mkutano lakini katika kuuliza masuali ilikuwa tunaita mtu mmoja mmoja na anaeleza masuali yake hadi mwisho ingawa hatukupenda mtu kumlazimisha kusema kila kitu lakini wengi wao wakiongea wakilia sana na kutuonesha makovu yao. Wenye majeraha ya risasi, kuna waliopigwa mikwaju, kuna waliobakwa na kuna ambao wameathirika kisaikolojia kutokana na vitendo walivyofanyiwa.

Najua machungu na athari za ubakaji, najua namna gani mtu ambaye anakuwa ameathirika kimwili na kisaikolojia katika jambo hilo, na pia nafahamu maumivu ya mtu ambaye anahadithia madhila yaliompata anapohadithia anaona kama kitendo kile anafanyia tena, hivyo maumivu yake yanakuwa makali zaidi kuliko mara ya kwanza kwa maana anapohadithia anakuwa na hisia kali (deep feeling).

Nikayakumbuka maelezo ya rafiki yangu mmoja wa kike kutoka Congo niliekuwa nikiishi naye bweni moja wakati nasoma nchini Kenya, aliwahi kubakwa namna ambavyo akinieleza madhila waliofanyiwa kabla ya ubakaji nikayafananisha na yale ambayo nilikuwa nikiyasikia kwa msichana mmoja wa Wete. Nililia sana na nilishindwa kuzuwia hisia zangu. Nilijisikia naumia sana. Niliporudi baada ya kazi nikamwambia Ally Saleh siamini nilichokisikia. Siamini kama haya yamewahi kutokea Zanzibar. Ally Saleh akanambia, “Naam! Yametokea.”

Siku ya pili nikakutana na mwanamke ambaye anaelezea namna ambavyo amebakwa au ameingiliwa kwa nguvu na wanaume wawili mbele ya mume wake ambaye alifungwa ukumbini kwake akiona huyu mkewe akibakwa. Alilia sana wakati ananielezea ingawa yeye baadae alijikaza, lakini mimi nilishindwa kumuangalia usoni. Uso wangu niliuinamisha chini nikifuta machozi mpaka anamaliza nilikuwa na masuali ya kumuuliza, lakini kila nikitaka kunyanyua uso nimuulize, nilishindwa.

Mwanamke mmoja ameanza na kuuliza suali, “jee mimi ndoa yangu ipo wakati nimeingiliwa na wanaume ambao sio waume zangu?” Anasema ameshindwa kumuelezea mumewe kama ameingiliwa kwa sababu mume wake alikuwa miongoni mwa wanaume waliokimbilia maporini kuishi huko.

“Nitaanza vipi au nitamtazama vipi mume wangu akijua kama nimevuliwa nguo na mtu asiyekuwa yeye. Siwezi hilo, siwezi kabisa. Namuomba Mwenyeenzi Mungu anisamehe makosa ambayo

RAIS Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa.

Inaendelea Uk. 6

Page 4: ANNUUR_1214

4 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Tahariri/Makala

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

TAYARI Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bw. Jecha Salum Jecha, ametangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio Zanzibar kuwa ni 20 machi 2016 siku ya Jumapili.

Bw. Jecha alisema watakaopigiwa kura hizo za marudio watakuwa ni wagombea walewale waliogombea nafasi ya Urais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani na kwamba hakutakuwa na kampeni za uchaguzi.

Tangazo hilo la Jecha limekuja baada ya awali kufuta uchaguzi wa Zanzibar Oktoba 28, 2015 na hatma ya kisiasa Zanzibar kubakia katika sintofahamu.

Kwa kipindi chote cha karibu miezi mitatu cha kufutwa uchaguzi huo, hakuna suluhu iliyopatikana kati ya pande mbili zilizokuwa zinachuana katika uchaguzi huo, yaani vyama vya CCM na CUF licha ya kufanyika mazungumzo pogo ya kusaka suluhu.

Mpaka Jecha analitangazia Taifa kuhusu tarehe ya marudio ya uchaguzi, msimamo wa CUF na mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad ni kutokubali kushiriki uchaguzi wa marudio. Ila Tume kumtangaza mshindi halali wa uchaguzi uliofutwa.

CCM na mgombea wake Dk. Ali Mohammed Shein, wamesimamia kurudiwa uchaguzi kama ilivyotangazwa na Tume huku wakiwashadidia wafuasi wao kuwa wawape ushindi wa kishindo!

Hata hivyo, pamoja na Bw. Jecha kutangaza tarehe ya kurejewa uchaguzi Zanzibar ili kutanzua mkwamo uliopo na kumaliza

Zanzibar inahitaji muafakana maridhiano

Kura si njia ya uhakika hitilafu iliyotokea, lakini tunachokiona ni kwamba, Zanzibar haina mazoea ya kutatua mizozo yake ya kisiasa kwa njia ya uchaguzi.

Zanzibar ilipofikia ina historia nzuri ya kumaliza mivutano yake ya kisiasa kwa njia ya muafaka na maridhiano, iwe ni masuala ya uchaguzi, ya kidola au kivyama.

Kwa sasa, ili kunusuru hali ya Zanzibar, kunahitajika muafaka wa namna yake kuliko wakati mwingine wowote, ili kupata suluhu ya kweli. Kutafuta suluhu na kuondoa mkwamo wa kisiasa kwa shuruti ya kurudia kupiga, tunaona kuna kila ishara ya kuongeza zaidi ombwe la mzozo wa kisiasa visiwani humo. Maana kwanza tujiulize, kwa nini ule wa awali ulifutwa? Mjadala wa kisheria, kikatiba na kisiasa ukionyesha kuwa kulikuwa na sababu za kufutwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, sheria za nchi na katiba yake, hapo sasa unaweza kuletwa ufumbuzi wa kurejea uchaguzi. Lakini kama umefutwa tu ‘kihuni’, kurudia uchaguzi haiwezi kuwa ufumbuzi.

Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini 1992, hakujawahi kutokea kufanyika uchaguizi mkuu Zanzibar, ukafanyika ukaisha na pasiwepo matatizo ya kisiasa. Tangu uchaguzi wa mwaka 1995, 2000, 2005.

Chaguzi zote hizo zimefanyika lakini hazikuweza kuondoa matatizo ya kisiasa Zanzibar. Hazikuisaidia Zanzibar kuwa na utulivu wa kisiasa unaostahiki. Tena unaweza kusema kuwa uchaguzi wa mwaka

uliopita ndio umefanyika kwa Amani na kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa kuliko miaka yote na bila malalamiko. Lakini ndio huo umefutwa! Sasa mwingine wa nini, kama sio kutaka kulazimisha jambo ambalo wananchi walishalikataa kwa kura zao?

Ni imani yetu kwamba pamoja na

kutangazwa tarehe ya kurejewa uchaguzi, bado tunaamini suluhu ya kweli na ya haki ya kisiasa Zanzibar haiwezi kuwa nje ya maridhiano ya pande husika. Kwa jinsi hali ilivyo sasa ambapo CCM wameshaweka msimamo wa kurejewa uchaguzi na CUF msimamo wa kutoshiriki uchaguzi wa marejeo, ni dalili tosha

kwamba hakuna suluhu kamili itakayopatikana kwa kura ya marudio.

Zaidi utashuhudiwa uchaguzi wa upande mmoja ‘wenye mabavu’, huku upande mwingine ukisusia. Na hapo tuna shaka ya kuhitimishwa ile serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoonyesha njia ya kutuliza shari za kisiasa na kuleta nuru Zanzibar.

Msiba mara mbili KisongeNI msiba mara mbili Kisonge. Kuondokewa na kijana wao na kukosa kumzika.

Ilikuwa wakitaka maiti ipelekwe Fuoni, wana-Kisonge wapate fursa kushiriki, lakini ndugu wakamuwahisha Barzakh kama zilivyo taratibu za Kiislamu.

Huo ni msiba wa Salum Bakari, kijana anayeishi Fuoni anayedaiwa kuwa ni miongoni mwa waandishi wa Ubao unaomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi, maarufu Bao la Kisonge, aliyefariki juzi ghafla.

Bakari aliumwa na tumbo ghafla na kukimbizwa hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ambapo wakati madaktari wakijitayarisha kumfanyia matibabu alifariki dunia.

Kwa mujibu wa daktari wa Mnazi Mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake alikiri kumpokea kijana huyo mchana na akasema alitakiwa kufanyiwa upasuaji, lakini kabla ya kufanyiwa alifariki dunia.

“Ni kweli aliletwa hapa hospitali na tukampokea akiumwa na tumbo na aliletwa mchana, lakini ilibidi afanyiwe operesheni kutokana na maumivu alokuwa akiyapata, bahati mbaya akafariki”, alisema daktari huyo ambaye alikataa kutajwa jina gazetini kwa madai ya kuwa yeye sio msemaji.

Pia daktari huyo alisema kutokana na hali ya nchi ilivyo anaogopa kuongea zaidi kwa kuwa

Na Mwandishi Wetu

hivi sasa serikali kama inawatafutia sababu tu, hivyo jambo lolote lisemwe na wahusika wenyewe kama Katibu Mkuu na Naibu Waziri.

Bakari ni mmoja wa watu ambao walikuwa ni waandishi wa maneno makali ya ubao huo wa Kisonge ambao zaidi huwa unawalenga wapinzani.

Moja ya maandishi yake aliyoandika wakati wa uhai wake ni kuwa ‘hata tukifa sote hatutoi nchi’, ambapo maandishi hayo huandikwa mara kwa mara tokea kufariki kwa mmoja wa wana CCM wahafidhina ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kutaka

kuvunja serikai ya umoja wa kitaifa Salmin Awadh Salmin ambaye naye alikufa ghafla muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha ndani cha ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui.

Salmin aliwahi kusema mara kadhaa kwamba atapeleka hoja binafsi ndani ya Baraza la Wawakilishi kutaka kuivunja serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Bao la Kisonge limekuwa likipata umaarufu kila siku kufuatia kuandika ujumbe ambao unawalenga wapinzani na kuwatupia vijembe jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele

Inaendelea Uk. 7

Page 5: ANNUUR_1214

5 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016MAKALA YA MTANGAZAJI

BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) , l ikiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi ka t ika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam.

Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.

Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. KWAMBA Uchaguzi M k u u w a Z a n z i b a r umeshafanyika tarehe 25 O k t o b a , 2 0 1 5 , a m b a p o kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali.

Kwa upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta uchaguzi huo.

2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.

AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR

3. KWAMBA linatoa wito k wa Wa z a n z i b a r i w o t e wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.

4. KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984.

Hakuna kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au S h e r i a ya U c h a g u z i ya Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa marudio.

5. KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe na matokeo yake kutangazwa.

6. KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu, vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza amani ya nchi yetu kwa kutaka

haki itendeke. Baraza Kuu linazihakikishia

taas is i na jumuiya h izo zote na pia kuwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete kat ika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

7. KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984.

Baraza Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.

8. KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi aliyoianza y a k u t a f u t a u f u m b u z i wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar.

Baraza Kuu l inamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.

9 . KWAMBA l ina laan i matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya

uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi kadhaa kisiwani Unguja.

1 0 . K WA M B A l i n a i t a k a jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.

11. KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu na kuwa watu l ivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha. Baraza Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la kura kwa njia za amani.

Baraza Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar.

12. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.

LIMETOLEWA NA:BARAZA KUU LA UONGOZI

LA TAIFATHE CIVIC UNITED FRONT(CUF – Chama Cha Wananchi)DAR ES SALAAM28 JANUARI, 2016

Page 6: ANNUUR_1214

6 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016Hoja ya Juma Kilaghai

BUFFET! Vyakula vya kila aina unajichagulia tu. Nyama za kila aina – ng’ombe, mbuzi, kuku, samaki, kamba, nakadhalika. Maandalizi: Ziko za kuchemsha, za kuoka, za ku’rost’, za kuchoma, nakadhalika. Huo ni upande mmoja. Upande wa kitoweo! Protini tupu. Upande wa pili kuna vyakula kama wali mweupe, biriani, pilau, viazi vya kusongwa (mushed potatoes), ndizi zilizopikwa rojo, chips za viazi, tambi, makaroni, chapati za kukanda, chapati za maji, nakadhalika. Huu ni upande wa ‘chakula!’ Wanga mtupu.

Upande wa tatu ni ule wa vitu ambavyo ‘siyo muhimu sana’. Hapa unaweza kukutana na mboga mbili tatu za majani; na matunda kama ndizi mbivu, tikiti, nakadhalika. Katika taaluma ya lishe, vyakula katika kundi hili ndivyo ambavyo ni muhimu sana kwa maana ya kuboresha afya. Ukichukulia gramu kwa gramu, vyakula hivi vimebeba virutubisho vingi sana (madini lishe, vitamini, ufumwele [fibers], vizuia vioksidishaji [anti oxidants], nakadhalika), ukilinganisha na vyakula vya protini na wanga. Hata hivyo, kimazoea vyakula hivi tunavipa umuhimu mdogo sana!

Haya ni mazingira ya buffet. Mara nyingi tunakutana na mazingira haya pale tunapokuwa wageni kwenye mahoteli makubwa, au tunapohudhuria sherehe

UCHANGANYAJI USIO SAHIHI WA VYAKULA zilizoandaliwa kwa bajeti kubwa, au tunapokuwa wageni kwenye makaazi ya matajiri. Katika mazingira yetu ya kawaida, iwe ni majumbani au ni kwenye migahawa, japo suala la mchanganyiko wa vyakula vingi halipo, lakini dhana ile ile ya ‘kitoweo’ na ‘chakula’ inaendelea kutawala. Mlo hukamilishwa kwa kuunganishwa kitoweo na ‘chakula’!

Kitoweo hapa ni nyama, kuku, samaki, dagaa na vitu vingine vyenye asili ya protini, wakati chakula ni ugali, ubwabwa, viazi, chapati, mihogo, magimbi, nakadhalika vyote vikiwa na asili ya wanga.

Watu wengi sana tuna tatizo la kujaa ‘gesi’ tumboni na kutopata haja kubwa vizuri. Ni tatizo ambalo tumeishi nalo kwa muda mrefu mno kiasi cha kuzoeleka na kuwa sehemu ya maisha. Kimsingi hili ni tatizo linalotokana na uchakataji (processing) mbovu kabisa wa chakula unaotokana na kuchanganya vyakula vya protini na wanga kwenye mlo mmoja.

Hali hii inatokana na ukweli kwamba watu wengi sana hatujui kuwa vyakula vya wanga na vile vya protini havitakiwi vichanganywe kabisa! Kama kuna haja ya kuchanganya vyakula vinavyotoka katika makundi haya na vyakula vingine, basi vyakula sahihi vinavyofaa kwa ajili ya kuchanganyia ni mboga za majani. Kwa maneno mengine,

wanga unaliwa kwa mboga za majani, na protini inaliwa na mboga za majani.

Kwa nini usahihi ni kula protini au wanga kwa mboga za majani pekee, na siyo vinginevyo? Kuna sababu mbili. Sababu ya kwanza ni kuwa vimeng'enya (enzymes) vinavyotakiwa kuchakata wanga ni tofauti kabisa na vile vinavyotakiwa kuchakata protini. Vimeng'enya hivi vimeundwa kwa namna ambayo hufanya kazi katika pH tofauti (vile vya wanga ni katika mazingira ya alkali, na vile vya protini ni katika mazingira ya tindikali). Sasa unapochanganya vyakula vinavyotoka katika makundi haya kwenye mlo mmoja, mwili unashindwa kuelewa kuwa ni vimeng'enya gani vitolewe ili kufanya Uchakataji.

