Top Banner
Uendeshaji manual
30

Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Oct 05, 2019

Download

Documents

dariahiddleston
Welcome message from author
This document is posted to help you gain knowledge. Please leave a comment to let me know what you think about it! Share it to your friends and learn new things together.
Transcript
Page 1: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Uendeshaji manual

Page 2: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea
Page 3: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

i

Hati miliki© 2019 Align Technology, Inc. Haki Zote Zimehifadhiwa.

Maelezo yaliyomo katika mwongozo huu yanaweza kubadilika bila ya taarifa.

Vifaa na programu iliyoelezwa katika mwongozo huu hutolewa chini ya makubaliano ya ununuzi au mpango wa ununuzi, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti yaliyotolewa au yanayoelezwa ndani yake, kwa mujibu wa vigezo na masharti ambayo Mteja amenunua Kifaa Chapa ya Nuru cha iTero Element Flex na vinaweza kutumika tu kulingana na makubaliano hayo.

Hakuna sehemu ya mwongozo huu inaoweza kutolewa tena, kurudufiwa, kuhifadhiwa katika mfumo wa kurejesha, au kusambazwa kwa namna yoyote (kielektroniki au kimakenika) kwa madhumuni yoyote isipokuwa matumizi ya kawaida ya mteja, bila idhini ya awali ya maandishi ya Align Technology Inc.

Mwongozo huu unaelezea iTero Kifaa Chapa ya Nuru cha Element Flex.

Toleo la lugha ya Kiingereza. Imesasishwa Januari 2019.

Alama za biasharaAlign, Invisalign, iTero, na iTero Element kati ya nyingine, ni alama za biashara na/au alama za huduma za Align Technology, Inc au moja ya matawi yake au makampuni husika na zinaweza kusajiliwa Marekani na/au nchi nyingine.

Alama zozote nyingine au alama za biashara zilizosajiliwa zinazoonekana katika mwongozo huu ni mali ya wamiliki husika.

Ofisi ya MarekaniMakao Makuu ya KampuniAlign Technology, Inc.2820 Orchard ParkwaySan Jose, California 95134

www.aligntech.com

Simu: +1 (408) 470-1000Faksi: +1 (408) 470-1010

Align Technology Ltd.3 Ariel Sharon BoulevardOr-Yehuda 6037606Israeli

Simu: +972 (3) 634-1441Faksi: +972 (3) 634-1440

Ofisi ya UholanziMakao Makuu ya Kimataifa Align Technology B.V.Arlandaweg 1611043 HS Amsterdam

Simu: +31 (0) 20-586-3600Faksi: +31 (0) 20-586-3751

Msaada kwa wateja Simu: +1 (800) 577-8767

Barua pepe: [email protected]

Barua pepe: [email protected]

Page 4: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

ii

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Inafuata matakwa ya Daraja la 1 la miale ya lezaKifaa hiki kimefuata: "21 CFR 1040.10" na "EN 60825-1".

Ukidhi wa matakwa ya CSAKifaa hiki kinakidhi wango cha CSA zifuatazo kwa Canada na Marekani: "UL Std No. 60601-1 - Vifaa vya Umeme vya Umeme Sehemu ya 1: Mahitaji ya Jumla ya Usalama"

Ukidhi wa matakwa ya FCCKifaa hiki kinakubaliana na Sehemu ya 15 ya Kanuni za FCC na uendeshaji wake unategemea masharti mawili yafuatayo:

1. Kifaa hiki hakiwezi kusababisha mwingiliano wa kudhuru.

2. Kifaa hiki lazima kikubali mwingiliano wowote kitakaopokea, ikiwemo mwingiliano unaoweza kusababisha uendeshaji usiotakiwa.

Onyo la Tume ya Shirikisho la Mawasiliano (FCC).Marekebisho kwa kifaa ambayo hayajakubaliwa kwa dhahiri na mtengenezaji huweza kusababisha kuondolewa kwa mamlaka yako ya kuendesha kifaa chini ya Kanuni za Tume ya Shirikisho la Mawasiliano (FCC).

Ukidhi wa matakwa ya EMCKifaa hiki kinakidhi viwango vifuatavyo vya EMC:

"IEC 60601-1-2 Vifaa vya umeme vya kitabibu - Sehemu ya 1-2: Mahitaji ya jumla ya usalama wa msingi na utendaji muhimu - Kiwango cha dhamana: Matukio ya umeme - Mahitaji na vipimo".

Ukidhi wa matakwa ya usalamaKifaa hiki kinakidhi viwango vifuatavyo vya usalama:

"IEC 60601-1 Vifaa vya umeme vya kitabibu - Sehemu ya 1: Matakwa ya jumla ya usalama wa msingi na utendaji muhimu."

Ukidhi wa matakwa ya CEKifaa hiki kinakidhi Maelekezo ya Mamlaka 93/42 / EEC kwa Vifaa vya Kitabibu.

Bidhaa ya Leza ya Daraja la 1

C US

Page 5: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

iii

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Alama Alama zifuatazo zinaweza kuonekana kwenye vipengele vya vifaa vya iTero Element Flex, na zinaweza pia kuonekana ndani ya mwongozo huu na maandiko mengine ya iTero Element Flex.

"Rx only"

Popote alama hii inapoonekana kwenye kifaa, inashauriwa kurejea mwongozo huu kwa habari kuhusu matumizi sahihi ya kifaa.

Zingatia: Alama hii hutumika kuonyesha ukweli kwamba kuna onyo maalum au tahadhari zinazohusiana na kifaa. Popote alama hii inaonekana kwenye kifaa, ni lazima kurejea taarifa zinazohusiana na usalama-zilizomo ndani ya muongozo huu wa utumiaji.

Mtengenezaji wa kifaa cha matibabu.

Nambari ya oda.

Inaonyesha ukomo wa joto ambao kifaa cha matibabu kinaweza kuhimili kwa usalama

Aina ya sehemu iliyowekwa ya BF. Sehemu yoyote ambayo alama hii inaonekana ni aina ya kutengwa ya umeme BF.

Sehemu au vifaa ambavyo alama hii hutokea havipaswi kutumiwa tena.

TAHADHARI: USIKANYAGE kwenye kitovu cha Flex!

Nambari ya mfuatano.

