Top Banner
al-Masa'ilu 'l-Islamiyyah (Sheria za Kiislamu) Kwa Mujibu wa Fatwa za Ayatullah al-Udhma Sayyid Sadiq Husaini Shirazi Mtarjumi: Abdul Karim J. Nkusui Kimechapishwa na: Ahlul Bayt Centre (ABC) S.L.P. - 7169, Arusha. Tanzania na Sayed Al-Shohada Charitable Committee S.L.P. - 15338, Kuwait
300

al-Masailu-l-Islamiyyah

Mar 30, 2016

Download

Documents

Ayatullah Shirazi amekua na kupambika umri wake kwa moyo wa ikhlasi, ucha Mungu, amali na fikra njema zinazokwenda sambamba na mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Ahlul Bait (a.s.).
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: al-Masailu-l-Islamiyyah

al-Masa'ilu 'l-Islamiyyah(Sheria za Kiislamu)

Kwa Mujibu wa Fatwa za

Ayatullah al-Udhma

Sayyid Sadiq Husaini Shirazi

Mtarjumi:

Abdul Karim J. Nkusui

Kimechapishwa na:

Ahlul Bayt Centre (ABC)

S.L.P. - 7169, Arusha. Tanzania

na

Sayed Al-Shohada Charitable Committee

S.L.P. - 15338, Kuwait

Page 2: al-Masailu-l-Islamiyyah

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:

Sayed Al-Shohadaa Charitable Committee

Kimetafsiriwa na:

Ustadh Abdul-Karim Nkusui

Barua Pepe: [email protected]

Toleo la kwanza: Augasti, 2008

Nakala: 3000

Kimechapishwa na:

Ahlul Bayt Centre (ABC)

S.L.P. - 7169, Arusha. Tanzania

na

Sayed Al-Shohada Charitable Committee

S.L.P. - 15338, Kuwait

Simu: +965 255 2560

Nukushi: +965 963 5403

DA’IYYAH - KUWAIT

Page 3: al-Masailu-l-Islamiyyah

YALIYOMO

Hukumu za Taqlid. “ Kufuata”.........................................................2

Hukumu za Tohara............................................................................6

Hukumu za Maji..............................................................................11

Hukumu za kujisaidia......................................................................13

Istibra...............................................................................................16

Adabu za kujisaidia.........................................................................17

Najisi...............................................................................................18

Njia za kuthibitisha Najisi...............................................................25

Namna ya kunajisika vitu vilivyo Tohara........................................26

Mas’ala............................................................................................28

Vinavyotoharisha.............................................................................30

Kupungua theluthi mbili za juisi ya zabibu mbivu.........................34

Hukumu za vyombo.........................................................................39

Kuosha mikono miwili....................................................................40

Kupaka kichwa................................................................................41

Kupaka miguu mwili.......................................................................41

Udhu wa Irtimasi “kuzamisha”........................................................42

Masharti ya udhu.............................................................................43

Hukumu za udhu..............................................................................45

Page 4: al-Masailu-l-Islamiyyah

D

Al-Masailul Islamiyah

Mambo ambayo yanapasa udhu.....................................................47

Vinavyobatilisha udhu.....................................................................48

Hukumu za udhu wa Jabirah (Bandeji)...........................................48

Josho za wajibu................................................................................49

Hukumu za Janaba...........................................................................50

Mambo ambayo ni haramu kwa mwenye Janaba...........................51

Mambo yaliyo makuruhu kwa mwenye Janaba..............................52

Mas’ala katika kuoga Janaba.........................................................53

Josho la mpangilio...........................................................................53

Josho la kuzama...............................................................................55

Hukumu za kuoga............................................................................55

Istihadha........................................................................................ . 58

Hukumu za Istihadha...................................................................... 59

Hedhi...............................................................................................65

Hukumu za Hedhi........................................................................... 68

Vigawanyo vya Hedhi.....................................................................72

Wenye Ada ya wakati na Idadi....................................................... 73

Nifasi.............................................................................................. 84

Kuoga josho la kugusa maiti...........................................................86

Hukumu za muhtadhari “anayekata roho”.......................................88

Hukumu baada ya mauti................................................................. 89

Page 5: al-Masailu-l-Islamiyyah

E

Al-Masailul Islamiyah

Hukumu za kuosha maiti.................................................................91

Hukumu za kumkafini maiti............................................................93

Hukumu za tahaniti “kupaka”..........................................................95

Hukumu za swala ya maiti...............................................................95

Namna ya kuswali swala ya maiti...................................................97

Yaliyo Sunna katika swala ya maiti................................................98

Hukumu za kuzika...........................................................................99

Tayamamu.....................................................................................105

Hukumu za swala...........................................................................110

Swala za wajibu.............................................................................111

Swala za wajibu za kila siku......................................................... 111

Wakati wa Swala ya Adhuhuri na Alasiri..................................... 112

Wakati wa Swala ya Magharibi na Isha....................................... 113

Wakati wa swala ya Asubuhi.........................................................113

Hukumu za wakati wa swala ....................................................... 115

Swala za Sunna..............................................................................119

Swala ya Usiku..............................................................................120

Swala ya Ghufaila......................................................................... 121

Hukumu za Kibla...........................................................................121

Kusitiri mwili katika Swala...........................................................122

Page 6: al-Masailu-l-Islamiyyah

Masharti ya vazi la mwenye kuswali............................................123

Sharti la kwanza...........................................................................123

Sharti la pili..................................................................................124

Sharti la tatu..................................................................................125

Sharti la nne..................................................................................125

Sharti la tano.................................................................................126

Sharti la sita..................................................................................127

Sehemu ambazo hazilamu tohara ya mwaili wa mwenye kuswali.127

Yaliyosunna katika vazi la mwenye kuswali.................................129

Yaliyo makuruhu katika vazi la mwenye kuswali.........................129

Sehemu ya mwenye kuswalio.......................................................129

Shari la kwanza..............................................................................130

Sharti la pili...................................................................................130

Sharti la tatu...................................................................................131

Sharti la nne...................................................................................131

Sharti la tano..................................................................................131

Sharti la sita...................................................................................131

Sharti la saba..................................................................................131

Sharti la nene.................................................................................132

Sharti la tisa...................................................................................132

Hukumu za misikiti. .................................................................... 133

F

Page 7: al-Masailu-l-Islamiyyah

Sharti la tano

Takbira ya kuhirimia swala.......................................................... 138

Sehemu Ambazo ni wajibu kukata Swala................................... 158

Shaka.............................................................................................157

Shaka zisizotiliwa maanani...........................................................160

Shaka ya kitu baada ya kupita sehemu yake.................................160

Shaka baada ya salamu..................................................................163

Mwingi wa shaka...........................................................................163

Shaka ya Imamu na Maamuma.....................................................163

Shaka zisizobatilisha swala........................................................... 167

Swala ya Ihtiyati............................................................................171

Sijida ya kusahau......................................................................... 172

Namna ya kuleta sijida ya kusahau.............................................. 174

Swala ya msafiri............................................................................176

Hukumu za makazi na kukaa siku kumi...................................... 183

Wajibu wa mtoto mkubwa kulipa swala zilizowapita wazazi waw-

ili....................................................................................................188

Swala ya Jamaa..............................................................................190

Hukumu za Jamaa......................................................................... 192

Sunna za swala ya Jamaa...............................................................193

Swala ya majanga..........................................................................197

G

Page 8: al-Masailu-l-Islamiyyah

Swala ya majanga..........................................................................197

Swala ya Idd mbili “Al-fitri na Al-adhihaa”.................................200

Hukumu za Saumu.........................................................................202

Panyeto”Kuchezea utupu”.............................................................207

Kumzulia uongo Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na Maimamu

(a.s)................................................................................................207

Kufika vumbi zito kwenye koo.................................................... 209

Kuzamisha kichwa kwenye maji...................................................210

Kubaki na Janaba au hedhi au Nifasi mpaka Alfajiri...................211

Hukumu ya vitenguzi.....................................................................216

Mambo ambayo ni wajibu kupa kadhaa na kutoa kafara...............217

Kafara za Saumu...........................................................................217

Mambo ambayo ni wajibu kulipa kadha ya saumu bila kafara......220

Hukumu za Saumu ya kadhaa....................................................... 222

Hukumu za Saumu ya msafiri........................................................224

Njia za kuthibiti mwanzo wa mwezi............................................226

Saumu ambazo ni Haramu na makuruhu ....................................277

Hukumu za Khumsi.......................................................................230

Hukumu za Zaka............................................................................231

Hukumu za Hija.............................................................................235

Umra Tamatui................................................................................238

H

Page 9: al-Masailu-l-Islamiyyah

Umra ya Mufrad............................................................................245

Hukumu za ndoa........................................................................... 248

Hukumu za Talaka.........................................................................260

Hukumu za kuchinja mnyama na kumuwinda kwake.................. 265

Njia ya kisheria ya kuchinja..........................................................266

Masharti ya kuchinja ....................................................................267

Hukumu za kuwinda kwa silaha...................................................269

Hukumu za kula na kunywa..........................................................273

Mambo ya Sunna wakati wa kula.................................................274

Hukumu za miradhi.......................................................................277

Talaqin ya maiti.............................................................................283

I

Page 10: al-Masailu-l-Islamiyyah

UTANGULIZI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehe-

mu, rehema na amani zimwendee kipenzi chetu Mtume Muhammad

(saww) na Aali zake wema, ama baad.

Taasisi ya Sayed Shohadaa (as) kwa moyo mkunjufu na furaha

kubwa inawaletea wasomaji wa lugha ya Kiswahili na hususan

kuitajirisha maktaba ya Kiswahili kwa Muhtasari wa Sharia ya

Kiislam kwa mujibu wa fat’wa za Ayatollah Al - Udhmaa As Sayed

Swadiq Al-Hussein As Shirazi - Mwenyezi Mungu aidumishe kazi

yake.

Tarjama hii ilioko mikononi mwako ni matunda ya jitihada na juhu-

di kubwa za waalimu wa Madrasatul - Wahdah Singida ambao

wametumia muda wao mwingi ili kufanikisha kazi hii nzuri; Kwa

hawa na kwa kila aliyeshiriki kwa namna moja au nyingine katika

kufanikisha kazi hii tunatoa shukrani zetu za dhati na tunawaombea

kila la kheri kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu awalipe malipo mema.

Imamu Swadiq Shirazi ametumia lugha rahisi na nyepesi jambo

ambalo tunamatumaini kuwa litawasaidia wasomaji na kuwafanyia

sahali katika kufuatilia na kujua hukumu za mas’ala ambayo aghlabu

wanayahitajia katika maisha yao ya kila siku bila ya ugumu wowote.

Tarjama hii imetoa kipaumbele katika mas’ala ambayo ni muhimu

zaidi kwa waumini ili kuwarahisishia kujua Sharia ya dini yao husu-

san mas’ala ya Swala, saumu, ndoa, talaka, mirathi n.k. Ni matara-

jio yetu kuwa wasomaji wetu watakipokea kwa mikono miwili na

J

Al-Masailul Islamiyah

Page 11: al-Masailu-l-Islamiyyah

watanufaika kwa kupata utatuzi wa mas’ala mengi mbali mbali kwa

njia nyepesi zaidi.

Tarjama hii haikuzingatia utaratibu wa namba za mas’ala kama

yalivyo katika kitabu cha asili bali mtiririko wa namba ni kulingana

na mas’ala yaliyochaguliwa, hivyo ukitaka kufuatilia lazima urejee

katika maudhui tajwa katika nakala ya asili ndio utajua namba ya

mas’ala husika. Nia yetu katika tarjama hii ni kutoa mas’ala ambayo

ni muhimu zaidi katika jamii pia hatukutaka kitabu kiwe ni kikubwa

sana.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atie wepesi na baraka katika kazi

hii ili iwafikie waumini kwa haraka kwani Yeye ndio mwenye

kuombwa msaada na taufiq

Wasalaam

S.S.Magwe

Sayed Shohadaa Trust

4 Rabiul Akhir 1428AH - 22 April 2007

K

Al-Masailul Islamiyah

Page 12: al-Masailu-l-Islamiyyah

L

DIBAJI

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema

Mwenye kurehemu.

Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe, rehema na

amani zimwendee kipenzi cha nyoyo zetu Mtume wetu Muhammad

(s.a.w.w.) na kizazi chake chema, masahaba wake na wote waliomfuata

kwa wema hadi Siku ya Kiyama.

SAYYED SHUHADAA CHARITABLE COMMITTEE ni taasisi ya

kidini inayojishughulisha na mambo ya waislamulimwenguni katika nyan-

ja mbalimbali za maisha yao ya kila siku. Pamoja na kujali sana mambo

ya waislamu pia inatoa kipaumbele katika suala la elimu kwa vijana wa

kiislamu na kuwaendeleza ili kuwajenga katika maadili mema ya kumtu-

mikia Mwenyezi Mungu na hatimaye wawe ni viongozi wazuri watakao-

hudumia jamii ya Kiislam na kuijenga kiroho, kimaadili na hatimaye

kuwawezesha kufikia lengo lao la kuwepo hapa dunia kwa wepesi.

Sambamba na hayo taasisi yetu pia inajishughulisha na mambo yafuatayo

katika jamii:-

- Ujenzi wa Miskiti

- Ujenzi wa Madrasa

- Kuwaangalia wazee wasiojiweza

- Kusaidia watoto yatima

- Kuwasaidia maskini

- Kutoa misaada ya kibinadamu wakati wa majanga

- Kukusanya na kugawa nudhur, kafara, chinjo katika mwezi wa Dhul-Hajj

na kutoa futari katika mwezi wa Ramadhani

- Kuendesha Majlis za Muharram na minasaba mbalimbali ya kidini kama

Page 13: al-Masailu-l-Islamiyyah

M

vile kuadhimisha Maulidi na Wafayaat ( vifo na mazazi )

- Kuchapisha vitabu mbalimbali vya kidini kama vile Misahafu, Juzuu

Amma, vitabu vya fikra, dua n.k.

- Na kuendesha na kusimamia semina mbalimbali za kidini.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe wepesi na atufanyie sahali katika

kufanikisha malengo yetu haya tuliyojiwekea, kwani Yeye ndiye

wakuombwa msaada

Wabillahi Tawfiq.

Page 14: al-Masailu-l-Islamiyyah

N

Page 15: al-Masailu-l-Islamiyyah
Page 16: al-Masailu-l-Islamiyyah

2

Al-Masailul Islamiyah

HUKUMU ZA TAQLID

“KUFUATA”

1.Mas’ala: Niwajibu itikadi ya mwislamu katika Usul- Dini “misingi ya

dini” iwe ni kutokana na dalili na hoja, na wala haijuzu humo kufanya

taqlid, kwa maana ya kwamba mtu asikubali maneno ya yeyote bila ya

dalili. Lakini katika hukumu za kidini na matawi yake ni wajibu ama awe

ni mujitahid anayeweza kuchambua hukumu kutoka katika naswi “ Aya au

Hadith” na ama awe ni mwenye kufanya taqlid kwa maana ya kwamba

afanye amali kutokana na fat’wa za mujitahid ambaye ametimiza mashar-

ti na ama awe anafanya amali kwa njia ya kufanya ihtiyat “tahadhari” kwa

namna ambayo atapata yakini kwamba ametekeleza wajibu. Kwa mfano

kama jopo la mujitahid limetoa fat’wa kuharamisha jambo na jopo jingine

limetoa fat’wa ya uhalali wa jambo hilo basi anachukua tahadhari ya kuto-

lifanya jambo hilo au kama baadhi wametoa fat’wa ya wajibu wa kufanya

amali na wengine wakatoa fat’wa ya kuwa kwake sunna basi anachukua

tahadhari ya kufanya jambo hilo. Na ambaye sio mujitahidi wala hawezi

kufanya ihtiyat “tahadhari” ni wajibu kwake kumfuata Mujitahid na

kufanya amali kulingana na fat’wa zake.

2: Kufanya taqlid katika hukumu ni kufanya amali kwa mujibu wa fat’wa

ya mmoja wa Mujitahidina. Ni wajibu Mujitahidi awe ni mwanaume,

baleghe, mwenyeakili timamu, Shia Ithina Asharia, mtoto wa halali, awe

hai, huru na mwadilifu. Mwadilifu ni mtu anayefanya yaliyo wajibu na

kuacha yaliyoharamu kwa kiasi kwamba lau kama ukiulizia hali yake kwa

jirani yake au kwa wanayeishi naye au watu wa mahali anapofanyia kazi

basi wangekupa habari za wema wake, na kwa tahadhari mujitahid huyo

awe ni mjuzi zaidi katika zama zake katika kufahamu hukumu na

kuzichambua.kuliko mujtahid mwengine

Page 17: al-Masailu-l-Islamiyyah

3

Al-Masailul Islamiyah

3: Mujitahid na mjuzi zaidi anafahamika kwa moja kati ya njia tatu:-

i – Mtu mwenyewe kupata yakini ya hilo, kwa yeye mwenyewe kuwa

ni kati ya wenye elimu na anaweza kumtambua mujitahid na mjuzi

zaidi kwa ujuzi wake.

ii - Wajuzi wawaili waadilifu kutoa taarifa juu ya hilo ambao

wanaweza kumtambua Mujitahid na mjuzi zaidi kwa sharti

wasipinge taarifa yao wajuzi wengine wawili.

iii Washuhudie hilo jopo la watu wenye elimu na ujuzi kati ya wanao

weza kumtambua Mujitahid na mjuzi zaidi na wanaoaminiwa, na

hukumu iliyo na nguvu zaidi ni kutosheleza taarifa ya mtu mmoja

ikiwa ni mkweli.

4. Ikiwa ni vigumu kumtambua mjuzi zaidi inalazimu kwa tahadhari ya

wajibu kumfuata anayedhaniwa kuwa yeye ni mjuzi zaidi, vivyo hivyo

atamfuata ambaye anadhana dhaifu juu ya kuwa kwake mjuzi zaidi na

anajua kutokuwepo kwa mjuzi zaidi mwingine asiyekuwa yeye kwa

tahadhari ya sunna, ama kama kundi litalingana katika ujuzi basi atam-

fuata mmoja kati yao, lakini ikiwa mmoja wao ni mchamungu zaidi basi

atamfuata yule mcamungu zaidi bila ya wengine kwa tahadhari ya

sunna.

5. Inawezekana kupata fat’wa na rai ya mujitahidi kwa moja kati ya njia

nne zifuatazo :-

Kusikia moja kwa moja kutoka kwa mujitahidi.

Kusikia kutoka kwa waadilifu wawili wakinukuu fat’wa ya Mujitahidi.

Kusikia kutoka kwa wanaoaminika na kutegemewa katika kunukuu kauli

yake.

Kupatikana fat’wa katika kitabu chake cha fat’wa, katika muundo unaole-

ta tumaini juu ya usahihi wa yaliyomo humo na usalama wake kutokana

Page 18: al-Masailu-l-Islamiyyah

4

Al-Masailul Islamiyah

na makosa.

6. Maadamu mwenye kufanya taqlid hajapata yakini ya kubadilika fat’wa

ya Mujitahidi na rai yake inajuzu kwake kufanya amali kulingana na

yaliyomo ndani ya kitabu chake cha fat’wa lakini akidhania juu ya

kuwepo mabadiliko katika fat’wa yake sio wajibu kuchunguza

isipokuwa kama dhana inakubalika kiakili.

7. Mujitahid mjuzi zaidi akitoa fat’wa katika mas’ala haijuzu kwa anaye

mfuta kumfuata mujitahidi mwingine katika mas’ala hayo kwa tahadha-

ri ya wajibu, lakini kama hajatoa fat’wa bali amesema. “ Kwa tahadha-

ri afanye kadha.” Kwa mfano akisema: “ kwa tahadhari alete tasbihi nne

mara tatu” inalazimu kwa mwenye kuqalid kufanya kulingana na tahad-

hari hii au afanye kulingana na fat’wa ya mujitahid mwingine, ikiwa

mujitahidi mwingine amesema inatosha kuileta mara moja basi anawe-

za kuileta mara moja, na hukumu ni hiyo hiyo ikiwa Marjii anayemfua-

ta atasema. “Mas’ala haya ni mahala pa kutafakari au ni mahala pa

mushkeli.”

8. Mujitahidi akitoa tahadhari baada ya kutoa fat’wa katika mas’ala mfano

mtu akisema “Chombo kilichonajisika kinatoharika kwa maji ya kuru

“birika” mara moja ingawa ni bora kukiosha mara tatu” haijuzu kwa

anayemfuata mujtahid kumrejea mujitahidi mwingine katika mas’ala

hayo na hii inaitwa tahadhari ya sunna.

9. Haijuzu kumfuata mujitahid aliyekufa kwa anayeanza taqlid, ama akifa

mujitahid ambaye mtu anamfuata inajuzu kwake kubaki katika taqlid ya

mujitahid aliyekufa katika mas’ala yote ambayo mwenye kuqalid

hajayafanya wakati wa uhai wa mujitahid.

10. Mtu akifanya amali fulani kwa fat’wa ya mujitahid, kisha mwenye

kufanya taqlid katika mas’ala hayo kwa fat’wa ya mujitahid aliye hai

baada ya kufa marja wake wa kwanza haitajuzu kwake kubadili kuto-

ka katika fat’wa ya mujitahid aliye hai kwenda kwenye fat’wa ya mar-

Page 19: al-Masailu-l-Islamiyyah

5

Al-Masailul Islamiyah

jaa wake wa awali aliyekufa katika mas’ala hayo. Vivyo hivyo ikiwa

mujitahid hakutoa fat’wa katika mas’ala hayo bali akatoa tahadhari na

mwenye kuqalid akafanya kulingana na tahadhari hiyo kwa muda hai-

juzu kwake kurejea katika fat’wa ya mujitahid aliyekufa.

11. Inajuzu kubadili taqlid kutoka kwa mujitahid aliyekufa kwenda kwa

mujitahid hai na wala haijuzu kubadili kutoka kwa mujitahid hai kwen-

da kwa mujitahid mwingine hai kwa tahadhari, isipokuwa ikiwa muji-

tahid wa pili ni mjuzi zaidi kuliko mujitahid wa kwanza au wa kwanza

akipoteza sifa ya uadilifu.

12. Ni wajibu kwa mukalafu “aliye baleghe na mwenyeakiili tiomamu”

kujifunza mas’ala ambayo aghlabu anayahitaji.

13. Yakitokea mas’ala ambayo mtu hajui hukumu yake ikiwa inawezeka-

na kusubiri ni wajibu wake kusubiri hadi apate fat’wa ya marjaa

anayemfuata na ikishindikana afanye kilicho wajibu kwake kwa

kuchukua tahadhari kama kuna uwezekano.

14. Kama mtu akinukuu fat’wa ya mujitahid kwa yeyote fat’wa ikibadili-

ka sio lazima kwake kumjulisha mabadiliko hayo, lakini akijua kuwa

alikosea katika kunukuu fat’wa ni lazima kumjulisha yale aliyoyanu-

kuu kwake kama kuna uwezekano.

15. Mukalafu akifanya amali kwa muda bila ya taqlid amali yake itasihi

ikiwa itaafikiana na fat’wa ya mujitahid ambaye ilikuwa ni wajibu

kwake kumfuata au ikiafikiana na fat’wa ya mujitahid ambaye imepa-

sa kumfuata, ingawa kwa tahadhari iafikiane na mujitahid anayetaka

kumfuata au akijua kwa njia nyingine kuwa amali zake zimeafikiana na

hali halisi na kwamba ametimiza wajibu wake.

16. Taqlid inahusu hukumu zote, katika ibada, mikataba, wajibu, haramu,

sunna, makuruhu na mubaha.

Page 20: al-Masailu-l-Islamiyyah

6

Al-Masailul Islamiyah

HUKUMU ZA TOHARA

Maji halisi na mudhafu

17. Maji ama ni mutlaq ‘halisi’ na ama ni mudhafu. Mudhafu ni ambayo

yamekamuliwa kutoka kwenye kitu, mfano maji ya komamanga, maji

ya waridi au yaliyochanganywa na kitu mfano maji yaliyochanganywa

na udongo n.k kiasi kwamba hayaitwi maji tu, na halisi ni yasiyoku-

wa hayo, nayo yamegawanyika sehemu tano:-

maji ya “kuru” birika

maji machache

maji yanayotiririka

maji ya mvua

maji ya kisima

Maji ya birika

18. Kuru “birika” ni ambalo lina ujazo wa shibiri 3 upana, urefu na kina au

ambalo jumla ya ujazo wake ni shibiri 27.

19. Maji ya birika hayanajisiki kwa kukutana tu na damu au mkojo au kitu

chochote kilicho najisi au kilichonajisika mfano nguo iliyonajisika ila

yakibadilika na kuchukua rangi ya najisi au harufu yake au ladha yake

na hayanajisiki ikiwa hayajabadilika.

20. Maji ya birika hayanajisiki ikiwa yatabadilika bila ya kupatwa na

najisi.

21. Kilicho najisi mfano damu kikikutana na maji yanayozidi kuru na

baadhi ya rangi yake ikabadilika au harufu yake, ikiwa yaliyobakia ni

Page 21: al-Masailu-l-Islamiyyah

7

Al-Masailul Islamiyah

machache kuliko kiwango cha kuru yote yatanajisika na ikiwa yaliy-

obakia ni kiwango cha kuru au zaidi ya kuru hayatanajisika yote bali

kiasi kilichobadilika tu.

22. Ikiwa maji ya bomba yameungana na birika maji yaliyonajisika yata-

toharika, lakini hayatohariki ikiwa yatadondokewa na matone tu, ila

kikiwekwa kitu kwenye bomba ili maji yake yaungane kabla hayajawa

matone na kuungana na maji yaliyonajisi, na kwa tahadhari ya sunna

yachanganyike maji ya bomba na maji yaliyonajisika.

23. Kama akiosha kitu najisi kwenye bomba la maji yaliyoungana na biri-

ka, maji yanayodondoka kutoka kitu kilicho najisi yatakuwa tohara

kama yataunganika na birika na hayajachukua rangi ya najisi au ladha

yake au harufu yake na ikiwa humo hakuna viini vya najisi.

24. Kama kitaganda kiasi cha maji ya birika na yaliyobaki yakawa sio

kiwango cha birika maji yaliyobaki yatanajisika kama yatakutana na

najisi, vivyo hivyo yatanajisika kila yatakapo yeyuka kutoka katika

barafu.

25. Maji ambayo yameshakuwa kuru ikitokea shaka kuwa yamepungua

kiasi cha kuru au laa basi hukumu yake ni kuru yaani ni tohara na

yanatoharisha na wala hayanajisiki kwa kukutana na najisi, na ambayo

yalikuwa sio kuru ikitokea shaka kuwa yamekuwa kuru au laa basi

hayatakuwa na hukumu ya kuru na kwa tahadhari ya lazima afanye

utafiti katika maudhui haya kisha aratibu atoe hukumu iliyotajwa

ikiwa hali halisi haitabainika.

26. Birika linathibitika kwa njia moja kati ya tatu:-

Mtu binafsi kupata yakini juu ya hilo

Watu wawili waadilifu watoe habari au mtu mmoja mkweli

Atoe habari ya hilo ambaye maji yako chini ya usimamizi wake kama vile

mwangalizi wa bafu akisema: Maji yaliyopo katika tanki la bafu ni birika

Page 22: al-Masailu-l-Islamiyyah

8

Al-Masailul Islamiyah

Maji machache

27. Maji machache ni maji ambayo hayatiririki ardhini na wala hayafikii

kiasi cha birika.

28. Maji machache yakimwagwa kwenye kitu najisi au yakikutana na naji-

si yananajisika, lakini kama yatamwagiwa kutoka juu, juu ya kitu kili-

cho najisi au kwa mkupuo, kina najisika kiasi kilichokutana na najisi tu

na kinachobakia kitakuwa tohara.

29. Maji machache yakimwagiwa kwenye kitu kilicho najisi ili kuondoa

kiini cha najisi humo, kisha maji yakajitenga nacho maji yanayojiten-

ga yatakuwa najisi na inalazimu kwa tahadhari ya sunna ajiepushe na

maji ambayo yanamwagiwa juu ya kitu kilicho najisika baada ya kuon-

doka kiini cha najisi humo.

30. Maji yanayooshewa sehemu ya haja kubwa na ndogo yatakuwa tohara

na wala hakitonajisika kitu kinacho kutana nayo kama masharti mata-

no yatatimia pamoja na kuchukua tahadhari:-

Kama hayatachukua rangi ya najisi, harufu yake au ladha yake.

Ikiwa hayatapatwa na najisi nyingine.

Ikiwa hayatapatwa na chembechembe za kinyesi zinazoonekana.

Ikiwa mkojo au kinyesi hakijatoka pamoja na damu.

Ikiwa haja ndogo au kubwa haitavuka sehemu yake ya kawaida inayoju-

likana.

Maji yanayotiririka

31. Maji yanayotiririka ni ambayo yanatoka ardhini na yanatiririka kama

maji ya chemchem na mifereji.

32. Maji yanayotiririka hata kama ni machache ni kama kuru yakipatwa na

najisi yatakuwa tohara maadam hayajabadilika rangi yake au harufu

Page 23: al-Masailu-l-Islamiyyah

9

Al-Masailul Islamiyah

yake au ladha yake kwa sababu ya najisi.

33. Najisi ikikutana na maji yanayotiririka kitanajisika kiasi cha maji kili-

chobadilika kwa sababu ya najisi tu, na ambayo yameunganika na

chemchem miongoni mwayo yatakuwa tohara hata kama ni machache

kuliko kuru. Ama maji mengine ya mto ikiwa yatakuwa katika kiwan-

go cha kuru au yakichanganyika na chemchem kwa njia ya maji

ambayo hayajabadilika yatakuwa tohara vinginevyo yatakuwa najisi.

34. Chemchem inayobubujika masika na inaacha kububujika wakati wa

kiangazi hukumu yake wakati inapotiririka ni hukumu ya maji yanay-

otiririka.

35. Maji ya chemchem ambayo hayatiririki lakini yanatoka kila yanapoc-

hotwa hukumu yake ni hukumu ya maji yanayotiririka, kwa maana

kwamba hayanajisiki kwa kukutana tu na kiini cha najisi maadamu

hayajabadilika rangi yake au ladha yake au harufu yake kwa sababu ya

najisi.

36. Maji yaliyotuama karibu na mto unaoungana nayo hukumu yake ni

hukumu ya maji yanayotiririka.

37. Maji ya hodhi za bafuni ikiwa yameungana na tanki basi ni kama maji

yanayotiririka katika hukumu, hata kama ni machache kuliko kuru,

kwa sharti tanki liwe na kiwango cha kuru.

38. Maji ya bomba ambayo yako katika bafu na majengo, ambayo yanami-

minika katika bomba na karo ikiwa yanaungana na kuru - kama vile

jokofu za maji ya kunywa- hukumu yake ni hukumu ya maji yanay-

otiririka.

39. Maji yanayotiririka juu ya ardhi lakini hayana chanzo toka ardhini

yakiwa chini ya kiwango cha kuru na yakakutana na najisi yatanajisi-

Page 24: al-Masailu-l-Islamiyyah

10

Al-Masailul Islamiyah

ka, ama ikiwa yanatiririka toka juu kwenda chini au kwa mkupuo na

yakakutana na najisi chini maji yaliyo juu hayatanajisika.

Maji ya mvua

40. Maji ya mvua yakinyeshea kitu kilicho najisi ambacho hakina kiini cha

najisi, kitu kilichonyeshewa na mvua kitatoharika, matone ya mvua

hayatoshelezi bali iwe kwa kiasi kwamba inaitwa mvua na inatiririka

ardhini na kwa tahadhari ya sunna mvua iwe ni kwa kiasi inatiririka

katika ardhi ngumu.

41. Hailazimu kukamua nguo, godoro n.k , sawa sawa likioshwa kwa maji

ya mvua au mengineyo.

42. Mvua ikinyeshea kiini cha najisi na kikasambaa hadi sehemu nyingine

matone yatakuwa tohara ikiwa hayaambatani na chembechembe za

najisi, harufu yake, rangi yake, au ladha yake, mvua ikinyeshea damu

na kusambaa ikiwa katika cheche kuna chembechembe za damu, haru-

fu yake au ladha yake zitakuwa najisi.

43. Mvua ikinyeshea paa la nyumba au juu ya jengo na ikawa juu yake

kuna kiini cha najisi maji yanayotiririka chini ni tohara hata kama

yatakuwa yamepata kiini cha najisi maadam mvua inaendelea kunye-

sha. Ama baada ya kukatika akijua kuwa maji yanayotiririka kutoka

kwenye paa yamepatwa na najisi basi yatakuwa najisi.

44. Ardhi iliyonajisi inatoharika kwa kunyeshewa na mvua , ikiwa mvua

itanyeshea ardhi kisha maji yakapenya katika sehemu iliyo najisi chini

ya paa sehemu hiyo itatoharika.

45. Udongo ulionajisi ambao kwa kunyeshewa na mvua unakuwa tope

utakuwatohara.

46. Maji ya mvua yakikusanyika sehemu yakaosha kitu kilichonajisika

Page 25: al-Masailu-l-Islamiyyah

11

Al-Masailul Islamiyah

wakati wa kunyesha mvua kitu hicho kinatoharika hata kama maji

yaliyokusanyika ni chini ya kuru, hii ni kwa sharti yasichukue rangi ya

najisi, harufu yake wala ladha yake.

47. Mvua ikinyeshea godoro tohara lililotandikwa juu ya ardhi iliyo najisi

na maji yakatiririka juu ya ardhi, ardhi najisi inatoharika na godoro hal-

itanajisika.

Maji ya kisima

48. Maji ya kisima yanayotoka ndani ya ardhi ni tohara hata kama ni

machache kuliko kuru maadam hayajabadilika rangi yake au harufu

yake au ladha yake kutokana na najisi, lakini ni sunna yanapokutana na

baadhi ya najisi yatolewe kiasi kilichotajwa katika vitabu vikubwa.

49. Najisi ikimwagiwa katika kisima ikabadili rangi yake au harufu yake

kama mabadiliko hayo yataondoka basi maji yakisima yatatoharika

ingawa kwa tahadhari ya sunna yachanganyike na maji mapya yanay-

otoka katika kisima.

50. Maji ya mvua au maji yoyote yakikusanyika katika shimo na yakawa

ni machache kuliko kuru yananajisika kwa kukutana na najisi.

HUKUMU ZA MAJI

51. Maji mudhafu(ambayo maana yake imeelezwa katika mas’ala 17) hay-

atoharishi kitu najisi na wala haisihi kutawadhia wala kuoga josho.

52. Maji mudhafu vyovyote yatavyokuwa mengi (lakini si kwa wingi wa

kisima cha mafuta) yananajisika kwa kukutana tu na najisi lakini kama

maji mudhafu yakikingwa kutoka juu, kwenye ya kitu najisi, yatana-

jisika yaliyokutana na najisi tu, bila ya kunajisika yaliyo juu, mfano

Page 26: al-Masailu-l-Islamiyyah

12

Al-Masailul Islamiyah

kama maji ya waridi yakimwagwa kutoka kwenye birika juu ya mkono

ulio na najisi yananajisika yaliyofika kwenye mkono na ambayo haya-

jafika yatakuwa tohara, vivyo hivyo lau yakisukumwa kutoka chini

kwenda juu kwa msukumo wa bomba na yakakutana na yaliyo juu

yaliyonajisika sehemu ya chini haitonajisika.

53. Maji mudhafu yakichanganyika na maji ya kuru au maji yanayotiriri-

ka kiasi ambacho hayasemwi kuwa ni mudhafu yanatoharika.

54. Maji ambayo yalikuwa mutlaq na wala hayajulikani kama yamegeuka

na kuwa mudhafu au laa yatahukumiwa kuwa ni mutlaq kwa maana

kwamba yanatoharisha najisi na inafaa kutawadha na kuoga kwayo.

Ama ambayo yalikuwa mudhafu mwanzo na wala haijulikani kabla ya

hapo yalikuwa mutlaq au ni mudhafu hayatoharishi kilichonajisika, na

kutawadha na kuoga kwayo ni batili lakini yakiwa kwa kiwango cha

kuru au zaidi yakikutana na najisi hayahukumiwi kuwa ni najisi.

55. Maji ambayo hayajulikani kuwa ni mutlaq au mudhafu wala haijulikani

je hapo kabla yalikuwa mutlaq au mudhafu, hayatoharishi kitu kilicho

najisika, na kutawadha na kuoga kwayo ni batili, lakini yakiwa kwa

kiwango cha kuru au zaidi yake na yakakutana na najisi hayahukumi-

wi kuwa yamenajisika.

56. Maji ambayo yamekutana na najisi mfano mkojo na damu yakabadili-

ka rangi yake au harufu yake au ladha yake kwa sababu hiyo yatana-

jisika hata kama yanatiririka au yako katika kiwango cha kuru, lakini

yakibadilika rangi yake au harufu yake au ladha yake kwa sababu ya

ukaribu wake na najisi iliyo nje – kama ikiwa mzoga umetupwa karibu

ya maji hayo ukabadili harufu ya maji – dhahiri ni kutonajisika kwake

na wala si wajibu kufanya tahadhari ingawa ni bora kufanya hivyo.

57.Maji ambayo yamekutana na najisi mfano wa mkojo na damu rangi

yake ikibadilika au harufu yake au ladha yake kwa sababu ya hiyo najisi

Page 27: al-Masailu-l-Islamiyyah

13

Al-Masailul Islamiyah

yananajisika japo yawe yanatiririka au kufikia kiwango cha kuru, laki-

ni endapo itabadilika rangi yake au harufu yake au ladha yake kwa ajili

ya ukaribu wake na najisi iliyo nje yake, kama vile utupwe mzoga

karibu na maji ukabadilisha harufu ya maji- kwa hukumu yenye nguvu

-hayanajisiki wala si lazima kufanya ihtiyati- tahadhari- japokuwa ni

bora.

58. Maji ambayo yameingia najisi mfano wa damu au mkojo ikabadilisha

harufu yake au ladha yake au rangi yake,yatatoharika yakikutana na

kuru au na maji yanayotiririka au yakinyeshewa na mvua moja kwa

moja au upepo ukipeperusha maji ya mvua na kuyaingiza humo au

maji ya mvua yametiririkia humo kutoka kwenye bomba la maji ya

mvua, hayo yote yatatimia kwa sharti ya kutoweka mabadiliko wake.

59. Mabaki ya maji yaliyonywewa na mbwa, nguruwe au kafiri ni najisi na

ni haramu kuyanywa, ama mabaki ya maji yaliyonywewa na mnyama

ambaye ni halali kuliwa ni tohara na sio makuruhu kuyanywa. Ama

mnyama aliye haramu kuliwa mabaki yake ni tohara ,lakini ni maku-

ruhu kuyanywa isipokuwa mabaki ya paka sio makuruhu kuyanywa.

60. Endapo kitu kilichonajisika kitaoshwa ndani ya kuru au maji yanay-

otiririka maji yanayoatuka kutoka kwenye kitu kilichooshwa yatakuwa

tohara.

HUKUMU ZA KWENDA HAJA

61. Ni wajibu- kwa mwanadamu- kustiri uchi wake - mbele ya kila aliye-

baleghe, wakati wa kujisaidia na mbele ya mtu mwingene hata kama

anayemuona ni mahram yake, kama vile dada yake, mama yake n.k.

Ni wajibu kustiri uchi mbele ya kichaa, mtoto mwenye kutambua zuri

na baya, lakini sio lazima kwa mke kusitiri uchi wake mbele ya mume

wake au kinyume chake.

62. Si wajibu kusitiri utupu kwa kitu makhsusi bali hata akiusitiri kwa

Page 28: al-Masailu-l-Islamiyyah

14

Al-Masailul Islamiyah

mkono wake inatosha.

63. Ni wajibu asielekee kibla wala kukipa mgongo wakati wa kujisaidia,

yaani sehemu ya mbele ya mwili wake; tumbo lake, kifua chake na

magoti yake yasielekee kibla au kinyume chake.

64. Endapo mwenye kujisaidia ameelekea kibla au amekipa mgongo haito-

tosha kwa kupindisha utupu wake mbali na upande wa kibla katika

hali zote mbili. Na ikiwa hakuelekea kibla wala kukipa mgongo afanye

ihtiyati ya wajibu kutoielekeza tupu yake upande wa kibla au kinyume

chake.

65. Na kwa tahadhari ya sunna asielekee mwenye kujisaidia wala

asielekeze mgongo kibla wakati wa kufanya istibraa (ambayo maelezo

yake yatakuja katika mas’ala 73) na wakati wa kujitoharisha sehemu ya

mkojo na ya haja kubwa pia.

66. Akilazimika kuelekea kibla au kukipa mgongo ili asionekane kwa

asiyekuwa mahram yake hakuna ubaya kukielekea kibla au kukipa

mgongo ,vivyo hivyo hakuna ubaya akilazimika kukielekea kibla au

kukipa mgongo kwa ajili ya sababu nyingine.

67. Hailazimu kuchukua tahadhari ya kutomkalisha mtoto mchanga kwa

namna ambayo atakuwa ameelekea kibla isipokuwa uharamu wa hilo

uwe kwa upande mwingine, na kama mtoto mwenyewe akielekea

kibla au akakipa mgongo hailazimu kumkataza kwa hilo.

68. Ni haramu kujisaidia katika sehemu tano:-

Vichochoro visivyopitika kama wenyewe hawaruhusu hilo,

vivyo hivyo katika njia zinazopitika (zisizo fungwa) katika

hali ya dharura kwa mpita njia. Miliki ambayo hairuhusiwi

kujisaidia humo.

Sehemu zilizowaqfu kwa watu mahsusi mfano katika madrasa za kidini

Page 29: al-Masailu-l-Islamiyyah

15

Al-Masailul Islamiyah

n.k. Juu ya kaburi la muumini kama hilo litamdhalilisha .Sehemu za hes-

hima ambazo haifai kujisaidia kutokana na heshima yake.

69. Sehemu ya haja kubwa haitohariki isipokuwa kwa maji katika hali tatu,

baadhi ya hizo ni kwa tahadhari:-

Kama itagusa sehemu ya haja kubwa najisi kutoka sehemu nyingine.

Kama itatoka pamoja na haja kubwa najisi nyingine kama vile damu.

Kama haja kubwa itavuka sehemu ya haja kubwa zaidi ya inavyojulikana.

Ama isiyokuwa katika hali zisizokuwa hizi inajuzu kutoharisha sehemu ya

haja kubwa kwa maji au tambara au mawe n.k, kama utakavyokuja ufafa-

nuzi wake ingawa kuosha kwa maji ni bora zaidi.

70. Sehemu ya haja ndogo haitohariki isipokuwa kwa maji na kama ikio-

shwa katika kuru au maji yanayotiririka mara moja baada ya kumalizi-

ka mkojo inatosha, lakini kwa maji machache inalazimu kuiosha mara

mbili na ni bora kuiosha mara tatu.

71. Inajuzu kutoharisha sehemu ya haja kubwa kwa mawe, changarawe na

mfano wake yakiwa makavu na tohara, na hakuna mushikeli ikiwa

yana unyevuvyevu kidogo kiasi kwamba hauhamii kwenye sehemu ya

haja kubwa, lakini ni wajibu afute kwa mawe yasiyopungua matatu na

asafishe sehemu ya haja kubwa mara moja au mara mbili.

72. Kwa tahadhari yasunna mawe yawe matatu au matambara ya kufutia

sehemu ya haja kubwa yawe matatu, jiwe kubwa lenye pembe tatu au

tambara refu moja linatosha, na kama najisi haitatoka kwa vipande

vitatu inamlazimu aongeze ambayo yatatosha kusafisha na kuondoa

najisi yote, na hakuna mushikeli katika kubakia chembechembe ndogo

sana zisizoonekana.

73 Haijuzu kufutia sehemu ya haja kubwa kwa vitu ambavyo ni wajibu

kuviheshimu, mfano karatasi ambayo ina jina la Mwenyezi Mungu,

manabii au mawasii (as) ,na kwa tahadhari ya sunna asifute kwa mifu-

Page 30: al-Masailu-l-Islamiyyah

16

Al-Masailul Islamiyah

pa wala kwa vinyesi vya wanyama, kama ataondoa haja kubwa kwa

vitu hivi ataasi na kupata dhambi, lakini dhahiri ni kwamba sehemu ya

haja kubwa itatoharika.

74. Akipata shaka kuwa sehemu ya haja kubwa imetoharika au laa, ni waji-

bu atoharishe, ama ikiwa ni kawaida yake kutoharisha sehemu ya haja

ndogo au kubwa haraka,basi ni kwa tahadhari ya sunna atoharishe.

75. Akishuku baada ya swala kwamba alitoharisha sehemu ya haja kubwa

kabla ya swala au laa, swala yake aliyoswali itasihi, lakini inamlazimu

kutoharisha kwa ajili ya swala zinazofuata, na kama atashuku ndani ya

swala ni wajibu akate swala na kutoharisha, ama ikiwa ni ada yake

kutoharisha sehemu ya haja mara tu baada ya haja basi itakuwa ni

sunna kufanya tahadhari kwa kutoharisha, na wala hatakakata swala

kwa ajili ya tahadhari hii ya sunna.

ISTIBRAA

76. Istibraa ni kitendo cha sunna wanachokifanya wanaume baada ya

kumaliza haja ndogo ili kuwa na yakini ya kutobakia mkojo katika njia

yake, na ina viwango, vilivyo bora zaidi ni kutoharisha sehemu ya haja

kubwa kwanza kama atakwenda haja kubwa baada ya mkojo kukatika,

kisha anakamua kwa kidole cha mkono wake wa kushoto kuanzia kati-

ka njia ya haja kubwa hadi kwenye shina la dhakari mara tatu kwa

nguvu, kisha anaweka kidole gumba juu ya dhakari na kidole cha sha-

hada chini yake kisha anakamua kwa nguvu hadi kwenye kichwa cha

dhakari mara tatu.

77. Maji yanayotoka kwa mwanaume baada ya kumchezea mwanamke

yanayoitwa madhii ni tohara, vivyo hivyo maji yanayotoka baada ya

manii ambayo huitwa wadhii ni tohara, vilevile maji yatokayo aghlab

baada ya mkojo ambayo huitwa wadii ni tohara kama hayajapatwa na

Page 31: al-Masailu-l-Islamiyyah

17

Al-Masailul Islamiyah

mkojo. Na mtu akifanya istibrai baada ya mkojo kisha akatokwa na

maji na akashuku kuwa ni mkojo au moja kati ya maji haya yaliyotaj-

wa basi yatakuwa tohara.

78. Mtu akishuku je, amefanya istibrai baada ya haja ndogo au laa, na aka-

tokwa na majimaji hajui ni najisi au ni tohara, hukumu yake ni najisi

na udhu wake unabatilika, lakini kama ni kawaida yake kufanya isti-

brai baada ya kukojoa. Au akishuku kuwa amefanya istibrai kwa njia

sahihi au laa, na yakatoka kwake maji maji hajui ni tohara au laa, yata-

kuwa tohara na udhu wake haubatiliki.

79. Ambaye hajafanya istibarai akiwa na yakini baada ya kupita muda

baada ya kukojoa kwamba hakuna mkojo katika njia ya mkojo, kisha

akaona maji maji na akashuku kuwa ni tohara au laa, yatakuwa tohara

na udhu wake hautabatiliki.

80. Kwa kuacha istibrai maji maji yanayoshukiwa kuwa ni mkojo yata-

hukumiwa kuwa ni najisi na yanatengua tohara, hata kama kuacha

kwake ni kwa dharura au kwa kughafilika.

81. Mwanamke hafanyi istibrai kutokana na mkojo, kama ataona maji maji

na akakushuku kuwa ni tohara au laa, basi yatakuwa tohara na udhu

wake au josho halitobatilika lake.

ADABU ZA KWENDA HAJA

82. Ni sunna wakati wa kujisaidia akae katika sehemu ambayo haonwi na

mtu yeyote, na atangulize mguu wa kushoto wakati wa kuingia choo-

ni, na atangulize mguu wa kulia wakati wa kutoka chooni.

83. Ni makuruhu kuelekea jua na mwezi wakati wa kujisaidia, lakini kara-

Page 32: al-Masailu-l-Islamiyyah

18

Al-Masailul Islamiyah

ha hii hutoweka akifunika tupu yake kwa kitu, na vivyo hivyo ni

makuruhu katika hali ya kujisaidia kuuelekea upepo, na ni makuruhu

kujisaidia katika njia, vichochoro, mbele ya majumba, chini ya miti ya

matunda, kula wakati wa kujisaidia, kukaa muda mrefu chooni na

kujitoharisha mahali pa haja kubwa kwa mkono wa kulia na vile vile

kuongea katika hali ya kujisaidia, na hakuna mushkeli kumtaja Mungu

au kuongea kwa dharura.

84. Ni makuruhu kukojoa katika ardhi ngumu, katika mashimo ya wadu-

du na katika maji hususan ikiwa yametuama, vivyo hivyo ni makuru-

hu kukojoa kwa kusimama. Lakini si makuruhu kukojoa wima katika

sehemu ambazo zimewekwa marumaru na changarawe zake.

85. Ni makuruhu kubana mkojo au haja kubwa, bali ni haramu ikiwa kuba-

na huku kutadhuru mwili madhara makubwa.

86. Ni sunna mtu kujisaidia haja ndogo kabla ya swala kisha atawadhe, au

kuoga na kuswali, vivyo hivyo ni sunna kujisaidia haja ndogo kabla ya

kulala, kabla ya kujaamiiana na baada ya kutoka manii.

NAJISI

87. Najisi ni kumi na moja:-

1. mkojo 4. mzoga 7. nguruwe 10. Pombe za kisasa

2. kinyesi 5. damu 8. kafiri 11. jasho la mnyama anayekula vinyesi

3. manii 6. mbwa 9. pombe za kienyeji

1 na 2 :Mkojo na kinyesi

88. Mkojo na kinyesi cha binadamu na cha kila mnyama aliye haramu

kuliwa ni najisi, lakini mkojo na kinyesi cha mnyama aliye haramu

kuliwa ambaye damu yake haitoki kwa kasi wakati wa kuchinjwa ni

tohara. Na vivyo hivyo mfano wa mbu, nzi -wanyama- wasio na

Page 33: al-Masailu-l-Islamiyyah

19

Al-Masailul Islamiyah

nyama. Ama mkojo na kinyesi cha mnyama aliye halali kuliwa ni toha-

ra.

89. Ni sunna kujiepusha na vinyesi vya ndege wasioliwa na hasa mkojo wa

popo na kinyesi chake.

90. Mkojo na kinyesi cha mnyama anayekula vinyesi ni najisi, vivyo hivyo

mkojo na kinyesi cha mnyama aliyeingiliwa na binadamu, vile vile

mkojo wa mnyama aliyenyonya kwa nguruwe na kunawiri kutokana na

maziwa yake.

3:Manii

91. Manii ya mwanadamu na ya mnyama anayetoka damu kwa kasi waka-

ti wa kuchinjwa ni najisi.

92. Maji ya aina tatu madhii, wadhii na wadii ni tohara.

4:Mzoga

93. Mzoga wa mnyama mwenye damu itokayo kwa kasi ni najisi, sawa

sawa amejifia mwenyewe au amechinjwa kwa njia isiyokuwa ya kisha-

ria. Samaki ambapo hana damu itokayo kwa kasi mzoga wake ni toha-

ra hata kama akifia kwenye maji.

94. Vitu visivyokuwa na uhai vinavyotokana na mnyama mfano sufi,

nywele, manyoya, mifupa na meno, vyote ni tohara isipokuwa vinavyo

tokana na mbwa na nguruwe.

95. Ikiwa sehemu ya mwili wa mwanadamu hai au mnyama hai mwenye

kutoka damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa itajitenga, basi nyama au

kipande au kitu kingine chenye uhai ni najisi.

96. Magamba mepesi yanayojitokeza kwenye midomo au mahali pengine

Page 34: al-Masailu-l-Islamiyyah

20

Al-Masailul Islamiyah

mwilini na ikiwa wakati wa kuanguka kwake umewadia, ni tohara japo

akiyang’oa - mtu - kwa hiyari, lakini ni bora kujiepusha kwa ihtiyati ya

sunna na magamba haya endapo yatang’olewa kabla ya wakati wa

kuanguka kwake.

97. Yai litokalo tumboni mwa kuku aliyekufa, endapo gamba lake la juu

litakuwa gumu ni tohara, lakini ni wajibu kulitoharisha kwa tahadha-

ri.

98. Kitoto kichanga cha kondoo au mbuzi kikifa kabla hakijala nyasi, kha-

mira (mazima aliyoyanyonya ambayo yako katika fuko la chakula)

iliyomo tumboni mwake ni tohara, lakini ni lazima kuitoharisha kwa

tahadhari.

99. Dawa ya mitishamba ya rojorojo, manukato, mafuta, rangi na sabuni

zinazoagizwa toka nchi zisizokuwa za kiislamu, hukumu yake ni toha-

ra maadamu tu mtu hajapata yakini ya unajisi wake.

100. Nyama, mafuta na ngozi zinazouzwa katika soko la waislamu ni toha-

ra, vivyo hivyo vilivyo katika miliki ya waislamu, lakini ikifahamika

kuwa mwislamu amevichukua kwa kafiri bila ya kuchunguza kuwa ni

kutoka kwa mnyama aliyechinjwa kisheria au laa, basi ni najisi.

5. Damu.

102. Damu ya binadamu na kila mnyama atokaye damu kwa kasi wakati

wa kuchinjwa ni najisi, na damu ya mnyama asiyetoka damu kwa kasi

wakati wa kuchinjwa mfano samaki, mbu au ambaye anashukiwa,

asiyejulikana kuwa anatoka damu kwa kasi wakati wa kuchinjwa au

laa, kama vile nyoka ni tohara.

103. Mnyama ambaye ni halali kuliwa akichinjwa kisharia na ikatoka

Page 35: al-Masailu-l-Islamiyyah

21

Al-Masailul Islamiyah

damu inayotakiwa kutoka, damu iliyobakia ndani ni tohara na inaju-

zu kula nyama yake bila ya kuiosha kutokana na damu, isipokuwa

shingo yake inapasa kuiosha halafu iliwe, lakini ikiwa kiasi cha

damu kutoka nje kitarejea hadi ndani ya nyama kutokana na kupu-

mua, au kichwa cha mnyama kuwa juu wakati wa kuchinja, damu

hiyo itakuwa najisi, ni wajibu kufanya tahadhari kufanya tahadhari

kwa kujiepusha na damu iliyobakia ndani ya mnyama aliye haramu

kuliwa kama atachinjwa kisheria.

104. Damu chache ambayo inaonekana katika yai la kuku ikiwa ganda lake

jepesi la juu halijapasuka, ikiwezekana kuitoa damu hiyo bila ya

kuchanganyika na yai basi yai litakuwa tohara.

105. Damu chache ionekanayo wakati wa kukamua maziwa wakati mwin-

gine inanajisisha maziwa – kwa tahadhari -

106. Damu inayotoka baina ya meno ikichanganyikana na majimaji ya

kinywa na kwisha ni tohara, lakini kwa tahadhari ya sunna asiyame-

ze.

107. Damu ambayo inaganda chini ya ngozi kwa sababu ya pigo kali, kama

haitosemekana kuwa ni damu basi ni tohara, na ikisemekana kuwa ni

damu basi ni najisi, na katika hali hii ngozi ikichanika au ukucha uki-

toboka inalazimu kutoa damu iliyoganda kwa ajili ya udhu na josho,

kama kutolewa hakutakuwa na tabu, na kama kutasababisha adha

inalazimu kuosha pembezoni mwake kwa namna ambayo haitasaba-

bisha kunajisika, kisha aweke kitambaa au mfano wake kisha anapa-

ka juu ya kitambaa na anatayamamu vile vile kwa tahadhari.

108. Kama hawezi kutambua kuwa hii damu iliyo chini ya ngozi imegan-

da au ni nyama imekuwa katika hali hiyo kutokana na kupigwa basi

itakuwa tohara.

109. Bonge la damu likitumbukia katika chakula wakati kimechemka,

Page 36: al-Masailu-l-Islamiyyah

22

Al-Masailul Islamiyah

katika chakula wakati kimechemka chakula chote kitanajisika na chombo

chake vile vile, na mchemko, joto au moto sio katika vitu vinavyotohari-

sha.

110. Maji ya njano yanayoonekana pembezoni mwa jeraha wakati wa

kukifungua kinapo pona, kama hatajua kuchanganyika kwake na

damu ni tohara, vivyo hivyo utando unaokuwa juu ya jeraha wakati

kinapopona na hufanya tabaka jeusi juu yake, hilo tabaka jeusi ni

tohara. kwa istihala « kubadilika.»

6 na 7 - Mbwa na nguruwe

111. Mbwa na nguruwe wa nchi kavu ni najisi hata nywele zao, mifupa yao

ma makucha yao na unyevunyevu wao. Lakini mbwa na nguruwe wa

majini ni tohara.

112. Wanyama wote walio haramu kuliwa ila mbwa na nguruwe inakuba-

lika kuchinjwa, kwa maana kuwa kama watachinjwa kisheria wataku-

wa tohara ingawa hawatakuwa halali kuliwa.

8- Kafiri

113. Kafiri ni najisi, naye ni ambaye anakanusha kuwepo kwa Mwenyezi

Mungu na anayemshirikisha au anaepinga utume wa Muhammad

(saww), vivyo hivyo kila anayekanusha wajibu katika wajibu wa dini,

mfano swala na saumu ambayo waislamu wanaizingatia kuwa ni

sehemu ya dini kwa sharti kuwa inalazimu kukanusha kwake huko

kumkanusha Nabii (saww), na awe anajua kuwa hii ni katika wajibu

wa dini, vinginevyo haitohukumiwa kuwa ni kafiri ingawa ni sunna

kufanya tahadhari kujiepusha naye. Na anayepinga siku ya kiyama na

madhambi makubwa, wajibu, nasibi, ghulati na khawariji wao wako

katika hukumu ya kafiri.

Page 37: al-Masailu-l-Islamiyyah

23

Al-Masailul Islamiyah

114. Ahlul- kitab, kama vile manaswara, mayahudi na majusi kwa - tahad-

hari ya wajibu ni kujiepusha nao katika sehemu zisizokuwa za dharu-

ra na shida, hata kama hawajanajisika kwa kunywa pombe, kula mizo-

ga na nyama ya nguruwe au kutumia kwao najisi zingine.

115. Mwili wote wa kafiri hata nywele, kucha na unyevunyevu vyote ni

najisi.

116. Ikiwa mzazi wa mtoto asiyebaleghe, mama yake, babu yake, bibi

yake, wote wakiwa ni makafiri basi mtoto pia atakuwa najisi, au ikiwa

mmoja wa hawa ni mwislamu basi mtoto atakuwa tohara.

117. Asiyejulikana kuwa ni kafiri au mwislamu akiwa katika nchi ya kiis-

lamu basi ni tohara, na hukumu zote za Uislamu zitatekelezwa kwake,

inajuzu kuoa mwislamu na kuzikwa katika makaburi ya waislamu.

118. Yeyote katika waislamu akimtukana Nabii (saww), Fatma Zahra au

mmoja wa maimamu kumi na mbili au akiwafanyia uadui basi ataku-

wa ni najisi.

9 -Pombe

119. Pombe na kila kileo cha asili ya majimaji ni najisi hata kama ataki-

gandisha kwa njia yoyote ile, ama kikiwa hakina asili ya majimaji

mfano bangi na hashishi ni tohara hata kama kikitumbukizwa kitu

humo ili iwe maji maji.

120. Polishi inayotumika kwa kupaka na kung’arisha milango, viti, meza

n.k. kama haijathibitika kuwa ni kileo basi ni tohara.

121. Zabibu mbivu au maji ya zabibu mbivu ikichemka yenyewe, ni hara-

mu kuila au kuinywa ni, lakini ni tohara na wala haijuzu kuitumia

(kuila na kuinywa) ila ikiwa siki, vivyo hivyo inaharamishwa kuitu-

Page 38: al-Masailu-l-Islamiyyah

24

Al-Masailul Islamiyah

mia ikiwa itachemshwa kwa njia ya kupikwa, na haijuzu kuitumia ila

baada ya kupungua theluthi mbili kwa kuichemsha kwa moto.

122. Tende, zabibu kavu na kishimishi na juisi zake, ni halali kama zita-

chemka zenyewe ingawa kwa tahadhari ya sunna hususani katika

zabibu na kishimishi ni kujiepusha kutumia.

10 - Bia.

123. Bia nacho ni kinywaji kinachotengenezwa kwa shairi ni najisi, lakini

maji yanayochukuliwa kutoka kwenye shairi kulingana na maelezo ya

daktari kwa ajili ya tiba na ambayo yanaitwa “maji ya shairi” vivyo

hivyo shairi inayopikwa katika mchuzi na shurbati ni tohara.

11 - Jasho la mnyama anayekula vinyesi

124. Kwa tahadhari ni wajibu kujiepusha na jasho la mnyama aliyezoea

kula vinyesi vya watu, na jasho la kila mnyama anayekula vinyesi vya

watu.

Jasho la janaba lililotokana na haramu

125. Jasho la janaba iliyotokana na haramu sio najisi ingawa ni bora

kuchukua tahadhari, ni sawasawa jasho limetoka wakati wa jimai au

baada yake, kwa mwanaume au kwa mwanamke, kwa zinaa au kwa

liwati, kwa kumwingilia mnyama au kwa kufanya punyeto. Na

punyeto ni mtu binafsi kukusudia kujitoa manii.

126. Mtu akimwingilia mke wake katika wakati ambao ni haramu kwake

kumwingilia, mfano akimwingilia wakati wa funga ya mwezi wa

Ramdhani au katika hedhi, kwa tahadhari ya sunna ajiepushe na jasho

lake.

Page 39: al-Masailu-l-Islamiyyah

25

Al-Masailul Islamiyah

127. Mwenye janaba linalotokana na haramu akitayamamu badala ya

kuoga kutokana na udhuru, kisha akatoka jasho baada ya kutayama-

mu, inajuzu kwake kuswali pamoja na nalo, lakini udhuru wake ukii-

sha kisha akatoka jasho haifai kwake kuswali na jasho hilo na ni juu

yake kujiepusha nalo kwa tahadhari ya sunna hadi aoge.

128. Akipata janaba kwa njia ya haramu kisha akamwingilia mke wake

kwa njia ya halali, kisha akapata janaba kwa njia ya haramu, basi -

kwa tahadhari ya sunna - ajiepushe na jasho lake vile vile.

NJIA ZA KUTHIBITISHA NAJISI

129. Najisi inathibitika kwa moja ya njia tatu:-

Mtu binafsi kuwa na yakini kwa kunajisika kitu, akidhani kunajisika kitu,

hailazimu kwake kujiepusha nacho, hakuna mushkeli kula katika migaha-

wa na magenge ambayo watu wamezoea na wanakula humo ambao hawa-

jali tohara na najisi ikiwa hajapata yakini kuwa chakula anachopewa ni

najisi.

Mmiliki au mtumiaji wa chombo anapotoa taarifa juu ya unajisi wa kitu,

kama vile mke au mtumishi akisema chombo hiki au kitu hiki kilichopo

mkononi na chini ya uangalizi wake ni najisi, basi inamlazimu kujiepusha

nacho, na hii inaitwa habari ya mmiliki.

Kutoa taarifa watu wawili kwa unajisi wa kitu, vivyo hivyo akitoa taarifa

mtu mmoja mkweli kuhusu unajisi wa kitu inamlazimu kujiepusha nacho-

kwa ilivyo na nguvu zaidi.

130. Ikiwa hajui unajisi wa kitu au utohara wake kwa kutokujua kwake

mas’ala, mfano kutojua kuwa jasho la janaba ya haramu ni najisi au

ni tohara, ni wajibu wake aulize ili ajue hukumu, lakini akipata shaka

juu ya unajisi wa kitu au kutokuwa kwake najisi pamoja na kujua

kwake mas’ala, mfano akishuku kuwa hii ni damu au sio damu? Au

Page 40: al-Masailu-l-Islamiyyah

26

Al-Masailul Islamiyah

akiwa hajui kuwa hii ni damu ya kiroboto au damu ya binadamu, basi

itakuwa tohara.

131. Kitu najisi ambacho anashaka kuwa kimekuwa tohara au laa kitabaki

kuwa ni najisi, na kitu tohara ambacho anashuku kuwa kimenajisika

au laa ni tohara, na kama anaweza kujua utohara wake au unajisi wake

haitomlazimu kuchunguza.

132. Akijua kuwa moja kati ya vyombo viwili au nguo mbili imenajisika,

na zote mbili alikuwa anazitumia na wala hajui ipi ndio imenajisika,

ni wajibu ajiepushe nazo zote, lakini ikiwa hajajua kwa mfano, kuwa

nguo yake ndio imenajisika au nguo ambayo haitumii kabisa na

ambayo ni nguo ya mwingine, haitomlazimu kujiepusha na nguo

yake.

NAMNA YA KUNAJISIKA VITU VILIVYO TOHA-

RA

133. Kitu najisi kikikutana na kitu tohara na vyote viwili au kimoja wapo

kina unyevunyevu kiasi kwamba unyevunyevu wa kimoja wapo una-

hamia kwa kingine, kitu tohara kinanajisika, ikiwa unyevunyevu ni

mdogo sana kiasi kwamba hausambai kwa kingine hakitonajisika.

134. Kitu tohara kikikutana na kitu najisi na akashuku je vyote au kimoja

wapo kilikuwa na unyevunyevu, kitu tohara hakitanajisika.

135. Kama kuna vitu viwili haijulikani kipi ni najisi na kipi ni tohara,

kimoja wapo kikigusa kitu tohara chenye unyevunyevu, kitu tohara

hakitanajisika, na kama kitu tohara kitagusa vyote viwili kitanajisika.

136. Ardhi, kitambaa na mfano wake kikiwa kimeloana inanajisika sehe-

Page 41: al-Masailu-l-Islamiyyah

27

Al-Masailul Islamiyah

mu ambayo inagusana na najisi, na iliyobaki itakuwa tohara vivyo

hivyo tikiti maji, tango n.k.

137. Mafuta, jamu na mfano wake ikiwa kwa namna ambayo kama ita-

chukuliwa, kiasi nafasi iliyopo itajaa haraka basi itanajisika yote kwa

kukutana tu na najisi, na ikiwa nafasi iliyopatikana kwa kupunguza

haijai haraka basi hainajisiki kwa kupatwa na najisi, isipokuwa sehe-

mu iliyokutana na najisi hadi nafasi hiyo ijae baadae, hivyo kinyesi

cha panya kikidondokea katika hali hii ya pili itanajisika sehemu

iliyogusana na kinyesi tu na iliyobaki itakuwa tohara.

138. Nzi au anayefanana naye katika wadudu akitua juu ya kitu najisi che-

nye unyevu nyevu, kisha akaruka na kutua juu ya kitu kingine toha-

ra, chenye unyevunyevu kitu tohara kina najisika kama itajulikana

kuwa nzi ana chembechembe za viini vya najisi,vivyo hivyo akipata

yakini juu ya kugandamana najisi katika mguu wa mnyama kisha

akapata shaka kuwa imeondoka au laa, ama ikiwa hakujua basi ni

tohara.

139. Sehemu ya mwili ikinajisika na ikawa na jasho, kisha jasho najisi

likatiririka kwenda sehemu nyingine, sehemu iliyofikiwa itanajisika,

na ikiwa halitiririka hadi sehemu nyingine basi sehemu ya mwili

iliyobaki itakuwa tohara.

140. Kamasi na makohozi yanayotoka puani na mdomoni yakiwa na damu

sehemu iliyogusana na damu ni najisi na iliyobaki ni tohara, kikitoka

kitu nje ya pua au kinywa sehemu ambayo anajua kuwa imegusana na

sehemu iliyonajisika ni najisi, na sehemu ambayo anashuku katika

kukutana na sehemu iliyonajisika itakuwa tohara.

141. Birika ambalo ndani yake kuna maji na chini yake kuna tundu iki-

wekwa juu ya ardhi iliyonajisika, na maji yatokayo kwenye lile tundu

yanajikusanya chini yake kiasi cha kuzingatiwa kuwa maji yaliyo

Page 42: al-Masailu-l-Islamiyyah

28

Al-Masailul Islamiyah

ndani ya birika na yale ya chini ni mamoja yaliyo ndani ya birika pia

yatakuwa yamenajisika. Na yakitiririka juu ya ardhi au yakipenya

humo, endapo tobo la birika likiwa limeungana na ardhi iliyonajisi

kiasi chakuwa inazuwia kububujika kwa majimaji ya ndani ya birika,

yatahukumiwa kuwa yamenajisika pia, lakini ikiwa tundu haikuunga-

na na ardhi iliyonajisika na wala hayahesabiki maji yaliyomo ndani ya

birika na yaliyo nje ni mamoja au maji yaliyo katika birika yakitoka

kwa nguvu na msukumo, yaliyo ndani ya birika hayatokuwa najisi.

142. Mtu akiingiza kitu mwilini na kikakutana na najisi, baada ya kukitoa

kikiwa hakikuchafuka na najisi, kitakuwa tohara. Akiingiza bomba

mahali pa kutokea haja kubwa au akidunga sindano au kisu na kitu

mfano wa viwili hivyo mwilini na baada ya kukitoa hakikuchafuka na

najisi hakitokuwa najsi, na vivyo hivyo mate au kamasi yakutanapo

na damu mdomoni na puani, kisha yakitoka bila ya kuchafuka na

damu yatakuwa tohara.

