AKIDA ILIOWEPESISHWA KUTOKANA NA QURAN TUKUFU NA SUNNA
ILIOTWAHIRIKA
MTUNZI
SHEKH DR.AHMAD BIN ABDULRAHMAN AL-QAADHI
CHUO KIKUU CHA QASIIM
KITIVO CHA AKIDA
MFASIRI
KHALID MUHAMMAD ALI DHALI
UTANGULIZI WA MTUNZI
Hakika sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu,twamuhimidi na
twamtaka msaada na twamtaka msamaha na twajilinda kwake kutokana na
shari ya nafsi zetu,kwani anaye muongoza hakuna wa kumpoteza na
ampotezae hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana Mola
apasaye kuabudiwa kwa haki ila ALLAH pekee hana mshirika aliesema:
(2) Yeye ndiye aliyeleta mtume katika watu wasiojua kusoma,awasomee
aya zake na kuwatakasa na kuwafunza kitabu na hikima,(ilimu
nyinginezo).Na kabla ya haya walikuwa katika upotofu(upotevu)ulio
dhahiri(AL-JUMA:2)na shuhudia ya kwamba Muhammad(swallallahu aleihi
wasallam) ni mjumbe wake na ni mtume wake ambaye kwamba
amewaneemesha waja wake kwa kutumilizwa kwake.Akasema:
(164)Hakika Mwenyezi Mungu amewafanyia Hisani kubwa Waislam
aliowaletea Mtume miongoni mwao,anayewasomea Aya Zake,na
anawatakasa na kuwafundisha kitabu na Hikima.Na bila shaka kabla ya
hapo walikuwa katika upotovu ulio dhahiri (AALI IMRAN:164)Ama baada
ya hayo;
Hakika Allah alimtuma mtume wake Muhammad (swallahu alaihi wa
salam ) kwa uwongofu na dini ya haki ili atoe watu kutoka katika
giza awapeleke katika muangaza,na kutoka katika upotevu uliowazi
awapeleke katika uongofu uliotimia,uongofu wenye kukunjua nyonyo na
kuleta utulivu wa nyonyo. Kwani (uongofu) ni elimu ya manufaa, na
(dini ya haki) ni matendo mema, na kwa nguzo hizi mbili ndio maisha
mazuri hupatikana. Na hakika amekusanya Allah katika kitabu chake
kitukufu yote wanayo yahitajia waja katika akida zao, ibada zao,
kutangamana kwao, tabia zao, na zikaja sunna za mtume(Sallallahu
alayhi wasallam) kufafanua yaliyo tajwa kijumla, na kueleza
lilofichamana na kueleza kwa upana yote yaliyoachiwa, kama
alivyosema mtume(S.A.W) jueni ya kwamba hakika yangu mimi nimepewa
Quran na kitu mfano wake pamoja (ambayo ni sunnah) imepokewa na Abu
Daud.Akida ya kiislamu ndio nguzo ya dini hii na msingi wake, na
ndio siri ya nguvu zake na ndio kudhihiri juu ya dini zote, kwa
sababu akida ya kiislamu imekusanya sifa za pekee. katika hizo
ni:-1.kumpwekesha Allah katika ibada na mtume (Sallallahu alayhi
wasallam) kwa kumfuata.
2.kukoma yaani hatupiti Quran wala hadithi za mtume (Sallallahu
alayhi wasallam)wala haiwi akida chimbuko lake ni rai wala
kiasi.
3.kuafikiana na maumbile ya Mwenyezi Mungu aliowaumbia watu
kabla ya kugeuzwa na shetani.
4.kuafikiana na akili iliyo wazi iliosalimika na utata na
mataminio.5.iliokamilika, yaani haijawacha sehemu yoyote ya maisha
ila imeifafanua.
6.iliofanana, kwani mengine husadikisha mengine na hakuna
mgongano katika akida za kiislamu wala sharia zake kabisa.
7.Ukati, yaani uislamu ni dini ya uadilifu hakuna kupita mipaka
na kuzidisha wala kupunguza baina ya mambo tofauti tafouti.
Na sifa hizi za akida ya kiislamu zimeleta matunda haya:-
1.kuhakikisha kwamba sote ni waja wake mola na walimwengu na
kutoka katika utumwa wa viumbe.
2.Kuhakikisha kumfuata mtume(Sallallahu alayhi wasallam) wa mola
wa walimwengu na kujitoa katika uzushi na wazushi.
3.Utulivu wa nafsi, na kumakinika kimoyo kwa kuwa na mahusiano
na Allah muumba, mpangaji wa mambo, mwenye hikma.
4.Kukinai kifikra na kusalimika na mgongano na mambo yasiokuwa
na asli.
5.Kutekeleza haja za roho na haja za mwili na kukamilishana
baina ya itikadi na tabia.
Na hawaja wacha wanavyuoni kuipa akida hamu zao, na kutoa juhudi
zao katika kuifundisha na kuipitisha. Mara wakieleza kiujumla akida
ya wema waliopita, na mara wakieleza jambo fulani katika akida, na
mara nyengine katika kuwajibu wazushi wenye kupoteza. Kwa hivyo
mimi nikaonelea kuyaleta karibu katika fahamu mambo au masala ya
akida,na kuyapanga kwa mpangilio wa mtume (Sallallahu alayhi
wasallam)na nguzo za imani sita zilizotajwa katika hadithi ya
Jibril iliyo mashuhuri, nikitegemea dalili za Quran na sunnah
iliyotahirika, na nikifanya chini ya kila msingi mambo yanayo
husiana nayo, pia nikitaja waliopotea katika masala hayo na
kuwajibu utata wao bila ya kurefusha.
Kwa hivyo hii akida ikadhihiri kwa msimamo wa kati baina ya
kurefusha na kufupisha, na ikapambanua kwa uwazi na wepesi, ili
waweze waislamu kunufaika nayo, na kupatikaniwe makusudio katika
kukusanya yote ambayo ni katika akida ya wema waliotangulia kwa
ibara nyepesi, na mpangilio wa kimaudhui nikakiita kitabu:AKIDA
ILIO WEPESISHWA KUTOKANA NA QURAN TUKUFU NA SUNNAH ILIYO
TAHIRIKA.
Namuomba Allah aijaalie kazi hii ni kwa ajili yake, yenye
kuwanufaisha waja wake na rehma na amani zimfikie mtume wetu
Muhammad na jamaa zake na maswahaba wake wote.
Kimeandikwa na Shekh Dr. Ahmed bin AbdulrahmanAlQaadhiUnieza
katika 17/2/1427
Peleka maoni katika
Barua pepe: al-aqida@al-aqida .com
Kitengo cha akida
kitivo cha sharia na msingi wa dini
unieza s.p 246 alama ya posta 51911.
UTANGULIZI WA MFASIRISifa njema zote ni za mwenyeezi
mungu,muumba wa mbingu na ardhi,na swala na salamu zimfikie mtume
wetu muhammad (Sallallahu alayhi wasallam) na maswahaba wake na
jamaa zake wote. Akida ni somo lenye kueleza kuhusu imani yetu kwa
mwenyeezi mungu,malaika wake,vitabu vyake,mitume yake,siku ya
mwisho,kadari na yanayo fungamana na hayo.
Hakika akida ndio msingi wa dini,kutengezeka akida ya mtu ndio
inamfanya awe mumini na apate maisha ya raha hapa duniani na
mashukio yake akhera itakuwa ni peponi, ama ikiharibika akida ya
mtu kwa kuingiliwa na shirki au venginevyo itapelekea mtu kutokuwa
na maisha ya raha hapa duniani na akhera mashukio yake itakuwa ni
motoni,kwasababu akida ni rasilmali yatu.
Kwasababu hizo zilizotangulia na kuona hali ya jamii zetu kwamba
utapata waislamu wengi hawayajui mambo muhimu katika akida yao na
imani yao,ujinga huu wenye kupelekea kufanya mambo yasiofaa,na
kupata pengo lililokuweko katika vitabu vya akida kwa lugha ya
kiswahili. Nikaona umuhimu wa kutafsiri kitabu cha akida na
kuwafafanulia waislamu mambo muhimu katika dini yao katika lugha
watakayo ifahamu. Vitabu vya akida viko sampuli tofauti lakini mimi
nikachagua kitabu hichi kwasababu mbili;
1-Muandishi wa kitabu amekusanya mambo mingi ya Akida chini ya
misingi sita ya Imani na akiwarudi mapote mapotevu katika kurasa
chache.
2-Wepesi wa utunzi wake na uwazi wa ibara zake.
Hakika kazi ya kufasiri haswa kitabu cha Akida si kazi
nyepesi,imenichukua mda na juhudi kubwa,lakini pamoja na udhaifu
wangu nikaweza kukamilisha kazi hii,yote haya ni taufik ya
ALLAH.
Kabla ya mwisho ,shukurani kwanza nawapelekea wazazi wangu
walionilea malezi mema,na nawashukuru mashekhe wangu wote
walioniwezesha kufika daraja hii.pia sisahau kuwashukuru ndugi
zangu walioweza kunisaidia na kila alienisaidia mpaka kitabu
kikafika mbele yenukatika walionipa nasaha, kunisaidia kuchapa na
wengineo. Mwisho ndugu zangu waislamu,mimi ni mja mdhaifu kwahivyo
ukipata makosa katika kitabu hichi usisite kunijulisha.
Ndugi yenu mdhaifu
KHALID MOHAMMAD ALI DHALI
27/6/1429
Sawa na
1/7/2008
s.p 83211
m.s.a
kenya
[email protected] AKIDA ILIOWEPESISHWA KUTOKANA NA QURAN
TUKUFU NA SUNNA ILIOTAHIRIKAMsingi wa akida ya kiislamu ni
kumuamini mwenyeezi mungu,na malaika wake na vitabu vyake,na mitume
yake na siku ya mwisho,na kadari kheri yake na shari yake.Amesema
Allah:
(177) Bali wema(hasa)ni (wa wale)wanaomwamini Mwenyezi Mungu na
siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii(AL BAQARAH:177)
Mtume Ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake,na
waislam,(pia wameamini hayo):wote wamemwamini Mwenyezi Mungu,na
Malaika wake,na Vitabu vyake,na Mitume yake,(AL BAQARAH:285) (136)
Enyi mlioamini! Mwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Kitabu
alichokiteremsha juu ya Mtume wake,Na Vitabu alivyoteremsha
zamani.Na mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu na Malaika wake na
Vitabu vyake na Mitume wake na Siku yaMwisho,basi bila shaka
amepotea upotofu(upotevu) ulio mbali(na haki). (AN NISA:136)Na
akasema mtume (Sallallahualayhi wasallam) kumwambia Jibril (alaihi
sallam) alipomuuliza kuhusu Imani ,Akasema Ni kumuamini mwenyezi
mungu na malaika wake,na vitabu vake,na mitume yake,na siku ya
mwisho,na kuamini kadari kheri yake na shari yake(yote yatoka kwake
Allah)
[Imepokewa na muslim].
KUMUAMINI MWENYEEZI MUNGU
Kumuamini Allah ni kuamini kwa kukata kwamba Allah yupo,na
kwamba yeye ndie mola wa kila kitu,anaestahiki kuabudiwa peke yake
pasi na mwengine,aliyesifika na sifa za ukamilifu,alietakasika
kutokamana na sifa za upungufu.KWANZA:KUAMINI KUWEPO KWAKE
Kuwepo kwake Allah (subhanahu wataala)ndio haki kubwaAmesema
allah:
(62)Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko,na wale wanaowaabudu
badala yake(Mwenyezi Mungu)hao ni batili,na Mwenyezi Mungu ndiye
aliye juu na ndiye aliye Mkubwa(AL-HAJJ:62)Na kuwa shaka kwa kuwepo
kwake Allah ni uzushi na ukanushaji,anasema Allah: (10)Mitume wao
wakasema:Je!Mnamfanyia shaka Mwenyezi Mungu.Muumba wa Mbingu na
Ardhi?Yeye anakuiteni akusameheni dhambi zenu na akupeni muhula
mpaka muda uliowekwa.Wakasema:Hamkuwa nyinyi ila ni watu kama
sisi.Mnataka tu kutuzuilia na yale waliokuwa wakiabudu babu
zetu.Basi tuleteeni hoja zilizo wazi.(IBRAHIM:10)Na kukanusha
kuwepo kwake Allah ni kiburi na ukafiri,Anasema Allaha: (102)
Akasema(Musa):umekwishajua kuwa hakuna aliyeteremsha(hoja)hizi
isipokuwa Mola wa Mbingu na Ardhi,kuwa dalili,(ila unajibanisha
tu).Na hakika mimi nakuona ,wewe Firauni umekwisha angamia(BANI
ISRAIL:102).Na akasema: (28) (29) (30) (31) (32) (Musa)akasema:Yeye
ndiye Mola wa Mashariki na Magharibi na vilivyomo baina yake;ikiwa
hamfahamu(jambo mtafahamu hili)(28).(Firauni)akasema:kama
ukishikilia (kuwa kuna) Mungu mwingine badala yangu kwa yakini
nitakufanya miongoni wa wenye kufungwa
gerezani(29).Akasema:Je!Ijapokuwa nitakuletea kitu kilicho
wazi,(hoja zilizo wazi za kuonyesha ukweli wa utume
wangu)?(30).Akasema:Kilete,akiwa ni miongoni mwa wasemao
kweli(31).Basi akaitupa fimbo yake,mara ikawa nyoka
dhahiri(32).(ASH-SHUARAA:28-32).Na inajulisha kuwepo kwake mambo
kadhaa;katika hayo:
1:Maumbile yaliyosalimika.Amesema Allah:
(30)Basi ueleke uso wako katika dini iliyosawasawa-ndiyo umbile
Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu,(yaani dini hii ya kiislam
inawafikiana barabara na umbile la binadamu).Hakuna mabadiliko
katika maumbile ya viumbe vya Mwenyezi Mungu.Hiyo ndiyo dini iliyo
haki,lakini watu wengi hawajui.(AR-RUM:30).Na amesema Mtume
Muhammad(Swallallah alayhi wasallama):Hakuna mtoto azaliwaye ila
huzaliwa katika maumbile(uislamu) kisha wazazi wake humfanya awe ni
yahudi au mnasara au majusi(wenye kuabudu moto).Imepokuwa na
bukheri basi kila kiumbe kinabaki katika umbile la uislamu la
asili,anahisi kila mtu katika nafsi yake kuwepo kwa Mungu,ila
litokezee lenye kuharibu maumbile hayo anasema Allah katika hadithi
Qudusii:(Mimi nimeumba waja wangu hunafaa(wenye kumpwekesha katika
ibada na kujiepusha na shirki),na hakika shaitwani aliwajia
akawapotoa kutoka katika dini yao,imepokewa na muslim.
