REPUBLIC OF KENYA MINISTRY OF HEALTH UNACHOHITAJI … · mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini. Chembechembe za rangi
Post on 29-Aug-2019
6 Views
Preview:
Transcript
KENCOKenyan Network of
Cancer Organisations
MINISTRY OF HEALTH
REPUBLIC OF KENYA
UNACHOHITAJI KUJUA KUHUSU SARATANI KWA MATUMIZI YA WAGONJWA NA WAUGUZI
Unachohitaji Kujua Kuhusu Saratani Kwa matumizi ya wagonjwa na wauguzI
DIBAJI Kijitabu hiki kimeandaliwa na Wizara ya Afya ya Kenya pamoja na Johns Hopkins Centre for
Communications Programs, kwa usaidizi kutoka kwa American Cancer Society.
Wawakilishi kutoka Wizara ya Afya ya Kenya, Kenyatta National Hospital, Moi Teaching and Referral Hospital, Aga Khan Hospital pamoja na Kenya Network of Cancer Organizations (KENCO) ambao pia
walitoa muongozo wa kiufundi na kusaidia katika usanifishaji wa maelezo ya kijitabu hiki kuambatana na utafiti mpana katika wagonjwa wa saratani na wahudumu wao wa afya.
Maelezo yaliyopo kwenye chati za saratani na muigo wa maelezo yaliyoopolewa kutoka kwa American Cancer Society. Baadhi ya maelezo kuhusu hali ya maisha pamoja na lishe yaliopolewa
kutoka kwa MacMillan Cancer Support, na taasisi ya U.S. National Cancer Institute. Waliohusika katika ruwaza na usanifishaji wa muundo walikuwa ni Avocado Design Studio.
© American Cancer Society, 2016.
Saratani ni Nini?
n Seli za kawaida zinajiongeza na kujizidisha kwa utaratibu mzuri. Saratani hutokea ikiwa seli hizo zinaanza kujiongeza bila mpangilio maalum.
n Seli zenye saratani huendelea kukua na kuunda seli mpya bila kikomo. Hali hii huupatia mwili wakati mgumu sana wa kufanya kazi jinsi inavyofaa
n KUELEZA SELI NI NINI: Seli ni sehemu ndogo zaidi katika mwili wa binadamu ambayo hutekeleza majukumu yote yanayohitajika ili aishi. Kwa kuwaida, seli huwa ni chembechembe ndogo zaidi zisizoonekana kwa macho ila tu kwa kutumia hadubini.
1
SELI ZA KAWAIDA
SELI YA SARATANI KUONGEZEA MARA DUFU UVIMBE UNAOSAMBAA
Saratani ni nini? 1
Mambo ya Kimsingi Kuhusu Saratani
n Saratani si ugonjwa wa aina moja tu, kuna aina nyingi za saratani.n Saratani inaweza kuanzia katika sehemu yoyote ya mwili. n Saratani inaweza kusambaa hadi katika sehemu nyinginezo za mwili, aidha
kupitia kwa mifumo ya limfu au mishipa ya damu na inapofanya hivyo huitwa metastasis.
n Saratani hutofautiana kutokana na jinsi inavyokua na kusambaa mwilini, na jinsi inavyopimwa na kutibiwa.
2
Mambo ya Kimsingi Kuhusu Saratani
MGAWANYIKO WA VIUNGO MBALI MBALI
UVIMBE WA AWALI
2
Saratani Maarufu Nchini Kenya
3
n KWA WANAUME
- Saratani ya Kibofu- Saratani ya umio - Saratani ya
mishipa ya damu na limfu
- Saratani ya tumbo- Satani ya bawasili
au utumbo (njia ya haja kubwa)
n KWA WANAWAKE:
- Saratani ya njia ya uzazi
- Saratani ya matiti- Saratani ya umio- Saratani ya tumbo- Saratani ya
mishipa ya damu na limfu
n KWA WATOTO:
- Limfoma- Saratani ya Damu
(Leukemia)- Uvimbekatikafigo- Uvimbe katika
macho - Saratani ya mifupa
Saratani Maarufu Nchini Kenya 3
SARATANI YA NJIA YA UZAZI
SARATANI YA MISHIPA YA DAMU NA LIMFU
SARATANI YA UMIO
SARATANI YA KIBOFU
SARATANI YA TUMBO
SARATANI YA BAWASILI AU
UTUMBO SARATANI YA MATITI
Je, Uvimbe Ndani ya Mwili (Tumor) ni Nini?
