-
ISSN 0856 - 3861 Na. 1183 RAMADHAN 1436, IJUMAA , JUNI 126-JULAI
2, 2015 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=
Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au
facebook:[email protected]
AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST
Kijana Usamah Abdullah Rahim...
Amiminiwa risasi na Polisi, afarikiApachikwa ugaidi kwa kukutwa
na kisu'John' auwa watu 9 kwa risasi wakisaliAambiwa labda alikosea
tu. Sio gaidi
Kamishna Magereza ashikilia uhai wa SheikhHajatoa uamuzi Sheikh
akatibiwe au laBassaleh, Kilemile wataka haki itendeke
Na Bakari Mwakangwale
Hali si shwari Zanzibar
Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha. Soma Uk. 8. Maalim Seif
Sharif Hamad.
WA K AT I m t u h u m i w a wa kesi ya ugaidi Said Amour,
akishindwa kufika Mahakamani kutokana na maradhi gerezani, juhudi
za kupata kibali kwa ajili ya matibabu yake zimekuwa
kitendawili.
Imeelezwa kuwa tangu kuwasilishwa kwa ombi la kupatiwa kibali
kwa ajili ya mtuhumiwa huyo kutibiwa
pia wameshindwa kufika Mahakama ya Kisutu, wiki iliyopita,
kutokana na kuwa wagonjwa.
Mshitakiwa namba 12 Said Amour, ni muda sasa hajahudhuria
Mahakamani
Inaendelea Uk. 2
KAMISHNA Mkuu wa Magereza Jonh Casmir Minja.
katika hospitali maalum, ni mwezi sasa kibali hicho
hakijatolewa.
Mbali na mtuhumiwa huyo, imedaiwa kuwa watuhumiwa wengine wawili
ambao ni mshitakiwa namba 16 Alawi Othman Amir na mshitakiwa namba
18 Amiri Hamisi Juma,
Usamah Abdullah Rahim
Mtume(saw) aliwahimiza Masahaba kuwahijia wenzao wasioweza kwa
ugonjwa au uzee na waliokufa katika Uislamu. Waislamu wengi
wanakufa bila kuhiji wakati waliwahi kupata uwezo wa kuhiji.
Umeshawaokoa wazazi wako na MOTO? Muda unakwisha! Gharama zote kwa
Hijja ni Dola 4,500. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,300. Karibuni Ahlu
Sunna Wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi:
Tanzania Bara: 0765462022;0782804480;
0717224437.Zanzibar:0777468018;0777458075;0777845010.
(14) WASITIRI WAZAZI WAKO!
Seif akataliwa kuingia Barazani Tuhuma nzito kwa Jecha, ZEC CUF
wampa orodha ya maluki
-
2 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015AN-NUUR
S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786Cel: 0784 370 208, 0713 110 148,
0755 260 087 , DSM.
www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]
zetu zipo: Manzese Tip Top
Usangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam
Tahariri/Habari
A M E S E M A k w e l i Mtume (s .a .w) : Lai t i watu
wangeaminiwa kwa madai yao tu, kuna watu wangedai damu na mali za
wengine.
Basi na iwe juu ya mwenye kudai, kuleta ushahidi wa madai
yake.
Kanuni hii ya Uislamu, ndiyo inayojenga msingi w a m w e n e n d
o w a mashitaka na kesi katika mahakama, katika nchi nyingi
zinazoongozwa kwa misingi ya Utawala Bora, Haki na Sheria.
Kuwa mtu atakuwa hana hatia mpaka atakapotiwa hatiani na vyombo
vya kisheria vinavyohusika na kutambulika.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, i n a m t u h u m u
S h e i k h Msellem Ali na wenzake kadhaa kuwa ni magaidi.
N i m wa k a wa p i l i sasa, serikali haijafikisha u s h a h i
d i w a k e mahakamani kuthibitisha madai yake.
Hata hivyo, kwa kipindi chote hicho, watuhumiwa wameendelea
kuteseka gerezani huku familia zao nazo zikiishi katika tabu kwa
kukosa wasimamizi na watafuta Rizki wakuu wa familia.
Hii ni dhulma ya wazi kwa misingi ya Kiislamu, Utawala Bora,
uadilifu na UBINADAMU kwa ujumla.
Ndio pale mafundisho ya Uislamu yakaagiza kuwa, yeyote mwenye
kumtuhumu mtu, basi haraka alete ushahidi kuthibitisha madai
yake.
Na ikatolewa sababu kuwa kwa maumbi le yake mwanadamu, lau
ataaminiwa tu kwa kila analosema, basi kuna watu watadai mpaka damu
ya watu wengine kuwa ni mali na haki yao.
Na ili kuepuka adhabu mbele ya Mwenyezi Mungu hiyo siku ya
Hukumu, ambayo inaanzia mara tu baada ya kutiwa kaburini, Uislamu
ukatoa angalizo
Vigogo wa Serikali wafutarishe familia za Masheikh wa Uamsho
na mwongozo muhimu sana:
Kuwa, ni bora mtu ukosee umwachie huru (usimuadhibu) mtu mkosaji
kwa kukosa ushahidi wa madhubuti, kuliko ufanye kosa la kumwadhibu
mtu asiye na hatia.
Na tunaambiwa Dua ya mwenye kudhulumiwa haina pazia baina yake
na Mungu wake.
Hivi wenye mamlaka na hasa walio Waislamu, a m b a o h i v i s a
s a watakuwa katika Funga ya Ramadhani, wanajisikiaje wakitia nia
ya funga na jioni wakifuturu huku wakijua kuwa kuna Waislamu wenzao
wasio na hatia wapo ndani, wanafunga na kuftari kwa chakula cha
gerezani wakati sio wafungwa!
Wanakosa tarawehe na Qiyamul Lail katika misikiti yao. Wanakosa
kuendesha darsa za Quran katika kipindi hiki cha Shahru Ramadhaan
ladhii unzila fiihi lQuran!
Ule ukarimu na huruma t u n a y o t a k i w a t u w e nayo
wakati wa Funga ya Ramadhani, ipo wapi iwapo tunafutari kwa kila
aina ya viliwa, vitafunwa na v inywewa, l ak in i haitupitikii kuwa
kuna akina mama na watoto ambao huenda hawakupata cha kuftaria kwa
sababu waume zao wapo ndani, sio kama wafungwa, lakini kwa tuhuma
tu!
Maadhali mwenzi wa Ramadhani umeanza, punde tu tutashuhudia
wanasiasa wakipigana vikumbo kuandaa futari, kuanzia za Ikulu,
Wakuu wa Mikoa, waliotangaza nia za Ubunge na Urais, mpaka za
mitaani.
Ni maoni yetu kuwa labda Masheikh wetu wa n g e wa e l i m i s h
a n a kuwashauri viongozi wetu hawa na wale watarajiwa, kuwa badala
ya kuandaa futari za kisiasa zisizo na tija mbele ya Mwenyezi
Mungu (ila kwa tija ya hapa hapa duniani tu), wangepeleka huruma
yao kwa akina mama, watoto na watu wazima wanaoteseka kwa vile
waume zao na vijana wao wanaowategemea wapo ndani. Wapeleke futari
zao za kisasia katika familia hizo.
Wa l i o m a d a r a k a n i w a k i o n y e s h a m f a n o
huo, hapana shaka na waliotangaza nia watafuata nyayo. Na hiyo
itakuwa msaada mkubwa kwa familia za watuhumiwa hao, japo
haitaondoa dhambi ya kuwafunga watu kwa tuhuma tu.
K i d u n i a t u n a w e z a kujifariji kuwa tunafuata sheria
(ya ugaidi), lakini kwa Mwenyezi Mungu, huo hautakuwa utetezi.
Mwenyezi Mungu anajua siri zilizomo katika vifua vyetu mpaka
sababu yenyewe ya kuwatuhumu huo ugaidi, kama ni tuhuma za kweli au
la. Anajua pia nia ya hao wababe waliobuni vita dhidi ya ugaidi ,
wanavyopiga propaganda na namna sisi tulivyotoswa kuitumikia agenda
hiyo (kwa malipo gani?)
Ni juzi tu tumemzika Mzee wetu, Sheikh Issa Shaaban Simba,
ambaye tunaambiwa katika moja ya usia wake aliagiza kuwa akifa
azikwe haraka kama Uislamu unavyoagiza.
Tunajua , kwa watu wema kaburi ni viwanja katika viwanja vya
Peponi. Lakini kwa watu waovu, waliodhulumu nafsi zao, kaburi ni
shimo katika
mashimo ya Moto wa Jahannam.
Wakati tukiwa tumo ndani ya Ibada hii kubwa ya Funga ya
Ramadhani, ni vyema kila mmoja wetu akajihesabu ni kwa namna gani
anafanya maandalizi, ili kaburi lake lije kuwa Bustani katika
Bustani za Peponi.
Lakin i p ia , n i kwa kiwango agani anajitahidi kuepuka yale
ambayo y a t a h e s a b i k a k u w a ni dhulma, iwe ni ya k u wa
f a n y i a we n g i n e au kuifanyia nafsi yake mwenyewe. Kwani
hayo n d i o y a t a m f u n g u l i a milango ya Jahannam mara tu
akiingia kaburini.
Tu m w o m b e A l l a h atutakabalie Funga zetu na Ibada zetu
kwa ujumla. Na atuepushe na kila aina ya dhulma.
Mkuu Magereza ashikilia uhai wa Sheikh SaidInatoka Uk. 1kutokana
na kusumbuliwa na maradhi, ambayo mpaka sasa hayajapatiwa tiba
inayostahili akiwa humo gerezani.
L a k i n i p i a k u n a washitakiwa namba 16 na 18 nao
hawakufika Mahakamani kwani pia ni wagonjwa.
A m e s e m a Wa k i l i wa watuhumiwa hao Abdul-fatah
Abdallah.
Akizungumzia suala la maombi ya kupatiwa kibali kwa ajili ya
kupatiwa rufaa mtuhumiwa namba 12 kwa ajili ya matibabu, Katibu wa
Kamati ya Maafa ya Shura ya Maimamu, Ustadhi Ally Mbaruku, alisema
suala hilo limekwamia kwa Kamishna wa Magereza.
A l i s e m a , k i l a wanapofuatilia wanapewa matumaini kwamba
kibali kinashughulikiwa kulingana na taratibu za Magereza, hata
hivyo alistaajibu kuona suala hilo linalohusu uhai wa mtu kupelekwa
kwa kasi ndogo.
Alisema, awali katika Ofisi hiyo ya Kamishna Mkuu wa Magereza,
waliwasilisha maombi ya aina mbili, kwa nyakati tofauti likiwemo
ombi la kupatiwa kibali cha kupeleka msaada katika gereza hi lo la
Segerea, ambapo ombi hilo lishajibiwa na misaada imeshapelekwa.
Alisema, maombi ya kibali cha matibabu ya Ust. Salumu, ndiyo
yalitangulia ambapo yalipelekwa mwanzoni mwa mwezi wa tano, mwaka
huu na maombi ya kibali cha kupeleka misaada kilipelekwa mwishoni
mwa mwezi huo wa tano.
Hatuelewi taratibu zao zikoje yaani maombi ya kibali cha
matibabu ndio
kilitangulia lakini mpaka sasa hakijatolewa na mtu anazidi
kuathirika kiafya, lakini hiki cha kupeleka msaada kimetoka haraka
wakati barua yake ilikwenda mwisho. Alisema mmoja wa wajumbe wa
Kamati hiyo.
Alisema, mara ya mwisho wal ie lezwa na maof i sa wa Ofisi ya
Kamishna wa Magereza, kuwa wanasubiri ripoti kutoka kwa daktari wa
Magereza ili wafahamishwe kuna wagonjwa wangapi, hata hivyo alisema
hadhani kama hiyo ni hoja ya msingi, kwani suala la Ust. Salumu,
lipo wazi na tatizo lake ni kubwa hata Mahakama, inalijua.
Katika barua hiyo kwa Ofisi ya Kamishna Jenerali w a M a g e r e
z a , y e n y e Kumbukumbu namba 009/KMS/2015, imeeleza hitajio la
Kamati hiyo kupatiwa kibali mtuhumiwa huyo apewe rufaa, ili
wampeleke katika hospitali yoyote kubwa.
Kamati ya Maafa Shura ya Maimamu (T) kwa heshima kubwa kabisa
tunaomba k iba l i i l i ndugu Sa id i , apatiwe rufaa katika
hospitali yoyote kubwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu na kamati
inachukua dhamana ya kul ip ia gharama za matibabu. Imesema sehemu
ya barua hiyo.
Barua hiyo inayoonesha kuwa ilipokelewa Mei 4, 2015, katika
Ofisi hiyo ya Kamishna wa Magereza, imeainisha k u w a S a i d A m
o u r n i mshitakiwa namba 12 katika kesi namba 29/2014, aliyepo
katika gereza la Segerea, ambaye kwa muda mrefu anasumbuliwa na
Korodani (Scrotal Swelling).
Hali ambayo inazidi kuwa tete siku hadi siku, pia wanalalamika
ya kuwa hawapatiwi matibabu ya kina.
Imesema barua hiyo ya Mei 4, 2015, ambayo An nuur, inayo nakala
yake iliyosainiwa na Katibu, Ally Mbaruku.
Kamati ya Maafa, ilifikia hatua ya kuwasilisha ombi hilo kwa
Kamishina wa Magereza, kufuatia watuhumiwa hao kulalamika mbele ya
Hakimu wa Mahakama ya Kisutu, Janet Kaluyenda, kuwa hawapati
matibabu.
Watuhumiwa hao mbele ya Mahakama hiyo, walikwenda mbali zaidi
wakidai kuwa wananyimwa mat ibabu yanayostahi l i kutokana na
Uislamu wao ambapo wa l i wa o m b a Wa i s l a m u kuwachangia i l
i wapate matibabu.
Waislamu wapo tayari kuwasaidia, ndio maana tulipeleka maombi
haraka kwa Kamishna wa Magereza ili atoe kibali cha kuruhusu
akatibiwe katika hospitali kubwa kwa gharama za Waislamu, lakini
bado kuna ugumu ni mwezi sasa toka tupeleke maombi hayo kibali
hakijatoka alisema Ust. Mbaruku.