Matokeo? Uchakataji wa chakula unakuwa ni mbovu kabisa na vyakula vilivyochanganywa kwenye mlo husika huishia kuoza na kuchachuka matumboni. Kuoza na kuchachuka huku kunazalisha gesi nyingi ya ajabu. Sababu ya pili ni kwamba vyakula vya protini vinatumia nishati nyingi sana kuchakatwa ukilinganisha na vile vya wanga. Kwenye mfuko wa tumbo kile chakula kinachohitaji nishati nyingi kuchakata ndicho ambacho kitaanza kuchakatwa. Hii ina maana kuwa kama mlo unajumuisha mchanganyiko wa wanga na protini, wanga utakaa kusubiri mzunguko wa

kuchakata protini ukamilike. Kwa kawaida uchakataji wa protini huchukua kati ya masaa 4 hadi 6. Kutokana na kuwa na asili ya sukari, wanga hauwezi kukaa kwa muda wote huo bila kuanza kuchachuka (ferment).

Matokeo ya kuchachuka kwa wanga wakati wa kusubiri uchakataji wa protini ukamilike ni gesi ya ajabu kuzalishwa! Kimsingi sababu hii ndiyo pia inayopelekea ishauriwe kuwa matunda yote matamu yaliwe walau nusu saa kabla ya kula chakula kingine. Hii ni kwa ajili ya kutoa nafasi kwa sukari yote iliyoko kwenye matunda hayo kuchakatwa na kufyonzwa mwilini kabla ya kukutana na vile vyakula vinavyochukua muda mrefu kuchakata.

Ukiondoa tatizo la kuzaliwa gesi nyingi tumboni pale mlo unapojumuisha protini na wanga, tatizo kubwa zaidi ni mwili kushindwa kupata virutubisho vya kutosha kutoka katika ‘huo mlo mchanganyiko’. Ili mwili uweze kufyonza virutubisho vilivyomo kwenye chakula kwa ufanisi, ni sharti chakula hicho kiwe kimesagwa vizuri, kitu ambacho hakipatikani pale mlo husika unapokuwa umejumuisha wanga na protini. Kwa bahati nzuri tatizo la uchanganyaji wa vyakula ni jepesi kutatua. Utatuzi wake hauhitaji gharama yoyote ya kifedha, bali ni suala la kubadilika zaidi kimtazamo.

(Kwa mawasiliano zaidi piga 0754281131/0655281131)

Karume ShujaaInatoka uk. 3nimefanyiwa bila ya ridhaa yangu.” Alisema mama huyo ambaye yeye ni kutokea maeneo ya Mkoani.

Yupo Bibi mmoja ambaye ni mtu mzima sana yeye nilimsifu kwa kujikaza, lakini akionesha uchungu namna alivyokuwa akieleza namna wajukuu zake walivyoingiliwa wakati yeye amefungwa kamba ukumbini, watoto walipelekwa chumbani na kuingiliwa.

“Nilikuwa nikisikia makelele ya wajukuu zangu ni watoto wadogo wale, nina hakika wamewabikiri kwa sababu wakipiga makelele sana sana”.

Inawezekana mambo hayo ya kuwabiriki watoto wadogo hasa wale waliokuwa wamemaliza sekondari yamefanyika kweli kwa makusudi kwa sababu baada ya miaka kadhaa tulipokwenda Pemba, baadhi ya waandishi wenzetu wa habari wakitwambia hadithi walizokuwa wakihadithiwa na wanajeshi wasio na maadili ambao wakijisifia kwamba waliwabikiri watoto wengi sana kipindi cha Januari 27, 2001 walipopelekwa Kisiwani Pemba. Na wakiomba hali

kama hiyo itokee ili wawapate tena. (Allah atuepushie mbali kwa fadhila zake na huruma yake).

Kwa kweli sitawacha kuyakumbuka yaliomkuta Mama mmoja wa Micheweni akielezea habari zake huku nikiwa mkono wangu ukishikilia shavu langu na kuona michirizi ya machozi ikichuruzika. Mama anasema alifukuzwa na majeshi na kuanguka chini na kisha kuingilia kinyume na maumbile kwa kuwa alikuwa na mtoto mchanga na aliwaeleza kwamba yeye ndio kwanza amejifungua yupo kwenye nifasi, lakini wakamwambia hivyo hivyo tukutie adabu.

Baada ya kumfanyia kitendo hicho akawa hawezi kutembea kwa maumivu aliokuwa akiyapata akaanza kukimbia kidogo kidogo na kupita kwenye bonde bahati mbaya huku akipepesuka akaja akakanyaga kama utelezi mtoto wake akadondoka kwenye matope.

Mama yule huku na khofu ya kunusuru roho yake kwa kuwa alisikia sauti za wanajeshi wengine wakiwatafuta watu waliojificha misituni, huku mtoto anazama katika tope. Uchungu wa mama ukachukua nafasi yake. Akaamua kuhangaika kumtoa mtoto katika tope hata kama wanajeshi watamkuta. Anainama anamtoa mwanawe kwenye matope anamuona mtoto wake hawezi kupumua na punzi za mbali kumbe anavuta pumzi za mwisho. Mtoto ameshakabwa na matope aloyameza. Mama akaanza kulia peke yake akaishiwa nguvu akakaa chini anaogopa kupiga kelele wanajeshi wasimsikie na huku anajaribu kumvuta yale matope kwa mdomoni lakini wapi. Kitoto kile kikafariki mikononi mwake!

Hiyo ni mifano michache tu kati ya watu ambao tumefanya nao mahojiano ambao wakati ule ambao ni kutoka katika maeneo

ya Wete, Chakechake, Micheweni na Mikoani kwa njia za mikutano na kuwauliza kwa kukaa nao kwa faragha kujua yaliowasibu ingawa baadhi yao walishindwa kueleza. Hawakupenda kuyaeleza wala kuandikwa yale mambo yaliowasibu wakisema yameshapita na yameshatendewa. Na ni mengi yanayofanana na hayo tuliohadithiwa na wengine wakianza kutueleza kwa kula viapo wakithibitisha maelezo yao.

Ni mambo mengi sana yalitokea, yanaumiza na yanatia uchungu sana. Lakini suali ni moja tu, jee tunataka haya yatufike tena? Na kama hatutaki, mbona dalili za kutokea haya zipo wazi? Mbona tunatafuta sababu za makusudi za kuturejesha huko tulipotoka?

Sio dhamira yangu kurejesha machungu kwa waathirika wala sio lengo langu kuwaumiza wale walioumia, lakini lengo langu ni kukumbusha kwamba huko tulishatoka na sasa tupo kwengine kabisa. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwamba aliwamiminia busara Rais Mstaafu Amani

Inaendelea Uk. 14

Page 7: ANNUUR_1214

7 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016Habari

Tatizo ni ‘majipu’ ya Kamati ya KutunukuBARAZA la Wakuu wa Shule za Kiislamu Tanzania, limeonyesha hofu katika uharaka wa mabadiliko ya kurejesha viwango vya ufaulu vya zamani uliofanywa na Waziri wa Elimu, Dk. Joyce Ndalichako.

Baraza hilo limesema kuwa, tatizo sio mfumo wa GPA wala Divisheni, bali utaratibu wa kutunuku usio na vigezo vilivyo wazi uliokuwepo wakati wa Dr. Joyce Ndalichako akiwa Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani.

Wamesema, wakati huo kulikuwa na kitu kinaitwa Kamati ya Kutunuku, ambao ndio walikuwa na mamlaka ya kutoa viwango vya ufauli kwa vigezo ambavyo walivijua wao wenyewe.

Wakafafanua kuwa alama za ufaulu zilikuwa ni siri kubwa ya Baraza la Mitihani na zenye kubadilikabadilika somo hadi somo na mwaka hadi mwaka.

Wasiwasi huo wa Wakuu wa Shule za Kiislamu, umekuja kufuatia hatua ya hivi karibuni ya Waziri Ndalichako kutangaza kurejesha mfumo wa zamani wa kukokotoa matokeo ya Mitihani ya Taifa chini ya Baraza la Mitihani la Taifa, na kuachana na mfumo mpya wa GPA.

Katika barua yao kwenda kwa Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa, Baraza hilo (BAWAKITA), limeonyesha wasiwasi wao huo baada ya Waziri wa Elimu, kusikiliza madai ya Chama cha Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Visivyo vya Serikali (Tangmosco) wakidai kuwa mabadiliko hayo kwenda katika mfumo wa GPA yameingia pasi ya kushirikishwa.

Barua hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wake Mwalim Hamisi Togwa, imesema hatua ya Waziri Ndalichako, kumtaka Katibu Mtendaji wa sasa Dr. Charles Msonde, aeleze kuhusu matumizi ya mfumo wa GPA kunaifanya jamii ione na kuelewa kwamba mfumo huo kaunzisha yeye.

BAWAKITA, imebainisha kuwa mfumo wa GPA, ulianza kutumika katika kutangaza matokeo kabla ya Katibu Mtendaji wa sasa, kwa watahiniwa wa Ualimu ngazi ya cheti na Diploma.

Kwa maana hiyo, Baraza hilo limemweleza Waziri Mkuu kwamba wana wasiwasi na uharaka wa Waziri wa Elimu, Mheshimiwa Dk. Ndalichako kurejesha mfumo wa zamani ambao ulibadilishwa baada ya kubainika kuwa na matatizo makubwa.

Na Bakari Mwakangwale

Ikifafanua hoja ya ushirikishwaji wa Tamongsco, katika maamuzi ya kutumia mfumo huo wa GPA, Baraza hilo limesema, walishirikishwa katika Tume iliyoongozwa na Profesa Sifuni Mchome, ambayo ilitoa ripoti yake Juni 15, 2015.

Imeeleza kuwa Tume hiyo ilikuwa na ushiriki mkubwa wa wadau mbalimbali wa Elimu ambapo mambo mengi yaliibuliwa na kuwa chachu ya mabadiliko katika sekta ya Elimu, ukilinganisha na tume tatu zilizo tangulia kati ya mwaka 2011 na 2013.

Ikifafanua zaidi barua hiyo, imesema kuwa kabala ya mabadiliko hayo kwa muda mrefu wadau wa elimu walikuwa hawafahamu mfumo sahihi wa ukokotoaji wa matokeo ya mitihani ya Taifa katika ngazi mbalimbali kama ilivyo bainishwa na ripoti ya Prof. Sifuni Mchome.

“Mh. Waziri Mkuu, ni Tume hiyo ndiyo iliyopendekeza ushirikishwaji wa wadau wa elimu katika kuboresha mfumo wa ukokotoaji wa matokeo, ambapo ilisambaza dodoso juu ya mapendekezo ya alama na madaraja ya ufaulu katika shule za Sekondari.” Imesema sehemu ya barua hiyo.

Ikaeleza kwamba kuuatia hatua hiyo, Baraza lilimuandikia barua Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, aliyepita wakiipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua katika kuwashirikisha wadau katika kuboresha mfumo wa ukokotoaji na kuondoa mfumo wa usiri chini ya Kamati ya Kutunuku, ambapo sasa kila mwalimu anajua wazi madaraja ya ufaulu na namna yanavyopatikana.

Baraza hilo, limeweka wazi kuwa kabla ya kuanza kutumika

kwa alama za ufaulu zilizopo, hakuna mdau yeyote anaweza kusema kwamba alama hizi ni ndogo na anataka zirejeshwe za zamani ambazo ni kubwa.

Wameeleza kuwa hiyo ni kutokana na kuwa alama za ufaulu zilikuwa ni siri kubwa ya Baraza la Mitihani na zenye kubadilikabadilika somo hadi somo na mwaka hadi mwaka.

Barua hiyo imebainisha kwamba, katika zama hizo ambapo vigezo vya ufaulu vilikuwa siri kubwa ya Kamati ya Kutunuku, ilikuwa pia zama ambapo shule za baadhi ya mashirika ya kidini zilidaiwa

KATIBU Mtendaji wa NECTA, Dr. Charles Msonde.

‘kutesa’ kila mwaka.Baraza hilo limesema ni wazi

kuwa mchakato wa uboreshaji wa Elimu katika nchi yeyote unahitaji muda na mikakati mbali mbali, kwani uwazi na ushirikishwaji katika elimu unaotekelezwa na Baraza la Mitihani hivi sasa ni kigezo na mkakati muhimu katika kutoa elimu bora.

Barua hiyo yenye Kumbukumbu namba BAWAKITA/OWT/ELIMU/2016/01/3, imemueleza Waziri Mkuu, kwamba wanapinga juhudi zozote zinazoweza kuwarudisha kule ambako wadau wa Elimu hawakujua mchango wa CA (Continuous Assessment) katika ufaulu wala alama za ufaulu.

Kurudi huko, imebainisha barua hiyo kuwa kunaweza kurudisha mfumo ambao unaweza kutoa mwanya kwa Kamati ya Kutunuku kuamua ni shule gani iongoze kwa kucheza na alama ya ufaulu kutoka somo hadi somo.

“Sisi hatupingi uboreshaji wowote wa majina ya madaraja iwe GPA au Division na hata kupandisha alama za ufaulu.”

“Cha msingi (Serikali) izingatie kanuni ilizojiwekea za utawala bora ambazo pamoja na mambo mengine, zinahitaji ushirikishwaji wa kina wa wadau wote na uwazi katika kufikia maamuzi.” Imeeleza barua hiyo ya Januari 21, 2016.

Msiba mara mbili KisongeInatoka Uk. 4sana na watu mbali mbali, viongozi wa dini na wanasiasa ambao wana khofu ya kuzuka machafuko kutokana na maneno yanayoandikwa katika ubao huo.

Wakati wa kampeni, jeshi la polisi lilipiga marufuku ubao huo kuandika ujumbe wowote ambao utachochea hamasa na kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Juzi Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alisema kuwa ujumbe unaoandikwa pale Kisonge ni mkali lakini hilo ni jukumu la vyama vya siasa na sio jeshi la polisi.

Kamanda Mkadam aliwataka wanasiasa kuwakataza vijana wao ili kuibakisha nchi katika hali ya amani kwani maneno yanaweza kuamsha hisia kali na hatimae kuzusha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Bakari amezikwa juzi katika

makaburi ya Uwanja wa Ndege Kiembe samaki na amesaliwa katika Msikiti wa Nassor Bachu Kikwajuni.

Kabla ya kuzikwa kulitokea mvutano kati ya wanafamilia na wafuasi wa CCM wa Kisonge wakati familia ikitaka azikwe haraka wakereketwa wenzake wakitaka apelekwe Fuoni kwa ajili ya kuzikwa siku ya pili ili wanachama wenzake wapate kuwahi maziko.

“Hatutaki azikwe na Kisonge, tutamzika sisi wenyewe, ndio wazee wake, ya Kisonge alipokuwa hai, sasa ameshafariki mwili wa marehemu upo mikononi mwa familia na familia ndio yenye jukumu la kumzika, tunaharakisha tukamsitiri haraka na ndio maana hatukutana kumpeleka Fuoni maana huenda yakaja maamuzi mengine, tukitoka hapa tunakwenda makaburini leo leo”, alisema Ustadh mmoja ambaye ni miongoni mwa wanafamilia.

WAZIRI wa Elimu, Dk. Joyce Ndalichako.