143. Kitu kilichonajisika kinanajisisha kama vile kiini cha najisi isipoku-

wa haitolazimu juu yake hukumu zake zote mfano kitu kikinajisika

kwa mkojo, inalazimu kurudiarudia kukitoharisha kama maji ni

machache na wala hailazimu kurudia rudia kwa kitu kilichokutana na

kitu kilichonajisika kwa mkojo.

MAS’ALA

144. Inaharamishwa kuitia najisi hati na maandishi ya Qur’an tukufu na ni

wajibu kuondoa najisi kwayo haraka pindi inaponajisika, lakini liki-

najisika jalada lake ni wajibu kulitoharisha ikiwa kuacha kwake kuna-

lazimu kuidharau, vivyo hivyo inaharamishwa kutia najisi (jalada

lake) na ni wajibu kutoharisha haraka msikiti, sehemu takatifu, turba

ya Imamu Hussein na hukumu ni hiyo hiyo katika turba ya Mtume

Page 43: al-Masailu-l-Islamiyyah

29

Al-Masailul Islamiyah

Mtukufu na Maasumina wengine kwa tahadhari.

145. Ni haramu kuweka Qur’an juu ya najisi mfano damu, na mzoga hata

kama ni mkavu kama itahesabiwa kuwa ni kudharau Qaur’an na ni

wajibu kuiondoa katika vitu hivyo haraka.

146. Inaharamishwa kuiandika Qur’an kwa wino najisi hata kama ni heru-

fi moja na kama akiandika ni wajibu kuifuta kwa kifuto au mfano

wake.

147. Ni haramu kumpa kafiri Qur’an tukufu kama hiyo itasababisha kuid-

harau Qur’an na ni wajibu kuichukua Qur’an kutoka kwake.

148. Karatasi ya Qur’an tukufu au kitu kingine ambacho ni wajibu kuki-

heshimu kama vile karatasi ambayo imeandikwa jina la Mwenyezi

Mungu, Nabii, Imamu au Fatma Zahra likiangukia chooni ni wajibu

kulitoa na kulitoharisha hata kama hilo litalazimu kutoa gharama, na

kama haiwezekani kuitoa basi kwa tahadhari ya wajibu aache kukitu-

mia choo hicho hadi apate yakini ya kuyeyuka na kumalizika maan-

dishi ya karatasi hiyo, vivyo hivyo turba ya Imamu Huseini ikiangu-

kia chooni na ikashindikana kuitoa ni wajibu kuacha kujisaidia katika

choo hicho hadi turba iyeyuke na kumalizika.

149. Ni haramu kula na kunywa najisi au kilichonajisika kama vile maji

yaliyonajisika, vivyo hivyo inaharamishwa kumlisha mwingine hata

kama ni mtoto lakini mtoto mwenyewe akila najisi si wajibu kumzuia

ikiwa najisi hiyo haina madhara kwake.

150. Hakuna mushakeli kuuza au kuazima kitu kilichonajisika ambacho

inawezekana kukitoharisha ikiwa muuzaji au mwazimishaji atatoa

taarifa juu ya unajisi wake.

151. Mtu akiona mtu anakula najisi au anaswali na nguo najisi haimlazimu

kumwambia.

Page 44: al-Masailu-l-Islamiyyah

30

Al-Masailul Islamiyah

152. Ikiwa sehemu ya godoro, mto au nyumba yake ni najisi na akaona

mgusano wa nguo za wanaoingia katika nyumba hiyo au miili yao au

kitu kingine na sehemu najisi nayo ikiwa na unyevunyevu ni lazima

kwake kuwaeleza kwa tahadhari ya wajibu ikiwa wamekuwa wageni

wake na wamekuja kwa wito wake.

153. Mwenye nyumba akijua wakati wa kula unajisi wa chakula ni wajibu

wake kuwaeleza wageni wake, ama akijua hilo mmoja wa wageni sio

lazima kwake kuwaeleza wengine.

VINAVYOTOHARISHA

154. Vinavyotoharisha vitu vilivyonajisika ni kumi na mbili:-

1. Maji 5. Kupungua theluthi mbili za juisi ya zabibu mbivu

2. Ardhi 6. Kuhama 8. Kuondoka kiini cha najisi

3. Jua 7. Uislamu 9. Kumtoharisha mnyama anayezoea

kula kinyesi

4. Kubadilika 10. Kufuata 11. Kutoweka kwa mwislamu

12. Kutoka damu kiwango kinachojulikana kwa mnyama.

MAJI

155. Maji yanatoharisha vitu kwa sharti nne:-

1- Yawe halisi

2- Yawe tohara

3- Yasiwe mudhafu wakati wa kutoharisha kitu kilicho najisika

4- Kusibaki baada ya kutoharisha kitu kilichonajisika kiini cha

najisi

156. Utoharishaji wa vitu vilivyonajisika kwa maji machache unasharti

zingine maelezo yake yatakuja baadae.

Page 45: al-Masailu-l-Islamiyyah

31

Al-Masailul Islamiyah

157. Ni wajibu katika kutoharisha chombo kilichonajisika kioshwe kwa

maji machache mara tatu kwa tahadhari, na inatosha kukiosha mara

moja katika kuru au maji yanayotiririka lakini chombo kilicho lamb-

wa na mbwa au alichonywea humo ni wajibu kwanza kukisugua kwa

mchanga tohara kisha kukitoharisha katika kuru au maji yanayotiriri-

ka mara mbili ama chombo kilicho dondokewa na ute wa mbwa au

maji maji yake ni bora kukisugua kwa mchanga na kukiosha mara

tatu.

158. Ikiwa mdomo wa chombo ambacho mbwa amelamba ni mfinyu na

ikashindikana kusugua ndani ya chombo kwa udongo itamlazimu iki-

wezekana kuzungusha tambara kwenye kijiti na kusugua ndani ya

chombo kwa mchanga kwa njia hiyo hiyo ikishindikana anamwagia

mchanga katika chombo na kutikisa kwa nguvu hadi mchanga ufike

sehemu zote za ndani.

159. Chombo ambacho kimelambwa nguruwe au kunywa humo ni wajibu

kukiosha kwa maji machache mara saba na inatosha kukiosha katika

kuru au maji yanayotiririka mara moja na wala hailazimu kusugua

kwa mchanga ingawa ni bora kusugua kwa mchanga.

160. Ikitakiwa kusafisha chombo kilichonajisika kwa pombe kwa maji

machache inatosha mara tatu ingawa kwa tahadhari ni bora zaidi

kukiosha mara saba kwa maji machache.

161. Mitungi na vyombo vya urembo vilivyotengenezwa kwa udongo ulio-

najisika au ambavyo maji najisi yamepenya ndani yake vikiwekwa

kwenye kuru au maji yanayotiririka na maji yakaenea sehemu zote

vitakuwa vimetoharika na ikitakiwa kutoharishwa ndani yake pia

inalazimu vibakie katika kuru au maji yanayotiririka kwa muda ili

maji yaenee sehemu zote za ndani.

162. Chombo kilicho najisi inawezekana kukitoharisha kwa maji

Page 46: al-Masailu-l-Islamiyyah

32

Al-Masailul Islamiyah

machache kwa njia mbili:-

1. Kwa kujaza chombo maji kisha anayamwaga mara tatu.

2. Au kuweka kiasi cha maji kisha anayazungusha humo kiasi cha

kufika sehemu zote zilizonajisika kisha anayamwaga na anaru-

dia mara tatu.

.

163. Kitu kikinajisika kwa mkojo wa mtoto mchanga ambaye hajaanza

kula chakula na hajanyonya maziwa ya nguruwe au kafiri, kikimwa-

giwa maji mara moja kiasi kwamba maji yanafika sehemu zote zili-

zonajisika kinatoharika lakini ni sunna kufanya tahadhari kwa

kumwgia maji mara mbili

2-Ardhi

164. Ardhi inatoharisha nyayo na viatu kwa sharti tatu :-

1. Ardhi iwe tohara

2. Iwe kavu

3. Kiini cha najisi kiondoke kama vile damu, mkojo au kilichonajisika

kama vile udongo ulionajisika ambao umegandamana katika sehemu za

nyayo au viatu kwa kutembea juu ya ardhi au kusugua juu yake kama

ambavyo inamlazimu katika kutoharisha kwa ardhi, ardhi iwe ni udon-

go au jiwe, vile vile sehemu ya chini ya nyayo au kiatu haitohariki kwa

kutembea juu ya godoro au jamvi, ama jiwe, changarawe, sementi iliyo-

tengenezwa kwa changarawe hukumu yake ni hukumu ya ardhi inato-

harisha.

165. Ni bora katika kutoharisha chini ya nyayo au viatu atembee juu ya

ardhi hatua kumi na tano au zaidi hata kama najisi itaondoka kwa

hatua chache kuliko hizo.

3 - Jua

166. Jua linatoharisha ardhi, majengo na mfano wake kama vile milango,

Page 47: al-Masailu-l-Islamiyyah

33

Al-Masailul Islamiyah

madirisha ya majengo yakinajisika vivyo hivyo hutoharisha misumari

iliyopigiliwa ukutani na hiyo ni kwa masharti matano baadhi yake ni

kwa tahadhari:-

1. Kitu najisi kiwe na unyevuunyevu kiasi kikigusana na kitu unyevu

nyevu wake unahamia kwake, kikiwa kikavu inalazimu kukiloanisha ili

kikaushwe na jua.

2.Kiini cha najisi kiondoshwe kabla ya kupigwa jua.

3. Jua lisizuiliwe na kitu, kama jua litazuiliwa na pazia, mawingu n.k na

likakausha (kitu hicho) hakitohariki, lakini kama mawingu au pazia ni

jepesi sana kiasi halizuii jua hakuna mushkeli.

4. Jua peke yake likaushe kitu najisi, jua halitotoharisha kama litasaidiwa

na upepo katika kukausha lakini hakuna mushikeli ikiwa upepo ni

mdogo sana kiasi inasemwa kimekaushwa na jua.

5. Jua likaushe jengo ambalo najisi imepenya kwa mara moja yaani kwa

mchomozo mmoja, ama jua likipiga juu ya ardhi na jengo lililonajisika

na likikausha nje ya jengo na ardhi kisha likapiga mara ya pili na

likakausha ndani yake itatoharika nje tu na ndani patabaki kuwa najisi.

4. Kubadilika

167. Kitu najisi kikibadilika kiasi kwamba kinaonekana katika sura ya kitu

tohara kinakuwa tohara na hii inaitwa “kubadilika”ni sawa kubadili-

ka ni kwa kiini cha najisi au kitu kilichonajisika mfano ubao uliona-

jisi kubadilika na kuwa majivu au mbwa kuzikwa katika ardhi ya

chumvi na kugeuka chumvi lakini hakitohariki ikiwa uhakika wa kitu

haujabadilika mfano ngano kuwa unga au kutengenezwa mkate au

maziwa yaliyonajisi kutengenezwa jibini au mgando.

168. Pombe ikibadilika yenyewe na kuwa siki au kwa kubadilishwa mfano

kuweka siki au chumvi humo inakuwa tohara.

169. Siki iliyotengenezwa kwa zabibu mbivu, kishimishi au tende najisi ni

najisi kwa tahadhari ya wajib

Page 48: al-Masailu-l-Islamiyyah

34

Al-Masailul Islamiyah

5 - Kupungua theluthi mbili za juisi ya zabibu mbivu

170. Maji ya za bibu mbivu hayanajisiki ikiwa yatachemshwa kwa moto

lakini ni haramu kuyanywa, na yakichemka na kupungua theluthi

mbili na ikabaki theluthi moja ni halali kuinywa, lakini ikichemka

yenyewe haiwi halali kuinywa isipokuwa ikigeuka siki.

171. Zikipungua theluthi mbili za juisi ya zabibu bila ya kuchemshwa

kama iliyobaki itachemka yenyewe au kwa moto ni haramu kuinywa

na ikitakiwa kuwa halali inalazimu kuchemshwa hadi ipungue the-

luthi mbili.

172. Punje ya zabibu ikitumbukia katika kitu kilichochemshwa kina-

chochemka kwa moto na punje ikichemka pamoja nacho sio wajibu

kujiepusha nacho.

173. Ikitakiwa kutengenezwa jamu katika viungu na masufuria tofauti

tofauti hakuna mushikeli katika kutumia mwiko katika chungu amba-

cho juisi yake imechemka katika viungu ambavyo havijachemka na

vikichemka vyote asitumie mwiko kwa sababu ya uharamu -katika

viungu ambavyo havijapungua theluthi mbili kwenye viungu

ambavyo vimepungua thelutghi mbili pamoja na kutobadilika,

vinginevyo hakuna mushkeli

6 - Kuhama

174. Inatoharika damu ya binadamu au mnyama anayetoka damu kwa kasi

wakati wa kuchinjwa ikihama kwenda katika mwili wa mnyama

asiyetoka damu kwa kasi na ikahesabika kuwa ni katika damu yake na

hii inaitwa “kuhama”, ama damu ambayo anainyonya luba kwa

mwanadamu ambapo haitwi damu ya luba bali damu ya binadamu

Page 49: al-Masailu-l-Islamiyyah

35

Al-Masailul Islamiyah

inakuwa ni najisi.

175. Mtu akiua kunguni kwenye mwili wake na hajui kuwa damu iliy-

otoka ya kunguni au ni ambayo ameinyonya kutoka kwake basi ni

tohara, vivyo hivyo akijua kuwa ni katika damu ya kunguni lakini

imeshakuwa ni sehemu ya mwili wake, ama ikiwa muda wa kuiny-

onya na kumuuwa kwake ni mchache sana kiasi kwamba inasemwa

kuwa hii damu ni damu ya binadamu au haijulikani kuwa ni damu ya

kunguni au damu ya binadamu itakuwa najisi kwa tahadhari.

7 - Uislamu

176. Kafiri akitamka shahada yaani akisema “Ash hadu an laa ilaaha ila

llah wa ash hadu anna Muhammadan rasulullah” anakuwa mwislam.

Mwili wake, mate yake, makamasi yake na jasho lake vinatoharika

baada ya kuslim. Lakini ikiwa kuna kiini cha najisi katika mwili

wake wakati wa kusilimu kwake itamlazimu kuondoa najisi na kuto-

harisha sehemu yake bali kiini cha najisi kikiondoka kabla ya kusil-

imu kwake kwa tahadhari ya sunna atoharishe sehemu iliyonajisika.

177. Kafiri akitamka shahada mbili na wala haijulikani kuwa uislamu

umeingia katika moyo wake au laa ni tohara lakini ikijulikani kuwa

uislam haujaingia moyoni ni najisi lakini mnafiki ambaye hajasilimu

kwa moyo lakini anatekeleza uislamu kivitendo ni tohara.

8. Kufuata

178. Kufuata: Ni kutoharika najisi kwa njia ya kutoharika kitu kilichona-

jisi kama vile kutoharika watoto kafiri wasiobaleghe kwa kusilimu

mmoja wa wazazi wawili au babu na bibi.

179. Pombe ikiwa siki chombo chake kinatoharika kwa kufuata kwake

hadi sehemu iliyofikia pombe vile vile kifuniko, kitambaa kina-

Page 50: al-Masailu-l-Islamiyyah

36

Al-Masailul Islamiyah

chowekwa kwenye mdomo wa chombo kama kitalowana kwa unye-

vunyevu huo lakini sehemu ya nje ya chombo hicho ikilowana kwa

pombe hiyo- kwa tahadhari ya sunna- ni kujiepusha nacho baada ya

kugeuka siki.

180. Ubao au jiwe ambalo amelazwa juu yake maiti na nguo ambayo ina-

funika mwili wake na mkono unaomuosha vyote vinatoharika baada

ya kukamalizika josha.

181. Anayetoharisha kitu mkono wake unatoharika baada ya kutoharika

kitu hicho kilichonajisika.

182. Maji yanayobaki katika nguo au mfano wake baada ya kuitoharisha

kwa maji machache na baada ya kutengana na maji ya kuoshewa ni

tohara.

9. Kuondoka kiini cha najisi

183. Mwili wa mnyama unatoharika - na unajumuisha viungo vyote vya

mwili wa mnyama hadi mdomo kwa upande wa ndege- kwa kuondo-

ka najisi kwake ikitapakaa najisi mfano damu au kilichonajisika

mfano maji, kisha kiini cha najisi au kilichonajisika kikaondoka una-

toharika, vivyo hivyo inatoharika sehemu ya ndani ya mwanadamu

kama vile tumbo, ndani ya pua na kinywa kwa kuondoa kiini cha

najisi kwayo, damu ikitoka baina ya meno na ikamalizika katika maji

maji ya kinywa haitomlazimu kutoharisha ndani ya kinywa vivyo

hivyo meno ya bandia yakinajisika ingawa ni bora zaidi kuyatohar-

isha.

184. Vumbi au mchanga najisi ukiangukia kwenye nguo au godoro au

mfano wake kisha akakung’uta au kutikisa kwa namna ambayo vumbi

najisi inaondoka kwa (kufanya hivyo) itakuwa tohara.

10. Kumtoharisha mnyama anayekula vinyesi

Page 51: al-Masailu-l-Islamiyyah

37

Al-Masailul Islamiyah

185.Mkojo na kinyesi cha mnyama - aliyezoea kula vinyesi vya binadamu

- ni najisi na ikitakiwa kumtoharisha ni lazima kumzuia mnyama huyo

kwa muda kutokana na kula vinyesi kiasi ambapo hatoitwa mnyama

anayekula vinyesi, na alishwe malisho tohara kwa muda huo.

186. Ngamia anazuiliwa siku arobaini, ng’ombe siku thelathini, kondoo na

mbuzi siku kumi, bata siku saba au siku tano na kuku ni siku tatu, na

mnyama atazuiwa kula najisi na alishwe chakula tohara katika muda

huu na lau ikithibiti anuani ya(mnyama mla kinyesi) baada ya muda

huu pia ni lazima azuiwiliwe kula najisi kwa muda mwingine ili asi-

itwe baada ya muda huo - mnyama anayekula kinyesi.

11. Kutoweka kwa mwislamu

187. Mwili wa mwislamu ukinajisika au nguo yake na kitu chake kingine

kama vile vyombo, godoro n.k. ambavyo viko katika milki yake kisha

akatoweka pamoja na vitu hivyo, vitu hivi vinahukumiwa kuwa ni

tohara kama yatatimia masharti sita baadhi yake ni kwa tahadhari:-

1. Mwislamu atapaswa aitakidi unajisi wa kitu hicho ambacho kimetia

najisi mwili wake au nguo yake n.k, ikiwa itagusa nguo yake au mwili

wake maji ya zabibu iliyochemka naye haitakidi kuwa ni najisi kisha

akatoweka basi kutoweka(kughibu) kwake hakutoharishi.

2. Mwislamu Ajue kufika najisi kwenye mwili wake au nguo yake au

kinacho shabihiana na hivyo.

3. Mwislamu aonekane baada ya kutoweka kwake anatumia vitu hivyo

katika amali ambazo zinatakiwa kuwa na tohara mfano kama anaswali

kwa nguo hiyo iliyonajisika.

4. Mwislamu mwenyewe kutambua kuwa tohra inatakiwa katika amali

Page 52: al-Masailu-l-Islamiyyah

38

Al-Masailul Islamiyah

hiyo ikiwa hatambui ulazima wa tohara kwa vazi la mweye kusali na

akasali kwa nguo hiyo haiwezi kuzingatiwa kuwa nguo hiyo ni tohara

kwa sabau ya kutoweka kwake.

5. Mwislamu huyo achukue jukumu la kutoharisha kitu hicho, akipata

yakini kwamba hajakitoharisha kitu hicho hakitazingatiwa kuwa ni

tohara, ama ikiwa hakuna tofauti baina ya tohara na najisi kwa mtazamo

wa mwislamu huyo basi kukizingatia kuwa ni tohara wakati huo ni

mahali pa mushikeli.

6. Mwislamu huyo awe baleghe - kwa tahadhari.

12. KUTOKA DAMU KWA KIWANGO KINACHOJULIKANA

KWA MNYAMA

188. Mnyama aliyehalali kuliwa akichinjwa kwa njia ya kisharia na kuto-

ka kwake damu kwa kiwango cha kawaida kinachojulikana, damu

iliyobaki katika mwili wake itakuwa tohara.

MAS’ALA

189. Mtu binafsi kuwa na yakini kwamba kitu kilichokuwa najisi kime-

shatoharika au wakitoa taarifa ya hilo watu wawiliwaadilifu inahuku-

miwa kuwa ni tohara, vivyo hivyo kama atatoa taarifa aliyetoharisha

kitu kilichokuwa najisi kama atapata matumaini kwa kauli yake au

ikiwa ndio mmiliki.

190. Mwakilishi wa mtu katika kutoharisha nguo yake kama atasema nguo

hii imetoharika basi nguo hiyo itakuwa tohara.

191. Mwenye wasiwasi (mwingi) naye ni ambaye hapati yakini kwa uto-

hara wakati wa kutoharisha kitu najisi inajuzu kwake kutosheka na

dhana au afanye kama wanavyotoharisha watu wa kawaida kwa kitu

najisi.

Page 53: al-Masailu-l-Islamiyyah

39

Al-Masailul Islamiyah

HUKUMU ZA VYOMBO

192. Chombo kilichotengenezwa kwa ngozi ya mbwa au nguruwe wa nchi

kavu au mfu ni najisi na inaharamishwa kulia na kunywea humo,

haifaikutawadhia wala kuogea na wala hakitumiki katika amali

ambayo tohara ni sharti humo bali kwa tahadhari ya sunna asitumie

ngozi ya mbwa au nguruwe au mfu hata kwa visivyokuwa vyombo.

193. Inaharamishwa kulia na kunywea katika vyombo vya dhahabu na

fedha na kwa tahadhari ya sunna ni kuacha kuvitumia kabisa hata

katika mapambo.

194. Chombo kilichopo katika milki ya asiyekuwa mwislamu ni tohara

maadamu mtu hajapata yakini ya unajisi wake.

195. Hakuna mushikeli kutumia vyombo vilivyochovywa dhahabu na

fedha.

UDHU

196. Yaliyo wajibu katika udhu ni: Nia, kuosha uso, kuosha mikono

miwili, kupaka maji utosini na juu ya miguu miwili.

KUOSHA USO

197. Ni wajibu kuosha uso kwa mapana na marefu kuanzia kwenye mao-

teo ya nywele hadi mwisho wa kidevu, na upana ni sehemu iliyozun-

gukwa na kidole gumba na kidole cha kati na kama hajaosha sehemu

katika kiasi hicho udhu wake utabatilika na ili apate yakini ya kufika

maji hadi kwenye kiasi hicho inamlazimu kuosha sehemu ya pembe-

zoni mwake vile vile.

Page 54: al-Masailu-l-Islamiyyah

40

Al-Masailul Islamiyah

198. Kama uso wa mtu au kiganja chake ni kikubwa au kidogo kuliko

maumbile ya watu wa kawaida inamlazimu atazame kiwango wana-

choosha nyuso zao watu wa umbile la kawaida na mikono yao kisha

aoshe, hukumu ni hiyo hiyo ikiwa nywele za utosi wa kichwa chake

zimevuka mpaka wa kawaida na kuteremka hadi kwenye paji au

ikiwa hana nywele kwenye utosi wa kichwa chake ni wajibu kuosha

paji la uso kwa kiwango cha watu wenye maumbile ya kawaida.

199. Ni wajibu kuosha uso na mikono miwili kuanzia juu kwenda chini

kama akiosha kuanzia chini kwenda juu udhu wake utabatilika.

200. Akiloanisha kiganja chake na akapaka kwacho uso wake na mikono

yake na ikiwa kiwango cha maji maji ya kiganja ni kwa kiasi kwam-

ba maji yanatiririka kidogo usoni na mikononi wakati wa kupaka

kwake inatosha.

KUOSHA MIKONO MIWILI

201. Baada ya kuosha uso ni wajibu kuosha mkono wa kulia kisha mkono

wa kushoto kuanzia kwenye kiwiko hadi kwenye ncha za vidole.

202. Ili kuwa na yakini kuwa ameosha kiwiko aoshe juu yake kidogo.

203. Anayeosha viganja vyake hadi kwenye vifundo viwili kabla ya

kuosha uso ni wajibu wake aoshe mikono yake hadi kwenye ncha za

vidole, na akiosha mikono yake hadi kwenye vifundo viwili na wala

asioshe viganja viwili udhu wake unabatilika.

204. Muosho wa kwanza wa uso na mikono miwili ni wajibu na wa pili ni

sunna, wa tatu na kuendelea ni haramu, ama ni muosho upi ni wa

kwanza au wa pili au wa tatu hiyo inategemea nia ya mwenye

kutawadha, kama atamwagia maji mara kumi kwa nia ya muosho wa

Page 55: al-Masailu-l-Islamiyyah

41

Al-Masailul Islamiyah

kwanza hakuna mushikeli na zote zinazingatiwa kuwa ni muosho wa

kwanza, na kama ataosha uso mara tatu kwa maana ya miosho mitatu

basi muosho wa tatu utakuwa haramu.

KUPAKA KICHWA

205. Baada ya kuosha uso na mikono miwili ni wajibu kupaka utosi wa

kichwa kwa unyevunyevu uliobaki kwenye kiganja, na kwa tahadhari

ya wajibu apake kwa kiganja cha kulia kuanzia juu kwenda chini.

206. Robo ya utosi wa kichwa inayoelekeana na uso ndio sehemu ya kupa-

ka, hivyo inatosha kupaka mahali na sehemu hiyo na kwa kiasi cho-

chote ingawa ni wajibu kupaka kiwango cha upana wa kidole, na kwa

tahadhari ya sunna urefu uwe kwa urefu wa kidole na upana uwe kwa

upana wa vidole vitatu vilioungana.

207. Sio wajibu kupaka ngozi ya kichwa bali inasihi kupaka juu ya nywele

za kichwa, lakini kama nywele za utosi wa kichwa chake ni ndefu

sana kiasi kwamba kama akizichana zitafika usoni au zinaangukia

sehemu ya pili kama za wanawake ni wajibu apake kwenye maoteo

ya nywele.

KUPAKA MIGUU MIWILI

208. Baada ya kupaka kichwa ni wajibu kupaka juu ya miguu miwili kwa

unyevunyevu ule ule wa udhu uliobakia katika viganja viwili kuanzia

kwenye ncha za nywele hadi kwenye kongo mbili, na kwa tahadhari

ya sunna ni kupaka hadi kwenye maungio ya mguu.

209. Kwa tahadhari ya sunna atangulize kupaka mguu wa kulia kabla ya

mguu wa kushoto vivyo hivyo apake mguu wa kulia kwa mkono wa

kulia na mguu wa kushoto kwa mkono wa kushoto.

Page 56: al-Masailu-l-Islamiyyah

42

Al-Masailul Islamiyah

210. Katika kupaka kichwa na sehemu ya juu ya miguu miwili ni wajibu

kupitisha mikono juu ya sehemu hizi, kama ataweka kiganja chake

juu ya kichwa chake na miguu yake, kisha akavuta kichwa na miguu

badala ya kupitisha mikono yake udhu wake utabatilika.

211. Ni wajibu sehemu ya kupakwa iwe kavu, ikiwa itakuwa na unyevu

nyevu kiasi ambacho unyevu nyevu wake unaathiri, unyevunyevu wa

kiganja hiyo itakuwa kinyume na tahadhari ya wajibu, lakini hakuna

mushkeli ikiwa unyevunyevu ni kidogo sana kiasi kuwa

utapoonekana unyevu nyevu utasemwa kuwa ni unyevunyevu wa

kiganja.

212. Kama unyevu nyevu wa kiganja utakauka na usibaki wa kupa kwayo,

haijuzu kuchukua unyevunyevu kutoka nje bali ni wajibu kuchukua

katika sehemu za udhu na kupaka kwa unyevunyevu huo.

213. Kupaka juu ya soksi na khuf ni batili, lakini hakuna mushkeli kupaka

juu yake ikiwa ni kutokana na baridi kali au hofu kutokana na wezi na

wanyama wakali na hakuweza kuvua soksi zake, na ikiwa juu ya soksi

kuna najisi inamlazimu kuweka kitu tohara juu yake kisha apakae, na

kwa tahadhari ya wajibu atayamamu vile vile.

214. Kama juu ya miguu kuna najisi na wala hawezi kutoharisha kwa ajili

ya kupaka juu yake itamlazimu kutayamamu.

UDHU WA IRTIMASI “KUZAMISHA”

215. Udhu wa itrimasi: Ni mwenye kutawadha kuzamisha uso wake na

mikono yake kwenye maji na kuutoa kwa nia ya udhu, na akiweka nia

wakati wa kuzamisha uso wake na mikono yake katika maji na

akabakia na nia yake hadi wakati wa kuitoa kwenye maji na akaende-

lea na nia yake hadi wakati wa kuutoa katika maji udhu wake unasi-

hi, vivyo hivyo unasihi udhu wake kama atazamisha mkono wake wa

Page 57: al-Masailu-l-Islamiyyah

43

Al-Masailul Islamiyah

kulia katika maji kwa nia ya udhu wa irtimasi na akaosha mkono wa

kushoto kwa nia ya udhu usio wa irtimasi.

216. Katika udhu wa irtmasi vile vile ni wajibu kuosha uso na mikono

kuanzia juu kwenda chini, anuie udhu wakati wa kuzamisha uso wake

na mikono yake katika maji, ni wajibu aingize uso wake kuanzia

kwenye paji la uso katika maji na mikono yake kuanzia kwenye

kiwiko, na anuie udhu wakati wa kutoa sehemu hizi kwenye maji, ni

wajibu atoe uso wake kuanzia upande wa paji na atoe mikono yake

kuanzia kwenye kiwiko.

217. Hakuna mushikeli kutawadha baadhi ya viungo vyake kwa irtmasi na

vingine kwa njia isiyokuwa ya irtimasi.

MASHARTI YA UDHU

218. Ili udhu usihi kuna masharti kumi na mbili:-

1. Maji ya udhu yawe tohara

2. Maji yawe halisi na sio mudhafu

3. Maji, chombo na sehemu anayotawadhia viwe mubaha “halali”

4. Chombo cha kutawadhia kisiwe cha dhahabu au fedha.

5. Viungo vya udhu viwe tohara wakati wa kuosha na kupaka

6. Wakati uwe unatosha kwa udhu na swala

7. Atawadhe kwa nia ya kujikurubisha, yaani kutekeleza amri ya

Mwenyezi Mungu mtukufu kama atatawadha kwa ajili ya kupa-

ta ubaridi au kwa nia nyingine udhu wake unabatilika.

219. Sio lazima kutamka nia ya udhu au kuipitisha katika moyo bali

inatosha kuwa mwangalifu wakati wa kutawadha kiasi kwamba lau

akiulizwa swali ghafla nini anachofanya angesema natawadha.

8. Achunge utaratibu katika vitendo vya udhu yaani aanze kwa

Page 58: al-Masailu-l-Islamiyyah

44

Al-Masailul Islamiyah

kuosha uso, mkono wa kulia, mkono wa kushoto, kupaka kich-

wa, kisha kupaka miguu miwili kama hatafuata utaratibu huu

udhu wake utabatilika.

9. Afanye vitendo vya udhu kwa mfuatano.

220. Kama atatenganisha baadhi ya vitendo vya udhu kwa muda kiasi

ambacho atakapotaka kuosha au kupaka kiungo kinachofuata viungo

vilivyotangulia vitakuwa vimeshakauka udhu wake utabatilika.

221. Kama atafuatisha baina ya viungo vya udhu kimoja baada ya kingine

bila ya kuchelewesha lakini unyevunyevu wa viungo vilivyotangulia

ukakauka kwa sababu ya joto la mwili udhu wake utasihi.

10. Atawadhe mwenyewe yaani aoshe uso wake, mikono yake na

apake sehemu za kupaka bila ya msaada wa yeyote na mtu

akimtawadhisha au akimsaidia katika kufikisha maji kwenye

uso wake au mikono yake au akapaka kichwa chake au miguu

yake, udhu wake utabatilika.

222. Asiyeweza kutawadha mwenyewe ni wajibu amuweke mtu wa kum-

tawadhisha na kama akitaka ujira ampe akiweza, lakini mwenye kuta-

wadhishwa anuie nia ya udhu na apake kwa mikono yake sehemu za

kupaka, kama hawezi amuweke mtu atakayeshika mikono yake na

kupaka kwayo sehemu za kupaka, na kama hilo haliwezekani ni waji-

bu mwakilishi wake achukue unyevunyevu kutoka katika kiganja cha

mwenye kutawadhishwa na apake kwayo sehemu zake za kupaka.

11. Asiwe na kizuizi cha kutumia maji

12. Katika viungo vya udhu kusiwe na kizuizi cha kuzuia maji

kufika kwenye ngozi

Page 59: al-Masailu-l-Islamiyyah

45

Al-Masailul Islamiyah

HUKUMU ZA UDHU

223. Ambaye anashuku sana katika vitendo vya udhu au sharti zake,

mfano utohara wa maji au uhalali wake au kwa ghasb(bila ya ridhaa

ya mwenyewe), ni wajibu asizingatie shaka yake.

224. Akishuku kuwa udhu wake umebatilika au laa, atahukumu kubaki

kwa udhu wake, lakini kama hajafanya istibrai baada ya haja ndogo

kisha akatawadha, na kisha akaona unyevunyevu baada ya udhu hajui

ni mkojo au kitu kingine, udhu wake utabatilika.

225. Anayeshuku kuwa ametawadha au laa, ni wajibu atawadhe.

226. Anayejua kuwa ametawadha kisha akapatwa na kinachobatilisha

udhu kama vile mkojo na wala hajui kipi kimetangulia, ikiwa ni kabla

ya swala ni wajibu atawadhe, na ikiwa ni ndani ya swala anaivunja na

kutawadha tena, na ikiwa ni baada ya swala , basi swala yake aliy-

oiswali itasihi, lakini atawadhe kwa swala zinazofuata.

227. Akishuku baada ya swala kuwa ametawadha kabla ya swala au laa,

swala yake aliyoisali itasihi, lakini ni wajibu atawadhe kwa swala

zinazofuata

228. Akishuku katikati ya swala kuwa ametawadha kabla ya kuingia

kwenye swala au laa, swala yake inabatilika na ni wajibu atawadhe

kisha aswali.

229. Akishuku baada ya swala kuwa udhu wake umebatilika kabla ya

swala au baada ya yake, swala yake aliyoswali itasihi.

230. Mwenye ugonjwa wa salasi (kutoka mkojo) au mabutun “asiyeweza

kuzuia haja kubwa” akitambua kuwa ugonjwa wake utampa fursa

mwanzo wa wakati wa swala hadi mwisho kwa kiasi cha kutosha

udhu na swala, ni wajibu aswali katika wakati huo, na kama fursa

Page 60: al-Masailu-l-Islamiyyah

46

Al-Masailul Islamiyah

hiyo haitoshi isipokuwa kufanya vitendo vya swala ni wajibu kufanya

vitendo vya wajibu tu na kuacha ya sunna kama vile kunuti, adhana

na kukimu.

231. Kama maslusi au mabtun hapati fursa ya kiasi cha kutawadha na

kuswali, bali mkojo au haja kubwa inadondoka wakati wa swala mara

nyingi, kama sio vigumu kwake basi atawadhe kila mara, aweke

chombo cha maji karibu naye na atawadhe kila unapotoka mkojo au

haja kubwa na akamilishe swala, lakini kwa tahadhari ya sunna aswali

swala ya pili kwa udhu mmoja hata kama udhu wake utabatilika

katikati ya swala asijali.

232. Maslusi au mabtun ambaye hawezi kujizuia kama itamuwia vigumu

kutawadha kila mara ni lazima kwake aswali kila swala kwa udhu

mmoja.

233. Ni wajibu kwa ambaye ana maradhi ya kutokwa na upepo afanye

kama anavyofanya maslus au mabtun, vivyo hivyo kwa asiyeweza

kujizuia na usingizi.

234. Maslusi ambaye anadondokwa na mkojo mfululizo ni wajibu ajihi-

fadhi mkojo usiruke hadi kwenye sehemu zingine za mwili wake kwa

kuweka kifuko chenye pamba au vitu vingine, na kwa tahadhari ya

wajibu atoharishe kifuko ambacho kina najisi, vivyo hivyo sehemu ya

haja ndogo kabla ya kila swala ikiwa hakuna usumbufu, na vivyo

hivyo inalazimu kwa mabatun.

235. Sio wajibu kwa maslusi au mabtun kulipa swala ambazo ameziswali

katika maradhi yake baada ya kupona kama atakuwa ameziswali

kama inavyotakiwa, lakini akipona ndani ya wakati wa swala ni bora

airudie swala aliyoiswali katika wakati huo.

Page 61: al-Masailu-l-Islamiyyah

47

Al-Masailul Islamiyah

MAMBO AMBAYO YANAPASA UDHU

236. Udhu ni wajibu kwa mambo matano:-

1. Swala za wajibu isipokuwa swala ya maiti

2. Sijida au tashahud iliyosahauliwa

3. Tawafu ya wajibu katika ka’aba tukufu

4. Akiweka nadhiri, kiapo au kumwahidi Mwenyezi Mungu kuwa

atatawadha

5. Akiweka nadhiri au akitaka kugusa, maandishi ya Qur’an kwa

mwili wake.

237. Sio wajibu kutawadha kwa ajili ya sijida ya kusahau isipokuwa

kutawadha katika sehemu hii ni jambo zuri.

238. Udhu ni wajibu ikiwa mtu atataka kutoharisha Qur’an iliyonajisika au

akitaka kuitoa chooni, lakini kama kuchelewa kuitoa itakuwa ni kuid-

harau Qur’an afanye upesi kuitoa bila ya udhu.

239. Ni haramu kugusa maandishi ya Qur’an kwa mwili bila ya udhu, na

kwa tahadhari ya wajibu asiguse kwa nywele zake isipokuwa zikiwa

ndefu, lakini hakuna mushikeli kugusa tarjama ya Qur’an ya lugha

yoyote.

240. Ni haramu kugusa jina la Mwenyezi Mungu kwa lugha yeyote bila ya

udhu, na kwa tahadhari ya wajibu asiguse jina la Nabii mtukufu na

Maimamu Masumini na Faatmah Zahra(a.s).

VINAVYOBATILISHA UDHU

241. Mambo yanayobatilisha udhu ni saba:-

1. Mkojo

Page 62: al-Masailu-l-Islamiyyah

48

Al-Masailul Islamiyah

2. Kinyesi

3. Upepo unaotoka katika sehemu ya haja

kubwa

4. Usingizi unaoshinda usikivu na kuona kiasi kwamba sikio hali-

sikii wala jicho halioni

5. Kila kinachoondoa akili kama vile ulevi, kichaa au kuzimia.

6. Istihadha utakuja ufafanuzi wake

7. Kila kinachowajibisha kuoga kama vile janaba na kugusa maiti

kwa tahadhari.

HUKUMU ZA UDHU WA BANDEJI

Bandeji ni ile ambayo inafungiwa jeraha au sehemu iliyoumia.

242. Ikiwa katika sehemu za udhu kuna jeraha, kidonda au mvunjiko na

hakuna kitu juu yake, na maji hayamdhuru ni wajibu atawadhe kama

kawaida.

243. Ikiwa sehemu kati ya sehemu za udhu kuna jeraha, kidonda au mvun-

jiko, na ikawa wazi na ikawa kumwagia maji juu yake kunadhuru,

lakini hakumdhuru kupitisha mkono wenye unyevunyevu juu yake,

basi kwa tahadhari ya wajibu ni kupitisha mkono wenye unyevunye-

vu juu yake, na kama hiyo pia inadhuru, au jeraha ni najisi haiweze-

kani kutoharisha, itamlazimu kuosha sehemu inayozunguka jeraha

kuanzia juu hadi chini, na kwa tahadhari ya wajibu aweke kitambaa

tohara juu ya jeraha na kupaka juu yake kwa mkono wenye unyevu-

nyevu, na ikiwa haiwezekani kwake kutoharisha itamlazimu kuosha

pembezoni mwa jeraha kisha atayamamu kwa tahadhari ya sunna.

244. Kama juu ya jeraha, kidonda au mvunjiko kuna bandeji, kama kuna

uwezekano wa kufungua na kusafisha na maji hasidhuru, ni wajibu

Page 63: al-Masailu-l-Islamiyyah

afungue na atawadhe kama kawaida, ni sawasawa bandeji iwe usoni,

mkononi, utosini au juu ya mguu.

245. Kama bandeji itafunika uso wote au mkono wote au mikono yote, ni

wajibu atawadhe udhu wa bandeji, na kwa tahadhari ya wajibu ataya-

mamu.

246. Kama bandeji imefunika viungo vyote vya udhu basi kwa tahadhari

ya wajibu atawadhe udhu wa bandeji na atayamamu vile vile.

247. Ikiwa katika viungo vya udhu hakuna jeraha, kidonda au mvunjiko,

lakini maji yanamdhuru ni wajibu atayamamu, na kwa tahadhari ata-

wadhe udhu wa bandeji.

248. Josho la bandeji ni kama udhu wa bendeji, lakini kwa tahadhari ya

wajibu aoge josho wa bandeji kwa utaratibu, hata kama anaweza

kuoga kwa kuzamia pamoja na masharti ambayo ni, tohara ya kiungo

na kutodhurika kwa maji, kama hayatapatikana masharti ya kuoga

kwa kuzamia basi aoge kwa utaratibu.

JOSHO ZA WAJIBU

249. Josho za wajibu ni saba:-

Kuoga josho la janaba

Kuoga josho la hedhi

Kuoga josho la nifasi

Kuoga josho la istihadha

Kuoga ikiwa umegusa maiti

Kuosha maiti.

Miogo ambayo inakuwa wajibu kwa sababu, kama vile nadhiri,ahadi n.k.

HUKUMU ZA JANABA

49

Al-Masailul Islamiyah

Page 64: al-Masailu-l-Islamiyyah

249. Janaba inapatikana kwa njia mbili:-

Kujamiana.

Kutokwa na manii, sawasawa akiwa usingizini au akiwa macho, yawe

yametoka machache au mengi, kwa kutamani au bila ya kutamani, kwa

hiyari au bila hiyari.

250. Ikiwa mtu atatokwa na unyevunyevu na ikawa hajui kuwa ni manii

au mkojo, ikiwa umetoka kutokana na matamanio, kwa nguvu na

kulegea kwa mwili baada ya kutoka kwake, basi hukumu yake ni

hukumu ya manii, na kama alama hizi tatu hazitokuwepo zote au

baadhi, basi hayatakuwa na hukumu ya manii, lakini kwa mtu

ambaye ni mgonjwa sio lazima unyevu nyevu huo utoke kwa nguvu,

ukitoka kwa shahawa na mwili kulegea baada ya kutoka basi

yatakuwa ni manii hata kama hayatatoka kwa nguvu.

251. Mtu akiingiza uume kwa kiasi cha kichwa au zaidi, ni sawasawa

aliyeingiliwa awe Mwanamke au mwanamume “Allah atulinde na

haya” iwe kwa mbele au nyuma, awe amebalehe au laa, manii ya

toke au laa, basi wote wawili watapata janaba na ni wajibu waoge.

252. Ikiwa mtu atashuku kuwa ameingiza uume kwa kiasi cha kichwa au

laa, sio wajibu wake aoge.

253. Akiingilia Mnyama – Mwnyezi Mungu atulinde na hayo - na akatok-

wa na manii kuoga kunatosheleza, na kama hajatokwa na manii na

alikuwa na udhu kabla ya kumwingilia mnyama, pia inatosha kuoga

peke yake, na kama alikuwa hana udhu basi ni kwa tahadhari ya

wajibu aoge na kutawadha.

254. Kama manii yatatikisika katika sehemu yake na hayakutoka, kisha

akashuku kuwa je, manii yametoka au laa, sio wajibu wake kuoga.

50

Al-Masailul Islamiyah

Page 65: al-Masailu-l-Islamiyyah

255. Mtu ambaye hawezi kuoga lakini anaweza kutayamamu, basi ina-

juzu kwake kumwingilia mke wake hata kama ni baada ya kuin-

gia wakati wa swala.

256. Kama mtu ataona manii katika nguo zake na anajua kuwa yameto-

ka kwake, kisha hajaoga, ni wajibu aoge, na ni wajibu alipe swala

ambazo ana yakini kuwa ameziswali baada ya kutokwa na hayo

manii na kabla ya kuoga. Lakini swala ambazo anadhani kuwa

ameziswali baada ya kutokwa na manii sio lazima kuzilipa.

MAMBO AMBAYO NI HARAMU

KWA MWENYE JANABA

257. Ni haramu kwa mwenye janaba mambo matano:-

Kugusa andiko la Qur’an tukufu au jina la Allah (swt) kwa mwili, na kwa

tahadhari ya wajibu asiguse majina ya Manabii, Maimamu waliotoharika

pia na Fatma Zahara (as).

Kuingia katika Msikiti Mtukufu wa Makka na msikiti wa Nabii (saww),

ni haramu hata kupita kwenye mlango na kutokea mlango mwingine.

Kusimama na kubakia ndani ya Msikiti mwingine, na vile vile katika

sehemu takatifu za Maimamu waliotoharika (as), lakini hakuna mushke-

li kupita mlangoni na kutokea mlango mwingine, na pia inajuzu kuingia

kwa ajili ya kuchukua kitu.

Kuingia msikitini kwa kusudi la kuweka kitu, bali ni haramu kwa tahad-

hari ya wajibu kuweka kitu ndani hata bila ya kuingia ndani.

51

Al-Masailul Islamiyah

Page 66: al-Masailu-l-Islamiyyah

Kusoma aya ya sajida katika moja ya sura “a’zaim” tukufu, nazo ni sura

za Qur’ani ambazo zina sajida ya wajibu nazo ni:-

Suratus Sajdah nayo ni sura ya 32

Sura ya Fuswilat nayo ni sura ya 41

Sura ya Najim nayo ni sura ya 53

Sura ya Alaq nayo ni sura ya 96

258. Ni haramu kwa mwenye janaba kusoma aya ya Sajida, bali ni kwa

tahadhari ya sunna asisome hata herufi moja katika sura hizi nne.

MAMBO YALIYO MAKURUHU

KWA MWENYE JANABA

259. Ni makuruhu kwa mwenye janaba mambo tisa yafuatayo:-

Kunywa na kula, lakini akitawadha au akiosha mikono yake kabla ya

kula na kunywa hapatakuwa na karaha

Kusoma aya za Qur’ani zaidi ya aya saba zisizokuwa katika sura za

sajida

Kugusa kwa mwili pembezoni mwa Qur’ani; jalada lake na baina ya maan-

dishi yake

Kuweka Qur’an tukufu na kuibeba

Kulala, lakini hakuna karaha akitawadha, au akitayamamu badala ya kuoga

kama hana maji

Kupaka hina n.k

Kujipaka mafuta

Kufanya jimai baada ya kujiotea usingizini.

52

Al-Masailul Islamiyah

Page 67: al-Masailu-l-Islamiyyah

MAS’ALA KATIKA KUOGA JOSHO LA JANABA

260.Kuoga josho la janaba ni sunna, na ni wajibu kwa ajili ya swala ya

wajibu n.k. Lakini sio lazima kuoga janaba kwa ajili ya swala ya maiti,

sajida ya kushukuru na sajida za Qur’an za wajibu, lakini ni bora kwa

tahadhari ya sunna kuoga kwa ajili ya swala ya maiti.

261. Sio lazima wakati wa kuoga kunuwia wajibu au sunna, inatosha

kunuwia kujikurubisha kwa Allah (swt) na kutekeleza amri yake.

262. Akiwa na yakini kuwa wakati wa swala umeingia na akanuwia kuoga

josho la wajibu, kisha ikambainikia kuwa ameoga kabla ya wakati

basi kuoga kwake kutasihi.

263. Josho la wajibu au sunna linagawanyika sehemu mbili:-

- Josho la mpangilio

- Josho la kujizamisha.

JOSHO LA MPANGILIO

264. Katika josho la mpangilio ni wajibu kuanza kichwa na shingo kwan-

za, kisha upande wa kulia kisha upande wa kushoto kwa nia ya kuoga,

na kama mwili wote uko ndani ya maji au chini ya bomba, atanuwia

kuoga kwa kuanza na kichwa na shingo kisha upande wa kulia kisha

upande wa kushoto. Kama atafanya kinyume na utaratibu huu kwa

makusudi au kutokujua mas’ala, basi kwa tahadhari ya wajibu josho

lake litabatilika.

265.Unapoosha upande wa kulia ni wajibu kuosha nusu ya kitovu na nusu

ya sehemu ya siri na nusu nyingine unaiosha unapoosha upande wa

kushoto, na kwa tahadhari ya sunna kuosha kitovu na sehemu ya siri

53

Al-Masailul Islamiyah

Page 68: al-Masailu-l-Islamiyyah

yote wakati unapoosha pande zote mbili.

266. Ili kupata uhakika kuwa umeosha sehemu zote tatu yaani kichwa,

shingo, upande wa kulia na upande wa kushoto, ni lazima kuzidisha

kila sehemu unapoosha. Bali kwa tahadhari ya sunna kuosha upande

wa kulia wote na upande wa kulia wa shingo na upande wa kushoto

wote pamoja na upande wa kushoto wa shingo.

267. Mtu akijua baada ya kuoga kuwa hajaosha sehemu katika mwili na

hajui ni wapi, basi lazima aoge kwa mara nyingine kwa tahadhari ya

wajibu.

268. Kama mtu akijua baada ya kuoga kuwa hajaosha sehemu katika

mwili, kama sehemu hiyo ipo upande wa kushoto inatosha aoshe

upande wa kushoto tu, na ikiwa itakuwa upande wa kulia ni kwa

tahadhari ya sunna baada ya kuiosha hiyo sehemu, aoshe upande wa

kushoto kwa mara nyingine, na kama itakuwa kichwani au shingoni

ni lazima aoshe hiyo sehemu, kisha upande wa kulia, kisha upande wa

kushoto kwa mara nyingine.

269. Kama atashuku kabla ya kumaliza kuosha upande wa kushoto

inatosheleza kuosha sehemu anayoishuku, lakini akishuku kuwa

hajaosha sehemu katika upande wa kulia basi ni kwa tahadhari ya

sunna kuosha sehemu aliyoishuku kisha aoshe upande wa kushoto

kwa mara nyingine, na akishuku kuwa hajaosha sehemu ya kichwa na

shingo, basi ni kwa tahadhari ya sunna baada ya kumaliza kuosha

hiyo sehemu, aoshe upande wa kulia kisha upande wa kushoto.

JOSHO LA KUZAMA

270. Katika josho la kuzamia ni wajibu maji yaenee mwili mzima kwa

mara moja, kama atazama katika maji kwa nia ya kuoga josho la

kuzama ni wajibu anyanyue miguu yake juu ya ardhi.

54

Al-Masailul Islamiyah

Page 69: al-Masailu-l-Islamiyyah

271. Katika josho la kuzamia sio lazima wakati wa nia baadhi ya mwili

uwe nje ya maji, bali anaweza kunuwia na mwili wote ukiwa ndani ya

maji.

272. Kama akijua baada ya kuoga josho la kuzamia kuwa kuna baadhi ya

sehemu za mwili hazijafikiwa na maji, sawasawa amejua hizo sehe-

mu au laa, ni wajibu arudie kuoga.

273. Kama wakati hautomtosha kuoga josho la mpangilio, lakini unam-

tosha kuoga josho la kuzamia, ni lazima aoge kwa kuzama.

274. Mwenye kufunga saumu ya wajibu au akihirimia hija au umra, hai-

juzu kwake kuoga kwa kuzama katika hali ya saumu au ihramu. Lakini

akioga kwa kusahau kuoga kwake utasihi.

HUKUMU ZA JOSHO

275. Katika kuoga josho la kuzamia ni lazima mwili wote uwe tohara,

lakini katika joshoo la mpangilio sio lazima mwili wote uwe na

tohara, na kama mwili wote utakuwa na najisi kisha akatoharisha kila

sehemu kabla ya kuiosha inatosheleza.

276. Mtu akizini kama akitaka kuoga kwa maji ya moto, na mwili wake

ukatoa jasho ,basi sio lazima aoge kwa maji ya baridi, japo ni bora

aoge kwa maji ya baridi.

277. Katika kuoga janaba usipoosha hata unywele mmoja wa mwili josho

lake litabatilika, lakini sio wajibu kuosha sehemu ambazo

hazionekani mfano ndani ya sikio na pua.

278 Sehemu ambayo inashukiwa kuwa ni ya ndani au ya nje ya mwili ni

lazima ioshwe kwa tahadhari.

55

Al-Masailul Islamiyah

Page 70: al-Masailu-l-Islamiyyah

279. Kama sikio lina shimo pana kwa kiasi kwamba kunaonekana ndani,

ni wajibu kuiosha na kama haionekani ndani sio lazima ioshwe.

280. Ni wajibu kuondoa kila uchafu unaozuia maji kufika mwilini, na

kama ataoga kabla ya kuhakikisha kuwa kuna kizuizi au laa, kisha

akabaini kuwa kizuizi hakijatoka, josho lake litabatilika.

281. Kama atashuku wakati wa kuoga, shaka inayokubalika kwa wenye

akili timamu, kuwa je kuna kizuizi kinachozuia maji kufika mwilini

au laa, basi ni wajibu afanye uchunguzi ili kuhakikisha kuwa hamna

kizuizi.

282. Katika kuoga ni lazima kuosha nywele ndogondogo ambazo zinah-

esabika kuwa ni sehemu ya mwili, na wala sio wajibu kuosha nywele

ndefu zaidi, bali ikiwezekana maji kufika mwilini bila ya kulowana

nywele josho litasihi. Lakini kama haitawezekana kufika maji mwili-

ni mpaka uoshe nywele ni wajibu kuziosha nywele ili maji yafike

mwilini.

283. Masharti yote ambayo yanafanya udhu usihi, mfano maji kuwa na

tohara na kuwa ya halali, vilevile masharti haya yanazingatiwa katika

kuoga, lakini sio lazima kuanza kuoga kuanzia juu mpaka chini,

vilevile sio lazima katika josho la mpangilio kuosha upande unaofua-

ta kwa haraka bila ya kuchelewesha,bali anaweza kuchelewesha

baada ya kuosha kichwa na shingo kisha baadaye aoshe upande wa

kulia na baada ya muda aoshe upande wa kushoto.

284. Anayeshindwa kuzuia mkojo au haja kubwa, kama maradhi yake

yatampa ahueni kidogo kwa kiwango cha kuoga na kuswali tu, basi ni

wajibu afanye haraka kuswali bila ya kuchelewesha, na vivyo hivyo

hukumu ni hii kwa mwanamke mwenye damu ya istihadha.

56

Al-Masailul Islamiyah

Page 71: al-Masailu-l-Islamiyyah

285. Mtu akikusudia kutomlipa malipo mwenye bafu au akinuwia kutolipa

taslimu josho lake litabatilika.

286. Kama mwenye bafu anaridhia malipo ya kuoga yacheleweshwe, laki-

ni mwenye kuoga akanuwia kutolipa kabisa au atalipa lakini katika

mali ya haramu, josho lake litakuwa na mushkeli.

287. Kama mtu akitaka kulipa malipo ya mwenye bafu katika mali ya hara-

mu au ambayo haijatolewa khumsi, joshoo lake litabatilika isipokuwa

mwenye bafu akiridhia kutochukua chochote.

288. Kama akishuku kuwa ameoga au laa ni wajibu aoge, lakini akishuku

baada ya kuoga kuwa ameoga sawasawa au laa, sio lazima arudie

kuoga.

289. Kama atatokwa na mkojo wakati anaoga, basi atakamilisha kuoga

kisha atatawadha au ataacha na kuanza kuoga upya kwa nia ya wajibu

ulio juu yake na kutawadha pia.

290. Kama akioga kwa ajili ya swala kwa kudhania kuwa wakati unam-

tosha kuoga na kuswali, kama wakati utatosha kuswali rakaa moja au

zaidi ndani ya wakati swala yake inasihi.

291. Mwenye janaba akishuku kuwa ameoga au laa, swala zake alizoswali

zitakuwa sahihi, lakini aoge kwa ajili ya swala zingine.

292. Mwenye kuwajibika kuoga josho nyingi, inajuzu aoge josho moja

kwa nia ya josho zote, au aoge kila mmoja kwa nia yake.

293. Kama ataandika kwenye mwili wake aya ya Qur’an au jina la Allah

ni wajibu kufuta kama itawezekana, na ikishindikana ni lazima

atawadhe na kuoga josho la kuzamia, na kama atataka kutawadha na

kuoga josho la mpangilio ni lazima maji yafike mwilini bila ya mkono

wake kugusa sehemu iliyoandikwa katika mwili wake.

57

Al-Masailul Islamiyah

Page 72: al-Masailu-l-Islamiyyah

294. Aliyeoga josho la janaba hatawadhi kwa ajili ya swala, ama josho

zingine za wajibu na sunna ni wajibu atawadhe kwa ajili ya swala,

kwa sababu josho hizi hazitoshelezi udhu, isipokuwa josho la wa jan-

aba tu.

ISTIHADHA

295. Damu ya istihadha ni moja ya damu ambazo zinatoka kwa

mwanamke, na mwanamke ambaye anatokwa na damu hii anaitwa

mustahadha.

296. Damu ya istihadha mara nyingi huwa ya njano, baridi, haichomi wala

haitoki kwa nguvu, inawezekana ikawa nyeusi au nyekundu ya moto

na nzito na inatoka kwa nguvu na kuchoma.

297. Istihadha inagawanyika sehemu tatu: Chache, wastani na nyingi.

Chache: Ni ambayo hailoanishi pamba anayoiweka mwanamke katika

uke.

Wastani: Ni ambayo inaloanisha na kupenya ndani ya pamba lakini

haitokezi nje ya kitambaa anachofungia pamba ili kuzuia damu isisambae

mwilini mwake.

Nyingi: Ni ambayo inapenya ndani ya pamba na kutokeza nje kwenye

kitambaa anachofungia pamba.

HUKUMU ZA ISTIHADHA

58

Al-Masailul Islamiyah

Page 73: al-Masailu-l-Islamiyyah

298. Katika istihadha chache ni wajibu mwanamke atawadhe katika kila

swala, abadilishe pamba na kutoharisha nje ya uke kama damu

itakuwa imefika.

298. Katika istihadha ya wastani ni wajibu mwanamke aoge katika swala

ya asubuhi josho la istihadha, kisha abadilishe pamba na kutoharisha

nje ya uke kama damu itakuwa imefika, na kama hataoga katika swala

ya asubuhi kwa makusudi au kwa kusahau ni wajibu kwake aoge kati-

ka swala ya Adhuhuri na Alasiri na kama hataoga kwa ajili ya

Adhuhuri na Alasiri basi aoge kabla ya swala ya Magharibi na Isha,

sawa sawa damu iwe imekatika au laa.

299. Katika istihadha nyingi ni wajibu aoge katika swala ya Asubuhi,

Adhuhuri na Alasiri, Magharibi na Isha yaani josho tatu, kisha abadil-

ishe pamba na kutoharisha nje ya uke. Na kama atatenganisha baina

ya Magharibi na Isha ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya Isha.

300. Damu ya istihadha ikiendelea kutoka mpaka karibu na wakati wa

swala, na kama mwanamke bado hajaoga na kutawadha, basi ni lazi-

ma kwake aoge na kutawadha wakati wa swala.

301. Mwenye istihadha ya wastani na nyingi ambaye ni wajibu kwake

kutawadha na kuoga, kama atatanguliza kutawadha au kuoga inasihi.

302. Mwenye istihadha chache ikiwa ya wastani baada ya sala ya Asubuhi

ni wajibu aoge kwa ajili ya sala ya Adhuhuri na Alasiri, na istihadha

ya wastani ikiwa nyingi baada ya sala ya Adhuhuri na Alasiri ni

wajibu aoge kwa ajili ya sala ya Magharibi na Isha.

303. Mwenye istadha chache au ya wastani ikiwa itakuwa nyingi baada ya

swala ya Asubuhi ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya Adhuhuri na

Alasiri, na aoge kwa mara nyingine kwa ajili ya swala ya Magharibi

59

Al-Masailul Islamiyah

Page 74: al-Masailu-l-Islamiyyah

na Isha.

304. Mwenye istihadha ya wastani au nyingi akioga kwa ajili ya swala ya

Asubuhi kabla ya kuingia wakati, josho lake litabatilika, lakini haku-

na tatizo kama ataoga kwa ajili ya swala ya usiku karibu na adhana

ya Alfajiri, na akaswali swala ya usiku, kisha wakati wa swala ya

Asubuhi ukaingia na akafanya haraka kuswali.

305. Mwanamke mwenye istihadha ni wajibu atawadhe katika kila swala,

iwe ya sunna au ya wajibu, na vile vile akitaka kurudia swala kwa

tahadhari au akitaka kurudia swala aliyoiswali furada kuiswali jamaa,

ni lazima afanye vitendo vyote anavyotakiwa kuvifanya mustadha.

Lakini sio lazima afanye vitendo anavyotakiwa kuvifanya mustadha

ikiwa anaswali rakaa ya Ihtiyati, sajda iliyosahauliwa, tashahudu

iliyosahauliwa na sajda ya kusahau, kama atavifanya hivi baada ya

swala bila kuchelewesha.

306. Ni lazima kwa mustahadha baada ya damu kukatika afanye vitendo

vya mustadha katika swala ya kwanza atakayotaka kuswali, baada ya

hapo sio lazima kuvifanya hivyo vitendo kwa ajili ya swala zingine.

307. Mustahadha kama hatambui yupo katika kundi gani ni lazima ajipime

ili ajijue yupo kundi gani, ataingiza pamba ukeni na kusubiri kidogo

kisha aitoe na baada ya kujua yuko kundi gani basi itakuwa ni isti-

hadha yake.

308.Mwenye istihadha akianza kusali bila ya kujua yupo kundi gani, kama

atakusudia kujikurubisha kwa Allah na akafanya vitendo vya mwenye

istadha chache sala yake itasihi, na kama hatakusudia kujikurubisha

kisha hajafanya wadhifa wake, akafanya wadhifa wa kundi lingine

mfano yeye ni wastani akafanya wadhifa wa chache sala yake itabati-

lika.

60

Al-Masailul Islamiyah

Page 75: al-Masailu-l-Islamiyyah

309. Mwenye istihadha kama hawezi kujua yuko katika kundi gani, mfano

hajui kuwa yeye yuko katika chache au wastani, basi ni lazima afanye

wadhifa wa istihadha chache, na kama hajui kuwa yuko katika isti-

hadha ya wastani au nyingi basi ni lazima afanye wadhifa wa isti-

hadha ya wastani, lakini kama alikuwa anajua yuko katika kundi gani

kati ya haya matatu, basi itabidi awe katika hilo kundi la zamani.

310. Damu ya istihadha ikibakia tumboni haibatilishi josho wala udhu,

na ikitoka hata kama ni chache inabatilisha udhu na josho.

311. Mwanamke mwenye istihadha kama hataona damu inajuzu asali

haraka na udhu alionao.

312. Mwenye istihadha akijua kuwa damu haijatoka tangu alipoanza

kutawadha au kuoga, inajuzu kwake kuchelewesha sala mpaka

wakati atakapokuwa tohara.

313. Mwenye istihadha akijua kuwa atatoharika kabisa kabla ya kumal-

izika wakati wa swala, au itakatika kwa muda wa kuweza kuswali

basi ni kwa tahadhari ya wajibu asubiri mpaka huo wakati na

kuswali atakapotoharika.

314. Kama itaonekana dhahiri kuwa damu imekatika na baada ya udhu na

kuoga , na mustahadha akajua kuwa akichelewesha swala kwa muda

wa kuweza kutawadha na kuoga atatoharika kabisa, ni wajibu

acheleweshe swala na arudie kutawadha na kuoga baada ya kuto-

harika, kisha aswali, na kama wakati utakuwa mfinyu sio lazima

arudie kutawadha na kuoga kwa mara nyingne, bali inajuzu aswali

na udhu na josho lile ile.

315. Mwenye istihadha nyingi na ya wastani anapotoharika kabisa ni

wajibu aoge, lakini kama akijua kuwa damu haijatoka kabla hajao-

ga sio lazima arudie kuoga.

61

Al-Masailul Islamiyah

Page 76: al-Masailu-l-Islamiyyah

316. Ni wajibu kwa mwenye istihadha chache baada ya udhu, na mwenye

istihadha nyingi na ya wastani baada ya kutawadha na kuoga wasali

bila ya kuchelewa, lakini hakuna tatizo kutoa adhana kukimu na

kusoma dua kabla ya swala, pia inajuzu kufanya mambo ya sunna

kama vile kunuti n.k.

317. Mwenye istihadha kama akichelewesha kusali baada ya kuoga, ni

lazima arudie kuoga na kusali bila ya kuchelewa.

318. Kama damu ya istihadha itaendelea kutoka bila ya kusimama, ni

lazima kwa tahadhari ya sunna kama hataogopa madhara kabla ya

kuoga na baada ya kuoga achukue pamba na kuingiza ukeni ili

kuzuia damu isitoke nje, lakini kama damu itakuwa haitiririki kila

wakati ni lazima baada ya udhu na kuoga azuie damu, na kama

atafanya uzembe kujihifadhi na akaacha damu inatoka ni lazima kwa

tahadhari ya sunna arudie kuoga na kutawadha na arudie swala kama

ameswali.

319. Kama damu haitakatika wakati wa kuoga, josho litasihi, lakini

mwenye istihahadha ya wastani akiwa mwenye istihahadha nyingi

wakati akioga, ni lazima aanze kuoga upya kwa tahadhari.

320. Kwa tahadhari ya sunna kwa mwenye istihahadha kuzuia damu isi-

toke mchana kutwa ambao atafunga saumu kwa kadiri atakavy-

oweza.

321. Mwenye istihahadha ambaye ni wajibu aoge, saumu yake itasihi

kama ataoga jinsi inavyotakiwa, mfano akioga kwa ajili ya swala

ya magharibi, kisha akaoga josho za mchana kwa ajili ya swala za

wajibu za siku hiyo. Lakini kama hataoga kwa ajili ya swala ya

magharibi na Isha na akaoga kwa ajili ya swala ya usiku kabla ya

adhana ya alfajir,i na akaoga josho za mchana kwa ajili ya swala

62

Al-Masailul Islamiyah

Page 77: al-Masailu-l-Islamiyyah

zake, saumu yake itasihi na kama atakuwa mustahadha baada ya

swala ya alasiri na hajaoga saumu yake itasihi.

322. Mwenye istihadha chache ikiwa ya wastani au nyingi kabla ya swala,

ni lazima afanye wadhifa wa istihadha ya wastani au nyingi, na

kama istihadha ya wastani ikiwa nyingi lazima afanye wadhifa wa

istihadha nyingi, na kama alikuwa ameoga kwa ajili ya istihadha ya

wastani haitosadia, bali ni wajibu arudie kuoga kwa ajili ya istihad-

ha nyingi.

323. Kama istahadha ya wastani itakuwa nyingi katikati ya swala basi ni

kwa tahadhari ya wajibu avunje swala, kisha aoge na kutawadha na

afanye vitendo vingine vya wajibu vya mwenye istihadha nyingi,

kisha aswali, na kama wakati hautatosha kutawadha na kuoga, ni

wajibu kwake atayamamu mara mbili, tayamamu moja ni badala ya

kuoga na nyingine ni badala ya kutawadha, na kama wakati hau-

tatosheleza kuoga na kutawadha basi ni wajibu kwake atayamamu

badala yake, na kama ataoga itabidi atayamamu badala ya udhu, na

kama atatawadha itabidi atayamamu badala ya kuoga, na kama

wakati hautatosha kwa vyote viwili, haijuzu kukata swala, bali

ataikamilisha kisha atalipa kwa tahadhari ya sunna.

324. Kama damu ikikatika katikati ya swala na mustadha hajui kuwa

imekatika tumboni au laa, kama atajua baada ya swala kuwa imekati-

ka ni wajibu kwake arudie kuoga, kutawadha na kuswali kwa mara

nyingine.

325. Kama mwenye istihadha nyingi ikiwa ya wastani, ni wajibu afanye

wadhifa wa istihadha nyingi katika swala ya kwanza, na wadhifa wa

wastani kwa swala zinazofuatia. Mfano mwenye istihadha nyingi

ikiwa ya wastani kabla ya adhuhuri, ni wajibu aoge kwa ajili ya

swala ya adhuhuri na atatawadha kwa ajili ya swala ya magharibi na

Isha, lakini kama hajaoga kwa ajili ya swala ya adhuhuri na ikawa

63

Al-Masailul Islamiyah

Page 78: al-Masailu-l-Islamiyyah

wakati unamtosha kuswali swala ya alasiri tu, basi ni wajibu kwake

aoge kwa ajili ya swala ya alasiri, na kama hataoga kwa ajili ya

swala ya alasiri pia, ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya

magharibi, na kama hataoga kwa ajili ya swala ya magharibi pia na

wakati ukawa hautoshi, basi ni wajibu aoge kwa ajili ya swala ya

Isha.

326. Kama damu ya istihadha nyingi itakatika kabla ya kila swala, kisha

akaona damu, ni wajibu aoge katika kila swala kwa tahadhari ya

wajibu.

327. Kama istihadha nyingi itakuwa istihadha chache ni wajibu kwake

afanye wadhifa wa istihadha nyingi katika swala ya kwanza, kisha

atafanya wadhifa wa istihadha chache katika swala zinazokuja, na

vile vile istihadha ya wastani ikiwa istihadha chache, atafanya wad-

hifa wa istihadha ya wastani katika swala ya kwanza, kisha atafanya

wadhifa wa istihadha chache katika swala zingine.

