Top Banner
1 AHLUL ~ KISAA Mkusanyiko wa sifa na tarehe za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Imamu Ali, Bibi Fatimah, Imamu Hassan na Imamu Hussein Kimetungwa na: Ahmad Badawy bin Muhammad Al-Husseiny Kimehaririwa na: Sheikh Harun Pingili Yamefuatia Mashairi ya MWENYE MANSABU Yaitwayo "KISHAMIA" Kimetolewa na Kuchapishwa na: BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA P.0. BOX 20033 DAR ES SALAAM - TANZANIA. www.allamahrizvi.com
58

AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

Feb 11, 2018

Download

Documents

vudat
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

1

AHLUL ~ KISAA

Mkusanyiko wa sifa na tarehe

za

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Imamu Ali, Bibi Fatimah,

Imamu Hassan na Imamu Hussein

Kimetungwa na:

Ahmad Badawy bin Muhammad Al-Husseiny

Kimehaririwa na:

Sheikh Harun Pingili

Yamefuatia Mashairi ya

MWENYE MANSABU

Yaitwayo

"KISHAMIA"

Kimetolewa na Kuchapishwa na:

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

P.0. BOX 20033

DAR ES SALAAM - TANZANIA.

www.allamahrizvi.com

Page 2: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

2

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:

Bilal Muslim Mission of Tanzania

ISBN 9976 956 48 7

Toleo la kwanza (Lilitolewa na Islamic research Organisation-

Mombasa, Kenya) 1964

Toleo la Pili 1989: Nakala 5,000

Toleo la Tatu 1998: Nakala 5,000

Kimetolewa na kuchapishwa na:

Bilal Muslim Mission of Tanzania

P.O. BOX 20033, DAR ES SALAAM

TANZANIA

www.allamahrizvi.com

Page 3: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

3

YALIYOMO

1. Dibaji...........................................................................

2. Utangulizi ..................................................................

3. Maana ya Ahlul - Kisaa ..............................................

4. Kuolewa kwake ..........................................................

5. Kifo Chake ................................................................

6. Imamu Ali .................................................................

7. Nasaba Yake ..............................................................

8. Kuzaliwa ........... ........................................................

9. Kusilimu Kwake .........................................................

10. Utukufu Wake ...........................................................

11. Ushujaa Wake ...........................................................

12. Kisa cha Anas bin Malik ............................................

13. Elimu ya Imamu Ali ............ ........................................

14. Sifa Zake ............................... .................................

15. Yeye na Ukhalifa .......................................................

16. Utawala Wake (Hitilafu Yake) ....................................

17. Vita vya Jamal (Ngamia) ............................................

18. Vita vya Siffin ............................................................

19. Uamuzi (Tahkim)........................................................

20. Kuuawa kwa Imamu Ali ...............................................

21. Familia Yake ..............................................................

22. Misemo Yake .............................................................

23. Imamu Hasan .............................................................

24. Ukarimu Wake ............................................................

25. Utukufu Wake ............................................................

26. Utawala Wake (Khilafa Yake) ......................................

27. Hassan Kuacha Ukhalifa .............................................

28. Muawiya Kumrithisha Mwanawe Yazid Utawala .........

29. Kifo cha Imamu Hassan ................................

30. Misemo Yake ...................................................

31. Imamu Hussein .............................................................

32. Hussein na Ukhalifa ....................................................

33. Kifo cha Muslim bin Akil na Haani bin Arwah ..............

34. Hussein Aihama Makkah ............................................

35. Karbala ......................................................................

36. Ashura .....................................................................

37 Hotuba ya Mwisho ya Hussein ....................................

38. Wakati wa vita ...........................................................

39. Kifo cha Imamu Hussein ..............................................

40. Safari ya Syria ............................................................

41. Watoto wa Imamu Hussein ............................................

42. Misemo Yake ..............................................................

43. Maana ya Masharifu ....................................................

www.allamahrizvi.com

Page 4: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

4

DIBAJI

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu. Kila sifa

njema na shukrani ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa Ulimwengu. Rehema na amani

zimshukie Mtume Muhammad, Jamaa (Aali) zake, na Sahaba zake.

Marhum Sheikh Abdullah Saleh Farsy amefanya kazi kubwa juu ya Uislamu kwa

kutunga MAISHA YA NABII MUHAMMAD (s.a.w.w.) - Sallallahu Alaihi wa Aalihi

wa sallam). Ni muhimu sana kwa kila Mwislamu kukijua kitabu hiki, kwa sababu

kimekusanya tarehe na sifa za Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

Kadhalika, Marhum Sheikh Muhammad Kasim Mazrui amefuatisha vitabu juu ya

Makhalifa wanne, baada ya Mtume (s.a.w.w.), navyo ni:

1) Maisha ya Abubakar Asiddik, 2) Maisha ya Umar Al-Faruk, 3) Maisha ya

Uthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. Vitabu hivi vinne ni muhimu

sana na nafuu kubwa kwa Waislamu wa Afrika Mashariki, kwa sababu vinaeleza

kwa Kiswahili tarehe ya Uislamu baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

Ninawahimiza sana Waislamu, wakubwa na watoto, wavisome vitabu hivyo vitano.

Mungu awalipe malipo mazuri Marhum Sheikh Abdullah Saleh Farsy na Marhum Sheikh

Muahammad Kasim Mazrui, na vizazi vyao, Ninamwomba duniani na Akhera - Amen.

Mimi nimeona vizuri nifuatishe vitabu hivyo kwa kutunga kitabu juu ya tarehe ya

AHLUL-BAYT (Watu wa Nyumbani mwa Mtume (s.a.w.w.) na nikakipa jina la

AHLUL-KISAA (Watu wa Kishamia). Sikutaja tarehe ya watoto wote wa Mtume, wala

tarehe ya Wake zake, (Radhiallahu Anhum Ajmaeen-R.A.A.) lakini nimetaja tarehe za

wale tu walioingizwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.) mwenye KISAA, nao ni Fatima,

Ali, Hassan na Hussein (Alaihimus Salaam - A.S).

Makusudio yangu ni kutaka radhi za Mwenyezi Mungu, ambaye alimwambia

Mtume wake awaambie Waislamu: “.... Sema (ewe Rasuli Wetu Muhammad); Kwa haya

(huku kukubalighishieni Ujumbe wa Allah) sikuombeni ujira wowote, ila mapenzi (yenu)

kwa jamaa (zangu)........"(Ash-shuura, 42:23)

Namwomba kila atakayeona makosa katika kitabu hiki, asahihishe na anipe habari,

kwani asiyekosa ni Mwenyezi Mungu tu.

www.allamahrizvi.com

Page 5: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

5

UTANGUIIZI

Natoa shukrani zangu kwa kila aliyekisadia kitabu hiki. Mara ya kwanza

kilichapishwa na ISLAMIC RESEARCH ORGANISATION, MOMBASA (KENYA),

mwenye mwaka 1964. Sasa, BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA imekubali

kukichapisha na kukieneza, ili watu waendelee kupata faida. Nimeruhusu kufanya

mabadilisho ya baadhi ya maneno ili wasomaji waweze kufahamu kwa urahisi.

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuni wezesha kukimaliza kitabu hiki.

Kadhalika nawashukuru walionisaidia kukipiga chapa kitabu hiki, na malipo yao yako

kwa Mwenyezi Mungu.

Namwomba kila asomae kitabu hiki, ajaribu kukitangaza na kuwatia hima wenziwe

kukisoma, kwani kusoma kwenu ndiko kutakapotupa hima sisi kutoa vitabu vingine vya

dini.

AHMAD BADAWY BIN MUHAMMAD AL-HUSSEINY,

S.L.P 81895, MOMBASA (KENYA)

23rd August, 1988(1Oth Muharram, 1409)

www.allamahrizvi.com

Page 6: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

6

MAANA YA AHLUL KISAA

Neno "KISAA" lina maana ya nguo ya kujitanda au kujifunika; Kiswahili ni kishamia,

shali au mharuma. ( آ��ء )

Kutamka "KISAA", kwa fataha ya kafu. Maana yake ni ubora na Utukufu ( آ��ء )

Kwa maana zote mbili hizo, neno hili ni sawa kwani hao ni watu wa kishamia, tena

wenye mifano bora na yenye utukufu. Lakini makusudio yake mwenye mada hii ni watu

wa kishamia.

Hadithi ya Kisaa (Watu wa Kishamia) ni mashuhuri sana, na imepokewa na

masahaba wengi na maimamu wa hadithi. Mmoja katika maimamu ni Imamu Muslim,

mwenye kitabu chake cha hadithi, kiitwacho SAHIHI MUSLIM, yeye amesema: "Mtume

(s.a.w.w.) aliwakaribisha (Imamu) Ali, Fatimah, Hassan na Hussein mwenye Kishamia.

kisha akaisoma aya hii:

….4 $ yϑΡÎ) ߉ƒ Ì� ムª! $# |= Ïδõ‹ ã‹ Ï9 ãΝà6Ζtã }§ ô_Íh�9$# Ÿ≅÷δ r& ÏMø�t7ø9 $# ö/ ä. t�Îdγ sÜムuρ #Z�� Îγ ôÜs? ∩⊂⊂∪

“……Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, Enyi watu wa nyumbani,

na kukutakaseni kabisa (Sura 33:33)

Vile vile Imamu Ahmad ameipokea hadithi hii kwa Sahaba Abu Said Al-Khudri

kuwa iliteremka aya hii kwa ajili ya Watukufu hawa wane, na Mwenyewe Mtukufu

Mtume (s.a.w.w.) ni wa tano. Kwa hivyo, mshairi amesema:-

"Kwanza ni Mtume, Ali na Al-Hasani.

Kisha Huseini, mama yao ndiye wa mwishoni,

Mkiwa na haja. kuu mno tawasalini.

Kwa watano hao, hujibiwa dua kwa hima”

Kadhalika mwenye hadithi nyingine, Mtume (s.a.w.w.) baada ya kuisoma aya hii

tuliyoitaja, aliongeza kusema: "Ewe Mola! Hawa ndio Ahlul Bait wangu khasa,

waondolee uchafu na uwatakase kabisa-kabisa, umnusuru mwenye kuwanusuru hawa, na

mpige vita mwenye kuwapiga vita hawa". Na hadithi nyingine tena mwenye Sahihi

Muslim ambayo aliyeipokea ni Ummu Salamah, mke wa Mtume (s.a.w.w.) baada ya

kuwakusanya Ali, Fatimah, Hassan na Husein", akasema: "ewe Mola, hawa ndio "Ahlu-

Bait" wangu, waondolee uchafu". Nikasema: Je na mimi ni pamoja nao ewe Mtume wa

Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w.) akanijibu: "kaa hapo hapo wewe ukatika kheri".

Kwa hadithi hii ya Imamu Muslim iliyopokewa kutoka kwa mke wa Mtume

(s.a.w.w.) na ya pili ni ile tuliyoitaja mwanzo iliyoeleza sababu ya kushuka Aya hii:

yatuonyesha wazi kuwa "Ahlul-Kisaa" ndio "Ahlul - Bait", nao ni hao niliowataja, watu

Page 7: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

7

wanne pamoja na Mwenyewe Mtume (s.a.w.w.)ni wa tano, na ingawa aya ya "Ahlul -

Bait" imeambatanishwa na aya (WAQARNA FI BUYUTI KUNNA...) kama aya moja

kwa maandishi lakini kipande cha mwisho kisemacho (INA MAA YURIIDU-LLAHU LI

YUDH'HIBA.....) Kwa mujibu wa riwaya zinazoeleza sababu ya kuteremka kwake

zaeleza kipande cha hii aya: (INA MAA YURIDULLAHU....) kiliteremka kwa watu

waliofunikwa Kishamia tu, Kisha Mtume (s.a.w.w.) aliwakusudia watu hawa na

akawaombea Mungu, kama hadithi ya Ummu Salamah, mkewe Mtume (s.a.w.w.):

ionyeshavyo, na nyingine ya Ummu Salamah, mkewe Mtume (s.a.w.w.): ionyeshavyo, na

nyiginezo kadha wa kadha. Nayatilia nguvu maneno haya kwa kisa cha Wanaswara

(Wakristo) wa Najran. Ujumbe wa Wakristo uliokwenda kumhoji Mtume (s.a.w.w.) kwa

habari ya Nabiy Issa kuwa si mja wa Mungu ni mtoto wa Mungu, hapo Mwenyezi

Mungu akamteremshia Mtume (s.a.w.w.) Aya hii:-

ô yϑsù y7§_ !%tn ϵ‹ Ïù .ÏΒ Ï‰÷è t/ $ tΒ x8u!% y zÏΒ ÉΟù=Ïè ø9 $# ö≅à) sù (#öθ s9$yè s? äíô‰tΡ $ tΡu !$ oΨö/r& ö/ä.u !$ oΨö/r&uρ $ tΡu !$|¡ ÎΣuρ

öΝä.u !$ |¡ÎΣuρ $ oΨ|¡ à�Ρr& uρ öΝ ä3|¡à�Ρr& uρ ¢Ο èO ö≅Íκ tJö6 tΡ ≅yè ôf uΖsù |MuΖ÷è©9 «!$# ’n? tã š Î/ É‹≈x6ø9 $# ∩∉⊇∪

"Mwenye kujadiliana (kushindana) nawe katika hilo (la Nabii Issa) baada ya

kukujia elimu (ujuzi kuwa Issa ni mja wa Mungu. Si mtoto wake), basi sema: Njooni !tu

waite watoto wetu na watoto wenu, na wake zetu na wake zenu, na nafsi zetu na nafsi

zenu (watu wetu na wenu); kisha tuombe kwa unyenyekevu na kuiweka "laana" (mateso)

ya Mwenyezi Mungu juu ya waongo". (Suura 3:61)

Hapo tena Mtume (s.a.w.w.) akatoka yeye na wajukuu zake ("ndio maana ya

watoto wetu") yaani Hassan na Husayn, akatoka binti yake Bibi Fatimah (ndiyo maana ya

"wake zetu"), akamchukua pamoja na hao Imamu Ali (ndiyo maana ya "nafsi zetu")

akatoka Mtume (s.a.w.w.) pamoja na watu wanne hao tu, akaenda nao mpaka mbele ya

hao Wakristo, akawaambia "Mimi ninaomba Dua na ninyi itikieni (Amin), lakini wapi,

ukweli ukisonga uwongo hujitenga; Nani anathubutu kupambana na watu hawa kwa

kuapizana! Wakaogopa, Walikatazwa na mkubwa wao, Aliwaambia: "Hawajaapizana

kaumu yoyote na Mtume ila kuangamia (hupotea wakafikiwa na mabalaa). Hapo tena

wakafanya sulhu kwa kutoa jiziya (kodi) kuwapa Waislamu. Hadithi hii imepokewa na

Imamu wa hadithi, bwana Abu Nuaim.

Tumeona kuwa Aya ya Qur'an imetaja "wake" na Mtume (s.a.w.w.) hakutoka na

mke yeyote miongoni mwa wake zake wala mwanamke yeyote ila alitoka na Bibi

Fatumah peke yake, kadhalika Aya imetaja " watoto "na Mtume (s.a.w.w.) hakutoka na

kijana wa jamaa yake wala wa yeyote bali alitoka na wajukuu zake Hassan na Husseyn.

Basi mabwana wanne hawa, Ali na mkewe na watoto wao; ndio alioamrisha

Mtume (s.a.w.w.) wapendwe kwa hadithi nyingi za Mtume (s.a.w.w.), na katika Qur-an

ni ile aya niliyoitaja mwanzo. Aya kamili, na maana yake nimekwisha kuieleza.

Na makusudio yake kuteremshwa aya hii ni kwa ajili ya watu wanne hawa, kwa

dalili waliyoipokea maimamu hawa: Imamu Ahmad, Tabrani na Hakim: wote

www.allamahrizvi.com

Page 8: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

8

wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema

ilipoteremka aya hii, Masahaba walimuuliza Mtume (s.a.w.w.) Wakasema: "Ewe Mtume

wa Mwenyezi Mungu! Ni nani hao walio karibu zake wapasikao juu yetu kuwapenda"

Mtume (s.a.w.w.) akasema: "Ni Ali, Fatma na watoto wao (Hassan na Hussein)".

Na walio karibu na Mtume (s.a.w.w.) yaani jamaa zake ni wengj, ni Banu Hashim

wote, hata na Makureish wote. Na wote hao Mtume (s.a.w.w.) aliamrisha wapendwe kwa

hadithi nyingi alizozisema juu ya watu hao, lakini walio bora kuliko wote na

aliowasisitiza sana Mtume (s.a.w.w.) wapendwe ni hawa watu wanne.

Nikiendelea kuzieleza sifa za watu hawa watukufu, nitakijaza kitabu chetu hiki

wala hakitatosha wala hatutawahi kusema mengine juu ya maisha yao, Hivyo naendelea

kusema: Imamu Muslim mwenye Sahihi yake ameipokea hadithi itolewayo kwa Sahaba

mkubwa Bwana Zaid bin Akram (R.A.) amesema: “Alisema Mtume (s.a.w.w.) mahali

paitwapo "KHAMM" baina ya Makkah na Madinah, Mtume (s.a.w.w.) akatoa khutuba.

Alimshukuru Mwenyezi Mungu kisha akasema' "amma Baad, Enyi watu! Hakika si

jingine (bali) mimi ni binadamu kama ninyi, nachelea kunijilia mjumbe wa Mola wangu

(Malaika wa mauti) nami nikamjibu (akaichukua roho): basi na mimi nawaachieni ninyi

vitu viwili (vitukufu): cha kwanza ni kitabu cha Mwenyezi Mungu (Quran) ndani yake

mna uongofu na nuru, basi shikamaneni nacho na mkitumie" Mtume (s.a.w.w.)

akasisitiza sana na kusogeleza juu ya Qur~an, kisha akasema: "Na Ahlul Baity", (watu

wa nyumba yangu) nawakumbusha kwa Mungu na Ahlul Baity "Alikariri mara tatu

tamko la Ahlul Baity" (Watu wa nyumba yangu).

Imepokewa hadithi na Addailamy, kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema:

"Wafundisheni adabu watoto wenu kwa mambo matatu.

1. Kwa kumpenda Mtume wenu (s.a.w.w.)

2. Na kuwapenda Ahlul Baity zake

3. Na kusoma Qur-ani.

Kadhalika Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia Sahaba zake

LAAH TUSWALII 'ALLAYYASW SWALAATAL BATRAA-A

Msinisalie sala ya mkato.

(Sahihi Bukhari na Sahih Muslim)

Masahaba wakamuuliza: “Ni ipi hiyo Sala ya MKATO”?

Akawaambia "Ni kusema:

Ewe Mola! Mrehemu Muhammad” Kisha mkanyamaza: Lakini semeni: "Ewe

Mola! Mrehemu Muhammad na “Aali” “Muhammad” Na Aali hapa ni walioamini katika

jamaa zake yaani Banu Hashim na Dhuriya zao wote. Kwa hiyo baadhi ya maimamu na

Wanavyuoni wamesema Sala juu ya Aali Muhammad mwenye tashahud (Attahiyyatu) ya

Mwisho ni wajibu, yaani ni lazima na ni miongoni mwa nguzo za sala kwa hadithi ile ya

Mtume (s.a.w.w.) aliposema kuwa asisaliwe sala ya “MKATO” kama nilivyoeleza

nyuma. Na wamechukulia maneno ya Imamu Shafii aliposema:-

Page 9: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

9

YAA AHLA BAYTI RASUULIL LAAHI?

HUBBUKUM FARADHUN MINALLAAHI FIIL QUR-AANI

ANZALAHU, KAFAAKUM MIN 'ADHWIIMIL QADRI

ANNAKUM MAN LAM

YUSWALI ALAYKUM LAA SWALAATA-LAHU".

Enyi Ahli-Bait wa Mtume wa Mungu: mapenzi yenu ni faradhi (lazima, juu ya

Waislamu) itokayo kwa Mwenyezi Mungu katika Qur-ani ameiteremsha. Yawatosha

ninyi kwa utukufu wa cheo, hakika yenu ninyi mtu asiye warehemu (katika sala) basi

hana maana ya: "Hana sala", yaani Sala kamili, si kuwa haikusihi la. Haya yote

niliyokutajieni ni kwa ufupi tu ya sifa za mabwana hawa.

Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) zatuonyesha kuwa Bibi Fatimah ni "bora" kuliko

wanawake wote lakini iko ikhtilafu baina ya wanavyuoni. Wengine wamesema bibi

Mariam ndiye wa kwanza, kisha ni Fatimah. Na wengine wamesema bibi Fatimah ndiye

wa kwanza na wengine wamesema Mariam ni bora kwa wakati wake; na Fatimah ni bora

kwa wakati wake; yaani wa Ummati Muhammad. Basi ikiwa ni hivi bila shaka Fatimah

ni bora kuliko Mariam; Sababu Ummati Muhammad ni bora kuliko Ummati wowote na

yeye ni bora wa wanawake wa Ummati Muhammad.

Vipi Mtume (s.a.w.w.) awe ni bora wa watu wote binti yake asiwe bora wa

wanawake wote! Mtume (s.a.w.w.) akisema: “kipenzi cha watu wangu kwangu ni

Fatimah” Akimwambia "Hakika! Mwenyezi Mungu huridhika kwa kuridhika wewe na

hukasiriki kwa kukasirika wewe".

Kadhalika amesema (s.a.w.w.): Itakapokuwa siku ya kiyama: atalingania mwenye

kulingania katika Arshi: "Enyi watu! Fungeni macho yenu mpaka apite Fatimah bint

Muhammad". Hapo tena atapita pamoja na wajakazi 70,000 katika Hurul-Ain, atapita

kama umeme".

Amepewa jina la "Zahraa" kwa ajili hakuingia katika Hedhi, kwani Asmaa binti

Umais asema: "Alikuja Fatimah na amembeba Hassan (baada ya kuzaa) na sikumuona na

damu, nikamuuliza Mtume (s.a.w.w.) kuwa Fatimah simuoni na damu ya hedhi wala ya

uzazi, Mtume (s.a.w.w.) akaniambia: Hujui wewe bint yangu kuwa ni twahara (safi)

haionekani hedhi wala damu ya uzazi"? Bibi Fatimah alikuwa amefanana sana na Mtume

(s.a.w.w.) kwa kila kitu, hata kwa mwendo na sauti pia alikuwa amempata baba yake

KUOLEWA KWAKE

Sayyedna Abubakar alipeleka ombi kwa Mtume (s.a.w.w.) akitaka kumposa Bibi

Fatimah (a.s.) lakini Mtume (s.a.w.w.) alikataa ombi hilo na akasema sijapata amri

kutoka kwa Mola wangu kumuoza. Akaenda Sayyidna Omar, vile vile akakataa

akajibiwa kama alivyojibiwa Sayyidna Abubakar (R.A.). Hapo tena Sayyidna Omar

(R.A.) akamwambia Imamu Ali! "Nenda wewe ukampose Fatimah” Imamu Ali akasema:

www.allamahrizvi.com

Page 10: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

10

Nikaenda mpaka nikaingia kwa Mtume (s.a.w.w.) nisiweze kusema naye, yeye

akaniuliza: "Umekuja kufanya nini"? Nikanyamaza, akaniambia:

Labda umekuja kumposa Fatimah?" Nikasema ndiyo akaniuliza unacho kitu cha

kumuolea”? Nikamwambia la, sina. Akaniambia: Iko wapi ile dir-i (nguo ya kuvaa ya

vita) niliyokupa Nikamjibu ninayo, akaniambia: "Nenda kaiuze kwa dirham mia nne

(400) ni mahri ya Fatimah" Hapa tena Imamu Ali akaenda akiuza dir~i yake kwa dirham

400.