n Saratani nyingi hufanya uvimbe unaoitwa (tumor) au seli yenye kitufe.n Uvimbe ambao si saratani huitwa “benign”. n Uvimbe ambao ni saratani huitwa “malignant” au uvimbe wenye kijicho.n Madaktari huchukua sehemu ndogo ya uvimbe huo na kuichunguza ili
kubaini iwapo ni saratani. Hatua hii huitwa bayopsia. Bayopsia nyingi hufanywa kwa kutumia sindano ndogo.
n Kuna aina fulani fuluni za saratani, kama vile Saratani ya damu (Leukemia) ambazo hazifanyi uvimbe. Hukua kwenye damu ama katika seli nyinginezo za mwili.
4
SELI ZA KAWAIDA
SELI ZINAZOSAMBAA
Je, Uvimbe Ndani ya Mwili (Tumor) ni Nini?
Uvimbe ndani ya mwili Utambuzi wa ugonjwa
4
Mbona Iwe Mimi?
n Iwapo unajiuliza swali “Nilikosea wapi?” au “Mbona ikawa mimi?” hauko peke yako.
n Unafaa ujue kwamba saratani si adhabu kwa mienendo yako ya hapo awali. Wala haisababishwi na mizengwe au nguvu zozote za giza kama vile uchawi.
n Saratani ni ugonjwa unaoweza kuathiri mtu yeyote, mahali popote, katika nchi yoyote ile, na wakati wowote.
n Saratani si kosa lako. Zingatia kujitunza vizuri sasa.
5
Mbona Iwe Mimi? 5Saratani unaweza kuathiri mtu yeyote Saratani haisababishwi na uchawi
Athari Zinazoambatana na Saratani
n Kwa hakika, madaktari hawajui kinachosababisha saratani. n Tunajua kwamba kuna vitu vinavyoitwa ‘ hali ya kuzua hatari’ ambayo
huathiri uwezekano wako wa kushikwa na magonjwa. n Baadhi ya hali hatari za saratani zinaweza kubadilishwa lakini nyingine
haziwezi. Hali hatari ambazo haziwezi kubadilishwa zinahusisha umri wako, jinsia yako, na historia ya familia yako.
n Hali zinazoweza kubadilishwa ni mambo unayofanya, kama vile iwapo unatumia tumbaku au pombe, aina ya chakula unachokula, na kiwango cha mazoezi unayofanya. Hali nyingine zinazozua hatari zinahusiana na vitu vilivyomo kwenye mazingira ambayo husababisha saratani.
6
Athari Zinazoambatana na Saratani 6
SodaSODA
wine
KIWANGO CHA MAZOEZI POMBE
VYAKULAUNAVYOKULA
TUMBAKU
UCHAFUZI WAMAZINGIRA
Dalili na Ishara za Ugonjwa
n Dalili ni ishara inayoonyesha kwamba kuna kasoro mwilini mwako.
n Matibabu hufanya kazi vizuri saratani inapogunduliwa mapema – ikiwa bado changa na uwezekano wake wa kusambaa hadi sehemu nyinginezozamwilinifinyu.
n Dalili za kawaida za saratani huwa ni pamoja na:- Kupungua kwa uzani
kusikoelezeka chanzo chake ni nini
- Maumivu- Mabadiliko ya ngozi- Joto jingi mwilini- Uchovu wa kila mara- Kuvuja damu kupita kiasi
n Saratani nyingi hazionyeshi dalili hadizinapofikiakiwangochajuunazinaweza tu kutambuliwa mapema kupitia ukaguzi.
Kumbuka sio kila mara dalili hizi humaanisha mtu aliye nazo ana saratani kwani zinaweza kuwa
dalili za magonjwa mengine tofauti.
7
Dalili na Ishara za Ugonjwa
Maumivu Mabadiliko ya ngozi
Joto jingi mwilini Uchovu wa kila mara Kuvuja damu kupita kiasi
Upunguaji wa uzani
7
Itikadi Zinazotumiwa Sana Ambazo ni za Uongo
n Saratani huambukizwa.n Saratani hutibiwa kwa dawa za kienyeji.n Si kweli kwamba hakuna kinachoweza kufanywa ili kuzuia kusambaa kwa
saratani mwilini.n Mjamzito aliye na saratani huzaa mtoto mwenye saratani.n Saratani ni ugonjwa wa wazee au matajiri pekee.n Saratani ni hukumu ya kifo.