Page 8: ANNUUR_1214

8 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Na Nizar Visram

Inaendelea Uk. 18

Makala

HABARI za hivi majuzi zinasema suala la Burundi litajadiliwa na kamati maalum ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linaloshughulikia utatuzi wa migogoro. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Abdullah Mwinyi amesema ujumbe wa Rais Pierre Nkurunziza umekubali kuhudhuria mkutano huo utakaofanyika mjini Arusha wiki hii. Kamati hiyo pia itatoa fursa kwa raia na asasi za kiraia kutoa maoni yao kuhusu mgogoro wa Burundi ambao umepelekea mamia ya watu kupoteza maisha yao. Moja ya asasi iliyosambaza risala yake ni jumuiya ya wanasheria wa Afrika (PALU) ambao wamependekeza kuwa Nkurunziza asiruhusiwe kushika uwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mpaka akubali kushiriki mikutano ya usuluhishi.

Kwa mujibu wa katiba ya EAC, uwenyekiti unatakiwa ushikwe na Nkurunziza baada ya Rais Magufuli kumaliza muda wake. Wengine wamediriki hata kusema kuwa Burundi ifukuzwe kutoka EAC

Wakati kamati ya EALA inapanga mkutano wa usuluhishi, tarehe 6 mwezi huu mawaziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Uganda, na Angola walihitimisha kikao cha faragha kuhusu Burundi uliofanyika mjini Arusha. Hii ni baada ya mazungumzo ya amani yaliyopangwa kufanyika Arusha kuahirishwa kwa vile ujumbe wa Nkurunziza ulikataa kuhudhuria wakisema hawatakaa meza moja na wale “wanaochochea vurugu nchini Burundi.”

Wakati huo huo, Rais Museveni ameteuliwa na marais wenzake wa EAC kuwa msuluhishi katika mgogoro wa Burundi. Yeye

Kwanini mabeberu wanachangamkia sana Burundi?

MWENYEKITI wa kamati maalum ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) , Abdullah Mwinyi.aliahidi kung’atuka baada ya mihula miwili lakini sasa anaendelea na muhula wa tano akiwa ametawala nchi kwa muda wa miaka 30. Sasa anatarajia kugombea urais mwezi ujao baada ya kubadili katiba iliyoweka kikomo. Alifanya mabadiliko hayo mnamo 2005 na tangu wakati huo amekuwa akisema “shamba ambalo nimelisafisha, kulipalilia na kulilima mwenywe sasa iweje niwaachie wengine walivune?” Kwa maneno mengine nchi imegeuzwa shamba lake.

Hata hivyo EAC imemteua kuwa msuluhishi wa Burundi , jambo ambalo limekubaliwa na AU, UN na wafadhili.

Kwa muda huu Rais Magufuli ni mwenyekiti wa EAC na ndio maana huwa anamtumia waziri wake wa mambo ya nje, Augustine Mahiga kushughulikia mgogoro wa Burundi. Mpaka sasa hajasafiri nje ya nchi na haieleweki iwapo atahudhuria mkutano mkuu wa EAC au wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika mjini Addis Ababa ili kuzungumzia mgogoro wa Burundi. Tanzania ina nafasi nzuri kwa vile Burundi imekuwa na uhusiano wa karibu na Tanzania. Wengi tutakumbuka wakati ule marais wa EAC walipokuwa wakikutana Tanzania na Burundi zilitengwa kwa sababu ilionekana sisi hatukuwa tayari kujiunga na miradi ya EAC. Wenzetu walijihesabu kama nchi zilizokuwa zinakubaliana (Coalition of the Willing - CoW).

Mgogoro wa Burundi ulianza pale mahakama

ya katiba ilipoamua kuwa Nkurunziza alikuwa na haki ya kugombea urais kwa muhula wa tatu, ingawa katiba iliyosainiwa na pande zote mjini Arusha iliweka kikomo cha mihula miwili. Ni kwa sababu muhula wa kwanza Nkurunziza alikuwa amechaguliwa na wabunge na sio kwa kura za wananchi. Hivyo muhula huo haukupaswa kuhesabiwa, ilisema mahakama. Katika jopo la majaji watano, mmoja alitofautiana kwa kusema kuwa hao wabunge waliwawakilisha wananchi kwa hiyo awamu ya kwanza ilipata ridhaa ya wananchi. Huyo jaji alilazimika kuikimbia nchi, baada ya kudai kuwa majaji wenzake walikuwa wamelazimishwa kumuunga mkono Nkurunziza.

Wapinzani wakadai kuwa hata hivyo mahakama hiyo ya katiba haiwezi kuwa huru kwa sababu majaji wake wameteuliwa na Nkurunziza. Kuna wanaosema kuwa hoja hii haina mashiko, kwani hata katika nchi za magharibi kama Ufaransa majaji wa mahakama ya katiba huteuliwa na rais. Hata Obama anawateua majaji wa mahakama ya juu. Hivyo, baada ya mahakama ya katiba kumruhusu, Nkurunziza aligombea urais mwezi Julai 2015 na akachaguliwa kuongoza muhula wa tatu kwa kupata asilimia 70 ya kura. Uchaguzi huo ulisusiwa na wapinzani. Marekani na EU wakakataa kutuma waangalizi wa uchaguzi.

Wakati Nkurunziza analaumiwa kwa kugombea urais muhula wa tatu, hatusikii lawama kutoka nchi

RAIS Museveni ameteuliwa na marais wenzake wa EAC kuwa msuluhishi katika mgogoro wa Burundi.

za magharibi zikielekezwa kwa marais wa Rwanda, Uganda na DRC (Congo) ambao pia wameongeza mihula yao. Kagame na Kabila nao, sawa na Nkurunziza, waliteuliwa kushika muhula wa kwanza na kwa hiyo wanadai hauhesabiki.

Kagame aliteuliwa kuwa rais mwaka 2000, kisha akachaguliwa kwa kishindo mwaka 2003 na 2010. Sasa awamu yake ijayo itakuwa ya nne lakini yeye anasema ni ya tatu. Pia anakusudia kuondoa kikomo ili aendelee kuchaguliwa bila kikomo. Kama ni kosa kwa Nkurunziza, kwanini isiwe kosa kwa Kagame na wengine?

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) lilipiga kura tarehe 12 Novemba mwaka jana na kupitisha azimio likilaani kile ilichokiita “mauaji, utesaji na ukandamizaji wa haki za binadamu” nchini Burundi. Ufaransa ndio ilitayarisha muswada wa azimio hilo na kuzihimiza nchi 15 wanachama wa baraza hilo kuunga mkono. Hapa inabidi tujiulize iweje azimio kuhusu nchi ya Kiafrika lipigiwe debe na nchi ya Ulaya badala ya Waafrika wenyewe?

Hata hivyo nchi za Kiafrika zikisaidiwa na Urusi zilipinga kipengele kinachotaka Burundi iwekewe vikwazo. Mwishowe azimio likapitishwa bila ya kipengele cha kikwazo. Sasa baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, ikatangazwa kuwa UN itafanya mipango ya kuhamisha baadhi ya askari wake kutoka DRC (Monusco) hadi Burundi. Wazo mbadala likatolewa kuwa badala ya UN kutuma majeshi yake, ni vizuri Umoja wa Afrika (AU) ikafanya kazi hiyo. Ikapendekezwa kuwa majeshi ya Monusco yanaweza yakaunganishwa na majeshi ya AU. Rais Obama wa Marekani akampigia simu Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na wakazungumzia hali ya Burundi.

AU ina sera ya kuwa na vikosi kila kanda barani Afrika. Hivyo, kwa upande wa Afrika Mashariki kuna kile kinachoitwa kikosi cha akiba cha Afrika Mashariki (East African Standby Force). Ni kikosi hiki ndicho kinachofikiriwa kupelekwa Burundi. Uamuzi wa

Page 9: ANNUUR_1214

9 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016Makala

JOSEPH "Jihad Jack" Terrence Thomas ni kijana ambaye aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na Mahakama Kuu ya Australia tarehe 31 Machi, 2006 kwa tuhuma za ugaidi. Ilidaiwa kuwa Joseph Thomas aliwahi kupewa pesa na magaidi wa Al Qaida na kwamba pesa hizo ilikuwa ni mtaji wa kuanzisha kundi la Al Qaida Australia. Joseph Terrence Thomas anatajwa kuwa raia wa kwanza wa Australia kushitakiwa na kuhukumiwa kwa sheria yenye utata ya kupambana na ugaidi (anti-terrorism laws) iliyowekwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 Marekani.

Ukitizama kwa undani na kuchambua tuhuma na baadae hukumu, unaweza kusema kuwa kama ni kosa, basi ilikuwa ni Thomas kusilimu na kuoa mke kutoka Pakistan.

Baada kusilimu na kuoa Mpakistan, Thomas aliondoka Australia Machi 2001 kwenda kwa wakweze,

Joseph "Jihad Jack"Sheikh Msellem Ali

Mhanga kama Herero, LumumbaUhuru anasema ana lengo muhimuLipi zaidi ya kutumikia ‘mabeberu?’

Na Omar Msangi kabla hata ya shambulio la Septemba 11. Kwa kutumia makachero na jeshi la Pakistan, Thomas alikamatwa huko huko akawekwa ndani ambapo aliteswa na kuandikishwa maelezo ya kukiri kuwa yeye ni Al Qaida na alikuwa akipokea pesa kutoka Al Qaida. Hata hivyo, baadae Mahakama ya Rufaa ilifutilia kwa mbali adhabu hiyo na kumuona hana hatia kwa sababu kilichodaiwa kuwa ni ushahidi kilipatikana baada ya Thomas kuteswa sana. Kwa maana nyingine ni kuwa kama ni kukiri, Mr Thomas alikiri kujinusuru kutokana na mateso makali aliyopewa akiwa rumande, mikononi mwa vyombo vya usalama.

Katika kufuatilia kesi ya mdogo wake, Les Terrence Thomas (kaka yake Joseph) anasema kuwa amekumbana na visa vya watu kuteswa bila ya kuwa na hatia au bila ya kuhukumiwa kwa tuhuma zinazowakabili. Amesema, kuna watuhumiwa wengi wa makosa ya ugaidi katika rumande za Melbourne na Sydney ambapo wanapewa

Inaendelea Uk. 10

UGAIDI una mifumo tofauti na sura nyingi, lakini baya zaidi kati yake ni ukatili. Tunaambiwa tuamini kuwa magaidi ni wehu na wakora, wanaozunguka na mabomu, bunduki nzito na mikanda ya milipuko. Ndiyo tunavyoambiwa tuwafikirie. Wengi wao

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidi

Na Andre Vitchek

Januari 22, 2016 'Mtandao wa Kupashana Habari,' na 'Counterpunch'

wana madevu; takriban wote wanaonekana 'kutokea nchi za nje, siyo 'Wazungu, siyo wa Magharibi. Kimsingi ni wapiga wake, wabaka watoto na wateketezaji sanamu za Kiyunani na Kirumi. (Hii ndiyo picha tunayopewa tuwaone kwayo kila anayetajwa kuwa ni gaidi. Ni jitu katili la kutisha.)

Hali halisi ni kuwa, wakati wa Vita Baridi (ushindani wa kiitikadi na tishio la vita kati ya Marekani na Urusi ya kikomunisti) kulikuwa na 'magaidi' wenye muonekano wa Kizungu. Walikuwa ni wanaharakati wakijumuika katika vikundi vya kimapinduzi, nchini Italia na kwingineko Ulaya. Ila ni wakati huu tu ambako tunajifunza kuwa matukio ya kigaidi walioyafanya, kumbe yalibuniwa na kutekelezwa na taasisi za himaya ya Marekani, serikali kadhaa za kupinga mageuzi barani Ulaya na mashirika ya kijasusi. Unakumbuka, nchi za NATO zilikuwa zinalipua

treni katika njia za mahandaki (chini ya ardhi), au kulipua vituo vizima vya treni (kisha kusingizia kuwa ni kazi ya magaidi.)

"Ilibidi ifanyike," ili kuharibu sifa ya wanaharakati, kuhakikisha tu kuwa watu hawapoteza mwelekeo na kupitia kura vyama vya Kikomunisti au vya Ujamaa wa dhati.

Pia kulikuwa na makundi kadhaa ya kigaidi Amerika ya Kusini - makundi ya uamsho wa kimapinduzi yakipigania uhuru na dhidi ya ukandamizaji, zaidi kupinga ukoloni wa Magharibi. Ilibidi wazungukwe, walainishwe, na kama walikuwa madarakani, wapinduliwe.

Lakini magaidi walianza tu kufahamika kwa kiwango kikubwa nchi za Magharibi baada ya kuteketea kwa Urusi na nchi za kikomunisti kwa jumla kupitia maelfu ya njia za kiuchumi, kijeshi na propaganda, na kufumba na kufumbua nchi za Magharibi

zikajikuta ziko kweupe, wako pekee yao bila mtu wa kupigana naye. Kwa njia moja au nyingine ilihisi kuwa zinahitaji kuhalalisha matendo yao ya kutisha barani Afrika, Mashariki ya Kati, Amerika ya Kusini na Asia.

Ilikuwa inahitaji adui mwingine mkubwa mwenye nguvu kuhalalisha bajeti zao kubwa sana za kijeshi na kijasusi. Ilikuwa haitoshi kupambana na vigaidi uchwara mia kadhaa katika mapori ya Colombia (FARC), Ireland ya Kaskazini (IRA) au Corsica (harakati ya kujitenga na Ufaransa). Ilibidi kuwa na kitu kikubwa, kitu kinacholingana na 'himaya ya uovu' inayotisha, kama ya Urusi.

Ni kwa kiasi kikubwa, kukosekana kwa tishio hili kulikuwa kunawakosesha usingizi (Wazungu mabeberu wa Ulaya na Marekani). Walitaka tishio pekee, siyo

Inaendelea Uk. 10

JIHAD Jack akiwa na mkewe.

Page 10: ANNUUR_1214

10 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

Makala

Inaendelea Uk. 11

Joseph "Jihad Jack"Sheikh Msellem Ali

Inatoka Uk. 9mateso ya kutisha wakati hawajahukumiwa kwa kosa lolote. Na wote hao ni Waislamu au watu kutoka Mashariki ya Kati na Asia.

Wiki iliyopita gazeti hili lilichapisha kisa cha kijana Saidi Michael Danieli alivyoteswa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola, yote kutaka akiri kuwa yeye ni gaidi/mshiriki wa jinai ya Sitakishari. Hata baada ya kuthibitisha kuwa hana hatia, bado polisi wakambambika tuhuma ya kukutwa na ‘sare’ walizodai ni za Al Shabaab. Katika kusimulia yaliyomsibu, Saidi Michael Danieli aligusia pia majaaliwa ya mwezake, marehemu sasa, aliyemtaja kwa jina moja la Khalfan ambaye aliteswa na kufariki.

“Aliponiona tu, alieleza kuwa amenitaja ili nifike nimuone katika hali aliyokuwa nayo, hata akifa ifahamike kuwa amekufa akiwa mikononi mwa Polisi. Kweli jamaa alifariki usiku wa saa nane, siku ile ile niliyoingia mimi.”

Anaelezea Saidi Michael Sheikh Msellem Ali Msellem

Danieli, akisimulia yaliyomkuta kijana Khalfan hadi mauti kumfika akiwa mikononi mwa polisi.

Haya anayosimulia Saidi, yaliyomkuta Khalfan na yale ya Joseph "Jihad Jack" Terrence Thomas, ndiyo majaaliwa ya Waislamu dunia nzima hivi sasa.