Msimbo wa kundi wa mtengenezaji

Mkusanyiko tofauti kwa takataka za umeme na vifaa vya umeme unahitajika. Kulingana na matakwa ya Mwongozo wa Ulaya kuhusu Takataka za Umeme na Vifaa vya Umeme (WEEE), usitupe kifaa hiki kwenye sehemu za takataka za nyumbani au manispaa. Kifaa hiki kina malighafi za WEEE. Tafadhali wasiliana na huduma ya EARN. Kiungo cha fomu ya ombi la mtandaoni http://b2btool.earn-service.com/aligntech/select.

TAHADHARI: Sheria ya Taifa la Marekani inaruhusu kifaa hiki kuuzwa na au kwa amri ya Daktari wa Meno mwenye kibali, Othodontisti au Mtaalamu wa Meno. Mfumo hutumika kama kifaa cha matibabu na unapaswa kuendeshwa na watoa huduma wa afya ambao wamekidhi vigezo pekee.

TAHADHARI: Kitovu cha Flex lazima kiwe kikavu!

Inaonyesha mwakilishi Aliyeidhinishwa katika Jumuia ya Ulaya.

Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea maelekezo ya matumizi.

REF

MLot

SN

Page 6: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

iv

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Maelekezo ya usalamaKabla ya kuanza kufanya kazi na mfumo, watumiaji wote wanatakiwa kusoma maelekezo haya ya usalama.

Mfumo hutolewa na kitovu cha Flex kilicho na umeme kwa kifaa cha kuskani. Kitovu cha Flex lazima kiwe kikavu na kilindwe dhidi ya kupasuka.

ANGALIZO - ili kuepuka hatari ya mshtuko wa umeme, kifaa hiki lazima tu kiunganishwe na ugavi wa umeme wenye kinga ardhini.

Ugavi wa nishati• Umeme kwenda kwenye skana hupelekwa kupitia kipitisha nishati

cha kiwango cha kitabibu ndani ya kitovu cha Flex.

Onyo la hatari ya umeme• Hatari ya mshtuko wa umeme! Hakuna sehemu za ndani za

kitovu cha Flex zinazoweza kurekebishwa na mtumiaji.

• Ili kuepuka hatari ya mshtuko wa umeme, iTero Element Flex inapaswa tu kuunganishwa na ugavi wa umeme wenye waya wa kinga ardhini.

• Unganisaha kitovu cha Flex kwenye kompyuta ambayo imeidhinishwa tu kulingana na IEC60950, na hadi UL60950-1. Kipakatalishi na vifaa vyake vyote viwe angaa mita 1.5 mbali na mgonjwa. Usimkague mgonjwa na kugusa kipakatalishi au kifaa chake chochote wakati huohuo

• Kifaa cha kuskania cha Align Technology na kipakatalishi zilizoidhinishwa pekee ziunganishwe kwenye soketi za USB za kitovu cha Flex.

• Kebo za umeme zilizoidhinishwa na Align Technology pekee ndizo zitumike kuunganisha kitovu cha Flex na soketi ya AC.

Uainishaji wa usalama• Aina ya ulinzi dhidi ya mshtuko wa umeme: Hatari ya 1.

• Kiwango cha ulinzi dhidi ya mshtuko wa umeme: Aina BF.

• Mfumo wa ulinzi dhidi ya uingiaji wa maji hatari: ya kawaida.

• Vifaa havifai kutumika kwa uwepo wa mchanganyiko wa nusukaputi inawaka.

• Muundo wa uendeshaji: Endelevu.

Kifaa cha afya kama tiba• Mfumo hutumika kama kifaa cha matibabu na unapaswa

kuendeshwa na watoa huduma wa afya ambao wamekidhi vigezo pekee.

Maangalizo ya Skana• Skana hutoa mwanga mwekundu wa leza (680nm Daraja la 1)

pamoja na utoaji wa LED nyeupe. Matumizi ya kawaida ya skana hayana hatari yoyote kwa jicho la mwanadamu. Hata hivyo, madaktari wanapaswa kuepuka kuangaza skana moja kwa moja kwenye macho ya mgonjwa.

• Epuka kukunja kebo, kuifunga vifundo, kuivuta, kukanyaga kebo.

• Wakati mfumo hautumiki, kifaa cha kuskani kiwekwe ndani ya kiunzitegemeo na nguzo ielekee chini ili kusiwe na mguso machoni na mwali wa leza katika mazingira yoyote.

• Daktari anapaswa kuamsha operesheni ya kuskani wakati tu nguzo ya skana iko mdomoni mwa mgonjwa.

• Madaktari wanapaswa kuepuka kuweka skana katika kiunzitegemeo wakati kazi ya kuskani inaendelea.

Kusafisha & kutoa maambukizi• Ili kuepuka maambukizo kutoka kwa mmoja kwenda kwa

mwingine, ni lazima kila baada ya kipindi na mgonjwa mmoja mkono vazi wa skana ubadilishwe na skana ifutwe vimelea.

• Utupaji wa mikono vazi ya skana ifuate taratibu za uendeshaji au maelekezo ya eneo husika ya utupaji wa takataka za kitabibu zenye vimelea.

Utoaji kashani & usimikaji• Mfumo unapaswa kutolewa kashani na kusimikwa kufuatana na

maelekezo ya ALign Technology.

Mazingira ya kazi • Mfumo lazima uhamishwe kati ya ofisi ndani ya kasha lake maalum

ili kuepuka uharibifu.

• Usizibe matundu ya hewa kwenye kifaa cha skana.

• Mfumo umekusudiwa kwa matumizi ya ndani tu. Haifai kuwekwa wazi kwenye jua moja kwa moja, joto kali au unyevu.

• Mfumo unapaswa kutumika tu kufuatana na joto sahihi la uendeshaji kama ilivyoelezwa katika Kiambatisho B.

• Ikiwa iTero Element Flex ndiyo kwanza imeletwa kwenye ofisi kutoka kwenye mazingira ya joto au baridi, inapaswa iwekwe kando mpaka iendane na halijoto ya chumba ili kuepusha mtonesho kwa ndani.