8
Itikadi Zinazotumiwa Sana Ambazo ni za Uongo
UONGO!
8
Viwango vya saratani
n Viwango hivi hutuonyesha jinsi na ambavyo saratani imesambaa kutoka ilikoanzia mwilini.
n Saratani nyingi huwa na viwango vinne.n Ufahamu wa viwango vya saratani husaidia daktari kuamua ni aina gani ya
matibabu yanayofaa na jinsi matibabu hayo yanavyoweza kutekelezwa na jinsi yanavyoweza kufanya kazi vizuri.
n Kama kawaida, kiwango cha chini (kama vile kiwango cha 1 au 2) humaanisha kuwa saratani haijasambaa sana mwilini.
n Ngazi ya juu (kama vile 3 au 4) humaanisha saratani imeenea zaidi. Hatua ya 4 ndiyo ya juu zaidi.
9
Ngazi za Saratani
KIWANGO CHA 0 Uvimbe katika kiungo Fulani
ndani ya mwili – saratani ikiwa
inaanza.
KIWANGO CHA 1Saratani
imeguduliwa katika kiungo
kimoja.
KIWANGO CHA 2Uvimbe unakua kwa kiasi, lakini mahala pamoja.
KIWANGO CHA 3Saratani imesambaa na kuwa
mafundo ya limfu na bila shaka kuvurugamkusanyiko
wa seli mwilini.
KIWANGO CHA 4saratani imesambaa katika sehemu nyingine za mwili.
Hapa inakaribia kufikia kiwango cha juu sana.
MSHIPA WA DAMU
FUNDO LA LIMFU
FUNDO LA LIMFU LIKIWANA SELI ZENYE SARATANI
AMBAZO ZIMESAMBAA KATIKA
KIUNGO FULANI CHA MWILI
9
Matibabu
n Matibabu yake yanaweza kuwa ya kutibu, kudhibiti, au kutibu matatizo yanayoisababisha.
n Matibabu maarufu ya saratani ni kufanyiwa upasuaji, kufanyiwa tiba ya kuchomwa (kemotherapi) na tiba ya miale yaani (radiation).
n Mtu anayeugua saratani huenda akahitaji mojawapo wa tiba hizi au aina zote na mara nyingi huduma kadhaa za matibabu huenda zikahitajika.
n Aina ya matibabu ambayo daktari wako atapendekeza itategemea:
- Aina ya saratani uliyo nayo;- Ngazi ya saratani;- Umri wako, hali ya afya kwa
jumla, na mahitaji ya mtu binafsi.
n Hakikisha kwamba unapata matibabu yako kutoka kwa kituo cha afya kinachojulikana vyema katika utoaji wa huduma za saratani.
10
Matibabu 10
Je, Upasuaji wa Saratani ni Nini?
n Baadhi ya Saratani zinaweza kuondolowa kupitia upasuaji.n Upasuaji unafaa kutumika katika eneo zenye uvimbe ambao haujasambaa
katika viungo vingine mwilini.n Upasuaji unaweza kutumika kutibu saratani, ama kutibu matatizo
mengine yaliyosababishwa na saratani hiyo.n Muulize Daktari wako sababu kamili ya upasuaji huo.
11
11Je, Upasuaji wa Saratani ni Nini?
Kemo ni Nini?
n Kemo hutumia dawa zenye nguvu ili kuua seli za saratani.n Kwa kawaida, dawa hizo huingizwa kwenye mishipa ya damu kupitia
chubu na sindano.n Baadhi ya dawa za kemo huweza kumezwa kama vidonge ama dawa ya
maji.n Kemo hutolewa kutibu saratani, au kumsaidia mgonjwa kuishi maisha
marefu zaidi au kumsaidia apate afueni.n Kemo hutumika kwa wagonjwa mbalimbali kwa kusudi mbali mbali.
Muulize muuguzi wako ni kusudi la kupewa tiba ya kemo.
12
12Kemo ni Nini?