Mtume (s.a.w.w.) alisema: "Ameniamrisha Mola wangu nimuozeshe Ali, Fatimah".

Mtume (s.a.w.w.) alipompa habari bibi Fatimah kuwa ataolewa na Imamu Ali, alimkuta

nyumbani mara moja akilia, akamwambia:

Ee Fatimah we! Unalia nini? Wallahi nimekuoza mtu aliye mwingi wa watu kwa

Ilimu, aliye mbora wao kwa upole, aliye wa kwanza kwa Kusilimu.

Basi tena ikatengenezwa harusi, akamuamrisha Mtume (s.a.w.w.) atengenezewe

Fatimah firasha na mito, akamuamrisha Asmaa bint Umais aitengeneze nyumba ya

Fatimah, na ulikuwa ni mwezi wa Mfungo tano mwaka wa pili wa Hijra.

Mtume (s.a.w.w.) akasoma khutuba akamuoza Imamu Ali. Ukaliwa Walimatul -

harusi kwa kondoo na tende zilizosongwa pamoja na samli: Mtume (s.a.w.w.)

akamwambia Imamu Ali: "Kabla hujazungumza na mkeo kwanza onana na mimi" Kisha

Mtume (s.a.w.w.) akaagizia maji yakaletwa akatawadha, yaliyo baki akayamimina katika

kifua cha Imamu Ali kidogo, kisha akasema: "Ewe Mola! Wabarikie hawa, vibarikie na

nasla (kizazi chao)". Baada ya sala ya Isha akapelekwa Bi Harusi nyumbani, alipelekwa

na Ummu Aiman na Bwana harusi akiwangojea. Hata Mtume (s.a.w.w.) alipokuja,

akaingia nyumbani akasema huyu Ndugu yako?

Ummu Aiman akamwambia: "Ndugu yako kisha umemuoza binti yako? Mtume

(s.a.w.w.) akamjibu: "Ee! yeye ni Ndugu yangu kwa daraja lakini hainizuii mimi

kumuoza binti yangu". Hapo tena Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Fatimah alete maji.

Fatimah akaenda akaleta maji huku akiona haya. Mtume (s.a.w.w.) akayamiminia katika

bakuli kisha akamwambia Fatimah asogee mbele.

Fatimah akasogea, Mtume (s.a.w.w.) akachukua maji kidogo akayapiga tama

(akayatia mdomoni) kisha akayarudisha (akayatema) Bakulini, kisha akayateka

akamnyunyizia nayo bibi Fatimah kifuani pake na huku akisema:

Ewe Mola! Hakika mimi namlinda huyu kwako pamoja na dhuriya (watoto) wake

(namlinda) na shetani aliye mbali na Rehema Zako". Kisha akamwambia Fatimah ageuke

kwa nyuma, akageuka akamnyunyizia tena maji kati ya mabega yake na akafanya kwa

Imamu Ali kama alivyo fanya kwa Bibi Fatimah kisha akamwambia Ali; "Ingia kwa watu

wako (mkeo) kwa jina la Mwenyezi Mungu na baraka zake".

Alharndulilah! Akashukuru Imamu Ali kwa kumpatia mke huyu, na sote

twamshukuru kwa neema kama hii. Ni furaha iliyoje ya bibi na bwana; Bwana kumpata

www.allamahrizvi.com

Page 11: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

11

mtoto wa Mtume (s.a.w.w.) na bibi kumpata nduguye Mtume (s.a.w.w.) kadhalika na

yeye mwenyewe Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ndiyo furaha yake kwa kumpa binti yake

ampendaye yeye mwenyewe (s.a.w.w.) na (kumpa Imamu Ali mke ampendaye yeye

mwenyewe (s.a.w.w.) baada ya kuwa Ali na Fatimah ni mtu na ami yake, kisha

wamelelewa pamoja, amewalea yeye Mtume (s.a.w.w.).

Bibi Fatimah alipopewa habari na Baba yake kuwa ataolewa na Imamu Ali, alilia,

hakulia kwa ajili kuwa hampendi laa, bali ni desturi ya Wanawali wote hasa wenye haya

na dini wakiposwa hulia. Je haya za wanawake kama kina bibi Fatima zi vipi! Allahu

Akbar, hazisemeki!

Ni juu ya Waislamu wote kwenda mwendo namna hii kama alivyofanya Mtume

(s.a.w.w.) yaani mume atafute mke "kufu" na mke au mkwe atafute mume "kufu" kama

alivyo sema Mtume (s.a.w.w.)

Mwanamke huolewa kwa mambo manne:-

1. Kwa ajili ya mali yake, au

2. Nasaba yake; au

3. Uzuri wake; au

4. Dini yake. (Basi wewe) jichukulie pato kwa mwenye dini. Usipofanya hivyo;

(fahamu) mikono yako itapata mtanga (utakorofika)!

Na hadithi nyingine Mtume (s.a.w.w.) amesema: "Awajiapo atakaye kuowa

ambaye mwaridhia "tabia" yake na "Dini" yake, basi muozeni, msipofanya hivyo

(mkakataa) au mukamuoza asiye kuwa na sifa hizo), basi patakuwa na fitina kubwa

katika nchi (mahali hapo)na uharibifu wenye kuenea".

Zama hizi ni wachache wafuatao mawili haya, kila mtu anataka mali na uzuri.

Ama Mtume (s.a.w.w.) kumkataa Sayyidna Abubakar na Sayyidna Omar ni kama

nilivyo tangulia kusema huko nyuma; kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hajapata amri

kutoka kwa Mola wake ya kumuoza Fatimah.

Basi tena wakakaa Bibi na Bwana kwa furaha mpaka Mwenyezi Mungu

akawaruzuku watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike, Hassan, Hussein na

Muhsin, lakini huyu alikufa mdogo sana. Na wanawake ni Zainabu na Ummu Kulthum.

ama Imamu Ali alipata watoto wengi kwa wake wengine aliowaoa kama utakavyo soma

mbele, lakini Imamu Ali hakuowa mke yeyote katika uhai wa bibi Fatirnah ila baada ya

kufa kwake.

KIFO CHAKE

Bibi Fatimah hakupata maisha ya haja, baada ya kufa baba yake alikuwa hana

furaha tena.

www.allamahrizvi.com

Page 12: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

12

Alipokufa Mtume (s.a.w.w.) Fatimah alikwenda kwa Sayyidna Abubakar

kumweleza urithi wake sababu ndiye Khalifa aliyeshika mambo yote, Sayyidna

Abubakar akakataa kumpa, Bibi Fatimah akamuuliza: "Ni yupi akurithiye wewe?

Akamjibu: “Ni mke wangu na watoto wangu" Akamwambia: kwa nini mimi nisimrithi

baba yangu"?

Sayyidna Abubakar akasema: Nimemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema:-

Sisi Mitume haturithiwi, tukiacha chochote ni Sadaka".

Hapo tena Bibi Fatimah akakasirika akatoka, na hakusema nae mpaka akafa. Lakini

wengine wasema kuwa Sayyidna Abubakar alikwenda mpaka nyumbani kwa bibi

Fatimah akasimama mlango akasema: Sitaondoka hapa mpaka binti ya Mtume (s.a.w.w.)

aniwie radhi: alipokuja Imamu Ali akasema naye mkewe mpaka akakubali akamsamehe.

Alipokuwa mgonjwa bibi Fatimah, maradhi ya mauti, aliyekuwa akimuuguza ni

Asmaa bint Umais. Siku ya kufa kwake Asmaa asema "Fatimah aliniambia mimi" Mimi

nikifa sipendi aingie yoyote, nikifa nioshe wewe na Ali". Kadhalika aliusia azikwe usiku.

Hata ilipofika usiku wa kuamkia Jumanne, 3Ramadhani, l1 Hijra, akafa na

akafanyiwa kama alivyousia na umri wake ulikuwa miaka 29 akazikwa hapo hapo

Madinah mahali paitwapo Bakiy. Mwenyezi Mungu amrehemu, Amin.

Sasa tumuache Bibi tumshike bwana ambaye ni wa tatu katika wale watano wa

kisaa, ambaye ni nduguye Mtume (s.a.w.w.) naye ni:-

IMAMU ALI

Imamu Ali (K. W) ni mashuhuri kwa lakab ya "Imamu" lakab hii hakuitwaa yeyote

kabla yake. Wale Makhalifa watatu walio mtangulia, walikuwa wakiitwa kwa "Khalifatu-

Rasulullah" na Sayyidna Omar akijulikana kama"Amirul Muuminiin".

Amma Imamu Ali kwa yote haya akijulikana, lakini zaidi ni hili la Imamu, kisha

tena likaenda baada yake kwa watoto wake kina Sayyidna Hassan na Sayyidna Hussein

na wajukuu zao hawa, ikaendelea mpaka kwa Maimamu wetu hata wanne. Imamu

Hanafy, Imamu Shafiy, Imamu Maliky na Imamu Hambaly. Kadhalika na Maimamu wa

hadithi wote, lakini asili ilianza kwa Imamu Ali.

NASABA YAKE

Yeye ni Ali bin Abu-Talib bin Abdil Muttalib bin Hashim. Yeye na Mtume

(s.a.w.w.) wanakutana kwa Abdul Muttalib yaani huyu ni babu yao wote wawili.

Kisha huyu Abi Talib baba yake Ali na Abdullah baba yake Mtume (s.a.w.w.)

mama yao ni mmoja, jina lake ni Fatimah bint Amri Al-Makazumiya, kwa hivyo ndipo

bwana Abdul-Muttalib alipokufa alimuusia Abu Talib kumlea Mtume (s.a.w.w.).

www.allamahrizvi.com

Page 13: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

13

Kadhalika na yeye Mtume (s.a.w.w.) akamchukua Imamu Ali kumlea ili

kumpunguzia uzito Ami yake, sababu Abi Talib alikuwa na watoto wengi naye alikuwa

maskini. Jina lake khasa ni Abdu Manaf, hili Abu Twalib ni kuniya, sababu alikuwa na

kijana akiitwa Talib, basi kwa hivyo akaitwa Abu Twalib yaani baba yake Talib, kama

Mtume (s.a.w.w.) akiitwa Abal Kassim na Abu Abdullah, sababu alikuwa nao hawa

watoto Kassim na Abdullah.

Lakini wakati mwingine huwa hana mtoto na hutengenezewa sifa ya kiutu au

mnyama. Kama Sahaba mmoja mashuhuri kwa jina la Abu-Huraira (baba yake paka)

hakika hakuwa na mtoto akiitwa "Paka" la yeye alikuwa akipenda kucheza na paka sana,

basi Mtume (s.a.w.w.) akamwita Abu-Huraira. Na hii si aibu ndiyo desturi ya Kiarabu.

Vile vile mara nyingi Mtume (s.a.w.w.) akimwita Imamu Ali Abu Turab (baba

yake Mchanga). Na sababu yake kumwita hivi, alikwenda Msikitini akamkuta amelala

mchangani akamwamsha kwa kumwita: "Ewe Aba Turab inuka".

Imamu Ali alikuwa na lakab nyingi (mafumbo ya majina), lakini mashuhuri ni

Asadullah, Raider. Assidikul-Akbaru na Yaasubul Ummah, haya mawili ya mwisho

alipewa na Mtume (s.a.w.w.) maana ya "Yaasub" ni Sayyid (Bwana) yaani yeye ni

Bwana wa Ummah. Na sababu ya kumwita "Siddikul-Akbar", ni hadithi yake Mtume

(s.a.w.w.) aliposema:

" Waliosadiki (mwanzo) ni watatu:-

(1) Habibun Najjar, katika watu wa Yaasiin aliye amini (wajumbe wa Nabii Issa

waliopelekwa katika kijiji cha watu wa Yaasiin kama ilivyo katika "Surati Yaasiin"

habari yao) ambaye alisema:-Enyi watu wangu! Waandameni wajumbe”

(2) Na Kharkil, aliye amini katika kabila la Firauni ambaye alisema "Mnamuuwa

mtu (kwa ajili) anasema: Mola wangu ni Mwenyezi Mungu"?

(3) Na Ali bin Abi Talib, na yeye ndiye bora wao".

Imamu Ali kun-ya zake vile vile ni nyingi, mashuhuri ni: Abu Turab, Abul

Hasanain, Abu Sibtain na Abur-Raihanatain. Yote haya ni maana ya "Baba wa

Hassan na Hussein, ila lile la Abu-Tarab tu, ni kama nilivyo eleza.

Na mama yake Imamu Ali ni Fatimah bint Asad bin Hashim, yaani yeye ni Banu

Hashim kwa Baba na mama, nani mtu wa mwazo kuzaliwa Banu Hashim pande zote

mbili na ni Sharaf kubwa hiyo aliyokuwa nayo Imamu Ali. Bibi huyu Fatimah binti Asad

ni katika wanawake walio amini mwanzo na akahama kwenda Madinah kumfuata Mtume

(s.a.w.w.) na yeye Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimpenda sana bibi huyu na kumtukuza

sababu ni mama yake wa kumlea.

Alipokufa bibi huyu, Mtume (s.a.w.w.) alilia sana, akamkafini (kumvisha sanda)

kwa kanzu yake mwenyewe (s.a.w.w.) Mtume akamsalia na alipofika kaburini kwanza

www.allamahrizvi.com

Page 14: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

14

akashuka yeye (s.a.w.w.) Mtume akalala ndani ya mwanandani kisha akamtia bibi huyu.

Mwenyezi Mungu amrehemu, Amin.

KUZALIWA

Imamu Ali (K.M.) Karamallah Wajhah) alizaliwa siku ya Ijumaa mwezi 13 Rajjab,

mwaka wa thalathini tangu kuzaliwa Mtume (s.a.w.w.) 600 A.D. yaani yeye ni mdogo

kuliko Mtume (s.a.w.w.) kwa miaka 30.

Alizaliwa Makkah ndani ya al-Kaaba, na hii ni Sharaf kubwa aliyoipata kwani

hakuna mtu yeyote aliyezaliwa mahali hapo patakatifu, basi huu ni mwanzo wake, na ni

mwisho wake, yaani mauti yake yalitokana na msikiti; alipigwa ndani ya Msikiti katika

masiku ya Lailatul - Kadri na akafa katika masiku hayo kama nitakavyo eleza katika kifo

chake.

Kama ulivyosoma nyuma ya kitabu chetu hiki kuwa Imamu Ali alilelewa na

Mtume (s.a.w.w.) basi hapana shaka alikuwa na tabia isiyo kuwa na mfano. Alikuwa

mpole, karimu, shujaa hakukubali kuonewa yeye wala yeyote. Alikuwa hodari tena

mwana chuoni kushinda masahaba wote kama tutakavyo soma mbele sifa zake moja

moja.

KUS1LIMU KWAKE

Imamu Ali alisilimu siku ya pili baada ya kupewa Utume Mtume (s.a.w.w.) Mtume

(s.a.w.w.) alipewa Utume siku ya Jumatatu yeye akasilimu siku ya Jumanne.

Kama ijulikanavyo katika tarekh ya Mtume (s.a.w.w.) kuwa alipokuwa katika Jabal

Hira akifanya ibada, akamjia Jibril na Wahyi, palepale alikwenda nyumbani kwa mkewe

na huku khofu imemjaa kwa mambo aliyoyaona, akamwambia bibi Khadija binti

Khuwaylid amfunike na akamueleza yote aliyoyaona, basi mtu wa kwanza aliyemuamini

alikuwa ni yeye bibi Khadija binti Khuwaylid. Hata siku ya pili akaingia Imamu Ali

akawakuta wanafanya ibada, akawauliza; "Mnafanya nini"?

Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: "Hii ni dini ya Mwenyezi Mungu ameichagua

mwenyewe, amewapeleka mitume wake, na mimi nakulingania kwa Mungu peke yake,

asiyekuwa na mshirika, na kumuabudu yeye na kuwachana na "Lata na Uza". Imamu Ali

akasema siwezi kukata jambo lolote pasi na kumpa habari baba yangu na hili ni jambo

jipya sijawahi kuliona au kulisikia.

Mtume (S.A.W.W,) akamuusia asilitangaze. Hapo Imamu Ali akaenda akampa

habari baba yake, naye akampa ruhusa akamfuata Muhammad kwa lolote lile

amwambialo.

Basi Ali akasilimu siku hiyo hiyo na umri wake ni miaka kumi au minane tu.

alisilimu kijana wala hakuabudu sanamu tangu utoto wake.

Page 15: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

15

UTUKUFU WAKE

Mtume (s.a.w.w.) alipata amri kutoka kwa Mola wake kuwa ahame pale Makkah

aende Madinah. akawapa habari sahaba zake, na wengine wakatangulia kwenda na

wengine wakabakia. Miongoni mwa waliobakia ni Sayyidna Abubakar na Imamu Ali.

Hata siku ile Makureish walipokusany ana katika Darin-Nad-wa wakakata shauri la

kumuuwa Mtume (s.a.w.w.), alishuka Jibril akamwambia Mtume (s.a.w.w.) kuwa asilale

usiku ule katika kitanda chake.

Hapo tena Mtume (s.a.w.w.) akamuamrisha Imamu Ali alale kitandani kwake na

ajifunike kishali chake (ili maadui wakija waone ni yeye, huku naye atoke).

Imamu Ali akalala, akawa ndiye mtu wa kwanza aliye inunua nafsi yake kwa

Mtume (s.a.w.w.).

Hata ilipofika usiku, Mtume (s.a.w.w.) akatoka na huku akisoma akawapita maadui

pale pale, nao wasimuone, akatoka (s.a.w.w.) salama akaenda mpaka kwa Sayyidna

Abubakar wakafuatana pamoja katika safari kama ijulikanavyo katika tarekh zote za

maisha ya Muhammad (s.a.w.w.).

Hata walipofahamu Makuraish wakajiona wametiwa mchanga vichwani mwao,

wakachungulia dirishani wakamuona amelala wakadhani ni Mtume (s.a.w.w.) wakarejea

kazi yao ya kushika zamu wamngojee atoke. Hata kulipo pambazuka asubuhi Imamu Ali

akainuka kitandani, walipo muona ni yeye wakamuuliza: " Yuko wapi Swahibu yako?

Akawajibu sijui, tena hapo wakajuwa kuwa Mtume (s.a.w.w.) ameokoka.

Imamu Ali akakaa Makkah kwa kazi aliyomuachia Mtume (s.a.w.w.) kurejesha

amana za watu, alipomaliza akaondoka haraka kuelekea Madinah peke yake, na alikuwa

akienda mchana na usiku hapumziki ila muda mchache tu. alipofika Madinah alikuwa

taabani miguu ikiwa imefura na kuchuruzika damu.

Mtume (s.a.w.w.) akalia kwa kumsikitikia kwa hali aliyokuwa nayo, akamtemea

mate na akamuombea Mungu. Basi haikumuuma tena miguu maishani mwake.

Mtume (s.a.w.w.) alipofika Madinah kazi ya kwanza aliyoifanya baada ya kujenga

Msikiti wa Quba, aliwafunga udugu masahaba wote-Muhajirina na Answari (wa Makkah

na Madinah) kila mtu akampa nduguye ila Imamu Ali hakumpa yeyote, pale pale Imamu

Ali akamwarnbia! Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!

Umefunga udugu baina ya Sahaba zako, kila mtu umempa nduguye ila mimi

hukunipa yeyote"? Mtume (s.a.w.w.) akamwambia:-

Wewe ni ndugu yangu 'Duniani na akhera". Mahali hapa Mtume (s.a.w.w.)

amemfanya Imamu Ali ni nduguye na katika "Mubahala" (kuapizana baina yake na

Wakristo) alimfanya ni "nafsi" yake kwa aya ya Qur'an kama tulivyo soma nyuma katika

hadithi ya "Wafd Najran".

Page 16: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

16

Kadhalika maneno haya yatiliwa nguvu na hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema:-

Ali ni katika mimi na mimi ni katika yeye". Maana yake Ali ni wangu nami ni wake.

Mahali pengine Mtume (s.a.w.w.) amemwita Imamu Ali "Waliy", nayo ni katika

hadith yake aliyoisema katika mahali paitwapo “Khum” katika kurudi kwake Mtume

(s.a.w.w.) kutoka Makkah pamoja na sahaba zake, kuhiji "Hijjatul - Widai".

Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya Sahaba mahali hapo, kisha akasimama akatoa

hutuba ndefu sana iliyo kali kabisa na ya kusikitisha, kuonyesha kuwa yeye hataonana

tena na Sahaba zake mwaka mwingine. Kisha akamshika Imamu Ali akamuinua mkono

juu kabisa watu wote wakarnuona kisha akasema "Sikuwa mimi ni "bora" kuliko nafsi

zenu? Wakasema (Masahaba) kwa nini Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! (kisha

Mtume (s.a.w.w.) akasema): Ambaye mimi ni "Maula" wake basi na Ali ni "Maula"

wake, Ewe Mola. Mtawalishe mwenye kumtawalisha Ali (au mnusuru mwenye

kumnusuru na teta naye mwenye kumteta Ali".

Tamko "Maula" sikulitafsiri kwa kiswahili chake vizuri, kwa sababu lina rnaana

mbili, ya kwanza ni "Mtukufu" au "mbora" na ya pili ni "Nasri" (mwenye kukunusuru).

Kadhalika tamko la "Mtawalishe" vile vile lina maana "mnusuru".

Basi kwa matamko haya ndipo pakawa na mzozo na ushindi baina ya sisi na"

Mashia" Sisi "Sunny" twalichukulia neno hili "Maula" ni "Nasir" (mwenye kukunusuru)

yaani kukusaidia na kukuhifadhi. Wao "Shia" wanalichukia neno hili "Maula" ni

"Mtawala" (Mtawala wa mambo) au "mtukufu".

Kwa hadithi hii ndipo waliposhikama "Shia" kuwa Mtume (s.a.w.w.) alimtawalisha

Imamu Ali, ipo na hadithi nyingine nitaitaja hapo baadaye.

Hadithi hiyo imepokelewa na Maimamu wa hadithi wengi mmoja ni Imamu

Muslim katika sahihi yake. Kadhalika na katika tafsiri ya Qur-an juzuu ya nne ya SAWI,

katika "Suuratil-Maarij" yaani Sura ya 70, ameitia hadithi hii, kisha ameendelea kusema

kuwa, baada ya Mtume (s.a.w.w.) kumaliza kusema, aliinuka mtu akamwambia Mtume

(s.a.w.w.) :-

Umetuamrisha kuamini tumeamini, umetuamrisha kusali tumesali, umetuamrisha

kufunga tumefunga, umetuamrisha kutoa zaka tumetoa, umetuamrisha Kuhiji tumehiji,

hukukubali ila kumfanya Ibn Ami yako (Ali) kuwa juu ya vichwa vyetu? Hili latoka

kwako au latoka kwa Mwenyezi Mungu? Ikiwa latoka kwa Mwenyezi Mungu, basi

naishuke adhabu hebu tuione!".

Mtume (s.a.w.w.) akamjibu kuwa latoka kwa Mwenyezi Mungu. Hapo hapo

kikashuka kijiwe kutoka mbinguni kikamuangukia mwilini akafa hapo hapo. Ndiyo

sababu ya kuteremka, "Sa-ala-Saailu".