Mwingiliano wa usumaku umeme• ONYO: Kifaa hiki kimejaribiwa na kinakidhi mahitaji ya vifaa vya

matibabu kulingana na kiwango cha EN60601-1-2. Kiwango hiki kimewekwa kutoa ulinzi wa kutosha dhidi ya mwingiliano wenye madhara katika vituo tiba vya kawaida. Hata hivyo, kutokana na ueneaji wa vifaa vitoavyo masafa ya redio na vyanzo vingine vya kelele za umeme kwenye mazingira ya vituo vya afya (kama vile, simu za mkononi, simu ya redio, vifaa vya umeme), inawezekana kwamba kiwango cha juu cha mwingiliano huo kutokana na ukaribu au nguvu ya chanzo, unaweza kusababisha mvurugiko wa utendakazi wa kifaa hiki.

• Ikitokea kushuka kwa kasi kwa volteji zinazoingia za mains, mfumo hautafanya kazi lakini utabakia salama kwa mtumiaji. Mfumo utarejea kwenye hali yake ya kiutendaji baada ya volteji kurejea kwenye hali yake ya awali.

Jumla• ANGALIZO: Hakuna mabadiliko ya kifaa hiki yanaruhusiwa.

Page 7: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea
Page 8: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea
Page 9: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

1

Jedwali la YaliyomoSura 1: Utangulizi 2

Kuhusu mwongozo huu wa uendeshaji 2

Matumizi yaliyopangwa 2

Faida za Mfumo wa iTero Element 2 2

Sehemu ya mtumiaji wa iTero Element 2 3

Sura ya 2: Vipengele vya msingi vya kifaa 4

Mwonekano wa mbele wa mfumo 4

Kifaa cha kuskani (kifimbo) 5

Ufungaji wa mfumo wa kuhamishika (kwa usafirishaji) 6

Kufunga mfumo 6

Sura ya 3: Uunganishaji na uwekaji programu 7

Hatua ya 1: Uunganishaji 7

Hatua ya 2: Pakua programu endeshi ya iTero Element Flex 8

Hatua ya 3: Mchakato wa Kuifanya Yangu 9

Sura ya 4: Maelekezo ya uendeshaji 10

Uwashaji na uanzaji wa kwanza 10

Kamera ya mtandaoni 10

Sura ya 5: Maelekezo ya utunzaji, usafishaji, na uondoaji vimelea kwenye skana 11

Utunzaji wa kifaa cha kuskani (kifimbo) 11

Utunzaji wa kebo ya kifaa cha kuskani 11

Namna bora zilizopendekezwa za kusafisha na kuua vimelea 11

Nyenzo za usafishaji na uondoaji vimelea kwa kifaa cha kuskani na kitako chake 12

Sura ya 6: Ubadilishaji mikono vazi kati ya mgonjwa mmoja na mwingine 13

Usafishaji na Uuaji vimelea kwenye kifaa cha kuskani (kifimbo) 13

Ubadilishaji mikono vazi 13

Mikono vazi ya skana 14

Sura ya 7: Miongozo ya mtandao wa LAN wa kliniki 15

Utangulizi 15

Maandalizi 16

Miongozo ya ruta 16

Firewall 16

Vidokezo vya Wi-Fi 17

Mapendekezo ya majina wenyeji ya Align 18

Kiambatisho A: Tamko la AMC 19

Kiambatisho B: Ufafanuzi wa vifaa 20

Page 10: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

2

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Sura ya 1:

UtanguliziKuhusu mwongozo huu wa uendeshajiMfumo wa iTero Element Flex hufikishwa kama kifaa cha mmiliki, cha kutumika katika ofisi ya daktari kinachotegemea kipakatalishi kwa ajili ya kuskani mdomoni. Mwongozo huu wa operesheni unaelezea jinsi ya kuwasha na kuzima mfumo, jinsi ya kushughulikia kitengo cha skanning / kifimbo na kebo, na jinsi ya kusafisha kifaa cha kuskani na kubadili mikono vazi yake kati ya wagonjwa.

Matumizi lengwaiTero Element Flex ni mfumo wa mwanga wa simu (CAD / CAM) unaotumiwa kurekodi picha za kiuchunguzi za meno na tishu za mdomoni. Mfumo unaweza kuunganishwa na vipakatalishi viliyoidhinishwa na Align Technology ili kupunguza matumizi ya nafasi ya ofisi na kuongeza urahisi uhamaji wa mfumo.

Data zinazoundwa kutokana na iTero zinaweza kutumika sambamba na uzalishaji wa vifaa vya kinywa (kama vile vilinganishi, vifungio, vyombo, n.k.) na vifaa.

Programu ya iTero Element Flex hutumika na skana ya iTero Element kudaka mwonekano wa 3D wa meno, tishu na miundo mdomoni, na uhusiano wa uumaji. Programu inasimamia uchakataji wa data, kuwezesha ushirikishaji wa data, na kusafirisha data kwa uundaji wa CAD / CAM wa marekebisho ya meno, vifaa vya Othodontiki, vitambaa, na vifaa. Mbali na kuskani data, habari mbalimbali za mgonjwa na mashauri zinaweza kuagizwa / kusafirishwa au kutumiwa kwa madhumuni ya uigaji. Uwezo mwingine unapatikana kwa ajili ya uthibitisho na matenegezo ya mfumo na hutumika kama kifaa cha kusimamia oda.

Faida za mfumo wa iTero Element FlexMfumo wa iTero Element Flex hutoa faida muhimu juu ya njia zilizopo za uzalishaji wa taji, ikiwa ni pamoja na kuskani bila poda, usahihi zaidi wa uzalishaji taji, na mrejesho wa haraka wakati wa mchakato wa kuskani.

Rejelea tovuti yetuhttp://www.itero.com kujifunza namna Huduma ya iTero inaweza kuwezesha biashara yako kwa kuongeza kuridhika kwa wateja wako, kuboresha matokeo ya kitabibu, na kuongeza ufanisi ofisini.

Maelekezo ya uwekaji programu endeshiTafadhali tazama orodha ya vipakatalishi na Vizuia Virusi vilivyoidhinishwa katikawww.iTero.com.

Ili kuhakikisha utendaji bora wa programu ya iTero, lazima vipakatalishi vilivyoidhinishwa pekee ndivyo vitumike na mfumo wa iTero Element Flex.