2:Akili iliowazi, anasema Allah:
(35)Je?Wameumbwa pasipo kitu,au wao ndio wamejiumba?
(AT-TUR:35).Kwani akili iliosalimika kutokana na mambo ya
shubha(utata) na matamanio inakubali moja kwa moja kwamba viumbe
lazima viwe na muumbaji kwa sababu viumbe haviwezi kujiumba
vyenyewe kwani kitu kisichikuwepo hakiwezi kufanya kitu kiwepo:basi
lazima kupatikaniwe muumba aliyopo naye ni Allh(subhanahu
wataala).Na ametolea ushahidi uwazi wa akili khatibu wa kiarabu
wakati wa ujahiliya(Qis bin Saidah Al-Iyaad)akasema:Choo cha ngamia
chajulisha kuwepo kwa ngamia na nyayo hujulisha juu ya mwendo kwani
mbingu zina nyota na ardhi ni yenye njia je,hayajulishi haya juu ya
Muumbaji mwenye Khibra?
3:Hisia zinaonekana,amesema Allah kuhusiana na Nabii Nuhu(Alayhi
ssalamu): (10) (11) (12) (13) (14)Ndipo akamuomba Mola wake
(akasema):Kwa hakika mimi nimeshindwa,basi ninusuru(10).Mara
tukaifungua milango ya Mbingu kwa maji yanayomiminika(kwa nguvu
kabisa)(11).Na tukazibubujisha maji chemchem zilizo katika ardhi,na
maji(ya juu na chini)yakakutana kwa jambo lililokadiriwa(na
Mungu)(12).Na tukamchukua(Nabii Nuhu)katika
ile(Jahazi)iliyotengenezwa kwa mbao na misumari(13).Ikawa inakwenda
mbele ya Macho yetu.Hii ni tunzo(tuzo)kwa aliyekuwa
amekataliwa(amekanushwa)(AL-QAMAR:10-14)Na akasema:) (63 (64) (65)
(66) (67)Mara tulimpelekea Wahyi Musa(Tukamwambia):Piga bahari kwa
fimbo yako.Basi ikatengana kila sehemu ikawa kama jabali
kubwa.(63).Na tukawaleta hapo wale watu wengine(na ni Firauni na
watu wake)(64).Na tukamuokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye
wote(65).Kisha tukawagharikisha wengine(66).Hakika katika hayo muna
mazingatio;na wengi katika wao si wenye
kuamini(ASH-SHUARAA:63-67)
Na akasema tena kulingamana na Nabii Isa (Alayhi wassalamu):
(49)
Na(atamfanya)Mtume kwa wana wa Israili,(kuwaambia):Nimekujieni
kwa hoja kutoka kwa Mola wenu,ya kwamba nakuumbieni,katika
udongo,kama sura ya ndege,kisha napuliza,mara anakuwa ndege,kwa
idhini ya Mwenyezi Mungu.Na ninawaponesha vipofu na wenye
mabalanga,na ninawafusha (baadhi ya) waliokufa,kwa idhini ya
Mwenyezi Mungu,na nitakuambieni mtakavyovila na mtakavyoweka akiba
katika nyumba zenu.Bila shaka katika haya imo hoja kwenu ikiwa
nyinyi ni watu wa kuamini(AALLI IMRAN:49)
Na akasema kiujumla surat (An-naml:62):
(62)Au Yule anayemjibu Yule aliyedhikika amwombapo na kuondoa
dhiki(yake)na kukufanyeni wenye kuendesha dunia(siyo bora?)Je,yuko
Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?Ni kuchache kuwaidhika kwenu
(AN-NAML:62).
Kwani miujiza ya Mitume na kujibu dua za waombaji na kuwaokoa
wenye matatizo ni dalili za kuhisika waliyafahamu haya pote la watu
kwa kushuhudia kuwepo kwa aliyewatuma na anayewajibu dua zao na
muokozi wao (Allah aliyetukuka)kushuhudia kwa yakini.4:Sharia
Sahihi:Amesema Allah: (82)Hawaizingatii nini,hii Qurani?Na kama
ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila shaka wangalikuta
ndani yake khitilafu nyingi(AN NISAA:82).
Na akasema tena: (174)Enyi watu!Imekufikieni dalili kutoka kwa
Mola wenu,na tumekuteremshieni nuru iliyo dhahiri (AN
NISAA:174).
Na akasema: (57)Enyi watu!Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola
wenu na poza la (dawa ya)yale yaliyomo vifuani,na uongofu
(mkubwa)na rehema kwa wanaoamini.(Nayo ni Qurani ambayo ikifuatwa
humtengenezea mtu dunia yake na akhera yake)(YUNUS:57)
Kwani yale yaliyoyakusanya Qurani kutokana na habari za Ghaibuna
Akida sahihi na Sharia adilifu na tabia njema ni dalili kwamba haya
yatoka kwa Allah,wala hayawezekani kutoka kwa mwingine katika
viumbe,ndiyo maana hajapinga kwa hakika kuwepo kwake Allah yeyote
katika wanadamu ila walitokeza baadhi ya mapote wenye kujifanyisha
katika mapagani wa kale na wa sasa.Kwa mfano:
1:Wenye kushikamana na zama:wenye kusema:
(24) Je! Na walisema:Haukuwa(uhai)ila ni uhai wetu huu wa
dunia,(haukuwa mwengine);tunakufa na tunaishi,wala hakuna
kinachotuangamiza isipokuwa(huu huu)ulimwengu;(kwani ndiyo ada yake
kufisha na kuhuisha).Lakini wao hawana ilimu ya
hayo(wanayoyasema)wandhania tu(AL-JATHIYAH:24).Wakidai kwamba
ulimwengu unakwenda peke yake na kwamba ulimwengu haujawacha wala
hauwachi kwenda pekee yake!Na wanasema matumbo hutoa watu na ardhi
humeza watu tu!Na hakuna kitu kituangamizacho ila kubadilika kwa
zama (yaani upite wakati Fulani wawe watu Fulani wawe wamemaliza
muda wao na wengine wakija ni hivyo hivyo,kwa hivyo mabadiliko ni
ya wakati tu).Wakawaweka mbali viumbe kutokana na muumbaji wao, na
Mungu aliwarudi kuwajibu hayo yao kwa kusema: (24)Lakini wao hawana
ilimu ya hayo (AL-JATHIYAH:24).
Si kwa akili wala kwa dalili wala kwa hisia wala kwa maumbile
bali ni dhana tu! (24)(wanayoyasema)wanadhania
tu(AL-JATHIYAH:24).
2:Wenye kushikamana na Asili(nature) wenye kusema kwamba
ulimwengu umepatikana kwa kitendo cha asili(maumbile) yaani dhati
ya vitu katika mimea au wanyama au vitu visivyokuwa na roho na sifa
zake vimejiumba vyenyewe na harakati(mienendo) zake na kuwajibu
hawa ni rahisi,nayo ni kwamba haiwezekani kitu kiwe ni kiumbe na
Muumbaji wakati mmoja anasema Allah: (35)Wameumbwa pasipo kitu,au
wao ndio waliojiumba(52:35).
Na hayo maumbile wanayotegemea kwamba ni jumla ya vitu visivyo
kuwa na harakati havisemi,wala havioni wala havisikii havina hisia
yoyote basi vitawezaje kuumba viumbe hai vyenye kusikia, kuona,
kuzungumza , kuhisi na vinahisi uchungu na kuwa na matarajio kwani
aliyekosa kitu hawezi kutowa .
3- wenye kushikamana na sudfa,wenye kusema kwamba viumbe
vilitokezea sudfa tu!kwa maana ya kwamba mkusanyiko wa vipande vya
vitu na viungo vyake vilipelekea kwa njia ya sudfa kutokeza uhai na
vikatengezeka viumbe tofauti tofauti bila ya mpangilio wowote
uliotangulia!Madai haya yanaanguka yenyewe kwa kujaribu kuyafikiria
tu!Kwani ukwasi katika kuumba na nidhamu zake za kimaumbile
zilizopangika na kuendelea juu ya muondoko huo huo kwa vipimo vya
sawa sawa vinakataa madai ya kwamba ulimwengu ulizuka kwa
sudfa.Amesema Allah: (88)Ndiyo sanaa ya Mwenyezi Mungu,(matengenezo
yake)aliyekitengeneza kila kitu(AN-NAML:85) Na akasema:
(12)Mwenyezi Mungu ni Yule ambaye aliyeziumba mbingu saba,na
ardhi kuwa mfano wake wa hizo.Amri(zake)zinashuka baina yao,ili
mujue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu,na
kwamba Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua(vilivyo kwa
ilimu yake) (AT-TALAQ:12).
4:Wakomunisti wenye kusema (hakuna Mola na maisha ni maada).
5:Watu wenye fikra za pekee katika historia kama firauni ambaye
aliyesema:
(23)Firauni akasema:Na nani huyo Mola wa walimwengu?
(ASH-SHUARAA:23).
Na namrudi (258)Hukumsikia Yule aliyehojiana na Ibrahim juu ya
Mola wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme?Ibrahimu
aliposema:Mola wangu ni Yule anayehuisha na kufisha,yeye
akasema:Mimi pia nahuisha na kufisha.Ibrahimu akasema:Mwenyezi
Mungu hulichomozesha jua mashariki,basi wewe lichomozeshe
magharibi.Akafedheheka Yule aliyekufuru,na Mwenyezi Mungu
hawaongozi watu madhalimu(AL BAQARAH:258)na hawa wanapingana na
nafsi zao.Wakanyusha maumbile yao kama alivyoshuhudia Allah kwa
kauli yake: Na wakazikanusha,na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini
nazo;(Kuwa ni kweli hayoaliyokuja nayo Nabii Musa.Lakini
walizikanusha tu),kwa dhulima na kujivuna.Basi angalia ulikuwaje
mwisho wa wafanyao ufisadi(AN-NAML:14)Ndio mana halikusimama lao la
kusimama na wala halikubaki lao la kubaki.
PILI:KUAMINI UBWANA WAKE ALLAH
Nayo ni kuitakidi kwa kukata kwamba Allah pekee ndio
mola,muumbaji,muamrishaji,na maana ya RABB :Ni bwana mfalme mwenye
kupeleka mambo,aliewalea walimwengu wote kwa neema zake amesema
Allah: (49) (50) )(Firauni)akasema:Mola wenu ni nani ewe Musa (49)
.(Musa )akasema: Mola wetu ni Yule aliyekipa kila kitu umbo lake
kisha akakiongoza(kufanya kinachowafiki umbo lake hilo(TA
HA:49-50)
Kwahivyo kuamini ubwana wake Allah ni juu ya haya mambo
matatu:
1)KUUMBA kwani Allah ameumba kila kitu,na venginevyo pasi na
Allah ni viumbe,amesema Allah:
(62Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu na yeye ndiye mlinzi
juu ya kila kitu(AZ-ZUMAR:62) na akasema: (2) Na ameumba kila kitu
na akakikadiria kipimo(chake)(AL-FURQAN:2)
Na kila kitu kilichoundwa na kuvumbuliwa kikitegemezwa kwa
kiumbe huwa ni kunasibisha tu!wala haimaanishi uumbaji kamili .Kwa
maana kazi yake huyo muundaji ni kuweka umbo ya hicho kitu na
utunzi na kukikadiria kitakuwa vipi ,lakini si kuanzisha(kutoka
kuwa kitu hakuna,bali yeye anakusanya vitu
vilivyokuwepo)Muanzishaji wa vitu vyote ni Allah kama ilivyo katika
aya hii: (14)Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa
waumbaji(AL-MUMINUN:14)
2)Kumiliki kwani ufalme ni wake Allah na venginevyo asiekuwa
Allah ni venye kumilikiwa na Allah.
Amesema Allah:
(107) Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye ufalme wa mbingu na
ardhi?Nanyi hamna mlinzi wala hamna msaidizi asiyekuwa Mwenyezi
Mungu(AL-BAQARAH:107)
(189)Na ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu,na
mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu(AALI IMRAN:189)
(26)Sema(katika kumsifu Mwenyezi Mungu):Ee Mola,uliyemiliki
ufalme wote!Humpa ufalme umtakaye,na humwondolea ufalme
umtakaye(AALI IMRAN:26) wala hana mshirika(wake)katika ufalme
)(BANI ISRAIL:111) (13) Huyo ndiye Mwenyezi Mungu,Mola wenu,mwenye
ufalme,na wale mnaowaabudu kinyume Chake,wao hawamiliki hata
utando(ugozi)wa koko ya tende(FATIR:13)na kila chenye kumilikiwa
kikinasibishwa kwa asiyekuwa Allah ni umilikaji usiokuwa kamili (ni
kunasibishiwa)tu!Umilikaji wenye mda kama alivyosema Allah:
(29)Enyi watu wangu!Leo mna ufalme mmeshinda katika
arhi(ghaafir:29)Na kama alivyosema: (3)Au(wawekeni Masuria)wale
ambao mikono yenu ya kiume imewamiliki(AN NISAA:3)
Na alivyosema:
(40)Bila shaka sisi tutairithi ardhi na walio juu yake.Na Kwetu
watarejeshwa (wote) (MARYAM:40)
3-Amri (kuamrisha)kwani kuamrisha ni kwa Allah na asiyekuwa yeye
ni mwenye kuamrishwa,amesema Allah: (154)Sema:Mambo yote ni ya
Mwenyezi Mungu(AALI IMRAN:154)Na akasema: (54) Fahamuni.kuumba ni
kwake tu Mwenyewe Mwenyezi Mungu.Na amri zote ni zake (Mwenyezi
Mungu).Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu,Mola wawalimwengu wote(AL
AARAF:54)
Na akasema: (210)Na lishe (mara moja)hilo jambo(la kuadhibiwa
kwao)?Na mambo yote hurudishwa kwa Mwenyezi Mungu(AL BAQARAH:210)
Na akasema kumwambia mtume wake: (128)Wewe huna lako katika shauri
hii(AALI IMRAN:128)Ikiwa mtume ni hivi itakuwaje kwa aliekuwa chini
yake kidaraja!Na akasema:
(4)Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla(yake)na baada(yake);na siku
hiyo Waislamu watafurahi(AR-RUM:4)
Kwani yeye Allah ndio muamrishaji wa pekee ju ya waja wake,na
kuamrisha kukitegemezwa kwa mwengine kama ilivyo katika aya hii:
(97)Lakini wao walifuata amri ya Firauni,na amri ya Firauni haikuwa
ni yenye uongofu(HUD:97
Basi huwa ni uamrishaji usiokuwa kamili bali ni kunasibishwa
tu!uamrishaji huo uko chini ya matakwa yake akitaka atapitisha amri
hiyo na akitaka atazuia. Na amri yaake Allah hukusanya amri ya
kisheria(kama amri yake ya swala)na amri ya kidunia(kama kifo na
venginevyo),ama amri zake za kidunia huwa bila ya pingamizi(hawana
hiari waja)nayo ni sawa na matakwa yake Allah,kama alivyosema
Allah:
(82)Hakika amri yake anapotaka chochote(kile kitokee)ni
kukiambia:Kuwa,basi mara huwa(YA-SIN:82)
Ama amri za dini huwa na hiari na kuchaguzwa(yaani Allah
hapeleki kumlazimisha ila amempatia chaguo na akifata atapata pepo
na akiwacha atapata adhabu)
Nazo hizo amri za dini ni sawa na mapenzi,huweza zikatokea au
huweza zisitokee,na yote hayo huwa chini ya matakwa yake ,kama
alivyosema:
(28) (29) Kwa Yule miongoni mwenu anyetaka kushika
njia(njema)(28).Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Mwenyezi
Mungu Mola wa walimwengu wote(AT-TAKWYR:28-29) Na sifa zake zengine
za ubwana wake zilizobaki zinaingia chini ya haya mambo
matatu,kuumba, ufalme, na kuamrisha jambo,kama kutoa rizki,
kuhuisha, kufisha, kuteremsha mvua ,kukuza mimea,kupeleka upepo,
kuvipeleka vyombo vya baharini,na kupishana usiku na mchana,kushika
mimba,na kumuwezesha mama kujifungua,kutoa afya,kumfanya mja
mgonjwa,kuwapatia nguvu waja,na kuwapatia udhalilifu,na sifa
nyenginezo.