Je, Tiba ya Miale ni Nini?
n Tiba inayotumia miale huwa ni matumizi ya miale ili kuua seli za saratani.n Vifaa maalum hutuma dozi kali za miale ili kumaliza saratani.n Miale hiyo pia inaweza kuathiri seli za kawaida zinazokaribiana na seli za
saratani. Lakini seli za kawaida zinaweza kujikarabati zenyewe na seli za saratani haziwezi kufanya hivyo.
n Tiba ya miale haina joto na pia haina uchungu.n Tiba ya miale inaweza kutumika kutibu saratani, au kuzuia kukua kwa
saratani.n Muulize muuguzi wako wa afya ni kwa nini unapewa tiba ya miale.
13
13Je, Tiba ya Miale ni Nini?
Madhara Andamizi ya Matibabu
n Kila matibabu yanaweza kuwa na athari zake.
n Baadhi yanaweza kuwa makali na mengine mepesi, lakini madhara mengi andamizi ya matibabu mengi ya saratani yanaweza kutibiwa.
- Kuchafuka roho na kutapika;- Kukosa hamu ya chakula; - Kunyonyoka nywele kwa muda;- Vidonda vya mdomo;- Hatari kubwa ya kupata
maambukizi;
- Kuvuja damu au kuchubuka kila unapojeruhiwa au kukatwa kidogo;
- Upungufu wa damu (kutokana na kupungua kwa seli nyekundu za damu), hali inayoweza kusababisha uchovu, kupumua kwa shida, ngozi iliyopauka, na dalili nyinginezo;
- Mwasho wa ngozi;- Uchovu wa kila mara.
n Madhara mengi andamizi humalizika baada ya kukamilika kwa matibabu.
n Madhara mengi ya saratani yanaweza kutibiwa.
14
Madhara Andamizi ya Matibabu
Kunyonyoka nywele Makovu kinywani Mwasho wa ngozi
14
Je, Nitaishi?
n Zipo sababu nyingi zinazoathiri urefu wa maisha atakayoishi mwathiriwa wa saratani.
- Aina ya saratani na mahali ilipo mwilini mwako; - Kiwangoambachosaratanihiyoimefikia; - Hali ya seli zenye saratani; - Umri wako na hali yako ya afya kabla ya
kupata saratani; - Jinsi mwili unavyoitikia matibabu.n Saratani nyingi zinaweza kutibiwa. n Ni vigumu sana kubashiri muda ambao mtu
anayeugua saratani ataishi.
Yanayompasa kujua mhudumu wa afya : Kuwa tayari kwa mazungumzo
halisi yanayohusu mgonjwa anayeugua
saratani..
15
Je, Nitaishi?
COMMUNITYCLINICJe,
Nitaishi?
15
Mapendekezo ya Lishe Wakati wa Matibabu
n Ulaji wa chakula kinachofaa kabla, wakati na baada ya matibabu, unaweza kukuwezesha kuhisi vizuri na kuongeza nguvu mwilini.
n PROTENI (NYAMA NA VIBADALA VYAKE): mimea jamii ya maharagwe, nayama ya ndege (k.m. kuku), nyama nyepesi, mayai, samaki, dagaa, bidhaa za maziwa, njugu na simsim na siagi.
n MAFUTA: - Asili nzuri ya mafuta ni: mafuta ya mboga kama vile yanayotokana na mahindi machanga,simsim, ufuta na
njugu. - Mlo mzuri haufai kuwa na mafuta yaliyotengenezwa kutokana na wanyama. - Jaribu kupunguza ulaji wa mafuta yabisi (yaliyogandamanishwa), kama vile siagi na mafuta yabisi ya kupikia.
Mafuta kama haya yanaweza kupatikana katika vitafunio na vyakula vya kuokwa.n STACHI (VYAKULA VYENYE WANGA): Aina za matunda, mboga za majani na nafaka. Mifani bora ni kama:
mahindi, mchele, maharage, viazi, mawele, mhogo, ngano, viazi mbatata, mtama, ndizi mbichi, pasta na nafaka.
n VITAMINI NA VIRUTUBISHI VYA MADINI: Vitamini na madini hutekeleza jukumu muhimu katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Chembechembe za rangi ya kijani kwenye mboga huwa na madini tele na vitamini.