Page 11: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

3

Sehemu ya mtumiaji wa iTero Element FlexMfumo wa iTero Element Flex hutoa sehemu ya mtumiaji inayofaa kwa kufanya skani za kidijitali kwa matumizi ya Urejeshaji au ya ki-Othodontiki. Daktari anaongozwa kwenye mtitiriko wa kuskani kwa kutumia visaidizi vya kuonyesha na vya maandishi. Skrini ya mguso na vitufe vya kwenye kifimbo hutumika kuitikia maelekezo ya skrini wakati wa mchakato wa kuskani.

Bofya kuingia Kituo cha Mafunzo au kuanza mafunzo

Bofya popote kwenye kioo kufunga muhtasari huu wa msaada

(Bofya kuanza shauri jipya)(Bofya kuona/kutafuta orodha

ya wagonjwa)

Bofya kufunga tarakilishi

Bofya kupangilia mapendeleo yako Bofya mara mbili kuunganishwa na wakala wa msaada kwa ajili ya utambuzi wa tatizo kutokea mbali (tafadhali piga simu kituo cha msaada kwanza)

Bofya ili kuona arifa, usasishaji na ujumbe mwingine kutoka Align Technology

Bofya kutazama hali ya oda zako

Kiwango cha betri ya kipakatalishi

Kubofya mara moja kwenye alama ya kiulizo utawezesha maelezo ya Msaada kutokea ambayo yatakupa muhtasari wa maelezo. Tafadhali zingatia kuwa alama ya Kifaa cha kichwani inatokea badala ya alama ya kiulizo kwenye mwonekano huu. Bofya popote kufunga skrini ya msaada na kurejea kwenye skrini husika.

Page 12: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

4

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Sura ya 2:

Vipengele vya msingi vya vifaa Mwonekano wa mbele wa mfumo

Kipakatalishi chenye kioo mguso

Kitovu cha Flex

Kifimbo na kiunzitegemeo

Page 13: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

5

Kifaa cha kuskani (kifimbo)

Kigao mguso

Mikono vazi ya kutumika mara moja

Kebo inayotoka ya kifaa cha kuskania na kiunganishi cha USB

Vitufe vya pembeni: Skani, washa/zima, kuwezesha kigao mguso

Matundu ya hewa

Page 14: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

6

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Ufungaji wa mfumo wa kuhamishika (kwa usafirishaji)

UsafirishajiTumia kasha lilitolewa ili kuhamisha mfumo kutoka ofisi moja kwenda nyingine.

Kuhamisha mfumoIli kuhakikisha ulinzi wa hali ya juu wa mfumo, inashauriwa mfumo uhamishwe kwa uangalifu. Fuata maagizo haya ya kuhamisha mfumo:

1. Weka mkono vazi wa bluu wa kinga kwenye kifimbo.

2. Hakikisha kifaa cha kuskania (kifimbo) kimekaa vizuri kwenye kasha.

3. Ondoa kitovu cha Flex na kebo za kipakatalishi za umeme za AC kutoka ukutani vizuri.

4. Weka vitu vyote katika kasha (tazama picha hapo juu).

5. Hakikisha kasha linabaki kavu ili kulinda vipengele vya mfumo dhidi ya unyevu.

Page 15: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

7

Sura ya 3:

Uunganishaji na uwekaji programu endeshi Hatua ya 1: Uunganishaji Tafadhali fuata maelekezo hapa chini ili kuunda skana yako ya iTero Element Flex: Kifimbo

(kifaa cha kuskania)

3.Unganisha kebo ya USB kwenye kitovu

6.Weka kebo ya umeme kwenye chanzo cha umeme cha AC

7.Usanidi wa mwisho/upangiliaji wa mfumo wa iTero Element Flex

1.Weka kifimbo kwenye kiunzitegemeo

4.Unganisha kebo ya USB kwenye kipakatalishi

2.Unganisha kebo ya umeme ya kitovu kwenye kitovu

5.Unganisha kebo ya kifimbo kwenye kitovu

Kitovu na kebo ya umeme ya kitovu

Kiunzitegemeo

Kifimbo na kebo ya kifimbo

Kebo ya USB ya kuunganisha kipakatalishi na kitovu

A

B

C

DA

B

CD

Mkondogeu wa umeme

Sehemu ya USB

Maelezo mawili muhimu:

• Kitovu kinapaswa kuunganishwa kwenye kitoa umeme wa mkondogeu ukutani wakati wote

• Kipakatilishi kinapaswa kuunganishwa kwenye mkondogeu wa umeme ukutani kwa ajili ya kuskani ndani ya kinywa

Page 16: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

8

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Hatua ya 2: Pakua programu endeshi ya iTero Element Flex Kwa ufungaji sahihi wa programu endeshi na upangiliaji wa skana yako ya iTero Element Flex, tafadhali hakikisha kifimbo chako cha iTero kiko imara kwenye kiunzitegemeo na kimeunganishwa kwenye kitovu, na kitovu kimeunganishwa kwenye kipakatalishi. Tafadhali hakikisha kipakatalishi chako kimeunganishwa ukutani kwenye chanzo cha nishati ya AC wakati wote wa uwekaji programu endeshi.

1. Kupangilia kipakatalishi

A. Washa kipakatalishi chako.

B. Sasisha Windows kwenye toleo la hivi karibuni zaidi.

2. Upakuaji wa programu endeshi ya iTero

A. Fungua sanduku la barua pepe iliyosajiliwa kwenye kivinjari. Tafuta baruapepe ya "iTero yako imetumwa" inayojumuisha maelekezo.

B. Bofya kwenye kiungo ili ufikie kwenye ukurasa na vipakuzi vya programu. au

C. Vinginevyo, fungua kivinjari na uende katika (andika anwani kwenye kivinjari chako) download.itero.com.

3. Uwekaji wa programu endeshi ya iTero

A. Bofya kwenye kitufe cha "Anza".

B. Fungua faili la kuwekwa lililopakuliwa.

C. Fuata maelekezo kwenye skrini kukamilisha upakuaji wa programu endeshi ya iTero.

Inashauriwa mara kwa mara kuangalia sasisho za Windows na kuziweka. Tafadhali wezesha sasisho.

