HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA 19 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 01 APRILI, 2015 I: UTANGULIZI (a) Masuala ya jumla Mheshimiwa Spika, 1. Leo tunahitimisha shughuli zilizopangwa za Mkutano wa 19 wa Bunge lako Tukufu. Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo. Mheshimiwa Spika, 2. Tarehe 17 Machi, 2015 wakati tunaanza Mkutano huu, ulitoa taarifa ya kusikitisha ya kumpoteza Mbunge mwenzetu Mheshimiwa Hayati Kapteni John Damian Komba, Mbunge wa Mbinga Mashariki aliyefariki tarehe 28 Februari, 2015 na kuzikwa nyumbani kwake Lituhi tarehe 03 Machi, 2015. 1
68
Embed
01.04.2015 Hotuba Ya Kuahirisha Bunge La 19 Dodoma Ya Pm Final Crested
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA 19 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 01 APRILI, 2015
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA 19 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 01 APRILI, 2015
I: UTANGULIZI
(a) Masuala ya jumla
Mheshimiwa Spika,
1. Leo tunahitimisha shughuli zilizopangwa za Mkutano
wa 19 wa Bunge lako Tukufu. Napenda kumshukuru
Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa
kutufikisha salama siku ya leo.
Mheshimiwa Spika,
2. Tarehe 17 Machi, 2015 wakati tunaanza Mkutano huu,
ulitoa taarifa ya kusikitisha ya kumpoteza Mbunge
mwenzetu Mheshimiwa Hayati Kapteni John Damian
Komba, Mbunge wa Mbinga Mashariki aliyefariki tarehe
28 Februari, 2015 na kuzikwa nyumbani kwake Lituhi
tarehe 03 Machi, 2015. Napenda nitumie fursa hii
kuungana na Waheshimiwa Wabunge wote kutoa pole
kwako, Wananchi wa Mbinga Mashariki na kwa
Watanzania wote kwa kuondokewa na ndugu yetu
1
mpendwa Hayati John Damian Komba. Kwetu sisi
tulioko ndani ya Bunge lako Tukufu hakuna asiyejua sifa
za Mheshimiwa Hayati Kapteni John Komba. Sote
tutaendelea kumkumbuka kwa yale yote aliyoyafanya kwa
faida na maendeleo ya Nchi yetu.
Mheshimiwa Spika,
3. Vilevile katika kipindi hiki tangu Mkutano wa mwisho
kulitokea majanga na ajali mbaya za Barabarani ambazo
watu wengi wamepoteza maisha. Nitumie nafasi hii ya
awali kabisa kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki
ambao wote wameguswa na misiba hiyo. Tuwaombee
kwa Mwenyezi Mungu roho za Marehemu zilale mahala
pema peponi. Kwa wale waliopata majeraha,
tunawaombea wapone haraka.
Mheshimiwa Spika,
4. Nitumie pia fursa hii ya mwanzo kuwapongeza
Mheshimiwa Dkt. Grace Khwaya Puja na Mheshimiwa
Innocent Rwabushaija Sebba kwa kuteuliwa na
Mheshimiwa Rais kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Uteuzi wao unaonesha imani
kubwa aliyonayo Mheshimiwa Rais katika utendaji wao.
Pamoja na kuwakaribisha Bungeni, tunawaahidi
ushirikiano wetu katika kutekeleza majukumu yao.2
b) Maswali
Mheshimiwa Spika,
5. Katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge walipata
fursa ya kuuliza maswali ya kawaida na jumla 156 ya
msingi na 425 ya nyongeza na kujibiwa na Serikali.