Na huku kuamini kwa Ubwana wake ni kitu kipo kimaumbile,hukijuwa
mwanadamu kwa akili,huhisika katika ulimwengu,na ushahidi wake
umejaa katika sharia na katika ushahidi wake katika Quran:
(164)Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi,na
(katika)kuandamizana usiku na mchana,na (katika mwendo wa) vyombo
ambavyo hupita katika bahari kwa(kuchukua vitu)viwafaavyo watu,na
(katika kumiminika)maji aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kutoka
mawinguni,na kwa (maji) hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa
kwake,na akaeneza humo(ulimwenguni kwa sababu ya maji hayo)kila
aina ya wanyama;na katika mabadiliko ya pepo,na mawingu
yanayoamrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi,bila shaka(katika
haya)zimo Ishara kwa watu wenye akili(kuwa yuko Mwenyezi Mungu na
ni Mmoja tu(AL BAQARA:164)
. (27)(Wewe)huingiza usiku katika mchana(ukawa mchana mrefu siku
za joto),na huuingiza mchana katika usiku(usiku ukawa mrefu siku za
baridi),na hutoa aliye hai kwa Yule asiye na uhai,na hutoa mfu
katika Yule aliye hai;na humpa riziki umtakaye bila hisabu(AALI
IMRAN:27)
(95) (96) (97) (98) (99) Mwenyezi Mungu ndiye
mpasuaji(mwoteshaji)wa mbegu na koko zikawa miti.Hutoa mzima katika
maiti,naye(pia)ndiye mtoaji maiti katika mzima.Huyo ndiye Mwenyezi
Mungu.Basi mnageuzwa wapi?(95).Ndiye anayepambazua mwangaza wa
asubuhi;na ameufanya usiku kuwa mapumziko,na jua na mwezi kwenda
kwa hisabu.Huo ndio mpimo (mtengenezo)wa Mwenye Nguvu na
ajuaye(96).Na yeye ndiye aliyekuumbieni nyota ili mwongoke kwazo
katika viza vya bara na bahari.Hakika tumeeleza vizuri(kila)Aya kwa
(nafuu ya) watu wnaojua(97).Na Yeye ndiye aliyekuumbeni katika
nafsi moja.Na pako (kwa ajili yenu)mahali pa kukaa milele.(Napo ni
akhera).na mahali pa kuwekwa muda mdogo tu(napo ni duniani).Hakika
tumezieleza Aya(hizi) kwa(nafuu ya)watu wanaofahamu(98).Na yeye
ndiye aliyeteremsha maji kutoka mawinguni;na kwayo tunaotesha mimea
ya kila kitu.Kisha tunapelekea kuchipua majani ya kijani
katika(mimea)hiyo;tukatoa ndani yake punje zilizopangana.Na katika
mitende(vinatoka)katika makole yake vishada vyenye
kuinama(vinakaribia kufika chini kwa vilivyotia,hata vimekuwa
vizito).Na anakuotesheni bustani za zabibu na zaituni na
makomango,yanayofanana na yasiyofanana.Angalieni matunda yake
yanapotoa na (angalieni kuiva kwake.Bila shaka katika hayo ziko
hoja (kubwa)kwa watu wanaoamini (AL AN-AM:95-99) (2) (3) (4)
Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua Mbingu bila nguzo:mnaziona
hivi.Kisha akastawi juu ya Arshi(Yake).Na akalitiisha (kwenu)jua na
mwezi(akavifanya vitii).Kila kimoja kinaendelea mpaka muda
uliowekwa.Yeye Ndiye anayeliendesha kila jambo.Anazipambanua Aya
hizi ili mupate yakini ya kukutana na Mola wenu(2).Na ndiye
aliyeitandaza ardhi na akaweka humo majabali na mito.Na katika kila
matunda akafanya humo namna mbili(dume na jike).Huufunika usiku juu
ya mchana(na mchana juu ya usiku).Hakika katika haya zimo
Ishara(kubwa kuwa Mwenyezi Mungu yupo);kwa watu wenye
kufikiri(3).Na katika ardhi muna vipande vinavyoungana(na kuzaa
kwake namna mbalimbali),na muna mabustani ya mizabibu,na mimea
mingine,na mitende ichipuayo katika shina moja na isiyochipua
katika shina moja.Vyote vinanoshelezwa(vinamiminiwa)maji yale
yale;na tunavifanya bora badhi yake vyengine katika
kula(utamu).Hakika katika haya zimo ishara kwa watu manaotia mambo
akilini(AR RAAD:2-4)
(3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16)
(17) (18) Ameziumba mbingu na ardhi kwa (ajili ya kudhihirisha)
haki;na ametukuka na ushirikina wao(hao makafiri)(3).Amemuumba
mwanadamu kwa tone la manii.Tahamaki amekuwa mshindani dhahiri(wa
kumkataa Mwenyezi Mungu)(4).Na (pia) amewaumba wanyama.Katika hao
mnapata(vifaa vitiavyoa)joto na manufaa(mengine);na wengine
mnawala(5).Na mnaona raha mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka
malishoni asubuhi(6).Na(wanyama hao pia)hubeba mizigo yenu kupeleka
miji msiyoweza kuifika isipokuwa kwa mashaka na taabu.Hakika Mola
wenu ni Mpole sana(na)Mwenye Rehema nyingi(7).Na (amewaumba Farasi
na Nyumbu na punda ili muwapande na(wawe)mapambo.Na ataumba
(vipando vyegine)msivyovijua.(Nayo ndiyo haya
mamotokari,meli,ma....)(8).Na ni juu ya Mwenyezi Mungu (kuonyesha)
njia (iliyo sawa).Na ziko(nyingine zisizo sawa).(basi nyinyi
fuateni hiyo njia ya sawa anyokuonyesheni Mwenyezi Mungu).Na kama
angalipenda bila shaka angali kuongozeni nyinyi nyote(mkitaka
msitake.Lakini kakupeni huria ya kuchaguaa mtakalo)(9).Yeye ndiye
anayekuteremshieni maji kutoka mawinguni;kwa hayo mnapata
kinywaji,na kwa hayo (inatoa) mimea ambayo humo mnalisha
(wanyama)(10).(Na kwa hayo) hukuotesheeni mimea(ya kila namna)na
mizeituni na mitende na mizabibu na kila matunda.na bila shaka
katika hayo imo ishara kwa watu wenye kufikiri(kuwa yuko Mwenyezi
Mungu)(11).Na amekutiishieni usiku na mchana .na jua na
mwezi.(vyote vimeumbwa kwa ajili ya maslaha yenu).Na (pia)nyota
zimetiishwa kwa amri yake.Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu
wenye akili(12).Na (akakuumbieni) hivi alivyovitawanya katika ardhi
vya rangi mbali mbali.Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu
wanaosikia mawaidha(13).Na yeye ndiye aliyetiisha bahari ili humo
mule daima kitoweo kipya(samaki),na mutoe humo mapambo
mnayoyavaa(ya lulu na marijani na yaliyo kama haya).na utaona
marikebu zikipasua humo,ili mtafute fadhila zake(kwa kufanya
biashara)na ili mupate kushukuru(14).Na akaweka katika ardhi milima
il(ardhi)isiyumbeyumbe nanyi.Na (akaweka)mito na mabara ili mpate
kuongoza(njia mnazozitaka)(15).Na(ameziweka)alama zingine.Na kwa
nyota(pia)wao wanafuata njia(16).Ati,yule anayeumba(naye ni
Mwenyezi Mungu)atakuwa sawa na wale wasiyoumba?Je
hamkumbuki?(17).Na mkihesabu neema za Mwenyezi Mungu hamtaweza
kuzihisabu.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe(na)Mwingi wa
kurehemu(AN NAHL:3-18) (11 (12)) (13) (14) (15) (16) (17) (18) (19)
(20) (21) (22) Ambao watarithi pepo;wakae humo milele(11).Na kwa
yakini tulimuumba mwanadamu kwa udongo ulio safi(12).Kisha
tukamuumba kwa tone la manii,(mbegu ya uzazi)lililowekwa katika
makao yaliyohifadhika(13).Kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande la
damu,na tukalifanya pande la damu hilo kuwa pande la nyama,kisha
tukalifanya pande la nyama hilo kuwa mifupa,na mifupa tukaivika
nyama,kisha tukamfanya kiumbe kingine.Basi ametukuka Mwenyezi Mungu
Mbora wa Waumbaji(14).Kisha hakika nyinyi baada ya hayo ni wenye
kufa(15).Kisha hakika nyinyi siku ya kiama mtafufuliwa(16).Na kwa
yakini tuliziumba juu yenu njia,(mbingu)saba.Nasi hatukuwa kwa
(hivi) viumbe (vyetu) ni wenye kughafilika(17).Na tumeteremsha
kutoka mawinguni maji kwa kiasi,na tukayatuliza
ardhini,(tukayahifadhi ndani ya ardhi).Na bila shaka sisi ni wenye
uweza wa kuyaondoa(18).Kwa maji hayo tukakufanyieni bustani za
mitende na mizabibu;mnapata humo matunda mengi,na katika hayo
mnakula(19).Na (kwa hayo akakufanyieni vile vile)mti utokao katika
mlima wa Sinai,unatoa mafuta na kuwa kitoweleo kwa walao.(nao ni
mzaituni)(20).Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika
wanyama:Tunakunywesheni katika vile vilivyomo matumboni mwao,na
mnapata katika hao manufaa mengi,na baadhi yao mnawala(21).Na juu
yao na juu ya marikabu mnabebwa(AL-MUMINUN:11-22)
(43) (44) (45) Je,huoni kuwa Mungu anayaendesha mawingu,kisha
huyaambatanisha pamoja, kisha huyafanya mirundo?Basi utaona mvua
ikitoka katikati yake;Naye huteremsha-kutoka juu katika milima ya
mawingu-mvua ya mawe,akamsibisha naye amtakaye na kumuepusha nayo
amtakaye;hukurubia mwanga wa umeme wake kupofoa macho(43).Mwenyezi
Mungu hubadiisha usiku na mchana;(baada ya mchana ukaja usiku na
baada ya usiku ukaja mchana);bila shaka katika hayo imo dalili kwa
wenye busara(ya kuonyesha hikima ya Mwenyezi Mungu)(44).Na Mwenyezi
Mungu amemuumba kila mnyama kwa maji(maji ndiyo asili ya viumbe
vyote).Wengine katika hao huenda kwa matumbo yao,na wengine wao
huenda kwa miguu miwili,na wengine wao huenda kwa mine;Mwenyezi
Mungu huumba ayatakayo.Hakika Mwenyezi Mungu Anao uweza juu ya kila
kitu(AN-NUR:43-45)
(45) (46) (47) (48) (49) (50) (51) (52) (53) (54) Jee,hukuona
Mola wako jinsi alivyokitandaza kivuli?Na angalitaka bila shaka
angekifanya kitulie tuli,(hakipunguki hakiongezeki);kisha
tumelifanya jua liwe dalili juu yake(45).Kisha tunakivulia kwenu
kidogo kidogo (mpaka kinaondoka kabisa)(46).Naye ndiye
aliyekufanyieni usiku kuwa nguo(la kukugubikeni),na usingizi kuwa
kama kufa,na akaufanya mchana uwe ndiyo kama kufufuka(47).Naye
ndiye azitumaye pepo kuwa habari njema kabla ya(kufika) Rehema
yake(ya mvua);na tunayateremsha kutoka mawinguni maji
safi(kabisa)(48).Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyokufa na
tuwanyweshe baadhi ya tuliowaumba;(nao ni)wanyama na watu
wengi(49).Na kwa yakini tunaigawa (hii mvua)baina yao(mara kwa
mara)ili wakumbuke;lakini watu wengi wanakataa ila kukufuru
tu(50).Na kama tungetaka tungewapelekea katika kila mji muonyaji
wao).(Lakini tumemleta Nabii Muhammad kwa watu wote)(51).Basi
usiwatii makafiri,na ushindane nao kwa(Quran)hii mashindano
makubwa(52).Naye (mwenyezi Mungu)Ndiye anayeziunganisha bahari
mbili;hii ni tamu,inayoondosha kiu,nahii ni yenye chumvi,kali;na
akaweka kinga kati yao na kizuizi kizuiacho(zisiharibiane ila pale
kiasi cha kukutana tu)(53).Naye ndiye aliyeumba mwanadamu kwa
maji,kisha akamfanyia nasaba(ya damu) na ujamaa wa ndoa.Na Mola
wako ni Mwenye uweza(wa kila jambo)(AL-FURQAN:45-54) (17) (18) (19)
(20) (21) (22) (23) (24) (25) (26) (27) Basi mtukuzeni Mwenyezi
Mungu mnapoingia katika nyakati za usiku(kwa kusali Magharibi na
Isha)na mnapoingia katika asubuhi(kwa kusali sala ya
alfajiri)(17).Na sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu mbinguni na
ardhini.Na (mtukuzeni)wakati wa alasiri na mnapoingia wakati wa
Adhuhuri(18).Hukitoa kilicho hai katika kilicho kufa,na hukitoa
kilicho kufa katika kilicho hai,na huihuisha ardhi baada ya kufa
kwake.Na hivyo ndivyo mtakavyofufuliwa(19).Na katika Ishara zake(za
kuonyesha uweza wake)ni huku kukuumbieni kwa udongo,kisha mumekuwa
watu mnaoenea(kila mahali)(20).Na katika Ishara zake(za kuonyesha
ihsani zake juu yenu)ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi
yenu ili mupate utulivu kwao,naye amejaalia mapenzi huruma baina
yenu.Bila shaka katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiri(21).Na
katika Ishara zake(za kuonyesha uweza wake)ni kuumba mbingu na
ardhi,na kukhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na(mengine yenu,na
hali ya kuwa muumbaji ni Huyo Huyo Mmoja).Kwa yakini katika haya
zimo Ishara kwa wenye ujuzi(22).Na katika Ishara zake(za kuonyesha
hikima yake) ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana,na kutafuta
kwenu fadhila Yake.Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu
wanaosikia(23).Na katika Ishara Zake(za kuonyesha nguvu zake) ni
kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni)hofu na tamaa ya(kuja mvua),na
kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni,kwayo huifufua ardhi
baada ya kufa kwake.Bila shaka katika haya Zimo Ishara kwa watu
wanaofahamu(24).Na katika Ishara zake (za kuonyesha uweza wake)ni
kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake;kisha atakapokuiteni
wito mmoja tu,(nyote) mtatoka ardhini(25).(Vyote) vilivyomo
mbinguni na ardhini ni vyake,na vyote humtii yeye(26).Na yeye ndiye
aliyevianzisha viumbe na ndiye atakayevirudisha(mara nyingine)na
(jambo) hili ni rahisi zaidi kwake;na ndiye mwenye sifa nzuri
mbinguni na katika ardhi,na ndiye Mwenye Nguvu,Mwenye Hikima
(AR-RUM:17-27) (1) (2) (3) (4) (5) (6) (7) (8) (9) (10) (11) (12)
(13) (14) (15) (16) (17) (18) (19) (20) (21) (22) (23) (24) (25)
(Mwenyezi Mungu) Mwingi wa rehema(1).Amemfundisha
Qurani(2).Amemuumba mwanadamu(3).Akamfundisha kunena(4).Jua na
mwezi(huwenda) kwa hisabu(yake)(5).Na miti midogo na mikubwa yote
inamnyenyekea(Mwenyezi Mungu) (6) .Na mbingu amezinyanyua juu na
ameweka uadilifu(insafu)(7).Ili msidhulumu katika kupima (na
mengineyo)(8).Basi pimeni kipimo kwa haki wala msipunguze
mizani(9).Na ardhi ameiweka(ameitandaza) kwa ajili ya
viumbe(10).Humo yamo matunda na mitende yenye
matunda(mafumba)(11).Na vimo vyakula vilivyo punje punje zenye
makapi,na mimea yenye harufu nzuri(12).Basi nyinyi viumbe namna
mbili-(binadamu na majini)-ipi katika neema ya Mola wenu
mnayoikanusha(kuwa si neema yake)?(13).Amemuumba mtu kwa udongo wa
mfinyanzi(utoao sauti) kama vyombo vya udongo(14).Na akawaumba
majini kwa ulimi wa moto(15).Basi ipi katika neema ya Mola wenu
mnayoikanusha (kuwa si neema yake)?(16).Mola wa mashariki mbili na
Mola wa magharibi mbili(17). Basi ipi katika neema ya Mola wenu
mnayoikanusha (kuwa si neema yake)?(18).Anazikutanisha bahari
mbili(ya maji ya chumvi na ya maji ya tamu)(19).Baina yao kuna
kizuizi,haziingiliani(zikaharibiana kabisa kabisa)(20). Basi ipi
katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema
yake)?(21).Katika hizo bahari mbili hutoka lulu na marijani(22).