328. Kama mustahadha ataacha kufanya moja ya wadhifa wake wa

wajibu, kama vile kuacha kubadilisha pamba basi swala yake inabati-

lika.

329. Mwenye istihadha chache kama anataka kufanya kitendo ambacho

ni sharti awe na udhu, mfano anataka kugusa maandiko ya Qur’an,

kama itakuwa ni baada ya swala basi ni wajibu kwake atawadhe.

330. Mustahadha kama ataoga josho za wajibu wake ataruhusiwa kuingia

msikitini, kusimama ndani yake, kusoma sura zenye sajda za wajibu

na kuonana kimwili na mume wake, hata kama hatafanya vitendo

vingine ambavyo ni wajibu avifanye kwa ajili ya swala, mfano

kubadilisha pamba na kitambaa.

331. Mwenye istihadha nyingi au ya wastani kama akitaka kusoma sura

yenye sajida ya wajibu au kuingia msikitini kabla ya swala, basi ni

64

Al-Masailul Islamiyah

Page 79: al-Masailu-l-Islamiyyah

kwa tahadhari ya wajibu aoge, na vile vile mume wake akimtaka

waonane kimwili, lakini akitaka kugusa Qur’ani ni wajibu kwake

atawadhe pia.

332. Swala ya majanga ni wajibu kwa mustahadha na ni wajibu kwake

afanye vyote ambavyo ni wajibu katika swala za kila siku.

333. Kama mustahadha atawajibika kuswali swala ya majanga katika

wakati wa swala za kila siku, ni wajibu kwake afanye kwa ajili ya

swala ya majanga kila kinachokuwa wajibu kwake kwa ajili ya

swala za kila siku, hata kama akitaka kuswali moja baada ya

nyingine na wala haijuzu kuswali swala zote mbili kwa josho moja.

334. Mustahadha kama akitaka kulipa swala zilizompita ni wajibu afanye

katika kila swala vyote ambavyo ni wajibu kwake kwa ajili ya swala

za adaa (swala zinazoswaliwa kwa wakati).

335. Mustahadha akijua kuwa damu inayotoka kwake sio damu ya jera-

ha au jipu na wala sio damu ya hedhi au nifasi kisheria, ni wajibu

afanye wadhifa wa mustahadha, bali hata akishuku kuwa ni damu ya

istahadha au ni katika damu zingine, kama haitakuwa na alama za

damu zingine, basi ni lazima kwake afanye wadhifa wa mustahad-

ha kwa tahadhari ya wajibu.

HEDHI

336. Damu ya hedhi ni damu ambayo inatoka kwenye mfuko wa uzazi

wa mwanamke katika kila mwezi kwa siku maalumu.

337. Damu ya hedhi mara nyingi huwa ni ya moto, nzito nyeusi au

nyekundu, inatoka kwa nguvu na inachoma.

338. Wanawake wa kikuraishi hukoma kutokwa na damu ya hedhi

wanapofikisha umri wa miaka sitini, na wasio kuwa makuraishi

hukoma kutokwa na damu ya hedhi wanapofikisha umri wa miaka

65

Al-Masailul Islamiyah

Page 80: al-Masailu-l-Islamiyyah

hamsini, na kama wataona damu baada ya hapo haitakuwa damu ya

hedhi hata kama ikiwa na alama za damu ya hedhi, bali itakuwa ni

damu ya istihadha.

339. Damu ambayo anaiona binti kabla hajatimiza miaka tisa au anay-

oiona mwanamke baada ya kufikia umri wa kutotokwa na hedhi

haitokuwa hedhi.

340. Mwanamke mwenye mimba na mwenye kunyonyesha anaweza

kupata hedhi.

341. Binti ambaye hajui kuwa ametimiza miaka tisa au laa, kama akiona

damu ambayo haina sifa za hedhi haitokuwa hedhi, na kama itakuwa

na sifa za hedhi basi itakuwa ni hedhi, inawezekana akawa ame-

timiza miaka tisa.

342. Mwanamke ambaye anashuku kuwa amekoma kutokwa na damu ya

hedhi au laa, na wala hawezi kujua umri wake ni miaka mingapi?

Kama ataona damu na wala hajui kuwa ni hedhi au laa, ni wajibu

ajalie kuwa hajakoma kutokwa na damu ya hedhi.

343. Muda wa hedhi haupungui siku tatu wala hauzidi siku kumi, kama

akiona damu kwa muda wa chini ya siku tatu hata kama ikiwa kido-

go haitakuwa hedhi, na muda mchache unaotenganisha baina ya

hedhi mbili ni siku kumi.

344. Ni wajibu siku tatu za hedhi ziwe kwa mfululizo, kama ataona damu

kwa muda wa siku mbili kisha akatoharika siku moja, kisha akaona

damu siku ya tatu, basi haitokuwa hedhi, ni juu yake kwa tahad-

hari ya sunna aache yaliyokatazwa katika hedhi na afanye vitendo

vya istihadha, yaani aache kuonana kimwili, kuingia msikitini,

kugusa maandiko ya Qur’ani, kugusa jina la Allah na kusoma sura

zenye sajida za wajibu, na wakati huo huo afanye yaliyo wajibu kwa

66

Al-Masailul Islamiyah

Page 81: al-Masailu-l-Islamiyyah

mustahadha, kutawadha, kuoga n.k, katika kila swala.

345. Sio lazima damu kutoka katika siku zote tatu, bali inatosha kuwepo

damu ndani ya uke, lakini akitoharika katikati ya siku tatu kwa

muda mfupi na muda huo uwe mfupi sana kwa kiasi kwamba

itasemwa kuwa damu ilikuwa ndani ya uke katika muda wa siku tatu

basi itakuwa hedhi.

346. Sio lazima aone damu katika usiku wa kwanza na usiku wa nne kwa

muda wa siku tatu, lakini ni lazima isikatike usiku wa pili na usiku wa

tatu, kama ataona damu kuanzia adhana ya Asubuhi ya siku ya kwan-

za na ikakatika wakati huo huo wa siku ya nne na haijakatika usiku

wa pili, wa tatu na wa nne, itakuwa ni hedhi.

347. Kama ataona damu kwa muda wa siku tatu mfululizo kisha akato-

harika, na kama ataona damu baada ya hapo na siku zote alizoona

damu na alizotoharika kama hazizidi siku kumi, basi zote zitakuwa

hedhi.

348. Kama ataona damu zaidi ya siku tatu na chini ya siku kumi na wala

hajui kuwa ni damu ya jipu au jeraha au damu ya hedhi, basi ni

wajibu aijalie kuwa ni hedhi, sawasawa atakuwa na yakini kuwa ni

hedhi au anashaka katika hilo.

349. Kama ataona damu na hajui kuwa ni damu ya jeraha au hedhi kabla

ya kupita siku tatu, basi kwa tahadhari ya wajibu afanye ibada zake na

aache kila kinachokuwa wajibu kuachwa na mwenye hedhi mpaka

itakapojulikana hali halisi.

350. Kama ataona damu kisha akashuku kuwa ni damu ya hedhi au ni

damu ya istihadha, basi ni wajibu aijalie kuwa ni hedhi, kama itakuwa

na alama za hedhi.

67

Al-Masailul Islamiyah

Page 82: al-Masailu-l-Islamiyyah

351. Kama ataona damu na akawa hajui kuwa ni damu ya hedhi au ni damu

ya bikira, basi ni wajibu afanye uchunguzi kwa kuingiza pamba ndani

ya uke na kusubiri kidogo kisha aitoe, kama damu haikuingia ndani

ya pamba bali ikachovya pembeni basi itakuwa ni damu ya bikira, na

kama damu itaingia ndani ya pamba yote basi itakuwa ni damu ya

hedhi, na hii ni ikiwa damu ya bikira sio nyingi inayoweza kufanana

na ya hedhi.

352. Kama ataona damu chini ya siku tatu na akatoharika, kisha akaona

damu kwa muda wa siku tatu zingine, basi damu ya mara ya pili ni

hedhi na ya kwanza sio hedhi hata kama itakuwa katika ada yake.

HUKUMU ZA HEDHI

353. Ni haramu kwa mwenye hedhi mambo yafuatayo:-

Ibada ambazo ni wajibu kutawadha au kuoga au kutayamamu, lakini ibada

ambazo hazihitaji udhu au kuoga au kutayamamu mfano swala ya maiti,

anaweza kuiswali akiwa katika hali ya hedhi.

Mambo yote ambayo ni haramu kwa mwenye janaba.

Jimai ni haramu kwa mwanaume na mwanamke, hata kwa kiasi cha kuin-

giza kichwa cha uume na kutotoka manii, bali ni kwa tahadhari ya wajibu

asiingize kichwa hata kidogo na asimwingilie mwanamke mwenye hedhi

kwa nyuma, lakini hakuna tatizo kumbusu.

354. Ni haramu kuonana kimwili kama hedhi itaendelea zaidi ya ada yake,

lakini ni wajibu azijaalie siku hizo kuwa ni hedhi, kama ataona damu

zaidi ya siku kumi ni wajibu ajalie ada za jamaa zake wa karibu kuwa

ni hedhi yake, na itakuwa haramu kwa mume wake kumuingilia.

355.Siku za hedhi zinagawanyika sehemu tatu

68

Al-Masailul Islamiyah

Page 83: al-Masailu-l-Islamiyyah

1 – Siku za mwanzo

2 - Siku za katikati

3 - Siku za mwisho

356. Kama mume wake atamwingilia kwa mbele katika siku za mwanzo

atatoa dinari moja kumpa fukara, na akimwingilia siku za katikati ata-

toa nusu dinari, na siku za mwisho atatoa robo dinari. Pia atatoa

kafara kama atamwingilia kwa nyuma akiwa katika hedhi.

357. Ni kwa tahadhari ya sunna kwa mwanamume kutoa kafara kama aki-

jua kuwa mke wake ana hedhi naye akamwingilia, lakini

akimwingilia katika hali ya hedhi naye hajui hatawajibika kutoa cho-

chote.

358. Sio wajibu kafara iwe ni dinari bali inaweza ikawa thamani yake.

369. Kama thamani ya kafara itatofautiana wakati alipomwingilia mke

wake mwenye hedhi na wakati wa kumpa fukara, ni wajibu atoe

thamani ya wakati anapompa fukara.

360. Kama mwanaume atamwingilia mke wake mwenye hedhi katika siku

za mwanzo za hedhi na za katikati na za mwisho itabidi atoe kafara

katika kila kundi kafara yake.

361. Mwanaume akimwingilia mke wake mwenye hedhi na akatoa kafara,

kisha akarudia tena kumwingilia atatoa kafara kwa mara nyingine.

362. Mwanaume akimwingilia mke wake mwenye hedhi zaidi ya mara

moja na hajatoa kafara wakati huo, basi ni kwa tahadhari ya sunna

atoe kafara moja katika kila mara aliyomwingilia.

363. Kama mwanaume atajua katikati ya jimai kuwa mke wake ana hedhi,

ni wajibu aache haraka na kama hataacha atalipa kafara kwa tahadhari

69

Al-Masailul Islamiyah

Page 84: al-Masailu-l-Islamiyyah

ya sunna.

364. Mwanaume akizini na mwanamke mwenye hedhi au akimwingilia

mwanamke ajinabia (asiyekuwa halali kwake) mwenye hedhi kwa

kudhania kuwa ni mke wake, basi ni kwa tahadhari ya sunna atoe

kafara.

365. Mtu ambaye hawezi kulipa kafara aombe msamaha kwa Allah (swt)

hii ikiwa hana uwezo kuanzia mwanzo, lakini kama alikuwa anauwe-

zo kisha akawa hana uwezo, basi kwa tahadhari ya sunna akipata

uwezo alipe kafara.

366. Talaka ya mwanamke akiwa katika hedhi ni batili.

367. Mwanamke akisema mimi nina hedhi au nimetoharika kutokana na

damu ya hedhi, kauli yake itakubalika ikiwa haijulikani kuwa ni

muongo.

368. Kama mwanamke atatokwa na hedhi wakati wa kuswali swala yake

itabatilika.

369. Kama mwanamke atashuku kuwa ametokwa na hedhi wakati wa

swala au laa, swala yake inasihi, lakini akijua kuwa alitokwa na hedhi

wakati wa swala basi swala yake itabatilika.

370. Baada ya mwanamke kutoharika kutokana na hedhi ni wajibu aoge

kwa ajili ya swala na ibada zingine ambazo ni sharti kuwa na udhu,

au kuoga, na kuoga josho la hedhi ni kama josho la janaba, lakini aki-

taka kuswali ni wajibu atawadhe kabla ya kuoga au baada ya kuoga.

371. Baada ya mwanamke kutoharika kutokana na damu ya hedhi akipewa

talaka inasihi hata kama bado hajaoga, vilevile inajuzu kwa mume

wake kumwingilia kabla ya kuoga, lakini kwa tahadhari ya sunna

aoshe uke wake kabla ya jimai, na kwa tahadhari ya sunna ajiepushe

na jimai kabla ya kuoga, ama mambo mengine ambayo yana-

70

Al-Masailul Islamiyah

Page 85: al-Masailu-l-Islamiyyah

haramishwa wakati wa hedhi mfano, kubakia msikitini, kugusa

maandiko ya Qur’an ambayo ni sharti awe na udhu haitakuwa ruhusa

kwake mpaka aoge au atawadhe.

372.Kama maji hayatoshi kutawadha na kuoga, lakini yanatosha ama

kuoga au kutawadha, basi ni wajibu aoge na atayamamu badala ya

udhu kwa tahadhari ya wajibu, na kama hayatoshi kuoga, basi ni

wajibu atawadhe halafu atayamamu badala ya kuoga, na kama hana

maji kabisa ni wajibu atayamamu mara mbili, moja ni badala ya kuoga

na nyingine ni badala ya udhu.

373. Mwanamke mwenye hedhi halipi swala za kila siku zilizopita wakati

wa hedhi, lakini ni wajibu alipe saumu za wajibu zilizompita wakati

wa hedhi.

374. Mwanamke akijua kuwa wakati wa swala umeingia na kama

akichelewesha swala atatokwa na hedhi, basi ni wajibu kwake aswali

haraka.

375. Kama atachelewesha swala mpaka wakati ukapita kwa kiwango cha

swala kisha akapata hedhi, ni wajibu ailipe hiyo swala, mwanamke

ambaye sio msafiri kama akichelewesha swala ya Adhuhuri kuanzia

mwanzo wa wakati kisha akapata hedhi baada ya kupita muda wa

kuweza kuswali rakaa nne, ni wajibu kwake ailipe, na kwa

mwanamke msafiri akichelewa kwa kiwango cha rakaa mbili ni

wajibu ailipe.

376.Kama mwanamke atatoharika mwisho wa wakati wa swala, na wakati

ukatosha kuoga na kutawadha na maandalizi mengine kwa ajili ya

swala na kuswali rakaa moja au zaidi ndani ya wakati, ni wajibu aswali

na kama hataswali ni wajibu ailipe

377. Kama wakati hautoshi kuoga na kutawadha lakini ukatosha kutaya-

71

Al-Masailul Islamiyah

Page 86: al-Masailu-l-Islamiyyah

mamu na kuswali, ni wajibu aswali hiyo swala, na vilevile kama wad-

hifa wake ni kutayamamu ni wajibu atayamamu na kuswali swala

hiyo.

378. Mwanamke mwenye hedhi akishuku kuwa wakati unamtosha kuswali

au laa, ni wajibu aswali swala hiyo.

379. Kama hajaswali kwa kudhania kuwa wakati haumtoshi kuswali rakaa

moja na kufanya maandalizi mengine, kisha ikabainika kuwa wakati

ulikuwa unatosha basi ni wajibu ailipe swala hiyo.

380. Ni sunna kwa mwanamke mwenye hedhi unapofika wakati wa swala

ajisafishe, abadilishe pamba na kitambaa kisha atawadhe au atayama-

mu kama hataweza kutawadha, kisha akae katika sehemu ya kuswalia

akielekea kibla na asome dhikiri, dua na kumswalia Mtume (saww)

381. Ni makuruhu kwa mwenye hedhi kusoma Qur’an tukufu, kuwa nayo,

kuibeba na kugusa pembeni mwa maandiko, vilevile ni makuruhu

kwake kupaka hina na n.k

VIGAWANYO VYA HEDHI

382. Wanawake wenye kutoka hedhi wamegawanyika katika sehemu sita;

1). Mwenye ada ya wakati na idadi:

Yaani anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo kwa wakati

maalumu na kwa idadi maalumu mfululizo mwanzo wa mwezi mpaka siku

ya saba.

2).Mwenye ada ya wakati:Yaani anaona damu ya hedhi katika miezi

miwili mfululizo kwa wakati maalumu, lakini idadi inatofautiana katika

mwezi wa kwanza na wa pili mfano; Anaona damu katika mwezi wa kwan-

za kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba, na mwezi wa pili

kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya nane.

72

Al-Masailul Islamiyah

Page 87: al-Masailu-l-Islamiyyah

3). Mwenye ada ya idadi: Yaani idadi ya hedhi katika miezi miwili inalin-

gana, lakini wakati wa kuona damu katika miezi miwili unatofautiana

mfano: Anaona damu katika mwezi wa kwanza kuanzia siku ya tano

mpaka siku ya kumi na mwezi wa pili kuanzia siku ya kumi na mbili

mpaka siku ya kumi na saba.

4). Asiokuwa na ada maalumu sio ya wakati wala ya idadi: Hapo

mwanzo alikuwa nayo lakini imeharibika, na wala haijatulia nakupata ada

mpya.

5). Anayeanza: Naye ni ambaye anaona damu kwa mara ya kwanza.

6). Aliyesahau ada yake.

WENYE ADA YA WAKATI NA IDADI

383. Wenye ada ya wakati na idadi wanagawanyika sehemu tatu:-

Mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo

kwa wakati maalumu na anatoharika kwa wakati maalumu mfano: Anaona

damu katika miezi miwili mfululizo kuanzia mwanzo wa mwezi na anato-

harika siku ya saba, ada yake inakuwa kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka

siku ya saba.

Mwanamke ambaye hatohariki kutokana na damu lakini anaona damu kati-

ka miezi miwili mfululizo na kwa siku maalumu damu yenye sifa ya hedhi,

lakini damu ambayo anaiona baada ya siku maalumu inakuwa na sifa za

damu ya istihadha. Mfano anaona damu yenye sifa ya hedhi kuanzia

mwanzo wa mwezi mpaka siku ya nane katika miezi yote miwili, kwa hiyo

hii ni ada yake kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya nane.

Mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo

kwa wakati maalumu na inaendelea kwa muda wa siku tatu au zaidi kisha

73

Al-Masailul Islamiyah

Page 88: al-Masailu-l-Islamiyyah

anatoharika siku moja au zaidi, kisha anaona damu kwa mara nyingine,

kama siku alizoona damu, na siku alizotoharika hazizidi siku kumi katika

kila miezi miwili, basi siku zote hizo zitakuwa ni ada yake mfano: Akiona

damu katika mwezi wa kwanza kuanzia mwanzo mpaka siku ya tatu, na

katika mwezi wa pili akiona kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya

tatu, kisha akatoharika kwa muda wa siku tatu au zaidi au pungufu ya tatu,

kisha akaona damu kwa mara nyingine kama siku alizoona damu, na siku

alizotoharika hazizidi siku tisa, kwa hiyo ada ya huyu mwanamke ni siku

tisa.

384. Mwanamke mwenye ada ya wakati na idadi kama akiona damu kabla

ya ada au baada ya ada kwa siku mbili au tatu kwa kiasi kwamba

itasemwa kuwa hedhi yake imetangulia au imechelewa, ni wajibu

kwake afanye wadhifa wa hedhi (afanye anayo yafanya mwenye

hedhi) hata kama damu haitakuwa na sifa za hedhi, na kama atajua

baadae kuwa haikuwa ni damu ya hedhi mfano: Akitoharika kabla ya

siku tatu basi ni wajibu kwake alipe ibada zilizompita.

385. Mwanamke mwenye ada ya idadi na wakati:-

kama akiona kabla ya ada yake na ikaendelea mpaka kwenye siku za ada

yake na baada ya ada, kama siku zote alizoona damu hazizidi siku kumi

basi zote zitakuwa ni hedhi.

Na kama zitazidi siku kumi basi damu aliyoiona katika siku za ada yake

zitakuwa ni hedhi, na damu ambayo aliona kabla na baada ya ada itakuwa

ni damu ya istihadha, na ni wajibu alipe ibada zilizopita katika siku zili-

zotangulia ada au baada ya ada.

Kama siku za ada na zilizotangulia ada hazizidi siku kumi basi zote

zitakuwa ni hedhi.

Na kama siku zitazidi siku kumi basi siku za ada peke yake zitakuwa ni

hedhi na damu aliyoiona kabla ya ada itakuwa ni damu ya istihadha, na ni

74

Al-Masailul Islamiyah

Page 89: al-Masailu-l-Islamiyyah

wajibu alipe ibada zilizompita.

Kama ataona damu katika siku za ada na baada ya siku za ada kama siku

zote hazitazidi siku kumi basi zote ni hedhi, na kama zitazidi siku kumi

basi siku za ada peke yake zitakuwa ni hedhi na zilizobaki ni istihadha.

386. Mwenye ada ya wakati na idadi :-

Kama ataona damu katika baadhi ya siku za ada yake na akaona kabla ya

ada, kama siku zote hazitazidi siku kumi, basi zitakuwa ni hedhi.

Na kama zitazidi siku kumi, basi siku alizoona damu katika siku za ada

yake zitakuwa ni hedhi, hata kama siku hizo zitakuwa chache au nyingi

kuliko ada yake, na zilizobaki zitakuwa ni istihadha.

Kama akiona katika baadhi ya siku za ada yake na baada ya ada na siku

zote hazizidi kumi basi zote ni hedhi.

Na kama siku alizoona damu zinazidi siku kumi ni wajibu ajalie siku zili-

zoingiliana na ada yake azifanye kuwa ni hedhi na zilizobaki ni istihadha.

387. Mwanamke mwenye ada ya wakati na idadi, kama akiona damu siku

tatu au zaidi kisha akatoharika, kisha akaona damu kwa mara

nyingine, na muda uliotenganisha baina ya damu mbili ni pungufu ya

siku kumi, kisha siku alizoona damu na siku alizotoharika zinazidi

siku kumi, mfano: aone damu kwa muda wa siku tano, kisha anaona

damu kwa mara ya pili kwa muda wa siku tano zingine, kwa hali hii

kutakuwa na sura zifuatazo:-

Damu aliyoiona kwa mara ya kwanza yote au baadhi ilingane na siku za

ada yake na wala hailingani na damu atakayoiona baada ya kutoharika na

siku za ada yake, basi hapa ni wajibu ajaalie kuwa ya kwanza ni hedhi na

ya pili ni istihadha.

75

Al-Masailul Islamiyah

Page 90: al-Masailu-l-Islamiyyah

Damu ya kwanza isilingane na siku za ada yake, damu ya pili yote au baad-

hi ilingane na siku za ada yake, hapa ni wajibu aifanye damu ya pili kuwa

ni hedhi na damu ya kwanza kuwa istihadha.

Baadhi ya siku za kwanza na za pili kulingana na siku za ada yake, na

damu ya kwanza iliyolingana na siku za ada isipungue siku tatu na damu

yote iliyolingana na ada na siku alizotoharika zisizidi siku kumi, na kwa

hali hii siku zote zitakuwa ni hedhi, na iliyotangulia ada na iliyochelewa

itakuwa ni istihadha. Mfano kama ada imeanza siku ya tatu ya mwezi

mpaka siku kumi na akaona damu katika moja ya miezi kuanzia mwanzo

mpaka siku ya sita, kisha akatoharika kwa muda wa siku mbili, kisha

akaona damu mpaka siku ya kumi na tano ya mwezi, basi atajaalia siku ya

tatu mpaka ya kumi ni hedhi na kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya

tatu, na kuanzia siku ya kumi mpaka siku ya kumi na tano ni istihadha.

Baadhi ya damu ya kwanza na ya pili ikilingana na siku za ada lakini baad-

hi ya damu ya kwanza iliyolingana na ada iwe pungufu ya siku tatu, basi

ni wajibu kwake katika hali hii ajiepushe na vilivyoharamu kwa mwenye

hedhi katika siku za damu mbili na siku alizotoharika, na wakati huo huo

atafanya vitendo vya mustadha na kufanya ibada kama ilivyo tajwa katika

hukumu za mustadha.

388. Mwenye ada ya wakati na idadi, kama hataona damu katika wakati wa

ada yake na akaiona wakati mwingine kwa kiwango cha ada yake, ni

wajibu aifanye kuwa hedhi, sawa sawa iwe kabla ya ada au baada ya

ada.

389. Mwenye ada ya wakati na idadi kama ataona damu wakati wa ada

yake lakini idadi ikawa pungufu au zaidi ya ada ya hedhi, na damu

aliyoiona kabla ya ada ikiwa na idadi ya ada, na kama kitenganishi

baina ya damu ni siku kumi au zaidi, atajaalia damu mbili kuwa ni

76

Al-Masailul Islamiyah

Page 91: al-Masailu-l-Islamiyyah

hedhi, na kama siku za damu mbili na siku alizotoharika hazizidi siku

kumi basi zote zitakuwa ni hedhi.

390. Mwenye ada ya wakati na idadi kama akiona damu zaidi ya siku

kumi, basi damu aliyoiona katika siku za ada itakuwa ni hedhi hata

kama haina sifa za hedhi, na damu aliyoiona baada ya siku za ada ni

istihadha hata kama ina sifa za hedhi, mfano: mwanamke ambaye ada

yake ni kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya saba, kama akiona

damu kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya kumi na mbili, ata-

jaalia siku saba za mwanzo kuwa ni hedhi na siku tano za mwisho

kuwa ni istihadha.

391. Wenye ada ya wakati wanagawanyika sehemu tatu:-

mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo

kwa wakati maalumu kisha anatoharika baada yake siku kadhaa, lakini

idadi ya siku katika kila mwezi inatofautiana. Mfano anaona damu katika

miezi miwili mfululizo kuanzia mwanzo wa mwezi, na mwezi wa kwanza

mpaka siku ya saba na mwezi wa pili mpaka siku ya nane, basi huyu ada

yake ni kuanzia mwanzo wa mwezi.

Mwanamke ambaye hatohariki kutokana na damu lakini damu ambayo

anaiona katika miezi miwili mfululizo kwa wakati maalumu inakuwa na

sifa ya hedhi, na damu anayoiona katika siku zingine inakuwa na sifa za

istihadha na idadi ya siku anazoona damu yenye sifa za hedhi katika miezi

miwili hailingani. Mfano damu anayoiona kuanzia mwanzo wa mwezi

mpaka siku ya saba ya mwezi wa kwanza na mwezi wa pili kuanzia mwan-

zo wa mwezi, mpaka siku ya nane inakuwa na sifa za hedhi na inayobaki

inakuwa na sifa za istihadha.

Mwanamke ambaye anaona damu ya hedhi katika miezi miwili mfululizo

kwa wakati maalumu kwa siku tatu au zaidi, kisha anatoharika kisha

anaona damu kwa mara nyingine, lakini idadi ya siku alizoona damu mbili

na alizotoharika hazizidi siku kumi, lakini katika mwezi wa pili inazidi

77

Al-Masailul Islamiyah

Page 92: al-Masailu-l-Islamiyyah

siku hizi au zinapungua kuliko mwezi wa kwanza mfano: katika mwezi wa

kwanza idadi ya siku ni nane na mwezi wa pili ni siku tisa, na huyu pia

mwanzo wa mwezi utakuwa ni ada yake.

392.Mwenye ada ya wakati kama akiona damu, kabla ya ada au baada kwa

siku mbili au tatu, ikiwa hedhi imetangulia au imechelewa ni wajibu

kwake afanye wadhifa wa hedhi hata kama hiyo damu haina sifa za

hedhi, na kama atatambua baadae kuwa haikuwa damu ya hedhi

mfano: akitoharika kabla ya siku tatu, ni wajibu alipe ibada zilizompi-

ta, nani bora kwake aache yaliyo haramu kwa mwenye hedhi na

kufanya yaliyo wajibu kwa mustahadha.

393. Mwenye ada ya wakati, kama akiona damu zaidi ya siku kumi na

akawa hawezi kutambua siku za hedhi kwa njia ya alama basi itabidi

ajalie ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake. Sawa sawa

jamaa zake wawe wa upande wa baba au wa mama, wako hai au maiti

kwa sharti ada zao wote ziwe sawa, lakini ada zao zikitofautiana

mfano: baadhi yao ni siku tano na baadhi yao ni siku saba, basi ina-

juzu kwake kujaalia ada ya waliowengi kuwa ni ada yake.

394. Mwenye ada ya wakati ambaye anafanya ada ya jamaa zake wa

karibu kuwa ni hedhi yake, basi ni wajibu afanye siku ambayo ilikuwa

mwanzo wa ada yake katika kila mwezi kuwa ni mwanzo wa hedhi

yake mfano: Mwanamke ambaye alikuwa anaona damu kila mwanzo

wa mwezi na anatoharika siku ya saba au ya nane, na kama ataona

damu katika moja ya miezi kwa muda wa siku kumi na mbili na ada

ya jamaa zake ni siku saba ni wajibu afanye siku saba kuanzia mwan-

zo wa mwezi kuwa ni hedhi na inayobaki kuwa istihadha.

395. Mwanamke ambaye ni wajibu kwake aifanye ada ya jamaa zake wa

karibu kuwa ni hedhi yake, kama hana jamaa au wakatofautiana ada

zao ni wajibu kila mwezi kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya

saba afanye kuwa ni hedhi na inayobaki kuwa istihadha lakini kama

78

Al-Masailul Islamiyah

Page 93: al-Masailu-l-Islamiyyah

alama za hedhi zitakuwa katika siku za katikati au za mwisho ni nyin-

gi zaidi kuliko siku zingine, basi ni wajibu afanye mwanzo wa siku

saba kuanzia katikati au kuanzia mwisho.

396. Wenye ada ya idadi wanagawanyika sehemu tatu:-

mwanamke ambaye idadi ya siku za hedhi yake katika miezi miwili mful-

ulizo zinakuwa sawa, lakini wakati wa kuona damu katika miezi miwili

unatofautiana, basi katika hali hii atajaalia siku zote alizoona damu kuwa

ni hedhi mfano: Kama akiona damu katika mwezi wa kwanza kuanzia

mwanzo mpaka siku ya tano, na katika mwezi wa pili kuanzia siku ya tano

na katika mwezi wa pili kuanzia siku ya kumi na moja mpaka siku ya kumi

na tano, ada yake itakuwa ni siku tano.

Mwanamke ambaye hatohariki kutokana na damu, lakini yeye anaona

damu katika miezi miwili mfululizo na katika siku maalumu damu yenye

sifa za hedhi na katika siku zingine anaona damu yenye sifa za istihadha,

na idadi ya siku amabzo ameona damu yenye sifa za hedhi katika miezi

inalingana lakini wakati unatofautiana. Katika hali hii siku zenye sifa za

hedhi zinakuwa ni ada yake mfano: Akiona damu kuanzia mwanzo wa

mwezi mpaka siku tano na katika mwezi unaofuatia kuanzia siku tano na

damu katika mida yote miwili inakuwa na sifa za hedhi na inayobaki

inakuwa na sifa za istihadha basi ada yake itakuwa siku tano.

Mwanamke anayeona damu katika miezi miwili mfululizo kwa muda wa

siku tatu au zaidi kisha akatoharika kwa muda wa siku moja au zaidi, kisha

akaona damu kwa mara nyingine lakini wakati wa kuona ukatofautiana

katika miezi miwili, kama idadi ya damu mbili na siku alizotoharika hazi-

jazidi siku kumi na idadi ya siku katika miezi miwili iko sawa, basi siku

alizoona damu na siku alizotoharika zinakuwa ni ada yake mfano: kama

akiona damu kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka siku ya tatu kisha akato-

harika kwa muda wa siku mbili kisha akaona damu kwa muda wa siku tatu

zingine, na katika mwezi wa pili akiona damu kuanzia siku ya kumi na

moja mpaka siku ya kumi na tatu, kisha akatoharika kwa muda wa siku

79

Al-Masailul Islamiyah

Page 94: al-Masailu-l-Islamiyyah

mbili au zaidi au pungufu kisha akaona damu kwa mara nyingine na siku

zote hazijazidi siku nane basi ada yake itakuwa siku nane.

397. Mwenye ada ya idadi kama akiona damu zaidi ya ada yake na ikazidi

kumi itakuwa kama ifuatavyo:-

Kama damu yote itakuwa ina sifa moja ni wajibu ajalie idadi ya siku

kuanzia wakati alipoona damu kuwa ada yake na inayobaki istihadha.

Kama sifa za damu zitatofautiana baadhi ikawa na sifa za hedhi na

nyingine za istihadha, kama damu yenye sifa za hedhi idadi yake italingana

na ada yake ni wajibu ajalie siku hizo kuwa ni hedhi na zinazobaki kuwa

istihadha.

Kama siku ambazo damu itakuwa na sifa za hedhi zinazidi siku za ada yake

atajalia idadi ya ada yake kuwa ni hedhi peke yake na inayobaki kuwa isti-

hadha.

Kama siku ambazo damu itakuwa na sifa za hedhi ni pungufu kuliko siku

za ada yake, ni wajibu aongeze siku zingine katika siku za ada yake kuwa

ni hedhi yake na zinazobaki ni istihadha.

398. Mwenye utata:Ni mwanamke ambaye anaona damu katika miezi

kadhaa lakini hana ada thabiti sio ya idadi wala ya wakati, kama

ataona damu zaidi ya siku kumi na damu yote ina sifa moja kama ada

ya jamaa zake wa karibu ni siku saba, basi afanye siku saba kuwa ni

hedhi na inayobaki kuwa ni istihadha, na kama ada yao ni chache

mfano: Ni siku tano, ataifanya kuwa ni hedhi na kwa tahadhari ya

sunna aache yaliyo haramu kwa wenye hedhi na kufanya wadhifa wa

mustadha, katika tofauti baina ya siku saba na ada zao, na kama ada

ya jamaa zake wa karibu ni zaidi ya siku saba, mfano ada yao ni siku

tisa kwa hiyo yeye atafanya siku saba kuwa ni hedhi na siku mbili zili-

zobaki ataacha yaliyoharamu kwa wenye hedhi na kufanya wadhifa

wa mustadha kwa tahadhari ya sunna.

80

Al-Masailul Islamiyah

Page 95: al-Masailu-l-Islamiyyah

399. Mwenye utata kama ataona damu zaidi ya siku kumi, na baadhi ya

damu ina sifa ya hedhi na nyingine ina sifa ya istihadha, kama damu

yenye sifa ya hedhi ni pungufu ya siku tatu au zaidi ya siku kumi ni

wajibu afanye kama tulivyotaja katika mas’ala yaliyopita, lakini kama

damu yenye sifa ya hedhi sio pungufu ya siku tatu wala zaidi ya siku

kumi basi yote itakuwa ni hedhi.

400. Anayeanza: Ni mwanamke ambaye anaona damu kwa mara ya kwan-

za, kama ataona damu zaidi ya siku kumi yenye sifa moja, basi ni

wajibu afanye ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni ada yake ambayo

ni siku saba na zinazobaki kuwa ni istihadha.

401. Anayeanza kama ataona damu zaidi ya siku kumi baadhi yake ina sifa

ya hedhi na nyingine ina sifa ya istihadha, kama damu yenye sifa ya

hedhi ni zaidi ya siku tatu na haijazidi siku kumi basi yote itakuwa ni

hedhi, lakini akiona damu kabla ya siku kumi kuisha damu yenye sifa

ya hedhi pia, mfano: Akiona damu nyeusi kwa muda wa siku tano, na

damu ya njano kwa muda wa siku tisa, kisha akaona damu nyeusi kwa

muda wa siku tano zingine, basi ni wajibu afanye ada ya jamaa zake

wa karibu kuwa ni hedhi yake na nyingine ni istihadha.

402. Anayeanza akiona damu zaidi ya siku kumi, na baadhi ya damu ina

sifa ya hedhi na nyingine ina sifa ya istihadha kama siku ambazo zina

sifa za hedhi ni chache kuliko siku tatu au zaidi ya siku kumi, basi ata-

jalia ada ya jamaa zake wa karibu kuwa ni hedhi yake na inayobaki

kuwa ni istihadha.

403. Aliyesahau: Ni mwanamke ambaye amesahau ada yake, kama ataona

damu zaidi ya siku kumi, ni wajibu ajalie siku ambazo zina sifa ya hedhi

kuwa ni hedhi, na ikiwa hataweza kupambanua kwa njia ya sifa na alama

ni wajibu ajaalie siku saba za mwanzo kuwa ni hedhi na zinazobaki kuwa

ni istihadha.

81

Al-Masailul Islamiyah

Page 96: al-Masailu-l-Islamiyyah

404. Anayeanza, mwenye utata, aliyesahau na mwenye ada ya idadi, kama

wataona damu yenye sifa ya hedhi au wakawa na yakini kuwa damu

itaendelea kwa muda wa siku tatu, ni wajibu kwao waache ibada, na

ikibainika baadae kuwa haikuwa ni hedhi ni wajibu kwao walipe

ibada zilizowapita, na kama hawajawa na yakini, na damu haikuwa na

sifa ya hedhi, basi ni lazima kwa tahadhari ya wajibu wafanye wad-

hifa wa mustadha kwa muda wa siku tatu na waache yaliyoharamu

kwa wenye hedhi, na kama hawatatoharika kabla ya siku tatu ni

wajibu waifanye kuwa ni hedhi.

405. Mwenye ada: Sawa sawa awe ni wa idadi au wakati au idadi na

wakati, kama wataona damu katika miezi miwili mfululizo inatofau-

tiana na ada zao kwa idadi au wakati au idadi na wakati na ilikuwa ni

ya aina moja katika miezi miwili katika idadi au wakati au katika

idadi na wakati, atarejea ada yake aliyoiona katika miezi hii miwili

Mfano: Kama alikuwa anaona damu kuanzia mwanzo wa mwezi mpaka

siku ya saba, kisha anatoharika lakini yeye akaona katika miezi miwili

mfululizo kuanzia siku ya kumi mpaka siku ya kumi na saba, kisha akato-

harika basi ada yake itakuwa kuanzia siku ya saba mpaka siku ya kumi na

saba.

406. Makusudio ya mwezi mmoja ni kuanzia kuonekana damu mpaka siku

ya thelathini, na wala sio mwanzo wa mwezi, labda hedhi ianze

mwanzo wa mwezi.

407. Mwanamke ambaye anaona damu katika mwezi mara moja, kama

ataona damu mara mbili na damu zote mbili zina sifa ya hedhi, kama

siku alizotoharika ni chache kuliko siku kumi ni wajibu azifanye

damu mbili kuwa ni hedhi.

408. Kama akiona damu kwa muda wa siku tatu au zaidi, damu yenye sifa

ya hedhi, kisha akaona damu kwa muda wa siku kumi au zaidi, damu

yenye sifa ya istihadha, kisha akaona baada ya muda wa siku tatu,

82

Al-Masailul Islamiyah

Page 97: al-Masailu-l-Islamiyyah

damu yenye sifa ya hedhi, basi ni wajibu ajalie damu ya kwanza na ya

pili zilizokuwa na sifa ya damu ya hedhi kuwa ni hedhi.

409. Mwanamke akitoharika kutokana na hedhi kabla ya siku kumi, na

akajua kuwa hakuna damu tumboni mwake, basi ni wajibu aoge kwa

ajili ya ibada zake, na akipta dhana kwamba ataona damu kwa mara

nyingine kabla ya siku kumi kwisha. Lakini kama atakuwa na yakini

kuwa ataona damu kwa mara nyingine kabla ya siku kumi kwisha,

basi asioge, bali damu ya kwanza na ya pili na siku ambazo zinakuwa

baina ya damu mbili zote zitakuwa ni hedhi.

410. Kama mwanamke akitoharika kabla ya siku kumi kwisha, na akadha-

nia kuwa bado kuna damu ndani ya tumbo, ni wajibu achukue pamba

na kuingiza ndani ya uke na asubiri kidogo kisha aitoe pamba, kama

pamba itakuwa ni safi basi ataoga na kufanya ibada, na kama pamba

haitakuwa safi mfano: Ikawa na rangi ya njano, haitakuwa ni hedhi

isipokuwa kama itakuwa katika siku za ada yake, bali hiyo itakuwa ni

istihadha. Lakini kama pamba itakuwa na damu na haikuwa katika

siku za ada yake au ada yake ni siku kumi, basi ni wajibu asubiri kama

atatoharika kabla ya siku kumi ataoga, laa sivyo ataoga mwanzo wa

siku ya kumi kama atatoharika mwanzo wa siku ya kumi, lakini kama

damu yake itazidi siku kumi na ada yake ni pungufu ya siku kumi,

kama akijua kuwa atatoharika kabla ya siku kumi au mwanzo wa siku

kumi basi asioge, na kama akidhania kuwa damu itaendelea mpaka

siku ya kumi basi kwa tahadhari aache ibada ikiwa damu ina sifa ya

hedhi, japo ni bora kuacha yaliyoharamu kwa mwenye hedhi na

kufanya wadhifa wa mustahadha, na kama atatoharika kabla ya siku

ya kumi au mwanzo wa siku ya kumi basi yote itakuwa ni hedhi, na

kama damu itazidi siku kumi basi ni wajibu afanye ada yake kuwa ni

hedhi na inayobaki kuwa ni istihadha, na atalipa ibada zilizompita

katika siku zilizozidi ada yake.

411. Kama atafanya baadhi ya siku kuwa ni hedhi kisha asifanye ibada,

83

Al-Masailul Islamiyah

Page 98: al-Masailu-l-Islamiyyah

halafu akatambua baadae kuwa haikuwa ni hedhi ni wajibu kwake

alipe swala na saumu zilizompita katika siku hizo, na kama atafanya

ibada kwa kudhania kuwa hana hedhi kisha akagundua kuwa alikuwa

na hedhi, basi ni wajibu kwake alipe saumu alizofunga katika siku

hizo.

NIFASI

412. Damu inayoanza kutoka baada ya sehemu ya mtoto kutokeza nje

kutoka tumboni na ikakatika kabla ya siku kumi au mwanzo ni mwa

siku kumi ni damu ya nifasi au “uzazi”.

413. Damu anayoiona mwanamke kabla ya kutokeza sehemu ya mtoto nje

kutoka tumboni sio damu ya nifasi.

414.Ili kuwa na uhakika wa damu ya nifasi sio lazima mtoto awe amekami-

lika kuumbwa, hata kama kikitoka kipande cha damu au mwanamke

mwenyewe akijua kuwa kilichotoka kama kingebakia tumboni

kingekuwa binadamu au wakunga wanne wakimwelezea kuwa kili-

chotoka kama kingebakia tumboni kingekuwa binadamu basi damu

atakayoiona kwa muda wa siku kumi ni damu ya nifasi.

415. Damu ya nifasi haizidi siku kumi.

416. Kama akishuku kuwa kilichotoka kwake kama kingebakia tumboni

kingekuwa ni binadamu au laa, basi ni kwa tahadhari ya wajibu

afanye uchunguzi. Kama akibakia katika hali ya shaka basi damu

inayotoka sio damu ya nifasi kisharia.

417. Ni haramu kwa mwenye nifasi kubakia msikitini, kugusa maandishi

ya Qur’an tukufu kwa mwili na kila kilichokuwa haramu kwa

mwenye hedhi, na mengineyo, kama ambavyo ni wajibu kwake

84

Al-Masailul Islamiyah

Page 99: al-Masailu-l-Islamiyyah

vilevile ni sunna kwake na makuruhu kwake yote ambayo ni wajibu

au sunna au makuruhu kwa wenye hedhi.

418. Haisihi kwa mwanamke kupewa talaka akiwa katika hali ya nifasi,

isipokuwa kwa masharti yatakayotajwa katika hukumu za talaka, pia

ni haramu kumwingilia kimwili, na kama mume wake atamwingilia

katika hali hiyo basi ni kwa tahadhari ya sunna atoe kafara kama

ilivyoelezwa katika hukumu za hedhi.

419. Ni wajibu kwa mwanamke aoge baada ya kutoharika kutokana na

damu ya nifasi kisha afanye ibada, na kama ataona damu kwa mara ya

pili, kama damu zote mbili na siku alizotoharika hazizidi siku kumi au

zikawa kumi basi zote zitakuwa ni nifasi, na kama alikuwa amefunga

katika siku alizotoharika ni wajibu alipe hiyo saumu.

420. Kama mwanamke akitoharika kutokana na damu ya nifasi na akadha-

nia kuwa kuna damu tumboni mwake, ni wajibu aingize pamba ukeni

na kusubiri kidogo, kama haijachovya chochote basi aoge kwa ajili ya

ibada zake.

421. Kama damu ya nifasi itazidi siku kumi, kama atakuwa na ada katika

hedhi basi atajalia kiwango cha ada yake kuwa nifasi na inayobaki

kuwa istihadha, na kama hana ada katika hedhi, atajalia kuanzia siku

ya kwanza mpaka ya kumi ni nifasi na siku zinazobaki kuwa istihad-

ha.

422. Mwanamke ambaye ada ya hedhi yake ni chini ya siku kumi, kama

ataona damu ya nifasi zaidi ya ada yake ya hedhi ni wajibu ajaalie

kiwango cha ada yake kuwa nifasi, na baada ya hapo aache ibada kwa

muda wa siku moja kwa tahadhari ya wajibu, na baada ya siku moja

mpaka siku ya kumi ni sunna kwake kufanya wadhifa wa mustahad-

ha, na kuacha kila kilichokuwa haramu kwa mwenye nifasi, na kiasi

kitakachozidi kumi itakuwa istihadha, na ni wajibu ajaalie siku baada

85

Al-Masailul Islamiyah

Page 100: al-Masailu-l-Islamiyyah

ya ada yake mpaka siku ya kumi kuwa istihadha, na atalipa ibada zili-

zompita katika siku hizo, mfano: mwanamke ambaye anakuwa na ada

katika hedhi siku sita ,kama ataona damu katika nifasi zaidi ya siku

sita ni wajibu ajalie siku sita kuwa ni nifasi na aache ibada katika siku

ya saba kwa tahadhari ya wajibu, na katika siku ya nane, tisa na kumi

ni sunna afanye wadhifa wa mustahadha mfano: Mwanamke ambaye

ada yake katika kila mwezi ni kuanzia siku ya ishirini mpaka ishirini

na saba, kama atajifungua siku ya kumi na damu ikaendelea kutoka

kwa muda wa mwezi au zaidi ya mwezi bila ya kukatika, ni wajibu

kwake ajalie siku ya kumi mpaka siku ya kumi na saba kuwa ni nifasi,

na baada ya kupita siku kumi zilizotajwa na kama damu anayoiona ni

katika siku za ada yake basi ni hedhi, sawa sawa iwe na sifa za hedhi

au laa.

423. Mwanamke ambaye hana ada katika hedhi, kama ataona damu baada

ya kujifungua kwa muda wa mwezi au zaidi, basi kumi la mwanzo ni

nifasi na kumi la pili ni istihadha, na atakayoiona baada ya hapo kama

ina sifa za hedhi basi ni hedhi la sivyo ni istihadha.

KUOGA JOSHO LA KUGUSA MAITI

424.Kama mtu atagusa mwili wa maiti uliopoa na haujaoshwa kwa mwili

wake ni wajibu kwake aoge josho la kugusa maiti, ni sawa sawa awe

amegusa usingizini au akiwa macho, kwa kutaka au laa, bali ni wajibu

kuoga kama amegusa ukucha kwa ukucha au mfupa kwa mfupa, laki-

ni sio wajibu kuoga kama atagusa mzoga wa mnyama.

425. Sio wajibu kuoga kama mtu atagusa maiti ya binadamu ikiwa hau-

japoa mwili wote, hata kama atagusa sehemu iliyopoa.

426. Kama mtu akigusa mwili wa maiti kwa unywele au akagusa unywele

wa maiti kwa mwili au akagusa unywele wa maiti kwa unywele wake,

kama nywele hazitakuwa ni ndefu sana kupita kiasi basi ni wajibu

86

Al-Masailul Islamiyah

Page 101: al-Masailu-l-Islamiyyah

aoge.

427.Ni wajibu kuoga josho la kugusa maiti, kama akigusa maiti ya mtoto

hata kama ikiwa ni kichanga cha miezi minne (umri wa kuwa tum-

boni), vilevile ataoga kwa tahadhari ya sunna, kama atagusa kichanga

chini ya miezi minne inamaana kuwa, akizaliwa mtoto mwenye umri

wa miezi minne akiwa maiti, kama mwili wake utakuwa wa baridi

wakati wa kutoka basi ni wajibu kwa mama yake aoge josho la kugusa

maiti kwa tahadhari ya wajibu, na kama umri wake utakuwa chini ya

miezi minne sio wajibu kwa mama aoge.

428.Mtoto ambaye amezaliwa baada ya mama yake kuwa maiti, kama

mwili wa mama yake utakuwa umepoa wakati wa kuzaliwa basi ni

wajibu kwa mtoto aoge josho la kugusa maiti akibaleghe kwa tahad-

hari.

429.Kama mtu akigusa maiti ambayo tayari imeshaoshwa josho zote

mitatu sio wajibu kwake kuoga josho la kugusa maiti.

430.Kama kichaa au mtoto akigusa maiti ni wajibu kwa kichaa aoge

akipona na kwa mtoto akibaleghe.

431. Kama sehemu ya mwili wa mtu aliye hai ikikatika au maiti ambaye

haijaoshwa na sehemu iliyokatika ina mfupa, na mtu akaigusa kabla

ya kuoshwa ni wajibu kwa aliyegusa aoge josho la kugusa maiti, laki-

ni kama sehemu iliyokatika haina mfupa sio wajibu aoge.

432. Ni kwa tahadhari ya wajibu kuoga josho la kugusa maiti, ukigusa

mfupa usiokuwa na nyama na haujaoshwa, sawa sawa umekatika

kutoka kwa maiti au kwa mtu hai, na vile vile ni lazima aoge akigusa

jino lililong’ooka kutoka kwa maiti kama maiti bado haijaoshwa,

lakini sio lazima aoge akigusa jino lililong’ooka kutoka kwa mtu hai,

na halina nyama au likiwa na nyama kidogo sana.

433. Josho la kugusa maiti ni sawa na kuoga janaba katika namna, lakini

87

Al-Masailul Islamiyah

Page 102: al-Masailu-l-Islamiyyah

mtu akioga josho la kugusa maiti akitaka kuswali ni wajibu kwake

atawadhe pia.

434.Kama atagusa maiti nyingi au akagusa maiti moja mara nyingi basi

inamtosheleza kuoga josho moja.

435. Hakuna tatizo kwa mwenye kugusa maiti ambayo haijaoshwa, kusi-

mama msikitini, kufanya jimai au kusoma sura zenye sajda ya wajibu,

lakini ni wajibu aoge na atawadhe kama akitaka kuswali n.k.

HUKUMU ZA MUHTADHARI

“ANAYEKATA ROHO”

436. Mwislamu anayekuwa katika hali ya kutokwa na roho ni wajibu

alazwe chali, nyayo za miguu yake zielekee kibla, sawa sawa awe ni

mwanaume au mwanamke, mkubwa au mdogo kama haitowezekana

kulazwa kwa mgongo, basi ni wajibu alazwe kwa mgongo kwa kadiri

itakavyowezekana, na kama haitawezekana kulazwa kwa kifua kifud-

ifudi ni wajibu akalishwe akielekezwa kibla na kama ikishindikana

hivyo pia ni lazima alazwe kwa upande wa kulia au wa kushoto

akielekezwa kibla.

437. Ni kwa tahadhari ya sunna kumwelekeza maiti kibla kama ilivy-

oelekezwa katika mas’ala iliyotangulia mpaka amalize kumuosha,

lakini akimaliza kumuosha ni bora alazwe kwa kama anavyolazwa

wakati anaposaliwa, mpaka atakapozikwa.

438. Kumuelekeza muhtadhari upande wa kibla ni wajibu kwa kila mwis-

lamu na wala haihitaji idhini ya mwenyemamlaka na maiti, na kama

baadhi (ya watu) watafanya haitakuwa wajibu kwa wengine.

439. Ni sunna kumsomea muhatadhari shahada mbili, majina ya maimamu

kumi na mbili n.k.

88

Al-Masailul Islamiyah

Page 103: al-Masailu-l-Islamiyyah

440. Ni sunna kumsomea dua muhtadhari.

441.Ni sunna kumuweka muhtadhari kwenye sehemu ya kuswalia pindi

anapozidiwa na uchungu wa kutokwa na roho.

442.Ni sunna kumsomea muhtadhari surat Yaasini, Swafaati, Ahzaabu,

Ayatul – kursiyi na Aya ya 54 katika surati A’raafu na Aya tatu za sura-

tul Baqara bali amsomee kila atachoweza katika Qur;an ili apate kus-

tarehe.

443. Ni makuruhu kumuacha muhtadhari peke yake, vile vile ni makuruhu

kumwekea kitu kizito juu ya tumbo, pia ni makuruhu kwa wenye

janaba na wenye hedhi kuhudhuria sehemu aliyopo muhtadhari,

kuongea, kulia sana, pia ni makuruhu wanawake kuachwa peke yao

sehemu aliyopo muhtadhari.

HUKUMU BAADA YA MAUTI

444. Ni sunna baada ya kufa kufumbwa macho ya maiti, mdomo wake na

kunyooshwa mikono yake na miguu yake, kisha afunikwe kwa shuka,

na kama atafariki usiku ni sunna kuwashwa taa katika sehemu

ambayo maiti ipo, pia waumini wapewe taarifa ili waje wasindikize

jeneza na wafanye haraka kuzika, lakini ni wajibu wasubiri mpaka

wapate yakini kuwa amefariki, vile vile ni wajibu kuchelewesha kuzi-

ka kama maiti ni mwanamke mweye mimba, na tumboni kwake kuna

mtoto hai apasuliwe upande wa kushoto kisha mtoto atolewe na

washone.

446.Ni wajibu wa kila mwislamu balaghe kuosha maiti ya mwiislamu, kui-

kafini, kuiswalia na kuizika hata kama maiti sio ya mwinathna

Asharia, na kama baadhi watafanya mambo haya basi haitakuwa waji-

89

Al-Masailul Islamiyah

Page 104: al-Masailu-l-Islamiyyah

bu kwa wengine.

Kama mtu ataanza kumwandaa maiti sio lazima kwa watu wengine kufa-

nya hivyo, lakini kama hatakamilisha basi itakuwa ni wajibu kwa wengine

kukamilisha.

447. Kama mtu atakuwa na yakini kuwa fulani ana mwandaa maiti, sio

wajibu kwake kufanya maandalizi, lakini akishuku au akidhani hivyo

basi ni wajibu kwakwe afanye hivyo.

448. Kama atatambua kuwa maiti amekosewa kuoshwa, kukafiniwa,

kuzikwa au kuswaliwa, ni wajibu arudie hayo kwa mara nyingine,

lakini akishuku au akidhania kuwa mambo hayo sio sahihi, sio lazima

kwake kufanya bali ajaalie kuwa ni sahihi.

449. Ni wajibu kuchukua idhini kwa walii wa maiti ili kumuosha kumka-

fini, kumswalia na kumzika.

450. Walii wa mwanamke ni mume wake na baada yake ni wanaume

wanaomrithi maiti kwa utaratibu uliopo katika mirathi.

451. Kama mtu atasema mimi ni walii au walii wa maiti au walii wa maiti

amenipa idhini ya kuosha maiti, kukafini na kuzika, kama watu

wataamini maneno yake na hakuna mtu aliyedai hivyo, basi ataachi-

wa afanye hivyo.

452. Mtu kama atabainisha mtu wa kumuosha kabla hajafa, kumkafini,

kumswalia na kumzika basi kwa tahadhari ya sunna achukue idhini

ya walii wa maiti, na wala sio lazima kwa mtu aliyeidhinishwa na

maiti kwa ajili ya maandalizi yake kukubaliwa wasia wake, lakini

wasia ukikubaliwa ni wajibu afanye hivyo.

HUKUMU ZA KUOSHA MAITI

90

Al-Masailul Islamiyah

Page 105: al-Masailu-l-Islamiyyah

453. Ni wajibu kuosha maiti josho tatu:-

Kwa maji yaliyochanganywa na sidri “majani ya mkunazi”

Kwa maji yaliyochanganywa na kafuri “karafuu maiti”

Kwa maji halisi.

454. Ni wajibu sidri na kafuri zisiwe nyingi sana mpaka kufanya maji

kuwa mudhafu vile vile ni wajibu zisiwe chache sana.

455. Kama sidri na kafuri haitoshi kwa kiwango kinachotakikana basi kwa

tahadhari ya wajibu ichanganywe na maji kiasi.

456. Mtu aliyevaa ihramu kwa ajili ya hija au umra kisha akafariki kabla

ya kukamilisha twawafu ya hija ni wajibu asioshwe na maji yaliy-

ochanganywa na kafuri, badala yake ataoshwa na maji halisi

457. Kama itakosekana kafuri na sidri au moja wapo au zikawa za wizi,

basi ni wajibu maiti aoshwe badala ya kila josho kwa maji halisi.

458.Ni wajibu anayeosha maiti awe ni muislamu wa madhehebu ya Shia

Ithinasharia, awe amebaleghe, awe na akili timamu, awe anajua

mas’ala ya kuosha pamoja na hukumu zake kama maiti hatakuwa ni

shia ithina asharia basi sio lazima kwa anayeosha kuwa ni shia ithi-

nasharia.

459. Ni wajibu kwa muoshaji akusudie kujikurubisha kwa Allah (swt)

wakati wa kuosha, yaani aoshe maiti kwa kujikurubisha kwa Allah

(swt) na kutekeleza amri yake (swt)

460. Ni wajibu maiti ya mtoto mwislamu ioshwe hata kama ni mtoto wa

zinaa, ama kuoshwa kwa kafiri na watoto wake kukafiniwa na kuzik-

wa haijathibiti katika sharia, mtu ambaye alikuwa na kichaa kuanzia

utotoni mpaka akabaleghe ni lazima aoshwe kama wazazi wake ni

waislamu au mmoja wao, lakini kama wote sio waislamu haijuzu

91

Al-Masailul Islamiyah

Page 106: al-Masailu-l-Islamiyyah

kuoshwa.

461.Ni wajibu kuosha kichanga chenye umri wa miezi minne au zaidi, laki-

ni kama kina umri chini ya miezi minne basi ni lazima afungwe na

kitambaa na azikwe bila ya kuoshwa.

462.Inajuzu kwa mwanaume kuosha maiti ya binti mwenye umri chini ya

miaka mitatu, vilevile inajuzu kwa mwanamke kuosha maiti ya mtoto

wa kiume ambaye umri wake haujavuka miaka mitatu.

463.Ni haramu kwa mwanaume kuosha maiti ya mwanamke, vilevile ni

haramu kwa mwanamke kuosha maiti ya mwanaume, lakini inajuzu

kwa mwanamke kuosha maiti ya mume wake, na mume pia kuosha

maiti ya mke wake, japo kwa tahadhari ya sunna mwanamke asimu-

oshe mume wake na mwanaume asimuoshe mke wake.

464. Kama hatopatikana mwanaume wa kuosha maiti ya mwanaume basi

inajuzu kwa mama yake, dada yake, shangazi yake, mama mdogo au

mkubwa wamuoshe.

465. Ni bora mwili wa maiti usifunikwe wakati wa kuoshwa isipokuwa

sehemu za siri ikiwa waoshaji na maiti ni jinsia moja.

466. Ni haramu kuangalia uchi wa maiti ila kwa mume na mke inajuzu

kuangalia na kama muosha maiti ataangalia uchi wa maiti atapata

dhambi, lakini haibatilishi josho la maiti.

467.Kama kuna sehemu najisi katika mwili wa maiti ni lazima itoharishwe

kabla hajaoshwa, na kwa tahadhari ya sunna mwili wa maiti wote uwe

na tohara kabla ya kuoshwa.

458.Namna yan kuosha maiti ni kama namna ya kuoga janaba kwa utarat-

ibu, na kwa tahadhari ya wajibu maiti asioshwe josho la kuzama, ikiwa

josho la utaratibu unawezekana.

92

Al-Masailul Islamiyah

Page 107: al-Masailu-l-Islamiyyah

469. Mtu akifa akiwa na janaba au hedhi sio lazima aoshwe josho la jana-

ba au la hedhi, bali inatosha aoshwe josho la maiti tu.

470. Sio haramu kuchukua malipo kwa ajili ya kuosha maiti ikiwa ni kwa

ajili ya kulingania, vinginevyo ni wajibu kutochukua, na kama ata-

muosha maiti kwa lengo la kuchukua malipo josho halitabatilika,

lakini sio haramu kuchukua malipo kwa ajili ya baadhi ya vitu kama

vile kuleta maji, sidri (majani ya mkunazi) au kafuri maiti.

471. Kama hakuna maji ya kuoshea maiti au kuna kizuizi cha kutumia maji

basi inatosha kumtayamimisha maiti, tayamamu moja badala ya josho

zote tatu, japo ni kwa tahadhari ya sunna kumtayamimisha tayamamu

tatu, kila tayamamu badala ya josho moja.

472. Katika kumtayamimisha maiti ni wajibu kwa aliye hai kupiga ardhi

kisha apake uso wa maiti na apake migongo ya viganja vya maiti.

HUKUMU ZA KUMKAFINI MAITI

473. Ni wajibu kumkafini maiti mwislamu kwa vipande vitatu vya nguo.

474. Kipande cha kwanza ni wajibu kianzie kwenye kitovu mpaka kwenye

magoti, lakini ni bora zaidi kianzie kifuani mpaka kwenye nyayo, na

cha pili ni wajibu kianzie mabegani mpaka kwenye miundi, na ni bora

mpaka kwenye nyayo, na cha tatu ni wajibu kiwe kirefu zaidi kwa

kiasi kwamba kinaweza kufunika mwili wote kwa urefu na upana.

475. Mali ya kununulia sanda ya maiti inachukuliwa kwenye theluthi ya

mali yake.

476. Sanda ya mke ni juu ya mume wake hata kama mke ni tajiri, vile vile

ni wajibu kwa mume kumtolea sanda mke wake aliyempa talaka

rejea- kama yatakavyokuja maelezo yake katika hukumu za talaka -

93

Al-Masailul Islamiyah

Page 108: al-Masailu-l-Islamiyyah

ikiwa atafariki kabla ya kumalizika eda yake, na ikiwa mume sio

baleghe au akiwa kichaa ni wajibu kwa walii wa mume kutoa sanda

kutoka katika mali ya anayemsimamia.

477. Sanda ya maiti sio wajibu kwa jamaa zake wa karibu.

478. Haijuzu kumkafini maiti na ngozi ya mzoga na sanda ya wizi hata

kama hakuna kitu kingine cha kumkafinia.

479. Haijuzu kumkafini maiti na sanda yenye najisi, hariri na kitambaa

kilichochovya dhahabu, ila katika dharura.

480. Haijuzu kumkafini maiti na sufi au nywele za mnyama ambaye ni

haramu kuliwa.

481. Kama sanda itanajisika na najisi ya maiti au na najisi nyingine, ni

wajibu itoharishwe au ikatwe sehemu yenye najisi hata kama maiti

atakuwa amewekwa kaburini, na kama haitawezekana kutoharishwa

au kukatwa ni wajibu abadilishiwe sanda nyingine ikiwezekana.

482. Mtu akihirimia kwa ajili ya Hija au Umra kisha akafa ni wajibu

akafiniwe kama wengine, wala hakutakuwa na tatizo kufunika uso na

kichwa.

483. Ni sunna kwa mtu wakati wa uhai wake kuandaa sanda, sidri na kafu-

ri (kwa ajili yake pindi atakapo kufa).

HUKUMU ZA TAHANITI “KUPAKA”

94

Al-Masailul Islamiyah

Page 109: al-Masailu-l-Islamiyyah

484. Ni wajibu kumpaka maiti kafuri maiti katika viungo vyake vya kusu-

judi

baada ya kumuosha.

485. Ni kwa tahadhari ya wajibu kupaka kafuri kuanzia paji la uso, kigan-

ja cha kulia na cha kushoto, goti la kulia na la kushoto, kidole gumba

cha kulia na cha kushoto.

486. Ni bora kumpaka maiti kafuri kabla ya kumkafini.

487. Mtu akihirimia Hija au Umra, kisha akifa kabla ya kumaliza sa’ayi na

kunyoa haijuzu kumpaka kafuri.

488.Mwanamke ambaye amefiwa na mume wake, kama akifa kabla ya

kumaliza eda basi ni wajibu apakwe kafuri.

489.Kama kafuri haitapatikana ya kutosha basi sio lazima kupakwa.

HUKUMU ZA SWALA YA MAITI

490. Ni wajibu kumswalia maiti hata kama ni mtoto, kama wazazi wake ni

waislamu au mmoja wao ni mwislamu na awe maiti huyo ametimiza

umri wa miaka sita.

491. Ni wajibu kumswalia maiti, baada ya kuoshwa, kupakwa kafuri na

kukafiniwa.

492. Sio lazima kwa anayetaka kuswali swala ya maiti awe na udhu au

aoge au atayamamu, japo ni bora awe na udhu au aoge na atayama-

mu.

493. Ni wajibu kwa anayetaka kuswali swala ya maiti aelekee kibla, kama

ilivyo wajibu kumlaza maiti kwa mgongo, kichwa chake kiwe upan-

95

Al-Masailul Islamiyah

Page 110: al-Masailu-l-Islamiyyah

de wa kulia wa mwenye kuswali na miguu yake iwe upande wa

kushoto wa mwenye kuswali.

494. Ni wajibu sehemu anayoswaliwa maiti isiwe ya kunyang’anya, pia ni

wajibu sehemu ya mwenye kumswalia isiwe juu zaidi ya sehemu ya

maiti.

495. Ni wajibu kwa mwenye kuswalia maiti asiwe mbali na maiti, lakini

kama maiti anaswaliwa jamaa hakuna tatizo mtu kuwa mbali na maiti,

kwa sharti safu za jamaa ziwe zimeungana.

496. Ni wajibu pasiwe na kizuizi baina ya maiti na mwenye kumswalia,

lakini hakuna tatizo kama maiti itakuwa kwenye sanduku n.k.

497. Ni wajibu mwenye kuswali swala ya maiti asimame usawa wa maiti,

lakini hakuna tatizo kwa mwenye kuswali jamaa kusimama pembeni

mwa maiti.

498. Ni wajibu kusitiri sehemu za siri za maiti wakati wa kumswalia, na

kama itashindikana kukafiniwa basi ni wajibu kusitiri sehemu za siri

hata kama ni kwa ubao au jiwe n.k.

499. Ni wajibu kuswali swala ya maiti kwa kusimama na iwe ni kwa ajili

ya kujikurubisha kwa Allah, na kubainisha katika nia maiti unayem-

swalia.

500. Mtu ambaye hawezi kuswali swala ya maiti kwa kusimama inajuzu

kuswali akiwa amekaa.

501. Ni makuruhu kurudia rudia kuswali swala ya maiti mmoja, lakini

hakuna karaha kurudiarudia kuswali swala ya maiti ya mwenye elimu

au mcha Mungu.

96

Al-Masailul Islamiyah

Page 111: al-Masailu-l-Islamiyyah

502. Kama maiti itazikwa bila ya kuswaliwa kwa makusudi au kwa kusa-

hau au kwa udhuru au ikijulikana baada ya kuzikwa kuwa swala ili-

kuwa ni batili, basi ni wajibu kuswali swala ya maiti, maiti akiwa

kaburini maadamu kaburi halijafutika kabisa.

NAMNA YA KUSWALI SWALA YA MAITI

503. Swala ya maiti ina takbira tano.

Takbira ya kwanza: Baada ya nia anasema “Ash hadu an laa ilaaha ila

llahu wa anna Muhammadan rasulullah”

Takbira ya pili anasema: Allahumma swali alaa Muhammad wa Aali

Muhammad waswali alaa jami’il – ambiyaai wal mursaliina”

Takbira ya tatu atasema: “ Allahumma ighfir lil muuminina wal muumi-

naat”

Takbira ya nne atasema: “Allahumma ighfir lihaadhal mayit” kama ni

mwanaume na akiwa mwanamke anasema “ Allahumma ighfir lihaadhihil

mayitah” kisha analeta takibira ya tano na swala inamalizika.

Katika takbira ya nne ikiwa maiti ni mtoto atasema: “ Allahumma ij’alhu

liabawayhi walanaa salafan wafartwan waajran” na kama hali yake haiju-

likani kuwa ni mwanaume au ni mwanamke atasema: “ Allahumma ighfir

liladhiyna tabuu watabi’u sabiylaka waqihim adhabal jahiym” na kama ni

mnafiki atalaaniwa katika takbira ya nne.

504. Ni wajibu kusoma takbira na dua kwa kufuatiliza ili hali swala isiha-

ribike.

505. Ni lazima kwa maamuma katika swala ya maiti naye asome takbira na

dua haitoshelezi Imamu peke yake kusoma.

97

Al-Masailul Islamiyah

Page 112: al-Masailu-l-Islamiyyah

506. Sio sharti kuwa na tohara wakati wa kuswali swala ya maiti, bali

inajuzu kwa mwenye kuswali, kuswali bila ya udhu na kuoga.

MAMBO YA SUNNA KATIKA SWALA YA MAITI:-

Mwenye kuswali awe na udhu, au aoge au atayamamu.