S a i d A m o u r , n i miongoni mwa Waislamu wanaotuhumiwa na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa makosa ya ugaidi, ambao
waliilalamikia Mahakama ya Kisutu kuwa walifanyiwa vitendo vya
ukatili wakiwa mikoni mwa Jeshi la Polisi, huku yeye (Said Amour )
inadaiwa aliminywa sehemu za siri na kumsababishia uvimbe.
Inaendelea Uk. 3
-
3 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari
Kumpachika Muislamu ukafiri ni ujingaHakuna dhana ya siasa kali
katika UislamuWafafanua Sheikh Kilemile, Doga, BassalehKUMPACHIKA
ukafiri Muislamu mwenzako, ni kielelezo cha ujinga na
jambo lisilokubalika katika Uislamu.
Aidha, Siasa kali au msimamo mkali, ni dhana ngeni katika
Uislamu kwani Dini hii ya haki inasema wazi kuwa ni ya kati na
kati, wema, uadilifu na upole.
Hayo yamebainishwa k a t i k a K o n g a m a n o lililoandaliwa
na Umoja wa Wanazuoni wa Tanzania ( H a y - a t - U l a m a a ) k
wa kushir ikiana na Umoja wa Wanazuoni wa Afrika, ambalo
lilifanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kat ika kongamano hilo, Sheikh Amran Kilemile,
alisema katika Uislamu hakuna kitu kinachoitwa Waislamu wenye
Msimamo Mkali.
Alisema, wamelazimika k u f a n y a K o n g a m a n o hilo kwa
kuwashirikisha Wanazuoni wa Kiislamu kwa lengo la kutoa elimu
kuhusu msamiati Msimamo mkali katika Uislamu na kwamba hakuna kitu
kama hicho katika Uislamu, kwani Uislamu una miongozo yake na
taratibu zake katika kuyaendea mambo yake.
Kutokana na baadhi ya Wais lamu kuwa na elimu ndogo, hupelekea
kuyachukua mambo ya Kiislamu kwa nguvu bila ya kuzama katika mambo
hayo na hii inatokana na ufahamu wao kuwa ni mdogo katika k u ya e
n d e a m a m b o ya Kiislamu. Alisema Sheikh Kilemile.
Alisema, Wanazuoni wa Kiislamu wanawanasihi vijana wa Kiislamu
ambao ndio wanao onekana kuingia zaidi katika mkumbo huo kuwa
makini na mitandao ya kijamii katika kuuendea Uislamu wao kwani
akasema, Uislamu unahitaji ukati na kati na kila jambo lina hatua
yake na utaratibu wake.
Alisema, mitandao ya kijamii ipo na haiepukiki k a t i k a U l i
m we n g u wa s a s a , l a k i n i k wa j i n s i hali ilivyo
sasa, inaweza ikakuingiza katika shari ya kuuangamiza Uislamu na
unaweza ukaitumia vizuri na ikakupeleka katika kheri ya kuuinua
Uislamu.
W e w e k i j a n a w a Kiislamu, huzuiwi kuwa katika mitandao
ya kijamii au kuitumia lakini itumie vizuri ili ilete kheri na
manufaa ikusaidie wewe na uisaidie jamii kwa ujumla. Alisema Shkh.
Kilemile.
A l i s e m a , m a k u n d i hayo yenye mtazamo na dhana ya
msimamo makali,
Na Bakari Mwakangwale
wa m e k u wa n a h a r a k a katika kuyaendea masuala ya dini
na kufikia mahali kuwakufurisha Waislamu wenzao, pale wanapojaribu
kuwakosoa kwa mujibu wa mafundiso ya Qur an.
B i l a y a m i z a n i unamkufurishaje Muislamu mwenzako, huu
ni uchache wa elimu na kuyafahamu mafundisho ya Uislamu, kwa sababu
ukiufahamu Uislamu huwezi kuwa na lugha za kukufurishana. Alisema
Shkh. Kilemile.
Sheikh Kilemile, aliwataka wadau na wanazuoni wa Kiislamu nchini
kushirikiana kukemea dhana ya Msimamo Mkali katika Uislamu kwani ni
jambo ambalo halipo katika Uislamu na katika zama hizi limesambaa
kwa kasi miongoni mwa Waislamu na kuleta sintofahamu.
S h k h K i l e m i l e akisherehesha mada yake akagusia baadhi
ya upotofu unaosambazwa akisema kuwa kuna watu wanadai kusoma elimu
ya shule ni ukafiri, huku wakiwalaz imisha Waislamu wengine
kutosoma na kuachana na elimu hiyo sambamba na kuwakataza Waislamu
kushiriki katika siasa kwamba kufanya hivyo ni ukafiri.
Akasisitiza kuwa huo ni upotofu na ujinga walio nao wanaosambaza
mawazo hayo.
Wakati huo huo, imeelezwa kuwa baadhi ya Waislamu wa m e k u wa
wa k i m b i l i a aya zenye Mutashabiha na
kuacha Muhakama, hivyo kusababisha migongano kwa Waislamu.
Hayo yamebainishwa na Sheikh Muharami Juma Doga, wakati akiongea
na Waislamu katika kongamano hilo ambapo alisema, lau Waislamu
wanashikamana na muhkamat, hakuna sababu ya kufarikiana.
Akasisi t iza kuwa aya mutashabihat, zinahitaji ujuzi, lakini
pia ifahamike kuwa uzito upo katika kufuata aya zilizo wazi ambazo
ndio zimebeba roho ya Dini.
Akisherehesha aya za Qur an na Hadithi za Mtume (s a w), Sheikh
Doga, alisema Uislamu unafundisha kuwa usijilazimishe kufanya jambo
lililo nje ya uwezo wako kwani kufanya hivyo ni hatari kubwa.
Alisema, makundi hayo yamekuwa yanatafuta njia zao za kuyaendea
mambo ya Uislamu katika mazingira ambayo yanahitaji ueledi na ina
le ta p icha kuwa h u e n d a wa n a m a l e n g o yao
waliyoyakusudia au w a n a t a k a w a o n e k a n e
wameleta kitu kipya katika jamii ya Waislamu jambo ambalo ni
hatari.
Ukifatilia nyendo zao u t a b a i n i wa n a ya e n d e a
masuala ya Kiislamu kwa njia zao, lakini Muhakama (a ina ya aya
ndani ya Qur an) hawazitaki, wao wa n a n g a n g a n a k a t i k a
Mutashabiha.
Bila shaka wana malengo yao waliyoyakusudia ima waonekane
wameleta kitu kipya katika jamii na hii ni hatari kubwa kabisa.
Alisema Shkh. Doga.
Mwanazuoni huyo katika dini ya Kiislamu, alisema hakuna kitu
kipya katika U i s l a m u b a d a l a y a k e wanaibuka watu
(Waislamu) wanodhani wataonyesha kitu ambacho wote hawakijui wala
hakuna anayekifanya huku wakitaka kuonyesha njia hiyo ndio njia
sahihi kumbe ni kupotoka.
A l i s e m a , k u t o k u j u a (ujinga) kwa Waislamu, ndio
chanzo cha upotoshaji unaotokea miongoni mwa Waislamu hivi sasa,
kwani yanayofanyika yanaashiria ni
ukosefu wa elimu na ufahamu wa mafundisho ya Uislamu.
N a ye D k t . H a m d u n i Suleiman, akichangia katika
Kongamano hilo, alisema yapo matatizo ya uelewa katika kuyaendea
masuala ya Uislamu na mbaya zaidi ni kule kijidhania kuwa wana
elimu ya Uislamu wakati hawana zaidi ya kuleta migongano miongoni
mwa Waislamu.
Ni vyema Waislamu hao kama wanafahamika waitwe katika hadhara
kama hizi zinazokutanisha Jopo la Wanazuoni wa Kiislamu ili wapate
majibu na ufafanuzi wa hoja na dhana zao hizo. Alisema Dkt.
Hamduni.
Akitoa maoni yake mara baada ya Kongamano hilo, Maalim Ally
Bassaleh, alisema mada mbalimbali zi l izo hudhurishwa na wanazuoni
kwa Waislamu zina umuhimu mkubwa kwa wakati uliopo ,hususan suala
la misimamo mikali katika Dini.
A l i s e m a , a n a u n g a n a na watoa mada wote na
wachangiaji juu ya kupinga vita dhana hiyo inayokuja kwa kasi
miongoni mwa Waislamu, sababu kubwa ikiwa ni ujinga (kutokujua)
unaotokana na mtu kutokuwa na elimu na jambo analo lifanya.
Sheikh Amran Kilemile.
Mkuu Magereza ashikilia uhai wa Sheikh SaidInatoka Uk. 2
W a k i w a z u n g u m z i a Waislamu hao walio gerezani kiasi
cha mwaka mzima sasa, Sheikh Amran Kilemile na Maalim Bassaleh, kwa
nyakati tofauti wameleza kuwa mamlaka husika ziwatendee haki kwa
mujibu wa sheria na katiba ya nchi.
Maalim Bassaleh, alisema watuhumiwa hao waliopo magerezani ni
Waislamu wenzao ambao wapo huko kwa muda mrefu bila sababu za
msingi kiasi kwamba sasa wanaamua kuchukua maamuzi ambayo s i ya
kawaida.
Maamuzi ya kugoma kula, kugoma kuingia Mahakamani na hata
kupanda juu ya mti, yote hiyo ni kutaka kuonyesha hisia zao, zaidi
ni kuona hawapati haki zao na hata kufikia kuomba waonane na baadhi
ya viongozi wa Serikali ili wapate kuwaeleza shida zao, lakini pia
inaonekana kama vile wanapuuzwa. Alisema Maalim Bassale.
A l i s e m a , w a l e n i wanadamu, hata kama wana makosa,
bado wanayo haki ya kusikilizwa lakini kwa hali inavyokwenda hata
mtu
wa kawaida mtaani anaona kuwa kinachotendwa dhidi ya watuhumiwa
hao ni dhulma.
A l i s e m a , m t u anapotuhumiwa huwa bado anakuwa hana
makosa mpaka pale Mahakama husika itakapo thibitisha, lakini
akasema Muislamu akituhumiwa tu ananyimwa dhamana si ajabu mwaka
mzima au zaidi kwa tuhuma zinazo stahili dhamana.
L a k i n i k u n a m t u mwingine mwenye imani ya Kikristo naye
ni kiongozi wa dini amekamatwa na silaha ya moto, na ikaelezwa
silaha yenyewe ina matatizo kwamba haijulikani kuwa ni ya halali au
la.
Lakini huyu pamoja na kukutwa na silaha yenye utata anapata
dhamana tena ya kujidhamini mwenywe lakini huyu Muislamu au Sheikh
hana kosa la kukamatwa na chochote, ni tuhuma tu lakini ananyimwa
dhamana. Alisema Maalim Bassaleh.
Akasema, mwenendo huo ni lazima Waislamu waone kuna uonevu
kutokana na tuhuma zao kusimamiwa kwa misingi ya dhulma ili hali
wengine wanafatiliwa kwa
misingi ya sheria na katiba ya nchi.
Kwa upande wake Sheikh Kilemile, alisema Masheikh na Waislamu
hao kama kweli wana kesi, basi ni bora izungumzwe na tatizo
lionekane, na kwamba kama unamtuhumu mtu, basi tuhuma zake uziweke
wazi.
E l e z a t u h u m a z a k e ziangaliwe kwa misingi ya haki na
kama ana makosa yaonekane, Mahakama zipo kwa ajili hiyo, makosa
yawe wazi yafahamike, kuliko hii hali ilivyo sasa dhidi ya Waislamu
hao. Alisema.
Sheria ya kesi ni kuwa inafikia mahali kesi yake inatakiwa
izungumzwe kisha Mahakama iamue kama anatuhuma au hana, kisha
mtuhumiwa apewe haki yake aidha kutumikia adhabu au aachiwe huru.
Aliongeza Sheikh Kilemile.
Akasema, Waislamu hao wanashikiliwa kwa muda mrefu sasa lakini
haieleweki sababu za msingi zinazo kwamisha kesi hiyo, huku siku
zinazidi kwenda na kupelekea watuhumiwa na umma hawajui hatima ya
suala hilo na kwamba hali hiyo haipendezi katika misingi ya utu na
haki.
-
4 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari
Amiminiwa risasi na Polisi, afarikiKIJANA Usamah Abdullah Rahim
amepigwa risasi na kuuliwa papo hapo na polisi.
Baada ya kumuuwa kijana huyo, Polisi walitoa taarifa wakidai
kuwa waliwahi kumuuwa ki jana huyo wa Kiislamu kwa sababu alikuwa
akipanga kuchinja Wakristo na hata Polisi.
Kama ushahidi, Polisi hao walionyesha kisu ambacho walidai kuwa
walimkuta nacho Rahim na kwamba walipotaka kumsimamisha il i
wampekue, Usamah Abdullah Rahim, aliwatisha k wa k i s u h i c h o
n d i o wakaamua kumpiga risasi.
Katika madai zaidi ya Pol is i inaelezwa kuwa m i o n g o n i m
w a w a t u ambao Usamah Abdullah Rahim, alipanga kuwachinja ni
pamoja na Bi Pamela Geller anayesifika kama manaharakati
anayeuchukia Uislamu.
Terror suspect killed by FBI 'planned to behead Pamela
Geller'
Usaama Rahim allegedly planned to kill anti-Islam activist
before his death in Boston on Tuesday.
Ndio baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti vikijitahidi
kuhalalisha m a u w a j i y a R a h i m yaliyotokea Boston mapema
mwanzoni mwa mwezi huu wa sita kwamba alikuwa kapanga kumuuwa
Pamela.
Jihadi Shot Dead in Boston was Plotting to Behead Cops, Another
Arrest Made.
Boston Beheading Plot Jihad in America: Enemy in our Midst.
Ndivyo vi l ivyokuwa v i m e p a m b wa v y o m b o vingine vya
habari vya Marekani vikielemea juu ya madai ya kitisho cha
kuchinjwa polisi.
The man shot and killed Tuesday by Boston police was plotting
with another suspect to behead a cop, a law enforcement source told
Fox News.
N d i v y o F O X N e w s walivyoripoti wakisherejesha kwa kudai
kuwa kijana huyo na watu wengine wal ikuwa wamepanga kuchinja
Wakristo na Polisi kwa kutumia mtindo wa magaidi wa ISIS.
Tunaamini walikuwa na nia ya kuchinja Polisi, alinukuliwa afisa
mmoja wa polisi akisema.