(c) Miswada
Mheshimiwa Spika,
6. Katika Mkutano huu, jumla ya Miswada 21 ilipangwa
kujadiliwa katika Mkutano wa 19. Miswada iliyowasilishwa
na kupitishwa katika hatua zote ni 14 ambayo ni kama
ifuatavyo:
i) Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa mwaka 2014 (The Non-Citizens Employement Regulation Bill, 2014);
ii) Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa Mwaka 2014 (The Firearms and Ammunition Control Bill, 2014);
iii) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014 [The Immigration (Amendment) Bill, 2014];
3
iv) Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 (The Tax Aministration Bill, 2014);
v) Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2014 (The Statistics Bill, 2014);
vi) Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa Mwaka 2014 [The Disaster Management Bill, 2014];
vii) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014 [The Wharehouse Receipts (Amendment) Bill, 2014];
viii) Muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa wa Mwaka 2015 (The National Payment Systems Bill, 2015);
ix) Muswada wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa Mwaka 2014 [The Drug Control and Enforcement Bill, 2014];
x) Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI wa Mwaka 2014 [The Tanzania Commision for AIDS (Amendment) Bill, 2014];
xi) Muswada wa Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2014 (The
Budget Bill, 2014);
4
xii) Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana Tanzania wa
Mwaka 2015 [The Youth Council of Tanzania Bill,
2015];
xiii) Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki wa
Mwaka 2014 (The Electronic Transaction Bill, 2015);
na
xiv) Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa Mwaka
2015 (The Computer and Cyber Crimes Bill, 2015).
Mheshimiwa Spika,
7. Miswada iliyoachwa kwa sababu mbalimbali ni:
xv) Muswada wa Sheria ya Wataalam wa Kemia wa
Mwaka 2014 (The Chemist Professionals Bill, 2014);
xvi) Muswada wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali wa Mwaka 2014 (The Government Chemistry
Laboratory Bill, 2014); na
xvii) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2014 [The Written Laws
(Miscellaneous Amendements) (No. 2) Bill 2014].
Mheshimiwa Spika,
5
8. Miswada ifuatavyo ilisomwa kwa mara ya Kwanza.
xviii) Muswada wa Sheria ya kupata Habari wa Mwaka
2015 (The Access to Information Bill, 2015);
xix) Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari wa Mwaka 2015 (The Media Services Bill, 2015);
xx) Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya
Ushindani wa Mwaka 2015 [The Fair Competition
(Amendment) Bill, 2015]; na
xxi) Muswada wa Sheria ya Tume ya Walimu wa Mwaka
2015 [The Teachers Servce Commission Bill, 2015].
d) Maazimio
Mheshimiwa Spika,
9. Katika Mkutano huu, pia Waheshimiwa Wabunge
walipata fursa ya kujadili na kuridhia Maazimio mawili
yafuatavyo:
i) Azimio la kuridhia Mkataba wa Msingi na Kanuni za
Utumishi wa Umma na Utawala Barani Afrika Mwaka
2011 (The African Charter and Principal of Public
Service and Administration, 2011); na
6
ii) Azimio la Kuridhia Makubaliano ya Msingi ya
Ushirikiano katika Bonde la Mto Nile (Agreement on
the Nile River Basin Co-operative Framework – CFA);
10. Napenda kuwapongeza sana Waheshimiwa Wabunge
wote kwa kazi kubwa iliyofanyika ya kujadili miswada
mingi kiasi hiki na kuipitisha pamoja na kuridhia maazimio
yote yaliyowasilishwa.