Andre Vltchek ameandika Makala aliyoipa jina “How the West Creates Terrorism”. Humo anaeleza na kuchambua jinsi nchi za Marekani na Ulaya zilivyounda zimwi hili ugaidi, zinavyotengeneza magaidi kila uchao na kuwatumia katika kufanikisha agenda zao za kibeberu. Andre Vltchek anasema, mabeberu wa Marekani na Ulaya, ndio magaidi wa kweli na wabaya wasio na mfanowe. Ni waharibifu, wanyonyaji,

waporaji na wauwaji. Sasa ili wasizomewe katika kuvamia, kuuwa na kupora, wametengeneza ugaidi bandia wakaupigia propaganda ukakubalika huku wao wakijitangaza kuwa ni wasamaria wema wanaoitakia mema dunia kwa kupambana na magaidi (walio waunda wenyewe). Kwa hiyo, wanapovamia Iraq na kuuwa watu kinyama Fallujah, inaonekana wanapambana na ‘magaidi’ sio wananchi wasio na hatia wa Fallujah. Hivyo hivyo wakifanya unyama wao Libya, Syria, Somalia na kila mahali wanapotaka mali kama walivyoshiriki kumuuwa Patrice Lumumba.

Hii ndiyo kawaida yao toka wakipambana na walichodai kuwa ni ‘evil’ Soviet “threat”, walipokuwa wakipambana na Fidel Castro na mikakati yao kwa ujumla katika uporaji Amerika ya Kusini kupitia “Operation Mongoose” na “Operation Northwoods” ambapo waliunda “Latin American ‘terror’ groups”.

“Ili kuufanya Uislamu uwe adui mwenye hadhi, Himaya

Inaendelea Uk. 11

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidiInatoka Uk. 9ushindani wa malengo ya usawa na maadili kimataifa.

Hivyo nchi za Magharibi (zikabuni na) zikaambatanisha ugaidi na Uislamu. Uislamu ambao ni moja ya tamaduni kubwa zaidi duniani, kwa lengo la kuwatisha mama wa nyumbani wa matabaka ya wenye fedha mitaa ya miji mikubwa ya nchi za Magharibi! Na zaidi ya hapo ilibidi Uislamu uzungukwe udhibitiwe kwani Uislamu ulikuwa na mwelekeo wa wazi mno wa Ujamaa na ulikuwa na amani kupita kiasi (kwa hiyo uvurugwe kuondoa Amani katika nchi za Waislamu na badala yake kupandikiza machafuko na mauwaji).

Wakati huo katika historia, viongozi wote muhimu wa mwelekeo wa siasa usio wa kidini na wa Kijamaa katika nchi za Kiislamu, kama Iran, Indonesia na Misri, walipinduliwa na nchi za Magharibi, urithi

wao kutemewa mate, au walipigwa tu marufuku.

Lakini hiyo haikutosha kwa nchi za Magharibi!

Ili kuufanya Uislamu uwe adui mwenye hadhi, Himaya (ya Marekani) ilibidi kwanza ielekeze hisia katika siasa kali na kuharibu asasi na taasisi za Kiislamu zisizohesabika. Halafu kuunda hizo mpya, hivyo kuzipatia mafunzo, kutoa silaha na fedha, ili

ziweze kuonekana zinatisha vya kutosha.

Bila shaka kuna sababu moja zaidi muhimu kwa 'ugaidi,' hasa 'ugaidi; (unaodaiwa kuwa) wa Kiislamu, kuwa ni wa lazima kwa kuhakikisha uendelevu wa fikra za nchi za Magharibi, utofauti wake na udhibiti wa dunia nzima: Inahalalisha dhana ya nchi za Magharibi ya ubora wake

usiopingika kitamaduni na kimaadili. (Kwa maana kuwa ukishaupaka matope Uislamu kuwa ni dini ya kigaidi na magaidi, unaacha Umagharibi (Ukristo?) kuwa ndio utamaduni bora na ustaarabu wenye maadili yanayofaa.)

Hivi ndivyo inavyofanya kazi

Kwa karne nyingi, nchi za Magharibi zimekuwa zikijitifua katika uwanda wa dunia kama dubu lenye kiu ya damu. Licha ya propaganda inayowafaa inayotolewa na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi vyenye njia za kuonekana kote duniani, ilikuwa inaanza kueleweka kuwa Himaya inabaka, kuua na kusomba mali kila sehemu duniani. Miongo michache mingine na dunia ingeziona nchi za Magharibi kama ugonjwa mbaya wenye simu. Hali kama hiyo ilibidi izuiliwe kwa njia zozote zile!

Hivyo wanaitikadi na wapropaganda wa Himaya wakaja na wazo jipya tena

WANAJESHI wa Kenya wakiwa wamebeba majeneza yenye miili ya wenzao waliuawa nchini Somalia hivi karibuni.

Page 11: ANNUUR_1214

11 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 201611 AN-NUURMakala

Inatoka Uk. 10 Joseph 'Jihad Jack' Sheikh Msellem Ali(ya Marekani) ilibidi kwanza ielekeze hisia katika siasa kali na kuharibu asasi na taasisi za Kiislamu zisizohesabika. Halafu kuunda hizo mpya, hivyo kuzipatia mafunzo, kutoa silaha na fedha, ili ziweze kuonekana zinatisha vya kutosha.”

Kuna mambo kadhaa ya kuchanganua hapa kutokana na maneno haya ya Andre Vltchek. Moja ni kuwa magaidi na ugaidi kama ulivyo katika sura yake ya sasa, ni jambo lililobuniwa na mabeberu. Ni mkakati na program inayoratibiwa na mabeberu wa Ulaya na Marekani katika kufanikisha malengo yao. Nitafafanua zaidi mbele. Pili, serikali yetu na serikali zote duniani, kadiri zitakavyojitahidi kutumia nguvu na mbinu mbalimbali kupambana na magaidi, magaidi wataendelea kuwepo na kunona zaidi. Ugaidi utakoma pale tu ambapo waliouanzisha watakapoutema kama walivyoacha ukoloni wa kuvamia na kukalia nchi Inaendelea Uk. 12

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidiInatoka Uk. 10la kufana: Na tuunde kitu ambacho kinaonekana na hata kusemwa vibaya zaidi yetu sisi, hivyo tunaweza kuitangazia dunia kuwa sisi bado ndiyo watulivu na wasikivu zaidi kitamaduni duniani kote!

Na tutengeze mlengwa halisi: na tupigane na kitu tunachokitengeneza wenyewe (ugaidi) - tupigane nacho katika jina la uhuru na demokrasia!

Ndivyo jinsi kizazi kipya, kizazi kipya cha 'ugaidi' kilivyozaliwa. Na kinaishi! Kinadunda vyema! Kinazaliana kama salamanda za Capek.

Ugaidi wa nchi za MagharibiUgaidi wa nchi

za Magharibi huwa hauzungumziwi, licha ya kuwa katika hali yake mbaya zaidi inapiga dunia bila kuvuta pumzi na kwa muda mrefu, maiti kwa mamia ya mamilioni zikijazana kila mahali.

WAKOLONI wa Kijerumani wakiwanyonga wananchi wa kabila laHerero nchini Namibia.

Hata vikosi vya nje na vya kukodiwa vya Himaya, kama Mujahiddin, Al Qaida au ISIS. haviwezi kufikia ukatili ambao umefikiwa mara kwa mara na wakubwa wao wa Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Ujerumani au Marekani. Ni kweli wanajitahidi sasa kuwafikia wakufunzi wao na wafadhili wao, lakini kimsingi ni kuwa hawana uwezo wa kufikia viwango vyao vya ukaliti na uuaji.

Inahitaji "utamaduni wa Magharibi" kuua watu takriban milioni 10 katika eneo moja tu la kijiografia, kwa muda mfupi tu vile! (Inaashiria kwa mfano Namibia, wakati ukoloni wa Ujerumani ulipozima uasi dhidi ya uvamizi wa kikoloni, ukateketeza kabila kubwa la wa-Herero ukawaua karibu wote. Kule Namibia alipelekwa jemadari wa cheo cha jenerali ndiyo maana alitenda atakavyo, hapa Tanganyika (Ujerumani ya Afrika Mashariki, Deutsch Ostafrika) aliletwa kamanda wa cheo cha Meja, yaani

Von Wissman, hivyo akawa mwangalifu zaidi asifikishwe mahakama ya kijeshi akivuka mpaka).

Hivyo ugaudi halisi ni upi, na ni kwa vipi ambako ISIS na wengine wangefuata uongozi wake? Wanasema kuwa ISIS inakata vichwa vya mateka wao. Ni vibaya

sana. Lakini ni nani mwalimu wao? Kwa karne nyingi, himaya za Ulaya zilikuwa zinaua, kutesa, kubaka na kukata viungo watu katika mabara yote duniani. Ambao hawakufanya hivyo moja kwa moja 'waliwekeza' katika kuunda vikundi vya misafara

Inaendelea Uk. 12

MAUAJI ya kutisha yaliyofanywa na Wajerumani nchini Namibia wakati wa ukoloni.

wakaja na ukoloni mambo leo.

Tatu, wengi wa wanaokamatwa kwa tuhuma za ugaidi, ni watu

waliotumbukizwa kwa ujinga wakidhani wanatumikia agenda njema kumbe wanamtumikia beberu kafiri. Na vijana wengi wa Kiislamu

wanaingia katika kundi hili. Hivi sasa kuna vijana wengi wa Kiislamu hufanya mijadala kuhusu habari za

Page 12: ANNUUR_1214

12 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 201612 Makala

Jinsi nchi za Magharibi zinavyotengeneza ugaidiInatoka Uk. 11ya wakoloni, au kupeleka watu kujiunga na vikosi vya maangamizi.

Mfalme Leopold II na mawakala wake waliua takriban watu milioni 10 katika eneo la Afrika ya Kati na Magharibi, ambayo sasa inajulikana kama Congo. Alikuwa akiwinda watu kama wanyama, akiwalazimisha kufanya kazi katika mashamba yake ya mpira. Kama alidhani hawajazi mapipa yake kwa haraka inavyotakiwa, hakusita kuwakata mikono, au kuwachoma moto wakazi wote wa vijiji katika vibanda vyao, wakiwa hai.

Wahanga milioni 10 walipotea. Milioni 10! Na hiyo haikutokea katika wakati wa mbali uliopita, katika "zama za giza," lakini katika karne ya 20 chini ya utawala unaoitwa ni ufalme wa kikatiba, na pia hujitangaza kuwa ni wa kidemokrasia. Inafananaje na ugaidi ambao unatawala katika maeneo yanayokaliwa na ISIS? Tulinganishe idadi na kiwango cha ukatili!

Na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo tangu 1995 imepoteza tena kiasi cha watu milioni 10 katika mzunguko wa kikatili wa vita na mauaji, ulioanzishwa

na mawakala wa nchi za Magharibi, Rwanda na Uganda (ona kiongezeo cha filamu ya mwandishi huyu ya Kamari ya Rwanda).

Wajerumani walifanya mauaji ya kimbari katika eneo la kusini magharibi ya Afrika, iitwayo sasa Namibia. Kabila la wa-Herero liliteketezwa, au kufikia kiasi cha asilimia 90

ya kabila lote. Watu kwanza walitolewa kwenye ardhi yao na kwenye nyumba zao na kutupwa katika jangwa. Kama walinusurika, vikundi vya wauaji waliowatangulia wa-Nazi vilifuata, vikitumia risasi na njia nyingine za mauaji ya halaiki. Majaribio ya kitiba juu ya binadamu yalifanywa, kuthibitisha

ubora wa taifa la Ujerumani na Wazungu kwa jumla.

Hawa walikuwa ni raia wa kawaida, watu ambao kosa pekee walilokuwa nalo ni kuwa hawakuwa Wazungu, na walikuwa wamekalia ardhi ambayo inavamiwa na kutwaliwa na Wazungu hao. Wapiganaji wa Taliban na hata ISIS hawajawahi kufikia hapo!

Hadi sasa, serikali ya Namibia inadai kurudishwa kwa vichwa visivyohesabika vya watu wa nchi hiyo, vichwa ambavyo vilikatwa na kupelekwa Chuo Kikuu cha Freiburg na mahospitali kadhaa jijini Berlin, kwa majaribio ya kitiba.

Hebu fikiria, ISIS ikate vichwa vya maelfu ya Wazungu, ili kufanya majaribio ya kitiba kuthibitisha kuwa Waarabu ni bora kuliko Wazungu. Ni jambo ambalo haliwezi kufikirika! (Ila jambo moja usisahau ISIS ni mtoto wa Wazungu hao hao anayekula na kupumua kwa pesa na silaha za Wazungu hao.)

(Makala hii: How the West Creates Terrorism, imeandikwa na Andre Vltchek na kutafsiriwa kwa Kiswahili na Anil Kija)

Joseph "Jihad Jack"Sheikh Msellem Ali

Inatoka Uk. 11‘Jihad’, Al Shabaab, Makafiri Vs Waislamu, na mambo kama hayo, kupitia Wasapu, Facebook na vitu kama hivyo, na wengine kufikia hatua ya kuhamasishana kufanya jinai kwa hoja ya kupambana na makafiri. Ukitafuta mzizi wa yote haya ni kutumbukizwa kijinga katika kile alichosema Andre Vltchek kwamba:

“In order to make Islam a worthy enemy, the Empire had to first radicalize and pervert countless Muslim movements and organizations, then create the new ones, consequently training, arming and financing them, so they could really look frightening enough.”

Anachotufahamisha Andre Vltchek ni baada ya mabeberu kumaliza vita baridi na Mrusi na baada ya kufanikisha mikakati ya ‘Mongoose’ na

‘Northwoods’, hivi sasa wapo kwa Waislamu. Wanaunda vikundi vya kigaidi katika nchi za Kiislamu kupitia mitaala ya kuwatia katika ‘siasa kali’ na ‘imani kali’, kisha huwapa mafunzo ya kigaidi, silaha na kuwawezesha kipesa na kuwatumia kwa mambo yao. Kijana akiona ‘Al Shabaab net au Jihad.com’ anaamini kuwa huu ni mtandao wa wana-Jihad na akisoma mjadala unaoendelea pale, huona hawa ndio Waislamu, ndio Mujahidina naye hujimwaga. Wengine wakishajuana huanzisha ‘Darsa Duara’ lao katika Wasapu, wanajipa majina kama AK-47 na vitu kama hivyo. Sasa hawa unaweza kusikia mmoja kadakwa na vyombo vya

Inaendelea Uk. 15

WANAWAKE wa kabila la Herero nchini Namibia.

WANANCHI wa kabila la Herero nchini Namibia.

Page 13: ANNUUR_1214

13 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016Makala

“ANAYEMFUATIA kwa ujasiri na msimamo alikuwa Salmin Awadh Salmini.

Kwa hakika CCM imeondokewa na majemadari, ambao kama kuna kuonana, hivi sasa wanaulizana ya ‘mitaa ya Barzakh’, sio tena ya ‘Kisiwandui!’

Na hapo ndipo yalipo mazingatio kwa kila Muislamu.

Kwamba, tunaweza kukataa kutoa serikali kwa ‘staili’ ya Jecha Salim Jecha, lakini hatuna ubavu wa kukataa kutolewa roho zetu na kuchukuliwa uhai wetu muda unapofika.”

Ni majira ya saa 11 Alfajiri nafungua simu yangu napata ujumbe ulioanza na:

“Innaa Lillahi Wainnaa Ilayhi Rajiuun. Asha Bakari hatunaye tena. Ameshatangulia mbele ya haki. Waarifu na wengine.” Ujumbe huo ukitokea Dubai.

Naam Alhamdulillah Mwenyeenzi Mungu ampokee na amsamehe mja wake huyo. Amin.