Page 17: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

17

Kwa hivi maneno ya Sawi yanatilia nguvu juu ya hadithi hii kuwa Mtume

(s.a.w.w.) alimtawalisha, kwani hakuwa na haja yule mtu kumhoji Mtume (s.a.w.w.) na

kumwambia kuwa amemuweka Ali juu ya vichwa vyao.

Kadhalika Mwenyezi Mungu amemwita Imamu Ali "Waliy" kwa neno lake

aliposema katika Qur-an:-

$ uΚΡÎ) ãΝä3–ŠÏ9 uρ ª! $# …ã& è!θß™u‘ uρ tÏ% ©!$#uρ (#θãΖtΒ#u tÏ% ©!$# tβθßϑ‹É) ムnο 4θn= ¢Á9 $# tβθ è?÷σ ムuρ nο 4θx. ¨“9 $# öΝèδuρ

tβθ ãèÏ.≡u‘ ∩∈∈∪

"Hakika si jingine, Waliy wenu ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na ambao

wameamini, ambao wanasali sala na kutoa zaka (Sadaka) na hali wao wako katika rukuu

(kusali)". (Sura 5:55.).

Sababu ya kushuka aya hii Imamu Ali, alikuwa akisali msikitini, akaja maskini

kuomba asimkute mtu ila Imamu Ali naye yuko katika sala, basi akamuashiria "pete"

yake aliyokuwa ameivaa kidoleni mwake akaja maskini akaitoa, yaani ndiyo sadaka

yake. Hapo ikateremka aya hii kwa Mtume (s.a.w.w.) kwa ajili ya Ali, kama ielezavyo

kuwa Waliy wenu ni Mungu na Mtume na wale wanao amini na kusali na kutoa sadaka

na ilhali wao wako katika sala na hili la kutoa Sadaka namna hii ni moja katika ukarimu

wake na ilhali naye kuwa ni maskini.

Kisa kingine cha ukarimu wake. Siku moja mkewe, bibi Fatimah alitengeneza

chakula chao na watoto wao, baada ya kumaliza tu kupika kabla hawajala mara akaja

"maskini" kuomba na hawana kitu ila kile chakula chao; Imamu Ali akamwambia

Fatimah akigawanye chakula kile sehemu tatu amletee sehemu moja. Akaenda bibi

Fatimah akakigawanya akamletea Imamu Ali akampa yule maskini. Sasa zimebaki

thuluthi mbili yaani mafungu mawili.

Haukupita muda mrefu mara akaja "Yatima" kuomba, Imamu Ali akachukua fungu

moja na akampa yule Yatima.

Sasa chakula chao kimebaki fungu moja tu, baada ya kitambo kidogo mara

akatokea "Asiir" (mtu aliyetekwa vitani). Imamu Ali akachukua lile fungu la tatu

lililobaki akampa yule "Asiir".

Wakabakia kulala na njaa, watoto wao Hassan na Hussein wakawa wanalia kwa

njaa nao bado wangali wadogo. Akawa mama yao akiwapumbaza na kuwahadaa kuwa

anawapikia chakula hadi ikaingia asubuhi.

Kwa ajili ya kitendo hiki kitukufu Mwenyezi Mungu akamteremshia Mtume wake

(s.a.w.w.) kwa ajili ya Imamu Ali aya tangu ya tano (5) katika sura ya 76 mpaka aya ya

21.

Page 18: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

18

Tuziache aya hizi tusitafsiri kwa sababu tunazo aya nyingi za kutafsiriwa atakaye

na atafute kalika tafsiri za Qur-an na aya hizi si dharura. Dharura ni ushahidi wa maneno

yetu nayo ni aya hizi:-

tβθ èùθ ム͑õ‹ ¨Ζ9 $$Î/ tβθ èù$ sƒ s†uρ $ YΒöθ tƒ tβ%x. …çν•� Ÿ° #Z�� ÏÜ tGó¡ãΒ ∩∠∪ tβθ ßϑÏèôÜ ãƒ uρ tΠ$ yè©Ü9$# 4’ n? tã ϵÎm7ãm

$ YΖŠ Å3ó¡ÏΒ $ VϑŠÏKtƒ uρ #·��Å™r& uρ ∩∇∪

(Hao watu wema ni ambao) watekeleza Nadhiri (wajibu wao) na wanaiogopa siku

ya kiama)... (Wema hao ni) walishao chakula hali ya kuwa wanakipenda (wakihitajia.

Wawalisha) maskini na yatima "asir" (aliyetekwa). (Suura 76:7-8).

Watu wengine: wakaanza kusema kuwa Imamu Ali amefanya hivi ili apate

kushukuriwa na kusifiwa, Zikateremka aya hizi:-

$ oÿ©ςÎ) ö/ ä3ãΚ Ïè ôÜçΡ Ïµô_ uθÏ9 «!$# Ÿω ߉ƒ Ì�çΡ óΟä3ΖÏΒ [ !#t“ y_ Ÿωuρ #·‘θä3ä© ∩∪ $ ¯ΡÎ) ß∃$sƒ wΥ ÏΒ $ uΖÎn/ §‘ $ ·Βöθtƒ

$ U™θç7tã #\�ƒÌ� sÜôϑ s% ∩⊇⊃∪ ãΝßγ9s%uθ sù ª! $# §�Ÿ° y7Ï9≡sŒ ÏΘöθ u‹ ø9 $# öΝßγ9 ¤)s9 uρ Zοu�ôØtΡ #Y‘ρ ç�ß  uρ ∩⊇⊇∪ Νßγ1 t“ y_uρ

$ yϑÎ/ (#ρç� y9|¹ ZπΖy_ #\�ƒÌ� ymuρ ∩⊇⊄∪

"Hakika si jingine, twawalisha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (peke yake) hatutaki

kwenu malipo wala shukrani. Hakika yetu sisi twaogopa kwa Mola wetu siku ya kukunja

uso (kwa taabu watakazo zipata watu tena siku hiyo) iliyo na shida (nayo ni siku ya

Kiama). Atawahifadhi Mwenyezi Mungu na shari la siku hiyo (ya kiyama au ile waliyo

lala na njaa) na atawakutanisha (Mola wao) kwa uzuri na furaha. Atawalipa kwa sababu

wamesubiri (nayo ni njaa wakalipwa) pepo na (mavazi ya) hariri" (Sura 76:9-12)

Zimeendelea aya kwa kusifiwa pepo kwa starehe zake na watakayo yakuta watakao

ingia mpaka karibu na mwisho wa Sura hii.

Hakika jambo la watu hawa "Maskini". "Yatima" na "Asiir" kumwendea Imamu

Ali wote kwa siku moja! Bila shaka hawakuwa ni watu, hawa walikuwa ni malaika,

walitumwa kwenda kumjaribu Imamu Ali kumuangalia atafanya au hatafanya. Naye

alifanya na Mwenyezi Mungu amemlipa.

Basi na Mwislamu yeyote akifanya haya baada ya faradhi yake kuitimiza, atayapata

haya aliyo yaagiza Mwenyezi Mungu katika sura hii.

Imamu Ali alihudhuria vita vyote vya Jihaad, vikubwa kama vita vya Badri na

Uhud na vidogo vyote.

Katika vita vya Badri yeye ni mmoja aliyechaguliwa na Mtume (s.a.w.w.) kwenda

kubariziana (Mubaaraza). Sababu Makafiri walitoka watu watatu kutaka mubaraza

Page 19: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

19

(kupambana mmoja mmoja) wakatoka katika Masahaba Ansari watatu, wale makafiri nao

ni- Utba bin Rubaia na Shaiba bin Rubaia, hawa ni ndugu, na wa tatu wao ni Walid bin

Utba. Hawa walipowaona watu waliotoka ni Ansar si makureish, wakamwambia:

"Muhammad! tutolee kufu zetu" (yaani Makuresh) hapo Mtume (s.a.w.w.) akaita: Ewe

Ubaida Ibnil Harith inuka na wewe Hamza inuka na wewe Ali inuka (hawa wawili ni

nduguze Mtume na mmoja ni Ami yake kisha ni nduguye wa kunyonya, naye ni Hamza)

Wakainuka wakabariziana na wale makafairi watatu. Makafiri wawili wakauliwa,

akabaki Ubaida na mtu wake Utba, akaumizwa Ubaida kwa dharba ya Utba, baadaye

Ubaida akafa shahidi (R.A.) na vile vile Utba aliuliwa.

Katika vita vya “Uhud” Imamu Ali ndiye aliyechukua bendera ya "Muhajirina"

(Waliohama kwenda Madinah) Mtume (s.a.w.w.) katika vita hivi aliwagawanya

Masahaba zake makundi matatu, mawili yalikuwa ni Ansar, nao ni "Aus" na "Khazaraj"

na moja "Muhajir" kadhalika na katika vita vya "Hunain" pia Imamu Ali ndiye aliye

kuwa na bendera ya Muhajirin. Na mahali kadhaa wa kadhaa tukitaja kitabu chetu

kitakuwa kirefu. Lakini nitataja vita vya "Khaibar" ambavyo walishindwa masahaba wote

kufungua (kushika mji) mpaka alipopewa Imamu Ali bendera akafungua. Na nitataja kwa

ufupi sana.

KHAIBAR ni mji uliombali na Madinah upande wa kaskazini kwa kiasi cha maili

96 za Kiarabu, na watu wake ni Mayahudi watupu, nao walikuwa ni watu wa vita na ni

mashujaa sana.

Akatoka Mtume (s.a.w.w.) na jeshi lake akawaendea. Akapigana nao kwa muda wa

siku saba, bado Mayahudi wamejikaza tu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na bendera yake

ikiitwa Ukaab na katika vita hivi kila siku akimpa ile bendera huyu na yule na wakirudi

bila ya kufungua (kushinda). Katika waliopewa bendera ni mabwana wakubwa Sayyidna

Abubakar na Umar (R.A.) pia wasiweze. Hata siku ya saba Mtume (s.a.w.w.) akasema:-

"Hakika Wallahi! Nitampa bendera kesho mtu ampendaye Mwenyezi Mungu na

Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda yeye". Yaani Mwenyezi

Mungu na Mtume wake wanampenda yeye naye anawapenda. Imamu BUKHARI NA

MUSLIM wamepokea hadithi hii.

Hapo tena masahaba wote wakawa wanangoja ni yupi, kila mmoja anaona atapewa

yeye, hata siku ya pili Mtume (s.a.w.w.) akauliza yuko wapi Ali? Akaambiwa ni

mgonjwa macho yanamuuma sana, akasema: "Mleteni".

Akaletwa Imamu Ali na huku amejifunga macho. Mtume (s.a.w.w.) akamfungua

akamtia mate machoni mwake kisha akamwambia "Haya nenda", akampa bendera yake

"Ukaab".

Tangu wakati huo alipo temewa mate na Mtume (s.a.w.w.) hakuugua tena macho,

kadhalika aliombewa Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.) asione joto wala baridi,

hakuwahi kushtakia maishani mwake joto wala baridi.

Page 20: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

20

Akatoka Imamu Ali naye amekwisha poa macho hayamuumi tena, akaenda mpaka

katika ngome ya Mayahudi akaisimamisha bendera nje chini ya ngome (mahali pa

kujihifadhi).

Hapo tena akatoka mkubwa wao naye ni Harithi naye alikuwa shujaa wao, hapo

Imamu Ali akamuua. Akatoka tena nduguye Harith naye ni Muhrib, wakapambana, kisha

ngao ya Ali ikamponyoka mkononi, akachukua mlango ambao ulikuwepo hapo katika

ngome akafanya ndiyo ngao yake, akapigana mpaka akafungua (akashinda) Basi tena

ukawa ushindi ni wa Waislamu.

USHUJAA WAKE

Tumekwisha soma nyuma ushujaa aliokuwa nao Imamu Ali, na ingekuwa vizuri

maneno yale kutiwa hapa, lakini kiko kisa kikubwa zaidi ambacho kitawatosha nacho ni

hiki:-

Katika vita vya "Khandak" shimo lililo zunguka Madinah kwa ajili ya kujihifadhi

na maadui, na aliyetoa shauri hili ni Salman Alfarsy kwa amri ya Mtume (s.a.w.w.),

Walikwenda Makuraish ili kuwapiga Waislamu, lakini wasiweze kuingia Madinah kwa

ajili ya hilo "Khandak”. Mwishowe akaruka shujaa mmoja mkubwa aitwaye "Amri bin

Abdi Wud" Ushujaa wake huyu ulikuwa hauna kiasi, katika mashujaa wa Kiarabu yeye

ni wa kwanza; ya kutosha kuwa yeye ameweza kuruka na Farasi wake katika Handaki

hilo, aliruka kwa upande wa pili kwenye masahaba, Wenzake wengine waliojaribu

walianguka wakafa.

Yeye akavuka salama akanadi tena: "Yuko mwenye kubariziana"? Masahaba wote

kimya, kana kwamba juu ya vichwa vyao ametua ndenge hatikisiki, na mashujaa wote

hapo wako kila mmoja amuogopa kwa ushujaa wake mtu huyo na nguvu zake akainuka

Imamu Ali (Simba wa Mungu) akamwambia Mtume (s.a.w.w.):-

"Mini na yeye Ewe Mtume wa Mungu" Mtume (s.a.w.w.) akamwambia "Hakika

huyo ni Amri", Mtume (s.a.w.w.) asimkubalie, akamwambia "Keti mahali pako" lile baba

likanadi mara ya pili na huku akitoa ufedhuli akisema:

"Nani atakaye pepo? Nani atakaye ghanimm? Nani aliyeshujaa? Pepo yenu ni huu

upanga wangu, na aje nimuuwe aingie peponi". Haya ni maneno aliyokuwa akiyasema

Amri na hapati jawabu lolote ila Imamu Ali ataka ruhusa kwa Mtume (s.a.w.w.) naye

hampi. Hata mara ya tatu akampa. Hapo tena akamtokea kijana umri wake hauzidi miaka

25 na Amri hapungui miaka 50, lile baba lilipo muona Imamu Ali alistaajabu kwa ujana

wake akamuuliza: "Ni nani wewe? Akamjibu: Ali, akamwambia "Bin Abdul Muttalib?

akamjibu bin Abi Talib akamwambia naona aibu kuimwaga damu yako kwa upanga huu.

Imamu Ali akamjibu: "Mimi sioni aibu kuimwaga damu yako kwa upanga wangu huu"

Na kabla ya hapo, Mtume (s.a.w.w.) alimpa Ali upanga wake "Dhul-Fikar" akamvisha

"Diri yake, akamvisha kilemba chake, kisha akamuombea dua akasema: "Ewe Mola!

msaidie. Ewe Mola wangu! Ulinichukulia Ubaida" siku ya Badri na "Hamza siku ya

Uhud na huyu Ali, kijana wa Ami yangu, usiniache pake yangu".

Page 21: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

21

Hapo tena Simba wa Mungu akapambana na simba wa Makuraish, kwanza Imamu,

Ali akapigwa dharuba akaikinga ikakata ngao yake ikampasua kichwa kidogo akaondoka

kwenda kujifunga vizuri damu isitoke, lile baba na wanafiki wakadhani kuwa Imamu Ali

amekwisha. Akawa yule Amri akinadi, mwingine mara hapo hapo Imamu Ali akamtokea,

likadanganywa, ukamtoka Ali tena Upanga ukampiga akaanguka, alipotaka kummaliza

kabisa, lile baba likamtemea mate usoni Imamu Ali. Hapo Imamu Ali akaona

akimmaliza, itakuwa ni kwa hasira zake si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, akamwita mtu

akamuua kabisa.

Hiki ni kisa mashuhuri katika tarekh zote, lakini baadhi ya waandikaji hawataki

kuwapa sifa wengine, kama sifa ya Imamu Ali na kueleza kisa hiki kwa urefu, bali hivi ni

ufupi, sababu zipo na nyimbo zake Imamu Ali alipokuwa akijisifu walipopambana na

Amri.

Muhammad Ridha aliyeandika Maisha ya Nabii Muhammad (s.a.w.w.) katika

kitabu chake: Kila katika vita vya Jihad amemsifu kila sahaba shujaa lakini katika vita ya

Khandak, mambo yote haya ya ushujaa wa Ali hakuyasema, ila amesema "Alitaka

Mubaraza Amri Imamu Ali akamuua!" Na ilhali ni mengi ya kusemwa! na hata katika

kitabu chake alichokiita Imamu ALI pia hakutaja kisa hiki wala chochote cha ushujaa.

Katika vita vya Uhud, Masahaba wote walikimbia na sababu ilitokana na wale

wenye kuwatilia vyembe walihalifu amri ya Mtume (s.a.w.w.) ameuawa. Basi tena hapo

hakukubakia ila watu wachache tu. Muhamad Ridhaa ameandika katika kitabu chake cha

Maisha ya Mtume (s.a.w.w.) kuwa:-Adui alifika mpaka alipokuwa Mtume (s.a.w.w.)

Mtume akaumia kwa mawe yao akaanguka akapotewa na fahamu. Ali na Talha ndio

walio muinua wakamsimamisha", Kisha amesema; katika walikuwa pamoja na Mtume

(s.a.w.w.) ambao hawakukimbia ni watii saba tu. Talha amemhesabu, Ali hakumtia! Na

kule nyuma amesema ndiye aliyekuwa pamoja na Talha wakimuinua Mtume (s.a.w.w.)

kisha amesema: ama Ali bin Abi Talib (R. A.) zimesihi hadithi kuwa yeye ni katika

waliothubutu (wasokimbia) na baadhi ya wapokeaji hadithi hawakumtaja, sababu alikuwa

ndiye mchukuaji bendera baada ya Musib".

Maneno haya yamo katika page (ukurasa) 232 na 234 katika kitabu chake

tulichokitaja. Vile vile katika ukurasa 198 katika vita vya Badri amesema: Aliulizwa Ali:

“Nani alieshujaa wa watu wote?" Akasema Abubakar, sababu yeye ndiye aliyekuwa

pamoja na Mtume (s.a.w.w.) katika (ARISH) kimwili.

Hapa hapaonyeshi ushujaa, panaonyesha kuwa Sayyidna Abubakar anapenda kuwa

pamoja na Mtume (s.a.w.w.), na vita vyote wapiganavyo watu huwa wanamlinda yeye.

Ama Imamu Ali kujibu namna hiyo ndiyo adabu kwani asipojibu hivyo ni sharti aseme:

"Shujaa ni mimi" kujibu namna hii licha ya yeye hata yeyote aliye mwerevu hawezi

kujibu.

Maneno hayakuwa Imamu Ali aliulizwa na akajibu hivyo, hakuthubutu kamwe

katika tarekh nyingine na angethubutu mahali pengine basi pia si ya kutolea hoja kama

hivyo.

Page 22: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

22

Basi kama tulivyo soma kuwa Imamu Ali alihudhuria katika vita vyote vya Jihad

na mara nyingi bendera ya Muhajirina Mtume (s.a.w.w.) alimpa yeye, ila katika vita vya

TAABUK vilivyokuwa mwaka wa tisa Hijra. Mtume (s.a.w.w.) hakumchukua Ali,

sababu alimuachia watu wake wa nyumbani. Hapo tena wanafiki wakaanza kutokwa na

maneno wakisema kuwa asingeachwa ila ni kwa uthakili wake, akatoka Imamu Ali

kwenda kumfuata Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza Mtume (s.a.w.w.) akamjibu kuwa; "Ni

waongo" nimekuachia watu wangu na wako, rudi mahala pangu. Kisha akamwambia:-

“Huridhiki Ewe Ali kuwa mbele yangu mimi una manzila kama ya Harun kwa

Musa? Isipokuwa hilo (la kuwa ) hapana (jinsi ya ) utume baada yangu! "Maana yake

hapana Mtume baada yake, lakini daraja zingine zote kama Ukhalifa, Uimamu yafaa

kuwa, Hadithi hii imetangaa katika vitabu vyote vya tarekh na vya hadithi na ni mmoja

katika watoleao hoja Mashia kuwa Imamu Ali ndiye Khalifa wa kwanza baada ya Mtume

(s.a.w.w.) lakini "Sunny" wamewajibu.

KISA CHA ANAS BIN MAL1K

Bw. Anas bin Malik. (R.A.) ni katika Sahaba, Ansari (wa Madinah) alikuwa

akimpenda Mtume (s.a.w.w.) na amepokea hadithi nyingi, moja ni hii hapa; amesema

mwenyewe:

"Aliletewa Mtume (s.a.w.w.) Hidaya (tunu) ya ndege wa kuchoma, alipowekewa

mbele yake alisema: “Ewe Mola! Niletee mimi apendezaye katika viumbe vyako kwako;

ale pamoja nami ndege huyu” Nikasema katika roho yangu. "Ewe Mola! nijalie mtu

(huyo) ni katika Ansar".

Akaja Ali akabisha mlango kwa taratibu. Nikauliza: Ni nani huyo? Akajibu; "Ni

mimi Ali" Nikamwambia Mtume (s.a.w.w.) yuko katika haja. Nikarudi kwa Mtume

(s.a.w.w.) naye akiomba ile dua yake. Akaja Ali mara mbili nami namrudisha. Hata

alipokuja mara ya tatu, Mtume (s.a.w.w.) akaniambia:

''Mfungulie mlango" nikamfungulia akapita akaketi pamoja na Mtume (s.a.w.w.)

Wakala pamoja yule ndege. Kisha Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali. "Ni lipi lililo

kuchelewesha? Akasema Ali" Hii ni mara ya tatu (kuja) na Anas akinirudisha'' Mtume

(s.a.w.w.) akaniambia. "Ewe Anas! Ni jambo gani lililokupa kufanya hivi? Nikasema:

Nikataraji mtu awe ni katika Ansar” Mtume (s.a.w.w.) akasema: katika Ansar yuko bora

kuliko Ali? Hadithi hii ya Bwana Anas, imepokelevva na Bw Abu Daud.

Tumeona mapenzi ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya Imamu Ali yalikuwa namna gani

katika kila jambo ataka ashirikiane naye; mapenzi ambayo akiyategemeza kwa Mola

wake, kwa kumwambia Mola wake: "Niletee apendwaye kwako katika viumbe vyako"

ELIMU YA IMAMU ALI

Page 23: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

23

Imamu Ali (K.W.) alikuwa bora wa Sahaba wote kwa elimu alivyo kuwa bora kwa

hoja kadhalika na kwa fasaha (uhodari wa kusema), mambo matatu haya hakushindwa na

yeyote baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni yeye. Ama katika Elimu, Mtume (s.a.w.w.)

amesema "Mimi ni mji wa elimu na ali ni mlango wake"(au ni nyumba). Amesema tena

“Mjuzi wenu kwa hukumu ya Ali”.

Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka Imamu Ali “Yemen” mara mbili ili kuwaongoza.

watu wa huko katika dini na awahukumu.

Imamu Ali akanena: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika wao (watu wa

Yemen) ni watu wazima na mimi ni kijana, pengine huenda nisisibu katika nitakalo

hukumu baina yao". Akamwambia (s.a.w.w.): "Nenda Mwenyezi Mungu atautia nguvu

moyo wako na auongoze ulimi wako" Kadhalika alipelekwa na Mtume (s.a.w.w.)

kuwalingania watu wa "Hamadan" na kwa "Banu Saad bin Bakr" na "Fulas", mahali kote

huku aliwalingania dini na wote wakaamini. Hapana nafasi ya kueleza kwa urefu.