Pia inashauriwa kuondoka kwenye Windows na kuzima kompyuta mwisho wa kila siku ili kuruhusu sasisho kuingia.

Kabla ya kuweka programu ya iTero Element Flex kwa mara ya kwanza, tafadhali weka usanikishaji wote wa Windows unaopatikana. Kompyuta mpya za Windows zinapaswa kuomba sasisho moja kwa moja.

Kuangalia masasisho ya Windows, fungua "Mipangilio" (Ufunguo wa Windows + I), chagua "Usasishaji na Usalama", na kisha "Usasishaji wa Windows". Bofya "Angalia masasisho" ili uone kama kuna masasisho mapya.

Inashauriwa kufunga programu nyingine wakati wa kutumia mfumo wa iTero Element Flex wa kuskani.

Page 17: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

9

Hatua ya 3: Mchakato wa Kuifanya Yangu

1.Chagua lugha uipendayo na bofya kwenye kitufe cha Ifanye Yangu ili kuanzisha Mchakato.

2.Fuata maagizo ya Kielekezi kwenye skrini ili kukamilisha uwekaji wa iTero Element Flex.

Page 18: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

10

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Sura ya 4:

Maelekezo ya uendeshajiUdhibiti kadhaa wa usalama umewekwa kwenye skana ili kutoa sehemu nzuri na salama kwa mtumiaji; programu ya kuzia virusi vya kompyuta ni moja ya udhibiti huo. Hivyo, Align inapendekeza sana programu za kuzuia virusi zipakiwe kwenye kompyuta.

Njia nyingine ya udhibiti wa usalama ni nywila ya mtumiaji wa Kompyuta. Ili kukidhi mahitaji ya chini zaidi ya usalama, inapendekezwa kutumia nywila inayokidhi matakwa yafuatayo:

1. Urefu wa angalau herufi 10

2. Angalau herufi moja kubwa (A-Z)

3. Angalau herufi moja ndogo (a-z)

4. Angalau tarakimu moja (0-9)

5. Angalau alama maalumu moja (vituo vya uandishi) - tafadhali zingatia kuwa hata nafasi huchukuliwa kuwa alama maalumu pia

6. Isizidi herufi 128 na si zaidi ya herufi 2 zinazofanana kwa mfuatano (kama vile, 111 au CCC hairuhusiwi)

Hakikisha kompyuta imeunganishwa kwenye umeme wa mkondogeu ukutani, ili kuhakikisha kiwango cha betri hakifiki chini mno, ambapo kuskani hakutawezekana tena

Kuanza programu ya iTero:

1. Washa kompyuta

2. Ingia kwenye programu za kompyuta yako kwa kuingiza nywila yako (ikiwa inahitajika)

3. Bofya mara mbili alama ya iTero

Inashauriwa kuweka mfumo katika uendeshaji wakati wa masaa ya kazi kuruhusu uhamishaji wa faili ya chini kwa chini kati ya ofisi ya daktari, maabara shiriki za daktari, na kituo cha Align Technology. Inashauriwa kuzima mfumo mwishoni mwa siku, na kuwasha upya asubuhi.

Kamera ya mtandaoniUnganisha kamera ya mtandaoni kwenye kipakatalishi kwa kufuata maelekezo ya bidhaa.

Page 19: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

11

Sura ya 5:

Maelekezo ya utunzaji skana, usafishaji, na uondoaji vimeleaUtunzaji wa kifaa cha kuskani (kifimbo)

• Kifaa cha kuskani kina sehemu laini na kinapaswa kutunzwa kwa umakini.

Utunzaji wa kebo ya kifaa cha kuskani

• Kebo ya skana inapaswa kutunzwa kwa umakini ili kuepuka uwezekano wa uharibifu.

• Epuka kunyonga, kuweka vifundo, kuvuta au kukanyaga kebo, n.k

• Kati ya vipindi tofauti vya wagonjwa, inashauriwa kufungua mikunjo na vifundo ili kuondoa kukakamaa kwenye kebo ya skana.

Namna bora zinazopendekezwa za kusafisha na kuua vimelea kwenye kifaa cha kuskania kati ya wagonjwa.

Ili kuepuka maambukizi kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine, tafadhali chukua hatua zinazohitajika na njia za kulinda kompyuta

• Usipulize viua vimelea moja kwa moja kwenye nyuso za mfumo wa skana

• Pulizia viua vimelea kwenye taulo, au tumia vifutio vya kuua vimelea kwa ajili ya kifaa cha kuskania.

• Onyo: kuweka viua vimelea kwa kuzidi kwenye nyuso za mfumo wa skana kunaweza kusababisha uharibifu, ikiwemo wa vifaa vya ndani.

• Fuata maelekezo ya wazalishaji wa viua vimelea kwa wakati unaofaa wa kuwasiliana. Ondoa mabaki ya vioevu vya kuua vimelea kwa kutumia kitambaa safi kisicho na nyuzi.

• Kumbuka: kufuata tahadhari za kawaida za ulinzi binafsi, kadri inavyofaa.

• Onyo: USIGUSE uso nuru wa kifaa cha kuskani (kifimbo).

Page 20: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

12

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Nyenzo za usafishaji na uuaji vimelea kwa kifaa cha kuskani na kiunzitegemeoNyenzo zifuatazo zinapendekezwa kusafishia na kuua vimelea kwenye kifaa cha kuskani na kiunzitegemeo.

Maelezo pH Mtengenezaji P/N Mtengenezaji

Birex® Vifutio vya kuua vimelea vya Quat 7.6 BI 240 Biotrol Intl.

CaviCide AF 12.7 13-800 Metrex

CaviCide AFCaviWipe

12.513-100013-1100

Metrex

CaviCide AFCaviWipe 1

12.513-500013-5100

Metrex

Huduma ya Afya ya Clorox® kioevu cha kuulia vimelea cha haidroksaidi peroksaidi

2-3 30828, 30829 Clorox® Huduma ya Afya™

Huduma ya Afya ya Clorox® vifutio vya kuulia vimelea vya haidrojeni peroksaidi

2-3 30824, 30825 Clorox® Huduma ya Afya™

Opti-Cide 3® kioevu 7.6 DOCS12-024, DOCP04-128 Biotrol Intl.

Opti-Cide 3® vifutio 7.6 DOCW06-100 Biotrol Intl.