II: MAAFA YALIYOJITOKEZA
a) Dhoruba ya Mtwara
Mheshimiwa Spika,
11. Usiku wa kuamkia tarehe 14 Januari 2015 kulitokea
mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali katika eneo la
Mnazi Bay, Mtwara; hali ambayo ilisababisha eneo la Nchi
kavu takribani mita 105 upana na mita 1,100 urefu
kumeguka na kuwa sehemu ya maji ya bahari. Eneo hili
limejengwa miundombinu ya gesi asilia kama ifuatavyo:-
i) Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom
Tanzania (M&P) kinachozalisha gesi ambayo inatumika
ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Awamu ya Pili ilianza
mwaka 2013 ikihusisha Wafanyabiashara waliosajiliwa
kutozwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Mheshimiwa Spika,
67. Katika utekelezaji wa zoezi hili, Serikali imelenga
kuingiza Walipa Kodi wapatao 250,000 kati ya Walipa
Kodi 1,500,000 ili waweze kutumia Mashine za
Kielektroniki za EFD. Walengwa wa utaratibu huu ni
Wafanyabiashara wenye biashara kubwa zenye Mtaji wa
kati ya Shilingi Milioni 14 na Shilingi Milioni 40. Katika
Awamu hizi mbili, Wafanyabiashara wanaoendesha
biashara zisizo rasmi kama vile, Wamachinga na wale
wanaotembeza bidhaa barabarani na Mama Lishe
hawahusiki na utaratibu huu.
Mheshimiwa Spika, 42
68. Napenda kusisitiza kuwa, Mfumo wa Matumizi ya
Mashine za Kielektroniki ni mzuri na unawasaidia
Wafanyabiashara kutunza kumbukumbu na kulipa Kodi
stahiki. Nawasihi Wafanyabiashara wajenge tabia ya
kutunza kumbukumbu za biashara zao ili waweze kulipa
Kodi Stahiki badala ya kutumia Mfumo wa Makadirio
ambao umepitwa na wakati. Serikali inaamini kuwa,
Matumizi ya Mashine za Kielektroniki zitaongeza
Makusanyo ya Kodi na kupunguza vishawishi vya Rushwa.
Mheshimiwa Spika,
69. Baada ya maelezo hayo, napenda kueleza hatua
zilizochukuliwa na Serikali kushughulikia Malalamiko ya
Wafanyabiashara pamoja na muhtasari wa makubaliano
baina ya Serikali na Wafanyabiashara katika maeneo
yanayolalamikiwa kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Spika,
70. Serikali ilikwishaanza kushughulikia Malalamiko ya
Jumuiya ya Wafanyabiashara tangu mwezi Januari, 2014,
hususan kuhusu kushughulikia changamoto zinazotokana
na Mfumo wa Mashine za Kielektroniki. Aidha, mwezi
Septemba, 2014 iliundwa Kamati ya Taifa ya Uhamasishaji
wa Matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD na Kamati
ya Ndogo ya Kiufundi ya kupitia mfumo wa uongoshaji wa 43
Mizigo Bandarini. Vilevile, Wizara ya Fedha imeunda
Kamati za Mikoa za kujadili changamoto mbalimbali
zinazowakabili Wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na
kuelimisha Umma kuhusu Matumizi ya Mashine za EFD.
Kutokana na hatua hizo kwa sasa mshine za kielektroniki
za EFD zimeboreshwa zaidi na kuipa Mamlaka ya Mapato
Tanzania uwezo mkubwa wa kusimamia mauzo ya
Wafanyabiashara. Aidha, zoezi la elimu kwa walipa kodi
linaendelea katika Mikoa yote Nchini.