Katika mwaka wa 9 Hijra, Mtume (s.a.w.w.) alimpeleka Sayyidna Abubakar katika

mwezi wa Hijra ili ahiji na watu. Kisha akamfuatisha Imamu Ali nyuma yake ili

awasomee watu wa Makkah ''Baraa-ah Kusitufiwe baada ya mwaka huo tupu tupu (bila

ya nguo kama ilivyo kuwa desturi yao) wala kafiri yeyote, asihiji, na mengineyo tena

akaenda Imamu Ali akasimama katika "Jamrah" (mahali pa kutupia mawe) siku ya Idd,

akatoa khutuba aliyo amrishwa na Mtume (s.a.w.w.).

Wakati wa khilafa ya Sayyidna Abubakar (R.A.) mara nyingi akishauriwa Imamu

Ali, kadhalika akipata Mushikil wowote Sayyidna Abubakar alikuwa akimuuliza Imamu

Ali. Hata mara moja alikuja mjumbe kutoka kwa mfalme wa Rome, akamuuliza Sayyidna

Abubakar. "Ni mtu gani ambaye hataraji pepo wala haogopi moto wala hamchi Mungu?

Harukuu wala hasujudu (wakati akiswali) anakula maiti na damu, na anashuhudia kwa

ambalo halioni, anapenda fitina na anasikia haki"?

Sayyidna Abubakar (R.A.) asiweze kujibu. Na Sayyidna Omar (R.A.) alikuwepo na

akakasirika juu ya yule mtu akamwambia "umezidisha ukafiri juu ya ukafiri wako"

akapelekewa habari hiyo Imamu Ali naye akaenda haraka akauliza yale maswali, kisha

akajibu hivi "Huyo ni mtu katika mawalii" wa Mwenyezi Mungu Yeye hataraji kuingia

peponi (kwa amali zake) wala hauchi moto lakini anamcha Mwenyezi Mungu. Wala

hamchi Mwenyezi Mungu (maana yake} hamchi na dhuluma zake bali anamcha kwa

uadilifu wake. Harukuu wala hasujudu katika "sala ya jeneza", anakula maiti na damu

(maana yake) anakula "nzige" "samaki" na "ini", anashuhudia kwa asiloliona (maana

yake) anashuhudia pepo na moto kuwa vipo naye hajaviona. Anapenda fitina (maana)

anapenda mali na watoto. Anachukia haki (maana) anachukia mauti". (Hakuna apendaye

kufa).

Basi ni mengi ya mushkil yaliyotokea kama namna hii, hasa katika Khilafa ya

Sayyidna Omar, hata Sayyidna Omar ikiwa usemi wake ni huu:-

Page 24: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

24

Ewe Mola wangu hakika najilinda na (mambo ya) Mushkil (mambo ya

kudanganyika) asipokuwepo Abal Hasan (Imamu Ali), "Maana yake asipokuwepo yeye

itakuwa hatari yakitokea maswali kama hayo.

Katika maneno yake Imamu Ali, kila mara alikuwa akisema:-

"Niulizeni kabla hamjanikosa (sijafa)", Khutuba zake na maneno yake ya maarifa,

yaani "Hekma" (Proverbs), hata vitabu 100 kama hivi havitoshi. Yeyote atakaye

kuzisoma hizo khutuba na kupata maarifa na asome kitabu "Nahjul - balaghah". Lakini

mwisho wa maneno yake, yaani baada ya kutaja kifo chake, nitataja kidogo katika

"Hekma" zake.

SIFA ZAKE

Imamu Ali ni nduguye Mtume (s.a.w.w.). Mtoto wa Ami yake, kisha ni mkwewe,

mumewe bibi Fatimah, tena ndiye baba wa dhuriya za Mtume (s.a.w.w.).

Yeye ni Mwislamu wa kwanza baada ya bibi Khadija. Yeye ni mtu wa kwanza

aliyeuza roho yake kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w.) wakati wa Hijra yake, akalala katika

firasha ya Mtume (s.a.w.w.). Yeye ndiye shujaa wa kwanza baada ya Mtume (s.a.w.w.).

Yeye ni mjuzi wa watu wote baada ya Mtume (s.a.w.w.) Yeye ni fasaha wa watu wote

baada ya Mtume (s.a.w.w.)

YEYE NA UKHALIFA (UTAWALA)

Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa mgonjwa (maradhi ya mauti) Imamu Ali alikuwa

haondoki nyumbani.

Mtume (s.a.w.w.) alipokufa walikusanyika Ansar (watu wa Madinah) katika jumba

lao mashauri (Bait Banu Saad) kumchagua Khalifa (mtu wa kushika mahali pa Mtume

(s.a.w.w.). Abu Ubaidah akapata habari hii, akatoka mbio mpaka kwa Sayyidna Omar,

akamwambia, upesi tukalipatilize jambo, Ansar wataka kumuweka Khalifa".

Wakaondoka wakaenda mpaka kwa Sayyidna Abubakar wakamwambia. Wote watatu

wakafuatana pamoja wakaenda kwenye mkutano wa Ansar.

Hapo Sayyidna Abubakar akatoa khutuba ndefu, katika maneno yake akawaonya

Ansar kuwa Khilafa ni ya Makuraish (watu wa Makkah).

Ukaendelea mjadala mrefu baina yao hata baadhi ya Ansar wakawahi kutoa panga

wakitaka kupigana, hawataki khilafa iwe kwa Makureish lakini mwisho wake upande wa

kina Sayyidna Abubakar ukashika nguvu, hapo tena akabaiwa (chaguliwa) Sayyidna

Abubakar lakini wengine wakakataa kumbai (kumchagua). Katika walio kataa mmoja ni

bwana mkubwa Saad bin Ubaad, bwana huyu hakumbai Sayyidna Abubakar mpaka

akafa.

Mambo haya yalipokuwa huko katika jumba la Ansar, akabaiwa Sayyidna

Abubakar, Masahaba kadhaa wa kadhaa hawakuwepo. Katika ambao hawakuwepo ni

Page 25: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

25

kina Sayyidna Uthman, Talha na Zubeir. Hawa ndio wakubwa wa Masahaba. Ama

Imamu Ali na Ami yake Sayyidna Abasi ndio waliokuwa wakimuosha Mtume (s.a.w.w.)

na kumkafini na Banu Hashim pia walikuwepo.

Imamu Ali na Ami yake na jamaa zao wote mara wakasikia kuwa amebaiwa

Abubakar, wao wote wakakataa na ulipita ushindani mkubwa baina yao na Sahaba.

Si kweli kuwa maswahaba wote walikuwa hawakumbuki kuwa nani inapasa awe

khalifa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au kuwa maswahaba hawakufahamu, ni yupi

aliye agizwa kuwa khalifa baada yake Mtume (s.a.w.w.) kauli mbili hizi si sahihi bali

maswahaba walikuwa wanamtambuwa mwenye haki zaidi ya kushika khilafa baada ya

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ili kuthibitisha hilo dondoo za baadhi ya waliyoyasema baadhi ya maswahaba.

Katika kikao cha kwanza cha mdahalo wa kumchagua khalifa kijulikanacho kwa

“HADITHI SAQIFA” WA KHILAAFATU ABUBAKARI kama ilivyo andikwa katika

tarehe ya AL-KAAMILU FI TARIKH YA IBUN ATHIRI:

Umar Bin Al-Khataab alifanya Bay’a ya Abi-Bakri akiwa mtu wa kwanza baada ya

mzozo mkali. Walisema Answari (watu wa Madina): LAA NUBAAYI-U ILLA

ALIYAN yaani hatuwezi kumfanyia Bai’a yeyote isipokuwa Aliy kisha aongeza kusema:

Hawakuwapo kwenye kikao kile cha Bai’a Aliy, na Baniy Haashimu, Zubair na Tal’ha na

alisema Zubair: Hatufanyi Bai’a isipokuwa ya Aliy. Ibun Athiri uk 325 Ama Ibun

Qutaiba ana nakili hivi: THUMMA INNA ALIYAN KARRAMA-LLAHU WAJIHAHU

ULITIYA BIHI ILAA ABIY BAKAR WA HUWA YA QULU: ANA ABDULLAHI

WA AKHU RASUULIHI.

Tarjuma yake: Kisha Aliy (a) aliletwa kwa Abi Bakari naye akisema: Mimi ni mja

wa Mungu na ni ndugu wa mjumbe wake. Kisha alipofikishwa kwa Abu Bakari

akaambiwa: Mfanyie Bai’a Aba Bakari Akasema (yaani Aliy): ANAA AHAQU

BIHADHAL-AMRI MINKUM. Mimi nina haki zaidi kwa jambo hili kuliko ninyi muna

paswa kunifanyia Bai’a mimi.

Ali aliendelea kusema: "'Mmelichukuwa hili Ma-Answari mukitowa hoja kwao

kuwa ninyi ni watu wakaribu wa Nabii (5) na mwauchukuwa (uongozi) kutoka kwetu

Ahlul-Bayt kwa nguvu."

Rejea uk 28-29 Kitabu Assiyasa wal-Imama pia hujulikana kwa jina la Taarikhul-

Khulafaa. Maelezo ya Imamu Aliy (a) yalikuwa ya wazi kabisa kuwajulisha maswahaba

kuwa yeye alikuwa na haki zaidi ya kuchaguliwa Khalifa kuliko Abu Bakari na Omar Bin

Al-Khatab.

Kati ya jumla ya mzozo huu wa kuchaguliwa Abu Bakari katika Saqifa Abdur-

Rah'man bin Aufi alisema kuwa shinikiza Answar wenyeji wa Madina: Ee ninyi Answar

hakika ingawaje munao ubora, lakini kati yenu hayupo mwenye ubora kama wa Abu'

Bakari, Umar na Aliy. Baada ya usemi huo alisimama Al-Mundhiru Bin Arqamu

Page 26: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

26

akasema: Hatupingi ubora wa ulio wataja kwa hakika kati yao kuna mtu lau angedai

jambo hili hangepingwa na yeyote. Amkusudia Aliy Bin Abi-Talib.

Tarehe ya Al-Yaaqoubiy uk 123 kichwa cha habari: "SAQIFA BANIY SAIDAH

WABAY-ATU-ABIY-BAKARI"

Tarehe hiyo hiyo uk 124. Imeandikwa:- Walikuwa muhajiruna na Answar hawana

shaka kumhusu Aliy. Walivyotoka nje ya Nyumba alisimama Abul-fadhili Bin Abbasi,

alikuwa ndio msemaji wa Maqureishi, akasema: "Ee ninyi Maqureishi haikuwa haki

kwenu kuchukuwa ukhalifa kwa njia ya udanganyifu, sisi ndio wenyewe sio ninyi na mtu

wetu ni mbora kwa ukhalifa kuliko ninyi".

Hapo usemi wa elekezwa kwa walio chukuwa khilafa toka kwa Answari na neno

mtu wetu ni bora, akusudiwa Aliy.

Kwa hiyo maswahaba hawakusahau wala si kweli kuwa walikuwa hawajui yupi

ashike khilafa!!

Sasa tutazame nini itakuwa, Abubakari ataweka wasia baada yake au naye

atawaacha kama wakati wa Mtume (s.a.w.w.), kwa maoni ya Masahaba kuwa aliacha tu,

hata alipokufa Sayyidna Abubakar (R.A.) ukaonekana wasia kuwa ameusia kuwa ashike

Sayyidna Omar. Hapo Omar Ibnul Khattaab (R.A.) akawa ndiye khalifa.

Sasa tutazame tena, Omar atafanya kama Abubakar atausia mtu Fulani, au ataacha

tu au atatumia maoni yake?

Alipo kurubia kufa Omar aliwahudhurisha masahaba sita watukufu “Ahul-Shuraa"

nao ni:- (1) Ali (2) Othman (3) Talha (4) Zuberi {5} Saad (6) Abdurahaman, wakawekwa

watu sita hawa, wao wamchague khalifa katika hawa sita bora wao ni Ali wakamchagua

Ali (a.s.) lakini katika shuruti alizoweka asikubali.

Imamu Ali alikubali kuhukumu kwa muujibu wa kitabu cha Mungu (s.w.t.) na kwa

Sunnah ya Mtume wa Mungu na alikataa kuhukumu kwa muujibu wa Sunnah ya

Sheikhaini (Abubakari na Omar).

Abdur-Rahiman bin Aufi Mwenyekiti wa Shuraa alimwambia Oth’man bin Affani

kuwa: Nitakupa Baia kwa Sharti ukubali kuwa utahukumu kwa mujibu wa kitabu cha

Mungu na Sunnah ya Mtume (s.a.w.w.) na Sunna Shekhayni Abubakar na Omari.

Othmani alikubali sharti hii bila kusita, Kwa hiyo Abdur Rahman Aufi akampa

Baya' Othman aliyekubaliana na Sharti za shuura. Hivyo Othman akawa Khalifa wa tatu.

Ili kuthibitisha hayo soma tarehe ya IBUN ATHIR V.3 - P – 71

Mwanzo mambo yakaenda vizuri, mara tu yakaharibika sharti zote zikavunjwa. Na

aliyeyaharibu ni Marwan Ibnu Hakam, Waziri wa Sayyidna Uthman. Ilikuwa mambo

yote matukufu na haki zote wapewe Banu Umayya.

Page 27: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

27

Hapo tena ikainuka "Thaura" (mapinduzi) kutaka kumuondoa Khalifa. Sayyidna

Uthman akakataa kujiuzulu, akakubali makosa yaliyopita na akayatengeneza, lakini

vilevile mambo yakazidi kuharibika ikawa fujo mpaka akauawa. na hakujulikana

aliyemuua, lakini yasemekana ni katika jeshi lililo kuja kutoka Misri. Kifo chake

chasikitisha sana. Hapo tena watu wakamuendea Imamu Ali awe Khalifa.

UTAWALA WAKE (KHILAFA YAKE)

Imamu Ali alibaiwa (chaguliwa) siku ya Ijumaa tarehe 25 mwezi wa Zul-hajj 35

Hijra, Juni 23, mwaka 656 AD (alibaiwa Madinah).

Mara tu baada ya kubaiwa Imamu Ali, Talha na Zubair walitoka kuelekea Makka

ambako Bibi Aisha alikuwa huko akihiji. Wakati Bibi Aisha alipokuwa akirudi zake

Madina, njiani alikutana na mtu mmoja jina lake Ubaid bin Abi Salama, akamuuliza. Je,

una habari gani? Yule mtu akajibu: “Uthman ameuawa” Akamuuliza: “Kisha wamefanya

nini?” Akasema: Watu wamembai Ali”.

Aisha akasema: “Laiti mbingu zingetengamana na ardhi! Nirudisheni, nirudisheni

(Makka)” Akarudishwa Makka na huku anakwenda akisema: “Wallahi ameuawa Uthman

madhlumu. Wallahi nitaitaka damu yake (kisasi).” Yule mtu akasema: “Kwa nini? Na

wewe ulikuwa ukisema muuweni Uthman.”

Basi Aisha akarudi Makka huko akakutana na Talha za Zubair kwa kutaka kisasi

cha Uthmani. Vita vikaandaliwa. Aisha akaandaliwa ngamia, na akaongoza vita dhidi ya

Imamu Ali akiwa amepanda ngamia huyo huko Basra. Ndipo vita hivyo vikajulikana kwa

jina la "Vita vya Jamal (Ngamia)"

VITA VYA JAMAL (NGAMIA)

Vita vya ngamia ilikuwa mfungo tisa, 36 Hijra, Bibi Aisha alitoka na jeshi lake

pamoja na zubeir na Talha wakenda mpaka Basra. Imamu Ali alipopata habari hii naye

akajifunga, akatoka na jeshi lake na masahaba watukufu kadha wa kadha hata ndugu yake

bibi Aisha yaani Muhamad bin Abubakar pia alikuwa upande wa Ali. Imamu Ali,

alikuwa amewanasihi kina Aisha, Talha na Zubeir wasisikie, kisha baadae wakakubali,

lakini baada ya kufa watu wengi na Talha (R A.) ameishauawa.

Hapo tena Zubeir akaacha vita akaenda zake. Pana mtu “Amri bin Jarmuz”

alimuona Zubeir akienda zake akamfuata akamwambia: Umeuwasha moto kisha

umeukimbia?! Akamuwinda kwa ghafla akamuua.

Na ulikuwa ni upande wa Bibi Aisha ndio ulioshindwa. Kisha Ali akamfungia

safari akampa na watu wa kumpeleka Aisha mpaka Madinah, na hapo tena vita vikaisha.

Sasa turudi nyuma tutazame baada ya kuuawa Uthmani ilikuwa nini Baada ya

kuuwawa tu. Mkewe alichukuwa kanzu ya mumewe na vidole vyake mwenyewe vilivyo

Page 28: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

28

katwa wakati wa kumkinga mumewe akavikusanya akaandika na barua akampa mtu

kuipeleka Sham (Syria) kwa Muawiya Liwali wa huko.

Muawiya bin Abi Sufiyan al- Amawiy ni yule aliyesilimu yeye na baba yake

pamoja katika "Fat-h – Makkah” ilipotekwa Makkah na Waislamu, 8 Ramadhan 8 Hijra

630 A.D. yaani wao waliukubali Uislamu baada ya kushindwa. Kusilimu kwao hata kufa

kwa Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni miaka miwili tu.

Muawiya akapokea kanzu ya "Khalifa Uthman" na vidole vya mkewe "NAILA"

pamoja na barua, alipomaliza kusoma barua, alichukua ile kanzu na vidole akavitundika

katika mimbari ya Msikiti. Kisha akawa anatoa khutuba kila mara kuwaona watu namna

gani khalifa alivyodhulumiwa na watu wa Madinah na hasa Banu Hashim (makusudio

yake ni Ali alipojua kuwa yeye ndiye Khalifa) na akawa anawahimiza watu wajiweke

tayari kutaka kisasi cha khalifa wao ili waende wakapigane na Ali.

Vilipokwisha vita vya" Jamal" Ali na Aisha. Imamu Ali aliondoka Basra kwenda

kukaa "KUFA" ambapo alipafanya" ASIMA" (Makao Makuu) yake, yote hiyo Basra na

Kufa ni katika Iraq. Imamu Ali kufika Kufa tu mara akasikia kuwa Muawiya na jeshi lake

la Sham la watu 60,000 (sitini alfu) limeondoka kuja kupambana naye.

Hapo tena naye akajifunga kwa jeshi la watu 50,000 (khamsini alfu) watu wa Iraq

wakaja na wengineo wote wakawa 90,000 (tisini alfu) zikatoka jeshi mbili la Muawiya na

la Ali yakapambana hapo mahali paitwapo "Siffin".

VITA VYA SIFFIN

Vita vya Siffin vilikuwa mfungo tano mwaka wa 37 Hijra, Julai 657 A.D hapo

"Siffin" karibu na mto wa Furat katika Iraq yalipambana majeshi ya pande mbili upande

wa Imamu Ali na upande wa Muawiya.

Kwanza Imamu Ali alimuuliza Muawiya hoja na sababu ya kuja kupigana

Muawiya akasema kuwa anataka damu (kisasi) ya Khalifa Uthman, ili Ali amtoe aliye

muuwa Uthman. Ali akawambia kuwa hamjui, ikiwa yeye anamjua amwambie fulani

apate kumuhukumu. Muawiya asimtaje ni yupi. Basi Imamu Ali akamwambia kuwa kuna

haja gani ya kumwaga damu ya Waislamu kwa ajili ya mtu mmoja! Tutoke mimi na

wewe tupambane" Hilo pia Muawiya asiliweze.

Baada ya mjadala mrefu na Imamu Ali kumsihi asisikie, akawa hataki ila ni vita.

Basi hapo tena vita vikaanza vikali kabisa, vikaendelea mara katika safu ya Imamu Ali

aliuwawa sahaba mtukufu naye ni Ammar bin Yaasir.

Alipouwawa mtu huyu, Amri Ibnil Aasi Waziri wa Muawiya alishangaa kupigana

na watu wengi wakamfuata wasipigane.

Muawiya akamuuliza "mbona hupigani?" Akamjibu nimemsikia Mtume (s.a.w.w.)

akisema "Kitamuuwa yeye (Ammar) kikundi kibaya". Nasi tumemuuwa mtu huyu

Page 29: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

29

yaonyesha sisi ni wabaya" Muawiya akasema: Sisi tumemuuwa? aliyemuwa ni

aliyemleta (yaani Ali), lakini sisi tumejitatua na yeye tu"

Namna gani watu hawa Muawiya na Amri, baada ya kusema wao wenyewe pia

wakawa hawaitaki haki?!

Imamu Ali aliposikia jawabu la Muawiya kwa kuuwawa Ammar, naye alisema:

"Na aliyemuuwa Hamza (katika vita vya Uhud) ni Mtume (s.a.w.w.). Kwa sababu yeye

ndiye aliye mpeleka".

Basi Muawiya na rafiki yake wakawa hawaitaki haki, wakaendelea na vita na

nguvu ziko katika jeshi la Ali. Likasonga jeshi lake mpaka kwenye Quba ya Muawiya. na

Amri, wakawa hawana la kufanya. Muawiya akamwambia rafiki yake, tufanye hila gani

sasa? Amri akajibu. Tuinue misahafu tuitundike juu ya mafumo, tuseme kitabu cha

Mwenyezi Mungu baina yetu na ninyi. Wakikubali hilo wao wote vita vitakwisha, na

wakikubali baadhi yao na baadhi wakikataa basi watakuwa wamegawanyika na kwa

kugawanyika kwao ndiyo faraji kwetu" Muawiya akafurahi kwa rai hiyo.

Basi hii ndiyo hila aliyoipika Amri, wakakataa haki wakafuata hila na makri

(vitimbi). Hapo tena wakaitundika misahafu na baadhi ya Jeshi la Ali likasimamisha vita.

Imamu Ali alipoona vile akawauliza watu wake sababu ya kusimamisha vita. Wakamjibu

kuwa wameinua Misahafu wanataka hukumu (sulhu) baina yetu. Imamu Ali akawaambia:

"Tusikubali hilo, hizo ni hila tu” kikaja kikundi kingine wakamwambia Ali kuwa lazima

tuwasikilize Imamu Ali akashangaa na akachelea fitina kwa watu wake kumuasi,

akasema: enyi waja wa Mungu endeleeni katika haki yenu na ukweli wenu na kupigana

na adui yenu.

Hakika ya "Muawiya na Ibnul Aas si watu wa dini wala Qur'an, mimi nawajua

zaidi kuliko nyinyi, nimesuhubiana nao tangu udogoni mpaka kufikia utu uzima, wakawa

ni wabaya utotoni na wabaya kwenye utu uzima wao.

“Wallahi wao hawakuinua misahafu ila ni hadaa na vitimbi”

Lakini wapi! Ndiyo yale yale tuliyoyasema kuwa khilafa ya Imamu Ali haimtaki.

Wakakataa kabisa kumsikiliza Imamu wao wakawa hawataki ila kufanya Hukumu.

Hukumu yenyewe ni kuchagua watu wawili wafanye sulhu watakalo pitistia wao ndilo

litakalo kubaliwa.

Muawiya akamchagua waziri wake (Amri) na watu wa Ali wakamchagua Abu

Musal-Ash~ari, na mtu huyu hakuwemo katika vita. Imamu Ali hakumkubali mtu huyu

akijua kwa yakini hawezi kupambana na Amri, ataviringwa tu, lakini vile vile watu wake

hawakumkubali yeyote ila huyo.