Tul i jua l i l ikuwa ni tishio la kweli na ilikuwa watekeleze
mpango huo Jumanne. Aliongeza afisa huyo.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Boston, Kamishna
William Evans alisema
Na Mwandishi Wetu
kuwa ilikuwa ni mapema kiasi saa moja asubuhi ambapo maofisa wa
kikosi maalum cha kupambana na ugaidi (Joint Terrorism Task Force)
walimsimisha Rahim wakimhoji mambo kuhusiana na mwenendo wake
unaotia shaka juu ya ugaidi.
Hata hivyo akadai kuwa Rahim alitoa kisu akitaka kumdhuru po l i
s i nd io wakamuwahi kumpiga risasi.
The terrorism plot was "very real" and "very dangerous."
Alidai Kamanda William Evans akijitahidi kuonyesha kuwa walikuwa
hawana n a m n a i l a k u m u u w a Usaamah Abdullah Rahim, kwa
madai kuwa ingekuwa hatari kama wasingefanya hivyo!
Ili kuthibitisha madai yao, polisi walidai kuwa upo mkanda wa
video ukionyesha tukio zima.
Hata hivyo, video iliyokuja kutolewa haithibitishi madai ya
polisi.
Ukiacha kuwa ki jana Rahim anaonekana kwa shida katika picha
hiyo ikionyesha kuwa ilipigwa toka mbali, lakini kisu hakionekani
kabisa au silaha ya namna yoyote.
Wa l a h i c h o k i t e n d o kinachodaiwa kuwa Rahim a l i t a
k a k u wa s h a b u l i a , hakionekani katika picha hiyo.
Hata vile vyombo vya habari ambavyo kwa kawaida hushabikia
taarifa za polisi juu ya madai ya kukamata au kuuwa magaidi,
viliandika vikisema kuwa video ya polisi haijibu maswali juu ya
tukio la kuuliwa Rahim na zaidi vikasema haithibitishi kwa namna
yoyote madai kuwa Rahim alipambana na polisi.
Ukiacha mapungufu hayo, ndugu, jamaa na waumini wa Msikiti
anaposwali Usamah, wanasema kuwa madai ya polisi na kikosi chao
maalum
cha kupambana na ugaidi ni urongo mtupu.
Na kwamba hata kama angekamatwa akiwa na kisu, bado hiyo sio
sababu ya kumpachika jinai ya ugaidi na kumuuwa papo hapo.
Wa n a s e m a , k a m a n i kitisho, basi waseme ni Uislamu wa
Usamah, lakini s i o k u m s i n g i z i a k u wa anapanga kuchinja
Wakristo na Polisi kwani kukutwa na kisu hilo ni jambo la kawaida
hasa kwa jamii ya Wamarekani Weusi, na hasa katika kipindi hiki
ambapo wanauliwa ovyo na polisi na hata wananchi wa kawaida Wazungu
ambao kila uchao wanazidi kuwa na chuki dhidi ya Weusi (racism)
Alisema Bi Karen, mmoja wa ndugu wa Usamah kwamba ingawa jamii
ya Wamarekani Weusi yote ipo katika kitisho, lakini unapokuwa Muis
lamu, kitisho kinakuwa kikubwa zaidi.
Hoja nyingine ya msingi Waislamu na ndugu wa Usamah wanahoji,
kama Polisi na hiyo Task Force yao ya kupambana na ugaidi wanadai
kuwa kijana huyo alikuwa na mpango wa kuchinja Wakristo, kwa nini
wasimkamate na kumfikisha mahakamani watoe ushahidi na pengine kwa
kumhoji m t u h u m i w a w a w e z e kuutambua mtandao wake wa
kigaidi na kuuvunja.
Wakati huo huo, Kijana wa Kizungu Dylann Roof aliingia katika
kanisa lijulikanalo kwa jina la Emanuel African Methodist Episcopal
Church kule Charleston, South Carolina, na kuwafyatulia risasi
waumini ambapo aliuwa watu 9 Wamarekani Weusi wakisali.
Hata hivyo, tukio hilo limechukuliwa kama uhalifu wa kawaida
nchini Marekani na hakuna namna kijana huyu anatuhumiwa kwa
ugaidi. Kinyume chake, baadhi
ya taarifa zikijitahidi kumtoa Dylann Roof katika jinai hiyo,
zimejaribu kuibua wasiwasi kuwa huenda kijana huyo alifanya tukio
hilo akiwa hayupo hadhiri. Kwamba labda kuna jambo lilimchanganya
akili ndio akaenda kanisani na kuuwa watu hao.
Shooters of Color Are Called 'Terrorists' and 'Thugs.' Why Are
White Shooters Called Mentally Ill'?
A n a h o j i m w a n d i s h i Anthea Butler akionyesha k u t o
k u r i d h i s h w a n a mwenendo wa vyombo vya habari na baadhi
ya maofisa wa v y o m b o v ya d o l a . Anasema, wakati kitendo
kilichofanyika ni ugaidi wa dhahiri dhidi ya watu Weusi na Makanisa
yao na kwamba sio tukio la mwanzo kwa Marekani, vyombo hivyo,
vinakuja na kauli ambazo ni kutaka kumfunika Dylann Roof na
kudunisha jinai aliyofanya.
Hili sio tukio la mwanzo katika historia ya Marekani. Makanisa
ya watu Weusi yamekuwa yaki lengwa na wabaguzi wa Kizungu (white
supremacists) ambao wamekuwa wakiyachoma moto makanisa hayo au
kuyalipua kwa mabomu kama namna moja wapo ya kuwat isha jami i ya
Weusi (terrorize the black communities).
Anasema Anthea Butler akitaja moja ya matukio mabaya ya kigaidi
dhidi ya Weusi kuwa ni pamoja na lile la kulipuliwa kanisa la
Wamarekani Weusi kule Birmingham, Ala., mwaka 1963 ambapo wasichana
wanne (4) waliuliwa.
W a l i o f a n y a j i n a i hiyo walitajwa kuwa ni wanachama
wa kundi la Ku Klux Klan (KKK), au kwa kifupi "the Klan".
Kundi lenye rekodi na historia chafu ya chuki, u b a g u z i u l
i o p i n d u k i a n a m a u wa j i d h i d i ya Wamarekani
Weusi.
Anasema Butler kuwa katika kuripoti tukio hilo la kuuliwa watu 9
ambalo kwa dhahiri kabisa ni la kigaidi, hutakuta vyombo vya habari
vikitia neno lolote kuwa huo ni ugaidi. Kinyume chake, pamoja na
kuwa hakuna taarifa zozote za kitabibu wala jamaa wa Dylann Roof
hawajaleta madai/utetezi kuwa kijana wao alikuwa na ugonjwa wa
akili, lakini vyombo vya habari mara tu baada ya kufanyika mauwaji
hayo v i l i anza ku ja na misamiati na misemo kama:
A victim of mistreatment or inadequate mental health resourceswe
dont know his
mental condition."Yote hii anasema, ni kutaka
kujenga hoja kumnasua kijana Dylann Roof katika jinai
inayomkabili.
Kwa upande mwingine kama Meya Joseph Riley wa Charleston
alivyosema, tukio hilo linaonekana kama jambo la bahati mbaya tu la
mtu binafsi aliye na matatizo fulani na halina uhusiano na kundi
lolote unaloweza kusema ni la kigaidi kama ambavyo matukio ya watu
wenye majina ya Kiislamu yanavyoburutwa yakatiwa katika kapu la
ISIS, Al Shabaab na Al-Qaida. Kwa watu kama Dylann Roof, wao
inakuwa ni kazi ya lone wolfs au "one hateful person".
Ni kutokana na hali kama hizi na ubalakala kama huu, wasomi na
wachambuzi wengi wa siasa za Marekani n a n c h i z a M a g h a r i
b i kwa ujumla, wanaitizama inayoitwa Vita dhidi ya ugaidi kama
tamthilia fulani na mzaha wa karne hii.
Ni picha na taswira ya kubuni ambayo inakolezwa na kuvurugwa na
wanasiasa.
K a m a a n a v y o s e m a mwandishi mchokozi wa Uingereza na
mchambuzi, Adam Curtis, hili "Ni wingu potofu la f ikra ambalo
limesambaa bila kuhojiwa miongoni mwa serikal i duniani kote,
majeshi ya usalama na vyombo vya habari."
Wakati nchi za Magharibi zikitumia Vita ya Msalaba dhidi ya
magaidi kuhalalisha uvamizi angamizi ili kupata masilahi yao ya
kibeberu, nchi kama yetu zinazochagizwa kushiriki katika Crusade
hii kama alivyoiita muasisi wake George W Bush, zinajikuta
zikijitosa kibubusa matokeo yake yakiwa ni maangamizi kwa watu wake
na nchi kwa ujumla.
Maangamizi kwa watu k w a s a b a b u , k w a n z a
watapandikizwa magaidi watakaoleta maafa kama i n a v y o t o k e a
N i g e r i a , Somalia, Yemen, Pakistan na Kenya.
P i l i , n i m a a n g a m i z i kwa nchi kwa sababu kwa
kutumia kisingizio cha kupambana na magaidi, mabeberu huingia
kikachero na kijeshi wakazidhibiti nchi wazitakazo zisiweze
kufurukuta wala kuwa na uhuru juu ya rasilimali zao na siasa za
nchi. Kila kitu wanapangiwa na kupewa maelekezo.
Kwa hiyo, wakati nchi lengwa ikiangamizwa pamoja na watu wake,
mabeberu wanavuna faida isiyo ya kawaida kiuchumi na kisiasa
kutimia azma yao ya Global hegemony.
Usamah Abdullah Rahim
-
5 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari za
Kimataifa
SERIKALI ya China imepiga marufuku wanafunzi, walimu na
watumishi wa umma katika eneo la Xinjiang lenye Waislamu wengi,
kutekeleza ibada ya Saumu katika mwezi h u u m t u k u f u w a
Ramadhani.
Serikali pia imezuia watu kuhudhuria shughuli zozote za kidini
ikiwa ni pamoja na ibada za usiku.
Taar i fa ya ser ika l i imetaka biashara kwenye h o t e l i n a
m i k a h a wa kufunguliwa nyakati za mchana kama kawaida.
Wa n a h a r a k a t i w a Kiislamu wamepinga agizo hilo la
serikali wakisema linalenga kuhujumu dini tukufu ya Kiislamu.
Ingawa serikali inasema lengo la kuweka sheria h iyo n i kuhak
ik i sha m a s u a l a y a d i n i hayavurugi muundo wa jamii, duru
za kuaminika zinasema sheria hiyo ina malengo ya kiuchumi, kwani
imewekwa i l i kuhakikisha nguvu kazi ya taifa haipungui katika
mwezi wa Ramadhani.
C h u o K i k u u c h a K i i s l a m u c h a A l -Azhar cha
nchini Misri kimepinga na kulaani dhulma na ukandamizaji wa kidini
unaolenga haki za msingi za Waislamu nchini China.
Al Azhar imeitaka jamii ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa
na asasi mbalimbali za haki za binadamu kulaani kitendo hicho.
Kwa miaka kadhaa sasa, serikali ya China imekuwa ikitekeleza
sheria hiyo ya kibaguzi na mwaka uliopita, watu kadhaa walifikishwa
m a h a k a m a n i k w a kufunga Ramadhani na kukaidi sheria hiyo.
(Irib)
MUFTI wa Uganda S h e i k h S h a b a n Ramadhan Mubajje, a m e
i t a k a s e r i k a l i n a m a s h i r i k a y a usalama ya nchi
hiyo y a n a y o c h u n g u z a mauaji ya viongozi wa Kiislamu,
kufanya kazi kwa uadilifu na kwa viwango vya juu vya utaalamu.
V y o m b o v y a habari vya Uganda vimemnukuu Mufti wa nchi
hiyo akiitaka serikali, hususan wale wanaohusika na masuala
Saudi Arabia inaendeleza na mashambulizi yake ya anga katika
maeneo mbalimbali ya Yemen, licha ya kutolewa wito m b a l i m b a
l i k a t i k a ukanda huo na kimataifa w a k u s i m a m i s h a
mashambuliz i hayo yanayouwa wananchi wasio na hatia kwa mamia ya
maelfu.
Mashambulizi ya anga ya muungano wa Saudia katika maeneo
mbalimbali ya Yemen yaliendelea wiki hii ; huku idadi kadhaa ya
Wayemeni wakiuawa na kujeruhiwa. M a s h a m b u l i z i h a y o y
a n a e n d e l e a h u k u makundi husika kwenye mgogoro wa Yemen
yakishindwa kufikia muafaka baada ya siku tano za mazungumzo mjini
Geneva Uswisi.
Saudi Arabia imesema k u w a k u o n d o k a wapiganaji wa
Mahouthi wa Ansarullah katika maeneo wanayoyadhibiti ni sharti la
usimamishwa vita huko Yemen.
Ismail Ould Sheikh A h m a d , M j u m b e Maalumu wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen, awali alijaribu k
u f a n ya j i t i h a d a z a kufikiwa makubaliano ya usitishaji
vita huko Yemen na baadaye makundi ya nchi hiyo yakaweza kuketi
kwenye meza ya mazungumzo huko Geneva.
Sambamba na juhudi h i z o z a k u u p a t i a ufumbuzi mgogoro
wa Yemen, lakini kutokana na mashambulizi ya Saudia ya n a y o e n
d e l e a k i l a uchao nchini humo, hali ya wananchi imekuwa mbaya
zaidi hivi sasa kwa kuzingatia uhaba wa chakula uliopo na kuendelea
kushambuliwa vituo vya afya na tiba nchini humo.
Wananchi wa Yemen h a w a p a t i h u d u m a
Licha ya Ramadhani Saudia yaendelea kuihujumu Yemen
Waharibu hospitali 62 na zahanati 115Wanaopambana wote wapo
kwenye swaumu
muhimu za kiafya na maji safi ya kunywa kutokana na kushtadi
mashambulizi ya utawala wa Aal Saud, huku uhaba wa mafuta pia
ukiwafanya raia hao wakabiliwe na hali ngumu ya kimaisha.
Ta m i m a l S h a m i , msemaji wa Wizara ya Afya ya Yemen
alisema
mwishoni mwa wik i kat ika mahoj iano na televisheni ya al
Mayadeen y a L e b a n o n k u w a , mashambulizi ya anga ya Saudia
huko Yemen hadi sasa yameharibu na kubomoa hospitali 62 na zahanati
115.