OPTIM 33TB kimiminika 2.5-3.5 OPT33-1GAL, OPT-33-1QT SciCan Inc.

vifutio vya OPTIM 33TB 2.5-3.5 OPT33-W10X10, OPT-33-W12 SciCan Inc.

ProSprayVifutio vya ProSpray

10PSC240PSW-1

Certol

Webcol® maandalizi ya alkoholivifutio

7 5110 Medtronic

Page 21: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

13

Sura ya 6:

Kubadilisha mikono vazi kati ya wagonjwaKusafisha na kuua vimelea vya kifaa cha kuskani (kifimbo)Kuepuka kuambukizana, ni muhimu kila baada ya mgonjwa mmoja unasafisha na kuua vimelea kwenye kifaa cha kuskani na mkono vazi wa kubadilishwa. Kwanza pulizia dawa ya kuua vimelea kwenye taulo au tumia vifutio vya kuua wadudu kusafisha skana na kiunzitegemeo cha skana. Kisha endelea na hatua zilizo chini ili kuondoa mkono vazi uliotumiwa na kuweka mkono vazi mpya.

ANGALIZO: Utupaji wa mikono vazi ya skana kulingana na taratibu zilizopo za utendaji au kulingana na taratibu za eneo husika za utupaji taka za kitabibu zenye vimelea.

Hatua ya 1Wakati wa KUTOA au KUWEKA mkono vazi, shikilia sehemu ya kati ya mkono vazi.

Hatua ya 2Bonyeza kidogo kwenye pande zote za mkono vazi wa kutumika mara moja, taratibu vuta mkono vazi kutoka kwenye kifaa cha kuskani na uitupe.

Hatua ya 3Taratibu sukuma mkono vazi mpya kwenye kifaa cha kuskani mpaka ukae sawa eneo lake.

ONYO: Uso nuru! USIGUSE uso nuru. Kugusa kunaweza kusababisha uharibifu Ikiwa kuna ulazima wa kusafisha, tumia vifutio maalumu na vitambaa visivyochubua vilivyomo kwenye kasha la mikono vazi ya skana. Kwa matumizi sahihi, rejea maelekezo yanayopatikana katika kasha la mikono vazi ya skana.

Ubadilishaji wa mikono vazi ya kutumika mara moja

Page 22: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

14

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Mikono vazi ya skanaKuna aina mbili za mikono vazi zinazotumiwa na kifaa cha skana (kifimbo):

Mikono vazi ya kutumika mara mojaMkono vazi mweupe ni wa kutumika mara moja tu katika kuskani mgonjwa. Daima badili mkono vazi mweupe kwenye kifaa cha skana kati ya mgonjwa mmoja na mwingine ili kuepuka maambukizi kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine Tafadhali tupa mkono vazi mweupe baada ya kila mgonjwa mmoja

Kisanduku cha mikono vazi ya skanaMikono vazi inaweza kuagizwa mtandaoni kutoka duka la iTero katika masanduku yenye idadi ya 25 www.store.itero.com, inapopatikana.

Mkono vazi wa kingaMkono vazi wa kinga wa bluu hutumika kulinda lenzi ya mwangaza wakati kifaa cha kuskani hakitumiki. Tafadhali weka mkono vazi wa bluu sehemu salama ili usipotee wala kuharibiwa.

Page 23: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

15

Sura ya 7:

Mtandao wa LAN wa klinikimiongozo ya mtandao UtanguliziSkana ya iTero Element inatumia muunganisho wa mtandao wa Wi-Fi ili kutuma na kurejesha skani kwenda na kutoka mtandao wa iTero.

Kama pendekezo, mara zote ni bora kuwa na teknolojia ya hali ya juu inayopatikana. Hapa ni baadhi ya miongozo ya kusaidia kupata muunganiko bora wa Wi-Fi:

Viwango vya Muunganiko wa Mtandao wa Wi-Fi

Bora >-50 dBm

Nzuri -50 hadi -60 dBm

Wastani -60 to -70 dBm

Dhaifu <-70 dBm

• MUHIMU: Ili kufikia utendaji bora wa skana yako ya iTero Element, hakikisha kuwa nguvu ya Wi-Fi yako ni "Bora" au angalau "Nzuri".

• TAHADHARI: Wakati unamskani mgonjwa, usiunganishe kebo ya mtandao wa LAN kwenye iTero Element - ni marufuku kwa sababu za hatari kwa usalama.

Page 24: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

16

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Maandalizi

• Modemu/Ruta inayohitajika inapaswa kupangiliwa na Usalama wa WPA2, ikiwemo nywila.

• Hakikisha mtaalamu wako wa Teknohama anakuwepo muda unaopanga kufanya usimikaji wa skana yako.

• Hakikisha sifa za SSID za Wi-Fi yako zinapatikana: Jina la Kuingilia na Nywila.

• Kiwango cha chini zaidi cha nguvu ya Wi-Fi kwa ajili ya mfumo kionyeshe angalau "mistari" miwili, kama ilivyoonyeshwa kwenye sura ya 2, juu).

• Kifaa cha utambuzi chini ya "Mipangilio", au Kifaa cha Muunganisho vinapendekezwa hapa chini.

• Jaribu muunganisho wako wa Wi-Fi kwa kompyuta yoyote, ukitumia kifaa cha muunganisho cha iTero (fanya jaribio karibu na kilipo kifaa cha kuskania kadri iwezekanavyo).

• Pakua Kifaa cha Muunganisho katika fc1.orthocad.com\download\AlignSupport\ConnectivityCheck2.0.exe

• Yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo kwa mtaalamu wa Teknohama wa ofisi, kuhusu kipi cha kuzingatiwa ili kuepuka matatizo kama vile yahusuyo ufikiaji au muunganisho kwenye/na skana ya iTero:

1. Mapendekezo ya jina mwenyeji kuhusiana na huduma za Align za milango ya kusikilizia ya 80 na 443.

2. Usizuie mawasiliano ya FTP kwani skana inatuma aina maalumu za mafaili (.3ds na.3dc/.3dm).

3. Lemaza wakala yoyote kwenye mawasiliano ya data kupitia TCP/IP.

4. Usiongeze skana kwenye kundi lolote la kikoa.

5. Usitumie sera yoyote ya kikundi kwenye skana kwani inaweza kuharibu utendaji wake sahihi.

Miongozo ya rutaViwango vya chini: 802.11N / 802.11AC

Miongozo ya uunganishwaji mtandaoIli kufikia utendaji bora wa skana yako ya iTero Element, hakikisha kwamba kasi yako ya kupakia intaneti ni angalau 1Mbps kwa kila skana. Pia, zingatia kwamba vifaa vingine vya ziada vinavyounganishwa kwenye mtandao sambamba na skana vinaweza kuathiri utendaji wa skana.