Muawiya akampanga mtu wake barabara (vizuri) na akamtia tamaa, akampa na

ahadi kuwa wakishinda atampa Misri na kumfanya Liwali (kama alivyokuwa Zamani za

Khilafa ya Umar, aliposhika Uthman akamuuzulu) Muawiya akamwambia Amri amghuri

Page 30: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

30

Abaa Musa ili amuuzulu Ali na yeye Amri amuondoe Muawiya kuwa si Liwali kisha

Waislamu wamchague Khalifa mwingine.

UAMUZI (TAHKIM)

Basi tena Amri akamuona Abuu Musa hata akakubali na wakishamaliza mashauri

kila mtu atamuuzulu mtu wake. Hata ilipokuwa siku ya hukumu, walikutana watu wote

kutoka kila upande wa Ali na Muawiya na vita vilikuwa vimesimama kwa muda wa siku

nyingi.

Alisimama Amri Ibni As akamtangaza Abu Musa ili aseme yeye kwanza akainuka

Abuu Musa akatoa khutuba kisha akasema: "tumeona Maslaha mimi na Amri kuwauzulu

watu wetu wawili, kisha ninyi mumchague mumtakaye, basi mimi namuuzulu Muawiya

na Ali" akaketi, akasimama Amri akasema - mmesikia Abaa Musa amuuzulu Ali nami

namuuzulu pia kuwa si khalifa, namthibitisha Muawiya sababu yeye ndiye mwenye haki

na atakaye kisasi cha khalifa Uthman".

Hapo tena ikadhihiri khiyana wakatukanana wao wawili na watu wengi

wakakasirika. Mara ghafla likatoka kundi jingine upande wa Imamu Ali wasiopungua

watu 10,000 wakawa wanasema: Hapana hukumu ila ni kwa Mungu’ Kikundi hicho

kikajiita "Khawariji' wakakufurisha vikundi vyote viwili cha Ali na Muawiya,

wakamfanya Imamu Ali kuwa ni kafiri kwa kukubali hukumu ile, wala naye hakukubali.

Au wao Khawariji kumfanya Imamu Ali ni kafiri au amepotea, amefanya makosa gani?

Kwani aliye hukumu ni yeye? Yeye si ndiye aliyekataa mwanzo wasisikie

wakamlazimisha akubali! Wala yeye hakukubali kumuuzulu. Vipi watamuuzulu watu

wawili naye amebaiwa Madinah na watu wote wa Iraq kadhalika.

Lakini Khawarij makusudi yao ni tamaa ya kupata dola nao kama aliyoipata

Muawiya Sham, Khawarij na mkubwa wao ni Abdullah bin Wahbu Raasibiy, wakawa

wakimpata mtu akitaka kumkufurisha Imamu Ali na Sayyidna Uthman kumuuwa. Ali na

Uthman kwao ni makafiri. Hapo Imamu Ali asiweze kustahimili akatoka na jeshi lake

kwenda kuwakomesha, akawanasihi sana wasisikie akawauwa, hawakubaki ila kidogo tu.

Basi zikaisha nguvu zao wakakoma.

Kisha Muawiya akaunda jeshi kwenda kuipiga Misri kuitoa katika mikono ya

Imamu Ali, Na wakati huo aliyekuwa Liwali wa huko ni Muhamad bin Sayyidna

Abubakar (yule aliye lelewa na Ali). Akaenda Amri na jeshi lake mpaka Misri. Jeshi la

Misri lilikuwa halina nguvu, likapata na khiyana ya fitina alizozitia Muawiya:

Imamu Ali wala Muhamad bin Abubakar hawana habari. Basi tena Muhamad bin

Abubakar akashindwa akauawa kisha akatiwa ndani ya matumbo ya punda akawashwa

moto. Yakatimu matakwa ya Amri akajikalia Misri.

Hii ndiyo kazi ya Amri Ibnul Aasi kwa mtoto wa Sayyidna Abubakar (R.A.)

kitendo kama hiki hata makafiri hawakufanya.

Page 31: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

31

Mara muda si muda, wakatoka watu watatu katika Khawarij wakafanya mashauri

wakalishana viapo katika Alkaaba ili wawauwe watu watatu kwa siku moja nayo ni siku

ya Lailatul Qadri” ili watu wapambazukiwe na furaha. Makhawarij watatu hao ni:-

1. Abbulrahman Ibnul Muljim, amuuwe Ali bin Abi Talib, Iraq.

2. Al-Bakr bin Abdulla Athimin, amuuwe Muawiya, Syria

3. Amri bin Bakri Athimmimiy, amuue Amri Ibnul Ass, Misri.

Hata siku ile ya miadi wote watatu kila mtu akaelekea upande wake, yule Amri bin

Bakri akaenda Misri, siku ile aliyokusudia kuuwa alfajiri yake, ikawafiki Amri hakutoka

kwenda Msikitini kusalisha alikuwa mgonjwa (au alipata habari kwa majasusi) akamtoa

mtu wake aitwaye Kharijah.

Wakati akiingia kiblani kusalisha, akapambana na upanga akafa, akashikwa yule

mtu akapelekwa kwa Amri alipoulizwa sababu ya kumuuwa yule akasema "Niliona kama

ni wewe Amri, kadhalika nakupa bishara kuwa Ali na Muawiya pia wameuawa, kisha

akauawa yule mtu.

Yule Al-Bakr bin Abdullah akaenda Sham (Syria) kwa Muawiya, lakini huyu pia

hakufaulu alimpiga dharuba ikampata ya matako ikamuumiza tu, pia naye alipoulizwa

alisema kuwa leo wakubwa watatu wamekusudiwa, tumeona kuwa wawili wamevuka

salama, sasa tutazame Imamu Ali bahati yake lakini haikuwa nzuri.

KUUAWA KWA IMAMU ALI

Abdurahaman Ibnu Muljim akawasili Kufa (au kufa) akaingoja ile siku hata

kulipopambazuka asubuhi mapema siku ya Ijumaa 17 Ramadhan. 40 Hijra 25 Januari

66O A.D. akatoka yeye na rafiki yake aitwaye Shabib bin Bujrah al-Ashjaiy waliagana

pamoja kuuwa, Wakaenda mpaka msikitini wakamngoja Imamu Ali, alipoingia kiblani tu

wote wawili wakamshambulia kwa panga lakini upanga wa Shabib haukumpata wala

naye hakupatikana kushikwa.

Ama upanga wa Ibnul Muljim ukampata Ali pembe ya kichwa naye akashikwa.

Ibnul Muljim alipofika Kufa alinunua upanga kwa elfu Dirham 1,000 na akautia

sumu kali ya kumuulia Imamu, alipambana na mwanamke Kitam binti Shahna ambaye ni

Khawarij, baba yake na mama yake walikufa katika vita vya Nahrawan (mahali

walipouawa Makhawaarij na Ali), alipopambana naye akampenda akataka kumuoa,

mwanamke huyu akamwambia Ibni Muljim “mahari yangu ni dirham elfu tatu na

kumuuwa Ali bin Abi Talib”, Ibn Muljim akakubali, lakini mawili hakuyapata alipata la

kumuua Imamu na kuuawa yeye na moto wa akhera unamngoja.

Basi aliposhikwa Imamu akausiya awekwe kisha: akasema: "Roho kwa roho nikifa

muuweni kama alivyoniuwa na nikibaki hai nitatizama maoni yangu, Enyi banil Mutaalib

msimwage damu ya Waislamu mkasema ameuawa Amiiril Muuminina”, Enyi fahamuni!

asiuawe ila aliye niuwa. Tazama ewe Hassan mimi nikifa na dharba hii, mpigeni dharuba

Page 32: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

32

kwa dharuba wala "Msimmathilishe" mtu (kumkata vipande vipande) kwani nimemsikia

Mtume (s.a.w.w.) akisema "Tahadharini na kumathilisha japokuwa ni kwa mbwa

auwaye".

Huu ndio wasia wa Imamu Ali kwa yule aliyempiga, hata baada ya siku tatu yaani

mwezi 20 Ramadhan usiku wa kuamkia 21, akawakusanya watoto wake Hassan, Hussein

na Mohamadul Hanafiya, kisha akawapa wasiya mrefu kwa ufupi ni hivi:-

"Nawausia kumcha Mwenyezi Mungu! Wala msiutake ulimwengu hata kama

ungewataka: akaendelea mpaka kisha akamkabili Alhanafiya akamwambia: Nakuusia

kuwaheshimu ndugu zako hawa (Hassan na Hussein) kwa utukufu wao walio nao (kuwa

mama yao Fatimah) na ni wakubwa zako" Kisha akawazungukia Hassan na Hussein

akawaambia. "Nawausia na ndugu yenu mdogo wenu mtoto wa baba yenu, na mwajua

kuwa baba yenu anampenda". Akaendelea kusema kwa kuwaamrisha watoto wake

waamrishe mema na wakataze mabaya, kisha akamaliza maneno yake Kwa kutoa

shahada akafa (R.A.)

Mauti ya Imamu Ali yalitabiriwa na Mtume (s.a.w.w.) aliposema:- "Ewe Ali!

Wajua nani aliyembaya?" (shakiy wa watu) wa kwanza? Imamu Ali akajibu:

“Aliyemuuwa “Ngamia” (wa Nabii Saleh)” akasema tena (s.a.w.w.) Na ni yupi mbaya

(Shakiy wa akhir zamani) wa watu wa mwisho?" Ali akajibu: "Mwenyezi Mungu na

Mtume wake ndio wajuao". Mtume (s.a.w.w.) atakaye kuuwa wewe" na alimuonyesha

mahali atakapopigwa.

Imamu Ali alioshwa na Hassan, Hussein na Abullah bin Jaafar, akasaliwa na

Hassan na alizikwa Najaf.

FAMILIA YAKE

Imamu Ali alikuwa na watoto thelathini na watatu, kumi na watano wanaume na

kumi na wanane wanawake. Na wote hawa aliwazaa kwa wake mbali mbali aliowaoa

baada ya kufa bibi Fatimah. 1. Hassan 2. Husein 3.Muhsin (aliyekufa mdogo) mama yao

ni Fatimah. 4. Abas 5. Abdullah 6. Jaffar 7 Uthman, mama yao ni Ummul Banin 8.

Muhamadul Akbar. Mama yake ni Khola bint Jaafar 9. Muhamadul Ausat, mama yake ni

Umma bint Abil Aas. 10. Muhamadul Asghar, mama yake ni Ummu Walad 11. Abubakr

12. Ubaidullah, mama yao ni Caila bint Mosood 13. Yahya 14. Aun mama yao ni Asmaa

bint Umais (mama yake Muhamad bin Abubakr) 15. Umarul Akbar. Mama yake ni

assahbaa Ummu Habib. Kadhalika kuna na Umarul Asghar na Abass Al Asghar na

Abdurahmaan, hawa watatu mama yao sikumjua.

Na wanawake ni:- 1. Zainabu 2. Ummu Kulthum, mama yao ni Bibi Fatimah 3.

Rukkaya 4. Ramla 5. Umm-Hani 6. Maimuna 7. Fatimah 8. Khadija 9. Ummul Kiram 10.

Ummu Salama 11. Ummu Jaafar 12. Jumana 13.Umama 14. Nafisa 15. Fakhita 16.

Musna 17. Amatuliah 18. Ummul Khair

Page 33: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

33

Imamu Ali alikufa akiwa na Umri wa miaka 63 kama umri aliofia Mtume

(s.a.w.w.) na Makhalifa wawili Sayyidna Abubakar na Umar, khilafa ya Imamu Ali

ilikuwa miaka mitano kupungua kidogo. Na kama tulivyo soma khilafa yake ilikuwa ya

taabu na balaa tangu mwanzo mpaka mwisho.

Tumeona Muawiya namna gani alivyompinga baada ya Imamu Ali kumnasihi

asisikie, kadhalika na haki akaiona wakati alipouawa Ammar bin Yasir, Amri Ibnul Aas

akamtolea hadithi ya ushuhuda wazi kuwa atauawa na kikundi kibaya: kadhalika na yeye

huyo aliyeitoa hadithi hiyo ya Mtume (s.a.w.w.) pia naye asiifuate! Allahu Akbaru!.

Isitoshe bughudha ya banu Ummaya kumchukia Imamu Ali, na Khawarji wakazidi

wakamfanya “kafir” Ibni Ami Rasulillah na mkewe Fatimah bint Rasul kufanya kafiri!

Pamoja na ushuhuda wote wa hadithi za Mtume (s.a.w.w.) juu ya Imani mahaba yake juu

ya Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.) lakini hii si ajabu kwani Mtume (s.a.w.w.)

alimpigia mfano Imamu Ali kuwa yeye ni kama mwana wa Maryam (Nabii Isa)

Mayahudi kwa kumchukia wamemfanya ni mwana wa haram, na manasara kwa

kumpenda wamemfanya ni mtoto wa Mwenyezi Mungu.

Basi na Imamu Ali ni vile vile Umayya wamemlaani na Khawarij wamemkufurisha

na baadhi ya madhehebu wamemfanya Mungu! “Wal-yaudhu Billah”.

MISEMO YAKE

Misemo ya Imamu Ali ni mingi sana lakini nitajaribu kuitaja hapa kidogo na

msomaji apate faida.

ULIMI

(a) Mwenye kuwa mtamu ulimi wake huwa wengi rafiki zake.

(b) Ulimi wa mwenye akili uko mbele ya moyo wake.

(c) Mtu amejificha chini ya ulimi wake.

(d) Semeni mpate kujulikana.

ELIMU

(a) Elimu humtukuza mtu mnyonge na ujinga humtweza mtukufu.

(b) Elimu ni bora kuliko mali elimu ya kulinda wewe, na wewe wailinda mali.

(c) Elimu ni hakimu na mali yahukumiwa.

(d) Ukafiri kuliko ufakiri ni ujinga.

(e) Neema ya mjinga ni kama bustani iliyo katika jalala (mahali pa kutupa

takataka).

WEMA

(a) Kwa wema (kutenda jema) muungwana utamfanya mtumwa.

(b) Hakuna ushindi pamoja na ubaya.

(c) Hakuna raha pamoja na husuda (kuwa hasidi) hakuna murua kwa muongo.

Page 34: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

34

(d) Hapana kusibu pasi na kushawir.

(e) Mneemeshe umtakaye utakuwa juu yake.

(f) Ubakhil ni makusanyo ya aibu zote.

KUMCHA MUNGU

(a) Hakuna utukufu kuliko kumcha Mungu.

(b) Hakuna maombezi yenye kuokoa kuliko toba.

(c) Mtumwa wa matamanio ya nafsi ni mnyonge kuliko mtumwa hasa.

(d) Mungu amrehemu mja aliyejua cheo chake.

(e) Jaala ikishuka udhuru kuondoka. (Jaala: kadari ya Mungu) ni njia iliyo kiza

usiiandame na ni bahari yenye uketo usiizamie, siri ya Mwenyezi Mungu

imefichikana usiitoe.

Katika kumlingania Mola wake alisema:- “Yanitosha mimi utukufu kuwa wewe ni

Mola wangu, na yanitosha mimi fakhari kuwa mimi ni mja wako".

Sasa hapa nakoma kuieleza tarekh ya Imamu Ali na sifa zake. Sasa nimuanze mtoto

wake wa kwanza na ambaye ni wanne katika wale" Ahlul - Kisaa ", naye ni:-

IMAMU HASSAN

Hassan bin Ali bin Abi Talib bin Abdil Muttalib bin Hashim, Mama yake ni

Fatimah bint Rasulillah, Muhamad (s.a.w.w.) kun-ya yake ni Abu Muhamad na lakab

yake ni Attaki, Al-Amin na Sibtir-Rasul.

Alizaliwa Jumanne ya katikati ya mwezi wa Ramadhan mwaka wa tatu wa Hijra

625 A.D. siku ya saba aliakikiwa na Mtume (s.a.w.w.) kwa mbuzi, akamnyoa nywele

zake akamtasadakia kwa uzani wake fedha, kisha akampa jina.

Imamu Ali asema: "Alipozaliwa Hassan alikuja Mtume (s.a.w.w.) akasema:

'Nionyesheni kijana changu je mmemwitaje? Nikasema nimemwita "Harb" akasema la

yeye ni "Hassan" na alipozaliwa Hussein tukamwita "Harb" akasema huyu ni "Hussein"

na alipozaliwa wa tatu tukamwita "Harb" akasema huyu ni "Muhsin" kisha akasema

nimewaita kwa majina ya Nabii Harun (watoto wake aliwaita): Shibri, Shabir na Mushbir

au Mushabbir."

Imamu Hassan alikuwa mweupe mzuri, na alikuwa amefanana sana na babu yake

(s.a.w.w.) kwa sura na upole, alikuwa karim mwenye heshima na murua, mwepesi

kusamehe na alikuwa hapendi fitina.

UKARIMU WAKE

Imamu Hassan alikuwa karim (wa kutoa mali) kupita kiasi, alimsikia mtu

akimuomba Mola wake ampe 10,000 Dir (Dirham elfu kumi) akaondoka Hassan akaenda

nyumbani akachukua zile Dirham akamletea yule mtu.

Page 35: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

35

Watu walimwambia Imamu Hassan "Namna gani wewe twakuona humrudishi

mwenye kuomba, na ingawa wewe pia ni muhitaji'? Akajibu: "Mimi kwa Mwenyezi

Mungu naomba tena najibembeleza kwake kwa hilo, nami naona haya kuwa kwake

naomba kisha nikamrudishe aniombaye na hakika! Mwenyezi Mungu amenizoeza mimi

ada (desturi), amenizoeza kunibubujishia neema zake juu yangu, nami nimezoea

kuwabubujiza (kuwapa kwa wingi) watu. Basi nachelea nikiondoa ada yangu; naye

Mwenyezi Mungu atazuia ada yake.

Haya ndiyo maneno ya majibu ya watu watukufu. Hivi ndivyo vitendo vya watu

wakarimu. Huu ndio mwendo wa Kiislam wanatakiwa waende mwendo huu na hasa

"masharifu" sababu ndio mwendo wa babu zao "Muacha lake huchekwa". Lakini wapi

sasa mambo haya yamekosekana kwa watu wote, na kwa pia tajiri ndiyo zaidi! Licha ya

kuendewa na mwenye haja ya kuomba hata ya kukopesha ni tabu. Na akitoa atoe maneno

na aeneze habari, na kutaka kujua atalipwa lini! Kana kwamba anaona mali ile ameipata

kwa uhodari kuliko yeye kwa kila kitu na hawazipati kupata si uhodari, wala kukosa si

ujinga.

“Fadhila (zozote – mali au jinginelo) ziko katika mamlaka ya Mwenyezi Mungu

humpa amtakaye”.

Uislamu umekuwa “mnyonge” dhaliil, na uko nyuma kwa elimu na kwa kila

jambo, si kwa lolote ni kwa pesa tu.

Ikiwa matajiri watazuia mikono yao hawafanyi yaliyo wajibu juu yao na sunna,

basi Waislamu watakwenda vipi mbele kwa elimu? na elimu yoyote si bure. Watakao

weza kusoma ni watoto wa kitajiri tu, hivi wasionao watasoma! Kila asomaye tarekh ya

Uislamu utaona kuwa Uislamu haukusimama kwa mdomo tu, la, bali umesimama kwa

mdomo na mali na kwa kutoa roho yake mtu.

Sisi tujiitao Waislamu wa kweli “Ahlul Sunna Wal-jamaa” Sunna yetu na jamaa

yetu ni katika kusali tu, lakini katika mengineyo la, hatuna haja. Yale makundi mengine

ya Kiislamu utaona mambo yao yote yanakwenda vizuri. Huwaoni Maimamu wao wa

Msikiti wala Masheikh wao kuwa ni masikini. Watoto wao wa kitajiri na wa kimaskini

wote wanakwenda mashuleni wala husikii kuwa mmoja katika wao amefukuzwa shuleni

kuwa hana ada ya shule. Enyi Waislamu Mwenyezi Mungu anatwaambia:-

$ pκ š‰ r'≈tƒ t Ï%©!$# (#θãΖtΒ#u ö≅yδ ö/ ä3—9 ߊ r& 4’ n? tã ;οt�≈pg ÏB / ä3ŠÉfΖè? ô ÏiΒ A>#x‹tã 8ΛÏ9 r& ∩⊇⊃∪ tβθ ãΖÏΒ÷σ è? «!$$ Î/

Ï& Î!θ ß™u‘uρ tβρ߉Îγ≈pgéB uρ ’Îû È≅‹Î6 y™ «!$# óΟ ä3Ï9≡uθ øΒr' Î/ öΝä3Å¡ à�Ρr& uρ 4 ö/ ä3Ï9≡sŒ ×�ö�yz ö/ ä3©9 βÎ) ÷Λ äΖä. tβθ çΗs>÷è s? ∩⊇⊇∪

“Enyi mlio amini! Ninawaonyesha (bishara hiyo ni) kumuamini Mwenyezi Mungu na

Mtume wake na mkafanya Jihad katika njia (dini) ya Mwenyezi Mungu kwa mali zenu na

nafsi (roho) zenu. Hilo (la jihad) kwenu, ndio bora kwenu ikiwa mnajua. (Sura 61:10-11)

Page 36: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

36

Aya za mbele baada ya hii zimeeleza habari ya malipo yao nayo ni pepo. Basi

shime jamaa! Nikiendelea kutaja visa vya ukarimu wa Imamu Hassan havitakwisha; Basi

"bora niendelee kutaja:-

UTUKUFU WAKE

Imamu Hassan na nduguye Hussein udogoni mwao wamelelewa na Mtume

(s.a.w.w.) na ukubwani wamelelewa na baba yao, basi bila shaka kila mambo matukufu

watakuwa nayo. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiwapenda; akisema:-

"Hawa wawili (Hassan na Hussein) ni watoto wangu na ni watoto wa binti yangu.

ewe Mola! Mimi nawapenda nawe wapende. Na umpende mwenye kuwapenda hawa".

Alikuwa Mtume (s.a.w.w.) akisali, katika kusujudu wakija Hassan na Hussein (au

mmojawapo wakimparaga juu ya maungo yake, watu wakitaka kuwaondoa Mtume

(s.a.w.w.) alikuwa akiwaashiria waache kisha akisema anipendae mimi na awapende

wawili hawa". Amesema tena (s.a.w.w.):-

“Hawa wawili ni watoto wangu mwenye kuwapenda amenipenda mimi na mwenye

kuwachukia hawa amenichukia mimi”.

Imamu Hassan na Hussein ni sawa fadhili zao (Matukufu yao) na mapenzi yao kwa

babu yao, Mtume (s.a.w.w.) namna alivyokuwa akiwapenda. Siku moja Mtume (s.a.w.w.)

alikuwa juu ya mimbar akikhutubu mara akawaona Hassan na Hussein wanakwenda

huku wakicheza, akaacha kukhutubu akashuka kutoka katika mimbari akawachukua

akawapakata.

Siku moja Hassan au Hussein alikuwa amebebwa na Mtume (s.a.w.w.) akapita mtu

mmoja akasema:-

"Neema ya mapando ni uliyoyapanda we! Kijana! Mtume (s.a.w.w.) akasema: "Na

neema ya aliyepanda (ni huyu kijana)" Imamu Bukhari amepokea hadithi kuwa Mtume

(s.a.w.w.) alikuwa juu ya mimbari na karibu yake alikuwepo Hassan, akasema:- Hakika

ya kijana wangu huyu ni bwana, hakika Mwenyezi Mungu atasahilisha kwa ajili yake kati

ya vikundi viwili vya Kiislam" SAHIHl BUKHARI VOL. 3, uk 244.