Imamu asimame usawa wa maiti wakati wa kumswalia maiti, na kama mtu

atamswalia furada pia asimame katikati ikiwa maiti ni mwanaume, ikiwa

maiti ni mwanamke asimame usawa wa kifua cha maiti.

Mwenye kuswali asiwe amevaa viatu.

Anyanyue mikono kila anaposoma takbira.

Mwenye kuswali asimame karibu sana na maiti, kwa kiasi upepo ukitikisa

nguo yake inaweza kugusa jeneza.

Ni sunna swala ya maiti kuswaliwa jamaa.

Imamu wa jamaa asome takibira na dua kwa sauti na maamuma wasisome

kwa sauti.

Maamuma asimame nyuma ya Imamu hata kama ni mmoja.

Amuombee maiti na waumini msamaha kwa Allah (swt) kwa wingi.

10.Aseme kabla ya swala “Aswalaatus swalaat, swalaat” mara tatu(badala

ya kukimu).

11.Swala ya maiti iswaliwe katika sehemu ambayo watu wamezoea

kuswalia maiti mara kwa mara.

12.Mwanamke mwenye hedhi akitaka kuswali swala ya maiti asimame

98

Al-Masailul Islamiyah

Page 113: al-Masailu-l-Islamiyyah

nyuma peke yake.

507. Inasihi kuswali swala ya maiti msikitini, na ingawa ni makuruhu laki-

ni sio makuruhu katika msikiti mtukufu wa Makka.

HUKUMU ZA KUZIKA

508.Ni wajibu maiti izikwe kwa kiasi kwamba harufu isienee, na wanya-

ma wasiweze kutoa mwili ndani ya ardhi, na kama itahofiwa kuwa

wanyama watafukua maiti basi ni lazima kaburi lijengewe.

509. Kama haiwezekani maiti kuzikwa, inajuzu kuwekwa kwenye jengo

au sanduku badala ya kuzikwa.

510. Ni wajibu maiti alazwe kwa upande wa kulia ili sehemu ya mbele

ielekee kibla

511. Kama mtu atafia kwenye meli ikawa mwili hautoharibika itabidi izik-

we ardhini na kama mwili utaharibika itabidi afungiwe kitu kizito

kisha izamishwe ndani ya maji

512. Mwanamke kafiri akifa na mtoto akafia tumboni au ikiwa bado

hajawa na uhai, kama baba wa mtoto ni mwislamu basi ni wajibu

mwanamke azikwe kwa kulazwa kwa upande wa kushoto ili mtoto

aliye tumboni aelekee kibla.

513. Haijuzu mwislamu kuzikwa katika makaburi ya makafiri, na haijuzu

kafiri kuzikwa katika makaburi ya waislamu.

514. Haijuzu kuzika mwislamu katika sehemu ambayo inasababisha

udhalili mfano, katika sehemu ambayo uchafu unatupwa.

99

Al-Masailul Islamiyah

Page 114: al-Masailu-l-Islamiyyah

515. Haijuzu kuzika katika ardhi ya kunyang’anya au waqfu, mfano ardhi

ya msikiti.

516. Haijuzu kuzika katika kaburi lingine, isipokuwa liwe ni la zamani

sana na limekwisha.

517. Sehemu yoyote ya mwili ikitengana na mwili ni lazima izikwe pamo-

ja na mwili, ni sunna katika uhai wa mtu anapokata kucha au kung’o-

ka meno ayazike.

518. Kama mtu atafia ndani ya kisima na haiwezekani kutolewa, basi ni

wajibu kisima kifukiwe na kuwa kaburi lake.

519. Kama mtoto atafia tumboni na kubakia kwake tumboni kukawa ni

hatari kwa maisha ya mama yake ni wajibu atolewe haraka.

520. Mwenye mimba akifariki na mtoto tumboni yuko hai ni wajibu apa-

suliwe upande wa kushoto kisha mtoto atolewe na kisha ashonwe

MAMBO YALIYO SUNN KATIKA KUZIKA

521.Ni sunna kuchimba kaburi sawa na urefu wa mtu wa kawaida

522. Ni sunna kuchimba kaburi kwa mustatili, na kuwekwa alama juu yake

ili kutofautisha na makaburi mengine, baada ya kumaliza kuzika ni

sunna kumwagia maji juu ya kaburi na kuweka vidole kaburini kisha

unasoma suratul Qadri mara saba na kumuombea msamaha maiti.

523. Ni sunna kubeba maiti ndani ya jeneza na kumwingiza kaburini tarat-

ibu na kusoma dua zilizopokelewa (kwenye kitabu) kabla ya kuzika

na baada ya kuzika, na kufungua sanda, baada ya kuwekwa katika

mwanandani shavu la maiti liwekwe juu ya ardhi na chini ya kichwa

chake pawekwe udongo, na kuwekwa udongo au tofali nyuma ya

mgongo wake ili asirudi nyuma, na kulala chali, na kabla ya kufuni-

100

Al-Masailul Islamiyah

Page 115: al-Masailu-l-Islamiyyah

ka mwanandani mzikaji apige bega la kulia la maiti, na anaweka

mkono wake wa kushoto juu ya bega la kushoto la maiti, na mdomo

wake ukaribie sikio la maiti, na kumtikisa kwa nguvu, kisha asome

talakini “talakini itakuja mwisho wakitabu Inshaallah.”

524.Ni sunna kuomboleza baada ya kuzika lakini kama muda umepita sana

ni bora kuacha kuomboleza ili usifanye msiba kurudia upya, ni sunna

kupeleka chakula kwenye nyumba ya msiba kwa muda wa siku tatu.

525. Ni sunna kwa mtu kufanya subira anapofiwa na jamaa zake wa

karibu, hasa anapofiwa na mtoto wake, ni sunna kusema “Innaa lilaah

wainnaa ilaihi raajiuuna” ni sunna kumsomea maiti Qu’ran tukufu na

kumwomba Allah haja zako katika kaburi la baba yako na la mama

yako, pia ni sunna kulijengea ili lisiharibike.

526 .Haijuzu kwa mtu kujirarua katika msiba, isipokuwa katika misiba ya

maasumina inajuzu kila aina ya maombolezo.

527. Haijuzu kupasua mifuko katika misiba isipokuwa katika msiba wa

baba na wa kaka, japokuwa ni bora kuacha pia.

528. Mwanamke kama atajirarua uso wake au akang’oa unywele wake basi

ni wajibu wake aache mtumwa huru, au alishe mafakiri kumi au

awape mavazi, na vile vile kwa mwanaume kama atachana mfuko au

nguo zake katika msiba wa mke wake au mtoto wake.

529. Ni bora kufanya tahadhari kutolia kwa sauti, lakini misiba ya maa-

sumini inajuzu kulia kwa sauti

SWALA YA WAHSHA

530. Ni sunna kuswali swala ya wahsha kwa ajili ya maiti baada ya kuzi-

101

Al-Masailul Islamiyah

Page 116: al-Masailu-l-Islamiyyah

ka kwa usiku wake, ni rakaa mbili unasoma katika rakaa ya kwanza

baada ya Al-hamdu ayatul kursiyi, mara moja, na katika rakaa ya pili

unasoma baada ya Al-hamdu suratul- Qadir mara kumi, na baada ya

swala unasoma Allahumma Swali alaa Muhammadi Waali

Muhammad, wab’athi thawabahaa ilaa Qabri Fulani na ni bora utaje

jina la maiti(mahala pa fulani).

531. Kama maiti atacheleweshwa kuzikwa au atapelekwa nchi nyingine,

basi swala ya wahsha isicheleweshwe mpaka usiku atakaozikwa

Kufukua kaburi

532. Ni haramu kufukua kaburi la mwislamu hata kama liwe ni la mtoto au

kichaa, lakini hakuna tatizo ikiwa mwili umekwisha kabisa na kuwa

udongo.

533. Ni haramu kufukua makaburi ya manabii, maimamu, watoto wao

mashahidi maulamaa, na watu wema hata kama imepita miaka mingi.

538. Sio haramu kufukua kaburi kwa mambo yafuatayo:-

Kama maiti atazikwa katika sehemu ya kunya’nganya na mwenyewe

hajaridhia kuzikwa maiti hapo.

Kama maiti atakafiniwa na sanda ya kunyang’anganya na mwenyewe

hajaridhika.

Kama maiti atazikwa bila kuoshwa au kukafiniwa au akioshwa kimakosa

au hajaelekezwa kibla.

Kama kuna haja ya kumuona maiti ili kuthibitisha haki.

Kama atazikwa katika sehemu inayo sababisha kudhalilika, mfano katika

102

Al-Masailul Islamiyah

Page 117: al-Masailu-l-Islamiyyah

makaburi ya makafiri au katika sehemu ya kutupia takataka.

Kama kufukuliwa kaburi ni kwa ajili ya jambo la kisharia muhimu zaidi

kuliko uharamu wa kufukua kaburi, mfano kutolewa mtoto hai aliye tum-

boni mwa mama yake aliyezikwa naye.

Ikiogopewa kuwa wanyama watafukua na kuitoa maiti nje ya kaburi au ita-

sombwa na maji au adui ataichukua.

Kama maiti hajazikwa pamoja na sehemu ya mwili wake iliyojitenga naye

na ikatakiwa kuzikwa pamoja naye, lakini kwa tahadhari ya wajibu sehe-

mu hiyo iwekwe bila ya kuonekana mwili wa maiti

Josho za sunna

539. Josho la Ijumaa: Wakati wake ni kuanzia adhana ya alfajiri mpaka

adhuhuri ya siku ya Ijumaa, na ni bora kuoga adhuhuri ikikaribia

Josho la mwanzo wa usiku wa kwanza wa Ramadhani, na kila usiku wa

witiri, mfano usiku wa tatu, wa tano, wa saba na wa tisa.

Ni sunna kuoga kuanzia usiku wa ishirini na moja mpaka mwisho wa

Ramadhani, sunna hii imetiwa mkazo zaidi katika usiku wa kwanza, usiku

wa kumi na tano, usiku wa kumi na saba, usiku wa kumi na tisa, usiku wa

ishirini na moja, usiku wa ishirini na tatu, usiku wa ishirini na tano, usiku

wa ishirini na saba, usiku wa ishirini na tisa katika mwezi wa Ramdhani

mtukufu.

Josho la siku ya Iddul -fitri na Iddul - Adhuha, na wakati wake ni kuanzia

adhana ya alfajiri mpaka magharibi, lakini ni bora kuoga kabla ya swala

ya Idd.

Josho la usiku wa kuamkia siku ya Idd ndogo na kubwa.

103

Al-Masailul Islamiyah

Page 118: al-Masailu-l-Islamiyyah

Josho la siku ya nane na ya tisa katika mwezi wa Dhul Hija, na ni bora

kuoga siku ya tisa kabla ya Adhuhuri.

Josho la siku ya kwanza, siku ya kumi na tano, siku ya ishirini na saba, na

siku ya mwisho katika siku ya mwezi wa Rajab.

Josho la siku ya Iddul - Ghadiri na ni bora kuoga kabla ya Adhuhuri

Josho la siku ya nne na siku ya ishirini katika mwezi wa Dhul -Hija.

Josho la siku ya Nairuzi, siku ya kumi na tano ya mwezi wa shambani na

siku ya tisa na siku ya kumi na saba ya mwezi na Rabiul-awal na siku ya

ishirini na tano ya mwezi wa Dhul Qa’ad.

Kuosha mtoto anapozaliwa.

Mwanamke kuoga baada ya kutumia manukato ambayo sio ya mume

wake.

Kuoga kwa mtu ambaye amekunywa pombe na akalala akiwa amelewa.

Kuoga josho la kugusa maiti ambaye hajaoshwa.

Josho la mtu ambaye hajaswali swala ya majanga kwa makusudi, hasa

swala ya kupatwa kwa jua na mwezi.

540. Ni sunna kuoga kwa mtu ambaye ameenda kuona mtu aliyesulubiwa,

lakini akimuona ghafla au ikiwa ameenda kutoa ushahidi sio lazima

kuoga.

541. Ni sunna kuoga kabla ya kuingia Makka, Msikiti mtukufu wa

Makka, Ka’aba, tukufu, na katika mji wa Madinatul Munawara, na

katika msikiti wa Mtume (saww) na katika sehemu takatifu za maima-

mu na ni sunna kuoga kwa ajili ya Ihramu.

542. Ni sunna kuoga kwa ajili ya kuwazuru Maimamu watukufu (as) iwe

104

Al-Masailul Islamiyah

Page 119: al-Masailu-l-Islamiyyah

kwa mbali au kwa karibu, na ni sunna kuoga kwa ajili ya kuomba haja

zako kwa Allah (swt), vile vile ni sunna kuoga kwa ajili ya kutubu na

kupata uchangamfu wa ibada.

543. Kama ikiwajibika kwa mtu kuoga josho nyingi za wajibu au baadhi

yake ni wajibu inatosha kuoga josho moja kwa nia ya josho zote.

TAYAMAMU

544. Ni wajibu kutayamamu badala ya kutawadha na kuoga katika

mambo saba:-

Kukosekana maji

Kama hutaweza kufika yaliko maji

Ikiwa maji yanamdhuru

Akihofia kiu

Maji aliyonayo kutotosha isipokuwa kutoharisha mwili na nguo

Maji yakiwa sio halali

Wakati wa swala ukiwa mfinyu.

Jambo la kwanza:

545.Mtu akiwa nyumbani ni wajibu atafute maji hadi akate tamaa, ndio

atayamamu.

546. Kama mtu ataacha kutafuta maji mpaka wakati wa swala ukabakia

mfinyu kisha akatayamamu, atakuwa ameasi lakini swala yake

itakuwa sahihi.

547. Mtu kama ana maji yanayotosha kutawadha au kuoga, na akajua

kuwa akiyamwaga hatapata maji, kama itakuwa ndani ya wakati wa

swala, basi ni haramu kuyamwaga, pia ni bora asiyamwage kabla ya

wakati wa swala

105

Al-Masailul Islamiyah

Page 120: al-Masailu-l-Islamiyyah

548. Mtu akijua kama hatapata maji kisha akabatilisha udhu wake baada

ya kuingia wakati wa swala, au akamwaga maji baada ya kuingia

wakati wa swala, atakuwa ameasi na kupata dhambi lakini swala

yake itasihi akitayamamu.

Jambo la pili:

549. Kama hutaweza kufika katika sehemu ambayo ina maji kwa sababu

ya uzee, basi ni wajibu utayamamu, pia ni wajibu utayamamu kama

kutumia maji kuna kudhuru.

550. Kama italazimika kununua ndoo au kamba ya kuvutia maji au

kukodisha basi ni wajibu anunue au akodishe.

551. Kama mtu hatapata maji mpaka akope hela za kununulia maji, basi ni

wajibu akope ili anunue maji.

552. Kama kuchimba kisima hakumpatii taabu basi ni wajibu achimbe illi

apate maji

553. Kama mtu atakupa maji bila masimango huna budi kuyachukua na

kutawadhia, lakini kama kuna masimango ni lazima usiyachukue

Jambo la tatu:

554. Akihofia kwamba kutumia maji kutamdhuru au akihofia maradhi

yake yatachukua muda mrefu au yatazidi au itakuwa vigumu kutibika

kwa sababu ya kutumia maji, basi ni wajibu atayamamu, lakini kama

maji yaliyochemshwa hayamdhuru ni wajibu atawadhe au aoge kwa

kutumia maji ya moto.

555. Sio lazima apate yakini kuwa maji yatamdhuru, bali hata akidhania

kuwa maji yatamdhuru na akawa na hofu basi ni wajibu atayamamu.

106

Al-Masailul Islamiyah

Page 121: al-Masailu-l-Islamiyyah

556. Mwenye ugonjwa wa macho kama maji yanamdhuru ni wajibu ataya-

mamu.

557. Kama atatayamamu kwa sababu ya kuwa na yakini kuwa maji

yatamdhuru, kisha akatambua kabla ya swala kuwa maji hayamdhu-

ru, tayamamu yake itabatilika, na akijua hivyo baada ya swala ni bora

arudie swala yake akiwa na udhu au aoge, na alipe ikiwa wakati

umepita.

558. Mtu akijua kuwa maji hayamdhuru kama ataoga au kutawadha, kisha

akajua baadae kuwa maji yanamdhuru basi josho lake na udhu wake

utasihi.

Jambo la nne:

559. Kama akihofia kutumia maji katika kutawadhia au kuogea atakufa

yeye au familia yake au rafiki yake au mtumishi, au kila aliye wajibu

kwake kuokoa maisha yake kutokana na kiu kali, basi ni wajibu ataya-

mamu badala ya kutawadha au kuoga.

560. Kama ana maji yaliyonajisika yanatosha kunywa yeye na familia yake

na yaliyotohara kwa ajili ya udhu au kuoga, basi ni wajibu maji yaliy-

otohara yawe ni ya kunywa na atayamamu kwa ajili ya swala, na aki-

taka kumnywesha mnyama wake maji amnyweshe maji yaliyonajisi-

ka.

Jambo la tano:

561. Kama mwili au nguo ikinajisika na maji aliyonayo ni machache,

mfano akitawadhia au kuogea hayatabaki, basi ni wajibu kwake ato-

harishe nguo au mwili wake kwa hayo maji kisha atayamamu kwa

ajili ya swala.

107

Al-Masailul Islamiyah

Page 122: al-Masailu-l-Islamiyyah

Jambo la sita:

562. Kama ana maji au chombo ambacho ni haramu kutumia, mfano maji

au chombo cha kunyang’anya basi ni wajibu atayamamu badala ya

kuoga au kutawadha.

563. Kama wakati wa swala utakuwa mfinyu kama akitawadha au kuoga

swala yote itakuwa nje ya wakati au baadhi, basi ni wajibu atayama-

mu.

Jambo la saba:

564. Kama atachelewesha swala kwa makusudi mpaka wakati ukawa hau-

toshi kutawadha au kuoga, atakuwa ameasi na kupata dhambi lakini

swala yake itakuwa sahihi.

565. Kama akishuku kuwa je wakati utabakia kwa ajili ya swala kama

atatawadha au kuoga, basi ni wajibu atawadhe au aoge.

Vitu ambavyo inasihi kutayamamu

566. Inasihi kutayamamu kwa udongo, mchanga na changarawe, yaani

vipande vipande vya udongo au vya mawe.

567. Inasihi kutayamamu kwa kutumia ukuta wa udongo, na ni bora

kuchukua tahadhari usitayamamu na ardhi au udongo mbichi na

wakati huo huo kuna mkavu.

Namna ya kutayamamu badala ya udhuNia.

Kupiga kwa viganja viwili kwa pamoja juu ya kitu ambacho kinasihi

kutayamamia

108

Al-Masailul Islamiyah

Page 123: al-Masailu-l-Islamiyyah

Kupaka paji la uso lote kwa viganja viwili kwa kuanzia kwenye maoteo ya

nywele mpaka juu ya pua.

Kupaka juu ya kiganja cha kulia kwa tumbo la kiganja cha mkono wa

kushoto kisha kupaka juu ya kiganja cha kushoto kwa tumbo la kiganja cha

mkono wa kulia, kuanzia kwenye vifundo mpaka kwenye ncha za vidole.

Namna ya kutayamamu badala ya kuoga

Katika tayamamu badala ya kuoga atanuia na kupiga ardhi kwa viganja

vyake kisha anapaka paji la uso, kisha atapaka mgongo wa kiganja cha

mkono wa kulia, kisha atapaka mgongo wa kiganja cha mkono wa

kushoto, kisha atapiga udongo tena na kupaka viganja vya mikono yake

kama ilivyotangulia.

Hukumu za kutayamamu

568. Ni wajibu kupaka paji la uso na mikono kwa kuanzia juu na kupele-

ka chini, na ni wajibu kutayamamu kwa kufuatilizia kiungo hadi kiun-

go kingine.

569. Ni wajibu wakati wa kutayamamu kubainisha nia kuwa unatayamamu

badala ya udhu au kuoga, pia ni wajibu kubainisha kuwa unatayama-

mu badala ya josho gani, josho la janaba au josho la hedhi n.k.

570. Ni wajibu wakati wa kutayamamu paji la uso na viganja vya mkono

viwe tohara.

571. Mtu ambaye hawezi kutayamamu mwenyewe ni wajibu atayaya-

mamishwe.

572. Mtu ambaye ametayamamu kwa sababu ya udhuru, kisha udhuru huo

109

Al-Masailul Islamiyah

Page 124: al-Masailu-l-Islamiyyah

ukaondoka basi tayamamu yake itabatilika.

573. Mambo ambayo yanatengua udhu yanatengua tayamamu pia.

574.Mtu ambaye hawezi kuoga, kama akiwajibika kuoga josho nyingi basi

tayamamu moja inamtosheleza

HUKUMU ZA SWALA

575. Swala ni katika amali iliyo bora kabisa katika dini na iliyo na

umuhimu mkubwa, bali swala ni nguzo ya dini, kama swala yako

itakubaliwa basi amali zako zingine zitakubaliwa, na ikikataliwa na

amali zako zingine hazitakubaliwa, mfano wa swala ni sawa na mtu

anayeoga kila siku mara tano, ambaye uchafu hautabaki katika mwili

wake. Vile vile mtu akiswali swala tano za faradhi atatakasika

kutokana na madhambi na machafu.

Na inapasa kwa mtu kuziswali swala zake mwanzo wa nyakati zake na

mwenye kuzipuzia swala zake na kuzembea ni sawa na mtu asiyeswali,

na atastahili adhabu akhera.

Mtume (saww) amesema: “ Hayupo katika dini yangu mwenye kupuuzia

swala yake”. Na Mtume (saww) amesema: “Hatapata maombezi yangu

mwenye kupuuzia swala yake, na wala hataingia katika hodhi yangu”.

Siku moja Mtume (saww) alikuwa msikitini, akaingia mtu mmoja na

akawa akishughulika na kuswali, lakini bila ya kutimiza rukuu yake na

sijda yake. Mtume (saww) akasema: “Huyu anadonoadonoa kama kun-

guru, lau akifa na hii ndio swala yake atakufa nje ya dini yangu”.

Basi inamlazimu mtu adumishe swala zake sana asiziswali harakaharaka,

110

Al-Masailul Islamiyah

Page 125: al-Masailu-l-Islamiyyah

na amnyenyekee Mola wake wakati wa swala, kwa hofu na heshima, na

ajue kwamba kuna ambaye anaongea nae ,na ajue kwamba yuko mbele

ya utukufu wa Mwenyezi Mungu na ufalme wake, awe dhalili na mnyonge,

na lau mwenye kuswali akiyajua haya wakati wa swala, basi nafsi yake

itayasahau mengine yote, na atajihisi kwamba yuko mbele ya Mwenyezi

Mungu (swt) kama ilivyotokea kwa kiongozi wetu Amirul Muuminina Ali

(as) walipoweza kumtoa mshale mguuni mwake bila ya yeye kuhisi wala

kutambua.

Hivi ndivyo yampasa mwenye kuswali atubie na kutaka istighifar kwa

Mola wake na kuelekea kwa Mola wake na kuacha madhambi na maasi

ambayo yanazuia kukubaliwa swala yake. Kama vile hasadi na kibri,

kusengenya, kula haramu na ulevi, na kuacha kuzuia kutoa khumsi na

zaka, bali kuacha maasi yote kwa ujumla. Pia yampasa aache vitendo

vyenye kupunguza thawabu za swala. Asisimame katika swala huku

akisinzia au akiswali huku akijizuia mkojo usimtoke au asiangalieangalie

juu, na hali yuko katika swala. Anatakiwa afanye vitendo vyenye

kumzidishia thawabu katika swala yake. Kama kuvaa pete ya akiki, kuvaa

nguo safi, kujipaka manukato, kupiga mswaki na kuchana nywele.

SWALA ZA WAJIBU576. Swala za wajibu ni:

1. Swala za kila siku

2. Swala za matukio (majanga)

3. Swala ya maiti

4. Swala ya tawafu ya wajibu ka’aba

5. Swala ya kuwalipia wazazi ambayo ni wajibu kwa mtoto mkub-

wa wa kiume

6. Swala inayokuwa wajibu kwa mtu kwa kuweka nadhiri au

ahadi au kiapo au kuajiriwa(kuswali kwa niaba ya mtu).

SWALA ZA WAJIBU ZA KILA SIKU

111

Al-Masailul Islamiyah

Page 126: al-Masailu-l-Islamiyyah

577. Swala za wajibu za kila siku ni tano, swala ya Adhuhuri na Alasir,

kila moja ina rakaa nne, na swala ya magharibi yenye rakaa tatu, na

swala ya Isha yenye rakaa nne, na swala ya asubuhi yenye rakaa

mbili.

Ni wajibu kupunguza swala zenye rakaa nne katika safari kwa masharti

ambayo ufafanuzi wake utaelezwa. Na maana ya kupunguza ni kuziswali

swala zenye rakaa nne, rakaa mbili mbili.

WAKATI WA SWALA YA ADHUHURI

NA ALASIRI

578.Swala ya Adhuhur na Alasir zina wakati mahsusi, na zina wakati wa

kushirikiana, ama wakati ulio mahsusi kwa swala ya adhuhuri ni pale

linapopinduka jua mpaka unapomalizika muda wa kiwango cha

kuswali swala ya Adhuhur. Basi ikiwa mtu yeyote ataiswali swala ya

Alasiri katika wakati huu kwa kusahau, swala yake itakuwa ni

batili. Ama wakati mahsusi kwa swala ya Alasir ni ule uliobakia

mpaka kuzama jua kwa kiwango cha kuweza kuswali rakaa nne za

Alasiri, kama mtu hakuswali swala ya Adhuhuri mpaka wakati huu

basi swala yake itakuwa ni kadhaa na ni juu yake kuiswali swala ya

alasiri muda huu, kisha ailipe swala ya adhuhuri.

Ama wakati wakushirikiana baina ya Adhuhuri na Alasiri ni muda ulio

baina ya wakati mahsusi kwa swala ya adhuhuri, na muda mahsusi wa

swala ya alasiri kiasi kwamba akiiswali swala ya alasiri katika muda

huu wa kushirikiana kabla ya kuiswali swala ya adhuhuri kwa kusahau,

swala yake itasihi na itahesabika kuwa ameswali alasiri, na ni wajibu wake

kuiswali adhuhuri baada yake.

579. Mtu akishughulika na kuswali swala ya alasiri kabla ya kuiswali

swala ya adhuhuri kwa kusahau, kisha akafahamu katikati kwamba

112

Al-Masailul Islamiyah

Page 127: al-Masailu-l-Islamiyyah

amekosea ikiwa hili litakuwa katika wakati wa kushirikiana baina ya

swala ya adhuhuri na alasiri ni wajibu kwake kubadili nia kwa kutia

nia ya swala ya adhuhuri, yaani yeye atanuia hali yuko katika swala

ya kwamba yote aliyofanya, na anayoyafanya sasa hivi na atakayoy-

afanya yatakuwa ni ya swala ya adhuhuri, na baada ya kukamilisha

swala ya adhuhuri, ataswali swala ya alasiri, ama ikiwa haya yote

aliyoyafanya ni katika wakati mahsusi kwa swala ya adhuhuri, basi

yote aliyoyafanya yatakuwa ni batili, sawasawa amefahamu makosa

yake katikati ya swala au baada ya swala.

WAKATI WA SWALA YA MAGHARIBI

NA ISHA

590. Magharibi huingia pale unapoondoka wekundu wa mashariki, nao ni

unaoonekana upande wa mashariki linapozama jua.

591. Kila swala ya magharibi na isha ina wakati wake mahsusi na zina

wakati wa kushirikiana baina ya swala hizi mbili. Ama wakati mah-

susi kwa swala ya magharibi ni mwanzo wa swala ya magharibi

mpaka kumalizika muda kwa kiwango cha kuiswali swala ya

magharibi, kiasi ambacho lau mtu msafiri akiswali swala ya isha

katika muda huu kwa kusahau swala yake itabatilika.

Ama wakati wa kushirikiana kati ya swala hizi mbili ni kati ya wakati

mahsusi kwa swala ya magharib na wakati mahsusi wa swala ya isha kiasi

kama mtu hakuiswali swala ya magharibi mpaka wakati huu itawajibi-

ka kuiswali swala ya isha kwanza kisha ataswali magharibi.

Ama wakati wa kushirikiana kati ya swala hizi mbili ni baina ya wakati

mahsusi kwa swala ya magharibi na wakati mahsusi kwa swala ya isha,

kiasi ambacho lau mtu akiiswali swala ya isha katika wakati huu wa

kushirikiana kabla ya kuswali magharibi kwa kusahau, kisha akafahamu

kuwa amekosea, swala yake itasihi na itamlazimu kuiswali swala ya

113

Al-Masailul Islamiyah

Page 128: al-Masailu-l-Islamiyyah

magharibi baada ya hapo.

592. Muda mahsusi na wa kushirikiana tuliouelezea katika mas’ala yaliy-

otangulia, unatofautiana kulingana na watu, kuhusu msafiri lau

ukipita muda wa mwanzo wa adhuhuri kwa kiwango cha kuswali

rakaa mbili, basi unaingia muda wa kushirikiana, ama kuhusu mtu

ambaye si msafiri ni lazima kwake upite muda wa mwanzo wa

adhuhuri kwa kiasi cha kuswali rakaa nne ndio ufike muda wa

kushirikiana.

593. Ikiwa mtu atashughulika kwa swala ya isha kabla ya swala ya

magharibi kwa kusahau na akafahamu katikati ya swala kuwa

amekosea, ikiwa atakuwa ameiswali swala yote au baadhi yake kati-

ka muda wa kushirikiana na ikawa hakuingia katika rukuu ya rakaa

ya nne, itamuwajibikia kubadilisha nia yake kwenda katika swala ya

magharibi, na atazingatia aliyoyasoma na kuyafanya ni ya swala ya

magharibi na hivyo itambidi akae ikiwa alikuwa amesimama pasi na

kwenda kwenye rukuu ya rakaa ya nne na kukamilisha swala, kisha

ataswali swala ya isha baada ya hapo. Na ikiwa atakuwa amekwenda

kwenye rukuu ya rakaa ya nne ni wajibu kukamilisha swala kisha

ataswali swala ya magharibi baada ya hapo.

Ama akiiswali swala katika wakati mahsusi kwa swala ya magharibi,

kama lau akiwa ni msafiri na akaswali Qaswir, swala yake itabatilika na

atawajibika kuswali swala ya magharibi kisha swala ya isha kwa

mpangilio.

594. Muda wa mwisho wa swala ya isha ni katikati ya usiku, hivyo ni laz-

ima tuanze kuhesabu usiku pindi jua linapozama mpaka adhana ya

alfajiri na sio kwa kuchomoza jua. Mwisho wa muda wa swala ya

magharibi na isha kwa mtu mwenye dharura au aliyesahau au kwa

aliyekuwa amelala au aliyechelewesha swala yake kwa ajili ya hedhi

ni mpaka adhana ya alfajiri.

114

Al-Masailul Islamiyah

Page 129: al-Masailu-l-Islamiyyah

595. Lau akichelewesha swala ya isha mpaka katikati ya usiku bila udhu-

ru, basi ni bora zaidi kuswali hata kabla ya swala ya alfajiri bila ya

nia ya adaai wala kadhaa

WAKATI WA SWALA YA ASUBUHI

596. Baada ya kutokeza weupe upande wa mashariki unaoelekea juu,

ambao unaitwa alfajiri ya mwanzo ya uongo, kisha weupe huu

hupanuka zaidi, wakati huo huwa alfajiri ya pili, “alfajiri ya kweli”

ama mwisho wa swala ya alfajiri ni kuchomoza kwa jua.

HUKUMU ZA WAKATI WA SWALA

597. Haijuzu kuanza kuswali mpaka uwe na uhakika wa kuingia muda wa

swala au baada ya kupewa tarifa na watu wawili waadilifu ya kuin-

gia wakati wa swala au kupata taarifa kwa mtu mmoja mwenye

kuaminika.

598. Ikiwa mtu hawezi kupata uhakika wa kuingia wakati wa swala kwa

kuwa yeye ni kipofu au kwa sababu ya mawingu au vumbi au kwa

sababu yuko ndani ya jela, ni wajibu kwake kuchelewesha swala

yake mpaka apate uhakika wa kuingia kwa wakati.

599. Ikiwa mtu atapewa taarifa na watu wawili waadilifu au akapata

uhakika mwenyewe wa kuingia wakati wa swala, akaanza kushughu-

lika na swala, kisha ikambainikia kwamba wakati wa swala bado

haujaingia basi swala yake itabatilika na vivyo hivyo itabatilika aki-

jua baada ya swala kwamba ameswali swala hiyo kabla ya kuingia

wakati, lakini akitambua kuingia wakati akiwa ndani ya swala, au

akatambua baada ya swala kwamba wakati wa swala umeingia na

yeye yuko ndani ya swala, swala yake itasihi.

115

Al-Masailul Islamiyah

Page 130: al-Masailu-l-Islamiyyah

600. Ikiwa mtu atapata uhakika wa kuingia wakati wa swala na akaanza

kuswali, kisha akashuku na hali yuko ndani ya swala kuwa je wakati

umeingia au bado? Basi swala yake itakuwa na mushkeli, ama akiwa

na yakini wakati wa kuswali na ana uhakika wa kuingia wakati wa

swala itasihi, lakini akijua kuwa swala yote ameiswali nje ya wakati

au akiwa hajui kuwa ameiswali ndani ya wakati au nje ya wakati

swala yake itabatilika, bali hata akijua kwamba wakati umeingia

akiwa anaswali ni wajibu arudie swala kwa tahadhari.

601 Mtu ambaye ana muda wa kuweza kuswali rakaa moja, ni wajibu

kwake kuiswali swala kwa nia ya adaai, lakini haijuzu kwake

kuichelewa swala kwa makusudi mpaka muda uwe mfinyu namna

hii.

602.Mtu ambaye si msafiri ikiwa ana muda wa kuweza kuswali rakaa tano

kabla ya kuzama jua ni wajibu kuswali swala ya adhuhuri na alasiri

wakati huo, lakini ikiwa muda ni mchache zaidi ya huo, itamuwa-

jibikia kuswali swala ya alasir peke yake, kisha ataiswali adhuhuri

kadha na vivyo hivyo atakapobakiwa na muda wa kuswali rakaa nne

kufikia nusu ya usiku, itampasa kuswali magharibi na isha katika

muda huo, lakini muda ukiwa ni mchache zaidi ya huo, itambidi

kuswali isha peke yake, kisha baada ya hapo ataswali swala ya

magharibi kadhaa, ila mwenye dharura ameongezewa muda mpaka

adhana ya alfajiri.

603.Msafiri aliyebakiwa na muda wa kuweza kuswali rakaa tatu kabla ya

kuingia magharibi, ni wajibu kuiswali swala ya adhuhuri na alasiri

katika muda huo. Na ikiwa muda ni mchache zaidi ya huo itamuwa-

jibikia kuiswali alasiri peke yake kisha ataswali adhuhuri kadha, na

ikiwa mtu amebakiwa na muda wa kuswali rakaa nne tu na kuingia

nusu ya usiku ni wajibu kuswali magharibi na isha wakati huo ama

akibakiwa na muda wa kuweza kuswali rakaa moja au zaidi ya rakaa

moja ndio ifike katikati ya usiku itamuwajibikia kuswali magharibi

haraka kwa nia ya adaai.

116

Al-Masailul Islamiyah

Page 131: al-Masailu-l-Islamiyyah

Ni sunna kwa mtu kuswali swala mwanzo wa wakati, na riwaya nyingi

zimepokelewa zikiusia jambo hili na kutilia mkazo sana na fadhila zina

kuwa nyingi zaidi kila swala inaposwaliwa mwanzo wa wakati wake ila

ikiwa kuchelewesha ni kwa ajili ya kutaka fadhila za kitu fulani, mfano

kusubiria mpaka aweze kuswali swala ya jamaa. Kama mtu ana udhuru

kiasi ambacho akitaka kuswali mwanzo wa wakati analazimika kutaya-

mamu kwa ajili ya swala au kuiswali swala kwa nguo iliyo na najisi,

ikiwa atajua kwamba udhuru wake utabakia mpaka mwisho wa wakati ita-

juzu kwake kuiswali swala mwanzo wa wakati, lakini akijua kuwa udhu-

ru wake utaondoka itamuwajibikia kusubiri mpaka udhuru wake uondoke

na kama udhuru wake haujaisha ataswali mwisho wa wakati, na wala hait-

omlazimu kusubiri kiasi cha kutokubakiwa na muda, ila kwa kiwango cha

kuweza kufanya wajibu wa swala bila ya mustahabu. Bali inajuzu

kuziswali swala katika muda wenye wasaa, ambapo anaweza kufanya

mustahabu mfano kuadhini, kukimu, kusoma kunuti pamoja na kutayama-

mu.

604. Mtu ambaye hajui taratibu za swala, hukumu za shaka na kusahau na

akashuku kuwa atatatizwa na moja wapo, ni wajibu kuchelewesha

swala yake mpaka mwisho wa wakati, ili aweze kujifunza lakini

akiwa na uhakika kwamba ataweza kukamilisha swala kwa njia sahi-

hi inajuzu kuswali mwanzo wa wakati, na kama hakutokewa na

mas’ala ambayo haelewi hukumu yake swala yake itasihi na aki-

tokewa na mas’ala ambayo hajui hukumu yake inajuzu afanye kwa

moja ya njia anazozijua na kukamilisha swala yake kisha ni wajibu

kwake kuuliza hukumu ile baada ya swala na kuirudia swala kama

aliiswali kinyume.

605. Ikiwa wakati wa swala ni mpana, na mwenye deni akamdai deni

lake ni wajibu kwake kumlipa deni lake kwanza kama itawezekana

kisha aendelee na swala, na vivyo hivyo ukimtokea wajibu mwingine

wa haraka, mfano akiona najisi msikitini, ni wajibu kusafisha msikiti

kwanza kisha ataswali na kama ataswali kwanza kisha aondoshe

117

Al-Masailul Islamiyah

Page 132: al-Masailu-l-Islamiyyah

najisi atakuwa ametaasi, lakini swala yake itakuwa sahihi.

SWALA AMBAZO NI WAJIBU KUZISWALI

KWA MPANGILIO

606. Ni wajibu kuiswali swala ya alasiri baada ya swala ya adhuhuri na

swala ya isha baada aya swala ya magharibi, na kama ataswali alasiri

kabla ya adhuhuri au isha kabla ya magharibi kwa makusudi basi swala

yake itabatilika.

607. Akianza kuswali kwa nia ya swala ya adhuhuri na wakati huo

akakumbuka kuwa ameswali adhuhuri haijuzu kwake kubadilisha nia

kwenda kwenye swala ya alasir na vivyo hivyo hukumu ni hii kati-

ka swala ya magharibi na isha.

608. Akipata uhakika akiwa katika swala ya alasiri kwamba hajaswali

adhuhuri, basi ni wajibu kwake kubadilisha nia kwenda kwenye

swala ya adhuhuri na kama akikumbuka baada ya hapo kwamba

ameswali adhuhuri kabla, itamlazimu kubadili nia yake kwenda

kwenye swala ya alasiri na swala yake itasihi ikiwa hakufanya kitu

katika swala iliyotangulia, kwa kusudio mahsusi kwa ajili ya

adhuhuri.

609. Ikiwa atashuku akiwa katika swala ya alasiri kwamba ameswali

swala ya adhuhuri, au laa, ni wajibu abadili nia yake kwenda kwenye

swala ya adhuhuri kisha ataswali alasiri lakini ikiwa wakati ni

mfinyu sana kiasi ambacho lau atatimiza swala na kutaka kuswali

alasiri wakati wa magharibi utaingia, itamuwajibikia kukamilisha

swala kwa nia ya alasiri na kwa sura hii ni juu yake ailipe adhuhuri

118

Al-Masailul Islamiyah

Page 133: al-Masailu-l-Islamiyyah

nje ya wakati kwa tahadhari.

610. Akishuku katika swala ya isha kabla ya kwenda rukuu ya rakaa ya

nne, kwamba ameswali magharibi kabla ya hapo au laa, ikiwa

wakati ni mfinyu kiasi ambacho lau akikamilisha swala itaingia

nusu ya usiku ni wajibu kukamilisha swala kwa nia ya isha, ama kama

wakati unawasaa inamuwajibikia kubadili nia kwenda swala ya

magharibi na kukamilisha rakaa tatu, kisha baada ya hapo ataswali

swala ya isha.

611. Akishuku ndani ya swala ya isha baada ya kufika kwenye rukuu ya

rakaa ya nne, kwamba ameswali magharibi kabla ya hapo au laa, ita-

muwajibikia kukamilisha swala yake kisha ataswali magharibi baada

ya hapo.

Kama atarudia swala aliyoiswali kabla kwa tahadhari, na katikati ya swala

akakumbuka kwamba hakuswali swala ambayo ilikuwa ni wajibu

kuiswali kabla ya hii swala, haijuzu kubadili nia yake kwenda kwenye

swala iliyotangulia, mfano kama alikuwa anarudia swala ya alasiri kwa

tahadhari na akakumbuka wakati huo kwamba hajaswali adhuhuri, haijuzu

kubadili nia yake kwenda kwenye adhuhuri.

612. Haijuzu kubadili nia kutoka kadha kwenda kwenye adai, wala kutoka

swala ya sunna kwenda kwenye swala ya wajibu.

Ikiwa wakati wa swala za adai, ni mpana inajuzu kubadilisha nia kutoka

swala za adai kwenda swala za kulipa ndani ya swala kama itawezekana

kubadilisha kwa mfano, kama mtu anaswali adhuhuri inajuzu kwake

kubadili nia yake kwenda swala ya asubuhi maadamu hajaingia katika

rakaa ya tatu.

SWALA ZA SUNNA

119

Al-Masailul Islamiyah

Page 134: al-Masailu-l-Islamiyyah

613. Swala za sunna ni nyingi na pia huitwa swala za “nawafil” na zili-

zotiliwa mkazo katika sunna za kila siku “zilizowekwa kwa

mpangilio” nazo ni za kila siku isipokuwa siku ya Ijumaa, ni rakaa

34 katika utaratibu ufuatao:-

-Sunna ya adhuhuri rakaa nane

-Sunna ya alasiri rakaa nane

-Suna ya magharibi rakaa nne

-Suna ya isha rakaa mbili

-Sunna ya swala ya usiku rakaa kumi na moja

SWALA YA USIKU

614. Wakati wa swala ya usiku unaanzia katikati ya usiku mpaka adhana

ya alfajiri, na ni bora zaidi kuswali swala ya usiku karibu na adhana

ya alfajiri.

615. Msafiri au mtu ambaye hawezi kuswali swala ya usiku baada ya

katikati ya usiku inajuzu kwake kuswali mwanzo wa usiku.

616. Swala ya usiku ina rakaa kumi na moja, rakaa nane kati ya hizo ni

sunna ya usiku, rakaa mbili ni shufaa, na rakaa moja ni witiri, na

katika kila rakaa mbili kuna salam ila rakaa ya witiri yenyewe peke

yake ina salam.

617. Ni sunna katika swala ya usiku kusoma sura ndefu katika rakaa ya

kwanza na sura fupi katika rakaa ya pili na ni sunna katika sunna ya

shufaa na witiri kusoma suratul – Falaq, Nnasi na Tauhidi au kuso-

ma suratu Tauhid katika rakaa zote.

618. Ni sunna katika kunuti ya witiri kuwaombea waumina 40 aseme:

“Ewe Mwenyezi Mungu msamehe fulani na fulani” uwataje kwa

120

Al-Masailul Islamiyah

Page 135: al-Masailu-l-Islamiyyah

majina yao, na aseme mara 70 “Astaghafirullaha rabbii waatuubu

ilaihi” na aseme mara saba “hadhaa maqamul – aaidhi bika mina

nnaari” na aseme mara 300 “al’afuwa”.

SWALA YA GHUFAILA

619. Miongoni mwa swala za sunna ni swala ya Ghufaila ambayo

huswaliwa baina ya Magharibi na Isha, nayo ina rakaa mbili na

huswaliwa kama ifuatavyo: Utasoma katika rakaa ya kwanza baada

ya Al hamdu “waddhannuun idhi dhahaba mughadhiban” iliyoko

katika sura ya 88 aya 87 na katika rakaa ya pili baada ya Al hamdu

“wa’indahu mafaatihul ghayib” mpaka mwisho wa aya iliyoko kati-

ka sura ya 6 aya ya 59

Na atasema katika kunuti “Allaahumma innii as,aluka bimafaatihil –

ghayibi allatii laa yaalamuhaa illa anta an tuswalliya alaa Muhammad

waali Muhammad” kisha unataja haja zako, kisha unasema “Allahumma

anta waliyu ni’imatiy wal- qaadiru alayi twalabatii ta’alamu haajatiy

faas’ aluka bihaq Muhammad waaalihi alaihi wa alaihimu ssalam lammaa

qadhwaytahaa lii”

HUKUMU ZA KIBLA

620.Kibla ni ka’aba tukufu iliyoko katika Mji wa Makka hivyo ni wajibu

kwa mwenye kuswali akiwa Makka kuilekea ka’aba yenyewe lakini

mtu alioko mbali aelekee upande wa kibla, vivyo hivyo kwa jambo

ambalo ni sharti kuelekea kibla kama vile kuchinja mnyama.

621. Mwenye kuswali swala zake za wajibu kwa kusimama ni wajibu

kuelekea kibla kwa uso wake, kifua chake, tumbo lake na sehemu

ya mbele ya miguu yake na kwa tahadhari ya sunna vidole vyake pia

vieleke kibla. Anayeswali kwa kukaa akishindwa kukaa katika hali ya

121

Al-Masailul Islamiyah

Page 136: al-Masailu-l-Islamiyyah

kawaida kuweka tumbo na miguu yake katika ardhi, ni wajibu

aelekeze uso wake, kifua chake na tumbo lake kibla, na kwa tahadhari

na miundi yake ielekee kibla.

622. Mtu ambaye hawezi kuswali kwa kukaa ni wajibu aswali kwa kulala

kwa ubavu wa kulia kwa kuelekeza sehemu ya mbele ya mwili wake

kibla, na kama hakuweza, basi aswali hali amelala kwa ubavu wa

kushoto, na akishindwa alale kwa mgongo kwa kuelekeza matumbo

ya miguu yake kibla.

623. Mwenye kutaka kuswali ni wajibu afanyejitihada ya kujua kwa yaki-

ni upande wa kibla, na inajuzu ategemee kauli ya watu wawili

waadilifu au mtu mmoja mkweli.

624. Kama akishindwa kupata yakini kwamba kibla kiko upande upi, na

hakupata mtu wa kuaminika wa kumwambia upande wa kibla, itam-

lazimu atumie dhana kwa kutazama mihrabu za miskiti ya waislam au

makaburi yao au njia zingine zitakazomuwezesha kujua upande wa

kibla.

625. Ambaye hakupata uhakika kibla kipo upande upi akitaka kufanya

amali isiyo kuwa swala ambayo ni wajibu kuelekea kibla, mfano aki-

taka kuchinja mnyama itamlazimu awe na dhana ulipo upande wa

kibla na akishindwa hilo atamchinja kumwelekeza upande wowote

atakaoafiki katika hali ya dharura juu ya amali hiyo.

KUSITIRI MWILI KATIKA SWALA

626. Ni wajibu kwa mwanaume kusitiri mwili wake katika swala hata

kama hakuna mtu yeyote anayemuona, na ni bora kusitiri kuanzia

kitovuni mpaka magotini.

627. Na ni wajibu kwa mwanamke wakati wa swala kusitiri mwili wake

wote hata kichwa na nywele, na kwa tahadhari ya sunna kusitiri chini

122

Al-Masailul Islamiyah

Page 137: al-Masailu-l-Islamiyyah

ya unyayo wake pia, lakini si lazima kusitiri vile viungo vinavy-

ooshwa katika udhu, yaani uso na viganja vya mikono mpaka kongo

mbili, na vile vile migongo ya miguu mpaka kwenye kongo mbili

lakini ili awe na yakini kwamba amesitiri yaliyowajibu kusitiriwa ni

wajibu kusitiri sehemu za pembeni za uso na kusitiri kongo za

viganja.

628. Kama mtu hakusitiri uchi wake katika swala kwa makusudi swala

yake inabatilika.

inajuzu kwa mwenye kuswali kusitiri uchi wake wakati wa swala kwa

karatasi au majani ya miti na ikiwa ana kitu kingine ambacho anaweza

kusitiri uchi wake kwa tahadhari ajisitiri kwa kitu hicho.

Inajuzu kwa mwenye kuswali kusitiri uchi wake kwa udongo.

VAZI LA MWENYE KUSWALI

629. Kuna masharti sita kwa vazi la mwenye kuswali:-

Lazima liwe tohara

Liwe la halali

Lisiwe limetokana na mizoga

Lisiwe limetokana na vitu vya wanyama ambao ni haramu kuliwa

Lisiwe la hariri halisi au dhahabu, ikiwa mwenye kuswali ni mwanaume,

ufafanuzi wake utakuja.

SHARTI LA KWANZA

630. Ni wajibu nguo ya mwenye kuswali iwe tohara na lau akiswali kwa

nguo au mwili ulio na najisi kwa makusudi swala yake inabatilika.

Mwenye kuswali na nguo au mwili ulio najisi naye hajui kwamba kuswali

katika hali ile inabatilisha swala, swala yake itasihi.

123

Al-Masailul Islamiyah

Page 138: al-Masailu-l-Islamiyyah

631. Kama hajui unajisi wa kitu kwa kutokujua mas’ala, mfano kama

hajui unajisi wa damu, kisha akaswali na nguo iliyo na najisi ya

damu swala yake inasihi.

632. Kama hajui kwamba mwili wake au nguo yake ina najisi na akatam-

bua hilo baada ya swala, swala yake itasihi.

633. Akiona damu katika mwili wake au vazi lake na akawa na uhakika

kwamba ile si katika damu zilizonajisi, mfano akiwa na uhakika

kwamba damu ile ni ya kunguni au ya mbu, na akafahamu baada ya

swala kwamba damu ile ni katika damu zilizo najisi ambazo hazifai

kuswali nazo, swala yake aliyoiswali itasihi.

634. Ambaye hana nguo nyingine isipokuwa hiyo yenye najisi, ni wajibu

kuswali na nguo hiyo, hasa kama hataweza kuvua nguo yake kwa

sababu ya baridi na mfano wa hilo swala yake itasihi.

635. Ambaye ana nguo mbili na akafahamu kwamba mojawapo ya nguo

zake mbili ina najisi, lakini hafahamu ni ipi kati ya hizo iliyo na

najisi, kama muda ni wasaa ni wajibu kuswali na nguo zake mbili,

mfano akitaka kuswali adhuhuri na alasir ataswali nazo katika kila

nguo moja, katika nguo hizo mbili lakini kama wakati hautoshi, ita-

muwajibikia kuswali na nguo mojawapo atakaeitaka lakini na kwa

tahadhari alipe swala hiyo baada ya wakati katika nguo tohara.

SHARTI LA PILI

636. Ni wajibu nguo ya mwenye kuswali iwe ya halali, na mwenye kujua

uharamu wa kuvaa nguo ya kunyang’anya lau akiswali na nguo ya

wizi au nguo yenye uzi au vifungo au kitu kingine cha kunyang’anya

swala yake inabatilika na hukumu hii pia ni kwa mtu ambaye hajui

na mwenye kupuuzia.

124

Al-Masailul Islamiyah

Page 139: al-Masailu-l-Islamiyyah

637. Anayejua uharamu wa kuvaa nguo ya kunyang’anya, lakini hajui

kubatilika kwa swala ya mwenye kuswali kwa nguo hiyo, kama

ataswali kwa nguo hiyo ya kunyang’anya kwa makusudi swala yake

itabatilika.

638. Kama hakujua au akisahau kwamba nguo yake ni ya wizi na

akaswali na nguo hiyo, swala yake itasihi lakini kama mtu

mwenyewe akinyang’anya nguo kisha akasahau kwamba nguo hii ni

ya kunyang’anya basi kwa tahadhari arudie swala hiyo kwa nguo

halali.

639. Kama mtu akiswali kwa nguo ya kunyang’anya kwa kulinda maisha

yake au kwa ajili ya nguo hiyo isiweze kubwa swala yake itasihi.

640. Akinunua nguo na pesa ambayo haijatolewa khumsi au zaka, na

akaswali na nguo hiyo, swala yake itakuwa na mushkeli

SHARTI LA TATU

641. Ni wajibu vazi la mwenye kusali lisiwe limechanganywa na vitu

vinavyotokana na mizoga ya wanyama ambao hutoka damu kwa kasi

wakati wa kuchinja kama vile mbuzi, na kwa tahadhari pia asiswali

na vazi lililotengenezwa na vitu vya mizoga ya wanyama ambao

damu zao hazitoki kwa kasi kama vile samaki na nyoka.

SHARTI LA NNE

642. Ni wajibu vazi la mwenye kuswali lisiwe limetokana na vitu vya

wanyama ambao ni haramu kuliwa na swala itabatilika kutokana na

vitu hivyo hata kama vazi hilo lina unywele mmoja.

643. Kama vazi lake lina kitu chochote kinachotokana na mate au mako-

hozi au kitu kingine chenye unyevunyevu unaotokana na wanyama

125

Al-Masailul Islamiyah

Page 140: al-Masailu-l-Islamiyyah

walio haramu kuliwa kama vile paka, kama vina unyevunyevu swala

yake itabatilika na vikiwa ni vikavu na najisi yake imeshaondoka

swala yake itasihi.

644. Akishuku kwamba vazi hili limetengenezwa kutokana na wanyama

ambao ni halali kuliwa au walioharamu kuliwa, itajuzu kuswali na

vazi hilo sawasawa limetengenezwa katika nchi za kiisalamu au

zisizokuwa za kiisalmu. Akiswali na nguo ambayo hajui au akisa-

hau kwamba imetokana na mnyama ambaye ni haramu kuliwa swala

yake itasihi.

SHARTI LA TANO

645. Ni haramu kwa mwanaume kuvaa nguo yenye nyuzi zilizochovya

dhahabu au vifungo vya dhahabu na itabatilisha swala, lakini haku-

na mushkeli katika hilo kwa wanawake katika swala na nje ya

swala. Ni haramu kwa mwanaume kujipamba kwa mapambo ya

dhahabu mfano kuvaa mikufu ya dhahbu shingoni au kuvaa pete au

saa ya dhahabu mkononi, na vitu vinayobatilisha swala, na ni

wajibu kujiepusha na kuvaa fremu za miwani kama ni za dhahabu,

lakini hakuna tatizo kujipamba mapambo ya dhahabu kwa

wanawake katika swala na nje ya swala.

646. Ikiwa mwanaume atasahau kwamba pete yake au vazi lake ni la

dhahabu, au akashuku na akaswali kwa pete au vazi hilo, swala yake

inasihi, lakini katika hali ya kushuku ni wajibu kwake afanye utafi-

ti na vivyo hivyo ni wajibu kufanya utafiti katika mas’ala mengine

yaliyobakia mbali na haya tuliyoyaeleza.

126

Al-Masailul Islamiyah

Page 141: al-Masailu-l-Islamiyyah

SHARTI LA SITA

647. Ni wajibu vazi la mwenye kuswali lisiwe limetokana na hariri hal-

isi hasa akiwa mwanaume na ni haramu pia kuvaa nje ya swala,

ama kofia, mkanda na mfano wa hivyo ni kinyume na tahadhari.

648. Nguo ambayo haifahamiki kuwa ni ya hariri halisi au laa, haina

mushkeli kuivaa wakati wa swala, hakuna tatizo katika leso iliy-

otengenezwa kwa hariri ikiwa ndani ya mfuko wa mwenye kuswali

na haitabatilisha swala. Hakuna tatizo kwa wanawake kuvaa hariri

ndani ya swala au nje ya swala. Hakuna kizuizi wakati wa dharura

kuvaa nguo ya kunyang’anya au iliyotengenezwa kwa hariri au

kuchanganywa na dhahabu au kutengenezwa kutokana na vitu vya

mizoga na inajuzu kuswali navyo.

SEHEMU AMBAZO HAZILAZIMU TOHARA YA

MWILI NA NGUO KWA MWENYE KUSWALI

649. Inasihi swala kwa kiwiliwili au nguo yenye najisi katika sehemu tatu:-

Ikiwa mwili au nguo ya mwenye kuswali itachafuka kwa damu iliyotoka

kwenye jeraha au kidonda au jipu kutoka katika mwili wake.

Mwili wake au nguo yake ikichafuka kwa damu iliyotoka kwa kiwango

kidogo sana.

Kama atalazimika kuswali kwa mwili au nguo iliyo na najisi.

650. Swala inasihi swala katika hali mbili ikiwa nguo za mwenye kuswali

tu zina najisi.

Ikiwa mavazi yake ni madogo mfano wa soksi au kofia vina najisi.

Ikinajisika nguo ya mwanamke anaelea kwa mkojo wa mtoto mchanga.

127

Al-Masailul Islamiyah

Page 142: al-Masailu-l-Islamiyyah

651. Kama katika mwili wa mwenye kuswali au nguo yake kuna jereha

au kidonda au jipu , itajuzu kwake kuswali kwa nguo hiyo mwilini

madamu jeraha au kidonda au jipu halijapona ikiwa kutoharisha

mwili au nguo au kubadilisha kwake kutakuwa na ugumu na pia

ikiwa katika mwili au nguo kuna matapishi yaliyotoka kwa

kuchanganyikana na damu au dawa iliyowekwa kwenye jeraha ikatia

najisi. Mtu ambaye mwili wake umejeruhiwa akiona katika mwili

wake au nguo yake damu na akawa hajui ni damu ya jeraha lake au

ni damu nyingine inajuzu kwake kuswali katika hali hiyo.

652. Ikiwa kwenye mwili wa mtu kuna majeraha mengi na yakawa

yamekaribiana kiasi cha kuhesabika kuwa ni jeraha moja hakuna

mushikeli kuswali na damu yake maadamu hajapona lakini kama

yametengana kiasi cha kuhesabika kila jeraha mahali pake basi kila

jeraha likipona itamlazimu kutoharisha nguo au mwili kwa ajili ya

swala kutokana na damu hiyo.

653. Ikiwa katika mwili au nguo ya mwenye kuswali kuna damu ya hedhi

au istihadha au nifasi au damu ya mbwa au nguruwe au damu ya

kafiri au mizoga swala yake itabatilika na pia kama kuna damu ya

mnyama ambaye ni haramu kuliwa, lakini hakuna tatizo katika

swala pamoja na damu zingine kama damu ya mtu au damu ya

mnyama aliye halali kuliwa japo itaenea sehemu za mwili wake au

nguo yake kwa sharti iwe damu yote hiyo ni chache sana.

YALIYO SUNNA KATIKA VAZI LA

128

Al-Masailul Islamiyah

Page 143: al-Masailu-l-Islamiyyah

MWENYE KUSWALI

654. Ni sunna katika vazi la mwenye kuswali mambo mengi miongoni

mwa hayo ni kuvaa kilemba, kuvaa joho, kuvaa nguo nyeupe, kuvaa

nguo iliyo safi zaidi, kujipaka manukato na kuvaa pete ya akiki.

YALIYO MAKURUHU KATIKA VAZI LA

MWENYE KUSWALI

655. Yaliyo makuruhu katika vazi la mwenye kuswali ni mengi, miongo-

ni mwa hayo ni kuvaa nguo nyeusi, ila kwa ajili ya kukumbuka misiba ya

maasumina (as) sio makuruhu bali ni sunna, na kuvaa nguo chafu, yenye

kubana, nguo za mwenye kunywa pombe, nguo za mtu ambaye hajiepushi

najisi, nguo yenye picha, nguo isiyo na vifungo na kuvaa pete yenye

picha.

SEHEMU YA MWENYE KUSWALI

656. Sehemu ya mwenye kuswali ina masharti tisa nayo ni:-

1. Iwe ya halali.

2. Iwe imetulizana isitikisike

3. Aweze kutimiza swala yake humo

4. Asiwe amekatazwa kubaki mle

5. Isiwe kusimama au kukaa sehemu ile ni haramu

6. Aweze kusimama, kurukuu na kusujudu humo

7. Asiwe mbele au amelingana na kaburi la maasum(as)

8. Sehemu hiyo isiwe na najisi yenye unyevunyevu

9. Paji lake la uso liwe limelingana na magoti yake na ncha za

dole gumba vya miguu yake.

129

Al-Masailul Islamiyah

Page 144: al-Masailu-l-Islamiyyah

Sharti la kwanza

657.Ni wajibu sehemu ya mwenye kuswali iwe ya halali, mwenye kuswali

katika sehemu iliyo nyang’anywa swala yake ni batili hata kama

ataswali juu ya godoro au kitanda lakini hakuna mushkeli kuswali

chini ya dari ya unyang’anyi na hema la unyang’anyi.

658. Mwenye kukaa katika sehemu ya msikiti kisha akaja mtu na akam-

nyanganya sehemu yake hiyo na akaswali, swala yake itakuwa na

mushkeli.

659. Kama mtu akijua kuwa sehemu hii ni ya kunyang’anya na hajui

kuwa kuswali katika sehemu hiyo kunabatilisha swala, kisha

akaswali hapo basi swala yake itabatilika kama hakufahamu kwa

kupuuzia. Mwenye kuwa na udhuru, na akaswali juu ya mnyama

kama mnyama huyo tandiko lake alotandikiwa juu ya mgongo wake

au ikiwa kiatu chake ni cha kunyang’anya swala yake ni batili, pia

hukumu ni hii hii kwa mwenye kuswali swala za sunna juu ya mnya-

ma huyo.

Sharti la pili

660. Ni wajibu sehemu ya mwenye kuswali iwe yenye kutulizana na

kama atalazimika kuswali katika sehemu yenye kutikisika kwa

sababu ya ufinyu wa wakati au sababu nyingine, mfano kuswali

katika gari au treni au ndege, itamuwajibikia kutokusoma wakati wa

mtikisiko na kutotulizana kwa mwili kama ataweza kufanya hivyo, hii

ni kama hataharibu utaratibu wa swala la sivyo asome wakati wa

mtikisiko, pia kama gari litageuka kutoka upande wa kibla kuelekea

upande mwingine ni wajibu yeye ageukie kibla.

Hapakatazwi kuswali katika gari au meli na vinginevyo vikiwa vimesima-

ma.

130

Al-Masailul Islamiyah

Page 145: al-Masailu-l-Islamiyyah

Sharti la tatu

661. Ni wajibu kwa mwenye kuswali aweze kumaliza swala, haijuzu

kuanza kuswali katika sehemu ambazo huna uhakika kwamba

utaweza kutimiza swala hapo, kwa sababu ya mvua au msongamano

au upepo mkali, lakini lau atashuku katika hilo au akawa na uhaki-

ka wa kutimiza swala, itajuzu kuanza kuswali, na ikikamilika swala

itasihi.

Sharti la nne

662.Nisharti asiswali katika sehemu ambayo ni haramu kubakia humo

kama vile kuswali chini ya dari inayokaribia kuanguka na kubomoka.

Sharti la tano

663. Ni sharti mtu asiswali juu ya kitu kilichokatazwa kusimama juu yake

au kukaa kama vile mswala ulioandikwa jina la Mwenyezi Mungu.

Sharti la sita

664. Ni wajibu asiswali katika paa liloinama sana kiasi kwamba hawezi

kusimama vizuri chini yake ama akilazimika kuswali katika sehemu

hii ni lazima asimame, arukuu na asujudu kadri atakavyoweza.

Sharti la saba

665. Ni wajibu asilitangulie kaburi la Mtume na maimamu wakati wa

kuswali vivyo hivyo asiswali kwa kulingana nalo kwa tahadhari ya

wajibu.

131

Al-Masailul Islamiyah

Page 146: al-Masailu-l-Islamiyyah

Sharti la nane

666. Ni wajibu sehemu ya mwenye kuswali isiwe na najisi yenye unyevu

nyevu unaohamia kwenye mwili wake au nguo yake na swala itabati-

lika ikiwa sehemu ya kusujudia ina najisi hata kama ni kavu na kwa

tahadhari ya sunna sehemu ya mwenye kuswali isiwe najisi kabisa.

Sharti la tisa

667. Ni wajibu sehemu ya paji lake wakati wa kusujudu isiwe juu au chini

zaidi kuliko. magoti yake na ncha za vidole gumba zaidi ya vidole

vinne vilivyounganishwa.

668. Si lazima mwanamke kusimama mbali ya mwanaume katika swala

isiyokuwa ya jamaa, wala mahali anaposujudia kuwa mbali kidogo

na mahali aliposimama mwanaume, ingawa ni bora kufanya hivyo.

669. Ni makuruhu kwa mwanamke kusimama mbele ya mwanaume au

kuwa sawasawa naye katika swala na kuanza kuswali pamoja lakini

haiwalazimu kurudia swala kama wakifanya hivyo. Kama kuna kizui-

zi kati ya mwanaume na mwanamke kiasi ambacho mmoja hamuo-

ni mwenzake au kati yao kuna umbali wa mita tano, au mmoja wao

kasimama sehemu ya juu sana kiasi ambacho haitasadikishwa kutan-

gulia kwa mwanamke au kuwa sawasawa, basi karaha huondoka. Ni

haramu kwa mwanaume na mwanamke ambao sio mahramu kukaa

chumba kimoja bila ya kuwa na mtu mwingine wa tatu na bila ya

kuonekana na yeyote, na kwa tahadhari ni kwamba swala yao hai-

tasihi katika sehemu hiyo, lakini kama mmoja ataswali na mwingi-

ne akaingia, swala yake haina mushkeli.

670. Kuswali sehemu ya kupigia muziki kama haihesabiki kuwa ni kusai-

dia kufanya katika maasi haina mushkeli.

132

Al-Masailul Islamiyah

Page 147: al-Masailu-l-Islamiyyah

SEHEMU ZILIZO SUNNA KUSWALI HUMO

671. Umepokewa msisitizo mkubwa katika sharia ya kiislamu kuhusu

kuswali katika misikiti na msikiti uliobora zaidi ni msikiti wa Makka,

kisha msikiti wa Mtume Madina kisha msikiti wa Al Kufa kisha msi-

kiti wa Al Aqswaa kisha kila msikiti mkuu wa kila mji, kisha msikiti

wa kila mtaa, kisha msikiti wa soko.

672. Ni bora kwa wanawake kuswali nyumbani lakini wakiweza kujilin-

da na wanaume ajinabiya basi itakuwa ni bora kuswali misikitini.

HUKUMU ZA MISIKITI

673. Ni haramu kutia najisi ardhi ya msikiti, dari yake, paa lake na sehe-

mu za ndani za kuta, na ni wajibu kwa atakayefahamu unajisi wa

moja ya sehemu hizo kuiondosha najisi haraka na kwa tahadhari ya

wajibu ni kwamba imeharamishwa kutia najisi sehemu za nje za msi-

kiti, na ikinajisika ni wajibu kwake kuiondosha haraka.

674. Kama hakuweza kusafisha msikiti au akihitajia msaada na hakupata

haitamuwajibikia kusafisha, lakini ni wajibu kwake kwa tahadhari ya

wajibu kumwambia mwenye uwezo wa kusafisha.

675. Sehemu ya msikiti ikinajisika na ikawa haiwezekani kutoharishwa

kwake ila kwa kuchimba shimo, basi ni wajibu kuchimbwa na ikila-

zimu kuvunja sehemu kwa ajili ya kutoharisha inajuzu kuvunja

sehemu hiyo. Ni haramu kutia najisi makaburi ya maimam, na lau

mojawapo likinajisika ni wajibu kulitoharisha. Ni haramu kuingiza

kiini cha najisi msikitini kama vile damu kama kutaudhalilisha msi-

kiti bali kwa tahadhari ya sunna kutoingiza kiini cha najisi msiki-

tini hata kama si kwa ajili ya kuudhalilisha msikiti lakini sio haramu

kuingiza kitu kilicho najisika msikitini, ila kama itakuwa ni kwa ajili

133

Al-Masailul Islamiyah

Page 148: al-Masailu-l-Islamiyyah

ya kuudhalilisha msikiti.

676. Haikatazwi kuweka mahema misikitini kwa ajili ya maatam na maji-

lisi za maombolezo ya maimamu. Pia haikatazwi kutundika na kui-

pamba kwa vitambaa vyeusi na kuingiza vitu vya kupikia chai kama

havitaleta madhara na havizui watu kuswali humo.

677. Haijuzu kuuza ardhi ya msikiti ikiwa msikiti umebomoka pia kuun-

ganisha na njia kuu au kuunganisha na milki ya mtu mwingine.

678. Ni haramu kuuza madirisha ya msikiti na milango yake na vitu vingi-

ne na kama msikiti ukibomoka basi ni wajibu kwa kiongozi wa kisha-

ria kuvitoa vitu na kuvitumia kuimarisha msikiti huo, na kama hai-

wezekani kuvitumia katika msikiti huo, ni wajibu kuvitoa katika misi-

kiti mingine, na ikishindikana katika misikiti mingine, itajuzu kuviu-

za kwa ajili ya kuimarisha misikiti mingine.

679. Inachukiza kuwaruhusu wasio na akili na watoto kuingia msikitini, ila

watoto kama kuingia kwao ni kwa ajili ya kujifunza swala na Qur’ani

na mas’ala ya kisharia, malezi, mafunzo ya kiislam na mengineyo,

pia inachukiza kwa mwenye kula vitunguu maji na saumu kama haru-

fu ya mdomo wake itawaudhi watu.

KUADHINI NA KUKIMU

680. Ni sunna kwa mwanaume na mwanamke kuadhini na kukimu kabla

ya swala za wajibu za kila siku, bali haifai kuacha kukimu lakini

kabla ya kuanza kuswali swala za wajibu zisizokuwa za kila siku

mfano swala za majanga ni sunna kusema mara tatu “As swalaatu

aswalatu aswalat”(badala ya kukimu).