Ta m i m a l S h a m i aliongeza kuwa, hakuna
shaka kuwa mashambulizi ya anga ya Riyadh ni sababu kuu ya
kuibuka matatizo ya kiafya na kitiba huko Yemen.
Umoja wa Mata i fa nao umedaiwa kuhusika katika kutokea maafa
hayo kwa hatua yake ya kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuikingia
kifua Saudi Arabia.
Uchunguzi wa mauaji ya Masheikh UgandaMufti aitaka serikali
iwafanye uadilifu
ya usalama kutumia utaalamu wa hali ya juu katika kazi zao kama
kweli wanataka kupata ufumbuzi wa kudumu wa mlolongo wa mauaji ya
viongozi wa Kiislamu nchini humo.
Mufti Mubajje alisema hayo wilayani Kamuli mwishoni mwa wiki
wakati wa uzinduzi wa eneo la Waislamu lililojengwa na shirika
lisilo la kiserikali NGO la Kamuli Good Hope lililogharimu shilingi
milioni 75.
Matamshi hayo ya Mufti Mubajje, yamekuja kufuatia wimbi la
mauaji ya Masheikh katika mkoa wa m a s h a r i k i , h u k u
mauaji ya karibuni kabisa yakiwa ni yale ya Sheikh Abdul Rashid
Wafula huko Mbale.
M u f t i M u b a j j e p i a amewataka Waislamu wa madhehebu
mbalimbali kuungana na kuweka pembeni tofauti zao ndogo ndogo na
kuwa mfano bora kwani Uis lamu inafundisha amani na kuishi na watu
kwa wema.
China yawazuia Waislamu Xinjiang kufunga
RAIA wa Yemen wakiwa wamebeba mtoto aliyejeruhiwa kutokana na
mashambulizi ya majeshi ya Saudi Arabia yanayoendelea nchini
humo.
-
6 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2,
2015Makala/Tangazo
Mafundisho ya Quran
Fethullah-Gulen
HIVI mnawaamrisha watu kufanya wema na hali mnaziacha nafsi zenu
na hali y a k u w a n y i n y i mnakisoma kitabu, hivi hamuelewi?.
[Al-Baqarah 44]
Pamoja na kwamba aya hii inawasemesha sehemu katika wana wa
Israel kwa sura ya moja kwa moja, lakini ni kwamba aya h i i i n a
wa s e m e s h a Waislamu vile vile.
K wa su r a h i i ya I s h a r a n a j a m b o ambalo
linakusudiwa hasa, ni kutuzinduwa j u u ya wa j i b u wa kupatikana
umoja na kutovunjana kati ya yale yanayosemwa na yale yanayotendwa.
Kwa maana ya umoja katika maneno na matendo.
Kwa sababu hiyo, tunaona kwamba aya nyingine inaelezea maana
haya kwa njia nyingine, inasema : Kwa nini mnasema yale ambayo
hamyatendi? [Assaf 2]
Usiwahamashishe w e n z a k o k u f a n y a wema, wakati wewe
mwenyewe unafanya kinyume chake.
N d i y o h a l i n a maneno au kusema na kutenda ni lugha yenye
pande mbili , kwa ajili ya kuinusuru haki na kuwakilisha, i t a k a
p o z u n g u m z a hii lugha yenye sura mbili na maonekano mawili,
kwa jina la haki na ikapiga kelele kwa hiyo haki taathira yake
itakuwa kubwa sana. Kwa sababu kunapasa j u u y a b i n a d a m u k
u ya t e k e l e z a ya l e
ambayo anawalingania wa t u we n g i n e . N a kusiwe na
kupingana kati ya maneno yake na matendo yake na kati ya hali yake
inayoonekana na maelezo yake.
Imekuja katika athari kwamba Mwenyezi M u n g u m t u k u f u
alimwambia Mtume Issa (a.s.):
Ionye nafsi yako kwanza, iwapo nafsi y a k o i t a y a k u b a l
i mawaidha, hapo wape (wengine) mawaidha yako. Na kama nafsi yako
haikukubali, basi ona haya kwangu.
Kwa msingi huo, i n a p a s a k u i s h i binadamu kufuatana na
anavyoamini na aakisi vina vya ulimwngu wake wa ndani miongoni mwa
fikra na hisia, itakuwa ni kitendo cha kuitakasa nafsi yake. Yule
ambaye hasimami usiku ni juu yake kutoizungumzia swala ya Tahajudi
na aone haya kufanya hivyo. Na yule ambaye hawezi kuswali kwa
unyenyekevu wote na kwa kujinyongesha na wala hatendi kwa adabu
mbele za Mwenyezi Mungu mtukufu, wala haimtishi na kuogopa
kumuogopa Mwenyezi Mungu, asizungumze kuhusu sifa kamili za swala.
Na akitokuwa ni mwenye ku j i toa muhanga, kunapasa kutozungumza
tamko moja kuhusu maudhui ya kuishi kwa ajili ya watu wengine.
Kwa sababu Mwenyezi M u n g u m t u k u f u a m e f u n g a m a
n i s h a kwa hekima fulani n g u v u ya k u a t h i r i yale
yanayosemwa, na mfumo wa utendaji wa msemaji.
H a p a k u n a p a s a kukumbusha jambo jingine, nalo ni kuja u
w e z e k a n o w a kuifahamu kimakosa aya hii:
N i k w a n i n i mnasema yale ambayo hamyatendi? [A-ssaf
2].
A y a h i i haifahamishi maana ya kuwa tahadhari kulikumbusha
jambo ambalo huishi nalo
kwa sababu kuishi ni ibada na kufikisha ni ibada nyingine. Yule
ambaye hakuyatekeleza yote mawili, amebeba dhambi mbili na amekaa
mbali na nguvu za kuathiri kwa hatua m b i l i , n a a m b a y e
hakulitekeleza moja la hayo mambo mawili, atabeba dhambi moja, na
amekuwa mbali na kuathiri kwa hatua m o j a . K wa s a b a b u
nguvu ya kuathiri kama tulivyosema inategemea juu ya kutekelezwa
yale yanayofikishwa.
Ndiyo, kwa hakika kuwaamrisha watu wengine kwa kufanya mema na
kuwakataza na maovu na kuacha
kuyatekeleza hayo juu ya nafsi huko, ni kuvunjana kuliko wazi.
Na mfano wa utendaji huu wenye makosa, unapunguza taathira ya mambo
chanya mengi, kama vile nguvu ya balagha na kuweka wazi na elimu.
Haya ndiyo ambayo yanatajwa na aya hii. Ila asije akatumbukia mtu
yeyote mwenye akili katika mfano wa kupinga huku na unamtaka
binadamu umakini na kufikiri katika kuishi, na kufikisha na yasiyo
kuwa hayo miongoni mwa upuuzi na maneno mengi yanayoondoa h a i b a
y a m w e n y e kuzungumza. Na hili lina maana kwamba
yeye ameiacha nafsi yake kikamilifu. Kwa sababu hiyo, imekuwa ni
juu ya mtoaji wa mawaidha, na juu ya mtoaji wa nasaha na mwenye
kuongoza, na mwenye kufikisha na mwenye kuandika, na mwenye kupanga
mambo, awe ni mkweli katika matendo ambayo anasimama nayo ili
yachukuliwe machukuo ya ukweli na kwa ajili yasipate kivuli
chochote cha shaka juu ya zile m a u d h u u a m b a z o
anazizungumzia na kuzitoa.
(Imenukuliwa kutoka Kitabu: Miyangaza y a Q u r a n k a t i k a
mbingu ya hisia, cha Muhammad Fethullah Gullen kilichotafsiriwa k
wa K i s wa h i l i n a Sheikh Sule iman Amran Kilemile)
-
7 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Habari
Profesa Ibrahim Noor Shariff
Propaganda za udini shuleni Tanzania-8
T U K U M B U K E p i a kuwa katika miaka hii tuliyonayo
hapatakuwa n a k u s h e r e h e k e a , kila mwaka, mauwaji y a k
i m a a f a k a m a wanavyosherehekea maafa ya Wazanzibari W a i s
l a m u w e n g i waliotolewa roho zao bure 1964. Yakitokea, jua
kuwa washiriki wengi watasakwa, kukamatwa n a k u p e l e k w a
mahakamani -- The Hague.
Nastaajabu, lakini sistaajabu sana kuona Waomani wamekaa kimya
maana kutokana na us taarabu wao , huwaoni kugombana ovyo na mtu
yoyote wala huwasikii kutukanana. Ni watu wakar imu sana kwa
vitendo na kwa maneno mazuri. Hivyo basi wanayasikia yasiyokuwa ya
kweli yanayosemwa dhidi yao na hawasemi kitu. Lakini, kama
ulivyoona wale wenye kutapakaza siasa kali za udini huwa kila
kukicha wanazidisha m a o n g o p e ya o n a kufikia hadi ya
kuonesha picha za utumwa hata West Indies, ambako Waarabu
hawakuweko, na kuonesha kuwa ni Waarabu waliokuwa na Watumwa hata
huko katika visiwa vilioko Amerika. Kwa ukosefu wa bahati, ukimya
wa Waomani unaotokana na ustaarabu wao wa hali ya juu kabisa wa
kutokujibu uwongo wa dhahiri unaosemwa dhidi yao na wenye siasa
kali za udini , kumewafanya wenye siasa hizo kuzidisha uwongo wao
kila leo.
Propaganda dhidi ya
Waislamu si jambo geni kwani zilianzia zaidi ya miaka elfu
iliyopita. Propaganda dhidi ya Waislamu wa Afrika Mashariki
zinazotokana n a w a k o l o n i n a w a m i s h i n a r i w a o p
i a s i j a m b o g e n i kwani zilianza tokea yalipowasili majeshi
y a K i p o r t u g i z i mwanzoni mwa karne ya 16 . Propaganda
hizi zilizidi kutia fora wakat i wa utawala wa Wa i n g e r e z a n
a Wajarumani mwishoni mwa karne ya 19. La kusikitisha ni kuona k u
wa wa m i s h i n a r i katika kusomesha kwao waliwafunza wanafunzi
wao wa Kiafrika ubaya wa Uislamu na wema wa Ukristo na kuwa dini ya
Kiislamu ni batili na dini yao ya Kikristo ndiyo ya kweli na ya
haki iliyoletwa Afrika Masharika na Kati kumkomboa Mwafrika na
ukatili na ubaya wa Uislamu na Waislamu.
W a k a t i h u o h u o w a l i p o k u w a wakiwasomesha haya
watoto wa Kiafrika, wakoloni wa Kizungu na wamishinari wao
waliziteka na kuzitia nchi za Afrika katika ukoloni wao ambao mara
nyingi ulisababisha v i f o v ya Wa a f r i k a wengi kwa mauwaji
ya kinyama kabisa na utiwaji wa Waafrika wengi utumwani katika n c
h i z a o we n ye we Waafrika, na mamilioni wengine ya Waafrika
waliotiwa utumwani walipelekwa kwenye nchi zilizotawaliwa na
Wazungu Wakristo.
Kama tulivyokwisha kutaja pia, chini ya utawala wa Mfalme
Leopord II (1835 1909) wa Ubiligiji aliwatia utumwani mamilioni ya
Wakongo katika m a s h a m b a ya m i t i y e n y e u t o m v u wa
kutengenezea mipira; na katika juhudi hizo a l iwauwa Waafr ika
wasiopungua milioni kumi, wengi walifungwa na kuadhibiwa vikali s a
n a , w a l i p i g w a mboko, wengine wengi walikatwa viganja vya
mikono yao walipokataa
kufanya kazi bila ya malipo. Soma vitabuni na fungua mitandao
uangalie mwenyewe n i n i w a m e a n d i k a wanahistoria kukhusu
u t u m w a h u u n a ukhabithi wake na idadi ya Waafrika
waliouliwa.
Lakini, wamishinari wa Kizungu jana na wamishinari wa Kiafrika
leo hawazungumzii utumwa huu na unyama wake, kwani kufanya h ivyo
kutawaweka Wakristo na Ukristo pahala pabaya sana. Na hili ndilo
jambo wanalolipiga chenga. Wao wamo kila leo k u s h i n d i l i a
k a t i k a bongo za wanafunzi wa Tanzania ubaya wa Waislamu tu
hata iwapo Uislamu na Waislamu hawakhusiki na ubaya h u o . K u f a
n ya h i l i kunayafanya masomo ya shule ya historia kuwa si masomo
yenye kuelezea ukweli uliotokea, bali huyafanya masomo hayo kutiwa
katika kumbo la propaganda; na la kusikitisha zaidi ni kuiona
Serikali ya Ta n z a n i a a m b a y o inajigamba kuwa haina dini
na haipendelei wala kuichukia dini yoyote kuwa inashiriki k iukami
l i fu ka t ika k u w a p a k a u c h a f u n a k u wa p i g a v i
t a Waislamu na dini yao na kuwapendelea Wakristo wenye siasa kali
za udini kwa kuachilia p r o p a g a n d a z e n ye ukweli finyu na
uwongo mwingi kusomeshwa katika shule za Tanzania mchana kweupe
bila ya kificho na bila ya kuona haya wala kuwa na khofu,
kunaifanya Serikali ya Tanzania kuwa mshiriki katika k u j e n g a
m s t a k b a l i mbaya kwa nchi ya Tanzania ambayo wao wameapa
kuilinda na kila ovu.
Wa n a p r o p a g a n d a waliopewa fursa ya kuandika vitabu
vya h i s t o r i a k w a a j i l i y a k u w a s o m e s h e a
wanafunzi wa shule za Tanzania wameitumilia fursa hiyo vibaya sana,
kwani wameonesha waziwazi mapendeleo yao juu ya Ukristo na Wakristo
na chuki
zao zinazotokana na vita vyao vya msalaba dhidi ya Uislamu na
Waislamu.
Vita hivi katika Afrika M a s h a r i k i k wa n z a v i l i a n
z i s h w a k w a maneno na wamishinari wa Kizungu na serikali zao
za kikoloni na z imepokelewa kwa utiifu mkubwa sana na wamishinari
wa Kiafrika ambao wamejibebesha vita hivyo vya msalaba na
kuviendeleza mbele kwa kadiri ambayo hata waalimu wao wa kikoloni
wanaonekana leo kama wanafunzi. Ingelikuwa hayo wanayoyaelezea w a
n a p r o p a g a n d a ni ya kwel i mtupu t u s i n g e l i g u t
u k a , l ak in i mengi za id i w a l i y o y a c h o r a n a k u y
a a n d i k a s i matokeo ya kwel i , kama tulivyokwisha
kudhihirisha.