Imamu Hassan amesoma Qur-an pamoja na tafsiri yake kwa baba yake basi bila

shaka naye ni hodari ni fasaha kama baba yake. Sasa tuendelee kutaja:-

UTAWALA WAKE (KHILAFA YAKE)

Baada ya kupigwa Imamu Ali na yule dhalimu Ibnil Muljim kama tulivyo soma

huko nyuma Imamu Ali aliusia kabla ya kufa, aliwausia watoto wake kumcha Mwenyezi

Mungu. Kisha akaingia mtu akamwambia: Ewe Amirul Muuminina! tukikukosa (ukifa)

Page 37: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

37

wala hatutakukosa (Inshaallah)! Je tumbai Hassan (tumpe ukhalifa mtoto wako)? Imamu

Ali akasema:- “Siwaamrishi wala siwakatazi, ninyi mwafahamu zaidi”.

Tumeona kuwa Imamu Ali hakuwausia watoto wala watu kwamba akifa khilafa

apewe mtoto wake na ilhali Hassan au Husein kwa wakati ule wao walikuwa bora kwa

kila kitu. Lakini Imamu Ali aliwaachia Umma wafanye watakalo, kisha asilaumiwe kwa

kuwalazimisha watu jambo wasilolipenda.

Hapo tena akabaiwa Imamu Hassan kuwa ndiye khalifa wa Waislamu baada ya

Imamu Ali. Alikuwa Khalifa mwezi wa Ramadhani mwaka wa 40, Hijra, 661 A.D.

Walimbai watu wapatao 40,000 (elfu arubaini) na aliyembai akiwa wa kwanza ni Kais

bin Saad Al- Ansariy.

Mambo aliyofanyiwa Imamu Ali na Muawiya tumeyaona, sasa tumtazame huyu

kijana wake, Khalifa mpya mjukuu wa Mtume (s.a.w.w.) atafanywa nini na Muawiya na

watu wake!.

Imamu Hassan baada ya kubaiwa tu, akapata habari kuwa Muawiya na jeshi lake la

watu wa Sham lipatalo 60,000 (elfu sitini), wameondoka kuja kupambana na Hassan na

jeshi lake la watu wa Iraq, wale waliombai watu 40,000. Elfu arobaini. Akatoka Hassan

na jeshi lake kwenda kupambana na Muawiya, naye alikuwa amepiga kambi mahali

paitwapo Maskini. “Na Imamu Hassan alikuwa amefika Madain (vijiji vya Iraq) na aliye

mtanguliza katika jeshi lake ni Kais bin Saad, yule aliyembai akiwa wa kwanza. Jeshi la

Hassan lilipofika hapo mara ghafla ukasikika ukelele kuwa yule Kais ameuawa, basi

kimbieni mwende zenu". Hapo tena jeshi la Hassan likaanza kukimbia baadhi ya watu, na

wakamuibia vitu vyake katika hema lake, na mtu mmoja aitwaye Jarah bin Asad

akamrukia Imamu Hassan kwa jambia kutaka kumuuwa, lakini lisimpate: "Mmemuuwa

baba yangu jana, na leo mwanirukia mimi kutaka kuniua?

Hii ndiyo hali ya watu wa Iraq kwa Hassan na tutaona mbele wakati wa Imamu

Hussein.

HASSAN KUACHA UKHALIFA

Imamu Hassan alipoona kuwa watu wa Iraq hawana ukweli, na khilafa haitatulia ila

mpaka kwa kumwaga damu ya Waislamu, basi akaona hapana haja tena kukaa katika

ukhalifa.

Akakubali kujiuzulu kumuachia Muawiya kwa masharti mengi miongoni mwa

masharti hayo ni: Asiusie khilafa baada yake Muawiya kwa mtoto wake (Yazid). Watu

wa Iraq na Hijra katika Shia (waliomnusuru Imamu Ali) wawe salama, asilaaniwe Ali,

Hassan achukue kisasi cha haja zake katika Baitul-mal ya kufa.

Muawiya akafurahi kwa Imamu Hassan kujiuzulu, na akakubali baadhi ya yale

masharti. Akatoa pesa nyingi sana akampa Sayyidna Hassan. Lakini kunyamaza

kumlaani Imamu Ali hakukubali.

Page 38: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

38

1. Mauwiya ndiye Khalifa wa kwanza (mfalme) wa Bani Ummaya na ndiye wa

kwanza aliyeweka "laana" kulaaniwa Imamu Ali, katika mimbari na kila mahali penye

ufalme wake na wa Bani Umayya, na mtu yeyote akataaye kulaani huuawa.

Jambo hili lajulikana na kila msomaji wa tarekh. Vitabu vyote vya tarekh vyasema;

kama tarekh ya Ibnul Athir Al-Masudy, Ikdul - Farid na nyinginezo kadha wa kadha.

lakini ajabu ni ya watu wengine ambao hawakushughulika na tarekh hata kidogo, licha

hii ya watu hawa hata ya Mtume (s.a.w.w.) hajui, wanajua kuwa alikuwa Mtume tu. Basi

watu hao wakafanya mambo kama haya, kuwa si kweli! Iwapo tarekh ni uwongo basi

hakuna lililo kweli. Kwani tarekh ni elimu na habari zilizopokelewa kutoka kwa watu wa

zamani - Mtume, Masahaba na wengineo.

1. Soma kitabu cha "Al Hassan Wal Hussein", kilichotungwa na Muhamad Ridhaa.

Imamu Hassan aliondoka katika Ukhalifa mwezi wa mfungo sita mwaka wa 41

Hijra. Yaani alikaa katika ukhalifa miezi sita tu. Imamu Hassan baada ya kujiuzulu na

Muawiya na rafiki zake wako katika mji wa KUFA. Amru Ibnul-Aas alimwambia

Muawiya: "Muamrishe Hassan ahutubu" kwanza akahutubu yeye Muawiya kisha

akamuamrisha Hassan ahutubu. Akainuka Hassan akamshukuru Mwenyezi Mungu kisha

akasema:-

Enyi watu! hakika Mwenyezi Mungu amewaongoza ninyi kwa mwanzo wetu

(Mtume (s.a.w.w.) babu yake). Akazuia damu (vita) yenu kwa mwisho wetu (ni yeye

Hassan) na kwa hakika lina jambo hili (khilafa) muda, na dunia ni mabadiliko (leo kwa

huyu kesho kwa yule). Mwenyezi Mungu aliyetukuka amemwambia Mtume wake: "Sijui

huenda hilo (Mlitakalo) likawa ni fitina kwenu na starehe mpaka muda maalum".

Alipomaliza kusema hivi Imamu Hassan, Muawiya alimwambia "keti"na

akamlaum Amri, sababu ndiye aliyemuashiria kusema. Na Imamu Hassan alikuwa

anataka kudhalilisha maovu yao ya kumpinga baba yake na yeye katika khilafa.

Imamu Hassan alikuwa haogopi kusema kweli mbele ya mtu yeyote, siku moja

walikusanyika watu wanne kwa Muawiya (mawaziri wake) nao ni:- Amru Ibnul Aas,

Walid bin Ukba, Utba bin Sufiyan na Mughaira bin Shuulba. Wakamwambia yeye na

baba yake (Ali) tumuonyeshe na kumkubalisha kuwa baba yake ndiye aliyemuuwa

Khalifa Uthman, wala hataweza kufanya lolote mbele yao.

Muawiya akakataa na akawaonya kuwa Hassan si mchache wa majibu wala

haogopi, lakini wasisikie, akaenda akaitwa akaja. Akasimama kila mtu katika wao mmoja

mmoja akamtukana Imamu Ali (naye hayuko duniani) hawakubakisha ubaya ila

walimbandika nao. Hata walipomaliza wote akainuka Imamu Hassan akawajibu kila mtu

akimpa lake la ubaya na tangu ukafiri wao ulivyokuwa wakati wakimpiga vita Mtume

(s.a.w.w.) wakati huo Imamu Ali ndiye aliyekuwa akimnusuru Mtume (s.a.w.w.) Imamu

Hassan akaendelea mpaka akawamaliza wote. Na alianza kumshambulia Muawiya

kwanza, na alipomshika Amru Ibnul As hayasemeki, sababu yeye ndiye aliyeanza na

aliyeyataka mambo yale.

Page 39: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

39

Alipomaliza Imamu Hasan akatoka na wao wameganda na kutosheka hawajui la

kufanya. Muawiya akawakasirikia sana na kuwasuta.

Imamu Hassan aliacha Khilafa kwa kutaka usalama na kuepukana na balaa za

hawa, lakini pia zisimtoke (Balaa zao) wakawa wanamtafuta kwa kila njia. Kisha Hassan

akaondoka Iraq akaenda zake Hijaz akakaa Madinah mpaka akafa huko.

MUAWIYA KUMRITHISHA MWANAWE YAZID UTAWALA

Imamu Hassan katika sharti alizompa Muawiya wakati alipomuachia Khilafa

alimshurutisha akifa amuachie yeye. Wakati walipokusanyika wajumbe wa kila nchi,

wakakusanyika Sham katika Dimishk (Damascus) Asima (Makao Makuu) ya Muawiya.

Na katika Waliohudhuria ni Ahnaf Bin Kais huyu ni mtu wa Iraq ambaye alikuwa pamoja

na Imamu Ali katika vita vya " SIFFIN".

Baada ya watu kuhudhuria, kwanza Muawiya alimwita Dhahhak Bin Kais

akamwambia. "Nitakapo maliza hutuba yangu, nitake ruhusa ya kusema, nitakapokupa.

Mshukuru Mungu kisha mtaje Yazid kwa vizuri na umsifu. Kisha unitake mimi

nimtawalishe (Khalifa) baada yangu: Kwani mimi nimefikiri na nimeona bora

kumtawalisha yeye. Kisha Muawiya akawaita watu wanne, akawaambia vile vile, ili

akisimama yule Dhahhak na wao watilie nguvu maneno yake ya kumtawalisha Yazid.

Alipomaliza Muawiya hutuba yake akainuka Dhahhak akatoa hutuba nzuri kabisa

ya kumsifu Yazid, na akamaliza maneno kama alivyo amrishwa. Na wale wengine wote

wakafanya vile vile. Akainuka Ahnaf Bin Kais akamuonya Muawiya kuwa watu wale

hawakumpa shauri nzuri (maskini hayajui yaliyopangwa). Na akasema kuwa si sawa,

wala watu wa Hijaz na Iraq hawaridhiki kumbai Yazid na ilhali Hassan yu hai bado.

Ukapita ushindani wa kujibizana muda mwingi na mtu ajibuye (kumtetea Hassan)

ni Ahnaf bin Kais peke yake. Basi yakaishia hapo hapo hakukuwa na jambo lolote.

Hata ulipofika mwaka wa 50 Hijra, Muawiya akaenda Madinah akawahudhurisha

Masahaba watukufu hao ni:-

Abdullah Bin Abasi, Bin Jaafar bin Abi Taalib, Abdullah bin Umar na Abdullah

bin Zubeir.

Walipo hudhuria, akatoa hutuba kwa kusema kuwa yeye amekuwa mtu mzima na

ajali yake imekurubia, na ameona bora kuwawekea wao Khalifa baada yake, mtoto wake

"Yazid" naye (Muawiya) akiturnai pia wao (kina Abdullah bin Abass) watakuwa radhi.

Kisha akasema: "Mrudishieni Amiril Muuminina kheri (Majibu mazuri) Mungu

atawarehemu".

Wote wale wanne wakamrudishia majibu Muawiya kila mtu kwa majibu yake

ambayo hayakumfurahisha Muawiya, kwani hakupata atakalo, wote walimkataa Yazid

Page 40: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

40

kuwa Khalifa kumtangulia Hassan na Hussein na wao pia ni vijana watukufu kuliko

Yazid.

Muawiya baada ya kupata majibu yao akakasirika na akasema: "Nimesema nanyi

mmesema, na mababa wameondoka wamebaki watoto. Mtoto wangu ni bora kuliko

watoto wao". Aliendelea kisha akasema: "Na hakika Mwenyezi Mungu amekutoa (katika

khilafa) wewe ibni Zubeir na wewe Ibn Umar ama hawa watoto wa Ami zangu wawili

hawa (Ibni Abas na ibni Jaafar) wamo katika rai yangu".

Haya ndiyo majibu ya Muawiya aliyo wajibu wale watoto wanne wa Masahaba,

Kisha Muawiya akasafiri akaenda zake Sham na kuzidi kufanya mashauri na watu wake

huko ili ambai Yazid kabla ya kufa yeye.

KIFO CHA IMAMU HASSAN

Imamu Hassan (R.A.) alikufa Madinah, siku ya Alhamisi, mwezi wa 7 wa mfungo

tano mwaka 49 Hijra 669 A.D. Baada ya kuishi miaka kumi katika ufalme wa Muawiya.

Aliyemuosha ni nduguye Hussein na nduguze Muhamad na Abas. Akazikwa BAKII

karibu na kaburi za wazee wake, Fatimah bint Rasul na Fatimah bint Asad (mama yake

na mamake babake) watu waliohudhuria katika mazishi yake ni wengi ajabu, hata

yasemekana kuwa hapo BAKII lau mtu angekuwa juu akaangusha sindano, basi

ingedondoka juu ya mtu.

Sababu ya kifo chake, Yazid alichelea baba yake asije akafa naye hajausia kupewa

yeye ukhalifa kisha ataushika Imamu Hassan. Yazid akapeleka salamu kwa mke wa

Hassan - Jaada bintul Ash-ath bin Kais Al-Kindy. Akamwambia kuwa ampe "Sumu”

Hassan kisha atamuowa yeye na atamjazi kwa 100,000 Dirham elfu mia, lakini wapi!

Haikuwa hivyo. Mke alimuua mumewe akakosa mwana na maji ya moto (Pesa na

kuolewa) na moto wamngojea Akhera.

Imamu Hassan alifahamu kuwa amepewa "Sumu" akamwita nduguye (Husein)

akamuusia akamwambia:-

Ewe ndugu yangu! Mimi nimepewa sumu mara tatu na sijaila mfano wa mara hii!:

Naona ini langu latoka", Hussein akamuuliza kuwa ni nani aliyekupa? Akajibu: "Wataka

kupigana naye? Wote njia yao ni kwa Mwenyezi Mungu (hawana pengine pa kwenda)"

kisha akasema Hassan:-

"Ewe Husein! Baba yetu Mungu amrehemu aliona jambo hili (la Khilafa) litakuwa

lake wakati alipokufa Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu akamuepushia!

limekwenda mpaka alipobaiwa yeye kisha akavuliwa (akapokonywa). Wallahi sioni mimi

kuwa Mwenyezi Mungu atakusanya kwetu sisi Ahlul Bait "Utume na Khilafa ". Basi

nakutahadharisha na masafihi wa KUFA (wasikucheze shere) nami niliomba kwa Aisha

(Ummul Muuminin) nikifa nizikwe nyumbani kwake (Pamoja na Babu yake s.a.w.w.) na

akakubali, lakini sioni ila watu watakukataza, basi wakikataa nizikeni BAKII.

Page 41: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

41

Maneno ya Imamu Hassan yalitimu kweli, alipokufa, Imamu Hussein alikwenda

kwa bibi Aisha akamwambia akakubali kwa furaha, lakini Marwan aliposikia akasema:

"Amesema uwongo (Hussein) na amesema uwongo (Aisha) Wallahi hazikwi huko

kabisa."

Imamu Hussein akataka kufanya vita, lakini kisha akakumbuka wasia wa nduguye.

Hii ndiyo kazi ya Banu Ummaya kuweza kumpa sumu mjukuu wa Mtume

(s.a.w.w.) kisha wakamkataza kuzikwa mahali pa babu yake! Mgala muuweni na haki

mumpe!

Imamu Hassan alikuwa mcha Mungu sana, amehiji hijja Ishirini. Alikuwa fasaha

sana kwa kusema, hutuba zake ni nyingi na ni nzito kuzitia katika kitabu hiki. Hii ni moja

katika hutuba zake baada ya kuuawa baba yake siku alipobaiwa msikitini aliinuka

akasema:

Mmelifanya hilo! Mmemuua Amiiril Muuminin. Wallahi ameuawa katika usiku

ulioteremshwa Qur-an (lailatul Qadr) na usiku ambao alikufa Nabii Mussa na

akarufaishwa Nabii Issa".

Kadhalika mithali yake ya Maneno ni nyingi, nitatia kidogo hapa:-

MISEMO YAKE

a) Uzuri wa suali (kuuliza) ni nusu ya Elimu.

b) Hapana adabu kwa asiyekuwa na akili.

c) Hapana haya kwa asiyekuwa na dini,

d) Mwenye kuanza Maneno kabla ya kutoa salamu msimjibu.

e) Maangamivu ya watu yako katika vitu vitatu:

"Kibri, Pupa na Hasadi". "Kibri" Ndiyo maangamivu ya dini na kwa hili

amelaaniwa "Iblisi" Na "Pupa" Ndiyo adui wa Roho, na kwa hili alitolewa Adamu

Peponi. Na Hasad" Ndio kiongozi wa mabaya: Na kwa hili Kaabil alimuua Haabil.

Hekima za maneno haya zatutosha tukizizingatia. Imamu Hassan alikuwa na

watoto kumi na moja:- (1) Zaid (2) Hasan (3) Qaasim (4) Abubakr (5) Abdullah. Hawa

waliuawa pamoja na Ami yao Imamu Hussein (6) Amru Ibnul Hassan (7) Abdurahman

(8) Husseinul Ashram (9) Muhamad (10) Yaakub (11) Ismail.

Tumeona Imamu Hassan amepata "Usuwa" wa baba yake: kwa kukosewa khilafa

na kuuawa. Sasa tumtazame Hussein atafanywa nini. Naye ndiye wa mwisho katika watu

wetu tuwatajao wa Ahlul Kisaa naye ni:-

IMAMU HUSSEIN

Hussein bin Ali bin Abi Talib bin Abdil Mutalib bin Hashim. Mama yake ni

Fatimah bint Rasulullah (s.a.w.w.). "Sibtu Rasulillah wa Raihaanatihi." Lakab zake ni:-

Sibtu - thani, Azzakiy, Ar-rashid, Attayib, Al-wafiy, Asayyid, al-Mubarak, na kun-ya

zake ni: Abdillah na Abu Shuhadaa.

www.allamahrizvi.com

Page 42: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

42

Alizaliwa Madina, siku ya Jumanne Mwezi nne Shabani, Mwaka wa nne 4 Hijra

yeye na nduguye ni mimba tu.

Mtume (s.a.w.w.) alimuakikia siku ya saba kwa mbuzi kama alivyofanya kwa

Hassan, Wengine wanasema waliakikiwa kwa kondoo wawili kila mtu.

Mtume (s.a.w.w.) alimuadhinia katika sikio lake na akamfunguza kinywa kwa mate

yake (s.a.w.w.) akamuombea Mungu, akamwita Hussein.

Imamu Hussein alikuwa mzuri kama ndugu yake, kadhalika alikuwa amefanana

sana na babu yake (s.a.w.w.) alikuwa mchaji Mungu, akipenda kufunga sana na amehiji

Hija 25 kwa miguu. Alikuwa karimu na mwingi wa kutoa sadaka. Kadhalika alikuwa

mwana chuoni na hodari wa kusema kwa ufasaha kama ndugu yake.

Ama ushujaa wake ni kama utakavyoona huko mbele: Katika vita wa Karbalaa.

Mapenzi ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na hadithi alizozisema juu ya Husen ni kama

nduguye Hassan, hapana haja ya kuzirejea tena lakini kwa Hussen ziko tena kidogo

ambazo ni zake tu, nazo ni hizi:-

Mtume (s.a.w.w.) Amesema: - Hussein ni katika Mimi, na Mimi ni katika

Hussein". Mwenyezi Mungu anampenda ampendaye Hussein "Mwenye kufurahika kwa

kutazama mtu katika watu wa peponi na amtazame Hussein."

Ewe Mola! mimi nampenda: Hussein nawe mpende” Haya ndiyo mapenzi ya

Mtume (s.a.w.w.) juu ya kijana huyu na nduguye, Hassan pia. Je kuwani hali gani kwa

wale wawachukiao watu hawa? Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kuwapenda namna hii kisha

akamuomba Mola wake pia awapende! Kinyume cha Mapenzi ni machukio. Na bila

shaka awachukiao hawa naye huchukiwa na Mtume (s.a.w.w.) na mwenye kuchukiwa na

Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu pia humchukia mtu huyu na achukiwaye na

Mwenyezi Mungu nyumba yake ni moto tu bila shaka”.

Ummu Salama, mke wa Mtume (s.a.w.w.) amesema: Mtume (s.a.w.w.) alikuwa

amelala nyumbani kwangu, akaja Hussein na huku anatambaa, mimi nikaketi mlangoni

na nikamzuia ili asije akaingia akamgutusha (Mtume). Kisha mimi nikaghafilika naye,

akatambaa mpaka akaenda akakaa juu ya tumbo la (babu yake) (s.a.w.w.) Mara nikasikia

sauti ya kilio cha Mtume (s.a.w.w.) nikaenda nikamwambia Ewe Mtume wa Mwenyezi

Mungu Sikujua Kama amekufikia akaniambia amekuja Jibril (a.s.) naye (Hussein) yuko

juu ya tumbo langu, akanambia:

"Wampenda huyo". Nikasema ndiyo akaniambia: Ummati (watu) wako watamuua.

Nikuonyeshe mchanga wa mahali atakapouliwa', Nikasema nionyeshe. Akapiga

ubawa wake, mara akaniletea (“mchanga huu”).

Ummu Salamah anasema “Mara nikaona mchanga katika mikono ya Mtume

(s.a.w.w.) naye akilia na huku akisema; "laiti namjua atakaye kuua baada yangu! Kisha

akasema:

Page 43: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

43

Ewe Ummu Salam Utakapogeuka mchanga huu ukawa damu. "damu" basi jua

kuwa mtoto wangu huyu ameuawa".

Ummu Salamah anasema: "Nikauchukua nikautia ndani ya chupa, hata siku

alipouawa Hussein nikautizama Umekuwa damu”? Nikauona umeshabadilika na kuwa

damu.

Imamu Hussein alikuwa na "karama" yeyote amwapizaye harudi salama, kama

tutakavyo soma katika vita vyake na kuuwa kwake.

HUSSEIN NA UKHALIFA

Tumesoma nyuma kuwa Muawiya alikuwa na hamu ya kumpa Ukhalifa mtoto

wake, Yazid, na akafanya kila namna ya hila na ilhali ameandikiana yeye na Irnamu

Hassan, ili akifa yeye (Muawiya) ashike Hassan. Na aliivunja ahadi hiyo, Hata alipokufa

Imamu Hassan kwa siku kidogo tu akamtawalisha Yazid. Na akaamrisha Maliwali wake

katika kila jimbo wachukue "baia" (ahadi) kwa watu.

Ama watu wa Madina wengi walikataa, na katika waliokataa wazi kabisa ni

Abdullah bin Zubair na Banu Hashim hata mmoja hakuna aliyembai Yazid.

Baada ya kufa Muawiya, Yazid alimtawalisha Ubeidullah bin Ziyad, Basra na

Nuuman bin Bashir, Kufa, na Walid bin Utba, Madinah, na Amri bin Saidi Ibnil-As,

Makkah.

Yazid alipotulia katika khilafa katika mwaka wa sitini, alimuandikia barua Walid

bin Utba, liwali wake aliyekuwa Madinah. Alimuarifu kuwa achukue baia kwa watu wa

Madinah na hasa kwa Hussein na Abdullah Ibnu Zubeir.