Mheshimiwa Spika,
71. Katika Kikao cha tarehe 27 Machi, 2015 Serikali
pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
tuliafikiana kwamba:
(a) Kamati ya Kitaifa ya Uhamasishaji wa Matumizi ya
Mashine za Kielektroniki (EFD) au Kamati ya pamoja
ya maridhiano baina ya Wafanyabiashara na Serikail
kuhusu matatizo ya kimfumo ya utozaji kodi na yale
yanayotokana na mfumo wa Mashine za Kielektroniki
za EFD; ikutane mapema iwezekanavyo kuanza
majadiliano ili kuyapatia ufumbuzi malalamiko,
changamoto na kero zinazowakabili Wafanyabiashara
na kuwasilisha mapendekezo yake Serikalini ndani ya
44
kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 28 Machi
2015. Kamati husika ikamilishe kazi yake kabla ya
mwisho wa mwezi Aprili, 2015;
(b) Ili kuwepo na uwakilishi mpana kwenye Kamati ya
Taifa ya pamoja ya Wafabiashara na TRA, Serikali
itateua Wajumbe wawili kutoka Wizara ya Viwanda na
Biashara na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge) wawe sehemu ya Kamati iliyoundwa
inayojumuisha Wajumbe Watatu (3) kutoka Jumuiya
ya Wafanyabiashara Tanzania na Wajumbe Watatu (3)
kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na
Mjumbe mmoja (1) kutoka Wizara ya Fedha;
(c) Kwa kuwa suala la Ongezeko la Kodi ya Mapato la
Asilimia 100 linatokana na Marekebisho ya Sheria ya
Fedha ya mwaka 2014/2015 ambayo imepitishwa na
Bunge, na linawahusu wale tu ambao hawatunzi
kumbukumbu zozote za mauzo ya bidhaa zao. Hivyo,
ufumbuzi wa suala hili unapaswa ufuate utaratibu wa
mchakato wa marekebisho ya Sheria husika kupitia
Bunge. Tuliafikiana kuwa, Jumuiya ya
Wafanyabiashara baada ya kujadiliana ndani ya
Kamati ya pamoja iwasilishe mapema mapendekezo
ya kurekebisha Mfumo wa Kodi unaolalamikiwa ili 45
maoni yao yajadiliwe kwenye Kamati ya Maboresho ya
Mfumo wa Kodi (Task Force on Tax Reforms) wakati
wa mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya Serikali ya
Mwaka 2015/2016 na kufanya marekebisho stahiki.
Hata hivyo, kwa kuwa suala hili litachukua muda
ninawashauri Wafanyabiashara waanze kulipa robo ya
kodi ilivyo sasa ili kuepuka kudaiwa malimbikizo
baada ya Sheria kurekebishwa;
(d) Kwa kuwa Mfumo wa Matumizi ya Mashine za
Kielektroniki una faida nyingi na manufaa makubwa
kwa Wafanyabiashara na Serikali; na kwa kuwa
Mfumo huo unatumika katika Nchi nyingi Duniani;
tumekubaliana kuwa, Jumuiya ya Wafanyabiashara
Tanzania (JWT) iendelee kuwahamasisha na
kuwaelimisha Wafanyabiashara wenzao kuhusu
umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara zao
kwa kutumia Mashine za Kielektroniki za EFD na
kulipa kodi stahiki. Serikali inaahidi kuwa itaendelea
kushughulikia changamoto za kimfumo na utawala
zilizopo za Matumizi ya Mashine za Kielektroniki za
EFD na tumesisitiza kuwa suala hili lijadiliwe kwenye
Kamati ya Kitaifa iliyoundwa ili kuzipatia ufumbuzi
kwa haraka;
46
(e) Kuhusu suala la Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Wafanyabiasha Nchini, Bwana Johnson Estomihi Minja
Kikao kilielezwa kwamba, Bwana Minja alishtakiwa
kwa makosa ya kuendesha Mikutano ya uchochezi ya
kuzuia matumizi ya Mashine za Kielektroniki na
kuhamasisha Wafanyabiashara kufunga maduka yao.
Tuliwaeleza Viongozi wa Wafanyabiashara kwamba
suala hilo lipo chini ya Mamlaka nyingine ambayo ni
Mahakama; na kwamba Mhusika alirejeshwa rumande
tarehe 26 Machi, 2015 kutokana na kukiuka mojawapo
ya masharti ya dhamana aliyopewa na Mahakama.