K w a w e n y e macho, na mwenye m a c h o h a a m b i w i
tazama, Tanzania imeshatumbukizwa katika vita vya udini na hawa
Watanzania wenye siasa kali za udin i . Tanzania n i nchi yenye
Waislamu w e n g i n a u b a y a mkubwa wanaoufanya wanapropaganda
hawa kwa propaganda zao dhidi ya Wais lamu n i kuwahamakisha
Waislamu na kupalilia mfarakano mkubwa wa kipumbavu kabisa baina ya
Wakristo na Waislamu wa Watanzania. Na hili ni jambo la khatari
kubwa sana kwa nchi nzima ya Tanzania, na Serikali ya Tanzania
ndiyo itakayokuja kulaumiwa na dunia kwa kushiriki ka t ika
propaganda hiz i kwa kuonesha kama hawayaoni na hayawakhusu hayo y
a n a y o s o m e s h w a s h u l e n i . V i t a v y a maneno
vimeanzishwa zamani, jee viongozi wenye busara Tanzania watapigania
kiungwana na kwa haki kuviondosha au watashika mirengo na
kuvipalilia vita hivi na raia wa kila upande k u k u t i s h wa m a
a f a kama waliyokutishwa Waruwanda, Wabosnia, W a z a n z i b a r
i n a wengineo?
Jambo moja wanafaa wenye akili zao timamu w a l i f i k i r i e
v i z u r i n i kuwa Wais lamu Tanganyika ni wengi na hawatakubali
wachinjwe huku wamelala chali. K i l a m we n ye a k i l i zake
timamu anaelewa fika kuwa kukianza chinjachinja Tanganyika, basi
watachinjwa watu wa dini zote wa pande zote na misiba itakuwa Ta n
g a n y i k a k o t e , hakuna atakayesalimika na ukoo wake wote.
Usia wangu ni kuwa w a t u w o t e w e m a wanaoipendelea mema
Tanzania watafute kila njia za kuungana na kuwapinga vikali sana
wenye kutapakaza siasa kali za chuki, za ukabila, udini na za aina
yoyote inayokhatarisha nchi.
K w a a j i l i y a propaganda za udini ziliomo ndani yake, v i
t a b u v y o t e v y a historia vinavyotumiwa shuleni Tanzania
leo, vinataka vichomwe moto ili kuondosha na kuuzika mmoja katika
mizizi mikuu ya fitina inayopaliliwa katika bongo za wanafunzi;
mzizi wa fitina ambao u n a e n d e l e a k u i l a Tanzania ndani
kwa ndani na siku moja itakuja kuleta khatari pevu. Inahitajia
badala yake viandikwe upya vitabu vya historia na mabingwa
wanaoijua historia vizuri sana n a w a s i o p e n d e l e a upande
wowote wala propaganda yoyote; mabingwa wa historia watakaoelezea
matokeo ya historia kwa ukweli k a m a u t a k a v y o -wezekana na
wana Adamu. Huu ndio usia wangu wa dhati. Ukiona nina-shambuliwa
mimi binafsi na watu fulani kwa ni l iyoyaelezea humu na kwa usia
huu nilioutoa, jua kuwa viumbe hao ama ni wale waliokwisha kupikwa
na kupikika vibaya sana na propaganda hizo nil izozielezea, a u n i
k a t i k a wa l e w a n a o n u f a i k a n a p r o p a g a n d a
h i z o ; v i u m b e a m b a o hawaipendelei mema Tanzania na watu
wake.
-
8 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2,
2015Habari/Tangazo
KAMATI YA MUUNGANO YA MASHINDANO YA SHULE ZA KIISLAMUAssalaam
alaykum warahmatullahi wabarakaatuhUmoja wa shule za msingi za
Kiislamu Tanzania (TIPSO) pamoja na
kamati ya pamoja ya kuhifadhi Quran inawatangazia wazazi,
walezi, walimu, wanafunzi na Waislamu wote kufanyika mashindano ya
tisa ya kuhifadhi Quran kwa shule za misngi za Kiislamu Tanzania
kama ifuatavyo:
Jumamosi 27/06/2015 katika Msikiti wa Kichangani Magomeni-Dar es
Salaam
Jumapili 28/06/2015-Fainali katika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar
es Salaam.
Muda ni kwa siku zote mbili kuanzia saa 2:00 Asubuhi 6:30
mchana. Wote mnakaribishwa.
Holy Quran Recitation Joint CommitteeMb: Mwenyekiti 0713 334
698, Katibu 0784 211673, Mweka hazina
(Treasurer) 0717 304 353 Email:[email protected]
MASHINDANO YA TISA YA KUHIFADHI QURAN
Hali si shwari ZanzibarWAKATI Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Z
a n z i b a r ( C C M ) wakimkataa Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim
Seif Sharif Hamad kuingia katika Baraza wakati wa kufungwa kwa
Baraza, ZEC imeshushiwa tuhuma nzito.
Tuhuma hizo ni ukiukwaji wa sheria na taratibu za uandikishaji
wapiga kura ambapo CUF wanadai kuwa ZEC inatumiwa na CCM
kuandikisha mamluki wa kukipa chama hicho tawala ushindi.
Katika kikao chake jana, Wawakilishi hao walikataa uwepo wa
Maalim Seif wakati Baraza hilo litakapofungwa leo na kuvunjwa rasmi
na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein.
Kwa mujibu wa sheria, Rais huingia ndani ya ukumbi wa Baraza
akiwa na wageni wake ambapo ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman
Makungu na Mshauri wake Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif
Hamad.
Kwa mujibu wa kanuni za Baraza hilo, wageni hao wanapoingia
ndani ya ukumbi huo, inabidi kutenguliwa kwa baadhi ya kanuni kwa
kuwa sio wajumbe wa Baraza.
Hivyo, Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho alitoa taarifa
ya kuwaarifu wajumbe juu ya ujio wa wageni hao na kutaka
waridhie.
Tunamtegemea Rais wa Zanzibar atakuja na ujumbe wake maalumu,
kwa hivyo tunamtegemea pia Jaji Mkuu, Jaji Makungu na tunamtegemea
Mshauri Mkuu mmoja wapo wa Rais ambaye ni Makamo wa Kwanza wa Rais,
Maalim Seif Sharif Hamad ambaye naye tunategemea kuingia humu
ndani.
Spika Kificho akaanza kuwahoj i wajumbe wa baraza hilo kwa mtu
mmoja mmoja, kati ya hao wageni watatu akianzia kwa Rais wa
Zanzibar, Jaji Mkuu na alipofika kumtaja Maalim Seif hali
ikabadilika.
M g e n i m w e n g i n e maalumu huyu ni mshauri wa Rais ambaye
ni Makamo wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad.
A l i p o a n z a k u m t a j a jina, wajumbe wakaanza kuongea
chini kwa chini ikaanza minongono ambapo Spika akaul iza mbona
anasikia minongono kama hawamtaki.
M b o n a n a s i k i a m i n o n g o n o k a m a hamumtaki..
nataka nisikie rasmi, aje au asiingie humu? Alihoji Spika
Kificho.
Hapo Wajumbe wakajibu kwa sauti kwamba asije.
Na Salma Alghaithiyyah, Zanzibar
Hawamtaki kuingia ndani ya ukumbi huo.
Spika akauliza tena, Ina maana Baraza halikuridhia Maalim Seif
kuingia humu ndani?
Wakajibu, ndio hatutaki asije humu ndani, hatumtaki.
Huku akicheka, Spika Kificho akasema kwa kawaida masuala haya
huwa hayana mjadala, na akawaambia wajumbe wa Baraza hilo kwamba
kwa kuwa yeye n d i ye a l i ye m u a n d i k i a barua Makamo wa
Kwanza kumualika katika kikao hicho, atalazimika kumuandikia barua
nyengine ya kutengua mualiko huo kutokana na wajumbe kumkataa
asiingie ndani ya ukumbi huo.
Kikawaida mimi ndiye niliyemuandikia barua ya kumualika kuja
hapa, kwa hivyo nitaandika nyengine kwa heshima zote kwamba
usije.
Alisema Spika huku wajumbe hao wakipiga makofi na kuongea kwa
furaha.
Inavyoelekea Wawakilishi h a w a k u p i t i a C C M ,
wamechukua hatua hi i kufuatia kitendo cha wenzao kupitia CUF
kususa vikao vya kumalizia Baraza.
M a p e m a w i k i h i i , W a w a k i l i s h i h a o kupitia
CUF wakiwemo mawaziri, walitoka nje ya kikao na kusema kuwa h a w a
t a h u d h u r i a h a t a kikao cha kuvunjwa Baraza kitakacho
hutubiwa na Mheshimiwa Rais Shein.
Walisema, wanafanya hivyo kusajili malalamiko yao kuwa upo
ukiukwaji mkubwa wa sheria, kanuni na taratibu katika uandikishaji
wapiga kura.
W a k a t i h u o h u o , Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,
Mheshimiwa, Jecha Salim Jecha, ametupiwa lawama nzito kuwa Tume ya
k e i n a f a n ya m a m b o ambayo yanaweza kuvuruga uchaguzi.
Moja ya tuhuma hizo ni madai kuwa ZEC inawekewa shinikizo
iongeze siku za uandikishaji kutoa fursa kwa CCM kukamilisha kazi
ya kuandikisha wapiga kura haramu.
Katika barua yao kwa Mwenyekiti Jecha, CUF wanadai kuwa wana
taarifa za kuaminika kwamba CCM kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa
na Wakuu wa Wilaya pamoja na Ofisi ya Usajili wa Vitambulisho vya
Mzanzibari Mkaazi iliandaa wapiga kura haramu ambao walipatiwa
vitambulisho vya ZAN ID ili kuwawezesha kuandikishwa kuwa wapiga
kura kwa lengo la kukisaidia CCM.
Hata hivyo wanadai kuwa, utolewaji na usambazaji wa vitambulisho
hivyo ulikwama na kupelekea vitambulisho hivyo kupatikana ikiwa
uandikishaji wa wapiga kura katika majimbo ya Wilaya ya Magharibi A
umeshamalizika.
Ni kutokana na hali hiyo, wanadai kuwa baada ya kupatikana ID
hizo, ndio zinafanyika njama kuongeza siku kutoa fursa kwa wenye ID
hizo kuandikishwa.
J u m l a y a Z A N I D zilizochapishwa kwa ajili ya uharamia
huu kwa Wilaya za Magharibi A na Magharibi B ni 39,500 na mpaka
jioni ya tarehe 23 Juni, 2015 walipatiwa ZAN ID 6,525 ambazo
walishindwa kuzi tumia kwa kukosa watu. Kati ya hizo, jumla ya ZAN
ID 1,200 zilipelekwa zikagawiwe katika jimbo la Bububu ambako muda
wa uandikishaji ulikwisha malizika wakati ZAN ID hizo zinawafikia
viongozi wa CCM.
Wanadai CUF katika barua yao kwa Mheshimiwa Jecha na kuongeza
kudai kuwa:
Baada ya kutofanikiwa kikamilifu, viongozi wa CCM jioni ya siku
hiyo hiyo ya tarehe 23 Juni, 2015 walikutana katika Ofisi yao ya
Mkoa wa Mjini iliyopo Amani na kupitisha maamuzi ya kuitaka Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar iongeze siku ili kuja kupandikiza wapiga kura
haramu kwa idadi ya mkakati iliyokuwa imepangwa.
Na kwamba, iliamuliwa k u w a Z A N I D h i z o zihamishiwe
katika majimbo
ya Wilaya ya Magharibi B katika uandikishaji ulioanza tarehe 24
Juni, 2015.
Katika barua hiyo ambayo nakala yake imesambazwa kwa Wahariri wa
Vyombo vya Habari, CUF kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu w a k e N a s
s o r A h m e d Mazrui wanadai kuwa, kazi ya kugawa ZAN ID kwa
makundi ya watu walioletwa kwa magari nje ya vituo vya uandikishaji
imefanyika ambapo waliambatanisha picha inayomuonesha mmoja wa watu
wa CCM akigawa ZAN ID hizo katika kituo cha Shakani, jimbo la
Dimani.
Kwa barua hii , CUF tunaitahadharisha Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar kuacha kuendelea kuitumikia CCM kwa kupokea ag izo la
kuongeza siku ili kusaidia kufanikisha mikakati ya CCM
inayoshindwa. Ilihitimisha barua hiyo ya CUF.
Katika barua yao nyingine kwa Mwenyekiti wa ZEC, Chama Cha
Wananchi, CUF wanadai kuwa wana taarifa kutoka vyanzo vya habari
vilivyomo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba kumeandaliwa
mpango wa kuvitumia vikosi kusaidia katika kuipa CCM ushindi.
W a m e d a i k u w a , utumikaji huo ni pamoja na kuandikishwa
katika maeneo ambapo sio wakazi pamoja na kutumika kuwadhibiti
mawakala wa CUF ambao w a n a h o j i w a n a p o o n a
w a k i l e t w a m a m l u k i au kuandikishwa watoto
wadogo.
Wanatoa mfano kuwa wapo watu wanaokuja na ID bandia kwa hiyo,
mashine zinakataa kuwatambua.
H a t a h i v y o , p o l i s i waliopo vituoni hutumika kulaz
imisha watu hao waandikishwe na Tume haichukui hatua, kuonyesha
kuwa wanajua mpango huo.
K a t i k a k i t u o c h a Chuini, jimbo la Mfenesini
vitambulisho 109 vilikataa kutambuliwa na mashine, hata hivyo nguvu
kubwa ilitumiwa na kuhakikisha k u w a w a t u h a o
wanaandikishwa. Hatua hiyo ilipelekea mzozo baina ya wananchi na
vikosi, na hivyo wananchi waliokataa ukiukwaji huo wa taratibu,
uliochochewa na Tume yako, walipigwa na kukamatwa kwa kuwekwa
katika vituo vya Polisi na kunyimwa dhamana.
Ilisema sehemu ya barua kwa Mwenyekiti wa ZEC na kuhitimisha kwa
kusema kuwa CUF itaendelea kutoa mashirikiano kwa Tume ya Uchaguzi
ya Zanzibar kwa mambo yote yanayofuata misingi ya katiba na sheria
na misingi ya uchaguzi huru na wa haki inayotambuliwa
kimataifa.