Walid alipopata barua hiyo alimshauri Marwan, naye akamwambia kuwa awaite

Hussein na Ibnu Zubeir usiku ule ule wapate kubai kabla ya watu: Sababu wao ndio

wakubwa wa nchi ya Madinah kwa wakati ule na baba zao ndio walikuwa wakubwa wa

Masahaba.

Imamu Hussein alipoendewa kuitwa usiku ule akatoka kwa kujifunga na kujiweka

tayari kwa vita vikitokea, Akatoka Imamu Hussein mpaka kwa Walid bin Utba akamkuta

amekaa na Marwan.

Hapo tena Walid akamsomea barua itokayo kwa Yazid. Imamu Hussein akamjibu

kuwa: Mfano wake yeye hafai kubai kwa siri, lakini watakapoitwa watu na ikatangazwa

bai ya Yazid hapo naye atabai.

Walid akamwambia: Basi nenda zako kwa jina la Mwenyezi Mungu mpaka

nitakapo ita Mkutano."

Page 44: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

44

Marwan akakasirika, akamwambia Walid: Akienda zake huyu saa hii tuliyonayo

humpati tena mpaka kwa vita: basi mzuie asiende mpaka abai au mkate shingo yake

akikataa kubai".

Imamu Hussein aliposikia maneno ya Marwan, aliruka na kumwambia:- Ee! Ni

wewe mwenye kuniua mimi au ni yeye? Wallahi Umesema Uwongo huthubutu tena

umepata madhambi (kwa neno hilo).

Akatoka Hussein akawapitia watu wake waliokuwa wakimngoja wakaenda zao

nyumbani, Na huku nyuma wale watu wawili (Walid na Marwan) wakawa

wanalaumiana.

Ama Ibni Zubeir hakuenda kwa Walid alitoa udhuru kuwa atakwenda asubuhi.

Akajifunga usiku ule ule akatoka akaenda zake Makkah.

Imamu Hussein naye usiku wa pili akatoka yeye na watu wake wote ila

Muhamadul-Hanafiya (Nduguye kwa baba) yeye hakuwahi kumfuata. akatoka Hussein

akaenda Makkah na ulikuwa ni mwezi wa Rajab, mwaka wa Sitini.

Imamu-Hussein alipofika Makkah, Wale Mashia wa babake (watu waliomnusuru

Imamu ALI) walioko Kufa (Iraq) walikutana wote wakamuandikia barua Hussein

kumuarifu kuwa aende Alkufa wapate kumbai, awe ndiye Khalifa wao. Na wakamuarifu

kuwa wao hawamtaki Yazid wala hawambai yule liwali wake aliyoko huko na Kufa,

naye alikuwa ni Numan bin Bashir. Baada ya siku mbili, wakampelekea tena. Imamu

Hussein barua ipatayo kurasa 150 kumhimiza aende haraka.

Wakampelekea tena mara ya tatu. Hata zilipokuwa nyingi barua zao za kumwita ili

aende Kufa: huko mji wa Iraq, hapo tena Hussein akawajibu barua isemayo hivi :-

Amma baadu: Nimefahamu yote mliyo niarifu. Na nimewaletea ndugu yangu na

(ambaye) ni mtoto wa Ami yangu na ni muaminifu katika watu wangu, Muslim bin Akil

na nimemuamrisha aniarifu mimi hali yenu na mambo yenu. Basi yeye atakapo niarifu

kuwa maoni yenu yamewafikiana na shauri lenu lirnekuwa moja kama ilivyokuwa katika

barua zenu mlizo niletea, basi mimi niko njiani naja haraka apendapo Mwenyezi Mungu.

Naapa kwa Umri wangu hafai kuwa Imamu (Mkubwa wa Umma au Khalifa) ila

aitumiaye Qur-an na kufanya uadilifu na kuifuata dini ya haki, Wassalaam.

Kisha Imamu Hussein akamwita Muslim bin Akil bin Abi Talib, Mtoto wa Ami

yake, akamfungia safari ya kwenda huko Al-kufa, na akamuamrisha pamoja na kumuusia

kumcha Mwenyezi Mungu na kwenda na watu kwa upole.

Akatoka Bwana Muslim bin Akil kuelekea Al kufa, hata alipofika wakawa Mashia

(watu wampendao Hussein) wamekusanyika na kusikiliza amri yake, liwali wa mji ule

Numan bin Bashir akapata habari ya yule mjumbe wa Hussein, Muslim bin Akil.

Page 45: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

45

Nuuman akawahutubia watu kuwaonya kuwa wasimkhalifu wala yeye hana vita

nao, lakini watakapomkhalifu na wakayasikiliza maneno ya Muslim bin Akil kuwa

asitiiwe Yazid atiiwe Hussein basi hapo atawachinja kwa upanga wake.

Haya ndiyo maneno ya Nuuman bin Bashir, naye alikuwa Sahaba, na alikuwa

liwali wa mji wa Al Kufa tangu wakati wa Sayyidna Uthman mpaka wakati ule wa

Yazid. Lakini kwa wakati ule wa utesi wa Hussein na Yazid na siasa ilivyokuwa kwa

Banu Umayya, na kwa ile hutuba yake haikuonyesha ukali na kumshambulia haraka

Muslim bin Akil, likampa Yazid kumuuzulu Nuuman na kumuweka Ubeidullah bin

Ziyad awe Liwali wa Al kufa na Basra.

Ibnu Ziyad alipofika Al kufa, alitoa hatuba kali yenye vitisho kuwatisha wale

wenye kuasi amri yake kutomkubali khalifa wao (Yazid) na atakaye sikiliza maneno yake

akamfuata, basi atakuwa katika amani. Na aliwatisha zaidi wale wakubwa na wazee wa

mji na akawapa tamaa kubwa kama ilivyo destruri ya wafalme wabaya au serikali mbaya

ikitaka kuharibu mila, dini na desturi za watu.

Kabla hatujaendelea mbele kutaja habari za mji wa Al-kufa, bora tutaje habari ya

huyu Ibnu Ziyad na Yazid, Ubaidullah Ibnu Ziyad bin Abi Sufiyani, yaani yeye na Yazid

ni ndugu kwa Ibni Ami, lakini tarehe nyingi, zinasema kuwa huyu Ziyad si mtoto wa Abu

Sufiyan, yaani ni Mwana haram" na aliyemfanya mwana halali ni Muawiya,

alimlahikisha na baba yake hapo tena akawa ni nduguye Muawiya. Mwenye kitabu cha

"Jawaahiral Adal" Juzuu ya pili anasema.:-

"Harith bin Kalda Athakafi tabibu wa Waarabu alikuwa na kijakazi akiitwa

"Sumayyah" akamfungisha urafiki na mtumwa wake aitwaye Abid, Sumayyah akapata

naye kijana naye ni huyu Ziyad.

Akawa kijana hodari shujaa. Imamu Ali wakati wa Khilafa yake alipata taabu kwa

watu wa Fursi, akamfanya Ziyad Amiri wa huko, hapo Fursi ikatulia, Hata alipo uawa

Imamu Ali, Muawiya akaogopa huyu Ziyad asije akaghiribu. Akamtuma Mushera bin

Shuuba akamwita akamfanya ni nduguye, akamlahikisha na nasabu ya baba yake akawa

anaitwa Ziyad bin Abid au (bin Sumayya au Ibnu Abid).

Yazid alikuwa mlevi, mzinifu tena mutribu kwa kuimba na kupiga vinanda kazi

yake ni kustarehe na wanawake na kuwinda tu, hizo ndizo shughuli zake.

Ama Ibni Ziyad alikuwa dhalimu zaidi kuliko Yazid. Sababu alipofika katika mji

wa Al kufa ni kama nilivyoeleza ujeuri alioufanya kwa watu na akawaua watu kadha wa

kadha, Miongoni mwa aliowaua ni Kais bin Mus-hir, Mjumbe aliyekwenda na barua ya

Imamu Hussein kuipeleka kwa watu wa Al kufa.

Ibnu Ziyad alimuamrisha huyu Kais apande Mimbari amtukane na amlani Imamu

Hussein. Alimwambia: "Mtukane muongo mtoto wa muongo". Akapanda Mimbari

akamsifu Hussein na akamlani Ibni Ziyad. Alipomaliza maneno yake. Ibni ziyad

akaamrishwa apandishwe juu ya ghorofa na akatupwa toka juu mpaka chini akafa.

Page 46: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

46

Muslim bin Akil alipofika mji wa Al-Kufa aliteremkia katika nyumba ya Mukhtari,

na mwanzo watu walimsikiliza kama tulivyosoma nyuma. Kisha alipo uzuliwa Nuuman

akawekwa Ibni Ziyad, na huyu Ibni Ziyad alipoingia mji wa Al kufa alijibadilisha, watu

wakawa hawamtambui wakaona ni Imamu Hussein, kwa kujua kwao kuwa yuko njiani

anakuja. Basi wakafikiri ni yeye, ikawa kila amuonaye anampa heshima ya mjukuu wa

Mtume (s.a.w.w.).

Ibni Ziyad akafanya hila hata akajua kuwa Muslim bin Akil yuko kwa Mukhtar.

akaanza tena hila zake za kuwatisha watu na kuwadanganya. Hata watu wote

wakamuepuka Muslim, asibakiwe na watu ila kidogo tu, Muslim, bin Akil akatoka kwa

Mukhtar akaenda kwa Haniy bin Arwa Al-Murady, Ibnu Ziyad akapata habari kuwa Ibni

Akil yuko huko.

Na huku nyumbani kwa Arwa alikuweko mtu katika Mashia (wampendao Hussein)

jina lake Sharik bin Aawar, naye alikuwa mgonjwa Ibni Ziyad akapeleka Salam kuwa

anakuja kumtazama mgonjwa. Sharik akamwambia Muslim bin Akil," Akija huyu

muuwe", kwani hii ni nafasi nzuri.

Lakini mwenye nyumba akakataa akasema: Sipendi auawe nyumbani kwangu.

Basi akaenda Ibni Ziyad akatoka salama na lau si yule Hani, mambo yangekwisha.

Ibni Ziyad kisha akajua kuwa Ibni Akil yuko kwa Hani, akampelekea Salam Hani aende

kwake. Hani akakataa lakini kisha akaenda. Alipofika, Ibni Ziyad akamwambia Hani

kuwa: amemchukua Muslim amemficha kwake. Hani akamwambia kuwa "Sikumficha

lakini alikuja akataka mahali nikamkaribisha". Ibni Ziyad akamtaka Hani amlete Muslim

kwake. Hani akajibu "Sitakuletea mgeni wangu ukamuuwe, kabisa hilo sitafanya.

Ibni Ziyad akaamrisha watu wamshike Hani wrampeleke mbele yake akashikwa

Hani na kupelekwa mbele yake akampiga kwa fito katika pua mpaka akamtoa damu na

fito ikavunjika.

Kisha Ibni Ziyad akaamrisha Hani afungwe.

Alipofungwa wakaja watu wake wakaizunguka nyumba, sababu walisikia kuwa

ameuawa, akatoka kadhi jina lake Shuraih akawatuliza watu wake akawaambia kuwa

hakuuawa. Wakaenda zao.

Bwana Muslim bin Akil akapata habari ile akawaita watu wake wote na wakawa

kitu kimoja wakaizunguka nyumba ya Ibni Ziyad naye yumo ndani na hana watu ila

thelathin tu. Akawa hana la kufanya mpaka ilipofika jioni wakawa wakubwa wanakuja

kumtazama kwa mlango wa nyuma.

Basi tena akawapanga wakubwa hao mpaka wakapangika, wakatoka wakiwatia

watu maneno na kuwatisha na kuwavunja vunja kwa pesa mpaka watu wakawa

wanamkimbia Muslim bin Akil, akawa hakubakiwa na watu ila thelathini tu.

Page 47: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

47

Hii ndiyo hali iliyofikia kwa watu wa al Kufa. Hii ndiyo kazi ya wanafiki, ndiyo

ahadi ya watu wa Iraq waliyompa Imamu Hussein na mjumbe wake!

Lakini si ajabu, haya waliyaanza kwa Imamu Ali na Hassan na sasa wanayamalizia

kwa Hussein.

KIFO CHA MUSLIM BIN AKIL

NA

HAANI BIN ARWAH

Bw. Muslim bin Akil alipoona hali ile iliyomfika kwa watu wake, akawa hajui la

kufanya. Akaenda mpaka kwenye nyumba ya Mwanamke wa kabila ya Kindly aitwaye

Twau-a Bibi huyu akamkaribisha vizuri na akamsaidia kwa kila alitakalo. Lakini wapi!

Majasusi walishapeleka habari kwa Bwana wao!

Ikazungukwa nyumba ya bibi yule, akatoka Muslim na upanga wake kujitetea,

lakini ataweza wapi mamia ya watu. Katika watu wa Ibni Ziyad waliokwenda kumshika,

mmoja wao ni Muhamad ibnil Ash-ath. Huyu alimpa Aman Ibnil Akil asiuawe pale,

wakamchukua mpaka kwa Ibni Ziyad, akaamrisha apandishwe juu ya ghorofa akatwe

kichwa.

Akadenguliwa kichwa kiwiliwili kikaviringika mpaka chini! na yule rafiki yake

ambaye alikuwa amefungwa Haaniy bin Arwah, akauawa. Viwiliwili vyao wote wawili

vikatundikwa!!

HUSSEIN AIHAMA MAKKAH

Kama tulivyosoma nyuma kuwa Imamu Hussein alimpeleka Muslim bin Akil kule

Al-Kufa ili akisha baiwa na watu wa huko na akipata barua yake naye ataondoka

Makkah.

Hussein akapata barua ya Ibnil Akil kuwa watu wamembai naye aende haraka.

Imamu Hussein naye akawaita na watu wake ili aende nao pamoja huko Iraq. Safari

hii haikuwapendeza watu wa Makkah wala wa Madinah, wakawa watu wengi wamsihi

Hussein asiondoke, jamaa zake na wasiokuwa jamaa zake. Hata mwisho Abduilah Ibni

Abass alimwambia:-

"Ikiwa huna budi na kwenda, basi usiende na wake zako na watoto wako. Wallahi

mimi nakuchelea usije ukauawa kama alivyo uawa uthman na watoto wake na wake zake

wanamtazama.

Wallahi umemfurahisha Ibni Zubeir kwa kumuachia Hijaz peke yake "Faragha ni

yake Sasa" Naapa kwa ambaye hapana Mola ila "Yeye"! Lau nashika nywele na upara

wako wa kichwa, utanisikiliza, basi ningefanya hilo".

Page 48: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

48

Hii ndiyo nasaha ya Ami yake lakini wapi! Hukumu ya Mwenyezi Mungu yataka

kupata, "Ajali haina kinga" Imamu Hussein akaona si sawa kuvunja ahadi, tena hasa kwa

kuwa amepata ukweli ile barua yake Ibnul Akil ya kumwita. Bali na yeyote mwenye

moyo safi na nia nzuri kwa umma wake ni lazima awasikilize kwa walitakalo. Kwa hiyo

ni lazima Imamu Hussein aondoke Makkah kwenda Al kufa-Iraq.

Imamu Hussein akatoa Makkah na watu wapatao 70, thelathini wenye farasi na

arobaini wa miguu. alipokuwa njiani akienda wakaongezeka watu wakafika 150.

Hata walipofika kitongoji kimoja kiitwacho Tha-alabiya, akapata habari ya kifo cha

Muslim bin Akil, na akaambiwa kuwa hana haja ya kwenda, akakubali kurudi, lakini

wale ndugu za Ibnul-Akil wakakataa mpaka nao waende wakafe.

Hapo tena Imamu Hussein akawaambia watu wake kuwa yeye hana dhamana ya

mtu yeyote, sababu watu wao huko Al-kufa wamewacheza shere, basi atakayekwenda

zake aende. Wale watu walio mkuta njiani wakenda zao akabakiwa na wale wale 70

aliotoka nao Makkah, mbali ya wanawake na watoto wadogo.

KARBALA

Katika safari yake Imamu Hussein alipambana na mjumbe wa Ibnul Ziyad aitwaye

Hur bin Yazid Attamimy, aliyeletwa kumzuia Hussein asifike Al kufa. Huyu Hur

alimuuliza Imamu Hussein jambo linalo mpeleka kule Iraq, akamjibu kuwa ni barua zao

za kumuita. Hur akastaajabu na akasema kuwa wao hawazijui barua hizo! Imamu

Hussein akamwambia "Mwaziandika barua kisha mnazikana!"

Imamu Hussein akataka kwenda zake lakini Hur akamkataza akamwambia.

Nimeambiwa na Amir Ibnu Ziyad nisikuache mpaka nikupeleke mbele yake". Hussein

akakataa kumfuata. Kisha Hur akamwambia asiondoke mpaka apeleke barua kwa Ibnu

Ziyad kunishauri Akaletewa barua na Ibnu Ziyad kuwa asimuache Hussein, wala

asimuweke mahali penye maji hapo tena Imamu Hussein akapelekwa mpaka "Karbala".

Karbala ni mahali katika Iraq karibu na mto wa Furat, lakini mto huo ulizungukwa

na jeshi la maadui wa Hussein ili asipate kunywa maji hayo, yeye wala watoto wake na

watu wake wote, Imamu Hussein akipiga kambi hapo akawa hana ruhusa ya kwenda

popote wala kuteka maji. Maji ya Mto yanywewayo na mbuzi, kondoo na mbwa:

anakatazwa Hussein na watu wake kunywa.

Jeshi hilo lililowekwa Karbala kumzuia Imamu Hussein Amir wake (General)

alikuwa ni Umar bin Saad Bin Abi Wakas ambaye baba yake alikuwa Sahaba mkubwa

katika masahaba.

Umar bin Saad kwanza alitumia upole kwa Imamu Hussein lakini yuko "Kabithi"

mmoja aitwaye Shamri bin Dhil-Jaushan akapeleka fitina kwa Ibnu Ziyad kuwa Umar

anambembeleza Hussein, ndipo Ibni Ziyad akamtuma yeye Shamri amwambie Umar bin

Page 49: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

49

Saad kuwa amlazimishe Hussein mpaka aende akasalimu amri kwake, laa si hivyo, basi

asimpe hata tone la maji na amuuwe ampelekee kichwa.

Asipofanya hivyo Umar, basi ameuzuliwa na badala yake ni Shamri.

Ujumbe huu ulipofika kwa Umar bin Saad ndipo alipotimiza amri ya Bwana wake,

japo si sawa na si haki, kwake ilikuwa bora kutii ya Ibni Ziyad na akamuasi Mola wake!

Imamu Hussein alikatazwa maji naye amechukua wanawake na watoto wake, na

katika watoto wake, mmoja alikuwa mgonjwa, naye aliitwa Ali (Aliyul Ausat). Mtoto

huyu akawa anaugua na kiu ya maji imemshika, hala machozi ya kilio cha Zainabu bint

Ali, Shangazi wa Mtoto huyu, yakawa ndiyo maji yake sababu wao walizuiliwa maji siku

tatu.

Hii ndiyo hali ya watu wa Iraq kuzuilia Waislamu maji, hata makafiri wakati wa

Jihad hawakuzuiliwa.

ASHURA

Hata siku ile ya tatu mwezi tisa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa Imamu Hussein

aliingia katika hema na akawakusanya watu wake wote akawatolea hotuba akawaambia:-

"Namsifu Mwenyezi Mungu uzuri wa Sifa, Namshukuru Yeye katika furaha na

taabu. Ewe Mola, nakushukuru kwa kututukuza sisi kwa Utume, na ukatufundisha sisi

Qur-an, na ukatufahamisha Elimu ya Dini, na ukatupa masikio (ya kusikia dini yako), na

Macho na nyoyo (za kuona haki): basi tujaalie sisi tuwe wenye kushukuru. Amma baadu.

Hakika yangu! Sijui marafiki watimizao "Ahadi" na waliobora kuliko rafiki zangu, wala

watu walio bora wazuri kuliko watu wangu (Ahlu Bait).

Mwenyezi Mungu atawalipa kheri, Basi fahamuni jueni! Nimewapa ruhusa nendeni

zenu nyote- hamna lawama kwangu (mkiuawa). Usiku huu umewafunika hamtaonekana,

basi shikeni njia mwende zenu".

Watu wa Imamu Hussein wote kwa umoja wao wakamwambia: "Kwa nini tufanye

hivyo sisi! Tubakie baada yako (tusife nawe?)! Mungu asituonyeshe hilo kabisa”!

Kisha Imamu Hussein akawaelekea watoto wa Ami yake akasema: Enyi watoto wa

Akil! yawatosha nyinyi kwa kifo cha Muslim (bin Akil) nendeni zenu nimewapa ruhusa.

Wakamjibu kwa Umoja wao:

"SUB- HANALLAH! Watasema nini watu, Watasema sisi tumemuacha shekhe

wetu na bwana wetu na watoto wa Maami tu ambao ni bora wa maami, wala

hatukuwatilia vyembe wala hatukupiga mapanga pamoja nao (kuwasaidia kupigana wala

tusijue wao wamefanywa nini? La! Wallahi kabisa hatutafanya hilo, lakini tutakukomboa

kwa roho zetu na mali zetu, na tupigane pamoja nawe. Mwenyezi Mungu afanye mabaya

maisha baada yako!

Page 50: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

50

Basi tena wakaendelea kwa maneno namna hii muda mrefu, kisha Imamu Hussein

akawashukuru, kisha kila mmoja akaenda mahala pake akalala.

Imamu Hussein akakaa mahala peke yake na usiku ukizidi kwenda akawa anauaga

usiku ule kwa nyimbo za kusikitisha na kuhuzunisha, kwani ndio usiku wake wa mwisho.

Zainab bint Ali, Ukhuti wake akaisikia sauti ya ndugu yake, akaenda akasema naye

na huku akilia. Hussein akamwambia:

Ewe ukhuti wangu we! Mche Mungu na uhuzunike kwa ajili yake (kwa ajili ya

dini), tena ujuwe, fahamu! walimwengu wote watakufa, wa mbinguni ndio watakaobakia,

na kila kitu kitaondoka na kuhiliki ila Mwenyezi Mungu peke yake, babu yangu ni bora

kuliko mimi, na mama yangu ni bora kuliko mimi na ndugu yangu ni bora kuliko mimi

(nao wote wamekufa). Na kila Mwislamu wa kweli ana kiigizo kizuri kwa Mtume

(s.a.w.w.).

HOTUBA YA MWISHO YA HUSSEIN

Imamu Hussein hakulala usiku ule, yeye wala watu wake, walikesha kwa kusali na

kuomba Mungu. Hata asubuhi akainuka Hussein akawapanga watu wake hao 70, kisha

akapanda farasi wake akawakabili wale maadui zake akawaita kwa sauti kubwa.

"Enyi watu wa Iraq" Wakamsikia watu wengi, wakangojea atakalo sema, Hussein

akawambia:-

Enyi watu nyie! Sikilizeni maneno yangu, wala msifanye haraka kwanza mpaka

niwape waadhi kwa ambalo ni wajibu wangu kuwapa.

Amma baadu: Ninasibisheni na mnitazame mimi ni nani? Kisha mzirejee nafsi

zenu mzilaumu. Zidini kufikiri yafaa kwenu kuniua mimi na kuvunja heshima yangu?

Siye mimi mtoto wa binti ya Mtume wenu (s.a.w.w.)? Na mtoto wa Wasiy wake na Ibni

Ami yake, na aliyemuamini kwanza Mtume (s.a.w.w.)?