781. Adhana ina vipengele ishirini navyo ni:-

Allahu akbar x 4

134

Al-Masailul Islamiyah

Page 149: al-Masailu-l-Islamiyyah

Ashahadu an llaa ilaaha illa llaah x 2

Ash hadu anna Muhammadan rasulullah x 2

Ash hadu anna Alliyyan waliyullah x 2

Hayya alaa swalaat x 2

Hayya alaal falah x 2

Hayya alaa khairil – amal x 2

Allah akbar x 2

Laa ilaaha illa llah x 2

683. Na iqama ina vipengele 19 yaani kwa kuondosha takbira mbili za

mwanzo na tahalili moja ya mwisho na kuongezea qadi qaamatis

swalaat mara mbili baada ya “Hayya alaa khairil – amali”

684. Haifai kutenganisha sana kati ya sentensi na vipengele vya adhana na

kukimu na akitenganisha sana kuliko kawaida basi atapaswa arudie

tena upya.

685. Akirudiarudia kwa kughani adhana na kukimu kiasi kwamba inakuwa

kama wimbo katika vikao vya upuuzi na michezo inakuwa ni hara-

mu.

686. Hakuna adhana katika swala za aina tano:-

Swala ya alasiri siku ya Ijumaa

Swala ya alasiri siku ya arafa, nayo ni siku ya 9 ya mfungo 3

swala ya isha usiku wa Idul -Adhuhaa kwa aliyoko muzdalfa

Swala ya alasiri na isha kwa mwenye istihadha

Swala ya alasiri na isha kwa asiyeweza kuzui mkojo au haja

kubwa, katika swala hizi huondoka adhana kama hakutenganisha

kati ya swala hiyo na Swala iliyotangulia.

687. Pakiadhiniwa na kukimiwa kwa swala ya jamaa, hawataadhini wala

kukimu wale watakaounga jamaa hawatolazimika kuadhini wala

kukimu tena.

688. Hakuna kukimu kama mtu akikuta watu wanaswali jamaa au jamaa

135

Al-Masailul Islamiyah

Page 150: al-Masailu-l-Islamiyyah

imemalizika na watu hawajaondoka katika safu, na akataka kuswali

peke yake au kuswali swala ya jamaa nyingine kwa masharti

matatu:-

Iwe pameadhiniwa na kukimiwa katika swala iliyotangulia

Isiwe swala ya jamaa iliyotangulia ni batili kuungana jamaa mbili ya

mwanzo na inayofuatia katika sehemu moja.

689. Ni sunna kwa anayechaguliwa kuadhini na kukim awe mwadilifu,

anayefahamu nyakati za swala mwenye sauti ya juu na aadhini kati-

ka sehemu iliyonyanyuka.

MAMBO YALIYOWAJIBU KATIKA SWALA

690. Wajibati za swala ni kumi na moja:-

Nia

Kisimamo

Takbira ya kuhirimia swala

Rukuu

Sijida

Kusoma

Dhikir

Tashahud

Kutoa salam

10.Kufuata utaratibu

11.Kufuatanisha

691. Baadhi ya wajibati za swala ni nguzo kwa maana kama mwenye

kuswali akiicha au akizidisha kwa makusudi au bila ya kukusudia

swala yake inabatilika, na baadhi ya wajibati siyo nguzo, kwa maana

kwamba swala inabatilika kwa kupunguza au kuzidisha kwa makus-

dui wala haibatiliki kwa kusahau.

692. Nguzo za swala ni tano

136

Al-Masailul Islamiyah

Page 151: al-Masailu-l-Islamiyyah

Nia

Takbira ya kuhirimia

Kisimamo wakati wa takbira ya kuhirimia na kisimamo kilichoun-

gana na rukuu (yaani kabla ya kurukuu)

Rukuu

Sijida mbili

NIA

693. Ni wajibu kwa mwenye kuswali atie nia katika swala kwa kujikuru-

bisha kwa Mwenyezi Mungu, na kutekeleza amri yake, wala hailaz-

imu kupitisha moyoni au kuitamka kwa ulimi wake, bali yatosha

kufahamu kwamba yeye anaswali rakaa nne za swala ya adhuhuri

kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

694. Akinuia katika swala ya adhuhuri au alasiri kwamba anaswali rakaa

nne lakini hakubainisha kwamba ni adhuhuri au alasiri basi swala

yake itakuwa na mushikeli na ni wajibu kwa ambaye ana kadha ya

adhuhuri na akataka kuswali adhuhuri kwa wakati au kadha katika

wakati wa adhuhuri kubainisha kwamba anaswali kadha au adaa

(kwa wakati).

695. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kubakia na nia yake tangu mwanzo

wa swala hadi mwisho na akighafilika wakati wa swala, kiasi lau

akiulizwa unafanya nini? Ikawa hajui aseme nini, swala yake ita-

batilika.

137

Al-Masailul Islamiyah

Page 152: al-Masailu-l-Islamiyyah

TAKBIRA YA KUHIRIMIA

696. Takbira ya kuhirimia yaani kusema: “Allah akbar” ni wajibu katika

kila mwanzo wa swala nayo ni nguzo katika swala na ni wajibu kufu-

atanisha kati ya neno “Allah” na neno “Akbar” pia ni wajibu kuy-

atamka kwa lugha ya kiarabu sahihi, na lau akitamka kwa kiarabu

chenye makosa au kwa lugha isiyokuwa ya kiarabu, takbira yake

haitasihi.

697. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kutulizana wakati wa kuleta takbira

ya kuhirimia, na kama akihirimia na hali anatikisika kwa makusudi,

takbira yake inabatilika.

698. Ni wajibu kuhirimia, na kusoma Al hamdu, sura, dhikiri na dua kwa

kiasi cha kusikia mwenyewe, kama ni kiziwi au asiyesikia vizuri au

kwa sababu ya makelele mengi, ni wajibu kuhirimia kwa kiasi

ambacho kama si kizuizi angesikia.

699. Bubu na mwenye matatizo ya ulimi yanayomfanya asiweze kutamka

takbira kwa njia sahihi, ni wajibu kutamka kwa namna atakayoweza,

na kama hakuweza kutamka chochote, itamlazimu kutamka kimoyo

moyo, na aashirie katika kuhirimia kwa kutikisa ulimi wake kwa

namna atakavyoweza.

700. Ni sunna kunyanyua mikono mpaka kwenye usawa wa masikio

wakati wa kuhirimia na katika takbira zingine wakati wa swala.

KISIMAMO

701. Kisimamo wakati wa kuhirimia na kisimamo kabla ya kwenda

kurukuu, visimamo hivi ni nguzo mbili, lakini kisimamo wakati wa

kusoma Al hamdu na sura na kisimamo baada ya rukuu si nguzo laki-

138

Al-Masailul Islamiyah

Page 153: al-Masailu-l-Islamiyyah

ni akiviacha kwa kusahau swala yake itasihi.

702. Ni wajibu kusimama kabla ya kuhirimia swala na baada ya kuhirimia

kwa kiwango cha kuwa na uhakika kwamba amehirimia wakati wa

kisimamo.

703. Akisahau kurukuu na akakaa baada ya Al hamdu na sura kisha

akakumbuka kwamba hajarukuu ni wajibu kusimama na kisha

arukuu, na akirukuu bila ya kusimama kwanza, swala yake inabatili-

ka kwa sababu hajasimama kabla ya rukuu.

704. Ni wajibu asitikise mwili wake wakati wa kisimamo na asiegemee

upande mmoja wala asiegemee kitu chochote, lakini hakuna tatizo lau

akifanya mambo haya kwa dharura, kama ambavyo hakuna tatizo

kama atatikisa miguu yake wakati wa kuinama kwenda kwenye

rukuu.

705. Akishindwa kusimama wakati wa kuswali ni wajibu kukaa na

akishindwa kukaa pia, ni wajibu kwake kulala lakini asisome cho-

chote mpaka atulizane.

KUSOMA

706. Ni wajibu kusoma Al hamdu na sura kamili katika rakaa mbili za

mwanzo katika swala za wajibu za kila siku. Kama wakati utakuwa ni

mfinyu na akalazimika kutokusoma sura, mfano lau ataogopa kuibi-

wa au kudhuriwa na wanyama wakali au litamsibu jambo jingine

kama atasoma sura, basi ni wajibu kwake asisome sura.

707. Akisoma sura kabla ya kusoma Al hamdu kwa makusudi swala yake

itabatilika. Na akifanya hivyo kwa kusahau na akakumbuka wakati

huo, itamlazimu kuacha sura kisha atasoma Al hamdu kisha atasoma

sura kuanzia mwanzo.

139

Al-Masailul Islamiyah

Page 154: al-Masailu-l-Islamiyyah

708. Akisahau kusoma Al hamdu na sura au akasahau mojawapo kisha

akakumbuka baada ya kufika kwenye rukuu swala yake itasihi.

709. Akikumbuka kabla ya kuinama kwenye rukuu kwamba hakusoma Al

hamdu na sura ni wajibu kuzisoma, pia akikumbuka kwamba haku-

soma sura peke yake, ni wajibu kuisoma, lakini akikumbuka katika

hali ile kwamba hakusoma Al hamdu ni wajibu kuisoma Al hamdu

kwanza kisha atairudia sura mara nyingine, na atafanya hivyo akijua

baada ya kuinama na kabla ya kufika katika rukuu kuwa hakusoma

Al hamdu na sura au mojawapo atarejea katika kisimamo na kusoma

Al hamdu aliyoisahau.

710. Akikusudia katika swala ya wajibu kusoma mojawapo ya sura zenye

sijda ya lazima swala yake itabatilika.

711. Ni wajibu kwa mwanaume kudhihirisha Al hamdu na sura katika

swala ya asubuhi, magharibi na isha na ni wajibu kwa mwanaume na

mwanamke kutokudhihirisha katika swala ya adhuhuri na alasiri.

712. Ni wajibu kwa mwanaume kudhihirisha kila neno la sura ya Al hamdu

na sura atakayoisoma katika swala ya asubuhi, magharibi na isha hata

herufi ya mwisho.

713. Inajuzu kwa mwanamke kutokudhihirisha au kudhuhirisha Al hamdu

katika swala ya asubuhi, magharibi na isha lakini hatodhihirisha

kama sauti yake itasikika na mtu ambaye si mahramu yake.

714. Mwanaume akikusudia kutokudhihirisha katika swala ambayo ni

wajibu kudhihirisha swala yake itabatilika lakini lau akifanya hivyo

kwa kusahau au kutokujua swala yake itasihi, na akifahamu kuwa

amekosea wakati wakusoma Al hamdu na sura, haimlazimu kurudia

aliyosoma kwa kukosea.

140

Al-Masailul Islamiyah

Page 155: al-Masailu-l-Islamiyyah

715. Akisoma kwa sauti ya juu sura ya Al hamdu na sura kinyume na sauti

zilizozoeleka, kama akisoma kwa kupiga makelele ya juu, swala yake

itabatilika.

716. Ni wajibu kujifunza swala ili asisome kwa makosa na ambaye hawezi

kujifunza kutamka sawa sawa, ni wajibu kuswali kwa njia atakay-

oweza lakini ni vizuri kuswali jamaa.

717. Ni sunna katika swala zote kusoma suratul – Qadir katika rakaa ya

kwanza na suratu tauhid katika rakaa ya pili.

718. Inachukiza kwa mtu kuacha kusoma suratu tauhid katika swala zake

za kila siku.

719. Inachukiza kuisoma suratu tauhid yote kwa pumzi mmoja bila ya

kusimama kwenye vituo.

720. Inachukiza kusoma katika rakaa ya pili sura aliyoisoma katika rakaa

ya kwanza isipokuwa kama atasoma suratu tauhid.

RUKUU

721. Ni wajibu kuinama baada ya kusoma katika kila rakaa kwa kiwango

cha kumuwezesha kushika magoti yaani kuweka viganja vya mikono

yake magotini.

722. Hakuna tatizo akiinama kwa kiwango cha kushika magoti hata kama

hakuweka viganja vyake juu ya magoti yake

723. Ni wajibu kuinama kuwe kwa nia ya kurukuu na akiinama kwa lengo

lingine kama kuweka kitu au kukinyanyua haitojuzu kuhesabiwa

kuwa ni rukuu.

730. Akirukuu kwa namna isiyoeleweka, kwa mfano lau akiinama kwa

kuelemea upande wa kulia au wa kushoto, rukuu yake haitosihi hata

141

Al-Masailul Islamiyah

Page 156: al-Masailu-l-Islamiyyah

kama mikono yake itafika kwenye magoti.

731. Ni bora kusema katika rukuu “Subhanallah” mara tatu au “Subhana

rabbiyal – adhiim wabihamdih” mara moja lakini kama muda ni

mfinyu au wakati wa dharura yatosha kusema “Subuhanallah” mara

moja.

732. Ni wajibu dhikri ya rukuu iwe kwa kufuatana na kwa kiarabu sahihi

na ni sunna kuikariri mara tatu au tano au zaidi.

733. Ni wajibu mwili wa mwenye kuswali kutulizana wakati wa kurukuu

kiasi cha kuweza kuitamka dhikri ya wajibu na pia wakati wa kutam-

ka dhikri ya sunna.

734. Akinyanyua kichwa chake makusudi kabla ya kukamilisha dhikiri ya

wajibu swala yake inabatilika.

735. Akisahau kurukuu na akakumbuka kabla ya kufika katika sijda ni

wajibu kusimama kisha alete rukuu na lau akisimama kwenye rukuu

kwa kuinama swala yake itabatilika.

736. Akikumbuka kuwa hakurukuu na hilo ni baada ya kuwa ameshafika

chini au baada ya kunyanyua kichawa chake kutoka kwenye sijda ya

kwanza, itamlazimu asimame wima kisha arukuu, kisha alete sijda ya

swala, kisha sijida ya sahau baada ya swala na kwa tahadhari arudie

swala yake mara ya pili.

KUSUJUDU

737. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kuleta sijida mbili baada ya rukuu,

katika kila rakaa za wajibu na sunna, maana ya kusujudu ni kuweka

paji la uso na matumbo ya viganja, magoti na vidole gumba vya

142

Al-Masailul Islamiyah

Page 157: al-Masailu-l-Islamiyyah

miguu juu ya ardhi.

738. Sijda mbili ni nguzo, kama mwenye kuswali akiziacha katika swala

ya wajibu kwa makusudi au kwa kusahau au akizidisha sijda mbili

zingine, swala yake itabatilika.

739. Akipunguza au akizidisha moja ya sijida mbili kwa makusudi swala

yake itabatilika

740. Kama hakuweka paji la uso wake ardhini kwa makusudi au kwa kusa-

hau sijda hiyo haitahesabika hata kama ameweka sehemu zingine za

kusujudia ardhini, lakini akiweka paji lake ardhini na hakuweka viun-

go vingine vya kusujudia sijda yake itasihi.

741. Ni wajibu kutulizana kwa mwili katika sijida kiasi cha kuleta dhikiri

ya wajibu na pia katika dhikiri ya sunna.

742. Akikusudia kuleta dhikri ya sijda kabla ya kufikisha paji la uso wake

ardhini na kutulizana mwili wake au akanyanyua kichwa chake kabla

ya kutimiza dhikri ya sijda kwa makusudi swala yake itabatilika.

743. Akileta dhikri ya sijida kabla ya kufikisha paji lake ardhini na mwili

wake kutulizana kwa kusahau na akafahamu makosa yake kabla ya

kunyanyua kichwa katika sijda atarudia dhikri na swala yake itasihi.

745. Akitambua baada ya kunyanyua kichwa katika sijda kwamba amele-

ta dhikri kabla ya kutulizana mwili wake au amenyanyua kichwa

kabla ya kutimiza dhikri ya sijida swala yake itasihi.

746. Akikusudia kunyanyua mojawapo ya viungo saba vya sijda wakati

wa kuleta dhikri ya sijda, swala yake inabatilika lakini hakuna tatizo

akinyanyua moja ya viungo vya sijda isipokuwa paji la uso katika

hali isiyokuwa ya kuleta dhikri ya swala kisha akarejesha kiungo

hicho ardhini mara nyingine.

143

Al-Masailul Islamiyah

Page 158: al-Masailu-l-Islamiyyah

VITU VINAVYOSIHI KUSUJUDIA JUU YAKE

747. Ni wajibu kusujudu juu ya ardhi na vinavyotokana na ardhi

“isipokuwa vile vinavyoliwa au kuvaliwa” kama vile mbao na majani

ya miti, wala haisihi kusujudu juu ya vitu vyenye kuliwa, kama vile

matunda na vyenye kuvaliwa kama vile pamba na vitu vya madini

kama vile dhahabu.

748. Haikatazwi kusujudu juu ya jani la zabibu likiwa kavu, kama sio kavu

na liko katika muda wa kuweza kuliwa, haitajuzu kusujudu juu yake.

749. Inasihi kusujudu juu ya vitu vinavyoota katika ardhi na vyenye kuli-

wa na wanyama kama vile majani, pumba n.k

750. Kilicho bora zaidi kusujudia ni turba ya Imam Hussein (as) kisha

udongo wa kawaida kisha jiwe kisha mimea.

751. Kama hana kitu chenye kusihi kusujudia juu yake au anacho lakini

akawa hawezi kusujudu juu yake kwa sababu ya baridi kali au joto

kali, basi kama ana nguo iliyotengenezwa kwa pamba au katani, ni

wajibu kwake kusujudu juu ya nguo yake, na ikiwa nguo yake ime-

tokana na vitu vingine ni wajibu kusujudu juu ya viganja vya mikono

yake au kitu cha madini kama vile pete ya akiki lakini ni bora asisu-

judu juu ya viganja vyake kama kunauwezekano wa kusujudu juu ya

kitu cha madini.

Kusujudu katika ardhi ambayo haitulizani ni batili.

752. Hakuna tatizo katika swala yake kama akifahamu baada ya kusujudu

kwamba amesujudu katika vitu ambavyo havisihi kusujudu juu yake.

753. Ni haramu kumsujudia asiyekuwa Mwenyezi Mungu na wanayofanya

144

Al-Masailul Islamiyah

Page 159: al-Masailu-l-Islamiyyah

baadhi ya waumini kwa kuweka mapaji ya nyuso zao katika dharihi

ya makaburi ya Maimamu watukufu hilo ni kwa ajili ya kumshuku-

ru Mwenyezi Mungu na hakuna mushkeli humo, ama kubusu ukuta

wa makaburi ya Maimamu jambo hilo linajuzu bali ni sunna na hilo

sio sijida

SUNNA ZA SIJDA NA MAKURUHU ZAKE

753. Ni sunna katika sijida mambo yafuatayo:-

Mwenye kuswali aseme Allahu akbar akiwa amesimama kabla ya kwenda

kusujudu, baada ya kunyanyua kichwa chake katika rukuu na kusimama

wima, pia kwa mwenye kuswali kwa kukaa baada ya kukaa wima.

Mwanaume kutanguliza mikono yake ardhini kwanza wakati wa kwenda

kusujudu kisha magoti yake.

Kuweka pua yake juu ya turba au kitu chenye kusihi kusujudia juu yake.

Kuviunganisha vidole vya mikono yake na kuiweka mikono yake usawa

wa ndwele za masikio yake kiasi kwamba ncha za vidole vyake vinakuwa

vimeelekea kibla

Kuomba katika sijida yake na kumwomba Mwenyezi Mungu kumkidhia

haja zake na aombe kwa dua hii “ Yaa khairal – masiuliina wa yaa khairal

– mu’utwiina, urzuqunii warzuqu iyaalii min fadhilika fainnaka dhul fad-

hilil adhiym”

Kukalia paja la kushoto anapotoka katika sijda na kuweka mgongo wa

mguu wa kulia juu ya tumbo la mguu wa kushoto.

Alete takibira baada ya kukaa katika kila sijda na mwili wake utulizane.

Aseme “Astaghafirullaha rabii waatubu ilaihi” Baada ya kukaa kutoka

sijda ya kwanza na mwili wake utulizane.

Arefushe sijida yake

Aweke mikono yake juu ya mapaja anapokaa

145

Al-Masailul Islamiyah

Page 160: al-Masailu-l-Islamiyyah

Alete takbira anapokwenda sijida ya pili katika hali ya kutulizana

Amswalie Mtume na kizazi chake katika sijida yake

Aweke mikono yake ardhini anapotaka kusimama

Mwanaume asikutanishe viwiko vya mikono yake na tumbo lake na asi-

ikutanishe na mbavu zake lakini mwanamke alaze viwiko vyake na tumbo

lake ardhini na kuvibana viungo vya mwili wake.

754. Inachukiza kupuliza sehemu ya kusujudia kwa ajili ya kuondosha

vumbi na lau ikitoka kutokana na kupuliza lafudhi ya herufi mbili

mfano akisema fuu, kwa makusudi swala yake itabatilika.

SIJDA ZA QUR’AN ZILIZO WAJIBU

755. Sijda za wajibu zinapatikana kila moja katika sura nne nazo ni:-

surat Najmi: aya ya 62, Al Alaq aya ya 19, Fusswilat aya ya 37 na As

Sajida aya ya 15 kila sura ina aya moja ya sijida ya wajibu na zinabainish-

wa katika misahafu mitukufu na ni wajibu kwa mtu atakapo isoma au

kuisikia asujudu baada ya kukamilika kusomwa aya kwa haraka, na kama

atasahau kusujudu wakati ule ule, basi asujudu akikumbuka.

Inawajibika kusujudu kama ikisomwa aya kamili ama lau ikisomwa nusu

haitolazimu kusujudu.

756.Akisikia aya ya sijda ikisomwa na mtoto ambaye hatofautishi jambo la

kheri na la shari au akasikia kwa mtu ambaye hakukusudia kusoma

Qur’ani, kwa tahadhari ya sunna asujudu, na pia akisikia aya ya sijda

katika kanda za kaseti au redioni.

Yatosha katika sijida ya Qur’an ya wajibu kuweka paji la uso ardhini kwa

lengo la kusujudu hata kama hakusoma dhikri lakini ni sunna kusoma

dhikri na ni bora kusema: “Laa ilaaha illa llahu haqan haqan, laa ilaha

illa llahu imanan wataswidiyqan, laa illaha illallaahu ubudiyatan

wariqan, sajadtu laka ya Rabi ta’abbudan wariqqan laa mustankifan

146

Al-Masailul Islamiyah

Page 161: al-Masailu-l-Islamiyyah

walaa mustakbiran bal anaa abdun dhalilun dhaiifun khaaifun mustaji-

irun”

TASHAHUD

757. Ni wajibu kukaa katika kila rakaa ya pili ya swala za wajibu na kati-

ka rakaa ya tatu ya swala ya magharibi na rakaa ya nne ya swala ya

adhuhuri, alasiri na isha na hilo ni baada ya kukaa kutoka sijida ya

pili, na kusema hali umetulizana mwili wake “Ash hadu an laa ila

ha illa llaahu wahadahu laa sharika lahu waash hadu anna

Muhammadan abduhu warasuluhu Allahumma swali alaa

Muhammadin waali Muhammadi”

758. Ni wajibu kuyasoma maneno ya tashahudi kwa kiarabu sahihi na kwa

kufuatana kama inavyofahamika.

759. Akisahau tashahud na akasimama kisha akakumbuka kabla ya

kurukuu kuwa hajaleta tashahud atakaa na kuleta tashahudi kisha

atasimama na kusoma yaliyo wajibu katika rakaa hiyo na kukamilisha

swala kisha ataleta sijda sahau baada ya swala kwa kusimama pasipo

mahala pake na akikumbuka ndani ya rukuu au baada ya salamu

atailipa tashahudi na kuleta sijia mbili za sahau kwa ajili ya tashahu-

di iliyo sahauliwa.

759. Ni sunna kwa mwanamke kubananisha mapaja yake wakati wa

tashahudi.

KUTOA SALAM

760. Mwenye kuswali atasema baada ya tashahud katika rakaa ya mwisho

ya swala na akiwa amekaa na kutulizana mwili wake “Assalaam

alaika ayyuha nnabiyyu warahmatullah wabarakatuh assalam

alainaa waalaa ibaadillah sswalihiyna assalaam alaikum warahmat-

147

Al-Masailul Islamiyah

Page 162: al-Masailu-l-Islamiyyah

ullah wabarakatuh”.

761. Akisahau salam na akawa hakukumbuka ila baada ya kumalizika

swala ni wajibu kwa tahadhari alete sijda mbili za sahau na ni vizuri

zaidi kuirudia swala yake.

MPANGILIO

762. Akiacha mpangilio wa swala kwa makusudi mfano akasoma sura

kabla ya Al hamdu au akasujudu kabla ya kurukuu swala yake ita-

batilika.

763. Akisahau nguzo miongoni mwa nguzo za swala kwa mfano akale-

ta sijida mbili kabla ya kuleta rukuu swala yake itabatilika.

764. Akisahau nguzo na akaleta kinachofuatia ambacho si nguzo, kwa

mfano akisahau sijida mbili na akaleta tashahudi ni wajibu alete

nguzo aliyoisahau kisha atarudia kusoma aliyoyasoma mwanzo

kimakosa au kwa kusahau.

765. Akisahau ambayo si nguzo na akaleta nguzo inayofuata, kwa mfano

lau akisahau Al hamdu na akashughulika na rukuu swala yake itasi-

hi.

766. Akileta sijida ya kwanza kwa kuamini kuwa ni sijida ya pili itah-

esabika kuwa ni sijda ya kwanza au akileta sijida ya pili k0wa

kuamini kuwa ni sijda ya kwanza itahesabika kuwa ni sijida ya pili na

swala yake itasihi.

KUFUATANISHA

767. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kuchunga mfuatano wa swala yaani

alete vitendo vya swala kama vile kurukuu, kusujudu na tashahud kwa

kufuatana na bila ya kutenganisha, pia achunge na afuatanishe katika

dhikir ambazo anazisoma kama inavyofahamika, na lau atatenganisha kati

148

Al-Masailul Islamiyah

Page 163: al-Masailu-l-Islamiyyah

ya mambo haya kiasi ambacho haitasemwa kwamba anaswali, swala

yake itabatilika.

768. Akitenganisha kati ya herufi na manaeno ya swala kwa kushau laki-

ni kutenganisha huko sio kwa kiasi cha kufuta utaratibu wa swala

kama hakushughulika na nguzo inayofuata ni wajibu kurudia kiso-

mo cha herufi na maneno yale kwa kufuatanisha na kwa njia yenye

kufahamika na lau kama ameshughulika na nguzo iliyofuata swala

yake itasihi.

769. Kurefusha rukuu na sijida na kusoma sura ndefu hakuvunji wala

hakuharibu mfuatano wake.

KUNUTI

770. Ni sunna kusoma kunuti katika swala zote za wajibu na za sunna na

hilo ni kabla ya kwenda rukuu ya rakaa ya pili bali ni vizuri

kutokuacha kunuti katika swala za wajibu na ni sunna kusoma kunuti

katika swala ya witiri japokuwa ni rakaa moja.

771. Katika kila rakaa ya swala ya ijumaa kuna kunuti na katika swala za

majanga kuna kunuti tano, na katika swala ya Iddi rakaa ya kwanza

ina kunuti tano na rakaa ya pili ina kunuti nne, na ni bora kutokuacha

kunuti za swala ya Iddil- Fitri na Adhuhaa.

772. Ni Sunna kwa mwenye kuswali kudhihirisha kunuti yake lakini ni

makuruhu kwa anayeswali jamaa kudhihirisha kunuti yake kama

Imamu atasikia sauti yake.

KUMSWALIA MTUME (SAWW)

773. Ni sunna kumswalia Mtume na watu wa nyumbani kwake pindi

149

Al-Masailul Islamiyah

Page 164: al-Masailu-l-Islamiyyah

usikiapo majina yake matukufu kama Muhammadi, Ahmadi au sifa

yake kama Mustwafaa au lakabu yake kama Abul – Qasim na hata

akisikia dhamiri inayomkusudia Mtume hata kama yupo kwenye

swala.

774. Ni sunna kuandika “kumtamkia rehema Mtume” pindi unapoandika

majina yake matukufu na pia kumtakia rehema Mtume na watu wa

nyumbani kwake anapowataja.

775. Namna ya kumtakia rehema Mtume ni kusema: “Allahuma swali

alaa Muhammadi wa Aali Muhammadi”

VINAVYO BATILISHA SWALA

776. Vitu vinavyobatilisha swala ni kumi na mbili:-

Kukosekana sharti miongoni mwa masharti ya swala.

Kutenguka udhu au josho

Kuweka mkono juu ya mwingine “juu ya tumbo”

Kusema “amina” baada ya Al hamdu

Kukipa kibla mgongo

Kuzungumza

Kukohoa

Kulia kwa ajili ya mambo ya kidunia

Kufutika sura ya swala

Kula na kunywa

Baadhi ya vifungu vya shaka

Ziada au upungufu katika nguzo za swala na zinginezo kwa ujumla.

YA KWANZA

777. Cha kwanza katika vinavyobatilisha swala ni kukosekana katikati

ya swala sharti miongoni mwa masharti yake, mfano atambue

katikati ya swala kuwa sehemu anayoswalia ni ya unyang’anyi na

150

Al-Masailul Islamiyah

Page 165: al-Masailu-l-Islamiyyah

hawezi kuhamia katika sehemu iliyohalali bila ya kufanya mambo

mengi ya kufuta sura ya swala.

YA PILI

778. Cha pili katika vinavyobatilisha swala ni kupatwa katikati ya swala

na moja ya vitenguzi vya udhu au josho, kwa kukusudia au kusahau

au kwa dharura mfano kutokwa na mkojo.

779. Al- masluus– Anayetokwa na mkojo kila wakati, au al – mabtun –

anayetokwa na haja kubwa mara kwa mara wakifanya kutokana na

wadhifa wao ambao tumeutaja katika hukumu za udhu swala zao

hazitabatilika. Na vile vile Mustahadha swala yake itasihi akitokwa

na damu katika swala akizingatia hukumu za istahadha.

780. Mwenye kughafilika na akalala bila ya hiyari kama hatajua amelala

ndani ya swala au baada ya swala, ni lazima arudie swala kwa

tahadhari ya wajibu ndani ya muda, na ni sunna alipe nje ya wakati.

781. Akitambua kuwa amelala kwa kutaka kwake na akasahau kuwa

amelala baada ya swala au katikati ya swala, swala yake itasihi.

782. Atakapoamka usingizini katika hali ya sijda na akashuku kuwa

amelala katika sijda ya mwisho ya swala au katika Sijida ya

kushukuru, “Baada ya swala” ni lazima arudie swala kwa tahadhari

ya wajibu ndani ya wakati, na ni sunna airudie nje ya wakati

YA TATU

783. Cha tatu katika vinavyobatilisha swala ni “takfiri” nayo ni kuwe-

ka moja ya mikono miwili juu ya mwingine kama wafanyavyo

wasiokuwa Shia.

151

Al-Masailul Islamiyah

Page 166: al-Masailu-l-Islamiyyah

784. Akiweka mkono juu ya mwingine ni lazima arudie swala na hata

kama hatafanya mfano wa takfiri zao, lakini hakuna tatizo kama

atafanya hivyo kwa kusahau, au kwa dharura au akifanya hivyo kwa

kujikuna na mfano wake.

YA NNE

785. Cha nne katika vinavyobatilisha swala ni kusema “Amin” baada ya

kusoma Al – hamdu ,na akisema hivyo kwa kusahau au taqiya swala

yake haitobatilika.

YA TANO

786. Cha tano katika vinavyobatilisha swala ni kukipa kibla mgongo kwa

kukusudia au kusahau au kwa kutokujua au akigeukia kulia au

kushoto mwa kibla, bali hata kwa makusudi kwa kiasi kwamba

haisemekani kuwa ameelekea kibla swala yake inabatilika hata kama

hajageuka kulia au kushoto.

787. Akigeuza kichwa chake mwelekeo wa kibla kwa kukusudia au kwa

kusahau kiasi kwamba anaweza kuona nyuma swala yake inabati-

lika, lakini akigeuza uso wake kidogo kwa kukusudia au kwa kusa-

hau swala yake haibatiliki

YA SITA

788. Cha sita katika vinavyobatilisha swala ni kutamka neno lenye

herufi mbili au zaidi hata kama halina maana lakini akifanya

hivyo kwa kusahau swala yake haibatiliki.

789. Akitamka neno lenye herufi moja na lenye maana mfano “Qi” amba-

cho ni kitendo cha amri ambacho kinatokana na “waqaa, yaqii” kwa

maana ya hifadhi, akifahamu maana ya kitendo hiki na akakusudia

kutamka, swala yake inabatilika, kwa tahadhari ya wajibu arudie

152

Al-Masailul Islamiyah

Page 167: al-Masailu-l-Islamiyyah

swala hata kama hakukusudia maana yake lakini alikuwa anatam-

bua kuwa maana yake ni hiyo.

790. Hakuna tatizo katika kukohoa, kucheua na kupiga miayo kwenye

swala, lakini kauli “akh” “ah” na zingine zenye herufi mbili zin-

abatilisha swala kama zikitamkwa kwa kukusudia.

791. Hakuna tatizo akitamka neno kwa kukusudia utajo mfano akisema:

“Allahu Akbar” kwa sauti ya juu ya kumzindua mwenzake katika

jambo fulani, na akitamka neno kwa kukusudia uzinduzi wa kufa-

hamisha jambo fulani na bila kukusudia kuwa ni dhikri swala ita-

batilika.

792. Hakuna tatizo kusoma Qur’an katika swala isipokuwa sura za

“Azaim” zenye sijida za lazima ambazo utajo wake umeshapita kati-

ka hukumu za janaba, na pia hakuna tatizo katika kutaja majina ya

Mwenyezi Mungu katika swala, na pia hakuna tatizo kwenye dua,

kwa tahadhari ya wajibu asiombe dua ila kwa kiarabu.

793. Hakuna tatizo katika kurudiarudia sehemu katika suratul - Hamdu au

sura au mengineyo miongoni mwa dhikri za swala mara nyingi kwa

tahadhari, pia hakuna tatizo akirudia rudia bila ya kukusudia au

kutenganisha, lakini akirudia rudia kitu kwa sababu ya wasiwasi

swala yake itaharibika kwa tahadhari

SALAMU KATIKA SWALA

794. Mwenye kuswali hatakiwi amsalimie yeyote lakini anaposalimiwa

ni wajibu arudishe salamu kama alivyosalimiwa , yaani arudishe

salamu kwa matamshi yale yale, mfano akiambiwa “Asalam

Alaykum” mwenye kuswali arudishe salamu kwa kusema “ Asalamu

Alaikum” lakini akisema “Alaikum Salam” kwa tahadhar aseme

“Asalam Alaykum”

153

Al-Masailul Islamiyah

Page 168: al-Masailu-l-Islamiyyah

795. Ni wajibu kurudisha salamu haraka katika swala au nje ya swala, na

akichelewa k`urudisha salamu kwa kukusudia au kwa kusahau kwa

muda kiasi kwamba akirudisha salamu haitahesabika kuwa ni

jawabu la ile salamu akiwa katika swala asirudishe salamu na akiwa

nje ya swala si wajibu kurudisha salamu.

796. Si wajibu alete jawabu la salamu kwa nia ya dua kwa kunuia kwa

kauli yake “Assalam alaikum” kuomba amani kutoka kwa Mwenyezi

Mungu kwa yule aliyemsalimia lakini inajuzu alete kwa kusudio la

kurudisha salamu.

797. Mwanamke akimsalimia mwanaume ajinabi katika swala au

mwanaume akimsalimia mwanamke ajinabiya katika swala au ikiwa

mwenye kusalimia ni mtoto wa kiume aliyepevuka, inajuzu kwa

mwenye kuswali bali ni wajibu wake arudishe salamu.

798. Mwenye kuswali asiporudisha salamu atakuwa ameasi na amepata

dhambi lakini swala yake inasihi.

799. Mtu akimsalimia mwenye kuswali kwa kukosea maneno kama ita-

hesabika kuwa ni salamu au kama atakosea katika matamshi yake

ni wajibu arudishe salamu na isipohesabika kuwa ni salamu si

wajibu kurudisha, bali haijuzu kurudisha salamu ndani ya swala.

800. Si wajibu kuitikia salamu kwa anayesalimia kwa mzaha au kejeli pia

haijuzu kumwitikia katika swala.

801. Mtu akisalimia kundi la watu ni wajibu kwa watu wale kuitikia sala-

mu, pia inatosha akiitikia mmoja wao.

802. Mtu anaposalimia watu na akaitikia asiyekusudiwa kurudisha salamu

haitaporomoka kwa waliokusudiwa bali ni wajibu wao kurudisha

salamu.

154

Al-Masailul Islamiyah

Page 169: al-Masailu-l-Islamiyyah

803.Mtu anaposalimia watu na mwenye kuswali akaitilia shaka kuwa

msalimiaji alimkusudia yeye au hakumkusudia, haijuzu kwa mwenye

kuswali kurudisha salamu, na pia akitambua kuwa msalimiaji

alimkusudia lakini wakajibu wengine inatosha, na akitambua kuwa

msalimiaji alimkusudia yeye halafu hakujibu hata mmoja ni lazima

yeye arudishe salamu.

804.Kuanza kusalimia ni sunna na imetiliwa mkazo kuwa mwenye kipan-

do aanze kumsalimia asiye na kipando, aliyesimama kwa aliyekaa na

mdogo amsalimie mkubwa ama kuitikia salamu ni wajibu.

805. Zikigongana salamu za watu wawili kwa tahadhari kila mmoja

aitikie salamu ya mwingine.

806. Ni sunna kurudisha salamu kwa iliyobora zaidi nje ya swala, mfano

mtu akisema “salam Alaykum” ajibu kwa kusema “salam alaikum

warahmatu llaahi”

YA SABA

807. Cha saba katika vinavyobatilisha swala ni kucheka kwa sauti, kwa

kukusudia au kwa dharura, ama akicheka kwa kusahau hakuna tatizo

katika swala, isipokuwa asitoke katika sura ya swala, ama

kutabasamu haibatilishi swala.

808. Ikibadilika hali yake kwa ajili ya kujizuia kudhihirisha sauti ya

kicheko mfano, rangi yake kuwa nyekundu kwa tahadhari ya sunna

arudie swala yake, lakini akitoka katika sura ya swala hapo atawa-

jibika kurudia swala.

YA NANE

809. Cha nne katika vinavyobatilisha swala ni kukusudia kulia kwa sauti

kwa ajili ya mambo ya kidunia, kwa tahadhari ya wajibu asilie kwa

155

Al-Masailul Islamiyah

Page 170: al-Masailu-l-Islamiyyah

ajili mambo ya kidunia hata bila ya sauti lakini hakuna tatizo kulia

kwa ajili ya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu au kwa ajili ya

mambo ya akhera kwa sauti ya juu au ya chini bali hili ni katika

vitu vizuri na pia inajuzu kwa dhahiri kulia kwa misiba ya Mtume

na watu wa nyumbani kwake “as.”

YA TISA

810. Cha tisa katika vinavyobatilisha swala ni kufanya kitendo kina-

chofuta sura ya swala kama kupiga makofi sana au kuruka sana

n.k. kwa kukusudia au kusahau lakini hakuna tatizo kufanya kitu

kisichofuta sura ya swala kama kuashiria kwa mkono.

811. Akinyamaza kwa muda mrefu kwenye swala kiasi kwamba haise-

mekani kuwa anaswali swala yake inabatilika.

812. Akileta kitendo katika swala au akinyamaza kwa muda, akitilia

shaka kuwa imefutika sura ya swala au laa swala yake inasihi.

YA KUMI

813. Kumi katika vinavyobatilisha swala ni kula na kunywa, akila au kun-

ywa katika swala kiasi kwamba haisemekani kuwa anaswali swala

yake inabatilika kwa kukusudia au kwa kusahau.

814. Anayetaka kufunga ikiwa anajishughulisha na swala ya witiri kabla

ya adhana ya alfajiri na akawa na kiu na akahofia kuingia Al fajiri

kama atakamilisha swala ya witiri na atabanwa na kiu inaruhusiwa

anywe maji katika swala kama maji yatakuwa mbele yake au karibu

kwa hatua chache na ajihadhari na vinavyobatilisha swala kama vile

kukipa kibla mgongo na mengineyo.

156

Al-Masailul Islamiyah

Page 171: al-Masailu-l-Islamiyyah

815. Akimeza mabaki ya chakula yaliyokuwepo katika meno au

mdomoni haibatiliki swala. Ikibaki sukari na yanayofanana na

sukari mdomoni kisha yakayeyuka katika swala kidogo kidogo na

kuingia tumboni pia swala haibatiliki

YA KUMI NA MOJA

816. Cha kumi na moja katika vinavyobatilisha swala ni kutilia shaka

katika swala za rakaa mbili, tatu au katika rakaa mbili za awali kati-

ka swala za rakaa mbili

YA KUMI NA MBILI

817. Cha kumi na mbili katika vinavyobatilisha swala ni kupunguza au

kuongeza nguzo miongoni mwa nguzo za swala na pia kuongeza au

kupunguza kwa kukusudia visivyokuwa nguzo lakini ziada ya takbi-

ratul ihram kwa kusahau haibatilishi swala.

818. Akitilia mashaka baada ya kumaliza swala kuwa ameleta kina-

chobatilisha swala au laa swala yake inasihi.

YALIYO MAKURUHU KATIKA SWALA

819. Ni makuruhu kugeuza uso wake kulia na kushoto au kufumba macho

au kugeuza macho kulia na kushoto au kuchezea ndevu au mikono

au kuliza (kubinya au kuvunja) vidole au kutema mate au kuangalia

hati ya Qur’an au kitabu au maandishi ya pete katika swala, vile vile

kunyamaza katikati ya kusoma Al – hamdu au sura nyingine au

kunyamza kwa ajili ya kusikiliza maneno ya mtu, bali ni makuruhu

kuleta chochote kinachotoa unyenyekevu na umakini unaotakiwa

katika swala.

157

Al-Masailul Islamiyah

Page 172: al-Masailu-l-Islamiyyah

820. Ni makuruhu kuswali wakati umebanwa na usingizi au mkojo au haja

kubwa na pia kuvaa soksi zinazobana miguu katika swala.

SEHEMU AMBAZO NI WAJIBU

KUKATA SWALA

821. Haijuzu kukata swala kwa hiyari, lakini hakuna kizuizi kukata swala

kwa ajili ya kuhifadhi mali au kuondoa madhara ya kimali na

kimwili.

822. Kama haiwezekani kwa mwenye kuswali kuhifadhi nafsi yake au

kuhifadhi ambao anawajibika kuwahifadhi, au kuhifadhi mali

ambayo ni wajibu kuihifadhi bila ya kukata swala, na pia ni maku-

ruhu kukata swala kwa kuhifadhi mali isiyokuwa na muhimu.

823. Akijishughulisha na swala katika muda mpana kisha akadaiwa na

anayemdai, ikiwezekana kulipa deni bila ya kukata swala alipe hali

ya kuwa katika swala, na kama haitawezekana kulipa deni bila ya

kukata swala, basi ni wajibu akate swala ili alipe deni, na kama

hatakata swala, swala yake itasihi japo kuwa atakuwa ameasi, kwa

kutokulipa deni.

824. Akifahamu katikati ya swala kunajisika msikiti, kama wakati wa

swala ni mfinyu ni wajibu akamilishe swala, na kama wakati ni

mpana ikiwezekana kutoharisha msikiti italazimu kuvunja swala, na

ikiwezekana kutoharisha msikiti baada ya swala basi haitaruhusiwa

kukata swala, na ikiwa kubakia najisi msikitini kunasabisha udhalili

kwa msikiti katika sura hii ni wajibu kukata swala ili atoharishe msik-

iti, kisha aswali na pia ni wajibu kukata swala kama haitawezekana

kutoharisha msikiti baada ya swala.

158

Al-Masailul Islamiyah

Page 173: al-Masailu-l-Islamiyyah

825. Mwenye kuwajibikiwa kukata swala kisha akaacha kukata na

akakamilisha atakuwa ameasi japokuwa swala yake itasihi.

826. Akikumbuka kabla ya kuinama kwa kiasi cha rukuu kuwa amesa-

hau adhana na iqama kama wakati utamruhusu ni sunna akate swala

kwa ajili ya kuleta adhana na iqama.

SHAKA

827. Shaka za swala zimegawanyika katika mafungu 23 nane kati ya hizo

zinabatilisha swala na sita ni wajibu zisizingatiwe na tisa hazibatilishi

swala.

828. Shaka zinazobatilisha swala ni kama zifuatazo:-

Shaka ya idadi ya rakaa katika swala za rakaa mbili kama swala ya asub-

uhi au swala ya msafiri lakini akitilia shaka katika idadi ya rakaa katika

swala za sunna zenye rakaa mbili na swala ya ihtiyati swala haibatiliki

kwa sababu yake.

Shaka katika idadi ya rakaa katika swala yenye rakaa 3

Akishuku katika swala ya rakaa nne kuwa ameswali rakaa moja au zaidi

Akishuku katika swala ya rakaa nne kabla ya kukamilisha sijida ya pili

kuwa ameswali rakaa mbili au zaidi.

Shaka baina ya rakaa mbili au tano au rakaa mbili au zaidi ya tano.

Shaka baina ya tatu na sita au tatu na zaidi ya sita .

Shaka katika idadi ya rakaa kiasi kwamba hajui rakaa ngapi ameswali.

Shaka baina ya rakaa nne na sita au baina ya rakaa nne na zaidi ya sita

kabla ya kukamilisha sijida ya pili lakini kama akishuku baada ya sijida

159

Al-Masailul Islamiyah

Page 174: al-Masailu-l-Islamiyyah

ya pili baina ya nne na sita au baina ya nne na zaidi ya sita kwa tahadhari

ajengee kuwa ameswali rakaa nne kisha akamilishe swala, baada ya hapo

alete sijida mbili za kusahau baada ya swala na pia arudie swala.

829. Mwenye kuswali akitokewa na moja ya shaka zinazobatilisha swala

inaruhusiwa kukata swala au afikirie mpaka sura ya swala ifutike na

akate tamaa ya kupata uhakika wa rakaa alizoziswali.

SHAKA ZISIZOTILIWA MAANANI

830. Shaka ambazo ni wajibu zisizingatiwe na wala zisitiliwe maanani ni

kama zifuatazo:-

Shaka ya kitu baada ya kupita sehemu yake mfano apate shaka katika

rukuu kuwa amesoma Al – hamdu au laa.

Shaka baada ya salamu

Shaka baada ya kupita muda wa swala

Mwingi wa shaka

Shaka ya Imam katika idadi ya rakaa wakikumbuka maamuma katika idadi

ya rakaa, na vile vile shaka ya maamuma kama Imam akikumbuka idadi ya

rakaa.

Shaka katika swala za sunna.

1 – SHAKA YA KITU BAADA YA KUPITA

SEHEMU YAKE

831. Akishuku katikati ya swala kuwa ameleta baadhi ya vitu

vilivyokuwa ni wajibu au hakuvileta mfano – akitilia shaka kuwa

amesoma Al – hamdu au laa, kama hajajishughulisha na yanayokuja

160

Al-Masailul Islamiyah

Page 175: al-Masailu-l-Islamiyyah

baada ya Al hamdu au baada ya alichokuwa akikishuku basi asizin-

gatie shaka yake.

832. Akitilia shaka katikati ya kusoma aya kuwa amesoma aya iliyopita au

laa au akitilia shaka katika aya anayoisoma kuwa amesoma mwanzo

wa aya au laa asizingatie shaka yake.

833. Akitilia shaka baada ya kurukuu na kusujudu kuwa ameleta baadhi ya

mambo ya wajibu katika swala kama vile dhikri, utulivu wa mwili au

laa, asizingatie shaka yake.

834. Akitilia shaka wakati anakwenda katika sijida kuwa ameleta rukuu

au laa au alisimama wima baada ya rukuu au laa asizingatie shaka

yake.

835. Akitilia shaka katika hali ya kunyanyuka kuwa ameleta sijida au

tashahudi au laa, asizingatie shaka yake.

836. Mwenye kuswali kwa kukaa au kulala akitilia shaka katikati ya

kusoma Al- hamdu au tasbihi nne kuwa ameleta tashahudi au sijida

au laa ni wajibu asizingatie shaka yake.

837. Kama akishuka katika kuleta sijida au tashahudi kabla ya kusoma

Al – hamdu au tasbihi, lazima alete alicho kitilia shaka.

838. Akishuku katika kutekeleza moja ya nguzo za swala kama atakuwa

ameshapita hiyo sehemu aliyoishuku basi asizingatie shaka yake,

kinyume na hapo kama alichotilia shaka atakumbuka baadae kuwa

alishaleta nguzo ya swala, basi swala yake itabatilika kwa kuongeza

nguzo ya ziada.

839. Akishuku katika kutekeleza kitu kisichokuwa ni nguzo kama atakuwa

amepita hiyo sehemu asizingatie hiyo shaka la sivyo ataleta alichoki-

161

Al-Masailul Islamiyah

Page 176: al-Masailu-l-Islamiyyah

tilia shaka, akikumbuka baada ya kuisoma kuwa alishaisoma kabla ya

hapo swala yake inasihi, kwa kutozidisha nguzo, na ataleta sijida

mbili za kusahau kwa tahadhari ya wajibu.

840. Akishuku katika kuleta moja ya nguzo za swala, kama amejishughul-

isha na ambacho kinafuata baada ya nguzo hiyo asizingatie shaka

yake mfano akitilia shaka katikati ya tashahudu kuwa ameleta sijida

mbili au laa, asizingatie shaka yake, ama akikumbuka kuwa hakule-

ta hiyo nguzo aliyoisahahu na kama atajishughulisha na nguzo

nyingine swala yake itakuwa imebatilika mfano akikumbuka kabla ya

kurukuu katika rakaa ifuatayo kuwa hajaleta sijida mbili katika rakaa

iliyopita basi alete hizo sijida mbili, na kama atakumbuka katikati ya

rukuu au baada ya rukuu swala yake inabatilika.

841. Akitilia shaka katika kutekeleza jambo ambalo si nguzo katika

matendo ya swala, na akajishughulisha na kitendo kifuatacho baada

ya hicho ni wajibu asizingatie shaka yake kwa mfano akitilia shaka

katika kusoma sura kuwa amesoma Al – hamdu au laa, ni wajibu

asizingatie shaka yake ama akikumbuka kuwa hakuleta kile kitendo

kabisa kama hajajishughulisha na kitendo ambacho ni nguzo ni

wajibu alete kitendo hicho alichokisahau, na kama atajishughulisha

na nguzo swala yake inasihi, kwa hiyo akikumbuka akiwa katika

kunuti kuwa hakusoma Al – hamduu ni wajibu asome Al – hamdu na

akikumbuka katika hali ya rukuu swala yake inasihi.

842. Akishuku kuwa ametoa salamu ya swala au laa, au akishuku kuwa

ameileta kwa usahihi au laa, kama shaka hizo mbili ni baada ya

kujishughulisha na nyuradi zinazofuatia baada swala kama vile dua au

kuanza swala nyingine, au baada ya kuleta kinachovunja swala na

kutoka katika hali ya mwenye kuswali au akawa anajiona kuwa hali

yake iko nje ya swala, basi asizingatie shaka yake ama shaka yake

ikiwa kabla ya vitu hivi ni wajibu atoe salamu upya.

162

Al-Masailul Islamiyah

Page 177: al-Masailu-l-Islamiyyah

2 SHAKA BAADA YA SALAMU

843. Akishuku baada ya salamu kuwa swala yake imesihi au laa, mfano

akitilia shaka kuwa amerukuu baada ya salamu, au akashuku baada ya

salamu katika swala ya rakaa nne kuwa ameswali rakaa nne au tano

asizingatie shaka yake, lakini ikiwa pande mbili hizi za shaka zin-

abatilisha swala mfano akishuku baada ya salamu katika swala ya

rakaa nne kuwa ameswali rakaa mbili au tano swala yake inabatilika.

3. SHAKA BAADA YA KUPITA WAKATI

844. Akishuku baada ya kupita muda kuwa ameswali au laa, akidhani

kuwa hakuswali kabisa, haimlazimu kuswali lakini akitilia shaka

kabla ya wakati kwisha kuwa ameswali au laa au akidhani kuwa

hakuswali kabisa ni wajibu aswali hata akidhani kuwa ameswali.

845. Akishuku baada ya kupita wakati kuwa ameswali kwa usahihi au laa

asizingatie shaka yake.

846. Akitambua baada ya kupita wakati wa adhuhuri na alasiri kuwa

ameswali rakaa nne tu, na hatambui kuwa ameziswali kwa nia gani ya

adhuhuri au alasiri ni wajibu aswali rakaa nne zingine za kadha kwa

nia ya yanayomuwajibikia.

847. Akitambua baada ya kupita wakati wa swala ya Magharibi na Isha

kuwa ameswali moja wapo kati ya swala hizi na hajui ameswali

rakaa tatu au nne ni wajibu alipe kadha ya Magharibi na Isha pamo-

ja.

4- MWINGI WA SHAKA

848. Mtu akishuku mara tatu katika swala moja au akishuku katika swala

tatu zinazofuatana kwa mfano asubuhi, adhuhuri na alasiri atahesabi-

163

Al-Masailul Islamiyah

Page 178: al-Masailu-l-Islamiyyah

ka kuwa ni mwingi wa shaka kwa hiyo haimlazimu kuzingatia shaka

yake kama wingi wa shaka zake unasababishwa na hasira, woga au

fikra nyingi.

849. Mwingi wa shaka akishuku katika kutekeleza jambo ikiwa jambo hilo

halibatilishi swala atajengea kuwa ametekeleza, mfano akishuku

kuwa amerukuu au laa atajengea kuwa amerukuu, na kama ikiwa

kutekeleza hilo jambo linabatilisha swala basi inabidi ajengee kuwa

hajafanya, mfano akishuku kuwa ameleta rukuu moja au zaidi ya

moja,anajengea kuwa hajaleta zaidi ya moja kwa sababu ziada ya

rukuu inabatilisha swala.

850. Mwingi wa shaka akishuku katika sehemu moja tu katika swala,

akishuku katika sehemu nyingine nje ya ile inatakiwa afanye kama

afanyavyo mwingi wa shaka, mfano akiwa mwingi wa shaka katika

sijida, kuwa amesujudu au laa, na akatilia shaka katika rukuu lazima

afanye kama anavyofanya mwingi wa shaka yaani atarukuu kama

alikuwa amesimama na hatazingatia shaka yake kama itakuwa baada

ya kwenda sijida.

851. Mwingi wa shaka akishuku katika swala maalumu pasina zingine

mfano akiwa anakithirisha shaka katika swala ya adhuhuri pasina

zingine na akishuku kwenye swala zingine kama swala ya alasiri kwa

mfano mwisho wa swala atafanya kama anavyofanya mwenye shaka

ya kawaida.

852. Mwingi wa shaka akishuku katika swala katika sehemu maalumu

pasina sehemu nyingine kama vile sehemu yenye makelele akiswali

sehemu nyingine ikamtokea shaka ni wajibu afanye kama afanyavyo

mwenye shaka ya kawaida.

853. Mwenye kushuku kwa sababu ni mwingi wa shaka ni wajibu afanye

kama afanyavyo mwenye shaka ya kawaida na mwingi wa shaka

164

Al-Masailul Islamiyah

Page 179: al-Masailu-l-Islamiyyah

asizingatie shaka yake maadamu hana uhakika wa kurudi katika hali

ya watu wa kawaida

954. Mwenye kushuku katika nguzo miongoni mwa nguzo za swala kisha

akawa hajazingatia shaka yake, kisha akakumbuka kuwa hakuileta ile

nguzo kama hajajishughulisha na nguzo nyingine ni wajibu alete

nguzo aliyoisahau, na ikiwa ameanza kujishughulisha na nguzo

nyingine swala itakuwa imebatilika, mfano akishuku kuwa amerukuu

au laa, akawa hajazingatia shaka yake, akikumbuka kabla ya sijida

kuwa haja rukuu, ni wajibu alete rukuu aliyoisahau ama akikumbuka

katika sijida ya pili swala yake inabatilika.

855. Mwingi wa shaka akishuku katika kuleta kisichokuwa nguzo na

akawa hajazingatia shaka yake, akikumbuka kuwa hajaleta kabisa kile

alichokuwa anakishuku, kama atakuwa hajapita hiyo sehemu lazima

akilete na kama atakuwa amepita hiyo sehemu swala yake inasihi,

mfano akishuku kuwa amesoma Al- hamdu au laa kisha akawa

hajazingatia shaka yake akikumbuka katika kunuti kuwa hajasoma Al

– hamdu ni wajibu asome Al – hamdu na akikumbuka katika rukuu

swala yake inasihi.

5- SHAKA YA IMAMU NA MAAMUMA

856. Imamu akishuku katika swala ya jamaa katika idadi ya rakaa mfano

akishuku kuwa ameswali rakaa tatu au nne, ikiwa maamuma

wanauhakika kuwa ameswali rakaa nne na wakamfahamisha Imamu

kuwa ameswali raka nne inamlazimu Imamu akamilishe swala, na

haitamlazimu kuswali swala ya ihityati, vile vile Imamu akiwa na

uhakika katika idadi maalumu za rakaa na maamuma akishuku katika

idadi ya rakaa ni lazima kwa maamuma asizingatie shaka yake.

6- SHAKA KATIKA SWALA YA SUNNA

857. Akishuku katika swala za sunna, ikiwa upande wa wingi wa shaka

165

Al-Masailul Islamiyah

Page 180: al-Masailu-l-Islamiyyah

unabatilisha swala atajengea katika uchache mfano ikimtokea shaka

katika sunna ya asubuhi kuwa ameswali rakaa mbili au tatu itamlaz-

imu ajengee kuwa ameswali rakaa mbili na ikiwa upande wa wingi

wa shaka haubatilishi swala, mfano akishuku kuwa ameswali rakaa

mbili au moja atafanya njia yoyote anayotaka yaani anaweza

kujengea kuwa ameswali rakaa mbili na kukamilisha swala au kujen-

gaea kuwa ameswali rakaa moja na kumalizia rakaa ya pili na swala

inasihi.

858. Upungufu wa nguzo unabatilisha swala ya sunna lakini ziada yake

haibatilishi swala, akisahau moja ya vitendo vya swala ya sunna na

hakukumbuka ila baada ya kuingia katika nguzo, atakuwa na haki ya

kuleta alichokisahau na kurudia ile nguzo mara nyingine mfano

akikumbuka katika rukuu kuwa hakusoma Al- hamdu na akawa ames-

imama wima basi utambidi asome Al- hamdu na kurukuu mara ya pili.

859. Akishuku katika kuleta moja ya matendo ya swala ya sunna iwe ni

katika nguzo au isiyokuwa nguzo itatakiwa alete alichokishuku,

maadamu hajapita sehemu yake na asizingatie shaka yake kama

atakuwa amepita hiyo sehemu.

860. Akidhani katika sunna ya rakaa mbili kuwa ameleta rakaa tatu au

zaidi ya tatu asizingatie dhana yake na swala itasihi na kama atadhani

kuwa ameleta rakaa mbili au chini ya mbili kwa tahadhari ya sunna

atafanya kutokana na dhana yake mfano akidhani kuwa ameswali

rakaa moja basi atakamilisha swala yake kwa kumalizia rakaa ya pili.

861. Akifanya katika swala ya sunna ambayo yanasababisha sijida ya

kusahahu au akisahau sijida au tashahudu, haitamlazimu baada ya

swala alete sijida sahau au kuleta kadha ya sijida iliyosahaulika au

tashahudi iliyosahaulika, na ingawa kwa tahadhari alete alichokisa-

hahu baada ya swala.

166

Al-Masailul Islamiyah

Page 181: al-Masailu-l-Islamiyyah

862. Akishuku kuwa ameswali swala ya sunna au laa kama swala hiyo

haitakuwa ya muda maalum kama swala ya “Jafari Twayaar” ata-

jengea kuwa hajaswali na vile vile atajengea kuwa hajaswali akitia

shaka katika swala za sunna za kila siku ambazo zinakuwa na muda

maalumu na ikiwa shaka yake ni kabla ya kupita muda na kama aki-

tilia shaka baada ya muda kupita basi hatazingatia shaka yake.

7. SHAKA ZISIZOBATILISHA SWALA

863. Ni wajibu kwa mwenye kuswali kutafakari haraka akishuku katika

idadi ya rakaa katika swala za rakaa nne na hiyo ni katika sura tisa, na

kama fikra yake itampelekea kupata yakini au dhana katika moja ya

pande mbili basi itabidi achukue ambayo inampelekea kupata yakini

au dhana yake katika upande huo na kukamilisha swala, na kama

mawazo yake na fikira zake hazitampa jawabu maalum basi atafanya

kutokana na kanuni ambazo ufafanuzi wake utakuja baadae

SURA YA KWANZA

864. Akishuku baada ya kunyanyua kichwa katika sijida ya pili kuwa

ameswali rakaa mbili au tatu katika sura hii ni wajibu ajengee kuwa

ameswali rakaa tatu, atasimama na kuleta rakaa nyingine na kukamil-

isha swala kisha ataleta baada ya swala rakaa moja ya swala ya ihtiy-

ati kwa kusimama na rakaa mbili kwa kukaa vilevile kama

utakavyokuja ufafanuzi wake baadaye

SURA YA PILI

865. Akishuku kati ya rakaa mbili au nne baada ya kunyanyua kichwa kati-

ka sijida ya pili hapo ni wajibu ajengee kuwa ameswali rakaa nne na

kukamilisha swala akiwa amekaa kisha ataleta rakaa mbili za swala ya

ihtiyati baada ya swala kwa kusimama kwa tahadhari

167

Al-Masailul Islamiyah

Page 182: al-Masailu-l-Islamiyyah

SURA YA TATU

866. Akishuku kati ya rakaa mbili, tatu na nne baada ya sijida ya pili yaani

hajui kuwa ameswali rakaa mbili, tatu au nne katika hali hii atajengea

kuwa ameswali rakaa nne na atakamilisha swala hali ya kuwa amekaa

kisha ataleta rakaa mbili za swala za ihtiyati kwa kusimama na rakaa

mbili kwa kukaa pia.

SURA YA NNE

867. Akishuku kati ya rakaa nne na tano baada ya kunyanyua kichwa

katika sijida ya pili, atajengea kuwa ameswali rakaa nne na kukamil-

isha swala hali ya kuwa amekaa na ataleta sijida mbili za kusahau

baada ya swala.

868. Ikitokea moja ya shaka hizi nne baada ya kuleta dhikri katika sijida

ya pili kabla ya kunyanyua kichwa katika sijida ya pili, basi atafanya

kutokana na hukumu za shaka zilizotajwa na atarudia swala kwa

tahadhari ya sunna na kama atarudia swala tu inatosha.

SURA YA TANO

869. Akishuku kati ya rakaa tatu na nne katika sehemu yeyote ya swala,

lazima ajengee kuwa ameswali rakaa nne na akamilishe swala, kisha

alete rakaa moja ya ihtiyati kwa kusimama au rakaa mbili kwa kukaa

kwa tahadhari

SURA YA SITA

870. Akishuku kati ya rakaa nne na tano akiwa katika hali ya kusimama,

lazima akae na atoe tashahudi na salamu na kukamilisha swala, kisha

ataleta rakaa moja ya ihtiyati kwa kusimama au mbili kwa kukaa na

kwa tahadhari ya wajibu alete sijida mbili za kusahau kwa ajili ya

kisimamo cha ziada.

168

Al-Masailul Islamiyah

Page 183: al-Masailu-l-Islamiyyah

SURA YA SABA

871. Akishuku kati ya rakaa tatu au tano katika hali ya kusimama itamlaz-

imu akae na atoe tashahudi na salamu na kukamilisha swala kisha

alete rakaa mbili za ihtiyati kwa kusimama kwa tahadhari na kuleta

sijida mbili za kusahau kwa ajili ya kisimamo cha ziada kwa tahad-

hari ya wajibu.

SURA YA NANE

872. Akishuku kati ya rakaa tatu, nne na tano katika hali ya kisimamo ita-

mlazimu akae na atoe tashahudi na salamu na ataleta baada ya salamu

sijida mbili za kusahau na kwa tahadhari ya wajibu alete sijida zingine

za kusahau kwa ajili ya kisimamo cha ziada.

SURA YA TISA

873. Akishuku kati ya rakaa tano na sita katika hali ya kisimamo itamlaz-

imu akae na alete tashahudi na salamu na ataleta baada ya salamu siji-

da mbili za kusahau na kwa tahadhari ya wajibu alete sijida zingine

mbili za kusahau kwa ajili ya kisimamo cha ziada

MAS’ALA MENGINE

874. Mwenye kuswali ikimtokea shaka isiyobatilisha swala itamlazimu

asikate swala kwa tahadhari, ama akianza swala nyingine baada ya

kuvunja ya mwanzo basi swala yake ya pili itasihi.

875. Ikimtokea moja ya shaka zinazosababisha swala ya ihtiyati,

akikamilisha swala yake na akianza swala nyingine bila ya kuleta

169

Al-Masailul Islamiyah

Page 184: al-Masailu-l-Islamiyyah

swala ya ihtiyati na akawa ameanza swala mpya kabla ya kuleta

kinachobatilisha swala, kama kugeuza uso pembeni mwa kibla,

swala yake ya pili itabatilika pia kwa tahadhari, ama akijishughulisha

na swala ya pili baada ya kuleta kinachobatilisha swala ya kwanza

swala ya pili itasihi.

876. Inapomtokea mwenye kuswali moja ya shaka zisizobatilisha swala ni

wajibu atulie na kufikiria kwa haraka kama ilivyotangulia, lakini aki-

tambua kuwa hatasahau kitu kwa kuchelewa kidogo inajuzu kwake

kufikiri kidogo baadae, mfano akishuku naye yuko katika sijida ina-

juzu kuahirisha kufikiria hadi baada ya sijida.

877. Dhana yake ikielemea moja kati ya pande mbili za shaka katika jambo

moja, kisha dhana yake ikalingana katika pande zote mbili kwa

mtazamo wake, ni wajibu afanye kulingana na hukumu za shaka na

pande zote mbili zikilingana kwa mtizamo wake tangu mwanzo basi

atajengea kutokana na kuelemea kwa moja ya dhana yake, na ni

wajibu afanye kilichowajibu kwake, lakini dhana yake ikielemea

moja ya pande mbili ni wajibu achukue upande ambao swala yake

itasihi na kukamilisha swala.

878. Ambaye hajui kuwa dhana yake imeelemea upande mmoja au pande

zote mbili, ni wajibu afanye kulingana na hukumu za shaka.

879. Akishuku katika tashahudi au baada ya kunyanyuka kuwa ameleta

sijida mbili au laa, kisha ikamtokea hapo hapo shaka isiyobatilisha

swala, ikitokea baada ya kukamilisha sijida mbili, mfano akishuku

kuwa ameswali rakaa mbili au tatu atafanya kulingana na wadhifa

tulioutaja na swala yake itasihi.

880. Akishuku katika hali ya kusimama kati ya rakaa tatu na nne au baina

ya rakaa tatu, nne na tano, na akakumbuka kuwa hajaleta sijida mbili

katika rakaa iliyopita swala yake inabatilika.

170

Al-Masailul Islamiyah

Page 185: al-Masailu-l-Islamiyyah

881. Ikiondoka shaka yake kisha ikamtokea shaka nyingine, mfano mwan-

zo alishuku kati ya rakaa mbili na tatu kisha akashuku mara ya pili

baina ya tatu na nne, atafanya kulingana na shaka yake ya pili.

882. Akishuku baada ya swala kuwa ameshuku kati ya rakaa mbili au nne

au kati ya tatu na nne ni wajibu afanye kwa shaka zote mbili.

883. Mwenye kuswali kwa kukaa akiweza kusimama katika kuleta swala

ya ihtiyati ni wajibu ailete kwa kusimama.

SWALA YA IHTIYATI

884. Ambaye amewajibikiwa na swala ya ihtiyati ni wajibu anuie kwa

haraka baada ya kumaliza swala, atahirimia na kusoma Al – hamdu tu

atarukuu na kuleta sijida mbili na akiwa katika wale waliowajibiki-

wa na rakaa moja ya ihtiyati ataleta tashahudi baada ya sijida mbili

na kutoa salamu, ama aliyewajibikiwa na rakaa mbili za ihtiyati atasi-

mama baada ya sijida mbili na kuswali rakaa ya pili, kisha ataleta

tashahud na kutoa salamu.

885. Katika swala ya ihtiyati hakuna sura wala kunut na lazima asidhi-

hirishe sauti wakati wa kusoam Al- hamdu wala asidhihirishe nia yake

na kwa tahadhari asidhihirishe hata bismillah pia.

886. Akitambua kabla ya swala ya ihtiyati kuwa swala yake ilikuwa sahi-

hi haimlazimu kuleta swala ya ihtiyati na akitambua hivyo katikati ya

swala ya ihtiyati haimlazimu kuikamilisha, bali inajuzu kuikatisha

popote alipo.

887. Akishuku kati ya rakaa mbili, tatu na nne katika hali ya kuleta rakaa

mbili za ihtiyati katika hali ya kusimama kabla ya kurukuu katika

rakaa ya pili kwamba swala yake ilikuwa ni rakaa tatu lazima akae na

kukamilisha swala ya ihtiyati rakaa moja.