Asubuhi ilipofika kila unapopita, taarifa zimeshasambaa na kauli unayoisikia katika vinywa vya watu ni hii “Nakwambieni nchi hii haipatikani kwa karatasi sisi tumepindua labda na nyie mpindue….hatutoi hatutoi hatutoi, wenye madaraka ni sie.”

Ni kauli ya Bi Asha Bakari wakati wa uhai wake ni kauli iliyompa umaarufu mkubwa katika siasa za Zanzibar ambayo imemalizia maisha yake.

“Sisi ndio wenye madaraka. Nawaambia tena jamaa zangu, wallaahi, wallaahi, wameshindwa kutawala 1995 hawatawali tena maisha yao yote na narudia tena na siogopi kusema. Serikali hii ni ya kimapinduzi si ya mchezo, hawawezi, hawawezi kutupindua…hatuwezi kukabidhi serikali kwa njia ya vikaratasi (kura)”.

Nchi haitolewi kwa ‘kura’, haya kuitisha uchaguzi kusumbua watu na kupoteza gharama zote hizo ya nini?

Hata hivyo, mtu unaweza kusema, hiyo ni kauli ya Asha Bakari si ya CCM wala Serikali ya Mapinduzi Zanziar. Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba aliyofanya Jecha ni kutafsiri kivitendo aliyosema Asha Bakari! Lakini maadhali CCM imemuunga mkono Jecha, ina maana kuwa huo ndio msimamo wa CCM na SMZ yake. Na kwa maana hiyo, hata tangazo la kurudia uchaguzi halina maana yoyote.

Vyovyote iwavyo, hayo ndiyo matamshi yaliompa umaarufu mkubwa Asha Bakari Makame na kuonekana jasiri hapa Zanzibar akijulikana zaidi kwa jina la ‘Mtama’ ambalo alipewa

Safari ni nzito!Tumkumbuke Asha kwa DuaAungana na Awadh BarzakhJecha anakazia tu kauli zao

Na Mwandishi Maalum, Zanzibar

na Baba yake Mzazi Bwana Bakari Makame. Anayemfuatia kwa ujasiri na msimamo wa namna hiyo alikuwa Salmin Awadh Salmini ambaye, naye alishatangulia mbele za haki. Kwa hakika CCM imeondokewa na majemadari, ambao kama kuna kuonana na kujuliana hali, hivi sasa wanaulizana ya ‘mitaa ya Barzakh’, sio tena ya “Mapinduziii!” Salmin Awadh alifikia mahali pa kuona kuwa hata kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ni kama wanasogelea katika kutaka kutoa nchi kwa ‘vikaratasi’ akataka kupeleka hoja binafsi Barazani, serikali hiyo ivunjiliwe kwa mbali. Bahati mbaya ‘jambo halikuwa’ mpaka akaondoka yeye.

Na hapo ndipo yalipo mazingatio kwa kila Muislamu na kwa hakika kwa kila binadamu. Kwamba, tunaweza kukataa kutoa serikali kwa

‘staili’ ya Jecha Salim Jecha, lakini hatuna ubavu wa kukataa kutolewa roho zetu na kuchukuliwa uhai wetu muda unapofika!

Asha Bakari (Allah amrehemu) alikuwa ni Mwanamke aliyekuwa mstari wa mbele katika kukihami na kukitetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uhai wake wote. Lakini kwa bahati mbaya, Chama iwe CCM, CUF au chochote, hakina uwezo wa kutetea uhai wa wanachama wake! Amekitumikia chama kwa muda mrefu na kukamata nyadhifa mbali mbali ndani ya chama hicho huku akiamini dhana ya uhafidhina ambayo ni viongozi wachache waliobaki ndani ya Chama Cha Mapinduzi waliobakia kutetea msimamo huo wa uhafidhina. Hao ni wale ambao hawataki demokrasia kufuata mkondo

wake na kung’ang’ania dhana ya mapinduzi daima zaidi kuliko uhalisia au lengo la Mapinduzi yenyewe ambalo limeasisiwa na aliyekuwa Rais wa Kwanza Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.

Lengo la Mapinduzi ni kukataa ubaguzi wa aina yeyote na kuwepo usawa kwa wananchi wote katika kupata huduma za kijamii kama elimu, afya na huduma nyenginezo zitolewazo na serikali.

Bi Asha pamoja na kuwa akipingwa na wengi kutokana na msimamo wake, lakini hakuvunjika moyo hata kidogo. Licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali, hasa kwa kuwa akitokea katika Kijiji Cha Mtambwe kijiji ambacho pia alichozaliwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.

“Mimi mwanangu Mtama, amejiunga na CCM muda mrefu tokea wakati wa ASP na anakipenda chama na anamaliza uhai wake akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM lakini sio lazima na mimi nimfuate yeye, mimi CUF na yeye ni CCM na hilo alilitambua awali”, alisema Mzee Bakari ambaye ni Baba yake Bi Asha.

Ujasiri wa Bi Asha na msimamo wake thabiti ndio uliompa umaarufu mkubwa ndani ya siasa za Zanzibar ambapo alionekana kama ni turufu muhimu mbele ya wapinzani wao wa CUF kwa kuwa anatokea Kisiwani Pemba. Lakini jengine kutoka kijiji kimoja na Maalim pia ilionekana kama ni nguvu kubwa ambayo ikitumika wazi wazi katika kumdhoofisha Maalim Seif kutokana na kutoka ndani ya kijiji na familia zilizo na mahusiano ya karibu.

Asha Bakari alizaliwa Disemba 25, 949 na kupata elimu yake ya msingi katika Shule ya Utaani mwaka 1957 hadi 1964 na kujiunga na Sekondari katika shule ya Fidel Castro mwaka 1965 hadi mwaka 1968. Baadae alijiunga na Chuo cha Uhazili mwaka 1970 kwa mwaka mmoja akisomea masomo ya sekretari katika ngazi ya cheti na kuongeza na miaka mengine miwili katika chuo hicho kwa kuendelea na kozi hiyo hiyo kwa ngazi ya Advence mwaka 1978 hadi 1979 na baadae kujiunga na kozi ya Diploma ya Political Science and Management mwaka 1984 hadi mwaka 1985 nchini Bulgeria.

Katika nafasi ambayo ameshikilia ndani ya serikali ni pamoja na uwalimu kuanzia mwaka 1969 hadi mwaka 1970, sekretari wa Wizara ya Elimu kuanzia mwaka 1970 hadi mwaka 1974, Sekretari wa Wizara ya Habari mwaka 1974 hadi mwaka 1980, na kisha

MAREHEMU Asha Bakari Makame.

Inaendelea Uk. 14

MAREHEMU Salmin Awadh Salmin

Page 14: ANNUUR_1214

14 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

MAKALA/MASHAIRI

Inatoka Uk. 7

Safari ni nzito!kuwa sekretari wa Baraza la Wawakilishi ambapo aliitumikia mwaka 1983 hadi 1985.

Baadae akateuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kuanzia mwaka 1985 hadi mwaka 1990 wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Usafiri na Mawasiliano mnamo mwaka 1990 hadi mwaka 1995 na baadae kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii, Vijana na Wanawake, mnamo mwaka 1995 hadi mwaka 2000 alikuwa Waziri wa Wanawake na Watoto na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi akitokea kwenye jumuiya za wanawake wa CCM Zanzibar.

Mbali na nafasi hizo za serikali, lakini Bi Asha alikuwa mstari wa mbele katika kukiendeleza Chama ambapo mnamo mwaka 1964 alikuwa ni Mjumbe wa Vijana wa Paunia kupitia Chama Cha ASP na baadae mwaka 1972 alijiunga na Afro Shirazi Youth League hadi hapo mwaka 1977 vyama vya TANU na ASP vilipoungana na kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) yeye akawa miongoni mwa wajumbe wa mwanzo wa chama hicho.

Tokea hapo mwaka 1978 kwenye jumuiya ya wanawake wa CCM kisha kuwa mjumbe wa JUWATA na baadae kuwa mjumbe wa Wazazi wa chama hicho cha CCM mwaka 1980 na akaanza kukamata nyadhifa nyengine mbali mbali ndani ya chama ikiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na 1992 hadi 2010 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) mwaka 2007 hadi anamaliza uhai wake yeye ni Makamo Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Katika uhai wake Bi Asha amaekabiliwa na changamoto mbali mbali lakini zaidi kwa wapinzani wake wa Chama Cha Wananchi (CUF) ambao alikuwa ni mpinzani wao mkubwa katika siasa. Bi Asha ambaye maarufu anajulikana kwa msimamo wake wa maneno alitokuwa akiyatoa mara kadhaa kuhusiana na Maalim Seif kushika dola yeye ni miongoni mwa wahafidhina wachache waliokuwa wakipinga na kusema kwamba “Hii ni nchi ya kimapinduzi na haitoki kwa karatasi”.

Matamshi yake hayo yakimaanisha hata mkipiga kura hamuwezi kushinda

“Labda na nyie mfanye Mapinduzi mpindue kama tulivyopindua lakini hatutoi..hatutoi…hatutoi”. Hizo ndo kauli zake ndani ya Baraza la Wawakilishi na hata katika Bunge Maalumu la Katiba.

Mbali ya ujasiri wake huo wa kusimamia uhafidhina, lakini Bi Asha pia alikuwa ni mtetezi mzuri wa maslahi ya Zanzibar kwa muda mrefu amekuwa akisimamia na kutetea suala la Zanzibar katika Muungano lakini kilichokuwa kikimponza na kuitwa msaliti ni kushikilia uhafidhina na umapinduzi tu.

Inawezekana wengi wakamuona Bi Asha ni mtu aliyekuwa anasimamia dhana isiyokubalika na wengi katika ulimwengu huu wa sasa, lakini ni miongoni mwa wanawake wachache ambao wameweza kusimama imara na kutetea kile wanachokiamini katika maisha yao.

Bi Asha kwenye Umapinduzi hajawahi kukengeuka hata siku moja. Ni miongoni mwa wengine walioipigia debe serikali ya umoja wa kitaifa kwa wakati ule ingawa kwa baadae akaungana na wenzake na kutaka kura ya maoni ya kuivunja kutokana na dhana ile ya uhafidhina na umapinduzi

kuwa mbele. Badhi ya wakati alikuwa na uzalendo na kuipenda nchi yake na linapokuja suala la kuitetea Zanzibar kwenye Muungano yeye ilikuwa kama anajifunga kibwebwe na kuanza ‘kucharura’ khasa akipaza sauti yake akisema na kutetea haki za Zanzibar na wakati mwengine aliungana na back benchers kwa kuikosoa serikali na kutaka kamati teule ziundwe katika kuwafichua wenye kufanya ubadhirifu ndani ya serikali.

Ukiacha ya kwenye siasa pia alikuwa ni mcheshi, mtu mwenye kupenda watu hodari na ni mzungumzaji mzuri na daima akipenda kutania muda wote. Binafsi nimejuana naye kwa muda mrefu akiniita ‘Mwanangu’ na kunitaka nimwite ‘Mama’ kutokana na mahusiano na urafiki wake na Baba yangu tokea wakiwa wadogo ambapo walicheza pamoja.

Kama ilivyo kwa binaadamu wengine hawakosi kuwa na makosa na kasoro katika maisha yake lakini tusahau yale mabaya yake na tumkumbuke kwa mema yake. Ni binaadamu kinachotakiwa sasa ni kumuombea katika safari yake hiyo nzito ya kurejea kwa Mola wake akielekea maisha ya Barzakh.

Karume Shujaa

Inatoka Uk. 6Abeid Karume na Maalim Seif Shariff Hamad, wakishauriwa na wazee wa CCM na CUF, wakatutoa huko katika shimo la moto kama walivyokuwa Aus na Khazraj. Lakini mbona tunataka kurejea tena kule tulipotoka ambapo tulikubaliana kutoka huko kabisa kwa Kusameheana, Kusahau yaliopita na Kusonga mbele na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa? Tukazika tofauti za kisiasa na kusahau yale yaliotangulia. Inakuwaje leo hali ya Zanzibar inaendelezwa kubaki katika khofu, woga na kiza kizito?

Ni wajibu wa viongozi kuyasoma haya na kuyafikiri huku wakijua wana dhima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Wana dhamana kubwa mbele ya jamii na wale watu waliowapa dhamana ya kuongoza. Ni jukumu lao, wasilikimbie. Waikumbuke siku ambayo wataitwa na kuulizwa na Mola wao juu ya uchunga wao. Kila mmoja ni mchunga na kila mchunga ataulizwa. Waliyasimamia vipi haya yasitokee? Wataulizwa ilikuwaje wakaamua na kutoa fursa kwa baadhi ya watu kuyatenda haya? Viongozi waliopo madarakani wana wajibu wa kuhakikisha usalama wa nchi na watu wake. Na njia ya kuleta usalama sio kuruhusu au kuweka mazingira yanayopelekea wananchi kufanyiwa yale waliyofanyiwa wanawake wa Wete, Mkoani na Micheweni.

Ningependa nisisitize kuwa, muhimu hapa sio kukumbushana machungu, lakini kutanabahishana kwamba kuna makosa tukifanya, yanaleta balaa, maafa na athari mbaya kwa wananchi. Katika Aya nilizozinukuu mwanzo, Waislamu wanatakiwa kurejea historia juu ya hali mbaya ya uhasama iliyokuwa baina ya Aus na Khazraj. Lakini Uislamu ukawaletea neema ya udugu na upendo wa dhati wakaepukana na balaa la

chuki, visasi na kuuwana. Tunaposoma aya hizi Wazanzibari, tukiwa katika vyama vyetu vya siasa vya CUF na CCM na tukiwa katika visiwa vyetu vya Unguja na Pemba, tujihisi kama walivyokuwa Aus na Khazraji. Allah (SWT) kwa huruma yake na Rehma zake akatuletea Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa kusimama kwa ubinadamu wetu na Uzanzibari wetu. Sasa hofu yangu ni kuwa, tusipojali na kuenzi neema hii, tunachotafuta ni balaa kuliko niliyoigusia kwa kifupi sana. Je, tunalitaka hilo?

Tukisimama na kutambua na kuheshimiana, awali ya yote, kama binadamu, pili kama Waislamu na Wakristo na tatu kama Wazanzibari na Watanzania, hatuwezi kuthubutu kufanyiana yale aliyofanyiwa yule mama wa Micheweni na kichanga chake!

Rafiki yangu mmoja alinambia Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Karume siku moja alisema ameingilia mlango mbaya lakini amejua kutafuta mlango mazuri wa kutokea. Kwa maana alipoingia tu madarakani, yakafanyika mauaji hayo ya Januari 26/27, 2001. Lakini ameiaga Ikulu kwa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa na kumaliza chuki na uhasama wa kisiasa.

Ni matarajio yangu, na kwa hakika ya wengi kuwa, maadhali Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein ameingia Ikulu na mguu wa kulia, kwa kukabidhiwa nchi ikiwa salama, atatuepusha na balaa linalotunyemelea.

Hii ndiyo dua yetu, na tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe ujasiri atuvushe salama, yasije kutokea tena yale yaliyowakuta akina mama na mabinti wa Pemba ambayo yakisimuliwa, hata ukiwa na roho ngumu kama jiwe au chuma, utajikuta ukitokwa na machozi.

DKT. Ali Mohamed Shein. Maalim Seif Sharif Hamad.