Basi ipi katika neema ya Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema
yake)?(23).Na yako katika Amri Yake haya yaliyotengenezwa yakawa
yanakwenda baharini;utadhani milima(24). Basi ipi katika neema ya
Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)? (AR-RAHMAN:1-25) (6)
(7) (8) (9) (10) (11) (12) (13) (14) (15) (16)Je!Hatukuifanya ardhi
kuwa tandiko?(6).Na milima kuwa kama vigingi(vya ardhi)(7).Na
tukakuumbeni wanaume na wanawake(8).Na tukaufanya usingizi wenu
kama kufa(9).Na tukaufanya usiku kama nguo (mnalofunikwa)(10).Na
tukaufanya mchana kama kufufuka(11).Na tukajenga juu yenu (mbingu)
saba madhubuti(12).Na tukaifanya taa ingarayo na yenye joto
kubwa(13).Na tukateremsha maji yaangukayo kwa kasi kutoka
mawinguni(14).Ili kwayo Tuoteshe (vyakula vilivyo) chembe chembe na
mimea(mengine)(15).Na mabustani yenye miti iliyosongana.(Basi sisi
tuliofanya yote haya inatushinda kufufua viumbe?) (AN-NABAA:6-16)
(27) (28) (29) (30) (31) (32) (33) Je,nyinyi ni wenye umbo la nguvu
zaidi au mbingu?Yeye amezijenga.(27).Akainua kimo chake na
akazitengeneza vizuri(28).Na akautia giza usiku wake na
akautokezesha mchana wake(29).Na ardhi baada ya hayo
Akaitandaza(30).Akatoa ndani yake maji yake na malisho yake(31).Na
milima akaisimamisha(32).(kafanya haya yote) kwa ajili ya
kuwastarehesheni nyinyi na wanyama wenu.(Basi aliyefanya yote haya
si muweza wa kufufua?)(AN-NAZIAT:27-33
(24) (25) (26) (27) (28) (29) (30) (31) (32)Hebu mwanadamu na
atazame chakula chake(24).Hakika sisi tume mimina maji kwa
nguvu(kutoka mawinguni)(25).Tena tukaipasua pasua ardhi(26).Kisha
tukaotesha humo(vyakula vilivyo) chembe chembe(27).Na mizabibu na
mboga(28).Na mizeituni na mitende(29).Na mabustani,(mashamba) yenye
miti iliyosongana bara bara(30).Na matunda na malisho(31).Kwa ajili
ya kukustarehesheni nyinyi na wanyama wenu(32).(ABASA:24-32) Na
jumla ya wanaadamu ni wenye kukubali ubwana wake Allah,kwamba yeye
ni muumbaji ,mfalme,mpangaji wa mambo.Hata washirikina wakiarabu
(makureshi) Mwenyeezimungu ameelezea kukubali kwao kwa ubwana
wake,katika sehemu kadha wa kadha katika Quran,kama alivyosema:
(84) (85) (86) (87) (88) (89) Sema:Ni ya nani ardhi na vilivyomo
ndani yake,kama nyinyi mnajua kitu?(84).Watasema:Ni ya Mwenyezi
Mungu.Sema:Basi je,hamkumbuki(kuwa Mwenyezi Mungu ni
muweza?(85).Sema:Ni nani Mola wa mbingu saba na Mola wa Arshi
kuu?(86).Watasema:Ni vya Mwenyezi Mungu.Sema:Basi
je,hamumuogopi?(87).Sema:Ni nani mkononi Mwake umo ufalme wa kila
kitu,Naye ndiye alindaye,na hakilindwi (chochote) Kinyume Naye,kama
mnajua(jambo nambieni hili)(88).Watasema:(Uweza huo) ni wa Mwenyezi
Mungu.Sema:Basi vipi mnadanganywa(na shetani
mkadanganyika?(AL-MUMINUN:84-89)
Na kama alivyosema:
(9)Na ukiwauliza:Ni nani aliyeziumba mbingu na ardhi?Kwa yakini
watasema:Ameziumba (Mwenyezi Mungu)-Mwenye
nguvu,Mjuzi(AZ-ZUKHRUF:9),Ila kulitokea upotevu katika baadhi ya
vipote tofauti tofauti ambavyo walishirikisha katika Ubwana
wake,mfano;1-Thanawi na Maanawiya katika majusi wenye kusema kwamba
Ulimwengu una waumbaji wawili ,mungu wa muangaza mwenye kuumba
kheri,na mungu wa giza-mwenye kuumba shari,na haya mapote
wanakubaliana kwamba muangaza ni bora kuliko giza , lakini
wanatafautiana katika giza ,Jee ni la tangu?au limezuka?
2-pili wakristo wenye kusema waungu watatu, wanamfanya mungu
mmoja ni misingi mitatu kwa madai yao;baba,mwana ,roho
mtakatifu.3-Baadhi ya washirikina wakiarabu (wakati wa
ujahiliya),wakiitakidi kwamba waungu wao wanaweza kuleta manufaa
Fulani au madhara Fulani,au ni wenye kupanga mambo Fulani .
4-kadaria wakanushaji wa kadari, wenye kusema kwamba mwanadamu
yuwaumba vitendo vyake,mwenyewe bila ya uumbaji wa Allah.
Na upotevu wote ni wenye kupingwa na hoja za kimaumbile
,kiakili,kwa hisia,na za kisharia na kwamba hoja hizi
zinathibitisha upweke wake Allah (alietukuka ) katika
kuumba,kumiliki,na kuamrisha.Amesema Allah: (91)Mwenyezi Mungu
hakujipatishia mtoto wala hakuwa pamoja Naye Mungu (mwingine) .
Ingekuwa hivyo basi kila mungu angaliwachukua aliowaumba;na baadhi
yao wangaliwashinda wengine(kwani lazima wangepigana kwani fahali
wawili hawakai zizi moja).Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa
wanazomsifu(nazo,zisizokuwa ndizo)(AL-MUMINUN:91)Kwani mola wa haki
lazima awe muumbaji mtendaji atakalo,na lau kama angekua na
mshirika angekuwa huyo mshirika pia akiumba na akifanya!na lingekua
moja katika mawili;*Ima kila Mungu angeenda na viumbe wake na awe
peke yake katika ufalme wake na uwezekano huu wakataliwa na
mpangilio wa ulimwengu ulivyo.
*Na ima ingetokea kushindana na kutawala juu ya mwengine, kama
mmoja ataka mwili ushughulike na mwengine ataka mwili utulie,
angetaka mmoja ahuishe kitu na mwengine ataka akifishe, basi ima
yatokee matakwa yote yao mawili au ya mmoja wao au yasitokee ya
wote, na uwezekano wa kwanza na wa tatu haiwezekani kwa sababu ni
kinyume,, hayawezi kukusanyika wala kuondoka, basi lazima itokee
uwezekano wa pili (nao ni kutokea matakwa ya mmoja wao) na yule
ambaye yatatokea matakwa yake basi yeye ndie Mungu mwenye uweza na
mwengine hafai kupata uungu basi haya yanapelekea kuthibitisha
Mungu mmoja na muumbaji mmoja na mfalme mmoja na mpangaji wa mambo
mmoja.
Tatu: kuamini uola wake Allah: nayo ni kuitakidi kwa kukata
kwamba Mwenyezi Mungu ndio mola wa haki anayesthiki ibada pekee
pasi na mwengine.Na maana ya ILLAH mola yaani ni mwenye kuabudiwa
ambae nyoyo zinamfanya mungu kwa mahaba na kumtukuza. Na hakika ya
ibada ni ukamilifu wa mapenzi kwa Allah pamoja na ukamilifu wa
kujidhalilisha kwake na kunyenyekea na kumtukuza na haya yote
hayawi ila kwa Allah pekee na imekuja imani hii kwa shahada kubwa
kutona na kwa Allah ( mkubwa mwenye kushuhudia) kwa kikubwa
kishuhudiwacho amesema Allah: (18)Mwenyezi Mungu ameshuhudia ya
kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye tu.Na malaika na wenye
elimu,(wote wameshuhudia hayo);(Yeye) Ndiye Mwenye kusimamisha
uadilifu.Hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye,Mwenye nguvu(na)
Mwenye hikima(AALI IMRAN:18)Na akasema:
(163)Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu,hakuna anayestahiki
kuabudiwa ila Yeye ambaye ni Mwingi wa rehma mwenye kurehemu(AL
BAQARAH:163)Na hakika ameumba Allah viumbe vyake vyote, kwa ajili
ya kumuabudu yeye pamoja ya kwamba Mwenyezi Mungu amejitosha nao
(hahitaji chochote kutoka kwa viumbe) amesema Allah:
(56) (57)Sikuwaumba majini na watu ila wapate
kuniabudu(56).Sitaki kwao riziki wala Sitaki wanilishe(
ADH-DHAARIYAT:56-57)
Na Allah ametuma mitume yake yote kwa watu ili waitikie imani
hii,na wawalinganie watu katika kumpwekesha katika ibada na kuondoa
shirki amesema Allah:
(36)Na bila shaka tulimpeleka Mtume katika kila uma ya
kwambaMuabuduni Mwenyezi Mungu na mwepukeni (Ibilisi) muovu.Basi
wako miongoni mwao ambao Mwenyezi Mungu amewaokoa,na wako miongoni
mwao ambao upotofu(upotevu) umethubutu juu yao.Basi tembeeni katika
ardhi na mwangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliokadhibisha(AN
NAHAL:36)Wakaanza kuwalingania jamaa zao kwa kusema: (75)Wakasema
wakuu wa kaumu yake waliotakabari,kuwaambia wale walio dhaifu wenye
kuamini miongoni mwao:Je,?Mnaitakidi ya kwamba Saleh
ametumwa(amepewa Utume) na Mola wake?Wakasema:Hakika tunayaamini
yale aliyotumwa(kuyafikisha)(AL AARAF:75)Na akasema Allah:
(25) Na hatukumtuma kabla yako Mtume yoyote ila tulimfunulia ya
kwamba hakuna aabudiwaye ila Mimi.basi Niabuduni(AL-ANBIYAA:25)Na
kupatikaniwa hili (kumpwekeshea Allah ibada) inalazimu kumfanyia
Allah sampuli zote za ibada yeye pekee, na yoyote atakae fanya
ibada yoyote kwa mwengine asie kuwa Allah basi huyo atakuwa
mshirikina na atakuwa kafiri.Nazo hizo ibada ziko sampuli
tofauti:
1.Ibada za kimoyo; kama mapenzi, amesema Allah:
(165)Na katika watu kuna wanaofanya waungu wasiyekuwa Mwenyezi
Mungu.Wanawapenda kumpenda Mwenyezi Mungu.Lakini walioamini
wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana.Na laiti waliodhulumu nafsi
zao wanaijua(balaa watakayoipata) watakapoiona adhabu(siku hiyo ya
Kiyama),kwa kuwa nguvu zote ni za Mwenyezi Mungu(siku hiyo-hakuna
masanamu wa kuwashufaia wala mengineyo)na kuwa Mwenyezi Mungu ni
mkali wa kuadhibu(AL BAQARAH:165)Na kuogopa amesema Allah:
(175)Basi msiwuogope;bali niogopeni Mimi mkiwa
waislamu(kweli)(AALI IMRAN:175)Na kutaraji amesema Allah:
(110)Waambie:Bila shaka mimi ni binadamu kama nyinyi (isipokuwa
nimeletewa wahyi tu,ndiyo tafauti yangu).Ninaletewa wahyi ya kwamba
Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu.Anayependa kukutana na (jaza ya) Mola
wake na basi afanye vitendo vizuri wala asimshirikishe yoyote
katika ibada ya Mola wake(AL-KAHF:110)Na kutegemea kwake Allah:
(23)Na tegemeeni juu ya Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wenye
kuamini(AL MAIDA:23)
Na uzuri wa moyo ndio asili ya uzuri wa mwili kama ilivyokuja
katika hadithi ((Juweni na kutanabahi! Ya kwamba katika mwili kuna
kipande cha nyama kikitengenea (kikiwa kizuri) umetengenea mwili
wote na kikiharibika umeharibika mwili wote. Juweni! Kipande hicho
ni moyo)) (Bukhari na Muslim).