171

Al-Masailul Islamiyah

Page 186: al-Masailu-l-Islamiyyah

888. Akishuku kuwa ameleta swala ya ihtiyati ambayo alitakiwa aswali au

laa, ikiwa ni baada ya wakati hatazingatia shaka yake, na kama wakati

bado upo na hakujishughulisha na kitu kingine na hajasimama sehe-

mu aliyokuwa anaswalia, na hakuleta kinachobatilisha swala itamlaz-

imu alete swala ya ihtiyat,i na kama ameleta kinachobatilisha au ame-

tenganisha kati ya swala aliyoiswali na shaka hiyo muda mrefu

hatazingatia shaka yake.

889. Akizidisha nguzo katika swala ya ihtiyati au akileta rakaa mbili

badala ya rakaa moja, swala yake ya ihtiyati inabatilika na ni wajibu

kurudia swala upya.

890. Hukumu ya dhana katika idadi ya rakaa ni hukumu ya yakini, ila

dhana ikiwa ni ya kitu kinachosababisha kubatilisha swala katika hali

hii, dhana haitakuwa na hukumu ya yakini, ama dhana katika vitendo

vya swala ingawa haiko mbali na kuiunganisha na yakini, lakini

pamoja na hivyo inalazimu kwa tahadhari ya sunna baada ya kuizin-

gatia dhana akamilishe amali na arudie swala

891. Hakuna tofauti katika hukumu ya shaka, kusahau na kudhani katika

swala za kila siku na swala zingine za wajibu, mfano akishuku katika

swala za majanga kuwa ameleta rakaa moja au mbili, kwa kuwa

swala ya majanga ina rakaa mbili hivyo shaka hiyo inabatilisha swala.

SIJIDA YA KUSAHAU

892. Ni wajibu kuleta sijida mbili za kusahau baada ya salamu kwa namna

ambayo ufafanuzi wake utakuja na hii ni kwa mambo matano:-

(i) Akizungumza katikati ya swala kwa kujisahau

(ii) Akitoa salamu sehemu isiyokuwa ya salamu, mfano akitoa

salamu katika rakaa ya kwanza kwa kujisahau

(iii) Akisahau moja ya sijida mbili

(iv) Akisahau tashahudi

172

Al-Masailul Islamiyah

Page 187: al-Masailu-l-Islamiyyah

(v) Akishuku baada ya sijida mbili katika swala ya rakaa nne

kuwa ameswali rakaa nne au tano.

893. Akikaa kwa kujisahau katika mahali pa kusimama, mfano akikaa kati-

ka hali ya kusoma Al-hamdu na sura kwa kukosea, au akasimama

katika mahali pa kukaa kama akisimama katika mahali pa tashahudi

kwa kujisahahu, itamlazimu kwa tahadhari ya wajibu alete sijida

mbili za kusahau, na kwa tahadhari ya wajibu alete sijida mbili za

kusahau katika kila ziada au upungufu.

Na hukumu za hali hizi zitatajwa katika mas’ala yajayo.

894. Mwenye kuswali akizungumza kwa kujisahau au akadhani kuwa

swala yake imekamilika, ni wajibu alete sijida mbili za kusahau.

895. Si wajibu kusujudu sijida ya kusahu kwa kutamka herufi ambayo

imesababishwa na kukohoa, kucheua na mengineyo, lakini akisema

Ah, au Akh, kwa kusahau ni wajibu alete sijida mbili za kusahau.

896. Mwenye kurudia kusoma vizuri kwa kukosea mara ya kwanza, haita-

mlazimu alete sijida ya kusahau kwa kukosea.

897. Akizungumza muda mrefu katika swala kwa kujisahau yatahesabika

maneno yake hayo kuwa ni neno moja inatosha alete sijida ya kusa-

hau baada ya swala.

898. Mwenye kuleta tasbihi nne zaidi ya mara tatu kwa kujisahau haitam-

lazimu alete sijida ya kusahau.

899. Akileta salamu nje ya sehemu ya salamu, mfano alete salamu tatu

zisizotajwa, inatosha alete sijida mbili za kusahau mara moja tu.

900. Asipoleta sijida mbili za kusahau baada ya salamu kwa kukusudia

173

Al-Masailul Islamiyah

Page 188: al-Masailu-l-Islamiyyah

atakuwa ameasi na atawajibika alete kwa haraka, na kama hataleta ni

lazima azilete wakati wowote atakapokumbuka na si lazima arudie

swala.

901. Akishuku kuwa imewajibika kwake sijida mbili za kusahau au laa,

haitamlazimu alete chochote.

902. Akitambua kuwa hakuleta moja ya sijida mbili za kusahau, itamlaz-

imu alete sijida zingine mbili za kusahau.

NAMNA YA KULETA SIJIDA YA KUSAHAU

903. Namna ya kusujudu sijida ya kusahau: Baada ya salamu anuie nia ya

sijida ya kusahau na kuweka paji la uso juu ya kinachosihi kusujudu

juu yake na kusema “Bismillah wa billah wa swala llahu alaa

Muhamadi wa aali Muhammad” au aseme “Bismillah wa billah

allahuma swali alaa muhamadi wa aali Muhamadi”. Na ni bora

aseme “Bismillah wabillah asalamu alayka ayuh nabiyu warahmatu

llah wabakatuh” Kisha anakaa kisha anasujudu tena na kusoma moja

ya dhikri hapo juu, atakaa na kuleta tashahudi na kutoa salamu moja.

KADHA YA SIJIDA AU TASHAHUDI ZILIZOSA-

HAULIKA

904. Ni sharti katika kadha ya sijida au tashahudi zilizosahaulika mambo

yote yanayoshurutishwa katika swala kama vile, tohara ya mwili na

mavazi na masharti mengineyo.

905. Akisahau sijida mara nyingi, mfano akisahau sijida katika rakaa ya

kwanza na sijida katika rakaa ya pili ni wajibu azilipe baada ya swala

174

Al-Masailul Islamiyah

Page 189: al-Masailu-l-Islamiyyah

ya pamoja na kuleta sijida mbili za kusahau kwa kila moja na hailazi-

mu kuainisha, ama akisahau sijida katika rakaa ya kwanza na ya mwi-

sho au akasahau tashahudi mbili, kwa tahadhari ya wajibu alete sijida

ya mwisho aliyoisahau kwanza, kisha analeta tashahudi na salamu na

baada ya hapo atalipa sijida ya kwanza, na vivyo hivyo itamlazimu

alete tashahudi iliyosahaulika mwisho na kutoa salamu, kisha atalipa

tashahudi ya kwanza, haya yote ni katika hali ya kutoleta kinachoba-

tilisha swala kwa kukusudia au kusahau, ama akileta kinachobatilisha

swala kwa kukusudia au kusahau ni lazima arudie swala.

906. Asipotambua kuwa amesahau tashahudi au sijida atawajibika kulipa

zote mbili pamoja, na hakuna tatizo kutanguliza moja kati ya hizi

mbili.

907. Akishuku kuwa amesahau tashahudi au sijida au laa, hatawajibika

kulipa kadha.

908. Akishuku kuwa baada ya swala alileta sijida au tashahudi zilizosa-

haulika au laa, ikiwa wakati bado upo itabidi arudie kulipa, na kama

wakati wa swala umeisha hatawajibika kuzilipa.

UPUNGUFU NA ZIADA KATIKA SEHEMU ZA

SWALA NA MASHARTI YAKE

909. Akizidisha au kupunguza katika wajibati za swala kwa kukusudia

swala yake inabatilika.

910. Akitambua katikati ya swala kuwa josho lake au udhu wake ulikuwa

batili au alijishughulisha na swala bila ya udhu au josho, swala yake

inabatilika, atairudia kwa udhu au josho, na akitambua baada ya swala

ni wajibu airudie kwa udhu au josho ikiwa wakati bado upo, na kama

175

Al-Masailul Islamiyah

Page 190: al-Masailu-l-Islamiyyah

wakati umekwisha ni lazima alipe kadha.

911. Akikumbuka kabla ya salamu kuwa amesahau rakaa katika mwisho

wa swala ni wajibu alete hiyo rakaa kwa haraka.

912. Akikumbuka baada ya salamu kuwa amesahau rakaa au zaidi ya

rakaa, akifanya kinachobatilisha swala kwa kusahau au kukusudia,

mfano kukipa kibla mgongo, swala yake inabatilika, na kama hajafa-

nya kinachobatilisha swala ni wajibu alete kwa haraka alichokisahau.

913. Akitambua kuwa ameswali kabla ya wakati au ameswali kwa kukipa

mgongo kibla au kuelekea kulia au kushoto mwa kibla ni wajibu aru-

die swala ndani ya wakati na kuilipa kama wakati umeisha

SWALA YA MSAFIRI

914. Ni wajibu kwa msafiri kupunguza katika swala za rakaa nne yaani

“Adhuhuri, Alasiri na Isha” na ataswali rakaa mbili badala ya rakaa

nne na hiyo ni pindi yakipatikana masharti nane yafuatayo:-

1. Masafa ya safari yawe ni farsakha nane ( kilometa 45)

2. Akusudie tangu mwanzo wa safari kukata farsakha nane

3. Asibadili nia yake

4. Asipitie katika mji wake, na asikusudie kukaa siku kumi

5. Asisafiri kwa ajili ya mambo ya haramu.

6. Asiwe ni katika watu wanaohamahama ambao hawatulii sehemu

moja.

7. Safari isiwe ndio kazi yake

8. Afike kwenye sehemu anayoruhusiwa kisheria kupunguza.

SHARTI LA KWANZA

176

Al-Masailul Islamiyah

Page 191: al-Masailu-l-Islamiyyah

915. Inatakiwa masafa anayosafiri yasipungue farsakha nane za kisheria na

farsakha moja ni sawa na kilometa tano na nusu takribani.

916. Mwenye kufikisha jumla ya masafa yake kwenda na kurudi farsakha

nane, akisafiri na kurudi siku hiyo hiyo, mfano akisafiri mchana aka-

rudi usiku wake, kama hayajapungua masafa ya kwenda farsakha nne

ni wajibu apunguze swala zake, lakini ikiwa kwenda ni farsakha tatu

na kurudi ni farsakha tano, dhahiri atapunguza swala zake, ingawa ni

kwa tahadhari ya sunna ni kukusanya baina ya kupunguza na kuka-

milisha.

917. Ikiwa safari yake kwenda na kurudi ni farsakha nane, na kama safari

yake haichukui siku kumi, kama akisafiri leo na akarudi kesho au

baada ya kesho au chini ya siku kumi ni wajibu apunguze swala zake

na asifunge bali atalipa kadha kama yuko katika mwezi wa

Ramadhani.

918. Ikiwa masafa hayajafika farsakha nane au msafiri hakujua kuwa safa-

ri yake inafika farsakha nane au haifiki hatapunguza swala zake. Ama

akishuku safari yake imefikia farsakha nane au haikufika, ni wajibu

wake afanye uchunguzi ili apate uhakika, na akipata habari kutoka

kwa waadilifu wawili au mmoja au inajulikana baina ya watu kiasi

cha kupata matumaini kuwa safari yake imefikisha farsakha nane

basi atapunguza swala zake.

919. Mwenye kupata uhakika kuwa safari yake imefika farsakha nane

kisha akapunguza swala zake, baada ya hapo akatambua kuwa safari

yake haikufikia farsakha nane, itamuwajibikia arudie swala za rakaa

nne ndani ya wakati au kadha kama wakati umepita.

920. Ikiwa safari ina njia mbili moja inafikisha farsakha nane na nyingine

haifikishi farsakha nane, akisafiri kwa ile njia inayofikisha farsakha

nane atapunguza swala, na kama atatumia njia ambayo haifikishi far-

sakha nane atakamilisha swala zake.

177

Al-Masailul Islamiyah

Page 192: al-Masailu-l-Islamiyyah

921. Ikiwa mji anaoishi una ukuta mwishoni mwa mji ni lazima aanze

kuhesabu masafa ya kisheria hapo, yaani farsakha nane kuanzia kwe-

nye ukuta wa mji, na kama hauna ukuta ni wajibu aanze kuhesabu

masafa ya kisheria mwisho wa nyumba za mji.

SHARTI LA PILI

922. Ni sharti akusudie kukata masafara ya farsakha nane kuanzia mwan-

zo wa safari, na kama atasafiri masafa ambayo hayafiki farsakha nane

kisha baada ya kufika hapo akakusudia kwenda sehemu nyingine

kiasi kwamba akijumlisha masafa mawili yatafikisha farsakha nane,

kwa kuwa hakukusudia tangu mwanzo wa safari kukata masafa haya

ni wajibu akamilishe swala yake.

923. Asiyejua kuwa safari yake itafikisha masafa kiasi gani, mfano akisa-

firi kwa ajili ya kutafuta kitu kilichopotea na hajui atasafiri masafa

kiasi gani mpaka akipate, ni wajibu akamilishe swala zake, na kama

wakati wa kurudi atasafiri farsakha nane au zaidi ni wajibu apunguze

swala zake.

924. Msafiri hapunguzi swala zake mpaka aazimie mwanzo wa safari

kukata masafa ya farsakha nane. Mwenye kukusudia kukata masafa

ya farsakha nane kama atapata rafiki, kama atakuwa na matumaini ya

kumpata rafiki ni wajibu apunguze swala zake, na kama hana matu-

maini ya kumpata rafiki atakamilisha swala.

925. Mwenye kukusudia kukata masafa ya farsakha nane ni wajibu aanze

kupunguza anapofikia kwenye sehemu asiyoona ukuta au kusikia

sauti ya adhana, na kama atasafiri kidogo sana kiasi kwamba haisadi-

ki kuwa ni msafiri ni wajibu wake akamilishe swala na kwa tahadha-

ri ya sunna apunguze swala

178

Al-Masailul Islamiyah

Page 193: al-Masailu-l-Islamiyyah

926. Ikiwa katika safari yake anamfuata mtu mfano mtumishi akisafiri

kwa kumfuata bwana wake, kama atatambua kuwa safari itafikisha

farsakha za kisheria atapunguza swala, na kama hatambui kwa tahad-

hari amuulize bwana wake.

SHARTI LA TATU

927.Ni sharti msafiri asibadilishe azima yake ya kukata masafa ya kisheria

njiani, akibadilisha lengo lake kabla ya kutimiza farsakha nne au aki-

sitasita baina ya kuendelea na safari au kurudi atawajibika kukamili-

sha swala.

928. Akibadili nia yake baada ya kumaliza farsakha nne ikiwa aliazimia

kukaa huko au kurudi baada ya siku kumi au akawa hana mwelekeo

baina ya kurudi au kubakia ni wajibu akamilishe swala.

929. Akibadili nia yake baada ya kumaliza farsakha nne na akawa ameazi-

mia kurudi siku ile ile ni wajibu kwake kupunguza hata kama akiru-

di kabla ya siku kumi.

930. Mtu akitoka kwenda sehemu maalum na akawa amekata sehemu fula-

ni ya masafa, baada ya hapo akakusudia kwenda sehemu nyingine,

kama jumla ya masafa ya sehemu anayoaanzia hivi sasa kwenda

sehemu ya pili aliyoikusudia mwishoni ni farsakha nane atapunguza

swala zake.

SHARTI LA NNE

931. Ni sharti msafiri asipitie kwenye mji wake kabla ya kufika farsakha

nane na asikae sehemu siku kumi au zaidi, kama atataka kupitia kwe-

nye mji wake kabla ya kukamilisha masafa ya kisheria au akitaka

kukaa sehemu siku kumi atakamilisha swala zake.

179

Al-Masailul Islamiyah

Page 194: al-Masailu-l-Islamiyyah

932. Asiye jua kuwa atapitia kwenye mji wake, au laa au atakaa zaidi ya

siku kumi au laa, ni wajibu akamilishe swala zake.

SHARTI LA TANO

933. Ni sharti asisafiri kwa ajili ya maasi au kitu cha haramu, kama atasa-

firi kwa ajili ya haramu kama vile kuiba, ni wajibu akamilishe swala

yake na vile vile atakamilisha swala kama safari yenyewe ni ya hara-

mu mfano kama inamdhuru au safari ya mke bila idhini ya mumewe,

au safari ya mtoto aliyekatazwa na wazazi wake pamoja na kupatika-

na maudhi kwa kuwakhalifu kwao ikiwa safari ya hawa sio ya waji-

bu. Lakini safari ya hija ya wajibu ni wajibu wapunguze katika swala

zao.

934. Ambaye safari yake sio ya haramu au hakusafiri kwa jambo la hara-

mu anapunguza swala zake hata akifanya maasi katika safari hiyo,

mfano kusengenya au kunywa pombe.

935. Akisafiri kwa ajili ya kuacha wajibu ni wajibu akamilishe swala

zake, aliyekuwa na deni na akawa na uwezo wa kulipa deni hilo

kisha akasafiri ili asilipe deni ni wajibu akamilishe swala, lakini

kama hakusafiri kwa ajili ya kuacha wajibu ni wajibu apunguze

katika swala zake, hata kama itaafikiana na kuacha wajibu kwa

sababu hiyo au italazimu hivyo.

936. Ikiwa safari yake si ya haramu lakini chombo alichosafiria ni cha

unyang’anyi au ardhi aliyotembelea juu yake ilikuwa ya

unyang’anyi atapunguza swala, na kwa tahadhari ya sunna akusanye

baina ya kupunguza na kukamilisha.

937. Mwenye kusafiri pamoja na dhalimu na ikiwa si lazima asafiri nae,

au amesafiri kwa ajili ya kumsaidia dhalimu ni wajibu akamilishe

180

Al-Masailul Islamiyah

Page 195: al-Masailu-l-Islamiyyah

swala. Ama kama kuna ulazima wa kusafiri nae au safari yake na

dhalimu ni kwa ajili ya kuwasaidia watakao dhulumiwa atapunguza

swala.

938. Ambaye amesafiri si kwa ajili ya maasi akikusudia katikati ya safa-

ri kumalizia masafa yaliyobakia kwa ajili ya maasi ni wajibu akami-

lishe swala zake, lakini swala zake alizoziswali kwa kupunguza

kabla ya hapo zitasihi.

SHARTI LA SITA

939. Ni shartia asiwe katika watu wa kuhamahama ambao wanahamahama

na wasio kuwa na makazi maalumu wanatembea na nyumba zao

wanapoona maji au majani wanapiga kambi hapo na yanapokwisha

huhama na kwenda sehemu nyingine hawa ni wajibu kukamilisha

swala zao.

940. Akisafiri mmoja wa watu hawa kwa ajili ya kutafauta malisho ya

wanyama wao hata kama safari yake ikifikia masafa ya kisheria ni

wajibu wake akamilishe swala hata kama hana mifugo yake.

941. Akisafiri miongoni mwa watu wanao hama hama kwa ajili ya hija,

ziara au biashara na mengineyo atapunguza swala zake.

SHARTI LA SABA

942. Ni sharti safari isiwe ni kazi yake na kama shughuli yake ni utingo,

dereva au baharia na wengineo atakamilisha swala kama safari yake

si ya kwanza, lakini katika safari ya kwanza atapunguza swala zake

hata kama safari yake itakuwa ndefu kiasi gani.

943. Ambaye safari ni kazi yake katika baadhi ya misimu ya mwaka,

kama vile dereva ambaye huendesha gari lake kiangazi au masika ni

181

Al-Masailul Islamiyah

Page 196: al-Masailu-l-Islamiyyah

wajibu akamilishe swala katika safari.

944. Ambaye shughuli yake ni safari akibaki kwenye mji wake siku kumi

au zaidi ni wajibu apunguze swala zake katika safari yake ya kwan-

za ambaye atasafiri baada ya kukaa siku kumi.

945. Mtalii katika miji ambayo hajaifanya kuwa ni makazi yake ni wajibu

akamilishe swala.

946. Ambaye safari si kazi yake na akawa anasafiri mara nyingi katika

miji au vijiji kwa ajili ya kuchukua bidhaa ni wajibu apunguze swala

zake.

SHARTI LA NANE

947. Ni sharti msafiri afike katika sehemu inayoruhusiwa kupunguza,

yaani awe mbali na mji kiasi kwamba haoni ukuta wa mji au hasikii

adhana.

948. Akisafiri na akifika sehemu anasikia adhana, lakini haoni ukuta wa

mji au anaona ukuta, lakini hasikii adhana akitaka kuswali atakami-

lisha swala.

949. Msafiri anayerudi kwenye mji wake ni wajibu akamilishe swala zake

pindi aonapo ukuta wa mji wake au asikiapo adhana, na msafiri

anayetaka kukaa sehemu siku kumi akiona kuta za sehemu hiyo au

akisikia adhana yake nilazima akamilishe swala.

950. Msafiri anayerudi kwenye mji wake ni wajibu akamilishe swala zake

anapoona ukuta wa mji wake au kusikia adhana, na pia msafiri

ambaye anataka kukaa kwenye sehemu siku kumi ataanza kukamili-

sha swala anapoona ukuta au kusikia adhana ya mahali anapoenda.

182

Al-Masailul Islamiyah

Page 197: al-Masailu-l-Islamiyyah

951. Akisafiri katika sehemu isiyokuwa na nyumba wala ukuta akifika

kwenye sehemu ambayo kwa kawaida kama kungelikuwa na nyumba

au ukuta zisingeonekana nilazima apunguze swala yake.

952. Ikiwa macho, masikio na sauti ya adhana si ya kawaida ni lazima

apunguze swala katika sehemu ambayo macho ya kawaida hayaoni,

au masikio ya kawaida hayasikii au sauti ya adhana ya kawaida haisi-

kiki.

953. Mwenye kwenda kwenye mji wake ni lazima akamilishe swala aona-

po ukuta wa mji au kusikia adhana.

HUKUMU ZA MAKAZI NA KUKAA

SIKU KUMI

954. Mwenye kuchagua mji kwa ajili ya kuishi utahesabiwa kuwa ni mji

wake hata kama hajazaliwa sehemu hiyo.

955. Akikusudia kuishi kwenye mji kwa muda maalum usiokuwa mji wake

kisha akahama hapo, haitahesabiwa kuwa ni mji wake ila anapotaka

kubaki muda mrefu kama mwaka au zaidi, kwa wanafunzi na wana-

chuo wanaosafiri kwa ajili ya kusoma huo mji unakuwa ni mji wao,

kwa hiyo wanalazimika kukamilisha swala na kufunga, na vivyo

hivyo hukumu ya Askari ambao wanapangiwa kukaa sehemu muda

mrefu.

956. Mahali ambapo amekusudia kuishi miaka minne au mitano itahesa-

bika kuwa ni mji wake, ikitokea safari kisha akarudi kwenye huo mji

atawajibika kukamilisha swala.

183

Al-Masailul Islamiyah

Page 198: al-Masailu-l-Islamiyyah

957. Mwenye sehemu mbili mfano akikaa sehemu moja miezi sita na sehe-

mu nyingine miezi sita, sehemu zote mbili zitahesabika kuwa ni miji

yake, na vile vile hukumu hii itakuwa kwa mwenye kuchagua miji

mingi kuwa makazi yake.

958. Akifika sehemu ambayo ilikuwa ni mji wake wakati uliopita lakini

alihama, hakamilishi swala hata kama bado hajapata mji mwingine.

959. Msafiri ambaye hajakusudia kuishi siku kumi lakini amenuia endapo

atapata rafiki sehemu nzuri atakaa siku kumi atapunguza swala zake.

960. Msafiri akikusudia kubaki sehemu siku kumi akibadilisha kusudio

lake la kubaki siku kumi kabla ya kuswali swala ya rakaa nne au

akawa hana mwelekeo kati ya kubaki au kuondoka ni wajibu apungu-

ze swala zake, na kama ataondoka hiyo sehemu au alikosa mwelekeo

baada ya kuswali swala ya rakaa nne, ni lazima akamilishe swala

maadamu yuko huko.

961. Msafiri akijishughulisha na swala kwa nia ya kukupunguza na kati-

kati ya swala akaazimia kukaa siku kumi ni lazima akamilishe swala.

962. Msafiri aliyekusudia kukaa sehemu siku kumi akikaa zaidi ya siku

kumi ni lazima akamilishe swala zake na haimlazimu kunuia upya

kukaa siku kumi zingine.

963. Msafiri aliyekusudia kukaa sehemu siku kumi ni wajibu wake kufun-

ga saumu za wajibu na za sunna na kuswali swala ya ijumaa.

964. Msafiri ambaye amebaki sehemu siku thelathini kwa kukosa mwele-

keo kuwa ataondoka lini, ni wajibu wake akamilishe swala baada ya

siku thelathini hata kama atakaa kidogo.

184

Al-Masailul Islamiyah

Page 199: al-Masailu-l-Islamiyyah

965. Msafiri ambaye hana mwelekeo kwa muda wa siku thelathini ni lazi-

ma akamilishe swala zake baada ya siku thelathini, kama siku thela-

thini amekaa sehemu moja, ama ikiwa zimeisha kwa kukaa sehemu

mbalimbali atapunguza swala zake hata baada ya siku thelathini.

MAS’ALA MENGINEYO

966. Inajuzu kwa msafiri akamilishe swala zake katika msikiti mtakatifu

wa Makka, msikiti wa Mtume, msikiti wa Kufah na kwenye kaburi la

Imamu Hussein (as) akiswali nje ya sehemu hizi au akiswali sehemu

ambayo iko na umbali kidogo kiasi cha mita ishirini na tano kwa

tahadhari ya sunna apunguze swala zake.

967. Anayetambua kuwa msafiri ni wajibu wake apunguze swala zake aki-

kamilisha kwa kujisahau swala yake inabatilika.

968. Msafiri asiyejua kuwa ni wajibu kwake kupunguza swala akikamili-

sha swala yake inasihi.

.

969. Akijisahau kuwa ni msafiri akakamilisha swala akitambua ndani ya

wakati atarudia swala yake na akitambua baada ya wakati halazimiki

kuswali kadha.

970. Ni sunna kwa msafiri baada ya kila swala aseme mara thelathini

“Subhana llah, wal hamdulillah, walaa ilaha ila llahu wa llah akbar”

imetiwa mkazo kuisema baada ya swala ya adhuhuri, alasiri na ishaa

na ni bora alete dhikri hii baada ya swala hizi mara sitini.

SWALA YA KADHA

971. Ambaye hakuswali swala ya wajibu katika wakati wake ni wajibu

185

Al-Masailul Islamiyah

Page 200: al-Masailu-l-Islamiyyah

ailipe hata kama alikuwa amelala wakati wote wa swala au wakati

umepita kwa sababu alikuwa amelewa, au kazimia, lakini mwanamke

halipi kadha za swala zilizompita katika hali ya hedhi na nifasi.

972. Akitambua baada ya wakati wa swala kuwa swala aliyoiswali ilikuwa

ni batili ni wajibu aswali kadha.

973. Ambaye ana kadha za swala zilizompita ni lazima asizembee wala

kupuuzia lakini sio wajibu kuzilipa kwa haraka.

974. Swala za kila siku zikimpita ambazo huwa na utaratibu kama adhu-

huri, alasiri au magharibi na ishaa katika siku moja ni wajibu azilipe

kwa utaratibu, ama nje na hapa ni kwa tahadhari ya sunna achunge

utaratibu.

975. Akitaka kulipa swala nyingi zisizo za kila siku kama swala za matu-

kio ambazo zimempita mara nyingi na akataka kulipa kadha za swala

za kila siku, si lazima kulipa kadha kwa utaratibu.

976. Akipitwa na swala ya adhuhuri kisha siku nyingine akapitwa na swala

ya alasiri au akapitwa na zote mbili na akawa hajui ni ipi iliyotangu-

lia kumpita, inatosha alete swala mbili za rakaa nne nne kwa kunuia

kuwa swala ya kwanza ni kadha ya siku ya kwanza na ya pili ni kadha

ya siku ya pili.

977. Akitambua kuwa amepitwa na swala ya rakaa nne na hatambui kuwa

ni adhuhuri au alasiri inatosha alete swala ya rakaa nne kwa nia ya

swala iliyompita.

978 Akipitwa na swala tano na hajui ya kwanza kumpita ni ipi itabidi azin-

gatie utaratibu ufuatao: Kwanza ataswali swala tisa kwa utaratibu,

ataanza na swala ya asubuhi, adhuhuri, alasiri, magaharibi na ishaa

kisha arudie upya swala ya asubuhi, adhuhuri, alasiri na magharibi na

vile vile akipitwa na swala sita itabidi aswali swala kumi kwa utarati-

186

Al-Masailul Islamiyah

Page 201: al-Masailu-l-Islamiyyah

bu huu huu na akipitwa na swala saba ataswali swala kumi na moja.

979. Mwenye kutambua kuwa amepitwa na swala ya asubuhi mara nyingi

au swala ya adhuhuri mara nyingi na hajui kuwa imepita mara ngapi

mara tatu au tano au sita, akilipa kadha kwa kiasi kidogo inatosha, na

kama anajua idadi yake lakini akasahau itabidi alete kadha ambayo

inampa uhakika, kama akiwa na uhakika kuwa swala ya asubuhi hai-

jampita zaidi ya mara kumi basi kwa tahadhari ya sunna inabidi alete

kadha ya swala ya asuhubi mara kumi.

980. Haijuzu kwa mtu mwingine kulipa kadha za swala zilizompita aliye

hai hata kama ameshindwa kuzilipa.

981. Inajuzu kuswali swala za kadha na jamaa hata kama swala ya imamu

ni adaa au kadha, hailazimu swala ya maamuma iafikiane na swala ya

imamu, hakuna tatizo kama akilipa kadha ya swala ya asubuhi na

imamu anaswali swala ya adhuhuri au alasiri.

982. Ni sunna kumhimiza mtoto na kumzoesha swala na ibada mbali

mbali, bali ni sunna pia kumhimiza kulipa swala zilizompita na inaju-

zu kwa watoto kusimisha swala ya jamaa na imamu wao awe ni

mtoto.

WAJIBU WA MTOTO MKUBWA KULIPA SWALA

ZILIZOWAPITA WAZAZI WAWILI

187

Al-Masailul Islamiyah

Page 202: al-Masailu-l-Islamiyyah

983. Ni wajibu kwa mtoto mkubwa kulipa kadha ya swala na saumu zili-

zompita baba yake, bali na hata mama pia kama hazikumpita kwa

kuasi na wakawa na uwezo wa kuzilipa, bali ni wajibu kulipa kadha

za wazazi wawili baada ya kufa kwao au kuajiri mtu wa kulipa kadha

zilizowapita, na zikiwapita swala na saumu bila ya udhuru wowote

kwa tahadhari mtoto mkubwa awalipie.

984. Mtoto mkubwa akishuku kuwa wazazi wake walipitwa na swala au

saumu sio wajibu wake kulipa kadha.

985. Kama mtoto mkubwa hafahamiki basi watoto wote watagawiwa

yaliyowapita wazazi wao au achaguliwe mmoja wao.

986. Kama maiti ameusia kuwa aajiriwe mtu wa kulipa yaliyompita haita-

wajibika kwa mtoto mkubwa baada ya aliye ajiriwa kulipa kadha kwa

njia sahihi.

987. Mtoto akitaka kulipa yaliyowapita wazazi wake ni lazima alipe kuto-

kana na wadhifa wake, mfano kudhihirisha sauti katika swala ya asu-

buhi na magharibi na isha hata kama analipa kadha ya mama yake.

988. Ikiwa mtoto mkubwa hajabaleghe au alikuwa ni kichaa wakati waza-

zi wake wanakufa atalipa kadha baada ya kubaleghe, na kichaa ata-

walipia atakapopona, na akifa mtoto mkubwa kabla ya kubaleghe

hatawajibika mtoto anayefuata.

989. Akifa mtoto mkubwa kabla ya kuwalipia wazazi wake si wajibu kwa

mtoto anayefuata kulipa.

KUTOA UJIRA KWA AJILI YA SWALA

ZA KADHA

188

Al-Masailul Islamiyah

Page 203: al-Masailu-l-Islamiyyah

990. Inajuzu kumwajiri mtu kwa ajili ya kulipa swala au ibada zingine na

kama atajitolea mtu bila ya ajira itasihi.

901. Ni wajibu kwa mwenye kuiajiri nafsi yake katika kulipa swala za

maiti awe ni mujitahidi au mwenye kujua hukumu za swala kwa uele-

wa na taqlidi sahihi.

902. Ni wajibu kwa muajiriwa amuainishe anayemuwalikilisha wakati wa

nia na si lazima atambue jina lake, na inatosha anuie hivi: “Ninaswali

kwa niaba ya yule nilioajiriwa kwa jili yake kwa kujikurubisha kwa

Mwenyezi Mungu”.

903. Akiajiriwa mtu kwa ajili ya kulipa kadha ya maiti ikifahamika kuwa

hajalipa kabisa au hajalipa kwa usahihi ni wajibu atoe ajira tena kwa

mwingine ikiwa ni wajibu kwake kuajiri.

904. Akishuku kuwa muajiriwa amelipa au laa, akisema muajiriwa kuwa

nimelipa na ni mkweli inatosha, na akishuku kuwa ametekeleza vili-

vyo au laa, si lazima aajiri upya mtu mwingine.

905. Haijuzu kumwajiri mtu mwenye udhuru kama vile mwenye wadhifa

wa kutayamamu au mwenye kuswali kwa kukaa n.k

906. Inajuzu mwanamke kulipa kadha za mwanaume pia inajuzu kwa

mwanaume kumlipia mwanamke na kila mmoja anafanya kulingana

na wadhifa wake.

SWALA YA JAMAA

907. Ni sunna kuswali swala za kila siku kwa jamaa na imetiliwa mkazo

kwenye swala ya asubuhi, magharibi na isha na hasa kwa aliyekaribu

na msikiti na mwenye kusikia adhana.

189

Al-Masailul Islamiyah

Page 204: al-Masailu-l-Islamiyyah

908. Mtu mmoja akiswali nyuma ya Imamu malipo ya kila rakaa ni sawa

na mwenye kuswali swala mia na hamsini, na kama watu wawili

watamfuata malipo yao ni sawa na kuswali swala mia sita, na idadi

inapoongezeka na malipo pia huongezeka mpaka kufikia kumi, wana-

pozidi kumi kama mbingu itakuwa ni katarasi na bahari kuwa wino na

miti kuwa kalamu kisha waandishi wawe ni majini, watu na malaika

hawataweza kuandika thawabu za rakaa moja.

909. Haijuzu kutohudhuria swala ya jamaa na haijuzu kuacha swala ya

jamaa bila ya udhuru.

910. Ni sunna kwa mtu kungoja jamaa, na swala ya jamaa baada ya waka-

ti wa mwanzo ni bora kuliko swala ya furada katika mwanzo wa

wakati.

911. Hakuna tatizo Imamu au Maamuma akitaka kurudia swala aliyokwi-

sha iswali kwa jamaa mara nyingine.

912. Ambaye hutokewa na wasiwasi katika swala ya furada na wasiwasi

wake huisha anaposwali jamaa itamlazimu kwa tahadhari ya wajibu

aswali jamaa.

913. Haijuzu kuswali swala za sunna kwa jamaa ila swala ya kuomba

mvua au swala ya wajibu iliyokuwa sunna kwa sababu fulani, kama

vile swala ya Iddil- ftiri, Iddil – Adhuha ambazo ni wajibu kwa kud-

hihiri Imamu (as) na ni sunna kwa kutokuwepo kwake, inajuzu kuzis-

wali jamaa.

914. Asiyetambua kuwa Imamu wa jamaa anaswali swala za kila siku

ambazo ni wajibu au swala ya sunna haijuzu kumfuata.

915. Safu za swala zikifika kwenye mlango wa msikiti swala inasihi kwa

yule aliyeswali mbele ya mlango.

190

Al-Masailul Islamiyah

Page 205: al-Masailu-l-Islamiyyah

916. Ambaye amesimama kwenye sehemu ambayo hapati mawasiliano na

safu ya mbele na kama hapati mawasiliano kwa imamu kwa kupitia

maamuma wengine kulia na kushoto, haijuzu kwake kujiunga na

imamu.

917. Hakuna tatizo kama sehemu ya maamuma iko juu zaidi kuliko sehe-

mu ya imamu.

918. Akitenganisha mtoto mwenye kutambua zuri na baya katika safu

moja, kama hawatambui kubatilika swala yake inajuzu kujiunga na

jamaa.

919. Akitambua kuwa swala ya imamu ni batili, kama akitambua kuwa

imamu hana udhu haijuzu kumfuata hata kama imamu hajajua hilo.

920. Akitambua maamuma baada ya swala kuwa imamu hakuwa muadili-

fu au alikuwa kafiri au swala yake ilikuwa batili kwa sababu mion-

goni mwa sababu mfano hakuwa na udhu swala inasihi.

921. Akinuia maamuma swala ya furada bila ya udhuru au pamoja na

udhuru baada ya Al – hamdu na sura haimlazimu kusoma Al hamdu

na sura lakini akinuia furada kabla ya kumaliza Al- hamdu na sura

inabidi asome kiasi ambacho imamu amesoma, na kwa tahadhari aru-

die kuzisoma kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

922. Akishuku maamuma kuwa amenuia swala ya furada au laa ni wajibu

ajengee kuwa hajanuia nia ya furada na ataendelea na swala ya

jamaa.

YALIYOLAZIMA KWA IMAMU

WA JAMAA

191

Al-Masailul Islamiyah

Page 206: al-Masailu-l-Islamiyyah

923. Lazima imamu wa jamaa awe baleghe, mwenye akili na awe ni shia

ithna asharia muadilifu, awe mtoto wa halali, awe anaswali swala kwa

usahihi, ni lazima imamu awe ni Mwanaume kama atafuatwa na

wanaume na hakuna tatizo kwa mtoto kufuatwa na watoto na pia

mwanamke kufuatwa na wanawake.

924. Mwenye kuwa na uwezo wa kuswali kwa kusimama haijuzu kumfua-

ta aliyekaa au aliyelala, ambaye anaswali kwa kukaa haijuzu kum-

fuata aliye lala, inajuzu kwa anayeswali kwa kulala amfuate aliyekaa

na aliyekaa kwa aliyesimama.

925. Inajuzu kumfuata imamu ambaye nguo yake ina najisi au wadhifa

wake ni kutayamamu au kwa udhu wa bandeji kama kuswali kwake

na nguo yenye najisi au tayamamu au udhu wa bandeji ni kwa saba-

bu ya udhuru.

926. Inajuzu kumfuata maslusi na mabtuni na pia inajuzu asiye kuwa mus-

tahadha kumfuata mustahadha.

927. Kwa tahadhari ya sunna wasifuatwe wenye ukoma na balanga na

yeyote.

HUKUMU ZA JAMAA

928. Ni wajibu kwa maamuma kumuainisha imamu katika nia, lakini hai-

lazimu kumjua imamu kwa jina inatosha kusema ninamfuata imamu

anayetuongoza.

929. Ni wajibu kwa maamuma alete vipengele vyote vya swala yeye mwe-

nyewe ila kusoma Al- hamdu na sura hiyo ni kazi ya imamu.

930. Ni wajibu kwa maamuma asisome Al- hamdu na sura katika swala za

asubuhi, magharibi na ishaa kama anasikia sauti ya imamu na hata

kama hasikii sauti ya imamu vizuri na kama hasikii kabisa lazima

192

Al-Masailul Islamiyah

Page 207: al-Masailu-l-Islamiyyah

asome kwa kutodhihirisha sauti.

931. Akirukuu kabla ya imamu kwa kujisahau na akajua kuwa nikirudi

katika kisimamo sitamuwahi imamu katika kusoma, akisuburi mpaka

imamu amkute kwenye rukuu swala yake inasihi. Na pia swala yake

inasihi kama atanyanyua kichwa chake kutoka kwenye rukuu kwa

lengo la kumfuata imamu kisha akarukuu na imamu mara ya pili.

932. Haijuzu kumfuata imamu akileta kunuti kwa kusahau katika sehemu

isiyo ya kunuti au akileta tashahudi katika sehemu isiyo ya tashahudi

kama ambavyo katika hali hii haijuzu kurukuu kabla ya imamu kuru-

kuu bali atasubiri kisha atakamilisha yaliyo bakia pamoja naye ila

akikusudia furada inajuzu kumkhalifu imamu.

SUNNA ZA SWALA YA JAMAA

933. Ni sunna kwa mamuma wa kiume asimame kulia mwa imamu na

kama maamuma ni wa kike atasimama kulia mwa imamu kiasi

kwamba sehemu yake ya kusujudia itakuwa sawa na magoti ya

imamu au miguu ya imamu kama maamuma ni mwanaume na mwa-

namke au mwanaume na wanawake wengi ni sunna maamuma wa

mwanaume asimame kulia mwa imamu na wanawake wasimame

nyuma ya imamu na kama ni wanaume wengi na wanawake wengi ni

sunna wanaume kuwa nyuma ya imamu na wanawake kuwa nyuma

ya wanaume.

934. Ikiwa imamu na maamuma ni wanawake ni bora wasimame kwa

usawa asitangulie imamu kwa maamuma.

935. Ni sunna kwa imamu kusimama katikati ya safu na wasimame wenye

elimu na ucha Mungu nyuma yake katika safu ya kwanza

936. Ni sunna safu ziwe zimenyooka na bila ya kuwepo na mwanya wala

193

Al-Masailul Islamiyah

Page 208: al-Masailu-l-Islamiyyah

kitenganishi chochote.

937. Ni sunna kwa waumini kusimama baada ya kauli ya imamu “Qad

Qaamati swaalat”

938. Ni sunna kwa imamu kuchunga udhaifu wa maamuma asirefushe

rukuu, kunuti na sijida ila akitambua kuwa wote wanapendezwa na

hali hiyo.

939. Ni sunna akitambua imamu kuongezeka kwa maamuma mwingine

arefushe rukuu mara mbili zaidi kisha asimame hata kama akitambua

kuongezeka mwingine.

VILIVYO MAKURUHU KATIKA

SWALA YA JAMAA

940. Ni makuruhu kwa maamuma kusimama peke yake katika safu moja

ikiwa katika safu zingine kuna sehemu zilizo wazi.

941. Ni makuruhu kwa maamuma kuleta baadhi ya dhikri kwa sauti kiasi

kwamba imamu anasikia.

942. Ni makuruhu kwa msafiri ambaye anapunguza swala zake kama

adhuhuri, alasiri na ishaa afuatwe na asiye kuwa msafiri na pia ni

makuruhu kwa asiye kuwa msafiri kumfuata msafiri.

SWALA YA IJUMAA

943. Swala ya ijumaa ni wajibu akiwepo Imamu (as) badala ya adhuhuri,

194

Al-Masailul Islamiyah

Page 209: al-Masailu-l-Islamiyyah

lakini katika zama ya ghaiba ya Imamu inakuwa ni wajibu wa hiari,

yaani mtu anakuwa na hiari katika siku ya Ijumaa kuswali adhuhuri

au kuswali ijumaa lakini kwa tahadhari ya sunna akiswali ijumaa kati-

ka wakati huu wa ghaiba ya Imamu aswali na adhuhuri pia.

944. Swala ya Ijumaa ina rakaa mbili mfano wa swala ya asubuhi na

imamu adhihirishe sauti yake katika kusoma Al- hamdu na sura na

imetiliwa mkazo asome suratul- jum’a katika rakaa ya kwanza na

suratul – munaafiquun katika rakaa ya pili, na ni sunna katika swala

ya ijumaa kuleta kunuti mbili katika rakaa ya kwanza kabla ya rukuu

na katika rukuu ya rakaa ya pili baada ya rukuu. Ni wajibu asirukuu

baada ya kunuti ya rakaa ya pili na akirukuu baada ya kunuti swala

inabatilika.

945. Shaka katika idadi ya rakaa kwenye swala ya ijumaa inabatilisha

swala.

946. Ni sharti katika swala ya ijumaa yanayoshurutishwa katika swala za

kila siku kwa kuongeza yafuatayo:-

1. Iswaliwe jamaa na si furada.

2. Iwe idadi ya wenye kuswali - imamu na maamuma - wawe saba

waliobaleghe kwa uchache na kwa tahadhari ya wajibu katika hao

asiwepo msafiri anayepunguza swala ikiwa imamu na mamuma ni

watano swala inasihi.

3. Imamu ahutubie kabla ya swala khutuba mbili kwa ufafanuzi uta-

kaokuja inshaallah.

4. Ikiwa kuna sehemu mbili za swala za ijumaa ni wajibu masafa

baina ya ijumaa mbili hizo yawe ni kilometa tano na nusu

5. Kama maamuma watatawanyika katikati ya khutuba ya swala au

195

Al-Masailul Islamiyah

Page 210: al-Masailu-l-Islamiyyah

kabla ya kuanza swala na idadi ikawa chini ya watu wanne swala

ya ijumaa haitasihi ni wajibu waswali adhuhuri, na wakitawanyi-

ka katikati ya swala ni wajibu kwa imamu kukamilisha ijumaa

kisha aswali adhuhuri.

947. Ni lazima vizingatiwe vitu vifuatavyo katika khutuba mbili:-

- Kumhimidi Mwenyezi Mungu – kumshukuru

- Kumtakia rehma Mtume “Muhammad (saww) na kizazi chake kituku-

fu

- Awalinganie watu katika kumcha Mwenyezi Mungu na kumuogopa

- Asome sura kamili katika khutuba ya kwanza

- Kuwatakia rehma maimamu na kuwataja kwa majina katika khutuba

ya pili

- Kuwaombea waumini maghfira

948. Ni lazima kumuhimidi Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma Mtume

Muhammadi (saww) na kizazi chake katika khutuba kwa lugha ya

kiarabu lakini mawaidha na kuwalingania inajuzu kwa lugha ya

waliohudhuria.

949. Ni lazima kwa imamu asome khutuba mbili mwenyewe, asisome

mwingine kama ambavyo anatakiwa azisome akiwa amesimama

kisha atenganishe khutuba ya pili kwa kukaa kikao kidogo na adhi-

hirishe sauti ya khutuba kwa uchache wasikie watu wanne

waliokamilisha masharti, na inapaswa waliohudhuria wote wasikie

khutuba mbili.

950. Ni lazima kwa maamuma kwa ubora kusikiliza khutuba ya imamu, na

wasizungumze mazungumzo yanayowafanya wasimsikilize imamu

na wala wasiswali swala za sunna na wakae mkao wa swala,

wasigeuke kulia na kushoto na wala wasigeuke geuke, na hakuna tati-

zo katika mambo haya baada ya khutuba na kabla ya swala.

196

Al-Masailul Islamiyah

Page 211: al-Masailu-l-Islamiyyah

951. Kama maamuma hawatasikiliza khutba mbili na wakawa wamegeuka

kulia na kushoto watakuwa wamefanya kinyume na tahadhari lakini

swala yao inasihi.

952. Si wajibu swala ya Ijumaa kwa asio baleghe, vichaa na wazee, wag-

onjwa, vipofu, wanawake, wasafiri na wanaokaa mbali na sehemu ya

kuswalia kwa farsakha mbili wala kwa yule ambaye ni vigumu

kuhudhuria katika swala wala katika wakati wa mvua, lakini mmoja

wa hawa akihudhuria swala yake inasihi.

953. Inajuzu kwa aliyechelewa khutba mbili ahudhurie ijumaa na kuswali,

na pia akimkuta imamu yuko kwenye rukuu ya rakaa ya pili itakuwa

rakaa yake ya kwanza na akitoa salamu imamu atasimama kwa ajili

ya rakaa ya pili na kukamilisha swala na ijumaa itakuwa imesihi.

SWALA YA MAJANGA

954. Ni wajibu kuswali swala ya majanga ambayo tutataja namna yake

baadaye kwa sababu ya mambo yafuatayo:-

1. Kupatwa kwa Jua, hata kama itapatwa sehemu tu na hajaogopa

yeyote

2. Kupatwa kwa Mwezi, hata kama itapatwa sehemu tu na hakuo-

gopa yeyote

3. Tetemeko, hata kama hakuogopa yeyote

4. Radi, ngurumo, kimbunga, kuvuma kwa upepo mweusi na

mwekundu n.k. ikiwa watu wengi wataogopa

955. Vikitokea vitu vingi ambavyo ni wajibu kuswali swala ya majanga ni

wajibu aswali kwa kila tukio swala ya janga mfano: Ikitokea kupatwa

kwa jua na likatokea tetemeko ni wajibu kuswali swala ya majanga

mara mbili.

197

Al-Masailul Islamiyah

Page 212: al-Masailu-l-Islamiyyah

956. Mwenye kuwajibikiwa na swala nyingi za majanga, mfano likipatwa

jua mara tatu na hakuswali kwa muda wake haitamlazimu wakati wa

kadha kuainisha ni swala ipi anayoiswali bali inatosha kuswali idadi

ya swala kulingana na idadi ya majanga yaliyompita.

957. Ni wajibu kuleta swala ya majanga tangu linapoanza kupatwa jua au

mwezi na kwa tahadhari ya sunna asicheleweshe hadi weupe uanze

kutokea.

958. Akiwajibikiwa na swala ya majanga katika wakati wa swala za kila

siku, kama wakati utakuwa ni mpana atachagua yeyote ya kutan-

guliza, na kama wakati utakuwa ni mfinyu itabidi aswali swala

ambayo muda wake ni mfinyu na kama wakati wa swala mbili hizi ni

mfinyu atatanguliza swala ya kila siku.

959. Akitambua katikati ya swala ya kila siku kuwa wakati wa swala ya

majanga ni mfinyu na wakati wa swala ya kila siku ni mpana

atakatisha swala ya kila siku na kuswali swala ya majanga.

960. Ikitokea kupatwa kwa jua, mwezi, tetemeko na mwanamke yuko kati-

ka hedhi au nifasi hatawajibikiwa na swala ya majanga wala kadha

yake lakini kwa tahadhari ya sunna aswali baada ya kutoharika.

NAMNA YA KUSWALI SWALA YA

MAJANGA

961. Swala ya majanga ina rakaa mbili na kila raka kuna rukuu tano namna

yake ni hii: “Alete takbira baada ya nia atasoma Al- hamdu na sura

kamili na kurukuu kisha anasimama na kusoma Al- hamdu na sura

kamili atafanya vivyo hivyo hadi mara tano na baada ya kusimama

kutoka kwenye rukuu ya tano anaenda kwenye sijida mbili kisha

anasimama kwa ajili ya rakaa ya pili, anafanya kama alivyofanya kati-

198

Al-Masailul Islamiyah

Page 213: al-Masailu-l-Islamiyyah

ka rakaa ya kwanza na kuleta tashahudi na kutoa salamu.

962. Katika swala ya majanga inajuzu baada ya nia na kusoma Al- hamdu

agawanye sura kwenye vifungu vitano atasoma aya au zaidi ya aya

kisha anarukuu kisha ananyanyuka anasoma kifungu cha pili cha sura

bila ya kusoma Al- hamdu kisha anarukuu vivyo hivyo mpaka rukuu

ya tano mfano: asome baada ya Al-hamdu (bismillah rahmani rahim”

kama anataka kusoma suratul – Ikhalas kisha anarukuuu kisha

ananyanyuka anasoma Qul huwallahu ahad – kisha anarukuu kisha

ananyanyuka anasoma Allahhu swamadu – anarukuu kisha anasoma

lam yalid walam yuulad kisha anarukuu kisha ananyanyuka anasoma

Walam yakun lahuu kufuwan ahad – anarukuu rukuu ya tano baada ya

kunyanyuka hapo anaenda kwenye sijida mbili kisha ananyanyuka

kwa ajili ya rakaa ya pili na anafanya kama alivyofanya kwenye rakaa

ya kwanza.

963. Ni sunna kuleta takbira kabla ya kurukuu na baada yake ama baada

ya rukuu ya tano na ya kumi ni sunna kusema “Samia llahu liman

hamidah”

964. Ni sunna kuleta Qunuti kabla ya rukuu ya pili, ya nne, ya sita, ya nane

na ya kumi na akileta Qunuti moja kabla ya rukuu ya kumi inatosha.

965. Kila rukuu katika rukuu za swala za majanga ni nguzo zinabatilisha

swala kwa kuongezeka kwake au kupungua kwa kukusudia au kusa-

hau.

966. Ni mustahabu kuleta swala ya majanga kwa jamaa na hapo

haitawalazimu maamuma kusoma Al- hamdu na sura .

199

Al-Masailul Islamiyah

Page 214: al-Masailu-l-Islamiyyah

SWALA YA IDD MBILI “AL – FITRI

NA AL – ADHIHAA”

967. Swala ya Idd mbili ni wajibu katika zama za kuwepo Imamu “as” na

ni lazima iswaliwe jamaa na ni sunna katika zama za “ghaiba”

kuswaliwa jamaa au furada.

968. Wakati wa swala ya Idd ni mwanzo wa kuchomoza jua mpaka jua

linapopetuka.

969. Ni sunna kuswali swala ya Idd ya adhuhaa baada ya kunyanyuka jua

kama ilivyo kwenye swala ya Iddil – fitri na atoe zaka kisha aswali

Idd.

970. Swala ya Idd mbili ina rakaa mbili kwanza analeta takbira ya ihram

kisha baada ya kusoma Al-hamdu na sura analeta takbira tano

anakunuti baada ya kila takbira, analeta takbira nyingine na kurukuu

kisha analeta sijida mbili, kisha anasimama kwa ajili ya rakaa ya pili

baada ya Al hamdu na sura analeta takbira nne na anakunuti baada ya

kila takbira kisha analeta takbira ya tano na kurukuu kisha analeta

sijida mbili baada ya rukuu na analeta tashahudi na kutoa salamu.

971. Na inatosha kuleta dua yeyote katika kunuti za idd mbili lakini ni bora

alete moja ya hizi dua mbili “Allahuma Ahlul kibriai wal

adhama.waahalul juudi wal jabarut waahalul ‘af’wi wa rahma

waahlu taqwaa walmaghifra as’aluka bihaqi hadhal yaumi alladhii

ja’al tahu lili muslimiina I’ydan, wali Muhammadin swala llahu alay-

hi waalihi dhukhran wa sharafan wakaramatan wa mazidaan, an

tuswaliya alaa muhammadin waali Muhammad, wa an tud khilanii fii

kuli khayrin adkhalta fiihi Muhammad waala muhammad wa

antukhirjanii min kuli suui akhrajta minhu muhammadan waala

200

Al-Masailul Islamiyah

Page 215: al-Masailu-l-Islamiyyah

Muhammadi swalawatuka alayhi wa alayhimu allahumma inii

as’aluka khayran maasaalaka minihu Ibaaduka swaalihuuna wa

waa’udhubika mimaa istadha minhu ibaadukal mukhliswuna”

972. Ni sunna kuleta khutba mbili katika ghaiba ya Imamu baada ya swala

na ni bora kutaja hukumu za fitri katika Iddil- fitri na hukumu za

kuchinja katika iddil adhiha

973. Hakuna katika idd mbili hizi sura maalumu ya kusoma lakini ni bora

asome katika rakaa ya kwanza suratu Shamsi (nayo ni sura ya 91)

na katika rakaa ya pili suratul ghashiya (nayo ni sura ya 88) au

asome katika rakaa ya kwanza suratul A’alaa (nayo ni sura ya 87)

na katika rakaa ya pili suratul Shamsi.

974. Ni sunna kuswali swala ya Idd mbili uwanjani lakini Makka ni

sunna kuswaliwa ndani ya msikiti mtukufu .

975. Ni sunna baada ya swala ya magharibi na isha, katika usiku wa idd il-

fitri na baada ya swala ya asubuhi na vile vile hata baada ya swala ya

Idd alete hizi takbira.

“Allahu akbaru Allahu akbaru laa ilaaha ila llaha wa llahu akbaru

walilahil hamdu,al-hamdu lilahi alaa maahadaanaa walahu shukri alaa

maa aulaanaa”

976. Na takbira ya Iddul – adhuhaa atesema baada ya kauli ya “alaa ma

hadaanaa” atasema “Allahu akbaru alaa maa razaqanaa min bahi-

imatil ana’am wal hamdulillah alaa maa ablaanaa” akiwa katika idd

ya kuchinja ni mustahabu alete takbira baada ya sala kumi na tano ya

kwanza ni swala ya adhuhuri katika siku ya Idd na ya mwisho ni

swala ya asubuhi ya siku ya kumi na tatu katika mwezi wa dhul –

hijja.

977. Akihudhuria maamuma na imamu yuko kwenye rukuu inajuzu kunuia

201

Al-Masailul Islamiyah

Page 216: al-Masailu-l-Islamiyyah

kisha ataleta takbiratul -ihram na anaenda kwenye rukuu na inah-

esabika kuwa ni rakaa.

978. Akisahahu tashahudi au moja ya sijida mbilli katika swala ya Idd kwa

tahadhari ya sunna alete kadha ya alichokisahau baada ya swala, na

akifanya kinacholazimu sijida ya kusahau ni lazima alete sijida ya

kusahau na akishuku katika Idadi ya rukuu na kunuti na akawa ame-

jishughulisha na kinachofuatia basi asizingatie shaka yake.

HUKUMU ZA SAUMU

979. Saumu ni kujizuia na vitu vyote ambavyo vinafuturisha ( ambavyo

vinamtoa mtu katika funga) kuanzia Adhana ya Alfajiri hadi Adhana

ya magharibi kwa kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu, tutataja

vinavyotengua saumu baadae

NIA

980. Si wajibu mfungaji kutamka kwa ulimi au kwa moyo mfano mtu

kusema “ nafunga kesho” bali inatosha kujizuia na vinavyobatilisha

saumu kuanzia adhana ya Alfajiri mpaka adhana ya magharibi kwa

kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu lakini ili awe na yakini kwam-

ba amefunga kwa muda wote inamlazimu kujizuia na vinavyobatil-

isha saumu kabla adhana ya Alfajiri kwa muda mchache na kufuturu

baada ya adhana ya magharibi kwa muda mchache vile vile.

981. Inajuzu mfungaji kunuia kwa kila siku katika siku za mwezi wa

Ramadhani kwa saumu ya siku inayofuata na ni bora kunuia katika

usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani kwa nia ya kufunga

mwezi mzima.

982. Muda wa nia ya funga ya mwezi wa Ramadhani ni mwanzo wa usiku

mpaka adhana ya asubuhi.

202

Al-Masailul Islamiyah

Page 217: al-Masailu-l-Islamiyyah

983. Muda wa nia ya saumu ya sunna ni mwanzo wa usiku mpaka kuza-

ma jua kwa kadri ya nia, ikiwa hajajishughulisha na kitu cha kuten-

gua saumu mpaka wakati wote huo na akanuia saumu ya sunna basi

saumu inasihi.

984. Mwenye kulala kabla ya adhana ya asubuhi bila ya kunuia saumu

akiamka kabla ya adhana na akanuia funga inasihi funga yake, iwe

funga yake ni ya wajibu au ya sunna na lau akiamka baada ya

adhuhuri haitatosha kunuia funga ya wajibu.

985. Akitaka kuleta saumu ambayo siyo ya mwezi wa Ramadhani ni

wajibu kwake kuiainisha saumu mfano anuie “ nafunga kadha au

nadhiri” lakini katika mwezi wa Ramadhani sio lazima anuie

“nafunga mwezi wa Ramadhani” bali akifunga kwa kutojua au

kusahau kwamba yuko katika mwezi wa Ramadhani na akanuia

vinginevyo anahesabiwa kuwa kafunga mwezi wa Ramadhani. Ikiwa

anajua ni mwezi wa Ramadhani na akanuia saumu isiyokuwa ya

mwezi wa Ramadhani kwa makusudi hata hesabiwa si katika mwezi

wa Ramadhani wala saumu nyingine ambayo amenuia.

986. Akifunga mfano kwa nia ya mwanzo wa mwezi wa Ramadhani,

kisha akatambua baadae kwamba ilikuwa siku ya pili au ya tatu ya

mwezi wa Ramadhani inasihi funga yake.

987. Akinuia kufunga kabla adhana ya Asubuhi kisha akazimia na kuzin-

duka katikati ya mchana, kwa tahadhari ya wajibu atimize saumu

ya siku hiyo na kuilipa kadha siku nyingine.

988. Akinuia kufunga kabla ya adhana ya asubuhi kisha akalala na asi-

amke ila baada ya magharibi, itasihi saumu yake.

989. Hakuna mushikeli mwenye kujiajiri kulipa kadha ya saumu ya maiti

kufunga saumu yake ya sunna, lakini kwa yule ambaye alikuwa na

203

Al-Masailul Islamiyah

Page 218: al-Masailu-l-Islamiyyah

kadha ya saumu iliyopita haijuzu kwake kuleta saumu ya sunna na

lau akifunga saumu ya sunna kwa kusahau akikumbuka kabla ya

adhuhuri inabatilika saumu yake ya sunna na inajuzu kubadili nia

yake ya sunna kwa nia ya saumu ya kadha ambayo ni wajibu wake

na lau akikumbuka baada ya adhuhuri itakuwa imebatilika saumu

yake ya sunna na lau akikumbuka baada ya magharibi itakuwa ime-

sihi saumu yake ya sunna

990. Kafiri akisilimu katika mwezi wa Ramadhani kabla ya Adhuhuri,

haitosihi saumu yake hata kama hajala kitu chochote kwa muda wote

huo na hata kama atakuwa amenuia kabla ya Adhuhuri.

991. Akifunga siku ya shaka kwamba ni mwisho wa Shaban au mwanzo

wa mwezi.wa Ramadhani kwa nia ya saumu ya kadha au saumu ya

sunna au vinginevyo kisha akajua wakati huo ni siku ya mwezi wa

Ramdahani inamuwajibikia abadili nia yake ya mwanzo aliyokuwa

nayo kwenda kwenye nia ya mwezi wa Ramadhani

VINAVYOTENGUA SAUMU

992. Vitenguzi vya saumu ni kumi:-

1. Kula

2. Kunywa

3. Jimai

4. Punyeto

5. Kumzulia Mwenyezi Mungu uongo au Mtume Muhammad (

saww) au Maimamu ( as) au Fatma Zahara (as)

6. Kufika vumbi zito kwenye koo

7. Kuzamisha kichwa chote kwenye maji

8. Kubaki na janaba au hedhi au nifasi mpaka adhana ya asubuhi

9. Kupiga bomba

10. Kujitapisha makusudi

204

Al-Masailul Islamiyah

Page 219: al-Masailu-l-Islamiyyah

1 na 2 Kula na kunywa

993. Akila mfungaji au akinywa kitu kwa makusudi basi saumu yake

inabatilika ni sawa kile kilicholiwa au kilichonywewa ni kili-

chozoeleka kama vile mkate, maji na mfano wake au visivyozoeleka

kama vile kula udongo na kunywa maji maji ya miti ni sawa kili-

choliwa au kilichonywewa ni kidogo sana au ni kingi inabatilika

saumu hata kwa kurudisha maji maji ya mswaki mdomoni baada ya

kuutoa kwake na kumeza maji maji yake kwa haraka isipokuwa yaki-

malizika maji maji ya mswaki katika maji ya mdomoni kiasi kwam-

ba haihesabiki kuwa amemeza maji maji ya kutoka nje.

994. Mfungaji akijua kuingia kwa Alfajiri na akawa anakula ni wajibu

ateme kile alichokitia mdomoni kwa haraka na lau akikimeza kwa

kusudi itabatilika saumu yake na inamuwajibikia kulipa kadha na

kutoa kafara. Akila mfungaji au akinywa kitu kwa kusahau, haito-

batilika saumu yake.

995. Ni vizuri zaidi mfungaji kujiepusha kutumia bomba kwa ajili ya tiba,

sindano zenye kuongeza lishe mwilini au kuongeza nguvu, hakuna

tatizo kutumia sindano zingine kwani hazibatilishi saumu kama sin-

dano za ganzi na sindano za dawa.

996. Mfungaji akimeza mabaki ya chakula yaliyobaki kwenye meno yake

kwa makusudi inabatilika saumu yake.

997. Mwenye kutaka kufunga si wajibu kwake kuondosha mabaki ya

chakula yaliyobaki kwenye meno yake kabla ya adhana ya Alfajiri

lakini akijua au akapata yakini kwamba mabaki yataingia kwenye koo

lake wakati wa mchana ikiwa hakutoa mabaki hayo kwenye meno

yake na kikaingia kitu katika mabaki ya chakula kwenye koo lake

inabatilika saumu yake kwa tahadhari.

205

Page 220: al-Masailu-l-Islamiyyah

998. Kumeza mate hakubatilishi saumu hata yakijikusanya mdomoni

kutokana na kuhisi athari ya uchachu na vinavyofanana na hivyo.

999. Mfungaji akipatwa na kiu kali kiasi kwamba anapatwa na matatizo au

akiogopa kupata madhara kwa sababu ya kiu, inajuzu kwake kunywa

maji kiasi cha kumwondoshea madhara lakini inabatilika saumu yake

na ni wajibu kujiepusha na vitu vingine vinavyobatilisha saumu

mchana wote ikiwa ni katika mwezi wa Ramadhani.

1000. Kumtafunia mtoto chakula au ndege na kuonja na mfano wake

ambapo kwa kawaida hakifiki mpaka kwenye koo haibatilishi

saumu hata kama ikifika kwenye koo ghafla lakini ikiwa alikuwa

anajua mwanzo kwamba chakula kitafika mpaka kwenye koo ita-

batilika saumu yake na inamlazimu ailipe na ni wajibu atoe kafara

pia.

JIMAI

1001. Jimai inabatilisha saumu hata kama hakuingiza ila kiasi cha kichwa

cha dhakari na ikawa manii hayajatoka . Akiingiza kiasi kidogo cha

kichwa cha dhakari na ikawa hayajatoka manii haibatiliki saumu

yake.

1002. Akitia shaka je ameingiza kiasi cha kichwa cha dhakari au laa inasi-

hi saumu yake.

1003. Akifanya jimai kwa kusahau kwamba amefunga au kulazimishwa (

kwa nguvu bila ya hiyari yake) saumu yake haibatiliki, lakini

akikumbuka aliye sahau au akaacha kulazimishwa ni wajibu

kuacha jimai na kama hataacha basi inabatilika saumu yake.

206

Al-Masailul Islamiyah

Page 221: al-Masailu-l-Islamiyyah

PUNYETO “ KUCHEZEA UTUPU”

1004. Mfungaji akifanya punyeto kwa kutumia njia ya kuchezea utupu

wake kujitoa manii na akajitoa manii saumu yake inabatilika.

1005. Yakimtoka mtu manii bila ya hiyari yake haibatiliki saumu yake,

lakini akifanya yale ambayo yanamfanya kutoka manii bila ya hiyari

inabatilika saumu yake.

1006. Akijua mfungaji kwamba akilala mchana ataota, haitomlazimu

kuacha kulala na akilala na akaota haitabatilika saumu yake.

1007. Akiamka mfungaji katika hali ya kutoka manii haimlazimu

kujizuia kutoka manii.

1008. Mfungaji aliyejiotea akijua kubakia manii katika njia ya mkojo na

kwamba asipokojoa kabla ya kuoga yatamtoka manii baada ya

kuoga, inalazimu kwa tahadhari ya sunna akojoe kabla ya kuoga

1009. Mfungaji akimchezea mtu kwa kusudi la kutoa manii inabatilika

saumu yake kwa tahadhari hata kama hayatamtoka manii.

1010. Mfungaji akimchezea mtu sio kwa kusudio la kutoka manii, ikiwa

anamatumaini kwamba manii hayatamtoka inasihi saumu yake,

hata kama yatatoka bila kutarajia, lakini ikiwa hakuwa na matu-

maini ya kutotoka manii saumu yake itabatilika kama yatamtoka

207

Al-Masailul Islamiyah

Page 222: al-Masailu-l-Islamiyyah

KUMZULIA MWENYEZI MUNGU UONGO,

MTUME (SAWW) NA MAIMAMU (AS).

1011. Akinasibisha mfungaji kwa makusudi uongo kwa Mwenyezi

Mungu au Manabii au Maimamu watukufu (as) kwa kutamka au

kuandika au kuashiria na mfano wake inabatilika saumu yake hata

kama atatubu haraka au akisema nimesema uongo, na kwa tahad-

hari ya wajibu kama atamsingizia Fatma Zahara ( as) vilevile

inabatilisha saumu.

1012. Akinukuu kitu kutoka kwa Mwenyezi Mungu au Nabii au Imamu

maasum (as) kwa itikadi kwamba alichokinukuu ni sahihi kisha

baadae akabaini kuwa sio sahihi, saumu yake haibatiliki.

1013. Ikiwa anajua kwamba kunasibisha uongo kwa Mwenyezi Mungu

au Mtume wake ( saww) inabatilisha saumu na akakusudia kunasi-

bisha kwa yale anayojua uongo wake, kisha akajua baadae kwamba

yale aliyoyasema yalikuwa ya kweli, atalipa kadha ya siku hiyo kwa

tahadhari ya wajibu.

1014. Akiulizwa mfungaji je, amesema Mtume ( saww) maudhui haya au

hapana? Na ilikuwa inampasa aseme hapana lakini yeye akajibu

kwa kusudi ndio badala ya hapana basi inabatilika saumu yake

1015. Akitoa habari kuhusu Mwenyezi Mungu au Mtume wake ( saww)

za kweli, kisha akasema nimesema uongo au akanasibisha juu yao

uongo usiku kisha akatilia mkazo katika mchana wa funga inabati-

lika saumu yake.

208

Al-Masailul Islamiyah

Page 223: al-Masailu-l-Islamiyyah

KUFIKA VUMBI ZITO KWENYE KOO

1016. Kufika vumbi zito kwenye koo kunabatilisha saumu, ni sawa likiwa

ni vumbi la kilicho halali kuliwa, kama vile vumbi la unga wa

ngano, au vumbi la kilichoharamu kuliwa, kama vile vumbi la udon-

go, na kwa tahadhari lisifike kabisa vumbi lisilokuwa zito kooni pia.

1017. Vumbi zito likitimka kwa sababu ya upepo na akawa hajazuia mfun-

gaji vumbi kufika kooni kwa kutokuwa mwangalifu bila ya kughafi-

lika na vumbi likafika kooni inabatilika saumu yake.