P.O. Box 90042, +255 713 586 186 au 713 455 255Dar es Salaam, Tanzania

NAFASI YA MAFUNZO YA USHONAJIChuo cha ushonaji Tanzania Islamic Centre kinawatangazia wanawake wote kuwa kinatoa mafunzo ya ushonaji (tailoring) na kudarizi (Embroidering) kwa ada nafuu sana. Chuo kina maadili na mazingira mazuri ya kujifunzia. Kipo Msikiti wa Kichangani, Magomeni Mapipa.Fomu zinapatikana hapa chuoni. Wanawake wote mnakaribishwa katika mafunzo.Wasiliana kwa simu No 0713586186 na 0713 455 255

Wabillah Tawfiq

Tanzania Islamic CentreManispaa ya Kinondoni

Page 15: ANNUUR_1214

15 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016Makala

Joseph 'Jihad Jack' Sheikh Msellem AliInatoka Uk. 11

dola na kisha kufuatia msururu wa kukamatwa kwa kila aliyekuwa katika mtandao huo. Hao ndio tunasema kuwa wamenaswa kwa ujinga kwa sababu, kwanza wanayojadili ukiyaweka katika mizani, yanakwenda kinyume kabisa na mafundisho yenyewe ya Uislamu. Pili, hayawezi kutatua matatizo ya Waisamu yaliyopo na tatu ni kuwa wanajadili mambo ya hatari bila hata ya kujua kuwa kwa utaalamu uliopo, wanayoandika si siri, kila wanachoandika kinasomwa na wengine bila wao kujua, wakiwepo polisi, wanausalama wa ndani na nje.

Ugaidi unavyowasaidia mbeberu

Mfalme Leopold II na wenzake, waliangamiza takribani Waafrika milioni 10 wa Congo hivi sasa, watu wakisakwa kama wanyama wa porini ili wakafanye kazi katika mashamba ya mpira (rubber plantations) ya mabeberu. Ndiyo yaliyojiri pia Namibia ambapo Wajerumani waliangamiza kabila la Herero kwa mauwaji ya halaiki (mass killing) ambapo manusura walitimuliwa katika majumba yao na mashamba yao wakakimbilia jangwani kuwapisha Wazungu. Mpaka leo mashamba yao yanatumiwa na Wazungu.

“Hawa walikuwa raia wasio na hatia ambao kama ni kosa, basi kosa lao lilikuwa kutokuwa Wazungu, halafu wakazaliwa katika ardhi safi kwa kilimo na yenye madini.”

Watu wa makabila ya Herero na Namaqua, Namibia, wakati huo German South-West Africa, walipinga ukoloni na ubeberu wa Ujerumani katika nchi yao. Kutokana na hilo wakatangaziwa ugaidi na uasi. Adhabu yao ikawa kuteswa na kuuliwa kwa kunyongwa, kupigwa risasi, kufanywa panya wa majaribio na kufukuzwa katika miji na vijiji vyao, wengi wakafa jangwani kwa kiu na njaa.

Zaidi ya kuwafanyisha kazi kitumwa, huku wakiwa wamewafunga minyororo, serikali ya Wazungu wa Ujerumani, haikutosheka, lakini ikawa inaleta wataalamu wake wa vyuo vikuu na hospitali

wakitaka kufanya utafiti, vinachukuliwa viungo vya watu wa Namibia. Ripoti ya Umoja wa Mataifa (United Nations' Whitaker Report) ya mwaka 1985, inataja mauwaji ya watu wa makabila ya Herero na Nama uliofanywa na Ujerumani, kwamba ndio mauwaji mabaya na ya mwanzo ya Kimbari katika karne ya 20. Hivi leo serikali ya Namibia inajaribu kuibana serikali ya Ujerumani irudishiwe mafuvu ya watu wake (Waafrika) waliokatwa vichwa na Wazungu vikapelekwa katika maabara ya Chuo Kikuu cha Freiburg na hospitali mbalimbali za Berlin kufanyia majaribio ya kisayansi!

Waliyofanya Wajerumani, ndiyo hayo hayo waliyofanya Uingereza, Ufaransa na Marekani katika ubeberu wao duniani. Leo mabeberu hao hao wanatuundia ISIS na akina Jihad John, ili kufunika unyama wao wanaoendelea kufanya katika nchi mbalimbali. (Tafuta: “Exposing Lies of the Empire”.)

Katika zama zile Ujerumani inaangamiza watu wa Namibia, inawezekana mji wa pili kutoka mahali wanapouliwa watu, wasijue kinachowapata wenzao. Leo ukifanya jambo dogo tu, dakika hiyo hiyo ulimwengu utajua na kupiga kelele. Sasa mabeberu hawawezi tena kufanya unyama kama ule wa Namibia bila ya kuzomewa. Walichofanya ni kuunda jinamizi la ugaidi. Ukitizama historia, yaliyowakuta watu makabila ya Herero na Namaqua, Namibia (German South-West Africa), ndiyo yaliyowakuta wananchi wa Fallujah, Iraq wakipinga uvamizi na uporaji wa Marekani. Lakini ulimwengu haukuwalilia wananchi wa Fallujah kwa sababu mabeberu walikwishatangaza kuwa wanapambana na magaidi. Katika Fallujah askari wa Marekani walilipua na kuuwa mpaka wagonjwa hospitalini na watu waliokuwa misikitini kisha wakazuiya chakula kuingia. Lakini nani wa kuisema

Marekani wakati inapambana na magaidi!!! Ugaidi kwa hakika limekuwa blanketi zito kabisa la kufunika mauwaji na uporaji wa mabeberu wa Kizungu ambao umekuwa ukifanyika toka wakati wa Mfalme Leopold II na wenzake.

Hivi karibuni Kenya ilitumbukia katika msiba mzito. Idadi kubwa ya askari wake walio Somalia waliuliwa na wapiganaji wa Al Shabaab. Akitoa salamu zake za rambi rambi, Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa jeshi la Kenya litaendelea kuwepo Somalia mpaka lengo lao la kwenda kule litimie.

Mtu utajiuliza, kwa lengo lipi Kenya ilikwenda Somalia zaidi ya kutumikia lengo la mabeberu? Kama ni uadui, Wasomali/Al Shabaab haikuwahi kuwa na uadui na Kenya. Ilikuwa na uadui na Marekani iliyopindua serikali yao ya Umoja wa Mahakama za Kiislamu na kuweka vibaraka.

Kama katika miaka ya 1800s mpaka mwanzoni mwa miaka ya 1990s wapo baadhi yetu walitumiwa na mabeberu wa Kizungu kuhilikisha kabila la Herero kule Namibia, wakatumiwa kukata vichwa vya wenzetu kuvipleka katika maabara za Ujerumani, wakatumiwa kuwauwa wazalendo kama Patrice Lumumba, leo tutakuwa na tofauti gani iwapo tunatumiwa na mabeberu wale wale wa Kizungu kutesa watu wetu na wengine kuwapeleka kufa Somalia kutumikia agenda ya Mmarekani?

WAJERUMANI waliwafunga minyororo kabila la Herero nchini Namibia kipindi cha ukoloni.

WANANCHI wa kabila la Herero waliokimbia makazi yao.

Page 16: ANNUUR_1214

16 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016Safu ya Ben Rijal

KAMA nilivyowahi kueleza huko nyuma kuwa Zanzibar ilikuwa ni kituo muhimu cha kueneza dini ya Kiislamu na wanafunzi waliokuwa wanaenda kusoma visiwani Zanzibar wakitoka katika maeneo ya Afrika ya Mashariki na wengine wakitokea katika maeneo ya Afrika ya Kati na Kusini mwa Afrika na walimu wao wengi walikuwa wenyeji ambao walielimika vya kutosha. Aidha, katika nyakati mbalimbali walitokea walimu kutoka Yemen, Misri, na Saudi Arabia.

Baadhi ya wasomi wa visiwani waliona kiu chao bado hakijakatika kwa maji walioyapata visiwani, kwa hio wakafunga safari kwenda Misri na Saudi Arabia kusoma kisha wakarudi kusomesha visiwani.

Jina litakustaajabisha, lakini hivyo Sheikhe ndivyo alivyokuwa akijinasibisha kwa jina lake. Sheikhe huyu alijinasibisha kuwa ni mkazi wa kutoka Lindi, asili ya kabila lake ni Mmakonde na ndivyo alivyokuwa akijulikana.

Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde alizaliwa katika mwaka wa 1307 AH (1890) akasoma kwao Lindi kwa Masheikhe wa huko kisha akapelekwa visiwani Zanzibar

Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde-12KATIKA safu yetu hii ya Masheikhe waliopita, wasomaji wamekuwa na kiu kutaka kujuwa juu ya Masheikhe waliopita wa Tanganyika, kwani watakuwa wa Tanganyika kwa wakati ambao ninawazungumza Masheikhe waliopita huko nyuma. Bahati mbaya kwa upande wa Tanganyika hakuna juhudi zilizofanyika kuwafanyia utafiti Msheikhe waliopita hata nilipowasiliana na Sheikhe wangu wa Tanga tarehe za Mwa hapo Tanga, alionambia kuwa hakuna maandishi ya kutosha ya Masheikhe hata wa karibuni kina Hemed bin Juma. Makala hii itamgusia kwa ufupi Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde aliotokea Lindi kusoma Unguja na kumalizikia na kusomesha

katika mji mkuu wake Unguja kwa Sheikh Issa bin Ahmad Msunjini. Hapa utaona kapelekwa kwa mtu mwenye asili ya visiwa vya Comoro.

Lindi na Msumbiji sio mbali na Wamakonde wengi wanatokea Msumbiji na watu wa visiwa vya Comoro katika nyakati tafauti kutokana na misukosuko ya maisha ya kuingia ukame na mabalaa mengine ya kimaumbile, walihama visiwa hivyo na kuhamia Msumbiji, Durban Afrika ya Kusini na visiwa vya Zanzibar. Watu wa maeneo ya Lindi, Mtawara, visiwa vya Comoro na Zanzibar walikuwa na maingiliano makubwa.

Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde alipelekwa kwa Sheikh Issa bin Ahmad Msunjini ambaye Sheikhe huyu ndio alioujenga Msikiti ujulikanao Msikiti Mabati uliopo katika mtaa wa Kisiwandui katika mwaka wa 1326 (1908). Sheikh Issa alimlea Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde na kumsomesha na kumpeleka kwa kila mwalimu ambaye atafaidika. Kwa hiyo ilivyokuwa yeye Sheikh Issa akisoma kwa gwiji wa elimu wa siku hizo Sheikh Abdalla Bakathir

naye Sheikh Said bin Abdalla Lindy alifaidika na kusoma kwa gwiji huyo.

Sheikh Said alitokea kuwa na hima ya kusoma na hakuwa mwenye kupoteza wakati wake zaidi ya kusoma na mlezi wake alipokabidhiwa, hakumfanya mtoto wa kumlea awe kazi yake kutumika na kumtuma, bali alitokea kumpenda zaidi hata ya wanawe na kwa hio hakuwa anampa kazi yoyote ile, iwe ya kuteka maji, kuchanja kuni au kazi zozote zile za nyumbani zaidi ya kumtaka kumuona kuwa ameelimika vya kutosha.

Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde aliichukua fursa hiyo vilivyo kwani alichukua ahadi alivyotoka nyumbani kuwa atasoma mwisho wa kipawa chake ahakikishe kuwa atalipata lengo alilolikusudia. Alikuwa akifwatana na mlezi wake katika kudarasisha.

Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde alikuwa na fani ya kuzungumza na kusomesha na akipenda kupita njia za mkato na kufanya ufupisho na hayo yakiwavutia vijana wenye kunyanyukia kupenda kuhudhuria

darsa zake. Alikuwa akisomesha Msikiti uliopo Vuga wa Maalim Murad ambapo vijana wa mji ndio maeneo waliokuwa wakiishi.

Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde katika mwaka wa 1372 AH (1953) aliomba ruksa ya kurudi Tanganyika nako huko ni kwao akasomeshe. Wajue wale ambao hawakumuona kama kweli alielimika. Hapo akawataka ruksa waliompokea kuwa wakati wa kurudi nyumbani umefika na Mtu ni kwao na walimpa ruksa hiyo kwa kuelewa lisilo budi hutendwa. Ni wakati wake umefika kurudi nyumbani.

Wengine husema Mtu ni kwao ugeni sio kitu chema, lakini Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde hakuyatamka hayo, ila alihisi ni vyema kurudi Tanganyika kwenda kuifanya kazi inayohitajika. Kwa hiyo katika mwaka huo wa 1372 AH (1953) alihamia Tabora na kupokewa na wenyeji wa hapo na kufanya kazi kubwa iliyostahiki kwa kusomesha watu wa rika mbalimbali.

Alipokuwa anadarasisha Tabora, wale ambao wakisema Kiarabu kama asili ya lugha yao, walikuja kufahamu kuwa wanahitajia kwenda kusoma kwake, chembelecho maneno ya vijana, kwani Sheikhe alikuwa akikisema Kiarabu kimbele kinyuma, ikimaanisha akikizungumza kwa njia za kisomi sio cha mtu aliozaliwa na lugha yake.

Kuhamia kwake Tabora kulimchukua miaka 4 kabla ya kufariki. Alifariki tarehe 19 Mfungo Tisa 1376 AH (January 1957) na kuwacha pengo kwani hapo Tabora wenyeji walifaidika naye vya kutosha. Tunamuomba Mola atupe juhudi kama alizokuwa nazo Sheikh Said Abdalla Lindy Mmakonde, Ameen.

WAZIRI Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameungana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku na Bernad Membe, kueleza kushangazwa kwake na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo.

Dkt. Salim amesema, hata Jumuiya za kimatifa nazo zilishtushwa na uamuzi huo.

Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo, baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana, ambapo siku chache zilizopita, Jecha ametangaza kuwa uchaguzi huo utarudiwa Machi 20 mwaka huu.

Dk. Salim amesema, kutokana na hali hiyo, kinachotakiwa hivi sasa ni

Zanzibar isipuuze ushauri wa wakongwehaki itendeke kwa kila kila upande kwa kukaa pamoja na kutafuta suluhisho la kudumu kwani Tanzania haijazoea migogoro ya siasa ambayo si jambo jema katika sura ya kimataifa.

Dk. Salim alitoa kauli yake wakati alipozungumza na MTANZANIA nyumbani kwake, Msasani, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Dk. Salim ambaye ana sifa ya kuwa msuluhishi wa kimataifa na ambaye amewahi kuwa Katibu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika OAU, (sasa AU), alisema kitendo cha kufutwa uchaguzi wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiwa wametoa ripoti za kuusifia.

Alisema, kufutwa na sasa tarehe Dk. Salim Ahmed Salim.MHE. Bernad Membe.Inaendelea Uk. 17

Dk. Salim, Membe, Butiku, wana funzo Tuache ubinafsi kwa maslahi ya wengi

Page 17: ANNUUR_1214

17 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

MAKALA/TANGAZ0

Inawatanganzia Waislam wote kuwa imeandaa safari ya Hijja mwaka 2016 sawa na mwaka 1437 Hijria kwa Dola US$ 3,555

Kutakuwa na punguzo la asilimia 16% kuanzia muda huu mpaka Feb 29/2016. Itakuwa Dola $2986 tu.

Kuanzia mwezi Machi 01-2016 mpaka Juni 12-2016 kutakuwa na punguzo la asilimia 6% sawa na Dola $3,341 tu.