2.Ibada za kauli( zenye kutekelezwa na ulimi), zenye
kutamkwa,kama dua amesema Allah:
(18)Na kwa hakika misikiti (yote) ni ya Mwenyezi Mungu,basi
msimuabudu yoyote pamoja na Mwenyezi Mungu(AL-JINN:18) Na kutaka
kuhifadhiwa amesema Allah: (1)Sema:Ninajikinga kwa Mola wa
ulimwengu wote(FALAQ:1)
(1)
Sema:Ninajikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea watu(NAAS:1)Na kutaka
kuokolewa amesema Allah: (9)(Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada
kwa Mola wenu,naye akakujibuni kuwa:Kwa yakini mimi nitakusaidieni
kwa Malaika elfu moja watakaofuata mfululizo(wanaongezeka tu). (AL
ANFAL:9)
3.Ibada za kimwili kama swala ,kuchinja, amesema Allah:
(162)Sema:Hakika sala yangu, na Ibada zangu(zote nyingine) na uzima
wangu,na kufa kwangu;(zote)ni kwa Mwenyezi Mungu.Muumba wa
walimwengu wote.(Likinisibu jambo limenisibu kwa kutaka Mwenyezi
Mungu si kwa kutaka viumbe vyake.Na yote ninayoyafanya nayafanya
kwa ajili yake (AL AN-AM:162) (2)Basi Sali kwa ajili ya Mola wake
na uchinje(kwa ajili ya Mola wako).(Na kila utakalolifanya lifanye
kwa ajili ya Mola wako,siyo mizimu wala mapango wala
makaburi)(KAWTHAR:2)4-Ibada za mali kama kutoa kwa ajili ya
ibada,kama zaka swadaka,nyasia,wakfu ,vipoa,(zawadi ambazo mtu
anatoa) amesema Allah: (99)Na katika Mabedui hao wako wanaomuamini
Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho,na wanaitakidi kuwa wanayoyatoa
ndiyo(sababu ya) kuwasogeza kwa Mwenyezi Mungu,na za (kupatia) Dua
ya Mtume.Sikieni!Ni hakika hayo (kweli kuwa ni) mambo ya kuwasogeza
kwa Mwenyezi Mungu .Mwenyezi Mungu atawaingiza katika Rehema
Yake.Bila shaka Mwenyezi Mungu ni mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa
Kurehemu(AT TAWBA:99) Na kulisha chakula amesema Allah: (8) (9) Na
huwalisha chakula masikini,mayatima na wafungwa,na hali ya kuwa
wenyewe wanakipenda(chakula hicho)(8).(Husema wenyewe katika nyoyo
zao wanapowapa chakula hicho):Tunakulisheni kwa ajili ya kutaka
radhi za Mwenywzi Mungu (tu) hatutaki kwenu malipo wala
shukurani(AD-DAHR:8-9) Na kuamini kwa uola wake Allah inalazimu
kuamini ubwana wake na yanayokusanywa na hayo.kwani yule
anayekubali kwamba Mwenyeezimungu ndio muumbaji mfalme mpangaji wa
mambo lazima akubali uola wake na ampwekeshe katika ibada.Na hoja
hii aliisimamisha mwenyeezimungu kwa washirikina kwa kukubali kwao
ubwana wake na kukataa uola wake,katika sehemu tofauti tofauti
katika kitabu chake Allah:mfano (21) (22)Enyi watu!Mwabuduni Mola
wenu ambaye amekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu,ili mpate
kuokoka(21).(Mwenyezi Mungu) ambaye Amekufanyieni hii ardhi kuwa
kama busati(mliotandikiwa mstarehe),na mbingu kuwa kama paa,na
akateremsha maji kutoka mawinguni,na kwa hayo Akatoa matunda yawe
riziki kwenu.Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika,na hali
nyinyi mnajua(kuwa hana mshirika)(AL BAQARAH:21-22) na akasema:)
(31) (32)Sema:Ni nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni (kwa kuleta
mvua) na katika ardhi (kwa kuotesha mimea)?Au ni nani anayemiliki
masikio(yenu) na macho(yenu)?Na nani amtoaye mzima katika wafu na
kumtoa mfu katika mzima?Na nani atengezaye mambo yote? Watasema:Ni
Mwenyezi Mungu.Basi sema:Je!Hamuogopi?(Mnawaabudu wengine pamoja
naye)!(31).Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu,Mola wenu wa haki.Na ni
nini kiko baada ya (kuacha) haki,isipokuwa upotofu(upotovu)?Basi
mnageuzwa wapi?(YUNUS:31-32
NA AKASEMA:
(59) (60) (62) (63) (64) Sema:Sifa njema ni za Mwenyezi Mungu,na
amani iwaendee watumwa wake aliowachagua.Je,Mwenyezi Mungu ni Bora
au wale wanaowashirikisha(na Mwenyezi Mungu ndiyo Bora)?(59).Au
Yule aliyeziumba mbingu na ardhi,na akakuteremshieni maji kutoka
mawinguni(siye bora?).Na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye
kupendeza(mashamba yenye kupendeza).Nyinyi hamna uweza wa kuiotesha
miti Yake hii.Je,yuko Mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu?Bali
hao(makafiri) ni watu wenye kwenda upogo,(kwenda upande)(60).Au
Yule aliyefanya ardhi kuwa mahali matulio(yenu),na akaweka ndani
yake mito na akaiweka milima,na akaweka kizuizi baina ya bahari
mbili,(bahari ya tamu na bahari ya chumvi,siye bora?).Je,yuko mungu
pamoja na Mwenyezi Mungu?Basi wengi katika wao
hawajui(jambo,wanajifuatia ovyo ovyo tu)(61).Au Yule anayemjibu
Yule aliyedhikika amwombapo na kuondoa dhiki (yake) na kukufanyeni
wenye kuendesha dunia (siye bora?).Je,yuko mungu pamoja na Mwenyezi
Mungu?Ni kuchache kuwaidhika kwenu(62).Au Yule anayekuongozeni
katika giza la bara na bahari,na azipelekae pepo kuleta habari
njema kabla ya Rehema Zake,(kabla ya kuja mvua,siye bora?).Je,yuko
mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Mwenyezi Mungu ametakasika na hao
wanaowashikirikisha naye(63).Au Yule aliyeanzisha viumbe,kisha
atavirudisha,na anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi,
(siye bora?)Je,yuko mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?Sema:Leteni
dalili zenu ikiwa mnasema kweli (kuwa yuko mungu mwengine pamoja na
Mwenyezi Mungu).(AN-NAML:59-64) Kwahivyo Allah akawasimamishia hoja
kwa kukubali kwao kumpwekesha Allah katika ubwana wake na kukataa
kumpwekesha katika uola wake.Pia mwenyeezimungu akavunja uungu wa
wola wao kwasababu hawasifiki na sifa zozote katika sifa za
ubwana(kama kuumba,kutoa rizki na sifa nyenginezo) Amesema
Allah:
(191) (192)) (193) (194) (195) (196) (197) (198Wanawashirikisha
(na mungu) wale ambao hawaumbi kitu,hali wao wameumbwa?(191).Wala
hawawezi kuwasaidia(hao wanaowaabudu),wala hawawezi kujisaidia
(wenyewe) nafsi zako?(192).Na kama hao (mnaowashirikisha na
Mwenyezi Mungu) mkiwaita katika uongofu hawatakufuateni(kwani
hawasiki lolote wala hawatambuichochote).Ni mamoja kwenu ikiwa
mtawaita au mtanyamaza kimya(hawana habari hawana lao
jambo)(193).Hakika wale mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni
waja(watumwa) kama nyinyi(bali nyinyi bora zaidi kuliko wao.Nyinyi
mna midomo ya kusemea,wao hawana).Hebu waiteni,nao wakuiteni,ikiwa
mnasema kweli(kama wao ni bora na wanayo haya)(194).(Nyinyi mna
miguu ya kwendea).Je,wao wana miguu ya kwendea?Au wanayo mikono ya
kushikia?Au wanayo macho ya kuonea?Au wanayo masikio ya
kusikilizia?Sema Nabii Muhammad uwaambie washirikina hawa): Waiteni
hao mnaowashirikisha na Mungu kisha nifanyieni kila vitimbi(vya
kuniangamiza) wala ,msinipe nafasi yoyote(mara moja niangamizeni
kama kweli wanaweza). (195).Mlinzi wangu wa(kunihifadhi) ni
Mwenyezi Mungu Aliteremsha kitabu(hiki kitukufu),naye ndiye
awalindae wafanyao wema(wote,si mimi tu).(196).Na wale mnaowaabudu
badala yake hawana uweza wa kukunusuruni wala wa kujinusuru
(wenyewe) nafsi zao(197).Na kama mkiwaita katika uongofu
hawasikii;na unawaona wanakutazama,lakini hawaoni.(masanamu
utayaona yamekodoa macho lakini kuona hapana)(AL AARAF:191-198)Na
akasema: (3) Na badala ya Mwenyezi mungu (wa haki),(wale makafiri)
wameshika miungu ambao hawaumbi chochote ila wao ndio
walioumbwa,wala hawajimilikii(kujiondoshea)
dhara wala(kujivutia)nafuu,wala hawamiliki mauti (kufisha)wala
uhai wala kufufua(alfurqan-3)na akasema:
( 22( (23)Sema:Waiteni mnaowadai uungu kinyume cha Mwenyezi
Mungu ;(wakusaidieni;hawawezi kukusaidieni kitu);hawamiliki(hata)
uzito wa mdudu chungu mbinguni wala ardhini,wala hawana ushirika(wa
Mungu);katika hizo(mbingu wala ardhi);wala Yeye hana msaidizi
miongoni mwao(22).Wala hautafaa uombezi mbele Yake(Mwenyezi Mungu )
ila kwa Yule aliyempa idhini.Hata inapoondolewa hofu nyoyoni
mwao,husema:Mola wenu amesema nini?.(Na wao) huwaambia:(Amesema
maneno ya) haki,Naye ndiye aliye juu,Mkubwa.(SABA:22-23)
Na ndio maana ikawa shirki katika ibada ni katika dhambi kubwa
na ni katika makosa makubwa ,amesema Allah:
(13)(wakumbushe),Luqumani alipomwambia mwanawe,na hali ya kuwa
anampa nasiha.Ewe mwanangu!Usimshirikishe Mwenyezi Mungu.maaana
shirki ndiyo dhuluma kubwa(LUQMAN:13)Na katika hadithi
iliyopokelewa na bukhari na muslim,amesema mtume(Sallallahualayhi
wasallam) jee nisiwajulisheni juu ya dhambi kubwa?
tukasema(maswahaba) kwani!ewe mtume wa
mwenyeezimungu,akasema:kumshirikisha Mwenyeezi
mungu..................hadith.na aliwauliza mtume (Sallallahualayhi
wasallam) ni dhambi gani kubwa?akasemani kumfanyia mwenyezimungu
mshirika na yeye ndie aliekuumba{bukhari na muslim}
Mweenyezimungu akaiwekea shirki kwasababu ya ukubwa ya uovu wake
hukmu za kidunia na za kiakhera,katika hizo;
1-kutosamehewa madhambi yao(washirikina) amesema Allah:
(48Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa;na husamehe
yasiyokuwa haya kwa amtakaye.Na anyemshirikisha Mwenyezi Mungu bila
shaka amebuni dhambi kubwa(AN NISAA:48)2-kuharamishwa kuingia pepo
na kuketi motoni milele. Amesema Allah:
(72) Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu,hakika Mwenyezi Mungu
atamharimishia pepo,na mahali pake(patakuwa) ni motoni.Na madhalimu
hawatakuwa na wa wasaidizi(wa kuwasaidia siku ya Kiama)(AL
MAIDAH:72)
3-Kupomoka matendo yao yote mema.Amesema Allah:
(65)Na kwa hakika yamefunuliwa kwako na kwa wale waliokuwa kabla
yako(maneno haya):-Kama ukimshirikisha(Mwenyezi Mungu) bila shaka
amali zako zitaruka patupu(hutazipatia thawabu japo ni amali
njema); na lazima utakuwa miongoni mwenye hasara.(AZ-ZUMAR:65) Na
ile miezi4-kutohifadhiwa damu zao na mali yao,amesema allah: (5) Na
ile miezi mitukufu itakapokwisha(Ile miezi mine waliyopewa),basi
waueni(piganeni na) washirikina popote muwakutapo,na wakamateni
matekakama wanavyokufanyieni) na wazungukeni na wakalieni katika
kila njia.Lakini wakitubu na wakasimamisha Sala na wakatoa
Zaka,basi iacheni njia yao(waacheni).Hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwingi wa kusamehe (na) Mwenye kurehemu(AT TAWBA:5)Na akasema mtume
(Sallah Alaihi Wasalam):(( Nimeamrishwa niwapige vita watu mpaka
waseme (Lailaha Illa llah), watakapo isema watahifadhika kutokana
na damu zao, mali yao, ila kwa haki yake)) Bukhari na Muslim.Na
wamepotea katika masala haya mapote tofauti tofauti katika
binadamu. Katika hao ni:
1.Wenye kuabudu masanamu pamoja na kutofautiana vitu
wanavyoviabudu katika miti, majini, mawe, binadamu na malaika,
nyota, wanyama na vitu ambavyo anawapoteza navyo shetani.2.Wenye
kuabudu makaburi na wakiweka nadhiri kwa makaburi na kujikurubisha
kwa kuchinja, na wakiomba makaburi hayo kuwapatia manufaa na
kuwaondelea madhara.