1018. Kwa tahadhari ya wajibu usimfikie mfungaji moshi mzito wa sigara

na tumbaku na mfano wake kwenye koo pia, hakuna mushikeli kati-

ka moshi mdogo wa kawaida uliopo katika bafu.

1019. Ikiwa mfungaji hakujihifadhi likaingia vumbi zito au moshi mzito

na mfano wake vikaingia kwenye koo ikiwa alikuwa na matumaini

au yakini ya kutofika mpaka kwenye koo inasihi saumu yake, na

ikiwa aliacha kujihifadhi kwa dhana ya kutoingia mpaka kwenye

koo basi inamlazimu kwa tahadhari kuleta kadha ya saumu hiyo.

1020. Akisahau kwamba amefunga na akaacha kujihifadhi kutofika vumbi

mpaka kwenye koo lake au kuingia vumbi na mfano wake vikain-

gia mpaka kwenye koo lake bila ya hiyari yake, haibatiliki saumu

yake.

209

Al-Masailul Islamiyah

Page 224: al-Masailu-l-Islamiyyah

KUZAMISHA KICHWA KWENYE MAJI

1021. Mfungaji akizamisha kichwa chake kwenye maji (Yaani akaingiza

kichwa chake chote kwenye maji ) kwa kusudi inabatilika saumu

yake na hakuna kafara juu yake, hata kama mwili wake umebaki nje

ya maji, lakini haitabatilika saumu yake lau akizamisha mwili wake

wote kwenye maji na kikabaki kichwa chake nje ya maji.

1022. Akiingiza nusu ya kichwa chake kwenye maji mara moja na akain-

giza nusu nyingine kwa mara nyingine haibatiliki saumu yake.

1023. Akishuku kwamba je ameingiza na amezamisha kichwa chake

chote katika maji au laa inasihi saumu yake.

1024. Akizamisha kichwa chake katika maji lakini zikabakia nywele za

kichwa chake nje ya maji inabatilika saumu yake.

1025. Kwa tahadhari ya wajibu asizamishe kichwa chake kwenye maji

mudhafu.

1026. Akianguka mfungaji kwenye maji bila ya hiyari yake na akaingiza

kichwa chake chote kwenye maji au akazamisha kichwa chake chote

kwenye maji kwa kusahau kwamba amefunga haibatiliki saumu

yake.

1027. Mfungaji akijiingiza mwenyewe kwenye maji na alikuwa na uhaki-

ka kwamba maji hayatofunika kichwa chake, yakifunika kichwa

chake haitobatilika saumu yake, ama ikiwa hakuwa na uhakika na

akajiingiza kwenye maji, na maji yakafunika kichwa chake inam-

lazimu alete kadha ya saumu hiyo kwa tahadhari ya wajibu.

1028. Akizamisha kichwa chake chote kwenye maji kwa nia ya kuoga na

akawa amesahau kwamba amefunga inasihi kuoga kwake na funga

210

Al-Masailul Islamiyah

Page 225: al-Masailu-l-Islamiyyah

yake.

1029 Akikusudia kuzamisha kichwa chake chote katika maji kwa ajili ya

kuoga na anajua kwamba amefunga, ikiwa saumu yake ni saumu ya

mwezi wa Ramadhani au ya wajibu maalumu inabatilika kuoga

kwake na saumu yake, na ikiwa saumu yake ni ya sunna au ya waji-

bu usio kuwa maalumu kwa wakati, mfano saumu ya kafara inasihi

kuoga kwake na inabatilika funga yake.

1030. Akizamisha kichwa chake chote katika maji kwa ajili ya kuokoa

(mtu) aliye zama kwenye maji inamlazimu kuleta kadha ingawa

kumuokoa yule mtu ni wajibu

KUBAKI NA JANABA AU HEDHI AU NIFASI

MPAKA ALFAJIRI

1031. Mwenye janaba asipooga mpaka adhana ya alfajiri kwa kusudi au

wadhifa wake ulikuwa ni kutayamamu na akawa hajatayamamu kwa

kusudi mpaka ikafika alfajiri inabatilika saumu yake katika mwezi

wa Ramadhani au kadha yake, ama zisizokuwa hizo katika funga za

wajibu na sunna haibatiliki, na kwa tahadhari ya sunna kutoacha

kuoga au kutayamamu kabla ya alfajiri, hasa katika wajibu maalum

kama vile saumu ya nadhiri ya siku maalum.

1032. Asipooga au asipotayamamu mpaka adhana ya Alfajiri katika

saumu ya wajibu ya wakati maalum kama vile saumu ya Ramadhani,

lakini sio kwa kusudi, au kama akizuiwa na mtu kuoga au kutaya-

mamu inasihi saumu yake.

1033. Mwenye janaba ambaye anataka kuleta saumu ya wajibu kama vile

211

Al-Masailul Islamiyah

Page 226: al-Masailu-l-Islamiyyah

saumu ya mwezi wa Ramadhani, ikiwa hajaoga kwa kusudi mpaka

wakati ukawa mfinyu ni wajibu atayamamu na afunge na saumu

yake itasihi, ingawa ni bora kwake alipe kadha ya saumu hiyo pia.

1034. Mwenye janaba akisahau kuoga katika mwezi wa Ramadhani na

akakumbuka baada ya kupita siku ni wajibu arudie saumu ya siku

hiyo, na akikumbuka baada ya siku nyigine inamlazimu kulipa

kadha ya siku ambazo anayakini kuwa alikuwa na janaba, mfano

kama hakujua amebaki na janaba siku tatu au nne ni wajibu alipe

saumu ya siku tatu kwa babu ndio kiasi alicho na yakini.

1035. Mwenye kukusudia kupata janaba katika siku za Ramadhani kati-

ka wakati usiotosheleza kuoga na kutayamamu inabatilika saumu

yake, na ni wajibu kwake kulipa kadha na kafara ,lakini akisababi-

sha kupata janaba katika wakati unaotosha kwa kutayamamu ni

wajibu kwake atayamamu na afunge ,na ni bora alipe kadha ya siku

hiyo.

1036. Mwenye kuwa na janaba katika usiku wa mwezi wa Ramadhani au

akajua kwamba lau akilala hataamka mpaka alfajiri, ni wajibu

kwake asilale, na akilala na asiamke mpaka alfajiri inabatilika

saumu yake na ni wajibu kwake kadha na fakara.

1037. Akilala mwenye janaba usiku katika mwezi wa Ramadhani inaju-

zu kwake kulala mara ya pili kabla ya kuoga ikiwa ni kawaida

yake kuamka kabla ya alfajiri, na ikiwa sio kawaida yake kuamka

inajuzu kwake kulala kabla ya kuoga lau akitarajia kuamka mara

ya pili kabla ya adhana ya Alfajiri, na kwa tahadhari asilale mpaka

aoge.

1038. Mwenye kuwa na janaba usiku katika mwezi wa Ramadhani aki-

tambua au ni kawaida yake kuamka kutoka usingizini kabla ya

adhana ya Alfajiri ikiwa amenuia kuoga baada ya kuamka kwake na

akalala na nia hiyo mpaka Alfajiri inasihi saumu yake.

212

Al-Masailul Islamiyah

Page 227: al-Masailu-l-Islamiyyah

1039. Mwenye janaba katika usiku wa mwenzi wa Ramadhani na ambaye

anajua au anatarajia kwamba ataamka kabla ya adhana ya Alfajiri

ikiwa hakutaka kuoga baada ya kuamka au akasitasita kwamba aoge

au laa lau akilala na asiamke inabatilika saumu yake na ni juu yake

kulipa kadha pamoja na kafara.

1040. Akijiotea mfungaji mchana sio wajibu kwake kufanya haraka kuoga

japo ni bora kufanya hivyo.

1041. Akiamka mfungaji katika mwezi wa Ramadhani baada ya adhana

ya Alfajiri akakuta amejiotea inasihi saumu yake hata kama aki-

tambua kuwa amejiotea kabla ya adhana

1042. Mwenye kutaka kulipa kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani

akibakia na janaba mpaka adhana ya Alfajiri inabatilika saumu yake

hata kama hakufanya hivyo kwa makusudi.

1043. Mwenye kutaka kulipa kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani

akiamka baada ya adhana ya Alfajiri na akakuta amejiotea na aka-

tambua kwamba amejiotea kabla ya adhana ikiwa wakati wa kadha

ni mfinyu, mfano ikiwa ni juu yake kulipa kadha ya siku tano na

haikubakia hadi mwezi wa Ramadhani ila siku tano tu, inamlazimu

afunge siku hiyo kwa tahadhari na afunge badala yake baada ya

mwezi wa Ramadhani vilevile, na ikiwa wakati wa kadha sio mfu-

nyu inabatilika saumu yake.

1044. Akibakia na janaba mpaka adhana ya Alfajiri katika saumu ya waji-

bu isiyokuwa saumu ya mwezi wa Ramadhani au kadha yake laki-

ni sio kwa makusudi ikiwa saumu hiyo ni ya wajibu maalumu kwa

wakati, mfano ikiwa aliweka nadhiri kufunga siku hiyo inasihi

saumu yake na ikiwa siyo ya wajibu maalumu mfano saumu ya

kafara basi kwa tahadhari ya sunna afunge badala ya siku hiyo siku

nyingine

213

Al-Masailul Islamiyah

Page 228: al-Masailu-l-Islamiyyah

1045. Akitoharika mwanamke kutokana na hedhi au nifasi kabla ya adha-

na ya Alfajiri na akawa hajaoga kwa makusudi au ilikuwa wadhifa

wake ni kutayamamu na akawa hajatayamam kwa makusudi inaba-

tilika saumu yake katika mwezi wa Ramadhani bali na katika kadha

na katika kila wajibu maalumu vile vile kwa tahadhari.

1046. Mwanamke ambaye anatoharika kutokana na hedhi au nifasi kabla

ya adhana ya Alfajiri pia mwenye janaba ikiwa wakati hautoshi

kwa kuoga, akitaka kufunga ni wajibu kwake kutayamamu na

inasihi saumu yake kwa ilivyo na nguvu zaidi, ni sawa sawa iliku-

wa ni saumu ya mwezi wa Ramadhani au ya wajibu maalumu au ya

sunna.

1047. Akitoharika mwanamke kutokana na damu ya hedhi au nifasi kabla

ya adhana ya Alfajiri na muda ukawa hautoshi sio kwa kuoga wala

kutayamamu, au akajua baada ya adhana kwamba alishatoharika

kabla ya adhana akitaka kufunga saumu ya wajibu maalumu kama

vile saumu ya mwezi wa Ramadhani inasihi saumu yake, vivyo

hivyo ikiwa saumu yake ni ya sunna au wajibu isiyo kuwa maalu-

mu kama vile saumu ya kafara, inasihi saumu yake kwa kauli yenye

nguvu zaidi.

1048. Akitoharika mwanamke kutokana na damu ya hedhi au nifasi baada

ya adhana ya Alfajiri au akaona damu ya hedhi au nifasi katikati ya

mchana inabatilika saumu yake hata kama imekaribia magharibi.

1049. Akisahau mwanamke kuoga josho la hedhi au nifasi na akakumbu-

ka baada ya siku au zaidi inasihi saumu ya siku alizofunga

1050. Mwanamke mwenye istahadha akileta josho zilizotajwa katika

hukumu za istihadha inasihi saumu yake.

1051. Mwenye kugusa maiti inajuzu kwake kufunga bila ya kuoga muogo

wa kugusa maiti na akigusa maiti katika hali ya kufunga haibatiliki

214

Al-Masailul Islamiyah

Page 229: al-Masailu-l-Islamiyyah

saumu yake.

KUPIGA BOMBA

1052. Kupiga bomba katika utupu wa nyuma kwa vitu vya maji maji

inabatilisha saumu na hakuna kafara juu yake hata kama ni dharu-

ra au ilikuwa ni kwa ajili ya tiba, hakuna tatizo katika bomba isiyo

ya maji maji japo ni bora kujiepusha nayo.

KUTAPIKA

1053. Akikusudia mfungaji kutapika hata kama akilazimika kwa ajili ya

maradhi na mfano wake inabatilika saumu yake na hakuna kafara

juu yake lakini akitapika kwa kusahau au bila hiyari yake inasihi

saumu yake.

1054. Akiweza mfungaji kuzuia kutapika inalazimu ajizuie, ikiwa haita-

sababisha madhara au matatizo juu yake.

1055. Akiingia mbu au mfano wake katika koo lake lazima amtoe ikiwe-

zekana na wala haibatiliki saumu yake, lakini akijua kumtoa kwake

itamsababisha kutapika haimlazimu kumtoa na inasihi saumu yake.

1056. Akicheua na kikapanda kitu mpaka kwenye koo lake au mpaka

kwenye kinywa chake ni wajibu akiteme nje na lau akimeza bila

hiyari yake inasihi saumu yake lakini ikiwa hakijafika kwenye koo

lake basi hakuna tatizo

HUKUMU YA VITENGUZI

215

Al-Masailul Islamiyah

Page 230: al-Masailu-l-Islamiyyah

1057. Akileta mfungaji moja ya vitenguzi kwa kusudi inabatilika saumu

yake na hakuna tatizo kwayo ikiwa sio kwa makusudi, lakini aki-

lala na janaba na ikawa hajaoga mpaka adhana ya Alfajiri inabatili-

ka saumu yake.

1058. Mtu yeyote akiingiza kitu katika koo la mfungaji kwa lazima au

akaingiza kichwa chake kwenye maji kwa kumteza nguvu haitaba-

tilika saumu yake, lakini akilazimishwa kubatilisha saumu yake

kama lau akiambiwa ikiwa huli chakula tutakudhuru kimali au kim-

wili akala kuepuka madhara inabatilika saumu yake.

1059. Inamlazimu mfungaji asiende sehemu ambayo anajua kwamba ana-

weza kulazimishwa kufungua na akifanya wakati huo kinachoten-

gua saumu kwa kulazimishwa inabatilika saumu yake.

YALIYO MAKURUHU KWA MFUNGAJI

1060. Ni makuruhu kwa mfungaji kufanya mambo yafuatayo:-

1. Kuweka dawa kwenye macho

2. Kupaka wanja, kama ladha yake au harufu yake itafika hadi kwe-

nye koo

3. Kufanya kila chenye kusababisha udhaifu kama vile kuumika au

kujisaidia kwa wingi

4. Kuvuta ugoro “puani” ikiwa hajui kufika kwake hadi kooni, na

kwa tahadhari ya wajibu ni kuacha hayo pamoja na kujua kuwa

utafika hadi kooni

5 .Kunusa mimea yenye harufu (manukato)

6. Mwanamke kukaa ndani ya maji

7. Kuingiza vitu (vikavu) katika njia ya haja kubwa

8. Kuloanisha nguo ambayo iko mwilini

9. Kun’goa jino na kila ambacho kinasababisha kutoka damu mdomoni

10. Kupiga mswaki kwa mti mbichi

216

Al-Masailul Islamiyah

Page 231: al-Masailu-l-Islamiyyah

11 .Kutia maji mdomoni au kisichokuwa maji mdomoni bila ya sababu

12 .Kumbusu mke bila kusudi la kutoka manii

13 .Kitendo ambacho kinachosababisha kuamsha matamanio na ikiwa ni

kwa kusudi la kutoka manii inabatilika saumu yake.

MAMBO AMBAYO NI WAJIBU KULIPA

KADHA NA KUTOA KAFARA

1061. Mfungaji akikusudia kutapika au kuzama katika maji au kujipiga

bomba kwa kitu cha maji maji mchana au akiwa na janaba usiku na

akaamka kama tulivyoeleza katika Mas’ala yaliyotangulia, kisha

akalala mara ya pili na akawa hajaamka mpaka adhana ya Alfajiri

ni wajibu kwake kadha tu, na lau akileta kitenguzi kingine kwa

makusudi ikiwa anajua kuwa jambo hili linabatilisha saumu yake ni

wajibu kwake kadha na kafara, lakini kafara katika kukusudia kuse-

ma uongo juu ya Mwenyezi Mungu au Mtume na Ahlul- bait wake

(as) ni katika upande wa tahadhari ya wajibu, na katika kukusudia

kutapika au kuzama kwenye maji au kupiga bomba kwa kitu cha

maji maji ni katika upande wa tahadhari ya sunna.

KAFARA ZA SAUMU

1062. Ambaye ni wajibu kutoa kafara ya saumu ya mwezi wa Ramadhani

inamlazimu kumuacha mtumwa huru au afunge miezi miwili mfu-

lulizo au alishe maskini sitini au ampe kila mmoja miongoni mwao

kibaba ( robo tatu ya kilo ) ya ngano au shairi au mfano wake, na

ikiwa hataweza hivi vitu anakuwa na hiyari baina ya kufunga siku

kumi na nane mfululizo au alishe mafukara kadri atakavyoweza, na

ikiwa hakuweza kufunga wala kulisha ni wajibu kwake alete isti-

ghifari kwa Mwenyezi Mungu kwa kusema mara moja (

Astaghafiru llaahi) na kwa tahadhari ya wajibu atoe kafara atakapo-

weza na kupata uwezo wa kimali.

217

Al-Masailul Islamiyah

Page 232: al-Masailu-l-Islamiyyah

1063. Mfungaji akifanya jimai mara nyingi wakati wa mchana wa mwezi

wa Ramadhani atatoa kwa kila mara kafara ikiwa amemwingilia

kwa halali, ama ikiwa kumwingilia kwake ni haramu ni wajibu

kwake kila mara atoe kafara zote tatu kwa pamoja.

1064. Akileta mfungaji kitenguzi kisichokuwa jimai kisha akamwingilia

mke wake kwa tahadhari ya wajibu atoe kafara ya kila moja katika

hayo.

1065. Akileta mfungaji kitendo cha halali ambacho kinabatilisha saumu

kisichokuwa jimai, kama vile kunywa maji, kisha akaleta kitendo

cha haramu kinachobatilisha saumu kisicho kuwa jimai pia, kama

lau akila chakula cha haramu inamtosha kafara moja kwa yote.

1066. Akicheua mfungaji na kikapanda kitu mpaka mdomoni kwake, aki-

kimeza makusudi inabatilika saumu yake na ni wajibu kwake kadha

na kafara pamoja, na ikiwa kile kitu kinaharamishwa kuliwa kwake

kama lau akicheua ikatoka damu mpaka mdomoni mwake kisha

akameza damu kwa kusudi inabatilika saumu yake na ni wajibu juu

yake kulipa kadha, na kwa tahadhari ya wajibu pia kutoa kafara ya

kukusanya zote.

1067. Akiweka nadhiri ya kufunga siku maalumu akibatilisha saumu

yake katika siku hiyo kwa makusudi ni wajibu wake amuache

mtumwa huru au afunge miezi miwili mfululizo au alishe masikini

sitini.

1068. Mfungaji akikusudia kubatilisha saumu yake kisha ukamtokea

udhuru usiokuwa wa hiyari kama hedhi au nifasi au maradhi sio

wajibu kwake kutoa kafara

1069. Akipata yakini kwamba ni mwanzo wa Ramadhani na akabatilisha

saumu yake kwa kusudi kisha akabaini kwamba ilikuwa mwisho wa

218

Al-Masailul Islamiyah

Page 233: al-Masailu-l-Islamiyyah

Shabani sio wajibu kwake kafara.

1070. Mfungaji akifanya jimai katika mwezi wa Ramadhani mke wake

ambaye amefunga, ikiwa amemlazimisha katika kumwingilia (

yaani hakuwa radhi) ni wajibu kutoa kafara yake na kafara ya (

mke wake) pia, ama ikiwa alikuwa ameridhia kuingiliwa ni waji-

bu kwa kila mmoja atoe kafara yake.

1071. Mfungaji akikimwingilia mke wake ambaye amefunga katika

mwezi wa Ramadhani hali akiwa amelala bila ya kuelewa ni

wajibu kwake kafara moja na inasihi saumu ya mke na siyo waji-

bu kwake kulipa kadhaa wala kafara.

1072. Ambaye hafungi kwa ajili ya safari au maradhi haijuzu kwake

kumlazimisha mke wake ambaye amefunga kufanya jimai, lakini

akimlazimisha kumwigilia sio wajibu kutoa kafara.

1073. Ni wajibu kutozembea kutoa kafara lakini sio wajibu kufanya hara-

ka.

1074. Ambaye analipa kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani

akikusudia kufanya kinachobatilisha saumu baada ya adhuhuri ni

wajibu juu yake kulisha maskini kumi, kila maskini kibaba na

akishindwa hivyo afunge siku tatu.

MAMBO AMBAYO NI WAJIBU KULIPA

219

Al-Masailul Islamiyah

Page 234: al-Masailu-l-Islamiyyah

KADHA YA SAUMU BILA KAFARA

1075. Ni wajibu kulipa kadha ya saumu bila kafara katika mambo yafu-

atayo:-

1. Akikusudia mfungaji kujitapisha au kuzama katika maji au kupiga

bomba za sindano za maji maji mchana wa mwezi wa Ramadhani haku-

na kafara ila katika upande wa tahadhari ya sunna.

2. Akiwa na janaba usiku wa mwezi wa Ramadhani na ikawa hakuzin-

duka katika usingizi wake mara ya pili mpaka adhana ya Alfajiri kwa

namna ya mifano ambayo imepita katika mas’ala yaliyotangulia.

3. Ambaye hajafanya kinachotengua saumu lakini hakunuia saumu au

amekusudia kutokufunga au anakusudia kufanya kinachobatilisha

saumu - kwa tahadhari.

4. Kusahau kuoga janaba katika mwezi wa Ramadhani na akafunga

pamoja na janaba siku moja au siku nyingi.

5. Mwenye kuleta kinachobatilisha saumu bila ya kuhakikisha kuwa ni

asubuhi katika mwezi wa Ramadhani kisha akabaini kuingia kwa asu-

buhi ni wajibu kwake kulipa kadha ya siku hiyo, na vile vile mwenye

kuleta kinacho batilisha saumu baada ya kuhakikisha kuwa ni asubu-

hi kwa kudhania kuingia asubuhi, bali hata mwenye kushuku kuingia

kwa asubuhi baada ya kuhakiki na akaleta kinachobatilisha kisha aka-

baini kuingia kwa asubuhi ni wajibu kwake kulipa kadha

6. Mtu kupewa taarifa kutoingia asubuhi akaleta vinavyobatilisha kwa

kauli ya mtoa habari kisha ikabainika kwake baada ya muda kwamba

ilikuwa asubuhi.

7. Akipewa taarifa na mtu kuingia kwa asubuhi akawa hajaamini haba-

ri aliyopewa na mtoa habari au akachukulia kuwa mtoa habari ana mfa-

220

Al-Masailul Islamiyah

Page 235: al-Masailu-l-Islamiyyah

nyia mzaha akaleta vinavyobatilisha kisha ikabainika kwake baada ya

muda kwamba ilikuwa asubuhi.

8. Akifungua kipofu kwa kutegemea habari ya mtoa habari kisha aka-

baini kutoingia kwa magharibi.

9. Akiwa na yakini kuingia kwa magharibi katika anga safi kwa sababu

ya giza akafungua kisha akabaini kwamba haikuwa imeingia maghari-

bi, lakini akiwa na matumaini ya kuingia magharibi katika anga lilofu-

nikwa kwa mawingu haimlazimu kulipa kadha pindi atakapofuturu

kisha ikabainika kutoingia kwa magharibi.

10. Akiingiza maji katika mdomo wake kwa kuleta ubaridi au bila ya

sababu yakaingia katika koo lake bila ya hiyari yake, na ama lau aki-

sahu kwamba amefunga akameza maji au akasukutua kwa ajili ya udhu

yakaingia maji katika koo lake bila hiyari yake hatolipa kadha.

1076. Akiingiza katika mdomo wake kitu kisichokuwa maji na kikaingia

katika koo lake bila hiyari yake au akisukutua kwa maji yakaingia

mpaka kwenye koo lake bila hiyari sio wajibu kwake kulipa kadha.

1077. Ni makuruhu kwa mfungaji kukithirisha kusukutua na akitaka

kumeza mate yake baada ya kusukutua ni bora ateme mara tatu kisha

ameze mate yake.

1078. Akipata shaka mfungaji je imeingia magharibi au laa , haijuzu

kwake kufuturu, lakini akishuku je imekuwa alfajiri au laa, inajuzu

kwake kufuturu baada ya kupata uhakika na kuchunguza

221

Al-Masailul Islamiyah

Page 236: al-Masailu-l-Islamiyyah

HUKUMU ZA SAUMU YA KADHA

1079. Kichaa akipona kichaa chake sio wajibu kwake kulipa kadha kwa

yaliyompita katika saumu siku za kichaa chake.

1080. Akisilimu kafiri siyo wajibu kwake kulipa kadha ya saumu iliyom-

pita katika siku za ukafiri wake, lakini lau akiritadi mwislam kisha

akasilim baada ya kuritadi ni wajibu kwake kulipa kadha kwa

yaliyompita katika saumu siku za kuritadi kwake.

1081. Ni wajibu kulipa kadha kwa yale yaliyompita katika saumu kwa

sababu ya kulewa au kwa kutumia kwake kitu cha kulevya kwa ajili

ya matibabu ya wajibu.

1082. Akifungua kwa siku nyingi kwa udhuru kisha akashuku wakati wa

kuondoka udhuru ikiwa ni kutokana na uzembe ni wajibu kwake

kwa tahadhari afunge siku nyingi zaidi kiasi cha kupata matumaini,

mfano lau akisafiri kabla ya mwezi wa Ramadhani na wala hajui

kwa uzembe, amerudi katika siku ya tano au ya sita katika mwezi wa

Ramadhani, ni wajibu wake afunge siku sita kwa tahadhari, ama

ikiwa hajui wakati wa kuondoka udhuru bila ya uzembe, inajuzu

kwake alete kadha kwa uchache yaani siku tano, ingawa kwa tahad-

hari ya sunna alipe kadha ya nyingi zaidi yaani siku sita.

1083. Ikiwa ni wajibu alipe kadha ya Ramadhani nyingi na akawa hajaai-

nisha katika nia kwamba anayoileta ni kadha ipi katika zile

Ramadhani, inahesabika kuwa ni kadha ya Ramadhani ya kwanza.

1084. Inajuzu kwa mwenye kufunga kadha ya mwezi wa Ramadhani

kufungua kabla ya adhuhuri ikiwa muda wa kadha sio mfinyu.

222

Al-Masailul Islamiyah

Page 237: al-Masailu-l-Islamiyyah

1085. Mtu akipitwa na saumu ya mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya hedhi

au nifasi au maradhi na akafa kabla ya kumalizika mwezi wa

Ramadhani sio wajibu kulipiwa kadha kwa yaliyompita katika

saumu ya mwezi huo.

1086 Akipitwa na saumu ya mwezi wa Ramadhani kwa ajili ya marad-

hi na yakaendelea maradhi yake mpaka Ramadhani nyingine hai-

tomuwajibikia kulipa kadha kwa yale yaliyompita katika saumu ya

mwezi huo, ni wajibu kwake ampe fakiri kwa kila siku kibaba cha

chakula, yaani ngano au mkate wake au kibaba cha shairi au mkate

wake, ama ikimpita saumu kwa ajili ya udhuru kama safari na

ukaendelea udhuru wake mpaka Ramadhani nyingine inalazimu

kwa tahadhari ya wajibu alipe saumu kwa siku ambazo zimempita

na ampe fakiri kibaba kwa kila siku.

1087. Ugonjwa ukichukua miaka mingi ni wajibu kwake kulipa kadha ya

Ramadhani ya mwisho tu baada ya kupona na atoe kibaba cha cha-

kula kwa kila siku iliyopita katika miaka iliyopita, yaani ngano,

shairi au mikate yake, tende au zabibu.

1088. Akichelewesha kadha ya saumu ya mwezi wa Ramadhani kwa

miaka mingi ni wajibu kwake kulipa kadha na kutoa fidia moja kwa

kila siku iliyompita.

1089. Akifungua katika mwezi wa Ramadhani kwa kusudi ni wajibu aili-

pe na afunge badala ya kila siku moja ( afunge) siku sitini au alishe

mafakiri sitini au amuache mtumwa huru, na ikiwa hatolipa

yaliyompita mpaka Ramadhani nyingine inamlazimu kutoa kibaba

kingine badala ya kila siku ambayo hakufunga ukiongezea na kafa-

ra, na inamlazimu vile vile kulipa saumu zilizompita.

1090. Ni wajibu kwa mtoto mkubwa kulipa yale yaliyompita baba yake

aliyefariki katika hali ya uhai wake katika saumu na swala kwa

223

Al-Masailul Islamiyah

Page 238: al-Masailu-l-Islamiyyah

mujibu wa maelezo ambayo yamepita katika mas’ala yaliyotangu-

lia, na vivyo hivyo amlipie mama yake baada ya kufariki kwake

yale yaliyompita katika uhai wake katika saumu na swala , kwa

tahadhari wajibu.

1091. Ikiwajibika kwa baba kulipa kadha ya saumu ambayo sio saumu ya

mwezi wa Ramadhani, mfano saumu ya nadhiri, inamlazimu mtoto

mkubwa kumlipia kwa tahadhari.

HUKUMU ZA SAUMU YA MSAFIRI

1092. Msafiri ambaye ni wajibu kwake kupunguza swala ni wajibu asi-

funge pia, na msafiri ambaye anakamilisha swala, mfano ambaye

safari ni kazi yake au safari yake ni safari ya maasia, ni wajibu afun-

ge.

1093. Hakuna mushikeli kusafiri katika mwezi wa Ramadhani lakini ni

makuruhu kusafiri ikiwa ni kwa ajili ya kukimbia saumu.

1094. Ikiwajibika kwa mtu funga maalum isiyokuwa saumu ya mwezi

wa Ramadhani kama vile saumu ya nadhiri maalum kwa wakati,

basi ni lazima asisafiri katika siku hiyo maadamu halazimiki kusa-

firi -tahadhari ya wajibu - na akisafari ni lazima akusudie kukaa

siku kumi na afunge kama inawezekana

1095. Akiweka nadhiri kufunga na akawa hajaainisha siku ambayo atafun-

ga kwayo haijuzu kuileta akiwa safarini, lakini lau akiweka nadhi-

ri kufunga siku maalumu katika safari basi lazima ailete katika safa-

ri, na vivyo hivyo akiweka nadhiri kufunga siku hiyo maalumu, ni

sawa akiwa katika safari au hayuko safarini ni wajibu kufunga siku

hiyo hata kama akiwa safirini.

224

Al-Masailul Islamiyah

Page 239: al-Masailu-l-Islamiyyah

1096. Inajuzu kwa msafiri kufunga sunna kwa siku tatu katika Mji wa

Madinatul- munawara kwa kuomba haja.

1097. Kwa yule ambaye hajui kwamba safari inabatilisha saumu akifunga

katika safari na katikati ya mchana akatambua hukumu, inabatilika

saumu yake, na asipotambua mpaka magharibi inasihi saumu yake.

1098. Akisahau kwamba yeye ni msafiri au akasahau kwamba saumu ya

msafiri ni batili na akafunga katika safari inabatilika saumu yake.

1099. Akisafiri mfungaji baada ya Adhuhuri ni wajibu akamilishe saumu

yake, na akisafiri kabla ya Adhuhuri na akakusudia kukata masafa

ya kisheria ( kama ilivyopita katika swala ya msafiri ) inalazimu

kutengua saumu yake pindi anapofika katika mpaka wa kupungu-

zia ( yaani kutokuonekana kuta za mji na kutosikika adhana yake),

na akibatilisha saumu yake kabla ya hapo ni wajibu kwake kafara

kwa tahadhari ya wajibu.

1100. Akifika mfungaji kabla ya adhuhuri katika mji wake au sehemu

ambayo anataka kukaa siku kumi hapo ikiwa hajaleta vinavyobati-

lisha saumu mpaka wakati huo ni wajibu afunge siku hiyo, na ikiwa

ameleta vinavyobatilisha saumu sio wajibu kwake kufunga siku

hiyo.

AMBAYE SIO WAJIBU KWAKE SAUMU

1101. Ikiwa hawezi kufunga saumu au saumu ina mletea matatizo kwa

ajili ya uzee sio wajibu kwake kufunga, lakini inamlazimu kutoa

kibaba cha chakula kwa maskini kwa kila siku kama yalivyotangu-

lia maelezo yake.

1102. Yule ambaye hawawezi kufunga kwa ajili ya uzee akiweza na aka-

pata upya uwezo wa kufunga baada ya mwezi wa Ramadhani inam-

lazimu alipe yale yaliyompita kwa tahadhari.

225

Al-Masailul Islamiyah

Page 240: al-Masailu-l-Islamiyyah

1103. Mwenye kiu ( ambaye anakuwa na kiu sana na hawezi kuvumilia

kiu au inamletea matatizo sana) sio wajibu kwake saumu na inam-

lazimu kutoa badala ya kila siku kibaba cha chakula kwa fakiri, kwa

mifano iliyopita maelezo yake na kwa tahadhari ya sunna asinywe

maji kwa wingi ila kwa kiwango cha dharura na inamlazimu kuli-

pa kadha kwa yaliyompita akiweza kufunga katika mwaka huo.

1104. Mwanamke anayenyonyesha mwenye maziwa machache, ni sawa

awe ni mama wa mtoto au ameajiriwa au ananyonyesha bila mali-

po, ikiwa saumu inamdhuru au inamdhuru anaye nyonya sio waji-

bu kwake kufunga, na ni wajibu atoe kwa fakiri badala ya kila siku

aliyofungua kibaba cha ngano au shairi au mikate yake, na ni waji-

bu alipe yaliyompita katika saumu akiweza kufunga katika mwaka

huo, na akijitolea mwenye kunyonyesha mtoto bila ya malipo au

akachukua ujira kwa baba wa mtoto au mama wa mtoto au mtu

mwingine akitoa ujira wake sio wajibu kwa mama kumpa mnyo-

nyeshaji mtoto, na kufunga.

1105. Mwanamke ambaye hawezi kufunga katika mwaka kwa sababu ya

kubeba mimba au kunyonyesha wala hakuweza kulipa katika

mwaka huo kwa sababu hiyo hiyo sio wajibu kwake kufunga wala

kulipa kadha, ni wajibu kutoa kwa maskini kwa kila siku vibaba

viwili vya chakula, kibaba baada ya mwezi wa Ramadhani na kiba-

ba kingine mwisho wa mwaka, yaani kabla Ramadhani ya pili.

NJIA ZA KUTHIBITI MWANZO

WA MWEZI

1106. Unathibiti mwanzo wa mwezi kwa mambo matano:-

1. Mtu mwenyewe kuuona mwezi mwandamo.

2. Kutoa habari ya kuonekana kwake watu ambao inapatikana yaki-

ni kutokana na maneno yao na vivyo hivyo kwa kila ambacho mtu

226

Al-Masailul Islamiyah

Page 241: al-Masailu-l-Islamiyyah

anapata yakini kwa sababu yake.

3. Kupata habari kwa ( watu wawili) waadilifu kwamba wameona

mwezi usiku, lakini wakihitalifiana katika wasifu wa mwezi hau-

tothibiti mwanzo wa mwezi.

4. Kumalizika kwa mwezi uliotangulia wa shabani siku thelethini,

hivyo unathibiti mwanzo wa mwezi wa Ramadhani na vivyo

hivyo kwa miezi mingine.

5. Kiongozi wa kidini akitangaza kuonekana kwa mwezi.

1107. Akihukumu kiongozi wa sharia “Marja’a” kuthibiti mwanzo wa

mwezi inalazimu kutekeleza hukumu yake hata kwa yule asiyemfu-

ata, ikiwa hakuhukumu kiongozi mwingine kupinga. Lakini

mwenye kujua kwamba kiongozi wa kisheria amekosea katika

hukumu yake basi hawezi kufanya kwa mujibu wa hukumu ya kion-

gozi huyo.

1108. Hauthibiti mwanzo wa mwezi kwa utabiri wa wanasayansi na wana-

jimu, lakini mtu akipata yakini kwa sababu ya habari yao ni

wajibu kufanya kwa mujibu wa habari yao.

1109. Ukithibiti mwezi mwandamo katika mji, haimaanishi kuthibiti kwa

watu wa mji mwingie ila ikiwa miji miwili imekaribiana au ikiju-

likana kwamba anga lao ni moja.

SAUMU AMBAZO NI HARAMU NA

MAKURUHU

1110. Inaharamishwa kufunga katika Iddil-fitiri na Idi Al- adhuha na vile

vile inaharamishwa kufunga katika siku ya shaka kwamba ni mwi-

sho wa shabani au ni mwanzo wa mwezi wa Ramadhani kama ata-

funga kwa nia ya mwanzo wa Ramadhani, na inaharamishwa kufun-

227

Al-Masailul Islamiyah

Page 242: al-Masailu-l-Islamiyyah

ga katika siku za tashiriqi (mibano) kwa mwenye kuwa Minaa.

1111. Inaharamishwa kwa mwanamke kufunga sunna ikiwa hiyo ni katika

kupoteza haki za mume wake na kwa tahadhari ya sunna asifunge

sunna bila ya idhini yake hata kama hadhuru haki yake.

1112. Inaharamishwa kwa mtoto kufunga sunna ikiwa inaleta maudhi kwa

wazazi wake au babu yake.

1113. Mwenye kujua kuwa saumu haimdhuru ni wajibu wake afunge hata

kama akiambiwa na daktari kuwa saumu inamdhuru, na mwenye

kuwa na yakini kwamba saumu inamdhuru au akadhani hivyo ni

wajibu asifunge hata kama akiambiwa na daktari kwamba saumu

haimdhuru na lau akifunga na hali ni hiyo saumu yake haitasihi

SAUMU YA SUNNA

1114. Ni sunna kufunga siku zote za mwaka ukiacha siku zilizotajwa

ambazo ni haramu au makuruhu kufunga na imetiliwa mkazo kufun-

ga baadhi ya siku ambazo ni: Siku ya Al hamisi katika mwanzo wa

kila mwezi, Al hamisi ya mwisho na Jumatano ya kumi la kwanza la

kila mwezi, na ikiwa hajafunga katika siku hizi ni mstahabu kwake

alipe, ikiwa hatalipa kadha pia ni mstahabu atoe kwa fakiri badala ya

kila siku - kibaba yaani gramu750 takribani - ya ngano au shairi au

unga wake au mikate yake au 6/12 ya uzito wa fedha halisi – gramu

moja na robo - na saumu ya siku ya kumi na tatu, kumi na nne na

kumi na tano katika kila mwezi. Na saumu ya mwezi wa Rajab,

Shabani na saumu ya siku ya Nairuzi na siku ya nne mpaka ya tisa

katika mwezi wa shawwali na siku ya ishirini na tano na ishirini na

tisa katika mwezi wa Dhil- qaad na siku ya kwanza mpaka ya tisa

katika mwezi wa Dhil-hija ( siku ya Arafa) lakini ikiwa udhaifu

unaosababishwa na saumu unamzuia kuleta dua siku ya Arafa ni

228

Al-Masailul Islamiyah

Page 243: al-Masailu-l-Islamiyyah

makuruhu kufunga siku hiyo, na saumu ya Iddil-ghadiri ( 18 Dhil-

hija) na siku ya Mubahala ( 24 Dhil –hija) na siku ya kwanza, ya

tatu na ya saba katika Muharam na siku ya kuzaliwa Mtume (saww)

( 17 Rabiul-Awwal) na saumu ya siku ya kumi na tano katika mwezi

wa Jamaadul-ulaa na siku ya kupewa utume Mtume (saww ) 27

Rajab.

1115. Lau akijishughulisha kwa saumu ya mustahabu sio wajibu kwake

kuitimiza mpaka magharibi, bali kama akialikwa na ndugu yake

muumini kwenye chakula ni mustahabu kuitika wito wake na kufun-

gua katikati ya mchana

SAUMU YA MAKURUHU

1116. Ni makuruhu kufunga siku ya Ashuraa na siku inayohisiwa kuwa niArafa au Iddul - Adhuha

WATU AMBAO NI SUNNA KUJIZUIA KULA

1117. Ni sunna kwa watu sita kujizuia kula katika mwezi wa Ramadhani

hata kama hawafungi:-

1. Msafiri ambaye amekula safarini kisha akarudi kwenye nchi

yake kabla ya Adhuhuri au akafika sehemu ambayo anataka

kukaa hapo siku kumi.

2. Msafiri ambaye anafika katika nchi yake baada ya adhuhuri au

sehemu ambayo anataka kukaa hapo kwa siku kumi.

3. Mgonjwa ambaye anapona kabla ya adhuhuri na akawa amek-

wisha kula kabla ya hapo.

4. Mgonjwa ambaye anapona baada ya adhuhuri, Mwanamke

229

Al-Masailul Islamiyah

Page 244: al-Masailu-l-Islamiyyah

ambaye ametoharika katika damu ya hedhi au nifasi katikati ya

mchana.

5. Kafiri ambaye anasilimu baada ya Adhuhuri.

1118. Ni sunna kwa mfungaji aswali magharibi na isha kabla ya kufuturu,

lakini kama kuna mtu ambaye anamsubiri mezani au anashauku sana

na chakula kiasi kwamba mawazo yake yote hayatakuwa kwenye

swala ni bora afuturu kwanza, lakini afanye haraka kuswali kwa

wakati wa fadhila kadri inavyowezekana.

HUKUMU ZA KHUMSI

1119. Khumsi ni wajibu katika vitu saba:-

1. Faida inayotokana na biashara

2. Madini

3. Kanzi

4. Mali ya halali iliyochanganyikana na mali ya haramu

5. Vito vya thamani vinavyotolewa baharini

6. Ngawira za vita

7. Ardhi anayoinunua kafiri dhimmiyi (aliye katika himaya ya

dola ya kiislam) kwa mwislamu

Faida inayopatikana kutokana na biashara

1120. Ni wajibu kutoa khumsi katika ziada, baada ya kutoa matumizi ya

mwaka mzima.

1121. Ni wajibu kutoa khumsi inapofikia kiwango maalum, itolewa moja

ya tano 20%.

1122. Kiwango maalumu cha madini ya dhahabu ni gramu 68, fedha ni

gramu 472 –kiwango hiki ni baada ya kutoa gharama zote.

230

Al-Masailul Islamiyah

Page 245: al-Masailu-l-Islamiyyah

1123. Ni wajibu khumsi igawanywe mafungu mawili:-

1. Fungu la maseyidi: Ni wajibu wapewe maseyidi maskini au

maseyidi mayatima ambao ni mafukara au msafiri ambaye ni

seyid.

2. Fungu la pili: ni la Imamu na katika zama hizi anapewa

Mujitahidi ambaye ametimiza masharti au linatumika katika

upande atakaotoa ruhusa litumike.

HUKUMU ZA ZAKA

1124. Zaka ni wajibu katika mambo tisa:-

1- Ngano 2 – Shairi 3 - Tende

4 - Zabibu 5- Dhahabu 6 - Fedha

7- Ngamia 8 -Ng’ombe 9 -Mbuzi na Kondoo

Masharti ya Zaka:-

1125. Zaka ni wajibu inapotimia kiwango maalum. Kiwango cha Ngano,

Shairi, Tende na Zabibu ni kilo gram 847 na gram 207 baada ya

kutoa gharama zote, na kiwango cha zaka yake ni 1/10 ikiwa ime-

nyeshewa na mvua na kama imemwagiliwa zaka yake ni 1/20

Kiwango cha Dhahabu

1126. Dhahabu ina viwango viwili:-

1- Kiwango cha kwanza ni gram 72 na zaka yake ni 1/40.

2- Kiwango cha pili ni gramu 4/14 yaani zikiongezwa gram 4/14 katika

gramu 72 ni wajibu kutoa 1/40 kutoka katika jumla ya gramu 4/86.

Kiwango cha Fedha

231

Al-Masailul Islamiyah

Page 246: al-Masailu-l-Islamiyyah

1127.Fedha ina viwango viwili:-

1. Mithiqal 105 ambayo ni sawa na gram 104 takribani na zaka yake ni

1/40.

2. Mithqal 21 ambayo ni sawa na gram 6/12 yaani inapoongezeka katika

kiwango cha awali na zaka yake ni 1/40.

Zaka ya Ng’ombe, Ngamia, mbuzi na Kondoo

1128.Katika wanyama kuna masharti mawili:-

1- Wasifanye kazi kwa muda wa mwaka mzima.

2- Wawe wanakula majani mbugani wenyewe wasikatiwe majani na kul-

ishwa.

Kiwango cha ngamia

1129. Kiwango cha kwanza ni ngamia watano zaka yake ni mbuzi mmoja.

Kiwango cha pili ni ngamia kumi zaka yake ni mbuzi wawili.

Kiwango cha tatu ni ngamia kumi na tano, zaka yake ni mbuzi

watatu. Kiwango cha nne ni ngamia ishirini zaka yake ni mbuzi

wanne. Kiwango cha tano ni ngamia ishirini na tano zaka yake ni

mbuzi watano. Kiwango cha sita ni ngamia ishirini na sita na zaka

yake ni ngamia ambaye ameingia mwaka wa pili. Kiwango cha

saba ni ngamia thelathini na sita na zaka yake ni ngamia aliyeingia

mwaka wa tatu. Kiwango cha tisa ni ngamia sitini na moja na zaka

yake ni ngamia aliyeingia mwaka wa tano. Kiwango cha kumi ni

ngamia sabini na sita na zaka yake ni ngamia wawili waloingia

mwaka tatu. Kiwango cha kumi na moja ni ngamia tisini na moja

zaka yake ni ngamia wawili walioingia mwaka wa nne. Kiwango cha

kumi na mbili ni mia na ishirini na moja na kuendelea, hapo atah-

esabu arobaini arobaini na atatoa kwa kila ngamia arobani ngamia

mmoja mwenye miaka mitatu au atahesabu hamsini hamsini na ata-

toa kwa kila ngamia hamsini ngamia mmoja mwenye miaka minne.

232

Al-Masailul Islamiyah

Page 247: al-Masailu-l-Islamiyyah

Kiwango cha Ng’ombe

1130. Kiwango cha kwanza ni ng’ombe thelathini na zaka yake ni

ndama aliyeingia mwaka wa pili. Kiwango cha pili ni ng’ombe

arobaini na zaka yake ni ndama aliyeingia mwaka wa tatu, idadi

ikiwa zaidi ya viwango hivyo zitahesabiwa thelathini thelathini au

arobaini arobaini na zaka yake ina tolewa kama tulivyotaja hapo juu.

Kiwango cha Mbuzi na Kondoo

1131.Kiwango cha kwanza ni mbuzi arobaini na zaka yake ni mbuzi

mmoja. Kiwango cha pili ni mbuzi mia na ishirini na moja na zaka

yake ni mbuzi wawili. Kiwango cha tatu ni mbuzi mia mbili na moja

na zaka yake ni mbuzi watatu. Kiwango cha nne ni mbuzi mia tatu na

moja na zaka yake ni mbuzi wanne.Kiwango cha tano ni mbuzi mia

nne na kuendelea, hapa atahesabu mia mia na kila mia zaka yake ni

mbuzi mmoja. Sio lazima kutoa zaka kutoka katika mbuzi wanao-

tolewa zaka bali inatosha kulipa kutoka kwenye mbuzi wake wengine

au kutoa kiasi cha thamani kinacholingana na kima chake au kutoa

kutoka katika aina nyingine.

1132. Wanaopewa zaka ni watu nane1 – Fakiri

2 - Masikini naye ni ambaye hali yake ni mbaya

zaidi kuliko fakiri

3- Anayekusanya zaka kwa amri ya Imamu au naibu wa Imamu

4-Wanaozoezwa nafsi zao nao ni:-

i) Makafiri ambao wakipewa zaka wanaelemea upande wa

Uislamu au watawasaidia waislamu katika vita

ii) Waislamu ambao nidhaifu wa imani

5- Kununulia watumwa na kuwaacha huru

233

Al-Masailul Islamiyah

Page 248: al-Masailu-l-Islamiyyah

6- Wenye madeni ambao wameshindwa kulipa

7- Katika njia ya Mwenyezi Mungu, katika mambo yenye manufaa

kwa waislamu wote mfano, kujenga misikiti, shule, hospitali n.k

8- Msafiri ambaye ameishiwa na masurufu ya safari.

1133. Ni wajibu anayechukua zaka awe Shia Ithna Asharia, kama akitoa

kitu kutoka katika zaka kwa yeyote kwa kuamini kuwa ni shia ni

wajibu arudie kutoa zaka, isipokuwa kama atampa kutoka katika

fungu la wanaozoezwa nyoyo zao.

Nia ya Zaka

1134. Ni wajibu kwa anayetoa zaka akusudie kujikurubisha kwa Allah

(swt) pia ni wajibu kubainisha anachokitoa kuwa ni zaka ya mali au

ni zaka ya Fitri. Lakini kama ikiwa ni wajibu wake kutoa zaka ya

ngano au shairi hailazimu kuainisha kwamba anayotoa ni zaka ya

ngano au shairi.

1135. Zaka ya fitri inakuwa wajibu kwa kila mtu ambaye ni baleghe,

mwenye akili timamu, mwelewa na sio fakiri, kutoa yeye na (kum-

tolea) kila mmoja katika familia yake kilo tatu takriban kwa fakiri,

za ngano, shairi, mtama n.k na kama akitoa thamani ya moja ya vitu

hivi inatosha.

1136. Ambaye hamiliki chakula chake cha mwaka mzima na wala hana

kazi ambayo inamuwezesha kupata chakula chake cha mwaka yeye

na familia yake anahesabiwa kuwa ni fakiri na wala sio wajibu

kwake zaka ya fitri.

1137. Ni wajibu kumtolea zaka ya fitri kila anayezingatiwa kuwa ni kati-

ka familia yake awe mdogo au mkubwa, mwislamu au kafiri, ni

wajibu kumpa mahitaji yake au laa, awe anaishi katika mji wa mtoa-

ji au laa.

234

Al-Masailul Islamiyah

Page 249: al-Masailu-l-Islamiyyah

1138. Ni wajibu kwa mwenyeji kumtolea zaka ya fitri mgeni anayekutem-

belea kabla ya magharibi kwa ridhaa yake.

Matumizi ya Zaka ya Fitiri

1139. Zaka ya fitiri inaweza kutumiwa katika moja ya mambo tuliyoyata-

ja katika zaka ya mali.

Nia ya Zaka ya Fitiri

1140. Ni wajibu wakati wa kutoa zaka ya fitri kunuia nia ya kujikurubisha

kwa Allah ( swt) na kutekeleza amri yake.

1141. Ikiwa mtu atatoa zaka ya fitri kabla ya mwezi wa Ramadhani

haitasihi na kwa tahadhari asiitoe ndani ya mwezi wa Ramadhani,

lakini kama akimkopesha fakiri mali kabla ya mwezi wa Ramadhani

kisha ikamuwajibikia zaka ya fitri baadae inajuzu kuhesabia deni

katika fitri.

HUKUMU ZA HIJA

1142. Hija ni wajibu kwa Muislamu mara moja katika maisha, ni wajibu

wa haraka kwa mwenye uwezo.

1143. Hija ya kiislamu ni wajibu kwa masharti manne:-

1. Mtu awe amebaleghe, si wajibu kwa mtoto ambaye bado haja-

baleghe lakini ni sunna kwa mtoto kuhiji akiruhusiwa na walii

wake.

235

Al-Masailul Islamiyah

Page 250: al-Masailu-l-Islamiyyah

2. Awe mwenye akili, si wajibu kwa mwendawazimu.

3. Awe huru si wajibu kwa mtumwa, lakini ni sunna kwa mtumwa

aende hija akiruhusiwa na walii wake.

4. Awe na uwezo na uwezo unamaanisha mambo yafuatayo:-

i) Awe na matumizi na nauli ya kutosha awe na uwezo wa kiafya

ambao unamruhusu kuhiji.

iii). Kusiwe na kizuizi njiani, muda uwe unatosha kufanya ibada

ya hija.

1144. Ni sunna kwa asiyekuwa na uwezo wa kimali kuhiji.

1145. Ambaye hajatimiza masharti na akahiji katika hiyo hali, wajibu wa

hija hautaondoka kwake bali ni wajibu ahiji atakapotimiza mashar-

ti.

1146. Hija ya kujitolea ni mtu kumuambia asiyemiliki kitu, mimi nitaku-

pa matumizi yako na ya familia yako maadamu upo katika hija,

wakati huo hija itakuwa wajibu kwake na kama atahiji katika hali

hii itakuwa imemtosheleza kuhiji na sio wajibu tena kuhiji hata

kama masharti yatatimia

1147. Aliyekuwa na uwezo katika miaka iliyopita kisha hakuhiji ni wajibu

ahiji vyovyote itakavyowezekana hata kama amekosa uwezo.

1148. Si wajibu kwa mtu kuuza nyumba yake, kipando chake au vyombo

vyake ili aende hija.

1149.Mwenye kuwa na mali ya kuhiji lakini hawezi kwenda hija kwa

sababu ya uzee au maradhi basi ni wajibu kumpa mtu mwingine

akahiji kwa niaba yake.

236

Al-Masailul Islamiyah

Page 251: al-Masailu-l-Islamiyyah

1150. Mtu akiweka nadhiri na akamuahidi Mwenyezi Mungu kwenda hija

ni wajibu aende hija hata kama alishaenda hija kabla.

1151. Inajuzu katika hija ya sunna mtu anuie kwa niaba ya Mtume (saww)

au Maimamu Maasumin (as) na wengineo waliokuwa hai au

waliotangulia mbele ya haki na ataandikiwa thawabu za hija kama

anavyoandikiwa aliyenuia hija kwa niaba yake.

1152. Mwanamke akitokwa na hedhi kabla ya ihramu, atahirimia katika

hali hiyo na akitoharika kabla ya kusimama arafa atawajibika alete

mambo ya umra, na kama hakutoharika mpaka muda wa kusimama

arafa ni wajibu abadili na anuie, “Hija ya Ifradi” na atasimama arafa

katika hiyo hali na kuleta matendo ya hija kisha analeta umra ya

mufradi, vile vile mwanamke akitokwa na hedhi au akipatwa na

nifasi baada ya Ihramu na kabla ya tawafu.

1153. Ikitokea tofauti baina ya shia na suni katika mwandamo wa mwezi

kama haitawezekana kuleta mambo ya hija kutokana na mtizamo wa

shia, basi itaruhusiwa kuleta kutokana na mtazamo wa suni na hija

itasihi.

MIGAWANYO YA HIJA

1154. Hija imegawanyika sehemu tatu:-

1. Hija ya tamatui

2. Hija ya Qiraan

3. Hija ya ifraad

1155. Hija ya tamatui ni wajibu kwa aliye mbali na mji wa Makka kwa

farsakha kumi na sita (16) au zaidi, hija ya Qiraan na hija ya Ifraadi

237

Al-Masailul Islamiyah

Page 252: al-Masailu-l-Islamiyyah

ni wajibu kwa wanaoishi mji wa Makka na aliyembali na mji huo

kwa chini ya farsakha 16.

1156. Ambaye wadhifa wake ni hija ya tamatui ni lazima alete umra kabla

ya hija na ambaye wadhifa wake ni hija ya Qiraan au Ifraad ni lazi-

ma alete umra baada ya hija.

Tofauti kati ya Qiraan na Ifraad ni kuwa mwenye kuhiji hija ya Qiraan

anavaa ihram akiwa na mnyama wake, lakini mwenye kuhiji hija ya ifraad

hawi pamoja na mnyama wake.

1157. Hija ya tamatui ina amali mbili:-

1. Umra tamatui

2. Na hija tamatui

UMRA TAMATUI

1158. Amali za umra tamatui ni tano nazo ni:-

1. Ihram

2 Kuzunguka ka’aba tukufu mara saba

3. Kuswali rakaa mbili za tawafu katika maqamu Ibarahim (as) au

nyuma yake

4. Kukimbia “sa’ayi” baina ya safa na mar’wa

mara saba.

5 Kupunguza nywele au ndevu au kukata kucha.

HIJA TAMATUI

1159. Hija tamatui ina amali kumi na tatu:-

1. Ihram

2. Kusimama arafa

3. Kusimama mash’ari - muzdalifa”

4. Kurusha mawe Aqaba - Mina

238

Al-Masailul Islamiyah

Page 253: al-Masailu-l-Islamiyyah

5.Kuchinja mnyama - Mina

6.Kunyoa au kupunguza nywele- Mina

7. Tawafu ya ziara

8. Rakaa mbili za swala ya tawafu ya ziara

9. Sa’ayi “kukimbia” kati ya safa na marwa

10. Tawafu nisaa

11. Rakaa mbili za tawafu nisaa

12.Kulala Mina usiku wa kumi na moja, kumi na mbili na waka-

ti mwingine ni wajibu kulala usiku wa kumi na tatu pia.

13. Kurusha mawe katika sehemu tatu Mina siku ya kumi na moja,

kumi na mbili na siku ya kumi na tatu kama akilala Mina.

AMALI ZA UMRA

Ihram

1160. Ihram ni amali ya kwanza katika amali za umra tamatui, wakati wa

ihram kwa ajili ya umra tamatui ni katika miezi ya hija (mfungo

mosi, mfungo pili na mfungo tatu).

MIQAATI (VITUO)

1161. Sehemu ya kuvalia ihramu huitwa Miqati na miqati ni moja ya sehe-

mu zifuatazo:-

1. Masjidi Shajara ni kituo cha watu wa Madina

2. Waadil aqiq ni kituo cha watu wapitao njia ya Iraki

3. Qurnul maanazil ni kituo cha watu wanaopita kutoka Twaif

4. Yalamlam ni kituo cha watu wanaopita kutoka Yemen

5. Al – Juhfa ni kituo cha watu wa Misri na Sham (Syiria na

239

Al-Masailul Islamiyah

Page 254: al-Masailu-l-Islamiyyah

Jodan).

1162. Ni wajibu kwa kila mtu ahirimie katika kituo chake kama tulivyo-

taja na inasihi kwa mtu kuhirimia kabla ya kufika katika kituo kwa

kuweka nadhiri.

VITU VILIVYO WAJIBU KATIKA

IHRAM

1153.Vilivyowajibu katika ihram ni vitu vitatu:-

1. Nia: Anuie hivi (Nahirimia kwa ajili ya umra tamatui kwa kuji-

kurubisha kwa Mwenyezi Mungu) ,na maana ya kuhirimia ni

kujilazimisha kuacha vitu ambavyo tutavitaja baadae.

2. Tal- biya (wito): alete tal- bia nne kama ifuatavyo: “Labaika

Allahumma labaika, labaika laa sharika laka labaika, innal-

hamda wa niamata laka wal - mulku, laa sharika laka”.

3. Kuvaa nguo mbili: Ni wajibu kwa wanaume, na si kwa wana-

wake, japokuwa ni kwa tahadhari ya sunna kwa mwanamke

angalau mwanzo tu.

1164. Ni wajibu nguo hizo ziwe tohara na zisiwe za hariri wala ngozi ya

mnyama ambaye ni haramu na zisiwe nyepesi kiasi kwamba mwili

unaonekana.

YALIYO WAJIBU KUJIEPUSHA WAKATI

WA IHRAM

1165. Ni wajibu kwa aliyevaa Ihram kujiepusha na vitu ishirini na nne:-

1. Kuwinda mnyama wa nchi kavu au kumsaidia anayewinda, kula

windo au kuchinja ila ikiwa ni wanyama wakali wa porini

240

Al-Masailul Islamiyah

Page 255: al-Masailu-l-Islamiyyah

ambao inaruhusiwa kujilinda nao kutokana na madhara.

2. Kuwakaribia wanawake kwa kuwaingilia au kubusu au kuwaan-

galia kwa matamanio.

3. Kuoa au kuozesha au kuwa shahidi.

4. Kujitoa manii kwa mkono (punyeto) au kitu chochote.

5. Kutumia manukato kama miski, zafarani au udi, kwa kula,

kunusa, kujipaka mafuta n.k, pia ni haramu kuziba pua kuto-

kana na harufu inayokarahisha.

6. Kuvaa nguo zilizoshonwa kwa wanaume, lakini inajuzu kuvaa

kimkoba cha kuhifadhia fedha hata kama kitakuwa kimeshon-

wa.

7. Kupaka wanja.

8. Kujitazama katika kioo.

9 Kuvaa soksi kwa mwanaume au chochote kinachofunika mguu.

10. Kufanya ufuska yaani kusema uongo, matusi au kujifakhari-

sha.

11. Kujadili – kuapa nayo ni kusema (laa wallaahi) – hapana wal-

lah na kwa tahadhari ya wajibu ni kujiepusha na viapo kabi-

sa.

12. Kuuwa wadudu kama viroboto, kunguni, chawa n.k.

13. kuvaa pete kwa kukusudia kuwa ni pambo.

14. Kutokuvaa mapambo kwa ujumla kama kujipaka hina au

kuvaa bangili, hereni, isipokuwa kama anavivaa muda wote .

241

Al-Masailul Islamiyah

Page 256: al-Masailu-l-Islamiyyah

15. Kufunika kichwa chote au sehemu ya kichwa au sikio kwa

wanaume bali ni haramu hata kujistiri kwa hina.

16. Mwanamke kusitiri uso wake kwa kitambaa kizito.

17. Kujipaka mafuta.

18 Kung’oa nywele kichwani au sehemu nyingine ya mwili hata

kama ni unywele mmoja na hakuna tatizo kama nywele zita-

dondoka wakati wa udhu.

19. Kujitoa damu hata kama kwa kupiga mswaki.

20. Kung’oa jino hata kama damu haitatoka.

21. Kukata kucha.

22. Kujifunika mwavuli kwa wanaume wakati wa kutembea laki-

ni hakuna tatizo kujifunika nyumbani.

23. Kukata mti au kun’goa mmea katika haram tukufu.

24. kubeba silaha kama bunduki au panga n.k.

KAFARA YA VITU VILIVYO HARAMISHWA

KATIKA IHRAM.

1166. Vitu ishirini na nne vilivyoharamu katika ihram vimegawanyika

katika sehemu tatu:-

1. Vilivyo haramu na ukivifanya kunawajibisha kafara tu.

2. Vilivyo haramu na ukivifanya hakuwajibishi kafara.

3. Vitu ambavyo kuvifanya kwake kunabatilisha hija na tunataja

baadhi ya kafara kwa muhtasari

1167. Kafara ya vitu vilivyoharam katika ihram:-

242

Al-Masailul Islamiyah

Page 257: al-Masailu-l-Islamiyyah

1. Kafara ya kuwinda imeelezwa kwa kirefu katika ibada ya hija.

2. Kafara ya kufanya jimai ni kutoa ngamia au ng’ombe au kondoo

kama ilivyoelezwa kwa ufafanuzi zaidi katika ibada ya hija.

3. Kafara ya kufunga ndoa kama mwanaume atamwingilia mwa-

namke ni ngamia kwa mwenye kufunga ndoa.

4. Kafara ya kufanya punyeto ni kama kafara ya kumwingilia mwa-

namke, na katika baadhi ya hali inabatilisha hija.

5. Kafara ya kutumia manukato ni kondoo.

6. Kafara ya kuvaa nguo iliyoshonwa ni kondoo.

7. Kafara ya kujipaka wanja ni kondoo.

8. Kafara ya kumtazama mwanamke ni kondoo.

9. Kafara ya kuvaa soksi ni kondoo.

10.Kafara ya ufuska ni kuomba msamaha.

11.Kafara ya kujadiliana ni ngamia au ng’ombe au kondoo.

12.Kafara ya kuua chawa ni kutoa sadaka ya kulisha maskini.

13. Kafara ya kujipamba ni kondoo kwa tahadhari.

14. Kafara ya kuvaa pete ni kondoo.

15. Kafara ya kufunika kichwa kwa wanaume ni kondoo.

16. Kafara ya mwanamke kufunika uso ni kondoo.

17. Kafara ya kujipaka mafuta ni kondoo.

18. Kafara ya kunyoa nywele ni kondoo au kufunga siku tatu au

kulisha maskini sita.

19. Kafara ya kujitoa damu ni kondoo.

20. Kafara ya kung’oa jino ni kondoo.

21. Kafara ya kukata kucha ni kondoo wawili.

22. Kafara ya kujifunika mwavuli kwa wanaume ni kondoo.

23. Kafara ya kukata mti au kung’oa mmea wa haram ni ng’ombe

au kondoo.

24. Kafara ya kuvaa silaha ni kondoo.

2. TAWAFU

243

Al-Masailul Islamiyah

Page 258: al-Masailu-l-Islamiyyah

1168. Mwenye kuhiji ataingia Makka baada ya kuhirimia umra na ataleta

amali ya pili ya umra ambayo ni kuzunguka ka’aba tukufu.

1169. Namna ya kutufu: Kaaba iwe mkono wake wa kushoto na kuzungu-

ka pembeni mwake mara saba na aanzie katika jiwe jeusi na amali-

zie hapo.

1170. Katika tawafu mambo yafuatayo ni sharti:-

1. Nia, atie nia kuwa anatufu

2. Tohara kutokana na hadathi kubwa kama vile janaba, hedhi,

nifasi na hadathi ndogo yaani awe na udhu

3. Tohara ya nguo na mwili

4. Mwanaume awe ametahiriwa

5. Kustiri uchi na ni wajibu kwa mwenye kujistiri yale yote

ambavyo ni wajibu kwa mwenye kujistiri katika swala

6. Tawafu: Iwe kati ya ka’aba tukufu na maqamu

Ibrahimu

7. Jiwe la Ismaili liwe ndani ya tawafu

8. Mwili wote uwe nje ya ka’aba.

3. SWALA YA TAWAFU

1171. Amali ya tatu ni kuswali swala ya tawafu katika

maqamu Ibarahim au nyuma yake.

1172. Swala ya tawafu ni kama swala ya asubuhi na

unatia nia ya kuswali swala ya tawafu.

4. SA’I

244

Al-Masailul Islamiyah

Page 259: al-Masailu-l-Islamiyyah

1173. Amali ya nne katika amali za umra ni sa’i yaani kukimbia baina ya

safa na mar’wa mara saba, na katika sehemu hii ni wajibu kwa

mwenye kuhiji akate masafa kati ya safa na mar’wa mara saba kwa

kuanzia safa na kumalizia mar’wa.

1174. Kutoka safa kwenda mar’wa inahesabika kuwa ni mzunguko mmoja,

na kurudi kutoka mar’wa kwenda safa ni mzunguko mwingine.

1175. Nia ya kukimbia sa’i.

5 - KUNYOA AU KUPUNGUZA

1176. Baada ya kukamilisha Sa’i ni wajibu kuleta amali ya tano ambayo ni

kupunguza nywele.

1177. Kupunguza: Inamaanisha kukata sehemu ya nywele za kichwa au

kukata kucha.

1178. Baada ya kunyoa, vitu vilivyokuwa haramu kwa ajili ya ihramu

vitakuwa halali ila viwili amabvyo uharamu wake ni kwa ajili ya

utukufu wa haram navyo ni :-

1. kuwinda

2. kukata mti au kung’oa mmea wa haram.

UMRA YA MUFRAD

1179. Akitaka mtu kuleta umra peke yake atafanya amali mfano wa amali

ya umra tamatui, lakini ataongeza tawafu nisai na swala ya tawafu

nisai.

AMALI ZA HIJA TAMATUI

245

Al-Masailul Islamiyah

Page 260: al-Masailu-l-Islamiyyah

1180. 1. Kuhirimia Hija

Mambo ya hija ni kumi na tatu kama tulivyosema na amali ya kwanza ni

kuvaa Ihramu, ni juu ya mwenye kuhiji baada ya kukamilisha mambo ya

umra, ahirimie mara ya pili kwa ajili ya hija, na tofauti ni kuwa kuhirimia

umra inakuwa katika moja ya vituo tulivyovitaja na kuhirimia hija

inakuwa Makka na ni sunna iwe katika msikiti mtukufu.

1181. Wakati wa kuhirimia hija ni baada ya kumaliza umra tamatui mpaka

wakati wa kusimama arafa.

2. KUSIMAMA ARAFA

1182. Amali ya pili katika amali za hija ni kusimama Arafa, yaani awe

katika uwanja wa Arafa kuanzia adhuhri katika siku ya Arafa (siku

ya tisa) mpaka kuzama kwa jua.

1183. Anuie katika kisimamo hiki.

3. KUSIMAMA KATIKA MASH’ARI “MUZDALI-DA”

1184. Ni wajibu kwenda Mash’ari baada ya kutoka Arafa baada ya kuza-

ma jua na awepo katika Mash’ari tangu mapambazuko ya Al-fajiri

mpaka kuchomoza kwa jua katika siku ya Idd ambayo ni siku ya

kumi.

1185. Inapokaribia kuchomoza kwa Al fajiri katika hiyo siku ni wajibu

mwenye kuhiji anuie na kusimama katika mash’ari.

4 – 6 AMALI ZA MINA.

246

Al-Masailul Islamiyah

Page 261: al-Masailu-l-Islamiyyah

KUTUPA MAWE, KUCHINJA NA KUNYOA

1186. Ni wajibu kwenda Mina baada ya kuchomoza jua katika siku ya Idd

na kufanya amali tatu:-

1. Kurusha mawe katika Aqaba (nayo ni jamaratul kubra) kwa

mawe saba madogo kwa taratibu moja baada ya jingine

2. Kuchinja ngamia au ng’ombe au kondoo

3. Kunyoa kichwa chote au kupunguza, kama hija yake ni ya

kwanza kwa tahadhari ya sunna anyoe kichwa chote.

7 – 11 – AMALI ZA MAKKA.