Miezi miwil i i l iopita akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kawake, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),
Salum Kassim Ali alieleza k u wa t u m e h i o h a i n a
mafungamano na taasisi yoyote hile katika ufanyaji kazi wake na
wamekuwa wakifanya kazi zao kwa ustadi mkubwa.
-
9 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Makala
WAISLAMU wa Tanzania leo hii wamepata msiba m k u b w a k u t o
k a n a n a k i f o c h a k i o n g o z i mkuu Sheikh Mkuu wa
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Issa Shaaban bin
Simba. Ikubalike kwamba Waislamu wa Tanzania wamempoteza kiongozi
wao mashuhuri sana, na labda haitakuwa rahisi kuziba pengo
aliloliacha. Alikuwa katika uongozi huo kwa muda mrefu hasa akiwa
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Bila sababu za msingi na vikiwa
vyombo v y e n y e m a d h u m u n i tofauti, lakini Katiba ya
BAKWATA inafanana sana na i le ya TANU/CCM. Unapata Sheikh wa
wilaya ikiwa Wilaya ya kiserekali hata kama wilaya ile ina Waislamu
wachache sana. Katika Uislamu, Wilaya ni sehemu kubwa sana ya nchi.
Idadi ya Waislamu katika Mkoa wa Shinyanga haifahamiki vizuri,
lakini inasemekana kuwa kwa D a a w a c h i n i y a A l -Marhum
Issa Bin Shaaban Simba, idadi hiyo ilikuwa ikiongezeka kidogo
kidogo.
Lakini wakat i fulani h u k o n y u m a , n i l i p a t a w a r
a k a k u t o k a k w a mwanaharakat i mmoja Muislamu aliyewahi
kuishi Shinyanga kwa muda mrefu tu. Waraka huu ulijaribu k u n i e
l i m i s h a k u h u s u mienendo ya Waislamu wa Shinyanga katika
jitihada ya kuusimamaisha Uislamu Mkoani humo. Kweli ama si ya
kweli , si dhamiri kuyanukuu hayo yaliyomo katika waraka huo. Hayo
si mada ya makala haya. Itoshe tu kusema kuwa kwa maoni ya huyu
Muislamu aliyeandika waraka ule, yeye aliona kulikuwa na kasoro
kubwa katika ule mwenendo w a k u w a h u d u m i a Waislamu wa
Shinyanga na wa Tanzania kwa jumla. Ningependa kusisisitiza tu
kwamba, kama kuna kasoro alizozitoa, hazikuwahusu viongozi wote wa
Shinyanga wa wakati ule.
Ni bahati mbaya sana kuwa katika uongozi wa Al Marhum Sheikh
Issa Bin Shaaban Simba, ni vigumu sana kutaja kwa uhakika ni wapi
Waislamu wanaweza kujivuna angalau kidogo hapa Uislamu na Waislamu
wamepiga hatua kubwa ya maendeleo. Wao wenyewe katika hali ya
kutaabad ama kujivuna kuwa Uislamu umekuwa na unaheshimika zaidi.
Yaani iwe katika daawa ama kwa mfano Waislamu sasa wameongeza shule
na vyuo kadhaa. Waislamu wa Tanzania wamshukuru kiasi gani
Bakwata leo na keshoNa Khalid S. Mtwangi
Rais Mstaafu Muheshimiwa Benjamin William Mkapa ambaye pamoja na
Ukatoliki wake, aliwaonea huruma Waislamu wa nchi hii na kuwapa
majengo walioweza kusimika Chuo Kikuu hapo Morogoro. Bahati nzuri
Chuo hicho hakimo mikononi mwa BAKWATA. Inasemekana kuwa kulikuwa
na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi waliomo Serekali , wale wasio
Waislamu. Wakati huo huo Kanisa Katoliki, kwa mfano, leo hii
wanaweza kujivunia vyuo vikuu zaidi kumi nchi humu. Labda itakuwa
si vibaya kusisitiza kuwa BAKWATA hawana hata Chuo Kikuu kimoja na
hii maana yake ni kwamba Waislamu nchini kila siku watakuwa nyuma
katika elimu.
Nadhani Waislamu wa Tanzania hata hawajasikia hiyo BAKWATA ina
mipango gani kuwaendeleza upande huo. Kweli ni baada ya ule mzozo
wa viwanja vya Changombe ndio Waislamu w a l i p o s i k i a k w a
m b a kutakuwa kiwanja mbadala cha kujenga chuo. Taarifa ambayo
haikuwa na msingi w o w o t e . L a b d a t o s h a tu Ustadh Issa
Ponda na wenzake wameteseka kwa kutetea mali ya Waislamu. Hiyo
ndiyo BAKWATA jana na leo. Kesho itakuwaje? Waislamu wasubiri
uchaguzi.
Ki fo cha Sheikh Bin Shaaban Simba, Sheikh Mkuu wa BAKWATA
kitaleta uongozi mpya pale kileleleni
ambao, ni mategemeo ya wengi, labda nao utalazimika k u l e t a
m a b a d i l i k o ya uongozi wote wa Chama hicho nchi nzima. Ni
hapo ndipo Waislamu wa Tanzania watakuwa wanatazamia mabadiliko
makubwa katika musakbali wa Uislamu nchini humu. Huko mbele kuna
nini? Watajiuliza.
Ni ukweli ambao ukubalike kuwa imekuwa vigumu sana huko nyuma
kuleta mageuzi katika uendeshaji na utawala wa chombo hiki BAKWATA.
Wakati akiwa Rais wa nchi hii Muheshimiwa Al Haj Ali Hassan Mwinyi
alijaribu kutaka kuleta mabadiliko ya uongozi humo BAKWATA k wa h i
y o u j e u t a wa l a mwingine; na mfumo pia ubadilike. Mzee
Rukhsa h a p a a l i k u t a k i z i n g i t i ambacho hakikumpa
rukhsa apite. Hakika bila shaka kutakuwa na wasomaji watakaokumbuka
hotuba ya Sheikh Mkuu wa wakati u le wakat i wa Maul id iliyosomewa
Shinyanga. Sheikh Mkuu yule alisikika akidiriki kusema huyu Rais
Mwinyi ataiweza wapi, BAKWATA ina wenyewe. Hakusema hapo wenyewe ni
kina nani. Kweli baadae Rais Mwinyi hakutaka kabisa kuigusa BAKWATA
ambao wao waliendelea kivyao na mambo yao kama kawaida.
H u k u W a i s l a m u wamebaki nyuma katika maendeleo ya nchi
hii, jambo ambalo linajulikana na kila Muislamu na kulalamikiwa
mara kwa mara kama sio kila siku. Naye Rais Jakaya
Kikwete alitoa malalamiko mengi dhidi ya BAKWATA mara baada ya
kushika hatamu za kuiendesha nchi hii Tanzania. Bila shaka wako
watakaokumbuka hutuba yake kule Arusha. Alisikika akiwashauri kwa
nguvu kabisa kuwa viongozi wa B A K WATA l a z i m a wabadilike na
mfumo wao pia ubadilike. Takriban miaka kumi baada ya ushauri huo
kutoka kwa Rais wa nchi hii, BAKWATA iko pale pale.
Ni kweli kuna wakati Al Marhum Sheikh Bin Shaaban Simba
alijaribu kutikisa kidogo uongozi wa Makao Makuu, kitendo ambacho
kwa muda kilileta tumaini la maendeleo . Wakati fulani al is ikika
akiwafokea wale waliokuwa wakipita wakisema ati kuwa BAKWATA ni
chombo cha CCM na Serekali. Huko nyuma, takriban miaka minne mitano
hivi, nilikutana na sheikh mmoja ambaye wakati huo alikuwa na
wadhifa hapo makao makuu ya BAKWATA. Kwa mbwebwe za kujiamini
kabisa, alinihakikishia kuwa BAKWATA aliyokuwemo yeye sio sawa na
BAKWATA ile ya zamani. Sasa inataka kuleta mapinduzi kweli kweli
katika harakati za kuwaletea maendeleo Waislamu wa Tanzania. Sheikh
huyu anisamehe sana ataposoma makala haya na kukuta nikiwajulisha
wasomaji wenzangu kuwa haukupita muda mrefu sheikh huyu alifukuzwa
katika uongozi.
Kuvuliwa kwake madaraka lilikuwa ni jambo baya sana kwa maoni
yangu kwa sababu huyu ni mmoja wa wale masheikh wana elimu na sifa
stahiki. Alikuwa ana Diploma ya Ualimu na leo ana degree ya fani
hiyo aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Na Sheikh Mkuu wa wakati ule alipowaambia Waislamu kuwa BAKWATA
ina wenyewe, hakuwataja hao ni kina nani. Hakika asingeweza kutaja
siri hiyo hadharani, lakini ni muhimu hao wenyewe watambue kuwa leo
hi ni mwaka 2015 hali yake katika nyanja nyingi sio sawa na 1968
BAKWATA ilipozaliwa pale Iringa huku Waislamu wakisimamiwa wakipewa
ulinzi na askari wenye ala zao kamili. Ukumbi mzima hapo
paliposimikwa uongozi mpya wa Waislamu wa BAKWATA, ulizungukwa na
hawa watumishi wa w a n a n c h i s i l a h a z a o (bunduki) zao
zikionyeshwa wazi wazi.
Nimewahi kuambiwa na Sheikh Khamis Mataka kwamba katika
utamaduni wa K i i s l a m u k i o n g o z i hachaguliwi kwa
kupigiwa kura. Panapotokea kiasi k i k u b wa c h a wa u m i n i
wakatoa hisia zao kwa sauti kubwa kumtaja wanayemtaka awe kiongozi
wao, basi ndiye huyo atakuwa amechaguliwa na waumini awe kiongozi
wao. Sio hivyo alivyopatikana Khalifa wa kwanza Sayyidna Abubakar
RA? Labda katika hali tuliyonayo, Waislamu nchini humu uteuzi wa
aina hiyo usiwezekane hasa kwa vile BAKWATA kwa mfano itatakiwa
kuviridhisha vyombo vingi vikiwemo vya Serekali kwamba uchaguzi wa
Sheikh Mkuu mpya wa BAKWATA umefuata misingi ya kidemokrasia kama
inavyoeleweka na Serekali na umeendeshwa kama katiba ya BAKWATA
inavotaka. Lakini muhimu ni kukumbuka kwamba wale Waislamu
wanaoongozwa na BAKWATA watambue kwamba wamepata nafasi nzuri adimu
sana ya kuweza kubadili mwenendo mzima wa utawala wa chama chao.
Mabadiliko ambayo yataweza kuwavutia labda Waislamu wengi, kama sio
wote wa Tanzania. Uje utawala ambao hakika utaleta maendeleo muhimu
na makubwa kwa Uislamu na Waislamu wa Tanzania.
Hapo BAKWATA itaweza kupata heshima kubwa sana labda miongoni
mwa Waislamu wote wa Tanzania na bila kuwaudhi wale wanaosemekana
kuwa ndio wenyewe.
ALIYEKUWA Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA), Al-Marhuum Sheikh Issa Shaaban bin Simba .
-
10 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 2015Makala
Inaendelea Uk. 12
TANGU enzi za kale jeshi lilikuwa na haja ya msaada wa
miundombinu ili kuweza kutekeleza aina yoyote ile ya shughuli za
kijeshi la uwanda mpana. Katika Roma ya zamani, mtandao mkubwa wa b
a r a b a r a u l i j e n g wa kuwezesha siyo biashara peke yake,
bali kuruhusu vikosi vya majeshi ya Roma kwenda haraka m a h a l i
wa l i p o k u wa w a n a h i t a j i w a . , n a kuwasilisha
mahitaji kwa ajili ya shighuli za kijeshi kufuatilia uwasilishaji
huo.
Kuelekea mwisho wa karne ya 18, jemadari wa Ufaransa, bingwa wa
mikakati ya kijeshi na kiongozi, Napoleon Bonaparte akaainisha kuwa
"jeshi linatembea kwa tumbo lake," akielezea upana wa miundombinu
unaohitajiwa kuwezesha jeshi kuwa na chakula cha kutosha, na hivyo
kuwa na uwezo wa kudumisha k i wa n g o c h a k e c h a kuendesha
mapigano.
K w a W a f a r a n s a , kushindwa kupeleka vifaa
vinavyohitajiwa kwa wakati kwa majeshi yake yaliyokuwa yakipigana
nchini Russia, na maamuzi ya Warussia kuchoma ardhi yao na
miundombinu ili isitumiwe na majeshi ya wavamizi, mwishowe
iliwezesha kushindwa kwa Wafaransa.
Ujerumani ya ki-Nazi ilifikia hatma hiyo hiyo wakati ilipotanua
vile vile kupita kiasi uwezo wake wa miundombinu wa k a t i wa u va
m i z i wake wa Russia katika Operation Barbarossa. Kama awali ,
majeshi ya uvamizi yalikwama yakiwa na uhaba wa vifaa kabla ya
kuzingirwa n a k u t e k e t e z w a a u kulazimishwa kurudi
nyuma.
Na katika nyakati za karibuni wakati wa Vita ya Ghuba mapema
miaka ya 1990, kuwepo kwa mkanda mrefu wa kuwasilisha vifaa kwa
majeshi ya Marekani ikijumlishwa na kutazamia kukutana n a s e h e
m u k u b w a
Darasa la Miundombinu: Ni wapi ISIS inapata bunduki zake?Na Tony
Cartalucci
Juni 10, 2015 - 'Mtandao wa Kupashana Habari'
'NEO'
ya majeshi ya Saddam Hussein, ilipunguza kasi ya uvamizi kasi
ambayo wengi walidhani ungefika Baghdad kama dhamira ya kisiasa
ingekuwepo. Nia ya kumpiga ilikuwepo, miundombinu ya kumpiga
ilikuwa hafifu.
M a f u n z o k u t o k a h i s t o r i a k w a k i a s i a m b
a c h o y a n a w e z a kuyakinishwa, yanaelekea kutokuwa na
undani, iwe ni kwa mbumbumbu a u u d a n g a n y i f u wa
kushangaza wa waweka sera na vyombo vya habari vya nchi za
Magharibi.
Miundombinu ya ISIS
Mfarakano mkubwa hivi sasa unaoiangamiza Mashariki ya Kati, hasa
katika nchi za Irak na Syria ambako kinachodaiwa ni 'Dola ya
Kiislamu\' (ISIS) kinajiendesha na papo hapo kupigana na kuyashinda
majeshi ya Syria, Lebanon, Irak na Iran, tunaambiwa, imejengwa kwa
miundombinu ya ulanguzi na malipo ya utekaji nyara.