3.Wachawi na warogi na makuhani, wale ambao wanaowaabudu majini
kwa sababu majini wanawaletea habari,ima wanawaletea wanavyovitaka
au wanafanya wanavyoambiwa.
Na kwa sababu ya shirki katika ibada mtume (Sallallah Alaihi
Wasalam) alihadhirisha njia za kupelekea hiyo shirki na akafunga
njia zote zitakazo sababisha shirki . katika mfano wa hayo ni:
1.Kuhadharisha kupita mpaka katika watu wema, akasema mtume
(Sallallah Alaihi Wasalam): (( Nawahadharisheni kutokana na kupita
mpaka, hakika waliangamizwa wale waliokuwa kabla yenu kutokana na
kupita mpaka)) Imepokewa na Ahmad na Tirmidhi na Ibni Mayah) na
akasema: (( musini tukuze kupita mpaka kama walivyopita mpaka
manaswara kwa Isa ibn Maryam, hakika mimi ni mja, semeni mja wa
Mwenyezi Mungu na mtume wake)) imepokewa na Bukhari.Na katika
kupita mpaka kwa watu wema ni kutawasali kupitia kwao kuliko
katazwa , nayo hiyo tawasuli iko sampuli mbili:i.Tawasuli ya
kishirikina yenye kumtoa mtu katika uislamu; nayo ni kuomba pasi na
Allah kwa kutaka kutekelezewa na kuondolewa majanga na matatizo
ii.Tawasuli ya kizushi; nayo ni kumuomba Mungu kupitia vitu
ambavyo havijawekwa na sharia, kama kuomba kupitia kwa watu wema,au
jaha zao (vyeo vyao) au heshima zao na mfano wa hayo.Na tawasuli
iliyoko kisharia inakuwa kwa kumuani Mwenyezi Mungu au kupitia kwa
jina katika majina yake au sifa katika sifa zake au kupitia kwa
jambo lake alilofanya au akaomba kuombewa Mungu kwa mtu mwema, kama
alivyosema Umar (Radhiallah anhu) ((Ewe mola tulikuwa sisi
tukipatwa na ukame tukitawasuli kwako kupitia mtume wetu
ukituteremshia mvua, na sisi twatawasuli kwako kupitia Ammi wa
mtume (Abbas) basi tuteremshie mvua)) Bukhari.
2.Akatutahadhirisha kutokamana na kufitinika na makaburi, na
mfano wa hayo ni:
i.Kuyafanya makaburi misikiti, kwani imepokewa na Aisha (R.A)
amesema: alipozidiwa mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) alikuwa
akijifunika shuka juu ya uso wake, akitulia kidogo hukifunguwa
shuka na akasema na yeye yuko hivyo(( laana ya Mungu iwe juu ya
mayahudi na manaswara, wameyafanya makaburi ya mitume yao
misikiti)) akihadharisha waliokuwa wakiyafanya na lau si hivyo
lingedhihiri na kuinuliwa kaburi lake ila yeye aliogopa kutofanywa
msikiti)) Bukhari na MuslimNa akasema: (( jueni walikuwa waliokuwa
kabla yenu wakifanya makaburi ya mitume yao misikiti, juweni
musifanye makaburi misikiti mimi nawakatazeni na hilo)) Muslim.
Na maana ya kufanya misikiti kukusudia humo hata kama
hakukujengwa msikiti kwa sababu msikiti ni sehemu ya
ibada.ii.Kuyajengea makaburi na kupakwa chokaa na rangi na
kuzidishwa mchanga mwengine kwani imepokewa kutoka kwa Abilhayaaj
Alasadi (Mungu amrehemu) alisema: alimwambia Ali bin Abi Twalib
(R.A) je nisikutume kwa lile alilonituma kwalo mtume (Sallallah
Alaihi Wasalam) ya kwamba nisiwache sanamu ila nimelivunja na wala
kaburi lililo inuliwa ila nimeliweka sawa) Muslimna imepokewa
kutoka kwa Jabir bin Abdillahi (R.A) amesema;( amekataza mtume
(Sallallah Alaihi Wasalam) kutia chokaa kaburi, na kukaliwa na
kujengewa)[Muslim], yaingia katika hayo yaliyokatazwa kujenga
makuba juu ya makaburi na kuyapamba na kuyarembesha.
iii.Kufunga safari kuyaendea makaburi; imekatazwa kutokana na
jumla la katazo la mtuma (Sallallah Alaihi Wasalam):musifunge
safari ya ibada ila kuelekea misikiti mitatu; Masjidil Haram
(Makkah), na msikiti wangu huu ( msikiti wa Madina), na msikiti wa
Aqswa (Falastin) Bukhari na Muslim.
iv.Kufanya kaburi lake ni idi ( yani lenye kuzuriwa mara kwa
mara) imepokewa na Abu Daud.
3.Kuhadharisha kujifananisha na washirikina, mayahudi, na
wakristo katika itikadi zao na ibada zao na ada zao zilizo husika
na wao pekee, amesema mtume (Sallallah Alaihi Wasalam):kuweni
kinyume na washirikinaBukhari na Muslim. Na akasema:kuweni kinyume
na majusi imepokewa na Muslim. Na akasema : kuweni kinyume na
mayahudi imepokewa na Abu Daud.
4.Kuhadharisha kutengeneza sura za watu,imepokewa na Aisha ya
kwamba Ummu Salama alimtajia mtume (Sallallah Alaihi Wasalam)
kanisa aliloliona Habashi na sura zilizokuwa zimetengenezwa akasema
mtume (Sallallah Alaihi Wasalam):hao akifa mtu mwema kwao hujenga
juu ya kaburi lake msikiti na wakatengeneza hizo sura hao ndio
viumbe waovu mbele ya Mwenyezi Mungu Bukhari na Muslim.
5.Kuhadharisha kutokana na matamko ya kishirikina, na mfano wa
hayo:
i.Kuapa kwa asiye kuwa Allah kwa dalili ya hadithi Yoyote ambaye
ataapa kwa asiye kuwa Allah kwa hakika amekufuru au
ameshirikishaimepokewa na Tirmidhi.
ii.Kusawazisha katika matakwa ya Allah na matakwa ya kiumbe
dalili yake ni kauli yake mtume (Sallallah Alaihi Wasalam)
alipomwambia mtu aliye mwambia ametaka Mwenyezi Mungu na ukataka
wewe (mtume) akasema mtume umenifanya mimi ni mshirika wa Mwenyezi
Mungu! sema ametaka Mwenyezi Mungu peke yake imepokewa na
Annasai.
iii.Kutegemeza vitendo vya Allah katika ulimwengu kwa asiye kuwa
Allah. Dalili yake imekuja katika hadithi Kudsi: Ama yule mwenye
kusema tumepata mvua kwa nyota fulani na fulani, basi huyo
amenikufuru mimi ameamini nyota Bukhari na Muslim.
6.Kutahadharisha kutokana na matendo ya kishirikina, na mfano wa
hayo:
i.Kuvaa kikuku au uzi katika mkono au katika shingo kwa lengo la
kujikinga kutokana na balaa au kuondoa balaa, dalili yake ni
hadithi ya Imran bin Huswein ya kwamba: mtume (Sallallah Alaihi
Wasalam) alipomuona mtu amevaa chuma katika mkono wake, mtume
(Sallallah Alaihi Wasalam) akamwambia ni nini hii? akasema nimevaa
kujizuia kutokana na ugonjwa akamwambia vua haitokuzidishia ila
ugonjwa kwani lau ukifa na bado unayo hautafaulu kabisa(yaani
huingii peponi) imepokewa na Ahmad na Ibn Hibban.
ii.Kujifunga hirizi, nyuzi zinazotiwa kaure, au nyuzi za kawaida
au vyenginevyo kujikinga kutokana na hasadi. Dalili yake mtume
(Sallallah Alaihi Wasalam) amesema: Yoyote mwenye kujifunga hirizi
basi Mungu asimtimizie mambo yake na yoyote mwenye kujifunga uzi wa
kaure basi Mungu asimpatie utulivu imepokewa na Ahmad na Ibn Hibban
na Hakim, na katika riwaya ilopokelewa na Ahmad na Hakim Yoyote
mwenye kujifunga hirizi basi hakika ameshirikisha na kwa hadithi
Musibakishe katika ngamia uzi uliofungwa (katika shingo zao) ila
umekatwa Bukhari na Muslim.
iii.Zunguo la kishirikina na dawa za mapenzi; kwa hadithi Hakika
zunguo ( la kishirikina) na hirizi na dawa za mapenzi ni shirki
imepokewa na Abu Daud.
iv.Kuchinja katika sehemu za ushirikina imekatazwa kwa neno lake
mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) alipomuuliza mtu aliye weka
nadhiri ya kuchinja ngamia Buwana ( ni jina la sehemu), mtume
(Sallallah Alaihi Wasalam) akamuuliza: Je kulikuwa na sanamu katika
masanamu ya jahiliya ya kiabudiwa? wakasema: hapana akamuuliza
(mtume) Je kulikuwa na idi katika idi zao wakasema hapana akasema
mtume (Sallallah Alaihi Wasalam): Tekeleza nadhiri yako imepokelewa
na Abu Daud.v.Kutowa fali mbaya na kuwa na itikadi kwa wanyama (
kubashiri vibaya ukiona kitu au mnyama fulani) kwa hadithi ya Ibn
Masud ameinyanyuwa kwa mtume (Sallallah Alaihi Wasalam) amesema:
Kutoa fali mbaya kwa ndege ni shirki imepokewa na Abu Daud na
TirmithiNNE: KUAMINI MAJINA YAKE NA SIFA ZAKE ALLAH.
Nayo ni kuamini kwa kukata bila ya shaka kwamba Allah ana majina
mazuri na sifa tukufu, na kumthibitishia aliyojithibitishia
mwenyewe Allah kwenye kitabu chake na aliyomthibitishia mtume wake
katika hadithi zake katika sifa za ukamilifu na sifa za utukufu
bila ya kumtolea mfano wala kumuekea sampuli na kumkanushia Allah
yale aliyojikanushia mwenyewe katika kitabu chake au aliyomkanushia
mtume wake katika hadithi zake, katika sifa za upungufu na za
kasoro, na kuwacha kumfananisha na viumbe bila ya kugeuza wala
kukanusha.amesema Allah: (180)Na Mwenyezi Mungu ana majina
mazuri;mwombeni kwayo.Na wacheni wale wanaoharibu utakatifu wa
majina yake.Karibuni hivi watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda(AL
AARAF:180) (11)Hakuna chochote mfano Wake;Naye ni Mwenye
kusikia,Mwenye kuona(ASH-SHURA:11)Na majina yake Allah na sifa zake
tukufu ni taukifia (yani tunafuata yale yailotejwa katika quran na
sunna pekee) haifai akili pekee kuithibitisha na hasifiwi Allah
isipokuwa sifa alizo jisifu nazo yeye mwenyewe au amemsifu nazo
mtume wake (Sallallah Alaihi Wasalam) . hatuchukuwi isipokuwa
katika quran na hadithi. Basi sifa alizozinyamazia Mwenyezi Mungu
na mtume wake ni lazima tuzinyamazie na kusimama hapo katika
kukanusha na kuthibitisha na kutaka ufafanuzi kwa msemaji
akikusudia maana sahihi itakubaliwa maana na tamko litaridishwa na
akitaja maana ambayo si sawa tamko litarudishwa na maana
pia.amesema Allah: (36)Wala usifuate(ukipita ukiyasema au
ukiyafanya) usio na ilimu (ujuzi) nayo.Hakika masikio na macho na
moyo;hivyo vyote vitaulizwa(BANI ISRAIL:36)Majina yake Mwenyezi
Mungu yamefikia upeo wa uzuri nayo ni majina yenye kumjulisha yeye
Allah na sifa zake. Sifa zake zimekamilika hazina upungufu kwa njia
yoyote,amesema Allah: (27)Na Yeye ndiye aliyeanzisha viumbe na
ndiye Atakayevirudisha(mara nyingine),na(jambo) hili ni rahisizaidi
Kwake;naye ndiye mwenye sifa nzuri mbinguni na katika ardhi,naye
ndiye mwenye nguvu,Mwenye hikima(AR-RUM:2)Nayo ni haki kwa hakika
yake, kwa hivyo ni lazima kuyapitisha vile yalivyo kwa dhahiri
yake, bila ya kuyageuza na haram kuyapotoa kwa kuyakanusha au
kuyafananisha au kuzusha majina ambayo Allah hajajiita nayo
mwenyewe au kuyatumia majina yake kumuitia mwengine.Na ya lazimu
kumuomba kupitia hayo majina katika ibada na katika dua, na
yatakiwa kuyajuwa idadi yake na kuyafahamu maana yake na
kuyafikiria athari zake na kufanya matakwa yake na hiyo ndio elimu
bora kabisa. Zagawanyika sifa zake Allah kulingana na kufungamana
haya majina na Allah vigawanyo viwili:
1.Sifa za dhati yake; nazo ni sifa zenye kushikamana na dhati
yake tukufu; kama uhai,kusikia, kuona, elimu, kudra (uweza),kutaka,
hikma, nguvu na nyenginezo ambazo kwamba hazimkiniki kuepukana nae
Allah.2.Sifa za vitendo; nazo ni sifa zilizofungamana na matakwa
yake na hikma yake, huzifanya atakapo na sampuli atakayo kulingana
na hikma yake kubwa; kama kustawi kwenye arshi, kushuka, kupenda ,
kuchukia, kufurahi, kuona ajabu, na kucheka, kuja na nyenginezo
zilizo kuja katika quran na zilizoswihi katika hadithi.