1187. Baada ya kukamilisha amali za Mina mwenye kuhiji anaweza kwen-

da Makka siku hiyo hiyo ya Idd na kufanya amali tano:-

1.Tawafu ya ziara mara saba

2. Rakaa mbili za tawafu ya ziara kwenye maqamu Ibrahimu au

nyuma yake

3. Sa’i “kukimbia” baina ya safa na mar’wa

4. Tawafu nisai, nayo ni kama tawafu ya hija

5. Rakaa mbili za tawafu nisai.

12. – KULALA MINA

1188. Ni wajibu kwa mwenye kuhiji kulala Mina siku ya kumi na moja,

kumi na mbili na ya kumi na tatu pia, na kiwango cha wajibu kulala

mina ni nusu ya usiku kuanzia mwanzo wake au mwisho wake, na

inajuzu kujishughulisha na ibada Makka badala ya kulala mina.

1189. Kama mwenye kuhiji hakulala ni wajibu atoe kafara kwa kila siku

kondoo na atahesabika ameasi akiacha kulala mina japokuwa hija

yake ni sahihi.

247

Al-Masailul Islamiyah

Page 262: al-Masailu-l-Islamiyyah

13. KUTUPA MAWE

1190. Ni wajibu kwa mwenye kuhiji kutupa mawe sehemu tatu katika

mchana wa siku alizolala mina, yaani siku ya kumi na moja, kumi na

mbili na siku ya kumi na tatu kama akilala mina, atatupa mawe saba

katika nguzo ya kwanza, mawe saba nguzo ya katikati mawe saba

na jamratul aqaba mawe saba, na kwa kufanya hivi atakuwa ame-

kamilisha amali za hija.

HUKUMU ZA NDOA

1191. Ni wajibu katika ndoa ya daima na ndoa ya muda kusoma swigha

“tamko” la ndoa na wala haitoshi kuchukuana kwa kuelewana, ama

wanaooana wasome wenyewe au waweke wakili atakayesoma kwa

niaba yao.

1192. Na wakili sio sharti awe mwanaume bali inajuzu awe mwanamke

kwa kumuwakilisha mwanaume au mwanamke.

1193. Haijuzu kwa mwanamke na mwanaume kuangaliana kama mume na

mke mpaka wapate yakini kuwa wakala wao tayari ameshafunga

ndoa, na dhana haitoshi.

1194.Inajuzu kwa mtu mmoja kusoma swigha ya ndoa kwa pande zote

mbili au kusoma swigha kwa niaba ya mwanamke kwa kujiozesha

mwenyewe, iwe katika ndoa ya daima au ya muda, lakini ni bora

kufanya tahadhari kwa kuwakilishwa na watu wawili.

Namna ya kufunga ndoa ya daima

1195. Ikiwa wenye kuoana watasoma swigha wenyewe basi mwanamke

atasema baada ya kubainishwa kiwango cha mahari “zawajtuka naf-

siy alaa swadaqil maalum” Nimekuozesha nafsi yangu kwa mahari

248

Al-Masailul Islamiyah

Page 263: al-Masailu-l-Islamiyyah

maalumu), kisha mwanaume aseme haraka “Qabitu nikaaha”

(Nimekubali kuoa). Kama waoaji watawakilishwa katika kufunga

ndoa, kama jina la mwanamke ni Fatma na jina la mwanaume ni

Ahmad basi wakili wa mwanamke atasema: Zawwajtuka muwaki-

latiy Fatwimah muwakilaka Ahmad alaswadaaqil maalum

“Nimemuozesha wakala wangu Fatma wakala wako Ahmad kwa

mahari maalum”, kisha wakili wa mwanaume atasema haraka

Qabiltu nikaha limuwakiliy Ahmad “Nimekubali nihaha kwa niaba

ya wakala wangu Ahmadi kwa mahari maalumu”.

Namna ya kufunga ndoa ya muda.

1196.Kama wanaooana watafunga ndoa wenyewe, basi mwanamke atase-

ma baada ya makubaliano ya mahari na muda: Zawajtuka nafsiy fiyl

mudatil maalumati wa alaa swadaqil maalum “Nimekuozesha nafsi

yangu kwa muda maalum na kwa mahari maalumu”, kisha

mwanaume atasema haraka: Qabiltu “nimekubali”, na ndoa inasihi,

na kama wataweka wakala basi wakala wa mwanamke atasema:

Zawajtu muwakilatiy muwakilaka fiy mudatil maalumati wa alaa

swadaqil maalum“Nimemuozesha wakala wangu, wakala wako kwa

muda maalumu na kwa mahari maalum”, kisha wakala wa

mwanaume atasema haraka: Qabiltu nikaha limuwakiliy

“Nimekubali ndoa kwa niaba ya wakala wangu”, ndoa inasihi.

1197. Masharti ya ndoa:-

Ndoa ifungwe kwa lugha ya kiarabu kwa kutamkwa kwa usahihi na

kama wanaooana hawajui kiarabu, basi waweke mtu wa kufunga

ndoa kwa niaba yao anayefahamu kiarabu vizuri, na kama

haitawezekana kabisa, basi ifungwe kwa lugha yeyote, lakini ni

wajibu waseme maneno yanayo maanisha: “Nimekuozesha na

nimekubali” katika lugha yao.

Ni wajibu ndoa ifungwe kwa kusoma swigha kwa pande mbili,

kwamba mwanamke akusudie kwa kusema: “Nimekuozesha nafsi

249

Al-Masailul Islamiyah

Page 264: al-Masailu-l-Islamiyyah

yangu kwamba nimekuwa mke wako, na mwanaume akusudie kwa

kusema: Nimekubali nikahi” nimeridhia hayo.

Wanaofunga au wanaofungisha ndoa wawe wamebaleghe.

Kama wakala atafungisha ndoa ni lazima ataje majina ya

wanaooana.

Wanaooana wawe wameridhia kuoana, kama mwanamke akilaz-

imishwa kukubali katika dhahiri, lakini ikajulikana kuwa ameridhia

moyoni ndoa inasihi.

1198. Kama atakosea kutamka hata herufi moja ndoa itabatilika kwa tahad-

hari kwamba itabadilisha maana yake.

1199. Kama mtu atamuozesha mwanamke kwa mawanaume bila ya rid-

haa yao, kisha wakaridhia baadae kwa kutamka, ndoa inasihi.

1200. Binti aliyebaleghe ambaye anaelewa masilahi yake kama akitaka

kuolewa, naye ni bikira ni bora achukue idhini kwa baba yake au

kwa babu yake kwa upande wa baba na wala sio lazima kuchukua

idhini kwa mama yake au kwa kaka yake.

1201. Kama baba na babu hawapo na binti sio bikira basi sio lazima kupa-

ta idhini kwa baba au kwa babu wa upande wa baba tu.

Kasoro ambazo inajuzu kuvunja ndoa

kwa ajili yake

1203. Kama mwanaume atajua baada ya ndoa kuwa mke ana moja kati ya

kasoro hizi inajuzu kuvunja ndoa:-

Wazimu

Ukoma

Mbalanga

250

Al-Masailul Islamiyah

Page 265: al-Masailu-l-Islamiyyah

Upofu

Kiwete

Njia ya mkojo na ya hedhi kuwa ni moja au sehemu ya haja kubwa

na njia ya hedhi kuwa moja

Kuota mfupa au nyama ndani ya uke na unazuia jimai

Kama mwanamke atajua kuwa mume wake amekatika uume au

hana nguvu za kiume au amehasiwa basi inajuzu kuvunja ndoa.

1204. Mume akivunja ndoa kwa moja ya kasoro tulizozitaja basi ni waji-

bu watengane bila ya talaka.

1205.Mwanamke akivunja ndoa kwa sababu mume wake hana nguvu za

kiume, basi ni wajibu kwa mume kumpa nusu ya mahari, lakini

kama mwanaume au mwanamke akivunja ndoa kwa moja ya aibu

tulizozitaja, kama hawajaonana kimwili sio wajibu kwa mwanaume

kumpa mwanamke chochote, na kama atamwingilia basi ni wajibu

ampe mahari yote.

Wanawake ambao ni haramu kuwaoa

1206. Ni haramu kuoa wanawake ambao ni mahramu mfano, mama, binti,dada, mama mkwe, shangazi, mama mkubwa au mdogo, bibi, mju-kuu, binti wa dada yako mke wa baba, na mke wa mtoto wako.

1207. Ukioa mwanamke kisha ukamwingilia basi, binti wa mke wako,

binti wa binti wa mke wako na binti wa mtoto wa kiume wa mke

wako wanakuwa ni mahramu wako na ni haramu kuwaoa.

1208. Haijuzu kuoa binti ambaye ni mchumba wa mtu mwingine maadam

bado anamafungamano naye.

1209. Wafuatao ni maharimu wa mwanaume: Shangazi wa baba yake,

mama mkubwa au mama mdogo wa baba yake, shangazi wa babu

yake, shangazi wa mama yake, mama mkubwa au mama mdogo wa

mama yake, shangazi wa bibi yake, mama mkubwa au mdogo wa

251

Al-Masailul Islamiyah

Page 266: al-Masailu-l-Islamiyyah

bibi yake.

1210. Wafuatao ni maharimu wa mwanamke: Mkwe, babu ambaye ni

mzazi wa wa baba mkwe, mtoto wa mume wake na mtoto wa mtoto

wa mume wake, wawe wamezaliwa au bado.

1211. Haijuzu kuoa binti wa dada wa mke na binti wa kaka yake bila ya

idhini ya mke, lakini akioa bila ya idhini ya mke wake na baadaye

akatoa idhini basi ndoa itasihi.

1212. Mtu akizini na shangazi na mama mkubwa au mdogo kabla ya

kumuoa binti wa shangazi au mama, basi haijuzu tena kumuoa huyo

binti.

1213. Mtu akimuoa binti wa shangazi au wa mama mkubwa au mdogo na

kabla ya kumwingilia akazini na shangazi au na mama mkubwa au

mdogo ni bora achukue tahadhari ajitenge nae.

1214.Mtu akizini na mwanamke ni bora achukue tahadhari asimuoe binti

wa huyo mwanamke aliyezini naye, kama mtu akioa mwanamke

kisha akamwingilia na baada ya hapo akazini na mama mkubwa,

basi mke wake hatakuwa haramu, japo ni bora atengane naye bila ya

talaka.

1215.Haijuzu mwanamke wa kiislamu kuolewa na kafiri, mkristo, myahu-

di au asiyekuwa hao. Haijuzu kwa mwislamu kuoa mwanamke

kafiri, lakini inajuzu kuoa mwanamke wa kikristo au wa kiyahudi

ndoa ya daima au ya muda.

1216.Kama atazini na mwanamke ambaye yuko kwenye eda ya talaka

rejea basi mwanamke huyo atakuwa haramu kwake, na akizini na

mwanamke ambaye yuko katika eda ya ndoa ya muda au katika eda

ya kufiwa basi inajuzu baada ya hapo kumuoa.

252

Al-Masailul Islamiyah

Page 267: al-Masailu-l-Islamiyyah

1217. Mtu akizini na mwanamke ambaye hana mume wala hayupo katika

eda inajuzu kumuoa, lakini ni bora achukue tahadhari ya kusubiri

mpaka huyo mwanamke aone damu ya hedhi kisha amuoe.

1218. Ni haramu kuoa mwanamke akiwa katika eda.

1219. Mtu akijua kuwa mwanamke huyu ana mume pamoja na hivyo

yeye akamuoa, basi ni wajibu watengane na asimuoe tena.

1220. Mtu akizini na mwanamke mwenye mume basi huyo mwanamke

hatakuwa haramu kwa mume wake hata kama hatatubu, japo ni

bora kwa mume wake ampe talaka lakini ni wajibu ampe mahari

yake yote.

1221. Mtu akimlawiti kijana basi mama wa huyo kijana, dada yake na

binti yake wanakuwa ni haramu kwa mwenye kulawiti

1222.Mtu akimlawiti mtu baada ya kumuoa mama yake au dada yake au

binti yake basi mke wake hatakuwa haramu kwake.

1223. Mtu aliyehirimia hija kisha akaoa hali ya kuwa amehirimia ndoa

inabatilika, kama alikuwa anajua kuwa ndoa katika hali ya Ihramu ni

haramu pamoja na hivyo akaoa basi mwanamke huyo atakuwa hara-

mu kwake milele.

1224. Ni haramu kuoa ukiwa katika hali ya Ihramu.

1225.Mwanaume kama hatafanya tawafu nisai katika hija basi mke wake

atakuwa haramu kwake, na vile vile mwanamke kama hatafanya

tawafu nisai mume wake atakuwa haramu kwake, lakini wakifanya

hiyo tawafu uharamu utaondoka.

253

Al-Masailul Islamiyah

Page 268: al-Masailu-l-Islamiyyah

1226. Mwanamke akipewa talaka tatu anakuwa haramu kwa mume wake,

lakini akiolewa na mume mwingine kisha akaachika au huyo mume

wake akifa, basi inajuzu aolewe na mume wake wa kwanza.

Hukumu za ndoa ya daima

1227. Mwanamke aliyeolewa ndoa ya daima haruhusiwi kutoka ila kwa

idhini ya mume wake, ni wajibu asimkatalie mume wake anapotaka

kustarehe naye, na asimnyime unyumba bila ya sababu ya kisheria,

na akimtii mume wake katika hilo, basi ni wajibu kwa mume wake

kumpatia chakula, mavazi na sehemu ya kukaa (nyumba), na kama

mwanaume hatamtimizia hayo itakuwa ni deni awe na uwezo au laa.

1228. Kama mwanamke akimnyima unyumba, basi hastahiki mavazi na

nyumba, lakini mahari atapewa.

1229. Haijuzu kwa mwanaume kumlazimisha mke wake kufanya kazi za

nyumbani.

1230. Mwanamke ambaye anamtii mume wake lakini hatoi matumizi, basi

inajuzu kwake katika hali hii achukue matumizi katika mali ya

mume wake bila ya idhini yake ikiwa anajiweza, lakini kama haji-

wezi basi sio wajibu kumtii mume wake wakati wa kutafuta riziki.

1231. Sio wajibu kwa mwanaume kulala kwa mke wake usiku katika kila

siku siku nne.

1232. Haijuzu kwa mwanaume kuacha kumwingilia mke wake zaidi ya

miezi minne. Ikiwa ni mmoja kwa shahiri

1233. Kama mahari haijabainishwa wakati wa kufunga ndoa, ndoa itasihi,

na mwanaume kama atamwingilia basi ni wajibu ampe mahari.

1234. Kama wakati wa kufunga ndoa hawatabainisha muda wa kulipa

254

Al-Masailul Islamiyah

Page 269: al-Masailu-l-Islamiyyah

mahari ya mke, basi inajuzu kwa mke kumnyima unyumba mume

wake mpaka apewe mahari, sawa sawa mwanaume awe na uwezo au

laa, lakini mke akiridhia kumpa unyumba kabla ya kupewa mahari

basi haijuzu kwake tena kumnyima unyumba baada ya hapo bila ya

udhuru wa kisheria.

Ndoa ya mut’a “Muda”

1235. Ni kwa tahadhari ya wajibu usiache kuonana kimwili na mke wa

muda zaidi ya miezi minne.

1236. Mke wa ndoa ya muda hana haki ya kupewa matumizi hata kama

amebeba mimba ya mume wake.

1237. Mke wa muda hana haki ya kumtaka mume wake kulala kwake

kama ambavyo hamrithi mume wake na mume pia hamrithi mke.

1238. Mke wa ndoa ya muda kama hajui kuwa hastahiki kupata matumizi

na hastahiki kumtaka mume wake kulala kwake ndoa itasihi, na

haimlazimu mume wake chochote kwa sababu ya kutokujua kwake.

1239. Inajuzu kwa mke wa muda kutoka bila ya ruhusa ya mume wake,

lakini kama kutoka kwake kutasababisha haki za mume wake

kupotea itakuwa ni haramu kutoka bila ruhusa.

1240. Mke wa ndoa ya muda kama atazawadiwa na mume wake muda

uliobakia, basi ni wajibu apewe mahari yote waliyoafikiana na hii

ni kama amemwingilia, na kama hajamwingilia atampa nusu ya

mahari.

1241. Inajuzu kwa mwanaume kufunga ndoa ya daima na mke wake wa

ndoa ya muda kabla ya muda wa ndoa ya muda kwisha, pia anaweza

kumuoa kwa mara ya pili ndoa ya muda, akiwa katika eda ya ndoa

ya muda ya kwanza.

255

Al-Masailul Islamiyah

Page 270: al-Masailu-l-Islamiyyah

Hukumu za kuangalia

1242. Ni haramu kwa mwanaume kuangalia mwili wa mwanamke ajin-

abiya, pia ni haramu kuangalia mwili wa binti ambaye umri wake

haujatimia miaka tisa, lakini anatambua baya na zuri, ni haramu

kuangalia hata nywele zake na kwa mwanamke pia ni haramu

kuangalia mwili wa mwanaume ajinabii.

1243. Hakuna tatizo kwa mwanaume kuangalia uso na viganja vya

mwanamke wa kikristo na wa kiyahudi.

1244. Ni wajibu kwa mwanamke kusitiri mwili wake pamoja na nywele

zake kwa mwanaume ajinabii, na kwa tahadhari asitiri mwili wake

kwa mtoto wa kiume ambaye hajabalehge lakini anaelewa kizuri na

kibaya.

1245. Ni haramu kuangalia uchi wa mwingine, hata uchi wa mtoto

anayetambua zuri na baya, lakini mume na mke inajuzu kwao kuan-

galiana mwili mzima.

1246. Ni wajibu kwa mwanaume asiangalie mwili wa mwanaume kwa

matamanio, na mwanamke asiangalie mwili wa mwanamke kwa

matamanio.

1247. Katika hali ya dharura inajuzu kwa nesi kumchoma sindano

mwanamke mwenzake au mwanaume ambaye sio mume wake, au

kusafisha uchi wa mwanamke mwenzake au uchi wa mwanume

ambaye sio mume wake, na kama akitaka kugusa uchi wa

mwanaume ni wajibu avae glovsi katika viganja vyake halafu aguse

au apige sindano au asafishe.

1248. Katika hali ya dharura inajuzu kwa mwanaume kumtibu mwanamke

ajinabiya kwa kumwangalia mwili wake au kumgusa, lakini kama

256

Al-Masailul Islamiyah

Page 271: al-Masailu-l-Islamiyyah

anaweza kumtibu bila ya kumwangalia au kumgusa ni lazima

asimwangalie au asimguse.

1249.Yeyote akilazimika kumtibu mwingine kuangalia uchi wake na haku-

na njia nyingine ila kuangalia uchi basi hakuna tatizo katika hilo.

Mas’ala katika ndoa

1250. Anayeogopa kufanya haramu kwa sababu hajaoa basi ni wajibu aoe.

1251. Mume akiweka sharti katika ndoa kuwa mke awe bikra, kisha

ikabainika kuwa hana bikra basi inajuzu kwake kuvunja ndoa.

1252. Ni haramu kwa mwanamke na mwanaume kukaa faragha katika

sehemu ambayo hakuna uwezekano wa mtu mwingine kuingia, sawa

sawa wawe katika ibada, katika maongezi mengine au wamelala au

wako macho, lakini ikiwa kuna uwezekano wa kuingia mtu

mwingine hakuna tatizo.

1253. Kama mwanaume atabainisha mahari wakati wa ndoa, lakini katika

nia yake hatompa hiyo mahari, ndoa itasihi lakini ni wajibu atoe hiyo

mahari.

1254. Mwislamu ambaye anakanusha kuwepo Allah au Nabii au siku ya

mwisho au hukumu katika hukumu za wajibu kama vile swala na

saumu, na anajua kuwa ni katika wajibu wa dini basi atakuwa ni

murtadi.

1255. Mwanamke akiritadi kabla ya kuingiliwa na mume wake basi ndoa

yake itabatilika, na kama ataritadi baada ya kuingiliwa naye ameko-

ma kutokwa na damu ya hedhi pia ndoa itabatilika, lakini kama

hajakoma kutokwa damu ya hedhi ni wajibu akae eda, na kama

atasilimu kabla ya muda wa eda kwisha ndoa yake haitabatilika, na

257

Al-Masailul Islamiyah

Page 272: al-Masailu-l-Islamiyyah

akibakia katika kuritadi kwake mpaka muda wa eda ukaisha basi

ndoa inabatilika.

1256. Mwanaume aliyezaliwa katika uislamu akirtadi mke wake anakuwa

haramu kwake, na ni wajibu kwa mwanamke akae eda ya kufiwa

ambayo ni miezi mnne na siku kumi.

1257. Mwanaume ambaye hajazaliwa katika uislamu kisha akasilimu,

halafu akaritadi kabla hajamwingilia mke wake basi ndoa inabatili-

ka, na kama ataritadi baada ya kumwingilia mke wake, kama mke

wake atakuwa katika umri wa kupata damu ya hedhi basi ni wajibu

wake akae eda ya kufiwa, na kama mume wake atasilimu kabla ya

muda wa eda haujaisha basi ndoa haibatiliki, la sivyo inabatilika

1258. Mwanamke akiolewa akiwa na binti wa mume mwingine, basi

mume wake wa pili anaweza kumuozesha huyo binti kwa kijana

wake wa mke wake mwingine, vile vile akimuozesha kijana wake

binti basi yeye anaweza kumuoa mama wa binti huyo.

1259. Kama mwanamke akizini kisha akapata mimba haijuzu kuitoa hiyo

mimba.

1260. Kama mwanaume atazini na mwanamke asiyeolewa wala hana eda,

kama atamuoa baada ya hapo kisha akazaliwa mtoto na hawajui

kuwa ni wa halali au ni wa haramu atakuwa ni mtoto wa halali.

1261. Kama mtu akioa mwanamke na hajui kuwa yuko katika eda au laa,

na mwanamke naye hajui, kisha akazaliwa mtoto atakuwa ni wa

halali kisheria, lakini kama mwanamke anajua kuwa yuko katika eda

basi mtoto atakuwa ni wa huyo mwanaume kisheria, lakini ndoa

itakuwa ni batili.

1262.Mwanamke akisema nimekoma kutokwa na damu ya hedhi au akise-

ma mimi sina mume, kauli yake itakubaliwa, lakini kama atakuwa

anatuhumiwa kwa uongo itabidi ufanyike uchunguzi.

258

Al-Masailul Islamiyah

Page 273: al-Masailu-l-Islamiyyah

1263. Mwanaume akioa kisha akaambiwa huyo mwanamke ana mume na

akasema mimi sina mume na kama haijathibiti kisheria kuwa

alikuwa na mume basi ni wajibu kauli ya mwanamke ikubaliwe.

1264. Haijuzu kwa baba kumtenganisha binti yake na mama yake kabla

hajatimiza miaka saba, na kwa mtoto wa kiume kabla hajatimiza

miaka miwili.

1265. Binti akibaleghe tu ni sunna kufanya haraka kumuozesha kwani

Imamu Swadiq (as) amesema: “Katika maisha mazuri ya mtu

asitoke hedhi binti yake nyumbani kwake”.

1266. Kama mwanamke ataelewana na mume wake asipewe mahari ili

mume wake asioe mwanamke mwingine basi ni wajibu kwa

mwanamke asiombe mahari, na ni wajibu kwa mwanaume asioe

mwanamke mwingine.

1267.Mtoto wa zinaa akioa na akapata mtoto atakuwa ni mtoto wa halali.

128. Mwanaume akimwingilia mke wake katika mwezi wa Ramadhani au

katika hedhi atakuwa ameasi na kupata dhambi, lakini mtoto

atakayezaliwa kutokana na hicho kitendo atakuwa ni wa halali.

1269.Mwanamke akipata yakini kuwa mume wake amefariki safarini na

baada ya eda ya kufiwa akaolewa, kisha akarudi mume wake wa

kwanza kutoka safarini, ni wajibu watengane na mume wa pili na

atakuwa halali kwa mume wake wa kwanza, lakini kama mume wa

pili alisha mwingilia ni wajibu kwa mwanamke baada ya kutengana

akae eda, na mume wa pili ampe mahari yote, lakini sio wajibu kwa

mume wa pili kumpa matumizi akiwa katika eda.

259

Al-Masailul Islamiyah

Page 274: al-Masailu-l-Islamiyyah

HUKUMU ZA TALAKA

1270. Ni sharti kwa mwanaume anayetoa talaka kwa mke wake, awe ame-

baleghe, awe na akili timamu, awe na hiyari, na kama atalazimish-

wa kutoa talaka, basi talaka itakuwa batili, ni sharti pia kukusudia

talaka kama atasema swigha ya talaka kwa mzaha haitasihi.

1271. Ni sharti wakati wa kutoa talaka mke awe ametoharika kutokana na

damu ya hedhi na damu ya nifasi na mume wake asiwe

amemwingilia katika hiyo tohara

1272. Talaka ya mke inasihi akiwa katika hali ya hedhi na nifasi katika

mambo matatu yafuatayo:-

Kama mume hajamwingilia baada ya ndoa.

Akijua kuwa ana mimba na kama hajajua kuwa ana mimba akam-

taliki katika hali ya kuwa na hedhi kisha baadae ikabainika kuwa

alikuwa na mimba, basi ni bora arudie talaka kwa mara nyingine

Kama mume akiwa mbali na mke akawa hajui kuwa ametoharika

kutokana na damu ya hedhi na nifasi au laa.

1273. Kama atampa mke wake talaka kwa kudhania hana hedhi, kisha

ikabainika baadaye kuwa alikuwa na hedhi wakati wa kupewa tala-

ka basi talaka itakuwa batili, na kama atatoa talaka kwa kudhania

kuwa ana hedhi lakini ikabainika baadae kuwa alikuwa tohara basi

talaka inasihi, anayejua kuwa ana hedhi au nifasi kisha akasafiri na

akataka kumpa talaka akiwa safarini ni wajibu asubiri atoharike

kutokana na hedhi au nifasi katika muda wake wa kawaida kisha

atamtaliki akitaka.

1274. Mwanaume akitaka kumpa talaka mke wake asiyepata hedhi kwa

ajili ya maradhi ni wajibu asimwingilie kwa muda wa miezi mitatu

260

Al-Masailul Islamiyah

Page 275: al-Masailu-l-Islamiyyah

tangu alipomwingilia kisha ampe talaka.

1275. Talaka ni lazima iwe kwa lugha ya kiarabu na isikilizwe na wanaume

wawili waadifilifu, kama mume mwenyewe akitaka kusoma swigha

ya talaka na jina la mke ni Fatma ni wajibu aseme “Zaujatiy

Faatwimat twaaliq”, na kama ataweka wakala ni lazima wakala

aseme “Zaujatu Muwakily twaaliq”

1276. Mwanamke wa ndoa ya muda hana talaka bali kutoka kwa mume

wake ni kumalizika kwa muda wa ndoa au azawadiwe muda ulioba-

ki, kwa mume kusema “wahabtukil- mudah”, na wala sio lazima

ishuhudiwe na mashahidi wawili na wala sio sharti asiwe na hedhi.

Eda ya Talaka

1277. Binti ambaye hajatimia miaka tisa na mwanamke ambaye amekoma

kutokwa damu ya hedhi hawana eda, na mume wake kama

atamwingilia kisha akampa talaka basi inajuzu kuolewa baada ya

kupewa talaka bila ya kukaa eda. Lakini haijuzu kumwingilia binti

mdogo.

1278. Mwanamke ambaye anapata hedhi akipewa talaka ni wajibu akae

eda yaani akipata hedhi mara tatu eda inaisha, lakini akipewa talaka

kabla hajaingiliwa basi hakai eda anaweza kuolewa tu baada ya

kupewa talaka.

1279. Mwanamke ambaye haoni damu yake ya hedhi na ana umri waku-

pata hedhi akipewa talaka na mume wake ni wajibu akae eda kwa

muda wa miezi mitatu.

1280. Mwenye mimba akipewa talaka eda yake inaisha akijifungua tu au

kwa mimba kuharibika mfano kama akipewa talaka kisha akajifun-

gua baada ya saa eda inaisha.

261

Al-Masailul Islamiyah

Page 276: al-Masailu-l-Islamiyyah

Eda ya ndoa ya muda

1281.Mwanamke ambaye aliolewa ndoa ya muda, muda ukiisha eda yake

ni kuona hedhi mbili na mwanamke ambaye hapati hedhi ni kwa

tahadhari ya wajibu asiolewe kwa muda wa siku arobaini na tano.

Eda ya mwanamke ambaye amefiwa na mume

1282. Eda ya mwanamke ambaye amefiwa na mume ni miezi minne na

siku kumi.

1283. Ni haramu kwa mwenye eda kuvaa nguo zenye mapambo, kupaka

wanja na kila aina ya mapambo.

Talaka ya bain na talaka rejea

1284. Talaka ya baain ikishatolewa haijuzu kwa mwanaume kumrejea

mke wake bila ya ndoa mpya.

1286. Talaka ya baain imegawanyika sehemu tano:-

Talaka ya binti ambaye hajatimia miaka tisa

Talaka ya mwanamke ambaye amekoma kutokwa damu ya hedhi

Talaka ya mke ambaye hajaingiliwa baada ya ndoa

Talaka ya kujivua na mubaraati

Talaka ya mke aliyepewa talaka tatu.

1287. Talaka rejea ni talaka ambayo inajuzu kwa mwanaume kumrejea

mke wake akiwa katika eda bila ya kufunga ndoa upya.

262

Al-Masailul Islamiyah

Page 277: al-Masailu-l-Islamiyyah

Hukumu za talaka rejea

1288. Mwanaume anaweza kumrejea mke wake kwa njia mbili:-

Atamke kauli inayomaanisha kuwa amemrejea

Afanye kitendo kinachoonyesha kuwa amemrejea.

1289. Mwanaume akimpa talaka mke wake talaka tatu na alikuwa anam-

rejea katika talaka ya kwanza na ya pili au alimwacha mara mbili

kisha akamuoa upya baada ya kila talaka anakuwa haramu kwake

mpaka aolewe na mwanaume mwingine, kama akipewa talaka na

mume wa pili inakuwa halali kumuoa baada ya hapo kwa masharti

yafuatayo:-

Mume wa pili amuoe ndoa ya daima.

Mume wa pili amwingilie kimwili na ni bora atokwe na manii.

Mume wa pili amtaliki au afe.

Eda ya talaka ya mume wa pili au eda ya kufiwa ya mume wa pili

imalizike.

Talaka ya kujivua

1290. Talaka ya kujivua ni mwanamke kumpa mume wake mali ili apewe

talaka.

1291. Mume mwenyewe akitaka kusoma swigha ya talaka basi atasema

“Zaujatiy Fatwimah khaala’atuha a’laa maa badhalat”

Talaka ya mubaraati

1292. Talaka ya mubaaraati ni mume na mke kuchukiana wote, basi mke

atampa mume wake mali ili apewe talaka.

263

Al-Masailul Islamiyah

Page 278: al-Masailu-l-Islamiyyah

1293. Kama mume mwenyewe atampa talaka basi atasema “Baaraatu zau-

jatiy Fatwimah a’ala mahariha fahiya twaliqu”

1294. Ni wajibu mali anayoichukua mume katika talaka ya mubaaraati isi-

zidi mahari, lakini hakuna tatizo kama itazidi katika kujivua.

Mas’ala katika eda na talaka

1295. Mwanaume akizini na mwanamke ajinabiya kwa dhana kuwa ni

mke wake ni wajibu kwa mwanamke akae eda.

1296. Mwanaume akizini na mwanamke na anajua kuwa sio mke wake

sio wajibu kwa mwanamke kukaa eda, iwe amejua kuwa

mwanaume sio mume wake au amedhania kuwa ni mume wake.

1297. Mwanaume akimhadaa mke wa mtu apewe talaka ili yeye amuoe

na mwanamke akafanya hivyo na mume wake akampa talaka, basi

talaka na ndoa zitasihi, lakini mume aliyemuoa na mwanamke wat-

apata dhambi kubwa sana.

1298. Mwanamke ambaye mume wake amepotea na anataka kuolewa na

mume mwingine ni wajibu arejee kwa mujitahidi mwadilifu au

wakala wake na kufanya kulingana na maoni yake.

Hukumu za kujivua na mubaaraati

1299.Talaka ya mubaaraati ni kama talaka ya kujivua katika hukumu zote

ila katika mambo matatu:-

Chuki katika mubaarati inakuwa katika pande zote mbili lakini kati-

ka kujivua chuki inakuwa kwa mwanamke tu.

Ni lazima mali anayoichukua mwanaume katika mubaraati isizidi

264

Al-Masailul Islamiyah

Page 279: al-Masailu-l-Islamiyyah

mahari lakini katika talaka ya kujivua inaweza ikazidi mahari.

Mwanaume akitoa talaka ya mubaaraati kwa lafdhi ya mubaaraati

basi ni kwa tahadhari ya sunna baada ya “Baar’atuki” aseme hara-

ka “Faanti twaaliqu” kinyume na talaka ya kujivua.

HUKUMU ZA KUCHINJA MNYAMA NA

KUMUWINDA KWAKE

1300. Akichinjwa mnyama ambaye ni halali kuliwa katika njia ambayo

tutaitaja baadae, nyama yake itakuwa halali na mwili wake ni tohara

awe wa porini au wa nyumbani.

1302. Mnyama aliyeingiliwa na mtu au mnyama aliyezoea kula vinyesi

vya watu asipotoharishwa kisheria nyama yake haitakuwa halali

baada ya kuchinjwa.

1303. Akiwinda wanyama wa porini ambao nyama zao ni halali kama

vile swala, au mnyama ambaye nyama yake ni halali ambaye

alikuwa wa nyumbani kisha akawa wa porini kama ng’ombe,

ngamia wa nyumbani akikimbia atakuwa ni tohara na halali, lakini

wanyama wa nyumbani kama mbuzi, kuku wa nyumbani na

wanyama halali wa porini wanao fugwa nyumbani hawawi tohara

wala halali kwa kuwindwa.

1304. Wanyama wa porini ambao ni halali kuliwa wanakuwa tohara au

halali kwa kuwindwa wanapokuwa na uwezo wa kukimbia au kuru-

ka, hivyo kifaranga cha ndege hakiwi halali kama hakiwezi kuruka

au mtoto wa swala hawi halali kama hawezi kukimbia.

1305. Mnyama ambaye ni halali kuliwa na asiyekuwa na damu inayotoka

kwa kasi kama samaki, akijifia atakuwa tohara lakini haijuzu kuli-

wa .

265

Al-Masailul Islamiyah

Page 280: al-Masailu-l-Islamiyyah

1306. Mnyama ambaye ni haramu kuliwa kama nyoka hawawi halali kwa

kuchinjwa lakini mzoga wake ni tohara.

1307. Mnyama akizaa mtoto amekufa au akitolewa tumboni amekufa ni

haramu kula nyama yake.

NJIA YA KISHERIA YA KUCHINJA

1308. Njia ya kisheria ya kuhalalisha mnyama ni kukata mishipa minne

chini ya shingo na haitoshi kukata kidogo bali ni wajibu kuikata

kwa ukamilifu.

1309. Akikata baadhi ya mishipa minne kisha akasubiri hadi akafa kisha

akamalizia mishipa mingine hata kama hajasubiri kwa muda mpaka

kufa kwa mnyama huyo akawa hajakata mishipa kwa mfuatano

kama ilivyozoeleka, kama atakata mishipa iliyobaki kabla ya kufa

kwa mnyama atakuwa ni halali, lakini kwa tahadhari ya sunna ni

kujiepusha na huyo mnyama.

1310. Mbwa mwitu akikata shingo ya mbuzi kiasi kwamba mishipa minne

haijabaki ambayo ni wajibu kuikata wakati wa kuchinja, huyo mnya-

ma atakuwa haramu, lakini kama akikata baadhi ya shingo au sehe-

mu nyingine na mishipa minne ikawa imebakia nyama yake

inakuwa tohara na halali kama atachinjwa kisheria.

MASHARTI YA KUCHINJA

1311. Kuchinja kisheria kuna masharti matano:-

Mchinjaji awe ni muislamu, mwanaume au mwanamke asiye dhi-

hirisha uadui kwa watu wa nyumba ya Mtume na kama atakuwa ni

mtoto wakiislamu anayejua zuri na baya inajuzu kuchinja.

266

Al-Masailul Islamiyah

Page 281: al-Masailu-l-Islamiyyah

Achinjwe mnyama kwa kisu kikali, kama hakitapatikana na mnya-

ma akataka kufa bila kuchinjwa inajuzu atumie kitu chochote kikali

kama chupa, jiwe n.k.

Amuelekeze kibla wakati wa kuchinja yaani (uso wa mnyama,

mikono, miguu na tumbo vielekezwe kibla na kama hakumuelekeza

kibla kwa kukusudia nyama itakuwa haramu, lakini akisahau au

akiwa hajui au akiwa hajui upande wa kibla au hakuweza

kumwelekeza mnyama kibla hapatakuwa na tatizo akimchinja kati-

ka hali hizi.

Akitaka kuchinja au kuweka kisu shingoni ataje jina la Mwenyezi

Mungu kwa nia ya kuchinja na inatosha kusema “Bismaillah” na

akitaja jina la Mwenyezi Mungu sio kwa nia ya kuchinja, mnyama

hatatoharika na nyama yake itakuwa haramu, na vile vile kama

hakutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kutojua lakini hakuna tatizo

kwa aliyesahau.

Ajitikise mnyama angalau mtikisiko mdogo baada ya kuchinjwa,

mfano kupepesa jicho, kutikisa mkia au miguu yake.

NJIA YA KISHERIA YA KUCHINJA NGAMIA

1312. Akitaka kumhalalisha ngamia ili awe tohara na halali ni wajibu kwa

kuongezea kuzingatia masharti yaliyo tangulia katika kuchinja atain-

giza kisu au kinachofanana na kisu katika “luba” nayo ni sehemu ya

juu iliyoingia ndani ambayo imekutana na shingo na hii inaitwa

“nahri”, kudunga inalazimu kumuelekeza kibla yaani uso wake

uelekee kibla.

1313. Ni bora wakati wa kumdunga ngamia awe amesimama na hakuna

tatizo kama atakuwa amelala kwa ubavu ila aelekee kibla.

14. Kama atachinjwa ngamia badala ya nahri au ikatumika nahri kwa

267

Al-Masailul Islamiyah

Page 282: al-Masailu-l-Islamiyyah

mbuzi au ng’ombe badala ya kuchinjwa nyama zitakuwa ni haramu na

mwili utakuwa ni najisi, lakini akikata mishipa ya ngamia kisha akatu-

mia njia ya nahri kwa njia tuliyoitaja nyama yake itakuwa halali na

mwili wake utakuwa tohara ,na pia mbuzi au ng’ombe ikitumika njia

ya nahri na kabla ya kufa ikakatwa mishipa minne nyama zitakuwa ni

halali na miili yao itakuwa ni tohara.

1315. Mnyama akiwa mkaili na ikashindikana kuchinjwa kwa njia iliy-

otajwa kisheria au akiangukia kisimani kiasi kwamba anataka kufa

huko na haikuwezekana kumchinja kisheria, inajuzu kumjeruhi kati-

ka sehemu yeyote ya mwili ili afe kwa sababu ya jeraha ,na atakuwa

halali na haimlazimu kumuelekeza kibla lakini lazima azingatie

masharti mengine tuliyoyataja katika kuchinja.

MAMBO YA SUNNA WAKATI WA KUCHINJA

1316. Ni sunna katika kuchinja mambo yafuatayo:-

1. Ni sunna katika kumchinja mbuzi amfunge mikono yake miwili na

mguu mmoja ama ng’ombe, ni sunna kumfunga mikono miwili na

miguu pia na anauacha mkia, ama ngamia ni sunna kumfunga mikono

na kwa ndege ni sunna amuache baada ya kumchinja ili afurukute.

2. Mwenye kuchinja aelekee kibla.

3. Ampe mnyama maji kabla ya kumchinja.

4. Asimtese mnyama, anoe kisu chake vizuri na afanye haraka kumch-

inja na asimuonyeshe kisu kabla ya kuanza kumchinja.

YALIYO MAKURUHU WAKATI WA KUCHINJA

1317. Ni makuruhu katika kuchinja mambo yafuatayo:-

1. Kukata mishipa kuanzia kisogoni

2. Kutenganisha kichwa cha mnyama na mwili kabla ya kutoka kwa

roho, lakini akifanya hivyo kwa kughafilika, au kwa sababu kisu ni

268

Al-Masailul Islamiyah

Page 283: al-Masailu-l-Islamiyyah

kikali mno na bila yakutarajia hivyo haitakuwa makuruhu

3. Kumchuna mnyama kabla ya kutokwa na roho

4. Kukata nyama yake kabla ya kutokwa na roho

5. Kumchinja mnyama na mwingine anamwangalia

6. Kumchinja mnyama usiku au mchana kabla jua halijapetuka katika

siku ya ijumaa, hakuna tatizo wakati wa dharura na haja

7.Mfugaji kumchinja mnyama aliyemlea mwenyewe.

HUKUMU ZA KUWINDA KWA SILAHA

1318. Akiwinda mnyama wa porini aliye halali kuliwa kwa silaha,

nyama yake inakuwa halali na mwili wake unakuwa tohara kwa

masharti matano:-

Silaha ya kuwindia iwe ni yenye kukata kama vile kisu, panga au

kitu kikali kama mshale ambao makali yake yanakata mwili wa

mnyama, mtu akiwinda kwa kutumia mtego au fimbo au jiwe na

mengineyo na mnyama huyo akafa kwa ajili hiyo, hatatoharika na

nyama yake itakuwa ni haramu.

Na kuwinda kwa silaha za moto kama vile bunduki kama risasi yake

ina makali ya kuweza kuchana mwili wa mnyama basi huyo mnya-

ma atakuwa tohara na nyama yake pia ni halali, na kama silaha haina

makali kiasi kwamba inaingia kwenye mwili wa mnyama kwa

nguvu na kumuua, kwa dhahari ni halali lakini akimuunguza kwa

joto lake na akafa kwa sababu hiyo utohara wake na uhalali wake ni

mahali pa mushikeli.

Ni wajibu muwindaji awe muislamu au mtoto wa muislamu mwenye

kutofautisha kati ya zuri na baya, na pindi anapowinda kafiri au

mwenye uadui na watu wa nyumba ya Mtume (saww) mnyama huyo

269

Al-Masailul Islamiyah

Page 284: al-Masailu-l-Islamiyyah

hatakuwa halali.

Atumie silaha ya kuwindia na kama atarusha risasi sehemu pasina

kukusudia kupiga mnyama kisha akapiga mnyama bila ya kutege-

mea mnyama hatakuwa halali na pia hatokuwa tohara.

Ataje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kutumia silaha na asipota-

ja jina la Mwenyezi Mungu kwa kukusudia mnyama huyo hatakuwa

halali, lakini akisahau hakuna tatizo.

Akute mnyama ameshakufa au amkute akiwa hai na wakati wa

kuchinja ukawa mfinyu, kama muda ulikuwa unamruhusu kuchinja

halafu akaacha kumchinja mpaka akafa nyama yake itakuwa ni hara-

mu.

1319. Wakishirikiana watu wawili katika kuwinda mmoja muislamu na

mwingine ni kafiri na mmoja akataja jina la Mwenyezi Mungu na

mwingine hakutaja kwa makusudi huyo mnyama hatakuwa halali.

1320. Akiwinda kwa silaha au mbwa wa wizi windo litakuwa ni halali

kwake, lakini atakuwa ameasi na ni wajibu wake atoe ujira kwa

mwenye silaha au mbwa.

1321 Akiwinda kwa upanga au mfano wake akawa amemkata mnyama

vipande viwili na kwa kuzingatia masharti, na mnyama akakatika

vipande viwili na kikabaki kichwa na shingo kwa kujitenga na

mwili, akikuta amekufa atakuwa halali vipande vyote na vile vile

akimkuta hai lakini hakupata wakati mpana wa kumchinja, ama

wakati wa kuchinja ukiwa mpana na ikawezekana kumchinja, basi

kipande kilichojitenga na kichwa kitakuwa haramu, na upande

wenye kichwa utakuwa halali kama atamchinja kisheria, la sivyo

huo upande pia uatakuwa haramu.

270

Al-Masailul Islamiyah

Page 285: al-Masailu-l-Islamiyyah

1322. Akiwinda mnyama na akamchinja na wakakuta tumboni mwa mnya-

ma kuna mtoto mfu, kama amekamilika kimaumbile na akawa

ameota manyoya au sufi na ikawa kifo cha mtoto kimesababishwa

na kuchinjwa kwa mnyama huyo, mtoto atakuwa tohara na halali.

KUWINDA KWA KUTUMIA MBWA

1323. Mbwa akiwinda mnyama wa porini ambaye nyama yake ni halali

utohara na uhalali wa huyo mnyama utatimia kwa masharti sita:-

1. Mbwa awe amefundishwa kiasi kwamba akitumwa anaenda na aki-

ambiwa simama anasimama na ikawa ni kawaida yake kiasi kuwa

hawezi kula kabla ya kufika mwenyewe na hakuna tatizo akimla mnya-

ma bila kutarajia

2. Atumwe na mwenyewe kushika mnyama na kama mbwa akiondoka

kushika mnyama bila ya kuamrishwa na mwenyewe huyo mnyama

atakuwa haramu.

3. Na anayemtuma mbwa awe ni muislamu au mtoto wa muislamu

mwenye kutofautisha kati ya kheri na shari, na kama anayemwamrisha

ni kafiri au ana chuki na watu wa nyumba ya Mtume (saww) windo la

huyo mbwa litakuwa haramu.

5. Ataje jina la Mwenyezi Mungu pindi anapomwamuru mbwa na kama

ataacha kutaja jina la Mwenyezi Mungu kwa kukusudia hilo windo

litakuwa haramu na kama atakuwa amesahau haitakuwa na mushikeli.

6. Mnyama afe kwa sababu ya kujeruhiwa na meno ya mbwa kama atam-

nyonga mnyama au akifa kwa kukimbia au kuogopa hatakuwa halali

7. Mwenye kumtuma mbwa amkute amekufa au akimkuta hai wakati wa

271

Al-Masailul Islamiyah

Page 286: al-Masailu-l-Islamiyyah

kuchinja ukawa ni mfinyu, kama wakati ukiwa unatosha kumchinja

mfano, amkute akiwa anapepesa macho yake au kutikisa mkia au miguu

kama hatomchinja mpaka akafa hata kuwa halali.

KUVUA SAMAKI

1324. Akivua samaki mwenye magamba kwenye maji na akafia nchi kavu

atakuwa ni tohara na nyama yake ni halali na akifia kwenye maji

atakuwa ni tohara lakini nyama yake ni haramu, ama samaki

ambaye hana magamba yeye ni haramu hata kama akitolewa

kwenye maji akiwa hai na akafia nchi kavu.

1325. Sio sharti mvuvi wa samaki awe muislamu na pia si wajibu kutaja

jina la Mwenyezi Mungu wala kuelekea kibla na kumchinja kwa

kisu, hivyo inajuzu kula samaki aliyevuliwa na kafiri lakini ni

wajibu muislamu azingatie kuvua kwake na ajue kuwa samaki ame-

vuliwa akiwa hai na amefia nchi kavu.

1326. Samaki aliyekufa ambaye hajulikani kuwa amevuliwa akiwa hai au

amekufa, kama samaki atakuwa kwa muislamu atakuwa halali na

kama atakuwa kwa kafiri atakuwa haramu hata kama akisema

amemvua akiwa hai, ila mtu akipata matumaini kwa maneno yake.

1327. Hailazimu kujiepusha kula samaki aliye hai.

KUWINDA SENENE/NZIGE

1328. Akimshika senene/nzige hai kwa mkono wake au kwa njia nyingine

atakuwa ni halali baada ya kufa kwake na si lazima aliyeshika

senene awe muislamu, na pia si lazima kutaja jina la Mwenyezi

272

Al-Masailul Islamiyah

Page 287: al-Masailu-l-Islamiyyah

Mungu wakati wa kuwashika, na ukiwapata senene kwa kafiri na

haijulikani kuwa amewachukua wakiwa hai au wakiwa wamekufa

hawatakuwa halali kuliwa hata kama akisema amewachukua waki-

wa hai, ila kama atapata matumaini kutokana na maneno yake.

HUKUMU ZA KULA NA KUNYW A

1329. Ni halali kula nyama ya kuku, njiwa, ndege wenye mwiba nyuma ya

mguu na ni haramu kula popo, tausi na kila ndege ambaye ana

makucha kama vile kipanga, mwewe na ambaye kupiga mabawa

wakati wa kuruka ni mara chache kuliko kutulizana, na kila ndege

asiye na mwiba nyuma ya mguu wake ila ikiwa kupiga mabawa ni

kwingi kuliko kutulizana basi atakuwa halali.

1330. Kama kipande cha nyama kikijitenga na mwili wa mnyama mfano:

Mkia au kipande cha nyama ambacho kinakatwa kwa mbuzi aliye

hai, kipande hicho ni najisi na ni haramu.

1331. Ni haramu vitu vifuatavyo kwa mnyama aliyechinjwa kisheria:-

1. Kinyesi

2. Damu

3. Uume

4.Uke

5. Mfuko wa kuhifadhi mtoto tezi na kokwa mbili

8. Kitu mfano wa punje katikati ya ubongo

9. Kandama

10. Mshipa wa uti wa mgongo

11. Makamasi nyongo kibofu

12. Mboni ya jicho mishipa iliyo baina ya kwato.

1332. Ni haramu kula chochote kinachomzuru mtu kwa madhara makub-

wa.

273

Al-Masailul Islamiyah

Page 288: al-Masailu-l-Islamiyyah

1333. Ni makuruhu kula nyama ya punda na farasi na kama mtu aki-

waingilia wanyama hawa nyama zao zitakuwa ni haramu, na ni

wajibu kuwatoa nje ya mji na kuwauza sehemu nyingine.

1334. Na mtu akimwingilia mnyama mwenye kuliwa kama ng’ombe na

mbuzi, basi mkojo na kinyesi chake kitakuwa najisi na maziwa

yatakuwa haramu kunywewa, na ni wajibu kumuuwa mnyama huyo

kwa haraka na mwenye kumwingilia alipe thamani yake kwa

mwenye ng’ombe.

1335. Ni haramu kukaa sehemu inayonywewa pombe au kileo chochote,

na pia ni haramu kula chochote katika meza inayonywewa pombe

juu yake.

1336. Ni wajibu kwa kila muislamu kumlisha na kumnywesha muislamu

mwenzake anayekaribia kufa kwa njaa au kwa kiu na kumuokoa

kutokana na mauti na kuhiliki, na vivyo hivyo kwa kila nafsi yenye

kuheshimika.

MAMBO YA SUNNA WAKATI WA KULA

1337. Ni sunna katika kula mambo yafuatayo:-

1. Kuosha mikono miwili kabla ya kula

2. Kuosha mikono miwili baada ya kula

3. Mwenye nyumba aanze kula kabla ya yeyote na amalize baada ya

kumaliza wote.

4. Kutaja jina la Mwenyezi Mungu unapoanza kula lakini kama kwenye

meza kuna vyakula vingi basi atataja jina la Mwenyezi Mungu katika

kila aina ya chakula.

5. Kula kwa mkono wa kulia

6. Ale kwa vidole vitatu au zaidi na asile kwa vidole viwili.

7. Ale kinachomuelekea katika chakula kama wanaokula ni wengi

274

Al-Masailul Islamiyah

Page 289: al-Masailu-l-Islamiyyah

8. Ale tonge dogo

9. Ale kwa muda mrefu na wala asifanye haraka katika kula

10.Atafune chakula vizuri

11.Alambe vidole vyake baada ya kula

12.Amshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kula

13.Achokonoe meno yake baada ya kula lakini asichokonoe kwa kijiti cha

mkomamanga, muwa wala kwa mti wa mtende.

14. Aokote mabaki ya chakula yaliyodondoka kwenye meza na kuyala na

kama atakuwa anakula porini au jangwani ni sunna kuwaachia ndege

na wanyama

15. Ale chakula mwanzo wa mchana na mwanzo wa usiku na asile katikati

ya mchana na katikati ya usiku

16. Aanze kula kwa chumvi na kumalizia kwa chumvi

17. Aoshe matunda kabla ya kuanza kula

18. Alale chali baada ya chakula na kuweka mguu wake wa kulia juu ya

mguu wa kushoto.

YALIYO MAKURUHU WAKATI WA KULA

1338. Yaliyomakuruhu wakati wa kula ni:-

1. Kula wakati umeshiba

2. Kula sana

3. Kuangalia uso wa mwenzako wakati wa kula.

4. Kula chakula cha moto

5. Kupuliza unachokula au unachokunywa

6. Kukata mkate kwa kisu

7. Kuweka mkate chini ya chombo

8. Kula nyama na kutobakisha kitu kwenye

mfupa

9. Kumenya matunda ambayo yanawezekana kuliwa bila kumenywa

10. kutupa tunda kabla ya kulila kwa ukamilifu.

275

Al-Masailul Islamiyah

Page 290: al-Masailu-l-Islamiyyah

MAMBO YA SUNNA WAKATI WA KUNYWA MAJI

1339. Yafuatayo ni sunna wakati wa kunywa:-

1. Anywe maji kwa kunyonya

2. Anywe maji mchana kwa kusimama na usiku kwa kukaa

3. Amtaje Mwenyezi Mungu kabla ya kunywa na baada ya kunywa

amshukuru Mwenyezi Mungu

4. Anywe maji kwa funda tatu

5. Awe na kiu ya maji na asinywe bila ya kuwa

na kiu.

6. Amkumbuke Imamu Hussein “as” na watu wa nyumba ya Mtume

na awalaani waliomuuwa Imamu Husein.

YALIYO MAKURUHU WAKATI WA

KUNYWA MAJI

1340.Ni makuruhu wakati wa kunywa mambo yafuatayo:-

1. Kunywa maji sana

2. Kunywa maji baada ya kula chakula chenye mafuta

3. Kunywa maji usiku kwa kusimama

4. Kunywa maji kwa mkono wa kushoto

5. Kunywa maji katika sehemu iliyovunjika au iliyo na mapengo

katika kikombe.

HUKUMU ZA MIRATHI

1341. Ambao wanarithi kwa nasaba ni tabaka tatu:-

Kwanza: Wazazi wa marehemu na watoto wake, kama hakuna watoto basi

watoto wa watoto wao na kuteremka chini, na anarithi kwao kila aliyeku-

276

Al-Masailul Islamiyah

Page 291: al-Masailu-l-Islamiyyah

wa karibu zaidi kwa marehemu na maadamu anapatikana mmoja katika

tabaka hili hatarithi yeyote kutoka katika tabaka la pili.

Pili: Babu, bibi na ndugu wa marehemu na kama hawapo basi watoto wao

wanarithi na kila aliye karibu zaidi na marehemu na maadamu anapatika-

na yeyote katika tabaka hili harithi yeyote kutoka katika tabaka la tatu.

Tatu: Ami, shangazi, mjomba na mama wadogo wa marehemu na watoto

wao na maadamu anapatikana yeyote kati ya ami, shangazi, mjomba na

mama wadogo hatorithi yeyote kati ya watoto wao, lakini kama marehemu

ataacha Ami wa upande wa baba tu na mtoto wa Ami wa upande wa baba

na mama, mtoto wa ami wa upande wa baba na mama atarithi bila ya Ami

wa upande wa baba tu.

1342. Kama marehemu hana ami, shangazi,mjomba na mama wadogo

wala watoto wao wala watoto wa watoto wao watarithi ami wa baba

yake na mama yake, shangazi zao na wajomba zao kama hawapo

watoto wao na kama hawapo basi wanarithi ami, shangazi, wajom-

ba na mama wadogo wa babu na bibi yao na kama hawapo basi

watarithi watoto wao.

1343.Mume na mke kila mtu anamrithi mwenzake kwa utaratibu utakao

kuja pamoja na kila tabaka katika matabaka matatu yaliyotajwa.

MIRATHI YA TABAKA LA KWANZA

1344. Marehemu akiacha mtu mmoja katika tabaka la kwanza kama vile

baba au mama au mtoto wa kiume au mtoto wa kike anarithi mali

yote na kama ataacha watoto wa kiume wengi au watoto wakike

wengi mali itagawanywa sawa baina yao, na kama ataacha mtoto

mmoja wa kiume na mtoto mmoja wa kike mali itagawanywa sehe-

mu tatu, mtoto wa kiume atapewa sehemu mbili na mtoto wa kike

atapewa sehemu mmoja, na kama ataacha watoto wa kiume wengi

na watoto wa kike wengi basi mali itagawanywa kwa namna

277

Al-Masailul Islamiyah

Page 292: al-Masailu-l-Islamiyyah

ambayo mtoto wa kiume atarithi mara dufu ya mtoto wa kike.1345. Kama marehemu ataacha wazazi wawili mali itagawanywa sehemu

tatu mzazi wa kiume atapewa sehemu mbili na mzazi wa kike ata-pewa sehemu moja, na kama marehemu ataacha pamoja na nduguwawili wa kiume au dada wawili au kaka na dada wawili na wotewakawa ni wa upande wa baba tu au wa upande wa mama waohawatarithi kwa marehemu maadamu marehemu ana baba na mamaisipokuwa mama wa marehemu kwa sabau yao atarithi moja ya sita“1/6” na mali iliyobaki atapewa baba wa marehemu.

1346. Marehemu akiacha wazazi wawili na binti mmoja kama marehemuhana kaka wawili wala dada wawili au dada wanne au kaka mmojana dada wawili wa upande wa baba mali itagawanywa sehemu tano,baba na mama kila mmoja atarithi sehemu moja na binti atarithisehemu tatu na kama marehemu ana kaka wawili au dada wanne aukaka na dada wawili wa upande wa baba mali itagawanywa sehemusita baba na mama kila moja atapata sehemu moja na binti atapewasehemu tatu, sehemu iliyobaki “1/6” itagawanywa sehemu nne babaatapewa sehemu moja na binti atapewa sehemu zilizobakia kwamfano kama itagawanywa mali ya marehemu sehemu 24 binti ata-pewa sehemu 15, baba atapewa sehemu 5 na mama atapewa sehemu4.

1347. Marehemu akiacha wazazi wawili na mtoto wa kiume mali itagawa-

nywa sehemu sita wazazi wawili kila mmoja atapewa sehemu moja

na sehemu nne atapewa mtoto wa kiume, na akiacha pamoja nao

watoto wengi wa kiume au watoto wengi wa kike mali itagawanywa

sawa baina yao, ama wakiwa ni watoto wa kiume na watoto wa kike

mali itagawanywa kwa namna ambayo mtoto wa kiume atachukua

mara dufu ya mtoto wa kike.

1350. Marehemu akiacha baba na mtoto mmoja wa kiume au mama na

mtoto mmoja wa kike mali itagawanywa sehemu sita sehemu moja

anapewa baba au mama na sehemu zilizobaki anapewa mtoto wa

kiume.

278

Al-Masailul Islamiyah

Page 293: al-Masailu-l-Islamiyyah

1351. Marehemu akiacha baba na mtoto wa kiume na binti au mama na

watoto wa kiume na binti mali itagawanywa sehemu sita, sehemu

moja anapewa baba au mama na sehemu zilizobakia zitagawanywa

kwa namna ambayo mtoto wa kiume atapata mara dufu ya binti.

1352. Marehemu akiacha baba na binti mmoja au mama na binti mmoja

mali itagawanywa sehemu nne sehemu moja atapewa baba au mama

na baki atapewa binti.

1353. Marehemu akiacha baba tu na watoto wa kike wengi au mama tu na

watoto wengi wa kike mali itagawanywa sehemu tano, sehemu moja

atapewa baba au mama na sehemu zilizobakia zitagawanywa kwa

watoto wa kike kwa usawa.

1354. Kama marehemu hajaacha mtoto wa kiume wala binti watarithi

watoto wa watoto wake wa kiume hisa ya watoto wa kiume hata

kama wao watakuwa ni wanawake, na watoto wa kike watarithi hisa

ya watoto wake wa kike hata kama watakuwa ni wanaume mfano,

kama marehemu ataacha mjukuu wa kiume wa binti yake na mjukuu

wa kike wa mtoto wake wa kiume mali itagawanywa sehemu tatu,

sehemu moja atapewa mtoto wa kiume wa binti yake na sehemu

mbili atapewa mtoto wa kike wa mtoto wake wa kiume.

MIRATHI YA TABAKA LA PILI

1355. Tabaka la pili linalorithi kwa nasaba ni babu, bibi, ndugu wa kiume

na wa kike wa marehemu na kama hajaacha ndugu wakiume na

wakike basi watoto wao ndio watarithi.

1356. Marehemu akiacha ndugu wa kiume tu au ndugu wa kike tu basi

mali yote ni yake, na wakiwepo ndugu wa kiume wengi na ndugu wa

kike wengi wa wazazi wawili mali itagawanywa baina yao kwa

usawa, na ikiwa ndugu wa kiume wengi na ndugu wa kike wengi

279

Al-Masailul Islamiyah

Page 294: al-Masailu-l-Islamiyyah

ndugu wa kiume watarithi mara dufu ya ndugu wa kike, mfano kama

ataacha ndugu wa kiume wawili na ndugu mmoja wa kike mali ita-

gawanywa sehemu tano kila ndugu wa kiume atapewa sehemu mbili

na ndugu wa kike atapewa sehemu moja.

1357. Kama marehemu ataacha ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa

wazazi wawili, ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa upande wa

baba tu hawatarithi, kama ataacha ndugu wa kiume au ndugu wa

kike wa upande wa baba tu atarithi mali yote, na akiacha ndugu wa

kiume kama ndugu wakiwa wengi wa upande wa baba tu mali ita-

gawanywa baina yao kwa usawa, na kama ataacha ndugu mmoja wa

kiume na ndugu wakike wengi mwanaume atarithi mara dufu ya

mwanamke.

1358. Marehemu akiacha ndugu wa kiume mmoja au ndugu wa kike

mmoja tu wa upande wa mama, atarithi mali yote na akiacha ndugu

wa kiume wengi au ndugu wa kike wengi wa upande wa mama tu

mali itagawanywa baina yao kwa usawa. Marehemu akiacha ndugu

wa kiume na ndugu wa kike wa wazazi wawili au ndugu wa kiume

na ndugu wa kike wa upande wa baba tu na ndugu wa kiume au wa

kike wa upande wa mama tu, ndugu wa upande wa baba tu hawata-

rithi na mali itagawanywa sehemu sita, sehemu moja atapewa ndugu

wa kiume na ndugu wa kike wa upande wa mama tu, na sehemu zili-

zobaki ni za ndugu wa kiume, na ndugu wa kike wa wazazi wawili

na wanaume watarithi mara dufu ya wanawake.

1359. Marehemu akiacha ndugu wa kiume na ndugu wa kike wa wazazi

wawili, ndugu wakiume na ndugu wakike wa upande wa baba tu na

ndugu wa kiume na ndugu wakike wa upande wa mama tu ndugu wa

kiume na ndugu wa kike wa upande wa baba hawatarithi na mali ita-

gawanywa sehemu tatu, sehemu itagawanywa baina ya ndugu wa

kiume na ndugu wa kike wa mama kwa usawa na iliyobakia wata-

pewa ndugu wa wazazi wawili na mwanaume atapata mara dufu ya

mwanamke.

280

Al-Masailul Islamiyah

Page 295: al-Masailu-l-Islamiyyah

1360. Marehemu akiacha kaka na dada wa upande wa baba tu na kaka au

dada wa upande wa mama tu mali itagawanywa sehemu sita, sehe-

mu moja ni ya kaka au dada wa upande wa mama, na iliyobaki ita-

gawanywa baina ya kaka na dada wa upande wa baba tu na mwa-

naume atapata mara dufu ya anayopata mwanamke.

1361. Marehemu akiacha kaka na dada na mke, mke atarithi kwa namna

ambayo utakuja ufafanuzi wake, na kaka na dada watarithi kwa

namna iliyotangulia kutajwa katika mas’ala yaliyotangulia, vivyo

hivyo akifa mke na akaacha kaka, dada na mume wake, mume ata-

rithi nusu ya mali na kaka na dada watarithi kwa namna iliyotajwa

katika mas’ala yaliyotangulia, lakini kurithi kwa mke au mume hai-

punguzi hisa ya kaka na dada wa wazazi wawili au wa upande wa

baba tu.

1362. Marehemu akiacha babu au bibi ni sawa awe wa upande wa baba au

wa upande wa mama tu, atarithi mali yote, babu akiwepo mzazi wa

babu hatarithi.

MIRATHI YA TABAKA LA TATU

1363. Tabaka la tatu ni Ami wa marehemu, wajomba, mama wadogo na

watoto wao kama hatakuwepo yeyote katika tabaka lililotangulia.

1364. Marehemu akiacha Ami, shangazi ni sawa awe ni wa upande wa

wazazi wawili au wa upande wa baba tu anarithi mali yote, na akia-

cha Ami wengi au shangazi wengi mali itagawanywa baina yao kwa

usawa.

1365. Marehemu akiacha mjomba au mama mdogo anarithi mali yote na

akiacha mjomba na mama mdogo na wote ni wa upande wa wazazi

wawili au wa upande wa baba tu mali itagawanywa baina yao kwa

usawa na kwa tahadhari waelewane katika kugawana.

281

Al-Masailul Islamiyah

Page 296: al-Masailu-l-Islamiyyah

MIRATHI YA MUME NA MKE

1366. Mke akifariki na akawa hajaacha watoto mume anarithi nusu ya mali

yake na inayobaki wanapewa watu wengine wa upande wa mke na

ikiwa ana watoto kwa huyo mume au kwa mume mwingine mume

anarithi robo ya mali yake na iliyobaki wanarithi wengine.

1367. Mume akifariki na akawa hajaacha watoto, mke anarithi robo ya

mali na iliyobaki wanarithi wengine na kama ana watoto kwa huyo

mume au kwa mume mwingine mke atarithi moja ya nane (1/8).

1368. Mke harithi ardhi na wala harithi nyumba, jengo na miti, lakini ana-

rithi thamani yake.

1369. Mke akitaka kurithi ardhi au kutumia vitu ambavyo havirithi ni waji-

bu atake idhini kwa warithi wengine na vivyo hivyo warithi wengi-

ne kwa tahadhari ya wajibu wasitumie vitu ambavyo mke anarithi

thamani yake kabla hawajampa hisa yake isipokuwa kama atatoa

idhini vinginevyo muamala utakuwa batili.

1370. Kama marehemu ana mke zaidi ya mmoja na hana watoto robo ya

mali yake itagawanywa kwa wake zake kwa usawa na kama ana

watoto (1/8) moja ya nane ya mali yake itagawanywa kwa wake

kwa usawa.

1371. Kama ataoa mke katika hali ya maradhi kisha akafa kwa maradhi

hayo mke wake atamrithi hata kama hakumwingilia.

1372. Mke akiachwa talaka rejea kisha akafa katika eda mume wake atam-

rithi, vivyo hivyo kama mume atafariki ndani ya eda yake mke ata-

rithi, lakini kama mmoja akifa baada ya kumalizika eda ya talaka

282

Al-Masailul Islamiyah

Page 297: al-Masailu-l-Islamiyyah

rejea au katika eda ya talaka bain hatamrithi.

1374. Mwislamu anarithi kwa kafiri lakini kafiri harithi kwa mwislamu

hata kama atakuwa ni mtoto wa marehemu au baba yake.

1375. Mtu akimuuwa yeyote kwa makusudi au kwa dhulma hatamrithi.

TALAQIN YA MAIT

283

Al-Masailul Islamiyah

Page 298: al-Masailu-l-Islamiyyah

284

Al-Masailul Islamiyah

Page 299: al-Masailu-l-Islamiyyah

285

Al-Masailul Islamiyah

Page 300: al-Masailu-l-Islamiyyah

BACK COVER

Historia fupi ya Ayatullah al-Udhmaa Sayyid Sadiq Shirazi (dama

dhilluhu).

Amezaliwa katika mwezi wa Dhilhijjah mwaka 1360 Hijria mwafaka namwaka 1948 Miladia katika mji mtukufu wa Karbala, Iraq.

Amesoma kwa marjaa taklidi na maulamaa wakubwa katika vyuo vikuu

vya kidini (hawza) hadi akafikia daraja la juu kabisa la kutoa fatwa na ijti-

hadi na kuwa mujtahidi.

Amelelewa katika nyumba kongwe ya ukoo wenye elimu kubwa na

uliobobea katika fikihi, ijtihadi, jihadi na kujitolea.

Ayatullah Shirazi amekua na kupambika umri wake kwa moyo wa ikhlasi,

ucha Mungu, amali na fikra njema zinazokwenda sambamba na

mafundisho ya Qur’ani Tukufu na Ahlul Bait (a.s.).

Ametunga vitabu vingi katika viwango mbalimbali ya ufahamu, miongoni

mwao vikiwepo:

Sharh al-‘Urwatu ‘l-Wuthqaa, Ijtiha wa Taqlid, Bayanu ‘l-Usul, Qa’idah

La Dharar Walaa Dhiraar, n.k.

Vivyo hivyo, ameandika vitabu vya masomo kwa ajili ya wanafunzi wa

Hawza, k.v. Rawdhah Fiy Sharh al-Lum’ah, Sharh al-Sharaa’i’, Sharh at-

Tabsirah, Sharh Suyuti, Sharh Samadiyyah, Mu’jazi Fiy Mantiq, n.k.

Zaidi ya miaka ishirini sasa, Ayatullah Sayyid Sadiq Shirazi amekuwa aki-

toa darsa za khariji za Usuli Fikihi ambazo ni darsa za juu kabisa katika

Hawza. Wanafunzi na hata maulamaa waliofikia daraja la ijtihadi ni mion-

goni wa wenye kuhudhuria darsa zake na kunufaika kwazo.