Uwezo wa kupigana wa ISIS ni wa serikali kamili. Inashikilia
eneo pana linalosambaa kote Syria
na Irak na siyo tu inaweza kulinda kijeshi na kupanua eneo h i l
i , l ak in i ina raslimali za kulisimamia eneo hilo, na hata
raslimali za kutawala makundi ya wakazi wa maeneo hayo i l iyoteka
, Kwa wachambuzi wa masuala ya kijeshi, hasa washiriki wa zamani wa
majeshi ya nchi za Magharibi, pamoja na washir ik i wa vyombo vya
habari vya nchi za Magharibi waliokuwa katika misafara ya malori ya
kijeshi ya mizigo iliyohitajika kwa ajili ya uvamizi wa Irak miaka
ya 1990 na halafu
mwaka 2003 , l az ima watashangaa hayo malori ya ISIS yako wapi
leo. Kwa hali yoyote, kama raslimali za kuwezesha uwezo wa
kuendesha shughuli za kijeshi ulioonyeshwa na ISIS ulikuwa
unapatikana katika maeneo ya Syria na Irak pekee, basi kwa hakika
majeshi ya Syria na Irak yangekuwa na uwezo wa kupigana kama huo au
zaidi lakini kimsingi hawana.
Na ingekuwa njia za kupeleka vifaa za ISIS zipo ndani ya maeneo
hayo ya Syria na Irak, basi kwa hakika majeshi ya Syria na Irak
yangeweza kutumia wanachowazidi ISIS, ndege za kivita - kuvuruga
uwezo wa ISIS kutumia njia hizo.
Lakini yote hii haitokei na kuna sababu kwanini.
M a g a i d i n a s i l a h a z i l i z o a c h w a k a t i k a
uvamizi wa Libya mwaka 2011 hima zilihamishiwa Uturuki na halafu
Syria - zikisimamiwa na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Marekani na mashirika ya kijasusi huko Benghazi - kituo cha ugaidi
kwa miongo kadhaa. Njia za kuwasilisha vifaa za ISIS zinatokea pale
ambapo Syria na Irak hazina uwezo wa kupeleka vita vya anga.
Kuelekea kaskazini kwa mashirika wa NATO, U t u r u k i , n a k u s
i n i mashariki kwa washirika wa Marekani wa Jordan na Saudia. Nje
ya mipaka hii kuna mtandao wa miundombinu unaoenea ukanda mzima
ikiwa ni pamoja na Ulaya Mashariki na Afrika Kaskazini.
Gazet i la ki la s iku la London Telegraph l i k a t a n g a z a
k a t i k a m a k a l a m wa k a 2 0 1 3 kuwa CIA inaendesha kituo
cha kupeleka silaha hapo Benghazi wakati ubalozi (wa Marekani)
unashambuliwa. Ilinukuu shirika la utangazaji la Marekani, CNN
likisema kuwa timu-kazi ya CIA il ikuwa ikifanya kazi zake kando ya
ubalozi huo kuandaa mradi wa kupeleka makombora kutoka maghala ya
silaha ya Libya kuelekea kwa waasi nchini Syria.
Silaha pia zimetokea Ulaya Mashariki, kwa
MAMA Usamah (katikati) na wanawake wenzake wakiswalia jeneza la
mwanae.
MAMA yake Usamah (katikati) baada ya mkutano na waandishi wa
habari.
-
11 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 201511
AN-NUURMakala
Ugaidi kama tamthiliya
Vi t a d h i d i ya u g a i d i inaendelea kuwa habari yenye
mashiko na ufanisi katika kukusanya hisia za watu pande mbili
zinazohusika. "Ugaidi wa kimataifa ni taswira ya kubuni ambayo
imekolezwa na kuvurugwa na wanasiasa," anaainisha mwandishi
mchokozi wa Uingereza na mchambuzi, Adam Curtis.
"Ni wingu potofu la fikra ambalo limesambaa bila kuhojiwa
miongoni mwa serikali duniani kote, majeshi ya usalama na vyombo
vya habari."
Kisiasa, nchi za Magharibi zimetumia vita hii ya msalaba dhidi
ya magaidi kuhalalisha uvamizi angamizi mara kadhaa pamoja na
ukiukwaji wa haki za binadamu ndani ya nchi na ng'ambo. Pia
inavuna
Tamthiliya pevu ya vita dhidi ya ugaidiNa Peter Bloom
KIJANA Usamah wakati akiwa shuleni.
HIVI karibuni katika eneo la Boston, kijana mweusi wa Kiislamu
mwenye umri wa miaka 26, alipigwa risasi na kuuawa na maofisa wa
Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na Idara ya Polisi ya Boston
(BDP). Kama ilivyoonyeshwa siku iliyofuata, vyombo vikubwa vya
habari kwa haraka, kwa mhemko na bila kutafakari, vikarudia madai
ya utekelezaji wa sheria za nchi (mara nyingine hutumwa bila
msemaji kujitaja) kuhusu k i l i c h o t o k e a : k u wa mtu huyo
aliyekufa, Usaamah Rahim, alikuwa anakaribia kutekeleza mauaji
yanayotokana na ushabiki wake kwa ISIS au kwa kuhusika na kundi
hilo la kigaidi, k u w a k a t a v i c h w a maofisa wa polisi bila
mpangilio halisi, akiwa anashirikiana na takriban watu wawili
wengine. Wakati Rahim anatembea kwenda kazini karibu na duka la
dawa la CVS majira ya saa moja asubuhi, maofisa hao wa polisi
walimfuata Rahim kumuuliza tu kuhusu
Maswali tata yatanda kuhusu kuuawa Boston kwa 'mkata kichwa' wa
ISISGlenn Greenwalld na Murtaza Hussain
mpango huo; ghafla, akatoa 'sime' au 'kisu cha kijeshi' ambacho
alikataa kukiangusha, na kuwalazimisha maofisa hao kumpiga r i sas
i
kichwani.K u l i k u wa n a k i l a
a i n a ya m a s wa l i ya wa z i ya s i y o e l e we k a kuhusu
madai haya , n a b a d o y a l i a c h w a
tu na kilichosikika ni k i w e w e k u w a ' I S I S iko
Massachusetts!' na m i h a n g a i k o m i n g i kuhusu watu
kukatwa vichwa. Hii ni moja ya mambo yanayosumbua sana kuhusu tukio
hili: polisi sasa wanaweza k u m s i m a m i s h a m t u b a r a b
a r a n i a m b a y e , kwa ushahidi wowote uliopo, hakuwa anafanya
lolote baya wakati huo, wamwue, halafu wapaze sauti tu "ISIS' na
'Gaidi' na 'kukatwa kichwa' n a k u r u d i a r u d i a n a hakuna
maswali yoyote yatakayoulizwa.
K u w a s h a w i s h i waandishi wa habari wakubali madai yao,
FBI na BDP walisisitiza kuwa kulikuwa na mkanda wa kamera ya
ufuatiliaji ambao ungeondoa shaka kuhusu ki l ichotokea, wakidai
kuwa "ufuatiliaji kwa kamera ya video u m e d h i h i r i s h a k i
l e maofisa walichosema." L a k i n i h a w a k u t o a mkanda huo,
na badala yake wakatumia karibu wiki mbili kulainisha na kuvuruga
akili za watu kwa kurudia madai kuhusu kile ambacho video hiyo
ambayo haijaonekana inachoonyesha.
Video hiyo mwishowe
ilitolewa. Kuiita video hiyo kuwa ni kichekesho, ingekuwa
upendeleo. Kamera ipo umbali wa mita 50 kutoka tukio l i l
ipotokea. Kioo cha kamera kimefichwa na matone ya mvua. Viwiliwili
vya watu vinatambulika kwa taabu. Hakuna silaha zinazoonekana,
ikiwa ni pamoja na silaha yoyote aliyokuwa nayo Rahim. Wa k a t i i
n a o n y e s h a kuwa Rahim hakupigwa risasi kwa nyuma kama kaka
yake alivyosema mwanzo (na baadaye akakiri kuwa hakuwa na ufahamu
sahih i ) , ha ionyesh i chochote k ingine . Kwa jumla , ha
iwezekani kusema nini kilitokea kutokana na video hii iliyopigiwa
chapuo sana , n je ya kuwa Rahim anaonekana alikuwa akitembea kwa
amani wakati alipofuatwa na watu kadhaa, ambao hawakuwa wamevaa
sare za polisi, katika mfumo wa kutishia, kijeshi:
Vyombo vya habari vilivyokuwa vinaikuza v i d e o h i y o k a m
a uthibitisho wa kile polisi wa l i c h o s e m a h a r a k a
wakaona kuwa inaonyesha kinyume chake. "Kutoa
faida isiyo ya kawaida ya fedha ambayo hatua hizo za uvamizi
zimewezesha baadhi ya makundi yenye nguvu ya maslahi katika nchi za
Magharibi.
Wakati huo huo, serikali za nchi za Magharibi na makundi ya
kiharakat i sawia yameendelea kutumia uzungumzaji huu kuelekea
malengo yao ya kisiasa na kiuchumi. Usawiri wa Vita dhidi ya Ugaidi
kama mapambano ya kimataifa "imefanya hata mashambulizi ya kigaidi
ya ndani ya nchi kuonekana kama sehemu ya mapambano haya mapana."
Kinacholeta wasiwasi kwa kiasi kikubwa pia ni kuwa mitandao hii ya
kimataifa i n a e n d e l e a k w a k a s i kubadilika kuwa
jitihada ya kuunda 'Dola ya Kiislamu (bandia)' ya kudumu katika o m
b we l i l i l o a c h wa n a uvamizi wa Marekani nchini Irak.
Pia, inabidi iainishwe kuwa kuuawa kwa Osama bin Laden na
kupunguzwa kwa kiasi kikubwa nguvu za Al Qaeda kama taaisi ya
kisiasa na kijeshi, haijaifikisha v i t a h i i k a t i k a t a m a
t i yake. Badala ya kufunga mitiririko ya fedha za vita, sasa kuna
"maadui" wapya kama ISIS ambao lazima wateketezwe. Vita dhidi ya
ugaidi imeondoka katika mfumo wa sinema kubwa ya mamilioni ya dola
za Marekani na kuwa mtiriririko wa tenda unaolipiwa kwa damu na
dhahabu.
Mpango halisi ni kuwa hakuna mpango kama huo. Ni ukweli
unaoonekana kuwa nchi za Magharibi na makundi ya washirika ni heri
waendeleze tamthiliya k u h u s u u g a i d i k u l i k o k u r u h
u s u n g u v u z a k e za kiuchumi na kisiasa kuingizwa mashakani
kwa kiwango kikubwa. Marekani
Inaendelea Uk. 17
na washirika wake wanaamini kuwa wanaweza kutesa, kuvamia, kuua,
kukandamiza na kulitumia tatizo hili la ugaidi lisionekane; kuwa
kinachohitajika tu ni kuua na kupiga marufuku wanasiasa kali wa
kutosha na ustawi wake (bila kuzungumzia kuendelea kui tamalaki
dunia) utahakikishwa.
Kinachotakiwa sasa ni habari mpya ya tumaini na harakati -
ambayo haitokani na hadithi tupu zenye vitendo vya kiharamia,
ambako taifa lenye nguvu zaidi ndiyo bora zaidi kimaadili, ila
ambalo badala yake linaangalia kwa ukweli nini kinachojificha nyuma
ya uhar ib i fu huu i l i kutekeleza mabadiliko ya kina kwa ajili
ya ustawi wa pamoja na uhuru halisi wa kisiasa.
T u n a c h o h i t a j i n i m t i r i r i k o w a f i k r a
ambacho kinachosukuma
maendeleo haya siyo taifa la kibeberu linaloendeleza vita ya
msalaba lenye dhamira isiyopindika ya kufikia 'haki' yake ya
kisasi, lakini makundi ya kidemokrasia na haki za kijamii
yakiunganika pamoja kubadili dunia kutoka chini hadi juu.
Bila kujali Bin Laden alikufa kwa njia gani, Vita dhidi ya
Ugaidi ndiyo hasa 'tamthiliya' inayohuzunisha.
(Hii ni sehemu ya makala Fairy Tale of the War on Terror kama
ilivyoandikwa na Peter Bloom. Peter Bloom ni mhadhiri katika Idara
ya Watu na Taasisi katika C h u o K i k u u H u r i a . Anaandika
katika fani za i t ikadi , mamlaka na siasa za ubepari na hivi sasa
anakamilisha tungo kuhusu 'Ubepari wa Ki imla Zama za
Utandawazi.')
-
12 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2, 201512
MAKALA
SWAUMU NA NDIMI ZETUUlimi tunu adhimu, ya MANANI kwa
insani,Ulimi tangu kadimu, kwa uneni namba 'wani',Ulimi MWEMA
mwalimu, na MUOVU kwa waneni,NDIMI zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI
Ramadhani.
Ulimi johari njema, tukufu yenye thamani,Ulimi kwa watu wema, u
lulu na marijani,Ulimi kwa taadhima, kwa kweli wakuthamini,NDIMI
zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi wainajisi, waovu yako thamani, Ulimi wanakutusi, kwa
kukupa sui nduni,Ulimi u IBILISI, eti mkubwa SHETANI,NDIMI zetu
TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi u sura mbili, kwa ya INSAFU mizani,Ulimi anokujali, kwa
KHERI wamuauni,Ulimi asokujali, kwa SHARI haumukhini,NDIMI zetu
TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi sasa kwanini, tuutie lawamani,Ulimi mimi sioni, ulaumiwe
kwanini,Ulimi kosale nini, nijuzeni ikhiwani,NDIMI zetu TUCHUNGENI,
WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi wa RAMADHANI, WAFUNGAJI uchungeni,Ulimi kwa QUR-ANI,
KUSOMA utumieni,Ulimi za ADINANI, kwao HADITHI someni,NDIMI zetu
TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi utumieni, kumdhukuru MANANI,Ulimi uzuieni, kuwasengenya
INSANI,Ulimi ukalifuni, mema unene JAMANI,NDIMI zetu TUCHUNGENI,
WAFUNGAJI Ramadhani.