Hakuwa Hamza. Bwana wa "Mashahidi" ni Ami yangu? Hakuwa Jaafar Attayar

aliyeko Peponi ni Ami yangu? Hamkusikia neno la Mtume (s.a.w.w.) alilosema kwa ajili

yangu na ndugu yangu (Hassan): "Hawa wawili ni Mabwana wa watu wa Peponi."

Basi mkinisadiki hilo nawaambia ni kweli. Wallahi sikuzoea kusema Uwongo! Na

mkinifanya mimi ni muongo basi wako ambao mkiwauliza watawaambia (kuwa Mtume

alisema kwa ajili yangu na ndugu yangu). Ikiwa mna shaka ya hilo lakini hamna shaka

kuwa mimi ni mtoto wa binti ya Mtume wenu.

Naapa kwa Mungu! Hapana kati ya Mashariki na Magharibi kijana wa binti ya

Mtume yeyote hivi sasa asiyekuwa mimi kwenu wala kwa wengine.

Page 51: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

51

Mateso ni yenu! Lo! Mwataka kwangu kisasi cha mtu wenu niliye Muuwa!? Au

mali yenu niliyo ipoteza? Au kisasi cha kidonda ambacho nimemtia mtu?"

Watu wa Iraq wakawa hawana la kusema: Wakajibu: Hatufahamu unayoyasema".

Kisha Imamu Hussein akamuona Hur-bin Yazid Attimimy akija mbele yake, Hur

akaenda mpaka kwa Hussein akatupa Silaha akamwambia:- Natubia kwa dhambi zangu

nilizozifanya.

Basi sasa niko pamoja na wewe kuwapinga maadui zako. “Je nimepata msamaha"?

Hussein akajibu "umepata".

Huyu ni yule aliyemzuia Imamu Hussein njiani akampeleka mpaka hapo Karbala.

Hur kisha aliwaelekea watu akawaambia:-

Enyi watu wa Al-Kufa! Wana kushukiwa huzuni nyingi na mkawakosa mama

zenu! Mmemwita huyu Bwana aliye mwema hata alipowajia mwamsalimisha kwa adui

yake? Na mlidai kuwa mtamnusuru na kumsaidia, sasa mwampiga vita na kutaka

kumuua? Mmezuilia njia amekuwa hana pa kwenda na mmemzuilia maji yeye na wake

zake na watoto wachanga? Maji ya mto wa Furat yanywewayo na Mayahudi na Majusi

na kuvurugwa na Nguruwe na Mbwa'?

Basi hao ndio watoto wao wameshikwa na kiu. Ni uovu ulioje, muufanyao kwa

kizazi cha Mtume! Mwenyezi Mungu asiwaonyeshe tone la maji siku hiyo ya kiu!”

Haya ndiyo maneno ya Hur-aliwaambia watu wa Al kufa, na hayakufaa lolote, bali

walizidi ushupavu na mara walianza wao vita.

WAKATI WA VITA

Maadui wa Imamu Hussein ndio walioanza vita, na aliyeanza kutupa mshale ni

Umar bin Saad bin Abi Waqas amiri wa jeshi la Ibnu Ziyad, ambalo jeshi hilo

halikupungua watu 4,000 (Elfu nne) wakapambana na jeshi la Hussein ambalo halikuzidi

watu 72 (Sabini nambili).

Vikaendelea vita kitambo kidogo yule Hur maskini akauawa. Panga zikawa

zafanya kazi pamoja na mishale, mpaka watu wa Hussein wote wakauawa wakabaki wale

ndugu na watoto tu. Hata kitambo kidogo mara na yule Aliyul-Akbar, Mtoto Mkubwa wa

Imamu Hussein akauawa, Umri wake ulikuwa miaka kumi na tisa.

Huyu ndiye mtoto mkubwa wa Imamu Hussein naye amekwisha kufa na baada ya

muda kidogo yule mtoto wa Hussein aliyemchanga aitwaye Aliyul Asghar, kiu ilimzidi

akaletwa kwa baba yake. Hussein akamchukua akaenda naye mpaka mbele ya maadui

kumuombea maji akawaambia:-

Enyi watu wa Al kufa! Muogopeni Mwenyezi Mungu na Mpeni maji huyu kijana,

ikiwa mimi katika maoni yenu ninamakosa - basi je kitoto hiki kichanga kina makosa

gani? Enyi watu nyie! Mcheni Mungu na mkumbuke adhabu iliyokali.

Page 52: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

52

Mtu mmoja katika wale maadui alitupa chembe juu ya mtoto na huku akisema:

Twa mnywesha!"

Baadala ya maji akatupiwa chembe, kikamuingia mtoto akafa palepale!!

KIFO CHA IMAMU HUSSEIN

Baada ya kuuawa kitoto kile, Imamu Hussein hakujifahamu tena, akawa

yuwapigana na watu wake wote wanauawa ila kidogo sana. Akapigana mpaka akabakiwa

na watu wawili tu, na haukupita muda na wale wawili nao wakamalizwa, sasa amebaki

peke yake.

Lau twaeleza ushujaa wake aliokuwa nao yeye na watu wake, basi wasomaji

wangeona ajabu, lakini kitazidi kuwa kirefu kitabu chetu.

Hussein alibaki kupigana peke yake na wale maadui wampigao kwa mapanga na

vyembe waliogopa kumsonga vizuri kila mmoja anakwenda anampiga na anarudi nyuma.

Kisha akaenda yule adui mkubwa Shamri bin Dhil-Jaushan, akawaambia watu:

"Mnangojea nini tena hamumuui huyu!"

Hapo hapo akapigwa panga akakatwa mkono wa kushoto kisha na wa kulia pia

hapo tena akaanguka akawa hana fahamu tena. Likaenda lile adui likamkata kichwa

Imamu Hussein! Allah Akbar!

Shimri akakichukua kichwa akampa mtu akamwambia: Kipeleke kwa Amir Umar

bin Saad". Aliuawa Imamu Hussein siku ya Ijumaa Mwezi kumi 10 (Ashura) Mfungo

nne, mwaka wa 61, Hijra.10 October, 680 C.E. (Christian Era) katika mahali hapo

paitwapo Karbala katika nchi ya Iraq.

Baada ya kuuawa Hussein usiulize hali walivyokuwa wanawake kwa vilio na

mgandano. Mtu yeyote akimuona maiti hutishika na huhuzunika, Je ikiwa maiti yule ni

wako, tena ameuawa hali hiyo. Kwani Hussein kifo chake kilikuwa hakijawahi kutokea

katika Tarekh. Mwili wake wote ulipatikana na alama za panga na mishale isiyo pungua

67, na mbali ya kukatwa mikono, isitoshe na kichwa kikakatwa.

Isitoshe maadui waliwaendea wanawake katika mahema yao, wengine walikosa

adabu wakataka kuwashika kama nyara! Allahu Akbaru! Banati za Mtume (s.a.w.w.)

wakataka kuwachukua nyara. Lakini wanawake waliwakaripia kwa kuwatahayarisha

wakatahari wakawaacha, lakini walichukua nyara vitu vyao.

Umar bin Saad akaenda akawakataza, lakini wengine hawakusikia walichukua.

Kisha wanawake pamoja na vile vichwa vya maiti waliouawa pamoja na kichwa cha

Imamu Hussein vikapelekwa Al-Kufa kwa Ibni Ziyad.

Kichwa cha Imamu Hussein kilipofika kwa Ibni Ziyad alikiweka akachukua fito

akawa anakichezea na kuyapiga meno ya Hussein kwa fito yake. Mahali hapo alikuwepo

Page 53: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

53

yule sahaba Mtukufu rafiki yake Mtume (s.a.w.w.) aitwaye Zaid bin Arkam alipomuona

akichezea kichwa Zaid bin Arkam, akamwambia Ibn Ziyad: Ondoa ufito wako katika

midomo ya huyu (Hussein) Naapa kwa Mungu ambaye hapana Mola ila yeye! Niliona

midomo ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya midomo ya huyu.”

Baada ya kusema hivi akawa analia huyu Mzee, Ibni Ziyad akamwambia: "Mungu

akulize! Walia kwa Fat-hi (Ushindi) wa Mungu? Lau Si utu uzima wako na kuwa huna

akili tena ningeikata shingo yako".

Haya ndiyo majibu ya huyu "Mal-un” Ibni ziyad juu ya rafiki wa Mtume (s.a.w.w.)

na vitendo vibaya juu ya Ahlul Bait Rasulillah”.

Isitoshe, Wakati walipoletwa wanawake, Ukhti wa Imamu Hussein na Banati zake,

yule bibi Zainabu Bint Ali, alikuwa amejibadilisha na amevaa nguo mbaya ili

asitambulikane. Akaingia Bibi Zanaibu kwa Ibni Ziyad pamoja na wanawake wengine

(wenzake) kama mateka! Ibni Ziyad alipomuona hali ile asimtambue akauliza: "Nani

huyu aliyejifunika?” Zainabu asimjibu. Akauliza mara tatu na Zainabu hakumjibu.

Mmoja katika vijakazi akasema: “Huyu ni Zainabu binti Fatimah bint Rasulillah."

Akainuka Ibni Ziyad akamuelekea Zainabu na huku "Kila Sifa njema ni za

Mwenyezi Mungu ambaye amewakashifu na kuwauwa na akawakadhibisha vitendo

vyenu!"

Zainabu akamjibu "Kila sifa njema ni za ambaye ametutukuza kwa Mtume wake

Muhamad (s.a.w.w.), Akatutakasa sisi na uchafu…

Hakika Mwenyezi Mungu humkashifu mtu fasiki (mchafu) na humkadhibisha mtu

mbaya naye huyo (mbaya) si katika sisi".

Ibni Ziyad akamwambia: "Umeonaje alivyofanya Mwenyezi juu ya watu wako?”

Zainabu akamjibu: "Mwenyezi Mungu amewaandikia mauti na wamejilalia katika

malazi yao, na atawakusanya Mwenyezi Mungu wewe na wao siku ya kiyama, na

watamshitakia uliyoyafanya."

Ibni Ziyad akakasirika kwa maneno yale, lakini wale waliokuwepo pale

wakamtuliza, kwani pia si ajabu angemuuwa Mwanamke.

Kisha Ibni Ziyad akamuona yule Ali Bin Hussein, ajulikanaye kwa jina la Aliyul-

Ausat na Zainul Abidiin, ambaye alikuwa mgonjwa.

Ibni Ziyad akasema; "Mwenyezi Mungu hajamuuwa tu Ali Bin Hussein?!” yule

mtoto akamjibu; "Nilikuwa na ndugu yangu aliitwa Ali (Aliyul- Asghar) Watu

wamemuuwa". Ibni Ziyad akasema:

“Aliyemuuwa ni Mungu (si watu) Ali akamjibu: Kwa aya ya Qur’ani isemayo hivi

maana yake:

Page 54: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

54

“Mwenyezi Mungu hufisha nafsi (roho) wakati wa mauti yake". Ibni Ziyad

akakasirika akaamrisha yule mtoto auwawe. Hapo tena Bibi Zainabu akamkumbatia

mtoto na kumwambia Ibni Ziyad:

“Wallahi simuachi, ukimuuwa na mimi uniue" kisha Ibni Ziyad akamuachia,

akainuka akatoka akaenda msikitini akatoa hotuba akasema:-

"Kila sifa njema ni za Mungu ambaye amedhihirisha haki juu ya watu wake, na

akamnusuru Amiril Muuminina Yazid bin Muawiya na watu wake, na akamuuwa

"Muongo wa Waongo" Hussein bin Ali na kikundi chake". Hii ndiyo jaza na uovu usio

kuwa na kiasi wa Ibni Ziyad kumuita Imamu Hussein na baba yake kuwa ni waongo!!

“Pale palikuwa na mtu ambaye ni katika Shia (kikundi) Wampendao kina Imamu

Ali, naye aitwa Abdullah bin Afif Ali-Azdy, akainuka akamwambia Ibni Ziyad: Ewe

mtoto wa Marjana wee!” Muongo wa waongo" ni wewe na baba yako na ambaye

amekutawalisha wewe: Wawaua watoto wa Mtume kisha ukasimama juu ya mimbari

ukasema maneno dhidi ya watu wa kweli”

Ibni Ziyad akakasirika akaamrisha auawe kwa kusurubiwa!

SAFARI YA SYRIA

Baada ya hapo ibn Ziyad aliamrisha kichwa cha Imamu Hussein pamoja na

wenzake vizungushwe katika mji wa Al-Kufa, kisha vipelekwe kwa Yazid huko aliko

Damascus mji mkuu wa Syria (Sham).

Vikazungushwa vichwa mjini Al-Kufa, kila mahali, mabarabarani na katika

masoko, kisha vikapelekwa huko Shamu kwa Yazid.

Kichwa cha Imamu Hussein kilipofika kwa Yazid alikiweka mbele yake akajifanya

anasikitika akahuzunika na huku akisema: "Wallahi Ewe Hussein lau ningekuweko

nisingelikuuwa.” Na alikuwa ameshika fito anachezea meno ya Hussein, palikuwa na mtu

akiitwa Abu Barza, akamwambia: “Wachezea meno ya Hussein kwa fito yako? Wallahi

imefanya jambo kubwa fito yako!

Mara nyingi nimemuona Mtume (s.a.w.w.) akimbusu kwa mdomo wake; Ama

wewe Yazid utakuja siku ya kiyama na Ibnu Ziyad ndiye muombezi wako na atakuja

huyu na Muhamad (s.a.w.w.) ndiye muombezi wake "

Yazid akatahayari asiweze kujibu kitu akaondoka.

Na mimi hapa nakoma na kisa hiki siwezi tena kuendelea mbele.

Moyo wangu wanipiga na kunichoma na mikono imeshikwa baridi na kutetemeka.

Kwani kifo cha Imamu Hussein hakijatokea Duniani kuuawa kwa kukatwa katwa viungo

mbali mbali, mikono mbali, kichwa mbali, mwili mbali. Kisha akazungushwa mji mzima

www.allamahrizvi.com

Page 55: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

55

tangu jimbo la Iraq mpaka Syria! Licha yeye Imamu Hussein ambaye ni mjukuu wa

Mtume (s.a.w.w.) hata yeyote hata kafiri ambaye ni kama Firaun, hata kama si

binaadamu ni mnyama kama paka na mbwa haifai kufanywa hivyo!

Je iwapo ni Hussein mtoto wa Fatimah bint Rasulillah! Babu yake ndiye aliye

waletea watu dini akawatoa katika ushenzi akawatia katika ustaarabu hata wakaipata hiyo

Dola.

Basi jaza ya mtu huyo ni kuuliwa wajukuu zake? Na wakadhalilishwa namna hiyo?

Basi mtu kama huyu Imamu Hussein ndiye wa kulilia na kuhuzunikia. Watu wengine

wanasema: "kwanini watu humlilia Imamu Hussein wasimlilie Mtume (s.a.w.w.).

Mtume (s.a.w.w.) wamlilie kitu gani na Ilhali amekufa kitandani pasi na kuuawa

wala kudhulumiwa wala dhalala yoyote, Hasha haikumpata! Basi aliliwe jambo gani, na

ilhali siku aliyokufa ndiyo tarehe aliyozaliwa?

Lakini Hussein ni kama tulivyo sema alipata taabu hata maji hakupewa akafa na

kiu na Ilhali maji akiyatazama na wasimpe!

WATOTO WA IMAMU HUSSEIN

Imamu Hussein alikuwa na watoto tisa wanaume nao ni hawa:-

1. Ali ndiye aitwaye Zeinul Abiduna. Na ndiye aliyetoa kizazi wakabakia mpaka

sasa.

2. Aliyul- Akbar, aliuawa Karbala pamoja na baba yake.

3. Aliyul - Asghar, aliyeuawa Karbala kwa mshale.

4. Abdullah, aliyeuawa Karbala pamoja na baba yake.

5. Jaafar, alikufa utotoni Madina

Na wanawake ni Wawili nao ni hawa:-1. Fatimah. 2. Sukaina

MISEMO YAKE

Imamu Hussein alikuwa fasaha kwa kusema kama babake na nduguye. Hapa chini

nitatia maneno yake ya hekima kidogo:-

a) Mwenye kuwa" karim (mpaji) huwa Bwana na bakhili (mgumu) huwa mnyonge.

b) Na mwenye kufanya haraka kwa jambo la kheri kumfanyia mwenzake atalipata

kesho (akhera) mbele ya Mola wake.

c) Mambo mabaya kwa Wafalme: Ni kuwa waoga kwa maadui na ukakamavu wa

ubaya juu ya wanyonge, na ubakhili.

d) Mali iliyobora ni yenye kuhifadhi cheo cha mtu (heshima)

Katika vita vya Karbala alikuwa akisema: Hakika mimi sioni mauti ila ni pepo

(Jannah) na Sioni uhai (maisha) pamoja na madhalimu ila dhambi".

Tumemaliza maisha pamoja na kifo cha Imamu Hussein naye alizikwa hapo

Karbala". Katika mji wa Al-kufa, Iraq ambapo ndipo penye kaburi lake na watu wana

zuru mpaka leo.

Page 56: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

56

Tumesoma kuwa watoto wa Imamu Hussein wote wanaume waliuawa na wengine

walikufa kabla yake yeye. Mtoto wake mwanaume aliyebaki ni yule mmoja tu aitwaye

Aliyul Ausat (Zainul Abidiyn); ambaye ndiye aliendelea na kizazi cha masharifu.

MAANA YA MASHARIFU

Swali hili lina mzozo mkubwa kwa watu, wengine wanauliza kwa hakika hawajui,

na wengine ni kwa dhihaka na shere na wengine wanawachukia na kuwakana kuwa

"Hakuna kabila la "Kisharifu"! Jawabu lake ni hili:-

Masharifu ni kizazi kilichotokana na Imamu Hassan na Imamu Hussein (watoto wa

Imamu Ali) na Mama yao ni bi Fatimah binti ya Mtume (s.a.w.w.) Ukoo utokao kwa

Imamu Hassan kwa ujumla huitwa "AL-HASANY" na ndani yake mna makabila kadha

wa kadha: kama Shekh Abdul Kadir AL-JEILANY, hakuitwa kwa kabila la "AL-

HASANY" naye atoka kwa Imamu Hassan: (amenasibishwa na Jeilany au GILAN ni mji

katika pande za Iran ("Jil-Karkuk") na ukoo utokao kwa Imamu Hussein kwa jumla

huitwa kwa "AL-HUSEINY". Makusudio ya Al-Huseiny hapo sio wale wajukuu wa

Sheikh Abubakar bin Salim, la na ingawa naye anatoka kwa Imamu Hussein. Shekh

Abubakar bin Salim alikuwa na mtoto aitwae Hussein kwa hiyo wajukuu zake wakaitwa

Al-Husseiny").

Amma kabila la Masharifu ni Banu Hashim, kabila ya babu zao (Hassan na

Hussein) na ya Mtume (s.a.w.w.) lakini Banu Hashim wataingia Banul Abbas na Banul

Muttalib na Watoto wa Imamu Ali ambao mama yao si Bi Fatimah hao wote si

masharifu: kwani kwa kidesturi "Shariff' ni aliyetoka kwa Fatimah. Na vile vile waitwa;

FATIMIYYIN, kama wajulikanavyo kwa ALAW1YYIN.

Atakaye ujuzi zaidi wa Masharifu na Makabila yao na akasome kitabu

MASHRAU-RUWY cha Sayyid Abubakar Ash-Shaly, na Ash-Sharaful Muabbad cha

Shekh Abdulla bin Mohamed Bakathir, Na vitabu vingi zimo habari zao. Kule kusema

masharifu ni watu gani au watoka wapi ni ujinga wa kutosoma au ni ufidhuli wa kutaka

kutukana watu. Au kusema kuwa waliuawa wote, hilo si kweli, sababu Imamu Hassan na

Hussein waliacha watoto kama tulivyoona.

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

ORODHA YA VITABU VYETU VYA KISWAHILI

1. Uislamu

2. Haja ya Dini

3. Mungu wa Uislamu

4. Uadilifu wa Mungu

5. Maisha ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.)

6. Uimamu

7. Ulul-Amr ni Nani

8. Fadhaali za Sayyidna Ali Ibni Abu Talib (a.s.)

9. Mtume wa Amani (s.a.w.w.)

10. Bibi Mwenye Nuru (a.s.)

11. Roho ya Matumaini - Imamu Ali (a.s.)

12. Mfalme wa Uvumilivu - Imamu Hassan (a.s.)

Page 57: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

57

13. Chem chem ya Uhuru - Imamu Hussein (a.s.)

14. Shujaa baada ya Karbala - Imamu Ali bin Husein (a.s.)

15. Mwanga wa Elimu - Imamu Baqir (a.s.)

16. Mwenge wa Ukweli - Imamu Jaafer Sadiq (a.s.)

17. Maadili ya Tabasamu - Imamu Musa Ibni Jaafar (a.s.)

18. Shahidi wa Mash-had-Imamu Ali Riza (a.s.)

19. Ukweli katika Minyororo-Imamu Muhammad Taqi (a.s.)

20. Nguzo ya Uchamungu-Imamu Ali Naqi (a.s.)

21. Mfungwa Adhimu - Imamu Hassan Askari (a.s.)

22. Anayengojewa - Imamu Mahdi (a.t.f.)

23. Imamu Zamana

24. Risaalatul-Huquq

25. Kitabu cha Sala

26. Kwanini Mashia husujudu juu ya udongo?

27. Kitabu cha Saumu

28. Kwanini Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alioa Wake wengi

29. Kwanini Uislam umeruhusu Mume kuoa Wake wengi

30. Mahojiano baina ya Mlahidi na Imamu Jaafar Sadiq (a.s.)

31. Umuhimu wa Hijabu

32. Mwenge wa Haki

33. Mafunzo ya Awali ya Uislamu

34. Historia ya Kislamu

35. Bwana Abu Talib

36. Ahlul Kisaa

37. Mambo yanayomhusu Maiti

38. Mambo yampasayo Mwislamu kuyajua na kuyaamini

39. Ushindi Usiozuilika

40. Madhehebu za Kishia

41. Maana na Chanzo cha Ushia

42. Huu ni Ushia

43. Muhimu wa Qurani

44. Taqiya ni Nini

45. Muhammad (s.a.w.w.) ni Nabii wa Mwisho

46. Ndoa katika Uislam

47. Kitabu cha Tajweed

48. Juzuu Amma

49. Bustani ya Elimu

50. Fitina za Wahhabi zafichuliwa

51. Mawahhabiyah na Wauaji wa Imamu Husein (a.s.)

52. Historia ya chanzo cha Mawahhabi

53. Shia na Qur'ani

54. Shia na Hadith

55. Shia na Sahaba

56. Nyama ya Nguruwe

57. Hadithul Quds

58. Ukiristo na Uislamu

Page 58: AHLUL Kisaa final - Allamah Rizvi · PDF fileUthman Ibn Affan, 4) Maisha ya Ali Ibn Abi Talib. ... wameipokea hadithi hii kutoka kwa bwana Abdullah bin Abass (R.A.), yeye amesema ilipoteremka

58

59. Masomo ya Kiislamu Kitabu cha Kwanza

60. Masomo ya Kiislamu Kitabu cha Pili

61. Masomo ya Kiislamu Kitabu cha Tatu

62. Masomo ya Kiislamu Kitabu cha Nne

www.allamahrizvi.com