Katika baadhi ya sifa hizo kama sifa ya kusema ni sifa
zilizofungamana na dhati yake na ni sifa ya kitendo, ni sifa za
dhati yake kulingana na asli ya sifa na sifa ya kitendo kulingana
na maneno yenyewe au husemwa sifa ya tangu na yenye kutokea
kulingana na maneno yenyewe. Na sifa zenginezo huitwa sifa za
habari; nazo ni ambazo ni kuthibitisha hiyo habari moja kwa moja
bila ya kufikiria kwa akili kama sifa ya uso, mikono, macho, mguu
na nyenginezo ambazo zimeswihi habari zake.Katika sifa zake
Mwenyezi Mungu zilizothibiti katika quran na sunna na Ijmaa:i.Sifa
ya kuwa juu (Uluuw) nayo ni sampuli tatu; kuwa juu kwa cheo chake,
ukubwa wa kushinda kwake na kuwa juu kwa yeye mwenyewe. Naye
Mwenyezi Mungu ni mshindi hakuna aliye juu yake katika viumbe wake,
amestawi katika arshi yake juu ya mbingu zake ameepukika na waja
wake hana chochote katika viumbe vyake wala hawana viumbe vyake
chochote katika yeye, ni sifa ya dhati yake (Uluuw).
ii.Sifa ya kustawi; nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu baada ya
kuumba mbingu na ardhi alistawi kwenye arshi yake; kwa maana
alikuwa juu yake na akastawi juu yake, kustawi ambapo uhakika wake
wafungamana na ukubwa wake na utukufu haiwi sawa na kustawi kwa
viumbe, kwa hivyo hii ni sifa ya kitendo.
iii.Sifa ya kusema: nayo ni kwamba Mwenyezi Mungu anazungumza
mazungumzo ya hakika yenye kusikika kwa herufi na sauti, hayafanani
maneno yake na maneno ya viumbe na yakwamba mwenyezi Mungu
anazungumza wakati atakao kwa maneno atakayo kwa sampuli aitakayo
kwa ukweli na uadilifu kwa vilima visivyoisha hakuacha na hajawacha
kusema Mwenyezi Mungu. Kwani ni sifa ya dhati yake kulingana na
asli yake na ni sifa ya kitendo kulingana na maneno.Hizi sampuli za
sifa zote ni haki kwa hakika yake Allah ni lazima kuzithibitisha na
kuzipitisha kama zilivyokuja, na kuzipitisha kwa dhahiri yake bila
ya kuleta sampuli na hili ni jambo ambalo lazima lizingatiwe katika
sifa zote, kuzizungumzia sifa Fulani ni kama kuzizungumzia sifa
zengine zilizobaki, sawa kwa sawa na yoyote atakaye tafautisha
amehukumu bila ya dalili.
Wamepotea katika masala ya majina yake mwenyeezimungu na sifa
zake,mapote tofauti tofauti nayo ni:
1-Watu wa kufananisha wale ambao waliopita mipaka katika
kuthibitisha hayo majina na sifa zake Allah,mpaka wakaingia katika
kumfananisha .Na utata wao katika hilo ni kwamba hilo ndio matakwa
ya dalili za sharia kwasababu mungu huwazungumzia watu kulingana
walivyozoea katika viumbe!Na kuwajibu watu hawa ni kwa njia
kadhaa:
(i)Mwenyeezimungu amekataa kuweko chochote mfano wake au sawa na
yeye au mshirika,kwa aya ambazo ni muhkam(hazina utata)ziko wazi
amesema Allah; (11) Hakuna chochote mfano Wake (ASH-SHURA:11)
(22) Basi msifanyie Mwenyezi Mungu washirika,na hali nyinyi
mnajua(kuwa hana mshirika)(AL BAQARAH:22) (4)Wala hana anayefanana
naye hata mmoja(IKHLAAS:4) Na wala hayawezi maneno yake mwenyeezi
mungu kugongana.(ii)Akili iliosalimika inakataa kusawazishwa Mungu
muumbaji aliekamilika na mja aliyeumbwa aliyempungufu. Basi kama
vile dhati yake Allah haifanani na dhati ya wengine,pia sifa zake
hazifanani na sifa za wengine.iii)Yakwamba mwenyezimungu
amewazungumzia waja kwa wanayo yafahamu kulingana asili ya
maana,wala hailazimishi kushirikiana katika maana ya kiujumla
kusawazisha katika hakika ya sifa na sampuli yake,ikiwa katika
viumbe kukitokea kuwafikiana majina ya viumbe venyewe haimaanishi
kufanana kwa viumbe hawa. Kama tamko la kusikia kuona na uweza,
basi baina ya Mwenyezi Mungu na viumbe ni mbali zaidi2.Watu wenye
kukanusha : wale waliopita mpaka katika kukanusha na utata wao eti
kuthibitisha sifa inalazimu kufananisha, kwa sababu sifa zile
kiumbe pia amesifika nazo basi italazimu tumuepushe nazo muumbaji,
wakathibitisha kuwepo kwake tu Allah bila ya sifa! Na mapote yaliyo
zidi kupita mpaka katika kukanusha ni (karamitwa baatinia) wale
ambao walimkanushuia Mwenyezi Mungu vinyume viwili, kisha (Jahmiya)
wale waliyo kanusha majina na sifa, kisha (Muutazila) wale ambao
walithibitisha majina na wakakanusha sifa zilizo kusanywa na hayo
majina
Kuwajibu haya mapote ni kwa njia kadhaa:
i.Kwamba Mwenyezi Mungu amejithibitishia nafsi yake majina
katika aya ambazo hazina utata, zilizo wazi na kutajwa kwake
kumeshikanishwa na kukanusha mfano wake kama neno lake Allah:
(11)Hakuna chochote mfano Wake ; Naye ni Mwenye kusikia,Mwenye
kuona(ASH-SHURA:11Na wala hayawezi kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu ni
yenye kugongana.ii.Ya kwamba kuthibitisha kuwepo kwake Allah tu
haiwezekani kumsifu kwa sifa ambayo haipo kikweli, bali ni jambo
ambalo lipo katika akili madai yao yanapelekea kukanusha
muumbaji.iii.Kwamba sifa kwa matamshi ya kiujumla kwa fulani
hailazimu kuthibiti sifa hiyo kwa mwengine, bali kila mmoja wao ni
kiungo katika hiyo sifa ya kiujumla kwa sababu sifa ikifunganishwa
na kitu au mtu au ikitegemezwa huondoka kushirikiana kwa nje.
3.Watu wa taawili wale waliyo itakidi kwamba dalili hazijulishi
sifa ambazo ni hakika kwa Allah, wakawa ni wenye kutafuta maana
nyengine ya hizo dalili bila ya hoja sahihi ambayo ya waruhusu
kuondoa maana kutoka katika udhahiri kupeleka katika maana
nyengine, wakiita kupendua kwao maana huku taawili!Kuwajibu hawa ni
kwa njia tafauti:
i.Kwamba Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa nafsi yake na ndio msemaji
kweli na ndio msemaji bora kuliko viumbe wote na
mtume(Sallallahualayhi wasallam) ndio mjuzi zaidi anayemjua Allah
na ndio msemaji kweli na mfasaha katika kusema kwake, na mwenye
kunasihi bora katika umma huu. Kisha atatokeaje mtu adai kutadaraki
(kutaja yaliyo achwa) na Mwenyezi Mungu na mtume wake, na ayafanye
maneno yao ni yenye kuleta utata na upotevu?
ii.Asili katika maneno yoyote ni kuyafahamu vile yalivyo katika
hakika yake, wala haifai kubadilisha maana ila kwa dalili ambayo
itaruhusu kugeuza maana ya hayo maneno na hakuna dalili.
iii.Kwamba mtume (Sallallahualayhi wasallam) amewaelezea watu
yaliyo teremshwa kwao na akafikisha kufikisha kulio wazi, basi
hawezi mtume (s.a.w) awache kuyaeleza mambo haya makubwa na maana
ya hizo sifa kama walivydai hawa wenye kubadilisha maana na kutunga
maana zao.
4.Watu wenye madai ya kutojulikana, wale walioitakidi kwamba
maana ya yale Mwenyezi Mungu aliyojielezea nayo nafsi yake au mtume
aliyo yaeleza maana yake haijulikani, hakuna ajuwae maana ya hayo
isipokuwa Allah wala hakuna mtu aweza kujuwa maana yake na
wanajiita watu hawa (Mufaawidha) wenye kumtegemezea Mungu na njia
yao ni tafwiidh- kumtegemezea Mungu.Kuwajibu hawa na kwa njia
kadhaa:
i.Haiwezekani iwe mlango wa elimu ya yaliyofumgamana na Mungu
ambao ni katika milango muhimu katika dini uwe imefungwa na wala
hakuna dalili wala akili zenye kukufikisha.
ii.Kwamba Allah ameteremsha quran katika ndimi za kiarabu
zilizowazi na akawa amrisha waja wake watie akilini maneno yake na
kuyazingatia na wala hakutoa chochote katika quran, basi hiyo
imejulisha kuwezekana kuwa na elimu ya maana ama sampuli na hakika
yake ni katika vitu vya ghaibu ambavyo elimu yake hutegemezwa kwa
Allah pekee.
iii.Mwenendo huu unapelekea kuwafanya wajinga wale wema
waliotangulia katika umma huu na kuwasifu kama kwamba wao hawajui
kusoma na hawajui kitabu ila ni matamanio tu! Kwao ni kama talasimu
na herufi pekee ambazo hazileti maana yenye kuingia akilini.
KUAMINI MALAIKA.Moja:Ni kuitakidi kwa kukata bila ya shaka
kwamba ni waja waliokirimiwa , waja wema, wenye kunyenyekea Mola
wao, wenye sikitiko hawana chochote katika sifa za uungu wala za
uola, amesema Allah:
(26) (27) (28)Na makafiri wakasema:(Mwenyezi Mungu) mwingi wa
rehema amejifanyia mtoto. Ametakasika :(Mwenyezi Mungu!)bali(hao
Malaika) ni waja wa :(Mwenyezi Mungu)
waliotukuzwa926).Hawamtangulii kwa neno(lake analosema) Nao
wanafanya amri zake(zote)(27). :(Mwenyezi Mungu) anayajua yaliyo
mbele yao(Hao Malaika) hawamuombei (yoyote) ila Yule
anayemridhia:(Mwenyewe Mwenyezi Mungu),nao kwa ajili ya kumuogopa
wananyenyekea(AL-ANBIYAA:26-28)Na akasema: (50)Wanamuogopa Mola wao
aliye juu yao,na wanatenda wanayoamrishwa(AN NAHL:50)Na akasema:
(6)Hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri Zake;na wanayatenda
wanayoamrishwa(yote)(AT-TAHRYM:6)Na akasema: (16)Watukufu,
Wachamungu.(abasa ;16) Na akasema: (40) (41)Na(wakumbushe) siku
atakayowakusanya wote,kasha atawaambia Malaika:Je!Hawa walikuwa
wakikuabuduni?(40).Waseme:umeepukana na kila upungufu!Wewe ndiye
kipenzi chetu,si hao;bali walikuwa wakiwaabudu majini;wengi wao
waliwaamini hao(majini).(34:40-41)
Na akasema: (32)Wakasema(Malaika):Utakatifu ni wako!hatuna ilimu
ila ile uliyotufundisha;bila shaka wewe ndiye Mjuzi na ndiye Mwenye
hikima.(Mwenye kuweka kila kitu mahala pake)(AL BAQARAH:32) Pili:Na
kuitakidi kwamba wao wameumbwa kutokana na nuru ( muangaza), wana
mbawa, katika umbile kubwa sampuli tofauti tofauti, amesema
mtume(Sallallahualayhi wasallam) wameumbwa malaika kutokana na nuru
(muangaza) imepokewa na Muslim na akasema Allah: (1)Sifa zote njema
ni zake Mwenyezi Mungu,Muumba wa mbingu na ardhi,aliyewafanya
Malaika kuwa wajumbe wenye mabawa,mbili mbili na tatu-tatu,na nne
nne.Huzidisha katika kuumba apendavyo.Bila shaka Mwenyezi Mungu ni
Mwenye uweza juu ya kila kitu(FATIR:1)Amesema Abdallah bin Masud
mtume (Sallallahualayhi wasallam) alimuona Jibril katika sura yake
ana mbawa mia sita, kila mbawa ni kiasi cha upeo wa muono, yapomoka
katika mbawa zake vitu vya rangi tafauti tafauti katika lulu na
yakuti.Na akasema Mtume: (Sallallahualayhi wasallam) Nimeruhusiwa
nizungumze kuhusiana na mmoja wa wabebaji wa arshi,baina ya ndewe
ya sikio lake mpaka kwenye bega lake ni mwendo wa miaka mia
saba.Wao ni viumbe wa kweli si nguvu tu za maanawia kama vile
walivyodai baadhi ya watiao shaka.Na malaika ni wengi hakuna ajuaye
idadi yake isipokuwa Mola wao, kwani imepokelewa katika hadithi ya
anas(iliyopokelewa na bukhari na muslim) katika kisa cha miraji,ya
kwamba mtume(Sallallahualayhi wasallam) alinyanyuliwa mpaka katika
baitul maamur katika mbingu ya saba,na ya kwamba wanaswali katika
hiyo nyumba(baitul maamur kila siku malaika elfu sabini,wanapotoka
hawarudi tena mpaka mwisho wake).Tatu:Kwamba wao malaika ni wenye
kupiga swafu wakimsabihi Mwenyezi Mungu,amewapatia Allah ilihamu ya
sampuli ya kumsabihi,na kutekeleza amri zake,na Akawapatia nguvu
kuzitekeleza amri hizo.Amesema Allah:
(164) (165) (166)Na (wanasema malaika katika kujua cheo
chao,kuwa:-)hakuna yoyote miongoni mwenu ila anapo mahali pake
mahsusi(ma-alum).(164).Na kwa yakini katika sisi wako wajipangao
safu(wakasali jamaa)(165).Na wako katika sisi wamtukuzao (Mwenyezi
Mungu kwa kumkanushia sifa zisizokuwa
zake)(AS-SAAFFAT:164-166).
Na akasema: (38)Na kama wakitakabari,(basi Mwenyezi Mungu hana
haja nao) kwani hao (viumbe watukufu)-(Malaika)-walioko kwako Mola
wako wanamsabahi usiku na mchana,wala hawachoki.(Basi kama nyinyi
hamuabudu yadhuru nini?)(HAA MYM SAJDAH:38).