Ulimi nanezo beti, zimefika ukingoni, Ulimi kwa KHAIRATI,
nifanye MWENZO mwandaniUlimi kwa SHURURATI, uwe ADUI mubini,NDIMI
zetu TUCHUNGENI, WAFUNGAJI Ramadhani
ABUU NYAMKOMOGI MWANZA
1.Leo naja na shauri , tusikilize usiaNi maneno ya Ghafuri,
yasiyopatwa na doaTukajitia kiburi, mwisho wetu ni balaaHalali
halali yetu, haramu tuikimbie
2.Mola ametudhukuri, bure hakutuachiaKatufunza ya fakhari, vya
halali kutumiaHaramu na vitu shari, laana vimetiliwaHalali halali
yetu, haramu tuichukie
3. Halali kitu kizuri, Allah ametuleteaHalali haina siri,
kweupeni hutokeaHalali hua dhahiri, haijifichi na juaHalali halali
yetu, haramu ichukieni
4.Tuitafute halali, popote ilipokaaIkibidi kwenda mbali, pembe
zote za duniaGharama tusizijali, muhimu ni manufaaHalali halali
yetu, haramu tuichukie
5. Haramu tusijadili, haifai kutumiaHaramu kwetu dajali, Mola
hakuiridhiaHaramu japo ni mali, acha ndugu nakwambiaHalali halai
yetu, haramu tuichukie
6. Halali iwe awali, tunapo pambaukiwaIsijekuwa ya pili, kinyume
tukachaguaHayo nayo tuyajali, yafaa kuzingatiwaHalali halali yetu,
haramu tuichukie
7. Machumo tutafakari, kabla ya kuchukuaTunakokwenda shubiri, na
muda umewadiaTukijifanya ayari, moto unatungojeaHalali halali yetu,
haramu ichukieni
8. Yatosha nilohubiri, ndugu kuwafikishiaYapo kwenye mstari, na
hayaja expireSi ya kale yalojiri, bado yanaendeleaHalali halali
yetu, haramu tuichukie
Mtunzi ni:-Zainab H. Mtima
Mbweni, Zanzibar0717 165 602
HALALI NA HARAMU
Darasa la Miundombinu: Ni wapi ISIS inapata bunduki zake?Inatoka
Uk. 10
mfano gazeti la New York Times likitoa taarifa mwaka 2013 katika
makala "Upelekaji wa silaha kwa waasi wa Syria wapanuka, kwa msaada
wa CIA," kwamba:
Kutoka katika ofisi za siri, maofisa wa kijasusi wa Marekani
wamesaidia serikali za nchi za Kiarabu kununua silaha, ikiwa ni
pamoja na manunuzi makubwa kutoka Croatia, na wamewapa kibal i
makamanda na vikundi vya waasi kuamua nani achukue s i laha hizo
wakati zikiwasili, kwa mujibu wa maofisa wa Marekani wakizungumza
kwa sharti la kutokutajwa.
Na wakati mashirika ya habari ya nchi za Magharibi wakati wote
yanazungumzia ISIS na makundi mengine yanayoendesha shughuli zao
chini ya mwavuli wa Al Qaeda kama 'waasi' au 'wenye siasa za
wastani,' ni wazi kama silaha zenye thamani ya mabilioni ya dola za
Marekani zinaelekezwa kwa 'wenye siasa za wastani,'ni wao, n a s i
y o I S I S a m b a o wangetamalaki katika eneo hilo.
Ta a r i f a z i l i z o v u j a s i k u z a k a r i b u n i
zilisema kuwa kuanzia mapema 2012 Wizara ya Ulinzi ya Marekani siyo
tu ilianza kuweka mkakati wa kuundwa kwa 'eneo la kisultani la
Salafi' linaloenea nchi za 'Syria na Irak, eneo ambalo hasa ndiyo
ISIS i l iko, i la i l ikaribisha ISIS kwa mikono miwili na
kuchangia kujenga mazingira yaliyoiwezesha kuzuka.
Njia za uwasilishaji vifaa za ISIS ni pana kiasi gani?
Wakati wadadisi wengi katika nchi za Magharibi wanapendelea
kusema kuwa hawajui ISIS hasa inapata mahitaji yake kutoka wapi ili
iweze k u e n d e l e z a u w a z o wake wa kushangaza wa kupigana,
baadhi ya waandishi wa habari wametembelea eneo hilo na kuchukua
picha na maelezo na kutoa taarifa
za milolongo ya magari ya vifaa yanayofikishwa kwa majeshi ya
kigaidi. Magari hayo yalikuwa yanatokea katika viwanda katika
maeneo yanayoshikiliwa na ISIS ndani kabisa ya nchi za Syria na
Irak? Katu. Yalikuwa yanatokea ndani kabisa ya Uturuki, kuvuka
mpaka wa Syria bila kusumbuliwa na kitu chochote, na kuendelea na
njia yake yakiwa na ulinzi usio rasmi wa vikosi vya majeshi ya
Uturuki hapo kando.
Majaribio ya Syria kushambulia misafara h i i n a m a g a i d i
wanaomiminika pamoja nayo, yamekabiliwa vikali na ulinzi wa anga wa
Uturuki.
Shirika la Utangazaji la Ujerumani, Deutsche We l l e ( D W ) l
i l i t o a mkanda wa sauti wa kwanza kutoka kianzio muhimu cha
habari nchi za Magharibi kuonyesha kuwa ISIS inapata vifaa siyo
kutoka 'ulanguzi wa mafuta' au 'malipo ya utekaji nyara', ila ni
vifaa vyenye thamani ya mabilioni ya dola za Marekani
vinavyopelekwa Syria kupitia mipaka ya mwanachama wa NATO, Uturuki,
kwa njia ya mamia ya malori kwa siku.
Ripot i h iyo yenye kichwa cha habari "Njia za kupokea vifaa za
ISIS kupitia Uturuki," i n a y a k i n i s h a k i l e ambacho
kilishatajwa na wachunguzi wa ramani ya kisiasa kuanzia hata 2001 -
kuwa ISIS inaishi kwa ufadhili mkubwa wa nchi kadhaa, ikiwemo bila
shaka, Uturuki yenyewe.
Ukiangalia ramani ya maeneo yaliyoshikwa n a I S I S n a k u s o
m a taarifa za mapito yake na mashambulizi kote katika ukanda huo
na hata mbali zaidi, mtu a n a w e z a k u d h a n i a kuwa mamia
ya malori kwa siku yangehitajika kuwezesha kiwango hiki cha uwezo
wa kupigana. Mtu angeweza kufikiria misa fara kama h iyo ikiingia
Irak kutoka Jordan na Saudia. Misafara kama hiyo ingeweza kuingia
Syria kutoka Jordan.
Kwa jumla, ukizingatia hali halisi ya miundombinu n a u m u h i
m u w a k e usioisha kwa kampeni za kijeshi katika historia y o t e
y a b i n a d a m u , hakuna maelezo mengine yanayokidhi kuhusu
uwezo wa ISIS kuendesha vita ndani ya Syria na Iraq, nje ya kiwango
kikubwa cha raslimali kinachopelekwa kwake kutoka ng'ambo.
Kama jeshi linatembea kwa tumbo lake , na tumbo la ISIS limejaa
vifaa kutoka NATO na nchi za Ghuba, ISIS itaendelea kutembea moto
mdundo kwa muda mrefu. Kiini cha kuweza kuvunja nguvu za ISIS ni
kuvunja uti wa mgongo wa njia zake za kupokea vifaa. Kufanya hivyo
hata hivyo, na ndiyo maana mgogoro huu umeendelea kwa muda mrefu,
Syria, Irak, Iran na wengine ingebidi hatimaye wafunge mipaka na
kuwalazimisha ISIS kupigana ndani ya mipaka ya Uturuki, Jordan na
Saudia, mkakati mgumu kuufikia kwani nchi kama Uturuki zimeunda
maeneo ya kujihami ya kudumu ndani ya Syria a m b a y o ya n g e h
i t a j i mkabiliano wa ana kwa ana na Uturuki yenyewe ili
kuyaondoa.
Huku Iran ikiingia katika mapambano hayo kwa kuhamisha maelfu ya
askari kuinua operesheni za kijeshi za Syria, kanuni muhimu za t
ishio la usalama zinaweza kuizuia Uturuki kutumia kwa dhamira
halisi maeneo hayo ya kujihami.
Tul ichobaki nacho wakati huu, ni NATO kimsingi ikiwa
imeshikilia eneo hilo nyara kwa u we z e k a n o wa v i t a mbaya
sana ya kikanda katika juhudi za kulinda na kuendeleza uharibifu u
l i o f a n y wa n a I S I S ndani ya Syria, ikiwa imefadhiliwa
kikamilifu kwa mtandao mkubwa wa miundombinu ikitoa katika maeneo
ya NATO.
( T o n y C a r t a l u c c i , anayeishi Bangkok, Thailand, ni
mtafiti wa ramani za kisiasa na mwandishi, hasa kwa jarida la
mtandao, "New Eastern Outlook.' Makala hii imetafsiriwa Kiswahili
na Anil Kija.)
-
13 AN-NUURRAMADHAN 1436, IJUMAA JUNI 26- Julai 2,
2015MAKALA/Matangazo
Hakuna jengo la Msikiti wala Madrasa, kuna kiwanja kilichotolewa
(WAQFU) miaka mitatu iliyopita. wanafunzi wanasomea Quran katika
majani kama wanavyoonekana katika picha. Pamoja na kuisoma Quran
katika mazingira magumu, lakini kwa kuwa huu ni mwezi wa Quran,
tumeandaa mashindano ya kuhifadhi Quran kwa vijana wote wa eneo la
Hondogo na maeneo ya jirani kuanzia Ramadhan 10-17. Lakini hatuna
mdhamini wa kutuwezesha zawadi kwa washindi watakaopatikana katika
shindano hilo.Hivyo basi tunaomba mchango wako wa chochote ulicho
nacho ili tununue zawadi kwa ajili ya watoto hao na kuzidi kuwatia
moyo na kuwa na mapenzi na Quran yao.kwa mawasiliano zaidi tupigie
simu No. 0715 259635 au 0757 375993
CHANGIA MASHINDANO YA QURAN AL MADRASATIL FADHAKIR HONDOGO
DAR
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), imeandaa Dua maalumu,
itakayowashirikisha Waislamu wote leo siku ya IJUMAA, katika
Msikiti wa Mtambani, Kinondoni.Waislamu wametakiwa kushiriki kwa
wingi ili kumlilia Allah (s.w) ndani ya Mwezi huu Mtukufu wa
Ramadhani kwa kuzingatia uzito na utufukufu wake, hii ni kufuatia
kadhia mbalimbali walizokutana nazo kabla ya Mwezi huu.Pia Viongozi
wa Jumuiya (Masheikh) watazungumzia: Waislamu na uchaguzi Mkuu wa
Urais na Madiwani.Dua itaanza mara baada ya mshuko wa Ibada ya
Swala ya Ijumaa, Msikitini hapo.
Sheikh Rajab Katimba.
Dua Maalum Masjidi Mtambani (Leo)
KUTOA ni jambo gumu sana kwa mwanadamu h a s a i w a p o n i k i
t u anachokipenda. Na vilevile ni jambo linalopendwa sana na
Uislamu. Kwa ajili hii, ndio tunaona kuwa Uislamu umelitilia nguvu
sana jambo hili na kuliandalia malipo makubwa.
Allah SW amelipangia njia tofauti jambo hili kwa kumfanya mtu
wepesi wa kumfanya na asiwe bakhili na hili ni kwa kumuekea njia ya
wajibu na njia za suna. Hakika kutoa kumeandaliwa malipo makubwa
ambayo ni tofauti na ibada nyengine na hili lipowazi.
Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu, ni
kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila
shuke zimo punje mia. Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na
Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua. (2:261.
Hili ni moja miongoni m w a f a i d a n y i n g i zipatikanazo
kwa kutoa sadaka. Nyengine miongoni mwa faida hizo, nikujenga
mahaba na mapenzi kati ya wanaopeana. Ndio Mtume SAW alivyozijenga
imani za Masahaba mpaka zikafikia daraja ya kupendana na kupeana
bila kujali, huku wakitarajia malipo makubwa mbele ya Allah SW.
Jambo hili la kutoa kwa hakika lina faida nyingi kubwa zaidi
katika hizo ni kufunikwa na kivuli cha Arshi ya Allah SW siku
ambayo hapatakuwa na kivuli ila hicho. Nayo ni s iku ya Kiama
ambapo jua litawakaribia viumbe kiasi ya shubiri moja juu ya vichwa
vyao. Kwenye hadithi iliopokewa na Imam Bukhari na Muslim
wamelezewa watu wa aiana 7 watakao funikwa nna kivuli hicho, mmoja
wao ni mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka ikafika kutojua mkono wa
kushoto kilichotoa mkono wa kulia.
Jambo hili tukufu tunapata fursa ya kujifunza katika mwezi huu
mtukufu wa Ramadhani na inapomalizika Ramadhani hugeuka hali zetu
tukawa wagumu wa kutoa kama kwamba wale waliokuwa wakitoa katika
mwezi wa Ramdhani sio sisi bali ni watu wengine. Inatakiwa kwa
Muislamu kuwa mwepesi wa kutoa kwani kila unachokitoa kwa a j i l i
ya Al lah SW h u wa h u j a p o t e z a b a l i ni akiba kubwa
ambayo umejiwekea ya kukusaidia siku ambayo hapana cha kukusaidia
isipokuwa kile u l i c h o k i t a n g u l i z a k wa mikono
yako.
Kuwa na subiraMuislamu anatakiwa
kuwa mwenye kusubiri baala zote zinazomkumba katika maisha yake
ya hapa duniani, kwa kiasi kile ambacho Muislamu anachokumbwa na
balaa na mitihani na akasubiri, ndio huwa daraja yake inapanda
mbele ya Allah SW. Ndio kwa maana hii akasema Mtume SAW:
Allah anapowapenda waja wake, huwajaribu kwa kuwapatia mitihani
ya kila
Ramadhani ni Darasa -Kutoa sadakaaina.
Na hili ni moja miongoni mwa faida nyingi zipatikazo katika
kusubiri kwa kuwa karibu na Allah SW hii ni faida nyengine
inayopatikana kwa kusubiri kwani Muislamu kiasi ambacho atakuwa ni
mwenye kumkumbuka Allah SW wakati wa raha hailingani na kiasi
atakavyo mja kumkumbuka Allah SW wakati atakapo kuwa na matatizo
kisha akawa ni mwenye kusubiri huku akifahanu wazi kuwa yote ni
yake yeye Allah SW, Hakika Allah y