MAMBO YATAKAYOGHARAMIWA

1. Semina za Hija, 2. Huduma za afya na kuchinja 3.Airport Charge na ticket za Ndege 4.Nyumba Makkah na Madina 5.Irham na Kuchinja kwa ajili ya Tama-tuu 6.Chakula wakati wote 7.Usafiri na ziara Makkah na Madina 8.Mahema Mina na Arafa.UMRA MWEZI WA RAMADHANI ITAKUWA NI DOLA US $1995

Fomu zinapatikana sehemu zifuatazo:-1.Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es Salaam Mtaa wa Dosi na Mkadini nyumba Namba 26 mkabala na Showroom ya magari Tell. 0713 730 444, 0773 804 101 ,0785 930 444 au 0773 930 444.2. Ofisi ya Ahlu Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484 982, 0777 413 987.3. Abubakr Maulana wa Markaz Kiwalani Dar es Salaam, Tel: 0784 453 8384. Abdallah Salehe Mazrui (Hoko) Dar es Salaam, Tel: 0715 724 444 5. Abdallah Hafidh Mazrui, Wete Pemba Tel: 0777 482 6656. Mohammed Hafidh Mazrui Mkoani Pemba 0777 456 9117. Sheikh Daud Khamis Shekha Tel: 0777 679 6928. Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) 0777 417 736WAHI KULIPIA1. Ofisi ya Ahlul Daawa Dar es salaam Tel: 0713 730444, 0773

804101,0785 930444.2. Ofisi ya Ahlul Daawa Zanzibar Rahaleo Tel: 0777 484982,

0777 413 987.Maalim Seif Humoud Hamed (Kijichi Zanzibar) Tel: 0777 417 736

TANBIH(a) Atakaemaliza taratibu zote mwanzo ndie

atakayeshughulikiwa mwanzo(b) Ili uwemo katika fungu la kwanza unatakiwa umalize

taratibu zote kabla ya punguzo (c) Kumbuka kikundi cha Ahlul Daawa kwa bei nafuu kuliko

wote na huduma kuliko wengi.Wabillah Tawfiq

Ahlu Daawa Hajj and Travel Agency

Zanzibar isipuuze ushauri wa wakongweInatoka Uk. 16ya kurejewa ikiwa imeshatangazwa, kumeibua sintofahamu kubwa katika nchi kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa, kwa uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini sasa bado suala hili halieleweki.

Hata hivyo Dk. Salim, alisema hadhani suala la kufutwa uchaguzi lilikuwa ni la mtu mmoja, kwamba hadhani ni la Jecha peke yake na kusema huo sio mustakabali mzuri visiwani humo.

Alisema, Zanzibar ni nchi ndogo lakini ina historia kubwa kisiasa, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika kufanyika kutatua mgogoro uliopo kwa maslahi ya Watanzania kwa ujumla.

Aliwataka Viongozi katika suala la Zanzibar haki itendeke na waache ushabiki wa vyama na kwamba, wote waweke ushabiki pembeni na watatue mgogoro huo kwa mustakabali wa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

Alishauri pande zote ziendelee kukutana hadi suluhu ya pamoja ipatikane, japo viongozi kadhaa wameshakutana na kufanya mazungumzo bila kupata suluhu.

Dk. Salim alitoa tahadhari kwamba nchi ipo katika hali mbaya na Watanzania hatujazoea na kwamba, suala la Zanzibar likiendelea linaweza kuzaa matatizo makubwa katika Taifa.

Akizungumzia kuhusu vitendo vya ubaguzi yakiwamo mabango yaliyokuwa yameandikwa ujumbe wa kibaguzi kwa maandishi makubwa katika sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, zilizoadhimishwa Januari 12, Dk. Salim alisema ameshangazwa na hali hiyo.

Alisema kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kubeba bango hilo hadharani kimeitia doa na ni aibu kwa Zanzibar na Tanzania wakati inafahamika kuwa suala la ubaguzi lilimalizika tangu mwaka 1964.

Aliongeza kuwa, kitendo kile ni jambo la kufedhehesha na halistahili kupewa nafasi hata kidogo.

Alisema wakianza kubagua, watakaoathirika wengi ni watoto wa viongozi na kwamba, ubaguzi huo ni ujinga na unaudhi.

Alisema kitendo cha wana-CCM kubeba bango hilo kinaonyesha wazi kuwa wameishiwa hoja kwa sababu suala la Hizbu lilikufa tangu mwaka 1964.

Hata hivyo, Dk. Salim alihoji kuwa iweje wanachama wabebe mabango yanayochochea ubaguzi katika sherehe za Mapinduzi na waliachwaje kufanya hivyo, hali ya kuwa viongozi walikuwapo na waliona.

Alisema, kama kuna mtu yeyote anaona hilo ni sawa, basi huyo ni sawa na kusema kafilisika kabisa.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2005 katika harakati za kuwania nafasi ya Urais ndani ya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu, Dk. Salim alidaiwa waziwazi na baadhi ya wana kambi wa CCM kuwa hakustahili kuwania kiti hicho kwa kuwa yeye alikuwa ni mwanachama wa Hizbu, chama

kilichokuwa kinaongoza serikali ya Zanzibar kabla ya Mapinduzi na kwamba ana asili ya Uarabu.

Kauli hizo za kibaguzi zilimuumiza sana Dk. Salim, ambaye wakati huo alikuwa akikubalika.

Mapema kabisa baada ya kufutwa uchaguzi wa Zanzibar, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, aliitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufanya kazi kwa kuzingatia katiba na sheria za nchi na kuacha kutanguliza mbele maslahi binafsi ya kisiasa.

Akizungumza na vyombo vya habari, Mzee Butiku, alisema amekerwa na tabia ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kusitisha uchaguzi na kushindwa kuwatangazia wananchi kiongozi wao waliomchagua, huku ikishindwa pia kuheshimu matakwa ya wananchi waliopiga kura katika visiwa vya Zanzibar.

Mzee Butiku bila kumung’unya maneno, aliitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kufanya kazi kwa weledi na kuheshimu maamuzi ya wananchi, badala ya kutanguliza mbele maslahi binafsi ya kisiasa, jambo ambalo inaweza kusababisha machafuko na umwagaji wa damu visiwani humo.

Pia aliwataka wananchi wa Zanzibar kutokubali kurudia tena upigaji wa kura, hadi hapo yatakapotolewa maelezo ya kuridhisha na wahusika waliosababisha uchaguzi huo kufutwa na watakaobainika kuharibu waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha Mzee Butiku aliwataka viongozi kuheshimu sheria na katiba ya nchi na kwamba, chama ambacho kinadhani kimeshindwa katika uchaguzi huo kikubali matokeo badala ya kuifanya Zanzibar ni mali ya chama fulani.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kadhalika alinukuliwa na vyombo vya habari akitoa maelezo ya kupinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar, akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu, kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe alionyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani.

Alisema, kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote badala ya yale yaliyobainika kuwa na matatizo.

Katika hatua za kujaribu kutatua mgogoro huo, inasemekana kuwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif tayari wameshakaa vikao tisa Ikulu Zanzibar, pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour na Dk. Amani Karume lakini bila kupatikana mafanikio, wala maelezo ya kina juu ya mazungumzo hayo.

Aidha, Rais John Magufuli naye ameshakutana na pande hizo mbili kwa nyakati tofauti, ambapo Maalim Seif alimtaka kuwa kinara wa kusuluhisha mzozo uliopo, lakini tangu wakati huo haonekani

kutilia mkazo.Tayari Katibu huyo Mkuu wa

CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Membe alifafanua zaidi kwamba, kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia na kwamba, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake.

Kwamba imeshangaza katika majimbo yote, hakuna hata moja lililofanya vizuri na hapo ndipo wengi wanapopata wasiwasi.

Aidha alisema haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk. Shein na Maalim Seif.

Alisema kama kuna mwanasiasa wanaodhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanafanya makosa makubwa kwani umoja uliopo Bara na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo.

Kwamba tatizo ambalo linaweza kuhatarisha usalama Zanzibar,

linaweza kusababisha matatizo katika Muungano hivyo wahusika wasikae kimya na kuangalia kitakachotokea.

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imesema haitashiriki uchaguzi huo.

Wakati matokeo ya uchaguzi yakiwa yametangazwa katika majimbo 32 na baadhi ya wagombea kukabidhiwa vyeti vya ushindi na matokeo kubandikwa vituoni huku matokeo hayo yakiendelea kutangazwa kwenye kituo kikuu cha kutangazia matokeo katika Hoteli ya Bwawani, ghafla zoezi hilo likasitishwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha, pale alipojitokeza kwenye kituo cha televisheni cha Taifa na kutangaza kufutwa kabisa uchaguzi Oktoba 28 mwaka jana.

Hatua hiyo ilipingwa vikali na CUF, vyama mbalimbali vya wanasheria na kushangaza Jumuia za kimataifa na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi.

Page 18: ANNUUR_1214

18 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

MAKALA

Kwanini mabeberu wanachangamkia sana Burundi?kupeleka wanajeshi 5,000 huko Burundi ulichukuliwa mnamo Disemba 2015 na Baraza la Amani na Usalama la AU. Nkurunziza alipewa muda wa kukubaliana na uamuzi huu, lakini akaupinga na kusema majeshi yake yatapambana na “kikosi cha uvamizi” cha AU.

Aghlabu tunapoongelea majeshi ya UN au ya AU, kisichotajwa ni kuwa majeshi hayo huwa yanafadhiliwa na mataifa makubwa kama Marekani. Bendera ni ya UN au AU na askari ni Waafrika, lakini Marekani na Ulaya wanatoa kila kitu kuanzia silaha hadi sare na posho.

Wakati AU imechachamaa kupeleka majeshi ya kulinda amani ili kuzuia mauaji nchini Burundi, wachunguzi wanahoji iweje AU hiyo hiyo ilikaa kimya wakati majeshi ya Ufaransa yalipoishambulia Ivory Coast mwaka 2010. Halafu kuna uvamizi wa Libya (2011), Mali (2012) na CAR (2013) uliofanywa na majeshi ya kigeni. Je yalikuwa wapi hayo majeshi ya AU ya

Inatoka Uk. 8

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusinikulinda amani?

Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza katika jumuiya ya EAC kuunga mkono upelekwaji wa majeshi ya kulinda amani nchini Burundi (Maprobu). Ingawa Nkurunzinza amesema hii itakuwa ni sawa na uvamizi wa nchi yake na majeshi

ya kigeni, Waziri Mahiga amesema lengo litakuwa ni kuwalinda raia na wala si kupambana na jeshi la nchi au na serikali yake. Suala hili lilizungumzwa na Mahiga alipokutana na mwenyekiti wa AU, Bi Nkosazana Dlamini-Zuma mjini Durban na mjini Addis Ababa. Baadae likatolewa tamko rasmi likimuomba Nkurunzinza kushirikiana na Maprobu. Mpaka sasa haieleweki ni nchi zipi zitatoa majeshi yake kuchangia hii Maprobu. Burundi yenyewe imetuma majeshi yake kulinda ‘amani’ huko Somalia na DR Congo. Sasa nayo inatakiwa ilindwe amani yake.

Ni vizuri tukajiuliza, kwanini mataifa makubwa yanachangamkia sana utumiaji wa majeshi ya usalama nchini Burundi? Suali hili linagusiwa na Charles Kambanda, mwanasheria kutoka Rwanda anayeishi Marekani. Aliwahi kuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Rwanda. Hivi karibuni akihojiwa na Idhaa ya Redio KPFA alisema mgogoro wa Burundi ni wa kisiasa na kiini chake ni maliasili ya nchi hiyo inayogombaniwa na mataifa makuu ulimwenguni.

Kambanda amesema, nchi za kibeberu zimenuia kuudhoofisha utawala wa Burundi ili iweze kuudhibiti. Kwa njia hii nchi hizi zitakuwa na nafasi ya kunyonya utajiri na maliasili za Burundi.

Anasema kinachofanyika nchini Burundi si tofauti na DRC, kwa vile kuna makampuni ya kimataifa yanayogombania maliasili

katika maeneo haya. Mbinu wanazotumia ni kutengeneza mazingira ili kurahisisha uporaji wa maliasili unaofanywa na makampuni ya kimataifa kupitia madalali wao wa kienyeji. Hii ndio hali ilivyo katika maeneo ya DRC Mashariki ambayo inapakana na Burundi. Na Burundi nayo inazalisha asilimia sita ya madini ya nikeli (nickel) duniani. Tayari makampuni ya kigeni yamewarubuni baadhi ya viongozi wa upinzani ambao ndio watakaokuwa madalali.

Kambanda anasema hii ndio sababu ya kimsingi inayozifanya nchi za Marekani na Ulaya kuhimiza na kuwezesha kile wanachokiita “kikosi cha kulinda amani” huko Burundi. Wamefaulu kuuza wazo hilo kwa AU ingawa EAC na SADC haziko tayari kuunga mkono. Badala yake zinataka yafanyike mazungumzo ili kufikia maridhiano.

Naye mwandishi Gearóid Ó Colmáin anasema Marekani na wenzake wa Ulaya wana mkakati wa kuidhibiti Burundi kwa kumuondoa Nkurunziza na kuuweka utawala utakaolinda maslahi yao. Hivi ndivyo ubeberu umekuwa ukifanya katika nchi nyingi za Afrika, Asia, Amerika Kusini na Mashariki ya Kati. Anasema mkakati huu umekuwa ukiendeshwa kupitia vyombo vya habari tangu 2005. Lengo lao ni kuchora upya mipaka ya nchi za Maziwa Makuu kama wanavyofanya katika nchi za Kiarabu. Katika nchi hizo mataifa ya kibeberu yalichora upya mipaka ya nchi na kuwatawaza wafalme vibaraka chini ya kile kinachoitwa makubaliano ya Simon-Picot. Hii ilifanyika baada ya Vita Kuu ya Kwanza na ingali inaendelea hadi leo.

Si ajabu, kwani hivi karibuni ilitangazwa kuwa mjumbe wa serikali ya Marekani anayeshughulikia Kanda ya Maziwa Makuu anatembelea Burundi. Kisha atafika Dar es Salaam, Rwanda, DRC na Addis Ababa. Akiwa mjini Addis atahudhuria mkutano wa kilele wa AU pamoja na wajumbe wenzake kutoka Marekani. Wanachokitafuta ni nini?

(0713-562181 [email protected])

RAIS Piere Nkurunzinza

TBC ni kuingilia uhuru wa habariInatoka Uk. 20zaidi.

Hata hivyo wakazi wengi wa jiji la Dar es Salaam wamesikitishwa na kutofurahishwa na hatua hiyo tofauti na alivyodai Nape, kwani walisema kitendo cha serikali kuingilia chombo cha habari na kuweka maamuzi yake ni kuingilia uhuru wa vyombo vya habari kwa mujibu wa sheria na vile vile kuzuia uhuru wa wananchi kupata habari.

Kurwa mkazi wa Mbagala alisema kutorushwa mijada ya Bunge moja kwa moja, kunatoa fursa kwa watendaji wa TBC kuhariri sehemu kubwa ya mijadala hiyo, hasa sehemu ambazo haiifurahishi serikali na kuruhusu ile ambayo kwao wanaona inawafaa, jambo ambalo ni sawa na kuwakatili wananchi.

Maide Omar, mkazi wa Manzese yeye alikwenda mbali zaidi na kuhoji kama TBC ni mali ya viongozi, ni mali ya serikali au mali ni ya umma wa Watanzania?.

Alihoji inakuwaje televisheni ya Taifa iwe na wasaa mrefu wa kurusha moja kwa moja hewani harusi ya mtu kwa maslahi ya familia Fulani, lakini ikose muda

wa kurushwa moja kwa moja vikao vya Bunge, jambo ambalo lina maslahi kwa umma.