FirewallMilango Wazi (ikiwa Firewall inafanya kazi):

a. 80 - HTTP - TCPb. 443 - HTTPS - TCP

Page 25: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

17

Vidokezo vya Wi-FiRuta za Wi-Fi zinakuwezesha kufikia mfumo wako wa mtandao kwa kutumia muunganisho wa Wi-Fi kutoka sehemu yoyote ndani ya eneo la uwezo wa mtandao wako wa bila waya. Hata hivyo, idadi, kina, na sehemu zilipo kuta, dari au vitenganishi vya ziada ambavyo mtandao wa bila waya utapaswa kusafiri kuvipita vinaweza kuzuia umbali na nguvu ya mtandao. Nguvu ya kawaida ya mtandao inatofautiana kutegemea na aina za nyenzo na kelele za chini za mawimbi ya redio kwenye nyumba au ofisi yako.

1. Hakikisha una idadi ndogo kabisa ya kuta na dari kati ya ruta na vifaa vingine vya mtandao. Kila kizuizi kinaweza kupunguza uwezo wa kufikia wa adapta yako kwa kati ya mita 1-3 (futi 3-9).

2. Hakikisha kuna mstari mnyoofu, usio na vitenganishi vyovyote baina ya vifaa vya mtandao. Hata ukuta unaoonekana kuwa mwembamba unaweza kuzuia nguvu ya mtandao kwa mita 1 (futi 3) ikiwa pembe ya ukuta imehamishwa hata kwa nyuzi mbili tu. Ili kupata mapokezi bora zaidi, weka vifaa vyote ili kwamba mawimbi ya Wi-Fi yanasafiri kwa unyoofu kupitia (900) ukuta au kitenganishi (badala ya kuwa kwenye pembe)

3. Nyenzo zilizotumika kujengea huleta utofauti Mlango mgumu wa chuma, au misumari, inaweza kuwa mizito sana kiasi cha kuwa na madhara kwa uwezo wa mawimbi ya Wi-Fi. Jaribu kuweka pointi za ufikiaji, ruta za mtandao wa bila waya, na kompyuta kwa namna inayoruhusu mawimbi kusafiri kupitia kuta kavu au njia wazi za milango. Nyenzo na vitu kama vile glasi, chuma, metali, kuta zenye kuhami joto, matenki ya maji (tangisamaki), vioo, makabati, matofali, na zege vinaweza kupunguza nguvu ya mawimbi ya mtandao wako wa bila waya.

4. Weka bidhaa yako ya iTero mbali (angalau futi 3-6 au mita 1-2) kutoka kwenye vifaa au vitu vinavyotoa kelele za mawimbi ya redio.

5. Ikiwa unatumia vifaa vya masikioni visivyotumia nyaya vya 2.4GHz au X-10 (vifaa visivyotumia nyaya kama vile feni za paa, taa za kuendeshwa mbali, mifumo ya usalama wa nyumbani), muunganisho wako wa bila waya unaweza kushuka sana au kukatika kabisa. Msingi wa vifaa vingi vya bila nyaya hutoa mawimbi ya redio, hata kama kifaa hakitumiki Weka vifaa vyako vingine vya bila nyaya mbali kadri iwezekanavyo kutoka kwenye skana na ruta yako.

6. Kwenye eneo lako, kunaweza kuwa na zaidi ya mtandao mmoja wa bila waya ulio hewani. Kila mtandao unatumia chaneli moja au zaidi. Ikiwa chaneli iko karibu na chaneli ya mfumo wako, mawasiliano yanaweza kuharibika kwa hali endelevu. Waambie idara yako ya teknohama kutazama hili, na ikibidi, badilisha namba ya chaneli inayotumiwa na mtandao wako.

Page 26: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

18

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Mapendekezo ya jina la mwenyeji wa AlignAlign daima inaboresha bidhaa na huduma zake. Hivyo, yaweza kujizatiti kwenye jina mwenyeji, lakini siyo katika IP fulani.

Orodha ifuatayo ya majina wenyeji iliundwa ili kuzipa skana za Align uwezo wa kutenda vizuri, ili kuweza kutumia uwezo wote wa hali ya juu wa utendaji wa skana.

Mapendekezo ya majina ya wenyeji wa Align:

Jina la mwenyeji Kiungio

Mycadent.com 80, 443

Myaligntech.com 80, 443

Export.mycadent.com 80, 443

Cboserver.mycadent.com 80, 443

Matstore.invisalign.com 80, 443

Matstore2.invisalign.com 80, 443

Matstore3.invisalign.com 80, 443

Matstore4.invisalign.com 80, 443

Matstoresg.invisalign.com 80, 443

Matstorechn.invisalign.com.cn 80, 443

Masafa ya IP ya AWS - Huduma za kimataifa za CDN za Amazon - Masafa ya anuani ya IP hubadilika kutegemea eneo ilipo skana.