Hivyo, siyo busara kwa Serikali kuingilia uhuru wa
Mhimili wa Mahakama. Serikali inaamini kuwa Mhusika
atatimiza masharti ya dhamana kesi yake
itakapotajwa tena leo tarehe 01 Aprili, 2015; na hivyo
kuachiwa huru. Taarifa zilizopatikana mchana wa leo
zinaonesha kwamba, Bwana Johnson Estomihi Minja
amepata dhamana na yuko huru jioni ya leo;
(f) Mwisho, tulikubalina kuwa kwa sababu Serikali
imeonesha nia njema ya kushughulikia mapema
iwezekanavyo malalamiko na changamoto
zinazowakabili Wafanyabiashara Nchini, ni vyema
Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara baada ya 47
Kikao kile, kwenda kutoa maelekezo kwa
Wafanyabiashara katika Mikoa yote Nchini kusitisha
mara moja mgomo unaoendelea na wawatake
Wafanyabiashara kufungua maduka yao ili Wananchi
wapate huduma na bidhaa muhimu.
Mheshimiwa Spika,
72. Serikali inathamini sana mchango wa
Wafanyabiashara katika Kukuza Uchumi na kuchangia
Mapato ya Serikali. Napenda kuwahakikishia
Wafanyabiashara na Wananchi wote kwamba, Serikali ipo
tayari kukaa pamoja na Wafanyabiashara kuzungumzia
changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa
haraka. Naomba nitumie fursa hii kutoa Wito kwa
Wafanyabiashara wote Nchini kufungua Maduka yao ili
waweze kutoa huduma muhimu za kuuza bidhaa kwa
Wananchi. Nasisitiza kwamba, utaratibu wa kutumia
Mashine za Kielektroniki haukuwekwa kwa nia mbaya, bali
unalenga kumrahisishia Mfanyabiashara kutunza
kumbukumbu za kila siku za biashara na kuwawezesha
kulipa Kodi Stahiki.
Mheshimiwa Spika,
48
73. Natoa Wito kwa Waheshimiwa Wabunge na Viongozi
wa ngazi zote kushirikiana na Serikali kuwaelimisha
Wananchi na Wafanyabiashara kuhusu manufaa ya
Matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD na kujenga
tabia ya kufanya biashara kwa kutunza kumbukumbu za
mauzo ili kwa pamoja tushirikiane kujenga Nchi yetu na
kuleta Maendeleo Endelevu kwa kulipa Kodi Stahiki.
X: MALALAMIKO KUHUSU USAJILI MPYA WA
BODABODA
Mheshimiwa Spika,
74. Pamoja na malalamiko hayo, yapo pia malalamiko ya
Wafanyabiashara wa Pikipiki na Bajaj ambao
wanailalamikia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
kwamba inawatoza Shilingi 250,000 hadi 300,000 kwa
kusajili upya Pikipiki moja. Wafanyabiashara ya Bodaboda
wamesema Mmiliki mpya wa Pikipiki au Bajaj anatakiwa
kulipia leseni yake ya barabara pamoja na kodi nyingine
ambazo ama Mmiliki wa zamani hakuzilipia; au
Makampuni yaliyowauzia Pikipiki na Bajaj hizo hawajalipa
kodi. Tulipokutana na Wafanyabiashara na Wenye
bodaboda wanauliza kwa nini Mamlaka ya Mapato
49
Tanzania, isiwatafute wale Wamiliki wa zamani na kuwadai
Kodi husika.
Mheshimiwa Spika,
75. Nilikutana na Wafanyabiashara husika pamoja na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambapo maelezo ya
Kitaalam tuliyopewa ni kwamba tangu tarehe 1 Julai, 2014
Serikali ilifuta Leseni ya barabara kwa Pikipiki na kuwataka
Wamiliki wote kufanya Usajili upya. Katika zoezi hilo,
Wamiliki wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wamelipa
ushuru na ada zifuatazo:-
Kwanza: Kulipa Kodi ya Usajili (Registration Fees)
ambayo ni Shilingi 10,000/= (kwa Wamiliki
Wapya);
Pili: Kulipia Ada ya Leseni ya Barabara (Road
Licence) ya Pikipiki mpya ambayo ni Shilingi
50,000 kwa Mwaka;
Tatu: Kulipa Ada ya Zimamoto ambayo Sh.10,000
kwa Mwaka;
Nne: Kulipa Ushuru wa Stampu (Stamp Duty) ambao
ni Asilimia moja (1%) ya thamani ya Pikipiki;
50
Tano: Kwa wale walionunua Pikipiki kutoka kwa
Wamiliki wa zamani wanatakiwa pia kulipa Kodi
ya Uhamisho wa Umiliki ambayo ni takriban
Shilingi 27,000/= pamoja na ushuru wa
Stempu (Stamp Duty) wa Asilimia moja (1%) ya
thamani ya pikipiki husika.