16
Mapendekezo ya Lishe Wakati wa Matibabu
YOGURT
MIZIZI
NAFAKA
MBOGA
MAHARAGWE NA NJUGU
MATUNDA
MAJANI
SAMAKI NA KUKU
NYAMA
YOGURTMAZIWA
KEKI
Wakati Mwingine
Vipimo Wastani vyakila siku hadi kila wiki
Mara kwa mara, angalau mara mbili kwa wiki
Pangilia kila mlo utumievyakula hivi
MAFUTA
16
Maji
n Maji au vinywaji ni muhimu kwa afya. Unafaa unywe angalau gilasi nane za vinywaji kila siku.
n Unaweza kuhitaji vyakula vya rojo-rojo zaidi iwapo unatapika, unaendesha, au hata ukiwa umepunguza kiasi cha chakula unachokula.
n Unaweza kuhitaji vinywaji zaidi hasa unapopokea matibabu ya kemo.
n Unafaa uepukane na vinywaji vilivyowekwa sukari kabla ya kuuzwa, pamoja na pombe.
17
Maji
121
2
3
4
56
7
8
9
10
11
17
Mapendekezo ya Mazoezi
n Shughuli za kutumia nguvu hukufanya kuwa imara. Zinaweza kusaidia kupunguza mzongo wa mawazo, jakamoyo, uchovu wa kila mara, kitefutefu, shida wakati wa haja kubwa inayotokana na upungufu wa maji mwilini. Zinaweza kuimarisha hamu yako ya chakula.
n Ratiba na aina ya mazoezi yatategemea hali ya kila mgonjwa. Mazoezi hayo yafaa kuwa ni jambo unalopenda kufanya.
n Unapaswa kutambua hali ya mwili wako na upumzike unapohitajika kufanya hivyo. Huu si wakati wa kujilazimisha kufanya mazoezi.
18
Mapendekezo ya Mazoezi
Kufanya kazi Kuruka kamba Kucheza
18
Mikakati ya Kuizoea Hali Mpya
n Waambiemarafikipamojanafamilia yako kuhusu saratani yako punde tu unapogundua kwamba unayo.
n Wafahamishe kwamba hauwezi kuwaambukiza. Waeleze kwamba unaendelea kupata matibabu ili kuimarisha afya yako.
n Waruhusumarafikinafamiliawakokukusaidia, na wafahamishe aina ya msaada unaohitaji.
n Kuna makundi mengi ya kuhimizana pia (mwelekeze mgonjwa na muuguzi wa afya kwenye kijitabu).
n Baadhi ya tiba badala huenda zikapunguza aina fulani ya dalili za saratani, kupunguza athari za matibabu, au kuimarisha hali yako ya afya. Lakini tiba za miti shamba na waganga huenda zikawa hatari kwa afya yako. Kila mara wasiliana na daktari wako au muuguzi kabla ya kutafuta tiba hizo.
19
Mikakati ya Kuizoea Hali Mpya 19
Haki za mgonjwa
20
n Haki zako kama mgonjwa ni pamoja na:
- Haki ya kupata matibabu.- Haki ya kupata matibabu ya dharura
katika kituo chochote cha afya.- Haki ya kukataa matibabu.- Haki ya kudumisha siri.- Haki ya kufahamishwa ili kukubali
matibabu.- Haki ya kupata maelezo. - Haki ya kutibiwa kwa heshima na
taadhima.- Haki ya kutafuta maoni tofauti ya
kimatibabu.- Haki ya kulalamika.
n Majukumu yako kama mgonjwa ni pamoja na:
- Kujishughulikia mwenyewe kuishi maisha bora kwa afya yako
- Kuwa na mtazamo chanya kuhusu afya na maisha yako
- Kuheshimu haki za watu wengine na kuepuka kuhatarisha maisha na afya yao
- Kuwapa habari zifaazo na sahihi wahudumu wa afya, ili kuwawezesha kukufanyia ukaguzi, matibabu na ushauri ufaao.
- Chunga stakabadhi zako za afya ulizonazo- Ili kutimiza ratiba ya kuonana na daktari,
chunga masaa na iwapo itakuwa vigumu kufikakwawakatiufaaowasilianamapemana mhudumu wako wa afya
- Ili kuzingatia maagizo, zingatia na wala usitumia vibaya madawa au matibabu uliyopewa.
Haki za mgonjwa 20
top related