80, 443

cloud.myitero.com 443

speedtest.tele2.net 80

alignapi.aligntech.com 80, 443

http://www.google.com 80, 443

http://www.microsoft.com 80, 443

http://www.yahoo.com 80, 443

iterosec.aligntech.com 80, 443

storage.cloud.aligntech.com 443

Page 27: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

19

Kiambatisho A:

Tamko la EMC Muhtasari wa matokeo ya majaribio ya EMC kwa iTero Element Flex

Jaribio Kiwango Ngazi / Kiwango cha ukali Matokeo

Nyaraka (IEC 60601-1-2 sehemu 4 na 5)

Matakwa ya jumla ya EMC kifungu cha 4.1 --Inatimiza matakwa

Lebo za nje kifungu cha 5.1 --Inatimiza matakwa

Uendanaji na mwongozo wa watumiaji kifungu cha 5.1 --Inatimiza matakwa

Usahihi wa maelezo ya kiufundi kifungu cha 5.2.2 --Inatimiza matakwa

Utoaji (IEC 60601-1-2 kifungu cha 7)

Utoaji uliofanyika Umbali wa masafa:150 kHz - 30 MHz

CISPR 11Kundi la 1 Daraja B230, 120 & 100 VAC mains @ 50 Hz;220 VAC mains @ 60 Hz

Inatimiza matakwa

Mnururisho unaotolewa Umbali wa masafa: 30 - 1000 MHz

CISPR 11 Kundi la 1 Daraja BInatimiza matakwa

Jaribio linganifu la utoaji mkondo wa umeme IEC 61000-3-2230 VAC mains @ 50 Hz & 220 V @ 60 Hz

Inatimiza matakwa

Mabadiliko ya volteji, mfumuko wa volteji na jaribio la mtetemeko IEC 61000-3-3230 VAC mains @ 50 Hz & 220 V @ 60 Hz

Inatimiza matakwa

Kinga (IEC 60601-1-2 kifungu cha 8)

Kinga kutokana na utokaji wa umeme (ESD) IEC 61000-4-28 kV utokaji kwa mguso & 15 kV utokaji kwa hewa

Inatimiza matakwa

Kinga dhidi ya sehemu za mnururisho wa umeme IEC 61000-4-310.0 V/m; 80 MHz ¸ 2.7 GHz, 80% AM, 1 kHz

Inatimiza matakwa

Kinga dhidi ya ukaribu wa kifaa cha mawasiliano cha mkononi IEC 61000-4-3Orodha ya masafa, kutoka 9 V / m hadi 28 V / m,PM (18 Hz au 217 Hz), FM 1 kHz

Inatimiza matakwa

Kinga kutokana na umeme upitao muda mfupi (EFT) IEC 61000-4-4± 2.0 kV - kwenye AC kuu;Tr/Th – 5/50 ns, 100 kHz

Inatimiza matakwa

Kinga kutokana na kuongezeka ghafla IEC 61000-4-5

±2.0 CM / ±1.0 kV DM kwenye 230 VAC kuu @ 50 Hz & 220 VAC kuu @ 60 Hz; Tr/Th – 1.2/50 (8/20) ms

Inatimiza matakwa

Kinga dhidi ya misukosuko itokanayo na mawimbi-ya redio IEC 61000-4-63.0, 6.0 VRMS kwenye 230 VAC mains & kebo ya kifimbo;0.15 ÷ 80 MHz, 80% AM @ 1 kHz

Inatimiza matakwa

Kinga dhidi ya kushuka kwa volteji, uingiliaji mfupi na utofauti wa volteji

IEC 61000-4-11

Kwenye 230 VAC & 100 VAC mains @ 50 Hz:Mzunguko wa 0% - 0.5 & mzunguko 1; Mizunguko wa 70% - 25; Mizunguko ya 0% - 250 Kwenye 220 VAC mains @ 60 HzMzunguko wa 0% - 0.5 & mzunguko 1; Mizunguko ya 70% - 30; Mizunguko ya% - 300

Inatimiza matakwa

Page 28: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

20

Mwongozo wa matumizi ya iTero Element Flex Kiswahili

Kipengele Maelezo

Kioo cha kutazamia Kioo cha kompyuta mpakato

SkanaSkana hutoa mwanga mwekundu wa leza (680nm Daraja la 1) pamoja na utoaji wa LED nyeupe.

Nguvu ya uendeshaji 100-240VAC- 50/60 Hz – 40VA (ukomo wa juu)

Joto lifaalo kwa uendeshaji 18°hadi 26°C / 64.4° hadi 78.8 ° F

Joto la Uhifadhi/Usafirishaji -5° hadi 50°C 23° hadi 122°F

Shinikizo & mwinuko ufaao kufanyia kaziShinikizo: 520 mmHg hadi 760 mmHg (~69 kPa hadi ~101 kPa)Mwinuko: futi 0 mpaka futi 10,000

Shinikizo & mwinuko wa Uhifadhi/Usafirishaji

Shinikizo: 430 mmHg hadi 760 mmHg (~57 kPa hadi ~101 kPa)Mwinuko: futi 0 mpaka futi 15,000

Unyevu wa kadri Uendeshaji: 40% hadi 70%; Uhifadhi: 30% hadi 90%

Vipimo

Kitovu cha iTero Element Flex:Urefu: 206 mm (~8 in)Upana: 94 mm (~3.7 in)Kina: 36.5 mm (~1.4 in)

Kifimbo cha iTero Element:Urefu: 338.5 mm (~13 in)Upana: 53.5 mm (~2 in)Kina: 69.8 mm (~3 in)

Kiunzitegemeo:Urefu: 262 mm (~10 in)Upana: 89 mm (~3.5 in)Kina: 52mm (~ 2 in)

Shauri:Urefu: 326.5 mm (~13 in)Upana: 455 mm (~18 in)Kina: 184 mm (~7 in)

Uzito halisikitovu cha iTero Element Flex: ~0.5 kg (~1 lbs)Kifimbo cha iTero Element: kg 0.47 (~1 lbs)Kasha tupu: ~2 kg (~4.5 lbs)

Uzito wa usafirishaji ~8 kg (~17.6 lbs)

Kiambatisho B:

Muainisho wa vifaa

Page 29: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea
Page 30: Uendeshaji manual - storagy-itero-production-us.s3 ...storagy-itero-production-us.s3.amazonaws.com/download/iTero-Element... · Jumuia ya Ulaya. Inaonyesha haja ya mtumiaji kurejea

Align, Invisalign, iTero, na iTero Element kati ya nyingine, ni alama za biashara na/au alama za huduma za Align Technology, Inc au moja ya matawi yake au makampuni husika na zinaweza kusajiliwa Marekani na/au nchi nyingine.

© 2019 Align Technology, Inc. Haki Zote Zimehifadhiwa. 205490 Rev B

Align Technology, Inc.2820 Orchard ParkwaySan Jose, CA 95134Marekani

Align Technology B.V. Arlandaweg 1611043HS AmsterdamUholanzi

Uendeshaji manual