Mheshimiwa Spika,
76. Ili kuwezesha Wamiliki wa pikipiki kulipa kodi hizo kwa
urahisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia
Sheria husika, ilitoa unafuu wa kumruhusu Mlipa Kodi,
kulipia Tozo na Ada hizo nilizozitaja kwa Awamu Nne (4)
kwa mwaka. Ukomo wa muda wa kulipia kodi hizo
ilikuwa imepangwa kuishia tarehe 31 Machi, 2015. Baada
ya Serikali kutatafakari kuhusu malalamiko hayo ya
Wamiliki wa bodaboda, imeamua kusogeza mbele muda
wa ukomo wa Usajili mpya wa Namba za Pikipiki
hadi Mwezi Desemba, 2015.
XI: HITIMISHO
Mheshimiwa Spika,
51
77. Kwa kumalizia na kama ilivyo ada, naomba nitumie
nafasi hii kuwashukuru wote waliosaidia kufanikisha
mkutano huu. Kipekee nikushukuru wewe binafsi
Mheshimiwa Spika, kwa kutuongoza vizuri na kwa busara
kubwa. Niwashukuru Wenyeviti wa Bunge kwa kazi nzuri
wanayofanya kila wanapopata nafsi ya kukalia kiti cha
Spika. Aidha, niwashukuru tena Waheshimiwa Wabunge
kwa kazi nzuri ya kujadili na kupitisha Miswada yote
iliyowasilishwa wakati wa Mkutano huu.
Mheshimiwa Spika,
78. Nitumie nafasi hii pia kumshukuru Katibu wa Bunge na
Wasaidizi wake wote kwa kazi nzuri ya kuhakikisha
mkutano huu unakamilisha shughuli zake kama
ilivyopangwa. Niwashukuru Wataalam wote wa Serikali na
Taasisi zake ikijumuisha Taasisi za Sekta Binafsi, kwa
misaada ya Kitaalam na huduma mbalimbali za
kufanikisha Mkutano huu.
79. Niwashukuru pia Waandishi wa Habari kwa kazi nzuri
walizofanya kuhakikisha kuwa taarifa za majadiliano na
maamuzi mbalimbali ya hapa Bungeni zinawafikia
Wananchi. Niwashukuru Madereva kwa kazi nzuri
waliyofanya ya kuwasafirisha kwa usalama Waheshimiwa
52
Wabunge, Viongozi mbalimbali, Wataalam na Wasaidizi
wote walioshiriki katika Mkutano huu.
Mheshimiwa Spika,
80. Nimalizie kwa kuwatakia wote safari njema
mnaporejea kwenye maeneo yenu ya kazi na katika
majimbo yenu. Ninaamini kwamba, Mwenyezi Mungu
atatulinda na kutuweka salama sote kama tulivyo hadi
kukutana tena katika Mkutano wa 20 wa Bunge lako
Tukufu ambao ni mkutano wa mwisho Kikatiba wa Bunge
la Kumi na ambao utakuwa mahususi kujadili Bajeti ya
Serikali.
Mheshimiwa Spika,81. Baada ya kusema hayo, naomba sasa kutoa Hoja kwamba, Bunge lako Tukufu liahirishwe hadi tarehe 12 Mei, 2015 saa 3:00 Asubuhi litakapokutana katika Mkutano wa 20 kwenye Ukumbi huu hapa Dodoma.