Hemed Diwani mkazi wa Kimara, alisema kuwa kwa jinsi TBC inavyendesha vipindi vyake, haifahamiki kama ni mali ya walipa kodi Watanzania na kama inaendeshwa kwa ruzuku inayotokana na kodi za wananchi wote.

“Kwa jinsi inavyoendeshwa na aina ya vipindi inavyovirusha, imekuwa kama ni mali ya watendaji wa serikali na chama tawala, wao wanaonekana kama vile ndio wahariri na waamuzi wa kipi kitangazwe na kipi kisitangazwe.

Alisema kwa jinsi inavyofanya kazi, haionekani kama watendaji wake wana uhuru wa kufanya maamuzi yao kwa kuzingatia uhuru wa weledi wa kitaaluma kwa mujibu wa sheria za habari na utangazaji.

Alitolea mfano wa kauli aliyoitoa Nape, na serikali kuwa, wao wanaonekana kuwa mamlaka na uwezo wa kuamua ni kipi kirushwe hewani na kipi kiachwe, bila kujali kuwa waathirika ni wananchi na walipa kodi wanaowafanya TBC wawepo hewani.

Page 19: ANNUUR_1214

19 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 2016

MAKALA

Afande Kova nyuma ya Pazia la UgaidiInatoka Uk. 20

wa Ugaidi bandia nchini jambo lililopelekea kukabiliana na mateso kutokana na uzito wa tuhuma, pasi ya kupelekwa Mahakamani. Ama kwa wale waliopelekwa Mahakamani kesi zao zimekuwa zikipigwa danadana kwa maelezo kuwa upelelezi hauja kamilika huku wakiendelea kusota rumande kutokana na dhamana zao kuzuiliwa.

“Wapo walio kamatwa kwa tuhuma hizo wakaishia kuteswa kisha wakaachiwa wakiwa wameathirika na wengine wakifariki muda mfupi baada ya kutoka rumande na wengine kupoteza wazazi wao kwa mstuko.” Amesema Uts. Awadhi.

Naye Ustadhi Abuu, alisema ipo haja ya kumwandikia Afande Kova, barua ya kumkaribisha uraiani na kumkumbusha kuwa cheo ni dhamana, na kwamba kila wakati mtu anatakiwa kuwa mwangalifu ili kupitia mikono yake na mamlaka yake asije kudhuru watu wasio na hatia.

“Tumkumbushe matukio yote ya kuwabambikia kesi Waislamu na alivyoyashadidia, lakini kwaTawfiq ya Allah (s.w) Waislamu tunashinda kesi na tuhuma hizo hizo bandia kila kukicha kwa kukosa ushahidi na kuamua kuzifuta au kuwaachia baada ya kuwatesa, bila kujua hiyo ni dhulma na ana dhima kubwa kwa Mwenyezi Mungu.” Alisema Ust. Abuu.

Alisema, ni vyema Waislamu wakifanya mchakato wa kumuandikia kitabu maalum ili vizazi vijavyo vimfahamu huku akipendekeza kuwa kitabu hicho kiitwe, ‘Afande Kova dhidi ya

Waislamu nyuma ya Pazia la Ugaidi.’

Alisema, pamoja na kufahamu kuwa Waislamu wanakamatwa na kudhaniwa kuwa ni magaidi, lakini wengi hawafahamu madhila yanayowapata na yanayoendelea kuwapata katika vituo vya Polisi, na zoezi hili lote lilikithiri chini ya ukamanda wa Afande Kova.

Kwa upande wake Sheikh Ally Yaqub amesema wakati Kamanda mstaafu Kova, akisema yapo mambo ambayo hatayasahau katika utumishi wake aelewe pia kuwa wapo Waislamu ambao hawatomsahau. Sasa inagekuwa nyema ikawa wanamkumbuka kwa Kheri.

Naye Ustadhi Hussein Mchomolo, aliye mkazi wa Masasi, ambaye ni muhanga aliyewahi kukamatwa, kuhojiwa kisha kuteswa, anasema yeye ni katika ambao jina la Kova litabaki katika kumbukumbu katika maisha yake yote. Alisema, awali baada ya kukamatwa akiwa kwao Masasi na kufikishwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi (Central Police) Jijini Dar es Salaam, bila kufahamu kosa lake akiwa na wenzake alihusiswa na tukio la ujambazi lililotokea Ikwiriri.

Ust. Mchomolo, alisema awali wakiwa hapo Polisi, ilitolewa amri kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kutoka Mkoani Mtwara, kuwa wasipatiwe chakula kinachotoka kwa ndugu zao.

Wakiwa humo mahabusu, alisema ulifika ugeni wa maafisa wa Jeshi la Polisi akiwemo IGP, Ernest Mangu, walilazimika kuukabili ugeni huo na kulazimisha kuongea nao.

“Mmeelezwa kuwa sisi ni watu

wa Ikwiriri, wakati mnafahamu kuwa tumetoka Mtwara, hivyo tuna matatizo tunataka tuwafikishieni na mtupatie majibu.”

“Hapo ndipo Afande Kova, akaniuliza ‘mnataka majibu sasa hivi au hata kesho? Nikamjibu kuwa yale yatakayo wezekana kujibuwa sasa mtatujibu na yale yatakayo hitaji hadi mkae shura mtajua ni wakati gani mtatujibu.”?

Alisema Ust. Mchomolo, akirejea maongezi yake baada ya kulazimisha kusikilizwa na IGP, mbele ya mwenyeji wake Afande Kova.

Alisema, hatua hiyo ilitoa fursa kwao kuruhusiwa kuongea na Afande Kova, ambapo alimchukua hadi katika ofisi ya RCO na kufanya mahojiano naye kwa ufasaha.

“Baada ya maongezi yetu alimwita Mkuu wa Kituo hicho na kumpa oda kuwa sasa chakula kinacholetwa na ndugu zetu kipokelewe na katika faili letu libadilishwe tuhuma, badala ya kuandikwa kuwa‘wauwaji wa Ikwiriri’ sasa liandikwe kuwa ni watuhumi wa ‘Ugaidi’ toka Mtwara”. Alisema Ust. Mchomolo, na kuongeza kuwa huyo ndiye Afande Kova na tuhuma zinazo wakabilia Waislamu, wakati wa uongozi wake, akidai kwamba alikuwa anaamua tu ni tuhuma ya aina gani apewe Muislamu.

Kufuatia hali hiyo, Ust. Mchomolo, alisema hiyo inatoa fundisho kuwa Waislamu wanao kamatwa na wengine kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za ugaidi ama uvamizi wa vituo vya Polisi, si kweli kuwa wamefanya makosa hayo.

“Mfano hai ni huo, kama ilivyokuwa kwetu, tumekamatwa

kwa tuhuma ya tukio la Ikwiriri, ulipokosekana ushahidi, tukazushiwa ya ugaidi, ina maana yeye ndiye alikuwa anaamua huyu au hawa wapewe tuhuma gani, sisi tulishangaa sana kwa hatua aliyoifanya Afande Kova, fikiria kwanza tulipewa tuhuma za mauaji ya Polisi wa kituo cha Polisi Ikwiriri, lakini akaja akaamua tupewe tuhuma za Ugaidi, huyo ndiye Afande Kova, hakika hatuwezi kumsahau.” Alieleza.

Kwa upande wake Maalim Yasin Khamis, alisema Afande Kova, ni binadamu na huu ni wakati muafaka wa kuelezwa wazi mabaya yake huenda ikamsaidia katika kipindi hiki ambacho yupo nje ya madaraka akatanabahi na kumrejea Muumba wake.

Alisema, pamoja na kuwa yapo matukio mengi, lakini anakumbuka kadhia ya uwanja wa Waislamu Chan’gombe, kuwa hatolisahau kutokana na kipigo kilichowakuta wanawake wa Kiislamu kutoka kwa Polisi, bila huruma wakiwa ndani ya Msikiti wa Markazi Chan’gombe.

“Uzuri wa bahati ni kwamba AfandeKova, yupo hai ni wakati muafaka kuelezwa madhila aliyo wasababishia Waislamu, angekuwa amefariki ingekuwa si sahihi kuyaeleza mabaya yake, lakini sasa aelezwe huenda akatanabahi na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe.”

Alisema Maalim Khamisi na kumalizia kwa kumkaribisha Afande Mstaafu Suleiman Kova katika maisha ya uraiani, waungane katika swala za jamaa Misikitini.

Hofu ya ugaidi inapopunguza uwezo wa kutumia akili UingerezaInatoka Uk. 20familia hiyo.

Kila kitu kilianzia katika zoezi la lugha darasani, mnamo Desemba 7 2015 katika shule moja ya msingi eneo la Lancashire, Kaskazini Mashariki ya Uingereza. Mvulana hiyo aliandika "naishi katika nyumba ya kigaidi" (I live in a terrorist house) badala ya "naishi katika nyumba yenye ngazi" (I live in a terraced house). Bila kuhangaika kuzungumza na mtoto huyo, uongozi wa shule hiyo haraka ukaitahadharisha polisi ambao waliingilia, asubuhi iliyofuata wakafika kwake kumhoji, ilisikika Paris Jumatano Januari 21.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, polisi na Halmashauri ya wilaya hiyo wanakiri kuwa ilikuwa ni "kosa kudhania kuwa mzozo huo unatokana na kosa tu la kuandika neno moja."

Taarifa hiyo inasema "shule hiyo na polisi walichukua hatua

zinazopasa na kwa kuwajibika." Hata hivyo, hakuna taarifa

inayoashiria kuwepo na msingi wa kuwa na wasiwasi imetolewa.

Akiwa amepata mshtuko mkubwa, mtoto huyo hathubutu tena kuandika tangu mkasa huo utokee, kwa mujibu wa familia hiyo.

Binamu yake aliema katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa 'kama mwalimu angekuwa na wasiwasi wa kufuatilia, ni kuhusu uwezo wa kuandika" wa mtoto huyo.

Tangu mwezi Julai mwaka jana, walimu nchini Uingereza wamepewa maelekeo ya kuarifu taasisi husika chochote ambacho kinaashiria siasa kali, kama inavyoainishwa katika sheria ya kupambana na ugaidi.

Matukio kadhaa ya aina hiyo yamefikishwa Baraza Kuu la Waislamu Uingereza ambalo limetoa taarifa kueleza "wasiwasi mkubwa" kuhusu matukio ya aina hiyo.

(Imetafsiriwa kutoka lugha ya Kifaransa na Anil Kija)

Page 20: ANNUUR_1214

20 AN-NUURRABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JAN 29-FEB 4, 201620 MAKALA AN-NUUR

20

Soma gazeti la AN-NUUR

KWA TSH 800/=kila Ijumaa

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

RABBIUTH THAN 1437, IJUMAA JANUARI 29 - FEBRUARI 4, 2016

WAKATI Kamanda Suleiman Kova akitangaza kustaafu utumishi katika Jeshi la Polisi, ametajwa kuingia katika kumbukumbu mbaya dhidi ya umma wa Kiislamu nchini wakati wa utumishi wake. Imeelezwa kuwa, hiyo ni kutokana na miaka ya hivi karibuni Waislamu kuwa wahanga wa tuhuma za ugaidi. Afande Kova amestaafu baada ya kufikia ukomo wa umri wa utumishi wa umma Serikalini, akiwa katika nafasi ya Kamanda wa Kanda Maalum Jijini Dar es Salaam tangu mwezi Juni 2008.

Kabla ya hapo amekuwa katika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi la Polisi nchini.

Afande Kova nyuma ya pazia la ugaidi

KWA kukosea kuandika neno moja kisarufi, mwanafuzi wa umri wa

Hofu ya ugaidi inapopunguza uwezo wa kutumia akili Uingereza

Wakati wewe hutosahau Sitakishari…, Waislamu nao hawatakusahau piaKaribu uraiani, karibu ‘Masjid mtaani’

Na BakariMwakangwale Akitangaza kustaafu kwake, mapema hivi karibuni katika viwanja vya Chuo Cha Maafisa wa Polisi Kurasini, Jijini Dar es Salaam, na kutambulisha Kamanda Simon Siro, kukaimu nafasi yake, aliyataja baadhi ya matukio kuwa kwake yatabaki kuwa ni kumbukumbu kichwani mwake. Kufuatia kauli hiyo ikawasukuma Waislamu nao kutoa maoni yao juu ya utumishi wake hususan kwa umma wa Kiislamu, kwamba ameondoka huku akiacha maumivu makali katika familia za Kiislamu na hawezi kusahaulika kutokana na madhila aliyo wasababishia.

Ustadhi Said Awadhi, alisema chini ya Kamanda Kova, baadhi ya Waislamu wamekuwa ni wahanga

Kamanda mstaafu Suleiman Kova.

Inaendelea Uk. 19

Na Mwandishi Maalum, SaphirNews, Paris

miaka 10 ameshuhudia polisi wakitinga nyumbani kwake kumhoji na kuangalia kompyuta inayotumiwa

na familia hiyo ili kufuatilia walichodai ni mahusiano na vikundi vya kigaidi katika

Inaendelea Uk. 19

SERIKALI imeondoa sehemu ya vipindi vya matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge vilivyokuwa vikirushwa na Televisheniya Taifa –TBC kutoka Dodoma.

Uamuzi huo wa serikali umetangazwa na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye katika kikao cha pili cha mkutano wa 11 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma Jumatano wiki

TBC ni kuingilia uhuru wa habariKuondoa matangazo ya Bunge:

Na Shaban Rajab hii. Kufuatia kauli hiyo

ya serikali, TBC sasa itakuwa ikirusha baadhi tu ya matangazo ya moja kwa moja ya vikao na mijadala ya Bunge, huku sehemu nyingine ya mijadala hiyo ikirekodiwa na kurushwa hewani katika kipindi maalum, ambacho Nape alikitaja kuwa kinaitwa “Leo katika Bunge”.

“Baadhi ya wananchi wameonyesha kuridhishwa na utaratibu huo na wameipongeza serikali.

Lengo la kuondoa baadhi ya vipindi vya moja kwa moja bungeni ni kupunguza gharama za uendeshaji kwa shirika.” Alisema Nape.

Wakati Nape akitoa kauli hiyo ya serikali, wabunge wengi, hasa wale wa vyama vya upinzani walikerwa na kupinga hatua hiyo na kudai hakutajadiliwa chochote bungeni hapo kabla ya kuwekwa sawa suala hilo la kuzuiwa TBC kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Hata hivyo Spika Job

Ndugai, alisema pamoja na kuonekana wabunge hao kutoridhishwa na hatua hiyo, kwa mujibu wa kanuni hawana uwezo wa kuzuia kauli iliyotolewa na serikali.

Bw. Nape alisifu hatua hiyo ya serikali na kusema kuwa kwa kurekodiwa na kutayarishwa matangazo ya vipindi vya mijadala ya Bunge na kurushwa majira ya saa nne usiku, kutatoa fursa kwa watu wengi kupata fursa ya kulitizama Bunge kwa kuwa muda mwingi wa mchana ambao TBC

ilikuwa ikirusha moja kwa moja matangazo ya vikao hivyo, watu wanakua maofisini na katika shughuli zao za uzalishaji hivyo kukosa kuona kinachoendelea Bungeni.

“Watanzania sasa watapata fursa zaidi, hasa wale ambao muda wa kurushwa moja kwa moja vipindi vya mijadala ya Bunge katika muda wa kawaida wanakuwa maofisini kazini au katika shughuli nyingine”. Alieleza Nape Bungeni na kuzua tafrani

Inaendelea Uk. 18