Na akasema: (20)Wanamtukuza usiku na mchana
hawanyongonyei(hawafanyi uvivu)(AL-ANBIYAA:20).Na imepokewa kutoka
kwa Hakimu bin Hizamu (R.a) amesema: tulipokuwa tumeketi mbele ya
Mtume (Sallallahualayhi wasallam) akasema: Mwasikia
ninachosikia?wakasema:Hatusikii cho chote,Akasema (Mtume
(s.a.w)):Mimi nasikia sauti ya mbingu,na wala hailaumuwi kutoa
sauti kwa sababu hakuna shubiri moja ila utapata malaika amesujudu
au amesimama(anafanya ibada)Imepokewa na twabrani na akasema Albani
ni sahihi kwa sharti ya muslim.
Nne:Kwamba wao hawaonekani kwani wao ni ulimwengu wa ghaibu
hawawezi kuhisika kwa hisia yoyote katika dunia kwa mwanaadamu
yoyote ila Yule aliyemtaka Mungu,kama kumuona Mtume wetu jibrili
kwa umbile lake lile aliloumbiwa.Bali hao malaika huonekana
akhera.
Amesema Allah: (22)Siku watakayowaona malaika haitakuwa furaha
siku hiyo kwa wenye makosa,(itakuwa ndiyo siku ya kutolewa roho
zao);na watasema(siku hiyo);(Mungu) Atuepushie mbali adhabu hii
iliyotukabili.(Lakini haitafaa kitu dua hiyo)(AL-FURQAN:22).Na
akasema:
(23)Na malaika wanawaingilia katika kila milango(AR
RAAD:23)Lakini Mwenyezi Mungu amewapatia uweza wa kujigeuza kwa
umbile la wanadamu, amesema Allah:
(17)Na aaweka pazia kujikinga nao.Tukampeleka Mhuisha Sharia
yetu(Jibril)-akajimithilisha kwake(kwa sura ya) binadamu aliye
kamili(MARYAM:17) Na akasema Allah: (69) (70)Na wajumbe
wetu(malaika kwa sura za kibinadamu) walimwendea Ibrahimu kwa
bishara(khabari njema kuwa atazaa na kujukuu na mengine
na)-wakasema:(Salam(alaykum-amani juu yenu).Akasema Ibrahimu:(Juu
yenu pia iwe amani. Na hakukaa (Ibrahimu) ila mara akaleta
ndama(aliyechomwa vizuri juu yam awe ya moto)(69).Basi alipoona
(Ibrahimu) mikono ya(watu) wale haifikilii (chakula kile)
aliwatilia shaka na akawaogopa(akadhani kuwa ni
maadui).Wakasema:Usiogope,hakika sisi tunapelekwa kwa watu wa
Luti(tukawaangamize na tukupe khabari wewe na mkeo,sara,kuwa mtazaa
na kujukuu nabado muhai(HUD:69-70)
Na akasema:
(77) (78)Na wajumbe wetu walipomjia(Nabii)Luti alihuzunika kwa
ajili yao(hao wageni kwa kuona kuwa watataabishwa wageni
hawa.Hawakujua kuwa ni malaika) na akaona taabu kwa ajili yao,na
akasema:Hii ni siku nguvu(kabisa)(77).Wakafika kaumu wake wakamjia
mbio(nyumbani kwake ili wafanye machafu wale wageni).Na kabla ya
haya walikuwa(daima) wakifanya maovu,akasema(Luti)Enyi kaumu
yangu!Hao binti zangu(binti wa umma wangu walioolewa katika nyumba
zenu) ndio wametakasika kwenu(kuwaingilia si waume wenzenu).Basi
Mcheni Mwenyezi Mungu wala msinifedheheshe mbele ya wageni
wangu.Je,miongoni mwenu hakuna mtu muongofu(hata
mmoja)?(HUD:77-78)Walikuwa hao malaika kwa umbile la waume. Pia
alipokuja Jibril (a.s) katika sifa ya mtu mweupe sana mwenye nyele
nyeusi sana na alikuwa mara nyengine akija katika sura ya dihya
alkalbi (r.a).Tano: Kwamba wao malaika wamepewa kazi tofauti
tofauti pamoja na kazi yao ya msingi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu na
kumsabihi katika hizo kazi:
i.Kuteremsha wahyi; nayo ni kazi ya Jibril (a.s) amesema
Allah:
(102)Sema:Roho takatifu(yaani Jibril)ameiteremsha kutoka kwa
Mola wako kwa haki,ili kuwathubutisha wale walioamini,na kuwa
uwongofu na khabari njema kwa waliosilimu(AN NAHL:102)
Na akasema: (192) (193) (194)Na bila shaka hii(Qurani)ni
Uteremsho wa Mola wa Walimwengu wote(192).ameteremsha haya Mhuisha
Sharia mwaminifu,(Jibril)(193).juu ya moyo wako,ili uwe miongoni
mwa Waonyaji(ASH-SHUARAA:192-194)ii.Kuchunga mtoto ( aliye tumboni)
kwa kumtia roho na kumuandikia rizki, mda wake, matendo yake na
atakuwa mwema au muovu.iii.Kumuhifadhi mwanadamu: amesema
Allah:
(11)Ana (kila mtu) kundi (la malaika) mbele yake na nyuma
yake:wanamlinda(na kuyadhibiti wanayoyafanya) kwa amri ya Mwenyezi
Mungu.Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka
wabadili wao yaliyomo katika nafsi zao.Na Mwenyezi Mungu
anapowatakia watu adhabu hakuna cha kuwazuia wala hawana Mlinzi
yoyote badala yake(Mwenyezi Mungu)(AR RAAD:11)
iv.Kuhifadhi matendo ya mwanadamu, amesema Allah: (17)
(18)Wanapopokea wapokeaji wawili,anayekaa kuliani na (anayekaa)
kushotoni,(malaika)(17).Hatoi kauli yoyote isipokuwa karibu naye
yuko mngojeaji tayaria(kuandika)(18)(QAF:17-18)
v.Kuwathibitisha waumini na kuwanusuru, amesema Allah:
(12)(Kumbukeni) Mola wenu alipowafunulia Malaika(akawaambia):Hakika
mimi ni pamoja nanyi,basi watieni nguvu wale walioamini;ninatia
woga katika nyoyo za makafiri.Basi wapigeni juu ya shingo(zao) na
kateli kila ncha za vidole vyao(AL ANFAL:12)
vi.Kuchukuwa roho, amesema Allah: (11)Sema:Atakufisheni malaika
wa mauti aliyewakilishwa kwenu,kasha mtarejeshwa kwa Mola
wenu(AS-SAJDAH:11)
vii.Kumuuliza maiti kaburini, kuhusu Mola wake, dini yake na
mtume wake na waulizaji hao ni wawili Munkar na Nakir.viii.Kupiga
baragumu siku ya kiama, nayo ni kazi ya Israfil (a.s), baragumu la
kwanza atapiga la kufisha na la pili ni la kufufua kama alivyosema
Allah:
(68)Na litapigwa baragumu watoke roho watu waliomo mbinguni na
waliomo ardhini ila Yule amtakaye Mwenyezi Mungu.Tena litapigwa
mara nyingine.Hapo watafufuka (wote);wawe wanatazama(nini
litatokea)(AZ-ZUMAR:68)xi.Walinzi wa moto, amesema Allah:
(31)Na hatukuweka walinzi wa huo moto ila
malaika(AL-MUDDATHTHIR:31)Na akasema: (77)Nao watapiga
kelele(kuwaambia yule malaika anayewaadhibu waseme:Ee
malik!Naatufishe Mola wako!(Malik)aseme:Bila shaka mtakaa humu
humu(AZ-ZUKHRUF:77)Na akasema: (6)Enyi mlioamini!Jiokoeni nafsi
zenu na watu wenu,na moto ambao kuni zake ni watu na
mawe.Wanausimama malaika wakali,wenye nguvu,hawamuasi Mwenyezi
Mungu kwa amri zake;na wanatenda
wanayoamrishwa(yote)(AT-TAHRYM:6)
x.Kuwatakia msamaha waumini, kuwaombea Mungu, kuwabashiria na
kuwakirimu katika pepo, amesema Allah: (7) (8) (9(Wale
wanaokichukua kiti cha Enzi (cha Mwenyezi Mungu ) na wale
wanaokizunguka,wanamtukuza Mola wao na kumsifu na wanamuamini na
wanawaombea samahani walioamini,(wanasema):Mola wetu!Umekienea kila
kitu kwa rehema na ilimu(Unakijua kila kitu).basi wasamehe
waliotubu na wakaifuata njia yako wa waepushe na adhabu ya
Jahanamu(7).Mola wetu:Waingize katika mabustani ya milele
uliyowaahidi.Na uwape pia haya waliyofanya mema miongoni mwa baba
zao na wake zao na watoto wao;Bila shaka wewe ndiye Mwenye
nguvu,Mwenye hikima(8).Na waepushe na maovu,kwani umuepushaye na
maovu siku hiyo,hakika umemrehemu;na huko ndiko kufuzu
kukubwa(AL-MUUMIN:7-9)
(30)Wale waliosema:Mola wenu ni Mwenyezi Mungu,kisha wakenda
mwendo mzuri,hao huwateremkia Malaika(wakati kutoka roho
wakawaambia):Msiogope wala msihuzunike,na furahini kwa pepo
mliyokuwa mkiahidiwa(HAA MYM SAJDAH :30)
(23) (24)Mabustani ya milele watayaingia wao(pamoja) na
waliofanya wema miongoni mwa wazee wao na wake wao na kizazi
chao.Na malaika wanawaingilia katika kila
milango(23).(Wanawaambia):Salamun Alaikum Iwe amani juu yenu kwa
sababu mlisubiri(mlistahmili kufanya mema na kuacha mabaya na
mkastahimiliana mkakaa vizuri na wenzenuBasi ni mema yalioje
matokeo ya nyumba(ya Akhera kwa wanaomcha Mungu)(AR RAAD:23-24)
KUAMINI VITABU.Nayo ni kuitakidi kwa kukata bila ya shaka kwamba
Mwenyezi Mungu aliwateremshia mitume wake vitabu kwa haki, vitabu
ambavyo ni muongozo kwa watu, na vime kusanya rehma kwa watu na ni
mawaidha kwao, na hoja kwao na vimekusanya ufafanuzi wa kila
jambo.
Kuamini hivo vitabu inakusanya mambo haya:
1.Kuamini vitabu tulivyovijua kwa majina yake na tusivyovijua
tuamini kiujumla.
Vitabu vitukufu katika hivyo ni vitatu:
i.Taurati ambayo aliteremshiwa musa (a.s), amesema Allah:
(144) (145) (Akasema Mwenyezi Mungu):Ewe Musa!Mimi nimekuchagua
juu ya watu wote kwa ujumbe wangu na kwa kusema nawe kwangu.Basi
pokeya haya niliyokupa,Na uwe miongoni mwa wanaoshukuru(144).Na
tukamwandikia katika mbao kila kitu-mawaidha(ya kila namna) na
maelezo ya kila jambo.Basi yashike kwa imara na uwaamrishe watu
wako wayashike bora haya.Karibuni nitakuonyesheni miji ya wavunjao
amri(zenu namna ilivyoharibika na nitakutawalisheni nyinyi(AL
AARAF:144-145)Na akasema: Hakika Tuliteremsha Taurati yenye uongozi
na nuru,ambayo kwayo Manabii waliojisalimisha (kwa Mwenyezi
Mungu)waliwahukumu Mayahudi,na watawa wa maulamaa pia(walihukumu
kwa hiyo taurati),kwa sababu walitakiwa kuhifadhi kitabu (hicho)
cha Mwenyezi Mingu; nao walikuwa mashahidi juu yake(AL
MAIDAH:44)ii.Injil ambayo Mwenyezi Mungu alimteremshia Isa (a.s),
amesema Allah:
(27)Kisha tukawafuatisha nyuma yao Mitume wetu(wengine) na
tukamfuatisha Isa bin Mariamu,na Tukampa Injili,na Tukaweka upole
na rehema katika nyoyo za wale waliomfuata.Na uruhubani(wanaume
kutooa na wanawake kutoolewa)wameubuni(wenyewe),Sisi
hatukuwaandikia hayo.(Wenyewe waliyafanya haya) ili kuitaka radhi
ya Mwenyezi Mungu.Lakini hawakuufuata(huo uruhubani wao) kama
inavyotakiwa kuufuata.Basi tukawapa wale walioamini miongoni mwao
ujira wao,na wengi wao ni maasi(AL-HADYD:27)
Na akasema: (46)Na Tukawafuatisha (mitume hiyo) Isa bin Maryamu
kuyahakikisha yaliyokuwa kabla yake katika Taurati,na tukampa
Injili iliyomo ndani yake uongozi na nuru na isadikishayo
yaliyokuwa kabla yake katika taurati,na uongozi na uongozi na
mawaidha kwa wamchao (wanaomwogopa)(AL MAIDA:46)iii.Quran ambayo
alimteremshia mtume Muhammad (Sallallahualayhi wasallam) , nacho
ndicho kitabu bora kuliko vyote, amesema Allah: (48)Na
Tumekuteremshia kitabu kwa (ajili ya kubainisha)
haki,kinachosadikisha vitabu vilivyo kabla yake,na kuvihukumia(kama
haya ndiyo yaliyoharibiwa au ndiyo yaliyosalimika).basi wahukumu
baina yao kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu,wala wasifuate
matamanio yao kwa kuacha haki iliyokufikia.Na kila (Uma) katika
nyinyi (binadamu )tumeujaaliwa sharia yake na njia yake.Na kama
Mwenyezi Mungu angalitaka angekufanyani kundi moja(la kufuata
sharia moja),lakini anataka kukujaribuni kwa hayo aliyokupani.Basi
shindaneni kuyafikilia mambo ya kheri.Nyinyi nyote marudio yenu ni
kwa Mwenyezi Mungu,Naye atakuambia (yote) yale mliyokuwa
mkikhitalifiana(AL MAIDAH:48)
Na katika vitabu vyake Mwenyezi Mungu alivyoteremsha ni;Zaburi
aliomteremshia Daud (a.s), amesema Allah: (55)Na Mola wako anawajua
sana wote waliomo katika mbingu na ardhi.Na kwa hakika
tuliwafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine(katika amali zao
zilizo bora zaidi kuliko za wenziwao),na Daudi tulimpa Zaburi(BANI
ISRAIL:55)Na kitabu cha Ibrahim, amesema Allah: (18) (19)Hakika
haya (mnayoambiwa humu katia Qurani) yamo katika vitabu
vilivyotanguliwa(18).Vitabu vya Ibrahimu na Musa(na
wengineo)(AL-ALAA:18-19)
2.Kuamini katika hivi vitabu ambayo hayajageuzwa, kwani Allah
ameeleza kwamba vitabu vya banu Isra